Page 1

Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Mfululizo wa Masuala ya Kifikihi

as - Sujuud ‘Ala ‘l-’Ardh ‘Alaa Dhaw’i ‘l-Kitaab wa ‘s-Sunnah

KUSUJUDU JUU YA UDONGO KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNA

Kimeandikwa na:

Sheikh Ja’far Subhani

Kimetarjumiwa na:

Hemedi Lubumba Selemani

Page A


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

'Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 9987 - 427 - 48 - 0

Kimeandikwa na:

Sheikh Jafar Subhani Kimetarjumiwa na:

Ustadh Lubumba Kimehaririwa na: Ustadh Abdallah Mohamed Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: Machi, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na:

Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Fax: +255 22 2127555 Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info

Page B


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page C

YALIYOMO Kusujudu juu ya udongo kwa mujibu wa kitabu na Sunna...............2 Kusujudu juu ya udongo.................................................................. 4 Tofauti za wanazuoni wa sheria kuhusu sharti za kitu cha kusujudu juu yake.............................................................................................5 Tofauti kati ya msujudiwa na kisujudio..........................................10 Sijda Kilugha (ya kiarabu).............................................................11 Siri ya kuachwa wazi paji la uso katika sijda.................................13 Suna ya Mtume katika kusujudu zama zake na baada yake.............16 Kipindi cha mwanzo: kusujudu juu ya ardhi....................................17 Kupoza changarawe ili kusujudu juu yake................................................................................................. 19 Amri ya kufikisha udongo kwenye paji...........................................20 Amri ya kuondoa kilemba kwenye paji la uso................................22 Mwenendo wa Mtume katika kusujudu...........................................23 Mwenendo wa maswahaba na Tabiina katika kusujudu..................25


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page D

Hatua ya pili: Kuruhusiwa kusujudu juu ya khumra na mkeka.............................27 Hatua ya Tatu: Kusujudu juu ya nguo kwa udhuru..................................................30 Matokeo ya uchunguzi.....................................................................33 Ni ipi siri ya kuchukua kipande cha udongo Tohara.......................35 Mwisho wa Safari............................................................................39

D


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page E

Neno la mchapishaji Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la: "Al-Sujuud Alal-Ardh" Sisi tumekiita: "Kusujudu juu ya udongo." Kitabu hiki, "Kusujudu juu ya udongo" ni matokea ya utafiti wa kielimu uliofanywa na Mwanachuoni wa Kiislamu, Sheikh Jafar Subhani. Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake. Wanachouni wa Kiislamu kama kawaida ya wanadamu wamehitilafiana katika hukumu ndogo ndogo katika matendo ya ibada, lakini kama ilivyo, tofauti ndogo kati ya wanachuo kwa wafuasi inakuwa ni mlima wa tofauti na kusababisha zongo lisilo na maana. Mambo ambayo wanachuo wetu wamehitilafiana si katika asili au misingi ya dini, na isitoshe ni mambo machache sana ukilinganisha na yale tunayokubaliana nayo. Kusujudu juu ya udongo ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu. Kwa hiyo hii sio hitilafu ya madhehebu, bali ni hitilafi ya wanachuo wa madhehebu zote wamehitilafiana juu ya suala hili. Lakini bahati mbaya Waislamu wengi hawaitambui hitilafu hii kwa usahihi na hivyo kuongelea katika dhana na kusababisha mizozo isiyokuwa na maana. Kutokana na hali hii Sheikh wetu, Jafar Subhani amelifanyia E


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page F

utafiti wa kina suala hili na kuweka wazi asaili ya hitilafu hii, kisha akamuachia msomaji mwenyewe kutoa uamuzi. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya ’Al-Itrah Foundation’ imeona ikitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yale yale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani (Lipumba) kwa kukubali jukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 2110640

F


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 1


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 2

Kusujudu juu ya udongo

KUSUJUDU JUU YA UDONGO KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNA Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu mlezi wa ulimwengu. Rehma na Amani zimfikie mbora wa viumbe na hitimisho la mitume Wake, pia kizazi chake kitakatifu ambacho ndio kasha la elimu yake na hazina ya mafunzo yake. Hakika Uislamu ni imani na sheria. Imani ni kuamini Mwenyezi Mungu, Mitume wake na Siku ya Mwisho. Na sheria ni hukumu za Mwenyezi Mungu ambazo zina jukumu la kumpa mwanadamu maisha bora na kumhakikishia mafanikio ya dunia na akhera. Sheria ya kiisilamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake, hivyo Mwenyezi Mungu akasema:

“Leo nimewakamilishia dini yenu na kuwatimizieni neema yangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu.�1 1 Al-Maida:3. 2


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 3

Kusujudu juu ya udongo Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanavyuoni wa sheria wametofautiana kwa sababu ya kutofautiana kwao kuhusu riwaya ambazo zimenasibishwa kwa Mtume. Jambo ambalo limepelekea kutofautiana kuhusu masuala madogo madogo ya sheria. Kwa kuwa ukweli hutokana na uchunguzi basi hakika katika mtiririko wa masomo haya tumejaribu kuliweka swala hili juu ya meza ya uchunguzi, kwani huenda ikawa ndio njia ya kuunganisha mtazamo na kupiga hatua katika uwanja huu. Kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dini hata ipelekee kuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyopo ni kuhusu riwaya zilizonasibishwa na Mtume, nalo ni jambo dogo ukilinganisha na mambo mengi ambayo tunaafikiana kati ya madhehebu za Kiislamu. Na muongozo wetu katika njia hii ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote kwa pamoja wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neema Zake mkawa ndugu.� (al-Imran; 3:103).

Sheikh Jafar Subhany Taasisi ya Imamu Sadiq (a.s.) Qum

3


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 4

Kusujudu juu ya udongo

KUSUJUDU JUU YA UDOGO Kati ya alama dhahiri zaidi za utumwa, unyenyekevu na udhalili wa kiumbe kwa muumba Wake ni kusujudu. Kupitia kusujudu muuminu hutilia nguvu utumwa wake kwa Mwenyeezi Mungu. Na Muumba aliyetukuka humkadiria mja Wake udhalili na utiifu na humtiririshia mwenye kusujudu mtiririko wa fadhila Zake na hisani Yake kubwa. Kwa ajili hiyo imepokewa ndani ya baadhi ya riwaya kuwa: Ndani ya sijda ndipo mja awapo karibu mno na Mola Wake . Kati ya ibada zote, Swala ndio ngazi pekee inayomtofautisha muumini dhidi ya kafiri, huku kusujudu kukiwa ni nguzo miongoni mwa nguzo zake, basi hakuna alama ya dhahiri mno katika kudhihirisha unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu kuliko kusujudu juu ya udongo, mchanga na changarawe, hii ni kutokana na unyenyekevu wa dhahiri na bayana unaopatikana hapo kuliko ule unaotokana na kusujudu juu ya mkeka na kirago, ukiachia mbali ule unaotokana na kusujudu juu ya mavazi ya kifahari, matandiko, dhahabu na fedha. Japokuwa katika hali zote hizo ni kusujudu, lakini utumwa unadhihirika mno katika fungu la mwanzo kwa kiwango kisichoweza kudhihiri katika fungu lingine. Shia Imamia hulazimika kusujudu juu ya udongo safarini na nyumbani, na wala hawana mbadala ila kile kiotacho toka aridhini kwa sharti kisiwe chenye kuliwa wala kuvaliwa, wala hawaoni ni sahihi katika hali ya kuswali, kusujudu juu ya kile kisichokuwa udongo wala kisichoota toka aridhini kwa kufuata Sunna iliyothibiti kwa wingi toka kwa Mtukufu Mtume na kizazi chake na maswahaba 4


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 5

Kusujudu juu ya udongo zake. Itadhihiri - ndani ya uchunguzi - kuwa kulazimika kusujudu juu ya udongo au kilichoota toka aridhini ilikuwa ndio Sunna ya maswahaba na kitendo cha kuacha Sunna hiyo kilizuka zama za baadaye.

TOFAUTI ZA WANAZUONI WA SHERIA KUHUSU SHARTI ZA KITU CHA KUSUJUDU JUU YAKE Waislam wote wameafikiana juu ya wajibu wa kusujudu ndani ya Swala, mara mbili ndani ya kila rakaa moja, pia hawajatofautiana juu ya msujudiwa kwani kwa hakika msujudiwa ni Mwenyezi Mungu ambaye husujudiwa na vile vilivyomo mbinguni na ardhini kwa kutaka na kutotaka2 Mbiu ya kila muislamu ni kauli ya Mwenyezi Mungu: “Msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba.”3 Ispokuwa wametofautiana juu ya sharti za kitu cha kusujudu juu yake; namaanisha kile anachotumia mwenye kusujudu kuweka paji lake juu yake. Kwa Shia Imamia kwao ni sharti kitu hicho cha kusujudu juu yake kiwe ni udongo (Ardhi) au kiotacho toka ardhini kisicholiwa wala kuvaliwa, kama vile mkeka na kirago na kinachofanana na hivyo. Madhehebu mengine yamewakhalifu juu ya hilo, na zifuatazo ni 2 Inaashiria kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Mwenyezi Mungu tu vikitaka visitake. Na vivuli vyao asubuhi na jioni. Ar-Raadi: 15 3 Fuswilat: 37

5


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 6

Kusujudu juu ya udongo nukuu za maoni tofauti: Sheikh Tusi4 amesema: - Anabainisha maoni ya Wanavyuoni wa sheria:- Pasipo na dharura haisihi kusujudu ila juu ya udongo au kiotacho aridhini kisicholiwa wala kuvaliwa kuanzia pamba hadi katani. Wanavyuoni wa kisunni wamekwenda kinyume kuhusu hilo, wao wameruhusu kusujudu juu ya pamba, katani, manyoya ya mnyama, sufu na mengineyo- mpaka akasema:- Haisihi kusujudu juu kitu kilicho mwilini kama vile kunjo la kilemba, sehemu ya joho na ukosi wa kanzu, na kauli hii ndio ya Shafi i na imepokewa toka kwa Ali, Ibnu Umar, Ubada bin Swamit, Malik na Ahmad bin Hambali. Abu Hanifa na wenzake wamesema: Iwapo atasujudu juu ya alichokibeba kama vile nguo iliyo mwilini basi itatosheleza. Na iwapo atasujudu juu ya kisichoachana naye, mfano atandike mkono wake na kusujudu juu yake basi itamtosheleza lakini kufanya hivyo ni karaha, hilo limepokewa toka kwa Al-Hasan Al-Basariyu5. Al-Allamah Al-Hilli6 amesema - Akibainisha maoni ya Wanavyuoni kuhusu kitu cha kusujudu juu yake: Haisihi kusujudu juu ya kitu kisicho udongo wala kisicho mmea wake kama vile ngozi na sufu, hili ni kwa wanavyuoni wetu wote. Wanavyuoni wote wa kisunni wamekubaliana kwa kuruhusu7. Mashia wamewafuata Maimamu wao katika hilo ambao wao ndio pacha wa kitabu na mwenza wake kwa mujibu wa Hadithi ya vizito 4- Ni mwanachuoni wa Kishia wa karne ya tano, ana vitabu na maandishi mbalimbali. Amezaliwa mwaka 385 na akafariki mwaka 460 A.H., ni mwanafunzi wa Sheikh Al-Mufid (336-413 Hijiriya) na As-Sayyid As-Sharifu Al-Murtaza (355436 Hijiriya) Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao. 5- Al-Khilafu: 1/357-358, suala la 112-113 kitabu cha Swala. 6 - Al-Hasan bin Yusuf bin Al-Mutahhari Al-Hilliy (348-726 A.H.) Na yeye ni kiongozi wa Mashia katika karne ya saba na karne ya nane. Hajaonekana katika zama mfano wake ila katika vipindi mahsusi. 7 At-Tadhkiratu: 2/434, suala la 100. 6


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 7

Kusujudu juu ya udongo viwili, hivyo sisi hapa tutakomea kutoa sehemu ndogo tu ya yale yaliyopokelewa toka kwao kuhusu upande huu: Amepokea As-Swaduq kwa njia yake toka kwa Hisham bin AlHakam kuwa alimuuliza Abu Abdillah: Nipe habari ni kitu gani inasihi kusujudu juu yake? Na ni kipi hakisihi kusujudu juu yake? Akasema: Haisihi kusujudu ispokuwa juu ya ardhi (udongo) au juu ya kilichoota aridhini ila tu kile kinacholiwa au kuvaliwa. Akamwambia: Mimi ni fidia kwako, niambie ni kwa sababu ipi? Akasema: Kwa sababu kusujudu ni unyenyekevu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hivyo haisihi sijda kuwa juu ya kinacholiwa au kuvaliwa kwa sababu watu wa duniani ni watumwa wa yale wanayokula na wanayoyavaa, na mwenye kusujudu, katika kusujudu kwake huwa yupo katika ibada ya Mwenyezi Mungu, hivyo anapokuwa katika sijda haipasi aweke paji lake juu ya wanachokitumikia watu wa dunia ambao wamehadaika kwa hadaa yake 8 As-Swadiq (a.s.) amesema: Kila kinachokuwa ni matumizi ya mwanadamu katika chakula chake au kinywaji chake au mavazi yake basi haisihi Swala juu yake wala sijda ila tu kile kinachokuwa ni kutokana na mmea wa ardhi usiokuwa tunda kabla haujakuwa nyuzi, ama ukiwa nyuzi haisihi kusujudu juu yake ispokuwa katika hali ya dharura�9. Hivyo haipasi kuwalaumu Mashia wanapowafuata Maimamu wao kwa kushikilia msimamo wa kusujudu juu ya ardhi au kile kioteshwacho na ardhi kisicholiwa wala kuvaliwa. Zaidi ya hapo ni kuwa yale waliyopokea masunni katika mada hii yanaunga mkono 8 Al-Wasailu: Juz: 3, Mlango 1 kati ya milango ya kitu cha kusujudu juu yake, Hadithi ya 1. Na kuna riwaya nyingine zenye madhumuni kama hayo zote zikionyesha kuwa lengo la kusujudu ambako ndio kujidhalilisha hakupatikani kwa kusujudu juu ya kisichokuwa ardhi au kisichoota kisicholiwa wala kuvaliwa, chunguza. 9 Al-Wasailu: 3, mlango 1 mlango wa kitu cha kusujudu juu yake, Hadithi ya 11. 7


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 8

Kusujudu juu ya udongo mtazamo wa Shia na hilo litakudhihirikia ndani ya Hadithi zitakazokuja kupitia njia zao na itakubainikia kuwa Sunna ya Mtume ilikuwa ni kusujudu juu ya ardhi kisha ikaja ruhusa ya kusujudu juu ya mkeka na kirago tu, na wala haijathibiti ruhusa ya tatu bali iliyothibiti ni kuzuwiliwa kwa ruhusa hiyo ya tatu kama utakavyoona. Mwanahadithi An-Nuuriyu ndani ya Al-Mustadrak amepokea kutoka kwenye (Daaimul-Islamu) toka kwa Jafar bin Muhammad toka kwa baba yake toka kwa babu zake toka kwa Ali (a.s.) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: Hakika ardhi ina huruma na nyinyi mnatayamamu kutokana nayo na mnaswali juu yake katika uhai wenu na yenyewe kwenu nyinyi ni sitara itoshayo kwa maiti wenu, hayo ni neema ya Mwenyezi Mungu ana kila sifa njema, hivyo kitu bora anachosujudu juu yake mwenye kuswali ni ardhi safi. 10 Pia imepokewa toka kwa Jafar bin Muhammad (a.s.) kuwa amesema: Inapasa mwenye kuswali aigusishe ardhi paji lake na aweke uso wake kwenye udongo kwa sababu kufanya hivyo ni kujidhalilisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. 11 As-Shaaraniy amesema: Makusudio ni kudhihirisha unyenyekevu kwa kichwa mpaka ardhi iguse uso wake ambao ndio kiungo bora mno kati ya viungo vyake, sawa agusishe kwa paji lake au pua yake bali inawezekana kwa wengine ikawa kuweka pua ni bora kwa kuwa (jina pua ndani ya kiarabu) limetokana na majivuno na kiburi, hivyo atakapoiweka aridhini atakuwa kama kwamba amejitoa kwenye kiburi ambacho ni sifa ya Mwenyezi Mungu, kwani hakika hadhara 10Mustadrakul-Wasailu: 4 mlango 10 mlango wa kitu cha kusujudu juu yake, Hadithi ya 1. 11 Mustadrakul-Wasailu: 4/14, mlango wa 10 mlango wa kitu cha kusujudu juu yake, hadithi ya 2. 8


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 9

Kusujudu juu ya udongo ya Mwenyezi Mungu ni haramu kuingia mtu mwenye chembe ya kiburi angalau ndogo. Hakika hadhara hiyo ndio pepo kubwa ya halisi, na Mtume amesema: Hatoingia peponi mtu yeyote mwenye chembe yoyote ya kiburi moyoni mwake. 12 Imamu Al-Maghribiy Al-Maliky Al-Raw daniy amenukuu kwa kuvusha toka kwa Ibnu Abbas: Mtu yeyote asiyeigusisha ardhi pua yake pamoja na paji lake pindi anaposujudu basi Swala yake haisihi 13 Kama ilivyo asili ya kitendo cha kiibada ni amri ielekezwayo na mtu mahususi, pia sharti zake na kanuni zake ni mambo mengine ambayo ni lazima yabainishwe na kufafanuliwa na mfafanuzi na mfikishaji wa sheria, na hapa tunamaanisha Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa sababu yeye ndiye kigezo kwa mujibu wa maelezo ya Qur ani tukufu na ndio mfafanuzi wa kitabu kitukufu na ni wajibu kwa waislamu wote wajifunze hukumu za dini yao na vipengele vya sheria yao toka kwake. Mwenyezi Mungu amesema: “Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na kumtaja Mwenyezi Mungu sana”14. “Na anachokupeni Mtume basi pokeeni na anachokukatazeni basi jiepusheni.”15 12Al-Yawaqiti wal-Jawahiri fi Aqaidil-Akabiri: Abdul-Wahabi bin Ahmad bin Ali Al-Answariy Al-Misriy maarufu kwa jina la As-Shaaraniy (Ni kati ya wanavyuoni maarufu wa karne ya kumi): 1/164. Chapa ya kwanza. 13 Muhammad bin Muhammad bin Sulaymani Al-maghribiy (Aliyefariki mwaka 1049) amekusanya kitabu Al-Fawaidu min Jaamiul-Usulu na Maj’maul-Zawaidi: 1/214 namba 1515. 14 Al-Ahzab: 21 15 Al-Hashri: 2. 9


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 10

Kusujudu juu ya udongo

TOFAUTI KATI YA MSUJUDIWA NA KISUJUDIO Mara nyingi hudhaniwa kuwa kukazania kusujudu juu ya ardhi au kiotacho toka aridhini ni bidaa; na udongo unaotumika kusujudu juu yake hufikiriwa kuwa ni sanamu, na hawa ndio wasiotofautisha kati ya msujudiwa na kisujudio. Na wanadai kuwa jiwe au udongo unaowekwa mbele ya mwenye kuswali ni sanamu analoliabudu mwenye kuswali kwa kuweka paji lake juu yake. Lakini si lawama juu ya Shia iwapo ufahamu wa mpinzani utakuwa finyu na akawa hajatofautisha kati ya mambo mawili na akadai kuwa kisujudio ndio msujudiwa, akalinganisha jambo la mwanatauhidi na jambo la mshirikina eti kwa hoja ya ushirikiano wa nje. Akashikilia muonekano na mtazamo ilihali kipimo ni kuchukua malengo na dhamira ya ndani, kwa sababu kwa muabudu masanamu, sanamu ni muabudiwa na msujudiwa, analiweka mbele yake na anasujudu na kurukuu kwa ajili yake. Lakini mwanatauhidi ambaye anataka kuonyesha udhalili mpaka kiwango cha mwisho yeye ananyenyekea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na anasujudu kwa ajili Yake anaweka paji lake na uso wake juu ya udongo, jiwe, mchanga na changarawe kudhihirisha kuwa yeye ni sawa na hivyo wakati wa kuthaminisha, akisema: Udongo si chochote mbele ya Mlezi wa walezi. Ndio, mwenye kusujudu juu ya udongo si mwenye kuuabudu bali yeye anajidhalilisha kwa Mola Wake kwa kusujudu juu yake, na atakayedhania kinyume na hivyo basi yeye amedhoofika kiakili na 10


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 11

Kusujudu juu ya udongo hilo litapelekea kuwatilia shaka wote wenye kuswali na kuhukumu ushirikina wao, hivyo anayesujudu juu ya busati na kitambaa na kingine lazima awe anakiabudu, kwa utaratibu huu inashangaza sana. Al-Amidiy amepokea toka kwa kiongozi wa waumini (a.s.) kuwa amesema: Kusujudu kimwili: Ni kuweka sharafu za nyuso juu ya udongo. 16

‘SIJDA’ KILUGHA (YA KIARABU) Hapana shaka kuwa kusujudu ni kati ya faradhi za sala na makundi yote mawili yamepokea toka kwa Ibnu Abbas kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Nimeamrishwa kusujudu kwa kutumia mifupa saba: Paji la uso, mikono miwili, magoti mawili na vichwa vya nyayo mbili. 17 Pamoja na hayo ni kuwa ukweli halisi wa sijda ni kuweka paji juu ya ardhi, ama vilivyobaki ni sawa na sharti za sijda na hilo linaonyeshwa na kauli za wanakamusi pale wanapotoa maana ya neno sijda kwani hawataji isipokuwa kuweka paji juu ya ardhi, hivyo ni kama kwamba viungo vingine ni sharti za sijda ambayo muweka sheria ameifaradhisha kisha akaiunganisha na ukweli wake halisi wa kilugha na kijamii. Ibnu Mandhur amenukuu toka kwa Ibnu Sayyidihi amesema: Kitenzi: ??? ???? ????? Sajada, yasujudu, sujudan (Kiarabu) ni ali16Ghurarul-hikam wa Duraril-Kalam: 1/107, namba 2234. 17Mashekhe wawili wameitoa, Bukhari: 1/206 na Muslim: 1/354. 11


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 12

Kusujudu juu ya udongo weka paji lake aridhini. Na kundi la watu ni: Sujadu na Sujudu18. Ibnu Al-Athiri amesema: Sijda ya Swala ni kuweka paji juu ya ardhi na wala hakuna unyenyekevu mkubwa mno kuliko huo 19 Ndani ya kamusi Tajul-urusi min Jawahiril-Qamusi: Sajada: Alinyenyekea na kati ya unyenyekevu ni sijda ya Swala nayo ni kuweka paji juu ya ardhi na wala hakuna unyenyekevu mkubwa mno kuliko huo na jina ni sijda 20. Maneno haya yaliyothibiti ndani ya vitabu vya lugha toka kwa waandishi wa kamusi na mfano wake yanaonyesha kuwa ukweli hasa na sijda halisi ni kuweka paji juu ya ardhi na laiti kama Mtume asingeamrisha kusujudu kutumia viungo saba basi ingetosha kuweka paji juu ya ardhi, lakini yeye katika kuweka sheria ameongeza mambo mengine na wajibu ikawa ni kusujudu kutumia viungo saba. Ikiwa hali ndio hiyo basi hakuna makosa kitendo cha kuweka paji kuwa na sharti mahususi la pekee lisilohusu viungo vingine, nalo ni sharti la kisujudio chake kuwa ni ardhi au kiotacho toka aridhini na wala haisihi kusujudu juu ya kitu kingine, na si viungo vingine.

18 Lisanul-Arabi: 6 neno Sajada. 19 An-Nihayatu: 2 neno Sajada. 20 Tajul-urusi: 8 neno Sajada. 12


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 13

Kusujudu juu ya udongo

SIRI YA KUACHWA WAZI PAJI LA USO KATIKA SIJIDA Na linaloonyesha hilo ni wanafiqihi wengi wa kisunni kuona ni lazima kuacha wazi paji na si viungo vingine, hivyo laiti kama viungo vingine vingekuwa na nafasi kama paji katika ukweli halisi wa sijda basi hukumu yake ingekuwa kama hukumu ya paji, ilhali ukweli ni tofauti. Ndani ya Muhtasari wa Abul-Qasim Al-Kharaqiy na ufafanuzi wake kuna: Wala si lazima kwake kugusa msala moja kwa moja kwa chochote ila kwa paji, kwa mujibu wa moja kati ya riwaya mbili. Na katika riwaya nyingine ni lazima kugusa msala kwa paji bila kizuizi, hilo limetajwa na Abul-Khitabi. Na Athramu amepokea akasema: Nilimuuliza Aba Abdillah kuhusu kusujudu juu ya kunjo la kilemba akajibu: Haisihi kusujudu juu ya kunjo lake bali kilemba huondolewa , na haya ndio madhehebu ya Shafi. Khababu amesema: Tulimlalamikia Mtume kuhusu joto la ardhi linavyounguza vipaji vyetu na viganja vyetu, lakini hakutujali akaendelea kusimulia mpaka akasema - na kutoka kwa Ali amesema: Iwapo mmoja wenu anaswali basi aondoe kilemba chake toka kwenye paji lake. Ameipokea Al-Bayhaqiy21. Ndani ya Al-Wajiza: Ni lazima kuacha wazi paji katika kusujudu kutokana na riwaya ya Khababu, amesema: Tulimlalamikia Mtume kuhusu joto la ardhi linavyounguza vipaji na viganja vyetu, lakini hakutujali, yaani tukaendelea kulalamika. Katika ufafanuzi amese21As-Sharhu Al-Kabiru ala matni Al-Kharaqiy: 1/557-558 kwenye hamishi ya AlMughniy 13


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 14

Kusujudu juu ya udongo ma: Wala si lazima kuacha paji lote wazi bali inatosha sehemu tu itakayothibiti jina la paji, hiyo ni kama katika kuweka paji. Na ni lazima sehemu itakayoachwa wazi iwe ni ile itakayowekwa juu ya ardhi, na iwapo ataiacha sehemu wazi kisha akaweka aridhini sehemu nyingine (isiyo wazi) basi haitosihi. Na hakika uwazi unapatikana pale ambapo kati ya paji na eneo la kusujudia hamna kizuwizi cha kuungana kinachoondoka kwa kuondoka yeye, hivyo iwapo atasujudu juu ya kiungo chake au kunjo la kilemba chake haitosihi kwa sababu hajagusa eneo la kusujudia kwa paji lake bila kizuizi. Tuna hadithi ya Khababu na pia amepokea kuwa Mtume alisema: Gusisha paji lako aridhini. 22 Ibnu Rushdi amesema: Pia wamekhitilafiana kuhusu je ni sharti mkono wa mwenye kusujudu uwe wazi na uwekwe juu ya kile unachowekwa uso juu yake? Au hilo si sharti lake? Malik amesema: Hilo ni miongoni mwa sharti la sijda; ameona kuwa ni sharti la kutimia kwake.23 Wengine wakasema: Hilo si miongoni mwa sharti la sijda. Kupitia mlango huu wametofautiana kuhusu kusujudu juu ya kunjo za kilemba na hapa watu wana madhehebu matatu: Wapo wanaozuwia, wapo wanaoruhusu, na wapo wanaotofautisha kati ya kusujudu juu ya kunjo kubwa la kilemba au dogo, na kutofautisha kati ya paji lake kugusa eneo dogo la ardhi au kutokugusa kabisa24. Al-Qafalu amesema: Iwapo kwenye paji lake kuna bandeji kwa tatizo fulani na akasujudu basi inatosha na wala halazimiki kurudia. Na 22 Al-Azizi, Sharhul-Wajizi ijulikanayo kwa jina la As-Sharhul-kabiru: 1 /521. 23 Maana yake si sharti la kusihi bali ni sharti la kukamilika. 24 -Bidayatul-Mujtahidi:1/139. 14


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 15

Kusujudu juu ya udongo miongoni mwa Wanavyuoni wetu wapo waliotoa kauli nyingine nayo ni ulazima wa kurudia kwa kupaka juu ya bandeji. 25 Ndani ya fiqihi ya madhehebu manne, Shafi wamesema: Inadhuru kusujudu juu ya kunjo la kilemba na mfano wake kama vile bandeji iwapo litafunika paji lote, na iwapo hatosujudu kwa paji lake lililo wazi basi Swala yake itabatilika iwapo tu amefanya makusudi huku anajua, isipokuwa tu kwa udhuru kama atakapokuwa na jeraha na akakhofu kupata maumivu makali iwapo ataondoa bandeji, basi katika hali kama hii kusujudu kwa paji hilo ni sahihi. 26 Dhahiri ni kuwa siri ya kulazimika kuacha wazi paji ni kugusanisha paji na udongo ili mwenye kuswali afikie kilele cha mwisho cha unyenyekevu na utumwa. Isipokuwa hawa wamehusisha kuacha wazi paji na kitendo cha kutokuwepo kizuizi juu ya paji kizuwiacho kusujudu, kama vile kunjo la kilemba na pande zake na bandeji na wameruhusu kusujudu juu ya zulia au tandiko. Kwa ajili hiyo wamebatilisha siri na faida ya ulazima wa kuacha paji wazi, basi hapo ndipo linapowaelekea swali lifuatalo: Ikiwa sijda juu ya tandiko na zulia inaruhusiwa basi kuna tofauti gani kati ya kusujudu juu ya hivyo na juu ya bandeji na kunjo la kilemba? Kwani kutofautisha kati ya mambo mawili hayo ni jambo la kushangaza. Kwani kwa hakika bandeji na kilemba hutengenezwa kwa uzi kama tandiko na zulia na kitendo cha kilemba na kunjo zake kubebwa na mwenye kuswali kinyume na tandiko na zulia hakulazimishi tofauti madamu kwa madai yao vinashirikiana katika kufanya sijda. 25 -Hil-yatul-ulamai fi maarifati madh habil-fuqahai:122. 26 Al-Fiqhu ala Madhahibul-Arbaa:1/233. 15


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 16

Kusujudu juu ya udongo Suala hii ni tofauti na pale tutakaposema: Siri ya kuacha wazi paji ni kugusanisha uso na ardhi, kwani hapo hakutakuwepo na tofauti kati ya bandeji na zulia, na huo ndio mtazamo wa Wanavyuoni wetu wote. Al-Allamah amesema: Ni lazima kuchomoza paji wakati wa kusujudu mpaka juu ya kile kinachosihi kusujudu juu yake. 27

SUNA YA MTUME KATIKA KUSUJUDU, ZAMA ZAKE NA BAADA YAKE Hakika Mtukufu Mtume na maswahaba zake walikuwa wakisujudu juu ya ardhi muda mrefu wakivumilia shida ya joto la ardhi, vumbi la udongo na unyevunyevu wa udongo miaka yote, na wala hakuna yeyote yule zama hizo aliyesujudu juu ya nguo na kunjo la kilemba bali hata juu ya mkeka, kirago na khumra28 wala juu ya tandiko na zulia. Utaratibu wa juu kabisa waliokuwa nao katika kuondoa udhia kwenye paji ulikuwa ni kupoza changarawe kwa viganja vyao kisha wanasujudu juu yake. Baadhi yao walimlalamikia Mtume kuhusu ukali wa joto lakini hakumjibu kwani hakuwa na uwezo wa kubadili amri ya Mwenyezi Mungu kwa matakwa yake mwenyewe mpaka pale ilipopatikana ruhusa ya kusujudu juu ya khumra29na mkeka, hivyo amri mpya ikawapa wasaa waislamu lakini ndani ya uzio maalumu, kwa mujibu wa hayo waislamu zama hizo walipitiwa na hatua tatu tu na si zaidi:

27 Muntahal-Matlabu: 5/154. 28 Mkeka mdogo wa kuswalia. 29 Mkeka mdogo wa kuswalia. 16


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 17

Kusujudu juu ya udongo Wakati ambao ilikuwa ni wajibu kwa waislamu kusujudu juu ya ardhi na aina zake mbalimbali kuanzia udongo, mchanga, changarawe na udongo laini na wala hawakuwa na ruhusa yoyote ile ya kusujudu juu ya kitu kingine. Kipindi ambacho ilipatikana ruhusa ya kusujudu juu ya mimea ya ardhi kuanzia mkeka, kirago na khumra ikiwa ni kuwarahisishia amri na kuwaondolea kero na tabu. Kipindi ambacho iliruhusiwa kusujudu juu ya vazi katika hali ya dharura na matatizo. Na ufuatao ni ufafanuzi wake:

Kipindi cha mwanzo: kusujudu juu ya ardhi Makundi yote mawili yamepokea toka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa alisema: Nimefanyiwa ardhi tohara na mahala pa kusujudia 30. Maana inayoeleweka toka ndani ya Hadithi hii ni kila sehemu ya ardhi ni mahala pa kusujudia na tohara, juu yake hufanywa sijda na tayamamu, kwa ajili hiyo ardhi hukusudiwa kwa mambo mawili: Mara kwa kusujudu na mara nyingine kwa kutayamamu. Hakika hadithi hii inathibitisha wazi kuwa ardhi, iwe ya udongo au majabali au changarawe ndio asili katika kusujudu na ndio inayowajibika kufanywa mahala pa kusujudia na wala hairuhusiwi kuvuka hapo isipokuwa kwa dalili nyingine. 30 Sahih Bukhari:1/91 kitabu cha Tayammam, hadithi ya 2. Sunanil-Bayhaqiy: 2/433 mlango: Popote sala itakapokukuta Swali kwani penyewe ni msikiti, na imepokewa pia na wengine kati ya waandishi wa Sahihi Sita na vitabu vya Sunna. 17


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 18

Kusujudu juu ya udongo Ama kutafsiri riwaya hii kuwa ibada na kusujudu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu haihusishi sehemu maalumu tu na kuacha sehemu nyingine bali ardhi yote ni mahala pa kusujudia waislamu, kinyume na wasio waislamu kwani wao wamehusisha ibada na mahekalu na makanisa tu. Maana hii haipingani na maana tuliyoitaja mwanzo, kwani iwapo ardhi yote ni mahala pa kusujudu mwenye kuswali basi inalazimu ardhi yote iwe inafaa kwa ibada, na hapo maana hii iliyotajwa ni maana muambata ya maana tuliyoitaja mwanzo. Na kinachoonyesha kuwa hayo ndio makusudio ni kule kutajwa tohara baada ya mahala pa kusujudia na kuyafanya maneno hayo mawili kuwa ni vitendwa vya kitenzi nimefanyiwa hivyo matokeo yake ni kuipa ardhi sifa mbili: Yenyewe kuwa ni mahala pa kusujudia na kuwa ni tohara, na hili ndilo alilofahamu Al-Jassasu akasema: Hakika yule aliyeifanya ardhi mahala pa kusujudia ndiye aliyeifanya tohara. 31 Na wengine mfano wake kati ya wafafanuzi wa hadithi. Basi iwapo udongo na changarawe ni tohara basi pia vyenyewe ni mahala pa kusujudia mwenye kuswali, hivyo kuwekwa kikomo ni hoja mpaka dalili nyingine ionyeshe ruhusa ya kuvuka kikomo hicho.

31 Ahkamul-Qur’ani: 2/389 iliyosambazwa Beiruti

18


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 19

Kusujudu juu ya udongo

Kupoza changarawe ili kusujudu juu yake 2. Toka kwa Jabir bin Abdillah Al-Answariy amesema: Nilikuwa nikiswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) Swala ya adhuhuri basi nikachukua fungu la changarawe mkononi mwangu na kuziweka mkono wa pili ili zipowe kisha naziweka kwa ajili ya paji langu ili nisujudu juu yake kwa jinsi joto lilivyokuwa kali32 Al-Bayhaqiy akaongeza kwa kusema: As-Sheikh amesema: Laiti ingeruhusiwa kusujudu juu ya vazi lililo mwilini basi hilo lingekuwa ni rahisi mno kuliko kupoza changarawe kwa viganja na kuziweka ili kusujudu33. Tunasema: Laiti ingeruhusiwa kusujudu juu ya nguo yoyote iliyo mwilini au iliyo nje ya mwili hilo lingekuwa ni rahisi mno kuliko kupoza changarawe na ingewezekana kubeba kitambaa au zulia au mfano wake kwa ajili ya kusujudu juu yake. 3. Anas amepokea akasema: Tulikuwa tukiswali pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku za joto basi kila mmoja wetu huchukua changarawe mkononi mwake ili kuzipoza na baadae huziweka na kusujudu juu yake34.

32 Musnadi Ahmad: 3/327 hadithi ya Jabir. Sunanil-Bayhaqiy: 1/439 mlango wa yaliyopokewa kuhusu kuiharakisha Swala kwa ajili ya ukali wa joto. 33 Sunanul-Bayhaqiy: 2/105. 34 Sunanul-Kubra: 2/106 19


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 20

Kusujudu juu ya udongo 4. Toka kwa Khabab bin Al-Arti amesema: Tulimlalamikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu joto la ardhi linavyounguza vipaji na viganja vyetu lakini hakutujibu35. Ibnu Athiri amezungumzia maana ya hadithi hii akasema: Hakika wao walipomlalamikia yale yanayowasibu kutokana na joto hilo hakuwapa nafasi ya kusujudu juu ya ncha kona za nguo zao 36 Riwaya hizi zinaonyesha sunna ya Mtume katika swala ilikuwa ni kusujudu juu ya ardhi tu mpaka Mtume hakuwapa nafasi waislamu waache na waende kwenye nguo za mwilini mwao au vitu vya nyuzi vilivyo nje ya miili yao, japokuwa Mtume ni mpole na mwenye huruma kwa waumini lakini aliendelea kuwawajibisha wagusanishe vipaji vyao na ardhi hata kama ukali wa joto lake utawaudhi. Hadithi zinazoamrisha kufikisha udongo kwenye paji zinaonyesha wazi jinsi waislamu walivyokuwa wakisujudu juu ya ardhi na jinsi Mtukufu Mtume alivyoshikilia msimamo wa kuweka paji juu ya udongo na wala si juu ya nguo ya mwilini kama vile kunjo la kilemba au isiyo mwilini kama vile vitambaa na mazulia. Riwaya hizo ni nyingi zaidi ya moja.

Amri ya kufikisha udongo kwenye paji 5- Imepokewa toka kwa Khalid bin Al-Jahaniy amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwona Suhaybu akisujudu huku akizuwia asipatwe na udongo, Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: Ewe Suhaybu, gusisha uso wako udongo 37. Kinachoonekana ni kuwa Suhaybu alikuwa anajikinga asipatwe na udongo kwa kusujudu juu ya nguo 35 Sunanil-Bayhaqiy: 2/105 mlango: Kuacha wazi paji la uso. 36 An-Nihayatu: 2/497, neno

Shaka. 37Al-Mutaqi Al-Hindiy: Kanzul-ummal: 7/465 namba 19810 20


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 21

Kusujudu juu ya udongo iliyo mwilini au isiyo mwilini, na kwa uchache ni kusujudu juu ya mkeka, kirago na mawe safi. Vyovyote vile itakavyokuwa ni kwamba hadithi hii ni ushahidi juu ya ubora wa kusujudu juu ya udongo kuliko kusujudu juu ya changarawe kama ilivyotangulia ruhusa ya kusujudu juu ya changarawe kinyume na kusujudu juu ya kisichokuwa ardhi. Ummu Salama amepokea kuwa: Mtume (s.a.w.w.) alimwona kijana wetu anayeitwa Af lahu akipuliza mahala pa kusujudia, akamwambia: Ewe Af lahu gusa udongo 38. Na katika riwaya nyingine: go 39.

Ewe Rabahu gusisha uso wako udon-

Abu Swaleh amepokea akasema: Niliingia kwa Ummu Salama kisha akaingia mtoto wa kaka yake na kuanza kuswali nyumbani mwake rakaa mbili, aliposujudu akapuliza udongo, hapo Ummu Salama akamwambia: Ewe mtoto wa kaka yangu usipulize kwani hakika mimi nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akimwambia mtumishi wake aliyeitwa Yasari: Gusisha uso wako udongo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. 40.

38 Al-Mutaqi Al-Hindiy: Kanzul-ummal:7/459 namba 19776 39 Al-Mutaqi Al-Hindiy: Kanzul-Ummal: 7/459 namba 19777 40 Al-Mutaqi Al-Hindiy: Kanzul-Ummal: 7/465 Na. 19810. Musnadi Ahmad: 6/301. 21


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 22

Kusujudu juu ya udongo

Amri ya kuondoa kilemba kwenye paji la uso Imepokewa kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiondoa kilemba kwenye paji lake anaposujudu.41 Imepokewa toka kwa Ali kiongozi wa waumini kuwa amesema: Iwapo mmoja wenu anasujudu basi aondoe kilemba kwenye paji ke inamaanisha ili asisujudu juu ya kunjo la kilemba42. Saleh bin Hayawani As-sabai amesema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwona mtu mmoja akisujudu ubavuni mwake na kilemba chake kikiwa kimefunika paji lake basi Mtukufu Mtume akakiondoa kwenye paji lake. 43 Iyadhi bin Abdullah Al-qarashiy amesema: Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwona mtu mmoja akisujudu juu ya kunjo la kilemba kilichoshuka kwenye paji lake, Mtume akamwashiria kwa mkono wake: Ondoa kilemba chako. 44 Riwaya hizi zinadhihirisha kuwa zama hizo waislamu hawakuwa na amri nyingine isipokuwa ni kusujudu juu ya udongo na wala hakuwa na ruhusa nyingine isipokuwa kupoza changarawe, na laiti kama kungekuwa na ruhusa nyingine basi wasingefanya hivyo na wala Mtume asingeamrisha kugusisha udongo wala kuondoa kilemba kwenye paji la uso. 41Tabaqatul-Kubra: 1/151 kama ilivyo kusujudu juu ya ardhi:41. 42Muntakhabu Kanzul-ummai iliyochapwa pembezoni mwa Al-Musnadi:3/194. 43As-Sunanil-Kubra: 2/105 44 As-Sunanil-Kubra: 2/105. 22


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 23

Kusujudu juu ya udongo

Mwenendo wa Mtume katika kusujudu Kutokana na riwaya nyingi inaonekana Mtume alikuwa akitilia umuhimu kusujudu juu ya ardhi na zifuatazo ni mfano wa riwaya hizo: 1-Al-Wailu bin Hajari amesema: Nilimuona Mtume (s.a.w.w.) anaposujudu huweka paji lake na pua yake juu ya ardhi. 45 2- Ibnu Abbas amesema: jiwe. 46

Hakika Mtukufu Mtume alisujudu juu ya

3- Aisha amesema: Sikuwahi kumuona Mtume (s.a.w.w.) akikinga uso wake na kitu. 47 Ibnu Hajar amesema: Katika hadithi hii kuna ishara kuwa kugusa ardhi bila kizuwizi katika sijda ndio asili kwa sababu kuna sharti la kutojiweza. 48 Hadithi hii inaonyesha ruhusa ya kusujudu juu ya vazi wakati wa dharura na kutokuruhusiwa katika hali ya kawaida, na hili ndilo lililopokewa toka kwa Maimamu wa Ahlul-baiti, kwani imepokewa toka kwa Uyaynatu Yubaul-Qaswabi amesema: Nilimwambia Aba Abdillah: Nikiingia msikitini siku yenye joto kali nikichukia kuswali juu ya changarawe nikitandika nguo yangu, je nisujudu juu yake? 45 Ahkamul-Qur’ani: 3/36. Musnadu Ahmad: 315,317. 46 As-Sunanil-Bayhaqiy: 2/102. 47 Al-Muswanafu:1/397. Kanzul-Ummal: 4/212. 48 Fathul-Bari: 1/414. 23


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 24

Kusujudu juu ya udongo Akajibu: Hakuna ubaya. 49 Na Al-Qasim bin Al-Fadhilu amesema: Nilimuuliza Ridha (a.s): Mimi ni fidia kwako, Je iwapo mtu anasujudu juu ya kunjo la kilemba chake kutokana na udhia wa joto na baridi. Akajibu: Hakuna ubaya.�50 Kuna riwaya na hadithi zinazoonyesha Mtukufu Mtume alikuwa akisujudu juu ya udongo na ardhi katika baridi kali na alikuwa akiswali kwenye shuka akijikingia mikono yake na miguu yake dhidi ya baridi ya ardhi na wala si paji lake. Na zifuatazo ni riwaya zionyeshazo hilo: 1- Wailu bin Hajar amesema: Siku moja nilimwona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiswali juu ya kitambaa cheupe na huku akiepusha mikono na miguu yake dhidi ya baridi ya ardhi kwa kitambaa hicho. 51 2- Thabit bin Swamit amepokea kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akiswali katika msikiti wa Bani Abdul-Ash hali aliweka mikono yake juu ya kitambaa alichojivingirishia kujiepusha na baridi ya mawe.52 3- Abu Huraira amesema: Mtume (s.a.w.w.) alisujudu siku ya mvua kali kiasi kwamba nikawa naona alama za sijda kwenye paji lake na pua yake. 53 49 Al-Wasailu: 3 mlango 4 kati ya milango ya kitu cha kusujudu juu yake, hadithi ya 1 50 Al-Wasailu: 3, mlango wa 4 mlango wa kitu cha kusujudu juu yake, hadithi ya 2. 51 As-Sunanul-Kubra lil-Bayhaqiy: 2:106. 52 Sunani Ibnu Majah: 1/329. 53 Maj’maul-Zawaidi: 2/126. 24


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 25

Kusujudu juu ya udongo Riwaya hizi na mfano wake zinaonyesha kitendo cha Mtukufu Mtume katika sijda yake siku za mvua na baridi na alikuwa akisujudu juu ya udongo na wala hakuuepusha uso wake kwa kitu chochote, na mara nyingine akiepusha mikono yake bila kuhusisha uso, huku umakini wa wapokezi kuhusu kubainisha kitendo cha Mtume kuepusha mikono yake kwa kitambaa dhidi ya baridi na udongo na wakiwa wameacha kutaja paji kunadhihirisha kuwa yeye hakuwahi kuepusha uso wake kwa chochote na laiti kama si hivyo basi wapokezi wangekitaja na wala wasingeghafilika.

MWENENDO WA MASWAHABA NA TABIINA KATIKA KUSUJUDU Kutokana na riwaya nyingi ni dhahiri kuwa mwenendo wa kundi la maswahaba ulikuwa ni kusujudu juu ya ardhi. 1- Abu Umayya amesema: Abu Bakr alikuwa akisujudu juu ya ardhi huku akijitandaza nayo.54 2- Abu Ubayda amesema: Ibnu Mas udi huwa hasujudu au amesema: Huwa hasali ila juu ya ardhi.55 3- Mas ruqu bin Al-Ajdau sahaba wa Ibnu Mas udi alikuwa haruhusu kusujudu juu ya kisichokuwa ardhi hata ndani ya jahazi na alikuwa akibeba kitu cha kusujudu juu yake ndani ya jahazi.56 54 Al-Muswanafu: 1/397 55 Al-Muswanafu: 1/367 56At-Tabaqatil-Kubra li-ibnu Saadi: 6/53. Na Al-Muswanafu Abdurazaqi: 2/583. 25


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 26

Kusujudu juu ya udongo 4- Ibrahimu An-Nakhaiy mwanachuoni wa Kufa aliyekuja baada ya maswahaba alikuwa akisimama juu ya busati la matete na kusujudu juu ya ardhi. Mpokezi akasema: Busati la matete ni nini? Akasema: Mkeka.57 Na katika tamko lingine alikuwa akiswali juu ya mkeka na kusujudu juu ya ardhi. 5- Umar bin Abdul-Aziz alikuwa hatosheki na khumra bali alikuwa anaweka udongo juu ya khumra na kusujudu juu yake.58 6- Ur watu bin Zubair alikuwa akichukia kuswali juu ya kitu kisichokuwa ardhi.59 7-Ali bin Abdallah bin Abbas alimuandikia Zurainu kuwa nitumie vipande vya mawe ya Mar wa ili niwe nasujudu juu yake.60 Matokeo ni kuwa kujidhalilisha na kunyenyekea mbele ya utukufu wa Mwenyezi Mungu kwa ubora kunapatikana kwa kuweka paji na pua juu ya udongo mkavu na mbichi huku ukisema: Udongo haulingani na bwana wa mabwana na udongo ni sawa na mimi, hali hiyo huwezi kuipata kwenye vitu vya viwandani. Na Allamah Al-Amini ana maneno ya maana sana, na yafuatayo ni maelezo yake: Na kinachofaa mno kufanyia sijda ambayo si chochote isipokuwa ni kujishusha na kujidhalilisha mbele ya utukufu wa Mwenyezi Mungu na heshima ya kiburi chake ni ardhi kufanywa mahala pa kusujudia 57 Al-Muswanafu Liabdirazaqi: 1397. 58 Fat-hul-Bari:1/410. 59 Fat-hul-Bari:1/410. 60 Akh-baru Maka lil-Azraqiy 26


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 27

Kusujudu juu ya udongo wakati wa kusujudu, huku mwenye kuswali akichafua shavu lake kwa udongo na kuidhalilisha pua yake ili mwenye kusujudu akumbuke udongo wake duni usio na thamani ambao ameumbwa kutokana nao, ambao atarudi tena na kutolewa mara nyingine ili awaidhike na awe na kumbukumbu ya uduni wa asili yake ili apatwe na unyenyekevu wa kiroho na udhalili wa ndani na mvunjiko wa nafsi na kuinuka kwa viuongo kuelekea kwenye utumwa huku akiachana na ujeuri na ubinafsi, na awe katika ujuzi kuwa kiumbe kitokanacho na udongo kinastahiki na kufaa udhalili na uduni na wala si kitu kingine. Katu kabisa siri hizi hazipatikani ndani ya vitu vya kutengenezwa kwa sufi, hariri na mfano wake miongoni mwa mambo ya raha na starehe ambayo yanamuonyesha mwanadamu ukubwa ndani ya nafsi yake. Vinamuonyesha heshima, utukufu, na cheo cha juu kwake na anapata ujeuri, kiburi na majivuno na hapo kujitoa kwenye udhalili na unyenyekevu.61

HATUA YA PILI KURUHUSIWA KUSUJUDU JUU YA KHUMRA NA MKEKA Hadithi na riwaya zilizotangulia zilizothibiti ndani ya Sahihi Sita na vitabu vya Musnadi na vingine vya hadithi vinaonyesha jinsi Mtume na maswahaba zake walivyoshikilia msimamo wa kusujudu juu ya ardhi na aina zake na wao hawakuacha kusujudu juu yake hata kama mambo yatakuwa magumu na joto likazidi. 61 Siratuna wasunatuna:125-126. 27


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 28

Kusujudu juu ya udongo Lakini kuna maelezo yanayoonyesha Mtume aliruhusu kusujudu juu ya mimea ya ardhi kwa wahyi toka kwa Mwenyezi Mungu, hapo likawa jepesi kwao suala la kusujudu na tabu na usumbufu wa joto na baridi na pale ardhi itakapokuwa imelowana vikaondolewa. Na yafuatayo ni hayo maelezo: 1-Anas bin Malik amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya khumra.62 2- Ibnu Abbas amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswalijuu ya khumra. Katika tamko lingine: Nabii alikuwa akiswali juu ya khumra.63 3- Aisha amesema: ya khumra. 64

Mtukufu Nabii (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu

4- Ummu Salama amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya khumra. 65 5- Maymuna amesema: anasujudu juu yake. 66

Mtukufu Mtume anasali juu ya khumra na

6- Ummu Sulaymu amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya khumra. 67 62 Abunaimil-Is’fihani: Ahk-baru Is’bihani: 2/141. 63 Musnadi Ahmad:1/269,303,309,358. 64 Musnadi Ahmad: 6/179 na pia mna alimwambia kijakazi wake akiwa msikitini: Niletee khumra. 65 Musnadi Ahmad: 6/30266 Musnadi Ahmad: 6/331-335. 67 Musnadi Ahmad: 6/377. 28


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 29

Kusujudu juu ya udongo 7. Abdallah bin Umar amesema: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya khumra.68 Baadhi ya waelekezaji ndani ya msikiti mtukufu walinikosoa pale waliponiona nikiendelea kusujudu juu ya mkeka na kunihoji sababu ya kufanya hivyo. Nikamwambia: Hakika Mtukufu Nabii alikuwa akiswali juu ya mikeka. Akasema: Hakika Swala ya Mtume juu ya mikeka na virago hailazimishi kusujudu juu yake kwani inawezekana akaswali juu ya mkeka na akasujudu juu ya kitu kingine. Nikamwambia: Hakika kutenganisha kati ya mambo hayo mawili hakulingani na lugha fasaha, kwani hakika kauli: Anaswali juu ya mkeka, inamaanisha anasali juu yake katika hali zake zote za Swala kuanzia kisimamo, rukuu na kusujudu na wala si aweke nyayo zake au magoti yake au mikono yake juu ya mkeka huku kaweka paji lake kwenye kitu kingine. Zaidi ya hapo kuna baadhi ya riwaya zimetamka wazi alikuwa akisujudu juu ya mkeka. 1. Abu Said Al-Khiduriy amesema: Nilikwenda kwa Mtukufu Mtume nikamkuta anasali juu ya mkeka na akisujudu juu yake. 69 2. Anas bin Malik amesema: Mtukufu Mtume alikuwa akiswali juu ya khumra na akisujudu juu yake.�70 68 Musnadi Ahmad: 2/92-98. 69 Sahih Muslim:2/62, Darul-fikri Beiruti. 70 Sahih Ibu Khuzaimati: 2/105, Al-Maktabu Al-Islamiyu chapa ya 2-1412 Hijiriyya. Al-Muujamu Al-Awsatu: 8/348. Al-Muujamu Al-Kabiru: 12/292.

29


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 30

Kusujudu juu ya udongo Ndani ya Hadithi zilizotajwa inabainika ruhusa ya kusujudu juu ya ardhi na udongo na baadhi ya vinavyoota aridhini mfano wa mkeka uliotengenezwa kwa magome ya mtende.

HATUA YA TATU KUSUJUDU JUU YA NGUO KWA UDHURU Tayari umeshazijua hatua mbili zilizopita na laiti kama ipo hatua ya tatu basi si nyingine bali ni hatua ya kuruhusu kusujudu juu ya kisichokuwa ardhi na kisichoota humo kwa udhuru na dharura. Na inaonyesha kuwa ruhusa hii ilikuja mwisho baada ya hatua hizo mbili, hiyo ni kama ulivyoona jinsi ambavyo Mtume hakujali malalamiko ya maswahaba dhidi ya ukali wa joto na ukali wa changarawe huku wakiendelea yeye na maswahaba zake kusujudu juu ya ardhi wakivumilia udhia na joto kali. Lakini Muumba Mtukufu akaruhusu kusujudu juu ya vazi kwa dharura na udhuru kwa lengo la kuondoa tabu. Na zifuatazo ni riwaya kuhusu hili: Anas bin Malik amesema: Tulipokuwa tukiswali pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kila mmoja wetu alikuwa hajimudu kuweka paji juu ya ardhi hivyo kila mmoja aliweka vazi lake na kusujudu juu yake. Na katika tamko lingine: Tulipokuwa tukiswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) kila mmoja wetu alikuwa akiweka baadhi ya vazi lake kwa sababu ya joto kali na iwapo atashindwa mmoja wetu kutuliza paji lake juu ya ardhi hutandika nguo yake. 30


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 31

Kusujudu juu ya udongo Katika tamko la tatu: Tulipokuwa tukiswali pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) baadhi yetu waliweka baadhi ya vazi mahala pa kusujudia kwa sababu ya joto kali.�71 Riwaya hii ambayo imenukuliwa na waandishi wa vitabu vya Sahih Sita, Sunani na Masanidi inadhihirisha ukweli wa baadhi ya riwaya zilizopokewa zikikusudia kuruhusu kusujudu juu ya nguo katika hali isiyo ya dharura. Hiyo ni kwa sababu riwaya ya Anas imeeleza ikihusisha ruhusa katika hali ya dharura tu, hivyo yenyewe inakuwa ni kihusisho cha makusudio ya riwaya hizi zisizo na sharti. Na zifuatazo ni baadhi ya hizo riwaya zilizopokewa katika hili: 1-Abdallah bin Muhrizu amepokea toka kwa Abu Huraira kuwa: Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya kunjo la kilemba chake.72 Hakika riwaya hii japokuwa inapingana na ile ya katazo la Mtume kuhusu kusujudu juu ya kunjo bado inachukuliwa kuwa ni wakati wa udhuru na dharura na hilo limetamkwa wazi na Sheikh Al-Bayhaqiy ndani ya Sunnan yake aliposema: Shekhe amesema: Ama riwaya zilizopokewa toka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuhusu hilo la kusujudu juu ya kunjo la kilemba hazithibitishi lolote kuhusu hilo, na sahihi mno miongoni mwa yale yaliyopokewa kuhusu hilo ni kauli ya Hasani Al-Basriy ambayo ni nukuu toka kwa maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.). 73 71 Sahih Bukhari: 1/101. Sahih Muslim: 2/109. Musnad Ahmad: 1/100. AsSunanul-Kubra: 2/106. 72 Kanzul-Ummal: 8/130 namba 22238. 73 Al-Sunnan Al-Kubra: 2/106. 31


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 32

Kusujudu juu ya udongo Na imepokewa toka kwa Ibnu Rashidi amesema: Nilimwona Makuhula akisujudu juu ya kilemba chake nikamwambia: Kwa nini unasujudu juu yake? Akasema: Nakinga meno yangu dhidi ya baridi .74 2-Riwaya iliyopokewa kutoka kwa Anas: Tulipokuwa tukiswali pamoja na Mtume mmoja wetu alikuwa akisujudu juu ya nguo yake .75 Riwaya hii inachukuliwa kuwa ni katika hali ya udhuru kwa kigezo cha riwaya tuliyopokea kupitia yeye mwenyewe na aliyoipokea Bukhari kupitia kwake yeye kuwa: Tulipokuwa tukiswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) kila mmoja wetu alikuwa hajimudu kuweka paji juu ya ardhi kwa sababu ya joto kali hivyo kila mmoja aliweka vazi lake na kusujudu juu yake. 76 Na inaungwa mkono na riwaya aliyoipokea An-Nasaiy: Tulipokuwa tukiswali Adhuhuri nyuma ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulisujudu juu ya mavazi yetu ili kujikinga na joto .77 Na kuna riwaya zisizo na hoja timilifu kiasi kwamba hazionyeshi isipokuwa ni kuwa Mtume aliswali juu ya kirago cha ngozi. Je? 74 Al-Muswanafu li-Abdil-Razaqi:1/400 kama ilivyo ndani ya Siratuna Wasunnatuna, na Al-Sijdatu ala Turbati: 93. 75 Al-Sunnanu Al-Kubra: 2/106 mlango wa atakayetandika nguo na kusujudu juu yake. 76 Bukhari: 2/64 Kitabu cha sala mlango wa kutandika nguo ndani ya sala kwa ajili ya kusujudu. 77 Ibnu Athiir: Jamiul-Usuul: 5/468 namba 3660. 32


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 33

Kusujudu juu ya udongo Alisujudu juu yake au la. Hakuna dalili ionyeshayo hilo. 3. Toka kwa Al-Mughira bin Shu ba: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiswali juu ya mkeka na ngozi yenye manyoya iliyotiwa dawa ili isioze.78

Riwaya hii japokuwa ni dhaifu kwa kuwemo Yunus bin Al-Harthi, bado haionyeshi kuwa alisujudu juu yake na wala hakuna mahusiano ya lazima kati ya kuswali juu ya ngozi na kusujudu juu yake, na hasa ngozi inapokuwa kipande kidogo kwani huenda (s.a.w.w.) aliweka paji lake juu ya ardhi au kiotacho toka aridhini, na hata kama tukijaalia kuwepo mahusiano ya lazima bado yenyewe na mfano wake hiyo haziwezi kuzishinda uzito riwaya tulizoorodhesha katika hatua mbili zilizopita.

MATOKEO YA UCHUNGUZI Hakika mwenye kufuatilia riwaya kwa kina ataona jahara kuwa suala la kusujudu ndani ya swala lilipitia hatua mbili au tatu, hivyo katika hatua ya kwanza faradhi ilikuwa ni kusujudu juu ya ardhi na waislamu hawakuruhusiwa kusujudu juu ya kisichokuwa ardhi, na katika hatua ya pili ikaja ruhusa ya kusujudu juu ya kinachoota toka aridhini na nyuma ya hatua hizi mbili hakuna hatua nyingine isipokuwa hatua ya kuruhusiwa kusujudu juu ya nguo kwa udhuru na dharura. 78 Abu Daud: As-Sunnan: mlango wa yaliyopokewa kuhusu kuswali juu ya khumra, namba 331. 33


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 34

Kusujudu juu ya udongo Hivyo maana iyonekanayo toka ndani ya baadhi ya riwaya zinazoruhusu kusujudu juu ya kirago cha ngozi na mfano wake huchukuliwa kuwa ni wakati wa dharura. Au hazina dalili kuwa alisujudu juu yake bali makusudio yake ni kuswali juu yake. Na hapa ndipo inapodhihiri jahara kuwa kitendo cha Shia kung ang ania kusujudu juu ya ardhi au kiotacho toka aridhini ndio kile kile kitendo kilicholetwa na Sunna tukufu ya Mtume (s.a.w.w.) na wala hawajakwenda kinyume hata kidogo. Na sisi tunawaomba kidogo mtazame kwa makini ili muone haki na muache uzushi (bidaa). Katu hakuna dalili inayoruhusu sijda juu ya matandiko, mazulia na mabusati yaliyotengenezwa kwa sufi, manyoya, hariri na mfano wake, na vazi lililomo mwilini, na ndani ya Sunna ya Mtume hamna mashiko yoyote yanayoruhusu hilo. Ni hizi hapa Sahihi sita zilizochukua dhamana ya kubainisha hukumu za dini, na hasa swala ambayo ndio nguzo ya dini, lakini ndani yake hamna hata hadithi moja wala neno moja linaloashiria wala kugusia ruhusa ya hilo. Hivyo kauli ya kuruhusu kusujudu juu ya matandiko na mazulia na kung ang ania hilo na kutandaza mabusati misikitini ili kusujudu juu yake kama ilivyozoeleka, suala hilo ni bidaa halisi na jambo lililozushwa nje ya sheria, na linapingana na mwenendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunna ya Mtukufu Mtume Wake (s.a.w.w.); â€œâ€Ś..na wala hamtokuta mabadiliko yoyote katika mwenendo wa Mwenyezi Mungu.â€?79

79 Siratuna Wasunnatuna: 133-134. 34


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 35

Kusujudu juu ya udongo

=6=

NI IPI SIRI YA KUCHUKUA KIPANDE CHA UDONGO TOHARA? Hapa limebaki swali ambalo mara nyingi hutolewa na ndugu zetu wengi wa kisunni kuhusu sababu ya Shia kuchukua kipande cha udongo tohara safarini na nyumbani na kusujudu juu yake na si kitu kingine. Huenda wenye akili duni wakadhani kuwa Shia hukisujudia kipande hicho na wala si kusujudu juu yake, na kuwa wanaabudu jiwe na kipande cha udongo, hilo ni kwa sababu masikini hawa hawatofautishi kati ya kusujudu juu ya kipande cha udongo na kukisujudia. Vyovyote vile ni kuwa jibu la swali hilo liko dhahiri kwani kilicho bora kwa Shia ni kuchukua kipande cha udongo tohara safi ili awe na yakini juu ya utohara wake, kipande hicho kichukuliwe ardhi yoyote ile na toka bara lolote lile kati ya pande za ulimwengu ni sawa kwao hamna tofauti. Kujali huku ni sawa tu na kile kitendo cha mwenye kuswali kujali tohara ya mwili wake, mavazi yake na msala wake. Ama siri ya kung ang ania kuchukua kipande cha udongo ni kwamba uhakika wa utohara wa kila ardhi -huwa humo, - na kukifanya mahala pa kusujudia, haupatikani kila eneo miongoni mwa maeneo anayokuwemo muislamu safarini na nyumbani, na itakuwaje awe na uhakika huo ilihali maeneo hayo yanafikiwa na aina tofauti za binadamu, waislamu na wasio waislamu, washikao misingi ya tohara na wasioshika misingi hiyo, hivyo katika hilo kuna taabu kubwa inayomfika muislamu katika swala yake, hivyo hana njia ya kukwepa kujichukulia kipande cha udongo tohara ili awe na imani na 35


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 36

Kusujudu juu ya udongo utohara wa kipande atakachosujudu juu yake wakati wa Swala yake ili kujitahadhari dhidi ya kusujudu juu ya uchafu na najsi na taka ambazo katu hazimkurubishi kwa Mwenyezi Mungu; na wala Sunna tukufu hairuhusu kusujudu juu yake, na wala akili timilifu haikubali, hasa baada ya kuwepo mkazo kamilifu wa hali ya juu kuhusu utohara wa viungo na mavazi ya mwenye kuswali na kukataza kuswali katika baadhi ya maeneo yakiwemo: Jalalani, machinjioni, mitaroni, bafuni na maeneo ya ngamia, bali imeamrishwa kutoharisha misikiti na kuinukiza manukato.80 Kanuni hii ilikuwa imethibiti kwa watu wema waliotangulia japokuwa historia ilighafilika kuinukuu kwani imepokewa kuwa: Mwanafunzi mmoja wa maswahaba mwanafiqihi Mas ruqu bin AlAjdau aliyefariki mwaka 62 A.H. alikuwa akitembea na tofali safarini tokea Madina na kusujudu juu yake, kama alivyotoa Ibnu Abu Shayba ndani ya kitabu chake Al-Muswanafu mlango wa aliyekuwa akibeba kitu ndani ya jahazi na akisujudu juu yake. Hapo ametoa kwa njia mbili kuwa Mas ruqu alikuwa akibeba tofali ndani ya jahazi na kusujudu juu yake pindi anapokuwa safarini.81 Mpaka hapa imebainika kuwa kitendo cha Shia kukazania kukifanya kipande cha udongo kuwa mahala pa kusujudia si chochote ila tu ni kumrahisishia mwenye kuswali awapo safarini na nyumbani kuhofia asije kukosa ardhi tohara au mkeka tohara na ikawa vigumu kwake kuswali, na jambo hili ni kama kitendo cha muislamu kuhifadhi udongo tohara kwa lengo la kutayamamia. Ama siri ya Shia kushikilia Sunna ya kusujudu juu ya udongo wa 80 Al-Allamatu Al-Amini: Siratuna Wasunatuna:158-159. 81 Abu Bakr bin Abu Shayba: Al-Muswanafu: 2/172. Darul-fikra -1409 Hijiriyya.

36


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 37

Kusujudu juu ya udongo Husein (a.s.) hakika hilo ni miongoni mwa malengo ya juu mno na makusudio ya kina mno, kati ya hayo ni: Pindi mwenye kuswali anapoweka paji lake juu ya udongo huo akumbuke kujitolea kwa Imam huyo katika njia ya imani na msingi wa dini na kung oa ujeuri na ufisadi, akiwa yeye mwenyewe na watu wa nyumbani kwake na wateule miongoni mwa maswahaba zake. Na kwa kuwa kusujudu ndio nguzo kubwa mno ya Swala kama ilivyo katika Hadithi: Katika hali ya sijda ndipo mja awapo karibu mno na Mola Wake hivyo inafaa mno awakumbuke kwa kuweka paji lake juu ya udongo huu mtakatifu wale ambao walifanya miili yao fidia kwa ajili ya haki na roho zao zikafikia heshima ya juu ili ahofie na kunyenyekea, na alazimike kujishusha na kujiinua kiroho huku akiidharau dunia hii danganyifu na mapambo yake ya kupita. Na huenda haya ndio makusudio ya kuwa kusujudu juu ya udongo huo huondoa vizuwizi saba kama isemavyo hadithi. Hivyo katika kusujudu huko kunakuwa na siri ya kukwea na kupanda toka kwenye udongo mpaka kwa bwana wa mabwana.82 Allamah Al-Amini amesema: Sisi tunachukua toka udongo wa Karbala vipande ving aravyo na vidonge tunavyosujudu juu yake kama alivyokuwa akifanya mwanachuoni wa fiq hi aliyetangulia Mas ruqu bin Al-Ajdau akibeba kipande toka udongo wa Madina na kusujudu juu yake, na mtu huyu ni mwanafunzi wa ukhalifa wema, mwanachuoni wa Madina na mwalimu wa Sunna ya Mtume (s.a.w.w.),yu mbali na bidaa. Hivyo katika hilo hamna aina yoyote ya kulazimisha maana au chochote kinachopingana na wito wa Qur ani, au kinachopingana na mwenendo wa Mwenyezi Mungu au kutoka nje ya maamuzi ya akili 82 Al-Ardhu wal-Turbatu Al-Husayniyatu: 24. 37


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 38

Kusujudu juu ya udongo na mantiki. Wala si faradhi kwa Shia kuufanya udongo wa Karbala mahala pa kusujudia, wala si wajibu wa kisharia na dini, na wala si jambo la lazima kimadhehebu, wala hamna yeyote miongoni mwao aliyetofautisha kati ya ruhusa ya kusujudu juu ya udongo huo na ile ya udongo wa eneo lote la ardhi, hilo ni tokea siku ya mwanzo ya udongo huo, kinyume na anavyodai asiyewajua Mashia na rai zao. Udongo wa Karbala si chochote kwao ila ni ubora wa kiakili na wala si jambo lingine, na ni kuchagua tu kilicho bora kusujudu juu yake kiakili na kimantiki kama ulivyosikia. Na kuna watu wengi wa madhehebu hii ndani ya safari zao wanachukuwa visivyokuwa udongo wa Karbala miongoni mwa vitu vinavyosihi kusujudu juu yake kama vile mkeka tohara na safi wanaoamini utohara wake, au khumra yenye hali kama hiyo na wanasujudu juu yake ndani ya Swala zao.83 Huu ni utambuzi wa jumla kuhusu suala hili la kifiqhi; ama ukamilifu wake umeachwa sehemu yake, na katika hilo tumetosheka na yale yaliyoandikwa na Wanavyuoni na wasomi wakubwa wa zama hizi. Miongoni mwao nawataja hawa tu: 1- Al-Muslihu-lkabiru Sheikh Muhammad Husein Kashiful-ghita (1295-1373 A.H.) ndani ya kitabu chake ‘Al-ardhu watur’batulHuseiniyatu’(Ardhi na udongo wa Husein). 2- Msomi mkubwa Sheikh Abdul-Husein Al-Amini mwandishi wa kitabu Al-Ghadir (1320-1390A.H.). Ameandika ujumbe kuhusu maudhui hii na kuchapwa mwisho wa kitabu chake Siratuna Wasunnatuna (Mwenendo wetu na Sunna yetu), 83 Siratuna wasunnatuna:116-167 Chapa ya Najaf tukufu. 38


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 39

Kusujudu juu ya udongo 3- As-Sujudu a’lal-ardhi (Kusujudu juu ya ardhi) cha mwanachuoni Sheikh Ali Al-Ahmadi na amekifanyia uchunguzi na utafiti bora. Tuliyoyataja katika suala hili ni matunda ya nuru ya elimu yao. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu Wanavyuoni wetu waliyotangulia na awahifadhi waliobaki. Hizi ndio riwaya tulizokomea na ambazo tumezitoa ndani ya muhtasari huu.

MWISHO WA SAFARI Tutataja mambo mawili: 1-Kulazimisha itikadi na vitendo juu ya mwenye kuzuru Katika maajabu ya dunia (Ishi uone maajabu ya dunia) ni kuondolewa uhuru ndani ya Haram mbili tukufu na mwenyekuzuru kulazimishwa itikadi na vitendo maalum ilihali toka karne na karne mwenendo ulikuwa ni kumpa mwenyekuzuru Haramu mbili tukufu uhuru wa itikadi na vitendo. Hakika kutabaruku na kuomba kupitia kwa Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bait ilikuwa ni Sunna iliyoenea katika karne zilizopita na wala hakukuwa na kizuizi chochote; huku Sahih Sita na Masanidi zikiwa zimelipokea hilo. Haram mbili Tukufu zilikuwa ni eneo la amani kwa mwenyekuzuru kama alivyotaka Mwenyezi Mungu zenyewe ziwe hivyo. Mwenyezi Mungu amesema: “Humo mna dalili zilizo wazi; katika hizo ni mahala aliposimama Ibrahim. Na mwenye kuingia 39


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 40

Kusujudu juu ya udongo humo huwa katika amani.”84 Na Mwenyezi Mungu amesema akisimulia dua ya Ibrahimu: Na aliposema Ibrahim: ‘Ewe Mola wangu ufanye mji huu uwe wa amani”.85 Lakini leo upande huo umekuwa ni kinyume na alivyouombea Ibrahim kwani Shia mwenye kuzuru anayefuata mafunzo ya vitendo vya Maimamu wa Ahlul-Bayt haachwi atekeleze ibada zake kwa uhuru kamili na wala azungumze chochote anachokiamini, na mfano wa hilo ni kulazimishwa kusujudu juu ya busati la nyuzi na kukatazwa kusujudu juu ya ardhi na udongo. Na sisi kwa nafasi yetu tunaitolea wito serikali iongozayo katika ardhi za Wahyi iwape uhuru wa kisheria Mahujaji wote ili watekeleze ibada zao kwa uhuru, kwani hakika hilo linatia nguvu misuli ya umoja na kusaidiana miongoni mwa waislamu bila kujali tofauti zao. 2- Sunna kugeuzwa bidaa Tayari umeshajua kuwa kusujudu juu ya ardhi au mkeka, kirago na mfano wake ni Sunna, na kuwa kusujudu juu ya matandiko, mazulia na mfano wake ni bidaa na hakuna chochote alichoteremsha Mwenyezi Mungu kuhusu hilo. Lakini kinachosikitisha ni Sunna kugeuzwa bidaa na bidaa kugeuzwa Sunna, hivyo laiti kama mtu atatenda Sunna misikitini na 84 -Al-Imran; 3: 97 85 -Al-Baqara; 2:126 40


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 41

Kusujudu juu ya udongo makaburini akasujudu juu ya udongo na mawe basi kitendo chake hiki huitwa bidaa na mtendaji huitwa mtu wa bidaa. Lakini katika mlango huu si hili tu pekee kwani tunaweza kuona mfano wake ndani ya fiqihi ya madhehebu manne: 1-Sheikh Muhammad bin Abdur-Rahmani Ad-Damashqi amesema: Sunna katika kaburi ni kusawazisha na ndio rai bora kwa madhehebu ya Shafi i. Abu Hanifa na Malik wamesema: Kuweka mwinuko ndio bora kwa sababu kusawazisha imekuwa ni alama ya Mashia. 86 Ar-Rafiiy amesema: Hakika Mtume (s.a.w.w.) alisawazisha kaburi la mwanae Ibrahim. Na Qasim bin Muhamad amesema: Niliona kaburi la Mtume na Abu Bakr na Umar yakiwa yamesawazishwa. Ibnu Abu Huraira amesema: Bora hivi sasa ni kuhama toka kwenye kusawazisha kwenda kwenye muinuko kwa sababu kusawazisha imekuwa ni alama ya Mashia na ni bora kuwakhalifu na kumkinga maiti, yeye na ndugu zake dhidi ya kutuhumiwa na bidaa. Na mfano wa hayo ni haya yaliyonukuliwa toka kwake: Hakika kudhihirisha Bismillahi kukigeuka na kuwa alama yao basi mustahabu ni kuificha ili kuwakhalifu, na akatoa hoja kupitia riwaya iliyopokewa kuwa: Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisimama lichomozapo jeneza ndipo akapewa habari kuwa mayahudi hufanya hivyo basi baada ya hapo akaacha kusimama ili kuwakhalifu. 86Al-Damash qiy: Rahmatul-Uma fi-Ikh-tilafil-umati: 1/88 na pia Allamatu AlAmini ameinukuu ndani ya Al-Ghadiri: 10/209. 41


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 42

Kusujudu juu ya udongo Na hii hapa ndio sababu aliyotumia kujibu ndani ya kitabu chake na ikamvutia Sheikh Abu Muhamad na akaifuata kadhi Ar-Rubaniy. Lakini wanavyuoni wengi wa kisunni wako katika mtazamo wa kwanza, wamesema: Laiti kama tutaacha mambo yaliyothibiti ndani ya Sunna kwa kuwa tu yanalingana na wanayoyafanya watu wa bidaa basi hilo litatupelekea kuacha Sunna nyingi.87 2- Al-Imamu Razi amesema: Al-Bayhaqiy amepokea toka kwa Abu Huraira amesema: Mtume alikuwa akidhihirisha Bismillahi Rahmani Rahimi ndani ya Swala yake na Ali (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa akidhihirisha Bismillahi na hilo limethibiti kwa wingi. Na Ali bin Abu Talib alikuwa akisema: Ewe ambaye utajo wako ni sharafu kwa wenye kukutaja. Jambo kama hili je inampasa mwenye akili kwenda mbio kulificha? Shia wamesema: Sunna ni kudhihirisha Bismillahi, sawa iwe ndani ya Swala za kudhihirisha au za kunong ona, na wanavyuoni wote wa kisunni wamewakhalifu - mpaka akasema - hakika Ali alikuwa akipindukia katika kudhihirisha Bismillahi hivyo ilipotua dola mikononi mwa Bani Umayyah wenyewe wakapindukia katika kuzuwia kudhihirisha, kwa lengo la kwenda mbio kubatilisha athari za Ali (Radhi za Allah ziwe juu yake). 88 3. Az-Zamakhshari ndani ya Tafsiir yake anapoitafsiri kauli ya Mwenyezi Mungu: Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake humtakia rehma Nabii amesema: Ukiniuliza unasemaje kumtakia 87. Al-Azizi Sharhul-Wajizi: 2/453. 88. Ar-Razi: Mafatihul-Ghaibi: 1/205-206. 42


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 43

Kusujudu juu ya udongo rehma mwingine? Nitasema: Inaruhusiwa kumtakia rehma kila muumini kwa ushahidi wa kauli ya Mwenyezi Mungu: Yeye ndiye ambaye huwatakia rehma, na kauli ya Mwenyezi Mungu: Watakie rehma hakika kuwatakia kwako rehma ni utulivu kwao, na kauli yake: Ewe Mwenyezi Mungu wafikishie rehma jamaa wa Abu Aufa. Lakini wanavyuoni wana ufafanuzi kuhusu hilo nao ni: Ikiwa dua hiyo itafuata baada ya ile ya Mtume kama ukasema: Ewe Mwenyezi Mungu! Mfikishie rehma Mtume na kizazi chake basi hakuna maneno. Na ama ukimtakia mmoja peke yake miongoni mwa watu wa nyumbani kwake, kwa namna ile ya kumtakia yeye (Mtume) peke yake basi kufanya hivyo ni makuruhu kwa sababu jambo hilo limekuwa ni alama ya utajo wa Mtume na linapelekea kutuhumiwa kuwa ni Shia89 4- Ndani ya Fat’hul-bari: Wametofautiana kuhusu kumtolea salamu asiye nabii baada ya kuafikiana kuwa ni sheria awapo hai, wapo waliyosema ni sharia bila sharti lolote, na wengine wakasema ni sharia kwa kufuatanisha na wala asimtolee peke yake kwa sababu kufanya hivyo imekuwa ni alama ya Mashia. Ameinukuu An-Nawawiy toka kwa Sheikh Abu Muhammad AlJuwayniy90 Maana yake ni kuwa hajapata kigezo kinachoruhusu kuacha yale yaliyofanywa kuwa sheria na uislamu ila ni matendo ya Mashia na 89 Al-Kashafu: 2/549. 90 Fat’hul-Bari: 14/11. 43


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 44

Kusujudu juu ya udongo Sunna tukufu za uislamu, na laiti hilo lingesihi basi ingewajibika kwa msemaji aache faradhi na Sunna zote ambazo hufanywa na mashia. Sema: Kila mmoja anangoja basi ngojeni, na mtajua ni nani mwenye njia iliyo sawa na ni nani aliyeongoka.�91 Imetarujumiwa na Hemedi Lubumba 0715-017178 0773-017178 0754-017178

91 At-Twaha: 135. 44


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 45

Kusujudu juu ya udongo

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23.

Qur’an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na sita Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur’an na Hadithi 45


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 46

Kusujudu juu ya udongo 24. 25. 26. 27. 28. 29.

Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur’an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii

30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46 47. 48.

Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n amavuko by ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur ani na husomwa kwa Jahara Maulidi Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kufungua Safarini Malumbano baina Sunni na Shia

46


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

10:52 AM

Page 47

Kusujudu juu ya udongo

BACK COVER Sheria ya Kiislamu ni ya kipekee kwa kuwa inahusika na kila jambo huku ikiweka utatuzi wa matatizo yote yanayompata mwanadamu katika sekta zote za maisha yake, hivyo Mwenyezi Mungu akasema: "Leo nimewakamilishieni dini yenu na kuwatimizieni neema Yangu na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu." (5:3). Isipokuwa kuna masuala madogo madogo ambayo wanazuoni wa sheria wamehitilafiana kwa sababu ya kutofautiana kwao kuhusu riwaya ambazo zimenasibishwa kwa Mtume. Jambo ambalo limesababisha kutofautiana kuhusu masuala madodo madogo ya sheria. Kwa kuwa ukweli hutokana na utafiti basi hakika katika mtiririko wa masomo haya mwandishi amejaribu kuliweka swala hili juu ya meza ya utafiti, kwani huenda ikawa ndio njia ya kuunganisha mtazamo na kusogeza hatua katika uwanja huu. Kwani tofauti iliyopo si katika asili na misingi ya dini hata isababishe kuwa na uadui na chuki, bali tofauti iliyopo ni kuhusu riwaya zilizonasibishwa na Mtume, nalo ni jambo dogo ukilinganisha na mambo mengi ambayo tunaafikiana kati ya madhehebu za Kiislamu. Na mwongozo wetu katika njia hii ni kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, mlipokuwa maadui na akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neema Zake mkawa ndugu." (3:103) Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation P.O. Box 19701, Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 47


Kusujudu juu ya udongo final edit S.Pingili.qxd

7/2/2011

Kusujudu juu ya udongo

48

10:52 AM

Page 48

Kusujudu juu ya udongo  

Kusujudu juu ya udongo ni suala ambalo wanachuo wetu wamehitalifiana; ndani ya madhehebu moja na kati ya madhehebu. Kwa hiyo hii sio hitilaf...