Afya ya uzazi

Page 1

WAJIBU WA WADAU WA ELIMU YA AFYA YA UZAZI 1. Wazazi – Kuwa tayari kuongelea masuala ya elimu ya afya ya uzazi bila kificho kwa watoto wao. 2. Wahudumu wa afya- kutoa taarifa sahihi kuhusu afya ya uzazi na huduma rafiki kwa vijana na kwa jamii kiujumla. 3. Shule na taasisi za elimu- kutoa elimu na huduma za afya ya uzazi kwa wanafunzi 4. Serikali – Kurekebisha sheria zinazozuia upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na kusimamia utekelezwaji wa sera na mipango. 5. Mashirika yasiyo ya kiserikali – kushirikiana na serikali kuanziasha na kusimamia miradi ya utoaji wa huduma na elimu ya afya ya uzazi kwa jamii. 6. Jamii – Kutambua, kutafuta, kushiriki na kutumia na kuzilinda huduma. Vituo vinavyo toa huduma ya elimu ya afya ya uzazi ni vipi? Huduma nyingi za afya ya uzazi hupatikana bure katika vituo vya afya vya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile TAWLA, AMREF, UMATI na MARIE STOPES.


Elimu ya afya ya uzazi ni nini?

E

limu ya afya ya uzazi ni suala linalohitaji uelewa wa kutosha kwa wote kwa sababu, afya ya uzazi na ujinsia huhusisha masuala yote yanayomzunguka mwanadamu katika hatua mbalimbali za maisha yake kuanzia kuzaliwa, ukuaji, uzazi, malezi na afya. Dhana ya kwamba elimu ya afya ya uzazi hukoma pale tu kijana anapokuwa ameshamaliza balehe na kuingia katika umri wa utu uzima sio sahihi. afya ya uzazi na ujinsia ni suala endelevu hadi mwisho wa uhai wa mwanadamu. Elimu ya afya ya uzazi inazungumzia: Taarifa sahihi za kuzuia na kutibu magonjwa ya zinaa na virusi vya UKIMWI Taarifa sahihi za uzazi wa mpango Taarifa sahihi za vijana na balehe Taarifa sahihi za madhara ya ukatili wa kijinsia Lengo la elimu ya afya ya uzazi ni: Kujifunza na kufahamu maana ya afya ya uzazi, ujinsia na umuhimu wake kwa jamii, mabadiliko wakati wa ukuaji kipindi cha balehe kwa vijana pamoja na kufahamu mahitaji na haki za afya ya uzazi.

Walengwa wa elimu ya afya ya uzazi Ni jamii kwa ujumla kuanzia kwa watoto wenye umri wa miaka 7 mpaka kwa watu wazima. Faida za elimu ya afya ya uzazi ni: Kusaidia kukabiliana na mimba za utotoni Kusaidia kujikinga na magonjwa ya zinaa na virusi vya UKIMWI Kuwa na malezi bora ya watoto Kusaidia kupata taarifa na huduma za uzazi wa mpango Kusaidia upatikanaji wa huduma ya ushauri nasaha Kusaidia kutambua mabadiliko wakati wa ukuajiBalehe Kusaidia kuzuia ukatili wa kijinsia mfano; ukeketaji Kusadia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kusaidia kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Kusaidia upatikanaji wa elimu ya stadi za maisha Sheria zilizopo katika elimu ya afya ya uzazi. Sheria ya kuzuia na kuthibiti ukimwi)ya mwaka 2008 ambayo imejaribu kwa sehemu kubwa kukataza mambo ambayo yamesababisha kuenea kwa UKIMWI ikiwa ni pamoja na tabia ya baadhi ya watu kuambukiza watu wengine VVU na UKIMWI kwa makusudi.

Sera ya taifa ya kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda mtoto ya mwaka 2002 Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) sura ya 16: Sheria hii imeainisha makosa yanayohusiana na utu katika sura ya kumi na tano kuanzia kifungu cha 129 – 159. Pia sheria hii inamlinda mtoto dhidi ya ukatili wa kimapenzi na imetoa katazo na adhabu kali kwa mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya ngono na mtoto wa chini ya miaka kumi na nane. kifungu namba 219 kinaeleza kosa la kuangamiza mtoto;sheria inasema kuwa mtoto mchanga anaweza kuzaliwa hai baada ya wiki 28 ya ujauzito tendo hilo la kuharibu mimba ni kinyume na sheria labda liwe linafanywa kwa “kulinda uhai wa mama” MAPUNGUFU KATIKA SHERIA ZINAZOHUSU AFYA YA UZAZI • Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 Sheria ya Ndoa inaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 15. Katika umri huo watoto wengi wanakuwa hawana elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo afya ya uzazi. Hali inayowapelekea kupata mimba za utotoni, kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo VVU na UKIMWI, vifo vinavyotokana na magonjwa ya zinaa na hata wakati wa kujifungua.


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.