Andrew Natsios, Mkurugenzi wa USAID wakati wa Utawala wa George W Bush, aligundua neon jipya “ Dhidi ya urasimu” – hiyo ni mifumu ya kirasimuna idara ambazo kusudi lake pekee ni kuhakikisha utiifu na kuwezesha upimaji wa mafanikio. Jukumu la awali la mifumo hii si kufanikisha mambo, bali kupunguza hatari. Hailengi kuwa mifumo ya kujifunza, wala haiazimii kuhakikisha maendeleo endelevu. Anajenga hoja kuwa USAID inakuwa haina ufanisi sana kwasababu ya mifumo hii.
‘Zile program za maendeleo ambazo ni sahihi na zinapimika kwa urahisi ni zile zenye mabadiliko madogo, na zile program ambazo zina mabadiliko sana ni zile zisizopimika kwa urahisi” Andrew Natsios
Uwezo wa kupimika (au uwajibikaji) haulingani na ufanisi wa maendeleo. Natsios anatoa mfano wa programu ya utoaji huduma wa dola billioni moja, mradi wa Malaria wa Bush. Mradi uliweza kufanikisha kile ulichobuniwa kukifanya: kupunguza viwango vya maambuzi. Lakini viwango hivi vidogo viliendelea kwasababu programu ilipuuzia maendeleo ya mashirika na taasisi wenyeji ili kuzitosheleza wakati wa baadae. Bila taasisi na mashirika ya ndani, jitihada za namna hii huwa zinakufa mara ufadhili unapokoma au kupungua, ingawa zilikidhi malengo yao yanayopimika. Michakato ya maendeleo ya mijadala ya sera na mageuzi, pamoja na usaidizi kwa taasisi na mashirika ya ndani kwa kawaida huwa na mafanio zaidi kuliko utoaji wa huduma. Hata hivyo, mafanikio yao, ambayo mara nyingi ni viwango si rahisi kuyapima kwa muda mfupi na hayawezi kuchangiwa moja kwa moja katika muda mrefu. USAID sio shirika pekee la kitaifa ambalo linazidi kukwazwa na urasimu. Ni ukweli kuhusu mashirika mengi ya kitaifa na mashirika mengi ya maendeleo ya kimataifa. Wanazijibu serikali ambazo zinajibu madai yanayokubalika ya walipa kodi kuonyesha kuwa zinatumia pesa vizuri. Lakini mashirika mengi ya maendeleo ya kitaifa yanatoa bajezi zake kubwa kwa mashirika mengine ya ndani naya kimataifa katika sura sura ya ruzuku. Madhara ya mtandao ni mfumo wa ripoti nyingi na zenye kuchukua muda mwingi ngazi hizo za juu hadi kuchukua muda mwingi wa ngazi ya chini jumuiya. Athari gani hii inazo katika kujifunza?
SURA YA 6: Matoleo ya dhati: utendaji wa wafadhili na kujifunza
79