Policy Brief: National Arts Policy_In Kiswahili

Page 1

MHUTASARI WA SERA MAPENDEKEZO YA MASWALA MUHIMU JUU YA SERA YA SANAA YA TAIFA 2016


Ufupisho Mhutasari huu wa Sera ni matokeo ya utafiti uliokusanya maoni ya wasanii kuhusu Sera ya Sanaa Ya Taifa ambayo inatayarishwa hivi sasa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM). Zoezi hili limewezeshwa kwa ufadhili wa Hivos East Africa. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM) imelikaribisha Baraza la Sanaa la Taifa/BASATA kama taasisi yenye mamlaka ya kukuza maendeleo ya sanaa, kutoa uchambuzi halisi utakaopendekeza umuhimu ya kuwa na Sera ya Sanaa. Kutokana na uchache wa muda na ufinyu wa bajeti BASATA ilitumia ujuzi uliotokana na uzoefu na kutoa mapendekezo yake kwenye Sera ya Sanaa. Hata hivyo kwa taasisi yenye mamlaka ya kuinua maendeleo ya Sanaa Tanzania, mchakato wa kisayansi uliyo jumuisha wasanii kama wadau wakuu ungehakiki hatua ikiwa mamlaka shirikishi katika utayarishaji wa Sera ya Sanaa. BASATA NA CDEA walikubaliana kufanya utafiti kwa pamoja ili kuanzisha na kuwawezesha wasanii kutoa maoni yao juu ya nini watakayopenda yajumuishwe kwenye Sera mpya ya Sanaa. BASATA NA CDEA walikubaliana kufanya utafiti kwa pamoja ili kuanzisha na kuwawezesha wasanii kutoa maoni yao juu ya nini watakayopenda yajumuishwe kwenye Sera mpya ya Sanaa. Wahusika wa kwanza wa mhutasari huu wa Sera ni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM) na BASATA. Hata hivyo Mhutasari huu utasambazwa kwa wadau wengine muhimu wakiwemo: • Wizara ya Fedha na Mipango • Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa • Wizara ya Elimu, Mafunzo ya Ufundi • Tume ya Taifa ya Takwimu • Wizara ya Maliasili na Utalii • Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za m itaa • Mamlaka ya Mawasiliano na Udhibiti Tanzania • UNESCO Tanzania • Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) • Wasomi • Mashirika ya Sanaa, Utamaduni na Ubunifu Mhutasari huu wa Sera unapendekeza mjumuisho wa Sera katika maeneo yafwatayo: • Kusaidia mifumo endelevu ya uongozi katika maendeleo ya Sanaa • Kufikia uwiano kwenye upatikanaji wa bidhaa na huduma na kuongezeka kwa Wasanii na Wataalamu wa utamaduni • Kujumuisha Sanaa kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa • Kukuza haki za binadamu na uhuru wa msingi 2. Taarifa ya Swala / Tatizo: Kwa sasa, Jamuuri ya Muungano wa Tanzania una Sera mbili za Utamaduni; Sera ya Utamaduni ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (1997) ambayo 1


inafahamika kama Sera ya Utamaduni ya ‘Taifa’. Utamaduni haujumuishwi katika maswala ya muungano na hivyo Zanzibar ina sera yake iitwayo Sera ya Utamaduni ya Zanzibar (2005). Kwa ujumla inakubalika kwamba maandishi ya Sera ya Utamaduni ya 1997 hayatoshelezi. Hili ni kwasababu mabadiliko mengi yamejitokeza yangu 1997. Kwa mfano, mwaka 2005 kulikuwa na hatua kubwa na mawazo mapana juu ya mifumo ya utamaduni na ubunifu wenye uwezo wa kuleta matokeo ya kimaendeleo barani Afrika. Pamoja na hayo, Tanzania iliridhia mikataba ya UNESCO ya mwaka 2003 na 2005 mnamo Oktoba 18, 2011 iliyoanza kazi rasmi Januari 18, 2012. Hususan, mkataba wa mwaka 2005 wa sheria za kimataifa ni mkataba unao hakikisha kuwa msanii, wataalamu wa tamaduni, washiriki na wanachi wote dunia nzima wanaweza kuunda, kutengeneza, kusambaza na kufurahia bidhaa, huduma na kazi mbali mbali zikiwemo zao wenyewe. Ni chombo pekee kinachorejea kwenye thamani ya bidhaa, huduma na kazi za kiutamaduni kibiashara. Hii haijaonyeshwa kwenye Sera ya sasa ya Utamaduni yamwaka 1997. Maendeleo ndani ya Serekali ya Jamuhuri ya Muungano waTanzania kwa sasa chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli ni kuanzishwa kwaWizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM). Hivyo kuna maslahi kuwa na Sera ya Sanaa ya Taifa ili kutoa mwongozo wa maendeleo ya Sanaa Tanzania. 3. Chanzo (cha tatizo) Kwa sasa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM) ipo kwenye mchakato wa kukusanya mawazo toka Wizara na taasisi nyingine ya maswala ya kujumuishwa kwenye rasimu ya Sera inayotayarishwa na wizara hiyo. Nakala imewekwa kwenye tovuti ya Wizara ili kurahisisha upatikanaji wa mrejesho kutoka kwa wadau mbali mbali wenye nia ya kufwatilia mchakato wa utungwaji wa Sera. • Sera ya Filamu ya Taifa • Sera ya Lugha ya Taifa • Sera ya Sanaa ya Taifa Kutokana na chanzo hiki, WHUSM imeliomba Baraza la Sanaa la Tanzania / BASATA kuwakilisha uchambuzi hali ambayo unatoa uhalali wa kuwa na Sera ya Sanaa ya Taifa. Kufwatia uchachewa muda na ufinyu wa bajeti, BASATA ilitumia ujuzi uliotokana na uzoefu na kutoa mapendekezo yake kwenye ya Sera ya Sanaa ya Taifa. Hata hivyo kwa taasisi yenye mamlaka ya kuinua maendeleo ya Sanaa Tanzania, mchakato wa kisayansi uliyo jumuisha wasanii kama wadau wakuu ungehakiki hatua ikiwa mamlaka shirikishi katika utayarishaji wa Sera ya Sanaa. Kufwatia ufadhili wa Hivos East Africa, CDEA iliweza kuungana na BASATA kufanya utafiti kwa pamoja ili kupata maoni ya wasanii juu ya nini wangependa kijumuishwe kwenye Sera mpya ya Sanaa. Madhumuni ya Utafiti: Kuisaidia BASATA kuwezesha ushirikishi wenye mamlaka wa wasanii kuchangia maoni yao kwa ajili ya Sera mpya ya Sanaa Tanzania mpaka Disemba 2016.

2


Matukio kujumuisha: 1. Kuandaa mbinu za utafiti 2. Kuwafundisha wakusanya taarifa 3. Utafiti wa kina kwa wasanii 4. Majadiliano ya Makundi maalumu 5. Uchambuzi wa taarifa 6. Uandishi wa ripoti na uhifadhi ya maswala muhimu kwenye video 7. Mikutano ya kifungua kinywa na wadau muhimu ( Walengwa: BASATA na Wizara) 8. Kuchapisha Mhutasari wa Sera 9. Kusambaza ujumbe waushawishi kupitia wasanii na mitandao ya kijamii. Matokeo ya Awali • BASATA kuhusisha ushiriki wenye mamlaka kwa wasanii kuchangia maoni yao kwa ajili ya Sera mpya ya Sanaa. Matokeo ya kati • Kwa sasa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM)imeviwekea vipaombele maoni ya BASATA na ya wasanii katika rasimu ya Sera ya Sanaa itakayo wakilishwa katika Baraza la Mawaziri na Bungeni Athari • Sera ya Sanaa inayozingatia mwenendo wa dunia na wa kikanda kwenye Sanaa na Utamaduni wenye kutoa miongozo ya maendeleo ya kisanii Tanzania. 4. Kauli ya Maslahi ya Asasi Kwenye Swala Hili: Culture and Development East Africa (CDEA)ni shirika la mitazamo ya kibunifu lililopo Dar es Salaam, Tanzania linalojishughulisha na kutoa huduma kwa wadau mbali mbaliwa Sanaa na utamaduni katikasekta ya maendeleo nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki. Kupitia programu ya Utamaduni na Utawala, tunaadhimia kushawishi kuwepo kwa mazingira wezeshaji kwa ajili ya sekta ya Utamaduni kupitia tafiti zinaozingatia viashiria na ushawishi Afrika Mashariki. Tunaamini ufanisi waSera unaweza kusababisha mazingira wezeshaji kwa ajli ya maendeleo ya Sanaa na kukua kwa uchumi wa kibunifu Afrka Mashariki. Tunatumaini kwamba maswala katika mhutasari huu wa Sera yatazingatiwa wakati wa maandalizi ya rasimu ya Sera ya Taifa ya Sanaa. 5. Sera Nyingine: 5.1Mapendekezo ya Sera Matokeo ya utafiti yamewekwa kwenye malengo manne, ambayo yanaendana na mkataba wa UNESCO wa 2005 ulioridhiwa na Tanzania mnamo tarehe 18/10/2011. 3


Jedali 1: Mapendekezo ya Sera Nyingine na Sera na Mchango wa Watunga Sheria Malengo muhimu ya kisera kujumuishwa kwenye Sera ya Sanaa ya Taifa

Mapendekezo ya Sera na mchango wa watunga sheria

• Kusaidia mifumo endelevu ya uongozi katika maendeleo ya Sanaa

Serekali iruhusu mazingira endelevu ya kidijitali yenye kuruhusu ubunifu Serekali kushirikiana na taasisi za kijamii kusaidia kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu Mkataba wa UNESCO wa 2005 ambao ni wa manufaa kwa wasanii Serekali kuweka mazingira bora ya uwekezaji kwenye maendeleo ya Sanaa Serekali kuinua na kutoa msaada kwa vituo vya mafunzo na huduma nyingine kwenye maeneo ya ubunifu kwa maendeleo ya sanaa Serekali kuinua na kutoa elimu ya Sanaa yenye kiwango, uhusiano kati ya utafiti na idara za Sanaa na Ubunifu

• Kufikia uwiano kwenye upatikanaji wa bidhaa na huduma na Kuongezeka kwa Wasanii na Wataalamu wa maswala ya utamaduni

Serekali kusaidia kuongezeka kwa Wasanii na Wataalamu wa maswala ya utamaduni Afrika Mashariki na kimataifa Serekali kusaidia upatikanaji wa bidhaa na huduma za kisanii ndani ya EAC, ACP na EU Serekali isaini mikataba na makubaliano ambayo yataendeleza na kulinda kazi za utamaduni na wasanii Serekali kusaidia kuongeza uwezo wa kukutanisha makampuni na wataalamu ndani ya sekta ya ubunifu

• Kujumuisha Sanaa kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa

Serekali kurejea Mpango mpya wa Maendeleo ya Taifa kipengele cha ubunifu na kutafakari tafsiri halisi na mchango wake katika maendeleo ya jamii na uchumi Serekali kutoa mkataba wa utafiti unaoendelea pamoja na WIPO ili kuangalia kwa ukaribu mchango wa Sanaa kwenye pato la taifa. MICAS, Tume ya Taifa ya Takwimu na Taasisi ya Takwimu ya UNESCO (UIS) zishirikiane katika kuandaa takwimu za kila mwaka za kwenye maswala ya utamaduni 4


• Kukuza haki za binadamu na uhuru wa msingi

Serekali itoe hatua za kisera zitakazo endeleza haki za kijamii na kiuchumi za msanii. Serekali kutoa miongozo ambayo itawawezesha wanawake wabunifu na wazalishaji wa bidhaa na huduma za utamaduni. Serekali kutoa miongozo itakayoendeleza fursa kwa wanawake kushiriki katika maswala ya utamaduni, kupata bidhaa na huduma.

5.2 Walengwa wa Awali CDEA wanatarajia kuipatia muhtasari huu wa Sera Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM) pamoja na BASATA. Wanatarajia mapendekezo ya Mhutasari huu waSera utachochea yafwatayo: (i) Kuwatambua wadau muhimu watakao wezesha utekelezaji wa Sera ya Sanaa ya Taifa (ii) Kuunganisha Sera ya Sanaa ya Taifa na ile ya Mpango wa Maendeleo na Utekelezaji wa Mikakati 5.3 Kundi la pili la Walengwa Wadau

Hatua za Kuchukuliwa

Wizara ya Fedha na Mipango

Kupitia upya kipengele cha ‘idara ya ubunifu’ kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa

Kutia sahihi makubaliano na mikataba ya kukuza na kulinda kazi za Sanaa

Wizara ya Elimu, Mafunzo ya Ufundi

Kuchunguza uborawa maswala ya Sera kwenye kiwango cha elimu ya Sanaa kuanzia shule za msingi mpaka taasisi za mafunzo ya juu na ufundi. Kuanzisha mafunzo ya sanaa ya muziki katika ngazi ya shule ya msingi

Tume ya Taifa ya Takwimu, Tanzania

Kukusanya mara kwa mara takwimu za utamaduni kwa kushirikiana na MICAS, Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi ya Utafiti ya UNESCO

Wizara ya Maliasili na Utalii

Kukuza maisha endelevu kupitia sanaa za Ufundi

Wizara ya Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa, Vyama vya Huduma na Utawala Bora

Kuhakikisha Kuanzishwa kwa sera ya Utamaduni kwa ngazi ya mitaa. 5


Mamlaka ya Mawasiliano na Udhibiti Tanzania(TCRA)

Kujenga mazingira endelevu ya kidijitali kuwapa wasanii nafasi kutumia tovuti, kushiriki katika ubunifu wa kidijitali kuunda na kupata soko

UNESCO Tanzania

Kutoa huduma za kiushauri katika maendeleo ya sera kwenye maeneo ya utamaduni na ubunifu.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)

Kujenga mazingira endelevu kwa wasanii kufurahia haki zao kwenye hifadhi za jamii kama ilivyopendekezwa na UNESCO kuhusuhadhi ya wasanii

Sekta Binafsi

Kuwekeza kwenye Idara za Utamaduni na ubunifu na maendeleo katika miundombinu ya sanaa

Wasomi

Kuchangia kwenye tafiti zinazozingatia viashiria na ushawishi kwenye sekta ya Utamaduni.

Mashirika ya Sanaa, Utamaduni na Ubunifu

Walengwa wa Sera ya Taifa ya Sanaa

6.0. Masuala Yaliyojitokeza Kipindi cha Majadiliano Yaliyotokea Kwenye Mkutano wa Kifungua Kinywa 1. Hakuna haja ya serikali kuwa na Sera ya Taifa ya filamu na Sera ya Taifa ya sanaa. Sera filamu lazima iwe kipengele kwenye Sera ya Taifa ya sanaa ambayo ndiyo sera kuu 2. BASATA inapaswa kutumia ya Mashirikisho ya sanaa ili kuweza kupata maoni zaidi kutoka kwa wasanii. 3. BASATA inapaswa kufanya uchunguzi ili kutambua kazi za kisanii zilizopo ili ziweze kujumuishwa katika sera. 4. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (WHUSM) inalazimika kuitisha mkutano wa kukusanya maoni kutoka kwa wasanii na si kutegemea tu maoni kwa njia ya barua pepe. 5. Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA aliwaonesha na kuwapatia washiriki chapisho juu ya sera Utamaduni barani Afrika lililoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Halmashauri za sanaa na Mashirika ya Utamaduni (IFACCA) ambazo zilionyesha jinsi nchi nyingine za Afrika ilivyotaja sera zao. Aliweza pia kuwapatia wawakilishi wa wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na BASATA muongozo kutoka UNESCO Sekretarieti ya 2005 ambao unaweza kuongoza Wizara ya jinsi ya kuandaa rasimu ya sera. Pia alisema kuwa Arterial Network ina chombo ambacho inaweza kusaidia kutoa huduma juu ya jinsi ya kuunda sera mpya sanaa 6.1. Mapendekezo Yaliyotolewa Wakati wa Majadiliano ya Yakutano wa Kifungua Kinywa • Jina la sera linapaswa kurekebishwa ili liweze kubeba kiini cha sanaa na nafasi yake ndani ya utamaduni • Kuna Hajaua kuwa na matamasha ya sanaa ya umma ili umma uweze kuipenda, kuitnamini na kufaihamu sanaa • Sera inapaswa kuongeza idadi ya wataalam katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (MICAS) na BASATA walio na historia kwenye fani ya saaa, ili waweze kufahamu na kukabiliana na changamoto za sekta 6


• Maendeleo ya Miundombinu ni muhimu katika sera kwa kuwaa hakuna maeneo ya umma na vifaa/nyenzo vya kuwawezesha wasanii na umma katika utoaji na upatikanaji wa sanaa • Pia Kuna haja ya kuendeleza sera ya utamaduni katika ngazi za mitaa na wilaya ambayo itawekwa sambamba na sera ya taifa ya sanaa • Sera ya sanaa iwanapaswa kuzingatia mwenendo wa kikanda na kimataifa kuhusiana na biashara ya bidhaa na huduma za kisanaa kuwa na haki miliki kama kipengele muhimu katika kibiashara ya sanaa 7. Vyanzo Vilivyochangia au Kupendekezwa: 1. Matokeo ya Utafiti,CDEA 2. Mpango mpya wa maendeleo 2016/17 – 2020/21, Serekali ya Tanzania 3. Mkataba wa UNESCO 2005 4. UNESCO, Kujenga Upya Sera za Utamaduni: Miaka Kumi ya Kuchangia Utofauti, Kauli za Maendeleo 5. Majadiliano wakati wa Mkutano wa Kifungua Kinywa baina ya CDEA, BASATA ,Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Wasanii

7


Kwa Tarfa zaidi kuhusu Mawasiliano ya BASATA: Bwana Godfrey L. Mngereza Gogereza Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa S.L.P Box. 4779 Dar Es Salaam Tanzania. Simu: +255 22 863784, Mobile: +255 713 644439 Fax: +255 22 86486 Barua Pepe: mngereza@yahoo.co.uk

Kwa Taarifa zaidi kuhusu Mawasiliano ya CDEA: Ayeta Anne Wangusa Mkurugenzi Mtendaji CDEA-Culture and Development East Africa, Kitalu No. 421, Nyumba No.1001, Mikocheni B, S.L.P 13355,Dar es Salaam, Tanzania. Simu.+255 22 2780087; Mob. +255 784856866 Barua Pepe. Ayeta.Wangusa@cdea.or.tz Ayeta_Wangusa@yahoo.com Cdea.Tanzania@yahoo.com


Utafiti Huu Umewezeshwa


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.