Skip to main content

11.c - Maria Kim

Page 1

huyu dem wa mtaa ni orphan anaye-raise bro wake, na huku anang’ang’ana na chuo. Ana-face challenges mob sana, Lakini hakubali anything kumzuia kuzima corruption. mafala pekee ndio hu-try kum-challenge. only the brave hujaribu kum-ask out!

Chuxx Arudi Ocha!

Manze alisema mimi ni kaa mtoi wake...

Lakini saa hizi ameniacha {hic!} Hata amesahau vitu alini-promise….niko alone. ALONE!

Siezi trust huyo Godpapa tena. Nita-change nianze life freshi.

18


Nitakuwa good boy! {hic!}

Wee! Ebu angalia kwenye unaenda!

Ah, msuper! Niaje? Cheki, uliniambia ukweli juu ya Godpapa, huyo msee hanijali.

Nishaamua, kuanzia saa hizi, nitakuwa good boy.

Nahitaji family. Nimekuchagua ukuwe wife wangu! Ulijuanga nina shamba ocha? Nita-visit budangu na ni-mshow ndio niirithi. Manze time yangu ishafika.

Chuxx ishia. Umelewa!

19


Mtoto wangu amerudi! Nduma! Umerudi? Ah, umenifurahisha sana!

Nimekuja ku-cheki urithi wangu. Baba, time yangu ikifika, nitaanza works kwa hii shamba.

Lakini unaona kijana, kazi ya shamba si rahisi. Ni lazima utie bidii kabisa.

20


Manze ina-bore! Nahitaji gauge initulize kiasi‌

hii ni first time nimewahi toa hiyo jacket yangu ya green... eh!!

unajua wase huni-enjoy ati hii t-shirt yangu maybe haina mgongo? eh, na hawa...? hawachoki?

Aki Baba, Nduma ni m-lazy tu vile alikuaga. Si-believe utamwachia shamba. acha nipige pose hapa kidogo

Rhoda, ndugu yako amechoka tu kwa sababu ya safari. Mwache apumzike kidogo. Shhh‌nyamaza wee kuku! Ni kutoka kwako ndio nita-get doh za ku-buy crate mzima ya gauge bariiiidi!

leta keg! patia kila mtu moja moja!

bosh... {hic!} we ni mshee wa nguvu!

21


Nduma, amka! Unaaibisha hii familia sana. Usidhani nitakuachia shamba yangu hivyo tu. Nimeifanyia kazi ngumu sana!

Ni miaka mob sana mimi na Baba tumekuwa tunafanya job hapa kwa shamba ndio ikuwe bizna ya maana. Wewe umekuja tu hivi na umetupotezea pesa mob sana kwa usiku moja tu!

Wewe ni mnoooono na uko greedy sana!

Mnanidisciminate tu juu nimenona?! mimi ndio first born son hapa!

Nonsense!

22

Hata nikikufa, Rhoda ndio atarithi hii shamba. Sio wewe. Ameweka bidii yake kujenga hii shamba.

Hebu ondoka kabisa!


Godpapa hawezi ni-discriminate, yeye ndio msee wa kabila yangu hapa mtaani…

Niaje DJB? Chuxx ana-complain juu budake alikataa kumpe shamba. Juu ya vile ako m-lazy, ame-loose opportunity ya kuwa na bizna ocha. Anajionaje? Ati sis wake hawezi rithi shamba juu ni dem?!

oh, umerudi? Hebu osha gari yangu!

Mayuts wengi wanawaste dooh mob kwa pombe na mwishowe wana-lose chances poa in life.

Niliuliza ma-fans juu ya hii noma Facebook na hivi ndio walisema…

BOY G Chuxx fanya bidii uwe na shamba yako. Budako akikunyima ni haki yake coz alifanya bidii na niyake. Sasa kama wewe ni mlevi na uko kwenye gang sidhani kama wataka kuji endeleza na hiyo plot. Kuna bob yako hapo kwa plot? Hauoni haya bado chaliii mkubwa una tegemea wazazi? Aibu hiyo bwana!

JARED I Chuxx a-relax a-buy yake coz huyu akipewa hiyo shamba, ataiuza. So buda asimpatie.
 
PETER B. L Kufikiria hio ploti ndo inafanya mjamaa awe mzembe. Fikiria out of the box; anza kuona vitu zingine muhimu kama kuuza makaa, panda skuma kwa gunia, fuga kuku….ni mob bana! FIKIRIA!

Lazima tukuwe responsible as mayuts kama tunataka ku-develop. Work hard ujitafutie kitu poa badala ya kutegemea wengine. Hatuwezi kuendelea kutumiwa na ma-leaders ati juu unataka easy money. Ni bidii yetu ndio itatuinua jo!

KATHY O. Hio ni sweat ya fathe na anakula sweat yake! Lazima Chuxx a-reap chenye yeye amepanda si ya baba yake! JOHN L. Ni right yake. Buda aachane na vijisababu. Apewe shamba ajiendeleze. Kama sivyo, buda naona yuko taabani. Chuxx ataterrorise ocha. Maybe anataka ku-invest ama ana-marry.

Ehe! Kama wewe ndio hao wasee wanangoja tu kurithi vitu, job yako ni pombe tu, ebu acha hiyo tabia mara that! Weka bidii!! Kaa gangare! Unatuaibisha jo! 23


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook