MTAMBO WA KUCHEMSHA MAJI KUTUMIA NISHATI YA JUA
KIELEKEZO CHA MWENYEWE
Yaliyomo
Mwongozo
3
Mwongozo............................................................................................3 Ujumbe za Usalama.............................................................................4
Maarifa ya Udhamini
Sheria za Udhamini..............................................................................6 Muda wa Udhamini...............................................................................6 Mwisho wa Dhima.................................................................................7 Yasiyokuwepo katika Udhamini............................................................7
Maelezo ya Bidhaa
6
8
Mwongozo............................................................................................8 Vipengele Vikuu....................................................................................9
Maagizo ya Utumizi
11
Skrini ya Kontrola...............................................................................11 Kuanza................................................................................................12 Kuwasha Mtambo...............................................................................12 Jinsi ya Kulipa / Kuongeza Credits.....................................................13 Jinisi ya kuangalia msalio wa Credits kutumia SMS..........................15 Utendaji wa Mtambo..........................................................................15
Maagizo ya Kudumisha
Maagizo ya Kudumisha......................................................................17 Vidokezo kwa Matokeo Bora..............................................................18
1
17
Yaliyomo
Utatuzi wa Shida
Shida za Kontrola...............................................................................19 Shida za Credits..................................................................................19 Utatuzi wa Shida za Mtambo..............................................................19
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara.............................................20
Maarifa ya Malipo
Chaguo A...........................................................................................21 Chaguo B...........................................................................................21
Anwani za Mawasiliano
Nambari ya Customer Care................................................................21 Nambari ya SMS (Bure)......................................................................21 Barua Pepe.........................................................................................21
19
20 21 21
2
MWONGOZO Asante kwa kununua mtambo wa kuchemsha maji kwa nishati ya jua ya ComIN iliyoundwa na BOSCH. Kielekezo hiki kinaelezea vipengele vikuu vya mtambo huu, jinsi ya utumizi, uwekaji na utatuzi wa shida unazoweza kuambatana nazo. Kwa maarifa zaidi, tafadhali piga simu kwa nambari ya Customer Care ya M-KOPA 0707 333 222 ama utume ujumbe bure wa SMS kwa 22363. Nambari ya Customer Care inapatikana 24/7. Tafadhali soma kijitabu hiki chote kabla ya kutumia kipengele chochote.
Yalitomo katika Mtambo wa Kuchemsha Maji kutumia Nishai ya Jua 5
4
3
2
8 7
1
3
6
1 Tenki ya maji baridi
5 Lango la kuthibiti maji
2 Pampu
6 Kontrola ya M-KOPA
3 Kikusanyo cha nishai ya jua
7 Solar panel
4 Tenki ya maji moto
8 Fremu
Ujumbe za Usalama
Kukosa kufuata maagizo yaliyomo katika kijitabu hiki kunaweza kusababisha uharibifu wa mali, kuumia au kuondolewa kwa udhamini wa bidhaa.
Usiwahi kubali Kontrola ya M-KOPA kugusa maji au itaharibika na kuweza kusababisha kuumia. Ikiwa Kontrola ya M-KOPA itashika maji, izime mara moja, toa maji yoyote na uiwache ikauke kabisa kabla ya kutumia tena.
Usichaji Kontrola ya M-KOPA bila kuikinga kutoka kwa jua kwa sababu betri inaweza kuharibika.
Usiwahi fungua au kujaribu kufanyia kipengele chochote ukarabati kwa sababu inaweza kusababisha kuumia, kuharibu mtambo na kuondolewa kwa udhamini wa bidhaa.
4
Maarifa ya Usalama
Ikiwa Kontrola ya M-KOPA itapata joto jingi zaidi inapochaji, itoe kwa chaja mara moja na pigia Customer Care simu kwa 0707 333 222 au tuma UJUMBE BURE kwa 22363.
Unganisha Kontrola ya M-KOPA kwa solar panel iliyothibitishwa na M-KOPA pekee. Kukosa kufuata maagizo haya kunaweza sababisha kuumia au kuharibika kwa Kontrola ya M-KOPA.
Utakapogundua hitilafu kwa bidhaa, tafadhali pigia Customer Care simu kwa 0707 333 222 au tuma UJUMBE BURE kwa 22363.
TAHADHARI!
Sehemu zifuatazo zinaweza kupata joto sana na huenda zikasababisha majeraha zikiguswa: - Kikusanyo cha nishai ya jua. - Tenki ya maji moto. - Maji moto kwenye mabomba na mfereji. - Mabomba amabayo hayajafunikwa na insulation.
5
MAARIFA YA UDHAMINI Sehemu hii inaelezea kuhusu sharti na sheria za udhamini wa bidhaa.
Sheria za Udhamini Kwa madai ya udhamini, lazima: ●• Bidhaa zikaguliwe na BOSCH kuhakikisha kwamba hitilafu ya mtambo imesababishwa na makosa katika kuundwa au vifaa vilivyotumika, katika muda wa udhamini. • Hakuna jambo lolote limefanyika ambalo limeondolewa kwa udhamini.
Muda wa Udhamini Muda wa udhamini ni MIAKA TATU (3) kutoka siku ya kununua bidhaa kwa vipengele hivi vya mtambo wa kuchemsha maji kutumia nishai ya jua: 1. Kikusanyo cha nishai ya jua 2. Tenki ya maji moto 3. Lango la kupitihsa maji 4. Thermo-mixing valve 5. Fremu 6. Mabomba ya maji na viunganishi Muda wa udhamini ni MIAKA MBILI (2) kutoka siku ya kununua bidhaa kwa vipengele hivi vya mtambo wa kuchemsha maji kutumia nishai ya jua: 1. Waya zote 2. Kontrola ya M-KOPA 3. Solar panel
6
Mwisho wa Dhima Udhamini ulioelezwa hapo juu ndio dhima yetu kamili. Kuongezea, BOSCH inakataa kukubali dhima yoyote kwa ajili ya uharibifu wa mali au majeraha yoyote yatakayotokea.
Yasiyokuwepo katika Udhamini Yafuatayo hayapo kwenye udhamini wa bidhaa: 1. Uharibifu wowote unaosababishwa na: • ‘Matendo ya Mungu’ au sababu lolte ambalo BOSCH haliwezi tawala. • Utumizi vibaya wa vipengele vya mtambo, pamoja na matumizi ya mtambo kwa kusudi lolote lisilo la kawaida kulingana na maagizo ya BOSCH. • Uhifadhi au utumizi vibaya wa vifaa vya mtambo. • Kuunganisha kwa nguvu za umeme isiyostahili. • Kujaribu kutengeneza au kufanyia ukarabati na mtu yeyote isipokuwa fundi waliothibitishwa na BOSCH. 2. Vifaa au vipengele vya mtambo vinavyoonyesha dalili za kufanyiwa ukarabati isiyostahili. 3. Vipengele vya mtambo ambavyo nambari ya serial imebadilishwa, imetolewa au kuharibiwa kiwango cha kukosa kusomeka. 4. Kusiha na kuzeeka kwa vipengele vya mtambo ya kawaida kwa muda, isipokuwa vipengele vinavyoonyesha dalili ya hitilafu katika uundaji.
7
MAELEZO YA BIDHAA
Kiunganishi cha bomba
Tenki la maji moto
Fremu
Bomba liliokingwa kupoteza joto
Kikusanyo cha nishai ya jua
8
Vipengele vya mtambo wa kuchemsha maji kutumia nishai ya jua Yaliyomo: 1. Kikusanyo cha nishai ya jua. 2. Tenki ya maji moto. 3. Kontrola ya M-KOPA, pamoja na PV panel. 4. Lango la kudhibiti maji. 5. Mabomba na viunganishi. 6. Fremu.
Kikusanyo cha nishai ya jua.
Tenki ya maji moto.
Kontrola ya M-KOPA
Chumba cha kuhifadhi Kontrola
9
Solar Panel
Mabomba na viunganishi
Waya
Lango la kudhibiti maji
Fremu
Pampu
Mahali msukumo wa maji hautoshi, mtambo unaambatana na pampu ili maji yaweze kupigwa kwenye tenki.
10
MAAGIZO YA UTUMIZI Skirini ya Kontrola ya M-KOPA Mwunganisha wa Kontrola ya M-KOPA na mitambo bora ya wakati ujao Chaji ya betri
Nguvu ya mtandao Kidude cha M-KOPA - kinaunganisha kwa mtandao - bonyeza kwa sekunde moja kuangalia credit
Kidude cha TV - bonyeza kidogo: zima mtambo wa kuchemsha maji - bonyeza sana: onyesha maarifa ya akaunti
Credits - Number of days device has been paid for and will work
Icon ya TV Imekatwa Inaunganisha Imeunganishwa
Idadi na tarehe ya malipo ya mwisho kwa M-KOPA
Tarehe credits zilizowekwa zinaisha
11
Idadi ya deni
Kuanza
Baada ya fundi wa BOSCH kumaliza kuweka mtambo wa kuchemsha maji, tafadhali chaji Kontrola ya M-KOPA kwa muda wa masaa 8. Kuchaji Kontrola, unganisha waya wa solar panel kwenye shimo la Kontrola llilio na icon ya jua. Hakikisha solar panel imewekelewa sawasawa kwenye paa au mahali popote pasipo na kivuli ndio iweze kupokea milae ya jua vizuri siku yote. Kuchaji itakapokamilika, icon ya betri itabadilika kutoka laini iliyovunjikavunjika na ikawa laini kamili. Laini iliyovunjikavunjika inaonyesha kwamba betri haijachaji kwa muda wa masaa 8.
Laini iliyo kamili inaonyesha kwamba betri imechaji kwa muda unaostahili wa masaa 8 na Kontrola iko tayari kutumiwa.
Baada ya kuchaji Kontrola kwa muda wa masaa 8, unganisha waya wa kuchemsha maji kwa shimo la TV ulio upande wa kulia wa panel.
Kuwasha Mtambo 1. Angalia credit zilizosalia kwa kubonyeza kidude cha M-KOPA kwenye Kontrola. 2. Bonyeza kidude cha TV kuwasha mtambo wa kuchemsha maji.
12
Jinsi ya Kulipa / Kuongeza Credits Malipo yanawezwa fanywa kutumia akaunti yoyte ya M-PESA. Futa maagizo yafuatayo ya kulipa au kuongeza credits.
1.
2.
Fungua orodha ya M-PESA (Safaricom SIM Toolkit) kwenye simu.
3.
4.
Bonyeza ‘Pay Bill’.
13
Bonyeza ‘Lipa na M-Pesa’.
Bonyeza ‘Enter Business No‘.
5.
6.
Weka business number ya M-KOPA: 333222.
Bonyeza ‘Account no.’
7.
8.
Weka nambari ya akaunti yako ya M-KOPA. Nambari hii ni kitambulisho ulichotumia kusajili na M-KOPA.
Weka idadi ya pesa unayotaka kulipa. Mfano: 500.
9.
Weka PIN yako ya M-PESA kisha bonyeza ‘OK’
10.
Hakikisha maarifa yote yako sawa kisha bonyeza ‘Send’ au ‘OK’.
14
11. 12. 13. 14.
Utapokea ujumbe wa SMS kutoka M-PESA ulio na maarifa ya malipo. Utapokea ujumbe wa SMS kutoka M-KOPA unaohakikisha idadi mpya ya credits zako. Credits zako mpya zitaonyeshwa kwenye skrini ya Kontrola katika muda wa masaa 24. Baada ya kupoea ujumbe wa SMS kutoka M-KOPA, bonyeza kidude cha M-KOPA kwa sekunde 1 kuonyesha idadi mpya ya credits.
KUMBUKA: USIWAHI lipa cash kwa mtu yeyote unapofanya malipo au kongezea credits. M-PESA ndio njia PEKEE ya kufanya malipo kwa M-KOPA.
Jinsi ya kuanagalia msalio wa M-KOPA kutumia SMS 1. 2.
Tuma ujumbe wa SMS ulio na neno ‘BAL’ kutoka nambari yako ya simu iliyosajiliwa na M-KOPA kwa nambari 22363. SMS kwa hii nambari ni bure. Subiri ujumbe wa kukujibu kutoka M-KOPA.
Utendaji wa Mtambo Utendaji wa mtabo unategemea eneo na hali ya hewa.
Eneo
Eneo linalofaa kuweka mtambio wa kuchemsha maji ni mahali pasipokuwa na kivuli. Pia, kikusanyo cha nishai ya jua inafaa kuwa inaangalia aidha kaskazini au kusini na sio mashariki au magharibi ili iweze kupokea miale ya jua siku yote.
Siku za Jua Utendaji wa mtambo ni bora kabisa siku zilizo na jua siku yote. Joto la maji linalotarajiwa ni kufikia 60°C.
15
Siku zilizo na Mawingu Kiasi Utendaji wa mtambo ni umepunguzwa kidogo kwa sababu ya mawingu yanayozuia miale ya jua. Joto la maji linalotarajiwa ni kufikia 50°C.
Siku zilizo na Mawingu au Mvua Kidogo Utendaji wa mtambo ni umepunguzwa zaidi kwa sababu miale ya jua yamezuiliwa. Joto la maji linalotarajiwa ni 40-50°C.
Siku zilizo na Mawingu bila Jua Utendaji wa mtambo ni umepunguzwa sana kwa sababu ya mawingu yanayozuia miale ya jua. Joto la maji linalotarajiwa ni 20-35°C.
Siku za Mvua Bila Jua Utendaji wa mtambo umeadhirika kabisa kwa sababu hakuna miale ya jua yanayoifikia. Hakuna maji yatakayochemshwa kwa hivyo joto la maji linalotarajiwa ni baridi au joto sawa na maji yaliyomo kwanye tenki ya maji baridi.
16
MAAGIZO YA KUDUMISHA Solar panel na kikusanyo cha nishai ya jua zinafaa kupanguzwa mara kwa mara ili kuondoa vumbi na chembe zinazoweza kuadhiri utendaji wa mtambo wa kuchemsha maji.
Solar panel na kikusanyo cha nishai zinafaa kuwekwa kwenye eneo wazi lisilo na kivuli chochote.
Ikiwa mtambo wa kuchemsha maji hautatumiwa kwa muda mrefu, funika kusanyo cha nishai kutumia kitambaa, turubai au plastiki isiyopitisha mwangaza ili kuzuia joto jingi kutokana na miale ya jua.
Kagua mabomba na viunganishi vyao mara kwa mara ili kutambua sehemu zinazoweza kuwa zinavuja maji.
17
Vidokezo kwa Matokeo Bora 1. Funga solar panel yako vizuri ili isipotee. 2. Panguza solar panel angalau mara moja kwa wiki ili kutoa vumbi na chembe zinazowea kuadhiri kuchaji kwa betri ya Kontrola.. 3. Credit moja ya M-KOPA linaweza kutumika kutoka saa sita usiku hadi saa sita usiku ya siku inayofuata. Hakikisha kwamba una credit za kutosha ili usikatizwe kutoka huduma la maji moto. 4. Hakikisha kwamba una salio ya angalau credit moja wakati wote ili upate maji moto. 5. Fanya malipo inavyostahili kulingana na mradi wa kulipa uliochagua. 6. Unavyolipa haraka ndivyo utakavyoweza kutumia mtambo wako wa kuchemsha maji BURE kwa haraka. 7. Lipa haraka ili umiliki mtambo kwa haraka na upewe punguzo ya bei kwa kumaliza malipo mapema. Ni muhimu kudumisha kufanya malipo wakati unaofaa ili uwe na rekodi bora ya malipo. 8. Kumbuka kununua credits mapema ili uweze kutumia huduma ya maji moto kwa muda mrefu uwezekanavyo kwa siku.
18
UTATUZI WA SHIDA Tatizo Hakuna maji
Linaweza Kusababishwa na
Hatua ya kuchukua
Hali ya hewa – mawingu au mvua
Hakuna la kufanya
Ukosefu wa maji
Chunguza supply ya maji
Lango la kuthibiti maji limefungwa
Chunguza ikiwa umenunua credits
Maji hayapiti kwa mabomba
Pigia Customer Care kwa 0707 333 222
Shida na
Ukosefu wa umeme
Pigia Customer Care kwa 0707 333 222
Kontrola
Hitilafu za kiumeme
Pigia Customer Care kwa 0707 333 222
moto
Tatizo Umelipa lakini credits
Linaweza Kusababishwa na
Hatua ya kuchukua
Credits hazisahihiki
Pigia Customer Care kwa 0707 333 222
Hali isiyostahili
Pigia Customer Care kwa 0707 333 222
bado hazionekani kwa Kontrola Skrini ya Kontrola haionyeshi chochote
19
MASAWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA 1.
Nitafanyaje ikiwa nimelipia credits kutumia M-PESA lakini Kontrola yangu haionyeshi malipo niliyofanya?
Ikiwa umelipia angalau credit ya siku moja kwa M-KOPA kutumia M-PESA, Kontrola inafaa kusahihisha idadi ya credits yenyewe katika muda wa masaa 12. La sivyo, tafadhali hakikisha kwamba umepokea ujumbe unaothibitisha malipo kutoka M-KOPA na pia M-PESA, na kwamba maarifa yote ya malipo yalikuwa sawa. Unaweza bonyeza kidude cha M-KOPA utakapopata ujumbe kutoka M-KOPA ili Kontrola lionyeshe salio la credits sahihi. Usipofaulu, pigia Customer Care simu. 2.
Niko na salio ya credits kwenye Kontrola yangu lakini mtambo wa kuchemsha maji haufanyi kazi.
Hakikisha kwamba Kontrola yako ina chaji ya kutosha, ilichaji kamili kwa muda wa masaa 8 (icon ya betri ni laini kamili wala sio kuvunjikavunjika), salio ya credit inaonekana kwenye skrini ya Kontrola na solar panel imaunganishwa. Iwapo bado kuna tatizo, pigia customer care kwa nambari 0707 333 222. 3.
Kontrola yangu itapokea credits kutoka kwa nyumba?
Kontrola yako ya M-KOPA inafaa iwe na mwunganisho kwa mtandao mahali popote simu ya kawaida inaweza kushika mtandao. Ikiwa mtandao wa Safaricom ni duni mahali ulipo, tafadhali piga simu kwa agenti wetu wa customer care ili usaidiwe. 4.
Nitafanya nini maji yakiwacha kuchemshwa?
Kwanza, chunguza hali ya hewa. Pia, hakikisha kwamba Kontrola yako ina idadi ya angalau credit moja. Iwapo shida haitatatulika, piga simu kwa nambari ya customer care ama utume ujumbe kwa nambari ya SMS ya customer care na utahudumiwa.. 5.
Je, mtambo wangu una udhamini?
Ndio. Vipengele kuu vina udhamini wa muda wa miaka 3. Kontrola na solar panel zina udhamini wa muda wa miaka 2.
20
MALIPO
Ukubwa:
Chaguo A (lita 200)
Chaguo B (lita 300)
Deposit:
KES 20,000
KES 30,000
Malipo:
KES 16,500 kila mwezi
KES 19,500 kila mwezi
Kiasi ya Micro-Payment:
KES 198,000
KES 234,000
Muda:
Miezi 12
Miezi 12
Jumla ya Gharama:
KES 218,000
KES 264,000
ANWANI ZA MAWASILIANO
Nambari ya Customer Care: 0707 333 222 Nambari ya SMS: 22363 (bure) Barua pepe: customercare@m-kopa.com
21