Page 1

Ee msupa, chill kidogo...

Sikuwa supposed kukwambia, lakini take care sweetness, kuna watu hawafurahishwi na kile unafanya.

Sema mresh, najua umenimiss.

Sasa Maria, naeza ongea na wewe?

Si-understand...

In private.

Mwambie kile unataka nikiwa hapa.

Twende J.K.

18

GRRRRRRRR!


Nimepata new info juu ya LATF na ina projects za constituencies kote nchini.

Last year, constituency yetu ilipata 4 Million na ikatumiwa kujenga library.

Hio ni poa, lakini sijaona laibu hapa. Iko?

si naweza kuwa nafanya homework kwa laibu?

Fathangu ni pastor. Twende tumuulize.

Unajua pale library iliojengwa iko?

Naijua. Twende niwaonyeshe.

19


Ndio hii library!

Siamini!!

4 million!

Mlitoa 4 million wapi? Hii library ilijengwa na 300,000 shillings!

Nilituma SMS kwa 3002 na kupata hiyo information.

Mmm... 3002. Nitajulisha congretation na watu wengine juu ya hio number kwa sermon ya Sunday. Elimu ni nguvu!

Yaani pesa za laibu zimetumika vibaya bila sisi wenyeji kujua?!

Asante sana.

20


Hatutakubali!

Wacha ku-jam hivo Maria, kumbuka fathangu alisema, knowledge is power.

LATF meeting ya next itakuwa September. Tunaweza julisha watu juu ya umuhimu wa kui-attend na juu ya 3002 SMS service. Then watu wanaweza jua venye LATF inatumiwa kwa area zao na ku-question maendeleo ya area yao.

Kwani ulikuwa ukitaka?

Kesho morning ni too late! Hebu tuziweke usiku!

Finally jobo imeisha.

Tutaweka hizi posters kesho morning.

Sawa, tuanze na sides gani?

21


Sunrise inapendeza. Kama wewe, Maria...

Thanks J.K! Tuchekiane baadaye

er... um... Hebu nicheki brathangu‌.

22


Nonsense!

Deal na huyu msichana once and for all! Hii ni serious bizness! Naskia unapenda huyu msichana. Nakupa advice, Pata pesa na wasichana wataifuata. Mnyamazishe mara moja!

Endeleza area yako through LATF Local Authority Transfer Fund/ LATF ilianzishwa 1999 kupitia LATF act No. 8 ya 1998 ili ku-improve huduma kwa local community kwa kuendeleza projects kwa wards kote nchini. A certain percentage ya budget kwa kila council huwa ni ya LATF. Mkutano hu-anncounce-iwa ili wanaward wa-attend. Mmoja wa community hu-appoint-iwa ku-chair mkutano wa ward. Kisha wana-ward hu-discuss venye wanaweza ku-solve shida zao kwa kuanzisha projects kwa ward. Hizi projects ni kama health, education, maji, na ingine itakayo benefit watu wa community. Community ina-prioritize projects tatu zitakazo anzishwa. Hizi proposed projects hu-forward-iwa kwa council committee inayo-forward kwa local council ili zipresent-iwe kwa Annual LATF Meeting. Kila mwaka, council huwa na Annual LATF Meeting inayo-announce-iwa through newspapers. Kwa annual LATF meet-

ing, wenyeji wa wards zote za council hukutana na ku-present projects zao ili ziwe-considered kwa plans za council. Hata kama hizi meetings hu-advertiseiwa, wananchi wachache hujua juu ya hizi meetings za ward na councils. Hii inafanya decisions kufanya na wachache. Miradi pia huchukuliwa na watu wanao ji-benefit wenyewe /cartels na impact ya miradi haifikii wenye kijiji. Ili LATF fund iweze kutumika ku-benefit local communities, ni kuhimu kwa wenyeji 1. Kupata info juu ya dates za mikutano kupitia posters badala ya newspapers sababu ni wachache hupata kuona announcement Annual LATF Meeting ya kupitia newspapers. Posters na mbinu zingine zinaweza kutumika. 2. Wananchi wachukue jukumu la ku-attend LATF meetings kwa wards wa-participate kwa ku-identify na ku-

run projects ili kuji-develop. In that way, watapata ku-own hizo projects. Ni responsibility yako ku-participate kwa maendeleo ya area yenu. Infonet imeunda SMS system ya kusaidia wananchi na info juu ya funds zilizo allocate-iwa kwa matumizi ya LATF kote nchini. Tuma SMS yako kwa 3002 iliyo na jina la ward na mradi/project na utapata amount iliotengwa kwa hiyo project. Hii info itasaidia kufanya viongozi kuwa accountable na transparent. Mfano: Rabai#Education. Tumia DJ B views na opinions juu ya hii storo ya LATF on 3002.

23

06.c - Maria Kim  

Chapta 6 - Maria Kim: Ana-Expose Ufisadi!

Read more
Read more
Similar to
Popular now
Just for you