RIZIKI Septemba/2026 - Novemba/2026
UFALME WA MUNGU NI HAKI TOLEO LA 3/2026
TAHARIRI
RIZIKI TOLEO 3, 2026
RIZIKI S.L.P. 2696, Arusha 0759 544 917 Barua pepe: editor.somabiblia@gmail.com Kamati ya Riziki: Mch. Elitegemeo Y. Mpumpa (mhariri) Mch. Anza Amen Lema Mch. Philip Bach-Svendsen Cathbert Msemo Mary Bura Magreth Mushi Mch. Gervas Meitamei Luhekelo Sanga Waandishi walioshiriki: Mch. Gideon Mumo Mch. Ernest William Kadiva Mary Lazaro Laiser Samwel Nyanda Layout: Cathbert Msemo Jalada: Cathbert Msemo ISSN 2683 - 6491 Nakala: 4500 Usambazaji:
SOMA BIBLIA
S.L.P. 2696, Arusha S.L.P. 12772, Dar es Salaam S.L.P. 1088, Iringa S.L.P. 6097, Mwanza S.L.P. 1062, Mbeya S.L.P. 4231, Dodoma S.L.P. 219, Makambako www.somabiblia.or.tz
Neno la Injili kwa rika zote Tanzania! Imechapwa na:
Imaging Smart - Dar es Salaam
Ufalme wa Mungu unaonekana katika haki Haki ni nini? Je, haki huamuliwa na sheria za wanadamu au na Mungu? Je, mtoto hutendewa haki anapolazimishwa kufuata mila na desturi? Je, mtu anaweza kujihesabia haki mbele za Mungu kwa matendo yake mwenyewe? Na ikiwa Ufalme wa Mungu ni haki, je, haki hiyo inaonekana katika maisha yetu ya kila siku? Maswali haya ndiyo msingi wa toleo hili la RIZIKI. Tunaishi katika ulimwengu “unaolilia haki”, kwa sababu mara nyingi hukutana na upendeleo, dhuluma na mifumo inayomweka mwanadamu mbali na kusudi la Mungu. Mungu hakai kimya. Injili inafunua habari njema kwamba haki ya kweli haianzi katika mahakama za dunia, bali katika kiti cha Mungu kupitia Yesu Kristo. Toleo hili linaanza mfululizo wa matoleo matatu yanayotafakari Warumi 14:17: “Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu.” Safari inaanza kwa kutazama haki kama msingi wa Ufalme wa Mungu, kabla ya kuendelea na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. Katika kurasa hizi utakutana na ushuhuda wa kupinga mila potofu, mafundisho kuhusu haki ya Kristo, wajibu wa wazazi katika malezi ya watoto, na nafasi ya Mkristo katika kujenga jamii yenye haki. Tunakualika usisome makala hizi kama maarifa tu, bali kama habari njema inayoaminika kuhusu Kristo Yesu kama haki yetu, na mwaliko wa kuishi maisha ya haki pamoja naye kama Bwana. Hapo ndipo familia hubadilika, jamii hujengwa, na Kristo hutukuzwa. Mch. Elitegemeo Y. Mpumpa
Yaliyomo: Uk. 3-5: Uk. 6-7: Uk. 8-9: Uk. 10-11: Uk. 12-13: Uk. 14-15:
Ufalme wa Mungu ni haki Nilivyopigania haki dhidi ya mila zisizofaa Mafarisayo: juhudi kwa ajili ya Mungu bila maarifa Kristo ndiye haki yetu Kuanzia haki hadi uwajibikaji katika yote Haki ni wajibu 2
MADA
RIZIKI TOLEO 3, 2026
Ufalme wa Mungu ni haki Dunia nzima ina changamoto ya kujua haki ni nini na inapatikana wapi. Watu wanauliza kama ipo kweli na kutendeka. Mara nyingi ninasikia maneno haya mtu anapofariki: “Amekwenda mbele ya haki”. Maana yake amekwenda kwa Mungu mwenye haki. Kauli hiyo inadokeza kuwa duniani hakuna haki, bali haki ipo kwa Mungu pekee. Biblia inathibitisha hiyo, ikisema kwamba miongoni mwa binadamu “hakuna mwenye haki hata mmoja” (Rum 3:10). Lakini “ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu” (Rum 14:17). Kwa nini kuna hali hiyo duniani? Biblia inajibu, ni kwa sababu “hakuna amtafutaye Mungu” (ling. Rum 3:10 na 11). Tukitaka mabadiliko na kuona haki kweli, Yesu ana ujumbe mzito unaotuambia waziwazi jinsi ya kufanya: “Utafuteni kwanza ufalme wake [Mungu] na haki yake; na hayo yote mtazisishiwa” (Mt 6:33).
ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (Mt 5:20). Wakati watu wengi huona maisha ya haki ndiyo yanayostahili urithi wao wa milele katika ufalme wa Mungu, Yesu anasema kwamba wenye njaa na kiu ya haki ndio walio heri, maana watashibishwa (Mt 5:6). Hao ndio walioona kwamba hawana haki wenyewe. Amri ni ya haki (Rum 7:12), lakini wameelewa haina nguvu ya kuwafanya wenye haki. Kwa hiyo wanaitafuta kwa Mungu wakiamini yeye ndiye mwenye haki. Na tumshukuru Mungu, wanaipata! Kwa sababu Mungu anaonyesha haki yake “pasipo sheria” (Rum 3:21), akimhesabu haki yeye amwaminiye Yesu (Rum 3:26). Hata Mungu anajisifu kwa kusema kwamba ndiye Mungu “ambaye huwahesabia waovu haki” wakiwa na imani hiyo tu “pasipo matendo” (Rum 4:5-6 NENO).
Maoni yanavyotofautiana
Yesu alipokuwa duniani, msisitizo wa mafundisho na huduma yake ulikuwa juu ya Ufalme wa Mungu. Mara nyingi alitumia mifano kufafanua juu yake. Alitumia taswira za kawaida kama vile mbegu, kondoo aliyepotea, na lulu. Mifano hii ilifanya kazi kama ‘madirisha’ kwa wasikilizaji waliokuwa tayari kuelewa, ikiwapa kuona ndani ya ufalme wa Mungu, na kama ‘vioo’ ili watafakari hali yao ya kiroho na maamuzi yao wenyewe. Sisi sote hupenda mfano wa mwana
Inakuwaje haki ya Mungu?
Mazungumzo ya kawaida kati ya watu siku hizi hutofautiana sana na Yesu alivyosema. Badala ya kila mtu kudai “haki yangu”, Yesu anasema juu ya “haki yake” Mungu. Badala ya sisi kutaka kuithibitisha haki yetu, Yesu anasema “msionyeshe haki yenu mbele ya watu” (tafsiri mbadala ya Mt 6:1). Hakuna kama Mafarisayo waliotafuta kuishi sheria ya Mungu, lakini Yesu anasema: “Haki yenu isipozidi hiyo haki 3
MADA
RIZIKI TOLEO 3, 2026
mpotevu, jinsi baba yake alivyompokea kwa upendo na kumrejeshea haki zote kama mwana, ingawa huyu alikuwa ameshazipokea mara moja na kuzitapanya kabisa. Kwa kweli hakuwa na haki yoyote tena. Lakini pamoja na kufurahia huruma ya baba, yabidi kuzingatia hoja ya yule mwana mkubwa, akimwambia baba yake: “Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona” (Lk 15:29-30). Je, hii ni haki kweli?
Mungu kwa sababu wanaona hawatendewi haki, ni kuwaambia wamtazame Mwanawe, Yesu Kristo. Yeye ndiye haki ya Mungu. Kwa sababu ya ustahimili wake, Mungu aliziachilia kwa muda mrefu zile dhambi zilizotangulia kufanywa. Lakini siku moja Mungu alisema: Ni mwisho; sasa haki itendeke! Lakini badala ya kutuhukumu sisi wenye dhambi, akamtoa Kristo Yesu awe dhabihu ya upatanisho (Rum 3:25). Alimweka kuwa “kiti cha neema” (Ebr 4:16; ling. tafsiri mbadala ya Rum 3:25), na sasa anatusihi tukutane naye hapo ili kupatanishwa naye, kwamba “yeye asiyejua dhambi, [Mungu] alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2 Kor 5:21).
Kristo Yesu alifanywa haki
Lakini haki duniani ikoje?
Jibu la Mungu kwao wanaofanana na mwana huyo mkubwa na kumlalamikia
Tunaposoma Biblia inavyosema juu ya
Mungu alimweka Yesu kuwa ”kiti cha neema”. Tafsiri hii mbadala ya Rum 3:25 inarejelea sanduku la agano, mahali pa upatanisho katika Agano la Kale. 4
MADA
RIZIKI TOLEO 3, 2026
Haki ni kuzawadiwa na kutenda mema
haki ya Mungu, bila shaka tunakubaliana na Yesu anaposema kwamba ufalme wa Mungu “si wa ulimwengu huu” (Yn 18:36). Haki iliyoelezwa hapo juu haina neno hapa duniani. Haki pasipo sheria wala matendo, hapana! Kama haki hiyo ya Mungu ingepata kutawala, jamii ingesambaratika kabisa! - Au vipi? Tukumbuke kwamba Yesu alipofundisha juu ya haki ya ufalme wa Mungu, hakumaanisha nchi ya kawaida yenye mfumo wa kisiasa na serikali inayoongoza kwa kutoa sheria. Alisema “ufalme wa Mungu umo ndani yenu” (Lk 17:21). Maana yake ni nini? Mtu anapompokea Yesu kwa imani kama haki yake, anazaliwa upya na Mungu (ling. Yn 3:1nk). Anakuwa mwana wa Mungu. Anapewa moyo mpya, moyo wa nyama badala ya wa jiwe, maana Mungu anamtia Roho wake mwenyewe ndani yake (Eze 36:26-27). Tena anaandika sheria yake katika moyo wa muumini huyo, akiahidi: Nitakuwa Mungu wako! (Yer 31:33) Je, wewe bado uko miongoni mwa hao wanaofikiri kwamba ufalme wa Mungu wenye haki hiyo hauendi duniani? Basi, sikiliza asemavyo Mungu mwenyewe: “Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka. Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu; msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao” (Isa 51:6-7).
Tusisubiri ‘kwenda mbele ya haki’ hadi kufa kwetu. Kuacha kuonana na Mungu kwenye kiti cha neema hadi tutakapokutana naye kwenye kiti cha hukumu, ni kudhihirisha moyo usio na toba na kujiwekea “akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu” (Rum 2:5). Basi, tutafute kukutana na Mungu kwenye kiti cha neema kama anavyotusihi kufanya. Hivyo tunaweza kuishi ndani ya ufalme wake kuanzia leo hii, na kuendelea hadi kufa kwetu kueneza ujumbe wa haki yake kwa njia ya ushuhuda wetu katika maneno na matendo mema. Haki ni zawadi kutoka kwa Mungu zawadi ambayo tumepewa bure. Basi, tutoe bure pia (ling. Mt 10:8). Mkristo hasemi “haki yangu, haki yangu”, bali hutafuta kuwatendea wengine kwa haki na kuwatetea wale wanaonyimwa haki zao. Kuna watu wanaotaka matendo kuliko maneno kwa sababu wanasisitiza kwamba haki itendeke, tena wanakumbusha kwamba “ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu” (1 Kor 4:20). Ni kweli, Yesu alisema neno juu ya watu kumtukuza Baba yetu aliye mbinguni, wakiyaona matendo yetu mema (Mt 5:16). Lakini pamoja na kujitahidi kutenda mema, tusisahau kwamba “neno la msalaba … kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu” (1 Kor 1:18). Tunaishi kwa ajili ya nini au nani?
Tunaishi katika mvutano uliopo kati ya Ufalme wa Mungu na ufalme wa uli.. inaendelea uk.7 5
USHUHUDA
RIZIKI TOLEO 3, 2026
Nilivyopigania haki dhidi ya mila zisizofaa Ninaitwa Mary Lazaro Laiser, mwenyeji wa wilaya ya Longido, mkoani Arusha. Nimepata elimu juu ya madhara ya ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni. Hiyo elimu ilinipa ujasiri. Kwanza nilimpambania binti yangu Nangidare Lengai Laizer kutokeketwa wala kuozwa
akiwa na umri mdogo. Ingawa haikuwa rahisi, nilifanikiwa. Nilimpa binti yangu elimu hiyo akiwa na umri wa miaka tisa na kumvusha rika akiwa na umri wa miaka 12 mwaka 2006. Sasa yeye ni mwalimu.
USHUHUDA
RIZIKI TOLEO 3, 2026 ... kutoka uk. 5
Kufundisha kuna manufaa
Sikuishia hapo, bali niliendelea kuwaelimisha baadhi ya wazazi wa eneo langu kupitia makusanyiko ya kanisani, sokoni, warsha, semina na vikundi mbalimbali. Kwanza niliwezeshwa na shirika la World Vision Tanzania (WVT). Baadaye shirika la Tembo limeniwezesha kuendelea hadi sasa. Imenifurahisha kuona kwamba baadhi ya wazazi wa Longido walioelewa elimu hii wamekubali kuwavusha binti zao rika pasipo kuwakeketa. Pia nimefanikiwa kutengeneza wawezeshaji wengine wa mradi katika eneo letu kupitia shirika la Tembo. Hivyo, sasa kuna Trainer of Trainees (TOT) katika vijiji vipatavyo vitano ambao wana uwezo wa kutoa elimu hii.
mwengu. Huu sio utofauti rahisi tu kati ya mema na mabaya. Badala yake, ni utofauti kati ya njia mbili tofauti kabisa za kuishi, mitazamo na mifumo ya imani miwili tofauti kabisa, na utiifu wa aina mbili tofauti kabisa. Je, tunatamani kuupata ulimwengu huu pamoja na kula na kunywa na kufurahia anasa yake yote, au tunamshukuru Mungu kwamba tumepata kuishi katika ufalme wake wenye baraka zake zote ya rohoni, yaani haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu? (Efe 1:3; Rum 14:17) Je, imani yetu iko katika maendeleo ya ufalme wa ulimwengu, au iko kwa Kristo Yesu, Mfalme wa amani na haki, kwamba aje katika ufalme wake? Je, tunaishi kwa ajili ya kuokoa vipande vilivyobaki vya ulimwengu huu wenye ukosefu wa haki, au tunaishi kama mashahidi wa Injili ya Kristo Yesu na haki yake, kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu kwa kila aaminiye? (Rum 1:16) Na vipi na utiifu wetu? Je, huu unatokana na hofu ya adhabu ya Mungu, au tunakwenda mbio katika njia ya maagizo yake, tukihubiri Injili, kuponya wagonjwa na kutoa pepo wachafu, kwa sababu Mungu ametukunjua mioyo yetu na kumimina pendo lake ndani yake? (Zab 119:32; Rum 5:5) Je, tunaitazamia kweli na hata kuihimiza ije siku ile ya Bwana Yesu atakapokuja katika ufalme wake mtukufu, tukio litakaloleta “mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”? (2 Pet 3:11-13)
Chanzo cha maarifa
Nilipokuwa nafanya kazi na WVT, nilikutana na wawezeshaji toka Soma Biblia. Kila asubuhi ikawa tuna kipindi cha sala, kipindi ambacho kilinijenga kiroho. Kipekee ninakumbuka somo toka Mwanzo 17:9-15 linalozungumza juu ya agano la Mungu na Ibrahimu juu ya tohara. Ni hapo Mungu alipoagiza kila mwanaume atahiriwe. Sarai, kwa upande mwingine, hakuhusika na tendo hilo, bali alipewa kuitwa Sara, jina jipya la heshima, na kubarikiwa kupata uzao. Kwenye msingi huo wa kibiblia, ambao haijaandika juu ya tohara ya wanawake, ndipo nilipopata ujasiri zaidi katika kuelimisha jamii kukataa ukeketaji na ndoa ya utotoni. Huu ndio msingi. Mary Lazaro Laiser 6
Mch. Dkt. Ernest William Kadiva 7
WATU WA BIBLIA
RIZIKI TOLEO 3, 2026
Mafarisayo: juhudi kwa ajili ya Mungu bila maarifa Kwa Wakristo wengi jina “Farisayo” linaleta picha hasi ya mtu asiyemjali Mungu wala mambo yake. Kama si kafiri kabisa, basi hakika ni mnafiki. Lakini ajabu sivyo! Mafarisayo ni kundi la kidini lililokuwa na ushawishi mkubwa sana katika historia ya Wayahudi hadi leo. Na wakati wa Paulo, Mafarisayo ndio waliokuwa kielelezo cha dini ya Kiyahudi iliyojengwa juu ya ujumbe wa Neno la Mungu. Siyo tu kwamba walikuwa makini kufuata sheria za Mungu, walikuwa pia wataalamu wa kuwabaini wengine na kuwashinikiza kutimiza sheria sawa na walivyoelewa wao.
Mungu, basi Paulo, anayejitambua kama Mfarisayo nambari moja, alihitimu sana (Gal 1:14). Sifa zake ni pamoja na kuwa mshiriki wa agano la Mungu akitahiriwa siku ya nane, kuwa Myahudi mwenye nasaba sahihi anayezungumza lugha ya asili ya Wayahudi, kufahamu sheria na kuitii kwa bidii ya Mafarisayo, na hata kuwa mkamilifu katika utakatifu. Zaidi ya hayo, juhudi zake za kidini zilimsukuma kuwatesa wazushi wa Kiyahudi (Mdo 22:15; 26:9-11; Flp 3:2-7). Ndivyo walivyokuwa Mafarisayo wengine pia. Je, walikamilika kweli?
Paulo na asili yake ya kifarisayo
Huku akisifu juhudi yao, Paulo pia anaonesha ukosefu mkubwa wa maarifa ya Mafarisayo. Walikuwa na juhudi ya kutafuta utakatifu kwa kufuata sheria kiasi cha kutothamini neema ya Mungu iliyofunuliwa katika Kristo Yesu. Walijitambua kama taifa teule la Mungu, lakini walikosa kutambua neema iliyowachagua. Walisisitiza maandiko yaliyofafanua sheria na utii wake, huku wakipuuza maandiko yaliyowaelekeza kwa Yesu Kristo kama yule ambaye Mungu alimtwisha dhambi zetu “ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye” (Isa 53:4-5; 2 Kor 5:21). Kama Paulo anavyoshudia baadaye, jitihada ya utii wa sheria hupuuza na hata kupinga mpango wa wokovu wa Mungu (Rum 10:2). Kwani badala ya kuwapokea wajumbe walioleta ujumbe huo mwema, Mafarisayo waliwakamata na kuwaua wakiamini hili lilimpendeza Mungu (Yn
Upungufu wa Mafarisayo
Paulo, ambaye alikuwa mmoja wao kabla ya kukutana na Yesu (Mdo 23:6; 26:5), anawatambua Mafarisayo kama watu walio na “juhudi kwa ajili ya Mungu” na kumwabudu “kwa bidii mchana na usiku” (Rum 10:2; Mdo 26:7). Kwa kweli walikuwa mstari wa mbele katika kushika sheria ya Mungu kuliko Wayahudi wengine. Kwa mfano, Farisayo asingeingia nyumbani mwa mtoza ushuru au kula na kunywa naye (Mk 2:14-17), na asingekula chochote kabla ya kunawa mikono (Mt 15:2). Kwa kufunga mara mbili kwa juma alifanya hata zaidi ya sheria ilivyodai (Mt 9:14; Lk 18:12). Kwa mtazamo wa tabia za nje, Mafarisayo walikuwa karibu na Mungu kuliko wengine wote. Je, ni kweli? Ukweli ni kwamba kama utii wa sheria ungempa yeyote haki mbele za 8
WATU WA BIBLIA
RIZIKI TOLEO 3, 2026
16:2). Walikuwa na macho ya kuona watu waliovunja sheria ndogo ndogo, lakini hawakuwa na macho ya kutambua makosa yao wenyewe wala kumtambua Yesu kuwa ni Kristo aliyefunuliwa katika mwili (Mt 7:3). Kwake Yesu waliona mwanadamu tu, mwana wa Yusufu na Mariamu, ambaye baadaye walimkamata na kumtundika msalabani (Yn 1:11).
anaumia kuona jinsi walivyopuuza uzito wa dhambi hiyo na kama tokeo lake pia kupuuza ufunuo wa mpango wa Mungu kuhusu wokovu wao. Kwa hiyo anaomba wageuzwe nia, na hivyo pia juhudi yao, hata wapate ujuzi wa kweli kwamba mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja tu, yaani Kristo Yesu (1 Tim 2:4-5). Anaomba watambue, kama alivyotambua mwenyewe, kwamba ufalme wa Masihi sio kwa waliozaliwa na Ibrahimu kimwili, bali waliohesabiwa haki ya Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo (Lk 2:30-32; Yn 3:3; 3:15, 36).
Uchungu wake Paulo kwa Mafarisayo
Ni kupotoka huko kunakomfanya Paulo awalilie akisema: “Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe (Rum 10:1). Paulo alitamani kuona wengi wa watu wake wakigeuka na kumwangalia Mungu badala ya kujiangalia wenyewe. Alitamani kuona wakitoka katika utumwa wa kujibidiisha siku zote bila kuufikia “ujuzi wa kweli” (2 Tim 3:7). Maana kama alivyofunuliwa Paulo mwenyewe, hakuna awezaye kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa njia ya matendo ya sheria (Rum 3:20).
Uhuru wa kweli
Mafarisayo walitarajia sana kuwa wenye haki mbele za Mungu, lakini juhudi yao kwa ajili ya Mungu iliwapofusha wasitambue haki yake. Hawakuelewa walihitaji uhuru kutoka utumwa wa dhambi na adhabu yake. Yesu anauelezea uhuru huu kuwa wa faida kuliko kupata ulimwengu wote na vyote viujazavyo (Mk 8:34). Ni uhuru wa kufanyika mwana wa ufalme wa Mungu kwa kupokea haki ya Mungu ipatikanayo kwa kumwamini Yesu Kristo pekee. Ombi la Paulo kwa Mafarisayo, mimi na wewe ni kwamba tupate kutambua kuwa hapana namna nyingine, ama njia nyingine, wala jina la mwingine awaye yote walilopewa wanadamu kupatia haki ya Mungu na wokovu wake (Mdo 4:12; Rum 3:24-26). Tiketi ya kuingia kwenye ufalme wa Mungu ni kupokea kwa imani haki ya Mungu ambayo ni sawa na Yesu Kristo, yeye pekee, na tendo la upatanisho wa Mungu katika yeye.
Utumwa wa Mafarisayo
Wayahudi wengi walimtarajia Masihi atakayewaokoa kutoka kwa utawala wa Warumi. Kwa Mafarisayo jambo hilo halikuwa na maana sana ikiwa tu walikuwa na uhuru wa kuishi sheria ya Mungu. Lakini ombi la Paulo linaonesha kwamba badala ya nafasi hiyo kuwaweka huru wa kuithibitisha haki yao wenyewe, walikuwa wamejiingiza kwenye utumwa mbaya zaidi. Walikuwa wameangukia utumwa wa dhambi ya kutojitia chini ya haki ya Mungu. Licha ya juhudi zao za kidini, Paulo
Mch. Gideon Mumo 9
IHUBIRI INJILI
RIZIKI TOLEO 3, 2026
Kristo ndiye haki yetu Mchango kwa maandalizi ya mahubiri juu ya Warumi 3:23-28 Je, mwanadamu anaweza kusimama mbele za Mungu kwa haki yake mwenyewe? Hili ndilo swali la msingi linalobeba kiini cha somo. Mtume Paulo anajibu kwa uthabiti: Hakuna mwanadamu atakayekuwa mwenye haki kwa matendo yake! Njia ni moja tu, nayo ni kuhesabiwa haki na Mungu, kwa neema yake, na hiyo yawezekana kwa sababu ya tendo lake la upatanisho katika Yesu Kristo.
la Mungu kwa tatizo la wanadamu wote: “Wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.” Injili inaweka wazi kuwa wokovu haupatikani kwa gharama ya fedha, mali wala jitihada za mwanadamu, bali ni zawadi ya bure kwetu. Lakini kwa Mungu ulikuwa na gharama kubwa mno: Ukombozi wetu ulimgharamia kifo cha kipatanisho cha Kristo Yesu.
Hakuna mwenye haki
Kiti cha rehema
Somo tajwa linaanza kwa kujibu hoja ya msingi iliyobainishwa wazi kuanzia Rum 1:18, kwamba kati ya wanadamu wote hakuna mwenye haki hata mmoja (3:10), bali ulimwengu wote ni chini ya hukumu ya Mungu (3:19). Ni “kwa sababu wote wamefanya dhambi” (m.23). Sheria ya Mungu yaweka wazi kuwa hakuna jitihada za mtu zinazoweza kumrejeshea hali ya kuwa mwenye haki mbele za Mungu. Aidha, mstari huo unaweka msingi wa tatizo hili la kiroho la mwanadamu kwa mtazamo mpana zaidi: “Wote wamepungukiwa na utukufu wa Mungu.”
M.25 unaeleza kazi ya Kristo kama dhabihu ya upatanisho. Kwa kawaida “upatanisho” ni tendo la kupatanisha pande mbili au zaidi zilizo na mgogoro; ni kurejesha maelewano au uhusiano uliovunjika. Fikiria mtu uliyemtendea kosa na kusababisha uadui kati yenu; unapoomba msamaha na anakusamehe, amani na maelewano hurejea. Lakini Injili siyo kwamba Mungu anaidhihirisha haki yake kwa kuziachilia, katika ustahimilivu wake, dhambi zote zilizotangulia kufanywa. Hata kama tungemwomba kwa moyo mnyenyekevu na wa toba, siyo haki kuziachilia tu, “maana mshahara wa dhambi ni mauti” (6:23). Paulo akiandika kwamba Mungu alimweka Yesu kuwa “upatanisho”, anamaanisha kifuniko kile cha sanduku la agano, ambapo damu ya dhabihu ya upatanisho iliponyunyizwa. Haki ya Mungu ni kifo cha Yesu badala yetu. Hivyo tu kuna uwezekano
“Lakini sasa …”
Kuanzia 3:21 Paulo anaanza kufafanua jinsi Injili ilivyo ya ajabu: Imedhihirisha haki ya Mungu, ambayo siyo ile anayodai katika sheria, bali ni haki anayoitoa kwa neema. “Neema” ni kutendewa tusivyostahili, kwa sababu tu Mungu ni upendo. Katika m.24 tunaona suluhisho la kipekee 10
IHUBIRI INJILI
RIZIKI TOLEO 3, 2026
Mpangilio wa Mahubiri
wa sisi kupatanishwa na Mungu. Haki ilitendeka katika Kristo Yesu. Ndiye haki ya Mungu.
Utangulizi
“Tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako” (Isa 43:26). Tumaini letu liko wapi tukiitwa hivyo na Mungu? Je, yawezekana kweli sisi kupata haki kwa Mungu? Haki yako ikoje?
Mungu aonyeshavyo haki yake
Mara mbili imeandikwa kuhusu Mungu kuonyesha haki yake. Mara ya kwanza ni hapo alipomweka Yesu kuwa “kiti cha rehema”. Mara ya pili ni wakati sisi tunapokuja kwenye kiti hicho, yaani, kumpokea Yesu kwa imani. Hapo Mungu anaonyesha haki yake akituhesabia Kristo Yesu kama haki yetu. Maana yake, haki yetu ni ya kigeni, siyo haki inayofungamana na sisi na maisha yetu, bali Yesu ndiye haki yetu.
Mada kuu 1. Hali yetu mbele za Mungu
Twahitaji kuokolewa kwa sababu - sote tumefanya dhambi (m.23) - hakuna sheria iwezayo kuhuisha uhusiano wetu na Mungu na kutufanya wenye haki (Rum 3:20; Gal 3:21) - toba na moyo mnyenyekevu haviokoi, maana si haki kuachilia tu dhambi (m.25-26; Rum 6:23)
Kwa wote waaminio
2. Injili inadhihirisha haki ya Mungu
Injili ni habari njema kwamba sote tuna nafasi ya kuhesabiwa haki kwenye kiti cha rehema cha Mungu, na kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu (ling. Tit 3:7). Inatuelekeza kumtegemea Kristo pekee, “hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki” (Gal 2:16). M.27-28 inahitimisha kwa kusisitiza kuwa hatuna sababu ya kujisifu kwa matendo yetu, kwani “huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria” (m.28). Ufalme wa Mungu ni haki kwa sababu msingi wake ni Kristo na kazi yake ya ukombozi. Ni haki “pasipo sheria” (3:21), lakini si kinyume na sheria, maana haki ile tunayodaiwa na sheria ya Mungu ilitendeka Yesu alipowekwa kuwa upatanisho.
- Aliionyesha alipomweka Yesu kuwa upatanisho (= kiti cha neema; m.25) - Anaionyesha anapomhesabia haki yeye amwaminiye Yesu (m.26; ling. Rum 4:5) 3. Twahesabiwa haki kwa imani
- Imani ni “pasipo matendo ya sheria” (m.28); madai ya sheria yalitendeka Yesu alipowekwa kuwa upatanisho - Imani ni “bure” (m.24) kwetu; Mungu ameshalipa gharama yote ya ukombozi - imani ni kuacha kujitegemea na kumtegemea Yesu pekee Hitimisho
- Haki ni ya kigeni, maana sisi hatuna ya kwetu, bali twahesabiwa haki na Mungu - Haki ni ya neema – ndivyo Mungu alivyoonyesha Golgatha na anavyoendelea kuonyesha anapowahesabia waovu haki (Rum 4:4-5) - Haki yapokelewa kwa imani katika Yesu ambaye ndiye haki ya Mungu.
Samwel Nyanda 11
KANISA LA NYUMBANI
RIZIKI TOLEO 3, 2026
KANISA LA NYUMBANI
RIZIKI TOLEO 3, 2026
Kuanzia haki hadi uwajibikaji katika yote Uhai mpya ni kitu maalumu, muujiza. Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa waliowazaa. Zawadi hii amewapa wazazi, ili watoto wawe na mahali maalumu penye nafasi ya pekee ya kukua kwenye mazingira ya upendo, usalama na kujifunza. Kama wawakilishi wa Mungu, wazazi ndio waliokabidhiwa wajibu huo, wakati Mungu mwenyewe yupo tayari kuwawezesha kuutekeleza. Pia ameweka jamaa, walezi, walimu na jamii kwa ujumla ili kuwasaidia wazazi.
Ulinzi dhidi ya madhara ya kimwili, kisaikolojia na kiroho ni wa lazima ili mtoto ajifunze vizuri. Maisha yanayompendeza Mungu huhitaji mazingira yenye haki, amani na furaha ili yajengwe na kukomaa. Kupitia elimu ya muda mrefu na mifano mizuri ya kuigwa, lengo ni kwamba mtoto awezeshwe kuwa mtu wa kujitegemea anayeshiriki kwa hiari yake katika maendeleo ya maisha ya kijamii.
malezi, ni lazima waheshimu na kuhakikisha haki za mtoto wao kwa kumpa kila kitu anachohitaji. Hatimaye, safari hii inapofikia mwisho na mtoto amekuwa kijana, bado wanapaswa kumwombea na kumpa ushauri na maarifa mazuri anapoomba msaada wao, lakini jukumu lao la kwanza ni kumruhu-
su aamue maisha yake mwenyewe katika nyanja zake zote. Heshima kubwa kwa wazazi ni pale lengo hili linapofanikiwa, na mtoto wao amekua hadi kuwa kijana anayemtumikia Mungu na kuwa baraka kwa watu wote. Riziki
Wajibu tunakulia kuushika
Tofauti na haki, wajibu hauji mara moja. Mtoto mchanga hawajibiki, ni mpokeaji Kama watu wote wengine, watoto nao tu. Huku haki ni kitu tunachozaliwa nawana haki za kiroho, binafsi na kimwili. cho, majukumu tunaongezewa kidogo Zawadi hii ya Mungu kidogo kulingana na wamezaliwa nayo. tunavyokua kimwili na Hutokana na hadhi kiakili. “Jambo muhimu yao kama viumbe waKwanza mtoto awatii lioumbwa kwa mfano katika ukuaji huu wa wazazi wake katika yote, wa Mungu, na jamii mtoto ni kujifunza lakini kadiri anavyokua yoyote inayowajibika anazidi kuwa na haki ya kwamba haki ya hutafuta kuziheshimu kuamua juu ya maisha haki hizo kupitia sheria uhuru na uwajibikaji yake mwenyewe. za nchi. Jambo muhimu huenda sambamba.” katika Haki ya kwanza ukuaji huu waliyo nayo watoto ni wa mtoto ni kujifukumjua Muumba wao na maisha yale ali- nza kwamba uhuru huenda sambayowakusudia kuishi hapa duniani. Malezi mba na wajibu. Lengo ni kwamba ya kweli hayaishii kuwapatia chakula na ajifunze kuelewa jamii na mazingimavazi. Watoto wajifunze na kuwezeshwa ra yake na kuwezeshwa kutumia vipawa kushiriki kama watu huru katika jamii ya vyake alivyozaliwa navyo ili aweze kukibinadamu, ambapo wote wanaheshimi- jitegemea katika yote afikiapo utu uzima ana, kujaliana na kusaidiana katika mfu- na kumtumikia Mungu kwa kuchangia mo wa kupokea na kutoa matendo ya upe- kwenye maendeleo ya familia na jamii. ndo. Haki yafungamana na kumtendea Wazazi wana jukumu kuu katika kila mtu kwa usawa. mchakato huu. Mwanzoni mwa safari ya Haki twazaliwa nayo
12
13
JAMII
RIZIKI TOLEO 3, 2026
JAMII
RIZIKI TOLEO 3, 2026
Haki ni wajibu Makala hii itahusu haki ya kijamii. Katika ulimwengu wa sasa, dhana ya haki mara nyingi huchukuliwa kama madai ya kupokea kutoka kwa wengine au kutoka kwenye mifumo ya kisheria. Nabii Mika anabadilisha mtazamo huu kabisa katika kitabu chake. Anatukumbusha kuwa msingi wa haki ya kijamii sio kitu tunachoweza kudai tu, bali ni wajibu mkuu ambao kila mmoja wetu amepewa na Mungu. Mika anasema: “Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako?” (Mik 6:8)
Kama mfano wa kwanza wa wajibu huo wa kutenda haki, Mika anataja kuishi kwa uaminifu. Humaanisha usawa kwa wote, yaani, kumpa kila mtu kile anachostahili bila ubaguzi. Wajibu huu unajitokeza katika maeneo yote ya maisha, kuanzia maisha ya kila siku hadi ya uongozi wa nchi, kama tunavyokumbushwa katika Mit 14:34: “Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote”. Kiongozi anayetenda haki hapokei rushwa wala hana ubaguzi, mfanyabiashara mwenye haki hatumii vipimo vya uongo wala kuuza bidhaa iliyoharibika, na raia atendaye haki analipa kodi zake na kuheshimu sheria za nchi. Na bila kujali hali ya kijamii ya watu, kila mmoja anawatendea haki majirani zake na jamii nzima inayomzunguka. Au vipi? Tukumbuke kwamba haki haitafutwi kwa maneno au kwa kusema “haki, haki”, bali kwa vitendo vya kila siku vinavyoonesha uadilifu, nidhamu na upendo. Hebu tuangalie siri ya kuishi namna hiyo.
Haki ni suala la vitendo
Maneno haya ya Nabii yanabeba siri kubwa ya jinsi mwanadamu anavyopaswa kuishi na kushirikiana na wengine.
Siri na.1: Hofu ya Mungu
Neno la Mika linahusu haki ya kijamii, haki miongoni mwa wanadamu. Hata hivyo Nabii anatukumbusha kwamba msingi wa haki uko 14
sehemu nyingine: “Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki”. Uadilifu na upendo huo unaotakiwa ili haki itendeke katika jamii, hutokana na hofu ya Mungu. Ni tunda la “kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako”. Unyenyekevu mbele za Mungu unamaanisha kutambua kuwa sisi si kitu bila Yeye, wala si kitu bila jirani yetu na jamii ile tunamoishi. Ni kutambua kwamba mamlaka, mali na akili tulizo nazo, zote ni zawadi kutoka Mungu; na kwamba nyingi kati ya zawadi hizi tumepewa kupitia watu wengine na kutokana na kuishi katika jamii yenye haki. Matokeo ya kutambua hivyo ni unyenyekevu, na unyenyekevu hutuepusha na kiburi ambacho huzaa tu vitendo vilivyo aibu kwa mtendaji mwenyewe na mzigo kwa wengine wote. Mnyenyekevu huacha kutumia nguvu zake kuwadhulumu, kuwaonea na kuwakandamiza wengine, au hata kuwaondoa kabisa.
kusamehe wale waliokosea na kuwasaidia wale waliotenda kwa nia nzuri ila wakashindwa kufikia kiwango fulani. Kupenda rehema ni kuwa na moyo wa huruma unaotafuta uwezekano wa kurejesha amani badala ya kuadhibu tu. Ni sehemu ya wajibu wetu wa kijamii kuangalia mahitaji ya wengine kwa jicho la upendo, ukarimu na utu. Tuwe tayari kunyoosha mkono ili kutoa msaada; na tupaze sauti pale ambapo sheria inatumika vibaya kuwanufaisha wenye nguvu na kuwakandamiza wanyonge. Haijawahi kuwa lengo la sheria yoyote ya haki kuhalalisha vitendo hivyo vibaya. “Amekuonyesha yaliyo mema”
Haki ya kijamii si suala la kusubiri kufanyiwa na wengine, wala hatuna haja ya kupitia mafunzo mengi kwanza. Nabii Mika anasema kwamba Mungu ameshatuonyesha yaliyo mema. Ndivyo alivyofanya katika Biblia, lakini pia kwa jinsi alivyotuumba na kututendea katika maisha yetu. Sheria za haki na hukumu za haki ni muhimu sana, lakini haki ya kijamii huanzia mahali pengine, yaani katika mioyo ya kila mmoja wetu. Basi, tukitaka haki itendeke, haki hii ni wajibu wetu wenyewe, na kuwajibika vizuri huanzia kwenye hatua ya unyenyekevu. Tunapotenda kwa haki na kupenda kuonesha rehema, tunachangia kwenye ujenzi wa jamii yenye usawa, amani na upendo wa kweli. Na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema?
Siri na.2: Rehema
Nabii Mika hadai tu haki itendeke, anasema pia kwamba “kutenda haki” hufungamana na “kupenda rehema”. Huwa tunahusisha haki na sheria zinazotudai matendo fulani, na kwamba lazima mtu adhibiwe anapozivunja. Ndivyo ilivyo katika jamii zote. Lakini haki bila rehema ni kali, na mara nyingi matokeo yake ni maumivu kuliko haki, kwa sababu tunasahau rehema tunapofuatilia haki. Tunasahau kwamba twapaswa kuwa jibu la vilio vya wanyonge na maskini wanaokandamizwa. Rehema inatufundisha kuwa na huruma, yaani, kutafuta uwezekano wa
Mwl. Magreth Mushi 15
RIZIKI TOLEO 3, 2026
Maisha Mazuri kwa Watoto Kila mtoto anastahili malezi bora, upendo na maisha yenye kusudi. Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, lakini kuwalea vizuri ni jukumu letu. Maisha Mazuri kwa Watoto ni kitabu kinachomsaidia mzazi na mwalimu kutafakari na kujifunza namna ya kumlea mtoto katika upendo, hekima, ulinzi na maadili mema. Ni mwongozo wenye msaada kwa wote wanaowalea watoto. Pata nakala yako dukani Soma Biblia.
Kristo Haki Yetu Kitabu kizuri kwa sala ya binafsi au sala ya kifamilia. Masomo yake 31 ni chakula bora na cha kiroho kwa moyo wako. Ukikisoma utazidi kumpenda Yesu.
SOMA BIBLIA 0759 544 917 S.L.P. 2696, Arusha editor.somabiblia@gmail.com www.somabiblia.or.tz
Soma RIZIKI “online”
www.issuu.com/riziki