Katika maisha haya watu wengi wanatumia damu ya Yesu kwa mambo mengi. Lakini je, matumizi haya yote ni sawa? Soma toleo hili lenye kichwa ‘Neema Yatosha’. Ndani yake kuna makala ya “Kwa damu ya Yesu” inatafakari swali hili zaidi.
Pia utasoma mada kuhusu damu ya Yesu ilivyo na maana kwa ushirika wetu kama Wakristo pamoja na ushuhuda wa kukutia moyo wakati unapoona ni kana kwamba Mungu hasikii maombi yako ya muda mrefu.
RIZIKI ni gazeti la Kikristo linalotolewa mara nne kwa mwaka. Gazeti hili limewalenga Wainjilisti na Wachungaji, lakini pia ni nzuri kwa wote wanaotafuta mafundisho mazuri katika maisha yao ndani ya kristo.
Lengo kuu la RIZIKI ni kuhamasisha na kufundisha wote wanaopeleka neno kwa watu, na kufikisha neno kwa usahihi wote ili kuwajenga watu.