Barefoot Guide 1 Kiswahili

Page 69

Lugha na tamaduni Uhusiano unaweza kukwamishwa au kuvunjika kwa sababu ndogo tu ya kutokuelewana. Uwezekano wa hali hii kutokea, huweza kuongezeka endapo tamaduni zetu ni tofauti. Ni muhimu kufahamu endapo kuna maana tofauti kwa maneno sawa katika tamaduni mbalimbali. Lugha ya mwili pia ni muhimu na jinsi ambavyo mambo hufanyika katika tamaduni tofauti. Umbali baina ya mtu na mtu wakati wamesimama na kuongea hutofautiana kulingana na tamaduni mbalimbali. Kusimama karibu sana au mbali sana na mtu kunaweza kutafsiriwa kwa namna tofauti tofauti kulingana na tamadumi husika. Katika nchi nyingine unaweza moja kwa moja kuanza kuongelea mada husika , lakini nchi nyingi zenye desturi za kitamaduni , kwa mfano , kama hutatumia mlolongo mrefu wa salamu , hoja na mapendekezo unazotoa zinaweza zisisikilizwe.

Usikivu makini Ni lini mara ya mwisho ulihisi umesikilizwa vizuri? Aina ya usikivu mbapo msikilizaji alikuwa hakushutumu au kutoa ushauri haraka haraka na alikuwa anamaanisha kuhitaji kusikia ulichotaka kusema, bila ajenda nyingine yeyote zaidi ya kutaka haswa kuelewa na kukusaidia.

RUBES ANAYO NYINGINE KWA AJILI YETU .... Nakumbuka katika tafrija moja , nilikutana na mtu ambaye hatujaonana kwa muda mrefu. Kama kawaida katika sherehe watu hufanya mazungumzo mepesi na kuzunguka zunguka kukutana na watu mbalimbali. Huyu rafiki yangu, alikuwa amepandishwa cheo muda sio mrefu, na kupewa nafasi ambayo ilikuwa na majukumu mengi zaidi na ilionekana wazi kuwa jamaa alikuwa amefurahia lakini pia alikuwa na hofu kuhusu nafasi hiyo mpya. Mazungumzo yetu yangeweza kufuata mielekeo miwili. Kwanza kazi yake ilinivutia sana na pia nilikuwa na uzoefu mzuri nayo. Kirahisi tu ningeweza kutawala mazungumzo na kumpa ushauri mzuri na kujigamba kwa uzoefu wangu katika nafasi kama hiyo. Lakini mwisho wa siku mazungumzo yetu yangeishia hapo na kila mmoja wetu kuendelea na mambo yake. Nikaamua kuchukua njia nyingine. Kwa kweli nilijitahidi sana kutulia na kumsikiliza kwa makini na kuzuia hisia ,mawazo na uzoefu wangu. Nilimuuliza maswali mara moja moja sana. Jamaa aliendelea kuongea , na kwa namna fulani nilianza kuvutiwa na tabia yangu ya usikivu. Licha ya kelele za watu wengine katika tafrija ile, mazungumzo yetu yalikwenda ndani kwa kiwango kikubwa na hata akafika hatua ya kuanza kujiuliza maswali , na kupata mbinu za kukabiliana na changamoto ya kimahusiano na mmoja wa wafanyakazi wake . Ndipo nikaweza kuanza kumpa mapendekezo kadhaa ambayo pengine aliyaona ya msingi au la. Tuliachana katika hali ya kuridhika kwa kukutana tena na rafiki yangu na tulitamani kukutana tena siku nyingine . Nilirudi nyumbani kwa furaha kuwa nimekutana na rafiki yangu wa zamani pia kujisikia vizuri kwamba niliweza kutoa mchango wangu katika mchakato wa maendeleo wa rafiki yangu – kwa kusikiliza kwa makini tu.

“Mahusiano yanaweza kuvunjika kwa kupishana kidogo tu. ”

KWA MAARIFA ZAIDI USISAHAU TOVUTI YETU: www.barefootguide.org

Kujaribu kwa dhati (na kwa nia) kusikiliza kunaweza kuwa ni jambo la maana kubwa na ni njia ya haraka ya kujenga mahusiano mazuri na watu wengine sambamba na kutuwezesha kujenga mahusiano mazuri na nafsi zetu wenyewe. SURA YA TATU: WATU NA WATU

61


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.