Page 1

A TOUR TO JOHANNESBURG , SOUTH AFRICA. Ilikuwa siku moja nikiwa katika daladala nikielekea posta na wakat safari ikiendelea huku nikitupa macho huku na kule ndipo nilipoona tangazo kuubwa kuhusu yale mashindano ya “Guinness Football Challenge� yakitangazwa kufanyika tena katika nchi yetu ya Tanzania ambapo tarehe ya kufanyika ilikuwa 14/11/2012 na mnatakiwa kuunda timu ya watu wawili wenye umri usiopungua miaka 18 ndipo nikamkumbuka tena kijana wangu abuu,nilikuwa na furaha baada ya kuona tangazo lile ndipo nikangoja mpaka niliporejea nyumbani na kumpigia simu abuu na kumueleza juu ya shindano lile ambapo na yeye alionekana ni mwenye hamu na shauku kubwa kushiriki kwenye shindano lile baada ya kumshawishi na kumpa moyo ya kuwa ni shindano jepesi mno na kwa uwezo wa soka aliokuwa nao basi ni wazi tutapata nafasi kirahisi. Ilipofika tarehe 14/11/2012 siku ya jumammosi nikampigia simu abuu na kukutana nae tayari kwa kuanza safari ya kuelekea katika viwanja vya leaders club ambapo ndo sehemu ambayo audition ilikuwa ikifanyika na bila kusita tukafika kituon kona na kupanda daladala mpaka ubungo japokuwa usafiri ulikuwa wa shida sana siku hiyo lakini tulifika ubungo na kupanda daladala mpaka magomeni ndipo tupate basi mpaka kinondoni manyanya ili tupande basi ambalo litatusuhusha kwenye viwanja hivyo vya leaders club eneo ambalo auditions zilikuwa zikifanyika kawa siku hiyo,tulichelewa kufika kidogo japo ilikuwa kinyume na matarajio yetu kuwa huenda tukakuta washamaliza kwa kuwa jua lilishaanza kupanda utosini yaani kuwa kali kiasi cha kuanza kuchoma japo hatukujali ukali wa jua lile na kutembea kwa haraka kutoka kituon mpaka kwenye viwanja hivyo vya leaders club ndipo tulipokuwa tukikaribia eneo hilo tulikuwa tukisikia kelele kubwa za muziki na kujionea vijana mbalimbali wakiwa wamekaa na wengine wakiendelea na mashindano na hapo ndipo tukapata moyo kuwa bado hatujachelewa ndipo tukasogea kwa ukaribu kabisa na kuuliza kuwa ukitaka kujisajili unakwenda wapi na hapo akatokea mmoja wa


waandaaji na kutuonyesha eneo la kuanzia kujisajili na hatimaye kuandikishwa majina yetu na kuingizwa katika list ya watu watakaochuana na vijana wengine wengi waliojitokeza siku hiyo na tukaamua kuipa jina timu yetu kwa kuiita “Ranger” maana ya jina hilo ni mlinzi wa kulinda wanyama katika mbuga au askari na lilitufaaa kwa kweli kwa wakati huo kwani tulikuwa tofauti na majina ya timu zoote zilizojitokeza pale kutokana na ukweli kwamba wengi wao walijiandikisha kwa majina ya vilabu vikubwa vya ulaya vyenye majina makubwa na vingine vyenye majina ya kawaida japo zinatokea ulaya pia,tulikabidhiwa namba ili tuninginize shingoni ili kuwa kama utambulisho kuwa ni washiriki kama washiriki wengie ndipo tukaelekezwa sehemu ya kukaa ili kusubiri zamu yetu itakapofika ili nasi tukaonyeshe kile tulichohitaji kuonyesha ili watu wafahamu na ulimwengu ujue juu ya vipaji tulivyojaaliwa na huku tukiwa pale tumeketi tulipata nafasi ya kuona vijana wengine wakichuana na kusema kweli tuliona vipaji mbalimbali vikionyesha uwezo wao juu ya kuuchezea mpira au gozi la ngombe kama inavyofahamika katika mitaa mingi ya dar es salaam na Tanzania kwa ujumla na kwa hakika vijana wengi wa kitanzania wana vipaji vya hali ya juu na kwa hakika nimejionea kwa macho yangu na huku tukiendelea kushangaa mimi na kijana wangu Abuu ndipo ghafla tukasikia jina la timu yetu likitajwa na ndipo tukasimama na mimi kuelekea kwenye sehemu ambayo wanauliza maswali kuhusiana na mchezo wa soka ulimwenguni kwa ujumla na ndipo nikaulizwa maswali kadhaa yakihusu ligi ya uingereza,ligi kuu bara ya Tanzania na ndipo nikajimwaga kwa kujibu kwa usahihi maswali mengi niliyoulizwa na ndipo nikamaliza na kwenda kumtazama Abuu akifanya yake pale katika kuzunguka “koni” yaan ilikuwa ni zoezi gumu japo kwa kijana huyu ilikuwa rahisi hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuuchezea mpira au gozi la ngombe kama wanavyoita wazawa na baada ya kumaliza zoezi hilo ndipo akelekea kwenye kiwanja flani kidogo kwa ajili ya kuuchezea mpira kwa kuonyesha ufundi wa kupiga danadana na kuonyesha michezo mingine kwa muda wa dakika kumi bila kudondosha chini na


hapo ndipo kijana Abuu alidhihirisha juu ya uwezo wake mkubwa kwani aliweza kukonga nyoyo za vijana wengi waliojitokeza eneo lile na kujikuta wakimshangilia sana kiasi cha kumshangza mchambuzi wa masuala ya soka nchini Tanzania na si mwingne bali ni “Ibrahim Masoud” au maarufu kwa jina la “Maestro” kwa kipaji kikubwa sana alichokuwa nacho kijana huyu mpole wa kitanzania mwenye umri mdogo kabisa na bila shaka aliwashangaza wengi nikiwemo mimi mwenyewe kwani sikuwa na matarajio juu ya mambo makubwa aliyoyafanya pale kwenye kile kiwanja na kwa bahati mbaya aliangusha mpira katika dakika kama ya nane hivi na zikiwa zimebakia au zimesalia dakika zisizopungua mbili hivi na haikuwa mbaya kwa upande wangu kwani alinifurahisha mno na baada ya kuanagusha mpira alipewa zoezi lingine na kupiga penalty katika magoli madogo sana na kufanikiwa kutumbukiza mipira miwili kati ya mitatu aliopatiwa na baada ya hapo nilienda kumpongeza na kumtia moyo kuwa amefanya vizuri sana na watu wengi walifurahia alichokuwa akikikifanya pale kwenye kile kiwanja kidogo maalumu kwa ajili ya zoezi lile la danadana na hapo ndipo tukenda kuketi ili kungoja kuitwa na wandaaji kwenda kuzungumza namna ya kupata matokeo na juu ya mambo kadhaa yanayohusu shindano lenyewe ikiwemo ruhusa ya wazazi na vipingamizi vyovyote juu ya safari ikitokea umepata nafasi ya kuiwakilisha nchi,tulitajiwa zawadi ya mwaka huo kuwa ni kitita kikubwa sana cha pesa kiasi cha 900,000$ sawa na billion 1 na 400 millioni pesa taslimu za kitanzania ni kiasi ambacho kijana yeyote angeshawishika kushiriki kwa kiasi hicho cha pesa kwani hali ya maisha nchini kwenu sio nzuri sana hasa kwa vijana kwani wengi wao hawajafanya vizuri shuleni japo wana vipaji vikubwa vya kuucheza mpira wa miguu.Tukamaliza kila taratibu zinazohitajika na hatimaye kuruhusiwa kuondoka na ilikuwa ishafika jioni majira ya saa kumi na tukiwa na uchovu mwingi lakini na furaha tele kwa kile tulichokifanya pale na kutimiza sehemu ya ndoto na hamu zetu za kushiriki mashindano yale makubwa katika ukanda huu wa Africa mashariki na barani afrika kwa ujumla na yalikuwa yakihusisha nchi za


Tanzania,Kenya na Uganda kwa upande wa mashariki mwa afrika na pia yalisemekana kuhusisha nchi za Cameroon na Ghana kama washiriki kutoka magharibi mwa afrika na hiyo ilikuwa siku nzuri sana kwangu na kurejea nyumbani salama huku nikijipa moyo kwa kusubiri matokeo baada ya muda wa wiki mbili baada ya siku ile ya jumamosi na imani yangu kuu ilikuwa kushinda na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi huko Johannesburg Afrika Kusini kwa mzee Madiba au Bondeni kama inavyofahamika hapa kwetu nyumbani Tanzania.

Wiki ya kwanza ikapita na ndipo usiku mmoja nikiwa natokea posta niko kwenye daladala ndipo nikapokea simu iliopigwa na mwanadada akijitambulisha kwa jina la Regina na kuniuliza kama nilishiriki shindano la Guinness Football Challenge na mimi bila kusita nikamjibu ndiyo na kuniuliza maswali kadhaa juu ya viambatanisho flani ikiwemo pass ya kusafiria yaani passport na kumjibu kuwa ninayo na akanambia nimtumie namba ya pass ya kusafiria na baada ya hapo nikaanza kuwa na maswali mengi juu ya simu ile niliopigiwa lakini baada ya muda kidogo Abuu akaja nyumbani kwetu na kunifahamisha kuwa na yeye kapigiwa simu kuulizwa maswali kadhaa kama yale nilioulizwa mimi na dada Yule na hatimaye kumjibu vyema na kwa usahihi mkubwa,tulijawa na furaha sana japo haikuwa dhahiri sana kwa kila mtu kwa kuwa hatukataka watu wafahamu kwani bado ilikuwa ni siri kati yangu mimi na Abuu kama tulivyokubaliana mpaka matokeo yatoke ndo tuwaambie baadhi ya watu wetu wa karibu ikiwemo wazazi wetu na ndugu zetu wengine wa karibu. Zilipokwisha wiki mbili ndipo nikiwa na mawazo juu ya report yangu ya field huko chuo ninakosoma ndipo ikapiga tena ile namba ya Yule dada anaitwa Regina na kwa akili ya haraka nikaikumbuka ile namba japokuwa sijaisave na nilipopokea tu nikaambiwa habari njema kuwa jina langu ni miongoni mwa majina yaliyochaguliwa kwa ajili ya kwenda johannessburg south afrika na furaha niliyokuwa nayo baada ya kupokea simu hiyo ikanisahaulisha kabisa kuhusu mawazo ya report yangu ya chuo na kuanza kuwaza juu


ya safari hiyo itakavyokuwa na mashindano yatakayokuwa japo sikuwa Napata picha kamili juu ya kile nitakachokikuta huko na nikaamua kumpigia simu Abuu kumpa habari njema ile na bila kutegemea na yeye akanambia kuwa alipigiwa simu na kuelekekezwa mahali zilipo ofisi zao kwa ajili ya kukutanishwa na washindi wengine,nakumbuka ilikuwa siku ya jumanne niliamka asubuhi na mapema na kuelekea huko mikocheni mahali zilipo ofisi hizo huku nikiwa bado sijiamini juu ya simu ile na hatimaye nikafika katika ofisi ile na kukuta baadhi ya washindi wakiwa wamefika na kuwangojea wengine ili wafike na hapo ndipo nikaamini kweli kuwa nimeshinda baada ya kukutana na washindi wengine na kupewa taarifa muhimu kuhusu safari ikiwemo juu ya kupatiwa pass ya kusafiria kwa wale wasiokuwa nazo,huku zoezi hilo likiendelea tulijitambulisha na kupeana namba za simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano baina yetu na kutangaziwa tarehe ya safari ambayo ilikuwa ni tarehe 12/01/2013 yaani mapema mwaka mpya utakapoingia basi na mimi nitaanza kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu kwa kutembelea nchi ambayo ilikuwa ni ndoto ya vijana wengi wa enzi hizo za miaka ya 90 kutua katika nchi hiyo wakiamini utakuwa na maisha bora huko. Tuliambiwa tarehe nyingne na siku ya kukutana kwa ajili ya kupewa maelezo ya jumla juu ya shindano zima na utaratibu wa safari utakavyokuwa kuanzia usafiri tutakaotumia kutoka hapa dar es salaam mpaka hatimaye kufika Johannesburg na sehemu tutakayofikia tukiwa huko na mambo mengine ya muhimu juu ya namna ya kuishi tukiwa huko na kuhusiwa sana kuhusu nidhamu hasa kwa team mate wako kwani tuliambiwa nidhamu ni kitu muhimu sana katika michezo na si hapo tu bali nidhamu ni kila kitu katika maisha ya binadamu hasa kijana,ndipo tukaambiwa kuwa kutakuwa na party katika moja ya kumbi nzuri na za kisasa katika jiji la dar es salaam na si kwingnine ni city sports lounge pale kwenye sanamu la bismini pale posta na hapo ndipo kutakuwa na waandishi wa habari za michezo kama sehemu ya shamrashamra za kutuaga na kututakia mafanikio katika safari yetu hiyo ya mafanikio sana na baada ya hapo kila mmoja alitawanyika ili


kujiandaa kwa safari kwa kuweka sawa mabegi na mavazi utakayoyatumia kwa muda wote tutakaokuwa huko afrika kusini huku tukingoja siku yenyewe ifike na ilikuwa tukipigiwa simu mara kwa mara kukumbushwa vitu vya muhimu vya kubeba kwa ajili ya safari na namna ya kuwahi siku ya safari ili tusije tukachelewa kulingana na ratiba ilivyopangwa na waandaaji hao.Baada ya kurejea nyumbani ndipo nikaamua kuwaambia wazazi kwa kuanza kumtaarifu mama yangu kwani ndio nilimkuta nyumbani juu ya safri nzima ilivyokuwa mpaka kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi na kwa haraka haraka ilikuwa ngumu kwake kuamini kuwa kijana wake naweza kupata nafasi kama hiyo kwani hakuwa akinidhania kama nina kipaji kiasi hiko na baba aliporejea toka kazini nikamueleza na yeye akanipa Baraka zake na kunitakia kheri katika mashindano hayo na hatimaye kukaa kwa amani na kungoja siku itimie ili nipate kusafiri lakini nilikuwa naona kama siku haziendi vile. Baada ya mwaka mpya kuingia yaani mwaka 2013 yaani hapo ndipo nilipoanza kuhisi ukweli juu ya yale tulioambiwa na waandaaji kwani muda ulikuwa ukikaribia sana,ndipo wiki moja kabla ya tarehe ya safari kufika tukaitwa ofisini kwa waandaaji mikocheni na ndipo tulipokutana kwa mara nyingne wale washindi wote na hapo ndipo kulikuwa na taarifa za mwisho kabisa juu ya safari ile na bila shaka ilikuwa siku ya furaha mno kwetu washindi wote kwani alikuja muandishi wa habari maarufu hapa jijini dar es salaam kwa jina la “michuzi� na alipiga picha nyingi na kuzituma katika mtandao wake na hatimaye dunia nzima iliniona mimi na washindi wengine na hapo ukurasa mpya ukafunguka kwani sikuwahi kutokea katika chombo kikubwa cha habari kama hiko tangu kuzaliwa kwangu mpaka umri huu niliofikia kwani yapata miongo miwili sasa tangu nimezaliwa na baada ya kutoka pale katika ile ofisi nilikwenda nyumbani na kijarida kimoja chenye maelezo yoote juu ya eneo tunalokwenda na namna mashindano yatakavyoendeshwa pamoja na uzuri wa sehemu tutakayofikia kwa kipindi chote cha mashindano na nilisoma vyema hiko kijarida kwa utulivu,picha zikatoka na baadhi ya rafiki na jamaa wakanipigia simu na


kunifahamisha kuwa wameniona na wengine hata sikutaraji kama wangeniona na kwa bahati nzuri mimi ndo nikachaguliwa kuwa kiongozi wa timu zote au mkuu wa msafara katika washiriki kumi tuliochaguliwa na nilifarijika sana kwa tukio lile kwani ilionyesha picha kuwa nakubalika japokuwa tuliiishi kwa muda mfupi au kufahamiana kwa muda mfupi mno na mimi niliridhia nafasi ile niliopatiwa na washiriki wenzangu pamoja na waandaaji wa mashindano kwa kuwa waliniamini kwa namna fulani. Maandalizi ya safari yaliendelea taratibu kwa kununua vitu ambavyo sikuwa navyo na vilikuwa sehemu ya safari kama vile begi la kusafiria na mahitaji mengine binafsi na haikuchukuwa muda mwingi kukamilisha mahitaji yangu yote na huku siku za safari zikiwa zinakaribia na kujiona kama vile nazaliwa upya kwa hamu na shauku kubwa ya kusafiri. Ilipofika siku ya jumamosi ya tarehe 11/01/2013 hiyo ndiyo ilikuwa tarehe rasmi ya safari na ilipangwa tukutane maeneo ya kinondoni moroco kama ndo makutano ya washiriki wote kwani hiyo sehemu ndio ilikuwa centre yaani kila mmoja wetu angefika kwa urahisi kabisa,ilipofika asubuhi ya siku hiyo niliamka mapema mno ili kuhakikisha kila kitu changu kinakwenda salama na hapo nilisalimiana na wazazi wangu na kumkumbusha baba yangu kuwa ile siku ya safari ndio imewadia na nilikuwa nataraji kusafiri usiku wa jumamosi na kwa kuwa nilihisi baada ya asubuhi ile tusingeweza kuonana tena na mzee wangu kwani angeondoka na kwenda kwenye majukumu ya kujenga taifa nikaamua kuchukua fursa hiyo ya kupeana nae mkono wa kheri na nasaha zake juu ya namna ya kuishi huko na kufanikiwa na nilifurahi sana baada ya kuagana nae nikatoka kwenda kariakoo kumuaga pia rafiki yangu anaejulikana kwa jina la khusaam na yeye pia alinipa baraka zake na pia nikaelekea kigamboni kuonana na mchumba wangu kwani yeye pia nilishampa taarifa za safari lakini hakuwa hakiniamini ndo sababu nikaenda kumuaga na yeye anipe baraka zake ili kuhakikisha hata nikiondoka basi yeye awe ameridhia na kubaki katika furaha huku akiniombea dua nifanikiwe ili mambo yawe mazuri baina yetu mimi na yeye na hapo ndipo nilimpa namba yangu ya simu


nitakayokuwa nikitumia huko ili kurahisisha mawasiliano kati yetu kwani namba yangu iliozoweleka itakuwa haipatikani kwa kipindi chote nitakachokuwa nje ya nchi na kwa bahati nzuri alinielewa na kuniamini lakini hakutaka niondoke na kurudi mikono mitupu kwani aliniagiza zawadi toka afrika kusini ili iwe kama sehemu ya ukumbusho huko siku za usoni na sio yeye tu bali kila mtu alitaka nimnunulie zawadi iwe kubwa au ndogo na wengi wao walitaka simu za mikononi tena zile za kisasa zaidi na kwa kuwa sikuwa na ujuzi wa bei za huko nilikubali kuwanunulia na kuwaahidi wote kuwa ningewaletea zawadi japo kidogo,nikaanza safari ya kurejea nyumbani kutoka kigamboni kwani ilikuwa ishafika mchana na ni karibu zaidi kufika ule muda ambao tulipanga kukutana moroco na baada ya muda flani na foleni za hapa na pale hatimaye nikafika nyumbani na kuanza kupanga vitu vyangu kwa kusaidiana na ndugu yangu mpenzi Dai na alikuwa akiniambiwa vitu gani niweke na vipi niviwache kwani begi lilikaribia kujaa na kupata uzito mkubwa kiasi lingenisumbua kwenye viwanja vya ndege na ukizingatia nitarejea na zawadi je ningepata wapi nafasi ya kuweka vitu vyote?nikaamua kumsikiliza na kupunguza baadhi ya vitu na huku muda ukikimbia sana,nikampigia simu Abuu ajiandae na tukutane nyumbani kwetu tayari kwa safari ya kuelekea moroco na baada ya muda Abuu alifika na kuandamana pamoja kuelekea sehemu ya makutano na kwa bahati mbaya tulichelewa kidogo japo haikuwa tatizo kwa waandaaji na tayari nilikuta washiriki wenzangu wakiwa wamefika na huku mshiriki mmoja hakuwa amefika na ilituchukuwa muda kumngoja kijana Lukwesa ambaye kuchelewa kwake ilikuwa kawaida sana na tukaamua kuondoka kuelekea hoteli maeneo ya kinondoni kanisani na tukafika katika hiyo hotel inaitwa sleep inn na kupewa vyumba na hakika palikuwa sehemu tulivu na maridhawa sana,tukaweka mabegi na kubadili nguo tayari kwa kuelekea posta katika mgahawa unaitwa city sports lounge ambapo majira ya jioni kutakuwa na hafla na waandishi wa habari za michezo wa magazeti na redio kama sehemu ya kuagana na kuonyesha jamii kuwa kweli safari ilikuwepo na ndipo baada ya nusu saa tukafika katika mgahawa huo


mwanana kabisa katika jiji la dar es salaam na kukuta mechi kadhaa za ligi ya uingereza zikiendelea na kila mmoja wetu akapoa katika meza yake na kuanza kuagiza vinywaji mbalimbali huku tukitazama mpira na mechi zilikuwa kali kwani chelsea ilikuwa ikicheza na miongoni mwa magoli ya siku hiyo yalifungwa na mchezaji toka senegal kwa jina la demba ba ambaye alikuwa punde tu amejiunga na club hiyo ya london,huku mechi zikiendelea na vinywaji vikiendelea na stori nyingi sana na washiriki wenzangu akiwemo Gullam Sosha na Abuu na wengineo.Baada ya muda flani muda wa hafla kuanza ukatangazwa kwani wageni wote walifika pale na watu walianza kujitambulisha kulingana na vyeo vyao pia washiriki tulipewa nafasi ya kujieleza na kueleza matarajio yetu katika mashindano hayo yatakayofanyika johannesburg afrika kusini na baada ya utambulisho kumalizika basi fursa ya kupata ya kupata chakula cha usiku ikawadia na hapo tulikula vyakula vizuri sana na kufurahi nafsi zetu kwa hakika na ilipofika majira ya saa tano usiku tulipanga kuanza safari ya kutoka posta na kurejea maeneo ya kinondoni,lakini kabla ya kuondoka eneo lile nikaitwa na kupewa maelekezo juu ya sehemu nitakazokuwa napita na namna ya kuwaongoza wenzangu ili tusije kupoteana kwenye viwanja vya ndege tutakavyopita kwa idadi ya viwanja vitatu mpaka tunamaliza safari yetu na nilisikiliza kwa makini kwani washiriki wote hakuna aliewahi kupanda ndege wala kufika airport na baada ya kupata maelekezo hayo muhimu ya safari basi tukaanza kurejea kwenye hoteli ili kupumzika kwa muda kabla ya saa saba usiku kufika kwani muda huo ndio tulipanga kuelekea airport,tukafika hotel na kupumzika kwa muda na kuja kuamshwa na dada Regina ambaye tulikuwa nae kwa karibu sana kwa muda wote wa maandalizi ya safari mpaka inakamilika na baada ya hapo kila mmoja aliamka na kuanza kujiandaa kwa kuoga na kuvaa nguo nzuri ili kwa kwenda uwanja wa ndege na tulipotoka nje ya hotel tulipiga picha nyingi kama sehemu ya ukumbusho na kupanda kwenye gari nzuri tulioandaliwa tayari kwa kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu julius kambarage nyerere ambapo tutapanda ndege ya shirika la ndege la kenya airways kuelekea NAIROBI na


haikutuchukuwa muda mwingi kufika airport kwa kuwa majira hayo ya usiku huwa foleni hakuna pia mji unakuwa umepoa na watu wanakuwa wamelala na kupumzika kwenye majumba yao na tulifanikiwa kufika salama katika uwanja wa ndege huo na kuingia ndani ya kiwanja tayari kwa ajili ya kuanza ukaguzi kwa ajili ya safari na tulipita sehemu ya kwanza ya ukaguzi salama na hatimaye kuingia ndani na kuambiwa tungoje katika viti fulani ili wafanyakazi wa ndege hiyo waanze kutuhudumia na baada ya dakika kadhaa nikaitwa mimi kiongozi wa msafara na kuambiwa kukusanya passport na yellow fever card za washiriki wote na kupeleka katika kaunta moja wapo na ndipo nikakutana na kijana mmoja mtanashati na kutusaidia kwa ukaribu zaidi na hatimaye kuambiwa nichukue mabegi yoote na kupewa vikadi flani vya utambulisho wa umiliki wa mzigo na kuambiwa kutoa vitu vyenye asili ya maji maji na kuweka katika begi moja ili kuepusha usumbufu wa hapa na pale pia kila mtu alipewa tiketi mbili yaani ya kutokea dar na kuelekea nairobi na ya kutoka nairobi kuelekea johannesburg,baada ya kumaliza process za awali ndipo tukaelekea uhamiaji na kugongewa visa za kutoka nje ya Tanzania na baada ya zoezi hilo tukapata fursa ya kuagana na dada Regina kwani asingeweza kwenda mbele zaidi ya hapo na kututakia kila la kheri kwenye safari yetu na hapo nikaongoza washiriki wenzangu kuelekea kwenye sehemu ya mwisho ya ukaguzi ili kupanda ndege ya kuelekea nairobi na hapo tulimaliza ukaguzi salama sana na kuambiwa kupumzika kwenye viti maalum ili kusubiri kuondoka na tulikaa kwa muda mrefu sana takribani saa moja na ilipotimu saa kumi usiku hatimaye tukaitwa kupanda ndege ndogo ya shirika la ndege la precision air ambao ni washirika wa kenya airways na baada ya dakika kumi na tano watu wote walikuwa wamekwisha keti katika siti zao wakipewa maelekezo na ndipo na mimi nilikuwa makini kusikiliza maelekezo ya usalama angani kwani ndio mara yangu ya kwanza kupanda ndege na nilikuwa na uoga flani hivi lakin nikaomba dua kabla ya safari na uoga ukapungua kidogo na nikajifunga mkanda na kuweka kiti vizuri na ndipo ndege ilipoanza safari taratibu na rubani akitangaza kuwa safari itakuwa ya muda wa saa


moja na kufika jijini nairobi saa kumi na mbili asubuhi na mapema punde tukatangaziwa ndege ipo tayari kupaa na ndipo ikaanza kwenda kasi kiasi cha kunishtua na baada ya kunyanyuka kuna hali flani ya utofauti nikaanza kuhisi yaani tumbo langu kama linataka kuuma lakin haliumi japo haikuchukuwa muda mwingi ile hali ikatulia na ndege ikakaa sawa na kutolewa tangazo la kufungua mikanda na kuanza kufurahia safari kwa kupitishiwa vinywaji na vyakula ili kupasha tumbo joto lakini kuna kitu sikukipenda katika ndege ile kwani ilikuwa na kelele sana kiasi cha masikio yangu kuzibuka na kutosikia vizuri kwa safari nzima na kuona safari chungu japo niliienjoy kiasi fulani ukizingatia ni mara ya kwanza kupanda ndege hasa inayokwenda nje ya nchi,vyakula vilinifikia na nikajaribu kula kiasi lakini sikushiba na kwa kuwa sikuwa na njia nyingne ya kufanya nikaamua kukaa kimya mpaka ntakaposhuka airport jomo kenyatta internantional airport ndipo nifanye mipango ya kula kwa wingi na wakati nikiwaza hayo yote mara punde nikamsikia rubani akitangaza kwa sasa tushaingia kenya na muda wowote tutatua nairobi na wahudumu wa ndege wakaanza kukusanya vyakula vilivyobaki ili kila mtu awe salama akingoja ndege itue kwani katika hatua hiyo usalama ni mdogo mno basi dakika chache nikasikia ndege ikishuka kwa kasi na tumbo kuanza kuuma na baada ya sekunde kadhaa nikasikia matairi yakisugua ardhi na kuchungulia nje dirishani nikaanza kuona majani na kugundua kuwa bila shaka tutakuwa tushafika ardhini na hatimaye kutua salama katika jiji kubwa la nairobi na kujionea mandhari nzuri ya uwanja huo wa ndege wa jomo kenyatta ambao ni wa kisasa zaidi kiasi cha kunishangaza mno kijana mie wa kitanzania ambae katika nchi yetu hakuna uwanja wa kisasa kama huu wa jomo kenyatta kwani kwa muda mchache niliokaa katika huo uwanja nilishuhudia ndege zaidi ya 50 zikiiingia na kutoka kwa muda huo mchache na nyingi zikiwemo za shirika la ndege la kenya airways,tukafanikiwa kushuka salama na wakati wa kushuka nyuma yangu niliona ndege kuubwa nikamuomba mmoja wa washiriki wenzangu akanipiga picha lakini kulikuwa na baridi kali sana katika uwanja huo siku hiyo lakini kwa wenyeji walidai kuwa ni kawaida kwa


jiji hilo kwa nyakati za asubuhi kama ile kuwa na baridi kali na liliniacha mimi na baadhi ya washiriki wenzangu tukijikumbatia kama vifaranga vya kuku kwa muda wote wa saa tatu tulizokaa katika uwanja huo kungoja ndege ya kwenda nayo moja kwa moja mpaka katika jiji la johannesburg afrika kusini au maarufu kama kwa madiba au “the land of madiba� na hatimaye tukafika katika passenger lounge tayari kwa kungoja ndege na kwenda kuuliza katika moja ya kaunta za kenya airways ili tupewe maelekezo ni wapi mahali kwa kusubiri ndege kwani tuliona watu wengi wakiwa busy na harakati zao za kuwahi ndege na wengine wakinunua zawadi katika maduka yaliyojaa ndani ya uwanja huo wa ndege na tukaelekezwa twende kaunta nambari 12 na hatimaye kufika katika kaunta hiyo ambayo saa tatu baadaye ndipo tutatumia kupitia ili kupanda ndege ya kwenda jozi,tukakubaliana na washiriki wenzangu kuwa kama kuna mtu anataka kutembea ndani ya kiwanja ruksa lakini itakapotimu saa mbili na nusu asubuhi wote tukutane katika kaunta hiyo na bila shaka walipokea maagizo yale kwa umakini na kila mmoja kutawanyika na ndipo mimi nikaenda msalani kutoa haja ndogo na kutafuta kiti tulivu na kuweka head phone zangu masikioni na kula muziki taratibu ili muda usogee na baada ya muda nikaamua kuweka radio ili nisikilize kinachoenedelea hapo nairobi au kenya kwa ujumla na kwa bahati mbaya na kukutana na redio nyingi zinazotangaza kwa kilugha yaani lugha za makabila na moja au mbili zikitangaza kiingereza na kiswahili na hapo ndipo nikaamini kuwa kenya ukabila umetawala sana na haikuwa dhamira yangu kuyafuatilia hayo yoote basi nikaamua kuachana na redio zao na kuamua kuendelea kusikiliza muziki wa kitanzania na wa huko marekani kiasi na hata baadhi ya nyimbo za kenya hasa kundi moja la vijana wanajulikana kwa jina la camp mulla vide yaani wamenivutia mno kwa mtindo wako wa mashairi na style ya uimbaji pia,huku muda ukisogea na nikiendelea kusikiliza muziki na kushangaa wanaopita na kwenda na kurudi huku nikitazama ndege zikiruka na kuingia hapo uwanjani na punde nikasikia first call ya wasafiri wanaokwenda johannessburg kwa ndege ya kenya airways na ndipo nikaanza kuona watu wengi wakipanga mstari ili kukaguliwa


tiketi zao na hatimaye kwenda kungoja ukaguzi wa mwisho na kupanda ndege,nikaanza kuwatafuta wenzangu ili niwafahamishe na ndipo nikakutana na kundi flani la vijana kama watatu wakitushangaa shangaa kumbe pia walikuwa washiriki wa shindano hilo hilo wakitokea kenya na bahati nzuri yupo mmoja wao alikuwa akizungumza kiswahili safi na alikuwa akiitwa Saddam au Awadh akiwa pamoja na wenzie na tulikuwa tukipanda ndege moja lakini hatukuwa tukijuana kusema kweli kwa kuwa wasafiri ni wengi na ndege yenyewe ni kubwa mno inabeba abiria takribani 345 kwa safari moja na mizigo pia na hakika ni ndege kubwa sana,wakati tukiwa katika mstari nikakutana na vijana kutoka Thailand tukawa tukizungumza huku tukicheka sana kwani wao waliniambia wanakwenda jozi kwa matembezi tu wakiwa na gitaa kwa kumaanisha wanapenda muziki na nikawaambia na mimi pia ni mpenz wa muziki na hatimaye kufurahia kukutana na kwenda pamoja mpaka kwenye ukaguzi na kufanikiwa kupita salama kwani sikuwa na mzigo wowote niliobeba zaidi ya passport yangu na card yangu ya yellow fever tu na baada ya muda tukaelekea katika viti kusubiri safari na huku nikitafakari juu ya safari itakavyokuwa kwani nilikuwa na hamu kubwa ya kufika jozi baada ya kukaa zaidi ya saa mbili hapa nairobi city,huku nikiwaza punde nikasikia second call ya kukaguliwa na kupanda kwenye ndege na hapo nikaanza kupata tumaini jipya la kusafiri na kupita katika ukaguzi kwa mara nyingine na hapo pia tukaanza kupita katika njia na kuingia katika basi fulani la kisasa ambalo litatutoa katika ngazi na kutupeleka mahali ndege ilipo kwani ni umbali kidogo na wakati tukielekea kwa mbali nikaona ndege moja kuubwa sana nikaanza kujipa moyo kuwa hiyo ndio itakuwa ndege tutakayopanda na wenzangu na kama nilipatia vile lile basi lilienda mpaka mita chache karibu na ile ndege na milango kufunguliwa na kuambiwa karibuni on board na kukaribishwa na tabasamu zuri na la bashasha la wahudumu wa ndege ile tayari kwa kuanza safari ya kuelekea jozi. Majira ya saa 3 asubuhi abiria wote wakiwa wameketi katika siti zao ndani ya ndege kubwa sana na ya kisasa ya kenya airways aina ya


boeing ndipo nikaanza kujionea tofauti kati ya precision air yenye kelele nyingi kiasi cha kunizibua masikio na hili ndege la kisasa ambalo kwanza siti zake ni kubwa pia ni very comfortable,screen kubwa na ya kutouch ipo mbele ya kiti nikapewa na head phone kubwa za kisasa kwa ajili ya kuenjoy muziki na filamu zilizokuwepo katika screen ile ya ndege kubwa na ya kisasa huku nikiwatazama washiriki wenzangu wakiwa nao wameketi na baadhi ya abiria wengine wakijiandaa kwa ajili ya safari na mimi nilipata bahati ya kukaa karibu na mtanzania mwenzangu ambae umri wake huenda ni sawa na baba yangu mzazi na tukawa tukizungumza mambo kadhaa ya utofauti kati ya ndege zetu yaani air tanzania na kenya airways na pia ubora wa viwanja vya ndege yaani jomo kenyatta na mwalimu nyerere international airport na kugundua tofauti kuubwa na za dhahiri baina ya nchi hizi mbili zilizo katika ukanda wa afrika mashariki na baada ya maongezi machache kila mmoja wetu akaanza kuwa busy na mambo yake na mimi nikachukua magazine flani niliokuta ndani ya ndege ikielezea mambo mbalimbali ya ndani ya kenya kuanzia biashara,uchumi,utalii,burudani na utamaduni. Mara tukasikia tangazo toka kwa rubani kuwa abiria wote mnakaribishwa katika ndege ile ambayo itakuwa ni ya muda wa saa nne angani na anategemea safari itakuwa nzuri na sio yenye kuchosha na kuwataka abiria wote safari njema na kufuata maelekezo ya usalama watakayopewa kwa muda wote watakaokuwa katika ndege ndipo tukaambiwa kufunga mkanda na kuweka viti sawa tayari kwa kuruka na kuliacha jiji la nairobi na kuelekea jozi kwa mzee madiba na hapo nikaanza kuona ndege ikiondoka taratibu na kuanza kushika kasi na hatimaye kupaa lakini safari hii tumbo halikunisumbua kwa kuwa nadhani nilinza kuzoea au ukubwa wa ndege pia ulichangia kwani ndege ile ilikuwa imetulia sana angani na hata kelele hazikuwepo badala yake air condition tu ndio ilikuwa kali sana kiasi cha kujikumbatia na kusikia njaa kali na hatimaye kujikuta dakika chache tu baada ya kupaa nikapata usingizi mzito na baada ya muda takribani saa mbili kupita nikaamshwa kwa kuwa chakula kilikuwa tayari kinagaiwa kwa abiria wote ndipo na mimi nikapatiwa chakula na


kuanza kula na baada ya kumaliza nikajihisi nimepata nguvu na uchovu umepungua kiasi na kuanza kutazama movie flani nzuri niliipenda mno na baada ya movie nikaanza kusoma tena ile magazine na ilifika mahali nikaona karibia ndege nzima wamelala na hiyo ilikuwa majira ya saa saba kwa saa za kenya na hiyo ilikuwa ikimaanisha kuwa safari ilikuwa ndefu kiasi na ukizingatia wengi katika washiriki wenzangu walikuwa wamekunywa pombe usiku wa jana na wengne wakiendelea kwenye ndege kunywa pombe pamoja na mapumziko hafifu tuliopata pia yalichangia wengi kuchoka,huku safari ikiendelea nikaanza kutazama kwenye screen na kuona maeneo au nchi tulizopita na tutakazopita mpaka kufika johannessburg na kwa haraka niliona tukipita kilimamjaro,zanzibar,malawi,msumbiji,zimbabwe na hatimaye tukatangaziwa kuwa tushaanza kuingia katika anga ya afrika kusini na wakati wowote tunaweza kutua na nikaanza kuchungulia nje na kujionea milima mikubwa sana japo sikupata kufahamu jina lake lakini kwa hakika ilipendeza sana machoni kwangu kiasi cha kuendelea kushangaa uzuri wa milima ile ambayo hata kwetu tanzania ipo tena mingi sana huko Morogoro,Iringa,Mbeya na kwingineko.Wakati huo likatolewa tangazo kuwa abiria wote tufunge mikanda sawa sawa na tuweke viti saambamba tayari kwa kutua katika uwanja wa ndege wa oliver tambo international airport na ndio airport kubwa na ya kisasa katika historia ya viwanja vya ndege katika bara la afrika kwa ujumla,punde si punde ndege ikagusa ardhi ya Afrika Kusini hususani mji wa jozi na kwa wakati huko ilikuwa saa sita mchana kwa majira ya afrika kusini na ilituchukua kama dakika kumi na tano mpaka kuanza kushuka na ndipo tulipokaribishwa kwa hali ya hewa nzuri na yenye utofauti mkubwa kati ya Dar es salaam na Nairobi pia yaani nilijihisi utofauti mkubwa na kuanza kuzunguka ndani ya kiwanja cha ndege hiko cha ukweli sana na kuanza kutembea katika ngazi za umeme huku tukicheka sana na washiriki wenzangu kwa ushamba ukitusumbua na tulitembea kwenye zaidi ya ngazi tatu za umeme yaani ilikuwa ni experience ya ukweli sana na ndipo tukaenda katika ofisi za uhamiaji za afrika kusini na tukapokelewa na tabasamu la bashasha la maofisa wa


uhamiaji lakini cha ajabu sikuulizwa nimekuja kufanya nini na baada ya muda kutazama passsport yangu nikapata kuona nimepewa viza ya miezi mitatu tena halali na baada ya kumaliza zoezi la visa ndipo tukasogea maeneo ya kuchukulia mizigo na ilituchukuwa muda kiasi sote kupata mizigo yetu lakini mwishoni tuliipata na kuanza kushangaa uzuri wa majengo ya ndani ya uwanja na kwenda moja kwa moja msalani kutoa haja ndogo na kutoa jasho la bongo huku tukifanya vituko vingi sana kule msalani na hatimaye kuanza kutoka nje ya kiwanja na punde tu tukafika nje na kujionea wenyewe uzuri wa kiwanja kile na sura mpya za kisouth na kwa bahati mbaya tunatoka nje hatukuwakuta wenyeji wetu na ikaleta maswali kidogo vichwani kwetu na ghafla akaja askari polisi mmoja na kuanza kutuuliza kuwa tumetokea wapi na kwanini tunashangaa sana eneo lile na ndipo wenzangu wakanitaka nizungumze nae na yule askari alitaka kujua ujio wetu pale na bila shaka nikamuelezea namna nzima na dhumuni la safari ile na katuelewa na kuomba namba za simu za wenyeji wetu ili awapigie kuwajulisha kama tumefika kwa kuwa sisi wote simu zetu za mkononi zilizuiliwa kupiga simu kabisa na kwa bahati nzuri akapiga simu na hatimaye kuwapata waandaaji na kuongea nao na kutupa jibu kuwa hawako mbali na tukae chini tupumzike na kweli baada ya dakika zipatazo tatu wakaja wale waandaaji wakiwa wamebeba bango limeandikwa “guinness football challenge� na ndipo hapo nikapata nafasi ya kumshukuru yule askari polisi kwa msaada wake japokuwa ni wajibu wake,hatimaye safari ikaanza ya kwenda katika hoteli tutakayofikia huko Midrand conference centre na eneo linaitwa Midrand na kwa kweli sikuwa nafahamu umbali halisi kutoka uwanja wa ndege mpaka midrand japokuwa kwa makadirio yaweza kuwa ni kama km 15 na muda ni kama dakika 30 mpaka kufika na tukiwa njiani tuliona mambo mengi ya kupendeza kuanzia majengo na kivutio kikubwa kilikuwa magari ya kisasa na barabara kubwa kubwa za njia sita au six ways na fly overs nyingi mno na pia kingine hakukuwa na traffic lights au humps nyingi katika barabara yaani ni moja kwa moja mpaka gari inaweza kutembea speed 120km/h kwa uzuri wa miundo


mbinu na kwa mwendo wa takribani nusu saa tukafanikiwa kufika hapo midrand na kukaribishwa na kukutana na ile timu ya kenya ikiwa imeshafika na kupewa vyumba na kuanza kupumzika na hapo ndipo na sisi kutoka tanzania na uchovu mkubwa tuliokuwa nao tukapewa vyumba na mimi nilikuwa chumba kimoja na team mate wangu kwa jina la Gullam Mikidadi au Sosha fundi wa mpira au mzee wa ndondo na baada ya kukabidhiwa funguo ndipo tukaenda moja kwa moja kujionea na kukuta chumba kizuri sana kikiwa na vitanda viwili,meza kuubwa,tv set yenye kingamuzi cha dstv na kama walijua tunapenda mpira basi yaani furaha ikazidi,choo na bafu vizuri,kiyoyozi kizuri sana,kabati zuri la kuhifadhia nguo na ndipo hapo nikaanza kutoa nguo zangu kwenye begi na kuanza kuzipanga kwenye kabati lile na hatimaye kuingia bafuni na kuoga ili kupunguza uchovu lakini sikupata maji ya moto na baridi lilianza kuwa kali kwa kuwa ilikuwa ishafika saa nane mchana lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kuoga na huku njaa ikiuma na baada ya kumaliza kuoga nikabadili nguo na kuvaa sueta na pensi na sandals ili nitoke nje kutazama mazingira huku nikingoja chakula kije tupate kula na bila kusahau usiku huo kulikuwa na mechi kali kati ya manchester united na liverpool iliokuwa ikitarajiwa kuanza saa 12 jioni majira ya afrika kusini pia watu wengi hasa tuliokuwa pale tulikuwa na hamu na shauku kubwa ya kutaka kutazama ile mechi ili kujua nani mbabe kati ya miamba hiyo miwili na bila shaka nikatoka kuonana na vijana au washiriki wengine kutoka Kenya na Uganda na kuanza kubadilishana mawazo juu ya mpira na hali za nchi zao kimichezo hasa mpira na kukuta vijana wenzangu wakiongea lugha tofauti na niliyozoea yaani wakawa wakisema kiingereza japokuwa si kwamba mimi sifahamu lugha hiyo ya mama mdogo yaani ya malkia la hasha lakini mazingira yangu si ya kuzungumza sana kiingereza japo na mimi nikaamua kujigeuza muingereza kwa kuanza kuongea kiingereza mara kwa mara kiasi cha kuanza kusahau kiswahili..hahahaha natania tu siwezi kusahau lugha ya mama yangu hata siku moja lakini mazingira humbadilisha mtu wakati mwingine japokuwa haikuwa rahisi kwangu kusahau lugha yangu hata chembe na kwa wakati huo ikafika saa 11


jioni kikaletwa chakula na ilikuwa ugali na kuku yaani kinyumbani kabisa kwa kuwa mazoea watanzania wengi mchana tunakula ugali japo watu wengi pale midland walilalamika kwani chakula kilichelewa sana na ukiachilia mbali kula muda huo pia ikifika saa 1 usiku chakula cha usiku au dinner itakuwa tayari kwa ajili ya kuliwa na ndipo wasimamizi wetu au chaperone wakasema hivyo vyakula vya usiku kila mtu atapewa chake aende nacho chumbani kwake ili ale saa yoyote akipenda na sio lazima muda ule na upate kukila chakula chako so muda wa mpira kuanza ukafika na baadhi ya watu wakaanza kuweka dau au kucheza kamali au bet kama wazungu wanavyoita ambapo pia vijana wengi huko nyumbani tanzania wameathiriwa na tabia ya bet au michezo ya kubashiri hasa game za mpira wa miguu huko barani ulaya kwa ujumla na mechi ikaanza kwa ushindani mkubwa sana hata hivyo ilipofika half time mimi nikazidiwa na uchovu na kwenda kulala hata mpira sikuumaliza na nikagundua wengi wetu tulikuwa na uchovu mwingi sana kiasi cha hata kutotaka kupiga story siku hiyo,baada ya mpira kuisha majira ya saa 2 usiku tukaitwa katika dinning hall kusikiliza juu ya mambo kadhaa ya kufanya kwa wakati wote tukiwa hapo hotelini na katika shindano lenyewe ndipo maelekezo yakaanza kutolewa na mtu mmoja ambaye anaitwa Trevor Mojela moja kati ya watu ambao nilipata kuwa nao karibu sana kwa siku za mbeleni kwa kuwa alikuwa akipenda kupiga story na kila mtu ambae alikuwa akihitaji kupiga story na tulikuwa karibu kiasi cha kuarrange sherehe ya siku yangu ya kuzaliwa na hata siku ya kwenda shopping tulinunua vitu sawa kama perfume na baadhi ya vitu vya mchumba wangu alivyoagiza,na baada ya kupewa maelekezo yoote kuwa kuanzia kesho asubuhi basi litakuja kutufuata na kutupeleka sehemu moja ikiitwa Alexandra na huko ndiko iliko studio inayoitwa Q STUDIOS ambayo inatumiwa na kampuni ya ENDEMOL kufanya shooting ya shindano zima la guinness football challenge na pia maelezo mengine kuwa muda mwingi tutatumia studio na hata chakula cha mchana tutakuwa tunakula huko studio na baada ya maelezo kuisha na baadhi ya maswali kuulizwa kuhusu shindano hatimaye kila mtu akapewa nafasi ya kwenda kulala ikiwa imefika majira ya saa 3 usiku na


kusema ukweli nilikuwa nasikia baridi na uchovu mwingi kiasi cha kushindwa kujizuia na kwenda kulala mpaka asubuhi ilipotimia na niliona usiku mfupi sana kwa utamu wa usingizi nilioupata. Ilipofika asubuhi ya tarehe 14/01/2013 yaani siku ya pili baada ya kutua jozi(johannesburg) niliamshwa mapema sana majira ya saa kumi na mbili na team mate wangu Gullam Sosha kwani hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza ya mashindano na ilipaswa tuamke mapema ili tupate muda mzuri wa kujiandaa na kwenda kupata breakfast katika dinning hall na kama kawaida nilikuta washiriki wengine wakiwa tayari washafika na kuanza kujipatia kifungua kinywa na niliposogea kwenye meza ya vyakula nilistaajabu sana kwa kukuta vyakula vya aina nyingi sana na vinginevyo sikuwahi hata kuviona au kuwahi kuvila na nilijitahidi kuchagua vyakula ninavyovifahamu tu kwa kuogopa kuaibika na mfumo wa kuchukua vyakula ulikuwa ni self service yaani unajihudumia chochote utakacho na baada ya kujisevia nikaenda kwenye meza moja kuubwa waliokaa washiriki wenzangu kutoka Tanzania na ama kwa hakika meza hiyo ilikuwa imejaa furaha sana kwa utani,vicheko na kila namna ya vioja na kuweka utofauti kati yetu na timu zingne zoote,baada ya kumaliza kupata breakfast mara anakuja chaperone mmoja na kutuambia basi limefika so tunahitajika kwenda kupanda na baada ya muda mchache washiriki wote tukawa tumepanda tayari kwa kuanza safari ya kwenda huko Alexandra kwenye studio inayoitwa Q STUDIOS na wakati tupo njiani kuelekea huko Alexandra tulipata fursa ya kujionea magari ya kifahari na majumba mazuri ya kupendeza machoni kwako na kujikuta saa zote ukishangaa hovyo lakini pia ilikuwa wakati mzuri wa kushangaa uzuri wa barabara na baada ya mwendo mfupi tu tukajikuta tunaingia kwenye geti kubwa na kuambiwa hapa ndio studio so tuvae vitambulisho wakati wote tutakaokuwa eneo lile na wengi wetu tulitii amri ile na kushuka kwenye basi na kuingia ndani na kuanza kutembezwa ndani ya eneo hilo na kujionea michezo mingi kama sehemu ya kupumzisha akili na miongoni mwa michezo hiyo ni roberto,table tennis na television kubwa yenye kingamuzi cha dstv kwa ajili ya kutazama matukio mbali mbali ya


michezo inayoendelea duniani kwa ujumla.Siku hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya rehearsal yaani kufanya mazoezi juu ya kile tutakachokuwa tunakifanya mapema baada ya mashindano kuanza na tulipata fursa ya kujionea washiriki kutoka TANZANIA,KENYA NA UGANDA wakipambana kama vile ilikuwa ndio siku ya shindano na kwa kweli tulianza kuona ugumu na kupata picha juu ya mashindano halisi yatakavyokuwa na baada ya saa kama tatu za mazoezi ndipo tukaenda mapumziko na kupata chakula cha mchana yaani lunch na baada ya lunch kuisha tukarejea tena katika studio na kuendelea na mazoezi na mpaka ilipofika saa kumi jioni ikawa ndio mwisho wa rehearsal kwa siku ya kwanza na kuanza safari ya kurejea MIDRAND tulipofikia na kwa muda huo magari yalikuwa mengi barabarani kwani watu wengi walikuwa wakitoka makazini so dereva hakuwa akienda mwendo mkubwa sana na kutufanya tuenjoy zaidi kwa kuwa tulipata fursa ya kuona vitu vingi zaidi na baada ya mwendo flani hivi tukafika hotelini na uchovu kiasi kwani hali ya hewa ilikuwa ni ya baridi na ni tofauti na dar tunapotoka ambapo kuna joto kali sana,tulifika majira ya saa kumi na moja na muda huo tulianza kuona vyakula vikiandaliwa kwa ajili ya mlo wa usiku na ilipotimu saa moja usiku tukaitwa kwenda kula chakula cha usiku na kama kawaida watanzania tulikuwa na meza yetu maalumu tuliojiandalia na kwa wakati wote tulikuwa tunakula huku stori na utani vikitawala katika eneo lile utandhani tupo nyumbani japokuwa tupo katika nchi ya watu tena mbali sana na kuanza kuona washiriki kutoka nchi nyingine wakianza kutamani mazingira tunayoishi sisi watanzania na kuanza kuulizana eti sisi tumetokea eneo moja?sisi tukawa tukicheka tu kwa kuwa tulikuwa tuna umoja na amani sana baina yetu utadhani ndugu wa baba mmoja au toka familia moja lakini ukweli ni kwamba kila mmoja wetu ametokea mazingira tofauti,tukapata mgeni katika meza yetu toka mombasa Kenya anaitwa Saddam au Awadhi akaja kujiunga nasi kwani alikuwa akizungumza kiswahili kizuri sana na baada ya kumdadisi kumbe ana asili ya zanzibar kwa hiyo nae alikuwa akijihisi kama kakutana na nduguze nasi tukampokea na kuanza kushirikiana nae katika mambo tofauti ndani ya


shindano lile mpaka tukawa tukienda chumbani kwake au yeye kuja vyumbani kwetu kwa nia ya kuzungumza tu,baada ya mlo wa usiku na baada ya story kiasi basi kila mmoja akaelekea kitandani kwake kwa ajili ya kujipumzisha ili kupata nafasi ya kufikiria juu ya siku inayofuata yaani siku ya pili ya rehearsal. Ikaingia siku mpya nayo ni asubuhi ya tarehe 15/01/2013 iikuwa siku ya jumanne na baridi lilikuwa kali mno siku hiyo kiasi cha kuamka na sueta zito kabisa na baada ya kuoga na kuvaa nguo zangu nzuri na mimi nikajongea dinning hall kupata breakfast na washiriki wenzangu na kwa bahati nzuri nikaanza kujifunza salamu kwa lugha za makabila ya south afrika na mfano ni lugha ya kizulu na kitswana na waliokuwa wakinifunza ni baadhi ya wahudumu wa hoteli ile ambao walikuwa wakarimu sana kwangu na kwa washiriki wote katika hoteli ile na baada ya kupakua vyakula navyotaka kula na kwa siku hiyo nilijaribu kula vyakula ambavyo sikuwahi kula na vilikuwa na ladha nzuri kinyume na matarajio yangu na nilienjoy sana asubuhi hii kwa kula vyakula vingi sana tofauti na jana kwani nadhani ugeni pia ulichangia na baada ya kumaliza kula ikatimu saa moja na dakika zake kadhaa na kupanda kwenye lile basi la kisasa aina ya marcopolo lenye uwezo wa kubeba watu 70 kwa wakati mmoja na baada ya washiriki wote kupanda katika basi safari ilianza tena ya kuelekea Alexandra kwenye studio zile ambazo shindano hufanyika na asubuhi hiyo tulipita njia tofauti na ile tuliopita jana na kujionea tena mambo mapya ikiwemo treni ya umeme yenye kwenda kasi sana kupita maelezo pia niliona msikiti kubwa sana kiasi cha kuvutiwa na kuupiga picha ili nipate kuwaonyesha ndugu na jamaa zangu waislamu ili kuona maendeleo ya waislamu wengine duniani na licha ya hivyo pia nikaona magari mapya ya kifahari yakikatisha huku na kule,punde tu tukafika katika studio ile na kwa siku ile ya pili ya mazoezi au rehearsal ndio siku ya mwisho ya mazoezi na kila kilichokuwa kikitaraji kufanyika siku hiyo ya pili ni uhalisia zaidi wa show itakavyokuwa kwa hiyo hata mavazi na umakini ulikuwa mkubwa hata sisi washiriki wengine hatukupewa nafasi ya kuingia studio na kuwa sehemu ya washangiliaji na badala yake tukaishia


kuketi kwenye chumba kimoja chenye viti vizuri na masofa na televisheni kuubwa ambayo ilkuwa ikionyesha kila kilichokuwa kikiendelea kule studio na huo ndio utakuwa utaratibu baada ya mashindano kuanza yaani kesho yake hatutapata fursa ya kuingia katika studio kama sio mshiriki kwa siku hiyo na badala yake utakuwa ukitazama kwenye tv tu japokuwa ilikuwa na uhalisia kiasi cha kuhisi na wewe upo mule ndani na baada ya kufika saa sita za mchana ukafika wakati wa lunch time na kujipatia vyakula vya aina tofauti huku tukipooza koo kwa juice,kahawa,maziwa na soda kubwa sana ili mradi tu kila mtu nafsi yake ifurahi na baada ya kumaliza kula tukarejea tena katika tv kupata kushuhudia kile kitakachokuwa kikiendelea pale studio na baada ya saa kadhaa kupita ikafika jioni na rehearsal kuisha na baada ya mazoezi kuisha tukapata fursa ya kutangaziwa timu zitakazoanza kuchuana hiyo siku ya kesho na kwa upande wa TANZANIA ilikuwa ni zamu ya AKIDA MWALIMU NA DANNY MSEKWA ambao walionyesha kujiamni sana wakati wa rehearsal kwa siku zote mbili na hiyo kesho ilikuwa ndio siku yao ya kuonyesha umwamba wao katika masuala ya soka kwa ujumla na baada ya kupewa majina ndipo tukaanza safari ya kurejea tena huko Midrand kwenye hotel na kiasi cha nusu saa tukajikuta tukifika salama katika eneo lile tulivu na lenye mandhari nzuri sana na kwa kuwa siku hiyo tulirejea mapema basi nikaamua kutumia wakati ule wa jioni kutembela baadhi ya maeneo ya hotel ile na kupiga picha kadhaa na kwa hakika zilipendeza sana picha zile kwa muonekano na kushuhudia ndege wazuri wakiimba majira yale ya jioni na jua kwa mbali likipotea na kushuhudia mataa yakianza kulipamba jiji lile la Johannesburg kwani mahali nilipokuwa ni kwa juu kiasi cha kuweza kuona mji mzima ukipendeza na kuvutia kwa mataa ya kila aina na kwa kuwa giza lilingia nikaamua kuelekea dinning hall na kukuta wenzangu wakiwa tayari washafika hapo kwa ajili ya kuchukua vyakula na kuanza kula na mimi pia nikapata nafasi ya kupakua vyakula ninavyohitaji kula,wakati tukiendelea kula mara yakaanza maongezi juu ya siku ya kesho itakavyokuwa na huku wengi tukipeana moyo juu ya siku ya kesho


kuwa watanzania tutashine katika mashindano yale kwa kuwa ari ilikuwa kubwa na uwezo wetu ulikuwa mkubwa pia so haikuwa tatizo sana na baada ya mashauriano kadhaa basi tukaitana katika chumba changu kwa kuwa mimi ndiyo nilikuwa kiongozi na baada ya kumaliza kula kila mmoja alikuja chumbani kwangu na kuanza kuwapiga msasa kina danny na akida juu ya maswali na namna ya kupata ushindi pia kuwaombea dua ili wafanye vyema na waamke na afya nzuri sana kwa ajili ya kushindana na baada ya maombi na dua tukapeana mikono na kila mmoja kaenda kwake chumbani kwa ajili ya kujipumzisha ili kesho apate kuamka mapema kujiandaa ili asije kuachwa na basi na hatimaye kutolewa katika shindano kama ilivyoelezwa hapo awali na waandaaji wa shindano lile. Niliamka mapema sana siku hiyo kwani ndiyo ilikuwa siku ya shindano lenyewe,ilikuwa siku ya jumatano ya tarehe 16/01/2013 na baada ya kuoga na kujiandaa nikamuasha mshiriki mwenzangu Sosha na kumwambia ajiandae na kuwa kushakucha na makucha yake na yeye pia kaenda kujiandaa na kabla hatujatoka akaja mshiriki mwenzetu kwa jina la Kheri kuja kutuamsha na kukuta tayari tushaamka na yote hii ni sababu shindano ndiyo linaanza na siku ile basi lilitaraji kuondoka mapema ili kuwahi kufika katika studio,baada ya kumaliza kujiandaa tukaenda sote kupata breakfast na kukaa pamoja na washindani wa siku hiyo Danny na Akida na kujaribu kuwapa moyo ili wapate kutulia na kufanya vyema na kwa kuwatazama walikuwa na hofu sana kiasi cha kushindwa kula vizuri na hata kupiga story kama ilivyo kawaida yao tukiwa katika meza ile au kilinge cha vijana wa kitanzania wenye furaha saa zote.Baada ya kumaliza kula basi likiwa lishafika nje ya geti mara washiriki tukaanza kupanda na baada ya chaperone kuhakiki uwepo wa kila mshiriki aliruhusu basi lianze safari ya kwenda Alexandra eneo ambalo kuna Q STUDIOS mahali kutakapofanyika shindano lile na baada ya mwendo wa dakika chache tukapita barabara kuu na kuingia ndani ya jengo la studio na baada ya kushuka timu ya Tanzania tukazungusha kiduara na kufanya maombi kwa ajili ya vijana wenzetu watakaopambana siku hiyo na baada ya maombi kuisha na kuwatakia


kila la kheri mara wakachukuliwa na kupelekwa katika dressing room na kupewa mavazi maalum yatakayokuwa yakitumika na washiriki kutoka Tanzania walipewa jezi za blue na trouser nyeusi,Kenya walipewa jezi nyekundu,nyeusi na trouser nyeusi,Uganda walipewa jezi za kijani na trouser nyeusi ili kuwapamba na kuwatofautisha wakiwa katika shindano na punde wakaingia studio ili kuanza kupambana na ghafla tukaanza kusikia kelele zikitokea nje toka katika chumba tulichokuwepo sisi washiriki ambao siku zetu za kupambana hazijafika na kutoka nje tukakutana na kundi kuubwa la vijana kumbe wale vijana ni watanzania wanaoishi kule South Africa na wengi wao wanatokea Pretoria walikuja na basi kwa ajili ya kushangilia na kuongeza ladha katika shindano lile na punde eneo lile likajaa furaha na kelele nyingi kwani baadhi ya washiriki walipata kuonana na majirani zao au jamaa zao na kubadilishana experience za maisha na muda walioishi katika nchi ile ya Afrika Kusini na baada ya dakika chache za kusalimiana wakaja kuitwa ili waingie studio ili zoezi zima la shindano lianze na baada ya dakika kupita tu tukaanza kuona katika televishen katika chumba kile maalum kwa ajili ya kutazama kinachoendelea ndani ya studio na tukiwa na hamu kubwa ya kuona shindano mara washiriki wakaanza kuingia katika studio tayari kwa kuanza shindano na punde shindano likaanza kwa round ya kwanza na timu kutoka Kenya ikaongoza,round ya pili ikaingia timu kutoka Tanzania ikaongoza,na ilipofika round ya tatu ikaongoza timu kutoka Kenya na baada ya hapo tukaenda mapumziko na kupata chakula cha mchana na bila shaka Danny na Akida walikuwa wakiendelea vizuri sana katika kupambana na kutetea nafasi yao ya kuibuka washindi na baada ya kumaliza kula lunch,shindano likaendelea tena kwa kuingia round ya nne na hatimaye washiriki toka Tanzania kufanikiwa kufika katika money wall na kupata kitita kizuri cha pesa na kwa kweli walistahili kwani walionyesha uwezo mkubwa sana siku ile na kwa juhudi zao wakatufanya hata sie tunaofuata kuwa na furaha na kujiamini na baada ya siku ile kuisha walipotoka nje ya studio tuliwapongeza sana na hata safari ya kurejea hotelini basi zima lilijaa kelele za watanzania kwani


shangwe ndiyo desturi yetu na kuwaacha washiriki wengine kimya kwa muda mpaka kufika hotelini na hata ulipofika wakati wa mlo wa usiku hali iliendelea kuwa ya furaha sana katika meza yetu kwa kila mtanzania na baada ya kumaliza kula tulijumuika tena chumbani kwangu kwa ajili ya kupiga maombi na dua na kupigana msasa kuhusu masuala ya soka na siku ya kesho ilikuwa zamu ya vijana wawili wenye vipaji vikubwa sana yaani IMA TEMU na SIMON MAESTRO ambao kwa bahati nzuri ni majirani huko Dar na wanafahamiana kwa ukaribu sana kiasi cha kuwapa kujiamini mno kwani kila mmoja anamuamini mwenzie katika kile anachokifanya kwa namna yake na baada ya maombi kumalizika basi kila mmoja alipata fursa ya kurejea katika chumba chake na kutuacha mimi na Sosha tukijadiliana mambo kadhaa juu ya shindano lile na tukiwa hatuna wasiwasi hata zamu yetu itakapofika,baada ya maongezi yale tukajikuta usingizi mzito na kuaga tayari kwa kupata kulala ili kesho panapo majaaliwa tukaone watanzania wenzetu wakipeperusha vyema bendera. Asubuhi mwanana na tulivu ilifika na ikatimu siku ya alhamisi ya tarehe 17/01/2013 na siku hiyo ilkuwa siku ya pili baada ya mashindano yale kuanza na jana yake baada ya kuwashuhudia kina Danny wakifanya vizuri basi leo ni zamu ya vijana wawili wengine toka maeneo ya jet karibu kabisa na uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK nyerere,si wengine bali ni IMA TEMU na SIMON MAESTRO wakitaraji kufanya mambo makubwa sana na punde baada ya mimi na washiriki wengine kuamka na kupata breakfast ya nguvu tukapanda basi na kuelekea katika Q STUDIO huko Alexandra na wakati tupo njiani siku hiyo kulikuwa na mvua kiasi jua halionekani kabisa yaani na baada ya mwendo fulani mrefu kwani siku hiyo magari yalikuwa mengi na hata mwendo haukuwa wa kasi sana sababu ya mvua na hatimaye tulifika pale studio salama na baada ya kushuka tukapiga maombi kama ilivyokuwa kawaida yetu na baada ya shindano kuanza tu tukaanza kuona vijana wa kitanzania wakijitahidi kujibu maswali kwa ufasaha katika round ya kwanza na hatimaye kufika round ya pili ndipo wakaanza kufanya vibaya mno kiasi cha kushindwa hata kuingiza mpira


mmoja katika nyavu na hivyo kutolewa katika mashindano mapema kinyume na matarajio ya wengi,zikabaki timu za kenya mbili na kuchuana kiasi na hatimaye timu moja kutoka kenya ikapata kufika katika money wall na kujivunia kiasi cha pesa kizuri tu na baada ya siku hiyo kuisha hofu ikaanza kutanda miongoni mwa timu zilizobaki kwani mashindano yalianza kuonekana magumu kwa upande fulani na hata wakati tupo njiani kuelekea hotelini huko MIDRAND tukitokea Q STUDIO ndani ya basi kulitawala ukimya mwingi sana kwani watanzania tulirudi vichwa chini kiasi cha kuwapa hofu hata washiriki wenzetu toka Kenya na Uganda na pia waganda wametoka mikono mitupu katika siku zote mbili,baada ya kufika hotel tulipata chakula cha usiku na kuelekea katika chumba changu ambapo kulikuwa na dua na maombi za kupigana msasa kama ilivyo ada na baada ya kumaliza nilihitaji muda mwingi wa kukaa peke yangu kwani kesho ndiyo ilikuwa siku yangu ya kupambana na pia kibaya zaidi nilipata maumivu ya tumbo na kuhara kiasi kwa saa kadhaa nadhani ilikuwa hofu tu na nilitaraji itakapofika asubuhi basi hali itakuwa nzuri na nilichofanya ni kuwapigia simu wazazi wangu kuwaeleza kuwa kesho ndiyo siku napambana so waniombee dua nifanikiwe na walinitakia kila kheri na hatimaye kupata nafasi ya kulala japo huku nikiwaza hali itakuwaje lakini mwenzangu SOSHA hakuwa na wasiwasi hata kidogo huku akinipa moyo kuwa tutafanya poa na ananiamini sana kwa juhudi zangu na tukaamua kulala ili tuamke mapema zaidi na baada ya kuagana tukalala. Niliamka mapema sana siku hii ya leo ya tarehe 18/01/2013 siku ya ijumaa kwani ilikuwa siku muhimu sana katika maisha yangu na ndio ilikuwa na umuhimu mno katika siku zote nitakazokaa hapa Johannesburg South Africa na bila shaka hii ndio siku nilikuwa na shauku nayo sana na baada ya kuamka na kuomba dua njema baada ya kutoka kitandani nikaenda zangu bafuni kuoga na sikutumia muda mwingi kama ilivyo kawaida yangu na badala yake muda mwingi niliutumia kuwaza na nikaoga haraka na kutoka ili kumpa nafasi mwenzangu Gullam Sosha na yeye kwenda kuoga mapema ili tupate


kujiandaa mapema kama unavyojua leo ndio mwali anatoka,baada ya kujiandaa tukaelekea dinning hall na kuwa miongoni mwa washiriki wa kwanza kupata breakfast na kwa umaarufu aliokuwa nao Sosha kwa muda mfupi tu tuliokaa pale hotel basi kila mtu alijua kama leo ni zamu yangu na Sosha kupeperusha bendera ya Tanzania na kusema kweli mambo yalikwenda vizuri mpaka tumemaliza kupata breakfast na hapo ndipo tukapata kupanda basi kwani muda wa kuondoka ukafika yaani siku hii ya leo naona kama muda unakwenda sana kiasi cha kila jambo nikawa naona linaenda haraka na hata breakfast sikuwa nimekula sana kama ilivyo kawaida yangu si unajua presha nying lakini moyoni nikawa nasema all is well and I am going to make it to the best. Tukafika salama hapo Q STUDIOS na kuzunguka kiduara na kupiga maombi na dua kama utaratibu wetu wa kila siku na baada ya kumaliza mamombi tukaenda moja kwa moja dressing room kubadili mavazi na kuvaa mavazi rasmi kwa ajili ya kupambana kwa kuvalia tisheti ya blue na trouser ya black na kwa hakika tulipendeza sana mimi na team mate wangu SOSHA na pamoja na timu zingine pia zilipendeza na kila mmoja alikuwa na hamu ya kutaka kuona tutafanya nini?Kweli tukaingia ndani katika studio tukiwa na furaha sana na hatimaye kukuta watu wengi sana yaani washangiliaji na wengi wao walikuwa wakimfahamu sosha kwa kuwa yeye ni mtoto wa kitaa na ashapiga ndondo nyingi sana mitaa tofauti na ukiachilia mbali umaarufu wake ndani ya hotel ile pale MIDRAND na hatimaye tukaanza kuingia kwa shangwe na kukaa katika podium kwa kujiamini huku kukiwa na camera zaidi ya 12 na watu ni wengi,kelele nyingi sana kiasi cha kukosa kujiamini kama ni muoga wa kuona camera mbele yako pia na mara ghafla likapulizwa vuvuzela flani kumaanisha shindano linaanza na likaulizwa swali la kwanza na kwa ajabu kabisa nikalijibu swali lile na kupata na SOSHA akapewa mpira apige kwa mfumo wa penalty na hatimaye kumfunga yule mystery goalkeeper na kujishindia 1000$ kwa hakika tulifurahi sana,round ya kwanza ikaanza na kushika nafasi ya tatu kwa timu yangu,round ya pili timu yetu ikashika nafasi ya kwanza,round ya tatu tukashika nafasi ya kwanza pia na baada ya hapo


zikabaki timu mbili tu yaani timu yangu na wakenya flani na kwa wakati huo ilikuwa imefika saa sita mchana na tayari kupata lunch au chakula cha mchana kama ilivyo kawaida na hapo ndipo nilipopata nafasi ya kuonana na washiriki wengine na kupewa hongera na matumaini mengi kwa uwezo tulioonyesha mimi na SOSHA na hata baada ya hapo tulipata kula na sikula kwa raha sababu ya presha ya shindano na chakula kilipoisha tukaja kuitwa tena ili kwenda kumalizia ungwe ya mwisho na tukaingia na kupewa gloves mimi na kuwa kama goalkeeper na punde tu nikasogea langoni na swali nikaanza kuulizwa nikapata na kupewa mpira GULLAM akamfunga yule kipa wa timu pinzani na hata hivyo mambo yaliendelea kuwa mazuri kila hatua japo ilifika kipindi nikaanza kukosa maswali bila kujijua na hatimaye mpaka muda unaisha timu yangu ikawa imeingiza mipira michache golini kwa wapinzani wetu na kuwapa nafasi ya kwenda kwenye money wall na kupata kitita kizuri cha pesa na kutuwacha mimi na SOSHA tukishangaa japo haikuuma sana kwani tumepata hata kitita cha kufutia machozi kusema kweli mashindano yalikuwa mazuri sana siku hiyo japokuwa hatukushinda.Baada ya kutoka nje ya studio watu wengi walitupa pole na kutupa moyo lakini hatukujutia kwa kile tulichofanya kwani tumekufa kijerumani na tai shingoni,maandalizi ya kurudi hotel yakaanza na hatimaye kufika hotel salama salmini na siku hiyo nilikuwa nimechoka sana na sikupata muda mwingi wa kukaa na watu na badala yake nilikula chakula cha usiku kwa haraka na kuingia kitandani mapema sana na baada ya hapo nikaanza kupakumbuka nyumbani kwetu,ndugu zangu na kitanda changu nyumbani. Siku hii ya nne tangu mashindano yameanza,ilikuwa jumamosi ya tarehe 19/01/2013 na siku hii ilikuwa nafasi nyingine kwa watanzania kuonyesha ukali wao na ikiwezekana kufuta matokeo mabaya tunayopata au tuliopata baada ya siku ya kwanza na leo ndiyo zamu ya vijana wawili hawa wanaocheza soka katika kituo kimoja cha soka jijini dar es salaam kinachomilikiwa na jeshi la kujenga taifa yaani JKT kinachoitwa TWALIPO SOCCER ACADEMY na hawa wana vipaji vikubwa sana na si wengine bali ni LUKWESA na HAMZA,tukapata


breakfast na baada ya hapo tukaondoka kuelekea studio kama ilivyo kawaida na katika washindani wa leo yaani Hamza alikuwa kijana mwenye kupenda kulalamika na kupenda utani kupitiliza halafu ni mwepesi sana kukasirika kupita maelezo japo hiyo tabia ndiyo ilimpa umaarufu sana katika kambi ile na baada ya kutua salama katika eneo la Alexandra kwenye Q STUDIOS na wao kina Hamza kwenda moja kwa moja dressing room na kubadili mavazi yao kwa ajili ya kuingia studio tayari kwa kuanza mashindano na walikuwa na furaha sana na kwa wakati huo mimi nipo zangu kwenye sofa kubwa na glass yangu ya juice nikingoja kuona vijana wakichuana wakati jana muda kama huo nami nilikuwa ndani ya studio nikipambana na kutazamwa na wenzangu. Shindano likaanza ni washiriki toka tanzania walionyesha umakini mkubwa na kupita katika round ya kwanza salama na kufika round ya pili mabapo hapo ndipo kulikuwa na ugumu kiasi na hatimaye kujikuta wakitupwa nje na kulia sana na kukosa raha japo haikuwa bahati yao hawa ndugu zangu wa kitanzania na kuwaacha wakenya wakifanya vizuri na kushinda kwa siku ya tatu mfululizo na kuwaacha waganda bila timu moja iliyofanya vizuri na kuanza kulalamika kuwa wakenya wamekuwa wakipendelewa na kuzua utata kiasi cha mashindano kusimama na kuitwa wadau wote ili mambo yawekwe sawa na hatimaye yakafankiwa na shindano kuendelea kama ilivyopangwa na mwishowe ikashuhudiwa wakenya wakishinda tena na baada ya kumalizika kwa shindano siku hiyo na kushuhudia kila mmoja wetu akipatiwa gift card ili kwenda kufanya shopping siku ya kesho yake jumapili kwani ndio ilichaguliwa maalumu kwa ajili ya kutembezwa katikati ya jiji la Johannesburg hasa katika kitongoji cha SOWETO kwenye uwanja mkubwa wa SOCCER CITY ambapo kwa wakati huo kulikuwa na mashindano ya AFCON yakiendelea kutimua vumbi so kwa wakati huo nchi hiyo ilikuwa imefurika wageni kwa ajili ya soka tu,baadae jioni tukarejea hotelini na siku hiyo niliamua kwenda kuogelea katika swimming pool japo sio mpenzi sana wa kuogelea kwa kuwa sina ujuzi mwingi japo natamani nifahamu kuogelea vyema na hapo ndipo nikakutana na Saddam na kuanza kunifundisha japo kichwa changu


kilikuwa kigumu kuelewa na kufanikiwa kujifunza kidogo katika vingi nilivyofundishwa na baada ya muda nikatoka na kwenda kuoga ili kwenda kupata chakula cha usiku na hata baada ya kula nikapata muda mzuri wa kuzungumza na washiriki wengine toka kenya na uganda na hata wenyeji wetu wa afrika kusini kwa kuzungumza mambo tofauti yanayohusu maisha na mpira kiasi,muda ulikuwa ukienda sana siku hiyo na sikuwa nikisikia usingizi na nilipiga story sana siku hiyo na ilipofika saa sita usiku nikaenda kulala kwani mwili ulikuwa umechoka mno na kwenda kulala ili kungoja asubuhi. Siku ya jumapili ilitimu na siku hiyo ya tarehe 20/01/2013 ndiyo ilikuwa siku ya kwenda kushangaa jiji na kwa maneno ya GODFREY mmoja kati ya chaperone aliniambia siku kama ya leo matajiri wengi huyatoa magari yao ya kifahari sana ambayo hawayatumii mara nyingi kutokana na msongamano wa magari au mafuta mengi yanayotumiwa na magari hayo na hali ya hewa ilikuwa nzuri sababu ya mvua kuwa inanyesha na kulikuwa na baridi kiasi,baada ya kuoga maji ya moto na kwenda kunywa chai nikaitafuta list ya vitu nilivyoagizwa na ndugu na jamaa pia mchumba wangu alitaka vitu vizuri vya kujipamba na baada ya watu wote kupata mlo wa asubuhi tukajiunga pamoja katika basi na siku hiyo tulikuwa na wasimamizi wengi kiasi ili kuhakikisha usalama wetu na baada ya mwendo mrefu sana na kupita sehemu tofauti tofauti tena ambazo hatujawah kupita nikawa najionea uzuri wa mji na mitaa yake na mazingira pia na tukajikuta tumefika katika sehemu inaitwa GREEN STONE SHOPPING CENTRE na mahali hapa kuna maduka ya kila aina na yanauza vitu vingi mno na kabla ya kushuka katika basi tulipewa onyo kali tusifanye any attemp of cheating or fraud or stealing sababu kuna cctv cameras kila sehemu zinazoona kila mtu na kila tukio na hatimaye kuachiwa kuanza kuzunguka na wakati nipo katika mizunguko niliona vitu vingi vizuri japo sikuweza kununua vitu vyoote japo vingi nilinunua nilivyoagizwa japo nilitumia pesa zangu mwenyewe kwa ajili ya kuwafurahisha wale ninaowapenda na kwa muda mwingi nimezunguka na kupata mahitaji yangu yote niliyotaka na kurudi kwenye basi ili kurudi tena hotelini kupumzika na hata hivyo


hatukuweza tena kwenda soccer city kwani barabara zilikuwa zimefungwa kupisha mechi ya Ghana iliokuwa ikichezwa jioni ya siku hiyo na kutunyima fursa hiyo adimu so tukarudi hotel na kupata nafasi ya kuangalia nilivyonunua na kwa hakika vitu vizuri na vitapendwa na ninaowapelekea,ikafika jioni nikapata chakula safi na kwenda kulala mapema kama ilivyo kawaida sababu mvua ilikuwa ikinyesha na nilikuwa nangoja sana kwa hamu kesho ifike ili nimuone kijana wangu ABUU ambae ndiye sababu ya mimi kuwa pale kwa muda ule. Tarehe 21/01/2013 ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya mashindano na pia ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kukaa katika hoteli ile na jiji lile la Johannesburg dah! Ilikuwa siku nzuri sana kwani kila kilichofanyika kilikuwa kizuri kwa kuwa hatutarudi tena katika hoteli ile isipokuwa kina DANNY na AKIDA ambao wamepata nafasi ya kurudi tena katika PAN AFRICAN ili kupambana zaidi na washindi wengine,asubuhi ile ilikuwa poa sana hata hali ya hewa ilikuwa tamu mno kiasi cha kunitamanisha kuendelea kubaki lakini nyumbani Tanzania nimeacha mambo mengi ya msingi yakiwemo masomo yangu ya chuo kikuu na ukizingatia ni mwaka wangu wa mwisho chuoni pia kuna family yangu nzuri na kikubwa mchumba wangu ninaempenda sana akiningoja kwa hamu kuubwa ukizingatia hajaniona kwa masiku tele. Nilipata breakfast kwa utulivu na siku hiyo nilikula sana kwani ni siku ya mwisho kula vizuri kiasi kile na baada ya kumaliza kula tukangoja kidogo na kupanda katika basi ili kuelekea studio ili kupata kushuhudia kijana wangu ABUU na KHERI wakitetea nafasi zao kwa siku hiyo kwani timu za Tanzania zilishindwa kutamba na kuwacha Kenya ikitawala katika hatua zote,baada ya kubadili mavazi na kuingia katika studio na kuanza kupambana sana kwa ajili ya kutetea nafasi na round ya kwanza ilipita na hatimaye kuingia round ya pili mpaka ya tatu na ya nne,ilipofika round ya nne walitolewa lakini kishujaa sana hata hivyo walijitahidi na kuwapa nafasi wakenya kwenda kwenye money wall na kupata kiasi kikubwa cha pesa na washindi wa siku hiyo kulikuwa na jamaa akiitwa Papaa huyu ni mjanja sana sijapata kuona mkenya mjanja kama huyu jamaa.Nakumbuka siku hiyo ndiyo ilikuwa closing day na


washiriki wote tulipata nafasi ya kupiga picha na waandaaji na washiriki wengine tayari kwa safari ya kurejea nyumbani na kuwa sehemu ya kumbukumbu ile kwani hapo baadaye show hiyo itaruka live katika television za Afrika Mashariki ili wananchi wapate kuona kilichojiri huko South Afrika na baada ya zoezi hilo la kupiga picha tukaanza kuagana na wapiga picha na wengineo walioko katika production crew na mungu akipenda tutaonana wakati mwingine,hatimaye kupanda basi na kurejea hoteli na majira hayo ilikuwa saa kumi na moja jioni kwa majira ya afrika kusini na usiku wake washiriki kutoka Tanzania tulikuwa tukitaraji kusafiri kurejea zetu bongo Dar es salaam na siku hiyo chakula cha usiku kilipikwa mapema na kwenda kula ili kuwahi ndege ili tusije kuchelewa na kuharibu mipango ya watu na nilikwenda kujiandaa na kuvaa shati langu zuri na sueta langu zuri la kupendeza na kujitia manukato na kuanza kupanga vitu vyangu katika mabegi yangu mawili makubwa yaliyokuwa yamejaa zawadi na baada ya muda yaani ilipofika saa mbili nikawa tayari nimejiandaa na kwenda kuagana na vijana wengine ambao wanatoka Kenya na Uganda na kubadilishana namba za simu pia account za facebook na twitter ili kurahisisha mawasiliano na mara tukatangaziwa ya kuwa basi lipo tayari kutuchukua na kutepelekaa uwanja wa ndege kwani ndege ilikuwa ikiondoka saa sita usiku ya jumanne itakuwa imeingia ya tarehe 22/01/2013 na wakati tunatoa mabegi yetu kupeleka kwenye basi nikawa natazama kwa uzuri eneo lile kwani itabaki kumbukumbu kichwani kwangu kwa mengi mazuri niliyoyapata kule ikiwemo siku yangu ya kuzaliwa kunikuta nikiwa kule na baadaye nilidumbukizwa katika pool la maji na kufanikiwa kuokolewa na Steven Mkenya huyu alinicheka sana baada ya kunitoa katika maji hata hivyo sikumlaumu mtu kwani ni sehemu ya shamra shamra za siku yangu ya kuzaliwa. Basi likaondoka na tayari kwenda airport ili kufanya process za kurejea home na hatimaye tukafika salama majira ya saa tatu usiku na kutoa mabegi yetu na kuagana na baadhi ya chaperones kwa kubadilishana namba za simu na emails na hatimaye kuingia ndani ya kiwanja na kwenda kudai kodi zetu tulizotumia lakini


kwa bahati mbaya walikuwa wamefunga na muda umeisha dah! ilituuma sana lakini ndiyo hivyo tena mambo ya nchi za watu na kutoka hapo kwenda kwenye counter za Kenya airways na kupatiwa boardinga pass na mizigo yetu kupimwa na kufungwa ili kuwekwa kwenye ndege na baada ya zoezi hilo kukamilika tukaagana na TREVOR MOJELA ambaye alikuwa mtu wangu wa karibu sana na kumshukuru sana kwa wema wake na kunipa no yake ya simu kama sehemu ya mawasiliano na hata hivyo tukapeana hug na kuingia ndani ya kiwanja kwa ajili ya kwenda kukaguliwa na kuingia uhamiaji na kugongewa visa ya kutoka na kwenda sehemu ya kungoja ndege na pia alitokea afisa mmoja wa uhamiaji akiwa anafahamu kiswahili kidogo akaanza kuchombeza maneno ya kiswahili baada ya kujua kuwa sisi tunatokea Tanzania na tulifurahi sana kuona kiswahili kinakubalika mpaka wageni wanajifunza na kusogea kwenye passenger lounge ili kusubiri ndege ya kurudi tz,tukangoja kwa muda wa saa mbili na hali ilikuwa ya baridi sana kwa muda huo na mimi nikiwa ndani ya sueta kubwa sikuwa na wasiwasi sana na mara ndege ikawasili na sisi kuanza kupanda kwenye ndege ile kwa haraka na ilipotimu saa sita na nusu safari ikaanza na ndege iliporuka na kuanza kuona taratibu tukiliacha jiji zuri la jozi kwa mataa yake mazuri na kumbukumbu nyingi zikibaki akilini na baada ya dakika kadhaa nikachukua blanket langu na kujifunika mpaka katikati ya usiku nikaamshwa kupewa chakula na baada ya hapo nikalala sana mpaka nilipoamshwa kuwa ndege inakaribia kutua NAIROBI, KENYA katika uwanja wa Jomo Kenyatta international airport na baada ya dakika chache tukatua katika ardhi ya Kenya salama salmini na wakati huo ilikuwa saa 11 alfajiri na sehemu hiyo ilikuwa na baridi sana kwa wakati huo na tukaenda moja kwa moja katika passenger lounge kungoja transfer ya kwenda DAR ES SALAAM, TANZANIA ni ilituchukua saa tatu kukaa katika uwanja huo wa ndege na nikiwa nimekaa katika moja ya siti nikiwa nimejifunika hood langu na kuweka head phones masikioni ndipo nikakutana na mzee mmoja wa kiarabu akidai anatokea London, UK kwa shughuli zake na kuanza kuniongelesha kiingereza akidhani mimi sifahamu kiswahili na ndipo


nikaanza kufunguka kiswahili tena cha mtaani ndipo akapata kufahamu na hapo ni kama nimemfungulia kwani aliongea sana tena mambo ya kipuuzi na matusi tele na kibaya zaidi alikuwa akinywa pombe na isitoshe kunikaribisha mimi na baadhi ya washiriki wenzangu soda za kopo alizoshuka nazo kwenye ndege na kwa story zake alisababisha tutake kuchelewa ndege mpaka kuanza kutangazwa majina yetu na kufanya haraka sana na kupanda katika basi na kupelekwa ndani ya ndege na punde tu ndege ilipojaa abiria ikaanza kuondoka kuelekea dar na kwa siku hiyo niliienjoy sana wakati nipo angani nikapata kuona Mlima Kilimanjaro kwa mbali pia kushuhudia filamu na kusikiliza muziki katika ndege kwa kuwa nilikuwa sina uchovu na nina hamu ya kufika nyumbani,ndani ya saa moja tukawa tumefika katika ardi ya Dar es salaam na kutua salama salmini na kumaliza process zote za uhamiaji na hatimaye kutoka nje ya uwanja na kukutana na dada Regina na babu kwa pamoja wakatuchukua na kuanza kuturejesha majumbani kwetu na hatimaye kupelekwa mpaka ubungo na kufika nyumbani kwa mara ya kwanza na kukutana na ndugu zangu na wazazi wangu na kwa hakika walifurahi sana kuniona na kuwaelezea mambo mazuri niliyoyaona na kuanza kugawa zawadi kwa wote niliowanunulia na kwa hakika ilikuwa nafasi nzuri kwangu kujifunza maisha na NAWASHUKURU SANA WOTE WALIOFANIKISHA SAFARI HII KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NA NINGEPENDA NIWATAJE KWA MAJINA LAKINI SITAMALIZA. -END-

A tour to johannesburg  

Guinness Football Challenge change my entire life.....

A tour to johannesburg  

Guinness Football Challenge change my entire life.....

Advertisement