Barefoot Guide 1 Kiswahili

Page 139

ATHALI ZA SILIKA Katika sura ya pili tulielezea silika nne. Kila silika huleta changamoto na michango fulani katika michakato ya mabadiliko: •

Silika ya moto mara nyingi haina subira kwa mabadiliko, na iko radhi kuthubutu. Hali hii inaweza kuleta hamasa nzuri kwenye mchakato wa mabadiliko lakini pia inaweza kuhatarisha zoezi zima endapo hatari ni kubwa sana.

Silika ya maji mara nyingi itapokea mabadiliko, ila inaweza kusita na hata kuonekana kama inapinga. Inawezekana kuwa wanasubiri muda muafaka kuchukua hatua, hutafuta njia rahisi ya kutokea.

Silika ya hewa inapenda mabadiliko na inaleta hali ya matumaini bila kutafakari sana ni kwa namna gani au kwa nini mabadiliko yanahitajika. Hali hii ikizidi kupita kiasi inaweza kuwa na hatari sana, lakini watu wenye wingi wa silika hii wanachangia matumaini na mtazamo chanya unaohitajika sana katika mchakato.

Silika ya Dunia hupokea mabadiliko kwa tahadhali na inahitaji kushawishiwa sana. Wanaweza kutoa mtazamo hasi kwa kiasi kikubwa lakini mashaka yao mara nyingi hutafsiriwa vibaya kama ukinzani hasi. Yamkini wameona vikwazo na wana maswali muhimu ya kuyazingatia ambayo yangeweza kuepusha shida nyingi mbeleni.

Kila sauti ina kitu cha kuchangia. Kama kiongozi au mwezeshaji unapofanya kazi na kundi la watu wa aina mbalimbali, inakupasa kutarajia, kuhamasisha na kuheshimu kila moja ya sauti hizo. Endapo hazijitokezi zenyewe, angalia kama unaweza kuzichimbua. Toa fursa kwa wasio na uvumilivu, wenye mashaka pamoja na wenye shauku kusikika.

KUTOKA UTEMEGEMEZI KUELEKEA KUJITEGEMEA Baada ya muda yamkini watu watataka kusimamia mchakato wa mabadiliko wao wenyewe pasipo wawezeshaji. Hii inaweza kuwa ishara kwamba kama wawezeshaji tumefanikiwa. Inaweza kuwa kwamba ‘’tukio’’ la mabadiliko limefanya kazi ya kutosha na kuwa watu wanaweza kuuendeleza mchakato wao wenyewe bila uongozi au uwezeshaji zaidi. Lakini inawezekana kuwa ingawa wamepata mwelekeo mpya na ujasiri, wanaweza kusumbuka katika utekelezaji wa mabadiliko waliyobainisha endapo watakosa msaada wa aina fulani. Tumebaini kuwa mara mafanikio muhimu yanapopatikana, mashirika huachana nasi sisi kama wawezeshaji wao, kama vile kazi kubwa na muhimu imekwishafanyika, na hutafuta njia zao wenyewe kutekeleza maamuzi yaliyotokana na zoezi tuliloliendesha. Mara nyingine bado kuna masuala ya gharama lakini tunajiuliza kama wametosheka na msaada wetu na kiongozi anataka kurudi katika nafasi yake ya kuongoza.

SURA YA SITA: Kutafuta makazi ya mabadiliko

131


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.