Barefoot Guide 1 Kiswahili

Page 168

KUPANGUSA VUMBI KATIKA MBINU YA KUJIFUNZA KUPITIA UZOEFU WA WENGINE Mbinu ya kujifunza kupitia uzoefu wa wengine ni nini na inahusiana vipi na aina nyingine za kujifunza? Tayari tulishaiangalia mbinu ya kujifunza kwa kutenda hapo awali.Ni kama zinakaribiana mengi tuliyoyasema kuhusu kujifunza kwa matendo ni ya kweli pia kwa upande wa kujifunza kupitia uzoefu wa wengine. Hakika, kujifunza kupitia jirani zetu na marafiki zetu ni mbinu ya kiasili na kongwe ya kujifunza kama ilivyo mbinu ya kujifunza kwa kutenda. Dhana ya kujifunza kwa kutenda pamoja na kujifunza kwa kupitia wengine kwa kawaida zinafungamana, mchakato ule ule – kaka yangu alinifundisha jinsi ya kurekebisha gata yake iliyoharibika , mkulima anamwelekeza jirani yake mbinu aliyotumia kudhibiti viwavi jeshi au mfanyakazi anamsimulia mwenzie jinsi walivyojipanga wakati alipokuwa katika kiwanda kingine ili kupata faida za madawa. Hii yote ni mifano ya mbinu zote mbili za kujifunza yaani kujifunza kupitia wengine na kujifunza kwa kutenda. Elimu ilipoingia katika mfumo wa walimu, wataalamu, madaktari, Wauguzi, wanasheria na maafisa ugani wa kilimo n.k – kwa watu wengi kama sehemu ya utawala wa kikoloni, matokeo ilikuwa kwamba imani waliyokuwa nayo watu kuhusu thamani ya uzoefu wao na uzoefu wa jirani zao pamoja na maarifa , fikra vilidharauliwa. Desturi na kanuni za kujifunza kutoka kwa wengine, kujifunza kwa pamoja, maarifa ya jamii zinakuwa zimezikwa nusu, na utegemezi wa kujifunza kupita wataalamu katika vizazi vichache vya zamani unaendelea kuimarishwa na jamii ya sasa. Ujuzi na kujifunza vimekuwa ni bidhaa za nje, na kuendelea kuondoshwa kwa kiasi kikubwa katika mifumo ya asili ya maisha ya jamii huku ikiwanyang’anya watu sio tu haki yao ya msingi ya kupata ujuzi na uwezo wao lakini pia kudhoofisha mahusiano ya kutegemeana yaliyodumu miaka mingi miongoni mwa wana jamii. Kurejesha au kujenga upya tamaduni na kanuni za mbinu za kujifunza kupitia watu wengine sambamba na kujifunza kwa kutenda vinakuwa msingi wa utendaji wa kimaendeleo, msingi wa kusudi au lengo.

“Kujifunza kupitia watu wengine kama ilivyo kujifunza kwa kutenda , ni mchakato wa kiasili wa kujifunza ambao tunaweza kuambatanisha na mabadiliko.” 160

Hii si kusema kuwa walimu na wataalamu hawana kazi muhimu. Mara nyingi wana uzoefu pamoja na maarifa ambavyo vyote vina nafasi muhimu katika kujifunza na ingekuwa ujinga kujinyima fursa hizi. Wanaweza kuleta ufafanuzi wa dhana wa thamani kubwa zaidi ya ule ulipo katika makundi ya marafiki tunayojifunza nayo. Kitu muhimu ni kujua muda gani na kwa jinsi gani utaalamu husika uletwe. Maarifa mapya yafanafaa kuletwa wakati tu maarifa na uzoefu walionao watu umeibuliwa, ili kwamba maarifa mapya au ufahamu wa kitaalamu uweze kuchangia na kupanua yale ambayo watu tayari wanafahamu, kuliko kupuuzia, na kukana au kubadilisha maarifa ya watu, kama inavyofanyika mara nyingi. Wazee katika jamuiya wana wajibu katika mchakato wa kujifunza kwa kuwa mahusiano yao na wale wanaowafundisha pamoja na muktadha mara nyingi ni wa karibu na wenye ugumu mchanganyiko. Kama wanajumuiya wa kutoka jumuiya moja, wanashirikiana vipengele vingi vya uhusiano wa kirafiki kama watu walioko ndani. WWW.BAREFOOTGUIDE.ORG


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.