BFG2: Mwongozo mguu peku wa desturi za kujifunza katika mashirika na katika mabadiliko ya kijamii

Page 142

Kutumia vielelezo katika kuelekea kujifahamu Kujichunguza, kubaini nini fikra , hisia pamoja na mashaka uliyo nayo. Kuweka kumbukumbu pamoja na kuelewa historia yako binafsi , haya ni mambo halisi tunayoweza kufanya kila wakati , kila mara. Hatuhitaji kutumia zana , vielelezo au nyezo ili kuweza kujifahamu. Ingawaje , vielelezo au zana zinaweza kusaidia kwa kiasi fulani. Katika aya ifuatayo tumependekeza vielelezo viwili tunavyo penda sana, lakini viko vielelezo vingine vingi vyenye kufaa pia. Angalizo moja kuhusu vielelezo :- Kutumia kielelezo ni kama kutazama ukweli wenye muonekano wa pande tatu kwa kutumia kifaa chenye kuweza kuona pande mbili. Kielelezo ni zana tu ya kutazamia ukweli au hali halisi na kutoa lughu moja ya kuzungumzia ukweli huo – Zana yenyewe sio ukweli tunao utafuta. Kwa mfano endapo utabaini kuwa staili yako ya kujifunza ni ile ya kinadharia , haina maana kuwa ni lazima ujitambue kama: mimi ni mnadharia. Ni hatari zaidi pale watu wanapo kuelezea kwa kusema wewe ni mnadharia. Wanadamu hawapendi kuwekewa mipaka. Hivyo tusitumie vielelezo kuwa wekea mipaka, ila vielelezo vitumike katika kuonesha mwelekeo wa ukuaji pamoja na maendeleo. Kwa kuwa nimebaini kuwa ninajifunza kwa staili ya mnadharia , sasa naweza kujaribu kutafuta na kutumia staili nyingine za kujifunza , na hivyo kuboresha mwenendo wangu. Na endapo utagundua kwa mtu mwingine anatumia staili ya mwanaharakati , unaweza kujaribu kumshawishi na kumsaidia kwa njia nzuri ili aweze kutumia staili nyingine. Usimkosoe au kurekebisha tabia fulani alizonazo, hali hii haipelekei kujifunza na mara nyingi husababisha upinzani.

‘

Kielelezo ni kizuri sio kwa majibu kinachotoa lakini ni pale kinapo tuwezesha kujiuliza maswali bora.

’

182

Kielelezo kizuri kinafaa sio kwa sababu ya majibu kinachotoa lakini ni pale kielelezo hicho kinapo tuwezesha kujiuliza maswali mazuri. Vielelezo ni hatari endapo tutavitumia kupata majawabuKatika maisha kila hali ni ya kipekee na vielelezo haviwezi kutoa majibu kwa maswali yote. Kwa muktadha wa mwongozo huu kuhusu kujifunza, pengine kielelezo cha staili za kujifunza ni mojawapo ya kitu cha kwanza kutazama. Katika sura ya 12 , yenye kichwa kisemacho tunajifunza kwa njia gani. Unaweza kupata ufafanuzi wa staili kadhaa. Ukurasa 36 wa mwongozo wa kwanza wa mguu peku unatupatia utangulizi , ufafanuzi wa kina pamoja na dhana kuhusu jinsi ya kutumia kielelezo cha silika nne. Katika ukurasa unaofuata tutakuelezea kielelezo cha mienendo ya mwanadamu na sifa za muhimu.

WWW.BAREFOOTGUIDE.ORG


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.