1 minute read

Siku ya Sabato

Baraka kuu zinafumbatwa katika utunzaji wa Sabato, na Mungu anatamani kwamba siku ya Sabato iwe siku ya furaha. Kulikuwa na furaha katika kuanzishwa kwa

Sabato. Mungu alitazama kwa kuridhika kazi ya mikono yake. Vitu vyote Alivyovifanya Alivitamka “vizuri sana.” Mbingu na nchi zilijawa na furaha. "Nyota za asubuhi ziliimba pamoja, na wana wote wa Mungu walipiga kelele kwa furaha."

Ingawa dhambi imeingia ulimwenguni ili kuharibu kazi yake kamilifu, Mungu bado anatupa Sabato kama ushuhuda kwamba Mmoja muweza wa yote, asiye na kikomo katika wema na rehema, aliumba vitu vyote. Baba yetu wa mbinguni anatamani kupitia utunzaji wa Sabato kuhifadhi miongoni mwa wanadamu ujuzi juu Yake. Anatamani kwamba Sabato ielekeze mawazo yetu kwake kama Mungu wa kweli na aliye hai, na kwamba kupitia kumjua Yeye tupate uzima na amani.

Hazina za Ushuhuda III, 16

Ellen G. White

This article is from: