Page 1

Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page A

KUWAONGOZA VIJANA WA KIZAZI KIPYA

Kimeandikwa na: Ustadh Murtadha Mutahhari

Kimetarjumiwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page B

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 9987 - 427 - 49 - 9 Kimeandikwa na: Ustadh Murtadha Mutahhari

Kimetarjumiwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: Februari, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na:

Al -Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Fax: +255 22 2127555 Email:alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page C

YALIYOMO Wasifu wa Al-Marhum Ayatullah Murtadha Mutahhari..............................2 Taratibu za Uongozi ni zenye kuhusiana na za muda.................................23 Sababu za tofauti miongoni mwa miujiza ya Mitume...............................27 Taratibu za Mitume....................................................................................30 Wanafunzi Bora.........................................................................................32 Ni kizazi cha vijana au kukomaa kwa akili za vijana................................37 Kuwa mwanachuoni kwa wakati ambamo unaishi....................................39 Mfano wa vizazi viwili............................................................................. 43 Vijana wa kisasa....................................................................................... 48 Matatizo ya kizazi hiki ni lazima yaeleweke.............................................50 Sababu za kwa nini watu wanavutika kuelekea kwenye kumkana Mungu...................................................................................................... 56 Ishara za maendeleo ya kielimu ................................................................57 Utelekezwaji wa Qur’ani Tukufu..............................................................59


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page D

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Vijana........................................................................................................ 63 Kuwafundisha Vijana ............................................................................. 66 Kutafuta Elimu ukiwa bado Kijana...........................................................67 Kijana na kujizuia kutokana na kutafuta Elimu.......................................68 Umashuhuri wa mtu kijana anayemuabudu Mwenyeezi Mungu..............70 Umashuhuri wa mtu anayetumia ujana wake katika utii kwa Mwenyezi Mungu...................................................................................................... 72 Maelezo ya sifa bainifu za kijana (Al-Fata)...............................................74

D


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page E

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

KUWAONGOZA VIJANA WA KIZAZI KIPYA

Abu Abdillah (amani juu yake) anasimulia kutoka kwa jadi yake (Maimam, amani juu yao wote) ambao wamesema yafuatayo: “Mtu mmoja alikuja kwa Mtukufu Mtume wa Allah, (rehema na amani juu yake na juu ya kizazi chake) na akasema, ‘Ewe Mtume wa Allah – elimu ni nini?’ Mtume akamjibu: ‘Ni kuwa kimya.’ Yule mtu akauliza tena, ‘Halafu nini?’ Mtume akamjibu: ‘Ni kusikiliza.’ Yule mtu akauliza, ‘Kisha nini?’ Mtume akasema: ‘Kisha ni kuwa na kumbukumbu.’ Yule mtu akauliza, ‘Kisha ni nini?’ Mtume akasema: ‘Kisha ni kuyatekeleza (yale mtu aliyojifunza).’ Yule mtu kisha akauliza tena, ‘Halafu nini tena, Ewe Mtume wa Allah?’ Mtukufu Mtume akasema, ‘Halafu ni kuyaeneza (yale ambayo mtu amejifunza).’”

Amani iwe juu yako Ewe Abul Fadhl al-Abbas Ibn Amiral-Mu’min Ali ibn Abi Talib.

E


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page F

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

“Ni mwema wa ajabu kiasi gani: Yule mwenye subira, mwenye kujitahidi’ Yule mlinzi, na msaidizi, Na ndugu anayemtetea ndugu yake, Mwenye kuwajibika katika utii kwa Mola Wake, Mwenye kutumainia yale ambayo wengine wameyakanusha, Miongoni mwa thawabu nyingi na sifa njema..........”

]Ziyaratil-Warith – ya Abbas ibn Ali (a.s.) Kwanza kabisa, tunamuadhimisha na kumpongeza Imam wetu mtukufu wa Zama, Imam al-Qaim al-Mahdi (a.l.t.f.) na watumishi wakweli wote, wa Allah (swt) katika maadhimisho haya matukufu ya 1400 ya ukumbusho wa kuzaliwa kwa yule Simba asiyehofu, mpiganaji shujaa, mtumishi asiye mbinafsi – ule Mwezi wa Bani Hashim, Hadhrat Abbas ibn Ali (a.s.) Hadharat Abbas (a.s.) ni mmoja wa mifano bora kabisa ya Shi’ah (wafuasi) wa Imam Ali (a.s.), na kutokana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ya kutimiza miaka 1,400, tunakitoa kitabu hiki kwa ajili ya nafsi hii mashuhuri na sharifu mno. Inatarajiwa kwamba, insha’allah, kwa kukisoma kitabu hiki, jamii ya Kiislamu - hususan vijana – itaongozwa na kusaidiwa katika jitihada zake za kuutambua Uislam halisi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kupania katika kuielewa njia hii nzuri kabisa ya maisha, kuwa watumishi halisi wa Allah (swt) na kuyatoa maisha yao katika njia ya Uislamu kama vile Hadharati Abbas ibn Ali (a.s.).

F


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page G

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya “Siwezi kulia juu ya kuipoteza dunia hii na kujaribu kukikwepa kifo wakati kitakaponijia. Bali, nitakikaribisha kifo kama kinanijia katika njia ya Mwenyezi Mungu. Nitakipokea kifo kwa uchangamfu, kwa shangwe na furaha, kwani Peponi ni makazi ya furaha zaidi kuliko dunia hii. Dunia hii sio mahali panapofaa kuishi. Mwenye bahati ni yule anayeKufa kwa ajili ya Uislamu.”

Hadharat Abbas ibne Ali (a.s.) Kasim Sumar Mwenyekiti, Meza ya Mtandao wa Vijana – Youth Network Desk [YND]

G


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page H

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

UTANGULIZI Na: Hasnain Walji “Tokea kwenye susu hadi kaburini, Maisha yaonekana bali ni kama njozini, Ni nzuri sana, awamu ile ya ujanani, Njozi hii hasa, ndio kubwa isiyo kifani.” Abu Faiyyaz

Kitabu hiki ni matunda ya moja kati ya hotuba nyingi za mwanafikara na mwanazuoni maarufu, Ayatullah Shahid Mutahhari (Qaddisa Sirruh - QS). Bado hapa tena, anaonyesha ile haja kubwa sana ya kufikiria upya ni vipi tunaweza kuzijibu changamoto zinazoletwa na zama hizi, zikitawaliwa na utamaduni wa kimagharibi na athari zinazoambatana nao. Huu ni mwendelezo wa utafutaji, maishani mwake mwote, kutaka kuziba ule ufa ambao unaelekea kutenganisha ile lugha asili ya dini na lugha ya usasa. Matokeo ya ufa kama huo yamesababisha kuzidi kwa fikira potovu ambazo zimegeuka kuwa ‘dhana.’ Mojawapo ya ‘dhana’ kama hizo inaitwa ‘tofauti kubwa ya vizazi.’ Baada ya kupata kutumika sana, fikira hii potovu ambayo sasa imekuwa ni dhana inayokubalika, na imechukua muundo wa utabiri unaojitosheleza wenyewe, kwa kweli umesababisha ‘tofauti’ kubwa sana kati ya vizazi. Imetoa kibali na heshima kwa kizazi cha vijana ‘kutofautiana.’ Kutumia msemo wa kisasa, imekuwa ‘poa’ kuvaa, kuwa na tabia na kutenda kwa kutofautiana kabisa. Hii ndio ramani ya barabara ambayo inayoendea kwenye MTV na nchi ya hip-hop. Jina la kitabu, ‘Kuwaongoza Vijana wa Kizazi Kipya’, linakuwa lenye H


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page I

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kufaa zaidi katika siku hizi na zama hizi za mikataba midogo midogo, baruapepe, milango ya mitandao na “kublogu” (kutoa maelezo binafsi kwa njia ya tovuti) – Fikra za kimagharibi na athari zake zinakubaliwa na kuidhinishwa duniani pote kwa shauku kubwa. Kuiga matakwa na mitindo ya kisasa kumeendelezwa sasa kwenye vituo vya mawasiliano katika nchi zinazoendelea ambapo vijana wa kiume na wa kike sasa wanaongea kwa ukokota maneno wa Texas na dakika inayofuata anakwenda kwenye lafudhi ya Uingereza Mpya akitoa huduma kwa muitaji kutoka Boston. Kwa vijana wa Kiislamu itakuwa vigumu sana kujikinga na kutoathirika na hili. Wasomaji, hususan wazazi, wanaotafuta maelekezo ya haraka au orodha ya majibu yaliyotayarishwa tayari kwa changamoto hizi watasikitika sana. Ingawa kitabu hiki kinazua maswali mengi zaidi kuliko yale kinayoyajibu, hata hivyo Ayatullah Mutahhari inauweka wajibu huo moja kwa moja juu ya kizazi kilichotangulia hivi karibuni tu na anasema: “Kila kizazi kina wajibu juu ya mwongozo wa kizazi kinachofuatia – hususan wale watu wanaotambulika rasmin kama ndio viongozi wa jamii – wao wana wajibu mkubwa zaidi .....” Wakati huo huo anatusihi tusizishughulikie changamoto za leo kwa utatuzi wa jana. Kuhusu suala hili, yeye anasema: “.......jambo la uongozi na mwongozo wa kizazi hiki unatofautiana katika njia na mbinu zake mwote katika vipindi mbalimbali vya nyakati na unatofautiana kulingana na vikundi au watu ambao tunashughulika nao. Hivyo ni lazima tuliondoe kabisa akilini mwetu, lile wazo kwamba hiki kizazi kipya lazima kiongozwe kwa kufuata njia zilizotumiwa na vizazi vilivyopita.” Ni katika muktadha huu ambamo kitabu hiki kinatakiwa kieleweke kama ni chenye kutoa maelekezo katika kuzijibu changamoto katika utaratibu unaohusika na wakati tunaoishi ndani yake. I


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page J

Mwanazuoni huyu marehemu, vilevile anatukumbusha Hadith ya Imam Ja’far Ibn Muhammad as-Sadiq, amani juu yake, kwamba: “Mtu ambaye anautambua vizuri wakatiiambamo anaishi ndani yake, kamwe hatajawa na utatanishi (juu ya yale mambo yaliyomzunguka).” Kwa hiyo, tukiwa watambuzi wa zama tunamoishi, tunahitaji kulenga kwenye ukamilifu wa vipengele vya kiakili, kijamii na kihisia ambavyo vinaathiri vijana wetu, na hususan wanafunzi katika vyuo na Vyuo Vikuu. Mahitaji ya zama hizi za sasa ni kutambua kwamba vijana wetu wanaendelea kupambana na ongezeko la uvunjikaji wa utaratibu wa kujifunza vivyo hivyo na mgawanyo wa nidhamu na kuhitilafiana yenye asili ya fikra kama mfumo wa utambuaji dini zaidi ya moja. Wanaishi katika zama ambayo inawelekeza kwenye itikadi nyingi zinazotofautiana na ambazo zinawataka maelezo yenye mantiki katika masuala ya imani. Utambuzi huu unaweza kutusaidia sisi kulea kizazi cha Waislamu ambacho nacho kitakujakuwa na uwezo wa kulea kizazi kitakachofuatia. Kwa kufunga, tunanukuu maneno ya mshairi wa Pakistan, Marhum Allamah Iqbal ambaye ameandika kama ifuatavyo: Ewe Mola, wajaalie Waislamu moyo wenye hamasa upya, Ambayo kwamba itaweza kuukunjua moyo na kuitikisa nafsi upya. Lifanye kila tone katika ummah wa Kiislam kutoa nuru tena, Ulibariki na dhamiri na ghera mpya tena. Wale waliopofushwa, wape maono mapya pia, Nilichokitambua mimi, waonyeshe na wao mawazo hayo hayo pia. Hasnain Walji Plano, Texas Jamadu Thani 1425/Agosti, 2004.

J


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page K

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kwa jina la: "Guiding the Youth of New Generation" Sisi tumekiita: "Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya" Kitabu hiki, "Kuwaongoza vijana wa kisasa" ni matokea yahotuba nyingi za mwanafikara na mwanachuoni maarufu, Ayatullah Shahid Mutahhari (Qaddisa Sirruh - QS). Vijana wetu siku hizi wametekwa nyara na tamaduni za magharibi na kuiga kila kinachotoka huko kuanzia mavazi mpaka fikira na mwelekeo wa kimaisha kiasi kwamba hawana habari na tamaduni zao, wamekuwa wapinzani wa kila lisiloafikiana na mawazo yao ya kimagharibi. Katika kitabu hiki mwachuoni huyu anajaribu kuzijibu changamoto zinazoletwa na zama hizi, hususan kutoka kwa vijana hawa wa kisasa. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, kwani kitakuwa kama kifungo macho na masikio kwa vijana wetu wale wanaotaka kuongozwa na kuongoka. Watu hawakatazwi kuiga, lakini wanatakiwa kuiga yale yaliyo mazuri tu, na maovu na mabaya kuwaachia wenyewe. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya 'Al-Itrah Foundation' imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu Ramadhani K. Shemahimbo, kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 2110640 K


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

L

Page L


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 1


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 2

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

Wasifu wa Al-Marhum Ayatullah Murtadha Mutahhari Ayatullah Murtadha Mutahhari (Quddisa Sirruh), mmoja wa wasanifu wakuu wa mzinduko mpya wa Kiislamu huko Iran, alizaliwa tarehe 2 Februari,1920 huko Fariman, wakati huo kikiwa ni kijiji na sasa hivi mji ulioko takriban kilometa sitini kutoka Mashhad, kituo maarufu cha Ziyarat na elimu cha Shi’ah kilichoko mashariki ya Iran. Baba yake alikuwa ni Muhammad Husain Mutahhari, mwanazuoni mashuhuri ambaye alisoma huko Najaf na akaishi miaka kadhaa huko Misri na Hijaz, kabla ya kurejea Fariman. Mutahhari mkubwa alikuwa ni wa tabaka tofauti la mawazo na mwanawe, ambaye kwa kila jambo alikuja kung’ara zaidi yake. Baba yake alikuwa na moyo sana na vitabu vya muhadithin mashuhuri, Mullah Muhammad Baqir Majlisi (q.s) ambapo shujaa mkubwa sana wa mwanawe, miongoni mwa wanazuoni wa Shi’ah wa zamani, alikuwa ni yule mwana teosofia (mwenye imani kwamba mwanadamu anaweza kumfahamu na kuwasiliana na Mungu kwa tafakari na utulivu mkubwa), Mullah Sadra (q.s). Hata hivyo, Ayatullah Mutahhari siku zote aliweka heshima na upendo mkuu kwa baba yake, ambaye alikuwa pia ndiye mwalimu wake wa kwanza, na alikitoa waqfu kimoja kati ya vitabu vyake maarufu, Dastan-e-Rastan (Utenzi wa Mwadilifu ), kwa ajili ya baba yake huyo, kilichochapishwa mara ya kwanza mwaka 1960, na ambacho baadaye kilichaguliwa kama kitabu cha mwaka na Kamisheni ya Taifa ya Iran kwa juu ya UNESCO mnamo mwaka 1965.

2


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 3

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Katika umri mdogo usiokawaida wa miaka kumi na mbili, Mutahhari alianza masomo yake rasmi ya kidini katika taasisi ya ufundishaji ya Mashhad, ambayo kwa wakati huo ilikuwa katika hali ya kulegalega, kiasi kwa sababu za ndani na kwa kiasi kingine, kwa sababu ya hatua za kionevu zilizoelekezwa na Ridha Khan, dikteta wa kwanza wa utawala wa Pahlavi dhidi ya taasisi zote za Kiislamu. Lakini hapo Mashhad, Mutahhari aligundua mapenzi yake makubwa juu ya falsafa, theolojia na mafundisho ya kumfikia Mungu kwa tafkira; mapenzi ambayo yalidumu pamoja naye maishani mwake na yakaja yakatengeneza mtazamo wake mzima wa juu ya dini: “Naweza kukumbuka kwamba wakati nilipoanza mafunzo yangu pale Mashhad na nikiwa bado ninashughulika na kujifunza kiarabu cha awali, wanafalsafa, masufi na wanatheolojia walinivutia zaidi sana kuliko wanazuoni na wanataaluma wengine, kama vile wavumbuzi na wagunduzi. Kwa kweli nilikuwa bado sijajizoesha na mawazo yao, lakini niliwaona wao kama mashujaa katika jukwaa la fikra.”1

Ilivyo hasa, mtu katika Mash’had aliyeamsha bidii kubwa kabisa ya Mutahhari alikuwa ni Mirza Mahdi Shahidi Razavi (q.s.), mwalimu wa falsafa. Lakini Razavi alifariki mnamo mwaka 1939, kabla Mutahhari hajawa mkubwa vya kutosha kushiriki kwenye darasa zake, na kwa kiasi fulani, kutokana na sababu hii, yeye aliondoka Mash’had mwaka uliofuatia kwenda kujiunga na idadi inayoongezeka ya wanafunzi wanaokusanyika katika taasisi ya mafunzo ya Qum. Shukurani kwa utawala mahiri wa Sheikh Abdul Karim Ha’iri (q.s.), Qum ilikuwa njiani kuja kuwa makao makuu ya kiroho na kielimu ya Iran ya Kiislamu, na Mutahhari aliweza kunufaika pale kutokana 1 ‘Ilal-e-Girayish ba Maddigari, uk. 9

3


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 4

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya na naelekezo ya uwanja mpana wa wanazuoni. Alisomea Fiqhi na Usul – masomo ya kiini cha mtaala wa kimapokeo – na Ayatullah Hujjat Kuhkamari (q.s) Ayattulah Sayyid Muhammad Damad (q.s.) Ayatullah Sayyid Muhammad Ridha Gulpayagani (q.s.) na Hajj Sayyid Sadr al-Din as-Sadr (q.s.). Lakini muhimu zaidi kuliko wote hawa alikuwa ni Ayatullah Burujerdi (q.s.), mrithi wa Ha’iri kama mkurugenzi wa mfumo wa mafunzo wa hapo Qum. Mutahhari alihudhuria mihadhara ya mafunzo yake tangu kuwasili kwake hapo Qum mwaka 1944 mpaka kuondoka kwake kuelekea Tehran mnamo mwaka 1952, na alistawisha heshima kubwa sana juu yake. Bidii kubwa yenye shauku na uvutiaji wa karibu viliainisha uhusiano wa Mutahhari na mshauri wake mkuu hapo Qum, Ayatullah Ruhullah Khumayni (q.s.). Wakati Mutahhari alipowasili Qum, Ayatullah Khumayni alikuwa ni mhadhiri kijana bado, lakini alikuwa amekwishabainishwa, kutokana na watu wa rika lake, kwa uzamaji na upeo wake mpana wa mtazamo wa kiislamu pamoja na uwezo wake wa kuufikisha kwa wengine. Sifa hizi zilidhihirishwa katika mihadhara, au hotuba zake maarufu juu ya maadili ambazo alianza kuzitoa ndani ya Qum mnamo miaka ya mapema ya 1930. Mihadhara yake ilivutia wasikilizaji wengi kutoka nje, na vilevile ndani ya ile taasisi ya mafunzo ya Kiislamu, na zilikuwa na athari nzito kwa wale wote waliozihudhuria. Mutahhari alifanya mafahamiano yake ya kwanza na Ayatullah Khumayni katika mihadhara hii: “Wakati nilipohama kwenda Qum, niliyaona madhumuni ya mahitaji yangu ndani ya mtu ambaye alikuwa nazo sifa zote za Mirza Mahdi (Shahidi Razavi) katika nyongeza ya sifa nyingine ambazo hizo kipekee zilikuwa ni zake binafsi. Nilitambua kwamba kiu ya nafsi yangu itaweza kutulizwa katika chemchemi halisi ya mtu yule. Ingawa nilikuwa bado sijamaliza hatua za awali za masomo yangu na bado nilikuwa sijafuzu kuingia katika 4


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 5

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya masomo ya elimu ya mantiki (ma’qulat), zile hotuba juu ya maadili zilizokuwa zikitolewa na mhadhiri mpendwa kila Alhamisi na Ijumaa hazikukomea kwenye maadili kwa maana ile ya kitaaluma tu, bali zilishughulika na elimu ya kuwasiliana na Mungu kitafkira na safari ya kiroho, na kwa hiyo, zilinilewesha mimi. Ninaweza kusema bila ya kutia chumvi kwamba hotuba zile ziliniamsha hisia za hali ya juu kiasi kwamba athari zake nilibakia nazo mpaka Jumatatu au Jumanne iliyofuatia. Sehemu muhimu ya hali yangu ya kiakili na kiroho ilianza kujijenga chini ya athari za hotuba zile na darasa nyingine nilizochukua katika kipindi cha miaka kumi na mbili pamoja na yule bwana wa kiroho (Ustadhi-Ilahi – kwa maana ya Ayatullah Khumayni)2

Mnamo kama mwaka 1946, Ayatullah Khumayni alianza kutoa darasa kwa kikundi kidogo cha wanafunzi kilichowajumuisha wote; Mutahhari na mkazimwenza chumbani mwake katika Madrassa ya Fayziya, Ayatullah Muntazari, juu ya vitabu viwili muhimu vya falsafa, Asfar al-Araba’a cha Mulla Sadra (q.s.) na Sharh-e-Manzuma cha Mulla Hadi Sabzwari (q.s.). Kushiriki kwa Mutahhari katika kikundi hiki, kilichoendelea kukutana mpaka takriban mwaka 1951, kulimuwezesha kuanzisha uhusiano wa karibu zaidi na mwalimu wake. Vilevile, mnamo mwaka 1946, kwa kutiwa moyo sana na Mutahhari na Muntazari, Ayatullah Khumayni alifundisha darasa lake rasmin, la mwanzo la Fiqh na Usul, akichukua ule mlango juu ya ushahidi wa kimatiki, kutoka kwenye juzuu ya pili ya Kifayatal Usul cha Akhund Khurasani kama kitabu chake cha kufundishia. Mutahhari aliyafuatilia masomo yake kwa bidii sana, huku akiwa bado anaendeleza masomo yake ya fiqh kwa Ayatullah Burujerdi. Katika miongo miwili ya kwanza ya baada ya vita, Ayatullah Khumayni alifundisha idadi kubwa ya wanafunzi hapo Qum, ambao walikuja wakawa viongozi wa mapinduzi ya Kiislamu na Jamhuri ya Kiislamu, ambao kwamba kwa kupitia kwao (na vilevile hata moja 2 Ibid. 5


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 6

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya kwa moja), sura ya shaksia yake ilionekana katika maendeleo yote muhimu ya muongo uliopita. Lakini hakuna hata mmoja miongoni mwa wanafunzi wake ambaye alichukua uhusiano wa karibu sana kwa Ayatullah Khumayni kama Mutahhari, ukaribu ambao kwamba Ayatullah Khumayni mwenyewe amekuwa shahidi juu yake. Mwanafunzi na mwalimu wake walikuwa na fungamano la kina kwenye mielekeo yote ya elimu ya desturi (ya siku zote), bila ya kuwa kwa namna yoyote ile, mateka wake (elimu hiyo); mtazamo mpana wa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha na imani, pamoja na umuhimu wa kipekee kupachikwa katika mwelekeo wa kifalsafa na kisufi; uwajibikaji halisi kwenye taasisi ya kidini, unaoimarishwa na utambuzi wa umuhimu wa mageuzi; haja ya mabadiliko makubwa ya kijamii na kisiasa, yakiambatana na hekima kubwa ya mkakati na mpangilio wa muda; na uwezo wa kufikia mbali zaidi nje ya duara la wachamungu wa kidesturi, na kupata usikivu na uwajibikaji wa wale walioelimishwa kisekula (kidunia). Miongoni mwa walimu wengine ambaye mvuto wake ulidhihirika kwa Mutahhari hapo Qum, alikuwa ni yule mfasiri wa Qur’ani na mwanafalsafa mashuhuri, Ayatullah Sayyid Muhammad Husain Taba’tabai (q.s.). Mutahhari alishiriki katika darasa zote za Taba’tabai juu ya Shifa’ ya Abu Ali Sina kutoka mwaka 1950 hadi 1953, na ile mikutano ya kila Alhamisi jioni ambayo ilifanyika chini ya maelekezo yake. Maudhui ya mikutano hii ilikuwa ni falsafa ya maada, chaguo mashuhuri kwa kikundi cha wanazuoni wa kizamani. Mutahhari mwenyewe alikuwa mwanzoni na shauku kubwa sana ya falsafa ya kuthamini mali, hususan U-maksi (Marxism), mara tu baada ya kuanza masomo juu ya elimu ya mantiki. Kwa mujibu wa kumbukumbu zake mwenyewe, mnamo karibu ya mwaka 1946 alianza kuzichunguza tarjuma za Kifursi juu ya fasihi 6


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 7

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya ya U-maksi zilizochapishwa na kikundi cha Tudeh, chama kikuu cha Umaksi ndani ya Iran na kwa wakati ule, nguvu muhimu katika medani ni kisiasa. Kwa nyongeza, alisoma maandishi ya Taqi Arani, mnadharia mkuu wa kikundi hicho cha Tudeh, na vile vile makala za U-maksi kwa lugha ya kiarabu kutoka Misri. Mwanzoni alipata ugumu katika kuyaelewa matini haya kwa sababu alikuwa hajazizoea istilahi za kifalsafa za kisasa, lakini kwa jitihada za kuendelea (ambazo zilihusisha utengenezaji wa mukhtasari wa Kanuni za Georges Pulitzer za Msingi wa Falsafa), alikuja kulimudu somo lote la falsafa ya kuthamini mali. Ustadi huu ulimfanya kuwa mchangiaji muhimu katika mizunguko ya Taba’tabai na baadae, baada ya kuhamia kwake Tehran, akawa mpambanaji madhubuti kabisa katika vita vya kiitikadi dhidi ya Umaksi na tafsiri za Uislamu zenye athari za ki-maksi. Makanusho yasiyo na idadi yameandikiwa insha nyingi katika ulimwengu wa kiislamu, kote, ndani ya Irani na kwingineko, lakini takriban, zote zimeshindwa kuvuka kwenda mbele zaidi, ya kutokupatana kwa dhahiri kwa umaksi na imani za kidini na kushindwa kwa kisiasa na kutowiana kwa vyama vya kisiasa vya kimaksi. Mutahhari, kwa kinyume chake, alikwenda kwenye mizizi ya kifalsafa ya jambo lenyewe na akadhihirisha kwa mantiki ya kisheria haswa na hali halisi ya kinadharia isiyo na msingi, ya kanuni kuu za umaksi. Maandishi yake ya kimjadala yanaainishwa zaidi kwa akili kuliko nguvu ya ufasaha wa usemaji au ya hisia za jazba. Hata hivyo, kwa Mutahhari, falsafa ilikuwa ni zaidi kupita kiasi cha kuwa chombo cha mjadala au kudhibiti akili; ilikuwa ni mtindo makhsusi wa udini, njia ya kuuelewa na kuundeleza Uislamu. Mutahhari anatokana, kwa kweli, na jadi ihusikanayo na falsafa ya ki-Shi’ah ambayo inarudi nyuma angalau, mpaka kwa Nasir ad-Din Tusi, mmoja wa mashujaa binafsi wa Mutahhari. Kusema kwamba 7


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 8

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya mtazamo wa Mutahhari juu ya Uislamu, ulikuwa wa kifalsafa sio kumaanisha kwamba hakuwa na thamani na mambo ya kiroho, au alikusudia kuuweka mfumo wa imani ulioteremshwa, chini ya tafsiri za kifalsafa na kuweka istilahi za kifalsafa juu ya nyanja zihusikanazo kidini; bali ina maana kwamba yeye alichukulia ule upatikanaji wa elimu na kuelewa kama ndio lengo kuu na manufaa ya dini na kwa sababu hiyo alitoa kwenye falsafa, kiasi fulani cha ubora miongoni mwa nidhamu zinazolelewa katika taasisi za kidini. Katika hili, yeye alikuwa katika kuhitilafiana na ile idadi kubwa ya wanazuoni ambao kwao wao, fiqh ilikuwa iwe ndio alfa na omega - mwanzo na mwisho wa somo, na watu wa kisasa, ambao kwao falsafa imewakilisha mdukizo wa kiyunani kwenye ulimwengu wa Kiislamu, na wale wote ambao kwamba kwao shauku ya kimapinduzi ilikuwa imefanywa kukosa subira kwa fikra makini za kifalsafa.3 Shule makhsusi ya falsafa ambayo Mutahhari alishikamana nayo ni ile ya Mulla Sadra, iliyoitwa Hikmat-i Muta’aliya - “Falsafa ya Juu” ambayo inatafuta kukusanya mbinu za umaizi wa kiroho na zile za matokeo ya tafsiri za kifalsafa. Mutahhari alikuwa ni mtu wa hali ya utulivu na shwari katika mwenendo wake wa kijumla na katika maandishi yake. Hata alipokuwa anashughulika na mijadala, alikuwa siku zote muungwana na kwa kawaida alijizuia kuwa na maneno yenye jazba na ya kejeli. Lakini alikuwa na utiifu mkubwa sana kwa Mulla Sadra kiasi kwamba angeweza kumtetea yeye kwa hisia kali hata dhidi ya shutuma ndogo au ya dharura, na alimchagulia mjukuu wake wa kwanza – na pia kwa ajili ya ile nyumba ya uchapishaji ya Qum ambayo ilitoa vitabu vyake – kuitwa kwa jina la Sadra. 3 Maelezo ya kuaminika juu ya maoni haya yalitolewa na Sayyid Qutb katika kitabu chake; Khasa’is al-Tasawwur al-Islami wa Muqawwimatuhu, Cairo, chapa nyingi, ambacho kilitarjumiwa kwa Kifursi na kilikuwa na kiasi cha athari juu ya maoni kuhusu falsafa. 8


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 9

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kwa kadiri ambavyo Shule ya Falsafa ya Sadra inavyojaribu kuunganisha zile mbinu za mwanga wa ndani na tafakari ya kiakili, haishangazi kwamba imekuwa yakupatwa na tafsiri zenye kutofautiana kwa upande wa wale walioelekea zaidi kwenye mbinu moja kuliko nyingine. Kuamua kutokana na maandiko yake, Mutahhari alikuwa anatokana na wale ambao kwamba, kwao mpanuko wa kielimu wa ile Shule ya Sadra ulikuwa umekwishazagaa; kuna kiasi kidogo sana cha hali ya wazi ya muujiza au ya kiroho iliyopatikana katika wale watetezi wengine wa dhana ya Sadri, labda kwa sababu Mutahhari aliuona uzoefu wake wa ndani kama usiopasika katika kazi ya mafundisho ambamo alikuwa ameshikamanishwa, au angalau kama siri ya ndani ambayo alipaswa kuificha. Linalowezekana sana hata hivyo, huu upendeleo wa mpanuko wa kweli hasa wa kifalsafa wa ile “Falsafa ya Juu” ulikuwa ni udhihirisho wa moyo na kipaji cha Mutahhari mwenyewe. Kwa hili, alitofautiana sana na mshauri wake maarufu, Ayatullah Khumayni, ambaye maelezo yake mengi ya kisiasa yanaendelea kuenezwa pamoja na lugha na shughuli za usufi na kiroho. Mnamo mwaka 1952, Mutahhari aliondoka Qum na kuelekea Tehran, ambako huko alimuoa binti ya Ayatullah Ruhani (q.s.) na akaanza kufundisha falsafa katika Madrassa ya Marwi, moja ya taasisi kuu za masomo ya kidini katika mji mkuu huo. Huu haukuwa ndio mwanza wa kazi yake ya ufundishaji, kwani tayari alipokuwa Qum alikuwa ameanza kufundisha baadhi ya masomo fulani – Mantiki, Falsafa, Masomo ya Dini (theologia) na Fiqh – akiwa yeye mwenyewe binafsi bado ni mwanafunzi. Lakini inaelekea Mutahhari alikuwa akikosa subira hatua kwa hatua na hali ya hewa iliyodhibitiwa ya Qum, pamoja na ugawanyikaji kimakundi uliokuwapo miongoni mwa baadhi ya wanafunzi na walimu wao, na pamoja na kujitenga kwao na shughuli za kijamii. Matarajio yake binafsi ya baadaye hapo Qum pia yalikuwa hayana uhakika. 9


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 10

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Hapo Tehran, Mutahhari alibaini uwanja mpana zaidi na wa kuridhisha wa shughuli za kidini, kielimu na mwishowe za kisiasa. Mnamo mwaka 1954, yeye aliitwa kufundisha falsafa katika Kitivo cha Theologia na Elimu za Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Tehran, ambapo alifundisha kwa miaka ishirini na mbili. Kwanza uhalalishaji wa ajira yake na kisha kupandishwa cheo kuwa profesa kulicheleweshwa na wivu wa washiriki wenzie duni na kwa fikra za kisiasa (kwani ukaribu wa Mutahhari kwa Ayatullah Khumayni ulikuwa unajulikana sana). Lakini kuwepo kwa mtu kama Mutahhari katika chuo kile cha kisekula (cha kilimwengu) kulikuwa ni muhimu na kunakofaa sana. Watu wengi wenye msingi wa madrasa walikuwa walikwishakuja kufundisha katika Vyuo vikuu, na mara nyingi walikuwa ni wenye maarifa makubwa. Hata hivyo, takriban wote, bila kumtoa hata mmoja, wao walikuwa wameiacha falsafa ya maisha, ya kiislamu, pamoja na vilemba na majoho yao. Mutahhari, tofauti na wao, alikuja chuoni hapo kama mfasiri mwenye uwezo na asiye na shaka, wa elimu hikma za Kiislamu, takriban kama balozi wa taasisi hiyo ya kidini kwa wale waliosomeshwa kidunia. Idadi kubwa ya watu walivutika kwake, kwani ule uwezo wa ufundishaji aliokuwa ameuonyesha mwanzo kule Qum, sasa ulikuwa umejitokeza wazi kabisa. Katika kuongezea kujenga sifa yake kama mhadhiri maarufu na mwenye nguvu wa Chuo Kikuu, Mutahhari alishiriki katika shughuli za jumuiya za kitaalamu nyingi za Kiislamu (Anjumanha) ambazo zilikuja kuwepo chini ya uangalizi wa Mahdi Bazargan na Ayatullah Taleqani (q.s.), akiwahadhiri madaktari, wahandisi na waalimu wao na kusaidia kuziratibu kazi zao. Idadi kadhaa ya vitabu vya Mutahhari vimekuwa na nakala zilizosahihishwa za mtiririko ya mihadhara yake iliyohadhiriwa kwenye jumuiya hizo za Kiislamu.

10


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 11

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Matakwa ya Mutahhari ya msambao mpana wa elimu ya kidini katika jamii na uwekezaji wa nguvu na wa kufaa wa wanazuoni wa kidini katika shughuli za kijamii kulimfanya mnamo mwaka 1960 atwae uongozi wa kikundi cha maulamaa wa mjini Tehran kilichojulikana kwa jina la “Anjuman-e-Mahana-yi Dini” (Chama cha Kidini cha kila Mwezi). Wajumbe wa kikundi hiki, ambacho kilikuwa ni pamoja na Ayatullah Beheshti (q.s.) mwanafunzi mwenzie Mutahhari huko Qum, walitayarisha hotuba za hadhara za kila mwezi, zilizoundwa sambamba na kuonyesha uhusiano wa Uislamu na shughuli za kisasa, na kuamsha fikra za kimageuzi miongoni mwa Ulamaa. Hotuba hizo zilichapishwa chini ya kichwa cha maneno: “Guftar-e-Mah” (Hotuba za kila Mwezi) na zikathubutu kuwa maarufu sana, lakini serikali ikazipiga marufuku mnamo mwezi wa Machi, 1963 wakati Ayatullah Khumayni alipoanza shutuma zake za wazi juu ya utawala wa Pahlavi. Jaribio muhimu sana mnamo mwaka 1965, la aina hiyo hiyo, lilikuwa ni kuanzishwa kwa Husayniya-e-Irshad, taasisi iliyokuwa Tehran kaskazini, iliyoundwa ili kupata utii kwenye Uislamu, wa vijana walioelimishwa kidunia. Mutahhari alikuwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya uongozi; yeye pia alihadhiri katika hiyo Husayniya-e-Irshad na kuhariri na kuchangia kwenye baadhi ya machapisho yake. Taasisi hiyo iliweza kuvuta makundi makubwa kwenye shughuli zake, lakini mafanikio haya – ambayo bila shaka yaliendeleza matumaini ya waanzilishi wake, yalizingwa na idadi fulani ya matatizo ya ndani. Mojawapo ya matatizo kama hayo lilikuwa ni yale mazingira ya kisiasa ya shughuli za taasisi, ambayo yalizusha maoni yanayokhitilafiana juu ya uwezekano wa kutoka nje ya uhadhiri wa kuleta mabadiliko na kwenda kwenye makabiliano ya kisiasa.

11


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 12

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Neno la kuzungumza kwa kawaida linabeba uzito wenye nguvu na wa haraka katika kuinua mabadiliko ya kimapinduzi kuliko neno la kuandikwa, na itawezekana kupanga mkusanyiko wa fasihi za hotuba, mawaidha na mihadhara muhimu ambayo yamebaba yale Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Lakini ubainishaji wa kadiri (iliyomo) au uwezo wa kiitikadi wa mapinduzi hayo na mipaka yake kutoka madhehebu pinzani au shindani umetegemea zaidi kwenye juu ya neno la kuandikwa, katika utungaji wa vitabu ambavyo vinaelezea kwa kinaganaga kanuni ya Kiislamu katika muundo wa hatua kwa hatua, pamoja na mazingatio maalum kwenye matatizo na shughuli za wakati huu. Katika nyanja hii mchango wa Mutahhari ulikuwa wa kipekee katika ukubwa na upeo wake. Mutahhari aliandika kwa uangalifu sana na kwa mfululizo, kuanzia siku za uanafunzi wake huko Qum hadi mwaka 1979, mwaka wa kifo chake cha kishahidi. Mengi ya matoleo yake yalitambulika kwa mwelekeo wake ule ule wa kifalsafa na msisitizo ambao umekwishafahamika, na huenda alikichukulia kuwa kama kitabu chake muhimu hiki, Usul-e-Falsafa wa Ravish-e-Ri’alism (Kanuni za Falsafa na Utaratibu wa Uhalisia), ambacho ni taarifa za maandishi za mihadhara ya Tabatabai kwenye mfululizo wa kila Alhamisi usiku huko Qum, yenye kijalizo cha maoni ya Mutahhari. Lakini hakuzichagua maudhui za vitabu vyake kwa shauku yake binafsi au upendeleo, bali kwa kutambua kwake ile haja, popote pale ambapo kitabu kilikuwa kinakosa mada muhimu za maslahi ya Kiislam ya wakati huu, yeye Mutahhari alijaribu kukipatia. Peke yake kabisa, yeye alianza kujenga misingi mikuu ya maktaba ya kisasa ya Kiislamu. Vitabu kama vile “Adl-e-Ilahi” (Uadilifu wa ki-ungu), “Nizam-e-Huquq-e-Zan dar Islam” (Mfumo wa Haki za Wanawake katika Uislamu), “Mas’ala-yi Hijab” (Masuala ya Hijabu), “Ashna’i ba Ulum-e-Islami” (Utangulizi juu ya Elimu za 12


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 13

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kiislamu), na “Muqaddima bar Jahanbini-yi Islami” (Utangulizi juu ya falsafa ya maisha ya Uislamu), vyote vilikusudiwa kukidhi haja, kuchangia kwenye uelewa sahihi na wa mpangilio wa Uislamu na matatizo yaliyoko ndani ya jamii ya Kiislamu. Vitabu hivi vinaweza kuchukuliwa hasa kama mchango wa kudumu na muhimu sana wa Mutahhari kwenye kuzaliwa upya kwa Iran ya Kiislamu, lakini utendaji wake pia ulikuwa na kiwango fulani cha kisiasa ambacho kwa hakika ni tegemezi, kisije kikaacha kutiliwa maanani. Wakati akiwa mwanafunzi na mwalimu asiye na uzoefu huko Qum, alijitahidi kudukiza utambuzi wa kisiasa katika watu wa rika lake na alikuwa karibu sana hususan na wale ambao miongoni mwao walikuwa wajumbe wa Fida’iyan-i Islam, chama cha kijeshi kilichoanzishwa mnamo mwaka 1945 na Nawwab Safawi. Makao makuu ya Fida’iyan hapo Qum yalikuwa ndio Madrasa-yi Fayziya, ambamo humo Mutahhari mwenyewe alikuwa akiishi, na alijitahidi sana bila mafanikio kuwazuia wasiondolewe kutoka kwenye Madrasah hiyo na Ayatullah Burujerdi ambaye alikuwa amejiweka kishupavu kabisa dhidi ya makabiliano yoyote ya kisiasa na utawala wa Shah. Wakati wa mapambano kwa ajili ya utaifishaji wa Biashara ya Mafuta ya Iran, Mutahhari aliunga mkono juhudi za Ayatullah Kashani (Quddisa Sirruh) na Dr. Muhammad Musaddiq, ingawa alimlaumu huyu Dr. Muhammad kwa kushikamana kwake na uzalendo wa kisekula. Baada ya kuhama kwake kwenda Tehran, Mutahhari alishirikiana na Chama cha Kupigania Uhuru cha Bazargan na Taleqani, lakini hakuwa kamwe mmoja wa watu mashuhuri wa kundi hili. Makabiliano yake mazito ya kwanza kabisa na utawala wa Shah yalikuja wakati wa maasi ya Khurdad 15 mwaka 1342 sawa na tarehe 6 Juni 1963, ambapo alijidhihirisha kuwa mfuasi wa Ayatullah Khomeini kisiasa na kielimu kwa kugawa matangazo yake na kuomba kuungwa mkono juu yake 13


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 14

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya katika hotuba alizozitoa.4 Matokeo yake alikamatwa na kushikiliwa kwa siku arobaini na tatu. Baada ya kuachiwa kwake, alishiriki kwa bidii sana katika vyama mbalimbali vilivyokuja kujitokeza katika kudumisha ile kasi ambayo ilikuwa ameanzishwa na yale maasi, cha muhimu sana kikiwa ni kile Chama cha Kijeshi cha Wanazuoni wa Kidini (Jami’a yi Ruhaniyat-eMubariz). Mnamo Novemba ya mwaka 1964, Ayatullah Khomein aliingia katika mwaka wake wa kumi na nne wa ukimbizi, aliokaa kwanza huko Uturuki na halafu huko Najaf, na katika kipindi chote hiki, Mutahhari alibaki kuwa na mawasiliano na Ayatullah Khomeini kwa njia zote, moja kwa moja – kwa kutembelea Najaf – na kwa njia zisizo dhahiri. Wakati mapinduzi ya Kiislamu yalipokaribia kilele chake cha ushindi katika majira ya baridi kali ya mwaka 1978 na Ayatullah Khomeini akaondoka Najaf kuelekea Paris, Mutahhari alikuwa miongoni mwa wale waliosafiri kwenda Paris kukutana na kuzungumza naye. Ukaribu wake na Ayatullah Khomeini ulithibitishwa na kule kuchaguliwa kwake kwenye Baraza la Mapinduzi ya Kiislamu, ambalo kuwepo kwake Baraza hilo kulitangazwa na Ayatullah Khomeini mnamo tarehe 12, Januari ya mwaka 1979. Huduma za utumishi za Mutahhari kwenye hayo Mapinduzi ya Kiislamu zilikatizwa kikatili kwa kule kuuliwa kwake mnamo Mei mosi ya mwaka 1979. Mauji haya yalifanywa na kundi moja lililojulikana kama Furqan, ambalo lilidai kuwa ni waongozaji wa “Uislamu wa Kimaendeleo,” kundi ambalo liko huru kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kupotosha mvuto wa wanazuoni wa kidini. Ingawa Mutahhari anaonekana kuwa mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Kiislamu wakati wa mauaji yake, lakini ilikuwa ni kama mwanafikra na mwandishi hivyo alivyouawa kishahidi. Mnamo mwaka 1972, Mutahhari alichapisha kitabu kilichoitwa ‘Illal-i 4 Jina la Mutahhari ni la tisa katika orodha ya watu wa kuwekwa kizuizini ya maandishi iliyotayarishwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa kijeshi mnamo Juni, 1963. Angalia nakala halisi ya maandishi hayo katika Dihnavi, Qiyaam-e-Khunin-i 15 Khurdad 42 ba

Rivayat-Asnad, Tehran, 1360Sh/1981, uk. 77. 14


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 15

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Girayish ba Maddagari’ (Sababu za Kugeukia kwenye Uyakinifu), kitabu muhimu kinachochambua usuli wa kihistoria wa uyakinifu (tamaa ya anasa) katika Ulaya na Irani. Wakati wa mapinduzi, aliandika utangulizi kwenye toleo na nane la kitabu hiki, akishambulia upotoshaji wa mawazo ya Hafidh na Hallaj ambayo yamekuwa ndio ya kimtindo katika sehemu za jamii ya Ki-Irani na kuzikanusha tafsiri fulani za kiyakinifu juu ya Qur’ani Tukufu. Chanzo cha tafsiri hizi kilikuwa ni lile kundi la Furqan, ambalo lilijaribu kuzikataa dhana za msingi za Qur’ani kama vile uwezo wa kimungu usio na mipaka na ule ukweli wa akhera. Kama kawaida katika masuala kama hayo, mwelekeo wa Mutahhari ulikuwa na mvuto na ushawishi, hana hasira au kushutumu, na alikaribisha pia majibu kutoka kundi la Furqan na makundi mengine yaliyotaka kutoa maoni juu ya kile alichokuwa amekiandika. Jibu lao pekee lilikuwa ni bunduki. Tishio la kuwauwa wote ambao walikuwa wanapingana nao lilikuwa tayari limo ndani ya machapisho ya Furqan, na baada ya uchapishaji wa toleo jipya la Illal-e-Girayish ba Maddigari, ni dhahiri kwamba Mutahhari alikuwa na jakamoyo kiasi fulani juu ya kuuawa kwake. Kulingana na ushahidi wa mwanawe, Mujtaba, namna fulani ya kutengwa kwenye shughuli za kidunia ulikuwa ukionekana juu yake, alizidisha swala na du’a zake za usiku na usomaji wa Qur’ani, na wakati mmoja aliota kwamba yuko mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Ayatullah Khomeini (Quddisa Sirruh). Siku ya Alhamisi ya tarehe 1 Mei, 1979, alikwenda kwenye nyumba ya Dr. Yadullah Sahabi pamoja na wajumbe wengine wa Baraza la Mapinduzi ya Kiislamu. Wakati wa takriban saa 4:30 usiku, yeye pamoja na mshiriki mwingine katika mkutano huo, Mhandisi Katira’i, waliondoka nyumbani kwa Sahabi. Akitembea peke yake kuelekea kwenye kichochoro cha karibu yake ambako ile gari ambayo ilikuwa imchukue kumpeleka nyumbani ilikuwa imeegeshwa, Mutahhari ghafla akasikia sauti ngeni asiyoifahamu ikimwita. Aligeuka kuangalia sauti hiyo imetokea wapi, na alipofanya hivyo, risasi ikampiga kwenye paji la uso, ikipenya chini ya ndewe ya sikio 15


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 16

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya la kulia na kutokea juu ya nyusi za jicho la kushoto. Alikufa takriban papo hapo, na ingawa alikimbizwa kwenye hospitali ya karibu, hapakuwa na chochote cha kuweza kufanywa isipokuwa kuomboleza kwa ajili yake tu. Mwili wake uliachwa pale hospitalini siku iliyofuatia, na kisha siku hiyo ya Alhamisi, katikati ya maombolezo yaliyotapakaa, ulichukuliwa kwa ajili ya kwenda kuswaliwa kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Tehran na halafu huko Qum kwa ajili ya mazishi, karibu na kaburi la Sheikh Abdul Karim Ha’iri (Quddisa Sirruh). Ayatullah Khomeini (r.a.) alilia wazi wazi hadharani wakati Mutahhari alipokuwa anazikwa hapo Qum, na akamwelezea kama “mwanangu mpendwa,” na kama “tunda la maisha yangu,” na “kipande cha nyama yangu.” Lakini katika taabini yake Ayatullah Khomeini pia alisema kwamba pamoja na kuuawa kwa Mutahhari, haiba yake haijapunguzwa, wala njia na lengo la mapinduzi halijavurugwa. “Wapenda maovu nawajue kwamba kwa kuondoka kwa Mutahhari – haiba yake ya Kiislamu, falsafa yake na elimu yake havijatutoka sisi. Vyama haviwezi kuharibu haiba ya Kiislamu ya mtu huyu mashuhuri wa Uislamu…….. Uislamu unakua na kuendelea kupitia mihanga na vifo vya kishahidi vya wale vipenzi wake. Tangu wakati wa kufunuliwa kwake hadi wakati huu wa sasa, Uislamu siku zote umeambatana na vifo vya kishahidi na ushujaa.”5 Umashuhuri na urithi wa Ayatullah Mutahhari kwa hakika vimedumu bila kusahaulika katika Jamhuri ya Kiislamu, kwa kiwango ambacho uwepo wake (kiroho) baada ya kufa kwake umekuwa na mvuto takriban kama mafanikio yake katika maisha yake. Maadhimisho ya kumbukumbu ya kuuawa kwa kishahidi yanaadhimishwa kama kawaida, na picha yake imeenea kote ndani ya Irani. Mengi ya maandishi yake yaliyokuwa hayajachapishwa sasa yanapigwa chapa kwa mara ya kwanza, na mkusanyiko 5 Maandishi ya taabini – maneno ya kusifu – ya Imam Khomeini katika kitabu Yadnama-yi Ustad-i Shahid Murtadha Mutahhari, uk. 3 – 5. 16


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 17

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya wote wa kazi zake sasa unasambazwa na kusomwa kwa kiwango kikubwa mno. Katika maneno ya Ayatullah Khamenei; Raisi wa Jamhuri ya Irani, vitabu vya Mutahhari vimekuja kuanzisha “muundombinu wa kielimu wa Jamhuri ya Kiislamu.” Juhudi hatimae zimo mbioni kueneza elimu ya maandishi ya Mutahhari nje ya nchi zinazozungumza Kifursi vile vile, na Wizara ya Uongozi wa Kiislamu imedhamini tafsiri ya vitabu vyake katika lugha mbali mbali kama ki-Hispania na ki-Malay. Kwa kuleta maana hata hivyo, itakuwa ni kumbukumbu inayofaa sana kwa Mutahhari kama Irani ya kimapinduzi itathibitisha kuweza kuunda serikali, jamii, uchumi na utamaduni ambavyo kiuhakika na kwa uaminifu kabisa ni vya Kiislamu. Kwani maisha ya Mutahhari yaliekezwa kwenye lengo ambalo linakuza zaidi motisha ya mtu binafsi, na kuuawa kwake kishahidi kulikuwa ndio onyesho la mwisho la kufichika huko kwa tabia.

“Walinganie watu kwenye njia ya Mola Wako kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora zaidi. Bila shaka Mola Wako anawajua vizuri sana wale waliopotea kutoka kwenye njia Yake na anawajua vema wale ambao wameongoka.” (Suratun-Nahl; 16:125) Kwa kweli, mjadala kwa ajili ya makala hii ambao utaelezwa chini ya maudhui ya “Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya” unahusiana hasa na wajibu wa kawaida ambao unawahusu Waislamu wote kwa jumla na hususan wale Waislamu ambao wanashikilia nafasi za uongozi rasmi wa kidini katika jamii. Kuna kanuni katika Uislamu ambayo wote tunaijua na inaeleza kwamba: Ndani ya chagizo tukufu la Uislamu, majukumu yamegawiwa miongoni mwa watu. Kwa hili tunamaanisha kwamba watu 17


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 18

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya ni wachunga na wanawajibika juu ya kila mmoja na tunashiriki katika wajibu huu kwa kila mmoja wetu.

“Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja atawajibika juu ya kile alichokichunga.� Bali hasa, kila kizazi ni mlezi na kinawajibika juu ya kizazi kingine. Kila kizazi kinawajibika juu ya kizazi kinachofuatia baada yao na kina wajibu wa kuhakikisha kwamba dini na mwongozo ambao umetolewa kwa kizazi kilichopita ambavyo vimelindwa na kupitishwa kutoka mkono hadi mkono na vikakifikia kizazi kilichofuatia, vinaweza kupitishwa kwa zamu na kupewa vizazi vijavyo. Kwa hiyo, kila kizazi kinachopita lazima kiwe tayari na kiwe kimeandaliwa kupokea mafundisho (ya dini) na kuyatumia vizuri iwezekanavyo. Kwa hiyo, mjadala wa uongozi wa vijana ni mjadala ambao pia unajumuisha majukumu ambayo sisi sote tunawajibika kuutimiza. Jambo ambalo tunalitanguliza katika mjadala huu kama nguvu isiyojulikana na ambayo ni lazima tufikirie kwa makini kuhusu nguvu hiyo na kujaribu kutafuta namna ya kuiboresha, inaweza kuelezewa kukwa ni kama ifuatayo: Uongozi na mwongozo wa mtu binafsi au hata wa kizazi kizima hauchukui sura katika namna na tabia zile zile ndani ya matukio na hali zinazobadilika (katika nyakati tofauti) – bali huwa ni tofauti. Hivyo muundo wa uongozi ni lazima pia uchukue mitindo na taratibu tofauti. Njia na namna zinazotu mika katika uongozi huu pia hutofautika, na agizo moja tu la jumla haliwezi kutolewa, ambalo litaweza kufanya kazi kwa watu wote na vizazi vyote vinavyoishi katika nyakati tofauti.

18


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 19

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kutokana na ukweli huu, katika kila zama na pale tunapoishi katika chini ya hali tofauti, ni lazima tufikirie kwa makini kuhusu jambo hili na kwa kutafakari, ni lazima tuone ni kwa namna gani uongozi na utawala unaweza kuchukua sura na ni agizo gani lazima litolewe kwenye jamii. Aina mbili za wajibu: Katika hotuba ambayo niliitoa katika uwanja huu huu chini ya mada ya “Amr bil Ma’ruf wa Nahi ‘Anil Munkar” (kuamrisha mema na kukataza maovu), niligusia kwenye nukta ambayo nitairudia hapa nayo hiyo ni: wajibu wetu wa kidini uko wa namna mbili – wajibu mwingine unahusiana na utendaji wa wa kazi ambao unapata sura katika mtindo au muundo maalum. Vipengele vyote muhimu vya kazi iliyobainishwa na sehemu zake moja moja zimeelezwa na dini ya Kiislamu na tumeambiwa kwamba ni lazima tutekeleze tendo maalum katika muundo wake ulioanishwa tukishikilia masharti yake mahususi. Bila shaka, tendo hilo mahsusi limeagizwa kutendwa (na Allah swt.) na kuna sababu juu yake hilo, hata hivyo hatuhusiki na matokeo au athari za kitendo hicho. Namna hizi za vitendo zinajulikana kama Ta’abudiyat (mambo ambayo yametungiwa sheria ambayo ni lazima tuyafuate kama matendo ya ibada). Ni aina hii ya matendo ambayo tunaweza pia kuyataja kama yale ambayo ni “Wajibu wa Mtindo na muundo wa Matendo.” Kwa mfano, Swala ni tendo ambalo lina kitendo tangulizi kinachohusiana nayo (Wudhu, Tayammam, Josho) na shuruti (zinazohusiana nayo); ina maandalizi fulani maalum na sehemu juu yake; yapo vile vile mambo yaliyoainishwa ambayo hayatakiwi kufanywa na mambo fulani yanayobatilisha Swala hiyo. Tumeamrishwa kutekeleza Swala bila kujali mazingira, na katika mtindo na muundo wake mahususi ndio muundo halisi kabisa wa kuzitii amri za Allah swt. Kwa hakika hata hivyo, hiki kitendo cha swala katika muundo wake maalum imeamriwa kwa ajili ya athari au matokeo – kuna matokeo ya moja kwa moja katika utekelezaji wa tendo 19


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 20

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya hili.

“Hakika swala humuweka mtu mbali na uchafu na maovu.” (Ankabut;29: 45) Sisi hasa tunawajibika tu na kulitekeleza tendo hili na hatuhusiki na matokeo ambayo tendo hili litasababisha. Endapo kama tunalifanya tendo hili katika ile njia sahihi na kamilifu kama tulivyoonyeshwa na jinsi tulivyoagizwa kulitenda, basi bila shaka hayo matokeo (ya kujiweka wenyewe mbali na maovu na uchafu) yatafuatia. Aina ya pili ya wajibu tulionao katika imani ya Uislamu unatajwa kama “Wajibu wa Matokeo.” Kwa hili tunayo maana kwamba matokeo au athari ya mwisho ya tendo pia ni wajibu wa mtu mwenyewe. Kama vile tu mtu wakati mwingine husema, “Ninataka kadha na kadhaa ya matokeo kwa ajili ya kitendo changu hiki.” Hata hivyo kuhusu ni jinsi gani matokeo hayo yatakavyojitokeza – kupitia njia gani na hatua zipi za mwanzo, kwa masharti gani na ni vipi yatakavyotekelezwa hayo – ni lazima tueleze kwamba yanapaswa kutekelezwa kwa njia bora zaidi iwezekanavyo, hata hivyo hakuna njia moja pekee, imara na yenye kuelezeka ambayo ni lazima ifanywe. Bali hasa, namna, taratibu na kupitia njia gani matokeo haya yanaweza kupatikana, zinabadilika pamoja na wakati na mahali. Ngoja nikupeni mfano. Hebu natuchukulie kwamba unalo tatizo fulani – kwa mfano, mmoja wa marafiki zako yuko jela. Kuna wakati ambapo unategemea kazi maalum ya kukamilishwa kutoka kwa mtu maalum kuhusiana na tatizo hilo ambalo mmo wewe na rafiki yako. Kwa mfano, rafiki yako anampa mtu mwingine barua na anamwambia kwamba ahakikishe kwamba anaitoa barua hiyo kwa mtu maalum – na hilo pia kwa wakati maalum. Ni wazi kwamba tunaweza kusema kuwa barua hii iliandikwa kwa madhumuni na lengo, hata hivyo yule mtu mwingine anahusika tu na 20


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 21

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya kuiwasilisha barua hiyo kwa yule mtu uliyemuanisha. Wakati mwingine, wewe unataka kuyafikia matokeo hayo wewe mwenyewe binafsi moja kwa moja na hivyo, huna haja ya hatua za mwanzo. Unamwambia rafiki yako kwamba unamtaka akusaidie kukutoa jela – hata hivyo, ni kwa kupitia njia na namna gani itakayotumika – haya hukuyaainisha wewe. Mtu huyo mwenyewe ni lazima aende na kuona ni njia gani bora ya kuitekeleza kazi hii. Kwa kawaida aina hizi za wajibu huchukua sura pale ambapo njia za kuifanyia kazi hiyo sio za namna moja – ikiwa na maana kwamba mtindo hubadilika. Katika mfano mmoja, mtu lazima atumie njia au utaratibu fulani, na katika wakati mwingine, ni lazima atumie utaratibu mwingine – umaalumu wa wakati na mahali ambapo alipo na kwa nyongeza, mambo mengine yanaweza yakatofautiana. Katika namna hizi za mifano, mtu lazima akae chini atafakari, afikiri na kupata njia bora zaidi iwezekanayo ya kuyafikia matokeo. Ndani ya dini ya Kiislamu, tunazo aina zote za wajibu. Swala, Saumu na matendo yote ya ibada huunda ule muundo wa kwanza wa wajibu; na mambo kama Jihadi (ule ulinzi mtakatifu wa Waislamu na nchi za Kiislamu) yanaunda ule muundo wa pili wa wajibu. Kuhusiana na Jihad, Waislamu wana wajibu wa kutetea kiini cha Uislamu na kulinda uhuru wa Waislamu – hata hivyo ni kwa kutumia njia gani? Je, wanailinda njia hiyo (Uislamu) kwa kutumia upanga, bunduki, au kitu kinginecho? Mambo haya hayakuainishwa na kimsingi, mambo ya namna hii hayawezi kuanishwa na kuwekewa matumizi ya jumla! Katika kila zama moja, Waislamu wanafaradhishwa kuchagua njia na taratibu bora za kutekelezea jukumu hili (la ulinzi):

21


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 22

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

“Na waandalieni nguvu kiasi muwezavyo, na kwa farasi waliofungwa (kwa maandalizi hayo) muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengine wasiokuwa wao, msiowajua, Mwenyezi Mungu anawajua. Na chochote ambacho mtakachokitoa katika nji ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa kamili na nyinyi hamtadhulumiwa. (al-Anfal; 8:60) Kwa hiyo ni lazima tuangalie – ni namna au taratibu gani wa muongozo katika kila wakati na kila zama? Jambo la mwongozo na uongozi linahusiana na ule muundo wa pili wa wajibu uliotajwa. Waislamu wanawajibika juu ya mwongozo wa kila mmoja wao kwa mwingine. Kila kizazi kinawajibika kwa mwongozo juu ya kizazi kinachofuatia – hususan wale watu ambao wanatambulika rasmi kama viongozi wa jamii – wao wana wajibu mkubwa zaidi. Kwa hali yoyote, matokeo haya – kwa maana ya yale ya kupata muundo na namna ya mwongozo – ni lazima yapatikane. Hata hivyo, kuhusu njia na taratibu ambazo ni lazima zitumike kufikia lengo hili, hizi zimeanishwa au kutengwa kwa ajili ya nyakati maalum na/au kwa kudumu. Aya tukufu za Qur’ani zinaeleza:

“Enyi mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na za watu wenu kutokana na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, ………. (at-Tahrim; 66:6) 22


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 23

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Ayah ii ina maana kwamba ni lazima tujilinde wenyewe na familia zetu kutokana na Moto wa Jahannam ambao kuni zake ni mawe na watu. Hivyo, tunaona kwamba kuna matokeo ambayo ni lazima tuyafikie, ambayo ni kujiokoa wenyewe na familia zetu, hata hivyo, njia ya kuyafikia matokeo haya haikuainishwa. Kakika Uislamu, hakuna utaratibu kamilifu, sahihi wa mia kwa mia wa mwongozo na uongozi ambao umeainishwa, ambao ndani yake sehemu zote – ikiwa ni pamoja na hatua za utangulizi, miundo na masharti, na mambo ambayo ni lazima yafanywe, ambao umetajwa. Kimsingi mambo haya hayawezi kuanishwa na kuwekwa mbele kwa vile yanatofautiana (kulingana na wakati na mahali ambapo mtu anaishi). Uongozi (wa jumla) wa watu sio sawa kama swala ambayo ni suala la utii kwa Mwenyezi Mungu swt., au kwa mfano usomaji wa manuizi au tahajia ambamo mtu anakariri kile ambacho anataka kukisoma kuwaroga na kuwadhibiti nge au nyoka pale wakati wowote nge au nyoka anapoweza kuja karibu ya mtu huyo, ataweza kusoma yale mambo ambayo ameyahifadhi kwa moyo kumfukuza au kumfuga mnyama mwindaji – ikiwa na maana kwamba hakuna utaratibu maalum ambao unaweza kuhusu mambo haya.

Taratibu za Uongozi ni zenye kuhusiana na za muda Kwa wakati na mahali fulani, inaweza ikawa ni kupitia jambo moja ambapo watu wanapata mwongozo, hata hivyo inawezekana kwamba katika wakati na sehemu nyingine, jambo lile lile linaweza likaongozea kwenye upotofu na kupotoshwa! Kama mantiki ile ile ambayo inamfanya mwanamke mzee asiye na elimu kuwa muumini wa kweli inatumiwa na mtu mwenye akili, mwenye elimu, 23


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 24

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya basi inaweza kwa kweli ikamfanya akawa amepotoshwa. Zaidi ya hayo, inawezekana kwamba kitabu ambacho kinakubaliana na mawazo ya wakati fulani na ambacho kinaungana na maoni ya wakati wa zama maalum na katika kiwango cha fikira zao, na ambacho kitaelekeza kwenye mwongozo wa watu (wa wakati huo), hicho kinaweza hasa kikaainishwa kuwa kama kitabu cha upotovu katika kipindi kingine cha wakati! Tunavyo vitabu ambavyo katika kipindi cha wakati wao, vilitimiza mahitaji na wajibu kwani wakati vilipoandikwa, na mamia na maelfu ya watu wakapata mwongozo kupitia vitabu kama hivyo, hata hivyo, vitabu hivyo hivyo – katika wakati wa zama zetu – havitaweza kumwongoza mtu yoyote! Vitabu hivi vinachukuliwa au kuonekana kwamba ni vyepesi sana na vinavyoweza kupelekea kwenye upotovu na kusababisha mashaka na mkanganyiko katika vichwa vya watu na hivyo, vinaweza kuanishwa kama vitabu vya upotofu – kitabu ambacho kununua na kuuzwa kwake, kuchapishwa na kusambazwa kwake hakutakosa kuwa na wasiwasi na mashaka! Inashangaza! Kitabu ambacho kimewaongoza maelfu – bali hasa mamia ya maelfu ya watu kwenye njia ya mwongozo wa kweli katika siku zilizopita, kinaweza sasa hivi kuainishwa kama kitabu cha upotofu? Ndiyo! Ukiacha kile Kitabu kitukufu (Qur’ani Tukufu) na maneno halisi ya Ma’asumin (a.s.), kitabu kingine chochote tunachozungumzia, kina ujumbe maalum ambao umelengwa kwenye muda wa kipindi maalum na chenye mipaka. Wakati zama hizo zinapokwisha, kitabu hicho tena kinakuwa hakina maana yoyote. Jambo hili ambalo nimelizungumza hivi punde tu, ni la muhimu sana, jambo la kawaida na hata siku hizi bado linaonekana kama halijulikani, geni na lisilofahamika ambalo ni lazima tulishinde, hata hivyo, jambo hili halijajadiliwa wala kutajwa. Sitarajii kwamba jambo hili litakuja kuwekwa wazi kabisa katika mkusanyiko wetu huu, kama mambo yalivyo ni lazima ielezwe kwa mwendelezo kwamba ni lazima tukubali kuwa njia za kwenye 24


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:56 AM

Page 25

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya mwongozo ni mahususi kwa vipindi vyao zenyewe. Hili likiwa limekwishasemwa, sasa tunataja uthibitisho kutoka kwenye vitabu vya Kiislamu, kuhusiana na mada hii, ili iweze kufahamika kwamba tunachokijadili hapa ni maoni yaliyoelezwa katika vitabu vya Kiislamu. Nilianza mjadala wangu kwa aya ya Qur’ani ambayo inasema:

“Uwaite watu kwenye njia ya Mola Wako kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola Wako ndiye anamjua sana aliyepotea katika njia Yake, naye ndiye awajuaye sana walioongoka. (Suratun-Nahl; 16: 125) Kutokana na makubaliano ya maoni ya wafasiri wa Qur’ani, aya hii inatuwasilishia njia tatu tofauti za kuwalingania watu, na inatupa sisi njia tatu za wazi za kuwangozea watu. Kila moja ya njia hizi tatu za mwongozo lazima zitumike katika matukio yao makhsusi. Aya hii inatuambia sisi kwamba ni lazima tuwaite watu kwenye njia ya Mola Wetu. Hili neno Mola (Rabi - ????) ni kauli maalum yenye maana ya mmoja ambaye anawajibika na malezi na uelimishaji. Kwa vile daraja hili la mwongozo ni daraja la ulinganiaji, au ualikaji na vile vile la malezi na uelimishaji, neno lililotumika hapa ni Mola. Kwa hiyo, tunaambiwa tuwaalike watu kwenye njia ya Mola Wetu – njia ambayo watu lazima waelimishwe na kufunzwa juu yake – lakini kwa kupitia namna gani? Ni lazima tutumie hekima (??????). Hekima imo katika maana ya hotuba yenye ushawishi na imara, ambayo haina imma dalili za mabishano, wala ambayo ndani yake yanaweza yakatokea mashaka. Katika istilahi za watu 25


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 26

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya wa mantiki na wanafalsafa, hii ni hotuba ambayo dibaji yake imeegemea kwenye uhakika wa mia kwa mia. Kwa hili tuna maana kwamba, watu lazima walinganiwe kwenye njia ya Mola kwa uthibitisho, hekima na ilmu ambayo ni halisi mia kwa mia, na ambayo haikuchafuliwa japo kidogo. Wafasiri wa Qur’ani Tukufu wameeleza kwamba kuwalingania watu kwa kutumia hekima ya kimantiki na kielimu, uthibitisho na ushahidi kumewekewa mipaka kwenye kundi moja maalum la watu ambao wana uwezo wa kuutumia utaratibu huu. Utaratibu wa pili ni kupitia mawaidha yenye ushawishi mzuri ??????) ikiwa na maana kwamba ni lazima tuwalinganie watu kwa Mola Wao kwa kutumia maneno mazuri, ushauri na maonyo ambayo kwamba mioyo yao na nafsi zao zitakubaliana nayo. Kuna baadhi ya watu ambao hawana uwezo wa kuzieleza imani zao kwa kutumia uthibitisho wao wa kielimu na kitaalamu, na endapo jambo la kisomi linatolewa mbele yao, mara moja wanakuwa wamechanganyikiwa. Hivyo, njia ya kuwaongoza hao ni kupitia ushauri mzuri na maonyo. Watu kama hao ni lazima waongozwe kwa kutumia hadith, simulizi na michapo juu ya matukio ya kweli, iliyoegemea kwenye hekima, na chochote kile ambacho kitaleta utulivu na kiliwazo kwenye nyoyo zao. Wajibu wa ushawishi na ushauri mzuri ni kufanya kazi kwenye moyo wa mtu, ambapo kazi ya elimu na uthibitisho wa kimantiki unashughulika na akili na uwezo wa mtu wa kufikiri. Idadi kubwa ya watu bado wako kwenye daraja la kutegemea mambo ambayo wanayaamini, juu ya nyoyo, nafsi na hisia, na hawako kwenye daraja la kutumia akili na fikra zao. Hatua ya tatu ni ile ya kujadiliana na watu kwa njia bora kiasi iwezekanavyo) ?????? ????? ?? ????). Hivyo, endapo mtu anawekwa ana kwa ana na mtu mwingine ambaye makusudio yake sio kufikia kwenye haki, na ambaye lengo lake sio kuelewa mambo ya ukweli yalivyo – bali amekuja, na yuko tayari kabisa kuzungumza, kuhojiana na kuleta mawazo ya ushindani – basi na huyo mwingine ni lazima pia abishane na mtu huyo kama anagombana naye. Hata hivyo, ni lazima tujadiliane na mtu huyo 26


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 27

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya kwa namna iliyo bora zaidi kiasi inavyowezekana kiasi kwamba majadiliano hayo hayapotoki kutoka kwenye njia ya haki na ukweli. Kwa hiyo, ni lazima tusikimbilie kwenye makosa na upotofu kwenye majadiliano, wala hatuwezi kukimbilia kwenye udanganyifu na mambo mengine kama hayo. Aya hii inatupa njia nyingi ambazo kwazo tunaweza kuwaongoza watu na kila njia imewekwa katika nafasi kwa ajili ya mfano maalum kwa wakati. Hivyo, ni wazi kwamba njia ambazo kwamba tunaweza kuwaongozea watu, zote hazifanani, na wala haziko sawa!

Sababu za tofauti miongoni mwa Miujiza ya Mitume Kuna Hadith ambayo kwa kiasi fulani inajulika vema, ambayo inaunga mkono madai yetu katika taratibu za mwongozo, kama inavyoonekana katika sababu za tofauti miongoni mwa miujiza ya Mitume mbalimbali waliotumwa. Ingawa Hadith hii ni kuhusu miujiza mbalimbali ya Mitume ambayo ilikuwa ya namna tofauti kulingana na vipindi tofauti vya nyakati, hata hivyo, bado inaunga mkono madai yetu (kuhusiana na taratibu za kuwaongoza vijana). Hadith hii kwa kweli ni majibu ambayo Ibne Sikkiyt (r.a.) aliyapokea kutoka kwa Imam al-Hadi (a.s.) – kiongozi wa kumi wa kidini aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu. Ibne Sikkiyt (r.a.) anafahamika sana miongoni mwa wataalamu wa Nahau ya Kiarabu. Jina lake linatajwa mara nyingi sana katika vitabu vya sintaksi (kanuni za lugha) na inaelezwa kwamba aliishi karibu katika kipindi cha Imam Ali ibn Muhammad al-Hadi (a.s.) – hivyo, ilikuwa takriban katika wakati huohuo kama kipindi cha utawala cha Mutawwakil. Ibne Sikkiyt (r.a.) vile vile alikuwa mfuasi wa imani ya Shi’ah na aliuawa mikononi mwa Mutawwakil. Imesemekana kwamba sababu za kwa nini ameuawa zilikuwa ni kwa sababu alikuwa na mapenzi makubwa kwa Imam Ali al27


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 28

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Hadi na familia yake (a.s.). Siku moja Ibne Sikkiyt (r.a.) alikuwa mbele ya Mutawwakil wakati watoto wa kiume wawili wa Mutawwakil walipoingia kwenye mkusanyiko huo. Mutawwakil, ambaye kuhusu yeye imeelezwa kwa kufahamika sana kuwa alikuwa ni mtu aliyekuwa na upanga ambao wakati wote ulikuwa kwenye msako wa damu, alimgeukia Ibne Sikkiyt (r.a.) na akamwambia, “Je, watoto wangu wawili hawa ndio bora, au watoto wa Ali – akiwa na maana ya Hasan na Husein (a.s.) wao ndio wabora?” Mtu huyu, Ibne Sikkiyt, mwenye elimu sana, alishangazwa sana na Mutawwakil, kiasi kwamba akamjibu mara moja, “Kwa maoni yangu mimi, Qambar (r.a.) pia ni bora zaidi kuliko baba wa watoto wako hawa wawili.” Kufikia hapo, Mutawwakil akatoa agizo kwa mtumwa wake wa Kituruki aingie ndani ya chumba hicho na akate ulimi wa Ibne Sikkiyt (r.a.) – na ilikuwa ni katika hali hii ambapo yeye alifariki. Kwa hali yoyote ile, mtu huyu alimuuliza Imam al-Hadi (a.s.): “Ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hivi ni kwa nini kwamba wakati Nabii Musa (a.s.) alinyanyuliwa kama Nabii, ishara zake na njia zake na miujiza ambayo aliitumia katika kuwalingania watu na kuwaletea mwongozo ilikuwa kupitia kwenye fimbo yake kugeuzwa kuwa nyoka, na mkono wake ambao uling’ara kwa Nuru Takatifu na mambo mengine kama hayo. Hata hivyo, wakati Nabii Isa (a.s.) aliponyanyuliwa kama Nabii, tunaona kwamba taratibu zake na miujiza ambayo aliitumia kuwalingania watu ilikuwa tofauti. Yeye aliponya watu ambao walikuwa wamezaliwa wakiwa vipovu; aliwatibia na kuwaponya wenye ukoma; aliwafufua wafu na mambo mengine kama hayo. Kama mambo yalivyokuwa, Nabii wetu (s.a.w.w.), wakati alipoteuliwa kama Mtume, namna ya muujiza wake haukuwa mmoja wa hii – kwa maana kwamba muujiza wake ulikuwa kwa maelezo na maneno – Qur’ani Tukufu?” Imam (a.s.) akamjibu kwamba, “Hii ilikuwa ni kutokana na tofauti katika nyakati ambapo mitume hawa walinyanyuliwa. Wakati wa Nabii Musa 28


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 29

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya (a.s.), watu walistaajabishwa na uchawi na uayari, hivyo, miujiza ya Musa (a.s.) ilifanana na mambo ambayo wengine walikuwa wakiyafanya, lakini tofauti ilikuwa kwamba Nabii Musa (a.s.) alileta muujiza wenye uthabiti juu yake, ambapo watu wengine walikuwa na uchawi na uganga tu. Na kuhusu wakati wa Nabii Isa (a.s.), zama zake zilikuwa ni zama ambazo ndani yake madaktari walikuwapo kwa wingi na walikuwa wana uwezo wa kutibia yale magonjwa mabaya zaidi na hili lilileta mshangao na bumbuazi kwa watu. Hivyo, Allah swt. akampa Isa (a.s.) miujiza ambayo itakuwa katika mwelekeo mmoja na kile watu wa wakati wake walichokuwa wakikifanya. Na kuhusu wakati wa Khatamin-Nabiin – mwisho wa Mitume (s.a.w.w.), wakati wake ulikuwa ni ule wa hotuba na mawasiliano ya mdomo, na mazingatio ya watu yaliyotolewa kwenye nguvu za ufasaha wa mazungumzo yalikuwa makubwa sana. Ni kwa sababu hii kwamba mafundisho makubwa sana ya Uislamu yaliletwa kupitia kwenye maneno matukufu, yaliyowekwa ndani ya vazi kamilifu la ufasaha na ufafanuzi (Qur’ani Tukufu).” Ibne Sikkiyt (r.a.) alinufaika sana kutokana na majibu aliyopewa na Imam (a.s.) na sasa kwa vile alielewa jambo hili, yeye alimwambia Imam, “Ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni ipi Hujjah ya Mwenyezi Mungu kwa sasa hivi?” Imam akamjibu, “ni Akili” na akamwambia:

“Hili, kwa jina la Mwenyezi Mungu, ndio jibu lenyewe.” Hivyo, ni dhahiri kwamba ile sababu ya tofauti katika miujiza ya Mitume ilikuwa kwamba, kupitia kila mmoja wao, walikuwa na uwezo wa kuwaongoza watu katika nyakati tofauti. Kama hali isingekuwa hivyo, basi inawezekana kwamba tangu Adam (a.s.) hadi Muhammad (s.a.w.w.) – kama Nabii Adam (a.s.) alikuwa na miujiza yoyote, na kama alikuwa ni 29


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 30

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Mtume (kwa vile wapo baadhi ya watu wanaosema kwamba yeye hakuwa Mtume) – kungekuwa na aina moja tu ya muujiza. Hata hivyo, tunaona kwamba hali sio hii na kwamba kila Mtume alileta pamoja naye, muujiza wake mwenyewe makhsusi, ambao ulikuwa wenye kufaa kwa ajili ya wakati na zama zake.

Taratibu za Mitume Kuna Hadith mashuhuri inayojulikana sana ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambayo imehifadhiwa ndani ya kitabu al-Kafi, na katika siku hizi chache za karibuni, kupitia kwa baadhi ya marafiki zetu ambao wanavyo vitabu vya Ahlus-Sunnah kwenye milki zao, na ambao wamefanya utafiti kupitia kwenye vitabu hivi, ni wazi kwamba Hadith hii imo pia kwenye vitabu vyao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwamba:

“Sisi, kusanyiko la Mitume wote, tumeamrishwa kuzungumza na watu kulingana na kiwango cha ufahamu wao.”6 Wakati wowote Mitume walipotaka kuongea na watu, waliongea nao kulingana na viwango vyao binafsi vya akili na walizingatia pia kiwango chao cha vipaji vyao, na wakazungumza nao katika njia iliyolingana vizuri na akili za watu. Ni lazima tukumbuke kwamba akili za Mitume (A.S.) ni kubwa sana kuliko za watu wengine wote, na wale watu waliokuwa karibu yao wana kiwango cha chini cha uelewa. Kwa hivyo, Mitume wasingezungumza mambo makubwa wala kutumia dhana kubwa kwa watu wa kawaida kwani hili litawafanya watu hao kuchanganyikiwa zaidi. Hali kadhalika, Mitume wasingejibu maswali ya mtu mwenye akili kwa namna ileile ambayo wangeweza kumjibu mtu mzee asiye na elimu. 6 al-Kafi, Juz. 1, uk. 23 30


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 31

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Mawlawi anagusia kwenye dhana iliyotajwa katika Hadith hiyo hapo juu katika shairi lake ambalo linasema: “Wanasema ni vibaya kuongeza kwenye akili za watu. Hili sio kasoro, bali ndio kazi ya Mtume.” Tofauti moja iliyopo kati ya taratibu za Mitume na zile za wanafalsafa ni kwamba, hao wanafalsafa wanatumia mfumo mmoja wa mantiki na mtindo mmoja wa kauli katika nyakati zote. Wanafalsafa wanayo aina moja tu ya bidhaa ‘kwa mauzo’ katika duka lao linalotambulika. Wale wanaokuja kwao ‘kununua vitu’ ni tabaka moja tu la watu – na hii ndio kasoro ya wanafalsafa kwani hawalioni lengo na madhumuni yao katika maisha, isipokuwa kujipamba wenyewe kwa mfululizo wa istilahi (za kifalsafa). Hivyo wanafalsafa wanalazimika kwenda kwenye sehemu moja tu ya jamii ambao wanatambua namna ya wanavyoongea na ambao wanaelewa maneno yao. Imeelezwa kwamba juu ya mlango wa ile shule inayofahamika sana ya Plato – ambayo kwa kweli ni bustani nje ya mji wa Athens, ambayo jina lake lilikuwa ni “Academy” na ambayo hadi leo, kutokana na mikutano ya kisayansi ambayo ilifanyika hapo, bado inajulikana kwa jina la Academy, kwamba kulikuwa na shairi lililokuwa limeandikwa hapo, ambalo linasema; “Yeyote yule ambaye hakujifunza jiometri haruhusiwi kuingia kwenye shule hii.” Katika shule na utaratibu ambao Mitume waliutumia, aina zote za wanafunzi wangeweza kunufaika kutokana na kile ambacho kilikuwa kinasemwa. Ni mahali hapa ambapo aina zote za watu zinaweza kupatikana – kuanzia yule wa juu sana kati ya walio juu (kielimu), ambao hata watu wa namna ya Plato wangeweza kujifunza kutoka kwao, hadi yule wa chini kabisa kati ya walio chini wa namna ambayo sio hata mzee, mtu wa kawaida anaweza kuwa na faida yoyote kwa mtu kama huyo! Haikuwa imeandikwa katika shule yoyote ile kati ya zile za Mitume kwamba, kama mtu yoyote alitaka kuja na kutumia manufaa ya mafundisho yao, ni lazima kwamba awe amesoma hadi kufikia kiwango hiki na kile. Bali, jinsi 31


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 32

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya ambavyo wamesoma zaidi, ndio ambavyo wangekuwa na ujuzi zaidi na kuwa tayari – hivyo kuwawezesha wao kupata manufaa zaidi katika mafundisho ya Mitume. Kama walikuwa wamejiandaa kwa kiasi kidogo kiakili, basi wangeweza kutumia manufaa ya mafundisho hayo kwa kipimo cha uwezo wao wenyewe, kama ilivyoelezwa:

“Sisi, kusanyiko la Mitume wote, tumeamrishwa kuzungumza na watu kulingana na kiwango cha ufahamu wao.”7

Wanafunzi Bora Kutoka kwenye nukta hii, tunatambua kwamba kuna jambo jingine ambalo tuna uwezo wa kulielewa, ambalo ni kwamba, wanafunzi bora wa wanafalsafa ni watu wale wale ambao waliishi katika zama zao na wakawaona – ambalo linatofautiana na wanafunzi bora wa Mitume na marafiki mwandani wa Allah (Awliyah – mawalii). Wanafunzi bora kabisa wa Plato, Aristotle au Abu ‘Ali Sina walikuwa wale ambao walikuwa moja kwa moja ndani ya duru la mafunzo yao. Watu ambao wanaelewa vizuri zile fikra za Abu ‘Ali walikuwa ni watu kama vile Bahmanyar au Abu ‘Abid Jawzjani. Hata hivyo, ni nani walikuwa wanafunzi bora wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Amirul-Mu’minin Ali ibn Abi Talib (a.s.) au Imam Ja’far asSadiq (a.s.)? Je, wanafunzi wao bora ni wale watu walioishi katika nyakati zao, na ambao waliishi pamoja nao? Hapana, hivi sivyo hali ilivyokuwa! Kuna jambo moja ambalo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliligusia katika moja ya hotuba zake. Inawezekana kwamba wale watu ambao waliishi wakati wa Mtume hawakuelewa vizuri ile maana halisi ya maneno haya (uki7 Ibid 32


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 33

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya waacha watu wachache kama Salman Farsi (r.a.), Abu Dhar (r.a.) na Miqdad (r.a.), wengine wanaweza wakawa hawakuyaelewa kikamilifu maneno yake). Mtume (s.a.w.w.) alisema:

“Mwenyezi Mungu amnusuru yule mja ambaye ameyasikia maneno yangu, akayaelewa hayo na kisha akayafikisha kwa yule mtu ambaye hayakumfika.”8 Katika riwaya zingine, Hadith hii imeelezwa kama hivi:

“Mwenyezi Mungu amnusuru mja ambaye ameyasikia maneno yangu …..” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) halafu akasema:

“Huenda (ikawa) mbeba fiqhi si faqihi, na huenda mbeba fiqhi akamfikishia aliye faqihi zaidi kuliko yeye. ngine mtu anakuwa na uelewa mkubwa sana wa elimu ya dini (fiqih) ambapo yeye mwenyewe sio Faqihi (mtu mwenye msingi thabiti wa elimu za Kiislamu), na inawezekana vipi kwamba wakati mwingine mtu anaweza akaihamisha elimu yake kwa mtu mwingine, lakini yule mtu mwingine kwa kweli anayo elimu zaidi kuliko yule anayeihamisha elimu.” Maana ya msamiati wa neno Fiqh katika dini ya Kiislamu kwa kweli inahusu hekima halisi na ya kweli ya dini, ambayo ni lazima ipatikane kwa kupitia kusoma kwa kina na fikra na hivyo, ile maana katika Hadith hii ni 8 Al-Amali cha Sheikh al-Mufid, kikao cha 23, uk. 186 33


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 34

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya ule ukweli na maneno ambayo watu wanayasikia moja kwa moja kutoka kwa Imam (a.s.). Hadithi hii inatuambia kwamba kuna watu wengi ambao wanayasikia maneno haya na kusikia ukweli wa dini moja kwa moja kutoka kwa Imam (a.s.) na kuuhifadhi, lakini sio watu wa kuelewa na kuchambua. Wapo pia watu wengi ambao wanayachukua maneno na ukweli wa dini na kuufikisha kwa watu wengine, lakini wale watu ambao wanaofikishiwa elimu hiyo ni wazuri zaidi na ni wabora zaidi katika kuelewa na kuifahamu elimu hii. Kwa mfano, mtu aliyasikia maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati aliposema:

“Usifanye kitu ambacho kitaleta madhara kwako wewe mwenyewe au kwa watu wengine.” Hata hivyo, yule mtu ambaye aliyasikia maneno hayo hakuwa na uwezo wa kuyaelewa maneno haya yalikuwa na uzito au undani kiasi gani. Hata hivyo, aliyahifadhi na kisha akayafikisha kwenye kizazi kilichofuatia, na kizazi hicho kilichofuata kikayaelewa vizuri zaidi kuliko yeye alivyoyaelewa – na kizazi hiki nacho pia kikayafikisha kwenye kizazi kingine kilichofuatia. Inawezekana kwamba hili litaendelea hadi kufikia kizazi cha kumi na mbili nacho kitayaelewa vizuri zaidi kuliko kile kizazi cha kwanza, cha pili, na cha tatu, kwa vile hiki kizazi cha kumi na mbili kitakuwa kimejiandaa vizuri zaidi kuyaelewa maneno hayo. Qur’ani ni ile ile. Hatuwezi kusema kwamba watu waliokuwepo zamani waliielewa Qur’ani vizuri zaidi (kuliko wengine) – bali hali ni kinyume cha hivyo. Muujiza wa Qur’ani uko kwenye ukweli kwamba Qur’ani siku zote iko hatua moja mbele ya tafsri ambazo zimeandikwa kuihusu – ikiwa na maana kwamba katika kila zama za wakati ambamo Qur’ani imefafanuliwa, pale elimu na uelewa wa watu unapoongezeka, watasonga mbele 34


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 35

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya katika kuitafsiri na kuielewa upya Qur’ani na wataona kwamba Qur’ani imezipita sherehe zao na imeendelea zaidi sana kuliko kile ambacho wamekiandika. Hatuhitaji kwenda mbali sana katika mjadala huu – kwa kifupi hebu iangalie ile Elimu ya Sheria (Ilmul-Usul). Bila shaka, wale masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wale wafuasi wa Amirul-Mu’minin Ali ibn Abi Talib (a.s.), wafuasi wa Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) na hata masahaba kama Zurarah na ibn al-Hakam (r.a.) walikuwa ni watu ambao walijifunza sheria za Fiqh imma moja kwa moja kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) au kwa mmoja wa Maimam (a.s.) lakini hata hivyo hawakuelewa, hawakuchambua na kuzichunguza kanuni za fiqh kama Muhaqqiq alHilli (q.s), Sheikh Murtadha (q.s.) na Sheikh Ansari (q.s.) walivyofanya. Kwa hiyo, kama tulivyoeleza – katika njia za wanafalsafa, ni mtu yupi ambaye ni mbora katika kuelewa maana za mwalimu wake? Ni yule mtu anayekwenda nyuma mbali sana (kwa mwalimu wake). Hata hivyo, katika shule ya Mitume na marafiki mwandani wa Mwenyezi Mungu swt., ni nani watakakuwa na wepesi bora zaidi wa kuwaelewa watu hawa watukufu? Ni wale watakaokuja baadae na kuwa na elimu zaidi na uelewa bora, na huu ni mmoja wa miujiza ya Utume. Katika Hadith ambayo inapatikana katika kifungu juu ya Tawhiid, imeelezwa kwamba, kwa vile Mwenyezi Mungu alijua kwamba katika mwisho wa wakati, watakuja kujitokeza watu ambao watazama kwa kina katika fikra na kuchimbua kwa kina katika kufikiria jambo, Yeye aliiteremsha Suratul-Hadid ambayo inajumuisha mambo makubwa na sahihi kabisa kuhusiana na Tawhiid. Kwa hili tuna maana ya kwamba watu katika wakati wa Mtume (s.a.w.w.) walikuwa hawastahili aya kama hizo. Hata hivyo katika siku za baadae, watu kama hao watakuja kutokea, ambao watastahili kupokea aya hizi za Qur’ani. Aya hizi ni kile kitakachotoa kirutubisho cha kiroho kwa watu wa 35


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 36

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya nyakati za baadae. Kwa kweli, kwa vile aya hizi zinaonyesha mipaka ya mwisho kabisa hasa ya kufafanua katika dhana ya Tawhiid, kama mtu alikuwa afanye ukaidi na kwenda kinyume na aya hizi, ni wazi kabisa kwamba yeye ataangamizwa. Huu ndio muujiza wa Utume na pia muujiza wa Qur’ani ambao ni:

“Mambo yake (Qur’ani) ya kushangaza kamwe hayaishi na ushangazaji wake hautakufa kamwe”9 Yote yale tuliyokwisha kuyaeleza hadi kufikia hapa yalikuwa ni kwa ajili ya madhumuni haya kwamba wakati tunapotaka kujadili jambo hilo na kuzungumzia kuhusu uongozi wa vijana, tusiweze kuwa na mtu atakayesimama na kusema, “Bwana! Mbona kana kwamba kuna tofauti kati ya mwongozo wa vijana na mwongozo wa kizazi cha wati wazima?! Kana kwamba Swala ambayo wanaitekeleza vijana na swala ambayo sisi watu wazima tunayoiswali ni tofauti, kiasi kwamba uongozi wao pia lazima uwe ni kitu tofauti? Kama vile ambavyo huko nyuma tulivyokuwa tukifanya mambo, hivyo pia ni lazima tuendelee kufanya kwa namna ile ile hata sasa. Siku zilizopita, vile tulivyokuwa tukitendeana na wakubwa zetu na mama zetu na baba zetu, na kama vile tulivyokuwa tukikaa pamoja katika mikusanyiko (Majlisi) na kusimulia matukio kuhusu ile mitihani na majonzi ambayo yaliwakabili Ahlul-Bayt (a.s.), na namna ambayo tulimtambua Mwenyezi Mungu swt., na kupokea mwongozo – vijana wa sasa pia ni lazima wafumbe macho yao (kwenye ukweli) na lazima waende kwenye sehemu zile zile ambazo sisi tulikwenda na kujifunza, na waongozwe kama vile ambavyo tulikuwa tumefundishwa na kuongozwa!”

9 Nahjul-Balaghah, Hotuba ya 150. 36


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 37

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

Ni Kizazi cha Vijana au Kukomaa kwa Akili za Vijana? Ni lazima nieleze hapa kwamba, wakati tunapotumia msemo huu “Kizazi cha vijana,” nia yetu sio kuainisha kiwango au umri wa vijana. Bali, nia yetu hasa ni kuongea na kile kiwango au kundi la watu ambao, kutokana na athari za masomo yao wenyewe na uzoefu wa ustaarabu huu mpya, wamekuza njia mahususi ya fikra na akili – iwe watu hawa watokee kuwa ni watu wazima au vijana. Hata hivyo wengi wa watu hawa wanatokana na kizazi cha machipukizi, na ni kwa sababu hii kwamba tunakitaja kama “kizazi cha vijana,” ambapo tunaona kwamba kunakuwepo pia na idadi kubwa ya “watu wazima” ambao wanayo namna hii mpya ya jinsi ya kufikiri, na wapo pia “vijana” wengi ambao muundo wao wa fikra na imani zao zinafanana na zile za vizazi vilivyopita. Kwa hali yoyote ile, kusudi letu ni kuzungumza kulingana na lile kundi la watu ambao wana mtindo huu mahususi wa fikra – jambo ambalo linaongezeka kila siku hadi siku. Huu ni mtindo wa fikra ambao watu wazima na vijana, wote wanaanza kuwa nao na huko baadae, na Mwenyezi Mungu aepushilie mbali, kama zile njia sahihi na taratibu za kuongoza na kuelekeza kizazi hiki zitakuwa hazitumiki, basi tutapoteza udhibiti kamili wa vizazi vya baadae. Jambo hili ni jambo muhimu sana katika nchi yetu (Irani) – na hata katika nchi nyingine za Kiislamu ambako nalo bado ni jambo muhimu – hata hivyo nchi hizi zililitambua jambo hili mapema kuliko tulivyofanya sisi na hivyo, waliliweka mbele jambo hili kwa umakini sana, ambapo sisi bado hatujalichukulia jambo hili kuwa la muhimu sana.

37


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 38

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kwa kuzungumza kwa kawaidi – machoni mwetu – hiki kizazi chipukizi ni kizazi tu cha watu ambao wamejipumbaza wenyewe na ambao wanaabudu tu tamaa zao duni. Tunadhani kwamba, wakati wanapozungumza nasi, tunaweza tu kuwafinyia nyuso, tukapitisha mizaha michache ya kejeli nje ya Mimbari, au kwamba tunaweza kukimbilia kuwalaani (kwa ajili ya makosa yao) na kuongea mambo mabaya kwao. Tunadhani kwamba tunaweza kuongea nao na kuwafanya watusikilize kwa kile tutakachokuwa tunakisema, tuwafanye wakicheke kile tunachowaambia na halafu kila kitu kitakuwa sawasawa. Tunadhani kwamba tunaweza kushangaa na kuwapigia mayowe: “Enyi mnaotoka kwenye shule (mbaya) kadha wa kadha” na tunafikiri kwamba hili litatua matatizo yetu yote. Yote haya ni maneno ya kujiliwaza tu ambayo tunayasema na yapo pale tu kwa ajili ya kutubakisha kwenye usingizi wetu na kutuzuia kufikiri hasa kuhusu namna na njia bora ya kuchukua. Ndani ya kitambo kidogo, tutaamka na kutambua kwamba sasa tumechelewa sana kurudi nyuma.

38


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 39

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

KUWA MWANACHUONI KWA WAKATI AMBAMO UNAISHI Kuna hotuba kutoka kwa Imam Ja’far ibne Muhammad as-Sadiq (a.s.) ambayo ni hotuba iliyo bora sana. Hadith hii imesimuliwa katika al-Kafi10 ambamo maneno yafuatayo yametajwa katika Hadith (ndefu):

“Mtu ambaye anatambua kwa ukamilifu kile kipindi ambamo yeye anaishi, kamwe hatazidiwa na kiwewe (cha mambo yaliyomzunguka yeye).” Hii ina maana kwamba, yule mtu anayejua, ambaye anatambua na kuelewa ule wakati au kipindi ambamo anaishi, yeye hawezi kusumbuliwa na mkanganyiko au wasiwasi kuhusu mambo yanayotokea katika mazingira yake yanayomzunguka. Neno “kuchanganyikiwa” lililotumika kwenye Hadith kwa kawaida katika ki-Farsi kwa maana ya shambulizi kubwa na la nguvu ambalo linalengwa dhidi ya mtu mwingine. Hata hivyo, katika lugha ya Kiarabu ni katika maana ya mtu ambaye amebeba kitu na ghafla, kutokana na kukosa uwezo kwake mwenyewe, au kutokutambua, anakuwa mzembe wa mazingira yake. Katika Hadith hii Imam (a.s.) ametwambia kwamba, “Kama mtu anatambua mazingira yake basi hatasumbuliwa kamwe na kuchanganyikiwa na kiwewe juu ya yale mambo ambayo yanamzunguka yeye, kiasi kwamba kwa wakati anaangalia na kusahau hata mikono na miguu yake mwenyewe, na akawa hana uwezo wa kuzitumia nguvu na nishati yake mwenyewe wala hana uwezo wa kukusanya mawazo yake kuweza kutatua tatizo.” Hii kwa hakika ni Hadith mashuhuri sana.

10 Al-Kafi; Juz. 1, uk. 26 - 27 39


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 40

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Viko vifungu vya maneno vingi vyenye umuhimu kama hiki katika Hadith hii ingawa sikuvihifadhi vyote, hata hivyo mstari mwingine unasema kwamba:

“Mtu ambaye hatumii akili yake hatakuwa mwenye kufanikiwa, na yule mtu ambaye kwamba hana elimu hataweza kuitumia akili yake.� Maana ya akil ?????) ni nguvu au uwezo wa kuhitimisha na kuangalia jambo kwa mantiki na kuanzisha uhusiano kati ya hoja mbili – ikiwa na maana ya kutoa masharti juu ya jambo na kufikia uamuzi. Akili huchukua chanzo cha msukumo kutoka kwenye elimu na hivyo, akili ni taa ambayo mafuta yake yanayoiendesha ni elimu. Hadith hii kisha inaendelea kusema:

Hii ina maana kwamba, yeyote anayeelewa (jambo fulani), basi matokeo yake ni kwamba atakuwa na tabia njema na ya kuheshimiwa kwani matokeo ya hazina au bidhaa isiyo na thamani ya bei ni kupitia ile kazi inayoitanguliza mbele. Kwa hili ina maana kwamba tusiwe wenye kuiogopa elimu na ni lazima tusiifikirie elimu kuwa kama ni kitu ambacho ni cha hatari. Hata hivyo kwa hali halisi, sisi ni maana tofauti kabisa na udhihirisho wa Hadith hii ambayo inasema:

Kutokea mwanzo hadi mwisho, kutoka juu hadi chini kutoka mlangoni (mwa Msikiti) mpaka kwenye Mihrab, sisi sote hatutambui zile zama ambamo tunaishi. Tumejikalia chini tu, bila ya kutambua mazingira yetu, huku tukisinzia. Wakati mmoja tunakabiliwa kwamba, kwa mfano, ardhi hii ni lazima igawanywe na kwamba ardhi hii ni lazima isafishwe na kulimwa (ili kuifanyia matumizi). Bila kujua, inakuwa kana kwamba 40


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 41

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya jambo hili (kuhusiana na usafishaji na ulimaji wa hiyo ardhi) linaanzisha machukizo juu yetu kwa vile hatuzitambui kabisa zile zama ambamo sisi tunaishi. Hatuna kule kuona mbali au makisio ya nini kinaweza kuja kutokea hapo baadae na hatukupanga lolote ili kuamua kwamba wajibu wetu utakuwa ni nini au ni kitu gani ambacho tunachotakiwa tuwe tunafanya. Sisi, katika hali halisi, hatujui ni nini kinachoendelea katika ulimwengu huu na ni nini kinachofanyika nyuma ya mapazia. Tumekabiliana ghafla na suala la haki za kijamii za wanawake. Hapa, hatuna muda wa kutosha kufikiri juu ya hili na kuchambua vipengele vyake vyote ili kubaini umuhimu wake. Hivi wale wanaozitetea hizi haki za kijamii za wanawake wamedhamiria ukweli? Hivi kweli wanataka kuvutia mashabiki wengi? Au kuna faida nyingine yoyote wanayonuia kuipata kutokana na kuibua masuala kama haya? Pamoja na haya, yatakuja kutokeza mambo mengine yenye mashaka na mageni yasiyojulikana kwetu sisi. Miaka sitini hadi mia iliyopita miongoni mwa nchi nyingine za Kiislamu, hili suala la kuwaongoza na kuwaelekeza vijana lilikuwa limekwisha kufikiriwa, lakini wamekuwa wakishughulika sana katika kulitafakari na kulijadili jambo hili kuliko sisi tulivyo sasa.

Ni nini ambacho ni lazima kifanyike? Kile ambacho ni muhimu sana kuliko kuandaa mpango kwa ajili ya uongozi wa kizazi hiki ni kwamba, ni lazima tuziimarishe imani katika vichwa vyetu wenyewe kwamba uongozi na mwongozo wa kizazi hiki ni tofauti katika utaratibu na mbinu zake, mwote katika vipindi mbalimbali vya nyakati, na unatofautiana kulingana vile vikundi vya watu ambao tunafanya kazi nao. Hivyo, ni lazima tuondoe kabisa yale mawazo kutoka vichwani mwetu, kwamba kizazi hiki kipya lazima kiongozwe kwa kufuata zile taratibu zilizotumiwa na vizazi vilivyotangulia.

41


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 42

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kwanza kabisa, ni lazima tukielewe vizuri kabisa hiki kizazi kipya, na Kufahamu ni aina gani za sifa bainishi na tofauti ambazo wanazo. Kuhusiana na kizazi hiki, kuna namna mbili za fikira ambazo ni za kawaida, na kwa kawaida kuna njia mbili ambazo zinaweza zikashughulikiwa kwazo. Kutokana na maoni ya baadhi ya watu, vijana hawa ni kundi la watu ambalo lisilojali na fidhuli, ambao wamedanganywa na kupendezwa mno na tamaa zao duni. Wao ni wenye kuabudu nafsi zao na wana maelfu (mengine) ya mapungufu. Hawa watu (wanaofikiria hivi juu ya kizazi hiki kipya) wakati wote wanawafinyia nyuso na kila mara wanazungumza vibaya juu ya kizazi hiki. Hata hivyo, vijana hawa wanajiona wenyewe kama wako kinyume kabisa na hali (picha) hii. Vijana hawajioni wenyewe kama ni wenye mapungufu yoyote. Wao wanajidhania kuwa ni sanamu (picha) la akili, sanamu la busara, sanamu la sifa za hali ya juu kabisa. Kizazi cha zamani kinafikiri kwamba kundi hili limeangukia kwenye kutoamini (ukafiri) na kwamba limetumbukia kwenye dhambi, ambapo hicho kizazi kipya kinadhani kwamba kizazi cha zamani wana akili nyepesi (mapunguani) na wajinga wasiojua kitu. Kizazi cha zamani kinawaambia kizazi kipya kwamba wamejishusha wenyewe kwenye kuabudu nafsi zao wenyewe na wamekuwa makafiri, ambapo hicho kizazi kipya kinawaambia kizazi cha zamani kwamba wao hawakijui kile ambacho wanakisema na kwamba hawawaelewi! Kuzungumzia kwa kawaida jinsi mambo yalivyo, inawezekana kwamba kizazi kimoja kinaweza kukiona kizazi kilichotangulia kana kwamba ni watu wenye haki lakini pia inawezekana kwamba wakawaona kama waliopotoka.

42


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 43

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

Mfano wa Vizazi Viwili Kuna aya katika Suratul-Ahqaf ambayo ilitajwa kabla sijaanza mjadala wangu. Kwa maoni yangu mimi, aya hii kwa kweli inafafanua mandhari ya vizazi viwili – yale ya kizazi chenye haki na mengine ya kizazi ambacho kimepotoka. Hatuwezi kusema kwamba bila shaka kila kizazi kinachopita kitakuwa ni kipotovu zaidi kuliko kizazi kilichotangulia, na kwamba dunia inasonga karibu kuelekea kwenye upotovu siku baada ya siku. Wakati huo huo, vilevile hatuwezi kusema kwamba vizazi vijavyo vitakuwa vikamilifu zaidi kuliko vilivyotangulia na kamwe havitaangukia kwenye makosa. Aya tunazotaka kuziangalia ni kama zifuatazo:

“Na tumemuusia mwanadamu afanye wema kwa wazazi, wake wawili, mama yake amechukua mimba yake kwa taabu na akamzaa kwa taabu, na kumbeba na kumwachisha ziwa ni miezi thelathini hata anapofikia balehge na akawa mwenye umri wa miaka arobaini, akasema: Ewe Mola Wangu! Niwezeshe nishukuru neema Zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na ili nifanye vitendo vizuri unavyovipenda, na unitengenezee watoto wangu. Kwa hakika ninatubu Kwako na hakika mimi ni miongoni mwa walionyenyekea. (Al-Ahqaf; 46:15) 43


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 44

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Aya hii ya Qur’ani inatudhihirishia njia moja ya kufikiri na kuelewa ya watu wa kizazi cha wenye haki. Imesemekana kwamba aya hii ilishuka kuhusiana na Sayyid ash-Shuhadaa Imam Husein ibne Ali (a.s.) – kama mambo yalivyo, yeye hasa ndiye ushahidi kamilifu wa aya hii, ingawaje aya yenyewe ni aya yenye kujumuisha kwa ujumla. Katika aya hii, kuna sifa tano ambazo zimetajwa, juu ya kizazi chenye uadilifu. Sifa ya kwanza ni kwamba nafsi ambayo ni yenye shukurani na inayotambua umuhimu na thamani ya neema na zawadi ya maumbile:

“Ewe Mola Wangu! Niwezeshe nishukuru neema Zako ulizonineemesha mimi...” (al-Ahqaf; 46:15) Mtu kama huyo anaziangalia zile neema na rehma ambazo Mwenyezi Mungu swt. amezitoa kwa wote pamoja (mama na baba) na kizazi kilichotangulia na anasema, “Ewe Allah! Nipe nguvu ya kuniwezesha kuifahamu haki na kuitambua thamani yake halisi. Nipe nguvu niweze Kufanya matumizi bora ya neema ambazo umezimimina juu yetu kwa kiasi ambacho nitazipata radhi Zako.” Kuwa wenye shukurani kwa neema yoyote ile kuna maana kwamba tunaitumia neema hiyo kama inavyopaswa kutumiwa. Baada ya hili, tunaomba kwamba Mwenyezi Mungu atupe uwezo wa kutenda matendo mema ambayo Yeye anaridhishwa nayo. Tunaomba kwamba sisi pia tuweze kupewa nafasi ya kutenda katika namna ambayo ni yenye manufaa kwetu wenyewe, na kwa wengine, na Kufanya yale mambo ambayo yataweza kutuchumia radhi za Mwenyezi Mungu swt.

“…..na ili nifanye vitendo vizuri unavyovipenda ” (al-Ahqaf; 46:15)

44


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 45

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Du’a ya tatu ni kwamba tugeuzie mazingatio yetu kwenye kizazi kijacho na kumuomba Mwenyezi Mungu swt. kwa ajili ya ubora wao na kwa wao kuwa waadilifu:

“…..na unitengenezee watoto wangu ……….” (al-Ahqaf; 46:15) Ombi la nne tunalotoa ni kwamba tuwe tunaruhusiwa kurejea kwa Mwenyezi Mungu swt. kwa ajili ya makosa yetu, kuteleza na kasoro zetu ambazo tumezitenda huko nyuma:

“…..Kwa hakika ninatubu Kwako…..” (46:15) Du’a ya tano na ya mwisho katika aya hii ni ile ya kwamba tunaomba tujaaliwe ile hali ya kunyenyekea kwenye haki na yale mambo ambayo Mwenyezi Mungu swt. ameyaainisha kwa ajili yetu kuhusiana na dunia ya kawaida na sheria za Kiislamu. Ni kwa njia ya kukengeuka mipaka iliyowekwa na Mwenyezi Mungu swt. ambako kunatupeleka kwenye kuangamia na kuteketea:

“…………na hakika mimi ni miongoni mwa walionyenyekea ….. (46:15) Kuhusiana na kizazi hiki kilichotajwa hapo juu, imeelezwa tena katika Qur’ani:

45


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 46

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

“Hao ndio tunaowakubalia vitendo vyao vyema walivyovitenda, na tunayasamehe makosa yao, na watakuwa ni watu wa Peponi, ahadi ya kweli waliyoahidiwa.” (Suratul-Ahqaf; 46:16) Katika kipande hiki cha aya, kiwakilishi nomio kinageuka na cha namna ya wingi na hivyo ni dhahiri kwamba sio cha kuhusika na mtu mmoja. Katika aya hii, imeelezwa kwamba, “Hao ndio tunaowakubalia vitendo vyao vyema na kuyasamehe makosa yao: (watakuwa) miongoni mwa watu wa Peponi, ahadi ya kweli waliyoahidiwa (katika maisha haya).” Hata hivyo aya ifuatayo ni ya kuhusu kizazi kiovu kilichopotoka, na inasema:

“Na ambaye anawaambia wazazi wake: Ah, Nanyi! Je, mnanitishia

kuwa nitafufuliwa na hali vizazi vingi vilikwishapita kabla yangu? Na hao wawili huomba msaada wa Mwenyezi Mungu, (nao humwambia mtoto wao): Ole wako! Amini, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, lakini yeye husema: siyo haya bali ni visa vya watu wa kale.” (al-Ahqaf; 46:17)11 Kizazi ambacho kina majivuno, kilichokanganyikiwa na kisichokomaa kiakili kitajifunza mambo machache, na halafu hawataamini kitu kingine chochote watakachosikia; hivyo wao watakoma kuwa watumwa wa Allah swt. Watawaambia baba na mama yao, “Ole 11 Ibid; Aya ya 17 46


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 47

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya wenu nyie!” Watawadhihaki wazazi wao na watakimbilia katika kuyacheka mawazo na imani zao. Kizazi kama hicho kitawaambia wazazi wao!

“Mnashikilia kunitisha kwamba nitafufuliwa?” (al-Ahqaf; 46:17) Kizazi kama hicho kinashangaa: “Hivi mnanitegemea mimi niamini kwamba kuna dunia nyingine baada ya hii, au kwamba kuna uhai mwingine baada ya huu ambapo tunaona kwamba vizazi vilivyotangulia vilikuja, vikaishi, vikafa na hiyo ndiyo hivyo!?” Hao baba na mama ni wenye kushika dini na hawako tayari kusikia kitu chochote kinachokwenda kinyume na dini na imani yao, hata hivyo wakati huo huo, wanaona kwamba yule kipenzi chao katika watu anazungumza nao kwa namna ambayo inawafanya wafadhaike na kuwalazimisha kumwambia mtoto wao:

“….. Ole wako! Amini, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli!”46:17 Moja ya mambo yanayouma sana kuliona, kwa baba na mama wanaoshika dini, ni mwanao wao mpenzi akienda bila lengo kuelekea kwenye kutoiamini dini, au kumuona akizikana imani hizo na kwenda kuelekea kwenye Kufr (ukafiri kamili).

47


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 48

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

“…..Na hao wawili huomba msaada wa Mwenyezi Mungu …..”46:17 Ni wakati huu ambapo kule kulilia na kuomba msaada kunaweza kusikika huko mbinguni wakati baba na mama wanapomuomba Mwenyezi Mungu swt. Hata hivyo, mtoto huyo anayajibu maombi yao kwa kusema kwamba:

“….. haya siyo chochote bali ni visa vya watu wa kale!” 46:17 Aya hii inatupa sisi picha ya vizazi viwili tofauti kabisa. Aya moja inatuonyesha kizazi kiadilifu, ambapo hii nyingine inatupa taswira ya kizazi kipotovu. Haya yakiwa yamekwisha kusemwa, hebu sasa tuangalie ni kundi lipi la kizazi chetu kichanga linaloangukia katika hili lifuatalo hapa chini.

Vijana wa Kisasa Kizazi chetu kichanga cha leo kina sifa zote nzuri na kasoro kadhaa ndani yao. Kizazi hiki kina mlolongo wa uelewaji na hisia ambazo vizazi vilivyotangulia havikuwa nazo na kwa hiyo, sisi lazima wakati wote tuwape faida ya mashaka yao. Wakati huo huo, wao wanayo mawazo potovu na sifa bainifu za 48


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 49

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya kimaadili za kinyume ambazo ni lazima ziondolewe kwenye tabia zao. Haiwezekani kuziondoa sifa bainifu hizi kutoka kwao bila ya kuzingatia na kuziheshimu zile sifa nzuri ambazo vijana hawa wanazo – kwa maana ya kwamba, kule kuelewa kwao na hisia zao, na sifa bainifu zao bora na tabia – hivyo ni lazima tuonyeshe heshima kwao kuhusiana na haya. Hakuna mwisho kabisa katika maisha. Katika vizazi vilivyotangulia, mawazo na akili za watu hazikuwa wazi kama za kizazi cha sasa. Hisia hizi na sifa nzuri hazikuwepo kwa watu wa siku za nyuma, na kwa hivyo ni lazima tuonyeshe heshima kwa vijana kwa ajili ya sifa zao bora – na ni Uislamu wenyewe, ambao umeonyesha heshima kwenye sifa bainifu hizi. Kama hatutaki kutoa mazingatio kwenye mambo haya, basi haiwezekani kufikiri kwamba tutakuwa na uwezo wa kutwaa madaraka na kuondosha huu upotofu wa kisomi na sifa bainifu za kimaadili zilizo kinyume kutoka kwenye vizazi vya baadae. Utaratibu ambao tumeuchukua kwa wakati huu tunapokabiliwa na kizazi hiki ni ule wa kuwafinyia nyuso, kuwashutumu, na kuwakashifu. Tunaendelea kuwakemea kwamba filamu za sinema ziko hivi, kumbi za maonyesho ziko vile, nyumba za wageni zilizoko kati ya Shamiran na Tehran (miji miwili ya Irani) ziko vile na vile; kumbi za dansi nazo ziko hivi, mabwawa ya kuogelea yako vile na hivyo tunafululiza kuendelea kuwakemea (kuhusu upotofu katika sehemu zote hizi) na ni lazima tujue kwamba huu sio utaratibu sahihi wa kufuata. Lazima turudi kwenye sababu ya asili ya upotofu unaopatikana katika sehemu hizi (na kwa nini kizazi hiki kipya wasiweze kwenda kwenye sehemu hizi).

49


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 50

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

Matatizo ya Kizazi hiki ni lazima yaeleweke Lengo letu kuu na umakinikaji ni kwamba ni lazima kwanza tutambue pale jitihada za kizazi hiki zilipotua. Ni lazima tuzitambue jitihada za kiakili, jitihada za kielimu – zile jitihada ambazo zitatuelekeza kwao tukiwa tunatambua (juu ya wajibu wao) – kwa maana ya yale mambo ambayo yanawasumbua vijana wa kisasa, ambayo hayakuwasumbua vijana wa siku zilizopita. Kuhusiana na haya, yule mshairi, Mawlawi; ameeleza kama ifuatavyo: “Huruma na unyenyekevu hutokea wakati wa maradhi: wakati wa maradhi wote ni kukesha tu (kwa dhamiri). Wale walioko macho zaidi, yeyote ni mwenye wingi zaidi wa maumivu; anakuwa mwenye utambuzi zaidi (wa Mungu), Mwenye kusawijika zaidi katika sura.”

Hapo zamani, milango ya kwenye matukio (yanayotokea duniani kote) ilikuwa imefungwa machoni mwa watu – wakati watu wanapokuwa wamefungiwa milango, basi maisha yakuwa rahisi – na madirisha pia yalikuwa yamefungwa. Hivyo hakuna mtu aliyejua ni nini kilichokuwa kinatokea huko nje (ya nyumbani kwao wenyewe). Wala hawakujua pia kilichokuwa kinatokea katika nchi nyinginezo. Leo hii, milango hii na madirisha (ya kwenye miji na nchi nyingine) iko wazi kabisa. Leo hii, watu wanaweza kuiona dunia yote na hatua ya maendeleo ambayo dunia imefikia. Wanaiona elimu ya dunia; wanauona uwezo 50


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 51

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya wa kiuchumi duniani kote; wanaziona nguvu za kisiasa na kijeshi za ulimwengu; wanaweza kuziona demokrasia za dunia; wanauona usawa unaochukua sura duniani kote; wanayaona mavuguvugu na machafuko na mapinduzi yote yanayotokea katika dunia. Vijana wanayaona mambo haya, hivyo hisia zao zinapanda juu, na wanayo haki ya kuyaona mambo haya na kujifikiria wenyewe na halafu waseme: “Kwa nini tumeachwa nyuma (licha ya maendeleo yote haya)?” Katika maneno ya mshairi: “Ni lazima niseme kweli kwamba siwezi kuvumilia kuona, Wapinzani wangu wakiishi vizuri wakati mimi nikiangalia tu.”

Kwa namna hii, dunia inasonga mbele kuelekea kwenye uhuru wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, na inaelekea kwenye umaarufu, ubora, heshima na uhuru hata hivyo sisi bado tumelala au tunashuhudia mabadiliko haya kwa mbali na tunapiga miayo. Vizazi vilivyotangulia havikuelewa mambo yote haya na havikuweza kuyatambua, hata hivyo hiki kizazi kipya kinayo haki ya kusema kwamba: “Kwa nini Japani, ambayo ni nchi ya waabudu masanamu, na Irani ambayo ni nchi ya Kiislamu, ndani ya mwaka huo huo na kipindi cha zama moja hiyo hiyo ya kuwepo, zinatambua haja, na zimeanzisha ustaarabu mpya na viwanda. Hata hivyo, tunaona kwamba Japani ilikuwa na uwezo wa kufikia hatua au kiwango ambacho wanao uwezo kirahisi kabisa wa kushindana na nchi za Magharibi, ambapo tunaiona hali ambayo Irani iko nayo?” “Layla na mimi tulikuwa tunasafiri pamoja kwenye njia ya mapenzi, Yeye alikifikia kile alichokuwa akikitafuta, ambapo mimi bado 51


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 52

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya inanibidi kufika huko.� Hivi kizazi hiki kipya hakina haki ya kuuliza maswali kama haya? Vizazi vilivyotangulia havikuwa na uzito mkubwa wa uingiliaji wa kigeni uliokuwa ukiwalemea kwenye mabega yao, kama ambao hiki kizazi cha sasa kinaopitia. Je, hii ni dhambi? Kwa kweli hapana! Hii sio dhambi hata kidogo! Bali kupitiwa na haya, kwa kweli ni ujumbe wa ki-mbinguni kutoka kwa Mwenyezi Mungu swt. Kama hisia hizi na uzoefu vingekuwa havipo, basi hii ingekuwa ni ishara ya kwamba sisi ni walengwa wa adhabu na uadabisho (wa Allah swt.) Kwa hiyo basi, sasa kwa vile hisia hizi zipo, hii ina maana kwamba Mwenyezi Mungu swt. anataka kutupatia sisi wokovu kutokana na uadabisho huu. Huko siku za nyuma, kiwango cha elimu kilikuwa cha chini sana na ni watu wachache sana waliokuwa na wasiwasi, kukanganyikiwa, na maswali (kuhusu dini), hata hivyo mtindo huu wa fikira sasa hivi umebadilika na watu wanauliza maswali mengi zaidi na zaidi. Ni kawaida kwamba pale elimu inapoongezeka, basi na maswali yataibuka kutoka akilini mwa watu, ambayo hayakufikiriwa kabla ya hapo, na wasiwasi na mchanganyiko huu lazima uondolewe kutoka kwenye akili za watu, na maswali wanayoyauliza, na mahitaji ya akili zao lazima yajibiwe. Haiwezekani kwamba unaweza kumwambia mtu kama huyo kwamba anapaswa kuyasahau maswali yake na arudie tu vile jinsi vizazi zamani vilivyokuwa – bali, hii ni fursa nzuri kabisa ya kuwafahamisha watu ule ukweli na mafundisho ya Kiislamu. Haiwezekani 52


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 53

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya kuelezea ukweli kwa mtu mjinga asiye na elimu, hivyo kuhusiana na mwongozo na uongozi wa kizazi kilichotangulia, ambacho kiwango chake cha fikra kilikuwa cha chini, ilikuwa ni muhimu kwetu sisi kuielezea dini na kuifikisha kwao katika namna maalum, kupitia mtindo maalum wa uandishi. Hata hivyo, leo, ule mtindo wa kizamani wa ulinganiaji na ule mtindo wa kizamani wa uandishi, yote haina maana wala thamani hata kidogo. Tuna lazima sisi, na hili ni muhimu sana, ya kujirekebisha sisi wenyewe na kuwa na ujenzi mpya wa kina katika sehemu hii ya matendo yetu. Ni lazima tuwe na ufahamu mzuri wa mantiki, fikira na lugha ya wakati huu, na ni lazima tushughlikie suala la mwongozo na uongozi wa watu kwa namna hii. Kiwango cha elimu cha kizazi kilichotangulia kilikuwa cha chini sana kiasi kwamba, kama katika mkusanyiko, mtu alikuwa azungumze mambo ambayo yalikwenda kinyume na mambo mengine ambayo aliyasema (katika mkusanyiko huo huo), basi hakuna hata mmoja ambaye angegundua au kulalamika kuhusu hilo. Hata hivyo leo, kama kijana wa makamu ambaye yuko kidato cha kumi au kumi na mbili angekuwa aende kukaa chini ya mimbari ya mhadhiri, atakuwa na uwezo wa kuokota makosa matano au sita, au pengine hata zaidi, kwa mhadhiri huyo. Ni lazima tuwe wasikivu kwenye mawazo na akili zao, na kwa hiyo, hatuwezi kuendelea kuwaambia wanyamaze na waache kupoteza wakati. Kama ujuavyo, haikuwa namna hii hapo nyuma. Katika siku za nyuma, mtu angeweza kusoma mistari elfu moja ya ushairi katika kikao kimoja, au maneno mengine ya sifa ambayo yalikuwa yanatofautiana kabisa, na hakuna hata mtu mmoja ambaye angeweza kuelewa kwamba kile alichokuwa akikisema mtu yule kilikuwa kinakwenda kinyume na maneno yake mwenyewe! Kwa mfano, mtu 53


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 54

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya atasema kwanza kwamba hakuna kitendo kinachoweza kutokea bila ya sababu au chanzo.

Mungu amekataa kuyapitisha mambo ila kwa sababu zake. “Mwenyezi Mungu ni Mkuu kuliko hivyo kwamba anaweza kuamuru mambo isipokuwa kwa sababu.” Mtu huyo ataeleza jambo hili na kila mtu atakubaliana naye, na kama hasa baada tu ya kuyasema haya, alikuwa aseme:

“Yanapofika maangamizo macho yanapofuka.” Kwa mara nyingine tena, kila mtu aliyaunga mkono madai haya na kuthibitisha ukweli wake! Kuna simulizi kwamba wakati Mfalme wa Nishabur12 alipokuwa amekuja Tehran, idadi kubwa ya watu ilikusanyika karibu yake chini ya mimbari kutokana na uzuri wa sauti yake aliyokuwa nayo. Kiongozi mashuhuri wa jumuiya hiyo akamwambia, “Kwa kuona ni jinsi gani idadi kubwa kama hii ya watu imekusanyika chini ya mimbari wakati unapozungumza, kwa nini usitamke maneno machache ya hekima mbele yao na ukaacha kupoteza wakati wao?”

12 Nishabur ni mji uliokuwa nje kidogo ya mji wa Mash’had ya sasa huko Iran. 54


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 55

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Mfalme huyo akajibu: “Watu hawa hawana uwezo wa kuelewa hotuba ya hekima. Maneno ya hekima yanaweza kuongewa tu kwa watu wenye elimu, na watu hawa hawana elimu!” Yule kiongozi akajibu kwamba yule mfalme amekosea katika kidokezo chake na hali haikuwa kama alivyosema. Mfalme akarudisha maneno kwamba hali ilikuwa ni kama alivyosema yeye hasa na kwamba angemthibitishia yule kiongozi. Siku moja wakati yule kiongozi alipokuwa kwenye mkusanyiko huo, yule mfalme akaanza kuongea juu ya mimbari kuhusu misiba iliyowafika Ahlul-Bayt (a.s.) katika mji wa Kufa huko Iraqi. Akasoma mashairi fulani kwa sauti nzuri, yenye kuhuzunisha ambayo iliwafanya watu hao watokwe na machozi. Halafu tena akasema, “Tulieni, tulieni, tulieni.” Baada ya kila mtu kutulia na kunyamaza, yeye akasema: “Ningependa kuwaelezeeni ile hali ya watoto wa Abu Abdillah (a.s.) wakati walipokuwa katika mji wa Kufa. Pale hao Ahlul-Bayt (a.s.) walipoingia kwenye mji wa Kufa, hali ya hewa ilikuwa ya joto sana. Jua lilikuwa linawachoma kiasi kwamba lilikuwa na hali kama moto uliokuwa umewekwa vichwani mwao. Wale watoto wadogo wa familia hiyo wote walikuwa na kiu, na kwa sababu ya joto hilo kali, wao walikuwa na miili ya moto sana. Halafu waliwekwa juu ya ngamia wasiokuwa na matandiko, na kwa vile ardhi ilikuwa imejaa barafu, wale ngamia waliendelea kuteleza katika barafu hiyo na hivyo, wale watoto wadogo wakaanguka kutoka kwenye ngamia hadi chini kwenye ardhi na wakaanza kulia: “???????” Oh, tuna kiu!”

55


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 56

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

Sababu za kwa nini watu wanavutika kuelekea kwenye kumkana Mungu Kwa kawaida, kuna watu wengine ambao wamekuwa na uwezo wa kuyatambua mambo ambayo yanakiuma kizazi hiki na wameweza kuwatumia vibaya vijana hawa na kuwapotosha. Ni njia gani mafundisho ya uyakinifu yaliyoyatumia – ambayo yametokea hata katika nchi hii (Irani) – ambayo yalikuwa na uwezo wa kuwafanya watu kujitoa muhanga maisha yao kwa ajili ya mambo haya na kwa ajili ya lengo la ukana Mungu? Mafundisho hayo yalitumia njia hii hii (ambayo tunaitafuta) kwa vile walijua kwamba kizazi hiki kilikuwa kinahitaji jambo fulani. Walijua kwamba walihitaji madhehebu ambayo ingeweza kujibu maswali yao, na kwa hivyo wakawasilisha kwao itikadi ya fikra kama hiyo. Walijua kwamba kizazi hiki kilikuwa na mlolongo wa maoni ya pamoja na malengo ambayo walitaka kuyafikia, na walitaka mambo haya kujithibitisha yenyewe kwamba ni ya kweli, na kwa hivyo, wayakinifu hawa wakayafanya hayo hayo kuwa ndio maoni na malengo yao. Hivyo, waliweza kuwavuta watu wengi upande wao wenyewe, na kwa aina gani ya kujitoa muhanga mwenyewe (kwa upande wao) na kwa namna gani ya ukaribu! Wakati mtu anapoonekana kuwa na mahitaji ya dhati juu ya jambo, huwa hafikirii juu ya uzuri na ubaya katika jambo hilo. Pale tumbo linapokuwa na njaa ya chakula, kwa kweli huwa halijali kuzingatia ni aina gani ya chakula linachokipata – litakula chochote kile litakachopata ili tu kuridhisha njaa hiyo. Nafsi nayo ni namna hiyo hiyo – 56


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 57

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya endapo inafikia hatua ambayo kwamba inakuwa na njaa kwa ajili ya madhehebu ya kufuata na madhehebu kama hiyo ambayo inaendeshwa kwa kanuni zilizobaishwa kabla na zenye kujulikana, ambazo zina uwezo wa kujibu maswali yanayotolewa, na ambazo zina uwezo wa kuyashuhulikia mambo yote ya dunia yenye kuchosha, na mambo ya kijamii ya pamoja yanayowekwa mbele yake, basi haitajali kama imani hizo zimeegemea kwenye mantiki yenye nguvu au hapana. Hivyo tunaona kwamba ubinadamu hautafuti hasa hotuba imara na yenye mantiki – bali unatafuta fikra au dhana iliyoratibiwa na kuandaliwa vizuri, ambayo itaweza kujibu maswali yote ya siku hadi siku ambayo yanajitokeza. Sisi, wanafalsafa, tulijua kwamba maneno yote haya ni upuuzi mtupu, na ingawa haikuwa na maana yoyote, falsafa hiyo iliyotajwa ilikuwa kwa kweli ni dharura yenye kuhitaji uangalifu ambayo ilijaza uwazi na ikajitengea nafasi kwa ajili ya mahali pake, na hivyo ikakubaliwa.

Ishara za Maendeleo ya Kielimu Baada ya mtoto kupitia kipindi cha kunyonyeshwa, na uwezo wa akili yake na uwezo wa utambuzi umekua, hapo sasa anaanza kuuliza maswali kuhusu mambo yaliyomzunguka yeye na lazima tuwe tayari kumjibu maswali yake kulingana na kiwango chake cha uelewa. Ni lazima tusije kumwambia kwamba, “Wacha kelele” au “linakuhusu nini?” au mambo kama hayo. Kuuliza maswali kwa mtoto ni ishara kwamba akili yake inakua na kwamba anafikiri. Maswali haya vilevile yanaonyesha kwamba nguvu zake za kiroho zimekua na zimechukua mshiko imara ndani yake yeye. Maswali haya ni dalili za asili; ni alama ya maumbile. Hayo maumbile 57


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 58

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya yanawatangazia wengine kwamba wakati wote yanahitaji kitu kipya ndani yake, hivyo wale watu ambao wako karibu na mtoto huyo ni lazima wampatie kile anachoomba. Jambo hilo hilo linaweza kusemwa juu ya jamii. Kama ndani ya jamii, hisia au uelewa mpya ukipatikana, basi hii pia ni dalili ya ustawi na maendeleo ya jamii hiyo. Hii pia ni dalili kwamba zile sehemu ndani ya jamii zina haja mpya ambayo ni lazima itimizwe. Mambo ya namna hii lazima yaonyeshwe kama ni mambo ambayo ni tofauti na tamaa duni na haja ya kuabudu nafsi, na hivyo tusije tukachukulia kamwe kwamba maswali haya ni namna ya uendekezaji wa tamaa duni. Hivyo, wakati mambo haya yanapojitokeza, ni lazima tuzingatie akilini haraka sana aya hii ifuatayo ya Qur’ani:

“Na kama ukiwatii wengi katika (hawa) waliomo duniani watakupoteza mbali na njia ya Mwenyezi Mungu. Wao hawafuati ila dhana tu, hawana ila (ni wenye kusema) uongo tu.” (alAn’aam; 6: 116) Na kwa nyongeza zaidi tunasoma hivi:

“Na kama haki ingelifuata matamanio yao, zingeharibika mbingu na ardhi na vilivyomo. Lakini tumewaletea ukumbusho wao, nao walijitenga mbali na ukumbusho huo.” (al-Muuminun; 23: 71)

58


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 59

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

Utelekezwaji wa Qur’ani Tukufu Leo hii, tunayo malalamiko ambayo ni lazima tuyazungumze kwa kukiambia kizazi hiki kipya, ambayo ni: Kwa nini hawana ufahamu wa Qur’ni? Kwa nini hawafundishwi Qur’ani katika shule zao? Hata kama tukienda kwenye Vyuo Vikuu, tunaona kwamba wanafunzi Waislamu wa vyuo hivyo hawawezi hata kusoma Qur’ani! Kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana kwamba hili limetokea, hata hivyo ni lazima tujiulize wenyewe, “Ni hatua gani tulizozichukua sisi ili kuwasaidia katika njia hii?” Je, tunachukulia kwamba yale masomo ya Fiqh, Shari’ah na Qur’ani ambayo yanafundishwa kwenye Madrasa za Kiislamu, kwamba hii inatosha kwa kizazi hiki kipya kuwa na ufahamu kamili wa Qur’ani? Kinachoshangaza zaidi ni kwamba vile vizazi vilivyotangulia pia viliwekwa mbali na vilikuwa vimeitelekeza Qur’ani – na halafu tunataka kulalamika kwa hiki kizazi kipya kwamba ni kwa nini hawakukuza uhusiano na Qur’ani!? Bila shaka, Qur’ani kwa kweli tumejitenganisha nayo sisi wenyewe na kisha bado tunategemea hiki kizazi kipya kushikamana na Qur’ani!? Kufikia hapa, tutawathibitishia wasomaji ni jinsi gani tumejitenga wenyewe na Kitabu hiki Kitukufu. Kama elimu ya mtu ni ile ya ujuzi wa Qur’ani – kwa maana ya kwamba yeye anafanya tafakari kubwa sana juu ya yaliyomo ndani ya Qur’ani, na kama anaijua tafsiri kamili ya Qur’ani, ni heshima kiasi gani anaweza akawa nayo mtu kama huyo miongoni mwetu? Hakuna kabisa! Hata hivyo, endapo mtu atakuwa akijue kitabu 59


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 60

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya “Kifayah”13 cha Akhund Mullah Kadhim Khurasani, basi ataheshimiwa na atachukuliwa kama mtu mwenye ukamilifu. Hivyo, kwa hakika Qur’ani haijulikani na imekuwa iko mbali na sisi na haya ndio malalamiko yale yale ambayo Qur’ani yenyewe itayatangaza! Sote tunajumuishwa kwenye malalamiko na uchungu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) wakati atakapolalamika kwa Mwenyezi Mungu swt:

“Na Mtume atasema: Ewe Mola Wangu! Kwa hakika watu wangu wameifanya Qur’ani hii kuwa ni kitu kilichoachwa.” (alFurqan; 25: 30) Takriban mwezi mmoja uliopita,14 mmoja wa wanachuoni wetu mashuhuri alikuwa amekwenda kwenye ile miji mitukufu (ndani ya Iraqi), na anasimulia kwamba alimtembelea Ayatullah Khu’i (Quddisa Sirruh). Alimwambia Ayatullah, “Kwa nini wewe umesimamisha yale masomo juu ya Tafsir ambayo ulikuwa ukiyatoa hivi karibuni?”15 Ayatullah akamjibu kwamba kulikuwa na vikwazo na matatizo mengi katika kutoa darasa hizo za Tafsir ya Qur’ani. 13 Hiki ni kimoja ya vitabu vikuu katika nyanja ya Usulul-Fiqh ambacho wanafunzi wa Seminari ya Theolojia wanahitaji kukisoma jinsi wanavyoendelea katika masomo yao ili kufikia kiwango cha juu cha usomi – Ba’thul Kharij. (Mfasiri) 14 Tokea pale hotuba hii ilipotolewa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1963. (Mfasiri). 15 Imesimuliwa kwamba Ayatullah Khu’i alikuwa akitoa darasa juu ya Tafsir ya Qur’ani miaka 8 au 9 iliyopita huko Najaf, baadhi yake ambazo zimechapwa katika muundo wa kitabu. 60


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 61

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Mwanachuoni huyu ndipo akamwambia Ayatullah Khu’i (Quddisa Sirruh) kwamba, “Allamah Taba’tabai (Quddisa Sirruh) ameziendeleza darasa zake za Tafsir ya Qur’ani huko Qum na hivyo, muda wake mwingi unatumika katika eneo hili la kuchunguza na kutafiti.” Ayatullah Khu’i akajibu, “Ayatullah Taba’tabai amejitoa muhanga mwenyewe – yeye amejitenga na jamii” na alikuwa sahihi. Inashangaza kwamba katika mambo nyeti kabisa ya dini, endapo tunamuona mtu ambaye amejitolea maisha yake yote katika kuichunguza Qur’ani, basi ataangukia kwenye maelfu ya shida na matatizo kutoka kwenye mtazamo wa chakula chake, maisha kwa jumla, tabia yake (ndani ya jamii), heshima yake na ataondolewa kutoka, na kunyimwa mambo mengi. Hata hivyo, kama angekuwa ayatumie maisha yake yote katika kusoma vitabu kama “Kifayah,” basi angekuwa mwenye kustahili kupata kila kitu! Hivyo, kwa mukhtasari, tunaweza kuwapata maefu ya watu ambao wanakijua kitabu cha “Kifayah” vizuri sana. Wao wanayajua vile vile majibu ya kwenye hoja zinazotolewa kutoka kwenya “Kifayah” na wanayajua pia majibu ya majibu yaliyotolewa – na wanayajua hata majibu ya majibu ya majibu ya “Kifayah” ingawa hata hivyo hatuwezi kupata hata watu wawili wanaoijua Qur’ani sawasawa! Kama utamuuliza mwanachuoni yoyote kuhusu aya ya Qur’ani, watasema kwamba ni lazima warudi na kuirejea kwenye Tafsir ya Qur’ani. Kile ambacho kinashangaza zaidi hata kuliko hiki ni kwamba kile kizazi kikongwe kimeshuhulika kwa namna hii kwenye Qur’ani, hata hivyo tulikuwa na matumaini makubwa kwamba hiki kizazi kipya cha vijana kingekuwa na uwezo wa kuisoma Qur’ani, kuielewa na kuifanyia kazi! Kama vizazi vilivyotangulia visingekuwa vimekengeuka kutoka 61


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 62

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya kwenye Qur’ani, basi bila shaka, hiki kizazi kipya vile vile kisingepotoshwa kutoka kwenye njia ya Qur’ani. Hivyo, ni sisi wenyewe ambao tumeshughulika katika namna hii na kujichumia ghadhabu na laana ya Mtume (s.a.w.w.) na Hiyo Qur’ani. Kuhusiana na Qur’ani, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:

Kwa hii tuna maana kwamba, mbele ya Mwenyezi Mungu swt. Qur’ani ni muombezi na huo uombezi wake utakubalika, na kuhusiana na wale watu ambao wanaipuuza Qur’ani, itakuja kulalamika (kwa Mwenyezi Mungu swt.) na malalamiko yake yatakuja kukubaliwa pia.16 Ni vizazi vyote, kile kikongwe na hiki kipya ambavyo havikutenda haki juu ya Qur’ani na vinaendelea kufanya hivyo. Ni kile kizazi kilichotangulia ambao wamelianzisha jambo hili la kuipuuza Qur’ani, na ni hiki kizazi kipya kabisa ambao wanaendelea katika nyayo zao. Kwa kulihitimisha hili; katika suala la uongozi wa vijana, zaidi ya jambo jingine lolote, kuna mambo mawili ambayo ni lazima tuyafanye: 1) Ni lazima tukitambue kile ambacho kinakitatiza kizazi hiki. Tutakapokuwa tumelifanya hili, ndipo tunaweza kuketi chini na kufikiri juu ya tiba na dawa kwa ajili ya matatizo yao, kwa vile bila kujua ni nini kinachowatatiza, itakuwa sio rahisi kusonga mbele na kuyatibu maradhi hayo. 16 al-Kafi, Juz. 2, uk. 599

62


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 63

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Jambo la pili ni kwamba kizazi cha zamani ni lazima kijisahihishe chenyewe. Kizazi hicho cha zamani lazima kiombe msamaha kwa ajili ya lile kosa kubwa sana ambalo wamelitenda na kwamba nalo hilo ni kwamba wameiacha na kuipuuza Qur’ani. Ni lazima sisi sote turejee kwenye hii Qur’ani na tuiweke Qur’ani hiyo mbele yetu, kisha tusonge mbele chini ya kivuli cha mwongozo wa Qur’ani ili tupate kuwa na uwezo wa kupata furaha na ukamilifu.

* * * * * VIJANA

1. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kipindi cha Ujana ni tawi miongon mwa wendawazimu.”17

2. Imam Ali ibne Abi Talib (a.s.) amesema: “Ujinga wa kijana una udhuru na elimu yake hudharauliwa ..”18

17 al-Ikhtisas, uk. 343. 18 Ghururul Hikm, Hadithi ya 4768 63


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 64

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

3. Imam Ali ibne Abi Talib (a.s.) amesema: “Kuna mambo mawili ambayo watu hawajui uzito wa umuhimu wao mpaka wayapoteze: ujana wao na afya njema.”19

4. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Wabora wa vijana wenu ni wale wanaofanana na walio wazee wenu20 na waovu wa wazee wenu ni wale wanaofanana na vijana wenu.”21.

19 Ibid, Hadithi ya 5764. 20 Mnapaswa kujua kwamba watu wako katika mafungu namna mbili ambayo kwamba kundi moja ni la kijana ambaye amejiweka mbali na kufuata tamaa za hisia zake duni na yuko mbali na ujinga ambao umeambatana na kipindi cha zama za kijana huyo. Anayo shauku ya kuelekea kwenye wema na kujiweka mbali na sifa mbaya, na kuhusu kwenye kundi la vijana wa namna hii ambalo Mtume (s.a.w.w.) amesema: ???? ??? ?? ??? ???? ?? ????

“Mola Wako anafurahiwa kuona na kijana ambaye amejiweka mbali na kufuata mambo ya kitoto-. matamanio ya hisia zake duni na yuko mbali na ujinga ambao umeambatana na zama za ujana wake.” 21Kanzul-Ummal, Hadithi ya 43058. 64


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 65

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

5. Imam Ja’far ibne Muhammad as-Sadiq (a.s.) amesema: “Wakati wowote Waraqah ibn Nawfil alipokuwa akienda kumuona Khadija binti Khuwaylid, alikuwa akimshauri yeye kama hivi: “Unapaswa kujua kwamba kwa hakika kijana ambaye ana tabia njema ni ufunguo wa kwenye mema yote na anawekwa mbali na maovu yote, wakati ambapo yule kijana mwenye tabia mbaya anatengwa mbali na mambo mema yote, naye ni ufunguo wa kwenye maovu yote.”22

6. Imam Ali ibne Abi Talib (a.s.) amesema: “Unapaswa kujua kwamba, Mwenyezi Mungu awe na rehma juu yenu; hakika mnaishi katika zama ambamo wale wasemao Haki humo ni wachache sana kwa idadi ……. Vijana wao ni wakaidi, na mabarobaro wao ni watenda dhambi, na wanachuoni wao ni wanafiki.”

22 Amali cha al-Tusi, uk. 302 na 598. 65


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 66

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

KUWAFUNDISHA VIJANA

7. Imam Ali ibne Abi Talib (a.s.) amesema: “Kwa hakika moyo wa kijana ni kama ardhi ambayo ni tupu itakubali chochote utakachotupa juu yake (na hicho ndicho kitakacho ota kutoka humo).” 23

8. Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) alimwambia sahaba mmoja aliyeitwa Al-Ahwal: “Je, umewahi kwenda Basra?” Mtu huyo akajibu, “Ndiyo.” Imam (a.s.) ndipo akamuuliza; “Ulizionaje shauku za watu kuhusiana na jambo hili (la Wilayah na Uimam wa Ahlul-Bayt) na kuukubali kwao?” Yule mtu akajibu; “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, hakika wale watu (ambao wanalifuata na kulikubali hili) ni wachache kwa idadi. Wanalifanyia kazi hili (kuilingania imani hii kwa wengine) ingawaje ni wachache kwa idadi.” Imam akamjibu akisema: “Ninakushauri kufanyia kazi juu ya vijana (katika kuwaelimisha juu ya mambo haya) kwa vile wao ni wepesi wa kukubali mambo yote mazuri.’”24 23 Tuhaful-Uqul, uk. 70 24Qurbul-Isnad, uk. 128 na 450. 66


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 67

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

KUTAFUTA ELIMU UKIWA BADO KIJANA

9. Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mtu anayetafuta elimu wakati akiwa kwenye ujana wake ni sawasawa na kitendo cha kuandika kitu juu ya jiwe; wakati ambapo yule mtu anayetafuta elimu pale anapokuwa ni mtu mzima ni sawa na kitendo cha kuandika kitu kwenye maji.”25

10. Imam Ali ibne Abi Talib (a.s.) amesema: “Kupata elimu katika ujana wake mtu ni sawa na kuandika kitu kwenye jiwe (kitabakia hapo siku zote).26

11. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kama mtu ambaye haitafuti elimu pale anapokuwa bado ni kijana, bali anakuja 25 Biharul-Anwar, Juz. 1, uk. 222; Hadith ya 6 na uk. 224, Hadith 13. 26 Ibid

67


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 68

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya kuitafuta wakati anapokuwa mtu mzima na akafariki akiwa katika hali hii, basi anafariki akiwa kama Shahid.”27

12. Nabii Ayyub (a.s.) amesema: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu hupandikiza hekima katika moyo wa kijana na mtu mzima. Kwa hiyo basi, kama Mwenyezi Mungu anamfanya mja kuwa mwenye hekima katika ujana wake, basi hataishusha hadhi yake mbele ya macho ya wenye elimu kwa vile tu ni wa umri mdogo kwani wao wataiona ile nuru tukufu ya Mwenyezi Mungu iking’ara kutoka kwa mtu huyu.”28

KIJANA NA KUJIZUIA KUTOKANA NA KUTAFUTA ELIMU

13. Imam Musa ibn Ja’far al-Kadhim (a.s.) amesema: “Kama ningekuwa nimuone kijana miongoni mwa vijana wa Shi’ah ambaye hajipatii elimu ya kina na uwezo wa kuelewa, kwa hakika nitampiga kwa upanga.”29 27 Kanzul-Ummal, Hadith ya 28843. 28 Tanbiyatul Khawatir, uk. 37 29 Fiqhul-Ridha, uk. 337 68


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 69

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

14. Imam Muhammad ibne Ali al-Baqir (a.s.) amesema: “Kama ningekuwa nimuone kijana miongoni mwa vijana wa Shi’ah ambaye hajishughulishi katika kujitafutia elimu na ufahamu wa kina (juu ya dini), basi mimi nitamkaripia vikali mno.”30

15. Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mimi sipendi kuwaona vijana kutoka miongoni mwenu isipokuwa kwamba yeye, awe mvulana au msichana, anayatumia maisha yake katika moja ya hali hizi mbili: imma kama mwanachuoni au kama mwanafunzi. Halafu basi, kama hayuko katika moja ya hali hizi, basi yeye ni mtu mmoja ambaye amepoteza au kufuja (kitu), na kwa kweli mwenye kufuja ni mtu ambaye ametumia vibaya kitu na kwa hakika kitendo cha kutumia kitu vibaya ni cha dhambi na mtu mwenye kutenda dhambi atakuwa na makao yake ndani ya Moto wa Jahannam – Ninaapa kwa yule ambaye alimteua Muhammad kwa Haki.” 31

30 Al-Mahasin, Juz. 1, uk. 357 na 760 31 Amali, ya al-Tusi, uk. 303 na 604 69


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 70

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

UMASHUHURI WA MTU KIJANA ANAYEMUABUDU MWENYEZI MUNGU

16. Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu, Aliye Juu, anampenda sana mtu kijana ambaye anatubia (kwa ajili ya dhambi zake).”32

17. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna kitu kinachopendeza sana kwa Mwenyezi Mungu, Aliye Juu, kuliko kijana ambaye anatubia (kwa ajili ya dhambi zake), na hakuna jambo lenye kuchukiza sana machoni mwa Mwenyezi Mungu, Aliye Juu kuliko mtu mzima ambaye anadumu katika kumuasi Yeye.”33

32 Kanzul-Ummal, Hadith ya 10185 33 Ibid; Hadith ya 10233 70


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 71

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 18. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hujisifia kwa Malaika Zake kuhusiana na mtu ambaye kijana ambaye ni mja Wake na Anasema, ‘Hebu muangalieni yule mja Wangu! Amejizuia kutokana na kufuata matamanio yake duni kwa ajili Yangu tu.”34

19. Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “ubora wa mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu ambaye ni kijana, na ambaye anamuabudu Mwenyezi Mungu katika hatua za ujana wake juu ya mtu mzima ambaye anamuabudu Mwenyezi Mungu baada ya kuwa amekuwa mzee, ni sawa na ubora wa mitume (Manabii na Mitume) juu ya viumbe wengine wote.”35

20. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kuna watu aina saba watakaopata hifadhi chini ya kivuli cha Kiti cha Enzi (Mamlaka) cha Mwenyezi Mungu, aliye Mtukufu na Mkuu katika hiyo siku ambapo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli Chake: kiongozi muadilifu ….. na kijana aliyeyatumia maisha yake 34 Ibid; Hadith ya 43057 35 Kanzul-Ummal, Hadith ya 43059.

71


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 72

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya katika kumuabudu Mwenyezi Mungu, Mtukufu na Mkuu.”36 UMASHUHURI WA MTU ANAYETUMIA UJANA WAKE KATIKA UTII KWA MWENYEZI MUNGU

21. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna kijana hata mmoja ambaye ataipa mgongo dunia yenye kupita na anasa zake kwa ajili tu ya radhi za Mwenyezi Mungu na akayatumia maisha yake ya ujana katika utii kwa Mwenyezi Mungu mpaka anafikia umri wa uzee wake, isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu atampatia malipo ya watu wakweli na waadilifu sabini na wawili.”37

22. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kwa hakika kiumbe kipenzi sana cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mkuu, ni yule kijana ambaye ni mdogo kwa umri na ambaye ni mtu mtanashati/mzuri na hata hivyo akauweka ujana na uzuri wake kwa Mwenyezi Mungu na katika kumtii Yeye peke yake. Hili ndio jambo ambalo kwalo Yeye Mwingi wa Rehma anajisifia nalo kwa Malaika Zake na anasema: “Huyu kwa hakika ni mja Wangu.’”38 36 al-Khisal, uk. 343, Hadith ya 8. 37 Makarimul-Akhlaq, Juz. 2, uk. 373. 38 Kanzul-Ummal, Hadith ya 43103 72


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 73

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

23. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu anampenda yule mtu kijana ambaye anayatumia maisha yake ya ujana katika utii kwa Mwenyezi Mungu, Aliye Mtukufu.”39

24. Amesema Nabii Ibrahim (a.s.) kwamba siku moja aliamka na akaona unywele mweupe katika ndevu zake na akasema: “Sifa zote njema ni za Kwake Mwenyezi Mungu, Mola wa ulimwengu wote, ambaye amenifanya mimi kufikia hatua hii katika maisha yangu, ambamo mimi sijawahi kumuasi Yeye Mwenyezi Mungu kwa kiasi cha angalau mpepeso wa jicho.”40

39 Kanzul-Ummal, Hadith ya 43060 40.40 Illulush-Shara'iyah, Juz. 2, uk. 104; Hadith ya 2. 73


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 74

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

MAELEZO YA SIFA BAINIFU ZA KIJANA {AL-FATA}

25. Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) alimuuliza Sulayman ibne Ja’far al-Hadhali kama ifuatavyo: “Ewe Sulayman, ni nini kinamaanishwa na neno kijana (al-Fata)?” Yeye akajibu akisema: “Najitowa kafara kwa ajili yako. Kwa maoni yetu sisi, kijana (alFata) ni babaru (Shababi).” Imam akaniambia, “Hata hivyo, unapaswa kujua kwamba kwa hakika wale Watu wa Pango (As’habulKahf) wote walikuwa ni watu wazima, hata hivyo mbona Mwenyezi Mungu anawataja kama vijana ambao wana imani ya kweli?! Ewe Sulayman, yule mtu anayemuamini Mwenyezi Mungu na akawa na utambuzi juu Yake basi huyo ni kijana.”41

41 Tafsir al-Ayashi, Juz. 2, uk. 323; Hadith ya 11. 74


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 75

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 26. Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) alimuuliza mtu mmoja: “Ni nini kinamaanishwa na neno kijana (al-Fata) kwa makisio yako wewe?” Yule mtu akajibu, “ni kijana.” Imam (a.s.) akamjibu, “Hapana, kijana (al-Fata) ni yule muumini wa kweli. Kwa hakika wale Watu wa Pango (As’habul-Kahf) wote walikuwa watu wazima, hata hivyo, Mwenyezi Mungu, Utukufu na Ukuu ni wake, anawaita wao ni vijana kwa imani yao.”42

Imam Hasan ibne Ali al-Mujtaba (amani iwe juu yake) amesema: “Kwa hakika leo ninyi ni vijana wa umma, na kesho, ninyi mtakuwa ndio viongozi wa jamii, hivyo, ni lazima juu yenu kuitafuta ilmu. Halafu basi, kama mtakuwa hamna uwezo wa kuyahifadhi yale yote mnayojifunza, basi ni lazima muyaandike na kuyahifadhi (kwa utunzaji wa salama) ili kwamba muwe mnaweza kuyarejea baadae (wakati mtakapoyahitaji).” Biharul-Anwaar, Juz. 2, uk. 152, Hadith ya 37.

42 al-Kafi, Juz. 8, uk. 395 na 595. 75


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 76

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1.

2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na Saba Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudhar Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 76


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 77

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur’an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillahi ni sehemu ya Qur’ani Sauti ya uadilifu wa Binadamu Kufungua Safarini. Kusujudu juu ya udongo. Maulidi Malumbano baina ya Sunni na Shia

77


Kuwaongoza vijana wa kisasa 2.qxd

7/2/2011

10:57 AM

Page 78

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya

BACK COVER Vijana wetu siku hizi wametekwa nyara na tamaduni za magharibi na kuiga kila kinachotoka huko kuanzia mavazi mpaka fikira na mwelekeo wa kimaisha kiasi kwamba hawana habari na tamaduni zao, wamekuwa wapinzani wa kila lisiloafikiana na mawazo yao ya kimagharibi. Katika kitabu hiki mwachuoni huyu anajaribu kuzijibu changamoto zinazoletwa na zama hizi, hususan kutoka kwa vijana hawa wa kisasa. Imamu Hasan Ibn Ali Ibn Abu Talib alisema: “Hakika leo wewe ni kijana wa taifa, na kesho mtakuwa viongozi wa umma, hivyo, inakuwajibikieni juu yenu kutafuta elimu. Ili kwamba kama huwezi kuyahifadhi yale yote unayojifunza, basi lazima uyaandike na kuyahifadhi ili baadae uweze kuyarejea (wakati ukuyahitaji).�

Biharul Anwar.J. 2, uk. 152. Hadithi 37. Hivyo, muhimu kwa vijana ni kusoma na kupata ujuzi wa kupambanua jema na ovu, na ili waje wawe viongozi wazuri na sio wasanii na waigizaji wa manbo ya hovyo ya nchi za magharibi. Kimetolewa na kuchapishwa na: Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 2110640

78

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya  

Vijana wetu siku hizi wametekwa nyara na tamaduni za magharibi na kuiga kila kinachotoka huko kuanzia mavazi mpaka fikira na mwelekeo wa kim...

Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya  

Vijana wetu siku hizi wametekwa nyara na tamaduni za magharibi na kuiga kila kinachotoka huko kuanzia mavazi mpaka fikira na mwelekeo wa kim...

Advertisement