Lakini kwa nini? na MC Chisholm

Page 1

MAZUNGUMZO KWA

WALE WANAOSITASITA KUPATA CHANJO... ... na wale wanaowapenda

MAZUNGUMZO KWA WALE WANAOSITASITA KUPATA CHANJO...

... na wale wanaowapenda

“Katika janga hili lote lengo letu limekuwa

kuwatumia wasanii ili kutusaidia kuelewa nyakati

hizi za sisizo za kawaida. Kwa hivyo, wakati Dr. Peter Centre ilipotufikia kuhusu kufanya kazi

katika mradi kuhusu watu wanaositasita kupata

chanjo, ilitubidi kusema ndiyo — kwa sababu

tunaona kwamba suala la chanjo linagawanya

marafiki, familia na jamii. Kama wasanii tunataka

kufanya sehemu yetu kuleta watu pamoja, na kupigana na kile tunachoona kama athari mbaya

zaidi ya janga hili — mafarakano na migawanyiko

inayoibuka katika sehemu nyingi za jamii.

Pamoja na Majadiliano ya Wanasitasita Kupata

Chanjo na Wale Wanaowapenda, tuliagiza waandishi

wanne wa tamthilia ambao mambo waliyokuwa

wamepitia maishani yangeweza kutoa maarifa na uelewaji kuhusu baadhi ya hali ngumu zaidi ambazo

sote tunakabili. Tunafikiria haya kama mazungumzo ya kuigiza yanayojumuisha hali ngumu ambazo

wengi wetu tunajikuta ndani yake. Iwe ni mjadala

unaofanya pamoja nawe mwenyewe, au mtu fulani

katika mduara wako, tunatumai michezo hii mifupi

itakusaidia kuabiri suala hili kwa fadhili na huruma.”

Boca del Lupo Boca del Lupo

1

KUHUSU BOCA DEL LUPO

Dhamira ya Boca del Lupo ni kutayarisha maonyesho yasiyo ya kawaida katika nafasi zisizo za kawaida. Kampuni imejitolea kwa ufikivu na inafanya kazi kupanua ushiriki, mtazamo na umuhimu wa utendaji wa kisasa ndani ya wingi wa tamaduni za Kanada. Ikiongozwa na Artistic

Director Sherry J. Yoon na Artistic Producer

Jay Dodge, Boca del Lupo imetengeneza zaidi ya kazi 60 mpya tangu kuanzishwa kwake mwaka wa

1996. Michezo ambayo kampuni hiyo imetayarisha

imeonyeshwa kitaifa na kimataifa na kampuni inaandaa programu mahiri ya ukuzaji wa wasanii inayojulikana kama SLaM. Wakati wa usimamizi wa hao wawili, kampuni imepokea tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na Jessies for Outstanding Design, Outstanding Production, Significant Artistic Achievement na Outstanding Performance; Critic’s Choice Award for Innovation; Alcan Performing Arts Award and The Patrick O’Neill Award, ambayo

ilishinda kwa Plays2Perform@Home, mradi wa ukumbi wa maonyesho wa nyumbani ambao ulihamasisha

Mazungumzo hayo kwa wale Wanaositasita Kupata

Chanjo na Wale Wanaowapenda.

Boca del Lupo inashukuru kutayarisha na kufanya

kazi kwenye eneo lisilojulikana la watu wa xwm θkw y m (Musqueam), Skwxwú7mesh (Squamish), na S lílw taɬ (Tsleil-Waututh). Bocadellupo.com

2

KIKAO

Jikoni lenye jua, na mimea mingi na sanaa nzuri, (sana sana Sanaa ya watoto!). Chanjo za Covid zimeidhinishwa kwa watoto wa miaka 5 hadi 11. Redio inacheza muziki wa ala kwa urahisi wa kusikiliza chinichini.

MAELEZO

Muigizaji anayecheza kama LINDA atacheza pia kama SPARKLES, ambaye mistari yake ni mapendekezo tu, tafadhali iyafanye yako. Ikiwa unajihisi huru zaidi kuongea, kupiga kelele... nguruwe mdogo, mtoto wa mbwa, nk... badilisha “paka” kwa aina yako. Niliandika haya kwa mchango muhimu kutoka kwa Dk. Elizabeth McLaughlin, mwanasaikolojia wa watoto. Alielezea umuhimu wa kusaidia ustahimilivu wa mtoto, na kuwasaidia kuelewa jinsi ya kukubali usumbufu ili kufikia lengo. Pia alinielekeza kwenye mfumo wa “CARD” wa kukabiliana na wasiwasi/hofu.

FARAJA

Saidia mtoto wako kukubali mawazo na hisia hasi. Wasaidie kujua kuwa haya ni ya kawaida na yatapita. Mfundishe mtoto wako kuwa jasiri na kuwa ‘bosi’ wa wasiwasi wake.

3

ULIZA

Sikilizaneni na mzungumze. Muulize mtoto wako jinsi anavyohisi na ujibu maswali yoyote ambayo anayo kwa uaminifu. Tumia maneno ambayo mtoto wako anaweza kuelewa kwa urahisi na kufuata mwongozo wake. Ikiwa mtoto wako hataki kuzungumza au hayuko tayari, ni sawa. Waambie wanaweza kuja kwako kila wakati ikiwa wana maswali.

STAREHE

Watoto huona na kuhisi kile ambacho wazazi wao wanafanya na mara nyingi hufanya vivyo hivyo. Mfano wa kustarehesha mtoto wako. Ongea na mtoto wako kwa sauti ya utulivu na ya kawaida ya kuzungumza.

VURUGA AKILI

Jaribu kuweka utaratibu wa kawaida na upunguze muda ambao mtoto wako huzingatia chochote kinachomfanya awe na wasiwasi.

4

KIM ni Baba mwenye umri wa miaka karibu 40. Anahangaika sana, akiwaza jinsi ya kuzungumza na binti yake wa shule ya msingi, anayeitwa SUZU, kuhusu yeye kupata chanjo. Ana wakati mgumu kupanga mawazo yake. Mama yake, LINDA, “Nana” amemaliza ziara ya Jumamosi asubuhi. Anadhani kizazi hiki cha wazazi kinajishughulisha sana. KIM anapunguza sauti ya redio huku akimwekea LINDA kahawa.

LINDA: Hiyo ni vizuri. Kim! Aaa, sipaswi kunywa kafeini, lakini napenda harufu ya kahawa sana siwezi kuiacha.

KIM: Naweza kutengeneza decaf—

LINDA: Yuck, sipendi hiyo kitu. Nani anayejua wanachoweka ndani yake ili kuondoa kafeini. Je, ulifanya miadi kwa ajili ya Suzu? Inachukua muda kwa chanjo kuanza.

KIM: Mama, najua jinsi inavyofanya kazi- nilipata chanjo haraka nilivyoweza.

LINDA: Ninataka kuwa salama nikiwa karibu na mjukuu wangu, pata chanjo na umalize hiyo.

KIM: Ana maswali mengi —

LINDA: Huo ni ujinga. Yeye ni mdogo sana hawezi kuelewa kabisa —

KIM: Kwa kweli Mama, mimi hushangazwa na jinsi anavyoelewa —

LINDA: Wewe ndiye unayemweleza mambo na ndio maana anakuwa na kila aina ya dhana. Kama hili jambo kuhusiana na sindano...

KIM: Watoto wengi wanaogopa sindano. Bado mimi nachukia sindano. Anapaswa kushirikishwa kuhusiana na maamuzi

5

yanayomhusu, haswa mwili wake.

LINDA: Mnalifanya kama jambo kubwa kitu kinachochukua sekunde mbili.

KIM: Ni jambo kubwa, Mama! Argh, usijali.

LINDA: Hapana niambie. Wewe sio mmoja wale wanaopinga —

KIM: Hapana, sikufikiria mara mbili juu ya kupata chanjo-kwangu. Lakini ni tofauti kufanya chaguo hilo kwa niaba yake, yeye ni mdogo sana ... asiye na nguvu, sio busara lakini vipi ikiwa... acha tu ninajaribu tu, kuelewa vizuri kwanza, ili niweze kumweleza.

LINDA: Ningepoteza akili kueleza kila kitu kwako na ndugu zako. “Kwa nini ninahitaji kwenda kulala?” “Kwa sababu kuna giza”, “Lakini kwa nini?” “Kwa sababu jua limepita”. “Lakini kwa nini?”. “Kwa sababu dunia inageuka”. “Lakini kwa nini?”

“Kwa sababu linafanya hivyo. Sasa nenda kitandani!”. ‘Lakini kwanini’ haziishi! Maliza haraka na kama atahangaika mnunulie ice cream baadaye. Hivyo ndivyo nilivyofanya nanyi.

KIM: Ndiyo. Nakumbuka nilitokwa na machozi, nikila aiskrimu ya ukungu wa mwezi kisha nikatapika.

LINDA: Ulikuwa na tumbo yenye matatizo kila wakati. Niliwapeleka ninyi watatu kubishana kwenye ofisi ya daktari, peke yangu —

KIM: Najua, ulijitahidi sana.

LINDA: Ee bwana, nilikutia kiwewe.

KIM: (akicheka) Ni sawa kabisa Mama. Kama sikuwa nikijaribu kujua jinsi ya kuzungumza na Suzu, nisingekumbuka

6

hata kutapika kila mahali kwa gari.

LINDA: Na pia kutapikia Kyle.

KIM: Ingawa, alistahili hivyo. Aliniambia kuwa sindano hiyo ingetoa damu yangu yote.

LINDA: Aaa, hiyo dogo — !

KIM: Labda ninafikiria hili kupita kiasi. Mimi sihisi kama nina majibu yote.

LINDA: La. Na hakuna wakati utakuwa nayo. Hiyo ni kuwa tu mzazi...

KIM: Ongezea?

KIM anaweka kahawa zaidi huku LINDA akiongea...

LINDA: Kim, kuhusu ulichosema— oh hiyo inatosha, wacha nafasi ya cream, asante— ulichosema, kuhusu watoto kuwa wadogo sana, kutokuwa na nguvu... Ninajua jinsi hilo linavyohisi. Ungenitazama kwa imani sana, ilikuwa inatisha.

Kwa hivyo, nilikusukuma haraka niwezavyo kwa sababu sikujua ni nini kingine cha kufanya. Naomba... msamaha. Nilikuwa nikitabasamu, lakini wewe ni baba mzuri sana. Kwa hivyo msikilize tu na umjibu kwa uaminifu. Dang, laiti ningerudi na kutumia ushauri wangu mwenyewe.

KIM: Asante Mama.

LINDA: Na—labda hii itasaidia—ilikua rahisi nilipogundua kwamba ilikuwa sawa kujibu baadhi ya hizo “Lakini Kwa nini?”

kwa kusema “sijui.”

KIM: Hm.

LINDA: Yuko wapi hata hivyo?

7

KIM: Huko juu kwa ghorofa akiwa na paka. (akimwita, na akipanda kwa ghorofa) Suzu?? Hey, Suuuzu...?

Tunapanda juu kwa ghorofa ambapo tunamkuta SUZU akiwa na paka wake kipenzi SPARKLES, akicheza katika matembezi kwenye kabati. SUZU anapekua rundo la vifaa vya ufundi akitafuta kitu. SPARKLES anaweza kulia, kuzomea na kukosoa— kukubali, kukataa, kuchanganyikiwa au kufurahisha...

SPARKLES: Mreoowrr? (unafanya nini?)

SUZU: Ninajaribu kutafuta kitu cha kukulinda. Kuna vitu nyingi sana kwenye kabati hili! Aa!

Hii itafanya! Simama sasa, lazima uvae hii.... Doo dooo do doo

SUZU ananguruma huku akifunga utepe kwenye upinde kwa shingo ya paka. SPARKLES hajali, amezoea mchezo wa kuvalishwa.

SUZU: Ta Da! Utepe huu ni utepe wa uchawi usioonekana wa... uchawi.

SPARKLES: Mrerp. (Mimi sitaki) Kwa hiyo SUZU anaeleza umihimu wake.

SUZU: Sparkles. Utepe huu utakufanya usionekane kwa sababu, ni ... ngao ya nguvu! Na virusi vya Covid vitasema, “Aaaarrrgghhghgh, nisaidie!!!–Nataka kuingia kwenye paka huyu, lakini hapana! Utepe huu wa kichawi una nguvu juu yangu, unanifanya, unanifanya... kulipuka!— Shaboooom! Brrrroom, Pyyoow!”. Hivyo ndivyo virusi vinavyosikika vinapolipuka. Na kisha— “EEEEEeeeek!” Zinaanguka chini. Zinakufa. Unapenda hivyo?

SPARKLES: Prrrrrrr (akitoa sauti ya ndiyo)

8

SUZU: Vema. Umelindwa. Na uko mrembo! Hm, kijiti changu kiko wapi? Kijana, baba anasema kweli, kabati langu halijapangwa. Ninataka fimbo yangu ili niweze— Sha-zing— kugeuza virusi vibaya vya Covid kuwa... kuwa... vifuniko vya theluji au— hapana, Sparkles, acha kukwaruza —utapoteza upinde wako wa kichawi! Unataka Covids ZIKUPATE?!

SPARKLES: Hissssst-rrrowr! (umefanya niogope!)

SUZU: Samahani, usiogope, ninajaribu tu kukulinda. Shh... kwa sababu wewe ni paka mdogo tu na mimi ni mkubwa kuliko wewe. Ninakupenda. Na ni kazi yangu kukutunza vizuri kwa sababu kuna hiki kitu ulimwenguni sasa, na ni Covid ambacho kinaumiza watu... SUZU anamfichulia siri SPARKLES. Unajua Lilly, rafiki yangu tunayesoma naye?

SPARKLES: Merwr. (“ndiyo”)

SUZU: Nyanya yake aliugua sana...

SPARKLES: Mrrwor?? (“Mgonjwa kiasi gani?”)

KIM: ... sana sana— alikuwa mgonjwa sana karibu afe. Sitaki nana wangu ... anapumua kwa nguvu

Kupitia mlango wa kabati tunasikia KIM akiita.

KIM: (kwa sauti ndogo) “Suzu??....Suuuuz...?

SUZU: Uhoh, shhh....

KIM anagongagonga mlango.

SPARKLES: MRRooowrR!! (anashangaa!!)

KIM: (kwa sauti ndogo) Je, uko ndani, Su? Ninaweza kuingia?

9

SUZU: Sawa.

Mlango unafunguliwa na KIM anaingia na kukaa kwenye sakafu.

KIM: Unafanya nini kwenye kabati?

SUZU: Sparkles aliogopa, anahisi salama akiwa humu ndani.

KIM: Na kwa nini anahitaji kujisikia salama?

SUZU: Sijui

KIM: Basi. Ni vizuri kuwa ako na wewe.

SUZU: Aha.

KIM: Suzu, umefikiria kuhusu tulichozungumza jana, kwamba watoto wanaweza kupata chanjo sasa, kwa ajili ya Covid?

SUZU: Ndiyo.

KIM: Unafikiria nini?

SUZU: Sidhani watoto wanapaswa kupata chanjo kwa sababu tayari nilizipata nilipokuwa mdogo, si ni kweli?

KIM: Ndio, kabla ya kuanza shule. Lakini hazikuwa za Covid. Je! unajua Covid ni nini?

SUZU: Haionekani na ni mbaya. Ni kidudu kibaya, kidogo, kinachokufanya mgonjwa kwa mishale.

KIM: Kweli, kwa sababu ina mishale inaitwa virusi vya Corona.

SUZU: Na inaogopa kuingia kwenye kabati.

10

KIM: (akicheka) Sikujua hilo! Kweli, kabati lako ni salama kwa sababu hakuna mtu anayeingia isipokuwa wewe na Sparkles.

SUZU: Na wewe, tunapolisafisha.

KIM: Inakufanya uhisi vipi ninapokuuliza kuhusu Covid?

SUZU: (Anapumua kwa nguvu). Aaa, huwa sipendi. Kila mtu wakati wote anazungumza kila wakati, blah, blah, blah Covid. Covid ondoka! Potelea mbali Covid, usiruhusu mlango ukugonge Covid! Kwaheliiiiiiiiiii

KIM: Wow, ingekuwa vizuri kama tungeweza kuiambia la kufanya. Lakini haiondoki, sivyo.

SUZU: Lakini kwa nini?

KIM: Kwa sababu vijidudu, virusi, hupitishwa kote, si ni kweli?

SUZU: Lakini kwa nini?

KIM: Kwa sababu watu huzibeba, huwa hawajui wanazibeba, lakini wanaweza kupitisha virusi kwa watu wengine.

SUZU: Kwa hivyo, kila mtu anapaswa kuacha kupitisha covids kwa watu wengine!!

KIM: Hiyo ndiyo sababu moja kwa nini tunapata chanjo. Ili tuwe na uwezekano mdogo wa kuwapa watu wengine. Una maoni gani kuhusu wewe kupata chanjo?

SUZU: Nafikiria chanjo ni za watu wakubwa na wazazi na nana na, na ... madereva wa mabasi aaaa na wazee wote, wazee na walimu wanaweza kupata chanjo. Na Sparkles na mimi tunaweza kukaa hapa ndani.

11

KIM: Je, hungechoka kama ungekaa humu ndani milele?

SUZU: (akiwa na hamu) Mnaweza kuninunulia TV kubwa na Playstation?

KIM: (akitabasamu) Hilo halitafanyika.

SUZU: Aww! (alijua angesema hivyo-ni mchezo kati yao)

KIM: Vipi kuhusu kila mtu shuleni? Je, hungehisi umewakosa?

SUZU: Kuna msichana fulani, msichana fulani mkubwa, anayeitwa Madison na alisema chanjo hazifanyi kazi.... Alituonyesha kwenye simu yake, kwamba watu walisema hivyo.

KIM: Sawa. Tumezungumza kuhusu mtandao na jinsi ilivyo ngumu kujua ukweli juu yake, si ni kweli?

SUZU: Ahuh.

KIM: Je, utaniahidi kwamba tutaangalia tu mambo pamoja? Na kama Madison au mtu yeyote atakuonyesha kitu utaniambia?

SUZU: Ndiyo, sikujua angetuonyesha mambo hayo! (anakasirika)

KIM: Sijakasirika, Suzu. Watoto wengine wana sheria tofauti katika familia zao. Lakini katika familia yetu, tutaangalia mambo pamoja, sawa?

SUZU: Sawa. Kwa hivyo, chanjo sio mbaya?

KIM: Hapana, wanasayansi wengi wameijaribu na wanapaswa kusema ukweli. Lakini wakati mwingine unapata athari. Baada ya kupata chanjo yangu, nilihisi kuchoka sana.

12

SUZU: Lakini kwa nini uliipata basi?

KIM: Kwa sababu sasa, ninaweza kufanya mambo ninayofurahia, kama vile kuona marafiki zangu bila kuwa na wasiwasi. Je, ungehisi umekosa marafiki zako kama ungekaa humu ndani?

SUZU: Lakini kwa nini, watoto wanapaswa kuipata?

KIM: Kwa sababu ingawa watu wengine hupata athari kutoka kwa chanjo, watu wengi zaidi huugua sana, huugua zaidi kutokana na Covid.

SUZU: Wanaugua kiasi gani?

KIM: Wanapata ugumu wa kupumua na wanahisi vibaya sana.

SUZU: Je, wanakufa?

KIM: Wakati mwingine tu. Na madaktari na wauguzi wanasaidia watu ambao wanaugua sana.

SUZU: Vipi kuhusu Nana, je ataugua?

KIM: Nana alipata chanjo na yuko makini. Unaweza kumsaidia yeye na kila mtu kuwa salama zaidi ukipata chanjo.

SUZU: Wanapaswa kuweka chanjo kwenye kidonge kidogo kwa watoto, kwa nini wasifanye hivyo?

KIM: Hilo ni wazo zuri na wangefanya kama wangeweza. Mimi sipendi sindano pia. Nilipopata chanjo ilinibidi kuvuta pumzi kubwa.

SUZU: Ulifanya hivyo?

KIM: Ndio, kama hivi ... unaweza kupumua pamoja nami, vuta

13

ndani kupitia pua lako na.... nje....

KIM na SUZU wanapumua kwa pamoja, wakitoa sauti ya kufoka wanapopumua kupitia midomo yao.

SPARKLES: Alaaaaaaa (“binadamu ni wa ajabu”)

KIM: Na muuguzi aliniambia baadhi ya watu huwa wanaangalia simu zao ili kurahisisha, nami nikasema, “Wazo zuri!” kwa hivyo nilitazama picha—zetu tukiwa ziwani.

SUZU: Ilifanya uhisi uchungu?

KIM: Sindano? Sikuhisi kwa sababu nilikuwa nikitazama picha yetu tukiwa kwenye mashua ya Kyle. Baadaye mkono wangu ulikuwa unauma kidogo. Uko sawa sasa.

SUZU: Sitaki kuwa mgonjwa...

KIM: Najua, lakini wewe ni mtoto mwenye afya nzuri, na watoto wengi hawaugui sana.

SUZU: Lakini kwa nini?

KIM: Mwili wako ni mchanga. ‘Mfumo wako wa kinga’— umesikia hilo?

SUZU: Ndiyo maana ninakula matunda na mboga. Ili kuweka mfumo wangu wa kinga imara.

KIM: Mfumo wa kinga, sawa. Wakati wewe ni mdogo na unakua, mfumo wako wa kinga ni wenye nguvu zaidi kuliko wa watu wakubwa.

SUZU: Lakini kwa nini ninahitaji kupata sindano basi?

KIM: Ndio njia bora ya kuwa salama zaidi na kusaidia kulinda wengine. Unaweza kufikiria jambo ambalo hupendi kufanya

14

lakini unajua kwamba baadaye, utafurahi kuwa ulifanya?

SUZU: Aa... Labda, kusafisha, sipendi kuifanya hivyo, lakini ninapenda baadaye, inapoonekana safi.

KIM: Wakati mwingine kuna faida ya kufanya kitu tusichokipenda. Je, kupata chanjo kunasikika kama jambo unaloweza kufanya?

SUZU: Labda...

SPARKLES anakwaruza shingo yake kwa mguu wake wa nyuma, whappawhappa .

KIM: Kuja, Sparkles— wacha tuondoe utepe huo....

SUZU: Hapana! Usitoe! Acha akae nayo!

KIM: Anajifunga nayo—

SUZU: Nilimfunga, ili kumlinda! Ninastahili kumtunza.

KIM: Sawa, nimeelewa. Kama vile ninavyopaswa kukutunza?

SUZU: Ndiyo.

KIM: Unafanya kazi nzuri... Na, ikiwa angehitaji kwenda kwa

daktari wa mifugo, ungeenda naye?

SUZU: Ndio, ningemwambia ni nzuri kwake, wakati mwingine tunafanya mambo ambayo ni magumu lakini ambayo

tutafurahia baadaye na ningempa zawadi ya kumsaidia.

KIM: Kama vile naweza kukusaidia, ikiwa tutaenda pamoja?

SUZU: Wewe na mimi Sparkles?

15

KIM: Sparkles pia? Apana Suzu, sidhani kama wanaruhusu vipenzi —

SUZU: Ninaweza kuonyesha Sparkles jinsi ya kupata sindano. Ili awe jasiri.

SPARKLES: Meow (nitakuwa jasiri)

KIM: Vizuri sana. Nitajaribu kutafuta kliniki ambapo tunaweza kwenda na Sparkles, lakini ikiwa sitapata, unaweza kutazama picha yake unapopata sindano?

SUZU: Labda yeye na Nana wangeweza kutazama kupitia zoom?

KIM: Aa! Unaweza kuzungumza na Nana ili amwonyeshe Sparkles jinsi ya kupata chanjo.

SUZU: Ndiyo. Ninaweza kufanya hivyo. Baba.... Kwa nini Covid haina huruma hivyo?

KIM: Ebu rudia?

SUZU: Kwa nini inataka kuumiza watu wazuri, kwa nini inataka kutuumiza?

KIM: Kwa sababu ni- ni um (akikumbuka ushauri wa Linda)...

Sijui. Labda tunaweza kuchunguza.

SUZU: Labda nitakuwa mwanasayansi wa virusi na kuchunguza.

KIM: Labda siku moja. Suzu, Nana Nana yuko jikoni na alileta vidakuzi.

SUZU: Vidakuzi! Twende Sparkles!

SPARKLES: Meowp (sawa!)

16

Wote wanainuka, SUZU anamwinua SPARKLES, sauti zao zikafifia huku wakielekea chini.

KIM: Unapaswa kumuuliza Nana akuelezee wakati aliponipeleka kupata chanjo nikiwa na umri wako, ni hadithi nzuri, mjomba wako Kyle yuko ndani na....

MWISHO!

17

MARY-COLIN CHISHOLM

Machi 2020: mchezo wangu wa A Belly Full (na M. Kash) ulifungwa wiki moja baada ya kufunguliwa. Matoleo matatu yaliyopangwa, kutia ndani kazi moja mpya, yalizabaratishwa na “mwaka bora zaidi kwa muda mrefu” uliotarajiwa ukatoweka. Shida yangu ya kibinafsi iliwekwa wazi haraka na hadithi za wale walioathiriwa moja kwa moja na Covid. Na nilikuwa mmoja wa wasanii wengi waliookolewa na shirikisho la CERB. Kwa hivyo, labda kama wewe, nilioka, nilitembea, niliota waziwazi, nilijifunga, nilipanda mbegu, na kugundua njia za zoom. Kupitia haya yote, nilijifunza kuona tena na kuthamini; fadhili, uhusiano, asili, uvumbuzi, na kupumua kwa njia ya kutokuwa na uhakika. Sina shukrani kwa Covid, au shukrani kwa masomo yake. Ni virusi vya nasibu, na iliumiza wengi sana, haswa walio hatarini zaidi, hazipaswi kamwe kupewa shukrani. Lakini tunapoelekea kwenye afya, nitakumbuka kukumbatia baraka zangu na kupenda vikali ulimwengu wetu wa pori na dhaifu wa kijani kibichi.

© 2021 MC CHISHOLM

Hakuna sehemu ya kitabu hiki inayoweza kunakiliwa kwa sehemu yoyote kwa njia yoyote ile—mchoro, kielektroniki, au kimitambo. Kwa ruhusa maalum, ikijumuisha madhumuni ya elimu, tafadhali wasiliana na Boca del Lupo at info@bocadellupo.com

DESIGN: Cabin + Cub Design

18

Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.