Skip to main content

08.c - Maria Kim

Page 1

hapo awali...

bro wa maria kim na friends zake walisaidia kuwajulisha watu juu ya latf meeting...

...ndio watu waliweza ku-attend na kumchagua pastor kuwa chairman wao...

...na wali-present shida zao za kupelekwa kwa latf for consideration...

Committee ya LATF imekubali ku-fund ujenzi wa latrine mpya!

Anafuatilia Asante sana Baba J.K. Chakula kilikuwa kitamu. Mimi nitaelekea home kunakuwa usiku.

Lazima tusherekee hii achievement! Twendeni dinner leo jioni?

Wa! Maria Kim amesahau purse yake.

Wacha niku-push.

Ah asante J-K. Lakini niko poa.

18


Hii ni last warning! Wachana na mambo hayakuhusu, ama life yako na bro yako itakuwa kwa danger!

Aki J.K! sijui ninge-do nini kama hungetokea!

19


Vitu zimekuwa worse...

Nilikuwa mjinga ku-think dame mdogo kama mimi anaweza change kitu yoyote.

Usi-give up manze! Wewe ni inspiration kubwa. Usiwawache wa-win.

Sitaki kuweka bro kwa risk zaidi.

Asante J.K. Goodnight.

baada ya weeks kadhaa...

Siz, umesikia news? Latrine imeshamaliza kujengwa!

20

Hio ni poa. Wacha nikaione.


Lazima unilipe ndio utumie choo!

Shika pesa zako.

?!

Huh? Maria Kim hakunitetesha juu ya kuwa-charge watu? Ni nini mbaya...?

Sasa mdem? Umebadilika! Huna problem na charge yetu?

Sijali siku hizi.

21


Bro yako ameshikwa na Chuux! Ati hajalipa kutumia choo!

baadaye... Maria Kim! Come haraka!

Nini? No one hurts my bro! Twende!

Mnafanya nini sasa? Mnavunja sheria hapa! Hii choo ni ya public.

Ilijengwa na pesa za LATF! Hamufai ku-force watu walipe kuitumia. Wacheni kuwa lazy na kudai pesa bure. Tafuteni kitu ya ku-do!

‌Ni responsibility yetu ku-maintain na kuchunga hii choo. Kama hatuishughulikii itachukuliwa na watu kama hawa.

Tuko pamoja?

Wachana na story za hii choo, na utuache vile umetupata!

ndio! tuko!

22


enda!!

toka hapa!!

wazi! maria kim is back!!

nitamtumia dj b text nim-show hii story

Life itakuwaje vijana waki-participate kwa LATF? Saseni wasee, mnajua juu ya LATF kuwa ni fund iliyo available kwa watu wote ili-wa-improve area yao. Lakini si watu wengi wanajua juu ya LATF. Kwa hivyo nili-meet na George Owuor wa Kenya Social Forum na nikamuuliza atueleze more juu ya hii fund... Alikuwa na haya ya kusema:

Maria Kim: KSF inafanya kazi gani ya LATF? George: Tumekuwa tuki-inform vijana na wenyeji wa Kisumu importance ya ku-participate kwa mambo ya LATF/ Local Authority Transfer Funds for 5 years. Maria Kim: Nini iliwafanya m-focus on LATF? George: Kwa new constitution, maendeleo yata-depend on participation ya watu, na dooh zitakuwa zikipitia LATF. Tuta-decide vile dooh zitatumika ili zitusaidie. Maria Kim: Mnatumia methods gani ku-inform watu wa Kisumu juu ya LATF? George: Tuna-hold seminars kwa community na ku-engage wenyeji kwa discussions za kuwa-help kujigundulia umuhimu wa kuparticipate kwa LATF meetings na projects. Vijana wanapata platform ya ku-discuss na ku-address issues za areas zao.

Maria Kim: Kwa hiyo 5 years KSF imekuwa in operation, mume-achieve mambo gani? George: Wenyeji wameanza ku-follow up maendeleo ya LATF kwa area yao, na kuaddress shida kwa area zao. Maria Kim: Na challenges, kuna any mmepata? George: Tumetishwa sababu ya ku-empower wenyeji ku-own projects na ku-ensure ufisadi unaisha na haijatuzuia. Watu few walijua na ku-attend LATF meetings sababu zina-announce-iwa kwa magazeti tu. KSF ina informers kwa council wanao-inform wenyeji meetings za LATF ili wa-participate. Thanks George Owuor kwa kubonga na mimi. Shujaaz fans, mumepata 1st hand information juu ya LATF. Unawezamake a difference kama Kenya Social Forum vile wame-succeed kwa area ya Kisumu.

Si ujaribu hii idea kisha utumie DJ B message kwa 3008 au facebook page yake on DJBOYIE SHUJAAZ juu ya hii story ya LATF.

23


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
08.c - Maria Kim by Shujaaz - Issuu