Skip to main content

09.b - Malkia

Page 1

yeye ni mhandi, mdosi, m-bright...

Yeye ni player!

alisema anapenda hair style yangu...

...na a+

yaani yeye ni the best! akanipa choku...

jipendo yaani huyo chali una-date ni teacher? ehe, kwani? ni serious kwa sababu ma-stude hawana ruhusa ya kuwa na relationships na teachers. julisha princie mara one!

shut up, uko jealous kuwa nina boyfie na huna! 9


niaje ma-fans nimepata sms kutoka kwa maria kim akiniambia kuwa beshte yake ame-rape-iwa na teacher wa shule yao. unataka ku-warn ma-dame wote wajichunge na wa keep safe!

ai! hiyo inaweza-happen kwa jipendo. lazima nifanye kitu nimsaidie.

10


jipendo! ngoja nikwambie! ?

aiiish! jiongeleshe!

aiii? ni nini? kwanini unalia? uli-fail?

nimekuwa fala. alisema nina hairstyle poa, akanipa choku. even nikapatiwa a+!

halafu akajaribu ku... ku... ni mbaya. yaani siamini nilifikiria kuwa mr.s ananipenda!!!

whaat! yani huyo mr.s ni player!

lazima tuambie princie!!

11


come in...

thank you, girls.

ms. mumbi, ita mr. s nataka. kumwongelesha mara moja. good morning principal. i hope you are well?

mr. s nimesikia some serious allegations against you. leave the school mpaka utakapo sikia kutoka kwa tsc... 12


i will not tolerate teachers being inapropriate with my students... but you children also need to take responsibility for your own safety...

if you feel that a teacher is behaving inappropriately, never accept a personal gift such as money, sweets or clothes from him or her. instead report the incident immediately.

siamini kuwa mr. s alikuwa player! oh, by the way thanks kwa kunisaidia ku-realize hivyo.

usini-thank, shukuru dj b! 13


Wasee, student mmoja leo amejipata pabaya kwa kuwa na relationship na teacher. Nilibonga na yeye na ku-discuss mambo tungetaka mjue juu ya kuwa sexually harassed.

Na ma-boys hu-harass-iwa?

Pia ma-boy’s huharass-iwa.

Naweza fanya nini niki-harass-iwa? Ambia yule anaku-harass awache anachofanya juu haikufurahishi. Unaweza enda na witness wakati unaongea na harasser. Wakati mwingine utapata kuwa hakuwa akijua kile anafanya kinakuudhi. Tuma complant kwa headteacher, deputy wake, teacher on duty au mzazi. Unaweza tuma barua. Hii complaint itafanyiwa investigations Weka record ya times ume-harassiwa pamoja na wapi kitendo kilifanyika, kama kuna-witnesses na vile uli-respond kwake. Ambia mtu una-trust kama mwalimu au classmate ili wakupatie emotional support. Unaweza report harassment kwa police au kuwapeleka kotini. Report cases za sexual harassment kwa kupiga simu kwa child line 116 na utasaidiwa! 14

Sexual harassment ina-involve kufanyiwa matendo yanayo-suggest sex na yanayo udhi mtu. Nitajuaje kama kitendo ni sexual harrassment?

Uta-trick-iwa na mtu kulala na yeye ili akupatie pesa, high grades, food au kuwa atakusaidia na family yako. Mwenye ku-harass anaweza kukupatia present, kukuandikia letter, kukukatia ama kufanya gestures. Jua kuwa harassment inaweza fanyika anywhere kama home, shule, ukitoka shule, kwa homes za watu wengine au public places kama bash. Sexual harassment sio kuongea na mtu, kukatiana, kuwa mabeshte au kuwa na crash na mtu mwingine na kuwa na chemistry kati ya watu wawili.

Na kuna sheria i nani-protect kutokana na sexual harassment? Ndio, Sexual Offenses Act. 24 inasema mtu anaweza kufungwa jela for minimum 10 years; Mtu yeyote awe headteacher, teacher, mfanyi kazi wa shule za prima ama seco au special institution anaye-take advantage of position yake kushawishi au ku-attract mwanafunzi kulala na yeye kama student au ku-commit offenses zingine za hiyo act kama sexual intercourse ambayo hailinganishwi na kosa la rape au kunajisiwa. Mtoto ni mtu yeyote below 18 years na penalties zingine hupewa makosa tofauti.

Ninaweza report juu ya kuwa sexually harassed? Shule inatakikana kufanya mambo haya ili kuifanya rahisi kwa mtu ku-report kama ame-harrass-iwa: Kusema jinsi za yeyote ku-report kesi kama ame-harass-iwa Create njia za ku-report harrasment in schools like reporting to their teachers in charge and their contacts Kuonyesha nani anaweza pewa report na anaye-harass-iwa Utaratibu wa kufanya investigations venye itakuwa na anaye-harass-iwa hatajulikana kwa wengine. Kutengeneza njia za ku-discipline anaye patikana aki- sexually harass wengine

Usinyamaze ukiwa sexually harassed, ongea. Kuna usaidizi!


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
09.b - Malkia by Shujaaz - Issuu