Skip to main content

CFCS VIII KUHAIRISHWA HADI MEI 2023

Page 1

KUHAIRISHWA KWA CFCS VIII! 14 hadi 19 Mei 2023


CHANGING FACES CHANGING SPACES Kwa Jamii na Washirika wetu, Mwaka uliopita tuliwaandikia habari za kusisimua kuwa tungeandaa CFCS VIII mwezi wa Oktoba 2022. Kama mjuavyo nyote, CFCS lilibuniwa kwa moyo wa badiliko la sura na badiliko katika fursa miongoni mwa mavuguvugu yetu na jamii zetu zote zikiwemo ndani ya jamii zetu tunamoishi. Kusikiliza kwetu katika UHAI ni Tendo la Kisiasa na tumekuwa tukisikiliza na baada ya kuzingatia kwa makini, tumeamua kuahirisha tarehe ya Kongamano la 8 la Changing Faces Changing Spaces linalofuata hadi 14-19 Mei 2023. Sasa katika mzunguko wake wa nane, kongamano hili, ambalo lilifanyika mwanzo katika 2007, na kutuumba, kama mfuko wa kwanza wa Uanarakati wa kiasilia wa kiafrika, unaendela kuhudumu kama jukwaa la harakati za mfanyakazi wa ngono na LGBTIQ+ wa Kiafrika na marafiki wao ili kujadili, kupanga mikakati na kubadilishana uzoefu ambao unaathiri harakati za jamii zetu. Kutokana na usuli wake wa kiuanaharakati na kuendelea kujitolea kwetu katika uongozi wa kiuanaharakati, CFCS kama nafasi ya harakati, inaendelea kutayarishwa na harakazi zilezile zilizoianzisha. Jopokazi la CFCS ambalo litaundwa na wanachama wa jamii zetu, litakuwa na wanachama wote kabla ya 31 Mei 2022. Tungependa kumshukuru kila mmoja ambaye alichukua muda wake wa kutuma ombi ili ajumuishwe katika jopokazi. Kama ilivyo desturi, tunathamini maoni yako na tunakualika kushiriki nasi maoni yako kuhusu yale ambayo ungependa kuona kama badiliko la sura na badiliko katika fursa ili tuweze kuunda kwa pamoja CFCS VIII ambalo linaleta taswira yako, jamii zetu na lile ambalo linazungumzia maisha halisi tuliyoisha. Tafadhali tufikia kupitia cfcs@uhai-eashri.org Kwa Upendo wa kimapinduzi Dkt. Stellah Wairimu Bosire na Mukami Marete


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
CFCS VIII KUHAIRISHWA HADI MEI 2023 by UHAI Communications - Issuu