BFG2: Mwongozo mguu peku wa desturi za kujifunza katika mashirika na katika mabadiliko ya kijamii

Page 26

Kujaribu kuibua ramani au picha ya utendaji wenu katika kikundi:

Before opening up for group conversations it is always useful to give people a little time to collect their thoughts, to think about what they want to say.

1. Kila mmoja aeleze nini hasa wanafanya . Toa muda kwa watu kujiandaa na zoezi hili( iwe mtu mmoja mmoja au kama timu). Watu wasimuliane kwa undani kuhusu za kazi zao za kawaida, hususani kazi ambayo imekwisha kamilika 2. Wakati maelezo yanapotolewa , wengine wanapaswa kusikiliza kwa makini , huku wakijiuliza maswali kadhaa akilini mwao, kwa mfano : Mabadiliko au utofauti unafanyika wapi? Ni mchango gani unatolewa hapa? Ni mahitaji gani ya msingi yanatimizwa ? Ni kazi gani inayotiliwa maanani zaidi? Kazi hii inafanyika vipi Ni nguvu gani inaendesha mchakato? 3. Baada ya mtu mmoja mmoja kukusanya mawazo yake , wanakikundi wanaweza sasa kutafakari ni jambo kati ya yale waliyosikia wameona ni la msingi, nini kilivuta hisia zao. 4. Ndiposa , hatua hii inaweza kuchochea majadiliano yanayo pelekea kutafuta majibu ya maswali yafuatayo: Kwa hiyo kimsingi tunafanya nini hasa – Kazi yetu halisi ni ipi hapa? Tunajali mambo gani? Hii inamaanisha nini kwa utendaji wetu kwa siku za zijazo? Zoezi hili linaweza kufanywa na kila mfanyakazi, kwa njia hii picha ya utendaji wa shirika hujengeka.Kuna njia nyingi mbalimbali za kufanya zoezi hili. Tungeweza kuwaomba watu kadhaa kuandaa mawasilisho na kukaribisha maswali na kuibua majadiliano. Tungeweza kutumia mchakato unaojulikana kama world café tembelea tovuti ili kubaini mahusiano mbalimbali na kazi tunayofanya. 5. Sasa tazama ni wapi pa kuelekeza nguvu zako katika kujifunza –Picha zilizo ibuka za utendaji wako , zitakusaidia kuamua ni wapi pa kuweka mkazo. Pengine unataka kuendelea kutoa maelezo ili kupata uelewa wa kina wa kazi mnayo fanya . Yamkini umebaini kuwa unahitaji kuwa wazi zaidi kuhusu mahitaji unayojaribu kutimiza na kutafakari kwa kina kuhusu madhumuni yako. Labda zoezi hili limedhihirisha haja ya kujenga ujuzi fulani ambao unakosekana.

18

WWW.BAREFOOTGUIDE.ORG


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.