Page 1

aenda shagz Tayari Malkia?! Out!

Habari Malkia? Asante kwa kunitembelea

Nitarudi jioni!!

9


Natayarisha kupanda maharagwe. Unajua kulima?

Nisaidie na kazi kidogo

Sawa nyanya

Hapana nyanya

Kukamua ng’ombe? Hapana nyanya

Huyu ng’ombe anatoa maziwa mEngi

KAAP!!

Ndio nyanya

Koo

twaa

Nyanya, kumbe unajua kuchongoa?!

Miguu kubwa kama meli!!

Nilikuwa nikichongoa nilipokuwa mdogo. Ingine inaenda, wewe ni mweusi mpaka kukiwa na giza unatafutwa na unga ya ugali

Mapua kubwa kama firimbi ya jakobo

Ha

! Ha!

Ha!

Ha

!

Ha

!

Una mdomo kubwa hadi ukiifunga inalia kama mlango. Ha ha ha ha

Ha

!

10

sh!

! aHa! HaH !


Twende tuchunge kondoo

Nyanya! Zitaniumiza!

Kondoo ni mnyama mtulivu, hawezi kukuumiza

Aaaaaa. Nakumbuka mamako alipokuwa mdogo

Alikuwa analipisha watoto wa kijiji na kuwabeba na kondoo Kweli?! Nitamcheka!

Asubuhi na mapema watoto walikuwa wanapanga laini kwa kondoo wakingojea mamako awafungulie

Mama na kondoo!! Haha ha ha ha

11


BAADAYE KWA NYANYA Mamangu alipenda wanyama gani? Na alisumbua walimu shuleni? Alikuwa na boyfriends wangapi

Uliza mamako, ndie anaweza kujibu maswali haya yote.

Mama hana wakati wa kuongea na mimi ninapotoka shule anashughuli nyingi

Pole, najua mamako anakupenda sana na anafanya kazi kwa bidii ili uwe na maisha mema. Sawa, nisaidie kufanya kazi ingine Niletee ile ndoo.

Nyanya maharagwe iko ndani ya maji

Niliziweka jana usiku ili ziwe tayari kupanda. Kuweka mbegu kwa maji kabla ya kupanda inasaidia mbegu zote kumea haraka wakati wa kiangazi na kupatia mavuno mapema. Ni rahisi sana. Twende shambani.

12


Sikuelewa sababu ya kuweka mbegu kwa maji

Nilikuwa napanda mbegu shambani chache ndio zilikua. Nilipata hasara hadi nilipoanza kuweka mbegu kwa maji usiku na kuzipanda asubuhi.

Mbegu ni kama mtoto, lazima uiTUNZE vizuri ili iwe na mazao mazuri. Mtoto asiye na afya hushikwa na magonjwa virahisi

Utajua kama nafaka itamea kwa uki iweka kwa maji na kutoa zile zina-float juu ya maji Kuweka mbegu kwa maji kunasaidia mbegu kupata joto, maji na hewa zilizo muhimu kwa mmea..Hii ni hakikisho kuwa mbegu zote zitakua

mmea

hours za ku-soak mbegu

mmea

hours za ku-soak mbegu

Wheat

12

Chickpea

6-8

Barley

12

Finger millet

8

Upland rice

12-18

Cow pea

8

Maize

12-18

Pigeon pea

8

Sorghum

10

Groundnut

8

Pearl millet

10 13


Asante kwa kunisaidia shambani

Nimefurahia kuwa na wewe

Mimi pia

Nitakuita unisaidie kuvuna maharagwe yetu Kwaheri nyanya

Kwaheri Malkia Nitakusaidia kuvuna

Kata hasara kwa kwa ku-soak mbegu kabla ya kupanda na utavuna haraka

Umewahi enda kwa shamba na kupata plants zikimea kwa patches? Hii ni sababu mbegu zingine zina-fail kugerminate. Wakati mwingine, mbegu zote zinaweza fail ku-germinate kabisa. Hii huwa hasara kubwa kwa wakulima. Ku-soak mbegu kabla ya kupanda ni simple na inahakikisha kuwa mbegu zitamea haraka ili kupata mavuno mapema. Ku-soak mbegu kabla ya kupanda hufanywa kwa areas zilizopata low rains na kwenye ardhi kavu. 14

Kwanini ni-soak mbegu zangu? a) Mbegu zote zina-grow kuwa mimea healthy. Ni expensive kupanda mbegu tena, na huna guarantee kuwa hizo mbegu zitamea this time round kuwa healthy. b) Zina-mature haraka na kuvunwa mbele ya zile hazijasoak-iwa. In that way, wakulima wanaweza panda mimea ingine hata kama ni off season. c) Zitamea haraka zaidi ya zile haziku-soak-iwa kwa maji. d) Inapunguza weeding sababu mimea ina-compete vipoa na weeds,

Jionee tofauti ya ku-soak mbegu na kuto-soak, kwa kupanda mbegu zime-soak-iwa na zile hazija-soak-iwa kwa separate containers. Steps za ku-soak mbegu 1. Weka mbegu kwa maji kwa masaa kadhaa 2. Kausha seeds. Unaweza ziweka for several days kabla ya kuzipanda.

Tumia DJ B views na opinions juu ya hii storo ya ku-soak seeds on 3008.

6.b - Malkia  

Chapta 6 - Malkia: Aenda Shagz