Page 1

NOT FOR SALE


hapo awali kilicho-happen na boyie...

‌na gang ili-arrest-iwa juu ya ku-disrupt rally... Boyie amwacha Dede aki-decide kama atajoin gang au kusaidia mamake‌

police station

boyie

mlishika jamaa anaitwa dede jana?

‌ na sasa Boyie anasumbuka ilimfika nini Dede...

wewe kijana, kaa mbali na wahalifu kama hao.

hakuna mtu na jina kama hiyo hapa.

lakini dede, kwani kumeendaje? haiya, hakuna mtu anachukua!

hakuna jibu. namba inaenda kwa mteja...

nani sasa atatutoa hapa, jo? yenyewe hatungewaamini na hizo pesa zao!

2

wametutumia!


dede! chapo zako zinatoka za round vipoa!

vipi boyie? umeshapiga kura? niliishia mapema juu niweze kurudi home nisaidie kina mathe hapa!

kweli! niliambia bwanangu atusaidie kwa hoteli pia badala ya kuwa kwa gang.

nafurahi sana kijana wetu amechagua kutusaidia kazi hapa. otherwise, angekua jela leo.

na Nimepata chance ya kutengeneza dooh bila stress!

bro wangu alikubali kunisaidia kuuza mboga zenye tulipanda.

inaonekana kuna njia zingine za kuepuka ghasia. lazima ni-share na vijanaa!

3


vipi ma-fans! beste yangu ameni-show story poa leo! ati PAL yake alifikiria kujiunga na gang fulani lakini akaamua kusaidia mathake na job instead.

akapata njia ya kutengeneza chapaa bila violence!

ma-youth, kuna njia poa ya kujijenga kuliko ma-gangs na hazikuwangi mbali!

tuwe GANGare!

4

Kuna choices zingine unaweza kumake badala ya ku-join gang! Ebu cheki kundi ya wamathe ‘The Kibera Women for Peace and Fairness’. Hawa wamathe walikuja pamoja baada ya noma ya post election. Wakasahau tofauti zao na kuamua kufikiria kama Wakenya. Hawa wamathe waliita mavijanaa ambao walikuwa kwa ma-gangs na kuwa-show watie zii maisha ya zamani waangalie future ilio na maisha ya amani. Wamama

waliunda vikundi za members kutoka makabila different, kama team ya foota, ambapo members wanafanya job pamoja kama team sio kama kabila. KWPF wanasema “Tunahimiza watu wahakikishe wame -vote kulingana na vile wanaamini ndani yao. Usilazimishwe na mtu kuchagua wanavyotaka. Kila mtu ana haki ya ku-vote anavyotaka bila kufurahisha mwingine”

Waweza kusoma zaidi kuhusu KWPF kwa website yetu….www.shujaaz.fm


hapo awalI...

Ex-prefects walipo-complain juu ya vile shule ina-run-iwa na School Council...

…Principal aliwaambia students wa-decide system wanayotaka…

…Both sides zika-present maoni yao, kisha students waka-vote...

Na sasa nitasoma matokeo ya kura…

Kura nyingi ni za…

…School council!

Chekini! Tulijua tutashinda! Yaay! 5


Nyinyi ma-cops mlidhani mtatushinda? Losers!

Hey! Tafadhali tujaribu kuelewana … Jameni! Hatufai kuchokozana! Si poa.

Nyinyi ni ma-students hapa chuoni kama sisi. Mna haki ya kupeana opinion zenu…

6

… na kutu-advise vipi twaweza-make chuo kuwa better. Hatufai ku-worry nani ameshinda ama ameshindwa...

… Tukifanya job pamoja, sote tunakuwa washindi!


Yenyewe hapo umebonda idea kali.…

Kama side yenye una-support inashindwa kwa kura haimaanishi eti all is lost. Each side huwanga na positive sides zake na each side inaweza benefit kila mtu. Hebu tusiwe na mentality ya lazima tushinde au sivyo kutakuwa kubaya sababu italeta chuki na mwishowe ni wachache wata-benefit. Ni bora kuwa na mentality ya ku-benefit pamoja ili tuweze kupeana opinions zetu vizuri na kushirikiana na wenzetu na kuleta maisha poa.

Poa! Tukutane kesho basi ku-discuss hizi issues…?

Mentality ya ku-benefit pamoja inamaanisha: Kutofikiria ‘ubinafsi’, ‘dhidi yao’, lakini kufikiria kuhusu ‘sisi pamoja’. Kusikiza na kuheshimu viewpoints za wengine. Kuheshimu tofauti za wenzetu. Kuelewa kuwa hakuna opinion ‘right’ ama ‘wrong’. Kuwa tayari kutofautiana.

Well Told Story © 2010 All rights reserved. No part of this publication may be reproduced, stored in any retrieval system or be transmitted in any form or by any means, electronic or mechanical without prior permission of the publishers. Although every effort has been taken to ensure the accuracy of information contained in this publication, in no event shall the publishers be liable for any incidental, indirect, consequential losses or damages of any kind without limitation arising out of or in connection with the use of the information in this publication. Shujaaz™ is published by Well Told Story Ltd. P.O. Box 1700 - 00502 Nairobi, Kenya. Tel. 020 603214 / 0719 407512. www.welltoldstory.co.ke. Printed on recycled paper Printed by Colourprint Limited. P.O Box 44466 – 00100, Nairobi, Kenya.

7


Hiyo risto ya kadhi courts kuwa included illegaly iliendaje? Ama me ndio nimebaki nyuma? – Fred M. Jumah

The information in this box is exclusively brought to you by the Committee of Experts on Constitutional Review and does not in any way reflect the views of the publishers or their partners

If YES wins in the referendum, afta what period of time will this new constitution begin its role? Provisions tofauti za constitution zitaanza ku-work kwa periods tofauti zinazo-guide-iwa na Schedules V na VI. - COE

Kadhi courts zimekuwa kwa current constitution na kwa sheria zetu. Kadhi courts hu-deal na divorce, marriage na inheritance kwa waislamu tu na sio kwa wale wasio waislamu. - COE

Refugees in camps, will they become Kenyans? - Kelvice Ambia Hakuna provision kwa proposed constitution inayokubali refugees kuwa wakenya. - COE

DJ B, Wat is the difference btwn private and public land? – Man Bonny. private land ni ardhi ilio kuwa owned na mtu private kwa ku-lease ama kuimiliki. Public land ni ile iliokuwa owned na serikali na agencies zake. - COE

Your Questions on

CONSTItUT

answered by th

Committee Of Ex

Big ups kwa mafans walionitumia maswali juu ya constitution. Haya ni majibu mengine kutoka kwa Commitee of Experts. NI-join pamoja na maelfu ya youth kwa facebook kwa “djboyie shujaaz” au kwa Twitter, “Shujaaz” au uni-SMS on 3008 ili tuendelee kujijenga na kujenga Kenya sisi mavijanaa!!!


How will da constitution msg be received and understood especially in da pastoral communities? Will there be voluntary youth groups available? Committee of experts ina cordinators waliowekwa kwa kila constituency na wafanya kazi wa Community-Based Organizations na kuhakikisha wakenya wamefundishwa juu ya constitution kabla ya referendum. - COE

n the

TION

he

xperts

Special thanks ni kwa Committee of experts waliojibu maswali yenu!

Je constitution ni mradi wa serikali? Mbona basi kuna ‘yes’ na ‘no’?

Mbona wata toa public holidays? - Jeff, Nairobi.

Constitution ni project ya Kenya na ya wakenya wote. Referendum inapatia wananchi option ya kukubali au kukataa constitution kwa ku-vote Yes au No. - COE

Proposed constitution itabakisha national days lakini parliament ina mamlaka ya ku-announce public holidays. - COE

Hiyo ni poa bt saga ya kupata id ukifika 16 iliendaje? – Thomas Tj Mbogho. Hakukuwa na proposal kama hiyo. - COE

Je committee imepitisha ma-youth watengewe dooh za kuboresha miradi yao? Article 55 inaprovisions za ku-allow youth kupata training, kuajiriwa na kupata nafasi ya ku-participate kisiasa, kiuchumi na maisha ya watu wote. - COE


ni, bele m o i za hap dith a h ka ule kati na y a j i k

Charlie na Rosie waliposikia hate speech… …walijaribu mara nyingi kui-record kwa simu iwe evidence…

…na kisha waka-succeed ku-pata recording ya kutuma kwa NCIC…

mara that that!

Eh, ulicheki sura zao results zilipo announce-iwa?

Hic…hehehe! Walikaa nyani zimenyeshewa!

Wanajua toka leo tumewamaliza!

Haya…

Nyote sasa mumekamatwa… Kwa kueneza semi za chuki.

10


Hii story ya semi za chuki zinafanya kila mtu ashuku mwenzake.

Cheki Rosie, kila mtu kijijini ana wasiwasi.

Najua! tuWA ambie uncle na brathako Kila mtu aje wa-organise tucheze ball na game ya foota! tusahau tofauti zetu!

Aiyaia! Rosie idea zako ni vi-deadly!

mwisho.

Hate speech ni makosa KWA SISI SOTE. Inaleta tension kati ya jamii. Zuia chuki kwa ku-recognise sisi sote tuko tofauti, na hizi tofauti ndizo zinafanya Kenya kuwa country poa! Michezo ni njia moja ya kuleta community ya watu wa kabila mbali mbali pamoja na kuwasaidia kujuana vipoa. Kuna community moja huko Baringo Central ilijaribu na ikatoboa, ilipoanzisha Community Development and Empowerment Forum. CODEF waliandaa na ku-sponsor game kadhaa za foota huko Ng’arua Division ya Laikipia West na Mochongoi 12 Division ya Baringo Central.

Timu ishirini walicheza kutoka hizo division mbili zikiwa na wachezaji kutoka jamii mbali mbali. Competition yenyewe ilichukua miezi mitatu, kisha fainali zenyewe zilichezwa na hatimaye mkutano wa amani kufanyika. Mkutano wa amani ulifanya ku-educate watu kuhusu umuhimu wa amani na ushirikiano. Ma-youth walikuwa encouraged kufanya mambo positive na kuacha mambo ya violence. Kumbuka kubonga kuchochea chuki yaani ‘hate speech’ utashikwa na

waweza kufungwa hadi miaka 5 ama upigwe fine ya hadi million moja…ama zote mbili!


hapo awali...

Maria-Kim na JK wali-suspect mambo mwana siasa alisema na waka-check facts...

…Despite Chuxx kujaribu kuwazuia waliambia wengine ukweli wa mambo…

…Usiku wa kuamkia referendum, Maria-Kim alilala akisumbuka vile mambo yatatokea...

no!

HII ILITENDEKA VIPI…?

amka...

maria-kim!

amka!

13


EH...? HAIYA…KWANI NILIKUWA NIMELALA?

jana NIliOTA VIBAYA, JK…ATI KILIUMANA NA KILA KITU KIKAHARIBIWA!

LAKINI, MARIA-KIM, SI UNACHEKI KILA KITU KIKO POA.

KWELI. YENYEWE WATU WAME-BEHAVE VIPOA.

Kumbuka VILE MA-LEADERS WALIPOJARIBU KUTUDANGANYA…

…HATUKUWABELIeVE TU HIVYO.

14


KISHA TUKA-DISCUSS ISSUES ILI KUZIELEWA VIPOA…

TULIJIKAZA KUJISOMEA KATIBA SISI WENYEWE…

… NA KUCHEKI MA-FACTS.

…HATA KAMA WALIJARIBU KUIFANYA IWE HARD KWETU.

ALAFU HATUKUKUBALI KUWA BRIBED…

…AMA KUDANGANYWA TWENDE KWA GHASIA.

NAFURAHI VILE KILA MTU AME-BEHAVE VIPOA! YENYEWE AT THE END OF THE DAY SOTE WAKENYA TUNAPENDA COUNTRY YETU NA TUNATAKA AMANI!

Ndio Inawezekana! the end.

This special edition has been produced at the request of National Cohesion and Integration Commission with the support of Committee Of Experts and GTZ, in collaboration with Safaricom and Saturday Nation. Factual content & technical info: National Cohesion and Integration Commission & Committee of Experts. Producer: Fatima Aly Jaffer. Layout design: Joe Barasa. Art: Daniel Muli, Eric Zoe Muthoga, Salim Busuru, Movin Were, Joe Barasa.


03 - Shujaaz NCIC Special Part 3 of 3  

Special 3 - part series commissioned by the National Cohesion and Intergration Commission.

03 - Shujaaz NCIC Special Part 3 of 3  

Special 3 - part series commissioned by the National Cohesion and Intergration Commission.

Advertisement