B8_pg01.pdf
1
11/09/2010
09:32:32
hapo awali...
chief aliwaambia gang wamtafute dj b na kufunga shujaaz.fm...
...lakini by mistake gang walimshika dj b mwingine aliyekuwa aki-play kwa concerts...
...na mamake dj b yule mwingine hakufurahia alipowapata kwa nyumba yake!...
...ni important sana tukatae pressure za gangs na wale wanataka kutunyang’anya biashara na pesa zetu.
BOYIE
kama ushawahi kuwa victim wa ma-gangs ni poa kuzungumza na mtu ako kwa...
Siku za mwizi ...mamlaka kama chief, ili ku-stop hii behaviour!
boosh, naenda kuambia chief vile wale vijana wakora walikufanyia! hatuwezi kuwaacha hivyo!
3
kazi yako ni kukaa kwa ofisi na kuzungusha makaratasi, huku wezi wanatuibia!
wewe chief! ni nini unafanya ili ku-control hizi gangs zinazo tuhangaisha?
walimfunga kijana wangu na kujaribu kumuibia vitu vyake vya muziki!
chief wa bure wewe!
huyo chief ni mzembe! hata hakuskia kitu chochote nilimwambia! afadhali ninge-shout zaidi! mum, hiyo si njia ya kuongelesha chief. Ndio sababu hakukusikiza kwa sababu ya ku-shout.
4
wacha ni-try kumuongelesha vi-politely.
gang fulani ya mavijanaa wali-break into my room wakanifunga kwa kiti ati niwaeleze kuhusu redio station yangu...lakini sina.
chief, naomba muda kidogo tu wako. nataka ku-report kesi ya kudhulumiwa.
na-hope utashughulikia hiyo kesi na haki ifanyike kwa hiyo gang.
mbona hao vijanaa walifikiria uko na redio station? mimi ni boosh najiita dj b. wanaweza kuwa walini-mistake dj b wa redio.
wajinga hao!
usijali kijanaa. nitajaribu kukufanyia justice. lazima hiyo gang ilipe kwa sababu ya crime zao.
askari! lazima tukamate hii gang ina-terrorise mitaa yetu. leo tunamaliza hio reign yao.
ndio wale!
5
karao! hepeni wasee!
weee! kujeni hapa!
kamata! nimempata, chief!
6
ninawashtaki kwa kujaribu kumwibia dj boosh.
haiya! lakini si ni wewe ulitu-show tutafute dj b!
wewe! sijui unaongelea nini? mumejaa uongo!
manze uta-regret kwa kutudanganya chief! uko alone na sisi ni kibao!
yaani hakuna mtu naweza trust? nitamtafuta dj b mwenyewe.
7
vipi ma-youth! nime-get text kutoka kwa jamaa anajiita dj b! inaonekana nina twin...lakini kumbukeni mimi ndio the one and only dj b kwa shujaaz.fm!
TIPS JuU YA KU-DEAL NA AUTHORITY Si rahisi kuongea na mtu aliye na mamlaka sababu yeye huwa na uamuzi wa hali yako. Lakini beshte yangu Boosh ana tips juu ya ku-communicate na kupata matokea uliyokuwa uki-expect kwa watu walio na authority. Kuwa umetulia kabla ya ku-meet na mtu aliye na mamlaka.
Kumbuka wakati tulikuwa shule vile tuli-treat walimu shuleni kama bad guys? Ukimfikiria mtu aliye na mamlaka kuwa adui yako, mtakaa kama mnashindana badala ya ku-discuss issues kama adults. 8
Vaa vizuri, kuwa msafi vile utaheshimika. Itasaidia ku-create impression poa na ku-demand respect. Usi-argue na mtu aliye na mamlaka. Kama umekosea, apologise ili isilete hasira juu ya kukana. Mwambie facts ukiwa calm na ume-tulia.
Kama ume ulizwa maswali, jibu kwa heshima na itazidisha chances ya kutapata results uliyokuwa ukitarajia.
Hebu tuambie vile ulim-get chief kusikia complaint yako!
Msalimie ili asifikiri unamchukia. Kumbuka yeye ni binadamu pia na kama wewe, anapenda apewe heshima. Ukimwongelesha vizuri, atataka kusikia mawazo yako and ku-respond.