Barefoot Guide 1 Kiswahili

Page 102

Katika uzoefu wetu ni mashirika machache sana yana ufahamu kuhusu mbinu yao ya msingi wanayotumia katika jitihada za kuleta mabadiliko. Matokeo yake kazi hufanyika kiholela na bila kuleta faida yoyote (katika hatua za mwanzo za ukuaji wa shirika, hili si tatizo kubwa, kwa kuwa shirika liko katika kipindi cha kufanya majaribio ya kazi zao.) Kufuatia uhitaji wa kuonesha mantiki ya miradi kama wanavyodai wahisani mashirika mengi yanajikuta yakichukua kusudi lao la msingi na kulikata vipande vipande ili kulingana na malengo na shughuli tofauti zisizo na uhusiano. (Kwa mfano bao mantiki) wakiamini kuwa vipengele hivi vikijumlishwa pamoja vitapelekea kutimiza lengo kuu la shirika. Mara nyingine endapo mazingira ya mabadiliko ni rahisi na yanayoweza kutabirika (Kama ilivyoelezewa katika sura ya 1 ukurasa wa 20) mfumo huu unaweza kufanya kazi vizuri. Lakini katika kazi nyingi za maendeleo utumiaji wa mfumo huu utahatarisha shirika kufanya kazi zilizogawanyika gawanyika ambazo mwisho wa siku hazina uhusiano na wala hazipelekei kuibua fursa mpya. Kutenga muda kila mara wa kufanya tafakari ya kina kuhusu kusudi, mbinu na mkakati wa shirika, huweza kuleta uhai halisi na uelewa wa kina katika utendaji kazi wa shirika. Hapa ndipo mfumo makini wa upangaji, ufuatiliaji na tathmini unapohitajika sana. Kuwa makini na kufahamu ni wapi kazi halisi ya shirika ilipo, unaweza kuepuka shughuli zisizo na mpangilio, na hivyo kuokoa muda mwingi, rasilimali na kuepuka matatizo yaliyoko mbele.

5. Shughuli, uwezo na rasilimali za program Kipengele hiki kina jumuisha kazi dhahiri zaidi za shirika. Pindi kusudi linapokuwa bayana, na pindi mbinu ya utendaji kazi pamoja na mkakati wa shirika zinapoainishwa, kipengele hiki cha mzunguko wa maisha ya shirika (asasi) huchukua jukumu la kutengeneza shughuli na kwa kupitia shughuli hizi mkakati wa programu utatekelezwa. Wakati huo huo, kipengele hiki huhamasisha uwezo wa rasilimali watu, kama vile ujuzi, mbinu na ufundi unaohitajika katika kutekeleza shughuli za mradi. Katika kipengele hiki pia kuna rasilimali vitu pamoja na mifumo ya utawala inayohitajika kusaidia utekelezaji wa program ofisini na nje ya ofisi.

6. Kujenga na kusimamia utendaji (ikijumuisha mizunguko ya kujifunza kwa vitendo – kupanga, kufuatilia na tathmini) Hebu tazama tena mchoro wa vipengele na mzunguko wa shirika. Utagundua kuwa kipengele hiki kinaungana na vipengele vingine vyote kupitia mizunguko ya kupanga, kufuatilia na tathmini. Mizunguko hii ni kama mzunguko wa damu katika mwili, ambao daima hulisha shirika ili liweze kujihuisha mara kwa mara na kuendelea kukua. Kipengele hiki pia kinawakilisha usimamizi wa vipengele vingine kupitia michakato ya kujifunza na kupitia mifumo na kanuni – kusimamia rasilimali watu, utendaji na kusimamia rasilimali za shirika. Kujifunza kwa vitendo ni msemo unaotumika kuelezea mzunguko endelevu wa kujifunza ili kuboresha kazi za shirika. Mashirika yote hujifunza na kutafakari kadri yanavyoendelea na kazi, kwa kujua au bila kujua, lakini mashirika makini hutenga muda wa mara kwa mara wa kujifunza.

94

WWW.BAREFOOTGUIDE.ORG


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.