

KITABU CHA MWAFAKA
CONCORDIA
1530
Kitabu Cha Mwafaka
Swahili Book of Concord
2nd edition printed 10,000 copies, October 2025
Copyright © 2011 Lutheran Heritage Foundation

Lutheran Heritage Foundation 51474 Romeo Plank Road Macomb, Michigan 48042, USA
www.LHFmissions.org info@LHFmissions.org
Translated from German and Latin texts.
The translation and publishing of this book has been made by Lutheran Heritage Foundation. All rights reserved. No part of this book may be reproduced, stored in a retrieval system, or transmitted, in any form or by any means, electronic, mechanical, photocopying, recording, or otherwise, without the prior written permission of Lutheran Heritage Foundation.
Funding for the publication of this volume was made possible by a grant from The Roy D. and Ingaborg G. Randolph Memorial Endowment Fund and the churches and individuals of the Lutheran Church-Missouri Synod Rocky Mountain District Longs Peak Circuit. Soli Deo Gloria!
To obtain more copies please contact: info@LHFmissions.org
LUTHERAN HERITAGE FOUNDATION - AFRICA
P.O. BOX 521 - 00502, KAREN, NAIROBI, KENYA
ISBN: 978-9914-713-00-8
Not for commercial use.
UTANGULIZI WA KITABU CHA MWAFAKA
Kitabu hiki kinaitwa “KITABU CHA MWAFAKA” kwa sababu ni mkusanyiko wa kiri tofauti za imani, ambazo huonyesha “mwafaka,” yaani, maafikiano ya mafundisho ambayo Kanisa la Kilutheri liliyahitimisha katika misingi ya Kibibilia wakati wa Matengenezo ya Kanisa na miongo iliyofuatia. Kwa kawaida, haya yalifanyika baada ya majadiliano mazito na mazungumzo marefu. Imekuwa hivyo daima katika historia ya Kanisa la Kikristo kwamba, popote Injili inapoangaza na Mungu anapopanda mbegu zake, Ibilisi hujaribu kupandikiza magugu yake. “KITABU CHA MWAFAKA” kilichapishwa mwaka wa 1580.1 Kinakuza na kufafanua ukweli muhimu na bora mno wa Injili na hazina ya mafundisho ambayo Luther na washirika wenzake waliyavumbua. Wale wote waliotaka kubaki kuwa waaminifu, waliuunga mkono urithi huu wa thamani.
Kwa sababu hiyo, Kiri za Kilutheri zilizomo katika kitabu hiki zina cheo na mamlaka ya kanuni za mafundisho ya Kanisa la Kilutheri. Hii ndiyo sababu, wakati wa kubarikiwa au kusimikwa kuwa wachungaji au kuwa wahudumu fulani wa Neno la Mungu katika Kanisa la Kilutheri, wanatakiwa kuiweka nadhiri. Hii inamaanisha kuwa, wanaahidi kwa unyenyekevu kwamba, kwa msaada wa Mungu,watafanya hivyo, na watakuwa waaminifu daima, siyo tu kwa Maandiko Matakatifu, bali pia kwa Kiri za Kanisa la Kilutheri. Kwa maneno mengine, wanaahidi ya kwamba, watahubiri na watafundisha daima kwa kufuatana na mafundisho ya Biblia jinsi yalivyoelezwa kinaganaga katika maandiko haya. Hii ni kwa sababu wanakubali na kukiri ya kwamba, Kiri za Kilutheri ni maelezo sahihi na ya wazi kulingana na yale ambayo Mungu ameyafunua katika Biblia.2
Kuna sehemu mbili katika “KITABU CHA MWAFAKA.” Sehemu ya kwanza
1 Inasemekana kwamba, Matengenezo ya Kilutheri yalianza mwaka wa 1517, wakati Martin Luther alipogongomelea hoja zake maarufu kwenye mlango wa Kanisa la Ngome kule Wittenberg ziitwazo “Hoja 95 zilizohusu Uweza wa Vyeti vya Upatanisho.” Yeye na wafuasi wake walikuwa karibu kuikiri na kuitetea imani yao hadharani. Walifanya vile katika hati tofauti ambazo kirasmi, zilichukuliwa na Walutheri kama Kiri zao za Imani. “Shauri la Mwafaka,” ambalo ni la mwisho, liliandikwa na kukubaliwa mwaka wa 1577. Kwa hiyo, kitabu kizima kilikuwa tayari kuchapishwa mwaka wa 1580. Kilitolewa rasmi tarehe 25, Juni mwaka huo, wakati wa maadhimisho ya ukumbusho wa miaka hamsini ya Ukiri wa Augsburg uliokuwa umetokea mwaka wa 1530.
2 Theologia ya Kilutheri hufundisha kwamba, Maandiko Matakatifu ndizo kanuni za mafundisho zinazoelekeza. (Kilatini: “Norma normans”) Huku Kiri zikiwa ni kanuni zilizoelekezwa (Kilatini: “Norma normata”). Kwa maneno mengine: Maandiko Matakatifu ndiyo kaida kuu na yenye mamlaka ya ukweli. Hata hivyo, hata kiri ni kanuni za kiwango cha pili lakini mafundisho yayo yanakubaliana kabisa na mafundisho ya Biblia.
Hii ndiyo sababu hayaonekani katika matini ya katekisimo jinsi yanavyoonekana katika “Kitabu cha Mwafaka.”
Luther alikuwa ameandika katekisimo zake kwa sababu alitaka ujumbe wa Biblia ujulikane kanisani, shuleni, na nyumbani mwa waumini. Zilitekeleza dhima maalumu kwa mujibu wa mafundisho ya Kikristo, lakini hakuzilazimishia kwao. Aliliacha Kanisa liwe huru kuzitumia njia na vifaa vingine ikiwa lilitaka kufanya hivyo, mradi tu lifundishe ukweli. Lakini vitabu hivi viwili vilijulikana kwa haraka sana na vikawa na sifa kubwa. Haraka sana, Makanisa ya Sachsen na kwingineko yaliweka masharti katika katiba zao kwamba, ilipasa vitabu hivyo vitumiwe kama miongozo ya kufundishia. Katika mazungumzo yao kuhusu mafundisho ya uongo na makosa ambayo yalijaribu kuingia katika Kanisa la Kilutheri, wachungaji na waalimu waliendelea kuzitetea. Baada ya kifo cha Luther, hasa mwaka wa 1563, Waprotestanti Wafuasi wa Calvin waliwasilisha kitabu kilichoitwa “Katekisimo ya Heidelberg” kama ukiri wao rasmi. Kwa hiyo, “Katekisimo Ndogo” na “Katekisimo Kubwa” kwa njia ya asili zilifanywa kuwa kiri rasmi na sanifu za Kanisa la Kilutheri. “Shauri la Mwafaka” linasema: “Kwa maafikiano, tunakiri pia Katekisimo Ndogo na Katekisimo Kubwa ya Dk. Luther, jinsi zilivyoshirikishwa katika maandiko yake yote, kama Biblia ya watu wa kawaida, ambayo katika hiyo, kila kitu kimeshirikishwa ambacho kilishughulikiwa kwa mapana katika Biblia, na ni za lazima kwa Mkristo kuzifahamu kwa ajili ya wokovu wake. Kulingana namwelekeo huu, jinsi ulivyotangazwa hapo juu, mafundisho yote yanayopaswa kuidhinishwa na lolote lililo kinyume nayo, linapaswa kukataliwa na kulaaniwa kulingana na azimio la imani yetu ya pamoja.” 51 Hadi sasa, Katekisimo Ndogo inatumika kote ulimwenguni kuwafundisha watoto na kuwaandaa kwa ajili ya kipaimara, angalau katika Makanisa ya Kilutheri yanayoamini Ukiri. “katika maadamu, zilipokubaliwa kwa ridhaa kuu na kutumiwa hadharani, kanisani, shuleni, na nyumbani na makanisa haya yote yanayodumu katika Ukiri wa Augsburg, kwa sababu katekisimo hizi hujumlisha kwa usahihi mafundisho ya Kikristo juu ya msingi wa Neno la Mungu kwa Wakristo wa kawaida katika muundo sahihi na sahili, lakini hasa kwa uwazi wa kutosha.”
Kwa kweli, bado kuna na kutakuwepo na watu ambao hawataithamini na wataipuuza “Katekisimo Ndogo.” Kwa kawaida, wao ni wapinzani wa ukweli wa kimapokeo. Ni watu ambao hawakubaliani na yaliyomo ndani yake. Lakini “Katekisimo Ndogo” ina wengi wanaoiheshimu kuliko wachongezi. Watu wanaoipenda kwa sababu ya ujumbe na yaliyomo ndani yake. Licha ya hayo,
51 “Shauri la Mwafaka, Tamko Thabiti, Muhtasari wa Mafundisho, Msingi, Kaida na Kanuni” 6.
xxvii
si maaskofu wala mapadre wa Kanisa kuu wanaojali jinsi maskini wanavyoishi au wanavyofariki. Hawa ni wale ambao hawaruhusiwi kumsikia akiongea nao kama Mchungaji wa kweli aliye na kondoo zake. Hii inanifanya nitetemeke na niogope kwamba, wakati fulani, Mungu anaweza kutuma sinodi ya malaika kwa Ujerumani, ituangamize kabisa kama Sodoma na Gomora kwa sababu tunamdhihaki sana kitukutu kwa njia ya sinodi”53 Haya ndiyo maneno ya Luther ya kuhitimisha dibaji yake kwa “Mafungu ya Smalkadi”: “ Ee Mpendwa Bwana Yesu Kristo! Mwenyewe uiitishe sinodi yako! Katika utukufu wako njoo uwaokoe watumishi wako! Papa na wafuasi wake hawafai. Hawakujali wewe hata kidogo. Fanya utusaidie sisi, tulio maskini na wahitaji tunatanafusi na kukuomba wewe kwa moyo, kulingana na neema yako uliyotupatia kwa njia ya Roho Mtakatifu, aishiye na atawalaye pamoja nawe na Baba, usujudiwe milele. Amina.”54
Luther wala watawala Walutheri hawakuwa tayari kuafikiana. Wakati ulikuwa umekwisha sauti ya upole ya Melanchthon ilipofaa. Ikiwa Papa alifikiri kwamba, watawala Walutheri wangerejeshwa kwa urahisi sana, angesikitika sana. Waliujibu mwaliko wake kwa masharti yafuatayo: 1. Lazima sinodi iwe huru, ambapo mambo yatazungumzwa vilivyo na kwa haki, na si mahakama ya Papa ambayo kwayo, kesi ingekuwa imeamuliwa kabla ya kusikilizwa. 2. Vyeo vya heshima vyote lazima vingewakilishwa na kushughulikiwa kwa usawa bila kuwashtaki Waprotestanti kuwa waasi ambao wajibu wao ulikwa ni kuyakana kabisa maoni ya Wakatoliki. 3. Msingi wa mchakato wote lazima uwe Biblia pekee na si uamuzi wa Upapa wa kibinadamu. 4. Afadhali, sinodi ifanyiwe Ujerumani.
Watawala Walutheri waliukataa mwaliko maana hii haikuwa aina ya sinodi waliyoitarajia. Lakini Luther alikuwa tayari kwenda ingawa hakututarajia lolote la maana kwa ajili ya Injili. Kwa upande wake, Papa alikuwa Mpinga Kristo kwani hakutaka kuisikiliza sauti ya Injili bali alipigana nayo kwa ukaidi. Ingawa alimkatalia uwezo wa haki takatifu ya kuitisha sinodi na kuuchukua wajibu kama jaji mkuu katika mambo yanayohusiana na mafundisho na imani, mtu angempa heshima ya kuliongoza baraza la aina hiyo kwa haki ya kibinadamu, jinsi hali ilivyokuwa katika Kanisa la Mwanzo. Yeye na wenzake waliamua kutoisusia sinodi ambayo wao wenyewe walikuwa wameiomba siku zote.
Karimu Mtawala Mchaguzi Yohana Fredrik (1503 -1554), mwana wa Yohana Mwaminifu, yeye binafsi alishawishika kwamba, wanatheologia wa Wittenberg hawakupaswa kuhudhuria Sinodi iliyopangwa. Tena, katika kumbukumbu
53 M. Luther, Mafungu ya Schmalkaldi, Dibaji, 10.11.
54 Mafungu ya Schmalkaldi, Dibaji,15.
xxix
iliyoandikwa Desemba tarehe 1, mwaka wa 1536, alimwomba Luther aorodheshe mambo ambayo kwayo, mapatano yoyote hayangewezekana. Ni mambo gani ambayo Luther hangeweza kuyajadili kamwe ambayo angekuwa tayari kuyakiri mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu wakati angetakiwa afe? Baadaye, orodha hii ingetiwa sahihi na wanatheologia wote wa Wittenberg. Mambo yaliharakishwa. Mtawala Mchaguzi alitaka matini hiyo iwe tayari katika lugha zote mbili, Kilatini na Kijerumani, kwa ajili ya ukumbusho wa siku ya kuongoka kwa Mtume Paulo, mnamo Januari tarehe 25, mwaka wa 1537. Ingetiliwa sahihi na wanatheologia wote wa chuo kikuu na kuwasilishwa kwa malodi Walutheri wote.
Luther alikuwa mgonjwa mahututi wakati huo na aliwaza kuwa, angakufa karibuni. Kwa hiyo, aliiandaa hati aliyokuwa ameombwa kuitunga kama ushahidi wake wa mwisho, wosia wake kwa wale ambao angewaacha hai na kwa ulimwengu wote. Anaandika tena katika Dibaji ya “Mafungu ya Schmalkaldi”: “Kwa sasa, nimeamua kuyachapisha mafungu haya katika maneno dhahiri yaliyopigwa chapa, ili, iwapo nitakufa kabla ya sinodi kukutana, jambo ninalotarajia na kutumainia kutokea, kwa sababu wale maayari wanauogopa mwanga na kuipinga nuru, hujikokota jinsi hiyo kuiahirisha na kuizuia Sinodi. Shabaha yangu ni kuuacha nyuma, ushuhuda na ukiri wangu pamoja na ukiri ule ambao nilitangulia kuutoa awali kwa jili ya wanaoishi na watakaokuwepo baada yangu. Mpaka sasa, nimesimama na, kwa neema ya Mungu, nitasimama katika ukiri huu.”55
Luther aliiwasilisha matini hiyo kwa wenzake wa Wittenberg: Yusto Yona, Yohana Bugenhagen, Filipo Melanchthon, Kaspar Cruciger, na baadhi ya wengineo miongoni mwao akiwemo Georg Spalatin, Nikolao von Amsdorf, na Yohana Agricola. Matini hiyo ilijadiliwa na kukubaliwa na wote. Hata Melanchthon dhaifu alikubali kuitia sahihi, mradi tu papa angepewa,“mamlaka kwa ajili ya haki ya kibinadamu kama angeikubali Injili. Pia, tungekubaliana naye kuwa na ukuu juu ya maaskofu ambao ameupata.”56
Yale yanayodaiwa kuwa “Mafungu ya Schmalkaldi” yaliwasilishwa kwa Mtawala Mchaguzi mnamo Januari tarehe 3, mwaka wa 1537. Mtawala Yohana Fredrik aliyasoma na akafurahishwa sana na yaliyokuwemo. Isitoshe, alifurahi kuona kwamba, yalitiwa sahihi na wanatheologia wote. Alimpongeza Luther kwa imani yake thabiti. Wachungaji wote wakuu wa Sachsen waliombwa pia kutia sahihi katika hati hiyo na kuifundisha vilivyo. Kwa kuwa Melanchthon
55 “Mafungu ya Schmalkaldi,” Dibaji 3. Ukiri uliotajwa hapa ni Ukiri wa binafsi kuhusu Ekaristi ulioandikwa na Luther mwaka wa 1528. Unaitwa “Ukiri Kuhusu Chakula Kitakatifu cha Kristo,” WA 20:894-1115.
56 “Mafungu ya Schmalkaldi”, sehemu ya mwisho ya sahihi.
xxx
alikosolewa vikali kwa kujitolea kwa dhati kumpa Papa mamlaka ya kibinadamu “iwapo angeikubali Injili,” ambayo ilikuwa, jinsi alivyosema mtu fulani, “sawa na kumwomba Ibilisi awe mtume,” mwishowe, alikubali kuyatupilia mbali maombi yake.
Kulikuwa na mkutano mkubwa mnamo Februari, mwaka wa 1537. Washiriki wote walitia sahihi kwenye ukiri isipokuwa wawakilishi wa Ujerumani Kusini ambao waliwaonea huruma wafuasi wa Kanisa la Waprotestanti lililoyazingatia mafundisho ya Kalvin huko Uswisi. Hii ndiyo sababu, ingawa “Mafungu ya Schmalkaldi” ni sehemu ya “Kitabu cha Mwafaka,” siku hizi, makanisa mengi ya Kilutheri ambayo yamefungua milango yao kwa Wanamabadiliko na Wanafalsafa wa umoja, wanayachukulia mafungu haya kama yale yaliyopitwa na wakati na yasiyokuwa na maana, lakini ambayo hayana mashiko katika yale yanayoyasema. Toleo la kwanza lilichapishwa kwa Kijerumani mnamo mwaka wa 1538 na likapokelewa katika “Kitabu cha Mwafaka,” sawasawa na toleo la Kilatini lililotolewa baadaye na Nikolao Selnecker.
“Mafungu ya Schmalkaldi” ni ukiri thabiti na jasiri sana uliotolewa na mtu aliyepoteza tumaini lolote la kuipatanisha imani ya Kilutheri na ya Roma kwa njia ya Sinodi ya Kikristo. Baada ya miaka kadhaa, Luther alikuwa amegundua kwamba, Melanchthon mwenye uangalifu kupita kiasi na mwenendo wake wa “Leisetreterei,”57 katika Baraza la Augsburg, alikuwa amepunguza tofauti kati ya mafundisho ya Kilutheri na Kiroma. Kwa hiyo, aliamua kutoa sura nyepesi yenye sifa bainifu za Ulutheri. Hivyo, “Mafungu ya Schmalkaldi” yangekuwa ishara ya mwisho ya kuuvunja uhusiano na Roma usiotangulika. Mafungu haya yanapatikana katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni fupi sana, inajishughulisha na “Mafungu Yanayohusu Utukufu wa Mungu” na yanayoelezea kwa sentensi kadhaa ukweli kamili wa utukufu wa Yesu Kristo. Sababu ya ufupi wa sehemu hii ni kwamba, hakukuwa na mabishano katika mafundisho haya. Sehemu ya pili inajishughulisha na “Mafungu Yanayorejea Huduma na Kazi ya Yesu Kristo au Ukombozi Wetu.” Haya ni maelezo kuhusu mafundisho ya kuhesabiwa haki. Hili linasemekana kuwa fungu muhimu sana la imani ya Kikristo. Linafuatiwa na fungu refu mno linalohusu Misa na Maombezi ya wafu watakatifu. Mafundisho haya ni ya uongo na yanapingwa vikali. Halafu fungu kuhusu Mikutano ya Mapdre na Makazi ya Watawa na fungu lingine kuhusu Upapa/Cheo cha Papa ambalo kwalo, Luther anaelezea kwamba, halikuanzishwa na Bwana, bali lilibuniwa na binadamu. Anaelezea kwa maneno makali sana kwamba, Papa si mtu binafsi tu, bali katika shughuli zake, ni Mpinga Kristo yule aliyezungumziwa na Mt. Paulo. 57 Neno hili la Kijerumani linamaanisha “kutembea polepole”.
xxxi
Sehemu ya tatu yenye mafungu 15 inajishughulisha na mafundisho kuhusu dhambi halisi, dhambi ya asili, Toba, Injili, Ubatizo, Sakramenti ya Madhabahu, Huduma za Funguo, Ukiri wa Mitume, Kutengwa na Kanisa, Kubarikiwa kuwa Mchungaji, Mwito, Kanisa, jinsi mtu anavyohesabiwa haki, Nadhiri za watawa na Tamaduni za Binadamu. Haya yote yalipingana vikali na mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Sehemu mojawapo muhimu mno katika “Mafungu ya Schmalkaldi” ni kuhusu yale ayasemayo Luther katika Fungu la Nane kuhusu Ulokole. Haya ni mafundisho ya uongo ambayo yanafundisha kwamba, Roho Mtakatifu hufanya kazi moja kwa moja katika mioyo ya wanadamu bila Vyombo vya Neema, yaani, mahubiri ya Injili, Ubatizo, na Chakula Kitakatifu. Luther anayashutumu mafundisho haya kama ya Ibilisi ambayo yanashikamana na Adamu na wanadamu wa asili. Wazo hili potovu linasemekana kuwa chanzo cha mafundisho yote ya uongo katika Ukristo.
Tuna “Mafungu ya Schmalkaldi” ya mwaka wa 1537. Luther aliyeugua ugonjwa mkali wa figo, alishawishika kuona kwamba, mwisho wa maisha yake ulikaribia. Kwa kweli, aliishi kwa miaka tisa zaidi. Hata hivyo, alikuwa tayari kufuata mwito wa Mungu wakati wowote. Aligundua kwamba, Kanisa la Kilutheri lingefikwa na nyakati ngumu. Halikutishwa tu na mamlaka ya uhasama ya kisiasa bali pia, na zaidi, mafundisho mengi ya uongo ambayo yangejaribu kulipotosha. Kwa hiyo, alitaka kusema kwa maneno makali na dhahiri kuhusu ukweli alioupigania na ni ukiri gani wa imani alioukiri ambao kwao, alikuwa tayari kukutana na Bwana na Muumba wake.
Katika mojawapo ya mahubiri yake, Luther anasema:
“Uzima wa milele kwa njia ya Neno la Mungu ni miliki kuu ambayo moyo wa binadamu hauwezi kuutambua. Kuhifadhi miliki hiyo, kunadai vita vikuu na vikali. Usiipuuze miliki hii. Usipolishikilia Neno lenye thamani kwa nguvu zako zote, utalipoteza milele. Usilidharau jinsi ulimwengu na baadhi ya roho pumbavu hufanya, zinadanganywa na Ibilisi kuhusu sakramenti na masuala mengine . . . Rafiki yangu, usinipendekezee amani na umoja iwapo nitalipoteza Neno la Mungu katika mchakato huo. Nikifanya hivyo, nitaupoteza uzima wa milele pamoja na kila kitu. Hakuna kusalimu amri au kushindwa katika jambo hili: la hasha, si kwa ajili ya upendo wako au wa mtu mwingine yeyote. Lazima wote walikubali Neno, awe rafiki au adui. Neno lilitujia kwa ajili ya uzima wa milele na si kwa kusudi la kueneza amani na umoja wa ulimwengu huu. Neno na mafundisho vitasababisha umoja na ushirika wa Kikristo. Pale ambapo vinatawala, mengine
xxxii
yote yatafuatia. Pale ambapo havipatikani, umoja hautadumu kamwe. Kwa hiyo, usizungumzie kuhusu upendo au urafiki wowote iwapo vinamaanisha kujitenga na Neno au imani. Maana haijasemekana kwamba, upendo huleta uzima wa milele, neema ya Mungu, na hazina za mbinguni. Neno tu ndilo linalofanya hivyo.”58
Kanisa la Kilutheri lilijua hatari iliyokuwepo, likasikiliza sauti ya Luther na likamfuata lilipoamua kukubali hati hii kama mojawapo ya Kiri zake rasmi.
Makala Kuhusu Mamlaka na Ukuu wa Papa
Watawala Walutheri walitaka wanatheologia wao pia wafundishe jambo fulani kuhusu Upapa na mamlaka yake. Hivyo, Melanchthon alikuwa ameombwa kutunga kilichodaiwa kuitwa “Makala Kuhusu Mamlaka na Ukuu wa Papa.” Hati hii ilikuwa tayari mnamo Februari tarehe 17, mwaka wa 1537. Melanchthon alikuwa amekana wazo la Ukuu wa Papa hata kwa “haki ya kibinadamu” ambayo kwayo, aliitetea hapo awali. Mara nyingine tena, alionyesha kwamba, angeweza kuwa thabiti wakati kila mmoja aliyekuwa karibu naye alikuwa hivyo, lakini alipopata nafasi alikuwa mpatanishi zaidi. Hakika, “Mafungu ya Schmalkaldi” yalikuwa ushindi kwa Melanchthon aliyekuwa mtaalamu mno, mwaminifu lakini dhaifu. Watawala na wanatheologia wengine walionekana kuwa wenye nguvu zaidi kuliko yeye.
Makala ya Melanchthon yanayozungumzia kuhusu, “Ukuu na Mamlaka ya Papa” na katika sehemu yake ya pili kuhusu “Mamlaka na Utekelezaji wa Sheria za Maaskofu,” yalitiwa sahihi na wanatheologia wote waliokuwepo huko
Schmalkaldi na baadaye yakatafsiriwa katika Kijerumani na Veit Dietrich.59
Hayajatajwa wazi kama Ukiri katika “Shauri la Mwafaka” lakini yalichukuliwa kama Nyongeza kwa “Mafungu ya Schmalkaldi.”
Katika “Makala” yake, Melanchthon anaelezea kwamba, madai kuwa Askofu wa Roma ni Papa, yaani, ni Kichwa cha Kanisa kwa mujibu wa haki ya kimungu ni uongo kabisa. Wala hakuna utawala msonge wa kikasisi ulioanzishwa na Mungu. Mitume walikuwa sawa, na walivyokuwa maaskofu ambao, awali walichaguliwa na kuitwa umma. Huduma ya pekee iliyoanzishwa kwa njia ya kimungu ni ile ya mitume na warithi wao, yaani, wachungaji, maaskofu, au wazee wa kanisa60 jinsi
58 Mahubiri kutoka mwaka wa 1531 (Oktoba 29), WA 34:II, 387.
59 Veit Dietrich (1506-1549) anastahili atajwe kwa umaarufu, kwa kuwa , alikuwa mwandishi wa hati mkato wa Luther ambaye aliandika mahubiri mengi ambayo Luther aliyahubiri Wittenberg. Baadaye alikuwa mchungaji huko Nürnberg mwaka wa 1547, alitimuliwa kutoka ofisini mwake kwa sababu alilipinga Suluhisho la Muda.
60 Πρεσβúτεροι, “wazee,” yaani wachungaji, sio wanakamati jinsi neno la “mzee” la kawaida linavyoeleweka
xxxiii
wanavyoitwa katika Agano Jipya. Melanchthon pia alionyesha kwamba, hakuna mamlaka yanayotoka katika nafsi ya mhudumu yeyote wa Kanisa, bali mamlaka ya pekee ambayo inafaa kutumiwa kanisani ni ile ya Neno la Mungu.
Mtunga “Makala” haya anasema mambo muhimu sana kuhusu huduma ambayo Yesu Kristo aliianzisha, aliiwekea msingi, aliijenga, aliliongoza Kanisa lake, na kuhusu uwezo na haki ya Kanisa kuwaita na kuwasimika wachungaji.
Maelezo yake nyeti hayafai kusahaulika wakati fundisho la huduma ni suala linalozungumziwa katika madhehebu mengi ya Kikristo, ikiwa ni pamoja na Kanisa la Kilutheri.
Shauri la Mwafaka
Kabla ya kuwasilisha “Shauri la Mwafaka,” ambalo ni ukiri wa mwisho na mpana wa Kanisa la Kilutheri, inafaa tuitoe habari fupi kuhusu hali ya dini ilivyokuwa huko Ujerumani ili tupate kuelewa maendeleo ya mwisho katika historia ya Ulutheri wa karne ya Kumi na Sita.
Martin Luther aliaga dunia mnamo Februari tarehe 18, mwaka wa 1546. Kifo chake kilikuwa dalili ya mwanzo wa vita vikali dhidi ya Kanisa la Kilutheri. Ni kana kwamba, maadui wa ukweli walikuwa wanangojea huyu mtetezi mkakamavu na hodari wa Injili ya wokovu wa Mungu aiage dunia. Maadui wake kutoka nje walikuwa ni Papa na Kaisari. Maadui wa ndani walikuwa wote ambao walitaka apoteze hazina yake yote, waliotaka wambadili awe Kanisa bila Ukiri ulio wazi kwa mafundisho yote yaliyowezekana. Wakati wa miaka yake ya mwisho, katika Kanisa la mapigano, kabla hajaingia lile la ushindi, Luther alihisi kwamba, mambo mabaya yangetokea, ugomvi ungezuka katika Chuo Kikuu cha Wittenberg, na kwamba, ujumbe wake ungeharibiwa. Aliteseka alipogundua kwamba, wenzake wengi walikuwa tayari kuviacha vita kwa ajili ya mafundisho safi. Tunaambiwa kwamba, kwenye mlango wa chumba chake cha kusomea aliandika maneno yafuatayo: “Tunahitaji kuwatahini maprofesa wetu kuhusu mafundisho ya Chakula Kitakatifu.” Alipoulizwa maana yake na mmoja wao aitwaye Yohana Major, alijibu: “Inamaanisha inayoyasema. Mnakuwa washukiwa kwa sababu ya kimya chenu. Iwapo mnadai kwamba, mnakiri uwepo kamili sawa na ninavyoukiri, basi mnapaswa kuukiri kanisani, katika mihadhara, katika mahubiri, na katika mazungumzo yenu ya binafsi. Ndugu wanahitaji kuimarishwa, wakosaji warejeshwe kwenye njia ya haki, na makosa yanapaswa kupigwa vita, la sivyo, ukiri wenu ni wa kuonekana tu na hauna thamani yoyote.”
kwa sababu ya mafundisho ya Kipresbyteri katika Afrika ya Mashariki.
xxxiv
Mnamo Juni tarehe 26, mwaka wa1546, Papa na Kaisari walihitimisha makala ambayo yalikusudiwa kuwalazimisha Waprotestanti wazitambue sheria za Sinodi ya Trento 1545-1563 na waunganishwe tena na Kanisa Katoliki. Watawala Waprotestanti walikuwa wameanzisha linalodaiwa kuwa Shirikisho la Schmalkaldi ili kumpinga Kaisari. Lakini walishindwa mnamo Aprili tarehe 24, mwaka wa 1547. Mtawala Mchaguzi wa Sachsen alifungwa na kuhukumiwa kifo. Ili kumwokoa, mji mkuu wa Wittenberg ulisalimu amri mnamo Mei tarehe 19.
“Suluhisho la Muda”61 lilitangazwa huko Augsburg mwaka wa 1548. Lilikuwa suluhisho la muda kabla ya Sinodi ya Trento na lilikusudiwa kuamua juu ya hali ya dini. Wachungaji wa Kilutheri waliruhusiwa kuoa na kushiriki Ushirika Mtakatifu katika mkate na divai. Lakini walihitajika kukubali desturi na sherehe za Kikatoliki, wakubali ukuu wa kimungu wa Papa na utawala msonge wa kikasisi ulioanzishwa na Mungu, wakubali mamlaka ya maaskofu, mafundisho ya mageuzo-uwamo (transubstantiatio), na maelezo kwamba, Kristo ameanzisha sakramenti saba tofauti.62 Isitoshe, walihitajika kukanusha madai kwamba, kuhesabiwa haki ni kwa njia ya imani pekee, mbali na matendo yote. Hili ndilo lililodaiwa kuitwa Suluhisho la Muda la Augsburg. Lililazimishwa kwa Makanisa ya Kilutheri katika Ujerumani. Wachungaji waliokataa kuliidhinisha waliteswa, wakapigwa marufuku au wakawekwa gerezani. Bado makanisa mengi yalilipinga sana. Kwa hiyo, lilifaulu nusu tu.
Kwa hiyo, “Suluhisho la Augsburg” lilibadilishwa kwa suluhisho lingine la muda lililoitwa Suluhisho la Muda la Leipzig. Hili lilitarajiwa lingekuwa kama aina ya maafikiano ambayo yangekubaliwa na Walutheri wote. Matini hii mpya iliidhinishwa na kukubaliwa na wanatheologia wa Wittenberg na Leipzig mnamo Desemba tarehe 20, mwaka wa 1548. Suluhisho hili lilihitaji mambo machache kuliko Suluhisho la Muda la Augsburg na lilijaribu kuyanusuru mafundisho maalumu ya Kilutheri. Wakati huo huo walifanya mkataba kuhusu “Adiaphora,” yaani, mambo ambayo si lazima kuyajali.63 Melanchthon alikuwa shabiki wake thabiti. Aliamini kwamba, mikataba fulani ingefanywa ili kuliokoa kanisa. Hakika, suluhisho jipya la muda halikuwa tu maafikiano kuhusu sherehe na kaida za dini, bali pia lilikuwa halisi kupuuza kwa mujibu wa mafundisho. Mafundisho
61 “Augsburg Interim.”
62 Fundisho la mageuzo - uwamo (Kilatini, “transubstantiatio”) ni kusema kwamba, mkate na divai hubadilika kwa mintarafu ya kiini na sifa zao kuwa kweli mwili na damu ya Kristo katika Chakula Kitakatifu kwa njia ya tendo la kasisi. Hata hivyo, sifa za nje za elementi (mkate, divai) hazibadiliki.
63 “Adiaphora” ni mambo ambayo hayajaandikwa, hayajaamriwa wala hayajakatazwa katika Biblia. Huwa hasa yanashughulikia kaida na sherehe.
xxxv
maalumu ya Kilutheri yaligeuzwa kuwa mambo ya Kikatoliki zaidi kuliko kuwa ya Ulutheri halisi. Suluhisho hili lilipingwa pia huko Wittenberg na kwingineko. Matthias Flacius Illyricus,64 mmoja wa kitivo huko Wittenberg, aliamua kuutoroka mji huo alipohofia usalama wake. Suluhisho la Muda la Leipzig lilipuuzwa katika sehemu nyingi za Ujerumani. Wale waliotaka kubaki kuwa waaminifu kwa mafundisho ya Luther, walisikitika sana walipogundua kwamba, mwandishi mkuu alikuwa mtu ambaye watu wote walimchukulia kuwa mrithi wa Luther, yaani, Philipp Melanchthon. Alipoteza heshima yake na mamlaka yote.
Wakati huo, kulikuwa na Mwinyi wa Sachsen, aliyeitwa Moritz. Alitawala sehemu nyingine za Sachsen kando na binamu yake, Mtawala Mchaguzi Yohana Fredrik. Alihongwa kwa kuahidiwa jimbo na cheo cha Mchaguzi. Alikuwa upande wa Wakatoliki na alimsaidia Kaisari kumshinda Yohana Fredrik.65 Lakini kwa kuogopa uwezo wa Kaisari ulioenea na akiogopeshwa na uovu aliotendewa baba mkwe wake, Filipo wa Hessen, alikula njama dhidi ya Karoli wa Tano, akapigana naye, akamtia mbaroni, na kutoka kwake akadai kwa lazima Maafikiano ya Passau mwaka wa 1552. Maafikiano haya yaliishia kuwafaa Walutheri sana. Walutheri na Wakatoliki sasa walikuwa katika kiwango sawa na walifurahia haki sawa katika ufalme. Kulingana na kanuni “Cuius regio, eius religio,”66 mtawala angeweza kuanzisha dini aliyoiunga mkono katika jimbo lake, na watu wote walioishi katika jimbo hilo walilazimika kumfuata. Huu ulikuwa mwanzo wa Makanisa ya Dola katika Ujerumani.
Wakati wa Suluhisho la Muda ulikwisha, lakini lilikuwa limeleta mabishano mengi ambayo yalidhoofisha mno Kanisa la Kilutheri. “Shauri la Mwafaka” ni ushuhuda ulio hai unaoonyesha jinsi hali ya mafundisho ilivyoenea kwa miongo mitatu au minne iliyofuatia kifo cha Luther. Vile vile, “Shauri la Mwafaka” ndilo ukiri wa mwisho wa Kanisa la Kilutheri, hati rasmi inayoelezea jinsi mabishano haya yalivyotatuliwa.
Mapigano kwa ajili ya mafundisho safi si kinyume cha wajibu wa Mkristo kudhihirisha upendo na kuishi kwa amani. Haya yanadhihirishwa wazi na “Shauri la Mwafaka.” Katika miongo iliyotangulia kuchapishwa kwake, wanatheologia wawili wakuu walilipinga, yaani, Flacius; mtetezi wa imani halisi na Melanchthon aliyewawakilisha wale waliotaka kuafikiana. Kulikuwa na mivutano mikali na
64 Matthias Flacius Illyricus (1520-1575) alikuwa mtetezi thabiti wa mafundisho halisi ya Ulutheri, lakini alikuwa mtu mkali na mara kwa mara alipigana kwa kina na mafundisho ya uongo. Alishutumiwa mara kwa mara kwa mtazamo wake, hata kutoka kwa wale waliokubaliana na ushawishi wake.
65 Kwa sababu hii alipata jina la “Yuda Iskariote wa Meissen.”
66 Maelezo haya yanamaanisha kwamba, lazima wananchi waifuate dini sawa na kumfuata mtawala wao.
xxxvi
yenye nguvu katika Kanisa iliyoohitaji kutulizwa. Kwa hiyo, ilipangwa mikutano mingi yenye majadiliano na mazungumzo marefu ambayo hayakufaulu. Lakini wanatheologia wawili, yaani, Yakobo Andreae67 na Martin Chemnitz68 walifanya walivyoweza kuanzisha tena umoja na amani.
Mwaka wa 1567, Andreae alitunga hati iliyoitwa “Mwafaka wa Schwaben.”69 Alitaka kuwasaidia Wanatheologia Walutheri waliokuwa wakigombana wayashinde mafarakano yao. Baada ya hati hiyo kufanyiwa marekebisho na Chemnitz na Daudi Chytraeus,70 ilichapishwa upya chini ya anwani; “Mwafaka wa Schwaben na Sachsen.” Mwaka wa 1576, mkutano muhimu ulifanyika huko Torgau. Kitabu kilichodaiwa kuitwa “Kitabu cha Torgau” kiliandikwa katika misingi ya “Mwafaka wa Schwaben na Sachsen” na katika baadhi ya hati zingine chache. Marekebisho ya mwisho yalifanywa na Andreae, Chemnitz, Chytraeus, Selnecker na wanatheologia wengine wawili, yaani, Musculus na Koerner. Hili ndilo linalodaiwa kuitwa “Tamko Thabiti,” ambalo ni sehemu ya pili na iliyo pana zaidi ya “Shauri la Mwafaka.” Sehemu ya kwanza ya huu Ukiri mpya wa Kilutheri na ya mwisho ni muhtasari wa “Tamko Thabiti” ulioandikwa na Andreae na ulioitwa “Muhtasari.” “Shauri la Mwafaka” lilitolewa rasmi huko Dresden mnamo Juni tarehe 25, mwaka wa 1580, wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini ya kumbukumbu ya “Ukiri wa Augsburg.” “Muhtasari” huu: 1) unaelezea hali ya kila ubishi, 2) unaelezea kwa ufasaha mafundisho ya kweli na 3) unayakataa mafundisho ya uongo. “Tamko Thabiti” haliufuati muundo huu, bali linaenda mara moja katika mazungumzo ya kina ya jambo linalojadiliwa. Kila mojawapo ya sehemu ya “Shauri la Mwafaka” ina utangulizi unaokiri kwamba, Maandiko Matakatifu tu ndiyo sheria ya imani na utekelezaji na huelezea mamlaka ya Kiri za Kilutheri zilizotangulia. Halafu mafungu kumi na mawili yanafuatia. Haya yanajishughulisha na mabishano kumi na mawili tofauti. Tutayawasilisha baadaye ili msomaji apate kuelewa kwa urahisi mambo ambayo yalikuwa hatarini na vile mabishano yametatuliwa.
Watu wengi hawalipendi “Shauri la Mwafaka.” Lina wakashifu hata katika Makanisa ya Kilutheri. Lakini bado linawangojea wale ambao wataweza kulikanusha. Njia bora zaidi ya kuonyesha sababu na roho ambayo kwayo,
67 Jakob Andreae (1528-1590) alikuwa mchungaji wa Stuttgart, alikuwa mrakibu wa Tübingen na mwishowe profesa na rais wa Chuo Kikuu cha Tübingen.
68 Martin Chemnitz (1522-1586) mwanafunzi wa zamani wa Melanchthon, alifundisha huko Wittenberg kabla ya kuwa mrakibu mkuu wa mji wa Braunschweig. Alikuwa mwanatheologia mwenye sifa kuu. Kawaida aliitwa “Martin wa Pili” aliyemfuata “Martin wa Kwanza,” yaani, Luther!).
69 Schwaben ni jimbo katika sehemu ya Kusini mwa Ujerumani.
70 David Chytraeus (1531-1600) mwanafunzi wa zamani, alitumika huko Rostock , alikuwa mhimili wa chuo kikuu. Ni mmoja wa waandishi wa “Shauri la Mwafaka.”
xxxvii
liliandikwa, ni kuidondoa aya yake ya hitimisho:
“Kutokana na haya maelezo yetu, marafiki, maadui, na kila mmoja atafahamu kabisa kwamba, hatuna nia ya kuikubali kazi bure ya ukweli wa milele wa Mungu na usiobadilika kwa ajili ya amani ya muda, utulivu na mapatano ya nje ambayo hatuna uwezo kuyatenda. Wala amani na mapatano ya namna hiyo hayatakuwa ya kudumu kwa kuwa, yamebuniwa dhidi ya ukweli na kwa ajili ya ukandamizwaji wa ukweli. Tunaelekea kuupamba na kuusitiri ufisadi wa mafundisho safi bado . . . Badala yake, tuufurahie ukweli na kuupenda kwa moyo wa ukunjufu mwafaka wa kweli unaolinda utukufu wa Mungu usiudhiwe, bila kupunguza lolote katika ukweli wa Injili Takatifu na bila kutoa nafasi kwa kosa hata kidogo. Kwa hiyo basi, wenye dhambi maskini wanaletwa katika toba halisi ya kweli, wanafufuliwa kwa njia ya imani, wanaidhinishwa katika utii mpya, na hivyo, wanahesabiwa haki na wenyewe wanaokolewa milele kwa njia ya ustahili wa pekee wa Kristo,”71
Ni wajibu wa Walutheri ambao ni mawakili wa muungano umpendezao Mungu na ulio na misingi yake katika ukiri wa ukweli wa kimungu, kuona kwamba, hazina aliyowapa Mungu katika “Shauri la Mwafaka” imehifadhiwa na imeenezwa kwa wengine. Wajibu huo, utaufanya ukweli wa wokovu ambao ameufunua katika Biblia Takatifu ujulikane. Hatimaye, Ukiri huu wa mwisho wa Kanisa la Kilutheri umeandikwa. Hivyo, “Mungu Mwenyezi na Baba wa Bwana wetu Yesu atupe neema ya Roho Mtakatifu wake ili sote tuwe pamoja katika yeye na daima tukae katika umoja wa Wakristo, ambao unampendeza yeye kweli.”72
Dhambi ya Asili:
Bishano la kwanza ambalo lilitatuliwa, lilihusu dhambi ya asili. Halikuwa bishano kuu lakini ndilo la kwanza kushughulikiwa na “Shauri la Mwafaka.” Mtu aliyeitwa Victorinus Strigel,73 sawa na Melanchthon, hakutofautisha kikamilifu kati ya theologia na falsafa. Akitumia sifa bainifu za kifalsafa74 alidai kwamba, dhambi ya asili ni ajali, tendo lisilo muhimu sana na hakika halimwathiri mtu. Hivyo basi, aliuchukua msimamo nusu wa Wapelagio au ule wa lazima ya kazi pamoja na Mungu na binadamu kwa ajili ya wokovu wa kutorithi dhambi ya asili.75 Alipingwa vikali na Flacius ambaye, akiitumia istilahi ileile ya kifalsafa
71 Shauri la Mwafaka, Tamko Thabiti 12, 95.96.
72 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 1, 23.
73 Victorinus Strigel (1524-1569) alikuwa mmoja wa wawakilishi wa kwanza kabisa wa kundi la Melanchthon. Alifundisha huko Wittenberg, Erfurt na Jena, halafu akaenda Leipzig na baadaye Heidelberg.
74 Utofautishaji kati ya kiini na ajali uliofanywa na mwanafalsafa Myunani maarufu sana, Aristotele aliyeishi kati ya karne nne kabla ya Kristo (“substantia-accidentia”)..
75 Pelagio alikuwa mtawa Mwingereza, aliyeishi mwanzoni mwa karne ya tano. Alikataa dhambi ya asili na alifundisha kwamba, kwa asili, mtu si mzuri wala si mbaya, lakini yeye ni mwenye uhuru wa kuchagua
xxxviii
alisema kwamba, dhambi ya asili si ajali bali inatokana na mwili wa mtu au asili yake. Ni kweli kwamba, kulingana na Biblia “mtu wa asili” amepotoshwa au mtu anapotoshwa na “asili” na kwamba, dhambi ya asili ni sehemu tu ya mtu aliyeanguka. Hili linamaanisha kwamba, watu wote huzaliwa na dhambi ya asili na dhambi hii hupenya kabisa katika uwepo wao. Hakika, mtu amepotoshwa kabisa na hana uwezo wa kiroho wa kumwezesha auchangie wokovu wake. Kwa hiyo, ni makosa kufundisha kama Strigel kwamba, Roho Mtakatifu humwongoa mtu mradi tu mtu huyo “atake,” “akubali” au “aamue” kuongolewa. Lakini ingawa Flacius alikusudia mema, aliivuka mipaka aliposema kwamba, dhambi ya asili inatokana hasa na kiini cha mwanadamu. Hii ingemaanisha kwamba, mtu hawezi kuwa mtu bila kuambukizwa dhambi ya asili. Falsafa hulitumia neno “kiini” kuonyesha kitu kinachokuwepo chenyewe. Kwa hiyo, kulingana na falsafa ya Aristotele, kiini cha mwanadamu ni kile kinachomfanya mtu kuwa mtu. Kwa hiyo, huwezi kukipoteza na bado uwe mtu. Hii ingemaanisha kwamba, kulingana na Flacius, mtu hawezi kuwa mtu bila dhambi ya asili, na kwamba, kabla ya kuanguka dhambini, Adamu alikuwa kiumbe kilichokuwa zaidi ya mwanamume na Hawa alikuwa kiumbe kilichokuwa zaidi ya mwanamke. Mwisho, ingemaanisha kwamba, Mungu ndiye mwanzilishi wa dhambi ya asili.
Flacius alipingwa na baadhi ya marafiki zake wa karibu na wawakilishi waaminifu zaidi wa Ulutheri halisi. Baadhi yao walikuwa: Moerlin, Chemnitz, Hesshusius na Wigand. Lakini alikuwa mkaidi kiasi kwamba, hakukubali kuwa alikuwa amekosea, ingawa alikuwa ametangaza kwamba atatumia istilahi nyingine.
Fungu la kwanza la “Shauri la Mwafaka” linaarifu jinsi Biblia inafundisha kuhusu dhambi ya asili na linakataa mafundisho yote mawili, yaani, fundisho la Strigel kuhusu kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu na fundisho la Flacius la kueleza kwa usahihi na kueleweka. Linasema: “Dhambi ya asili si dhambi ambayo mtu anaitenda, bali inashikamana na asili, kiini na ariki yake. Ingawa hakuna fikira mbovu zinazoweza kutokea katika moyo wa mpotovu, hakuna maneno ya bure yaliyosemwa, hakuna matendo maovu yaliyotendwa, na hata hivyo, bado asili haijapotoshwa kwa njia ya dhambi ya asili.76 Tena, kwa upande mwingine, “Mafundisho haya yanayodai kwamba, utofautishaji usiwepo kati ya yote mawili. Mt. Agostino alipinga kwa ukali mafundisho ya Pelagio. Yanakataliwa pia na Ukiri wa Augsburg. Upelagio nusu ni mafundisho ambayo hayana kina kile, lakini wao hufundisha kwamba, kwa usaidizi wa Mungu, mtu anaweza kuchagua kati ya yote mawili. Kiini cha suala hili ni: je, katika mambo ya wokovu, mtu ana hiari au la? Mafundisho ya Kanisa la Roma yanafuata nyayo za Wapelagio wasio wakweli.
76 Shauri la Mwafaka, Muhtasari,1,: 21.
xxxix
kati ya asili yetu ya ubinadamu na dhambi ya asili yanagongana na mafungu makuu ya imani yetu ya Kikristo kuhusu uumbaji, ukombozi, utakaso, na ufufuo wa miili yetu, na hayawezi kuishi pamoja chanjari.”
Kanisa litaweza kujifunza nini kutoka katika bishano hili? Ni kweli kwamba, ni muhimu sana kupinga mafundisho ya uongo, hasa mafundisho ambayo ni hatari sana na yanayoenezwa kote kama fundisho kuhusu mchango wa kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu.77 Lakini pia ni muhimu kuepuka kueleza kwa usahihi na kueleweka kunakovuka mipaka ya yale yanayofundishwa na Maandiko Matakatifu. Mara nyingi, wanatheologia wengi wenye nia njema, kwa kawaida, huanguka katika mtego huu wakati bishano kali limechacha. Hii ni kama maji kwenye kinu cha wale wanaojaribu kueneza mawazo ya kupotosha. Haya yamefanyika siku baada ya nyingine katika historia ya Kanisa la Kristo. Mfano mmoja: Biblia hufundisha kwamba, Yesu Kristo alijinyenyekeza alipofanyika kuwa mwanadamu ili auokoe ulimwengu. Hata hivyo, ingekuwa makosa makubwa kuhitimisha kwamba, aliuacha uungu wake mbinguni na kuwa, alikuwa mwanadamu wa kawaida na mwanadamu tu alipokuwa ulimwenguni. Vile vile ingekuwa makosa kusema kwamba, kwa kuwa, alikuwa mwanadamu kweli na Mungu kweli, basi hakujinyenyekeza kamwe bali aliendelea kuzitumia asili za uungu wake wote lakini kwa njia ya kujificha. Hakika, mafundisho halisi ya Biblia yanatufundisha kwamba, akiwa mwanadamu na Mungu wakati huo huo, kwa kweli hakutumia utimilifu kwa njia ya utukufu wa asili yake ya Kimungu.
Fundisho la msingi la mabishano haya ni kwamba, kweli zinazofunuliwa katika Biblia hubaki kuwa miujiza ambayo akili ya mwanadamu haiwezi kuifumbua wala hakuna lugha ya mwanadamu au ya kifalsafa au isiyokuwa ya kifalsafa inayoweza kuifunua. Tunaweza na ni lazima tukifikie kiwango cha Biblia lakini si zaidi. Huu ndio unyenyekevu wa Kikristo. Mtume Paulo anasema, “Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana” (1 Kor. 13,12).
Hiari /Nia Huru:
Jinsi tulivyokwisha kuona, kuna mafundisho ya uongo yaitwayo “synergeia,” yaani, kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu. Istilahi hii inatokana na lugha ya Kiyunani na inamaanisha “ushirikiano.” Kama jinsi imeelezewa tayari, linaitwa fundisho la Wapelagio wasiokamilika. Hivyo basi, 77 Kiyunani συνεργεια (Synergism).
xl
kulingana na mafundisho haya, licha ya anguko lake, dhambi ya asili, uwezo wa kiroho na nguvu, na uwezo wa kushirikiana na neema ya Mungu kwa njia ya msaada wake, anaufanikisha wongofu, kuzaliwa tena, kuhesabiwa haki na wokovu wake.
Luther alikuwa mtetezi thabiti wa kazi ya Mungu inayojitosheleza na ya pekee katika wokovu78 ambayo ni kinyume cha ‘Synergism’. Mojawapo ya maandiko yake makuu ni makala yanayoitwa “Utumwa wa Hiari” (1525/1526). Katika kitabu hiki, Luther anaelezea kwamba, kiasili, mwanadamu amepotoshwa kabisa na yu mfu kiroho, angalau kwa mujibu wa wokovu wake. Anamtegemea Mungu na neema yake kabisa. Melanchthon alipokuwa mwalimu chipukizi, alikubaliana na madai hayo ya Luther jinsi yanavyoshuhudiwa na mafungu mengi aliyoyaandika mwaka wa 1530 katika “Ukiri wa Augsburg.” Lakini baadaye aliibua wazo kwamba, kuongoka kunaletwa na mambo matatu: Roho Mtakatifu, Neno la Mungu, na idhini ya mwanadamu. Mambo haya matatu yanafaa kuelezea kwa nini baadhi ya watu wanaongoka na wengine hawaongoki. Haitoshi tu kulisikia Neno la Mungu bali pia unahitajika kuufungua moyo wako kwa Roho Mtakatifu na kumkubali yeye ili afanye kazi ndani yako. Lazima hiari yako ikubali na ishirikiane na Roho wa Mungu kwa njia fulani.
Melanchthon alingojea hadi Luther akafariki kabla ya kuyaeleza mawazo yake wazi.79 Aliitunga fomula inayosema kwamba, mwanadamu ana “uwezo wa kuiomba neema,” wakati ambapo Luther alifundisha daima kwamba, mwanadamu ni mlegevu hadi Mungu peke yake amwongoe na augeuze moyo wake. Moyo huu mpya peke yake ndio unaweza kumkubali Mungu na hiari yake. Kabla ya kuongoka na kuzaliwa upya, hawezi kufanya lolote kwa ajili ya kuingia katika ushirika na Bwana na neema yake. Yafuatayo ni maelezo machache ya Melanchthon: “Sababu tatu za matendo mema zinaafikiana” Neno la Mungu, Roho Mtakatifu na hiari ya mwanadamu inayokubali na si ile inayokataa Neno la Mungu . . . Wakati nafsi inayojisikia na inayojihimili haipingi yenyewe, haioni haya, lakini Roho Mtakatifu anayesaidia, anayeitia bidii kukubali, katika mapambano kama hayo, hiari huwa si legevu . . . Mungu huzivutia akili zetu, lakini lazima tukubali na tusikatae.”80 “Mungu mwenye rehema hajishughulishi na mwanadamu kama kipande, bali humvuta kwa njia ambayo hiari yake hushiriki pia.”81 Hili lilikuwa jaribio la kuelezea kwa nini watu wote wanaosikia
78 Nisharti ya kipekee; Kiyunani μονεργεια, kinyume kabisa cha συνεργεια.
79 Alifanya vile katika mafungu aliyoyaandika katika Kilatini na akayaita “Loci Communes” hasa katika toleo la 1548.
80 FilipoMelanchthon, Loci Communes, 1543, uk. 658.917.
81 Loci Communes, 1548, uk. 260.
xli
Injili hawaongolewi na kuletwa katika imani. Kwa nini mtume Petro aliokolewa, ilihali Yuda alipotea kabisa? Kwa nini wewe ni Mkristo na jirani yako ambaye pia aliisikia Injili hajaamini bado?
Melanchthon alisalimu amri kuhusiana na kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu alipokuwa akiyatafuta majibu kwa maswali haya. Kuna mafundisho ya uongo na ya kutisha yanayofundisha kwamba, Mungu hataki kuwaokoa watu wote. Badala yake, ameamua kutowaokoa watu fulani milele. Haya ndiyo yaliyokuwa mafundisho ya Yohana Calvin yaliyoitwa “Kudura Maradufu.”82 Kwa kweli, Melanchthon alikataa kuyakubali. Kwa hiyo, alifikiria kwamba, iwapo kosa halikuwa upande wa Mungu, lazima lilikuwa upande wa mwanadamu. Haya yamaanisha kwamba, ikiwa wote hawataokoka, ni kwa sababu wote hawafanyi wanayohitajika kuyafanya. Kuna watu wanaokataa kushirikiana na neema ya Mungu. Vile vile, haya ni mafundisho ya uongo. Kusema kweli, ni mafundisho ya uongo yaliyoandikwa moyoni mwa wanadamu. Ni sehemu ya hali ya asili ya akili ya wanadamu wote kuamini kwamba, wanaweza na lazima wastahili wokovu kwa njia moja au nyingine. Wazo hili linapatikana katika dini zote zilizobuniwa na wanadamu. Isipokuwa dini ya Kikristo tu ulimwenguni ambayo hufundisha kwamba, mwanadamu hawezi kufanya lolote na hawezi kujikomboa mwenyewe kwa njia yoyote. Badala yake, Ukristo unafundisha kuwa, mwanadamu amekombolewa kwa njia ya neema na Mwana wa Mungu ambaye anampa wokovu wa bure na asioustahili. Msamaha wa dhambi na maisha ya milele haviwezi kustahiliwa kwa matendo yetu binafsi wala kwa mtazamo wetu binafsi wakati Injili inapotujia kwa njia ya ujumbe wake mtukufu, ingawa yanaweza kuonekana sawa machoni mwetu. Si kwamba ninaweza kusema “La” kwa Injili, vivyo hivyo ninaweza kusema “Ndiyo.” Mtume Paulo anasema, “Mtu wa kiasili hapokei karama za Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.” (1 Kor. 2:14). Biblia inasema wazi kwamba, Bwana “aliufungua” moyo wa Lidia ili “ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo” (Mdo. 16:14). Mungu asipoifungua mioyo yetu, hatuwezi kuipokea Injili yake na kuiamini. Tendo hili la kufungua mioyo yetu ni karama yake Mungu mwenyewe.
Mabishano ya wazi yalitokea wakati Yohana Pfeffinger83 alipochapisha mfululizo wa hoja kadhaa akitetea kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu mwaka wa 1555. Aliungwa mkono na Viktorino Strigel ambaye, tumekwishaona, kwamba tayari alikuwa ameyatetea mafundisho ya dhambi
82 Kilatini, “Praedestinatio duplex”.
83 Yohana Pfeffinger (1493-1573) alikuwa profesa wa theologia katika Chuo Kikuu cha Leipzig.
xlii
ya asili, pamoja na mwanatheologia mwingine aliyeitwa Hugel. Walipingwa vikali na Flacius, Amsdorf, Gallus, Hesshusius ambao walitangaza kwamba, mafundisho haya hayakulingana na alivyofundisha Martin Luther katika makala yake yaitawayo, “Utumwa wa Hiari.” Ni makosa kusema kwamba, mwanadamu wa asili ni mgonjwa kwa njia ya kiroho. Yeye siyo mgonjwa kiroho tu bali ni mfu kiroho, kiasi kwamba, Biblia inachukulia kuongoka kuwa `kuzaliwa kupya kabisa (Yn. 3:1 Pet. 1:23) au ufufuo wa kiroho (Efe. 2:4-7; Kol. 2:12-13). Sisi tunaweza kughairi tu kwamba, mtu kama Melanchthon, aliyetazamiwa na kila mtu kuwa mrithi halali wa Luther, alishindwa kwa makosa kama hayo. Yaani, alishindwa na aina ya mafundisho ya Wakatoliki Wapelagio wasiokamilika, isipokuwa, badala ya kuelezea kushiriki kwa mwanadamu katika wokovu wake kwa njia ya matendo yake, yanasifu moyo wake Injili inapomuita katika imani. Biblia inasema kwamba, wokovu ni bure, na unaposemwa kuwa ni bure, ni bure kabisa. Ni 100% bure kwa sababu ni karama ya Mungu 100%!
Fungu la pili la “Shauri la Mwafaka” lilikataa mafundisho ya kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu, katika miundo yote iliyokuwa imechukua katika mabishano haya: “Kabla ya mwanadamu kuelimishwa, kuongolewa, kuzaliwa upya, kufanywa mpya, na kuvutwa na Roho Mtakatifu, mwenyewe anaweza na kwa nguvu zake za asili anaweza kuanza kazi au kukubaliana kufanya kazi katika mambo ya kiroho na katika kuongoka au kuzaliwa upya kwake kiasi kidogo sawa na jiwe au boriti au tofali . . . Maandiko Matakatifu yanahesabu kuongoka, imani katika Kristo, kuzaliwa, kufanywa mpya, na yote yanayohusiana na mwanzo na mwisho unaofaa, si kwa ajili ya uwezo wa mwanadamu wa hiari ya asili, wala kamilifu, wala nusu, wala katika hali yoyote ile, hata iliyo ndogo zaidi au sehemu isiyo na thamani zaidi, bali katika ‘solidum,’ yaani, kwa ajili ya kazi ya kimungu tu na Roho Mtakatifu, jinsi Utetezi unavyosema.”84
Haki ya imani mbele za Mungu:
Luther alikuwa amekiri kuhusu fundisho la kuhesabiwa haki katika “Mafungu ya Schmalkaldi” yasemayo: “Hakuna lolote katika fungu hili linaloweza kushindwa ama kujisalimisha, hata kama mbingu na dunia na vyote ambavyo havitadumu vinapaswa kuangamia.”85 Lakini alihofia kwamba, fundisho hili muhimu mno la Biblia lingeharibiwa baada ya kifo chake. Hakukosea. Mwaka wa 1549, Andrea Osiander86 alidharau fundisho la kuhesabiwa haki kama
84 Shauri la Mwafaka, Tamko Thabiti, 2, 24.25.
85 Mafungu ya Schmalkaldi, 2, 1, 5.
86 Andreas Osiander (1498-1552) alianzisha Matengenezo ya Kanisa katika mji mkuu wa Nürnberg , baadaye
xliii
kisingizio tu kwa mwumini cha haki na stahili za Kristo. Alirudi katika dhana ya Kikatoliki kuhusu “neema inayomiminiwa.”87 Alifundisha kwamba, mtu anahesabiwa haki kwa njia ya Kristo anayeishi ndani yake, yaani, kwa njia ya “kumiminiwa” kwa njia ya haki ya kimsingi ya asili yake ya kimungu. Hii ilimaanisha kwamba, kuhesabiwa haki ni zaidi ya kutangazwa kuwa mwenye haki, kuondolewa dhambi zako, kwamba kuhesabiwa haki ni sawa na kufanywa mpya moyoni au utakaso. Kwa maneno mengine, si “Kristo kwa ajili yetu,” bali ni “Kristo ndani yetu”88 anayetuokoa. Mwenye dhambi anaokolewa kwa njia ya mabadiliko ambayo Kristo anayatenda ndani yake. Osiander alifundisha kwamba, haki inayotuhesabia haki, hakika ni utakatifu ulio katika kufanyika upya kwa mwanadamu, katika karama za neema, katika maisha ya kiroho, na katika asili ya mwanadamu aliyezaliwa upya. Aliandika: “Yeyote atakayehesabiwa haki, lazima aamini. Lakini kama ataamini, lazima tayari awe amezaliwa na anaishi. Kwa hiyo, Kristo hajatuhesabia haki, lakini tumekombolewa . . . Mungu pia anatamani kutuhesabia haki kwa njia ya imani katika Kristo, kwa njia ya kutumiminia kuhesabiwa haki au kwa njia ya haki.” Hivyo, dhambi “ambayo tayari imesamehewa, lakini bado inaishi na kushikamana na miili yetu, labda yote itaoza - itaweza kukanwa - na kuharibiwa ndani yetu. Kwanza kabisa, hili ndilo tendo la kuhesabiwa haki.”89
Osiander alishambuliwa na Joachim Mörlin90 aliyemkumbusha kwamba, kulingana na Biblia na Martin Luther, mwanadamu anahesabiwa haki kwa njia ya “haki ya kigeni,” yaani, haki ya mwingine. Haki yetu ni kwa njia ya kuhesabiwa haki kwa ajili ya Kristo. Huku kuhesabiwa haki kamili peke yake kunamruhusu mwumini ahakikishiwe wokovu wake. Mörlin alimshambulia Osiander hadharani katika mahubiri yake, akisema kwamba, mafundisho ya uongo kama hayo hayangeweza kuvumiliwa katika Kanisa la Kilutheri. Alilalamika kwamba, haya yalikuwa mafundisho ya Kikatoliki ya kuhesabiwa haki katika mavazi mapya. Lakini Osiander alitilia mkazo na akaaga dunia wakati mabishano haya yalishika moto.
Mtu aliyeitwa Francesco Stankaro91 alipendezwa na mawazo ya Luther. Ole wake! Alikuwa mtu mkaidi na kigeugeu ambaye alisababisha shida na matatizo akafundisha theologia katika Chuo Kikuu cha Königsberg.
87 Kilatini: Gratia infusa.
88 Kilatini: Christus pro nobis – Christus in nobis.
89 Andreas Osiander, Mpatanishi Peke yake, 1551.
90 Joachim Mörlin (1514-1571) alikuwa atoroke kwa sababu alilipinga Suluhisho la Muda. Aliitwa tena, akawa askofu wa Kanisa la Kilutheri.
91 Francesco Stancaro (ca. 1510-1574) alikuwa mtawa aliyetoka Italia. Alifanya kazi yake kule Italia, Uswisi, Ujerumani, Poland na Hungaria.
xliv
kila pahali. Alijitahidi kumshambulia Osiander, lakini alilitenda kosa lililokuwa kinyume, alipotangaza kwamba, mwenye dhambi huhesabiwa haki kwa njia ya haki ya kibinadamu ya Kristo, badala ya haki yake ya kimungu. Yeye ni Mpatanishi wetu kama mwanadamu na si kama Mungu, kulingana na asili yake ya kibinadamu mbali na asili yake ya kimungu. Hivyo, Stankaro aliiondoa asili ya kimungu ya Kristo kutoka katika kazi yake ya ukombozi ambayo ni uongo kabisa. Kama mwanadamu, Kristo alilazimika kama mwanadamu mwingine yeyote kuitimiza Sheria ya Mungu, na mwanadamu mwenye haki hawezi kamwe kuwaokoa wengine kwa njia ya haki yake. Damu inayotusafisha ni damu ya Mwana wa Mungu (1 Yoh. 1:7), damu ya mwanadamu ambaye wakati huo huo, ni Mungu wa kweli. Uasi wa Stankaro uliharibu umoja wa Yesu Kristo na akatutia mashaka kuhusu ukombozi na kuhesabiwa haki kwetu.
Fungu la Tatu la “Shauri la Mwafaka” linayakataa mafundisho yote mawili, yaani, la Osiander na Stankaro. Linasema: “Dhidi ya makosa haya mawili yaliyosimuliwa punde tu, tunaamini kwa pamoja ifuatavyo: tunafundisha na kukiri kwamba, Kristo ni haki yetu, si kulingana na asili ya kimungu, wala si kulingana na asili ya kibinadamu peke yake, bali ni Kristo mzima kulingana na asili zote mbili. Isitoshe, ni katika utii wake ambao, kama Mungu na kama mwanadamu alionyesha heshima hadi alipokufa. Kwa hiyo, kwa ajili yetu, alitustahilia msamaha wa dhambi na uzima wa milele. . . Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kuwa, kulingana na matumizi ya Roho Mtakatifu, neno ‘kuhesabia haki’ linamaanisha ‘kuondokana na dhambi,’92 yaani, ni kuutangaza uhuru kutoka dhambini93 katika fungu hili.”
Fungu hili linatukumbusha umuhimu wa kuyahifadhi mafundisho safi ya kuhesabiwa haki. Maafikiano yoyote yana matokeo ya kuharibu, kwa sababu yanamwalika muumini kuuweka msingi wake wa uhakika wa wokovu si katika Kristo peke yake, bali katika yale Kristo amemfanyia na analoendelea kulifanya katika yeye. Hayo yanamaanisha kwamba, msingi wa wokovu wetu unahusu yote mawili: lililofanyika msalabani wakati mmoja na lile linalofanyika sasa ndani mwetu. Kwa maneno mengine, kuhusu msamaha wa Kristo na kuhusu mabadiliko yanayotendeka ndani yetu. Mtu anahitaji tu kusikiliza baadhi ya mahubiri katika madhehebu mbalimbali ya Kikristo ili aweze kugundua kwamba, wokovu kwa njia ya yanayofanyika kwa wanadamu, kwa njia ya mabadiliko yanayotokea kwao na mema wanayoyafanya maishani mwao ni mahubiri ya kawaida sana, yaani ni mchanganyiko wa Sheria na Injili. Makanisa ya Kilutheri
92 Kijerumani: ‘absolvieren’; Kilatini: ‘absolvere’. 93 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 3,1.5.
xlv
yaliyolitia sahihi “Tangazo la Pamoja Kuhusu Mafundisho ya Kuhesabiwa Haki,” linaonyesha kwamba, wao ni waathiriwa wa kosa hili.
Matendo Mema:
Mabishano haya yalihusu matendo mema ya Mkristo. Wajibu wa hayo ulikuwa ni upi kulingana na theologia ya Kilutheri? Mwaka wa 1535, Melanchthon alikuwa ametangaza kwamba, matendo mema ni “lazima kwa ajili ya uzima wa milele.”94 Alilotaka kulisema kwa lazima ni kwamba, (hayo matendo mema) yalitakiwa yafuate upatanisho na kuhesabiwa haki. Jambo ambalo ni la kweli! Yeyote ambaye hayafanyi matendo mema, huonyesha kwamba yeye si muumini wa kweli. Isitoshe, njia hii ya kuyasema mambo inaweza na imeweza kueleweka visivyo. Hii ndiyo sababu iliyomfanya Luther asiitumie kamwe. Mnamo Juni tarehe 1, mwaka wa 1537, katika mabishano ya hadhara huko Wittenberg, alikuwa ameyakataa, huku akishikilia kwamba, utakaso lazima ufuate kuhesabiwa haki.
Mabishano haya yalionekana kama yaliyotatuliwa wakati Georg Major95 alipoliibua tena. Ingawa Melanchthon alikuwa amemwonya asiyatumie maneno, “lazima kwa ajili ya wokovu,” kwa sababu, kwa urahisi, yangemaanisha kwamba, ustahili unaambatanishwa na matendo mema. Major alishawishika kwamba, hakika, yalistahili kwa kiasi fulani. Alikanwa na watu kama Nicholas von Amsdorf,96 Flacius, Gallus na wengineo. Major alijibu kwamba, hakuwa amefundisha kwamba, matendo mema ni ya lazima kwa ajili ya kupata wokovu. Hata hivyo, aliamini kuwa, matendo hayo ni ya lazima ili “kuuhifadhi” wokovu upatikanao kwa njia ya imani peke yake. Georg Major aliungwa mkono na Yusto Menius,97 lakini karibu wachungaji wote wa Sachsen walilalamika. Hawakuwa tayari kuyatumia maelezo ya aina hiyo yenye utata ambayo yangekubaliwa na Kanisa Katoliki. Kueleza kwa utaratibu kuhusu mafundisho kunapohitaji maelezo yasiyokuwa na mwisho ili kuepuka kueleza vibaya, hakuwezi kulifundisha na kulijenga Kanisa. Fundisho la Luther kuhusu kuhesabiwa haki kwa njia ya imani peke yake, bila matendo ya Sheria, lilikuwa hazina ya thamani zaidi kuweza kufichuliwa kwa njia ya sintofahamu. Kusema kwamba, imani peke
94 Filipo Melanchthon “Loci Communes”, toleo la mwaka wa 1535. “Loci Communes” ni maneno ya Kilatini ambayo yanamaanisha “pahali pa kawaida.” Mafundisho ya kanuni yaligawanywa katika “mahali” (Kilatini, “locus”) yaani sura. Taarifa sawa na hiyo inapatikana katika toleo la 1537. Lakini kwenye toleo la 1543, alikomesha maneno “kwa wokovu,” alitangaza kwamba, matendo mema ni ya lazima katika maisha ya Mkristo.
95 Geog Major (1502-1574) alikuwa mwanafunzi wa Melanchthon mwenye bidii. Alifundisha theologia huko Wittenberg.
96 Nicholas von Amsdorf (1499-1558), alikuwa rafiki wa dhati wa Luther, aliteuliwa kuwa askofu wa Naumburg na Mtengenezaji Kanisa (1542).
97 Justus Menius (1499-1558) alikuwa mrakibu wa Gotha.
xlvi
yake inahesabia haki, lakini kuwa, imani hiyo hiyo daima huzaa matendo mema ni jambo moja. Isitoshe, kudai kwamba, matendo haya mema ni ya lazima kwa wokovu ni jambo jingine. Ni kweli kusema kwamba, imani huzaa matendo mema daima, lakini hili halimaanishi kwamba, uwepo wa matendo haya mema kunaipa imani uwezo wa kuhesabia haki. Imani haihesabii haki kwa sababu inazaa matunda, bali inahesabia haki kama njia sahili ya kupokea msamaha wa dhambi na wokovu, njia iliyo karama ya Mungu.
Ingawa aliahidi kwamba hangesema tena kwamba, “matendo mema ni ya lazima kwa ajili ya wokovu,” kwa sababu yangefasiriwa kwa njia mbaya, Major hakukubali kamwe kwamba, alikuwa amekosea. Kwa hiyo, mabishano yaliendelea hadi alipoaga dunia mwaka wa 1574. Huenda ni kweli kwamba, kama Flacius angekuwa mpole kiasi kuhusu alivyomtendea Major, mabishano yangekuwa yamemalizika kabla ya hayo. Lakini hata Chemnitz aliyekuwa mpole, alisema kwamba, hangeweza kukubaliana na Major.
“Shauri la Mwafaka” liliunga mkono kabisa maelezo ya mafundisho ya Flacius kuhusu suala hilo na likakataa istilahi tata iliyotumiwa na Melanchthon, Major na Menius. Anasema, “aina za hotuba zilizotajwa hapo juu hazipaswi kufundishwa, kutetewa, au kuwiwa radhi, bali zinapaswa kutupwa kutoka katika makanisa yetu na kuzikana kama za uongo na zisizo sahihi.”98 “Neno ‘lazima’ halipaswi kutumiwa kuhusu utiifu mpya.” Lakini “hili lisieleweke kana kwamba, liko katika hiari ya mtu aliyeongoka kutenda au kuvumilia kuyatenda mema atakapo, na kwamba, hata hivyo, anaweza kuiweka imani kama atavumilia katika dhambi kwa kudhamiria.”99
Kadhalika, kuna maelezo mengine ambayo yalikataliwa na “Shauri la Mwafaka.” Maelezo kwamba, matendo mema ni “yanaudhuru kwa wokovu:” “Tunayakataa na tunayalaani kama ya uchokozi na yenye kuleta hasara kwa nidhamu ya Mkristo, tangazo la kwamba: Matendo mema yanaudhuru wokovu.”100 Yalivyo ya kushangaza ni kwamba, haya ndiyo yaliyokuwa majibu ya Nicholas von Amsdorf kwa Georg Major. Hili ndilo linalotokea wakati mabishano yamechacha. Unapoteza udhibiti na unavuka mipaka ya unayopaswa kuyasema na unayoweza kuyasema, kulingana na kweli ya misingi ya Maandiko Matakatifu. Matendo mema hayakudhuru wokovu kwa njia yoyote. Yanadhuru tu mtu anapoyatumainia na anapotafuta faraja kwayo na uhakika wa wokovu. Ni jambo la kusikitisha sana, mtu anapoyapigania mafundisho ya kweli kwa dhati
98 Shauri la Mwafaka, Tamko Thabiti, 4, 29.
99 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 4, 2.6.
100 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 4, 17.
xlvii
halafu anaanguka katika makosa yaliyo kinyume anapoyakanusha makosa. Ama angalau, anaanguka katika njia isiyo ya furaha ili kuyaelezea mafundisho ya Biblia. Kwa bahati mbaya, haya ni mambo ambayo hufanyika kila mara katika Wakristo waliomo duniani/Kanisa la mapambano.101
Sheria na Injili:
Tofauti sahihi kati ya Sheria na Injili ilikuwa suala muhimu sana katika theologia ya Martin Luther. Alikuwa akisema kwamba, angekuwa tayari kumpa mtu yeyote shahada ya udaktari ambaye angeweza kuyatofautisha haya mawili kwa usahihi. Mabishano ya awali kuhusu kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu na wajibu wa matendo mema, yalionyesha wazi kwamba, wanatheologia wengi Walutheri hawakuweza tena kufanya hivyo. Hili pia ni kweli kuhusu bishano jingine linaloitwa “bishano linalopinga sheria.”102 Fungu la Tano la “Shauri la Mwafaka” linashughulikia jambo hili.
Kulikuwa na bishano jingine la kwanza linalopinga sheria wakati wa maisha ya Luther, lililochochewa na Yohana Agricola103 mwaka wa 1527 lakini lililokomeshwa haraka na Luther. Agricola alilirudia kuelekea mwaka wa 1540. Alisema kwamba, toba inafuliwa na Injili na siyo na Sheria. Aliendelea kusema kwamba, Sheria haina nafasi katika Kanisa la Kikristo, kwa sababu Wakristo wamewekwa huru kutoka katika nira yake. Alisema kwamba, pahali panapofaa sheria ni ukumbi wa mji au mahakama ya mji lakini si katika Kanisa la wanaokombolewa. Agricola alimshambulia Melanchthon kwa kuyakosoa maandiko yake kuhusu, “Maagizo kwa Wageni wa Makanisa ya Sachsen.” Luther, akigundua makosa ya Agricola katika “Maoni na maelezo fafanuzi kuhusuWaraka kwa Wagalatia,” anatangaza kwamba, wajibu wa Sheria ni kutisha dhamiri ili zijitayarishe kumkubali Yesu Kristo anayetangazwa katika Injili.
Mnamo Desemba tarehe 1, mwaka wa 1537, Luther alikataa na kuukanusha msimamo wa Agricola. Kwa kuwa hakukubali, Luther alitishia kumfukuza kama hakukana msimamo wake. Agricola aliukana Januari tarehe 12, mwaka wa 1538. Lakini kwa kuwa ukanaji wake haukuwa wa kweli, mkutano mwingine uliitwa Septemba ya mwaka huo huo kwa kusudi la kulitatua suala hilo. Ni kutokana na muktadha huu Luther aliandika makala yake: “Dhidi ya Wapinga Sheria.” Ukweli ni kwamba, Agricola hakuubadilisha msimamo wake kamwe. Kulikuwa
101 Kanisa lililo vitani ni kanisa lililo ulimwenguni ambalo linakiri na kupigania Bwana wake. Kinyume chake ni Kanisa la Ushindi lililo kule mbinguni.
102 Neno “Antinomianism” humaanisha “dhidi ya Sheria.”
103 Johannes Agricola (1492-1566), mmoja wa marafiki wa kwanza wa Luther, alifundisha katika Chuo Kikuu cha Wittenberg kabla ya kuwa mhubiri wa kitala cha Brandenburg.
xlviii
na baadhi ya watu waliomuunga mkono. Baada ya kifo cha Luther, wapinzani wake wakali walikuwa Flacius, Moerlin, Wigand104 na Westphal.105
Agricola aliipinga sheria kabisa. Alidai kwamba, sheria ilikuwa ufunuo wa Mungu katika Agano la Kale. Nafasi yake ilichukuliwa na Injili katika Agano Jipya. Baadhi ya Wanatheologia wengine kama Melanchthon na wafuasi wake hawakukifikia kiwango hicho. Badala yake, walifundisha kwamba, Injili, kinyume na Sheria, ina mwito wenye nguvu zaidi kuhusu toba kushinda Sheria. Hotuba hii ilikanganya sana kiasi kwamba, mambo yalihitaji kuwekwa wazi zaidi.
Haya yalifanywa katika Fungu la Tano la “Shauri la Mwafaka.” Tofauti ifuatayo inatolewa: “Tunaamini, tunafundisha, na kukiri kwamba, Sheria hasa ni mafundisho ya kimungu yanayofundisha yaliyo sahihi na yanayompendeza Mungu. Tena, Sheria inakikemea kila kitu kilicho dhambi na kilicho kinyume cha mapenzi ya Mungu . . . Lakini, kwa kufaa, Injili ni aina ya mafundisho yanayofundisha kile ambacho mwanadamu ambaye, hajazitii sheria na aliyelaaniwa nazo, anapaswa kuamini kwamba, Kristo amelipia na amefanya ridhaa kwa ajili ya dhambi zote. Isitoshe, mwanadamu huyo bila stahili zake zozote amepata, msamaha wa dhambi, haki inayofaa mbele za Mungu na uzima wa milele.”106 Inasemekana kwamba, Injili inaweza kutumika kuwa na maana pana kwa ajili ya yale yote ambayo Kristo ameyafundisha. Maana hii pana ni mwito kwa ajili ya toba. Lakini inapingana na Sheria inapotumika kuwa na maana finyu, “Tunaamini, tunafundisha, na kukiri kwamba, Injili si mahubiri ya toba na shutuma, bali, kwa kufaa, ni mahubiri ya faraja na habari njema mno. Injili hii haishutumu wala haitishi, bali inazifariji dhamiri dhidi ya vitisho vya Sheria. Peke yake, inaonyesha ustahili wa Kristo, na inazichangamsha tena dhamiri kwa njia ya mahubiri ya kupendeza ya neema na fadhili za Mungu zipatikanazo kwa njia ya stahili za Kristo.”107
Kwa vyovyote, ugomvi huu haukuwa suala sahili la istilahi ya jinsi neno lile lile linavyoweza kutumika kwa njia tofauti. Hatari ilikuwa ni matumizi bora ya Sheria na Injili. Tofauti kali lazima ifanywe na utata wowote lazima uepukwe, ili Sheria isigeuzwe kuwa Injili wala Injili kuwa Sheria. Zote mbili zina nafasi zao katika Kanisa la Kikristo. Sheria inahitaji kuhubiriwa ili watu wazikubali
104 Johannes Wigand (1523-1587) alikuwa mtetezi thabiti wa Ulutheri katika mabishano mengi maishani mwake.
105 Joachim Westphal (1510-1574) alikuwa mwanafunzi wa Luther na Melanchthon, alishiriki katika mazungumzo mbalimbali ya kitheologia, aliwapinga Melanchthon na Major, baadaye alimpinga Calvin na wafuasi wake.
106 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 5, 2.4
107 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 5,Ş 6.
xlix
dhambi zao na watubu. Injili lazima itangazwe ili iwaambie watu kwamba, Kristo amewakomboa na wanaokolewa kwa njia ya imani katika yeye. Kisha, inakuwa ni wajibu wa Sheria kuwaonyesha waumini wanavyoweza kumtumikia Bwana wao. Hivyo, ingawa Sheria haiwezi kumshtaki na kumhukumu muumini tena, kwa kuwa amefanywa huru kutokana na laana ya Sheria, bado anaihitaji kama kanuni inayomwambia jinsi ya kumtumikia Bwana wake. Pahali pa Sheria siyo tu katika ukumbi wa mji na mahakama, bali pia katika Kanisa la Kikristo. Ingawa wamehesabiwa haki kabisa kwa njia ya damu ya Kristo, Wakristo bado wanambeba Adamu wao wa kale. Kwa hiyo, bado wanahitaji kuisikia sauti ya Sheria ambayo inawaonyesha dhambi zao na kuwaelekeza kwenye toba kila siku. Isitoshe, wanahitaji kuisikia sauti ya Sheria ili wakumbushwe mapenzi ya Mungu daima na waambiwe jinsi ya kumtumikia, ingawa kutaka na uwezo wa kumtumikia vinatokana na Injili tu. Kutokana na maelezo haya, tayari tuko katikati ya mabishano yafuatayo.
Matumizi ya tatu ya Sheria:
Maneno machache yatatosha kuyaelezea haya mabishano mapya, kwa kuwa yalihusiana kwa karibu na hayo yaliyotangulia. Wakati mwingine yanaitwa Mabishano ya Pili ya Upingaji wa Sheria. Kadhalika, yanashughulikia Sheria, hasa katika kile kinachoitwa matumizi ya tatu. Baadhi ya Wanatheologia kama Andreas Poach, Anton Otto, na Andreas Musculus,108 walikataa kwamba, Sheria ilikuwa na wajibu wowote katika utakaso wa Mkristo. Swali lifuatalo linaulizwa: Waumini wanahitajika kufanya matendo gani mema? Ilisemekana kwamba, Sheria kama ufunuo wa Mungu katika Agano la Kale ilifundisha jinsi Waisraeli walipaswa kuishi kama watu wa Mungu. Lakini Sheria haikushughulika na matendo mema ambayo Wakristo wanaoishi katika Agano Jipya wanapaswa kuyatenda.
Hii si kweli. “Shauri la Mwafaka” linaelezea kwamba, Sheria ya Mungu ina kazi tatu tofauti. “1. Sheria inatunza nidhamu inayoonekana dhidi ya watu wakaidi na wasio watiifu. 2. Sheria inawafundisha watu kuzifahamu dhambi zao. 3. Baada ya wao kuzaliwa upya, na ingawa wanaishi katika mwili, Sheria inawawezesha kuwa na kanuni thabiti ambayo kwayo, wanaweza kuyatawala na kuyaelekeza maisha yao yote.”109 Matumizi haya ya tatu ya sheria yametiliwa mashaka na wengine. Hata hivyo, inasemekana kwamba, ingawa Kristo ametukomboa kutoka katika laana ya Sheria, hajaipiga marufuku Sheria. Kwa
108 Andreas Poach (1516-1585) na Anton Otto (1505-?), Andreas Musculus (1514-1581) wahudumu katika miji tofauti ya Ujerumani, walimwunga mkono Johannes Agricola katika bishano lililotangulia.
109 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, Fungu 6, 1.
l
kuwa, kuongolewa na kufanyika upya kwa Mkristo hakujakamilika katika maisha haya, bado dhambi imo ndani yake na kuna vita vya mara kwa mara dhidi ya mwili. Kwa hiyo, bado anahitaji kusikia mapenzi ya Mungu ni yepi kutoka katika Sheria. Asipofanya hivyo, haraka sana atajianzishia kanuni zake mwenyewe katika maisha.
Kwa kawaida, haya ndiyo yanayofanyika siku hizi. Kuhusu masuala magumu ya maadili, kuna makanisa mengi yanayodai kwamba, masuala yanayohusiana na maadili, yaliyosemwa na Biblia miaka elfu mbili iliyopita, si ya lazima siku hizi. Kwa hiyo, kaida na tabia kwa ajili ya maisha ya Kikristo vinaweza kutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine au kutoka utamaduni mmoja hadi mwingine. Maadili ya Biblia, yanaakisi misimamo ya nyakati na tamaduni za kale. Mambo yaliyozingatiwa na Wayahudi kuwa ya kweli na bora kabla ya na wakati wa Yesu, si lazima yawe ya maana katika siku hizi. Kwa hiyo, utohozi kwa ajili ya matarajio ya siku hizi ni halali kuhusiana na masuala kama ngono kabla ya ndoa, kudumu kwa ndoa, utoaji mimba, au tohara, tukitaja haya machache tu. Huu ndio mtazamo wa kawaida sana siku hizi hata miongoni mwa Wakristo.
Huu si msimamo wa “Shauri la Mwafaka.” Linaelezea wazi kabisa kwamba: Kanuni za tabia za Mkristo na maisha ya kila siku si yale mimi kama muumini au jamii ambamo ninaishi inayazingatia kuwa sahihi na bora. Hata hivyo, yaliyo sahihi na bora ni yale ambayo Mungu hufundisha katika Biblia yake, maana Biblia daima ni Neno lake, na kila pahali huyafunua mapenzi yake ya milele. Hili ni jambo muhimu sana kwa ajili ya Kanisa la Kikristo, hasa siku hizi zilizojaa changamoto za dunia ya kisasa ambamo Wakristo wanaishi na majaribu mengi yanayowazingira. Kuishi kama Mkristo si kutenda tu jinsi kila mtu anatenda, bali ni kutenda jinsi Mungu anavyotufundisha katika Neno lake. Yeyote anayedai kuwa na uwezo na haki ya kuamua mabaya na mazuri kulingana na dhamiri yake, huichukua hadhi ya Mungu na hujifanya kana kwamba yeye mwenyewe ni Mungu. Kwa hiyo, ingawa Sheria ya Mungu haiwezi kuwashtaki na kuwalaani Wakristo tena, inabaki kuwa kanuni na kawaida katika maisha yao ya kila siku maana wanahesabiwa haki kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.
Chakula cha Bwana na Nafsi ya Kristo:
Fungu hili pia linaitwa “Mabishano ya Wakalvini Wasiri.”110 Neno ‘Crypto’ lina maana ya “-a siri.” Hivyo basi, “Mabishano ya Wakalvini Wasiri” yalikuwa mabishano ambayo kwayo, baadhi ya watu walijitahidi kuyaficha mafundisho ya Kikalvini ya Chakula Kitakatifu katika istilahi ya Kilutheri. Kwa hiyo, mabishano 110 Kilatini: “Cryptocalvinismus.” Neno “crypto” linamaanisha“ kitu kilichofichwa.”
li
haya hayakuwa hatari tu bali pia maovu zaidi.
Watu ambao waliandika na kutia sahihi kwenye “Shauri la Mwafaka,” walishawishika kwamba, walikuwa warithi wa kiroho wa Martin Luther. Hawakukusudia tu kuyainamia mamlaka ya huyu mtu bali walitaka wabaki kuwa waaminifu kwa mafundisho ya Biblia aliyokuwa amewafundisha Luther katika mambo yote. Haya ni kweli hasa kuhusiana na Fungu la Saba na Fungu la Nane yanayoshughulikia Chakula Kitakatifu na nafsi ya Kristo. Haya ndiyo mambo mawili katika muktadha huu ambayo yana uhusiano wa karibu sana.
Fungu la Saba linafundisha wazi uwepo halisi wa mwili na damu yake Kristo katika Ekaristi. Yaani, umoja wao wa kisakramenti kwa ajili ya mkate na divai vilivyofanywa vitakatifu. Muungamo huu unaitwa “wa kisakramenti” kwa sababu ni maalumu kwa ajili ya Sakramenti Takatifu. Ni uwepo halisi na si uwepo wa kienyeji. Hii inamaanisha kwamba, mwili na damu ya Kristo havipatikani kienyeji katika mkate na divai. Tena, vinapokelewa hakika kwa njia ya kinywa. “Uwepo Halisi” unamaanisha kwamba, mwili na damu ya Kristo vipo kweli, na vinapokelewa na washiriki wote. Shauri la “Muungamo wa Kisakramenti” linakusudia hasa kuelezea kwamba, hili ni fumbo lisiloweza kuvumbuliwa kwa njia ya akili ya mwanadamu na haliwezi kuelezewa kabisa kwa maneno ya mwanadamu.
Fungu la Nane linaukiri muungamo binafsi wa asili ya kimungu na wa asili ya kibinadamu katika nafsi ya Kristo. Asili zote mbili zinaunganishwa pamoja na zinashiriki asili au sifa zao. Haya ndiyo yanayofundishwa na Biblia na haya ndiyo yanayoufanya uwepo halisi kuwezekana, ingawa hayawezi kuelezewa kwa njia ambayo akili ya mwanadamu inaweza kuyafahamu.
Mafungu haya mawili yalikusudiwa kuyazuia Mafundisho ya Wafuasi wa Kalvini kuhusu uwepo wa mwili na damu ya Kristo kama ishara tu yasiingie katika Kanisa la Kilutheri. Kalvini na Zwingli walishiriki mafundisho sawa kama yanavyoshuhudiwa katika kinachodaiwa kuitwa “Mwafaka wa Zürich”.111 Hii ni hati ambayo watu wengi walitamani kuikubali kama msingi wa mafundisho ya Uprotestanti wa Ulaya nzima ya wakati huo, ikiwa ni pamoja na, Uswisi, Ufaransa, Uingereza, Uholanzi na maeneo mengi ya Kusini mwa Ujerumani. Kuna baadhi ya tofauti kati ya mafundisho ya Zwingli na ya Kalvini kuhusu Chakula Kitakatifu. Kwake Zwingli, chakula hiki kilikuwa tu tendo la kiishara la kukumbuka kifo cha Kristo na kukumbuka ushirika wa waumini. Kwake Kalvini, chakula hiki kilikuwa zaidi ya hayo. Kilikuwa chombo cha neema kwa 111 Kilatini “Consensus Tigurinus”. Mwafaka huu uliyotungwa katika mwaka wa 1549.
lii
njia fulani. Hata hivyo, hawa viongozi wote wawili wa Kanisa waliukataa uwepo halisi. Wote wawili walielezea kwamba, mwili halisi na damu halisi ya Kristo havipo. Wanaendelea kudai kuwa, haviwezi kuwepo kwa sababu Kristo alipaa mbinguni. Kwa hawa wanamatengenezo Waswisi, Zwingli na Kalvini, kuna uwepo wake kila pahali katika asili yake ya kimungu, lakini uwepo wake wa mwili wa kibinadamu na damu haupo kila pahali. Haya yanaelezea uhusiano wa dhati uliopo baina ya Chakula Kitakatifu na Kristologia. Kalvini aliitumia istilahi ambayo ilikuwa karibu sana na ile ya Kilutheri,112 wakati huo huo aliwapinga vikali Walutheri.
Wachungaji na washiriki wengi wa Kanisa Kusini mwa Ujerumani na hata huko Sachsen walitaka kuyakubali mafundisho ya Kalvini kisiri. Hii ndiyo sababu waliitwa “Wakalvini Wasiri.” Jinsi tumekwisha kuona, Melanchthon alikuwa mtetezi mwenye juhudi ya msimamo wa Luther mwanzoni. Pole pole baadaye, alishawishika kwamba, Luther hakuwa sahihi na alitafuta aina ya maafikiano na upande wa Uprotestanti wa mafundisho ya Kalvini. Jinsi wakati ulivyoendelea, ndivyo alivyokuwa dhaifu siku baada ya nyingine. Kwa hiyo, aliyabadilisha maneno ya “Ukiri wa Augsburg” mara nyingi, ingawa ukiri huo ulikuwa umekubaliwa rasmi katika toleo lake la mwaka wa 1530. Kwa sababu hiyo, mtu anashangaa kama kweli alikuwa na imani halisi jinsi alivyodai mara kwa mara.
Mwaka wa 1552, Yoakimu Westphal aliwatahadharisha wenzake kwamba, Melanchthon alikuwa amewabadilisha wanafunzi wake kuwa Wakalvini Wasiri na kwamba, mafundisho ya Kalvini kuhusu Chakula Kitakatifu yalikuwa yameingia katika Kanisa la Kilutheri. Alilia kwamba, wakati ulikuwa umewadia wa kuichukua hatua. Hivyo, alikuwa mmoja wa watetezi muhimu katika vita dhidi ya Wakalvini Wasiri. Aliungwa mkono na Yohana Brenz113 na Martin Chemnitz. Lakini Ukalvini ulikuwa umepenya Uprotestanti wa Kijerumani kiasi kwamba, haungeng’olewa tena kutoka katika sehemu nyingi za nchi hiyo. Hata mji wa Wittenberg, uliokuwa ngome ya Ulutheri, ulikuwa umeathiriwa nao sana. Wanatheologia wengi wa Sachsen waliyapendelea mafundisho ya Kalvini, ingawa walidai kwamba, walikuwa waaminifu kwa “Ukiri wa Augsburg.” Walimchochea Mtawala Mchaguzi dhidi ya Walutheri waaminifu, hasa Flacius na wakauweka Mji wa Sachsen mikononi mwa Kalvini. Wachungaji waliombwa
112 Calvin alisema angetia sahihi kwa Confessio Augastana Variata, Ukiri wa Augsburg uliobadilishwa.
113 Johann Brenz (1499-1570) alikuwa mmoja wa wafuasi wa kwanza wa Luther. Alitekeleza Matengenezo ya kanisa katika ufalme wa Württemberg. Alikuwa muhubiri wa kiutendaji na aliandika vitabu vingi vilivyokusudiwa kuwafundisha watu na kujenga Kanisa.
liii
kutia sahihi “Corpus Philippicum.” Huu ulikuwa mkusanyiko wa hati mbalimbali ikiwa ni pamoja na maandiko ya Melanchthon. Wale waliokataa kuutia sahihi, walifukuzwa, wakapigwa marufuku au wakapelekwa gerezani.
Mwishowe, Mtawala Mchaguzi Agostino alikubali kuyapanga makabiliano kati ya Walutheri halisi na Wakalvini Wasiri. Ilidhihirika wazi kwamba, Wakalvini Wasiri waliyakataa mafundisho ya uwepo kila pahali.114 Mafundisho haya yalielezea kwamba, Kristo yupo kila pahali kimwili kwa msaada wa uungu wake. Kadhalika, Wakalvini walikataa kile kinachoitwa katika Kilatini, “manducatio impiorum” au “manducatio indignorum,” yaani, kauli ya kawaida ya Kilutheri kwamba, washiriki wote, hata wale wasiomcha Mungu na wenye mioyo migumu, hupokea mwili kweli na damu kweli ya Kristo katika Sakramenti. Lakini kwa ajili ya ugumu wao wa mioyo, wanavipokea kwa ajili ya hukumu yao. Sasa hali ya mambo imekuwa wazi. Wafuasi wa Melanchthon walikuwa Wakalvini
Wasiri. Aliposhinikizwa na Mfalme wa Denmaki, Mwinyi wa Württemberg na wengineo, Mtawala Mchaguzi wa Sachsen aliurudisha Ulutheri huko Sachsen. Hoja za makubaliano ziliwasilishwa na zilitiwa sahihi katika Baraza la Torgau Septemba, mwaka wa 1574. Huu ulikuwa mwisho wa mabishano ya Wakalvini Wasiri huko Sachsen.
Fungu la Saba la “Shauri la Mwafaka” linaelezea jinsi mabishano yalivyotokea, linasema hatari iliyokuwepo, na linataja baadhi ya mambo mengine mengi: “Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, Chakula Kitakatifu, mwili na damu ya Kristo, vipo kwa kweli na kimsingi na vinagawanywa na kupokewa kwa kweli katika mkate na divai.” Halafu, “Shauri la Mwafaka” linaelezea kwamba, Mungu, yaani, umwilisho wa Yesu Kristo una “aina anuai za kuwa pahali popote” na kwamba, mwili na damu ya Kristo vimo katika Sakramenti: “Sisi hatupokei mwili na damu ya Kristo kiroho kwa njia ya imani tu, bali pia kwa kinywa; tena si kwa njia ya Kikapernaumu115 ila kwa njia ya Mungu wa mbinguni, kwa sababu ya muungano wa kisakramenti.” “Shauri la Mwafaka” linasema ifuatavyo kuhusu washiriki wa sakramenti wasiostahili: “Tunaamini, tunafundisha na kukiri kwamba, siyo tu waumini wa kweli na wasiostahili, bali wasiostahili na wasioamini wote hupokea mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo. Hata hivyo, si kwa ajili ya kuwapa uzima na faraja, bali kwa ajili ya hukumu na laana
114 Kilatini: “Ubiquitas”.
115 Wapinzani wa mafundisho ya Kilutheri waliwashtaki walimu Walutheri kwamba, jinsi watu wa Kapernaumu walivyotafsiri maneno ya Yohana 6:26.52 kumaanisha kula kwa njia ya kimwili tu, vivyo hivyo, walidai kwamba, mafundisho ya Kilutheri yalimaanisha kuwa washiriki “wanachana nyama ya Kristo kwa meno yao na kuisaga kama chakula kingine chochote.” Wengine pia walithubutu kubuni kwamba, Walutheri ni watu wala watu.
iwapo hawaongoki na hawatubu.” 116 Mabishano kuhusu Chakula cha Bwana yalizaa kutoafikiana miongoni mwa baadhi ya wanatheologia kuhusu asili na tabia mbili za Kristo. Haya yalitatuliwa na Fungu la Nane la “Shauri la Mwafaka” linaloelezea kwamba, ushirika halisi wa asili na sifa hizi mbili za Kristo si kwa majina tu kama zilivyofundishwa na Wakalvini. Hii inamaanisha kwamba, lolote analolifanya Kristo, analifanya kama mwanadamu kweli na kama Mungu kweli. “Kwa hiyo, tunaamini, tunafundisha na tunakiri kwamba, Mariamu hakuchukua mimba na hakuzaa mwanadamu wa kawaida tu na hakukuwa na zaidi, bali aliichukua mimba na akamzaa Mwana wa Mungu kweli. Kwa hiyo, anaitwa Mama wa Mungu kwa haki na hakika. Kwa hiyo, pia tunaamini, tunafundisha na kukiri kwamba, hakuwa mtu wa kawaida tu aliyeteseka, aliyekufa, aliyezikwa, aliyeshuka kuzimuni, aliyefufuka kutoka kwa wafu, na aliyepaa mbinguni, kwa njia ya utukufu na enzi kuu ya Mungu kwa ajili yetu, bali ni mwanadamu ambaye asili yake ya kibinadamu ni muungano na ushirika na Mwana wa Mungu wenye maana sana na usioelezeka ambao ni nafsi moja pamoja na yeye.”117 Sifa za kimungu za Kristo haziwi asili yake ya kibinadamu, na vivyo hivyo, sifa zake za kibinadamu haziwi asili zake za kimungu. Tena, tabia zake safi za asili yake ya kimungu zinatolewa kwa njia ya umwilisho kwa ajili ya asili yake ya kibinadamu, ili mwili wake uwepo kila pahali na kwa hiyo, huwepo kweli katika Sakramenti.
Tukichunguza jinsi hali ilivyo sasa katika ulimwengu wa Uprotestanti, tunagundua jinsi mafungu haya mawili yalivyo muhimu. Siku hizi, makanisa mengi ya Kilutheri yametupilia mbali mafundisho ya Luther na ya “Shauri la Mwafaka” kuhusu Chakula Kitakatifu. Au kwa njia sahili, tunaweza kusema, kwao, fundisho la uwepo halisi jinsi linavyoelezewa na Biblia na kuelezewa kwa utaratibu na Kiri za Kilutheri, si muhimu vya kutosha kulidumisha kwa gharama yoyote na kulizingatia kama kizuizi kwa ajili ya ushirika wa kanisa. Vinginevyo, hawangekuwa na mkataba na Makanisa ya Kikalvini kwa kutia sahihi maandiko ambayo yanaonyesha wazi kwamba, yanaafikiana na mafundisho ya Zwingli au ya Kalvini. “Hoja za maafikiano” za kitheologia ambazo zimetolewa wakati wa miongo iliyotangulia zingetiwa sahihi na washiriki wote. Hali haingekuwa vile kama Makanisa hayo hayo ya Kilutheri yangekuwa yanafuata nyayo za Luther. Ingawa hatuwezi kusema kwamba, maandiko yote kuhusu mafundisho au matangazo ya maafikiano ambayo yametolewa karibuni yanaonyesha wazi wazi mafundisho ya uongo, mambo yameelezewa kwa utaratibu kiasi kwamba, yanaweza kuidhinishwa na washiriki wote. Kwa kawaida, mafundisho ya kweli yanapuuzwa na kufifishwa mara kwa mara, ili kila mtu aweze kuzifafanua hati
116 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 7,1.4.5.7.
117 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 8, 7.8.
lv
hizi kwa njia ambayo dhamiri yake itanyamazishwa. Basi, ukweli unatolewa kwa urahisi sana, kama vile dhabihu katika madhabahu ya itikadi ya umoja.
Kushuka Kuzimuni kwa Kristo:
Biblia inafundisha kwamba, baada ya Yesu Kristo kuuawa, “Roho yake ikahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea Roho waliokaa kifungoni, akawahubiri” (1 Pet. 3:18.19). Hii ndiyo inayoitwa kushuka kuzimuni kwa Kristo. “Mahubiri” haya hayakunuiwa kuwaongoa wale walio kuzimuni, kwa kuwa kulingana na Biblia, ni wazi kwamba, hakuna nafasi ya kuongoka baada ya kifo. Alienda huko kutangaza ushindi wake dhidi ya kifo na jehanumu.
Maneno machache yatafaa kuelezea sifa za mabishano kuhusu kushuka kuzimuni kwa Kristo. Mwaka wa 1533, Luther alikuwa amefundisha katika mahubiri aliyoyahubiri huko Torgau kwamba, Kristo alikuwa amekwenda kuzimuni kulingana na nafsi zote mbili, yaani, mwili wake na nafsi yake. Tendo hili ndilo lililokuwa hatua ya kwanza katika utukufu wake. Alikuwa ameenda kuzimuni kuutangaza ushindi wake dhidi ya Ibilisi na pepo wabaya wote. Ilikuwa aina ya maandamano ya kuutangaza ushindi wake katika ufalme wa Shetani. Kalvini na wafuasi wake walikuwa na dhana nyingine tofauti kuhusu kushuka kwake kuzimuni. Waliamini kwamba, ilikuwa sehemu ya hali yake ya udhalilishwaji, njia ya mfano au ya kiishara ya kusema kwamba, alikuwa na aliteseka kuzimuni alipokuwa akifa msalabani.
Yohana Aepinus,118 mhubiri mmoja katika Kanisa la Hamburg, alikubaliana na mafundisho ya Wakalvini katika suala hili. Alifundisha kwamba, kushuka kwake kuzimuni kulikuwa sehemu ya mateso ya Kristo. Aliendelea kufundisha kwamba, kwenda kwake kuzimuni kulimaanisha kuwa alivumilia laana na mateso ya kuzimuni kwa niaba yetu. Hayo ndiyo aliyowaelezea wachungaji wa Hamburg alipokuwa akiwafundisha. Aepinus aliwasilisha kukataa kwao. Wapinzani wa Aepinus walidai kwamba, kabla ya kufa, Kristo alisema: “Imekwisha” (Yn. 19:30). Hii ilimaanisha kwamba, ukombozi wa ulimwengu umekamilishwa msalabani. Kwa hiyo, kushuka kuzimuni kwake kulifanyika baada ya tamko hilo na kulikuwa sehemu ya utukufu wake.
Baraza la mji wa Hamburg liliutaka ushauri wa Melanchthon. Aliwaambia kwamba, msimamo wa Luther kuhusu suala hili ulijulikana na mtu anapaswa kufuatwa. Aepinus alifariki mwaka wa 1553, lakini bado kulikuwa na baadhi ya maswali miongoni mwa wachungaji. Baadhi yao walielekea kuukubali mtazamo 118 John Aepinus (1499-1553) alikuwa mfuasi wa Matthias Flacius na Walutheri halisi.
lvi
wa Kalvini. Kwa hiyo, waandishi wa “Shauri la Mwafaka” waliamua kurudia imani ya Luther na wakaelezea: “Inatosha kujua kwamba, Kristo alishuka kuzimuni, aliiharibu kuzimu kwa ajili ya waumini wote, na aliwakomboa kutoka kwa mamlaka ya kifo, ya Ibilisi, ya laana ya milele, na kutoka kwa mapatilizo ya kuzimu.”119 Pia ilisemekana kwamba, masuala yote yasiyokuwa na maana na ya uzushi kuhusu ni lini hakika haya yalifanyika, hayakufaa na yanapaswa kuepukwa kwa sababu hayakuwa na nafasi katika Kanisa.
Kaida za Kanisa au kinachodaiwa kuitwa Mambo Ambayo si Lazima Kuyajali.
“Adiaphoron” ni neno la Kiyunani ambalo lamaanisha “kutojali.” Wingi wake ni “adiaphora.” “Adiaphora” ni mambo ya kutojali, mambo ambayo Biblia haiyaamrishi wala haiyakatazi. Kwa kawaida, neno hili linatumika katika kuhusiana na desturi, kaida na sherehe.120
Jinsi tumekwishaona, “Suluhisho la Muda la Leipzig” (1548)121 lilitekeleza baadhi ya maafikiano kuhusu mambo yanayohusiana na mafundisho na lilihitaji kwamba, Walutheri waanzishe tena kaida za Katoliki katika Makanisa yao kwa mfano: Mpako Mtakatifu, uimbaji wa Kigregoriano, mavazi ya kipadre, na sherehe mbalimbali za liturgia kama vile karamu za Mariamu. Haya yalisababisha shida nyingi katika Kanisa la Kilutheri. Mabishano yaliyoitwa “Mabishano yasiyojaliwa” yalikuwa yanaendelea. Suala lilikuwa iwapo Walutheri wangeweza tena kuleta sherehe za Kikatoliki kanisani kwa dhamiri nzuri. Sherehe zilizoathiriwa na mafundisho ya uongo ziliachwa. Lakini je, sherehe na kaida ambazo hazikuwa na uhusiano na mafundisho ya Kilutheri zingefanyiwa nini? Je, zingeweza kuanzishwa tena bila kuyaingiza mafundisho matatani kwa njia yoyote, hasa yaliyolazimishwa na mamlaka ya raia? Je, yangeweza kufanywa bila kuukana uhuru wa Mkristo na kukashifu maadui na marafiki hasa wale ambao ni dhaifu katika imani?
Mara nyingine tena, Melanchthon na Flacius ndio waliokuwa wapinzani wakuu katika mabishano haya. Melanchthon ambaye aliipa kipaumbele amani katika Kanisa na dola, alifikiria kwamba, Suluhisho la Muda la Leipzig lingeweza kutekelezwa bila hatari yoyote, mradi tu ukweli wa Biblia usikiukwe. Flacius alikuwa na mtazamo tofauti. Bila shaka, sherehe ambazo zilikuwa kinyume
119 Shauri la Mwafaka, Muhtasari,9, 4.
120 Kiyunani, αδιαφορον
121 Maafikiano mawili yalilazimishwa na Kaisari na Mtawala Moritz wa Sachsen kwa Walutheri baada ya Vita vya Schmalkald 1546-1547, yaani Suluhisho la Augsburg Kusini mwa Ujerumani na lile la Leipzig katika Sachsen.
lvii
cha Biblia ziliondolewa kutoka mwanzoni. Lakini hakutaka kuanzisha mambo ya kutojali, yaani kaida ambazo hazikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mafundisho ya Kanisa. Kwa kuwa, hazihitajiki wala hazikatazwi na Maandiko Matakatifu, kwa kawaida, zingeachwa tu sawa na kukubaliwa. Lakini wakati ukiri wa imani ya kweli u hatarini, hizi zinaweza kuwa jambo la dhamiri, hasa zinapolazimishwa kwa waumini na hivyo basi kuwanyima uhuru wao wa Kikristo na kuwaweka chini ya nira ya mwanadamu. Au wakati zikianzishwa, zinaweza kutafsiriwa na wengine kama kuukataa ukweli. Hivi ndivyo hali ya mambo ilivyokuwa katika “Suluhisho la Muda la Leipzig.” Dhamiri nyingi zilikuwa zimekashifiwa na kudhoofishwa. Kwa urahisi, watu wangeweza kuhisi kwamba, Walutheri walikuwa wamekosea kwa njia nyingi na kwamba, mwishowe, walisahihisha makosa yao mengi kwa njia ya kukubali anuai kulikofanywa na Roma.
Hakika, wafuasi wa Suluhisho la Muda walipinga kwamba, walikuwa wakweli, na waliichukua hatua kwa dhamiri safi kwa ajili ya amani. Si hata Martin Luther hakuvumilia baadhi ya kaida za Kikatoliki kwa sababu alitaka kuwaokoa waliokuwa dhaifu? Bila shaka, ndiyo, lakini maadui wa Suluhisho la Muda walijibu kwamba, muktadha na hali havikuwa sawa. Ilimbidi Luther awashughulikie Wakristo dhaifu. Alikuwa amependelea kuvumilia desturi fulani mradi tu akitumainia kwamba, bado maafikiano na Roma yangewezekana. Wakati huu ulikuwa umekwisha kabisa na Kanisa Katoliki lilidhihirisha wazi kwamba, maafikiano hayangewezekana wala hata hayakutakiwa. Mwishowe, mambo ambayo Luther aliyakubali kwa unyofu, sasa yalilazimishwa kwa watu. Wakristo hawawezi kunyamaza wakati mambo yanalazimishwa kwao kama yaliyo ya lazima kwa ajili ya wokovu. Kukubali hakuruhusiwi kama unataka tu kuepuka ulipizaji kisasi na mateso. Ukiukataa ukweli kwa ajili ya amani, unamchukiza Bwana.
Mwishowe, Flacius alishinda kesi. Msimamo wake uliidhinishwa na Fungu la Kumi la “Shauri la Mwafaka:” “Kwa kusudi la kuhitimisha mabishano haya, tunaamini, tunafundisha na kukiri kwamba, sherehe au kaida za Kanisa hazijaamriwa wala kukatazwa katika Neno la Mungu. Badala yake, zimeasisiwa peke yake kwa ajili ya nidhamu na utaratibu bora, na zenyewe haziwi ibada ya kimungu.” “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” (Mt. 15:9). . . Tunaamini, tunafundisha na kukiri kwamba, Kanisa la Mungu122 “lina uwezo, kulingana na hali zake, kuzibadilisha sherehe za aina hiyo kwa njia inayoweza kuwa ya manufaa zaidi na ya kuyarekebisha maadili kwa 122 Kufuatana na andiko la Kilatini. Kijerumani, ‘Geimende’ (‘Jumuiya’).
lviii
ajili ya usharika wa Mungu.” Lakini “wakati wa mateso, ambapo ukiri dhahiri wa imani unahitajika kutoka kwetu, hatupaswi kukubali kushindwa na maadui katika mambo kama hayo ambayo si ya lazima kujali . . . Maana, katika hali ya namna hiyo, si suala linalohusu mambo ya kutojali tena, bali ni jambo linalohusu ukweli wa Injili na uhuru wa Kikristo. Hali kadhalika, linahusu uzuiaji wa makosa ya walio dhaifu katika imani.”123
Hili pia ni funzo kwa Kanisa la Kilutheri la wakati wote. Ni muhimu sana kutofautisha kati ya mafundisho na mambo ya kutojali. Yaani, kati ya mambo ambayo yanadhihirishwa wazi katika Neno la Mungu na yale ambayo hayajaamrishwa wala kukatazwa. Kutojali, yaani, “adiaphoron,” ni kutojali . Tusisubuthu (kutojali) kulazimisha kwa Kanisa au kwa dhamiri za Wakristo. Vile vile kusikomeshwe bila sababu bora. Lakini pia ni kweli kwamba, iwapo jambo ambalo Kanisa lina haki ya kulitekeleza, linaweza kueleweka vibaya na kufafanuliwa visivyo na washirika dhaifu au watu kutoka nje, basi lazima liepukwe. Mtume Paulo ameandika katika muktadha tofauti lakini ulio sawa kwa njia fulani: “Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo” (1 Kor. 10:23). Daima, lazima maswali yawe: Je, jambo ambalo tungependa kulianzisha katika Kanisa linaweza kumtukuza Bwana na kuyarekebisha maaadili ya waumini? Je, ni kwa ajili ya asili kama hiyo ambapo ukweli wa Mungu unahifadhiwa, unatangazwa na unaheshimiwa?
Majaliwa ya milele au Uteuzi wa Mungu.
Mafundisho ya majaliwa ya milele au uteuzi wa Mungu kuhusu wanadamu ulikuwa mdahalo wa mwisho uliotatuliwa na “Shauri la Mwafaka.” Kwa kweli, hayakuwa mabishano ndani ya Ulutheri jinsi yalivyokuwa katika makanisa ya mafundisho ya Kalvini. Hata hivyo, mambo hayakuwa wazi akilini mwa watu wengi. Upande mmoja ulikuwa na mafundisho ya Kalvini kuhusu majaliwa maradufu ya milele, yanayosema kwamba, hata kabla ya Mungu kuumba ulimwengu, alikuwa ameamua kwamba, angewaokoa baadhi ya watu na angewatelekeza wengine milele. Si mapenzi yake kuwa wenye dhambi wote wapate uzima wa milele kwa njia ya Yesu Kristo. Haya ni maelezo ya kutisha. Hata hivyo, haya ndiyo mafundisho rasmi ya Kalvini na ya Kikalvinisti. Mafundisho haya hayakupata wafuasi katika Kanisa la Kilutheri. Kinyume chake, kulikuwa na waliofundisha kuhusu kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu124 katika Kanisa la Kilutheri. Kwa kweli, hawa walifundisha kwamba,
123 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 10, 1.2.4.
124 Kilatini: Synergismus.
lix
Mungu angependa kuwaokoa watu wote, lakini kwamba, hili halitoshi. Ili kuuleta wokovu, utashi wa mwanadamu lazima ushirikiane na utashi wa Mungu. Isitoshe, wanadamu wana dhima yao ya kutekeleza. Wote hawana mwenendo sawa, na tofauti hii katika mienendo yao inaelezea sababu ya wengine kuokolewa na wengine kutookolewa.
Maswali ni: Je, Ni ni lipi huja kwanza, uteuzi au imani? Kwa maneno mengine, je, katika milele yote, ninaamini kwa sababu Mungu aliniteua kabla ya kuuweka msingi wa ulimwengu? Je, ninaamini kwa sababu ameamua kuwa, angenileta katika imani na hivyo aniokoe? Kutokana na maswali haya, wongofu na imani ni matokeo ya moja kwa moja ya kudura ya Mungu. Au ni kinyume chake: Imani yangu inatangulia kudura? Yaani, katika milele yote, Mungu ameamua kuniokoa, hata kabla ya kuniumba? Alijua kwamba, ningeipokea Injili yake na niiamini? Ikiwa ni hivyo basi, uteuzi wangu ungekuwa matokeo ya moja kwa moja ya imani ambayo Mungu aliiona mbeleni katika milele yote. Hali hiyo ingemaanisha kwamba, uteuzi na wokovu wangu vimewekwa mikononi mwangu, kumaanisha kwamba, hivyo viwili havingekuwa vya bure na hiari kabisa. Kwa kuwa Kalvini alisema: wokovu ni kwa njia ya neema pekee yake, maana yake ni kwamba, kwa kuwa siyo watu wote wanaookolewa, Mungu hataki kabisa kuwaokoa wote. Kauli kuhusu mafundisho ya kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu inaelezea jambo tofauti kabisa. Kauli hii inafundisha kwamba, Mungu anataka kuwaokoa watu wote, lakini kwamba, si wote wanaookoka kwa sababu neema peke yake haitoshi. Ni lazima mwanadamu achukue hatua ya kuikubali Injili. Mwanzoni, Mungu aliwateua wale aliojua kwamba, wangeikubali na kuiamini Injili. Inasemekana kwamba, hii ndiyo sababu iliyomfanya Mfalme Daudi aokolewe, ilhali Mfale Sauli alipotea. Kwa nini Petro alizitubu dhambi zake na akaokolewa ilhali Yuda Iskariote alikataa kuzitubu dhambi zake na hivyo akalaaniwa?
Kulikuwa na mwanzo wa mabishano katika mji wa Strasbourg ambapo Walutheri na Wafuasi wa Kalvini waliishi pamoja. Yohana Marbach125 aliuanzisha Ulutheri halisi lakini alikuwa na hasimu aliyeitwa Hieoronimo Zanchi126 ambaye alikuwa Mkalvini Msiri. Mdahalo wa huko Strasbourg uliwachochea waandishi wa “Shauri la Mwafaka” kuongezea Fungu la Kumi na Moja katika ukiri wao. Walitaka kuyahifadhi yote mawili, yaani, “sola gratia” na “gratia universalis.”
125 Johann Marbach (1521-1581) alikuwa mchungaji mkuu wa Strasbourg ambapo alifanya kazi ya kurudisha mafundisho ya Matengenezo ya Kanisa na mafundisho ya Kilutheri.
126 Hieronymus Zanchi (1516-1590) mtawa wa zamani wa Daraja la Kiagostno kule Italia, alishawishiwa sana na Calvin huko Geneva ambapo alifundisha theologia kabla ya kwenda Strasbourg ambapo alijishughulisha na mabishano tofauti.
lx
Yaani madai kwamba, watu wanaokolewa kwa njia ya neema ya Mungu peke yake na kwamba, neema hii ni kwa watu wote. Kwa hiyo, waliisababisha tofauti kali kati ya ufahamu wa mapema wa Mungu unaoenea kwa watu wote, walio wacha Mungu na waovu, na majaliwa yake yanayoshughulikia tu wateule na kuufanya wokovu wao upatikane. Hata hivyo, ingawa Mungu huyaona yote mbeleni, ikiwa ni pamoja na maovu yatendwayo na wanadamu, yeye si msababishi wa maovu na dhambi.127
Uteuzi wa Mungu ni wa bure na usiostahilika kabisa. Kwa sababu ya uteuzi huu uliochukuliwa na Bwana katika milele yote, wanadamu wanaletwa katika imani, wanaongolewa, wanahesabiwa haki, na wanahifadhiwa katika imani mpaka wafe na kuingia katika uzima wa milele. Yale yote anayoyafanya Mungu maishani mwao ili awaokoe ni matokeo ya majaliwa yao. Wenye dhambi wanaokolewa kwa neema peke yake na Mungu anawataka wote waokolewe. Hata hivyo, siyo watu wote wanaochaguliwa kwa ajili ya uzima wa milele. Maelezo haya mawili yanapingana. Hakika, hakuna jawabu kwa maswali yafuatayo: Ikiwa wokovu ni kwa neema peke yake, ikiwa neema hii ni kwa ulimwengu wote, na ikiwa neema hii inatolewa kwa watu wote, kwa nini wote hawaokolewi? Mwisho, kama Mungu anataka kuwaokoa watu wote, kwa nini hakuwateua wote waingie katika uzima wa milele? Hili ndilo fumbo ambalo “Shauri la Mwafaka” halitarajii kulitatua. Ni miongoni mwa mafumbo ambayo Luther na Ulutheri halisi uko tayari kuishi nalo.
Hapa kuna maelezo machache ya kawaida kutoka katika “Shauri la Mwafaka:” “Majaliwa au uteuzi wa milele wa Mungu unahusu tu wachaji, watoto wake wapendwa, naye Mungu kama chanzo cha wokovu wao . . . Majaliwa haya hayapaswi kuchunguzwa katika mawaidha ya siri ya Mungu, bali haina budi kutafutwa katika Neno lake ambamo inafunuliwa.”128 Hii inamaanisha kwamba, uteuzi wa Mungu ni sehemu ya Injili inayomtangaza Yesu Kristo: “Kristo anawaita kwake wenye dhambi wote na anawaahidi furaha. Kwa bidii, angependa kwamba, watu wote waje kwake na wateseke wenyewe ili waweze kusaidiwa129. . . Hatuna budi kujifunza mafundisho haya kuhusu majaliwa, kutoka katika Injili takatifu juu ya Kristo peke yake.”130
Mafundisho ya majaliwa ya Mungu hayajafunuliwa ili tuwe na fumbo la kulitafakari na kujaribu kulifafanua, bali yamefunuliwa kwa ajili ya faraja yetu. Si wajibu wetu kuibua uzushi kuhusu hili, lakini kwa upole, tunaalikwa kuamini
127 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 11, 1.2.
128 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 11, 4.5.
129 Mt. 9:2, 9, 22, 29, 35, 37; 11:28.
130 Shauri la Mwafaka, Muhtasari, 11, 7.9.
lxi
kwamba, iwapo tunamtumainia Yesu Kristo sasa, ni kwa sababu Mungu ameamua kutuokoa milele kwa njia ya Yesu Kristo. Hii siyo “amri ya kutisha” ambayo Kalvini aliizungumzia, bali ukweli wa ajabu kwamba, tu mikononi mwa Mungu na atafanya lolote kulitimiza aliloliamua kwa ajili yetu. Uhakika huu ni kwa ajili ya waumini wanyenyekevu na siyo kwa ajili ya wasioamini au walio Wakristo kwa jina tu. Uhakika huu ni chanzo cha furaha, na siyo utiaji moyo kwa ajili ya uzembe kiroho, unafiki kidini, na usalama kimwili. Kanisa la Kilutheri huamini, hufundisha, na hukiri yote mawili kwamba, wokovu ni karama ya bure ya Mungu iliyokusudiwa kwa ajili ya wote, na kwamba, “wengi wameitwa bali wachache wameteuliwa,” bila kujaribu kuyapatanisha kabisa yote mawili.
Kwa kweli, mafundisho ya Kibiblia kuhusu majaliwa ya milele ya Mungu humtukuza Bwana na huisifu neema yake vizuri. Lolote liendalo zaidi ya ukweli huu uliofunuliwa katika Biblia ni tupu, lisilokuwa na manufaa, na lenye uzushi hatari zaidi! Watoto wa Mungu wanaombwa na Baba yao aliye Mbinguni waamini ufunuo wake hata wakati hawauelewi kabisa. Yale yanayowapa shida kuyafahamu sasa, watayafahamu kabisa mara tu watakapokuwa mbinguni.
Haya yanalingana kabisa na aliyoyaandika Martin Luther mwaka wa 1526 katika makala kuu inayoitwa “Utumwa wa Hiari.”131 Katika kitabu hiki, aliyatoa maelezo makuu machache ambayo yanastahili kutolewa hapa:
• Mwanadamu yu huru katika upeo ambao Mungu
• Mwanadamu anaweza kumpinga “Deus revelatus,” yaani, “Mungu aliyefunuliwa.” Huyu ni Mungu ambaye amejifunua mwenyewe katika Maandiko Matakatifu, bali si “Deus absconditus,” yaani, “Mungu aliyefichwa.” Huyu ni Mungu aliye katika enzi yake kamili na asiyechunguzika. Pale ambapo Mungu hajajifunua mwenyewe, anautumia utashi wake mkuu.
• Mungu anayatumia mamlaka yake kwa njia ya wasiomcha, lakini yeye si mwanzilishi wa uovu wanaoutenda. Sifa mbovu za matendo ya wanadamu ni sehemu ya upotovu wao wa asili.
• Mungu ndiye mwanzilishi wa wokovu wetu. Angependa kuwaokoa watu wote. Hii inamaanisha kwamba, iwapo baadhi yao wataangamia, haitakuwa wajibu wake bali
131 Martin Luther, “Utumwa wa Hiari”, toleo la St. Louis, toleo la Kijerumani W2 18, p. 1668-1969. Kichwa cha asili cha Kilatini cha kitabu ni “De Servo Arbitrio.” Yalikuwa jibu kwa makala yaliyoitwa “Uhuru wa Hiari”, yaliyoandikwa na mtaalamu mkuu wa elimu ya ubinadamu wa siku hizo, Desiderius Erasmus wa Rotterdam (1466-1536).
lxii
• “Kwa neema pekee”132 peke yake yanaweza kutoa uhakika wa wokovu. Kwa kiasi kidogo, iwapo wokovu wetu ungetegemea na tabia zetu, hatungekuwa na hakika nao kamwe. Luther alikumbuka matukio mabaya aliyokumbana nayo katika jumba la watawa alipokuwa haifahamu Injili ya kweli.
• Watu huuliza maswali mengi: Kwa nini Mungu aliwaruhusu wanadamu kuanguka dhambini? Je, hangeweza kuzuia kuanguka huko? Kwa nini aliwaruhusu wanadamu wote kuambukizwa dhambi ya asili? Kwa nini haubadilishi utashi mwovu wa wanadamu kuwa utashi mwema kabla hawajazaliwa?
• Maswali mengi kuhusu Mungu aliyefichwa hayapati majibu kutoka katika Neno lake. Mwishowe, hatujui sababu yake, maana wote wamepotoka na wako chini ya laana ileile. Vile vile, hatujui kwa nini wengine wanaokolewa na wengine wanaangamia. Lakini sisi ni nani kuweza kupingana na Mungu na kuweza kuihoji haki yake na wema wake? Hakuna mkanganyiko katika Mungu, na linaloonekana kuwa utashi wake usioeleweka na unaokanganya, litapata suluhisho siku moja.
Kuna wanatheologia wanaoshikilia kwamba, kuna tofauti katika mafundisho ya majaliwa baina ya Luther na Kiri za Kilutheri. Wanaendelea kusema kwamba, Luther aliikaribia dhana ya Kalvini kuliko ya wafuasi wake. Kwa urahisi, tutakubali kwamba, aliyasema mambo kwa njia thabiti kuliko walivyosema. Hata hivyo, Luther ni Luther! Hakuna mkanganyiko kati yake na yale waliyoyasema waandishi wa “Shauri la Mwafaka.” Waliyoyasema yamekubaliwa rasmi kama mafundisho ya Kanisa la Kilutheri. Wale wanaodai vinginevyo, bado wanatuwia thibitisho la madai yao.
Uasi na Madhehebu Mengine:
Mafungu Kumi na Moja ya kwanza ya “Shauri la Mwafaka” yanaonyesha kwamba, maafikiano yalikuwa yamefikiwa katika Kanisa la Kilutheri kuhusiana na idadi fulani ya mafundisho yaliyobishaniwa. Mwaka wa 1580, Kanisa hili liliamini na kufundisha ukweli ule ule lililoukiri mwaka wa 1530 katika Baraza la Augsburg. Wakati huo, dini na madhehebu mengi yaliibuka, mengi yao yakiwa ya kundi la Waanabaptisti. Hawa walikuwa wale waliofundisha kuhusu kazi ya mwanadamu pamoja na Mungu kwa ajili ya wokovu. Walifundisha kwamba, mwanadamu ana uwezo, kwa njia ya uamuzi wa binafsi, kushirikiana na kuzaliwa 132 Kilatini, “sola gratia”.
lxiii
mara ya pili. Miongoni mwa mambo mengine, walikataa Ubatizo wa watoto na wajibu wa waumini katika kuyakubali mamlaka ya kiraia. Wakatoliki wengi walilichukulia Kanisa la Kilutheri kuwa, liliwajibika kwa ajili ya ueneaji wa vikundi hivi. Kwa hiyo, ilikuwa muhimu sana kwa Kanisa la Kilutheri kutangaza hadharani kwamba, halikutaka kuhusishwa kabisa na wao na kwamba, kulikuwa na mambo muhimu sana ambayo hawakuafikiana kabisa.
Kwa hiyo, “Shauri la Mwafaka” lina sura ya mwisho ambapo mafundisho tofauti ya uongo yanayofundishwa na Waanabaptisti, yanatambuliwa na kulaaniwa. Mafundisho ambayo yanakataliwa ni yale yanayokana kuzaliwa kwa Yesu na Bikira, uungu, dhambi ya asili, na yanayokana haja ya Ubatizo wa watoto. Au yanayodai kwamba, mamlaka ya kiraia imeanzishwa kwa ajili ya wasioamini na kwa ajili ya waovu katika ulimwengu huu, lakini kwamba,Wakristo hawalazimishwi kuitii.
Miongoni mwa watu hawa, kuna mtu mmoja anayetajwa kwa njia maalumu katika “Shauri la Mwafaka.” Mtu huyu ni Caspar Schwenkfeld133 aliyekuwa Mkristo wa kawaida aliyeshawishiwa na mawazo ya Luther. Alitekeleza wajibu muhimu katika Matengenezo ya Kanisa huko Silesia. Alikuwa mtu mwenye nafsi huru na aliyapinga Matengenezo ya Kanisa la Kilutheri kuhusiana na masuala mengi sana. Masuala hayo ni kama: mafundisho kuhusu kuhesabiwa haki, kushikilia Maandiko Matakatifu bila masharti kama asili na kanuni ya imani tu, mafundisho ya huduma iliyoanzishwa kimungu au kuamini katika ufanisi wa sakramenti kama vyombo vya neema. “Shauri la Mwafaka” linataka kuelezea wazi kwamba, Walutheri hawahusiki na mawazo haya mapya. Wala hawahusiki na na mafundisho yanayokataa Utatu Mtakatifu, kuzuka tena kwa uasi wa kale wa Ario unaokataa uungu wa Kristo na Utatu Mtakatifu na uliokuwa unataka kujitokeza tena.
Shuhuda za Mababa - Orodha ya Shuhuda
Hii si sehemu ya “Shauri la Mwafaka,” lakini iliongezwa kama kiambatisho cha “Kitabu cha Mwafaka.” Sehemu hii iliandikwa na Jacob Andreae na Martin Chemnitz na ilipokelewa katika “Kitabu cha Mwafaka” kwa njia ya pendekezo la Chemnitz mnamo Januari, mwaka wa 1580. Wanatheologia wengi Wakalvinisti Wasiri walidai kwamba, “Shauri la Mwafaka” lilikuwa limeanzisha katika Fungu linalohusu nafsi ya Kristo na katika Chakula Kitakatifu “maelezo mageni, ya ajabu, yaliyobuniwa na mtu binafsi, yasiyokuwa ya kawaida, na mapya kabisa.”
133 Caspar von Schwenkfeld (ca. 1489-1561) alikuwa mshauri katika kitala la Mwinyi wa Liegnitz, Silesia, nchi ndogo katika Ulaya wa Kati.
lxiv
Orodha hii inajumlisha madondoo mengi kutoka kwa Sinodi Kuu za kwanza za Kanisa Katoliki134 na madondoo mengi ya akina Baba wa Kanisa135 waliosifika na wenye ushawishi mkubwa. Madondoo haya yote yanaelezea kwamba, Kristo ana asili mbili. Yaani, asili ya kimungu na asili ya kibinadamu na kwamba, kuna ushirika kamili kati ya asili hizo kiasi kwamba, tabia zao zote za kimungu na za kibinadamu zinakuwa za nafsi nzima ya Kristo. Madondoo haya pia yanaonyesha kwamba, tabia za asili yake ya kimungu zinawasiliana na asili yake ya kibinadamu. Hii inamaanisha kwamba, mwili wa Kristo unashiriki katika sifa za asili yake ya kimungu, kwa mfano, kama uwepo wake kila pahali. Kwa hiyo, uwepo halisi wa mwili na damu yake kunawezekana. Hata hivyo, Kanisa la Kilutheri haliyahusishi mafundisho na Kristologia ya Biblia, bali linayahusisha maneno yale aliyoyasema Kristo alipokianzisha Chakula Kitakatifu. Hivyo basi, “Shuhuda za Mababa” zilikusudiwa kudhihirisha kwamba, madai ya maadui yalikuwa ya uongo. Isitoshe, shuhuda hizo zinadhihirisha kwamba, Kanisa la Kilutheri halikiri tu mafundisho sawa na yale yanayofundishwa na kukiriwa na Kanisa la Kikristo la Kwanza, bali pia linakiri kwa njia ya istilahi ile ile.
Hitimisho:
Huu ndio mwisho wa Utangulizi wetu wa “Kitabu cha Mwafaka.” Kuna wanatheologia wengi siku hizi wanaotangaza kwamba, Kiri za Kanisa la Kilutheri ni hati muhimu na za thamani za kitheologia za karne ya kumi na sita. Hasa zinatoa ushuhuda wa yale Kanisa la Kilutheri liliamini na kukiri wakati huo. Lakini, kama ilivyoelezewa katika toleo la Kifaransa la “Kitabu cha Mwafaka,” “mambo ambayo Ukiri wa Imani unayatangaza siyo kweli ambazo lazima zikubaliwe kwa ajili yazo zenyewe. Ni Neno la Mungu lisilobadilika na kamili linaloupata msemo wake katika Ukiri wa imani. Msemo huu unauchukua muundo wa ushuhuda wa kibinadamu, yaani, ule wa neno pungufu . . . Kama maoni na maoni na maoni na maelezo fafanuzi kuhusu Maandiko Matakatifu, Kiri wa Imani ni hati za imani zilizohusishwa na hali halisi ya kihistoria na ufahamu kifasili wa wakati huo. Wanatheologia wa kisasa wakikumbana na Kiri hizi, wanayazua masuala mengi hatari. Baadhi ya maelezo, moja kwa moja hutegemea hali halisi ya kihistoria ya wakati huo . . . Hata maelezo ambayo hayaonekani kuhusiana na muktadha wa wakati huo - kuhusu Kristologia au kuhesabiwa haki kwa njia ya imaniyanafaa kukaguliwa tena kulingana na ugunduzi wa ufasili wa karibuni.”136
134 Sinodi ya Efeso (431) na Khalkedon (451).
135 Miongoni mwao Eusebio, Athanasιο, Epiphanio, Kirillo, Theodoreto, Yohana wa Dameski, Basileio Mkuu, Ambrosio, Khrisostomo, Gregorio wa Nyssa na wengineo.
136 Maana na Mamlaka ya Kiri za Imani, katika La Foi des Ėglises Luthériennes, 1991, p.19.
lxv
Hii inamaanisha kwamba, mamlaka ya Kiri za Kanisa za Kilutheri ni finyu na kwamba, yanayoyasema yanahitaji kufikiriwa, kuhakikiwa na ikiwezekana yaandikwe upya.”
Hili ni suala ambalo hatuwezi kukubaliana nalo, na tunathubutu kulisema waziwazi. Tunaamini kwamba, Biblia peke yake ndilo Neno la Mungu lenye lililofunuliwa na lisilokosea. Vile vile tunaamini kwamba, Kiri za Kilutheri “siyo shuhuda za muda fulani” kuhusu yale Biblia inayoyasema, bali ni uwasilishwaji sahihi na wa kweli wa mafundisho ya Biblia. Siyo kwamba tunataka isisitizwe tu, bali pia ithibitishwe iwapo tutakosea. Hakika, Kiri za Kanisa letu si zenye ufunuo jinsi yalivyokuwa maandiko ya manabii na mitume. Badala yake, zinazoyasema yanajumlisha ufunuo wa Mungu katika Maandiko Matakatifu, katika yote yanavyosema na yanayoyakataa. Changamoto za kitheologia za siku hizi zinahitaji mtazamo na mkazo tofauti. Hata hivyo, Walutheri ambao wamekata kauli kubakia kuwa waaminifu kwa yale ambayo Biblia inayafundisha na yale mbayo akina baba walikiri wakati wa karne ya kumi na sita, hawataruhusu mamlaka ya kiri za kanisa yaharibiwe hata kidogo.
Kiri za Kanisa la Kilutheri ni na zinabaki kuwa za lazima katika maelezo yote kuhusu mafundisho. Ingawa mambo yangeweza kusemwa vinginevyo kuliko yanavyosemwa, lazima yabaki bila kubadilishwa katika yale ambayo zilitaka kusema hakika na zinabakiza mamlaka yao ya lazima. Mara kwa mara, inadaiwa kwamba, uvumbuzi wa ufasili mpya unahitaji Kiri kusomwa tena kwa umakini. Maswali ni: Je, Ufasili wa uvumbuzi huu mpya ni nini? Ni jinsi gani ufasili wa siku hizi unahitaji kufikiri na kuandika tena yale yaliyosemwa katika “Kitabu cha Mwafaka?” Bado tunangojea ushahidi wa madai hayo. Inasemekana kwamba, Ulutheri kote ulimwenguni ni “jamii ya kimataifa ya Makanisa yaliyo katika ushirika kamili wa Kanisa,” na kwamba, “Katika Shirikisho la Makanisa ya Kilutheri Duniani, sote ni Kanisa moja lililounganika katika maelewano sawa ya imani na ya Maandiko.”137 Mwandishi wa utangulizi wa sasa anathubutu kusema: “kwa bahati mbaya, haya siyo kweli.” Ulutheri ulimwenguni haupo pamoja tena katika imani sawa.
Haya yangekuwa tu hivyo kama Walutheri wote wangekuwa tayari kuamini kwamba, Biblia ni kanuni kuu mno ya imani na maisha ya Kikristo na isiyokosea na kwamba, Kiri za Kilutheri ni shuhuda zilizo zaidi ya shuhuda za muda fulani kulingana na yale Walutheri waliyaamini miaka 400 au 500 iliyopita. Kiri hizo ni kanuni za kufundishia zilizo za lazima, ingawa zimewasilishwa kwa ajili ya zile za Biblia. Ni kanuni za lazima siyo “kwa kiasi kwamba,” mimi binafsi 137 o. c., p. 20.
lxvi
ninazichukulia kuwa sahihi, bali “kwa sababu” ni maelezo sahihi ya mafundisho ya Biblia.138
Kanisa aminifu la Kilutheri ni Kanisa ambalo linaweza kusema pamoja na ukiri wa “Shauri la Mwafaka:” “Hivyo basi, mbele za Mungu na mbele za Wakristo wote wa sasa na vizazi vyetu vijavyo, tungependa kushuhudia kwamba, maazimio haya yaliyowasilishwa kuhusu mafungu yaliyobishaniwa hapo juu na yaliyoelezewa, ndiyo imani, mafundisho, na ukiri wetu, na si mengineyo. Kwa neema ya Mungu, tungependa kuonekana mbele ya kiti cha hukumu cha Yesu Kristo tukiwa wenye mioyo thabiti na tukiitoa hesabu ya imani yetu.” 139
Prof. Dr. Wilbert Kreiss
Woerth, Ufaransa
138 Utofautishaji umefanywa kati ya kile theologia inakiita katika Kilatini, “quatenus – subscription” na “quia –subscription” ambayo yanamaanisha mchango “hadi” na mchango “ kwa sababu,” ni kuwasilisha sahihi kwa ajili ya mafundisho ya Biblia katika mafungu yaliyobishaniwa. 139 Shauri la Mwafaka, Tamko Thabiti, 12, 40.
lxvii
‘CONCORDIA’
Mwafaka
Ukiri wa mafundisho na imani ulio wa Kikristo, uliorudiwa na ulio wa kauli moja, uliotolewa na watawala wachaguzi, watawala wengine na vyeo vya heshima140 na wanatheologia wao ambao hukubali Ukiri wa Augsburg, na pia wanatheologia wao. Tamko thabiti limeambatanishwa kutoka katika Maandiko Matakatifu kama kanuni na amri ya ukweli peke yake kuhusu mafungu kadhaa yaliyoleta mashindano na mabishano baada ya kufariki kwake dunia kwa uanaheri, kwa Dk. Martin Luther. Haya yote yamechapishwa kwa mujibu wa maafikiano na agizo la kauli moja ya watawala hawa wachaguzi, watawala wengine na vyeo vya heshima kwa ajili ya mafundisho na maonyo kwa makanisa na shule zao, na pia kwa kumbukumbu ya vizazi vya baadaye.
1580
140 Wachaguzi walikuwa watawala (Kijerumani: Kurfürst’) waliomchagua kaisari wa Dola la Ujerumani: Maaskofu Wakuu wa Köln, Mainz na Trier, Pfalzgraf wa Rhein, Mtawala wa Sachsen, Markgraf wa Brandenburg na Mfalme wa Bohemia. Wakati wa Enzi ya Kati uwakalishi wa jamii katika baraza la dola ulikuwa tofauti kuliko uwakilishi wa w kisasa wa kidemokrasia. Watu wote wa jamii walikuwa wamegawanyika katika tabaka fulani (Kijerumani: ‘Stand’) kulingana na asili, mali na weledi. Tabaka za jamii zilitangulia umuhimu wa mtu binafsi: Malodi, makasisi wa kanisa na miji maalumu wa dola. Tabaka za uwakilishi katika Baraza la Dola ziliitwa ‘Vyeo vya heshima’ (Kijerumani: ‘Reichsstände’).
lxviii
UTANGULIZI
Sisi watawala wachaguzi, watawala wengine na vyeo vya heshima vya Dola
Takatifu la Roma la Taifa la Kijerumani ambao tumetajwa kwa majina hapa chini, tunatoa na kutangaza mbele yenu kwa moyo wote na kufuatana na hadhi na cheo cha kila mmoja tamko hili rasmi la huduma, urafiki na afya kwa wasomaji wetu wote kama ifuatavyo:
Fadhili kubwa mno ya Mungu Mwenyezi na huruma yote141 ni hivi kwamba amemimina nuru ya Injili safi na ya kweli katika nyakati hizi za mwisho za ulimwengu wetu unaopita, na pia ametupatia Neno lake ambalo ndilo pekee liletalo wokovu wetu, kwa kutuangaza upendo wake usiopimika, kwa neema na huruma zake kwa walimwengu. Haya yalitokea baada ya giza la ushirikina wa kipapa uliokuja katika nchi yetu pendwa ya Ujerumani. Kwa sababu hii, ukiri huu mfupi wenye maneno machache yaliyo wazi uliandaliwa kutoka katika Neno la Mungu, yaani, Maandiko Matakatifu mno ya manabii na mitume. Ukiri huu ulitolewa pia katika lugha ya Kijerumani na Kilatini na watangulizi wetu wacha Mungu sana na waliosifika kwenye lile Baraza la Augsburg la mwaka wa 1530 kwa Kaisari Karolo V na vyeo vya heshima, na hatimaye ukaenezwa hadharani kwa watu wote wanaokiri mafundisho ya Kikristo hata kuenea na kujulikana kwa kuongelewa na kuhubiriwa ulimwenguni mwote.
Hatimaye makanisa mengi na vyuo vya elimu ya juu vilikubali na kuupokea ukiri huu kama ukiri wa kisasa142 uliotolewa katika mafungu maalumu ya imani, hasa katika majadiliano dhidi ya Waroma143 na upotovu wa kila aina dhidi ya mafundisho ya kimbingu. Walirejea kwenye ukiri huu na kuutetea kwa mwafaka wa kudumu, bila mabishano au mashaka yoyote.
Waliangalia mafundisho yaliyomo ndani yake kuwa mafundisho kamili kufuatana na shuhuda thabiti za Maandiko Matakatifu kwa mujibu wa kiri za kale zilizokubaliwa. Walitambua kikamilifu mafundisho haya kuwa kweli rai iliyo pekee na ya daima ya Kanisa la Kristo ambayo inakubaliana na kanuni za kanisa. Makubaliano haya yalitetewa dhidi ya mafundisho mengi yenye kupotosha na ya uzushi. Hata hivyo, yalirudiwa tena.
Jambo lililo wazi kwa kila mtu ni jinsi gani matukio ya hatari na ya usumbufu yaliikumba nchi yetu tuipendayo ya Ujerumani muda mfupi tu baada ya kufariki
141 Kilatini: ‘Deus Optimus Maximus’, Kijerumani: ‘Gott der Allmächtige’
142 Katika lugha ya Kilatini ‘Ukiri’ ni kama confessio, professio na symbolum. Neno hili la ‘symbolum’ linatumika hapa
143 Yaani, wafuasi wa Papa wa Roma.
dunia na uchaji mkubwa mno kwa shujaa yule mwenye fahari kuu, yaani, Dk. Martin Luther. Katika hali hii ya maumivu na mfarakano wa serikali, adui wa binadamu alitenda kazi yake baramaki144 kwa kutawanya mbegu yake ya mafundisho ya uongo ya mafarakano na kuuleta uharibifu na mgawanyiko katika makanisa na mashule kwa kusudi la kuuhimiza ugomvi na chuki na kuuchafua usafi wa mafundisho ya kimbingu, kukiharibu kifungo cha upendo wa Kikristo na mwafaka mtakatifu, na kwa njia hii, kuzuia na kuchelewesha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Injili Takatifu mno.145
Kilammoja pia anajua jinsi maadui wa ukweli wa kimbingu walivyochukua nafasi ya kuyapotosha makanisa na vyuo vyetu vya elimu ya juu, kuyafunika makosa yao na kuwapotosha walio na dhamiri changa kutoka mafundisho safi ya Injili na kuwafanya wabebe na kuistahimili kongwa ya utumwa wa Papa na kuyakubali makosa mengine yanayopingana na Neno la Mungu.
Hakuna jambo lolote la kutupendeza zaidi kuliko tulilosisitiza kwa bidii sana na kumwomba Mungu Mwenyezi na huruma yote kwamba, makanisa na shule zetu ziweze kukaa ndani ya mafundisho safi ya Neno la Mungu na katika mwafaka mtakatifu wa nafsi, na kuendelea kuongozwa kulingana na kanuni za Neno la Mungu kama wakati wa Dk. Martin Luther alipokuwa bado angali hai.
Lakini tunaona wazi kwamba, kama jinsi ilivyokuwa wakati wa mitume watakatifu pia, ndugu wa uongo walipenyeza mafundisho yao potovu katika makanisa mengine ambayo mitume wenyewe walipanda mbegu ya Injili ya Kristo. Kwa jinsi hii, Mungu aliyekasirika kwa sababu ya dhambi zetu na ulegevu wa nyakati hizo,146 aliruhusu misiba hii iingilie makanisa yetu pia.
Tukikumbuka huduma hii ambayo Mungu ametukabidhi, sisi tunaangalia kuwa wajibu na jukumu letu kuu ni kuyaondoa mafundisho ya uasi yaliyosambaa katika mikoa na maeneo yetu. Mafundisho haya ni yale yaliyotuingia zaidi na zaidi hata kutambulika kama desturi za watu. Kusudi letu ni kwamba raia wa dola yetu wapate kuendelea kwa njia na katika ujuzi wa uchaji wa kweli na wavumilie daima katika mafundisho ya kimbingu yaliyositirika bila kuruhusu kushawishiwa kuyaacha.
Pamoja na hayo na kwa kusudi hili, watangulizi wetu waliosifika sana pamoja na baadhi yetu, katika mwisho wa mkutano wa watawala wachaguzi
144 Yaani, kwa hila.
145 Kilatini: Sacrosanctum evangelium’.
146 Maandiko ya Kijerumani: “… umb unserer und der undankabaren Welt Unbussfertigkeit und Sünde willen …”; yaani: “Kwa sababu ya dhambi ya ulimwengu wetu usiokuwa na shukrani wala toba.”
lxx
kule Frankfurt ya Main147 mwaka wa Kristo 1558148 tumeamua kwa kura zote kwamba inatubidi kuwa na mkutano maalumu kwapamoja ambapo tungeweza kuzungumza sisi wenyewe kwa haja na kwa uzoefu juu ya mambo mbalimbali, ambayo washindani wetu wameyatumia vibaya kwa chuki na kwa uzushi dhidi ya makanisa na vyuo vyetu vya elimu ya juu.
Baada ya majadiliano haya, watangulizi wetu wengine bora sana wenye kumbukumbu ya uchaji na na baadhi yetu sisi tulikutana kule Naumburg katika mkoa wa Thüringen.149 Tulirudia tena kuzungumza juu ya Ukiri wa Augusburg –ambao tulikwisha kuutaja mara nyingi - uliowekwa mbele ya Kaisari Karolo V na wachaguzi wengi wa dola katika baraza la dola liliyofanyika huko Augsburg katika mwaka wa 1530, na tena kwa kauli moja tulitilia sahihi zetu katika ukiri huu mtakatifu uliojengwa juu ya shuhuda dhahiri za ukweli usiobadilika wa Neno la Mungu. Kusudi letu lilikuwa kuvionya na kuvilinda vizazi vyetu vya baadaye, kama tuwezavyo kuwa mifano na wasimamizi, dhidi ya mafundisho ya uasi yanayopingana na Neno la Mungu. Tumefanya hili ili tushuhudie na kutamka mbele ya Enzi yake Kaisari, Bwana wetu mwenye huruma na kwa wanadamu wote, kwamba haikuwa nia yetu kuyapokea, kuyatetea au kueneza mafundisho mengine mapya au yasiyo sawa. Badala yake, nia yetu ilikuwa kwa msaada wa Mungu kubaki katika ukweli ambao hapo mwanzo tuliukubali na kuukiri kule Augsburg katika mwaka wa 1530.
Bila mashaka yoyote tulitarajia kuwa maadui wa mafundisho safi ya Kiinjili wapate kuacha kabisa maneno ya kashfa na mashtaka yaliyobuniwa dhidi yetu na pia ili watu wengine wenye nia njema waweze kuhimizwa na kutiwa moyo na ukiri huu uliorudiwa hata waweze kuuliza na kuchunguza kwa makini ukweli wa kimbingu ambao peke yake unaweza kutupatia wokovu. Kwa njia hii wao wenyewe wapate kujikabidhi na kukubaliana na ukweli huu hata kuutafuta ndani yake wokovu wa nafsi zao na heri zao za milele pasipo majadiliano na
147 Iko miji miwili kule Ujerumani inayoitwa Frankfurt, yaani Frankfurt ya mto wa Oder kule mashariki, na Frankfurt ya mto wa Main kule magharibi mwa Ujerumani.
148 Kusudi kuu la mkutano huu uliokutana miezi ya Februari na Machi 1558 lilikuwa kumchagua rasmi kaisari mpya, yaani, Ferdinando I (1503-1564, kaisari 1556-1564) baada ya Kaisari Karolo V (1500-1558, kaisari 1519-1556) aliyeng’atuka kwenye cheo cha kaisari 1556.
149 Mkutano wa Naumburg kule Thüringen ulikutana tangu tarehe 20 mwezi wa Januari hadi tarehe 1 mwezi wa Februari katika mwaka wa 1561. Majadiliano ya watawala Walutheri yalihusu misimamo wao kwenye Ukiri wa Augsburg uliobadilishwa (Kilatini: ‘Confessio Augustana variata’) na Philipp Melanchthon (14971560) katika mwaka wa 1540 kwa upande wa mafundisho ya Roma (k.m. mafundisho ya mageuzi ya kiini ya elementi za Ekaristi, Kilatini: ‘transsubstantiatio’) na, Ukiri wa asili au usiobadilika wa Augsburg 1530 (Kilatini: ‘Confessio Augustana invariata’). Watawala wengi pamoja na watawala wachaguzi wawili na miji mingi ilitia sahihi. Watawala wa Württemberg, Sachsen na Sachsen za Chini pamoja na wajumbe wa miji mingine ya pwani walikataa.
lxxi
mafarakano zaidi.
Lakini kwa upande wetu, tuligundua kwa masikitiko kuwa, wapinzani wetu hawakujali hata kidogo tamko letu wala marudio ya ukiri mtakatifu.150 Kwa hiyo, sisi wenyewe pamoja na makanisa yetu hatukupata uhuru toka kwa uzushi wa madhara yaliyoenezwa dhidi yetu miongoni mwa umma. Wapinzani wa imani ya kweli151 walitafsiri kusudi na maamuzi yetu yaliyo bora mno kwa maana iliyo mbaya kana kwamba hatukuwa na uhakika kuhusu imani yetu. Kwa sababu hiyo, wamesema kwa uongo, tuliibadilisha sana mara kwa mara kiasi kwamba sisi na wanatheologia wetu hatujui ni toleo lipi la ukiri uliotolewa awali kwa Kaisari kule Augusburg.152
Mashtaka ya wapinzani yamewashtusha na kuwatenganisha watu wengi wema kutoka kwa makanisa, vyuo, mafundisho, imani na ukiri wetu.
Zaidi ya hayo, hasara hii imeingia kwasababu, yale mafundisho yaliyopingana na asasi ya Chakula Kitakatifu cha mwili na damu ya Kristo yameingizwa kila mara kwa kisingizio cha Ukiri Augsburg na mawazo mengine mapotovu pote katika makanisa na vyuo vyetu.
Watu wengine wacha Mungu, waliopenda amani na mwafaka, hasa wanatheologia wataalamu153 walipotambua maendeleo hayo, waliona waziwazi kuwa hakuna njia iliyo nzuri ya kukabiliana na uzushi pamoja na mabishano ya kidini yaliyokuwa yakikua zaidi na zaidi, walitaka kwamba mafungu ya majadiliano haya yachunguzwe na kufafanuliwa yamkini na kamili kabisa kwa msingi wa Neno la Mungu. Hali kadhalika, walitaka mafundisho ya uasi yaachwe na yahukumiwe na ukweli wa Mungu kukiriwa kwa uwazi kabisa. Kwa njia hii, midomo ya adui iweze kunyamazishwa na waumini wa kawaida na wacha Mungu wapate kuiona njia na kuwa na maelezo sahihi ili waweze kuwa wazuri mbele ya mabishano haya na wakati ujao wayaepuke mafundisho ya uasi kwa msaada wa neema ya Mungu.
Basi, mwanzoni, wanatheologia hawa waliwasiliana miongoni mwao kwa maandiko fasaha yaliyotokana na Neno la Mungu kuhusu mbinu hodari na bora kabisa za kuyatuliza na kuyaondoa mabishano haya ambayo yaliyaletea makanisa
150 Kilatini: ‘pia’ ; maana yake: -a uchaji.
151 Kilatini: ‘religio vera’, yaani, ‘dini ya kweli’. Lakini mababa wa Matengenezo ya Kanisa walilitumia neno la ‘dini’ (‘religio’) kama kisawe cha ‘imani’.
152 Sentensi hii inayahusu majadiliano kati ya wafuasi wa Philipp Melanchthon waliokubaliana na mabadiliko ya Ukiri wa Augsburg (‘Confessio Augustana variata’) na ‘Walutheri wa Asili’ (Kijerumani: ‘Gnesiolutheraner’) walioshika kabisa ukiri wa asili wa 1530 (‘Confessio Augustana invariata’).
153 Hasa Yakobo Andreae, Martin Chemnitz na Nikolao Selnecker .
lxxii
hasara. Hata hivyo, bila kuumiza hata kidogo ukweli wa Injili na hasa, kwa njia hii, wapinzani watanyang’anywa nafasi kwa kisingizio chochote cha uzushi.
Halafu waliyachukua mafungu yenye kujadiliwa kwa kusudi la kuyachunguza na kuyatathmini kikamilifu kwa njia ya kumwogopa Mungu. Mwishowe waliitunga hati ambapo mabishano haya yangeweza kutulizwa kwa njia sahihi na ya Kikristo.
Sisi basi, tulipoelezwa juu ya shughuli hii ya Kikristo ya wanatheologia, hatukuridhika tu bali tulijisikia kuwajibika kuieneza na kuitangaza kwa juhudi zetu zote kulingana na mamlaka na huduma tuliyo nayo ambayo tumekabidhiwa na Mungu.
Ndipo, mimi, Mtawala Mchaguzi wa Mkoa wa Sachsen n.k., kwa mashauri ya watawala wachaguzi na watawala wengine pia wanaokubaliana na imani yetu pamoja nasi, kwa neema ya Mungu niliwaalika wanatheologia wengine walio bora sana na bila tuhuma, wenye uzoefu na utaalamu, kufika kule Torgau katika mwaka wa 1576 kwa kusudi la kueneza mwafaka kati ya walimu wengine wa kanisa.
Walipokutana walizungumza pamoja kwa njia ya Kikristo juu ya mafungu haya yenye kujadiliwa na juu ya maandiko kuhusu suluhu ambayo tuliirejea awali.
Hatimaye, baada ya maombi matakatifu kwa Mungu Mwenyezi na mwenye huruma zote kwa ajili ya sifa na utukufu wake, mambo yote yaliyoonekana kuhusu majadiliano haya na yaliyo muhimu sana, yalikusanywa kwenye maandiko maalumu kufuatana kwa utaratibu na urahisi bora mno154 kwa msaada wa Roho wa Bwana na neema zake.
Baada ya hayo, kitabu hiki kilipelekwa kwa baadhi ya watawala wachaguzi, watawala wengine na vyeo vya heshima ambavyo viliukiri Ukiri wa Augsburg. Wanatheologia mashuhuri, maarufu na wataalamu wao waliombwa kwamba wakisome kwa uangalifu mkubwa na kwa moyo wa uchaji hata kukichunguza kila kipengele kwa juhudi. Kisha, watueleze kwa maandishi juu ya maoni na lawama zao pamoja na urazini wao kuhusu kila sehemu na hoja maalumu bila wasiwasi wowote.
Tulipopokea lawama hizi tuliiona miongozo mingi mizuri na ya Kikristo iliyowezesha utoaji na uthabiti wa mafundisho sahihi ya Kikristo kwa shuhuda 154 Kitabu cha Torgau kilichotungwa katika Ngome ya Hartenberg tangu tarehe 9 Aprili mpaka tarehe 7 Juni 1576. Yakobo Andreae alikifupisha kitabu hiki kuwa ‘Epitome (‘Muhtasari’) Formulae Concordiae’.
lxxiii
za Neno la Mungu dhidi ya uharibifu na mikengeuko yoyote, ili mafundisho ya uasi yasipate kufichwa kwa kisingizio chao, bali azimio la mafundisho safi liweze kufundishwa kwa vizazi vijavyo bila machafuko yoyote.
Shauri la Mwafaka wa Kikristo (“Formula Concordiae”) lilikamilika kwa msaada wa miongozo hiyo katika umbo linalotolewa hapa.
Halafu, baadhi yetu tulikisimulia kitabu hiki kwa uwazi na ufasaha kabisa kwa wanatheologia wote na kwa wachungaji wa makanisa na shule katika mikoa na majimbo yetu. Kwa sababu ya vikwazo fulani sisi sote hatukuweza kufanya hivyo hadi wakati huo. Tuliwahimiza wachungaji hawa kuzichunguza sehemu za yaliyomo ya kitabu hiki kwa jitihada na uangalifu sana.
Walipoona kwamba maelekezo haya ya majadiliano yalilingana hasa na Neno la Mungu, na pia na Ukiri wa Augsburg, walikipokea kwa hiari kitabu hiki kama maelezo matakatifu na sahihi ya Ukiri wa Augsburg. Walikubali na kulitilia sahihi zao na kwa jinsi hii walishuhudia hadharani kwa mioyo, midomo na mikono yao. Kwa sababu hiyo, mapatano haya ni mwafaka na makubaliano ya kudumu ya wachungaji wote na kila mmoja, wa makanisa yetu na pia ya walimu wakuu walioko katika mikoa na majimbo, wala si ya wanatheologia wetu wachache peke yake.155
Mapatano haya yaliyotajwa hapo juu ambayo yalitolewa kwa kusudi zuri yaliyofikiwa na watangulizi wetu waheshimiwa na sisi wenyewe kule Frankfurt ya Main na kule Naumburg yalishindwa kufikia lengo lililokusudiwa la mwafaka wa Kikristo. Baadhi ya watu walijaribu kuyatumia kwa kusudi la kuyasitiri makosa na mafundisho yao ya uasi. Ingawa sisi hatukuwa na nia hiyo hata kidogo katika mawazo yetu kuiingiza katika maandiko yetu aina yoyote ya mafundisho mapya na ya uasi, kuyasifia na kuyathibitisha kwa kifuniko chochote, au hata kutengana na ukiri ule wa Augsburg kama ulivyotolewa katika mwaka wa 1530. Wale baadhi yetu tulioudhuria amali zile za Naumburg tulijiwekea haki na ahadi kwamba tutakielezea kwa uthabiti na bila kusita kila kitu kitakachoweza kuhitajika au kudaiwa hatimaye na hali ya lazima. Kwa sababu hiyo basi, tumechanganua kwa makubaliano makubwa na kwa uchaji katika hiki “Kitabu cha Mwafaka” azimio la mapenzi yetu ya kudumu na marudio ya imani yetu ya Kikristo na ukiri wetu. Kwa sababu hiyo, watu wasivumilie kuhangaishwa na visingizio viliyobuniwa na wapinzani wetu kwamba sisi pia hatuyajui yaliyomo ya kweli na ya halisi ya Ukiri wa Augsburg. Kinyume chake, watu wa wakati wetu na hata vizazi 155 Idadi ya vyeo vya heshima vya dola vilivyokubaliana na Kitabu cha Muafaka ilikuwa 86 na idadi ya wanatheologia waliolitilia sahihi zao ilikuwa kama 8000-9000.
lxxiv
vitakavyokuja wapate kufundishwa kinaganaga na kwa kweli na kuwa na uhakika kwamba ukiri wetu huu mtakatifu na wa makanisa na shule za majimbo yetu yote daima ni upi. Kulingana na ukweli safi na madhubuti wa Neno la Mungu tunaushika Ukiri ule wa Augsburg peke yake uliotolewa kwa Kaisari Karolo V katika mwaka wa 1530 katika baraza lile maarufu na bila kuufadhili mwingine. Tumethibitisha jambo hilo kwa uwazi kabisa. Nakala za ukiri huu zinapatikana kwenye nyaraka156 za watangulizi wetu mashuhuri waliotoa wenyewe ukiri huu kwa Karolo V katika baraza lile. Tulitaka kwamba watu bora kabisa walinganishe nakala hizi sawasawa na maandiko yale yaliyotolewa kwa kaisari na yanayohifadhiwa kwenye nyaraka za Dola Takatifu la Roma. Tuna uhakika kwamba yaliyomo ya nakala yetu na pia nakala za Kilatini na Kijerumani yanafanana kabisa. Kwa sababu hii, tulitaka kuuingiza ukiri huo uliotolewa wakati ule, kwenye azimio letu lililofuata, yaani Kitabu cha Mwafaka, kwa kusudi la watu wote wapate kuelewa kwamba katika majimbo, makanisa na shule zetu hatuyavumilii mafundisho mengine yoyote isipokuwa yale yaliyokubaliwa na watawala wachaguzi, watawala wengine na vyeo vya heshima vya dola kwa ukiri makini kule Augsburg katika mwaka wa 1530.
Tutaushika ukiri huu wenye heri wa maisha haya hadi mwisho kwa msaada mwema wa Mungu, tutakapohamia katika nchi yetu ya mbinguni na kuonekana mbele ya mahakama ya Bwana wetu Yesu Kristo wenye nafsi bora na jasiri na dhamiri safi.
Tena ni tumaini letu kwamba kuanzia sasa na kuendelea wapinzani wetu wataacha kututilia shinikizo zito mno sisi na makanisa yetu na wachungaji wetu kwa udanganyifu wao wa kusema kwamba, sisi hatuwezi kuwa na hakika yoyote kuhusu imani yetu hata kuitunga kiri mpya karibu karibu kila mwezi, kila mwaka na zaidi.
Kuhusu toleo la pili la Ukiri wa Augsburg,157 lililotajwa pia katika mafungu ya Naumburg, tumeona kwamba – jinsi inavyojulikana kwa watu wote - wengine walijaribu kuzitenga na kuzificha potovu zao kuhusu Chakula158 na makosa mengine kwa kisingizio cha maneno ya toleo hili la pili. Watu hawa walijaribu kuukinza umma wa kawaida kwa vitabu vyao vilivyochapishwa hadharani. Walifanya hivyo bila kuyazingatia maneno dhahiri ya Ukiri wa Augsburg
156 Yaani, maktaba ya hati rasmi. Maandiko ya asili ya Kilatini na Kijerumani hayapatikani zaidi. Hata hivyo, wataalamu walizitafuta nakala zaidi ya 50 toka mwaka wa 1530, hata kuweza kufikia uamuzi kuhusu maandiko kamili ya Ukiri wa Augsburg katika lugha ya Kilatini na Kijerumani.
157 Ukiri wa Augsburg uliobadilishwa (‘Confessio Augustana variata’) 1540 uliotungwa na Philipp Melanchthon, Fungu la Kumi.
158 Yaani, Chakula cha Bwana.
lxxv
yaliyokana makosa yale zamani. Maana ya maneno haya ilikuwa tofauti kabisa na maoni yao.
Kwa kuwa basi, tunataka sasa kushuhudia na kuwaaminisha wote kwa maandiko haya, kwa wakati ule au huu kwamba hatukutaka hata kidogo, kuitetea, kuiwia radhi au kuiafiki kwa kisingizio cha mafundisho ya Kiinjili, mifumo ya imani na maoni ya uasi ambayo yangeliweza kusitiriwa chini ya maneno mengine.
Kwa kweli, sisi hatukukubali kamwe toleo la pili kwa namna nyingine yoyote kuliko Ukiri wa kwanza wa Augsburg kama ulivyotolewa.
Tuliona pia kwamba hatuna sababu yoyote ya kuvihukumu na kuvikana vitabu vingine vya Dk. Philipp Melanchthon, au vya Yohana Brenz, Urbano Regio, na vya huyu aliyetoka Mkoa wa Pommern,159 na vya wengine kama vikikubaliana na kanuni ile iliyosimuliwa katika Kitabu cha Mwafaka.
Ingawa wapinzani walifaulu kushawishi baadhi ya wanatheologia na pia Luther mwenyewe, kujadiliana kuhusu Chakula cha Bwana juu ya muungano wa binafsi160 wa nafsi mbili za Kristo. Lakini wanatheologia wetu wanathibitisha dhahiri katika Kitabu cha Mwafaka na yaliyomo yake kuwa kanuni ya mafundisho safi sana na maoni yetu na kitabu kile cha kudumu kwamba watu wachaji hawana msingi mwingine wowote katika majadiliano kuhusu Chakula cha Bwana isipokuwa urithi wa maneno ya asasi ya Bwana wetu Yesu Kristo. Naam, kwa kuwa Kristo ni mwenyezi na mnyofu, ataweza pia kuvifanikisha vile ambavyo alivianzisha na aliviahidi kwa Neno lake.
Kwa kuwa msingi huu umeshambuliwa sana na wapinzani, hawakujadiliana juu ya maoni mengine ya hoja hii, bali waliyashika kwa imani ya kweli na kwa uimara maneno dhahiri mno ya Kristo. Kauli hii ni bora na ya kueleweka kwa watu wa kawaida wanaohitaji kufundishwa kwa kuwa hawawezi kuyaelewa majadiliano haya vizuri.
Wapinzani hulishambulia dai letu thabiti kuhusu maana sahili ya maneno ya urithi wa Kristo hata kuikataa kama uasi uliopinga imani ya kweli, hasa mafungu ya Imani ya Mitume (Mwana wa Mungu kufanyika mwili, kupaa kwake na kuketi kwake katika mkono wa kulia wa Mungu Mwenye Nguvu na Enzi). Kwa hiyo, hatuna budi kuonyesha kwa ufafanuzi thabiti na wa kweli kwamba maoni yetu yanaafiki kabisa maneno ya Kristo na mafungu yale ya imani.
Tukiangalia sentensi na namna za kuyatumia maneno161 katika Kitabu hiki
159 Yaani, Yohana Bugenhagen.
160 Kilatini: ‘Unio personalis’.
161 Kilatini: ‘Modus loquendi´’; istilahi ya kibalagha.
lxxvi
cha Mwafaka kuhusu enzi ya nafsi ya kibinadamu ya Kristo162 aliyewekwa na kuinuliwa katika mkono wa kulia wa Mungu, mashaka yote ya kisirani na chuki zote zinazotoa maana tofauti za neno la ‘abstractum’163 (jinsi shule za mababa zilivyoitumia istilahi hii) zitaweza kuondolewa toka kwetu. Wanatheologia wetu hutaka kujulisha kwa maneno bora na dhahiri sana, kwamba enzi ya nafsi ya kibinadamu ya Kristo isifikiriwe kamwe nje ya muungano wa binafsi. Isikubaliwe pia kwamba nafsi ya kibinadamu iwe na enzi au asili ileile katika muungano wa binafsi kwa njia ya kiini, umbo, hali na unafsi, tukitumia lugha ya wataalamu.164Tukifuata basi, namna hii ya msemo na mafundisho, tabia za nafsi ya kimungu na kibinadamu zitachanganywa na nafsi ya kibinadamu itafanywa kuwa sawa165 na nafsi ya kimungu kwa upande wa kiini na tabia zake hata kukanushwa kabisa.
Wanatheologia hawa huona kwamba inatubidi kulitambua jambo hili kwa njia na kwa utofautishaji wa muungano wa kiini,166 jinsi ilivyofundishwa zamani kwa tahadhari, kwa kuwa ni siri inayopita nguvu zote za asili na akili zetu.
Tumetangaza katika azimio letu na maelezo yote ya mifumo ya imani yaliyoleta mabishano makusudi na dhahiri mno, hukumu, lawama na kukataliwa kwa mifumo ya imani ya kukufuru, hasa yale yanayohusu Chakula Kitakatifu. Sisi hatukufanya hivyo peke yake kwa kusudi kwamba watu wote waiepuke mifumo hii iliyolaaniwa ya imani, bali kwa sababu zingine pia ambazo haziwezi kusahauliwa. Hata hivyo si shauri na kusudi letu kamwe kuwahukumu wale wanaokosea kama majuha na ambao hawawezi kuangaliwa kama wale waliokufuru mafundisho ya ukweli wa kimbingu. Wala hatuyahukumu makanisa yote yaliyomo katika Dola la Roma la Taifa la Ujerumani au kwingineko. Kinyume chake, katika azimio letu tulimaanisha zaidi maoni ya walokole na walimu wao wapotovu na makafiri (ambao hatutaki kuwavumilia katika majimbo, makanisa na shule zetu). Basi ni kusudi letu, kuyakaripia hadharani makosa yanayopinga Neno la Mungu dhahiri bila uwezekano wa kulinganishwa nalo. Aidha, tulichukua hatua za kuwaonya wacha Mungu ili wapate kuyaepuka makosa haya kwa bidii. Hatuna mashaka yoyote ya kwamba watu wengi wacha Mungu au wasio wabaya hupatikana katika makanisa yale ambayo bado hayajakubaliana nasi. Naam, wanafuata unyofu wao, hawayatambui vizuri masuala haya. Watu wa namna hiyo hawawezi kuzivumilia
162 Kilatini: ‘Maiestas humanae naturae in persona Christi’.
163 Rejeo kwa jadiliano baina ya Yohana Wigand na Tileman Hesshus kuhusu matumizi ya istilahi hii katika uchanganuzi wa uhusiano wa nafsi za Kristo.
164 Kilatini: Essentialiter, formaliter, habitualiter, subiective. Istilahi hizi zinatoka muundo wa falsafa ya Aristotele (384-322 K.K.)
165 Kilatini: ‘Exaequaretur’.
166 Kilatini: ‘Unio hypostatica’.
lxxvii
hata kidogo dhihaka zilizopayukwa dhidi ya Chakula Kitakatifu. Kwa mintarafu ya chakula hiki tunamaanisha kile kilichoadhimishwa katika makanisa yetu kwa mujibu wa agizo la Kristo na kinachokubaliwa na mwafaka mkubwa wa watu wengi bora kulingana na maneno ya wosia wake.
Tuna matumaini makubwa kwamba kwa msaada wa Roho wa Bwana watu hawa watakubali ukweli usiobadilika wa Neno la Mungu pamoja nasi na makanisa na shule zetu, kama wakifundishwa kwa usahihi juu ya mambo haya. Kwa kweli, ni wajibu wa wanatheologia na watumishi wote wa makanisa, hasa wale waliohudhuria mashauriano haya, kuwafundisha kiasi wale waliokosea ukweli kwa sababu ya urahisi au ujinga wowote juu ya hatari iliyopo juu ya wokovu wao na kuwazatiti167 dhidi ya mafundisho ya uasi, ili wote wasipotee na ikwa mtu aliye kipofu akamuongoza kipofu mwingine.168
Kwa sababu hiyo, tunataka kushuhudia mbele za Mungu na mbele ya kanisa zima kwamba haikuwa azima169 yetu kutoa mwanya na hatari kwa azimio letu hili la mapatano kwa watu wacha Mungu walioadhibiwa siku hizi. Kama vile upendo wa Kikristo ulivyotuweka tangu zamani tuwe na huruma na watu hawa kwa ajili ya mateso yao, vivyo hivyo tunachukia na kukirihi sana usumbufu na ukatili mkali mno uliopo juu ya hawa maskini.
Sisi hatutaki hata kidogo kuwa na hatia kwa damu ile, itakayolipiziwa kisasi kikali bila shaka kwa watesaji wao katika hukumu ile ya Bwana ya kutisha na mbele ya mahakama ya Kristo. Kwa kweli, hawatakuwa na budi kutoa hesabu pale kwa ajili ya ukatili wao na kujiweka chini ya adhabu za kuogofya kabisa.
Wakati wote, azima yetu sisi imekuwa kama jinsi tulivyokwisha kukumbusha hapo juu kwamba, hakuna mafundisho mengine isipokuwa yale yaliyowekwa juu ya msingi wa Neno la Mungu na yaliyomo katika Ukiri wa Augsburg na Utetezi wake,170 kufuatana na maana yake sahihi ni uvume na ufundishwe kikamilifu katika nchi, majimbo, shule na makanisa yetu. Kusudi kuu la mwafaka huu la kuileta amani limekuwa kuyazuia mafundisho yanayopinga maoni sahihi.
Kwa sababu hii, tunakiri na kushuhudia mbele za Mungu na wanadamu171 wote kwamba hatumaanishi kwa azimio letu lenye mafungu yaliyoleta utata, ukiri wowote mpya au tofauti kuliko ule uliotolewa kwa marehemu Kaisari Karolo V
167 Yaani, kuandaa.
168 Lk. 6:39.
169 Yaani, kusudio, nia.
170 Yaani, Utetezi wa Ukiri wa Augsburg, Kilatini: ‘Apologia Confessionis Augustanae’.
171 Kilatini: ‘Mortales’; maana yake: ‘Wote ambao hufa’.
lxxviii
katika mwaka wa 1530. Kinyume chake, tumetaka sana kuyaongoza makanisa na shule zetu kwenye chemchemi ya Maandiko Matakatifu na kiri za zamani na pia Ukiri wa Augsburg uliotajwa tayari.
Tunaazimia kwa uzito kabisa kwamba, vijana watakaosoma kwa kusudi la kuingia katika huduma za makanisa na shule wafundishwe kwa uaminifu na kwa uangalifu, ili mafundisho sahihi na ukiri wa imani uhifadhiwe na uhubiriwe kwa msaada wa Roho Mtakatifu, kwa vizazi vyetu vya baadaye pia, hadi kurudi kwake Mkombozi na Mwokozi wetu Yesu Kristo katika utukufu wake.
Kwa sababu hizo, sisi tuna hakika katika nafsi zetu kwa msaada wa Roho Mtakatifu kuhusu ukiri wetu uliotokana na maandiko ya manabii na mitume na dhamiri zetu zilikuwa zimethibitishwa sana. Hivyo, tumefikiri kwamba wakati umekuja kukitoa Kitabu hiki cha Mwafaka katika mwangaza wa mchana.
Ilionekana kuwa muhimu mno kuyapata maelezo na mapatano ya mabishano haya yote yanayotokana na Neno la Mungu, miongoni mwa makosa, chuki, mabishano na migawanyiko mingi zaidi na ya muda mrefu, ili mafundisho sahihi na mafundisho ya uasi yaweze kutambuliwa na kutofautishwa kabisa.
Juu ya hayo, ni muhimu kwamba watu wanaopenda ghasia na mabishano hata kutovumilia kigwe chochote cha umbo la mafundisho safi, wasipate nafasi zozote za kuyaanzisha kwa majadiliano yenye uzushi mwingi na kuyatetea mafundisho ya uasi kwa makusudi.
Matokeo ya haya yote ni kuwa hatimaye mafundisho sahihi yatavurugwa kabisa na kupotea hata vizazi vijavyo havitapata kitu ila mawazo yasiyo dhahiri na wayowayo za wataalamu.172
Zaidi ya hayo, tunaelewa kwamba kwa ajili ya huduma tuliyopata kutoka kwa Mungu tunawajibika kuyatunza kwa jitihada zote yapasayo faida ya maisha haya na maisha yajayo ya raia wetu. Inatubidi kuchukua hatua ili jina na utukufu wa Mungu upate kuenea pamoja na Neno lake ambalo peke yake hututolea tumaini la wokovu, na makanisa na shule zetu zipate amani na utulivu na dhamiri zilizosumbuliwa vibaya zipatiwe maonyo na faraja. Hasa tuna hakika kwamba watu wengi wenye madaraka makubwa na madogo, walio bora na hodari, wamekingojea kwa majonzi makubwa na hamu kubwa kitabu hiki mabruki173 cha mwafaka wa Kikristo. Tumeona tangu mwanzo wa majadiliano haya na tunaendelea kuwa na maoni haya ya kwamba kitabu hiki mabruki na muhimu
172 Maandiko ya Kilatini: Εποχαι academicae; Kijerumani: “Zweifelhaftige, disputierliche Wahn und Meinungen”.
173 Kilatini: ‘Salutaris’.
lxxix
mno cha mwafaka kisifichwe mbali kutoka katika macho ya watu hata kuiweka nuru ile ya ukweli wa kimbingu chini ya pishi au meza.174 Kwa sababu hiyo, hatupaswi kusimamisha au kuahirisha zaidi uchapishaji wake.
Hatuna mashaka yoyote kwamba wacha Mungu wote wanaoupenda ukweli wa kimbingu na mwafaka huu unaompendeza Mungu, wataupokea shughuli hii mabruki pamoja nasi na ya manufaa na takatifu na muhimu mno bila kuruhusu kitu chochote kuzuia kwa njia yoyote azima hii inayokuza utukufu wa Mungu na heri ya umma katika mambo ya milele na ya dunia hii.
Hatimaye basi, tunataka kurudia kusema tena kabisa kwamba nia yetu siyo kuyatunga mambo yoyote mapya kwa mwafaka huu wala kukengeuka toka ukweli wa kimbingu uliotambuliwa na kukiriwa na watangulizi wetu wacha Mungu maarufu sana na sisi wenyewe pia.
Tunamaanisha mafundisho yaliyojengwa juu ya maandiko ya manabii na mitume na kujumuishwa katika kiri tatu za zamani, Ukiri wa Augsburg mwaka wa 1530 uliopatiwa kwa marehemu Kaisari Karolo V, halafu Apologia iliyounganishwa nao, Mafungu ya Smalkaldi, katekisimo zote mbili za mtu bora mno Dk. Luther.
Kwa sababu hiyo, sisi hatutaki kukengeuka hata kidogo kwa upande wa mambo yenyewe au sentensi za yaliyomo yake, bali tumekata shauri kustahimili kwa msaada wa Roho wa Bwana kwa uthabiti na kwa makubaliano makuu katika mwafaka huu mtakatifu na tutayapima mabishano yote kwa kanuni hii ya kweli na azimio la mafundisho safi.
Halafu pia, tumeamua kwamba tunataka kuitunza amani na mwafaka pamoja na watawala na vyeo vya heshima vyote vingine vya Dola Takatifu la Roma na wafalme, watawala na wakwasi wa serikali175 zingine kufuatana na katiba za Dola Takatifu na maafikiano tuliyo nayo. Tumeazimia kwa niaba ya huduma zetu zote kumwonyesha ukarimu na ridhaa kila mmoja kulingana na heshima na cheo chake.
Zaidi ya hayo, tunataka kuchukua hatua kwa bidii kusudi majimbo yetu yasaidiwe na ziara zenye mwangaza za makanisa, shule na kaguzi za matbaa176 na njia zingine mabruki tulizo nazo na kufuatana na hali ya mahali maalumu, kukitetea Kitabu hiki cha Mwafaka kwa nguvu na uzito mkubwa.
Ikiwa mizozo ya kisasa iliyotulizwa tayari kuhusu dini yetu ikichipuka upya
174 Mt. 5:15.
175 Kilatini: Res publica’.
176 Yaani, udhibiti wa vitabu, hasa katika maeneo ya Braunschweig.
lxxx
au mizozo mipya kujitokeza, tuna ushupavu pia wa kuituliza na kuitatua mapema kabla haijaenea na kuleta madhara ili kila aina ya kashfa ziweze kutulizwa na kuondolewa kwa wakati wake.
Kama ushuhuda wetu wa mambo haya tumetia sahihi za majina yetu kwa mwafaka mkuu na kuipiga mihuri yetu.
Ludwig Lodi wa Upalatinati177 wa Rhein, Mtawala Mchaguzi
Augusto Mwinyi178 wa Sachsen, Mtawala Mchaguzi
Yohana Georg Lodi179 wa Brandenburg, Mtawala Mchaguzi
Joachim Fredrik Lodi wa Brandenburg, Mkurugenzi wa Dayosisi Kuu ya
Magdeburg
Yohana Askofu wa Meissen
Eberhart Askofu wa Lübeck, Mkurugenzi wa Dayosisi ya Verden.
Philipps Ludwig Lodi wa Upalatinati.
Fredrik Wilhelms Mwinyi wa Sacsen kupitia kwa walezi wao
Yoansen Mwinyi wa Sachsen
Yohana Kasimir Mwinyi kupitia kwa walezi wao
Yohana Ernstens Mwinyi wa Sachsen
Georg Fredrik Lodi wa Brandenburg
Yulio Mwinyi wa Braunschweig na Lüneburg
Otto Mwinyi wa Braunschweig na Lüneburg
Henrik Mdogo Mwinyi wa Braunschweig na Lüneburg
Wilhelm Mdogo Mwinyi wa Braunschweig na Lüneburg
Wolf Mwinyi wa Braunschweig na Lüneburg
Ulriki Mwinyi wa Mecklenburg
Yohansen Mwinyi wa Mecklenburg kupitia kwa walezi wao
Sigismund Augusto Mwinyi wa Mecklenburg
Ludwig Mwinyi wa Wirtemberg
Ernst Lodi wa Baden kupitia kwa walwzi wao
177 Kilatini: ‘Comes Palatinus’, Kijerumani: ‘Pfalzgraf’. Watawala wa Upalatinati walikuwa wasimamizi wa mali na hati rasmi za mfalme na waliukagua utawala wa watawala mamwinyi.
178 Kijerumani: ‘Herzog’; Kiingereza: ‘Duke’.
179 Kijerumani: ‘Markgraf’., yaani, mtawala wa maeneo ya mipaka ya dola mwenye wajibu maalumu wa ulinzi.
lxxxi
Yakobo
Lodi wa Baden
Georg Ernst Lodi na Bwana180 wa Hennenberg
Fredrik
Hans Günther
Lodi wa Wirtemberg na Mümpelgart
Lodi181 wa Schwarzburg
Wilhelm Lodi wa Schwarzburg
Albrecht
Emich
Lodi wa Schwarzburg
Lodi wa Leiningen
Philipps Lodi wa Hanau
Gottfried Lodi wa Öttingen
George Lodi na Bwana wa Castell
Henrik
Hans Hoier
Lodi na Bwana wa Castell
Lodi wa Mansfeld
Bruno Lodi wa Mansfeld
HoierKristof Lodi wa Mansfeld
Peter Enrst Mdogo
Lodi wa Mansfeld
Kristof Lodi wa Mansfeld
Otto Lodi wa Hoya na Burghausen
Yohana Lodi wa Oldenburg na Delmenhorst
Albrecht Georg Lodi wa Stolberg
Wolf Ernst Lodi wa Stolberg
Ludwig Lodi wa Gleichen
Karolo Lodi wa Gleichen
Ernest Lodi wa Reinstein
Boto Lodi wa Reinstein
Ludwig Lodi wa Lewenstein
Henrik Bwana wa Limpurg huru daima
Georg Bwana wa Schönburg
Wolf Bwana wa Schönburg
180 Yaani, ‘Bwana Huru’, Kijerumani: ‘Freiherr’; Kilatini na kufuatana kwa Kiingereza: ‘Baro(n). Cheo cha chini cha malodi. Baadaye katika karne ya 15 jina la ‘Bwana’ lilibadilishwa kuwa ‘Baron’ kule Ujerumani.
181 Katika aina hii ‘Lodi’ ni tafsiri ya neno la Kilatini ‘Comes’, Kijerumani ‘Graf’ na Kiingereza ‘Count’.
lxxxii
Anarck Fredrik Bwana wa Wildenfels
Meya na Halmashauri ya Jiji la Lübeck.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Landau.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Münster kule Mt. Georgental.
Halmashauri ya Jiji la Goslar.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Ulm.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Esslingen.
Halmashauri ya Jiji la Reutlingen.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Nördlingen.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Rothenburg karibu Tauber.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Schwäbisch-Hall.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Heilbronn.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Memmingen.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Lindau.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Schweinfurt.
Halmashauri ya Jiji la Donawerda.
Mkurugenzi na Halmashauri ya Jiji la Regensburg.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Wimpfen.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Giengen.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Bopfingen.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Aalen.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Kaufbeuren.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Isna.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Kempten.
Halmashauri ya Jiji la Hamburg.
Halmashauri ya Jiji la Göttingen.
Halmashauri ya Jiji la Braunschweig.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Lüneburg.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Leutkirch.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Hildesheim.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Hameln.
Meya na Halmashauri ya Jiji la Hannover. Halmashauri ya Mühlhausen.
Halmashauri za Erfurt.
Halmashauri za Jiji la Einbeck.
Halmashauri za Jiji la Northeim.
KIRI TATU KUU au
IMANI YA KIKRISTO
inayotumiwa katika makanisa kwa ridhaa kuu
TRIA SYMBOLA CATHOLICA
sive oecumenica
KIRI TATU KUU ZA IMANI ZINAZOTUMIWA KATIKA MAKANISA
KWA RIDHAA KUU
1. UKIRI WA MITUME182
Namwamini Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia.
Namwamini Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, Bwana wetu, aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Mariamu, akateswa wakati wa Pontio Pilato, akasulibiwa, akafa na akazikwa, akashuka kuzimuni. Siku ya tatu akafufuka kutoka kwa wafu; akapaa mbinguni, ameketi katika mkono wa kulia wa Mungu Baba Mwenyezi, kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Namwamini Roho Mtakatifu, Kanisa Takatifu la Kikristo183 ushirika wa watakatifu, ondoleo la dhambi, kufufuliwa kwa mwili, na uzima wa milele. Amina.
2. UKIRI WA NIKEA184
Namwamini Mungu mmoja, Baba Mwenyezi. Muumba wa mbingu na dunia, na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Namwamini Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu, aliyezaliwa na Baba kabla ya ulimwengu wote, mwana wa azali, Mungu wa Mungu, Mwanga wa Mwanga, Mungu kweli wa Mungu kweli, aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye asili moja na Baba, ambaye katika yeye vitu vyote viliumbwa: alishuka kutoka mbinguni, kwaajili yetu wanadamu na kwaajili ya wokovu wetu, alifanyika mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu katika Bikira Mariamu, na alifanyika mwanadamu: ambaye pia, kwa ajili yetu, alisulibiwa wakati wa Pontio Pilato, aliteswa na kuzikwa: katika siku ya tatu alifufuka kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kulia wa Baba: atakuja tena na utukufu kuwahukumu walio hai na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.
Namwamini Roho Mtakatifu, Bwana mtoa uzima, atokaye kwa Baba na
182 Symbolum Apostolicum/Apostolorum’ au ‚Symbolum Romanum.
183 Neno la Kilatini: ‘catholica’ (‘ecclesia catholica, fides catholica‘) limetafsiriwa kuwa ‘Kikristo’ ili kuepuka utata baina ya Kanisa la Roma na makanisa mengine.
184 “Symbolum Nicaeno-Constantinopolitanum.” Ukiri huu ni ukiri ambatani wa Sinodi ya Nikea wa mwaka wa 325 na Sinodi ya Konstantinopoli ya mwaka wa 381. Kaisari wa Roma, Konstantino Mkuu (306-337), aliyewakomboa Wakristo mwaka wa 313 baada ya udhalimu wa nyakati za karne tatu katika Dola la Roma, aliita sinodi ya maaskofu mnamo 250-300 kukutana katika mji wa Nikea huko Bithinia mwaka wa 325. Sinodi hii iliukubali ukiri wa maaskofu Aleksandro wa Aleksandria, Markello wa Ankara, na Hosio wa Cordoba. Sinodi iliyalaani mafundisho ya Ario. Baada ya mabishano mengi ya kitheologia na kisiasa, Sinodi ya Konstantinopoli ilithibitisha ‘Ukiri wa Nikea‘ kama ukiri halisi wa imani ya Kikristo. Katikati ya Sinodi ya Nikea na Sinodi ya Konstantinopoli, kulikuwa na vita vikali vya kanisa kuhusu uungu wa Kristo. Mwishowe, imani iliyokiriwa huko Nikea iliyashinda mafundisho ya Ario na wafuasi wake mbalimbali.
Mwana185: ambaye pamoja na Baba na Mwana anaabudiwa na kutukuzwa: aliyenena kwa vinywa vya manabii. Naliamini Kanisa moja takatifu la Kikristo na la kimitume. Naukiri Ubatizo mmoja kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Natazamia kufufuliwa kwa wafu na uzima wa ulimwengu ujao. Amina.
3. UKIRI WA ATHANASIO186
uliotungwa dhidi ya Waariano187
1. Yeyote apendaye kuokolewa, lazima aishikilie imani ya kweli ya Kikristo kuliko vitu vyote.
2. Ambaye haishikilii imani kikamilifu pasipo kuitangua, bila shaka ataangamia milele.
3. Hii ndiyo imani ya Kikristo ya kweli ya kwamba, tunamwabudu Mungu mmoja katika nafsi tatu na nafsi tatu katika Mungu mmoja
4. Bila kuchanganya nafsi wala kutenganisha asili.
5. Kwa sababu kuna nafsi moja ya Baba, nafsi nyingine ya Mwana, na Roho Mtakatifu ni nafsi nyingine.
6. Lakini kuna Uungu mmoja wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sawasawa na katika utukufu na enzi ileile ya milele.
7. Jinsi Baba alivyo, ndivyo Mwana alivyo, na pia ndivyo alivyo Roho Mtakatifu:
8. Baba hakuumbwa, Mwana hakuumbwa, Roho Mtakatifu hakuumbwa,
9. Baba hana mwisho, Mwana hana mwisho, Roho Mtakatifu hana mwisho, 10. Baba ni wa milele, Mwana ni wa milele, Roho Mtakatifu ni wa milele,
11. na ingawa ni hivyo, si wamilele watatu bali ni mmoja wa milele:
12. jinsi wasivyokuwa watatu wasioumbwa na wasio na mwisho, hivyo ni mmoja asiyeumbwa na asiye na mwisho.
185 186 ‘Symbolum Quicumque.’ Askofu Mkuu wa Aleksandria Athanasio Mkuu (296-373) hakutunga ukiri huu mwenyewe. Jina hili linamheshimu kama shujaa mkuu wa imani halisi kuhusu uungu wa Yesu Kristo.
187 Ario (mnamo 250 - 336) kutoka Libya, alikuwa mchungaji katika Aleksandria, Misri. Alifundisha kwamba, nafsi ya Kristo ni tofauti na ile ya Mungu Baba. ‘Sinodi ya Nikea’ (325) iliyakataa mafundisho yake.
13. Vivyo hivyo, Baba ni Mwenyezi, Mwana ni Mwenyezi, Roho Mtakatifu ni Mwenyezi,
14. na hata hivyo, si kana kwamba ni watatu ambao ni wenyezi bali mwenyezi mmoja.
15. Hivyo basi, Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu, Roho Mtakatifu ni Mungu,
16. na ingawa ni hivyo, hakuna Miungu watatu bali Mungu mmoja.
17. Hivyo basi, Baba ni Bwana, Mwana ni Bwana, na Roho Mtakatifu ni Bwana, 18. na hata hivyo, si Mabwana watatu bali Bwana mmoja.
19. Jinsi inavyotulazimu kwa ukweli wa Kikristo kukiri kila nafsi pekee kama Mungu na Bwana, hivyo pia tunakatazwa, na dini/imani ya Kikristo kusema kuwa kuna Miungu watatu au Mabwana watatu.
20. Baba hakufanywa au hakuumbwa au hakuzaliwa na yeyote.
21. Mwana hakufanywa au hakuumbwa, bali alizaliwa na Baba peke yake.
22. Roho Mtakatifu hakufanywa au hakuumbwa au hakuzaliwa, bali hutoka kwa Baba na Mwana.
23. Basi, kuna Baba mmoja, si Baba watatu, kuna Mwana mmoja, sio Wana watatu, kuna Roho Mtakatifu mmoja, si Roho Watakatifu watatu.
24. Na katika Utatu huu, hakuna nafsi inayojitokeza kwanza au inayofuata nyingine, hakuna iliyo kubwa kuzidi/kuliko nyingine au iliyo ndogo kuliko nyingine,
25. lakini nafsi zote tatu zinalingana na ziko pamoja milele, jinsi ilivyokwisha kutajwa hapo juu, nafsi tatu lazima ziabudiwe katika Utatu katika Umoja, na Umoja lazima uabudiwe katika Utatu.
26. Hivyo, yeyote atumainie kuokolewa lazima afikiri hivyo kuhusu Utatu Mtakatifu.
27. Pia, kwa ajili ya wokovu wa milele, lazima kila mtu aamini kwa uaminifu kuwa, Bwana wetu Yesu Kristo alifanyika mtu halisi.
28. Hii ni kufuatana na imani ya kweli kwamba, tunaamini na kukiri kuwa, Bwana wetu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, wakati huo huo ni Mungu na mwanadamu:
29.ni Mungu wa asili ya Baba, aliyezaliwa kabla ya nyakati, na ni mwanadamu wa asili ya mama yake aliyezaliwa duniani.
30.Mungu halisi na mwanadamu halisi, mwenye nafsi yenye akili ya kibinadamu, na mwenye mwili wa kibinadamu,
31.sawasawa na Baba kuhusu Uungu, mdogo kuliko Baba kuhusu uanadamu wake.
32.Ingawa ni Mungu na mwanadamu, si Kristo wawili, bali ni Kristo mmoja.
33.Mmoja: ndiyo kusema, bila kubadilisha Uungu kuwa katika mwili, bali kwa kuuchukua uanadamu katika Mungu;
34.Mmoja kabisa, si kwa ajili ya kuchanganya asili, bali kwa ajili ya umoja wa nafsi.
35.Jinsi nafsi yenye akili na mwili ni mwanadamu mmoja, vivyo hivyo, Mungu na mwanadamu ni Kristo mmoja.
36.Aliyeteswa kwa ajili ya wokovu wetu, akashuka kuzimuni, akafufuka kutoka kwa wafu,
37.Akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kulia wa Baba, kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
38.Wakati wa kuja kwake watu wote watafufuka, tena wakiwa na miili yao nakutoa hesabu kuhusu matendo yao wenyewe.
39.Na wale waliofanya mema wataingia katika uzima wa milele, na wale waliotenda mabaya wataingia katika moto wa milele.
40.Hii ndiyo imani ya Kikristo; yeyote asiyeamini kwa uaminifu na kwa uthabiti hawezi kuokolewa.
UKIRI WA AUGSBURG
Ukiri wa Imani wa Watawala na Miji Fulani Uliowasilishwa kwa
Enzi yake Kaisari huko Augsburg mwaka wa 1530
Confessio Fidei
“Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, wala sitaona aibu”
Zab. 119: 46
UTANGULIZI188
1. Mfalme Mkuu asiyeshindwa, Kaisari Augusto, bwana mwenye huruma nyingi! Enzi yako Kaisari, uliliagiza baraza kukutana huko Augsburg ili kushauriana juu ya misaada dhidi ya Uturuki, alioye adui mkuu na mkali sana, tangu zamani kwa jina au kwa dini ya Kikristo: pia kupanga jinsi ya kuendelea kuyapinga mashambulio yao makali. 2. Licha ya hayo, kujadili juu ya kutokupatana kwa dini yetu takatifu na imani yetu ya Kikristo. Katika mwanzo huu wa dini, kumekuwepo na kutosikilizwa wazi kwa maoni na imani za vyama kadhaa miongoni mwetu, kueleweka na kufikiria kati yao kwa upendo, huruma na upole wao kwa wao. 3. Kuhusiana na kupata, suluhisho la wazi na lenye ukweli na umoja wa Kikristo katika mambo haya, kwa njia ya kuyarekebisha maandiko ya pande zote mbili yasiyolingana ili dini moja, safi na ya kweli ifuatwe nasi sote. 4. Jinsi tulivyo chini ya Kristo mmoja tu na tunapigana chini yake. Kusudi letu pia ni tuweze kuishi katika Kanisa la Kikristo katika umoja na utengemano. 5. Nasi tuliozitia sahihi na tulioitwa kwenye baraza hili pamoja na wachaguzi,189 watawala wadogo wa jadi katika vyeo vya heshima, tumefika Augsburg mapema kwa kulitii agizo la Kaisari pasipo kujisifu tu miongoni mwa waliotangulia kufika.
6. Kwa sababu ya Enzi yako Kaisari, miongoni mwa mambo mengine hapa
188 Kulingana na andiko la Kilatini.
189 Wachaguzi walikuwa watawala (Kijerumani: ‘Kurfürst’) waliomchagua Kaisari, Maaskofu Wakuu wa Köln, Mainz na Trier, Pfalzgraf wa Rhein, Mtawala wa Sachsen, Markgraf wa Brandenburg, na Mfalme wa Bohemia.
Augsburg, mwanzoni mwa baraza ulitoa pendekezo kwa wachaguzi, watawala, na kwa vyeo vya heshima vya dola190 kwamba, kwa nguvu ya amri ya Kaisari, vyeo vyote vya heshima vya dola vitoe maoni na kauli zao hadharani kwa Kijerumani na Kilatini. 7. Hivyo, baada ya majadiliano ya Jumatano, iliamuliwa kwamba, tunatakiwa leo (Ijumaa) tutoe utimilifu wa ukiri wetu kwa Kijerumani na Kilatini kulingana na matakwa yako Kaisari. 8. Basi, ili kuyafuata mapenzi ya Enzi yako Kaisari, tunautoa ukiri wa wachungaji wetu na ukiri wetu sisi wenyewe ili kuweka wazi, aina ya mafundisho wanayoyatoa katika Maandiko Matakatifu na Neno safi la Mungu miongoni mwetu hadi sasa katika mwanzo huu wa dini
9. Iwapo wachaguzi wengine, watawala, na vyeo vya heshima vya dola wameyatoa pia maandiko ya namna hiyo katika Kijerumani na Kilatini kuhusu maoni na kauli zao. 10. Tutakuwa tayari kutii Enzi yako Kaisari, bwana wetu mpole sana, na kujadiliana kwa urafiki na watawala waliotajwa, marafiki zetu, na vyeo vya heshima, juu ya njia nzuri za kukubaliana na kuridhiana kwa haki kwa kadiri linavyowezekana. Kwa hiyo, tutakutana tukiwa na maandiko ya maoni ya pande zote mbili. Kisha, jambo hili litashughulikiwa kwa amani na upendo. Mungu akiruhusu, hata vikao hivyo virudi katika dini moja iliyo ya kweli. Kadhalika, hatuna budi kuishi, bila kupigana chini ya Kristo mmoja, kumkiri Kristo mmoja kulingana na agizo la Enzi yako Kaisari, kuyaweka yote katika ukweli wa Mungu, tukimwomba Mungu kwa sala za kutoka moyoni ili atusaidie na atuletee amani.
12. Wachaguzi, watawala, na vyeo vya heshima vingine vya chama kingine hata wasiotaka kuenenda kulingana na agizo la Enzi yako Kaisari, pia hata matunda yasipokuwepo, 13. tunataka kukuhakikishia kwamba, hatutakataa lolote ambalo litaweza kuleta mapatano ya Kikristo, jinsi inavyoruhusiwa na Mungu na dhamiri safi. 14. Kwa hisani yako, Enzi yako Kaisari, wachaguzi na vyeo vya heshima vya dola na wote wapendao dini ya kweli kwa juhudi, pamoja na watakaosikiliza kwa roho nzuri mwanzo huu, mkubali na mtambue mwanzo huu kutoka kwa ukiri wetu na wa wenzetu.
15. Hapo awali, Enzi yako Kaisari ulitoa matumaini, si mara moja, bali mara nyingi, na zaidi kwa maneno ya tangazo la Baraza la Spires la mwaka wa 1526. 16. Kwa sababu fulani, wachaguzi, watawala, na vikao vya wawakilishi vya dola vilidai kwamba, kwa Enzi yako, hukutaka zilizotolewa wakati huo wa kukata shauri katika mazungumzo haya ya imani yetu takatifu. 17. Kisha, 190 (Cheo cha heshima cha dola); Kilatini: ‘status imperii,’ Kijerumani: ‘Stand,’ muundo wa uwakili katika Baraza la Dola. Wakati huo watu walitazamiwa kwanza kama wawakilishi wa cheo cha binadamu katika shirika la umma, kama malodi, mapadre, wenyeji wa miji au wakulima. Kidemokrasia, wananchi hawakuwa na haki binafsi.
ukataka kumshawishi Kuhani Mkuu wa Roma191 aitishe sinodi. Mwaka uliopita, jambo hilo hilo lililetwa tena katika Baraza la Spires. 18. Hapo, Enzi yako Kaisari ulijulisha kulingana na maagizo kwa Bwana Ferdinand, Mfalme wa Bohemia na Hungaria, rafiki na bwana wetu mpole, na kisha, kwa msemaji na wajumbe wa Kaisari kwamba, Enzi yako Kaisari umefikiria kabisa mpango wa kuita sinodi kuu. 19. Mpango huo ulitolewa na Kaimu wa Kaisari na mwenyekiti wa washauri wa utawala na wajumbe wa vikao vingine katika baraza lao huko Regensburg. Enzi yako Kaisari, pia ulifikiria mpango huu uwe wa manufaa. Kwa kuwa mambo hayo yaliyozungumzwa kati ya Enzi yako Kaisari na Kuhani Mkuu wa Roma, yalionekana kukaribiana sana na patano na suluhisho la Kikristo. Enzi yako Kaisari haukushuku kwamba, Kuhani Mkuu wa Roma angeweza kushawishika kuitisha sinodi kuu. 20. Kwa hiyo, Enzi yako Kaisari ulitangaza kwa upole kwamba, utachukua hatua ili Kuhani Mkuu wa Roma akubali kuita sinodi kuu ya namna hiyo haraka iwezekanavyo kwa kutuma barua za mwaliko.
21. Mifarakano hii isipoweza kutatuliwa kwa urafiki na mapatano kati yetu na chama kingine, tunatoa msimamo wetu kwa utiifu wote mwingi mno mbele ya Enzi yako Kaisari kwamba, tu tayari kabisa kuhudhuria sinodi kuu ya namna hiyo ya Kikristo na huru. 22. Kuita sinodi ya aina hiyo kumeafikiwa kwa umoja mkubwa na wachaguzi, watawala, na vikao vya wawakilishi vya ufalme kila wakati juu ya mazungumzo mazito ya mabaraza yote ya falme za miaka ya utawala wa Enzi yako Kaisari. Kisheria, hapo nyuma, tulikata rufaa mara nyingi katika mwanzo huu muhimu sana wa muda mrefu na mzito mno kwa halmashauri hiyo na kwa Enzi yako Kaisari. 23. Tunaendelea kusisitiza rufaa hii na hatutaki wala hatuwezi kuiacha iwapo majadiliano haya au mengine hayatatatuliwa kwa urafiki kati yetu na upande mwingine kulingana na barua ya Kaisari na mapatano ya Kikristo. 24. Licha ya hayo, tunatoa ushuhuda wetu ifuatavyo mbele ya umma.
191 ‘Kuhani Mkuu wa Roma,’ tafsiri kutoka kwa Kilatini: ‘Pontifex Maximus,’ jina maalumu la heshima la Askofu wa Roma lenye asili ya dini ya kale ya Waroma. Jina hili la heshima limetumiwa tangu karne ya kumi na nne.
MAFUNGU HALISI YA IMANI NA MAFUNDISHO193
L = Kilatini (Lingua Latina)
G = Kijerumani (Lingua Germanica)
I. Mungu L
1. Makanisa miongoni mwetu, kwa ridhaa kuu hufundisha kwamba, kanuni ya sinodi ya Nikea kuhusu umoja wa asili moja ya kimungu na nafsi tatu katika asili hii moja ya kimungu ni lazima iaminiwe kweli bila mashaka yoyote. 2. Yaani kwamba, kuna asili ya kimungu moja iitwayo Mungu, na ambayo ni Mungu wa milele, asiye na mwili, asiyegawanyika, aliye na nguvu, hekima na uzuri usiokuwa na mwisho, na Muumba na mhifadhi wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. 3. Hata hivyo, kuna nafsi tatu zenye asili hiyo hiyo na nguvu hizo hizo, ambazo ni za milele: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. 4. Neno ‘nafsi’ linatumika kwa jinsi hii katika maana iliyotumiwa na waandishi wa Kanisa. Halimaanishi sehemu au sifa ya lingine, bali linaloishi peke yake.
5. Yanahukumiwa mafundisho yote ya uongo yanayojitokeza dhidi ya fungu hili, 6. miongoni mwa hayo ni kama yale ya wafuasi wa Mani walioweka kanuni mbili, moja nzuri na nyingine mbaya. Isitoshe, akina Valentino, Ario, Eunomio, Waislamu, na wengine kama hawa.194 Yanahukumu pia akina Samosata, wa zamani na wapya, wababaikao kwamba, kuna nafsi moja tu, wanaoshindana kwa maneno kwa hila na kukufuru kwamba, Neno na Roho Mtakatifu, si nafsi tofauti, kwa sababu “Neno” linamaanisha neno linalosemwa au sauti, na kwamba ‘Roho Makatifu’ ni mwendo unaofanywa kwa viumbe na kwamba, Neno na Roho Mtakatifu, si nafsi tofauti, kwa sababu “Neno” linamaanisha neno linalosemwa
192 Kichwa katika Kilatini. Kila fungu la ‘Ukiri wa Augsburg’ linatolewa kwanza kulingana na andiko la Kilatini, kisha kulingana na andiko la Kijerumani.
193 Kichwa katika Kijerumani.
194 Mani (mnamo 216-276) alianzisha dhehebu lake lenye asili ya maoni ya Ugnostiki katika pande za Uajemi na Uhindi. Valentino (135-160) alifundisha huko Roma kulingana na maoni ya Ugnostiki kwamba, Mungu wa kweli hakuumba mbingu na dunia, bali shetani mwingine aliyeitwa ‘Demiurgo.’ Eunomio ( alifariki mwaka wa 394), askofu mwasi wa Antiokia tangu mwaka wa 260, akaondolewa mwaka wa 268. Alifundisha asili moja ya Yesu ya kibinadamu. Wakristo wa Kanisa la Zamani sawa na akina Baba wa Matengenezo ya Kanisa pia waliangalia Uislamu kama dhehebu moja la mafundisho ya uongo sawa na yale ya Ugnostiki na Waariano.
na “Roho” ni mwendo unaofanyika katika viumbe.195
I. Mungu G
1. Kwanza, kwa ridhaa kuu tunafundisha na kushikilia kwamba, kulingana na kanuni ya Sinodi ya Nikea, kuna asili moja ya kimungu ambayo kiukweli inaitwa Mungu. 2. Pia kuna nafsi tatu 3. Wote watatu ni wa asili moja ya kimungu, waishio milele bila kugawanyika, na mwisho, wenye uweza, hekima, na wema usiokuwa na kikomo. Muumba mmoja na mhifadhi ndiye wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. 4. Neno “nafsi” linafaa kueleweka kama jinsi akina baba walivyolitumia neno hili, si kama sehemu au sifa ya lingine bali linaloishi peke yake.
5. Kwa hiyo, mafundisho yote ya uzushi yanayolipinga fungu hili yanakataliwa kabisa. 6. Baadhi ya haya ni mafundisho ya uzushi wa wafuasi wa Mani waliofundisha kwamba, kuna miungu wawili ambao mmoja ni mwema na mwingine ni mwovu. Kadhalika, kuna mafundisho ya wafuasi wa Valentino, Ario, Eunomio, Waislamu, na wengine kama hao. Kuna pia wafuasi wa zamani na wafuasi wapya wa Samosata wanaoshikilia nafsi moja tu. Wao hufanya upotoshaji juu ya nafsi hizo mbili. Yaani, Neno na Roho Mtakatifu wanaposema kwamba, hao wengine wawili si lazima wawe nafsi tofauti bali Neno linamaanisha neno lenye nguvu au sauti. Roho Mtakatifu ni mwendo unaofanyika katika viumbe.
II. Dhambi ya Asili L
1. Makanisa yetu pia hufundisha kwamba, tangu anguko la Adamu, wanadamu wote wanaozaliwa kimaumbile wanazaliwa na dhambi. Hii ni kusema, wanazaliwa bila hofu ya Mungu, bila tegemeo kwa Mungu na wenye hali ya kutamani.196 2. Ugonjwa huu au kosa la asili ni dhambi kweli, ambayo hata sasa inalaani na inasababisha mauti ya milele kwa wasiozaliwa mara ya pili kwa njia ya Ubatizo na Roho Mtakatifu.
3. Yanawahukumu Wapelagio197 na wengine wanaokataa uovu wa asili kuwa
195 Paulo wa Samosata, Askofu wa Antiokia katika karne ya tatu. Uasi wake ulitangulia wa Nestorio, ambao uliukazia zaidi ubinadamu wa Kristo hata kufundisha kwamba, Kristo alikuwa Mungu kadiri ya kupata uwezo wa Mungu kama mwanadamu. ‘Wasamosata wapya,’ yaani, Yohana Campano aliyezuru kitala cha Mtawala Mchaguzi wa Sachsen huko Torgau mwaka wa 1530. Yohana huyu aliukataa pia Uungu wa Roho Mtakatifu.
196 (Hali ya kutamani), Kilatini: ‘consupiscentia.’ Istilahi hii ilikuwa muhimu sana katika anthropologia ya Mt. Agostino.
197 Pelagio, mtaalamu wa theologia kutoka Uingereza aliyefundisha theologia huko Roma mwanzo wa karne ya nne. Wapelagio waliamini hiari katika wokovu na walikataa dhambi ya asili. Agostino wa Hippo (354-430) huko Afrika Kaskazini, askofu na Baba wa Kanisa la Zamani aliyapinga mafundisho ya Wapelagio kwa bidii
ni dhambi na wanaoficha utukufu wa ustahili na fadhili za Kristo kwa kushindana kwa maneno kwamba, binadamu anaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa nguvu na akili zake.
II. Dhambi ya asili G
1. Pia miongoni mwetu inafundishwa kwamba, tangu anguko la Adamu, wanadamu wote wanaozaliwa kwa njia ya asili ya wazazi wao, wanatungwa mimba na kuzaliwa wakiwa na dhambi. Hii inamaanisha kwamba, wanadamu wote wanajawa na tamaa na mielekeo miovu kutoka katika tumbo la uzazi. Kwa nguvu za asili, wanashindwa kuwa na hali ya hofu ya Mungu kweli, na imani ya kweli katika Mungu. 2. Licha ya hayo, ugonjwa huu wa kuzaliwa nao na dhambi ya asili ni dhambi ya kweli na inawahukumu katika ghadhabu ya milele ya Mungu wote wasiozaliwa mara ya pili kwa njia ya Ubatizo na Roho Mtakatifu.
3. Hivyo, wanapingwa Wapelagio na wengineo wanaoikanusha dhambi ya asili kuwa dhambi. Kwa hiyo basi, wao hufanya asili yetu kuwa wacha Mungu kwa uweza wa asili na kukashfu mateso na ustahili wa Kristo.
III. Mwana wa Mungu L
1. Kadhalika, makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, Neno, yaani, Mwana wa Mungu, aliyachukua maumbile ya kibinadamu katika tumbo la Bikira Mariamu Mbarikiwa. 2. Hivyo, asili hizo mbili, ya kimungu na ya kibinadamu ziliungana katika umoja wa nafsi bila kugawanyika: 3. Kristo mmoja, Mungu kweli na binadamu kweli, aliyezaliwa na Bikira Mariamu, akateseka kweli, akasulibiwa, akafa, na akazikwa ili atupatanishe na Baba ili awe dhabihu si kwa hatia ya asili peke yake, bali kwa makosa yote wanayoyafanya wanadamu. 4. Alishuka kuzimuni pia, na siku ya tatu akafufuka kweli, na siku ya tatu akapaa mbinguni na ameketi mkono wa kulia wa Baba, na amiliki na atawale daima juu ya viumbe vyote. 5. Isitoshe, awatakase wamwaminio kwa kumtuma Roho Mtakatifu mioyoni mwao ili awatawale, awafariji, awahuishe, na awatetee dhidi ya Ibilisi na nguvu za dhambi. Kristo huyo huyo atarudi tena wazi kuwahukumu walio hai na wafu, kama ilivyoelezwa katika Ukiri wa Mitume.
III. Mwana wa Mungu G
1. Kadhalika, fundisho ni kwamba, Mungu Mwana alifanyika kuwa mwanadamu, akazaliwa na Bikira safi Mariamu. 2. Asili hizo mbili, ya kimungu sana. Kanisa la Magharibi lilikataa mafundisho haya na liliwaharamisha Wapelagio katika karne ya tano.
na ya kibinadamu hajizagawanyika kamwe katika umoja wa nafsi moja ya Kristo ambaye ndiye Mungu wa kweli na binadamu wa kweli. 3. Alizaliwa kwa kweli, akateswa, akasulibiwa, akafa, na akazikwa ili awe dhabihu, si kwa dhambi ya asili tu bali kwa dhambi zingine zote na airidhishe ghadhabu ya Mungu. 4. Kristo huyo, alishuka kuzimuni, na hakika, siku ya tatu akafufuka kutoka kwa wafu, akapaa mbinguni, na anakaa mkono wa kulia wa Baba ili atawale na amiliki viumbe vyote kwa shabaha kwamba, 5. kwa njia ya Roho Mtakatifu awatakase, awasafishe, awawezeshe, awafariji wote wanaomwamini, awape uzima, vipawa, mali za aina zote, awalinde, na awakinge dhidi ya Ibilisi na dhambi. 6. Kadhalika, mwishowe, huyo Kristo Bwana, atarudi tena hadharani kuwahukumu walio hai na wafu, na kadhalika, kulingana na Ukiri wa Mitume.
IV. Kuhesabiwa Haki L
1. Kadhalika, makanisa yetu hufundisha kwamba, wanadamu hawawezi kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa nguvu zao, stahili zao, au kwa kazi zao, 2. bali wanahesabiwa haki bure kwa ajili ya Kristo kwa imani wanapoamini kwamba, wanapokelewa katika neema na dhambi zao zinasamehewa kwa ajili ya Kristo, ambaye kwa kifo chake, alifanyika ridhaa kwa dhambi zetu. 3. Mungu anaihesabu imani hii kuwa haki mbele zake (Rum. 3 na 4).
IV. Kuhesabiwa Haki G
1. Fundisho ni kwamba, hatuwezi kupata msamaha wa dhambi na haki mbele za Mungu kwa stahili zetu, matendo, au ridhaa yetu, 2. bali tunaupokea msamaha wa dhambi na tunakuwa wenye haki mbele za Mungu kwa neema, kwa ajili ya Kristo, na kwa imani wakati tunaamini kwamba, Kristo aliteseka kwa ajili yetu, na kwa ajili yake mwenyewe, tunasamehewa dhambi zetu, tunazawadiwa haki ya Mungu, na uzima wa milele. 3. Jinsi Mt. Paulo asemavyo katika Warumi sura ya tatu na ya nne, Mungu anaitazamia na anaihesabu imani hii kuwa haki mbele zake mwenyewe.
V. Huduma ya Kanisa L
1. Huduma ya kufundisha Injili na kuzitunza Sakramenti ilianzishwa ili tuipokee imani hii. 2. Naam, kwa njia ya Neno na Sakramenti kama vyombo, Roho Mtakatifu anayetekeleza imani katika wanaoisikiliza Injili anatolewa mahali na wakati unaompendeza Mungu. 3. Hii ni kusema kwamba, si kwa ajili ya kustahili kwetu, bali kwa ajili ya Kristo, Mungu anawahesabu wenye haki wanaoamini na kupokelewa katika neema, Gal. 3:14: “Ili . . . tupate kupokea
ahadi ya Roho kwa njia ya imani.”
4. Makanisa yetu yanawahukumu Waanabaptisti na wengine wanaofikiri kwamba, Roho Mtakatifu anawashukia wanadamu bila neno la nje, kwa njia ya matayarisho yao na kazi zao.
V. Huduma na Mahubiri G198
1. Ili tuipokee imani kama hiyo, Mungu aliianzisha huduma ya mahubiri kuwapatia watu Injili na sakramenti. 2. Kwa njia ya hivi kama vyombo vyake, Mungu anatupatia Roho Mtakatifu anayetekeleza imani katika wanaoisikiliza Injili, mahali na wakati inampendeza Mungu. 3. Injili inafundisha kwamba, tuna Mungu mwenye huruma, si kwa ustahili wetu bali kwa ustahili wa Kristo tunapoyaamini haya.
4. Waanabaptisti na wengine wanahukumiwa kwa kuwa wanafundisha kwamba, tunampokea Roho Mtakatifu kwa matayarisho, mawazo, na matendo yetu wenyewe bila Neno la mwili la Injili.
VI. Utii Mpya L
1. Kadhalika, makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, imani hii inapaswa kuyazaa matunda mema na inapaswa itende matendo mema yaliyoamriwa na Mungu. Lazima tufanye hivyo kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu na si kwa kuyategemea ili kustahili haki mbele za Mungu kwa ajili ya matendo hayo 2. kwa sababu ondoleo la dhambi na kuhesabiwa haki hupokelewa kwa imani kama jinsi maneno ya Kristo yanavyoshuhudia: “Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, sisi tu watumwa wasio na faida” (Lk. 17:10). 3. Kadhalika, inafundishwa na akina baba wa Kanisa la Zamani kwamba, Ambrosio199 anasema: “Imeagizwa na Mungu kwamba, yeyote amwaminiye Kristo, ataokolewa, si kwa matendo bali kwa imani peke yake na atapokea ondoleo la dhambi kwa neema.”
VI. Utiifu Mpya G
1. Kadhalika, fundisho juu ya utiifu mpya ni kwamba, imani ya jinsi hiyo haina budi kuyazaa matunda mema na matendo mema. 2. Ni lazima tufanye matendo
198 Kijerumani: Predigtamt.
199 Ambrosio (339 -397), zamani alikuwa askofu maarufu wa Milano, baba wa kiroho wa Agostino. Hata hivyo, dondoo hili halitoki kwa Ambrosio mwenyewe bali limetoka kwa mkusanyiko wa ufafanuzi wa vitabu vya Agano Jipya katika karne ya nne. Tayari, maandiko haya yalitazamiwa kutoka kwa Ambrosio.
mema jinsi Mungu ametuamrisha na kwa ajili ya Mungu mwenyewe. Hata hivyo, tusiyategemee matendo ya namna hii kana kwamba, kwayo, tungeweza kustahili neema mbele za Mungu. Sisi tunaupokea msamaha wa dhambi na haki kwa njia ya imani katika Kristo jinsi Kristo mwenyewe anavyosema: “Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, sisi tu watumwa wasio na faida” (Lk. 17: 10). 3. Kadhalika, akina baba wa Kanisa wanafundisha, kwa mfano, Ambrosio anasema: “Imeagizwa na Mungu kwamba, yeyote amwaminiye Kristo, ataokolewa na atapata msamaha wa dhambi, si kwa matendo bali kwa imani peke yake bila ustahili wowote.”
VII. Kanisa L
1. Kadhalika, makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, kanisa moja takatifu litakuwepo daima. Basi, kanisa ni mkusanyiko wa watakatifu ambao kwao, Injili inafundishwa kwa ufasaha na Sakramenti zinaadhimishwa sawasawa. 2. Kwa umoja wa kweli wa Kanisa, inatoshea kukubaliana kuhusu mafundisho ya Injili na kuhusu utunzaji wa Sakramenti. 3. Si lazima mapokeo ya binadamu au kanuni za dini na sherehe zilizoanzishwa na wanadamu zifanane kila mahali. 4. Jinsi Mt. Paulo asemavyo, “Imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote . . .” (Efe. 4:5-6).
VII. Kanisa G
1. Pia inafundishwa miongoni mwetu kwamba, lazima kanisa moja takatifu liwepo na lidumu daima. Huu ni mkusanyiko wa waumini wote miongoni mwa ambao Injili safi inahubiriwa na sakramenti takatifu zinatunukiwa kulingana na Injili.
2. Naam, inatoshea kwa umoja wa kweli wa makanisa ya Kikristo kwamba, Injili inahubiriwa kwa ridhaa kulingana na ufahamu safi na sakramenti takatifu zinasimamiwa kulingana na Neno la Mungu. 3. Kwa umoja wa kweli wa kanisa, si lazima kaida zilizoanzishwa na mwanadamu zinapaswe kuzingatiwa kwa usawa katika maeneo yote. 4. jinsi Paulo anavyosema katika Efe. 4: 4-5: “. . . mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja. imani moja, ubatizo mmoja . . . ”
VIII. Kanisa ni nini? L
1. Kusema kweli, kanisa ni mkusanyiko wa watakatifu wanaoamini kweli. Hata hivyo, kwa ajili ya maisha haya, wanafiki wengi na watu wabaya
wamechanganyika na wanaoamini. Hivyo, inakubalika kutumia sakramenti zilizotunzwa na watu waovu kulingana na asemavyo Kristo, “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa . . .” (Mt. 23:2). 2. Sakramenti na Neno la Kristo kuhusu agizo na uanzishwaji wake ni vyenye nguvu kwa kuwa vilianzishwa na kuagizwa na Bwana hata kama vinaadhimishwa na watu waovu.
3. Makanisa yetu yanawahukumu Wadonatio200 na wengine kama hao ambao wamekataa huduma ya watu waovu katika kanisa na kufikiria kwamba, huduma ya watu waovu haina faida wala matokeo yoyote.
VIII. Kanisa ni nini? G
1. Kadhalika, ingawa Kanisa la Kikristo ni mkusanyiko wa waumini na watakatifu wote, kwa ajili ya maisha haya, Wakristo wengi waongo, wanafiki, na hata wakosaji wa wazi wanaendelea kukaa miongoni mwa wacha Mungu. Hata hivyo, Sakramenti ni halisi ingawa wachungaji wanaozitunuku si wacha Mungu. Kristo mwenyewe anaarifu: “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa . . .” (Mt. 23:2). 3. Hivyo wanahukumiwa Wadonatio na wengine wote ambao wameshikilia mtazamo tofauti.
IX. Ubatizo L
1. Makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, Ubatizo ni lazima kwa wokovu kwa maana neema ya Mungu inatolewa kwa njia ya Ubatizo na kwamba, 2. watoto lazima wabatizwe. Kwa kuwa wanapokabidhiwa kwa Mungu kwa njia ya Ubatizo, wanapokelewa katika neema yake.
3. Makanisa yetu yanawahukumu Waanabaptisti201 ambao wanakataa Ubatizo wa watoto na kusema kwamba, watoto wanaokolewa bila Ubatizo.
IX. Ubatizo G
1. Fundisho ni kwamba Ubatizo, ni lazima kwa wokovu na Neema inatolewa kwao (Ubatizo). 2. Inawabidi watoto wachanga pia wabatizwe kwa kuwa wanakabidhiwa kwa Mungu katika Ubatizo wa namna hiyo na watakubaliwa naye.
200 Wadonatio waliokuwa wafuasi wa Askofu Donato Mkuu katika karne ya tatu. Walikuwa dhehebu moja katika Afrika Kaskazini katika karne ya nne. Waliukataa uwezo wa maaskofu walioanguka wakati wa udhalimu kwa Wakristo, japo walitubu baadaye. Walimpinga vikali Mt. Agostino. 201 Waanabaptisti (Anabaptists) walikataa Ubatizo wa watoto na waliwabatiza mara ya pili tena waliokuwa wamebatizwa wakiwa watoto.
3. Kwa hiyo, wanakataliwa Waanabaptisti ambao hufundisha kwamba, Ubatizo wa watoto wachanga si halali.
X.
Chakula cha Bwana L
1. Makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, mwili na damu ya Kristo vipo hapa kwa kweli, na vinatolewa kwa wanaokishiriki Chakula cha Bwana. 2. Yanawakataa wanaofundisha vinginevyo.
X. Chakula Kitakatifu cha Bwana G
1. Fundisho ni kwamba, mwili na damu halisi ya Kristo vipo hapa kwa kweli katika Chakula cha Bwana katika sura ya mkate na divai na vinagawanywa na kupokelewa. 2. Kwa hiyo, mafundisho yanayoyapinga haya yanakataliwa.
XI. Ungamo L
Makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, ungamo la faragha lazima liendelezwe katika makanisa. Hata hivyo, si lazima kutaja dhambi zote katika ungamo. Kwa kuwa haiwezekani kufanya hivyo kulingana na Zaburi, “Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake?” (Zab. 19:12).
XI. Ungamo G
Miongoni mwetu inafundishwa kwamba, ondoleo la faragha lihifadhiwe na lisiachwe ingawa si lazima kuyataja makosa na dhambi zote katika ungamo kwa kuwa haiwezekani kufanya hivyo, Zab. 19: 12, “Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake?”
XII. Toba L
1. Makanisa miongoni mwetu hufundisha kuhusu toba kwamba, walioanguka baada ya Ubatizo wanaweza kuupata msamaha wa dhambi wakati wowote wanapoongoka. 2. Na kwamba, Kanisa halina budi kuwatangazia ondoleo la dhambi202 wanaorudi kwa njia ya toba. 3. Kwa kweli, toba ina sehemu mbili: 4. kwanza ni majuto, yaani, hofu kuu inayoipinga dhamiri kwa njia ya ufahamu wa dhambi; 5. pili ni imani inayozaliwa kutokana na Injili au msamaha wa dhambi na kuamini kwamba, dhambi zinasamehewa kwa ajili ya Neema ya Kristo na
202 Taz. Tofauti kati ya isitlahi hizi “msamaha wa dhambi,” (Kilatini: ‘remissio peccatorum’) na “ondoleo la dhambi” (Kilatini: ‘absolutio’). Ondoleo la dhambi ni sehemu moja ya kaida ya ungamo.
imani hii inaifariji dhamiri na kuiondoa kutoka katika hofu. 6. Halafu, inabidi matendo mema yafuatie ambayo ni matunda ya toba.
7. Makanisa yetu yanawahukumu Waanabaptisti wanaokataa kwamba, waliohesabiwa haki mara moja wanaweza kumpoteza Roho Mtakatifu. Kadhalika, wanaobabaika kwamba, wengine wanaweza kupata ukamilifu katika maisha haya na hivyo hawawezi kutenda dhambi. 9. Nao Wanovatiano203 wanahukumiwa kwa maana hawataki kuwasamehe walioanguka baada ya Ubatizo ingawa walirudi kwa njia ya toba. Pia wasiofundisha kwamba, ondoleo la dhambi linapatikana kwa njia ya imani wanakataliwa, lakini wanatulazimisha kustahili kuipokea neema kwa kazi zetu za upatanisho.204
XII. Toba G
1. Miongoni mwetu inafundishwa kwamba, waliotenda dhambi baada ya Ubatizo, 2. wao huupokea msamaha wa dhambi, Kanisa lisiwakataze kushiriki ondoleo la dhambi wakati wowote wanapotubu. 3. Kusema ukweli, Toba ya kweli ni majuto, majonzi makubwa, au hofu kuu kwa ajili ya dhambi na wakati huo huo ni kuiamini Injili na ondoleo la dhambi. 5. Yaani, kwamba, dhambi zote zimesamehewa na neema imetolewa kwa njia ya Kristo. Imani hii inaufariji na kuutuliza moyo. 6. Kisha, uboreshaji wa maisha ufuate na uache dhambi kwa kuwa matendo haya yanapaswa kuwa matunda ya toba jinsi Yohana anavyosema katika Mt. 3:8, “Basi zaeni matunda yapasayo toba . . .”
7. Hapa, wanakataliwa wanaofundisha kwamba, watu waliokuwa wacha Mungu hawapaswi kuanguka tena.
9. Kinyume chake, wanalaaniwa wafuasi wa Donatio ambao waliwakataza watu waliotenda dhambi wasipokee ondoleo la dhambi.
10. Wanakataliwa pia wasiofundisha kwamba, mtu anapokea msamaha wa dhambi kwa imani, bali kwa matendo ya upatanisho unaofanywa na mwanadamu.
203 Novatiano, mchungaji huko Roma katika karne ya tatu, alitengwa kwa sababu ya mafundisho yake ya ushupavu kuhusu toba. Aliuawa katika udhalimu wa Kaisari Valeriano 257-258. Kanisa la Novatiano liliendelea mpaka karne ya sita.
204 Kilatini: ‘Satisfactiones nostras.’ Kulingana na mafundisho ya Roma, mkosaji hupatanisha sehemu ya matokeo ya dhambi zake baada ya padre kumtangazia msamaha wa dhambi, kwa matendo mema au matendo ya upatanisho kwa njia ya kuufanya ubia pamoja na neema ya Mungu. Katika kazi hii, alisaidiwa na Kanisa lililoweza kuitumia hazina ya stahili za Kristo na watakatifu wote (Kilatini: ‘thesaurus ecclesiae’) kwa faida ya waliozitubu dhambi zao.
XIII. Matumizi ya Sakramenti L
1. Makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, sakramenti hazikuanzishwa kuwa alama za kukiri kati ya wanadamu peke yao, bali ziwe alama na shuhuda wa mapenzi ya Mungu kwetu ili kuhuisha na kuimarisha imani kati ya wanaozitumia.
2. Kwa hiyo, sakramenti hazina budi kutumiwa kwa lengo maalumu kwamba, imani inategemea ahadi zinazotolewa na zinazoonyeshwa.
XIII. Matumizi ya Sakramenti G
Miongoni mwetu inafundishwa kwamba, sakramenti hazikuanzishwa tu kuwa alama za kutambua Wakristo kwa njia ya nje peke yake, bali ni alama na ushuhuda wa Mungu kutuhusu ili kuiamsha na kuiimarisha imani yetu. Kwa hiyo, zinahitaji imani na zinatumiwa kwa njia halisi zinapopokelewa kwa imani na kwa madhumuni ya uimarishaji wa imani.
XIV. Utaratibu wa Kanisa L
Makanisa miongoni mwetu hufundisha kuhusu utaratibu wa Kanisa kwamba, yeyote asihubiri hadharani, kanisani, wala asiadhimishe sakramenti, isipokuwa awe ameitwa kwa utaratibu.205
XIV. Utaratibu wa Kanisa G
Miongoni mwetu nafundishwa kwamba, yeyote asifundishe, au asihubiri, au asizitunuku sakramenti hadharani bila wito halisi.
XV. Kaida za Kanisa206
1. Makanisa miongoni mwetu hufundisha kuhusu kaida za Kikanisa kwamba, taratibu hizo zihifadhiwe ambazo zinaweza kuhifadhiwa bila dhambi na zinazofaa kwa amani na utaratibu bora katika Kanisa kama sikukuu fulani na sherehe.
2. Hata hivyo, watu wanaonywa wasizilemee dhamiri zao kwa mambo kama hayo, kana kwamba, taratibu za namna hii ni za lazima kwa wokovu.
3. Watu wanaonywa zaidi miongoni mwetu kwamba, mapokeo ya wanadamu ambayo yameanzishwa ili kumpatanisha Mungu, kustahili neema, na kutenda upatanisho kwa ajili ya dhambi ni kinyume cha Injili na cha mafundisho kuhusu imani kabisa. Kwa hiyo, nadhiri207 na mapokeo kuhusu vyakula na siku na
205 Kilatini: ‘Rite vocatus.’
206 Kijerumani: ‘Von Kirchenordnungen;’ Kilatini: ‘De ritibus ecclesiasticis.’
207 ‘Nadhiri,’ yaani, viapo vya kidini.
kadhalika, vilivyoanzishwa ili kustahili neema na kufidia makosa, si kitu dhidi ya Injili.
XV. Kaida za Kanisa
Fundisho ni kwamba, kaida za Kanisa zilizoanzishwa na wanadamu zinazoweza kutunzwa bila dhambi na zinazohudumia utaratibu bora na amani katika Kanisa, kama sikukuu fulani, sherehe, na nyingine kama hizo, zitunzwe. Hata hivyo, watu wanaonywa wasizilemee dhamiri zao kwa mambo kama hayo, kana kwamba, taratibu za namna hiyo ni lazima kwa wokovu. Licha ya haya, fundisho ni kuwa, taratibu na mapokeo yote yaliyoanzishwa na watu ili kumpatanisha Mungu na kustahili neema kwayo, yanaipinga Injili na mafundisho ya imani katika Kristo. Hivyo, nadhiri za utawa na mapokeo mengine kuhusu utofautishaji wa vyakula, siku, na kadhalika, vinavyokusudiwa kwa ajili ya kuistahili neema, havina maana yoyote na vinaipinga Injili.
XVI. Mambo ya Jamii L
1. Makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, miundo halali ya jamii ni kazi njema za Mungu, na imewapasa Wakristo kuzisimamia huduma za jamii, 2. kuhudumu kama mahakimu, kuamua mambo kulingana na sheria za ufalme wa kaisari na sheria zingine zilizopo, kama kutoa adhabu za haki, kujishughulisha katika vita vya haki, kutumika kama askari, kufanya mikataba halali, kuwa na mali, kula viapo wakihitajiwa na hakimu, kuoa, na kuolewa.
3. Yanawalaani Waanabaptisti wanaowakataza Wakristo wasifanye huduma hizi za jamii.
4. Yanawalaani pia wasiouweka ukamilifu uletwao na Injili katika kumwogopa Mungu na katika imani na badala yake wanauweka katika kususia wajibu wa jamii. Injili inafundisha haki ya moyo ya milele na haiharibu serikali au jamii. Kinyume chake, inashurutisha sana zihifadhiwe kama taratibu za Mungu na matumizi ya upendo katika mambo haya ya jamii. Kwa hiyo, Wakristo hawana budi kuwatii wakuu wao na sheria isipokuwa pale wanapoamriwa kutenda dhambi, hapo imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu (Mdo. 5:29).
XVI. Serikali na Madaraka ya Dunia208 G
1. Miongoni mwetu inafundishwa kwamba, mamlaka zote kuu hapa duniani, utawala, na sheria halisi, ni utaratibu bora ulioumbwa na kuanzishwa na Mungu. 2. Wakristo wanaweza kuhudumia katika ofisi ya mamlaka kuu kama kuwa mtawala na hakimu bila dhambi, kutoa hukumu kulingana na haki ya Kaisari au haki zingine halisi, kuwaadhibu wahalifu kwa upanga, kuongoza vita vilivyosadikishwa, kupigana katika vita, kununua na kuuza, kula kiapo, kumiliki rasimali, kuoa, kuolewa na kadhalika.
3. Walaaniwe Waanabaptisti wanaofundisha pia kwamba, mambo haya yaliyotangualia si ya Kikristo.
4. Walaaniwe pia wanaofundisha kwamba, ukamilifu wa Kikristo unahitaji kuiacha nyumba na kaya kwa njia ya kimwili, mwanamke, na mtoto na kuyakataa mambo haya yote yaliyotajwa kana kwamba, kufanya hivyo ndio ukamilifu halisi, hofu halisi ya Mungu, na imani halisi katika Mungu.209 Kusema kweli, Injili haifundishi haki ya nje na ya wakati huo bali hali na haki ya ndani ya moyo na ya milele. Injili haipindui madaraka ya dunia, serikali, na hali ya ndoa bali inataka kwamba, watu wote wayatazame haya yote kuwa utaratibu wa kweli wa uungu. 5. Kila mmoja na katika vyeo vya namna hiyo aonyeshe upendo wa Kikristo na matendo mema ya kweli kulingana na wito wake. 6. Kwa hiyo, inawabidi Wakristo kuwa raia wa mamlaka iliyo kuu na kutii maagizo na sheria zao katika mambo yote yakiweza kutendeka bila dhambi. Lakini wakati amri ya mamlaka kuu haiwezi kutendeka bila dhambi, 7. mtu amtii Mungu kuliko wanadamu (Mdo. 5:29).
XVII. Kurudi kwa Kristo kwa Hukumu L
1. Kadhalika, makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, Kristo ataonekana katika ukamilisho wa ulimwengu akihukumu na atawafufua wafu wote. 2. Atawapatia uzima wa milele na furaha isiyokuwa na mwisho wanaomcha na wateule, lakini wasiomcha Mungu na mashetani atawahukumu wapate kuteseka bila mwisho.
4. Makanisa yetu yanawahukumu Waanabaptisti wanaofikiri kwamba, kutakuwa na mwisho wa mateso ya ghadhabu kwa waliohukumiwa pamoja na
208 Kijerumani: ‘Polizei.’ Neno hili halimaanishi ‘Polisi,’ bali linatokana na neno la Kiyunani: ‘πολιτεια,’ yaani, muundo wa serikali, Kilatini: ‘politia.’
209 Ukamilifu wa namna hiyo, yaani, maisha ya watawa, ulifundishwa katika Kanisa la Roma na pia miongoni mwa baadhi ya vikundi vya Waanabaptisti.
mashetani.210
5. Yanawahukumu pia wengine wanaotangaza maoni ya Kiyahudi kwamba, watakatifu watapata mamlaka ya dunia kabla ya ufufuo wa wafu, pia wasiomcha Mungu wakiwa wanagandamizwa kila mahali.211
XVII. Kurudi kwa Kristo kwa Hukumu G
1. Fundisho ni kwamba, Bwana wetu Yesu Kristo 3. Atawapatia wanaoamini na walioteuliwa uzima na furaha ya milele. Atawalaani wasiomcha Mungu na mashetani kwenda kuzimuni kuipokea adhabu ya milele.
4. Wanakataliwa Waanabaptisti wanaofundisha kwamba, mashetani na watu waliolaaniwa hawatapokea mateso na dhiki ya milele.
5. Kadhalika, yanakataliwa mafundisho fulani ya Wayahudi yanayojulikana hata leo kwamba, watakatifu kabisa watashika madaraka ya dunia na wasiomcha Mungu watagandamizwa kabla ya ufufuo wa wafu.
XVIII. Hiari212 Huru L
1. Makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, hiari ya binadamu ina uhuru fulani wa kuifuata haki ya jamii na kuchagua kati ya mambo yaliyomo katika sehemu ya akili ya binadamu. 2. Hata hivyo, haina uwezo kutimiza haki ya Mungu au haki ya kiroho bila Roho Mtakatifu, kwa kuwa mwanadamu wa tabia ya asili hayatambui mambo ya Roho wa Mungu (1 Kor. 2:14). 3. Lakini haki hii inazaliwa moyoni wakati Roho Mtakatifu anapokelewa kwa Neno. Katika kitabu cha tatu cha “Hypognostikon,”213 kwa maneno kadhaa Agostino anasema: “Tunakubali kwamba, watu wote wana hiari huru inayowawezesha kukata mashauri kwa ajili ya akili. Hata hivyo, kuhusu mashauri haya ya akili haiwezekani kutimiza mambo ya kumpendeza Mungu bila Mungu. Kwa maana, ni katika matendo ya maisha haya ndipo wana hiari kuchagua mema au mabaya. Kusema “mema” kunamaanisha matendo mema yanayotokana na wema katika maumbile. Yaani, kuwa na moyo wa kulima mashamba, kula, kunywa, kuwa
210 Mafundisho haya yanaitwa ‘αποκαταστασις,’ Kiingereza: ‘universalism.’
211 Tabiri za Melkior Rinck huko Worms. Baada ya ‘Ukiri wa Augsburg,’ Waanabaptisti wengine walianzisha “Ufalme wa Mungu,” huko Münster, Westfalen, jinsi walivyouita, chini ya utawala katili mwaka wa 15321535.
212 Kilatini: ‘arbitrium.’ Neno hili linamaanisha zaidi ya “kutaka,” “kupenda,” au “kutamani.” Neno ‘arbitrium’ linamaanisha kutaka na pia kuweza kukata shauri na kulitekeleza. Kwa hiyo, tunalitumia tu neno “hiari” badala ya “nia.”
213 Kitabu kiitwacho, ‘Hypomnesticon contra Pelagianos et Coelestianos’ kilihesabiwa Agostino katika mikusanyiko ya zamani ya maandiko na vitabu vyake.
na rafiki, kujivika, kujenga nyumba, kuoa, kufuga ng’ombe, kujifunza ufundi mzuri mbalimbali, au kulitenda lolote zuri linalohusiana na maisha haya. Haya yote hayawezekani kuwepo bila majaliwa ya Mungu. Naam, haya yote yapo, tumeyaona kwake na kwa njia yake. Kwa upande mwingine, kwa kutaja neno “ovu” anamaanisha mambo kama utashi wa kuabudu sanamu, utashi wa kuua, na kadhalika.”
XVIII. Hiari G
1. Pia inafundishwa miongoni mwetu kwamba, binadamu ana kiwango fulani cha hiari. Yaani, kuishi maisha ya nje ya kuheshimika na kufanya uamuzi katika mambo yanakubalika kwenye akili. 2. Lakini bila neema, msaada, na mvuto wa Roho Mtakatifu, mtu hawezi kumpendeza Mungu, kumwogopa, au kumwamini Mungu kwa moyo wake, au kuziondoa tamaa mbaya za maumbile kutoka moyoni mwake. 3. Haya yote yanatekelezwa na Roho Mtakatifu ambaye anapatiwa kwa njia ya Neno la Mungu. Naam, Paulo anasema katika 1 Kor. 2: 14: “Mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu.”
4. Ili idhihirike kwamba, hatufundishi mambo mapya hapa, haya ndiyo maneno dhahiri ya Agostino kuhusu hiari yanayonukuliwa kutoka Kitabu cha Tatu cha “Hypognostikon:” “Tunakubali kwamba, watu wote wana hiari inayowawezesha kukata mashauri kwa ajili ya akili. Hata hivyo, kuhusu mashauri haya ya akili haiwezekani kutimiza mambo ya kumpendeza Mungu bila Mungu. Kwa maana, ni katika matendo ya maisha haya ndipo wana hiari kuchagua mema au mabaya. Kusema “mema” kunamaanisha matendo mema yanayotokana na wema katika maumbile. Yaani, kuwa na moyo wa kulima mashamba, kula, kunywa, kuwa na rafiki, kujivika, kujenga nyumba, kuoa, kufuga ng’ombe, kujifunza ufundi mzuri mbalimbali, au kutenda lolote zuri linalohusiana na maisha haya. Haya yote hayawezekani kuwepo bila majaliwa ya Mungu. Naam, haya yote yapo, tumeyaona kwake na kwa njia yake. Kwa upande mwingine, kwa kutaja neno “ovu” anamaanisha mambo kama utashi wa kuabudu sanamu, utashi wa kuua, na kadhalika.”
XIX. Chanzo cha Dhambi L Makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, ingawa Mungu anaumba na kuitunza asili, chanzo cha dhambi ni nia ya mwovu, yaani, Ibilisi na watu wasiomcha Mungu. Bila msaada wa Mungu, nia ya waovu itamgeukia mwovu na si Mungu jinsi Kristo anavyosema katika Yn. 8:44: “Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe.”
XIX. Chanzo cha Dhambi G
Inafundishwa miongoni mwetu kwamba, ingawa Mungu Mwenyezi ameyaumba na bado anaitunza asili yote, hata hivyo, nia mbaya inatenda dhambi katika watu waovu wanaomdharau Mungu. Hii ndiyo nia ya Ibilisi na ya watu wote wasiomcha Mungu. Wakati Mungu anatoa tegemeo lake tu, nia inatoka kwa Mungu na kuugeukia uovu, jinsi Kristo asemavyo katika Yohana 8:44: “Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe.”
XX. Imani na Matendo Mema L
1. Wenzetu wanashtakiwa kwa uongo kwa kuyakataza matendo mema. 2. Maandiko yao kuhusu Amri Kumi na mengine kama hayo yanashuhudia kwa pamoja kwamba, wamefundisha kwa njia ya manufaa kuhusu hali na wajibu wote wa maisha, wakionyesha hali zipi za maisha na matendo yepi yampendezayo Mungu katika miito kadha wa kadha. 3. Zamani, wahubiri waliyafundisha mambo haya kidogo. Badala yake, waliyahimiza matendo ya kitoto na yasiyohitajika, kama sikukuu maalumu, mifungo iliyoamriwa, madaraja ya udugu, hija, ibada kwa ajili ya watakatifu, rozari, umonaki na kadhalika. 4. Kwa sababu wapinzani wetu wameonywa kuhusu mambo haya, sasa wanayaacha hata hawahubiri kama awali kuhusu matendo haya yasiyokuwa na faida. 5. Hata wameanza kutaja zaidi imani ambayo waliinyamazia. 6. Wao hufundisha kwamba, tunahesabiwa haki si kwa matendo tu lakini kwa kuiunganisha imani na matendo. Isitoshe, wanasema kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani na matendo. 7. Mafundisho haya yanaweza kuvumiliwa kuliko yale yaliyotajwa mwanzoni. Vile vile, yanaweza kumpatia mtu faraja kuliko mafundisho yao ya zamani.
8. Kwa hiyo basi, mafundisho kuhusu imani ambayo yanapaswa kuwa mafundisho maalumu katika Kanisa, yalikuwa yameachwa kwa muda mrefu sana bila kujali. Ni muhimu kila mmoja akubali kwamba, kumekuwepo na ukimya mkubwa kuhusu haki ya imani katika mahubiri ambayo mafundisho kuhusu matendo yameshughulikiwa katika Kanisa. Wenzetu wameyaelimisha makanisa miongoni mwetu kuhusu imani ifuatavyo:
9. Tunaanza kufundisha kwamba, matendo yetu hayawezi kutupatanisha na Mungu au kustahilisha ondoleo la dhambi na neema. Badala yake, tunapokea ondoleo la dhambi na neema kwa imani tunapoamini kwamba, tunapokelewa katika neema kwa ajili ya Kristo ambaye peke yake amewekwa kuwa Mpatanishi na Msuluhishi na ambaye kwake, Baba anapatanishwa nasi. 10. Kwa hiyo, anayetegemea kwamba, anastahili neema kwa matendo yake, anaidharau stahili na
neema ya Kristo, anatafuta njia ya kumwendea Mungu kwa nguvu za kibinadamu bila Kristo, ingawa, kuhusu yeye mwenyewe, Kristo amesema: “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima” (Yn. 14:6).
11. Mafundisho haya kuhusu imani yanaelezwa kila mahali katika maandiko ya Paulo (Efe. 2:8): “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani , wala si kwa matendo.”
12. Yeyote asije akadai kwa hila kwamba, tumeyatunga maelezo mapya ya Paulo. Tunasema, jambo hilo lote lina ushuhuda wa akina baba. 13. Katika vitabu vingi, Agostino anaitetea neema na haki ya imani dhidi ya stahili za matendo. 14. Ambrosio anayafundisha hayo hayo katika “Wito wa Mataifa” (‘De vocatione gentium’) na penginepo kwa maana katika “Wito wa Mataifa” anasema: “Ukombozi wa damu ya Kristo ungekuwa bila thamani yoyote na huruma ya Mungu haingetangulia matendo ya binadamu kama kuhesabiwa haki, ambako kunatimizwa kwa neema, kungetegemea stahili zilizotangulia hata kutokuwa zawadi ya bure ya mpaji, bali itakuwa mshahara wa mtenda kazi.”
15. Ingawa mafundisho haya yanadharauliwa na watu wasio na uzoefu katika majaribu, dhamiri za wacha Mungu na wanaoogopa hupata kujua kwa uzoefu kwamba, yanaleta faraja isiyokuwa na mwisho kwa sababu dhamiri za watu haziwezi kupata utulivu kwa matendo yoyote ila tu kwa imani wanaposadiki hakika kwamba, kwa ajili ya Kristo, wana Mungu aliyepatanishwa nao, 16. jinsi Paulo afundishavyo katika Rum. 5:1: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu.” 17. Mafundisho haya yote yanahusiana na mapigano ya dhamiri yenye hofu na hayawezi kueleweka bila mapigano haya. 18. Hii ndiyo sababu wasiokuwa na uzoefu na watu wa ulimwengu huota ndoto kwamba, haki ya Kikristo si zaidi ya haki ya jamii au falsafa.
19. Zamani, dhamiri ziliteswa na mafundisho ya matendo wakati ambapo hakukusikika faraja ya Injili. 20. Watu wengine walisukumwa na dhamiri zao kwenda jangwani au katika nyumba za watawa wakiwa na matumaini ya kustahili neema kwa njia ya maisha ya utawa. 21. Wengine walivumbua matendo mengine ili kustahili neema na ondoleo la dhambi. 22. Kwa hiyo, kulikuwa na hoja kubwa ya kutoa na kufanya upya mafundisho haya ya imani katika Kristo ili kuwezesha dhamiri yenye mahangaiko isipungukiwe na faraja. Badala yake, ijue kwamba, neema na ondoleo la dhambi vinaeleweka kwa imani katika Kristo.
23. Watu wanaonywa pia kwamba, maneno haya “ondoleo la dhambi,” kwa “imani” hayamaanishi maarifa ya kihistoria peke yake (jinsi ilivyo ndani ya asiyemcha Mungu na Ibilisi), lakini yanamaanisha imani ya kuamini. Si historia
tu, bali pia matokeo ya historia, yaani, kwa njia ya fungu hili linalohusu ondoleo la dhambi kwa ajili ya Kristo, tuna neema, haki, na ondoleo la dhambi.
24. Yeyote basi, anayejua kwamba, ana Baba aliyepatanishwa naye kwa njia ya Kristo, kweli anamjua Mungu. Anajua kwamba, anamtunza na anamwita Mungu. 25. Hakosi kuwa na Mungu kama watu wa mataifa, kwa maana Ibilisi na watu wasiomcha Mungu hawawezi kuliamini fungu hili la ondoleo la dhambi. Hivyo, wanamchukia Mungu kama adui, hawamwiti na hawatarajii mema yoyote kutoka kwake. 26. Kadhalika, Agostino anawaonya wasomaji wake kwa njia hii kuhusu neno “imani” anapowafundisha kwamba, katika Biblia, neno “imani” haliwezi kueleweka kama maarifa yaliyo ndani ya wasiomcha Mungu, lakini kama ujasiri unaoifariji na unaohimiza mioyo yenye hofu sana.
27. Wenzetu wanaendelea kufundisha kwamba, ni sharti kufanya matendo mema, si kwamba, tutategemea kustahili neema kwa hayo, lakini kwa sababu ya mapenzi ya Mungu. 28. Ni kwa imani tu tunapata ondoleo la dhambi na neema. 29. Pia kwa njia ya imani, Roho Mtakatifu anapokelewa. Basi, mioyo inahuishwa na inapata mawazo mapya ili kuweza kuyazaa matendo mema. 30. Ambrosio anasema: “Imani ni mzazi wa nia njema na tendo la haki.” 31. Kwani bila Roho Mtakatifu, nguvu za wanadamu zinajaa mawazo yasiyompa Mungu heshima na ni duni kutenda matendo mema mbele za Mungu. 32. Mbali na hayo, ni chini ya nguvu za Ibilisi anayewahimiza wanadamu katika dhambi mbalimbali, maoni mabaya, na manza214 ya wazi. 33. Hali hii inaonekana katika maisha ya wataalamu wa falsafa waliojaribu kuishi maisha ya uadilifu. Hata hivyo, hawakuweza kulitimiza kusudi lao. Badala yake, walitiwa najisi katika aina nyingi za uhalifu wa wazi. 34. Unyonge wa binadamu ni wa aina hii. Yaani, mtu anapojiongoza kwa nguvu za binadamu peke yake bila imani na Roho Mtakatifu.
35. Ni rahisi kuona kwamba, hatuna sababu yoyote ya kuyashtaki mafundisho haya kuwa yanazuia matendo mema. Kinyume chake, tuna sababu ya kuyasifu kwa kuonyesha jinsi tunawezeshwa kuyatenda matendo mema 36. kwani bila imani, asili ya binadamu haiwezi kutenda matendo ya Amri ya Kwanza au ya Pili. 37. Bila imani, kumwita Mungu hakutarajii lolote kutoka kwake, au kubeba msalaba, bali hutafuta na kutegemea msaada wa binadamu. 38. Basi, bila imani na tegemeo katika Mungu, moyo wa binadamu unatawaliwa na tamaa mbaya zote na mashauri ya kibinadamu. 39. Kwa hiyo, Kristo anasema, “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote” (Yn. 15:5), 40. Nalo Kanisa linaimba: Pasipo kuwepo kwako mwanadamu hana kitu licha ya hatia.215
214 Yaani, makosa.
215 Dondoo kutoka kwa wimbo maarufu wa Pentekoste ‘Veni Sancte Spiritus’ - ‘Njoo Roho Mtakatifu,’
XX. Imani na Matendo Mema G
1. Wenzetu wamekuwa wakishtakiwa uongo kwa kuyakataza matendo mema. 2. Maandiko yao juu ya Amri Kumi na maandiko mengine yanaonyesha kwamba, wameyatunga maarifa na mashauri yenye faida sana kuhusu hali halisi ya maisha na matendo ya Kikristo. 3. Kabla ya wakati huo, mambo haya yalifundishwa kidogo tu. Badala yake, mahubiri karibu yote yalishughulikia matendo ya kitoto yasiyokuwa na faida kama rozari, ibada kwa ajili ya watakatifu, umonaki, hija, mifungo iliyoagizwa, sikukuu, madaraja ya udugu na kadhalika. 4. Wapinzani wetu hawayasifu zaidi matendo ya namna hiyo yasiyokuwa na faida jinsi walivyofanya awali. 5. Wamejifunza pia kuzungumza kuhusu imani ambayo hawakuihubiri kamwe zamani. 6. Hawafundishi zaidi kwamba, tunahesabiwa haki kwa ajili ya matendo peke yake. Badala yake, wanaongezea pia imani katika Kristo na wanasema kwamba, imani na matendo vinatufanya wenye haki mbele za Mungu.
7. Nyongeza ya namna hiyo inaweza kufariji zaidi kuliko mafundisho ya kuyategemea matendo tu.
8. Kwa sababu mafundisho kuhusu imani ambayo ni fungu kuu la Ukristo, yalikerwa kwa muda mrefu sana - jinsi inatubidi kukubali - wakati hakuna kitu kingine chochote kilichohubiriwa popote isipokuwa matendo tu, watu wetu wameshauriwa kwa njia ifuatayo:
9. Kwanza, matendo yetu hayawezi kutupatanisha na Mungu na hayatufanyi kuistahili neema. Hili linafanyika tu kwa imani tunapoamini kwamba, dhambi zetu zitasamehewa kwa ajili ya Kristo ambaye ndiye Mpatanishi anayetusuluhisha na Baba. 10. Mtu ambaye hudhania kwamba, anaweza kuyafanikisha haya na kustahili neema kwa matendo, anamdharau Kristo na anatafuta njia yake mwenyewe kupambana na Injili na kumwendea Mungu.
11. Mafundisho haya kuhusu imani yanatendeka kwa njia ya wazi na dhahiri pahali pengi jinsi Mt. Paulo asemavyo hasa katika Efe. 2: 8-9: “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”
12. Hapa hakuna uchambuzi mpya ambao umekuwa ukiingizwa. 13. Tunaweza kuushuhudia huu kwa Agostino ambaye alilitenda jambo hili kwa bidii na aliyefundisha kwamba, tunapokea neema na kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa imani katika Kristo na si kwa matendo jinsi kitabu chake kiitwacho, uliotungwa na Stephen Langton (+1228), Askofu Mkuu wa Canterbury.
“Roho na Herufi”216 kinavyodhihirisha.
15. Hata hivyo, mafundisho haya yanadharauliwa sana na watu ambao hawajajaribiwa, ila yanakuwa ya baraka kweli na yenye faraja kwa watu wenye dhamiri zinazomwogopa Mungu na zenye hofu. 16. Dhamiri haiwezi kupata utulivu na amani kwa njia ya matendo bali kwa imani peke yake inapoamini imara kwamba, ina Mungu mwenye huruma kwa ajili ya Kristo jinsi Mt. Paulo anavyosema katika Rum. 5:1: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu.”
19. Faraja hii haikusikika zamani katika mahubiri bali dhamiri dhaifu zilisukumwa kutegemea juhudi zao na kila aina ya matendo. 20. Wengine waliendeshwa na dhamiri zao kwa kujiunga na nyumba za watawa kwa tumaini kwamba, wangeweza kuistahili neema kwa kuishi maisha ya watawa. 21. Wengine walitazamia matendo mengine ili kupata stahili na kupatanishwa kwa ajili ya dhambi. 22. Wengi wao waligundua kwamba, mtu hawezi kupata amani kwa njia hii. Kwa hiyo basi, ilikuwa lazima kuyahubiri na kuyatumia mafundisho haya kuhusu imani katika Kristo ili watu wapate kujua kwamba, tunapewa neema ya Mungu kwa njia ya imani peke yake bila stahili zetu.
23. Tunafundisha pia kwamba, hapa, hatuzungumzii kuhusu imani ya aina inayochukuliwa na Ibilisi na watu wasiomcha Mungu pia wanaoamini kihistoria tu kwamba, Kristo aliteseka na akafufuka kutoka kwa wafu. Badala yake, tunaizungumzia imani ya kweli inayoamini kwamba, kwa njia ya Kristo, tunapata neema na msamaha wa dhambi.
24. Basi, yeyote anayefahamu kwamba, katika Kristo, ana Mungu mwenye huruma, anamfahamu Mungu, anamlilia kwa maombi, na haishi bila Mungu jinsi Wapagani wanavyofanya. 25. Yaani, watu wasiomcha Mungu na Ibilisi hawaliamini fungu hili la msamaha wa dhambi. Kwa hiyo, wanaendelea kuwa maadui wa Mungu, hawawezi kumwomba na hawatarajii jema lolote kutoka kwake. Maandiko Matakatifu yanaizungumzia imani na hayamaanishi ujuzi mtupu ambao ni imani ya Ibilisi na watu wasiomcha Mungu jinsi tunavyoonyesha sasa. Ebr. 11:1 inafundisha kwamba, imani si ujuzi mtupu wa kihistoria tu, bali ni tegemeo kwa Mungu na utimizo wa ahadi zake. 26. Agostino anatukumbusha pia kwamba, inatubidi kulielewa neno “imani” katika Maandiko Matakatifu kuwa na maana ya tegemeo kwa Mungu, kuwa thibitisho kwamba, Mungu ndiye mwenye huruma kwetu na si kuwa na maana ya ujuzi mtupu wa kihistoria unaofahamika kwa Maibilisi pia.
216 Kilatini: ‘De Spiritu et littera.’
27. Pia inafundishwa kwamba, matendo mema lazima yatendeke ingawa hatuna budi kuyatenda lakini bila tegemeo kwamba, kwayo tungestahili neema. Badala yake, tunayatenda matendo mema kwa ajili ya Mungu na kwa sifa zake. 28. Daima, imani peke yake ndiyo inashika neema na msamaha wa dhambi. 29. Wakati Roho Mtakatifu anatolewa kwa imani, moyo unahimizwa kuyatenda matendo mema. 31. Awali, bila Roho Mtakatifu, 32. moyo ulikuwa dhaifu chini ya mamlaka ya Ibilisi ambaye huiendesha asili maskini na ya ubinadamu, hufanya dhambi nyingi 33. jinsi tunavyoona katika wanafalsafa wengi waliojisingizia maisha maaminifu na maadilifu. Lakini walishindwa kufanya hivyo na wakaanguka kadamnasi katika dhambi mbaya. 34. Mambo haya yanajiri katika maisha ya mtu asiyekuwa na imani, Roho Mtakatifu, na anayetawaliwa na nguvu za kibinadamu tu.
35. Kwa hiyo basi, mafundisho haya kuhusu imani yasilaumiwe kwamba, yanakataa matendo mema. Badala yake, yasifiwe sana kwa kuwa yanafundisha kutenda matendo mema na kutusaidia kufahamu jinsi tungeweza kuyashika haya matendo. 36. Kwa kuwa, asili na nguvu ya binadamu vi nje ya imani na Kristo, vi dhaifu zaidi hata kuweza kutenda matendo mema, 37. kumwomba Mungu, kuvumilia katika dhiki, kuwapenda majirani zetu, kuhudumia kwa bidii katika huduma zilizoamriwa, kutii, kuepuka tamaa mbaya na kadhalika. 38. Matendo hayo makuu na ya kweli ya jinsi hiyo hayawezi kutendeka bila msaada wa Kristo 39. jinsi anavyosema mwenyewe katika Yn. 15:5: “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”
XXI. Ibada ya Watakatifu L
1. Makanisa miongoni mwetu hufundisha kwamba, inafaa kuwa na kumbukumbu ya watakatifu na isisitizwe ili tuige imani zao na matendo yao mema kulingana na wito wetu. Hivyo, kaisari anaweza kuiga mfano wa Daudi katika vita kwa kuwafukuza Waturuki kutoka katika nchi yetu, kwani Kaisari ni mfalme kama alivyokuwa Daudi. 2. Lakini, Biblia haitufundishi kuwaomba watakatifu au kutafuta msaada wao bali inatuelekeza tuutafute kwa Kristo peke yake aliye Msuluhishi, Mpatanishi, Kuhani Mkuu na Mwombezi. 3. Ni lazima yeye aombwe na ametuahidi kuyasikia maombi yetu. Kristo anaikubali ibada ya namna hiyo, yaani, kwamba, aombwe katika mateso yote. 4. “Kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba . . .” (1 Yoh. 2:1).
XXI. Ibada ya Watu Watakatifu G
1. Kadhalika, inafundishwa miongoni mwetu kwamba, watakatifu wanafaa kukumbukwa ili imani yetu iimarike wakati tunaiona neema waliyopokea na jinsi walivyoimarishwa na imani. 2. Licha ya hayo, matendo yao mema ni mifano bora kwetu katika wito wa kila mmoja wetu. Enzi yake Kaisari unapaswa kuufuata mfano wa Daudi kwa njia ya heri na ya kimungu anapowapiga vita Waturuki, maanaa hawa wawili ni wenye huduma ya kifalme inayohitaji himaya na ulinzi wa raia wao. Hata hivyo, haiwezi kuonyeshwa katika Maandiko Matakatifu kwamba, watakatifu wanaombwa au msaada unatafutwa kutoka kwao. “Mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu” (1 Tim. 2:5). Yeye ndiye Mwokozi pekee, Kuhani Mkuu pekee, Kiti cha Neema na Mwombezi mtetezi mbele za Mungu (Rum. 8:34). Yeye peke yake aliahidi kuyasikiliza maombi yetu. 3. Kulingana na Maandiko Matakatifu, ibada kuu mno ni kumtafuta Yesu Kristo kwa moyo wote katika matatizo na haja zote. 4. “Kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki” (1 Yoh. 2:1). * * *
Muhutasari wa sehemu ya kwanza L
1. Hii ni kuhusu muhtasari wa mafundisho yetu. Kama inavyoonekana katika haya kwamba, hatuna jambo lolote linalopingana na Biblia au na Kanisa Katoliki au Kanisa la Roma, kulingana na Kanisa la Zamani jinsi linavyojulikana kwetu kutokana na waandishi wake. Kwa hiyo, hao wanahukumu vikali mno wanapodai kwamba, walimu wetu wahesabiwe kuwa wazushi. 2. Mfarakano huu wote unahusu matumizi machache mabaya ambayo yameingizwa katika makanisa bila mamlaka maalumu. Ingawa kungekuwa na tofauti katika haya, maaskofu wangefaa kuwa na upole hata kutustahimili kulingana na ukiri wetu ambao tumeuweka, kwani hata kanuni si kali kiasi cha kudai kwamba, 3. ibada zifanane kila mahali ilihali ibada za makanisa hazijakuwa sawa wakati wowote. 4. Kwa kiasi kikubwa, tunafuata ibada za zamani kwa ukamilifu. Hivyo, ni uwongo na visingizio kabisa kushtaki kwamba, desturi na taratibu zote za zamani zimeondolewa kutoka makanisa yetu. 5. Lakini malalamiko ya kawaida yamekuwepo kwamba, matumizi mabaya mengine yanahusiana na ibada za kawaida. Sehemu za haya zimerekebishwa kwa sababu hazingekubaliwa kwa dhamiri safi.
Muhutasari wa sehemu ya kwanza G
1. Huu ni muhtasari tu wa mafundisho yanayohubiriwa na kufundishwa katika makanisa yetu kama mafundisho halisi ya Kikristo, faraja ya dhamiri na uboreshaji wa wanaoamini. Kwa kweli, hatutaki kuziathiri vibaya nafsi na dhamiri zetu mbele za Mungu kwa njia ya kulitumia vibaya jina au Neno lake. Hatutaki pia kuwarithisha watoto wetu na vizazi vijavyo mafundisho mengine yoyote isipokuwa haya yanayokubaliana na Neno safi la Mungu na ukweli wa Kikristo. Kwa kuwa mafundisho haya yana msingi wa wazi katika Maandiko Matakatifu na hayapingi au hayaendi kinyume na Kanisa la Katoliki la Kikristo au hata Kanisa la Roma, jinsi yanavyojulikana kwetu kutoka kwa akina baba wake. Tunashawishika kwamba, wapinzani wetu hawana budi kukubaliana nasi kuhusu mafungu yaliyoelezewa hapo juu. Kwa hiyo, wanaofikiria kukataa, kuepuka na kujitenga na makanisa yetu kana kwamba, mafundisho yetu yanakuwa mafundisho ya uzushi, yanafanywa kwa njia ya tahariki na isiyokuwa na mema kupambana na umoja na upendo wote wa Kikristo. Wao hufanya hivyo bila msingi imara wowote wa agizo la Mungu au Maandiko Matakatifu. 2. Kwa kiasi kikubwa, majadiliano na mabishano yanahusu mapokeo na matumizi mabaya mbalimbali. Kuhusiana na mafungu makuu, hakuna neno lisilokuwa na msingi au ambalo lingepungukiwa vibaya, na kwa kuwa ukiri wetu unaonekana kuwa wa kimungu na wa Kikristo, inawabidi maaskofu kufanya kazi zao kulingana na haki zote na wawe wenye upole zaidi. Hata hivyo, hatungepatikana katika mapokeo fulani. Hivyo, tunatumaini kutoa misingi na sababu imara za kuyabadilisha mapokeo na matumizi fulani mabaya.
MAFUNGU YENYE MAELEZO KUHUSU MATUMIZI MABAYA
YALIYOREKEBISHWA
(L)
1. Makanisa miongoni mwetu hayapitii pembeni mwa Kanisa Katoliki katika fungu lolote la imani. Badala yake, yameondoa matumizi mengine mabaya ambayo ni mapya na yanapambana na nia ya kanuni kwa sababu ya makosa ya nyakati. Ni ombi letu Enzi yako Kaisari, usikilize kwa upole, yote yaliyobadilishwa na sababu za kutoulazimisha umati kuyafuata matumizi haya mabaya dhidi ya dhamiri zao. 2. Enzi yako Kaisari usiwaamini wanaohimiza chuki ya watu dhidi yetu na kuvieneza visingizio vya ajabu katika umma. 3. Baada ya kuichochea mioyo ya watu wema, kwanza, walitayarisha nafasi ya ugomvi huu na kwa njia
iyo hiyo wanajaribu kuongezea fitina. 4. Enzi yako Kaisari, utagundua bila shaka kwamba, muundo wa mafundisho na desturi tulizo nazo zinakubalika kuliko maneno ya watu wasiomcha Mungu na wakorofi. 5. Ukweli hauwezi kupatikana katika uvumi ndani ya umma au katika mashtaka ya wapinzani wetu. Hata hivyo, Ni rahisi kuelewa kwamba, hakuna lolote linaloweza kuendeleza heshima ya desturi kuhusu kutunzwa na kuistawisha hofu takatifu na uchaji katika umma kama matumizi ya desturi za ibada yanayofuata utaratibu katika makanisa.
MAFUNGU YA KUJADILIWA YANAYOELEZEA MATUMIZI
MABAYA YALIYOREKEBISHWA (G)
Mafungu ya imani hayafundishwi kila pahali katika makanisa yetu kinyume na Maandiko Matakatifu au kinyume na mafundisho ya Kanisa. Badala yake, matumizi mabaya fulani tu yalibadilishwa. Sehemu moja ya matumizi haya mabaya iliingizwa kanisani miaka kadhaa ya kale. Sehemu nyingine iliingizwa kwa nguvu na ujeuri. Tunawajibika kwa sababu ya haja yetu kubwa kuyaelezea matumizi haya mabaya na kuzionyesha sababu za kuyaruhusu mabadiliko haya ili Ufalme wake mkuu Kaisari upate kuelewa kwamba, hatukuendelea hapa kwa njia isiyokuwa ya Kikristo au kwa upuuzi bali tulilazimishwa kuyaruhusu mabadiliko ya namna hiyo na Agizo la Mungu ambalo ndilo linatazamiwa kuwa juu ya kila uzoefu.
XXII. Aina zote Mbili L
1. Wakristo wa kawaida hupewa aina zote mbili za sakramenti ya Chakula cha Bwana kwa kuwa desturi hii ina agizo la Bwana katika Mt. 26:27: “Nyweni nyote katika hiki.” 2. Kristo aliagiza wazi kwamba, wote wanywe katika kikombe.
3. Mtu yeyote asiweze kusisitiza tofauti ndogo kwamba, jambo hilo lilihusu wachungaji peke yao. Katika 1 Kor.11:20, Mt. Paulo anatoa mfano unaoonyesha kwamba, ushirika wote ulitumia aina hizi zote mbili. 4. Desturi hii iliendelea katika Kanisa kwa muda mrefu. Haijulikani ni lini au ni nani aliyeigeuza ingawa Kadinali Cusano217 anasema ni lini mabadiliko yalithibitishwa. 5. Sipriano218
217 Nicolaus Cusanus (1401-1464), kutoka Ujerumani alikuwa mtaalamu maarufu wa aina ya falsafa ya Platoni katika Kanisa la Magharibi, kisha akawa askofu katika cheo cha kadinali. Aliendeleza sana majaribio ya kuliunganisha Kanisa la Mashariki na sehemu nyingine pamoja na Kanisa la Magharibi chini ya ukuu wa Papa wa Roma. Kama mtaalamu wa historia, alikana asili ya hati nyingine za Kanisa la Roma kuhusu ukuu wa Papa. Kulingana na Kadinali Kusano, matumizi ya aina moja ya sakramenti ya Ekaristi yaliimarishwa katika Sinodi ya Laterano ya Nne, huko Roma mwaka wa 1215.
218 Sipriano (Cyprianus +258 ), Askofu wa Karthago huko Afrika Kaskazini, aliyefariki katika udhalimu uliofanywa kwa Wakristo chini ya Kaisari Valeriano.
anashuhudia penginepo kwamba, damu ilitolewa kwa washirika. 6. Kadhalika, inashuhudiwa na Hieronimo219 aliyesema: “Daraja la wachungaji linatunza Ekaristi na linatoa damu ya Kristo kwa watu.” 7. Hata Papa Gelasio220 aliagiza sakramenti isigawanywe” (Dist. 2. de consecratione, c. Comperimus). 8. Ni desturi ya pekee isiyokuwa ya zamani inayoshikilia tofauti. 9. Lakini inaonekana wazi kwamba, desturi iliyoanzishwa kinyume cha maagizo ya Mungu isikubaliwe kama inayoshuhudiwa na kanuni (Dist. 3. c. “Veritate” na sura zinazofuatia).
10.Lakini desturi hii imepokelewa, si dhidi ya Biblia tu lakini pia dhidi ya kanuni za zamani na mfano wa Kanisa. Kwa hiyo, 11. waliopendelea kutumia aina zote mbili za sakramenti hawangelazimishwa kufanya tofauti na kisha kuikosea dhamiri. 12 Kwa kuwa ugawaji wa sakramenti haukubaliani na agizo la Kristo, maandamano yaliyokuwepo pia yameachwa miongoni mwetu.221
XXII. Aina zote Mbili za Sakramenti G
1. Miongoni mwetu, Wakristo wa kawaida hutunukiwa sakramenti katika aina zote mbili. Sababu yake ni agizo na amri dhahiri ya Kristo katika Mt. 26:27: “Nyweni nyote katika hiki.” 2. Kristo anaamuru kwa maneno dhahiri kwamba, inawabidi wote kunywa katika kikombe.
3. Ili yeyote asisalie na kuyatafsiri maneno haya kumaanisha mapadre tu, Mt. Paulo anaonyesha katika 1 Kor. 11:20 kwamba, ushirika mzima wa Kanisa la Korintho ulitumia aina zote mbili. 4. Desturi hii iliendelea katika kanisa kwa muda mrefu, kama inavyoweza kuonyeshwa kutoka kwenye historia na maandiko ya mababa. 5. Sipriano anaeleza kwamba katika wakati wake kikombe kilitolewa kwa watu wa kawaida. 6. Pia Mtakatifu Jerome anaeleza kuwa mapadre waliosimamia sakramenti waligawa damu ya Kristo kwa watu. 7. Papa Gelasio alitoa agizo kwamba Sakramenti si yakutenganisha. 8. Hakuna kanuni hata moja iliyopo inayoelekeza mapokezi ya aina moja tu. Hakuna anayefahamu ni lini au kupitia kwa nani desturi hii ya kupokea aina moja tu ilianzishwa, ingawa Kadinali Cusano anataja wakati ambao matumizi haya yalipitishwa. 10. Ni dhahiri kwamba desturi hiyo, iliyotolewa kinyume na amri ya Mungu na pia
219 Hieronimo (+420) alikuwa mtaalamu maarufu na Baba wa Kanisa la Magharibi. Alitafsiri Biblia katika Kilatini. Tafsiri hii ya ‘Versio Vulgata’ (Toleo la Watu Wote) inaendelea kuwa Biblia rasmi ya Kanisa Katoliki.
220 Papa wa Roma katika mwaka wa 492-496.
221 Maandamano ya mwili wa Kristo (Corpus Christi) yaliainishwa Alhamisi iliyofuatia Jumapili ya Utatu. Sherehe hii ilianzishwa katika Kanisa la Magharibi kwa ajili ya agizo la Papa Urbano IV mwaka wa 1264. Papa Urbano IV aliufuata ushawishi wa madai ya maono ya mmonaki Juliana huko Ubelgiji, mwaka wa 1230. Wawakilishi Walutheri katika Baraza la Augsburg walikataa kushiriki katika maandamano haya wakati huo. Sherehe haikufanywa na wakuu wa Matengenezo ya Kanisa kabisa kwa sababu ya mafundisho mabaya kuhusu aina moja ya sakramenti ya Chakula cha Bwana.
kinyume na kanuni za kale, sio ya haki. 11. Kwa sababu hiyo haifai kuzibebesha mizigo dhamiri za wale wanaopenda kuishiriki sakramenti kulingana na utaratibu wa Kristo au kuwalazimisha kutenda kinyume na mpango wa Kriso Bwana wetu. 12. Kwakuwa kuitenganisha sakramenti ni kinyume na utaratibu wa Kristo, pia tumeachana na desturi ya kubeba Sakramenti kwenye maandamano.
XXIII. Ndoa kwa Wachungaji L
1. Kumekuwa na malalamiko mara kwa mara kuhusu wachungaji wasioweza kuzizuia tamaa zao za kimwili. 2. Kuhusu jambo hilo, imesemekana kwamba, Papa Pio222 alisema kwamba, kulikuwepo na sababu zingine ambazo ziliwafanya wachungaji wasioe. Hata hivyo, sasa kuna sababu nzito zaidi kuliko hizo ambazo zinalifanya jambo hili lirudishwe. Naam, Platina223 aliandika kuhusu jambo hili. 3. Ili kuiepuka kashfa hiyo, wachungaji walio miongoni mwetu walijichukulia wake zao na wakafundisha kwamba, ni halali kwao kuoa. 4. Kwanza, haya yalifanywa kwa sababu Mt. Paulo anasema: “Kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe” (1 Kor. 7:2), pia anasema: “Maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa” (1 Kor. 7:9). 5. Pili, Kristo anasema: “Si wote wawezao kulipokea neno hili” (Mt. 19:11). Kwalo, aliagiza kwamba, si wanadamu wote wanaoweza kukaa katika hali ya useja kwa sababu Mungu alimwumba mwanadamu apate kuzaa (Mwa. 1:28). 6. Asili ya mwanadamu haina mamlaka kuubadilisha uumbaji wake bila karama na kazi maalumu ya Mungu. 8. Hii ndiyo sababu wasioweza kukaa bila kuoa wanaweza kuoa. Maana hakuna asili ya ubinadamu iliyo na mamlaka ya kubadilisha amri na maagizo ya Mungu. 9. Kwa hiyo, wachungaji wetu hufundisha kwamba, ni halali kwao kuoa.
10. Ni dhahiri kwamba, katika Kanisa la zamani, wachungaji walioa. 11. Mt. Paulo anasema kwamba, mwanamume ambaye ameoa achaguliwe kuwa askofu (1 Tim. 3:2). 12. Awali, karne nne zilizopita, wachungaji walilazimika kukaa katika hali ya useja huko Ujerumani. Kusema kweli walitoa upinzani wa namna hiyo hata askofu mkuu wa Mainz alikuwa karibu kuuawa katika maasi ya wachungaji waliokuwa wameghadhibika wakati alikuwa karibu kutangaza amri ya Kuhani Mkuu wa Roma kuhusu jambo hilo.224 13. Hatima ya jambo hili ilikuwa katili sana. Haikutoshea kukatazwa tu kuoa wakati ujao, bali ndoa zilizokuwepo pia zilivunjwa ingawa tendo hilo lilipingana na sheria zote za kimungu na za
222 Papa Pio II (1458-1464).
223 Mtaalamu kutoka Italia, Bartolomeo Platina, katika kitabu chake kiitwacho, “Historia ya akina Papa” mwaka wa 1479.
224 Siegfried, Askofu Mkuu wa Mainz, katika sinodi za Mainz na Erfurt za mwaka wa 1075.
binadamu. Isitoshe, lilipingana na kanuni zote zilizotungwa na akina papa, na zilizotungwa na sinodi maarufu mno.225
14. Kadiri ulimwengu unavyozidi kuzeeka, ndivyo asili ya ubinadamu nayo inavyozidi kuwa na udhaifu. Hivyo, inafaa kuchukua tahadhari dhidi ya uanzishwaji wa uovu zaidi nchini Ujerumani.
15. Licha ya hayo, Mungu aliianzisha ndoa ili iwe tiba dhidi ya unyonge wa binadamu. 16. Kanuni zenyewe zinasema kwamba, kila wakati lazima ukali wa zamani utulizwe kwa ajili ya unyonge wa watu. Inatumainiwa kwamba, hili linalohusu ndoa za wachungaji litekelezwe katika shauri hili. 17. Pia inaonekana kwamba, makanisa yatakosa wachungaji hivi karibuni iwapo ndoa zitaendelea kukatazwa.
18. Ingawa agizo la Mungu linaendelea kuwepo, nayo desturi ya Kanisa inajulikana vizuri na zaidi, huu useja mchafu unaendelea kuzaa kashfa, uzinzi, na maasi mengine yastahiliyo adhabu kulingana na sheria. Ndoa za wachungaji zinapingwa vikali zaidi kuliko jambo lingine lolote. 19. Mungu aliagiza kwamba, ndoa ifanyike kwa heshima. 20. Sheria za jamii zote zilizopangwa na kukaa vizuri, hata miongoni mwa watu wa mataifa, zinaiheshimu ndoa kwa sifa kuu. 21. Hata hivyo, watu huteswa kikatili kwa hukumu ya kifo, hata wachungaji, kinyume cha kusudi la kanuni, bila sababu nyingine yoyote isipokuwa ndoa.
22. Mt. Paulo nakataza ndoa kuitwa fundisho la mashetani katika (1 Tim. 4,3). 23. Hili linaweza kueleweka vizuri kwa kuwa katazo la ndoa linahifadhiwa kwa adhabu za namna hizo.
24. Jinsi sheria ya binadamu isivyoweza kubatilisha agizo la Mungu, vivyo hivyo, kiapo nacho hakibadilishi agizo la Mungu.
25. Kwa hiyo, Sipriano anahimiza kwamba, wanawake wasioiweka ahadi ya ubikira jinsi walivyoahidi waolewe. Haya ni maneno yake katika kitabu chake cha kwanza cha nyaraka (Ep. XI): “Wale wasiotaka au wasioweza kuvumilia, afadhali waolewe kuliko kuanguka katika moto kwa ajili ya tamaa zao; kwa vyovyote vile wasiwakwaze ndugu na dada zao.”
26. Kanuni pia zinauonyesha uadilifu wa kiasi fulani kwa waliotoa nadhiri kabla ya umri maalumu na jinsi ilivyokuwa kawaida nyakati za awali.
225 Mathalani Sinodi ya Nikea.
XXIII. Ndoa za Wachungaji226 G
1. Kumekuwa na malalamiko makubwa ulimwenguni kote kati ya watu wote wenye vyeo vikuu au vya chini kuhusu uzinzi mkuu na maisha ya uhuni usiokuwa na haya wa mapadre wasioweza kuzuia tamaa za kimwili na walioendelea hata kujiingiza katika uovu wa kuchukiza mno. 3. Ili kuzizuia dhambi zisizofaa, uzinzi, na uasherati wa aina zote, wachungaji wengine wameingia katika ndoa. 4. Wametoa sababu zao za kuoa kwamba, walisukumwa na kulazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na mateso makubwa ya dhamiri zao. Hasa, kwa kuwa, Maandiko Matakatifu yanasema wazi kwamba, asasi ya ndoa ilianzishwa na Bwana Mungu kwa shabaha ya kuuzuia uzinzi. Katika 1 Kor. 7:2 Mt. Paulo anasema: “Kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe.” Vile vile anasema katika 1 Kor. 7:9: “Maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.” 5. Licha ya hayo, katika Mt. 19:11, Kristo anaposema: “Si wote wawezao kulipokea neno hili,” anadokezea kwamba, ni watu wachache ambao wana kipawa cha kuishi katika hali ya useja na hakika, alikuwa anajua asili ya ubinadamu. Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke kulingana na Mwanzo 1:27. 6. Kwa vyovyote vile, uzoefu umedhihirisha zaidi kwamba, maendelezo au mabadiliko ya uumbaji wa Mungu aliye Enzi Kuu mno, hayapatikani kwa njia ya azimio au uamuzi wa binadamu katika nguvu na uweza wa binadamu bila kipawa au neema maalumu ya Mungu. Je, ni matokeo gani mazuri? Je, maisha safi na yenye kuaminika au njia jalili na sahihi ya watu wengi ni ipi? Inajulikana wazi kwamba, watu wengi wamehisi dukuduku na dhiki ya kuogofya sana ya dhamiri katika kitanda cha mauti na wengi pia wameungama hivyo. 8. Kwa kuwa, Neno la Mungu na agizo lake haviwezi kubadilishwa kwa nadhiri au kwa sheria za binadamu, wachungaji na 9. makasisi wetu wengineo wamejichukulia wake kwa sababu hii na sababu zinginezo.
10. Vitabu vya historia na maandiko ya mababa yanaonyesha kwamba, makanisa ya zamani yalifuata matumizi kwamba, makasisi na mashemasi walikuwa na wake zao. 11. Kwa hiyo, Mt. Paulo anasema katika 1 Tim. 3:2: “Askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja.” 12. Ilikuwa karne nne tu zilizopita wakati makasisi katika maeneo ya Ujerumani walilazimishwa kuziweka nadhiri za useja kwa nguvu. Uamuzi huu ulitendeka kwa njia kali na ngumu sana. Kwa hiyo, Askofu Mkuu mmoja huko Mainz aliyekuwa ametangaza
226 Istilahi za waliobarikiwa kwa huduma ya mitume wa kanisa lililohitilafiana. Ukiri wa Augsburg unatumia “sacerdos” na “Priester” (kuhani) au ‘Geistlichen’ (wa hali ya kiroho). Baadaye jina la huduma hii lilikuwa miongoni mwa Walutheri ‘Pfarrer’ au ‘Pastor’ (Mchungaji). Kwa sababu ya kihistoria, istilahi katika fungu hili zinafuata mitindo ya Kikatoliki na Kianglikana: “Padre” na “Kasisi.” Hata hivyo, ili tusichafue mawazo ya msomaji wa kitabu hiki, tutatumia jina, “Mchungaji” katika kichwa cha fungu hili.
tangazo jipya la Papa alikuwa karibu kuuawa wakati wa maasi ya jumuiya yote ya mapadre.227 Katazo hilo lilitendeka hima na bila busara yoyote. Hata Papa wa wakati huo hakukanusha tu ndoa za mapadre za wakati ujao bali alizivunja ndoa zilizodumu kwa muda mrefu. Hatua hii haikupinga tu haki ya kimungu ya asili na ya dunia bali pia ilizipinga kabisa kanuni zenyewe za upapa na sinodi mashuhuri sana.228
13. Watu wengi wa vyeo vikuu, wacha Mungu na wenye busara, wametoa maoni yayo hayo na mashaka yao kwamba, useja wa namna hiyo uliolazimishwa na katazo la ndoa iliyoanzishwa na Mungu mwenyewe na aliyempa binadamu uhuru, haukuzaa mema yoyote bali ulitoa nafasi ya uovu mkubwa na kashfa nyingi. Jinsi wasifu wake unavyodokezea, hata mojawapo ya akina papa wa Roma, Pio wa II, alikuwa akisema mara kwa mara na hasa aliruhusu kuandikwa kwamba, ikiwa kuna sababu za kukataza ndoa ya makasisi, sasa kuna sababu muhimu, bora na nzito za kuiruhusu ndoa tena. Hakuna tashwishi kwamba, Pio wa II kama mtu hodari na mwenye hekima, alitoa kauli hii kwa sababu ya mashaka mazito.229
14. Kwa hiyo basi, tunataka, kama raia wa mfalme mkuu Kaisari, kukutegemea wewe ambaye ni Kaisari Mkristo na wa kusifika sana kwamba, uzingatie kwa fadhila kwamba, nyakati hizo, mwisho wa dunia utakuwa mbaya na wanadamu watazidi kuwa dhaifu na hafifu jinsi Maandiko Matakatifu yanavyotabiri.
15. Kwa hiyo, kulingana na Ukristo, ni muhimu na ni manufaa kulitambua kabisa jambo hili la kuikanusha ndoa ili lisisababishe maovu na uasherati mwingi wa aibu kuenea katika mikoa ya Ujerumani. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuyabadilisha au kuyapanga mambo haya kwa njia bora au yenye hekima kuliko Mungu mwenyewe, aliyeanzisha ndoa kuusaidia udhaifu wa binadamu na kuuzuia uasherati.
16. Kanuni za zamani230 zinasema pia kwamba, wakati mwingine ni muhimu sana kuutuliza ukali na ugumu kwa ajili ya unyonge wa binadamu ili kuzuia na kuepuka kashfa kubwa zaidi.
Hakika, katika kesi hii, urahisishaji uwe wa lazima na wa Kikristo. Ni vipi hali
227 Askofu Mkuu Siegfried wa Mainz katika sinodi za Erfurt na Mainz za mwaka wa 1075.
228 Decr. Grat. I dist. 82, c. 2-5; dist. 84, 4. Sinodi ya Nikea ilikataa useja wa makasisi; Historia ya Kanisa ya Evagrio 1, 11.
229 Mtaalamu Bartolomeo Platina huko Italia, katika historia yake ya akina papa mwaka wa 1479. Pio II 14581464.
230 Gratiano, Decr. 1, dist. 34, c. 7; 2, c. 1, q.7, c. 5.
ya ndoa ya makasisi na mapadre, hasa wachungaji na wengineo wanaohudumia Kanisa, inaweza kuwa ya hasara kwa makanisa ya Kikristo? 17. Iwapo ukali huu wa kuizuia ndoa utaendelea, kuna uwezekano wa kuwepo na uhaba wa makasisi na wachungaji wakati ujao.
18. Nafasi hii kwamba, mapadre na makasisi wanapaswa kuoa ina msingi wake katika Neno la Mungu na agizo lake. Vitabu vya historia vinaonyesha kwamba, mapadre walikuwa wakioa na kwamba, nadhiri ya useja imesababisha kashfa nyingi zisizokuwa za Kikristo, imesababisha uzinzi, uhuni wa kuogofya sana na usiosikika, na uovu wa kuchukiza mno. Hata baadhi ya mapadre wa makanisa makuu na Kitala cha Roma wameyakubali haya mara kwa mara na kuteta kwamba, maovu kama haya mabaya sana ya kupita kiasi yapatikanayo miongoni mwa makasisi wa Kanisa yanaweza kuiamsha ghadhabu ya Mungu. Kwa hiyo, ni hali ya kusikitisha sana kwamba, ndoa ya Kikristo haijakatazwa tu bali imeadhibiwa kwa haraka kana kwamba, ni udhalimu mkubwa, 19. ingawa katika Maandiko Matakatifu, Mungu aliamuru ndoa ifanyike kwa heshima. 20. Hali ya ndoa inasifiwa katika haki ya dola na falme zote zenye sheria na haki. 21. Ni nyakati zetu tu ambapo watu wasiokuwa na hatia huadhibiwa hasa makasisi bila sababu yoyote isipokuwa kwa kuoa tu na hasa makasisi ambao inawapasa wahurumiwe kuliko wengine wote. Hatua hizi zinachukuliwa siyo tu kama kinyume cha sheria ya kimungu bali pia kama kinyume cha kanuni za Kanisa. 22. Katika 1 Tim. 4:1,3, Mtume Paulo anayaita mafundisho ya kuikataza ndoa kuwa mafundisho ya mashetani. Katika Yn. 8:44, 23. Kristo mwenyewe anasema kwamba, Ibilisi ni mwuaji tangu mwanzo. Taarifa hizi mbili zinalingana vyema kabisa kwa kuwa lazima kukataza ndoa kuwe mafundisho ya Ibilisi na ujasiri wa kudumisha mafundisho kama hayo wakitumia umwagaji damu.
24. Jinsi sheria ya binadamu isivyoweza kubadilisha au kukomesha Sheria ya Mungu, vivyo hivyo, nadhiri hazibadilishi agizo la Mungu. Kwa hiyo, 25. Mtakatifu Sipriano anahimiza kwamba, wanawake ambao hawakuweza kuziweka nadhiri zao za ubikira kama walivyoahidi, waolewe. Katika barua yake ya kumi na moja aliandika ifuatavyo: “Wale wasiotaka au wasioweza kuvumilia, afadhali waolewe kuliko kuanguka katika moto kwa ajili ya tamaa zao; kwa vyovyote vile wasiwakwaze ndugu na dada zao.”
26. Pamoja na hayo, kanuni zote zinaonyesha upole na haki kwa waliotoa nadhiri zao katika ujana wao na wengi wa makasisi na watawa waliokabidhiwa vyeo vyao wakiwa vijana wasiokuwa na ujuzi.
XXIV. Misa L231
1. Makanisa yetu yanashtakiwa kwa uongo kwamba, yameondoa misa.232 Kusema kweli, misa imehifadhiwa miongoni mwetu na inaadhimishwa kwa heshima kuu. 2. Karibu desturi zote zimehifadhiwa na zinafuatwa isipokuwa nyimbo zingine za Kijerumani na za Kilatini zimeongezewa hapa na pale ili kuufundisha umma. 3. Desturi za ibada zinahitajika hasa kwa kusudi hili moja la kuwafundisha wasiokuwa na elimu. 4. Mtume Paulo aliagiza (1 Kor. 14:2, 9) lugha wanayoielewa watu itumike kanisani. 5. Watu wamezoea kupokea sakramenti wakiwa pamoja wanapostahili kufanya hivyo. 6. Jambo hili linaongezea heshima na sifa kwa desturi za hadharani za ibada kwao. Hakuna wanaokubaliwa kushiriki isipokuwa wawe wamehojiwa kwanza na wamechunguzwa.233 7. Watu pia huonywa kuhusu umuhimu na matumizi ya sakramenti, faraja inayotoa kwa dhamiri zenye hofu ili zijifunze kumwamini Mungu na zipate kutarajia na kumwomba Mungu mema yote. 8. Ibada ya aina hii inampendeza Mungu. Matumizi kama hayo ya sakramenti yanaongeza uchaji mbele za Mungu. 9. Kwa hiyo, haionekani wazi kwamba, misa zinasherehekewa miongoni mwa wapinzani wetu kwa bidii kubwa kuliko miongoni mwetu.
10. Lakini imejulikana wazi kwamba, watu wote wema wamelalamika sana hadharani na kwa muda mrefu kuhusu jambo hili kwamba, misa zilikufuriwa vibaya hata kwa malengo ya kupata faida. 11. Si kusema kwamba, haijulikani hata kidogo jinsi matumizi haya mabaya yameenea katika makanisa yote. Si kusema kwamba, haijulikani Misa zinasherehekewa na watu wa aina gani ili walipwe mshahara au ujira tu, na ni wangapi huzisheherekea misa kinyume cha katazo la kanuni. 12. Lakini Mtume Paulo, katika 1 Kor. 11:27, anawatishia vikali wanaoishiriki ekaristi isivyostahili anaposema: “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.” Kwa hiyo, wachungaji wetu walipoonywa kuhusu kosa hilo, misa za faraghani234 hazikuendelea miongoni mwetu kwa kiwango hicho. Misa hizo hazikusherehekewa miongoni mwetu kwa sababu nyingine kama vile kupata faida.
14. Maaskofu hawakuwa wasioelewa juu ya dhulma hizi. Wangeyarekebisha
231 Kiyunani: ‘Ευχαριστια,’ jina la ibada yenye Chakula cha Bwana.
232 Mathalani Johann Eck (1486-1543) aliyekuwa Profesa wa Ingolstadt, adui mkuu wa Martin Luther.
233 Mwishoni mwa mwaka wa 1520, huko Wittenberg, Wakristo walilazimika kwenda kuungama kabla ya Chakula cha Bwana.
234 (Misa ya Faraghani), ‘Missa Votiva’ ilikuwa aina maalumu ya misa zilizosherehekewa kama kumbukumbu ya wafu ili kutuliza hali ya nafsi za waliokuwa Purgatorio ili kusafishwa dhambi zao ndogo. Misa za aina hii zilisherehekewa hata bila ushirika na zilileta faida kubwa kwa makanisa.
kwa muda unaofaa, ugomvi huu ungepungua. 15. Kwa sababu ya uzembe wao, uovu mwingine uliachwa ujipenyeze katika Kanisa. 16. Sasa, baada ya wakati kupita wanaanza kulalamika kuhusu shida za Kanisa kwa kuwa maovu yaliyokuwa yanatendeka yalikuwa dhahiri kabisa na hayakuweza kuvumiliwa tena. 17. Kumekuwa na mifarakano mikubwa kuhusu misa na sakramenti. 18.Labda kukufuru kwa misa kwa muda mrefu kama huu kunasababisha adhabu kwa ulimwengu, kwa kuwa kulistahimiliwa katika makanisa kwa karne kadhaa na waliokuwa na mamlaka na jukumu la kukuondoa. 19. Imeandikwa katika Amri Kumi za Mungu: “Maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure” (Kut. 20:7). 20 Basi, inaonekana kwamba, tangu mwanzo wa ulimwengu, hakuna agizo la Mungu lililotumiwa vibaya kwa ajili ya faida kama misa.
21. Licha ya hayo, wazo lililoongezea misa za faragha bila mwisho liliongezeka. Yaani, kwamba, Kristo ameipatanisha dhambi ya asili kwa mateso yake, na aliianzisha misa ili kuitoa dhabihu kwa makosa ya kila siku. Yaani, makosa ya mauti sawasawa na ya kusameheka.
22. Mawazo yameenea hadharani kwamba, misa kama tendo lenyewe235 inayafuta makosa ya walio hai na wafu na inajitosheleza katika jambo hili. 23. Kuhusu haya, watu walianza kuhojiana kama misa moja iliyotajwa kwa watu wengi inastahili sawa na misa maalumu kwa watu binafsi. Mabishano haya yalizaa idadi kubwa ya misa zisizokuwa na mwisho.
24. Kuhusu mashauri haya, wenzetu wameonya kwamba, mawazo hayo ni kinyume cha Biblia kabisa na yanaupunguza utukufu wa mateso ya Kristo. 25. Naam, mateso ya Kristo yalikuwa toleo na suluhu, si kwa ajili ya hatia ya dhambi ya asili peke yake, lakini pia kwa sababu ya dhambi zote zilizobaki 26. jinsi Mtume Paulo alivyoandika katika Waraka kwa Waebrania 10:10: “. . . tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.” 27. Pia katika Ebr. 10:14 imeandikwa: “Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.”
28. Kadhalika, Biblia inafundisha kwamba, tunahesabiwa haki mbele za Mungu kwa imani katika Kristo. 29. Sasa basi, misa ikiondoa dhambi ya walio hai na wafu, kwa tendo la nje, haki itatokana na matendo ya misa na si kwa imani wakati Maandiko Matakatifu hayaruhusu hivyo.
30. Basi, Kristo anatuagiza tufanye hivyo kwa ukumbusho wake (Lk. 22:19), kwa kuwa misa ilianzishwa ili imani ya wanaoishiriki sakramenti ikumbuke 235 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
fadhila inayopokea kutoka kwa Kristo ili kuihimiza na kuifariji dhamiri yenye hofu. 31. Kumkumbuka Kristo ni kuzikumbuka fadhila zake na zaidi kuelewa kwamba, zinatolewa kwetu kwa kweli. 32. Haitoshi kuikumbuka historia peke yake kwa kuwa Wayahudi na wasiomcha Mungu pia wanaweza kuikumbuka. 33. Basi, misa itumiwe ili kuitoa sakramenti kwa wanaohitaji faraja. Naye Ambrosio anasema: “Kwa sababu ninaendelea kukosa kila wakati, sina budi kuipokea dawa.”
34. Kwa kuwa misa ni ushirika wa namna hiyo wa sakramenti, misa moja ya kawaida inafanyika kwetu kila sikukuu, na katika siku nyingine pia, wengine wakitaka, itatolewa kwao wanaoiomba. 35. Desturi hii si mpya katika Kanisa. Kwa sababu wa zamani kabla ya wakati wa Gregorio236 hawataji misa za faraghani, bali huzungumzia zaidi kuhusu misa za kawaida. 36. Krisostomo anasema kwamba, mchungaji husimama kila siku katika madhabahu kuwaalika watu kadhaa katika ushirika na kuwakataa wengine. 37. Kutokana na kanuni za zamani inajulikana kwamba, mtu mmoja alisherehekea misa na wazee237 na mashemasi wengine wote walipokea mwili wa Bwana kutoka kwake. 38. Vivyo hivyo, maneno ya kanuni ya Nikea yanasema: “Baada ya wazee, mashemasi wapokee kwa utaratibu Ushirika Mtakatifu kutoka kwa askofu au kutoka kwa mzee.” Katika 1 Kor. 11:33, 39. kuhusu usharika Mtume Paulo anaagiza kwamba, wengine wangojeane ili washiriki pamoja.
40. Basi, kwa kuwa miongoni mwetu misa inakubaliwa na mfano wa Kanisa unavyoonekana kutoka kwenye Biblia na mababa, tuna imani kwamba, haiwezi kukataliwa, hasa kwa sababu desturi za imani za kawaida zimetunzwa kwa kiasi kikubwa hadi sasa. Jumla ya misa zinazofanyika ni tofauti. Hivyo, ingekuwa bora kupunguza idadi kwa sababu ya matumizi makubwa na mengi mabaya. 41. Naam, zamani hata katika makanisa yaliyohudhuriwa zaidi, misa haikusherehekewa kila siku jinsi inavyoshuhudiwa katika Historia Tripartita238 (Kitabu cha 9, sura ya 33): “Tena katika Aleksandria, Maandiko yanasomwa kila Jumatano na Ijumaa, halafu walimu huyafafanua na yote yanasherehekewa bila kumbukumbu ya kuadhimisha ya dhabihu.”
236 Papa Gregorio I (590-604).
237 ‘Πρεσβυτερος’ yaani, “mchungaji.”
238 (Historia ya Sehemu Tatu), (Kilatini: ‘Historia tripartita’) iliandikwa na mmonaki Kassiodoro (480-570) huko Roma.
XXIV. Misa G
1. Makanisa miongoni mwetu yanashtakiwa bila sababu kwamba, yameondoa misa.239 Bila majivuno yoyote, ni dhahiri kwamba, misa imehifadhiwa miongoni mwetu kwa uchaji na uzito kuliko wapinzani wetu. Zaidi ya hayo, umma unafundishwa mara nyingi kwa bidii kuu kuhusu Sakramenti Takatifu, shabaha ya uanzishwaji wake na njia za kuitumia. Yaani, kama faraja ya dhamiri zinazoogopa kiasi kwamba, watu wavutwe kwa ushirika wa misa. Pia watu wanapewa mawaidha kuhusu mafundisho yasiyokuwa ya kweli kuhusu sakramenti. Kuhusu kaida za misa za hadhara, hatuna mabadiliko adhimu isipokuwa mahali fulani nyimbo zinaimbwa kwa Kijerumani ili umma upate kujifunza na kuzoea kuimba kando ya nyimbo za Kilatini kwa kuwa, maana kuu ya kaida zote ni umma kujua mambo ambayo yanaibidi kujifunza kuhusu Kristo.
10. Awali, kabla ya wakati wetu, misa ilitumiwa vibaya kwa njia nyingi jinsi inavyojuliakana wazi. Misa ilibadilishwa kuwa bidhaa ya soko kuu, bidhaa iliyonunuliwa na kuuzwa karibu katika makanisa yote kwa ajili ya fedha. Matumizi haya mabaya yalilaumiwa mara nyingi na watu wenye elimu na wacha Mungu kabla ya nyakati zetu.240 12. Wakati wahubiri wetu walikuwa wamehubiri kuhusu mambo haya na wachungaji walikuwa wamekumbushwa kuhusu jukumu la kuogofya sana ambalo kweli, linapasa kumhusu kila Mkristo – yaani, yeyote anayetumia sakramenti isivyostahili atakuwa na hatia ya mwili na damu ya Kristo - 13 misa zile za kukodiwa na za mahali pa siri241 zilizoshurutishwa kusherehekewa mpaka sasa, kwa ajili ya malipo na ujira, zimekomeshwa kabisa.
21. Wakati huo huo, uzushi wa kuchukiza mno ulilaaniwa. Yaani, mafundisho kwamba, kwa kifo chake, Bwana wetu Yesu Kristo alikwisha kufanya suluhisho la dhambi ya asili peke yake na alianzisha misa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi zingine. 22. Hivyo, misa ilifanyika kuwa dhabihu kwa ajili ya walio hai na wafu ili kuondoa dhambi na kumpatanisha Mungu kwayo. 23. Kisha, mjadala ulifuatia zaidi kwamba, misa moja iliyofanywa kwa ajili ya wengi ingestahili sawa na misa maalumu iliyosherekewa kwa ajili ya mtu mmoja. Kutokana na hali hii, kukawa uzidishaji wa misa ambazo kwazo, katika utendaji wao, watu walitarajia kupata lolote walilolitaka kutoka kwa Mungu. Wakati huo huo, imani katika Kristo na ibada ya kweli ya Mungu vilisahaulika.
24. Kwa hiyo, mafundisho yaliyohitajika yalitolewa bila shaka hasa ili
239 Rejea Yohana Eck, Hoja 404, 269-278.
240 Nikolao Kusano, Yohana Tauler, Jean Gerson, Gabriel Biel.
241 Kijerumani: ‘Kaufmesse’ na ‘Winkelmesse.’ (Misa ya Mahali pa Siri) na (Misa ya Faragha).
watu wapate kuyajua matumizi halisi ya sakramenti. 26. Kwanza kabisa, watu walifundishwa kwamba, mahali pengi Maandiko Matakatifu yanaonyesha kwamba, hakuna dhabihu ya dhambi ya asili wala za dhambi zingine zozote isipokuwa kifo kimoja cha Kristo. 27. Kwa kuwa, imeandikwa katika Waraka wa Waebrania kwamba, Kristo mwenyewe alijitoa mara moja na toleo likafanya utakaso wa dhambi zote. 25. Ni fundisho jipya kabisa katika mafundisho ya Kanisa kudai kwamba, kifo cha Kristo kingefanya utakaso wa dhambi ya asili peke yake na si dhambi zingine. Vivyo hivyo, tutarajie kwamba, kila mtu aelewe kuwa, uzushi huu ulilaaniwa kwa haki.
28. Pili, Mt. Paulo anafundisha kwamba, tunapokea neema kutoka kwa Mungu kwa njia ya imani na si kwa njia ya matendo. 29. Kinyume chake kabisa ni kwamba, mafundisho haya ni matumizi ya misa na watu wanaodhania kwamba, neema inapokelewa kwa njia ya tendo hili la misa lenyewe. Inajulikana wazi kwamba, misa inatumiwa kwa shabaha ya kuziondoa dhambi na kuipata neema na fadhila mbalimbali kutoka kwa Mungu, si kwa padre mwenyewe tu bali kwa ulimwengu wote na watu wengine wote walio hai na wafu.
30. Tatu, Sakramenti Takatifu haikuanzishwa kwa madhumuni ya kutengeneza dhabihu kwa ajili ya dhambi kwa sababu dhabihu hii imekwisha kutolewa. Badala yake, shabaha yake ni kuiamsha imani yetu na kuzifariji dhamiri zetu wakati tunafahamu kwamba, neema na msamaha wa dhambi vimeahidiwa kwetu na Kristo. Vivyo hivyo, sakramenti inadai imani na pasipokuwa na imani inatumika bure.
34. Kwa kuwa, misa si dhabihu ya kuziondoa dhambi za wengine, wawe hai au wafu, bali lazima uwe ushirika ambapo mchungaji na wengine huipokea sakramenti wao wenyewe, inasherehekewa miongoni mwetu kwa njia ifuatayo: wakati wa sikukuu na siku zingine, wakati washiriki wapo, misa hutolewa na wanaoitamani hushirikishwa.242 35. Hivyo basi, misa inatumiwa miongoni mwetu kwa njia halisi kama jinsi ilivyosherehekewa nyakati za kale kanisani. Matumizi haya yanashuhudiwa na Mt. Paulo katika 1 Kor. 11:20 na maandiko mengi ya akina Baba wa Kanisa. 36. Krisostomo anasema kwamba, makasisi husimama kila siku ili kuwahimiza wengine kushiriki na kuwazuia wengine wasiende mbele243 kushiriki. 37. Kanuni za zamani pia zinaonyesha kwamba, mtu mmoja aliongoza na kuwashirikisha makasisi wengine na mashemasi. 38. Kwa
242 M. Luther, ‘Formula Missae et Communionis’ WA 12, kuanzia ukurasa wa 215; ‘Deutsche Messe,’ WA 19, kuanzia ukurasa wa 97.
243 Johannes Khrysostomos, (347-407), Askofu Mkuu wa Konstantinopoli. Hom. 3 in Ep. Ad Eph. Hom. 17 in Ep. As Hebr.: ‘In tremendo illo silentio vehementer vociferans alios quidem vocat, alios vero arcet sacerdos.’
kuwa, maneno ya kanuni ya Nikea yanasema: “Baada ya makasisi, mashemasi watapokea sakramenti kwa utaratibu kutoka kwa askofu au kasisi.”244
40. Basi, kwa kuwa hakuna jambo jipya lililowasilishwa ambalo kwalo, halikuwa katika Kanisa na hakuna mabadiliko wazi yaliyofanywa kuhusu kaida za hadhara za misa isipokuwa misa zingine ambazo zilisherehekewa zaidi ya misa za ushirika, labda kwa sababu ya matumizi mabaya, zilikomeshwa. Njia hii ya kuisherehekea misa haifai kulaaniwa kama uasi na si njia ya Kikristo. 41. Naam, zamani hata katika makanisa makubwa yenye watu wengi, misa haikusherehekewa kila siku watu walipokusanyika. Kulingana na “Historia ya Sehemu Tatu,”245 Kitabu cha Tisa, Maandiko Matakatifu yalisomwa na kuelezewa huko Aleksandria kila Jumatano na Ijumaa na haya yote yalifanywa bila misa.
XXV. Ungamo L
1. Ungamo halikutanguliwa katika makanisa yetu. Kwa kuwa si kawaida kutunukiwa mwili wa Kristo ila kwa waliohojiwa tayari na walioondolewa dhambi zao. 2. Watu wanafundishwa kwa umakini kuhusu imani ya ondoleo la dhambi, jambo ambalo halikusemwa sana kabla ya wakati huu. 3. Watu wetu hufundishwa kulithamini ondoleo la dhambi kwa sababu ni sauti ya Mungu inayotangazwa kwa agizo la Mungu. 4. Mamlaka ya funguo yanasifiwa sana, na watu hukumbushwa kuhusu faraja kubwa inayoletewa dhamiri zenye hofu, na zaidi kwamba, Mungu anadai imani inayoamini ondoleo la dhambi kuwa kama sauti inayosikika kutoka mbinguni na kwamba, imani ya namna hii inaupokea na inaupata msamaha wa dhambi. 5. Zamani matendo ya ridhaa yaliadhimishwa bila kipimo, lakini hakuna lililosemwa hata kidogo kuhusu imani, ustahili wa Kristo na haki ya imani. 6. Hivyo, makanisa yetu hayana kosa kuhusu jambo hili, hata wapinzani wetu hawana budi kukiri kwamba, wenzetu wameutoa mwanga kuhusu mafundisho ya toba na wameyatoa kwa uangalifu.
7. Kuhusu ungamo, hufundishwa kwamba, kuhesabu dhambi fulani si lazima. Dhamiri zisifadhaishwe na shaka la kuhesabu dhambi fulani fulani kwa kuwa haiwezekani kabisa kuzitaja dhambi zote. 8. (Zab. 19:12) unashuhudia: “Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake?” Kadhalika, (Yeremia 17:9) anasema: “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, . . . nani awezaye kuujua?” 9. Lakini, dhambi zisiposamehewa licha ya zile zilizotajwa, dhamiri hazingepata
244 Can. 18.
245 ‘Historia Tripartita’ iliandikwa na mmonaki Kassiodoro (480-570) aliyetoka Roma. Hapa Kassiodoro alidondoa historia ya Kanisa la Sokrate, 5, 22.
amani kwa kuwa makosa mengi mno hayawezi kuonekana au kukumbukwa. 10. Waandishi wa kale pia wanashuhudia kwamba, si lazima kuyahesabu. 11. Naye Krisostomo246 amenukuliwa katika kanuni, akisema: “Sisemi kwamba, inakubidi ujifunue faraghani au ujishtaki mbele ya wengine, walakini ninataka umtii nabii asemaye: ‘Umkabidhi BWANA njia yako’ (Zab. 37:5). Basi, katika sala zako, ungama dhambi zako mbele za Mungu, hakimu wa kweli. Ungama dhambi zako si kwa ulimi wako, bali kwa ukumbusho wa dhamiri yako,” 12. na kadhalika. Maelezo kuhusu Toba (Glossa de poenitentia Dist. 5 in Cap. Consideret)247 yanakiri kwamba, ungamo la namna hiyo ni la haki ya binadamu. 13. Hata hivyo, tumelishika ungamo kwa sababu ya baraka kuu ya ondoleo la dhambi na kwa sababu linailetea dhamiri faida.
XXV. Ungamo G
1. Kwa upande wetu, kuungama hakujakomeshwa na wahubiri wetu. Tumeihifadhi desturi hii ya kutokutoa sakramenti kwa ambao hawakuhojiwa na kuondolewa dhambi zao kabla ya misa. 2. Wakati huo huo, watu wanafundishwa kwa uangalifu kuhusu faraja ya Neno la ondoleo la dhambi248 ili walichukulie ondoleo la dhambi kama kitu kikubwa na cha thamani sana. 3. Ondoleo la dhambi si sauti au neno la mtu ambaye ananena, bali ni Neno la Mungu ambaye anasamehe dhambi. Kwa kuwa, Neno hili linatangazwa kwa niaba ya Mungu na kwa agizo lake. 4. Agizo hili linafundishwa kwa jitihada kubwa kuhusu mamlaka ya funguo jinsi yanavyofariji na yalivyo muhimu kwa dhamiri zenye hofu. Tunafundisha zaidi kwamba, Mungu anadai tuliamini ondoleo hili kana kwamba, sauti yake ingesikika kutoka mbinguni ili tujifariji kwa furaha na ondoleo la dhambi na tujue kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi kwa imani hiyo. 5. Hapo zamani, wahubiri waliofundisha sana juu ya ungamo, hawakutaja hata neno moja kuhusu jambo hili muhimu sana bali walitesa dhamiri kwa njia ya orodha ndefu za dhambi, matendo ya kipatanisho, vyeti vya upatanisho, hija, na mambo kama hayo. 6. Wapinzani wetu wengi wamekubali wenyewe kwamba, tumeshughulikia na kuandika kuhusu fungu hili la toba ya kweli ya Kikristo kwa njia inayofaa sana kuliko ilivyokwisha kufanywa kwa muda mrefu.
7. Tunafundisha kuhusu ungamo kwamba, hakuna anayefaa kushurutishwa
246 Johannes Khrysostomos, alikuwa mhubiri maarufu mno katika Kanisa la Zamani. Kwa hiyo, Khrysostomos alimtaja: ‘kama mwenye kinywa cha dhahabu.’ Aliteswa chini ya Kaisari wa Roma Mashariki kwa sababu, katika mahubiri yake, alizilaumu dhambi za mke wa Kaisari, yaani, Eudokia na wa kitala cha Kaisari. Alikufa kama mfungwa kwa sababu ya ushuhuda wake wa Kikristo.
247 ‘Glossa’ maelezo ya sheria za kanuni za kanisa.
248 Kilatini: ‘absolutio;’ Kijerumani: ‘Absolution.’
kuorodesha dhambi zake kwa utaratibu kwa kuwa haiwezekani 8. jinsi anasemavyo mtunga Zaburi: “Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake?”249 9. Kadhalika, Yeremia anasema: “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote . . . nani awezaye kuujua?”250 Asili yetu dhaifu ya kibinadamu imezama ndani ya kina kirefu cha dhambi hata kutoweza kuziona au kuzifahamu dhambi zote. Tungeondolewa dhambi zile tu ambazo tungeweza kuzitaja, hali hii ya mambo ingetusaidia kidogo sana. Kwa hiyo, hakuna haja ya kuwashurutisha watu kutoa maelezo ya kina ya dhambi zao. 10. Huu ulikuwa pia mtazamo wa mababa wa Kanisa ambao unaweza kuonekana katika “Dist. 1 De poenitentia” 11. ambapo maneno haya ya Krisostomo yalinukuliwa: “Sisemi kwamba, inakubidi kujifunua faraghani au kujishtaki mbele ya wengine, lakini ninataka umtii nabii asemaye, “Umkabidhi BWANA njia yako.”251 Ungama kwa sala dhambi zako kwa Bwana Mungu aliye hakimu wa kweli. Ungama dhambi zako si kwa ulimi wako bali katika dhamiri yako.” Hapa tunaona dhahiri kwamba, Krisostomo hawashurutishi watu kuzitaja dhambi kwa majina yao. 12. Maelezo ya pembeni252 katika “De poenitentia, Dist. 5” pia yanafundisha kwamba, ungamo la jinsi hiyo halijaamrishwa na Maandiko Matakatifu bali lilianzishwa na makanisa. 13. Wahubiri wa upande wetu bado wanafundishwa kwa jitihada kuu kwamba, ungamo lazima lihifadhiwe kwa ajili ya ondoleo la dhambi, ambalo ndilo sehemu kuu muhimu sana kwa ajili ya kufariji dhamiri ambazo ni zenye kuogofya na pia kwa sababu zingine.
XXVI. Upambanuaji wa Vyakula L
1. yamekuwa maoni ya kawaida, si ya umma tu lakini pia ya waliofundisha katika makanisa kwamba, kutofautisha vyakula na desturi za namna hii za binadamu ni matendo yenye faida kwa shabaha ya kustahilisha neema na radhi za dhambi. 2. Na iwapo ulimwengu ulifikiria hivyo, inaonekana wazi kutokana na hilo kwamba, taratibu mpya, madaraja mapya ya watawa, sikukuu mpya, mifungo mipya vilianzishwa siku kwa siku na walimu katika makanisa walidai matendo haya yawe ibada ya faradhi253 ili kuistahilisha neema na kuogofya dhamiri za watu walioacha baadhi ya mambo haya. 3. Kutokana na nia ya desturi hii, madhara mengi yametokea katika Kanisa.
4. Kwanza, mafundisho ya neema na haki ya imani yalifichwa. Naam, sehemu maalumu ya Injili iliyohitajika kusimama na kujulikana zaidi katika
249 Zab. 19: 12.
250 Yer. 17: 9.
251 Zab. 37: 5.
252 ‘Glossa’
253 ‘Faradhi,’ yaani, jambo la lazima kufanywa, wajibu radhi, yaani, hali ya nafsi kuridhika.
Kanisa ili ustahili wa Kristo ujulikane vyema, nayo imani inayoamini kwamba, dhambi zimesamehewa kwa ajili ya Kristo, iinuliwe juu ya kazi zote. 5. Kwa hiyo, Mtume Paulo pia anaweka mkazo zaidi katika kanuni hii, hata kuziondoa sheria na desturi za binadamu ili kuweka wazi kwamba, haki ya Kikristo ni tofauti kabisa na matendo ya namna hii. Yaani, imani inayoamini kwamba, kwa ajili ya Kristo, tunapokelewa katika neema. 6. Lakini mafundisho haya ya Mtume Paulo yamefunikwa karibu yote na mapokeo yaliyozaa wazo kwamba, ni sharti kustahili neema na haki kwa njia ya kuvichagua vyakula na ibada kama hizo. 7. Katika maelezo ya toba, imani haikutajwa ila tu matendo ya ridhaa254 ndiyo yaliyopendekezwa na toba yote ilifikiriwa kwamba, ina mambo haya.
8. Pili, desturi hizi ziliyaficha maagizo ya Mungu kwa njia ya kuyaweka mapokeo haya juu sana kuliko maagizo ya Mungu. Kwa jumla, Ukristo ulifikiriwa kuwa jambo la maadhimisho ya sikukuu fulani fulani peke yake, taratibu za ibada, mifungo na mavazi. 9. Maadhimisho haya yalikuwa na majina ya heshima ya maisha ya kiroho au maisha makamilifu. 10. Ambapo maagizo ya Mungu kuhusu mwito wa kila mmoja yalikuwa bila adhama,255 jinsi baba anavyowaelimisha watoto wake kwamba, mama aliwazaa watoto, na mtawala huiongoza serikali. Mambo haya yalihesabiwa kuwa kazi ya ulimwengu na kazi zisizokuwa kamili na chini sana zikilinganishwa na maadhimisho ya fahari. 11. Kosa hili lilizitesa sana dhamiri za wacha Mungu waliosikitika kwamba, walifungwa katika daraja la maisha lisilokamilika kama ndoa, kazi za hakimu, au kazi nyingine za serikali. Waliwastahi sana watawa na wengine kama hao, wakifikiria kimakosa kwamba, maadhimisho ya watu hao yalikuwa yanampendeza Mungu zaidi.
12. Tatu, mapokeo yaliashiria hatari nyingi kwa dhamiri kwa sababu haikuwezekana kuyaadhimisha yote. Hata hivyo, watu walifikiria kwamba, maadhimisho hayo yalikuwa ibada za faradhi. 13. Gerson256 anaandika kwamba, wengi walikufa moyo, pia wengine walijiua kwa kuwa walifikiria kwamba, hawakuweza kuyatimiza mapokeo kwa sababu hawakuwa wamesikia kuhusu faraja ya neema na haki ya imani. 14. Tunaona kwamba, “summistae”257 na wanatheologia wanazikusanya desturi na wanazitafuta njia za kuzipunguza ili kuzituliza dhamiri. Hata hivyo, hawaziendelezi dhamiri vya kutosha, lakini wakati mwingine wanaitengeneza mitego zaidi. 15. Shule na mahubiri yameshughulika
254 Hali ya kutosheka na jambo. Kulingana na mafundisho ya Kanisa la Roma, matendo ya ridhaa au upatanisho pamoja na toba vilihitajika.
255 Utukufu, heshima.
256 Jean le Charlier de Gerson (1363-1429) kutoka Ufaransa, mwandishi maarufu wa Kanisa la Magharibi wakati wake.
257 ‘Waandishi wa vitabu vya ungamo;’ ‘Summistae’ kutoka ‘summa;’ maana yake: “muhtasari:” waliandika vitabu vya ungamo vyenye mashauri mbalimbali kuhusu mambo ya kiroho na ya dhamiri.
sana kuyakusanya mapokeo haya hata kutokuwa na nafasi ya kuyagusa Maandiko Matakatifu au kuyatafuta mafundisho zaidi yenye faida kuhusu imani, msalaba, matumaini, heshima ya mambo ya serikali na faraja ya dhamiri zilizojaribiwa sana. 16. Kwa hiyo, Gerson na wanatheologia wengine walilalamika sana kwamba, walikwazwa vibaya na mabishano haya kuhusu mapokeo hata wakashindwa kujihusisha na aina bora ya mafundisho. 17. Agostino pia anakataa kuziudhi dhamiri kwa maadhimisho ya namna hiyo. Anamshauri Yanuario258 kwa busara ili ajue kwamba, yataadhimishwa kama mambo yasiyokuwa muhimu, kwa sababu haya ni maneno yake.
18. Kwa hiyo, walimu wetu wasilaumiwe kana kwamba, walilichukua jambo hili bila kufikiria au kutokana na chuki dhidi ya maaskofu jinsi wengine wanavyodhania kimakosa. 19. Kulikuwa na haja kubwa kuyaonya makanisa kuhusu makosa haya yaliyotokana na mapokeo yaliyoeleweka vibaya. 20. Kwa sababu katika makanisa Injili inatulazimisha kuyazingatia mafundisho kuhusu neema na haki ya imani, ambayo hata hivyo hayaeleweki, watu wakifikiria kwamba, wanastahili neema kutokana na maadhimisho ya mambo wanayojichagulia.
21. Kwa hiyo, walimu wetu wamefundisha kwamba, hatuwezi kustahili neema au kuhesabiwa haki kwa maadhimisho ya mapokeo ya binadamu. Kwa hiyo, isifikiriwe kwamba, maadhimisho kama haya ni matendo ya ibada yaliyo ya lazima. 22. Wanaongezea shuhuda kutoka kwa Maandiko Matakatifu. Katika
Mt. 15:3, 11 Kristo anawatetea mitume wasioadhimisha mapokeo ya desturi ya kawaida, hata ambayo hayakuwa desturi haramu, ambayo yalionekana kuwa ya kisheria na yenye uwiano na utakaso wa torati na anasema: “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.” 23. Basi, Kristo hadai tendo la ibada lisilokuwa na faida. Baadaye kidogo anaongezea: “Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi.” 24.Kadhalika imeandikwa katika Rum. 14:17: “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa,” 25. na katika Kol. 2: 16; 20-21: “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato.” Kadhalika: “Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, msishike, msionje, msiguse? . . .” 27. Petro anasema katika Mdo. 15:10-11: “Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. Bali twaamini kwamba, tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.” 28. Hapa Petro anakataa kuitwisha dhamiri mizigo kwa desturi nyingi za ibada ziwe za Musa au za wengine. 29. Pia 258 Barua ya Agostino kwa rafiki yake aliyeitwa Januarius (Ep. 54).
katika 1 Tim. 4:1, 3 Mtume Paulo analiita katazo la vyakula kuwa mafundisho ya mashetani kwa sababu kuyaagiza au kuyatenda matendo ya jinsi hiyo ili kustahili neema kunapingana na Injili kuwa dhahiri kwamba, haki ya Ukristo haiwezi kuwepo bila matendo ya ibada ya jinsi hiyo.
30. Wapinzani wetu hapa wanakataa wakisema kwamba, walimu wetu kama Yoviniano259 wanaikana nidhamu na mambo ya kuufisha mwili. 31. Lakini mambo tofauti kabisa yanaweza kueleweka katika maandiko ya walimu wetu, kwa maana kila wakati, wamekuwa wakifundisha kuhusu msalaba kwamba, Wakristo hulazimika kuyapata mateso. 32. Kuyastahimili mateso mbalimbali na kusulubiwa pamoja na Kristo ni jambo la kweli na halisi kuliko makusudi ya kubuni.
33. Mbali na hayo, wao hufundisha kwamba, kila Mkristo anahitaji kuudhibiti260 mwili wake au kujizoesha na kujishurutisha kwa mazoezi na kazi za mwili ili asijaribiwe na shibe au uvivu wa kuitenda dhambi, lakini si kwamba, tungestahili neema au kupata ridhaa kwa ajili ya dhambi kwa mazoezi ya namna hiyo. 34. Nidhamu ya kimwili ya jinsi hiyo inahitaji kuhimizwa kila wakati, si kwa siku chache na zilizopangwa tu 35. kama Kristo anavyofundisha katika Lk. 21:34: “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi . . .,” 36. kadhalika Mt. 17:21: “Namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.” 37. Naye Paulo anasema katika 1 Kor. 9:27: “Nautesa mwili wangu na kuutumikisha.”
38. Hapa anaonyesha wazi kwamba, aliutesa mwili wake, si ili astahili msamaha wa dhambi kwa hiyo nidhamu, lakini ili awe na mwili uliowekwa chini ya utii na uliofaa kwa mambo ya kiroho na kuitoa huduma yake kulingana na wito wake. 39. Kwa hiyo, lililoshutumiwa si kufunga kwenyewe, bali ni mapokeo yanayohatarisha dhamiri yakiielezea aina fulani ya siku na vyakula kana kwamba, kazi za namna hiyo ni matendo ya lazima kwa ibada.
40. Hata hivyo, mapokeo mengi yametunzwa miongoni mwetu kama utaratibu wa masomo katika Misa na sikukuu, ambayo yana faida kwa ajili ya kuuweka utaratibu unaofaa katika Kanisa. 41. Wakati huo huo, watu wanafundishwa kwamba, desturi za namna hiyo si kwasababu ya kuhesabiwa haki mbele za Mungu na hakuna dhambi ambayo imefanywa kama iliyoepukwa bila maasi. 42. Uhuru wa namna hiyo ulijulikana kwa mababa, 43. kwani Pasaka iliadhimishwa huko Mashariki wakati tofauti na Roma, na Waroma walipolishtaki Kanisa la Mashariki kwamba, kwa ajili ya tofauti hii, waliousababisha mfarakano wa 259 Jovinianus, mtawa kutoka Roma, aliyefundisha mwaka wa 385 dhidi ya maoni ya wamonaki wengi kwamba, watu wangeweza kustahili neema kwa matendo ya jinsi hiyo. Melanchthon, aliandika andiko la ‘Ukiri wa Augsburg’ akiyafuata maoni ya Hieronimo aliyemshtaki kwa uongo Yoviniano. 260 Yaani, kulinda au kutunza.
Kanisa, walionywa na wengine kwamba, desturi za namna hiyo hazikuhitaji kufanana kila mahali.261 44. Na Ireneo262 anasema: “Kutopatana kuhusu mfungo hakuharibu umoja wa imani.” Naye Papa Gregorio anaarifu katika Dist. XII kwamba, tofauti ya namna hiyo haiuharibu umoja wa Kanisa. 45. Katika “Historia Tripartita” kitabu cha tisa, mifano mingi ya tofauti za desturi za ibada imekusanywa, na maneno yafuatayo yamesemwa: “Hayakuwa malengo ya mitume kuziweka sheria za lazima kuhusu sikukuu, bali kuhubiri uchaji kwa Mungu na mazungumzo mazuri miongoni mwa watu.”
XXVI. Tofauti za Vyakula G
1. Awali, watu walifundishwa, walihubiriwa na kuandikiwa kwamba, upambanuzi wa vyakula na mapokeo ya namna hiyo yaliyoanzishwa na binadamu yalikusudiwa kustahilisha neema na kuridhisha dhambi kwayo.263 2. Kutokana na msingi huu, mifungo mipya, taratibu mpya, madaraja mapya, na mambo kama hayo yalibuniwa kila siku na yaliendelezwa kwa bidii na ukali kana kwamba, mambo hayo yangeweza kuwa ibada ya lazima kwa shabaha ya kustahili neema. Mtu asingeyaadhimisha mambo kama haya, ilitazamwa kwamba, aliitenda dhambi kubwa. 3. Kutokana na hili makosa mengi yenye madhara yametokea katika kanisa.
4. Kwanza, neema ya Kristo na mafundisho kuhusu imani264 yanafichwa kwa njia hii. Hata hivyo, Injili inatuhimiza kwa uzito mkubwa kuuchukulia ustahili wa Kristo kuwa kitu kikubwa na wenye thamani sana na kujua kwamba, imani katika Kristo ilikuwa zaidi ya matendo yote kabisa. 5. Kwa hili, Mt. Paulo alipinga kwa nguvu Sheria za Musa na mapokeo ya binadamu ili sisi tupate kujifunza kwamba, hatutakuwa wacha Mungu mbele zake kwa matendo yetu wenyewe bali kwa imani peke yake katika Kristo ili tuipate neema kwa ajili ya Kristo peke yake. 6. Mafundisho ya jinsi hiyo yalikuwa karibu kuzimika kwa sababu watu walifundishwa kustahili neema kwa mifungo iliyoagizwa, upambanuzi wa vyakula, mavazi na kadhalika.
8. Pili, mapokeo yaliyotajwa yametia giza maagizo ya Mungu kwa sababu mapokeo haya yaliwekwa mbali na maagizo ya Mungu. 9.Matendo haya yalitazamiwa kuwa maisha ya Kikristo peke yake: mtu yeyote aliyeadhimisha
261 Mabishano kuhusu wakati wa Pasaka katika karne ya pili kati ya Kanisa la Magharibi na Kanisa la Mashariki.
262 Ireneo (mnamo 130 - 200), Baba Myunani wa Kanisa la Zamani, alifariki kama askofu wa Lyon huko Ufaransa.
263 Tomaso wa Akuino (mnamo 1225-1274), ‘Summa theologica’ 2, 2. q 147, a, 1 c.
264 Yaani, haki ya imani.
sikukuu kwa njia hii, akasali kwa njia hii, akafunga kwa njia hii na akavalia kwa njia hii alisemekana kwamba, alikuwa na maisha ya kiroho na ya Kikristo. 10. Kwa upande mwingine, matendo mengine ya kazi muhimu sana yalitazamiwa kuwa matendo ya dunia, yasiyokuwa ya kiroho sawa na kazi mtu yeyote anawajibika kuifanya kulingana na wito wake: kazi za bwana wa kaya kuwalisha mke na watoto wake na kuwaongoza katika hofu ya Mungu, kazi ya mke kuwazaa watoto na kuwatunza vizuri, wajibu wa mtawala na mamlaka yaliyo makuu kutawala juu ya nchi na raia na kadhalika. 11. Kazi za jinsi hiyo, zilizoamriwa na Mungu zilitazamiwa kuwa kazi za dunia na zilizokuwa mbali na ukamilifu wakati mapokeo yalitajwa kwa majina yenye fahari sana kuwa matendo matakatifu na timamu peke yao. Kulingana na hayo, hakukuwa na kikomo au mwisho katika kutengeneza mapokeo kama hayo.
12. Tatu, mapokeo yaliyotajwa yamekuwa mzigo mzito wa dhamiri. Naam, haikuwezekana kuyaadhimisha mapokeo yote. Hata hivyo, watu walidhania kwamba, mapokeo yalikuwa ibada ya faradhi ya Mungu. 13. Gerson265 anaandika kwamba, watu wengi walikufa moyo na baadhi yao walijiua kwa sababu hawakuisikia faraja yoyote ya neema ya Kristo. 14. Katika vitabu vya “Summistae” na wanatheologia tunaweza kuona jinsi dhamiri za watu zilivyovurugika kwa kuwa walijitolea kuyalinganisha mapokeo na wakazitafuta njia za kupunguza ili kuzituliza dhamiri. 15. Lakini walikuwa wamejishughulisha kwa juhudi kiasi kwamba, hawakujali mafundisho yote mazuri ya Kikristo kuhusu mambo mengine yaliyokuwa muhimu sana kama imani, faraja, miongoni mwa dhiki kubwa na kadhalika. 16. Kabla ya wakati wetu, wataalamu wengi wacha Mungu walilalamika sana kwamba, mapokeo yalizaa mabishano mengi katika Kanisa na watu wacha Mungu walizuiwa kuujia ufahamu halisi wa Kristo. Gerson na wengine wengi walilalamika vikali kwa ajili ya hali hii.266 17. Kusema kweli, hata Agostino mwenyewe alikerwa na hali hii kwamba, dhamiri nyingi ziliudhiwa na mapokeo mengi na akafundisha kuhusiana na haya kwamba, watu wasiyatazame mambo ya lazima kushikwa.267
18. Kwa hiyo, wenzetu hawakufundisha kuhusu mambo haya kwa sababu ya uovu au dharau ya mamlaka ya kiroho. 19. Ni haja kubwa iliyodai kutoa mafundisho kuhusu makosa yaliyotajwa hapo juu, makosa ambayo yalichipuka kutoka kwa sifa za uongo za mapokeo. 20. Injili inadai kwamba, inapasa na ni lazima kwamba, mafundisho ya imani yanatumika katika makanisa walakini mafundisho haya hayawezi kueleweka jinsi inavyodhaniwa kwamba, neema
265 Jean le Charlier de Gerson (1363-1429) mkuu wa Chuo Kikuu cha Pari.
266 Gerson, ‘De vita spirituali animae,’ lect. 2. Opp. 2. ed. (1728) 3, 16 n.k.
267 Ep. 54, 2. 2 ‘ad Januarium.’
inapatikana kwa njia ya matendo ya hiari ili kuistahili neema.
21. Kwa hiyo, inafundishwa kwamba, neema haiwezi kustahiliwa au Mungu hawezi kupatanishwa na dhambi haziwezi kuridhishwa kwa njia ya kuyaadhimisha mapokeo ya binadamu. Kwa hiyo, si halali kubuni ibada kwa mambo haya. 22. Kama sababu, tunayarejea Maandiko Matakatifu katika Mt. 15:9 ambapo Kristo aliwawia radhi mitume wake wasiofuata mapokeo ya kawaida na akasema: “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”
23. Kwa sababu, Kristo anayaita mapokeo haya kuwa ibada bure, basi, si ya lazima. Baadaye kidogo anasema, “Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi.”268 24. Kadhalika Mtume Paulo anaandika katika Rum. 14:17: “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa,” 25. na katika Kol. 2:16 anasema: “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu . . .” 27. Petro anasema katika Mdo. 15:10: “Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.” 28. Petro anakataa kuitwisha dhamiri mizigo ya taratibu za nje kuwa kaida za Musa au za mwingine. 29. Katika 1 Tim. 4: 1,3 katazo kuhusu vyakula au ndoa linaitwa mafundisho ya mashetani. Kwa kuwa, kuyaanzisha matendo ya namna hiyo au kuyatenda kwa shabaha ya kustahili msamaha wa dhambi au kuwa na wazo kwamba, yeyote hawi Mkristo ila awe ametenda kaida hizo, ni kinyume cha Injili kabisa.
30. Ingawa walimu wetu wanashtakiwa kwamba, wao hukana hatua za kuutesa mwili na kuifuata nidhamu kama Yoviniano,269 maandiko yao yanaonyesha yaliyomo tofauti kabisa. 31. Wakati wote yaliendelea kufundisha kuhusu Msalaba Mtakatifu, yaani, kwamba, Wakristo huwajibika kuteseka. 32. Kuteseka huku ni nidhamu ya kweli si maadili yaliyobuniwa tu.
33. Walimu wetu wanafundisha pia kwamba, ni wajibu wa kila mtu kufanya mazoezi ya mwili kama kufunga na matendo mengine ili asiipatie dhambi nafasi, si kana kwamba, angestahili neema kwa matendo ya namna hiyo. 34. Mazoezi haya ya mwili yasifanyike tu katika siku maalumu zilizoamriwa bali wakati wote. 35. Katika Lk. 21:34, Kristo anasema yafuatayo kuhusu haya: “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi.” 36. Kadhalika Mt. 17:21: “Namna hii ya mashetani haitoki ila kwa kusali na kufunga.” 37. Mtume Paulo anasema kwamba, anautesa mwili wake na kuutumikisha. 38. Kwa hiyo, anaonyesha
268 Mt. 15: 11.
269 Mashtaka ya Hieronimo dhidi ya Yoviniano (mnamo 385) hayakuwa na msingi wowote. Yoviniano alipinga mafundisho ya kustahili neema kwa matendo, si nidhamu na maadili ya Kikristo. Kwa bahati mbaya, hapa, Melanchthon alizifuata kashifa za Hieronimo.
kwamba, kusudi la nidhamu hii si kustahili neema bali kuitunza hali ya mwili ili isizuie watu kufanya huduma za wito wao. Mifungo yenyewe haiachwi pia. 39. Lakini tunakataa kabisa mapokeo ya kufanya mifungo kuwa mambo ya siku na vyakula maalumu kwa sababu kufanya hivyo kunazichanganya dhamiri.
40. Kaida nyingi na mapokeo mengi yalihifadhiwa miongoni mwetu kama utaratibu wa misa, nyimbo,270 sikukuu, na kadhalika ambayo yanasaidia kutunza utaratibu bora katika makanisa. 41. Licha ya hayo, umma unaendelea kufundishwa kwamba, ibada hii ya nje haiwezi kumfanya mtu yeyote kuwa mcha Mungu na iadhimishwe bila kuisumbua dhamiri. Yaani, kuiacha dhambi iwapo itafanyika hivyo bila kashfa. 42. Mababa wa kale waliudumisha uhuru huu kuhusu kaida za nje. 43. Huko Mashariki, Pasaka ilisherehekewa wakati tofauti271 kuliko Roma. Ingawa wengine walionelea tofauti hizi kama kuligawanya Kanisa, walionywa na wengine kwamba, haikuwa lazima kudumisha umoja katika desturi za namna hiyo. 44. Ireneo alisema: “Kutopatana kuhusu mfungo hakuharibu umoja wa imani.” Kuna pia maelezo katika Dist. 12 kuhusu upungufu wa umoja katika mapokeo ya binadamu kwamba, jambo hili halipingi umoja wa Ukristo. 45 “Historia ya Sehemu Tatu” Kitabu cha Tisa, inakusanya mifano mingi ya matumizi tofauti ya Kanisa na inaongezea msemo wa Kikristo wenye faida: “Kusudi la mitume halikuwa kuanzisha sikukuu bali kufundisha imani na upendo.”272
XXVII. Nadhiri za Utawa L
1. Mafundisho yetu kuhusu nadhiri273 za utawa yanaweza kueleweka vizuri ikiwa yeyote ataikumbuka hali za nyumba za watawa zilivyokuwa, na ni mambo mangapi yalitendeka katika nyumba hizo kila siku ambayo yaliyopingana na kanuni. 2. Wakati wa Agostino, nyumba za watawa zilikuwa shirika za hiari. 3. Baadaye nidhamu ilipoharibika, nadhiri ziliongezwa kila mahali ili kuitengeneza upya nidhamu sawa na gereza lililopangwa vizuri. Hatua kwa hatua, maadhimisho mengine yaliongezwa kwa wingi juu ya nadhiri. 4. Minyororo ya jinsi hii iliwekwa juu ya wengi wasiokuwa na umri wa kutosha kinyume cha kanuni za Kanisa. 5. Wengi waliingia katika maisha ya namna hiyo kwa kutofahamu. Ingawa hawakupungukiwa na miaka, walishindwa kuzipima nguvu zao. 6. Waliotegwa hivyo, walilazimika kubakia ingawa baadhi yao wangeweza kuwa huru kama wangelalamika kulingana na kanuni. 7. Haya yalitendeka zaidi katika nyumba za wanawali kuliko za watawa wa kiume ingawa udhaifu wa kike ungestahili
270 Nyimbo hizi zilikuwa nyimbo za liturgia kutoka kwa Biblia zinazoitwa ‘canticulum.’
271 Nisan tarehe 14, katika kalenda ya Wayahudi.
272 Kassiodoro katika ‘Historia Tripartita’ 9, 38 kulingana na Sokrate Hist. Eccl. 5, 22.
273 “Nadhiri,” yaani, viapo vya dini.
kuangaliwa kwa makini. Ukali huu haukuwapendeza watu wengi wazuri kabla ya nyakati hizi. 8. Waliona kwamba, wasichana na wavulana walitupwa katika nyumba za watawa kwa ajili ya kuyapata maisha. Waliyaona matokeo mabaya yaliyotokana na mashauri haya, aina za kashfa zilizotokea na mitego iliyowekewa dhamiri. 9. Walijuta walipoona kwamba, mamlaka ya kanuni yalidharauliwa na yalitengwa kabisa katika jambo muhimu mno. 10. Licha ya ufisadi huu, ushawishi uliongezeka, hata zamani nadhiri hazikuwapendeza watawa wenye busara zaidi jinsi ilivyojulikana vyema.
11. Walifundisha kwamba, nadhiri zilikuwa sawa na Ubatizo,274 na kwamba, kwa maisha ya aina hii, watu walistahili ondoleo la dhambi na haki mbele za Mungu. 12. Licha ya hayo, waliongezea kwamba, maisha ya utawa hayakustahili tu haki mbele za Mungu. Badala yake, yaliyashika zaidi maagizo na ‘mashauri ya kiinjili’275 pia. 13. Hivyo, waliwashawishi watu kuamini kwamba, kazi ya utawa ilikuwa nzuri zaidi kuliko Ubatizo, na kwamba, maisha ya utawa yalikuwa ya sifa kuliko maisha ya hakimu, wachungaji na wengineo wanaohudumu katika wito wao kulingana na maagizo ya Mungu, na si ibada zingine zilizoanzishwa na watu. 14. Hakuna lolote katika haya ambalo lingeweza kukataliwa kwani linaonekana katika vitabu vyao.
15. Je, nini kilichotendeka baada ya watu kama hao kujiunga na nyumba za watawa?. Awali, kulikuwa na shule za Maandiko Matakatifu na malezi mengine ambayo yalikuwa ya faida kwa Kanisa nao wachungaji na maaskofu walipatikana katika nyumba hizo. Sasa, kila kitu kimebadilika. Si lazima kuyarudia mambo yanayojulikana vizuri. 16. Awali, watu walikusanyika pamoja katika nyumba za watawa ili kujifunza. Sasa, wanashikilia kwamba, maisha ya jinsi hii yalianzishwa ili kustahili neema na haki. Kweli, wao huhubiri kwamba, ni hali ya ukamilifu na wanaiinua juu zaidi kuliko aina zote za maisha yaliyoanzishwa na Mungu. 17. Mambo haya tumeyakariri bila maongezeko ya makuruhu276 ili mafundisho yetu kuhusu jambo hili yaweze kueleweka vizuri zaidi.
18. Kwanza, kuhusu wanaoifunga ndoa, tunafundisha kwamba, ni halali kwa watu wote ambao hawafai useja kuifunga ndoa, kwa kuwa nadhiri haziwezi kuondoa utaratibu na agizo la Mungu. 19. Hili ni agizo la Mungu: “Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe” (1 Kor. 7:2). 20. Si agizo tu, bali uumbaji na utaratibu wa Mungu unawalazimisha kushiriki ndoa wasiokatazwa na kazi fulani ya Mungu. Haya ni kulingana na somo la
274 Mathalani, Tomaso wa Akuino.
275 Akina Baba wengine wa Kanisa la Zamani waliotofautisha kati ya “Maagizo ya Mungu” (‘praecepta Dei’) na “mashauri ya kiinjili” (‘consilia evangelica’).
276 Yaani, mambo ya kuchukiza sana.
Mwa. 2:18: “Si vema mtu huyo awe peke yake.” 21. Hivyo, wanaolitii agizo hili na utaratibu huu wa Mungu, hawatendi dhambi.
22. Je, lipi litayapinga haya? Yeyote anaweza kulizidisha dai la nadhiri kadiri atakavyo. Hata hivyo, haiwezekani uwekaji nadhiri iliondoe agizo la Mungu. 23. Kanuni zinataja kwamba, kila nadhiri i chini ya haki ya aliye mkuu. Inashangaza kuona kwamba, nadhiri zilizo kinyume cha agizo la Mungu zina thamani.
24. Sasa basi, kama wajibu wa nadhiri ungeweza kubadilika, Makuhani Wakuu wa Roma hawangeweza kuibadilisha, kwani si halali kwa mtu kuutangua277 tu wajibu wa sheria ya Mungu. 25. Lakini Makuhani Wakuu wa Roma wamehukumu kwa busara kwamba, inabidi kuufuata utaratibu kuhusiana na wajibu huu. Hivyo, tunasoma kwamba, waliibadilisha nadhiri mara nyingi. 26. Historia ya mfalme wa Aragoni aliyerudishwa kutoka nyumba ya watawa278 inajulikana vizuri na hata kuna mifano mingine kutoka wakati wetu.
27. Basi, mbona wapinzani wetu huuzidisha zaidi wajibu au matokeo ya nadhiri, huku wakikaa kimya kuhusu asili ya nadhiri yenyewe, ambayo kwa hiari, inapasa kuchaguliwa kwa uhuru wa mawazo?279 28. Uwezo wa binadamu kubaki katika usafi kijinsia haujulikani. 29. Wachache kiasi gani walioiweka nadhiri kwa hiari na kwa kukusudia hivyo! Wasichana na wavulana hushawishiwa, wakati mwingine hulazimishwa pia kuiweka nadhiri kabla ya kuamua vizuri. 30. Kwa hiyo, si vizuri kubishana kwa nguvu kuhusu wajibu wakati watu wote hukubali kwamba, ni kinyume cha asili ya nadhiri kuifanya ahadi isiyokuwa ya hiari na yakukusudiwa.
31. Kanuni nyingi zaidi zinazifuta nadhiri zilizowekwa kabla ya umri wa miaka kumi na mitano. Kabla ya umri huo, mtu haonekani kuwa na uamuzi wa kutosha wa kukata shauri kuhusu maisha yake ya baadaye. 32. Kanuni nyingine, tena yenye ridhaa zaidi ya unyonge wa binadamu, inaongezea miaka michache ili mtu akatae kuiweka nadhiri kabla ya kutimiza umri wa miaka kumi na minane. 33. Basi, tuifuate ipi? Watawa wengi zaidi wana sababu za kuziacha nyumba za watawa kwa kuwa wengi wao wameweka nadhiri kabla ya kutimiza umri huo.
34. Mwishowe, ingawa ubadilishaji nadhiri unaweza kulaumiwa, hauonekani kufuata moja kwa moja kwamba, ndoa za watu wa jinsi hiyo zivunjike. 35. Kwa kuwa Agostino anakana kwamba, zisivunjike (“27., quaest. I, cap. Nuptiarum”).
277 Tangua – kuvunja kanuni au maafikiano.
278 Ramiro II alijiunga na watawa. Baada ya kufariki kwa ndugu yake asiyekuwa na watoto, aliyaacha maisha ya utawa ili awe mfalme wa Aragoni.
279 Mathalani, Tomaso wa Akuino katika kitabu chake kiitwacho, ‘Summa Theologica’ 2, 2. q. 88.
Mamlaka yake si hafifu ingawa wengine wametofautiana naye baadaye.
36. Ingawa inaonekana kwamba, amri ya Mungu kuhusu ndoa inawaweka wengi huru kutoka kwa nadhiri zao, bado wenzetu wamezitoa hoja nyingine kuhusu nadhiri kuonyesha kwamba, hazina maana. Kila ibada ya Mungu iliyoanzishwa na watu ili kustahili haki na neema bila agizo la Mungu ni kufuru, kwani Kristo anasema: “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” (Mt. 15:9). 37. Naye Paulo anafundisha kila mahali kwamba, haki haitolewi kutokana na maadhimisho na ibada ambazo ni mawazo ya binadamu. Badala yake, inapokelewa kwa imani na wanaoamini kuwa wamepokelewa na Mungu kwa ajili ya Kristo.
38. Inaonekana wazi kwamba, watawa wamefundisha kwamba, maadhimisho yaliyobuniwa yanaifanya ridhaa ya dhambi hata kustahili neema na haki. Hili ni lipi lingine isipokuwa kuupunguza utukufu wa Kristo, kuificha na kuikana haki ya imani? 39. Basi, inafuatia kwamba, nadhiri za kawaida zimekuwa ibada mbovu. 40. Kwa hiyo, zimekuwa batili kabisa, kwa kuwa nadhiri mbovu iliyofanywa kinyume cha agizo la Mungu haifai. Jinsi kanuni isemavyo ni kwamba, hakuna nadhiri inayopaswa kuwafunga watu kwa uovu.
41. Paulo anasema: “Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema” (Gal. 5:4). 42. Hivyo, wanaotaka kuhesabiwa haki kwa nadhiri, wametengwa na Kristo na wameanguka kutoka katika hali ya neema 43. kwa sababu wanajihesabia haki kwa nadhiri zao. Huhesabu kwa matendo yao wenyewe hasa yaliyo ya utukufu wa Kristo. 44. Haiwezekani pia kupingwa kwamba, watawa wameendelea na mafundisho ya kuhesabiwa haki na kustahili kwao ondoleo la dhambi kwa nadhiri na maadhimisho. Kusema kweli, wameutunga upuuzi mkuu kwa kusema kwamba, wangeweza kuwashirikisha wengine pia katika matendo yao. 45. Yeyote akimtaka mwingine ayatie chumvi mambo haya kwa kusudi baya, ni mangapi mengi ataweza kuyakusanya, ambayo kwayo, hata watawa wenyewe wanayaonea aibu! 46. Mbali na haya, waliwashawishi watu kwamba, desturi za dini za binadamu ndizo hali ya ukamilifu wa Kikristo. Je, ni lipi lingine ila kuihesabu haki kwa matendo? 47. Ni jambo la kukosesha na lisilokuwa rahisi katika Kanisa kuwapendekezea watu ibada maalumu iliyoanzishwa na watu bila agizo lolote la Mungu na kuendelea na mafundisho kana kwamba, ibada ya jinsi hiyo inawahesabia watu haki. 48. Maana haki ya imani ambayo inahitajika kufundishwa katika Kanisa inafichwa wakati macho ya watu yanapofushwa na desturi hizi za maadhimisho ya malaika, unafiki huu wa umaskini, unyenyekevu na useja.
49. Licha ya hayo, maagizo ya Mungu na ibada kweli ya Mungu vinafichwa pale watu wanaposikia kwamba, watawa peke yao ndio wenye ukamilifu. Kwani, huu ndio ukamilifu wa Kikristo: kumwogopa Mungu kweli, na wakati huo huo kuwa na imani kuu na kutegemea kwamba, kwa ajili ya Kristo, tuna Mungu aliyepatanishwa nasi, kumwomba Mungu na kutarajia kweli msaada kutoka kwake katika mambo yote kulingana na wito wetu. Wakati huo huo, kuwa waangalifu katika kuyatenda matendo mema na kuudhihirisha wito wetu. 50.Katika mambo haya, kuna ukamilifu wa kweli na ibada ya kweli ya Mungu. Si katika useja, uombaji au mavazi machafu,280 51. bali raia wanayawaza mawazo mengi yenye madhara kutoka kwa sifa hizo danganyifu za maisha ya utawa. 52. Wao huisikia sifa ya useja isiyokuwa na kifani. Kwa hiyo, wao hukaa katika maisha ya unyumba wakiwa na dhamiri yenye kuhangaisha. 53. Wao husikia kwamba, watawa waombaji peke yao ndio wakamilifu. Kwa hiyo, wanapojihusisha na mali au wanapojishughulisha na biashara huwa na dhamiri iliyosumbuliwa. 54.Wao husikia kwamba, kutolipiza kisasi ni shauri la kiinjili tu, kwa kuwa wengine hawaogopi kulipiza kisasi katika maisha yao binafsi wanaposikia kwamba, hili hukatazwa, ni ushauri tu na si agizo. 55. Wengine hukata shauri kwamba, kazi ya mahakama na huduma zote za serikali hazistahili kwa Wakristo.
56. Tunasoma mifano ya watu walioiacha ndoa, waliouacha utawala wa nchi na kujiunga na nyumba za watawa. 57. Tendo hili waliliita “kujitoa ulimwenguni” na “kuyatafuta maisha matakatifu.” Hawakutambua kwamba, Mungu anahitaji kutumikiwa katika maagizo aliyoyatoa yeye mwenyewe, na si katika maagizo yaliyobuniwa na watu. 58. Aina bora na kamilifu ya maisha ni yenye kutokana na agizo la Mungu. 59. Ni muhimu kuwakemea watu juu ya mambo haya.
60. Kabla ya nyakati hizi, Gerson alilikaripia kosa la watawa kuhusu ukamilifu na alishuhudia kwamba, jambo hili lilikuwa jipya kabisa kwamba, maisha ya utawa ni ya hali ya ukamilifu.
61. Basi, kuna maoni mengi maovu yanayohusiana na nadhiri: kwamba, zinamfanya mtu kuwa mwenye haki kwamba, zinathibitisha kuwa zinamwezesha mtu kuwa na ukamilifu wa Kikristo kwamba, watawa wanayaadhimisha mashauri na maagizo na hata kuyafanya matendo zaidi ya kadiri ya haki. 62. Kwa kuwa yote haya ni uongo na hayana faida, yanaifanya nadhiri kuwa batili na potovu.
280 Mavazi machafu yalikuwa katika madaraja mengine ya utawa kama alama ya unyenyekevu wa kweli.
XXVII. Nadhiri za Utawa G
1. Kwanza, katika mazungumzo, ni lazima kufikiria kuhusu nadhiri za utawa, maoni yaliyoshikiliwa kuhusu nadhiri hizo, na maisha waliyoishi watawa katika nyumba zao. Isitoshe, kila siku, mambo mengi hayakulipinga Neno la Mungu tu bali pia haki za Upapa. 2. Wakati wa Mtakatifu Agostino, hali ya watawa ilikuwa huru. Baadaye wakati nidhamu ya kweli na mafundisho yalipotoka, nadhiri za utawa ziliundwa na jaribio likafanywa kuirejesha nidhamu kwa njia ya nadhiri hizi kana kwamba, ilikuwa jela iliyobuniwa vyema.
3. Zaidi ya nadhiri za utawa, matakwa mengine mengi yalishurutishwa. 4. Minyororo ya namna hiyo na mizigo iliwekwa kwa wingi hata kabla ya umri wa kufaa.
5. Hivyo, watu wengi walijiunga na maisha ya utawa kwa ujinga. Hata hivyo, watu hawa hawakuwa vijana sana, hawakutambua au kufahamu vya kutosha uweza wao. 6. Waliokamatwa na kutekwa hivyo waligandamizwa na kulazimishwa kubaki ijapokuwa hata haki ya Upapa ingeweza kuwaweka wengi wao huru. 7. Hali ya mambo ilikuwa ngumu katika nyumba za watawa mabikira kuliko nyumba za watawa wanaume. Hata hivyo, ingepasa sana kuwaangalia wanawake kama vyombo dhaifu. 8. Zamani, ukali na uzito wa jinsi hiyo haukuwapendeza watu wengi wacha Mungu kwa kuwa waliona kwamba, wavulana na wasichana walitupwa katika nyumba za watawa ili watengenezwe. Waliyaona pia matokeo mabaya yaliyotokana na mpango huu, kashfa na aina gani ya mizigo ya dhamiri! 9. Watu wengi walilalamika kwamba, kanuni hazikufuatwa kikamilifu katika kesi za namna hiyo. 10. Licha ya hayo, nadhiri za utawa zilipata sifa jinsi inavyojulikana kwamba, watawa wengi hata wenye ufahamu haba waliudhika.
11. Ilidaiwa pia kwamba, nadhiri za utawa zilikuwa sawa na Ubatizo na kwamba, kwa njia ya maisha ya watawa, mtu angeweza kuupata msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki mbele za Mungu.281 12. Licha ya haya, waliongezea kwamba, maisha ya watawa hayakustahili haki na uchaji, bali kwa njia ya maisha haya pia maagizo na mashauri ya Injili yalifuatwa. 13. Hivyo basi, nadhiri za utawa zilisifiwa zaidi kuliko Ubatizo. Ilidaiwa pia kwamba, stahili zaidi ziliweza kustahiliwa kwa maisha ya watawa kuliko hali zote zingine za maisha zilizoanzishwa na Mungu kama huduma ya padre na mhubiri, mtawala, bwana mkuu na kadhalika. Hata hivyo, hawa wote wanahudumia katika wito wao uliopangwa kulingana na Neno na agizo la Mungu bila uchaji uliobuniwa tu. 14. Hakuna lolote ambalo lingeweza kukataliwa kwani linaonekana katika vitabu
281 Tomaso wa Akuino, ‘Summa theologica’ 2, 2. q. 189, a. 3 ad 3.
vyao wenyewe.
15. Licha ya hayo, waliokamatwa na wakavutiwa kwa werevu kujiunga na nyumba za watawa, walijifunza kidogo tu kuhusu Kristo. Zamani, nyumba za watawa ziliongoza shule za Maandiko Matakatifu na masomo mengine yaliyokuwa kwa faida ya makanisa ya Kikristo. Hivyo, wachungaji na maaskofu waliteuliwa kutoka kwa nyumba za watawa. Sasa, hali ya mambo imekuwa tofauti. 16. Zamani, watu walikusanyika na waliishi katika nyumba za watawa ili kujifunza Maandiko Matakatifu. Sasa, inadaiwa kwamba, maisha ya utawa ni hali ya aina yake kiasi kwamba, inastahili neema ya Mungu na uchaji mbele zake. Kwa kweli, inaitwa hali ya ukamilifu282 na inatazamiwa sana kuwa juu ya hali zingine zote zilizoanzishwa na Mungu. 17. Haya yote yanaonyeshwa hapa wazi bila tafsiri mbaya ili kuwasaidia watu kuelewa vizuri zaidi mambo ambayo wenzetu huyafundisha na kuyahubiri.
18. Kwanza, wao hufundisha miongoni mwetu kuhusu wote wanaotamani kuoa na kuolewa, wasiopatanishwa na useja kwamba, wana uweza, haki, na mamlaka ya kuoa na kuolewa kwa sababu nadhiri haziwezi kuubatilisha utaratibu na agizo la Mungu. 19. Agizo la Mungu linasikika katika 1 Kor. 7:2: “Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.” 20. Hili si agizo la Mungu tu linalotuhimiza, linalotushurutisha na kutulazimisha kufanya hivyo. Badala yake, ni uumbaji na utaratibu wa Mungu pia unaowaongoza wote kuoa na kuolewa, ambao hawajajaliwa na karama ya ubikira kutokana na tendo la pekee la Mungu kulingana na msemo huu katika Mwa. 2:18: “Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.”
22. Je, lipi litayapinga haya? Hakuna maana kuzisifu zaidi nadhiri na wajibu wake. Hakuna maana kuziinua juu sana. Licha ya haya, mtu hawezi kushurutisha kwamba, Agizo la Mungu libatilike kwayo. 23. Wataalamu wanasema kwamba, nadhiri inayopinga kanuni za Upapa haiwezi kufungwa.283 Je, ni kwa udogo upi nadhiri zingeweza, kuwa halisi na zenye mamlaka wakati zinalipinga Agizo la Mungu?
24. Iwapo hakuna sababu yoyote inayopatikana kuruhusu kuubatilisha wajibu wa nadhiri, akina papa wa Roma hawangetoa na kufungua watu kutokana na wajibu kama huo. Hakuna mtu yeyote aliye na haki kuubatilisha wajibu
282 Tomaso wa Akuino, ‘Summa theological’ 2, 2.q. 186 a. 1 c.
283 Decr. Grat. P. 2, c. 20. q. 2: ‘Monacho non licet votum vovere sine consensus abbatis sui, si autem voverit, frangendum erit.’ (Mtawa hapaswi kuweka nadhiri bila makubaliano ya mkuu wake. Basi, akiweka nadhiri yake, ivunjwe.)
unaotokana na haki ya kimungu. 25. Kwa hiyo, akina papa wa Roma walikuwa wakielewa vyema kwamba, wajibu huu unafaa kufanyiwa marekebisho kiasi ili uwe mzuri zaidi na mara kwa mara walitoa kibali, 26. jinsi ilivyokuwa kwa mfalme wa Aragonia284 na wengine wengi. Iwapo kibali kilitolewa kwa ajili ya mambo ya dunia hii, ni vipi kibali kinafaa kutolewa kwa sababu ya haja ya nafsi za binadamu?
27. Basi, mbona wapinzani wetu wanaendelea kusisitiza kwamba, nadhiri lazima zihifadhiwe bila kuhakikisha kama nadhiri hizo zinastahili? Kwa kuwa lazima nadhiri ihusishe linalowezekana na la hiari na sharti lisiwe la kushurutishwa. 28. Inajulikana wazi kwa vipi ubikira wa milele unategemea nguvu na uweza wa binadamu. 29. Wanaume na wanawake wachache tu wameweka nadhiri za utawa kwa kujitolea wao wenyewe bila kusita na baada ya kutafakari kunakostahili. Kabla ya kufikia ufahamu unaofaa, walishawishiwa kuweka nadhiri za utawa na wakati mwingine walishurutishwa na kulazimishwa kufanya hivyo. 30. Kwa hiyo, si vizuri kubishana kwa nguvu bila subira kuhusu wajibu wa nadhiri kwa mujibu wa mwafaka wa wengi kwamba, kufanya hivyo kunaipinga hulka na asili ya nadhiri kuwa kitu cha hiari kinachofaa kuwekwa tu baada ya kutafakari kunakostahili na ushauri.
31. Kanuni nyingi na haki ya Upapa zinabatilisha nadhiri ambazo ziliwekwa kabla ya umri wa miaka kumi na mitano.285 Ilitazamiwa kwamba, kabla ya umri huu, mtu hana uelewa wa kutosha wa kuamua au kupanga utaratibu wa maisha yake yote. 32. Kanuni nyingine inakubali miaka mingine zaidi kwa ajili ya udhaifu wa binadamu, kwa kuwa kanuni hii inakataa kuweka nadhiri za utawa kabla ya mtu kutimiza miaka kumi na minane.286 33. Kwa hiyo, kukawa na sehemu kubwa ya vibali na sababu za kuondoka nyumba za watawa kwa kuwa wengi wao waliingia nyumba za watawa wakati wa utoto kabla ya kufikisha miaka hii iliyoainishwa.
34. Mwishowe, ingawa uvunjaji wa nadhiri za utawa ungeweza kulaumiwa, kwamba haukufuatia, ndoa za watu waliozivunja nadhiri zao zingevunjika pia. 35. Kwa kuwa, Agostino anasema katika “27, quest. 1, cap. Nuptiarum” kwamba, ndoa ya jinsi hiyo isivunjike. Mtakatifu Agostino ni mwenye heshima isiyodharauliwa katika Kanisa la Kikristo. Hata hivyo, wengine walitofautiana naye.
36. Hata hivyo, amri ya Mungu kuhusu hali ya ndoa ni huru kabisa
284 Mfalme Ramiro wa II alikuwa mtawa aliyeruhusiwa kuiacha nyumba ya watawa na kuwa mfalme wa Aragoni baada kifo cha ndugu yake ambaye hakutaka kumwachia mrithi yeyote Aragoni.
285 Decr. Grat. P. 2, C. 20. q. 1. c. 10.
286 Pahali papo papo pa Gratiano, c. 5.
ikilinganishwa na nadhiri za utawa na inawaweka watu huru. Wenzetu wanazitoa sababu zaidi za kuonyesha kwamba, nadhiri za utawa ni batili kabisa na hazina maana. Aina zote za ibada zilizoanzishwa na watu bila agizo na amri ya Mungu kwa shabaha ya kupata haki na neema ya Mungu, zinampinga Mungu na Injili Takatifu na ni kinyume cha Agizo la Mungu kabisa. Kristo mwenyewe anasema katika Mt. 15:9: “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo wanadamu.” 37. Mtakatifu Paulo anafundisha kila mahali kwamba, mtu asitafute haki katika maagizo yetu na ibada zetu zilizobuniwa na watu. Haki na uchaji mbele za Mungu vinatokana na imani na tegemeo katika jambo hili kwamba, Mungu anatupokea katika neema yake kwa ajili ya mwanawe wa pekee, Yesu Kristo.
38. Inajulikana wazi kwamba, watawa waliendelea kufundisha na kuhubiri kwamba, maisha yao ya kiroho yaliyobuniwa yanaridhisha dhambi na kupata neema na haki ya Mungu. Hili ni lipi lingine isipokuwa kuupunguza utukufu na sifa ya neema ya Kristo na kukanusha haki ya imani? 39. Kutokana na hili, inafuatia kwamba, nadhiri za kawaida zilikuwa ibada za Mungu zisizokuwa halali na za bandia. 40. Kwa hiyo, nadhiri hizo hazifungamani kwa kuwa nadhiri inayolipinga agizo la Mungu ni ya kufuru sana na batili kabisa. Hata kanuni zinafundisha kwamba, nadhiri isiwe mnyororo wa dhambi.287
41. Mtakatifu Paulo anasema katika Gal. 5:4: “Mmtengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.” 42. Hali kadhalika, wote wanaotaka kuhesabiwa haki kwa njia ya nadhiri wametengwa na Kristo na wameanguka kutoka neema ya Mungu kwa kuwa wanamwibia Kristo heshima yake na kuitawaza heshima hii kwa nadhiri zao na kwa maisha ya utawa. 43. Hata hivyo, ni Kristo pekee anayetufanya kuwa wenye haki.
44. Hatuwezi kukataa kwamba, watawa wameendelea kufundisha na kuhubiri kwamba, walihesabiwa haki na kuupata msamaha wa dhambi kwa nadhiri zao, kwa maisha yao ya utawa na kwa maadhimisho yao. Kusema kweli, waliyabuni madai mengine ya upuuzi na ya aibu kana kwamba, wangeweza kuyatumia matendo yao mema kwa ajili ya watu wengine. 45. Mtu akitaka kuyahesabu madai haya yote ili kuwagombeza kwayo, je, ni vipengele vingapi vingeweza kukusanywa ambavyo watawa wenyewe wanavionea aibu na wangetamani kwamba, havingetokea kabisa. 46. Mbali na haya yote, waliwashawishi watu kwamba, hali iliyobuniwa ya madaraja ya kiroho ni hali ya ukamilifu wa Kikristo.
287 Decr. Grat. 2, C. 22. q. 4. c. 22: ‘Iuramentum non ob hoc fuisse institutum, invenitur, ut esset vinculum iniquitatis.’ Sentensi hii hailengi hasa nadhiri za utawa bali viapo vyote vya kidini.
47. Kusema hivyo ni utukuzaji wa matendo kana kwamba, matendo ndiyo njia ya kufikia kuhesabiwa haki. 48. Hii si kashfa ndogo katika makanisa ya Kikristo kwamba, watu hutolewa aina ya ibada ya Mungu ambayo ilibuniwa na watu bila agizo la Mungu hata kufundishwa kwamba, ibada kama hiyo itawafanya watu kuwa wacha Mungu na wenye haki mbele za Mungu. Kwa kuwa haki ya imani inayopaswa kusisitizwa wakati wote kuliko mambo mengine katika Kanisa la Kikristo inatiwa giza wakati macho ya watu yanayopigwa na butwaa kwa huu uchaji wa kiroho wa kimalaika pamoja na umaskini, unyenyekevu na useja bandia.
49. Licha ya hayo, maagizo ya Mungu na ibada ya kweli na halisi vinatiwa giza wakati watu wanasikia kwamba, wamonaki peke yao ndio wanaweza kuwa wenye ukamilifu. Ukamilifu wa Kikristo ni kumwogopa Mungu kwa moyo wa kweli, ni tegemeo, imani na tumaini la moyo kwamba, tunao kwa ajili Kristo Mungu mwenye neema na huruma. Hivyo, tunaweza na inatubidi pia kumwuliza na kumwomba Mungu mambo yote tunayohitaji, na kwa ujasiri kutegemea msaada wake katika dhiki zote zinazohusiana na wito na hali yetu maalumu katika maisha haya. Wakati huo huo, tufanye matendo mema kwa watu wengine na tushughulike kwa juhudi na wito wetu. 50. Ukamilifu wa kweli na ibada halisi ya Mungu ni vya jinsi hii. Si uombaji au kuuvalia ukaya mweusi au wa rangi ya kijivu na kadhalika. 51. Hata hivyo, watu wa kawaida wanaposikia hali ya useja ikisifiwa kupita kiasi, wanayawaza mengi ya kudhuru kutokana na utukuzaji wa bandia wa maisha ya utawa, 52. kwa kuwa dhamiri zao zinataabika kwa sababu wameoa. 53. Wakati mtu wa kawaida anasikia kwamba, watawa waombaji peke yao ndio wenye ukamilifu, hana hakika kama anaweza kumiliki rasimali yake na kujishughulisha na biashara bila kutenda dhambi. 54. Watu wakisikia kwamba, kutolipiza kisasi ni shauri la Injili tu, ni kawaida kwamba, wengine wanahimiza kwamba, si dhambi kulipiza kisasi nje ya shughuli zao za ofisi. 55. Wengine wanadhania kwamba, si halali Wakristo kuyaadhibu mabaya katika shughuli za mamlaka kuu.
56. Maarifa katika vitabu fulani yanasema kwamba, wanaume waliaacha wake, watoto, na pia waliziacha ofisi zao za serikali na kuzikimbilia nyumba za watawa. 57. Kuhusu haya walidai kwamba, ni kujitoa ulimwenguni na kuyatafuta maisha yanayompendeza Mungu kuliko mengine. Walishindwa kuelewa kwamba, inambidii mtu kumtumikia Mungu kwa amri ambazo alipewa na Mungu na si kwa maagizo mengine yaliyobuniwa na watu. 58. Hiyo ndiyo hali ya maisha yaliyokuwa makamilifu na mazuri ambayo yanaungwa mkono na maagizo ya Mungu. Kwa upande mwingine, hali ya maisha isiyoagizwa na
Mungu ni hatari sana. 59. Ilikuwa lazima kuwapa watu mafundisho halisi kuhusu mambo kama haya.
60. Zamani, Gerson aliyakaripia makosa ya watawa kuhusu ukamilifu na akaonyesha kwamba, ilikuwa uvumbuzi wa wakati wake kuzungumzia maisha ya watawa kama hali ya ukamilifu.288
61. Hivyo, maoni mengi yasiyokuwa ya uchaji wa kweli wa Mungu na makosa mengi yanaambatana na nadhiri za utawa. Yanawahakikishia watu kuwa na haki na uchaji mbele za Mungu. Yanadai kuufanyiza ukamilifu wa Kikristo hata watu waweze kutimiza kwazo mashauri ya Injili na amri za Mungu. Yanafanyiza pia matendo zaidi ya kiwango289 ambayo watu hawawajibiki kumtendea Mungu. Basi, Kwa sababu mambo haya yote ni uongo, hayana faida, na ni ya kubuniwa tu, nadhiri za utawa ni batili kabisa na hazina maana.
XXVIII. Mamlaka katika Kanisa L290
1. Nyakati zilizopita, pamekuwa na mjadala kuhusu mamlaka ya maaskofu na baadhi yao wameyachanganya madaraka ya Kanisa na ya upanga. 2. Kutokana na mkanganyiko huo, vita vikali pamoja na machafuko vimetokea. Maaskofu wamesukumwa kwa nguvu za funguo, hawakuzianzisha tu taratibu mpya za ibada na kuuleta uzito wa dhamiri kwa kuzinyamazia kesi kadha wa kadha pamoja na utengaji katili, bali pia wamefaulu kuzigeuza falme za ulimwengu huu na kumwondolea Kaisari himaya yake. 3. Kwa muda mrefu sasa, maovu haya yamekemewa katika Kanisa na watu wasomi na wamchao Mungu. 4.Kwa hiyo, walimu wetu wakitaka kuzifariji dhamiri za watu, wanalazimika kuionyesha tofauti kati ya mamlaka ya Kanisa na nguvu za upanga, na kufundisha kwamba, zote mbili hutokana na agizo la Mungu. Hivyo, zote mbili zishikiliwe kwa unyenyekevu na heshima kama zawadi kuu za Mungu duniani.
5. Lakini wazo lao ni kwamba, nguvu za funguo, au mamlaka ya maaskofu jinsi yalivyo katika Injili, ni nguvu au amri ya Mungu, kuihubiri Injili, kusamehe au kuifungia dhambi, na kuzitunza sakramenti. 6. Kwa maana kwa kuitumia amri hii, Kristo aliwatuma mitume wake, akisema katika Yn. 20:21: “. . . kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.”
288 Gerson aliyapinga mafundisho ya Tomaso wa Akuino kuhusu “hali ya ukamilifu” (‘status perfectionis’). Gerson 2, uk. 680.
289 Kilatini: ‘opera supererogationis,’ Tomaso wa Akuino, ‘Summa Theologica’ 2, 2. q. 85. a. 4. c.
290 Kilatini: ‘De potestate clavium,’ yaani, (mamlaka ya funguo).
7. Pia alisema kama ilivyoandikwa katika Mk.16:15: “Enendeni . . . mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.”
8. Mamlaka haya yanatumiwa tu kuifundishia au kuihubiria Injili na kuzitunza sakramenti kwa wengi au mtu mmoja mmoja na kutegemea mwito wa mtu. Kwa sababu katika hivi hutolewa, si vitu vya kimwili tu, bali vya milele, kama vile haki ya milele, Roho Mtakatifu na uzima wa milele. 9. Vitu hivi haviwezi kuwepo ila kwa huduma ya Neno na Sakramenti, kwa sababu Paulo anasema katika Rum. 1:16: “Injili . . . ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye,” pia Zab.119:50 inasema: “. . . ahadi yako imenihuisha.” 10. Kwa hiyo, kwa kuwa mamlaka katika Kanisa huvileta vitu vya milele, na hutumiwa katika huduma ya Neno peke yake, huiingilia serikali ya nchi kwa kiasi kidogo sawasawa na sanaa ya uimbaji inavyoingilia serikali ya nchi. 11. Hii ni kwa sababu serikali kamili huyashughulikia mambo mengine kuliko kuishughulikia Injili. Serikali haiilindi mioyo ila miili pamoja na vitu vinavyoonekana visipate madhara dhahiri na kuwazuia watu kwa upanga na kwa adhabu za kimwili ilihali Injili huilinda nafsi dhidi ya uzushi, Ibilisi, na kifo cha milele.
12. Kwa hiyo, mamlaka katika Kanisa na mamlaka ya serikali yasichanganywe. Mamlaka katika Kanisa yana agizo lake. Yaani, kuifundisha Injili na kuzitunza sakramenti. 13. Yasiachwe yavunje na kuingia katika ofisi nyingine, yasizihamishe milki za dunia, yasizibadilishe sheria za watawala wa nchi, yasiufute utii halali, yasiingilie hukumu, sheria au maafikiano ya nchi, na yasiwatengenezee watawala wa nchi sheria za kutengeneza miundo inayopaswa kuanzishwa na serikali. 14. Kristo anasema: “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu” (Yn. 18:36); 15. pia husema: “Ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?” (Lk. 12:14). Paulo pia aliandika katika Flp. 3:20: “Wenyeji wetu uko mbinguni,” na katika 2 Kor.10:4-5: “Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome,” na kadhalika.
18. Kwa hiyo, walimu wetu wanaionyesha tofauti kati ya wajibu wa mamlaka haya mawili kwa kuyaheshimu na kuyatambua kama zawadi na baraka za Mungu.
19. Iwapo maaskofu wana mamlaka ya upanga, nguvu hizo walizo nazo si kama maaskofu chini ya agizo la Injili, ila kwa sheria ya binadamu baada ya kuzipokea kutoka kwa wafalme na makaisari kwa madhumuni ya usimamizi wa serikali ya nchi yao. Lakini hii ni kazi nyingine mbali na huduma ya Injili.291
291 Wakati huo, maaskofu walikuwa watawala wa milki huko Ujerumani, walikuwa na mamlaka ya serikali katika mikoa yao. Akina Baba wa Matengenezo ya Kanisa walitaka kuyaweka mamlaka haya mbali kabisa na huduma ya kiroho ya maaskofu.
20. Hivyo basi, swali linapohusu utawala wa maaskofu, mamlaka ya nchi hayana budi kutofautishwa na mamlaka ya Kanisa. 21. Mara nyingine tena, kulingana na Injili – ama jinsi wasemavyo kwa haki ya kimungu - hakuna utawala ambao ni wa maaskofu kwa kuwa ni maaskofu - yaani, ni kwa wao waliokabidhiwa huduma ya Neno na sakramenti - isipokuwa kuisamehe dhambi, kuyakataza mafundisho yanayokwenda kinyume cha Injili, na kuwaondoa watu waovu kutoka ushirika wa Kanisa, ambao uovu wao unajulikana, wakiyafanya haya yote bila kuyatumia mamlaka ya binadamu ila tu kwa neno. 22. Makanisa yanalazimishwa na sheria ya kimungu kuwatii maaskofu sawasawa na inavyoonekana katika Lk. 10:16: “Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi.” 23. Lakini maaskofu wanapofundisha au kuamuru lolote kinyume cha Injili basi, hapo makanisa yana amri ya Mungu inayowakataza kutii, “Jihadharini na manabii wa uongo” (Mt. 7:15); 24. “Ijapokuwa . . .malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe” 25. (Gal.1:8); “Hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli,” 26.pia, “. . . uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa” (2 Kor. 13:8,10). 27. Ndivyo pia kanuni za Kanisa zinavyoamuru (II.Q. VII. Cap., Sacerdotes, na Cap. Oves).292
28. Naye Agostino (Contra Petiliani Epistolam): “Wala hatulazimiki kuwatii Maaskofu Wakatoliki293 wakidiriki kukosa, au kushikilia kitu chochote kinyume cha Maandiko Matakatifu ya Kanuni ya Mungu.”294
29. Iwapo maaskofu wana nguvu nyingine yoyote au mamlaka, katika kusikiliza na kuamua kesi kama za ndoa, matoleo ya zaka na kadhalika, wanazo kwa haki ya kibinadamu. Kawaida inaposhindikana, watawala wa mikoa wanalazimika, kutoa haki kwa raia wao kinyume na mapenzi yao ili kuweza kuilinda amani.
30. Licha ya hayo, kuna mabishano ikiwa kama maaskofu au wachungaji wana haki ya kuingiza sherehe kanisani, na kuitunga sheria juu ya vyakula, sikukuu, na vyeo, yaani, viwango vya wachungaji na kadhalika. 31. Wale wanaowapa maaskofu haki hii wanarejea ushuhuda huu, “Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote” (Yn. 16:12-13).
292 Gratiano (+ mnamo 1159) kutoka Italia, baba wa haki ya kanuni katika Kanisa la Magharibi. Aliyakusanya katika kitabu chake kiitwacho, ‘Concordia Discordantium Canonum’ takriban maandiko 4,000 mbalimbali kuhusu kanuni za Sheria ya Kanisa. Kitabu hiki kilikuwa msingi wa sheria ya Kanisa la Magharibi ‘Corpus Iuris Canonici.’
293 ‘Maaskofu Wakatoliki;’ maana yake: maaskofu wa Kanisa lote kinyume cha maaskofu Wadonatio, wakati wa farakano la Kidonatisti huko Kaskazini mwa Afrika katika karne ya 3 na 4.
294 Agostino, ‘De Unitate Ecclesiae,’ (‘Umoja wa Kanisa’). Kitabu hiki kilikuwa jibu la Agostino kwa waraka wa askofu Mdonatio aliyeitwa Petiliano.
32. Wao pia wanaurejea mfano wa mitume, waliowaamuru watu kukaa mbali na damu pamoja na vitu vilivyonyongwa (Mdo. 15:29). 33. Wanairejea kubadilishwa kwa siku ya Sabato kuwa Siku ya Bwana, kinyume cha Amri Kumi inavyoelezea. Wala hakuna mfano wowote wa kusisitiziwa kuliko huo wa badiliko la Sabato. Hivyo ndivyo wanavyoyasisitiza zaidi juu ya mamlaka ya Kanisa wanaposema kwamba, yana nguvu kubwa, kwa kuwa yameitangua mojawapo ya Amri Kumi!
34. Kuhusu swali hili, walimu wetu wanadai, jinsi ilivyoonyeshwa hapo juu kwamba, maaskofu hawana nguvu ya kutoa amri yoyote kinyume cha Injili. Kanuni za Kanisa zinafundisha jambo hilo hilo (Dist. IX). 35. Sasa, ni kinyume cha Maandiko Matakatifu kuyaweka au kudai kuyafuata mapokeo yoyote makusudi kwamba, kwa ufuasi wa jinsi hiyo, tuweze kufanya fidia ya dhambi au kustahili kuhesabiwa haki. 36. Kwa maana utukufu wa ustahili wa Kristo unaumizwa tunapofikiria kwamba, tunahesabiwa haki kwa desturi ya namna hiyo. 37. Lakini ni wazi kwamba, kwa imani ya jinsi hiyo, mapokeo yameongezeka kanisani kupita kiasi, wakati mafundisho kuhusu imani pamoja na haki vipatikanavyo kwa imani vinakandamizwa. Kwa maana muda baada ya muda sikukuu zaidi ziliteuliwa, kufunga kuliagizwa, sherehe na madaraja mapya yalianzishwa kwa kuwa waanzilishi wa vitu vya aina hii walidhania kwamba, kwa matendo haya, wangepata kustahili neema. 38. Hivyo basi, siku zilizopita, kanuni za toba ziliongezeka na bado tunaweza kuziona baadhi ya dalili hizo zinazoonekana kidogo katika kanuni za ridhaa.
39. Tena, watengenezaji wa mapokeo wanakwenda kinyume cha amri za Mungu wanapozihusisha dhambi na vyakula, siku na mambo ya aina hiyo, na kulitwika utumwa wa sheria kana kwamba, ni lazima miongoni mwa Wakristo. Ili kustahili kuhesabiwa haki, ibada kama ya Kilawi ziwepo kana kwamba, utaratibu wake ulikabidhiwa na Mungu kwa Mitume na maaskofu. 40. Ndiyo sababu baadhi yao wanaandika: kwa kiwango fulani, Makuhani Wakuu wa Roma, wanaelekea kupotoshwa na Sheria ya Musa. 41. Hivyo, inakuwa ni mizigo kama wanaifanya kuwa dhambi ya mauti hata bila kuwaudhi wengine kama vile, kuzifanya kazi za mikono siku za sikukuu ni dhambi ya mauti, vyakula fulani vinachafua dhamiri, mafungu mengine yasiyokuwa ya asili lakini yaliyobuniwa ni kazi zinazompendeza Mungu, ni dhambi ya mauti kuziruka saa zilizopangiwa sala katika kanuni295 kwamba, dhambi iliyohusu kesi iliyofichwa haiwezi kusamehewa isipokuwa na aliyeisitiri, wakati Kanuni zenyewe zinazungumzia tu
295 Saa saba au nane zilizopangiwa sala za kanuni kwa wamonaki na wengine: ‘matutina’ na ‘laudes’ (alfajiri), ‘ad primam’ na ‘ad tertiam’ ( saa moja na saa tatu asubuhi), ‘ad sextam’ (adhuhuri), ‘ad nonam’ (saa tisa za alasiri), ‘vesper’ (jioni), ‘completorium’ (usiku)
kusitiriwa kwa adhabu ya Kanisa na wala hazizungumzii kusitiriwa kwa hatia.296
42. Maaskofu wamepata wapi haki ya kulitwika Kanisa mapokeo haya na kuiwekea dhamiri mizigo wakati Mt. Petro anakataza kuiweka nira kwenye shingo za wanafunzi (Mdo. 15:10), na Mt. Paulo anasema katika 2 Kor. 13:10, kwamba, mamlaka aliyopewa ni kwa ajili ya maongozi mema, na si kwa kuumiza? Kwa nini basi, wanaiongeza dhambi katika mapokeo haya?
43. Lakini kuna shuhuda za wazi zinazokataza uundaji wa mapokeo kama hayo, kwa makusudi ya kumridhisha Mungu au kana kwamba, yalikuwa ya lazima kwa wokovu. 44. Katika Kol. 2:16-23, Paulo anasema: “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato . . . 45. Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani. Msishike, msionje, msiguse; mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa; hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima.” 46. Pia katika Tito 1:14, Paulo anasema: “Wasizikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu wajiepushao na yaliyo kweli.”
47. Kuhusu hao wanaodai mapokeo, Kristo anasema katika Mt. 15:14: “Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu.” 48. Huzikemea ibada hizo, akisema: “Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa” (Mt. 15:13).
49. Iwapo maaskofu wana haki ya kuyalemeza makanisa kwa mapokeo ya jinsi hiyo, kwa nini Maandiko Matakatifu mara nyingi hukataza utungwaji wa mapokeo? Kwa nini yanayaita “mafundisho ya mashetani?” (1 Tim. 4:1). Je, Roho Mtakatifu aliifanya kazi ya bure kuyatoa maonyo dhidi ya mambo haya?
50. Kwa kuwa basi, sheria ziliwekwa kana kwamba ni za lazima, au ziliwekwa ili kustahili neema, ni kinyume cha Injili. Inamaana kwamba, si halali kwa askofu yeyote kuanzisha au kuzidai ibada kama hizo kana kwamba, ni za lazima. 51. Fundisho kuhusu uhuru wa Kikristo lazima lihifadhiwe katika makanisa, ili iwe wazi kwamba, utumwa wa sheria si jambo la lazima kwa kuhesabiwa haki, 52. jinsi ilivyoandikwa katika Waraka kwa Wagalatia: “Wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa” (Gal. 5:1). Ni lazima kabisa kwamba, fundisho kuu la Injili lihifadhiwe. Yaani, tunaipokea neema bure kwa imani katika Kristo na si kwa kuyafuata mambo fulani au matendo ya ibada yaliyobuniwa na watu.
296 Kulingana na sheria ya Kanuni za Kanisa ‘Lex canonica,’ Kuhani Mkuu wa Roma au maaskofu peke yao ndio waliruhusiwa kulitangaza ondoleo la dhambi fulani fulani.
53. Hivyo basi, tufikirie nini kuhusu Jumapili na mambo mengine ya dini yanayofanywa ndani ya nyumba ya Mungu? Jibu: ni halali kwa maaskofu au wachungaji kupanga kanuni za kufuatwa ili mambo yafanyike kwa utaratibu katika Kanisa; lakini si kwamba kwa njia hiyo, tuweze kustahili neema au kufidia dhambi, au dhamiri zilazimike kuzihesabu kuwa ibada za lazima. 54. Hivyo, Paulo anaagiza: “Wanawake wafunike vichwa vyao wakati wa mkutano wa ibada” (1 Kor. 11:5). Katika 1 Kor.14:30 pia anasema kwamba: “Watafsiri waseme kwa utaratibu ndani ya Kanisa,” yaani, mmoja baada ya mwingine.
55. Ni vyema kama makanisa yatayafuata maagizo kama hayo kwa ajili ya upendo na utulivu, na wayashike mradi mtu asimkwaze mwingine, ili mambo yote yafanyike kwa uzuri na kwa utaratibu katika Kanisa na bila fujo (1 Kor.14:40; linganisha na Flp. 2:14). 56. Lakini dhamiri zisilemezwe kwa kusadikishwa kwamba, ni lazima kwa wokovu, au kuamua kwamba, wanaoyaacha maagizo haya bila kuwakwaza wengine wanatenda dhambi. Hakuna asemaye kwamba, mwanamke hutenda dhambi akitembea hadharani bila kukifunika kichwa chake.
57. Sawa na desturi za kuitunza Siku ya Bwana (Jumapili), Pasaka, Pentekoste, pamoja na sikukuu nyinginezo na matambiko mengine ya ibada sawa na mambo ya aina hii. 58. Hao wanaodai kwamba, kwa mamlaka ya Kanisa, kuiadhimisha Siku ya Bwana badala ya Siku ya Sabato kuliagizwa kama jambo la lazima, wanakosea. 59. Ni Maandiko Matakatifu yaliyoitangua Siku ya Sabato na si Kanisa. 60. Kwa kuwa, ilikuwa lazima kuiweka siku fulani ili watu wajue ni lini wanapaswa kukusanyika pamoja. Inaelekea kwamba, Kanisa liliichagua Siku ya Bwana kwa kusudi hili. Siku hii inaelekea kuwa imechaguliwa pia kwa sababu ya ziada kwamba, watu wawe na mfano wa uhuru wa Kikristo, na wapate kujua kwamba, si lazima kuitunza Siku ya Sabato au siku nyingine.
61. Kuna majadiliano mabaya mno yanayohusu ubadilishaji wa sheria, sherehe za sheria mpya, kubadilishwa kwa siku ya Sabato ambayo yote yalianzia kwenye imani potovu kwamba, ni lazima kuwa na ibada kama ile ya Kilawi kanisani na kwamba, Kristo aliwaagiza mitume na maaskofu kuzibuni sherehe mpya ambazo zingekuwa za lazima kwa wokovu. 62. Makosa haya yaliingia kanisani polepole wakati haki ya imani haikufundishwa kwa uwazi ulivyostahili. 63. Wengine wanadai kwamba, kuiadhimisha Siku ya Bwana si sharti la kimungu hasa ila ni kama lilikuwa sharti la kimungu na wanaelezea ni kiasi gani cha kazi kinachoweza kufanywa wakati wa sikukuu takatifu. 64. Mabishano hayo yanaweza kuwa lipi lingine isipokuwa mtego wa dhamiri? Kwa maana ijapokuwa wanajitahidi kuyawekea mapokeo mabadiliko madogomadogo, hata hivyo, manufaa yake hayawezi kufaulu iwapo maoni yanaendelea kubaki kwamba, maadhimisho ni
ya lazima. Wazo hili lazima libakie pale ambapo haki ya imani na Uhuru wa Kikristo havijulikani.
65. Mitume waliamuru kwamba, mtu aiepuke damu (Mdo. 15:20). Nani alifuataye agizo hili leo? Wasiolifuata hawatendi dhambi kwa maana mitume wenyewe hawakutaka kuzibebesha dhamiri utumwa wa aina hiyo, lakini waliukataza ulaji huo kwa muda ili kukiepuka kikwazo.297 Kuhusu agizo hilo, inakuwa lazima mtu azingatie lengo la kudumu la Injili ni lipi.
67. Ni vigumu sana kudai kwamba, kanuni yoyote inafuatwa kikamilifu na siku kwa siku zinatoweka hata miongoni mwa wanaoyatetea mapokeo. 68. Wala dhamiri haziwezi kutunzwa bila uboreshwaji huo kwamba, tunajua kuwa, kanuni zinafuatwa bila kuzihesabu kuwa za lazima na kwamba, hakuna madhara yanayozipata dhamiri hata wakati mapokeo yanaacha kutumiwa kwa kutokuwa na sababu ya kuyatumia.
69. Maaskofu wangeweza kuudumisha utiifu wa watu kwa urahisi kama wasingeng’ang’ana mapokeo yafuatwe ambayo hayawezi tena kufuatwa kwa dhamiri nzuri. 70. Sasa, wanauamuru useja, hawamkaribishi yeyote katika huduma yao asiyeapa kuwa hatafundisha mafundisho halisi ya Injili. 71. Makanisa hayamaanishi kuwataka maaskofu kuuleta tena umoja kwa kuyatoa mhanga heshima yao, jambo ambalo hata hivyo, ni halali kwa wachungaji wema kulifanya. 72. Lakini, yanawaomba tu waiondolee mbali mizigo ya udhalimu ambayo ni mipya na imepokelewa kinyume cha mazoea ya Kanisa Katoliki. 73. Inaweza kuwa kwamba, mwanzoni iliwezekana kuwepo sababu za kukubalika kwa ajili ya baadhi ya kanuni hizi na bado hazijarekebishwa ili zifae kuendana na nyakati za baadaye. 74. Ni wazi pia kwamba, kanuni kadha wa kadha ziliingizwa kimakosa. Ingefaa huruma ya maaskofu iyatulize mapokeo makali sasa kwa sababu mabadiliko ya jinsi hiyo hayawezi kuudhoofisha umoja wa Kanisa. Kwa maana mapokeo mengi ya binadamu yamebadilishwa jinsi wakati unavyopita jinsi kanuni zenyewe zinavyoonyesha. 75. Lakini ikiwa haiwezekani kuupunguza ufuasi wa kanuni ambao hauwezi kufanyika bila dhambi, tunalazimika kulifuata agizo la mitume, linalotuamuru, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu” (Mdo. 5:29).
76. Petro anawakataza maaskofu kuwa mabwana na kuyatawala makanisa hivyo (1 Pet. 5:3). 77. Si kusudi letu kwamba, maaskofu wayaache mamlaka yao
297 Kulingana na Martin Luther, kusudi la amri hii ya upendo wa Kikristo lilikuwa kuyazuia mabishano kati ya Wakristo Wayahudi na Wakristo wa Mataifa katika ibada na sherehe za Kanisa ili Wakristo wa Mataifa wasiwakwaze, kwa vyakula vyao. Wakristo Wayahudi waliozishika amri za Musa kuhusu kutokula damu (‘Von Konziliis und Kirchen’ – “Sinodi na Makanisa,” 1539).
ya kutawala, lakini hili moja tunaliomba kwamba, wairuhusu Injili ifundishwe kwa usahihi na kwamba, waulegeze ufuasi wa hapa na pale ambao hauwezi kufuatwa bila dhambi. 78. Lakini wasipokubali lolote, inakuwa jukumu lao kuona namna watakavyojieleza mbele za Mungu kwa kuuleta msingi wa farakano kwa ujeuri wao.
XXVIII. Mamlaka ya Maaskofu G298
1. Mambo kadhaa na mengi yaliandikwa nyakati za zamani kuhusu mamlaka ya maaskofu. Baadhi ya waandishi hawa walichanganya vibaya mamlaka ya maaskofu na mamlaka ya upanga. 2. Kutokana na mkanganyiko huu, vita vingi vikali, uasi na taharuki vilitokea kwa sababu ya maaskofu, kwa kisingizio cha mamlaka waliyopewa na Kristo, hawakuanzisha tu aina mpya za ibada na kuzisumbua dhamiri kwa mamlaka ya kesi zilizohifadhiwa299 na kwa adhabu kubwa na jeuri za kutengwa na Kanisa. Isitoshe, walithubutu hata kuweka na kuondosha madarakani wafalme na makaisari kwa hiari yao. 3. Ukatili wa jinsi hiyo ulilaumiwa kwa muda mrefu na wataalamu na wacha Mungu katika Ukristo. 4. Kwa hiyo, wenzetu hawakuwa na budi kuelezea tofauti kati ya mamlaka ya kiroho na mamlaka ya kidunia, kati ya upanga na madaraka ya kiroho na kidunia kwa ajili ya faraja ya dhamiri. Wamefundisha kwamba, madaraka na mamlaka viheshimiwe na vithaminiwe kwa uchaji wote kwa ajili ya agizo la Mungu kama zawadi kuu mbili za Mungu hapa duniani.
5. Basi, wenzetu hufundisha kwamba, mamlaka ya ufunguo au mamlaka ya maaskofu yanalingana na Injili, mamlaka na agizo la Mungu kuihubiri Injili, kusamehe na kufunga dhambi, kuzitunuku na kuzitunza sakramenti. 6. Kwa kuwa Kristo aliwatuma mitume wake kwa agizo hili katika Yn. 20: 21-23: “Kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi . . . Pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.”
8. Mamlaka haya ya funguo au ya maaskofu yanatumiwa na kutendeka tu kwa mafundisho na mahubiri ya Neno la Mungu kwa kutoa sakramenti300 kwa watu wengi au kwa mtu binafsi kulingana na wito wake. Kwa hiyo, mambo na vitu vya mielele si vipawa vya kimwili vinavyogawanywa, yaani, haki ya milele, Roho Mtakatifu na uzima wa milele. 9. Vipawa hivi haviwezi kupokelewa isipokuwa
298 Andiko la Kijerumani: ‘Von der Bischofen gewalt,’ yaani, “mamlaka ya maaskofu.”
299 Kilatini: ‘Reservatio casuum.’ Kanisa la Roma linafundisha kwamba, katika kesi maalumu za ungamo la dhambi, ondoleo la dhambi linahifadhiwa kwa maaskofu au kwa Papa wa Roma.
300 Andiko la Kijerumani: ‘mit Handreichung der Sakramente,’ yaani, “kwa mkono.”
kwa njia ya ofisi ya mahubiri na ugawaji wa sakramenti. Naam, Mtakatifu Paulo anasema: “Injili . . . ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye.”301 10. Kwa kuwa mamlaka katika makanisa au mamlaka ya maaskofu yanatupatia mali za milele na kwa njia ya utendaji wa ofisi ya mahubiri peke yake, mamlaka haya hayajiingizi popote katika serikali au mamlaka ya dunia. 11. Mamlaka ya dunia inahusika na mambo tofauti kuliko Injili. Mamlaka ya dunia hailindi roho, lakini kwa upanga na adhabu za kimwili inalinda mwili na vitu kutoka katika nguvu za wengine.
12. Kwa hiyo, mamlaka hizi mbili,302 yaani, mamlaka ya kiroho na ya dunia, zisichanganywe na zisiwekwe pamoja. Mamlaka ya kiroho ina agizo lake la kuihubiri Injili na kutoa sakramenti. 13. Kwa hiyo, mamlaka hizi zisiingilie madaraka ya ofisi nyingine kwa njia ya kuweka na kuwaondoa wafalme madarakani, yasibatilishe sheria kuhusu mambo ya dunia. 14. Kristo mwenyewe alivyokwisha kusema: “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu.”303 15. Kadhalika, “Ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?” (Lk. 12:14). Katika Wafilipi 3:20, 16. Mtakatifu Paulo anasema pia: “Wenyeji wetu uko mbinnguni.” 17. Katika 2 Kor. 10:4-5: “Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome . . . na kila kitu . . . kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu.”
18. Hivyo, wenzetu hutofautisha kati ya mamlaka na kazi za madaraka hayo mawili na kuelekezea kwamba, yote mawili yaheshimiwe kama vipawa vikuu vya Mungu hapa duniani.
19. Katika hali ambapo maaskofu wamepokea madaraka ya dunia na upanga, wanaendelea kumiliki si kama maaskofu kulingana na haki ya kimungu, bali kulingana na haki ya kibinadamu ya kifalme, waliyokabidhiwa madaraka haya na makaisari na wafalme wa Roma kwa shabaha ya maongozi ya dunia ya maeneo yao. Ofisi hii ni tofauti kabisa na ofisi ya Injili.
21. Kulingana na haki ya kimungu ofisi ya askofu ndiyo ofisi ya kuihubiri Injili, kusamehe dhambi, kuhukumu juu ya mafundisho, na kukataa mafundisho yaliyo kinyume cha Injili na kuwaondoa katika usharika wa Kikristo watu wasiomcha Mungu ambao hujulikana wazi katika uovu wao. Haya yote yafanywe kwa nguvu za Neno la Mungu pekee na sio ya binadamu. 22. Wachungaji na makanisa yanawajibika kuwatii maaskofu kulingana na neno la Kristo katika Luka 10:16: “Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi.” 23. Lakini pale ambapo maaskofu
301 Rum. 1: 16.
302 Kijerumani: ‘Regiment.‘
303 Yn. 18: 36.
hufundisha, huweka na kuanzisha lolote kinyume na Injili, katika tokeo hili, sisi tuna agizo la Mungu kwamba, hatupaswi kuwatii, jinsi ilivyo katika Mt. 7:15: “Jihadharani na manabii wa uongo.” 24. Mtakatifu Paulo anaandika pia katika Gal. 1:8: “Ijapokuwa . . . malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi Injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.” 25. Kadhalika anaandika katika 2 Kor. 13:8: “Hatuwezi kutenda neno lo lote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli.” 26. Isitoshe, katika aya ya kumi anasema: “Uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.” 27. Sheria ya kanuni inadai jambo hilo hilo katika 2, q. 7, sura ya “Sacerdotes” na katika sura ya “Oves.”304 28. Mtakatifu Agostino anaandika katika waraka wake dhidi ya Petiliano kwamba, watu wasifuate hata maaskofu waliochaguliwa kulingana na uratatibu wa kanuni kama watakosa au watafundisha au kulianzisha lolote kinyume na Maandiko Matakatifu.
29. Maaskofu wakiwa na mamlaka na utendaji wa sheria katika mambo fulani kama mambo ya ndoa na zaka, watapokea mamlaka haya kulingana na haki ya binadamu. Hata hivyo, maaskofu wakizembea wajibu wao wa ofisi, watawala watawajibika, wapende wasipende kulazimika kutoa haki kwa raia kwa ajili ya amani na ili kuzuia mifarakano na machafuko makubwa katika nchi zao.
30. Licha ya hayo, kuna mabishano iwapo maaskofu wana mamlaka ya kuanzisha kaida katika makanisa au kuanzisha kanuni kuhusu vyakula, sikukuu, na madaraja mbalimbali ya watumishi wa Kanisa. Ambao wanakubaliana na mamlaka ya jinsi hiyo ya maaskofu, wanaurejea msemo wa Kristo katika Yn. 16: 12,13: “Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote.” Pamoja na haya, wanataja mfano kutoka Matendo ya Mitume 15: 20,29, ambapo palikatazwa kula damu na nyama ya wanyama walionyongwa. Isitoshe, wao hukata rufaa kwa tendo la kuibadilisha Sabato iwe Jumapili jinsi wasemavyo, ni kinyume cha Amri Kumi za Mungu. Hakuna jambo lingine lolote linalokatiwa rufaa na kusisitizwa sana kwa msisitizo kama ubadilishaji wa Sabato, ambao kwao, wanataka kusisitiza kwamba, mamlaka ya Kanisa ndiyo makubwa kwa sababu Kanisa liliachana nakubadilisha sehemu ya Amri Kumi za Mungu.
34. Wenzetu wanafundisha kuhusu suala hili kwamba, maaskofu hawana mamlaka kuamuru au kuanzisha lolote kinyume na Injili, jinsi ilivyoonyeshwa hapo juu na jinsi haki ya kanuni inavyofundisha katika sehemu nzima ya
304 Decr. Grat. P. 2. q. 7 c. 8. na c. 13.
Utofautishaji wa Tisa.305 35. Ni kinyume kabisa cha Agizo la Mungu na Neno lake kuzitunga sheria kutokana na maoni yetu wenyewe au kudai zifuatwe ili kufanya ridhaa kwa ajili ya dhambi na kuipata neema. 36. Utukufu wa ustahili wa Kristo unakufuriwa wakati tunadhania kustahili neema kwa amri kama hizo. 37. Inajulikana wazi kabisa kwamba, maagizo ya binadamu yameongezeka bila kipimo katika Ukristo wote wakati mafundisho kuhusu imani na haki ya imani yalikuwa karibu kukomeshwa. 38. Karibu kila siku, sikukuu mpya, mifungo mipya, kaida mpya, na ibada mpya za watakatifu ziliagizwa ili neema na mema yote yastahilishwe kwa matendo ya jinsi hiyo.
39. Kadhalika, wanaoanzisha maagizo ya kibinadamu, wanafanya hivyo kinyume cha Agizo la Mungu wanapoihusisha dhambi na vyakula, sikukuu na mambo kama haya. Isitoshe, wanausumbua Ukristo kwa utumwa wa sheria kana kwamba, ibada ya jinsi hiyo lazima ipatikane miongoni mwa Wakristo kwa shabaha ya kuistahili neema ya Mungu. Jinsi wengine walivyoandika, ibada hii inayofanana na ibada ya Kilawi, ilianzishwa na Mungu na jinsi wanavyodai iliamriwa naye kwa mitume na maaskofu. 40. Inapasa kuaminika kwamba, maaskofu fulani walikuwa wamedanganya kwa mfano wa Torati ya Musa. 41. Maagizo yaliendelea kuongezeka bila kikomo kana kwamba, itakuwa dhambi ya mauti mtu akifanya kazi ya mikono wakati wa sikukuu hata bila kashfa yoyote kwa watu wengine, itakuwa dhambi ya mauti mtu akipuuza kuhudhuria sala saba za kanuni, kwamba vyakula fulani vingeweza kuichafua dhamiri, kwamba kufunga ni kazi ambayo kwayo Mungu hupatanishwa na kana kwamba, katika kesi306 inayohifadhiwa, dhambi haiwezi kusamehewa. Lazima kumtafuta mtu mwenye mamlaka ya kesi ya jinsi hiyo mbali na hakika kwamba, haki ya kanuni haisemi lolote kuhusu kuhifadhiwa kwa hatia bali kuhusu kuhifadhiwa kwa adhabu ya marudi.
42. Maaskofu walipata wapi haki na nguvu kuulazimishia Ukristo kwa madai ya jinsi hiyo ya kuziumiza dhamiri za watu? Katika Mdo. 15, 10 Mtakatifu Petro anakataza kuweka nira juu ya shingo za wanafunzi. Mtakatifu Paulo anasema kwa Wakorintho kwamba, mamlaka yaliyotolewa ni ya kujenga wala si ya kubomoa. Basi, mbona wao huongezea dhambi kwa madai kama hayo?
43. Hata hivyo, kuna kauli wazi za Maandiko Matakatifu zinapatikana zinazokataa kabisa kuweka madai hayo kwa shabaha ya kuistahili neema ya Mungu au kama kuwa ya lazima kwa wokovu. 44. Hivyo, Mtakatifu Paulo anasema katika Ko. 2:16: “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au
305 Decr. Grat. 1, d. 9. c. 8 sqq. ‘Utofautishaji,’ katika Kilatini: ‘distinctio.’ 306 Kilatini: ‘reservatio casuum.’
vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.” 45. Tena katika Kol. 2: 20-23 anasema: “Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani. Msishike, msionje, msiguse, mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa; hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo haya yote yanaonekana kana kwamba yana hekima.” 46. Vile vile katika Tito 1:14 Mtakatifu Paulo anakataa kusikiliza hadithi za Wayahudi, wala maagizo ya watu yajiepushao na kweli.
47. Kristo mwenyewe anasema hivi katika Mt. 15:14 kuhusu wanaojenga juu ya maagizo ya binadamu: “Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu.” Anakataa ibada za jinsi hiyo katika Mt. 15:13: “Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.”
49. Iwapo maaskofu wana mamlaka ya kuyatwika makanisa mizigo kwa maagizo yasiyopimika na kuzisumbua dhamiri, basi, kwa nini Maandiko ya Kimungu mara kwa mara yatakataa kuyatengeneza na kuyashika maagizo ya binadamu? Kwa nini maandiko haya yanayaita mafundisho ya jinsi hiyo mafundisho ya mashetani? Je, inawezekana kwamba, Roho Mtakatifu alionya dhidi ya mambo haya bure tu?
50. Kwa vile maagizo hayo yamewekwa kuwa ya lazima ili kumpatanisha Mungu na kuistahili neema, ni kinyume na Injili kabisa, maaskofu hawapaswi kudai ibada za jinsi hiyo. 51. Ni lazima kuyahifadhi mafundisho kuhusu uhuru wa Kikristo katika Ukristo, yaani, kwamba, utumwa wa sheria si lazima kwa kuhesabiwa haki. 52. Katika Gal. 5:1 Mtakatifu Paulo anaandika: “Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.” Fungu kuu la Injili lazima lihifadhiwe, yaani, kwamba sisi tunaipokea neema ya Mungu kwa njia ya imani katika Kristo bila stahili zetu wenyewe. Hatuwezi kustahili neema kwa ibada zetu zilizoanzishwa na wanadamu.
53. Basi, tufikiri nini kuhusu Jumapili na kanuni na taratibu zingine za kanisa? Wenzetu hujibu kwamba, maaskofu au wachungaji wanaweza kuyapanga mambo ili yote yaweze kufanyika kwa utaratibu mzuri katika Kanisa. Lakini shabaha ya utaratibu huo si kuipokea neema ya Mungu au kuziridhisha dhambi au kuzifunga dhamiri kwao kana kwamba ibada hizo ni za lazima hata kuhesabu kwamba, kutozijali ibada za jinsi hiyo ni kutenda dhambi. Hata hivyo, kufanyike bila kashfa zozote. 54. Katika 1 Kor. 11:5 Mtakatifu Paulo anaelekeza kwamba, wanawake
wanafaa kuvifunika vichwa vyao wakiwa kwenye ushirika. Anaelekeza pia kwamba, wahubiri wasiongee wote pamoja katika mkutano wa ushirika bali kwa utaratibu mzuri, mmoja baada ya mwingine.
55. Ushirika wa Kikristo unafaa kuudumisha utaratibu wa jinsi hiyo kwa ajili ya upendo na amani na Wakristo wanapaswa kuwatii maaskofu na wachungaji katika mambo haya na kuyafuata ili mtu mmoja asimkasirishe mwingine ili kusiwe na machafuko au mwenendo usiofaa katika kanisa. 56. Lakini dhamiri zisisumbuliwe na madai kwamba, mambo hayo ni ya lazima kwa wokovu, kana kwamba, watenda dhambi wangevunja mojawapo bila kashfa yoyote kwani hakuna yeyote angesema kwamba, mwanamke aliyefanya dhambi bila hatia yoyote angeenda nje bila kukifunika kichwa chake.
57. Hali kadhalika, ni uzingatifu wa Jumapili, Pasaka na sherehe na desturi za aina hiyo. 58. Ambao hudhania kwamba, Jumapili ilipangwa badala ya Sabato kuwa ya lazima, wao hukosea vibaya, 59. kwa sababu Maandiko Matakatifu yaliitangua Sabato na yanafundisha kwamba, baada ya ufunuo wa Injili, taratibu zote za Agano la Kale zinaweza kuachwa. 60. Hata hivyo, kwa sababu ilikuwa lazima kuichagua siku fulani ili watu wajue ni lini walipaswa kukutana, Kanisa la Kikristo lilichagua Jumapili kwa shabaha hiyo. Mabadiliko haya yalilipendeza na kulifurahia zaidi kwa kuwa watu walipata mfano wa uhuru wa Kikristo ili wajue kwamba, si uzingatifu wa Sabato wala wa siku nyingine ambao ni wa lazima.
61. Majadiliano mengi yasiyokuwa halisi yalitokea kuhusu ubadilishaji wa sheria, taratibu za Agano Jipya na kubadilishwa kwa Sabato. Mambo haya yote ni maoni ya uzushi na yenye makosa, kwamba Ukristo hauna budi kuwa na ibada kulingana na ibada ya Walawi au ya Wayahudi na kwamba, Kristo angeamuru mitume na maaskofu kubuni taratibu mpya ambazo zingekuwa za lazima kwa wokovu. 62. Makosa haya yaliingizwa katika jumuiya ya Ukristo wakati haki ya imani haikufundishwa na kuhibiriwa kwa uwazi na usanifu. 63. Wengine wanadai kwamba, ingawa Jumapili haiadhimishwi kulingana na haki kimungu, hata hivyo, iadhimishwe kama inayoikaribia haki ya kimungu. Wanashauri namna na kiasi cha kazi inayoweza kufanywa siku ya mapumziko. 64. Ni nini majadiliano ya jinsi hiyo isipokuwa mitego ya dhamiri? Ingawa wanajitokeza kung’arisha na kupunguza maagizo ya kibinadamu, hakuna kiasi307 au urahisishaji wakati maoni haya yanadumu na kubaki kwamba, uzingatiaji wake ni wa lazima. Lazima maoni haya yatadumu ilimradi uelewano kuhusu haki ya imani na uhuru wa Kikristo.
307 Kijerumani: ‘epieikeia’ kulingana na neno la Kiyunani: ‘επιεικεια.’
65. Mitume waliagiza kwamba, mtu ajiepushe na damu na nyama ya wanyama walionyongwa. Sasa, ni nani anayelifuata katazo hili? Ambao hawalifuati hawatendi dhambi kwa maana mitume wenyewe hawakutaka kuzibebesha dhamiri utumwa wa aina hiyo, lakini walikataza ulaji kwa muda ili kuzuia kikwazo. 66. Lazima kuangalia sehemu kuu ya mafundisho ya Kikristo katika agizo hili. Sehemu hii kuu haitatanguliwa nalo.308
67. Ni kwa nadra sana, kanuni hata moja ya zamani inafuatwa kikamilifu. Maagizo mengi yanatelekezwa siku kwa siku hata katika maisha ya wanaoyafuata kwa bidii sana. 68. Haiwezekani kushauri au kusaidia dhamiri isipokuwa kwa njia ya kuyang’arisha maagizo haya ili watu waelewe kwamba, maagizo hayo yasitazamwe kuwa ya lazima na hata kuyapuuza hakudhuru dhamiri.
69. Maaskofu wangeweza kudumisha utiifu wa watu kwa urahisi kama hawangesisitiza uzingatiaji wa maagizo hayo amabayo hayawezi kuhifadhika bila dhambi. 70. Wao wanatoa Sakramenti kwa namna moja na hukataa aina zote mbili za Sakramenti Takatifu. Wanazikataa ndoa za makasisi na hawamruhusu yeyote katika huduma takatifu isipokuwa baada ya kiapo cha kutohubiri mafundisho haya ambayo, bila shaka, yanafuata Injili Takatifu. 71. Makanisa miongoni mwetu hayaombi kwamba, maaskofu wahifadhi amani na umoja kwa hasara ya heshima na cheo chao. Hata hivyo, maaskofu hufanya hivyo katika hali ya dharura. 72. Makanisa miongoni mwetu yanaomba tu kwamba, maaskofu wapunguze mizigo fulani isiyo na maana, isiyopatikana katika Kanisa nyakati za kale. Mizigo hii iliingizwa kanisani dhidi ya mapokeo ya makanisa ya Kikristo. 73. Labda mizigo hii ilikuwa na maana fulani ya kuingizwa katika Kanisa lakini haina maana wakati wetu. 74. Wala haiwezi kukanushwa kwamba, maagizo mengine yalikubaliwa kwa ajili ya ujinga. Kulingana na hayo, maaskofu wanapaswa kuwa wenye fadhila hata kuyapunguza maagizo haya, hasa kama mabadaliko yaliyodaiwa hayavunji umoja wa makanisa ya Kikristo. Naam, maagizo mengi ya binadamu yalitelekezwa katika matumizi na si lazima jinsi haki ya Kipapa yenyewe inavyoshuhudia.309 75. Hata hivyo, kama hii haiwezekani, kama hawataweza kushawishika kupunguza au kutangua maagizo ya binadamu ambayo hayawezi kufuatwa bila dhambi, hatuna budi kuifuata kanuni ya mitume inayotuamuru kumtii Mungu kuliko wanadamu.310
76. Mtakatifu Petro anawakataza maaskofu kutawala kwa ubwana311 kana kwamba, wana madaraka ya kuyashurutisha makanisa kulingana na nia zao. 77.
308 Mdo. 15: 23-29.
309 K.m. kanuni kuhusu toba.
310 Mdo. 5: 29.
311 1 Pet. 5: 2.
Hatuna kusudi la kutafuta njia za kuwapokonya maaskofu madaraka yao. Badala yake, inatakiwa na inaombwa kwamba, wasitushurutishe kutenda dhambi. 78. Wasipotaka kufanya hivyo au wakilidharau ombi letu, waacheni wafikiri jinsi watalazimishwa kumtolea majibu mbele ya macho ya Mungu, kwani kwa ukaidi wao, watasababisha mifarakano na utengano, ambavyo kwa kweli wanapaswa kusaidia kuvizuia.
Hitimisho L
1. Sasa, tumeyasimulia mafungu makuu ambayo yanaonekana kuwa ya ubishi. 2. Maana, ijapokuwa shutuma zaidi zingetajwa ili kuepuka kuurefusha wakati, tumeyaonyesha mambo muhimu ambayo yanaweza kuonekana kama msingi wa mengine. Pamekuwapo na manung’uniko mengi kuhusu vyeti vya upatanisho,312 kuenda hija, na kutumia vibaya mamlaka ya kuwatenga watu na Kanisa. Sharika zimesumbuliwa vibaya na wahubiri wanaoviuza vyeti vya upatanisho.313 Kulikuwako na mashindano yasiyokuwa na mwisho kati ya wachungaji na wamonaki kuhusu haki za mitaa, sharika, toba, mazishi, na mengine mengi yasiyoweza kuorodheshwa. 3. Tumeyaruka mambo ya aina hii. Hivyo, yaliyo muhimu katika jambo hili, baada ya kuelezwa kwa ufupi, yanaweza kueleweka kwa urahisi zaidi. 4. Hakuna lililosemwa au lililohusishwa hapa kwa lengo la kumshutumu yeyote. 5. Ni mambo hayo yaliyoelezewa tu, tuliyoyafikiria kuwa lazima yasemwe kusudi yaeleweke kwamba, katika mafundisho na sherehe, hakuna lililopokelewa kwa upande wetu kinyume cha Maandiko Matakatifu au Kanisa Katoliki. Kwa maana ni wazi kwamba, tumekuwa waangalifu mno kuyazuia mafundisho mapya na yasiyokuwa ya kimungu kuruhusiwa kunyemelea na kuingia ndani ya makanisa yetu.
6. Hivyo, tunataka kuyaweka mbele mafungu ya hapo juu kulingana na amri yako Enzi Yako Kaisari, ili kulionyesha ungamo letu na watu wapate kuuona
312 ‘Cheti cha Utapatanisho,’ Kilatini: ‘indulgentia:’ Akina Baba wa Matengenezo ya Kanisa waliyapinga mafundisho ya Roma kuhusu toba. Waliozitubu dhambi zao walisamehewa dhambi kwa neema ya Mungu na kwa ajili ya upatanisho wa Yesu Kristo. Licha ya hayo, mkosaji alihitajika kuutoa upatanisho wa matokeo ya dhambi zake kuhusu hatia ya muda pia. Kulingana na mafundisho ya Roma, mkosaji aliipatanisha sehemu ya matokeo ya dhambi zake kwa njia ya kuufanya ubia pamoja na neema ya Mungu. Katika kazi hii, alisaidiwa na Kanisa lililoweza kuitumia hazina ya stahili za Kristo na watakatifu wote (Kilatini: ‘thesaurus ecclesiae) kwa faida ya waliozitubu dhambi zao. Wakati huo, akina Papa wa Roma waliviuza vyeti vya upatanisho fulani ili kuzikusanya fedha kwa ajili ya jengo kubwa la Basilika la Mtakatifu Petro huko Roma. Martin Luther alisimama hadharani dhidi ya biashara ya namna hiyo kwa hoja zake 95 katika mji wa Wittenberg huko Ujerumani Oktoba 30, mwaka wa 1517.
313 Wahubiri maalumu (Kilatini: ‘questor’ au ‘stationarius’) tangu mwanzo wa karne ya 11. Sinodi ya Trento iliyakataa mahubiri ya namna hiyo mwaka wa 1546 katika Kanisa la Roma. Huduma hii ilitanguliwa kabisa mwaka wa 1562.
muhtasari wa mafundisho ya walimu wetu.
7. Kama kuna lolote ambalo yeyote anaweza kulitaka liwemo katika ukiri huu, tuko tayari, ikimpendeza Mungu, kuiweka mbele taarifa iliyopanuliwa zaidi kulingana na Maandiko Matakatifu.
Hitimisho G
1. Sasa, tumeyasimulia mafungu makuu ambayo yalitazamwa kuwa sababu ya mabishano. Hata hivyo, matumizi mabaya na maovu mengi zaidi yangeweza kutajwa, tutaka kuuepuka urefu wa kuchosha. Badala yake, tuliyaonyesha mambo makuu tu ambayo yanaweza kuyapima mengine kwa urahisi. Nyakati za zamani, manung’uniko mengi yalisikika kuhusu vyeti vya upatanisho, hija, na kutumia vibaya mamlaka ya kuwatenga watu na Kanisa. Sharika zimesumbuliwa vibaya na wahubiri wanaoviuza vyeti vya upatanisho. Kulikuwako na mashindano yasiyokuwa na mwisho kati ya wachungaji na wamonaki kuhusu haki za mitaa, sharika, toba, mazishi, na mengine mengi yasiyoweza kuorodheshwa. Mambo ya aina hii tumeyaruka baada ya kuyaelezea kwa ufupi ili mafungu makuu yaweze kueleweka kwa urahisi zaidi. Hakuna lililosemwa au lililohusishwa hapa kwa lengo la kumshutumu yeyote. Ni mambo hayo yaliyoelezewa tu, tuliyoyafikiria kuwa lazima yasemwe ili yaeleweke kwamba, katika mafundisho na taratibu, hakuna lililopokelewa kwa upande wetu kinyume cha Maandiko Matakatifu au Kanisa Katoliki. Kwa maana ni wazi kwamba, tumekuwa waangalifu sana kuyazuia mafundisho mapya dhidi ya uchaji yasiruhusiwe kunyemelea na kuingia ndani ya makanisa yetu.
6. Hivyo, tunataka kuyaweka mbele mafungu hayo hapo juu, kulingana na amri yako Enzi Yako Kaisari, ili kuuonyesha ukiri wetu na watu wapate kuuona muhtasari wa mafundisho ya walimu wetu. Kama kuna lolote ambalo yeyote anaweza kulitaka liwemo katika ukiri huu, tuko tayari, ikimpendeza Mungu, kuiweka mbele taarifa iliyopanuliwa zaidi kulingana na Maandiko Matakatifu.
Raia wako Waaminifu Enzi yako Kaisari
Yohana
Mtawala Mchaguzi wa Sachsen
Georg Lodi wa Brandenburg
Ernst Mwinyi wa Lünenburg
Filipo Mtawala wa Hessen
Johann Fredrik Mtawala wa Sachsen
Franz Mwinyi wa Lünenburg
Wolf Mtawala wa Anhalt
Baraza na Meya wa mji wa Nürnberg
Baraza la Reutlingen314
314 Yohana Mvumilivu (Johann der Beständige, 1525-1532), nduguye Mtawala Fredrik mwenye Busara. Georg von Brandenburg-Ansbach (Markgraf). Ernst Shahidi (Ernst der Bekenner, 1520-1546). Filipo Mkarimu (Philipp der Grossmütige, 1519-1567). Yohana Fredrik Mkarimu (Johann Friedrich der Grossmütige, 15321554), mwana wa Zohana Mvumilivu. Franz, nduguye Ernst (+ 1549). Wolf, yaani, Wolfgang von Anhalt (+ 1566). Wajumbe wa Nürnberg walikuwa Christoph Kress und Klemens Volkamer. Mjumbe wa Reutlingen alikuwa meya Jos Weiss. Baada za mwezi mmoja, miji ya Windsheim, Heilbron, Kempten, na Weissenburg/Nordgau iliunga mkono.
UTANGULIZI
Salamu za Filipo Melanchthon315 kwa Msomaji
1. Baada ya Ukiri wa watawala wetu kusomwa hadharani, baadhi ya wanatheologia na watawa walitunga Hoja316 dhidi ya hati yetu. Enzi ya Kaisari iliamuru Hoja hii isomwe mbele ya baraza la watawala. Halafu alidai watawala wetu waikubali Hoja hii.
2. Wenzetu waliomba waonyeshwe hadharani nakala ya Hoja yenyewe. Maana walikuwa wamesikia kwamba, yalikatazwa mafungu mengi ambayo hayakuweza kuachwa bila kuziudhi dhamiri. Walitaka kuyaona mafungu yale ambayo wapinzani wetu waliyalaani ili kuzikanusha sababu zao za kimsingi. Walifikiri kwamba, wapinzani wetu wangependa kulitoa andiko hilo bila kusita kwa maana jambo hilo lilihusu dini na maelezo ya dhamiri za binadamu. Walakini wenzetu hawakuweza kulipata isipokuwa kwa masharti yenye hatari kubwa mno.317
3. Halafu, suluhu ilitafutwa. Ilionekana wazi kwamba, wenzetu
315 Philipp Melanchthon (1497-1560): Melanchthon ni jina la Kiyunani lililotafsiriwa kutoka kwa jina la asili la jamaa; yaani, ‘Schwarzerd’ (Udongo Mweusi). Mtaalamu maarufu wa Matengenezo ya Kanisa na msaidizi muhimu sana wa Martin Luther. Alisomea katika vyo vikuu vya Heidelberg na Tübingen. Profesa wa Kiyunani katika Chuo Kikuu cha Wittenberg tangu mwaka wa 1518. Alishiriki baraza la Speyer mwaka wa 1529 na la Augsburg mwaka wa 1530 na katika majadiliano ya Marburg mwaka wa 1529. Alitunga kitabu cha elimu ya Imani ya Kikristo kiitwacho, ‘Loci Communes’ (‘Masharti Yote’) mwaka wa 1521. Alitunga sehemu nyingi za ”Ukiri wa Augsburg,” “Utetezi wa Ukiri wa Augsburg” wote, na “Makala kuhusu Ukuu wa Papa.” Elimu yake ilikuwa muhimu zaidi katika kuyatunga maandiko ya Matengenezo ya Kanisa na katika kutafsiri Biblia katika Kijerumani. Melanchthon hakuwa shujaa wa vita vya kiroho kama Martin Luther, bali alikuwa mtu wa elimu mwenye mwenendo mwema, na mtu wa maafikiano. Hata angekosa msimamo thabiti katika mambo muhimu sana kuhusu pande za Roma na wafuasi wa Zwingli. Kwa sababu hiyo, alikubali ‘Ukiri wa Augsburg Uliobadilika’ (‘Confessio Augustana variata’) mwaka wa 1540 kama mwafaka pamoja na wafuasi wa Zwingli na ‘Interim of Augsburg’ (Hati ya Muda ya Augsburg) mwaka wa 1548 kama mwafaka pamoja na Roma. Melanchthon alitunga “Utetezi wa Ukiri wa Augsburg” katika Kilatini. Yusto Yona aliutafsiri baadaye kidogo katika Kijerumani. Wenye vyeo vya heshima vya Kilutheri walitia sahihi zao katika “Utetezi” huko Smalkaldi mwaka wa 1537. Andiko la Kiswahili lilitafsiriwa kutoka Kilatini.
316 Kilatini: ‘Confutatio pontificia.’ Maana ya hoja hii ni kuupinga ‘Ukiri wa Augsburg’ na kujaribu kubainisha dhahiri makosa yake.
317 Katazo la Kaisari la Agosti 5, kwa ajili ya jibu la Walutheri.
hawakutazamia mzigo wowote kuwa mzito zaidi ambao ungeweza kukubaliwa licha ya ile iliyoweza kuziudhi dhamiri. 4. Lakini, kwa ghasia, wapinzani wetu waling’ang’ania tukubali matumizi mabaya na makosa yaliyokuwa wazi. Tuliposita, Enzi ya Kaisari ilirudia kudai watawala wetu waikubali Hoja. Hata hivyo, watawala wetu walikataa kabisa kufanya hivyo. Basi ni kwa njia gani, wangeweza kukubali andiko lisiloonekana katika masuala ya dini? Walisikia pia kwamba, baadhi ya mafungu yalikuwa yale yaliyolaaniwa. Ungekuwa uhalifu mkubwa kuzipokea hukumu za wapinzani wetu.
5. Watawala wetu waliniamuru mimi na wengine kuuandaa Utetezi wa Ukiri wetu ili kuielezea Enzi ya Kaisari madhumuni ya kutoweza kuikubali Hoja na kuyatoa kabisa yale ambayo wapinzani wetu walituletea kama pingamizi. 6. Wakati wa kusomwa, baadhi yetu tuliandika mambo makuu juu ya hoja yake na majadiliano.318 7. Waliutoa utetezi huu mbele ya Enzi ya Kaisari ili kumuonyesha sababu kubwa na nzito zilizotuzuia kuikubali Hoja. Walakini Enzi ya Kaisari haikuyapokea maandiko yaliyoletwa. 8. Baadaye, kulitokea tangazo lingine, ambalo kwalo wapinzani wetu walijisifu kuwa wameukanusha ukiri wetu kwa njia ya Maandiko Matakatifu.
9. Sasa basi, msomaji mpendwa, una utetezi wetu. Utakuonyesha yale ambayo wapinzani wetu wameyahukumu, kadiri tulivyoyawasilisha kwa nia nzuri. Utaona pia mafungu kadhaa ambayo waliyalaani katika upinzani wa andiko dhahiri la Roho Mtakatifu, ilihali hatuwezi kuzimomonyoa aya zetu kwa Maandiko Matakatifu.
10. Ingawa mwanzoni tulianzisha kazi ya utetezi huu pamoja na wengine, lakini ilivyotokea katika uchapaji ni kwamba, niliongezea mambo fulani. Kwa sababu hiyo, ninalitoa jina langu ili yeyote asiweze kulalamika kuwa kitabu kilichapishwa bila jina la mwandishi kujulikana. 11. Wakati wote wa mabishano haya, nimezoea kusisitiza kwa kadri iwezekanavyo muundo wa mapokeo wa mafundisho ili kuirahihisha fursa ya mwafaka. Ninafuata desturi hii bila kwenda kando sana, ingawa ningeweza kuwaongoza watu wa wakati huo wajitenge na maoni ya wapinzani wetu. 12. Walakini wapinzani wetu wanaonyesha kwa matendo yao kwamba, hawatafuti ukweli wala mwafaka, bali wana hamu ya kuimwaga damu yetu.
13. Sasa niliandika kadiri nilivyoweza. Kama misemo yoyote inaonekana kuwa mikali zaidi, sina budi kusema kwamba, ninabishana pamoja na wanatheologia na watawa walioiandika Hoja, wala sibishani na Kaisari au watawala ambao 318 Hasa mtaalamu Yoakimu Kamerario, rafikiye Melanchthon aliyetoka Nürnberg.
inanibidi niwaheshimu sana. 14. Lakini nimeiona karibuni Hoja, ambayo nilitambua kuwa imeandikwa kwa njia ya kudhuru, kwa siri, na kwa uzushi kiasi kwamba, pahali pengine maalumu panaweza kuwadanganya hata wasomaji waangalifu. 15. Sikuzijadili ghiliba zao zote kwa maana kazi hii haingemalizika. Badala yake, nimekusanya hoja maalumu ili ushuhuda wetu uenee kwa mataifa yote kwamba, tunaitafakari Injili ya Kristo kwa usahihi na uchaji.
16. Sisi hatufurahii ugomvi. Tunaielewa hatari yetu dhahiri kwa kuwa upana wake, iko wazi kwa sababu ya hali ya chuki iliyochochewa na wapinzani wetu. Lakini hatuwezi kuusalimisha ukweli ambao ni wazi na wa lazima kwa kanisa. Kwa sababu hiyo, tunaamini kwamba, lazima tuvumilie shida na hatari kwa ajili ya utukufu wa Kristo na wema wa Kanisa. Tunaamini kwamba, Mungu atakubali huduma hii yetu, na tunategemea kwamba, vizazi vijavyo vitatuhukumu kwa haki zaidi. 17. Bila mashaka yoyote, wenzetu wamezileta wazi aya za Mafundisho ya Kikristo ambayo Kanisa linayahitaji kwa kweli. Haipaswi kuelezewa hapa jinsi zilivyofichwa ndani ya mawazo hatari ya watawa, makasisi wa makanisa makuu, na wanatheologia wapotoshaji.
18. Watu wema wengi wameshuhudia hadharani na kumshukuru Mungu kwa ajili ya baraka hizi kubwa za mafundisho bora katika masharti mengi muhimu sana kuliko lile linaloenea kwenye maandiko ya wapinzani wetu.
19. Sasa tunaikabidhi sababu yetu mikononi mwa Kristo ambaye siku moja atayahukumu mabishano haya. Tunamwomba ayaangalie makanisa yake yaliyo matesoni na yaliyotawanyika ili ayarudishe katika mwafaka wa kudumu wa Kristo.
UTETEZI WA UKIRI
Fungu la Kwanza: Mungu
1. Wapinzani wetu wanaliafiki fungu la kwanza la Ukiri wetu. Katika hilo tunatangaza kwamba, sisi tunaamini na kufundisha kuwa kuna asili moja ya kimungu isiyogawanyika n.k. Hata hivyo, zimo nafsi tatu tofauti za milele katika asili hiyo moja ya kimungu, yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. 2. Kila wakati tumelifundisha na kulitetea fungu hili. Tunasadiki kwamba, Maandiko Matakatifu hulishuhudia fungu hili kwa uthabiti, uhakika, na bila kulikanusha. Tunatamka daima kwa dhati kwamba, wale wanaoamini tofauti, wako nje ya Kanisa319 la Kristo, ni waabudu sanamu, na wanamkufuru Mungu.
319 Kilatini: ‘Extra ecclesiam.’
Fungu la Pili: Dhambi ya Asili
1. Wapinzani wetu wanaliafiki fungu la pili kuhusu dhambi ya asili, lakini wanaukaripia ufafanuzi wetu wa kuishinda dhambi ya asili. Mwanzoni kabisa, Enzi ya Kaisari imeweza kuona mara moja kwamba, watunzi wa Hoja hii siyo wamekosa busara tu bali hata unyofu pia. Wakati tunataka kuyaelezea mara moja, kwa moyo safi, yale yanayohusu “dhambi ya asili,” wanataka kuyakengeusha kwa ufasiri wa uchungu ambao waliubuni kwa nia mbaya. Wanadai hivi: Kutokuwa na hofu ya Mungu na kutomwamini Mungu ni dhambi halisi. Hivyo basi, wanakataa kwamba, ni dhambi ya asili.320
2. Bila shaka, mabishano haya matupu yametoka kwa wanatheologia wenye utata, wala si kutoka kwa baraza la madiwani wa Kaisari. Ni rahisi sana kukanusha aina hii ya udanganyifu. Lakini ili watu wote wema wapate kuelewa kwamba, mafundisho yetu kuhusu suala hili si ya upuuzi, tunawaomba wachunguze kwanza maandiko ya Kijerumani ya “Ukiri.” Ukiri huu unatuondoa hatiani kabisa kutoka kwa mafundisho mapya: “Pia inafundishwa miongoni mwetu kwamba, tangu anguko la Adamu, wanadamu wote wanaozaliwa kwa njia ya asili, wanachukuliwa mimba na wazazi wao na kuzaliwa wakiwa wenye dhambi. “Hii inamaanisha kwamba, wanadamu wote wanajaa tamaa na mielekeo miovu kutoka katika tumbo la uzazi. Kwa nguvu za asili, wanashindwa kuwa na hofu ya kweli na imani ya kweli katika Mungu.” Aya hii hushuhudia kuwa sisi tunakataa kabisa kwamba, wale waliozaliwa kulingana na asili ya kimwili wangeweza kuwa na tendo la hofu lenyewe na tegemeo kwa Mungu au uwezekano na kipawa cha kulizaa. Kwa nini basi, ingewezekanaje tulaumiwe katika jambo hili? Angalau sasa, tunafikiria kuwa mbele ya watu wengine bora kama wasiokuwa na waa. Aya ya Kilatini huukataa uwezo wa asili katika maana hiyo. Yaani, vipawa na nguvu ya kuzaa hofu na tegemeo kwa Mungu na vile vile matendo ya watu wazima. Tunapoitaja “ashiki,”321 hatumaanishi matendo au matunda yake peke yake, bali mwelekeo wa kudumu wa asili.
4. Kusudi letu ni kuonyesha mbele kidogo, kwa maneno mengine zaidi kwamba, maelezo yetu yanakubaliana na fasili ya zamani na ya mapokeo. Kwanza, lazima tuonyeshe kwa nini tunayatumia maneno haya hapa. Wapinzani wetu wasomi hukubaliana kwamba, kwa upande wa kiini, dhambi ya asili ni ashiki.322 Kwa
320 Kilatini: ‘culpa actualis,’ ‘culpa originalis.’
321 Kilatini: ‘Concupiscentia.’ Istilahi hii ilikuwa jambo la kimsingi katika theologia ya Mt. Agostino wa Hippo (354-430) na ya Dk. Martin Luther, aliyemfuata.
322 “Minatarafu ya kiini,” Kilatini: ‘materiale.’ Istilahi ‘materia,’ (kiini) , na ‘forma,’ (umbo), zinatokana na falsafa ya Aristotele (384-322 K.K.). Tomaso wa Akuino (1225/6-1274): ‘Peccatum originale materialiter quidem est concupiscentia, formaliter vero defectus originalis iustitiae’ - Dhambi ya asili ni mintarafu ya kiini ashiki, lakini mintarafu ya umbo lake ni dosari ya haki ya asili (Summa Theologica 2, 1.q 82 a. 3 c
sababu hiyo basi, tulipolielezea jambo hilo, haikuwezekana kuyaepuka maneno haya, hasa wakati huo ambapo wengi waliitumia falsafa badala ya dini kuhusu hoja hiyo.
5. Kuna baadhi yao ambao husema kwamba, dhambi ya asili siyo hatia au upotovu katika asili ya mwanadamu. Badala yake, wanadai kuwa dhambi hiyo ni aina ya utumwa tu au hali ya kuweza kufa ambayo wafuasi wa Adamu huipitia bila kosa lao wenyewe kwa sababu ya hatia ya mtu mwingine.323 Wanaendelea kusema kwamba, mtu hahukumiwi kifo cha milele kwa sababu ya dhambi ya asili, bali kama watoto wanaozaliwa katika utumwa. Hawakupata hali hii kwa sababu ya makosa ya asili yao, bali kwa ajili ya akina mama zao.
6. Ili kuonyesha wazi kwamba, wazo hili la kukufuru sana halitupendezi hata kidogo, tuliitaja ashiki. Kama kidokezo kizuri zaidi, tumeitaja kuwa kama ugonjwa na kuelezea kwamba, wanadamu huzaliwa wakiwa na asili ya uovu na makosa.
7. Sisi hatukutaja tu tamaa bali pia kutokuwepo na hofu ya Mungu na imani. Tumefanya hivyo kwa sababu Madaktari Wanazuoni324 wanaipunguza kabisa fasili ya akina Baba325 juu ya dhambi ya asili kwa sababu ya kutoielewa vya kutosha. Wanaendelea kujadiliana juu ya vifaa vya dhambi vya moto, “fomes,”326 iwapo ni tabia ya kimwili. Wanajiuliza kwa njia yao ya kijinga, kama vimeambukizwa kwa njia ya tufaha au pumzi ya nyoka,327 na zaidi kama kuna dawa ya kujinusuru. Wameificha hoja yenyewe katika maswali kama hayo.
8. Basi, wanapoizungumzia dhambi ya asili, hawakumbuki maovu mabaya zaidi ya asili ya binadamu kama kutomfahamu na kumdharau Mungu, kukosa hofu na tegemeo kwa Mungu, kuichukia hukumu yake, kuitoroka hukumu yake, kukata tamaa kuhusu neema yake, kuyategemea mambo ya ulimwengu huu n.k. Madaktari Wanazuoni hawayatambui magonjwa hayo ambayo yanapingana
323 Pelagio, mtaalamu wa theologia kutoka Uingereza aliyefundisha theologia huko Roma katika mwanzo wa karne ya tano. Wafuasi wa Pelagio waliamini kwamba, mwanadamu ana hiari katika wokovu na walikataa dhambi ya asili. Kanisa la Magharibi lilikataa mafundisho haya na liliwaharamisha Wapelagio katika karne ya nne kwa ajili ya uwezo wa Mt. Agostino wa Hippo. Wakati wa Enzi ya Kati, katika Kanisa la Magharibi, Yohana Duns Scotus (mnamo mwaka wa 1265-1308) na Gabriel Biel (mnamo mwaka wa 1420-95) walifundisha kwamba, ashiki si dhambi ya asili. Wakati wa Matengenezo ya Kanisa, Huldrych Zwingli (1484-1531) alifundisha kwamba, ni uambukizwaji wa asili wa mauti, si dhambi na hatia.
324 Kilatini: ‘Scholastici doctores.’
325 Yaani, akina Baba wa Kanisa.
326 Petro Lombardo, ‘Fomes peccati’ au vifaa ya dhambi vya moto, ni istilahi ya theologia ya wanazuoni. ‘Fomes’ ilifikiriwa kuwa kama salio la dhambi ya asili na kama kisawe cha ashiki, yaani, ‘concupiscentia.’ Pia ‘languor naturae,’ yaani, unyong’onyevu wa asili.
327 Gabriel Biel na Gregorio wa Rimini, ‘Doctor authenticus,’ mfuasi wa William wa Okam, + 1358. Gregorio wa Rimini alipata kauli yake kutoka kwa ufafanuzi wa Biblia wa Mt. Agostino.
kabisa na sheria ya Mungu. Kinyume chake, wanayahesabu, kama asili ya binadamu, kuwa na nguvu zisizodhulumika za kumpenda Mungu katika mambo yote na kuzitii amri zake kutokana na kiini cha matendo yenyewe.328 Hawauoni mgongano wowote! 9. Ni kipi kingine basi, isipokuwa haki ya asili kuweza kumpenda Mungu zaidi kuliko vitu vyote kwa uwezo wa mtu mwenyewe na kuzitii amri zake? 10. Iwapo asili ya mwanadamu yenyewe ina nguvu kamili hata kuweza kumpenda Mungu zaidi kuliko vitu vyote, sawa na wanazuoni watamkavyo kwa dhati, basi, dhambi ya asili ni ipi? Ni kwa kusudi gani neema ya Kristo ingehitajika iwapo tungeweza kuwa wenye haki kwa haki yetu wenyewe? Ni kwa kusudi gani Roho Mtakatifu anahitajika iwapo nguvu za binadamu zenyewe zingeweza kumpenda Mungu zaidi kuliko vitu vingine vyote na kuzitii amri zake? 11. Ni nani asiyeweza kuuona upuuzi wa maoni ya wapinzani wetu? Wao huyatambua magonjwa madogo ya asili ya kibinadamu bila kuyatambua yale yaliyo mazito zaidi. Hata hivyo, Maandiko Matakatifu hutuonya kila mahali na manabii hunung’unika daima kuhusu hayo kama; usalama wa kimwili, kumdharau na kumchukiza Mungu, na makosa mengine kama hayo ambayo tumezaliwa nayo. 12. Lakini baadhi ya wanazuoni walianza kuyachanganya mafundisho ya Kikristo na mawazo ya kifalsafa kuhusu ukamilifu wa asili na hiari na matendo yake kupita kiasi na kufundisha kwamba, watu huhesabiwa haki mbele za Mungu kwa nguvu ya haki ya kifalsafa au ya kiraia, ambayo kwa namna fulani tumeikubali kwa kiasi kuwa chini ya akili na kutawaliwa nasi. Walishindwa kabisa kuiona najisi ya ndani ya asili ya mwanadamu. 13. Najisi hii haiwezi kutambuliwa kwa njia nyingine isipokuwa kwa Neno la Mungu ambalo mara nyingi wanazuoni hawalitumii katika mijadala yao .
14. Hii ndiyo sababu iliyotufanya tuitaje pia ashiki na kukanusha nguvu za asili za binadamu katika maelezo yetu kuhusu dhambi ya asili, hofu na tegemeo kwa Mungu. Yaani, tulitaka kuonyesha kuwa dhambi ya asili hujumuisha makosa haya pia: Kutomfahamu na kumdharau, kukosa kumwamini na kumtegemea, na kutoweza kumpenda Mungu. Haya ni makosa maalumu ya asili ya binadamu yanayoupinga hasa Ubao wa Kwanza wa Amri Kumi za Mungu.329
15. hatujasema jambo lolote jipya. Ikieleweka vyema, fasili ya zamani husema vivyo hivyo: “Dhambi ya asili ni upungufu wa haki ya asili.”330 Basi, haki ni nini? Hapa wanazuoni hujadiliana kuhusu maswala ya kipembuzi331 bila kuelezea hata kidogo haki ya asili ni ipi. 16. Kwa hiyo, katika Maandiko, haki siyo tu ubao
328 Kilatini: ‘Quoad substantiam actuum’; k.m. Gabriel Biel na Yohana Duns Scotus.
329 Yaani, amri 1-3 kuhusu kumpenda Mungu.
330 Anselm wa Canterbury (1033-1109).
331 Kilatini: ‘Questiones dialecticae.’
wa pili wa Amri Kumi za Mungu, bali hata ule wa kwanza pia unaotufundisha kumwogopa, kumwamini na kumpenda Mungu. 17. Hivyo, maana ya haki ya asili siyo tu kukusudia upatanisho sawa bora wa kimwili,332 bali pia vipawa hivi: Ufahamu wa kweli wa Mungu, kumwogopa Mungu, tegemeo kwa Mungu, au mwelekeo na uwezo safi wa kuyafikia mambo haya. 18. Hali kadhalika, Maandiko Matakatifu hushuhudia hivyo yasemapo kuwa, mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa sura yake.333 Ni nini zaidi ya kuwa sanamu ya hekima na haki iliyopandikizwa katika mwanadamu ili apate kumtambua Mungu na katika Mungu apate kumwakisi? Maana yake: mwanadamu alizipokea karama za ufahamu wa Mungu, za kumwogopa Mungu, na za tegemeo kwa Mungu n.k. Hivyo basi, Ireneo na Ambrosio huifafanua sura ya Mungu.334 19. Baada ya kuyasema mambo mengi kuhusu sentensi hii akasema: “Nafsi hiyo siyo katika mfano wa Mungu ambapo Mungu hakuwepo daima.” 20. Katika nyaraka zake kwa Waefeso na Wakolosai335 Paulo pia anaonyesha mfano wa Mungu kuwa ni ufahamu wa Mungu, haki, na ukweli. 21. Petro Lombardo anathubutu kusema kwamba, haki ya asili ni mfanano wenyewe wa Mungu ambao aliupandikiza kwa mwanadamu.336 22. Tunazidondoa sentensi za walimu wa kale ambazo hupatana kabisa na ufafanuzi wa Agostino kuhusu mfano wa Mungu.337
23. Hali kadhalika, fasili ya kale isemayo kuwa dhambi ni upungufu wa haki, haikatai tu utii wa mamlaka ya chini ya mwanadamu, lakini hukataa pia mwanadamu kuwa na ufahamu wa mungu, tegemeo la hofu ya Mungu, na upendo kwa Mungu, au uwezo wowote wa kuyatenda hayo. Hata wanatheologia wanazuoni hufundisha kuwa mambo haya hayawezi kutendwa bila vipawa maalumu na msaada wa neema.338 Ili kupata kulielewa jambo hili sawasawa, tumevitaja vipawa hivi: ufahamu, hofu, na tegemeo kwa Mungu. Kutokana na haya, ni dhahiri kabisa kwamba, fasili ya kale husema yale yale tuliyoyasema,
332 Kilatini: ‘Aequale temperamentum gualitatum corporis.’ Matokeo ya Adamu Kuanguka Dhambini ‘inordinata dispositio partium animae,’ yaani, “tabia isiyokuwa makini katika sehemu za nafsi” ; Tomaso wa Akuino katika ‘Summa Theologica 2, 1, q. 82a na 85a.’
333 Mwa. 1:27, Fasiri ya ‘Union Version’ inalitumia neno ‘mfano’ mara mbili kumaanisha “ZLM” (zäläm), “mfano,” Kilatini: ‘imago,’ na “DMVT” (demut), “sura” au “mfanano,” Kilatini: ‘similitudo.’
334 Ireneo (mnamo 130-200), Baba Myunani wa Kanisa la Zamani. Alifariki dunia kama Askofu wa Lyon huko Ufaransa. Ambrosio (339-397), zamani alikuwa askofu maarufu wa Milano huko Italia, na baba wa kiroho wa Agostino.
335 Ef. 5 : 9; Kol. 3 : 10
336 Petrus Lombardus (mnamo 1100-1160). Kitabu chake maarufu sana kiitwacho, ‘Sententiarum libri quattuor’ (Vitabu Vinne vya Ufafanuzi) kilikuwa mkusanyiko wa fafanuzi za akina Baba wa Kanisa kulingana na utaratibu wa mifumo ya imani. Sent. II, dist. 16 c.
337 Agostino, “Utatu” (De Trinitate 12, 7.12.14.).
338 Msaada wa neema katika hali ya asili, Kilatini: ‘auxilium gratiae au adiutorium gratiae au donum superadditum au donum supernaturale au gratia gratum faciens’: Mt. Agostino, wanatheologia Wafranskiskano, Tomaso wa Akuino, Yohana Duns Scotus.
tulipoikataa hofu ya Mungu na tegemeo kwake. Siyo tendo lenyewe tu bali pia vipawa na nguvu ya kuyatenda.
24. Fasili ya Agostino ni ile ile ambayo huifafanua dhambi ya asili kama ashiki. Yeye humaanisha kwamba, ashiki iliingia mahali pa haki iliyopotea. Kwa maana, asili katika udhaifu wake isipoweza kumwogopa na kumpenda Mungu au kumwamini Mungu, hutamani na huyapenda mambo ya anasa; ama inadharau hukumu ya Mungu katika usalama wake mbaya au huichukia ambayo imejaa hofu. Hivyo, Agostino huunganisha dosari pamoja na hali ya uovu ulioifuata. 25. Ashiki siyo tu uharibifu wa ubora wa mwili, bali ni mwelekeo mbaya wa nguvu aula339 katika mambo ya anasa. Hawayaelewi hata kidogo maneno ya wale wanaosisitiza wenyewe kwamba, mara moja, mwanadamu huweza kuwa pamoja na ashiki isiyonyimwa bado na Roho Mtakatifu na huweza kumpenda Mungu zaidi kuliko vitu vyote.
26. Tumeielezea kwa usahihi fasili yetu kuhusu dhambi ya asili katika pande zote mbili, yaani, dosari zile za kutoweza kumwamini au kumpenda Mungu. Hali kadhalika, kuna ashiki ambayo huyatamani mambo ya anasa kinyume na Neno la Mungu. Maana yake: ashiki hutamani siyo tu anasa za mwili, bali pia hekima na haki za mwili na kuzitegemea hizi na kumdharau Mungu. 27. Walimu walioyafundisha haya siyo wanatheologia wa kale tu, bali hata wengine wapya hodari ambao hufundisha kwamba, dhambi ya asili ni dosari kweli zilizotajwa awali na ashiki. Tomaso asema: “Dhambi ya asili ni dosari ya haki ya asili na pamoja na hii ni tabia isiyokuwa makini ya sehemu za nafsi.340 Kwa hiyo, siyo dosari peke yake bali ni hali ya uharibifu.” 28.Bonaventura341 huandika: “Watu wakiuliza dhambi ya asili ni nini, jibu halisi litakuwa kwamba, ni ashiki isiyokuwa na kiasi. Jibu halisi pia ni kusema kwamba, ni dosari ya haki tunayowiwa kweli. Mojawapo ya majibu haya hujumuisha jibu lingine.” 29. Hugo342 alikubali aliposema kwamba, dhambi ya asili ni ujinga wa nafsi na ashiki ya mwili. Anamaanisha kwamba, sisi huzaliwa tukiwa wajinga kuhusu Mungu, vile vile huwa hatumwamini, hatumtegemei, tunamdharau, na kumchukia Mungu. Ameyaweka haya yote pamoja katika neno `ujinga.` 30. Hoja hizi zinakubaliwa na Maandiko Matakatifu. Wakati mwingine Paulo huitaja dosari hii katika 1 Kor.
339 Yaani, bora.
340 Kilatini: ‘Inordinata dispositio partium animae.’
341 Bonaventura, Giovanni di Fidanza (mnamo 1217-74) mwanatheologia wa Kifransiskano, ‘Doctor seraphicus.’ Aliupinga uwezo wa falsafa ya Aristotele katika theologia. Dondoo, Sent. lib. 2, dist. 30. q un. Art. 2c
342 Hugo wa Mt. Viktor (+ 1142) Mmonaki wa Kiagostino katika Pari huko Ufaransa. ‘De sacramentis’ 1, 7. c. 28.
2:14 ifuatavyo: “Basi mwanadamu wa tabia343 ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu.” Pahali pengine katika Rum. 7:5 anataja kuwa ashiki iliyokuwako hutenda kazi katika viungo vyetu na kuyazaa matunda ya uovu. 31. Tungeweza kunukuu pahali pengi kutoka katika pande zote mbili, lakini katika jambo hili dhahiri, hatuhitaji ushahidi mwingine zaidi. Msomaji mwenye busara ataweza kuona kwa urahisi kwamba, kuikosa hofu na imani siyo makosa ya matendo bali hizi ni dosari za kudumu katika asili isiyofanyika upya.
32. Basi, maoni yetu kuhusu dhambi ya asili hayahitilafiani ama na Maandiko Matakatifu au Kanisa la Katoliki.344 Badala yake, tumezitakasa na kuziweka nuruni sentensi nzito mno za Maandiko Matakatifu na za mababa zilizofichwa na majadiliano ya wanatheolojia wa wakati huu. Jambo lenyewe ni dhahiri lakini wanatheologia wa kisasa, hakika hawazingatii walilomaanisha mababa wa Kanisa kuhusu dosari. 33. Utambuzi wa dhambi ya asili ni wa lazima, wala sisi hatuwezi kuufahamu ukubwa wa neema ya Kristo isipokuwa kwa ujuzi wa makosa yetu. Haki yote ya mwanadamu ni unafiki mtupu mbele za Mungu tusipotambua moyo usiokuwa na upendo, hofu, na tegemeo kwa Mungu. 34. Hivyo nabii anasema: “Baada ya kufundishwa kwangu, nalijipiga pajani.”345 Vile vile: “Mimi nilisema kwa haraka yangu, wanadamu wote ni waongo.”346 Yaani, hawana mtazamo sawa kumhusu Mungu.
35. Hapa, wapinzani wetu pia humchapa kiboko Luther aliyeandika: Dhambi ya asili hubaki hata baada ya Ubatizo.347 Wanaongezea kusema kuwa, fungu hili limehukumiwa ipasavyo na Leo X.348 Enzi ya Kaisari itautambua uongo ulio wazi hapa. Naam, wapinzani wetu hufahamu ni ufafanuzi gani alioumaanisha Luther kwa msemo huu kwamba, dhambi ya asili hubaki hata baada ya Ubatizo. Amekuwa akiandika daima kwamba, Ubatizo huondoa hatia ya dhambi ya asili, japo jinsi wanavyodai, kiini chake, yaani ashiki hubaki. Kuhusu kiini, aliongezea pia kwamba, Roho Mtakatifu atolewaye katika Ubatizo huanza kuinyima ashiki na huunda misukumo mipya ndani ya mtu. 36. Agostino hakuzungumzia jambo lile lile aliposema: “Dhambi husamehewa katika Ubatizo, siyo kwamba, haipo tena, bali haihesabiwi.349 Hapa anashuhudia wazi kuwa dhambi hubaki japo haihesabiki. Ufafanuzi huu ulivipendeza vizazi vilivyofuata kadiri ya
343 Kilatini: ‘Homo animalis.’
344 Yaani, Kanisa zima la Kikristo, si Kanisa la Roma peke yake.
345 Yer. 31: 19
346 Zab. 116: 11
347 Hoja ya pili ya majadiliano ya Leipzig ya mwaka wa 1519.
348 Tangazo la Papa Leo X la Juni 15, mwaka wa 1520: “Makosa ya Martin Luther.”
349 Ndoa na ashiki 1, 25.
kudondolewa katika mifumo ya Kanisa.350 Dhidi ya Yuliano, Agostino husema pia: “Sheria iliyomo katika viungo vyangu imeondolewa kwa wongofu wa kiroho na hubaki katika mwili wenye kufa. Imeondolewa kwa sababu hatia yake imeondolewa na sakramenti ambayo kwayo, waumini huzaliwa mara ya pili. Lakini hubaki kwa sababu sheria huziunda tamaa na wale waumini hupingana nazo.”351 37. Wapinzani wetu wanajua vizuri kwamba, hivyo ndivyo anavyoamini Luther na kufundisha. Lakini, kwa sababu hawawezi kulikana jambo lenyewe, wanayapotosha maneno ili wapate kumshinda mtu asiye na hatia kwa udanganyifu huu.
38. Lakini wapinzani wetu wanashindana kwamba, ashiki ni adhabu na wala siyo dhambi, wakati Luther husisitiza kuwa ashiki ni dhambi. Hapo awali, tulitangulia kusema kwamba, hata Agostino huifasili dhambi ya asili kuwa ashiki. Waacheni sasa, wabishane na Agostino kama mkazo huu hauwafurahishi! Licha ya hayo, Paulo anasema: “Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingelisema, usitamani” (Rum. 7: 7). Kadhalika anasema: “Lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.” (Rum. 7: 23). Hakuna mzaha unaoweza kuubadilisha ushahidi huu. Kwa maana, unataja wazi ashiki kuwa dhambi, japo haihesabiwi kwa wale walio katika Kristo. Kwa asili, jambo lenyewe hustahili kifo kama halikusamehewa. Zamani, hii ndiyo ilikuwa kauli ya mababa wa Kanisa kuhusu mabishano haya. Kwa mjadala mrefu, Agostino aliyakataa maoni ya wale waliodhania kuwa ashiki haikuwa uovu, bali jambo lisilosimamia upande wowote, sawa na rangi ya ngozi au afya mbaya.352
42. Wapinzani wetu wakidai kwamba, vifaa vya dhambi vya moto353 ni mambo ya kawaida tu, siyo aya nyingi za Maandiko Matakatifu peke yake zitakazoyapinga mafundisho ya kauli hiyo, bali hata Kanisa zima. Japo hakuna mwafaka kamili uliopatikana, ni nani anayethubutu kusema kwamba, mambo haya yawe ya kawaida, yaani, mashaka kuhusu ghadhabu, neema, na Neno la 350 Mfumo, Kilatini: ‘decretum,’ barua ya Papa wa Roma iliyohusu suala maalumu la mafundisho au usimamiaji haki katika Kanisa la Magharibi. Mkusanyiko wa kwanza wa mifumo ya Papa ulitolewa na Dionisio Exiquus mwaka wa 520. Mtawa Gratiano (+ mnamo 1159) aliyefundisha katika Chuo Kikuu cha Bologna huko Italia, aliutoa mkusanyiko ulio muhimu sana kabla ya mwaka wa 1139. Alivipanga vifaa vya maandiko ya mifumo karibu 4,000 kulingana na utaratibu wa kisheria katika kitabu kiitwacho, ‘Concordantia Discordatium Canonum,’ kawaida tu ‘Decretum Gratiani.’ Baadaye kitabu hiki kilikuwa sehemu ya kwanza ya mkusanyiko rasmi wa Sheria ya Kanuni za Kanisa la Roma, yaani, ‘Corpus Iuris Canonici’ katika mwaka wa 1917.
351 Agostino, ‘Contra Iulinamum’ (‘Dhidi ya Yuliano’) 2, 3.
352 Kiyunani: ‘αδιαφορον.’
353 Kilatini: ‘fomes.’
Mungu? Vile vile, kuikasirikia hukumu yake, kuudhika kwa sababu Mungu hataki kutuokoa mara moja kutoka kwa dhiki, kuhangaika kwa sababu watu waovu huwa na bahati nzuri kuliko watu wema, kuwashwa na hasira, ashiki, kiburi, mali n.k. Wacha Mungu wamekiri mambo haya, 43. jinsi Zaburi na manabii wanavyoonyesha. Lakini madaktari wanazuoni wameyaazima mawazo mageni kabisa kutoka kwenye falsafa kwamba sababu ya hisia zetu sisi sio wema wala wabaya, hatupaswi kusifiwa wala kulaumiwa354. Hali kadhalika wanasema, hakuna lolote ambalo ni dhambi isipokuwa lifanyike makusudi. Sentensi hizi za wanafalsafa ziliitaja haki ya serikali wala siyo hukumu ya Mungu. Wajinga hawa huthubutu kuzibuni sentensi zingine kama hizo kwamba, asili siyo ovu. Sisi hatutaikaripia kauli hii. Lakini siyo halali kuipindisha ili kuipunguza dhambi ya asili. Bado sentensi za namna hiyo zinapatikana katika maandiko ya Madaktari Wanazuoni ambao wamechanganya falsafa au maadili ya serikali na Injili kwa njia isiyofaa. 44. Mambo haya hayakujadiliwa katika vyuo vikuu peke yake bali yaliufikia umma. Vishawishi hivi viliendelea kutawala na kulielimisha imani kwa nguvu za kibinadamu na kuuzuia ujuzi wa neema ya Kristo. 45. Hivyo, Luther alipotaka kuuarifu ukubwa wa dhambi ya asili na udhaifu wa binadamu, alifundisha kuwa, kwa upande wa asili yao, mabaki ya dhambi siyo mambo ya kawaida katika mwanadamu. Yanahitaji neema ya Kristo ili yasihesabiwe355 na Roho Mtakatifu ili yaaibishwe.
46. Japo madaktari wanazuoni huyafifiliza haya mawili, yaani, dhambi na adhabu wanapofundisha kwamba, mwanadamu anaweza kuzitii amri za Mungu kwa uwezo wake mwenyewe, Kitabu cha Mwanzo huelezea adhabu tofauti iliyotolewa kwa sababu ya dhambi ya asili: Asili ya binadamu haipo tu chini ya kifo na mateso mengine ya kimwili, bali ipo pia chini ya utawala wa Ibilisi. Kwa maana, hukumu ya kuogofya sana imetangazwa: “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino” (Mwa. 3: 15). 47. Upungufu356 na ashiki ni dhambi sawasawa na jinsi mauti, mateso mengine ya mwili, na udhalimu wa Ibilisi ulivyo adhabu maalumu. Asili ya binadamu imetawaliwa na imeshikwa mateka na Ibilisi anayeipumbaza kwa mawazo na makosa ya kukufuru na kuichochea katika aina zote za dhambi. 48. Hivyo, jinsi Ibilisi asivyoweza kushindwa pasipo msaada wa Kristo, vivyo hivyo, kwa nguvu zetu hatuwezi kujinasua wenyewe kutoka katika utumwa huo. 49. Historia ya ulimwengu wenyewe huonyesha uwezo wa
354 Tomaso wa Akuino alikirejelea kitabu cha Aristotele (mnamo 384-322 K.K) ‘Elimuadili ya Nikomakhos.’
355 Yaani, yasihesabiwe kuwa hatia mbele za Mungu. 356 Yaani, upungufu wa kuzitii kamili Amri za Mungu.
utawala wa Ibilisi. Ulimwengu unaendelea kujaa kufuru dhidi ya Mungu na maoni yasiyokuwa ya kumcha Mungu na kwa vifungo hivi ibilisi amewafunga wenye hekima na haki machoni pa ulimwengu. Makosa mabaya zaidi huonekana katika watu wengine. 50. Basi, Kristo ametolewa kwa shabaha ya kuyachukua makosa na adhabu hizo na kuuharibu ufalme wa Ibilisi, dhambi, na mauti. Basi, fadhili hizi za Kristo haziwezi kutambuliwa pasipo kuutambua uovu wetu. Hivyo basi, wahubiri wetu wameyafundisha mambo haya kwa jitihada. Hawakuanzisha lolote jipya, bali waliyaendeleza Maandiko Mtakatifu na mafundisho ya mababa watakatifu wa Kanisa.
51. Tunaamini kwamba, yaliyotangulia yataitosheleza Enzi ya Kaisari kuhusu upuuzi wa kitoto na zisizo na maana ambazo wapinzani wetu wameutumia kulikashifu hili fungu letu. Tunafahamu vizuri kwamba, kauli yetu ni halali na inakubaliana kabisa na Kanisa Katoliki la Kristo. Basi, wapinzani wetu wakiyaanzisha mabishano haya tena, miongoni mwetu hatutakosa watakaowajibu na kuutetea ukweli. Maana, mara nyingi, wapinzani wetu hawaelewi walisemalo katika jambo hili. Mara kwa mara wao husema mambo ya ukinzani, hushindwa kabisa kuelezea kwa ufasaha na kwa upembuzi357 kuhusu urasmi358 wa dhambi ya asili au linalotajwa kuwa kasoro zake. Upande wetu, tumesita kushiriki mabishano haya yao kwa kina. Tumeridhika tu kusimulia, katika maneno ya kawaida, maoni ya mababa watakatifu ambayo hata sisi tunayafuata.
Fungu la Tatu: Kristo
1. Wapinzani wetu wanakubali Fungu letu la tatu, ambapo tunakiri kwamba, kuna asili mbili katika Kristo, yaani, Neno alichukua asili ya binadamu katika umoja wa nafsi yake. Kristo yule yule aliteswa na kufa ili ampatanishe Baba nasi; Alihuishwa ili atawale, awahesabie haki, na awatakase wale wanaomwamini n.k., sawa na jinsi Ukiri wa Mitume na wa Nikea unavyosema.
Fungu la Nne: Kuhesabiwa Haki
1. Wapinzani wetu wanatulaani katika fungu la nne, tano, na sita na baadaye katika lile la ishirini kwa sababu ya mafundisho yetu kwamba, watu hawapokei msamaha wa dhambi kwa njia ya stahili zao, bali huupokea bure kwa ajili ya Kristo na kwa imani359 katika Kristo. Wanayalaani mafundisho yote mawili, yaani kwa
357 Kilatini: ‘Dialectice.’
358 Kilatini: ‘Formale.’
359 Tafsiri ya ‘Union Version’ inastahabu kusema, (kwa njia ya imani) badala ya (kwa imani). Lakini (kwa
sababu sisi hukana kwamba, watu hawaupokei msamaha wa dhambi kwa stahili zao, na kwa sababu tunakiri kuwa watu huupokea msamaha wa dhambi kwa imani na huhesabiwa haki kwa imani katika Kristo. 2. Tunaisihi Enzi ya Kaisari itusikilize kwa upole kuhusu mambo haya makubwa mno, kwa sababu mabishano haya yanahusu mfumo maalumu wa imani ya Kikristo, ambao ukieleweka vema, unaangaza na kukuza utukufu wa Kristo na kuziletea dhamiri za wachaji faraja tele wanazozihitaji. 3. Kwa kuwa, wapinzani wetu hawafahamu hata kidogo msamaha wa dhambi wala imani wala neema wala haki, wanaikanganya kauli hii vibaya na kuuvuruga utukufu na fadhili za Kristo na kuzinyang’anya dhamiri za wacha Mungu faraja waliyopewa katika Kristo. 4. Ili tuweze kuuthibitisha ukiri wetu na kuzipinga hoja za wapinzani wetu, kuyatoa mambo kadhaa kama utangulizi ili marejeo ya aina zote mbili za mafundisho ya imani ya wapinzani wetu na yetu wenyewe yaweze kueleweka.
5. Katika Maandiko Matakatifu yote, inatubidi kutofautisha kati ya kauli hizo maalumu mbili, yaani, sheria na ahadi. Katika sehemu moja yanafundisha sheria. Kadhalika katika sehemu nyingine yanafundisha ahadi kuhusu Kristo. Kwa upande mmoja yanaahidi kwamba, Masihi anauahidi msamaha wa dhambi, haki, na uzima wa milele kwa ajili yake. Kwa upande mwingine, katika Agano Jipya, Kristo aliyekuja aliahidi msamaha wa dhambi, haki, na uzima wa milele. 6. Katika mjadala huu, sisi huiita sheria Amri Kumi za Mungu popote ipatikanapo katika Maandiko Matakatifu. Sasa, hatusemi lolote kuhusu taratibu za ibada na utimizaji wa sheria za raia za Musa.
7. Kutoka sehemu hizo mbili za Maandiko Matakatifu, wapinzani wetu huzichagua sheria, kwa sababu akili ya binadamu hufahamu sheria kwa kiasi fulani kwa kawaida ya asili yake. Yaani, haki ya kimungu imeandikwa katika dhamiri.360 Kwa sababu hiyo na kwa njia ya sheria, wanadamu hutafuta msamaha wa dhambi na haki. 8. Lakini Amri Kumi za Mungu hazidai tu matendo ya nje ya ambayo angalau sheria inaweza kuyazaa bali, zinadai pia yale yanayopita uwezo wa akili kabisa. Yaani, kumwogopa kweli, kumpenda kwa kweli, kumwomba kwa kweli, na kumsadiki Mungu kwa kweli kwamba anatusikia na tunautumainia msaada wake katika kifo na katika dhiki zote. Mwisho, Amri Kumi za Mungu hudai utiifu kwa Mungu katika kifo na mateso yote tusije tukajaribu kuyakimbia mambo haya au kuyatupilia mbali wakati Mungu anayaweka.
9. Hapa Madaktari Wanazuoni wamewafuata wanafalsafa wanaofundisha tu haki ya akili, yaani, matendo ya kiraia na kudhania kwamba, akili inaweza imani) inatangamana kamili na kusudi na matumizi ya Martin Luther 360 Rum. 2: 14-15
kumpenda Mungu kuliko vitu vyote bila Roho Mtakatifu. Mradi nafsi ya mtu imetulia na haihisi ghadhabu au hukumu ya Mungu, anaweza kufikiria kwamba anataka kumpenda na pia kuyatenda mema kwa ajili ya Mungu. Wao hufundisha kwamba, watu hustahili msamaha wa dhambi kwa njia hii, yaani, kufanya kulingana na nguvu zao. Yaani, akili ikisikitikia dhambi, inatokeza tendo la kumpenda Mungu au kutenda mema kwa ajili ya Mungu. 10. Kwa kuwa mtazamo huu huwapendeza wanadamu, imejitokeza na kuzidisha aina nyingi za ibada kanisani, kama vile nadhiri za watawa na matumizi mabaya ya misa; 11. Kwa ajili ya mtazamo huu, ibada fulani na desturi za kuzishika kanuni zilianzishwa daima na mtu fulani ili kulielimisha na kulizidisha tegemeo la matendo ya jinsi hiyo, walithibitisha kwamba, kwa lazima Mungu humpa neema yake atendaye hivyo. Lazima hiyo ni ya utaratibu usiobadilika na siyo wa shurutisho.361
12. Kutokana na mtazamo huu kuna makosa mengi makubwa na yenye madhara, ambayo yangeweza kuchukua muda mrefu kuyaorodhesha. Hivyo msomaji mwenye busara alizingatie tu hili: iwapo ndilo haki ya Kikristo, kuna tofauti gani kati ya falsafa na mafundisho ya Kristo? Iwapo tutastahili msamaha wa dhambi kwa matendo yetu haya yaliyotajwa, basi, Kristo anafanya nini? 13. Iwapo tutaweza kuhesabiwa haki kwa njia ya akili zetu na kwa matendo yetu, tutakuwa na haja gani na Kristo na kuzaliwa upya? Kutokana na misingi ya maoni haya, mambo yametokea kwamba, hata watu wengi wanatudhihaki kwa kufundisha kwamba, wanadamu hawana budi kuitafuta haki fulani zaidi ya ile ya falsafa. 14. Tuna habari za baadhi ambao waliiweka Injili kando katika mahubiri yao na waliifafanua elimumaadili ya Aristotele. Iwapo maoni ya wapinzani wetu ambayo wao huyatetea kuwa ni sahihi, hawakukosea hata kidogo walipofanya hivyo. Maana, Aristotele aliandika kwa njia ya maarifa sana kuhusu maadili ya raia kwamba hakuna haja ya kuliongezea lolote zaidi. 15. Tunayaona maandiko yaliyotolewa na yanayoweka misemo fulani fulani ya Kristo pamoja na yale ya Sokrate, Zeno362 na wengine kana kwamba, Kristo alikuwa amekuja kutoa aina za sheria fulani ambazo kwazo tunastahili msamaha wa dhambi, badala ya kuupokea bure kwa ajili ya stahili za Kristo. 16. Hivyo, tukiyapokea mafundisho ya wapinzani wetu kwamba, sisi hustahili msamaha wa dhambi na haki kwa matendo ya akili, hapatakuwepo na tofauti yoyote baina ya haki ya kifalsafa au ya Kifarisayo na haki ya Kikristo.
361 Kilatini: ‘Necessitas coactionis’ (shurutisho) na ‘necessitas immutabilis’ (utaratibu wa Mungu usiobadilika); hizi ni istilahi za theologia za madaktari wanazuoni wa shule ya Kifransiskano kama Gabriel Biel na Bonaventura.
362 Sokrate, Σωκρατης, mwanafalsafa na mfano wa Platoni na wengine huko Athena (mnamo 470-399 K.K.). Zeno, Ζενων, wa Elea (mnamo 490-430), na Zeno Mdogo wa Kitiono (mnamo 335-263 K.K.), mwanzilishi mmoja wa Shule ya Stoa.
17. Hata hivyo, wapinzani wetu huudai ufahamu wa kihistoria kuhusu Kristo ili wasimkwepe kabisa na kumtukuza kwamba, kwa njia yake tunastahili kupewa hali fulani au jinsi waiitavyo “neema ya kwanza.” Wao huelewa kwamba, hali hii ni mwelekeo wa kumpenda Mungu kwa wepesi zaidi. Lakini hali hii haionekani kuwa ya maana sana kwa sababu wao hudhania kwamba, vitendo vya nia ya mtu kabla ya hali hii na baada yake ni vya aina moja. Wanadhania kwamba, nia inaweza kumpenda Mungu, lakini hali hii inaiamsha itende hivyo kwa radhi zaidi. Licha ya hayo, wao hudai tuistahili hali hii ya kwanza kwa stahili zilizotangulia.363 Kisha, wao huamuru tustahili ongezeko la hali hiyo na uzima wa milele kwa matendo ya sheria. 18. Kwa hiyo, wao humzika Kristo na kuwafanya watu wasimtumie kama Mpatanishi na waamini kwamba, kwa njia yake, wanapokea bure msamaha wa dhambi na suluhisho. Badala yake, wao huwafanya waote kwamba, wanastahili msamaha wa dhambi na wanahesabiwa haki mbele za Mungu kwa utimizo wao wa sheria. Ingawa sheria haiwezi kutosheka kamwe, na akili huyatenda matendo fulani ya nje, akili haimwogopi Mungu wala haiamini kwa kweli kuwa Mungu hujali. Ingawa wao huizungumzia hali hiyo, lakini bila haki ya imani, upendo wa Mungu hauwezi kupatikana wala hauwezi kufahamika na wanadamu.
19. Wanapoudhania uweza wao unaotofautisha kati ya stahili ya ulinganifu na stahili ya cheo,364 wanacheza ili tu wasionekane kuwa sawa na Wapelagio moja kwa moja.365 Maana, ikiwa Mungu humpa mtu stahili ya ulinganifu kama jambo la lazima, haitakuwa stahili ya ulinganifu bali stahili ya heshima. Basi, hawaelewi wanalolizungumzia. Wao hudhania kuwa baada ya upendo kwa Mungu, mwanadamu anapata stahili ya heshima. Hata hivyo, wao humfanya mtu kuwa na mashaka kuhusu uwepo wa hali hii. Basi, mtu anawezaje kujua iwapo ana stahili ya ulinganifu au ya heshima? 20. Lakini suala hili zima limezushwa na watu wazembe wasiofahamu jinsi msamaha wa dhambi hupatikana au jinsi hukumu ya Mungu na vitisho vya dhamiri huliondoa kabisa tegemeo letu katika matendo. Wanafiki wasiokuwa na hofu husadiki daima kwamba, wana stahili za heshima bila kujali kama hali hii ipo au haipo. Kwa kuwa, kawaida watu huitegemea haki yao wenyewe. Lakini dhamiri zilizotishika huyumba, hujaa mashaka, hutafuta, na kisha hujilimbikizia matendo mengine ili zijipatie amani. Dhamiri hizo hazifikirii kamwe kwamba, zina stahili ya heshima na hukata tamaa kwa kishindo zinapoyasikiliza mafundisho ya sheria zaidi ya yale ya Injili ambayo ni ya msamaha wa dhambi wa bure na wa haki ya imani.
363 Kilatini: ‘Merita praecedentia.’
364 ‘Stahili ya cheo,’ Kilatini: ‘meritum de congruo:’ stahili ya mtu kwa kadiri ya matendo yake. “Stahili ya hadhi,” Kilatini: ‘meritum de condigno:’ Stahili ambayo huja kutoka nje kuhusu matendo ya mtu.
365 Taz. ‘Ukiri wa Augsburg,’ fungu la pili.
21. Hivyo basi, wapinzani wetu hawafundishi kitu ila haki ya akili au sheria. Wanaikodolea macho jinsi Wayahudi walivyouangalia uso wa Musa uliofunikwa. Wanawahimiza wanafiki, ambao hufikiri kwamba, wanairidhisha sheria katika ufidhuli wao, majivuno, matendo yao, na katika kuidharau neema ya Kristo, wakati wanaziweka dhamiri zenye hofu kwenye hali ya kukata tamaa kwasababu, wanapokuwa na mashaka hawataweza kamwe kuona imani ni nini na inaleta matokeo gani. Hivyo, mwishowe hukata tamaa kabisa.
22. Kwa upande wetu, tunaitafakari kwamba Mungu anataka haki ya akili. Kwa ajili ya amri ya Mungu, lazima tuyatende yale yanayoagizwa na Amri Kumi za Mungu, jinsi ilivyoandikwa katika Gal. 3: 24: “Hivyo torati imekuwa kiongozi,” na 1 Tim. 1: 9: “Sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, . . . ” Maana, kwa nidhamu ya kiraia Mungu hutaka kuwashurutisha watu wanaoyatii mapenzi ya mwili366 na ili kuihifadhi nidhamu hii, ametupa sheria, ustaarabu,367 utaalamu, hakimu, na adhabu. 23. Kwa kiasi fulani, akili inaweza kuitekeleza haki hii kwa nguvu zake, ingawa mara nyingi inashindwa na udhaifu wa kibinadamu na Ibilisi anayeiingiza katika kashfa za wazi. 24. Kwa upande wetu, tunataka sana kuikiri heshima ya haki ya akili, kwa kuwa asili yetu ya uharibifu haina mema yoyote kuliko hii kama anavyosema Aristotele: “Hakuna ng’andu368 ya jioni wala ya alfajiri iliyo na urembo zaidi kuliko haki.”369 Mungu hata huizawadia baraka za mwili. Hata hivyo, tusiitukuze kwa fadhila ya Kristo.
25. Ni uongo kudhania kwamba, tunastahili msamaha wa dhambi kwa matendo yetu.
26. Kadhalika ni uongo kwamba, mtu anahesabiwa haki mbele za Mungu kwa ajili ya haki ya akili.
27. Ni uongo kabisa kudhania kwamba, kwa nguvu zake zenyewe akili inaweza kumpenda Mungu kuliko vitu vyote na kuitekeleza sheria yake. Yaani, inaweza kumwogopa Mungu kweli na kumsadiki kweli kwamba yeye husikia maombi. Pia kwamba, inaweza kumtii Mungu wakati wa kifo na mapatilizo yake mengine na kutotamani mali ya wengine. Lakini akili inaweza kutekeleza matendo ya kiraia.
28. Ni uongo kabisa pia na fedheha kwa utukufu wa Kristo kudhania kwamba,
366 Kilatini: ‘Carnales.’
367 Kilatini: ‘Litteras.’ Maana yake ni (herufi), (barua), (vitabu), (fasihi). Kulingana na maoni ya Wayunani na Warumi wa kale, fasihi ni dalili maalumu ya ustaarabu wa taifa au ufalme au dola.
368 Nyota maalumu ya jioni na alfajiri inayoitwa katika Kilatini, Kingereza n.k. ‘Venus,’ yaani, mungu wa kike mrembo wa upendo wa Warumi wa kale.
369 Elimumaadili ya Nikomakhos 5, 3.
watu wanaotekeleza Amri Kumi za Mungu bila neema hawatendi dhambi.
29. Msimamo huu wetu una ushuhuda siyo katika Maandiko Matakatifu tu bali pia katika maandiko ya mababa wa Kanisa. Kwa kupingana na Wapelagio, Agostino ameelezea sana kwamba, neema haitolewi kwa ajili ya stahili zetu. Katika kitabu chake kiitwacho “Asili na Neema”370 anasema: “Ikiwa uwezekano wa asili utasaidiwa na hiari, utatosha ili kugundua namna mtu anavyopaswa kuishi, na pia kwa maisha yaliyo bora. Basi, Kristo alikufa bure na hivyo pia, kashfa ya msalaba imebatilika.371 30. Kwa nini basi, mimi pia nisilalamike hapa? Lakini nitapaza sauti ili kuwakaripia kwa huzuni ya Kikristo: “Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa asili;372 mmeanguka na kutoka katika haki ya neema,” kwani “Wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.” Kadiri Kristo alivyo “mwisho wa sheria,” vivyo hivyo ni Mwokozi wa asili ya mwanadamu iliyopotoka kwa ajili ya haki kwa “kila aaminiye . . .” 373 31. Yn. 8: 36: “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.” Kwa hiyo basi, akili haiwezi kutuweka huru na dhambi zetu wala kutustahilisha kupata msamaha wa dhambi. Tena katika Yn. 3: 5 imeandikwa: “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” Lakini ikiwa inatubidi tuzaliwe upya kwa Roho Mtakatifu, basi, ni dhahiri kwamba, haki ya akili haituhesabii haki mbele za Mungu na haitekelezi sheria. 32. Pia katika Rum. 3: 23 tunasoma: “. . . wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu,” yaani, wamepungukiwa hekima na haki ya Mungu inayomfahamu na kumheshimu. Pia Rum. 8: 7-8 inasema: “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.” 33. Nikitumia maneno ya Agostino alipolijadili jambo hili, maneno haya ni ushuhuda wazi kiasi kwamba, hayahitaji kutafakari ila tu msikilizaji makini afanye hivyo. Kwa kuwa, nia ya mwili ni uadui dhidi ya Mungu, ni dhahiri kwamba, mwili hutenda dhambi hata utendapo shughuli za kawaida za kiraia. Mwili usipokuwa chini ya Sheria ya Mungu, hakika huzitenda dhambi hata unapoyatoa matendo mazuri sana na yenye sifa nzuri machoni pa wanadamu. 34. Wapinzani wetu huzitazama amri za kibao cha pili, zinazozingatia haki za kiraia zinazoweza kueleweka kwa njia ya akili. Wanaofikiria kwamba wanatimiza sheria ya Mungu wanajiridhisha kwa hayo. Kumbe, hawakioni vyema kibao cha kwanza cha Amri Kumi za Mungu kinachotuamuru tumwogope
370 Kilatini: ‘De natura et gratia.’
371 Gal. 2 : 21
372 Paulo: ‘Sheria’; hapa ni jambo lilo hilo lenye maana sawa na ‘asili.’
373 Gal. 5:4; Rum. 10: 3-4
na tumpende Mungu kweli, tusadiki hakika kwamba, anaichukia dhambi, na tuwe na hakika kwamba Mungu hutusikia. Lakini nafsi ya mwanadamu isiyokuwa na Roho Mtakatifu wala hofu ama inayoidharau hukumu ya Mungu, hukimbia na kuchukia hukumu yake. Kwa hiyo, haikitii kibao cha kwanza cha Amri Kumi za Mungu. 35. Mwanadamu ana asili ya kumdharau Mungu na ya kutilia mashaka kuhusu neno lake, vitisho, na ahadi zake. Kwa sababu hiyo, wanadamu hutenda dhambi kweli hata wanapotenda mambo maadilifu bila Roho Mtakatifu, kwa maana huyafanya hayo kwa moyo mwovu jinsi tunavyosoma: “Kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.”374 Watu wa jinsi hiyo humdharau Mungu wanapotenda mambo haya, jinsi Epikuro375 alikataa kuamini kuwa Mungu alimjali, alimstahi na alimsikiliza. Kwake Mungu, dharau hii inachafua matendo maadilifu maana Mungu huihukumu mioyo.
36. Hatimaye, wapinzani wetu walikuwa wakiandika mambo ya ujinga sana waliposisitiza kwamba, watu wenye hatia ya ghadhabu ya milele wanapaswa kustahili msamaha wa dhambi kwa njia ya kivutio cha tendo la upendo kwakuwa haiwezekani kabisa kumpenda Mungu bila imani kuupokea kwanza msamaha wa dhambi. Moyo usiohisi ghadhabu ya Mungu kweli hauwezi kumpenda isipokuwa huonekana kuwa Mungu amepatanishwa nao. Anapotutisha na anapoonekana kuwa anatutupa kwenye mauti ya milele, asili ya kibinadamu haiwezi kutiwa moyo wa kumpenda Mungu wa ghadhabu, wa hukumu, na wa adhabu. 37. Ni rahisi sana kwa wazembe wasiokuwa na kazi kuzibuni ndoto hizi kuhusu upendo wa mtu mwenye hatia ya dhambi ya mauti, kumpenda Mungu kuliko vitu vyote. Kwakuwa hawaielewi hata kidogo ghadhabu wala hukumu ya Mungu. Lakini wakati wa maumivu ya dhamiri na mashindano ya ndani, dhamiri inaugundua upuuzi huu wa ulanguzi wa falsafa ulivyo batili. 38. Paulo anasema: “Sheria ndiyo ifanyayo hasira.”376 Hasemi kwamba, kwa njia ya sheria watu hustahili msamaha wa dhambi. Maana, daima, sheria huzishtaki na kuzitisha dhamiri. Sheria haimhesabii mtu haki kwa sababu dhamiri iliyotishwa na sheria huikimbia hukumu ya Mungu. Kwa hiyo, wanaotegemea kustahili msamaha wa dhambi kwa njia ya sheria na matendo yao wenyewe hukosea sana. 39. Sasa, maneno haya, yamekwisha kutoshea kuhusu haki ya akili au sheria kama wafundishavyo wapinzani wetu. Baadaye, tutakapofafanua msimamo wetu kuhusu haki ya imani, tutalazimishwa na jambo lenyewe kutoa ushahidi mwingi zaidi. Ushahidi huu utasaidia pia kuyapinga yale makosa ya wapinzani wetu
374 Rum. 14: 23
375 Epikuro, mwanafalsafa Myunani (341-270 K.K.), alifundisha kwamba, maana ya maisha ya binadamu ni anasa, utulivu na furaha.
376 Rum. 4: 15
tuliyokuwa tukiyadondoa.
40. Kwa kuwa, wanadamu hawawezi kuitekeleza sheria ya Mungu kwa nguvu zao wenyewe, wote wanatawaliwa na dhambi, ni wenye hatia ya ghadhabu ya milele na mauti, hawataweza kujiweka huru mbali na dhambi wala kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria. Lakini, ahadi ya msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki vilitolewa kwa sababu ya Yesu Kristo aliyetolewa kwa ajili yetu kuridhika kwa dhambi za ulimwengu na ameteuliwa awe Mpatanishi na msuluhishi. 41. Ahadi hii haina sharti lolote la stahili zetu bali inautoa msamaha wa dhambi bure na kuhesabiwa haki, jinsi Paulo asemavyo: “Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena . . .”377 Pahali pengine anasema: “Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria.”378 Maana yake ni kwamba, msamaha wa dhambi hutolewa bure. Upatanisho hautegemei stahili zetu kamwe. 42. Kama msamaha wa dhambi ungetegemea stahili zetu na kama upatanisho ungekuwepo kwa njia ya sheria, hapo, usingefaa kitu. Kwa sababu sisi hatuitekelezi sheria, kamwe tusingeishika ahadi ya upatanisho. Kwa ajili ya hayo, Paulo anatoa hoja hii katika Warumi 4: 14 kwamba: “Maana ikiwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika.” Maana, kama ahadi ingekuwa na sharti la stahili zetu na sheria ambazo kamwe hatuzitekelezi, hapo ahadi ingekuwa haina maana.
43. Basi, kwa kuwa tunahesabiwa haki kwa ahadi ya bure, inafuatana na kwamba sisi hatuwezi kamwe kujihesabia haki. Basi, vinginevyo, ahadi inahitajika kwa kusudi gani? Kwa kuwa, ahadi haiwezi kupokelewa isipokuwa kwa imani, hasa, Injili iliyo ahadi ya msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki kwa ajili ya Kristo, inaihubiri haki ya imani katika Kristo, ambavyo sheria haivifundishi, wala hii siyo haki ipatikanayo kwa njia ya sheria. 44. Maana, sheria inadai matendo yetu na utimilifu wetu wenyewe. Lakini kwetu sisi tulioonewa na dhambi na mauti, ahadi inatoa upatanisho bure kwa ajili ya Kristo ambao tunaupokea kwa imani tu wala siyo kwa matendo. Imani hii inaleta tegemeo kwa Mungu ambalo halitokani na stahili yetu, bali lililo katika ahadi ya rehema ya Kristo peke yake. 45. Imani hii maalumu ya mtu binafsi,379 ambayo kwayo mtu yeyote akiamini kuwa dhambi zake zimesamehewa kwa ajili ya Kristo na kwamba, Mungu amepatanishwa na kuridhishwa kwa ajili ya Kristo, imani hii itaupokea msamaha wa dhambi na ikutuhesabia haki. Wakati wa toba, yaani miongoni mwa hofu kuu, imani hii itaifariji mioyo na kuitia hamasa, itatuzaa upya na kutupa Roho Mtakatifu ili
377 Rum. 11: 6
378 Rum. 3: 21
379 Kilatini: ‘Fides specialis,’ yaani imani ya binafsi (maalumu) kinyume cha ujuzi wa nje wa kihistoria (malimwengu).
tuweze kuitekeleza sheria ya Mungu. Yaani, kumpenda Mungu, kumwogopa kweli, kuwa na uhakika kwamba, anatusikiliza, kumtii Mungu miongoni mwa dhiki zote, kuziharibu tamaa n.k. 46. Kwa njia hii, imani ambayo huupokea bure msamaha wa dhambi, humweka Kristo aliye Mpatanishi na mtoa ridhaa dhidi ya ghadhabu ya Mungu na sio stahili zetu au upendo wetu. Basi imani hii, ni ufahamu wa kweli wa Kristo, inatumia fadhili zake, baraka za Kristo, hata huizaa mioyo upya na inautangulia utumizo wetu wa sheria. 47. Hakuna hata silabi moja ya imani hii inayopatikana katika mafundisho ya wapinzani wetu. Kwa hiyo basi, tunawakaripia wapinzani wetu kwa kufundisha kwao haki ya sheria badala ya haki ya Injili, ambayo huihubiri haki ya imani katika Kristo.
Ni Imani ipi Inayokufanya kuwa Mwenye Haki?
48. Wapinzani wetu hudhania kwamba, imani ni ile tu ya ujuzi wa kihistoria na kufundisha zaidi kwamba, imani hii inaweza kupatikana pamoja na dhambi ya mauti. Basi, hawasemi neno lolote kuhusu imani ambayo kwayo, jinsi asemavyo Paulo mara nyingi kwamba, binadamu huhesabiwa haki, kwa kuwa wanaohesabiwa haki mbele za Mungu hawaishi katika dhambi ya mauti. Imani inayomhesabia mtu haki, siyo tu ujuzi wa kihistoria, bali ni kuidhinisha ahadi ya Mungu yenye ahadi ya msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki. Kusudi hakuna mtu mwingine adhaniaye kuwa ni ujuzi tu tunaongezea kwamba, imani inamaanisha kutamani na kupokea ahadi ya msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki.
49. Ni rahisi sana kutambua tofauti kati ya imani ya jinsi hii na haki ya sheria. Imani ni ibada380 inayopokea fadhili zinazotolewa na Mungu. Haki ya sheria ni ibada381 inayomtolea Mungu dhabibu za stahili zetu wenyewe. Mungu anataka kuabudiwa kwa imani, yaani, kwa njia ya kutuwezesha tupokee lolote analoliahidi na analolitoa.
50. Paulo anaelezea wazi kwamba, imani haimaanishi tu ujuzi wa kihistoria, bali ni imani inayoidhinisha ahadi kama alivyosema: “Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba, ile ahadi iwe imara . . .”382 Ni msimamo wake kwamba, ahadi haiwezi kupokelewa isipokuwa kwa njia ya imani. Kwa hiyo, anaunganisha ahadi na imani na anavifanya viwiane. 51. Itakuwa rahisi zaidi kubainisha imani ni ipi kama tukiuangalia Ukiri wa Imani ambao hulitangaza kwa
380 Melanchthon anatumia neno la Kiyunani ‘λατρεια’ kutoka Warumi 9: 4,12.
381 Taz. rejeo lililotangulia.
382 Rum. 4: 16
makini fungu hili: Msamaha wa dhambi!383 Hivyo, haitoshi kuamini kwamba, Kristo alizaliwa, akateswa, kisha akafufuka, bila kuliongezea fungu hili, yaani, msamaha wa dhambi ambalo ndilo lengo la historia nzima.384 Mengine ni lazima tuyaunganishe na fungu hili hapa: Msamaha wa dhambi umetolewa kwa ajili ya Kristo na siyo kwa ajili ya stahili zetu. 52. Kama stahili zetu zingeweza kuitoa ridhaa kwa ajili ya makosa yetu, kwa nini basi ilikuwa lazima kumtoa Kristo kwa ajili ya makosa yetu?
53. Kila mara katika kuzungumzia imani iletayo haki, itatubidi pia kuyajua sawia mambo haya matatu: Kwanza, ahadi yenyewe, pili, zawadi peke yake, na tatu, stahili za Kristo ambazo ni kama malipo na ridhaa. Ahadi hupokelewa na imani; Zawadi ya bure inatupilia mbali stahili zetu na inamaanisha kwamba, fadhili inatolewa kwa ajili ya rehema. Stahili za Kristo ni malipo, kwa sababu ni lazima kuwe na upatanisho fulani kwa ajili ya makosa yetu. 54. Maandiko Matakatifu yamejaa maombi ya rehema. Mababa watakatifu walisema mara nyingi kwamba, tunaokokewa kwa rehema. 56. Kila mara rehema inapotajwa, basi, inatubidi tukumbuke kwamba, imani inayopokea ahadi ya rehema inahitajika hapo. Kwa upande mwingine, wakati wowote tutakapotaja imani, tutataka kabisa kwamba, lengo lake lenyewe ambalo ni ahadi ya rehema lifahamike. Imani haimfanyi mtu ahesabiwe haki au aokolewe kwa njia ya kuwa na imani yenyewe bali ni kwa kuwa yenyewe peke yake (imani) inapokea rehema iliyoahidiwa.
57. Ibada hii385 husifiwa pote katika vitabu vya manabii na zaburi, ingawa sheria haifundishi msamaha wa dhambi utolewao bure. Lakini Mababa386 walifahamu ahadi kuhusu Kristo, yaani kwamba, kwa ajili ya Kristo Mungu alikusudia kuzisamehe dhambi. Kama walivyotambua kwamba, Kristo atakuwa malipo ya makosa yetu, walifahamu vizuri kwamba, matendo yetu hayawezi kuwa malipo ya jambo hili lililo kubwa mno. Hali kadhalika, walipokea kwa imani rehema na msamaha wa dhambi bure, kama jinsi ilivyo kwa watakatifu wa Agano Jipya. Haya ndiyo marudio mengi ya rehema na imani kutoka kwa zaburi na manabii yanayofungamana na: “Bwana, kama wewe ungehesabu maovu, ee Bwana, nani angesimama?”387 Basi, anaungama makosa yake bila kuzirejea stahili zake. Anaongezea pia: “Lakini kwako kuna msamaha ili
383 Ukiri wa Mitume, Fungu la Tatu: “Namwamini Roho Mtakatifu, Kanisa tatatifu la Kikristo lililo moja tu, msamaha wa dhambi . . .”
384 Maandiko ya Kilatini: ‘Resuscitare,’ yaani. “huishwa tena.” Andiko la Kijerumani: ‘Auferstehen,’ yaani, “kufufuka.” “Lengo la historia,” Kilatini: ‘Causa finalis,’ istilahi ya falsafa ya Aristotele. Tafsiri ya Kijerumani inapungukiwa na istilahi kamili: ‘Darum das alles geschehen:’ “Kwa ajili yake, yote yalitendeka.”
385 Kiyunani: ‘Λατρεια.’
386 Akina Baba wa Agano la Kale.
387 Zab. 130: 3
wewe uogopwe.”388 Hapa anajifariji kwa tegemeo lake kwa rehema ya Mungu. Ananukuu ahadi pia: “Nafsi yangu inangojea neno lake, nafsi yangu inamtumaini Bwana.”389 Maana yake: Kwa kuwa wewe umeahidi msamaha wa dhambi, mimi ninaishika ahadi yako. Hivyo, mababa pia hawakuhesbiwa haki kwa sheria, bali kwa njia ya ahadi na kwa imani. Inatushangaza sana kwamba, wapinzani wetu wanaipunguza imani kwa kiwango hiki, japo wanaona kwamba, inasifiwa pote kama aina bora ya ibada, kama ilivyo katika Zaburi 50: 15: “Ukaniite siku ya mateso; nitakuokoa, na wewe utanitukuza.” Hivyo ndivyo Mungu anavyopenda kujulikana na kuabudiwa. Anafanya hivyo kwa njia ya kupokea fadhili zake kwa ajili ya huruma yake, siyo kwa sababu ya stahili zetu. Hii ndiyo faraja kubwa katika dhiki zote. Wapinzani wetu huziondoa faraja za aina hiyo wanapoipunguza na kuidharau imani wakifundisha watu wamkaribie Mungu kwa matendo na stahili tu.
Imani katika Kristo Huhesabia Haki
61. Kwanza kabisa, mtu yeyote asifikirie kwamb tunazungumzia ujuzi wa kihistoria tu usio na maana. Tunalazimika kuelezea jinsi imani inavyotokea na baadaye tutaonyesha jinsi imani inavyohesabia haki na maana yake. Kisha, ndipo tutayabatilisha mabishano ya wapinzani wetu. 62. Katika sura ya mwisho ya Luka, Kristo anaamuru kwamba, toba na msamaha wa dhambi vihubiriwe kwa jina lake.390 Injili huelezea kwamba, wanadamu wote wako chini ya dhambi na wanastahili ghadhabu na mauti ya milele. Licha ya hayo, inauahidi (Injili) msamaha wa dhambi kwa ajili ya Kristo na haki ambao hupokelewa kwa imani. Mahubiri ya toba yanayoithibitisha hatia yetu, huogopesha dhamiri zetu kwa vitisho vikubwa na vya kweli. Wakati wa vitisho hivi, mioyo lazima ipate faraja. Faraja hii itapokelewa pia, wakiiamini ahadi ya Kristo inayotutawala, yaani kwamba, kwa ajili yake Kristo tuna msamaha wa dhambi. Imani hii huleta amani, hutufariji, hupokea msamaha wa dhambi, hutuhesabia haki na kutuhuisha. Yaani, faraja hii ni uzima mpya na wa kiroho. 63. Mambo haya ni wazi na dhahiri yenye ushuhuda wa Kanisa na yanayofahamika kwa wacha Mungu. Wapinzani wetu hawawezi kamwe kusema njia ya kumpata Roho Mtakatifu. Wanadhania tu kwamba, sakramenti zinatutolea Roho Mtakatifu kwa njia ya tendo lenyewe391 bila mwenendo ulio halali katika wale wanaompokea, kana kwamba, zawadi ya Roho Mtakatifu inakuwa jambo lisilo na maana.
388 Zab. 130: 4
389 Zab. 130: 5
390 Lk. 24: 47
391 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
100
64. Lakini sisi tunazungumzia kuhusu imani isiyokuwa mawazo matupu, bali ile inayotuweka huru mbali na kifo, inayootesha maisha mapya ndani ya mioyo, na iliyo kazi ya Roho Mtakatifu. Kamwe, imani hii haiwezi kudumu pamoja na dhambi ya mauti, bali pale inapoonekana huzaa matunda mema, kama tutakavyoelezea baadaye. 65. Basi, tunawezaje kusema kwa urahisi zaidi na kwa uwazi mkuu zaidi kuhusu uongofu wa waovu au kuzaliwa upya? Basi, angalau wajaribu kuutoa ufafanuzi mmoja wa fasihi ya “Sentensi”392 kutoka umati huu mkubwa mno ya waandishi, ikielezea jinsi kuzaliwa upya kunavyotokea. 66. Wanapozungumzia kuhusu hali ya upendo, hudhania kuwa mtu anaweza kuistahili kwa matendo. Hawafundishi, jinsi Waanabaptisti walivyofanya pia wakati huo, kwamba, hali hii inapokelewa kwa njia ya neno.393 67. Lakini kwa kuwa hatuwezi kumshika Mungu, na hatuwezi kumfahamu isipokuwa kwa njia ya Neno. Kwa sababu hiyo, haki inatekelezwa pia kwa njia ya neno, kama Paulo asemavyo: “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye,. . .” na “Basi imani, chanzo chake ni kusikia. . .”394 Hapa tunaweza kuitumia hoja hii kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani, kwa maana ikiwa haki hutekelezwa kwa njia ya neno peke yake, na neno hupokelewa kwa njia ya imani tu, basi, linalofuatia ni kuwa imani huhesabia haki. Lakini, bado tuna hoja zingine zenye mvuto. 69. Hayo tuliyoyasema mpaka sasa ilikuionyesha namna ya kuzaliwa upya na pia, imani tuliyokuwa tukiizungumzia ni ipi.
69. Sasa, tutaelezea jinsi imani inavyohesabia haki. Mwanzo wa yote, inatubidi kuwakumbusha wasomaji kwamba, tuataishikilia hoja isemayo, “Kristo ni Mpatanishi” ndipo tuitetee hoja isemayo, “imani huhesabia haki.” Kwa njia gani, basi, Kristo anaweza kuwa mpatanishi tusipomtumainia kama Mpatanishi, tusipofikiri kwamba, tunahesabiwa haki kwa ajili yake? Maana ya kuamini ni kuzitegemea stahili za Kristo, yaani kwamba, hakika kwa ajili yake Mungu anataka aridhike nasi. 70. Hali kadhalika, ni muhimu kuitetea hoja hii kwamba, “kando ya sheria ahadi ya Kristo ni ya lazima,” kisha tunalazimika kuitetea hoja isemayo, “imani huhesabia haki.” Naam, sheria haifundishi kuwa msamaha wa dhambi hupatikana bure. Pia, hatuwezi kuitimiza sheria mpaka kwanza tumpokee Roho Mtakatifu. Kwa sababu hiyo, hatuna budi kuitetea hoja hii kwamba, ahadi ya Kristo ni ya lazima. Ahadi hii haiwezekani kupokelewa isipokuwa kwa imani tu. Kwa hiyo, yeyote anayekana kwamba, imani haihesabii haki huwa anafundisha sheria tu na huiweka mbali Injili na Kristo.
392 Kilatini: ‘Sententiae.’ Sentensi ni mafundisho ambayo ni ya kuaminika, hata hivyo, bila idhini rasmi.
393 Taz. ‘Ukiri wa Augsburg,’ Fungu la Tano.
394 Rum. 1: 16; 10: 17
71. Labda wengine wakisikia kuwa imani huhesabia haki, wataielewa kama mwanzo kana kwamba, imani ni mwanzo wa haki au maandalizi ya kuhesabiwa haki, siyo ambayo kwayo wenyewe tunapokelewa na Mungu, bali ni matendo yatakayoifuata. 72. Wao hufikiria kwamba, imani inatukuzwa mno kwa sababu ni aina ya chanzo. Mwanzo huwa na maana sana sawa na msemo wa kawaida usemao, “mwanzo ni nusu ya kila kitu.”395 Ni kama kusema kwamba, masomo ya msingi396 huwafanya madaktari wa fani zote kwa kuwa huwaandaa, ingawa ni fani yenyewe inayomwandaa kila mmoja awe msanii. Sisi hatuufuati msimamo huo kuhusu imani. Badala yake, tunatetea mafundisho haya kwamba, tunahesabiwa haki au tunapokelewa na Mungu kwa ajili ya Kristo, hasa na hakika kwa imani peke yake. “Kuhesabiwa haki” kunamaanisha kuwafanya wakosaji wenye hatia wawe na haki, wazaliwe upya, watangaziwe na wahesabiwe kuwa wenye haki. Kwa maana, Maandiko Matakatifu huzungumzia njia hizo mbili. Kwa hiyo, kwanza, tunataka kuelezea wazi: Imani peke yake humfanya mwenye hatia kuwa na haki; maana yake ni kwamba, imani hupokea msamaha wa dhambi.
73. Neno hili dogo “tu”397 huwaudhi baadhi ya watu, ingawa Paulo anasema: “Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria”398; kadhalika katika Waefeso. 2: 8-9: “. . . ni kipawa cha Mungu wala; si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” Kadhalika katika Warumi 3: 24: “Wanahesabiwa haki bure . . .” Wasipolipenda neno hili la pekee “tu,” basi, wawe tayari kuyaondoa pia maneno mengine ya pekee ya Paulo kama “bure” “si kwa matendo” “ni kipawa” n.k. Maana, hata maneno hayo ni ya pekee kabisa. Kwa upande wetu, sisi tunaoondoa dai la ustahilifu, na siyo neno au sakramenti, kama wapinzani wetu wanavyodai kwa hila. Tumetangulia kusema kwamba, imani inatokana na neno, na hivyo ndivyo ilivyo. Tunaitukuza sana Huduma ya Neno.399 74. Upendo na matendo mema lazima viifuate imani. Kwa hiyo, haviondolewi kwa maana ya kuifuata imani. Lakini tegemeo lote la ustahilifu wa upendo au matendo mema linaondolewa kwenye kuhesabia haki. Tutaielezea hoja hii kwa uwazi zaidi.
395 Kiyunani: ‘Αρχη ημισυ παντος,’ Platoni ‘Sheria’ 6, 753 E.
396 Kilatini: ‘Grammatica,’ aina ya kwanza ya masomo ya shahada ya kwanza, yaani, sanaa za lugha, balagha au usemaji, upembuzi na muziki, Kilatini: ‘Artes liberales.’
397 Kilatini: ‘Sola fide,’ “imani peke yake,” “imani tu.”
398 Rum. 3: 28
399 Taz. ‘Ukiri wa Augsburg,’ Fungu la Tano.
Tunaupata Msamaha wa Dhambi kwa Imani katika Kristo peke yake
75. Tunahisi kwamba, hata wapinzani wetu wanakubali kwamba, kwanza, msamaha wa dhambi ni wa lazima katika kuhesabiwa haki.400 Maana, sisi sote tunapatikana chini ya dhambi. Kwa hiyo, tunatoa hoja ifuatavyo:
76. Kwanza, kuupokea msamaha wa dhambi ni sawa na kuhesabiwa haki jinsi ilivyoandikwa: “Heri aliyesamehewa dhambi.”401 77. Tunapokea msamaha wa dhambi kwa imani tu katika Kristo, wala siyo kwa upendo, wala siyo kwa sababu ya upendo au matendo, ingawa upendo huifuata imani. Kwa hiyo, tunahesabiwa haki kwa imani tu. 78. Hapa, kuhesabiwa haki hueleweka kuwa haki inayomfanya mtu awe mwenye hatia, mwenye haki, au azaliwe upya.
79. Itakuwa rahisi kuifafanua sentensi hii ndogo tukifahamu namna kusamehewa dhambi kunavyotokea. Wapinzani wetu wajinga wanabishana sana. Je, msamaha wa dhambi na kumiminiwa kwa neema ni mabadiliko yale yale? Katika swali hili waatu wasiokuwa na hofu hawakuwa na neno la kusema. Ni lazima hofu za dhambi na mauti ya milele vishindwe mioyoni mwetu kwa msamaha wa dhambi, kama Paulo anavyoshuhudua katika 1 Kor. 15:56-57? “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.” Hii ni kusema kwamba, inatishia dhamiri, naam, hii hutokea kwa njia ya sheria ambayo huifunua ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi. Lakini Kwa njia gani tunashinda katika Kristo? Kwa imani, tunapojifariji kwa tegemeo la rehema iliyoahidiwa kwa ajili ya Kristo. 80. Hivyo ndivyo ilivyo, tunapoithibitisha sentensi hii ndogo kama ifuatavyo. Ghadhabu ya Mungu haitaweza kutulizwa tukiyaweka mbele zake matendo yetu wenyewe, kwa kuwa Kristo amewekwa awe Mpatanishi, ambaye katika yeye Baba anapatanishwa nasi. Ni kwa imani tu Kristo anafahamika kama Mpatanishi. Kwa hiyo, kwa imani tu, tutaupokea msamaha wa dhambi tukiifariji mioyo yetu kwa tegemeo katika rehema iliyoahidiwa kwa ajili ya Kristo. 81. Ndivyo Paulo asemavyo katika Warumi 5:2: “Ambaye kwa yeye tumepata kumfikia Baba,” na anaongezea: “kwa imani.”402 Kwa njia hiyo, tutapatanishwa na Baba na tunaupokea msamaha wa dhambi tukifarijika kwa kuitegemea rehema iliyoahidiwa kwa ajili ya Kristo. Wapinzani wetu wanaelewa kuwa Kristo, akiwa kama Mpatanishi na Mtulizaji kwa njia hii, ameistahili
400 Hasa Yohana Duns Scotus (mnamo 1265 - 1308) na wafuasi wake, wakati msamaha wa dhambi ulikuwa katika muundo wa kitheologia wa Tomaso wa Akuino, hatua ya nne baada unyweshwaji wa neema, mwenendo wa hiari wa kumwelekea Mungu na mwenendo wa hiari dhidi ya dhambi.
401 Zab. 32: 1
402 Melanchthon, ‘Per fidem,’ yaani, “kwa imani” katika maana ya kuwa zana. ‘Union Version,’ “Kwa njia ya imani” katika maana ya hali.
hali ya upendo. Hawatuamuru kumtumia kama Mpatanishi badala yake, kana kwamba wamekwisha kumzika Kristo, wanadhania tunayo njia ya kumwendea Mungu kwa matendo yetu na kuistahili hali hii ya kimsingi. Hivyo, tunamfikia Mungu kwa njia ya upendo huu. Je, hii siyo kumzika Kristo kabisa na kuyatupilia mbali mafundisho yote ya imani? Kinyume chake, Paulo hufundisha kwamba, tunamfikia Mungu kwa ajili ya Kristo aliye Mpatanishi. Ili kuonyesha jinsi inavyotendeka, anaongezea kwamba, tunamfikia Mungu kwa imani. Hivyo, kwa imani na kwa ajili ya Kristo tunaupokea msamaha wa dhambi. Kamwe, hatuwezi kuweka upendo wetu au matendo yetu mbele ya ghadhabu ya Mungu.
82. Pili, ni hakika kwamba, dhambi zinasamehewa kwa ajili ya Kristo aliye Mpatanishi kulingana na Warumi 3: 25: “Ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho,” na hapo Paulo anaongezea, “kwa imani.” Kwa hiyo, Mpatanishi huyu hutufaa tukiishika ahadi ya rehema kwa imani iliyo katika yeye na kuiweka mbele ya ghadhabu na hukumu ya Mungu. Kuna kauli inayofanana na hiyo katika Waebrania 4: 14-16: “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu . . . basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri.” Anatuamuru tumkaribie Mungu kwa ajili ya tegemeo katika Kristo, aliye Kuhani Mkuu, na siyo kwa ajili ya tegemeo katika ustahili wetu, kauli hii inahitaji imani.
83. Tatu, katika Matendo ya Mitume 10:43 Petro anasema: “Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.” Huyo Petro angewezaje kusema kwa uwazi zaidi? Anasema kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi kwa jina lake, yaani, kwa ajili yake, na siyo kwa ajili ya stahili zetu, kwa toba, kwa majuto,403 kwa upendo, na kwa ajili ya ibada au matendo yetu. Anaongezea, “tunapomwamini.” Basi, anadai imani. Yaani, hatuwezi kulishika jina la Yesu ila kwa imani. Licha ya hayo, anataja mwafaka wa manabii wote. Madai ya namna hiyo yanataja kwa hakika mamlaka ya Kanisa. Tutayarudia haya baadaye tutakapozungumzia kuhusu toba.
84. Nne, msamaha wa dhambi ni jambo lililoahidiwa kwa ajili ya Kristo. Hivyo basi, haliwezekani kupokewa isipokuwa kwa imani tu. Naam, ahadi haiwezi kupokelewa isipokuwa kwa imani peke yake. Warumi 4:16: “Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba, ile hadi iwe imara kwa wazao wote,” kwa maana kwamba: “Kama ingetegemea stahili zetu, ahadi ingekuwa isiyoaminika na isiyokuwa na maana kwa sababu tusingeweza kamwe kuamua kama tulistahili vya kutosha.” Dhamiri zenye uzoefu zinaweza kuelewa. Kwa hiyo, Paulo anasema katika G. 3:22: “Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa 403 Kilatini: ‘Contritio’ na ‘attritio.’
imani ya Yesu Kristo.” Hapa, anatunyima ustahilifu wowote, kwani anasema kwamba, wanadamu wote ni wenye hatia na hufungwa chini ya dhambi. Kisha, anaiongezea ahadi, yaani ahadi ya msamaha wa dhambi na ya kuhesabiwa haki, hata kuiongezea njia ya kupokelewa kwa ahadi hiyo, yaani kwa njia ya imani. Hoja hiyo, ambayo ni mahususi, inatokana na asili ya ahadi na mara kwa mara unarudiwa na Paulo.404 Hakuna hoja nyingine zaidi ambayo mtu anaweza kuiunda au kuidhania itakayokanusha hoja ya Paulo. 85. Hivyo, mioyo bora isiruhusu kufarakishwa na kauli hii kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi kwa imani tu kwa ajili ya Kristo. Hapa, (imani) ina faraja ya hakika na imara dhidi ya vitisho vya dhambi, dhidi ya mauti ya milele, na dhidi ya milango yote ya Jehanamu.405
86. Kwa kuwa tunaupokea msamaha wa dhambi na Roho Mtakatifu kwa imani peke yake, ni imani hiyo peke yake ambayo hutuhesabia haki. Wale waliopatanishwa wanahesabiwa kuwa wenye haki na watoto wa Mungu, siyo kwa sababu ya usafi wao bali kwa rehema na kwa ajili ya Kristo, mradi tu waishike rehema hii kwa imani. Hali kadhalika, Maandiko Matakatifu hushuhudia kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani. Basi, tunauongezea ushuhuda mwingine unaotangaza wazi kwamba, imani ndiyo haki yenyewe ambayo kwayo tunahesabiwa haki mbele za Mungu. Siyo kana kwamba, imani inakuwa kama tendo lenye ustahili, bali kwa sababu inapokea ahadi ya Mungu kwamba, kwa ajili ya Kristo Mungu hupendelea kuwa mwenye kuridhika kwa wale wanaomwamini Kristo. Kusema kweli, inatambua (imani) kwamba, “Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi.”406
87. Katika waraka wake kwa Warumi, Paulo anajadili hasa kuhusu aya hii na anasema kwamba, tunahesabiwa haki bure kwa imani tunapoamini kuwa kwaajili ya Kristo Mungu amepatanishwa nasi. Katika sura ya tatu, anautoa msimamo huo mkuu ambao ni jumla ya majadiliano yote: “Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.”407 Wapinzani wetu hufafanua haya kumaanisha taratibu za Walawi. Lakini hapa, Paulo anamaanisha sheria nzima, na siyo tu taratibu za kiibada. Kwa maana, baadaye kidogo, ananukuu Amri Kumi za Mungu: “Usitamani.”408 Kama matendo maadilifu yangestahilisha msamaha wa dhambi na haki, kusingekuwako na haja yoyote ya Kristo na ahadi, na yote ayasemayo Paulo kuhusu ahadi yangepinduliwa kabisa. Pia angekuwa amekosea vibaya alipowandikia Waefeso: “Tunaokolewa bure
404 Rum. 4: 16; Gal. 3: 18
405 Mt. 16: 18
406 1 Kor. 1: 30
407 Rum. 3: 28
408 Rum. 7: 7
kwa kipawa cha Mungu wala si kwa matendo. ”409 Paulo pia anamtaja Ibrahimu na Daudi waliokuwa na amri ya Mungu kuhusu tohara.410 Kama matendo yawayo yote yangehesabiwa haki, ni dhahiri kwamba, matendo haya yangeweza kuhesabiwa haki yaliyotokana na agizo. Lakini Agostino alifundisha hakika kwamba, Paulo anazungumzia kuhusu sheria nzima kama alivyoielezea kwa kirefu katika makala yake ya “Roho na Andiko” akisema mwishoni kuwa: “Kwa hiyo, baada ya kutafakari na kujadili mambo haya kadiri ya uwezo ambao Bwana aliona utafaa kutujulia, tunajumlisha kwa kusema kwamba, mtu hahesabiwi haki kwa njia ya kuyashika maagizo ya maisha mema, bali kwa imani katika Yesu Kristo.” 411
88. Ili tusifikirie kwamba, Paulo alikosea kidogo bila kukusudia, katika kuandika, “imani huhesabia haki,” alitoa hoja na alithibitisha katika mjadala mrefu katika Waraka kwa Warumi, sura ya nne, na kisha akazidi kuurudia katika nyaraka zake zote. 89. Anasema hivyo katika Warumi 4:4-5: “Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.” Hapa anasema wazi kabisa kwamba, imani peke yake ndiyo inahesabiwa kuwa haki. Kwa hiyo, imani ni jambo lile ambalo Mungu analitangaza kuwa haki. Anaongezea kwamba, linahesabiwa bure na kukana kwamba, lingewezekana kuhesabiwa bure kama lingekuwa ni malipo kwaajili ya matendo. Kwa sababu hiyo, anatupilia mbali pia matendo kulingana na sheria za maadili, kwa kuwa kama katika hayo tunapata kuhesabiwa haki mbele za Mungu, hapo imani isingehesabiwa haki bila matendo. 90. Pia baadaye Mt. Paulo anasema: “Kwa kuwa twanena ya kwamba kwake Ibrahimu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki.”412 91. Katika sura ya tano anasema kuwa, “Basi, tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu.” Maana yake: Dhamiri zetu zinatulia na kujaa furaha mbele za Mungu. 92. Katika Warumi 10:10 tunasoma: “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki . . .” Anatangaza hapa kwamba, imani ni haki ya moyo. Katika 2:16 anasema: “. . . sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria . . .” 93. Katika Waefeso 2:8-9 anasema: “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”
409 Efe. 2: 8
410 Rum. 4: 1-6
411 Kilatini: ‘De spiritu et littera’ 13, 22.
412 Rum. 4: 9
94. Katika Yohana 1:12-13 tunasoma: “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.” 95. Katika Yohana 3:14-15 tunasoma: “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa, ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.” 96. Kadhalika, katika Yohana 3:17-18 tunasoma: “Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.”
97. Kadhalika, katika Matendo ya Mitume 13:38-39 anasema: “Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi; na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.” Je, ni lipi lingeweza kuelezea bayana zaidi huduma ya Kristo na kuhesabiwa haki? Anasema: Torati haihesabii haki. Kwa sababu hiyo, Kristo ametolewa kwa kusudi tuamini kwamba tunahesabiwa haki kwa ajili yake. Dhahiri, anainyang’anya torati haki. Kwa hiyo, tunahesabiwa haki kwa ajili ya Kristo tunapoamini kuwa Mungu amepatanishwa nasi kwa ajili yake Kristo. 98. Katika Matendo ya Mitume 4: 11-12 tunasoma: “Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” Lakini jina la Kristo linashikwa/ linapokewa kwa imani tu. Kwa hiyo, tunaokolewa kwa ajili ya tegemeo katika jina la Kristo, na siyo kwa ajili ya tegemeo katika matendo yetu. Lakini hapa, “jina” linamaanisha kile kinachotajwa kuwa chanzo cha wokovu. Kulitaja jina la Yesu ni kulitegemea kama chanzo au gharama ambayo tunaokolewa kwayo. 99. Katika Matendo ya Mitume 15:9 tunasoma: “. . . akiwasafisha mioyo yao kwa imani.” Kwa hiyo, imani wanayoizungumzia mitume siyo maarifa matupu, bali ni kitu kinachompokea Roho Mtakatifu na kutuhesabia haki.
100. Katika Habakuki 2:4 tunasoma: “. . .mwenye haki ataishi kwa imani yake.” Hapa nabii anaonyesha kwamba, kwanza wanadamu wanahesabiwa haki kwa imani kwa kuwa wao huamini kwamba, Mungu ni mwenye huruma, na anaongezea kuwa imani ile ile huhuisha kwa maana inaleta amani moyoni, furaha, na uzima wa milele.
101. Katika Isaya 53:11 tunasoma: “Kwa maarifa . . . atawafanya wengi kuwa wenye haki.” Lakini maarifa kuhusu Kristo yana maana gani ila kuzifahamu
fadhili za Kristo, naam ahadi ambazo kwazo amezieneza kwa njia ya Injili ulimwenguni kote? Hakika na kwa kweli, kumwamini Kristo ni kuzifahamu fadhili hizi, kuamini kwa hakika kwamba, Mungu atayatimiza kabisa yale aliyoyaahidi katika Kristo.
102. Maandiko Matakatifu yanajaa ushuhuda wa aina hiyo. Kwa upande mmoja, yanafundisha sheria na, kwa upande mwingine, yanafundisha ahadi kuhusu Kristo, msamaha wa dhambi, na ridhaa bure kwa ajili ya Kristo.
103. Kuna ushuhuda wa aina ile ile, hapa na pale, katika maandiko ya Mbaba.413 Katika waraka Ambrosio anasema kwa Ireneo fulani414: “Lakini ulimwengu umewekwa chini yake Mungu kwa sheria. Amri ya sheria inawahusu wote na hakuna yeyote mwenye kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria. Maana yake: Dhambi inatambuliwa kwa njia ya sheria lakini hatia yake inabaki. Sheria inaonekana kutia hasara inapowafanya wote kuwa wakosaji, lakini Bwana Yesu aliwasamehe wote kwa kuja kwake na kwa kumwaga damu yake ameifuta hatia iliyokuwa ikitushtaki.415 Hili ndilo Mtume Paulo alisemalo: “Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;”416 kwa Kristo. Kwa maana, baada ya ulimwengu mzima kuwekwa nchini ya sheria, aliziondoa dhambi za ulimwengu, jinsi Yohana ashuhudiavyo anaposema: “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”417 Kwa hiyo, mtu yeyote asijisifie matendo, kwani hakuna anayeokolewa kwa matendo yake. Lakini mwenye haki ameipata hiyo kama zawadi kwa sababu alihesabiwa haki baada ya kuoshwa.418 Ni dhahiri kuwa imani ndiyo iwaekayo huru wanadamu kwa njia ya damu ya Kristo; maana, “Heri aliyesamehewa dhambi, na kusitiriwa makosa yake.”419 104. Haya ndiyo maneno ya Ambrosio yanayotetea waziwazi msimamo wetu. Anachukulia matendo haki kabisa na kuipa imani yenye kutukomboa kwa damu ya Kristo. 105. Kama utawakusanya pamoja wale waliotunga vitabu vya Sentensi waliotiwa madoido fahari ya majina yote, maana baadhi wanaitwa wa “kimalaika,” wengine “mwerevu” na “asiyekatalika”,420 lakini hawa wote pamoja na waliosomwa tena na tena hawasaidii katika kumwelewa Paulo kama ilivyo sentensi hii moja kutoka
413 Yaani, akina Baba wa Kanisa.
414 Ep.73, 16, 1307 n.y. Ireneo, huyu siye Baba wa Kanisa mwenye jina lilo hilo.
415 Kol. 2: 14
416 Rum. 5: 20
417 Yn. 1: 29
418 Andiko la Kijerumani: ‘In der Tauf in Christo’ (Katika Ubatizo katika Kristo).
419 Zab. 32: 1
420 Tomaso wa Akuino aliitwa ‘doctor angelicus,’ yaani, mwalimu wa kimalaika, Yohana Duns Scotus ‘subtilis,’ yaani, mwerevu na Aleksander wa Hales ‘irrefragabilis,’ yaani, asiyekatalika.
kwa Ambrosio.
106. Agostino aliandika sana dhidi ya Wapelagio kwa mujibu wa msimamo huo. Katika kitabu chake kiitwacho “Roho na Andiko”421 anasema: “Kwa hiyo basi, haki ya sheria inaonyeshwa kuwa tamko lisemalo kwamba, yeyote aitimizaye sheria ataishi kwayo, ili katika kuutambua udhaifu wake apate kumfikia anayehesabia haki, siyo kwa juhudi zake mwenyewe wala kwa herufi ya sheria yenyewe, kwa maana haiwezekani kufanyika hivyo, bali kwa imani inayompatanisha naye hata kuitenda sheria na kuishi kwayo. Tendo halali ambalo kwalo mtu anapata kuishi, halipatikani ila katika mtu aliyehesabiwa haki. Basi, kuhesabiwa haki kunafanikishwa kwa imani.” Hapa anaelezewa wazi kwamba, yeye anayehesabia haki anapatanishwa kwa imani na haki inafanikishwa kwa imani. Baadaye kidogo anasema: “Kwa upande wa sheria, tunamwogopa Mungu na kwa upande wa imani tunamtumainia Mungu. Bali kwao wanaoiogopa adhabu neema imefichwa. Lakini nafsi inayojikokota chini ya hofu hii, ikimbilie rehema ya Mungu kwa imani ili atoe lile aliloliamuru.” Hapo basi, anafundisha kwamba, mioyo yetu inaogopeshwa na sheria, lakini hupata faraja kwa njia ya imani. Anafundisha kwamba, afadhali kuishika rehema kwa imani kabla ya kujaribu kuitenda sheria. Baadaye kidogo tutayanukuu matamko mengine kadhaa.
107. Inashangaza sana kuona kwamba, wapinzani wetu hawavutwi na sehemu nyingi za Maandiko Matakatifu zinazopatia imani haki wazi na kuyakataa matendo. 108. Je, wanadhani kwamba, hili linarudiwa mara kwa mara bila sababu? Je, wanadhani pia kwamba, maneno haya yalianguka kutoka kwa Roho Mtakatifu bila kujua? Lakini, kwa hila, wamebuni kisingizio chao. 109. Naam, wao husema kwamba, inapaswa (haki) kuihusu “imani iundwayo na upendo,” yaani, hawaihusishi haki na imani, isipokuwa kwa ajili ya upendo.422 Zaidi ya hayo, hawapatii imani haki hata kidogo, bali upendo tu, kwa sababu wanadhania kwamba, imani inaweza kudumu na dhambi ya mauti. 110. Mafundisho haya yanaishia wapi kama siyo kukomesha ahadi na kuirudia sheria? Imani ikipokea msamaha wa dhambi kwa ajili ya upendo, daima, msamaha wa dhambi utabaki katika mashaka, kwa kuwa hatupendi jinsi tunavyopaswa. Kwa kweli, hatuwezi hata kidogo kupenda ipasavyo mpaka pale mioyo yetu inakuwa na uhakika kwamba, msamaha wa dhambi umekwisha kutolewa kwetu. Kwa njia hii, wapinzani wetu wanapodai tegemeo kwa upendo wetu kama sharti la msamaha wa dhambi na haki, wanaibatilisha kabisa Injili ya ondoleo la dhambi bure.
421 Kilatini: ‘De Spiritu et litera 29, 51.’
422 Kilatini: ‘Fides caritate formata.’
Maana, binadamu hawawezi kutoa wala kuelewa upendo huu bila kuamini kwamba, msamaha wa dhambi unapokelewa bure.
111. Hata sisi tunasema kuwa lazima upendo uifuate imani kama Paulo asemavyo: “Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.”423 112. Lakini kulingana na hili hatupaswi kufikiria kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi kwa kutegemea upendo huu au kwa ajili ya upendo huu, sawasawa na hili kwamba, hatupokei msamaha wa dhambi kwa matendo mengine yanayofuatia imani, bali kwa imani peke yake.424 Ni kwa njia ya imani, katika maana yake maalumu, ambayo hupokea msamaha wa dhambi kwani ahadi haiwezi kupokelewa ila kwa imani tu. 113. Imani, katika maana yake maalumu, hukubali ahadi na Maandiko Matakatifu yanayozungumzia kuhusu imani hii. 114. Maana, imani inaupokea msamaha wa dhambi na hata hutupatanisha na Mungu. Tunatangulia kuhesabiwa haki kwa imani kwa ajili ya Kristo kabla ya kupenda na kuishika sheria ingawa lazima upendo ufuatie. 115. Imani ya jinsi hii siyo maarifa ya bure, wala haiwezi kuwepo pamoja na dhambi ya mauti, bali ni kazi ya Roho Mtakatifu inayotuweka huru na mauti ikizifariji na kuzifufua akili zilizo na hofu. 116. Kwa kuwa, imani hii peke yake ndiyo ipokeayo msamaha wa dhambi na hutufanya tukubalike mbele za Mungu na humleta Roho Mtakatifu, hivyo, inapaswa kuitwa “neema inayotufanya kukubalika”425 kuliko kuuita upendo ambao ni matokeo ya neema.
117. Kwa kadiri hiyo, tumeonyesha tele kwa njia ya ushuhuda wa Maandiko Matakatifu na kwa hoja zinazotokana na Maandiko Matakatifu, ili jambo hili lipate kuwa dhahiri zaidi kwamba, tunapokea msamaha wa dhambi kwa imani tu kwa ajili ya Kristo. Isitoshe, tunahesabiwa haki kwa imani tu, yaani, katika/huwafanya wakosaji kuwa wenye haki na kuzaliwa upya. 118. Ni rahisi sana kuuhukumu umuhimu wa ufahamu wa imani hii, kwani kwa imani hiyo tu tunatambua huduma ya Kristo na kuzipokea fadhili zake na imani hii peke yake inatoa faraja ya hakika na imara kwa wacha Mungu. 119. Kwa hiyo, lazima mafundisho haya yawepo Kanisani ili wacha Mungu walipokee tumaini imara la wokovu.426 Wapinzani wetu huzitunza nafsi za wanadamu vibaya wanapowatafadhalisha wawe na mashaka kama waliopokea msamaha wa dhambi. Ni kwa njia gani wao ambao wanaamini kuwa na mashaka kuhusu msamaha wa dhambi ni lazima
423 Gal. 5 : 6
424 Kilatini: ‘Sola fide.’ Neno hili ni maarufu pamoja na maneno mengine mawili ya shime ya Kilutheri: “Maandiko Matakatifu peke yake” – ‘Sola Scriptura,’ na “kwa neema peke yake” – ‘Sola gratia.’
425 Kilatini: ‘Gratia gratum faciens.’
426 Hapa kuna mafundisho dhahiri ya Kilutheri kuhusu yakini ya wokovu dhidi ya mafundisho ya Roma kuhusu lazima ya wasiwasi ya wokovu. Msingi yakini wa wokovu ni Neno la Mungu lililo imara na dhahiri.
saa ya kifo, watastahimili iwapo hawajasikia lolote kuhusu imani hii? 120. Zaidi ya hayo, lazima Injili ya Kristo ibaki ndani ya kanisa, yaani, ahadi kuwa dhambi imesamehewa bure kwa ajili ya Kristo. Wale wasiofundisha hata kidogo kuhusu imani hii tunayoizungumzia wanaitangua kabisa Injili. 121. Madaktari Wanazuoni hawatoi neno lolote kuhusu imani hii. Wapinzani wetu huwafuata na kutoikubali imani hii. Wanashindwa kabisa kutambua kwamba, kutokubali imani hii kunaiangamiza ahadi yote ya msamaha bure wa dhambi na ya haki ya Kristo.
Upendo na Utimizaji wa Sheria
122. Hapa, waoinzani wetu wanahimiza sababu dhidi yetu kwa maneno haya: “Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.” Zaidi ya hayo wanasema: “Wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki,”427 na aya zingine kama hizo zinazohusu sheria na matendo. Kabla ya kuzijibu aya hizi, lazima tuseme yale tunayoamini kuhusu upendo na utimizaji wa sheria.
123. Imeandikwa katika kitabu cha nabii Yeremia: “Nitatia sheria yangu ndani yao . . .”428 Katika Warumi 3:31 Paulo anasema kwamba, imani haifutilii mbali sheria, bali inaiimarisha. Kristo anasema, “Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri”429 Kadhalika anasema: “Kama sina upendo, si kitu mimi.”430 124. vifungu hivi navingine vinashuhudia kwamba, lazima sheria ipate kukua katika sisi zaidi na zaidi. Hapa, hatuzungumzii kuhusu taratibu za ibada, bali Amri Kumi ambazo zinahusika na miendo ya moyoni. 125. Kwa kuwa, imani inatuletea Roho Mtakatifu na kuyazaa maisha mapya mioyoni, lazima izae pia misukumo ya kiroho mioyoni. Ni misukumo gani hiyo nabii anaionyesha anaposema: “Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika . . .”431 Baada ya kuhesabiwa haki na kuzaliwa upya kwa njia ya imani, tunaanza kumwogopa na kumpenda Mungu, kumwomba na kutazamia msaada kutoka kwake, kumshukuru na kumtolea sifa na kumtii katika huzuni. Tutaanza pia kuwapenda majirani zetu kwa kuwa mioyo yetu ina misukumo ya kiroho na takatifu.
126. Mambo haya hayawezi kutokea isipokuwa baada ya kuhesabiwa haki kwa imani na kuzaliwa upya, ndipo tunampokea Roho Mtakatifu. Kwanza kabisa, haiwezekani sheria itekelezwe bila Kristo. Kadhalika, haiwezekani sheria itekelezwe bila Roho Mtakatifu. 127. Lakini Roho Mtakatifu hupokelewa kwa njia ya imani, kulingana na maneno ya Paulo kwa Wagalatia: “Tupate
427 Mt. 19: 17; Rum. 2: 13
428 Yer. 31: 33
429 Mt. 19: 17
430 1 Kor. 13: 2
431 Yer. 31: 33
kupokea ahadi ya Roho kwa imani” (Wagalatia 3: 14). 128. Zaidi ya hayo, ni kwa njia gani basi, moyo wa mwanadamu unaweza kumpenda Mungu unaposikia kwamba, amekasirika vikali hata anatulemea kwa majanga ya wakati huo na ya milele? 129. Sheria inatushtaki daima na mara zote inatuonyesha Mungu alivyo mwenye ghadhabu. Hatuwezi kumpenda Mungu kamwe mpaka tutakapopokea rehema yake kwa njia ya imani. Baada ya haya, ndipo, Mungu anaweza kuwa wa kupendwa.
130. Ingawa kwa kiasi fulani inawezekana kufanya matendo mema ya kijamii bila Kristo wala Roho Mtakatifu, yaani, matendo ya nje ya kisheria, hata hivyo ni wazi, maana tulivyosema ni kwamba, yale ambayo ni kiini cha sheria ya Mungu, yaani, misukumo ya moyo ya kumpenda Mungu, iliyofundishwa katika ubao wa kwanza, haiwezi kupatikana bila Roho Mtakatifu. 131. Lakini wapinzani wetu ni mabingwa wa theologia! Wao huangalia ubao wa pili wa Amri Kumi za Mungu na matendo ya kisiasa. Hawaujali hata kidogo ule wa kwanza, kana kwamba, si kitu kuhusu jambo lenyewe au kudai zaidi matendo ya nje ya ibada. Wanaipuuza kabisa sheria ya milele iliyo juu kabisa ya hisi na akili za viumbe vyote: “. . . mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote.”432
132. Lakini Kristo ametolewa ili, kwa ajili yake tuweze kupokea zawadi ya msamaha wa dhambi na Roho Mtakatifu, ili azae ndani yetu haki ya milele na maisha mapya na ya uzima wa milele. Hivyo, sheria haiwezi kutimizwa sawasawa isipokuwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, ambaye tunampokea kwa imani. Kwa sababu hiyo, Paulo anasema kwamba, imani haitupilii mbali sheria, bali huiimarisha, maana sheria inaweza kutekelezwa pale tu Roho Mtakatifu anapotolewa.433 133.Katika 2 Kor.o 3:15-17, Paulo anafundisha kwamba, utaji uliofunika uso wa Musa hauwezi kuondolewa isipokuwa kwa njia ya imani inayompokea Roho Mtakatifu. Maana, hivi ndivyo anavyosema, “Ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. Lakini wakati wowote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa. Basi ‘Bwana’ ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.” 134. Kwa njia ya “utaji,” Paulo anamaanisha maoni ya kibinadamu kuhusu sheria nzima, yaani Amri Kumi za Mungu na taratibu za ibada. Maana wanafiki hudhani kuwa matendo ya nje na ya kijamii yanairidhisha sheria ya Mungu na kuwa dhabihu na matendo ya kiibada iwapo matendo yenyewe434 yanastahilisha mtu ahesabiwe haki mbele za Mungu. 135. Bali utaji huu unaondelewa kutoka kwetu, na ukosefu huu unaondolewa Mungu anapotudhihirishia moyoni mwetu uchafu wetu na
432 Kum. 6: 5
433 Rum. 3: 31
434 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
ukubwa wa dhambi zetu. Yakishafanyika hayo, hapo ndipo tunatambua tulivyo mbali na kushika sheria. Halafu tunakubali kwamba, katika hali yake isiyokuwa na hofu na ulegevu, mwili haumwogopi Mungu, au hauamui kamwe kutunzwa kwetu naye, bali hudhani kuwa watu huzaliwa na kufa kwa bahati mbaya. Ndipo tunaugundua upungufu wetu wa kuamini kuwa Mungu anatusikiliza na kutusamehe. Lakini tukisha kuisikiliza Injili ya msamaha wa dhambi na hata kuhimizwa kwa njia ya imani, tutapokea Roho Mtakatifu ili tuweze kumfikiria Mungu sawasawa, tutamwogopa na kumwamini n.k. Kutokana na haya, ni wazi kwamba, bila Kristo wala Roho Mtakatifu hatuwezi kuitimiza sheria.
136. Hivyo, sisi tunakiri kwamba, ni lazima utimizaji wa sheria uanzie kwetu na halafu uendelee kukua zaidi na zaidi. Lakini tunamaanisha kujumuisha pande zote mbili, yaani, misukumo ya kiroho ya ndani na matendo mema ya nje. Wapinzani wetu wanapotuzushia husema kwamba, wenzetu hawafundishi matendo mema wakati hawayadai matendo haya tu, bali huonyesha jinsi yanavyoweza kufanyika. 137. Matokeo hudhihirisha wanafiki wanaojaribu sana kuitimiza sheria kwa nguvu zao wenyewe bila kufanikiwa kufikia lengo lao. 138. Maana, kwa nguvu yake, asili ya mwanadamu ni dhaifu mno kuweza kumpinga Ibilisi awatekaye wote ambao hawajawekwa huru kwa imani. 139. Nguvu ya Kristo inahitajika dhidi ya Ibilisi tunapojua kwamba, tunasikilizwa na tuna ahadi yake kwa ajili ya Kristo. Kwa hiyo, tunaomba Roho Mtakatifu atutawale na atutetee, tusiweze kudanganywa na kukosea au kushawishika kutenda lililo kinyume cha mapenzi ya Mungu. Hivyo, zaburi hufundisha hivi, “. . . umeteka mateka, umepewa vipawa katikati ya wanadamu . . . ” (Zaburi 68:18). Yaani, Kristo alimshinda Ibilisi na alitupatia ahadi yake na Roho Mtakatifu, ili sisi wenyewe tushinde pia kwa msaada wa Mungu. Katika 1 Yohana 3: 8 tunasoma: “Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” 140. Kwa hiyo basi, hatufundishi tu namna sheria inavyoweza kutimizwa bali kwamba, Mungu anapendezwa tunapoitimiza sheria - si kwa njia ya kumridhisha kwa sheria bali kwa kuwa tumo katika Kristo, kama tutakavyoonyesha baadaye kidogo. Inajulikana wazi kwamba, tunadai matendo mema. 141. Hasa tunaongeza kwamba, haiwezekani kutenga imani na upendo wa Mungu, hata kama upendo ni mdogo kiasi gani, kwa kuwa tunamfikia Baba kwa njia ya Kristo. Baada ya kuupokea msamaha wa dhambi tunakuwa na hakika kwamba, tuna Mungu, yaani anayetujali, tunayemwita, tunayemshukuru, tunayemwogopa, na tunayempenda jinsi Yohana anavyofundisha katika waraka wake wa kwanza anaposema: “Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza” (1 Yohana 4:19), yaani, kwa sababu Mungu alimtoa Mwanawe kwa ajili yetu na akatusamehe dhambi zetu. Inamaanisha kwamba, imani hutangulia na upendo hufuatia. 143. Hali kadhalika,
ile imani tunayoizungumzia inapatikana katika toba, yaani, inazaliwa katika hofu kuu ya dhamiri ambayo husikia ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi zetu na kuutafuta msamaha wa dhambi na kuwekwa huru kutoka dhambini. Imani hii inapaswa kukua na kuimarika katika hofu hizi na mateso mengine. Kwa sababu hii, imani haiwezi kuwemo kwa watu wanaoishi kwa njia ya kuufuata mwili, na wanaofurahia na kuzitii tamaa zao. Kwa sababu hiyo, Paulo anasema: “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.”435 Pia anasema: “Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.”436 144. Kwa hiyo, imani iliyopokea msamaha wa dhambi katika moyo uliofanywa kuogopa na pia kuikimbia dhambi, haidumu katika watu wanaofuata tamaa zao, wala haipatikani pamoja na dhambi ya mauti.
145. Wapinzani wetu huinua tokeo mojawapo la imani ambalo ni upendo na kufundisha kwamba, upendo huhesabia haki. Kutokana na hili ni wazi kwamba wao hufundisha sheria tu. Hawafundishi kwamba, hatuna budi kwanza kuupokea msamaha wa dhambi kwa njia ya imani. Wala hawafundishi kwamba, kwa njia ya Kristo mpatanishi, tuna Mungu mwenye neema. Wanafikiri hii ni kwasababu ya upendo wetu Hata hivyo, hawasemi upendo huu ni wa aina gani. 146. Wanahubiri kushika kwao sheria, japo sifa hii inastahili hasa kuwa ya Kristo. Wanaliweka tegemeo katika matendo yao wenyewe wakipingana na hukumu ya Mungu. Maana wanasema kwamba, wanastahili neema na uzima wa milele kwa hadhi.437 Tegemeo hili ni potovu na batili kabisa. Katika maisha haya, hatuwezi kuitimiza sheria kwa sababu hali yetu ya kimwili haikomi kuzaa tamaa mbaya, ingawa Roho aliye ndani yetu huendelea kuzizuia.
147. Lakini mtu fulani anaweza kuuliza: Sisi pia tunakubali kwamba, upendo ni tendo la Roho Mtakatifu na pia ni haki, kwa kuwa ni utimizaji wa sheria. Ikiwa ni hivyo, kwa nini basi, tusifundishe kwamba, upendo huhesabia haki? Lazima tujibu swali hili kuwa: Kwanza kabisa, ni hakika kwamba, hatupokei msamaha wa dhambi kwa njia ya upendo au kwa sababu ya upendo wetu, bali kwa ajili ya Kristo kwa njia ya imani tu. 148. Imani peke yake438 iliyotazamia ahadi na kuthubutu kwa uhakika kabisa kwamba, Mungu anasamehe kwa sababu Kristo hakufa bure n.k. Imani hii hushinda hofu kuu za dhambi na mauti. 149. Mtu akiwa na mashaka kama dhambi zake zinasamehewa, anamtukana Kristo kwa
435 Rum. 8: 1
436 Rum. 8: 12-13
437 Kilatini: ‘Meritum de condigno.’
438 Kilatini: ‘Sola fide.’
maana, anakisia dhambi yake kuwa kubwa au ya kufaa zaidi kuliko kifo na ahadi ya Kristo japo Paulo anasema kwamba, neema ilizidi zaidi kuliko dhambi,439 na kwamba, rehema ni yenye nguvu zaidi kuliko dhambi. 150. Mtu akidhani kwamba, ataupokea msamaha wa dhambi kwa kuwa ana upendo, anamtukana Kristo na katika hukumu ya Mungu ataona kwamba, kwa haki yake mwenyewe, tegemeo lake ni potovu na tupu. Kwa hiyo, hapana budi kuwepo na imani ipatanishayo na kuhesabia haki. Hatupokei msamaha wa dhambi kwa maadili yoyote ya kisheria au kwa ajili yavyo - iwe uvumilivu, usafi au utiifu wa kiraia n.k. - hata kama maadili hayo hayana budi kuyafuata. 151. Hali kadhalika, hatupokei msamaha wa dhambi kwa ajili ya upendo kwa Mungu, hata kama huo pia hauna budi kuufuata.
152. Jinsi tamathali isemavyo, wakati fulani sababu na matokeo huungana pamoja katika neno lile lile.440 Katika Luka 7: 47, Kristo anasema: “Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana.” Lakini anafafanua mwenyewe maneno yake aongezeapo: “Imani yako imekuokoa.”441 Kristo hakutaka kwamba, kwa tendo lile la upendo, mwanamke aonekane kustahili kujipatia msamaha wa dhambi. 153. Kwa sababu hiyo, alisema wazi: “Imani yako imekuokoa.” Lakini basi, imani ndiyo inaishika bure huruma kwa ajili ya neno la Mungu. Kama fulani akikana kwamba, hii siyo imani, haelewi kabisa asili ya imani. 154. Historia hii nzima inaonyesha hapa anachokiita kuwa “upendo.”
Mwanamke alifika akiwa mwenye tegemeo hili kuhusu Kristo kwamba, msamaha wa dhambi unapatikana kwake. Ibada ya namna hiyo ni ibada kuu kabisa ya Kristo. Hakuna jema lolote kuu ambalo aliweza kumpatia Kristo. Hakika, kutafuta kwake msamaha wa dhambi kulikuwa kumkiri Kristo kama Masihi. Kuamini kweli ni kumfikiria Kristo kwa namna hiyo, kumwabudu na kumshika. Lakini Kristo alilitumia neno “upendo” siyo pamoja na mwanamke bali dhidi ya Mfarisayo, alipolinganisha utukufu mzima alioupata kutoka kwa Mfarisayo na ule wa mwanamke. Anamkemea Mfarisayo kwa sababu ya kutokumkiri yeye kuwa Masihi, ingawa alimonyesha Yesu huduma za nje za ukarimu kama kwa mtu aliye mkuu na mtakatifu. Alimwelekeza mwanamke huyu dhaifu na kuihubiri ibada yake, yaani kumpaka kwake mafuta na machozi yake n.k. Hayo yote yalikuwa alama na ukiri wa imani kwa sababu alikuwa akitafuta msamaha wa dhambi kutoka kwake Kristo. Hakika, mfano huu ni mkubwa uliosababisha hata Kristo amkemee Mfarisayo, mtu mwenye hekima na heshima lakini aliyekosa
439 Rum. 5: 20
440 Melanchthon anatumia istilahi ya Kiyunani: ‘κατα
Maana yake: Kuelewa mambo mawili pamoja bila kuitaja istilahi tegemezi.
441 Lk. 7: 50
imani. Anailaumu kufuru yake na kumhimiza kwa njia ya mfano wa mwanamke huyu dhaifu. Ni aibu kubwa kuona mwanamke asiyeelimika akimwamini Mungu ilhali mtaalamu wa sheria hakumwamini wala hakumkubali Masihi au kutafuta kutoka kwake msamaha wa dhambi na wokovu. 155. Kwa jinsi hii, Yesu analisifu tendo zima la mwanamke kumwabudu442 yeye na kama Maandiko Matakatifu yafanyavyo, kwa kuweka mambo mengi kwenye kifungu kimoja cha maneno. Baadaye, tutaonyesha zaidi aya zile zile za jinsi hiyo, kwa mfano: “Lakini, toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu.” 443 Hadai sadaka peke yake bali hata haki ya imani. Kwa hiyo, anasema hapa: “Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana.” Maana yake ni kwamba, mwanamke ameniabudu hakika kwa njia ya imani na kwa matendo na ishara za imani. Kwa njia hii basi, anajumuisha tendo zima la ibada. Wakati huo huo, anafundisha kwamba, ni imani hasa inayopokea msamaha wa dhambi kwa usahihi, ingawa upendo, ukiri na aina nyingine za matunda mema yanapaswa yafuate. Kwa sababu hiyo, hamaanishi kwamba, matunda haya ni gharama au ridhaa ambayo hulipia msamaha wa dhambi ili kutupatanisha na Mungu. 156. Tunajadiliana kuhusu suala lenye uzito, utukufu wa Kristo na chanzo cha faraja ya hakika na dhabiti kwa watu wenye mioyo ya wacha Mungu ikiwa tunapaswa kuweka tumaini letu kwa Kristo au katika matendo yetu wenyewe; 157. Ikiwa tunaliweka katika matendo yetu, tunamnyang’anya Kristo heshima yake ya kuwa Mpatanishi na Msuluhishi wetu. Basi, katika hukumu ya Mungu tutafahamu kwamba, tegemeo hili ni batili na dhamiri zitatumbukia katika kukata tamaa. Maana, kama msamaha wa dhambi na upatanisho havipatikani bure kwa ajili ya Kristo, bali kwa ajili ya upendo wetu, hakuna mwanadamu hata mmoja atakayepokea msamaha wa dhambi mpaka aitimize sheria nzima, kwa kuwa, sheria haihesabii haki mradi inaweza kutushtaki. 159. Ni dhahiri kwamba, kuhesabiwa haki ni upatanisho kwa ajili ya Kristo. Tunahesabiwa haki kwa njia ya imani kwa kuwa ni hakika kabisa kwamba, msamaha wa dhambi unapokelewa imani pekee.
159. Sasa tujibu pingamizi lile wapinzani wetu walilolitaja hapo juu.444 Hakika, wapinzani wetu hawakosei wanapodai kwamba, upendo ni kushika sheria, na kuitii sheria bila shaka ni haki. Lakini wanakosea sana wanapofikiri kwamba, tunahesabiwa haki kwa njia ya sheria. Sisi hatuhesabiwi haki kwa
442 Melanchthon analitumia neno la Kilatini ‘cultus,’ yaani, ‘ibada,’ na tena katika andiko la Kijerumani ‘Dienst,’ yaani, ‘huduma.’
443 Lk. 11: 41
444 147: “Lakini mtu fulani akizungumza: Sisi pia tunakubali kuwa upendo ni tendo la Roho Mtakatifu na pia haki, kwa kuwa ni utimizaji wa sheria. Basi, iwapo ni hivyo, kwa nini tusifundishe kwamba, upendo huhesabia haki?”
sheria, bali tunaupokea msamaha wa dhambi na upatanisho kwa imani kwa ajili ya Kristo, siyo kwa ajili ya upendo au utimizaji wa sheria. Kutokana na hili, inakuwa hakika kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani katika Kristo.
160. Kisha kushikwa huku kwa sheria na kuitii sheria kunapokuwa kwa ukamilifu, hakika ni haki, lakini kwetu, huo bado huwa mnyonge na mchafu. Kwa sababu hiyo, haimpendezi Mungu na haikubaliki kwa ajili yake yenyewe.
161. Kutokana na hayo tuliyosema hapo juu, ni wazi kwamba, kuhesabiwa haki hakumaanishi tu mwanzo wa ukarabati, bali upatanisho ambao katika huo, tunakubaliwa baadaye. Hata hivyo, ni dhahiri zaidi sasa kwamba, mwanzo wa utimizaji wa sheria hauhesabii haki, kwa sababu hukubaliwa tu kwa ajili ya imani. Basi, lazima tusitegemee kwamba, tunahesabiwa haki mbele za Mungu kwa ukamilifu wetu wenyewe na kwa utimizaji wa sheria na siyo kwa ajili ya Kristo.
162. Hii ni kweli kwa sababu, kwanza: baada ya kufanywa upya kwetu, Kristo hakomi kuendelea kuwa Mpatanishi. Wanakosea kabisa wale wanaodhani kwamba, alistahili ”neema ya kwanza” tu. Na kwamba, baada ya hapo, sisi tunampendeza Mungu na kujistahilisha kupata uzima wa milele kwa utimizaji wa sheria. 163. Kristo anabaki kuwa Mpatanishi. Lazima daima tuwe na hakika kwamba, kwa ajili yake, tuna Mungu mwenye neema licha ya kutostahili kwetu. Paulo anafundisha hili wazi anaposema: “Maana sijui sababu ya kujishtaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo . . .”445 Bali anaamini kwamba, anahesabiwa haki kwa ajili ya Kristo kulingana na tamko hili: “Heri waliosamehewa makosa yao, na waliositiriwa dhambi zao.”446 Msamaha huu hupokelewa daima kwa imani. Kadhalika, kuhesabiwa kuwa mwenye haki ya Injili kunatokana na ahadi na kunapokelewa kwa imani. Kwa hiyo, inatubidi daima kusadiki kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani kwa ajili ya Kristo. 164. Iwapo wale waliozaliwa upya wanatakiwa kuamini baadaye kwamba watakubaliwa kwa kuwa wameitenda sheria, dhamiri yetu itawezaje kuwa na hakika kwamba, inampendeza Mungu, maadamu kamwe hatuitimizi sheria? 165. Kwa hiyo, inatubidi kuirudia tena na tena ahadi na kuutunza udhaifu wetu kwayo hata kusadiki kuwa tunahesabiwa haki kwa ajili ya Kristo: “Naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.”447 Mtu yeyote akifikiri kwamba, tayari ana haki na anakubalika kwaajili yake mwenyewe kwa kutimiza kwake sheria na si kwa sababu ya ahadi ya Kristo, anamtukana huyu kuhani mkuu. Haiwezekani kuelewa jinsi mtu anavyoweza kumwacha Kristo aliye Mtulizaji na
445 1 Kor. 4: 4
446 Zab. 32: 1; Rum. 4: 7
447 Rum. 8: 34
Mpatanishi, na kisha adhanie kuwa ana haki mbele za Mungu.
166. Tena majadiliano marefu yanafaa nini? Maandiko Matakatifu yote na Kanisa zima hutangaza kwamba, sheria haiwezi kutimizwa. Mwanzo wa utimizaji wa sheria wenyewe haumpendezi Mungu, bali ni kwa ajili ya imani katika Kristo. 167. Vinginevyo, bila imani, daima sheria inatushitaki. Kwani ni nani ampendaye au amwogopaye Mungu kiasi cha kutosha? Nani avumiliaye kwa utulivu mateso yaletwayo na Mungu? Ni nani asiye na mashaka, mara nyingi, kama mambo ya wanadamu huongozwa na mashauri ya Mungu au hutokea kwa bahati tu? Ni nani asiyekuwa na mashaka mara kwa mara kama Mungu anamsikia? Ni nani asiyekasirika kwa sababu waovu hustawi zaidi kuliko wacha Mungu, na kwa sababu waovu wanawatesa wacha Mungu? Ni nani aliyetimiza madai ya wito wake? Ni nani aliyempenda jirani yake kama nafsi yake? Ni nani asiyeudhiwa na tamaa? 168. Hivyo basi, Paulo anasema: “Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.” Kadhalika: “. . . mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”448 Pia Daudi anasema: “Wala usimhukumu mtumishi wako, maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.”449 Hata huyu mtumishi wa Mungu pia anamwomba Mungu kutupilia mbali hukumu yake. Kadhalika: “Heri BWANA asiyemhesabia upotovu.”450 Basi, katika hali ya unyonge wetu, daima kuna dhambi ambayo ingeweza kuhesabiwa kwetu. Kuhusu hili, baadaye anasema kidogo kuwa: “Kwa hiyo kila mtu mtauwa, akuombe wakati unapopatikana.”451 Anaonyesha hapa kwamba, hata watakatifu hawana budi kuomba msamaha wa dhambi.
169. Hao ni vipofu sugu wasioamini kwamba, tamaa za kimwili ni dhambi, ambayo kwayo Paulo anasema: “Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na roho hushindana na mwili.”452 170. Mwili haumsadiki Mungu na hutegemea mambo ya muda. Wakati wa misiba mikubwa, hutafuta misaada kutoka kwa watu, hata huyapinga mapenzi ya Mungu na kukimbia mateso ambayo unapaswa kuyavumilia kwa ajili ya agizo la Mungu. Isitoshe, unashuku rehema ya Mungu. Roho Mtakatifu hupambana mioyoni mwetu na hisia za aina hii ili kuyakomesha, kuyaangamiza na kutupatia misukumo mipya ya kiroho. 171. Baadaye hapa chini tutaorodhesha ushuhuda mwingi zaidi kuhusu suala hili, ingawa tayari unaonekana kokote, siyo tu katika Maandiko Matakatifu, bali hata
448 Rum. 7: 19, 25
449 Zab. 143 : 2
450 Zab. 32 : 2
451 Zab. 32 : 6
452 Gal. 5 : 17
katika maandiko ya Mababa watakatifu.
172. Agostino anasema vizuri sana kwamba: “Amri zote za Mungu zinatimizwa pale ambapo upungufu wao unasamehewa.”453 Hivyo, hata katika matendo mema anaitaka imani yetu ili tuamini kwamba, tunampendeza Mungu kwa ajili ya Kristo na kwamba, matendo yenyewe hayana stahili zozote za kumpendeza Mungu. 173. Hieronimo akiwapinga wafuasi wa Pelagio anaandika: “ Basi, tuna haki tunapoungama kwamba, tu wenye dhambi na haki yetu haitegemei ustahili wetu, bali rehema ya Mungu.”454 174. Hivyo, katika mwanzo wa utimizaji wa sheria lazima tuwe na imani iliyo na hakika kwamba, tuna Mungu wa rehema anayeridhika kwa ajili ya Kristo. Maana rehema haiwezi kupatikana pasipo imani jinsi awali tulivyokwishataja mara nyingi. 175. Hivyo, Paulo anaposema kwamba, sheria inathibitishwa kwa imani,455 msemo huu usieleweke tu kwamba, wale waliozaliwa upya hupokea Roho Mtakatifu na misukumo yao hukubaliana na sheria ya Mungu. Muhimu zaidi, tunapaswa kutambua jinsi tulivyo mbali na ukamilifu wa sheria. 176. Kwa sababu hiyo, sisi hatuwezi kufikiri kwamba, tunahesabiwa haki mbele za Mungu kwa njia ya kuitimiza sheria. Badala yake, ili dhamiri yetu iweze kutulia lazima tutafute kuhesabiwa haki mahali pengine.. Mradi tunapoikimbia hukumu ya Mungu na kumkasirikia, sisi si wenye haki mbele zake. 177. Kwa hiyo, tunahitimisha kwa kusema kwamba, sisi tuliopatanishwa kwa imani kwa ajili ya Kristo, tunahesabiwa kuwa na haki, si kwa sababu ya sheria au matendo yetu, bali kwa kuwa mwanzo huu wa utimizaji wa sheria humpendeza Mungu kwa ajili ya imani, na pia kwamba, kwa ajili ya imani, upungufu wa utimizaji wa sheria hauhesabiwi, ingawa kuwepo kwa uchafu wetu hututisha kwelikweli. 178. Kwa hiyo basi, hatuna budi kuitafuta haki kwingineko, maana upendo na matendo yetu havihesabii haki. Mbali na usafi wetu, na hata mbali na sheria yenyewe, lazima pawekwe kifo na ridhaa ya Kristo, vilivyotolewa kwetu ili tutambue kwamba, tunaye Mungu mwenye rehema kwa sababu ya ridhaa hii na siyo kwa sababu ya utimizaji wetu wa sheria.
179. Katika Wagalatia 3:13, Paulo anafundisha: “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu.” Maana yake: Sheria inawahukumu watu wote, lakini Kristo asiye na dhambi alijiweka chini ya adhabu ya makosa, na kufanyika dhabihu kwa ajili yetu. Aliondolea mbali haki ya sheria ili isiwashtaki na kuwahukumu wamwaminiye. Maana, yeye mwenyewe ni ridhaa kwa hao na kwa ajili ya ridhaa hii, sasa wanahesabiwa haki. Lakini hata kama hawajaitimiza sheria yenyewe kwa kweli, wanapohesabiwa haki, sheria
453 ‘Retractationes’ 1, 19, 3.
454 ‘Dialogus adversus Pelagianos’ 1, 13. 455 Rum. 3: 31
haiwezi kuwashtaki wala kuwahukumu. Paulo anaandikia kwa Wakolosai (Kol. 2: 10) kauli ile ile: “Na ninyi mmetimilika katika yeye . . .” Ni kana kwamba anasema: “Ingawa mko mbali na utimilifu wa sheria, hata hivyo masalio ya dhambi hayawaletei hukumu. Maana, kwa sababu ya Kristo, tuna upatanisho wa hakika na imara kwa njia ya imani, ingawa dhambi huendelea kuganda katika miili yetu.”
180. Daima, inatubidi kuiweka ahadi ya Mungu mbele ya macho yetu. Kwa ajili ya ahadi yake na kwa ajili ya Kristo, Mungu anapenda kuwa na mwelekeo mzuri kwetu na kutuhesabia haki, si kwa sababu ya sheria au matendo yetu. Inazibidi dhamiri zenye hofu kuutafuta upatanisho na haki katika ahadi hii. Kwa njia ya ahadi hii, hazina budi kustahimili (dhamiri) na kuwa na hakika kwamba, kwa ajili ya Kristo na kwa ajili ya ahadi yake zina Mungu mwenye rehema. Hivyo basi, matendo hayawezi kuituliza dhamiri kamwe, bali ni ahadi peke yake tu iwezayo kufanya hivyo. 181. Kadhalika, iwapo lazima kutafuta haki na amani ya dhamiri kwingineko nje ya upendo na matendo yetu, itafuatia kwamba, upendo na matendo havistahili kuhesabiwa haki ilihali bado ni maadili mema na haki kulingana na sheria, alimradi yanaitimiza sheria. Mpaka hapo utiifu wa sheria huhesabia haki kwa masharti ya haki ya sheria. Lakini haki hii isiyo kamili haikubaliwi na Mungu isipokuwa kwa ajili ya imani. Kwa hiyo, haki hii haiokoi, yaani, yenyewe haipatanishi, haizai upya wala haitufanyi kustahili mbele za Mungu.
182. Kutokana na haya ni wazi kwamba, tunahesabiwa haki mbele za Mungu kwa imani tu. Maana, tunaupokea msamaha wa dhambi kwa imani tu, na upatanisho kwa ajili ya Kristo, kwani upatanisho au kuhesabiwa haki ni jambo lililoahidiwa kwa ajili ya Kristo na siyo kwa ajili ya sheria. Hivyo, msamaha wa dhambi unapokelewa kwa imani peke yake, japo utimizaji wa sheria hufuatana na kipawa cha Roho Mtakatifu.
Jibu kwa Hoja za Wapinzani wetu
183. Baada ya kuichunguza misingi ya suala hili, yaani, kutofautisha kati ya sheria na ahadi au Injili, itakuwa rahisi kukanusha pingamizi za wapinzani wetu. Maana wao hurejea misemo inayohusu sheria na matendo na kuiacha misemo inayohusu ahadi. 184. Lakini tunaweza kujibu mara moja matamko yao yote kuhusu sheria: Sheria haiwezi kutimizwa bila Kristo, na matendo mema ya kiraia yakitendwa bila Kristo hayampendezi Mungu. Kwa hiyo, matendo yakihubiriwa,456 hakuna budi kuongezea kwamba, imani ni ya lazima, na kuwa 456 Kilatini: ‘Praedicantur ‘Kijerumani: ‘Lehren oder predigen.’ Tafsiri mbalimbali, k.m. Tappert:
matendo yanahubiriwa kwa ajili ya imani, kwa maana matendo ni matunda au ushuhuda wa imani. 185. Masuala yenye maana nyingi na hatari huibua masuluhisho mengi tofauti. Kwa maana maneno ya mshairi wa kale ni kweli: “Neno baya linalougua lenyewe, linahitaji tiba ya busara.”457 Lakini katika masuala mema na imara, elezo moja au mawili yaliyochukuliwa kutoka kwenye vyanzo, yatarekebisha kila kitu kinachoonekana kuwa cha wasiwasi. Hivyo ndivyo ilivyo katika mjadala wetu. Kanuni niliyoitaja hapo juu hufafanua misemo yote inayotajwa kuhusu sheria na matendo. 186. Tunakubali kwamba, pahali pengine Maandiko Matakatifu hufundisha sheria na pahali pengine hufundisha Injili iliyo ahadi ya msamaha wa dhambi iliyo ya bure kwa ajili ya Kristo. Lakini wapinzani wetu huitoa kabisa ahadi ya bure wanapokataa kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani na kufundisha kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi na upatanisho kwa ajili ya upendo na matendo yetu. 187. Kama msamaha ungetegemea matendo yetu, usingekuwa wa kweli kabisa na ahadi ingebatilika. 188. Kwa sababu hiyo, tunazihimiza nafsi za uchaji wa Mungu kutafakari kuhusu ahadi, na tunafundisha kuhusu msamaha wa dhambi na upatanisho wa bure kwamba, unapatikana kwa njia ya imani katika Kristo. Ndipo, baadaye tutaongezea fundisho kuhusu sheria. Ni lazima tupambanue kati ya haya, jinsi Paulo asemavyo.458 Lazima tuangalie vizuri kile Maandiko Matakatifu yanapatia sheria na ahadi. Maana maandiko hayo yanayasifia matendo kiasi cha kutoiondoa ahadi ya bure.
189. Matendo mema lazima yatendwe kwasababu Mungu ameyaamuru ili kwayo tuizoeze imani yetu, na pia kwa ajili ya ukiri na matendo ya shukrani kwa Mungu. Kwa sababu hizo, matendo mema lazima yatendwe. Matendo haya yanatendeka katika mwili ambao bado sehemu yake haijatakaswa kabisa na huzuia zile Roho Mtakatifu anazochochea na hata kuzichafua kwa uchafu wake. Hata hivyo, matendo haya ni matakatifu, ya kimungu na dhabihu kwa ajili ya imani na ufalme wa Kristo, unaoonyesha utawala wake mbele ya ulimwengu. Maana kwa matendo haya, Kristo anaitakasa mioyo na kumgandamiza Ibilisi. Ili kuidumisha Injili miongoni mwa wanadamu, Kristo anauweka hadharani ukiri wa watakatifu dhidi ya ufalme wa Ibilisi na hata anautangaza uwezo wake katika udhaifu wetu. 190. Hatari, kazi na mahubiri ya Paulo, Athanasio, Agostino na walimu wengine wa Kanisa ni matendo matakatifu, sadaka za kweli na zinazokubalika mbele za Mungu, mapambano ambayo kwayo Kristo amemdhibiti Ibilisi na kumfukuzia mbali na waumini. 191. Kazi za Daudi katika vita na katika kuitawala serikali
‘Yakisifiwa’ 457 Euripide (485/4 au 480 –406 K.K.), mwandishi wa michezo wa Kiyunani katika mchezo wake wa ‘Wanawake wa Foinikia‘ aya za 474-5: ‘Ο
458 2 Tim. 2: 15: ‘ορθοτομειν.’
ni matendo matakatifu, dhabihu safi, mapambano ya Mungu akililinda taifa lililokuwa na Neno lake dhidi ya Ibilisi, ili ufahamu wa wake Mungu usitoweke kabisa duniani.
192. Tunahisi vivyo hivyo kuhusu kila aina ya kazi duni mno na katika maisha ya kibinafsi. Kwa njia ya matendo haya, Kristo anaushangilia ushindi wake dhidi ya Ibilisi. Jinsi ambavyo ugawaji wa sadaka uliofanywa na Wakorintho ulivyokuwa tendo takatifu la “huruma,”459 dhabihu na pambano la Kristo dhidi ya Ibilisi ambaye anajikokota kuzuia sifa zozote zisitolewe kwa Mungu. 193. Kuyakashifu matendo kama ukiri wa mafundisho ya imani, mateso, huduma za huruma, na kujinyima kimwili kungekuwa sawa na kuudharau utawala wa Kristo unaoonekana miongoni mwa wanadamu. Acheni tuliongezee neno hapa kuhusu tuzo na stahili. 194. Tunafundisha kwamba, tuzo zimetolewa na kuahidiwa kwa ajili ya matendo ya waaminifu. Tunafundisha kwamba, matendo mema ni yenye kustahili, siyo kwa ajili ya kustahili msamaha wa dhambi, neema, au kuhesabiwa haki – ( maana tunazawadiwa haya kwa imani tu ) – bali kwa ajili ya tuzo zingine za kimwili na kiroho katika maisha haya na yajayo, jinsi asemavyo Paulo: “Lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.”460 Kwa hiyo, huko kutakuweko na tuzo tofauti kwa ajili ya kazi mbalimbali. 195. Lakini msamaha wa dhambi ni ule ule na ulio sawa kwa watu wote jinsi Kristo alivyo mmoja, na msamaha huu unatolewa bure kwa wote wanaoamini kwamba, dhambi zao zimesamehewa kwa ajili ya Kristo. Msamaha wa dhambi na haki hupokelewa kwa imani tu, wala siyo kwa matendo yoyote. Hili ni dhahiri katika vitisho vya dhamiri, maana hatuwezi kuyaweka matendo yetu yoyote juu ya ghadhabu ya Mungu, jinsi Paulo asemavyo waziwazi: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani.”461 196. Aidha, kwa kuwa imani inatufanya kuwa wana wa Mungu, vile vile inatufanya kuwa warithi pamoja na Kristo. Kwa kuwa, kwa matendo yetu hatustahili kuhesabiwa haki inayotufanya kuwa wana wa Mungu na warithi pamoja na Kristo, hatustahili uzima wa milele kwa matendo yetu. Ni imani tu inayolipokea hili maana inatuhesabia haki na ina Mungu mwenye neema. Maisha ya milele ni kwa wale waliohesabiwa haki. Haya kwa mujibu wa msemo usemao: “. . . wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.”462 197. Paulo anaisifu amri ya kuwaheshimu wazazi huku akiilenga thawabu inayohusiana na amri hiyo.463 Hana
459 1 Kor. 16: 1; Kilatini: ‘Elemosyna,’ Kiyunani: ‘Ελημοσυνη.’
460 1 Kor. 3: 8
461 Rum. 5: 1-2
462 Rum. 8: 30
463 Efe. 6: 2-3
maana ya kusema kwamba, utiifu kwa wazazi wetu unatufanya tuhesabiwe haki mbele za Mungu, bali kwamba, utiifu huo unapotokea kwa wale waliohesabiwa haki huwastahilisha thawabu zingine kubwa. 198. Tena, Mungu huwatumia watakatifu wake kwa njia tofauti na mara nyingi huziahirisha thawabu za matendo ya haki ili wajifunze kutotegemea haki yao wenyewe bali wajifunze kuyatafuta mapenzi ya Mungu kuliko thawabu, jinsi inavyoonekana wazi katika Ayubu, Katika Kristo, na katika watakatifu wengine wote. Zaburi nyingi hutufundisha hivyo zikitufariji kuhusu sudi464 ya wale wasiokuwa wenye haki, jinsi tusomavyo katika Zab. 37: 1: “Usiwahusudu wafanyao ubatili.” Pia Kristo anasema: “Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; maana ufalme wa mbinguni ni wao.”465 Bila shaka, sifa ya jinsi hii inawahimiza waaminifu kuyatenda matendo mema. 200. Wakati huo huo mafundisho ya toba yanahubiriwa kwa waovu, ambao matendo yao ni maovu na ghadhabu ya Mungu inafunuliwa, ikiwatishia wote wasiotubu.
201. Kwa hiyo, tunasifu na kuyadai matendo mema na tunatoa sababu nyingi za kuonyesha kwa nini yanapaswa kufanywa.
Paulo anafundisha vivyo hivyo kuhusu matendo anaposema kwamba, Ibrahimu hakupokea tohara ili ahesabiwe haki.466 Tayari alikuwa amekwisha kuhesabiwa haki kwa imani lakini tohara iliongezewa kusudi awe na alama iliyochorwa kwenye mwili wake ambayo kwayo, aweze kukumbushwa na kukua katika imani, na kwa njia ya ushuhuda wake akiri imani yake mbele ya watu wengine na awavute ili waamini.
202. “Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhahibu iliyo bora . . .”467 Kwa sababu alikuwa mwenye haki kwa imani, dhabihu yake ilimpendeza Mungusiyo kwa ajili ya kuustahili msamaha wa dhambi na neema kwa njia ya kazi hii, bali kwa kuitumia na kuionyesha imani yake kwa wengine, akiwaalika waamini.
203. Hata hivyo, matendo mema hayana budi kuifuata imani kwa njia hii. Mtu asiyeweza kuamini au kuwa na hakika moyoni mwake kwamba, anasamehewa bure kwa ajili ya Kristo, na kuwa ana Mungu wa rehema aliyeridhika kwa ajili ya Kristo, yeye huyatumia matendo kwa njia tofauti kabisa. Mtu kama huyo ayaonapo matendo ya watakatifu, huchukulia kibinadamu kwamba, kwa matendo haya watakatifu walistahili msamaha wa dhambi na neema. Ndipo huyaiga haya na kufikiri kwamba, kwa matendo hayo hayo atastahili neema na msamaha wa dhambi, ataituliza ghadhabu ya Mungu, na atapata kuhesabiwa haki kwaajili ya matendo haya. Tunalilaani wazo hili potovu kuhusu matendo. 204. Kwanza, 464 Bahati nzuri, furaha, ustawi.
465 Mt. 5: 10
466 Rum. 4: 9-22
467 Ebr. 11: 4
wazo hili linauvuruga utukufu wa Kristo, kwa kuwa watu huyaweka matendo haya mbele za Mungu kama gharama na upatanisho. Kwa njia hiyo, ile heshima iliyo ya Kristo pekee inatolewa kwa matendo yetu. Pili, bado huwa hawapati amani ya dhamiri katika matendo haya, Lakini wakati wa kitisho halisi, wao huyalimbikiza matendo na hatimaye wanakata tamaa, kwa kuwa hawawezi kupata vya kutosha matendo yoyote yaliyo safi. Daima, sheria huwashtaki na kuwaletea ghadhabu. Tatu, watu wa jinsi hiyo hawawezi kuupata ufahamu wa Mungu, kwa maana katika hasira yao wanaikimbia hukumu ya Mungu na kamwe hawaamini kwamba, anawasikia. 205. Lakini imani huutoa uhakika kuhusu uwepo wa Mungu inapokuwa na hakika kwamba, yeye hutusamehe bure na kutusikiliza.
206. Daima, wazo potovu kuhusu matendo huushikilia ulimwengu. Watu wa mataifa wana dhabihu ambazo walizipokea kutoka kwa mababa zao. Waliyaiga matendo yao bila kuishika imani yao. Badala yake, walijiaminisha kuwa matendo haya ni gharama na upatanisho iliyowapatanisha wao na Mungu. 207. Taifa la Torati468 liliziiga dhabihu hizi likiwaza kwamba, lilikuwa na Mungu wa rehema aliyeridhika kwa ajili ya matendo yao, yaani kwa ajili ya matendo yenyewe.469 Hapa tunaona jinsi manabii walivyoukemea umma kwa ukali (Zab. 50:8): “Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako.” Na Yeremia 7:22: “Sikuwaamuru kwa habari za sadaka za kuteketezwa . . .” Hakika, vifungu kama hivyo havihukumu matendo yaliyoagizwa na Mungu kwa ajili ya desturi za nje katika jamii hiyo. Lakini zinaulaani ushawishi huu wa kukufuru sana kwamba, kwa matendo haya wangewaza kuwa, , waliituliza ghadhabu ya Mungu kwa kuiweka imani kando. 208. Kwa kuwa, hakuna matendo yoyote yanayoweza kuituliza dhamiri, waliendelea kuzibuni aina mpya za matendo zaidi ya yale yaliyoamriwa na Mungu. Taifa la Israeli liliwaona manabii wakitoa dhabihu katika mahali pa juu. Mifano ya watakatifu inawavutia sana wale wanaotumainia kuwa, wakitenda walivyotenda (watakatifu) wanaweza kuipokea neema. Kwa hiyo, watu walijitahidi kuliiga tendo hili kwa raghba470 isiyoaminika ili wapate kustahili neema, haki, na msamaha wa dhambi. Lakini manabii hawakutoa dhabihu katika mahali pa juu ili kuistahili neema na msamaha kwa ajili ya tendo hili, bali kwa kuwa walikuwa wakifundisha katika pahali hapo na hivyo waliutoa ushuhuda wa imani yao. 209. Watu walisikia kwamba, Ibrahimu alikuwa amemtoa mwanawe kama dhabihu. Hivyo, kwa tendo hili la ukatili na chungu, hata wao waliwachinja wana wao ili waweze kuituliza ghadhabu ya Mungu.471
468 Kilatini: ‘Populus in lege’ (taifa la sheria). Andiko la Kijerumani: ‘Die Israeliten,’ yaani, Waisraeli.
469 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
470 Moyo, kero.
471 Mwa. 22; Law. 20: 2; 2 Fal. 23: 10; Yer. 7: 31; 19: 5; 32: 35
Lakini Ibrahimu hakumtoa mwanawe kama dhabihu akitazamia kwamba, tendo hili lingekuwa gharama au upatanisho/utulizaji ambao kwao angehesabiwa haki. 210. Hivyo, Chakula cha Bwana kilianzishwa Kanisani ili imani yetu iimarishwe kwa kutukumbusha ahadi za Kristo kwa njia ya alama hii. Alama ambayo ni kumbukumbu ya ahadi, na kuweza kuishuhudia imani yetu hadharani huku tukizihubiri fadhili za Kristo, jinsi asemavyo Paulo: “Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.”472
Lakini wapinzani wetu wanadai kwamba, misa ni tendo linalohesabia mtu haki kama tendo lenyewe na huiondoa hatia na adhabu kutoka kwa wale ambao kwao misa inatolewa jinsi Gabriel Biel anavyoandika.473
211. Antonio, Bernardo, Dominiko, Fransisko, na mababa watakatifu wengine waliichagua aina fulani ya maisha kwa ajili ya kujifunza au kwa ajili ya mazoezi mengine ya manufaa. Wakati huo huo waliamini kwamba, walihesabiwa haki kwa njia ya imani na kwamba, walikuwa na Mungu wa rehema aliyeridhika kwa ajili ya Kristo na wala siyo kwa ajili ya mazoezi yao ya kiroho yenyewe.474 Lakini tangu hapo, umma uliiga, siyo imani ya mababa bali mienendo yao tu bila imani yao ili kwa matendo kama hayo wastahili msamaha wa dhambi, neema na haki. Hawakuamini kwamba, tayari waliyapokea hayo bure kwa ajili ya Kristo aliye Mpatanishi? 212. Kwa njia hii, ulimwengu huyahukumu matendo yote kwamba, ni upatanisho ambao kwao Mungu hutulizwa, na gharama ambayo kwayo tunahesabiwa haki. Ulimwengu hauamini kwamba, Kristo ndiye mpatanishi, au kwamba, tunahesabiwa haki bure kwa imani kwa ajili ya Kristo. Lakini, kwa kuwa matendo hayawezi kuituliza dhamiri, daima watu huyachagua matendo mengine, yaani, taratibu mpya, nadhiri mpya, na madaraja mapya ya watawa zaidi ya amri ya Mungu kwa matarajio ya kupata tendo jipya kubwa ambalo wanaweza kulitumia dhidi ya ghadhabu na hukumu ya Mungu. 213. Wapinzani wetu hudumisha mawazo haya mapotovu kuhusu matendo ambayo hayatokani na Biblia. Je, hili ni lipi lingine isipokuwa kumpokonya Kristo heshima ya kuwa Mpatanishi na Mtulizaji, iwapo tutayaamini matendo yetu kuwa upatanisho/ utulizaji na kudai kwamba, tunastahili kuupokea msamaha wa dhambi na neema na kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa ajili ya matendo na siyo kwa ajili ya Kristo kwa njia ya imani? 214. Hata hivyo basi, tunaamini na kufundisha kwamba, matendo mema hayana budi kutendwa, kwa kuwa mwanzo wetu wa kuifuata sheria lazima ufuate imani; Lakini bado tunampa Kristo heshima yake. Tunaamini na kufundisha kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani mbele za
472 1 Kor. 11: 26
473 Gabriel Biel (mnamo 1420 - 1495 ), katika ‘Expositio canonis missae’ 26, 81.
474 Mt. Antonio (251? - 356 ), Bernardo wa Clairwaux (1090 - 1153 ), Dominiko (mnamo 1174 - 1223 ). Fransisko wa Asisi (1181/2 - 1226 ).
Mungu kwa ajili ya Kristo na kwamba, hatuhesabiwi haki kwa ajili ya matendo yetu bila Kristo aliye Mpatanishi. Hatustahili kuupokea msamaha wa dhambi, neema, na haki kwa njia ya matendo. Hatuwezi kuyaweka matendo yetu dhidi ya ghadhabu na hukumu ya Mungu. Kwa kuwa, matendo yetu hayawezi kuvishinda vitisho vikuu vya dhambi bali ni imani peke yake iwezayo kuvishinda. Ni Kristo pekee, Mpatanishi awezaye kupambanuliwa kwa njia ya imani dhidi ya ghadhabu na hukumu ya Mungu. Hili ndilo tunaloliamini na kulifundisha. 215. Yeyote aaminiye tofauti hampi Kristo heshima anayostahili, Maana, amewekwa kuwa Mpatanishi ambaye kupitia kwake tunaweza kumfikia Baba. 216. Hapa tunazungumzia haki ambayo kwayo tunajishughulisha na Mungu, na tunashikilia neema na amani ya dhamiri wala hatuwazungumzii wanadamu. 217. Lakini dhamiri haiwezi kuwa na amani mbele za Mungu isipokuwa kwa imani peke yake, ambayo kwayo dhamiri hiyo inahakikishiwa kwamba, Mungu amepatanishwa nasi kwa ajili ya Kristo, kulingana na neno hili: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani.”475 Kuhesabiwa haki ni tendo ambalo limeahidiwa bure tu kwa ajili ya Kristo. Kwa hiyo, linapokelewa mbele za Mungu kwa imani peke yake.
218. Sasa basi, tutayajibu mafungu ambayo wapinzani wetu wananukuu ili kuthibitisha kwamba, tunahesabiwa haki kwa upendo na matendo. Wao hunukuu 1 Kor. 13:2 usemao: “. . . nijapokuwa na imani timilifu..., kama sina upendo, si kitu mimi.” Hapa, wapinzani wetu huushangilia ushindi mkuu! Mbele ya kanisa zima wao wanasema, Paulo anadai kwamba imani peke yake haihesabii haki. 219. Kwa kuwa sasa tumeonyesha tunaloliamini kuhusu upendo na matendo, jibu litakuwa rahisi. Katika andiko hili, Paulo anahitaji upendo. Hata nasi pia tunahitaji upendo Tumetaja hapo juu kwamba, lazima tufanywe upya na tuanze kuitimiza sheria, kulingana na kauli hii isemayo: “Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika;...”476 Yeyote atupiliaye mbali upendo, hataweza kudumu katika imani yake, hata iwe kubwa sana, kwa maana hatamshika Roho Mtakatifu.
220. Lakini katika kifungu hiki, Paulo hazungumzii namna ya kuhesabiwa haki. Anawaandikia watu ambao, baada ya kuhesabiwa haki, walihitaji kuhimizwa kuzaa matunda mema wasije wakampoteza Roho Mtakatifu. 221. Wapinzani wetu huendelea kwa njia iliyo kinyume, yaani, isiyokuwa na mantiki: wao wananukuu andiko hili moja ambalo Paulo anaitumia kufundisha kuhusu matunda. Wao wanayaruka maandiko mengine mengi ambayo kwa utaratibu anaijadili namna ya kuhesabiwa haki. Licha ya hayo, daima wanaongezea masahihisho
475 Rum. 5: 1
476 Yer. 31: 33
katika maandiko mengine yanayozungumzia kuhusu imani kwamba, ni lazima zieleweke kwa kurejelea maana ya “imani iliyoumbwa.”477 Hapa hawaliongezei sahihisho lolote lisemalo: tunahitaji imani ili tuweze kuhesabiwa haki kwa ajili ya Kristo, aliye mpatanishi. Hivyo, wapinzani wetu humtenga Kristo katika kuhesabiwa haki na huifundisha tu haki ya sheria. Lakini acheni turudi kwake Paulo! 222. Hakuna mtu arazinishaye kifungu hiki zaidi kuliko kwamba, upendo ni wa lazima. Tunakubaliana nalo kabisa. Vile vile ni lazima kutoiba. Lakini itakuwa udanganyifu mbaya mtu akishikilia: kwa kuwa ni lazima kutoiba, basi, kutoiba humwesabia mtu haki. Maana, kuhesabia haki, siyo kibali cha tendo fulani bali ni kibali cha mtu kwa jumla. Hivyo, kifungu hiki kutoka kwa Paulo hakipingani nasi, ila tu wapinzani wetu hawapaswi kujiongezea mawazo yao. Maana, Paulo hasemi kwamba, upendo huhesabia haki, bali kwamba “mimi si kitu.” Yaani, imani inazimika bila kujali ilikuwa kubwa kiasi gani. Paulo hasemi kwamba, upendo huvishinda vitisho vikuu vya dhambi na mauti; kwamba, tunaweza kuutumia upendo dhidi ya ghadhabu na hukumu ya Mungu; kwamba, upendo wetu huiridhisha sheria ya Mungu, kwamba, kwa upendo wetu tunaweza kumkaribia Mungu hata bila Kristo aliye mpatanishi; na kwamba, kwa upendo wetu, tunaipokea ahadi ya msamaha wa dhambi. Paulo hasemi lolote miongoni mwa mambo haya. Yeye haamini kwamba, upendo huhesabia haki, kwa sababu tunahesabiwa haki tu tunapomshikilia Kristo, mpatanishi na kuamini kwamba, kwa ajili yake, Mungu aliyeridhika ni mwenye rehema kwetu. Wala tusiote ndoto kuhusu kuhesabiwa haki kamwe pasipo Kristo, aliye Mpatanishi wetu!
223. Waacheni wapinzani wetu waondoe kabisa ahadi kuhusu Kristo, waacheni waibatilishe Injili iwapo Kristo hahitajiki na iwapo, kwa upendo wetu tunaweza kuyashinda mauti bila Kristo na kumkaribia Mungu bila Kristo kama Mpatanishi wetu. 224. Wapinzani wetu huvigeuza vifungu vingi kwa sababu wao huyaingiza mawazo yao katika vifungu hivi badala ya kuchukua maana kutokana na vifungu vyenyewe. Hakuna tatizo katika kifungu hiki iwapo tutauondoa ufafanuzi ambao wapinzani wetu wameuweka ndani yake kwa maana hawaelewi kuhesabiwa haki ni nini au jinsi inavyotokea. Kwa kuwa, Wakorintho walikuwa wamehesabiwa haki awali na kuzipokea karama bora sana. Kama kawaida, mwanzoni walikuwa na hamasa/ari nyingi. Baadaye, mafarakano yalizuka kati yao na jinsi Paulo anavyoonyesha, walianza kuwachukia walimu bora. Paulo anawakanya kuhusiana na haya na kuwaita warejee kwenye majukumu ya upendo. Ingawa haya ni ya lazima, ingekuwa ndoto ya kijinga kudhani kwamba, tunahesabiwa haki mbele
477 Yaani, “imani iliyoumbwa na upendo,” Kilatini: ‘Fides caritate formata.’ Kitenzi “umba” kisieleweke hapa kuwa na maana ya ‘creatio,’ (uumbaji), bali ‘forma,’ (umbo), (sura).
za Mungu kwa matendo ya ubao wa pili478 ambao kwa huo tunajishughulisha na wanadamu na siyo hasa na Mungu. Lakini katika kuhesabiwa haki, hatuna budi kujishughulisha na Mungu. Isitoshe, ghadhabu yake lazima itulizwe na dhamiri ipate amani mbele zake. Hakuna lolote kati ya haya linalotokea kwa njia ya ubao wa pili wa Amri Kumi za Mungu.
225. Wao wanapinga kwamba, upendo unapendekezwa kuliko imani na tumaini kwani Paulo anasema: “Lililo kuu ni upendo.”479 Kwa hiyo, inaonekana kuwa matokeo yake ni kwamba, wema mkuu na maalumu kuliko vyote lazima uhesabie haki. 226. Lakini, katika fungu hili, Paulo anazungumzia hasa kuhusu upendo kwa jirani na kusema kwamba, lililo kuu kuliko yote ni upendo kwa sababu huyazaa matunda mengi mno. Imani na tumaini vinahusika na Mungu peke yake, ilihali upendo una wajibu wa nje usio na mwisho kwa wanadamu. Hata hivyo, tunawahakikishia wapinzani wetu kwamba, upendo wa Mungu na wa jirani ndiyo sifa kuu bora zaidi kwa sababu amri kuu inasema: “Mpende Bwana Mungu wako.”480 Lakini kwa sababu gani watahitimisha kwamba, upendo huhesabia haki? Wao husema kwamba, wema mkuu hutuhesabia haki. 227. Lakini hata Amri ya Kwanza au ya Pili ya sheria haihesabii haki, wala maadili makuu ya sheria hayawezi kufanya hivyo. Lakini maadili yale yamshikayo Kristo ndiyo yahesabiwayo haki, yakitujulisha sisi wema wa Kristo na ambao kwayo tunaipokea neema na amani kutoka kwa Mungu. Maadili haya ni imani. Jinsi tulivyosema mara nyingi, imani siyo tu ufahamu, bali ni hamu ya kupokea na kushika yale yaliyotolewa katika ahadi ya Kristo. 228. Lakini utiifu huu kwake Mungu, hamu hii ya kuipokea ahadi iliyotolewa, ni tendo la kumwabudu Mungu481 jinsi ulivyo upendo. Ni mapenzi ya Mungu tumwamini na tuzipokee fadhili kutoka kwake; Analitangaza hili kuwa ni ibada ya kweli.
229. Wapinzani wetu huuona upendo kuwa matokeo ya haki kwa sababu kila mahali wao hufundisha na kudai haki ya sheria. Hatuwezi kukana kwamba, upendo ndilo tendo kuu zaidi la sheria. Hekima ya mwanadamu huitazamia sheria na kutafuta haki ndani yake. Hivyo, Madaktari Wanazuoni waliokuwa watu wakuu na stadi, walihubiri tendo kuu la sheria na kwalo, walihusisha kuhesabiwa haki. Lakini wakidanganywa kwa busara za kibinadamu, hawakuweza kuuona uso halisi wa Musa, bali waliona uso wake uliotiwa utaji,482 sawasawa na wafanyavyo Mafarisayo, wanafalsafa na Waislamu. 230. Kwa upande wetu, tunahubiri upuuzi
478 Yaani, ubao wa pili wa Amri Kumi za Mungu, hasa amri ya 4-10.
479 1 Kor. 13: 13
480 Mt. 22: 37
481 Hapa, Melanchthon analitumia neno la Kiyunani ‘λατρεια,’ yaani, “ibada.”
482 2 Kor. 13: 2-15
wa Injili, ambao huifunua haki ya aina nyingine, yaani kwamba, kwa sababu ya Kristo, Mpatanishi, tunahesabiwa haki tunapoamini kuwa, kwa ajili ya Kristo, Mungu mwenye rehema kwetu, anatuhurumia. Tunajua wazi kwamba, mafundisho haya yanachukiza urazini na sheria na vile vile tunajua wazi kwamba, mafundisho ya sheria kuhusu upendo yanakubalika zaidi; Maana, fundisho hili ndilo busara ya mwanadamu. Lakini hatuuonei haya upuuzi wa Injili. Tunautetea kwa sababu ya utukufu wa Kristo na kumsihi Kristo atoe msaada wa Roho Mtakatifu aifanye (Injili) kuwa wazi na dhahiri.
231. Katika Hoja wapinzani wetu wameinukuu dhidi yetu aya ya Wakolosai 3:14: “Upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.” Kutokana na aya hii, wao huhalalisha kwamba, upendo huhesabia haki kwa kuwa huwafanya watu kuwa wakamilifu. Ingawa tungeweza kutoa majibu mengi kuhusu ukamilifu, tutaonyesha tu maana yake kwa mujibu wa Paulo. Bila shaka, Paulo anajadili kuhusu upendo kwa jirani yetu. Hatuna haki kufikiri kwamba, Paulo angeweza kuhusisha ama haki au ukamilifu mbele za Mungu katika matendo ya Ubao wa Pili kuliko Ubao wa Kwanza wa sheria. Ikiwa ni upendo ambao huwafanya watu kuwa waadilifu, basi Kristo, Mpatanishi, hatakuwa na maana. Ni imani pekee ndiyo inayomshika Kristo aliye mpatanishi. Kamwe, Paulo asingemkubali Kristo, Mpatanishi atengwe na kwa hivyo, mtazamo huu u mbali kabisa na kusudi la Paulo. 232. Hivyo, Paulo hazungumzii ukamilifu wa mtu binafsi bali kuhusu ushirika katika Kanisa. Anasema kwamba, upendo ni kifungo na mnyororo usiokatika unaowaunganisha washarika wengi wa Kanisa na mtu mwingine. Kadhalika, katika familia na jumuiya zote maelewano yanapaswa kustawishwa kwa kuhudumiana maana, siyo rahisi kuudumisha utulivu mpaka watu wafunike na kusamehe makosa fulani miongoni mwao. Kwa njia iyo hiyo, Paulo anaamuru kwamba, upendo uwepo Kanisani ili kudumisha mwafaka, Haja ikiwepo, kuwe na kuuvumilia mwenendo mpotovu wa ndugu, ili kuyasitiri makosa madogo madogo, Kanisa lisije likasambaratika katika mafarakano mbalimbali, chuki, makundi, na aina za uzushi unaosababishwa na mafarakano kama hayo. 233. Maana, lazima mwafaka utasambaratika, iwapo maaskofu watautwika umma mizigo mizito zaidi au kutojali unyonge wake. Wakati mwingine, mafarakano hutokea umma unapohukumu tabia za makasisi wao wa Kanisa la Kikristo kwa ukali sana au kuwadharau kwa ajili ya makosa madogo. Matokeo yake baadaye huwa ni kutafuta aina nyingine ya imani na makasisi wengine wa Kanisa la Kikristo. 234. Kwa upande mwingine, ukamilifu, (yaani, uadilifu wa Kanisa), utahifadhiwa Wakristo wenye nguvu wakiwa pamoja na wanyonge, umma ukistahimili upungufu wa makasisi wa Kanisa la Kikristo na maaskofu wanapozingatia unyonge wa umma. 235. Vitabu vingi vya wataalamu wenye
busara nyingi vimejaa mafundisho ya uadilifu ili, miongoni mwetu, tuyavumilie mengi katika maisha ya kila siku kwa ajili ya amani ya pande zote mbili. Paulo hufundisha kuhusu jambo hili hapa na penginepo. Kwa sababu hiyo, si sawa kwa wapinzani wetu kubishana kuhusu msingi wa neno “ukamilifu” ambao upendo unahesabia haki, Wakati Paulo anapozungumzia umoja na amani ya umma katika kanisa. Ambrosio huifafanua andiko hili ifuatavyo: “Sawasawa na jinsi jengo linavyopaswa kuwa kamili na zima ikiwa sehemu zake zote zinashikamana sawasawa.”483 236. Wapinzani wetu wanahubiri kwa shingo upande sana kuhusu upendo ambao hawauonyeshi kamwe katika matendo. Wanafanya nini sasa? Wanayafarakanisha makanisa. Wanazitunga sheria kwa damu na wanamwomba Kaisari, mtawala mwenye huruma nyingi, azitangaze rasmi. Wanawachinja wachungaji na watu wema wengine, iwapo walithubutu kutangaza kutokubaliana kwao na baadhi ya matumizi mabaya yaliyokuwa wazi. Haya yote hayalingani na sifa zao za upendo; Kama wapinzani wetu wangezifuata, wangeileta amani katika Kanisa na serikali. Misukosuko hii ingetoweka ikiwa wapinzani wetu wangeacha kukazia, kwa ukali, desturi fulani zisizokuwa na maana kwa ajili ya uchaji. Isitoshe, nyingi hazifuatwi hata na wale wanaozitetea kwa bidii. Wanasameheana wenyewe kwa urahisi, ila siyo kwa wengine, jinsi mshairi anavyoandika kuhusu mtu huyo: “Mimi ninajisamehe mwenyewe, anasema Maenio.”484 237. Lakini hili ni tofauti kabisa na sifa hizo za upendo wanazozikariri kutoka kwa Paulo. Hawana ufahamu zaidi ya kuta zinazorudisha nyuma mwangwi.
238. Wao huinukuu kauli hii kutoka kwa Petro: “Upendano husitiri wingi wa dhambi.”485 Bila shaka, Petro vile vile anazungumzia kuhusu upendo kwa jirani, maana anaihusisha kauli hii na amri ya kupendana. Isingeweza kuingia mawazoni mwa mtume yeyote kuwa upendo wetu unaishinda dhambi na kifo; Au kwamba, badala ya Kristo, Mpatanishi, upendo ni upatanisho ambao, unampatanisha Mungu nasi; au kwamba, upendo hou ni haki bila Kristo Mpatanishi. Hata kama kungekuwapo upendo wa namna hii, ungekuwa upendo wa haki ya sheria badala ya kuwa haki ya Injili ambayo inatuahidi upatanisho na haki ikiwa tunaamini kwamba, kwa ajili ya Kristo, mpatanishi, Baba ni mwenye rehema kwetu, na kwamba, stahili za Kristo zimetolewa kwetu. 239.Kadhalika, mapema kidogo, Petro alituamuru tumwendee Kristo na kujengwa juu yake. Pia anaongezea kusema: “Na kila amwaminiye hatatahayarika.”486 Upendo wetu hautuondolei aibu wakati Mungu anapotuhukumu na kutushtaki, lakini imani
483 Rejeo hili halipatikani katika maandiko ya Ambrosio yanayofahamika.
484 Qu. Horatius Flaccus (65 - 8 K.K.) katika ‘Satirae‘ 1, 3, 23.
485 1 Pet. 4: 8
486 1 Pet. 2: 4-6
katika Kristo hutuweka huru miongoni mwa hofu hizi kwa kuwa tunajua kwamba, tunasamehewa kwa ajili ya Kristo.
240. Licha ya hayo, tamko hili kuhusu upendo limenukuliwa kutoka Mithali 10: 12, mahali kinyume chake kinaelezea dhahiri maana yake kuwa: “Kuchukiana huondokesha fitina; bali kupendana husitiri makosa yote.” 241. Aya hii inafundisha jambo lile lile jinsi Paulo asemavyo katika Kol. 3: 13, yaani, mafarakano yakitokea yamalizwe kwa utulivu na upole/uvumilivu. Anasema kwamba, mifarakano hukua kwasababu ya chuki, jinsi tuonavyo mara nyingi majanga makubwa zaidi yanatokana na makosa madogo madogo. Mabishano madogo yalizuka kati ya Kaisari Gaio Yulio na Pompeyo, ambayo hayangezusha vita vya wenyewe kwa wenyewe, kama kila upande ungekubali kushindwa kwa kiasi kidogo. 242. Wakati kila mmoja alikubali amri kwa chuki yake, ghasia kubwa ilizuka kutokana na suala lisilokuwa na maana. Uzushi mwingi umetokea Kanisani kutokana tu na chuki za makasisi wa Kanisa la Kikristo. Kwa hiyo, katika andiko hili, Petro hazungumzii kuhusu makosa yake mwenyewe bali ya watu wengine anaposema: “Bali kupendana kusitiri makosa yote,” yaani, makosa ya watu wengine na yale yaliyotendeka baina ya watu. Maana yake: Ingawa dhambi hizi hutokea, upendo huzisitiri, husamehe, huzaa matunda, husalimu amri, na haifikii kikomo cha sheria. Petro, hamaanishi kwamba, upendo hustahili msamaha wa dhambi mbele za Mungu; kwamba, badala ya Kristo mpatanishi, upendo ni upatanisho wetu; au kwamba, upendo huzaa upya na huhesabia haki. Anamaanisha kwamba, katika mahusiano ya kibinadamu, upendo usiwe wenye wepesi wa kukasirika, mkali, au usiosamehe; Badala yake, upendo usitiri baadhi ya makosa ya marafiki zake; na kwamba, uyatetee kabisa hata makosa makubwa ya wengine jinsi methali ya kawaida isemavyo: “Fahamu, lakini usizichukie, tabia za rafiki.”487 243. Mara nyingi, mitume hawazungumzi bila sababu kuhusu wajibu huu wa upendo ambao wafalsafa huuita ‘kiasi’ (επιεικεια). Wema huu ni wa lazima kwa ajili ya kuuhifadhi mwafaka kwa jamaa ambao hauwezi kudumu pasipo wachungaji na makanisa kuyasahau na kuyasamehe mambo mengi.
244. Wananukuu andiko hili Kutoka kwenye Waraka wa Yakobo: “Mwaona kwamba, mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.”488 Hakuna fungu lingine linalopaswa kupingana zaidi na msimamo wetu, lakini jibu lake ni rahisi na wazi. Maneno ya Yakobo hayataleta shida yoyote iwapo wapinzani wetu hawaingizi mawazo yao kuhusu ustahilifu wa matendo. Popote matendo yanapotajwa, wapinzani wetu huongezea maoni
487 Horatio, ‘Satirae’ 1, 3, 32. 488 Yak. 2: 24
yao mapotovu kwamba, tunastahili msamaha wa dhambi kwa matendo mema; kwamba, matendo mema ni upatanisho na gharama ambayo kwayo Mungu anapatanishwa nasi; kwamba, matendo mema yanashinda vitisho vya dhambi na mauti; kwamba, matendo yanakubalika mbele za Mungu kwa ajili ya ubora wake; na kwamba, hatuhitaji rehema na Kristo, Mpatanishi. Ingawa wapinzani wetu huyatetea haya yote kwa kisingizio cha sentensi ya Yakobo. Hakuna lolote kati ya haya lililowahi kuingia akilini mwa Yakobo.
245. Kwanza, lazima tuelewe kwamba, andiko hili linawapinga zaidi wapinzani wetu kuliko sisi. Wapinzani wetu hufundisha kwamba, mwanadamu anahesabiwa haki kwa upendo na matendo, lakini hawasemi lolote kuhusu imani ambayo kwayo tunamshikilia Kristo, Mpatanishi. Hawaishutumu tu imani hii kwa kauli na maandiko yao bali kuitupilia mbali na Kanisa kwa njia ya upanga na adhabu ya kifo. Mafundisho ya Yakobo ni mema kiasi gani! Maana haiachi imani wala hatukuzi upendo badala yake, bali anaidumisha (imani) ili Kristo ambaye ni mpatanishi, asije akatengwa na kuhesabiwa haki. Vivyo hivyo, hata Paulo anaunganisha imani na upendo anapotoa muhtasari wa maisha ya Kikristo katika 1 Tim 1:5: “Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.”
246. Pili, muktadha489 wa kifungu hiki unaonyesha kwamba, matendo yanayozungumziwa hapa ni yale yanayoifuata imani na kuonyesha kwamba, imani haijafa bali ni hai na inatenda kazi moyoni. Basi, Yakobo hakushikilia kwamba, tunastahili msamaha wa dhambi na neema kwa njia ya matendo yetu mema. Anayazungumzia matendo ya wale waliokwisha kuhesabiwa haki, ambao tayari wamekwisha kupatanishwa, wamekubaliwa na kuupokea msamaha wa dhambi. Kwa hiyo, ni udanganyifu kwa wapinzani wetu kubishana kutokana na andiko hili kwamba, Yakobo anafundisha kuwa, sisi tunastahili msamaha wa dhambi na neema kwa matendo mema na kwamba, kwa matendo yetu, tunaweza kumkaribia Mungu bila Kristo aliye Mpatanishi
247. Tatu, tayari Yakobo amesema kwamba, kuzaliwa upya kunafanyika kwa njia ya Injili. Anasema: “Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.”490 Anaposema kwamba, tumezaliwa upya kwa njia ya Injili, anafundisha kwamba, tumezaliwa upya na kuhesabiwa haki kwa njia ya imani. Maana, ni imani tu inayoishikilia ahadi ya Kristo tunapopinga vikali vitisho vikuu vya dhambi na kifo. Hivyo, Yakobo hamaanishi kwamba, tunazaliwa upya kwa matendo yetu.
489 Yaani, mazingira ya aya maalumu katika maandiko. 490 Yak. 1: 18
248. Kutokana na hili ni wazi kwamba, Yakobo hayupo kinyume nasi anapobainisha kati ya imani iliyokufa na imani hai na anakaripia nafsi zembe na zinazoota ndoto kwamba, zina imani na kumbe hazina. 249. Alisema kwamba, imani isiyozaa matunda mema imekufa, lakini imani ni hai inapozaa matendo mema. Tayari, tumekwisha kuonyesha vya kutosha kile tunachomaanisha kwa imani. Hatuzungumzii maarifa yasiyofaa ambayo hata mashetani wanayo, bali tunazungumzia imani ambayo inapinga vitisho vikubwa vya dhamiri na kisha kutia moyo na kufariji mioyo iliyo na hofu. 250. Imani ya jinsi hiyo siyo rahisi kama jinsi wapinzani wetu wanavyofikiri; wala, imani hiyo si uwezo wa kibinadamu, bali ni utakatifu wa Mungu unaotufanya kuwa hai na kutuwezesha kushinda kifo na Ibilisi. Jinsi Paulo asemavyo katika Wakolosai kwamba, kwa nguvu za Mungu, imani ni madhubuti na inashinda mauti (Wakolosai 2: 12): “Katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu.” Kwa kuwa, imani hii ni maisha mapya, lazima izae misukumo mipya na matendo mapya. Kwa hiyo, ni sahihi Yakobo kukana kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani bila matendo. 251. Lakini anaposema kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani na matendo, hakika hamaanishi kwamba, tunazaliwa upya kwa matendo. Wala hasemi kwamba, kwa sehemu fulani, upatanisho wetu ni kwa ajili ya Kristo, na kwa sehemu nyingine upatanisho huo ni kwa ajili ya matendo yetu. Wala haelezei namna ya kuhesabiwa haki, bali anaelezea tu asili ya waliohesabiwa haki ambao tayari wamehesabiwa haki na kuzaliwa upya. 252. “Kuhesabiwa haki” hapa hakumaanishi kwamba, mwenye dhambi anafanywa kuwa mwenye haki, bali anatangaziwa kuwa mwenye haki kwa njia ya kimahakama491 jinsi ilivyo katika kifungu kifuatacho: “Bali ni wale waitendao sheria watahesabiwa haki.”492 Jinsi maneno haya yasemavyo, “bali ni wale waitendao sheria watahesabiwa haki,” hayana lolote lililo kinyume na msimamo wetu, hali kadhalika tunayadumisha hayo hayo kuhusu maneno ya Yakobo: “Mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake,” 493 maana watu walio na imani na matendo mema bila shaka wanatangaziwa haki. Jinsi tulivyosema, matendo mema ya watakatifu ni ya haki na yanampendeza Mungu kwa ajili ya imani. Yakobo anahubiri tu matendo yanayozaliwa na imani peke yake, jinsi anavyoonyesha anapomzungumzia Ibrahimu: “Imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake.”494 Inasemwa katika sentensi hii: “Waitendao sheria watahesabiwa haki,” yaani, wanaomwamini Mungu kutoka moyoni na wanaozaa matunda mema,
491 Kilatini: ‘Usu forensi iustum pronuntiari.’ Sentensi hii ni moyo wa mafundisho ya Kilutheri kuhusu kuhesabia haki mbele za Mungu.
492 Rum. 2: 13
493 Yak. 2: 24
494 Yak. 2: 22
yanayompendeza kwa ajili ya imani, na kwa hiyo kuwa watimizaji wa sheria, hao Mungu huwatangazia haki. 253. Maneno haya yaliyosemwa kwa urahisi, hayana makosa, lakini wapinzani wetu wanayapindua kwa kuingiza ndani mwao maoni yao mapotovu. Hayahalalishi hitimisho lolote kati ya haya: matendo hustahili msamaha wa dhambi; kwamba, matendo huifanya mioyo yetu izaliwe upya; kwamba, matendo ni upatanisho; kwamba, matendo humpendeza Mungu bila Kristo, Mpatanishi; na kwamba, matendo hayamhitaji Kristo, Mpatanishi. Yakobo hasemi lolote miongoni mwa haya, ambayo wapinzani wetu bila aibu wanayahitimisha kutokana na maneno yake.
254. Ili kutupinga, wanazirejea kauli zingine zinazohusu matendo (Luka 6:37): “. . . achilieni, nanyi mtaachiliwa;” Isaya 58: 7, 9: “Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako . . . Ndipo utaita, na Bwana ataitika;” Danieli 4:27: “Ukaache dhambi zako kwa kutenda haki.” Mathayo 5:3,7: “Heri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao . . . Heri wenye rehema; maana hao watapata rehema.” 255. Lakini kama wapinzani wetu wasingeyaingiza maoni yao ya uongo ndani ya aya hizi zote, kusingekuwepo na lolote linalokwenda kinyume nasi. Aya hizi zina mambo mawili. La kwanza ni mahubiri ya sheria au toba ambayo huwahukumu watenda mabaya na kuwaamuru watende mema. Lingine ni ahadi inayoongezwa. Katika mambo haya mawili hawaongezi kuwa dhambi zinasamehewa bila imani au kwamba, matendo haya yenyewe ni upatanisho. 256. Lakini sheria inapohubiriwa, lazima mambo haya mawili yakumbukwe. Kwanza, hatuwezi kuitimiza sheria tusipozaliwa upya kwa njia ya imani katika Kristo, jinsi asemavyo: “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”495 Ingawa wanadamu wanaweza kutenda matendo fulani ya nje, tamko hili kwa watu wote lazima liruhusiwe kuifafanua sheria nzima: “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.”496 Pia ni lazima tuishike ahadi ya Injili kwamba, kupitia Kristo tuna njia ya kumfikia Baba.497 257. Ni wazi kwamba, hatuhesabiwi haki kwa sheria. Vinginevyo, ikiwa mahubiri ya sheria yenyewe yangetosha, Kristo na Injili ingehitajika kwa kusudi gani? Kwa sababu hiyo, haitoshi kuihubiri sheria katika mahuhubiri ya toba, yaani Neno lile linaloshtaki kwa ajili ya dhambi.498 Kwa maana, sheria huiamsha ghadhabu; hushtaki; huzitisha dhamiri. Dhamiri haziwezi kutulia mpaka zisikie sauti ya Mungu, ikitoa wazi ahadi ya msamaha wa dhambi. Hivyo, ni muhimu kuongezea ahadi ya Injili kwamba, kwa ajili ya Kristo, dhambi zinasamehewa na kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi kwa
495 Yn. 15: 5
496 Ebr. 11: 6
497 Rum. 5: 2
498 Au, linaloonyesha dhambi.
njia ya imani katika Kristo. Iwapo wapinzani wetu wataiondoa Injili ya Kristo kutoka kwa mahubiri ya toba, basi, wanastahili kuitwa wanaomkufuru Kristo.
258. Haya yanadhihirika wazi Isaya anapohubiri kuhusu toba anaposema: (Isaya 1: 16-18) “Acheni kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; . . . ” Hivyo, nabii anahimiza toba na anaongezea ahadi. Itakuwa ni upumbavu kuyaangalia matendo haya pekee katika kauli hii: “Takeni hukumu na haki,. . . mpatieni yatima haki yake.” Mwanzoni kabisa anasema, “Acheni kutenda mabaya” akiishutumu mioyo isiyomcha Mungu na kuidai imani. Nabii hasemi kwamba, kwa njia ya matendo haya - “takeni hukumu na haki,. . . mpatieni yatima haki yake” - yangeweza kustahili msamaha wa dhambi kwa matendo yenyewe,499 bali anayaamuru matendo haya kuwa ya lazima kwa ajili ya maisha mapya. Wakati huo huo, anataka msamaha wa dhambi upokelewe kwa imani. Kwa sababu hiyo, anaongeza ahadi. 259. Inatubidi tuzifafanue aya zingine zinazofanana na hii na kwa njia hiyo hiyo. Kristo anahubiri toba anaposema, “achilieni” na analiongezea neno la ahadi, “nanyi mtaachiliwa.”500 Hasemi kwamba, tunaposamehe, hustahilisha msamaha wa dhambi kwa tendo lenyewe,501 bali anadai maisha mapya, ambayo kwa hakika ni ya lazima. Wakati huo huo, anataka msamaha wa dhambi upokelewe kwa imani. Kadhalika, nabii Isaya anaposema: “Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako,”502 anadai maisha mapya. Wala nabii hazungumzii tendo hili peke yake, bali kuhusu toba nzima kama andiko linavyoonyesha; Isitoshe, wakati huo huo, anataka msamaha wa dhambi upokelewe kwa imani. Maana ni hakika kwamba, wala milango ya kuzimu haitalishinda (Mathayo 16,18), kwamba, katika mahubiri ya toba, mahubiri ya sheria hayatoshi kwa sababu sheria hutenda ghadhabu na daima hushtaki. Lazima mahubiri ya Injili yaongezwe, yaani, kwamba, msamaha wa dhambi unatolewa kwetu iwapo tunaamini kwamba, kwa ajili ya Kristo dhambi zetu zinasamehewa. Kama si hivyo, kungekuwa na haja gani ya Kristo wala ya Injili? Inatubidi tuyazingatie daima mafundisho haya muhimu. Kwa njia hii, tunaweza kuwapinga wanaomkataa Kristo, wanaoiharibu Injili, na wanaoyageuza Maandiko Matakatifu kwa hila ili yalingane na nadharia iliyobuniwa na wanadamu kwamba, tunaununua msamaha wa dhambi kwa matendo yetu.
499 Kilatini: ‘Ex opere operato’
500 Lk. 6: 37
501 Kilatini: ‘Ex opere operato’
502 Isa. 58: 7
261. Hivyo, katika mahubiri ya nabii Danieli imani inahitajika. Danieli hakumaanisha tu kusema kwamba, mfalme anapaswa kutoa zaka, bali anajumuisha toba yote anaposema: “. . . ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini . . .”, yaani, ukaache maovu kwa kubadilika moyo na matendo.503 Hili linahitaji imani. Danieli alimhubiria mfalme mambo mengi kuhusu ibada ya Mungu mmoja wa Israeli na akambadili siyo kwa ajili ya kutoa zaka tu bali hasa kwa kuwa na imani. Maana, hapa kuna ukiri safi wa mfalme kuhusu Mungu wa Israeli: “... kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii.”504 Kwa hiyo, mahubiri ya Danieli yana sehemu mbili. Sehemu moja inafundisha kuhusu maisha mapya na matendo yake. Katika sehemu nyingine Danieli anamuahidi mfalme msamaha wa dhambi. Ahadi hii ya msamaha wa dhambi siyo mahubiri ya sheria, bali sauti ya kinabii na ya kiinjili ambayo, kwa hakika, Danieli aliitaka ipokelewe kwa imani. 262. Danieli, alitambua kwamba, msamaha wa dhambi katika Kristo haukuahidiwa kwa Waisraeli tu bali uliahidiwa kwa mataifa yote. Vinginevyo, asingeweza kumuahidi mfalme msamaha wa dhambi. Hasa katikati ya vitisho vya dhambi, mwanadamu lazima awe na neno la Mungu imara ili ajifunze kuhusu mapenzi ya Mungu, yaani, kwamba, Mungu hana hasira tena. Katika lugha yake mwenyewe, maneno ya Danieli yanaelezea kwa ufasaha zaidi kuhusu toba kamili na yanaitoa ahadi wazi zaidi yakisema: “Ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini.” Maneno haya yanajishughulisha na mawanda mazima ya toba. Yanamwamuru mfalme awe mwenye haki, kisha atende mema na kuwatetea maskini dhidi dhuluma kwani huo ulikuwa wajibu wa mfalme. Haki ni imani iliyomo ndani ya moyo. 263. Dhambi zinaondolewa kwa toba, yaani, sharti au hatia inaondolewa kwa kuwa Mungu huwasamehe wale wanaotubu, jinsi ilivyoandikwa katika (Ezekieli 18: 21-22). Hatuwezi kujitetea kutokana na hili kwamba, Mungu husamehe kwa ajili ya matendo yanayofuata, au kwa sababu ya zaka, bali kwa ajili ya ahadi yake yeye huwasamehe wao waishikao ahadi hiyo. Hawaishiki ahadi isipokuwa waiamini na waishinde dhambi na kifo kwa njia ya imani. Wakiwa wamezaliwa hivyo upya kwa namna hii, huzaa matunda yapasayo toba jinsi Yohana Mbatizaji anavyosema.505 Hivyo, ahadi inaongezewa “Tazama, utaweza kuondolewa uovu wako.”506 264. Hapa Hieronimo aliongezea kishirikishi kidogo kinachoelezea mashaka na katika maelezo yake alishikilia kwa mamlaka haba kwamba, hakuna uhakika katika msamaha wa dhambi.507
503 Dan. 4: 24, 27
504 Dan. 3: 29
505 Mt. 3: 8
506 Dan. 4: 27
507 Hieronimo alitumia neno la Kilatini: ‘forsitan,’ yaani, “labda:” “Labda utaweza kuondolewa uovu wako.”
Tukumbuke kabisa kwamba, Injili huahidi msamaha wa dhambi kwa uhakika. Itakuwa upigaji marufuku wazi wa Injili ikiwa tutakana kwamba, hakika, msamaha wa dhambi lazima utolewe kwa njia ya ahadi. Acheni tumpuuze Hieronimo kabisa katika ufafanuzi wake wa andiko hilo, japo hata ahadi inahusika wazi katika neno “komboa.” Linamaanisha kwamba, msamaha wa dhambi unawezekana, kwamba, dhambi zinaweza kuondolewa, kwamba, sharti au hatia ya deni inaweza kuondolewa, na kwamba, ghadhabu ya Mungu inaweza kutulizwa. Kila mahali, wapinzani wetu wanaziacha ahadi na kuzitazama amri tu wakiongezea nadharia ya mwanadamu kwamba, msamaha wa dhambi unategemea matendo. Andiko halisemi hivyo. Badala yake linadai imani. Kila palipo na ahadi, hapo imani huhitajika. Ni imani tu iwezayo kuipokea ahadi.
265. Machoni pa mwanadamu, matendo yanavutia macho sana. Kwa desturi, sababu za kibinadamu, huwavutia; kwa sababu huona matendo tu na hauangalii wala hauelewi imani. huota kwamba, stahili ya matendo haya huleta msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki. Kwa kawaida, wazo hili la kisheria huambatana na akili za wananadamu na haliwezi kuondolewa mpaka tuwe tumefundishwa na Mungu. 266. Lazima akili igeuzwe kutoka kwa maoni kama hayo ya kimwili hadi kwa Neno la Mungu. Tunaona kwamba, Injili na ahadi ya Kristo vimetolewa kwetu. Haitupasi kuikana ahadi ya Kristo sheria inapohubiriwa na matendo kuamriwa. Kinyume chake, lazima kwanza tuishike ahadi ili tuweze kuyatenda mema na kwamba, matendo yetu yaweze kumpendeza Mungu, jinsi Kristo anavyosema: “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”508 Kadhalika, iwapo Danieli angesema: “Uache maovu yako kwa toba,” wapinzani wetu wangepita fungu hili. Anatumia maneno mengine kuelezea wazo hihi hili, na wapinzani wetu mara moja wanayageuza maneno yake ili yalete maana iliyo kinyume cha mafundisho ya neema na imani, wakati Danieli anataka sana kkuijumuisha imani. 267. Basi, hivi ndivyo tunavyoyajibu maneno ya Danieli: Kwa kuwa anapohubiri toba, hafundishi juu ya matendo tu, bali hata juu ya imani pia, jinsi masimulizi yenyewe katika kifungu hicho hicho yanavyoshuhudia. Pili, kwa kuwa Danieli anaitoa ahadi dhahiri, bila shaka anaidai imani, ambayo huamini kwamba, Mungu anasamehe dhambi bure. Ingawa anataja matendo yanayohusiana na toba, kwa hiyo, Danieli hasemi kwamba, kutokana na matendo haya tunastahili msamaha wa dhambi. Danieli hazungumzii kuhusu ondoleo la adhabu peke yake, kwa sababu ni kazi bure kulitafuta ondoleo la adhabu mpaka moyo uwe umepata kwanza ondoleo la hatia. 268. Iwapo wapinzani wetu watamwelewa Danieli kama anayerejelea tu ondoleo la adhabu peke yake, andiko hili halitadhibitisha lolote dhidi yetu, kwa sababu, itawabidi kukubali kwamba, kwanza msamaha 508 Yn. 15: 5
wa dhambi huja na kuhesabiwa haki bila matendo. Jinsi tunavyokubali bila wasiwasi, baadaye adhabu zinazotuadhibu zinapunguzwa kwa njia ya sala zetu na matendo mema, hasa kwa toba yetu kamili, kulingana na maneno yasemayo: “Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa,” “Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza,” “Nirudieni mimi . . . nami nitawarudia ninyi” na “Ukaniite siku ya mateso, nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”509
269. Kwa hiyo, kila matendo mema yanaposifiwa na sheria inahubiriwa, sharti tuzishike kabisa kanuni hizi: kwamba, sheria haitimizwi bila Kristo, jinsi alivyosema mwenyewe: “Pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote”510 na kuwa, “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.”511 Hakika, mafundisho ya sheria hayakusudiwi kuiondoa Injili na kumwondoa Kristo, mpatanishi. Basi, walaaniwe kabisa wapinzani wetu, hao Mafarisayo, wanaoifafanua sheria kwa namna ambayo wanauhusisha utukufu wa Kriristo kwa njia ya matendo na kwa kuyafanya matendo yawe upatanisho unaostahili msamaha wa dhambi. Hivyo basi, inafuata kwamba, matendo yanatukuzwa kwa kumpendeza Mungu kwa ajili ya imani, kwa kuwa hayampendezi bila Kristo, Mpatanishi: “Ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii,”512 kwake Baba, siyo kwa njia ya matendo bila Kristo, Mpatanishi. 270. Katika kauli isemayo: “Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri,”513 hatuna budi kutambua kwamba, hakuna mtu awezaye kuzishika amri au kumpendeza Mungu bila Kristo. Hivyo, Amri ya Kwanza katika Amri Kumi za Mungu yenyewe inasema: “Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.”514 ikielezea ahadi tele ya sheria. Lakini sheria hii haitimizwi bila Kristo. Daima huishtaki dhamiri ambayo haitimizi sheria. Kwa sababu hiyo, dhamiri huikimbia kjwa hofu hukumu na adhabu ya sheria: “Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira.”515 Lakini sheria inatimizwa mara tu mtu asikiapo kwamba, Mungu amepatanishwa nasi kwa ajili ya Kristo ingawa hatuwezi kuitimiza sheria. Imani inapomshika Kristo, Mpatanishi, moyo hutulia, huanza kumpenda Mungu na kuitimiza sheria. Inajua kwamba, sasa inampendeza Mungu kwa ajili ya Kristo, Mpatanishi, ingawa mwanzo wake wa utimizaji sheria ni najisi na mchafu mno. Kwa njia hii atuna budi kuyaangalia mahubiri ya toba. 271. Ingawa wanazuoni hawajasema lolote kuhusu imani katika mafundisho yao
509 1Kor. 11: 31; Yer. 15: 19; Zek. 1: 3; Zab. 50: 15
510 Yn. 15: 5
511 Ebr. 11:6
512 Rum. 5: 2. Andiko la Melanchthon: ‘Kwa Mungu.’
513 Mt. 19: 17
514 Kut. 20: 6
515 Rum. 4: 15
kuhusu toba, lakini tunafikiri kwamba, hakuna hata mmoja wa wapinzani wetu aliyeghadhibika kiasi cha kukana kwamba, ondoleo la dhambi ni sauti ya Injili. Ondoleo la dhambi lazima lipokelewe kwa njia ya imani ili lichangamshe dhamiri iliyojaa hofu.
272. Kwa sababu mafundisho ya toba hayadai tu matendo mapya bali pia yanaahidi msamaha wa dhambi, lazima yahitaji imani. Ni imani tu inayopokea msamaha wa dhambi. Katika mafungu haya yanayohusu toba, ni muhimu sana kufahamu kwamba, imani inahitajika, wala siyo matendo tu, jinsi ilivyo katika Mathayo 6: 14: “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.” Hapa tendo linahitajika na ahadi ya msamaha wa dhambi inaongezwa, siyo kwa kuyategemea matendo bali kwa kumtegemea Kristo kwa imani. 273. Hivyo, Maandiko Matakatifu hushuhudia katika mahali pengi kama katika Matendo ya Mitume 10, 43: “Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.” 1 Yohana 2: 12 inasema: “. . . kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.” Waefeso 1: 7: “Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi.” Je, kwa nini mafungu yakaririwe? 274. Hili ndilo tangazo muhimu la Injili kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi kwa njia ya imani kwa ajili ya Kristo wala siyo kwa ajili ya matendo yetu. Wapinzani wetu hujaribu kulinyamazisha tangazo hili la Injili kwa kuyageuza vibaya yale mafungu yanayofundisha sheria au matendo. Ni kweli kwamba, katika kufundisha matendo ya toba yanahitajika, kwa kuwa maisha mapya yanahitajika. Lakini, kwa ukorofi, wapinzani wetu wanashikilia hapa kwamba, tunastahili msamaha wa dhambi au haki kwa matendo kama hayo. 275. Hata hivyo, mara kwa mara Kristo anaihusisha ahadi ya msamaha wa dhambi na matendo mema. Hamaanishi kwamba, matendo mema ni upatanisho – maana yanafuata upatanisho – bali anafanya hivyo kwa sababu mbili. Kwanza, ni kwamba, matunda mema yanapaswa kufuata kwa lazima. Hivyo, anaonya kwamba, toba ni ya kinafiki na ya uongo ikiwa matunda mema hayataifuata. Sababu nyingine ni kwamba, tunahitaji ishara za nje za ahadi hii kubwa kabisa zinazoonekana,516 maana, dhaniri iliyo na hofi inahitaji faraja kubwa. Kwa mfano, Ubatizo na Chakula cha Bwana ni alama ambazo mara kwa mara huonya, huchangamsha, na kuimarisha nafsi zenye hofu ili zipate kuamini kwa dhati kwamba, dhambi zao zimesamehewa. Ahadi hii hii imeandikwa na kuonyeshwa katika matendo mema, ambayo yanatuhimiza tuzidi kuamini kwa
516 Kilatini: ‘Externa signa.’ Ni muhimu sana kuelewa maneno haya “dalili zinazoonekana” kulingana na mafundisho mazima ya Kilutheri kuhusu sakramenti. Kwa kweli, sakramennti ni alama au dalili zinazoonekana lakini zisizokuwa alama au dalili tupu katika maana ya mifano bali ni alama au dalili zinazojaa kuwepo kwa Kristo na neema ya Mungu.
uthabiti. Wale wanaoshindwa kutenda mema, hawajibidiishi wenyewe kuamini bali wanazidharau ahadi hizi. Lakini wacha Mungu huzikumbatia ahadi hizo na hufurahia kuwa na ishara na ushuhuda wa ahadi hii kuu. Hivyo, hujizoeza wenyewe katika ishara na katika shuhuda hizi. Jinsi ambavyo Chakula cha Bwana chenyewe hakihesabii haki kama tendo lenyewe517 bila imani, vivyo hivyo utoaji wa sadaka hauhesabii haki kama tendo lenyewe bila imani.
277. Kauli ya Tobiti (4: 11)518 inapaswa pia kueleweka kwa njia ile ile: “Utoaji wa sadaka unatuweka huru kutoka kwa makosa yote na kifo.” Hatutasema kwamba, huu ni mbalagha,519 bali hivyo ndivyo inavyopaswa kueleweka ili utukufu wa Kristo usije ukapunguzwa, ambaye mamlaka yake binafsi ni kuweka watu huru kutoka kwenye dhambi na mauti. Inatubidi kuirudia kanuni hii kwamba, mafundisho ya sheria hayatafaa bila Kristo. 278. Hivyo Mungu hupendezwa na utoaji ule unaofuata kuhesabiwa haki au upatanisho, siyo kwa ule unaotangulia Kwa hiyo, utoaji sadaka haumuweki huru yeyote kutoka kwa dhambi na mauti, siyo kama matendo yenyewe. Jinsi tulivyosema awali kuhusu toba ni kwamba, hatuna budi kuzingatia imani na matunda pamoja. Hivyo, kuhusu utoaji sadaka, tunasema kwamba, ni upya kabisa wa maisha ambao huokoa. Utoaji sadaka ni zoezi la imani hiyo inayoukubali msamaha wa dhambi na kuyashinda mauti jinsi inavyozidi kuwa yenye nguvu zaidi kwa njia ya mazoezi kama hayo. Pia tunakubali kwamba, sadaka hustahilisha baraka nyingi za Mungu, hupunguza adhabu zetu na hustahilisha utetezi kwa ajili yetu katika hatari za dhambi na mauti, kama jinsi tulivyoelezea mapema kwa ujumla kuhusu toba. 279. Kauli nzima ya Tobia ikichunguzwa inaonyesha kwamba, imani inahitajika kwanza kabla ya utoaji wa sadaka: “Mwanangu, uwe mwaminifu kwa Bwana Mungu wetu siku zote za maisha yako,” na baadaye anasema: “Umtukuze Bwana Mungu wako siku zote. Umwombe aongoze njia zako na kuzifanikisha shughuli zako . . .”520 Kwa kufaa, matendo haya ni vya aina ya imani ambayo tumekuwa tukiizungumzia, imani ambayo huamini kuwa Mungu aliyeridhika anapatanishwa kwa ajili ya rehema yake mwenyewe na inayotaka kuhesabiwa haki, kutakaswa na kutawaliwa na Mungu. 280. Lakini wapinzani wetu, walio mahiri, wanazichagua aya zinazopotosha ili kuziwasilisha kwa watu wasio na uzoefu. Kisha, wao huyaongezea kitu kutoka kwa maoni yao wenyewe. Inatubidi kuzingatia vifungu katika muktadha wao, maana kulingana na maoni ya watu wote, siyo halali kutoa hukumu au kujibu kifungu kimoja katika mabishano, bila kuizingatia sheria
517 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
518 Kitabu kimoja cha Agano la Kale kisichotambuliwa kuwa chenye mamlaka kuhusu mafundisho ya imani.
519 Yaani, jamblo la kutia chumvi.
520 Tob. 4: 5,19
nzima. Mara nyingi vifungu vinapozingatiwa katika muktadha wao wenyewe, hutoa fafanuzi zao.521
281. Luka 11: 41 vile vile imenukuliwa katika hali iliyopotoka: “Lakini, toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu.” Bila shaka wapinzani wetu ni viziwi. Ni mara ngapi tumekwisha kusema kwamba, lazima Injili ya Kristo iongezewe kwenye mahubiri ya sheria, kwamba, matendo mema humpendeza Mungu kwa ajili ya Kristo. Lakini kila mahali, humwacha Kristo nje na hufundisha kwamba, tunastahili kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria. 282. Uchunguzi wa aya hii nzima unaonyesha kwamba, imani inahitajika. Kristo anawakemea Mafarisayo kwa kuwaza kwamba, wamesafishwa mbele za Mungu, yaani, wanahesabiwa haki kwa kutawadha mara kwa mara. Vivyo hivyo, Papasina hakika ni yupi - alisema kuwa kunyunyizia maji yaliyotiwa chumvi “huosha na kutakasa watu.” Maelezo yanasema kwamba, maji ya chumvi yanasafisha makosa madogo madogo. 522 Hayo pia yalikuwa mawazo ya mafarisayo. Kristo aliyakataa haya na badala ya usafishaji huu wa uono anaweka usafi maradufu, yaani ule wa ndani na mwingine wa nje. Anawaamuru watakaswe kwa ndani na kisha anaongezea usafi wa nje: “Toeni sadaka kwa mali iliyosalia na hivyo vitu vyote vitakuwa safi kwa ajili yenu.” 283. Wapinzani wetu hukifafanua visivyo kishirikishi kinachoenea pote ”-ote.” Kristo analiongezea hitimisho hili kwa vifungu vyote viwili: Vitu vyote vitakuwa safi iwapo wewe ni safi kwa ndani na iwapo utazitoa sadaka. Anamaanisha kwamba, usafi wa nje utapatikana katika matendo yaliyoamriwa na Mungu. Usafi huo haupatikani katika mapokeo ya kibinadamu kama kutawadha katika nyakati hizo au kunyunyizia maji kila siku wakati wetu, mavazi ya watawa, kutofautisha vyakula na majivuno ya aina hiyo. Lakini wapinzani wetu wanaipindisha maana yake wanapohamisha, kwa njia ya ghiliba, kishirikishi cha ulimwengu wote hadi kuwa sehemu moja tu: “Vitu vyote vitakuwa safi mtakapokuwa mmetoa sadaka.” 284. Walakini Petro anasema kwamba, mioyo hutakaswa kwa imani.523 Uchunguzi wa fungu zima unaonyesha kwamba, unakubaliana na Maandiko mengine Matakatifu; kwa maana, ikiwa mioyo ni safi na kisha sadaka nje inaongezwa, (yaani, matendo yote ya upendo), basi, watu wote ni safi kabisa, siyo ndani tu, bali nje pia. Zaidi ya hayo, mbona mahubiri haya hayatolewi yote? Onyo dogo lina sehemu nyingi za makaripio, zingine zinaamuru imani na zingine zikiamuru matendo. Msomaji mwaminifu hatazichagua amri kuhusu matendo tu na kuziruka aya zinazohusu imani.
521 Kanuni kuu ya ufafanuzi wa Kilutheri wa Biblia: ‘Scriptura Sacra sui ipsius interpres,’ yaani, Maandiko Matakatifu yanajifafanua yenyewe.
522 Decr.Grat. 3. De consecr. d. 3. c. 20. Pseudo-Alexander I. 523 Mdo. 15: 9
285. Mwisho, tungependa kuwakumbusha wasomaji wetu kwamba, wapinzani wetu wanazishauri vibaya sana dhamiri za wacha Mungu wanapofundisha kwamba, matendo yanastahili msamaha wa dhambi. Sababu yake ni kwamba, dhamiri inayotafuta msamaha wa dhambi kwa njia ya matendo haiwezi kuwa na hakika kwamba, tendo lake litamridhisha Mungu. Dhamiri hiyo daima inasumbuliwa na inayabuni matendo mengine na huduma zingine na mwishowe hukata tamaa kabisa. Akiuelezea mchakato huu katika Rum. 4:14 na kuendelea, Paulo, anathibitisha kwamba, ahadi ya haki haitegemei matendo yetu kwa sababu tusingeweza kuwa na hakika kwamba, tuna Mungu mwenye rehema aliyeridhika kwa kuwa daima sheria inashutumu. Hivyo, ahadi haingekuwa na maana na ya hakika. Anahitimisha kwamba, siyo matendo bali imani inakubali msamaha wa dhambi na haki iliyoahidiwa. Kwa hakika, hili ndilo Paulo alimaanishalo hakika. Hili linatoa faraja kuu mno kwa dhamiri za waaminifu na huumulika utukufu wa Kristo, ambaye kwa hakika alitolewa kwetu ili, kwa ajili yake, tuwe na neema, haki na amani.
286. Mpaka hapa, tumechunguza mafungu maalumu ambayo wapinzani wetu huyarejelea dhidi yetu wakibisha kwamba, imani haihesabii haki, na kwamba, kwa matendo yetu, tunastahili kupata neema na msamaha wa dhambi. Tunatarajia kwamba, tumeonyesha kwa njia ya dhamiri za wacha Mungu kiasi cha kutosha kwamba, mafungu haya hayapingani na msimamo wetu. Wapinzani wetu huyapindisha Maandiko Matakatifu kwa nia mbaya ili yalingane na maoni yao wenyewe. Wanayanukuu mafungu mengi katika umbo la kupotosha. Wanaviruka vifungu vya Bibilia vilivyo dhahiri zaidi vinavyohusu imani. Badala yake, wanachagua vifungu vya Maandiko Matakatifu vinavyohusu matendo na hata wanayapotosha haya. Kila mahali wanayaongezea mawazo ya kibinadamu kwenye maneno ya Maandiko Matakatifu. Wanaifundisha sheria kwa namna inayoificha Injili ya Kristo. Tunatumaini kwamba, tumeyaonyesha yote haya kwa ajili ya kuzitosheleza dhamiri zinazomcha Mungu. 287. Mfumo mzima wa wapinzani wetu unatokana na akili ya kibinadamu au mafundisho ya sheria badala ya Injili. Wao hufundisha njia mbili za kuhesabiwa haki. Moja ambayo msingi wake ni sabau za kibinadamu na nyingine ambayo msingi wake ni sheria. Hakuna yoyote ambayo msingi wake ni Injili au ahadi ya Kristo.
288. Kulingana na wapinzani wetu, namna ya kwanza ya kuhesabiwa haki ni kwamba, wanadamu hustahili neema kwa matendo mema. Kwanza, kwa ajili ya stahili kwa kadiri ya matendo, na pili kwa ajili ya stahili ya hadhi.524 Namna hii
524 Stahili kwa kadiri ya matendo yenyewe – ‘meritum de congruo;’ stahili ya hadhi kwa ajili ya wema maalumu wa matendo – ‘meritum de condigno.’
ni mafundisho ya urazini. Unapokuwa hauoni uchafu wa moyo, ufahamu hudhani kwamba, unampendeza Mungu ukiwa unatenda mema. Lakini watu wanapokuwa katika hatari kuu, huongeza aina nyingine za ibada ili waepukane na vitisho vya dhamiri. Watu wa mataifa na Waisraeli waliwatoa dhabihu wanadamu na walijishughulisha na kazi za kuumiza mno ili kuituliza ghadhabu ya Mungu. Baadaye, watu waliyabuni madaraja ya watawa, ambayo yalishindana katika ukali wa kanuni za dini zao ili kuvipinga vitisho vya dhamiri na ghadhabu ya Mungu. Kwa kuwa aina hii ya kuhesabiwa haki ina maana na inajishughulisha na matendo ya nje, kwa kiasi fulani inaweza kueleweka na mahitaji yake yanaweza kutimizwa. Kwa sababu hii, wataalamu wa sheria za Kanisa walizipindisha kanuni za Kanisa la Kikristo. Hawakuelewa sababu zilizowafanya mababa kuzitunga. Siyo kwamba, tunatakiwa kutafuta haki kwa matendo haya, bali kwamba, kwa ajili ya utulivu wa jamii, utaratibu fulani unapaswa kuwepo katika Kanisa. Kwa njia hii ya kuhesabia haki, wamepotosha pia sakramenti, hasa Misa, ambayo kwayo wanajitafutia haki, neema, na wokovu kama tendo lenyewe.
289. Namna nyingine ya kuhesabiwa haki iliyotolewa na Wanatheologia Wanazuoni inafundisha kwamba, tunahesabiwa haki kwa njia ya tabia fulani ambayo imewekwa na Mungu, yaani, upendo.525 Kwa msaada wa tabia hii, tunaitii sheria ya Mungu kwa nje na kwa ndani. Utii wa sheria wa jinsi hiyo, unastahili neema na uzima wa milele. Bila shaka, haya ni mafundisho ya sheria. Inavyosema sheria ni kweli: “Nawe mpende BWANA, Mungu wako,” na “Bali umpende jirani yako kama nafsi yako . . .”526 Kwa hiyo, upendo ni utimizaji wa sheria.
290. Mkristo anaweza kuzitathmini namna zote mbili, kwa kuwa zote zinamwacha Kristo na kwa sababu hiyo, zote hazina budi kukataliwa kabisa. Namna ya kwanza isiyomcha Mungu ni dhahiri kwa sababu inafundisha kwamba, matendo yetu ni upatanisho wa dhambi. Namna ya pili ina madhara mengi ambayo ni hatari. Haitufundishi kujitolea wenyewe kwa Kristo katika kuzaliwa upya kwetu. Haifundishi kwamba, kuhesabiwa haki ni msamaha wa dhambi. Haifundishi kwamba, msamaha wa dhambi huutangulia upendo wetu, bali hudhania kwamba, tunalionyesha tendo la upendo ambalo kwalo tunastahili msamaha wa dhambi. Haifundishi kwamba, tunashinda vitisho vya dhambi na mauti kwa njia ya imani katika Kristo. Bila haki yoyote, inafundisha kwamba, wanadamu humjia Mungu kwa utimizaji wa sheria wao wenyewe bali siyo kwa njia ya Kristo, mpatanishi. Kisha inafikiri kwamba, utimizaji huu wa sheria
525 Kilatini: ‘Iusti simus per quendam habitum a Deo infusum, qui est dilectio.’ 526 Kum. 6: 5; Law. 19: 18
pamoja na Kristo, Mpatanishi, ni haki inayostahili neema na uzima wa milele, ingawa, kwa nadra, utimizaji wa sheria hata miongoni mwa watakatifu huwa dhaifu na mnyonge.
291. Mtu akitafakari kwamba, Injili haikutolewa ulimwenguni bure, kwamba, Kristo hakuahidiwa, hakufunuliwa, hakuzaliwa, hakuteswa, na hakuhuishwa bure, ataelewa kwa urahisi sana kwamba, hatuhesabiwi haki kwa njia ya sababu wala kwa njia ya sheria. Basi, hatuna budi kutofautiana na wapinzani wetu kuhusu kuhesabiwa haki. Injili huonyesha njia nyingine. Inatulazimisha kumtumia Kristo katika kuhesabiwa haki. Inatufundisha kwamba, kupitia Kristo, tuna njia ya kumfikia Mungu kwa njia ya imani.527 Inafundisha kwamba, tunapaswa kumweka Kristo, Mpatanishi na Mtulizaji, dhidi ya ghadhabu ya Mungu. Inafundisha kwamba, kwa njia ya imani katika Kristo tunapokea msamaha wa dhambi, upatanisho na ushindi juu ya vitisho vya dhambi na kifo. 292. Hivyo, Paulo anasema pia kwamba, haki haipatikani kwa njia ya sheria bali kwa njia ya ahadi, ambayo kwayo Baba ameutoa uhakikisho kwamba, anataka kusamehe na kupatanishwa nasi kwa ajili ya Kristo. Ahadi hii inapokelewa kwa njia ya imani tu,528 jinsi Paulo anavyoarifu katika Rum. 4:13. Imani peke yake ndiyo ipokeayo msamaha wa dhambi, ihesabiayo haki, na izaayo upya. Kisha, upendo na matendo mengine mema hufuatia. Kama tulivyotaja awali, tunafundisha kwamba, mtu anahesabiwa haki wakati, dhamiri yake inapotishwa kwa mahubiri ya toba, anajipa moyo na kuamini kwamba, ana Mungu mwenye rehema kwa ajili ya Kristo. 293. Imani hii inahesabiwa haki mbele za Mungu (Rum.. 4: 3, 5). Moyo unapohimizwa na kuhuishwa na imani kwa njia hii, unampokea Roho Mtakatifu. Kwa njia ya kufanywa upya naye, (Roho Mtakatifu) tunaweza kuitimiza sheria, kumpenda Mungu na Neno lake, kumtii Mungu katikati ya mateso, kuwa safi, kumpenda jirani n.k. Ingawa matendo haya yako mbali sana na ukamilifu wa sheria, yanampendeza Mungu kwa ajili ya imani yenye kuhalalisha kwamba, kwa ajili ya Kristo, tuna Mungu mwenye rehema aliyeridhika. Mambo haya ni wazi kabisa na yanapatana na Injili, na yeyote mwenye akili timamu anaweza kuyaelewa vizuri. 294. Kutokana na fungu hili la msingi, ni wazi kufahamu sababu inayotufanya tuihusishe haki na imani badala ya upendo, ingawa upendo huifuata imani kwa kuwa upendo ni utumizaji wa sheria. Paulo hufundisha kwamba, tunahesabiwa haki siyo kwa njia ya sheria bali kwa njia ya ahadi inayopokelewa kwa imani tu. Basi, hatuwezi kumwendea Mungu bila Kristo, Mpatanishi, wala hatupati msamaha wa dhambi kwa ajili ya upendo wetu bali kwa ajili ya Kristo. 295. Kamwe, hata hatuwezi kumpenda Mungu mwenye hasira; Daima, sheria
527 Rum. 5: 1-2
528 Kilatini: ‘Sola fide.’
hutushtaki na hivyo, hutuonyesha Mungu mwenye hasira. Kwa hiyo, hatuna budi kuishika kwanza ahadi kwa njia ya imani, kwamba, kwa ajili ya Kristo, Baba amepatanishwa nasi na anasamehe. Baadaye tunaanza kuitimiza sheria. 296. Tofauti kabisa na ufahamu wa mwanadamu, tofauti kabisa na Musa, inatulazimu tuelekeze macho yetu kwa Kristo na kuamini kwamba, alitolewa kwa ajili yetu ili kwa yeye tuhesabiwe haki. Hatuwezi kamwe kuiridhisha sheria katika mwili. Kwa hiyo, hatuhesabiwi haki kwa ajili ya sheria bali kwa ajili ya Kristo ambaye tunatunukiwa stahili zake tukimwamini. 297. Basi, kuna mambo mawili ya msingi, hatuhesabiwi haki kwa sheria - kwa sababu asili ya binadamu haiwezi kuitimiza sheria ya Mungu wala haiwezi kumpenda Mungu; na pili kwamba, tunahesabiwa haki kwa njia ya ahadi, ambayo kwayo tunaahidiwa upatanisho, haki, na uzima wa milele kwa ajili ya Kristo. Tunatakiwa kutafakari kwamba, Kristo hakuahidiwa, hakufunuliwa, kuzaliwa, kusulubiwa na kuhuishwa bure; Ahadi ya neema ya Kristo haikutolewa bure, pia kabla ya kutolewa kwa sheria na nje ya sheria tangu mwanzo wa ulimwengu. Ahadi hiyo inapaswa kupokelewa kwa njia ya imani, jinsi Waraka wa Yohana usemavyo: “Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. Naa huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.”529 Kristo anasema: “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.”530 Paulo anasema: “Ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii.” Anaongezea pia anaposema: “Kwa njia ya imani”531 Kwa hiyo, tunaipokea ahadi ya msamaha wa dhambi na haki kwa njia ya imani katika Kristo. Hatuhesabiwi haki mbele za Mungu ama kwa sababu au kwa njia ya sheria.
298. Mambo haya yako wazi kabisa na ya ushuhuda kwamba, tunashangaa kuwaona wapinzani wetu wakiyakataa kwa kelele. Uthibitisho532 ni dhahiri; kwa kuwa hatuhesabiwi haki mbele za Mungu kwa njia ya sheria ila tu kwa njia ya ahadi. Haki lazima ipatikane kwa njia ya imani. Je, ni hoja gani, ambayo mtu yeyote anaweza kuitoa dhidi ya udhibitisho huu, kama sio anataka kumpiga marufuku kabisa Kristo na Injili ? 299. Utukufu wa Kristo hung’aa pale tunapowafundisha watu kumtumia kama Mpatanishi na Mtulizaji wao. Katika mafundisho haya dhamiri za wacha Mungu huiona faraja kamili itolewayo kwao. Wanafundishwa
529 1 Yoh. 5: 10-12
530 Yn. 8: 36
531 Rum. 5: 2
532 Melanchthon anatumia neno la Kiyunani: ‘αποδειξις.’
kuamini na kuitegemea kweli ya hakika kwamba, wana Baba aliyepatanishwa nao kwa ajili ya Kristo, siyo kwa ajili ya haki zetu533 wenyewe, bali kwa sababu Kristo bado hutuwezesha kuitimiza sheria. 300. Wapinzani wetu huzipata baraka kama hizo kutoka kwa Kanisa wanapolaani na kujaribu kuharibu mafundisho kuhusu haki kwa njia ya imani. Kwa hiyo, acheni watu wote wema wajihadhari wasije wakasalimu amri kwa mashauri yao yasiyomcha Mungu. Mafundisho ya wapinzani wetu hayatuambii jinsi tunavyotakiwa kumtumia Kristo dhidi ya ghadhabu ya Mungu, kana kwamba wenyewe tungeweza kuishinda ghadhabu ya Mungu kwa njia ya upendo wetu au kwa kumpenda Mungu mweye hasira. 301. Juu ya mambo haya dhamiri zaimeachwa na mashaka. Iwapo zinatakiwa kuamini kwamba, zina Mungu mwenye rehema kwa kuwa zinapenda na kuitimiza sheria, itazibidi kutilia shaka kama zina Mungu mwenye rehema. Jinsi wapinzani wetu wanavyokubali, labda dhamiri hazihisi upendo huu kamwe, au zinahisi kwa hakika kwamba, upendo huo ni dhaifu sana. Mara nyingi sana wanaikasirikia hukumu ya Mungu, anayeitaabisha asili ya mwanadamu kwa maovu mabaya sana, mateso katika maisha haya na hofu kuu ya ghadhabu ya milele. Basi, ni lini dhamiri itatulia? Ni lini itapata amani? Ni lini itampenda Mungu katikati ya mashaka na vitisho hivi? Fundisho hili la sheria ni nini isipokuwa kukatisha tamaa? 302. Mwache mpinzani wetu yeyote ajitokeze kuuelezea upendo ambao kwao anampenda Mungu! Wapinzani wetu hawaelewi lolote wanalolizungumza. Wanalitamka neno “upendo” bila kulielewa, sawa sawa na mwangwi wa kuta za nyumba ufanyavyo. Jinsi mafundisho yao yalivyochanganyikiwa na kutoeleweka! Fundisho hili linamaanisha utukufu wa Kristo hadi kwa matendo ya wanadamu; Huziongoza dhamiri hadi kwenye kiburi au kwenye ukataji tamaa. 303. Tunatumaini kwamba, nafsi za wacha Mungu zitaelewa mafundisho yetu na kwamba, yataleta faraja ya uchaji na mabruki534 kwa dhamiri zilizotishiwa. Wapinzani wetu wanalikwepa suala muhimu kwamba, hata watu wengi waovu na mashetani pia huamini.535 Tumekwisha kusema mara nyingi kwamba, tunaizungumzia imani katika Kristo, yaani, imani katika msamaha wa dhambi, imani ambayo kweli na kwa moyo wote inaikubali ahadi ya neema. Imani hii haipatikani bila mapambano makali moyoni mwa wanadamu. Watu wenye busara wanaweza kutambua kwa urahisi kwamba, imani inayoamini kwamba, Mungu anatujali, anatusamehe, na kutusikia siyo ya dunia hii.536 Maana, nafsi ya binadamu yenyewe haiamini jambo kama hilo kuhusu Mungu. Kwa hiyo, waovu wala mashetani hawawezi kuwa na aina ya imani tunayoizungumzia hapa.
533 Yaani, matendo ya haki.
534 Kutoa afya na baraka, Kilatini: ‘Salubris.’
535 Yak. 2: 19
536 Juu ya asili, Kilatini: ‘Supra naturam.’
304. Mpotoshaji anaweza kulikwepa jambo muhimu hapa kwamba, haki imo katika hiari ya mtu na kwa sababu hiyo haiwezi kuhusishwa na imani, ambayo imo akilini. Jibu kwa wazo hili ni rahisi sana kwa kuwa hata Madaktari Wanazuoni hukubali kwamba, hiari ya mtu ndiyo inayoiamuru akili ilikubali Neno la Mungu.537 Tunaelezea wazi zaidi kwamba, vitisho vya dhambi na kifo haviwi mawazo katika akili tu, bali pia ni misukosuko mibaya ya hiari ya mtu inapokuwa inaikimbia hukumu ya Mungu. Vivyo hivyo, imani siyo tu maarifa akilini, bali pia ni tegemeo katika hiari ya mtu, yaani, kutamani na kupokea yale ambayo yanayotolewa na ahadi: Upatanisho na msamaha wa dhambi. Hivyo ndivyo Maandiko Matakatifu yanavyolitumia neno “imani,” kulingana na jinsi kauli hii ya Paulo inavyoonyesha: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na muwe na amani kwa Mungu.”538 305. Katika fungu hili, “kuhesabiwa haki,” kwa njia ya kimahakama,539 kunamaanisha “kumhukumu mtu kuwa hana hatia na kumtangazia kuwa mwenye haki, lakini kwa ajili ya haki ya kigeni,540 yaani, haki ya Kristo. Haki hii ya kigeni hupitishwa kwetu kwa njia ya imani.541 306. Kwa kuwa haki yetu katika fungu hili ni kuhesabiwa haki ya kigeni, inatubidi kuzungumzia hapa kuhusu haki kwa njia iliyo tofauti na uchunguzi ule wa kifalsafa au wa kimahakama wa haki ya mtu mwenyewe, ambayo kwa hakika inaishi katika hiari ya mtu. Paulo anasema: “Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi,” pia, “yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.”542 307. Basi, kwa kuwa haki ya Kristo inatolewa kwetu kwa njia ya imani, kwa hiyo, imani ni haki ndani yetu kwa njia ya kuhesabiwa haki.543 Ikimaanisha kwamba, kwa njia ya kuhesabiwa huko haki, tunakubaliwa na Mungu kwa ajili ya kuhesabiwa haki na sheria za Mungu, jinsi Paulo asemavyo: “Imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.”544 308. Tunalazimika kusema kwa ufundi545 kwa ajili ya wale wengine wanaogombania mambo madogomadogo: Hakika, imani ni haki kwa sababu ni utiifu kwa
Injili. Inajulikana kwamba, utiifu wa amri ya mkuu, bila shaka, ni aina ya haki inayomgawia kila mmoja chake.546 Matendo yetu mema au utiifu kwa sheria
537 Tomaso wa Akuino katika STh 2, 1.q.56 a. 3. c: ‘Nullus enim credit nisi volens’ – “Hakuna mtu anayeamini bila hiari.”
538 Rum. 5: 1
539 Kilatini: ‘Forensi consuetudine.’
540 Kilatini: ‘Aliena iustitia.’
541 Kilatini: ‘quae aliena iustitia communicatur nobis per fidem.’
542 1 Kor. 1: 30; 2 Kor. 5: 21
543 Kilatini: ‘Imputative.’
544 Rum. 4:5
545 Melanchthon, ‘Τεχνολογικως.’
546 Kilatini: ‘Species distributivae iustitiae.’
vinaweza kumpendeza Mungu tu kwasababu utiifu huu kwa Injili unamshikilia Kristo, Mpatanishi, na unaishughulikia haki. Kamwe hatuitoshelezi sheria, lakini kwa ajili ya Kristo tunasamehewa kwa hilo, jinsi Paulo asemavyo: “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.”547 309.Imani hii inamtukuza Mungu na inampa Mungu kinachomstahili. Kwa utiifu, inazikubali ahadi zake. Jinsi Paulo asemavyo katika Rum. 4:20: “Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu.” 310. Hivyo, λατρεια, yaani, ibada ya Injili, ni kuzipokea karama njema kutoka kwa Mungu, ilhali ibada ya sheria ni kumtolea na kumtunukia Mungu vitu vyetu. Hatuwezi kumtolea Mungu chochote mpaka kwanza tupatanishwe naye na tuzaliwe upya. Faraja iliyo kubwa sana inatokana na mafundisho haya kwamba, ibada kuu sana katika Injili ni hamu ya kupokea msamaha wa dhambi, neema, na haki kutoka kwa Mungu. Katika Yn 6:40 Kristo anasema yafuatayo kuhusu ibada hii: “Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele . . .” Na Baba anasema: “Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.”548 311. Wapinzani wetu huzungumzia utiifu kwa sheria; hawazungumzii utiifu kwa Injili. Hata hivyo, hatuwezi kuitii sheria mpaka tuwe tumezaliwa upya kwa njia ya Injili. Isitoshe, hatuwezi kumpenda Mungu mpaka tuwe tumeupokea msamaha wa dhambi. 312. Maadamu tunahisi kwamba Mungu anatukasirikia, asili ya mwanadamu huikimbia ghadhabu na hukumu yake. Mtu fulani anaweza kubishana kwamba, ikiwa ni imani inayokipenda kile kitolewacho na ahadi, basi, tabia za imani na tumaini zitaonekana kukanganywa, kwa sababu ni imani inayotarajia kukipokea kilichoahidiwa. Tunalijibu hili kwamba, kwa kweli, hisia hizi haziwezi kugawanywa jinsi zilivyo katika fikira zembe za Madaktari Wanazuoni. Katika Ebr. 11:1 imani imeelezewa kuwa “hakika ya mambo yatarajiwayo.” Hata hivyo, iwapo mtu anataka kuyatofautisha mambo, tunasema kwamba, lengo la tumaini ni tukio la siku zijazo, ilhali imani inajishughulisha na mambo ya siku zijazo na ya sasa na kwa sasa inapokea msamaha wa dhambi ambao hutolewa na ahadi.
313. Kutokana na hili, tunatumaini kwamba, hali ya imani itaeleweka dhahiri. Isitoshe, kuna sababu zinazotulazimisha kushikilia kwamba, tunahesabiwa haki, tunapatanishwa, na kuzaliwa upya kwa imani, iwapo kweli tunataka kufundisha haki ya Injili wala siyo haki ya sheria. Wale wanaofundisha kwamba, tunahesabiwa haki kwa upendo hufundisha haki ya sheria, hawatuelimishi kumtumia Kristo kama Mpatanishi wetu katika kuhesabiwa haki. 314. Ni dhahiri
547 Rum. 8: 1
548 Mt. 17: 5
kwamba, tunavishinda vitisho vya dhambi na kifo kwa imani na siyo kwa upendo. Sababu yake ni kwamba, hatuwezi kutumia upendo na utimizaji wetu wa sheria dhidi ya ghadhabu ya Mungu jinsi Paulo asemavyo katika Rum. 5: 2, “Ambaye kwa yeye (Kristo) tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii.”549
Tunaisisitiza kauli hii mara kwa mara kwa sababu iko wazi kabisa. Inaijumlisha hali yetu vyema kabisa na kuizingatia kwa kwa makini kutatufundisha mengi juu ya suala zima na kuleta faraja kwa nafsi zilizofadhiliwa. Kwa hiyo, inafaa sana kuwa nayo tayari na kuiweka akilini siyo tu kwa ajili ya kuyapinga mafundisho ya wapinzani wetu kwamba, tunamfikia Mungu kwa njia ya upendo na stahili bila Kristo, Mpatanishi, bali pia ili kujifurahisha wenyewe katikati ya vitisho na kuitumia imani yetu. 315. Pia ni wazi kwamba, bila msaada wa Kristo hatuwezi kuitimiza sheria, kama jinsi yeye mwenyewe asemavyo: “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”550 Hivyo, kabla ya kuitimiza sheria, lazima mioyo yetu iwe imezaliwa upya kwa imani.
316. Kutokana na hili, inaeleweka vizuri sababu yetu ya kuyakataa mafundisho ya wapinzani wetu kuhusu stahili ya hadhi551. Uamuzi huu ni rahisi. Kwanza, wapinzani wetu hawataji imani hata kidogo au ukweli kwamba, kwa ajili ya Kristo tunampendeza Mungu kwa njia ya imani. Badala yake, wao hudhania kwamba, matendo mema yakisaidiwa na “mamlaka” ya upendo ni haki ifaayo inayompendeza Mungu yenyewe na hustahili uzima wa milele bila haja ya Kristo, Mpatanishi wetu. 317. Je, hii ni nini kama siyo kuuhamisha utukufu wa Kristo kuwa matendo yetu, na uharibifu wa utukufu wake kama mpatanishi, iwapo tunataka kumpendeza Mungu kwa matendo yetu na wala siyo kwa ajili ya Kristo? Hii pia ni kumpokonya Kristo utukufu wake kama Mpatanishi. Yeye ni Mpatanishi daima wala hawi tu mwanzoni mwa kuhesabiwa haki. Pia Paulo anasema kwamba, iwapo mtu aliyehesabiwa haki katika Kristo lazima aitafute haki yake mahali pengine, atamfanya Kristo kuwa “mtumishi wa dhambi,” maana yeye hawezi kuhesabia haki kikamilifu.552 318. Ni upuuzi kabisa wapinzani wetu wanapofundisha kwamba, matendo mema hustahili neema kwa ajili ya hadhi, kana kwamba, dhamiri zetu zinapotutisha baada ya kuhesabiwa haki, jinsi zifanyavyo mara kwa mara, inatupasa tuitafute neema kwa njia ya tendo jema na siyo kwa njia ya imani katika Kristo.
319. Pili, mafundisho ya wapinzani wetu huziacha dhamiri zetu katika mashaka, ili zisiweze kutulizwa kamwe; Maana, sheria hutushtaki daima hata
549 Rum. 5: 2
550 Yn. 15: 5
551 Kilatini: ‘Meritum de condigno.’
552 Gal. 2: 17
katika matendo mema. Mwili siku zote hu hutamani ukishindana na Roho.553 Ni kwa njia gani dhamiri itapata amani pasipo imani ikiamini kwamba, inapaswa kumpendeza Mungu kwa tendo lake lenyewe, na wala siyo kwa ajili ya Kristo. 320. Je, italipata tendo gani ambalo italichukulia kwamba, linafaa uzima wa milele, iwapo hakika tumaini linapaswa kuhimiliwa kwa njia ya wema? Dhidi ya mashaka haya Paulo anasema: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu ”554 Inatupasa kuwa na hakika kabisa kwamba, tunapewa haki na uzima wa milele kwa ajili ya Kristo. Vile vile kuhusu Ibrahimu anasema: “Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa. ”555
321. Tatu, je, dhamiri itajuaje wakati tendo limefanyika chini ya ushawishi wa moyo huu wa upendo, ili iwe na hakika ya kustahili neema ya hadhi? Walakini tofauti hii kati ya ustahili wa watu kwa kadiri ya matendo yao556 na stahili ya hadhi umebuniwa tu ili kuyakwepa Maandiko Matakatifu. Maana, jinsi tumekwisha kusema hapo juu kwamba, lengo la mtendaji halitofautishi baina ya aina mbili za stahili. Wanafiki wajipendao huamini tu kwamba, matendo yao yanafaa vya kutosha kuweza kuwahesabia haki. Ilhali, dhamiri zenye kutishwa huwa na mashaka kuhusu matendo yao yote na kwa sababu hiyo, huendelea kutafuta matendo mengine mapya bila kukoma. Kuweza kupata stahili za hadhi kunamaanisha haya: Kuwa na mashaka na kutenda kazi bila imani hadi kufuatie kukata tamaa. Kwa kifupi ni kwamba: Mafundisho yote ya wapinzani wetu kuhusu suala hili yamejaa makosa na hatari.
322. Nne, Kanisa zima hukiri kwamba, uzima wa milele unapatikana kwa njia ya rehema. Akizungumzia kuhusu matendo yafanywayo na watakatifu baada ya kuhesabiwa haki, Agostino anasema yafuatayo katika kitabu chake “Neema na Hiari:”557 “Mungu hatuongozi sisi hadi katika uzima wa milele kwa stahili zetu, bali kwa njia ya rehema yake.” Isitoshe, Agostino anasema yafuatayo katika kitabu cha tisa cha “Maungamo”558 (9: 13): “Ole kwa maisha ya wanadamu hata kama ni yenye kusifiwa sana, iwapo yatahukumiwa bila rehema.” Katika fafanuzi za Sala ya Bwana Sipriano anasema: “Mtu asije akajipendekeza mwenyewe kwamba, yeye hana hatia na kwa njia ya kujivuna mwenyewe aangamie hata zaidi. Anaagizwa na kufundishwa kwamba, anatenda dhambi kila siku, maana anaagizwa kuomba kila siku kwa ajili ya dhambi zake.”559 323.
553 Gal. 5: 17
554 Rum. 5: 1
555 Rum. 4: 18
556 Kilatini: ‘Meritum de congruo.’
557 ‘De gratia et libero arbitrio’ 9, 21.
558 Confessiones.’
559 ‘De oratione dominica’ 22.
Suala hili linaeleweka vizuri na lina ushuhuda mwingi ulio wazi mno katika Maandiko Matakatifu na katika mababa wa kanisa, wanaohubiri kwa umoja kwamba, hata tukiwa na matendo mema, tutahitaji rehema katika matendo hayo. 324. Tukiitazama rehema hii, imani inatutia moyo na kutufariji. Wapinzani wetu wanafundisha vibaya wanapotukuza stahili kwa njia ambayo haiongezei chochote imani hii inayoshikilia rehema. Jinsi tulivyosema hapo juu ni kwamba, ahadi na imani vinawiana na kwamba, ni imani tu iwezayo kuishikilia ahadi. Hivyo, hapa tunasema kwamba, rehema iliyoahidiwa, inahitaji imani, na kwamba, ni imani tu iwezayo kuishikilia rehema hii. Hivyo basi, tunalikataa ipasavyo fundisho kuhusu stahili ya hadhi kwa kuwa halifundishi lolote kuhusu kuihesabia imani haki na kuficha utukufu na huduma ya Kristo, Mpatanishi? 325. Mtu yeyote asije akafikiri kwamba, tunafundisha jambo lolote jipya katika suala hili wakati mababa wa Kanisa wametoa fundisho hili kwa wazi kwamba, tunahitaji rehema hata katika matendo yetu mema.
326. Maandiko Matakatifu yanalisisitiza jambo hili mara nyingi. Zab. 143:2 inasema, “Wala usimhukumu mtumishi wako, maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.” Jambo hili linawanyima watu wote, hata watakatifu na watumishi wa Mungu, utukufu wowote katika haki ya mwanadamu iwapo Mungu hasamehei bali huhukumu na kulaani mioyo yao. Mahali pengine Mfalme Daudi anapojivunia haki yake, anazungumzia daawa560 yake dhidi ya watesi wa Neno la Mungu, wala siyo usafi wake mwenyewe. Anaomba akitetea kazi na utukufu wa Mungu, jinsi ilivyoandikwa katika Zab. 7:8 “BWANA, unihukumu mimi, kwa kadiri ya haki yangu, sawasawa na unyofu nilio nao.” Vivyo hivyo, katika Zab. 130: 3 anasema kuwa hakuna mtu atakayeweza kustahimili hukumu ya Mungu akichunguza dhambi zetu: “BWANA, kama wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama?” 327. Ayubu 9: 28: “Mimi huyaogopa matendo yangu yote561; kadhalika: “Ingawaje najiosha kwa maji ya theluji, na kuitakasa mikono yangu kwa sabuni; lakini utanitupa shimoni.”562 Mithali 20: 9: “Nani awezaye kusema, nimesafisha moyo wangu;563nimetakasika dhambi yangu? 328. 1 Yoh. 1: 8: “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Pia katika Sala ya Bwana watakatifu huomba msamaha wa dhambi. Hivyo, watakatifu wana dhambi pia. 329. Hes.14: 18: “. . . naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa . . .” Kum. 4: 24: “Kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, ni moto ulao.” Zek. 2: 13: “Nyamazeni, ninyi
560 Yaani, kesi, ajili.
561 ‘Union Version,’ (Huzuni zangu zote).
562 Yaani, shimoni mwa matope; aya za 30-31.
563 ‘Vulgata’: ‘Mundum est cor meum’; yaani, “moyo wangu ni safi.”
nyote wenye mwili, mbele za BWANA;” Isa. 40: 6-7: “Wote wenye mwili ni majani, na wema wake wote ni kama ua la kondeni; majani yakauka, au lanyauka; kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake.” 330. Katika (Yona 2: 8), Yona anasema: “Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo hujitenga na rehema zao wenyewe,” yaani, tegemeo lote ni ubatili isipokuwa tegemeo katika rehema. Rehema hutuokoa, lakini stahili na jitihada zetu havituokoi. Kwa hiyo, katika 331. Dan. 9: 18-19, Danieli anaomba ifuatavyo: “Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie;, fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi. Ee, Bwana, usikie; Ee Bwana, usamehe; Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako.” Hivyo, Danieli anatufundisha tuishike rehema tunapoomba, yaani, tunapokuwa mbele za Mungu tuitegemee rehema yake na siyo stahili zetu. 332. Tunashangaa wanachokifanya wapinzani wetu wanapoomba, ikiwa kweli watu hawa wa ulimwengu humwomba Mungu kitu chochote! Ikiwa wanatangaza kwamba, wanastahili kwa sababu wana upendo na matendo mema, na huidai neema, kana kwamba, waliistahili, basi, wanaomba sawa na alivyofanya Mfarisayo katika Luka 18: 11 akisema: “Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine.” Sala ya aina hiyo inayoitegemea haki yake yenyewe na siyo rehema ya Mungu, inamfedhehesha Kristo, anayetuombea kama Kuhani wetu Mkuu. 333. Hivyo, sala zetu zinategemea rehema za Mungu tunapoamini kwamba, ametusikia kwa ajili ya Kristo aliye Kuhani Mkuu, jinsi yeye mwenyewe asemavyo: “Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.”564 Anasema: “Kwa jina langu” kwa sababu hatuwezi kumkaribia Baba bila Kuhani huyu Mkuu.
334. Hapa, kauli ya Kristo kutoka Lk. 17: 10 inahusika pia: “Mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, sisi tu watumwa wasio na faida; ” Maneno haya yanasema wazi kwamba, Mungu huokoa kwa njia ya rehema na kutokana na ahadi yake, siyo kama deni analotuwia kwa ajili ya matendo yetu mema. 335. Katika hatua hii wapinzani wetu wanayachezea maneno ya Kristo kwa njia ya kushangaza sana. Wanabishana kwamba, ikiwa hatufai japo tumefanya kila kitu, tunapaswa kusema kwamba, hatufai japo tumeamini kila kitu. Kwanza, wao hufanya mazingaombwe,565yaani, kuyageuza maneno dhidi yetu. Wanasema kwamba, maneno yanapaswa kusema: ”Mtakapokwisha kuamini yote, semeni, sisi ni watumwa wasio na faida.” Halafu wao huongezea kwamba, matendo yetu hayana faida kwa Mungu, bali yanatuletea sisi faida. 336. Tazameni jinsi ujinga
564 Yn. 16: 23
565 Melanchthon: ‘αντιστρεφοω,’ yaani, ulinganisho wa pande mbili.
huu wa kitoto unavyowafurahisha wapinzani wetu! Ingawa mambo haya ya upuuzi hayastahili kukanushwa, hata hivyo, tutayajibu kwa kifupi. Hoja hii ya wapinzani wetu kuhusu αντιστρεφον ni yenye kasoro kabisa.
337. Kwanza, wapinzani wetu wanakosea sana kuhusu neno “imani.” Ikiwa lilimaanisha tu maarifa ya kihistoria ambayo hata waovu na mashetani pia wanayo,566 mabishano yao kwamba, imani haina maana ingekuwa sahihi wanaposema: “Mtakapokuwa mmeamini kila kitu, semeni, sisi tu watumwa wasio na faida.” Hata hivyo, sisi hatuzungumzii maarifa ya kihistoria, bali imani567 katika ahadi ya Mungu na rehema yake. Tegemeo hili katika ahadi hukiri kwamba, sisi ni watumwa wasiostahili. Hakika, ukiri huu kwamba, matendo yetu hayafai kitu, ni sauti yenyewe ya imani, jinsi inavyoshuhudiwa kutoka kwa mfano wa Danieli kama unavyotajwa hapo juu: “Maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, . . . ” n.k.568 338. Naam, imani huokoa kwa kuwa inaishika rehema na ahadi ya neema, ingawa matendo yetu hayana faida. Kwa maana hii, hatuhangaishwi na hoja569 hii: “Mtakapokuwa mmeamini kila kitu, semeni, sisi tu watumishi wasio na faida.” Maana matendo yetu hayana faida, na pamoja na Kanisa zima tunafundisha kwamba, tunaokolewa kwa njia ya rehema. 339. Kadhalika, wakitaka kurazinisha kwa njia ya tashbihi570 kutoka kwa kauli: “Utakapokwisha kuamini kila kitu, usitegemee matendo yako,” hadi kwa kauli: “Ukiisha kutegemea kila kitu, usitegemee ahadi ya Mungu.” Kauli hizi mbili haziambatani kwa kuwa ni tofauti mno. Sababu na madhumuni ya tegemeo katika kauli iliyotangulia ni tofauti kabisa na ya pili inayofuatia.571 Kwanza, tegemeo ni tegemeo katika matendo yetu wenyewe; ilhali pili, tegemeo ni tegemeo katika ahadi ya kimungu. Kristo hulaani tegemeo katika matendo yetu wenyewe, halaani tegemeo katika ahadi yake. Hataki tukate tamaa kuhusu neema na rehema ya Mungu. Anayashutumu matendo yetu kwamba hayana faida lakini hashutumu ahadi inayotoa rehema za bure. 340. Hapa, Ambrosio amesema wazi: “Neema itambuliwe bila kutojali asili.”572 341. Inatulazimu kutegemea ahadi ya neema, siyo asili yetu wenyewe. Lakini wapinzani wetu hupotosha kauli za imani zilizotolewa ili kuiunga imani mkono kama desturi. Lakini tunavirudishia vyuo vyao maswali haya magumu. 342. Porojo hizi ni
566 Yak. 2: 19
567 Kilatini: ‘Fiducia.’
568 Dan. 9: 18
569 Melanchthon, ‘αωτιστρεφον.’
570 Mlinganisho.
571 Kilatini: ‘Propositio prior – propositio posterior.’
572 Kilatini: ‘Agnoscenda est gratia, sed non ignoranda natura;’ ‘Expositio evangelii secundum Lucam’ 8, 52.
kukwepa jambo muhimu wanapoyafafanua maneno “watumwa wasio na faida” kumaanisha kwamba, matendo hayana faida mbele za Mungu bali yana faida kwetu sisi. Kristo anaizungumzia faida hiyo ambayo kwayo Mungu hujiwajibisha mwenyewe ili aidumishe neema yake, ingawa haifai hapa kuzungumzia lililo na faida na lisilo na faida. “Watumishi wasio na thamani” humaanisha “watumishi wasiotosheleza” kwa kuwa hakuna yeyote amwogopaye, ampendaye au amwaminiye Mungu jinsi impasavyo. 343. Tuyaacheni kabisa mapepe haya ya wapinzani wetu ambayo watu wenye ujuzi wanaweza kuyahukumu kwa urahisi yanapofunuliwa. Wanazamia pia kuuona mvunjiko katika maneno yaliyo wazi na dhahiri mno. Kila mtu anaweza kutambua kwamba, aya hii hulaani tegemeo katika matendo yetu wenyewe.
344. Kwa hiyo, tuacheni tuushike ukiri wa Kanisa kwamba, tunaokolewa kwa ajili ya rehema. Hapa mtu asifikiri: tukiokolewa kwa rehema kabla ya wokovu, “tumaini litakuwa lisilo na uhakika iwapo hakuna suala litakalowatofautisha wale waliookolewa na wale ambao hawajaokolewa”. Tunapaswa kulitoa jibu lifaalo kwa ajili ya hili. Kwa ajili ya suala hili, inaonekana kwamba, Madaktari Wanazuoni waliibuni neno “stahili ya hadhi.”573 Hili linaweza kuwa tatizo kubwa kwa akili ya mwanadamu. 345. Kwa hiyo, tutalijibu kwa kifupi. Kusudi tumaini liwe la hakika na ili tutofautishe baina ya wale waliookoka na wale wasiookoka, hatuna budi kukubali kwamba, tunaokolewa kwa njia ya rehema. Tukisema hivyo wazi bila udhibitisho, kauli hii itaonekana kuwa upuuzi. Maana, katika mahakama ya hukumu ya wanadamu haki au hatia ni vya hakika, wakati huruma haina uhakika. Lakini hukumu ya Mungu ni tofauti kabisa. Hapa, huruma ina ahadi na amri ya Mungu iliyo wazi na yenye hakika. Kusema kweli, Injili ni agizo la kutuaminisha kwamba, tuna Mungu mwenye rehema aliyeridhika kwa ajili ya Kristo: “Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi n.k ”574 346. Basi, kila tupozungumzia kuhusu huruma, lazima imani katika ahadi iongezewe hapo. Imani hii huzaa tumaini la hakika, maana inategemea Neno na Amri ya Mungu. Iwapo tumaini letu lingetegemea matendo, lingekuwa na mashaka kwa kuwa matendo hayawezi kuituliza dhamiri jinsi tulivyotaja mara nyingi hapo juu.
347. Imani hii hubainisha kati ya wale waliookolewa na wale wasioookolewa. Imani huleta tofauti kati ya watu wanaostahili na wasiostahili kwa sababu uzima wa milele umeahidiwa wao waliohesabiwa haki na ni imani inayohesabia haki.
348. Hapa, wapinzani wetu watasisitiza kwamba, matendo mema hayahitajiki
573 Kilatini: ‘Meritum condigni.’
574 Yn. 3: 17-18
kama hayastahili uzima wa milele. Tumekwisha kuupinga uzushi huu hapo awali. Bila shaka, matendo mema ni ya lazima. Tunasema kwamba, uzima wa milele umeahidiwa wale waliohesabiwa haki, lakini wale waishio kwa kuzifuata tamaa za miili, hawawezi kuipokea imani wala haki kamwe. Tunahesabiwa haki hasa kwa kusudi hili hili kwamba, tukiwa wenye haki, tutaweza kuanza kuyatenda matendo mema na kuitii Sheria ya Mungu. 349. Tumezaliwa upya na kumpokea Roho Mtakatifu ili maisha haya mapya yaweze kuzaa matendo mapya, misukumo mipya ya nafsi, yaani kumwogopa na kumpenda Mungu, na kuzichukia tamaa mbaya n.k. Imani tunayoizungumzia inapatikana katika toba. 350. Inapaswa kuimarika na kukua zaidi miongoni mwa matendo mema, majaribu, na hatari ili tuweze tuimarike zaidi katika kusadiki kwamba, Mungu anatujali, anatusamehe, na huyasikia maombi yetu kwa ajili ya Kristo. Hakuna yeyote ajifunzaye mambo haya bila mapambano mengi makali. Basi, ni mara ngapi dhamiri zetu zinatushtaki na kutukatisha tamaa kabisa zinapotukumbusha dhambi za zamani na mpya au uchafu wa asili yetu? Hati hii ya mashtaka575 haifutwi bila migongano mikali ambayo kwayo uzoefu hushuhudia jinsi imani ilivyo suala gumu.
351. Tunapoendelea kutiwa moyo na farajiwa katikati ya vitisho vikuu, misukumo mingine ya kiroho inaongezeka kama vile ufahamu wa Mungu, uchaji Mungu, tegemeo, na upendo wa Mungu. Hivyo, tumezaliwa upya jinsi Paulo asemavyo, “mkivaa utu mpya,” na “tukiurudisha utukufu wa Bwana... tunabadilishwa tufanane na mfano huo huo,”576; yaani, tunaupata ufahamu wa kweli wa Mungu unaotuwezesha kumcha kweli na kutumaini kwamba, anatulinda na kutusikia. 352. Kuzaliwa upya huku ni mwanzo wa uzima wa milele, jinsi Paulo asemavyo: “Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.”577 Tena: “Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.”578 353. Kutokana na kauli hizi, msomaji mwenye nia ya haki anaweza kuhukumu kwamba, tunayadai matendo mema kwa uzito kabisa, kwa sababu tunafundisha kwamba, imani hii hutokana na toba na inapaswa kukua daima katika toba. Hapa ndipo pana ukamilifu wa Kikristo na wa kiroho kwamba, toba na imani katikati ya toba hukua pamoja. Wacha Mungu wanaweza kuyaelewa haya mafundisho vizuri zaidi kuliko wanayoyafundisha wapinzani wetu kuhusu usufii579 au ukamilifu. 354.Jinsi ambavyo kuhesabiwa
575 Kol. 2: 14
576 Kol. 3: 10; 2 Kor. 3: 18
577 Rum. 8: 10
578 2 Kor. 5: 2-3
579 Kilatini: ‘Contemplatio,’ yaani, kutafakari sana, taamuli.
haki ni kwa imani, vivyo hivyo hata uzima wa milele ni wake. Jinsi Mt. Petro asemavyo: “Katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu.”580 Wapinzani wetu hukubali kwamba, wenye haki ni watoto wa Mungu na warithi pamoja na Kristo.581 355. Ndipo, baadaye matendo yanayompendeza Mungu kwa njia ya imani hustahilisha thawabu zingine za kimwili na kiroho. Kutakuwepo na tofauti katika utukufu wa watakatifu.
356. Hapa, wapinzani wetu husisitiza kwamba, uzima wa milele ni thawabu, na kwa hiyo hustahilishwa kwa stahili ya utu kwa njia ya matendo mema. Tutalijibu hili kwa kifupi na kwa wazi sana. Paulo anauita uzima wa milele “karama” (Rum. 6: 23) kwa sababu haki tuipokeayo kwa ajili ya Kristo wakati huo huo hutufanya wana wa Mungu na warithi pamoja na Kristo.582 Jinsi Yohana asemavyo: “Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele.”583 Agostino na waandishi wengi waliomfuata wanasema: “Mungu hutawaza karama zake ndani yetu.”584 Lakini mahali pengine imeandikwa: “Thawabu yenu ni kubwa mbinguni.”585 Iwapo kauli hizi zinaonekana kuwa na mgongano kwa wapinzani wetu, waacheni wazichunguze. 357. Lakini, kwa nadra sana, wao huwa mahakimu wenye haki kwa sababu wanaliacha neno “karama.” Pia wanakiacha kiini cha suala lenyewe. Badala yake, wao hulichagua neno “thawabu” na katika maelezo siyo tu wanakiuka Maandiko Mtakatifu bali hata matumizi ya lugha yenyewe. Wanaendelea kubishana kwamba, neno “thawabu” likitajwa, lazima matendo yetu yahesabiwe kuwa gharama ya uzima wa milele. Basi, kwa hiyo, matendo yanastahili neema na uzima wa milele bila kuhitaji rehema au Kristo, Mpatanishi au imani. Kwa kweli, upembuzi586 huu ni mpya kabisa. 358. Tunaisikia hili neno “thawabu;” hivyo, hatuhitaji Kristo, Mpatanishi wala imani inayotupeleka kwa Mungu kwa ajili ya Kristo, na siyo kwa ajili ya matendo yetu. Ni nani asiyetambua kwamba, hili ni hitimisho bila msingi587 wowote? 359. Hatubishani kuhusu neno “thawabu.” Tunalobishania ni suala hili: je, matendo yenyewe hustahili neema na uzima wa milele au yanampendeza Mungu tu kwa ajili ya imani peke yake inayomshikilia Kristo, Mpatanishi? 360. Wapinzani wetu hudhania kwamba, matendo hustahili neema na uzima wa milele. Wanaendelea kuchukulia kwamba, wao wana stahili za ziada ambazo wanaweza kuzitoa kwa
580 1 Pet. 1: 9
581 Rum. 8: 17
582 Rum. 8: 17
583 Yn. 3: 36
584 ‘De gratia et libero arbitrio’ 6, 9, 15.
585 Lk. 6: 23
586 Kilatini: ‘Dialectica.’
587 Melanchthon: ‘Ανακολοθον,’ yaani, uamuzi bila hoja zinazoweza kuuthibitisha.
wengine ili wapate kuhesabiwa haki, jinsi watawa wa kiume wanavyouza stahili za madaraja yao kwa wengine. Wanalifikia hitimisho la ajabu kwa mbinu ya Krisippo588 wanaposikia kutajwa kwa neno hili moja “thawabu.” Kwa hiyo, tuna matendo ambayo yana thamani ya kutosha kuweza kupata thawabu hiyo; Kwa hiyo, matendo yenyewe humpendeza Mungu, siyo kwa ajili ya Kristo, Mpatanishi. Kwa sababu mtu mmoja ana stahili zaidi kuliko mtu mwingine, hivyo, baadhi yao wana matendo yenye stahili za ziada. Watu wenye matendo yanayostahilli wanaweza kuwagawia wengine stahili zao. Msomaji mpendwa, jihadhari maana bado hujasikia hitimisho lote. 361. Inatubidi tuongezee madai589 fulani kuhusu utoaji huu, kama jinsi ambavyo joho la mtawa wa kiume linawekwa juu ya maiti n.k. Fadhili za Kristo na haki ya imani vinatiwa giza kwa mfululizo wa mabishano kama hayo ya stahili.
362. Sisi hatuyatoi mabishano ya maneno590 matupu kuhusu neno “thawabu.” Iwapo wapinzani wetu watakubali kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani kwa ajili ya Kristo na kwamba, matendo mema yanampendeza Mungu kwa ajili ya imani, basi hatungebishana sana kuhusu neno “thawabu.” Tunakubali kwamba, uzima wa milele ni thawabu kwa sababu ni jambo tunalowiwa kwa ajili ya ahadi, siyo kwa ajili ya stahili zetu. Tumeonyesha hapo juu kwamba, kuhesabiwa haki kumeahidiwa, na ni karama ya Mungu kabisa. Ahadi ya uzima wa milele imeongezewa kwa karama hii kulingana na maneno haya: “Na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.”591363. Maneno ya Paulo yanaleta maana ile ile: “Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile;” n.k.592 Wale waliohesabiwa haki wanawiwa taji kwa ajili ya ahadi. 364. Inawabidi watakatifu kuifahamu ahadi hii. Ahadi hii siyo kichocheo kwa faida yao wenyewe, bali wao wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Ili wasikate tamaa katikati ya mateso inawabidi kujua kwamba, ni mapenzi ya Mungu kuwasaidia, kuwaokoa na kuwanusuru. 365. Wenye nguvu husikia tangazo la adhabu na thawabu kwa njia moja na wanyonge kwa njia nyingine. Maana, wanyonge hutenda kazi kwa faida yao wenyewe. Hata hivyo, mahubiri ya thawabu na adhabu ni ya lazima. Mahubiri ya adhabu yanafungamana na toba kwa kuwa yanatangaza ghadhabu ya Mungu. Neema inafunuliwa katika
588 Krisippo alikuwa mwanafalsafa wa Skuli ya Stoa wakati wa karne ya tatu K.K. Krisippo ni mfano wa mtaalamu aliyekuwa hodari katika majadiliano lakini asiyeweza kufafanua kauli zake kwa njia ya maandiko hata kidogo.
589 Kilatini: ‘Sacramentum’: hapa, neno hili halimaanishi Ubatizo au Ekaristi, bali linamaanisha matendo fulani ya kaida za binadamu katika Kanisa.
590 Melanchthon, ’Λογομαχια.’
591 Rum. 8: 30
592 2 Tim. 4: 8
mahubiri ya thawabu. Maandiko Matakatifu yanapozungumzia matendo mema, mara nyingi yanahusisha imani, kwa kuwa hupenda kuihusisha haki ya moyo pamoja na matunda yake. Hali kadhalika, wakati mwingine Maandiko Matakatifu hutoa neema na thawabu nyinginezo, kama ilivyo katika Isa. 58: 8-9 na mara kwa mara katika aya zingine za manabii. 366. Tukubali pia, na tumeshuhudia mara nyingi kwamba, ingawa kuhesabiwa haki na uzima wa milele vinafungamana na imani, bado matendo mema hustahili thawabu zingine za kimwili na kiroho katika viwango tofauti tofauti jinsi inavyoandikwa: “Lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.”593 Haki ya Injili inayojishughulisha na ahadi ya neema, hupokea bure haki na uzima wa milele. Utimizaji wa sheria unaoifuata imani hujishughulisha na sheria, ambayo kwayo thawabu inatolewa na kuwiwa, siyo bure bali kwa ajili ya matendo yetu. Wale wanaostahili hili hutangulia kuhesabiwa haki kabla ya kuitimiza sheria. Kwa hiyo, kwanza, wanakuwa “wamehamishwa na kuingizwa katika ufalme wa Mwana wa pendo lake Mungu” jinsi Paulo asemavyo, “na warithio pamoja na Kristo.”594367. Lakini kila tunapojadili ustahili, wapinzani wetu huutumia mara moja kwa ajili ya haki na siyo kwa thawabu zingine. Ingawa Injili huitoa haki bure kwa ajili ya stahili za Kristo, na siyo zetu, stahili za Kristo hutolewa kwetu kwa imani. Matendo na mateso hayastahili kuhesabiwa haki ila thawabu zinginezo, jinsi thawabu hutolewa kwa njia ya matendo katika mafungu haya: “Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.”595 Hapa ni wazi kwamba, kiwango cha thawabu hupimwa kulingana na kiwango cha kazi. “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi.”596 368. Vile vile hapa, sheria huitoa thawabu kwa kazi fulani. Ingawa utimizaji hivyo wa sheria hustahili thawabu, kwa sababu thawabu hasa ni ya sheria, bado inatubidi kukumbuka kwamba, Injili inatoa kuhesabiwa haki bure kwa ajili ya Kristo. Hatuitimizi wala hatuwezi kabisa kuishika sheria kabla hatujapatanishwa na Mungu, hatujahesabiwa haki na hatujazaliwa upya. Utimizaji huu wa sheria haungempendeza Mungu mpaka tuwe tulikubalika kwa ajili ya imani. Kwa kuwa watu hukubaliwa kwa njia ya imani, mwanzo huu wa utimizaji wa sheria humpendeza Mungu na una thawabu yake katika maisha haya na ya baadaye. 369. Tungeweza kusema mengi zaidi kuhusu neno ‘thawabu’ kwa kulingana na asili ya sheria, lakini kwa kuwa kufanya hivyo kungechukua muda mrefu, tutaielezea mahali pengine kwa upana.
593 1 Kor. 3: 8
594 Kol. 1: 13; Rum. 8: 17
595 2 Kor. 9: 6
596 Kut. 20: 12
370. Wapinzani wetu wanahimiza sana kwamba, matendo mema hasa hustahili uzima wa milele, kwa sababu katika Rum. 2: 6 Paulo anasema: “Atamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.” Kadhalika: “Bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema.”597 Yn. 5: 29: “Wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima;” Mt. 25: 35: “Kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula,” n.k. 371. Aya hizi na zingine zote za namna hii ambapo kwazo matendo yanasifiwa katika Maandiko ni lazima zieleweke kwamba, hazimaanishi tu matendo ya nje bali hata imani ya moyoni. Maana, Maandiko Matakatifu hayazungumzii unafiki bali haki ya moyoni na matunda yake. 372. Kila mara sheria na matendo vinapotajwa, inatupasa kufahamu kwamba, Kristo, Mpatanishi, hapaswi kutengwa. Yeye ndiye mwisho wa sheria598 na yeye mwenyewe anasema: “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote”599 Kama tulivyotaja hapo awali,600mafungu yote yanayohusu matendo yanaweza kufafanuliwa kulingana na kanuni hii. Kwa hiyo, uzima wa milele unapotolewa kwa matendo, unatolewa kwa wale waliohesabiwa haki. Maana, wanadamu hawawezi kutenda matendo mema isipokuwa tu wale waliohesabiwa haki, na wanaoongozwa na Roho wa Kristo.601 Isitoshe, matendo mema hayawezi kumpendeza Mungu bila Kristo, Mpatanishi na imani, kwa kulingana na kifungu hiki: “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.”602Paulo anaposema: “Atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake,” inatupasa tuelewe kwamba, siyo matendo yanayoonekana tu bali ni kwa wenye haki au udhalimu wote. Yaani, “utukufu ni kwa kila mtu atendaye mema”,603 yaani, kwa ajili ya mtu mwenye haki. “Mkanipa chakula” - hili limetajwa hapa kama tunda na ushuhuda wa haki ya moyo na wa imani, na kwa hiyo, uzima wa milele unatolewa kwa haki. 374. Kwa njia hii hii, Maandiko
Matakatifu hujumlisha pamoja haki ya moyo na matunda yake. Mara nyingi, Maandiko Matakatifu hutaja matunda kusudi watu wasio na uzoefu wapate kuelewa wazi zaidi na pia kuonyesha kwamba, maisha mapya na kuzaliwa upya kunahitajika wala siyo unafiki. Basi, kuzaliwa upya kwa jinsi hiyo hutokea kwa njia ya imani katikati toba.
375. Hakuna mtu mwenye akili timamu awezaye kuhukumu vinginevyo. Hapa, hatutaki kuufuata upambanuzi wa hila katika kutofautisha kati ya haki ya moyo na matunda yake. Iwapo wapinzani wetu wangeweza kukubali kwamba,
597 Rum. 2: 10
598 Rum. 10: 4
599 Yn. 15: 5
600 Utetezi, Kuhesabiwa haki 255, 266, 314.
601 Rum. 8: 14
602 Ebr. 11: 6
603 Rum. 2: 10
matunda humpendeza Mungu kwa ajili ya imani na Kristo, Mpatanishi, lakini matunda yenyewe hayastahili kupata neema na uzima wa milele. 376. Hili ndilo tunalolilaani katika mafundisho ya wapinzani wetu kuwa wanapofasiri aya zile za Maandiko Matakatifu kwa njia ya kifalsafa au ya Kiyahudi wanaiondoa haki ya imani na Kristo, Mpatanishi. Kutokana na aya hizi, wao hutoa sababu kwamba, matendo haya hustahili neema, kulingana na wema wa ulinganifu au mengine hulingana na stahili ya utu, na kwamba, upendo utaongezewa hapo; Maana yake: kwa kuwa matendo huhesabia haki na kwa sababu haya ndiyo haki, yanastahili uzima wa milele. Uasi huu unaondoa wazi haki ya imani inayosadiki kwamba, tuna njia ya kumwendea Mungu kwa ajili ya Kristo na siyo kwa matendo yetu. Haki hii inasadiki kwamba, tunaongozwa hadi kwa Baba kwa njia ya Kuhani na Mpatanishi aliye Kristo na tuna Baba mwenye rehema aliyepatanishwa, kama tulivyosema vya kutosha hapo juu. 377. Mafundisho haya ya haki ya imani yasipuuzwe kamwe katika Kanisa la Kristo; kwa kuwa bila haya, huduma ya Kristo haiwezi kueleweka na mafundisho mengine ya kuhesabiwa haki ni mafundisho ya sheria peke yake. Hivyo, inatulazimu kuishika sana Injili na mafundisho ya ahadi iliyotolewa kwa ajili ya Kristo.
378. Basi, hatujadiliani hapa na wapinzani wetu kuhusu jambo lililo dogo. Hatujaribu kuwa wenye hila tunapowakaripia, hawa wanaofundisha kwamba, tunastahili uzima wa milele kwa matendo, wakiacha imani inayomshika Kristo, Mpatanishi. 379. Kuhusu imani hii inayoamini kwamba, tuna Baba mwenye rehema aliyeridhika kwa ajili ya Kristo, haipatikani kabisa silabi hata moja katika mafundisho ya Madaktari Wanazuoni. Wao hudhania kila pahali kwamba, tumekubalika na sisi ndio wenye haki kwa ajili ya matendo yetu, yawe yametendeka kwa akili au angalau kwa mhemuko wa upendo wanaozungumzia. 380. Hata hivyo, wamechukua baadhi ya misemo ya waandishi wa zamani kama maagizo ya kanuni,604 na wanaikengeusha kabisa kwa fafanuzi zao. 381. Wataalamu wanashikilia katika vyuo vyao kwamba, matendo mema humpendeza Mungu kwa ajili ya neema, na hivyo, yatupasa kuitegemea neema ya Mungu. Hapo wanafafanua neema kama hali ambayo kwayo tunampenda Mungu, kana kwamba, watu wa kale walimaanisha kwamba, sisi tunapaswa kuwa na ujasiri kwa kuutegemea upendo wetu, ambao tunajua, kutokana na uzoefu kuwa ni dhaifu na mchafu. Hata hivyo, ni jambo la kushangaza sana ambalo wanafundisha na wanatuamuru kuutegemea upendo ilihali wao hufundisha kwamba, hatuwezi kujua kwa hakika kama upendo upo.605 Basi, mbona hawadhihirishi hapa neema
604 Kilatini: ‘Apothegmata’; yaani, sentensi rasmi ya Sheria ya Kanuni.
605 Gabriel Biel, Sent. 2 d 27 q. un. a. 3 dub 5Q: “Ni vigumu zaidi kujua kuwa tuna upendo na kwa upande wa asili haiwezekani kabisa. Kwa hiyo, tukijua kwamba, tunampenda Mungu, hata hivyo, hatutaweza kujua wazi
na rehema ya Mungu kwetu sisi? Kila mara neema na rehema vinapotajwa inapaswa hapo kuongezea imani na rehema. Kwa kuwa ni kwa njia ya imani tu kwetu sisi tunaishika ahadi ya rehema, upatanisho na upendo wa Mungu. Iwapo waliyaelewa hivyo, wangekuwa sahihi waliposema kwamba, lazima tutegemee neema na kwamba, matendo mema yanampendeza Mungu kwa ajili ya Neema; maana imani huishikilia neema. 382. Madaktari Wanazuoni wanashikilia pia kwamba, matendo yetu mema yanakubaliwa kwa ajili ya nguvu ya mateso ya Kristo. Hivyo ndivyo ilivyo kabisa! Basi, mbona hawaiongezei imani? Yaani Kristo ni upatanisho kwa imani jinsi Paulo anavyosema.606 Mateso ya Kristo yametuletea faida wakati dhamiri zenye hofu zinafarijiwa kwa imani na zinaamini kwamba, dhambi zetu zimeondolewa kwa kifo cha Kristo na kuwa Mungu amepatanishwa nasi kwa sababu ya mateso ya Kristo. Ikiwa fundisho la imani limeachwa, ni bure kusema kwamba, matendo yetu yanakubaliwa kwa ajili ya mateso ya Kristo.
383. Wanatheologia Wanazuoni wanazipotosha sentensi fulani katika vyuo vyao vikuu hasa, kwa sababu hawafundishi haki ya imani. Wao huifafanua imani kama ujuzi wa kihistoria tu au wa mifumo ya imani,607wala siyo kama uwezo uishikao ahadi ya neema na haki, kwa nguvu zinazoufufua moyo ulio katikati ya hofu kuu za dhambi na mauti. Paulo anasema: “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” 608384. Hapa tunafikiria kwamba, wapinzani wetu watakubali kuwa tendo la kuungama tu haliwezi kuokoa au kuhesabia haki, bali linaokoa kwa ajili ya imani ya moyoni peke yake. Paulo anasema kwamba, kukiri kunaokoa ili kuonyesha ni imani ya namna gani inayopokea uzima wa milele, yaani, imani iliyo imara na inayofanya kazi.
385. Hakuna imani iliyo imara ambayo haijitokezi katika ukiri. Hivyo, matendo mengine mema humpendeza Mungu kwa ajili ya imani, jinsi maombi ya Kanisa yaombavyo kuwa mambo yote yakubaliwe kwa ajili ya Kristo na kuyaomba yote kwa ajili ya Kristo. Inajulikana wazi kwamba, kila sala humalizika kwa maneno haya: “Kwa ajili ya Kristo Bwana wetu.” 386. Kwa hiyo, tunahitimisha kwamba, tunahesabiwa haki mbele za Mungu, tunapatanishwa naye, na kuzaliwa upya kwa imani inayoishika ahadi ya neema kwa kutubu na kuihuisha nafsi yenye hofu kuu
hali yake. (‘Difficillimum autem est scire, se habere illam dilectionem. Et forte naturaliter impossibile. Quia et si scire possumus nos diligere Deum, non tamen evidenter scire possumus illam circumsantiam.’).
606 Rum. 3: 25
607 ‘Imani isiyokuwa na sura,’ ‘fides informis’ kupambana na ‘imani iliyoumbwa na upendo,’‘ides caritate fromata.’ Kulingana na falsafa ya Aristotele, kitu chenyewe ni ‘materia’ au yakinifu inayohitaji kuwa imeumbwa na ‘forma’ au sura, umbo, ili kiweze kulifuata na kulitimiza kusudi lake. Katika hali yakinifu kitu kiwe uwezekano tu, lakini kikipata umbo au sura yake, kitajitambulisha na kitafanikiwa.
608 Rum. 10: 10
hata kuaminishwa kwamba, Mungu anapatanishwa nasi na kutupendelea kwa ajili ya Kristo. Kwa njia ya imani hii, Petro anasema, “sisi tunalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata tupate wokovu ulio tayari kufunuliwa.”609387. Ufahamu wa imani hii ni wa lazima kwa Wakristo. Unaleta faraja tele katika adha zote na hutuonyesha huduma ya Kristo. Basi, wale wanaokataa kwamba, wanadamu huhesabiwa haki kwa imani, hukana kuwa Kristo ni Mpatanishi na Mtulizaji, na hukana ahadi ya rehema na Injili. Wao hufundisha ama mafundisho ya haki kwa njia ya akili au sheria.
388.Tumeonyesha hapa chanzo cha mgongano huu kadiri ya uwezo wetu na tumeyafafanua masuala yaliyokuwa vipingamizi kwa wapinzani wetu. Haya yatakuwa rahisi kwa watu wema kutathmini iwapo watakumbuka, wakati wowote kuhusu upendo au matendo zinaponukuliwa kwamba, sheria haiwezi kutimizwa bila Kristo na kwamba, hatuhesabiwi haki kwa sheria bali kwa njia ya Injili, iliyo ahadi ya rehema katika Kristo. 389. Ingawa mjadala huu ni mfupi, tunatumai kwamba, watu wema wataimarishwa katika imani, na dhamiri zao zitafundishwa na kufarijiwa. Tunajua kwamba, tuliyoyasema yanapatana na Maandiko ya manabii na mitume, ikiwa ni pamoja na yale ya mababa Watakatifu kama Ambrosio, Agostino na wengineo wengi pamoja na Kanisa zima la Kristo linalokiri bila shaka kwamba, Kristo ni Mpatanishi na Mtenda haki.
390. Tusidhanie moja kwa moja kwamba, Kanisa la Roma hukubali kila jambo ambalo Papa, au makadinali, au maaskofu, au baadhi ya wanatheologia na watawa wa kiume wanalikubali. Inajulikana wazi kwamba, Makuhani Wakuu610 wanajali zaidi mamlaka yao wenyewe kuliko Injili ya Kristo. Kila mmoja anajua kwamba, wengi wao ni wapenda anasa hadharani zaidi kama akina Epikuro.611 Pia ni dhahiri kwamba, wanatheologia wengi wamechanganya kupita kiasi falsafa na mafundisho ya Kikristo. 391. Mamlaka yao hayapaswi kuheshimiwa zaidi kiasi cha kutoweza kuafiki kamwe mabishano yote, hasa wakati makosa yao mengi ni ya wazi, kiasi cha kuweza kumpenda Mungu kuliko vitu vyote kwa nguvu za binadamu peke yake. Mfumo huu wa mafundisho umejaa makosa mengi ambayo ni uongo dhahiri. 392. Maandiko Matakatifu, mababa Watakatifu na hukumu ya waaminifu wote wanayapinga mafundisho haya kabisa. Kwa hiyo, ijapokuwa Makuhani Wakuu, au baadhi ya wanatheologia, na watawa wa kiume katika Kanisa wametufundisha tuutafute msamaha wa dhambi, rehema na haki
609 1 Pet. 1: 5
610 Kilatini: ‘Pontifex maximus.’
611 Kilatini: ‘Epicuraei.’ Epikuro (342 – 270 K.K.), mwanafalsafa Myunani aliyekataa kabisa kuwepo kwa miungu. Kwa sababu ya ukanaji wa Mungu alifundisha kwamba, shabaha ya maisha ya binadamu ni kutafuta starehe na anasa kwa njia hii au nyingine.
kwa njia ya matendo yetu na ibada mpya, ambazo zinazuia huduma za Kristo zisionekane na hivyo kumfanya Kristo kuwa mtunga sheria peke yake na siyo Mpatanishi na Mtenda haki. Hata hivyo, ufahamu wa Kristo, umebaki miongoni mwa baadhi ya waaminifu daima.
393. Licha ya hayo, Maandiko Matakatifu yalitabiri kwamba, kwa njia hii, mapokeo ya wanadamu na mafundisho ya matendo vitaficha haki ya imani. Jinsi Paulo anavyolalamika mara nyingi612 kwamba, hata wakati huo, baadhi ya waalimu walifundisha kwamba, badala ya haki ya imani, watu wanapatanishwa na Mungu na kuhesabiwa haki, kwa njia za matendo na ibada zao wenyewe na siyo kwa njia ya imani kwa ajili ya Kristo. Kwa njia ya asili, wanadamu huamua kwamba, Mungu anapaswa kuridhishwa kwa matendo. 394. Akili ya binadamu haioni haki nyingine isipokuwa haki ya sheria ambayo inaeleweka kama uadilifu wa kisheria. Kwa sababu hiyo, daima, walimu waliofundisha tu haki hii inayoonekana, wameendelea kuwepo hapa ulimwenguni, huku wakiitenga haki ya imani na madaktari wa namna hiyo watakuwepo daima. 395. Ilitokea hivyo pia miongoni mwa Taifa la Israeli. Waisraeli wengi zaidi walidhania kwamba, waliustahili msamaha wa dhambi kwa matendo yao. Kwa sababu hiyo,wakaongeza dhabihu na aina za ibada. Kinyume chake, manabii walilaani maoni haya na waliifundisha haki ya imani. Matokeo ya Taifa la Israeli ni mfano wa yale ambayo, yangetokea katika Kanisa la baadaye.
396. Kwa hiyo, nafsi za wacha Mungu zisisumbuliwe na umati wa wapinzani wetu wanaoyapinga mafundisho yetu. Ni rahisi sana kuzitathmini nafsi zao, kwa sababu, katika baadhi ya mafundisho yao, wameuhukumu ukweli ulio bayana na dhahiri kabisa ili uzushi/uovu uwe wazi. 397. Tangazo rasmi la Papa Leo wa Kumi613 limelaani fungu lililo muhimu mno ambalo Wakristo wote hawana budi kulishika na kuliamini. Yaani, Tunapaswa kusadiki kwamba, tumeondolewa dhambi siyo kwa ajili ya toba/majuto yetu bali kwa ajili ya Neno la Kristo, “Lo lote utakalolifunga” n.k.614398. Sasa, katika mkutano huu, waandishi wa Hoja615 wametulaani kwa maneno dhahiri kwamba, imani ni sehemu ya toba, ambayo kwayo, tunaupata msamaha wa dhambi, tunashinda vitisho vikuu vya dhambi na tunaipokea amani kwa ajili ya dhamiri yetu. Basi, ni nani asiyeona kwamba, fundisho hili la kuupokea msamaha wa dhambi kwa njia ya imani ni la kweli, hakika na muhimu mno kwa Wakristo wote? Vizazi vyote vya baadaye, vinaposikia kwamba, fundisho la jinsi hii lilihukumiwa, vitawezaje kuuona
612 Gal. 4: 9; 5:7; Kol. 2: 8, 16-17; 1 Tim. 4: 2-3
613 ‘Exsurge Domine.’
614 Mt. 16: 19
615 ‘Confutatio.’
ufahamu wowote wa Kristo katika watunga laana hii. 399. Mtu anaweza pia kuhukumu nafsi zao kutokana na ukatili usiosikika ambao unajulikana kwa kila mtu kuwa ulitendwa kwa watu wengi wacha Mungu. Tumesikia katika hii halmashauri ya dola616 kwamba, wakati maoni yalipokuwa yakitolewa kuhusu Ukiri wetu, mheshimiwa padre mmoja alisema kwamba, hakuna shauri lililoonekana kuwa bora kwake kuliko kuliandika jibu kwa damu dhidi ya ukiri wetu ulioandikwa kwa wino. Je, Phalaris617 angesema lipi ambalo lingekuwa katili kuliko hili? Kwa sababu hiyo, baadhi ya watawala waliyachukulia maelezo haya kama yasiyofaa kuzungumziwa katika mkutano wa namna hiyo wa kupinga maadili kabisa.
400. Ingawa wapinzani wetu hudai wenyewe kuwa ni Kanisa, hata hivyo, tunajua kwamba, Kanisa la Kristo linapatikana miongoni mwa wale waifundishao Injili ya Kristo, siyo wale wanaotetea maoni mapotovu yanayoipinga Injili, jinsi Bwana asemavyo: “Kondoo wangu waisikia sauti yangu.”618 Agostino anasema: “Swali ni, Kanisa liko wapi? Tutafanyaje basi? Je, tulitafute katika maneno yetu wenyewe au katika maneno yake aliye kichwa chake, yaani, Bwana wetu Yesu Kristo. Ninadhani kwamba, inatubidi kulitafuta katika maneno yake aliye ukweli na aufahamuye mwili wake vizuri kabisa.” 619 Hukumu za wapinzani wetu hazitatuhangaisha kwa maana wanayatetea maoni ya wanadamu yaliyo kinyume cha Injili, kinyume cha mamlaka ya kiroho ya mababa Watakatifu, na kinyume cha ushuhuda wa nafsi za wacha Mungu.
Fungu la Saba na Nane: Kanisa
1. Wapinzani wetu wanalilaani Fungu la Saba la Ukiri wetu tunaposema kwamba, Kanisa ni Ushirika wa Watakatifu. Wameongezea maneno mengi yanayosema kwamba, waovu wasitengwe na Kanisa kwa maana Yohana alilinganisha Kanisa na sakafu ya kupuria nafaka ambapo makapi na ngano hurundikwa pamoja,620na Kristo alilinganisha na wavu ambao ndani yake kuna samaki wazuri na wabaya n.k.621
2. Bila shaka, msemo usemao kwamba, hakuna dawa dhidi ya wazushi ni wa kweli kabisa. Hakuna lolote ambalo linaweza kusemwa kwa uwazi kiasi kwamba, lingeweza kuuepuka upotoshwaji. 3. Kwa sababu hiyo hiyo,
616 Kilatini: ‘Senatus imperii.’
617 Phalaris alikuwa mdhalimu mkali mno wa Akraga huko Sisilia mnamo mwaka wa 560 K.K.
618 Yn. 10: 27
619 Ep. ad cath. contra Donatistas (De unitate ecclesiae).
620 Mt. 3: 12
621 Mt. 13: 47
tuliliongezea Fungu la Nane, kusudi tuepukane na mawazo kwamba, tunabagua watu waovu na wanafiki kutoka katika ushirika wazi wa Kanisa, au kukataa ufanisi wa sakramenti inayohudumiwa na watu waovu au wanafiki.622 Hivyo, hatuhitaji kujitetea wenyewe kwa kirefu dhidi ya uzushi huu. Fungu la Nane linatosha kabisa kutuweka huru. Naam, tunakubali kwamba, katika maisha haya, wanafiki na watu waovu wamechangamana na Kanisa na ni washiriki wa Kanisa kulingana na ushirikiano wa alama za Kanisa unaoonekana. Yaani, neno, maungamo, na sakramenti, hasa kama hawajatengwa na Kanisa. Sakramenti hazipotezi ufanisi wake zinapotolewa na watu waovu. Kwa sababu hiyo, tunaweza kuzitumia sakramenti ambazo zinatunukiwa na watu waovu.623 4. Pia Paulo anatabiri kwamba, Mpinga Kristo “hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu,”624yaani, atatawala na kwamba, atakuwa na madaraka kanisani. 5. Hata hivyo, Kanisa siyo tu muungano wa ushirika unaoonekana na taratibu fulani za dini kama serikali zingine za kiraia, bali kimsingi ni muungano wa imani na wa Roho Mtakatifu mioyoni mwa watu. Ili uweze kujulikana, ushirika huu una alama zinazoonekana, yaani, mafundisho safi ya Injili, na utoaji wa sakramenti kulingana na Injili ya Kristo. Kanisa hili peke yake linaitwa mwili wa Kristo, ambalo Kristo hulihuisha, hulibariki na hulitawala kwa njia ya Roho Mtakatifu, jinsi Paulo ashuhudiavyo katika Efe. 1: 22-23 anaposema: “Akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” Hivyo, kwa wale ambao Kristo hafanyi kazi ndani yao siyo viungo vya Kristo. Wapinzani wetu pia huyakubali haya kwamba, waovu ni washiriki wafu 625katika Kanisa. 6. Kwa sababu hiyo, tunashangaa sana kwa nini wapinzani wetu wanayakosoa maelezo yetu yanayozungumzia juu ya washiriki hai wa Kanisa.
622 Jinsi Wadonatio walivyosadiki na kufanya Kaskazini mwa Afrika wakati wa karne ya tatu na nne.
623 Mapokezi ya sakramenti kutoka mikononi mwa wachungaji waovu yanatazamiwa hapa kutoka kwa upande wa Wakristo wa kawaida. Mchungaji mwovu akihudumia kulingana na utaratibu wa Kanisa, ataweza kuwahudumia Wakristo wa kawaida ili wasipoteze sakramenti. Kutoka upande wa Kanisa, jambo hili ni tofauti. Jinsi Melanchthon alivyorudia tena na tena kusema katika Utetezi huu, watu waovu ambao huendelea kuishi katika dhambi za mauti hawana imani ya kweli na Roho Mtakatifu. Kwa sababu hiyo, ni wajibu wa Kanisa kujitetea kwa njia ya kuwaweka chini ya marudi ili wapate nafasi ya kutubu kweli na dhambi zao zisienee katika Kanisa (1 Kor 5). Kwa hiyo, Melanchthon ameandika maneno haya: “Hasa kama hawakutengwa na Kanisa” (‘Presertim si non sint excommunicati’). Marudi, yaani, mamlaka ya funguo (Ukiri wa Augsburg 28) ni alama moja ya Kanisa la Kikristo. Siku hizi makanisa mengi yasiyotumia mamlaka ya funguo, yamejitetea kwa fungu hili la ‘Utetezi wa Augsburg’ bila kutofautisha baina ya haki ya Wakristo wa kawaida ya kuipokea sakramenti na wajibu wa Kanisa kutumia funguo zote mbili za mbinguni dhidi ya dhambi katika Kanisa, hasa miongoni mwa huduma yake.
624 2 The. 2: 4
625 Makapi; Mt. 3: 12
7. Hatujasema lolote jipya. Paulo analifafanua Kanisa kwa jinsi hiyo hiyo katika Efe. 5: 25-27, akisema kwamba lazima kususdi litakaswe ili liwe takatifu. Kadhalika, aliongezea alama zinazoonekana, yaani, Neno na sakramenti. Anasema: “Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na hila wala kinyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.” Tumeirudia kauli hii karibu kwa maneno yaleyale katika Ukiri wetu. Kadhalika, Fungu la Ukiri wa Mitume linafasili Kanisa kwa njia hii likitufundisha kuamini kuwa kuna Kanisa moja takatifu la ulimwenguni mwote.626 8. Bila shaka, waovu siyo Kanisa takatifu! Kifungu hiki, “Ushirika wa watakatifu” kinaonekana kuongezewa ili kifafanue Kanisa ni nini. Yaani, mkusanyiko wa watakatifu ambao hushiriki katika Injili au mafundisho na Roho Mtakatifu yule yule ambaye hufanya upya, hutakasa na hutawala mioyo yao.
9. Tunaliweka Fungu hili kwa sababu ya muhimu sana. Tunaziona hatari zisizopimika zinazotishia kuliangamiza Kanisa kabisa. Katika Kanisa lenyewe, kuna idadi isiyopimika ya watu wasiomcha Mungu na wanaolikandamiza; Hata hivyo, Kanisa litadumu ingawa tunajua kwamba, kuna kundi kubwa la waovu. Kristo atalipatia Kanisa karama zake ambazo ameziahidi, yaani, msamaha wa dhambi, kuyajibu maombi, na karama ya Roho Mtakatifu. Ukiri unatupatia faraja hizi ili tusikate tamaa bali tuweze kuyajua haya yote. 10. Unasema, “Kanisa Katoliki” – tusije tukauchukulia kuwa na maana ya serikali fulani ya mataifa inayoonekana. Badala yake, Unaundwa na watu waliotawanyika ulimwenguni kote ambao hukubaliana na Injili, na walio na Kristo, Roho Mtakatifu, na Sakramenti zile zile, iwe zina mapokeo yale yale ya kibinadamu au la. Ufafanuzi mmoja wa mifumo627 unasema kwamba, katika maana pana, Kanisa628 lina wacha Mungu na waovu. Basi, waovu ni kiungo cha Kanisa kwa jina tu na siyo kwa kweli, ilihali wacha Mungu ni kiungo cha Kanisa kwa kweli na kwa jina. 11. Mababa wa kanisa, wanalisema hilo hilo katika maeneo mengi. Kwa mfano, Hieronimo anasema: “Mkosaji aliyechafuliwa na dhambi yoyote hawezi kuitwa kiungo cha Kanisa wala hawezi kuitwa mfuasi wa Kristo.”629
12. Hata hivyo, wanafiki na watu waovu wanahusishwa na kanisa la kweli kwa kadiri ya taratibu za nje. Lazima kulifasili Kanisa kuwa lile ambalo ni mwili hai wa Kristo, yaani, Kanisa kwa jina na uhakika wake. 13. Lazima tuelewe vizuri ni jambo gani hasa linalotufanya, kuwa viungo na, washiriki hai wa Kanisa. Ikiwa
626 Kilatini: “. . . sit sancta catholica ecclesia;” Kanisa Takatifu na la Katoliki.
627 Mfumo, ‘decretum,’ ufafanuzi, ‘glossa.’ Decr. Grat. II. C. 33. q. 3. d. L. De poen. C. 70.
628 Kilatini: ‘Ecclesia large dicta,’ au, ‘ecclesia quandoque large sumitur.’
629 Hieronimo bandia, siye Hieronimo mwenyewe, Pseudo-Hieron. Ep ad Eph 5:24
tukilifasili Kanisa kuwa kama shirika la nje tu la watu wema na waovu, watu hawangeelewa kwamba, Ufalme wa Kristo ni haki ya moyo na karama ya Roho Mtakatifu. Badala yake, wangefikiri kwamba, Kanisa ni pahali pa kuzifuata taratibu za nje za ibada fulani na desturi za kidini. 14. Basi, kutakuwa na tofauti gani kati ya Taifa la Torati630 na Kanisa kama Kanisa likiwa tu shirika la nje? Basi, Paulo hutofautisha kati ya Kanisa na Taifa la Agano la Kale, kuwa Kanisa ni taifa la kiroho, lisilotengwa na wapagani kwa taratibu za kiraia, bali kwamba, kweli ni Taifa la Mungu, lililozaliwa upya na Roho Mtakatifu. Naam, Watu wa Agano la Kale, wale waliozaliwa kwa mwili walikuwa na ahadi kuhusu mambo ya kimwili, mambo ya kisiasa n.k. pamoja na ahadi kuhusu Kristo. Kwa sababu ya ahadi hizi, hata wale walio waovu miongoni mwao waliitwa Watu wa Mungu, kwa sababu Mungu aliutenganisha uzao huu wa kimwili kutoka kwa mataifa mengine kwa njia ya maagizo ya nje na ahadi kadhaa. Hata hivyo, watu hawa waovu hawakumpendeza Mungu. 15. Lakini Injili haileti kivuli cha mambo ya milele, bali mambo ya milele yenyewe, yaani, Roho Mtakatifu na haki631 ambayo kwayo tunahesabiwa haki mbele za Mungu.
16. Kwa hiyo, kulingana na Injili watu hao, kwa kweli, ni Taifa la Mungu linaloipokea ahadi ya Roho Mtakatifu. Licha ya hayo, Kanisa ni Ufalme wa Kristo kinyume na Ufalme wa Ibilisi. Ni kweli kabisa kwamba, walio waovu wamo katika utawala wa Ibilisi na ni washiriki wa Ufalme wa Ibilisi, jinsi Paulo anavyofundisha katika Efe. 2: 2 anaposema kuwa Ibilisi, “ni yule atendaye kazi sasa katika wana wa uasi.” Kristo aliwaambia Mafarisayo waliokuwa na ushirika wa nje na Kanisa, yaani, pamoja na watakatifu katika Taifa la Torati, kwa maana walishika nyadhifa za juu, walitoa dhabihu na kufundisha: “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi.”632 Hivyo, kusema kweli, Kanisa ambalo kweli ni Ufalme wa Kristo, ni ushirika wa watakatifu. Waovu wanatawaliwa na Ibilisi na ni mateka wake; Hawatawaliwi na Roho wa Kristo.
17. Je, kwanini tuhitaji maneno zaidi katika jambo lililo wazi? Iwapo Kanisa ambalo ni ufalme wa kweli wa Kristo umetofautishwa na Ufalme wa Ibilisi, ni lazima tufuate kuwa watu waovu ni wa Ufalme wa Ibilisi, siyo wa Kanisa. Kwa sababu, Ufalme wa Kristo bado haujafunuliwa, bado hao wamechangamana na Kanisa633 na wanashika huduma za Kanisa. 18. Watu waovu hawamo katika Ufalme wa Kristo ikiwa ufalme huu bado haujafunuliwa. Daima sehemu ile aihuishaye kwa Roho wake ni Ufalme wa Kristo, iwe imefunuliwa au imefichwa
630 Agano la Kale.
631 Ebr. 10: 1
632 Yn. 8: 44
633 Kilatini: ‘Sint admixti ecclesiae.’
chini ya msalaba, sawa na Kristo alivyo yule yule, awe ametukuzwa sasa au aliteswa awali. Mifano ya Kristo ianakubaliana na hili. 19.Katika Mt. 13: 38 anasema wazi kuwa: “Zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu.” Anasema, shamba ni ulimwengu na siyo Kanisa. Hivyo, Yohana anazungumzia juu ya taifa zima la Wayahudi na kusema kwamba, Kanisa la kweli litatenganishwa na taifa lile.634 Kwa hiyo, aya hii inapingana na wapinzani wetu kuliko kuwatetea kwani inaonyesha kwamba, watu wa kweli na wa kiroho watatengwa na watu wa kimwili. Kristo pia anazungumzia juu ya aina ya Kanisa anaposema kwamba, ufalme wa Mungu ni kama wavu, au sawa na wanawali kumi.635 Anatufundisha kwamba, Kanisa limefichwa chini ya kundi la watu waovu ili kikwazo hiki kisije kikawaumiza wacha Mungu nasi tupate kuelewa kwamba, Neno na sakramenti vina nguvu hata pale waovu wanapovisimamia. Wakati huo huo, yeye hufundisha kwamba, ijapokuwa watu hawa waovu hushiriki alama za nje, bado wao siyo wa ufalme wa kweli wa Kristo na viungo vyake, maana wao ni viungo vya Ufalme wa Ibilisi.
20. Pia sisi hatuoti ndoto juu ya Serikali ya Platoni,636jinsi wengine wanavyodai kwa njia ya kukufuru, bali tunaelezea kwamba, ndani ya Kanisa hili hupatikana, linafanywa na waumini wa kweli, watu wenye haki waliotawanyika ulimwenguni pote. Pia tunaongezea alama zake, yaani, mafundisho safi ya Injili na sakramenti. Kwa hakika, Kanisa hili linaitwa “nguzo ya ukweli”637kwa maana huitunza Injili safi, kwa kile Paulo anakiita , “msingi,”638yaani, ufahamu kweli wa Kristo na imani. Hata hivyo, pia kuna watu dhaifu ndani yake ambao hujenga katika msingi huu kwa mabua, yaani, mawazo yasiyo na faida. Kwa kuwa mawazo haya hayawezi kuupindua msingi, watu hawa wanasamehewa au hata kurekebishwa. 21. Maandiko ya Mababa Watakatifu yanashuhudia pia kwamba, mara nyingine hata wao walijenga kwa mabua juu ya msingi, lakini hiyo haikubatilisha imani yao. Lakini mambo mengi ambayo wapinzani wetu wanayatetea, yanaibatilisha imani, kama wanavyolaani mafundisho kuhusu msamaha wa dhambi. tunavyoeleza kwamba, msamaha wa dhambi hupokelewa kwa imani. Pia ni na uovu wa wazi wapinzani wetu wanapofundisha kwamba, watu hustahili msamaha wa dhambi kutokana na upendo wao kwa Mungu kabla ya neema. Kadhalika, hii inamaanisha kuuondoa msingi, yaani, Kristo. Vilevile, kwa kusudi gani imani inahitajika iwapo sakramenti kama matendo yenyewe zinatufanya wenye haki bila mwelekeo mwema wa yule anayezitumia? 22.
634 Yaani, Yohana Mbatizaji katika Mt. 3: 12
635 Mt. 13: 47, Mt. 25: 1
636 Kitabu maarufu cha Platoni ( 427 - 347 K.K.)
637 1 Tim. 3: 15
638 1 Kor. 3: 12
Kanisa lina ahadi kwamba, daima litakuwa na Roho Mtakatifu. Pia lina maonyo kwamba, kutakuwepo na walimu wasiomcha Mungu na mbwa mwitu. Lakini kwa kweli Kanisa ni lile ambalo lina Roho Mtakatifu. Ingawa mbwa mwitu na walimu wasiomcha Mungu walisumbua Kanisa sana, kwa kweli, wao siyo Ufalme wa Kristo. Ndivyo Lyra639 anavyoshuhudia anaposema: “Kanisa halikuundwa na watu kwa ajili ya mamlaka au cheo chao Kanisani au ulimwenguni, kwa sababu watawala wengi na makuhani wakuu, kadhalika wengine walio chini, wameasika. Kwa hiyo, Kanisa linaundwa na watu walio na ufahamu kweli fika na ukiri wa imani na ukweli.” Ni lipi lingine tulilolisema katika ukiri wetu ambalo ni tofauti anayoyasema hapa Lyra?
23. Labda wapinzani wetu wanadai kwamba, Kanisa ni kama ufalme wa nje upatikanao ulimwenguni pote ambamo hata Kuhani Mkuu wa Roma lazima awe na mamlaka yasiyokuwa na kikomo.640bila kumwajibikia mtu yeyote. Kwa sababu hiyo, ana mamlaka ya kuthibitisha mafungu ya imani, kutangua maandiko kwa ruhusa yake, kuanzisha ibada na kafara. Hali kadhalika, kutoa sheria apendavyo, kutoa kibali kutoka sheria zote, ziwe za kimungu, au za serikali au za kanuni sawasawa na matakwa yake. Kaisari na wafalme wote hupokea mamlaka na uwezo wa kutawala kwa amri ya Kristo, kwa kuwa kama Mungu Baba alivyompa Kristo kila kitu, hivyo, sasa hatuna budi kuelewa kwamba, haki hiyo imekabidhiwa kwa Papa. Hivyo, Papa lazima awe bwana wa ulimwengu wote na falme zote za dunia, na mambo yote ya binafsi au rasmi. Lazima awe na mamlaka kamili katika mambo ya ulimwengu na ya kiroho na panga mbili za roho na dunia. 24. Sasa, fasili hii ni fasili ya ufalme wa Kuhani Mkuu wa Roma na siyo wa Kanisa la Kristo. Imetungwa siyo na wataalamu wa Sheria ya Kanuni peke yake, bali na Kitabu cha Danieli (Dan. 11: 36-39).641
25. Iwapo tungefasili Kanisa kwa njia hiyo, labda tungeweza kuwa mahakimu waadilifu. Naam, maandiko mengi yametolewa ambayo yameandikwa kwa mtindo mpotovu na wa kukufuru kuhusu mamlaka ya Kuhani Mkuu wa Roma ambayo hakuna mtu aliyewahi kuhukumiwa. Sisi pekee tunalaumiwa kwa kuwa tunaihubiri fadhili ya Kristo ambayo kwayo tunaupokea msamaha wa dhambi kwa njia ya imani katika yeye na siyo kwa njia ya ibada alizozibuni huyo kuhani mkuu. 26 Licha ya haya, Kristo, manabii na mitume hulifasili Kanisa kwa njia tofauti kabisa kuliko utawala wa Upapa. 27. Wala yasinenwe kuhusu ukuhani huu yale yanayohusu Kanisa la kweli, kwamba, li nguzo ya imani na kwamba
639 Nikolao wa Lyra (mnamo 1270 - 1349) kuhusu Mt. 16: 10
640 Melanchthon anatumia Kiyunani ‘ανυπευθυνον.’
641 Hapa Melanchthon anatumia kejeli: Dan. 11: 36-39 ni mafungu muhimu ya Agano la Kale kuhusu mafundisho kuhusu Mpinga Kristo.
hawakosei. Wangapi kati yao hujali lolote kuhusu Injili au wanaona kuwa inafaa kusomwa? Wale walio wengi hudhihaki dini zote waziwazi, au iwapo hulikubali lolote lile, hulikubali lile linalokubaliana na akili ya kibinadamu na kuchukulia mengine kama hadithi, sawa na michezo ya watunga mashairi.
28. Kwa sababu hiyo, sisi tunasisitiza kulingana na Maandiko Matakatifu kwamba, katika maana halisi,642 Kanisa ni ushirika wa watakatifu ambao kweli wanaiamini Injili ya Kristo na wenye Roho Mtakatifu. Hata hivyo, tunakubali kwamba, wanafiki na watu waovu wengi ambao wamechangamana nao katika maisha haya hushiriki pamoja katika alama za nje. Nao ni washiriki wa Kanisa kulingana na jumuia hii ya alama za nje. Hivyo basi, wana huduma Kanisani. Sakramenti hazipotezi nguvu zao zinapotolewa na watu wasiostahili, kwa maana hawawakilishi nafsi zao zenyewe bali Kristo, kwa ajili ya wito wa Kanisa, kama Kristo anavyoshuhudia: “Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi.”643 Wanapolitoa Neno la Kristo au sakramenti, wanafanya hivyo kwa niaba ya Kristo na badala yake. Sauti ya Kristo inatufundisha hili kusudi tusikwazwe na wachungaji wasiostahili.
29. Tumelielezea suala hili kwa uwazi wakutosha katika ukiri wetu kwamba, hatukubaliani na Wadonatio na wafuasi wa Wycliffe ambao huamini kwamba, watu hutenda dhambi wanapopokea sakramenti kutoka kwa watu wasiostahili Kanisani.644 Kwa sasa, hili linaonekana kutosha kutetea maelezo yetu kuhusu Kanisa. Hatuoni pia jinsi linavyoweza huelezwa kwa namna tofauti kuliko maelezo yetu kwa maana Kanisa linaitwa mwili wa Kristo. Ni wazi kwamba, watendao maovu ni wa ufalme na mwili wa Ibilisi awaendeshae na kuwashika mateka. Haya yote ni dhahiri kabisa kama jua la alasiri; Basi, iwapo wapinzani wetu bado wataendelea hukota uzushi, tutakuwa tayari kuwajibu tena kwa undani. 30. Kadhalika, wapinzani wetu hulaani sehemu ya Fungu la Saba lisemalo: “Kwa umoja na ukweli wa Kanisa, inatosha kukubaliana kuhusu mafundisho ya Injili na utunzaji wa sakramenti. Siyo lazima mapokeo ya kibinadamu, matendo ya dini, na ibada zinazoanzishwa na watu zifanane kokote.” Hapa wao hutofautisha baina ya ibada za kokote na ibada maalumu hata kukubali fungu letu kwa tafsiri ya ibada maalumu. Lakini tukimaanisha ibada za kokote, hawatakubali. 31. Tuna shida sana kuelewa shabaha ya wapinzani wetu. Sisi huzungumzia kuhusu umoja wa kweli, yaani, ule wa kiroho. Bila umoja huo hapawezi kuwa na imani wala haki moyoni mbele za Mungu. Kwa ajili ya umoja huu, tunasema, siyo
642 Kilatini: ‘Ecclesia proprie dicta.’
643 Lk. 10 : 16
644 ‘Ukiri wa Augsburg’ 7, hata hivyo, hakuna neno kuhusu wafuasi wa John Wyckliffe.
lazima kuwa na usawa wa taratibu za ibada za kibinadamu, ziwe zile za kokote au maalumu kwa kuwa haki kwa njia ya imani haifungamani na desturi fulani, kama haki ya sheria ilivyofungamana na ibada za Musa, kwa sababu haki ya moyoni ni jambo ambalo huhuisha moyo. Mapokeo ya kibinadamu yawe yale ya kokote au maalumu, hayajengi lolote, wala hayazaliwi na Roho Mtakatifu, kama ilivyo usafi, uvumilivu, hofu ya Mungu, kuwapenda majirani, na matendo ya upendo.
32. Kwa kweli, tulikuwa na sababu nzito za kulitunga fungu hili, kwa maana ni wazi kwamba, mawazo mengi mapumbavu kuhusu mapokeo yamejipenyeza ndani ya kanisa. Baadhi ya Wakristo wanafikiri kwamba, mapokeo ya wanadamu ni ibada za lazima ili kuhesabiwa haki. Halafu wanajadiliana ni kwa sababu gani ilitokea kwamba, Mungu huabudiwa kwa njia nyingi sana, kana kwamba, matendo haya yalikuwa ya ibada za kweli badala ya kupaswa kuwa maagizo tu ya nje na ya kisiasa. Yasiyohusiana hata kidogo na haki ya moyo au kumwabudu Mungu. Kwa sababu nzuri na halali hutofautiana kulingana na hali au kwa njia moja au nyingine. Vilevile, baadhi ya makanisa yameyatenga makanisa mengine kwa sababu ya desturi za namna hiyo, kama zile za maadhimisho ya Pasaka, matumizi ya sanamu, na mengineyo mengi.645 Kutokana na sababu hiyo, wale wasiokuwa na ufahamu mzuri wamehitimisha kwamba, imani au haki ya moyoni haiwezi kupatikana mbele za Mungu bila maadhimisho haya. Juu ya suala hili, kuna vitabu vingi viovu kuhusu ungamo la dhambi646 na mengineyo.
33. Kutokana na kwamba, tofauti kati ya mida ya usiku na mchana haziwezi kuudhuru umoja wa Kanisa, hivyo tunaamini kwamba, namna mbalimbali za ibada zilizoanzishwa na wanadamu haziwezi kuudhuru umoja wa kweli wa Kanisa, ingawa inatupendeza kwamba, ibada za kokote zihifadhiwe kwa ajili ya amani. Hivyo, katika makanisa yetu, sisi pia tumehifadhi kwa hiari utaratibu wa misa, Siku ya Bwana, na sikukuu zingine muhimu. Tumeyachukua maagizo ya kale kwa moyo wa shukrani mno, hasa yale yaliyo na nidhamu inayotumika kuelimisha na kufundisha watu wasio na uzoefu. 34. Sasa hatujadiliani iwapo inatubidi kuyahifadhi maagizo haya kwa ajili ya amani au ya faida ya kimwili. Masuala mengine kabisa yanajadiliwa. Basi, inahojiwa iwapo ufuasi wa mapokeo ya wanadamu ni ibada inayohitajika kwa ajili ya kuhesabiwa haki mbele za
645 Mwisho wa karne ya pili B.K., Kanisa la Roma lilitenga Kanisa la Asia kwa sababu Wakristo wa Asia waliifuata tarehe ya Kiyahudi badala ya kalenda ya Roma kuhusu wakati wa Pasaka. Mwaka wa 769 Sinodi ya Laterano ililaani Sinodi ya Konstantinnopoli (754) kwa sababu ya ugomvi wa wapinzani wetu wa sanamu takatifu au ‘ikoni’ Katika mwaka wa 1054 Papa wa Roma alililaani Kanisa la Byzantio. 646 Vitabu vya wanatheologia waliotunga mashauri ya ulaghai kuhusu njia ya kuungama dhambi mbele ya kasisi, kama kitabu cha Raimundo wa Pennaforte katika karne ya kumi na mbili ‘Summa de casibus conscientiae.’
Mungu. Jambo hili ni hoja kuu647 katika mjadala huu. Baada ya hoja hiyo, ndipo itawezekana kuamuliwa iwapo ni lazima mapokeo ya wanadamu yafanane kokote kwa umoja wa kweli wa Kanisa. Ikiwa mapokeo ya wanadamu siyo ibada za lazima kwa ajili ya kuhesabiwa haki mbele za Mungu, basi, inafuatia kwamba, watu wanaweza kuwa wenye haki na watoto wa Mungu hata kama hawayashiki mapokeo yaliyokuwa yamepokelewa mahali pengine. Mavazi ya mtindo wa Kijerumani yasipokuwa ibada ya lazima kwa ajili ya kuhesabiwa haki mbele za Mungu, basi wanadamu wanaweza kuwa wenye haki na kuwa watoto wa Mungu na kuwa kweli Kanisa la Kristo hata kama labda wangevalia sawa katika mtindo wa Kifaransa na siyo wa Kijerumani.
35. Paulo anafundisha kuhusu mambo haya wazi katika Kol. 2: 16-17 anaposema: “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au Sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.” Vilevile: “Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani? Msishike, msionje, msiguse; (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe.”648 36. Maana yake: Haki ya moyoni ni jambo la kiroho linalohuisha mioyo yetu. Inajulikana wazi kwamba, mapokeo ya wanadamu hayahuishi mioyo, na siyo matokeo ya Roho Mtakatifu kama vile upendo kwa majirani, usafi wa kimwili n.k. Matokeo ya namna hiyo siyo vyombo ambavyo kwavyo Mungu huiwezesha mioyo kuamini (ambavyo ni Neno na sakramenti zilizoanzishwa na Mungu) bali ni matumizi ya mambo yasiyohusu mioyo na “huangamia zinapotumika.” Hivyo, tusidhani kwamba, ni za lazima kwa shabaha ya kuhesabiwa haki mbele za Mungu. Paulo pia anasema vivyo hivyo katika Rum.14: 17: “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.”
37. Lakini siyo lazima kutaja shuhuda nyingi kwa kuwa ziko wazi popote katika Maandiko Matakatifu na tulizikusanya nyingi zaidi katika mafungu ya mwisho ya ukiri wetu. Hatuna budi tuibue tena na kujadili kwa ukamilifu zaidi hoja kuu649 ya mjadala huu huko mbele, yaani, kama mapokeo ya wanadamu ni ibada zinazohitajika ili kuhesabiwa haki mbele za Mungu. Tutajadiliana kuhusu jambo hilo kwa undani.
647 Melanchthon, ‘κρινομενον,’ yaani, kauli ya kuonyesha kiini cha mjadala. 648 Aya za 20-23. 649 ‘Κρινομενον.’
38. Wapinzani wetu husema kwamba, mapokeo ya kokote lazima yafuatwe kwa kuwa yanadhaniwa kuwa yalitoka kwa mitume wenyewe. Ole wenu, ninyi watu wa dini! Wanataka kuyahifadhi mapokeo yaliyopokelewa kutoka kwa mitume na siyo mafundisho yao! 39. Inatubidi kuyapima mapokeo hayo sawa na jinsi mitume wenyewe walivyofanya katika maandiko yao. Mitume hawakutaka tuamini kwamba, tunahesabiwa haki kwa taratibu za namna hiyo au kwamba, taratibu hizi ni za lazima kwa njia ya haki mbele za Mungu. Mitume hawakutaka kuibebesha dhamiri mzigo kama huo, Hawakutaka kuiunganisha haki na dhambi pamoja na maadhimisho ya siku, vyakula, na mengineyo. 40. Kinyume chake, Paulo anayaita maoni kama haya kuwa “mafundisho ya mashetani.” Kwa sababu hiyo, ili kujua matakwa na nia ya mitume inatubidi kuyachunguza maandiko yao na siyo, haitoshi tu kuurejea mfano wao. Walifuata siku fulani, siyo kwa sababu ufuasi huu ulikuwa wa lazima kwa ajili ya kuhesabiwa haki bali kuwajulisha watu wakati wa kukusanyika. Walifuata pia taratibu nyingine za ibada walipokutana, kama utaratibu wa masomo. Mara kwa mara, watu walizishika desturi fulani za Mababa650 ambazo mitume walizibadilisha kwa mujibu wa historia ya Injili, kwa mfano Pasaka na Pentekoste. Walifanya hivyo ili kuziendeleza kumbukumbu za matukio makuu mno kwa mifano pia na siyo kwa mafundisho peke yake, hata kwa ajili ya vizazi vya baadaye. 41. Lakini kama mapokeo haya yangekuwa ya lazima kwa ajili ya kuhesabiwa haki, basi, mbona maaskofu waliyabadilisha mengi yao baadaye? Kama yalikuwa mambo ya haki ya kimungu, 651haingeruhusiwa kuyabadilisha kwa mamlaka ya wanadamu.
42. Kabla ya Sinodi ya Nikea, Pasaka ilisherehekewa na watu fulani nyakati fulani, lakini tofauti hii haikudhuru imani. Baadaye ilipangwa kwamba, Pasaka yetu isisadifu wakati wa Pasaka ya Wayahudi ingawa mitume waliyaamuru makanisa kuiadhimisha Pasaka na ndugu ambao walikuwa wameongoka kutoka Uyahudi. Kwa sababu hiyo, baada ya Sinodi ya Nikea, mataifa kadhaa yalishikilia desturi hii na kuifuata kalenda ya Kiyahudi.652 Lakini kama maneno ya amri hii yanavyoonyesha, mitume hawakutaka kuweka amri juu ya makanisa
650 Yaani, akina baba Wayahudi.
651 Kilatini: ‘Iure divino.’
652 Kanisa la Zamani lilishuhudia mabishano mengi kuhusu wakati wa Pasaka: 1. ‘Quartodesimani,’ Wakristo wa zamani hasa katika maeneo ya Asia Ndogo waliofuata kalenda ya Wayahudi na kuiadhimisha Pasaka tarehe 14 mwezi wa Nisan (Melito wa Sardis, Apollinario wa Hierapolis, Polikarpo wa Smyrna, Ireneo). Askofu Viktor wa Roma aliyatenga makanisa ya ‘Quartodesimani’ ya Asia na Kanisa la Roma kwa ajili ya tofauti kuhusu tarehe ya Pasaka katika mwisho wa karne ya pili. 2. Tofauti baina ya Kanisa la Antiokia na Aleksandria katika kuuhesabu mwezi wa Pasaka. Kanisa la Antiokia lilifuata kalenda ya Wayahudi kwa maana Aleksandria iliweka mwezi wa Pasaka kuwa baada ya siku mlingano ya majira ya kuchipua. Sinodi ya Nikea ilikubali kalenda ya Aleksandria katika mwaka wa 325. Vikundi vingine vilitoroka Kanisa kwa sababu ya uamuzi huo kama lile la Audiani na Protopaschites. Baadaye, mabishano kuhusu tarehe ya Pasaka yaliendelea mpaka Enzi ya Kati.
kwa maana kwamba, waliwakataza watu kujali iwapo ndugu zao walikosea kuhesabu muda kwa usahihi waliposherehekea Pasaka. Epifanio653 alihifadhi maneno ya amri hii: “Msihesabu nyakati, bali sherehekeeni pamoja na ndugu zenu wa tohara, sherehekeeni wakati huo huo pamoja nao, maana ingawa wamekosea, msifadhaishwe.” Epifanio aliandika kwamba, maneno haya ni yale ya mitume yaliyoandikwa katika agizo lao kuhusu Pasaka. Basi, kutokana nayo, msomaji mwenye busara anaweza kuona kwa urahisi kwamba, mitume walitaka kuuondolea umma maoni ya upuuzi kuwa kuzingatia muda ni jambo la lazima, walipowakataza kufadhaika ingawa watu wangekosea kuhesabu kwa usahihi. 43.Kulikuwako na wengine huko Mashariki walioitwa Waaudiano654 kutoka kwa mwanzilishi wa mafundisho yao; Walisisitiza kuwa ni lazima Pasaka isherehekewe pamoja na Wayahudi kwa sababu ya maagizo haya ya mitume. Ili kuwakanusha, Epifanio aliyatukuza maagizo na kusema kuwa hakuna lolote lililokuwa kinyume cha imani au kanuni ya Kanisa. Aliwakosoa Waaudiana kwa sababu ya kutoelewa msemo huu.655 Alifafanua sawa na tufanyavyo: Mitume hawakukusudia kurejelea wakati ambapo Pasaka ilipasawa kusherehekewa, bali, kwa ajili ya mwafaka, walitaka wengine wote wafuate mfano wa ndugu mashuhuri ambao walikuwa wameongoka kutoka katika dini ya Kiyahudi na kuhifadhi desturi zao. 44. Mitume walimwonya msomaji kwa busara kwamba, asiuharibu uhuru wa kiinjili, wala asiilazimishe dhamiri; maana waliongezea kwamba, msomaji asijali hata kama atakosea kuhesabu nyakati kwa ukamilifu.
45. Mifano mingi ya namna hiyo inaweza kukusanywa kutoka katika historia mbalimbali. Kulinagana na hii, inaonyesha wazi kwamba, tofauti ya ufuasi wa taratibu ya wanadamu haidhuru umoja wa imani. Lakini kwa sababu gani tujadiliane? Wapinzani wetu hawaelewi hata kidogo, haki ya imani ni ipi na ufalme wa Kristo ni upi, iwapo wataamua kwamba, ulinganifu katika vyakula, siku, mavazi na mambo kama haya ni ya lazima, bila amri ya Mungu. Lakini angalieni wapinzani wetu walivyo watu wa dini kabisa!656 46. Kwa ajili ya umoja wa Kanisa, wanahitaji ulinganifu katika ufuasi wa taratibu za kibinadamu ijapokuwa wao wenyewe wamelibadilisha agizo la Kristo kuhusu matumizi ya Chakula cha Bwana, ambayo,hapo awali, yalikuwa matumizi ya kokote. Lakini iwapo maagizo ya ulimwengu wote ni ya lazima, basi, kwa nini walilibadilisha agizo kuhusu Chakula cha Kristo, ambalo silo agizo la kibinadamu bali la 653 Epifanio wa Salamis (mnamo 315-403) katika kitabu chake kiitwacho, ‘Panairion,’ yaani, ‘Ukanushaji wa Nyasi Zote,’ 70, 10: ‘Υμεις
654 Kilatini: ‘Audiani.’
655 Melanchthon: ‘το ρητον.’
656 Kilatini: ‘Hominus religiosus,’ lugha ya kejeli.
kimungu? Lakini baadaye itatubidi kuzungumzia mjadala huu mzima.
47. Wamekubali Fungu la Nane zima ambapo tunakiri kwamba, wanafiki na watu waovu wamechanganyikana na Kanisa na kwamba, sakramenti zina nguvu ingawa zinatunzwa na makasisi waovu, kwa maana wachungaji hufanya kazi kwa niaba ya Kristo. Hawawakilishi nafsi zao wenyewe, kwa mujibu wa maneno haya: “Awasikilizaye ninyi anisikiza mimi.”65748. Lazima walimu waovu wakataliwe kwa sababu, kamwe, hawafanyi kazi kwa niaba ya Kristo, bali ni Wapinga Kristo658 Yesu anasema: “Jihadharini na manabii wa uongo”659 Kadhalika Paulo anasema: “Mtu awaye yote akiwahubiri ninyi Injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.”660
49. Aghalabu, Kristo ametuonya katika mifano yake kuhusu Kanisa661 kwamba, tusichukizwe na uovu binafsi wa makasisi au umma hata tufanye mafarakano kama Wadonatio walivyofanya kwa uovu. 50.Lakini tunawachukulia kama wachochezi kabisa waliofanya mafarakano kwa sababu waliwanyima makasisi haki ya kumiliki mali na rasilimali. Haki ya kumiliki mali ni utaratibu wa kiraia. Wakristo wanapaswa kuzitumia taratibu za kiraia jinsi watumiavyo hewa, mwanga, chakula na kinywaji. Kwani kama vile ulimwengu wote na mienendo thabiti ya nyota, kwa hakika, ni utaratibu wa Mungu na hata huhifadhiwa na Mungu mwenyewe, vivyo hivyo, muundo halisi wa jamii ni utaratibu wa kweli wa Mungu na huhifadhiwa na kutetewa na Mungu mwenyewe dhidi ya Ibilisi.
Fungu la Tisa: Ubatizo
1. Fungu la Tisa limekubaliwa. Katika fungu hili tunakiri kwamba, Ubatizo ni wa lazima kwa wokovu. Kwa hiyo, watoto wabatizwe na zaidi kwamba, Ubatizo wa watoto siyo wa bure bali ni wa lazima na ufaao kwa wokovu. 2. Kwa kuwa, Injili inafundishwa miongoni mwetu kwa utakatifu na kwa bidii, tumepokea pia tunda hili la Injili kwa baraka ya Mungu, kwamba, hakuna Waanabaptisti wapatikanao katika makanisa yetu. Watu wetu wameandaliwa kwa Neno la Mungu kujihami dhidi ya kikundi hiki cha kukufuru na chochezi cha hawa wanyang’anyi. Tunapoyalaani maasi mengi ya Waanabapisti tunaulaani pia uasi huu kwamba, Ubatizo wa watoto hauna maana. Ni hakika kabisa kwamba, ahadi ya wokovu inawahusu hata watoto wachanga. Lakini haiwahusu wale walio nje
657 Lk. 10: 16. Hapa, ‘Utetezi wa Augsburg’ unafundisha wazi kwamba, huduma ya uchungaji inamwakilisha
Kristo mwenyewe.
658 Kilatini: ‘Antichristi.’
659 Mt. 7 : 15
660 Gal. 1 : 9
661 Mt. 13 : 24-30, 36-44, 47-50
ya Kanisa la Kristo, ambako hakuna Neno wala sakramenti kwa sababu Kristo huzaa upya kwa Neno na sakramenti. Kwa hiyo, kuwabatiza watoto wachanga ni lazima kwa sababu ahadi ya wokovu inawahusu wao pia kulingana na agizo hili la Kristo: “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.”662 Jinsi wokovu unavyotolewa kwa watu wote, ndivyo Ubatizo unavyotolewa kwa wanaume, wanawake, vijana na watoto wachanga wote. Basi, ni wazi kwamba, inawapasa watoto wachanga wabatizwe kwa sababu wokovu unatolewa kwa njia ya Ubatizo.
3. Pili, inajulikana wazi kwamba, Mungu anaukubali Ubatizo wa watoto wachanga. Kwa hiyo, Waanabaptisti wanakukufuru sana wanapolaani Ubatizo wa watoto wachanga. Kuwa Mungu anakubali Ubatizo wa watoto wachanga, inaonyeshwa hapa na ukweli kwamba Mungu huwapa Roho Mtakatifu wale waliobatizwa kwa njia hii. Basi, Ubatizo huu ukiwa hauna maana, Roho Mtakatifu hangekuwa ametolewa kwa yeyote. Hakuna ambaye angeokolewa, na mwishowe, hakuna Kanisa ambalo lingekuwepo. Sababu hizi peke yake zinatosha kuthibitisha nafsi bora za wacha Mungu dhidi ya maoni ya kukufuru na ya kilokole ya Waanabaptisti.
Fungu la Kumi: Chakula Kitakatifu
1. Fungu la Kumi linakubaliwa tunapokiri maoni yetu kwamba, mwili na damu ya Kristo vipo kweli katika Chakula cha Bwana na kwa uthabiti663 na vinatolewa pamoja na vitu vinavyoonekana, yaani, mkate na mvinyo, kwa wale wanaopokea sakramenti. Baada ya kuchunguza kwa makini na kuelezea wazi; tunautetea msimamo huu kwa ukakamavu. Maana, Paulo anasema kwamba, mkate ni “kushiriki mwili wa Kristo,” n.k. Kwa ajili ya haya, mkate hautakuwa ushirika katika mwili wa Kristo bali katika roho yake tu, ikiwa mwili kweli wa Bwana haupo. 2. Tunajua kwamba, siyo tu Kanisa la Roma linalokiri uwepo wa mwili wa Kristo, bali Kanisa la Kiyunani pia linakiri hivyo tangu zamani na hata wakati huo. Kanuni yao ya misa ni ushahidi wa hili, ambapo kasisi huomba wazi kwamba, mkate ubadilishwe na uwe mwili wa kweli wa Kristo.664 Kadhalika, Mwanatheologia kutoka Bulgaria,665ambaye huonekana kwetu kuwa mwandishi hodari, anasema dhahiri kwamba, mkate sio tamathali666 tu bali unabadilika kuwa
662 Mt. 28 : 19
663 Kilatini: ‘Vere et substantialiter.’
664 Liturgia ya Yohana Krisostomo (mnamo 347-407 B.K.): ‘Ufanye mkate huu kuwa mwili wa thamani wa Kristo wako.’
665 Theofilakto, mtaalamu Myunani wa Biblia na mfuasi wa Yohana Krisostomo, tangu mwaka wa 1078, Askofu Mkuu wa Akhrida katika maeneo ya Wabulgari.
666 Mfano, taswira.
mwili kweli. 3. Ufafanuzi mrefu wa Kirillo667 unapatikana katika Yohana sura ya 15 ambapo anafundisha kwamba, Kristo hutolewa kwetu kama mwili katika Chakula Kitakatifu. Anasema: “Hatukatai kwamba, tunaunganishwa na Kristo kwa njia ya roho kwa imani ya kweli na upendo mnyofu. Lakini tunakataa kabisa kuwa hatuunganishwi naye kwa njia ya mwili. Tunasema kwamba, jambo hili ni kinyume kabisa na Maandiko Mtakatifu. Nani aliye na mashaka kwamba, Kristo ni mzabibu na sisi ni matawi kweli yawezayo kujipatia uzima kutoka kwake? Msikilize Paulo asemavyo: “Sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo”668 kwani “Sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.”669 Au mwingine anafikiriaje kwamba, labda hatusikii matokeo ya baraka hii ya fumbo? Kwa kuwa yamo ndani yetu, basi, usharika huu uliotolewa na mwili wa Kristo unakuwaje kwamba, Kristo hukaa ndani yetu?” Baadaye kidogo Kirillo anasema: “Kwa sababu hiyo inatubidi kufikiri kwamba, Kristo yumo ndani yetu, siyo tu katika hali ya nafsi inayotambuliwa kama upendo, bali kwa njia ya kushiriki katika asili yake.” n.k. 4. Hatukuyanukuu haya yote ili kuanzisha hapa mjadala kuhusu suala hili kwa kuwa Enzi ya Kaisari inalikubali fungu hili. Bali, ili wasomaji wetu wote wapate kuelewa wazi kuwa, sisi tunayatetea mafundisho haya katika Kanisa zima kwamba, mwili na damu ya Kristo vipo katika Chakula cha Bwana kweli na kwa uthabiti na vinatolewa kweli pamoja na vitu vinavyoonekana, yaani, mkate na mvinyo. Tunazungumzia juu ya kuwepo kwa Kristo aliye hai kwa sababu tunajua kabisa kwamba, ‘kifo hakina tena mamlaka dhidi yake’.670
Fungu la Kumi na Moja: Ungamo la Dhambi
1. Fungu la Kumi na Moja linalouhifadhi msamaha wa dhambi katika Kanisa linakubaliwa. Lakini wapinzani wetu wanaongezea sahihisho kwamba, kanuni ya “Omnis utriusque”671lazima ichunguzwe: ungamo lazima lifanywe kila mwaka, na hata kama dhambi zote haziwezi kutajwa, juhudi zifanywe kabisa ili kuzikumbuka na kuzitaja zile zinazoweza kukumbukwa. Baadaye kidogo, tutalizungumzia fungu hili zima zaidi tutakapokuwa tukielezea mafundisho mazima kuhusu toba. 2.Inajulikana wazi kwamba, tumeeleza na kusifu sana
667 Kirillo wa Aleksandria (+ 444 B.K.), alikuwa Askofu Mkuu wa Aleksandria tangu mwaka wa 412, mtaalamu mashuhuri. Alitetea vikali Uungu halisi wa Kristo dhidi ya mafundisho ya Nestorio (+ 451 B.K.) aliyekuwa Askofu Mkuu wa Konstantinnopoli.
668 Rum. 12: 5
669 1 Kor. 10: 17
670 Rum. 6: 9
671 Kanuni ya Papa Gregorio IX (Decr.Greg. IX. Lib. V. tit. 38 c.12.) iliyoamuliwa katika Sinodi ya nne ya Laterano katika mwaka wa 1215.
baraka ya msamaha wa dhambi na mamlaka ya funguo kwamba dhamiri nyingi zilizoteseka zimefarijika kwa ajili ya mafundisho yetu. Zimesikia kwamba, kwa njia ya amri za Mungu na sauti halisi ya Injili, tunausadiki msamaha wa dhambi na kutazamia kwa hakika kwamba, tunazawadiwa bure ondoleo la makosa672 yetu kwa ajili ya Kristo na kuona kwa kweli kwamba, tunapatanishwa na Mungu kwa imani hii. Fundisho hili limewatia moyo wengi walio wacha Mungu, na mwanzoni, liliwashawishi watu wengi wema kumfuata Luther, maana linaonyesha faraja ya hakika na thabiti kwa dhamiri. Awali, uwezo wote wa msamaha wa dhambi ulilemewa na mafundisho kuhusu matendo, wakati Madaktari Wanazuoni na wamonaki hawakufundisha chochote juu ya imani na msamaha wa bure.
3. Kuhusiana na wakati, kwa hakika, watu wengi mno katika makanisa yetu hushiriki sakramenti, ondoleo la dhambi na Chakula cha Bwana mara nyingi katika mwaka. Pia, wale wanaofundisha juu ya thamani na matunda ya sakramenti huelekeza kwa njia ya kuwaalika watu kutumia sakramenti mara kwa mara. Kuhusu suala hili, yapo maandiko mengi yaliyoandikwa na wenzetu na wapinzani wetu Iwapo wao ni watu wema, bila shaka wataweza kuyakubali na kuyasifu. 4. Waovu waziwazi na wapotoshaji wa sakramenti wametengwa. Tunafanya haya kulingana na Injili pamoja na kanuni za kale. 5. Lakini hakuna muda fulani unaoamriwa kwa sababu si wote waliostahili katika hali na muda huo huo. Licha ya hayo, iwapo watu wote wangekurupuka katika muda huo huo, wasingeweza kusikilizwa na kuelekezwa ipasavyo. Kanuni na mababa wa kale hawakuuteua muda fulani. Kanuni husema tu kuwa: “Wakiwepo watakaoingia Kanisani mwa Mungu na watakaoonekana kuwa hawashiriki kamwe, basi, waonywe. Iwapo wataendelea kutoshiriki, basi, waambiwe watubu. Wakishiriki, basi, wasijihini daima. Wasipotubu, basi, wajihini.”673 Kristo anasema kwamba, wale wanaozishiriki sakramenti bila kustahili, hupokea hukumu juu yao wenyewe.674 Hivyo basi, wachungaji wetu hawawalazimishi wale wasiostahili kuzipokea Sakramenti.
6. Kuhusu sharti la kutaja dhambi moja kwa moja katika ungamo, tunafundisha watu ili dhamiri zao zisitegwe kabisa. Hata hivyo, inafaa kwamba, watu wasiokuwa na tajiriba675 washauriwe kutaja baadhi ya makosa moja kwa moja ili wapate kufundishwa ipasavyo. Basi, sasa tunajadiliana kuhusu yale
672 “Msamaha wa dhambi,” Kilatini: ‘Absolutio;’ “ondoleo la dhambi,” Kilatini: ‘Remissio peccatorum.’
673 Decr. Gratiani III. De consecr. D. 2. c.20.
674 1 Kor. 11 : 27, 29. Ufafanuzi wa Melanchthon unamaanisha kwamba, mafundisho ya Paulo kuhusu sakramenti, kwa kweli, ni maneno ya Kristo mwenyewe. 675 Uzoefu.
yaliyo ya lazima kulingana na haki ya kimungu.676 Kwa sababu hiyo, hakuna haja wapinzani wetu kunukuu kanuni ya “Omnis utriusque,” dhidi yetu ambayo tunaifahamu fika.677 Heri wangeonyesha kwa haki ya Mungu kwamba, kutaja dhambi moja kwa moja ni lazima kwa ajili ya kuupokea msamaha wa dhambi. 7. Kanisa zima huko Ulaya kote linajua kabisa ni minyororo gani ilizifunga dhamiri kwa njia ya hii kanuni inayodai kuzitaja dhambi zote moja kwa moja. Andiko lenyewe halikufanya uharibifu sana sawa na yale yaliyoongezewa baadaye na “summistae,”678 yaani, waandishi wa vitabu vya ungamo kuhusu hali mbalimbali za dhambi. Njia gani za mzingo, maumivu makali yapi zaidi kwa njia ya nafsi njema zaidi! Vitisho hivi havikushurutisha lolote kwa majambazi na wenye kukufuru. 8. Tanzia gani zilitendeka baina ya makasisi na ndugu watawa wa kiume kwa sababu ya agizo hili679 kuwa ni lazima kila mmoja kuungama mbele ya padre wake mwenyewe. Ndugu hawa watawa wa kiume hawakuwa ndugu wa kweli walipopigana kuhusu mamlaka ya maungamo. Kwa upande wetu, sisi tuna msimamo kwamba, kulingana na haki ya kimungu, si lazima kutaja makosa moja kwa moja, na msimamo huu ulikubaliwa na Panormitano680 na mabingwa wengine wa Sheria za Kanisa. Sisi hatutaki kuiwekea sharti kanuni ile ya “Omnis utriusque” katika dhamiri za wenzetu. Msimamo wetu kuhusu kanuni hii ni huo huo kuhusu mapokeo mengine ya wanadamu: siyo ibada ya lazima kwa ajili ya kuhesabiwa haki. Kanuni hii hudai mambo yasiyowezekana kabisa kwamba, tuungame makosa yetu yote. Ni hakika kwamba, hatukumbuki wala hatuelewi dhambi zetu nyingi kwa mujibu wa tamko hili: “Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake?”681
9. Wachungaji wema wakipatikana wataelewa ilivyo na faida kuwahoji wasiokuwa na uzoefu. Basi, sisi hatutaki kuruhusu mateso makali ya waandishi wa vitabu vya ungamo. Waandishi hawa wangeweza kuvumiliwa kwa vyovyote, iwapo wangeongezea neno hata moja juu ya imani ambayo huifariji na kuitia moyo dhamiri. Basi, hakuna silabi hata moja inayopatikana kuhusu imani hii ambayo huupokea msamaha wa dhambi katika uchungu huu mkubwa wa kanuni
676 Kilatini: ‘Iure divino.’
677 Kabisa kabisa.
678 “Summistae” kutoka Kilatini “summa.” Maana yake ”muhtasari.” Wanatheologia wa namna hii waliandika vitabu vya ungamo vyenye mashauri mbalimbali kuhusu mambo ya kiroho na dhamiri.
679 Uamuzi wa Sinodi ya Nne ya Laterano mwaka wa 1215.
680 Nikolao wa Tudeschis, Askofu Mkuu wa Palermo (+ 1445) na mfafanuzi maarufu wa Sheria ya Kanisa la Roma.
681 Zab. 19: 12
za katiba,682 maelezo ya sheria ya Kanisa,683 vitabu vya toba684 na nyaraka za kitubio.685 Hakuna neno lolote juu ya Kristo. Wanarudia tu orodha za dhambi. Sehemu kubwa mno hujishughulisha na makosa dhidi ya mapokeo ya wanadamu, ambayo ni upuuzi usiopimika. 10. Mafundisho haya yamesababisha nafsi nyingi za wacha Mungu kukata tamaa kwa sababu waliamini kwamba, kulingana na haki ya kimungu, ni lazima kuzitaja dhambi moja kwa moja, wakati huo huo wakiona kwamba, haiwezekani. Kuna mafundisho mengine ya wapinzani wetu juu ya toba yenye makosa makubwa, hivyo tutayajadili hapa.
Fungu la Kumi na Mbili: Toba686
1. Wapinzani wetu wanakubali sehemu ya kwanza ya Fungu la Kumi na Mbili, ambapo tunaelezea kwamba, wale walioanguka baada ya Ubatizo wana nafasi ya kuupokea msamaha wa dhambi wakati wowote na kila mara wanapoongoka. Wanailaani sehemu ya pili tusemapo kwamba, majuto na imani ni sehemu za toba, na wanakataa imani kuwa sehemu ya pili ya toba. 2 Tutafanya nini hapa, Karolo, Kaisari asiyeshindwa kabisa? Naam, hii ni sauti halisi ya Injili kuwa tunaupokea msamaha wa dhambi kwa njia ya imani. Waandishi wa Hoja687 wanailaani sauti hii ya Injili. Kwa hiyo, kwa vyovyote, hatuwezi kuikubali Hoja. Hatuwezi kuilaani sauti mabruki688 mno ya Injili na ituleteayo faraja tele. Je, ni jambo lipi lingine la kuikana vibaya damu na kifo cha Kristo zaidi ya kukataa kwamba, tunapata msamaha wa dhambi kwa njia ya imani? 3. Basi, kwa sababu hii, tunakuomba Karolo, Kaisari asiyeshindwa, kutusikiliza kwa ustahimilivu na kwa umakini katika suala hili lililo kuu kabisa. Linalishika fungu maalumu la Injili, ufahamu wa kweli wa Kristo, na ibada ya kweli ya Mungu. Watu wote wema wataelewa vizuri kwamba, katika jambo hili mahsusi, tumefundisha lile ambalo ni la kweli, takatifu, lenye afya, na la lazima kwa Kanisa la Kristo ulimwenguni mote. Wataona kwamba, maandiko ya wenzetu yameng’aa nuru zaidi kuliko Injili na yameyarekebisha makosa mengi maovu ambayo zamani yalificha kabisa mafundisho kuhusu toba,689kwa maoni ya Madaktari Wanazuoni na wataalamu wa sheria za Kanisa.
682 Kilatini: ‘Constitutio.’
683 Kilatini: ‘Glossa.’
684 Kilatini: ‘Summa.’
685 Kilatini: ‘Epistula confessionalis.’
686 Kilatini: ‘Poenitentia’; Kijerumani: ‘Busse.’
687 Kilatini: ‘Confutatio.’
688 Yenye afya.
689 Kilatini: ‘Canonista,’ yaani bingwa wa sheria ya kanuni za Kanisa la Magharibi, ‘Corpus iuris canonici.’
4. Kabla ya kuanza kuutetea msimamo wetu, tunapaswa kusema mambo fulani kama dibaji. Watu wote wema katika vyeo vyote vya heshima, hata wanatheologia wenyewe, hukubali kwamba, kabla ya maandiko ya Luther, mafundisho kuhusu toba yalikuwa katika hali ya mchafuko kabisa. 5. Vitabu vya ufafanuzi690 vyenye maswali yasiyokuwa na mwisho ambayo wanatheologia hawakuweza kuyaelezea vya kutosha vinapatikana. Umma haukuweza kuelewa kiini cha jambo zima wala matakwa maalumu ya toba au chanzo cha amani ya dhamiri. 6. Kwa hiyo, mmoja wa wapinzani wetu asonge mbele na atuambie ni wakati gani msamaha wa dhambi unafanyika. Mungu wangu, hili ni giza totoro! Wanashangaa kama msamaha wa dhambi upo katika majuto madogo au majuto makubwa691 Kama msamaha wa dhambi ukipatikana kwa ajili ya majuto makubwa, kwa nini ondoleo la dhambi lihitajike, mamlaka ya funguo yafanye nini ikiwa dhambi zimesamehewa tayari? Hapa wanatoa jasho zaidi wanapopunguza mamlaka ya funguo kwa njia ya kukufuru. 7. Baadhi yao wanafikiri kwamba, mamlaka ya funguo hayasamehi dhambi bali yanazibadili tu adhabu za milele kuwa za muda. Hivyo, mamlaka hiyo yenye nguvu iwe huduma ya ghadhabu na adhabu tu na siyo ile ya uzima na ya Roho. Wengine wenye tahadhari zaidi hudhania kwamba, mamlaka ya funguo yanasamehe dhambi mbele ya Kanisa lakini siyo mbele za Mungu.692 Mafundisho ya namna hii pia ni kosa lenye madhara. Maana, iwapo mamlaka ya funguo hayawezi kutufariji mbele za Mungu, ni jambo gani mwishowe linaloweza kuituliza dhamiri? Kitakachofuata ni mkanganyiko mkubwa. 8. Wanafundisha kwamba, tunastahili neema kwa njia ya majuto makubwa.693 Mtu fulani anaweza kuuliza, kwa nini Sauli, Yuda na watu kama hao hawakupata neema ingawa walijutia kwa njia ya kutisha kabisa?
Kulingana na imani na Injili, hatuna budi kujibu kwamba, Yuda hakuamini wala hakuinuka kutoka kwenye anguko lake kwa nguvu ya Injili na ahadi ya Kristo. Kwa maana, imani inaonyesha tofauti baina ya majuto ya Yuda na yale ya Petro. Lakini wapinzani wetu hujibu kwa njia ya kisheria kwamba, Yuda hakumpenda
Mungu bali aliiogopa adhabu. 9. Lini basi, dhamiri iliyo na hofu, hasa miongoni mwa hofu kuu za kweli zinazoelezewa katika Zaburi na manabii na zinazowapata wale wanaoongoka kwa kweli, inaweza kuamua kwa hakika kama imwogope
Mungu kwa ajili yake mwenyewe au izikimbilie ghadhabu za milele? Mihemuko hii mikubwa ya nafsi inaweza kutofautishwa kitaaluma lakini, kwa kweli, jambo lenyewe haliwezi kutenganishwa na maisha ya kweli jinsi hawa Madaktari
690 Kilatini: ‘Libri sententianiorum.’
691 Kilatini: ‘Attritio’ na ‘contritio’; utofautishaji wa kitheologia wa Aleksandro wa Hales (mnamo 1186-1245) aliyekuwa daktari wa fafanuzi za Petro Lombardo (mnamo 1100-1160).
692 Gabriel Biel (mnamo 1420-1495), kwa mafundisho ya fafanuzi za Petro Lombardo.
693 ‘Contritio.’
Wanazuoni wajanja wanavyofikiria. 10 Hapa tunakata rufaa kwa ajili ya hukumu ya watu wote wema na wenye busara. Bila shaka watakubali kwamba, majadiliano ya wapinzani wetu yamejaa mikanganyo na yamekuwa yenye utata sana. Hata hivyo, haya yote yanahusu jambo lililo kuu mno ambalo ni kiini cha Injili, yaani, msamaha wa dhambi. Kwa upande wa wapinzani wetu, mafundisho haya yote kuhusu masuala haya ambayo tumeyaelezea, yanajaa makosa na unafiki hata kuificha baraka ya Kristo, mamlaka ya funguo, na haki ya imani.
11. Haya yote hutokea katika hatua ya kwanza. Nini kitatokea tutakapofika katika ungamo?694 Ni majadiliano kiasi gani yamefanyika kuhusu kutaja dhambi zote moja kwa moja bila mwisho? Kwa sehemu kubwa, makosa haya yalihusu mapokeo ya wanadamu! Ili kuzitesa zaidi nafsi za wacha Mungu, wanabuni kwamba, haki ya kimungu inadai kuziorodhesha dhambi zote. 12. Wanapodai vikali orodha hii ya makosa kwa kisingizio cha haki ya kimungu, huwa wana maneno yaliyopoa tu kuhusu msamaha wa dhambi, ambao kwa kweli ni wa haki ya kimungu. Wanabuni kwamba, sakramenti hutoa neema kama tendo lenyewe695 bila mtazamo sahihi wa mpokeaji na hawaitaji imani inayotambua msamaha na kuifariji dhamiri kwa neno lolote. Hii ndiyo kweli inayoitwa “kuondoka kabla ya usirisiri.”696
13. Hatua ya tatu imebaki kuhusu matendo ya upatanisho. Hapa, majadiliano kuhusu hoja yao ni shaghalalabaghala697 kabisa. Wanabuni kwamba, adhabu za milele zinabadilishwa kuwa adhabu za moto wa Purgatorio.698Jinsi wanavyofundisha ni kwamba, sehemu ya adhabu hizi inasamehewa kwa njia ya nguvu ya mamlaka ya funguo na sehemu nyingine inakombolewa kwa njia ya matendo ya ridhaa. 14.Wanaongezea zaidi kwamba, matendo ya ridhaa ni ya lazima, ni ya zaidi ya kiwango,699na haya ni pamoja na matendo matupu ya ufuasi wa kipumbavu wa mapokeo mbalimbali kama kuhiji, kutumia rozari au kuadhimisha mambo kama hayo ambayo hayana agizo la Mungu. 15. Kadiri walivyonunua fursa ya kuingia Purgatorio kwa matendo ya ridhaa, walibuni pia mbinu ya kuyafidia matendo hayo kwa faida kubwa mno. Naam, wao waliuza
694 Kabla ya kuelezea toba ya Injili, hapa Melanchthon alifuata hatua tatu za toba ya Enzi ya Kati, yaani, majuto makubwa (‘contritio’ 5-10), ungamo (‘confessio’ 11-12) na upatanisho au ridhaa (‘satisfactio’ 13-16). Papa Gregorio Mkuu (mnamo 540-604) alikuza sana mafundisho kuhusu matendo ya ridhaa katika toba.
695 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
696 Katika Kanisa la Zamani wakatekumeni waliamriwa kuondoka katika liturgia kabla ya sehemu ya Sakramenti ya Madhabahu. Kiyunani: ‘Απιεναι προ των μυστηριων.’
697 Kukanganya mambo vibaya sana.
698 Kilatini: ‘Purgatorium.’
699 Kilatini: ‘Opera supererogationis.’ Tomaso wa Akuino katika ‘Summa’ yake II, 1. q. 87 a.5. III q. 86 a. 4.
vyeti vya upatanisho700 ambavyo walivielezea kuwa fidia kwa ajili ya matendo ya ridhaa. Kwa njia hii, walikusanya mapato, siyo tu kutoka kwa wale walio hai bali zaidi kutoka kwa wale waliofariki dunia. Wanayakomboa matendo ya upatanisho ya wale waliofariki dunia siyo tu kwa vyeti vya upatanisho, bali pia kwa dhabihu ya misa.70116.Mwishowe, kazi yote ya matendo ya ridhaa, haina mwisho. Basi, sisi hatuwezi kuziorodhesha kashfa hizo zote. Mafundisho haya ya kuchukiza ya mashetani yanaficha mafundisho ya haki ya imani na ya baraka za Kristo. Kwa sababu hiyo, watu wote wema hufahamu kwamba, ni heri na inafaa kuyashutumu mafundisho ya toba kama yalivyofundishwa na Madaktari Wanazuoni na wataalamu wa kanuni za Sheria za Kanisa. Mafundisho yafuatayo ni uongo dhahiri usiopatana na Maandiko Matakatifu mababa wa Kanisa pia:
17. 1. Kulingana na Agano la Mungu, tunastahili neema kwa matendo mema yatendwayo nje ya neema.
18. 2. Tunastahili neema kwa majuto madogo.702
19. 3. Inatosha kuichukia dhambi, Ili kufuta dhambi.
20. 4. Tunaupokea msamaha wa dhambi kwa sababu ya majuto, na siyo kwa njia ya imani katika Kristo.
21. 5. Mamlaka ya funguo yanaweza kusamehe dhambi mbele ya Kanisa, na siyo mbele za Mungu.
22. 6. Mamlaka ya funguo hayasamehi dhambi mbele za Mungu bali yalianzishwa ili yabadilishe adhabu za milele kuwa za muda, yalazimishie dhamiri matendo ya upatanisho, yaanzishe ibada mpya na yashurutishe dhamiri kwa matendo ya upatanisho na ibada za namna hiyo.
23. 7. Sawa na wanavyoamuru wapinzani wetu, kuorodheshwa kwa dhambi katika maungamo ni lazima kulingana na haki ya kimungu.
24. 8. Matendo ya upatanisho yaliyoamriwa na kanuni za Sheria za Kanisa ni ya lazima ili kukombolewa kutoka kwenye adhabu za moto wa Purgatorio au kufaidi kama fidia ya kufuta hatia. Hivi ndivyo watu wasio na uzoefu wanavyoielewa.
25. 9. Kuipokea Sakramenti ya Kitubio ni sawa na kuipata neema kwa njia ya tendo lenyewe bila mtazamo sahihi wa mpokeaji, yaani, bila imani katika Kristo.
26. 10. Mamlaka ya funguo, kwa njia ya vyeti vya upatanisho huokoa nafsi
700 Cheti cha upatanisho, Kilatini: ‘indulgentia.’
701 Kilatini: ‘Sacrificium missae.’
702 Kilatini: ‘Attritio.’
kutoka katika moto wa Purgatorio.
27. 11. Katika kesi zilizohifadhiwa,703lazima kuihifadhi hati na siyo tu adhabu ya kisheria ya mtu aliyeongoka kwa kweli.
28. Ili kuziongoza dhamiri za wacha Mungu kutoka kwa njia za mzingo wa Madaktari Wanazuoni, tumethibitisha kwamba toba ina sehemu mbili, Yaani, majuto ya kweli704 na imani. Mtu akitaka kuiongezea sehemu ya tatu, yaani, matunda halisi ya toba,705na mabadiliko ya maisha yote na tabia, hatutampinga. 29. Kuhusu majuto, tumeyaondoa mazungumzo yale yasiyokuwa na faida na yasiyokoma kwamba, lini tunajutia kwa sababu tunampenda Mungu na lini kwasababu tunaiogopa adhabu. Tunasema kwamba, majuto ni hofu ya kweli ya dhamiri ambayo husikia ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi na kujutia kwa sababu ya kutenda dhambi. Majuto haya hutokea wakati Neno la Mungu linapokemea dhambi. Kwa maana muhtasari wa mahubiri ya Injili ni kuishutumu dhambi, kutoa msamaha wa dhambi na haki kwa ajili ya Kristo. Hali kadhalika, kutupatia Roho Mtakatifu na uzima wa milele ili tuzaliwe upya na hata tuyatende mema. 30. Kristo anajumlisha Injili katika sura ya mwisho ya Injili ya Luka anaposema: “na kwamba, mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi” (Lk. 24: 47). Maandiko yanazungumza juu ya hofu hizi kubwa.
31. Kwa mfano, katika Zab. 38:4, 8 tunasoma: “Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa, kama mzigo mzito zimenilemea mno . . . Nimedhoofika na kuchubuka sana, nimeugua kwa fadhaa za moyo wangu.” Katika Zab. 6:23: “BWANA, unifadhili, maana ninanyauka; BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. Na nafsi yangu imefadhaika sana; na Wewe, BWANA, hata lini?” Katika Isaya 38: 10,13, “Nalisema, Katika ustawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu . . . Nitajituliza hata asubuhi; kama simba, aivunja mifupa yangu yote; tangu mchana hata usiku wanimaliza.” 32. Katika hofu hizi kubwa dhamiri husikia ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi. Ghadhabu hii haijulikani kwa watu bila hofu706 kwa wanaotembea kimwili.707 Dhamiri inaona upotovu wa dhambi na kusikitika kwa kweli kwamba, imetenda dhambi; Wakati huo huo inakimbilia ghadhabu ya kutisha ya Mungu, 703 Kilatini: ‘Reservatio casuum;’ makosa makubwa mno yalihifadhiwa katika mahakama za maaskofu au Papa wa Roma mwenyewe na wale waliotenda uhalifu huo hawakuweza kuamini kwamba, wangeweza kupata msamaha wa dhambi bila ya kusafiri mbali kutoka nyumbani ama katika mji wa askofu au mji wa Roma. Kwa hiyo, watu wengi walikata tamaa na kupotea bila matumaini yoyote ya kusamehewa.
704 Kilatini: ‘Contritio.’
705 Mt. 3: 8
706 Pasipo hofu ya Mungu; Kilatini: ‘securus.’
707 K.m. Rum. 8: 1
kwa maana asili ya mwanadamu haiwezi kuivumilia isipokuwa kwa msaada wa Neno la Mungu. 33. Paulo anasema: “Maana mimi kwa njia ya sheria naliifia sheria.”708 Kwa maana sheria hushtaki tu na kutisha dhamiri. Katika vitisho hivi, wapinzani wetu hawasemi lolote juu ya imani. Badala yake, wanalitoa tu neno ambalo huishtaki dhambi, haya ni mafundisho ya sheria peke yake, na siyo ya Injili. Wanasema kwamba, watu hustahili neema katika huzuni na vitisho hivi iwapo wanampenda Mungu. Lakini ni kwa njia gani watu wanaweza kumpenda Mungu hasa katikati ya vitisho vikuu vya kweli wakati wanasikia ghadhabu ya Mungu ya kutisha na isiyoelezeka? Wanafundisha nini isipokuwa kukata tamaa, wakati wanaionyesha sheria tu katikati ya vitisho kama hivi?
35. Basi, katika ufafanuzi wetu, tunaongezea sehemu ya pili ya toba, yaani, imani katika Kristo. Kwa kuwa ni lazima kuionyesha dhamiri Injili ya Kristo katika vitisho hivi, ambavyo huahidi msamaha wa dhambi bure kabisa kwa ajili ya Kristo. Wanapaswa kuamini kwamba, kwa sababu ya Kristo, dhambi zao zimesamehewa bure. 36. Imani hii huimarisha, huhimili na kuhuisha wenye majuto kulingana na aya hii: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu.”709 Imani hii huupokea msamaha wa dhambi. Imani hii hutufanya kuwa wenye haki mbele za Mungu, jinsi aya hiyo hiyo isemavyo: “Tunaokolewa kwa imani.” Imani hii huonyesha tofauti baina ya majuto ya Yuda na ya Petro, na yale ya Sauli na Daudi. Majuto ya Yuda na Sauli hayakufaa kwa sababu yalikosa imani ambayo huutoa msamaha wa dhambi uliotolewa kwa ajili ya Kristo. Lakini majuto ya Daudi na Petro yalifaa kwa sababu yalikuwa na imani iliyopokea msamaha wa dhambi kwa ajili ya Kristo. 37. Wala upendo haupo kabla ya kupatanishwa kwa njia ya imani. Kwa maana sheria haiwezi kutekelezwa bila Kristo jinsi neno lisemavyo: “kwa Kristo tumepata . . . kuifikia neema.”710 Imani hii hukua polepole na hupambana na dhambi katika maisha yote ili ishinde dhambi na mauti. Lakini upendo hufuata imani, kama tulivyokwisha kusema hapo juu. 38. Hivyo basi, woga wa mtoto unaweza kuelezwa dhahiri kama wasiwasi uliounganika na imani, pale ambapo imani hufariji na kuhimili moyo wenye wasiwasi. Woga wa mtumwa unakosa imani iliyohimili moyo wenye wasiwasi.
39. Mamlaka ya funguo husimamia na huidhihirisha Injili kwa njia ya ondoleo la dhambi ambayo ndiyo sauti ya kweli ya Injili. Kwa sababu hiyo, tukizungumzia imani, tutaweka ondoleo la dhambi ndani yake kwa maana “imani, chanzo chake
708 Gal. 2: 19
709 Rum. 5: 1
710 Rum. 5: 2
ni kusikia,” jinsi Paulo anavyosema.711 Baada ya kusikia Injili, baada ya kupokea ondoleo la dhambi, dhamiri huimarika na kufarijika. 40. Kwa sababu Mungu huhuisha kweli kwa Neno, hivyo, kweli funguo husamehe dhambi mbele zake, sawa na tamko hili: “Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi.”712 Kwa hiyo, lazima kuiamini sauti ya mchungaji anayelitangaza ondoleo la dhambi sawa na sauti inayotoka mbinguni. 41. Ondoleo la dhambi lingeweza kuitwa vizuri Sakramenti ya Toba, jinsi wasemavyo pia Madaktari Wanazuoni wenye elimu zaidi.713 42. Wakati huo huo, imani hii inaimarishwa katikati ya majaribu kwa njia ya kutangaziwa Injili na matumizi ya sakramenti. Hizi ni ishara za Agano Jipya. Yaani, ishara za msamaha wa dhambi. Basi, zinautoa msamaha wa dhambi jinsi maneno katika Chakula cha Bwana yashuhudiavyo dhahiri: “Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu . . . Kikombe hiki ni agano jipya.”714 Hivyo, imani huzaliwa na kuthibitishwa kwa njia ya ondoleo la dhambi, sauti ya Injili, na matumizi ya sakramenti hata kutoshindwa inapopambana na vitisho vikuu vya dhambi na mauti. 43. Ufahamu huu wa toba ni wazi na sahihi na unaongezea heshima ya mamlaka ya funguo na sakramenti. Hata unaonyesha fadhili ya Kristo na kumkimbilia kama mpatanishi na msuluhishi wetu.
44. Kwa kuwa hoja unatuhukumu kwa sababu tumezitoa sehemu hizi mbili za toba, inatubidi kuonyesha kuwa Maandiko Matakatifu ndiyo yanayozifanya sehemu hizi maalumu kuwa za lazima katika toba au kuungama kwa mkosaji.
Katika Mt. 11: 28 Kristo anasema: “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Kuna sehemu mbili hapa. Yaani, kusumbuka na kulemewa. Maana yake ni majuto, wasiwasi na vitisho vya dhambi na mauti. Kumfikia Kristo kunamaanisha kuamini kwamba, kwa ajili yake dhambi zimesamehewa. Tunapoamini, Roho Mtakatifu huhuisha mioyo kwa Neno la Kristo. 45. Hivyo kuna sehemu mbili hapa; toba na imani. Katika Mk.1: 15 Kristo anasema: “. . . tubuni, na kuiamini Injili.” Katika sehemu ya kwanza, anapokaripia kwa ajili ya dhambi, katika sehemu ya mwisho anatufariji na kutuonyesha msamaha wa dhambi. Kwa maana, kuiamini Injili siyo kuamini kwa jumla tu jinsi hata mashetani wanavyofanya,715 bali hasa ni kuuamini msamaha wa dhambi uliotolewa kwetu kwa ajili ya Kristo; Injili inayafunua haya. Hapa pia tunaziona sehemu mbili zilizounganishwa: yaani, majuto, wakati dhambi inashutumiwa na imani wakati inatamkwa, “amini Injili.” Hatutakataa mtu akisema kuwa Kristo anaunganisha pia matunda ya toba au maisha mapya.
711 Rum. 10: 17
712 Lk. 10: 16
713 Yohana Duns Scotus, Comm.in sent. IV, d. 16, q. 1,7.
714 Lk. 22: 19-20
715 Yak. 2: 19
Inatosha kwetu kuzitaja sehemu hizi maalumu, majuto na imani kama sehemu kuu za toba..
46. Karibu kila Paulo anapoelezea kuhusu uongofu na kufanywa upya, anataja sehemu hizi mbili. Yaani, kuuawa na kuhuishwa jinsi ilivyo katika Kol. 2: 11: “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.” Kisha, baadaye kidogo: “Mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu.”716 Kuna sehemu mbili hapa. Moja ni kuweka mbali mwili wa dhambi, na nyingine ni kufufuliwa kwa njia ya imani. Maneno kama kuuawa, kuhuishwa, kuweka mbali, kuchochewa, yasieleweke kwa njia ya falsafa ya Platoni kama mfano tu wa mabadiliko; bali kuuawa kunamaanisha vitisho vya kweli sawa na vile vya kifo ambavyo huwa asili haiwezi kustahimili bila msaada wa imani. Hivyo, yale tunayoyaita majuto, Paulo huyaita “kuuvua mwili wa dhambi” kwa sababu katika matatizo haya tamaa zetu za asili717 husafishwa. Kuhuishwa kusieleweke kama maono ya falsafa ya Platoni bali kama faraja kweli inayoyadumisha maisha yaliyokimbia kutoka katika majuto. 47. Hivyo, kuna sehemu mbili. Yaani, majuto na imani. Kwa kuwa, dhamiri haiwezi kutulizwa isipokuwa kwa imani, vivyo hivyo imani peke yake huhuisha sawa na neno hili: “mwenye haki ataishi kwa imani.”718
48. Anasema zaidi katika Waraka wa Wakolosai Kol. 2: 14 kwamba, Kristo amefuta ile hati719 iliyokuwa adui yetu kwa nguvu ya kisheria. Hapa pia kuna sehemu mbili. Hati ya kutushtaki na kufutwa kwake. Hati ya kutushtaki ni dhamiri inayotulaumu na kutulaani. Sheria ni neno linaloyashtaki na kuyahukumu makosa. Basi, sauti inayosema, “nimemfanyia BWANA dhambi,”720 jinsi ilivyomwambia Daudi ni hati ya kutushtaki. Watu wasiokuwa wacha Mungu na wasiokuwa na hofu ya kimungu hawasemi hili kwa makini, kwa maana hawaoni wala kusoma adhabu ya sheria iliyoandikwa mioyoni mwao. Adhabu hii inaeleweka tu katikati ya majuto na vitisho vya kweli. Hivyo, hati hii ni majuto yanayotuhukumu. Utangulizi wa hati hii ni kuiondoa sentensi hii ambayo kwayo, sisi hutangaza kwamba, tumehukumiwa na kuiandika ndani yetu sentensi ambayo kwayo, tunafahamu kuwa tumekombolewa kutoka katika hukumu. Sentensi hii mpya ni imani inayoiondoa hukumu iliyotangulia na kuupatia moyo amani na uzima.
49. Lakini kwa nini tuutaje ushuhuda mwingi wakati kuna nyingi zaidi katika Maandiko Matakatifu? Zab. 118:18 inasema: “BWANA ameniadhibu sana,
716 Kol. 2: 12
717 Kilatini: ‘Concupiscentia.’
718 Hab. 2: 4; Rum. 1: 17
719 Mwandiko wa hati ya mkono, Kilatini: ‘Chirographum.’
720 2 Sam. 12: 13
lakini hakuniacha nife.” Nayo Zab.119: 28 inasema: “Nafsi yangu imeyeyuka kwa uzito, unitie nguvu sawasa wa na neno lako.”721 Sehemu ya kwanza ina majuto, wakati sehemu ya pili inaelezea namna tunavyohuishwa katika majuto kwa Neno la Mungu linalotupatia neema. Hii hudumisha na kuhuisha mioyo. 50. 1 Sam. 2: 6 inasema: “BWANA huua, naye hufanya kuwa hai; hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.” Katika sentensi hizi, sehemu ya kwanza humaanisha majuto na ya pili imani. 51. Isaya 28: 21 inasema: “Maana BWANA ataondoka . . ., ataghadhibika . . .; apate kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu; na kulitimiza tendo lake, tendo lake la ajabu.” Isaya anaiita kazi Mungu ya kutisha kuwa kazi ya kigeni722 kwa sababu kazi halisi ya Mungu ni kuhuisha na kufariji. Lakini anasema kwamba, Mungu hutisha ili nafasi ya faraja na uhuishaji ipatikane, kwa maana mioyo ambayo haisikii ghadhabu ya Mungu katika uasi wao, huidharau faraja. 52. Maandiko Matakatifu huyaunganisha mambo haya mawili kwa njia hii, yaani, hofu kuu na faraja, ili yafundishe haya kuwa sehemu kuu za toba, majuto, na imani inayoleta faraja na kuhesabiwa haki. Hatuwezi kuona asili ya toba ikionyeshwa kwingine kwa njia uwazi na sahili zaidi.
53. Haya ni matendo mawili ya Mungu yaliyo ya muhimu sana kwa wanadamu, yaani, kutisha, kuhesabia haki na kuhuisha wale walo na hofu kuu. Maandiko Matakatifu yote yanagawanyika kulingana na kazi hizo mbili. Sehemu moja inahusu sheria ambayo hufunua, hushutumu na kulaani dhambi. Sehemu ya pili inahusu Injili, yaani, ahadi ya neema iliyotolewa katika Kristo. Ahadi hii imerudiwa mara kwa mara katika Maandiko Matakatifu. Kwanza ilitolewa kwa Adamu, baadaye ikatolewa kwa mababa wa Imani, ikaelezewa na manabii, ikahubiriwa na kufunuliwa na Kristo katikati ya Wayahudi, na mwishowe ikaenezwa na mitume ulimwenguni kote. 54. Watakatifu wote wamehesabiwa haki kwa njia ya imani katika ahadi hii wala siyo kwa majuto yao madogo au makubwa.
55. Sehemu hizi mbili zinaonekana pia katika maisha ya watakatifu. Adamu alikaripiwa baada ya dhambi yake na kuogopa. Haya ni majuto. Baadaye Mungu aliahidi neema na kusema kwamba, pangekuwepo na uzao ambao ungeharibu ufalme wa Ibilisi, mauti na dhambi! Hapa, anautoa msamaha wa dhambi. Hizi ni sehemu kuu. Ingawa bado adhabu iliongezewa baadaye, adhabu hii haistahilishi msamaha wa dhambi. Tutazungumzia aina hii ya adhabu baadaye.
56. Isitoshe, Daudi anakemewa na Nathani na katika hofu yake anasema:
721 Idadi za Zaburi katika Toleo la ‘Vulgata’ ni 117: 18 na 118: 28. 722 Kilatini: ‘Opus alienum.’ ‘Union Version,’ “Kazi ya ajabu.”
“Nimemfanyia BWANA dhambi.”723 Haya ni majuto. Baadaye analisikia ondoleo la dhambi: “BWANA naye ameiondoa mbali dhambi yako; hutakufa.”724 Sauti hii ilimtia Daudi nguvu za kuidumisha imani, kumhesabia haki na kumhuisha. Adhabu pia inaongezewa hapa, japo haistahilishi msamaha wa dhambi. 57. Adhabu maalumu hazitaongezewa daima, lakini daima majuto na imani lazima vitakuwa katika toba, jinsi ilivyo katika Luka 7: 37 n.k. Mwanamke aliyekuwa mwenye dhambi alikuja kwa Kristo akiwa mwenye machozi ambayo yalionyesha majuto yake. Baadaye alitangaziwa ondoleo la dhambi: “Umesamehewa dhambi zako . . . Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani”.725 Hii ni sehemu ya pili ya toba, imani ambayo ilimtia moyo na kumfariji. 58.Kutokana na haya yote, wasomaji wacha Mungu wanaweza kuona wazi kwamba, tumeiweka toba katika sehemu zake ambazo ni katika uongofu au kuzaliwa upya na msamaha wa dhambi. Kadhalika, matunda yafaayo adhabu hufuatia kuzaliwa kupya na msamaha wa dhambi. Tumeziweka sehemu hizi mbili ili tuweze kuikazia imani tunayohitaji sana katika toba. Itakuwa rahisi kuelewa ni imani ipi inayohubiriwa na Injili ikifanyika kuwa kinyume cha majuto na kuuawa.
59. Kwa kuwa wapinzani wetu hupinga hasa fungu hili kwamba, watu hupata msamaha wa dhambi kwa njia ya imani, tunaongezea baadhi ya vidhibitisho ambavyo kwavyo, inawezakana kueleweka kwamba, msamaha wa dhambi hautokani na tendo lenyewe na majuto, bali kwa imani ile ambayo kwayo mtu binafsi anaamini kuwa dhambi zake zimesamehewa. Naam, fungu hili ni kuu kabisa ambalo kwalo tunagombana na wapinzani wetu na ambalo tunaamini kuwa Wakristo wote lazima walielewe. Kwa kuwa ni wazi kwamba, tumesema vya kutosha juu ya hili mapema, hapa tutasema kwa ufupi kwa maana mafundisho ya toba na kuhesabiwa haki yanakaribiana sana.
60. Wapinzani wetu wanapozungumzia imani na kusema kwamba, inafuata toba, hawamaanishi imani ile ya kuhesabiwa haki, bali imani ya jumla ambayo huamini kuwa Mungu yupo, na kuwa adhabu inawakalia wakosaji n.k. Basi, kwa upande wetu, kinyume na imani ya namna hiyo, tunadai kwamba, inampasa kila mmoja aamini kwamba, dhambi zake zimesamehewa. Tunajadiliana juu ya imani hii maalumu. Tunaiweka imani hii kinyume cha maoni ambayo hutuamuru tuyategemee majuto, ungamo na matendo ya upatanisho kama tendo lililotendeka726 na siyo katika ahadi ya Kristo. Imani hii hufuatia vitisho vikuu hata kuvishinda na kupata dhamiri iliyotulizwa. Imani hii inahesabia haki na
723 2 Sam. 12: 13
724 v 2 Sam. 12: 14
725 Lk. 7: 48, 50
726 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
huzaa upya kwa maana hutufungua kutoka kwenye hofu kuu na kuzaa amani, furaha na maisha mapya moyoni. Sisi tunaitetea imani hii kwamba, ni ya lazima kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Kwa sababu hiyo, tunaiweka kama sehemu mojawapo ya toba. Kanisa la Kristo halina msimamo tofauti kinyume na madai ya wapinzani wetu.
61. Mwanzoni kabisa, tunawauliza wapinzani wetu iwapo kupokea ondoleo la dhambi ni sehemu ya toba au la. Iwapo hawa wajuzi wa utofautishaji wanajaribu kulitofautisha na ungamo, basi, tunashindwa kuona faida ya ungamo bila ondoleo la dhambi. Kwa upande mwingine, iwapo hawatautenganisha upokeaji wa ondoleo la dhambi na ungamo, hawatakuwa na budi kukubali kwamba, imani ni sehemu ya toba kwa maana ondoleo la dhambi halitapokelewa bila imani. Paulo anathibitisha katika Rum. 4: 16 kwamba, ondoleo la dhambi halitapokelewa bila imani kwa kuwa ni imani tu iwezayo kuipokea ahadi. Ondoleo la dhambi si lolote bali ni ahadi ya msamaha wa dhambi. Kwa sababu hiyo, linadai lazima imani iwepo. 62. Hatuelewi pia hata kidogo jinsi mtu anaweza kuupokea msamaha wa dhambi bila kuukubali moyoni mwake. Kutolikubali ondoleo la dhambi ni nini isipokuwa kumshutumu Mungu kuwa mwongo? Moyo uwapo na mashaka, hudhania kwamba, ahadi za Mungu hazina uhakuka na tupu kabisa. Kwa sababu hiyo, imeandikwa katika 1 Yoh. 5: 10: “Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.”
63. Pili, tunahisi, wapinzani wetu watakubali kwamba, ondoleo la dhambi ni sehemu ya toba au shabaha yake – yaani, kile wakiitacho “kikomo cha mwisho.”727 Hivyo basi, yule anayepokea ondoleo la dhambi lazima aunganishwe kama sehemu mojawapo ya toba. Lakini ni hakika kabisa, ingawa milango yote ya Jehanumu728 italia kwa sauti kuu dhidi yake kwamba, ondoleo la dhambi linaweza kupokelewa kwa imani peke yake,729ambayo inaamini kwamba, dhambi zinasamehewa kwa ajili ya Kristo, Rum. 3: 25: “ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake.” Kadhalika, Rum. 5: 2: “Ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema.” 64 Kwa kuwa, dhamiri iliyotishwa haiwezi kuweka matendo yetu au upendo wetu kinyume na ghadhabu ya Mungu, bali mwishowe itatulia inapomshika
Kristo aliye mpatanishi na kuamini kwamba, ahadi zimetolewa kwa ajili yake. Wale wote wanaoota kwamba, moyo unaweza kuipata amani bila imani katika
Kristo Yesu, hawawezi kuelewa msamaha wa dhambi ni upi na unatujia kwa
727 Kilatini: ‘Terminus ad quem;’ Tomaso wa Akuino STh. II 1. q. 113 a 6 c.
728 Mt. 16: 18
729 Kilatini: ‘Sola fide.’
njia gani. 65. Katika 1 Pet. 2: 6, Petro ananukuu maneno ya Isa. 28: 16: “Na kila amwaminiye hatatahayarika.” Hivyo basi, wanafiki wanaoamini kuupokea msamaha wa dhambi kwa kazi zao wenyewe na siyo kwa ajili ya Kristo, hawana budi kuaibika. Petro pia anasema katika Mdo. 10: 43: “Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba, kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.” Hakuweza kulizungumzia hili wazi zaidi aliposema “kwa jina lake,” ndipo anaongezea “kila amwaminiye.” Basi, tunaupokea msamaha wa dhambi kwa jina la Kristo peke yake. Maana yake ni kwamba, kwa njia ya Kristo na siyo kwa sababu ya stahili zetu zozote au matendo yetu yoyote. Hili linafanyika tunapoamini kwamba, dhambi zetu zinasamehewa kwa njia ya Kristo.
66. Wapinzani wetu hupiga kelele sana kwamba, wao wenyewe ni Kanisa na wanaufuata mwafaka wa Kanisa. Lakini hapa Petro anatuonyesha pia mwafaka wa Kanisa katika huu msimamo wetu: “Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba, kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi n.k.” Kwa kweli, mwafaka wa manabii lazima uelezewe kama mwafaka wa Kanisa zima. Sisi hatukubali kwamba, Papa ama Kanisa wawe na mamlaka ya kutoa uamuzi wowote kinyume na mwafaka huu wa manabii. 67. Hata hivyo, tangazo la Papa Leo730 linalaani, kwa uwazi kabisa, fungu hili la msamaha wa dhambi jinsi wapinzani wetu wanavyolilaani katika hoja yao. Jambo hili linaonyesha dhahiri Kanisa lao lililohukumu jinsi hiyo lilikuwa la aina gani na linaundwa na watu wa aina gani. Katika matamko yao wanalaani kwamba, fundisho hili kuwa tunapata msamaha wa dhambi kwa imani kwa ajili ya Kristo na siyo kwa njia ya matendo yetu, bali wanaamuru kwamba, mafundisho haya yatupiliwe mbali kwa nguvu na upanga, na kwamba, watu wema wanaokubali imani hii wauawe kwa ukatili wa namna yoyote.
68. Kwa upande wao, wanatheolojia wenye majina ya vyeo vikuu sana kama vile Duns Scotus, Gabriel731 na wengineo pamoja na misemo ya mababa iliyofupishwa na iliyonukuliwa kutoka katika matamko yao. Kwa kweli, kama mamlaka hii ingehesabiwa yote, wangekuwa sahihi kabisa; Kwa maana, kuna umati mkubwa mno wa waandishi wajinga wanaojihusisha na “Sentensi” ambao, jinsi ilivyo katika njama, huzitetea fikra potofu kuhusu stahili za majuto madogo, matendo na mengine yanayofanana nayo, jinsi tulivyokwisha kuyanukuu hapo juu. 69. Basi, mtu asishawishiwe na idadi hii bwa ya nukuu, bali akumbuke kwamba, hakuna uzito mkuu katika ushuhuda wa wanatheologia wa baadaye ambao hawakutengeneza maandiko yao wenyewe bali waliyatunga tu kutoka
730 ‘Bulla’ au tangazo la ilani la Papa Leo wa Kumi dhidi ya Martin Luther katika mwaka wa 1520 ‘Exsurge Domine’ 15.
731 Yohana Duns Scotus (+1308), Gabriel Biel (+1495), walikuwa Madaktari Wanazuoni maarufu.
kwenye vitabu vya wale waliowatangulia na kuyahamisha mawazo haya kutoka kitabu kimoja hadi kingine. Hapo hawakuhukumu lolote bali, kama maseneta wa cheo cha chini, waliyapitisha makosa ya wakubwa wao kimyakimya bila kuyaelewa. 70. Basi, sisi tunaiweka sauti ya Petro inayotoa mwafaka wa manabii wa kuvipinga vikosi vyovyote vya waandishi wa sentensi bila mashaka yoyote. 71. Ushuhuda wa Roho Mtakatifu uliongezewa katika mahubiri haya ya Petro, maana maandiko yanasema: “Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.”732
72. Basi, dhamiri za wacha Mungu sharti zifahamu kwamba, agizo la Mungu ni kuamini kuwa, kusamehewa dhambi ni bure kwa ajili ya Kristo na siyo kwa ajili ya matendo yetu. Inawapasa kujiimarisha kwa agizo hili la Mungu dhidi ya kukata tamaa na dhidi ya hofu kuu za dhambi na mauti. 73. Inawabidi wajue kwamba, hivi ndivyo nwatakatifu walivyoamini tangu mwanzo wa ulimwengu. Petro anaonyesha wazi mwafaka wa manabii; Maandiko ya mitume yanashuhudia wazi kwamba, wanakubaliana kabisa; Pia, ushuhuda wa mababa wa Kanisa haupunguki. Kwa maana, Bernardo husema vivyo hivyo kwa maneno dhahiri kabisa: “Mbele ya mambo mengine lazima kuamini kwamba, huwezi kupata msamaha wa dhambi isipokuwa kwa huruma za Mungu; lakini uongezee hapo pia kwamba, unaamini kusamehewa dhambi zako kwa ajili yake. Roho Mtakatifu anauleta moyoni mwako ushuhuda huu akisema: ‘Dhambi zako zimeondolewa.’
Ndiyo sababu mtume anatafakari kwamba, mwanadamu anahesabiwa haki bure kwa njia ya imani.733 74. Maneno haya ya Bernardo huelezea, kwa njia ya ajabu sana, hoja yetu kwa sababu hataki tuamini tu kwamba, dhambi zinasamehewa kwa huruma, bali anaamuru tuiongezee imani ya kibinafsi ambayo kwayo tunaamini wenyewe kuwa dhambi zetu zimesamehewa. Anatufundisha pia jinsi tunavyokuwa na uhakika kuhusu msamaha wa dhambi, yaani, wakati mioyo yetu inahimizwa na inatulia kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Je, wapinzani wetu watadai nini zaidi? Je, bado wanathubutu kukataa kwamba, tunaupata msamaha wa dhambi kwa njia ya imani, au kuwa imani ni sehemu ya toba?
75. Tatu, wapinzani wetu wanasisitiza kwamba, dhambi zinasamehewa kwa njia hii: Mtu mwenye majuto madogo au makubwa734 analifanya tendo la upendo kwa Mungu. Hivyo, kwa tendo hili, anastahili kuupokea msamaha wa dhambi. Hili si lingine lolote isipokuwa kuifundisha sheria pamoja na kuondolewa kwa Injili na kufutwa kwa ahadi ya Kristo. Wanadai tu sheria na matendo yetu kwa sababu sheria hudai tu upendo. Mbali na hayo, wanatufundisha kutegemea kuwa
732 Mdo. 10: 44
733 Bernardo wa Clairwaux, “Mahubiri kuhusu maadhimisho ya Bikira Mariamu” I, 1.
734 Kilatini: ‘Attritus seu contritus.’
tunapata msamaha wa dhambi kwa ajili ya toba na upendo. Basi, hili ni lipi lingine isipokuwa kuyaweka matumaini yetu kwenye matendo yetu mbali na Neno la Mungu na ahadi yake kuhusu Kristo? Ikiwa sheria inatosha kwa ajili ya kuupata msamaha wa dhambi, Injili itahitajika kwa ajili gani? Kuna haja gani ya Kristo ikiwa tunapata msamaha wa dhambi kwa matendo yetu? 76. Kinyume chake, kwa upande wa Injili, tunazishauri dhamiri za watu kugeuka kutoka kwa sheria, kutoka kwa tegemeo la matendo yetu wenyewe, hadi kwa upande wa tegemeo la ahadi na Kristo. Maana, Injili inatufunulia Kristo na kuuahidi msamaha wa dhambi bure kwa ajili yake. Injili inatuamuru kuitegemea ahadi hii kwamba, tunapatanishwa na Baba kwa ajili ya Kristo na siyo kwa sababu ya majuto au upendo wetu. Kwa maana, hakuna mpatanishi mwingine au mwenye kuturidhisha isipokuwa Kristo. Sisi hatuwezi kuitenda sheria isipokuwa, kwanza tuwe tumepatanishwa na Kristo. Hata kama tungetenda lingine lolote, bado tunapaswa tukumbuke kwamba, hatupokei msamaha wa dhambi kwa sababu ya matendo haya bali kwa ajili ya Kristo, aliye Mpatanishi na mwenye kuturidhisha.
77. Tutamuudhi Kristo na kuitangua Injili kama tukifikiria kwamba, tunaupata msamaha wa dhambi kwa ajili ya sheria au kwa njia nyingine tofauti na imani katika Kristo. Awali, tumekwisha kuzungumzia uwiano735 huu kuhusiana na kuhesabiwa haki tuliposema kwamba, sababu ya kutoa kauli yetu ilikuwa kwamba, wanadamu huhesabiwa haki kwa imani na siyo kwa upendo. 78. Kwa sababu hiyo, mafundisho ya wapinzani wetu ni mafundisho ya sheria tu wanapofundisha kwamba, watu huupata msamaha wa dhambi kwa majuto na upendo wao, na hutegemea majuto na upendo huo. Ni mafundisho ya sheria tu isiyoeleweka sawa na Wayahudi walivyouangalia uso wa Musa uliokuwa umefunikwa kwa shela. Tukibuni iwapo upendo utapatikana, na iwapo matendo yatakuwepo, ilihali wala upendo au matendo haviwezi kuwa upatanisho wa dhambi. Haviwezi kuwekwa dhidi ya ghadhabu na hukumu ya Mungu kulingana na kifungu hiki: “Wala usimhukumu mtumishi wako, maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.”736 Kamwe haturuhusiwi kuihamisha sifa ya Kristo hadi kwenye matendo yetu.
79. Kwa sababu hizi, Paulo hukataa kwamba, tunahesabiwa haki kwa njia ya sheria. Kinyume cha sheria, anaiweka ahadi ya msamaha wa dhambi inayotolewa kwa ajili ya Kristo. Anafundisha kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi bure kwa njia ya imani na kwa ajili ya Kristo. Katika ahadi hii, Paulo anatuita kutoka katika sheria. Anatuagiza tuitazame ahadi hii ambayo isingekuwa na maana iwapo tungetangulia kuhesabiwa haki kwa sheria kabla ya ahadi, au iwapo
735 Kilatini: ‘Ratio.’
736 Zab. 143: 2
tungepata msamaha wa dhambi kwa ajili ya haki zetu. 80. Lakini inajulikana wazi kwamba, ahadi ilitolewa na Kristo ambaye amefunuliwa kwa sababu hatukuweza kuitimiza sheria. Kwa sababu hiyo, lazima tupatanishwe kwa njia ya ahadi kabla ya kuitimiza sheria. Imani peke yake huipokea ahadi. Hivyo, kwa njia ya imani, wale wanaotubu hawana budi kuishika ahadi ya msamaha wa dhambi iliyotolewa kwa ajili ya Kristo na kuwa na hakika kwamba, wana Baba aliyepatanishwa bure kwa ajili ya Kristo. 81.Huu ndio msimamo wa Paulo anaposema katika Rum. 4: 16: “Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba, ile ahadi iwe imara kwa wazao wote,” na katika Gal. 3: 22: “Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, kusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.” Maana yake ni kwamba, watu wote wako chini ya dhambi, na hawawezi kuwa huru kwa njia yoyote isipokuwa waishike ahadi ya msamaha wa dhambi kwa njia ya imani. 82. Kwahiyo, ni lazima tuupokee msamaha wa dhambi kwa imani kabla ya kuitimiza sheria, japo jinsi tulivyosema awali, upendo hufuatia imani, kwa sababu wale waliozaliwa upya humpokea Roho Mtakatifu na ndipo wanaanza kuitimiza sheria.
83. Tungeeleza shuhuda nyingi zaidi kama hazingekuwa wazi kwa kila msomaji aliye mwaminifu wa Maandiko Matakatifu. Hatutaki pia kurefusha kauli hii ili iweze kueleweka kwa urahisi zaidi. 84. Hakuna mashaka yoyote kwamba, huu ndio msimamo wa Paulo tunaoutetea: tunaupokea msamaha wa dhambi kwa njia ya imani kwa ajili ya Kristo na kwamba, kwa imani, inatupasa kumwamini Kristo aliye Mpatanishi na siyo kuyaweka matendo yetu dhidi ya ghadhabu ya Mungu. Nafsi za wacha Mungu hazipaswi kusumbuliwa iwapo wapinzani wetu wataipindisha misemo ya Paulo, kwa maana hakuna lolote litakalosemwa kwa njia dhahiri ambalo haliwezi kupotoshwa. Tunajua kwamba, ile ambayo tumeisema ndiyo sentensi ya Paulo ya kweli na halisi; Tunajua kwamba, msimamo wetu huziletea faraja thabiti dhamiri za wacha Mungu, ambayo pasipo hiyo, hakuna awezaye kuvumilia mbele ya hukumu ya Mungu.
85. Kwa sababu hiyo, tunakataa maoni ya Kifarisayo ya wapinzani wetu kwamba, hatuupokei msamaha wa dhambi kwa njia ya imani. Badala yake tunastahili msamaha huu kwa upendo na matendo yetu na kwamba, tunapaswa kuweka upendo na matendo yetu dhidi ya ghadhabu ya Mungu. Hili ni fundisho la sheria wala si la Injili, kufikiria kwamba, kwanza, lazima mwanadamu ahesabiwe haki kwa njia ya sheria kabla ya kupatanishwa na Mungu kwa njia ya Kristo, ingawa Kristo anasema: “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. . . maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”73786. Lakini, wapinzani
737 Yn. 15: 5
wetu hufikiria kwamba, sisi ni matawi lakini yale ya Musa na siyo ya Kristo. Wanapendelea kutangulia kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria na kuutoa upendo wetu na matendo kwa Mungu kabla ya kupatanishwa na Mungu kwa njia ya Kristo, kabla ya kuwa matawi ya Kristo. Kinyume chake, Paulo anasisitiza kwamba, hatuwezi kuitimiza sheria bila Kristo. Hivyo, lazima tuikubali ahadi ili tuhesabiwe haki kwa njia ya imani ili tupatanishwe na Mungu kwa ajili ya Kristo kabla ya kuitimiza sheria. 87.Tunafikiri kwamba, hili liko wazi vya kutosha kwa dhamiri za wacha Mungu na kutokana na hili wanaelewa jinsi tulivyokiri hapo juu kwamba, watu wanahesabiwa haki kwa njia ya imani na siyo kwa upendo na kwamba, hatuna budi kumwamini Kristo aliye Mpatanishi, kwa maana hatupaswi kuweka upendo au matendo yetu dhidi ya ghadhabu ya Mungu au kutegemea matendo au upendo wetu. Lazima tutangulie kuishika ahadi ya msamaha wa dhambi kabla ya kuitimiza sheria.
88. Mwisho: Ni lini dhamiri zitatulia tukiupokea msamaha wa dhambi kwa ajili ya upendo wetu au tukiitimiza sheria? Maana, daima sheria itatushtaki kwa sababu hatuiridhishi sheria ya Mungu kamwe. Jinsi Paulo asemavyo: “sheria ndiyo ifanyayo hasira.”738 Krisostomo anauliza kuhusu toba: “Tunawezaje kuwa na hakika kwamba, dhambi zetu zimesamehewa?”739 Wapinzani wetu huuliza swali hilo hilo katika sentensi zao. Hili haliwezi kujibiwa wala dhamiri haziwezi kutulia isipokuwa tufahamu kwamba, ni amri ya Mungu na Injili yenyewe inayoweza kuridhika hakika kwamba, dhambi zao zinasamehewa bure kwa ajili ya Kristo, bila mashaka yoyote. Ikiwa mtu yoyote akiwa na mashaka, anamfanya Mungu kuwa mdanganyifu katika ahadi yake, jinsi Yohana asemavyo.740 Sisi tunafundisha kwamba, uhakika wa imani ulio wa namna hiyo unahitajika katika Injili. Wapinzani wetu wanaziacha dhamiri zikiyumba na kutokuwa na uhakika. 89. Dhamiri hazitaweza kutenda lolote kwa njia ya imani zikiwa na mashaka daima iwapo zimesamehewa au la. Zinawezaje kumwomba Mungu kwa mashaka haya, zinawezaje kuridhika kwa uhakika kwamba, zinasikilizwa? Hivyo, maishayao yote hayana Mungu na hayana ibada ya kweli ya Mungu. Hili ndilo Paulo alisemalo: “Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.”741 Kwa kuwa, daima wanapatikana katika hali ya mashaka, hawawezi kutambua kamwe imani ni nini. Kwa sababu hiyo, mwisho inatokea kwamba, wao hushindwa na kukata tamaa. 90. Haya ndiyo mafundisho ya wapinzani wetu, ndiyo mafundisho ya sheria, batili ya Injili, na mafundisho ya kukata tamaa. Kwa upande wetu,
738 Rum. 4: 15
739 Ad. Theod. Laps. I, 5.
740 1 Yoh. 5: 10
741 Rum. 14: 23
tunafurahia sana kuwapa watu wote wema ushauri kuhusu fungu hili la toba. Halina uvunguvungu wowote kabisa. Wataweza kutangaza iwapo mafundisho yetu au yale ya wapinzani wetu yanaonekana kuwa ya kimungu na ya kuipatia dhamiri uzima. Mafarakano kama haya kamwe hayatufurahishi kanisani. Hivyo, kama hatungekuwa na sababu kuu na muhimu sana za kutokubaliana na wapinzani wetu, tungependa sana kunyamaza. Lakini kwa vile wanaulaani ukweli ulio wazi, siyo halali kwa upande wetu kuacha chanzo ambacho ni cha Kristo na Kanisa.
91. Taryari tumesema sababu za kuzishikilia sehemu hizi mbili za toba. Yaani, majuto na imani. Tumefanya hili hasa kwa kuwa misemo mingi ya Mababa wa Kanisa kuhusu toba inazunguka inanukuliwa na wapinzani wetu kwa namna iliyo mbaya na potofu. Hawa wapinzani wetu huvuruga misemo hii ili kuifanya imani iwe gizani. Kwa mfano: “Toba inamaanisha kuomboleza maovu yaliyopita na kutotenda tena matendo ambayo yanahitaji kuombolezwa.”742 Kadhalika: “Toba ni aina ya kulipia kisasi kwa mtu anayesikitika, akijiadhibu mwenyewe kwa kusikitikia yale aliyoyatenda.”743 Matamko haya hayataji lolote juu ya imani. Yalipofafanuliwa katika vyuo vikuu, hayakuwa na neno lolote kuhusu imani! 92. Kwa sababu hiyo, tumeihesabu imani kuwa sehemu ya toba ili mafundisho ya imani yawe wazi zaidi. Kwa maana, misemo hii inayodai majuto makubwa au matendo mema bila kuitaja imani, inayohesabiwa haki, ni hatari kubwa iliyo wazi. 93 Kiukweli ni haki kuhitaji busara za wale waliokusanya vipande vya sentensi744 na amri hizi. Kwa kuwa, mababa wa Kanisa wakati fulani huizungumzia sehemu moja, na wakati mwingine sehemu nyingine ya toba na siyo kama sehemu moja tu, bali sehemu zote mbili, yaani majuto na imani. Ingefaa sana kuchagua na kuziunganisha sentensi hizi.
94. Tertulliano anazungumzia kwa upeo sana kuhusu imani hasa akisifu kiapo katika kitabu cha nabii: “Waambie, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu; na kuiacha njia yake mbaya, akaishi.”745 Kwa kuwa, anapotoa kiapo kuwa, hafurahii kifo cha mtu mkosaji, Mungu huonyesha kwamba, anahitaji imani ambayo kwayo tunamwamini anapoapa na kusadiki kwa uhakika kwamba, anatusamehe. Lazima mamlaka ya ahadi za kimungu yenyewe ithaminiwe kati yetu. Basi, sasa, ahadi hii inathibitishwa kwa kiapo. Hivyo, mtu yeyote akisisitiza kwamba, hatasamehewa, anamshtaki Mungu kwa ajili ya kosa la kusema uongo kwamba Mungu hakuapa kweli. Kufuru hii ni kali mno kuliko inavyofikirika. Hivi ndivyo
742 Decr.Grat. II. C. 33.q.3. De poen. D. 3. c. 1.
743 Decr. Grat. II. C. 33. q. 3. De poen. d. 3. c. 4.
744 Fetwa.
745 Eze. 33: 11
Tertulliano asemavyo: “Anatukaribisha katika wokovu kwa zawadi na pengine katika kiapo. Mungu anaposema, ‘kama niishivyo,’ angependa aaminiwe. Heri wale ambao Mungu hukitoa kiapo kwa ajili yao! Ole wetu wenye baa mno kama hatutamwamini Bwana hata atokiapo kiapo!”746
95. Imani hii sharti isadiki kabisa kwamba, Mungu anatusamehe bure kwa ajili ya Kristo, kwa ajili ya ahadi yake, na siyo kwa ajili ya matendo, majuto, toba au ridhaa zetu. Maana, imani ikitegemea matendo haya, mara moja itakosa uhakika kwa sababu dhamiri yenye hofu huyaona matendo haya kuwa yasiyo na thamani yoyote. 96. Kuhusu toba, Ambrosio anasema ifuatavyo kwa njia iliyo wazi kabisa: “Basi, inatulazimu kuamini kutubu ndipo tusamehewe kwa njia hii ambayo tunategemea msamaha kwa imani sawa na imani ipatikanayo kwenye makubaliano yaliyoandikwa.”747 Tena: “Ni imani tu ambayo huzifunika dhambi zetu.”74897. Kwahiyo kuna sentensi za mababa wa Kanisa zinapatikana katika maandiko yao, siyo kuhusu majuto na matendo tu, bali pia kuhusu imani. Lakini kwa sababu wapinzani wetu hawaelewi asili ya toba na hata lugha ya mababa wa Kanisa, wanachagua misemo ya sehemu moja ya toba kuhusu matendo kwa sababu hawaelewi misemo mingineyo kuhusu imani na hivyo basi, huiruka.
Ungamo na Matendo ya Upatanisho 98. Watu wema wanaweza kuelewa kwa urahisi umuhimu wa kuyatunza mafundisho sahihi kuhusu sehemu za toba tulizozizungumzia hapo juu Yaani, majuto na imani. Kwa sababu hiyo, tumeuweka mkazo kwenye mafungu haya bila kujadiliana sana kuhusu ungamo na matendo ya upatanisho.749 99. Kwa maana, sisi pia tunashika ungamo, hasa kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Yaani, Neno la Mungu ambalo linatangaziwa watu binafsi kwa mamlaka ya funguo. 100. Kwa hiyo, ni jambo la kukufuru kuondoa kanisani ondoleo la binafsi750. 101. Wale wanaodharau ondoleo la binafsi hawaelewi kamwe msamaha wa dhambi au mamlaka ya funguo. 102. Vinginevyo, kama tulivyosema awali, , hatuamini kwamba, kulingana na haki ya kimungu ni lazima, kutaja dhambi zetu zote moja kwa moja katika ungamo. 103. Jambo ambalo linabishaniwa na wengine kuwa hakimu hana budi kuifahamu kesi kamili kabla ya kuitangaza hukumu, halihusu jambo hilo hata kidogo kwa sababu huduma ya ondoleo la dhambi ni baraka au neema, na siyo hukumu au sheria. 104. Kwa sababu hiyo, wachungaji kanisani
746 ‘Tertulliano, De poenitentia’ 4.
747 ‘De poenitentia adversus Novatianos’ 2, 9.
748 Apologia proph. David 13, 63. Dondoo hili halitoki kwa Ambrosio.
749 Kilatini, “Satisfactiones.”
750 Kilatini: ‘absolutio,’ (Ondoleo), Kilatini: ‘remissio,’ (Msamaha).
wana mamlaka ya kusamehe dhambi; Hawana mamlaka ya kuchunguza dhambi za siri. 105. Tunaondolewa hata dhambi zile ambazo hatuzikumbuki. Kwa hiyo, ondoleo la dhambi ambalo ni sauti ya Injili ya kusamehe dhambi na kufariji dhamiri, halihitaji uchunguzi maalumu.
106. Ni upumbavu kabisa kuurejea hapa msemo wa Suleimani usemao: “Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako.”751 Suleimani hazungumzii ungamo bali alikuwa akitoa tu ushauri mdogo tu kwa ajili ya uchumi kwa mkuu wa kaya akimwambia awe makini kuhusu mali yake mwenyewe. Inampasa ajihini mali ya jirani hata amwagize kuitunza lakini asiiache hofu ya Mungu au imani au kutojali Neno la Mungu kwa njia hii. Lakini wapinzani wetu huigeuza misemo ya Maandiko Matakatifu kwa namna ya ajabu kumaanisha kitu chochote wanachotaka kumaanisha. Kulingana na tafsiri yao, “kujua” kunamaanisha kusikiliza ungamo, na “hali” maana yake ni siri za dhamiri na siyo tabia ya nje. “Kundi” linamaanisha watu. Hakika, ufafanuzi huu ni nadhifu kabisa kwa watu hawa ambao wanadharau masomo ya sarufi. Hata hivyo, mtu akitaka kurejea katika shauri hili kama mfano kutoka kwa bwana wa kaya, kumaanisha mchungaji, lazima aifafanue “hali” kama tabia ya nje. Usawa wa namna hiyo angalau utakuwa na maana zaidi.
107. Tuyaacheni mambo yalivyo. Zaburi hutaja ungamo mara kwa mara. Kwa mfano, “Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA; nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.”752 Ungamo la dhambi la namna hii lililotolewa kwa Mungu, lenyewe ni majuto. Maana, ungamo litolewapo kwa Mungu, lazima litoke moyoni na siyo tu kwa sauti vile wanavyofanya wachekeshaji katika michezo. Kwa hiyo, ungamo la jinsi hiyo ni majuto. Katika hali hii tunaisikia ghadhabu ya Mungu na tunakiri kwamba, Mungu ana hasira ya haki na hawezi kutulizwa kwa matendo yetu. Na hivyo, tunatafuta huruma kwa ajili ya ahadi ya Mungu. 108.Ungamo ni la namna hii: “Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, . . . na kuwa safi utoapo hukumu.”753 Maana yake: ninakiri kwamba, mimi ndimi mkosaji anayestahili hukumu ya milele na siwezi kutekeleza haki au stahili zangu kinyume na hukumu yako. Hivyo, ninatangaza kwamba, wewe ndiwe mwenye haki unapotuhukumu na kuadhibu. Ninatangaza kwamba, unashinda wakati wanafiki wanapokuhukumu na kusema kwamba, huna haki ya kuwaadhibu, au kuwahukumu wale waliostahili sana. Hata stahili zetu haziwezi kutekelezwa kinyume na hukumu yako. Badala yake, tutahesabiwa haki, ukituhesabia haki, na ukituangalia kama wenye haki kwa njia ya huruma yako. 109. Labda mtu
751 Mit. 27: 23
752 Zab. 32: 5
753 Zab. 51: 4
angetaka kuinukuu Yakobo 5: 16: “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi.” Lakini ungamo linalotolewa kwa makasisi halizungumziwi hapa bali suluhisho kati ya ndugu na ndugu, kwa maana ungamo linaamriwa kuwa baina ya wote wawili.
110. Wapinzani wetu wanasisitiza kwamba, kutaja makosa moja kwa moja katika ungamo ni lazima kulingana na haki ya kimungu. Wanaamini kwamba, watakuwa wakiwashutumu wanatheolojia wengi waliokubalika mno. Japo, tunalikubali ungamo na kuona kuwa, kwa kiasi fulani, uchunguzi unafaa ili watu wapate kufundishwa vizuri zaidi, lazima uchunguzi utumiwe kwa kiasi, ili dhamiri zisitekwe kabisa. Hazitaweza kuwa na amani kama zikidhania kwamba, haziwezi kupata msamaha wa dhambi bila dhambi zao zote kuhesabiwa kikamilifu. 111. Ni uongo mtupu kusisitiza kama jinsi wapinzani wetu wafanyavyo katika hoja yao kwamba, ungamo kamili ni la lazima kwa ajili ya wokovu. Haiwezekani kabisa! Dhamiri za watu zinawekewa minyororo ya jinsi gani wanapolidai ungamo kamili!754 Ni lini basi, dhamiri zinaweza kujihakikishia kwamba ungamo lake limekamilika? 112. Waandishi wa Kanisa hulitaja ungamo lakini kwa njia ya kuelezea juu ya ungamo la hadharani,755na siyo juu ya jambo hilo la kutaja dhambi za siri. Kwa sababu wale waliokuwa watovu wa imani au wakosaji wa hadharani hawakupokelewa bila matendo ya upatanisho, waliungama kwa wachungaji756 ili matendo haya ya upatanisho yalingane na makosa yao. Haya yote hayahusu hata kidogo majadiliano haya ya kutaja makosa moja kwa moja tunayoyazungumzia. Ungamo la namna hiyo lilifanyika, siyo kwamba, matendo ya upatanisho na msamaha wa dhambi havitakuwepo mbele za Mungu, bali hawakuweza kuamuru matendo haya ya upatanisho bila kuifahamu aina ya kosa. Naam, Makosa tofauti yalikuwa na kanuni tofauti.
113. Neno hili “upatanisho,”757ni kumbukumbu ya lile ungamo la hadharani. Mababa watakatifu hawakupenda kuwarudisha kundini wale waliokuwa watovu wa imani au waliokosa hadharani isipokuwa toba zao zilichunguzwa kwanza na kutazamwa hadharani kwa kadiri ilivyowezekana. Inaonekana walikuwa na sababu nyingi kwa ajili ya matumizi ya namna hiyo. Maonyo kwa wale waliokuwa watovu wa imani yalitumiwa kama mfano kwa wengine wote jinsi ufafanuzi wa kanuni758 unavyosema. Haikuwa pia uadilifu kuwapokea wakosaji
754 Kilatini: ‚Confessio integra.‘
755 Kilatini: ‘Ritus publicae poenitentiae.’ Kawaida, Kanisa la Zamani lilitumia ungamo la hadharani peke yake na si ungamo la siri.
756 Kilatini: ‘Presbyteri,’ Kijerumani: ‘Priester,’ yaani, makasisi au mapadre.
757 Kilatini: ‘Satisfactio,’ maana yake: ridhaa, suluhisho.
758 Glossa in Decr. Grat. II. C. 24. q. 3. c. 18.
hadharani katika Ekaristi mara moja. Mapokeo haya yalipitwa na wakati kabisa na hayakuhitaji kurudishwa tena kwa sababu hayakuwa ya lazima mbele za Mungu kwa ajili ya msamaha wa dhambi. 114. Mababa wa Kanisa pia hawakuamini kwamba, watu hustahili msamaha wa dhambi kwa mapokeo ya matendo kama haya. Kwa kawaida basi, desturi za namna hii huwashawishi wasio wazoefu kufikiri kwamba, matendo haya hustahili msamaha wa dhambi mbele za Mungu. Yeyote anayeliamini hili anaamini kwa njia ya Kiyahudi na ya Kipagani. Mataifa pia yalikuwa na matendo kadhaa ya kufidia makosa ambayo kwayo walidhania kuwa walipatanishwa na miungu yao. 115. Hata hivyo, mapokeo haya hayafuatwi zaidi. Neno “upatanisho” bado limebaki pamoja na desturi ya kuyaamuru matendo fulani ya upatanisho katika ungamo. Matendo haya yanafasiliwa kama matendo yasiyoshurutishwa.759 Sisi tunayaita matendo ya upatanisho wa kikanuni.760116. Msimamo wetu kuhusu matendo haya ni huo huo, kuhusu kutaja dhambi katika ungamo la dhambi moja kwa moja, kwamba, matendo ya kikanuni siyo ya lazima kwa ajili ya msamaha wa dhambi kulingana na haki ya kimungu. Hali kadhalika, mapokeo yale ya kale kuhusu matendo ya upatanisho katika ungamo la hadharani hayakuwa ya lazima kwa ajili ya msamaha wa dhambi kulingana na haki ya kimungu. Hatuna budi kuyashika mafundisho ya imani, kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi kwa imani kwa njia ya Kristo na siyo kwa matendo yetu, ama yatangulie au yafuate. Kwa sababu hiyo, tumejadili vya kutosha kuhusu mafundisho ya matendo ya upatanisho wa ridhaa, watu wasianze kuyatenda ili kuitia giza haki ya imani, wasifikiri pia kwamba, kwa ajili ya matendo haya, wanapokea msamaha wa dhambi. 117. Misemo mingi ya Madaktari Wanazuoni ya kufasili matendo ya upatanisho imeyaunga mkono makosa haya kwa mfano, tendo la upatanisho linafanyika ili kuituliza ghadhabu ya Mungu.761
118. Wapinzani wetu bado hukubali kwamba, matendo ya upatanisho hayafai lolote katika kuoindoa hatia. Badala yake, wao hufikiri kwamba, yanaweza kuchangia katika ukombozi wa adhabu za Purgatorio au adhabu nyinginezo. Naam, wao hufundisha kwamba, Mungu huondoa hatia anaposamehe dhambi. Hata hivyo, kwa sababu kosa linabidi kuadhibiwa kwa haki ya kimungu, adhabu za milele zinapaswa kubadilishwa kuwa za muda. Wanaongezea zaidi kwamba, sehemu ile ya adhabu ya muda husamehewa na mamlaka ya funguo, na masalio lazima yakombolewe kwa matendo ya upatanisho. Haiwezekani kuelewa ni adhabu zipi zinasamehewa na mamlaka ya funguo, isipokuwa wanamaanisha sehemu za adhabu za Purgatorio. Kwa jinsi hiyo, matendo ya upatanisho
759 Kilatini: ‘opera non debita.’
760 Kilatini: ‘satisfactiones canonicae.’
761 Gabriel Biel, In sent. IV. D. 16. q. 2. a. 1. C.
yangeweza kukomboa adhabu za Purgatorio peke yake. Wanasisitiza zaidi kwamba, matendo haya ya upatanisho yatahalalika hata yakitendwa na wale walioanguka tena katika dhambi ya mauti,762kana kwamba, wale walio katika hali ya dhambi ya mauti wangeweza kuituliza ghadhabu ya Mungu. 119. Nadharia hii yote ni hadithi tu iliyobuniwa hapo awali bila mamlaka ya Maandiko Matakatifu au waandishi wa kale wa Kanisa. Hata Petro Lombardo mwenyewe hasemi hivyo kuhusu matendo ya upatanisho. 120. Madaktari Wanazuoni waliona kwamba, matendo ya upatanisho yalipatikana kanisani bila kuelewa kwamba, mapokeo haya ya hadharani yalianzishwa ili yawe mifano na yawajaribu wale walioomba kupokelewa katika Kanisa, yaani kwamba hawakuliona hili kuwa nidhamu na hata kuwa jambo la kijamii.763 Hivyo, kwa uzushi walidhania kwamba, mapokeo haya yalifuatwa, sio kwa ajili ya nidhamu katika Kanisa, bali ili kumtuliza Mungu. Na kama ilivyo kila pahali, wamechanganya mambo ya kiroho na ya kijamii,764ilihali wamekosea vibaya kuhusu mafundisho ya matendo ya upatanisho. 121. Lakini ufafanuzi wa kanuni mara nyingi huonyesha kwamba, mapokeo haya yalianzishwa kwa ajili ya nidhamu ya kanisa.
122. Basi, angalieni jinsi wapinzani wetu waziteteavyo hadithi zao hizi za uongo katika Hoja ambayo wanathubutu kuisisitiza kwa Enzi ya Kaisari. Wananukuu misemo mingi ya Maandiko Matakatifu ili kulipamba jambo hili mbele ya watu wasiokuwa wazoefu kana kwamba, lina mamlaka katika Maandiko Matakatifu, japo halikufahamika wakati wa Petro Lombardo. Hizi ni aya wanazonukuu: “Basi zaeni matunda yapasayo toba;”765 “Vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki.”766 Hali kadhalika, Kristo alihubiri kuhusu toba: “Tubuni.”767 Kristo aliwaamuru mitume wahubiri toba.”768 Petro alihubiri toba katika Mdo. 2:38. Baadaye wanainukuu misemo kadhaa ya mababa wa Kanisa na kanuni na kuhitimisha kwamba, matendo ya upatanisho yasiondolewe kutoka kanisani kinyume na neno dhahiri la Injili na amri za masinodi na mababa wa Kanisa. Wale walioondolewa na kasisi wanapaswa wafanye toba iliyoamriwa pia, kulingana na msemo wa Paulo: “Ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.”769
762 Kilatini: ‘peccatum mortale.’
763 Kilatini: ‘res politica.’
764 Melanchthon, ‘Πολιτικα.’
765 Mt. 3: 8
766 Rum. 6: 19
767 Mk. 1: 15
768 Lk. 24: 17
769 Tito 2: 14
123. Mungu na awaadhibu hawa madaktari wanazuoni wanaopotosha , kwa uovu kabisa, kulivuruga Neno la Mungu kulingana na njozi zao potovu! Ni vipi mtu mwema hangechochewa na ufidhuli huu? Kristo anasema: “Tubuni!” Mitume wanahubiri toba. Kwa hiyo, adhabu za Purgatorio hulipia adhabu za milele! Hivyo, funguo zina mamlaka kuondoa sehemu ya adhabu ya Purgatorio! Basi, matendo ya upatanisho huzikomboa adhabu za Purgatorio! Basi, ni nani aliyewafundisha hawa punda upembuzi wa namna hiyo? Lakini haya siyo upembuzi au ustaarabu, bali ni ghiliba kabisa. Wanalinukuu neno “tubuni” ili wale wasioelimika wakiusikia msemo huu ukirejewa dhidi yetu wahitimishe kwamba, sisi tunaiondoa toba nzima. Kwa ujanja wa namna hiyo, wanajaribu kufarakisha nafsi za watu na kuchochea chuki ili wale wasioelimika waanze kupiga kelele dhidi yetu: “Wale wazushi waliolaaniwa na wanaokataa toba, waondolewe katikati ya wanadamu!”
124. Tunatumaini kwamba, miongoni mwa watu wema, usingiziaji huu hautafaulu. Pia Mungu hatavumilia ufidhuli na uovu huu kwa muda mrefu zaidi. Jambo muhimu sana ni kwamba, Kuhani Mkuu wa Roma haitunzi vizuri heshima yake anapowatumia watetezi hawa na kuzikabidhi hukumu zao. Kwa maana, kwa njia ya ukiri wetu, tumeshughulikia karibu muhtasari wa mafundisho yote ya Kikristo. Ingefaa sana kuwatumia mahakimu wenye mafundisho na imani ya kuaminika kuliko hawa Madaktari Wanazuoni walioandika Hoja hii. Mahakimu hao wangeweza kutoa uamuzi wao kuhusu mambo haya makubwa na tofauti sana.
125. Kulingana na busara yako, ilikuwa juu yako wewe Campeggi770 kuhakikisha kwamba, mtu asiandike chochote kuhusu mambo haya makubwa ambayo sasa au baadaye yangeweza kupunguza heshima ya Kiti cha Roma.771 Kama kiti cha Enzi ya Roma kikiona kwamba, ni vizuri mataifa yote kukubali kuwepo kwake kama mwalimu mkuu wa imani, kinapaswa kuangalia kwa makini kwamba, wasomi na waadilifu wanachunguza masuala ya kidini. Pengine ulimwengu utasemaje iwapo andiko la wapinzani wetu litawekwa nuruni?772 Kizazi kijacho kitafikiri nini kuhusu kashfa hizo? 126. Unaona, Campeggi, kwamba huu ndio wakati wa mwisho ambao Kristo aliutabiri kuwa na hatari sana kwa uchaji wa kweli. Hivyo basi, ingewabidi ninyi mnaoketi katika mnara wa doria na kuyaongoza mambo ya kidini, kulazimika kufuata busara na jitihada zisizokuwa za kawaida nyakati hizo. Msipoangalia vizuri, kuna ishara nyingi ambazo zitaionyesha mapinduzi katika Dola ya Roma. 127.Utakosea kama
770 Lorenzo Campeggi (1474-1539) alikuwa balozi wa Papa wa Roma katika Baraza la Augsburg, alimtaka Kaisari awang’oe Walutheri kwa ajili ya vurugu.
771 Yaani, Kiti cha Enzi cha Askofu wa Roma.
772 Hoja ya ‘Ukiri wa Augsburg’ mwishowe ilitolewa rasmi mwaka wa 1573.
ukifikiri kwamba, makanisa yataweza kutawaliwa kwa nguvu na silaha tu. Watu wanahitaji mafundisho ya imani. Unadhani ni watu wangapi watapatikana, siyo tu katika Ujerumani, bali huko Uingereza, Uhispania, Ufaransa, Italia na mwishowe hata mjini Roma kwenyewe, ambao walipoona majadiliano yaliyotokea kuhusu mambo haya makubwa mno, walianza kuwa na mashaka kuhusu vifungu kadhaa? Je, ni wangapi wamekasirika kimya kimya kwasababu, mmekataa kuyachunguza mambo haya makubwa na kuyahukumu kwa njia halisi? Hamyaelezei mambo haya kwa dhamiri zilizotetereka. Badala yake, mnatuamuru sisi tudhulumiwe na kuangamizwa kwa silaha. 128. Kuna watu wengi wema ambao, mashaka kama haya ni makali kushinda kifo. Unakosea kutozingatia vya kutosha imani,773ikiwa unadhani, watu wema hukerwa kwa kiasi kidogo tu pengine wakianza kuwa na mashaka kuhusu mfumo mwingine wa imani. Mashaka kama haya hayana budi kuzaa chuki kali zaidi dhidi ya hao. Wakiwa na wajibu wa kutunza dhamiri, watakataa kuruhusu hata kidogo suala lifafanuliwe. 129. Hapa hatusemi kwamba, mnapaswa kuiogopa hukumu ya Mungu, kwa maana Makuhani Wakuu hufikiri kwamba, wanaweza kulichukulia jambo hili kuwa rahisi maana wanashika funguo, na hivyo, wenyewe wataweza kujifungulia mbingu kwa hiari. Tunazungumzia juu ya hukumu za wanadamu na madai ya kimya ya mataifa yote; Sasa, wanadai kwamba masuala haya yachunguzwe na kuwekwa sawa kabisa ili nafsi za watu wema ziponywe na kuwekwa huru kutoka katika mashaka yote. Wewe mwenye busara, utaweza kutambua kwa urahisi ni nini kitakachotokea wakati ujao iwapo chuki hii itazuka kwenu? Lakini mtaweza kuyavutia mataifa yote kwa fadhili hii ikiwa mtaziponya dhamiri zenye mashaka, maana wote wenye busara wanalichukulia jambo hili kuwa la thamani sana. 130. Hatusemi hivyo kwasababu tuna mashaka kuhusu ukiri wetu. Tunajua kwamba, ukiri wetu ni wa kweli, mtakatifu na wenye manufaa kwa dhamiri za wacha Mungu. Lakini, labda kuna watu wengi mahali pengine wenye mashaka mazito kuhusu mambo muhimu lakini hawawasikilizi walimu bora ambao wanaweza kuziponya dhamiri zao.
131. Basi, turudi tena katika nchachonge774 ya suala hili! Vifungu vya Maandiko Matakatifu vilivyonukuliwa na wapinzani wetu havisemi lolote kuhusu matendo ya upatanisho wa kanuni au mawazo ya Madaktari Wanazuoni kwa kuwa inajulikana kwamba, mambo haya yalitokea tu hapo awali.775 Kwa sababu hiyo, mawazo yao ni upotoshaji mtupu na uvunjaji tu wa Maandiko Matakatifu. Sisi tunasema kwamba, toba, yaani, kuongoka, na kuzaliwa upya, lazima vifuatiwe
773 Kilatini: ‘religio,’ yaani, “dini.” Katika muktadha huu, ina maana sawa na “imani.”
774 Kilatini: ‘propositum.’
775 Tangu Petro Abailard (1079-1142).
na matunda na matendo mema katika maisha yote. Ugeuzaji na majuto hauwezi kuwa wa kweli pale ambapo mwili hautaudhiwa na matunda mema hayatazaliwa. Vitisho vya kweli na huzuni za kweli za nafsi haviwezi kuendekeza anasa. Imani ya kweli haiwi bila shukrani kwa Mungu wala haizidharau amri zake. Yaani, hakuna toba ya ndani ambayo haionekani katika nidhamu ya mwili. 132. Hiki tunachosema ndiyo shabaha ya Yohana anaposema: “Basi, zaeni matunda yapasayo toba.”776 Hali kadhalika, Paulo anaposema: “vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki,”777 jinsi anavyosema penginepo: “itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu”778 n.k. Kristo asemapo, “tubuni,”779 kwa hakika anazungumzia toba iliyo kamili, yaani, upya wote wa maisha na matunda yake. Hazungumzii matendo ya upatanisho wa kinafiki ambao Madaktari Wanazuoni huufikiria kufidia adhabu za Purgatorio au adhabu zingine ingawa zinatoka kwa watu wanaoishi katika dhambi za mauti.
133. Sababu nyingi zinaweza kukusanywa kwa shabaha ya kuonyesha kwamba, misemo hii ya Maandiko Matakatifu haifungamani hata kidogo na matendo ya upatanisho ya Madaktari Wanazuoni. Wanadhania kwamba, matendo ya upatanisho siyo matendo ya lazima. Lakini Maandiko Mataktifu yanahitaji matendo ya lazima katika sentensi hizi. Sauti hii ya Kristo ni sauti ya agizo kabisa: “Tubuni!” 134. Kadhalika, wapinzani wetu huandika kwamba, mtu atubuye akikataa kukubali matendo ya upatanisho, hatendi dhambi bali atalazimika kulipia adhabu katika Purgatorio. Hivyo, bila shaka, vifungu hivi ni maagizo yaliyofungamana na maisha haya: “Tubuni,” “. . . zaeni matunda yapasayo toba, “ “. . . vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki.” Kwa sababu hiyo, haviwezi kugeuzwa ili vimaanishe matendo ya ridhaa, ambayo yanaweza kukomeshwa kwa hiari, kwa maana mtu hawezi kukataa maagizo ya Mungu.. 135. Tatu, vyeti vya upatanisho huondoa matendo ya upatanisho780 kama sura ya juu ya ‘Toba na msamaha’ inavyofundishwa katika mwanzo wa maneno haya: “Maadamu kutoka hili . . .”781 Lakini vyeti vya upatanisho havituondoi kutoka katika maagizo kama: “Tubuni” na “zaeni matunda yapasayo toba.” Hivyo, inajulikana wazi kwamba, misemo hiyo ya Biblia imegeuzwa vibaya hata kuwa matendo ya upatanisho wa kanuni. Basi, litazameni litakalofuatia! 136. Kama adhabu za Purgatorio ni matendo ya upatanisho au mateso ya upatanisho782 au
776 Mt. 3: 8
777 Rum. 6: 19
778 Rum. 12: 1
779 Mt. 4: 17
780 Matendo ya kanuni, si ya Biblia.
781 Decr. Greg. IX, V. 38. c. 14.
782 Neno la Kilatini lililobuniwa na Philipp Melanchthon, ‘satispassiones.’
iwapo matendo ya upatanisho ni fidia za adhabu za Purgatorio, mbona basi, sentensi hizo haziamuru nafsi ziadhibiwe katika Purgatorio? Kwa kuwa, hili linatokana na wapinzani wetu kwamba, hatuna budi kuzifafanua sentensi hizi kwa njia mpya kabisa: “Zaeni matunda yapasayo toba” na “tubuni” zitamaanisha, kuteswa na adhabu ya Purgatorio baada ya maisha haya. 137. Lakini ni karaha kubwa kupoteza wakati zaidi kuupinga upumbavu mwingi zaidi wa wapinzani wetu. Ni wazi kwamba, Maandiko Matakatifu yanazungumzia kuhusu matendo ya lazima, juu ya upya wote wa maisha, na wala siyo jitihada hizi za matendo yasiyo ya lazima wayazungumziayo wapinzani wetu. Hata hivyo bado kwa hadithi hizi za uongo wanatetea kabisa madaraja ya watawa, mauzo ya misa na maadhimisho yasiyo na mwisho kwajili ya kuridhisha adhabu, kama siyo hatia.
138. Kwa kuwa, nukuu zao za Maandiko Matakatifu hazizungumzii kuwa matendo yasiyokuwa ya lazima783 yafidie adhabu za milele; wapinzani wetu husisitiza kwa njia ya jinai kwamba, matendo ya upatanisho wa kanuni yanafidia adhabu hizi. Funguo hazina agizo la kubadilisha baadhi ya adhabu au kuziondoa sehemu zake. Ni wapi Maandiko Matakatifu yanalizungumzia hili? Kristo anazungumzia kuhusu msamaha wa dhambi anaposema: “yo yote mtakayoyafungua . . .”784 n.k. Kifo cha milele kimeondolewa kwa msamaha na uzima wa milele umetolewa. Kristo hazungumzii hapo kuhusu kuagiza adhabu anaposema “yo yote mtakayoyafungua” bali anabakiza dhambi za wale wasiogeuka. 139. Sentensi ya Petro Lombardo785 kuhusu sehemu za adhabu ambazo zinabidi zisamehewe zimetolewa kutoka upande wa adhabu za kanuni ambazo wachungaji walizisamehe sehemu yake. Basi, hata hivyo, tunaamini kwamba, lazima toba izae matunda mema kwa ajili ya utukufu na amri ya Mungu na kwamba matunda mema haya, kama kufunga na kuomba kwa kweli, sadaka za kweli, yanatokana na maagizo ya Mungu. Lakini hakuna mahali popote katika Maandiko Mtakatifu tunaambiwa kwamba, adhabu za milele hazisamehewi isipokuwa kwa ajili ya adhabu ya Purgatorio au matendo ya upatanisho wa kanuni. Yaani, kwa ajili ya matendo maalumu yasiyokuwa ya lazima au kwamba, mamlaka ya funguo yana amri ya kuzibadilisha adhabu, au kuzisamehe sehemu zake. Ulikuwa wajibu wa wapinzani wetu kulidhibitisha jambo hilo.
140. Kifo cha Kristo ndicho ridhaa zaidi, Siyo tu kwa ajili ya hatia bali pia kwa ajili ya kifo cha milele kulingana na aya hii: “ewe mauti, nitakuwa kifo chako.”786 Kwa hiyo, ni udubwana mkubwa kusema kwamba, ridhaa ya Kristo
783 Kilatini: ‘Opera non debita.’
784 Mt. 18: 18
785 Sent. IV. D. 18. 7.
786 Hos. 13: 14. Sentensi hii imedondolewa kulingana na Toleo la Vulgata. ‘Union Version,’ “Ewe mauti, ya
hukomboa hatia lakini adhabu zetu hukomboa kifo cha milele. Basi, kulingana na kifungu (Hos. 13:14) “nitakuwa kifo chako,” yanapaswa yachukuliwe kwa kutokumaanisaha Kristo bali matendo yetu, na wala hata siyo matendo yaliyoamriwa na Mungu bali taratibu batili za dini zilizobuniwa na wanadamu. Hizo zinakisiwa kuyaondoa mauti japo zinatendeka katika dhambi ya mauti. 141. Tunasikitika kupita kiasi tunapousimulia upumbavu huu wa wapinzani wetu. Mtu yoyote akiuchunguza, hana budi kukasirika kabisa kuhusu mafundisho ya kishetani ambayo Ibilisi mwenyewe ameyapakaza kanisani ili kuukandamiza ufahamu wa sheria na Injili, toba, uhuishaji, na baraka za Kristo. 142. Kuhusu sheria wanasema: Mungu ameukubali unyonge wetu na ameweka mpaka fulani ambao mtu anapaswa kuushika kwa makini, yaani, amri787 ili, juu ya haya, apate kuridhisha makosa yaliyotendeka kwa matendo yazidiyo kiwango.788 Hapa, wanadhania kwamba, sisi tunaweza kuitimiza sheria zaidi kuliko inavyohitajika. Lakini Maandiko Matakatifu mahali pote yanasema kwamba, tunapungukiwa sana sana katika ukamilifu ule unaohitajiwa na sheria. Watu hawa hufikiria kwamba, Sheria ya Mungu hushughulikia haki ya nje na ya kiraia. Hawaoni kwamba, sheria inatuhitaji tumpende Mungu kwa “mioyo yetu yote”789 n.k. na kuilaani, katika asili, tamaa yote790 mbaya. Kwa hiyo, hakuna atendaye kulingana na sheria inavyohitaji. Katika ujinga wetu tunafikiria kwamba, tunaweza kutenda hata zaidi. Ingawa tunaweza kutenda matendo ya nje ambayo Mungu hakuyaamuru katika sheria yake, ni tegemeo la bure na la kukufuru kuamini kwamba, tukifanya hivyo sheria ya Mungu inaweza kuwa imetimizwa.
143. Maombi ya kweli, sadaka za kweli, na kufunga kwa kweli vina amri ya Mungu; Vinapokuwa na amri ya Mungu, haviwezi kuwa bila dhambi. Basi, matendo hayo yasipoagizwa na sheria ya Mungu, ila yameundwa kutokana na mapokeo ya binadamu, ni matendo ya mapokeo ya wanadamu ambayo kwayo Kristo anasema: “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”791 Hii ni mifungo fulani iliyoanzishwa, siyo kwa kuutawala mwili, bali kama Scotus792 asemavyo, ili kumtolea Mungu heshima na kufidia kifo wapi mapigo yako?” 787 Mafundisho ya Uwazuoni katika Kanisa la Roma yalitofautisha amri (‘praecepta’) na mashauri ya Kiinjili (‘consilia evangelica’). Kwa mafundisho ya Uwanazuoni – k.m. mtaalamu wa Kifransiskano Bonaventura (Giovanni di Fidanza, mnamo 1217-1274) “Daktari wa Kiserafi” (‘Doctor seraphicus’) – amri zinawahusu watu wote kikamilifu wakati mashauri yanawahusu watu maaalumu. Yaani, walioweza kuistahili neema kwa njia ya kuyafuata mashauri haya, kama useja, umaskini, utiifu maalumu n.k. Kawaida, mashauri yalibadilika katika madaraja ya wamonaki kuwa amri halisi, na Amri halisi za Mungu kuwa mashauri tu.
788 Kilatini: ‘Opera supererogationis.’
789 Kum. 6: 5
790 Kilatini: ‘Concupiscentia.’
791 Mt. 15: 9
792 Yohana Duns Scotus (mnamo 1265-1308) , ‘Doctor subtilis’ au ‘Doctor Marianus’ alikuwa mwanatheologia
cha milele. Kadhalika, idadi fulani ya sala, namna fulani ya sadaka vikitendeka kama matendo yenyewe793 ili kuwa ibada za Mungu, vinampatia Mungu heshima yake kama tendo lenyewe la kufidia kifo cha milele. Wanayapatia matendo haya ustahili wa upatanisho kama matendo yenyewe, kwa maana wanafundisha kwamba, huwasaidia hata wale wanaopatikana katika hali ya dhambi ya mauti. 144. Matendo mengine, kama hija, yanaenda mbali zaidi na Amri za Mungu. Kuna aina nyingi za hija, mtu mmoja anaweza kusafiri akiwa amevaa silaha, na mwingine akawa anatembea kwa miguu mitupu. Kristo huyaita matendo haya, ibada zisizokuwa na maana. Kwa sababu hiyo, hayafai katika kuituliza ghadhabu ya Mungu kama wapinzani wetu wanavyodai. Hata hivyo, wanayapamba matendo haya kwa majina adhimu. Yanaitwa matendo yazidiyo kiwango.794 Wanayapatia heshima ya kustahili kuilipia gharama ya mauti ya milele. 145. Hivyo, hata matendo ya Amri za Mungu yanastahabiwa. Kwa njia hii, Sheria ya Mungu inavurugwa maradufu: kwanza, kwa njia ya kudhania kwamba, matendo ya nje ya kiraia huitimiza Sheria ya Mungu, na pili, kwa njia ya kuyaongezea mapokeo ya wanadamu ambapo matendo yao yana cheo juu ya matendo ya Sheria ya Mungu.
146. Licha ya hayo, toba na neema vinafanyika giza. Naam, mauti ya milele hayawezi kufidiwa kwa matendo ambayo ni fidia ya bure na hayawezi kudhukiwa katika maisha haya yenye ladha ya kifo. Hatuna budi kuyaweka mambo tofauti kabisa dhidi ya kifo kinapotushambulia. Hali kadhalika, ghadhabu ya Mungu inashindwa na imani katika Kristo. Vile vile, imani katika Kristo inashinda kifo kama jinsi Paulo anavyosema: “Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.”795 Hasemi: “Atupaye kushinda tukiweka matendo yetu ya upatanisho dhidi ya kifo.” 147. Wapinzani wetu wanahusika na uvumi usio na kazi kuhusu msamaha wa hatia. Hawaoni ni kwa jinsi gani moyo utawekwa huru katika ghadhabu ya Mungu na kifo cha milele kwa imani katika Kristo, hatia ikisamehewa. Basi, kwa kuwa kifo cha Kristo ni ridhaa ya mauti ya milele na wapinzani wetu wenyewe hukubali kwamba, matendo ya upatanisho siyo matendo ya lazima, bali matendo ya mapokeo ya wanadamu, ambayo Kristo huyaita matendo ya ibada yasiyokuwa na maana,796 tunaweza kutamka kwa dhati kwamba, matendo ya upatanisho wa kanuni siyo ya lazima kulingana na haki ya kimungu kwa msamaha wa hatia ama kwa adhabu ya milele au adhabu ya wa Uwanazuoni wa Daraja la Kifransiskano. Alisisiza umuhimu wa upendo na nia kuliko ujuzi na akili jinsi Tomaso wa Akuino alivyosisitiza. In sent. IV. D. 15. q. 1. a. 3.
793 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
794 Kilatini: ‘Opera supererogationis.’
795 1 Kor. 15: 57
796 Mt. 15: 9
207
Purgatorio.
148. Wapinzani wetu wanapinga kwamba, kisasi au adhabu ni ya lazima kwa toba kwa sababu Agostino anasema: “Toba ni kisasi kinachoadhibu” 797 n.k. Tunakubali kwamba, kisasi au adhabu ni ya lazima katika toba, lakini siyo kama ustahili au malipo kama jinsi wapinzani wetu wanavyoyafikiria kuwa matendo ya upatanisho. Kwa kuwa adhabu imetajwa, wanaipotosha wakimaanisha tendo la upatanisho. Agostino hakuona kwamba, majuto ni malipo ya msamaha wa dhambi. Alijua kabisa kwamba, dhambi zinasamehewa bure kwa njia ya Kristo. Alijua kabisa kwamba, kifo cha Kristo ni dhabibu kwa ajili ya dhambi. Kwa sababu hiyo, daima inatubidi kuzielewa kwa njia iliyo halisi dondoo kuhusu kisasi na adhabu, tusiuvuruge msamaha bure wa dhambi au kuufanyia giza ustahili wa Kristo hata kuwatoa watu kwenye matumaini katika Kristo hadi kwenye adhabu inayosimama dhidi ya dhambi, lakini bila kuwa sababu za msamaha. Tunakubali kwamba, adhabu inapatikana katika toba lakini siyo kama malipo. Adhabu inapatikana kwa njia rasmi katika toba kwa sababu kuzaliwa upya kwenyewe hufanyika kwa kuifisha asili yetu ya kale. Hofu kuu na misukumo mingine inajiinua dhidi ya dhambi lakini siyo kama sababu za msamaha. Kwa hivyo, imani isipopatikana, majuto haya yangetoa tu kifo cha milele. Labda msemo wa Scotus ni mzuri anaposema kwamba, toba inatajwa kwa sababu ya adhabu798 alimradi adhabu isieleweke kuwa malipo ya msamaha. Zaidi ya hayo, Agostino hazungumzii adhabu zilizosamehewa kwa mamlaka ya funguo. Kwa sababu hiyo, siyo halali kuugeuza msemo huu ili kumaanisha matendo ya upatanisho. Anazizungumzia adhabu za kweli, yaani, hofu kuu na huzuni za kweli za nafsi katika toba. 149. Hata hivyo, katika mawanda haya, hatutoi dhiki ya nje ya mwili kwa sababu inafuata huzuni za moyo kwa hiari yake. Wapinzani wetu watakosea sana wakidhania kwamba, matendo ya upatanisho wa kanuni ni adhabu za kweli kuliko hofu kuu za kweli moyoni. Ni upuuzi kabisa kulivuruga neno “adhabu” kumaanisha matendo yale yasiyo na maana ya upatanisho bila kurejea vitisho vitishavyo dhamiri, ambavyo Daudi anavielezea akisema: “Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka.”799 Nani asiyependa kuvalia silaha na kutafuta Kanisa la Yakobo Mtakatifu au Basilika la Petro Mtakatifu,800 kuliko kuvumilia nguvu ya
797 Agostino bandia, “Toba ya kweli na ya uongo” 19, 35.
798 Katika Kilatini istilahi ‘poenitentia’ (toba), inakaribiana sana na istilahi ‘poena’ (adhabu); In. Sent. IV, d. 14, q. 1, a. 3.
799 2 Sam. 22 : 5
800 Santiago de Compostela kutoka kaskazini magharibi mwa Uhispania. Pahali hapo palidhaniwa kuwa kaburi la Yakobo Mtakatifu, nduguye Yesu na wakati wa Enzi ya Kati, palikuwa pahali muhimu pa hija. Wakristo walianza kuhama kutoka kituo hiki cha kidini na kurudia tena sehemu za Uhispania zilizokokuwa chini ya mamlaka ya Waarabu. Kanisa Kuu la Mt. Petro lilijengwa pia pahali muhimu pa hija.
huzuni isiyoelezeka hata katika toba ya kweli inayowajia hata watu wa kawaida?
150. Wapinzani wetu wanasema kwamba,kuadhibu dhambi ni kulingana na haki ya Mungu. Kwanza kabisa, wanaposisitiza kwamba, dhambi inapaswa kuadhibiwa, wanaonyesha vya kutosha kwamba, wanaidharau fadhili ya Kristo. Mungu amepanga kuwa, kifo cha Mwana wake ni malipo kwa ajili ya dhambi zetu, siyo kwa ajili ya adhabu zetu wala matendo yetu ya upatanisho. Ni ubwege wa jinsi gani kuyajali matendo yetu ya upatanisho wa Kristo! Zaidi ya hayo, Mungu akituadhibu kwa ukali mkubwa sana, hatupaswi kudhania kwamba, tunapatiwa msamaha wa dhambi kwa sababu ya adhabu ya namna hiyo. Kuna sababu mbili: kwanza, kutoiharibu fadhili ya Kristo; pili, dhamiri kutotulizwa kwa msamaha wa dhambi isipokuwa msamaha huo uwe wa bure. Mwishowe, Mungu akiadhibu kwa ukali mkubwa sana, adhabu hizo hazitahusika hata kidogo na funguo. Funguo hazina agizo lolote la kutoza au kusamehe adhabu ambazo ni matendo ya Mungu. Kwanza, tunaadhibiwa katika majuto makubwa anapoidhihirisha ghadhabu yake kwa njia za hofu kuu za toba. Daudi analishuhudia hili aasemapo: “BWANA, usinikemee kwa hasira yako.”801 Vile vile, Yer. 10: 24 inasema: “Ee BWANA, unirudi kwa haki; si kwa hasira yako, usije ukaniangamiza.” Hapa, adhabu kali zaidi huzungumziwa. Wapinzani wetu pia hukubali kwamba, toba inaweza kuwa kubwa kiasi cha kutohitaji tendo la upatanisho. Hivyo basi, majuto ni adhabu ya kweli kuliko tendo lolote la upatanisho. 151. Licha ya hayo, watakatifu wako chini ya kifo na mateso yote ya kawaida, jinsi Petro asemavyo katika 1 Petro 4: 17: “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii Injili ya Mungu utakuwaje?” Hata hivyo, kwa kawaida, mateso haya ni adhabu za dhambi kuhusu wacha Mungu na yana kusudi lingine tofauti, yaani, kuuwa dhambi, kwa sababu yanakomesha na kuuwa tamaa katika watakatifu. Maana, kifo kinadumu katika watakatifu ili kuuwa asili hii chafu. Hivyo, Paulo anasema: “Miili yenu iumekufa kwa sababu ya dhambi.”802 Maana yake: mwili unaharibiwa kwa sababu, wakati huo, dhambi inabaki ndani yake. 152. Kwa sababu hiyo, msalaba siyo adhabu bali ni mazoezi na matayarisho ya kufanywa upya. Kwani dhambi inapofishwa, na tunapojifunza kutafuta msaada wa Mungu na hata kufahamu uwepo wake katikati ya majaribu, tutaungama upungufu wetu wa kutokuamini uliomo mioyoni mwetu zaidi na zaidi na tutatiwa moyo na imani. Basi, kwa njia hii, kufanywa upya kwa roho kunakua jinsi Paulo asemavyo: “Bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.”803 Hali kadhalika,
801 Zab. 6:1
802 Rum. 8:10
803 2 Kor. 4:16
Paulo akizungumzia juu yake mwenyewe anasema: “Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu; ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu” (2 Kor. 1: 9). Isaya anasema: “BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.”804 Aidha, kifo ni adhabu kweli wakati moyo wenye hofu unahisi ghadhabu ya Mungu kulingana na aya hii: “Uchungu wa mauti ni dhambi.”805 153. Hata hivyo, baada ya imani kuzishinda hofu kuu za dhambi kwa watakatifu, kifo hakitakuwa adhabu kwa maana halisi pasipo msisimko huu wa ghadhabu. 154. Licha ya hayo, funguo hazitoshi wala haziwezi kusamehe adhabu hizi. Kwa sababu hiyo, matendo ya upatanisho hayahusu adhabu hizi, kwani funguo haziondoi kifo wala sehemu ya mateso yetu ya kawaida. Iwapo wanafidia adhabu hizi kwa matendo ya upatanisho sasa, mbona wanatuamuru tutende upatanisho katika Purgatorio?
155. Wanayakanusha mafundisho yetu kwa mifano ya Adamu na Daudi aliyeadhibiwa kwa sababu ya uzinzi wake.806 Wanaifanya mifano hii kuwa kanuni kwa watu wote kwamba: Kuwe na adhabu maalumu za muda zinazolingana na dhambi fulani na kuwekwa kwa njia ya mamlaka ya funguo. 156.Tumekwisha kusema hapo awali kwamba, watakatifu huvumilia adhabu ambazo ni kazi ya Mungu, kama vile toba au hofu kuu za dhamiri, yakiwemo matatizo mengine ya kawaida. Kadhalika, wengine huvumilia adhabu maalumu zilizowekwa na Mungu ili wawe mfano. Adhabu hizi hazihusu funguo hata kidogo kwa sababu funguo haziwezi kuziweka wala kuziondoa adhabu hizi, bali Mungu huziweka na kuziondoa mbali na huduma za funguo.
Kutokana na haya, kanuni ya kila pahali hailingani na hii kwamba, Daudi alipokea adhabu maalumu kwa sababu, mbali na mateso ya kawaida, kuna adhabu maalumu katika Purgatorio ambapo adhabu maalumu zinatangamana na matabaka maalumu. 157. Maandiko Matakatifu yanafundisha wapi kuwa hatuwezi kuwekwa huru kutoka katika mauti ya milele isipokuwa kwa fidia ya adhabu maalumu zipitazo mateso ya kawaida? Kinyume chake, daima Maandiko Matakatifu yanafundisha kabisa kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi bure kwa njia ya Kristo ambaye ni Mshindi wa dhambi na kifo. Hivyo, hatupaswi kuchanganya sifa za upatanisho na hili. Japo mateso bado yapo, Maandiko Matakatifu yanayafafanua kuwa kazi ya kuuwa, dhambi za wakati huo siyo fidia au malipo ya mauti ya milele.
804 Isa. 26: 16
805 1 Kor. 15: 56
806 Mafundisho ya Nikolao Ferber (Herborn) katika ‘Enchiridion‘ yake ya 24.
158. Ayubu hana hatia: Mateso yake hayakutokana na makosa yake mabaya yaliyopita. Hivyo, daima, mateso siyo adhabu au alama za ghadhabu. Kwa hiyo, dhamiri zenye hofu inapaswa zifundishwe kwamba, mateso yanasababisha mambo mengine ili zisifikirie kwamba, zimeachwa na Mungu, kwa maana, katikati ya mateso, dhamiri hazioni lolote zaidi ya adhabu na ghadhabu ya Mungu. Zinapaswa kuzitafakari shabaha hizi zingine muhimu, yaani kwamba, Mungu anatenda kazi yake ya kigeni ili aweze kutenda kazi yake halisi, jinsi Isaya anavyofundisha katika mahubiri yake marefu: Isa. 28: 21. 159. Wanafunzi walipouliza kuhusu kipofu kuwa ni nani aliyefanya dhambi, Kristo alijibu kwamba, dhambi haikuwa sababu ya upofu huo bali “kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.”807 Katika Yeremia imeandikwa: “wasioandikiwa kunywea kikombe, watakinywea.”808 Kwa sababu hizo, manabii, Yohana Mbatizaji, na watakatifu wengine wengi waliuawa. 160. Kwa hiyo, daima, mateso siyo adhabu kwa ajili ya matendo maalumu yaliyopita, bali ni matendo ya Mungu yaliyokusudiwa kwa faida yetu ili uwezo wa Mungu uonekane zaidi katika unyonge wetu.
Hivyo, Paulo anasema: “maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.”809 Kwa sababu hiyo na kwa mapenzi ya Mungu, lazima miili yetu itolewe kama dhabihu kuonyesha utiifu na siyo kufidia kifo cha milele. Maana, Mungu ana malipo mengine, yaani, kifo cha Mwana wake. 161. Hivi ndivyo Gregorio alivyofafanua adhabu ya Daudi asemapo: “Kama Mungu alikuwa amemtisha kwa sababu ya dhambi ili Daudi afedheheshwe na mwana wake kwa njia hii, kwa nini aliendelea kumtisha hata dhambi ilipokuwa imesamehewa? Jibu ni kwamba, dhambi ilisamehewa ili mtu asizuiwe kuupokea uzima wa milele. Hata hivyo, mfano wa tisho ulifuatia ili uchaji wa mtu uzoezwe na ujaribiwe hasa kwa njia ya fedheha. Ndipo, Mungu akamuweka mtu kwa njia ya kifo cha mwili kwa sababu ya dhambi. Hata baada ya msamaha wa dhambi, hakukiharibu kwa ajili ya kuizoeza haki ili haki ya wale waliotakaswa izoezwe na kujaribiwa.”810
162. Kwa kweli, mateso ya kawaida hayawezi kuondolewa kwa njia ya matendo ya upatanisho wa kanuni. Maana yake: kwa njia ya matendo ya mapokeo ya wanadamu, ambayo wao husema kuwa yanahalalishika kama matendo yenyewe, yangetendeka katika hali ya dhambi ya mauti, yangeweza kufidia adhabu. 163. Wanabishania kauli ya Paulo isemayo: “Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa na Bwana.”811 Lakini neno “hukumu” linarejea mchakato wote
807 Yn. 9: 3
808 Yer. 49: 12
809 2 Kor. 12: 9
810 Agostino, ‘De peccatorum meritis et remissione’ 2, c. 34, 56. (Stahili na msamaha wa dhambi).
811 1 Kor. 11: 31
wa toba na matunda yanayotazamiwa na siyo kuhusu “matendo yasiyokuwa ya lazima.” Wapinzani wetu wanalipa adhabu kwa kuidharau sarufi wanapolifafanua neno “hukumu” kama “hija” kwa maana ya silaha nzima ya kuliendeleza Kanisa la Mtakatifu Yakobo, au kutenda matendo kama hayo. “Hukumu” humaanisha toba nzima. Pia humaanisha kuishutumu dhambi. 164. Lawama ya namna hiyo inatendeka katika majuto makubwa na maisha yaliyobadilika. Toba nzima, yaani, majuto, imani, matunda mema hupunguza adhabu na mateso ya hadhara na ya kibinafsi kama jinsi Isaya afundishavyo katika Isa. 1: 16-19: “acheni kutenda mabaya; jifunzeni kutenda mema; . . . Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; . . . Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi.” 165. Tamko hili ambalo ni zito na mabruki812 mno kuhusu toba nzima na matendo yanayohitajika na yaliyoamriwa na Mungu, lisihamishiwe kwenye matendo ya upatanisho na utendaji wa mapokeo ya wanadamu. Ni vyema kufundisha kwamba, maovu yetu ya kawaida yanapunguzwa kwa toba yetu na matunda yake yaliyo ya kweli. Yaani, matendo mema yafanyikayo katika imani, lakini si kama jinsi watu hawa wanavyodhania kuwa ni matendo yafanyikayo katika dhambi ya mauti. Mfano wa wakazi wa Ninawi unalihusu hili. 166. Kwa ajili ya toba yao - tunamaanisha toba nzima - walipatanishwa na Mungu na waliuepusha mji wao813 na maangamizi.
167. Kama tulivyokwisha kusema hapo awali, mababa wa Kanisa walipotaja matendo ya upatanisho na sinodi zilipotunga kanuni, mambo haya yalikuwa masuala ya nidhamu ya Kanisa yaliyoundwa kwa ajili ya kuutoa mfano. Basi, hawakuifikiria nidhamu hii kuwa ya lazima kwa msamaha wa dhambi au wa adhabu. Hapa, waliporejea Purgatorio, hawakulifafanua jambo hili kama fidia ya adhabu ya milele au tendo la upatanisho, bali kama kuzisafisha nafsi zisizokamilika. Hivyo, Agostino anasema kwamba, dhambi zinazosameheka zinamalizika.814 Maana yake: kufuru kuhusu Mungu na mihemuko kama hiyo inaharibiwa kabisa.
168. Mara nyingine, waandishi walilihamisha neno “upatanisho” kutoka ibada ya hadharani na kulitumia kumaanisha kufishwa kwa kweli. Kwa hiyo, Agostino anasema: “upatanisho wa kweli unamaanisha kuzing’oa asili za dhambi, yaani, kuufisha mwili na kadhalika, kuushurutisha, siyo kufidia adhabu ya milele bali kuuzuia mwili ili usivutiwe kutenda dhambi.”815
812 Yaani, kutia afya/uzima.
813 Yona 3 : 10
814 Agostino, ‘De Civitate Dei’ 21, 26,4 (Mji wa Mungu).
815 Agostino bandia, yaani, Gennadio wa Massilia, “Mafundisho ya Kanisa,” yamedondolewa kutoka katika Decr. Grat. II. C. 33. q. 3. De poen. 3. c
169. Hivyo, kuhusu fidia,816 Gregorio anasema kwamba, toba ni ya uongo isipowatosheleza wale ambao tumechukua mali yao. Yeyote anayeendelea kuiba hatubu kweli kwa sababu ameiba au amenyang’anya Maana bado ni mwizi na mnyang’anyi kwa kuwa bado anamiliki mali ya mtu mwingine kinyume cha sheria. Fidia ya raia ni ya lazima jinsi ilivyoandikwa: “Mwibaji asiibe tena.”817 170. Kadhalika, Krisostomo anasema: “Majuto moyoni, ungamo midomoni, matendo yenye unyenyekevu kamili.”818 Hili halitupingi hata kidogo. Lazima, matendo mema yafuate toba, na toba siyo hila bali mageuzi ya maisha yote.
171. Kadhalika, Mababa wa Kanisa wanaandika kwamba, wakati wa maisha, inatosha kutubu hadharani au kwa makini mara moja ilivyoagizwa na kanuni kuhusu matendo ya upatanisho. Kutokana na hilo ni wazi kwamba, kanuni hizo si za lazima kwa ajili ya msamaha wa dhambi maana mara nyingi wanazidai, tofauti na ungamo la hadharani, yaani, toba za aina nyingine zisizoamriwa na kanuni.
172. Waasisi819 wa Hoja wanaandika kwamba, haitavumilika matendo ya upatanisho yaondolewe kabisa kinyume cha Injili iliyo wazi. Basi, mpaka sasa, tumeonyesha kwamba, matendo ya upatanisho wa kanuni, yaani, matendo yasiyokuwa ya lazima, yasitendeke kwa ajili ya kufidia adhabu, kwa kuwa hayana agizo la Injili. Suala hili lenyewe liko wazi. 173. Basi, iwapo matendo ya upatanisho siyo ya lazima, kwa nini wanataja “Injili iliyo wazi?” Injili ingeamuru kufidia adhabu kwa matendo ya namna hiyo, matendo hayo yangekuwa ya lazima kabisa. Lakini wanayazungumzia ili kuwadanganya wale wasiojua kwa njia ya kunukuu ushuhuda kuhusu matendo yaliyokuwa ya lazima ingawa, katika matendo yao ya upatanisho, wanaamuru matendo yasiyokuwa ya lazima. Licha ya hayo, katika vyuo vyao vikuu, wanakubali kwamba, mtu anaweza kukataa matendo ya upatanisho bila kutenda dhambi. Wanapotosha kabisa wanapoandika kwamba, tunashurutishwa na mafundisho kuhusu “Injili iliyo wazi” kuyakubali matendo hayo ya upatanisho wa kanuni.
174. Licha ya hayo, tumeshuhudia mara nyingi kwamba, toba lazima izae matunda mema. Amri820 zinafundisha matunda haya ni yapi, yaani, maombi, sadaka, ukiri wa Injili, mafundisho ya Injili, kuwatii wazazi, kuyatii mamlaka
816 Kilatini: ‘Restitutio.’ Maana yake ni kurudisha mali yaliyoibiwa na kufidia uharibifu uliotendwa. Dondoo la Gregorio katika Decr. Grat. II. C. 33. q. 3. De poen. d.. 6. c. 6. 817 Efe 4:28
818 Krisostomo bandia katika Decr.Grat. 2. C. 33. q. 3.
819 Tafsiri ya Kijerumani: ‘Esel,’ yaani, “punda.”
820 Amri Kumi za Mungu.
yote yaliyo makuu,821 mtu kuhudumu katika wito wake, kuepuka uchungu, na kutoiridhia hasira. Badala yake, tuwe na amani, tuwape wale wanaohitaji kulingana na uwezo wetu, tusizini, tusiwe wagoni, bali tuushurutishe, tuuzuie na tuuadhibu mwili. Haya yote yanafanyika, siyo ili kufidia adhabu ya milele, bali ili kutomtii Ibilisi, kutomwudhi Roho Mtakatifu, kusema ukweli na kadhalika. Matunda haya yameamriwa na Mungu. Hivyo, lazima yatendeke kwa utukufu wake, na kwa sababu ya amri yake, yana thawabu zao. Lakini Maandiko Matakatifu hayafundishi kwamba, adhabu za milele zinasamehewa kwa ajili ya fidia za mapokeo maalumu au Purgatorio. 175. Zamani, vyeti vya upatanisho vilikuwa milki au ukubalifu822 wa ungamo la hadharani ili watu wasilemewe sana na mizigo mizito. Ikiwa mamlaka ya kibinadamu yanaweza kuyaondolea matendo ya upatanisho na adhabu sasa, basi, fidia hii siyo ya lazima kulingana na haki ya kimungu. Naam, haki ya kimungu haitanguliwi na mamlaka ya kibinadamu.823 Aidha, kwa kuwa desturi yenyewe imepitwa na wakati, na kwamba haina vipingamizi vyovyote kutoka kwa maaskofu, hakuna haja ya misamaha hii. Hata hivyo, limebaki neno vyeti vya upatanisho. Matendo ya upatanisho yasieleweke kama nidhamu ya raia bali kama fidia ya adhabu. Hali kadhalika, vyeti vya upatanisho vimeelezewa vibaya kama viwezavyo kuzikomboa nafsi za binadamu kutoka Purgatorio.
176. Ufunguo hauna mamlaka yoyote isipokuwa kufunga na kufungua hapa duniani kulingana na maneno yafuatayo: “Lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.”824 Kama tulivyokwisha kusema hapo juu, ingawa funguo hazina mamlaka ya kutoa adhabu au kuanzisha ibada fulani, zina agizo tu la kusamehe dhambi za wale walioongoka na pia kuwashutumu na kuwatenga wale wasiotaka kuongoka. Hali kadhalika, “kufungua” kunamaanisha kusamehe dhambi, na “kufunga” kunamaanisha kutosamehe dhambi. Naam, Kristo anauzungumzia ufalme wa kiroho. 177. Agizo la Mungu ni kwamba, Wahudumu wa Injili wasamehe wale wanaoongoka kulingana na maneno haya: “Kwa ajili ya mamlaka yetu, tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha.”825 Kwa sababu hiyo, kesi zilizohifadhiwa ni masuala ya kidunia. Kesi hizi zinahusu adhabu ya kanuni, siyo hatia mbele za Mungu katika maisha ya wao walioongoka
821 Kilatini: ‘Magistrates,’ (mahakimu).
822 Kilatini: ‘Condonatio’ (condonamentum).
823 Kilatini: ‘Ius divinum non tollitur humana auctoritate;’ msimamo wa kimsingi wa Matengenezo ya Kanisa. Mamlaka ya binadamu yanashika pia kanuni zote za Kanisa zisizokuwa na msingi wa Neno la Mungu, yaani, Biblia.
824 Mt. 16:19
825 2 Kor. 10:8
kweli. Kwa hiyo, wapinzani wetu wanahukumu vizuri wanapokubali kwamba, katika saa ya kifo, kesi zilizohifadhiwa hazipaswi kuzuia ondoleo la dhambi.
178. Hapa, tumeelezea ujumla wa mafundisho yetu kuhusu toba. Kwa hakika tunajua kwamba, mafundisho haya ni matakatifu na yanafaa kwa nafsi bora. Watu wacha Mungu wakilinganisha mafundisho yetu na mabishano shaghalabaghala826 ya wapinzani wetu, wataona dhahiri kwamba, wapinzani wetu wamepuuza kufundisha imani yanayotuhesabia haki na kuifariji mioyo ya wacha Mungu. Wataona vilevile kwamba, wapinzani wetu wamebuni mambo mengi kuhusu ustahili wa majuto madogo,827 kuyahesabu makosa na matendo ya upatanisho pasipo mwisho, jinsi wanavyosema kuhusu, “mambo yasiyogusa dunia wala mbingu,”828 ambayo wapinzani wetu wenyewe hawawezi kuyaelezea ipasavyo.
Fungu la Kumi na Tatu: Idadi na Matumizi ya Sakramenti829
1. Katika Fungu la Kumi na Tatu, wapinzani wetu wanakubali tulilosema kwamba, sakramenti siyo tu ishara za kukiri miongoni mwa wanadamu kama jinsi wengine wanavyodhania,830 bali ni ishara na ushuhuda wa mapenzi ya Mungu kwetu, ambao kwao Mungu anaigusa mioyo ili iamini. 2. Lakini hapa, wanatuamuru kwamba tuhesabu, sakramenti saba. Basi, tunaamini kwamba, hatuna budi kutenda na siyo kuyapuuza mambo na ibada zozote zilizoanzishwa katika Maandiko Matakatifu hata kama ni za kiasi gani. Hatufikirii kwamba, ina maana kubwa iwapo itakuwa kwa madhumuni ya kufundisha ingawa idadi itatofautiana ilimradi mapokeo ya Maandiko Matakatifu yahifadhiwe kwa sahihi. Hata wazee hawakuzihesabu sakramenti kwa njia iyo hiyo.831
3. Ikiwa tutaifafanua sakramenti kuwa ibada zenye Agizo la Mungu na ahadi ya neema, itakuwa rahisi kuzihukumu sakramenti katika maana halisi. Kwa kuwa, ibada zilizoanzishwa na watu, hazikuanzishwa kwa njia hii ya sakramenti katika maana halisi, kwa vile wanadamu hawana mamlaka ya kuahidi neema. Kwa hiyo,
826 Machafuko.
827 Kilatini: ‘Attritio.’
828 ‘Ουτε
methali ya Kiyunani iliyotumiwa na Lukiano (mnamo 120 B.K. – mnamo 180 B.K.), aliyekuwa mwanafalsafa na mwandishi wa tashtiti ya michezo katika Kiyunani. Sentensi hii ilidondolewa kutoka kwa hoja yake “Aleksandro nabii wa uongo” mwaka wa 180 B.K. dhidi ya Aleksandro wa Abonuteikho. Katika kujifunza kumfahamu mwaka wa 164 B.K., Lukiano aliyahatarisha maisha yake pakubwa. Watu wa kawaida waliamini kwamba, Aleksandro alikuwa mtendaji mkuu wa miujiza.
829 Kijerumani: (Sakramenti na matumizi yao halisi).
830 Hyldrych Zwingli (1484-1531) alitoka Zürich, Uswisi, na wafuasi wake. Zwingli alitohoa ufafanuzi wa ishara kuhusu sakramenti mwaka wa 1523. Kwa hiyo, majadiliano baina ya Luther na Zwingli yalishindwa huko Marburg, Ujerumani, mwaka wa 1529 na Matengezo ya Kanisa katika Bara la Ulaya yaligawanyika katika medani mbili.
831 Sakramenti zilihesabiwa kuwa saba tangu wakati wa Petro Lombardo (mnamo 1100-1160).
ishara zilizoanzishwa bila Agizo la Mungu siyo ishara thabiti za neema, ingawa zingewafundisha watu wasiokuwa na elimu. 4. Hivyo basi, sakramenti halisi ni Ubatizo, Chakula cha Bwana, na Ondoleo la Dhambi ambalo ni sakramenti ya toba. Maana ibada hizi zina Agizo la Mungu na ahadi ya neema, ambazo ndizo halisi zilizomo katika Agano Jipya. Mioyo yetu inapaswa kuwa na uhakika tunapobatizwa, tunaposhiriki damu na mwili wa Bwana, tunapoondolewa dhambi zetu, kwamba, Mungu anatusamehe kweli kwa ajili ya Kristo. 5. Wakati huo huo, Mungu anaigusa mioyo kwa Neno na ibada ili mioyo iamini na kuipokea imani, jinsi Paulo asemavyo: “Basi imani, chanzo chake ni kusikia.”832 Kadiri Neno linavyoingia kupitia masikioni na kuisukuma mioyo, kadhalika, ibada zinaingia kupitia machoni na kuigusa mioyo. 5. Neno na ibada hizo zina matokeo hayo hayo, kulingana na msemo maarufu wa Agostino kuwa sakramenti ni “neno lionekanalo.”833 Kwa maana, ibada inapokelewa kwa macho na ni kama taswira ya Neno yenye maana hiyo hiyo sawa na neno lenyewe. Hivyo, haya yote yana matokeo sawa.
6. Kipaimara na Mpako Mtakatifu ni ibada zilizopokelewa kutoka kwa mababa wa Kanisa. Hata Kanisa halidai kwamba, ibada hizi ni za lazima kwa wokovu kwa maana hazina Agizo la Mungu. Hivyo, inafaa kuzitofautisha ibada hizi na zile zilizo za awali ambazo zina agizo mahususi la Mungu na ahadi ya wazi ya neema.
7. Wapinzani wetu hawatambui kwamba, ukuhani au utoaji wa sakramenti kwa wengine ni Huduma ya Neno. Badala yake, wanaitambua huduma ya kutoa dhabihu, kana kwamba, ingekuwa lazima katika Agano Jipya kuwa na ukuhani sawa na ule wa Walawi waliotoa dhabihu kwa niaba ya umma na kuustahilisha msamaha wa dhambi kwaajili ya watu wengine.834 8. Tunafundisha kwamba, dhabihu ya kifo cha Kristo msalabani ilitosha kwa ajili ya dhambi za dunia nzima na hatuhitaji tena dhabihu zingine kana kwamba, hiyo ya Kristo haikutosha kwa ajili ya dhambi zetu. 9. Kwa sababu hiyo, watu hawahesabiwi haki kwa ajili ya dhabihu nyingine zozote, bali kwa ajili ya dhabihu hii moja ya Kristo, wakiamini kwamba, wamekombolewa nayo. Kwa sababu hiyo, makuhani hawaitwi ili wazitoe dhabihu kwa niaba ya umma ili ziustahilishe msamaha wa dhambi kama jinsi ilivyo katika Torati. Badala yake, wanaitwa kuifundisha Injili na kutoa sakramenti kwa watu. 10.Waraka kwa Waebrania unafundisha wazi kwamba, hatuna ukuhani kama ule wa Walawi.835 11. Kama kubarikiwa kwa
832 Rum. 10 :17
833 Kilatini: ‘Verbum visibile,‘ Tract. 80 in Jn 3
834 Petro Lombardo Sent. IV. D. 24, 9.
835 Ebr. 7:9
wachungaji kunaelezewa kuhusiana na Huduma ya Neno, basi, kweli hatusiti kuita sakramenti. Huduma ya Neno ina agizo la Mungu na ahadi ya neema: “Injili . . . ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye” (Rum. 1: 16). Tena: “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma”(Isa. 55: 11). 12. Ikiwa kubarikiwa kwa wachungaji kunaelezewa katika maana hii, hatusiti kamwe kuita kuwekea mikono kuwa sakramenti. Naam, Kanisa lina mamlaka ya kuwateua wachungaji; jambo hili lazima litufurahishe mno kwa kuwa tunajua kwamba, Mungu anaikubali huduma hii na yumo ndani yake. 13. Ni vyema sana kuitukuza Huduma ya Neno kwa kila aina ya sifa dhidi ya walokole ambao huota ndoto kwamba, Roho Mtakatifu hatolewi kwa njia ya Neno bali kwa sababu ya matayarisho yao wenyewe.Wanakaa wakiwa legevu gizani na kungojea mwangaza, sawa na walokole wa zamani836 walivyofundisha awali na jinsi Waanabaptisti wanavyofundisha sasa.
14. Ndoa haikuanzishwa katika Agano Jipya, bali mwanzoni kabisa mwa uumbaji wa mwanadamu. Ina amri ya Mungu na pia ina ahadi yake lakini siyo kuhusu Agano Jipya bali kuhusu maisha ya kimwili. Kwa sababu hiyo, mtu yoyote akitaka kuiita sakramenti, lazima aitofautishe na zile zilizotangulia, ambazo katika maana halisi, ni ishara za Agano Jipya na ndio ushuhuda wa neema na msamaha wa dhambi. 15. Lakini ndoa ikiitwa sakramenti kwa sababu ina amri ya Mungu, basi, vyeo au huduma zingine zenye Agizo la Mungu pia zinaweza kuitwa sakramenti kama mahakimu.
16. Mwisho, iwapo ni lazima kuyaorodhesha mambo yote yenye Amri ya Mungu kama sakramenti ambayo yameongezea ahadi kwayo, je, kwa nini tusiongezee sala ambayo, kwa kweli, inawezekana kabisa kuitwa sakramenti? Ina Amri ya Mungu na ahadi nyingi. Kama ingewekwa kati ya sakramenti katika tabaka la heshima zaidi, ingeweza kuwahimiza watu kusali zaidi. 17. Pia, sadaka zingeweza kuorodheshwa hapa pamoja na majaribu ambayo yenyewe ni ishara ambazo kwazo Mungu ameiongezea ahadi. Lakini na tuyaache haya! Hakuna mtu mwenye akili atakayebishana sana kuhusu idadi ya sakramenti au neno hili kama kweli mambo yenye Agizo na Ahadi ya Mungu yanahifadhiwa.
18. Ni muhimu zaidi kujua jinsi ya kuzitumia sakramenti. Hapa tunailaani jumuiya nzima ya Madaktari Wanazuoni ambao hufundisha kwamba, sakramenti isiyokuwa na kizuizi chochote, hutoa neema kama matendo yenyewe bila
836 Melanchthon, ‘Ενθουσιασται;’ maana yake: “Kuwa na Mungu.” Katika Kanisa la Magharibi, mwenendo wa namna hiyo uliitwa “hesikasti” (kimya). Waliutafuta kwa njia ya “Sala ya Yesu” na kwa njia ya mkao maalumu wa kimwili kuuona mwangaza wa utukufu wa kimungu.
mwelekeo mzuri wa wale wanaozitumia. Mafundisho haya ni uyahudi mtupu kudhania kwamba, tunahesabiwa haki kwa njia ya kaida iliyotendeka tu bila mwelekeo mzuri wa mioyoni mwetu, yaani, bila imani. Hata hivyo, mafundisho haya ya kukufuru na mapotovu, yanafundishwa kwa heshima na mamlaka kuu kote katika utawala wa Kuhani Mkuu wa Roma. 19. Kinyume chake, Paulo anapinga na kukataa kwamba, Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya tohara. Badala yake, anasema kwamba, tohara ilikuwa ishara iliyotolewa kwa ajili ya kuonyesha imani. Hivyo, tunafundisha kwamba, lazima imani iwepo katika matumizi ya sakramenti ambazo zinaamini ahadi hizi na kuyapokea mambo yaliyoahidiwa na kutolewa katika sakramenti. 20.Sababu yake ni wazi na imara kabisa. Ahadi haina maana isipokuwa inapokelewa kwa imani. Sakramenti ni ishara za ahadi. Kwa sababu hiyo, lazima imani iwepo ili kila mmoja anayekishiriki Chakula cha Bwana akishiriki kwa njia hii. Kwa kuwa hii ni sakramenti ya Agano Jipya, jinsi Kristo anavyosema wazi,837 lazima mtu awe imara kwamba, anapokea mambo yaliyoahidiwa katika Agano Jipya, yaani msamaha wa bure wa dhambi . Analipokea jambo hili kwa imani, kuifariji dhamiri yenye hofu na husadiki kabisa kwamba, ushuhuda huu si wa uongo bali ni wa kweli, jinsi ambavyo Mungu, kwa njia ya muujiza mpya, anaahidi kutoka mbinguni kwamba, anapenda kusamehe. 21. Lakini miuzija na ahadi hizi zinamnufaisha nini mtu asiyeamini? Hapa tunazungumzia kuhusu imani maalumu inayoamini ahadi inayotolewa badala ya kuamini tu kwa ujumla kwamba Mungu yupo. Basi, inaamini kwamba, kweli msamaha wa dhambi unatolewa. 22. Matumizi haya ya sakramenti yanazifariji nafsi za wenye hofu na wacha Mungu.
23. Hakuna mtu yeyote awezaye kuelezea ni matumizi mangapi mabaya yaliyozaliwa kanisani na kauli hii ya kilokole kuhusu “opus operatum.” Yaani, tendo lenyewe lililotendeka bila mwelekeo mwema wa mtu anayezitumia sakramenti. Unajisi wa Misa usiokuwa na mwisho unatokea hapo, ambao tutauzungumzia baadaye kidogo.838 Hakuna neno hata moja ambalo linaweza kutolewa kutoka katika vitabu vya waandishi wa zamani ili kuwatetea Madaktari Wanazuoni. Kwa hakika, Agostino anasema kinyume kabisa kwamba, ni imani katika sakramenti, na siyo sakramenti inayotuhesabia haki. Na tamko la Paulo linajulikana wazi: “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki.”839
Fungu la Kumi na Nne: Utaratibu wa Kanisa
1. Wanakubali Fungu la Kumi na Nne tusemapo kwamba, hakuna anayeruhusiwa
837 1 Kor. 11: 25
838 Taz. Fungu la Ishirini na Nne.
839 Rum. 10: 10
kutunza sakramenti na Neno kanisani isipokuwa awe ameitwa kwa utaratibu.840 Wanakubali kwa sharti kwamba, tunawabariki wachungaji kwa utaratibu wa kanuni. Tumelishuhudia jambo hili mara nyingi katika baraza kwamba, tunatamani sana kuudumisha uongozi wa Kanisa841 pamoja na vyeo mbalimbali vya mamlaka katika Kanisa ingawa, kwa sharti, vimeundwa na mamlaka ya kibinadamu.842 Tunajua vizuri kwamba, Mababa wa Kanisa walianzisha nidhamu ya Kanisa kwa kusudi bora na lenye manufaa kama jinsi inavyoelezewa na kanuni za kale. 2. Walakini maaskofu wanawashurutisha makasisi wetu ama kukataa na kulaani aina ya mafundisho tuliyoyakiri au wanawaua watu maskini na wasio na hatia kwa ukatili ambao haujawahi kusikika. Sababu hizi zinawazuia makasisi wetu kuwakubali maaskofu kama hao. Hivyo, ukatili wa maaskofu ni sababu kwamba, mahali fulani, uongozi wa kikanuni unavunjwa licha ya upande wetu, kutamani sana kuuhifadhi uongozi huu. Maaskofu wataona wenyewe ni kwa njia gani watatoa hesabu kwa Mungu kwa sababu ya kulivunja Kanisa.
3. Dhamiri zetu hazina shaka lolote kuhusu kauli hii kwa kuwa tunajua kabisa kwamba, ukiri wetu ni wa kweli, ni wa uchaji na wa Ukatoliki. 4. Kwa sababu hiyo, hatulazimishwi kukubali ukatili wa wale wanaoyakandamiza mafundisho haya. Tunajua pia kwamba, Kanisa linapatikana miongoni mwa wale ambao hufundisha Neno la Mungu na kutoa sakramenti kwa ufasaha. Kanisa halipatikani miongoni mwa wale ambao hujaribu kuliharibu Neno la Mungu, siyo tu kwa amri zao, bali kwa njia ya kuwachinja wale wanaofundisha hilo ambalo ni sahihi na la kweli. Ingawa kanuni zenyewe ni za upole sana kwa wale wanaozivunja. 5. Licha ya hayo, tunataka kushuhudia tena nia yetu ya kuuhifadhi uongozi na Kanisa la kikanuni,843 mradi tu maaskofu waache ukatili wao dhidi ya makanisa yetu. Utayari wetu huu utakuwa utetezi wetu mbele za Mungu, na kati ya mataifa yote na hadhi hata miongoni mwa vizazi vya sasa na vitakavyokuja dhidi ya mashtaka kwamba, tumeyavunja mamlaka ya maaskofu, ili watu wakisoma na kusikia kwamba, licha na ushuhuda wetu dhidi ya ukatili wa maaskofu usiokuwa wa haki, hatukuweza kupata haki.
Fungu
la
Kumi
na Tano: Mapokeo ya Binadamu katika Kanisa844
1. Wapinzani wetu wanaikubali sehemu ya kwanza ya Fungu la Kumi na Tano
840 Kilatini: ‘Rite vocatus.’
841 Kilatini: ‘Politia ecclesiastica.’
842 Melanchthon alithibitisha kauli hii katika mazungumzo yake pamoja na Balozi wa Papa, Lorenzo Campeggio huko Augsburg.s
843 Kilatini: ‘Politia ecclesiastica et canonica’
844 ‘Ukiri wa Augsburg‘ 15, “Kaida za Kanisa’
tunaposema kwamba, tunapaswa kuadhimisha taratibu zote za Kanisa ambazo zinaweza kuadhimishwa pasipo dhambi na ambazo zinaleta utulivu na utaratibu bora kanisani. Wanailaani kabisa sehemu ya pili tusemapo kwamba, mapokeo ya wanadamu yaliyoanzishwa ili kumtuliza Mungu, kuistahili neema na kuifanya ridhaa kwa ajili ya dhambi ni kinyume kabisa cha Injili. 2. Ingawa tumezungumzia mapokeo kwa urefu katika kifungu cha ishirini na sita cha ungamo, tunapaswa kuyarudia mambo machache hapa.
3. Hata hivyo, tulifikiria kwamba, wapinzani wetu waliyatetea mapokeo ya wanadamu kwa sababu zingine. Hatukudhania hata kidogo kwamba, wangelaani fungu hili: kwamba sisi hatustahili msamaha wa dhambi au neema kwa njia ya kuyaadhimisha mapokeo ya wanadamu. Baada ya fungu hili845 kulaaniwa, kesi yetu hii ni rahisi jinsi ilivyo mrama. 4. Hapa, wapinzani wetu wanayafuata wazi mafundisho ya Kiyahudi; wanaipinga wazi Injili kwa mafundisho ya mashetani. Naam, Maandiko Matakatifu yanayaita mapokeo kuwa “mafundisho ya mashetani”846 inapofundishwa kwamba, mapokeo ya aina hii ni ibada zinazofaa katika kustahili msamaha wa dhambi na neema. Basi, mafundisho haya yanaficha kabisa Injili, fadhili za Kristo na haki ya imani. 5. Injili inatufundisha kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi na kupatanishwa na Mungu bure kwa imani katika Kristo. Kwa upande mwingine, wapinzani wetu wanamtengeneza mpatanishi mwingine, yaani, mapokeo haya. Kwa ajili ya mapokeo haya, wanataka sana kuupata msamaha wa dhambi, na kwa mapokeo haya, wanataka kuituliza ghadhabu ya Mungu. Walakini Kristo anasema wazi: “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”847
6. Hapo awali tulijadiliana sana kwamba, watu wanahesabiwa haki kwa imani bure wanapoamini kuwa wana Mungu aliyetulizwa kwa ajili ya Kristo, siyo kwa sababu ya matendo yetu. Hili ndilo fundisho la kweli la Injili, kwa sababu Paulo anasema wazi katika Efe. 2: 8: “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.” 7. Basi, wapinzani wetu husema kwamba, watu huustahili msamaha wa dhambi kwa njia ya kuyaadhimisha mapokeo haya ya wanadamu. Je, hili hii ni nini isipokuwa kumtengeneza mwadilifu mwingine na mpatanishi mwingine badala ya Kristo? 8. Paulo anasema kwa Wagalatia (Gal. 5: 4): “Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria . . . “ Maana yake: mkidhania kuwa mtastahili kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa njia ya kuifuata sheria, Kristo hatawafaidi lolote. Basi, kwa kusudi gani wao hudhania kumhitaji Kristo ikiwa
845 Andiko la Kijerumani: ‘Unverschämt,‘ yaani, “kwa ukavu mkuu.”
846 1 Tim. 4: 1
847 Mt 15, 9
wanaamini kuwa wenye haki kwa ufuasi wao wa sheria? 9. Mungu alimteua Kristo kuwa mpatanishi, kwa kuwa, kwa ajili ya Mpatanishi huyu, alipenda asulubiwe kwa ajili ya matendo ya haki yetu wenyewe. Lakini watu hawa huamini kwamba, Mungu ametulizwa na kuridhishwa kwa ajili ya mapokeo na siyo kwa ajili ya Kristo. Hivyo basi, wanamnyang’anya Kristo heshima yake kama Mpatanishi.
10. Basi, hakuna tofauti kati ya mapokeo yetu na taratibu za Musa kuhusu jambo hilo. Kwa hiyo, Paulo anazilaani taratibu za Musa jinsi anavyolaani mapokeo kwa sababu yalifikiriwa kuwa matendo yanayostahili haki mbele za Mungu. Kwa njia hiyo, huduma ya Kristo na haki ya imani inafichwa. Kwa hiyo, kwa njia ya kuondoa sheria na mapokeo, anadai kuwa msamaha wa dhambi umeahidiwa siyo kwa ajili ya matendo yetu, bali bure kwa ajili ya Kristo, ilimradi tuupokee kwa imani , kwani ni imani tu ambayo kwayo ahadi inapokelewa. 11. Kwa kuwa tunaupokea msamaha wa dhambi kwa imani, na kuwa tuna Mungu aliyeridhishwa kwa ajili ya Kristo, ni uzushi na kosa la kumkufuru Mungu kushikilia kwamba, tunaustahili msamaha wa dhambi kwa matendo ya maadhimisho haya . 12. Mtu akisema hapa kwamba, hatustahili msamaha wa dhambi isipokuwa wale ambao tayari wamekwisha kuhesabiwa haki wataistahili neema kwa kuyazingatia mapokeo haya, Paulo anajibu tena kwamba Kristo angekuwa “mtumishi wa dhambi” (Gal. 2: 17) ikiwa ingetupasa kuamini kwamba, baada ya kuhesabiwa haki hatuhesabiwi kuwa wenye haki kwa ajili ya Kristo bali hatuna budi kwanza kustahili kwa matendo mengine ya maadhimisho ili tuhesabiwe haki: “Agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye.”848 Hali kadhalika, wosia wa Mungu unatuahidi kwamba, angependa kuridhishwa kwetu kwa ajili ya Kristo, kusiongezewe hili, kuwa kwanza inatubidi kustahili kwa matendo haya ya maadhimisho ili tuhesabiwe na kukubaliwa na kuhesabiwa wenye haki.
13. Basi, kuna haja gani kuwa na mjadala mrefu? Mababa Watakatifu hawakuanzisha mapokeo yoyote ili kuustahilisha msamaha wa dhambi au haki. Waliyaanzisha kwa ajili ya utaratibu bora na utulivu kanisani. 14. Mtu akitaka kuyaanzisha matendo fulani ili austahili msamaha wa dhambi au ahesabiwe haki, atajuaje kwamba, matendo haya yanampendeza Mungu pasipo ushuhuda wa Neno la Mungu? Atawezaje kuwaimarisha watu kuhusu mapenzi ya Mungu bila mamlaka ya Neno la Mungu? Je, Mungu hakatazi kabisa kuzianzisha ibada bila agizo lake popote katika vitabu vya manabii? Katika Eze. 20: 1819 imeandikwa: “Msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao. Mimi ni BWANA, Mungu wenu; 848 Gal. 3: 15; ‘Union Version,’ “Agano“ badala ya “wosia”
endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda.” 15. Kama watu wakiruhusiwa kuzianzisha ibada na kuistahili neema kwa matendo hayo, ibada za dini za mataifa yote zitakubaliwa, pamoja na ibada zilizoanzishwa na Yeroboamu849 na wengineo juu ya Torati. Kuna tofauti gani iwapo tunaruhusiwa kuzianzisha ibada zinazonufaisha katika kustahili neema na haki? Basi, mbona Wapagani na Waisraeli hawakuruhusiwa kufanya hivyo? 16. Kwa kweli, ibada za Wapagani na Waisraeli ziliachwa kwa sababu walidhania kwamba, wanaweza kuustahili msamaha wa dhambi na haki kwa matendo haya bila kuifahamu haki ya imani. 17. Hatimaye, ni jinsi gani tunahakikishiwa kwamba, ibada zilizoanzishwa na wanadamu bila mamlaka ya Mungu zinatufanya tuwe na haki, ambapo haiwezekani kulihalalisha lolote kuhusu mapenzi ya Mungu bila Neno la Mungu? Itakuwaje iwapo Mungu hatazikubali ibada hizo? Ni vipi wapinzani wetu watathibitisha sasa kwamba, zinatufanya tuwe wenye haki? Jambo hilo haliwezi kuthibitishwa bila Neno na ushuhuda wa Mungu. Paulo anasema: “Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.”850 Kwa kuwa, ibada hizi hazina ushuhuda wowote wa Neno la Mungu, dhamiri hazina budi kuwa na mashaka kama kweli zinampendeza Mungu.
18. Kuna haja gani ya maneno katika jambo lilo wazi kabisa? Wapinzani wetu wakizitetea ibada za kibinadamu kuwa zinastahilisha kuhesabiwa haki, neema na msamaha wa dhambi, watajenga kabisa ufalme wa Mpinga Kristo. Kwani ufalme wa Mpinga Kristo ni njia mpya ya kumwabudu Mungu iliyobuniwa na mamlaka ya kibinadamu ili kupambana na Kristo. Hali kadhalika, utawala wa Muhammadi una taratibu za ibada. Una matendo ambayo kwayo unajaribu kutafuta kuhesabiwa haki mbele za Mungu ukikataa kwamba, wanadamu wanahesabiwa haki bure mbele za Mungu kwa imani kwa ajili ya Kristo. Kwa hivyo, pia Upapa851 utakuwa sehemu ya ufalme wa Mpinga Kristo ukiendelea kuyatetea mafundisho haya kwamba, taratibu za ibada za wanadamu zinatuhesabia haki. Naam, wanajitwalia heshima ya Kristo wanapofundisha kwamba, hatuhesabiwi haki bure kwa imani, kwa ajili ya Kristo, bali kwa taratibu hizo za ibada, hasa wanapofundisha kwamba, ibada za namna hiyo siyo tu za kufaidi katika kuhesabiwa haki, bali pia ni za lazima, jinsi walivyodhania awali katika Fungu la Nane ambapo wanatulaani kwa sababu ya kusema kwamba, kwa umoja wa kweli wa Kanisa siyo lazima mapokeo yaliyoanzishwa na wanadamu yafanane kila mahali. 19. Katika sura ya kumi na moja ya kitabu chake (Dan. 11: 38) Danieli anaelekeza kwamba, taratibu mpya za ibada za wanadamu zitakuwa
849 1 Fal. 12: 26-27
850 Rum. 14: 23
851 Kilatini: ‘Papatus.’
muundo na sera ya utawala852 wa Mpinga Kristo. Naam, anasema: “Lakini katika mahali pake atamheshimu mungu wa ngome;853 na mungu ambaye baba zake hawakumjua atamheshimu, kwa dhahabu, na fedha, na vito vya thamani, na vitu vipendezavyo.” Anaelezea hapa ibada mpya anaposema kwamba, ataabudiwa Mungu ambaye Mababa hawakumjua.
20. Japo Mbaba watakatifu wenyewe walikuwa na taratibu, ibada, na mapokeo, hata hivyo, hawakudhania kwamba mambo haya yangenufaisha au yangekuwa ya lazima kwa ajili ya kuhesabiwa haki. Hawakuficha utukufu au huduma ya Kristo bali walifundisha kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani kwa ajili ya Kristo na wala siyo kwa ajili ya ibada zile za wanadamu. Aidha walizifuata taratibu za kibinadamu kwa sababu ya faida ya nidhamu ya kimwili ili umma upate kujua nyakati za kukutana na ili uwe mfano jinsi mambo yanavyotakiwa kufanyika makanisani kwa utaratibu na kwa uungwana. Mwishowe, watu wa kawaida wapate mafundisho fulani. Naam, hitilafu za nyakati na mabadiliko ya taratibu yamesaidia sana kuwakumbusha watu wa kawaida.854
21. Kwa sababu hizi, Mababa walizihifadhi taratibu za ibada jinsi Epifanio855 anavyoshuhudia dhahiri katika majadiliano yake dhidi ya Waenkratito 856 ambao walikuwa wa aina hiyo hiyo sawa na wamonaki wetu. Naam, walikuwa na mashirikisho yaliyoyachukua mapokeo fulani. Waliacha divai hata wakati wa Chakula cha Bwana, na hawakula nyama au samaki. Kwa ajili ya nidhamu hii, waliwashinda hata Wadominikani.857 Waliipinga ndoa, ingawa bado hawakuupinga urafiki na wanawake. Yaani, Epifanio anawashutumu kadamnasi858 kuwa akina mama wengi waliwafuata katika maisha hayo hayo. Hali kadhalika, siku hizi, karibu pote, watawa wa kiume wanaishi katika nyumba zinazopakana na za watawa wa kike. Aidha, walidhania kwamba, matendo haya ya adhimisho yalikuwa ibada za kweli za Mungu na haki ambayo ilikuwa sababu ya kukubaliwa na Mungu na kuituliza ghadhabu yake. Epifanio hakuyakubali maoni haya. Alionyesha kwamba, shabaha za mapokeo zilikuwa tofauti kabisa. Alisema kwamba, mapokeo yaliweza kukubaliwa ili kuutesa mwili, kuwakandamiza wale
852 Melanchthon, ‘πολιτεια.’
853 Melanchthon, ‘Deus Maosim,‘ katika Kiebrania. ‘Maosim;’ lina maana sawa na “misa.”
854 Yaani, kuhusu historia takatifu katika Kijerumani: ‘Dienen das Volk in Zucht zu behalten und zu erinnern der Historien’
855 Epfanio wa Salamis (mnamo 315-403), askofu na mwandishi wa Kikristo.
856 Dhehebu kali wakati wa Kanisa la Zamani lililojaribu kuufuata uzingatifu ‘ενκρατειν‘ mno wa Torati.
857 Pamoja na Wafransiskano, daraja la Kidominikano lililoanzishwa katika miaka ya 1220 na 1221, lilikuwa maarufu kwa ajili ya kazi, mahubiri, elimu na nidhamu yake na pia kwa ajili ya wataalamu wakuu, kama Alberto Mkuu na Tomaso wa Akuino.
858 Mbele ya watu.
wasio na elimu au kwa ajili ya muundo wa kiraia. Sisi pia tunaona kwamba, mapokeo yanaweza kuhifadhiwa kweli kwa sababu zinazofuatia. Watu wa kawaida wanaweza kujishughulisha na mambo matakatifu kwa njia halisi zaidi jinsi Yehoshafati na Mfalme wa Ninawi walivyotangaza mifungo.859 Utaratibu na uongozi wa Kanisa unaweza kuwaelezea, wale wasio na elimu, madai ya kila wakati. Kwa sababu hiyo, kuna sherehe za Krismasi, Pasaka, Pentekoste n.k. Hilo ndilo Epifanio alisemalo kuwa mapokeo yaliyoanzishwa kwa sababu za watu. Yaani, kwa ajili ya utaratibu bora. Utaratibu huu unaweza kuwafundisha watu kuhusu historia na fadhili za Kristo. Kwa kuwa, inafaa zaidi kuyatumia mambo ya kuonekana yaliyoonyeshwa katika taratibu na desturi kwa mafundisho ya watu wa kawaida kuliko matumizi ya maandiko. Shabaha ya mapokeo ni kuipa taswira na kuionyeshea umma mambo. Lakini wapinzani wetu wanazishikizia shabaha hizo kufuatana na ushawishi wa mambo tofauti Kifarisayo. Yaani kwamba, matendo haya ya maadhimisho yanastahili msamaha wa dhambi, kuwa taratibu za namna hiyo ni za lazima kwa wokovu, na kuwa watu huhesabiwa haki mbele za Mungu kwa ajili ya mambo haya ya wanadamu. Ni wazi kabisa kwamba, haya ni sawa na kumsifu Mungu kwa dhahabu, fedha, na johari. Yaani, kudhania kwamba, Mungu anaweza kutulizwa kwa njia za mavazi, mapambo na vitu kama hivyo, bila mwisho katika mapokeo ya wanadamu au pia kudhania kwamba, ibada ya Mungu inafanyika kwa kuhitilafiana na nyakati, vyakula au mavazi.
22. Katika Kol. 2: 23, Paulo anaandika kwamba, mapokeo “yana hekima” na kweli yanayo. Utaratibu860 huu unafaa sana kanisani na hivyo ni wa lazima. Walakini, kwa kuwa asili ya binadamu haielewi haki ya imani, upande wa asili yake inadhania kwamba, matendo ya jinsi hiyo yanawahesabia watu haki na yanawapatanisha na Mungu. 23. Umma wa Waisraeli ulifikiria kwa njia hii na hata ukaongezea taratibu za namna hiyo kwa maoni haya kama jinsi yalivyoenezwa miongoni mwetu katika nyumba za watawa. 24. Hivyo ndivyo akili ya binadamu inavyotathmini kufunga na nidhamu ya kimwili. Ingawa shabaha yao ni kuuzuia mwili, akili inajishikiza shabaha nyingine, kuwa, ibada inayohesabia haki jinsi Tomaso alivyoandika: “Kufunga kunafaa kwa kuharibu na kuzuia hatia.”861 Haya ndiyo maneno ya Tomaso. Hivyo, sura ya hekima na haki inawadanganya wanadamu katika matendo kama hayo. Pia hapo, mifano ya watakatifu inaongezeka. Watu wanapojaribu kuiiga mifano hii, aghalabu wanayaiga matendo yao ya nje badala ya kuiiga imani yao.
859 2 Nya. 20:30; Yn. 3:7
860 Melanchthon, ‘ευταχια.’
861 Tomaso wa Akuino STh. II, 2 q. 147. a. 3. c.
25. Hapo, sura hii ya hekima na haki inapokuwa imewadanganya watu, aina zote za matatizo yasiyohesabika hufuata: Injili ya haki ya imani katika Kristo inafichwa na badala yake, inachukuliwa na imani batili katika matendo hayo. Halafu Amri za Mungu zinafichwa kwa kuwa matendo haya yanachukuliwa kuwa na cheo cha maisha kamili na ya kiroho na yatapendelewa zaidi na watu kuliko matendo yaliyoagizwa na Amri za Mungu. Yaani, matendo ya wito wa kila mmoja, himaya ya serikali, himaya ya uchumi, maisha ya ndoa, na malezi ya watoto. 26.Yakilinganishwa na taratibu zile za ibada, yataonekana kuwa ya malimwengu, kwamba yanatendwa na watu wengi, na kuwa yana kiasi cha mashaka ya dhamiri. Inajulikana wazi kwamba, watu wengi wameiacha nyadhifa zao za utawala serekalini na ndoa zao ili kuyafuata matendo haya kwa kudhani kuwa yangekuwa mazuri na matakatifu zaidi.
27. Wala hili halitoshi. Pale ambapo ushawishi huo huzihangaisha nafsi za watu kuwa maadhimisho hayo ni ya lazima kwa ajili ya kuhesabiwa haki, dhamiri zinateswa vikali kabisa kwa sababu haziwezi kuyatekeleza matendo yote ya uzingatifu kwa undani kabisa. Ni nani awezaye kuziorodhesha (nafsi) zote? Kuna mabuku862 makubwa zaidi, hata maktaba mazima, bila silabi hata moja kuhusu Kristo au imani katika yeye, au kuhusu matendo mema ya wito wa kila mmoja? Badala yake, vitabu na maktaba hizi zimekusanya mapokeo pamoja na fafanuzi zao zinazofanya matendo haya kuwa magumu au kuwa rahisi zaidi wakati mwingine. 28. Gerson,863 aliye mtu bora sana, anateswa kiasi gani anapotafuta viwango na mipaka ya maagizo! Hata hivyo, hawezi kurekebisha hali inayoupunguza uzito864 kwa kiwango chochote! Wakati huo huo analalamika sana kuhusu hatari za dhamiri za wacha Mungu kwa ajili ya huo ufafanuzi mkali wa mapokeo.
29. Basi, tunajiimarisha kwa Neno la Mungu dhidi ya sura ile ya hekima na haki katika desturi za kibinadamu za kuwadanganya watu. Kwanza, tunajua kwamba, desturi hizi hazistahilishi msamaha wa dhambi wala kuhesabiwa haki mbele za Mungu kamwe, na kwamba, haya si ya lazima kwa ajili ya kuhesabia haki. 30. Awali, tulinukuu baadhi ya ushuhuda kuhusu jambo hili. Ushuhuda huu unapatikana tele katika nyaraka za Paulo. Anasema wazi katika Kol. 2: 1617: “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au Sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.” Hapo, anaiunganisha Sheria ya Musa na mapokeo ya wanadamu ili wapinzani wetu wasiweze kuukwepa ushuhuda
862 Vitabu.
863 Jean Gerson, “Maisha ya Kiroho” Lect. 2, III, 16. 864 Melanchthon, ‘επιεικεια.’
huo kwa tabia zao za kusema kwamba, Paulo anaizungumzia Sheria ya Musa tu. Lakini anashuhudia hapa wazi kabisa kwamba, anazungumzia mapokeo ya wanadamu. Hivyo, wapinzani wetu hawalioni walisemalo. Iwapo Injili itakataa taratibu za Musa zilizoanzishwa na Mungu ili kuhesabia haki, basi, ni jinsi gani mapokeo ya wanadamu yatahesabia haki zaidi!
31. Wala maaskofu hawana mamlaka ya kuanzisha ibada fulani kana kwamba, zilihesabia haki au zilikuwa za lazima kwa ajili ya haki. Hata katika Mdo. 15: 10 mitume wanasema: “Mbona mnamjaribu Mungu kwa kuweka kongwa n.k.” Petro anaisuta sinodi hii kwa ajili ya dhambi kubwa ya kuliwekea Kanisa mzigo huo. Katika Gal. 5: 1, Paulo anawaonya wasinaswe: “chini ya utumwa.” 32. Basi, mitume walitaka sana uhuru huo ubakie kanisani. Ili kwamba namna ya ibada isichukuliwe kuwa ya lazima jinsi desturi zilivyokuwa za lazima kwa njia ya sheria au mapokeo kwa muda. Shabaha yake ni kwamba, haki ya imani isifichwe ikiwa watu wanaamini kwamba, ibada hizo zinastahili haki au zinakuwa za lazima kwa kuhesabia haki. 33. Kwa njia mbalimbali, wengi hutazamia nafasi za kuyapunguza mapokeo865 ili kuzistarehesha dhamiri bila kupata viwango vya hakika ambavyo kwavyo wangekuwa huru kutoka kwa minyororo hii. 34. Basi, jinsi Aleksandro, baada ya kushindwa kulifundua fundo lile huko Gordioni, alilikata kwa upanga wake mara moja.866 Hali kadhalika, mitume waliziweka huru dhamiri kutoka kwa mapokeo mara moja, hasa yalipotolewa ili yastahili kuhesabiwa haki. Basi, mitume wanatulazimisha kuyapinga mafundisho haya kwa njia ya mafundisho na kwa mifano. Wanatulazimisha kufundisha kwamba, mapokeo hayahesabii haki; kwamba, siyo ya lazima kwa ajili ya kuhesabiwa haki; kwamba, hakuna mtu yeyote anayepaswa kuunda au kukubali mapokeo kwa wazo kwamba, yanastahilisha kuhesabiwa haki. 35. Basi, mtu yeyote akiyafuata, na atende hivyo tu kama mwenye anazifuata desturi za jamii bila madai haramu,867 mbele za Mungu, jinsi ambavyo hakuna thamani mbele za Mungu katika kuziadhimisha desturi za ulimwengu, iwapo askari wanavalia aina moja ya sare na madaktari aina nyingine. 36. Mitume waliyakiuka mapokeo, na walisamehewa na Kristo. Kwa mfano huo, Mafarisayo walionyeshwa kwamba, ibada zao hazikuwa na maana.868 37. Kama wenzetu wanayaacha baadhi ya
865 Melanchthon, ‘επιεικεια.’
866 Aleksandro Mkuu (356 – 323 K.K.), mfalme wa Makedonia, aliyepambana na Uyunani nzima, Asia (Uturuki Mamboleo), Shamu, Misri na Uajemi, mpaka Pakistani. Katika mji wa Gordion huko Asia, alionyeshwa ama katika ngome ya mfalme Gordios au katika hekalu, gari la farasi lililofungwa na mfumo wa mafundo ambao haukuwezekana kufunguliwa na mtu yeyote. Kulingana na misendu, Aleksandro alipoliona fundo hilo, badala ya kujaribu kulifungua, alishika upanga wake na kulikata kabisa wakati wa bamvua mwaka wa 333 K.K. Kwa njia ya misendu hii, tendo hili la ghafla lilionekana kuwa kama utabiri wa ushinde wa Asia nzima.
867 Yasiyokuwa halali.
868 Mt. 12 : 1-8
mapokeo yasiyokuwa na maana, wana udhuru vya kutosha kwa kuwa haya yalidaiwa kwa sababu ya kustahilisha kuhesabiwa haki. Naam, wazo la namna hiyo kuhusu mapokeo ni la kukufuru.
38. Licha ya hayo, tungependa kuyafuata mapokeo ya kale yaliyoanzishwa katika Kanisa kwa ajili ya faida yao na kwa sababu yaliongezea utulivu. Isitoshe, tunayafafanua kwa maana iliyo bora mno,869 tukiliondoa wazo linaloshikilia kwamba, yanahesabia haki. 39. Maadui zetu hutushtaki kwa uongo kwamba, tunatangua taratibu bora na nidhamu katika Kanisa. Kiukweli tunaweza kudai kwamba, liturgia ya makanisa yetu870 ni nyoofu zaidi kuliko yao. Mtu akitaka kulichunguza jambo hili kwa makini, ataona kwamba, sisi tunazifuata kanuni kwa uamninifu zaidi kuliko wapinzani wetu. 40. Miongoni mwa wapinzani wetu, makuhani871 wa kukalifu na wafanyakazi wa kukodiwa huiongoza misa kwa ajili ya mshahara tu. Wanaimba Zaburi, siyo kwa kufundisha au kusali, bali kwa ajili ya ibada peke yake, kana kwamba, kazi hii ni ibada halali na ya kweli kwa sababu ya mshahara. Watu wengi kati yetu hukishiriki Chakula cha Bwana kila Jumapili, lakini baada ya kufundishwa, kuhojiwa na kuondolewa dhambi. Watoto huimba Zaburi ili kujifunza. Watu huimba kwa ajili kujifunza au kusali. 41 Miongoni mwa wapinzani wetu, hawana mafundisho yoyote ya katekisimo kwa watoto, hata ingawa kanuni imeyaagiza. Miongoni mwetu, wachungaji na wahudumu wa makanisa wanatakiwa kuwafundisha na kuwahoji vijana, desturi ambayo huyazaa matunda mema mno. 42.Miongoni mwa wapinzani wetu, kuna mikoa mingi ambapo mwaka mzima hakuna mahubiri, isipokuwa wakati wa Kwaresima, ilihali ibada maalumu ya Mungu ni mafundisho ya Injili. Wapinzani wetu wanapohubiri, wanazungumzia kuhusu mapokeo ya wanadamu, ibada za watakatifu, na mambo mengine hafifu ambayo, kwa hakika, yanadharauliwa na watu ambao wanatelekeza baada ya somo la Injili. Wachache ambao ni bora kwa kiasi, sasa wanaanza kuzungumzia matendo mema, lakini hawasemi lolote kuhusu haki ya imani au kuhusu imani katika Kristo au faraja ya dhamiri. Hata wanaishambulia sehemu hii muhimu mno ya Injili kwa kashfa zao. 43. Kwa upande mwingine, mahubiri yote katika makanisa yetu yanahusu mada kama vile: toba, kumwogopa Mungu, imani katika Kristo, haki ya imani, faraja ya dhamiri kwa imani, mazoezi ya imani, maombi – yaani, yawe ya aina gani, na uhakika kuwa ni ya kufaa na ya kusikika, msalaba, heshima kwa watawala, amri
869 Melanchthon, ‘Προς το ευφημοτερον,’ yaani, maana iliyo bora mno.
870 Kilatini: ‘Publica forma ecclesiae.’
871 Kilatini: ‘Sacrificulus;’ jina la makuhani wapagani waliotoa dhabihu hasa kwa niaba ya wafalme. Katika Kanisa la Magharibi, ‘sacrificium,’ yaani, “dhabihu,” ilimaanisha wakati wa Enzi ya Kati wa misa iliyoeleweka kuwa dhabihu mbele za Mungu. Makasisi maalumu waliathiriwa kuongoza Misa za namna hiyo ili kukusanya stahili mbele za Mungu na kufidia matendo ya upatanisho.
zote kwa ajili ya raia, tofauti baina ya ufalme wa Kristo - au ufalme wa kiroho –mambo ya kisiasa, ndoa, elimu na mafundisho ya watoto, usafi, na kazi zote za upendo. 44. Kutokana na maelezo haya juu ya hali ya makanisa yetu, ni wazi kwamba tunatunza nidhamu ya Kanisa, desturi takatifu na mila nzuri za Kanisa kwa bidii mno.
45. Tunafundisha kuhusu kufishwa kwa mwili na nidhamu ya mwili sawasawa na maneno ya Ukiri kwamba, kujifisha kweli kusikokuwa kwa bandia kunafanyika kwa njia ya msalaba na mateso ambayo kwayo Mungu anatuzoeza. Katika yote haya, lazima tuyatii mapenzi ya Mungu, jinsi Paulo asemavyo: “Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai.”872 46. Haya ni mazoezi ya kiroho ya hofu na imani. Mbali na unyonge huu wa mwili unaoletwa kwa njia ya msalaba, kadhalika, aina ya matendo ya hiari ni ya lazima. Kuhusu hilo, Kristo anasema: “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi.”873 Naye Paulo anasema: “Bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha.”874 47. Inatupasa kujitolea katika mazoezi haya, siyo kama ibada zitakazotuhesabia haki, bali kama kinga kwa ajili ya miili yetu, tusije tukashindwa na shibe na kuridhika mno na kuwa wazembe. Kwa sababu hiyo, tusije tukajiendekeza na kujidekeza kwa tamaa za miili yetu.
Jitihada hii lazima idumu kwa kuwa ina agizo la Mungu875 lisilokoma. 48. Lakini maagizo kuhusu vyakula na majira maalumu, hayasaidii lolote katika utiifu wa mwili. Wakati wa kufunga, vyakula vyao ni vitamu na vya anasa kuliko karamu nyinginezo na wapinzani wetu hata hawazingatii maagizo ya kisheria.
49. Mada hii kuhusu mapokeo ina mijadala mingi na migumu. Tunafahamu kutokana na uzoefu halisi kwamba, mapokeo ni mitego kweli ya dhamiri. Yanapodaiwa kama mambo ya lazima, yanaziumiza dhamiri ambazo zimeliacha tendo fulani la kuadhimisha. Kwa upande wingine, kufutwa kwake kunahusisha utata na maswali yake. 50. Lakini sababu yetu ni rahisi na wazi kwa sababu wapinzani wetu wanatulaani kwa kuwa tunafundisha kwamba, mapokeo ya wanadamu hayastahili msamaha wa dhambi. Hali kadhalika, wanayadai wanayoyaita “mapokeo ya ulimwenguni kote,” kuwa ya lazima kwa ajili ya kuhesabia haki. Hapa Paulo ni mlezi wetu thabiti anayepambana popote akisisitiza kwamba, matendo haya ya uzingatifu kamwe hayahesabii haki wala siyo ya lazima na hayapo juu wala zaidi ya haki ya imani. 51. Hata hivyo, tunafundisha kwamba, uhuru utumike kwa kiasi katika mambo haya ili watu wasiokuwa na
872 Rum. 12 : 1
873 Lk. 21 : 34
874 1 Kor. 9 : 27
875 Hapa, Melanchthon anamaanisha kufunga lakini bila sheria au kanuni zozote.
tajriba876 wasije wakabadilika kuwa maadui wa mafundisho ya kweli ya Injili kwa sababu ya matumizi mabaya ya uhuru. Jambo lolote lisibadilishwe katika desturi za zilizozoeleka bila sababu nzuri. Badala yake, desturi za zamani zifuatwe, ili kuyalea makubaliano ambayo yanaweza kutunzwa bila dhambi au usumbufu mkubwa. 52.Tumeonyesha katika mkutano huu877 kwa kiasi kikubwa kwamba, tunasita kuifuata miafaka pamoja na wengine wote, kwa ajili ya upendo, mambo yasiyo ya kujali878 ilihali ingetusumbua. Tuliamua kwamba, mwafaka wa hadhara, usiokuwa na hasara yoyote kwa dhamiri lazima upendelewe zaidi ya manufaa mengine yote. Tutasema zaidi kuhusu suala hili zima tutakapojadili nadhiri na mamlaka ya Kanisa.
Fungu Kumi na Sita: Utaratibu wa Kisiasa
1. Wapinzani wetu wanalikubali Fungu la Kumi na Sita bila ukinzani. Katika fungu hili tunakiri kwamba, Mkristo anapaswa kuhudumu serikalini kihalali, kutoa maamuzi kwa sheria za dola au sheria nyinginezo zilizokubaliwa, kuamuru adhabu halali, kuanzisha vita vya haki, kuhudumu jeshini, kuafikiana kwa njia ya sheria, kuwa na mali ya binafsi, kula kiapo inapohitajika na serikali, kuoa na kuolewa. Kwa kifupi, amri halali ya kiraia ni maagizo mema ya Mungu na amri takatifu ambazo Mkristo anaweza kujihusisha bila mashaka. 2. Suala hili zima kuhusu tofauti baina ya Ufalme wa Kristo na ufalme wa kisiasa, limemulikwa kwa njia inayofaa katika maandiko ya wanatheologia wetu. Ufalme wa Kristo ni wa kiroho; ni maarifa ya Mungu moyoni, kumwogopa Mungu na imani, mwanzo wa haki na uzima wa milele. Wakati huo huo, kwa nje, unaturuhusu kutumia amri halali za kisiasa za taifa tunaloishi, jinsi unavyoturuhusu kutumia dawa, usanifu majengo, chakula, kinywaji au hewa. 3. Injili haianzishi sheria mpya kuhusu milki ya raia, bali inatuamuru kuzitii sheria zilizopo, ziwe zimepitishwa na Wapagani au wengineo. Vile vile kwa utiifu huu inatuhimiza kuutekeleza upendo. Ilikuwa ni uwendawazimu kwa Karlstadt879 kujaribu kuziweka kwetu sheria za kimahakama za Musa. 4. Wanatheologia wetu wameandika kwa kina zaidi kuhusu mada hii kwa sababu watawa wa kiume walikuwa wameyaeneza mawazo mengi ya hatari kanisani. Waliita kumiliki mali kwa pamoja taifa la
876 Uzoefu.
877 Majadiliano ya Agosti, mwaka wa 1530 yenye shabaha ya kuyatafuta maafikiano baina ya wahusika wote.
878 Melanchthon,‘αδιαφορον.’
879 Andreas Bodenstein au Karlstadt (mnamo 1480-1541) alikuwa profesa huko Wittenberg hadi mwaka wa 1524. Alijaribu kutekeleza Matengezo ya Kanisa kwa njia ya mapinduzi, k.m. kwa njia ya kuondoa kabisa mapokezi ya liturgia, mavazi ya ibada na kadhalika. Alianza kumpinga Luther zaidi na zaidi na hata aliungwa mkono na walokole wa Matengenezo ya Kanisa.
kiinjili, waliita kutomiliki mali shauri la kiinjili na walikataa kwenda mahakamani. Mawazo haya yanaifunika sana Injili na mamlaka ya kiroho; pia, yanakuwa hatari kwa serikali. 5. Kwa maana, Injili haiharibu asasi za kijamii au kiuchumi bali inaziidhinisha kabisa, na inatuamuru kuzitii kama amri takatifu, siyo kwa sababu ya kuiogopa adhabu bali “kwa sababu ya dhamiri.”880
6. Yuliano Mwasi, Kelso881 na wengineo wengi waliwapinga Wakristo kwa kuwalaumu kwamba, Injili inaiharibu serikali kwa njia ya kukizuia kisasi kisheria na kufundisha mengine ambayo hayalingani na mahusiano ya kiraia. Maswali haya yaliwasumbua sana Origene, Nazianzo882 na wengineo japo itakuwa rahisi kuyajibu tukijua kwamba, Injili haipitishi sheria kuhusu hali ya kiraia bali ni msamaha wa dhambi na mwanzo wa uzima wa milele mioyoni mwa waumini. Licha ya hayo, haizikubali serikali za ulimwenguni bali inatufundisha zaidi kujitolea kwazo.883 Jinsi ambavyo tunapaswa kutii kwa lazima kanuni asilia za majira, na katika mabadiliko ya kipupwe na kiangazi kama amri za Mungu. 7. Injili inakataza kisasi binafsi, na Kristo hulisisitiza jambo hili mara nyingi mitume wasije wakafikiria kwamba, inawapasa kuwanyang’anya mamlaka yao wenye utawala serikalini jinsi ilivyokuwa katika ndoto ya Wayahudi kuhusu ufalme wa Masihi. Badala yake, aliwataka waufahamu wajibu wao wa kufundisha kwamba, ufalme wa kiroho hauibadilishi serikali ya kiraia. Kwa sababu hiyo, kisasi binafsi kinakatazwa, siyo kama ushauri wa kiinjili bali kama amri (Mt. 5: 39; Rum. 12: 19). Kisasi cha hadharani kupitia kwa hakimu, hakikatazwi bali kinaamriwa kabisa na kulingana na Paulo, ni kazi ya Mungu (Rum. 13: 1 n.k.). Aina za visasi vya hadhara ni maamuzi ya mahakama, adhabu, vita, na huduma ya jeshi. 8. Jinsi ambavyo hukumu za waandishi wengi zimekuwa na kiwango hafifu katika mambo haya, ni ushahidi kutokana na mtazamo wao wenye makosa kwamba, Injili ni tukio la nje, la kigeni na ni aina ya muundo wa serikali ya utawa. Hawakuona kwamba, Injili huileta haki ya milele mioyoni, na wakati huo huo, inaiidhinisha serikali ya kiraia.
9. Pia ni uongo kudai kwamba, ukamilifu wa Kikristo unamaanisha kutokuwa na mali. Ukamilifu wa Kikristo haupatikani katika kuzidharau amri za kiraia bali ni katika mitazamo ya moyo, kama vile kumcha Mungu sana, na katika imani
880 Rum. 13: 5
881 Julianos Apostata, Kaisari (361-363). Alikufa vitani kwa maneno haya: ‘Umenishinda Mnazareti!’ Kitabu chake kinachoitwa, ‘Dhidi ya Wakristo’ 2, 12. Kelso (Kelsos) mwanafalsafa Mpagani katika karne ya pili. Baba wa Kanisa la Origene alimpinga kwa maandiko yake, ‘Dhidi ya Kelso’ 7, 58, II. 882 Gregorio wa Nazianzo (mnamo 329- 395), askofu na mwanatheologia Myunani, mmojawapo wa akina
Baba maarufu wa Kapadokia waliotetea ‘Ukiri wa Imani wa Nikea’ dhidi Waariano pamoja na Athanasio Mkuu, Askofu Mkuu wa Aleksandria.
883 Rum. 13: 1
thabiti. Ingawa Ibrahimu, Daudi na Danieli walikuwa wenye mali na mamlaka ya juu, hawakupungukiwa katika ukamilifu wao kuliko mtawa yeyote. 10. Lakini watawa wa kiume waliwavutia watu kwa unafiki huu wa nje na waliwapofusha wasione kiini cha ukamilifu wa kweli. Naam, ukamilifu wa kweli unapatikana katika mambo gani! Wamesifu kiasi gani kuhusu kushikamana na mali kuwa jambo la Kiinjili! 11. Sifa ya jinsi hii ni hatari mno, hasa, kwa sababu inayapinga Maandiko Matakatifu. Maandiko Matakatifu hayafundishi ushirika wa mali bali yanaamuru: “usiibe.” Amri Kumi za Mungu zinatambua haki ya umiliki na zinamwagiza kila mmoja awe na mali yake mwenyewe. Wyckliffe alikosea vibaya sana alipodai kwamba, mapadre hawakuruhusiwa kumiliki mali zao wenyewe.884 12. Majadiliano yasiyokuwa na mwisho kuhusu mikataba, kamwe hayatatosheleza dhamiri njema, isipokuwa tu yatambue kanuni kwamba, Mkristo anaweza kuzitumia kihalali amri za kiraia na sheria. Kanuni hii huzilinda dhamiri kwa kuwa inafundisha kwamba, iwapo mikataba inaidhinishwa na mahakimu au na sheria, vivyo hivyo, inakuwa halali mbele za Mungu.
13. Wanatheologia wenzetu wamelielezea suala hili zima kwa uwazi kuhusu mambo ya kisiasa. Walifanya hivyo kwani karibu watu wote wema waliojishughulisha na siasa na biashara wameshuhudia jinsi walivyosaidiwa sana baada ya nadharia za watawa wa kiume kuwasumbua na kuwafanya wawe na mashaka iwapo Injili iliruhusu shughuli za jinsi hiyo za umma na za binafsi. Tumeurudia tena msimamo wetu ili watu wa nje wapate kuelewa kwamba, mafundisho tunayoyafuata hayadhoofishi bali yanayaimarisha mamlaka ya mahakimu na heshima ya amri za kiraia kwa jumla. Umuhimu wa suala hili uligubikwa na maoni ya kijinga ya nadharia za watawa wa kiume ambazo ziliupendelea sana umaskini na unyenyekevu wa kinafiki kuliko jamii na uchumi, ingawa mambo haya yameamuriwa na Mungu ilihali mafundisho ya ushirika wa Platoni haujaamuriwa na Mungu.
Fungu la Kumi na Saba: Kristo Kuja Kuhukumu
1. Wapinzani wetu wanalikubali Fungu la Kumi na Saba bila kikwazo. Hapa tunakiri kwamba, Kristo atatokea mwishoni mwa ulimwengu, atawahuisha wafu wote, atawapa wacha Mungu uzima wa milele na furaha ya milele. Atawahukumu wanaokufuru wateswe pamoja na Ibilisi bila mwisho.
884 ‘De Ecclesia’ 8.
Fungu la Kumi na Nane: Hiari Huru
1. Wapinzani wetu hulikubali Fungu la Kumi na Nane kuhusu hiari huru lakini wanaongezea baadhi ya ushuhuda ambao, kwa kiasi kidogo sana, unalingana na kusudi lao.885 Wanaongezea pia tahadhari kwamba, mengi yasije yakatolewa kwa hiari huru, jinsi ilivyo katika imani ya Pelagio, au uhuru wote ukatazwe kama jinsi ilivyo katika Uwamani.886 2. Vyema kabisa; lakini kuna tofauti gani baina ya Wapelagio na wapinzani wetu, kwa maana haya makundi yote mawili huamini kwamba, watu huweza kumpenda Mungu na kutimiza “kiini cha matendo,”887 kinachohitajiwa na amri za Mungu na kwamba, bila Roho Mtakatifu wanadamu huweza kustahili neema na kuhesabiwa haki kwa matendo ambayo akili huyazaa yenyewe? 3. Ni kiasi gani cha upuuzi kinachofuatia dhana hizi za Wapelagio ambazo zinafundishwa katika vyuo vyao kwa mamlaka makuu kabisa! Agostino, aliyemfuata Paulo, anazikanusha dhana hizi kwa nguvu. Awali, tayari tuliidondoa kauli yake katika fungu linalohusu kuhesabiwa haki.
4. Basi, sisi hatukatai kabisa uhuru wa hiari ya mwanadamu. Hiari ya mwanadamu ina uhuru wa kuchagua kati ya matendo na mambo yanayoeleweka kwa akili ya kibinadamu. Kwa kiasi fulani, inaweza kuitimiza haki ya raia au haki ya matendo. Inaweza kuzungumzia kuhusu Mungu na kumwabudu kwa matendo ya nje. Inaweza kuwatii mahakimu na wazazi. Kwa nje, inaweza kuchagua kuacha mauaji, uzinzi, au wizi. Kwa kuwa asili ya mwanadamu bado ina ufahamu na hukumu kuhusu mambo yanayohusu hisia, pia hubakiza hiari katika mambo haya, ikiwa ni pamoja na uhuru na uwezo wa kuitimiza haki ya raia. Maandiko Matakatifu yanaiita haki hii ambayo, asili ya mwili au akili inaweza kuitimiza bila Roho Mtakatifu, kuwa haki ya mwili. 5 Hata hivyo, nguvu ya tamaa mbaya888 ni kubwa mno kiasi kwamba, watu huzitii tamaa zao mbaya zaidi kuliko sauti za hukumu yao. Wakati huo huo, kulingana na asemavyo Paulo,889 Ibilisi afanyaye kazi katika wana wa kuasi, haachi kuuchochea udhaifu huu wa asili kwa njia ya makosa mbalimbali. Kwa sababu hizo, hata haki ya kiraia imeadimika sana miongoni mwa wanadamu, jinsi tunavyoona kwamba, hata wanafalsafa walioonekana kuitaka haki hii, hawakuipata. 6. Aidha, ni uongo kabisa kusema kwamba, mtu hatendi dhambi akiyatenda matendo ya amri nje ya
885 1 Kor. 7: 37; Sir 31: 10; Mwa. 4: 7; Isa. 1: 19-20; Yer. 3: 5; Eze. 18: 31-32; 1 Kor. 14: 32; 2 Kor. 9: 7; Mk. 14: 7; Mt. 23: 37
886 Mani (mnamo 216 - mnamo 277 B.K.) Mwalimu Mwajemi aliyeanzisha dini yake iliyofundisha ugavi mkali baina ya wema na ubaya. Baba wa Kanisa, Agostino wa Hippo, kwa muda, alikuwa mfuasi wa dini hii.
887 Kilatini: ‘Quoad substantiam actuum.’
888 Kilatini: ‘Concupiscentia.’
889 Efe. 2: 2
neema. Licha ya hayo, wanaongezea kwamba, kwa wema wa ulinganifu kwa matendo haya,890 mwanadamu hupokea msamaha wa dhambi na haki. Bila Roho Mtakatifu, mioyo ya wanadamu haina hofu kwa Mungu wala tegemeo kwa Mungu wala imani kwamba, Mungu huwasikia, huwasamehe, huwasaidia, au huwaokoa. Kwa hiyo, wao siyo wachaji kwa maana: “Mti mwovu hauwezi kuzaa matunda mazuri;” na “pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.891
7. Japo tunakubaliana na hiari huru, uhuru, na uwezo wa kutenda matendo ya nje ya sheria, hata hivyo, hatuihesabu hiari huru kuwa na uwezo wa kiroho kwa ajili ya: kumcha Mungu kweli, imani ya kweli katika Mungu, maarifa na tegemeo kwamba, Mungu hutuzingatia, hutusikia, na hutusamehe. Haya ndiyo matendo ya kweli ya ubao wa kwanza892 ambayo Moyo wa mwanadamu hauwezi kuyatekeleza bila Roho Mtakatifu. Jinsi Paulo anavyosema: “mwanadamu wa tabia ya asili,” akimaanisha mtu ambaye huutumia tu welekevu wa asili, “hawezi kuyafahamu mambo ya Roho wa Mungu.”893 8. Jambo hili linaweza kuamuriwa vizuri ikiwa watu watazingatia kile ambacho mioyo yao huamini kuhusu mapenzi ya Mungu: je, wanaamini kweli kwamba, Mungu huwajali na huwasikia? Ni vigumu hata kwa watakatifu kuitimiza imani hii maana, kwa wasiomcha Mungu haiwezekani kabisa. Jinsi tulivyosema awali, inazaliwa wakati mioyo iliyotishwa inaisikia Injili na kuipokea faraja.
9. Hivyo, inafaa sana kutofautisha kati ya haki ya kiraia inayohesabiwa kwa hiari huru na haki ya kiroho inayohesabiwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu katika wale waliozaliwa upya. Hivyo, nidhamu ya nje inahifadhiwa kwa sababu watu wote wanapaswa kuelewa kwamba, Mungu anahitaji haki hii ya raia na kwamba, tunaweza kuitimiza kwa kiasi fulani. Wakati huo huo, inaonyesha tofauti kati ya haki ya binadamu na haki ya kiroho. Yaani, tofauti kati ya mafundisho ya kifalsafa na mafundisho ya Roho Mtakatifu, na inaonyesha sababu ya kumhitaji Roho Mtakatifu. 10. Tofauti hii siyo uvumbuzi wetu bali ni mafundisho sahihi ya Maandiko Matakatifu. Agostino pia huizungumzia na hivi karibuni Guilelmo wa Pari894 ameizungumzia vizuri zaidi. Lakini wale walioota ndoto kwamba, watu wanaweza kuitii Sheria ya Mungu bila Roho Mtakatifu na kwamba, Roho Mtakatifu anatolewa kwao bila kuijali stahili ya utiifu huu, wameyakandamiza haya mafundisho sahihi kijinai.
890 Kilatini: ‘De congruo.’
891 Mt. 7: 18; Ebr. 11: 6
892 Yaani, mbao mbili za mawe zenye Amri Kumi za Mungu.
893 1 Kor. 2: 14
894 Guilelmo wa Pari au Peraldus (+ kabla 1270), mtawa, mwandishi na mhubiri kutoka daraja la Kidominikano; ‘Summa de virtutibus. De iustitia 5’ mwaka wa 1492. Hapa, Melanchthon alimrejea Agostino Bandia ‘Hypomnesticon’ 3, 4, 5.
Fungu la Kumi na Tisa: Chanzo cha Dhambi
1. Wapinzani wetu wanalikubali Fungu la Kumi na Tisa. Hapa tunakiri kwamba, Mungu pekee yake alianzisha asili nzima na huvitunza vitu vyote vilivyopo. Hata hivyo, chanzo cha dhambi ni mapenzi ya Ibilisi na watu wanaojitenga na Mungu, jinsi Kristo alivyosema juu ya Ibilisi: “Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe.”895
Fungu la Ishirini: Matendo Mema
1. Katika Fungu la Ishirini, wanaeleza maneno haya wazi kwamba, wanakataa na hawalikubali tamko letu kuwa watu hawastahili msamaha wa dhambi kwa matendo mema. Wanatangaza dhahiri kwamba, wanakataa na hawalikubali fungu hili. Tunaweza kusema nini kuhusu suala lililo wazi? 2. Hapa, watunzi wa Hoja wameonyesha nafsi yao ya kweli. Ni jambo lipi lililo wazi zaidi kanisani kuliko hili yakwamba, msamaha wa dhambi unatolewa bure kwa ajili ya Kristo, na kwamba, Kristo ndiye mpatanishi kwa ajili ya makosa na siyo matendo yetu? jinsi Petro anavyosema: “Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.”896 Tungependa kukubaliana na Kanisa hili la manabii kuliko wale waandishi wa Hoja waliolaaniwa ambao wanamkufuru Kristo kwa ujeuri sana. 3. Hata hivyo, kulikuwa na wanatheologia wengine walioshikilia kwamba, watu wanahesabiwa haki mbele za Mungu baada ya kusamehewa dhambi, siyo kwa sababu ya imani bali kwa njia ya matendo yao wenyewe. Hawakudhamiria kwamba, msamaha wa dhambi wenyewe unatolewa kwa sababu ya matendo yetu, na siyo bure kwa ajili ya Kristo.
4. Kwa hiyo, kufuru ya kuhusisha heshima ya Kristo kwa matendo yetu haivumiliki kabisa. Wanatheologia hawa hawana aibu yoyote kabisa kama wakithubutu kuingiza dhana hii kanisani kwa njia ya magendo. Tuna hakika kuwa Kaisari Mheshimiwa mno na watawala wengi zaidi wangekuwa wamekataza kubakia kwa kauli hii ya Hoja ikiwa umakini wao ungekuwa umevutwa kwa hilo. 5. Hapa, tungeweza kunukuu shuhuda zisizokuwa na mwisho kutoka kwa Maandiko Matakatifu na Mababa wa Kanisa. Hata hivyo, tumekwisha kusema vya kutosha kuhusu mada hii hapo juu. Lakini mtu ajuaye Kristo ametolewa kwa sababu gani, ajuaye pia kwamba, Kristo ni mpatanishi kwa ajili ya dhambi zetu, hana haja yoyote ya ushuhuda mwingi zaidi. Isaya anasema: “BWANA ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.”897 Basi, wapinzani wetu wanafundisha kinyume
895 Yn. 8: 44
896 Mdo. 10: 43
897 Isa. 53: 6
chake kwamba, Mungu ameziweka dhambi zetu katika matendo yetu na siyo juu yake Kristo. Hatuelekei kuyataja matendo wanayoyadai hapa. 6. Tunaona kwamba, amri ya kutisha sana imeelekezwa kwetu sisi, ambayo ingetutisha zaidi ikiwa tungekuwa tunabishana kuhusu mambo yenye mashaka na na ya upuuzi. Sasa, katika dhamiri zetu tunaona kwamba, wapinzani wetu wanaulaani ukweli ulio wazi kabisa ambao lazima Kanisa liutetee na unaozidisha utukufu wa Kristo.
Tunaweza kuvidharau kwa urahisi vitisho vikuu vya ulimwengu na kuyastahimili kwa ujasiri mateso yoyote kwa ajili ya Kristo na kwa ajili ya maendeleo ya Kanisa. 7. Ni nani ambaye hatafurahia kufa katika ukiri huu na mafungu yake kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi bure kwa imani, kwa ajili ya Kristo na siyo kwa stahili za matendo yetu? 8. Dhamiri za wachaji hazitakuwa na msingi imara wakati zinapotishwa na dhambi na mauti, na Ibilisi anazishawishi zikate tamaa isipokuwa zifahamu kwamba, lazima ziamini katika msamaha wa dhambi unaotolewa bure kwa ajili ya Kristo. Imani hii inahimili na kuihuisha mioyo katika mapambano yake makali dhidi ya kukata tamaa.
9. Suala hili ni la thamani sana. Kwamba, kwalo tunajiepusha na hatari yoyote: “Usishindwe na uovu; endelea bila hofu!”898 Linamhusu kila mmoja wenu aliyekubali ukiri wetu wakati wapinzani wetu wanatumia vitisho, maumivu makali na adhabu ili kujaribu kuwaondolea ninyi hii faraja kubwa iliyotolewa kwa Kanisa zima katika fungu letu hili. 10. Kila achunguzaye suala hili hatapungukiwa na ushuhuda mwingi unaoimarisha nafsi yake katika Maandiko Matakatifu. Kwa maana Paulo anapiga kelele katika Rum. 3 na 4 kwamba, dhambi zinasamehewa bure kwa ajili ya Kristo. Hivyo, anasema: “Wanahesabiwa haki bure kwa neema yake;” “ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote.”899 Maana yake: Ahadi ingetegemea matendo yetu, haingehakikishwa. Ikiwa msamaha wa dhambi ungetolewa kwa ajili ya matendo yetu, ni lini tungejua kuwa tumeupata? Ni lini dhamiri iliyotishwa ingepata tendo ambalo ingedhania kuwa linatosha kuituliza ghadhabu ya Mungu? 11. Lakini tumekwisha kuzungumzia suala hili zima hapo juu. Msomaji anaweza kuupata ushuhuda wetu hapo. Njia ya aibu ambayo kwayo wapinzani wetu wamelichukulia suala hili imetulazimisha kuliwasilisha shtaka kuliko kulitunga kanusho la hatua kwa hatua. Wameingia katika kumbukumbu wakiikataa imani yetu kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi siyo kwa ajili ya matendo yetu bali bure, kwa imani, kwa ajili ya Kristo.
12. Kando na kulilaani fungu letu, wapinzani wetu wamezinukuu aya kadhaa za Maandiko Matakatifu. Inafaa kuzichunguza baadhi ya hizo. Wanamrejea
898 Vergilio, Aeneis 6, 95. 899 Rum. 3: 24; 4: 16
Petro: “Jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu.”900 Msomaji mpendwa, sasa unaona kwamba, wapinzani wetu hawakupoteza wakati wowote kujinufaisha kwa njia ya kimantiki kwa kuwa wamejifunza hila za ajabu sana za kulifikia hitimisho lolote kiholela kutoka kwa Maandiko Matakatifu. “Uthibitishe wito wako kwa matendo mema,” Kwa hiyo, matendo hustahili msamaha wa dhambi! Kwa madai hayo hayo, tungeweza kusema kwa mtu aliyehukumiwa kifo na kisha akasamehewa,: hakimu anaamuru kwamba, kuanzia sasa na baadaye usiibe mali ya watu wengine, kwa hiyo, umesamehewa. 13. Hoja ya jinsi hiyo ni kuyafanya matokeo kuwa sababu. Naam, Petro anazungumzia kuhusu matendo yanayoufuata msamaha wa dhambi. Anafundisha kwamba, matendo haya yanapaswa kutendwa ili kuuthibitisha wito wao. Maana yake: wasije wakaanguka kutoka katika wito wao kwa kutenda dhambi tena. Fanyeni matendo mema ili kudumu katika wito wenu na wala msipoteze karama zake ambazo mlipewa kabla ya matendo yenu na siyo kwa sababu ya matendo hayo ambayo sasa yanatimizwa na imani. Imani haibaki ndani ya wale ambao wamempoteza Roho Mtakatifu na kuikataa toba; kama jinsi tulivyosema awali kwamba, imani inapatikana katika toba.Wanauongezea ushuhuda mwingine usiohusika kabisa.
14. Mwishoni, wanasema kwamba, wazo hili lililaaniwa miaka elfu moja iliyopita wakati wa Agostino. Dai hili ni uzushi kabisa! Daima, Kanisa la Kristo limeamini kwamba, msamaha wa dhambi unapokewa bure; kwa kweli, Wapelagio walilaaniwa kwa kushikilia kwamba, neema inatolewa kwa ajili ya matendo yetu.901 Licha ya hayo, hapo juu, tumeuonyesha vya kutosha msimamo wetu kwamba, matendo mema lazima yaifuate imani. Sisi hatuibatilishi sheria jinsi Paulo asemavyo,902 bali tunaithibitisha, kwa maana tunapopokea Roho Mtakatifu kwa imani, utimizaji wa sheria lazima ufuatie ambao kwao, upendo, uvumilivu, usafi wa maisha na matunda mengine yote ya Roho yanazidi kuzaliwa.
Fungu la Ishirini na Moja: Ibada ya Watakatifu
1. Wanalilaani kabisa hili Fungu la Ishirini na Moja kwa sababu hatuhitaji ibada ya watakatifu. Hakuna popote ambapo wanatumia ujuzi wa mwingi hivyo, lakini wanaloweza kulithibitisha ni kwamba, watakatifu wanapaswa kuheshimiwa. Hali kadhalika, watakatifu walio hai wanapaswa kuwaombea watu wengine kana kwamba, kwa sababu hiyo, kuwaomba watakatifu waliokufa kunakuwa kwa lazima. 2.Wanamrejea Sipriano aliyemwomba Kornelio
900 2 Pet. 1: 10
901 Sinodi za Karthago na Mileve ya mwaka wa 416 huko Kaskazini mwa Afrika na Sinodi ya Efeso ya mwaka wa 431 huko Asia.
902 Rum. 3: 31
alipokuwa bado hai awaombee ndugu zake baada ya kufariki dunia.903 Wanautaja mfano huu, ili kuithibitisha ibada ya wafu! Vilevile wanaurejelea mgongano kati ya Hieronimo na Vigilantio na kusema: “Katika medani904 hii Hieronimo alimshinda Vigilantio905 miaka elfu kumi na moja iliyopita.” Hivyo, wapinzani wetu wanaushangilia ushindi kana kwamba, tayari vita vimekwisha. Punda hawa hawaoni kwamba, mgongano huu kati ya Hieronimo na Vigilantio hauna silabi hata moja kuhusu watakatifu. Badala yake, unazungumzia tu kuhusu kuwaheshimu na wala siyo kuwaomba watakatifu. Hata waandishi wengine wote wa kale kabla ya Gregorio906 hawakutaja ibada ya watakatifu. 3. Kusema kweli, nadharia ya ibada ya watakatifu pamoja na nadharia za wapinzani wetu wanaofundisha kuhusu matumizi ya stahili, hazina ushuhuda wowote wa waandishi wa kale.
4. Ukiri wetu unakubali kuwaheshimu watakatifu. Heshima hizo ni za aina tatu. Heshima ya kwanza ni shukrani: Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa ajili ya kuonyesha mifano ya huruma yake, kwa ajili ya kuyafunua mapenzi yake ya kuwaokoa wanadamu, na kwa ajili ya kuwatuma walimu na karama nyingenezo kwa Kanisa. Karama hizi kubwa mno zinapaswa kuhimidiwa sana. Hali kadhalika, watakatifu wenyewe wanapaswa kusifiwa kwa sababu ya kuzitumia karama hizi kwa uaminifu, jinsi Kristo anavyowasifu watumwa waaminifu.907 5.Heshima ya pili ni kuimarisha imani yetu: Tunapomwona Petro akisamehewa baada ya kukana kwake, tunahimizwa kuamini kwamba, kweli, neema ni nyingi zaidi ya dhambi.908 6. Heshima ya tatu ni kuiga: kwanza, kuiiga imani yao na baadaye kuyaiga maadili yao ambayo kila mmoja anapaswa kuyaiga kadiri ya mwito wake. 8. Wapinzani wetu hawahitaji heshima hizi za kweli. Badala yake, wanajadiliana tu kuhusu ibada ya watakatifu, ambayo, kwa kweli, ingawa haikuwa hatari, siyo ya lazima.
8. Licha ya hayo, tunakubali kwamba, malaika hutuombea. Jambo hili linashuhudiwa katika Zek. 1: 12 ambapo malaika anasali akisema: “Ee BWANA wa majeshi, hata lini utakataa kuurehemu Yerusalemu, na miji ya Yuda uliyoikasirikia miaka hii sabini?” 9. Tunakubali pia kwamba, watakatifu walio mbinguni, huliombea Kanisa zima kwa jumla jinsi walivyoliombea Kanisa la ulimwenguni kote walipokuwa hai. Hata hivyo, hatuna ushuhuda wowote katika
903 Sipriano Ep. 60, 5.
904 Yaani, uwanja wa vita.
905 Vigilantio wa Akvitania (Ufaransa, mnamo 400) alipinga ibada ya watakatifu na masalio yao, pia aliupinga useja wa mapadre dhidi ya Hieronimo.
906 Papa Gregorio Mkuu (mnamo 540-604). Wakati wa Kanisa la Zamani, akina Baba walitofautisha baina ya ibada ya Mungu ‘λατρεια’ na huduma ya watakatifu ‘δουλεια.’
907 Mt. 25: 21,23
908 Rum. 5: 20
Maandiko Matakatifu kuhusu maombi ya wale waliokufa, isipokuwa ile njozi iliyoandikwa katika kitabu cha pili cha Wamakabayo 15: 14.
10. Ingawa watakatifu wanaliombea Kanisa kwa juhudi, haimaanishi kwamba, lazima waabudiwe. Lakini, ukiri wetu unalithibitisha jambo hili kwamba, Maandiko Matakatifu hayatufundishi kuwaabudu watakatifu wala kuuomba msaada wao. Maana, hakuna amri, wala ahadi, wala mfano wowote unaoweza kuonyeshwa kutoka katika Maandiko Matakatifu kuhusu ibada ya watakatifu; Kutokana na hili, inafuata kwamba, dhamiri haziwezi kuwa na uhakika wowote kuhusu maombi ya namna hiyo. Kwa kuwa sala haina budi kutokana na imani, tunawezaje kujua iwapo Mungu anakubali maombi ya namna hiyo? Bila ushuhuda wa Maandiko Matakatifu, tunawezaje kujua kwamba, watakatifu huyasikia maombi ya mtu binafsi? 11. Kuna ushahidi kwamba, baadhi ya wataalamu huwachukulia watakatifu kuwa na sifa wazi za kimungu, yaani, uweza wa kuyatambua mawazo ya akili zetu yasiyotamkwa. Wanajadiliana kuhusu maarifa ya asubuhi na jioni, kwa sababu, labda kwa sababu hawana uhakika iwapo watakatifu hutusikia asubuhi ama jioni.909 Hawajalibuni hili ili kuwaheshimu watakatifu, bali kuzitetea ibada zao za kujinufaisha. 12. Kwa kuwa ibada ya watakatifu haiwezi kuthibitishwa kwa Neno la Mungu, wapinzani wetu hawawezi kulitoa lolote dhidi ya hoja hii. Hatuwezi kuthibitisha kwamba, watakatifu wanayasikia maombi yetu, na hata kama wanayasikia, kwamba, yanakubaliwa na Mungu. 13. Kwa hiyo, wapinzani wetu wasitulazimishe kukubali jambo lisilo hakika, maana sala bila imani siyo sala. Wanapouelekeza mfano huu kwa Kanisa, itajulikana wazi kwamba, hii ni desturi mpya kabisa katika Kanisa. Sala za zamani hazikuwaomba watakatifu910 ijapokuwa ziliwataja. Licha ya hayo, ibada hii mpya katika Kanisa si sawa na ibada ya watu binafsi. 14. Wapinzani wetu hawaidai tu ibada ya watakatifu katika staha yao, bali wanazitumia hata stahili za watakatifu kwa wengine na kuwafanya watakatifu kuwa wapatanishi na pia waombezi. Madai haya hayawezi kuvumilika kabisa, kwa kuwa, kwa njia hii, heshima ya pekee ya Kristo inahamishwa hadi kwa watakatifu. Wapinzani wetu wanawafanya watakatifu kuwa wapatanishi na watulizaji ingawa wanatofautisha kati ya wapatanishi wa uombezi na wapatanishi wa wokovu, ni wazi kwamba, wanawafanya watakatifu kuwa wapatanishi wa
909 Nadharia ya Uwanazuoni kuhusu ujuzi wa malaika kutokana na mawazo ya Agostino katika Maelezo ya Kitabu cha Mwanzo ‘De Genesi ad litteram’ 4, 24.29-32). Ujuzi wa asubuhi ‘cognitio matutina’ ni ujuzi upitao asili, ujuzi wa Mungu na ufunuo wake. Ujuzi wa jioni ‘cognitio vespertina’ ni ujuzi utokanao na asili.
910 Sala ya kwanza ya Misa, Kilatini: ‘Collecta;’ sala fupi za siku. Sala hizi zinazobadilika siku kwa siku katika liturgia daima zimemwelekeza Mungu peke yake.
wokovu. 15. Wanayasema hayo bila ushuhuda wa Maandiko Matakatifu kwa kuwaita wapatanishi wa maombezi. Tukitumia lugha nyepesi, mafundisho haya pia yanaivuruga huduma ya Kristo, na huyahamisha matumaini tunayopaswa kuyapata katika rehema ya Kristo hadi kwa watakatifu. Wanadamu hudhania kwamba, Kristo ni mkali sana na watakatifu wanaweza kufikiwa kwa urahisi zaidi. Kwa sababu hiyo, wanaitegemea zaidi huruma ya watakatifu kuliko huruma ya Kristo na wanamtoroka Kristo na kuwakimbilia watakatifu. Hivyo, kweli, wanawafanya watakatifu kuwa wapatanishi wa wokovu.
16. Sasa tutadhibitisha kwamba, kweli, wanawafanya watakatifu siyo tu kuwa waombezi bali pia wapatanishi. Maana yake: wapatanishi wa wokovu. Kwa sasa, hatutayazungumzia matumizi mabaya ya umma bali tutayajadili maoni ya wanatheolojia. Watu wasiokuwa na elimu wanaweza kuyahukumu yaliyobakia.
17. Mpatanishi anapaswa kuwa na sifa mbili. Kwanza kabisa, lazima awe na Neno la Mungu linalotuhakikishia kwamba, Mungu anataka kuwahurumia na kuwasikia wale wamwombao kwa njia ya mpatanishi huyu. Kwa ajili ya Kristo, kuna ahadi ya jinsi hiyo: “Tena . . . Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.”911 Hakuna ahadi yoyote kama hiyo kwa watakatifu. Kwa sababu hiyo, dhamiri haziwezi kuwa na hakika kwamba, zitasikilizwa kwa ajili ya maombi ya watakatifu. Kwa hiyo, msingi wa maombi ya jinsi hiyo, haupatikani katika imani. 18. Isitoshe, tuna amri ya kumwomba Kristo kulingana na maneno haya: “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao.”912 Kwa kweli, maneno haya yanatuhusu sisi. Katika Isa. 11: 10, Isaya anasema: “Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese, lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta.” Zab. 45:12 inasema: “Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako.” Zab. 72:11,15 inasema: “Naam, wafalme wote na wamsujudie; na baadaye kidogo: “Na wamwombee daima.” Katika Yohana 5: 23, Kristo anasema: “Ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba.” Katika 2 The. 2: 16-17, Paulo anaomba: “Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, . . . awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.” Je, ni agizo au mfano gani wapinzani wetu wanaweza kuuonyesha kutoka katika Maandiko Matakatifu kuhusu ibada ya watakatifu?
19. Sifa ya pili kwa mpatanishi ni hii: sifa zake lazima ziidhinishwe913 ili kuwafanya watu wengine kuridhika na kutolewa kwa njia ya hesabu ya Kimungu,
911 Yn 16, 23
912 Mt 11, 28 913 Yaani, na Mungu.
ili tuweze kuhesabiwa haki kwazo kana kwamba, stahili hizo zilikuwa zetu wenyewe. Iwapo fulani atalipa deni kwa ajili ya rafiki yake: mdaiwa anakuwa huru kwa wema wa mwingine kana kwamba, ni mali yake. Hali kadhalika, tunapomwamini Kristo, stahili zake zinatolewa kwetu ili tuhesabiwe haki kwa njia ya tegemeo la stahili za Kristo kana kwamba, zilikuwa stahili zetu wenyewe.
20. Kwa hivyo, vyanzo vya imani katika huruma ni ahadi na kutolewa kwa stahili. Imani kama hiyo iliyo katika ahadi ya Mungu na stahili za Kristo lazima iwe msingi wa maombi. Hatuna budi kuwa na hakika kabisa kwamba, tunasikiwa kwa ajili ya Kristo na tuna Baba mwenye rehema aliyepatanishwa kwa stahili zake Kristo.
21. Kwanza, wapinzani wetu wanatuamuru tuwaombe watakatifu, ingawa hawana ahadi ya Mungu, wala amri, wala mfano kutoka katika Maandiko Matakatifu. Lakini, wangetutaka tutegemee zaidi katika huruma ya watakatifu kuliko katika huruma ya Kristo, japo Kristo alituamuru tumwendee yeye na siyo kuwaendea watakatifu. 22. Pili, wanatutaka tuzitegemee stahili za watakatifu. Wanazitumia stahili hizi kwa watu wengine sawa na afanyavyo Kristo, kana kwamba, tulihesabiwa haki kwazo, jinsi tunavyohesabiwa haki kwa stahili za Kristo. Hatuyatoi mashtaka ya uongo hapa. Wanasema kwamba, wanazitumia stahili za watakatifu katika vyeti vya upatanisho.914 23. Gabriel Biel anathubutu kuarifu kuhusu ufafanuzi wa Kanuni za Misa: “Kwa utaratibu ulioanzishwa na Mungu, inatubidi kuutafuta msaada wa watakatifu ili tuokolewe kwa stahili na nadhiri zao.”915 Haya ndiyo maneno ya Gabriel mwenyewe. Hata hivyo, kuna upuuzi mkubwa zaidi katika vitabu na mahubiri ya wapinzani wetu hapa na pale. Je, hili ni lipi isipokuwa kuwafanya watakatifu kuwa wapatanishi? Ikiwa itatupasa kuwaamini kwa ajili ya wokovu wetu, basi, wanawekwa katika kiwango sawa na Kristo.
24. Ni wapi basi, ambapo Mungu ameweka amri hii kwamba, “inatubidi kuutafuta msaada wa watakatifu” kama asemavyo mtu huyu? Mwache, autoe mfano au fundisho angalau moja kutoka katika Maandiko Matakatifu! Labda wanaupata utaratibu huu kutoka katika majumba ya wafalme ambapo marafiki walitumiwa kama watetezi. Lakini iwapo mfalme amemteua mtetezi fulani, hataki tena aombwe rufaa kwa njia ya wengine. Kwa sababu hiyo, kwa kuwa Kristo ameteuliwa kuwa mwombezi wetu na Kuhani Mkuu, mbona tuwatafute wengine?
914 Tangazo ‘Unigenitus’ la Papa Klementi wa Sita mwaka wa 1343.
915 Gabriel Biel katika kitabu chake kiitwacho, ‘Ufafanuzi wa Kanuni za Misa Tatakatifu’ ‘Sacri canonis missae expositio’ mwaka wa 1488.
25. Mtindo huu wa ondoleo la dhambi hutumiwa pahali pengine: “Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo, stahili za Bikira Aali mno Mariamu na watakatifu wote ziwe nawe kwa ajili ya msamaha wa dhambi!”916 Kulingana na tangazo hili la kuachiliwa, tunapatanishwa na kuhesabiwa haki, siyo kwa stahili za Kristo peke yake, bali pia kwa stahili za watakatifu wengine. 26. Baadhi yetu tumemwona mtawa wa kiume mmoja, mwanatheologia, aliyeitwa kumfariji daktari fulani wa theologia aliyekaribia kufa. Hakufanya lolote isipokuwa kuitaja sala hii kwa daktari anayefariki: “Mama wa neema, utulinde na yule adui na utupokee saa ya kufa kwetu.”
27. Iwapo Mariamu Aali huliombea Kanisa, je, huzipokea nafsi kifoni, anakishinda kifo, au anahuisha? Kristo anafanya nini iwapo Mariamu Aali anayafanya haya yote? Ingawa anastahili heshima tele, hataki kuwekwa katika kiwango sawa na Kristo, bali anatutaka tuuzingatie mfano wake na kuufuata. 28. Jambo la kweli ni kwamba, katika maoni ya umma, Bikira Aali ameichukua nafasi ya Kristo kabisa. Watu wamekuwa wakimwomba, wameitegemea huruma yake, na wamejaribu kumtuliza Kristo kwa njia yake, kana kwamba, Kristo siye Mpatanishi, bali yeye ni hakimu mkali na mlipiza kisasi tu. 29. Msimamo wetu ni kwamba, tusitegemee stahili za watakatifu zihamishiwe kwetu kana kwamba, tunapatanishwa, tunahesabiwa haki, au tunaokolewa na Mungu kwa ajili ya stahili hizo. Tunaupokea msamaha wa dhambi kwa stahili za Kristo peke yake tunapomwamini. Kuhusu watakatifu wengine imesemwa: “Lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.”917 Maana yake: hawawezi kutoleana stahili zao wao kwa wao, sawasawa na watawa wa kiume wanavyozieneza stahili za madaraja yao. 30. Kuhusu wanawali wapumbavu Hilario anasema: “Kwa kuwa wanawali wapumbavu hawangeweza hutoka nje wakiwa na taa zilizozimika, waliwaomba wale wenye busara wawaazime mafuta. Hao waliwajibu kwamba, hawangeweza kuwapa kwa sababu, labda hayangewatosha wote. Hakuna awezaye kusaidiwa kwa matendo au stahili za mwingine, kwa kuwa kila mmoja lazima anunue mafuta kwa taa yake mwenyewe.”918
31. Wapinzani wetu wanafundisha kwamba, inatupasa tuitegemee ibada za watakatifu, ingawa hawana Neno la Mungu wala mfano kutoka katika Maandiko Matakatifu. Wanazitumia stahili za watakatifu sawasawa na stahili za Kristo na kwa njia hiyo, wanaihamisha kwa watakatifu heshima ambayo ni yake Kristo. Hivyo basi, hatuwezi kukubaliana ama na mawazo yao kuhusu kuiheshimu ibada 916 Mtindo huu ulitumiwa k.m. katika Dayosisi Kuu ya Pari. 917 1 Kor. 3: 8 918 Hilario, “Ufafanuzi wa Injili kutokana na Mathayo 27: 5. ”
ya watakatifu au desturi ya kuwaomba. Tunajua kwamba, inatulazimu kuyaweka matumaini yetu katika maombezi ya Kristo kwa sababu haya tu ndiyo yaliyo na ahadi ya Mungu. Tunajua kwamba, stahili za Kristo ndio upatanishi wetu pekee. Kwa ajili ya stahili za Kristo tunahesabiwa haki tunapomwamini, jinsi andiko lisemavyo: “Na kila amwaminiye hatatahayarika.”919 Hatupaswi kuamini kwamba, tunahesabiwa haki kwa stahili za Bikira Aali au watakatifu wengine.
32. Hata wanatheolojia wanalishikilia kosa kwamba, kila mtakatifu ana shughuli yake maalumu aliyopewa: Mt. Anna920 huutoa utajiri, Sebastiano921 huyaepusha maradhi ya kuambukiza, Valentino922 huponya kifafa, na Georgio923 huwalinda mashujaa malodi, wapanda farasi. Asili ya dhana za jinsi hiyo ni za kipagani. Warumi walifikiria kwamba, Yuno aliutoa utajiri, Febriso aliiepusha homa, na Kasto pamoja na Poluksi waliwalinda mashujaa malodi wapanda farasi n.k.924 33. Hata ibada ya watakatifu ingefundishwa kiasi, matokeo yake bado yangekuwa hatari. Kwanini kulitetea jambo ikiwa halina agizo au ushuhuda katika Neno la Mungu? Kiukweli, hakuna ushuhuda wa hilo katika waandishi wa kale. 34 Jinsi nilivyotangulia kusema, ufahamu wetu wote wa Kristo hupotea tunapowatafuta wapatanishi wengine na kuwategemea badala ya Kristo. Tulichunguze suala hili la hakika jinsi lilivyo. Inaonekana dhahiri kwamba, watakatifu walipotajwa kwa mara ya kwanza katika sala za kale, tendo hilo halikushutumiwa. Baadaye, kukafuata ibada ya watakatifu, pamoja nayo, kukawa na matumizi mabaya zaidi hata kushinda yale ya kipagani. Baada ya ibada ya watakatifu, kukafuatia picha za watakatifu. Watu waliziheshimu picha hizo na walifikiria kwamba, zilikuwa na nguvu fulani za kimiujiza, sawa na jinsi wachawi walivyofikiria kwamba, nyota zenye taswira za unajimu zilizochongwa nyakati maalumu, zilikuwa na nguvu fulani. Katika jumba moja la watawa wa kiume, tuliona sanamu ya Bikira Aali iliyokuwa imetengenezwa kama mwanasesere aliyecheza peke yake925 na ilionekana ikisema Ndiyo au Hapana kwa waombaji.
35. Lakini masimulizi yote haya ya ajabu kuhusu sanamu na picha, hayawezi kulinganishwa na hadithi za kizimwi kuhusu watakatifu zilizofundishwa hadharani kwa mamlaka ya juu kabisa. Katikati ya mateso yake, Barbara926 aliomba
919 Rum. 9: 33
920 Anna au Hanna, mama wa Bikira Mariamu alitukuzwa kama msaidizi wa maskini.
921 Kulingana na hadithi za zamani, ofisa wa Jeshi la Roma, shahidi wa Kikristo wakati wa Kaisari Diokletiano katika karne ya nne.
922 Mmisionari wa kwanza katika Mkoa wa Retia, huko Austria katika karne ya tano.
923 Askari na shujaa kutoka Kapadokia, shahidi wa Kikristo wakati wa Kaisari Diokletiano.
924 Baba wa Kanisa, Agostino wa Hippo alihakiki vikali dini ya Warumi wa kale kwa sababu ya shughuli mbalimbali ya miungu katika maisha ya watu; (Mji wa Mungu) ‘De civitate Dei’ 4, 8.10.
925 Melanchthon, ‘αυτοματον.’
926 Kulingana na “Hadithi ya dhahabu” ‘Legenda aurea’ iliyotolewa na Yakobo wa Voragine huko Kaskazini
thawabu kwamba, yeyote amwombaye yeye asife bila Ekaristi. Mtu mwingine alizikariri zaburi zote kila siku akiwa amesimama kwa mguu mmoja. Mtu fulani stadi aliichora picha ya Kristoforo927 kwa namna ya kuiashiria nguvu kubwa ya kiroho inayohitajika kwa wale ambao wangemwamini Kristo. Yaani, wale ambao wangefundisha na kuikiri Injili, kwa kuwa wangekumbana na hatari kubwa. Kisha, watawa wa kiume wajinga waliwafundisha watu wamwombe Kristoforo, kana kwamba, hakika, wakati wowote, alikuwepo Polifemo928 wa jinsi hiyo. Hakuna yeyote aliyeikusanya historia ya kweli kuhusu watakatifu. 36. Mambo makubwa waliyoyafanya watakatifu yamekuwa kama mifano kwa watu katika maisha yao hadharani929 au katika maisha ya binafsi. Mambo hayo yamekuwa kama njia ya kuidhibitisha imani yao na kama kivutio cha kuwaiga katika mambo ya hadhara. Hakuna mtu aliyeyatafuta haya katika hadithi za kweli kuhusu watakatifu. Lakini inafaa sana kusikia jinsi watakatifu walivyozihudumia serikali mbalimbali, walivyokumbana na matatizo na hatari, walivyowasaidia wafalme wakati wa hatari kubwa, walivyofundisha Injili, na walivyopambana na wazushi. Baadhi ya mifano ya huruma inafaa sana kama tunapoona na kusikia jinsi Petro alivyosamehewa dhambi ya kumkana Kristo, jinsi Sipriano930 alivyosamehewa dhambi ya kuwa mchawi, jinsi Agostino alivyoipata nguvu ya imani wakati wa ugonjwa na daima alithibitisha kwamba, Mungu huyasikia maombi ya waumini. Ingefaa sana kuikumbuka mifano ya jinsi hii inayohusu imani au woga au utawala wa mambo ya umma. 37. Lakini watunzi wapumbavu wasiokuwa na ujuzi wowote kuhusu imani au mambo ya serikali, walizibuni hadithi hizi zinazoiga tenzi na kuleta tu mifano ya ushirikina wa sala fulani, mifungo fulani, na taratibu nyingine za dini za kuleta faida. Hakuna haja kuorodhesha hapa miujiza ya sala za rozari walizozibuni, kaida zingine sawa za dini, au hekaya, jinsi wanavyoziita. Vioo na rozari vyote huwa na mambo mengi yanayofanana na “Hadithi za kweli” za Lukiano.931
38. Maaskofu, wanatheologia, na watawa wa kiume wanazifurahia sana hadithi hizi za kuchukiza na za kukufuru kwa sababu wanajipatia faida.932 Lakini mwa Italia mwaka wa 1266, Barbara baada ya kuongoka huko Nikomedia, alitolewa na babake kwa maofisa wa Roma ili kuhukumiwa na kuuawa.
927 Jina la Kristoforo linamaanisha “Mbeba Kristo.” Hadithi hii pia ilitokea katika kitabu cha “Hadithi ya dhahabu.”
928 Shujaa wa kale katika hadithi za Wayunani, zimwi lenye jicho moja katika matukio ya Odysseo kulingana na mashairi ya Homero; baadaye shujaa wa uigaji katika michezo ya kuchekesha.
929 Kilatini: ‘Res publica.’
930 Askofu wa Antiokia katika karne ya pili.
931 Lukiano wa Samosata alitunga vitabu vya tashtiti juu ya matapeli wa dini katika karne ya kwanza B.K.
932 Melanchthon, ‘προς τα αλφιτα.’
hawawezi kutuvumilia kwa sababu hatuhitaji ibada ya watakatifu, na tunalaani matumizi mabaya katika sala za watakatifu ili kuitilia mkazo heshima na kazi ya Kristo. 39. Watu wema kila mahali wamekuwa wakitumaini sana kwamba, maaskofu wangeyatumia mamlaka yao na wahubiri wangeutekeleza wajibu wao katika kuyarekebisha haya matumizi mabaya; Lakini, katika Hoja yao, wapinzani wetu wanajitia hamnazo kuhusu makosa mabaya yaliyo wazi, kana kwamba, wanakusudia kutulazimisha tuipokee Hoja yao, na kutushurutisha tuyaridhie hata matumizi mabaya zaidi.
40. Hoja hii ni hati ya udanganyifu iliyotungwa kwa njia ya werevu sana, siyo hapa tu, bali karibu kila pahali. Hakuna mahali popote wanapotofautisha kati ya mafundisho yao ya imani na makosa mabaya yaliyo wazi. Hata hivyo, yeyote mwenye busara katika ushirika wao angekubali kwamba, mafundisho mengi ya Madaktari Wanazuoni na Wakanonisti933 ni batili na kwamba, matumizi mengi mabaya yameruhusiwa kanisani kwa sababu ya ujinga na uzembe wa wachungaji. 41. Luther hakuwa mtu wa kwanza kuyalalamikia matumizi mabaya ya hadhara. Watu wengi mashuhuri na wenye utaalamu waliyachukia matumizi mabaya ya Misa kwa muda mrefu. Imani katika adhimisho la utawa, ibada za watakatifu kwa ajili ya faida, mkanganyiko katika imani ya toba ambayo ilipaswa kuwa wazi na dhahiri iwezekanavyo kanisani. Wenyewe tumewasikia wanatheologia bora sana wakiomba vizuizi vya mafundisho ya Uwanazuoni kwa sababu yanafaa zaidi katika ubishi wa kifalsafa kuliko uchaji.934 Hata hivyo, Madaktari Wanazuoni wa kale, mara kwa mara walikuwa karibu na Maandiko Matakatifu kuliko wale wapya. Kwa njia hii basi, theologia ya wapya imeshuka zaidi na zaidi. Kwa sababu hii, tangu mwanzo, watu wengi bora waliompenda Luther walifanya hivyo kwa sababu waliona kwamba, aliziweka huru nafsi za watu kutoka katika mikanganyiko ya labirinthino935 na mabishano yasiyokoma ya wanatheolojia, Madaktari Wanazuoni na ya Wakanonisti na kwamba alikuwa akiyafundisha mambo yenye manufaa kwa uchaji.
42. Kwa hiyo, wapinzani wetu hawakuwa waaminifu walipoyapuuza haya matumizi mabaya na kututaka tuikubali Hoja hii. Iwapo hakika walikuwa wakilitakia Kanisa mema, wangemshauri Kaisari bora mno kuzichukua hatua za kuyasahihisha haya matumizi mabaya. Kwa kuwa ni wazi kwamba, anawahangaikia sana kulipatanisha na kulistawisha Kanisa. Badala ya kuyakubali
933 Wataalamu wa kanuni za sheria za Kanisa.
934 Labda Melanchthon alimaanisha Profesa Wendelin Steinbach katika Tübingen au kitabu cha Erasmaso wa Rotterdam, ‘Encomium moriae’ (Sifa za juu za ujinga) mwaka wa 1508.
935 Njia za mzingo, ujenzi katika hadithi za zamani za Wayunani. Watu walioingia ujenzi huu walipoteza njia, hawakuweza kurudi na mwishowe waliangamia.
mapenzi haya ya heshima na matakatifu ya Kaisari bora mno, wapinzani wetu wanajaribu kwa namna yoyote kutukandamiza. 43. Wanaonyesha ishara nyingi za kutoijali sana hali ya Kanisa. Hawafanyi jitihada zozote kuutoa muhtasari yakini wa mafundisho ya imani ya Kanisa kwa watu. Wanayatetea wazi matumizi mabaya kwa ukatili mpya ulio kinyume cha sheria. Hawawavumilii hata kidogo wachungaji wenye uwezo katika makanisa. Njia hii ya kutenda mambo haisaidii mamlaka yao wala ya Kanisa na watu wema wanaweza kupima matokeo yake kwa urahisi. Baada ya madaktari hodari kuuawa na mafundisho ya kweli kuangamizwa, nafsi kali za walokole936 zitatokea ambazo wapinzani wetu hawataweza kuzizuia. Watalitaabisha Kanisa kwa mafundisho yao ya kukufuru na watausambaratisha utaratibu mzima wa Kanisa937 tunaoutazamia kuudumisha.
44. Kwa hiyo, Kaisari Karolo bora mno, kwa ajili ya utukufu wa Kristo, ambao tunafahamu kwamba, unapenda kuutukuza na kuuendeleza, tunakusihi usikubaliane na mashauri makali ya wapinzani wetu. Badala yake, zitafute njia zingine stahifu za kuuanzisha mwafaka ili dhamiri za wacha Mungu zisitwikwe mizigo wala watu maasumu938 kuteswa vikali, kama jinsi ilivyotendeka awali, wala mafundisho mabruki939 yasidhulumiwe kanisani. Ni jukumu lako kubwa zaidi kuliko yote mbele za Mungu kuyadumisha na kuyaeneza mafundisho safi kwa vizazi vijavyo na kuwalinda wanaoyafundisha kwa njia halisi. Mungu analidai hili anapowaheshimu wafalme kwa jina lake mwenyewe na anawaita miungu: “Mimi nimesema Ndinyi miungu . . .”940 Maana yake: Inawapasa kuyadumisha na kuyaeneza mambo ya kimungu duniani. Yaani, Injili ya Kristo na kama wawakilishi wa Mungu kuyalinda maisha na usalama wa watu wasio na hatia.
Fungu la Ishirini na Mbili: Aina zote Mbili za Sakramenti
1. Hakuna mashaka yoyote kwamba, matumizi ya aina zote mbili za Chakula cha Bwana ni ya kimungu na yanalingana na utaratibu wa Kristo na maneno ya Paulo. Kwa maana, Kristo alizianzisha aina zote mbili. Hakufanya hivyo tu kwa ajili ya sehemu ya Kanisa tu, bali kwa ajili ya Kanisa zima. Siyo Wapresbiteri941 tu, bali kanisa zima huitumia sakramenti kwa mamlaka ya Kristo na siyo kwa
936 Kilatini: ‘Fanatici spiritus.’
937 Kilatini: ‘Ecclesiastica politia.’
938 Wasiokuwa na hatia.
939 Hukota afya, yenye heri na baraka.
940 Zab. 82: 6
941 Wapresbiteri au wazee walikuwa wachungaji na si wanakamati wa Kanisa. H. Zwingli, J. Calvin, Waanabaptisti na wafuasi wao walimfafanua mpresbyteri au mzee kumaanisha mwanakamati wa Kanisa.
mamlaka ya mwanadamu. Tunatarajia kwamba, wapinzani wetu watalikubali hilo. 2.Ikiwa Kristo alianzisha kwa ajili ya Kanisa zima, mbona aina moja inakataliwa katika sehemu ya Kanisa? na Mbona matumizi yake yanakataliwa?
Mbona agizo la Kristo linabadilishwa, hasa kwa vile yeye mwenyewe analiita agano lake? Iwapo siyo halali kutangua agano la mwanadamu, haiwezekani kabisa kuutangua wasia942 wa Kristo. 3. Paulo anasema kuwa aliyapokea kutoka kwa Bwana aliyokuwa akitupatia. Yeye alitupatia matumizi ya aina zote mbili jinsi andiko linavyoonyesha dhahiri katika 1 Kor. 11: 23-24: “Fanyeni hivi.” Kwanza, Kristo anazungumzia kuhusu mwili wake. Baadaye anayarudia maneno hayo hayo kuhusu kikombe. Kisha anasema: “Mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe” (1 Kor. 11: 28). Haya ndiyo maneno yake yeye aliyeianzisha sakramenti. Alitangulia kusema kwamba, wale watakaoshiriki Chakula cha Bwana lazima washiriki pamoja. 4. Kwa hiyo, kuna ushahidi wa kutosha kwamba, sakramenti ilianzishwa kwa ajili ya Kanisa zima. Bado desturi hii inadumishwa katika Kanisa la Kiyunani, na wakati mmoja ilishamiri katika Kanisa la Kilatini, jinsi Sipriano na Hieronimo wanavyoshuhudia. Hieronimo anayasema yafuatayo katika ufafanuzi wake kuhusu Kitabu cha Zefania: “Makasisi ambao huitunukia Ekaristi, na kuigawa damu ya Bwana kwa watu n.k.”943 Sinodi ya Toledo inautoa ushuhuda huo huo.944 Isitoshe, haitakuwa vigumu kukusanya rundo kubwa la ushuhuda. 5. Hapa hatutii chumvi, ila tunamwachia msomaji mwenye busara aamue ambalo anapaswa kuliamini kuhusu agizo la Mungu.
6. Katika Hoja hii, wapinzani wetu hawajaribu kulielezea Kanisa sababu ya wao kuizuia sehemu ya pili ya sakramenti. Haya ndiyo yawapasayo watu wema wa dini kuyafanya. Walipaswa kulipatia Kanisa maelezo halali ili kuwafundisha wale walioipokea sehemu moja tu ya sakramenti. Watu hawa wanashikilia kwamba, ni halali kukataza matumizi ya sehemu moja na wanakataa kuruhusu matumizi ya sehemu zote mbili. 7. Hawawezi kuutoa mfano wowote wa awali ili kuuthibitisha ubunifu wao kwamba, mwanzoni mwa Kanisa, ilikuwa ni desturi katika baadhi ya sehemu kuruhusu matumizi ya sehemu moja tu. Wanazirejea aya zinazotaja mkate kama Lk. 24: 35, isemayo kwamba, wanafunzi walimtambua Kristo alipoumega mkate. Wanazirejea pia aya zingine zinazotaja umegaji mkate. Hatupingi sana iwapo mtu atazichukulia aya hizi akirejea sakramenti. Hata hivyo, bado haimaanishi kwamba, sehemu moja ndiyo ilitolewa. Maana, katika matumizi ya kawaida ya lugha, kuitaja sehemu moja pia kunaashiria ile nyingine.
942 Kiyunani: ‘Διαθηκη’; neno hili linaweza kutafsiriwa kama “agano” au “wasia.” Luther alilitafsiri neno hili kumaanisha “wasia” kulingana na Mt. Paulo.
943 Hieronimo, “Ufafanuzi wa Kitabu cha Zefania” sura ya tatu. 944 Huko Uhispania mwaka wa 633.
8. Vile vile wanaurejea “ushirika wa Wakristo wa kawaida.” Lakini huu haukuwa matumizi ya sehemu moja. Wakati makasisi waliamriwa kutumia ushirika wa Wakristo wa kawaida, hii ilimaanisha kwamba, walikuwa wameondolewa kutoka katika huduma ya uchungaji945 na hawakuruhusiwa kuviweka wakfu vitu hivyo . Wapinzani wetu wanalijua hili vizuri, lakini huwatupia mchanga machoni wale wasiojua ambao wanaposikia neno “ushirika wa Wakristo wa kawaida,” mara moja wanafikiri kwamba, inamaanisha desturi yetu ya sasa ya kuwapa Wakristo wa kawaida sehemu tu ya sakramenti.
9. Utazame ufidhuli wa watu! Gabrieli anasema kwamba, miongoni mwa sababu zingine za kutokutolewa aina zote mbili ni kuwa, inapasa iwepo tofauti kati ya Wakristo wa kawaida na makasisi. Hii ndiyo sababu maalumu ya kuaminika sana ya kutetea katazo la sehemu moja ili kukiinua cheo cha makasisi kwa taratibu za kidini. Tukisema kwa upole iwezekanavyo, hii ni hila ya kibinadamu na shabaha yake inajulikana wazi. 10. Katika hii Hoja, wanarejea kesi ya wana wa Eli. Baada ya kuupoteza ukuhani mkuu, walipaswa kuomba sehemu moja iliyokuwa ya makuhani (1 Sam. 2: 36). Wapinzani wetu wanasema kwamba, hilo linaonyesha matumizi ya sehemu moja, na wanaongezea kusema: “Hivyo Wakristo wetu wa kawaida wanapaswa waridhike na sehemu moja inayotunukiwa na makuhani, yaani, aina moja ya sakramenti.” Wapinzani wetu ni dhahiri wanachekesha wanapoitumia hadithi ya wana wa Eli katika sakramenti. Hadithi hii inaelezea adhabu ya Eli. Je, wanataka pia kusema kwamba, ni adhabu kwa Wakristo wa kawaida kukatazwa sehemu moja? Sakramenti ilianzishwa ili kuzifariji na kuziimarisha nafsi zilizotishwa zinapoamini kwamba, mwili wa Kristo uliotolewa kwa ajili ya maisha duniani, ni chakula chao na kwamba, wanahuishwa wanapounganishwa na Kristo. Walakini wapinzani wetu wanabisha kwamba, ni adhabu kwa Wakristo wa kawaida kukatazwa aina moja. Wanasema: Hawana budi kuridhika! Amri ni amri kabisa! 11. Lakini kwa nini wanapaswa kuridhika? Hawapaswi kuuliza sababu. Lolote walisemalo wanatheolojia na liwe sheria! Haya ni mabaki wazi ya Eck.946 Naam, tunazitambua dhahiri sauti hizi za Thraso,947 na kama tungependa kuwajibu, tungekuwa na mengi ya kusema. Utizame ufidhuli mkubwa wa mtu huyu! sawa na dhalimu katika michezo ya
945 Sinodi la Orleans mwaka wa 538.
946 Melanchthon, ‘εωλοκρασια Ecciana.’ Yohana Eck (1486-1543) kutoka Ingolstadt alikuwa mpinzani mkali wa Martin Luther, mwanatheologia wa mabishano dhidi ya Luther na wafuasi wake.
947 Thraso alikuwa askari mwenye majigambo katika michezo ya Terentio Aferi mwaka wa 160-166 K.K. huko Roma. Msemo huu unatokana na Martin Luther aliyetumia mfano huu mara ya kwanza katika barua yake ya heshima kwa Papa Leo X mwaka wa 1520 kwa ajili ya kitabu chake kiitwacho, ‘Uhuru wa Kikristo.’ Inaonekana kwamba, Eck alikuwa mlimi wa kujitangaza sana kwa sababu, baadaye, katika ufafanuzi wake wa ‘Kitabu cha Ufunuo,’ alimlinganisha Luther na chura katika Ufu. 16: 12-14 mwaka wa 1530.
kuigiza anaamuru anaposema: “Wapende wasipende, lazima waridhike!” 12. Sidhani kwamba, katika hukumu ya Mungu, sababu hizi anazozitoa zitawaondolea hatia wale wanaozuia sehemu ya sakramenti na kuwakasirikia watu wema ambao hutumia sakramenti nzima. 13. Wakiyazuia matumizi ya sakramenti nzima kwa sababu ya kuweka tofauti kati ya madaraja, sababu hii peke yake lazima itufanye tusikubaliane na wapinzani wetu, ingawa tungependa kuidumisha desturi yao. Kuna tofauti nyinginezo za daraja kati ya kasisi na Wakristo wa kawaida, lakini sababu inayowafanya waitetee tofauti hii kwa bidii zaidi iko wazi kabisa. Lakini ili kuepukana na wazo kwamba, tunaidharau heshima halisi ya daraja la makasisi, hatutasema zaidi kuhusu miundo yao ya hila.
14. Wanarejea pia hatari ya kuimwaga divai sakafuni kutoka kikombeni na mambo yanayofanana na hayo yasiyokuwa na nguvu za kutosha kuweza kulibadilisha agizo la Kristo. 15. Ikiwa tutaruhusu uhuru wa kutumia aina moja au zote mbili, wanawezaje kuamrisha katazo la matumizi ya sehemu moja? Hata hivyo, Kanisa lenyewe haliwezi kujitwalia uhuru wa kulifanya agizo la Kristo kuwa mambo ambayo si lazima kuyajali.948 16. Sisi hatulilaumu Kanisa ambalo limeathirika vibaya kwa sababu halikuweza kuwa na sehemu zote mbili, lakini tunawalaumu waandishi wanaotetea uhalali wa katazo la kuitumia sakramenti nzima, na hata wanalitenga Kanisa na kuwatesa vibaya wanaotumia sakramenti nzima. Waache wafikirie watakavyowajibika mbele za Mungu kwa ajili ya maamuzi yao. 17. Wala hatuthubutu kudhani kwamba, Kanisa linaidhinisha mara moja au linakubali lolote wanaloliamua Mapapa, hasa pale ambapo Maandiko Matakatifu yanatabiri kuhusu maaskofu na wachungaji kwa maneno ya Ezekieli: “Sheria itampotea kuhani.”949
Fungu la Ishirini na Tatu: Ndoa za Wachungaji
1. Licha ya sifa mbaya sana ya useja wao ulionajisiwa, wapinzani wetu wanathubutu, siyo tu kuitetea sheria ya Kuhani Mkuu wa Roma kwa kisingizio cha jina la Mungu, bali wanamhimiza Kaisari na watawala wasiruhusu ndoa za makasisi, Dola la Roma lisije likaaibishwa na kufedheheshwa. Haya ndiyo hasa wayasemayo.
2. Katika historia, ni wapi unaweza kusomwa ufidhuli mkubwa zaidi kuliko huo wa wapinzani wetu? Punde, tutazihakiki hoja zao. Kwanza, mwache msomaji mwenye akili atafakari ni wapi ufidhuli wa watu hawa wapotovu unaelekea ambao husema kwamba, ndoa huiaibisha na kuifedhehesha dola, kana kwamba, Kanisa
948 ‘Adiaphora.’ 949 Eze. 7: 26
linapambwa kwa fedheha ya umma. Yaani, tamaa mbaya za mababa watakatifu wanaofanana na Kurio na wanaishi kama Bakhanali.950 Mambo mengi ya uasherati mkuu kabisa wayatendayo watu hawa hayawezi hata kutajwa bila kuona haya. Wanakuomba wewe Kaisari Karolo uzilinde hizi tamaa zao kwa mkono wako safi wa kulia! Wewe ambaye, hata unabii wa kale unakutaja kuwa mfalme mwenye uso wa adabu, kwa maana msemo juu yako unaonekana: “Mtu mwenye uso usiokuwa na majivuno atatawala kila mahali.”951 3.Wanadai uitangue ndoa kinyume cha haki ya kimungu, cha sheria za mataifa, na cha kanuni za Kanisa za sinodi. Kwa ajili tu ya ndoa zao, wanadai uwaadhibu vikali watu wasio na hatia, uwaue makasisi ambao hata watu washenzi wanawahurumia kwa heshima, na uwafukuze wanawake na watoto mayatima walioachwa. Wanapendekeza kwako, Kaisari bora mno, uzipitishe sheria ambazo hakuna nchi yoyote ya washenzi au katili ingeweza kuzizingatia. 4. Lakini kwa kuwa mwenendo wako hauna fedheha wala ukatili, tunatumaini kwamba, utatushughulikia kwa upole, hasa unapojifunza kwamba, kwa ajili ya cheo chetu, tuna sababu nzito kutoka katika Neno la Mungu, wakati wapinzani wetu wenyewe wanatoa hoja zao za kipumbavu na mawazo matupu.
5. Lakini hawautetei useja kwa makini. Wanajua vizuri kwamba, wachache tu huufuata usafi wa kimwili. Badala yake, wanaitumia dini kama kisingizio cha kuyadumisha mamlaka yao, ambayo wanafikiria kwamba, useja huyazidisha. Sasa tunauona usahihi wa onyo la Petro kwamba, manabii wa uongo watawapotosha watu kwa hadithi zao.952 Kuhusu jambo hili zima wapinzani wetu hawatasema, hawataandika au hawatatenda kwa ukweli, dhahiri na kwa uwazi. Wanayapigania mamlaka yao kwa kuwa wanadhania kwa uongo kwamba, yamo hatarini na wanajaribu sana kuyaimarisha kwa kisingizio kiovu cha kumcha Mungu.
6. Sisi hatuwezi kuiidhinisha sheria ya useja inayotetewa na wapinzani wetu kwa sababu inaipinga haki ya kimungu na ya asili953 na inapingana na amri za sinodi.954 Ni wazi kabisa kwamba, sheria hii inahatarisha sana dini na maadili, kwa kuwa inazaa kashfa, dhambi na ufisadi wa maadili ya umma usiokwisha. Mabishano yetu mengine yanahitaji mazungumzo ya madaktari, lakini jambo hili 950 Msemo wa zamani unaopatikana katika michezo za Yuvenali 2, 3. Curius Dentatus alikuwa ofisa mkuu katika jeshi la Roma. Alijulikana kuwa mtu mwenye tabia ya kiasi. Bakhanali zilikuwa sherehe kwa heshima ya mungu wa divai, yaani, Bacchus (Kiyunani: ‘Διονυσιος’). Katika sherehe hizi, wanaume na wanawake walifuata tamaa mbaya za mwili katika hali ya ulevi.
951 Uaguzi wa Sibylla 8, 169-170. Waandishi Wayahudi na Wakristo waliongezea ubashiri na masimulizi yao wenyewe katika uaguzi wa zamani wa Kipagani huko Uyunani. Baadhi ya akina Baba wa Kanisa walivisadiki vitabu hivi kuwa ubashiri halisi wa Sibylla.
952 2 Pet. 3 : 2
953 Kilatini: ‘Ius divinum et naturale.’
954 K.m. Sinodi ya Nikea
ni dhahiri kabisa kwa pande zote mbili kiasi kwamba, halihitaji mazungumzo zaidi. Linahitaji tu uamuzi wa mwanadamu mnyofu na mcha Mungu. Tunapokuwa tumeutetea ukweli ulio wazi, wapinzani wetu wamezibuni hila zingine ili kuzibeza955 hoja zetu.
7. Kwanza, Mwa. 1: 28 inafundisha kwamba, watu waliumbwa ili wazaane na kwamba, jinsia moja lazima iitamani nyingine. Sisi hatuzungumzii hapa kuhusu tamaa mbaya956 ambayo ni dhambi, bali kuhusu wanachokiita “hamu ya asili,” 957 yaani, hamu iliyokusudiwa kuwa katika hali isiyochafuliwa. Kwa kweli, upendo huu wa jinsia moja kwa nyingine ni agizo la kimungu. Kwa kuwa, agizo hili la Mungu haliwezi kutanguliwa bila tendo maalumu la Mungu, inafuatia kwamba, haki ya kuoa na kuolewa haiwezi kutanguliwa na sheria wala nadhiri.
8. Wapinzani wetu wanajibu kwa hoja ya kipumbavu sana wakisema kwamba, mwanzoni kulikuwepo na amri ya kuujaza ulimwengu, lakini kwa kuwa ulimwengu umejazwa sasa, ndoa haiamriwi tena. Utazame ubishi wao mwerevu kabisa! Neno la Mungu liliiumba asili ya mwanadamu izaane, siyo tu mwanzoni mwa uumbaji, bali bado inaendelea kuzaana alimradi asili yetu hii ya kimwili ipo. Vivyo hivyo, nchi nayo izae kwa nguvu ya Neno hili: “Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, . . . kwa jinsi yake . . . ”958 Kutokana na agizo hili, nchi haikuzaa mimea mwanzoni tu, bali kila mwaka mashamba yanapambwa alimradi nchi inaendelea kuwepo. Jinsi sheria za wanadamu haziwezi kuibadilisha asili ya nchi, kadhalika, nadhiri wala sheria za kibinadamu haziwezi kuibadilisha asili ya mwanadamu bila tendo maalumu la Mungu.
9. Pili, kwa sababu uumbaji huu au agizo la Mungu ndani ya mwanadamu ni haki ya asili, wanasheria wamesema kwa busara na kwa usahihi kwamba, muungano baina ya mwanamume na mwanamke ni kwa haki ya asili.959 Kwa kuwa, haki ya asili haibadiliki, basi, haki ya kufunga ndoa lazima ibakie daima. Lazima ibakie kwani, pale ambapo asili haibadiliki, agizo ambalo Mungu amelijenga katika asili hiyo, na sheria za wanadamu haziwezi kulitangua. 10 Hivyo, ni dhihaka kabisa kwa wapinzani wetu kusema kwamba, mwanzoni ndoa iliamriwa lakini sasa haiamriwi tena. Hii ni sawa kabisa na kusema kwamba, zamani watu walizaliwa wakiwa na jinsia na sasa hawana, au zamani walizaliwa wakiwa wenye haki ya asili na sasa hawana. Hakuna mhunzi960 awezaye kubuni
955 Kudhihaki.
956 Kilatini: ‘Concupiscentia.’
957 Melanchthon, “Στοργη φυσικη,” Cicero Attica 10, 8, 9.
958 Mwa. 1: 11
959 Kilatini: ‘Ius naturale.’
960 Kilatini: ‘Faber.’ Mtunzi mmoja wa Hoja aliitwa Faber, aliyekuwa Askofu Mkuu wa Wien huko Austria
zaidi udanganyifu wowote kuliko upumbavu huu, uliovumbuliwa ili kuizuia sheria ya asili. 11. Acheni basi, tuuweke ukweli huu akilini uliofundishwa na Maandiko Matakatifu na wanasheria wameuelezea kwa busara: muungano wa mwanamume na mwanamke ni kwa haki ya asili. 12. Hakika, haki ya asili ni haki ya kimungu, kwa sababu ni agizo la kimungu lililoumbwa katika asili. Kwa kuwa, haki hii haiwezi kubadilishwa bila tendo maalumu la Mungu, haki hii ya mkataba wa kuoa na kuolewa lazima ibaki, kwa kuwa tamaa ya asili baina ya jinsia moja na nyingine ni agizo la Mungu na kwa hiyo, ni haki; Vinginevyo, kwa nini jinsia hizi mbili ziliumbwa? 13. Kama jinsi tulivyokwisha kusema hapo awali, hatuzungumzii kuhusu tamaa mbaya ambayo ni dhambi bali kuhusu hamu iliyoitwa “hamu ya asili” ambayo haiondolewi na tamaa mbaya kutoka katika asili bali iliwaka tu. Sasa, inahitaji dawa zaidi, na ndoa ni ya lazima kwa ajili tiba na pia kwa uzazi. Mambo haya ni wazi na thabiti kabisa kiasi cha kutopingika.
14. Tatu, Paulo anasema: “Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe.”961 Amri hii ya moja kwa moja inawahusu wote wasiofaa kwa useja. 15. Wapinzani wetu wanadai waonyeshwe amri inayowataka makasisi waoe, kana kwamba mapadre siyo wanadamu. Tunasisitiza kwamba, lolote linalohusu asili ya mwanadamu kwa jumla, linawahusu pia makasisi. 16. Je, si Paulo anafundisha hapa kwamba, wale ambao hawana kipawa cha kuitawala tamaa waoe? Baadaye, anajielezea mwenyewe zaidi anaposema: “ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa”962 Naye Kristo anasema wazi: “Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.”963 Tangu anguko la mwanadamu, mambo haya mawili, yaani, tamaa ya asili na tamaa mbaya iichocheayo hamu ya asili hutokea pamoja. Hivyo, ndoa inahitajika zaidi sasa kuliko katika hali ya usafi. Kwa sababu hiyo, Paulo anaizungumzia ndoa kama dawa na anaamuru kuoa kwa sababu ya tamaa hizi ziwakazo. Kwa kuwa, mamlaka yoyote ya kibinadamu, sheria wala nadhiri haviwezi kutangua asili wala tamaa mbaya, vivyo hivyo, haviwezi kuitangua kauli hii: “Ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.” Hivyo, kila mmoja anayewaka tamaa ana haki ya kuoa. 17 Amri ya Paulo isemayo: “kwa sababu ya zinaa, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe,” inawahusisha wote ambao hawawezi kuitawala tamaa kabisa. Kuliamua suala hili, kunategemea dhamiri ya kila mtu.
18. Hapa wanawaamuru watu kumwomba Mungu nguvu ya kuitawala tamaa na kuidhibiti miili yao kwa njia ya taabu na kufunga. Je, kwa nini wenyewe baadaye.
961 1 Kor. 7: 2
962 1 Kor. 7: 9
963 Mt. 19: 11
hawazitumii amri hizi kuu? Jinsi tulivyokwisha kusema awali, wapinzani wetu wanachekesha tu; Hawalichukulii suala hili kwa uzito. 19. Iwapo kutawala tamaa kungewezekana kwa kila mmoja, hakungehitaji kipawa maalum. Kristo anaonyesha kwamba, kutawala tamaa kunahitaji kipawa maalum. Kwa hiyo, siyo kwa kila mmoja. Mungu anawataka watu wengine wote waitumie sheria ya wote ya asili ambayo ameiweka. Kwa kuwa hataki kabisa tuyadharau maagizo yake, yaani, viumbe vyake. Anapenda watu wawe safi kwa njia ya dawa aitoayo, jinsi apendavyo kuyalisha maisha yetu kwa njia ya chakula na kinywaji. 20. Gerson anashuhudia kwamba, watu wengi wema wamejaribu kuidhibiti miili yao lakini bila kufaulu sana.964 Kadhalika, Ambrosio anasema kwa usahihi: “Ubikira unaweza kupendekezwa tu na siyo kuamriwa; ni jambo la hiari zaidi kuliko kuwa la lazima.” 21. Ikiwa mtu atalipinga hili kwa kusema kwamba, Kristo aliwasifu wale, “matowashi waliojifanya kuwa matoashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni,”965 akumbuke kwamba, Kristo anawasifu wale walio na kipawa cha kuitawala tamaa na hivyo anaongezea: “Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.” 22. Useja usiokuwa safi haumpendezi Kristo. Sisi pia tunapongeza kutawala mwili kweli. Basi, sasa tunazungumzia kuhusu sheria na kuhusu wale ambao hawana kipawa cha kuitawala tamaa. Jambo hili halina budi kuwa huru kabisa na walio dhaifu hawapaswi kuwekewa mitego kwa njia ya sheria hii.
23. Nne, sheria ya Upapa haikubaliani kabisa na kanuni za Kanisa za sinodi. Yaani, kanuni za Kanisa za kale hazikatazi wala hazitangui ndoa zilizokwisha kufungwa, ingawa ziliwaondoa kwenye huduma wale waliooa wakiwa ofisini. Nyakati hizo, kuondolewa kwa jinsi hiyo kulitazamiwa kuwa fadhili tu. Hizi kanuni mpya za Kanisa haziwakilishi uamuzi wa sinodi, bali hukumu za binafsi za akina Papa katika baraza. Zinakataza kuoa na kuolewa na zinazitangua zile ambazo zimekwisha kufungwa, na yote haya ni kinyume cha waziwazi cha amri ya Kristo: “Aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.”966 24. Katika Hoja yao, wapinzani wetu wanapiga kelele wakisema kwamba, sinodi zimeuamuru useja. Hatuzipingi misimamo za sinodi, kwa kuwa misimamo hii inairuhusu ndoa kwa masharti fulani. Badala yake, tunazishtaki sheria zilizopitishwa na akina papa wa Roma, kinyume cha mamlaka yao tangu nyakati za sinodi za kale,. Akina papa wanayadharau mamlaka ya sinodi, ilihali wanawataka wengine wayakubali kama jambo tukufu mno. 25. Hivyo, sheria kuhusu useja wa kudumu ni ngeni kwa huu udhalimu mpya wa Upapa. Danieli
964 Labda kitabu chake kiitwacho, ‘De coelibatu’ (Kuhusu Useja) 3.
965 Mt. 19: 12
966 Mt. 1:9, 6
anayachukulia madharau kwa wanawake967 kuwa alama ya utawala wa Mpinga Kristo.
26. Tano, ingawa wapinzani wetu hawaitetei sheria hii kwa sababu za kidini, kwa kuwa wanajua vizuri kwamba, haifuatwi, bado wanaifunika kwa kwa misemo yenye sauti ya uchamungu ili kuipa mwelekeo wa kidini. Wanadai kwamba, wanauhitaji useja kwa kuwa ni safi, kana kwamba, ndoa ni chafu na yenye dhambi au kana kwamba, useja ulistahili kuhesabiwa haki zaidi kuliko ndoa. 27. Kwa sababu hii, wanazirejea taratibu za Torati ya Musa iliyoelezea kwamba, wakati wa huduma zao, makuhani wa Agano la Kale walitengwa na wanawake wao. Kwa kuwa makuhani wa Agano la Jipya wanapaswa kuomba bila kukoma; wanalazimika pia kuishi katika hali ya kuitawala tamaa siku zote. Ulinganifu huu hafifu unawasilishwa kama thibitisho la kuwalazimisha makasisi kuingia katika useja wa kudumu, ingawa, katika ulinganifu huu, ndoa inaruhusiwa na kujamiana kunakatazwa wakati wa huduma. Licha ya hayo, sala ni jambo moja na huduma ni jambo jingine. Watakatifu walisali hata walipokuwa hawaendelei na huduma yao kwa watu, na kujamiiana katika ndoa hakukuwazuia kusali.
28. Tutaujibu vyema uongo huu uliobuniwa mmoja baada ya mwingine. Kwanza, wapinzani wetu hawana budi kukubali kwamba, ndoa ni safi kwa waumini kwa sababu imetakaswa kwa Neno la Mungu. Yaani, ni jambo linaloruhusiwa na kuidhinishwa kwa Neno la Mungu, jinsi Maandiko Matakatifu yashuhudiavyo kwa wingi. 29. Kristo anaiita ndoa muungano mtakatifu anaposema: “Aliowaunganisha Mungu.”968 30. Paulo anasema kuhusu ndoa, chakula na vitu vya jinsi hiyo,: “Vimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”969 Maana yake: kwa njia ya Neno linaloihakikishia dhamiri kwamba, kwa njia ya sala, yaani, kwa njia ya imani, inayokitumia kwa furaha, Mungu anaviidhinisha kama karama yake. 31. Katika 1 Kor. 7: 14 anasema: “Mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe,” yaani, matumizi ya ndoa yanaruhusiwa na ni matakatifu kwa ajili ya imani katika Kristo jinsi matumizi ya vyakula yanavyoruhusiwa n.k. 32. Kadhalika, katika 1 Tim. 2: 15, anasema: “Ataokolewa kwa uzazi wake.” Ikiwa wapinzani wetu wangeweza kuitoa aya ya jinsi hiyo kuhusu useja, wangeweza kuusherehekea ushindi wa ajabu. Paulo anasema kwamba, mwanamke anaokolewa kwa uzazi wake. Kinyume cha unafiki wa useja, ni heshima gani angeweza kuitoa kuliko kusema kwamba, mwanawake anaokolewa kwa njia ya huduma zenyewe za ndoa, kwa njia ya kujamiana katika ndoa, kwa kuwazaa watoto na kwa shughuli zake nyinginezo za nyumbani? Paulo anasema nini? Hebu msomaji atambue
967 Dan. 11: 37
968 Mt. 19: 6
969 1 Tim. 4: 5
vizuri kwamba, anaiongezea imani na hazisifu shughuli za nyumbani mbali na imani. Anasema: “ikiwa anadumu katika imani.” Analizungumzia tabaka la akina mama kwa jumla. Zaidi ya hayo yote, anahitaji imani ambayo kwayo, mwanamke anaupokea msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki. Halafu anaiongezea kazi maalumu ya wito wake; kwa maana, utendaji wa kazi za wito maalumu lazima ufuate imani ya kila mmoja, akimpendeza Mungu kwa ajili ya imani. Hivyo, shughuli za mwanamke zinampendeza Mungu kwa ajili ya imani, na mwanamke anayeamini anaokolewa iwapo anahudumu kwa uaminifu katika majukumu haya ya wito wake.
33. Aya hizi zinafundisha kwamba, ndoa ni jambo la halali. Usafi ukimaanisha kwamba, jambo fulani limeruhusiwa na limeidhinishwa na Mungu, basi, ndoa ni safi kwa kuwa imeidhinishwa kwa Neno la Mungu. 34. Kuhusu mambo yaliyo halali, Paulo anasema: “Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi,”970 yaani, kwa wanaoamini na waliohesabiwa haki kwa imani katika Kristo. Iwapo ubikira si safi kwa wasiomcha Mungu, vivyo hivyo, ndoa ni safi kwa wacha Mungu, kwa njia ya Neno la Mungu na imani.
35. Pili, kinyume halisi ni kati ya tamaa mbaya na usafi unaofahamika kama usafi wa moyo na kuitawala tamaa mbaya. Hii ni kwa kuwa sheria haikatazi ndoa pekee bali tamaa mbaya, zinaa na uzinzi. Kwa hiyo, useja si lazima uwe usafi. Usafi wa moyo unaweza kupatikana ndani ya mwanamume aliyeoa kama Ibrahimu au Yakobo, kuliko kwa wengine wengi zaidi ambao, hakika, wanaitawala tamaa.
36. Mwisho, iwapo wapinzani wetu wanaufafanua useja kama usafi unaostahili haki zaidi kuliko ndoa, tutapinga kabisa. Hatuhesabiwi haki kwa ajili ya ubikira au ndoa, bali tunaipata bure kwa ajili ya Kristo tunapoamini kwamba, kwa ajili yake, Mungu anatuhurumia. 37. Labda hapa watalia kwamba, tumeiweka ndoa katika kiwango sawa na ubikira jinsi alivyofanya Yoviniano.971 Lakini makaripio kama hayo hayatatufanya tuuache ukweli wa haki ya imani jinsi tulivyoelezea hapo juu. 38. Hatuiweki ndoa katika kiwango sawa na ubikira. Maana, kipawa kimoja kinakishinda kingine. Hivyo, unabii huishinda balagha,972 sayansi ya vita huishinda ya kilimo, na balagha huushinda usanifu majengo. Vivyo hivyo, ubikira ni kipawa kiishindacho ndoa. 39. Lakini jinsi ambavyo ufasaha haumfanyi mzungumzaji kuwa mwenye haki zaidi mbele za Mungu kuliko majengo yanavyoweza kumfanya msanifu majengo kuwa mwenye haki. Vivyo
970 Tit. 1: 15
971 Yoviniano (+ 405) mtawa aliyeuweka ubikira na ndoa kuwa katika kiwango sawa. Alikuwa pia na mashaka kuhusu ubikira wa milele wa Bikira Mariamu. Alihukumiwa na sinodi za Roma na Milano. Hieronimo na Agostino waliandika dhidi ya mafundisho yake. 972 Ulumbaji, Ubora, fahari ya lugha, hotuba.
hivyo, bikira hastahili haki zaidi kwa ajili ya ubikira wake kuliko mtu aliyeoa afanyavyo, kwa kuyatenda majukumu yake ya ndoa. Inambidi kila mmoja kuhudumu kwa uaminifu katika kipawa chake akiamini kwamba, kwa njia ya imani, anapata msamaha wa dhambi na anahesabiwa haki mbele za Mungu kwa ajili ya Kristo.
40. Kristo wala Paulo hawausifu ubikira kwa sababu unamfanya mtu kuhesabiwa haki, bali kwa sababu ni wa manufaa na hausumbui katika shughuli za nyumbani wakati wa maombi, mafundisho, na utumishi. Hii ndiyo sababu Paulo anasema: “Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana.”973 Anausifu ubikira kwa ajili ya kutafakari na kusoma. Vivyo hivyo, Kristo hawasifu tu ambao wenyewe hujifanya matowashi bali anaongezea: “kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.”974 Hii inamaanisha kupata nafasi ya kujifunza au kuifundisha Injili. Hasemi kwamba, ubikira unastahili wokovu au msamaha wa dhambi.
41. Kuhusu ulinganifu na makuhani Walawi, tayari tumekwisha kujibu kwamba, si lazima kuulazimisha useja wa kudumu kwa makasisi. Isitoshe, sheria za Walawi kuhusu unajisi hazituhusu. Kujamiana kulikuwa unajisi kinyume na sheria hizi. Hata hivyo, sasa si unajisi kwa maana Paulo anasema: “Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi.”975 Naam, Injili inatuweka huru kutoka katika sheria hizi za Walawi kuhusu unajisi. 42. Mtu yeyote akiitetea sheria ya useja ili kuzitwika dhamiri mizigo kwa uzingatifu huu wa Walawi, lazima tumpinge kabisa jinsi mitume, katika Mdo. 15, walivyowapinga waliodai tohara na waliojaribu kulazimishia Torati ya Musa kwa Wakristo.
43. Wakati huo huo, watu wema wanajua jinsi ya kuishi kwa kiasi katika ndoa, hasa wanapojishughulisha na huduma za umma ambazo, mara nyingi, zinawalemea watu wema kiasi cha wao kusahau shida za nyumbani. Watu wema pia hulifahamu hilo kwamba, Paulo anamwamuru kila mmoja amtunze mkewe kwa utakatifu (1 The. 4:4).976 Wanajua pia kwamba, wakati mwingine lazima watengane ili wapate nafasi ya kusali, lakini Paulo hapendi jambo hili liwe lakudumu.977 Kuitawala tamaa jinsi hiyo ni rahisi kwa wacha Mungu na wenye
973 1 Kor. 7: 32
974 Mt. 19: 12
975 Tit. 1: 15
976 1 The. 4: 4. ‘Union Version:’ “Kila mmoja wenu ajue kuuweka mwili wake katika utakatifu na heshima.” Hali kadhalika, toleo la R. Kolb na T.J. Wengert. Maandiko ya Utetezi wa Ukiri wa Augsburg (Kilatini na Kijerumani) yanalitumia neno ‘vas’ (Kilatini) na ‘Fass’ (Kijerumani) na katika Kiyunani: ‘σκευοζ,’ yaani, “chombo”. Neno “chombo” linaweza kumaanisha ama mwili au mke. Utetezi wa Ukiri wa Augsburg unalitumia neno “chombo” katika maana ya “mke,” si katika maana ya “mwili” jinsi ‘Union Version’ inavyolitafsiri. Taz. mstari wa 20.
977 1 Kor. 7: 5
shughuli nyingi. 44. Lakini ni wazi kwamba, umati mkubwa wa makasisi wavivu kundini mwao, ambamo wanaweza kuishi kwa hiari, hawawezi hata kutimiza kutawala tamaa huku kwa Walawi. Sote tunaufahamu ubeti huu vizuri: “Huyu kijana Amor, aufuataye uzembe daima, huwachukia wale walio na shughuli n.k.”978
45. Waasi wengi wameielewa vibaya Sheria ya Musa. Hivyo, wanaidharau ndoa na kuusifu useja. Epifanio analalamika kwamba, tabia hiyo ya Waenkratito iliwavutia wapumbavu. Tumekwisha kuwazungumzia hapo awali.979 Pia inajulikana wazi kwamba, kulingana na desturi zao, wamonaki/watawa wa kiume walieneza matangazo yenye imani ya uchawi kuhusu useja yaliyozisumbua dhamiri nyingi za wacha Mungu kuhusu uhalali wa kuoa au kuolewa. Si vigumu hata kidogo kuusimulia ushuhuda wao. Kwa kweli, wamonaki/watawa wa kiume hawa hawakuilaani ndoa kabisa kwa ajili ya uzazi. Hata hivyo, waliuona upungufu mwingi kama namna ya maisha yasiyompendeza Mungu, angalau kwa ajili ya uzazi. Lakini waliusifu useja kana kwamba, ni wa hali ya maisha ya malaika. Walihubiri kwamba, useja ni dhabihu ya kumpendeza zaidi Mungu, ni kustahili msamaha wa dhambi, ni tuzo za dhahabu, ni kuzaa matunda kwa mia, na mambo mengine mengi yasiyokuwa na mwisho.980 Paulo anakataa kabisa “kuabudu malaika” katika Wakolosai.981 46. Hii ni kwa sababu anadai kuwa kufanya hivyo kunaukandamiza ufahamu wa Kristo kwa kuwafanya watu waamini kwamba, wao ni safi na watahesabiwa haki kwa ajili ya unafiki wa jinsi hiyo na siyo kwa ajili ya Kristo. 47 Licha ya hayo, inaficha utambuzi wa amri na karama za Mungu ambazo anatutaka tuzitumie kwa uchaji. 48. Hii ni kwa sababu matendo mapya ya ibada yanaongezewa na kustahabiwa kuliko Amri za Mungu. 49 Hivyo, maoni haya potovu kuhusu useja lazima yapingwe daima katika Kanisa mpaka dhamiri za wacha Mungu zipate kujua kwamba, ndoa inampendeza Mungu na zijue ni ibada za jinsi gani zinazokubaliwa na Mungu.
50. Wapinzani wetu hawataki useja kwa sababu za kidini, kwa kuwa wanajua vizuri kwamba, kwa kawaida, usafi haufuatwi. Lakini wanaitumia hii sababu ya kidini kama kisingizio cha kuwadanganya wasiojua. Kwa hiyo, wanadharauliwa kuliko Waenkratito, ambao huonekana kuwa wamepotoka kwa njia fulani ya dini. Lakini Wasardanapalo982 hawa huitumia dini kama kisingizio tu.
978 Ovidio (43 K.K. – mnamo 17 B.K.), mshairi wa Kilatini. ‘Remedia amoris’ (Tiba ya Upendo). Huko Roma Mungu wa upendo aliitwa ‘Amor’ na alisawiriwa kama kijana.
979 Utetezi 15, 21.
980 K.m. Tomaso wa Akuino STh 2, 2, q. 186, a. 4 na 7.
981 Kol. 2: 18
982 Sardanapalo, mfalme wa Assyria alijulikana kwa sababu katika maisha yake, alijihusisha na anasa mbalimbali.
51. Sita, tuna sababu nyingi zaidi za kukataa sheria ya useja wa kudumu. Ingawa hii si sheria ya haki, ni hatari kwa ajili ya maadili ya umma na ya binafsi. Hii peke yake lazima iwazuie watu wema kutoidhinisha mzigo ambao umeziangamiza nafsi nyingi.
52. Watu wema wamekuwa wakiulalamikia mzigo huu kwa muda mrefu ama kwa ajili yao wenyewe au kwa ajili ya waliowaona kuwa hatarini. Lakini hakuna hata mmoja wa hawa Mapapa aliyeyasikiliza malalamiko hayo. Siyo siri ambavyo sheria hii imeyahatarisha maadili ya umma na jinsi inavyouzaa ufisadi na tamaa mbaya za aibu. Katika kejeli zake, bado Roma inazisoma na kuzitambua taswira na maadili yake yenyewe.
53. Hivyo, Mungu hulipiza kisasi kwa wale wanaodharau karama na agizo lake na wanaoizuia ndoa. Kwa kuwa imekuwa desturi kuzibadilisha sheria nyinginezo iwapo manufaa ya wote yalidai hivyo. Basi, kwa nini haikufanyika hivyo hivyo kwa sheria hii? Kuna sababu nyingi nzito zinazodai mabadiliko, hasa katika nyakati hizi za mwisho. Asili inazeeka na kudhoofika kidogo kidogo, hivyo, tunapaswa kuzitumia tiba tulizopatiwa na Mungu. 54. Tunaona kwamba, Mungu inaidhihirisha ghadhabu yake dhidi ya uovu wa binadamu katika gharika ya wakati wa Nuhu na katika kuiteketeza miji mitano.983 Uovu wa jinsi hiyo hiyo umetangulia maangamizi ya miji mingine mingi, kama vile Sibariso na Roma.984 Hizi ni taswira za wakati wa mwisho. 55. Kwa hiyo, wakati kama huo, ilibidi kuilinda ndoa kwa sheria kali sana na mifano na kuwashawishi watu waoe na waolewe. Huu ni wajibu wa watumishi wa serikali, wanaopaswa kuidumisha nidhamu ya umma. Wakati huo huo, inawapasa madaktari wa Injili wayafanye haya mambo mawili: wawashawishi watu wasioweza kuitawala tamaa waoe na kuolewa, na wawahimize wengine wasikidharau kipawa cha kuitawala tamaa.
56. Kila siku, akina Papa huzitoa na kuzibadilisha baadhi ya sheria nzuri; wamekuwa wagumu kama chuma na wasiobadilika juu ya sheria hii moja ya useja, ingawa, bila shaka, hili ni suala rahisi la haki ya binadamu. 57. Sasa wanaifanya sheria hii isivumilike zaidi kwa njia nyingi. Kanuni za Kanisa zinaamuru kwamba, makasisi wa namna hiyo985 wasimamishwe kwa muda. Lakini watengeneza hizi kanuni za Kanisa wasiokuwa stadi hawasimamishwi kwa muda kwenye huduma tu bali pia katika msalaba.986 Wanawaua kikatili watu wengi wema kwa sababu
983 Sodoma na Gomora na miji mingine katika Mwa. 18 na 19.
984 Sybaris, mji wa kale wa Kiyunani Kusini mwa Italia ulijulikana kwa sababu ya maisha yake ya kutafuta anasa.
985 Makasisi waliooa. Kanuni 11 za Sinodi ya Roma ya mwaka wa 1078.
986 Mchezo wa maneno: ‘Suspendere ab officio – suspendere ab arboribus.’ Neno ‘suspendere’ linamaanisha “kusimamisha” na “kuangika,” yaani, kunyonga: “kuwasimamisha kutoka hudumani - kuwanyonga kwenye
wameoa! 58. Mauaji ya jinsi hiyo ya mapadre987 yanaonyesha kwamba, sheria hii ni mafundisho ya mashetani.988 Kwa kuwa Ibilisi ni mwuaji,989 anaitetea sheria yake kwa njia ya mauaji haya.
59. Tunajua kwamba, hatujikingi dhidi ya shtaka la mifarakano kwa sababu tunaonekana kutengana na wale wanaotambuliwa kama maaskofu wa kawaida. Lakini dhamiri zetu zina amani. Ijapokuwa tunatamani kuuanzisha mwafaka kwa bidii mno, tunafahamu kwamba hatuwezi kuwaridhisha wapinzani wetu isipokuwa tuukane ukweli ulio wazi kabisa. Itatubidi tule njama na wapinzani wetu katika kuitetea sheria hii isiyokuwa ya haki. Yaani, kuzivunja ndoa zilizopo, kuwaua makasisi wanaokataa kusalimu amri, na kuwafukuza wanawake maskini na watoto yatima. Kwa kuwa, hakika masharti haya hayampendezi Mungu, hatusikitiki hata kidogo kwamba, hatuungani katika vita990 na wapinzani wetu wanaowaua wenzao.
60. Tumeelezea kwa nini hatuwezi kukubaliana, kwa uaminifu, na wapinzani wetu wanaoitetea sheria ya akina Papa kuhusu useja wa kudumu. Sheria hii inapingana na haki ya asili ya Kimungu, hata haikubaliani na kanuni za Kanisa, ni ya ushirikina, na yenye hatari kubwa. Mwishowe, suala hili zima ni hila. Sababu halisi ya sheria siyo dini bali ni mamlaka, ambapo dini ni kisingizio kiovu tu. Hakuna mtu mwenye akili awezaye kubishana dhidi ya hoja hizi thabiti mno. 61. Injili inairuhusu ndoa kwa wanaoihitaji, lakini haimshurutishi yeyote aoe ambaye angependa kuitawala tamaa, mradi tu aitawale kweli tamaa. Msimamo wetu ni kwamba, makasisi wapewe uhuru huu. Hatutaki kumshurutisha mtu yeyote kuishi katika useja au kuzivunja ndoa zilizopo.
62. Katika kuzielezea hoja zetu, kinasibu, tumezikariri na kuzikataa hoja za kipumbavu za wapinzani wetu. Sasa tutazihakiki kwa kifupi hoja zao muhimu katika kuitetea sheria. Kwanza, wanasema kwamba, imefunuliwa na Mungu. 63. Watazame hawa wajinga wahuni wakubwa! Wanathubutu kudai kwamba, sheria ya useja wa kudumu imefunuliwa na Mungu ingawa inapingana na ushuhuda wazi wa Maandiko Matakatifu yanayomwamuru kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe kwa sababu ya zinaa.991 Kadhalika, yanazuia kuzivunja ndoa992 zilizopo. Paulo anamuonyesha mwandishi halisi wa sheria ya jinsi hii anapoiita miti.”
987 Hapa, Melanchthon analitumia neno ‘parricidium;’ kumaanisha ‘mauaji ya baba au ndugu.’ ‘Padre’ ni ‘baba.’
988 1 Tim. 4: 1-3
989 Yn. 8: 44
990 Melanchthon, ‘Συμμακχια.’
991 1 Kor. 7: 2
992 Mt. 19: 6
“mafundisho ya mashetani.”993 Mwandishi halisi anaonekana kwa matunda yake: tamaa mbaya za kuchukiza sana na mauaji ya wenzao yanayotekelezwa chini ya kisingizio cha sheria hii.
64. Hoja ya pili ya wapinzani wetu ni kwamba, inawabidi makasisi wawe safi. Kauli hii ni kulingana na (Isa. 52: 11), “Iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.” Wanazirejea pia aya nyingi ili kuitetea fetwa/hoja hii. Tayari, tumekwisha kuipinga hii hoja ambayo wanaichukulia kuwa ya fahari mno.994
Tumekwisha kusema kwamba, bila imani, ubikira si safi mbele za Mungu, na kwamba, ndoa ni safi kwa sababu ya imani kulingana na (Tit. 1:15), “Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi.” Tumesema pia kwamba, mambo haya ya kaida/taratibu na sheria za usafi wa nje ya Agano la Kale hayafai hapa kwa kuwa Injili inautaka usafi wa moyo na siyo usafi wa taratibu za sheria. Inawezekana kwamba, mioyo ya waliooa kama Ibrahimu na Yakobo, ambao walikuwa na wake wengi,995 wenye mitala ilikuwa safi zaidi na iliwaka tamaa kidogo zaidi kuliko mioyo ya waseja wengi ambao hakika wanaitawala tamaa. Maneno yafuatayo ya Isaya: “Iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA,” lazima yachukuliwe kumaanisha usafi wa moyo na toba kamili. 65. Licha ya hayo, watakatifu watajua thamani ya kadiri ya kujamiana katika ndoa na lile Paulo aliitalo kuutawala mwili katika utakatifu na heshima.996 66. Mwisho, ni haki kuwashauri wale ambao hawawezi kuitawala tamaa katika useja waoe ili wapate kuwa safi, kwa kuwa ndoa ni safi. Hivyo, sheria hii hii “Iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA,” inawataka waseja wasiokuwa safi wawe waume safi.
67. Hoja yao ya tatu ni ya kutisha sana: ndoa ya makasisi ni uzushi wa Yoviniano. Maneno matamu kabisa! Hili ni shtaka jipya kwamba, ndoa ni uzushi! Wakati wa Yoviniano, bado ulimwengu hauikujua sheria ya useja wa kudumu. Hivyo, ni uongo fidhuli kabisa kusema kwamba, ndoa za makasisi ni za uzushi wa Yoviniano au kusema kwamba, Kanisa liliilaani ndoa wakati huo. 68. Kauli za jinsi hiyo zinaonyesha shabaha ya wapinzani wetu ya kuiandika Hoja. Waliamua kwamba, njia bora sana ya kuwachochea wasioelimika ilikuwa ni kuyaanzisha mashtaka ya uzushi dhidi yetu mara kwa mara. Isitoshe, waliyatoa mawazo kwamba, sababu yetu ilijaribiwa na kuhukumiwa na mabaraza mengi ya awali ya Kanisa na kupatikana na hatia. Kwa hiyo, mara nyingi wanayageuza maamuzi haya ya Kanisa. Wanalijua jambo hili vizuri; hivyo, hawataki kutuonyesha nakala hata moja ya Hoja, ulaghai na usingiziaji wao usije ukafichuliwa. 69.
993 1 Tim. 4: 1
994 Melanchthon, ‘Ευπροσωπον.’
995 Melanchthon, ‘Πολυγαμοι.’
996 1 The. 4: 4
Tumetangulia kutoa msimamo wetu kuhusu mabishano ya Yoviniano kuhusiana na thamani ya ulinganisho wa ndoa na ubikira. Hatuiweki ndoa na ubikira katika kiwango kimoja, lakini ubikira wala ndoa haistahili kuhesabiwa haki.
70. Wanaitetea sheria mbovu na yenye utovu wa maadili kwa mabishano ya uongo kama haya. Kwa sababu kama hizi, wanawashawishi watawala wauchukue msimamo ulio kinyume cha hukumu ya Mungu, ambaye atawataka watoe hesabu ya kuzivunja ndoa, kuwatesa na kuwaua makasisi. Msiwe na mashaka kwa kuwa, kama jinsi damu ya Habili ilivyolia kifoni,997 vivyo hivyo pia damu ya waathiriwa wengi wasio na hatia waliotendewa unyama italilia mbinguni. Mungu mwenyewe atalipiza kisasi dhidi ya ukatili huu. Ndipo mtaelewa ubatili wa ubishi wa wapinzani wetu na kufahamu kwamba, katika hukumu ya Mungu hautasimama upotovu wa Neno la Mungu, kama jinsi Isaya asemavyo katika (Isa. 40: 6): “Wote wenye mwili ni majani, na wema wake wote ni kama ua la kondeni.”
71. Hata iweje, watawala wetu wataweza kuwa na dhamiri safi kuhusu suala hili. Hata kama makasisi walikuwa wamekosea walipooa, hakika, ni kinyume cha Neno na mapenzi ya Mungu kuzivunja ndoa na kuyatoa makatazo ya sheria shenzi na katili. Shani998 na shari999 hazitawafurahisha watawala wetu kwa ajili ya kufanya hivyo tu. Badala yake, wanaiheshimu kauli ya Neno la Mungu kuliko kulifuata jambo lingine lolote, hasa linapokuwa liko wazi kabisa.
Fungu la Ishirini na Nne: Misa
1. Tukianza, inatubidi kurudia tamko la utangulizi kwamba, hatuitangui misa bali tunailinda na kuitetea kwa uchaji. Misa zinasherekewa katika makanisa yetu kila Jumapili na nyakati nyinginezo za sikukuu. Wakati wa misa hizo, sakramenti hutolewa kwa wanaotaka kuipokea baada ya kuchunguzwa na kuondolewa dhambi zao. Tunayahifadhi Mapokeo ya kawaida kama vile maumbo ya liturgia, masomo, sala, mavazi ya makasisi, n.k.
2. Katika makemeo marefu kuhusu matumizi ya lugha ya Kilatini katika misa, wapinzani wetu werevu huyatumia maneno ya ulaghai juu ya jinsi msikilizaji asiyekuwa na elimu kuhusu imani ya Kanisa anafaidika kutokana na kuisikiliza misa asiyoielewa. Inavyoonekana, wanafikiria kwamba, kuisikiliza misa tu hata bila kuielewa ni tendo la ibada. 3. Hatutaki kuendelea kulisisitiza sana suala hili, bali tunamwacha msomaji autoe uamuzi wake. Tunalitaja hili kwa kulipitia tu ili 997 Mwa. 4: 10 998 Upya. 999 Ugomvi.
kuonyesha kwamba, masomo na sala za Kilatini zimehifadhiwa katika makanisa yetu.
Shabaha ya kuzifuata taratibu za ibada ni kuwafanya watu wajifunze Maandiko Matakatifu, na walioguswa na Neno waipokee imani, wamche Mungu, na pia waweze kusali. Hivyo, tunakihifadhi Kilatini kwa ajili ya hao wanaojifunza na kukielewa, na tunaziingiza nyimbo za Kijerumani ili watu wa kawaida wapate kujifunza, na hali hiyo itachochea imani na uchaji wao. 4. Daima, hii imekuwa desturi katika makanisa. Japo, mara kwa mara nyimbo za Kijerumani zimekuwa zenye mabadiliko mengi katika kuimbwa, hata hivyo, karibu kila mahali, watu waliimba nyimbo katika lugha zao wenyewe. 5. Hakuna aliyewahi kuandika au kupendekeza kwamba, watu wafaidike kwa kusikiliza masomo wasiyoyaelewa, au wakisikiliza taratibu za ibada ambazo haziwafundishi wala haziwaonyi, bali zinatendeka1000 tu kwa njia ya kufanya au kutazama tu. Zilaaniwe kabisa dhana za Kifarisayo za jinsi hiyo!
6. Desturi yetu hii ya kuiadhimisha misa ya umma au ya ushirika tu, hailipingi Kanisa Katoliki hata kidogo. Mpaka leo, sharika za Wayunani hazina misa za binafsi bali zina misa moja tu ya umma siku ya Jumapili au sikukuu za sherehe. Misa ya umma inaadhimishwa kila siku katika majumba ya watawa. Desturi hizi ni masalia ya mapokeo ya kale. Mababa wa Kanisa kabla ya Gregorio1001 hawazitaji misa za binafsi. 7.Kwa sasa, mjadala kuhusu asili za misa za binafsi utakomea hapa. Ni wazi kwamba, baada ya wamonaki waombaji1002 kuanza kutawala, idadi ya misa za binafsi iliongezeka. Misa hizo zimekuwa za ushirikina na zenye tamaa ya fedha mno kiasi kwamba, kwa muda mrefu, watu wote wema wametaka ziwekewe mipaka fulani. Ingawa Mt. Fransisko1003 alijaribu kulirekebisha jambo hili kwa agizo kwamba, kila siku, kila jumuia lazima iridhike na misa moja tu ya umma, mpango huu ulibadilishwa baadaye kwa sababu ya ushirikina au faida ya fedha. 8. Kwa hiyo, inapowapendeza wao wenyewe, wanazibadilisha asasi za Mababa, kisha, wanayanukuu mamlaka ya Mababa hao dhidi yetu. Epifanio aliandika kwamba, huko Asia, hakukuwepo na ibada za kila siku, bali Ushirika Mtakatifu1004 ulipokewa mara tatu kwa wiki na kwamba, desturi hii ilikuwa mapokeo ya mitume wenyewe. Anasema: “Mikutano kwa ajili ya Ushirika Mtakatifu iliagizwa na mitume ifanyike siku ya nne, ya Mkesha wa Sabato na
1000 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
1001 Papa Gregorio Mkuu wa Roma (+ 604 B.K.).
1002 Kilatini: ‘Monachi mendicantes.’
1003 Fransisko wa Asisi (1181/2-1226) mwanzilishi wa Daraja la Kifransiskano au “Ndugu Wadogo” (Kilatini, ‘Fratres minores’ au “Ndugu Weupe;” iliyokubaliwa na Papa Inokentio III mwaka wa 1209-1210.
1004 ‘Synaxis’ au ‘συναξις,’ (ushirika), (jumuia), sawa na “sinagogi” lakini katika maana ya Kikristo peke yake; pia ibada ya Ekaristi.
Siku ya Bwana.”1005
9. Wapinzani wetu wameukusanya ushuhuda mwingi hapa ili kuonyesha kwamba, misa ni dhabihu. Lakini nukuu zote wanazozitoa kutoka kwa Mababa na kutoka kwa ubishi zinanyamazishwa kwa jibu hili moja: misa kama tendo lenyewe tu haitoi neema wala, kwa wengine, haistahilishi msamaha wa dhambi ya kusameheka, ya mauti, ya hatia, au ya adhabu. Jibu hili moja linayakana mapingamizi yote wayatoayo wapinzani wetu, siyo katika Hoja hii tu bali pia katika maandiko yao yote kuhusu misa.
10. Wasomaji wetu lazima tuwakumbushe kuhusu hali halisi. Aiskino/ Aiskhines1006 aliwakumbusha Wayahudi kwamba, katika mabishano, sehemu zote mbili lazima zijishughulishe tu na suala lililo mbele yao na siyo kujishughulisha na mengineyo ya kando, jinsi mabondia hupigana wasimamampo bila kumwacha mpinzani. Vivyo hivyo, wapinzani wetu wanapaswa kulijadili suala lililo mbele yetu. Suala halisi la ubishi1007 likiwa dhahiri, itakuwa rahisi sana kuzitathmini hoja ambazo zimewasilishwa na pande zote mbili.
11. Katika Ukiri wetu, tumeelezea msimamo wetu kwamba, Chakula cha Bwana hakitoi neema tendo lenyewe tu na kwa wengine, walio hai au wafu, hakistahilishi msamaha wa dhambi, wa hatia au wa adhabu tendo lenyewe tu.1008 12. Msimamo huu umeimarishwa na kuthibitishwa na jambo hilo kwamba, haiwezekani kabisa kuupokea msamaha wa dhambi kwa ajili ya jitihada zetu tendo lenyewe tu, bali lazima tuvishinde vitisho vikuu vya dhambi, vya mauti, na tuifariji mioyo yetu kwa ufahamu wa Kristo kwa njia ya imani. Hivyo, kwa ajili ya Kristo, tunasamehewa dhambi na stahili na haki zake vimewekwa juu yetu (Rum. 5: 1): “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani.” Mambo haya ni imara na ya kweli kiasi kwamba, yanaweza kuishinda milango yote ya kuzimu.1009
13. Kama hili lingekuwa tatizo zima, kesi hii ingesuluhishwa. Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu awezaye kuikubali dhana hii ya Kifarisayo na ya kipagani kuhusu utendaji wa misa tendo lenyewe tu. Lakini dhana hii imeushinda umma na imezidisha idadi za misa nyingi mno. Wanafikiria kwamba, wanaweza kuituliza ghadhabu ya Mungu, kuupokea msamaha wa hatia na adhabu, na wanaweza kukipata chochote wakitakacho katika maisha haya, na hata wanaweza
1005 ‘Συναξεις
Epif. Haer. 3. 22. 522.
1006 Mbalagha Myunani (390/389 - mnamo 315); ‘Κατα
1007 Kilatini: ‘Status controversiae.’
1008 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
1009 Mt. 16: 18
(Dhidi ya Ktesifon) 206.
kuwaweka wafu huru kwa njia ya matendo ya Misa hizi. Watawa wa kiume na madaktari wanazuoni wameileta na kuifundisha dhana hii ya Kifarisayo kanisani.
14. Japo tayari tumeshaielezea kesi yetu, inatubidi tuongezee mambo machache kwa kuwa wapinzani wetu wamezipotosha aya nyingi za Maandiko Matakatifu kwa njia ya kuyatetea makosa yao. Hoja imeyasema mengi kuhusu dhabihu, ingawa katika Ukiri wetu, tumeliepuka neno hii makusudi kwa sababu ya utata wake. Tayari tumekwisha kuelezea uelewa wa sasa wa dhabihu kati ya wale watu tunaowakosoa kwa sababu ya matumizi yake mabaya. Kwanza kabisa, hatuna budi kuelezea maana ya dhabihu ili kuzifafanua aya za Maandiko Matakatifu waliyoyapotosha vibaya. 15. Kwa mwongo mmoja uliopita, wapinzani wetu wameandika vitabu visivyokuwa na mwisho kuhusu dhabihu, lakini hakuna hata kitabu kimoja kinachoifafanua dhabihu. Wanaichukua tu hili neno “dhabihu” kutoka katika Maandiko Matakatifu au Mababa wa Kanisa. Kisha, wanaigeuza kwa kuziongezea dhana zao kana kwamba, inamaanisha chochote wanachopenda imaanishe.
Asili na Aina za Dhabihu
16. Sokrate anasema katika kitabu cha Platoni, yaani, “Faidro” kwamba, yeye hupenda sana utofautishaji kwa sababu bila kupambanua hakuna linaloweza kuelezwa au kueleweka katika mazungumzo. Na kwamba ikiwa atamuona yeyote mwenye ujuzi mzuri wa kupambanua atazifuata nyayo zake sawa na kuzifuata zile za Mungu.1010 Anashauri pia mtu anayetofautisha mambo kukata washiriki kwenye muunganiko, si kama mpishi asiye na ujuzi amtengapo mshiriki mahali pabaya. Basi, wapinzani wetu wanayadharau mashauri haya sana hata kwamba, Platoni aliwaita wapinzani wetu “wapishi wabaya”1011 wanaokatakata sehemu za dhabihu hata kuziharibu jinsi tutakavyoona tukianza kuzijadili aina tofauti za dhabihu. 17.Wanatheologia hutofautisha kwa njia halisi kati ya Sakramenti na dhabihu. Jinsi inayofanana pande zote, ingelikuwa “kaida ya dini” au “tendo takatifu.” 18 Sakramenti ni kaida ya dini au tendo ambalo kwalo Mungu anatutolea yale ambayo anatuahidi katika kaida ya dini. Hivyo, Ubatizo si tendo ambalo tunalomtolea Mungu, bali ambalo kwalo Mungu anatubatiza, yaani, kupitia mchungaji anayetenda kwa niaba yake. Hapa Mungu anatutolea na kututunukia msamaha wa dhambi n.k. kwa mujibu wa ahadi: “Aaminiye na kubatizwa ataokoka.”1012 Kinyume chake, dhabihu ni kaida au tendo tunalolitoa kwa Mungu ili kumheshimu.
1010 Sokrate mwanafalsafa Myunani (mnamo 380-450 K.K.).
1011 Melanchthon, ‘κακοι μαγειροι.’
1012 Mk. 16:10
19. Kimsingi, kuna aina mbili tu za dhabihu na si zaidi. Aina ya kwanza ni dhabihu ya upatanisho. Hili ni tendo la ridhaa kwa ajili ya hatia na adhabu ili kutupatanisha na Mungu au kuituliza ghadhabu yake, au kustahilisha msamaha wa dhambi kwa wengine. Aina ya pili ni dhabihu ya shukrani.1013 Dhabihu hii haistahilishi msamaha wa dhambi au upatanisho, bali inatolewa na wale waliopatanishwa ili kutoa au kuonyesha shukrani zetu kwa ajili ya msamaha wa dhambi na fadhili nyinginezo zilizopokelewa.
20. Ni lazima kabisa kuona dhahiri na kuweka mtazamo mbele katika mabishano haya na majadiliano mengine, aina hizo mbili na kuwa na kuwa waangalifu sana ili tuzisichanganye. Kama kitabu hiki kingeruhusu, tungeongezea sababu za utofautishaji huu. Ushuhuda mwingine wa mwingi wa utofautishaji huo unapatikana katika Waraka wa Waebrania na kwingineko.1014 21 Dhabihu zote za Walawi zinaweza kupambanuliwa chini ya mojawapo ya mada hizi. Naam, Torati ilizitaja baadhi ya dhabihu kuwa zile za upatanisho kwa ajili ya kile walichomaanisha au usawa wake, siyo kwa sababu ya kuustahilisha msamaha wa dhambi mbele za Mungu, bali ni kulingana na haki ya sheria; hivyo wale ambao dhabihu hizi zilitolewa hawakupaswa kutengwa na umma. Kwahiyo, dhabihu ziliitwa za upatanisho kwa ajili ya dhambi, au za kuteketezwa1015 kwa ajili ya hatia. Dhabihu za shukrani1016 zilikuwa sadaka ya unga, dhabihu, sadaka ya vinywaji, sadaka ya shukrani, malimbuko ya kwanza, na zaka (Law. 1-7).1017
22. Lakini dhabihu moja ya upatanisho imetolewa ulimwenguni, yaani kifo cha Kristo, kama Waraka kwa Waebrania ufundishavyo: “Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.”1018 Baadaye kidogo tunaelezwa kuhusu mapenzi ya Kristo: “Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Kristo Yesu mara moja tu.”1019 23. Isaya anafafanua Torati ili tupate kujua kweli kwamba, kifo cha Krsto ni ridhaa ya kweli au upatanisho wa dhambi zetu, haikuwa kama taratibu za torati; kwa sababu hiyo, anasema: “Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, ataona uzao wake, ataishi siku nyingi.”1020 Neno alilotumia hapa, (asam) linamaanisha sadaka ya hatia.1021
1013 Melanchthon, ‘Sacrificium ευκριστικον.’
1014 Ebr. 10: 5-16; Kut. 32:6; 2 Sam. 6: 17
1015 Melanchthon, ‘Holocaustum.’ Aina hii maalumu ya dhabihu inatafsiriwa katika, Union Version nje ya Kitabu cha Walawi kwa maneno kama: matoleo, ‘‘dhabihu, ‘‘sadaka, bila kuelekezea kamili aina yake maalumu.
1016 Melancthon, ‘ευκαριστικα.’
1017 Law. 1 – 7
1018 Ebr. 1: 4
1019 Ebr. 10: 10
1020 Isa. 53: 10
1021 Taz. Law. 5
Katika Torati, sadaka hii ilimaanisha kwamba, sadaka itakuja itakayoridhisha hatia za dhambi zetu na kumpatanisha Mungu, kusudi watu waweze kujua kwamba, Mungu anataka kupatanishwa nasi kwa ajili ya stahili za mtu mwingine, yaani Kristo, na siyo kwa ajili ya matendo yetu ya haki.1022 Paulo anafafanua neno hilo hilo “asam” kumaanisha “dhambi” katika Rum. 8: 3: “Kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;” yaani, kwa njia ya dhabihu kwa ajili ya dhambi.
Tunaweza kuelewa maana ya neno hili kwa urahisi zaidi tukiangalia desturi za Wapagani ambazo tunaona katika mahubiri ya Mababa wa Kanisa kwamba, zimechukuliwa kutoka kwa ufahamu ulio potofu. Katika Kilatini sadaka ya hatia iliitwa “hostia.” Ilitolewa ili kumtuliza Mungu aliyeonekana kuwa amekasirika mno wakati wa balaa kubwa.1023 Nyakati zingine wanadamu walitolewa kama dhabihu, labda kwa sababu walisikia kwamba, dhabihu ya kibinadamu itaweza kumtuliza Mungu na wanadamu wote. Wayunani waliita ‘biwi’ au “jalala.”1024 Isaya na Paulo wanamaanisha kwamba, Kristo amefanyika kuwa sadaka ya hatia, yaani “hostia,” dhabihu ya ridhaa, ili ampatanishe Mungu kwa njia ya stahili zake, siyo kwa stahili zetu. Kwa hiyo, hili libakie katika suala hili kwamba, kifo cha Kristo peke yake ni dhabihu ya kweli ya upatanisho. 24. Naam, dhabihu za upatanisho za Walawi ziliitwa tu kuwa za upatanisho kwa ajili ya upatanisho wa baadaye. Kwa njia ya mlinganisho, zilikuwa upatanisho kulingana na haki ya sheria ili wakosaji wasitengwe kabisa na umma. Lakini baada ya ufunuo wa Injili, zilitakiwa kukomeshwa kwa kuwa hazikuwa upatanisho wa kweli, kwa sababu Injili iliahidiwa ili kuufunua upatanisho wa kweli.
25. Dhabihu zilizobaki ni sadaka za shukrani.1025 Zinaitwa dhabihu za sifa, mahubiri ya Injili, imani, sala, matendo ya shukrani, ukiri wa imani, mateso ya watakatifu na hata zaidi, matendo yote mema ya watakatifu. Sadaka hizi zote si utoshelevu kwa wale wanaozitoa, wala haziwezi kutumiwa kwa ajili ya watu wengine kuwastahilisha msamaha wa dhambi au upatanisho kwa ajili ya matendo yenyewe tu. Sadaka hizi zinatolewa na wale ambao tayari walishapatanishwa. 26. Dhabihu za Agano Jipya ni za aina hii, jinsi Petro afundishavyo katika 1 Pet. 2: 5: “Ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za Roho.” Dhabihu za kiroho zinapingana siyo tu na dhabihu za wanyama, bali pia na matendo ya wanadamu yaliyotendeka kwa ajili ya matendo haya yenyewe. Kwa maana, neno hili la “kiroho” linamaanisha, 1022 Kilatini: ‘Propter nostras iustitias;’ (kwa ajili ya haki zetu), yaani, matendo ya haki kama katika Ufu. 19: 8 1023 Dhabihu ya ‘piaculum,’ yaani, ile ya ridhaa ilikuwa dhabihu kuu katika ibada rasmi ya serikali ya Roma.
1024 Kiyunani: ‘καθαρματα’ au ‘περιπσηματα;’ taz. 1 Kor. 4: 13 1025 Wal. 3: 7, 11-17 (sadaka za shukrani); Zab. 56:12 (dhabihu za shukrani). Melancthon, ‘Sacrificia, ευκηαριστικα’
mienendo ya Roho Mtakatifu ndani yetu. Paulo anafundisha katika Rum. 12:1 “Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” “Ibada yenye maana” inamaanisha ibada ambayo nafsi inamfahamu Mungu na kumshika, jinsi inavyotokea katika mienendo ya hofu na tegemeo kwa Mungu. Hivyo, basi, haiko kinyume cha ibada za Walawi tu ambapo ng’ombe walichinjwa, bali pia kinyume cha ibada zote ambapo inabuniwa kumtolea Mungu tendo lenyewe tu kwa nguvu ya kutendeka. Waraka kwa Waebrania unafundisha jambo hilo hilo (Ebr. 13: 15): “Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima,” Waraka huu unaongezea ufafanuzi wake: “Yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.” Waliamriwa hapa kuzitoa sifa, yaani, maombi, shukrani, ukiri, na mengine kama hayo. Haya yananufaisha, siyo kama matendo yenyewe, bali kwa ajili ya imani. Tunaliona jambo hili katika kauli hii: “Kwa njia yake na tumtolee,” yaani, kwa njia ya imani katika Kristo.
27. Kwa ufupi, ibada ya Agano Jipya ni ibada ya kiroho. Ibada hii ni haki ya imani moyoni na matunda ya imani. Kwa hiyo, inafuta ibada za Walawi. Kristo anasema katika Yn. 4: 23-24: “Waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Naam, Baba mwenyewe anatafuta wale ambao humwabudu. Mungu ni roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” Aya hizi zinalaani wazi maoni kuhusu dhabihu zinazotungwa kunufaisha kama matendo yenyewe tu. Badala yake, zinafundisha kuabudu katika roho, yaani, kwa misukumo ya moyo na imani. 28. Hali kadhalika, manabii wa Agano la Kale pia walililaani wazo la umma kuhusu matendo yaliyotendeka tu na kufundisha haki na sadaka za kiroho. Yer. 7: 22-23, inasema: “Maana sikusema na baba zenu, wala sikuwaamuru kwa habari za sadaka za kuteketezwa na dhabihu1026, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, lakini naliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru, mpate kufanikiwa.” Kwa njia gani tungefikiri kwamba, Wayahudi walikubali hotuba hii iliyoonekana kupingana na Musa hadharani? Naam, ilifahamika kwamba, Mungu aliwaamuru Mababa kumtolea sadaka za kuteketezwa pamoja na dhabihu, lakini Yeremia analaani wazo lao kuhusu dhabihu ambayo haitoki kwa Mungu. Yaani, ibada za namna hiyo zilimpendeza Mungu kama matendo yenyewe tu. Lakini anaongezea amri ya Mungu kuhusu imani: “Sikilizeni;” maana yake: Ninyi aminini kwamba, mimi ndimi Mungu wenu ndivyo ninavyotaka, mnanifahamu kuwa mwenye kuwahurumia na kuwasaidia kwa maana sizihitaji dhabihu zenu. Amini kwamba, mimi ndimi Mungu, anayewahesabia haki, Mungu Mwokozi, siye kwa ajili ya 1026 Kilatini: ‘Holocaustis et victimis.’
matendo, bali kwa ajili ya Neno na ahadi yangu. Ombeni na kuutarajia msaada wangu kwa kweli na kwa moyo!
29. Hali kadhalika, Zab. 491027 inalaani wazo la matendo yenyewe tu na kudai maombezi baada ya kuikataa dhabihu: “Je! nile nyama ya mafahali n.k. . . . Ukaniite siku ya mateso; nitakuokoa, na wewe utanitukuza.” Hii inashuhudiwa kuwa tukimwomba Mungu kwa mioyo yetu yote ni ibada ya kweli na heshima,
Kadhalika Zab. 39:6 1028: “Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, masikio yangu umeyazibua.” Maana yake: wewe umenipa Neno la kusikia, na ahadi zako na kutaka niliamini kwamba unapenda sana kunihurumia, kunisaidia n.k. Zab. 50:181029: “Maana hupendezwi na dhabihu1030… dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu hutaudharau.”
Kadhalika Zab. 4:6: “Toeni dhadihu za haki, na kumtumaini BWANA.” Zaburi inatuamuru tumtegemee hata inasema kwamba, hiyo ndiyo dhabihu ya haki, na inamaanisha kwamba, dhabihu zingine si za kweli na za haki. Pia Zab. 115:17: “Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; na kulitangaza jina la BWANA”. Sala inatajwa kuwa dhabihu ya shukrani.
30. Maandiko Matakatifu yamejaa ushuhuda wa jinsi hiyo unaofundisha kwamba, dhabihu kama matendo yenyewe tu hazitupatanishi na Mungu. Kwa hiyo, Maandiko Matakatifu yanafundisha kwamba, baada ya kubatilishwa kwa ibada za Walawi, dhabihu mpya na safi zitatolewa ambazo ni imani, sala, shukrani, ukiri na mahubiri ya Injili pamoja na mateso kwa sababu ya Injili, n.k.
31. Kuhusu dhabihu za namna hiyo Malaki anasema: “Kwa maana tokea mawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika Mataifa, na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi”1031 Wapinzani wetu wanaipotosha aya hii kumaanisha misa kwa njia ya kuwanukuu Mababa wa Kanisa. Lakini ni rahisi sana kuwapa jibu. Ingawa aya hii ingemaanisha misa, haitafuata kwamba, misa kama tendo lenyewe tu lililotendeka litaweza kutufanya kuwa wenye haki au kustahili msamaha wa dhambi n.k. ikitumika kwa ajili ya watu wengine. Nabii hasemi lolote kuhusu mambo haya yaliyobuniwa kwa njia fidhuli na watawa na wataalamu wa ghiliba. 32. Mbali na hilo, maneno yenyewe ya nabii yanatoa maana yake. Kwanza, maneno haya yanasema kwamba, jina la Bwana litakuwa
1027 ‘Vulgata;’ ‘Union Version,’ Zab. 50: 13,15
1028 ‘Union Version,’ Zab. 40
1029 ‘Union Version,’ Zab. 51
1030 Kilatini: ‘Holocaustum’
1031 Mal. 1: 11
kuu kabisa. Hili linafanyika kwa njia ya mahubiri ya Injili, yanayofanya jina la Kristo na huruma ya Baba iliyoahidiwa katika Kristo ijulikane vizuri. Mahubiri ya Injili yanazaa imani kwa watu wanaoipokea Injili. Watu hawa wanamwomba Mungu, wanamshukuru, wanayavumilia mateso katika kuungama, na kuyatenda matendo mema kwa ajili ya utukufu wa Kristo. Hivi ndivyo, jina la Bwana litakavyofanyika kuwa kuu kati ya mataifa. Kwa hiyo, “ubani” na “dhabihu safi” havimaanishi desturi kama tendo lenyewe tu lililotendeka bali dhabihu zile zote ambazo kwazo, jina la Bwana linatukuzwa. Hizo ni kama imani, sala, mahubiri ya Injili, maungamo n.k. 33. Mtu akipenda kuambatanisha hapa kaida ya dini, tutaweza kulivumilia hilo kwa urahisi kama hamaanishi kaida peke yake au kufundisha kwamba, kaida hunufaisha kama tendo lenyewe tu lililotendeka. Naam, tunahesabu kati ya dhabihu za sifa, yaani, sifa za Mungu, na mahubiri ya Neno. Hivyo ndivyo, sifa ya Mungu inavyoweza kuwa tendo la shukrani kwa njia ya kukipokea Chakula cha Bwana. Lakini shukrani hii haiwezi kuhesabia haki kama tendo lenyewe tu, au kutumika kwa ajili ya watu wengine ili kustahili msamaha wa dhambi. Lakini tutaelezea baadaye kidogo jinsi kaida za dini zinaweza kubatilishwa kuwa dhabihu. Kwa kuwa, Malaki anazungumzia kuhusu ibada zote za Agano Jipya na si Chakula cha Bwana peke yake, na halitoi wazo la kifarisayo kuhusu sherehe za tendo lenyewe tu lililotendeka. Hivyo, Malaki hatupingi hata kidogo, bali anatuunga mkono. Kwa maana, anahitaji ibada za moyo ambazo kwazo, jina la Bwana linatukuzwa sana na kuwa kuu kabisa.
34. Wanarejea aya nyingine kutoka Malaki: “Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha, nao watamtolea BWANA dhabihu katika haki.”1032 Aya hii wazi inahitaji dhabihu za wenye haki; Kwa sababu hiyo, haielezei wazo kuhusu tendo lenyewe tu lililotendeka. Naam, dhabihu za wana wa Lawi, yaani, za wale wanaofundisha katika Agano Jipya, ni mahubiri ya Injili na matunda mema ya mahubiri haya jinsi Paulo anavyosema katika Rum. 15: 16: “Ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanye Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.” Hii inamaanisha kwamba, Wapagani watakuwa dhabihu zinazokubalika kwa Mungu kwa imani, n.k. Uchinjwaji wa wanyama katika Agano la Kale lilimaanisha kifo cha Kristo na mahubiri ya Injili, ambayo kwayo, lazima tuufishe mwili huu wa kale na kuanza maisha mapya na ya milele ndani yetu.
Lakini kila mahali, wapinzani wetu hulipotosha neno dhabihu kumaanisha kaida ya dini pekee. Wanayaruka kabisa mahubiri ya Injili, imani, maombi na
1032 Mal. 3: 3
mambo mengine kama hayo, ijapokuwa kaida za dini zilianzishwa kwa sababu ya mambo haya. Agano Jipya lazima liwe na dhabihu za moyo, na siyo kaida za dini zilizotendeka kwa mtindo wa makuhani Walawi.
35. Wapinzani wetu huirejea pia dhabihu ya kila siku,1033 jinsi ilivyokuwa dhabihu ya kila siku katika Torati. Hali kadhalika, lazima misa iwe dhabihu ya kila siku katika Agano Jipya. Wapinzani wetu watafaulu vizuri iwapo tutawaacha watushinde kwa mafumbo. Lakini inajulikana wazi kwamba, mafumbo hayazai uthibitisho imara. Hata hivyo, kwa urahisi tunakubali kwamba, misa inafahamika kuwa dhabihu ya kila siku, mradi tu inamaanisha misa nzima. Yaani, kaida ya mahubiri ya Injili, imani, sala, na shukrani. Naam, haya yote yanaambatana na dhabihu ya kila siku ya Agano Jipya kwa kuwa kaida za dini zilianzishwa kwa ajili ya mambo haya na hazipaswi kutenganishwa nayo. Kwa hiyo, Paulo anasema: “Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.”1034 Lakini kutokana na mfano huu wa Walawi, haitokei hata kidogo kwamba, kaida ya dini ni tendo lenyewe tu lililotendeka ili kuhesabia haki au kutumika kwa ajili ya wengine ili kuwastahilishia msamaha wa dhambi n.k. 36. Kwa upande wingine, mfano wa Walawi hauonyeshi tu kaida peke yake bali mahubiri ya Injili. Kitabu cha (Hesabu 28:4 n.k.) kinaorodhesha sehemu tatu za dhabihu hii ya kila siku, yaani, ile ya kondoo wa kuteketezwa, dhabihu ya kinywaji, na dhabihu ya unga. Torati ilionyesha taswira au vivuli vya mambo yale yatakayokuja baadaye. Kwa sababu hiyo, mandhari haya yanamwelezea Kristo na ibada nzima ya Agano Jipya. Kuteketezwa kwa kondoo kunamaanisha kifo cha Kristo. Dhabihu ya kinywaji inamaanisha waaminio ulimwenguni walionyunyiziwa damu ya Mwana Kondoo, yaani, kwa njia ya mahubiri ya Injili. Tendo hili ni la kutakaswa, jinsi Petro asemavyo: “Kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutiifu na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo.”1035 Dhabihu ya unga ni alama ya imani, sala na shukrani ndani ya mioyo. 37. Kwa hiyo, kadiri tunavyoona kivuli katika Agano la Kale,1036 vivyo hivyo, katika Agano Jipya, inatubidi tutafute jambo limaanishwalo1037 na siyo alama nyingine inayohusu dhabihu.
38. Ingawa kaida ya dini ni kumbukumbu ya kifo cha Kristo, kwa hivyo, yenyewe siyo dhabihu ya kila siku. Ukumbusho wenyewe ni dhabihu hii ya kweli ya kila siku, yaani, mahubiri na imani inayoamini kweli kwamba, Mungu
1033 Kut. 29: 38-39; Dan. 8: 11-12; 12: 11
1034 1 Kor. 11: 26
1035 1 Pet. 1: 2
1036 Kol. 2 : 17; Ebr. 10 : 1
1037 Kilatini: ‘Res significata’
amepatanishwa nasi kwa kifo cha Kristo. Hapo lazima pawepo dhabihu ya kinywaji. Hivyo ndivyo kusema, matokeo ya mahubiri kunyunyiziwa damu ya Kristo na Injili. Zinatakiwa pia sadaka za unga, yaani shukrani, ungamo na mateso.
39. Hivyo, baada ya kulikana wazo hili la Kifarisayo kuhusu tendo lenyewe tu lililotendeka, tunaelewa kwamba, ibada ni ibada ya kiroho ya kila siku na dhabihu ya moyo. Maana, katika Agano Jipya, inatubidi kutafuta kiini cha mambo, yaani, Roho Mtakatifu, anayetufisha na kutuhuisha. 40. Katika mambo haya Inajulikana wazi vya kutosha kwamba, mfano wa dhabihu ya kila siku haitupingi hata kidogo, bali unatuunga mkono kwa sababu tunataka mambo yote yanayoambatana na dhabihu ya kila siku. Wapinzani wetu huota ndoto ya uongo kwamba, inamaanisha kaida peke yake na siyo mahubiri ya Injili, kufishwa na kuhuishwa kwa moyo.
41 Sasa basi, watu wema wanaweza kuhukumu kwa urahisi kuwa mashtaka haya ni ya uongo kabisa, kwamba, tunaiondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.1038 Uhalisia unaonyesha akina nai ni Antioko wanaolitawala Kanisa. Watu hawa kisingizio cha dini, wananyakua mamlaka ya dunia, na wanatawala bila kujali dini na mafundisho ya Injili. Wanaviendeleza vita mithili ya wafalme wa dunia, na kuanzisha ibada mpya kabisa kanisani. 42. Kwani, wapinzani wetu huhifadhi kaida ya misa tu na kuibadilisha hadharani kuwa chukizo la uharibifu ili kujikusanyia fedha. Kisha, wanabuni kwamba, tendo hili linaweza kutumika kwa ajili ya wengine ili kuwastahilisha neema na kila aina ya wema. 43. Wakihubiri hawafundishi Injili au kuzifariji dhamiri au kuonyesha wazi kwamba, dhambi zinasamehewa bure kwa ajili ya Kristo. Badala yake, wanazungumzia ibada za watakatifu, matendo ya upatanisho wa wanadamu, mapokeo ya kibinadamu na kuthibitisha kwamba, haya huwahesabia haki wanadamu mbele za Mungu. Hata hivyo, baadhi ya hayo ni ya kukufuru hadharani. Wanaliteta jambo hili kwa udhalimu. Baadhi ya wahubiri wanaotaka kuonekana kuwa wenye ustaarabu zaidi, wanatoa masuala ya kifalsafa ambayo umma hauyaelewi wala hayaeleweki kwa wao pia wanaoyatambulisha. Mwishowe, hao ndio wanaostahimilika kidogo huifundisha sheria bila kusema chochote kuhusu haki ya imani.
44. Katika Hoja, wapinzani wetu wanaomboleza kwa njia ya ajabu sana kuhusu “uharibifu wa mahekalu”1039 kuwa, madhabahu hubaki bila mapambo, bila mishumaa wala sanamu. Wanayaita mambo haya yasiyokuwa na maana,
1038 Dan. 11 : 31; matendo ya Mfalme wa Shamu, Antioko Epifane IV miaka ya 169 na 167 K.K. Matendo haya yalikuwa mfano wa ujeuri wa Mpinga Kristo utakaokuja. 1039 Rejea Mpinga Kristo.
mapambo ya makanisa. 45. Danieli anayaelezea tofauti akiita “chukizo la uharibifu”1040 yaani, ujinga wa Injili. Umma uliojazwa mapokeo na mawazo mengi mbalimbali hata haukuweza kuelewa mafundisho makuu ya Kikristo. 46. Ni nani kati ya watu wa kawaida aliyewahi kuelewa mafundisho yale ya toba yaliyotolewa na wapinzani wetu? Hata hivyo, aya hii ndiyo kuu kabisa katika mafundisho ya Kikristo.
Dhamiri za watu ziliteswa kwa hesabu ya dhambi na matendo ya upatanisho. Wapinzani wetu hawakutaja kamwe imani, ambayo kwayo, tunapokea bure msamaha wa dhambi. Vitabu vyao vyote na mahubiri yao yote yalikuwa kimya kabisa kuhusu mapigano ya imani katika hali ya kukata tamaa na juu ya msamaha wa dhambi wa bure kwa ajili ya Kristo. 47. Licha ya haya, ilikuja najisi ya kutisha ya misa na ibada nyingi potovu katika makanisa. Hili ndilo “chukizo la uharibifu” analolielezea Danieli.
48. Kinyume chake na kwa fadhili ya Mungu, makasisi katika makanisa yetu wanazingatia Huduma ya Neno, wanafundisha Injili kuhusu fadhili za Kristo, kuuonyesha msamaha wa dhambi upatikanao bure kwa ajili ya Kristo. Mafundisho haya yanaipatia dhamiri faraja ya kweli. Licha ya haya, yanafuata mafundisho yaliyoamriwa na Mungu kuhusu matendo mema. Pia wanazungumzia kuhusu thamani na matumizi ya sakramenti.
49. Iwapo “dhabihu ya kila siku” ingemaanisha matumizi ya sakramenti, tungeitunza vizuri zaidi kuliko wapinzani wetu kwa sababu, kati yao, mapadre wanaitunza sakramenti kwa ajili ya malipo tu. Sakramenti inatumiwa kati yetu kwa bidii na kwa njia ya uchaji zaidi. Umma unapokea sakramenti baada ya kufundishwa na kuchunguzwa. Naam, watu hufundishwa kuhusu matumizi ya kweli ya sakramenti kwamba, imeanzishwa ili iwe muhuri na ushuhuda wa msamaha bure wa dhambi. Hali kadhalika, lazima dhamiri zenye hofu zihimizwe kutegemea na kuamini kwamba, zinasamehewa dhambi zao bure. Hivyo, kwa kuwa tunayatunza mahubiri ya Injili pamoja na matumizi halisi ya sakramenti, bado “dhabihu ya kila siku” inadumu kati yetu.
50. Kwa upande wa mwonekano wa nje, mahudhurio katika makanisa yetu ni mengi kuliko wapinzani wetu, kwa kuwa wasikilizaji huhimizwa kabisa na mahubiri ya kupata faida na kuwa dhahiri. Lakini si umma wala Madaktari Wanazuoni walioyaelewa abadani mafundisho ya wapinzani wetu. 51. Mapambo ya kweli ya Kanisa ni mafundisho matakatifu, yenye faida na dhahiri, matumizi ya dhati ya sakramenti, bidii ya sala na mengine kama hayo. Mishumaa, 1040 Dan. 11: 31; 12: 11
vyombo vya dhahabu na mapambo kama hayo yanarembesha, lakini hayawi urembo halisi wa Kanisa. Ikiwa wapinzani wetu watasisitiza maana ya ibada kuwa katika mambo kama haya, mbali na mahubiri ya Injili, imani na mapigano yake, itawabidi wahesabiwe katika wale wanaoelezwa na Danieli (2: 38), yaani, wanaomwabudu Mungu kwa njia ya dhahabu na fedha.1041
52. Wanarejea pia Waraka kwa Waebrania: “Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabibu kwa ajili ya dhambi.”1042 Kutokana na aya hii, wanabuni kwamba, kwa kuwa Agano Jipya lina makuhani wakuu na makasisi, inaelekea kwamba, lazima dhabihu ya aina nyingine ipatikane kwa ajili ya dhambi. Kauli hii inawavutia sana wajinga, hasa iwapo fahari ya kuwa kuhani na dhabihu za Agano la Kale zinawekwa mbele ya macho yao. Ulinganifu huu huwadanganya wajinga na kufikiria kirahisi kwamba, hatuna budi kufanya kaida fulani au dhabihu zitakazotumika kwa ajili ya makosa ya watu wengine sawa na ilivyofanyika katika Agano la Kale. Ibada za misa na sera zingine za Papa siyo chochote isipokuwa sera ya Walawi iliyoeleweka vibaya.
53. Ingawa kauli yetu ina ushuhuda maalumu katika Waraka kwa Waebrania, wapinzani wetu huzipotosha aya zilizofunuliwa katika waraka huo dhidi yetu, jinsi inavyosemwa: “kila kuhani mkuu amewekwa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi.” Maandiko Matakatifu yenyewe yanaungana na Kristo kama Kuhani Mkuu. Maneno yaliyotangulia yanazungumzia kuhusu ukuhani wa Walawi yanayomaanisha kwamba, ukuhani wa Walawi ulikuwa mfano wa ukuhani wa Kristo. Kwa kuwa, dhabihu za Walawi hazikustahili msamaha wa dhambi mbele za Mungu. Zilikuwa tu mfano wa dhabihu ya Kristo ambayo ilikuwa dhabihu moja ya upatanisho kama tulivyokwisha kusema. 54. Kwa hiyo, sehemu kubwa ya waraka inazungumzia kwamba, ukuhani wa kale na dhabihu za zamani havikuanzishwa ili kuustahili msamaha wa dhambi au upatanisho mbele za Mungu, bali kuiashiria dhabihu moja pekee ya Kristo itakayokuja. 55. Naam, iliwabidi watu watakatifu wa Agano la Kale kuhesabiwa haki kwa ahadi ya msamaha wa dhambi uliotolewa kwa ajili ya Kristo mithili ya watu watakatifu wa Agano Jipya. Iliwabidi watu watakatifu wote tangu mwanzo wa ulimwengu, kuamini kwamba, Kristo aliyeahidiwa atakuwa dhabihu na ridhaa kwa ajili ya dhambi, jinsi Isaya afundishavyo (Isa. 53: 10): “Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kuwa dhambi.”
56. Kwa kuwa, dhabihu za Agano la Kale hazikustahili upatanisho, isipokuwa
1041 Dan. 11: 38, yaani, Mpinga Kristo. 1042 Ebr. 5: 1
kwa maana ya kuashiria tu. Yaani, zilistahilisha upatanisho wa kiraia peke yake, kumaanisha, dhabihu itakayokuja. Kwa hiyo, sasa inafuata kwamba, dhabihu ya Kristo iliyotumika kwa ajili ya makosa ya wengine ndiyo ya pekee. Hakuna dhabihu nyingine iliyobakia katika Agano Jipya itakayotumika kwa ajili ya makosa ya wengine isipokuwa dhabihu moja ya Kristo msalabani.
57. Wale wanaofikiria kwamba, dhabihu za Walawi ziliustahilisha msamaha wa dhambi mbele za Mungu na kudai kwa mfano huu kwamba, ilipasa dhabihu zitumike kwa ajili ya wengine katika Agano Jipya mbali na kifo cha Kristo, wanakosea kabisa. Ubunifu huu unatangua kabisa ustahili wa mateso ya Kristo na haki ya imani. Isitoshe, huyavunja mafundisho ya Agano la Kale na ya Agano Jipya na kuwaweka wapatanishi na wasuluhishi wengine kama Makuhani Wakuu na makuhani wa sadaka1043 badala ya Kristo, ambao huuza kazi zao makanisani kila siku.
58. Kwa hiyo, mwingine akidai lazima Agano Jipya liwe na kuhani atoaye dhabihu kwa ajili ya makosa, hoja hii itaweza kukubaliwa ikihusiana na Kristo pekee. Waraka mzima kwa Waebrania unauthibitisha utatuzi huu. Tukidai ridhaa nyingine kwa shabaha ya kutumika kwa ajili ya makosa ya wengine na kumpatanisha Mungu nasi mbali na kifo cha Kristo, itakuwa na maana ya kuwaweka wapatanishi wengine. 59. Licha ya hayo: ukuhani wa Agano Jipya ni huduma ya Roho Mtakatifu, jinsi Paulo anavyofundisha katika 2 Kor. 3: 6. Kwa sababu hiyo, dhabihu ya pekee ya ridhaa kwa ajili ya dhambi za watu wengine ni dhabihu ya Kristo. Hakuna dhabihu nyingine sawa na zile za Walawi ambazo zingeweza kutumika kwa ajili ya wengine kama matendo yenyewe tu yaliyotendeka. Kinyume chake, huduma hii inawapa watu Injili na sakramenti ambazo kwazo, wanaipokea imani na Roho Mtakatifu na kwa kufishwa na kuhuishwa. Naam, huduma ya Roho Mtakatifu hulipinga kabisa jambo hili kuwa matendo yenyewe tu kwa ajili ya wengine. Naam, ni huduma ya Roho ambayo kwayo, Roho Mtakatifu huifanya kazi yake mioyoni mwa watu. Kwa hiyo, huduma yake hii huwafaidisha watu kwa njia ya kufanya kazi yake ya kuwapa uzao mpya na kuwahuisha. Hili halifanyiki kwa njia ya kutumia tendo la mwingine kwa ajili ya wengine kama matendo yenyewe tu yaliyotendeka.
60. Sasa basi, tumeonyesha kwa nini misa haihesabii haki kama tendo lenyewe tu na iliyotumika kwa ajili ya wengine kuwastahilishia msamaha wa dhambi kwa kuwa mambo haya mawili yanaipinga haki ya imani. Haiwezekani kabisa kuupata msamaha wa dhambi, kuzishinda hofu za dhambi na kifo kwa tendo lolote au kwa kitu chochote isipokuwa kwa njia ya imani katika Kristo, 1043 Kilatini: “Pontifex” na “sacrificulus, majina ya Kirumi ya Kipagani.
kulingana na haya: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na imani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.”1044
61. Pia tumeonyesha kwamba, aya za Maandiko Matakatifu zilinukuliwa ili kutupinga, kwa kiasi kidogo sana zinayalinda maoni mapotovu ya wapinzani wetu kuhusu tendo lenyewe tu lililotendeka.1045 Watu wema kati mataifa yote wanaweza kulihukumu jambo hili. 62. Kwa sababu hiyo, tunakana kabisa kosa la Tomaso anaposema: “Mwili wa Bwana, uliotolewa msalabani mara moja kwa ajili ya deni la dhambi ya asili, unatolewa kila siku madhabahuni kwa ajili ya makosa ya kila siku ili Kanisa liwe na kipawa ili lijipatanishe na Mungu.”1046 63. Inabidi tuyakane makosa mengine yote ya kawaida ya uongo kwamba, Misa humpatia mtendaji neema kwa nguvu ya tendo lenyewe tu. Inabidi tuyakane makosa ya kwamba, Misa kama tendo lenyewe tu lililotumika kwa ajili ya watu wengine, hata wale wasiomcha Mungu na wasiotoa kikwazo, huwastahilishia ondoleo la dhambi, hatia, na adhabu. Mafundisho haya yote ni ya uongo na ya kukufuru yaliyobuniwa hapo awali na watawa wajinga. Yanauvuruga utukufu wa mateso ya Kristo na haki kwa imani.
64. Makosa haya yamezaa mengine mengi yasiyokadirika. Kwa mfano, kwa kiasi gani misa zilizotumika mara moja kwa ajili ya wengi, zitafaidi, na kwa kiasi gani misa iliyotumika kwa ajili ya mtu mmoja itafaidi? Wataalamu waghilibu1047 wana orodha za stahili sawa na wenye benki zinazopima dhahabu au fedha. Kisha, wanaziuza misa sawa na wanavyouza bidhaa zinazotarajiwa: kwa wafanyibiashara kwa ajili ya biashara bora, kwa wawindaji kwa ajili ya uwindaji bora, na mambo kama haya yasiyokadirika.1048 Mwishowe, zinatumiwa kwa ajili ya wafu na kuziweka nafsi huru kutoka katika adhabu ya Purgatorio kwa njia ya matumizi ya sakramenti, ingawa bila imani misa haina faida kwa walio hai. 65. Wapinzani wetu hawawezi kutoa silabi hata moja kutoka katika Maandiko Matakatifu ili waweze kuzitetea hadithi zao ambazo hufundishwa kanisani kwa mamlaka makuu bila msingi wowote wa Kanisa la Zamani wala Mababa wa Kanisa.
Maoni ya akina Baba wa Kanisa kuhusu Dhabihu
66. Tumekuwa tukielezea aya za Maandiko Matakatifu zinazonukuliwa dhidi yetu. Inatubidi kutoa jibu letu kuhusu Mababa wa Kanisa. Sisi hatujali
1044 Rum. 5: 1
1045 Kilatini: ‘De opere operato.’
1046 Tomaso wa Akuino Opuscula 58, ‘De venerabili sacramento altaris’ c. 1.
1047 Kilatini: ‘Sophistae.’
1048 Misa zilizotolewa kwa ajili ya shabaha maalumu; Kilatini: ‘Missa votiva.’
kwamba, Mababa wa Kanisa huiita misa kuwa dhabihu, lakini hawakumaanisha kwamba, misa kama tendo lenyewe tu inaweza kutoa neema iliyotumika kwa ajili ya wengine kuwastahilishia msamaha wa dhambi, hatia, na adhabu. Ni wapi basi, Mababa wa Kanisa wanazungumzia mambo haya ya kutisha? Wanaelezea wazi kwamba, wanazungumzia kuhusu shukrani. Kwa sababu hiyo, wanaiita ευχηαριστια.1049 67. Tumekwisha kusema hapo juu kwamba, dhabihu ya shukrani haistahilishi upatanisho, bali hutoka kwa wale waliopatanishwa, sawa na mateso yasiyopatanisha bali yanakuwa dhabihu shukrani1050 wakati waliopatanishwa wanayastahimili.
Jibu hili linalohusu, aghalabu, misemo ya Mababa wa kanisa ni kitu cha kututetea dhidi ya wapinzani wetu. Ni hakika kabisa kwamba, hadithi kuhusu ustahili wa matendo yenyewe tu yaliyotendeka haupatikani popote katika maandiko ya Mababa wa kanisa. Ili tuweze kulielewa suala zima dhahiri, tutazungumzia kuhusu matumizi ya sakramenti, mambo yale yanayokubaliana na Mababa wa kanisa pamoja na Maandiko Matakatifu.
Matumizi ya Sakramenti na Dhabihu
68. Baadhi ya watu wacheshi1051 wamebuni kwamba, Chakula cha Bwana kilianzishwa kwa sababu mbili: kwanza, kiwe alama na ushuhuda wa cheo, kama aina fulani ya mavazi ya watawa ilivyokuwa alama maalumu ya daraja la watawa. Pili, wao hufikiria kwamba, alama ya namna hiyo hasa humpendeza Kristo kama mlo mkuu ulio alama ya muungano thabiti na urafiki kati ya Wakristo kwasababu karamu ina ishara za mapatano na urafiki. Lakini hili ni wazo la dunia ambalo halionyeshi matumizi maaalumu ya mambo yaliyotolewa na Mungu. Linaelezea tu juu ya upendo, ulioeleweka kiasi na watu wa dunia na wa ulimwengu pia. Hakuna neno kuhusu imani. Naam, wako watu wachache tu wanaoielewa.
69. Sakramenti si ishara pekee kati ya watu, bali ni ishara za mapenzi ya Mungu kwetu. Hivyo, sakramenti zinafafanuliwa kwa usahihi katika Agano Jipya kuwa ishara za neema. Basi, sakramenti ina sehemu mbili: ishara yenyewe na neno. Katika Agano Jipya, neno ni ahadi ya neema. Ahadi ya Agano Jipya ni ahadi ya msamaha wa dhambi, jinsi maandiko yasemavyo kuwa: “Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu . . . ”; “Hii ndiyo damu yangu ya agano imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa msamaha wa dhambi.”1052 70. Basi, Neno
1049 Kiyunani: ‘Shukrani.’
1050 Melanchthon, ‘Sacrificia ευχαριστικα.’
1051 Kilatini: ‚Belli Homines;‘ Kijerumani: ‘Fürwitzige Gelehrten.‘ Melanchthon anapiga kijembe kuhusu utaalamu wa H. Zwingli na maoni ya wafuasi wake. Taz. ‘Ukiri wa Augsburg,‘ Mafungu ya 10, 13. 1052 Lk. 22: 19; Mt. 26: 28
linatoa msamaha wa dhambi. Kaida yenyewe ni taswira au muhuri wa neno, jinsi Paulo asemavyo1053 kwamba, inaonyesha ahadi. Jinsi ahadi haina maana imani isipokuwepo, inaamini kabisa kwamba, msamaha wa dhambi unatolewa hapo. Imani ya jinsi hiyo inazihimiza nafsi zenye majuto makubwa. Vile vile, neno limetolewa ili kuihimiza imani hii. Hivyo, sakramenti imeanzishwa ili sura inayoonekana mbele ya macho iguse mioyo ili iamini. Naam, Roho Mtakatifu hufanya kazi yake kwa haya. Yaani, kwa njia ya Neno na Sakramenti.
71. Ibada ya Agano Jipya ni matumizi haya ya sakramenti, ambapo imani inahuisha mioyo yenye hofu kuu. Agano Jipya lina misukumo ya kiroho, yaani, kufishwa na kuhuishwa. Kristo alianzisha sakramenti kwa matumizi haya kama anavyoamuru yafanywe kwa ukumbusho wake.”1054 Kumbuka, Kristo si mtazamo wa kizembe wa tamthiliya au mithili ya kusherehekea kumbukumbu za Herakle au Odiseo1055 katika michezo ya tanzia. Ni ukumbusho wa fadhili za Kristo na kuzipokea kwa imani, ili zituhuishe. Zaburi inasema: “Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; BWANA ni mwenye fadhili na rehema. Amewapa wamchao chakula . . . ”1056 Kaida hiyo inamaanisha kwamba, inatubidi kutambua mapenzi na huruma ya Mungu kwayo. 73. Imani inayotambua huruma huhuisha. Basi, haya ni matumizi makuu ya sakramenti ambapo inajulikana wazi wanaokubaliwa katika sakramenti yaani, dhamiri zenye hofu kuu na jinsi zinavyopaswa kuitumia.
74. Dhabihu inakuja kwa sababu ya haya, kwa maana tendo moja linaweza kuwa na shabaha nyingi. Dhamiri iliyohimizwa na imani ikitambua ni hofu gani iliyoiweka huru, itatoa shukrani kweli kwa ajili ya fadhili na mateso ya Kristo. Inatumia kaida yenyewe kama sifa ya Mungu ili kuonyesha shukrani ya utiifu na kushuhudia kwamba, karama za Mungu ni kubwa. Hivyo, kaida itakuwa dhabihu ya shukrani.
75. Mababa wengi huzungumzia pia athari za aina mbili: faraja ya dhamiri na shukrani au sifa. Athari ya kwanza inahusu asili ya sakramenti na ya pili inahusu dhabihu. Kuhusu faraja Ambrosio anasema: “Enendeni kwake ili mwondolewe dhambi, kwa maana yeye mwenyewe ni msamaha wa dhambi. Labda mnauliza: yeye yu nani? Sikilizeni anavyosema yeye mwenyewe: ‘Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu
1053 Rum. 4: 11
1054 1 Kor. 11: 24
1055 Herakle alikuwa shujaa katika visasili vya Kiyunani. Odysseo alikuwa shujaa katika tenzi za Homero (katika karne ya saba K.K.); alitangatanga baharini kwa jahazi yake baada ya maangamizi ya Troa miaka mingi kabla ya kufika nyumbani.
1056 Zab. 111: 4
kamwe.”1057 Hapa inashuhudiwa kwamba, msamaha wa dhambi unatolewa katika sakramenti, na kwamba, ni lazima kuupokea kwa imani. Mababa wa kanisa wana kauli nyingi za aina hii, lakini wapinzani wetu wanazigeuza kumaanisha tendo lenyewe tu lililotendeka na kutumika kwa ajili ya wengine. Kinyume chake, Mababa wa kanisa wanahitaji imani waziwazi na huzungumzia kuhusu faraja ya mtu binafsi, yaani, matumizi kwa ajili ya wengine.
76. Licha ya haya, kuna misemo kuhusu shukrani. Msemo wa Sipriano kuhusu washiriki wacha Mungu ni mzuri sana: “Uchaji wa kweli unatofautisha baina ya yale yaliyotolewa na yale yaliyosamehewa na kumshukuru mpaji karimu kwa ajili ya fadhili zake tele.”1058 Maana yake: uchaji wa kweli unatazama yale yaliyotolewa na yaliyosamehewa na kulinganisha ukubwa wa fadhili za Mungu pamoja na ukubwa wa ubaya wetu, yaani, dhambi zetu na kifo chetu na unatoa shukrani n.k. Kutokana na hayo, neno “Ekaristi”1059 lilitokea katika Kanisa. Kaida yenyewe siyo shukrani ambayo inaweza kutumiwa kwa ajili ya wengine kama tendo lenyewe tu ili kuwastahilishia msamaha wa dhambi n.k. ili nafsi za wafu ziwe huru. Maoni ya namna hiyo kwamba, kaida bila imani zinaweza kunufaisha ama mtendaji au wengine yanapingana na haki ya imani.
Majina ya Misa
78. Wapinzani wetu wanairejelea pia sarufi. Wanatumia majina ya misa, ambayo hayahitaji mjadala mrefu. Hata hivyo, misa inapoitwa dhabihu, haimaanishi kwamba, lazima itoe neema kama tendo lenyewe tu lililotendeka na kustahili msamaha wa dhambi likitumiwa kwa ajili ya wengine. 79. Wanasema kwamba, “liturgia”1060 inamaanisha “dhabihu” na Wayunani huiita Misa “liturgia.” Basi, mbona hawalitumii neno la zamani la “ushirika”1061 ambalo linaonyesha kwamba, zamani misa ilikuwa ushirika kwa wengi? Sasa, tuacheni tuzungumzie “liturgia.” Neno hili halimaanishi hasa dhabihu bali huduma ya jumuia. Hivyo, linaafikiana vizuri na maana yetu kuwa mchungaji mmoja anayebariki anawapa watu mwili na damu ya Bwana jinsi mchungaji mmoja afundishaye anawapa watu Injili, kama jinsi Paulo asemavyo: “Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.”1062 Maana yake: kwa njia za Neno na Sakramenti kulingana na 2 Kor. 5: 20: “Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, 1057 Yn. 6: 35; Ambrosio, Ufafanuzi wa Zab. 118
1058 Sipriano Bandia, yaani, Mtawa Mkuu Arnold von Bonneval (+ 1156) wa Daraja la Wabenedikto.
1059 Melanchthon, ‘Ευχαριστια.’
1060 Melanchthon, ‘Λειτουργια.’
1061 Kiyunani: ‘Συνακσις.’
1062 1 Kor. 4: 1
kana kwamba, Mungu anaishi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.”
81. Hivyo, neno “liturgia” linalingana vizuri na “huduma.” Neno hili la zamani lilitumika katika huduma za umma za serikali na kwa Wayunani lilimaanisha majukumu ya umma, sawa na kodi zilizokusanywa ili kulitunza kundi la manowari n.k., Kama jinsi hotuba ya Demostene kwa Lepitine ishuhudiavyo.1063 Yaliyomo kuhusu hotuba hii nzima ni majadiliano yanayohusu dhima na maondoleo ya jumuiya. Anasema kwamba, baadhi ya watu wasiostahili wameepuka wajibu wa umma kwa kinga iliyobuniwa. Vivyo hivyo, wakati wa Warumi walisema, jinsi agizo rasmi la Pertinakso lionyeshavyo katika sheria kuhusu kinga, 1. Semper: hata hivyo idadi ya watoto haiwezi kuwapa wazazi kinga kuhusu shughuli zote za umma.1064 Mfafanuzi1065 wa Demostene aliandika kuwa “liturgia” ni aina moja ya kodi, gharama ya michezo ya hadhara, kujenga manowari, utunzaji wa jumba la mazoezi, sawa na majukumu mengine ya jumuiya. Paulo analitumia neno hili katika 2 Kor. 9: 12 kumaanisha matoleo. 82. Huduma hii ya kuchanga msaada haitoshelezi tu mahitaji ya watakatifu, bali pia inawafanya watu wengi zaidi wamshukuru Mungu. Katika Flp. 2: 25, alimwita Epafrodito kuwa “mhudumu wa mahitaji yangu”1066 ambayo, kwa hakika, haimaanishi kasisi mtoa dhabihu. 83. Shuhuda zaidi hazihitajiki hapa kwa kuwa kila asomaye kuhusu waandishi wa Kiyunani anaweza kupata mifano dhahiri ya matumizi ya neno “liturgia” popote yenye maana za wajibu wa jumuiya au huduma fulani. Kwa sababu ya irabu unganifu ??, wanaisimu hawafikii hitimisho kwamba, asili yake ni λιτε, yenye maana ya sala, bali inatokana na neno λειτα, lenye maana ya mali za jumuiya.1067 Kwa sababu hiyo basi, kitenzi λειτουργεω kinamaanisha: ninakimu, ninatunza mali ya jumuiya.
84. Ni jambo la dhihaka kabisa kusisitiza kwamba, kwa maana Maandiko Mtakatifu yanataja madhabahu, misa lazima iwe dhabihu. Hata hivyo, Paulo anatumia umbo la madhabahu kwa ajili ya kutoa mfano. 85 Wanadhani pia kwamba, neno misa limetoholea kutoka kwa neno mizbeach, neno la Kiebrania litajalo madhabahu. Je, walikuwa na sababu nyingine ya kuitafuta etimologia1068 isipokuwa kuonyesha ufahamu wa Kiebrania? Je, walikuwa na sababu yoyote ya kwenda nje ya etimologia wakati neno hili linapatikana katika Kum. 16:10, 1063 1, 457,7.
1064 Kilatini: ‘Rescriptum.’ Kaisari Pertinax (+193 B.K.) alimpa kinga mtu mwenye watoto 16.
1065 Jina lake peke yake linajulikana, yaani, Ulpiano.
1066 Kiyunani: ‘Λeitourgos.’
1067 Asili ya neno hili ni λειτος, yaani, “kuhusu umma au taifa.”
1068 Elimu ya asili na historia ya maana ya maneno.
ambapo linamaanisha matoleo au zawadi za umma na siyo dhabihu ya kuhani? Iliwabidi watu binafsi waliofika katika sikukuu ya Pasaka kupeleka zawadi fulani kama mchango wa ishara. Wakristo walihifadhi desturi hii mwanzoni. 86. Jinsi Kanuni za Mitume1069 zionyeshavyo, Wakristo walipokutana walileta mkate, mvinyo, na vitu vingine. Kisha, sehemu yake ilichukuliwa na kubarikiwa, na sehemu iliyobakia iligawanywa kwa maskini. Kulingana na desturi hii, waliliweka neno “misa” kumaanisha matoleo. Inaonekana kwamba, kwa sababu ya matoleo ya namna hiyo, mahali fulani misa iliitwa “Chakula cha Upendo,”1070 isipokuwa jina hili litazamiwe kutumika kwa ajili ya karamu ya pamoja. Lakini wacha sasa tupitie mambo haya hafifu! 87. Ni jambo la dhihaka kabisa kuwa wapinzani kuibua mizozo kama hii kuhusu suala hili kubwa sana. Kwa kuwa ingawa Misa inaitwa dhabihu, kwa njia gani basi, neno lenyewe linaweza kuafikiana na upuuzi huo wa “ex opere operato”1071 na kutumika ili kuwastahilishia watu wengine msamaha wa dhambi, kama jinsi wanavyootea? Kwa kweli, misa inaweza kuitwa sadaka, kama inavyoitwa Ekaristi, hasa kwa sababu maombezi, shukrani na ibada nzima inayoitwa shukrani1072 hutolewa huko. Lakini mapokeo wala maombezi kama matendo yenyewe tu hayawezi kunufaisha bila imani. Lakini hapa hatujadiliani kuhusu maombi, bali hasa kuhusu Chakula cha Bwana.
88. Kanuni ya Kiyunani kuhusu ibada pia inazungumzia sana kuhusu dhabihu, lakini inaonyesha wazi kwamba, haizungumzii kuhusu mwili na damu ya Bwana, bali kuhusu ibada nzima, maombezi na shukrani. Inasema ifuatavyo:
1073 Tukiyaelewa haya kwa njia iliyo sahihi, hatutakuwa na jambo lolote linaloweza kuiudhi akili. Basi, tunaombwa kustahili kumtolea dhabihu za sala, maombi ya bidii na dhabihu zisizokuwa na damu kwa ajili ya watu wote. Kanuni hii inataja maombi kuwa dhabihu zizisokuwa na damu. Baadaye kidogo inasema: “Tunakutolea ibada hii ya maana na isiyo na damu.” Ni kazi isiyokuwa na weledi kuielezea “dhabihu yenye maana” kwa njia ya kuihusisha na mwili wenyewe wa Kristo wakati ambapo kanuni inazungumzia ibada nzima. “Ibada yenye maana,”1074 kwa maneno ya
1069 Kilatini: ‘Consitutiones Apostolorum,’ sehemu ‘Canones Apostolorun 2-5.’ ‘Consitutiones Apostolorum’ (Katiba za Mitume), mkusanyiko wa sheria za Kanisa wenye vitabu vinane kutoka Shamu mwishoni mwa karne ya 3.
1070 ‘Αγαπη.’
1071 Yaani, kwa nguvu ya tendo lenyewe tu bila imani.
1072 ‘Ευχαριστια.’
1073 Dondoo kutoka mwanzo wa ibada ya waumini katika liturgia ya Yohana Krisostomo (mnamo 347-407). Krisostomo alianzisha matengenezo ya liturgia ya Kanisa la Mashariki. Kazi hii iliongezewa baadaye hata ikawa liturgia ya Kanisa la Mashariki zima, yaani, Konstantinopoli, Uyunani, Urusi n.k.
1074 ‘Λογικη λατρεια.’
Paulo,1075 ni ibada ya nafsi, hofu, imani, maombezi, shukrani n.k. na inasimama dhidi ya “opus operatum,” yaani, tendo lenyewe peke yake.
Misa kwa Ajili ya Wafu
89. Wapinzani wetu wanaendelea kuyatetea matumizi ya misa ili kuzifanya huru nafsi za wafu. Kwa njia hii, wanaendelea kukusanya faida zisizikuwa na mwisho lakini bila ushuhuda wowote na agizo lolote kutoka katika Maandiko Matakatifu. Ni kosa kuzianzisha ibada kama hizi kanisani bila amri ya Mungu, bila mfano wa Maandiko Matakatifu, na katika matumizi kutia, , Chakula cha Bwana ambacho kimeanzishwa kwa ajili ya ukumbusho na mahubiri kati ya walio hai, kwa ajili ya wafu. Haya ni matumizi mabaya ya jina la Mungu dhidi ya Amri ya Pili.
Kwanza kabisa, kuitukana Injili ni kuamini kwamba, kaida ya dini kama tendo lenyewe tu bila imani ni dhabihu ya kutupatanisha na Mungu na kutoa ridhaa kwa ajili ya dhambi. Ni mahubiri ya kukufuru kabisa kulihesabu tendo la padre kuwa na thamani sawasawa na kifo cha Kristo. Pili, dhambi na kifo haviwezi kushindwa isipokuwa kwa imani katika Kristo, jinsi Paulo afundishavyo: “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu.”1076 Kwa sababu hiyo basi, adhabu ya Purgatorio haiwezi kushindwa kwa matumizi ya matendo ya mtu mwingine.
90. Tayari tumeacha aina za ushahidi wa wapinzani wetu kuhusu Purgatorio, maoni yao kuhusu adhabu zinazotakiwa kuwa Purgatorio, sababu waletazo katika mafundisho ya ridhaa, na ambayo tulikwisha kuonyesha awali kuwa lisilo na ukweli. Tunalisema tu jambo hili: Ni kweli kabisa kwamba, Chakula cha Bwana kimeanzishwa kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Kwa kuwa, kinatoa msamaha wa dhambi, ni lazima kuelewa kama hatia halisi. Hata hivyo, misa haitoi ridhaa kwa ajili ya hatia; isije ikawa sawa na kifo cha Kristo. Msamaha wa hatia unaweza kupokelewa kwa imani peke yake. Hivyo, misa siyo ridhaa bali ahadi na sakramenti inayohitaji imani.
91. Kwa hakika watu wote wacha Mungu watashikwa na uchungu mkali mno, wakitafakari kwamba, sehemu kuu ya misa imehamishwa kwa wafu kwa ajili ya kuwa ridhaa ya adhabu. Kufanya hivyo kunamaanisha kuiondoa dhabihu ya kila siku kanisani. Kufanya hivyo kunamaanisha udhalimu wa Antioko1077
1075 Rum. 12: 1
1076 Rum. 5: 1
1077 Antioko IV Epifane (+ 163 K.K.), mfalme wa Shamu tangu mwaka wa 175 K.K. Alijaribu kuziunganisha sehemu tofauti za ufalme wake kwa njia ya kuzitoza utamaduni wa Kiyunani. Utamaduni huu uliathiriwa kutoka
unaobadilisha ahadi mabruki1078 mno za msamaha wa hatia na imani na mawazo matupu kuhusu matendo ya upatanisho. Kufanya hivyo ni kuichafua Injili na kuyapotosha matumizi ya sakramenti. Wanaofanya hivyo ni wale ambao Paulo anawaita wanaojipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.1079 Wameyakandamiza mafundisho ya imani na wameugeuza msamaha wa hatia, mwili na damu ya Bwana kwa kisingizio cha matendo ya upatanisho kuwa biashara yao ya kukufuru. Siku moja watalipia adhabu ya ukafiri huu. Kwa sababu hiyo, dhamiri zetu na za wacha Mungu wote ni sharti zisiyakubali matumizi mabaya ya wapinzani wetu.
92. Lakini, acheni tulirudie suala lenyewe. Kwa kuwa misa, kama tendo lenyewe tu na, bila imani siyo upatanisho au ridhaa kwa ajili ya adhabu au hatia, hivyo, matumizi yake kwa ajili ya wafu hayana maana. Hakuna sababu hapa ya kuendelea na mjadala mrefu. Inajulikana wazi kwamba, matumizi haya ya misa kwa ajili ya wafu hayana ushuhuda wowote kutoka katika Maandiko Matakatifu. Licha ya hayo, ni hatari sana kuanzisha ibada kanisani bila mamlaka ya Maandiko Matakatifu. Basi, ikihitajika baadaye, tutajadili kwa kina zaidi kuhusu suala zima. Kuna sababu yoyote kubishana na wapinzani wetu ambao hawaelewi maana ya dhabihu, sakramenti, msamaha wa dhambi wala imani?
93. Kanuni ya ibada ya Kiyunani haitumii dhabihu kama ridhaa kwa ajili ya wafu kwa sababu inaitumia kuungana na Mababa Wakuu, manabii na mitume. Jambo hili linaonyesha kwamba, Wayunani huitoa kama dhabihu ya shukrani na siyo kama matumizi ya upatanisho kwa ajili ya adhabu. Hata hivyo, hawazungumzii kuhusu dhabihu ya mwili na damu ya Bwana peke yake, bali hata sehemu nyingine za ibada hasa maombi na shukrani. Kwa maana, baada ya kuvibariki vyombo vya sakramenti, wao huomba washiriki wanufaike, na hawazungumzii kuhusu wengine. Kisha, wao huongezea: “Tunakutolea ibada hii yenye maana kwa ajili ya wafu katika imani, wahenga, akina baba, Mababa Wakuu, manabii, mitume n.k.”1080 “Ibada yenye maana” haimaanishi tu mkate wenyewe, bali maombi na mambo yote yanayohusu ibada. 94.Wapinzani wetu wanapoirejea misemo ya Mababa wa Kanisa kuhusu dhabihu kwa ajili ya wafu, sisi tunajua vizuri kwamba, wahenga wa zamani walizungumzia sala kwa ajili Mashariki, hasa kutoka Shamu, Uajameni, Uhindi na Misri wakati wa Mfalme wa Makedonia, Aleksandro Mkuu (+ 323 K.K.). Utamaduni huu ulidai ibada ya miungu wengi. Kwa hiyo, Antioko alijaribu kubadilisha ibada katika hekalu la Yerusalemu kulingana na mitindo ya kipagani. Alilishambulia hekalu miaka ya 169 na 167 K.K. na alichafua maeneo yake kwa ibada na dhabihu za Kipagani. Imani na kaida za Wayahudi zilikataliwa kwa tisho la hukumu ya kifo. Mwishowe, Wayahudi walihalifu na kumshinda Antioko aliyehamia pande za Uajameni ambapo alifia. Unabii na historia hii inasimuliwa katika vitabu viwili vya Wamakabayo.
1078 Yaani, hukota afya.
1079 1 Kor. 11: 27
1080
ya wafu. Kwa upande wetu, hatulikatai hili, lakini tunakataa kabisa matumizi ya Chakula cha Bwana kama tendo lenyewe tu kwa ajili ya wafu. Watu wa kale hawatetei mafundisho ya wapinzani wetu kuhusu nguvu ya tendo lenyewe tu. Hata kama, wanaungwa mkono na Gregorio na wanatheologia wa hivi karibuni, tunawapinga kwa Maandiko Matakatifu yaliyo wazi kabisa. Hata hivyo, maoni ya Mababa wa Kanisa yanahitilafiana sana. 95 Naam, walikuwa wanadamu tu na waliweza kuanguka na kukosea. Iwapo wangehuishwa sasa na kuona jinsi misemo yao inavyogeuzwa ili kutetea uongo ulio wazi ambao wapinzani wetu huufundisha kuhusu matendo yenyewe tu yaliyotendeka, wangefafanua wenyewe tofauti kabisa.
96. Wapinzani wetu wananukuu pia kwa uongo lawama ya Aerio1081 dhidi yetu, ambaye anasema kwamba, tunalaaniwa kwa sababu ya kukataa dhabihu za Misa kwa ajili ya wale wanaoishi na wafu. Mara nyingi, wanayatumia mandhari haya, yaani, uzushi wa kale na kuulinganisha kwa uongo na msimamo wetu ili wapate kuitatiza hali yetu kwa upambanuzi huu. Epifanio anashuhudia kwamba, Aerio aliamini kuwa maombezi kwa ajili ya wafu hayakuwa na maana1082 na tunamlaumu kwa sababu hii. Sisi hatumtetei Aerio. Tunawapinga ninyi kwa sababu ya utetezi wenu mbaya wa uzushi, unaopingana wazi na manabii, mitume, na Mababa watakatifu. Yaani, misa kama tendo lenyewe tu1083 inatuhesabia haki, inatustahilishia msamaha wa hatia na adhabu na hata kwa waovu ambao kwao inatumika, kama wasipopinga. Tunakataa kabisa makosa haya mapotovu ambayo huuudhi utukufu wa mateso ya Kristo na kuharibu kabisa mafundisho ya haki ya imani.
97. Imani ya wasiomcha Mungu wakati wa Torati ilikuwa hiyo hiyo. Yaani, wanastahili msamaha wa dhambi kwa njia ya dhabihu kama matendo yenyewe tu na siyo kuupokea bure kwa imani. Kwa sababu hiyo, waliongezea idadi ya ibada na dhabihu, walianzisha ibada ya Baali katika Israeli na hata huko Yuda walitambika kwenye vimisitu. Kwa sababu hiyo, manabii waliilaani imani hii, na kuwapinga, siyo tu walioabudu Baali, bali pia makuhani waliotekeleza dhabihu zilizoamriwa na Mungu huku wakiwa na imani hii ya kukufuru.1084 Lakini imani hii hushikamana na ulimwengu na itaendelea kushikamana kuwa ibada na dhabihu ni matendo ya upatanisho. Watu wa kimwili hawastahimili wakati dhabihu ya Kristo peke yake ikipewa utukufu wa kuwa upatanisho kwa
1081 Aerio alikuwa mchungaji aliyeishi katika karne ya nne katika mji wa Sebaste katika pwani ya Bahari Nyeusi. Alikataa sheria ya Kanisa ya kufunga na maombi kwa ajili ya wafu.
1082 Pan. haer. 75, 2. 3. 7.
1083 Kilatini: ‘Ex opere operato.’
1084 Yer. 2: 8, 26; 17: 1
282
sababu hawaelewi haki ya imani bali huhesabu heshima hiyo hiyo kwa ibada na dhabihu zingine zote. 98. Hali kadhalika, imani ya uongo kuhusu dhabihu ilishikamana huko Yuda na makuhani wapotovu. Hali kadhalika, katika Israeli, walistahimili ibada za Baali, ambapo Kanisa la Mungu lililokuwepo, lilikataa ibada potovu. Hivyo, ibada ya Baali inashikamana na utawala wa Papa, yaani, matumizi mabaya ya misa ili kustahilisha msamaha wa hatia na adhabu kwa wapotovu. Basi, inaonekana kwamba, ibada hii ya Baali itadumu pamoja na utawala wa Papa mpaka Kristo aje katika hukumu na kuuangamiza utawala wa Mpinga Kristo kwa utukufu wa kuja kwake. Kwa sasa, wanaoiamini kweli Injili hawana budi kutokubali ibada hizi potovu zilizobuniwa dhidi ya agizo la Mungu na kuuficha utukufu wa Kristo na haki ya imani.
99. Tumeyasema haya kwa ufupi kuhusu misa ili watu wote wema kati ya mataifa yote wapate kuelewa jinsi tuitunzavyo kwa jitihada kuu heshima ya Misa, kwa njia ya kuonyesha matumizi yake halisi. Tuna sababu za haki mno kutokubaliana na wapinzani wetu. Tunataka pia kuwaonya watu wote wema ili wasiwasaidie wapinzani wetu wanapotetea kufuru ya Misa wasije wakajifunga wenyewe pamoja kwa dhambi za watu wengine. Daawa1085 hii ndiyo kubwa, jambo hili ndilo kubwa hata kushinda kazi duni ikilinganishwa na ya nabii Eliya alipoipinga ibada ya Baali. Sisi tumeiwasilisha daawa hii iliyo nzito zaidi kwa staha mno na kujibu bila kutoa lawama yoyote. Lakini kama wapinzani wetu wakitulazimisha kuyahesabu matumizi yote mabaya ya misa, haitawezekana kulichukulia jambo hilo kwa upole huo huo.
Fungu la Ishirini na Saba: Nadhiri za Watawa
1. Miaka thelathini iliyopita katika mji wa Eisenach huko mkoani Thüringen, mtawa mmoja Mfransiskano aliyeitwa Yohana Hilten aliishi miongoni mwetu. Daraja lake mwenyewe lilimuweka gerezani kwa sababu aliyakemea baadhi ya matumizi mabaya yaliyojulikana wazi. Tumeyaona maandiko yake, na kutokana na haya, asili ya mafundisho yake inaweza kueleweka sawa sawa.1086 Waliomfahamu wanashuhudia kwamba, alikuwa mzee mpole, makini lakini si mwepesi. Aliyatabiri mambo mengi. 2. Baadhi yao yamekwisha tayari kutokea, na mengine yanaonekana kukaribia. Hatupendi kuyarudia hapa isije wengine wakachukulia kwamba, tunayasimulia kwa ajili ya chuki au kwa upendeleo wa mtu yeyote. Mwishoni, alipokuwa mgonjwa labda kwa sababu ya umri wake au hali duni ya gereza, alimwita mwangalizi wake ili amwelezee kuhusu ugonjwa
1085 Sababu, kesi, daawa.
1086 Melanchthon alisoma ufasiri wa Yohana Hilten kuhusu ‘Kitabu cha Danieli.’
wake. Lakini mwangalizi alipoingia gerezani alianza kwa chuki ya Kifarisayo kumshtaki mtu kwa ajili ya mafundisho yake yaliyoonekana kuudhuru hata uchumi wao.1087 Kisha Hilten aliacha kusema chochote kuhusu afya yake na akasema kwamba, alikuwa anayavumilia mateso hayo kwa upole kwa ajili ya Kristo kwa sababu hakulifundisha au kuliandika lolote ambalo liliitishia hali ya watawa. Alikuwa amepinga tu matumizi fulani mabaya yaliyojulikana wazi.
3. Alisema tu: “Bali mwingine atakuja katika mwaka wa Bwana wetu 1516 atakayewaangamiza ninyi na hamtaweza kumzuia.” Baadaye, marafiki zake waliipata sentensi hii kuhusu maangamizi ya utawala wa watawa na idadi kamili ya miaka aliyokuwa ameandika katika fafanuzi/fasiri zake zipatikanazo mahali maalumu katika Kitabu cha Danieli.
4. Hata hivyo, matokeo ya wakati ujao yataonyesha, ni kwa kiasi gani, sauti yake hii itaaminiwa. Kuna dalili zingine zenye uhakika sawa na maneno ya utabiri yaliyotishia mabadiliko katika utawala wa watawa. Basi, kiasi cha unafiki wa tamaa ya makuu, uchoyo, kiasi cha ujinga na ukatili walionao watu hawa wasiokuwa na elimu, upuuzi katika mahubiri, na kutafakari daima njia mpya za kutafuta fedha, vinajulikana. Pia kuna maovu mengine ambayo hatupendi kuyazungumzia. 5. Zamani, nyumba za watawa zilikuwa shule za mafundisho ya Kikristo. Lakini zimeharibika kutoka hali ya dhahabu mpaka hali ya chuma, au kutoka mchemraba tele wa Platoni mpaka sauti zisizolingana kabisa, ambazo Platoni alisema zinasababisha maangamizi.1088 Baadhi ya nyumba za watawa zilizojaa utajiri hulisha tu kikundi cha wazembe ambacho, kwa kisingizio kibaya cha dini, wanatafuta anasa tu kwa sadaka za jumuia za Kanisa. 6. Lakini Kristo anaonya kwamba, chumvi iliyopoteza ladha yake haifai: “Ila kutupwa nje na kukanyagwa.”1089 Hivyo, kwa mitindo hii watawa wenyewe huimba nyimbo zao za mauti1090. 7. Ishara nyingine inaongezeka kwamba, wakati fulani watawa ni wauaji wa watu wema. Bila shaka, hivi karibuni, Mungu atalipiza kisasi kwa ajili ya mauaji haya. 8 Hatuwashtaki watu wote. Naam, tunafikiri kwamba, baadhi ya watu wema wanapatikana hapa na pale katika nyumba za watawa ambao wana maoni ya wastani kuhusu ibada na matendo ya kibinadamu, kama jinsi baadhi ya waandishi wanavyotaja. Hawakubali kabisa ukatili ambao wanafiki miongoni mwao huuonyesha.
1087 Andiko la Kijerumani: ‘Dass solche Predigt nicht wollt in der Küche nütz sein.‘ Yaani, “Mahubiri ya namna hiyo hayatafaidi jikoni.”
1088 Platoni, Timaio 98 C. Mchemraba wa Platoni uliomaanisha muundo wa kifalsafa ambamo vyema vyote vinaunganika pamoja vizuri.
1089 Mt. 5: 13
1090 Andiko la Kijerumani: ‘Ihr eigen requiem.’
9. Hapa, tunazungumzia aina ya mafundisho ambayo waasisi wa Hoja wanaitetea sana sasa, na sio suala kuwa nadhiri lazima ziwekwe au la. Maoni yetu ni kwamba, nadhiri za halali ziwekwe, lakini tunajadiliana mambo mengine yanayofuatia: Je, ibada za namna hiyo zinastahilisha msamaha wa dhambi au kuhesabiwa haki? Je, nadhiri ni matendo ya upatanisho kwa ajili ya dhambi? Je, ni sawa na Ubatizo? Je, ni ushikaji wa amri na mashauri? Je, ni ukamilifu wa Kiinjili? Je, zina stahili zaidi ya kiwango? Je, stahili hizi zinaweza kuokoa wengine zinapohamishiwa kwao? Je, ni halali kutoa nadhiri hizi kwa mwenye maoni ya namna hiyo? Je, ni halali kutoa nadhiri kwa kisingizio cha dini, ilihali zimetolewa kwa ajili ya tumbo na uzembe tu? Je, nadhiri zinazogandamizwa na watu wakaidi ni za kweli, au wale wasioweza kuhukumu vizuri aina ya maisha haya kwa sababu ya umri wao, watu waliotupwa katika nyumba za watawa na wazazi au marafiki ili walishwe kwa kibali cha jumuiya bila wao kupoteza urithi wa binafsi? Je, nadhiri ni halali ikiwa zinawasukuma hadharani watu kwenye mwisho mbaya ama kwa sababu udhaifu unazuia utendaji wao au kwa sababu washiriki wa madaraja haya wanalazimishwa kukubali matumizi mabaya ya Misa, ibada za kukufuru za watakatifu na kukubali na kusaidia hila za ukatili dhidi ya watu wema? Basi, tunajadiliana kuhusu maswali haya! 10. Katika Ukiri, tumezungumzia mengi kuhusu nadhiri hizi ambazo hata kanuni za Papa zinazikataa, ilihali wapinzani wetu bado wanapuuza kila kitu tulichokionyesha. Haya ndiyo maneno waliyoyatumia hasa.
Ni vyema kusikia jinsi wanavyozikosoa hoja zetu bila msingi na jinsi wanavyojaribu kuiunga mkono kesi yao. Kwa kusudi hili, tutapitia hoja zetu kwa ufupi na kufutilia mbali mara moja visingizio vya wapinzani wetu. Kwa kuwa, kesi hii nzima imefanywa kwa bidii na ni tele katika kitabu cha Luther kiitwacho ‘Nadhiri za Watawa,’1091 tunataka kurejea tena kitabu hiki hapa.
11. Kwanza, ni kweli kabisa kwamba, nadhiri ya namna hiyo ambayo kwayo, mtu anayeitoa atadhania kuwa sasa anastahili msamaha wa dhambi mbele za Mungu au kufanya ridhaa kwa ajili ya dhambi mbele za Mungu, haitakiwi. Ni wazi kuwa jambo hili linaishusha heshima ya Injili ifundishayo kwamba, msamaha wa dhambi unatolewa kwetu bure kwa ajili ya Kristo, jinsi ilivyosemwa kwa wingi hapo juu. Hivyo, tulizinukuu aya za Paulo kwa Wagalatia: “Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.”1092 Wale wanaotafuta msamaha wa dhambi bila imani katika Kristo, bali kwa njia ya matendo ya watawa, wanampokonya Kristo heshima
1091 ‘De votis monasticis iudicium’ mwaka wa 1521. 1092 Gal. 5: 4
yake na kumsulubisha tena. Walakini, sikilizeni basi, jinsi mafundi hawa wa Hoja wanavyodai hapa. 12. Wanaelezea kwamba, aya ya Paulo inahusu Sheria ya Musa peke yake. Wanaongezea pia kwamba, watawa hutenda usikivu huu wote kwa ajili ya Kristo na kujaribu sana kuishi kadiri ya Injili ili waustahili uzima wa milele. Kisha wanaongezea hitimisho la kuogofya sana kwa maneno haya: “Kwa hiyo, haya yote yaliyowekwa kupambana na utawa ni mambo ya kukufuru.”
13. Ewe Kristo! Mpaka lini utaendelea kuwavumilia maadui zetu wanaovunja hii heshima ya Injili yako? Tulisema katika Ukiri kwamba, msamaha wa dhambi unatolewa bure kwa njia ya imani na kwa ajili ya Kristo. Kama hii siyo sauti ya Injili yenyewe, na kama silo Neno la Baba wa milele uliloufunulia ulimwengu, wewe unaekaa kifuani mwa Baba - basi ni hakika tunashutumiwa kweli. Lakini kifo chako ni ushuhuda, ufufuo wako ni ushuhuda, Roho Mtakatifu ni ushuhuda, na Kanisa lako zima ni ushuhuda kwamba, hili ndilo fundisho la kweli la Injili. Yaani, tunaupokea msamaha wa dhambi, siyo kwa ajili ya stahili zetu, bali kwa ajili yako, kwa imani.
14. Kwa kuwa, Paulo anakataa kwamba, kwa sheria ya Musa, watu hawastahili msamaha wa dhambi, anaipunguza zaidi sifa hii ya mapokeo ya wanadamu, kama ashuhudiavyo wazi katika Kol. 2:16. Iwapo sheria ya Musa ambayo Mungu mwenyewe aliifunua, haikustahilisha msamaha wa dhambi, itawezekanaje namna za maadhimisho haya ya kijinga1093 zinazohitilafiana na desturi za jamii zistahilishe msamaha wa dhambi?
15. Wapinzani wetu hudhania kwamba, Paulo aliitangua Sheria ya Musa na kwamba, Kristo alichukua mahali pake. Hivyo, Kristo hatoi msamaha wa dhambi bure bali kwa ajili ya matendo mengine ya sheria ambayo sasa labda yamebuniwa. 16. Kwa kupitia dhana hizi zilizokithiri na kukufuru, wanaipindua fadhili ya Kristo. Kisha, kati yao wenyewe wanadhania kwamba, watendao sheria ile ya Kristo, watawa wanaenda mbele zaidi kuliko wengine kwa sababu ya umaskini, utakatifu na utiifu wao wa unafiki kwa maana haya yote yamejaa uigaji. Wanajivunia umaskini katika wingi wa mali. Wanajivunia utiifu ingawa hakuna kundi lolote la watu lenye uhuru mkubwa kuliko watawa. Kuhusu useja, afadhali tusizungumze. Gerson anaweza kuonyesha hali ya usafi huo ulivyo hasa kwa waliojaribu kuzuia tamaa. Basi, ni wangapi kati yao wanaojaribu kufanya hivyo?
17. Hivyo, watawa huishi kwa uigaji huo katika Injili! Kristo hakuchukua nafasi ya Musa ili kutusamehea dhambi kwa ajili ya matendo yetu, bali aliziweka
1093 Andiko la Kijerumani: Utawa, rosari n.k.
stahili zake na upatanisho wake dhidi ya ghadhabu ya Mungu ili tusamehewe bure. Basi, yeyote awekaye upatanisho wa Kristo kwa njia ya kutojali ustahili wake dhidi ya ghadhabu ya Mungu, na kujaribu kuupata msamaha wa dhambi kwa ajili ya ustahili wake mwenyewe ama kwa njia ya kutenda matendo ya Sheria ya Musa au ya Amri Kumi au ya Katiba ya Benedikto1094 au Agostino au katiba nyinginezo - ametangua ahadi ya Kristo, amemtupilia mbali Kristo na amepotea kutoka kwenye neema. Haya ndiyo maamuzi ya Paulo.
18. Sasa, Kaisari Karolo mwenye huruma nyingi mno tazama, watawala tazameni, vyeo vyote vya heshima tazameni ufidhuli huu wa wapinzani wetu! Japo tuliinukuu aya ya Paulo katika kulihakikisha hili, wameandika wenyewe: “Haya yote yaliyowekwa kupambana na utawa ni mambo ya kukufuru.” 19. Lakini ni lipi lenye uhakika zaidi ya haya kuwa watu huupokea msamaha wa dhambi kwa imani kwa ajili ya Kristo? Walaghai hawa wana ujasiri kuliita neno hili kuwa la kukufuru. Hatuna mashaka kwamba, iwapo tayari ungekuwa umeambiwa kuhusu fungu hili, ungeona kwamba jambo hili la kukufuru zaidi liondolewe kutoka katika Hoja.
20. Kwa kuwa tumeonyesha kwa kina hapo juu sana kuwa, wazo hili ni la kukufuru sana kwamba tunaupokea msamaha wa dhambi kwa ajili ya matendo yetu, tutalijadili hapa kwa kifupi. Kutokana na hayo, msomaji hodari ataweza kupambanua kwa urahisi kwamba, hatustahili msamaha wa dhambi kwa matendo ya utawa. Kwa sababu hiyo, kufuru hii haiwezi kuvumilika ambayo tunasoma katika Tomaso kwamba, nadhiri ya watawa ni sawa na Ubatizo. Ni upuuzi kabisa kuweka mapokeo ya wanadamu yasiyokuwa na amri wala ahadi ya Mungu kuwa sawa na agizo la Kristo lenye amri na ahadi ya Mungu na lenye agano la neema na uzima wa milele.
21. Pili, utiifu, umaskini na useja visipokuwa vichafu, ni mazoezi ya mambo ambayo si lazima kuyajali.1095 Kwa sababu hiyo, watakatifu wanaweza kuvitumia bila dhambi, sawa na Bernardo, Fransisko na watu wengine watakatifu. Walivitumia kwa faida ya mwili ili wapate nafasi za kutosha kufundisha pamoja na huduma zingine takatifu, siyo kwamba, hayo matendo yenyewe tu yawe ibada ya kuhesabia haki au ya kustahilisha uzima wa milele. Hatimaye, haya yote yanakuwa aina ambayo Paulo anaizungumzia: “Kujitokeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo.”1096 22. Inawezekana kwamba, hapa na pale katika 1094 Benedikto wa Nursia; katiba yake ilikuwa mfano wa kanuni zote za utawa huko Magharibi mwa Ulaya, ‘Sancti Benedicti regula monachorum’ mwanzoni mwa karne ya sita huko Italia. Katiba ya watawa wa daraja la Kiagostino kutoka kwa Agostino mwenyewe iliaminiwa mwishoni mwa Enzi ya Kati. 1095 Melanchthon, ‘Αδιαφορα.’ 1096 1 Tim. 4: 8
nyumba za watawa bado kuna watu wema wanaohudumia neno na wanaofuata matendo ya maadhimisho haya bila mawazo maovu. 23. Lakini dhana kwamba, maadhimisho haya ni ibada ambayo kwayo, tunahesabiwa haki mbele za Mungu na tunastahili uzima wa milele hupingana na Injili ya haki ya imani ifundishayo kwamba, tunapewa haki na uzima wa milele kwa ajili ya Kristo. Wazo hili linaupinga pia msemo wa Kristo usemao: “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”1097 Linapinga pia kauli hii: “Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.”1098 Kwa hiyo basi, ni vipi wanaweza kuimarika bila ushuhuda wowote wa Neno la Mungu kwamba, ni ibada zinazokubaliwa na Mungu kuwa haki mbele zake?
24. Lakini uangalieni ufidhuli wa wapinzani wetu! Hawafundishi tu kwamba, maadhimisho haya ni ibada zinazomhesabia mtu haki bali wanaongezea pia kwamba, ibada za namna hiyo ni timilifu zaidi kuustahilisha msamaha wa dhambi na haki kuliko hali zingine za maisha. Maoni mengi ya uongo na mapotovu yanaingia hapa. Wanawaza kwamba, wanashika amri na mashauri.1099 Kisha, watu hawa karimu sana wanaoota ndoto kuwa na stahili zaidi ya kiwango huwauzia wengine stahili hizo. Mambo haya yote yamejaa ubatili mtupu wa Kifarisayo. 25. Ni kufuru kubwa mno kuamini kwamba, wanatimiza Amri Kumi kiasi cha kubakia na stahili, wakati amri hizi huwashtaki watakatifu wote: “Mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho zako zote, na kwa nguvu yako yote,” na tena: “Usiitamani.” Nabii anasema: “Wanadamu wote ni waongo.”1100 Maana yake: hawafikirii vilivyo kuhusu Mungu wala hawamwogopi na hawamwamini Mungu vya kutosha. Kwa sababu hiyo, watawa hujigamba kwa uongo kwamba, wanaishika amri kwa kuyazingatia maisha ya kitawa na hata kuliko amri.
26. Kisha, ni uongo kabisa kudai kwamba, matendo ya uzingatifu wa kitawa ni matendo ya mashauri ya kiinjili kwa maana Injili haifundishi matumizi ya nguo na vyakula tofauti wala kuacha mali binafsi. Haya ni mapokeo ya wanadamu ambayo zaidi ya yote yamesemwa kwayo: “Lakini chakula hakituhudhuru mbele za Mungu.”1101 Kwa sababu hiyo mambo haya siyo ibada zinazohesabia haki wala ukamilifu. Kinyume chake: yanapopendekezwa chini ya mada hizi, ni
1097 Mt. 15: 9
1098 Rum. 14: 23
1099 Wanatheologia wa Enzi ya Kati walitofautisha kati ya Amri za Mungu zilizokuwa za lazima kwa Wakristo wote na mashauri ya Kiinjili yasiyokuwa ya lazima na yaliyotoa stahili kama matendo zaidi kuhusu kiwango.
1100 Kum. 6: 5; Kut. 20: 17; Zab. 116: 11 1101 1 Kor. 8: 8
“mafundisho ya mashetani’” tu.1102
27. Ubikira unapendekezwa lakini kwa wale tu wenye kipawa hiki, kama ilivyokwisha kutajwa hapo juu. Lakini ni uzushi wenye madhara sana kuamini kwamba, ukamilifu wa kiinjili unapatikana katika mapokeo ya wanadamu. Kama ingekuwa hivyo, hata watawa Waislamu wangeweza kujigamba kwamba, wana ukamilifu wa Injili. Ukamilifu huu haupatikani katika mambo ambayo siyo lazima kuyajali.1103 Kwa sababu ufalme wa Mungu ni haki na uzima moyoni,1104 hivyo, ukamilifu unamaanisha kukua katika hofu ya Mungu, kutegemea huruma iliyoahidiwa katika Kristo na kujali kwa utiifu wito jinsi Paulo anavyotoa wasifu kikamilifu: “Tunabadilishwa tufanane na mfano huo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.”1105 Hasemi: “Tunachukua kanzu ya watawa baada ya nyingine, ama kubadhi au mishipi.”1106 Inasikitisha sana kusoma na kusikia kanisani sauti za Kifarisayo na za Kiislamu kwamba, ukamilifu wa kiinjili na wa ufalme wa Kristo, ambao ndio uzima wa milele, unalinganishwa na maadhimisho hayo ya kipumbavu kuhusu mavazi na takataka kama hizo.
28. Afadhali kuisikia sasa kauli duni ya maamuzi ya hawa Waareopagi1107 waliyoitunga katika Hoja. Hivi ndivyo wasemavyo: “Imetajwa wazi katika Maandiko Mtakatifu kwamba, maisha ya watawa hustahilisha uzima wa milele iwapo unafuatwa kwa uzingatifu upasao, na kila mtawa anaweza kufanya hivyo kwa neema ya Mungu. Kwa kweli, Kristo ameahidi hili tele kwa walioacha nyumba na ndugu zao n.k.”1108 29. Haya ni maneno ya wapinzani wetu, ambayo yanasisitiza ufidhuli huu kwamba, Maandiko Mtakatifu yanafundisha maisha ya utawa kuustahilisha uzima wa milele. Ni wapi Maandiko Matakatifu yanazungumzia kuhusu maisha ya watawa? Hii ndiyo njia ya wapinzani wetu ya kuendeleza kesi yao. Hivi ndivyo wapuuzi wasiofaa lolote wanavyonukuu Maandiko Matakatifu. Ingawa kila mmoja anajua kwamba, maisha ya utawa ni uvumbuzi wa siku hizi, bado wanayarejea mamlaka ya Maandiko Matakatifu hata wanadai kwamba, tamko lao limetajwa katika Maandiko Matakatifu. 30. Kwa kuongezea, wanamtukana Kristo wanaposema kwamba, watu wanastahili uzima wa milele kwa njia ya maisha ya utawa. Hata Mungu mwenyewe
1102 1 Tim. 4: 1
1103 ‘Αδιαφορα.’
1104 Rum. 14: 17
1105 2 Kor. 3: 18
1106 Hapa, Melanchthon anayachezea maneno ya Kilatini, ‘cucullus, calceus, cingula.’
1107 Rejea tashititi katika Mdo. 17: 22, 34
1108 Mt. 19: 29
haipatii sheria yake heshima hii ya kustahilisha uzima wa milele, jinsi asemavyo wazi katika Eze. 20:25: “Tena naliwapa amri zisizokuwa njema, na hukumu ambazo hawakuweza kuishi kwazo.” 31.Kwanza, ni kweli kabisa kwamba, maisha ya utawa hayastahilishi msamaha wa dhambi kwa maana tunaupokea bure kwa njia ya imani, jinsi ilivyokwisha kutajwa hapo juu. 32. Kisha, uzima wa milele unatolewa kwa rehema kwa ajili ya Kristo kwa wanaoupokea msamaha wa dhambi kwa njia ya imani bila kuweka stahili zao kinyume cha hukumu ya Mungu jinsi Bernardo asemavyo pia kwa nguvu kuwa: “Kwanza watu wote hawana budi kuamini kwamba, huwezi kuupata msamaha wa dhambi mbali na huruma ya Mungu. Kisha, huwezi kuwa na matendo yoyote mema isipokuwa matendo haya yatolewe bure.” Mwishowe, huwezi kuustahili uzima wa milele kwa matendo yoyote isipokuwa uzima huu uzawadiwe kwako. Hapo juu, tumeyarejea mambo mengine yaifuatiayo kauli hii. Mwishoni, Bernardo anaongezea: “Mtu na asijidanganye mwenyewe, kwa maana akifikiri kwa makini, atagundua kwamba, hata akiwa na askari elfu kumi hawezi kusimama mbele za Mungu amjiaye na ishirini elfu.”1109 33. Kwa vile hatustahili msamaha wa dhambi au uzima wa milele kwa matendo ya sheria ya Mungu, hivyo, lazima tutafute zaidi rehema iliyoahidiwa katika Kristo. Sembuse heshima hii ya kuustahilisha msamaha wa dhambi au uzima wa milele ihesabiwe matendo ya uzingatifu wa utawa ambayo ni mapokeo matupu ya wanadamu.
34. Hivyo, wale wafundishao kwamba, maisha ya watawa yanastahilisha msamaha wa dhambi au uzima wa milele, wanaivunja kabisa Injili ya msamaha wa dhambi bure na rehema iliyoahidiwa katika Kristo. Wanalihamisha tegemeo lililostahikiwa katika Kristo hadi kwenye uzingatifu ule wa kijinga. Wanaziabudu kanzu zao na uchafu wao badala ya Kristo. Japo hata wao wenyewe wanahitaji huruma, wanamkosea Mungu wanapodhania kuhusu stahili zinazozidi kiwango1110 na kuziuza kwa wengine.
35. Tumeyazungumzia mambo haya kwa ufupi, kwa maana tulikwisha kuyazungumzia hapo awali kuhusu mafungu ya kuhesabiwa haki, toba, na mapokeo ya wanadamu. Sasa, inajulikana wazi na vya kutosha kabisa kwamba, nadhiri za utawa si bei ambayo kwayo, hutolewa msamaha wa dhambi na uzima wa milele. Kwa kuwa Kristo anayaita mapokeo kuwa “ibada zisizokuwa na maana,” kamwe hayawezi kuwa ukamilifu wa Kiinjili.
36. Lakini inaonekana kwamba, wapinzani wetu wanajaribu kupunguza
1109 Bernardo wa Clairwaux/Kleawaksi, Mahubiri ya Sikukuu ya Tangazo la Malaika Gabrieli kwa Mariamu. Rejea Lk. 14: 31-32 1110 Kilatini: ‘Merita supererogationis.’
kwa hila maoni ya kawaida kuhusu ukamilifu. Wanakataa kwamba, maisha ya utawa ni makamilifu, lakini wanasema kuwa ni hali ya kuupata ukamilifu. Usemi mzuri kabisa! Tunakumbuka kwamba, sahihisho hili linatoka kwa Gerson.1111 Inaonekana kwamba, watu wenye busara wamechukizwa na sifa hizo za juu kupita kiasi kuhusu maisha ya watawa. Kwa vile hawathubutu kuikana kabisa sifa yake ya ukamilifu. Waliongezea sahihisho1112 hili kwamba, ni hali ya kuupata ukamilifu. 37. Tukilifuata wazo hili, maisha ya watawa hayatakuwa hali ya ukamilifu kuzidi maisha ya mkulima au msanii. Hizi pia ni hali za kuupata ukamilifu. Inawabidi watu wote kuutafuta ukamilifu katika wito wao. Yaani, katika hofu ya Mungu, katika imani, katika upendo kwa jirani, na katika maadili ya kiroho kama hayo.
38. Katika nyadhifa za wamonaki wa jangwani, kuna mifano ya Antonio1113 na ya wengineo ambayo huziweka hali mbalimbali za maisha katika tabaka moja. Imeandikwa kwamba, Antonio alimwomba Mungu amwonyeshe maendeleo aliyokuwa akiyafanya katika hali yake ya maisha. Ndotoni, Mungu alimtaka ajilinganishe na mshona viatu mmoja katika jiji la Aleksandria. Siku iliyofuatia, Antonio alifika jijini na alienda kwa huyo mshona viatu ili kutafiti mazoezi na vipawa vyake. Alipozungumza naye hakusikia lolote isipokuwa hili kwamba, kila asubuhi aliuombea mji mzima kwa maneno machache na baadaye aliizingatia kazi yake kwa makini. Hivyo, Antonio alipata kuelewa kwamba, hali ya maisha aliyokuwa ameanza kuifuata1114 haingehesabiwa haki.
39. Ingawa sasa wapinzani wetu wanazipunguza sifa zao kuhusu ukamilifu, kwa kweli, wanaamini vinginevyo kuhusu jambo lenyewe. Naam, wanaendelea kuuza stahili na kuzihamisha kwa wengine kwa kisingizio hiki kwamba, wanatimiza amri na mashauri na kwa sababu hiyo, wanadhania kwamba, wana hakika ya stahili zilizobakia. Ni lipi lingine isipokuwa kujikweza kuwa na ukamilifu? Katika Hoja yenyewe, inadaiwa kwamba, watawa hushindania sana kuishi kikamilifu zaidi kulingana na Injili. Japo watawa wataishi kikamilifu zaidi kulingana na Injili kwa sababu hawana mali binafsi, wanaishi katika useja, wanazitii kanuni kuhusu mavazi, vyakula, na takataka za namna hiyo, ukamilifu wa mapokeo ya wanadamu hautawahesabia haki.
1111 Jean Gerson, ‘De consiliis evangelicis et statu perfectionis’ 2, 679 (Mashauri ya Kiinjili na Hali ya Ukamilifu).
1112 Melanchthon, ‘επανορθωσις.’
1113 Antonio Mkuu, mtawa wa jangwani huko Misri (mnamo mwaka wa 251-356) aliyekuwa maarufu kutokana na wasifu wake uliotungwa na Askofu Mkuu wa Aleksandria, Athanasio (Maisha ya Antonio). Mfano wa Antonio uliwavutia watu wengi zaidi kujiunga na utawa.
1114 ‘De vitis patrum’ (Maisha ya akina Baba) 3. ‘Verba seniorum’ (Misemo ya Wazee) 130.
40. Kadhalika, Hoja inasema kwamba, watawa hustahili uzima wa milele mwingi zaidi kwa kuyanukuu Maandiko Matakatifu: “Kila mtu aliyeacha nyumba,” n.k.1115 Hapa pia Hoja inajipachika juu ya ukamilifu kwa matendo bandia ya dini. Lakini aya hii haihusu maisha ya watawa hata kidogo. Naam, siyo mapenzi ya Kristo tuwaache wazazi, mke, au ndugu zetu kwa kuwa, tendo hili halistahilishi msamaha wa dhambi wala uzima wa milele. Kinyume chake, kufanya hivyo ni kukufuru sana. Mtu akiwaacha wazazi na mke wake ili austahili msamaha wa dhambi au uzima wa milele, atamkashifu Kristo.
41. Kuna aina mbili za kuacha. Moja hutokea bila wito wala amri ya Mungu. Kristo haikubali hiyo kwa maana matendo tunayojichagulia ni “ibada batili.”1116 Tunaona wazi zaidi kwamba, Kristo hakubali kukimbia mke na watoto anapoelezea kuhusu kuacha kwa namna hiyo. Tunajua kwamba, amri ya Mungu inatukataza kumwacha mke na watoto. Lakini njia nyingine ya kuwaacha ni ile itolewayo na amri ya Mungu wakati mamlaka au maonevu yanapotulazimisha ama kuikimbia au kuikana Injili. Hapa tuna amri ya kuvumilia dhuluma , kupokonywa siyo tu mali, mke, na watoto bali maisha yenyewe. Kristo anakubali sana hasara ya namna hiyo. Kwa sababu hii, anaongezea maneno haya: “Kwa ajili ya Injili.”1117 Ili kuonyesha kwamba, hazungumzii kuhusu wafanyao madhara kwa wake na watoto bali kwa wavumiliao mateso kwa sababu ya ukiri wa Injili. 42. Vile vile, tunapaswa kuiacha miili yetu kwa ajili ya Injili. Lakini ni dhihaka sana kufikiria kwamba, kujiua na kuiacha miili yetu bila amri ya Mungu ni ibada kwa Mungu. Kwa hiyo, ni dhihaka kabisa kusema kwamba, ni ibada kwa Mungu kuacha mali, marafiki, mke na watoto wetu bila amri ya Mungu.
43. Inajulikana wazi kwamba, usemi wa Kristo umepotoshwa kumaanisha maisha ya utawa, isipokuwa labda pengine tamko lisemalo kwamba, watapokea zaidi ya mara mia katika maisha haya. Wengi zaidi huwa watawa, si kwa ajili ya Injili, bali kwa ajili ya chakula na burudani; badala ya urithi wa kiasi wanajipatia mali tele kabisa. 44. Kwa vile maisha ya utawa yamejaa uongo, wananukuu ushuhuda wa Maandiko Matakatifu kwa kisingizio cha uongo. Hivyo, wanakosea maradufu kuwadaganya watu na kufanya hivyo kwa kisingizio cha jina la Mungu.
45. Wananukuu aya nyingine kuhusu ukamilifu: “Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hizina mbiguni; kisha njoo unifuate.”1118 Aya hii imewahangaisha watu wengi waliodhania kwamba, ukamilifu unamaanisha kuacha mali na udhibiti wa mali. 46. Basi,
1115 Mt. 19 : 29
1116 Mt. 15: 9
1117 Mk. 10: 29
1118 Mt. 19: 21
tuwaruhusu tu wanafalsafa wamhubirie Aristipo aliyetupa shehena kubwa ya dhahabu baharini!1119 Mifano kama hiyo haina uhusiano wowote na ukamilifu wa Kikristo. Ugavi, usimamiaji, na umilikaji wa mali ni taratibu za kijamii zinazokubaliwa na Neno la Mungu katika amri hii “Usiibe.”1120 Kujitenga na mali hakuamriwi wala hakushauriwi katika Maandiko Matakatifu. Umaskini wa Injili1121 haumaanishi kuachana na mali, bali ni kutokuwepo kwa uchoyo na uaminifu katika utajiri jinsi Daudi alivyokuwa maskini katika utawala tajiri sana. 47. Kwa sababu hiyo, kuachana na mali ni mapokeo ya kibinadamu tu na ni ibada isiyofaa. Sifa za juu zinazopita kiasi kabisa katika kanuni za “Extravagantes.”1122 Kanuni hizi zinasema kwamba, kuukataa umilikaji wa mali zote kwa ajili ya Mungu ni stahili, utakatifu, na njia ya ukamilifu. Ni hatari mno kukumbatia, sifa hizo kupita kiasi juu ya jambo lolote linalopingana na utaratibu wa kijamii. 48. Lakini Kristo analiita jambo hili ukamilifu! Ndiyo, lakini wanalivuruga andiko hili wanapolinukuu kwa njia isiyostahili. Ukamilifu unapatikana katika maneno haya ya Kristo anapoongezea: “Nifuate!” 49. Yanaonyesha mfano wa utiifu katika wito. Kwa maana miito inatofautiana. Hivyo, wito huu haumaanishi kila mmoja, bali tu mtu ambaye Kristo anamzungumzia hapa. Kwa hivyo, wito wa Daudi kuwa mfalme au wa Ibrahimu kumchinja mwanawe, siyo mifano ya kuigwa nasi. Miito ni ya kibinafsi kama jinsi shughuli zingine zinavyotofautiana kulingana na muda na watu, lakini mfano wa utiifu ni wa mahali pote. 50. Kijana huyo angeushika ukamilifu ujao, angeuamini na kuutii wito huu. Hivyo, ukamilifu wetu ni kuwa na imani ya kweli na kuutii wito wa kila mmoja.
51. Tatu: nadhiri za watawa zinaahidi usafi. Tumekwisha kusema hapo juu kuhusu ndoa za makasisi kwamba, sheria ya asili iliyomo ndani ya wanadamu haiwezi kutanguliwa kwa nadhiri au sheria mbalimbali. Kwa kuwa, kila mtu hana kipawa cha useja. Ni wengi wanaoshindwa katika kuitawala tamaa mbaya kwa sababu ya udhaifu wao. Wala hakuna nadhiri au sheria iwezayo kubatilisha amri ya Roho Mtakatifu: “Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe.”1123 Kwa sababu hiyo, nadhiri ya aina hiyo siyo halali
1119 Aristipo (mnamo 435-366 K.K.) aliyetoka Kurene, alianzisha shule ya falsafa iliyofundisha kwamba, anasa za mwili ni shabaha kuu ya maisha ya binadamu. Alizitupa dhahabu zake baharini zisikamatwe na haramia (Dionisio Laerte II, 77). Rejea andiko la Kijerumani. Baada ya Aristipo, mwanafalsafa mwingine, yaani, Diogene, aliyaacha maisha ya kawaida na akaishi katika chombo kikubwa badala ya nyumba halisi.
1120 Kut. 20: 15
1121 Mt. 5: 3
1122 Kilatini: Extravagans,’ (kitu kinachotembea nje;) kanuni za akina papa zisizopatikana katika mikusanyiko ya Sheria za Kanuni za Kanisa la Roma. Kanuni ya Papa Yohana XXII (1316-1334) inayodondoa katiba ya Papa Nikolao III (1277-80).
1123 1 Kor. 7: 2
kwa yeyote asiyekuwa na kipawa cha kujizuia ambao huathiriwa kwa ajili ya udhaifu wao. 52. Tumekwisha kuzungumza vya kutosha kuhusu mada hii hapo awali. Inashangaza kweli kuwa wapinzani wetu wakiona hatari na kashfa hizo mbele yao, wanatetea mapokeo yao kinyume cha amri ya Mungu iliyoko wazi. Hawaathiriwi hata kidogo na sauti ya Kristo inayowalaumu Mafarisayo kwa ajili ya luzidisha mapokeo ya kuliko amri za Mungu
53. Nne: wote wanaoishi katika nyumba za watawa wako huru kuiabudu ibada potovu kama vile unajisi wa misa, ibada za watakatifu zenye dhambi maradufu, kwa ajili ya wafu, ili kukusanya fedha kwa njia ya maombi. Katika ibada hizi, watu watakatifu huichukua sehemu ya Kristo na kuabudiwa kwa njia ya kukufuru. Kwa mfano Wadominikano, wametengeza sala ya rozari ya Bikira Mbarikiwa ambayo ni payo-payo1124 tu, ujinga na upotovu wa kulieneza tumaini lisilokuwepo kabisa. Upotovu huu unatumika tu kwa ajili ya kukusanya fedha. 54. Hawasikilizi wala hawaiuhubiri Injili ya msamaha wa bure wa dhambi kwa ajili ya Kristo, haki ya imani, toba ya kweli, na kuhusu matendo ambayo yana amri ya Mungu. Lakini wanatumia muda wao ama katika mazungumzo ya kifalsafa au katika mapokeo ya kaida yanamfunika Kristo.
55. Hapa hatuzumgumzii hiyo ibada yao ya kaida nzima kama masomo, nyimbo na mengine1125 kama hayo. Mambo hayo yangeweza kuvumiliwa iwapo yangetumika kama mazoezi sawa na mafundisho shuleni yalivyo na shabaha ya mafundisho kwa wasikilizaji, na kama njia ya kufundisha kuwasukuma baadhi yao katika kuogopa au kuamini. Lakini sasa wanadhania kwamba, matendo haya yanayostahilisha msamaha wa dhambi kwao na kwa wengine ni ibada ya Mungu. Hii ndiyo sababu wanaongezea idadi ya kaida hizi. Kama wangezitumia ili kuwafundisha au kuwaasa wasikilizaji, masomo mafupi na kamili yangefaa zaidi kuliko payo-payo1126 hizo zisizokuwa na mwisho. 56. Kwa hiyo, maisha mazima ya watawa yamejaa unafiki na mawazo ya uongo. Kuhusiana na haya, hatari hii inaongezeka kwamba, wote walio katika jamii hizi wanashurutishwa kukubaliana na watesaji wa ile kweli. Hivyo basi, kuna sababu nyingi na nzito kabisa za kuwaweka huru watu wema kutoka katika aina hii ya maisha.
57. Mwishowe, kwa ajili ya kanuni zenyewe, watu wengi walioapa nadhiri zao bila kuelewa vya kutosha kwa sababu wamedanganywa na hila/hoja za watawa au kwa sababu wameshurutishwa na marafiki zao, wamekuwa huru. Nadhiri za namna hiyo hazitangazwi hata na kanuni zenyewe kuwa nadhiri halisi. Kutokana
1124 Mt. 6: 7; Melanchthon, ‘βαττολογια.’
1125 Masomo, zaburi, kantiko (Nyimbo za Agano Jipya), antifoni, responsorio na sehemu zingine za liturgia katika kitabu cha breviario cha Kanisa la Roma tangu karne ya kumi. 1126 Melanchthon, ‘βαττολογια.’
na haya yote, inafahamika wazi kwamba, kuna sababu nyingi zinazotuelezea kwamba, nadhiri zilizotolewa mpaka sasa, si nadhiri halisi. Hivyo, ni bora kuachana na maisha haya yaliyojaa unafiki na mawazo mapotovu.
58. Ili watupinge, wanaurejea hapa mfano wa Wanadhiri kutoka Torati1127. Lakini watu hawa hawakujichukulia nadhiri zao wenyewe, mawazo ambayo, kama tulivyosema, tumeyakaripia katika nadhiri za watawa. Kaida ya Wanadhiri ilikusudia mazoezi au ukiri wa imani mbele ya wanadamu na siyo kuustahilisha msamaha wa dhambi wala haikuhesabia haki mbele za Mungu. Kisha, kama jinsi tohara au machinjo ya dhabihu hayawezi kuwa ibada sasa, vivyo hivyo kaida ya Wanadhiri haipaswi kupendekezwa kuwa ibada, bali inaweza tu kutambuliwa kama jambo ambalo si lazima kulijali. Hivyo basi, siyo sahihi kulinganisha utawa uliobuniwa bila Neno la Mungu kama ibada inayostahilisha msamaha wa dhambi na kuhesabia haki, pamoja na kaida ya Wanadhiri yenye Neno la Mungu na iliyotolewa siyo ili kuustahilisha msamaha wa dhambi bali ili yawe mazoezi ya nje kama kaida zingine za Torati. Vile vile hayo yanaweza kusemwa kuhusu nadhiri zinazotolewa katika Torati.
59. Wanawarejea pia Warekabu wasiokuwa na mali wala wasiokunywa divai yoyote ambao Yeremia anawazungumzia katika sura yake ya 35:6. Barabara kabisa! Mfano wa Warekabu unawahusu watawa wetu vizuri ambao makao yao ni ghali zaidi kuliko makasri ya wafalme ambao huishi maisha ya anasa. Lakini Warekabu walikuwa wameoa katika umaskini wao wa kila kitu. Watawa wetu wana kila aina ya anasa na wanadai kuwa waseja.
60. Mbali na hayo, inatupasa kuifafanua mifano hii kulingana na ngazi, yaani, kulingana na maandiko yaliyo thabiti na dhahiri, siyo kinyume cha ngazi au maandiko yenyewe. 61. Ni jambo la hakika kabisa kwamba, matendo yetu hayastahilishi msamaha wa dhambi au kuhesabiwa haki. Warekabu wanapotukuzwa, lazima tuelewe kwamba, hawakushikilia mitindo yao ili kustahili msamaha wa dhambi kwayo, au kwamba, tendo lenyewe tu la ibada lilikuwa tendo lililohesabia haki au kwamba, kwa sababu yake, tunapata uzima wa milele na siyo kwa sababu ya rehema ya Mungu, kwa ajili ya uzao ulioahidiwa.1128
Lakini kwa sababu walikuwa na amri iliyotoka kwa wazazi wao, wanasifiwa kwa ajili ya utiifu wao ambao Mungu aliuamuru: “Waheshimu baba yako na mama yako.”1129
62. Kisha, desturi hii ilikuwa na shabaha maalumu: kwa kuwa wao
1127 Hes.6: 2-21
1128 Mwa. 3: 15
1129 Kut. 20: 12
walikuwa watu waliohamahama na siyo Waisraeli. inaonyesha kwamba, baba yao alitaka kuwatofautisha kwa alama fulani kutoka kwa watu wengine wa aina yake ili wasifanane na wenzao katika upotovu wa ibada ya sanamu. Alitaka kuwakumbusha kwa alama hizi kuhusu mafundisho ya imani na uzima usio na mwisho. Shabaha ya namna hiyo ni halali kabisa. Lakini shabaha za utawa ni tofauti kabisa kulingana na mapokeo yake. Wanadhania kwamba, matendo ya utawa ni ibada. Wanadhania kwamba, ibada hizi huustahilisha msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki. Hivyo basi, mfano wa Warekabu ni tofauti sana na utawa. Hatutazungumzia uovu mwingine uliomo siku hizi katika nyumba za watawa.
64. Vile vile wananukuu 1Tim. 5: 11-12 kuhusu wajane waliolitumikia Kanisa na waliokuwa wametunzwa kwa mfuko wa umma jinsi inavyosema: “Wanapotaka kuolewa, nao wanapopambana na kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza.” 65. Kwanza, acheni tuseme kwamba, mtume anazungumzia nadhiri hapa. Hata hivyo, aya hii haikubaliani na nadhiri za watawa zinazotumiwa kwa shabaha za ibada za kukufuru na kwa wazo hili kwamba, zinastahilisha msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki. Yaani, Paulo anazilaani kwa sauti kuu ibada zote, sheria zote na matendo yote yatendekayo kwa ajili ya kuustahilisha msamaha wa dhambi au ambayo kwayo, tunaupata uzima wa milele badala ya rehema kwa ajili ya Kristo. Kwa sababu hiyo, kama kuna nadhiri za wajane, ziko tofauti na nadhiri za watawa.
66. Licha ya hayo, wapinzani wetu wasipokoma kuivuruga aya hii kuhusu nadhiri, itawalazimu waivuruge aya nyingine inayokataza kumchagua mjane isipokuwa umri wake uwe umefikia miaka sitini.1130 Hivyo, nadhiri zilizofanywa kabla ya umri huo zitakuwa haramu. 67.Lakini Kanisa bado halikuzijua nadhiri hizi. Paulo aliwashutumu wajane, siyo kwa ajili ya kuwa waliolewaanawaamrisha vijana waoe - bali kwa sababu walikuwa hawazuiliki walipokuwa wanatunzwa kwa fedha za umma na hivyo kuipoteza imani. Hii ndiyo aiitayo “imani ya kwanza,” siyo nadhiri za utawa, bali za Kikristo. Anatumia imani kwa njia hiyo hiyo pia katika sura hiyo hiyo : “Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani.”1131 68. Naam, anazungumzia imani tofauti na wataalamu wa ghiliba. Yeye haaihesabu imani kwa watu wanaopatikana katika dhambi ya mauti; Kwa sababu hiyo, anasema kwamba, wale wasiowatunza jamaa zao wanaikataa imani. Kwa namna hiyo hiyo anasema, wanawake wasiozuilika waliikana imani.
1130 1 Tim. 5: 9
1131 1 Tim. 5: 8
69. Tumepitia baadhi ya madhumuni yetu na kuyakanusha mapingamizi ya wapinzani wetu. Tumeyatunga haya, siyo kwa ajili ya wapinzani wetu tu, bali hata zaidi kwa ajili ya nafsi za wacha Mungu ili wapate kuona wazi sababu ambazo kwazo, inawalazimu kukataa unafiki na ibada zilizobuniwa za watawa ambazo Kristo anazifuta kwa sauti hii moja anaposema: “Nao waniabudu bure . . . yaliyo maagizo ya wanadamu.”1132 Kwa sababu hiyo, nadhiri zenyewe pamoja na uzingatiaji wa vyakula, masomo, nyimbo, mavazi, viatu, mikanda, haya yote ni ibada zisizokuwa na faida mbele za Mungu. Nafsi zote za wacha Mungu zinapaswa zitambue kweli kuwa wazo hilo ya kwamba uzingatiaji wa namna hiyo hustahilisha msamaha wa dhambi na kwamba, kwa ajili yake, tunahesabiwa haki, tunapata uzima wa milele kwayo, na siyo kwa rehema kwa ajili ya Kristo, ni la Kifarisayo na la kulaaniwa hakika. 70.Watu watakatifu walioishi katika aina hizo za maisha lazima wangekataa tumaini lolote la uzingatiaji huu, wakijifunza kwamba, waliupokea msamaha wa dhambi bure kwa ajili ya Kristo, na kwamba, wataweza kuupata uzima wa milele kwa rehema kwa ajili ya Kristo na siyo kwa ajili ya ibada kama hizo, na kwamba, Mungu anazikubali tu ibada zilizoanzishwa kwa Neno lake na kufanyika katika imani.
Fungu Ishirini na Nane: Mamlaka Kanisani
1. Wapinzani wetu wanapiga kelele hapa sana kuhusu faida kubwa na kinga za cheo cha Kanisa, hata kuongezea hitimisho hili: “Haya yote ni haramu yanayotolewa katika fungu hili kupinga kinga za makanisa na makasisi.” 2. Haya ni usingiziaji tu, kwa maana katika fungu hili, tumekuwa tukizungumzia mambo mengine tofauti. Zaidi ya hayo, mara nyingi tumekuwa tukishuhudia kwamba, hatuilaumu michango na kinga za watawala.
3. Laiti wapinzani wetu wangesikiliza malalamiko ya makanisa na nafsi za wacha Mungu! Kwa ushujaa, wapinzani wetu hulinda vyeo na mali zao wakati huo hawajali hali za makanisa, na hawaangalii vizuri mafundisho ya makanisa na huduma ya sakramenti kwa uaratibu.1133 Wanawapokea watu wowote kwenye huduma ya upadre bila ubaguzi. Baadaye, huwatwika mizigo isiyovumilika, kana kwamba wanafurahia wengine waangamie. Wanadai uzingatiaji kamili wa mapokeo yao kuliko Injili. 4. Katika mabishano haya mazito na magumu, umma una hamu kubwa na moyo wa kuelekezwa ili uwe na hakika kuhusu njia ya kuifuata. Badala ya kuzisaidia nafsi zinazoteswa vikali na mashaka, wanazihimiza kwa kelele za kutiana shime vitani. Licha ya hivyo, katika mambo haya yaliyoko
1132 Mt. 15: 9
1133 Kilatini: ‘Sacramenta rite tractari;’ taz. ‘Ukiri wa Augsbug,’ Fungu la Kumi na Nne.
wazi, wanayatoa maagizo yaliyoandikwa kwa damu, wakiwatisha watu kwa adhabu kali wasipotenda wazi kinyume na amri za Mungu. 5. Lakini, kwa upande wenu, inawabidi kuona machozi ya wanaoteseka na kusikia malalamiko ya uchungu ya watu wengi wema. Bila shaka, Mungu anayaona na kuyasikia, na wakati fulani mtaitoa hesabu ya uwakili wenu mbele zake.
6. Tumezijumuisha sehemu mbalimbali ndani ya Ukiri na fungu hili. Lakini jibu pekee la wapinzani wetu ni kwamba, maaskofu wana mamlaka ya kutawala na kurudi kwa njia ya kudhibiti1134 ili kuwaelekeza walio chini yao katika lengo la furaha ya milele. Uwezo wa kutawala unahitaji nguvu ya kuhukumu, kufasili, kutofautisha na kuamua mambo yatakayosaidia au kuboresha shabaha iliyokukwisha kutajwa hapo juu. Haya ni maneno ya Hoja ambayo kwayo, wapinzani wetu hutufundisha kwamba, maaskofu wana mamlaka ya kutunga sheria ambazo zinafaa katika kuupata uzima wa milele. Mjadala mzima unahusu jambo hili.
7. Inatubidi kuyashika mafundisho haya kanisani, kwamba, tunaupokea msamaha wa dhambi bure kwa ajili ya Kristo kwa imani. Vile vile, inatubidi kuyashika mafundisho kwamba, mapokeo ya wanadamu ni ibada zisizokuwa na maana. Kwa sababu hiyo, hakuna dhambi wala haki katika chakula, kinywaji, mavazi, na mambo ya jinsi hiyo. Kristo alitaka matumizi ya vitu hivyo yawe huru anaposema: “Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi.”1135 Na Paulo anaposema: “ Maana ufalme wa Mungu si kula au kunywa.”1136 8. Kwa sababu hiyo, maaskofu hawana haki ya kupitisha mapokeo mbali na Injili kana kwamba, yangestahilisha msamaha wa dhambi au yangekuwa ibada ya kumpendeza Mungu kama haki. Mapokeo hayo yanaweza pia kuisumbua dhamiri kana kwamba, kuyaacha kunakuwa dhambi. Haya yote yanafundishwa na aya moja katika Matendo ya Mitume 15:9, ambapo mitume wanasema kwamba, mioyo inasafishwa kwa imani. Kisha, wanakataa watu wasitwishwe nira, wakionyesha jinsi hatari ya jambo ilivyo, na ukubwa wa dhambi ya wanaolitwisha Kanisa mzigo. Wanasema: “Kwa nini mnamjaribu Mungu?”1137 Lakini radi hii haiwatishi wapinzani wetu wanaotetea kwa ujeuri mapokeo na maoni ya kukufuru.
9. Hapo juu, walililaani Fungu la Kumi na Tano ambapo tulidai kwamba, mapokeo hayawezi kustahilisha msamaha wa dhambi. Hapa wanasema kwamba, mapokeo yanafaidi kwa ajili ya uzima wa milele. Je, yanaustahilisha kweli msamaha wa dhambi? Je, ni ibada zinazokubaliwa na Mungu kama haki? Je, 1134 Yaani, kushurutisha.
1135 Mt. 15: 11
1136 Rum. 4: 17
1137 Mdo. 15: 10
yanahuisha mioyo? Katika Waraka kwa Wakolosai, Paulo anakataa faida ya mapokeo kwa ajili ya haki na uzima wa milele, kwa maana chakula, kinywaji, mavazi, na mengineyo ni vitu vinavyoharibika kadiri vinavyotumika.1138 Badala yake, uzima wa milele unatekelezwa moyoni na mambo ya milele, yaani, Neno la Mungu na Roho Mtakatifu. Hebu sasa wapinzani wetu watueleze jinsi mapokeo yanavyofaa kwa uzima wa milele!
11. Basi, Injili inashuhudia wazi kwamba, Kanisa lisilazimishiwe mapokeo ili kustahilisha msamaha wa dhambi au kuwa ibada zinazokubaliwa na Mungu kama haki au kuzisumbua dhamiri kwa mizigo hii kwamba, kutoyajali mapokeo haya kunahesabiwa kuwa dhambi. Wapinzani wetu kamwe hawataweza kuonyesha kwamba, maaskofu wana mamlaka ya kuanzisha ibada kama hizi.
12. Katika Ukiri, tumeelezea Injili inawapa maaskofu aina gani ya mamlaka. Wale ambao ni maaskofu sasa hawazitunzi huduma zao za kiaskofu kulingana na Injili. Wawe tu maaskofu kulingana na madaraka ya Kanisa ambayo hatuyalaumu. Lakini sisi tunazungumzia huduma ya kiaskofu kulingana na Injili. 13 Tunaupenda utofautishaji wa zamani kati ya mamlaka ya kuwabariki mapadre na mamlaka ya utimizaji wa sheria.1139 Kwa hiyo, askofu ana mamlaka ya kuwabariki wachungaji, yaani, Huduma ya Neno na sakramenti. Kadhalika, ana mamlaka ya utimizaji wa sheria, yaani, mamlaka ya kuwatenga wenye hatia ya jinai za umma na kuwaondolea dhambi walioongoka na kuomba ondoleo la dhambi. 14. Basi, hawana mamlaka ya uonevu, yaani, kutawala bila sheria fulani, wala mamlaka ya kifalme, yaani, kutawala juu ya sheria, lakini wana amri ya uhakika, Neno la Mungu hakika ambalo kwalo wanapaswa kulifundisha na wanapaswa kutekeleza mamlaka yao. Hata hivyo, tukisema maaskofu wana mamlaka fulani ya utimizaji wa sheria, haimaanishi kwamba, wanaweza kuanzisha ibada mpya, kwa maana ibada hazihusiani na utimizaji huo. Wana Neno, wana amri. Kulingana na mamlaka haya, wanapaswa kuitekeleza sheria, yaani, wakati mmojawapo anatenda jambo kinyume cha Neno ambalo wamelipokea kutoka kwa Kristo.
15. Katika Ukiri, tumeongezea pia namna ya wao kuweza kuyapitisha mapokeo. Lakini mapokeo haya hayapaswi kufikiriwa kuwa ibada za lazima bali njia ya kulinda utaratibu kanisani kwa ajili ya amani. Haya hayapaswi kuitega dhamiri kana kwamba, wangeamrisha ibada za lazima. Hivi ndivyo Paulo afundishavyo anaposema: “Katika ungwana huo Kristo alituweka huru; kwa
1138 Kol. 2: 20-23
1139 Kilatini: ‘Potestas ordinis’ na ‘potestas jurisdictionis.’
hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.”1140 16. Kwa hiyo, matumizi ya mipango ya namna hiyo lazima yaachwe huru - isipokuwa tu kashfa ziepukwe - na yasitambuliwe kama ibada za lazima. Hivyo, hata mitume waliyaamuru mambo mengi yaliyobadilika kwa kuzifuata nyakati. Hawakuyatoa mambo haya kwa jinsi hii ili yasiweze kubadilishwa. Hawakuyapitia maandiko yao wenyewe, katika wanayoyaelezea kwa bidii sana ili Kanisa lisitaabishwe na maoni kwamba, kaida za wanadamu ni ibada za lazima.
17. Haya ndiyo mafundisho ya wazi kuhusu ufafanuzi juu ya mapokeo. Yaani, tujue kwamba, mapokeo siyo ibada za lazima. Hata hivyo, tuyafuate kwa nafasi zake bila maono haramu, ili kuepukana na kashfa. 18. Wataalamu wengi na watu wakubwa walifikiria hivyo kanisani. Hatuoni ni jambo gani linaweza kupingwa hapa. Ni dhahiri kabisa kwamba, kauli hii, “awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi,”1141 haizungumzii kuhusu mapokeo bali kinyume cha mapokeo kabisa. Siyo “madaraka kamili”1142 jinsi wanavyoyaita, bali ni “shauri maalumu,” “udhamini maalumu,”1143 yaani, ushuhuda uliotolewa kwa mitume ili tuwaamini kwa ajili ya neno la mwingine na siyo kwa ajili ya neno lao wenyewe. Kwa maana, Kristo anataka kututhibitishia kadiri ilivyohitajika ili tupate kujua kwamba, neno lililotolewa kwa watu lina nguvu na tusitazamie neno lingine kutoka mbinguni. 19. Maneno haya, “awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi,” hayawezi kutumiwa kwa njia ya mapokeo. Naam, hapa Kristo anahitaji wafundishwe kwa njia ambayo sauti yake mwenyewe itasikika dhahiri, kwa sababu anasema, “anisikilizaye mimi.” Kwa hiyo, anataka sauti yake, neno lake lisikike, siyo mapokeo ya wanadamu. Maneno haya yanayotutetea sanasana na kutuletea mafundisho yenye faraja kuu yanavurugwa na punda hawa kuwa mambo batili kama tofauti za vyakula, mavazi na mengine kama hayo.
20. Wananukuu pia Ebr. 13:17: “Watiini wenye kuwaongoza.”1144 Kauli hii inahitaji utiifu wa Injili. Haitoi madaraka kwa maaskofu mbali na Injili. Maaskofu hawapaswi kupitisha mapokeo kinyume cha Injili, wala kufafanua mapokeo yao dhidi ya Injili. Wanapofanya hivyo tunakatazwa kuwatii kulingana na neno hili: “Iwapo yeyote atawahubiri Injili nyingine tofauti, alaaniwe.”1145
21. Hali kadhalika, tunaijibu aya hii: “Yoyote watakayowaambia myashike
1140 Gal. 5: 1
1141 Lk. 10: 16
1142 Kilatini: ‘Mandatum cum libera.’
1143 Kilatini: ‘Cautio de rato.’
1144 Ebr. 13: 17
1145 Gal. 1: 8
na kuyatenda.”1146 Inajulikana wazi kwamba, hapa hatuamriwi kukubali kila kitu, kwa kuwa mahali pengine Maandiko Matakatifu yanaamuru tumtii Mungu zaidi ya wanadamu.1147 Wanapofundisha mambo ya kukufuru yasisikilizwe. Mambo haya maovu kabisa ni mafundisho kwamba, mapokeo ya wanadamu ni ibada za Mungu; kwamba, ni ibada za lazima, na zinastahilisha msamaha wa dhambi na uzima wa milele.
22.Wanatushtaki pia kwa jili ya kashfa za umma na ghasia zilizoibuka kwa kisingizio cha mafundisho yetu. Tutalijibu hili kwa ufupi. 23. Ikiwa makosa yote yakiwekwa pamoja, bado fungu moja la msamaha wa dhambi tunaoupata bure kwa imani na kwa ajili ya Kristo, litatuletea mema ya kutosha kuyaficha maovu yote. 24. Kwa asili, jambo hili lilimfanya Luther kuwadhihaki, siyo tu wakereketwa wetu, bali na wengine wengi wanaotupinga sasa. “Ukereketwa wa zamani unalala, na wanadamu wafao ndio wasahaulifu,” alisema Pindaro.1148 Basi, hatutaki kuuacha ukweli ulio wa lazima kwa Kanisa, wala kukubaliana na wapinzani wetu wanaoulaani. 25. Lazima tumtii Mungu zaidi kuliko wanadamu.1149 Wao hawatakuwa na budi kutoa hesabu kwa ajili ya mgawanyiko huu, ambao, kwa asili, waliulaani ukweli ulio wazi, na sasa wanauadhibu kwa ukatili mno ukweli huu. Je, hakuna kashfa zilizotokea dhidi ya wapinzani wetu? 26. Ni mabaya gani yaliyotokea kutokana na kuikufuru misa kwa njia ya kukusanya fedha? Kuna aibu gani katika useja! Lakini tuuacheni mlinganisho! 27. Haya ni majibu yetu ya kisasa kwa Hoja. Sasa watu wote wacha Mungu wahukumu kama wapinzani wetu wanastahili kujisifu kwamba, kweli wameukanusha Ukiri wetu kwa Maandiko Matakatifu.
1146 Mt. 23: 3
1147 Mdo. 5: 29
1148 Pindaro (522/518-446 K.K.), mshairi Myunani aliyetoka Kinoskefalai. Miongoni mwa vitabu vyake kumi na saba, ni vitabu vinne tu vilivyohifadhiwa. Katika vitabu hivyo, anaimba kuhusu sherehe za Wayunani.
(Isth. 8, 25).
1149 Mdo. 5: 29
Mwisho
MAFUNGU YA SMALKALDI
Mafungu ya mafundisho ya Kikristo ambayo yalikuwa yawasilishwe nasi katika Sinodi ya Mantova, au mahali popote ambapo sinodi hii ingefanyiwa. Yanaonyesha wazi mambo ambayo tunaweza au hatuwezi kuyapokea, kuyakubali ama kutoyakubali.
Yameandikwa na Dk. Martin Luther mwaka wa 1537
DIBAJI YA DK. MARTIN LUTHER
1. Papa Paulo, anayeitwa Paulo wa Tatu, alitangaza kwamba, anataka aiitishe sinodi ikutane huko Mantova1150 mwaka uliopita katika majira ya Pentekoste. Kisha, aliihamisha sinodi hii kutoka Mantova na haijulikani alikonuia au alikoweza kuiitisha.1151 Kwa upande wetu, hatuna budi kujitayarisha kwamba, tutahukumiwa katika sinodi hii, iwe tuna wito au hatuna wito wowote. Kwa sababu hiyo, niliagizwa kutoa na kukusanya mafungu ya mafundisho yetu. Daawa hii ikifanyika katika sinodi, lazima tutajua ni wapi na ni kwa kiasi gani tungeweza au tungetaka kukubaliana na wafuasi wa Papa na ni mambo yepi tungeyashikilia na kuyadumisha mpaka mwisho.
2. Kwa hiyo, nimeyakusanya mafungu haya na kuyatoa kwa wawakilishi wetu. Wenzetu waliyakubali na kuyakiri Mafungu haya kwa maafikiano kabisa na kuamuliwa kwamba, lazima yatolewe hadharani kama ukiri wa imani yetu iwapo, kwa nia njema, Papa na wafuasi wake watathubutu kuitisha sinodi huru kama jinsi anavyowajibika kufanya bila udanganyifu au usaliti.
3. Lakini mahakama ya Roma inaogopa sana sinodi huru na inaiepuka nuru kwa njia ya aibu kabisa. Hata inapoteza tumaini la wenzao kwamba, Mahakama ya Roma, itavumilia sinodi huru bila yenyewe kuitisha sinodi ya namna hiyo. Wamechukizwa na kutaabishwa sana kwani wanaona kwamba, Papa anapenda
1150 Mji huko Kaskazini mwa Italia katika Mkoa wa Lombardia. 1151 Papa Paulo III aliahirisha sinodi tarehe 20 Aprili, mwaka wa 1537 mpaka tarehe 1 Novemba, mwaka uo huo. Baadaye, sinodi iliahirishwa mpaka tarehe 1 Mei, mwaka wa 1538 na kuitwa mjini Vicenza. Mwishowe, sinodi iliahirishwa tena kwa muda tarehe 21Mei, mwaka wa 1539.
zaidi kuona Wakristo wote wakiangamia na nafsi zote zikilaaniwa kuliko yeye mwenyewe na wafuasi wake kuvumilia na kuruhusiwa kwa vizuizi kuwekwa katika udhalimu wake.
Hata hivyo, nimeamua kuyatoa mafungu haya hadharani kwa njia ya kuchapishwa ili kama nitakufa kabla ya sinodi. (ambayo ninaitarajia itatokea, kwa sababu matapeli hao wanauogopa mwanga na kuipinga nuru na hujikokota dhahiri kabisa wapate kuiahirisha na kuizuia sinodi) Shabaha yangu ni kuuacha ushuhuda na ukiri wangu kwa watakaoishi baada yangu, pamoja na ukiri ambao nilitangulia kuutoa. Mpaka sasa, nimesimama katika ukiri huu1152 na nitaendelea kusimama kwa neema ya Mungu.
4. Niseme nini? Kwa nini nilalamike? Bado ninaishi. Bado ninaandika, ninahubiri, na ninahutubu kila siku. Hata hivyo, kuna watu wengine wenye sumu – sio tu miongoni mwa wapinzani wetu, bali pia ndugu wasiokuwa wakweli miongoni mwa wenzetu. Hawa huthubutu kunipinga kwa ajili ya maandiko na mafundisho yangu. Hata hivyo, niko hapa kuona kwa macho yangu na kusikia kwa masikio yangu. Wanajua vizuri kwamba, mimi ninafundisha tofauti kabisa. Kwa njia hii, wanataka kuieneza sumu yao katika kazi yangu ili wapate kuwashawishi watu maskini kwa jina langu. Basi, nini zaidi kitatokea baada ya kifo changu?
5. Nijibu kila suala wakati bado ninaishi? Lakini niwezeje kuvifunga vinywa vyote vya Ibilisi? Haya yote yanaineza sumu hasa yale wasiyotaka kuyasikia au kuyang’amua, yaani, yale tunayoyaandika. Watu hawa wanajishughulisha sana kughushi na kupotosha kila hati ya maneno yetu. Mwishowe, nitamruhusu Ibilisi mwenyewe ama ghadhabu ya Mungu kuwajibu jinsi wanavyostahili.
6. Mara nyingi ninamfikiria jalali1153 Gerson,1154 aliyekuwa na mashaka kama mtu anaweza kuandika hadharani lolote lililo zuri. Kama lisipofanyika, nafsi za wengi ambazo zingeweza kuokolewa zitapotea. Kwa upande mwingine, likifanyika, Ibilisi atakuwepo mara moja na vinywa vyake vingi, vibaya, na vyenye sumu ili kukipotosha kila kitu na hata kulizuia tunda lolote.
7. Hata hivyo, wanachokitimiza watu hawa ni wazi kabisa. Ingawa wameendelea kusema uongo kwa kututukana kwa aibu na wamejaribu kuwatawala watu kwa njia ya uongo, Mungu ameendelea kuiruhusu kazi yake ishamiri vizuri. Amekipunguza kikundi chao na kukizidisha chetu zaidi. Amewafanya wao na
1152 Luther anakirejea hapa kitabu chake : ‘Von Abendmahl Christi Bekenntnis,’ (‘Chakula cha Kristo –Ukiri’) mwaka wa 1528.
1153 Yaani, mtu bora na mwenye heshima.
1154 Jean le Charlier de Gerson (1363-1429): kutoka Ufaransa, mwandishi maarufu wa Kanisa la Magharibi wakati wake. Kitabu chake ‘De laude scriptorum’ (‘Sifa ya Waandishi’) XI.
uongo wao kutiwa aibu tena na tena.
8. Niruhusu, nilisimulie tukio la kihistoria. Daktari mmoja alizuru Wittenberg kama balozi wa Ufaransa.1155 Alitueleza hadharani kwamba, mfalme wake alishawishiwa bila mashaka yoyote kwamba, hali ya mambo ilivyokuwa, ni kama hakukuwa na Kanisa, hakukuwa na serikali, na hakukuwa na ndoa miongoni mwetu. Badala yake, sote tunaishi kiholela kama ng’ombe na kila mtu hufanya alipendalo. Fikiria wao watakavyotuona mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo siku ya mwisho. Katika maandiko yao, wao wameusema uongo mbaya kabisa kwa mfalme na nchi za kigeni kana kwamba, ulikuwa ukweli. Kristo, Bwana na hakimu wetu sote, anajua vyema kwamba, wamesema uongo na wanaendelea kusema uongo. Nina hakika kwamba, hawana budi kuisikia hukumu dhidi yao. Mungu awaongoze wale wanaoweza kuongoka kwa njia ya toba. Wengine waliosalia, Huzuni na ‘Ole’ vitakuwa fungu lao milele.
10. Nikilirudia tena suala lenyewe, kwa kweli, ningependa sana kuiona sinodi itakayokutana ili watu wengi wenye mambo mengi wapate kusaidiwa. Wenyewe hatuihitaji kwa sababu kwa neema ya Mungu makanisa yetu yameelimishwa, kwa Neno safi, kwa matumizi halisi ya sakramenti, wamekuwa na ufahamu wa miito mbalimbali,1156 na matendo halisi. Kwa sababu hiyo, hatuitamani sinodi. Hatuna sababu ya kutumainia au kutegemea kwamba, sinodi itarekebisha lolote kuhusu masuala haya. Badala yake, katika dayosisi za maaskofu, tunaona sharika nyingi zilizoachwa na nafasi nyingi za makasisi zilizokuwa wazi kiasi kwamba, mioyo yetu inavunjika kwa huzuni.1157 Hata sasa, siyo maaskofu wala mapadre wa makanisa1158 makuu wanaojali hata kidogo jinsi watu masikini wanavyoishi au wanavyokufa, ingawa Kristo aliwafia wao pia. Watu hao hawawezi kumsikia Kristo kama Mchungaji wao Mwema jinsi anavyosema kwa kondoo zake. 11. Kwa sababu hiyo, inanikera na kunitisha kwamba, anaweza kuitisha sinodi ya malaika ihukumu Ujerumani na kutuangamiza kabisa kama Sodoma na Gomora kwa sababu tunamdhihaki kwa aibu sana kwa sinodi hii.
12. Mbali na masuala muhimu ya Kanisa, kuna masuala mengi makuu ya kijamii yasiyohesabika yanayohitaji marekebisho. Watawala na vyeo vya heshima hupigana. Ulaji riba na ulafi vimechipuka kama gharika na kujipa sura ya haki. Isitoshe, kuna udhalimu, uzinzi, kiburi, anasa katika mavazi, ulafi,
1155 Gervasius Waim, balozi wa Mfalme Fransisko I wa Ufaransa, alisomea chini ya adui yake Luther, yaani, Yohana Eck, alizuru Wittenberg mwaka wa 1531.
1156 Yaani, vyeo vya kijamii au wito.
1157 Mwaka wa 1538, ilielezwa kwamba, katika Dayosisi ya Würzburg pekee, sharika tajiri mia sita zilikuwa bila mapadre.
1158 Kilatini: ‘Canonicus,’ Kijerumani: ‘Domherr .’
kamari, fahari isiyofaa, aina zote za uovu, ufisadi, ukaidi wa raia, wa watumishi, wa wafanyakazi na mafalahi (wakulima wadogo) unyanganyi katika kila aina ya biashara. Ni nani awezaye kuyaorodhesha yote? Uovu huu umezidi kupita kiasi kwamba, sinodi kumi na baraza hata ishirini hazingeweza kuyarekebisha mambo tena. 13. Ikiwa wajumbe wa sinodi wakitaka kuzitumikia hizo hisa kuu za vyeo vya kiroho na kidunia zilizo kinyume na mapenzi ya Mungu, mikono yao itajaa kiasi cha kuisahau michezo ya kitapeli na ya kipumbavu wa joho, vipara utosini, mishipi mipana, kofia na fimbo za maaskofu na makadinali, na upuuzi unaofanana na hayo. Tukichunguza vizuri kama amri na maagizo ya Mungu yanafuatwa vizuri katika maisha ya Kanisa na jamii, tutapata muda wa kutosha kuzirekebisha kanuni kuhusu vyakula, mavazi, vipara utosini, na kasumba. Lakini tukikubali kuwameza ngamia na kuwasita mbu, tukiiruhusu boriti isimame na kuvihukumu vijiti,1159 tutaweza pia kuridhika na sinodi hii.
14. Kwa hiyo, nimeyatunga baadhi ya mafungu, kwani, mbali na hayo, Mungu ametupatia shughuli nyingi kanisani, serikalini, na katika familia ambazo hatuwezi kuzikamilisha kamwe. Je, shughuli hizo za kuyakubali maagizo na kanuni nyingi katika sinodi zina faida gani, hasa wakati masuala haya makuu yaliyoamriwa na Mungu hayawekwi au hayatiliwi maanani? Je, inambidi Mungu akubaliane nasi tunapojipumbaza kwa kuzikanyagia chini amri zake za taadhima. Dhambi zetu zinatukandamiza na kumzuia Mungu kuwa mwenye huruma kwetu kwani hatutubu. Badala yake, tunajaribu kulitetea kila chukizo la uharibifu.
15. Mpendwa Bwana Yesu Kristo, iitishe sinodi yako mwenyewe! Njoo katika utukufu wako uwaokoe watumishi wako! Papa na wafuasi wake hawawezi kusaidiwa. Hawakujali wewe hata kidogo. Lakini utusaidie sisi maskini, dhalili, na tunaokukosea, tunapokulilia wewe kwa moyo, jinsi ulivyotupatia neema yako kwa njia ya Roho Mtakatifu, ambaye pamoja nawe, na Baba aishiye na kumiliki, asifiwe milele. Amina.
SEHEMU YA KWANZA
Mafungu Yanayohusu Enzi ya Mungu:
1. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, nafsi tatu tofauti katika ariki na asili moja ni Mungu mmoja, aliyeziumba mbingu na nchi n.k.
2. Baba hakuzaliwa na yeyote, Mwana alizaliwa na Baba, na Roho Mtakatifu alitoka kwa Baba na Mwana.
1159 Mt. 23: 24, Mt. 7: 3-4
3. Mwana peke yake alikuwa mwanadamu, na siyo Baba wala Roho Mtakatifu.
4. Mwana alikuwa mwanadamu kwa njia hii: alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu bila ushirikiano wa mwanadamu, na alizaliwa na Mariamu aliye safi, mtakatifu, na Bikira Daima.1160 Kisha aliteswa, akafa, akazikwa, akashuka Jehanumu, akafufuka kutoka kwa wafu, na akapaa mbinguni; ameketi katika mkono wa kulia wa Mungu, atakuja kuwahukumu walio hai na wafu, jinsi Ukiri wa Mitume, Ukiri wa Athanasio na katekisimo ya kawaida ya watoto vinavyofundisha.
Hakuna majadiliano au mabishano kuhusu mafungu haya kwa sababu pande zote mbili zinayakiri. Kwa hiyo, siyo muhimu kuyaelezea kwa kina zaidi.
SEHEMU YA PILI
Huduma na Kazi ya Yesu Kristo, au Ukombozi Wetu
Fungu la Kwanza Lililo Kuu
1. Yesu Kristo, Mungu wetu na Bwana wetu, “alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki” (Rum. 4:25). 2.Yeye peke yake ni “Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yn.1:29).
“Na BWANA ameweka juu yake maovu yetu sisi sote” (Isa. 53:6). 3. Zaidi, “Wote wamefanya dhambi, wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; katika damu yake n.k.” (Rum. 3:23-25).
4. Haya lazima yaaminiwe na hayawezi kupokelewa au kufahamika kwa tendo lolote, sheria yoyote, au stahili yoyote. Kwa sababu hiyo, ni dhahiri na kweli kabisa kwamba, imani hii peke yake inahesabia haki, jinsi Mt. Paulo anavyosema: “Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria” (Rum. 3:28). Tena: “[Mungu] ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu” (Rum. 3:26).
5. Hakuna lolote katika fungu hili linaloweza kuachwa ama kubadilishwa, hata kama mbingu na dunia na vitu vya muda, vinaweza kuangamia, jinsi Mt. Petro asemavyo: “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Mdo. 4:12). “Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona” (Isa. 53:5).
1160 Kilatini: ‘Semper virgo.’
Mafundisho na maisha yetu yote yanasimama juu ya fungu hili na kwalo, tunampinga Papa, Ibilisi, na dunia. Hatuna budi kuwa imara kabisa juu ya haya. La sivyo, yote yatapotea, hivyo Papa, Ibilisi na wapinzani wetu wote watakuwa na uhalali wa kutushinda kabisa.
Fungu la Pili: Dhabihu ya Misa
1. Misa1161 iko chini ya Upapa, ni chukizo kubwa mno, na ni uharibifu hasa unaopinga fungu hili kuu. Hata hivyo, imekuwa ibada kuu na yenye kuthaminiwa zaidi ya zingine zote miongoni mwa ibada za miungu ya Upapa. Kwa kuwa inasisitizwa kwamba, tambiko hili au tendo hili la misa – ingawa inaongozwa na fisadi yeyote- linamuweka mtu huru kutoka dhambini, katika maisha ya sasa duniani na huko Purgatorio. Hata hivyo, lazima jambo hili litendwe na MwanaKondoo wa Mungu peke yake, jinsi ilivyoelezwa hapo juu. Hatuwezi kuliepuka au kuliachilia fungu hili hata kidogo, kwa kuwa fungu la kwanza haliruhusu jambo la namna hiyo.
2. Ili wapatikane wafuasi wa Papa walio na busara, mtu angeweza kuongea nao ifuatavyo kwa njia ya kirafiki:
Mbona wanang’ang’ania sana misa zao?
Mbali na yote, ni ubunifu tu wa kibinadamu bila amri ya Mungu. Tunaweza kuuacha ubunifu wote wa kibinadamu kwani Kristo anasema: “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” (Mt. 15:9).
3. Misa haihitajiki. Kwa hiyo, inaweza kuachwa bila kutenda dhambi wala kuwa hatarini.
4. Sakramenti inaweza kupokelewa vizuri zaidi na kwa njia ya heri kulingana na ilivyoasisiwa na Kristo peke yake. Mbona basi, dunia yote inapelekwa kwenye huzuni na matesoni kwa ajili ya mambo yasiyokuwa muhimu na ya kubuniwa, wakati sakramenti inaweza kutolewa kwa njia nyingine na ya heri zaidi?
5. Waacheni watu wahubiriwe hadharani kwamba, misa iliyobuniwa na wanadamu, inaweza kuachwa bila kutenda dhambi. Hakuna mtu atakayehukumiwa kwa ajili ya kutoifuata. Kinyume chake, mtu anaweza kuokolewa vizuri zaidi bila misa. Itakuwaje iwapo misa itaanza kudhoofika, siyo tu kwa umma fidhuli,1162 bali pia kwa mioyo ya watu wote wacha Mungu, walio Wakristo, wenye busara, 1161 Kumbukeni vizuri kwamba, hapa, “misa” inamaanisha dhabihu ya Misa, siyo ibada halisi ya neno na sakramenti jinsi inavyofundishwa katika Ukiri wa Augsburg katika Fungu la Ishirini na Nne (Misa). 1162 Kijerumani: (Chakari mpumbavu).
na wanaomwogopa Mungu? Itakuwaje, hasa wakisikia kwamba, misa ni tendo hatari lililotungwa na kubuniwa bila mapenzi na Neno la Mungu?1163
6. Kwa kuwa, matumizi mabaya yasiyohesabika na yasiyosemezeka yamejitokeza katika dunia nzima kwa ajili ya biashara za misa, yaani, kuuzwa na kununuliwa kwa misa, itakuwa busara kuziacha kabisa. Hii ni kwa sababu ya kuyazuia matumizi mabaya, ingawa zingekuwa na mambo ya kufaa na mazuri. Kama tunaweza kuwa na mambo yote yanayohitajika kwa njia ya lazima, ya kufaa, na imara bila Misa yenyewe, basi, kuna sababu kubwa zaidi za kuziacha daima ili kuyazuia matumizi mabaya mengine kama haya kwani misa yenyewe siyo ya lazima, haina faida yoyote, na ni hatari.
7. Kanuni ya Misa1164 na vitabu vyote vya ufafanuzi wake vinaonyesha kwamba, misa haiwezi kuwa tendo lolote isipokuwa kazi ya wanadamu, kazi ya watu wabaya ambayo kwayo, mwanadamu anajaribu kujipatanisha yeye mwenyewe na wengine na Mungu na kupata na kuustahili msamaha wa dhambi na neema. Watu hufikiria hivyo wanapojaribu kuipatia maelekezo mema. Je, Misa ingeweza kutolewa kwa kusudi gani lingine? Kwa sababu hiyo, lazima ihukumiwe na iachwe kabisa. Kwasababu, inalipinga fungu la kimsingi wazi kabisa, ambalo linasisitiza kwamba, dhambi zetu zinaondolewa na Mwana Kondoo, Mwana wa Mungu1165 na siyo na mtu mbaya au mcha Mungu anayeiongoza misa na matendo yake.
8. Mtu yeyote akitoa kisingizio kwamba, anatamani kujishirikisha kibinafsi kwa sababu ya uchaji wake mwenyewe, hawezi kuyasema haya kwa dhati. Akitaka kushiriki kwa kweli, ataweza kuipokea sakramenti inavyostahili na ilivyo kama jinsi Kristo alivyoiasisi. Kujishirikisha binafsi hakuna uhakika na siyo kwa lazima na kunakataliwa. Mtu anayefanya hivyo, hajui analolifanya kwa sababu anafuata maoni na fikira potovu za wanadamu bila Neno la Mungu.
9. Hivyo, siyo halali, (ingawa mambo mengine yote ni sawa) kwa mtu binafsi kuitumia sakramenti ya Kanisa zima kwa ibada yake binafsi na anaitumia vibaya bila Neno la Mungu na nje ya usharika wa Kanisa.
10. Fungu hili kuhusu misa litakuwa hoja kuu ya sinodi. Ingawa wafuasi wa Papa watakubaliana nasi katika mafungu mengine yote, hawataweza kukubaliana na fungu hili jinsi Kampegio1166 alivyosema huko Augsburg: Angependa zaidi 1163 Aya hii iliingizwa katika toleo la mwaka wa 1538. 1164 Kilatini: ‘Canon missae,’ sehemu kuu ya Misa yenye maneno ya Kristo iliyosomwa kimya.
1165 Yn. 1: 29
1166 Lorenzo Campeggio (1474-1539): askofu Mkuu wa Bologna huko Italia; alihudumu mara nyingi kama balozi wa Papa huko Uingereza na Dola la Ujerumani, diwani wa Kaisari Karolo V wakati wa Baraza la Augsburg la mwaka wa 1530.
308
kuraruliwa kabisa kuliko kuiacha misa. Kwa upande wangu na kwa msaada wa Mungu, ningeruhusu kuchomwa moto hadi niwe majivu kuliko kumruhusu kasisi anayeongoza misa kwa matendo yake – awe mwema au mbaya – astahili kuwa sawa na Mwokozi wangu, Yesu Kristo, au awekwe kuwa juu yake. Hivyo basi, tutabakia tumegawanyika milele na kupingana mmoja na mwingine. Wanaelewa jambo hili vizuri: ambapo misa itakapoanguka, Upapa utaangamia pia. Kabla ya kuliruhusu hili litokee, ikiwezekana watatuua sote.
11. Mbali na haya, mkia huu wa joka,1167 yaani, misa, umeuleta uzao wa funza wengi na ibada mbalimbali za miungu na sanamu.
12. Kwanza ni Purgatorio. Walikuwa wamejikita hasa Purgatorioni na katika misa kwa ajili ya wafu, na ibada za mikesha, na misa za baada ya siku ya saba, na siku thelathini, na mwezi mzima baada ya kifo. Kisha, kulikuwa na misa za wiki baada ya Siku ya Mikaeli,1168 Siku ya Nafsi Zote,1169 na kuoshwa nafsi.1170 Misa ilikuwa inatumiwa hasa kwa ajili ya wafu tu, ingawa Kristo aliianzisha sakramenti kwa ajili ya wanaoishi. Kwa sababu hiyo, lazima tuichukulie Purgatorio pamoja na fahari yake yote, ibada, na biashara kuwa udanganyifu mtupu wa Ibilisi kwa maana inalipinga pia fungu kuu kwamba, ni Kristo peke yake aliye msaada wa nafsi na siyo matendo ya mwanadamu. Licha ya hayo, hatuna amri yoyote ya kuabudu kwa ajili ya wafu. Kwa sababu hiyo peke yake, Purgatorio itupiliwe mbali kwani ni uzushi na ibada ya kukufuru.
13. Hapa, wafuasi wa Papa humrejea Agostino na baadhi ya akina Baba wa Kanisa ambao inasemekana kuwa waliandika kuhusu Purgatorio. Wanafikiri kwamba, sisi hatuelewi ni kwa madhumuni na upeo gani waandishi hawa wameandika hivyo matamko yao. Mt. Agostino haandiki kwamba, Purgatorio ipo. Isitoshe, haonyeshi andiko lolote la Maandiko Matakatifu lililoweza kumlazimisha akubaliane nayo hivyo nmeiacha bila ufumbuzi wowote. Anasema tu kwamba, mama yake alimwomba amkumbuke madhabahuni na wakati wa sakramenti.1171 Mambo haya yote yamekuwa maoni ya watu binafsi na hayawezi kulianzisha fungu lolote la imani. Mungu peke yake ana haki ya kufanya hivyo. 14. Lakini wafuasi wetu wa Papa huliingiza neno la kibinadamu katika mambo haya ili watu waliamini soko lao kuu1172 la kashfa, la kukufuru na kulaaniwa kabisa, yaani, uchuuzi wa misa za nafsi na dhabihu kwa ajili ya Purgatorio n.k.
1167 Ufu. 12: 3; 20: 2 1168 Septemba 29. 1169 Novemba 2.
1170 Kuoga kwa watu maskini kulifikiriwa kuwa tendo la ustahili.
1171 Agostino, “Maungamo” (Confessions) 9, 11, 13, 27, 36.
1172 Kijerumani: ‘Jahrmarkt,’ yaani, “soko la mwaka.”
Hawawezi kamwe kupata ushuhuda wa mafundisho haya kutoka kwa Agostino. Kwanza, walifunge soko lao kuu la Misa za Purgatorio, ambalo Mt. Agostino hakulifikiria hata kidogo, ndipo tuweze kujadiliana nao ikiwa tungeweza kuvumilia tamko la Mt. Agostino lisilotokana na Maandiko Matakatifu kuhusu iwapo inawapasa wafu kuadhimishwa katika sakramenti. 15 Siyo halali kulitunga fungu la imani kwa matendo au maneno ya akina Baba Watakatifu. Vinginevyo, vyakula walivyovila, mavazi waliyoyavalia, aina za nyumba walimoishi n.k. vingekuwa mafungu ya lazima ya imani kama ilivyotendeka katika masalio ya watakatifu. Neno la Mungu linapaswa kuwa msingi wa fungu la imani na siyo la mwingine yeyote, hata awe malaika.1173
16. Pili, kwa sababu ya haya, mashetani wameuanzisha uhuni mwingi unaoonekana kama nafsi za wanadamu zinazodai misa, mikesha, hija na sadaka zingine1174 kwa uongo na ujanja usioelezeka. 17. Sisi sote tuliuona uhuni huu kama mafungu ya imani na tuliishi kulingana nayo. Papa aliyathibitisha pia mambo kama haya, misa na machukizo mengine yote. Hapa pia, makubaliano wala maafikiano hayataweza kuwepo.
18. Tatu, ni hija.1175 Hapa pia, watu walitafuta misa, msamaha wa dhambi, na neema ya Mungu kwani misa ilikitawala kila kitu. Ni hakika kabisa kwamba, hija bila Neno la Mungu hazikuamriwa na hazihitajiki kwa sababu tunaweza kutenda mambo mengine mema bila dhambi na hatari. Mbona basi, wanazitelekeza sharika zao wenyewe, Neno la Mungu, wake na watoto, ambavyo ni vya lazima na agizo la Mungu na baada ya hayo, hukimbia kuitafuta hii mianga ya moto wa Ibilisi isiyohitajika, isiyo na hakika, na yenye hasara? 19. Wanafanya hivyo kwa sababu Ibilisi amemchochea Papa kusifia na kukubaliana na matendo haya ili umma mkubwa umwache Kristo na kuanguka katika matendo yao wenyewemabaya zaidi ya yote – ya kuwa waabudu miungu na sanamu. Licha ya hayo, ni jambo lisilohitajika, lisiloamriwa, lisiloshauriwa, lisilokuwa la hakika, na lililo la hasara sana. Kwa hiyo, hapa pia makubaliano wala maafikianao hayataweza kuwepo. Badala yake, ihubiriwe kwamba, hija hazihitajiki na ni hatari sana. 20. Halafu tutaona ikiwa zitadumu au la.
1173 Gal.1: 8. Aya hii iliingizwa katika toleo la mwaka wa 1538.
1174 Kwa mfano, Papa Gregorio Mkuu (mnamo 540-604) na Dk. Petro Damiano (mnamo 1007-1072) walielezea kuhusu njozi za namna hiyo
1175 Kilatini: ‘Peregrinatio,’ Kijerumani: ‘Wallfahrt.’
21. Nne, ni Udugu. Hapa, Nyumba za watawa, taasisi,1176 mapadre wadogo,1177 na makasisi wamejiwajibisha wenyewe kuzitoa misa zote kwa mapatano ya kibiashara, matendo mema n.k kwa faida ya watu walio hai na wafu. Mambo haya yote siyo tu ubunifu wa mwanadamu usiokuwa na Neno la mungu, bali pia hayahitajiki na hayaamriwi. Badala yake, yanalipinga Fungu la Kwanza kuhusu wokovu. Kwa hiyo, hayawezi kuvumiliwa kwa hali yoyote.
22. Tano, ni masalio ya watakatifu. Kuhusiana na hili, udanganyifu na upuuzi mwingi umezuliwa kuhusu mifupa ya mbwa na farasi. Mambo hayo yamemfanya hata Ibilisi mwenyewe acheke. Ingawa yalikuwa na mambo mengine mazuri, masalio ya watakatifu yalipaswa kushutumiwa tangu zamani. Hayatokani na Neno la Mungu, hayana amri, hayajashauriwa, hayahitajiki kabisa, na hayana faida yoyote! 23. Hata hivyo, jambo lililo baya zaidi ya yote ni dai la kwamba, masalio ya watakatifu huleta upatanisho na msamaha wa dhambi mithili ya misa na kwamba, matumizi yake ni matendo mema na huduma ya Mungu.
24. Sita, ni vyeti vyenye thamani vya upatanisho.1178 Vinavyotolewa – kwa pesa - kwa ajili ya walio hai na wafu. Hapa, Papa dhalili, aliye Yuda Iskarioti, anauza stahili za Kristo, stahili tele za watakatifu wote, na za Kanisa zima. Haya hayawezi kuvumiliwa hata kidogo! Biashara hii haitokani na Neno la Mungu, haihitajiki na haina amri maalumu. Licha ya hayo, inalipinga Fungu la Kwanza. Maana, stahili za Kristo haziwezi kununuliwa kwa matendo yetu wala kwa hela zetu. Badala yake, zinapokelewa kwa imani, kwa neema peke yake, na bila fedha au stahili yoyote. Hazipokelewi kwa njia ya uwezo wa Papa bali kwa njia ya mahubiri ya Neno la Mungu.
Maombezi ya Watakatifu
25. Maombezi ya watakatifu ni mojawapo ya matumizi mabaya ya Mpinga Kristo. Yanalipinga kabisa Fungu Kuu la Kwanza na yanadhoofisha kabisa ufahamu wa Kristo. Maombezi haya ya watakatifu hayakuamriwa wala hayakushauriwa na Maandiko Matakatifu. Hatuna mfano wake wowote. Ingawa maombezi ya namna hii yalikuwa na thamani, (ambayo hayana) tuna kila lililo jema mara elfu katika Kristo.
1176 Taasisi maalumu zilianzishwa tangu karne ya nane katika nyumba fulani za watawa na katika makanisa makuu ya dayosisi fulani. Wajumbe wa taasisi za namna hiyo waliokuwa mapadre na Wakristo wa kawaida pia, waliwajibika kwa mapatano rasmi, kusali kwa ajili ya ndugu wafu na kutenda matendo mema kwa ajili ya nafsi zao.
1177 Kilatini: ‘Vicarista,’ Kijerumani: ‘Vikarist:’ waliitwa pia ‘Altaristen,’ “mapadre wa madhabahu,” waliokuwa mapadre wa cheo cha chini katika makanisa makuu.
1178 Kilatini: ‘Indulgentia.’
26. Kweli, mbinguni malaika wanatuombea jinsi Kristo mwenyewe anavyofanya, na jinsi watakatifu wanavyofanya pia hapa duniani na labda huko mbinguni. Lakini hilo, halimaanishi kwamba, tunapaswa kuwaomba malaika na watakatifu, kufunga kwa ajili yao, kuadhimisha sherehe kwa ajili yao, kuziongoza misa, kuwatolea sadaka, kuyaanzisha makanisa, kuyaanzisha madhabahu, na ibada kwa ajili yao, kuwatumikia, kuwachukulia kama wasaidizi wakati wa shida, kudhania kwamba, wanatupatia misaada mbalimbali na kwamba, kila mmoja ana aina maalumu ya msaada, jinsi wafuasi wa Papa wanavyofundisha na kutenda. Haya yote ni kuiabudu miungu na sanamu. Ni Mungu peke yake anayestahili heshima kama hiyo. 27. Kama Mkristo na mtakatifu hapa duniani, unaweza kuniombea, siyo tu katika aina moja ya shida bali katika matatizo yote. Lakini kwa sababu hiyo, haimaanishi kwamba, ninapaswa kukuabudu, kukuomba, kufunga, kuadhimisha sherehe, kuiongoza misa, kuzitoa sadaka kwa heshima yako, au kukutegemea kwa ajili ya wokovu wangu. 28. Ninaweza kukuheshimu, kukupenda na kukushukuru kwa njia zingine katika Kristo. Malaika na wafu watakatifu wakinyimwa heshima hii ya kukufuru, heshima inayobakia haitakuwa na hasara yoyote na itasahauliwa upesi.1179 Wakati faida, msaada wa kiroho na wa kimwili hautatarajiwa, watakatifu watakoma kusumbuliwa makaburini mwao au mbinguni, kwani, labda hakuna atakayewakumbuka sana, atakayewaheshimu, na atakayewaenzi bure au kwa ajili ya upendo wakati hakuna matarajio ya kupata manufaa.
29. Muhtasari: Hatuwezi kuivumilia bali lazima tuilaani misa na yote iliyoyazaa na yanayofungamana nayo. Tunafanya hivyo ili tupate kuihifadhi sakramenti takatifu katika usafi na uhakika wake kulingana na kuanzishwa na Kristo kwamba, tunaweza kuitumia na kuipokea katika imani.
Fungu la Tatu:
Taasisi za Kanuni za Makanisa Makuu na Nyumba za Watawa
1. Taasisi za kikanuni na nyumba za watawa zilizoanzishwa zamani kwa kusudi jema, yaani, kuwaelimisha wanaume wasomi na wanawake wa staha, lazima zirudishwe tena katika matumizi ya asili ili tupate wachungaji, wahubiri, na wahudumu wengine wa Kanisa. Isitoshe, ili tupate pia watumishi wa serikali tawala katika miji na mikoa. Kadhalika, wasichana waliostaarabika vizuri wawe akina mama, watunzaji wa nyumba n.k.
1179 Kilatini: ‘Collegium canonicorum,’ mashirika ya mapadre wasiokuwa watawa katika makanisa makuu ya dayosisi zenye shabaha za kutunza shule.
2. Kama hawakubali kuhudumu hivyo, itafaa kuziacha taasisi na nyumba hizo za watawa au kuzibomoa kabisa. Hatuwezi kuzihifadhi nyumba hizi na ibada zao za kukufuru zilizobuniwa na wanadamu zinazodai kuwa bora zaidi kuliko Ukristo wa kawaida, kuliko huduma, na kuliko wito wa maisha ulioanzishwa na Mungu. Mambo haya yote yanapingana na Fungu Kuu la Kwanza linalohusu wokovu katika Yesu Kristo. Licha ya hayo, kama ubunifu mwingine wa mwanadamu, haya yote hayajaamriwa na Mungu, hayahitajiki, na hayana faida. Isitoshe, husababisha jitihada hatari zisizokuwa na mwisho na kwa sababu hiyo, manabii wanaita ibada ya mungu ya jinsi hiyo “aven,” yaani, “ubatili.”1180
Fungu la Nne: Upapa
1. Kulingana na haki ya kimungu yaani, Neno la Mungu Papa si mkuu wa Ukristo wote. Kwa maana cheo hiki ni cha mtu moja tu aitwaye Yesu Kristo.1181 Papa ni askofu tu na mchungaji mkuu wa makanisa katika Roma na makanisa mengine yaliyojiunga naye kwa hiari au kwa njia ya asasi za kibinadamu, yaani, serikali ya dunia. Makanisa haya hayakuchagua kuishi chini yake kama chini ya kabaila fulani, bali yalichagua kusimama pamoja naye kama ndugu Wakristo na washirika kulingana na udhibitisho wa sinodi za zamani na za wakati wa Mt. Sipriano.1182 2. Lakini siku hizi, hakuna askofu anayethubutu kumwita papa “ndugu” kama jinsi ilivyokuwa desturi wakati huo. Badala yake, anamwita papa, “bwana mwenye huruma nyingi,” kana kwamba, yeye alikuwa Kaisari au mfalme. Hatutataka, hatutawajibika na hatutaweza kuzitwika dhamiri zetu mzigo huu. Mtu anayetaka kufanya hivyo, afanye tu lakini bila kututegemea!
3. Kwa sababu hiyo, inaelekea kwamba, mambo yote yaliyotekelezwa na kuanzishwa na Papa kwa mamlaka yake bandia, ya kuchukiza, ya kukufuru, na ya kujitwalia, yamekuwa, na bado yanaendelea kuwa matendo na hila tupu za Ibilisi. Kwa njia hii basi, ameendelea kuliharibu Kanisa Takatifu lote na kulikataa Fungu
Kuu la Kwanza linaloelezea kuhusu wokovu uliotekelezwa na Yesu Kristo, kwa nguvu zake zote, isipokuwa mambo yanayohusu serikali ya dunia ambapo, wakati mwingine, Mungu huyaruhusu mazuri mengi kuja kwa njia ya wadhalimu na watu waovu.
4. Kama ushuhuda wa hali ya mambo, matangazo na vitabu vyote vya Papa vina maandiko ambayo kwayo, ananguruma kama simba jinsi malaika
1180 Isa. 1: 13; 29: 20; 41: 29; Zek. 10: 2; Hab. 1: 3
1181 Efe. 1: 22; 4:15; 5: 25; Kol. 1: 18
1182 Sipriano, Askofu Mkuu wa Karthago Kaskazini mwa Afrika aliyeuawa kwa ajili ya imani yake mwaka wa 258. Kulingana na mafundisho ya Sipriano, Askofu wa Roma alistahili heshima maalumu. Hata hivyo, bila mamlaka yoyote juu ya maaskofu wengine wote.
anavyopendekeza katika sura ya kumi ya Kitabu cha Ufunuo.1183 Anadai kwamba, hakuna Mkristo yeyote anayeweza kuokolewa isipokuwa amtii Papa na ajitiishe kwake katika yote anayoyataka, anayosema, na anayoyafanya. Hii ni kama kusema: “Ingawa unamwamini Kristo, na katika yeye una kila kitu unachokihitaji kwa ajili ya wokovu, haya ni bure na si kitu kabisa isipokuwa unihesabie mimi kama mungu wako, unitii, na unitegemee.”1184 Lakini ni wazi kwamba, Kanisa Takatifu lilikuwa bila Papa kwa karibu karne tano na zaidi.1185 Mpaka sasa, Kanisa la Ugiriki na makanisa ya mataifa mengine, kamwe hayajawa chini ya Papa. 5 Jinsi ilivyosemwa mara nyingi, ni dhahiri kabisa kwamba, upapa ni jambo lililobuniwa na wanadamu. Halijaamriwa na Mungu, halihitajiki, na halina maana kabisa. Kanisa Takatifu la Kikristo linaweza kudumu vyema bila kiongozi wa namna hiyo na kwa hakika, lingebakia kuwa imara zaidi kama kiongozi wa jinsi hiyo asingeinuliwa na Ibilisi. 6. Upapa haulifaidishi Kanisa hata kidogo kwa sababu hautumii huduma yoyote ya Kikristo. Kwa hiyo, Kanisa lazima liendelee kuwepo bila Papa.
7. Chukulia kwamba, Papa angekoma kudai kwamba yeye ni kiongozi mkuu wa Kanisa kwa haki ya kimungu, au kwa amri ya Mungu; chukulia kwamba, tungehitaji kiongozi ambaye wengine wote wangeshikamana naye ili kuulinda umoja wa Ukristo dhidi ya madhehebu fulani na uzushi; chukulia kwamba, wanadamu wangemchagua kiongozi huyo, chukulia kwamba, wangekuwa na haki na hiari ya kumbadilisha au kumwondoa madarakani. Hii ndiyo njia iliyofuatwa na Sinodi ya Konstanzo.1186 Iliwaondoa mapapa watatu mamlakani na kumteua wa nne.1187 Nikisema, Papa na Kiti cha Roma wangeliafiki na kulikubali hili, ambalo haliwezekani, inamaanisha kwamba, mamlaka na cheo chake vingeangushwa na kuharibiwa kabisa, pamoja na haki zake zote na kujidai. Kwa ufupi, hawezi kufanya hivyo. Hata kama ingewezekana, Ukristo usingesaidiwa kwa njia yoyote.
8. Kinyume chake, idadi ya madhehebu mbalimbali ingeongezeka zaidi kuliko zamani. Kwa sababu siyo, lazima kuwa chini ya kiongozi huyo kwa ajili ya agizo la Mungu, lakini kwa sababu ya anasa ya mwanadamu, kiongozi huyu
1183 Ufu. 10: 3. Luther aliandika sura ya 12 ya Ufunuo wa Yohana. Kosa hili lilirekebishwa hapa.
1184 Tangazo la Papa Bonifasio VIII mwaka wa 1302 ‘Unam sanctam’ (Kanisa moja takatifu): ‘Porro subesse Romano pontifici omni humanae creaturae . . . omnino esse de necessitate salutis’ – (Hasa kuwa chini ya Kuhani Mkuu wa Roma ni lazima kwa kila binadamu kwa ajili wokovu).
1185 Luther aliuhesabu muda huu hadi upapa wa Gregorio Mkuu (590-604).
1186 Huko Ujerumani miaka ya 1414-1418.
1187 Papa Yohana XXIII aliuzuliwa Mei20, mwaka wa 1415. Papa Gregorio XII aling’atushwa upapa Julai 4, mwaka wa 1415. Benedikto XIII aliondolewa madarakani Novemba 11, mwaka wa 1417.
atadharauliwa kwa urahisi sana na upesi na mwishowe atabakia bila wafuasi wowote. Mkuu wa jinsi hiyo hatahitajika daima kubakia huko Roma au mahali penginepo pa kudumu.1188 Badala yake, mahali hapo pangeweza kuwa popote na katika kanisa lolote ambapo Mungu angemwinua mtu hodari kwa huduma hiyo. Hii ingekuwa ni hali ya kuchanganya na kutatiza kwa namna gani!
9. Kwa sababu hiyo, Kanisa haliwezi kutawaliwa na kudumishwa vyema zaidi, isipokuwa sote tuwe chini ya kiongozi mmoja, yaani, Kristo, maaskofu wote wawe sawa katika huduma yao, ingawa vipaji vyao vinatofautiana, waunganishwe kwa juhudi katika umoja wa mafundisho, imani, sakramenti, sala na matendo ya upendo. Mt. Hieronimo mwenyewe anaandika1189 kwamba, makasisi wote waliyaongoza makanisa huko Aleksandria kwa pamoja. Mitume walifanya vivyo hivyo na baada yao, maaskofu wote katika mataifa yote ya Wakristo walizifuata nyayo zao mpaka Papa alipokiinua kichwa chake juu yao wote.
10. Fungu hili linaonyesha kwa uwezo mkubwa kwamba, Papa ndiye Mpinga Kristo1190 halisi ambaye amejiinua mwenyewe na kujiweka kinyume na Kristo. Kwa kuwa, Papa hatawaruhusu Wakristo waokolewe isipokuwa kwa mamlaka yake, ambayo hayana maana kabisa kwa vile hayakuasisiwa wala hayakuamriwa na Mungu.1191 11. Haya ndiyo hasa Mt. Paulo aliyoyaita kujiinua mwenyewe juu ya na dhidi ya Mungu. Hata Waturuki ama wakaidi wengine,1192 ambao wana uadui mkubwa dhidi ya Wakristo, hawafanyi hivyo. Wao humruhusu kila mmoja anayetaka kumwamini Kristo, na wanaipokea sifa ya kimwili1193 na utiifu kutoka kwa Wakristo.
12. Lakini, Papa hatairuhusu imani ya jinsi hiyo bali anadai kwamba, lazima mtu amtii ili aweze kuokolewa. Hatutalikubali hili hata kama itatupasa kufa kwa ajili ya jina la Mungu. 13. Haya yote ni matokeo ya Papa kutaka kuwa kiongozi wa Kanisa la Kikristo kwa njia ya haki ya kimungu.1194 Kwa sababu hiyo, mwenyewe alilazimika kujiweka katika cheo sawa na cha juu zaidi kuliko Kristo. Isitoshe, alitaka ajitangaze mwenyewe kama kiongozi na bwana wa Kanisa, na
1188 Kitala cha Papa kilikaa huko Ufaransa katika mji wa Avignon miaka ya 1309-1377 kwa sababu mfalme wa Ufaransa Mrembo Filipo IV alimshika Papa na alimfunga katika Avignon, Mkoa wa Provence, Kusini mwa Ufaransa. Wakati huu ambapo Papa alikuwa chini wafalme wa Ufaransa, uliitwa “Mateka ya Babeli.”
1189 Comm. In Ep. Ad Titum 1, 56; Ep. 146.
1190 Luther anatumia istilahi mbili hapa. ‘Endchrist,’ yaani, “Kristo wa wakati wa mwisho,” na ‘Widerchrist,’ yaani, “Mpinga Kristo.”
1191 2 The. 2: 4
1192 Luther, ‘der Turke noch Tatter.‘ Waturuki ni taifa moja la makabila ya Watartari. Kwake Luther, ‘Waturuki na Watartari’ ni istilahi moja inayomaanisha maadui Waislamu wa Ukristo.
1193 ‘Jizya.’ ‘Jizya.’
1194 Kilatini: ‘Iure divino.’
kama mtawala wa dunia yote. Hatimaye, aliudai uungu wa dunia hii na hata alithubutu kuwaamrisha malaika wa ufalme wa mbinguni.1195
14. Basi, tunapotofautisha baina ya mafundisho ya Papa na Maandiko Matakatifu, ama yanapolinganishwa, inadhihirika kwamba, mafundisho ya Papa, hata yakiwa bora zaidi, yametokana na sheria za upagani wa kaisari wa Roma. Isitoshe, ni mafundisho yanayohusu shughuli na hukumu za kidunia jinsi mikusanyiko ya matamko yake rasmi1196 inavyoonyesha. Mafundisho haya ya papa yanatolewa kuhusu sherehe za makanisa, mavazi, vyakula, wahudumu, michezo ya watoto, shere za vinyago/mazingaombwe, michezo ya upumbavu na mengine mengi yasiyohesabika, bila kumtaja Kristo, imani na amri za Mungu.
Hatimaye, jinsi Ibilisi mwenyewe alivyojiinua dhidi ya Mungu, ni kama Papa anavyoyatangaza mambo dhidi ya uongo wake kuhusu misa, Purgatorio, maisha ya utawa, matendo ya kibinadamu, na ibada zilizobuniwa na wanadamu,. Haya yote ni kiini cha Upapa na yaliyo kinyume na Mungu. Papa wa Roma huendelea kuwalaani, kuwaua, na kuwatesa Wakristo wote wasioyasifu na kuyaheshimu machukizo yake ya mambo yaliyotajwa hapo juu. Kwa hiyo, hatuwezi kumwabudu Ibilisi mwenyewe kama bwana au Mungu wetu. Vivyo hivyo, mtume wake, Papa au Mpinga Kristo hawezi kututesa wala hawezi kututawala kama kiongozi au bwana. Hii ni kwa sababu, utawala wake ni wa uongo, uuaji, na maangamizi ya milele ya mwili na nafsi jinsi nilivyoelezea katika vitabu vingi.
15. Mafungu haya manne yatakuwa na mambo ya kutosha ya kulaaniwa katika sinodi yao. Maana, hawataweza wala hawatakubaliana nasi kuhusu kipengele kidogo sana cha mafungu haya. Hatuna budi kuliamini jambo hili na kutumainia kwamba, Bwana wetu Yesu Kristo amewashambulia maadui zake na atalikamilisha kusudi lake kwa njia ya Roho wake na kuja kwake. Amina.
16. Hatutasimama katika sinodi mbele ya Kaisari au mamlaka ya dunia, jinsi tulivyofanya katika Baraza la Augsburg, ambapo tuliitwa kwenye shauri kwa barua rahimu ya Kaisari, na ambapo tulisikilizwa kwa uadilifu. Badala yake, tutasimama mbele ya Papa na Ibilisi mwenyewe, ambaye hakusudii kutusikiliza bali kutuhukumu, kutuua, na kutushurutisha tuziabudu sanamu. Kwa sababu hiyo, hapa, hatupaswi kuibusu miguu yake au kusema, “Wewe u bwana wangu rahimu!” Lakini, hatuna budi kusema jinsi malaika alivyosema kwa Ibilisi katika
1195 Tangazo la Papa Klemens VI la mwaka wa 1346 lililoelezea kwamba, Papa aliwaamrisha malaika wa mbinguni kubeba nafsi za Wakristo watakaokufa wakati wa hija kwenda Roma mwaka maalumu wa 1350.
1196 “Tamko rasmi,” Kilatini, ‘Decretum.’ Mikusanyiko ya matamko ya papa iliitwa ‘Decretales.’
kitabu cha Zekaria: “BWANA na akukemee Ewe Shetani” (Zek. 3:2).
SEHEMU YA TATU
Mafungu yafuatavyo yanashughulikia masuala ambayo huenda tutayajadili na wataalamu na watu wenye busara, au hata miongoni mwetu wenyewe. Kwa kuwa, Papa na ufalme wake haujali lolote kuhusu masuala haya. Hajishughulishi na masuala ya nafsi, bali fedha, heshima na mamlaka peke yake.
I. Dhambi
1. Kwanza ni kuhusu dhambi: hapa hatuna budi kukiri jinsi Mt. Paulo asemavyo katika Rum. 5:12, kwamba, dhambi imetokana na mwanadamu mmoja, yaani, Adamu. Kwa ajili ya kukaidi kwake, wanadamu wote wamekuwa wenye dhambi na wamewekwa chini ya kifo na Ibilisi. Hii inaitwa dhambi ya asili au dhambi kuu.
2. Matunda ya dhambi ya asili ni matendo maovu ambayo yanakatazwa na Amri Kumi za Mungu. Nayo ni kutoamini, imani potovu, kuabudu sanamu, kutomcha Mungu, kiburi, kutomtumainia Mungu, kukata tamaa, na upofu wa kiroho. Kwa ufupi, ujinga na kutomjali Mungu. Pili ni uongo, kuapa vibaya kwa jina la Mungu, kuliacha Neno la Mungu, kuacha kuomba, kutoliitia jina la Mungu, kulidharau Neno la Mungu, kutowatii wazazi, mauaji, uchafu, wizi, udanganyifu n.k.
3. Dhambi hii ya asili ni upotovu mkubwa na mbaya zaidi kiasi kwamba, hatuwezi kuutambua kwa akili zetu, bali lazima tuamini kwa njia ya ufunuo wa Maandiko Matakatifu (Zab. 51:5; Rum. 5:12 n.k; Kut. 33:20; Mwa. 3:6 n.k). Kwa sababu hiyo, mafundisho ya Madaktari Wanazuoni1197 ni uzushi na upofu mtupu kabisa wa kupambana na fungu hili:
4. i. yaani kwamba, baada ya kuanguka kwa Adamu, uwezo wa asili ya mwanadamu unabakia kuwa timamu bila kupotoshwa na kwamba, kutokana na asili yake, mwanadamu ana akili nzuri na nia njema kama jinsi wanafalsafa wanavyofundisha.
5. ii. kadhalika, mwanadamu ana hiari huru1198 ya kuamua ama kuyatenda
1197 Kilatini: ‘Scholastici doctores,’ Kijerumani: ‘Schultheologen.’
1198 Kijerumani: ‘der freie Wille,‘ Kilatini: ‘liberum arbitrium.‘ Istilahi ya Kilatini ‘arbitrium‘ inamaanisha “uamuzi.” Maana ya isitilahi hii ni zaidi ya mwenendo wa nia ya binadamu peke yake; ‘arbitrium.‘ Ni pamoja na nia ya kutamani na uwezo wa kuamua kati ya mambo mema na mabaya, bila lazima ya dhambi ya asili.
6. iii. kadhalika, mwanadamu anaweza, kwa nguvu zake za asili, kuzishika na kuzitimiza amri zote za Mungu.
7. iv. kadhalika, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu kuliko vitu vyote na jirani yake kama nafsi yake mwenyewe kwa nguvu zake za kiasili.
8. v. kadhalika, mwanadamu akifanya awezavyo, Mungu atamjalia neema yake kweli.
9. vi. kadhalika, mtu anapokwenda kwenye sakramenti, hahitaji kuwa na makusudio mema. Inatosha kwamba, hana makusudio mabaya ya kutenda dhambi, kwa vile huo ndio wema wa asili ya mwanadamu na hiyo ndiyo nguvu ya sakramenti.
10. vii. Kwamba haijaandikwa katika Maandiko Matakatifu kuwa, Roho Mtakatifu na vipawa vyake ni muhimu kwa ajili ya kutenda tendo jema.
11. Madai haya na mengine mengi yanatokana na upungufu mzima wa ufahamu na ujuzi wa dhambi na Kristo aliye Mwokozi wetu. Upungufu wa namna hii ni mafundisho ya kipagani kabisa, ambayo hatuwezi kuyavumilia. Kama mafundisho haya yangekuwa ya kweli, Kristo angekuwa amekufa bure, kwa kuwa tatizo ama dhambi yoyote haingekuwemo ndani ya mwanadamu ambayo lazima Kristo angeifia. Au vinginevyo, angekufa kwa ajili ya mwili tu na siyo nafsi ilihali nafsi ingekuwa nzima na mwili tu ndio ungekuwa chini ya kifo.
II. Sheria
1. Kwanza kabisa, hapa tunasisitiza kwamba, sheria ilitolewa na Mungu ili kuzuia dhambi kwa upande mmoja, kwa vitisho vya kuogofya vya adhabu na kwa upande nwingine, kwa ahadi za neema na fadhili. Lakini shabaha hii ilishindikana kabisa kwa sababu ya uovu ambao dhambi iliuleta ndani ya mwanadamu. 2. Kwa upande mwingine, watu wengine wamekuwa waovu zaidi kwa sababu ya uadui wao wa kupambana na sheria, kwa kuwa inawakataza yale wapendayo kuyafanya na kuyaamuru yale wasiyopenda kuyafanya. Kwa sababu hiyo, wanaendelea zaidi na zaidi kutenda kinyume na madai ya sheria kwa vile wanaweza kufanya hivyo bila hatari ya adhabu. Hawa ni watu wakorofi na waovu wafanyao uovu wakati wowote wanapopata nafasi. 3. Wengine huwa vipofu kwa ajili ya kiburi wakiwaza kwamba, wanaweza kushika sheria kwa nguvu zao wenyewe, jinsi ilivyoelezewa hapo juu kuhusu madaktari wanazuoni. Wao hujisingizia tu unafiki na utakatifu bandia kabisa.
318 mema au kuyaacha yaliyo mabaya.
4. Lakini kazi au nguvu kuu ya sheria ni kukashifu dhambi ya asili pamoja na matunda yake na kumwonyesha mwanadamu kina kisichopimika cha anguko la asili yake na uharibifu wake. Kwahiyo, sheria lazima imwambie kwamba, hana Mungu bali anaiabudu miungu ya kigeni, jambo ambalo hangeliamini kabla na bila ujuzi wa sheria. Kwa njia hii basi, anaanza kuogopa, kunyenyekea, kukata tamaa, na kufa moyo. Ana hamu sana ya kupata msaada lakini bila kujua atakapoupata msaada huu. Anaanza kumchukia Mungu na kunung’unika. Hii ndiyo maana ya Rum. 4:15: “Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira,” na ya Rum. 5:20: “Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana.”
III. Toba
1. Agano Jipya linahifadhi na kutekeleza huduma hii ya sheria kama jinsi Paulo pia afanyavyo na kusema katika Rum. 1:18: “Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu!” na katika Rum. 3:19-20: “Na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria.” Kristo anasema pia katika Yn. 16:8: “Naye akiisha kuja, huyo ataudhibitishia ulimwengu kwa habari ya dhambi.”
2. Hii ndio radi ya Mungu ambayo kwayo, anawaangusha katika chungu kimoja wote watendao dhambi hadharani na wanafiki pia na kutomruhusu mtu yeyote kujihesabia haki na kuwafanya wote wawe katika hali ya hofu kuu na kufa moyo. Hii ndiyo nyundo ambayo Yeremia anaizungumzia anaposema: “Je! Neno langu si kama moto? asema BWANA; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?” 1199 Hii siyo toba iliyobuniwa, yaani, “activa contritio”-(majuto ya bandia), bali ni “passiva contritio” – (majuto ya yanayotendwa kweli), yaani, maumivu makali ya kweli moyoni, mateso, na maumivu ya kifo.
3. Huu ndio mwanzo wa toba ya kweli. Hapa, mtu hana budi kuisikia hukumu: “Ninyi nyote ni ubatili tu mkiwa wakosaji au watakatifu. Hamna budi kubadilishwa kabisa na kuwa tofauti na mlivyo sasa na kutenda tofauti kuliko sasa bila kujali ninyi ni nani, kuwa wakuu kiasi gani, kuwa wenye hekima, kuwa na mamlaka, na kuwa watakatifu mlivyojifikiria. Hapa hakuna hata mmoja mwenye haki.”
4. Lakini Agano Jipya linaunganisha kwa mara moja faraja na ahadi ya neema ya Injili na huduma hii ya sheria ambayo ni ya kuaminiwa jinsi Kristo asemavyo katika Mk. 1:15: “Tubuni, na kuiamini Injili,” yaani, “ni afadhali kubadilika
1199 Yer. 23: 29
na kutenda tofauti na kuiamini ahadi yangu.” 5. Yohana aliyemtangulia Kristo, anaitwa pia mhubiri wa toba lakini kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Yaani, ilimpasa Yohana awashutumu wote na kuwathibitishia kuwa wenye dhambi ili wapate kujua hali yao mbele za Mungu. Yaani, wajitambue kuwa watu waliopotea. Kwa njia hii, watakuwa wametayarishwa kwa Bwana, yaani, watakuwa tayari kuipokea neema, kuongoka, na kuupokea msamaha wa dhambi kutoka kwake. 6. Kadhalika, Kristo mwenyewe anasema katika Lk. 24:47: “Na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi.”
7. Lakini pale ambapo sheria peke yake inaitunza huduma yake bila Injili, kuna kifo na jehanumu tu na mwanadamu hana budi kufa moyo kama Sauli na Yuda.1200 8. Mt. Paulo anasema kwamba, sheria inaleta mauti kwa njia ya dhambi.1201 Kinyume chake, Injili huleta faraja na msamaha, siyo kwa njia moja tu, bali kwa Neno na Sakramenti n.k.; kama jinsi tutakavyosikia zaidi kwamba, kwake Mungu kuna ukombozi mwingi kutoka katika gereza la dhambi jinsi Zab. 130:71202 inavyosema.
9. Sasa basi, inatubidi kulinganisha toba bandia ya wataalamu wa ghiliba1203 wanaopambana na toba ya kweli ili hizi zote mbili ziweze kueleweka vizuri.
Toba Bandia ya Wafuasi wa Papa
10. Wafuasi wa Papa hawakuweza kabisa kufundisha kuhusu toba kwa usahihi kwa sababu hawakufahamu dhambi ni nini hasa. Jinsi ilivyoelezewa hapo juu, hawakuwa na mafundisho halisi kuhusu dhambi ya asili. Badala yake, wao husisitiza kwamba, welekewu wa asili wa mwanadamu umeendelea kuhifadhiwa kuwa mzima na usio na uharibifu wowote. Hivyo, Akili ina uwezo wa kuelezea vizuri na nia inaweza kutenda vizuri ipasavyo. Lakini, kwa hakika, Mungu anaitoa neema yake jinsi mtu anayefanya kadiri awezavyo kutenda kulingana na hiari yake huru.
11. Kutokana na mafundisho haya, inafuata kwamba, watu walitubu tu makosa ya matendo mabaya kama mawazo mapotovu waliyoyakubali na pia maneno na matendo mabaya, ambayo nia huru ingeweza kuyaepuka. Msukumo mbaya, tamaa mbaya na mwelekeo havikuchukuliwa kuwa dhambi. 12. Waliigawanya
1200 1 Sam. 28: 20; 31: 34; Mt. 27: 3-5
1201 Rum. 7: 10
1202 Toleo la Vulgata, Zab. 129
1203 Kijerumani: ‘Sophist,’ Kilatini: ‘Sophista.’ Awali, istilahi hii ilimaanisha “mwanafalsafa” na “mwalimu wa balagha” huko Uyunani. Katika majadiliano ya Sokrate na wanafunzi wake (manamo 470-399), istilahi hii ilipata maana yake mbaya. Luther aliitumia istilahi hii ili kumaanisha madaktari wanazuoni.
toba kama hii katika sehemu tatu: majuto makubwa,1204 ungamo, na upatanisho. Faraja na ahadi viliambatishwa hapo: mtu akitubu kwa njia iliyo sawa, akiungama dhambi na kufanya upatanisho, ataustahili msamaha wa dhambi na atakuwa amezilipia dhambi zake mbele za Mungu. Hivyo ndivyo, walivyowaongoza watu wayategemee matendo yao wenyewe kama wakitubu. 13. Kutoka hapo, neno hili lililosemwa mimbarini wakati wa ungamo la hadhara, likisomwa: “Bwana Mungu, uongeze wakati wa maisha yangu mpaka nitakapopata fursa ya kutubu dhambi zangu na kuyarekebisha maisha yangu.”1205
14. Hapa, hakuna wazo lolote kuhusu Kristo wala imani. Badala yake, watu walitarajia kwamba, wangeupata ushindi na wangezifuta dhambi zao mbele za Mungu kwa matendo yao wenyewe. Sisi pia tulikuwa makasisi na watawa kwa lengo hili ili wenyewe tuweze kuipinga dhambi.
15. Majuto makubwa1206 yalifanyika hivi: kwa kuwa hakuna yeyote aliyeweza kuzikumbuka dhambi zake zote, angalau zile alizozitenda mwaka mzima, waliukimbilia mwanya wao: yaani dhambi iliyofichika ikigunduliwa baadaye, lazima pia itubiwe na iungamwe n.k. Lakini wakati huo huo, mtu mwenye dhambi aliwekwa chini ya neema ya Mungu.
16. Kwa kuwa hakuna mtu aliyejua ni kiasi gani cha majuto kilichoweza kutosha mbele za Mungu, watu walifarijiwa hivi: mtu asiyeweza kuwa na majuto makubwa (‘contritio’) angalau lazima awe na majuto madogo (‘attritio’) ambayo ninaweza kuyaita toba nusu au chimbuko lake. Hata mmoja hakuelewa wala bado haelewi maana ya maneno haya jinsi mwenyewe nisivyoyaelewa pia. Hata hivyo, majuto haya madogo yalikubaliwa kuwa kipimo cha kuyapimia majuto makubwa.
17. Mtu akisema kwamba, hakuweza kutubu au kujutia dhambi zake, k.m. uasherati kulipiza kisasi, au mengineyo, aliulizwa kama angetamani au angetaka kutubu akasema “ndiyo,” (kwani ni nani isipokuwa Ibilisi ambaye angesema hapana), waliuruhusu ukubalifu huu kuhesabiwa kama majuto makubwa na walimsamehe dhambi zake kwa ajili ya tendo hili. Walilalama hapa kama jinsi alivyofanya Mt. Bernardo.1207
1204 Kilatini: ‘Contritio.’
1205 Kilatni: ‘Prolonga, Deus, vitam meam, donec pro meis peccatis satisfecero et vitam meam emendavero.’ Ombi hili lilitumiwa angalau karne ya kumi na lilitolewa na padre kwa niaba ya usharika mwishoni mwa hotuba yake.
1206 Kijerumani: ‘Reu.’
1207 Bernardo wa Clairwaux (1090-1153): huko Ufaransa; kitabu chake kiliitwa, ‘Tractatus de gratia et libero arbitrio 4, 0. ’
18. Hapa, tunaona wazi kabisa jinsi akili ya mwanadamu huyapapasa mambo ya Mungu, ikiitafuta faraja katika matendo yake mwenyewe, kulingana na giza la nafsi yake, bila kujali Kristo na imani. Tukiyaangalia haya katika mwanga, tutaona kwamba, majuto kama haya ni wazo lililobuniwa na kutungwa na nguvu za mwanadamu mwenyewe bila imani na bila kumfahamu Kristo. Mkosaji maskini mwenye majuto haya bandia, alipotafakari tamaa au mapatilizo yake, pengine angecheka kwanza badala ya kulia, isipokuwa wale waliokuwa wamenaswa kweli na sheria au waliokuwa wameteswa bure na Ibilisi kwa nafsi ya huzuni. Mbali na haya, hakika, majuto ya namna hiyo yalikuwa unafiki kabisa usioiua tamaa ya dhambi. Naam, watu hawakuwa na budi kutubu, lakini wangependa kutenda dhambi zaidi kama wangeruhusiwa tu kufanya hivyo.
19. Hivi ndivyo ungamo lilivyotendeka: kila mtu lazima kuzisimulia dhambi zake zote jambo ambalo ni muhali kabisa. Kwa kweli, ni maumivu makali kabisa! Dhambi zilizosahaulika zilisamehewa kwa sharti hili tu kwamba, zitaungamwa mara zitakapokumbukwa.
Kwa hiyo, mtu hakuweza kujua kamwe ni lini angeungama na kuwa safi vya kutosha ama ni lini kuungama kungekuwa na mwisho wake. Wakati huo huo, alishauriwa kuyatumainia matendo yake mwenyewe na kuambiwa kwamba, kadiri alivyozidi kuungama dhambi zake na kuona aibu, ndivyo angejiaibisha mwenyewe mbele ya kasisi, na ndivyo ingekuwa kuharakisha upatanisho wa dhambi zake vizuri. Unyenyekevu wa namna hii unaweza kustahili neema ya Mungu.
20. Hapa, hakuna mahali pa imani wala Kristo! Hakuna maarifa ya nguvu za ondoleo la dhambi! Faraja ya mtu ilibakia tu katika kutaja dhambi zake na kuona aibu kwa ajili yazo. Haiwezekani kuzisimulia aina zote za mateso, udanganyifu, na ibada za miungu mingine zilizozaliwa na toba ya namna hiyo.
21. Lakini upatanisho ulikuwa sehemu changamano zaidi ya toba. Hakuna mtu yeyote aliyeweza kujua hakika, angelipa kiasi gani kwa ajili ya dhambi moja mbali na dhambi zake zote. Lakini hapa walilibuni shauri bora ya upatanisho mdogo na rahisi, iliamriwa, kama vile kusema Sala ya Bwana mara tano, kufunga siku moja n.k. Sehemu ya toba iliyobakia ilirejeshwa Purgatorio.
22. Hapa, hakukuwa na lolote ila uchungu na taabu. Wengi waliogopa kwamba, hawangetoka Purgatorio kwa sababu, kulingana na kanuni za zamani za Kanisa, miaka saba ya toba ilihitajika kwa dhambi moja ya mauti. Hata hivyo, tumaini liliwekwa katika kazi za upatanisho za mwanadamu. Kama upatanisho ungekuwa mkamilifu, watu wangeutumainia peke yake bila kuhitaji imani
wala Kristo. Lakini toba kama hii ni bandia kabisa. Ingawa mtu angeendelea kutubu kwa muda wa miaka mia, hangeweza kujua kama angetubu kwa kiasi kinachotakiwa. Kwa hiyo basi, daima, watu waliendelea kutubu bila kufaulu kweli.
24. Basi, Kiti Kitakatifu cha Roma kililisaidia Kanisa maskini na kukibuni cheti cha upatanisho.1208 Kwa njia ya cheti hiki, matendo ya upatanisho yalisamehewa na kuondolewa. Kwanza, kwa miaka saba au miaka mia moja. Mamlaka ya namna hiyo yaligawanywa miongoni mwa makadinali na maaskofu ili, mmoja wao aweze kugawa vyeti vya upatanisho kwa miaka mia moja, na mwingine kwa siku mia moja. Papa alijiwekea yeye peke yake mamlaka ya kuyaondoa matendo yote ya upatanisho.1209
25. Kwa kuwa, shughuli hii ilianza kuleta fedha na biashara ya matangazo ya Papa yakawa na faida, Papa aliubuni mwaka wa dhahabu na akaliweka adhimisho lake huko Roma. Jambo hili lilimaanisha msamaha wa adhabu na hatia zote.1210 Halaiki ya watu ilikimbia huko Roma, kwani kila mmoja alitamani kujiepusha na mzigo mzito usiobebeka. Maana yake: kutafuta na kuwa na nguvu kuhusu hazina ya dunia.1211 Papa alikimbia mbele kwa haraka na akaagiza mwaka wa dhahabu baada ya mwingine.1212 Lakini kadiri alivyozimeza fedha zaidi na zaidi, ndivyo umio wake ulivyotanuka. Kwa sababu hiyo, aliwatuma mabalozi wake ng’ambo katika nchi mbalimbali mpaka makanisa yote na kila nyumba ikajaa mwaka wa dhahabu. 26. Mwishowe, alilazimisha kuingia prugatorio miongoni mwa waliofariki dunia. Kwanza, kwa kuanzisha misa na mikesha,1213 kisha pamoja na vyeti vya upatanisho na mwaka wa dhahabu. Hatimaye, bei za nafsi zilipungua zaidi na ziliachiliwa kwa sarafu moja.1214
27. Lakini haya yote hayakuwa na msaada wowote, kwa kuwa Papa huyo huyo, aliyewafundisha watu kujikabidhi na kukitegemea cheti cha upatanisho, alileta mashaka tena alipotangaza ifuatavyo katika matangazo yake: “Yeyote atakayefaidika kutokana na cheti cha upatanisho au mwaka wa dhahabu, lazima
1208 Kijerumani: ‘Ablass,’ Kilatini: ‘Indulgentia.’
1209 Kijerumani: ‘Plenarablass,’ Kilatini: ‘Indulgentia plenaria.’ Kwa mara ya kwanza, Papa Urbano II aliahidi cheti kamili cha upatanisho kwa wote walioenda katika vita vya msalaba huko Yerusalemu mwaka wa 1095.
1210 Kilatini: ‘Remissio poenae et culpae.’ Msemo huu ulitumiwa hadi wakati wa Sinodi ya Konstanzo (14141418).
1211 Rejea Dan. 11:43. Wakati wa Enzi ya Kati, Wakristo wa Ulaya waliamini aghalabu kwamba, Ibilisi atamwonyesha Mpinga Kristo hazina zote zilizofichwa ardhini ili aweze kuwapotosha watu wote.
1212 Miaka ya 1300, 1350, 1390, 1423, 1450, 1475, 1500, 1525.
1213 Kilatini: ‘Vigilia.’
1214 Msemo wa kawaida wa waliouza vyeti vya upatanisho, hasa wa Yohana Tetzel (1465-1519): “Iwapo sarafu itaanguka sandukuni, nafsi ya mtu itaruka kutoka Purgatorio hadi mbinguni.”
atubu, aungame na alipe fedha.”1215 Hapo juu tumeona kwamba, toba na ungamo lao ni unafiki usiokuwa na uhakika wowote. Licha ya hayo, hakuna mtu aliyejua nafsi zilizopatikana huko Purgatorio zilikuwa za nani, hakuna aliyejua ni zipi kati ya hizo zilitubiwa kweli na kuungama sawasawa humo Purgatorio. Vivyo hivyo, Papa alipokea fedha na kuwafariji watu kwa mamlaka yake na vyeti vyake vya upatanisho lakini aliwaongoza tena katika matendo yao wenyewe yasiyokuwa na uhakika.
28. Walikuwepo pia Wengine ambao hawakufikiri walikuwa na hatia ya dhambi za mawazo, za maneno wala za matendo. Mimi na wengine kama mimi tulitaka kuishi kama watawa na makasisi katika nyumba za watawa na taasisi za kanuni za makanisa makuu. Tulijilinda dhidi ya mawazo mabaya kwa njia ya kufunga, kukesha, kusali, misa, mavazi ya kukwaruza na vitanda vigumu. Tulijaribu kwa kweli na kwa nguvu zetu zote kuwa watakatifu. Kama bado uovu uliorithiwa, kwa njia ya kuzaliwa, uliyafanya yale ambayo ni asili yake kufanywa, wakati mwingine tulipokuwa tumelala, jinsi Mt. Agostino, Mt. Hieronimo na wengine walivyokiri,1216 hata hivyo, tulifikiri, kulingana na mafundisho yetu kuwa wengine, miongoni mwetu waliokuwa, , watakatifu kabisa pasipo dhambi na wamejaa matendo mema. Hivyo basi, tuligawanya na kuuza, wenyewe kwa wenyewe, matendo yetu mema tuliyotenda zaidi ya yale tuliyoyahitaji kwa ajili ya kwenda mbinguni. Huu ndio ,ukweli kabisa, na kuna muhuri, barua na mifano ya kuyadhamini haya.
29. Watu kama hawa hawakuhitaji toba, kwani wangejutia nini ikiwa hawakuyakubali mawazo maovu? Wangeungamia nini ikiwa waliliepuka neno moja lililo baya? Wangeutoa upatanisho gani ikiwa walikuwa na matendo yao bila hatia yoyote hata kuweza kuuza haki yao tele kwa wengine, yaani, wakosaji maskini? Wakati wa Kristo, waandishi na Mafarisayo pia walikuwa watakatifu na wanafiki wa namna hiyo.
30. Hapa anamwingilia “malaika mwenye moto,”1217 yaani, Yohana Mbatizaji, mhubiri wa toba ya kweli. Anawapiga kwa radi moja na kuwaharibu hawa wote wawili. Yaani, wale wanaochuuza na kununua matendo anasema: “Tubuni.” 31. Kwa upande mwingine, kuna wengine ambao hufikiri: “Tayari tumekwisha kutubu,” na kwa upande mwingine kuna wale ambao hudhania: “Hatuhitaji kutubu.” Lakini Yohana anasema: 32. “Tubuni ninyi nyote, yaani, wenye toba ya bandia na watakatifu wa uongo. Ninyi nyote mnauhitaji msamaha wa dhambi,
1215 Kwa mfano, tangazo la vyeti vya upatanisho mwaka wa 1517. 1216 Agostino, Conf. 2, 2; 10, 50; Hieronimo, Epist. ad Eustochium 22, 7. 1217 Mal. 3: 1
kwa kuwa bado, hamjui dhambi ni nini na hamjui kutubu au kujiepusha nayo. Hakuna hata mmoja wenu aliye mwema. Nyote mmejaa kutoamini, upofu na kutomfahamu Mungu na mapenzi yake. Kwani Mungu akiwepo na kutokana na ukamilifu wake wote, tumeipokea neema kwa neema.1218 Hakuna mwanadamu anayeweza kuwa mwenye haki mbele za Mungu bila yeye. Mkitaka kutubu, tubuni sawasawa. Toba yenu haikamilishi lolote. Nanyi wanafiki mnaofikiri kwamba, hamhitaji kutubu, ninyi wazao wa nyoka wenye sumu kali, ni nani aliyewahakikishia kuwa mtaepuka ghadhabu inayokuja?1219
33. Mtakatifu Paulo anahubiri hivyo hivyo katika Rum. 3:10-12: “Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.” 34. Kadhalika, katika Mdo. 17:30 anasema: “Bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.” Anasema, “watu wote,” na anafanya hivyo kwa maana ya watu wote kabisa. 35. Toba kama hii inatufundisha tuitambue dhambi, yaani, tukubali kwamba, tumepotea kabisa, kwamba, kutoka upande mmoja hadi mwingine hakuna wema ndani yetu, na kwamba, lazima tufanyike wapya na kuwa watu tofauti kabisa.
36. Toba hii siyo yenye tafsiri, duni na haimaniki kama toba ya dhambi halisi, kwa sababu haijadili kuwa, ipi ni dhambi na ni ipi siyo dhambi, bali inakusanya kila kitu pamoja na kusema kwamba, mambo yetu yote ni dhambi tupu. Mbona tupoteze muda kuyapekua, kuyagawanya na kuyatofautisha mambo? Kwa sababu hiyo, toba ya namna hii si yenye mashaka yoyote, kwa kuwa hakuna lililobakia tunaloweza kulifikiria kuwa zuri kiasi cha kulipia dhambi zetu. Jambo linalobakia ni hakika hii kwamba, hatuwezi kuweka tumaini letu juu ya chochote kwetu, kuhusu fikra zetu, misemo na matendo yetu n.k.
37. Kwa hiyo, toba haiwezi kuwa ya bandia kama kazi ya kutia kiraka isiyokuwa ya hakika. Kwani mtu anayeungama kwamba, yeye ni mwenye dhambi kabisa, anazingatia makosa yote bila kutaja wala kusahau hata moja. 38. Wala ridhaa yetu haiwezi kuwa ya hakika, kwa kuwa siyo kwa kazi zetu tuzitendayo zenye mashaka na dhambi, bali ni mateso na damu ya Mwana Kondoo wa Mungu asiye na hatia aichukuaye1220 dhambi ya ulimwengu.
39. Hii ndiyo toba ambayo Yohana aliihubiri, Kristo aliihubiri, na Injili ambayo tunaihubiri pia. Kwa njia ya toba hii, tunamtupilia mbali Papa na kila kitu
1218 Yn. 1:16. Luther alitafsiri ‘χαριν αντι χαριτος’ kuwa (neema kwa neema) ‘Gnade umb Gnade,’ si (neema juu ya neema) jinsi ‘Union Version’ ilivyotafsiri.
1219 Mt. 3: 7 1220 Kijerumani: ‘trägt,’ (aichukuaye), Kilatini: ‘tollit,’ (aiondoaye).
kinachoandamana na matendo yetu mema, kwa kuwa yote yanayoitwa “matendo mema” au “sheria” yamejengwa juu ya msingi mbovu uliooza. Hakuna tendo jema hata moja, bali kazi za uovu ndizo zilizopo na hakuna anayeitimiza sheria – jinsi Kristo asemavyo katika Yn. 7,19 - bali wote wamepotoka. Kwa sababu hiyo, jengo hili limejengwa pande zake, ni takatifu, ni lenye fahari sana kwa udanganyifu, uongo na unafiki mtupu kabisa.
40. Toba ya Wakristo itadumu hadi kifo, kwa kuwa inaipinga dhambi iliyobakia katika mwili wakati wa maisha yote. Katika Rum. 7:23, Mt. Paulo anaipiga vita sheria katika viungo vyake, na anafanya hivyo, siyo kwa nguvu zake mwenyewe, bali kwa karama ya Roho Mtakatifu ambayo hufuatia msamaha wa dhambi. Karama hii daima huing’oa na kuifagia dhambi ambayo imebakia na hufanya kazi kwa bidii ili kumwezesha mwanadamu kuwa safi na mtakatifu kabisa.
41. Papa wa Roma, wanatheologia, wanasheria, na watu wote hawaielewi toba hii hata kidogo. Ni mafundisho yatokayo mbinguni, yaliyofunuliwa katika Injili, na bado yanaitwa kuwa uasi na watakatifu wasiomcha Mungu.
42. Kwa upande mwingine, watu wenye nafsi za mifarakano1221 wanaweza kutokea na labda wengine tayari wapo kama wale niliowaona kwa macho yangu wakati wa maasi1222 - wanaoshikilia kwamba, mara tu wanapopokea roho au msamaha wa dhambi, au mara tu wanapoamini, watadumu katika imani hata wakitenda dhambi baadaye na dhambi kama hiyo haitawadhuru tena. Wao hupiga mayowe: “Fanya unalolitaka! Kama unaamini kwamba, dhambi zote husamehewa kabisa kwa imani” n.k. . Wanaongezea kwamba, iwapo mtu yeyote atatenda dhambi baada ya kupokea imani na Roho Mtakatifu, hakuwa kweli na Roho Mtakatifu na imani. Basi, nimekutana na watu wengi wapumbavu kama hao na ninaogopa kwamba, mashetani wa namna hiyo bado wanaendelea kukaa miongoni mwa baadhi yao.
43. Kwa hiyo, ni muhimu sana kuelewa na kufundisha kwamba, wakati watakatifu, hasa wenye dhambi ya asili na bado wanaoihisi, wanaotubu kila siku, wanaopambana nayo, huanguka katika dhambi ya kadamnasi1223 jinsi Daudi alivyoanguka katika uzinzi, mauaji, na kufuru, huwa hawana imani na Roho Mtakatifu. Kwani, Roho Mtakatifu hairuhusu dhambi kutawala na kushinda, bali Roho Mtakatifu huikandamiza na kuizuia dhambi isifanye inachotamani. Dhambi ikifaulu kuyatenda inayoyatamani, hakuna Roho Mtakatifu wala imani jinsi Mt. 1221 Kijerumani: ‘trägt,’ (aichukuaye), Kilatini: ‘tollit,’ (aiondoaye). 1222 Maasi makubwa ya mafalahi mwaka wa 1525. 1223 Mbele ya watu.
Yohana asemavyo: “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi!”1224 Wakati huo huo ni kweli pia, jinsi Mt. Yohana huyo huyo anavyoandika: “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.”1225
IV. Injili
Sasa tuirudie Injili, ambayo huutoa ushauri na msaada dhidi ya dhambi kwa njia zaidi ya moja kwa kuwa Mungu ana utajiri wa neema isiyokuwa na kifani. Kwanza, kwa njia ya maneno ya vinywa wakati msamaha wa dhambi unahubiriwa katika dunia nzima. Hii ndiyo huduma halisi1226 ya Injili. Pili, kwa njia ya Ubatizo. Tatu, kwa njia ya Sakramenti Takatifu ya Madhabahu. Nne, kwa Mamlaka ya Funguo na pia kwa njia ya mazungumzo na kutiwa moyo miongoni mwa ndugu: “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao” (Mt. 18: 20).
V. Ubatizo
1. Ubatizo siyo kitu kingine zaidi ya Neno la Mungu katika maji, ulioamriwa na kuanzishwa naye au jinsi Paulo asemavyo: “Uogaji katika neno”1227 “Kujisafisha kwa maji katika neno,” jinsi Agostino pia anavyonena: “Neno linaingia katika elementi na kuwa sakramenti.”1228 Kwa hiyo, hatukubaliani na Tomaso na wanatheologia wa Kidominikano wanaolisahau Neno ambalo ndilo uasisiwaji wa Mungu na kusisitiza kwamba, Mungu ameiunganisha nguvu ya kiroho na maji ambayo huosha dhambi kwa maji. Pia hatukubaliani na Scotus/Skotaso na Wafransiskano wanaofundisha kwamba, Ubatizo huosha dhambi kwa msaada wa utashi wa Mungu, maana utashi wa Mungu peke yake huosha na siyo neno au maji.1229
Ubatizo wa Watoto
Tunafundisha kwamba, watoto lazima wabatizwe kwa kuwa wao pia huushiriki wokovu ulioahidiwa na kutekelezwa katika Kristo. Kanisa halina budi kuwapa
1224 1 Yoh. 3: 9; 5:18 1225 1 Yoh. 1:8
1226 Kilatini: ‘officium proprium.’
1227 Luther katika Kilatin:‘Lavacrun in verbo.‘ Efe. 5:26. ‘Toleo la Vulgata’; ‘lavacrum aquae in verbo.’
1228 Luther katika Kilatin:‘Lavacrun in verbo.’ Efe. 5:26. ‘Toleo la Vulgata’; ‘lavacrum aquae in verbo.’
1229 Tomaso wa Akuino (1225-1274) katika ‘Summa theologiae‘ p. 3 q. 62 art. 4. Daraja la Kidominikano liliitwa “Daraja la Wahubiri.” Duns Scotus (1266-1308): alikuwa mwanatheologia katika Daraja la Kifransiskano lililoitwa pia “Daraja la Pekupeku.”
Ubatizo na wokovu huu.
VI. Sakramenti ya Madhabahu
1. Kuhusu Sakramenti ya Madhabahu tunasema kwamba, mkate na divai katika Chakula cha Bwana ni mwili na damu ya kweli ya Kristo. Vinatolewa na kupokelewa siyo na wacha Mungu tu bali pia na Wakristo waovu.
2. Sakramenti ya aina moja peke yake isitolewe. Hatuhitaji hekima ya fahari1230 ya Sinodi ya Konstanzo na wataalamu wa ghiliba kutufundisha kwamba, mkate peke yake una kitu sawa kama mkate na divai pamoja.1231 3. Hata kama ingekuwa kweli kwamba, aina moja ina kitu sawa kama aina zote mbili, aina moja tu haiwezi kutekeleza utaratibu na uanzishwaji wote wa Kristo. 4. Hasa tunawahukumu na kuwalaani, kwa jina la Mungu, sio tu wale ambao hawaziachi tu aina zote mbili za Chakula cha Bwana, bali pia hukataa, huhukumu na huzomea, kwa njia ya kashfa sana, matumizi ya aina zote mbili kama yaliyo uasi. Kwa njia hiyo, wao humpinga Kristo aliye Bwana na Mungu wetu na kujiweka wenyewe juu yake kabisa.
5. Kuhusu mafundisho ya mageuzo-uwamo, hatujali hata kidogo ghiliba ya madaktari wanazuoni.1232 Wao hufundisha kwamba, mkate na divai hupoteza kiini chao cha asili na hubakia na sura na rangi tu ya mkate na siyo mkate halisi. Ni vyema kusema pamoja na Maandiko Matakatifu kwamba, mkate unabakia kuwa mkate jinsi Mt. Paulo mwenyewe anavyonena: “Mkate ule tuumegao” (1 Kor. 10:16), na tena “Na hivyo aule mkate” (1 Kor. 11:28).
VII. Funguo
1. Funguo ni huduma na mamlaka itolewayo kwa Kanisa na Kristo ili kufunga katika dhambi na kufungua kutoka katika dhambi.1233 Mamlaka haya hayahusu tu dhambi kubwa na zilizo wazi bali pia zile ambazo ni za hila, za siri na ambazo ni Mungu peke yake anayezijua. Kwa kuwa imeandikwa: “Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake” (Zab. 19:12). Paulo mwenyewe analalamika katika (Rum. 7:23) kwamba, katika mwili wake anatumikia “ile sheria ya dhambi.” 2. Ni mamlaka ya Mungu peke yake na siyo mamlaka yetu kuamua ni mambo gani ambayo ni dhambi na tena ni dhambi gani kubwa au ni ngapi kama ilivyoandikwa:
1230 Kijerumani: ‘hohe Kunst,’ Kilatini: ‘Doxosophia,’ hapa istilahi ya dhihaka ya sayansi.
1231 Makataa ya Sinodi ya Konstanzo tarehe 15, Juni mwaka wa 1415.
1232 Katoliki, inayaita mafundisho haya ‘mageuzo-uwamo.’ 2000, (Fungu la 1376). ‘Mageuzo ya elementi,’ Kilatini: ‘transsubstantiatio,’ “Katekisimu ya Kanisa
1233 Mt. 18: 18
“Wala usimhukumu mtumishi wako, maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki” (Zab. 143:2). 3. Paulo mwenyewe anasema katika (1 Kor. 4:4): “Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo.”
VIII. Ungamo
1. Kwa kuwa, ondoleo la dhambi au mamlaka ya funguo yaliasisiwa na Kristo katika Injili, ni faraja na msaada dhidi ya dhambi na dhamiri mbaya. Kwa vyovyote, ungamo au ondoleo la dhambi visiruhusiwe kupotea katika Kanisa. Ungamo linahitajika hasa kwa ajili ya dhamiri yenye uoga na pia, kwa ajili ya vijana wasiofundishwa wanaohitaji kuchunguzwa na kufundishwa katika mafundisho ya Kikristo.
2. Hata hivyo, hesabu ya dhambi lazima iachwe kwa hiari ya kila mtu kuzitaja au kutokuzitaja dhambi zake apendavyo. Tunapoishi katika mwili, hatutasema uongo tukidai: “Mimi niliye maskini na mwenye dhambi kabisa.” Pia: “Lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali.” (Rum. 7:23). Kwa sababu ondoleo la dhambi analotangaziwa mtu binafsi linatokana na huduma ya funguo, hatupaswi kulidharau. Kinyume chake, lazima liheshimiwe na lithaminiwe sana, kama huduma zingine za Makanisa ya Kikristo.
3. Katika mambo haya yanayohusu Neno la nje linalohubiriwa, lazima tuushike kwa uthabiti ukweli huu usemao kwamba, Mungu hampatii yeyote Roho Mtakatifu wake au neema yake isipokuwa kwa njia ya na pamoja na Neno la nje linalotangulia yote ili tupate kukingwa dhidi ya walokole. Yaani, roho 1234 zinazojigamba kuwa na Roho Mtakatifu bila Neno na kabla ya Neno. Kwa hiyo, roho hizo zinayahukumu, zinayafafanua na zinayapindisha Maandiko Matakatifu au Neno la kinywa kwa kulingana na mapenzi yao. Müntzer1235 alifanya hivyo na wengine bado wanafanya hivyo hivyo siku hizi. Wanataka kutofautisha kwa ukali kati ya herufi na Roho Mtakatifu bila kuelewa wanalolisema au wanalolifundisha. 4. Upapa wa Roma wenyewe pia siyo lolote mbali na ulokole mbaya. Kwa kuwa Papa hujisifu kwamba, “sheria zote zimo ndani ya kisanduku cha moyo wake.”1236 Kwa hiyo, anadai kwamba, lolote analoliamua na analoliamuru katika kanisa lake ni roho na haki, hata kama liko juu ya Maandiko Matakatifu na Neno linalohubiriwa. 5.Haya yote ni uovu wa Ibilisi wa kale, yule nyoka wa kale1237 aliyewaongoza Adamu na Hawa katika ulokole mbaya kwa mawazo yao
1234 Kilatini: ‘Enthusiastae,’ Kijerumani: ‘Enthusiasten.’
1235 Tomaso Müntzer (1490-1525): alikuwa mmoja wa viongozi wa maasi makubwa ya mafalahi.
1236 Corpus iuris canonici, Liber Sextus’ 1, 2 c.1: ‘Pontifex, qui iura omnia in scrinio pectoris sui censetur habere.’
1237 Ufu. 12: 9
wenyewe. 6. Hata sasa analitumia Neno la nje jinsi walokole wetu wanavyoliacha Neno la nje lakini hawataki kuwa kimya. Badala yake, wanaendelea kupayuka na kuyatunga maneno yao wenyewe na kuujaza kwayo ulimwengu wote. Ni kana kwamba Roho Mtakatifu hangeweza kuja kwa njia ya maneno ambayo yameandikwa na kusemwa na mitume, bali kwa njia ya maandiko na maneno ya walokole wenyewe. Mbona hawaachi kabisa mahubiri na maandiko yao? Mbona hawasubiri mpaka Roho Mtakatifu aingie ndani ya watu bila na kabla ya kuandika kwao jinsi wanavyojigamba kwamba, amewajia wao bila mahubiri ya Neno la Maandiko Matakatifu? Hakuna nafasi hapa kutafakari zaidi kuhusu jambo hilo. Mahali pengine tumelizungumzia kwa utoshelezi kabisa.1238
7. Hata wale walioamini kabla ya Ubatizo au wameamini wakati wa Ubatizo, huipata imani kwa Neno la nje ambalo lilitangulia. Hali kadhalika, watu wazima lazima kwanza wasikie: “aaminiye na kubatizwa ataokoka,”1239 hata kama hawakuamini tangu mwanzo na hawakumpokea Roho Mtakatifu na hawakubatizwa mpaka baada ya muongo mmoja. 8. Kornelio katika (Mdo. 10:2,22) alikwisha kusikia kwa muda mrefu sana, kutoka kwa Wayahudi, kuhusu Masihi atakayekuja. Kwa njia hii, alikuwa mwenye haki mbele za Mungu. Kwa ajili ya imani ya namna hiyo, sala na sadaka zake vikakubalika mbele za Mungu. Kwa sababu hiyo, Luka anamwita “mcha Mungu” na ‘anayemwogopa Mungu.’ Lakini hangeweza kuamini na kuwa mwenye haki kama Neno la kusikika halikutangulia. Hata hivyo, ilimbidi Petro amfunulie kwamba, Masihi ambaye alimwamini amekwisha kuja tayari. Imani yake katika Masihi haikupaswa kutekwa na ugumu wa Wayahudi wasioamini. Badala yake, ilimbidi kujua kwamba, ilimpasa aokolewe kwa njia ya Masihi aliyepo na siyo kumkana au kumtesa pamoja na Wayahudi.
9. Kwa ufupi: magonjwa ya mlipuko ya ulokole yamejisitiri katika Adamu na uzao wake kutoka mwanzo wa dunia hadi mwisho wake. Joka yule wa zamani1240 aliiambukiza na kuitawanya sumu hii na kuwa chanzo, nguvu na uwezo wa uasi wote, jinsi ulivyo uasi wa Upapa na Muhammad. 10. Kwa sababu hiyo, hatuna budi kuushika kwa uthabiti, ukweli huu kwamba, Mungu hajihusishi nasi isipokuwa kwa njia ya Neno la nje na sakramenti. Lolote linalosifiwa kuwa la Roho Mtakatifu mbali na Neno na sakramenti ni la Ibilisi. Mungu alijifunua kwa Musa kwa njia ya moto kichakani na kwa njia ya Neno la kinywa chake.1241
1238 Kwa mfano, kitabu cha Dk. Martin Luther kiitwacho, ‘Dhidi ya Manabii wa Mbingu’ (15241525).
1239 Mk. 16: 16
1240 Mwa. 3: 1,14; Ufu. 12: 3,9 1241 Kut. 3: 2
330
Hakuna nabii, awe Eliya au Elisha, aliyempokea Roho Mtakatifu bila Amri Kumi za Mungu. Yohana Mbatizaji hakuchukuliwa mimba bila kutanguliwa na neno la malaika Gabrieli wala hakurukaruka tumboni mwa mama yake kabla ya sauti ya Mariamu.1242 Mt. Petro anasema kwamba, manabii walibashiri kama wanadamu wa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu na siyo kwa hiari ya mwanadamu.1243 Lakini hawakuwa watakatifu bila Neno la nje. Haiwezekani kwamba, Roho Mtakatifu asingewasukuma kutabiri wakati hawajawa watakatifu. Petro mwenyewe anasema kwamba, walikuwa watakatifu, kwa sababu Roho Mtakatifu alisema kupitia kwao.
IX. Kutengwa na Kanisa
Tunaichukulia adhabu kubwa ya Papa wa Roma ya Kutengwa na Kanisa kuwa adhabu ya kawaida ya raia ambayo haituhusu sisi wahudumu katika Kanisa.1244 Lakini adhabu ndogo ya Kutengwa na Kanisa1245 ni adhabu ya kweli ya Kikristo. Yaani, kutowaruhusu wale ambao ni wakosaji wa hadharani wasiotubu, kuja kwenye sakramenti na kushiriki katika mambo mengine ya Kanisa mpaka watakapozitengeneza njia zao na kuziepuka dhambi. Wachungaji hawapaswi kuchanganya adhabu ya raia pamoja na adhabu hii ya kiroho ya Kutengwa na Kanisa.
X. Kubarikiwa kuwa Mchungaji na Wito wa Uchungaji
1. Ikiwa maaskofu wangetaka kuwa maaskofu wa kweli na kulitunza Kanisa na Injili vizuri, tungeweza kukubali (kwa ajili ya upendo na umoja lakini si kwa lazima) kwamba, wawabariki na kuwasimika wahubiri wetu, kwa sharti kwamba, wangefanya hivyo bila unafiki na majivuno yasiyokuwa ya Kikristo. Walakini, sasa wao siyo maaskofu wa kweli na hawapendi kuwa maaskofu wa namna hiyo bali ni mabwana wakuu na watawala wa dunia. Hawahubiri, hawafundishi, hawabatizi, hawakitunzi Chakula cha Bwana wala hawafanyi kazi au huduma yoyote katika Kanisa. Kinyume chake, wanawatesa na wanawahukumu wale ambao wameitwa kufanya huduma ya namna hiyo. Lakini Kanisa halipaswi kuachwa bila wahudumu kwa ajili ya hao maaskofu.
3. Kwa sababu hiyo basi, tunataka na inatubidi kuifuata mifano ya kale ya
1242 Lk. 1: 8-19, 41-44
1243 2 Pet. 1: 21
1244 Luther mwenyewe aliwekwa chini ya adhabu kubwa ya kutengwa na Kanisa (‘excommunicatio maior’) na baadaye wakati wa Baraza la/Sinodi ya Worms, mwaka wa 1521, aliwekwa chini ya Laana ya Dola iliyokuwa adhabu ya raia.
1245 ‘Excommunicatio minor.’
Kanisa na akina baba zake kuwabariki sisi wenyewe watu wanaostahiki huduma hii. Wafuasi wa papa hawana haki kutukataza au kutuzuia kufanya hivyo hata kwa mujibu wa sheria zao. Kwa kuwa zinasema kwamba, wale waliobarikiwa na waasi kuwa wachungaji watatambuliwa kama waliobarikiwa na watabakia hivyo. Mt. Hieronimo anaandika pia kuhusu Kanisa la Aleksandria kwamba, mwanzoni lilitawaliwa na makasisi na wahubiri kwa makubaliano bila maaskofu.
XI. Ndoa ya Wachungaji
1. Wafuasi wa Papa wamepiga marukufu ndoa kwa daraja la kimungu la wachungaji na kuliwekea mzigo wa useja wa kudumu usiokwisha bila mamlaka au haki yoyote. Kinyume chake, walitenda hivyo kama wahalifu wagumu, dhalimu wa Mpinga Kristo. Kwa njia hii basi, walitoa nafasi kwa kila aina ya dhambi zote za kutisha, za kuchukiza na zisizohesabika, ambazo kwazo, bado wanahusika. 2. Madhali sisi wala wao hawajapewa uwezo wa kumfanya mwanamume kuwa mwanamke au mwanamke kuwa mwanamume au kuzitangua kabisa tofauti za kijinsia, wao hawakuwa na uwezo wowote wa kuvitenganisha viumbe vya Mungu kama hivyo au kuwazuia kuishi pamoja kwa uaminifu katika ndoa. 3. Kwa hiyo, hatudhamirii kukubaliana na useja wao wa kuchukiza wala hatutaweza kuuvumilia. Kinyume chake, tungependa sana ndoa iwe huru, jinsi Mungu alivyoiamuru na kuiasisi. Sisi hatutaki kuingilia kati na kulizuia tendo la Mungu, kwa sababu Paulo anasema kwamba, kufanya hivyo ni mafundisho ya mashetani.1246
XII. Kanisa
1. Sisi hatukubaliani kamwe na wafuasi wa papa kwamba, wao ni Kanisa, maana wao siyo Kanisa. 2. Wala hatutayasikiliza yale wanayotuamuru au wanayotukataza kwa jina la Kanisa. Tunamshukuru Mungu, maana, mtoto wa umri wa miaka saba anajua Kanisa ni nini. Yaani, ndilo waumini watakatifu na “kondoo wanaoisikia sauti ya Mchungaji wao.”1247 Kwa hivyo, watoto huomba: 3. “Ninaliamini Kanisa moja takatifu la Kikristo.” Utakatifu wake hautegemei vitu vya utani, vipara vya utosini, kanzu au kaida zao zingine walizozibuni nje ya Maandiko Matakatifu, bali unasimama katika Neno la Mungu na imani ya kweli.
1246 1 Tim. 4: 1
1247 Yn. 10: 3
XIII. Jinsi Mwanadamu Anavyohesabiwa Haki mbele za Mungu na Matendo yake Mema
1. Sioni sababu yoyote ya kuyabadilisha mafundisho ambayo mpaka sasa nimeendelea kuyafundisha daima kwa imani, jinsi Mt. Petro asemavyo kwamba, tunaupata moyo mpya ulio safi na kwamba, Mungu anapenda kuhesabu na ndiyo anatuhesabu sisi wenye haki na utakatifu mbele zake kwa ajili ya Kristo, Mpatanishi wetu. Ingawa dhambi haikuondolewa kutoka katika mwili wetu wala mauti, Mungu hataihesabu wala kuijali.
2. Kisha, matendo mema huifuata imani ya jinsi hiyo, mageuzi mapya, na msamaha wa dhambi. Lolote linalobakia kama dhambi au lisilokuwa kamili katika matendo haya, halitahesabiwa kama dhambi au kasoro kwa ajili ya Kristo. Mintarafu ya binafsi na matendo yake, mtu mzima ataitoa hesabu ya kuwa mwenye haki na mtakatifu kwa njia ya neema na huruma safi zilizomiminwa kwetu kwa wingi na Kristo ili ziwe kinga yetu. 3. Kwa sababu hiyo, hatutaweza kujivunia ustahili mkuu katika matendo yetu iwapo utachukuliwa kuwa nje ya neema na huruma za Mungu. Badala yake, tunafuata kama jinsi ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: “Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana” (1 Kor. 1:31). Yaani, tuko salama iwapo tutajigamba kwamba, tuna Mungu mwenye neema. Tunaliongezea hili kwamba, matendo mema yasipofuatia, imani yetu ni ya bandia na siyo ya kweli.
XIV. Nadhiri za Utawa
Kwa kuwa nadhiri za utawa zinalipinga Fungu Kuu la Kwanza, lazima ziwekwe kando kabisa. Ni kwa ajili ya haya Kristo anasema katika Mt. 24,5: “Mimi ni Kristo.” Mtu anayeweka nadhiri ya maisha ya utawa huamini kwamba, ameingia katika mfumo wa maisha ambao ni bora kuliko maisha ya Mkristo wa kawaida. Kwa matendo yake mwenyewe, anakusudia kujisaidia na kuwasaidia wengine kwenda mbinguni. Hii ni kumkana Kristo kabisa. Wafuasi wa Papa hujivunia Mt. Tomaso1248 wao kwamba, nadhiri ya utawa ni sawa na Ubatizo. Hii ni kufuru.
XV. Mapokeo ya Binadamu
1. Hoja ya wafuasi wa Papa ni kufuru kabisa kwamba, mapokeo ya wanadamu yanaendeleza msamaha wa dhambi na huzaa heri ya milele. Jinsi Kristo asemavyo: “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya 1248 Tomaso wa Akuino, ‘Summa theologiae’ P. 2, 2 qu 189 art. 3 ad 3.
wanadamu.”1249 Kadhalika, imeandikwa katika Tit. 1:14: “Watu wajiepushao na yaliyo kweli.”1250 Siyo halali kusema kama jinsi wanavyofanya kwamba, ni dhambi ya mauti1251 kuvunja maagizo haya ya wanadamu.
3. Haya ndiyo mafungu ambayo kwayo lazima nisimame na ambayo kwayo nitasimama Mungu akipenda hadi kifo changu. Sielewi jinsi ninavyoweza kulibadilisha au kulikubali lolote katika hayo. Mtu akitaka kuyafanyia maafikiano yoyote, mwache afanye hivyo kwa hatari ya dhamiri yake mwenyewe.
4. Mwisho, limebakia gunia la mazingaombwe ya Papa linalojaa mafungu ya kipuuzi na ya kitoto, kama vile kuweka wakfu makanisa, ubatizo wa kengele, ubatizo wa mawe ya madhabahu pamoja na mwaliko wa wadhamini na zawadi zao n.k. Kubatiza kwa namna hiyo ni dhihaka na kashfa ya Ubatizo Mtakatifu na hakuwezi kuvumiliwa. Licha ya hayo, kuna baraka za mishumaa, mitende, viungo, shayiri, keki za Pasaka, n.k. Hizi haziwezi kuitwa baraka, na siyo baraka bali ni dhihaka tupu na ulaghai. Hila hizo zisizohesabika tunaziacha ziabudiwe na wao wenyewe na mungu wao mpaka watakapowachoka. Sisi hatutaki kuhusishwa nazo hata kidogo.
Sahihi katika Mafungu ya Smalkaldi:
Dk. Martin Luther, alitia sahihi
Yusto Yona, Dk., mwalimu mkuu, alitia sahihi kwa mkono wake mwenyewe
Yohana Bugenhagen, wa Pommern, alitia sahihi
Caspar Creutziger Dk., alitia sahihi
Nikolao Amsdorf, wa Magdeburg, alitia sahihi
Georgio Spalatin, wa Altenburg, alitia sahihi
Mimi, Philipp Melanchthon, ninakubaliana na mafungu ya hapo juu kuwa ni halisi na ni ya Kikristo. Hata hivyo, kuhusu Papa, ninaona kwamba, kama angeyaruhusu mahubiri ya Injili, tungeweza pia kukubaliana naye kuwa na ukuu juu ya maaskofu ambao ameupata kwa haki za kibinadamu. Kufanya makubaliano haya ni kwa ajili ya amani na umoja wa jumla miongoni mwa Wakristo ambao wako chini yake sasa na watakaokuwa baadaye.
Yohana Agrikola, wa Eisleben, alitia sahihi.
1249 Mt. 15: 9
1250 Kilatini: ‘Aversantium veritatem.’
1251 Kwa mfano, Yohana Cochlaeus (1479-1552).
Gabriel Didimo alitia sahihi.
Mimi, Urbano Rhegio, Dk., msimamizi mkuu wa makanisa katika Lüneburg, ninatia sahihi kwa jina langu na kwa majina ya ndugu zangu na la Kanisa la Hannover.
Mimi, Stefano Agricola, Mhubiri wa Hof, ninatia sahihi.
Pia mimi, Yohana Draconites, Profesa na mhubiri katika Marburg, ninatia sahihi
Mimi, Conrad Figenbotz, kwa utukufu wa Mungu ninatia sahihi yangu kwamba, nimeamini hivyo na bado ninaendelea kuamini na kuhubiri kwa uthabiti jinsi ilivyo hapo juu.
Mimi, Andrea Osiander, Mchungaji katika Nürnberg, ninatia sahihi
M. Vitus Dietrich, Mhubiri katika Nürnberg.
Mimi, Erhard Schnepf, Mhubiri katika Stuttgart, ninatia sahihi
Conrad Oettinger, wa Pforzheim, mhubiri wa Mwinyi Ulrich.
Simon Schneeweiss, Mchungaji wa Kanisa la Koethen.
Yohana Schlagenhaufen, mchungaji wa Kanisa la Köthen.
Bwana Georgio Helt, wa Forchheim.
Bwana Adam wa Fulda,
Bwana Antonio Korvino, mmoja wa wahubiri katika Hessen
Tena mimi, Yohana Bugenhagen wa Pommern, Dk., ninatia sahihi kwa niaba ya Bwana Yohana Brenz aliyeniamuru kwa kusema na kwa andiko alipoondoka Smalkaldi ambalo nimewaonyesha ndugu hawa ambao wametia sahihi
Mimi, Dionisio Melander, ninaukubali Ukiri, Utetezi, na Mwafaka katika mafundisho kuhusu Ekaristi
Paulo Rhodio, Mrakibu Mkuu wa Stettin.
Gerardo Oemcken, Mrakibu Mkuu wa Kanisa la Minden.
Mimi, Briksio Northano, mchungaji wa Kanisa la Kristo huko Soest, ninatia sahihi kwa mafungu ya Baba mheshimiwa Martin Luther, na ninakiri kwamba, hadi sasa nimeamini na kufundisha, na kwa Roho wa Kristo nitaendelea kuamini na kufundisha.
Mikaeli Saelio, Mhubiri katika Mansfeld, alitia sahihi
Bwana Petro Geltnero, Mhubiri katika Frankfurt, alitia sahihi
Wendalino Faber, Mchungaji wa Seeburg katika Mansfeld
Yohana Aepino, alitia sahihi na kukubali pamoja na wahubiri wote wa Hamburg maoni ya Dk. Philipp yaliyoongezewa mwishoni kuhusu Ukuu wa Papa.
Kadhalika, mimi Yohana wa Amsterdam, kutoka Bremen
Mimi, Frederik Maikonio, Mchungaji wa Kanisa la Gotha, Thüringen, ninatia sahihi kwa jina langu mwenyewe na kwa niaba ya Yusto Menio wa Eisenach
Mimi, Yohana Lango, Daktari na mhubiri wa Kanisa la Erfurt, ninatia sahihi kwa jina langu mwenyewe na kwa niaba ya wahubiri na watenda kazi wenzangu wengine katika Injili, majina yao:
Bwana mtaalamu mwenye leseni Ludoviko Platzio toka Melsungen, Mch. Bwana Sigismund Kirchner,
Bwana Wolfgang Kiswetter, Bwana Melchior Weittmann, Bwana Yohana Thall, Bwana Yohana Kilian, Bwana Nikolao Faber, Bwana Andrea Menser, ninatia sahihi kwa mkono wangu wenyewe na Mimi, Egidio Melcher, ninatia sahihi kwa mkono wangu wenyewe.
MAKALA KUHUSU MAMLAKA NA UKUU WA PAPA1252
De potestate et primatu papae tractatus
yaliyotungwa na wanatheologia waliokusanyika Smalkaldi mwaka wa 1537
Askofu wa Roma hujitwaza kwamba, amewekwa juu ya maaskofu wote na wachungaji wote kwa njia ya haki ya kimungu.1253 2. Licha ya hayo, anaendelea kudai kwamba, ana haki ya kimungu kwa panga zote mbili, yaani, mamlaka ya kuwateua na kuwaondoa wafalme madarakani.1254 3. Tatu, anasema kwamba, ni lazima kuyaamini mambo haya kwa ajili ya wokovu.1255 Kwa sababu hizo, Askofu wa Roma anajiita wakili wa Kristo hapa duniani.1256 4. Tunaangalia na kukiri kwamba, masharti haya matatu ni ya kinafiki na ya kukufuru, dhalimu na yenye madhara kwa Kanisa. 5. Ili ushuhuda wetu ueleweke, kwanza, tunalifafanua jambo hilo wanalodai kwamba, yeye ndiye aliye juu ya maaskofu wote kwa njia ya sheria ya kimungu. Wao humaanisha kwamba, Papa ni askofu wa kila mahali na wa kiekumeni kama wanavyodai. Hivyo, inawabidi maaskofu na wachungaji wote wa ulimwengu kumwomba baraka na uthibitisho kwa huduma zao. Ana mamlaka ya kuwachagua, kuwabariki, kuwathibitisha na kuwaondoa madarakani maaskofu wote.1257 6. Licha ya hayo, yeye hujipatia mamlaka ya kutunga sheria kuhusu ibada, mabadiliko ya sakramenti, na imani.1258 Anadai sana, masharti, makatazo1259 na sheria zake ziheshimiwe kama masharti ya imani au maagizo ya Mungu yanayozishurutisha dhamiri, kwa kuwa amejipatia mamlaka ya haki ya 1252 Kulingana na andiko la Kilatini makala haya yalitungwa na Philipp Melanchthon. 1253 “Haki ya kimungu,” Kilatini: ‘Iure divino.’ Kinyume chake ni ‘iure humano,’ yaani, “kwa haki ya binadamu.” Linganisha na Gratiano (‘Decr. Gratiani P.I.D. 21 c. 3, D. 22 c. 1-2’) na Gregoriano IX (‘Decr. Gregoriani IX.5, 33. C. 26’). Gratiano, aliyeishi katika karne ya kumi na moja, alitoka Bologna huko Italia na alikusanya maandiko mbalimbali karibu 4,000 kuhusu usimamiaji wa haki ya Kanisa. Kitabu chake kilikuwa msingi wa kitabu cha sheria ya Kanisa la Magharibi, yaani, ‘Corpus iuris canonici.’ Papa Gregoriano IX (mnamo 1148-1241) alimteua Raimundo wa Penafort, aliyetoka nchi ya Uhispania (1185-1275), kuitimiza kazi ya Gratiano kwa maagizo mengine ya Kanisa. Toleo la Raimundo lilitolewa kati ya miaka ya 1230 na 1234.
1254 Kulingana na tangazo la Papa ‘Unam sanctam’ la Papa Bonifasio VIII (mnamo 1234-1303) mwaka wa 1301.
1255 Sinodi ya Konstanzo iliimarisha maoni ya namna hiyo katika mwaka wa 1418.
1256 Kilatini, ‘Vicarius Filii Dei.’ Akina Papa waliendelea kukitumia cheo hiki tangu Papa Inokentio III (11981216).
1257 Kilatini: ‘Plenitudo potestatis’ (ukamilifu wa mamlaka). ‘Decr. Gratiani P.I.D. 21 c. 1, 8.’
1258 Kilatini: ‘Doctrina,’ yaani, yaliyomo ya imani kama mafundisho rasmi ya Kanisa.
1259 Kilatini: ‘Decretun,’ yaani, tamko rasmi.
kimungu. Licha ya haya, anataka mamlaka yake yatangulie maagizo ya Mungu. Jambo la kutisha zaidi ni yeye kuongezea kwamba, ni lazima kuyaamini haya yote kwa ajili ya wokovu.1260
USHUHUDA KUTOKA MAANDIKO MATAKATIFU
7. I. Kwanza kabisa, basi, acheni tuonyeshe kutoka katika Injili kwamba, Askofu wa Roma si aliye juu ya maaskofu na wachungaji wote kwa haki ya kimungu. Katika Luka 22:24-27, Kristo anaukataa wazi ubwana miongoni mwa Mitume. 8. Maana, hili ndilo suala wafuasi wake Kristo walibishania alipoyazungumzia mateso yake: nani angekuwa kiongozi, na kama ilivyokuwa, nani angekuwa naibu wa Kristo baada ya kuondoka kwake? Kristo aliwakemea mitume wake kwa ajili ya kosa hili na akawafundisha kwamba, hakuna anayepaswa kuuchukua ubwana au ukuu miongoni mwao, lakini kwamba, mitume wote walitumwa kwa usawa na iliwabidi kuitumikia Injili pamoja. Kwa hiyo alisema: “Wafalme wa Mataifa huwatawala, lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo.”1261 Tabaini11262 hapa inaonyesha kwamba, ubwana haukubaliki. Jambo hilo hilo linafundishwa katika mfano wa ubishi uliofanana na huu kuhusu ufalme. Kristo alimweka mtoto katikati ya wafuasi wake,1263 akionyesha kwamba, ukuu miongoni mwa watumishi haukutakiwa, jinsi ambavyo mtoto hatafuti wala hajichukulii ukuu binafsi.
9. II. Katika Yohana 20:21, Kristo aliwatuma wanafunzi wake kama watu walio sawa, bila kuwabagua aliposema: “Kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.” Aliwatuma kila mmoja peke yake. Alisema, yeye mwenyewe alitumwa kwa njia hiyo hiyo. Kwa sababu hii, hakumpa yeyote haki au ubwana juu ya wengine.
10. III. Katika Wagalatia 2:2, 6, Paulo anathibitisha bayana kwamba, hakubarikiwa wala hakupata udhibitisho kutoka kwa Petro, wala hamtambui Petro kama mmoja ambaye udhibitisho unapaswa kutafutwa kwake. Kutokana na ukweli huu, yeye anasema kwamba, wito wake haukutegemea mamlaka ya Petro. Lakini wajibu wake ungekuwa kumkubali Petro kama mkuu wake kama Petro angekuwa mkuu wake kwa haki ya kimungu. Hata hivyo, anasema kwamba, yeye aliweza kuihubiri Injili mara moja bila kumwuliza Petro: “Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo,” anasema, “haina tofauti yoyote kwangu; Mungu
1260 ‘Decr. Gratiani P.I.D. 15 c. 2, D. 19 c. 2.6., D. 20 c. 1.’
1261 Lk. 22: 25-26
1262 Kilatini: ‘antithesis.’
1263 Mt. 18: 1-4
hapokei uso wa mwanadamu.” Tena:“hao wenye sifa hawakuniongezea kitu.”1264
Wale waliokuwa na sifa hawakuongezea chochote kwangu. Kwa kuwa Paulo anashuhudia wazi kwamba, hakuwa na haja ya kuutafuta udhibitisho kutoka kwa Petro, hata baada ya yeye kumjia, anafundisha kwamba, mamlaka ya kimitume yanategemea Neno la Mungu, kwamba, Petro hakuwa mkuu kuliko mitume wengine na kwamba, kubarikiwa au udhibitisho havingetafutwa kwa Petro peke yake.
11. IV. Katika 1 Kor. 3:4-8, Paulo anawaweka wahudumu1265 katika tabaka lililo sawa na anafundisha kwamba, Kanisa liko juu ya wahudumu. Kwa hiyo, hamhesabii Petro ukuu au mamlaka juu ya Kanisa au juu ya makasisi wengine. Kwa maana anasema: “Kwamba, ni Paulo, au Apolo, au Kefa, . . . vyote ni vyenu.”1266 Hivyo ni kusema kwamba, Petro au watumishi wengine hawapaswi kuchukua ubwana au mamlaka juu ya Kanisa, au kulilemea Kanisa kwa mapokeo. Mamlaka ya mtu yeyote yasipewe kipaumbele zaidi ya Neno wala mamlaka ya Kefa yasiwekwe juu ya mamlaka ya mitume wengine. Hata hivyo, wakati huo walifikiria hivi: Kefa analitekeleza hili. Yeye ni mtume wa hadhi ya juu. Kwa hivyo, Paulo na wengine wanapaswa kulitekeleza hili: Paulo anampokonya Petro unafiki huu na kukataa kwamba, mamlaka ya Petro ni makubwa kuliko ya wengine au ya Kanisa. 1 Pet. 5:3 inasema: “Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya makasisi wa kanisa.” 1267
USHUHUDA KUTOKA HISTORIA
12. V. Aidha, Sinodi ya Nikea iliamua kwamba, Askofu wa Aleksandria ayatunze makanisa katika Mashariki, na Askofu wa Roma ayatunze makanisa yaliyokuwa chini ya Mji wa Roma. Yaani, yale ambayo yalikuwa katika mikoa ya Roma huko Magharibi.1268 Kwa hiyo, mwanzoni mamlaka ya Askofu wa Roma yalitokana na uamuzi wa sinodi na ambao ni haki ya binadamu, kwa maana ikiwa Askofu wa Roma alikuwa na mamlaka kwa haki ya kimungu, haingekuwa halali kwa sinodi kumpokonya haki yoyote na kuihamisha kwa Askofu wa Aleksandria.
1264 Gal. 2: 6
1265 Kilatini: ‘minister;’ Kijerumani: ‘Kirchendiener,’ yaani, (watumishi wa Kanisa).
1266 1 Kor. 3: 21-22
1267 Kiyunani: “μηδ”
Kilatini: ‘Non dominantes in clero.’ Maandiko ya Kiyunani na Kilatini humaanisha hasa uhusiano wa wachungaji katika Kanisa, si uhusiano wa mchungaji na usharika wake jinsi toleo la ‘Union Version’ linavyotafsiri: “Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao.”
1268 Kanuni ya 6 ya Sinodi ya Nikea ya mwaka wa 325. “Yale yaliyo chini ya Mji wa Roma;” Kilatini: ‘Ecclesiae suburbanae,’ kulingana na fasiri ya Rufinus Turranius (345-410) katika Historia yake ya Kanisa I, 6: Mikoa ya nchi ya Italia, yaani, Kampania, Toskana, Umbria, Piseno, Sisilia, Apulia, Kalabria, Brutii, Lusania, Samnio, Sardinia, Korsika, Valeria.
Hakika, maaskofu wa Mashariki wote wangepaswa daima kutafuta baraka na udhibitisho kutoka kwa Askofu wa Roma.
13. VI. Tena, Sinodi ya Nikea iliamua kwamba, maaskofu wote wanapaswa kuchaguliwa na makanisa yao mbele ya askofu mmoja au zaidi walio jirani.1269 14. Hili pia lilitekelezwa katika nchi za Magharibi na katika makanisa ya Kilatini kama Sipriano na Agostino wanavyoshuhudia.1270 Kwani Sipriano anasema katika barua yake ya nne kwa Kornelio: “Basi sharti utekeleze kwa makini na utende kulingana na desturi ya kimungu na katika matumizi ya kimitume lile ambalo sote tumelitekeleza, takriban katika mikoa yote. Kwa mfano, adhimisho kamili la kuwabariki maaskofu jirani kutoka katika mkoa huo huo wanapaswa kukusanyika pamoja na watu ambao mkuu wao atabarikiwa. Kisha, askofu anapaswa kuchaguliwa mbele ya umati mkubwa kabisa unaoyafahamu maisha ya kila mgombeaji – jinsi tulivyoona ikitekelezwa miongoni mwenu alipobarikiwa mwenzetu Sabino – kiasi kwamba, kura za ndugu wote na kwa njia ya uamuzi wa maaskofu wote waliokusanyika mbele yao, uaskofu uweze kutolewa na mikono iwekwe juu ya anayehusika.” 15. Sipriano anaiita desturi hii kuwa desturi ya kimungu na matumizi ya kimitume, na anatetea kwamba, ilitekelezwa, takriban mikoa yote. Hivyo, kuanzia hapo, siyo baraka wala udhibitisho vilivyotafutwa kutoka kwa Askofu wa Roma. Katika sehemu kubwa ya ulimwengu iwe ni katika makanisa ya Kiyunani au Kilatini, ni wazi kwamba, makanisa hayakuelekeza ukuu na ubwana kwa Askofu wa Roma.
16. VII. Ukuu wa jinsi hiyo hauwezekani. Kwa maana, askofu mmoja hawezi kuwa mwangalizi wa makanisa yote ulimwenguni au makanisa yaliyo mbali huko vijijini yatafute kubarikiwa na yeye peke yake. Inadhihirika kwamba, ufalme wa Kristo umeenea katika sehemu zote ulimwenguni na kwamba, kuna makanisa mengi Mashariki wakati huu ambayo hayatafuti baraka au kibali kutoka kwa Askofu wa Roma. Inavyoelekea ni kwamba, jinsi haikuwezekana kwa ukuu, na makanisa katika eneo kubwa la ulimwengu haikutambua au kulitekeleza jambo hili, ni wazi kwamba, halikuasisiwa.
17. VIII. Sinodi nyingi za zamani zilikutana bila Askofu wa Roma kuzisimamia - kama vile Sinodi ya Nikea na nyinginezo nyingi. Hili pia linaonyesha kwamba, Kanisa halikuutambua ukuu wala umaarufu wa Askofu wa Roma.
18. IX. Hieronimo anasema: “Ikiwa ni mamlaka unayoyataka, dunia ni
1269 Kanuni ya 4 ya Sinodi ya Nikea.
1270 Sipriano katika barua yake ya 67 kwa mchungaji Feliksi na shemasi Aelio. Barua hii ilihesabiwa katika matoleo ya zamani kwa Kornelio. Agostino katika kitabu chake kiitwacho, ‘De baptismo contra Donatistas’ 2, 2 (Kuhusu Ubatizo dhidi ya Wafuasi wa Donato).
kubwa kuliko mji mkuu.1271 Popote alipo askofu - iwe ni Roma au Eugubio au Konstantinopoli au Regio au Aleksandria ana hadhi na ukasisi huo huo.1272 Ni nguvu ya utajiri au unyenyekevu wa umaskini unaomfanya askofu kuwa mkuu au mdogo.”
19. X. Gregorio alipomwandikia Askofu wa Aleksandria alikataa kuitwa askofu wa ulimwengu wote.1273 Katika taarifa1274 anasema kwamba, katika Sinodi ya Khalkedon ukuu ulitolewa kwa Askofu wa Roma lakini hakuuitikia.
20. XI. Mwisho, Papa anawezaje kuwa juu ya Kanisa lote kwa haki ya kimungu, kwa kuwa anachaguliwa na Kanisa na desturi ilienea polepole kwamba, maaskofu wa Roma walikipokea kibali chao kutoka kwa Kaisari?1275
HOJA ZA WAPINZANI KUKANUSHWA
21. Aidha, kulipokuwa na mzozo wa muda mrefu baina ya maaskofu wa Konstantinopoli na Roma kuhusu ukuu, hatimaye, Kaisari Fokasi aliamua ukuu upewe Askofu wa Roma.1276 Lakini kama Kanisa la kale lingekubali ukuu wa Makuhani wa Roma, mzozo huu haungetokea wala agizo la kaisari halingekuwa la lazima.
22. Hapa, kauli fulani zilitumiwa ili kutupinga: “Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu.” Tena: “Nami nitakupa wewe funguo.”
Tena: “Lisha kondoo zangu,” na kauli fulani nyinginezo.1277 Kwa maana, ubishi huu wote umeelezwa na kushughulikiwa vya kutosha katika vitabu vya wanatheologia wetu na maelezo yote hayawezi kurudiwa tena, tunayarejea maandiko hayo na kunuia kwamba, yahesabiwe kama yalivyorudiwa. Hata hivyo, tutayajibu kwa kutumia ufananuzi wake. 23. Katika kauli hizi zote, Petro ni mwakilishi wa kundi lote la mitume kama inavyodhihirika katika muktadha wenyewe. Maana, Kristo hakumwuliza Petro peke yake bali anasema: “Nanyi mwaninena mimi kuwa ni
1271 Kilatini : ‘Orbis maior est urbe.’
1272 Wakati wa Kanisa la Asili, Roma na Aleksandria ilikuwa miji mikuu ya Kaisari. Eugubio (Gubbio) na Regio (Reggio) ilikuwa miji midogo.
1273 Papa Gregorio Mkuu (mnamo 540-604). Ep. Lib. 8 ep. 30 barua kwa Eulogio, Askofu wa Aleksandria.
1274 Kilatini: ‘regestae.’
1275 Kaisari wa Byzantio (Konstantinopoli) alithibitisha uchaguzi wa Askofu wa Roma wakati wa utawala wa Byzantio kuhusu Italia hadi mwaka wa 781. Kaisari Lotaro I (824) na Otto I Mkuu (962) walipatana na Papa kuhusu suala hilo.
1276 Wakati wa Papa Bonifasio III mwaka wa 607.
1277 Mt. 16: 18; Mt. 16: 19; Yn. 21: 17. Wapinzani wa Matengenezo ya Kanisa walivutiwa na aya hizi walipojaribu kutetea Ukuu wa Papa, yaani, Yohana Eck, Hieronimo Emser, Silvester Prierias na Agostino Alveldo.
nani?”1278 Na lile linalozungumziwa katika umoja hapa - “nami nitakupa wewe funguo na lo lote utakalolifunga,” - limetajwa kwingineko katika wingi: “Yo yote mtakayoyafunga,” n.k. Imeandikwa pia katika Yohana: “Mtakaowaondolea dhambi” n.k.1279 Maneno haya yanashuhudia kwamba, funguo zilipeanwa kwa mitume wote sawa na kwamba, mitume wote walitumwa kwa usawa. 24. Kwa kuongezea, ni heri kutambua kwamba, funguo siyo mamlaka ya mtu binafsi lakini ni mamlaka ya Kanisa zima jinsi inavyodhihirishwa na hoja nyingi zilizo wazi na zenye nguvu. Kwani, baada ya kuzungumzia kuhusu funguo katika Mt. 18:19, Kristo alisema: “Wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote,” n.k. Kwa hiyo, anatoa funguo hasa na papo hapo kwa Kanisa. Kwa sababu hiyo, Kanisa lina haki ya wito. Kwa hiyo, katika kauli hizi, ni lazima kumtambua Petro kama mwakilishi wa kundi lote la mitume. Kwa sababu hiyo, kauli hizi hazimpatii Petro hiari yoyote au ukuu au utawala wowote.
25. Katika usemi: “Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu,”1280 ni hakika kwamba, Kanisa halikujengwa juu ya mamlaka ya mtu binafsi bali juu ya huduma ya ukiri alioutoa Petro alipomkiri Yesu kuwa Kristo, Mwana wa Mungu. Kwa hiyo, Kristo anamwita Petro kama mtumishi na kusema, “juu ya mwamba huu,” yaani, juu ya huduma hii. 26. Kando na hili, huduma ya Agano Jipya haikufungwa katika mahali na watu fulani jinsi huduma ya Walawi ilivyo bali imesambazwa ulimwenguni mwote, inapatikana popote ambapo Mungu anatoa vipawa vyake, kwa mitume, manabii, wachungaji na walimu. Huduma siyo halali kwa ajili ya mamlaka ya mtu yeyote binafsi lakini kwa sababu ya Neno lililotolewa na Kristo. 27. Mababa watakatifu wengi kama vile Origene, Ambrosio, Sipriano, Hilario na Beda huutafsiri usemi “juu ya mwamba huu” kwa njia hii na siyo kumaanisha nafsi au ukuu wa Petro.1281 28. Kwa hiyo, Krisostomo anatangaza kwamba, Kristo anasema “juu ya mwamba huu” na siyo “juu ya Petro.” Kwani, alilijenga Kanisa lake siyo juu ya mtu bali juu ya imani ya Petro. Imani hii ilikuwa ipi zaidi ya “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”1282 29. Hilario anasema: “Baba alimfunulia Petro kwamba, alipaswa kusema
1278 Mt. 16: 15
1279 Yn. 20: 23
1280 Mt. 16: 18
1281 Mtaalamu na shahidi Origene (mnamo 185-254) katika ufafanuzi wake juu ya Mathayo (Comment. In Matth. 12: 11. Askofu Ambrosio (mnamo 338-97). Imekuwa dhahiri kwamba, mkusanyiko wa maandiko ulioitwa ‘Ambrosiaster’ hautokani na kalamu ya Askofu Ambrosio. Mkusanyiko huu una ufafanuzi za Waraka wa Mtume Paulo (Comment. katika Eph. 2: 20). Sipriano, Askofu wa Karthago na shahidi (+ 258) ‘De catholica ecclesiae unitate’ (Umoja wa Kanisa Katoliki) cap. 4. Askofu Hilario wa Poitiers (mnamo 315-67) aliitwa “Athanasio wa Kanisa la Magharibi” katika kitabu chake kiitwacho, ‘De Trinitate’ (Kuhusu Utatu) 6, 36-37. Beda Mheshimiwa (Kilatini: ‘Venerabilis’) (mnamo 673-735) mtaalamu wa Biblia na historia huko Uingereza. Exp. Ev. Math. (Ufafanuzi wa Mathayo) 3: 16. 1282 Mt. 16: 16
“Wewe ni Mwana wa Mungu aliye hai.” Juu ya mwamba wa ukiri huo, Kanisa limejengwa. Imani hii ndiyo msingi wa Kanisa.”
30. Kauli hizi: “Lisha kondoo zangu” na: “Je, wewe wanipenda kuliko hawa?”1283 siyo busara kuhitimisha kwamba, zinauweka ukuu maalumu kwa Petro. Kwani Kristo anamwita Petro awalishe kondoo, yaani, alihubiri Neno au aliongoze Kanisa kwa Neno. Petro anaubeba utume huu akiwa pamoja na mitume wengine.
31. Fungu la pili linaeleweka wazi zaidi kuliko lile la kwanza. Hii ni kwa sababu Kristo aliwapa mitume mamlaka ya kiroho peke yake. Yaani, aliwapa amri ya kuihubiri Injili, kuutangaza msamaha wa dhambi, kuzitunza sakramenti na kuwatenga waovu na kanisa bila kutumia nguvu za kimwili. Hakuwapa nguvu ya upanga au haki ya kuanzisha, kumiliki au kuhamisha falme za ulimwengu. Maana, Kristo alisema: “Basi, enendeni, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.”1284 Kadhalika: “Kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.”1285 Zaidi inadhihirika kwamba, Kristo hakutumwa kutumia upanga wala kumiliki ufalme wa ulimwengu kwani alisema: “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu.”1286 Vile vile Paulo alisema: “Si kwamba tunatawala imani yenu.”1287 Tena: “Silaha za vita vyetu si za mwili,”1288 n.k. 32. Kwani, katika mateso yake, Kristo alivikwa taji la miiba, na kwamba, aliongozwa kwenda kudhihakiwa ndani ya vazi la kifalme lenye rangi ya zambarau. Hii ni ishara kwamba, nyakati zitakuja baada ya ufalme wake wa kiroho kupuuzwa – yaani, baada ya Injili kuhangaishwa - wakati ufalme mwingine wa dunia utabuniwa kwa unafiki wa nguvu za Kanisa. 33. Kwa sababu hiyo, katiba ya Bonifasio VIII, tofauti ya sura ya “Omnes,” na matamshi mengine ya jinsi hiyo yanayodai kwamba, kulingana na haki ya kimungu, Papa ni mtawala wa falme za dunia ni za uongo na kufuru.1289 34. Dhana hii imesababisha giza la kutisha kulishukia Kanisa na baadaye machafuko zaidi kutokea katika Ulaya. Vivyo hivyo, huduma ya Injili ilipuuzwa kabisa. Elimu ya imani na ya ufalme wa kiroho vilizimwa. Haki ya Kikristo ilifikiriwa kuwa ile ya utawala wa nje ambao Papa alikuwa ameuanzisha. 35. Kisha, Mapapa walianza kujinyakulia falme, kuhamisha falme,1290 na kuwahangaisha watawala, takriban
1283 Yn. 21: 17 na Yn. 21: 15
1284 Mt. 28: 19-20
1285 Yn. 20: 21
1286 Yn. 18: 36
1287 2 Kor. 1: 24
1288 2 Kor. 10: 4
1289 Tangazo la Papa Bonifasio VIII ‘Unam Sanctam’ la mwaka wa 1301.
1290 Akina Papa waliweka wafalme wapinzani wanne katika Ujerumani: 1077 Papa Gregorio VII, 1246 na 1247 Papa Inokentio IV, 1346 Papa Κlemenso VI. Papa Aleksandro VI, wakati wake, alipanua maeneo ya nchi za Upapa. Kwa kisingizio chake, alinena hati iliyobuniwa, yaani, “Msaada wa Kaisari Konstantino” (Donatio/
mataifa yote ya Ulaya. Hasa kaisari wa Ujerumani,1291 walihangaishwa kwa matangazo ya utengano1292 na vita visivyokuwa vya haki.1293 Wakati mwingine haya yalifanyika ili kuikalia miji ya Italia na wakati mwingine kuwafanya maaskofu wa Ujerumani kuwa chini ya uwezo wao na kuwapokonya watawala haki ya kuwateua maaskofu.1294 Kweli, imeandikwa hata katika “Klementina:” “Milki ikiwa wazi, Papa ndiye mrithi halali.”1295 36. Kwa hiyo, Papa hakujitwalia tu mamlaka ya utawala kinyume cha amri ya Kristo bali hata alijitukuza kwa jeuri juu ya wafalme wote1296. Tendo lenyewe si la kushutumiwa peke yake katika suala hilo. Lililo kufuru zaidi ni kwamba, kama kisingizio chake, alinena kuwa ana mamlaka ya Kristo, hata ya kubadilisha funguo1297 kuwa vitu vya mamlaka ya dunia na kuambatanisha wokovu kwenye maovu haya na fikira potovu kwa kutetea kwamba, kwa ajili ya wokovu, ni lazima kuamini kwamba, utawala huo ni milki ya Papa kwa haki ya kimungu. 37. Makosa haya makubwa mno yaliyoliweka giza juu ya wokovu na Ufalme wa Kristo, yasipuuzwe kabisa. Matokeo yanaonyesha kwamba, yamekuwa balaa kubwa kanisani.
38. Hili lazima liongezewe katika Fungu la Tatu: Hata kama Askofu wa Roma ataushika ukuu na ubora kwa haki ya kimungu, utiifu hautalazimika kuwepo kwa wale makuhani wanaotetea aina za ibada zisizokuwa za kimungu, wanaoziabudu sanamu, na mafundisho yanayopingana na Injili. Kinyume chake, makuhani wa jinsi hiyo na mamlaka ya aina hiyo yanapaswa kutambuliwa kama yaliyolaaniwa. Kwa hiyo, Paulo anafundisha wazi: “Ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.”1298 Tena imeandikwa katika Matendo ya Mitume: “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.”1299 Vivyo hivyo kanuni za Kanisa zinafundisha wazi kwamba, haifai
Constitutum Constantini). Hati hii ilibuniwa katika karne za nane na tisa katika Milki ya Wafranko huko Ulaya ‘Regnum Francorum’ tangu karne ya tano hadi karne ya tisa) . 1291 Wakati wa Enzi ya Κati kaisari wa Ujerumani na akina Papa walipingana kwa ajili ya utawala wa Italia, hasa wakati wa nasaba ya kifalme ya Hohenstaufer hadi mwaka wa 1268. 1292 Kaisari na wafalme wa Ujerumani: 1076 na 1080 Papa Gregorio VII, 1094 Papa Urbano II, 1118 Papa Gelasio, 1160 Papa Aleksandro III, 1201 na 1210 Papa Inokentio III, 1227 na 1239 Papa Gregorio IX, 1245 Papa Inokentio IV, 1267 Papa Κlemenso VI, 1324 na 1327 Papa Yohana XXII, 1346 Papa Klemenso VI. Mfalme wa Uingereza:1208 na 1212 Papa Inokentio III. Ufaransa: 1303 Papa Bonifasio VIII.
1293 Papa Aleksandro VI dhidi ya Karolo VIII wa Ufaransa 1495/6, Papa Yulio II dhidi ya Louis XII wa Ufaransa 1511/13, Papa Klemenso VII dhidi ya Kaisari Karolo V 1526/9.
1294 Mabishano ya usimikaji 1075-1122.
1295 Corp.iur.can. Clementinae II, 11 c. 2
1296 Papa Aleksandro VI aliongoza vita dhidi ya Louis XII wa Ufaransa 1511/13 na Papa Klemenso dhidi ya Kaisari Karolo V 1526/29.
1297 Yaani, funguo za mbinguni, mamlaka ya Kanisa ya kufunga na kufungua duniani, naam, kuwaondolea na kuwafungia watendao dhambi (Mt. 16 : 19; 18 : 18; Yn. 20: 23).
1298 Gal. 1: 8
1299 Mdo. 5: 29
344
kumtii Papa mwasi.1300 Kuhani mkuu wa Walawi alikuwa kuhani bora kuliko wote kulingana na haki ya kimungu. Hata hivyo, haikuwa lazima kuwatii makuhani wakuu waovu jinsi Yeremia na manabii wengine walivyokataa kuwatii. Isitoshe, mitume hawakukubaliana na Kayafa na hawakuwa na masharti yoyote ya kumtii.
ALAMA ZA MPINGA KRISTO
39. Lakini ni alama wazi ya Mpinga Kristo kwamba, Makuhani wa Roma na wafuasi wao huyatetea mafundisho na madhehebu yasiyomcha Mungu. Alama za “Mpinga Kristo”1301 zinalingana na zile za ufalme wa Papa na wafuasi wake. Kwa kuwa, anapomwelezea “Mpinga Kristo” katika Waraka wa Wathesalonike, Paulo anamwita: “Yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba, yeye ndiye Mungu.”1302 Anamzungumzia mmoja anayetawala ndani ya Kanisa na siyo wafalme wa mataifa. Anamwita huyu “Mpinga Kristo” kwa sababu atabuni mafundisho ambayo yanaipinga Injili na atajitwaza kuwa mwenye mamlaka ya kimungu. 40.Kwa upande mmoja, ni dhahiri kwamba, Papa anatawala katika Kanisa na amejenga mamlaka haya kwa ajili yake kwa kisingizio cha mamlaka ya Kanisa na udhalimu. Kama kisingizio cha kuuficha ukweli, waliyatumia maneno haya: “nitakupa wewe funguo.”1303 Halafu, mafundisho ya Papa yanaipinga Injili kwa njia nyingi. Papa anajitwalia aina tatu za mamlaka ya kimungu. Kwanza: kwa sababu mwenyewe amejiwekea haki ya kuyabadilisha mafundisho ya Kristo na aina za ibada zilizoasisiwa na Mungu, na anataka mafundisho na ibada zake mwenyewe zitazamwe kuwa takatifu. Pili: kwa sababu amejichukulia siyo tu nguvu za kufungua na kufunga katika maisha haya, lakini pia amejichukulia mamlaka juu ya nafsi baada ya maisha haya. Tatu: kwa sababu Papa hataki mambo yake yaamuliwe na Kanisa au yeyote na anayainua mamlaka yake kuwa juu ya uamuzi wa sinodi na Kanisa lote.1304 Kutotaka uamuzi utolewe na Kanisa au na yeyote ni kujifanya kuwa Mungu. Mwisho: yeye huyatetea makosa haya ya kutisha sana na ya kukufuru kwa ukatili mkuu na hata huwaadhibu wale wasiokubali1305 kwa njia ya kifo.
1300 Decr. Grat. Pt. 1 Dist. 40 c. 6.
1301 Kilatini: ‘Antichristus.’
1302 2 The. 2: 4
1303 Mt. 16: 19
1304 Decr.Grat. P.I D.40 c. 6. Papa Gelasio I (+ 496): ‘Papa a nemine iudicatur’ (Papa asihukumiwe na yeyote). Tangazo la Papa Leo X la mwaka wa 1516 lililoitwa ‘Aeternus Pastor’ (Mchungaji wa Milele) liliyahukumu maoni yote kwamba, sinodi za Kanisa zina mamlaka juu ya Papa.
1305 Heinrich Voss na Johannes van den Esschen huko Brüssel (Ubelgiji) 1.7.1523; Kaspar Tauber huko Wien (Austria); Heinrich von Zutphen huko Ditmar 10.12.1524, Johann Heuglin huko Meersburg (Ujerumani) 10.5.1527; Leonhard Kaiser huko Scharding 16.8.1527; Lambert Thorn huko Brüssel 15.9.1528, Adolf
41. Kwa sababu hii ndiyo hali ya mambo ilivyo, Wakristo wote wanapaswa kujihadhari kwa kutoshiriki mafundisho ya uongo, kufuru na ukatili wa Papa usiokuwa na haki. Hawana budi kumwacha na kumlaani Papa na wafuasi wake kama ufalme wa Mpinga Kristo jinsi alivyoamuru Kristo: “Jihadharini na manabii wa uongo.”1306 Naye Paulo aliamuru kwamba, walimu wasiokuwa wachaji wanapaswa kuepukwa na kuchukiwa kama waliolaaniwa.1307 Pia katika 2 Kor. 6: 14 anasema: “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini,1308 kwa jinsi isiyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya nuru na giza?
42. Kutokukubali muafaka kwa nchi nyingi na kuitwa watu wa mafarakano ni jambo zito. Lakini mamlaka ya kimungu yanawaamuru watu wote wasijihusishe na wasiunge mkono kufuru na ukatili usiokuwa na haki. Kwa sababu hiyo, dhamiri zetu zimetolewa hatiani. Makosa ya utawala wa Papa ni dhahiri kabisa. Maandiko yote yanatangaza, kwa sauti kuu, makosa haya kuwa mafundisho ya mashetani na ya Mpinga Kristo.1309 43. Ibada za miungu ya uongo katika kuitia misa najisi ni dhahiri. Maana, kwa kuongezea dhulma zaidi, wanajishugulisha katika kujipatia faida zenye fedheha bila aibu. 44. Mafundisho kuhusu toba yamechafuliwa kabisa na Papa pamoja na wafuasi wake ambao wanafundisha kwamba, dhambi zinasamehewa kwa ajili ya stahili za matendo yetu. Halafu, wanatufanya tuwe na mashaka ikiwa kama ondoleo la dhambi linapatikana. Hawafundishi popote kwamba, dhambi zinasamehewa bure kwa ajili ya Kristo na kwamba, kwa imani hii, tunaupokea msamaha wa dhambi. Kwa haya, wanautia giza utukufu wa Kristo, wanazinyang’anya dhamiri faraja iliyo imara, na wanazipiga marufuku ibada za kweli, yaani, kuitumia imani inayoshindana dhidi ya kukata tamaa.
45. Wameyatia giza mafundisho kuhusu dhambi. Wameibuni desturi ya kuzihesabu dhambi zote katika ungamo. Desturi hii imesababisha makosa mengi na ukataji tamaa. Isitoshe, wamezibuni ridhaa kwa njia ambazo zimetia giza zaidi katika fadhili ya Kristo. 46.Kutokana na haya, kulitokea vyeti vya upatanisho ambavyo si kitu bali uongo uliobuniwa kwa kusudi la kuleta faida.1310 47. Halafu, kuna ibada za watakatifu. Ibada hizi zimesababisha mabaya mangapi na ibada za
Clarenbach na Peter Fliesteden huko Köln (Ujerumani) 28.9.1529. Mashahidi hawa wa Matengenezo ya Kanisa walitangulia maelfu na maelfu walioteswa na baadaye kuuawa katika Ulaya na wafuasi wa Papa kwa sababu ya imani na ukiri wao wa Biblia.
1306 Mt. 7: 15. Taz. pia Ukiri wa Augsburg, Fungu la 28, 22-28.
1307 Tit. 3: 10
1308 Kulingana na Andiko la Kijerumani lililofuatia ‘Vulgata.’ Andiko la Kilatini: ‘Ne sitis consortes infidelium’ ( Msiandamane na wasioamini).
1309 I Tim. 4: 1
1310 Taz. ‘Ukiri wa Augsburg,’ Mafungu ya 11 na 25.
sanamu za kutisha kiasi gani?1311 48. Ni vitendo vingapi vya uasherati vilivyotokana na mafundisho ya useja?1312 Mafundisho kuhusu nadhiri yameifunika Injili giza kwa kiasi gani? Hapa wamesingizia kwamba, nadhiri zinaleta haki mbele za Mungu na zinaustahilisha msamaha wa dhambi.1313 Kwa hiyo, wameihamisha stahili ya Kristo hadi kwa desturi za wanadamu na wameyazima kabisa mafundisho kuhusu imani. Wamesingizia, kwa uongo kwamba, desturi hizi zilizo hafifu mno ni ibada na ukamilifu wa Mungu. Wamezipendelea hizi kuliko kazi zinazotendwa kwenye wito ambao Mungu anautaka na ameuamuru. Makosa kama hayo yasipuuzwe kwa kuwa yanapunguza utukufu wa Mungu na yanaleta maangamizi kwenye nafsi. Kwa hiyo, hayawezi kutokutiliwa maanani.
49. Hivyo, dhambi mbili kubwa sana lazima ziongezewe juu ya makosa haya. Kwanza, ni kwamba, Papa anayatetea makosa haya kwa ukatili usiokuwa na haki na kwa adhabu ya kikatili. Pili, ni kwamba, Papa analiondolea Kanisa uamuzi na haruhusu mabishano ya Kanisa la Kikristo yatatuliwe kwa njia inayofaa. Kwa hakika, anadai kwamba, yuko juu ya sinodi na anaweza kuyafuta makatazo ya sinodi, kama jinsi wakati mwingine kanuni za Kanisa zinavyotangaza kwa ushupavu.1314 Mifano inaonyesha kwamba, makuhani watakatifu waliyatekeleza haya kwa ufidhuli mwingi zaidi. 50. Suala la tisa la kanuni ya tatu linasema: “Kiti Kikuu kisihukumiwe na mtu yeyote. Maana hakimu hawezi kuhukumiwa na Kaisari au daraja la mapadre wote au wafalme au umma.”1315 51. Kwa hiyo, Papa huutumia udhalimu kwa njia mbili. Anayatetea makosa yake kwa nguvu na kwa mauaji ya wanadamu na anaukataa uchunguzi wa sheria. Jambo hili la pili linaumiza zaidi kuliko adhabu zozote, kwa kuwa wakati utaratibu wote wa sheria umekiukwa, makanisa hayawezi kuondoa mifumo na ibada za kukufuru. Kwa hiyo, nafsi zisizohesabika zinapotea kizazi baada ya kizazi.
52. Kwa hiyo, waacheni wacha Mungu wayafikirie makosa haya mengi ya utawala wa Papa na udhalimu wake. Kwanza, inawapasa wafahamu kwamba, makosa haya ni lazima yakataliwe na mafundisho sahihi yafuatwe kwa utukufu wa Mungu na wokovu wa nafsi za wanadamu. 53. Pili, inawapasa wafahamu jinsi ilivyo jinai kubwa kuunga mkono ukatili usiokuwa wa haki katika kuwaua watakatifu ambao, bila shaka, Mungu atalipiza kisasi kwa ajili ya damu yao.
1311 Taz. ‘Ukiri wa Augsburg,’ Fungu la 21.
1312 Taz. ‘Ukri wa Augsburg,’ Fungu la 23.
1313 Taz. ‘Ukiri wa Augsburg,’ Fungu la 27.
1314 Decr. Grat. O. 1 D. 16, 17, 19, 21. Decr. Greg. 9. I, 6 c. 4.
1315 Decr. Grat. P. 2 C. 9 q. 3 c. 13. Tangazo la Papa Pio II ‘Execrabilis’ (Makuruhu) mwaka wa 1460 lililaani ukataji rufaa wa sinodi za wakati ujao.
54. Inawapasa hasa walio viungo maalumu vya Kanisa,1316 yaani, wafalme na watawala, kuyatazama maslahi ya Kanisa na kuhakikisha kwamba, makosa yameondolewa na dhamiri zimeponywa. Mungu anawashauri wafalme: “Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, enyi waamuzi wa dunia, mwadhibiwe.”1317 Maana, utunzaji mkuu wa kwanza wa wafalme unapaswa kuwa kuuinua utukufu wa Mungu. Kwa sababu hiyo, itakuwa aibu kwao kuyatumia mamlaka na utawala wao kwa ajili ya kuziimarisha ibada za sanamu na jinai nyingine nyingi zisizohesabika na kwa mauaji ya watakatifu.
55. Ingawa Papa anapaswa kufanya sinodi, Kanisa litawezaje kutakaswa kama Papa hawezi kuliruhusu lolote liamuriwe kinyume na mapenzi yake na hampatii yeyote haki ya kulielezea wazo isipokuwa wafuasi wake ambao amewafunga kwa viapo na laana za kuogofya ili kuutetea udhalimu na maovu yake bila kulijali Neno la Mungu.1318 56. Kwa kuwa maamuzi ya sinodi ni yale ya Kanisa na siyo yale ya makuhani, inawapasa wafalme wauzuie ukware1319 wa makuhani na kuhakikisha kwamba, Kanisa halinyanganywi nguvu za kuhukumu na kuamua kulingana na Neno la Mungu. Kama Wakristo wengine, inawabidi kuyachunguza makosa mengine ya Papa. Hawana budi pia kumkemea Papa anapokwepa na anapozuia ufahamu na uamuzi wa kweli wa Kanisa.
57. Kwa sababu hiyo, ingawa Askofu wa Roma alikuwa na ukuu kwa haki ya kimungu, hapaswi kumtii iwapo anazitetea ibada za kufuru na mafundisho yanapingana na Injili. Kinyume chake, ni lazima kumpinga kama Mpinga Kristo.
58. Makosa ya Papa ni ya wazi na siyo madogo. Ukatili wake ni dhahiri na anautumia pia dhidi ya wacha Mungu. Tunaijua dhahiri amri ya Mungu kwamba, inatupasa kuzikimbia ibada za sanamu, mafundisho ya kufuru, na udhalimu usiokuwa na haki.1320 Kwa hiyo, wacha Mungu wote wana sababu kubwa, za lazima, na wazi kabisa za kutokumtii Papa. Sababu hizi muhimu ni faraja kwa wacha Mungu wakati, wanashutumiwa kwa ajili ya kashfa, mafarakano na mabishano kama jinsi inavyotokea mara nyingi. 59. Kwa upande mwingine, 1316 Kilatini: ‘Praecipua membra ecclesiae.’ Ni muhimu sana kuona kwamba, Melanchthon hasemi hapa kuwa wafalme na watawala ni wakuu wa Kanisa jinsi Wakristo wengi walivyofikiria baadaye wakati wa muundo wa Kanisa la serikali huko Ulaya. Mamlaka ya wafalme na ya watawala si mamlaka ya kuliongoza Kanisa bali ni kipawa cha kulisaidia Kanisa kutoka kwa hali mbaya ili liweze kuwa Kanisa la Kikristo tena.
1317 Zab. 2:10
1318 Zamani maaskofu wakuu peke yake walikula kiapo cha utiifu kwa Papa. Baadaye maaskofu wote walilazimika kula kiapo cha utwana kwa Papa aliyejiinua kuwa Lodi Mkuu kulingana na aina za haki ya Enzi ya Kati huko Ulaya.
1319 Tamaa ya kiume au kike isiyozuiwa, nyege
1320 Isa. 48: 20; 52: 11; Yer. 51: 45; 2 Kor. 6: 17; Ufu. 18: 4; Taz. pia Mt. 24: 15-18; Mk. 13: 1416.
348
wale wanaokubaliana na Papa na wanaoyatetea mafundisho yake na ibada zake za kukufuru, wanajinajisi kwa ibada za sanamu na mawazo ya kukufuru, wanajifanya kuwa na hatia ya damu za wacha Mungu ambao Papa anawaadhibu na wanaupunguza utukufu wa Mungu. Vile vile, wanauzuia ustawi wa Kanisa kwa njia ya kuyaimarisha makosa na dhambi, ili kuyalazimisha kwa vizazi vyote vya baadaye.
MAMLAKA NA UTEKELEZAJI WA SHERIA WA MAASKOFU
Katika Ukiri na Utetezi, kwa kawaida, tumeyafafanua yale tunayoweza kuyasema kuhusu mamlaka katika Kanisa.1321
60. Injili inawataka wanaoyaongoza makanisa waihubiri Injili, wautangaze msamaha wa dhambi, wazitunze sakramenti, na licha ya hayo, waitekeleze sheria, yaani, wawatenge na Kanisa wenye makosa ya wazi na kuwatangazia msamaha wa dhambi wanaotubu. 61. Kulingana na ukiri wa wote, hata ule wa maadui zetu, ni dhahiri kwamba, mamlaka haya ni haki ya kimungu kwa wote wanaoyaongoza makanisa iwe wanaitwa wachungaji au wazee au maaskofu wa Kanisa.1322 62. Kwa hiyo, Hieronimo anafundisha wazi katika nyaraka za mitume kwamba, wale wote wanaoyaongoza makanisa ni maaskofu na wazee wa kanisa. Ananukuu yafuatayo kutoka katika Waraka wa Tito: “Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru.” Anaonyesha kwa maneno haya yafuatayo: “Na askofu awe mume wa mke mmoja”1323 Kadhalika, Petro na Yohana wanajiita wazee.1324 Kisha, Hieronimo anaongezea: “Baadaye, mtu mmoja alichaguliwa ili kuwaongoza wengine wote. Jambo hilo lilikusudiwa kuyazuia mafarakano, watu kadhaa wasije wakajikusanyia makundi tofauti na kuliharibu Kanisa la Kristo. Kwa kuwa, huko Aleksandria, tangu wakati wa Marko Mwinjilisti hadi nyakati za maaskofu Ezra na Dionisio,1325 kila wakati wazee walimchagua mmoja wao, wakampa hadhi ya juu, na kumwita askofu. Aidha, vivyo hivyo, jeshi huweza 1321 ‘Ukiri wa Augsburg’ 28. ‘Utetezi wa Ukiri wa Augsburg’ 28. 1322 Taz. Mdo. 20: 17,28: wachungaji, wazee, viongozi, na maaskofu ni majina ya huduma iyo hiyo, yaani, majina ya daraja la uchungaji. Kadhalika, katika Waraka kwa Tit. 1: 5-7: Mzee ni jina sawa na la askofu. Wakati wa Matengezo ya Kanisa katika karne ya 16 jina “mzee,” (Kiyunani: ‘presbyteros’) lilibadilika miongoni mwa Waanabaptisti na wafuasi wa H. Zwingli na J. Calvin kumaanisha mwanachama wa kawaida asiyekuwa mchungaji wa kamati ya usharika wa Kanisa. Kwa ajili ya misioni ya makanisa ya Kipresbiteri na Kianabaptisti, maana hii ya jina “mzee wa Kanisa” isiyokuwa sahihi, ilienea Afrika ya Mashariki yote. Taz. marejeo yanayofuatia.
1323 Hieronimo: Waraka wa 146 kwa Euangelo (Euagrio) na Waraka wa 69 kwa Okeano. Tit. 1: 5-7.
1324 1 Pet. 5: 1; 2 Yoh. 1; 3 Yoh. 1
1325 Dionisio Mkuu, Askofu Mkuu wa Aleksandria, huko Misri, (+264).
kumchagua Amiri Jeshi Mkuu wake. Mashemasi nao huweza kumchagua kutoka miongoni mwao, anayejulikana kuwa mashughuli na kumwita Shemasi Mkuu.1326 Maana, mbali na kuwabariki wachungaji, ni lipi ambalo askofu hulifanya, ambalo mzee wa Kanisa halifanyi?”
63. Kwa hiyo basi, Hieronimo anafundisha kwamba, tofauti iliyoko kati ya daraja la maaskofu na wazee au wachungaji1327 ni mamlaka ya kibinadamu. Ukweli wenyewe unalishuhudia hili, kwa Maana, kimamlaka wao ni sawa jinsi nilivyosema. 64. Baadaye, jambo moja lilileta tofauti kati ya maaskofu na wachungaji, yaani, haki ya kuwabariki wachungaji katika Kanisa. Maana, iliamuliwa kwamba, askofu mmoja anapaswa kuwabariki wachungaji katika makanisa mengi. 65. Lakini kwa kuwa tofauti kati ya maaskofu na wachungaji siyo kwa haki ya kimungu, ni dhahiri kwamba, kubarakiwa kunakotolewa na mchungaji katika Kanisa lake ni halali na kunadumu katika haki ya kimungu.
66. Hivyo basi, maaskofu wa kawaida wanapokuwa maadui wa Injili na hawataki kuwabariki wachungaji, makanisa yenyewe yana haki ya kuwabariki. 67. Kwa kuwa, popote Kanisa lilipo, haki ya kuihudumia Injili pia ipo. Kwa sababu hiyo, ni lazima Kanisa lihifadhi haki yake ya kuwaita, kuwachagua, na kuwabariki wachungaji. 1328
Haki hii ni kipawa maalumu kinachotolewa kwa Kanisa peke yake. Hakuna mamlaka ya kibinadamu inayoweza kukitoa kwa Kanisa jinsi Paulo anavyoshuhudia katika Waefeso anaposema: “Alipopaa juu akawapa wanadamu vipawa.”1329 Anawahesabu wachungaji na walimu kuwa miongoni mwa vipawa maalumu vinavyotolewa kwa Kanisa peke yake. Pia anaongezea kwamba, vinatolewa kwa kazi ya huduma na kwa kuujenga mwili wa Kristo. Basi, palipo na Kanisa la kweli, haki ya kuwachagua na kuwabariki makasisi lazima iwepo pia. Kwa hivyo, wakati wa dharura, hata Mkristo wa kawaida anatangaza ondoleo la dhambi na anakuwa kasisi au mchungaji wa mwingine jinsi Agostino anavyotoa mfano kuhusu Wakristo wawili waliokuwa melini. Mmoja alimbatiza
1326 Baadaye katika historia ya Kanisa, cheo hiki cha ushemasi kilihesabiwa kuwa cheo cha daraja la mapadre na jina la Shemasi Mkuu lilikuwa la Kasisi Mkuu, kwa mfano, katika Makanisa ya Kianglikana.
1327 Yaani, mchungaji au kasisi wa usharika.
1328 Kwa mfano, huko Bohemia, maaskofu wote waliacha makanisa yao na kukataza makanisa baraka za makasisi kabisa. Luther aliwaandikia waraka au makala yenye mashauri yake ‘De Instituendis Ministris Ecclesiae’ (Kuwabiriki Wahudumu wa Kanisa) mwaka wa 1523. Kulingana na makala haya, kuwabariki wachungaji ni wajibu wa askofu kwa niaba ya viumbe vyote vya mwili wa Kristo. Maaskofu wakikataa wajibu huu kwa sababu zisizolingana na Biblia, kasisi yeyote anaweza kumbariki mchungaji kwa wito wa Kanisa lingine.
1329 Efe. 4: 8,11-12.
mkatekumeni mwenzake1330 na aliyebatizwa, akamtangazia aliyembatiza ondoleo la dhambi.1331 68. Hapa, maneno ya Kristo yanafaa yanayoshuhudia kwamba, funguo zilitolewa kwa Kanisa na siyo kwa watu fulani: “Walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo hapo hapo katikati yao.”1332
69. Mwisho, hili linathibitishwa na kauli ya Petro: “Ninyi ni ukuhani wa kifalme.”1333 Maneno haya yanahusu Kanisa la kweli ambalo, kwa sababu ndilo lililo na ukuhani peke yake, hakika, ndilo ambalo lina haki ya kuwachagua na kuwabariki wachungaji. 70. Desturi ya kawaida mno katika Kanisa inalishuhudia hili pia. Zamani umma uliwachagua wachungaji na maaskofu. Baadaye, askofu wa Kanisa hilo au wa Kanisa jirani aliletwa kumthibitisha aliyechaguliwa kwa kumwekea mikono. Kubarikiwa kuwa mchungaji hakukuwa lolote zaidi ya uthibitisho huo. 71. Baadaye, sherehe mpya ziliongezewa ambazo Dionisio anazielezea; Lakini yeye ni mwandishi bandia wa karibuni, hata awe nani, jinsi maandiko ya Klemenso yalivyo ya bandia.1334 Tena, waandishi wa karibuni zaidi waliongezea maneno: “Ninakupa wewe mamlaka ya kutoa dhabihu kwa ajili ya walio hai na wafu.”1335 Lakini hata hili halipatikani katika Dionisio!
72. Kutokana na hakika hizi zote, kuna ushahidi kwamba, Kanisa linashikilia haki ya kuwachagua na kuwabariki makasisi. Kwa sababu hiyo, maaskofu wanapokuwa waasi au wanapokataa kuwabariki wachungaji, 81. makanisa yenyewe yanalazimika kuwabariki wachungaji na makasisi kwa haki ya kimungu. Uovu na udhalimu wa maaskofu husababisha mfarakano na kutokuelewana. Maana, Paulo anaamuru kwamba, maaskofu wanaofundisha na kutetea
1330 Mwanafunzi katika daraja la ubatizo. 1331 Waraka wa Agostino kwa Fortunato. Decr. Grat. P. 3 D. 4 c. 36. Kulingana na mafundisho ya Martin Luther katika makala yake ya ‘De Instituendis Ministris Ecclesiae,’ kila Mkristo ana mamlaka ya kusali, kulitangaza Neno la Mungu, kubatiza na kulitangaza ondoleo la dhambi katika hali ya dharura, kwa sababu matendo haya ni ya lazima kwa wokovu. Hata hivyo, Wakristo wa kawaida hawawezi kuitunza Sakramenti ya Chakula cha Bwana. Mchungaji aliyebarikiwa asipokuwepo, lazima wasubiri hadi kasisi aliyebarikiwa awepo kwa sababu kuitunza Sakramenti ya Ekaristi ni wajibu wa mapadre na sakramenti hii si ya lazima kwa wokovu.
1332 Mt. 18: 20
1333 1 Pet. 2: 9
1334 Maandiko bandia chini ya jina la Dionisio Mwareopago (Mdo. 17:34) yalitungwa mwishoni mwa karne ya nne huko Shamu ‘Περι
(Uongozi wa Kasisi wa Kanisa). Luther anamaanisha andiko bandia la Klemenso aliyekuwa Askofu wa Roma (+ mnamo 100). Wakati wa Matengenezo ya Kanisa, andiko moja tu lililojulikana lilitungwa mwishoni mwa karne ya kwanza: ‘Recognitionum libri X ad Jacobum Fratrem Domini’ (Vitabu Kumi vya Uchunguzi wa Yakobo Ndugu yake Bwana). Baadaye, maandiko mengine bandia ya Klemenso yalijulikana.
1335 Maneno ya askofu anapotoa vyombo vya Ekaristi kwa anayebarikiwa kuwa mchungaji. Kiraa hiki kililetwa katika liturgia ya kumbariki mchungaji katika Kanisa la Magharibi katika karne ya tisa.
81 Andiko la Kijerumani, ‘Tüchtige Personen‘ (Watu hodari).
82 Gal. 1: 7-9. Kiyunani: ‘αναθημα.‘
mafundisho na mifumo ya ibada za kukufuru wachukuliwe kama waliolaaniwa.82
73. Tumezungumzia kubarikiwa kwa wachungaji ambalo ni jambo moja –jinsi Hieronimo asemavyo - linalowatofautisha maaskofu na makasisi wengine. Hivyo basi, hakuna haja ya kuzijadili huduma zingine za maaskofu, si lazima kuzungumzia kipaimara wala kubarikiwa kwa kengele, ambayo ndiyo karibu mambo pekee1336 waliyojiwekea. Hata hivyo, lazima tuseme jambo kuhusu utekelezaji wa sheria.
74. Ni hakika kwamba, wachungaji wote wana mamlaka ya kawaida ya kuwatenga na Kanisa wenye hatia ya makosa ya wazi. Maaskofu wamejiwekea mamlaka haya peke yao na wameyatumia kwa ajili ya faida. Inajulikana wazi kwamba, maofisa wa maaskofu1337 (jinsi wanavyoitwa) - wakiyatumia masharti yasiyovumilika na pengine kwa ukatili au kwa uchoyo au tamaa nyinginezo, wamewadhulumu watu na kuwatenga na Kanisa bila utaratibu wa haki ya sheria. Ni udhalimu wa namna gani kwa maofisa wa maaskofu katika miji kuwa na mamlaka ya kutenga watu na Kanisa kiholela bila haki ya sheria? 75. Ni katika mambo gani wameyatumia vibaya mamlaka haya! Siyo katika kuyaadhibu makosa halisi, bali katika kushughulikia mifungo au sherehe na mambo hafifu yanayofanana na hayo. Ili wawe na hakika, nyakati zingine waliwaadhibu watu waliojihusisha na uzinzi. Lakini kuhusiana na hili, mara nyingi waliwahangaisha watu wasio na hatia na waaminifu. Licha ya hayo, kwa kuwa hili ni shitaka baya mno, hakuna mtu anayepaswa kuhukumiwa bila haki ya sheria. 76. Kwa hiyo, kwa kuwa maaskofu wenyewe wamejiwekea utekelezaji huu wa udhalimu wa sheria na wanautumia vibaya, hakuna haja kuwatii maaskofu kwa sababu ya utekelezaji huu wa sheria. Kwa kuwa tuna sababu nzuri za kutowatii, ni haki kuurejesha utekelezaji huu wa sheria kwa wachungaji wacha Mungu na kuhakikisha kwamba, unatumika vyema kwa ajili ya matengenezo ya maadili na kwa utukufu wa Mungu.
77. Kumebakia utekelezaji wa sheria katika kesi ambazo, kulingana na Kanuni ya Kanisa, zinahusiana na mahakama za Kanisa la Kikristo (jinsi wanavyoyaita) hasa kesi kuhusu ndoa. Kuhusiana na haya pia, maaskofu wana mamlaka kwa haki ya kibinadamu tu na hawajawa nayo kwa muda mrefu. Hii ni kwa sababu yanaonekana katika Mfumo wa Sheria wa Yustiniano katika katiba zilizoitwa “Codex” na “Novellae,”1338 kwamba, awali, kesi za ndoa ziliamuliwa na hakimu.
1336 Taz. ‘Mafungu ya Smalkaldi’ 3, 15: “Mapokeo ya binadamu.”
1337 Kilatini: ‘Officiales;’ maofisa wa askofu kwa utekelezaji wa kisheria katika Kanisa, k.m. katika kesi za nidhamu, na usimamiaji wa ndoa.
1338 Yustiniano I (483-565) Kaisari wa Byzantio (Konstantinopoli). Alitangaza mfumo wa kisheria ‘Codex Iustiniani’ mwaka wa 529, kulikuwepo pia na ongezeko la mfumo wa kisheria wa Kaisari Theodosio II (401-
Kwa haki ya kimungu, mahakimu wa dunia wanalazimika kuitoa hukumu iwapo maaskofu wanazembea. Kanuni za Kanisa zinalikubali hili1339 kwa hiyo, siyo lazima kuwatii maaskofu kuhusiana na utekelezaji huu wa sheria. 78. Na kwa kuwa wamezibuni sheria fulani zisizokuwa za haki kuhusu ndoa na wanazitumia katika mahakama zao, kuna sababu zaidi za kuanzisha mahakama zingine. Kwa kuwa, desturi kuhusu “undugu wa kiroho” siyo ya haki.1340 Vile vile, desturi isiyokuwa ya haki1341 ni ile inayomzuia mtu asiyekuwa na hatia asioe baada ya talaka.
Pia kwa jumla, sheria isiyokuwa ya haki,1342 ni ile inayoidhinisha ndoa zote za siri na za uchumba wa udanganyifu katika ukiukaji wa haki ya wazazi. Vivyo hivyo, sheria kuhusu useja wa makasisi siyo ya haki. Pia kuna mitego mingine ya dhamiri katika sheria zao ambayo haitakuwa na faida kuichambua yote hapa. Imetosha kuonyesha kwamba, kuna sheria nyingi za Papa zisizokuwa za haki katika masuala ya ndoa, na kwamba, kwa sababu ya haya, inawapasa mahakimu kuzianzisha mahakama zingine.
79. Kuna sababu nyingi za kutosha zinazoyalazimisha makanisa yasiwatambue kama maaskofu. Hii ni kwa sababu, maaskofu ambao ni wafuasi wa Papa wanayatetea mafundisho na mifumo ya ibada za kukufuru na hawaweki walimu wacha Mungu. Badala yake, wanauunga mkono ukatili wa Papa. Licha ya hayo, wamewapokonya wachungaji utekelezaji wa sheria na wanautekeleza peke yao kwa udhalimu. Mwisho, wao huzifuata sheria zisizokuwa za haki katika maswala ya ndoa. 80. Wao wenyewe inawapasa kukumbuka kwamba, maaskofu wamepewa mali kama sadaka kwa ajili ya usimamizi na manufaa ya makanisa, jinsi sheria isemavyo: “Karama inatolewa kwa ajili ya huduma.”1343 Kwa sababu hiyo, hawawezi kuzimiliki sadaka hizi kwa dhamiri njema. Wakati huo huo, wanazipora fedha za Kanisa, ambalo linazihitaji kwa msaada wa makasisi, kuyastawisha masomo, kuwatunza maskini, na kuzianzisha mahakama hasa zinazohusu kesi za ndoa.1344 81. Aina na idadi ya ugomvi kuhusu mambo ya 450) mwaka wa 438. Mfumo wa kisheria wa Kaisari Yustiniano ulikuwa msingi wa maarifa ya sheria ya Kirumi, hasa katika Magharibi ya Ulaya. Kulingana na ‘Codex Iustiniani’ mamlaka yamegawanyika katika ‘imperium’ (dola) iliyohusiana na mambo ya dunia na ‘sacerdotium’ (ukuhani) uliohusiana na mambo ya kimungu. Dola na ukuhani vilichukuliwa kuwa mambo ya kutegemeana. ‘Codex Iustiniani’ ilikuwa pia msingi wa haki ya Kanisa la Magharibi, yaani, Sheria ya Kanuni.
1339 Decr. Greg. 9. V, 26 c. 2.
1340 Marufuku kuhusu ndoa kati ya wadhamini wa Ubatizo; Decr.Greg. 9. 4, 11.
1341 Akina Baba wa Kanisa walitoa hoja ya marufuku hii katika Mt. 5: 32; Mk. 10: 11; Lk. 16: 18
1342 Martin Luther alipingana vikali na wanasheria huko Wittenberg kuhusu suala hilo.
1343 Corp.iur.can. 6. 1, 3 c. 15 (Mfumo wa Sheria ya Kanuni).
1344 Mahakama ya namna hiyo ya Kanisa yalianzishwa huko Wittenberg mwaka wa 1539.
ndoa ni makubwa kiasi kwamba, yanahitaji mahakama maalumu. Lakini mali za Kanisa zinahitajika ili kuweza kuyaanzisha. 82. Petro alitabiri kwamba, wakati ujao, kutatokea maaskofu waovu watakaozifuja sadaka za Kanisa kwa anasa badala ya kuzitunza huduma zao. Acheni wanaolilaghai Kanisa wafahamu kwamba, Mungu atawaadhibu kwa ajili ya uhalifu wao.
ORODHA YA MADAKTARI NA WAHUBIRI WALIOTIA
SAHIHI UKIRI NA UTETEZI 15371345
Kwa agizo la watawala maarufu mno na vyeo vya heshima na vya miji, inayokiri mafundisho ya Injili, tumerudia kuyasoma tena mafungu ya Ukiri uliotolewa kwa Kaisari katika Baraza la Augsburg.1346 Kwa fadhili za Mungu, wahubiri wote ambao wamehudhuria mkutano huu wa Smalkaldi, wanakiri kwa muafaka kwamba, wanakubaliana na mafungu ya Ukiri wa Augsburg na Utetezi wake katika makanisa yao. Pia Wanakiri kwamba, wanakubaliana na fungu kuhusu ukuu wa Papa na mamlaka yake na pia kuhusu utekelezaji wa maaskofu, lililowasilishwa kwa watawala waliokuwa hapa Smakaldi. Kulingana na hayo, wanazitia sahihi zao.
Mimi Dk. Yohana Bugenhagen wa Pommern ninatia sahihi katika mafungu ya Ukiri wa Augsburg, Utetezi wa Ukiri wa Augsburg na fungu kuhusu upapa lililotolewa kwa watawala huko Smalkaldi.
Pia mimi Dk. Urbano Rhegio, mrakibu mkuu wa makanisa katika Mkoa wa Luneburg, ninatia sahihi.
Nikolao Amsdorf wa Magdeburg alitia sahihi.
Georg Spalatino wa Altenburg alitia sahihi.
Andrea Osiander ninatia sahihi.
M. Veit Dietrich wa Nürnberg, alitia sahihi.
Stephano Agrikola Mhubiri wa kitala, alitia sahihi kwa mkono wake mwenyewe.
Yohana Draconites wa Marburg alitia sahihi.
Kondrad Figenbotz aliyatia sahihi yote.
1345 Kulingana na andiko la Kijerumani: ‘Concordia’ (Mwafaka) na idhini ya wahubiri waliokuwepo katika mkutano wa Smalkaldi. “Ukiri” unamaanisha ‘Ukiri wa Augsburg’ (‘Confessio Augustana’) na Utetezi wake unamaanisha (‘Apologia’).
1346 Mwaka wa 1530.
Martin Bucer1347
Erhard Schnepff ninatia sahihi.
Paulo Rhodio Mhubiri wa Stettin.
Gerdt Oemken mrakibu mkuu wa Kanisa la Minden.
Briksio wa Noirde Mhubiri wa Soest.
Simon Schneeweiss Mchungaji wa Crailsheim.
Tena mimi Pomeranus1348 ninatia sahihi kwa jina la M. Yohana Brenz, jinsi alivyoniamuru.
Philipp Melanchthon alitia sahihi kwa mkono wake mwenyewe.
Antonio Korvino alitia sahihi kwa niaba yake mwenyewe na kwa niaba ya Adamu wa Fulda kwa mkono wake mwenyewe.
Yohana Schlagenhaufen alitia sahihi kwa mkono wake mwenyewe.
Georgio Helt wa Forchheim
Mikaeli Selio, mhubiri wa Mansfeld.
Petro Geltnero, mhubiri wa Kanisa la Frankfurt.
Dionisio Melander alitia sahihi.
Paulo Fagio1349 wa Strasbourg
Wendalono Faber Mchungaji wa Seeburg katika Mansfeld
Konrad Ötinger wa Pforzheim, mhubiri wa Ulrich, Mtawala wa Württemberg.
Bonifasio Wolfhart1350 Kasisi wa Neno wa Kanisa la Augsburg.
1347 Martin Bucer (1491-1551), alitoka Schlettstadt. Mtawa wa Daraja la Kidominikano 1506-1521. Alikutana na Martin Luther katika majadiliano ya Heidelberg mwakas wa 1518. Mchungaji wa Weissenburg 1522 na Strassbourg 1523-1540, ambapo aliendesha Matengenezo ya Kanisa sana. Alijaribu kuunganisha Walutheri na wafuasi wa Huldrych Zwingli, na baadaye mwenyewe alikuwa mfuasi wa mafundisho ya Zwingli. Alihamia Uingereza mwaka wa 1549 baada ya ‘Interim of Augsburg’ (Hati ya Muda ya Augsburg) na aliendelea kufanya kazi huko Cambridge, alipofariki dunia na alipozikwa. Alitoa mashauri mengi kwa Askofu Mkuu wa Canterbury Tomaso Cranmer kuhusu liturgia na mafundisho ya Ekaristi kulingana na maoni ya Zwingli.
1348 Yaani, Bugenhagen.
1349 Paulus Fagius (mnamo 1504-1549), alitoka Rheinzabern. Mwalimu wa shule ya Isny mwa wa 1527. Alifundisha masomo ya theologia katika Chuo Kikuu cha Strassbourg 1536-1537. Mchungaji wa Isny 15381543. Alipanga Kanisa la Konstanzo 1543-44. Profesa na mhubiri katika Strassbourg 1544-1549. Baada ya ‘Interim of Augsburg’ (Hati ya Muda ya Augsburg) mwaka wa 1548, alihamia huko Uingereza pamoja na Martin Bucer.
1350 Bonifacius Wolfhart Lycosthenes (+ 1543), alitoka Buchheim huko Franken. Aliungwa mkono na Zwingli na Oekolampadius katika Basel. Tangu mwaka wa 1525 alikuwa huko Strasbourg ambapo alikuwa mhubiri
Yohana Aepino mrakibu mkuu wa Hamburg, n.k., alitia sahihi kwa mkono wake mwenyewe.
Kadhalika alimfanya Yohana wa Amsterdam na wa Bremen kutia sahihi.
Yohana Fontano1351 mrakibu mkuu wa Hessen ya Chini, alitia sahihi.
Frederiko Myconio alitia sahihi yake na kwa niaba ya Yusto Menio.
Ambrosio Blaurero.1352
wa Kanisa la Mt. Anna. Baadaye mhubiri wa Kanisa la Mt. Moritz huko Augsburg. Alikuwa mfuasi wa H. Zwingli.
1351 Johannes Fontanus au Fontius (+ 1539, alitoka Wetter. Alipata shahada ya pili katika chuo kikuu, alikuwa mchugaji wa Homberg/Etze miaka ya 1529-1535, Mrakibu Mkuu wa Dayosisi ya Kassel miaka ya 15361538.
1352 Ambrosius Blaurerus (1492-1564), alitoka Konstanzo. Mtawa wa Daraja li Kibenediktino. Aliiacha nyumba ya watawa mwaka wa 1522. Mhubiri Mlutheri wa Konstanzo mwaka wa 1525. Aliitwa mwaka wa 1534 na Mtawala Ulrich wa Württemberg kutekeleza Matengenezo ya Kanisa huko Württemberg pamoja na Erhard Schnepff. Kuhusu mafundisho ya Ekaristi aliungwa mkono na Martin Bucer. Tangu mwaka wa 1538 alihamia Augsburg na alifukuzwa kwa sababu ya upinzani wake dhidi ya ‘Interim of Augsburg’ (Hati ya Muda ya Augsburg) ya mwaka wa 1548.
KATEKISIMO NDOGO
DK. MARTIN LUTHER
Utangulizi wa Luther
Neema, huruma, na amani katika Yesu Kristo, Bwana wetu, kutoka kwa Martin Luther kwa wachungaji na wahubiri wote wenye moyo wa uchaji.
1. Nililazimishwa na hali ile mbaya kabisa niliyokutana nayo juzijuzi nilipoyazuru makanisa fulani, kuitunga katekisimo hii fupi, wazi, na sahili mno. 2. Mungu wa milele! Ni msiba wa namna gani niliouona pale! Umati wote wa kawaida, hasa ule wa mashambani, na pia wachungaji wengi zaidi, hawakuwa na ujuzi wowote juu ya mafundisho ya Kikristo. Hata kulisema jambo hilo kwenyewe kunatutahayarisha kabisa. Japo hawaelewi Sala ya Bwana, Ukiri wa Mitume, na Amri Kumi za Mungu, hawawezi kusema maneno yao. Hata hivyo, wao wote huitwa Wakristo kulingana na jina lile takatifu la Kristo na wanaendelea kupokea Sakramenti Takatifu pamoja nasi. Kwa ufupi, hawahitilafiani na wanyama hata kidogo. Sasa, Injili inapoendelea kufundishwa popote, wamejifunza pia kutumia vibaya uhuru wa Kikristo.
4. Maaskofu, mtamjibuje Kristo kuhusu hayo mtakapodaiwa kuitoa hesabu kwa Mungu? Msiba huu wa dini ya Kikristo ni madaraka yenu pekee. Ninyi mliwaacha watu kupotoka kwa njia hii ya aibu. Mna hatia kabisa kwa sababu ya kutotunza huduma yenu kwa njia hii wakati wowote. Mimi siwatakii ubaya wowote. Je, si ukosefu wa uchaji mkuu, si aibu kuu kabisa kuishurutisha aina moja tu ya Sakramenti na mapokeo yenu, na tena kutotunza kabisa hata kuwadharau wale waliokabidhiwa kwenu kwa kusudi la utunzaji wa imani: hawashiki Sala ya Bwana, Ukiri wa Mitume, au Amri Kumi za Mungu. Ole, ole, wenu!
6. Kwa hiyo, ninawasihi kwa moyo na ninawaapisha ninyi wachungaji na
wahubiri kwa ajili ya Mungu. Fanyeni huduma yenu kwa bidii na watunzeni vizuri wale waliokabidhiwa kwenu na Mungu. Mtafanya vizuri kutusaidia katika kazi hii ya kuufundisha umati katekisimo hii kwa nguvu, hasa kwa wale ambao ni vijana. Wasiwatahayari wale wasiokuwa na ujuzi wa mambo haya, kuujulisha mfano huo tulioutunga neno kwa neno kwa wasikilizaji wao ifuatavyo:
7. Kwanza kabisa, wahubiri waangalie vizuri wasizifundishe Amri Kumi za Mungu au Sala ya Bwana au Ukiri wa Mitume au Sakramenti kwa njia tofauti mara kwa mara. Badala yake, watumie daima mfano ule ule wanapofundisha na wanapoueleza umati. Ninataka kulitoa shauri hilo kwa sababu ya kujua kwamba, si rahisi kuwafundisha watu wasiokuwa wasomi sana au vijana, tusipoutumia na kuukiri mfano ule ule wa maneno tena na tena. Ukiitumia njia ile, na nyingineyo, watu wasiokuwa wasomi sana watafadhaishwa kwa urahisi na shughuli zote za mafundisho yako zitakuwa maangamizi.
8. Mababa watakatifu waliliona jambo hilo pia. Naam, walitaka pia kuwa na mfano mmoja wenye maneno halisi ya Amri Kumi za Mungu, Ukiri, na Sala ya Bwana katika Kanisa. Inatubidi kuuiga uangalifu wao. Hatuna budi kuwafundisha wale wasiokuwa wasomi sana na vijana bila kuibadilisha hata silabi moja wakati wowote wa mafundisho ili muundo wa kazi hii uwe ule ule daima. Basi, ushike daima mfano ule wa kuhubiri juu ya katekisimo uliouteua bila kuhitilafiana nao. 9. Ukiifundisha Injili katika mkutano wa wataalamu, mambo yatakuwa tofauti.
Hapo utapata nafasi ya kuutumia ustadi na usemaji wako. Mimi sipingi hata kidogo ukiyabadilisha maneno kwao, ukiubadilisha muundo wa mafundisho yako hata ukibuni nyuso mbalimbali uwezavyo kwa maneno yako. Lakini wewe, uutumie daima mfano uliotungwa kwa maneno halisi kwa watu wa kawaida. 10. Kazi hii inabidi kuwa ya kwanza. Fundisha Amri Kumi za Mungu na Ukiri na Sala ya Bwana neno kwa neno kwa njia ya kufahamika sana. Halafu, wale walioyasikiliza haya mara nyingi zaidi wajifunze kuyakiriri pia.
11. Watu wengine wakiidharau dini kwa sababu ya kutopenda kujifunza mambo haya, itawabidi wakumbushwe kwamba, wanamkana Kristo na kwamba, wao si Wakristo. Wasikaribishwe katika Sakramenti ya Madhabahu, na wasikubaliwe kuwa wadhamini katika Ubatizo wa watoto. Wasikubaliwe kutumia sheria ya uhuru wa Kikristo kulingana na mapenzi yao. Afadhali warudishwe kwa Papa na hakimu wa dayosisi. Kusema kweli, kwa Shetani mwenyewe. 12. Licha ya hayo, wazazi na wazee wa jamaa wakatae kuwapa riziki. Wangefanya vizuri pia kuwajulisha watu washenzi wa aina hii kwamba, watawala wana rai kuwafukuza wao kutoka nchi yao ili waende mahali pengine.
13. Ijapokuwa hatuwezi wala haiwezekani na hatulazimiki kumshurutisha yeyote kuamini, hata hivyo, inafaa watu wayashike mambo halali. Isitoshe, wajue yale yasiyoruhusiwa kulingana na haki ya watu hao wa mahali wanapoishi na kujipatia riziki yao. Inampasa yeyote ajue na afuate haki za mji ambao anataka kuzitumia faida zake, awe anajali au hajali kama mlaghai au mjanja yeyote.
14. Pili, baada ya watu wasiokuwa wasomi kujifunza kunena maneno ya katekisimo vizuri, wafundishwe maelezo yake ili wapate kuyaelewa kabisa. Unaweza kuutumia mfano huo wetu uliochapishwa hapa au mfano mwingine pia. Kwa kuwa ni lazima kuifundisha katekisimo wazi kwa umati kwa maneno yale yale daima jinsi nilivyohimiza tayari. Kadhalika, ninataka kwamba, maelezo yake yawe yale yale bila mabadiliko ya silabi hata moja. Utumie wakati wa kutosha kwa jambo hilo. Huhitajiki kuyajulisha mambo yote mara moja. Ufuate utaratibu wa maelezo yanayofuatana kwa zamu. Baada ya kueleweka maana halisi ya Amri ya Kwanza, Amri ya Pili ifuatie. Yakifundishwa hivyo yote kwa zamu, tutaiepuka taabu kwamba, akili za watu zilizochanganyikiwa na kuvurugwa na mambo mengi mno, hazitayapoteza yote.
17. Tatu, baada ya kumaliza kuyafundisha maelezo ya katekisimo hii fupi, uongezee maelezo marefu ili wasikilizaji wapate kuyaelewa yote zaidi. Ifafanue kila amri, sehemu zote za Ukiri na Sala ya Bwana kwa mifano. Yataje matendo, matunda na faida zake mbalimbali. Kadhalika, zitaje hatari na laana zinazotupata tusipoyafuata hayo. Yafuate maelezo ya mambo haya yaliyoandikwa maridhawa katika vitabu vya wacha Mungu. 18. Zisisitize mno amri ambazo watu wa mahali pako wanaonekana kuzikiuka zaidi. Nitatoa mifano ya mambo haya: isisitize Amri ya Saba kwa wafanya biashara na kwa wafanyakazi wa mikono. Isisitize amri hii kwa ustadi kwa wakulima na kwa watumishi wote kwa kuwa wao huwashughulikia watu kwa udanganyifu na uhalifu. Kadhalika, ifundishe Amri ya Nne kwa watu wasiokuwa wajuzi na kwa watoto pia kwa kusudi la usalama, ili wajishughulishe kuwa waaminifu katika mambo yote, wawatii mahakimu, wazazi, na wasiivuruge amani ya taifa. Mafundisho ya namna hiyo yanaweza kufafanuliwa kwa kuitumia mifano ya Maandiko Matakatifu, jinsi Mungu alivyowapa adhabu kubwa waliovunja amri hii, na jinsi walioitii walivyobarikiwa katika kazi zao zote kwa njia ya ajabu sana.
19. Pamoja na hayo, wahimize watawala, mahakimu, na wazazi kuhusu huduma zao, ili wazitunze huduma za taifa kwa uangalifu, na wayaangalie vizuri masomo ya watoto wao. Basi, wahimizwe jinsi wanavyoweza kuelewa kwamba, wanalazimika kuyatenda haya kwa ajili ya agizo la Mungu. Wasipotahadhari, watakosea sana mbele za Mungu. Naam, kwa njia hii, wanauondoa utawala wa
Mungu na ule wa binadamu na wanaonekana kuwa maadui wakali mno wa Mungu na wa binadamu. 20. Uwaonyeshe na waone katika taswira ubaya wautendao kwa serikali wasipoyaangalia vizuri masomo ya watoto wao. Kwa maana, hawa pia watakuwa wachungaji, watumishi wa Neno la Mungu, na watumishi wa serikali. Maisha haya kwao hayawezi kupungukiwa bila hasara kubwa mno. Uongezee pia kwamba, Mungu atawaadhibu vikali sana wazazi kwa sababu ya kosa la aina hiyo. Mimi silijui kabisa jambo lingine linalohitaji uangalifu wa namna hiyo. Basi, haiwezekani, baadhi ya wakuu, mahakimu, na wazazi wengine kuambiwa jinsi wanavyolipuuza jambo hili wakati huu. Bila shaka, mambo haya hutoka kwenye mashauri ya Shetani mwenyewe ili kuiepusha Ujerumani na msiba mkubwa mno.
21. Mwisho, ingawa udhalimu wa Papa umepungua na umeharibika tayari; bado unaona watu wengi, karibu kila mahali, hawaendi kwenye Sakramenti siku zote. Wao huidharau kama jambo bure lisilokuwa na faradhi. Hawa pia washawishiwe na wahimizwe kuyaacha maoni ya namna hiyo. Sipendi hata kidogo kumshurutisha mtu mwingine kwa imani au kwa Sakramenti. Wale wanaoamuru sheria, hufanya vibaya sana, nyakati fulani, mahali fulani na mambo kama haya. 22. Lakini walio katika huduma ya Neno la Mungu hawana budi kufundisha kwamba, wasikilizaji wao, walioshurutishwa na mapenzi yao, watakuja kwetu na watatushurutisha sisi, watumishi wa Neno la Mungu, kuwapa Sakramenti bila sheria zetu zozote. Itafanyika kwa mafundisho haya kwamba, ni hatari kubwa kuidharau Sakramenti. Wasioshiriki Sakramenti, angalau mara nne kwa mwaka, katika kundi la Wakristo, hawastahili kuhesabiwa katika kundi hilo. Badala yake, wahesabiwe katika kundi la Wakristo wasioamini na wasioisikiliza Injili. Kristo hakusema, “Ondoa hili” au “Dharau hili,” lakini alisema, “Fanyeni hivi, kila mara mnywapo,” n.k. (1 Kor. 11:25). Kweli alitaka tulitende hili, tusiliache wala tusilidharau. “Fanyeni hivi,” alisema.
23. Fulani akiidharau Sakramenti, kwa hali hiyo anadokeza kwamba, hana dhambi, hana mwili, hana Shetani, hana ulimwengu, hana kifo, hana hatari, na hana jehanumu. Yaani, yeye haamini lolote katika mambo hayo ingawa amezama kabisa ndani ya haya na anakuwa mfungwa wa mamlaka mazito zaidi ya Shetani. Anadokeza kwamba, hahitaji neema, uzima, paradiso, mbinguni, Kristo, Mungu, wala fadhili yoyote. Kwa maana, akiamini kwamba, aligharikiwa sana na makosa hata akakosa neema, bila shaka asingeidharau Sakramenti hii yenye tiba dhidi ya makosa na hazina tele ya fadhili kwetu. Sheria zingine hazihitajiki hata kidogo kuwashurutisha watu waishiriki Sakramenti. Wao wenyewe wangekimbia kwa hiari yao kwa sababu ya mzigo wa makosa yao, wangekushurutisha uwape Sakramenti.
24. Basi, hapa, tusiifanye sheria jinsi Papa alivyoifanya. Jambo linalohitaji kufanywa ni kuelezea waziwazi faida na hasara, hatari na Baraka, pamoja na manufaa ya Sakramenti, ili watu wenyewe wafike kwa hiari yao bila ya kuhitaji ushawishi. Lakini, ikiwa wanakataa kuja, waachwe, na waambiwe kwamba, wote wasiohisi na wasiotambua mahitaji yao muhimu na msaada wa neema ya Mungu, wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani. 25. Ushauri wa jinsi hii usipotolewa kwa watu, ni kosa linalowapa watu nafasi ya kuidharau Sakramenti. Je, watu watakuwa waangalifu namna gani iwapo watumishi wa Neno la Mungu hawafanyi wajibu wao, bali wanakaa kimya? Kwa hiyo, huu ni wajibu wa mchungaji na mhubiri. 26. Huduma ya Neno la Mungu imebadilika kabisa kutoka ile ya wakati wa uongozi wa Papa. Sasa, huduma hii ni ya neema na wokovu. 27. Ndio maana ni ngumu na nzito, yenye hatari na majaribu na haina thawabu au shukrani mbele ya ulimwengu. Lakini Kristo mwenyewe ndiye atakayekuwa thawabu ikiwa kazi hii itafanywa kwa uaminifu. Baba wa neema yote ayajalie haya! Kwake iwe sifa na shukrani milele, katika Kristo Bwana wetu. Amina.
1. AMRI KUMI
Utaratibu wazi ambao bwana wa nyumba atafundishia wenzake1353
Amri ya Kwanza
1. “Usiwe na miungu mingine.”1354
2. Hii ina maana gani?
Imetupasa kumwogopa, kumpenda na kumtegemea Mungu kuliko vitu vyote.
Amri ya Pili
3. “Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.”
4. Hii ina maana gani?
Imetupasa kumwogopa na kumpenda Mungu, ili tusilitaje jina lake kwa kulaani, kuapa tukifanya uganga, tukisema uongo, au tukidanganya, ila kila wakati wa haja tuliite, tuliombe, tulitukuze, na kulishukuru.
Amri ya Tatu
5. “Ikumbuke siku ya sabato uitakase.”1355
6. Hii ina maana gani?
Imetupasa kumwogopa na kumpenda Mungu, ili tusilidharau Neno lake na mahubiri ya jinsi hiyo, ila tulitakase na kwa furaha tulisikie na kujifunza Neno lake.
Amri ya Nne
7. “Waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi.”
8. Hii ina maana gani?
1353 Kulingana na andiko la Kijerumani.
1354 Kut. 20:2-17; Kum. 5:6-21. Katika matoleo mengine (mathalani Nűrnberg 1531, 1558) maneno haya yametanguliwa; “Mimi ni Bwana, Mungu wako.”
1355 Mababa wa Matengenezo ya Kanisa hawakukubali uzingatifu wa Jumamosi kama Siku ya Sabato sawa na Wayahudi na Wakristo wa madhehebu mengine wanavyofanya. Tazama Ukiri wa Augsburg fungu la 28:5760.
Imetupasa kumwogopa na kumpenda Mungu, ili tusiwadharau wazazi na wakubwa wetu, wala tusiwakasirishe, ila tuwaheshimu, tuwatumikie, tuwatii, tuwapende, na kuwastahi.
Amri ya Tano
9. “Usiue.”
10. Hii ina maana gani?
1Imetupasa kumwogopa na kumpenda Mungu, ili tusiyahatarishe maisha ya jirani yetu wala tusimwumize, ila tumsaidie na kumstawisha katika kila haja ya maisha.
Amri ya Sita
11. “Usizini.”
12. Hii ina maana gani?
Imetupasa kumwogopa na kumpenda Mungu, ili kuwa na maisha matakatifu na safi katika neno na tendo, kila mmoja akimpenda na kumheshimu mke wake au mume wake.
Amri ya Saba
13. “Usiibe.”
14. Hii ina maana gani?
Imetupasa kumwogopa na kumpenda Mungu, ili tusitwae fedha au mali ya jirani yetu, wala tusimpunje au kufanya kwa njia yoyote ambayo haistahili, ila tumsaidie kuyaongeza na kuyalinda mapato na mali yake.
Amri ya Nane
15. “Usimshuhudie jirani yako kwa uwongo.”
16. Hii ina maana gani?
Imetupasa kumwogopa na kumpenda Mungu ili tusiseme uongo juu ya jirani yetu, wala kumsaliti, kumsingizia, au kumpotezea heshima, badala yake, tumwombee msamaha, tumsemee mema, na tumsaidie sifa yake isiharibike.
Amri ya Tisa
17. “Usiitamani nyumba ya jirani yako.”
18. Hii ina maana gani?
Imetupasa kumwogopa na kumpenda Mungu, ili tusifanye hila ya kujipatia urithi au nyumba ya jirani yetu, wala kuvipata vitu vyake kwa kuitumia vibaya sheria, ila tumhudumie, na kumsaidia ili apate kuvitunza vilivyo vyake.
Amri
ya Kumi
19. “Usimtamani mke wa jirani yako, au mtumishi wake wa kiume, au mtumishi wake wa kike, au ng’ombe wake, au punda1356 wake au chochote kilicho cha jirani yako.”
20. Hii ina maana gani?
Imetupasa kumwogopa na kumpenda Mungu, ili usimnyang’anye, tusimchukize au kushawishi mke, watumishi au ng’ombe wa jirani yetu, ila tuwasaidie kukaa na kuendelea kumtumikia kwa kuutekeleza wajibu wao.
Mwisho
21. Mungu anasema nini kuhusu amri hizi zote?
Anasema, “Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.” [Kut. 20:5-6]
22. Maana yake ni nini?
Mungu anaogofya na kuwaadhibu wote wanaoziasi amri hizi. Hivyo, tuiogope ghadhabu yake, na tusiziasi amri hizi. Kwa upande mwingine, anawaahidia neema na kila baraka wote wanaozitunza. Kwa hiyo, tumpende, tumtegemee, na tufanye alivyoagiza kwa furaha.
1356 ‘Mifugo’ katika andiko la Kijerumani.
2. UKIRI WA IMANI
Utaratibu wazi ambao bwana wa nyumba atafundishia wenzake
1. Fungu la Kwanza: UUMBAJI
“Namwamini Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia.”
2. Hii ina maana gani?
Ninaamini ya kwamba, Mungu ndiye aliyeniumba mimi na vyote, kwamba, amenipa na anahifadhi mwili na roho yangu, viungo vyote na akili, mawazo yangu, na uelekevu wangu wote wa akili.
Tena, hunipa mavazi na chakula, nyumba na makao, jamaa na milki; siku kwa siku hunipa kwa wingi riziki itoshayo mwili na maisha haya.
Hunilinda dhidi ya hatari zote, hunilinda na kunihifadhi nisipatwe na uovu wowote.
Hayo yote hunifanyia kwa sababu ya wema na rehema yake ya kimungu iliyo kama ya baba. Sikuyastahili mimi; kwa hivyo vyote imenipasa kumshukuru na kumsifu, kumtumikia na kumtii.
Hii ni kweli kabisa.
3. Fungu la Pili: UKOMBOZI
“Namwamini Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, Bwana wetu, aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Mariamu, akateswa zamani za Pontio Pilato, akasulibiwa, akafa na akazikwa. Akashuka kuzimuni. Siku ya tatu akafufuka kutoka kwa wafu. Akapaa mbinguni, na ameketi mkono wa kuume wa Mungu, Baba Mwenyezi. Kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.”
4. Hii ina maana gani?
Ninaamini kwamba, Yesu Kristo ni Mungu wa kweli, Mwana wa pekee wa Baba tangu milele, na pia mwanadamu wa kweli, aliyezaliwa naye Bikira Mariamu, huyu ndiye Bwana wangu, aliyeniokoa, mimi niliyepotea na kustahili kuhukumiwa, amenikomboa na kunitoa kutoka katika dhambi zote, mauti na nguvu za Ibilisi; hakunikomboa kwa dhahabu au fedha, ila kwa damu yake takatifu na kwa mateso na kifo chake, bila hatia, kusudi niwe wake, na niishi
chini yake katika ufalme wake na kumtumikia katika haki ya milele bila hatia na heri, kama alivyofufuka kutoka wafu, anaishi na kutawala pasipo mwisho.
Hii ni kweli kabisa.
5. Fungu la Tatu: UTAKASO
“Namwamini Roho Mtakatifu, kanisa takatifu la Kikristo lililo moja tu, ushirika wa watakatifu, ondoleo la dhambi, ufufuo wa mwili, na uzima wa milele. Amina.”
6. Hii ina maana gani?
Ninaamini kwamba, kwa akili au nguvu zangu mwenyewe siwezi kumwamini Yesu Kristo, Bwana wangu, wala kumfikia. Lakini Roho Mtakatifu ameniita kwa njia ya Injili ameniangaza amenipa vipaji vyake, amenitakasa na kunilinda ili niishike imani ya kweli.
Vivyo hivyo, huliita, hulikusanya, huliangaza, na kulitakasa kanisa la Kikristo lote duniani na kulilinda likae katikaYesu Kristo katika imani moja tu ya kweli.
Katika kanisa hili la Kikristo hunisamehe dhambi zangu kila siku, huwasamehe dhambi zao wote waaminio dhambi zetu kila siku.
Siku ya mwisho atanifufua pamoja na wafu wote, na anipe uzima wa milele katika Kristo pamoja na wote wamwaminio.
Hii ni kweli kabisa.
3. SALA YA BWANA
Utaratibu wazi ambao bwana wa nyumba atafundishia wenzake
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litakaswe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu; na utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea; na usitutie majaribuni, lakini utuokoe kutoka uovu. Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu hata milele. Amina.
Utangulizi
1. “Baba yetu uliye mbinguni”1357
2. Hii ina maana gani?
Kwa maneno haya Mungu anatuhimiza kwa ukarimu tuamini ya kuwa Yeye ni Baba yetu wa kweli na kwamba, sisi ni wanawe wa kweli, ili kwa ujasiri wote na matumaini tuweze kumwomba kama watoto wapendwa wamwombavyo baba yao mpendwa.
Ombi la Kwanza
3. “Jina lako litakaswe.”
4. Hii ina maana gani?
Jina la Mungu lenyewe ni takatifu kwa hakika, lakini tunaomba katika ombi hili kwamba, liweze kuwa takatifu miongoni mwetu pia.
5. Jina la Mungu linatakaswaje?
Jina la Mungu linatakaswa Neno la Mungu linapofundishwa katika ukweli na usafi wake, na sisi, kama wana wa Mungu, pia tunaishi maisha matakatifu kufuatana nalo. Tusaidie kulitenda hilo, mpendwa Baba uliye mbinguni! Lakini yeyote anayefundisha au anayeishi kinyume cha Neno la Mungu hulikufuru jina hilo lake miongoni mwetu. Tukingie hili, Baba uliye mbinguni!
Ombi la pili
6. “Ufalme wako uje.”
7. Hii ina maana gani?
Bila shaka, ufalme wa Mungu huja wenyewe bila sala zetu, lakini tunaomba katika ombi hili kwamba, uje kwetu pia.
8. Ufalme wa Mungu hujaje?
Ufalme wa Mungu Baba aliye mbinguni anapotupatia Roho wake Mtakatifu ili kwa neema yake, tuliamini Neno lake takatifu na kuishi maisha ya kimungu hatimaye hapa na huko baadaye milele.
1357 Martin Luther hakuyaandika maingizo haya katika Kilatini. Yalichapishwa baadaye mwaka wa 1531 katika Kijerumani pekee. Sala ya Bwana ni kufatana na Mt. 6:9-13.
Ombi la Tatu
9. “Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni.”
10. Hii ina maana gani?
Mapenzi ya Mungu mema na ya rehema hutendeka yenyewe hata bila ombi letu, lakini tunaomba katika ombi hili kwamba, yaweze kutendeka kwetu pia.
11. Mapenzi ya Mungu yanatendekaje?
Mapenzi ya Mungu hutendeka anapozuia nakuharibu kila shauri na kusudi baya la Ibilisi, la ulimwengu, na asili yetu ya dhambi, ambavyo hutuzuia kulitakasa jina la Mungu au kuuzuia ufalme wake usije; na anapotupatia nguvu na kutuimarisha katika Neno lake na imani yake mpaka tufe. Haya ni mapenzi yake mema na yenye rehema.
Ombi la Nne
12. “Utupe leo riziki yetu.”
13. Hii ina maana gani?
Hakika, Mungu humpatia kila mmoja mkate wa kila siku, bila maombi yetu, hata kwa walio wabaya, lakini tunaomba katika ombi hili kuwa Mungu atuwezeshe kulifahamu hili na tuupokee mkate wetu wa kila siku kwa shukrani.
14. Nini maana ya riziki yetu?
Riziki yetu ni kila kitu kinachohusu tegemeo na mahitaji ya kimwili kama: chakula, kinywaji, mavazi, viatu, nyumba, makazi, shamba, mifugo, fedha, mali, mume au mke anayemcha Mungu, watoto wachaji, watumishi wachaji, watawala waaminifu na wacha Mungu, serikali nzuri, majira mema ya hali ya hewa, amani afya, udhibiti binafsi, sifa njema, marafiki wema, majirani waaminifu, na kadhalika.
Ombi la Tano
15. “Na utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea.”
16. Hii ina maana gani?
Tunaomba katika ombi hili kwamba, Baba yetu aliye mbinguni hatazitazama dhambi zetu, au kuyakataa maombi yetu kwa ajili yazo. Hatustahili wala hatukustahili lakini tunaomba kwamba, atatupatia vyote kwa neema maana
tunatenda dhambi kila siku na hatustahili lolote ila adhabu. Vivyo hivyo, nasi pia tutawasamehe wanaotukosea kwa moyo na kwa furaha, na tuwatendee mema.
Ombi la Sita
17. “Na usitutie majaribuni.”
18. Hii ina maana gani?
Mungu hamjaribu yeyote. Tunaomba katika ombi hili kwamba, Mungu aweze kutuhifadhi na kutulinda ili Ibilisi, dunia, na asili yetu ya dhambi visiweze kutudanganya au kutupotosha, kuuamini uongo, kukata tamaa, na aibu zingine kubwa na uovu. Ingawa tunajaribiwa na vitu hivi, tunaomba tuweze kuvishinda na kuwa washindi hatimaye.
Ombi la Saba
19. “Lakini utuokoe kutoka uovu.”
20. Hii ina maana gani?
Tunaomba katika ombi hili, kwa kifupi kwamba, Baba yetu aliye mbinguni aweze kutuokoa kutokana na kila uovu wa mwili na moyo, mali na sifa, na mwishowe, wa saa yetu ya kufa ikiwadia, aweze kutupa mwisho wenye Baraka, na kwa rehema atuondoe kutoka bonde hili la huzuni na kutupokea mwenyewe kwake mbinguni.
Mwisho
21. [“Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu hata milele.”]1358 “Amina.”
22. Hii ina maana gani?
Maana yake ni kwamba, inanipasa kuhakikishiwa kuwa maombi haya yanampendeza Baba yetu aliye mbinguni, na kwamba, anayasikia, kwa kuwa Yeye mwenyewe ametuagiza tuombe hivi na ameahidi kutusikia. Amina, amina, maana yake ni “ndiyo, ndiyo, na iwe hivyo.”
1358 Sehemu hii ya Sala ya Bwana haipatikani katika maandiko ya zamani sana ya Agano Jipya. Hii ndiyo sababu haikutumika pia katika utaratibu wa asili wa ibada. Baadaye sehemu hii ya sifa ilipokelewa katika Kanisa. Toleo la Nűrnberg la mwaka wa 1558 na matoleo mengine yaliingizwa baadaye katika Katekisimo Ndogo.
4.
SAKRAMENTI YA UBATIZO MTAKATIFU
Utaratibu wazi ambao bwana wa nyumba atafundishia wenzake
1. Ubatizo ni nini?
KWANZA
2. Ubatizo si maji matupu, bali ni maji yanayotumika kulingana na amri ya Mungu na kuchangamana na Neno la Mungu.
3. Neno hilo la Mungu ni nini?
4. Katika sura ya mwisho ya Mathayo, Kristo Bwana wetu husema: “Basi enendeni mkayafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.” [Mathayo 28:19]
PILI
5. Ubatizo huzitoa faida gani?
6. Huutoa msamaha wa dhambi, na huokoa kutoka mautini, Ibilisi, na huutoa wokovu wa milele kwa wote wanaouamini, kama maneno na ahadi za Mungu zinavyotangaza.
7. Maneno haya na ahadi hizi za Mungu ni zipi?
8. Sura ya mwisho wa Marko, Bwana wetu Yesu Kristo husema: “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa.” Marko 16:16]
TATU
9. Maji yanawezaje kuyatenda matendo haya makubwa?
10. Hakika, si maji yayatendayo matendo haya, bali Neno la Mungu linalochangamana na maji, pamoja na imani inayoliamini neno hili la Mungu katika maji. Kwa kuwa pasipo Neno la Mungu, maji nimaji matupu na si Ubatizo. Lakini yanapochangamana na Neno la Mungu huwa Ubatizo, yaani, maji yahuishayo, yajaayo neema na kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili katika Roho Mtakatifu, kama Mtume Paulo asemavyo katika Tito sura ya tatu: “Alituokoa kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya katika Roho Mtakatifu, ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele
kama lilivyo tumaini letu. Ni neno la kuaminiwa.” [Tit. 3:5-8]
NNE
11. Kubatizwa kwa maji kuna maana gani?
12. Kunaashiria kwamba, Adamu wa Kale aliye ndani yetu, anapaswa, kwa majuto makubwa na toba, kuzamishwa hadi kufa pamoja na dhambi zote na tamaa mbovu, na kwamba, mtu mpya anapaswa kuibuka na kuinuka kila siku na kuishi milele mbele za Mungu katika haki na usafi.
13. Haya yameandikwa wapi?
14. Katika Warumi sura ya sita, Mt. Paulo huandika: “Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.” [Warumi 6:4]
5. UNGAMO LA DHAMBI
Utaratibu wazi ambao bwana wa nyumba atafundishia wenzake
15. Ungamo ni nini?
16. Ungamo lina sehemu mbili:
Kwanza, ni kwamba, tuziungame dhambi zetu; na pili, ni kwamba, tunalipokea ondoleo la dhambi, yaani, msamaha kutoka kwake mchungaji kama kutoka kwake Mungu mwenyewe, bila kushuku, bali kuamini kwa uthabiti kwamba, kwa ondoleo hilo dhambi zetu zinasamehewa mbinguni mbele za Mungu.
17. Tunapaswa kuziungama dhambi za namna gani?
18. Mbele za Mungu tunapaswa kuziungama dhambi zetu zote, hata zile ambazo hatuzifahamu, kama tufanyavyo katika Sala ya Bwana, lakini mbele ya mchungaji tunapaswa kuungama dhambi zile tu ambazo tunazifahamu na tunazozihisi mioyoni mwetu.
19. [Dhambi] hizi ni zipi?
20. Jichunguze kwa makini maishani mwako kufuatana na Amri Kumi: Je, wewe ni baba, mama, mwana, binti, mume, mke, au mfanya kazi? Umekuwa mkaidi, mzinifu au mzembe? Umekuwa mwenye hasira kali, mjeuri, au mgomvi? Umemwudhi fulani kwa maneno au matendo? Umeiba, umekuwa asiyejali,
mharibifu wa chochote, au umeitenda dhuluma yoyote?
Ofisi ya Funguo
Ofisi ya Funguo ni nini?
Ofisi ya Funguo ni yale mamlaka maalumu ambayo Kristoamelipatia Kanisa lake duniani kuwaondolea dhambi wenye dhambi wanaotubu, lakini kuwafungia dhambi wasiotubu mradi wawe hawataki kutubu.
Haya yameandikwa wapi?
Haya ndiyo Mwinjilisti Mtakatifu Yohana ameyaandika katika sura ya ishirini: Naye akiisha kusema hayo akawavuvia, akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.” [Yohana 20:22-23]
Unaamini nini kufuata na maneno haya?
Ninaamini kwamba, wakati wahudumu wa Kristo walioitwa hutushughulikia kwa amri yake ya kimungu, hasa wanapowatenga watenda dhambi waziwazi wasiotubu na ushirika wa Kikristo na kuwasamehe wanaotubu dhambi zao na wanataka kufanya vizuri zaidi, hili ni halali na hakika hata mbinguni, kana kwamba, Kristo Bwana wetu mpendwa anajishughulisha nasi mwenyewe.
6. SAKRAMENTI YA MADHABAHU
Utaratibu wazi ambao bwana wa nyumba atafundishia wenzake
1. Ni nini Sakramenti ya Madhabahu?
2. Sakramenti ya Madhabahu ni mwili wa kweli na damu ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo katika mkate na divai, iliyoanzishwa na Kristo mwenyewe katika kula na kunywa kwa ajili yetu Wakristo.
3. Haya yameandikwa wapi?
4. Wainjilisti watakatifu Mathayo, Marko, Luka, na Mtakatifu Paulo pia wameandika:
Bwana wetu Yesu Kristo usiku ule alipotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega akawapa wanafunzi wake, akisema: “Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu uliotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”
Na vivi hivi pia baada ya kula akakitwaa kikombe, akawapa, akisema: “Nyweni nyote katika hiki. Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili yenu kwa ondoleo la dhambi. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu.”
5. Manufaa ya kula na kunywa huku ni yapi?
6. Maneno haya, “Uliotolewa na iliyomwagika kwa ajili yenu kwa ondoleo la dhambi,” hutuonyesha kwamba, katika Sakramenti ondoleo la dhambi, uzima, na wokovu hutolewa kwetu kwa njia ya maneno haya. Kwa kuwa palipo na ondoleo la dhambi, hapo pana uzima na wokovu pia.
7. Kula na kunywa kimwili kunawezaje kuyatenda mambo makubwa kama hayo?
8. Hakika, kula na kunywa tu haviyatendi mambo haya bali maneno yaliyoandikwa hapa: “Uliotolewa na iliyomwagika kwa ajili yenu kwa ondoleo la dhambi.” Maneno haya, pamoja na kula na kunywa kimwili, ni maneno muhimu katika Sakramenti. Ayaaminiye maneno haya, ana lile yanayolisema: “ondoleo la dhambi.”
9. Ni nani hupokea Sakramenti hii kwa kustahili?
10. Kwa kweli, kufunga na maandalizi ya kimwili ni mazoezi mazuri ya kinje. Lakini mtu huyo ambaye ana imani katika maneno haya anastahili kweli na amejitayarisha vilivyo: “Uliotolewa na imwagikayo kwa ajili ya ondoleo la dhambi.”
Lakini yeyote asiyeyaamini maneno haya au ayatiliaye mashaka hastahili na hajajiandaa, kwa sababu maneno “kwa ajili yenu” huhitaji nafsi zote kuamini.
7. SALA ZA KILA SIKU
Utaratibu wazi ambao bwana wa nyumba atafundishia wenzake kuomba
Sala ya Asubuhi
1. Asubuhi, unapoamka, ufanye alama ya msalaba na kusema: Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
2. Halafu, ukiwa umepiga magoti au umesimama, useme Ukiri wa Mitume na Sala ya Bwana. Kisha unaweza kusema sala hii fupi:
Nakushukuru wewe Baba wa mbinguni kwa Mwana wako mpendwa Yesu Kristo, kwa kuwa umenilinda usiku huu dhidi ya maumivu yote na hatari zote. Nakusihi kwamba unilinde pia siku hii ya leo dhidi ya dhambi na uovu wote, ili matendo yangu na maisha yangu yote yaweze kukupendeza. Mikononi mwako nakabidhi mwili wangu na nafsi yangu na vyote nilivyonavyo. Malaika wako mtakatifu awe pamoja nami ili yule Ibilisi asinishinde. Amina.
3. Kisha uende kazini mwako kwa furaha ukiimba na kumshukuru Bwana
Sala ya Jioni
4. Jioni, unapokwenda kulala, ufanye alama ya msalaba na useme:
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
5. Halafu, ukiwa umepiga magoti au umesimama useme Ukiri wa Mitume na Sala ya Bwana. Kisha, unaweza kusema sala hii fupi ukipata nafasi:
“Nakushukuru wewe Baba wa mbinguni kwa Mwana wako mpendwa, Yesu Kristo, kwa kuwa umenilinda siku hii kwa huruma yako. Nakusihi kwamba unisamehe dhambi zangu zote kadri nilivyotenda makosa, na unilinde usiku huu kwa huruma yako. Mikononi mwako nakabidhi mwili wangu na nafsi yangu na vyovyote nilivyonavyo. Malaika wako mtakatifu awe pamoja nami ili yule Ibilisi asinishinde. Amina.”
Kisha unapaswa kulala salama pasipo hofu.
Utaratibu wazi ambao bwana wa nyumba atawafundishia wenzake kubariki na kushukuru mezani.
Baraka ya Mezani
7. Inawabidi wanafunzi (watoto na wote waliomo nyumbani) kuketi mezani kwa makini na kushikamanisha mikono yao na kusema:
8. Macho ya watu wote yanakuelekea Wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake. Waufumbua mkono wako, wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake. [Zab. 145:15-16]
9. Halafu Sala ya Bwana isemwe na kisha ombi hili:
Bwana Mungu Baba wa mbinguni utubariki kwa vipaji vyako hivi ulivyotupatia, tuvitumie kwa ukarimu wako, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Amina.
Shukrani
10. Inabidi baada ya kula tena kushikamanisha mikono kwa makini kwa njia ile ile na kusema:
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema: kwa maana fadhili zake ni za milele. Kila chenye mwili akipa chakula chake. Humpa mnyama chakula chake, wana–kunguru waliao. Hapendezwi na nguvu za farasi, wala hairidhii miguu ya mtu. Bwana huwaridhia wao wamchao, na kuzitarajia fadhili zake. [Zab. 136: 1, 25; 147:9 - 11]
11. Halafu Sala ya Bwana isemwe, kisha ombi hili:
Tunakushukuru Bwana Mungu, Baba yetu, kwa fadhili zako zote, kwa Yesu Kristo Bwana wetu aishiye na kutawala milele na milele. Amina.
8. MAJEDWALI YA WAJIBU
1. Vifungu fulani vya maandiko matakatifu kuhusu madaraja au vyeo vitakatifu kwa kusudi la kumhimiza kila mmoja kuzitunza huduma na shughuli zake
Kwa Maaskofu, Wachungaji, na Wahubiri
2. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu. 1 Tim. 3: 2-4
Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. 1 Tim. 3: 6
Akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga. Tit. 1:9
Wasikilizaji Wanachowawia Wachungaji Wao.
3. Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili. 1 Kor. 9:14
Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.
Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Gal. 6:6-7
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake. 1 Tim. 5:17–18
Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi. 1 The. 5:12-13
Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala sio kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi. Ebr. 13:17
Kwa Serikali
4. Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo imeamuriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema nawe utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Rum. 13:1-4
Kwa Wananchi
5. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. Mt. 22:21b
Kwa hiyo, ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. Rum. 13:5-7
Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri,
nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu. 1 Tim. 2: 1-3
Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema. Tit. 3:1
Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema. 1 Pet. 2:13- 14
Kwa Wanaume
6. Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe. 1 Pet. 3:7
Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. Kol. 3:19
Kwa wake
7. Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Efe. 5:22
Maana hivyo ndivyo walivyopamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote. 1 Pet. 3:5–6
Kwa Wazazi
8. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. Efe. 6:4
Kwa watoto
9. Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. “Waheshimu baba yako mama yako” -amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi- “Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.” Efe. 6:1-3
Kwa Watumishi wa Kila Aina
10. Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo; wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekezao kwa wanadamu; bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; kwa nia njema
kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu; mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana, kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru. Efe. 6:5-8
Kwa
Waajiri na Wakaguzi
11. Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo. Efe. 6:9
Kwa Vijana
12. Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake. 1 Pet. 5:5–6
Kwa Wajane
13. Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku. Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai. 1 Tim. 5:5-6
Kwa kila Mtu
14. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Rum. 13:9
Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote. 1 Tim. 2:1
9. MASWALI YA KIKRISTO NA MAJIBU YAKE
YALIANDALIWA NA DK. MARTIN LUTHER KWA
WANAOKUSUDIA KUSHIRIKI SAKRAMENTI.
Baada ya ungamo na maelezo katika Amri Kumi, Ukiri, Sala ya Bwana na Sakramenti za Ubatizo na Chakula cha Bwana, mchungaji anaweza kuuliza, au Wakristo wanaweza kujiuliza maswali haya:
1. Je, unaamini kuwa u mwenye dhambi?
Ndiyo, naamini hivyo. Mimi ni mwenye dhambi.
2. Unalijuaje hili?
Kutokana na Amri kumi, ambazo sikuzishika.
3. Je, unasikitika kwa ajili ya dhambi zako?
Ndiyo, nasikitika kuwa nimetenda dhambi dhidi ya Mungu.
4. Umestahili nini kutoka kwake Mungu kwa ajili ya dhambi zako?
Ghadhabu yake, kutopendezwa, kifo cha muda, na hukumu ya milele. Taz. Rum. 6:21-23
5. Je, unatumaini kuokolewa?
Ndiyo, hilo ndilo tumaini langu.
6. Unamwamini nani?
Namwamini Yesu Kristo Bwana wangu mpendwa.
7. Kristo yu nani?
Mwana wa Mungu, Mungu kweli na mwanadamu kweli.
8. Kuna Mungu wangapi?
Mmoja tu, lakini kuna nafsi tatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
9. Kristo alikufanyia nini ili uweze kumtegemea?
Alikufa kwa ajili yangu na alimwaga damu kwa ajili yangu pale msalabani kwa ajili ya msamaha wa dhambi.
10. Je, Baba alikufa pia kwa ajili yako?
Hapana hakufanya hivyo. Baba ni Mungu tu, kama alivyo Roho Mtakatifu; lakini Mwana ni Mungu kweli na mwanadamu kweli. Alikufa kwa ajili yangu na alimwaga damu yake kwa ajili yangu.
11. Unalijuaje hili?
Kutokana na Injili, kutokana na maneno ya kuianzisha Sakramenti, na mwili na damu yake iliyotolewa kwa ajili yangu kama ishara katika Sakramenti.
12. Maneno ya kuibariki Sakramenti ni yapi?
Bwana wetu Yesu Kristo usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha
kushukuru akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, “Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu uliotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Na vivi hivi baada ya kula pia akakitwaa kikombe, akawapa, akisema, “Nyweni nyote katika hiki. Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Fanyeni hivi, kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.”
13. Basi, unaamini kwamba, mwili na damu ya kweli ya Yesu Kristo vimo katika Sakramenti?
Ndiyo naamini hivyo.
14. Nini kinakushawishi kuamini hivyo?
Neno la Kristo: Twaeni, ule, huu ni mwili wangu; nyweni nyote katika hiki, hu ndiyo damu yangu.
15. Tufanye nini tunapokula mwili wake na kunywa damu yake, na twapata ahadi yake kwa njia hii?
Inatupasa kukumbuka na kutangaza kifo chake na umwangikaji wa damu yake, kama alivyotufundisha. Fanyeni hivi, kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.
16. Lazima tukikumbuke na kukitangaza kifo chake?
Kwanza, ili tujifunze kuamini kwamba, hakuna kiumbe kinachoweza kuridhisha dhambi zetu. Kristo tu, Mungu na mwanadamu kweli, aweza kufanya hivyo. Pili, ili tuweze kujifunza kutishwa na dhambi zetu, na kuzifikiria kama za hatari. Tatu, ili tupate furaha na faraja katika Kristo tu, na kwa njia ya yeye tupate kuokolewa.
17. Ni msukumo upi uliomfanya Kristo kufa na kulipa deni lote kwa ajili ya dhambi zetu?
Upendo wake mkuu kwa Baba yake na kwangu na wenye dhambi wengine, kama ilivyoandikwa katika Yn. 14; Rum. 5; Gal. 2 na Efe. 5.
18. Mwisho, kwa nini unapenda kushiriki Sakramenti?
Ili niweze kujifunza kuamini kuwa Kristo, kwa upendo mwingi, alikufa kwa ajili ya dhambi zangu, na pia kujifunza kutoka kwake kumpenda Mungu na jirani yangu.
19. Nini kinapasa kumwonya na kumtia moyo Mkristo kupokea Sakramenti
kila mara?
Kwanza, vyote amri na ahadi za Kristo Bwana. Pili, hitaji lake mwenyewe lenye mkazo, kwa sababu ya kile ambacho amri, kutia moyo, na ahadi vimetolewa.
20. Lakini ufanye nini ikiwa huna hakika ya hitaji hili na huna njaa na kiu kwa ajili ya Sakramenti?
Kwa mtu wa namna hiyo hakuna ushauri mzuri zaidi unaoweza kutolewa kuliko huu: kwanza, lazima aguse mwili wake ili kuona kama bado ana nyama na damu. Kisha lazima aamini kile ambacho Maandiko Matakatifu husema juu yake katika Gal. 5 na Rum. 7.
Pili, lazima aangalie huku na kule kuona kama yuko bado ulimwenguni, na kumbuka kwamba, hapatakuweko kutokuweko kwa dhambi na taabu, kama
Maandiko Matakatifu yasemavyo katika Yn. 15–16 na katika 1 Yoh. 2 na 5.
Tatu, bila shaka atakuwa na Ibilisi pia akimzunguka, ambaye akiwa na siku yake ya uongo na usiku atamfanya asiwe na amani, ndani au nje, kama
Maandiko Matakatifu yanavyomchora katika Yn. 8 na 16; 1 Pet. 5; Efe. 6; na 2 Tim. 2.
ANGALIZO
Maswali haya na majibu si mchezo wa mtoto, bali yanawekwa pamoja kwa uangalifu wa kusudi kubwa na mheshimiwa na mwenye bidii Dk. Luther kwa ajili ya vijana na wazee. Kila mmoja na azingatie na kulifikiria kuwa jambo la maana; kwa kuwa Mt. Paulo huwaandikia Wagalatia, katika sura ya sita (6:7): “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi.”
KIJITABU KIDOGO CHA KUFUNGISHA NDOA KWA WACHUNGAJI WA KAWAIDA1359
Martin Luther
1. “Nchi nyingi na tamaduni nyingi,” huzisema methali maarufu kuhusu ndoa. Kwa sababu harusi na ndoa ni mambo ya dunia, sisi “watu wa kiroho” 1360 au watumishi wa Kanisa, kwa vyovyote, hatuwezi kuamrisha chochote kuhusu ndoa, bali tunalolifanya ni kuruhusu kila mji na nchi kuyazingatia mapokeo yake. Baadhi ya watu humleta Bibi Harusi kanisani mara mbili, jioni na asubuhi, ilihali wengine humpeleka kanisani mara moja tu. Wengine hutangaza hadharani na kuyasoma matangazo ya ndoa mimbarani majuma mawili au matatu kabla ya harusi yenyewe kufanyika. Haya yote ninayaachia watawala na mabaraza ya miji husika ziweze kuweka na kupanga watakavyo. Mambo haya hayanihusu mimi hata kidogo.
2. Hata hivyo, watu wanapotuomba tuwabariki mbele au hata ndani ya Kanisa kwa kuwaombea au hata kufungisha ndoa zao, hatuna budi kufanya hivyo. Kwa hiyo, ninataka kutoa mashauri haya na utaratibu huu kwa wale ambao hawajui jinsi ya kuyaendeleza haya yote na huenda wakauzingatia utaratibu huu ufuatao pamoja nasi. Wengine, ambao wana ujuzi zaidi - yaani, wale ambao hawawezi kufanya lolote na ambao wanadhania kwamba, wanayajua yote - hawauhitaji utaratibu wangu huu ninaoutoa hapa. Ninautoa tu kwa ajili ya kuuboresha na kuutengeneza kwa ujuzi mwingi zaidi. Hakika, wanapaswa kuwa na tahadhari kubwa ili wasizifuate kaida za watu wengine. Mtu anaweza hata kudhania kwamba, amejifunza jambo bora kutoka kwa mtu mwingine! Je, hiyo haitakuwa aibu kubwa?
3. Mpaka sasa, watawa wa kiume na wa kike wameendelea kuwekwa wakfu katika hali zao kwa ufahari mkubwa ingawa hali zao ni za kukufuru sana na za ubunifu wa kibinadamu usiokuwa na msingi wowote katika Biblia. Basi, ni kwa jinsi gani inatupasa zaidi tuiheshimu hali takatifu ya ndoa! Inastahiki kupambwa kwa njia nzuri zaidi kwa maombi na baraka. Ingawa ndoa ni suala la kidunia,
1359 Makala haya pia yalichapishwa kuwa kijitabu kidogo mwaka wa 1529 na pia yalikuwepo katika matoleo mengi ya kijitabu cha ‘Katekisimo Ndogo’ kilichochapishwa nyakati za Martin Luther kuanzia mwaka wa 1529. Vile vile katika angalau toleo moja la ‘Kitabu cha Mwafaka’ cha mwaka wa 1580. 1360 Kijerumani: ‘Geistliche.’
hata hivyo inaelezwa wazi katika Neno la Mungu na si ubunifu wa kibinadamu kama jinsi hali ya maisha ya watawa wa kiume na wa kike ilivyo. Kwa hiyo, inapaswa kutambuliwa kuwa hali ya kiroho mara mia zaidi kuliko hali ya utawa ambao, hakika, lazima uonekane kuwa hali ya kidunia na ya kimwili kuliko vyote kwa sababu ulibuniwa na kuanzishwa na mwili na damu kutokana na akili na maelewano ya kidunia peke yake kabisa.
4. Ndoa inahitaji kubarikiwa pia kwa ajili ya vijana ili wapate kuichukulia kwa umakini, waipe hadhi ya juu kama tendo na amri kuu kutoka kwa Mungu, wasije wakaipuuza kiasi cha kuicheka au kuikejeli kwa namna fulani. Hili ni jambo linaloshuhudiwa siku hizi. Watu huichukulia ndoa na huifanya arusi kuwa tendo la kimchezo tu. Kwa kweli, wale ambao walianzisha desturi ya kuwaleta Bibi na Bwana Harusi kanisani, hawakulichukulia jambo hilo kimchezo bali waliliona kuwa jambo lenye umuhimu mkubwa. Bila shaka, walitaka kuzipokea baraka za Mungu pamoja na maombi ya usharika.1361 Hawakuwa na shabaha ya kuwachezea watu kwa vitimbi vya kima vya Kipagani.1362
5. Jambo hili ni la wazi kabisa. Kwa kuwa, mtu akimwomba baraka mchungaji au askofu,1363 ataonyesha katika ombi lake, ingawa hatasema kwa uwazi kwamba, atajitolea katika hatari na anahitaji baraka za Mungu na sala za usharika kwa ajili ya hali hii ya maisha ambayo anaitazamia. Uzoefu wa kila siku unaonyesha ni taabu gani ambazo Ibilisi anaweza kusababisha katika ndoa: uasherati, uzinzi, ugomvi, na dhiki za kila aina.
Kwa hiyo, Bwana Harusi na Bibi Harusi wanapotamani na kuomba wahudumiwe, tunataka kuwashughulikia kwa njia ifuatayo:
6. Kwanza, ndoa itangazwe mimbarani kwa maneno yafuatayo: “Yusufu na Mariamu1341364 wanataka kuungana pamoja katika ndoa takatifu jinsi Mungu alivyoagiza. Wanataka wapate maombi ya Kikristo ya usharika wote ili ndoa yao ipate kuanza kwa jina la Mungu na iweze kufanikiwa. Sasa iwapo mtu yeyote ana sababu yoyote ya kuipinga ndoa hii, hebu aiseme sasa. La sivyo, basi na akae kimya daima. Mungu awape baraka zake. Amina.”
7. Kufungisha ndoa kufanyike mbele ya Kanisa1365 kwa maneno yafuatayo:
1361 Luther alimaanisha maombi ya usharika yanayofanywa na Wakristo wote katika ibada.
1362 Kijerumani: ‘heidnisch Affenspiel.’
1363 Kulingana na Luther, mchungaji mkuu wa usharika ana cheo cha askofu.
1364 Istilahi ‘Hans und Greta,’ majina ya kawaida kwa ajili ya waliooana, lakini pia ni majina ya wazazi wa Luther.
1365 Kulinagana na Luther, watu walipaswa kuoana punde tu baada ya uposaji. Kwa sababu viapo vya ndoa vilikuwa mambo ya kisheria, sehemu hii ilifanyiwa mlangoni mwa Kanisa.
“Wewe Yusufu, je, unakubali na kutaka kumwoa huyu Mariamu awe mke wako?”
Aseme: “Ndiyo.”
“Mariamu, unakubali na kutaka kuolewa na huyu Yusufu awe mume wako?”
Aseme: “Ndiyo.”
8. Hapa wanapaswa kupewa nafasi ya kupeana pete. Mchungaji anaiunganisha mikono yao ya kulia pamoja, na kusema: “Basi, aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.” 1366
Kisha mchungaji awaambie wote waliohudhuria:
9. “Kwa kuwa Yusufu na Mariamu wanataka kuungana pamoja katika ndoa na wameungama jambo hili mbele za Mungu na hapa mbele ya watu na kama alama ya maneno waliyoahidiana, wamepeana mikono na pete za harusi, ninatangaza hadharani kuwa wameungana katika ndoa, katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.”
10. Hapo mbele ya madhabahu1371367 mchungaji na awasomee Bwana na Bibi Arusi Neno la Mungu kutoka Kitabu cha Mwanzo 2: 18, 21–24.
BWANA Mungu akasema, si vyema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.1368 BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
11. Kisha mchungaji na awageukie wote wawili na kuwaambia ifuatavyo: “Kwa kuwa nyote wawili sasa mmeungana pamoja katika ndoa katika jina la Mungu, hebu sikilizeni kwanza amri ya Mungu kuhusu ndoa. Mtume Paulo1369 anasema hivi:
12. “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda
1366 Mt. 19: 6
1367 Hili linadhihirisha mwanzo wa ibada.
1368 Katika toleo la 1536 la ‘Katekisimo Ndogo,’ nakala hii inalingana na toleo kamili la Biblia ya Luther ya mwaka wa 1534. Nakala za zamani zinasema: “atakayekuwa mwenzi wake.”
1369 Efe. 5: 25-29, Efe. 5: 22-24
Kanisa,1370 akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika Neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na doa wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.”1371
13. “Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.”
14. “Pili, sikilizeni pia juu ya msalaba ambao Mungu anawapa wote wanaoungana katika ndoa. Mungu akamwambia mke hivi: ‘Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”
“Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”1372
15. “Tatu, hii ni faraja kwenu, kuwa mjue na kuamini jinsi ndoa yenu inavyoridhisha na ilivyo yenye baraka machoni pa Mungu. Maana imeandikwa:1373 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, wanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.”
Kwa hiyo, Sulemani pia anasema:1374
“Apataye mke apata kitu chema; naye ajipatia kibali kwa BWANA.”
16. Sasa mchungaji na aiinue mikono yake juu yao na aombe:1451375 “Ee 1370 Kijerumani: ‘Gemeine,’ yaani, “usharika.”
1371 Kabla ya mwaka wa 1536: “Alidhihirishe Kanisa lenye utukufu kwa ajili yake mwenyewe.”
1372 Mwa. 3: 16-19
1373 Mwa. 1: 27-28, 31
1374 Mit. 18: 22
1375 Ombi lifuatalo limetokana na ombi la utamaduni lililofanywa katika ibada za ndoa wakati wa Luther.
Bwana Mungu, uliyewaumba mume na mke na uliyeamuru waungane pamoja katika ndoa, na uliyewabariki pia na kuwapatia tunda la tumbo, na kwa njia hiyo umeonyesha umuhimu wa siri ya Mpendwa Mwanao Yesu Kristo na Kanisa,1376 lililo Bibi Harusi wake: Tunakuomba wema wako usiokuwa na mwisho uwepo kwamba, hutaruhusu uumbaji wako, agizo na baraka kuondolewa au kuharibiwa, bali, kwa neema, iendelee kuwepo miongoni mwetu kwa njia ya Yesu Kristo BWANA wetu. Amina.”
1376 Efe. 5: 32
KIJITABU CHA UBATIZO KILICHOTAFSIRIWA KATIKA KIJERUMANI NA KUDURUSIWA1377
Martin Luther
Kwa wasomaji Wakristo wote: Neema na amani katika Kristo Bwana wetu!
1. Kila siku ninaona na kusikia jinsi sakramenti kuu, takatifu, na yenye faraja sana, yaani, Ubatizo, unavyotekelezwa kwa watoto wadogo kwa uzembe na pasipo ustahifu, nisije nikasema kwa njia ya kutojali. Nadhani sababu yake ni kwamba, wale wanaohudhuria hawaelewi lolote linalosemwa au linalotendwa. Kwa hiyo, ninaona kwamba, ni jambo lenye manufaa sana na la maana kuwabatiza watu katika lugha ya mama. Hivyo, niliutafsiri utaratibu wa Ubatizo katika Kijerumani. Nimeanza pia kuwabatiza watu kwa Kijerumani ili wadhamini na wote wanaohudhuria wapate kuamka katika imani yakini na ya uchaji zaidi. Isitoshe, wachungaji wanapaswa kuwa waangalifu zaidi kwa ajili ya wasikilizaji wao.
2. Kwa jina la uaminifu katika Kristo, ninawasihi wote wanaobatiza, wadhamini na wanaohudhuria Ubatizo: jaribuni kuuelewa umuhimu na uzito wa tendo hili! Sababu ni kwamba, katika maneno ya maombi, mtasikia wazi jinsi Kanisa linavyomleta mtoto mchanga mbele za Mungu kwa dhati na hata kuungama mbele zake bila shaka wala tashwishi zozote, kwamba mtoto amefungwa na Ibilisi na yu chini ya dhambi. Hivyo basi, wanamsihi Mungu apate kumsaidia na kwa njia ya Ubatizo huo, wanamwomba Mungu amwokoe na amfanye mtoto wake.
3. Kwa hiyo, unapaswa kuona kwamba, si jambo la mzaha kumshambulia Ibilisi. Sisi hatumfukuzi tu Ibilisi kutoka kwa mtoto, bali tunamchochea adui huyu mkuu kumsumbua huyu aliyebatizwa katika maisha yake yote. Kwa sababu hiyo, ni muhimu sana kumsaidia mtoto huyo maskini, kwa moyo wote, kwa imani kuu, na kumsihi Mungu kwa bidii tuwezavyo, kulingana na maombi haya, ili Mungu asimweke tu mtoto huru kutoka katika uweza wa Ibilisi bali pia ampatie nguvu ili mtoto aweze kumpinga Ibilisi kwa ushujaa na kwa nguvu zote katika maisha yake yote na hata katika kifo. Kwa kuwa, watu waliobatizwa
1377 Kijitabu hiki cha Ubatizo kinachohusu taratibu za Enzi ya Kati za Ubatizo kilichapishwa mara ya kwanza mwaka wa 1523 (WA 12, 42-48; LW 53, 95-103). Mnamo mwaka wa 1526, toleo la pili lilichapishwa (WA 19, 537-541; LW 53:106-109 na 101-103), ambalo ndilo msingi wa fungu hili. Kiliingizwa katika toleo la pili la Katekisimo Ndogo mwaka wa 1529, katika matoleo yote yaliyofuatia katika Wittenberg nyakati za Luther, na katika baadhi ya matoleo ya mwaka wa 1580 ya “Kitabu cha Mwafaka.”
wataweza kupotoka mara nyingi na kuwa wabaya sana, ninaona kwamba, Ubatizo ulitekelezwa kwa njia ya kutojali sana na ya baridi na kwamba, watu walimwombea huyu aliyebatizwa bila maana ya kweli.
5. Kumbuka pia kwamba, mambo ya nje hayana maana sana katika Ubatizo, kama kupulizwa macho, kuweka alama za msalaba, kuweka chumvi mdomoni au kuweka mate au udongo masikioni na puani, kutiwa mafuta kifuani na mabegani, kupakwa mafuta matakatifu kichwani, kuvalia mavazi meupe, kuweka mshumaa uwakao mkononi mwa mtoto, au lolote ambalo limewekwa na watu liwe ishara ya Ubatizo. Ukweli ni kwamba, Ubatizo unaweza kuwepo hata bila ya haya yote, maana hayo siyo mambo yanayomfanya Ibilisi atetemeke na akimbie. Yeye anayathubutu makuu hata kuliko haya! Hapa, lazima mambo yatendeke kwa dhati.
6. Badala yake, hakikisha kwamba, unasimama imara katika Ubatizo wenye imani ya kweli, unalisikiliza Neno la Mungu, na kwamba, kipindi chote, unaomba kwa dhati. Maana, kila mchungaji anaposema, “Tuombe,” yeye anakutaka uombe pamoja naye. Isitoshe, wadhamini wote na wote wanaoshuhudia wanapaswa kusema sala hizi kwa Mungu mioyoni mwao pamoja na mchungaji.
7. Kwa hiyo, mchungaji anapaswa kuzisema sala hizi waziwazi na polepole, ili wadhamini wapate kuzisikia na kuzielewa. Inawabidi wadhamini kukubaliana na mchungaji kusali pamoja mioyoni mwao, kumwelezea Mungu kuhusu taabu za mtoto, na kumpiga vita Ibilisi kwa nguvu zao zote kwa niaba ya mtoto. Wafanye hivyo kwa dhati yote kwa sababu vita hivi vya Ibilisi si mchezo.
8. Kutokana na hili, ni vizuri na inafaa kuwakataza wachungaji walevi na wasiomcha Mungu wabatize na wala tusiwachague wadhamini wasiokuwa makini. Badala yake, tunapaswa kuwa na wachungaji wema, wenye maadili, waliomakinika, na walioongoka. Nao wadhamini wanaochaguliwa wanapaswa wawe wamemakinika, na wenye imani ya kweli ili hii sakramenti iliyo muhimu sana isichukuliwe kama kejeli ya Ibilisi na kumvunjia Mungu heshima. Katika sakramenti hii ya Ubatizo, tunamiminiwa kwa wingi neema kuu ya Mungu na isiyokuwa na mwisho. Yeye mwenyewe anaiita sakrementi hii “kuzaliwa upya.1378” Kwa njia yake, tunakombolewa kutoka katika nguvu za Ibilisi na kutoka katika nguvu za dhambi, kifo, na Jehanumu. Tunakuwa watoto wa uzima wanaorithi vyote kutoka kwa Mungu. Tunakuwa watoto wa Mungu mwenyewe na ndugu na dada katika Kristo.1379
1378 Yn. 3: 3,5 1379 Neno kwa neno, “ndugu.”
9. Enyi, Wakristo wapendwa, tusiichukulie hii heshima kuu hivi hivi tu! Maana, Ubatizo ndiyo njia yetu ya pekee ya kuipata faraja na ndicho kiingilio cha pekee cha kuupata urithi wetu kutoka kwa Mungu na kuupata ushirika wa watakatifu wote. Mpaka hapa Mungu atusaidie. Amina.
11. Anayebatiza atasema:
“Ondoka, ewe roho mchafu na mwache Roho Mtakatifu aingie.”
12. Kisha ataweka alama ya msalaba usoni na kifuani na kusema: “Pokea ishara ya msalaba mtakatifu usoni na kifuani.”
“Tuombe: Ee Mungu Mwenyezi uishiye milele, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ninakuomba kwa niaba ya huyu mtumishi wako, N. ambaye anaomba abatizwe na anayetaka kupata neema yako ya milele kwa kuzaliwa upya kiroho. Mpokee BWANA, na kama ulivyosema, ‘Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.’1380 Hivyo, mpe sasa baraka yeye ambaye anakuomba na abishaye, ili aweze kupata baraka ya milele ya kuoshwa kwa maji ya mbinguni,1381 na kupokea ufalme ulioahidiwa uutoao kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.”
14. “Tuombe: “Mwenyezi Mungu wa milele ambaye, kulingana na hukumu yako ya dhati, uliwalaani wote wasioamini duniani kwa kuleta gharika na, kwa ajili ya huruma zako kuu, ukamwokoa Nuhu na watu saba wa familia yake. Wewe uliyemzamisha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu na kuwaongoza watu wako wa Israeli katika nchi kavu katika bahari hiyo na uliyetupa mfano wa Ubatizo wako mtakatifu. Kwa njia ya Ubatizo wa mpendwa Mwanao, BWANA wetu Yesu Kristo, uliutakasa na kuutenga mto Yordani na maji yote kuwa baraka kuu ya kuziosha dhambi: tunaomba kwa ajili ya hii huruma yako kuu kwamba, utamlinda N. na kumbariki kwa imani ya kweli katika Roho Mtakatifu ili, kwa njia ya mafuriko haya ya namna ile ile ya wokovu, yote yale yaliyozaliwa ndani yake kutoka Adamu au dhambi zozote alizozipata zioshwe na kuzamishwa, na kwamba, akiwa ametengwa kutoka kwa wale wasioamini, aweze kutunzwa na kuwa salama katika safina takatifu. Yaani, Kanisa la Kikristo – ili wakati wote apate kuwa na moyo safi na furaha ya kulitumikia jina lako; kwamba, pamoja na waumini wote katika ahadi yako, aweze kuurithi uzima wa milele kwa njia ya Yesu Kristo BWANA wetu. Amina.”
15. “Ninakuagiza, ee roho mchafu, katika jina la Baba (+) na la Mwana (+)
1380 Mt. 7: 7
1381 Tit. 3: 5
na la Roho Mtakatifu (+) utoke na uondoke kutoka kwa mtumishi huyu wa Yesu Kristo.1382 Amina.”
“Hebu tuisikie Injili takatifu ya Mt. Marko:1383
16. “Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni, ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa. Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabarikia.”
17. Kisha, mchungaji ataiweka mikono yake juu ya kichwa cha mtoto na ataomba Sala ya Bwana pamoja na wadhamini wakiwa wamepiga magoti:
“Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litakaswe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni, utupe leo riziki yetu, utusamehe makosa yetu, kama sisi nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Amina.”
18. Baada ya haya, mtoto huyo mchanga ataletwa katika chombo cha Ubatizo.1384 Kisha mchungaji atasema:
“BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, tangu sasa na hata milele.” 1385
19. Mchungaji atamwapisha mtoto, kwa njia ya wadhamini wake, na kusema:
20. “N., Je, unamkataa Shetani?”
Jibu: “Ndiyo.”
21. “Na kazi zake zote?”
Jibu: “Ndiyo.”
22. “Na njia zake zote?”
Jibu: “Ndiyo.”
Kisha, mchungaji atauliza:
23. “Je, unamwamini Mungu Baba mwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi?”
1382 Ishara ya msalaba ilifanywa kwa mtoto mara tatu.
1383 Mk. 10: 13-16
1384 Kulingana na imani za kale, upungaji wa pepo wachafu, Kilatini: ‘abrenuntiatio,’ ulifanyiwa mlangoni mwa Kanisa na mengine yaliyofuatia hayo yalikuwa katika sinia la Ubatizo. 1385 Zab. 121: 8
390
Jibu: “Ndiyo.”
24.“Je, unamwamini Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, Bwana wetu, aliyezaliwa, akateswa na akafa?”
Jibu: “Ndiyo.”
25.“Je, unamwamini Roho Mtakatifu, Kanisa moja takatifu la Kikristo, umoja wa watakatifu, msamaha wa dhambi, kufufuka kwa mwili, na baada ya kifo uzima wa milele?”
Jibu: “Ndiyo.”
26.“Unataka kubatizwa?”
Jibu: “Ndiyo.”
27.Sasa mchungaji anamchukua mtoto na kumweka kwenye chombo cha Ubatizo na kusema:
28.“Ninakubatiza katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.”
29.Kisha wadhamini watamshikilia mtoto huyu mchanga juu ya chombo cha Ubatizo, pamoja na mchungaji, (na akimvalisha mtoto vazi la ubatizo) na kusema:
30.“Mwenyezi Mungu na Baba wa BWANA wetu Yesu Kristo, aliyekufanya uzaliwe tena kwa mara ya pili kwa njia ya maji na Roho Mtakatifu na aliyekusamehe dhambi zako zote, tunaomba akupatie nguvu kwa neema yake upate uzima wa milele. Amina.”
31.“Amani iwe pamoja nawe.”
Jibu: “Amina.” 1386
1386 Matoleo mbalimbali ya Katekisimo Ndogo pia huongezea maandiko mengine. Matoleo yaliyochapishwa katika Wittenberg wakati wa maisha ya Luther mnamo mwaka wa 1529 yalikuwa pamoja na: ‘Litania ya Kijerumani’ (WA 30/3, 29-36; LW 53:163-69); mwaka wa 1536, 1537 na mwaka wa 1539: ‘Te Deum na Magnificat,’ zote hizo katika Kijerumani (WA 35, 458-59); mwaka wa 1543: Sala dhidi ya Waturuki (WA 51, 608, 6/24-610, 15/34).
391
KATEKISIMO KUBWA
DK. MARTIN LUTHER
1529
UTANGULIZI WA MARTIN LUTHER1387
1. Sababu yetu ya kuishughulikia Katekisimo katika mahubiri na hata kuwahimiza na kuwaapiza wengine kufanya hivyo siyo duni. Pia, kwa masikitiko tunaona kwamba, wachungaji na wahubiri1388 wengi ni wazembe sana katika jambo hili. Hawaziheshimu huduma zao na mafundisho haya. Wengine wanafanya hivyo kwa ajili ya utaalamu mkubwa, cheo cha juu jinsi wanavyodhania, uvivu na ulafi peke yake, na kuvishughulikia vitambi vyao. Wanautilia mkazo uhusiano wa jambo hili kana kwamba, walikuwa wachungaji na wahubiri kwa ajili ya matumbo yao na hawakuwa na lingine lolote la kufanya isipokuwa kuyagharamia na kuyatumia mapato yao siku zote za maisha yao jinsi walivyozoea kufanya chini ya Upapa.
2. Kila kitu wanachopaswa kukihubiri na kukifundisha sasa kinawekwa mbele yao kwa wingi, wazi, na kwa urahisi katika vitabu vingi vizuri na maarufu mno na vyenye msaada, kwa mfano, “Mahubiri Yanayojihubiri Yenyewe,” “Ulale Salama,” “Tayari,” “Hazina,”1389 kama vilivyoitwa zamani. Hata hivyo, hawawi
1387 Tafsiri ya Katekisimo Kubwa inalifuata aghalabu andiko la Kijerumani lililoandikwa na Martin Luther mwaka wa 1529 na lililoongezewa/lililopanuliwa mwaka wa 1530 kwa jina la ‘Katekisimo ya Kijerumani.’ Tafsiri ya Kilatini ilitolewa mwaka wa 1529. Toleo la pili la Kilatini la mwaka wa 1544 lilitafsiriwa na mtaalamu Vincent Obsopeus. Inaufuata mtindo mzuri mno wa Kilatini.
1388 “Wachungaji,” Kilatini: ‘parochius,’ Kijerumani:‘Pfarrherr’ walikuwa na mamlaka yote ya usharika. “Wahubiri,” Kilatini: ‘Concionator,’ Kijerumani:‘Prediger’ walihubiri katika makanisa bila mamlaka kuhusu usharika.
1389 Mikusanyiko ya mahubiri iliyokuwa tayari, Kijerumani:‘Postille’ kwa wahubiri. Majina haya ya mzaha yaliwadhihaki wahubiri wazembe waliopenda kuyasoma mahubiri yaliyoandaliwa tayari katika vitabu badala
wema na waaminifu kwa kuvinunua vitabu hivi, au kwa kuwa navyo. Isitoshe, hata hawavichunguzi wala hawavisomi. Hivyo, ni wazi kwamba, wao ni walafi wasiokuwa na aibu na watumishi wa matumbo yao waliostahili zaidi kuwa wachunga nguruwe na watunza mbwa kuliko kuwa watunza nafsi za watu au kuitwa wachungaji.
3. Kwa kuwa wamewekwa huru sasa kutokana na mzigo usionufaisha wa kelele za saa saba za sala za kanuni,1390 badala yake, ingekuwa bora kama wangesoma angalau ukurasa mmoja au kurasa mbili kutoka katika Katekisimo, Kitabu cha Sala, Agano Jipya au kwingineko katika Biblia, na wangeisema Sala ya Bwana kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya washarika wao asubuhi, adhuhuri, na jioni. Kwa njia hii, wangeweza kuonyesha heshima na shukrani kwa Injili, ambayo kwayo, wamewekwa huru kutokana na mizigo na usumbufu mwingi. Wangeona aibu kidogo kwa sababu, kama nguruwe na mbwa, hawaikumbuki tena Injili kuliko ukware mzembe wa aibu wenye makuruhu ya kimwili!1391 4. Inavyoonekana, umma unaichukulia Injili kijuujuu zaidi, na hakuna la maana tunalolifanya hata kama tungezitumia bidii zetu zote. Basi, ni lipi litakalofaulu iwapo tutalegea na kuwa wavivu jinsi tulivyokuwa chini ya Upapa?
5. Licha ya hili, kumeongezeka uovu wa aibu na ambukizo la kisirisiri la kujihisi salama na kuridhika. Yaani, wengi wanaichukulia Katekisimo kuwa fundisho duni na hafifu wanaloweza kulipitia, kulisoma haraka, na kulijua mara moja. Baada ya kuisoma mara moja, huitupa pembeni kana kwamba, wangeona aibu kuisoma tena. 6. Naam, hata miongoni mwa malodi wenye vyeo,1392 kuna watu washenzi na bahili wanaothubutu kudai kwamba, hakuna tena haja ya wachungaji ama ya wahubiri tangu sasa na kuendelea kwani kuna kila kitu katika vitabu, na kila mmoja anaweza kujifunza mwenyewe kwa urahisi. Kwa hiyo, wako radhi kuziacha sharika zioze na kudidimia katika uharibifu, na wachungaji na wahubiri waumie sana kwa dhiki na njaa, jinsi Wajerumani wenye wazimu wafanyavyo. Kwa maana, sisi Wajerumani tuna watu wa namna hiyo wanaoleta aibu ambao imetupasa kuwavumilia.
7. Lakini mimi mwenyewe ninasema: mimi pia ni daktari, mhubiri, msomi na mwenye uzoefu, angalau sawasawa na wanavyoweza kuwa hao wote ambao wana majivuno na ujasiri wa namna hiyo. Hata hivyo, ninajifanya kama mtoto anayefundishwa Katekisimo. Kila asubuhi na kila mara ninapopata nafasi, ya kuyaandaa yao wenyewe kwa bidii.
1390 Taz. Ukiri wa Augsburg 28, 41 rejeo la 61.
1391 Naam, ukware ni istilahi itumiwayo katika ‘Uhuru wa Kikristo.’
1392 Kilatini: ‘nobil,’ Kijerumani: ‘Adligen,’ Kiingereza: ‘nobility,’ watu wenye mamlaka ya mikoa ya kurithiwa.
ninaisoma na kuikariri neno kwa neno, Sala ya Bwana, Amri Kumi za Mungu, Ukiri wa Imani, Zaburi, n.k. 8. Inanipasa kuisoma na kujifunza kila siku, na bado sijaijua kwa kiwango nikitakacho, isipokuwa kubakia kuwa kama mtoto na mwanafunzi wa Katekisimo, na ninafanya hivyo kwa furaha. Kumbe, hawa jamaa wateuzi na wanaokirihi sana, hudhania kuwa madaktari walio juu ya madaktari wote, kwa kuisoma mara moja tu kwa haraka na wanajua kila kitu na hawahitaji lolote. Vyema, hakika, hii pia ni ishara kwamba, wanaidharau, siyo tu huduma yao, bali pia nafsi za watu, naam, hata Mungu na Neno lake. Hawahitaji kuanguka kwani wamekwisha kuanguka vibaya sana tayari. Wanahitaji kufanyika watoto na kuanza kujifunza upya alfabeti zao japo wanafikiria kwamba, wamekua na waliziacha zamani.
9. Hivyo, ninawasihi wenye vitambi hawa wavivu,1393 watakatifu, na wanaojivuna wakubali kusadikishwa na kuamini kwa ajili ya Mungu kwamba, hakika kabisa, wao siyo wasomi au madaktari wakubwa jinsi wanavyofikiria. Wasithubutu kamwe kudhania kwamba, wamemaliza kujifunza sehemu hizo zote1394 au kuzijua vyema vya kutosha, ingawa wanajisifu kuwa wanaijua vizuri sana. Hata kama wangeijua na kuielewa kikamilifu kabisa–kwa vyovyote, jambo ambalo haliwezekani katika maisha haya–kuna manufaa na matunda ya aina nyingi ambayo bado yatapokewa, iwapo itasomwa kila siku na kufanyiwa mazoezi katika mawazo na maneno. Yaani, Roho Mtakatifu atakuwa katika usomaji wa namna hii wa kurudia na kutafakari. Yeye huigawa nuru na uchaji ambao ni mpya daima, wa ziada, wa kuthaminiwa, na wa kufurahiwa zaidi, jinsi Kristo anavyoahidi katika Mt. 18:20: “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”
10. Zaidi ya hayo, ni msaada wenye matokeo makubwa sana dhidi ya Ibilisi, dunia, mwili, na mawazo maovu yote kujishughulisha mwenyewe na Neno la Mungu, kulisoma na kulitafakari. Zaburi ya Kwanza huwaita wenye heri hao“ambao sheria yake huitafakari mchana na usiku.” Bila shaka, huwezi kuufukiza ubani zaidi au harufu nyingineyo kali dhidi ya Ibilisi kuliko kuyashughulikia maagizo ya Mungu na maneno yake kwa kuyasema, kuyaimba na kuyatafakari. Kwa maana, haya ndiyo maji halisi, ya kweli, matakatifu, na alama takatifu ambayo Ibilisi huikimbia, na ambayo kwayo, anaweza kufukuzwa.
11. Sasa basi, kwa sababu hii peke yake, inakupasa kuyasoma, kuyasema, kuyawaza na kuyatafakari kwa furaha mafungu haya, hata kama hungekuwa na faida nyingine yoyote na matunda kuweza kumfukuza Ibilisi na mawazo mabaya.
1393 Yaani, walafi na wazembe, Kijerumani: ‘faule Wänste,’ Kilatini: ‘ignavos ventres.’ 1394 Naam, sehemu zote za Katekisimo.
Naam, hawezi kulisikia na kulivumilia Neno la Mungu. Si hadithi ya upuuzi kama ile ya Dietrich wa Bern1395 lakini jinsi Mt. Paulo asemavyo katika Rum. 1:16: “Ni uweza wa Mungu.” Hakika, ni uweza wa Mungu ambao humchoma Ibilisi na kutupatia nguvu nyingi sana, faraja, na msaada.
12. Niseme nini zaidi? Nikitaka kuzisimulia faida zote na matunda yote yaliyotokana na Neno la Mungu nitapata wapi karatasi na muda wa kutosha? Ibilisi anaitwa bwana wa aina elfu za hila. Lakini tutaliita nini Neno la Mungu, linalomfukuza huyu bwana wa dunia mwenye elfu za hila na kumbatilisha yeye pamoja na hila na nguvu zake zote? Basi, inalibidi kuwa hodari mara elfu mia moja hata zaidi ya hapo. 13. Je, kwa upuuzi, tudharau aina hii ya nguvu, faida, uweza, na matunda hasa sisi tunaodai kuitwa wachungaji na wahubiri? Kama ni hivyo, hatutastahili kupewa chakula chochote. Badala yake, tutafukuzwa nje na mbwa na kutupiwa samadi.1396 Kwa kweli, sisi hatuyahitaji haya yote kila siku kadiri tunavyohitaji chakula chetu cha kila siku. Lakini ni lazima pia tuyatumie haya kila siku dhidi ya mashambulio na hila za Ibilisi, mwenye hila mia elfu.
14. Kama hili halitoshi kutushawishi kuisoma Katekisimo kila siku, inastahili tujisikie kulazimishwa vya kutosha na amri ya Mungu yenyewe. Katika Kumbukumbu la Torati (Kum. 6:6-8) anaamuru kwamba, kila siku mioyoni mietu, inatupasa kuzitafakari sheria zake, tupoketi, tupotembea, tuposimama, tupolala chini, au tunapoamka. Isitoshe, inatupasa tuwe nazo machoni petu na mikononi mwetu kama alama na ishara ya wakati wote. Bila shaka, hakulidai na kulilazimisha hili pasipokuwa na lengo. Naam, anazijua hatari na shida zetu, mashambulio makali ya kila mara na kila wakati, na majaribu ya Ibilisi. Hivyo, anataka kutuonya, kutuandaa, na kutulinda dhidi yao kwa “kuizima mishale yote yenye moto,”1397 na kwa dawa zuri dhidi ya maambukizo na vishawishi vyake viovu. 15. Ole wetu, sisi ni wapumbavu na wakosa akili jinsi gani! Inatulazimu kuishi na kuwa miongoni mwa maadui wenye nguvu nyingi jinsi maibilisi walivyo. Lakini, bado tunazidharau silaha za ulinzi wetu, na tunakuwa wavivu mno kuzitazama au kuzifikiria!
16. Wafanye nini watakatifu hawa wenye karaha na wenye kiburi ambao hawataki au hawajitahidi kuisoma na kujifunza Katekisimo kila siku? Wanajifikiria
1395 Jina la mtu maarufu katika hadithi za kale za Wajerumani. Mtu wa asili wa hadithi hizo alikuwa mfalme wa Wagothi wa Mashariki, Teoderiko Mkuu 489/493-526 aliyetawala Roma na aliyeyang’ang’ania sana madhehebu ya Waariano. ‘Bern,’ jina la mji huko Uswisi, awali lilikuwa ‘Verona’ huko Italia na lilibadilika baadaye kuwa ‘Bern.’ Katika maandiko ya Martin Luther, Dietrich wa Bern ulikuwa mfano wa hadithi za uongo na michezo tu.
1396 “Samadi,” yaani, kinyesi cha wanyama wanaocheua. 1397 Efe. 6:16
kuwa wataalamu zaidi kuliko Mungu mwenyewe, malaika wake watakatifu, manabii, mitume, na Wakristo wote! Mungu mwenyewe haoni aibu kuifundisha kila siku, maana hajui lingine zuri zaidi au jambo tofauti la kufundisha. Licha ya hayo, anaendelea kulifundisha kila siku jambo lilo hilo, bila kulibadilisha na lingine jipya. Watakatifu wote hawalijui lolote zuri na la kufaa zaidi, pia hawajui kujifunza kwa ukamilifu. Je, sisi hatutakuwa mafundi wa ajabu sana, tukidhania kwamba, baada ya kuisoma au kuisikia mara moja, tunajua kila kitu na hatuhitaji kuisoma na kujifunza zaidi! Tunawezaje kumaliza kujifunza katika muda wa saa moja jambo ambalo Mungu mwenyewe halimalizi kulifundisha? Kusema kweli, amekuwa akilifundisha tangu mwanzo na ataendelea hadi mwisho wa dunia. Manabii wote na watakatifu wamekuwa na kazi nyingi ya kujifunza na daima wamebaki kuwa wanafunzi na wanalazimika kuendelea kuwa hivyo!
17. Ni hakika kwamba, mtu anayezijua Amri Kumi za Mungu kikamilifu, kwa lazima, anayajua Maandiko Matakatifu yote. Katika mambo yote na hali zote, anaweza kushauri, kusaidia, kufariji, kuhukumu, na kuamua kati ya mambo ya dunia na mambo ya kiroho. Anastahili kuhukumu kuhusu elimu yote ya imani, vyeo, roho, haki, na vingine vyote vilivyomo duniani.
18. Kwa hakika, Zaburi nzima ni nini isipokuwa mawazo na mazoezi kuhusu Amri ya Kwanza? Sasa ninajua kwa hakika kwamba, wenye vitambi wavivu au nafsi zenye karaha hazielewi zaburi hata moja, sembuse Maandiko Matakatifu yote. Hata hivyo, bado wanajifanya kuwa wanaijua na huidharau Katekisimo ambayo ni mkusanyiko na ufupisho wa Maandiko Matakatifu yote.
19. Kwa hiyo, ninawasihi tena Wakristo wote na hasa wachungaji na wahubiri wasiwe madaktari upesi mno na kudhania kwamba, wanakijua kila kitu. Fikira batili, sawa na nguo mpya, hunywea sana.1398 Badala yake, wajizoeze vyema katika mafunzo haya kila siku na daima watende kulingana nayo. Licha ya hayo, waacheni wajichunge kwa uangalifu mwingi dhidi ya jasho la sumu na maambukizo ya ujasiri wa mafundi wa mazingaombwe. Wasome kwa uthabiti, wafundishe, wajifunze, wafikiri, na kutafakari. Wasiache mpaka wawe wamemwua Ibilisi kwa mafundisho yao na wajidai kuwa na elimu zaidi kuliko Mungu mwenyewe na watakatifu wake wote.
20. Wakionyesha juhudi za namna hiyo, basi, ninawaahidi–na ujuzi wao utanishuhudia–kwamba, watayapata matunda mengi na Mungu atawafanya kuwa watu bora sana. Baada ya muda, wao wenyewe watakiri kwamba, jinsi wanavyojifunza Katekisimo kwa kina, ndivyo wanavyozidi kukiri jinsi 1398 Methali ya zamani ya Kijerumani. “Nywea”–hali ya kitu kuwa kifupi kuliko kilivyokuwa.
wasivyoielewa, na kuzidi kuyaona mengi ya kuendelea kujifunza. Hapa tu, hakika, wenye njaa na kiu watalifurahia lile ambalo kwa sasa hawawezi kulivumilia kwa ajili ya kula mno na kuvimbiwa. Kwa lengo hili, Mungu na aijaze neema yake! Amina.
UTANGULIZI MFUPI1399
1. Hubiri hili liliandaliwa awali kwa mafundisho ya watoto na ya wasiokuwa na elimu. Hivyo, tangu zamani, katika Kiyunani yaliitwa, “Katekisimo,” yaani, “mafundisho ya watoto.” 2. Yaliyomo yake ni elimu ambayo lazima kila Mkristo aijue. Yeyote asiyekuwa na elimu hiyo asihesabiwe kati ya Wakristo wala asiruhusiwe kushiriki sakramenti yoyote. Fundi asiyezijua kanuni na matumizi ya sanaa yake anakataliwa na kuonekana kuwa asiyefaa. 3. Kwa hiyo, vijana lazima wafundishwe kujifunza vyema sehemu za Katekisimo au mahubiri kwa watoto. Wajizoeze, kwa juhudi, kutenda kulingana na mafundisho haya.
4. Kwa hiyo, ni wajibu wa kila mmoja aliye baba wa kaya kuwauliza maswali na kuwajaribu watoto wake na watumishi, angalau, mara moja kwa juma na kuhakikisha kuwa wameyajua yale waliyojifunza. Iwapo hawayajui, awahimize wafanye bidii kwa uaminifu kufanya hivyo. 5. Ninakumbuka vizuri walipokuwepo wazee mafidhuli ambao hawakulijua lolote kuhusu mambo haya. Kweli, hata sasa, tunawaona kila siku. Hata hivyo, wanakwenda kwa Ubatizo na kwa Chakula cha Bwana na kukitumia kila kitu ambacho ni cha Wakristo, japo wale wanaoshiriki Chakula cha Bwana inawapasa kujua na kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa mafundisho yote ya Kikristo kuliko watoto na wale wanaoanza shule. Kwa ajili ya watu wa kawaida, tunaridhishwa na sehemu tatu zilizodumu katika Ukristo tangu zamani, japo zimefundishwa kidogo sana na kutunzwa kikamilifu hadi watoto na wazee wote wanaotaka kuwa Wakristo, wapate kufundishwa vizuri na kuzijua.
1. AMRI KUMI ZA MUNGU
1. Usiwe na miungu mingine ila mimi.1400
2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.
3. Ikumbuke siku ya sabato uitakase.
4. Waheshimu baba yako na mama yako.
5. Usiue.
1399 Utangulizi huo mfupi unayafuata mahubiri ya Martin Luther kuhusu Katekisimo ya Mei18, mwaka wa 1528.
1400 Katika matoleo mengine maneno haya yametanguliwa: “Mimi ni Bwana Mungu wako.”
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usimshuhudie jirani yako uongo.
9. Usitamani nyumba ya jirani yako.
10. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake, wala mifugo yake wala cho chote alicho nacho.1401
II. MAFUNGU MAKUU YA IMANI YETU
11. Namwamini Mungu, Baba, Mwenyezi, Muumba mbingu na dunia.
12. Namwamini Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, Bwana wetu, aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Mariamu, akateswa wakati wa Pontio Pilato, alisulibiwa, akafa akazikwa, akashuka kuzimuni; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kulia wa Mungu, Baba Mwenyezi, kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na walio wafu.
Namwamini Roho Mtakatifu, Kanisa Takatifu la Kikristo lililo moja tu, ushirika wa watakatifu, ondoleo la dhambi, kufufuka kwa mwili na uzima wa milele. Amina.
III. SALA, AU “BABA YETU,” ILIYOFUNDISHWA NA KRISTO
14. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litakaswe,1402 ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu ya kila siku. Utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyosamehe waliotukosea, na usitutie majaribuni, lakini utuokoe kutoka uovu.1403 Amina.
15. Haya ndiyo mafungu ya lazima. 16. Mkristo yeyote anapaswa kujifunza na kuyarudia neno kwa neno. Watoto wetu wanapaswa kufundishwa uzoefu wa kuyanena kimoyomoyo kila siku wanapoamka asubuhi, wanapoketi chakulani, na wanapokwenda kulala usiku. Wasipewe chakula chochote wala wanachokinywa mpaka wameyarudia. 17. Vivyo hivyo, kila baba wa kaya anawajibika kufanya
1401 Ng’ombe au punda. 1402 ‘Union Version:’ ‘Litukuzwe.’ Lakini kitenzi ‘kutakasa’ ni tafsiri kamili ya kitenzi cha Kiyunani ‘αγιαεσθαι;’ Kijerumani: ‘geheiliget,’ Kilatini : ‘sanctificetur.’ 1403 Sehemu ya mwisho ya Sala ya Bwana haipatikani katika maandiko ya zamani ya Agano Jipya. Hii ndiyo sababu haikutumika pia katika utaratibu wa asili wa ibada. Baadaye sehemu hii ya sifa ilipokelewa katika Kanisa.
101Mt. 28:19; Mk. 16:16. Dondoo la Mathayo linafuatia toleo la ‘Textus Receptus,’ lililotumiwa na Luther na wataalamu wote wakati wa karne ya 16.
hivyo kwa watumishi wake wa kiume na wa kike. Asiwe nao katika nyumba yake kama hawayajui na hawataki kujifunza mambo haya. 18. Naye mtu yeyote ambaye ni fidhuli na mkaidi kiasi kwamba, hataki kujifunza mambo haya asivumiliwe. Kwa sababu, kila jambo tulilonalo katika Maandiko linaonekana humo kwa ufupi na katika lugha wazi na rahisi. 19. Kwa maana hiyo, akina baba wapendwa au mitume, hata wawe nani, kwa njia hii ya mafundisho ya maisha, wamejumlisha hekima na tabia ya Wakristo ambayo wanasema na kuzingatia na ambayo wanahusishwa nayo.
20. Baada ya mafungu haya matatu kueleweka, inatupasa pia kujua tuseme nini kuhusu sakramenti ambazo Kristo mwenyewe alizianzisha. Yaani, Ubatizo, na Mwili na Damu takatifu ya Kristo, kulingana na maneno ambayo ni kumbukumbu katika Mathayo na Marko101 mwishoni mwa Injili zao wanapoelezea jinsi Kristo alivyowaaga na kuwatuma.
UBATIZO
21. “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” 1404
22. Elimu hii ya mafundisho ya Biblia kuhusu Ubatizo inatosha sana kwa Mkristo asiyekuwa na elimu. Kadhalika, maneno machache na sahihi kuhusu sakramenti ya pili yanapasa kutumiwa. Naam, maneno ya Mt. Paulo.1405
SAKRAMENTI
23. “Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, ‘Huu ndio mwili wangu uliotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.’ Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, ‘Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.”
24. Hivyo, kwa jumla, tuna sehemu tano za elimu yote ya Kikristo, ambazo tunapaswa kuzitumia na kuwataka vijana kuzisema neno kwa neno kimoyomoyo. Kwa maana, haiwezekani kudhania kwamba, vijana watajifunza na kubakia na mambo haya kutokana na mahubiri tu. 25. Watu watakapokuwa wamejifunza sehemu hizi vyema, wanaweza pia kuweka mbele yao zaburi chache au nyimbo zilizotungwa kutokana na sehemu hizi kwa kuuongezea na kuuimarisha ujuzi
1404 Kulingana na Mt. 28:19 na Mk. 16:15 katika ‘Toleo la Vulgata.’ 1405 1 Kor. 11:23-35
wao. Hivyo, vijana wetu wataongozwa kuingia katika Maandiko Matakatifu ili wapate kuendelea kila siku.
26. Walakini haitoshi tu kujifunza neno kwa neno na kulirudia kimoyomoyo. Vijana lazima wayahudhurie mahubiri pia, hasa mahubiri yanayohusu Katekisimo1406 ili waweze kuyasikia maelezo yake na waweze kujifunza maana ya kila sehemu. Halafu, wataweza pia kuyarudia waliyoyasikia, na wakiulizwa, waweze kulitoa jibu sahihi ili mahubiri yasikose faida na matunda. 27. Kwa maana, sababu ya kuwa waangalifu kuhubiri kuhusu Katekisimo mara nyingi ni kuwafundisha vijana wetu, siyo kwa hali ya juu na elimu ya juu, ila kwa ufupi na kwa njia iliyorahisishwa sana ili iwaingie maanani mara moja na kubakia katika kumbukumbu zao. Kwa hiyo, sasa tutayachukua mafungu yaliyotajwa hapo juu moja baada ya jingine na tuyaseme mengi iwezekanavyo kuyahusu, kwa njia wazi.
FUNGU LA KWANZA: AMRI KUMI ZA MUNGU
AMRI YA KWANZA
“Usiwe na miungu mingine.”
1. Ndiyo kusema, inakubidi unitukuze mimi peke yangu kama Mungu wako. Maana ya maneno haya ni ipi na ielewekeje? Maana ya Mungu ni nini au Mungu ni nani?
2. Jibu: Maana ya Mungu ni chimbuko tunalotazamia mema yote na kimbilio katika dhiki. Kuwa na Mungu siyo lingine lolote isipokuwa kumtegemea na kumwamini kwa mioyo yetu yote. Kama nilivyokwisha kusema mara nyingi ni kwamba, tegemeo na imani ya moyo peke yake humfanya Mungu na sanamu ya kuabudiwa. 3. Ikiwa imani yako na tegemeo ni sahihi, basi, Mungu wako ni Mungu wa kweli. Kwa upande mwingine, iwapo tegemeo lako ni la uongo na ovu, basi, huna mungu wa kweli. Maana hivi viwili ni mamoja, yaani, imani na Mungu. Basi, ninasema, unalolitolea moyo wako na kuliamini, hakika, ndiye Mungu wako.
4. Hivyo basi, lengo la amri hii ni kuidai imani ya kweli na tegemeo la moyo lililotulia juu ya Mungu mmoja ambaye ni wa kweli na kushikamana naye peke
1406 Kanisa la Magharibi lilifuata ratiba ya wiki nne maalumu za kufunga ‘quatember,’ yaani, wiki ya tatu ya mwezi wa tisa, Jumapili ya tatu ya wiki iliyofuatia katika majira ya Majilio, Jumapili ya kwanza ya wiki iliyofuatia katika majira ya Kwaresima na Jumapili ya Pentekoste ya wiki iliyofuatia.
400
yake. Maana yake: Hakikisha unaniacha Mimi peke yangu kuwa Mungu wako, na usimtafute mwingine kamwe. Yaani: Lolote jema unalopungukiwa nalo, ulitazamie kutoka kwangu na ulitafute wakati wowote unapoumizwa na dhiki na taabu, ujikabidhi kwangu na ushikamane nami. Mimi ndiye nitakayekutosheleza na kukuondolea kila shida, mradi tu uhakikishe kwamba, hutauacha moyo wako umpende au utulie kwa mwingine.
5. Ili kuizingatia amri hii, itanibidi nilielezee hili kwa ukali kidogo zaidi, kwa mifano ya kushindwa kwa kawaida ili liweze kufahamika na kukumbukwa. Mtu, jinsi wengi wafanyavyo, hufikiri ana Mungu na kila kitu kwa wingi wakati ana pesa na mali. Hutegemea na hujivunia mali kwa uthabiti na uaminifu kiasi kwamba, hamhitaji yeyote. 6. Hapana shaka, mtu wa namna hiyo ana mungu, aitwaye Mamoni/Utajiri. Yaani, pesa na mali anamouweka moyo wake wote. Ni sanamu ya kawaida sana ya kuabudiwa duniani. 7. Mwenye pesa na mali anajiona kuwa salama, kuwa ana furaha, asiyekuwa na mahangaiko kana kwamba, ameketi katikati ya Paradiso. 8. Kwa upande mwingine, mchochole huwa na mashaka na hukata tamaa kana kwamba, hakulisikia lolote kuhusu Mungu. 9. Ni wachache sana wenye furaha, na ambao hawahuzuniki wala kulalamika wanapokuwa hawana Mamoni/Utajiri. Haya1407 hushikamana na kuing’ang’ania asili yetu hadi kaburini.
10. Pia, yeyote akiutegemea na akijivunia wingi wa maarifa, hekima, utawala, fadhili, urafiki na heshima na kuvitegemea, naye pia ana mungu asiyekuwa wa kweli. Hili hutokea tena unapong’amua jinsi watu walivyo wajuvi,1408 salama, na wenye kiburi kwa sababu ya kuwa na vitu kama hivyo na wanavyosononeka wakati havipo tena au vinapokuwa vimeondolewa kwao. Hivyo, ninarudia kwamba, ufafanuzi mkuu wa hoja hii ni kwamba, kuwa na Mungu hasa ni kuwa na kitu ambacho moyo unakitegemea kabisa.
11. Licha ya hayo, fikiria tulivyozoea kufanya hadi sasa katika upofu wetu chini ya Upapa. Kama yeyote aliumwa na jino alifunga na kumwabudu Mt. Apolonio. Kama alipatwa na woga wa moto, aliutafuta msaada wa Mt. Laurentio kama mlezi wake wakati wa shida. Kama aliihofia tauni aliiweka nadhiri kwa Mt. Sebastiano au Rocco1409/Rocho. Machukizo mengine yasiyohesabika yalikuweko na kila mmoja alijichagulia mtakatifu wake, akamwabudu, na kumwita amsaidie
1407 Yaani, masumbuko na tamaa ya fedha.
1408 “Mjuvi.”
1409 Apolonio, Laurentio na Sebastiano walikuwa mashahidi katika Kanisa la Asili. Meno ya Apolonio (+ 248/49) yalivunjwa alipoteswa; Laurentio (+ 258) alichomwa katika nguzo ya moto; Sebastiano (+ mwanzo wa karne ya tatu) alipigwa mishale. Rochus (1295-1327) aliwaponya watu wenye tauni kwa njia ya kuwaombea karibu na msalaba wenye sanamu ya Kristo huko Italia.
wakati wa shida. 12. Katika tabaka hili, kuna wale wafanyavyo jinsi wachawi na walozi hufanya, ambao ibada yao ya mungu inachukiza kupita kiasi, na wanaolifanya agano na Ibilisi ili awape fedha nyingi sana, awasaidie wapate wapenzi, awalindie mifugo yao, na awasaidie wapate mali iliyopotea n.k. Hawa wote wanaiweka mioyo yao yote na tegemeo mahali pengine na siyo kwa Mungu wa kweli. Hawalitazamii wala hawalitafuti lolote kutoka kwake.
13. Hivyo, unaweza kuelewa kwa urahisi hali na kusudi la amri hii. Inadai moyo wote wa binadamu na matumaini yake yote yawekwe kwa Mungu peke yake na siyo kwa mwingine yeyote. Fahamu kwamba, kuwa na Mungu, siyo kumshika kwa mikono yako au kumweka mfukoni au kumfungia sandukuni. 14. Basi, tuna Mungu mioyo yetu inapomkubali na inapomshikilia yeye. 15. Lakini kumshikilia yeye kwa mioyo yetu siyo lingine zaidi ila kumwamini kabisa. Kwa sababu hiyo, anataka kutuepusha na lolote na kisha anatuvutia kwake mwenyewe. Kwa sababu, yeye peke yake, ndiye aliye mwema wa milele. Ni kana kwamba, alisema: “Mlivyovitafuta awali kutoka kwa watakatifu au mlivyovitumainia kuvipata kutoka kwa Mamoni/Utajiri au mahali pengine popote, vitafuteni vitu hivyo vyote kwangu na nihesabuni kama mmoja peke yake atakayewasaidia na kuwamwagieni vyote vilivyo vyema kwa utajiri.”
16. Tazameni, hapa una maana ya heshima na ibada ya kweli impendezayo Mungu na anayoiamuru chini ya adhabu ya hasira ya milele. Yaani, moyo usijue faraja au tumaini lingine lolote isipokuwa lile lipatikanalo kwake, usijiruhusu kubanduliwa kutoka kwake ila unapaswa kuhatarisha na kutothamini lolote duniani kwa ajili yake. 17. Kwa upande mwingine, unaweza kuamua kwa urahisi jinsi dunia inavyojizoeza katika ibada ya uongo na kuiabudu miungu. Hapajakuwepo watu ambao wamepotoka kiasi kwamba, hawajaiweka na kuifuata njia fulani ya kuabudu. Kila mmoja amemweka mungu wake binafsi anayemtegemea kwa baraka, kwa msaada, na kwa faraja.
18. Kwa mfano, watu wa dini za mapokeo wanaoweka tegemeo lao katika nguvu na utawala walimpandisha Yupita1410 cheo cha kuwa juu ya miungu yote. Wengine waliotafuta, kwa nguvu, utajiri, furaha, au anasa, na maisha rahisi, walimtukuza Herkulo, Merkurio, Veno au wengine. Isitoshe, wanawake wajawazito, walimwabudu Diana au Lukina, na kadhalika.1411 Kila mmoja alilifanya lile ambalo moyo ulifikiri kuwa mungu wake. Hata katika mawazo ya walio na miungu ya mapokeo, kuwa na mungu kunamaanisha kutegemea 1410 Kilatini: ‘Iuppiter.’ 1411 Waroma wa zamani waliamini kwamba, Merkurio ‘Mercurius’ na Herkulo ‘Hercules’ walileta usitawi. Veno ‘Venus’ alikuwa mungu wa upendo, na Diana alikuwa mungu wa uwindaji. Lukino ‘Lucina’ alikuwa mungu wa kuzaa.
402
na kuamini. 19. Tatizo ni kwamba, tegemeo lao ni uongo na uovu kwa maana halikujengwa juu ya Mungu mmoja, ambaye zaidi yake, hakika, hakuna Mungu mwingine mbinguni au duniani. 20. Kwa hiyo, watu wa dini za mapokeo wanazifanya dhana na ndoto zao kuhusu Mungu katika sanamu na kutegemea lile ambalo ni tupu lisilokuweko. Ndivyo ilivyo kwa ibada zote za miungu ya uongo. 21. Kuiabudu miungu hakuko katika kuisimamisha sanamu na kuiabudu. Kupo hasa moyo unapokimbilia na kutafuta msaada na faraja kutoka kwa viumbe, watakatifu, au maibilisi, bila kumjali Mungu wala kutazamia vitu vizuri kutoka kwake, wala kutotegemea hasa kwamba, yeye anataka kusaidia, wala moyo hauamini kwamba, jema lolote linalopatikana linatoka kwa Mungu.1412
22. Licha ya hayo, kuna ibada ya uongo. Hii ni ibada ya miungu ya uongo ambayo inapita kiasi, ambayo imeendelea kufanyika hadi sasa na bado ipo duniani. Madaraja yote ya kidini yamejengwa juu yake. Hiyo ibada inahusu dhamiri itafutayo msaada pamoja na faraja na wokovu katika kazi zake zenyewe. Kisha, hudhania kuiteka mbingu kutoka kwa Mungu. Huhesabu mara ngapi imetoa mchango, mara ngapi imefunga, mara ngapi imeongoza misa n.k. Inavitegemea vitu kama hivyo na kujivunia vitu hivyo kiasi kwamba, haikubali kulipokea lolote kutoka kwa Mungu kama zawadi, lakini hupenda kujipatia au kustahili kila kitu katika kazi kana kwamba, Mungu anatutumikia au ana deni letu nasi tu mabwana wanaomtawala. 23. Hilo ni lipi isipokuwa kumfanya Mungu kuwa sanamu? Naam, mungu chale,1413 au kumfanya kuwa kama Mungu? Lakini jambo hili li kali kidogo na halifai kwa wanafunzi chipukizi.
24. Lakini watu wasiokuwa na elimu, nao waambiwe hili ili wapate kuiona na kuikumbuka maana ya amri hii: Imetupasa kumtegemea Mungu peke yake, na kuvitarajia vitu vizuri kutoka kwake, kwa maana ndiye atupatiaye mwili, uhai, chakula, tunachokinywa, malisho, afya, ulinzi, amani, na fadhili zote za muda na za kudumu. Yeye atulindaye na kutuokoa na mwovu, hututoa katika uovu wowote unapotupata. Nimerudia mara nyingi kuwa ni Mungu peke yake ambaye, katika yeye, tunapata yote yaliyo mema na ambaye, katika yeye, tunaokolewa kutoka maovu yote. 25. Kwa sababu hiyo, sisi Wajerumani, tangu nyakati za kale, tumemwita Mungu kwa fahari na kwa jina lenye fahari na thamani kuliko lugha nyingine zozote. Jina linalotokana na neno “wema,” kwa sababu yeye ni chemchemi ya milele inayobubujika kwa wingi na inayoyatiririsha yote yaitwayo na yaliyo mema.1414
1412 Lawama hii ya Luther kuhusu ibada ya miungu inafanana na ya maandiko ya Agostino kuhusu historia na dini ya Waroma katika kitabu kiitwacho, ‘De Civitate Dei’ 1,2 (Mji wa Mungu) miaka ya 413-425.
1413 Kijerumani: ‘Apfelgott;’ (mungu tufani) mfano mmoja wa kanivali. 1414 Kijerumani: ‘Gott’ ni (Mungu)‚‘gut,’ (zuri) au (jema).
403
26. Ingawa mengi mazuri hutujia kutoka kwa wanadamu, tunayapokea yote kutoka kwa Mungu kwa agizo lake na kulingana na mpango wake. Mungu ameamuru kwamba, wazazi wetu na watawala wote watutendee kila aina ya wema. Kadhalika, inambidi kila mmoja amtendee mema jirani yake. Hivyo, tunaipokea mibaraka hii siyo kutoka kwao ila kutoka kwa Mungu kwa njia yao. Viumbe ni mikono tu, mifereji, na njia anazozitumia Mungu kuzitoa karama zote. Kwa mfano, anampatia mama matiti na maziwa ampe mtoto wake. Anazitoa nafaka na aina zote za mazao kutoka udongoni yawe chakula cha mwanadamu, vitu ambavyo kiumbe chenyewe hakiwezi kuvizalisha. 27. Hivyo basi, mtu yeyote asidiriki kukichukua au kukitoa kitu chochote isipokuwa jinsi Mungu alivyoamuru. Lazima tuvitambue vitu vyote kama karama za Mungu na kumshukuru kwa ajili yavyo jinsi amri hii inavyodai. Kwa sababu hii, nyenzo hizi za kuvipokelea vipaji vizuri kwa njia ya viumbe si za kudharauliwa wala kiburi kisitufanye kutafuta mantiki na njia zingine ambazo Mungu hakuziagiza. Maana, huko hakutakuwa kuipokea mibaraka kutoka kwa Mungu, bali kutakuwa kuitafuta kutoka kwetu wenyewe.
28. Hivyo basi, mwache kila mmoja ahakikishe kwamba, ameitukuza amri hii na kuiinua kabisa kuliko vitu vyote wala asiidhanie kuwa utani. Utafute na kuuchunguza moyo wako kwa juhudi na utaona kama unamshikilia Mungu peke yake au la. Ukiwa na moyo ambao hautazamii lolote kutoka kwake isipokuwa lililo zuri, hasa wakati wa shida na mahitaji na unalikataa na kuliacha kila ambalo si Mungu, basi, una Mungu wa kweli. Kinyume chake, moyo wako ukilishikilia lingine ambalo unalitumainia litoe wema na msaada mwingi zaidi kuliko Mungu, na unamtoroka, ila unamkimbilia wakati wa dhiki, basi, wewe una mungu wa uongo, mungu mwingin.
29. Kwa sababu hiyo, ili Mungu aonyeshe kwamba, hataiacha amri hii ipuuzwe na, badala yake, atailinda kwa hali yoyote, kwanza, ameiambatanisha na tisho kali, halafu ameitoa ahadi nzuri na yenye faraja. Mambo haya mawili lazima yasisitizwe na kuhimizwa akilini mwa vijana ili waweze kuyatia maanani na kuyakumbuka.
[Maelezo ya Nyongeza ya Amri ya Kwanza]
30. “Mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.” (Kut. 20:5-6)
31. Ijapokuwa maneno haya yanazihusu amri zote–kama tutakavyoona baadaye–bado yameunganishwa na amri hii kuu kwa maana ni jambo muhimu sana watu kuwa na kichwa kinachofaa. Kwa maana, kichwa kikifaa, maisha yote hayana budi kufaa au kuwa mema na maisha mema yanakuwa na kichwa kinachofaa. 32. Basi, jifunze kutoka kwa maneno haya jinsi Mungu anavyokuwa na hasira kuhusu hao wanaolitegemea lingine lolote isipokuwa yeye. Tena, jinsi alivyo mzuri na mwenye rehema kwa wale wanaomtegemea na kumwamini yeye peke yake kwa moyo wote. Hasira yake haimaliziki hadi kizazi cha nne. 33. Kwa upande mwingine, baraka na wema wake unawafikia maelfu wengi, watu wasije wakaishi kama wenye usalama na kujikabidhi kwa bahati tu, jinsi watu wa mioyo katili wanavyofikiria kwamba, ni mamoja tu jinsi wanavyoishi. 34. Ni Mungu ambaye hataacha bila kulipiza kisasi iwapo watu watamwacha, na hataacha kuwa na hasira hadi kizazi cha nne, naam, hadi wote wameteketezwa. Hivyo, hupenda aogopwe na asidharauliwe.
35. Amelithibitisha hili katika historia kwa visa vyote mbalimbali, jinsi Maandiko Matakatifu yanavyoonyesha kikamilifu na jinsi uzoefu wa kila siku unavyotufundisha bado. Tangu mwanzo, amezing’oa kabisa ibada zote za sanamu na kuziharibu zote za wanaoabudu miungu na za Kiyahudi; jinsi anavyozipindua ibada zote za uongo sasa ili wote watakaobakia humo lazima wateketee hatimaye. 36. Kwa hiyo, hata sasa, kuna wanaojivuna ulimwenguni, wenye nguvu, na matajiri–Wasardanapaluse na Waphalaridesi wanaozidi hata Waperisi kwa utajiri1415–wanaojigambia uasi na utajiri wao na huamini kwamba, wanaweza kuhimili ghadhabu ya Mungu pasipo kujali iwapo Mungu amewakasirikia au amewatabasamia lakini hawatafaulu. Kabla hawajajua, wataangamizwa na vyote walivyovitegemea; sawasawa na wengine wote waliopotea ambao walijifikiria kuwa na hali ya juu na wenye nguvu.
37. Kwa sababu ya vichwa vigumu tu wanadhania kwamba, Mungu hajali na anawaruhusu kupumzika kwa usalama kana kwamba, hana habari kabisa jinsi mambo yalivyo. Lazima atawaharibu na kuwaadhibu vikali kiasi kwamba, hatasahau hasira yake mpaka kwa watoto wa watoto wao. Anakusudia kwamba, kila mmoja atavutiwa na kuona kwamba, huu siyo utani kwake. 38. Kwa maana, hawa ndio anaowazungumzia anaposema: “Wananichukia,” yaani, wanaoendelea katika uasi na kiburi chao. Wanakataa kuyasikiliza yanayohubiriwa au wanayoambiwa. Wanapokemewa ili waweze kuyajua wenyewe na kutubu
1415 Sardanapalus: Mfalme wa hadithi za kale wa Assyria. Kwa sababu ya maisha yenye anasa na tabia zake za kuwapenda wanawake, alikuwa mfano wa mfalme laini sana. Kulingana na hadithi alijiulia mbali na kwao. Phalaris: Dhalimu Myunani wa mji wa Akragas 570-554 K.K. Alikuwa mfano wa mdhulumu mkali.
kabla ya adhabu kuwashukia, wanakasirika na kuwa wajinga kiasi kwamba, kwa haki, wanastahili ghadhabu wanayoipokea. Tunaliona jambo hili kila siku kwa maaskofu na watawala.
39. Pamoja na kwamba, vitisho hivi ni vya kuogofya sana, kuna faraja katika ahadi yenye nguvu zaidi inayowahakikishia huruma hao wanaomshikilia Mungu peke yake–na huahidi wema na baraka, siyo tu kwa ajili yao wenyewe bali pia kwa watoto wao na kwa watoto wa watoto wao hata vizazi maelfu na maelfu. 40. Hakika, hili linastahili kutuamsha na kutusukuma tuitayarishe mioyo yetu katika tumaini lililokamilika katika Mungu iwapo tunayataka mema yote katika maisha haya na ya milele. Kwa kuwa, Enzi Tukufu hutujia na neema kubwa, vivutio vya kufurahisha, na ahadi zilizo tajiri sana.
41. Hivyo basi, mwache kila mmoja alitahadhari hili, lisije likaonekana kana kwamba, lilisemwa na mtu. Kwa maana, linakuletea baraka ya milele, furaha, na wokovu, au litakuletea hasira ya milele, tabu na huzuni. Ni lipi la ziada ambalo ungeliomba au kulihitaji zaidi ya ahadi ya Mungu yenye neema ya kwamba, atakuwa pamoja nawe na kila baraka, na atakulinda na kukusaidia katika kila hitaji? Tatizo ni kwamba, dunia hailiamini lolote katika haya wala kulihesabu kuwa ni Neno la Mungu. 42. Kwa sababu dunia inaona kwamba, wale wanaomtegemea Mungu pasipo kutegemea mali, hupata masikitiko na wana upungufu. Isitoshe, Ibilisi huwapinga, hushindana nao, hawana pesa, fadhili, wala heshima, na wanafanikiwa kuyahimili maisha kwa shida kubwa. Wakati uo huo, wanaotumikia Mamoni/Utajiri wana uwezo, fadhili, heshima, mali, na kila aina ya starehe machoni pa ulimwengu. Kwa sababu hii, maneno haya hayana budi kutambuliwa kama yaliyotumiwa kuupinga udanganyifu huu. Hatuna budi kuyahesabu kwamba, hayasemi uongo wala hayadanganyi. Bado yatathibitisha kuwa ya kweli.
43. Tafakari juu ya wale waliojitolea kwa uangalifu na juhudi zote kujirundikia mali, fedha, au waulize wamefikia wapi hatimaye. Utaona kwamba, juhudi na kazi zao zimekuwa bure. Iwapo wamefaulu kuzirundika hazina nyingi, hizo zote zimepotea na kutoweka mwishowe. Wao wenyewe hawakuweza kuzifurahia mali zao ambazo hazikutosha kuwa urithi wa kizazi cha tatu.1416 44. Utapata mifano ya kutosha katika hadithi mbalimbali za historia na kutoka vinywa vya wazee wenye uzoefu sana. Yatafakari tu na uyajali. 45. Sauli alikuwa Mfalme Mkuu, mcha Mungu na aliyechaguliwa na Mungu mwenyewe. Lakini baada ya kuyaimarisha mamlaka yake, kulipenda taji na mamlaka yake zaidi, aliuacha 1416 Methali ya Kilatini, ‘De male quaesitis non gaudet tertius heres.’ Kiswahili, Mrithi wa tatu hataweza kuzifurahia mali zilizokusanywa kwa ubaya/ufisadi.
moyo wake ukamtelekeza Mungu kwa kuuandama ubaya. Kwa sababu hiyo, hakuwa na budi kuangamia na vyote alivyokuwa navyo. Hatimaye, hakuna mtoto wake hata mmoja aliyebaki. 46. Kwa upande mwingine, Daudi alikuwa mtu maskini, aliyedharauliwa, aliyewindwa, aliyedhulumiwa, na maisha yake hayakuwa na usalama popote. Hata hivyo, aliendelea kuvumilia hasira ya Sauli na akawa mfalme. Maneno haya lazima yadumu na yathibishe kuwa ya kweli kwani Mungu hawezi kusema uongo au kudanganya. Basi, usimwache Ibilisi, dunia, na mwangaza wake, ambavyo hudumu kwa muda na mwishowe hutoweka kabisa, vikudanganye.
47. Acheni tujifunze vyema Amri ya Kwanza ili tupate kuona isivyowezekana Mungu kukivumilia kiburi chochote au kulitegemea jambo jingine lolote. Halidai lolote kubwa kuliko tegemeo litokalo moyoni kwa fadhili zake zote. Hivyo, tutakuwa katika njia bora na kuendelea kutembea na kuyatumia mema yote ambayo Mungu huyatoa jinsi mshona viatu anavyoitumia sindano yake, msharasi1417 na uzi wake kuifanyia kazi, na halafu huviweka kando. Au jinsi msafiri atumiavyo nyumba ya wageni, chakula, na kitanda kwa hitaji la muda tu. Mwache kila mmoja aishi katika imani maishani mwake kulingana na agizo la Mungu na pasipo kukiruhusu hata mojawapo ya vitu hivi kuwa bwana wake au sanamu ya kuabudiwa.
48. Yaacheni haya yatoshee kuhusu Amri ya Kwanza ambayo ilitubidi kuielezea kwa maneno mengi kwa sababu ni muhimu sana. Jinsi nilivyokwisha kusema, pale ambapo moyo umeelekezwa vyema kwa Mungu na amri hii inafuatwa, utimizaji wa amri nyingine zote utafuatia kwa hiari yake.
AMRI YA PILI
49. “Usilitaje jina la Bwana Mungu bure”
50. Jinsi Amri ya Kwanza ilivyouhekimisha moyo na kuifundisha imani, vivyo hivyo, amri hii inatuongoza na kuielekeza midomo na ulimi kuwa katika uhusiano mzuri na Mungu. Kwa maana, mambo ya kwanza yanayotoka na kujionyesha kutoka moyoni ni maneno. Jinsi nilivyokwisha kufundisha hapo juu namna ya kujibu swali, ina maana gani kuwa na Mungu, vivyo hivyo, inakupasa ujifunze kuelewa na kuishika kwa usahihi maana ya amri hii na amri nyinginezo zote.
51. Ukiulizwa: Vipi unavyoielewa Amri ya Pili? Kulitaja bure au kulitumia 1417 ‘Msharasi’ – chombo cha seremala kinachotumiwa kutobolea vitundu vidogo katika mbao.
vibaya Jina la Mungu kuna maana gani? Wajibu ifuatavyo kwa ufupi: “Ni kulitumia vibaya Jina la Mungu ikiwa tutamwita Bwana Mungu pasipo kujali, kwa kuusisitiza uongo au kosa la aina yoyote.” Kwa hiyo, lile ambalo amri hii hulikataza ni kutolikimbilia jina la Mungu kwa uongo, au kulitaja kutoka kinywani wakati moyo unajua hakika au unapaswa kujua kinyume chake. Kwa mfano, ambapo watu huapa mahakamani na mtu mmoja husema uongo dhidi ya mwingine. 52. Jina la Mungu haliwezi kutumiwa vibaya kwa kuuimarisha uongo na udanganyifu. Iache hii ibakie kuwa maana dhahiri na sahili ya amri hii.1418
53. Kutokana na hili, kila mmoja anaweza kutambua ni lini na ni mara ngapi jina la Mungu linatumiwa vibaya, japo haiwezekani kuyahesabu matumizi mabaya yote. Hata hivyo, kwa ufupi, kila matumizi mabaya ya jina la Mungu hutokea hasa katika shughuli za dunia zinazohusu fedha, mali, na heshima. Shughuli hizi hutokea hadharani mahakamani, sokoni, au pengine popote ambapo watu wanaapa kwa uongo wakilitumia jina la Mungu. Au wanapoziweka rehani nafsi zao kwa ajili ya jambo lolote. Hili linatokea mara nyingi katika mambo ya unyumba, ambapo watu wawili huchumbiana kwa siri na baadaye huyavunja mapatano yao yaliyofanyika kwa kiapo.
54. Lakini matumizi mabaya zaidi ya yote hutokea katika mambo ya kiroho ambayo yanaihusu dhamiri, wakati wahubiri wa uongo wanauweka na kuutoa ubatili wao kuwa sawa na Neno la Mungu.
55. Tazama, haya yote ni jaribio la kujirembesha mwenyewe katika jina la Mungu, au kujifanya wa kuvutia, au kujihesabia haki mwenyewe katika shughuli za kawaida za dunia, au katika mambo ya imani yaliyo bora sana na magumu na katika elimu ya imani. Miongoni mwa waongo kuna pia wenye kukufuru na siyo wale wabaya mno tu wanaojulikana kwa watu wote kuwa wanaliaibisha jina la Mungu bila kuogopa–hawa hawatuhusu ila huwahusu chakari wahalifu ili wapate nidhamu– lakini pia wale wanaokufuru hadharani ukweli na Neno la Mungu na kulitoa kwa Ibilisi. Hakuna haja tena kulizungumzia hili zaidi.
56. Basi, tuacheni tujifunze kwa kweli na tuuweke moyoni umuhimu mkubwa wa amri hii ili tuichunge kwa juhudi kubwa na kuyaepuka sana matumizi mabaya ya jina takatifu, ambayo ni dhambi kubwa kuliko zote inayoweza kufanywa hadharani. Kwa maana, kuusema uongo na kudanganya ni dhambi kubwa, lakini inakuwa kubwa zaidi tunapojaribu kuitetea na kutaka kuithibitisha kwa njia ya kuliita jina la Mungu na kulitumia kama kifuniko cha kufunikia aibu. Hivyo, ikatokea kwamba, uongo hutokea mara moja, maradufu, kisha mara nyingi.
1418 Sentensi hii inayafuata maandiko ya Kilatini. Maandiko ya Kijerumani: ‘Das lasse das Deutsch und leichtisten Verstand dieses Gebots bleiben.’
57. Kwa sababu hiyo, Mungu ameiongezea amri hii tisho la uchaji:“Maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.” Maana yake ni kwamba, yeyote atakayeikiuka hatasamehewa wala hataachwa bila kuadhibiwa. Jinsi Mungu asivyoacha kuuadhibu moyo ulioasi hata kidogo, hataliruhusu jina lake litumiwe kuufunika uongo hata kidogo. 58. Kwa bahati mbaya, ni janga la mara kwa mara katika dunia nzima kwamba, kuna wachache sana wasiolitumia jina la Mungu kwa madhumuni ya kusema uongo na uovu wa kila aina, sawasawa na walivyo wachache wanaomtegemea Mungu peke yake kwa moyo wao wote.
59. Kwa asili, sote tuna wema huu mzuri ndani yetu kwamba, tufanyapo kosa, tungependa kuifunika na kuirahisisha aibu yake, ili isionekane na kujulikana kwa yeyote. Hakuna hata mtu mmoja mwenye kiburi awezaye kujivunia uovu alioufanya mbele ya ulimwengu. Tunapenda kutenda kwa siri bila mtu yeyote kufahamu tulifanyalo. Yeyote akigunduliwa, Mungu na jina lake huingizwa katika jambo hilo ili ulaghai uonekane kuwa uchaji na aibu kuwa heshima. 60. Hii ndiyo njia ya kawaida ya ulimwengu, na kama gharika kuu, imezigharikisha nchi zote. Hivyo, tunapata tunalostahili: tauni, vita, njaa, moto, mafuriko, wake wajeuri, watoto, watumishi na masumbuko ya aina zote.1419 Dhiki kubwa za namna hii zingetoka wapi? Ni huruma kubwa sana kwamba, bado dunia inatuvumilia na kutuhimili.
61. Kwa hiyo, licha ya yote, vijana wetu wanapaswa kulazimishwa na kufundishwa, kwa juhudi, ili wapate kuiheshimu sana amri hii kama amri nyinginezo. Kila wanapokosea, tuwarudi kwa kiboko mara moja na kupambana nao kwa kuitumia na kuisisitiza kwao ili tuweze kuwalea siyo kwa rada tu bali pia katika kicho na kumwogopa Mungu.
62. Hivyo, sasa unafahamu ina maana gani kulitumia vibaya jina la Bwana Mungu. Kurudia kwa ufupi: ni ama kuusema uongo tu na kulithibitisha lile lisilokuwa kweli kwa jina la Mungu, au kulaani, kuapa, kusihi, na kwa ufupi, kuufanya uovu wa aina yoyote.
63. Licha ya hayo, inakubidi pia kujua jinsi ya kulitumia jina la Mungu inavyostahili. Kwa kuyatumia maneno: “Usilitaje bure jina la Mungu,” wakati uo huo, Mungu anatuelekeza pia kulitumia vyema kwa sababu limefunuliwa na kutolewa kwetu kwa lengo la kutumiwa kwa manufaa yetu. 64. Kwa kuwa, tumekatazwa kulitumia jina takatifu kwa uongo au uovu, kwa upande mwingine 1419 Miaka ya 1527-1528, tauni iliathiri Wittenberg; Kaisari Karolo V alipigana na Waingereza, Wafaransa, Papa wa Roma, na miji ya Milano na Venezia; Waturuki walitaka kuvianzisha vita tena; bei zilipanda/mfumko wa bei ulizidi, na Mto Elbe ulifurika sana.
inafuatia kwamba, tunaamriwa kulitumia kwa ajili ya ukweli na uzuri wote. Kwa mfano, tunapoapa kwa haki inapokuwa lazima na inapohitajika. Isitoshe, tunapolifundisha vizuri, tunapoliita jina lake wakati wa shida au kumtukuza na kumshukuru wakati wa mafanikio n.k. Haya yote yameagizwa kwa ufupi katika Zab. 50:15: “Ukaniite siku ya mateso; nitakuokoa, na wewe utanitukuza.” Shabaha ni kulitumia jina lake katika huduma ya kweli na katika njia iliyobarikiwa. Hivyo, jina lake litakaswe, jinsi tunavyoomba katika Sala ya Bwana.
65. Hapa, jumlisho la amri nzima limeelezewa. Hivyo, iwapo umeielewa, umelitatua kwa urahisi swali ambalo limewasumbua sana walimu wengi: kwa nini kiapo kimekatazwa katika Injili ilihali Kristo, Mt. Paulo, na watakatifu wengine walikula viapo.1420 66. Kwa ufupi, maelezo ni haya: Hatupaswi kuapa ili kuuimarisha uovu, yaani, uongo au ambapo hakuna haja wala faida. Badala yake, tuape kwa kuimarisha ukweli na kwa manufaa ya jirani. Hakika, hii ni kazi nzuri ambayo kwayo, Mungu anatukuzwa, kweli na haki vinaimarishwa, uongo unakanushwa, amani inaletwa miongoni mwa watu, utiifu unaonyeshwa, na mapigano yanatulizwa. Kwa maana, hapa, Mungu mwenyewe anaingilia kati na kubainisha kati ya mema na mabaya, mazuri na maovu. 67. Kama mtu mmoja katika ugovi anaapa kwa uongo, hataiepuka adhabu. Ingawa itachukua muda mrefu, hatafanikiwa. Kila kitu ambacho atakipata kwa kiapo cha uongo kitamponyoka kutoka mikononi na hatakifurahia kamwe. 68. Nimeliona hili katika wengi walioapa kwa uongo katika kiapo chao cha ndoa. Kamwe, hawakupata kuwa na furaha hata saa moja wala siku njema baadaye. Hivyo, waliteketea vibaya katika mwili, roho, na mali zao zilipotea kwa njia ya mikasa.
69. Kwa hiyo, ninashauri na kuomba jinsi nilivyofanya hapo awali kwamba, kwa njia ya maonyo, vitisho, vizuizi, na adhabu, watoto wafundishwe mapema kuuepuka uongo. Waepuke hasa kuliingiza jina la Mungu katika uongo. Kwa maana, wanaporuhusiwa kufanya wapendavyo, hakuna zuri litakalotoka kwao. Ni dhahiri kabisa kwamba, siku hizi dunia imekuwa mbaya zaidi kuliko ilivyopata kuwa. Hakuna utawala, hakuna utiifu, hakuna uaminifu, na hakuna imani. Badala yake kuna ukaidi tu, na watu wasiokuwa na nidhamu ambao hawawezi kusaidiwa kwa njia ya mafundisho au adhabu. Haya yote ni hasira na adhabu za Mungu kwa ajili ya kuidharau amri hii makusudi.
70. Kwa upande mwingine, inawapasa watoto wahimizwe na kuchochewa kuliheshimu jina la Mungu na kila mara wawe nalo midomoni mwao daima katika kila jambo litakalowapata au litakaloonekana kwao. Kwa maana, heshima ya kweli ya jina lake ni kuwa na matazamio nalo kwa ajili ya faraja zote. Hivyo, 1420 Mt. 26:63-64; Gal. 1:20; 2 Kor. 1:23
kama tulivyosikia hapo juu, moyo humtolea Mungu heshima anayoistahili kwa imani, na baadaye humkiri kwa midomo.
71. Hii ni tabia iliyobarikiwa, yenye manufaa, na inafaa sana kwa kumpinga Ibilisi ambaye daima yu katika mazingira yetu ili atuingize katika dhambi, aibu, maafa, na masumbuko. Huchukia sana kulisikia jina la Mungu, na hawezi kubakia kwa muda mrefu, pale ambapo linatajwa na kuitwa kwa moyo. 72. Naam, maafa mengi mabaya na ya kutisha yangetupata kama hatungeliita jina la Mungu naye akatulinda. Mimi mwenyewe nimejaribu na kujifunza kwa uzoefu kwamba, mara nyingi, nimeepushiwa mara moja na kuondolewa janga kubwa na la ghafla nilipomwita Mungu. Ninasema, ili tumuudhi Ibilisi, inatupasa tuwe na jina hili takatifu midomoni mwetu daima ili asiweze kutujeruhi atakavyo.
73. Kwa sababu hii, amri hii inatusaidia kuiunda tabia na kujikabidhi kwa Mungu kila siku. Yaani, nafsi na mwili, mke, watoto, watumishi, na vyote tulivyonavyo dhidi ya kila shida inayoweza kutokea. Hivyo, miongoni mwetu, kumetokea mazoea ya kusema sala wakati wa chakula na sala nyinginezo za asubuhi na jioni. 74. Vilevile, kuna mazoea ya watoto kuifanya alama ya msalaba wakati jambo baya mno na la kuogofya linaonekana au linasikika na wanalia kwa sauti kubwa wakisema: “Bwana Mungu, tuokoe!” “Tusaidie, mpenzi Bwana Yesu!” Hali kadhalika, yeyote akipata bahati njema ambayo hakuitazamia, ingawa ni ndogo namna gani, anasema: “Mungu asifiwe na ashukuriwe!” “Mungu amenitunukia hili!” Watoto walizoea kufundishwa kufunga na kumwomba Mt. Nikolao na watakatifu wengineo. Hili lingependeza zaidi na kukubaliwa na Mungu kuliko umonaki/utawala mkuu wote na utawa wa Wakerthuso.1421
75. Kwa njia hii, tunaweza kuwalea vijana wetu kwa njia za kitoto na michezo kama hii katika hofu na heshima ya Mungu. Hivyo, inapasa amri ya kwanza na ya pili ziweze kushikwa vyema na katika mazoezi ya kudumu. Hivyo, kiasi fulani cha uzuri kinaweza kuota mizizi, kukua, na kuyazaa matunda. Yaani, watu wakue ambao nchi nzima inaweza kujivunia na kuwafurahia sana. 76. Hii ndiyo ingekuwa njia ya kuwalea watoto vyema ili waweze kufundishwa kwa upole na furaha. Kwa maana, wenye kulazimishwa kwa viboko na makofi tu hawatakuwa na tabia nzuri. Watabakia tu kuwa watu wazuri wakati kiboko kinaiangukia miili yao.
77. Lakini aina hii ya mafundisho huisambaza mizizi yake mioyoni ili
1421 Daraja la Wakerthusi lililoanzishwa mwaka wa 1084 na Bruno (1032-1101) huko Ufaransa katika Grand Chartreuse. Wamonaki/Watawala wakuu wa daraja hilo waliifuata nidhamu kali ya kujinyima anasa za mwili. Luther alilitumia daraja hili mara nyingi kama mfano wa kuelekezana kwa ajili ya uhuru wa Injili.
wamwogope Mungu kuliko kiboko na mangumi. Hili ninalisema kwa urahisi wa namna hii kwa sababu ya vijana, ili lipenye katika akili zao. Kwa maana, tunapowahubiria watoto, inatubidi pia kuisema lugha yao. Hivyo, tutayazuia matumizi mabaya na kuyafundisha matumizi mema ya jina la Mungu, jambo ambalo halipo katika maneno tu, lakini pia katika utendaji na katika maisha. Hii ni kwa sababu inawapasa wajue kwamba,Mungu anapendezwa na matumizi mazuri ya jina lake; naye atayazawadia kwa utajiri jinsi atakavyoyaadhibu vikali matumizi mabaya.
AMRI YA TATU
“Uikumbuke siku ya Sabato uitakase”
79. Asili ya “siku takatifu” au “pumziko” ni neno la Kiebrania “shabbath” ambalo maana yake halisi ni kupumzika, yaani, kuiacha kazi. Hivyo, neno kwa neno tumezoea kusema “kuiacha kazi” kumaanisha kuishika/kuitakasa siku takatifu au sikukuu. 80. Katika Agano la Kale, Mungu aliitenga siku ya saba na kuiweka kwa mapumziko. Aliiamuru ihesabiwe kuwa takatifu kuliko nyingine zote. Kuhusu utii wa jambo hili la nje, amri hii ilitolewa kwa Wayahudi peke yake. Walipaswa kuziacha kazi za nguvu na kupumzika ili mtu na mnyama waweze kurudishiwa nguvu upya na wasidhoofishwe kwa kazi za mfululizo. 81. Hata hivyo, baadaye waliiwekea mipaka myembamba mno na kuitumia vibaya. Walimchongea Kristo wakashindwa kumvumilia kwa ajili ya kuzifanya kazi izo hizo ambazo wao wenyewe walizoea kuzifanya siku hiyo, jinsi tunavyosoma katika Injili–kana kwamba, amri ingeweza kutimizwa kwa kuiacha kazi yoyote ya kulima. Hii haikuwa maana yake bali tutakavyosikia ni kwamba, ilimaanisha kuitakasa siku takatifu au siku ya mapumziko.
82. Basi, upana wa amri hii ukieleweka, haituhusu sisi Wakristo. Ni jambo la nje, jinsi yalivyo maagizo mengine ya Agano la Kale ambayo yaliambatana na mapokeo, watu, nyakati na mahali fulani fulani. Sasa tumekuwa huru kwa hayo yote kwa njia ya Kristo.
83. Ili kuyafafanua mapenzi ya Mungu, katika amri hii, kwa watu wasiokuwa na elimu, tunadokeza kwamba, hatuiadhimishi sikukuu kwa sababu ya Wakristo wenye ujuzi na elimu kwani wao hawaihitaji. Kwanza, tunaitakasa kwa sababu ya mahitaji ya kimwili. Asili hufundisha na kudai kwamba, kwa siku moja nzima, umma, watumishi, watwana, na wajakazi ambao wamekuwa wakihudumu kazini wiki nzima, waziache kazi na wapate kupumzika na kuburudika. 84. Pili na la msingi zaidi, tunaitakasa siku hii ya kupumzika–kwa kuwa hatuwezi kuwa na
wakati mwingine–ili uhuru na muda vipatikane kuihudhuria ibada ili tuje pamoja kusikia, kuzungumza kuhusu Neno la Mungu, na halafu tumsifu Mungu kwa nyimbo na sala.
85. Licha ya hayo, ninasema, hilo halikulazimishwa sana kwa wakati maalumu, jinsi ilivyokuwa kwa Wayahudi kwamba, itakuwa siku hii au siku fulani. Kwa maana, hakuna siku inayoishinda nyingine kwa umuhimu. Kusema kweli, ibada ingefanyika kila siku. Hata hivyo, kwa kuwa umma hauwezi mahudhurio ya jinsi hiyo, angalau pawe na siku moja iliyotengwa katika juma kwa ajili ya shughuli hiyo. Kwa sababu Jumapili imewekwa kwa ajili hiyo tangu zamani, tusiibadilishe. Kwa njia hii, utaratibu unaohusu wote utakuwepo na yeyote asiilete vurugu kwa kuyazusha mambo mapya.
86. Hivyo basi, maana dhahiri ya amri hii ni: kwa kuwa tunaiadhimisha sikukuu kwa vyovyote, maadhimisho hayo yangetumiwa kwa kulisikia Neno la Mungu. Kazi ya pekee ya siku hii iwe ni huduma ya mahubiri kwa sababu ya wadogo na umma wa kawaida. Lakini maadhimisho ya mapumziko yasitafsiriwe kuwa mawazo finyu mno kiasi cha kujizuia kuifanya kazi ya ghafla inayoweza kuzuka au kazi ya dharura.
87. Basi, unapoulizwa maana ya “Uitakase siku takatifu,” jibu: “Inamaanisha kuihesabu kuwa takatifu.” Lakini inamaanisha nini kuihesabu kuwa takatifu? Ni kuitengea maneno matakatifu, kazi takatifu, na maisha matakatifu. Siku yenyewe haihitaji kutakaswa kwa sababu imeumbwa ikiwa takatifu. Lakini Mungu anaitaka iwe takatifu kwako. Hivyo basi, hufanyika takatifu au najisi kutegemea na unavyoitumia kuyatenda mambo matakatifu au machafu.
88. Utakaso huo hufanyikaje? Haufanyiki tunapoketi karibu na jiko na kutozifanya kazi za nje au kujipamba kwa mataji na kuzivalia nguo nzuri sana ila, kama ilivyokwisha kusemwa, tunapojishughulisha na Neno la Mungu na kujizoeza kwalo.
89. Naam, sisi Wakristo tunapaswa kuifanya kila siku kuwa takatifu na kujitolea wenyewe kwa kuzitenda shughuli takatifu. Yaani, kila siku tujishughulishe na Neno la Mungu, na tuwe nalo mioyoni mwetu na midomoni mwetu. Hata hivyo, jinsi tulivyokwisha kusema kwamba, watu wote hawana wakati huo mwingi wa kazi rasmi, tunapaswa kuzitumia saa kadhaa katika juma kwa ajili ya vijana, au angalau siku nzima kwa ajili ya umma wote ili kuyatunza mambo haya peke yake: kuzifundisha Amri Kumi za Mungu, Ukiri wa Imani, na Sala ya Bwana. Tunaweza kuyarekebisha maisha na utu wetu wote kulingana na Neno la Mungu. 90. Wakati wowote haya yanafanyika na kukaririwa, hakika, siku takatifu inaadhimishwa.
Hayo yasipofanyika, haitaitwa siku takatifu ya Wakristo. Wasiokuwa Wakristo wanaweza pia kuziacha kazi na kuwa walegevu tu sawa na kundi letu lote la mapadre wasimamao kila siku makanisani wakiimba na kupiga kengele bila kuitakasa siku takatifu. Kwa maana, hawahubiri wala kujizoeza Neno la Mungu ila wanalifundisha na kuishi kinyume cha neno lenyewe. 91. Neno la Mungu ni masalio matakatifu kushinda masalio yote.1422 Naam, sisi Wakristo tunalikubali hilo moja tu. Japo tungekuwa na mifupa yote ya watakatifu wote au mavazi matakatifu yote yaliyowekwa wakfu na kukusanywa katika rundo moja, havingeweza kutusaidia katika lolote. Maana, vyote ni vitu vilivyokufa au visivyokuwa na uhai na ambavyo haviwezi kumtakasa yeyote. Lakini Neno la Mungu ni hazina inayovitakasa vitu vyote. Kwalo, watakatifu wenyewe wote walitakaswa. 92. Wakati wowote Neno la Mungu linafundishwa, linahubiriwa, linasikilizwa, linasomwa, au linatafakariwa, hapo ndipo mtu, siku, na kazi vinatakaswa kwalo. Siyo kwa sababu ya kazi ya nje bali kwa ajili ya Neno ambalo linatufanya sisi sote kuwa watakatifu. Kwa hiyo, daima ninasema tena kwamba, maisha yetu yote na kazi zetu havina budi kuongozwa na Neno la Mungu iwapo vitakuwa vitakatifu au vitampendeza Mungu. Pale ambapo hili linafanyika, amri hii inatumika na inatimizwa.
93. Kinyume chake, kila mwenendo au kazi inayofanywa bila Neno la Mungu si takatifu mbele za Mungu, hata iwe ya fahari vipi au hata kama imegubikwa kwa masalio ya watakatifu, jinsi yalivyo madaraja ya kiroho yanayobuniwa ambayo hayajui lolote kuhusu Neno la Mungu lakini huutafuta utakatifu katika kazi zao zenyewe.1423
94. Basi, kumbuka kwamba, nguvu na mamlaka ya amri hii vinaonekana siyo katika kupumzika bali katika utakaso, ili siku hii iwe na kazi yake takatifu ya pekee. Kwa sababu aina nyingine za kazi na shughuli hazifai kuitwa takatifu isipokuwa mtu mwenyewe awe mtakatifu kwanza. Lakini hapa, inabidi kazi itakayomtakasa mtu ifanywe; nayo–jinsi tulivyosikia–hufanyika kwa nguvu ya 1422 Kulingana na maandiko ya Kijerumani: “Hekalu lililo juu ya mahekalu yote.” Masalio matakatifu ni sehemu mbalimbali za maiti au nguo za Wakristo maarufu waliofariki dunia. Wakristo walifundishwa na waliamini katika Kanisa la Roma kwamba, masalio yalikuwa na stahili maalumu za watakatifu mbele za Mungu. Stahili hizo ziliiongezea hazina ya stahili ya Kanisa kulingana na imani ya namna hiyo. Wakristo waliweza kuipata rehema kutoka kwa hazina hiyo ya Kanisa kwa njia ya ungamo na kazi za upatanisho ili kuiepuka au kuifupisha Purgatorio, yaani, mahali pa mateso ya muda baada ya kufariki dunia. Walimu wa Matengenezo ya Kanisa waliyaacha na kuyalaani mafundisho ya namna hiyo kama kufuru dhidi ya stahili na haki ya Kristo.
1423 Mwaka wa 1522, Luther aliandika kitabu kiitwacho ‘Wider den falsch genannten geistlichen Stand des Papsts und der Bischoe.’ Maana yake: (Dhidi ya Madaraja ya Papa na Maaskofu Yaliyoitwa ya Kiroho kwa Uongo).
Neno la Mungu peke yake. Kwa hiyo, mahali, nyakati, watu, na utaratibu mzima wa nje wa kuabudu vimeanzishwa na kuteuliwa ili mamlaka ya Neno la Mungu yaweze kudhihirika hadharani.
95. Neno la Mungu linategemewa sana kiasi kwamba, hakuna siku inayoweza kutakaswa bila neno lenyewe. Hatuna budi kufahamu kwamba, Mungu anausisitiza utiifu mkali wa amri hii na atawaadhibu wote watakaodharau, watakaokataa kusikiliza na kujifunza neno lake, hasa wakati ulioamriwa kwa ajili hiyo.
96. Hivyo basi, amri hii huvunjwa na wanaoitumia au wanaoinajisi siku takatifu isivyostahili, jinsi wafanyavyo hao wasiojali kulisikiliza Neno la Mungu kwa ajili ya tamaa yao au upuuzi wao. Isitoshe, kuna wanaolala katika vilabu vya pombe na kulewa sana kama nguruwe. Pia kuna kundi lingine linalolisikiliza Neno la Mungu, jinsi linavyoisikiliza burudani yoyote, wanaokuja katika mahubiri kwa ajili ya mazoea tu, na wanaondoka tena wakiwa na ujuzi mdogo sana wa Neno la Mungu mwishoni mwa mwaka jinsi walivyokuwa mwanzoni mwa mwaka.
97. Wazo limekuwepo kwamba, Jumapili ilitakaswa iwapo mtu alisikiliza Misa au Injili ikisomwa. Lakini hakuna aliyeuliza kuhusu Neno la Mungu wala hakuna aliyelifundisha. Kwa kuwa sasa tuna Neno la Mungu, bado tunashindwa kuyaondoa matumizi mabaya ya siku takatifu kwa sababu tunaruhusu kuhubiriwa na kuonywa lakini tunasikiliza bila kujali sana.
98. Basi, kumbuka kwamba, inakupasa kulisikiliza Neno, kujifunza, na kulishika. Usilichukulie kuwa jambo la hiari au lisilokuwa na umuhimu mkubwa kwako. Ni amri ya Mungu na atataka kujua ulivyosikiliza, ulivyojifunza, na ulivyoliheshimu Neno lake.
99. Vile vile, wenye kiburi wanaopenda kuchaguachagua hawana budi kukemewa. Hawa ni wale ambao, baada ya kusikiliza hubiri moja au mahubiri mawili, huugua na kuchoka wakifikiria kwamba, wanayajua hayo yote vyema na hawamhitaji mwalimu au daktari yeyote wa ziada. Hii ndiyo hasa dhambi iliyoorodheshwa miongoni mwa dhambi za mauti, na inaitwa ??????, yaani, ulegevu au ridhaa yenye nia mbaya na upotovu ambao Ibilisi huutumia kuiloga na kuidanganya mioyo ya wengi ili, kwa siri, atuvamie na kuliondoa Neno la Mungu kutoka kwetu.
100. Niache nikuambie hili: ingawa tayari unalijua Neno kikamilifu na umekuwa mtaalamu walo, bado u katika utawala wa Ibilisi kila siku. Mchana na usiku hataacha kamwe kuiba bila ufahamu wako, hataacha kuchochea kutokuamini mioyoni mwenu, na hataacha kuchochea mawazo maovu dhidi ya amri zilizotangulia na zingine zote. Hivyo, inakupasa kuliweka Neno la Mungu
moyoni, midomoni, na masikioni mwako siku zote. Kwa maana, moyo ulegeapo na neno halisikilizwi, Ibilisi huvunja, huingia, na huyasababisha madhara kabla hatujayatambua. 101. Kinyume chake, tunapolitafakari sana, tunapolisikiliza, na tunapolitumia Neno, lina nguvu ya kuyazaa matunda. Daima linauamsha ufahamu mpya, furaha mpya, na moyo mpya wa ibada. Isitoshe, daima linautakasa moyo na mawazo yake. Maana neno hili si zembe au halijafa, bali lina nguvu na li hai. 102. Ingawa hakuna raghba au mahitaji yoyote yaliyotuleta kwa Neno, bado kila mmoja anapaswa kuelewa kwamba, kwa njia hii, Ibilisi anafukuzwa na anatoroka. Hivyo, amri hii inatimizwa, na Mungu anafurahishwa na hayo kuliko fahari ya matendo yoyote ya unafiki hata yakiwa adhimu vipi.
AMRI YA NNE
103. Mpaka sasa tumekwisha kujifunza amri tatu za kwanza ambazo zinamhusu Mungu. Kwanza, katika maisha yetu yote, inatupasa tumtegemee, tumwogope, na tumpende Mungu kwa moyo wetu wote. Pili, inatupasa tusilitumie vibaya jina lake takatifu katika kuuimarisha uongo au kazi yoyote mbaya ila tulitumie kwa sifa ya Mungu, kwa faida na kwa wokovu wa jirani, na wetu wenyewe. Tatu, katika sikukuu na wakati wa mapumziko, inatupasa tujishughulishe kwa juhudi na Neno la Mungu, ili matendo yetu yote na maisha yetu yote yatawaliwe nalo. Sasa, zinafuatia nyingine saba zinazomhusu jirani yetu. Miongoni mwazo, iliyo kubwa kuliko zote ni:
104. “Waheshimu baba yako na mama yako”
105. Miongoni mwa asasi zote, Mungu amekitunukia sifa maalumu cheo cha baba na cha mama mzazi. Anatuamuru tuwapende na kuwaheshimu wazazi wetu. Kuhusu ndugu, madada, na majirani zetu kwa jumla, anaamuru tuwapende. Hivyo, anawabainisha baba na mama juu ya watu wengine wote duniani na anawaweka karibu naye. Kwa maana, kuheshimu ni jambo muhimu zaidi kuliko kupenda. 106. Heshima inajumlisha upendo, staha, unyenyekevu, na adabu kwa ajili ya enzi inayofichwa ndani yazo. 107. Inatuamrisha tuwazungumzie kwa upendo na kicho,1424 kwa moyo na kwa mwili, na tuwaonyeshe kwa matendo yetu kwamba, tunawaheshimu sana na kwamba, tunawahesabu kuwa wa pili baada ya Mungu. Kwa maana, yeyote tunayemheshimu kwa moyo wote, inatupasa tumstahi kama aliye juu na mkubwa kweli. 108. Kwa hiyo, lazima vijana wafundishwe kuwaogopa wazazi wao kama wawakilishi wa Mungu. Isitoshe, lazima wakumbuke kwamba, hata kama wazazi wao ni wa hali ya chini 1424 “Kicho” – hali ya kuogopa.
namna gani, maskini, dhaifu, na wenye kushangaza, wao ni baba na mama ambao Mungu amewapa. Hawapaswi kunyang’anywa heshima yao kwa jinsi walivyo au kwa ajili ya kushindwa kwao. Hivyo, tusiufikirie utu wao jinsi walivyo bali tuyafikirie mapenzi ya Mungu aliyewaumba na kuwaweka kuwa wazazi wetu. Naam, katika hali nyingine zote, sisi sote tu sawa mbele za Mungu. Hata hivyo, lazima pawe na jinsi hii isiyokuwa ya usawa na yenye tofauti maalumu miongoni mwetu. Hivyo, Mungu anakuamuru uwe mwangalifu, unitii kama babako,1425 na uyakubali mamlaka yangu.
109. Kwanza basi, jifunze amri hii inadai nini kuhusu heshima ya wazazi. Unapaswa kuwaweka katika ngazi tofauti na ya juu zaidi kama hazina yenye thamani kubwa kuliko zote duniani. 110. Licha ya hayo, uwe na adabu kwa njia ya maneno yako mbele zao, usiwazungumzie kwa kiburi na kwa kuasi. Badala yake, watiini na uzuie ulimi wako, hata kama watakukasirisha. 111. Tatu, inakubidi pia kuwaheshimu kimatendo, yaani, uwatumikie kwa mwili na mali, uwasaidie, uwatunze wakizeeka, wakiugua, wakidhoofika, au wakiwa maskini. Inakupasa uyafanye haya yote kwa furaha, unyenyekevu na kicho, kana kwamba unayafanya mbele za Mungu. Yeye anayewajali wazazi wake, hataruhusu wateseke kwa kupungukiwa au kwa njaa. Atawaweka juu kuliko yeye mwenyewe, atawaweka ubavuni mwake, na atashiriki nao kila alichonacho kulingana na uweza wake.
112. Pili, tazama jinsi kazi waliyopewa watoto ilivyo kubwa, nzuri, na takatifu. Ole wao, wameidharau na kuipuuza na hakuna anayeitambua kama amri ya Mungu au kama neno takatifu na agizo la Mungu. Kwa maana, tungeihesabu hivyo, ingekuwa wazi kwa wote kwamba, walioishi kulingana na maneno haya, lazima pia wawe watu watakatifu. Kisha, hakungekuwa na haja ya kuuanzisha utawa au mashirika ya watawa. Kila mtoto angebaki kuwa mwaminifu kwa amri hii, na angeweza kuielekeza dhamiri yake kwa Mungu akisema: “Ikinipasa kuzifanya kazi nzuri na takatifu, silijui lolote zuri zaidi kuliko kuitoa heshima na utii wote kwa wazazi wangu kwa maana Mungu mwenyewe ameitoa amri hii. 113. Linaloamriwa na Mungu halina budi kuheshimiwa mno kuliko lolote tunaloweza kulibuni wenyewe. Kwa kuwa hakuna mwalimu mwingine mkuu au bora kuliko Mungu, fundisho zuri zaidi kuliko lake haliwezi kuwepo. Sasa, analifundisha kikamilifu litupasalo kulifanya tukitaka kweli kuyafanya matendo mema na anapoyaamuru, anaonyesha kwamba, anapendezwa nayo. Basi, iwapo hii ni amri ya Mungu, na inajumuisha busara yake kubwa zaidi, basi, sitaifanya kuwa nzuri zaidi kamwe.”
114. Unaona, kwa njia hii, tungekuwa na watoto wacha Mungu waliofundishwa 1425 Mt. 5:48
vyema na kulelewa katika baraka ya kweli, wangebakia nyumbani katika utiifu na huduma kwa wazazi wao, na tungekuwa na fundisho maalumu katika uzuri na furaha. Lakini watu hawakuhisi waliolazimika kuitanguliza amri ya Mungu katika utukufu wake mkamilifu. Waliweza kuidharau na kuiacha bila kujali. Kwa hiyo, watoto hawakuweza kuiweka moyoni. Waliachama1426 kwa mshangao katika mipangilio yote ambayo tumeibuni bila hata kuiomba idhini ya Mungu.
115. Hivyo, kwa ajili ya kumpenda Mungu, acheni tuwafundishe vijana wetu kuitanguliza amri hii na kuyaweka mbali mambo mengine yote. Iwapo wanataka kumtumikia Mungu kwa matendo mema kweli, inawapasa wayafanye yanayowapendeza akina baba na mama zao, au kwa wenye majukumu ya wazazi. Kila mtoto ajuaye na alifanyaye hili, kwanza kabisa, ana faraja kubwa moyoni mwake na anaweza kujivuna kwa furaha mbele ya wote wanaojishughulisha na kazi walizojichagulia: “Tazama, kazi hii inampendeza Mungu wangu mbinguni. Hili ninalijua hakika.” 116. Waacheni wote wajitokeze na kujivunia kazi zao kubwa, nyingi, zinazotaabisha, na zilizo ngumu. Tutaona kama wataionyesha kazi hata moja ambayo ni kubwa na nzuri zaidi kuliko utiifu kwa baba na mama, ambao Mungu ameuagiza na ameuamurisha uwe karibu na utiifu kwa ajili ya utukufu wake. Kama Neno na mapenzi ya Mungu vinahesabiwa kuwa vya kwanza na kutimizwa, hakuna litakalodhukuriwa kuwa muhimu zaidi ya mapenzi na neno la wazazi. Bora tu haya pia yawe chini ya utiifu ulioelekezwa kwa Mungu na yasiende kinyume cha amri zilizotangulia.
117. Kwa hiyo, inakupasa ufurahie moyoni na kumshukuru Mungu kwamba, amekuchagua na kukupa hadhi ya kufanya kazi ambayo ni ya thamani jinsi hiyo na ya kumpendeza. Ijapokuwa inahesabiwa kuwa duni na inadharauliwa, hakikisha unaichukulia kuwa kubwa na ya thamani, siyo kwa sababu ya kustahili kwako lakini kwa sababu ina mahali pake ndani ya hicho kito1427 na hiyo hazina takatifu, yaani, Neno na amri ya Mungu. 118. Ee, Wakerthusi, watawa wa kiume, na watawa wa kike wangelipa gharama kubwa kiasi gani iwapo, katika utendaji wao wa kidini, wangeweza kuleta mbele za Mungu kazi moja waliyoifanya kulingana na amri yake, na mbele yake wangeweza kusema kwa moyo wa furaha: “Sasa ninajua kwamba, kazi hii inakupendeza Wewe.” Je, watu hawa maskini na wanyonge watajificha wapi watakapotahayari1428 mbele za Mungu na ulimwengu wote? Wataaibika mbele ya mtoto ambaye atakuwa ameishi kulingana na amri hii na kulazimika kukiri kwamba, kulingana na stahili za maisha yao yote, hawafai kumpa maji ya kunywa? 119. Wanalistahili hili kwa sababu ya upotovu wao wa 1426 “Achama” – fungua kinywa kwa mshangao.
1427 “Kito” – jiwe la thamani. 1428 “Kutahayari” – kuona haya baada ya kulitenda jambo la aibu.
kiibilisi na kwa kuikanyagia chini amri ya Mungu kiasi cha kulazimika kujitesa bila manufaa kwa kazi zao walizozibuni wenyewe, na wakati uo huo, wapokee dharau na shida kama ujira wao.
120. Si moyo ungerukaruka na kuyeyuka kwa furaha wakati wa kwenda kufanya kazi na kufanya lililoamriwa ukisema: “Tazama, hii ni nzuri zaidi kuliko utakatifu wote wa Wakerthusi, ingawa wanafunga hadi kufa na wanapiga magoti yao kwa sala bila kukoma?” Kwa maana, hapa una matini hakika na ushuhuda mtakatifu ambao Mungu ameuagiza. Hajaliamuru hata neno moja kuhusu hayo mambo mengine. Hii ndiyo hali mbaya na upofu duni wa dunia kwamba, hakuna anayeyaliamini jambo hili. Hivyo, Ibilisi ametudanganya kabisa kwa utakatifu wa uongo na kiinimacho cha matendo yetu wenyewe.
121. Kwa hiyo, ninarudia kusema, ningekuwa na furaha sana kama tungeyafumbua macho na masikio yetu na kuliweka hili moyoni ili tusipotoshwe tena kutoka kwa Neno safi la Mungu na kupelekwa kwa ubatili wa Ibilisi unaotudanganya. Halafu, yote yangekuwa mema. Wazazi wangekuwa na furaha zaidi, upendo, wema, na uelewano ndani ya nyumba zao. Nao watoto wangeipendeza mno mioyo ya wazazi wao. 122. Kwa upande mwingine, wanapokaidi na kutofanya linalostahili hadi kiboko kitumiwe, wanamkasirisha Mungu na wazazi wao pia. Hivyo, wanajinyima hazina hii na furaha ya dhamiri na kujiwekea balaa tupu. 123. Hivyo ndivyo mambo yanavyotendeka duniani sasa, jinsi kila mmoja anavyolalamika. Vijana pamoja na wazee ni wakaidi, wakorofi, hawana staha, hawaitambui heshima, hawalifanyi lolote hadi walazimishwekwa makonde, na wanaharibiana majina na kupunguziana hadhi1429 kwa siri wawezavyo. Kwa hiyo, Mungu huwaadhibu kiasi kwamba, wanazama katika kila aina ya uchafu na dhiki. Aghalabu, wala wazazi wao hawawezi kuyafanya mengi, maana, mjinga mmoja humfundisha mwingine na jinsi wao walivyoishi ndivyo waishivyo watoto wao baada yao.
125. Ninasema, hili linapaswa kuwa shauri la kwanza na muhimu kuliko yote lituhimizalo kuishika amri hii. Kwa mujibu wa amri, kama hatungekuwa na baba na mama, tungetamani Mungu aliweke gogo au jiwe mbele yetu ambalo tungeliita baba na mama. Tungefurahia kiasi gani zaidi kuwaonyesha heshima na utii kwani ametupa wazazi hai. Kwa maana tunajua kwamba, inaufurahisha mno Utukufu wa Mungu na malaika wote na kuwaudhi maibilisi wote, na licha ya hayo, ni kazi ya thamani kuliko zote tuwezayo kuifanya, inayoikaribia ibada takatifu ya kumwabudu Mungu iliyoelezewa katika amri zilizotangulia. 126. Hata utoaji zaka na kila tendo jema kwa jirani haliwezi kulinganishwa na hii. Kwa maana, 1429 “Hadhi” – cheo, utukufu, heshima.
Mungu ameliinua tabaka hili la wazazi juu ya mengine yote. Naam, ameliweka liwe mwakilishi wake hapa duniani. Mapenzi haya na furaha ya Mungu vinastahili kuwa sababu na kichocheo cha kutosha kulifanya tunaloliweza kwa uchangamfu na furaha.
127. Licha ya hili, ni wajibu wetu machoni pa ulimwengu kuonyesha shukrani kwa ajili ya wema na vitu vyote vizuri ambavyo tumevipokea kutoka kwa wazazi wetu. 128. Lakini hapa tena Ibilisi anaitawala duniani: watoto wanawasahau wazazi wao jinsi sote tunavyomsahau Mungu, na hakuna hata mmoja anayefikiria jinsi Mungu anavyotulisha, anavyotulinda, anavyotukingia hatari, na anavyotukirimia mema mengi ya ajabu ya mwili na ya nafsi. Hasa saa ya uovu inapofika, tunakasirika na kulalamika bila subira na kuyasahau mema yote tuliyoyapokea maishani mwetu. Hivyo ndivyo tunavyowatendea wazazi wetu na hakuna mtoto anayelitambua au kulidhukuru hili isipokuwa Roho Mtakatifu awe amemwongoza kwalo.
129. Mungu anajua vizuri sana upotovu huu wa dunia. Hivyo, kwa njia ya amri, yeye humkumbusha na kumhimiza kila mmoja wetu atafakari aliyofanyiwa na wazazi wake. Hivyo, kila mmoja hutambua kwamba, kutoka kwao amepata mwili, uhai, na kwamba, amelishwa na kupewa malezi nao, la sivyo, angekuwa ameangamia mara mia katika uchafu wake yeye mwenyewe. 130. Wahenga hawakukosea waliposema: ‘Deo, parentibus et magistris non protest satis gratiae rependi.’ Maana yake: Mungu, wazazi, na walimu hawawezi kushukuriwa na kulipwa vya kutosha kamwe. Anayeliona suala hili jinsi hii atakuwa na heshima yote kwa wazazi wake bila kulazimishwa na atawasifu kama waliotumiwa na Mungu kumfanyia mema yote.
131. Zaidi na licha ya haya yote, kichocheo kingine kikubwa ambacho kingetuamsha zaidi kuishika amri hii ni kwamba, Mungu ameiambatanisha amri hii na ahadi nzuri: “Siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.” 132. Unaona mwenyewe jinsi Mungu alivyo makini kuhusu amri hii. Anatangaza kwamba, amri hii ni ya furaha, ni ya kupendeza kwake, ni chombo kwa ajili ya ustawi wetu mkubwa zaidi inayotuongoza katika maisha ya utulivu, mazuri, na yenye baraka. Kwa hiyo, Mtume Paulo pia anaikweza1430 sana na kuisifu amri hii anaposema katika Efe. 6:2-3: “Amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.” Ijapokuwa amri nyingine nazo zina ahadi inayodokezewa, hakuna nyingine kamwe iliyoelezewa wazi na dhahiri kuliko hii.
1430 “Kweza” – pandisha/patia hadhi ya juu.
134. Basi, hili ndilo tunda na zawadi kwamba, yeyote atakayeitii amri hii, atakuwa na siku za furaha, fanaka, na usitawi. Kwa upande mwingine, adhabu kwa atakayeikaidi ni hii kwamba, ataangamia haraka na hatayafurahia maisha kamwe. Kwa maana, katika Maandiko Matakatifu, kuwa na maisha marefu kunamaanisha kuzeeka, na kuwa na kila kitu katika maisha marefu kama vile afya nzuri, mke, na watoto, riziki, amani, serikali nzuri n.k., ambavyo, vikikosa, maisha haya hayawezi kufurahiwa kwa ukunjufu wala hayatadumu sana. 135. Hivyo, usipowatii baba na mama na kuwa chini ya nidhamu yao, basi, mtii chakari, na usipomtii yeye, basi, mtii mnyosha mifupa,1431 yaani, kifo! 136. Kwa ufupi, haya ndiyo anayoyataka Mungu: mtii, mpende, na mtumikie naye atakupa zawadi na kila baraka. Kwa upande mwingine, ukimuudhi, atakasirika, atakupelekea kifo na chakari. Kwa nini tuna wahalifu wengi jinsi hii ambao lazima watiwe kitanzi kila siku, wakatwe shingo, au wavunjwevunjwe katika gurudumu1432 kwa ajili ya kutotii? Hawatakubali kulelewa kwa wema. Matokeo yake ni kwamba, kwa njia ya adhabu ya Mungu, wanajipatia taabu na masikitiko, mambo tunayoyaona. Kwa maana, ni nadra sana waovu kama hao kufa kifo cha kawaida au cha wakati unaofaa.
137. Hata hivyo, wachaji na watiifu wana baraka hii. Wanaishi muda mrefu katika amani na utulivu. Huwaona wajukuu wao kama tulivyosema hapo juu,“hadi kizazi cha tatu na cha nne.” 138. Tena, kulingana na tujuavyo kutokana na uzoefu, ambapo kuna jamaa ya heshima na ya zamani wanaoendelea vizuri na kuwa na watoto wengi, hakika, wana misingi yao katika ukweli huu kwamba, baadhi yao walilelewa vizuri na waliwastahi wazazi wao. Kwa upande mwingine, kuhusu waovu imeandikwa katika Zab. 109:13: “Wazao wake waangamizwe, jina lao likafutwe katika kizazi cha pili.” 139. Hivyo basi, jifunze vyema jinsi utiifu ulivyo jambo muhimu sana machoni mwa Mungu. Kwa kuwa anaupatia hadhi ya juu sana, anapendezwa nao mno, na anaupatia thawabu1433 ya utajiri mkubwa. Licha ya hayo, Mungu ni mkali mno katika kuwaadhibu wanaoivunja amri hii.
140. Ninasema, haya yote yanaweza kuwashawishi vijana, kwa maana hakuna anayeamini jinsi amri hii inavyolazimu, ambayo awali, haikutiliwa maanani wala haifundishwa chini ya Upapa. Haya ni maneno ya kawaida na rahisi, na kila mtu anadhania amekwisha kuyajua tayari. Kwa hiyo, watu huyaweka kando rahisi, huielekeza mioyo yao kwenye mambo mengine, na kisha hushindwa kutambua
1431 Kijerumani: ‘Streckebein;’ Kiyunani: ‘θαωατω πανδαματορι, των κακων παιδων διδασκαλω,’ yaani, (kifo, aliye mwalimu wa wanafunzi waovu mwenye enzi).
1432 Wakati huo, wahalifu wabaya walifungiwa kwenye magurudumu makubwa ya mbao na walivunjwa mifupa moja kwa moja kwa gongo kubwa.
1433 “Thawabu,” malipo mema ayapatayo mtu kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kuzitii amri Zake.
na kuamini jinsi wanavyomfanya Mungu akasirike wakati hawaijali amri hii na jinsi ilivyo jambo la thamani na la kukubalika wanapolifuata.
141. Kuhusiana na amri hii, kuna mengi ya kusemwa juu ya aina mbalimbali za utiifu kwa watu wenye mamlaka, watu wenye wajibu wa kuamuru, na wanaotawala. Kutoka kwa mamlaka ya wazazi, mamlaka mengine yote yanapatikana na kustawishwa. Kwa maana, baba peke yake anaposhindwa kumwelimisha mtoto wake, humwajiri mwalimu amfundishe. Akiwa dhaifu mno, anauomba msaada wa marafiki na majirani zake. Akifariki, anayatoa na kuyatunuku mamlaka ya utawala wake kwa wengine ambao wameteuliwa kwa kazi hiyo. 142. Vile vile, chini yake, lazima awe na watumishi wa nyumbani, wanaume kwa wanawake kwa madhumuni ya kuitunza nyumba. Basi, wote waitwao mabwana wana cheo cha wazazi na lazima wapate nguvu na mamlaka yao ya kutawala kutoka kwacho. Hivyo, wote wanaitwa baba katika Maandiko Matakatifu kwa sababu, katika utawala wao, wanautekeleza wajibu wa baba, na wanapaswa kuwa na moyo wa ubaba kwa walio chini yao. Jinsi ilivyokuwa tangu zamani, Warumi na mataifa mengine waliwaita mabwana na mabibi wenye nyumba “patres et matres familiae,” yaani, baba na mama wa kaya.Tena, waliwaita watawala na mabwana “patres patriae,”1434 yaani, baba wa nchi. Ni aibu kubwa kwetu Wakristo ambao hatuwaiti vivyo hivyo, au angalau, hatuwathamini na kuwaheshimu vivyo hivyo.
143. Lolote mtoto anawawia baba na mama, ndilo wengine wote wanaloiwia kaya nzima. Kwa hiyo, watwana na wajakazi wanapaswa kuwa waangalifu kuwatii mabwana na mabibi zao na kuwaheshimu kama baba na mama zao wenyewe. Isitoshe, wanapaswa kukifanya kila kitu wanachokijua kuwa kinatazamiwa kutoka kwao siyo kwa lazima na kwa kusita, bali kwa furaha na kwa uchangamfu na lazima walifanye jambo hilo kwa sababu iliyotajwa hapo juu. Yaani, ni amri ya Mungu na inampendeza yeye kuliko matendo mengine yote. 144. Hata inawapasa kuyalipa marupurupu kwa kazi walizopewa na wafurahie kuwa na mabwana na mabibi ili waweze kuwa na dhamiri nzuri jinsi hiyo, na wajue jinsi ya kuzifanya kazi ambazo hakika ni za thamani kubwa mno. Awali, kazi hizi zilitelekezwa na kudharauliwa. Badala yake, katika jina la Ibilisi, kila mtu alikimbilia nyumba za watawa, alikwenda katika hija, alivitafuta vyeti vya upatanisho kwa hasara yao na kwa dhamiri mbaya.
145. Kama ukweli huu ungeweza kuwekwa mioyoni mwa watu maskini, basi, mjakazi angeruka, angemsifu, na angemshukuru Mungu. Kwa kazi yake ya uangalifu ambayo kwayo, huipokea riziki na mshahara, angepata hazina ambayo 1434 ‘Pater patriae;’ Marcus Tullius Cicero (106-43 K.K.), alilipata jina hili la heshima huko Roma alipoifichua njama ya Katalina.
hata wanaohesabiwa kuwa watakatifu wakubwa kuliko wote hawajaipata. Je, si jambo la ajabu kujigamba mwenyewe kwa kusema: “Nikiifanya kazi yangu ya kila siku kwa uaminifu, tendo hilo ni zuri kuliko utawa wote na maisha ya kujinyima ya watawa wa kuime?” 146. Licha ya hayo, una ahadi kwamba, utastawi na kuendelea katika mema yote. Unawezaje kuwa na heri zaidi na maisha matakatifu kuhusiana na kazi zako? 147. Hakika, imani ndiyo inayomfanya mtu kuwa mtakatifu mbele za Mungu. Imani peke yake humhudumia yeye wakati kazi zetu zinawahudumia watu. 148. Hapa una kila jambo jema, makazi na ulinzi katika Bwana, dhamiri yenye furaha na Mungu mwenye rehema pia, atakayekupa thawabu mara mia moja. Wewe ni lodi1435 wa kweli ukiwa mcha Mungu na mtiifu. Iwapo wewe si mtiifu, utapokea hasira na ghadhabu za Mungu. Hutakuwa na amani moyoni, na hatimaye utakuwa na kila aina ya masumbuko na taabu.
149. Yeyote ambaye hatashawishiwa na hili, na ambaye hatauegemea uungu, tunamkabidhi kwa chakari na kwa mnyosha mifupa.1436 Hivyo, mwache kila mtu anayeweza kuukubaki ushauri. Akumbuke kwamba, Mungu asidharauliwe na kwamba, Mungu anasema nawe na anaudai utiifu. Ukimtii Yeye, wewe u mtoto wake mpendwa. Ukiidharau amri hii, basi, pokea aibu, dhiki, na majuto kama thawabu yako
150. Yayo hayo pia hayana budi kusemwa kuhusu utiifu kwa mamlaka makuu,1437 ambayo–jinsi tulivyosema–yamejumlishwa katika cheo cha ubaba, yaani, uhusiano mpana sana kuliko uhusiano mwingine wowote. Kwa hiyo, mtu ni baba wa kaya, wa kadiri ya idadi ya wakazi, wananchi, na watawaliwa wake. Kwa maana, Mungu anatupatia chakula, nyumba, makazi, ulinzi, na usalama kwa kuwatumia watawala wa umma sawa na anavyowatumia wazazi wetu. Hivyo, kwa kuwa wamepatiwa jina hili na cheo kwa heshima zote kama adhama yao kubwa kabisa, ni wajibu wetu kuwaheshimu na kuwakuza kama hazina na johari yenye thamani kubwa kuliko zote duniani.
151. Aliye mtiifu, anayekubali, na aliye tayari kuhudumia, na kwa uchangamfu wote anaitoa heshima yote inapohitajika, anajua kuwa anampendeza Mungu na kwamba, anaipokea furaha na shangwe kama zawadi yake. Kwa upande mwingine, asipofanya hivyo kwa upendo, na badala yake, akiwadharau, akiwapinga, na akiasi dhidi ya mamlaka yao, mwache ajue kwamba, hatapata upendeleo wala baraka kutoka kwa Mungu. Anapofikiria kwamba, atazipata rupia kwa kutokuwa mwaminifu, atazipoteza kumi mahali pengine. Isitoshe, atakuwa mhanga kwa
1435 Kijerumani:‘Junker;’ mtu mwenye cheo kikubwa katika mashariki ya Ujerumani ya zamani.
1436 Kijerumani: ‘Streckebein,’ yaani, (kifo). Msemo wa kawaida wa Luther uliotoka mkoani Niedersachsen.
1437 Kijerumani: ‘Obrigkeit.’
423
chakari, au ataangamia vitani, au kwa tauni, au kwa njaa, au watoto wake watakuwa waovu, na atayaona maumivu, ataikosa haki, na atayapata mapigo ya ujeuri mikononi mwa watumishi wake, majirani, wageni, na wadhalimu. Kisha, atalipwa kwa kisasi analolitafuta na analolistahili.
152. Kama tungeacha tushawishiwe kwamba, kazi za utiifu zinampendeza Mungu na zina thawabu kubwa, tungegharikishwa kabisa na baraka nyingi na tungepata kila ambalo mioyo yetu inalitaka. Lakini Neno na amri ya Mungu vinadharauliwa kana kwamba Yeye ni mpuuzi. Hata hivyo, tuacheni tuone kama wewe ni mtu wa kumpinga. Unadhani itakuwaje vigumu kwake kukulipa? 53. Kwa hiyo, hakika utaishi vizuri zaidi kwa hisani ya Mungu, amani, na baraka kuliko kuishi na chuki na dhiki. Unafikiri ni kwa nini sasa dunia imejaa kutokuamini, fedheha, taabu na mauaji? 154. Ni kwa sababu kila mmoja anataka kuwa bwana anayejitawala mwenyewe, hataki kuyajali maslahi ya wengine, anataka kuwa huru kama Kaisari asiyekuwa chini ya mamlaka yoyote, na hulifanya analolitaka. Kwa hiyo, Mungu anamwadhibu mlaghai mmoja kwa kumtumia mwingine. Unapompunja au kumdharau bwana wako, mtu mwingine anakuja na anakutendea vivyo hivyo. Naam, katika nyumba yako lazima utalipa mara kumi zaidi kutoka kwa mke, watoto au watumishi wako wenyewe.
155. Naam, kwa makini, tunazihisi balaa zetu, tunanung’unika, na kulalamika kwa kutokuamini, uhalifu wa kutumia nguvu, ujeuri, na ukosefu wa haki. Hata hivyo, hatutaki kuona kwamba, sisi wenyewe ni wahalifu waliostahili adhabu sana na kwamba, hatufanywi bora hata kidogo kwayo. Tunaidharau hisani na furaha. Hivyo, ni haki tu kwamba, tuna balaa bila huruma. 156. Bila shaka, bado kuna mahali fulani ulimwenguni ambamo kuna wacha Mungu, la sivyo, Mungu hangeendelea kutupatia mema mengi! Kwa ajili ya stahili zetu wenyewe, hatungekuwa na hata senti nyumbani wala jani kondeni. 157. Nimelazimika kuyahimiza haya yote kwa maneno mengi kwa matumaini kwamba, mtu fulani anaweza kuyaweka moyoni ili tuweze kukombolewa kutoka kwa upofu na dhiki ambamo tumetumbukia sana, na tuweze kuelewa kweli Neno na mapenzi ya Mungu na kuvipokea kwa uaminifu. Kwa maana, kutokana na Neno la Mungu, tungeweza kujifunza jinsi ya kujipatia furaha, shangwe, na wokovu hapa na ahera.
158. Hivyo, tuna baba wa aina tatu waliowasilishwa katika amri hii: akina baba wa damu, akina baba wa jamaa/kaya, na akina baba wa nchi. Licha ya hawa, kuna pia akina baba wa kiroho, siyo kama hao wa Upapa waliojiita hivyo wenyewe bila kuutekeleza wajibu wowote wa huduma ya ubaba. Maana akina baba wa kiroho ni wale tu wanaotutawala na kutuongoza katika Neno la Mungu. 159. Mt. Paulo anajivuna kwamba, yeye ni baba katika 1 Kor. 4:15 anaposema: “Maana
424
mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.” 160, Kwa kuwa watu kama hao ni akina baba, wanastahili kuheshimiwa hata kuliko wengine wote. Lakini huipokea heshima kwa nadra sana. Kwa maana, njia ambayo dunia inawaheshimu ni kuwateka nyara kutoka katika nchi na kuwanyima kipande cha mkate. Kwa ufupi, jinsi Mt. Paulo1438 asemavyo: “Tumefanywa kama takataka za dunia, na tama ya vitu vyote hata sasa.”
161. Kuna haja kuuhimiza umma kwamba, watakaoitwa Wakristo wanawajibika mbele za Mungu kuionyesha “heshima maradufu”1439 kwa wale wanaozihudumia nafsi zao, wawafanyie mema, na kuwatunza. Mungu atawaongezea baraka za kutosha watendao hivyo na hatawaacha wakose mahitaji. 162. Lakini katika jambo hili, kila mmoja hulipinga na kuliasi. Wote wanaogopa kwamba, vitambi vyao vitapungua/watapungukiwa. Hivyo, hawawezi kumtunza mhubiri hata mmoja anayeheshimika, ingawa awali waliyajaza matumbo ya vitambi kumi. 163. Kwa sababu hii, Mungu anastahili kutunyang’anya Neno na baraka zake, na tena awaruhusu wahubiri wa uongo kuinuka na kutuongoza hadi kwa Ibilisi, ambaye, licha ya hayo, atainyonya jasho na damu yetu.
164. Hata hivyo, wanaotumainia mapenzi na amri ya Mungu wana ahadi kwamba, kwa kila watakachowapa akina baba wa kimwili na wa kiroho, na kwa heshima watakayowapa, watazawadiwa pakubwa. Wao watakuwa na mkate, nguo, fedha kwa mwaka mmoja au miwili, pia watakuwa na maisha marefu, riziki, amani, utajiri na baraka milele. 165. Hivyo, wewe ufanye wajibu wako na mwache Mungu akutunze na akupatie mahitaji yako yote. Kwa kuwa ameliahidi hilo, hajapata kudanganya kamwe wala hatakudanganya wewe.
166. Hili linapasa kututia moyo kabisa na kuilainisha mioyo kwa furaha na upendo kwa ambao tunawawia heshima kiasi cha kuiinua mikono yetu kwa furaha katika kumshukuru Mungu kwa kutupatia ahadi kama hizo. Inatupasa kukimbia hadi miisho ya dunia ili tuzipate. Kwa maana, japo jitihada za dunia yote zitaunganika, haziwezi kutuongezea hata saa moja katika maisha yetu au kuiotesha punje moja ya ngano kutoka ardhini. Lakini Mungu anaweza na ataweza kukupa yote kwa wingi kabisa kulingana na matakwa ya moyo wako. Yeye anayeyadharau na kuyabeza haya hastahili kamwe kulisikia neno kutoka kwa Mungu.
167. Mengi yamesemwa kuliko inavyopasa kwa hao ambao amri hii inawahusu. Licha ya hayo, ingekuwa vizuri kuwahubiria wazazi kuhusu asili ya huduma yao wajue namna ya kuwatendea walio chini ya mamlaka yao. Ijapokuwa wajibu wa 1438 1 Kor. 4:13 1439 1 Tim. 5:17
wakubwa haujaelezewa kinaganaga katika Amri Kumi za Mungu, umeagizwa mara kwa mara katika aya nyingi za Maandiko Matakatifu na Mungu anautaka ujumlishwe katika amri hii ambayo kwayo, anazungumzia kuhusu baba na mama.
168. Mungu hataki kuwa na walaghai na wadhalimu katika huduma hii ya utawala1440 na wajibu wala hataki kuwapa heshima hii–yaani, nguvu na mamlaka ya kutawala–wanaweza tu kusujudiwa. Lakini wazazi wanapaswa kutambua kwamba, wanamwia Mungu utiifu na kwamba, zaidi ya yote, wanapaswa kuutekeleza wajibu wao kwa bidii na kwa uaminifu. Wanapaswa pia kuwatunza na kuwapa mahitaji ya kimwili watoto wao, watumishi, raia, na vile vile kuwalea ili wamtukuze na kumheshimu Mungu. 169. Kwa hiyo, usifikirie kwamba, asasi ya mzazi ni jambo la furaha na haja. Hii ni amri kali na agizo la Mungu ambaye pia anakutaka uwajibikie amri hii.
170. Lakini tatizo hapa ni kwamba, hakuna hata mmoja anayelielewa au kulisikiliza hili. Kila mmoja hutenda kana kwamba, Mungu alitupatia watoto kwa lengo la furaha na burudani. Alitupatia watumishi ili tuwatumikishe kama ng’ombe au punda kwa ajili ya kazi tu. Alitupatia raia tuwafanyie tupendavyo kana kwamba, halikuwa jukumu letu kuhusiana na wanavyojifunza au wanavyoishi. 171. Hakuna anayetaka kutambua kwamba, hii ni amri ya Enzi ya Mungu, ambaye hutuita kwa ukali tuitoe hesabu yetu na kutuadhibu kwa ajili ya kuipuuza. Wala umuhimu wake hautambuliwi ili kuyatoa makini ya dhati kwa vijana. 172. Iwapo tunataka watu bora na hodari katika utawala wa raia na Kanisa, lazima tutumie juhudi, muda, na gharama zote katika kuwafundisha na kuwaelimisha watoto wetu ili waweze kumtumikia Mungu na wanadamu. Isitoshe, hatupaswi kufikiria tu jinsi ya kurundika fedha na mali kwa ajili yao. 173. Mungu anaweza kabisa kuwatunza na kuwatajirisha jinsi afanyavyo kila siku bila sisi. Lakini ametupatia watoto na amri hii kwamba, tuwafundishe na kuwatawala kulingana na mapenzi yake. La sivyo, Mungu hangekuwa na haja ya kuwatoa baba na mama. 174. Basi, mwache kila mmoja ajue kwamba, ni wajibu wake mkuu kuwalea watoto wake katika hofu na maarifa ya Mungu. La sivyo, kuna hatari ya kuipoteza neema ya Mungu wetu. Iwapo watoto wamejaliwa akili nyingi, tuwape nafasi ya kujifunza na kusoma kwa bidii ili waweze kutumikia wanapohitajika.
175. Hili lingefanyika, Mungu angetubariki kwa wingi na kutupatia neema ili tuwaelimishe watu ambao wangekuwa wa manufaa kwa nchi na watu. Kadhalika, tungekuwa na wananchi walioelimishwa vyema, wanawake wanyofu, hodari, na wapendao nyumba ambao wangewalea watoto na watumishi wacha Mungu. 176. Fikiria madhara ya kufisha unayoyafanya unapodharau na kushindwa kuwalea 1440 Kijerumani: ‘Ampt und Regiment.’
426
watoto wako ili waweze kuwa na manufaa na ucha Mungu. Unajiletea dhambi na ghadhabu na unajipatia kuzimu1441 kama ujira wa jinsi umewalea watoto wako hata kama utakuwa mchaji na mtakatifu jinsi gani katika mambo mengine. 177. Kwa kuwa amri hii imepuuzwa, Mungu anaiadhibu dunia kwa njia ya kutisha. Hivyo, hakuna tena nidhamu ya raia, amani, au heshima kwa watawala. Sote tunalalamika kuhusu hali ilivyo, lakini hatuoni kuwa ni kosa letu. Kwa sababu ya jinsi tunavyowafundisha, tuna raia walioharibika na wasiotii.
178. Haya yanatoshea kuwa kama maonyo; maelezo ya kina zaidi yatangojea wakati mwingine.
AMRI YA TANO
179. “Usiue”
180. Sasa tumekwisha kuushughulikia utawala wa kiroho na wa duniani, yaani, mamlaka ya Mungu, ya baba, na utiifu. Katika amri hii, tunaziacha nyumba zetu na kwenda kwa majirani zetu kujifunza binafsi jinsi mwenendo wetu unavyotakiwa kuwa miongoni mwa wanadamu wenzetu. Kwa hiyo, Mungu wala serikali haijumlishwi katika amri hii na bado haki ya kuua haujabatilishwa. 181. Mungu ameikabidhi serikali mamlaka ya kuwaadhibu watenda maovu badala ya wazazi, ambao hapo awali, walitakiwa kuwapeleka watoto wao hukumuni na kuwahukumu kwa kifo1442 jinsi tusomavyo katika maandiko ya Musa. Kwa hiyo, linalokatazwa hapa linamhusu mtu binafsi katika mahusiano yake wala siyo serikali.
182. Amri hii ni sahili vya kutosha na imetumika mara nyingi. Tunaisikia ikielezewa kila mwaka katika Injili ya Mathayo 5:21ambapo Kristo mwenyewe anaielezea kwa ufupi, yaani, hatupaswi kuua, kwa mkono, moyo, mdomo, ishara, makonyezo, msaada, wala kwa njia ya ushauri. Kwa hiyo, kila mmoja anakatazwa hapa kukasirika, isipokuwa–kama tulivyokwisha kusema–kwa hao wanaomwakilisha Mungu, yaani, wazazi na serikali. Kwa maana, ni haki kwa Mungu na kwa kila anayemwakilisha kukasirika, kukemea, na kuadhibu na haya yanatekelezwa dhidi ya wanaoivunja amri hii pamoja na zingine.
183. Lakini sababu na haja ya amri hii ni kwamba, Mungu anajua vyema kwamba, dunia ni ovu na kwamba, maisha haya yamejaa dhiki nyingi. Kwa hiyo, ameiweka amri hii na amri zingine kama mpaka kati ya mema na mabaya. Kuna uhalifu mwingi dhidi ya amri hii sawa na ulivyo dhidi ya amri zingine zote. Hivyo, 1441 Kuzimu – ahera, mahali pa mateso ya milele ziendapo nafsi za watu baada ya hukumu. 1442 Kum. 21:18-20
kuhusu amri hii, hatuna budi kuishi miongoni mwa watu wengi wanaotudhuru, na kwa hiyo, tuna sababu ya kuwa na uhasama nao. 184. Kwa mfano, jirani yako anakuonea wivu kuwa una nyumba na kaya nzuri, mali nyingi zaidi, na fanaka kutoka kwa Mungu kumshinda. Kwa hiyo, ananuna, anakuonea wivu, na hasemi mema juu yako.
Hivyo, kwa uchochezi wa Ibilisi, unakuwa na maadui wengi wanaokuonea wivu kwa jema lolote unalipata kimwili au kiroho. Tunapowaona watu wa namna hii, mioyo yetu hughadhabika na tunakuwa tayari kuimwaga idamu na kulipiza kisasi. Kisha, matusi na makonde yanafuatia, ambayo hatimaye, matunda yao huwa dhiki na mauaji. 185. Hapa, Mungu, kama Baba mpole, anaingilia kati na kuyataka magomvi yasuluhishwe kwa ajili ya usalama wa wote wanaohusika ili mtu mmoja asimdhulumu mwingine. Kwa jumla, anataka kila mmoja alindwe, awe huru, na awe na amani dhidi ya uovu na mashambulizi makali ya wengine. Ameitoa amri hii iwe kama ukuta, ngome, na kimbilio la jirani yetu ili tusimjeruhi na kuumiza mwili wake.
186. Basi, linalofundishwa na amri hii ni kwamba, mtu yeyote asimdhuru mwingine kwa ajili ya tendo lolote ovu hata kama anastahili kudhuriwa. Kwa maana, mauaji yamekatazwa na kila linaloweza kusababisha mauaji. Watu wengi, ijapokuwa hawaui, hulaani na kuyatamka mabaya kuhusu maadui zao ambayo kama yangetimia, yangewamaliza mara moja. 187. Kila mmoja wetu ana moyo wa kulipiza kisasi. Ni kawaida kwamba, hakuna mtu anayetaka kuteseka mikononi mwa mwingine. Kwa hiyo, Mungu anataka kuiondoa mizizi na chanzo cha mioyo hii ya uchungu dhidi ya majirani zetu. Anatutaka tuitimize amri hii na daima tuitumie kama kioo cha kujionea wenyewe ili tuweze kuyazingatia mapenzi yake na tumkabidhi yeye ovu lolote linalotupata kwa kujiamini moyoni na kwa sala. Kisha, tutaridhika kuwaruhusu maadui zetu kughadhibika, kukasirika sana, na kuyafanya mabaya kuliko yote. Hivyo, tupate kujifunza kuituliza hasira yetu, na badala yake, tuwe na moyo wenye uvumilivu na upole, hasa kwa wanaotukasirisha, yaani, maadui zetu.
188. Kwa ufupi basi, umuhimu wa amri hii inayouzuia umma usiue ni kutomdhuru mtu yeyote. Kwanza, hii inamaanisha, tusimdhuru mtu yeyote kwa mkono, kwa matendo, kwa kwa ushauri wa maneno, na hatupaswi kuzitumia mbinu zozote zenye nia ya kumdhuru mtu yeyote. Mwisho kabisa, mioyo yetu isiwe na chuki au nia ya kumdhuru mtu yeyote kwa kuwa na hasira au chuki naye. Hivyo, tusiwe na lawama mbele ya watu wote kimwili na kiroho, hasa kwa ambaye anatutakia mabaya au anatutendea maovu. Kwa maana, kumtendea mabaya mtu ambaye anakutakia na anakufanyia mema ni uovu mno bali siyo utu.
428
189. Pili, amri hii haivunjwi mtu anapolifanya ovu tu, bali pia anaposhindwa kumfanyia jirani yake mema. Au, licha ya kuwa na nafasi, anashindwa kulizuia ovu, kumlinda, kumtetea, na kumwokoa kutokana na madhara yote ya mwili ama jeraha. 190. Basi, iwapo utamwacha mtu aende zake akiwa uchi, wakati ungeweza kumpa nguo, basi, umemfanya afe kwa baridi kali. Ukimwona mtu mwenye njaa na usimpe chakula, umemfisha kwa njaa. Pia, ukimwona asiyekuwa na hatia akihukumiwa kifo au dhiki inayofanana na hiyo, na usimwokoe, japo unajua njia na mbinu za kufanya hivyo, umemwua. Haitakusaidia kujitetea kwamba, hukuwa na uwezo wa kumpatia msaada wowote, ushauri au ufadhili kwa ajili ya kifo chake, kwa maana, umemnyima upendo wako na umemkosesha manufaa ambayo kwayo, maisha yake yangeokolewa.
191. Kwa hiyo, Mungu huwaita wauaji, watu wote wasioshauri na wasiotoa msaada kwa watu wenye haja na hatari ya mwili na uhai. Atawatolea hukumu ya kutisha siku ya mwisho jinsi Kristo mwenyewe atangazavyo akisema: “Nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.1443 Yaani: “Mngeniacha mimi na walio wangu kufa kwa njaa, kiu, na baridi. Mngetuacha turaruliwe na wanyama wakali, tuozee kifungoni, au tuangamie katika shida.”
192. Kuna lingine lipi isipokuwa kuwasuta watu kama hao kama wauaji na mbwa wa mawindoni? Hata hivyo, ijapokuwa hujayafanya haya yote, umemwacha jirani yako ateseke na aangamie katika dhiki zake. Ni sawa na kumwona mtu akitapatapa katika maji yenye kina kirefu au aliyeanguka motoni na ningeweza kumnyoshea mkono nimvute na kumwokoa, lakini nikatae kumfanyia hivyo. Ningeonekanaje machoni pa ulimwengu isipokuwa kuwa mwuaji na mhalifu?
193. Kwa hiyo, lengo halisi la Mungu ni kwamba, tusimruhusu mtu yeyote aumie bali tumwonyeshe kila mtu wema na upendo wote. 194. Jinsi nilivyosema, wema huu umeelekezwa tu kwa walio maadui zetu. Kwa maana, kuwaonyesha marafiki zetu wema ni maadili ya ukafiri jinsi asemavyo Kristo katika Mt. 5:4647.
195. Hapa tena tuna Neno la Mungu ambalo kwalo, anataka kututia moyo na kutuhimiza tuyatende matendo ya haki, bora, na ya kukwezwa kama vile upole, uvumilivu, na kwa ufupi, upendo, na huruma kwa maadui zetu. Daima anatukumbusha tutafakari kuhusu Amri ya Kwanza, kwamba, yeye ni Mungu wetu, yaani, kwamba, anataka kututia nguvu, kutusaidia, na kutulinda ili aweze
1443 Mt. 25:42-43
kuizima tamaa yetu ya kulipiza kisasi.
196. Iwapo haya yangezingatiwa katika mawazo yetu, mikononi mwetu tungekuwa na matendo mema mengi. 197. Lakini haya yangekuwa mahubiri kwa wamonaki/watawa wa kiume, yangeidhalilisha asasi ya kiroho na kuuingilia utakatifu wa Wakerthusi. Kiutendaji, yangehesabiwa kuwa sawa na kuyakataza matendo yao mema na kuzipiga marufuku nyumba za watawa. Kwa maana, katika mafundisho haya, maisha ya kawaida ya Wakristo yangehesabiwa kuistahili hali iyo hiyo na hata zaidi. Kila mtu angeona jinsi wamonaki/watawa wa kiume wanavyoifanyia mzaha na kuipotosha dunia kwa onyesho la utakatifu wa uongo na unafiki, wakati wameitupilia mbali amri hii na nyinginezo. Wanazihesabu kuwa si za lazima, kana kwamba, hazikuwa amri bali mashauri1444 tu. Licha ya hayo, bila aibu, wamejivunia na kujigambia wito wao wa kinafiki na matendo kama “maisha makamilifu kushinda yote,” ili wapate kuishi maisha mazuri na rahisi bila msalaba na bila mateso. Kwa sababu hiyo, waliyakimbilia makao ya watawa ili wasilazimike kuteseka kwa ajili ya baya lolote kutoka kwa yeyote au kumfanyia yeyote jema lolote. 198. Fahamu kwamba, haya ndiyo matendo yaliyoagizwa na Neno la Mungu, matendo yaliyo ya kweli, matakatifu, na ya kimungu, ambayo kwayo, Yeye huyafurahia na malaika wake wote. Kinyume chake, utakatifu wote wa binadamu ni uvundo mbaya sana na uchafu unaostahili ghadhabu na laana.
AMRI YA SITA
199. “Usizini”
200. Amri zinazofuatia ni rahisi kueleweka kutokana na zile zilizotangulia. Zote zinatufundisha tusiwafanyie majirani zetu madhara yoyote. Zimepangwa kwa njia ya kupendeza sana. Kwanza, zinaishughulikia nafsi ya mtu mwenyewe. Kisha, zinaelekea kwa mtu aliye karibu sana naye, yaani, mke wake, aliye mpenzi wake kuliko wote, ambaye ni mwili na damu moja naye. Hivyo, tusimfanyie dhara kubwa zaidi katika miliki yoyote ambayo ni yake. Hivyo basi, umekatazwa hapa wazi usimfedheheshe mke wake. 201. Uzinzi umetajwa hasa, kwa sababu miongoni mwa Wayahudi, kila mmoja aliagizwa na kuamriwa aoe. Vijana walioana wakiwa wadogo ilivyowezekana. Hivyo, ubikira ulikuwa na thamani 1444 Mafundisho ya zamani ya Kanisa la Roma yalitofautisha baina ya ‘praecepta’ (amri) na ‘consilia evangelica’ (mashauri). Kulingana na mafundisho haya, amri zinawahusu watu wote kikamilifu ilihali mashauri yanawahusu watu maalumu waliostahili neema kwa njia ya kuyafuata mashauri kama useja, umaskini, utiifu maalumu n.k. Luther aliyahakiki maoni haya sana kwa sababu mashauri yalibadilika katika madaraja ya wamonaki/watawala wakuu na kuwa amri halisi nazo amri halisi za Mungu zilibadilika na kuwa mashauri tu.
430
ndogo. Isitoshe, umalaya na uchafu wa kimwili havikuvumiliwa kama sasa katika jamii hiyo. Kwa hiyo, uasherati ulikuwa uhalifu wa kawaida miongoni mwao.
202. Kwa kuwa miongoni mwetu kuna desturi mbalimbali za aibu na takataka halisi za maovu yote na uchafu, amri hii inahusishwa na kila aina ya uzinzi. Siyo kwamba, tendo la nje tu limekatazwa, bali kila aina ya sababu, nia, kishawishi, na njia yoyote. Hivyo, moyo, midomo, na mwili wako mzima uwe safi na usitoe nafasi yoyote ya msaada ama ushawishi wa uasherati. 203. Licha ya hayo, unapaswa umtetee, umlinde, na kumwokoa jirani yako kila mara anapokuwa katika hatari au shida. Kwa upande mwingine, umsaidie na umshauri ili apate kuidumisha heshima yake. 204. Unapopuuza kufanya hivyo, japo ungelizuia ovu, au unapoliachilia kana kwamba, halikuhusu wewe, basi, hakika unakuwa mwenye hatia sawasawa na aliyelitenda tendo lenyewe. 205. Kwa ufupi, kila mmoja anahitajika kuishi kwa unyofu na amsaidie jirani yake kuishi kama yeye. Hivyo, kwa amri hii, Mungu anataka kumlinda kila mume na mke ili asiingiliwe na yeyote.
206. Lakini kwa kuwa amri hii inawahusu hasa watu wanaoishi katika asasi ya ndoa1445 na kuna nafasi ya kuizungumzia, acheni kwanza tutambue kwa makini jinsi Mungu anavyoyasifu na kuyatukuza sana maisha ya unyumba kwa kuyaidhinisha na kuyalinda. Aliyaidhinisha tayari katika Amri ya Nne: “Waheshimu baba yako na mama yako.” Lakini–jinsi nilivyokwisha kusema hapa– ameihifadhi na kuilinda. 207. Kwa hiyo, anatutaka pia tuiheshimu, tuidumishe, na kuitunza kama asasi takatifu na iliyobarikiwa. Ni muhimu kwamba, aliianzisha kama asasi ya kwanza miongoni mwa nyingine zote. Isitoshe, alimwumba mume na mke kwa nia tofauti–jinsi ilivyo wazi–si kwa mwenendo mchafu, bali wawe waaminifu mmoja kwa mwenzake, waneemeke, wawazae watoto, wawatunze, na wawalee kwa utukufu wa Mungu. 208. Kwa sababu hiyo, Mungu ameibariki sana asasi hii kuliko zingine zote. Licha ya hayo, ameikirimia na kuijalia kila kitu duniani ili iweze kuyakimu mahitaji yote vya kutosha kabisa. Maisha ya ndoa si utani wala mzaha bali ni asasi1446 njema mno na ambayo Mungu mwenyewe anaipa hadhi kubwa. Ni jambo muhimu kabisa kwake kwamba, watu wafunzwe kuihudumia dunia na kuyaendeleza maarifa ya Mungu, maisha ya uchaji, mema yote, na kupambana na uovu na Ibilisi.
209. Kwa hiyo, nimefundisha kila mara kwamba, cheo hiki cha ndoa kisidharauliwe wala kisionewe aibu jinsi dunia pofu na mapadre wa uongo wanavyofanya. Badala yake, kiangaliwe katika Neno la Mungu ambalo kwalo,
1445 Kijerumani: ‘Ehestand.’ 1446 Kijerumani: ‘Ehestand,’ Kilatini: ‘Ordo matrimonii.’
kimepambwa na kutakaswa. Hii siyo asasi inayowekwa katika kiwango sawa na zingine. Inazitangulia na kuzishinda zote, iwe ile ya Kaisari, watawala, maaskofu au yeyote yule. Kwa kuwa vyeo vya Kanisa/kiroho na vya raia ni muhimu, wanaovishikilia hawana budi kunyenyekea na kuwaruhusu watu wote washiriki katika asasi hii ya ndoa jinsi tutakavyosikia. 210. Hii siyo asasi ya kipekee lakini ni nzuri zaidi kuliko zote, inaenea miongoni mwa Wakristo wote, na inapatikana na kuenea ulimwenguni kote.
211. Pili, kumbuka pia kwamba, ni asasi ya heshima, ya lazima, na iliyoamriwa kwa mkazo mkubwa na Mungu. Kwa jumla, katika hali zote, wanaume kwa wanawake waliumbwa kwa madhumuni hayo, yaani, lazima washiriki asasi hii. Bado kuna wengine kadhaa wasioruhusiwa - japo ni wachache-ambao Mungu amewaacha hasa wasijiingize katika maisha ya ndoa. Baadhi ambao hawafai kwa maisha ya ndoa na wengine ambao amewapa kipaji cha juu sana kinachopita uweza wa binadamu amewaachilia ili waweze kuwa nje ya asasi hii. 212. Mahali, ambapo asili inatawala, jinsi ilivyoumbwa na Mungu, haiwezekani kuishi bila kuoa. Maana mwili na damu vinabaki kuwa mwili na damu, na mielekeo ya asili na vichocheo vina njia zao bila kizuizi, jinsi uchunguzi na uzoefu wa kila mtu anavyoshuhudia. Basi, ili iwe rahisi zaidi kwa mtu kuepukana na zinaa kwa kiasi fulani, Mungu ameianzisha ndoa ili kila mmoja awe na sehemu yake aliyotengewa na aridhike nayo ingawa hapa pia, neema ya Mungu inahitajika ili moyo uwe safi.
213. Kutokana na haya, unaona jinsi kundi la akina papa, mapadre, wamonaki/ watawa wa kiume, na manoni/watawa wa kike wanavyoupinga mpango na amri ya Mungu wanapoidharau na kuikataza ndoa, wanapojisifu na kuapa kwamba, wataudumisha ubikira/utakatifu wa maisha daima. Licha ya hayo, wanaudanganya umma kwa maneno ya uongo na sura ya ulaghai. 214. Kwa maana, hakuna hata mtu mmoja aliye na upendo haba na mielekeo ya ubikira/utakatifu kama ambao, kwa ajili ya utakatifu mkubwa, wanaiepuka ndoa, na ama wanatumbukia katika uzinzi wazi na usiokuwa na aibu, ama wanayafanya hata yaliyo mabaya zaidi kwa siri, mambo maovu sana kuweza kutajwa, jinsi yalivyothibitishwa kikamilifu mno, kwa bahati mbaya. 215. Kwa ufupi, ingawa waliepukana na tendo hilo, bado mioyo yao ilijaa mawazo ya uzinzi na tamaa mbovu kiasi kwamba, wanaugua uchu mkali sana mfululizo na mateso ya siri, ambayo yanaweza kuepukwa katika maisha ya ndoa. 216. Hivyo basi, viapo vyote vya usafi vya kuyaepuka maisha ya ndoa vinalaaniwa na kufutiliwa mbali na amri hii. Naam, ruhusa huru inatolewa, hata amri inatolewa kuhusu dhamiri zote duni zilizodanganywa na viapo vyao vya kimonaki kuziacha hali za uzinzi na kuyaingia katika maisha ya ndoa. Hata hivyo, ingawa maisha ya kimonaki yangekuwa ya kimungu, hawangekuwa na
uwezo kuudumisha uongofu, na wakibakia humo, itawabidi waivunje amri hii zaidi na zaidi.
217. Sasa, ninayasema mambo haya ili vijana wetu waweze kuongozwa kuyapenda maisha ya ndoa na kujua kwamba, ni asasi iliyobarikiwa na inayompendeza Mungu. Hivyo, maisha ya ndoa yatarudishiwa heshima yake halisi wakati upasao na kutakuwa na upungufu wa matendo machafu, mapotovu, na mwenendo mbaya ambavyo sasa vimeleta vurugu duniani kote katika umalaya wazi na maovu mengine ya aibu yatokanayo na kuyadharau maisha ya ndoa. 218. Kwa hiyo, ni wajibu wa wazazi na watawala kuhakikisha kwamba, vijana wetu wanaelekezwa kuwa na nidhamu, kuwaheshimu watawala, na watakapofikia utu uzima, wawaandalie ndoa katika kumcha Mungu na kwa heshima. Naye Mungu atawaongezea baraka na neema ili binadamu wawe na furaha na shangwe katika maisha yao ya ndoa.
219. Basi, katika hitimisho, niache niseme kwamba, amri hii inamtaka kila mmoja aishi kwa uadilifu katika mawazo, maneno, na matendo katika hali yake halisi, yaani, katika asasi ya ndoa. Isitoshe, kila mmoja ampende na kumheshimu mume au mke wake aliyepewa na Mungu. Kwa maana, usafi wa mume na mke unashinda vitu vyote vya lazima na kwamba, inawapasa mume na mke waishi pamoja kwa kila njia, wapendane na kupatana, kila mmoja akimtunza mwenzake kutoka moyoni na kwa uaminifu wote. 220. Hii ndiyo njia ya kimsingi mojawapo inayoufanya usafi uvutie na utamanike. Katika hali kama hizo, uongofu unafuatia bila amri yoyote. Hii ndiyo sababu, kwa juhudi kubwa, Mt. Paulo anawashauri mume na mke wapendane na kuheshimiana.1447 Hapa una tendo jingine jema la thamani. Naam, una matendo mengi makubwa unayoweza kujivunia kwa furaha dhidi ya “asasi zote za kiroho” zinazochaguliwa bila Neno na amri ya Mungu.
AMRI YA SABA
222. “Usiibe”
223. Baada ya nafsi yetu wenyewe, mwenzi wetu, mali yetu ya dunia hii ni ya manufaa makubwa sana kwetu. Hii nayo Mungu anataka ilindwe. Ametukataza tusimnyang’anye au kuzidokoa1448 mali za jirani yetu. 224. Maana kuiba siyo jambo jingine isipokuwa kujipatia mali ya mwingine kwa njia haramu. Kwa ufupi, hii ni pamoja na kumpunja jirani yetu katika mapatano yoyote yanayomletea hasara. Wizi ni ubaya wa kawaida unaotapakaa lakini watu wengi hawaujali sana
1447 Efe. 5:25-33; Kol. 3:18-19 1448 Dokoa, chukua kidogo kidogo kwa kuiba.
na tatizo lote linashindikana sasa. Iwapo wote ambao ni wezi, japo hawakubali kuwa, wangenyongwa kwa viunzi1449 vya kunyongea, karibuni dunia haingekuwa na watu, na kungekuwa na upungufu wa chakari na wa viunzi vya kuwanyongea. Jinsi nilivyokwisha kusema tayari ni kuwa, mtu huiba anapochukua kitu kutoka kwa sefu ya mtu, mfuko wake, anapompunja jirani yake sokoni, katika duka la vyakula, duka la nyama, sela1450 la mvinyo na bia, kiwandani, na kwa ufupi, popote ambapo biashara hufanyiwa na pesa hubadilishwa kwa mazao au kazi.
225. Acheni tuyafanye dhahiri zaidi ili umma uweze kuona jinsi tulivyo waaminifu. Kwa mfano, iwapo mtwana au mjakazi si mwaminifu katika kazi zake za nyumbani na huufanya uharibifu au huuruhusu uharibifu utokee ambapo ungeweza kuepukika. Au iwapo, kwa ajili ya uvivu, kutojali, au ubaya, mtumishi anaviharibu na kuvipuuza vitu hata mwajiri wake wa kiume au wa kike achukizwe na kukerwa. Haya yanapofanywa makusudi–kwa maana siyazungumzii yasiyonuiwa au yasiyopangwa–mtumishi anaweza kumwibia mwajiri wake sarafu za dhahabu1451 thelathini au arobaini au zaidi kwa mwaka. Kama mwizi angekichukua kiasi kama hicho angenyongwa kwa kamba ya kunyongea, lakini mtumishi anaweza hata kuwa mwasi na mjeuri na kumtaka yeyote athubutu kumwita mwizi!
226. Jambo lilo hilo lazima lisemwe kuhusu mafundi, wafanyakazi, na vibarua. Hawa wanatenda kazi kwa ujeuri na hawajui kamwe njia zinazofaa za kuwatoza watu viwango vya juu kupita kiasi na bado hawajali na hawaaminiki katika kazi zao. Hawa wote ni wabaya zaidi kuliko wezi wa kunyemelea, ambao tunaweza kuwazuia kwa kufuli na komeo, au tukiweza kuwakamata tunaweza kuwaadhibu wasilirudie kosa lao. Lakini kwa wengine, hakuna anayeweza kuwalinda, hata hakuna anayeweza kuwatazama kwa ukali au kuwashtaki kwa ajili ya wizi. Badala yake, mtu huona ni afadhali azipoteze mara kumi pesa alizo nazo katika mkoba wake. Kwa maana, hawa ndio majirani zangu, marafiki zangu wema, watumishi wangu wenyewe, ambao kutoka kwao ninayatazamia mema. Hata hivyo, wao ni wa kwanza kunighilibu.
227. Licha ya hayo, udanganyifu uo huo huendelea kwa nguvu zote sokoni na katika shughuli za kila siku. Mtu mmoja humdanganya mwingine wazi kabisa kwa bidhaa zenye kasoro, vipimo vya uongo, mizani za udanganyifu, sarafu mbaya, na humpunja kwa kila hila za siri, desturi za uerevu, na shughuli za ujanja. Tena, mtu humpunja mwingine katika biashara, humwibia kwa ujanja, humchuna, na
1449 Kiunzi, mwimo wa mlango.
1450 Sela, ghala lililo chini ya ardhi.
1451 Kijerumani: ‘Gulden’ kutokana na ‘Gold,’ yaani, dhahabu.
434
kumtesa kabisa makusudi. Nani awezaye kuyaelezea au kuyadhania haya yote? 228. Kwa ufupi, wizi ndiyo shughuli ya kawaida sana na shirika kubwa kuliko yote duniani. Tukimchunguza mwanadamu katika hali zake zote, yeye si lolote isipokuwa banda kubwa na pana lililojaa wezi wakubwa.
229. Watu hawa wanaitwa wadanganyifu waungwana au wafanyakazi wakubwa.1452 Mbali na kuwa wachokonozi1453 wa makufuli na wezi wa kunyemelea wanaovimimina visanduku vya pesa, wanaketi katika viti maofisini, wanaitwa mabwana wakubwa, wananchi waheshimiwa, wanaudai wema, na kumbe, wananyang’anya na kuiba kwa njia ya kuuonyesha uhalali mkubwa wa sheria.
230. Naam, hapa tunaweza kunyamaza kuhusu aina nyingi za wezi wadogowadogo, ili tuyaanzishe mashambulizi dhidi ya wezi wakuu, wezi mashuhuri na wenye nguvu, wanaoshirikiana na mabwana na watawala na kuupunja mji mmoja, miwili, na Ujerumani nzima kila siku. Naam, ingekuwaje kwa kichwa na mlinzi mkuu wa wezi wote, Kiti Kitakatifu huko Roma na wafuasi wake wote, ambacho kimepunja na kuziiba hazina zote za dunia nzima na kuziweka hadi sasa?
231. Kwa ufupi, hii ndiyo hali ya dunia. Wale wanaoweza kuiba na kunyang’anya wazi wako salama na huru, hawasumbuliwi na yeyote, na hata wanadai heshima kutoka kwa binadamu. Wakati uo huo, wezi wadogowadogo wa kunyemelea, waliolitenda kosa moja, lazima waibebe aibu na adhabu ili kuwafanya wengine wawe wema na wenye heshima. Lakini hawa nao wangeambiwa kwamba, machoni pa Mungu, wao ni wezi wakubwa kuliko wote, na kwamba, atawaadhibu kulingana na wanavyostahili.
232. Amri hii ni yenye athari nyingi jinsi tumekwisha kuonyesha. Kwa hiyo, ni lazima kuisisitiza na kuielezea kwa umma ili ulafi wao uweze kuzuiwa na kwamba, mbele ya macho yao, waweze kuiona daima na kwa dhati hasira na ulipizaji kisasi wa Mungu. Maana, ni lazima kulihubiri hili, siyo kwa Wakristo, bali hasa kwa wajanja na waovu, ijapokuwa ingestahili zaidi kama jaji, au chakari1454 angeyafanya mahubiri hayo. 233. Mwache kila mmoja ajue kwamba, ni wajibu wake kutomwumiza jirani yake, kutompunja, au kutomdanganya kwa shughuli yoyote isiyokuwa ya kweli au ya hila asije akaipata ghadhabu ya Mungu. Licha ya hilo, anawajibika kuilinda mali ya jirani yake kwa uaminifu na kuyazidisha manufaa yake, hasa anapoupokea ujira kwa huduma kama hizo.
1452 Kijerumani: ‘Stuhlräuber.’
1453 “Uchokonozi” – hali ya kukitia kitu chenye ncha tunduni ili kukitoa kilichomo ndani. 1454 Luther, ‘Meister Hans,’ (Fundi Hans), yaani, chakari/mnyongaji.
234. Mtu anayeidharau amri hii makusudi, anaweza kumtoroka na kumwepuka kabisa chakari lakini hataiepuka hasira na adhabu ya Mungu. Ingawa ataiandama njia yake ya uasi na kiburi kwa muda mrefu, bado atabakia kuwa mzururaji na mwombaji na atakumbana na aina zote za matata na balaa. 235. Sasa wewe mtumishi unapaswa kuzitunza mali za bwana au bibi yako wanaokuwezesha ujipatie riziki. Lakini unaifuata njia yako mwenyewe, unajichukulia ujira wako kama mwizi, na hata unatazamia kuheshimiwa kama malodi. Wengi wenu pia ni wajeuri kwa mabwana na mabibi zenu na hampendi kuwafanyia hisani na huduma ya kuwalinda wasipate hasara. Lakini tazama mnachokifaidi. 236. Unapotajirika mwenyewe, unapokuwa na nyumba yako mwenyewe ambayo Mungu atakuwezesha kuipata kwa njia haramu, siku itakuja ya kuitoa hesabu na ya mapatilizo. Maana, kwa kila senti ambayo umeichukua, na kwa kila sarafu ambayo umeiharibu itakubidi ulipe mara thelathini.
237. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mafundi na kwa vibarua ambao, kutoka kwao, tunalazimika kuteseka kwa ajili ya ujeuri kama huo usiovumilika. Wanajifanya kana kwamba, wao walikuwa mabwana wa mali za wengine na wana haki kwa lolote wanalolidai. Waacheni tu waendelee kujitwalia mali ya watu kwa ujasiri na ujanja mwingi wanavyoweza. 238. Mungu hataisahau amri yake. Atawalipa wanalolistahili. Atawatundika wao siyo katika kiunzi cha mti mbichi, bali katika kiunzi cha mti mkavu.1455 Hawatastawi wala kulifaidi lolote katika maisha yao yote. 239. Naam, kama serikali yetu ingeongozwa vizuri, ujeuri wa namna hii ungezuiwa haraka. Kwa mfano, Warumi wa kale waliwashika kikosini mara moja wakosaji wa jinsi hiyo ili wengine wapate maonyo.
240. Ajali iyo hiyo itawapata wanaoligeuza soko huru la watu wote kuwa pango la nyama iliyooza na la wanyang’anyi. Maskini wanapunjwa kila siku. Wanatwikwa mizigo mipya na bei za juu. Kila mmoja analitumia soko visivyo kwa njia yake makusudi, kwa majivuno, na kwa kiburi, kana kwamba, ilikuwa haki na faida yake kisheria kuyauza mazao yake kwa bei za juu apendavyo bila kukosolewa. 241. Tutasimama kando na kuwaacha watu wa jinsi hiyo waibe kwa ujanja, wapokonye, na walimbikize. 242. Lakini tutamtegemea Mungu ambaye hujichukulia mwenyewe mambo mikononi mwake. Baada ya wao kubania na kukwangua kwa muda mrefu, atawatangazia baraka ya aina hii: “Nafaka zako zitaharibikia ghalani, bia yako itaharibikia selani, na ng’ombe wako watafia zizini. Naam, ambapo umemdanganya au umempunja yeyote sarafu moja, malimbikizo yako yote yataangamizwa kwa kutu ili usiyafurahie kamwe.”
243. Naam, kila siku tuna ushuhuda wa moja kwa moja machoni petu 1455 Kukatwa kichwa ni kifo kikali kuliko kunyongwa.
kwamba, mali yoyote iliyopatikana kwa njia mbaya haitastawi. Ni watu wangapi wanakwangua na kukwaruza mchana na usiku na bado utajiri wao hauongezeki hata kwa sarafu moja. Japo wanajikusanyia malimbikizo makubwa, lazima watateseka kwa matata na balaa kiasi kwamba, kamwe hawataweza kuyafurahia au kuyapokezana kwa watoto wao. 244. Lakini kwa kuwa tunayapuuza haya na kujifanya kuwa hayatuhusu kamwe, Mungu lazima atuadhibu na atufundishe maadili kwa njia tofauti. Hutupatia dhiki moja baada ya nyingine au, hututumia kikosi cha askari. Katika saa moja, kinasafisha akiba na pochi zetu hadi sarafu ya mwisho. Kisha, kama shukrani yao, wanazichoma na kuziharibu nyumba na makao, wanayatenda maovu, na wanawaua mke na watoto.
245. Kwa ufupi, unavyozidi kuiba, kuwa na hakika kwamba, kiasi icho hicho kitaibwa kutoka kwako. Yeyote anayenyang’anya na kuvichukua vitu vya watu kwa nguvu na udanganyifu, lazima amvumilie mwingine mwenye tabia kama hiyo. Kwa maana, Mungu ni stadi hodari wa sanaa hii. Kwa kuwa kila mtu anamnyang’anya na kumwibia mwingine, anamwadhibu mwizi mmoja kwa kumtumia mwingine. La sivyo, hatungekuwa na viunzi na kamba za kutosha kuwanyongea?
246. Yeyote anayetaka kujifunza, mwache ajue kwamba, hii ni amri ya Mungu na haipaswi kufanyiwa utani kamwe. Mnaotudharau, mnaotupunja, mnaotuibia, na mnaotunyang’anya, tutawavumilia. Tutakivumilia kiburi chenu na kuwaonyesheni msamaha na huruma, jinsi Sala ya Bwana inavyofundisha. Wakati uo huo, wenye haki hawatapungukiwa na kitu na utajitesa mwenyewe zaidi kuliko wengine. Jihadhari unavyowafanyia maskini ambao ndio wengi sasa. 247. Iwapo, unakutana na mtu maskini hohehahe anayeishi maisha ya kijungujiko, unajifanya kana kwamba, kila mtu anaishi kwa hisani yako, unamchuna na kumkwaruza hadi kwenye mfupa, na unamfukuza kwa kiburi kikubwa badala ya kumsaidia. Ataondoka akiwa amedhalilishwa na akiwa mwenye huzuni, na kwa kuwa hana mwingine wa kumlalamikia, atalilia mbinguni. Jihadhari na hili, ninarudia, sawa na kujihadhari na Ibilisi mwenyewe! Upigaji kite na vilio vya mtu vya namna hiyo havitakuwa jambo la utani. Vitakuwa na athari kubwa mno kwako na kwa dunia nzima kuvihimili.1456 Kwa maana, vitamfikia Mungu anayezilinda nafsi maskini zenye huzuni, na hatakosa kuzilipia kisasi. Lakini ukilidharau na kulikataa hili, tazama ni nani umejiletea mwenyewe. Ukifanikiwa na kusitawi, unaweza kumwita Mungu na mimi waongo mbele ya dunia nzima.
248. Sasa tumetoa maonyo na ushawishi wa kutosha. Asiyelisikia au kuliamini hili anaweza kwenda njia yake mwenyewe hadi atakapojifunza kwa uzoefu. 1456 Himili, chukua yaliyo mazito/vumilia.
Lakini vijana wanahimizwa wawe macho na wasiufuate umma uliozeeka, na mpotovu. Badala yake, waikazie amri ya Mungu macho yao, ghadhabu na adhabu visije vikawapata pia. 249. Wajibu wetu ni kufundisha na kukaripia tu kwa njia ya Neno la Mungu. Kuuzuia uhalifu wazi ni wajibu wa watawala na mahakimu. Wanapaswa kuwa macho na kuwa na uthabiti wa kutosha kuanzisha na kudumisha amani katika maeneo yote ya biashara na uchumi ili maskini wasilemewe, wasidhulumiwe, na wasishtakiwe kwa ajili ya dhambi za watu wengine.
250. Yaliyosemwa yametosha kuhusu asili ya wizi. Hautapewa maana finyu1457 ila hauna budi kuhusishwa na mahusiano yetu yote na majirani zetu. Kwa jumla, jinsi tulivyofanya katika amri zilizotangulia: kwa upande mmoja, tunakatazwa kumwumiza jirani yetu au kumfanyia ubaya wowote kwa njia yoyote ile inayoweza kufikirika, iwe ni kuziharibu, kuzizuia, au kuziingilia miliki na mali zake. Hata hatupaswi kuidhinisha au kuruhusu jambo la namna hiyo. Badala yake, tulikinge na kulizuia. 251. Kwa upande mwingine, tumeamriwa kuyaendeleza na kuyazidisha manufaa ya jirani yetu, na akipungukiwa tumsaidie, tushiriki naye, na tuwakopeshe maadui na marafiki wote.
252. Yeyote atafutaye na atakaye matendo mema, ataipata nafasi nzuri hapa kuyafanya mambo yanayokubalika kwa ukunjufu na ya kumpendeza Mungu. Licha ya hayo, kwa neema, yeye huwapa baraka nyingi mno kwa ukarimu.
Tutalipwa kwa wingi kwa ajili ya msaada wote au huruma tunaomwonyesha jirani yetu, jinsi afundishavyo mfalme Sulemani katika Mithali 19:17 kwamba: “Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.” Hapa una Bwana tajiri. 253. Hakika anatosha kwa mahitaji yako na hatakuacha upungukiwe au ukikose kitu chochote. Hivyo, kwa dhamiri yenye furaha, unaweza kufurahia mara mia moja kuliko ambavyo ungevikusanya pamoja kwa ujanja, na kwa udhalimu. Yeyote asiyehitaji baraka hii, ataipata ghadhabu na balaa ya kutosha.
AMRI YA NANE
244. “Usimshuhudie jirani yako kwa uongo”
255. Mbali na mwili wako wenyewe, mke wako au mume wako, na mali yako ya duniani, una hazina moja yenye thamani kwako. Yaani, heshima yako na jina lako zuri, kwa maana, haivumiliki kuishi miongoni mwa watu katika aibu na madharau. Kwa hiyo, Mungu hapendi jirani yetu anyang’anywe sifa yake nzuri, 1457 Finyu, isiyokuwa pana.
438
heshima, tabia, pesa, na mali yake. Anamtaka kila mtu aidumishe heshima yake mbele ya mke wake, watoto, watumishi, na majirani. 256. Katika maana yake ya kwanza na sahili kabisa, jinsi maneno yanavyodhihirisha–“Usishuhudie kwa uongo”–amri hii inayafaa mahakama ya haki ya watu wote, ambapo mtu maskini na asiye na hatia anashtakiwa na kusingiziwa na mashahidi wa uongo na mwishowe anaadhibiwa mwilini, mali au heshima yake.
258. Tatizo hili linaelekea kutuhusu kidogo tu sasa, lakini miongoni mwa Wayahudi lilikuwa tatizo la kila mara. Taifa hilo lilikuwa na serikali nzuri mno yenye utaratibu. Hata sasa, ambapo kuna serikali ya namna hiyo, mifano ya dhambi ya namna hii bado inatokea. Sababu ni kwamba: ukweli wa mielekeo ya dunia ulivyo, ambapo mahakimu, meya, wakuu, au wengine wenye madaraka wanaketi kuhukumu, kila wakati tunaona kwamba, binadamu hawataki kumwudhi mtu yeyote mwenye hadhi. Badala yake, wanazungumza bila haki wakitaka kupata upendeleo, pesa, matarajio au urafiki. Hivyo, mtu maskini hudhulumiwa kwa lazima, hushindwa katika kesi yake na huteseka kwa adhabu. Ni adha ya kila mahali duniani kwamba, mara chache sana, watu waadilifu huyasimamia mahakama ya sheria. Kwa kila hali, hakimu anatakiwa kuwa mtu mwaminifu, mwenye haki, mwenye busara, mpole, jasiri, na asiyeogopa. Kadhalika, shahidi awe mtu asiyeogopa, na licha ya hilo, awe mtu mwenye haki.
259. Mwenye kusimamia haki kwa usawa katika kesi zote, mara nyingi huwakasirisha marafiki wazuri, jamaa yake, majirani, matajiri, na wenye nguvu ambao wana uwezo wa kumsaidia au kumwumiza. Hivyo, lazima awe kipofu sana, ayafunge macho na masikio yake kutokana na kila jambo, isipokuwa kwa ushahidi unaotolewa na autoe uamuzi wake inavyostahili.
260. Matumizi ya kwanza ya amri hii ni kwamba, kila mmoja amsaidie jirani yake kudumisha haki zake. Analazimika kutoziruhusu haki hizi kuzuiwa au kupotoshwa ila aziendeleze, azilinde kwa moyo mmoja, awe hakimu au shahidi, na ayaache matokeo yawe yatakavyokuwa.
261. Hapa tuna lengo kwa wanasheria wetu, toeni hukumu ya haki na usawa katika kila kesi. Wanapaswa kuiacha haki ibakie kuwa haki, wasiipotoshe, wasiifiche kwa hila, wasiligandamize lolote kwa sababu ya pesa, mali, heshima, au uwezo wa mtu yeyote. Hiki ndicho kipengele kimoja cha amri hii, na maana yake ya wazi kuliko zote, inapohusishwa na yote yanayotokea mahakamani.
262. Yanayofuata ni mapana sana yanapotumiwa katika mamlaka au utawala wa kiroho. Hapa pia, kila mmoja anamshuhudia jirani yake kwa uongo. Popote ambapo pana wahubiri na Wakristo wachaji, inawabidi wavumilie ulimwengu
439
unapowata wazushi, wapotovu, na wenye kuchochea uasi dhidi ya serikali na walaghai waliolaaniwa. Licha ya hayo, Neno la Mungu halina budi kuona mateso ya aibu kubwa sana, yenye chuki, na kufuru. Neno hili linapingwa, linapotoshwa, linatumiwa vibaya, na linatafsiriwa visivyo. Lakini liache hili lipite. Ni asili ya ulimwengu kulaani na kuitesa kweli pamoja na watoto wa Mungu na bado hulidhukurii hili kuwa dhambi.
263. Kipengele cha tatu cha amri hii kinatuhusu sisi sote. Inazikataza dhambi zote za ulimi ambazo kwazo, tungeweza kumwumiza au kumwudhi jirani yetu. Ushuhuda wa uongo ulio wazi, ni kazi ya ulimi. Mungu analikataza kila tendo linalomwudhi jirani. 264. Hili linawahusu wahubiri wa uongo, mafundisho yao mabovu na kufuru, mahakimu na mashahidi wa uongo, tabia zao mbaya mahakamani, uongo, na masengenyo yao ya nje ya mahakama. Inahusu hasa dhambi inayochukiza, ya aibu, ya kuchongea au kukashifu ambayo kwayo, Ibilisi huvivizia. Mengi yanaweza kusemwa kuhusu hili. Ni dhambi ya kawaida, ya asili, ya binadamu kwamba, kila mmoja angependelea zaidi kusikia maovu kuliko mema kuhusu jirani yake. Hapa, japo sisi ni waovu, hatuwezi kuvumilia kusikia uovu unaotuhusu. Tunataka sifa nzuri kama dhahabu kutoka kwa dunia yote. Hata hivyo, hatuwezi kuvumilia kusikia mazuri kabisa yakisemwa kuhusu wengine.
265. Basi, ili kuliepuka ovu hili, inatupasa kukumbuka kwamba, hakuna aliye na haki ya kumhukumu na kumkemea jirani yake hadharani, hata kama ameiona dhambi aliyoifanya, isipokuwa kama amepewa mamlaka ya kuhukumu na kukemea.
266. Kuna tofauti kubwa kati ya kuihukumu dhambi na kuwa na ujuzi wa dhambi. Unaweza kuijua dhambi, lakini huwezi kuihukumu. Ninaweza kuona na kusikia kuwa jirani yangu hufanya dhambi, lakini sina agizo lolote la kulifanya jambo hili liwe chanzo cha mazungumzo. Nikilishika na kulikatia shauri, nitaanguka katika dhambi kubwa kuliko yake. Unapoupata utambuzi wa dhambi, lifanye tu sikio lako kuwa kaburi na uizike hadi utakapoteuliwa kuwa hakimu na kupewa mamlaka ya kutoa adhabu kwa mujibu wa wajibu wako.
267. Hao wasioridhika kujua tu bali hukimbilia kuhukumu wanaitwa wachochezi. Wakijifunza kidogo kuhusu umbeya wao, wanausambaza hadi kila pembe, wanauona utamu, na kufurahia kama nguruwe wanaojiviringisha matopeni na kuchimba humo kwa pua zao. 268. Hili si lingine isipokuwa kumnyang’anya Mungu hukumu na mamlaka yake, na kuitamka hukumu na adhabu kali kuliko zote. Kwa maana, hukumu kali kuliko zote ambayo hakimu anaweza kuitamka
ni kumwita mtu mwizi, muuaji, au haini n.k. Basi, yeyote anayediriki kumshtaki jirani yake, hujichukulia madaraka yafananayo na ya Kaisari na mahakimu wote. Japo huuchomoi upanga, unautumia ulimi wako wenye sumu kumfedhehesha na kumwumiza jirani yako.
269. Kwa hiyo, Mungu anakukataza kusema maovu kuhusu mwingine hata kama unajua hakika kwamba, amekosea. Licha ya hayo, ni vibaya zaidi ya katazo hili iwapo huna hakika isipokuwa umepata uvumi tu. Lakini ukisema: “Kwa nini nisizungumze iwapo ni ukweli?” 270. Ninajibu: “Kwa nini usiulete ukweli huo mbele ya hakimu wa kawaida?” “Ee, siwezi kuthibitisha hadharani. Ninaweza kuitwa mwongo na kufukuzwa kwa aibu.” Je, sasa unaweza kuishuku hatari? Iwapo hujiamini kuutoa ushahidi wako mbele ya mamlaka yaliyo halali, basi, uzuie ulimi wako na unyamaze. Jiwekee ujuzi wako mwenyewe na usiutoe kwa wengine. Maana, unapozitoa habari usizoweza kuzithibitisha, ingawa ni za kweli, unaonekana kuwa mwongo. Licha ya hilo, unafanya hivyo kama mjanja, maana hakuna mtu anayestahili kunyang’anywa heshima na jina lake zuri isipokuwa kwanza, haya yawe yameondolewa kutoka kwake hadharani.
271. Kila maarifa yasiyoweza kuthibitishwa vya kutosha ni ushahidi wa uongo. 272. Yeyote asidai mbele ya umma, kama kweli, lile ambalo halithibitishwi hadharani. Kwa ufupi, lililo siri linapasa kubakia kuwa siri au angalau, likemewe faraghani jinsi tutakavyosikia baadaye. 273. Hivyo, ukikumbana na mtu mwenye ulimi usiofaa, anayepiga domo/mwenye umbeya na anayemsingizia mwingine, mkemee mara moja ana kwa ana na mfanye atahayari kwa aibu. Hivyo, utawanyamazisha wengi ambao wangemwingiza mtu maskini katika aibu ambayo kwayo, hangeweza kujiondoa mwenyewe. Kwa maana, heshima na jina jema vinaweza kuondolewa kwa urahisi, lakini si rahisi kurudishwa.
274. Hivyo, unaona kwamba, tunakatazwa kabisa kusema maovu kuhusu jirani yetu. Hata hivyo, ipo tofauti kuwahusu mahakimu, wahubiri, na wazazi, kwa maana inatupasa tuifafanue amri hii kwa njia ambayo italifanya ovu liadhibiwe. Tumekwisha kuona kwamba, Amri ya Tano inatukataza tusimwumize mtu mwilini isipokuwa mnyongaji/chakari. Kulingana na wajibu wake, hamtendei jirani yake wema ila madhara na ovu tu. Hata hivyo, hafanyi dhambi dhidi ya amri ya Mungu, kwa maana Mungu ameianzisha huduma hiyo kwa hiari yake. Jinsi anavyoonya katika Amri ya Tano, Yeye mwenyewe amejiwekea haki ya kuitoa adhabu. Hali kadhalika, katika nafsi yake mwenyewe, hakuna ambaye ana haki ya kumhukumu na kumlaani mtu yeyote. Hata hivyo, ambao wana wajibu wa kufanya hivyo wakishindwa, hufanya dhambi sawasawa na wanaojichukulia sheria mikononi mwao bila agizo kama hilo. 275. Lazima hii inamtaka mtu
kuuripoti uovu, kuyatoa mashtaka, kuthibitisha, kuchunguza, na kushuhudia. Haitofautiani na daktari amponyaye mgonjwa. Wakati mwingine hulazimika kumchunguza na hata kumgusa sehemu zake za siri. Vivyo hivyo, serikali, wazazi, ndugu, madada, na marafiki wa karibu wanawajibika, mmoja kwa mwenzake, kuyakemea maovu inapokuwa lazima na kwa manufaa ya anayehusika.
276. Lakini njia bora ya kulishughulikia suala hili ingekuwa ni kuuchunga utaratibu uliowekwa na Injili katika Mt. 18:15 ambapo Kristo anasema: “Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu.”1458 Hapa, una kanuni bora, ya thamani, na ya kuutawala ulimi unaostahili kutambuliwa kwa uangalifu iwapo tutayaepuka haya matumizi mabaya ya kuchukiza. Basi, liache hili liwe sheria yako kwamba, hutakuwa mwepesi kueneza kashfa na umbeya juu ya jirani yako ila umwonye kwa siri ili aweze kujirekebisha. Vivyo hivyo, mtu yeyote akikunong’onezea kuhusu alililofanya mtu huyu au yule, mfundishe. Iwapo aliliona kosa, mwambie aende mwenyewe na kumkemea mtu huyo, la sivyo, anyamaze.
277. Unaweza kujifunza somo hili kutokana na usimamizi wa kaya wa kila siku. Mwenye nyumba anapomwona mtumishi ameshindwa kuutekeleza wajibu wake, anamkabili mwenyewe. Akiwa mjinga kiasi cha kumwacha mtumishi nyumbani na kwenda mitaani kunung’unika kwa majirani, bila shaka angeambiwa: “Mjinga we! Hilo halituhusu. Kwa nini usimwambie mwenyewe?”
280. Hilo lingekuwa jambo la udugu la kusema, kwa kuwa uovu ungesahihishwa na heshima ya jirani ingedumishwa. Jinsi Kristo mwenyewe asemavyo katika aya iyo hiyo: “Akikusikia, umempata nduguyo.” Hivyo, utakuwa umeifanya kazi kubwa na nzuri sana. Unafikiri ni jambo lisilokuwa na thamani kumpata ndugu? Waacheni wamonaki/watawa wa kiume wote na madaraja matakatifu yote yajitokeze na kazi zao zote zilizorundikwa, na uone kama wataweza kujigamba kwamba, wamempata ndugu mmoja!
279. Kristo anaendelea kufundisha katika (Mt.18:16): “Kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.” Hivyo, mtu anayehusika akabiliwe badala ya kusengenywa wakati hayuko. 280. Basi, kama hili halitasaidia, lilete suala hilo mbele ya hadhara, mbele ya mahakama ya serikali, au mbele ya Kanisa. Na hapo husimami peke yako. Una mashahidi utakaowatumia kumtia mwenye makosa hatiani na ambao hakimu atatumia ushuhuda wao kama msingi wa uamuzi wake na hukumu. Huu ndio utaratibu bora wa kumzuia na kumrudi mtu mwovu. 281. Lakini ukimsengenya mtu katika kila pembe na kuuchimbuachimbua uchafu 1458 Maandiko ya Luther: Mt. 19
442
wake, hakuna mtu atakayerekebishwa. Licha ya hayo, unapoitwa kuwa shahidi, inawezekana ukane kwamba, hukulisema lolote. 282. Ingefaa mchezo wa wambeya kama hao uharibiwe, kama onyo kwa wengine. Iwapo unaushughulikia ustawi wa jirani yako au kutokana na upendo wa kweli, hutamnyemelea kwa siri ukiiepuka nuru ya mchana.
284. Haya yote yanahusu dhambi za siri. Lakini dhambi ikionekana hadharani kiasi kwamba, hakimu na dunia nzima wanaijua, bila dhambi, unaweza kumwepuka na kujitenga na mtu huyo kama aliyejiletea fedheha, na unaweza kutoa ushuhuda hadharani juu yake. Kwa maana, jambo linapojulikana kwa kila mtu, haiwezekani kuwa na suala la kashfa, utovu wa haki, au ushuhuda wa uongo. Kwa mfano, tunamlaumu Papa na mafundisho yake sasa, ambayo yamekuwa wazi vitabuni, na yameenezwa kwa kelele sana duniani kote. Ambapo dhambi ni wazi, adhabu inastahili kuwa wazi ili kila mmoja aweze kujua jinsi ya kujikinga dhidi yake.
285. Sasa tuna muhtasari na dutu ya amri hii. Hakuna yeyote atakayemwumiza jirani yake, kwa ulimi wake, awe rafiki au adui. Hakuna atakayemsengenya, iwe kwa ukweli au kwa uongo, isipokuwa hayo yafanywe na mamlaka husika au kwa manufaa yake. Mtu autumie ulimi wake kuyasema mema tu kuhusu kila mtu, kuzisetiri dhambi na udhaifu wa jirani yake, kuusamehe, kuufunika, na kuuficha kwa heshima yake mwenyewe. 286. Sababu yetu kubwa ya kufanya hivyo lazima iwe ile iliyodokezewa na Kristo katika Injili, na ambamo anatutaka tuzitimize amri zote kuhusu jirani yetu: “Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo” (Mt. 7:12).
287. Hata asili hutufundisha lilo hilo katika miili yetu yenyewe jinsi Mt. Paulo asemavyo katika 1 Kor. 12:22-23: “Vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi; na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi.” Hakuna mtu anayefunika uso, macho, pua, na kinywa chake. Hatuhitaji kufanya hivyo kwa sababu ni viungo vyetu vyenye heshima kubwa kabisa. Lakini viungo dhaifu, ambavyo tunavionea aibu, tunavificha kwa uangalifu. Mikono yetu na macho, hata na mwili mzima, hauna budi kusaidia kuvifunika na kuvificha. 288. Hivyo, katika mahusiano ya mtu na mwingine, tunapaswa kufunika hitilafu na udhaifu wowote tunaouona katika jirani yetu, tukifanya bidii tuwezavyo kumhudumia na kumsaidia kuiinua heshima yake. Kwa upande mwingine, tunapaswa kuzuia kila jambo linaloelekea kumfedhehesha. 289. Ni maadili mazuri, ya pekee, na yenye uadilifu hasa kuyatoa maelezo mazuri daima kuhusu yote tunayoweza kuyasikia juu ya jirani yetu, mradi yasiwe maovu bayana. Isitoshe, tunapaswa kumtetea dhidi ya ndimi
443
zenye sumu za wanaojishughulisha popote wadadisipo na kulikimbilia lolote ili kumkosoa jirani yao, wakipotosha na kugeuza maneno kwa njia mbaya zaidi. Hili ndilo linalotendeka sasa, hasa kwa Neno tunu la Mungu na wahubiri wake.
290. Amri hii inahusu wingi wa matendo mema yampendezayo Mungu sana na yaletayo baraka nyingi sana, iwapo tu ulimwengu mpofu na watakatifu wa uongo wangezitambua. Hakuna chochote kuhusu mtu au ndani ya mtu kinachoweza kufanya wema au ubaya mkubwa zaidi katika mambo ya kiroho au ya dunia hii kuliko hiki kiungo kidogo na dhaifu miongoni mwa viungo vyake vyote, yaani, ulimi.1459
AMRI YA TISA NA YA KUMI
292. “Usiitamani nyumba ya jirani yako”
“Usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumishi wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.”
293. Amri hizi mbili zikichukuliwa katika maana halisi, zilitolewa kwa Wayahudi peke yao. Kwa kiasi, zinatuhusu pia. Wayahudi hawakuzifafanua kwa kuzihusisha na uasherati au wizi, kwa kuwa dhambi hizi zilikwisha kufundishwa vya kutosha katika amri zilizotangulia. Walifikiria kwamba, walizitimiza amri walipoyatii maagizo na makatazo yapatikanayo ndani yazo. Mungu aliziongezea amri hizi mbili ili kuwafundisha kwamba, ni dhambi kumtamani mke au mali ya jirani, au kuwa na mipango yoyote nazo. 294. Amri hizi zilihitajika hasa kwa sababu watumishi wa kiume na wa kike hawakuwa huru, jinsi ilivyo sasa katika utawala wa Wayahudi, kutumikia kwa mishahara kulingana na mapenzi yao. Sababu ni kwamba, miili, mifugo, na vyote walivyokuwa navyo vilikuwa mali za mabwana zao. 295. Pia, kila mwanamume alikuwa na uwezo kumfukuza mke wake hadharani kwa njia ya kumpa hati ya talaka na kumchukua mke mwingine.1460 Kwa hiyo, kulikuwa na hatari miongoni mwao kwamba, kama mmoja alivutiwa na mke wa mwingine, alimfukuza mke wake kwa sababu yoyote isiyokuwa muhimu na kumfarakisha mke wa mwingine ili aweze kumchukua kisheria. Walifikiria kwamba, hilo halikuwa dhambi au aibu tena kuliko ilivyo sasa ambapo bwana anawafukuza watumishi wake na kumshawishi wa jirani yake amwache.
296. Kwa hiyo, ninasema, walizifafanua amri hizi kikamilifu–japo pia zina
1459 Yak. 3:5
1460 Kum. 24:1-4; Mt. 5:31; 19:7
matumizi mapana na ya hali ya juu zaidi–kumkataza mtu yeyote, hata mwenye kujipendekeza, asitamani, asipende kwa hila, au asiteke kilicho cha jirani yake kama vile mke wake, watumishi, nyumba, mashamba, makonde, au wanyama. Basi, hapo juu, Amri ya Saba inakukataza usiteke au usizuie mali za mwingine ambazo huna haki kuwa nazo. Lakini hapa imekatazwa pia usikishawishi chochote kitoke kwa jirani yako, japo mbele ya dunia, ungeweza kufanya hivyo kwa heshima bila mashtaka, lawama, au kwa njia ya matendo ya ulaghai.
297. Hivyo ndivyo asili yetu ilivyo kwamba, tunaona uchungu sote mtu akiwa na kitu kama sisi. Kila mmoja hujipatia yote anayoweza na kuwaacha wengine wajijali wenyewe. Na bado sisi sote tunajifanya kuwa wanyofu. 298. Tunajua namna ya kuuonyesha uso mzuri ili kuuficha ulaghai wetu. Tunaubuni ukwepaji stadi na ubaya wa hila - njia zinazofaa zaidi na zaidi zinagunduliwa siku kwa sikukatika kisingizio cha haki. Tunathubutu kujivunia hali hizo wazi na kusisitiza kwamba, zisiitwe uhuni bali busara na ufahamu wa mambo.
299. Katika hili, tunasaidiwa na mawakili na wanasheria wanaoisongonyoa na kuiongezea sheria ili iwafae, na wanaoitumia kwa visingizio bila kujali usawa au hali ya jirani. Kwa ufupi, yeyote aliyepiku ujanja na werevu zaidi katika mambo kama hayo, hupata manufaa zaidi kutokana na sheria, kwa maana inadaiwa kwamba: “Vigilantibus iura subveniunt–“Sheria huwahifadhi waangalifu.”1461
300. Basi, amri hii ya mwisho haiwahusu ambao dunia inawahesabu kuwa majambazi waovu, bali inahusu wale walio wanyofu kabisa - watu wanaotaka wasifiwe kuwa wa kweli na waadilifu kwa maana hawajazivunja amri zilizotangulia. Wayahudi walidai hasa kuwa wa kundi hili, sawasawa na watu wengi mashuhuri wa cheo cha malodi, wakuu, na watawala walivyo sasa. Umma u chini zaidi ngazini, ambapo Amri ya Saba inahusika, kwa kuwa hawajihusishi sana na masuala ya heshima na haki inapokuwa jambo la kujipatia mali.
301. Hali hii hujitokeza zaidi katika kesi ambapo mtu mmoja hunuia kujipatia na kukiminya kitu kutoka kwa jirani yake. Kwa mfano, wakati watu wanazozana na kupigana mwereka kwa ajili ya urithi mkubwa, shamba, na kadhalika, wanatumbukia katika hoja zozote zisizokuwa za haki. Hivyo, huzipaka na kuzipamba ili sheria iziunge mkono. Isitoshe, wanapewa mamlaka ya usalama kuhusiana na mali hiyo ili kuizuia isinung’unikiwe na kubishaniwa. 302. Vivyo hivyo, mtu mmoja akitamani ngome, mji, nchi, au kitu kingine kikubwa, anatumia hongo kwa njia ya ushirikiano wa kirafiki, na kwa mbinu zingine zozote zilizo wazi kwake, hadi aichukue mali kutoka kwa mwenyewe na apewe kisheria kwa 1461 Methali ya Kilatini.
njia za hati za serikali na muhuri wa mtawala ukishuhudia kwamba, ilipatikana kihalali.
303. Jambo lilo hilo hutokea katika mambo ya biashara za kawaida ambapo mtu mmoja hukichomoa kitu kutoka mkononi mwa mwingine kwa ujanja na mdhulumiwa hukosa la kufanya amzuie. Au akiuona mwanya wa faida–tuseme iwapo mtu hajiwezi kwa sababu ya ugonjwa au deni, huendelea kuimiliki sehemu yake ya mali au kuiuza bila kujali–humhangaisha na kumsumbua mpaka aichukue nusu au zaidi yake. Bado, hii haitahesabiwa kuwa imepatikana kinyume cha sheria, lakini itachuliwa kana kwamba, ilinunuliwa kwa haki. Hivyo, kuifanya misemo ifuatayo isadifu: “Mwenye kuwahi hutangulia kudhulumiwa/Anayewahi kwa mtemi huambua mzoga” na “Kila mtu na wake kwanza wengine wajitegemee.”
304. Nani ana akili ya kutosha kuwaza kwamba, ataweza kujipatia nini kwa kujisingizia nafasi kama hiyo? Ulimwengu haulihesabu hili kuwa makosa, na hauoni kwamba, jirani anadhulumiwa na kulazimishwa kutoa mhanga kile ambacho hawezi kukiacha bila kupata hasara. Kisha, bado hakuna mtu anayetaka hili limpate yeye mwenyewe. Kutokana na hili, ni wazi kwamba, hizi sababu zote na kujifanya ni uongo mtupu.
305. Hivi ndivyo hali ilivyokuwa zamani kuhusu wanawake walioolewa. Waliijua hila kama hii. Iwapo mtu alivutiwa na mwanamke mwingine, kwa njia yoyote ile, aidha alidiriki peke yake, au kupitia kwa wengine, alimfanya mume wake achukizwe naye, au aanze kuwa mkorofi mno na mgumu kuishi naye kiasi kwamba, mume wake alilazimika kumruhusu na kumwachia mume mwingine. Bila shaka, tendo la namna hiyo liliendelea wakati wa sheria, kwa maana tunasoma hata katika Injili1462 kwamba, Mfalme Herode alimchukua mke wa ndugu yake wakati ndugu yake alikuwa hai. Isitoshe, bado alijionyesha kama mheshimiwa na mnyofu, jinsi Mt. Marko anavyoshuhudia. 306. Ninategemea kwamba, mifano ya namna hii haitaonekana miongoni mwetu, isipokuwa mtu aweze kulitumia hili kumshawishi bibi arusi tajiri na kumwachisha mwingine. Kwa maana, katika Agano Jipya,1463 watu waliooana wanakatazwa kutalikiana. Lakini si jambo gumu sana miongoni mwetu mtu kumtenga mtumishi wa kiume au wa kike wa mwingine na kumfanya amwache au kumshawishi kwa maneno ya kuvutia.
307. Mambo haya na yawe yalivyo. Inakupasa ujifunze kwamba, Mungu hataki umnyang’anye jirani yako kitu chochote kilicho chake. Wala usimwachie hasara wakati unaufurahisha ulafi wako ingawa mbele ya ulimwengu unaweza
1462 Mt. 14:3-4; Mk. 6:17 1463 Mt. 5:31-32; 19:3-9; Mk. 10:2-12; Lk. 16:18; 1 Kor. 7:10-11
446
kubaki na mali hiyo kwa heshima. Kufanya hivyo ni uovu wenye giza wa kichinichini, na jinsi tunavyosema, yote yanafanyika “chini ya kofia”1464 ili usigunduliwe. Ijapokuwa utajifanya kama mtu ambaye hakumtendea mtu yeyote jambo baya, umeingilia haki za jirani yako. Inawezekana isiitwe kuiba au ghiliba, bado ni kutamani–yaani, unakuwa na makusudi kuhusu mali ya jirani yako, ukiiondoa kwa hila kutoke kwake kinyume cha matakwa yake, na kukionea wivu alichopewa na Mungu. 308. Hakimu na umma wanaweza kukuacha nacho lakini Mungu hatakuacha. Maana anauona moyo wako mwovu na udanganyifu wa ulimwengu. Ukitoa kidole/inchi kwa dunia, itachukua yadi na hatimaye dhuluma wazi na vurugu hufuatia.
309. Basi, ziacheni amri hizi zibakie na matumizi yao ya jumla. Tunaamriwa tusimtakie jirani yetu madhara, tusiyasababishe, na tusiyape nafasi. Badala yake, tuwe radhi kumwachia kilicho chake, na kuendelea kulinda chochote ambacho ni cha faida na manufaa kwake jinsi tunavyomtaka yeye atufanyie. 310. Hivyo, amri hizi zinalenga hasa wivu na tamaa mbaya. Kusudi la Mungu likiwa ni kuiharibu mizizi yote na sababu za madhara kwa majirani zetu. Kwa hiyo, anatangaza kwa maneno wazi: “Usitamani.” Licha ya yote, anataka mioyo yetu iwe safi, ingawa katika maisha yetu yote hatuwezi kuufikia ukamilifu huo. Hivyo, amri hii inabakia kama zingine. Daima inatushtaki na kuonyesha hakika jinsi tulivyo wanyofu mbele za Mungu.
HITIMISHO LA AMRI KUMI
311. Basi, hapa tuna Amri Kumi za Mungu, muhtasari wa mafundisho ya kimungu kuhusu yanayotakiwa tuyatende ili tufanye maisha yetu yote yampendeze Mungu. Ni chemcemi ya kweli ambayo kutoka kwayo, matendo mema lazima yabubujike. Ni chombo cha kweli ambacho kwacho, matendo mema lazima yapitie. Mbali na Amri hizi Kumi, hakuna tendo wala tabia inayoweza kuwa nzuri au ya kumpendeza Mungu, hata kama ni kubwa au ya thamani namna gani mbele ya ulimwengu.
312. Tuone sasa, jinsi watakatifu wetu wakubwa wanavyoweza kujivunia madaraja yao ya kiroho, na matendo makubwa na mazito waliyoyabuni. Wameacha amri hizi kana kwamba, zilikuwa za thamani ndogo sana na zilikwisha kutimizwa zamani.
313. Ninadhania kwamba, tutakuwa na shughuli tele za kuzitii amri hizi, kuushika upole, uvumilivu, upendo kwa maadui, unyofu, huruma, na yote 1464 Methali ya Kijerumani iliyomaanisha kofia ya mchawi.
447
yanayohusika na mema haya. Lakini matendo ya namna hiyo si muhimu na hayavutii hata kidogo mbele ya dunia. Si ya kawaida, si ya fahari, hayawekewi mipaka kutumiwa nyakati, mahali, ibada, na sherehe maalumu. Bali ni matendo ya kawaida, ni kazi za nyumbani za kila siku kati ya jirani na mwenzake na yasiyokuwa na heshima yoyote. 314. Kwa upande mwingine, matendo hayo mengine huyavutia macho na masikio ya watu sana. Yakisaidiwa na majivuno makuu, fahari, na majengo adhimu sana, yanarembwa sana kiasi cha kukifanya kila kitu king’ae na kumetameta zaidi. Watu hufukiza ubani, huimba, hupiga kengele, huwasha mishumaa, taa, hadi chochote hakiwezi kuonekana wala kusikika. Padre aliyevalia kasula ya dhahabu1465 akisimama au Mkristo wa kawaida akipiga magoti kanisani siku nzima, hilo huchukuliwa kuwa tendo la tunu kubwa lisiloweza kutukuzwa vya kutosha. Lakini mwali maskini akimtunza mtoto mchanga na kuyafanya yalivyoamriwa kwa uaminifu, hayo huonekana kuwa bure kabisa. Vinginevyo, kwa nini wamonaki/watawa wa kiume na wa kike wahamie makazi ya watawa?
315. Fikiria tu. Je, si kiburi cha kiibilisi kwa watakatifu waliokata tamaa kuthubutu kubuni maisha na madaraja bora na matakatifu kuliko mafundisho ya Amri Kumi? Jinsi nilivyosema, wao husisitiza kwamba, maisha haya ni ya watu wa kawaida, walakini yao ni kwa watakatifu na kwa watimilifu. 316. Watu hawa vipofu na wanyonge hawaoni kwamba, hakuna mtu yeyote aliyeweza kuendelea hata kuitimiza mojawapo ya Amri Kumi kabisa. Inatubidi Ukiri wa Imani na Sala ya Bwana itusaidie–jinsi tutakavyosikia–ili tutafute na tusali kwa mambo ya aina hii na tuyapokee wakati wote. Kwa sababu hiyo, majivuno yao yote ni sawa na iwapo ningejigamba: “Naam, sina sarafu yoyote, lakini ninaahidi kulipa gilda kumi.”1466
317. Mimi ninayasema haya na kukariri tena kuyasema ili watu waache matumizi haya mabaya yasiyokuwa rahisi kutolewa na yaliyowashikilia watu wote. Isitoshe, wajifunze katika hali zote za maisha kuzitunza na kuzisikiliza amri hizi. Kwa maana, kwa muda mrefu, watu hawatatunga mafundisho au hali ya maisha yaliyo sawa na Amri Kumi, kwa kuwa amri hizi ni kuu mno. Kwa sababu hiyo, wanadamu hawawezi kuzitimiza kwa nguvu za kibinadamu. Yeyote akiweza kuzitimiza, atakuwa mtu wa mbinguni. Naam, mtu mtakatifu aliye juu ya utakatifu wote wa dunia. 318. Jishughulishe tu nazo, jijaribu kabisa, na fanya uwezavyo. Hakika utayapata mengi ya kujishughulisha nayo kiasi kwamba, 1465 Vazi maalumu linalotumika katika Ibada za Ekaristi, yaani, misa. Hapa, Luther anamaanisha misa za binafsi zilizosherehekewa kwa ajili ya wafu ili kuliletea Kanisa faida. 1466 Sarafu ya Kijerumani ‘Groschen.’ Thamani ya gilda - yaani, ‘Gold,’ ilikuwa ni ‘Groschen’ 21 baada ya “dhahabu.”
448
hutatafuta au kuzisikiliza kazi zingine au utakatifu mwingine.
319. Haya yanatosha kuhusu sehemu ya kwanza kwa ajili ya mafundisho na maonyo. Hata hivyo, inatubidi tuyakariri maandiko tuliyoyajadili mapema kuhusu Amri ya Kwanza, ili kuonyesha juhudi anazozitaka Mungu tuzitenge kwa ajili ya kujifunza jinsi ya kufundisha na kujizoeza Amri Kumi za Mungu.
320. Mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.1467
321. Ingawa kimsingi kiambatisho hiki kinahusishwa hasa na Amri ya Kwanza–jinsi tulivyosikia awali hapo juu–kilinuiwa kuhusishwa na amri zote pia. Kwa hiyo, zote zinapaswa kuhusishwa na kuelekezwa kwayo. Kwa sababu hiyo, ninasema kwamba, inatubidi kuiweka amri hii mbele ya vijana na kuisisitiza ili wajifunze na waishike. Kisha wataelewa kwa nini tunashurutishwa na kulazimishwa kuzitimiza hizi Amri Kumi. Watu waelewe kwamba, kiambatisho hiki kinahusiana na kila mojawapo ya amri, kikiingia na kuzipenya zote.
322. Jinsi tulivyosema awali, maneno haya hizo hapo juu yana tisho kali na maneno karimu ya ahadi ili kututisha, kutuonya, kutushawishi, na kututamanisha ili tulizingatie Neno lake kwa uzito wa kimungu na kuliheshimu. Kwa kuwa mwenyewe anadhihirisha umuhimu wa amri kwake, atazichunga kwa ukali kabisa akiwaadhibu vikali na kwa njia ya kutisha zaidi wote wanaozidharau na kuzivunja amri zake. Kinyume chake, atawazawadia tele, atawabariki, na kuwapa mema yote wote wanaoziheshimu, wanaopenda kutenda, na kuishi kulingana nazo. 323. Vivyo hivyo, Mungu anadai kwamba, matendo yote ya utimizaji wa amri yatoke katika moyo unaomwogopa na kumheshimu peke yake. Kwa ajili ya hofu hii, moyo huo huacha mambo yote yanayokiuka mapenzi ya Mungu ili usimkasirishe. Badala yake, huo moyo humtegemea peke yake, hutenda yote yanayompendeza kwa sababu Mungu hujionyesha mwenyewe kama Baba karimu anayetupatia neema na baraka zote.
324. Hii ndiyo maana kamili na ufafanuzi halisi wa amri ya kwanza na kuu kabisa. Amri zote zinatokana na zinatitirika kutoka kwa amri hii. Maneno haya, “usiwe na miungu mingine” humaanisha tu: “Inakubidi kuniogopa, kunipenda, na kunitegemea peke yangu kama Mungu wako kweli.” Moyo wa mwanadamu ukiwa wa namna hiyo kumhusu Mungu, huwa umetimiza amri hii na amri zingine zote. Kwa upande mwingine, mtu yeyote akiogopa na kukipenda kitu kingine chochote huko mbinguni au hapa duniani, hataitii amri hii au amri zingine 1467 Kut. 20:5-6
449
326. Hivyo, Amri ya Kwanza inabidi iangaze na itoe nuru yake kwa amri zingine zote. Kwa sababu hiyo, lazima uyaruhusu maneno ya hitimisho hili, yapitie katika amri zingine zote, kama bizimu au kifundo cha shada la maua kinachofungisha mwanzo na mwisho pamoja na kulishikilia shada lote. Vivyo hivyo, watu waikariri wakati wote bila kuisahau. Naam, upendo na tegemeo linalotokana na Amri ya Kwanza hudai tumwogope Mungu kulingana na Amri ya Pili, tusilitumie jina lake vibaya kwa kulaani, kusema uongo, kulaghai, na kwa kuzitenda aina zingine za hila na maovu. Badala yake, tulitumie jina lake vizuri katika sala, sifa, na shukrani. Vivyo hivyo, uchaji, upendo, na tegemeo vinapaswa kutulazimisha tusilidharau Neno lake. Badala yake, tujifunze, tulisikilize kwa fuhara, tulitakase, na kuliheshimu.
327. Hivyo, kwa njia ya amri zinazofuatia zinazomhusu jirani yetu, kila kitu kinatokana na nguvu ya Amri ya Kwanza. Tunapaswa kuwaheshimu, kuwanyenyekea, na kuwatii baba na mama, mabwana, na wote wenye mamlaka kwa ajili ya Mungu. Kwa maana hupaswi kuwaheshimu au kuwaogopa baba na mama kwa makosa ukiyafanya au ukiacha kuyafanya mambo ili uwapendeze tu. Afadhali umwulize Mungu anachotaka ukifanye na atakachokudai hakika. Ukiliacha hilo, una hakimu mwenye hasira. Ukilifanya hilo, una baba mwenye huruma.
328. Kadhalika, inakubidi usimtendee jirani yako madhara, uharibifu, au ugomvi. Isitoshe, usimsumbue kwa njia yoyote, binafsi, mke wake, mali yake, heshima yake, au haki yake, hata kama utakuwa na nafasi na udhuru wa kufanya hivyo bila kuadhibiwa na mtu yeyote. Kinyume chake, ni lazima uwatendee mema watu wote, uwasaidie, na uyaendeleze masilahi yao, kwa hali yoyote na unapoweza kutokana na mapenzi ya Mungu tu ili umpendeze, ukiwa na matumaini kwamba, atakuzawadia kwa wingi yote uyafanyayo. Hivyo, unaona jinsi Amri ya Kwanza ilivyo chimbuko kuu na chemchemi zinamotoka zingine zote. Tena, zote zinairudia na kuitegemea kiasi kwamba, mwisho na mwanzo vimehusishwa na kufungamanishwa pamoja.
1468 Zab. 147:11
450 zozote. 325. Basi, Maandiko Matakatifu yote yamehubiri na yameifundisha amri hii kila mahali, yakisisitiza mambo haya mawili: uchaji na tegemeo kwa Mungu. Hasa nabii Daudi anafanya hivyo tena na tena katika Kitabu cha Zaburi anaposema:“BWANA huwaridhia wao wamchao, na kuzitarajia fadhili zake.”1468 Inaonekana kwamba, ameielezea amri nzima katika aya moja kana kwamba, anasema: “BWANA anawapenda wale wasiokuwa na miungu mingine.”
330. Mimi ninarudia kusema kwamba, ni faida na lazima kuwafundisha, kuwahimiza, na kuwakumbusha vijana haya yote wakati wote ili walelewe, siyo kwa mapigo na lazima tu, kama mifugo, bali katika uchaji na kicho cha Mungu. Haya siyo mambo madogomadogo ya watu lakini ni amri ya Mungu aliye juu zaidi, anayezilinda kwa juhudi kuu, anayeitoa wazi ghadhabu yake kwa wanaozidharau. Kinyume chake, anawazawadia tele wanaozitii. Watu wanapotafakari jambo hili na kuliweka moyoni, kutatokea mhemuko wa hiari na shauku ya kufanya mapenzi ya Mungu kwa furaha. 331. Kwa sababu hii, Agano la Kale haliwalazimishi watu bure kuziandika Amri Kumi juu ya kila ukuta na pembe, na hata nguoni mwao.1469 Tusifanye hivyo kama maonyesho tu, jinsi walivyofanya Wayahudi,1470 bali tuziweke siku zote mbele ya macho yetu na katika mawazo yetu daima, na kuzifuata kabisa katika kazi na njia zetu zote. 332. Kila mmoja azifanye kuwa mazoezi yake ya kila siku katika hali zote, katika mambo yake yote na shughuli zake kana kwamba, zimeandikwa kila mahali anakoangalia, na kila mahali anakokwenda au kokote anakosimama. Kwa hiyo: mwenyewe akiwa nyumbani kwake, na akiwa nje miongoni mwa majirani zake, atakuwa na wasaa wa kutosha wa kuzishika Amri Kumi, na hakuna anayelamizika kuzitafuta kutoka mbali.
333. Kutokana na haya yote, ni wazi mara nyingine tena jinsi inavyostahili Amri hizi Kumi ziadhimishwe sana na kusifiwa kuliko maagizo yote, amri, na matendo yanayofundishwa na kutimizwa mbali nazo. Tunaweza kutoa changamoto hapa: Waacheni wenye hekima wote na watakatifu wajitokeze na kutoa, kama wanaweza, kazi yoyote kama ile ambayo Mungu anadai kwa moyo na kuamuru katika amri hizi katika tisho la ghadhabu na adhabu yake kuu. Wakati uo huo, anaongezea ahadi zenye utukufu mkuu kwamba, atatuzawadia kwa wingi vitu vyote vizuri na mibaraka. Kwa hiyo, inatupasa kuziheshimu mno na kuzithamani kuliko mafundisho mengine yote kama hazina kuu ambayo Mungu ametupatia.
SEHEMU YA PILI: UKIRI WA IMANI1471
1. Kufikia hapa, tumeisikia sehemu ya kwanza ya mafundisho ya Kikristo. Ndani yake, tumeona yote ambayo Mungu anataka tuyafanye au tusiyafanye. Ukiri hufuata ipasavyo, ukielezea vyema yote tunayopaswa kuyatazamia na kuyapokea kutoka kwa Mungu. Kwa ufupi, unatufundisha kumjua yeye kikamilifu. 2. Umetolewa ili utusaidie kuyafanya ambayo Amri Kumi zinayahitaji kutoka kwetu.
1469 Kum. 6:8-9; 11:20
1470 Mt. 23:5
1471 Kilatini: ‘De symbolo fidei,’ (Ukiri wa Imani).
Kwa maana, jinsi tulivyosema hapo juu, zimewekwa katika kiwango cha juu kiasi kwamba, uweza wote wa mwanadamu ni duni mno na dhaifu kuzitimiza. Kwa hiyo, ni lazima kujifunza sehemu hii sawa na sehemu nyinginezo ili tupate kujua ni wapi na ni vipi tunapata nguvu kwa kazi hii. 3. Iwapo tungeweza kuzishika Amri Kumi ipasavyo, kwa nguvu zetu wenyewe, hatungehitaji Ukiri wala Sala ya Bwana. Lakini kabla hatujaelezea manufaa na lazima ya Ukiri, inatoshea kama watu wa kawaida watajifunza kuuelewa Ukiri wenyewe kama hatua ya kwanza.
5. Kwanza, Ukiri ulikuwa umegawanywa katika mafungu kumi na mawili.1472 Naam, iwapo fikira zote zipatikanazo katika Maandiko Matakatifu na zilizo katika Ukiri zingekusanywa, kungekuwa na mafungu mengi zaidi ambayo hayangeweza kuelezewa yote katika maneno machache jinsi hii. 6. Lakini, ili uwe wazi na sahili kabisa kwa ajili ya kuwafundishia watoto, tutaujumlisha Ukiri wote katika mafungu matatu kulingana na nafsi tatu za Mungu, ambaye yote tunayoyaamini yanamhusu. Fungu la kwanza linalomhusu Mungu Baba, huelezea uumbaji. Fungu la pili linamhusu Mwana, yaani, ukombozi. Fungu la tatu linamhusu Roho Mtakatifu, yaani, utakaso. 7. Hivyo, ukiri unaweza kufupishwa katika maneno haya machache: “Ninamwamini Mungu Baba, aliyeniumba. Ninamwamini Mungu Mwana, aliyenikomboa. Ninamwamini Roho Mtakatifu, anitakasaye.” Kuna Mungu mmoja na imani moja lakini nafsi tatu. Kwa hiyo, kuna mafungu matatu au kiri tatu. 8. Acheni tuyafafanue maneno haya kwa ufupi:
FUNGU LA KWANZA
9. “Namwamini Mungu Baba, Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia.”
10. Maneno haya yanatupatia maelezo mafupi kuhusu Mungu Baba, asili yake, mapenzi yake, na matendo yake. Kwa kuwa, Amri Kumi zimetuelezea kwamba, hatupaswi kuwa na miungu mingine isipokuwa Mungu mmoja, swali ni: “Je, Mungu ni nani? Au yeye hufanya nini? Tunawezaje kumsifu, kusimulia juu yake au kumwelezea ili apate kufahamika?” Fungu hili na mafungu yanayofuatia hulifundisha jambo hili. Kwa hiyo, Ukiri ni itikio na ungamo la Wakristo ambalo msingi wake ni Amri ya Kwanza. 11. Ungemwuliza mtoto mdogo: “Mvulana wangu, una Mungu wa namna gani? Unajua nini juu yake?” Angeweza kusema, “Kwanza, Mungu wangu ndiye Baba, aliyeziumba mbingu na dunia. Mbali na 1472 Ugavi huu katika mafungu kumi na mawili ulifuatia mafundisho ya zamani tangu karne ya 5. Papa Leo Mkuu (440-461), katika barua yake kwa Pulcheria (Ep. 31), aliandika: ‘Catholici symboli brevis et perfecta confessio, quae duodecim apostolorum totidem est signata sententiis’ – (Ukiri mfupi na halisi wa imani ya Katoliki uliotungwa kwa sentensi za mitume wote kumi na wawili).
yeye peke yake sina mungu mwingine, kwani hakuna mwingine yeyote ambaye angeweza kuumba mbingu na dunia.”
12. Hata hivyo, kwa wataalamu walioendelea zaidi na wasomi, mafungu yote matatu yanaweza kutunzwa kikamilifu zaidi na kugawanywa katika sehemu nyingi inavyowezekana kuyapata maneno. Lakini kwa wanafunzi wadogo, inatoshea kuyaonyesha mambo muhimu tu, yaani, jinsi tulivyosema kwamba, fungu hili linaushughulikia uumbaji. Inatupasa kuyasisitiza maneno “Muumba wa mbingu na dunia.” 13. Ni nini maana ya maneno, “Ninamwamini Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba?” Jibu: Ninashikilia na kuamini kwamba, mimi ni kiumbe cha Mungu; yaani, amenipa na daima huhimili mwili wangu, nafsi, uhai, viungo vyangu vidogo kwa vikubwa, akili zote, maana na welekevu wangu. Licha ya hayo, amenipa chakula changu, kinywaji, nguo, mapato, mke, watoto, watumishi, nyumba, na maskani. 14. Isitoshe, huufanya uumbaji wote usaidie kutupatia viburudisho na mahitaji ya lazima kwa uhai–jua, mwezi, nyota za angani, mchana, usiku, hewa, moto, maji, vyote vitokavyo ardhini, ndege, samaki, wanyama, nafaka, na aina zote za mazao. 15. Aidha, hutupatia baraka zote zinazoonekana na za muda–serikali thabiti, amani, na usalama. 16. Kwa hiyo, tunajifunza katika fungu hili kwamba, hakuna hata mmoja wetu aliye na uhai wake yeye mwenyewe, chochote kilichotajwa hapa, kinachoweza kutajwa, wala mwenyewe hawezi kuhifadhi chochote miongoni mwa vitu hivyo, viwe vidogo au duni kiasi gani. Yote haya yanafahamika katika neno “Muumba.”
17. Aidha, tunakiri kwamba, Mungu Baba ametupatia vyote tulivyo navyo, tuvionavyo kwa macho yetu, anatulinda kila siku, anatukinga dhidi ya uovu, balaa, hatari, na kutuepushia aina zote za maafa. Yeye huyafanya haya yote kutokana na upendo na wema wake halisi, bila stahili zetu, kama Baba karimu anayetujali ili tusipatwe na uovu wowote. 18. Hata hivyo, mdahalo zaidi kuhusu jambo hili utajadiliwa katika sehemu zingine mbili za fungu hili, ambapo tunasema “Baba Mwenyezi.”
19. Hivyo, vyote tulivyo navyo na vyote vipatikanavyo mbinguni na duniani, hutolewa na huhimiliwa na Mungu kila siku. Basi, inafuatia kwamba, hakika tunawajibika kumpenda, kumsifu, na kumshukuru bila kukoma. Kwa ufupi, tuyatende haya yote kwa ajili ya utumishi wake, jinsi alivyodai na kutuagiza katika Amri Kumi.
20. Mengi yangeweza kusemwa kama tungefafanua kwa utondoti jinsi watu wachache wanaliamini fungu hili. Sisi sote tunalipitia tu, tunalisikiliza, na kulikariri. Hata hivyo, hatuoni wala hatutilii maanani ambalo maneno hayo
yanatuagiza tulifanye. 21. Kwa kuwa, tungeliamini fungu hili kwa mioyo yetu yote, tungetenda itupasavyo pia. Hatungejigamba, kujisifu, na kujivuna kana kwamba, sisi wenyewe tuna uhai, mali, nguvu, heshima, na vitu vyetu wenyewe kama hivyo, kana kwamba, sisi wenyewe ilitupasa tuogopwe na tutumikiwe. Hivyo ndivyo dunia hii dhalili na potovu inavyofanya. Huzama katika upofu wake, ikitumia vibaya baraka na karama zote za Mungu kwa ajili ya kiburi, ulafi, anasa, starehe, na bila kumgeukia Mungu kamwe ili kumshukuru au kumtambua kama Bwana na Muumbaji.
22. Kwa hiyo, fungu hili lingetunyenyekesha na kututisha sote kama tungeliamini. Kwa maana, tunafanya dhambi kila siku kwa macho, masikio, mikono, mwili, nafsi, pesa, mali, na kwa vyote tulivyo navyo. Haya ni ya kweli hasa kwa ambao hata wanapingana na Neno la Mungu. Lakini bado Wakristo wana manufaa haya kwamba, wanajitambua katika wajibu wa kumtumikia na kumtii kwa ajili ya haya yote.
23. Kwa hiyo basi, inatupasa tujifunze fungu hili kila siku na kuliingiza akilini mwetu. Kila kitu tukionacho na kila baraka tuipatayo inapasa kutukumbusha hilo. Tunapoepuka dhiki au hatari, inatupasa tutambue kwamba, haya ni matendo ya Mungu. Anatupatia vitu hivi vyote ili tuweze kuhisi na kuona moyo wake wa ubaba kwavyo na upendo wake usiokuwa na mipaka kwetu. Hivyo, mioyo yetu itaamshwa na kuchochewa na shukrani kwake Mungu na kutaka kuzitumia baraka hizi zote kwa utukufu na sifa zake.
24. Kwa ufupi, hii ndiyo maana ya fungu hili. Ni lile tu ambalo watu wa kawaida wanahitaji kujifunza mwanzoni, kuhusu tulivyo navyo na tunavyovipokea kutoka kwa Mungu, na kuhusu tunachomwia kama malipo. Haya ni maarifa mazuri mno na hata hazina kubwa zaidi. Kwani, hapa tunaona jinsi Baba amejitolea mwenyewe kwetu na kwa viumbe vyake vyote. Isitoshe, ametujazia hazina hiyo tele katika maisha haya, na licha ya hayo, ametumiminia mali za milele zisizoelezeka kwa njia ya Mwanawe na Roho Mtakatifu, jinsi tutakavyosikia.
FUNGU LA PILI
25. “Namwamini Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee Bwana wetu: aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Mariamu; akateswa wakati wa Pontio Pilato; alisulubiwa, akafa na kuzikwa: alishuka kuzimuni, siku ya tatu alifufuka toka kwa wafu, alipaa mbinguni, na anakaa mkono wa kulia wa Mungu, Baba
454
Mwenyezi, kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.”
26. Hapa tunajifunza kufahamu nafsi ya pili ya Mungu. Tunaona yale yote tunayoyapokea kutoka kwa Mungu zaidi ya vitu vya muda viliyotajwa hapo juu, yaani, alivyojitolea kwetu kikamilifu kabisa bila kutuhini lolote. Fungu hili ni tajiri sana na muhimu mno. Lakini, ili tulielezee kwa ufupi na kwa urahisi, tutauchukua msemo mmoja unaojumlisha dutu ya fungu hili. Katika huo tutajifunza jinsi tunavyokombolewa. Tutayamakinikia maneno haya, “Katika Yesu Kristo, Bwana wetu.”
27. Ukiulizwa: “Unaamini nini katika Fungu la Pili kuhusu Yesu Kristo?” Jibu kwa ufupi: “Ninaamini kwamba, Yesu Kristo, Mwana kweli wa Mungu, amekuwa Bwana wangu.” Ina maana gani “kuwa Bwana?” Ina maana kwamba, ameniokoa kutoka dhambini, kutoka kwa Ibilisi, kutoka mautini, na kutoka kwa maovu yote. Kabla yake, sikuwa na Bwana na Mfalme bali nilikuwa mtumwa chini ya nguvu ya Ibilisi. Nilihukumiwa kifo na kutatanishwa katika dhambi na upofu.
28. Tulipoumbwa na Mungu Baba, na kupokea vitu vizuri vya kila aina kutoka kwake, Ibilisi alikuja na kutuongoza hadi kwenye kutotii, dhambi, mauti, na maovu yote. Tulikaa chini ya ghadhabu na hasira ya Mungu tukiwa tumehukumiwa katika laana ya milele jinsi tulivyostahili. 29. Hapakuwa na ushauri, msaada, wala faraja kwetu hadi huyu Mwana wa pekee na wa milele wa Mungu akaja kutoka mbinguni kutusaidia. Katika uzuri wake usiopimika, alikuwa na huruma kuhusu taabu na unyonge wetu. 30. Hawa wadhalimu na walinzi wa gereza sasa wamefukuzwa, na nafasi yao imechukuliwa na Yesu Kristo, Bwana wa uzima, wa haki, wa kila jema, na wa baraka. Ametunyakua, sisi viumbe maskini tuliopotea, kutoka kwenye maafa ya Jehanumu, ametushindia, ametuweka huru, na ameturudisha kwa fadhila na neema ya Baba yake. Ametuchukua kuwa wake, chini ya ulinzi wake ili atutawale kwa haki yake, hekima, nguvu, uhai, na uanaheri.
31. Uache huu uwe muhtasari wa fungu hili kwamba, neno hilo dogo BWANA, linamaanisha tu Mkombozi. Yaani, aliyeturejesha kutoka kwa Ibilisi na kutupeleka kwa Mungu, kutoka mautini hadi uzimani, kutoka dhambini hadi kwenye haki, na sasa anatutunza katika usalama. Sehemu zinazobakia za hili fungu, zinatumika tu kuelezea kwa uwazi na zinaonyesha jinsi na kwa njia gani wokovu huu ulifanikishwa. Yaani, ulimgharimu Kristo nini, alichokilipa, na jinsi alivyojihatarisha ili kutushindia na kutuweka chini ya utawala wake. Yaani, alifanyika kuwa mwanadamu, akachukuliwa mimba, akazaliwa na Bikira Mariamu bila dhambi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili awe Bwana juu ya dhambi. Aidha, aliteswa, alikufa, na akazikwa ili aweze kuwa ridhaa kwa ajili
yangu na kulilipa deni langu, siyo kwa fedha wala dhahabu, bali kwa damu yake ya thamani. Hayo yote yalifanyika ili awe BWANA wangu. Maana, hakulifanya lolote miongoni mwa haya kwa ajili yake mwenyewe wala hakuyahitaji. Baadaye alifufuka tena kutoka kwa wafu, akayameza na kuyamaliza mauti.1473 Mwishowe, akapaa mbinguni na kuyachukua mamlaka katika mkono wa kulia wa Baba. Kwa hiyo, Ibilisi na nguvu zake zote lazima awe na alale chini ya miguu yake hadi siku ya mwisho, atakapotugawanya kabisa na kututenga na dunia ya maovu, Ibilisi, mauti, dhambi, na kadhalika.
32. Lakini mahali pazuri pa kuyaelezea mambo haya yote yaliyo tofauti siyo katika mahubiri mafupi kwa watoto. Ni katika mahubiri marefu ya mwaka mzima, hasa nyakati zilizotengwa kushughulikia, kwa kirefu, mafungu kama kuzaliwa, mateso, ufufuo, na kupaa kwa Kristo.
33. Naam, Injili yote tunayoihubiri inategemea kulielewa vyema fungu hili. Ndilo lililo msingi wa wokovu wetu wote na uanaheri, na ni tajiri mno, pana, na hatuwezi kamwe kujifunza fungu hilo kikamilifu.
FUNGU LA TATU
34. Namwamini Roho Mtakatifu, kanisa takatifu la Kikristo, ushirika wa watakatifu, ondoleo la dhambi, ufufuo wa mwili, na uzima wa milele. Amina.
35. Jinsi nilivyosema, siwezi kulipatia fungu hili kichwa bora zaidi kuliko “Utakaso.” Ndani yake, kazi ya Roho Mtakatifu inaelezewa na kuonyeshwa, yaani, kututakasa. Kwa hiyo, lazima tuimakinikie sana istilahi “Roho Mtakatifu.” Ni kamilifu sana kuweza kupata kibadala chake. 36. Aina nyingine nyingi za roho zimetajwa katika Maandiko Matakatifu kama vile roho ya binadamu,1474 roho za mbinguni,1475 na za maibilisi.1476 Lakini Roho wa Mungu peke yake ndiye anayeitwa Roho Mtakatifu, yaani, ambaye ametutakasa na bado anatutakasa. Jinsi Baba anavyoitwa Muumba na Mwana anavyoitwa Mkombozi, kwa sababu ya kazi yake, Roho Mtakatifu lazima aitwe Mtakasaji, yaani, atakasaye. Utakaso huu unafanyikaje? 37. Jibu: Jinsi Mwana anavyopata mamlaka kwa kutununua kwa kuzaliwa, kifo, na ufufuo wake, vivyo hivyo, Roho Mtakatifu huutekeleza utakaso wetu kwa: ushirika wa watakatifu au Kanisa takatifu la Kikristo, ondoleo
1473 Isa. 25:5
1474 1 Kor. 2:11 1475 Yaani, malaika. 1476 1 Sam. 16:14, 23; Mdo. 19:12, 15
la dhambi, ufufuo wa mwili, na uzima wa milele. Yaani, yeye hutuongoza kwanza hadi katika jumuia takatifu lake, anatuweka kifuani mwa Kanisa, anakotuhubiria na kutuleta kwake Kristo.
38. Wewe wala mimi hatungeweza kujua chochote kamwe kuhusu Kristo, hatungweza kumwamini, na hatungeweza kumpokea kama Bwana wetu. Hayo yangewezekana tu kama yangetolewa kwetu kwanza na kuwekwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu kwa njia ya mahubiri ya Injili. Kazi imemalizika na kutimizwa, Kristo ameitwaa na kuishinda hazina kwa ajili yetu kwa njia ya mateso, kifo, na ufufuo wake. Lakini iwapo kazi hiyo ingebakia kufichwa na hakuna aliyeijua, basi, yote yangekuwa yamefanyika bure na kila kitu kingepotea. Ili hazina hii isizikwe bali itumiwe na kufurahiwa, Mungu amelifanya Neno lichapishwe na kuhubiriwa. Kwalo, amemtoa Roho Mtakatifu atoe na atupatie hazina hii ya wokovu. 39. Kwa hiyo, kutakasa ni kutuleta kwa Kristo BWANA, na kuipokea baraka hii ambayo hatungeweza kujipatia wenyewe.
40. Basi, jifunze fungu hili kwa uwazi iwezekanavyo. Ukiulizwa maneno “ninamwamini Roho Mtakatifu” yanamaanisha nini? Unaweza kujibu: “Ninaamini ya kuwa Roho Mtakatifu hunitakasa, jinsi jina lake linavyodokezea.”
41. Yeye analifanyaje hilo? Analifanya kwa njia gani? Jibu: “Kupitia kwa Kanisa Takatifu la Kikristo, ondoleo la dhambi, ufufuo wa mwili, na uzima wa milele.”
42. Kwanza, ana jamii ya pekee ulimwenguni. Ndiye mama ambebaye na kumzaa kila Mkristo kwa Neno la Mungu. Roho Mtakatifu hulifunua na kulihubiri Neno hilo na kwalo, huiangaza na kuichochea mioyo ili ilielewe, ilipokee, ilishikilie, na ivumilie ndani yalo.
43. Ambapo Roho Mtakatifu halisababishi Neno kuhubiriwa na hauchochei ufahamu mioyoni, kila kitu hupotea. Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa chini ya Upapa, ambapo imani iliwekwa pembeni na hakuna hata mmoja aliyemtambua Kristo kama Bwana, au Roho Mtakatifu kama Mtakasaji. Yaani, hakuna aliyeamini kwamba, Kristo ni Bwana wetu kwa maana kwamba, alitushindia hazina hii bila matendo yetu, stahili zetu, na alitupatanisha na Baba. Ni lipi lililokosekana hapa? 44. Hapakuwa na Roho Mtakatifu wa kuufunua ukweli huu na kuufanya uhubiriwe. Watu na roho mbovu zilikuwepo, zikitufundisha kuipata neema na kuokolewa kwa matendo yetu. Kwa hiyo, Kanisa la Kristo halikuwepo. 45. Kwa maana, ambapo Kristo hahubiriwi, hakuna Roho Mtakatifu wa kuumba, wa kuita, na wa kulisanya Kanisa la Kikristo. Nje ya Roho Mtakatifu, hakuna awezaye kuja kwa Kristo Bwana. 46. Liache hili litoshee kuhusu ujumbe wa fungu hili. Lakini kwa kuwa mambo kadha wa kadha katika fungu hili si dhahiri kwa watu wa kawaida, tutayapitia pia.
47. Ukiri huliita Kanisa Takatifu la Kikristo, “communio sanctorum,” “ushirika wa watakatifu.”1477 Maelezo yote mawili yana maana sawa. Nyakati za mwanzoni, msemo wa pili ulikosekana, na hauleti maana katika tafsiri yetu. Iwapo utatafsiriwa kinahau (maneno yenye maana maalumu), ni lazima tuuelezee vinginevyo kabisa. 48. Neno “ecclesia,” dhahiri linamaanisha, “kusanyiko.” Hata hivyo, sisi tumezoea neno “Kirche,” yaani, “kanisa,” ambalo watu wa kawaida hulifahamu, si kama kundi la watu bali kama jengo au nyumba iliyowekwa wakfu. Lakini nyumba haipaswi kuitwa kanisa isipokuwa kwa sababu hii moja kwamba, kundi la watu hukusanyika humo. Kwa maana, sisi tunaokusanyika huchagua mahali pa pekee na huipa nyumba jina lake kwa ajili ya kusanyiko. Hivyo, neno “Kirche,” (kanisa) hakika linamaanisha kusanyiko la kawaida. Neno hili si la asili ya Kijerumani bali ni la asili ya Kiyunani, sawa na neno “ecclesia.” Neno hilo ni “?????,” katika Kiyunani, na “curia” katika Kilatini. Hivyo, katika Kiswahili, linapaswa kuitwa “kusanyiko la Wakristo” au “mkutano,” au bora na dhahiri zaidi, “Wakristo watakatifu.”
49. Kadhalika, neno “communio” lililoambatishwa, lisingetafsiriwa kuwa “ushirika” bali “jamii.” Ni maoni au ufafanuzi ambao kwao, mtu fulani alinuia kuelezea maana ya Kanisa la Kikristo. Lakini wengine kati yetu wasiofahamu Kilatini au Kijerumani wamelitafsiri kuwa “ushirika wa watakatifu,” ingawa hakuna Mjerumani ambaye angetumia au angefahamu maana ya usemi wa namna hiyo. Kinahau (maneno yenye maana maalumu), tunapaswa kusema “jamii ya watakatifu,” yaani, jamii iliyo na watakatifu tu, au wazi zaidi, “jamii takatifu.” 50. Ninalisema hili ili usemi huu uweze kueleweka. Hata hivyo, umeimarika katika matumizi kiasi kwamba, hauwezi kung’olewa. Hivyo, kulibadilisha neno kutakaribia uasi.
51. Hii ndiyo jumla na kiini cha usemi huu: Ninaamini kwamba, duniani kuna kundi takatifu dogo au jamii safi ya watakatifu iliyo chini ya kichwa kimoja, yaani, Kristo. Inakusanywa na Roho Mtakatifu katika imani, nia, na welekevu mmoja. Ina aina mbalimbali za vipaji, na bado inaunganishwa katika upendo bila dhehebu wala mafarakano. 52. Mimi pia ni sehemu, kiungo, mshiriki, na mwenzi katika mibaraka yote inayomilikiwa na jamii hii. Nililetwa kwayo na Roho Mtakatifu na kuunganishwa kwayo kwa ukweli kwamba, nimelisikia na bado ninalisikia Neno la Mungu ambalo ndilo hatua ya kwanza ya kuiingilia katika jamii hii. Kabla ya kufika hapa, tulikuwa wa Ibilisi kabisa na hatukujua kitu kuhusu Mungu na Kristo. 53. Roho Mtakatifu hubakia na jamii takatifu au Wakristo hadi siku 1477 Msemo, ‘Communio sanctorum’ unamaanisha mambo mawili: yaani, Ushirika wa Watakatifu na usharika wa mambo matakatifu kama sakramenti. Luther alizijua maana hizi mbili, lakini aliitilia mkazo maana ya Ushirika wa Watakatifu.
458
54. Licha ya hayo, tunaamini kwamba, katika hili Kanisa la Kikristo, tuna msamaha wa dhambi ambao unatolewa katika sakramenti takatifu, ondoleo la dhambi, na maneno yote yanayofariji ya Injili nzima. Kwa ufupi, kila kitu kinachohubiriwa kuhusu sakramenti, Injili nzima, na wajibu wa Ukristo, kinaelekezwa kwenye msamaha. Msamaha unahitajika kila wakati kwa maana, ingawa neema ya Mungu imepatikana kwa ushindi wa Kristo, na utakatifu umetendwa na Roho Mtakatifu kwa njia ya Neno la Mungu katika umoja wa Kanisa la Kikristo, kwa kuwa bado tunatatizwa na matamanio ya kimwili, tuna dhambi.
55. Hivyo basi, kila jambo katika Kanisa la Kikristo limepangwa kiasi kwamba, tunaweza kupokea msamaha wa dhambi kila siku kwa njia ya Neno na ishara zilizowekwa kufariji na kufufua dhamiri zetu wakati wote tunaishi. Ingawa tuna dhambi, Roho Mtakatifu huhakikisha kwamba, hazituumizi kwa sababu tu katika Kanisa la Kikristo, ambapo kuna msamaha wa dhambi tele. Mungu hutusamehe, nasi tunasameheana, tunavumiliana, na kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.
56. Walakini, nje ya Kanisa la Kikristo, yaani, ambapo hakuna Injili, msamaha wala utakatifu haupo. Kwa hiyo, wote wanaotafuta kuustahilisha utakatifu kwa njia ya matendo yao na siyo kwa njia ya Injili na msamaha wa dhambi, wamejifukuza na kujitenga wenyewe na Kanisa.
57. Wakati uo huo, kwa kuwa utakatifu umeanza na unaendelea kukua kila siku, tunangojea wakati miili yetu itauuwa, itazikwa na uchafu wote, itahuishwa ikiwa yenye utukufu zaidi, na itafufuka katika utakatifu mkamilifu katika maisha mapya na ya milele. 58. Sasa tuko safi na watakatifu nusu tu. Lazima Roho Mtakatifu aendelee kufanya kazi yake ndani yetu kwa njia ya Neno akitusamehe kila siku hadi tutakapoufikia uzima ambapo hapatakuwepo na msamaha tena. Katika maisha haya, kutakuwa na watu safi kikamilifu, watakatifu kabisa, waliojaa wema na haki, wasiokuwa na dhambi, maovu yote, na wasiokufa, wanaoishi katika miili mipya ya milele na iliyotukuzwa.
59. Basi, haya yote ndiyo huduma na matendo ya Roho Mtakatifu. Kuanzisha na kuzidisha utakatifu duniani siku zote kwa njia hizi mbili, Kanisa la Kikristo na msamaha wa dhambi. Kisha, tutakapotoka katika maisha haya, ataukamilisha utakatifu wetu mara moja na atatuhifadhi humo milele kwa njia ya sehemu mbili za mwisho za fungu hili.
459 ya mwisho. Kwa njia ya jamii hii, Roho Mtakatifu hutukusanya, hutufundisha, na kulihubiri Neno. Kwa njia ya jamii hii, yeye huumba na kuzidisha utakaso, akiufanya ukue kila siku, uimarike katika imani, na katika matunda ya Roho.
60. Hata hivyo, maneno “ufufuo wa mwili,” hayakuteuliwa vyema. Sisi Wajerumani tunapoyasikia maneno “Auferstehung des Fleisches” hatulifikirii lolote isipokuwa duka la nyama. Kinahau (maneno yenye maana maalumu), tunaweza kusema, “ufufuo wa mwili.” Hata hivyo, hili si muhimu sana, mradi tu maneno yafahamike vyema.1478
61. Basi, hili ndilo fungu ambalo lazima tulitumie daima. Uumbaji umetimia na wokovu umefanikishwa lakini Roho Mtakatifu anaiendeleza kazi yake siku zote mpaka siku ya mwisho. Kwa hiyo, ameuteua ushirika1479 wake ulimwenguni ambao kwao, ananena na kuzifanya kazi zake zote. 62. Maana, bado hajawakusanya Wakristo wote wala hajaumaliza utoaji wa msamaha. Hivyo, tunamwamini yeye ambaye kila siku anatuleta katika ushirika huu kwa njia ya Neno. Isitoshe, yeye huarifu, huongeza, na huimarisha imani kwa Neno lilo hilo na msamaha wa dhambi. Kazi yake inapokuwa imekwisha na tunakaa katika hiyo, kwa kuwa tutakuwa tumekufa kwa kuutumikia sana ulimwengu na maovu yote, mwishowe yeye atatufanya watakatifu kamili na milele. Sasa tunalingojea hili lifanikishwe kwa imani kwa njia ya Neno.
63. Katika Ukiri huu, asili, mapenzi, na kazi za Mungu zote zimesawiriwa vizuri sana kwa maneno machache lakini yenye nguvu. Katika hayo, kuna hekima yetu yote, ipitayo hekima zote, welekevu, na akili za binadamu. Ingawa ulimwengu wote umejaribu kwa juhudi kubwa kumfahamu Mungu, anayoyafikiria, na anayoyatenda, lakini haujafanikiwa kamwe. Lakini hapa una kila kitu tele. 64. Katika haya mafungu matatu, Mungu mwenyewe ametufunulia na kutufungulia vina vikubwa mno vya moyo wake wa ubaba, upendo wake tu usioelezeka. Yeye alituumba ili atukomboe na atutakase. Aidha, baada ya kutupatia vitu vyote mbinguni na duniani, ametupatia Mwanawe na Roho wake Mtakatifu, ambao kwao, yeye hutuleta kwake. 65. Jinsi tulivyoelezea awali, hatungeweza kutambua kamwe hisani na neema za Baba bila Kristo Bwana ambaye ndiye kioo cha moyo wa Baba. Mbali na yeye, hatulioni lolote isipokuwa hakimu mkali na wa kutisha. Wala hatungeweza kulijua lolote kuhusu Kristo kama Roho Mtakatifu hangemfunua.
66. Kwa hivyo, mafungu haya ya Ukiri wa Imani yanatugawanya na kutubainisha sisi Wakristo na watu wengine wote ulimwenguni. Wapagani, Waturuki,1480 Wayahudi, Wakristo wa uongo, na wanafiki, wote wako nje ya Kanisa la Kikristo. Ingawa wanamwamini, wanamwabudu Mungu mmoja wa 1478 ‘Auferstehung des Fleisches;’ maana yake: ufufuo wa nyama, Kijerumani: ‘Fleisch’ = (nyama). Msemo ‘ufufuo wa mwili’ unafuata kamili shabaha ya maelezo ya Martin Luther. 1479 Kijerumani: ‘Gemeine.’ 1480 Yaani, Waislamu.
460
kweli, hawaujui kamwe mtazamo wake ulivyo kuwahusu. Hawawezi kujiamini kuhusu upendo na baraka zake. Kwa hiyo, wanabaki katika ghadhabu na laana ya milele kwa kuwa hawana Kristo Bwana. Isitoshe, hawajaangazwa na kubarikiwa kwa vipaji vya Roho Mtakatifu.
67. Sasa unaona kwamba, Ukiri wa Imani ni fundisho tofauti sana na Amri Kumi. Amri Kumi hutufundisha tunayopaswa kuyafanya. Ukiri wa Imani hutuambia ambayo Mungu hutufanyia na kutupatia. Aidha, Amri Kumi zimeandikwa katika mioyo ya watu wote. Hakuna hekima ya mwanadamu inayoweza kuufahamu Ukiri wa Imani. Lazima ufundishwe na Roho Mtakatifu peke yake. 68. Kwa hiyo, Amri Kumi zenyewe hazitufanyi Wakristo, kwani ghadhabu za Mungu na hasira zake bado hubaki juu yetu kwa sababu hatuwezi kuyatimiza madai yake. Lakini Ukiri wa Imani huleta neema safi peke yake na utufanya wanyofu na wenye kumpendeza Mungu. 69. Kwa njia ya maarifa haya, tunapenda na kufurahia Amri za Mungu zote kwa sababu tunaona kwamba, Mungu hujitolea mwenyewe kwetu kabisa, kwa njia ya vipaji vyake vyote, nguvu zake, na hutusaidia kuzitimiza Amri Kumi. Baba hutupatia uumbaji wote, Kristo hutupatia kazi zake zote, na Roho Mtakatifu hutupatia vipaji vyake vyote.
70. Kwa sasa, haya yametosha kuhusu Ukiri wa Imani ili watu wa kawaida wawekewe msingi bila kuwalemeza. Baada ya kufahamu maana yake halisi, wanaweza kujifunza zaidi wao wenyewe, wakiyahusisha mafundisho yote ya Katekisimo na wanayojifunza katika Maandiko Matakatifu. Hivyo, waweze kuendelea kuimarika na kukua zaidi katika welekevu. Wakati wote tunaishi, tutakuwa na mambo ya kutosha kuhubiri na kujifunza kuhusu imani.
SEHEMU YA TATU: SALA YA BWANA
1. Tumekwisha kusikia litupasalo kulitenda na kuliamini. Maisha mema zaidi na yenye uheri tele yanakuwa na asili yake katika mambo haya. Inayofuatia sasa ni sehemu ya tatu kuhusu itupasavyo kusali. 2. Wanadamu wako katika hali ambayo hakuna yeyote awezaye kuzitunza Amri Kumi za Mungu kikamilifu ingawa ameanza kuamini. Licha ya hayo, Ibilisi, ulimwengu, na miili yetu, hupingana na jitihada zetu kwa nguvu zote. Kwa sababu hiyo, hakuna jambo ambalo ni la lazima kama kumwita Mungu na kuleta sala zetu masikioni mwake bila kukoma ili aweze kutupatia, kutuhifadhia, na kutuzidishia imani yetu na utiifu kwa Amri Kumi. Pia atatuondolea yote yanayotuzuia kuzitimiza ili tuweze kujua tuombe nini na tusali vipi. 3. Kristo Bwana wetu mwenyewe ametufundisha njia zote mbili na maneno kama tutakavyoona.
4. Kabla ya kuielezea sehemu kwa sehemu ya Sala ya Bwana, lazima kabisa kuwatia moyo na kuwavuta watu katika sala jinsi Kristo na mitume1481 walivyofanya pia. 5. Jambo la kwanza la kufahamu ndilo hili: Ni wajibu wetu kusali kwa ajili ya amri ya Mungu. Tuliambiwa katika amri ya pili: “Usilitaje bure jina la Mungu.” Kwa hiyo, tunapaswa kulitukuza jina takatifu na kuomba au kuliita katika mahitaji yote. Maana, kuliita si lolote bali ni kusali. 6. Hivyo basi, sala imeamriwa kabisa pia kwa uchaji kama amri nyinginezo, kama vile kutokuwa na miungu, kutoua mwingine, kutoiba, na kadhalika. Mtu awaye yote asifikirie kwamba, hakuna tofauti akiomba au asipoomba, jinsi wafanyavyo wapotovu ambao katika kujidanganya kwao husema: “Kwa nini nisali? Nani anajua kama Mungu husikia sala yangu au hujali kuisikia? Nisipoomba, mwingine ataomba.” Hivyo, wao huingia katika desturi ya kutosali kabisa, wakisingizia kwamba, kwa sababu tunakana sala za uongo na unafiki, basi tunafundisha kwamba, hakuna wajibu wala haja ya kuomba.
7. Ni kweli kabisa kwamba, aina ya kubwata na mingurumo iliyohesabiwa kuwa sala kanisani wakati wa maombi haikuwa sala halisi. Ukariri wa nje wa namna hiyo, ungetumika vizuri, unaweza kufaa kwa mazoezi ya watoto wadogo, wanafunzi, na watu wa kawaida. Ingawa unaweza kuitwa wimbo au zoezi la kusoma, lakini si sala ya kweli. 8. Kama amri ya pili inavyofundisha, kusali ni kumwita Mungu katika kila shida. Mungu hulidai hili. Hajaiachia hiari yetu. Ni wajibu na kanuni yetu kuomba ikiwa tunataka kuwa Wakristo, jinsi ilivyo wajibu na kanuni yetu kuwaheshimu baba na mama zetu na mamlaka makuu. Katika maombi na sala, jina la Mungu hutukuzwa na kutumika kwa lengo jema. Tunapaswa kulitazama jambo hili juu ya yote ili tuweze kuyanyamazisha na kuyarudisha nyuma mawazo yoyote yanayoweza kutuzuia na kutukataza kuomba. 9. Isingestahili kijana kumwambia babake: “Inanifaidi nini kuwa mtiifu? Nitaenda nitende ninavyotaka. Kwani kuna tofauti gani?” Lakini amri hii inadumu: “Lazima utatii!” Vivyo hivyo, haijaiachia hiari yangu kusali au kutosali. Ni wajibu na kanuni yangu huku nikichelea ghadhabu na hasira ya Mungu.1482
1481 Mt. 7:7; Lk. 18:1; 21:36; Rum. 12:12; Kol. 4:2; 1 The. 5:17; 1 Tim. 2:1; Yak. 1:6; 5:13; 1 Pet. 4:8; Yud. 20 1482 Aya za 10-11 hazipo katika Toleo la asili la Jena: 12. Haya hayana budi kutiliwa maanani kuhusu mambo yote ili tuweze kunyamazisha na kuyarudisha nyuma mawazo ambayo yangetuzuia au yangetukataza kuomba kana kwamba, haingekuwa tofauti kubwa sana ikiwa hatusali au kana kwamba, sala iliamriwa tu kwa ambao ni watakatifu zaidi na wenye majaliwa ya Mungu kutushinda. Kwa kweli, kwa asili yake, moyo wa mwanadamu ni wenye upotovu wa kukata tamaa kiasi kwamba, kila siku unamtoroka Mungu, ukifikiria kwamba, hataki wala hajali maombi yetu kwa sababu sisi ni wenye dhambi na hatustahili chochote ila ghadhabu. Kinyume chake, ninasema, tunapaswa kuiheshimu amri hii na kumgeukia Mungu tusije tukaighadhabisha hasira yake kwa kutotii kwa namna hiyo. Katika amri hii, yeye anatuhakikishia kwamba, hatatutupa nje wala hatatufukuza
462
12. Kutokana na huu ukweli kwamba, maombi yameamriwa, tunapaswa kutanabahi kwamba, kwa njia yoyote ile, mtu yeyote hapaswi kuyadharau maombi yake bali anapaswa kuyathamini sana. Uchukue mfano kutoka amri nyinginezo. 13. Mtoto asije akadharau kamwe kumtii babake na mamake, lakini kila mara afikirie: “Hili ni tendo la utiifu na lolote nilifanyalo lisiwe na lengo lingine isipokuwa tu kuuafiki utiifu na amri ya Mungu. Ninaweza kulitumainia hili, kulitegemea, na kuliheshimu mno. Si kwa sababu ya dhamana yangu, lakini kwa sababu ya amri.” Ndivyo ilivyo na hapa pia. Inafaa tulihesabu tuliombalo na sababu yake kama lililoamriwa na Mungu lifanyike kwa ajili ya utiifu kwake. Lazima tufikirie: “Kwa ajili yangu binafsi, sala hii haina maana, lakini ni muhimu kwa sababu ni amri ya Mungu.” Hivyo, si hoja aliombalo mtu, kila mmoja lazima amkaribie Mungu daima katika utiifu wa amri hii.
14. Kwa hiyo, tunaharakisha kuomba na kumwonya kila mmoja kuyaweka maneno haya moyoni na asiyadharau maombi kwa njia yoyote ile. Sala ilifundishwa wakati fulani katika jina la Ibilisi kwa kuwa hakuna yeyote aliyeisikiliza. Watu walidhania kwamba, ilitosha ikiwa ilitendwa hata kama Mungu aliisikia au la. Lakini hiyo ni kuingia katika sala kwa kubahatisha na kunung’unika bila lengo lolote. Sala kama hiyo haina thamani. 15. Tunajiruhusu wenyewe kuzuiliwa na kukatazwa na mawazo kama haya: “Mimi si mtakatifu au mstahiki vya kutosha. Kama ningekuwa mchaji na mtakatifu kama Mt. Petro au Mt. Paulo, basi ningeomba.” Yaache kabisa mawazo kama hayo! Amri iyo hiyo iliyomfaa Mt. Paulo inanifaa hata mimi. Amri ya pili ilitolewa kwa ajili yangu sawasawa na kwa ajili yake. Hawezi kujisifia amri nzuri zaidi au takatifu zaidi kuliko mimi. 16. Kwa hivyo, inafaa useme: “Sala niitoayo ni yenye thamani, takatifu, na inampendeza Mungu kama zile za Mt. Paulo aliye mtakatifu zaidi miongoni mwa watakatifu. Hii ndiyo sababu: Ninakubali wazi kwamba, yeye ni mtakatifu zaidi kwa kuuhesabu utu wake, lakini si kwa sababu ya amri. Mungu hatazami maombi kwa ajili ya mtu bali ni kwa ajili ya Neno lake na kwa ajili ya kulitii. Juu ya amri hii, ambayo sala za watakatifu wote zinaitegemea, nami zangu zitaitegemea pia. Aidha, ninaliombea lile lile waliloliombea wote.”
17. Hili ni jambo la kwanza muhimu sana kwamba, maombi yetu yote yautegemee utiifu kwa Mungu bila kuangalia utu wetu, tuwe wenye dhambi, watakatifu, wafaao, au wasiofaa. 18. Tujifunze kwamba, Mungu hataki amri hii ichukuliwe kama mzaha, ila ataghadhabika na kutuadhibu tusipoomba ingawa tu wenye dhambi. Badala yake, anapenda kutuvutia kwake mwenyewe ili tujinyenyekeze mbele zake, tuuomboleze unyonge wetu na hali yetu mbaya, na tuiombe rehema na nusura. Hivyo, tunasoma katika Maandiko Matakatifu kwamba, yeye ana hasira kwa sababu waliopigwa kwa ajili ya dhambi zao hawakumrudia ili waitulize ghadhabu yake na waitafute neema kwa sala zao.
jinsi anavyoyaadhibu maasi mengine yote. Wala hatayaruhusu maombi yetu yabatilishwe au yapotee, kwani kama hakuwa tayari kukujibu, hangekuamuru kuomba na kisha kuifuatisha amri kali jinsi hii. 19. Jambo la pili, sisi sote tunapaswa kuwa na hamu kubwa na kutiwa moyo kusali kwa sababu Mungu ametuahidi kwamba, sala zetu zitajibiwa hakika, kama asemavyo katika Zab. 50:15: “Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa,” naye Kristo anasema katika Mt. 7:7-8: “Ombeni, nanyi mtapewa” . . .“Kwa maana kila aombaye hupokea.” 20. Kwa kweli, ahadi kama hizi zinafaa ziamshe hamu na upendo wa kusali katika mioyo yetu. Kwani Mungu, kwa Neno lake hushuhudia kwamba, sala zetu zinampendeza na kwa hakika zitasikika na kukubaliwa, ili tusije tukaidharau, tukaibeza, au tukasali kwa mashaka. 21. Hivyo, unaweza kumkabili nalo na kusema: “Naja kwako ee Baba mpendwa na kusali, si kwa hiari yangu au kwa ustahiki wangu mwenyewe, bali kwa amri na ahadi yako, ambayo haiwezi kuniadimikia au kunidanganya.” Mtu awaye yeyote asiyeamini ahadi hii, kwa mara nyingine anapaswa kufahamu kwamba, anamkasirisha Mungu, anapomdharau sana na kumshtaki kuwa mwongo.
22. Licha ya hayo, tunapaswa kutiwa moyo na kuvutiwa kuomba kwa sababu, zaidi ya amri na ahadi hii, Mungu hulichukua jukumu la kuyaweka vinywani mwetu maneno tuyatumiayo kusali. Hivyo, tunaona jinsi alivyo mwaminifu kweli kwa kujihusisha na mahitaji yetu. Hatuwezi kuwa na shaka kamwe kwamba, sala yetu inampendeza na kwa hakika ataisikia. 23. Hivyo, sala hii ni kubwa kushinda nyingi zote tunazoweza kuzitunga wenyewe. Kwani katika hiyo ya mwisho, dhamiri zetu zitakuwa na mashaka zikisema, “Nimesali, lakini nani anayefahamu kama imempendeza, au nimeufikia utaratibu na mwelekeo ulio bora?” Yaani, hakuna sala iliyo kuu ulimwenguni kuishinda, kwani ina ushuhuda bora zaidi kwamba, Mungu hupenda kuisikia. Hatupaswi kuibadilisha na mali zote ulimwenguni.
24. Kwa sababu hii, imeagizwa pia kwamba, tunapaswa kutafakari kuhusu mahitaji yetu ambayo yanafaa kutuvuta na kutushurutisha kusali bila kukoma. Mtu anayetaka kusali lazima aonyeshe haja yake, ataje na aombe analolitaka; la sivyo, haitakuwa sala. 25. Hata hivyo, kwa haki tumezikataa sala za wamonaki/ watawa wa kiume na makasisi wanaosoma na kunguruma kwa hofu mchana na usiku. Hakuna hata mmoja wao anayefikiria kuliomba hata lililo dogo sana. Kama tungeweza kukusanya makanisa yote na mapadre wote, wangeweza kuungama kwamba, hawakupata kusali kwa moyo wote kwa ajili ya hata tone moja la divai. Hakuna hata mmoja wao aliyechukua jukumu la kusali kwa ajili ya utiifu kwa Mungu na kwa kuamini ahadi zake au kutokana na fikira kuhusu mahitaji yake
464
mwenyewe. Licha ya hayo, walifikiria kutenda mema kama malipo kwa Mungu bila kuwa na nia ya kulipokea lolote kutoka kwake, bali kumpatia kitu tu.
26. Lakini, palipo na sala ya kweli lazima pawe na uhalisi. Lazima tuyahisi mahitaji yetu, shida inayotuhimiza, na kutusukuma kulia. Ndipo, sala itatoka kwa hiari ipasavyo, na hatutahitaji kufundishwa jinsi ya kujitayarisha kwayo au jinsi ya kuuamsha uchaji. 27. Hitaji linalotuhusu sisi na wengine limeonyeshwa dhahiri katika Sala ya Bwana. Kwa hiyo, inaweza kutukumbusha na kututia moyo tusije tukawa wazembe kusali. Sote tuna upungufu wa kutosha, lakini shida ni kwamba, hatuuhisi wala kuuona. Basi, Mungu anakutaka uomboleze na uzielezee haja na matakwa yako. Si kwamba, hayajui bali ili uweze kuufanya moyo wako uyachangamkie matakwa magumu na makubwa zaidi, kisha ulikinge joho lako na kulipanua ili uyapokee mengi.
28. Kutoka ujana wake, kila mmoja wetu anapaswa kuikuza tabia ya kusali kila siku kwa ajili ya mahitaji yake yote. Wakati wowote atambue lolote linalomsumbua au linalowasumbua wengine katika mazingara yake, kama vile wahubiri, mahakimu, majirani, na watumishi. Jinsi tulivyosema, kila mara mtu anapaswa kumkumbusha Mungu amri na ahadi zake, akijua kwamba, hazitapuuzwa. 29. Ninalisema hili kwa sababu ningependa kuona watu wakirudishwa katika kusali vizuri. Wasiyatende mambo bila adabu na kwa mzizimo hata wakawa wapuuzi wa maombi siku kwa siku. Haya tu ndiyo mapenzi ya Ibilisi nayo ndiyo anayoyashughulikia kwa nguvu zake zote. Maana, anafahamu vizuri sana uharibifu na madhara anayoyapata wakati maombi yanatumika vizuri.
30. Lazima tulifahamu hili kwamba, usalama na ulinzi wetu uko katika sala tu. Sisi tu dhaifu sana. Hatuwezi kushindana na Ibilisi, nguvu zake zote, na majeshi yake ambayo yamepangwa dhidi yetu kujaribu kutukanyagia chini ya miguu yao. Kwa hiyo, ni lazima Wakristo wachague, kwa uangalifu sana, silaha zinazowafaa kuzitumia ili waweze kusimama dhidi ya Ibilisi. 31. Je, unafikiri ni lipi lililoleta matokeo makubwa jinsi hii, wakati uliopita, ili kukinga makusudi hila za maadui zetu na kukomesha nia zao zinazofisha na kuleta uasi wao ambao kwao, Ibilisi alitazamia kutuponda na Injili? Licha ya hayo, maombi ya wacha Mungu wachache yamesimama upande wetu kama ukuta wa chuma? La sivyo, wangeshuhudia matukio tofauti sana: Ibilisi angekuwa ameiharibu Ujerumani katika damu kabisa. Sasa wanaweza kudhihaki na kusimanga kwa uthabiti. Lakini kwa sala peke yake tutawashinda wao na Ibilisi, ikiwa tu tutavumilia kwa juhudi na bila kuwa walegevu. 32. Kwani, wakati wowote Mkristo mchaji akiomba: “Ee Baba, mapenzi yako yatimizwe,” Mungu hujibu kutoka juu: “Ndiyo, mwanangu mpendwa, yatatimizwa licha ya Ibilisi na ulimwengu wote.”
465
33. Liache hili lisemwe kama jambo la maonyo ili watu wapate kujifunza kuhusu yote, waithamini sala kama kitu bora na chenye manufaa makubwa, watofautishe kikamilifu kati ya kupayukapayuka na kusali kwa ajili ya kitu kikamilifu. Kwa njia yoyote, hatuikatai sala, lakini tunashutumu kabisa kilio kikali na manung’uniko yasiyokuwa na maana, jinsi Kristo mwenyewe anavyoyakataa na kuyakataza maneno mengi. 34. Sasa tutaielezea Sala ya Bwana kwa ufupi na dhahiri kabisa. Katika mafungu au maombi saba yanayofuatana, kunatambuliwa mahitaji yote yanayotusumbua, na kila moja ni kubwa kiasi cha kutushurutisha kuliomba bila kukoma katika maisha yetu yote.
OMBI LA KWANZA
35. “Jina lako litakaswe”
36. Sentensi hii si dhahiri wala si nahau (maneno yenye maana maalumu) safi ya Kijerumani. Katika lugha yetu tungesema: “Baba wa Mbinguni, ruhusu kwamba, jina lako peke yake liwe takatifu!” 37. Lakini kusali kwamba, jina lake litakaswe kunamaanisha nini? Je, jina hilo si takatifu tayari? Jibu: Ndiyo, lenyewe ni takatifu lakini siyo jinsi tunavyolitumia. Tulipewa jina la Mungu tulipofanywa Wakristo wakati wa Ubatizo. Hivyo, tunaitwa watoto wa Mungu na tunazifurahia sakramenti, ambazo kwazo, mwenyewe anatushirikisha ili lolote lake liwe kwa ajili ya huduma yetu. 38. Hivyo, tunapaswa kutambua kwamba, tunalazimika pakubwa kuliheshimu jina la Mungu, kulitukuza, kulifanya takatifu ipasavyo, kulihesabu kuwa tunu kuu, na lililo takatifu kuliko yote tuliyo nayo. Tusali kama watoto wazuri kwamba, jina lake ambalo tayari ni takatifu huko mbinguni, litakaswe nasi duniani na ulimwenguni kote.
39. Linatakaswaje miongoni mwetu? Jibu wazi kabisa ni: Wakati mafundisho na maisha yetu yanakuwa ya kimungu na ya Kikristo. Kwa kuwa, katika sala hii, tunamwita Mungu Baba yetu. Ni wajibu wetu kuwa na tabia ya watoto wazuri, katika njia zote, ili aweze kuipokea heshima na sifa kutoka kwetu badala ya fedheha. 40. Sasa, jina la Mungu linanajisiwa nasi katika maneno au matendo. Yote tuyafanyayo ulimwenguni yanaweza kuainishwa kama neno au tendo, maneno, au matendo. 41. Kwanza, linanajisiwa watu wanapohubiri, wanapofundisha, na wanaponena lolote lisilokuwa la kweli, wakilitumia jina la Mungu, ili kuupamba uongo na kuufanya ukubalike. Hii ndiyo njia mbaya kuliko zote ya kulinajisi na kulifedhehesha jina lililo takatifu. 42. Vivyo hivyo, linanajisiwa wakati watu wanalitumia jina la Bwana isivyofaa ili kusetiri aibu yao kwa kuapa, kulaani, kufanya mizungu na kadhalika. 43. Linanajisiwa pia
466
kwa kuishi maisha machafu na matendo maovu hadharani, wakati waitwao Wakristo na watu wa Mungu wanakuwa waasherati, walevi, walafi, wenye wivu, na wenye kukashifu. Hapa tena jina la Mungu hunajisiwa na kukufuriwa kwa sababu yetu. 44. Jinsi ilivyo aibu na fedheha kwa baba wa kimwili kuwa na mtoto mbaya mkaidi, anayemchokoza kwa maneno na matendo akiwa na sababu kwamba, kwa ajili yake, baba hupata dharau na shutuma. Hivyo ndivyo Mungu anavyodharauliwa iwapo sisi tunaoitwa kwa jina lake na tunaofurahia baraka zake nyingi, tutashindwa kufundisha, kunena, na kuishi kama watoto wachaji wa mbinguni. Matokeo yake yatakuwa kwamba, atasikia tukiitwa watoto washenzi wa Ibilisi badala ya kuitwa watoto wa Mungu.
45. Kwa hiyo, unaona kwamba, katika ombi hili, tunaomba moja kwa moja jambo lilo hilo ambalo Mungu analidai katika Amri ya Pili: kwamba, jina lake lisitajwe bure kwa kuapa, kulaani, na kudanganya. Badala yake, litumike ipasavyo kwa sifa na utukufu wa Mungu. Mtu awaye yote akilitumia jina la Mungu kwa lolote baya, hulinajisi na kulikufuru jina hili takatifu. Ilivyokuwa zamani ni kwamba, Kanisa lilisemekana kunajisiwa iwapo mauaji au uhalifu wa aina yoyote ulifanyiwa humo, na wakati chombo cha mkate wa maonyesho,1483 kwa ajili ya kusujudu au masalio1484 yalinajisiwa. Hivyo, kukifanya kichafu ambacho chenyewe ni kitakatifu kwa matumizi mabaya. 46. Basi, ombi hili ni rahisi na wazi mara tu tukielewa lugha kwamba, “kutakasa” katika lugha yetu kunamaanisha, “kusifu, kuhimidi, na kuheshimu” kwa maneno na matendo. 47. Tazama jinsi haja ya sala ya namna hii ilivyo kuu! Kwa kuwa, tunaona kwamba, ulimwengu umejaa madhehebu na waalimu wa uongo. Hao wote hulivalia jina takatifu kama joho na kama haki ya mafundisho yao ya kiibilisi. Lazima tupige kelele bila kukoma dhidi ya wote wanaohubiri na kuamini uongo. Pia lazima 1483 Kilatini: ‘ostensorium,’ Kingereza: ‘Monstrance;’ chombo maalumu cha mikate ya Ekaristi iliyobarikiwa ambayo ilibaki baada ya misa. Kwanza, mikate hii iliabudiwa kama mwili wa Kristo katika chombo cha kawaida cha mikate, yaani ‘ciborium.’ Baadaye, mikate hii iliyobarikiwa iliwekwa katika chombo chicho hicho maalumu, yaani, ‘ostensorium.’ Akina Baba Walutheri wa Matenegenezo ya Kanisa walifundisha kikamilifu kwamba, mikate na divai iliyobarikiwa wakati wa Chakula cha Bwana viishe kabisa wakati wa ibada. Hata hivyo, masalio yoyote ya mikate au divai iliyobarikiwa kuwa sakramenti, yawekwe kwa heshima katika vyombo maalumu ili yatumiwe katika ibada nyingine itakayofuatia. Historia ya mzozo wa Mch. Simon Wolferinus katika mji wa Eisleben, huko Ujerumani mwaka wa 1543, inatuelezea mambo haya kuhusu matumizi ya liturgia ya sakramenti. Martin Luther aliyarekebisha vikali mafundisho ya Wolferinus katika barua zake mbili: Mchungaji akitaka kuongezea mikate au divai wakati wa Chakula cha Bwana, hana budi kusema maneno ya mwanzoni tena kwa sauti. Wachungaji wazimalize elementi za sakramenti wakati wa ibada. Isipowezekana, masalio ya sakramenti–‘reliquum sacramenti’–yatunzwe kwa heshima, kwa kuwa masalio haya pia yanaendelea kuwa sakramenti baada ya matumizi hayo. WA Bfw. 10, 3888, uk. 340. WA Bfw. 3894, uk. 347 nk.
1484 Kilatini: ‘scrinium,’ Kingereza: ‘shrine,’ sanduku maalumu katika kanisa au mahali pa hija lenye masalio ya watakatifu. Akina Baba wa Matengenezo ya Kanisa waliiacha ibada ya masalio kwa kuwa ilikuwa ibada ya sanamu.
467
tupige kelele dhidi ya wanaoishambulia na kuitesa Injili yetu, mafundisho yetu safi, na kujaribu kuikandamiza, jinsi wafanyavyo maaskofu, wadhalimu, walokole, na wengineo. Kadhalika, ombi hili ni kwa ajili yetu tulio na Neno la Mungu, lakini ambao hatuna shukrani na tunashindwa kuishi ipasavyo kwalo. 48. Ukilisali ombi hili kwa moyo wote utakuwa na hakika kwamba, Mungu anapendezwa. Kwani, hakuna lingine lolote ambalo angependa kulisikia kuliko kupewa utukufu wake, sifa yake kuinuliwa juu ya yote, Neno lake kufundishwa katika usafi, kutunzwa, na kuthaminiwa.
OMBI LA PILI
“Ufalme wako uje”
49. Tuliomba katika sehemu ya kwanza kuhusu heshima na jina la Mungu kwamba, aweze kuuzuia ulimwengu usiutumie utukufu wake na jina lake ili kusetiri uongo na maovu yake. Badala yake, jina lake litakaswe na liheshimiwe sana kwa mafundisho na katika maisha ili apate kusifiwa na kukwezwa miongoni mwetu. Hapa tunaomba kwamba, ufalme wake uje. 50. Jinsi jina la Mungu lenyewe lilivyo takatifu, bado tunaomba liwe takatifu miongoni mwetu. Vivyo hivyo, ufalme wake huja wenyewe bila sala zetu na bado tunauomba uje kwetu. Yaani, tunauomba uweze kudumu na kuenea miongoni mwetu ili tuweze kuwa sehemu ya ambao kwao, jina lake linatakaswa na ufalme wake unastawi.
51. Je, ufalme wa Mungu ni nini? Jibu: Ni yale tuliyojifunza tu katika Ukiri wa Imani. Yaani, Mungu alimtuma ulimwenguni mwanawe, Kristo Bwana wetu, kutuokoa na kutuweka huru kutokana na nguvu za Ibilisi na kutuleta kwake mwenyewe ili atutawale kama mfalme wa haki, wa uzima, na wa wokovu dhidi ya dhambi, mauti, na dhamiri mbaya. Alitupatia Roho Mtakatifu wake pia kutufundisha hili, kutuangaza, na kutuimarisha katika imani kwa nguvu yake kupitia Neno lake takatifu. Kwa sababu hiyo, mwanzoni tunaomba kwamba, haya yote yanaweza kufanikishwa miongoni mwetu na kwamba, jina la Mungu lipate kusifiwa kwa njia ya Neno lake takatifu na katika maisha yetu ya Kikristo. 52. Tunaliomba hili, ili sisi ambao tumeliamini, tubakie kuwa waaminifu na kukua siku kwa siku ndani yalo, na ili lipate kutambuliwa na kuwavutia wafuasi miongoni mwa watu wengine, na kuendelea kwa nguvu ulimwenguni kote. Hivyo, tunaomba kwamba, wengi wanaweza kufika kwenye ufalme wa neema, na kuwa washiriki wa wokovu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu ili sisi sote tuweze kubakia pamoja milele katika ufalme huu ambao umeonekana sasa miongoni mwetu.
468
53. Ufalme wa Mungu hutujia kwa njia mbili: kwanza, ufalme huu hutujia hapa wakati wa dahari hii kwa njia ya Neno na imani; pili, unatujia kupitia ufunuo wa mwisho1485 milele. Sasa tunayaombea haya mawili kwamba, ufalme uwajie ambao bado hawako ndani yake na kwamba, uweze kutujia tulio ndani yake kwa njia ya kukua kila siku, na baadaye katika uzima wa milele. 54. Haya yote ni sawa na kusema tu: “Ee, Baba mpendwa! Tunakusihi, utupe Neno lako, ili Injili ipate kuhubiriwa kwa uaminifu ulimwenguni kote; iweze kupokelewa kwa imani na iweze kufanya kazi yake na kuishi ndani yetu. Hivyo, tunaomba kwamba, ufalme wako uweze kuenea miongoni mwetu kwa njia ya Neno na nguvu ya Roho Mtakatifu kwamba, ufalme wa Ibilisi uangushwe na asiwe na haki au nguvu juu yetu, mpaka hatimaye ufalme wa Ibilisi utakapoangamizwa kabisa. Isitoshe, mpaka dhambi, mauti, na Jehanumu imalizwe, nasi tupate kuishi milele katika haki na heri iliyokamilika.”
55. Unaona hapa kwamba, hatuuombi ukoko wa mkate au sadaka ya maskini au mali za muda zinazoharibika. Tunaomba hazina ya milele yenye gharama kuu na kila kitu alicho nacho Mungu mwenyewe. Lingekuwa jambo lililo kuu sana kwa moyo wa mtu kuthubutu kuwa na shauku nayo ikiwa Mungu mwenyewe hakutuamuru tuiombe. 56. Lakini kwa kuwa yeye ni Mungu, anadai heshima ya kutoa kwa wingi zaidi na kwa ukarimu kuliko mtu awaye yote anavyoweza kuelewa, kama chemchemi ya milele isiyomalizika, ambayo kadiri inavyozidi kububujika na kufurika, ndivyo inavyozidi kutoa. Kutoka kwetu, Yeye hataki lingine lolote zaidi ya kuomba vitu vingi na vikubwa kutoka kwake. Kinyume chake, anaudhika iwapo hatuombi na kudai kwa kujiamini. 57. Mfikirie Kaisari tajiri sana na mwenye mamlaka mengi mno ambaye amemwalika mwombaji maskini kuomba lolote ambalo angependa kuwa nalo naye yu tayari kumpa zawadi kubwa ya kifalme. Huyo mpumbavu amwombe tu bakuli la supu ya maskini.1486 Kwa kweli, angechukuliwa kama jangili na mlaghai aliyeidhihaki amri ya Enzi ya Kaisari na asiyestahili kufika mbele yake. Vivyo hivyo, ni aibu kubwa na fedheha kwa Mungu ikiwa sisi ambao ametuahidi na kutupatia dhamana ya baraka zisizoweza kuelezeka, tutazidharau au tutakosa kujiamani kwamba, tutazipokea, na kwa nadra, tutathubutu kuomba mmego wa mkate. 58. Hatia inategemea kabisa ule upungufu wa imani wenye fedheha usiomtazamia Mungu hata kwa kidogo kishibishacho tumbo, licha ya kutegemea baraka za milele kutoka kwa Mungu bila mashaka. Basi, lazima tujiimarishe wenyewe dhidi ya kutoamini na tuuruhusu ufalme wa Mungu kuwa jambo la kwanza la kuomba. Ndipo kweli, tutapata tele vitu vingine vyote jinsi afundishavyo Kristo: 1485 Yaani, ufunuo wa Kristo atakapokuja mara ya pili. 1486 Aina ya supu rojorojo iliyopatikana tayari katika majumba ya kifalme kwa ajili ya waombaji.
469
“Utafuteni kwanza ufalme wake, na hayo yote mtazidishiwa.”1487 Kwani Mungu angeturuhusuje tuteseke kwa kukosa vitu vinavyoharibika wakati ametuahidi kile cha milele kisichoharibika?
OMBI LA TATU
59. “Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni”
60. Kufikia sasa, tumeomba kwamba, jina la Mungu litakaswe nasi na ufalme wake uenee miongoni mwetu. Mambo haya mawili hujumuisha yale yote yanayohusu utukufu wa Mungu na wokovu wetu, ambao kwao, tunamfaa Mungu na hazina zake zote. Lakini bado kuna hitaji kubwa linalotutaka tuyatunze mambo haya mawili kwa makini na tusijiruhusu wenyewe kutenganishwa nayo kamwe. 61. Katika serikali bora, kuna haja ya kuwa na wajenzi, watawala, watetezi, walinzi, na walezi waangalifu. Kadhalika, japo tumeomba kwa ajili ya yaliyo muhimu sana–Injili, imani, na Roho Mtakatifu ili aweze kututawala sisi tuliokombolewa kutoka kwa mamlaka ya Ibilisi–lazima tuombe ili mapenzi ya Mungu yafanyike. Tukijaribu kuzishikilia sana hazina hizi, lazima tuumie kwa njia ya mashambulizi na uvamizi wa kushangaza kutoka kwa wote wanaothubutu kuzuia na kuzipinga ahadi za utimizaji wa maombi mawili ya kwanza.
62. Ni jambo lisiloaminika jinsi Ibilisi anapinga na kuzuia utimizaji wa hayo maombi. Hawezi kuvumilia mtu yeyote aamini au afundishe inavyotakiwa. Inamwumiza zaidi wakati uongo na machukizo yake yenye kuheshimiwa, hufunuliwa, huwekwa wazi kwa aibu yote, hutolewa nje ya mioyo ya wanadamu, na wakati ufa hutokea katika ufalme wake chini ya visingizio vya kujipendekeza sana vya jina la Mungu. Kwa hiyo, sawa na adui mwenye hasira, hughadhabika, hupayapaya kwa nguvu na uwezo wake wote. Isitoshe, huwaongoza wafuasi wake wote, huushirikisha ulimwengu, na miili yetu yenyewe kama wasaidizi wake. 63. Kwa maana, miili yetu yenyewe ni yenye uovu na hujisalimisha kwa mwovu, hata tunapokuwa tumeliamini Neno la Mungu. Kadhalika, ulimwengu wote ni mkaidi na mpotovu. Huyavuruga haya kwa kuipepea na kuichochea miale ili kutuzuia, kutufukuza, kutujeruhi, na kutufanya tuwe chini ya himaya yake kwa mara nyingine tena. 64. Hii ndiyo shabaha, matakwa, na wazo lake la pekee. Kwa ajili hii, anakazana usiku na mchana bila kupumzika, akitumia sanaa, hila, njia, na mbinu yoyote awezayo kuibuni.
65. Tukitaka kuwa Wakristo, tutapaswa kujua hakika kwamba, Ibilisi, malaika
1487 Mt. 6:33; Lk. 12:31
wake wote,1488 na ulimwengu ni maadui wetu ambao hututesa kwa kila msiba na huzuni. Kwa maana, mahali Neno la Mungu linahubiriwa, linakubaliwa, linaaminiwa, na linazaa matunda, hapo msalaba mtakatifu hautakuwa mbali. Basi, mtu yeyote asifikirie kwamba, atakuwa na amani. Lazima atakitoa kila kitu alicho nacho ulimwenguni, yaani, mali, heshima, nyumba, makazi, mke, watoto, mwili, na uhai. 66. Sasa, hili huuzunisha mwili na Adamu wetu wa kale. Kwa hiyo, inamaanisha kwamba, lazima tubaki kuwa imara, tuvumilie mateso yoyote yanayotujia, na tukiruhusu chochote kinachochukuliwa kutoka kwetu.
67. Kwa hiyo, kuna hitaji ilo hilo katika suala hili jinsi lilivyo katika masuala mengine, yaani, kusali bila kukoma: “Mapenzi yako yatimizwe, Babangu mpendwa, na siyo mapenzi ya Ibilisi au maadui wetu, na wala si ya hao watakaolitesa na kuligandamiza Neno lako takatifu au kuuzuia ufalme wako usije. Utujalie tuweze kuvumilia na kushinda kwa utulivu ili miili yetu maskini isijisalimishe au isianguke kwa ajili ya udhaifu au uzembe katika yale tutakayolazimika kuteswa kwayo.”
68. Kumbuka kwamba, katika maombi haya matatu, maslahi yanayomhusu Mungu mwenyewe yameelezewa kwa urahisi sana. Hata hivyo, tumesali kwa niaba yetu wenyewe. Tuyaombayo yanatuhusu wenyewe tu tunapoomba kwamba, vinginevyo yanayoweza kufanyika bila sisi, yaweze kufanyika pia katika sisi. Jinsi jina la Mungu lazima litakaswe na ufalme wake lazima uje, hata pasipo sala yetu, vivyo hivyo, mapenzi yake lazima yafanyike na kudumu ingawa Ibilisi na jeshi lake lote litatushambulia na kughadhabishwa vikali dhidi ya ufalme katika kujaribu kabisa kuitangua Injili. Lakini kwa ajili yetu wenyewe, lazima tuombe kwamba, mapenzi yake yatendeke kwetu bila kizuizi, bila kujali ghadhabu yao ili wasiweze kuambulia lolote, na tubaki kuwa imara mbele ya vurugu na mateso tukiyanyenyekea mapenzi ya Mungu.
69. Sasa, ombi kama hilo lazima liwe kinga na ngao yetu katika kufukuza na kuponda yote ambayo Ibilisi, maaskofu, wadhalimu, na waasi wanaweza kuyatenda dhidi ya Injili yetu. Waacheni waghadhabike, watende ubaya wao kupindukia, wale njama, wapange jinsi ya kutukandamiza na kutuangamiza ili mapenzi na hila zao ziweze kushinda. Mkristo mmoja au wawili wakijihami kwa sala angalau moja, watakuwa boma letu ambalo kwalo, wengine watajivunja vipandevipande. 70. Ni faraja na majivuno yetu kwamba, mapenzi, makusudi ya Ibilisi, na ya maadui wetu wote lazima yashindwe na kuwa batili haidhuru yalivyo na kiburi, salama, na yenye nguvu. Kwa maana, mapenzi yao yasingevunjwa na kukatishwa tamaa, ufalme wa Mungu usingedumu duniani wala jina lake 1488 Mt. 25:41
halingetakaswa.
OMBI LA NNE
71. “Utupe leo mkate wetu wa kila siku”
72. Hapa tunafikiria kapu tupu la mkate. Yaani, mahitaji ya miili yetu na maisha yetu hapa ulimwenguni. Neno hili ni fupi na rahisi lakini lenye maana pana. Unapoomba “mkate wa kila siku,” unaomba kila kitu cha lazima ili upate na ufurahie mkate wa kila siku. Kinyume chake, ni lazima tuombe dhidi ya kila kitu ambacho huingilia furaha yetu. Hivyo, lazima uyapanue na uyakuze mawazo yako yafikirie joko au pipa la unga/kapu la mkate, mashamba makubwa, na nchi nzima inayozaa na kuutoa mkate wetu wa kila siku na aina zote za riziki. Kwa maana, kama Mungu hangeiruhusu ngano/nafaka kukua, hangeibariki, na hangeitunza shambani, hatungeupata mkate wa kuuandaa mezani kutoka jokoni.
73. Kwa ufupi, sala hii inajumlisha kila kitu ambacho kinahusiana na maisha yetu katika ulimwengu huu. Kwa ajili ya hayo, tunahitaji mkate wa kila siku. Hivyo sasa, maisha yetu hayahitaji chakula, mkate, na mahitaji mengine kwa ajili ya miili yetu.1489 Vile vile yanahitaji amani, maelewano katika shughuli zetu za kila siku, na katika ushirikiano wa kila maelezo na watu wengine ambao tunaishi na kutenda mambo nao. Kwa ufupi, kila kitu kinachohusiana na taratibu za nyumbani mwetu, masuala yetu ya raia au ya kisiasa. Kwa maana, mahusiano haya mawili yanapoingiliwa na kuzuiwa kutenda kazi ipasavyo, hapo mahitaji ya lazima ya maisha yanaingiliwa, na maisha yenyewe hayawezi kudumishwa kwa kipindi chochote kirefu. 74. Naam, hitaji kubwa zaidi kushinda yote ni kuiombea serikali yetu na wenye mamlaka makuu. Kwa maana, kupitia kwao hasa, Mungu hutupatia mkate wetu wa kila siku na faraja zote za maisha haya. Japo tumepokea tele mambo yote mazuri kutoka kwa Mungu, hatuwezi kubakiza mojawapo au kuyafurahia kwa usalama na furaha mpaka atupatie serikali imara na yenye amani. Maana, ambapo pana mfarakano, mapambano, na vita, hapo mkate wetu wa kila siku hupunguzwa au huondolewa kabisa.
75. Kwa hiyo, ingefaa iwapo nembo ya kila mtawala mchaji ingepambwa kwa boflo ya mkate badala ya simba au shada la waridi au boflo ya mkate kupigwa chapa sarafuni ili kuwakumbusha watawala na wafuasi wao kwamba, tunafurahia ulinzi na amani kwa njia ya huduma zao. Si hivyo tu, bila wao, hatungekuwa na chakula au baraka thabiti za mkate mtamu wa kila siku tuupendao.1490 Watawala
1489 1 Tim. 6:8 1490 Taswira ya nembo ya mkoa wa Sachsen ilikuwa ni shada la waridi, taswira ya nembo za mikoa ya
wanastahili heshima zote, na tunalazimika kuitoa huduma yoyote itupasayo na kutenda tuwezalo kwa ajili yao. Kwa maana, tunafurahia mali zetu kwa amani na utulivu kwa ajili yao. Vinginevyo, hatungeweza kuitunza hata sarafu moja. Aidha, tunapaswa kuwaombea kwamba, kwa ajili yao, Mungu aweze kutumiminia zaidi baraka na mambo mazuri.
76. Acheni tuorodheshe kwa ufupi jinsi ombi hili linavyojumlisha kwa undani mahusiano yote ulimwenguni. Bila ombi hili, mtu anaweza kuitoa sala ndefu, akiorodhesha kwa maneno mengi, mambo yote inayoyajumlisha. Kwa mfano, tunaweza kumwomba Mungu atupatie chakula, kinywaji, nguo, nyumba, kaya, afya njema, na awezeshe ngano/nafaka na matunda ya shambani kukua na kuzaa tele. Isitoshe, tunaweza kumwomba atusaidie kuzitunza jamaa zetu vyema, atupatie na awahifadhi wake, watoto, na watumishi wazuri. Aziwezeshe kazi zetu, ufundi au shughuli, iwayo itakavyokuwa, kustawi na kufanikiwa. Atupatie majirani waaminifu na marafiki wazuri na kadhalika. 77. Tena, tunamwomba Mungu awajalie busara, nguvu, na ufanisi Kaisari, wafalme, vyeo vyote vya heshima, hasa watawala, mawakili, mahakimu, na maofisa wetu watawale vizuri na kuwashinda Waturuki na maadui wetu wote.1491 Awawezeshe watawaliwa wao na watu wote kwa jumla kuishi pamoja kwa unyenyekevu, amani, na maelewano. 78. Kwa upande mwingine, atukingie shida zozote dhidi ya miili, na maisha yetu kutokana na dhoruba, mvua ya mawe, moto, mafuriko, sumu, ndwele yoyote yenye kufisha, tauni, vita, umwagaji damu, njaa, wanyama wakali, na watu waovu. 79. Ni vyema kuwahimiza watu wa kawaida wote ili wajue kwamba, vitu hivi vyote hutoka kwa Mungu na ni lazima tuviombe.
80. Lakini ombi hili hasa limeelekezwa dhidi ya adui wetu mkuu, yaani, Ibilisi, ambaye nia na tamaa yake kubwa ni kuyaondoa au kuyaingilia yote tuliyoyapokea kutoka kwa Mungu. Haridhiki kuyapinga na kuyapindua mamlaka ya kiroho ili aweze kuwadanganya watu kwa uongo wake na kuwaweka chini ya uwezo wake. Lakini pia, yeye huzuia na kukwamisha uanzishwaji wa serikali yoyote au mahusiano ya amani na ya kuheshimika duniani. Hii ndiyo sababu inayomfanya asababishe ubishi, mauaji, uasi, na vita. Ndiyo sababu anatuma
Meissen na Thüringen ilikuwa ni simba. Sarafu za mikoa ya Sachsen na Braunschweig zilikuwa na alama ya simba.
1491 Dola la Uturuki au Dola la Waotomani lilianzishwa na Mfalme Osman I Ghasi (1258-1326) na liliendelea hadi mwaka wa 1922. Waturuki waliziteka sehemu nyingi za Uarabuni, Misri na Ulaya. Mwaka wa 1453, Waturuki walilishinda na walilimaliza kabisa Dola la Baizantio (Konstantinopoli, siku hizi Istanbul). Kaisari wa Uturuki waliziteka nchi zote za Balkani na mara nyingi, waliitishia Austria na sehemu za moyo wa Ulaya. Tisho hili lilikuwa pia la kidini kwa sababu Waturuki waliueneza Uislamu kwa nguvu. Basi, mapigano haya yalikuwa kati ya Ukristo na Uislamu, ya taifa, na ya kisiasa. Tisho la mamlaka ya Uturuki lilikuwa lile lililokuwepo dhidi ya ‘Uhuru wa Kikristo.’ Hii ndiyo sababu jina ‘Uturuki’ lilikuwa kisawe cha ‘Uislamu’ katika lugha ya Martin Luther.
dhoruba na mvua ya mawe kuangamiza mazao, mifugo, na huitia hewa sumu na kadhalika. 81. Kwa ufupi, anaumia anapoona kila mtu akipokea funda la mkate kutoka kwa Mungu na kulila kwa amani. Kama ingekuwa uwezo wake, hakika hatungekuwa na mabua shambani, sarafu hata moja nyumbani, uhai wetu angalau kwa saa moja tu, kama sala zetu kwa Mungu, hasa wale tulio na Neno la Mungu na tupendao kuwa Wakristo, hazingemzuia.
82. Hivyo, unaona jinsi Mungu anavyopenda kutuonyesha kwamba, anatujali katika mahitaji yetu yote, na hutupatia maisha yetu ya kila siku kwa uaminifu. 83. Japo hutupatia na huzitoa baraka hizi tele hata kwa watu waovu na majangili, bado hututaka tuziombe ili tujue kwamba, tumezipokea kutoka mkononi mwake na, katika hizo baraka, tuutambue wema na ubaba wake kwetu. Anapouondoa mkono wake kutoka kwetu, hakuna linaloweza kustawi au kudumu muda mrefu, jinsi tuonavyo kweli na tunavyoshuhudia kila siku. 84. Kuna shida kiasi gani duniani sasa kwa sababu ya sarafu bandia? Naam, kwa sababu ya unyonyaji wa kila siku, riba katika biashara ya umma, shughuli, na kazi kwa wanaowagandamiza maskini tele na kuwapokonya mkate wao wa kila siku! Naam, hatuna budi kulivumilia hili, lakini waacheni wanyonyaji na wagandamizaji watahadhari wasije wakapoteza sala ya kawaida ya maombezi ya Kanisa.1492 Waacheni wajihadhari hii Sala ya Bwana isije ikageuzwa dhidi yao.
OMBI LA TANO
85. “Na utusamehe madeni yetu, kama sisi tunavyosamehe wadeni wetu”
86. Ombi hili linahusu maisha yetu duni na ya tabu. Japo tuna Neno la Mungu, tunaamini, tunatii, tunayanyenyekea mapenzi yake, na tunahimiliwa na karama na baraka za Mungu, haimaanishi kwamba, hatuna dhambi. Bado tunajikwaa na kukosea kila siku kwa sababu tunaishi ulimwenguni miongoni mwa watu wanaotuudhi kabisa, wanaotufanya tusivumilie, tuwe na hasira, tulipize kisasi na kadhalika. 87. Licha ya hayo, Ibilisi yu nyuma yetu akituzingira kila upande jinsi tumesikia. Yeye anayaongoza mashambulizi yake dhidi ya maombi yote yaliyotangulia. Hivyo, si rahisi kwetu kusimama imara katika migongano kama hiyo isiyokoma. 88. Kadhalika, hapa kuna haja kubwa ya kumwita Mungu na kusali: “Babangu mpendwa, utusamehe madeni yetu!” Hii haimaanishi kwamba, Yeye hatusamehi dhambi zetu kabla na bila maombi yetu. Alitupatia Injili ambamo kuna msamaha kabla ya kuomba na hata kuifikiria. Lakini jambo muhimu kabisa hapa kwetu ni kutambua na kukubali msamaha huu. 89. Kwa 1492 Lugha ya methali: kuadhiri.
maana, mwili ambamo kwamo, tunaishi kila siku, ni wa asili isiyomtegemea na kumwamini Mungu. Mara nyingi, huchochewa na matamanio na hila mbovu. Hivyo, tunatenda dhambi kila siku kwa maneno, matendo, na katika matendo yaliyoagizwa na yasiyoagizwa. Hivyo, dhamiri zetu hazitulii, badala yake, huogopa hasira na chuki ya Mungu. Kisha, zinapoteza faraja na tumaini la Injili. Kwa hiyo, ni muhimu kuligeukia ombi hili daima kwa ajili ya faraja itakayoziponya dhamiri zetu.
90. Ombi hili linafaa nia ya Mungu ya kukivunja kiburi chetu na kutufanya wanyenyekevu. Amejiwekea haki hii kwamba, iwapo mtu yeyote atajisifia uchaji wake na kuwadharau wengine, anapaswa kujichunguza mwenyewe kwa mujibu wa ombi hili. Atagundua kwamba, yeye si mchaji zaidi kuliko wengine kwamba, wanadamu wote hawana budi kujinyenyekeza mbele za Mungu, na wafurahi kwamba, wanaweza kuupata msamaha wa dhambi. 91. Mtu yeyote asije akafikiria kwamba, anaweza kukifikia kiwango ambacho hatauhitaji huu msamaha wa dhambi. Kwa ufupi, Mungu asipotusamehe bila kukoma, tutapotea kabisa.
92. Hivyo, ombi hili hasa ni rufaa kwake Mungu ili asizihesabu dhambi zetu na asituadhibu tunavyostahili kila siku. Badala yake, atushughulikie kwa huruma, atusamehe jinsi alivyoahidi, atupatie dhamiri zenye furaha na changamfu ili tuweze kusimama mbele zake katika sala. Ambapo moyo si mnyofu kwa Mungu, na hauwezi kulipokea tumaini hilo, hautathubutu kusali. Lakini moyo wenye furaha na tumaini jinsi hiyo, unatokana tu na maarifa kwamba, dhambi zetu zimesamehewa.
93. Kwa sasa, sharti muhimu sana na lenye faraja limeongezewa: “Kama tunavyowasamehe wadeni wetu.” Mungu ametuahidi kwa uhakikisho kwamba, kila dhambi imesamehewa kwa masharti kwamba, sisi pia tunawasamehe majirani zetu. 94. Tunaendelea kumkosea sana Mungu kila siku na bado anaendelea kutusamehe kwa neema. Kadhalika, inatubidi kuwasamehe majirani zetu wanaotufanyia madhara, vurugu, udhalimu, na wanaotuonea kijicho. 95. Usiposamehe, usifikirie kwamba, Mungu atakusamehe! Lakini ukisamehe, una faraja na uhakikisho kwamba, umesamehewa huko mbinguni. 96. Hilo halitafanyika kwa ajili ya msamaha wako, bali kwa kuwa Mungu anatutendea hivyo bure, kwa neema peke yake, jinsi alivyoahidi, na jinsi Injili inavyotufundisha. Lakini, amelitoa sharti hili kwa uimarishwaji na uhakikisho wetu kama ishara pamoja na ahadi ambayo inakubaliana na ombi hili: “Achilieni, nanyi mtaachiliwa” (Lk. 6:37). Kisha, Kristo anairudia mara tu baada ya Sala ya Bwana katika Mt. 6:14 anaposema:“Kwa maana mkiwasamehe watu makosa
yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.”
97. Hivyo, ishara hii imeambatishwa kwenye hili ombi ili tunapoomba, tuweze kuikumbuka ahadi hii na kufikiria: “Baba mpendwa, nimekujia niombe msamaha, siyo kwa mawazo kwamba, ningeweza kukuridhisha na kuustahili msamaha, bali kwa sababu umeitoa ahadi na kuiwekea muhuri, ikienda yakini sawa na msamaha uliotangazwa na wewe mwenyewe.” 98. Lolote linaloweza kutimizwa na Ubatizo na sakramenti,1493 mambo yaliyoteuliwa kuwa alama za nje, basi, ishara hii inaweza kuziimarisha na kuzifurahisha dhamiri zetu. Imeanzishwa hasa kwa ajili yetu ili tuitumie na tuifanyie mazoezi kila saa na tuiweke daima.
OMBI LA SITA
99. “Usitutie majaribuni”
100. Sasa, tumesikia vya kutosha kuhusu mahangaiko na jitihada zinazohitajika ili kulinda na kuvumilia katika karama zote tunazoziombea. Hata hivyo, hili halifanikiwi bila makosa na kujikwaa. Aidha, haya ndiyo maisha kwamba, japo tumepata msamaha, dhamiri safi, na tumeondolewa dhambi kabisa, inatokea kwamba, mtu husimama leo na kuanguka kesho. Kwa hiyo, ingawa sasa sisi ni wanyofu na tunasimama mbele za Mungu tukiwa wachaji wenye dhamiri safi, hatuna budi kuomba ili asituruhusu kuanguka tena na kuyakubali majaribio na majaribu. 101. Kuna majaribu ya aina tatu:1494 ya mwili, ya dunia, na ya Ibilisi. 102. Tunaendelea kuishi katika mwili na tuna yule Adamu wa kale anayening’inia shingoni mwetu. Yeye hufanya kazi na anatushawishi kila siku ili tuingie katika uasherati, uzembe, ulafi, ulevi, uroho, udanganyifu, ulaghai, na ghiliba dhidi ya majirani zetu. Kwa ufupi, anatushawishi tujihusishe na tamaa zote za uovu ambazo, kwa asili, zimo ndani yetu, na ambazo zinachochewa na jumuiya, mifano ya watu wengine, tuyaonayo, na tuyasikiayo. Haya yote huumiza na huchochea hata moyo usiokuwa na hatia. 103. Pili, kuna dunia ambayo hutushambulia kwa maneno, matendo, na hutuelekeza kwenye hasira na kutovumilia. Kwa ufupi, ina: chuki, wivu, uadui, vurugu, dhuluma, uhaini, ulipizaji kisasi, laana, shutuma, uchongezi, kiburi, majivuno, kupenda anasa, heshima, umaarufu, na mamlaka. Hata hakuna anayependa kuwa wa mwisho bali kila mtu anataka aketi katika pahali pa juu ili watu wote wamwone. 104. Kisha, huja Ibilisi anayetuchokoza na kutusumbua kutoka pande zote, lakini hujitukuza mwenyewe hasa ambapo dhamiri na mambo ya kiroho yako hatarini. Nia yake ni kutufanya tupuuze,
1493 Yaani, sakramenti ya Chakula cha Bwana. 1494 Kijerumani: ‘Bekörunge,’ Jinsi watu wa mkoa wa Sachsen wanavyoyaita tangu zamani.
tutadharau Neno na matendo ya Mungu, tuwe mbali na imani, tumaini, na upendo. Badala yake, anataka atuingize katika kutoamini, usalama wa uongo, ukaidi, ukataji tamaa, ukanaji Mungu, kufuru, na dhambi nyingine nyingi za kuchukiza mno zisizohesabika. Hii ni mitego na nyavu. Naam, “mishale yenye moto”1495 halisi ambayo imevurumishwa mioyoni mwetu kwa njia ya chuki, siyo kwa damu na mwili bali na Ibilisi mwenyewe.
105. Hizi ndizo hatari na majaribu makubwa na makali ambayo kila Mkristo lazima ayavumilie hata kama yatamjia moja baada ya jingine. Kwa kuwa, bado tunaishi katika maisha haya yenye aibu sana, tunashambuliwa, tunawindwa, tunasumbuliwa kutoka pande zote, tunazuiwa kupaza sauti na kuomba kila saa kwamba, Mungu asituruhusu tunyong’onyee, tuchoke, turudi tena katika dhambi, aibu, na kutoamini. Vinginevyo, haiwezekani kuyashinda hata majaribu madogo mno.
106. Hii ndiyo maana ya “kutotutia majaribuni.” Yaani, Mungu anapotupatia uwezo na nguvu za kuyazuia, hata kama majaribu hayo hayaondolewi au hayamaliziki. Kwa maana, hakuna yeyote awezaye kuyaepuka majaribu na vishawishi kama tungali tunaishi katika mwili na tuna Ibilisi anayetuwinda. Hatuna budi kuyavumilia majaribu hata kuzongomezwa nayo. Lakini tunaomba kwamba, tusianguke na kuangamia katika hayo. Kwa maana, kuna tofauti kati ya kuyahisi majaribu na kuyaruhusu na kujisalimisha kwayo.1496 107. Sisi sote hatuna budi kuyahisi, japo siyo kwa kiwango icho hicho. Baadhi wana majaribu ya mara kwa mara na makali sana kuliko wengine. Kwa mfano, vijana wanajaribiwa hasa na mwili, na watu wazima, na ulimwengu. Wengine, yaani, Wakristo imara, wanaohusika na mambo ya kiroho wanajaribiwa na Ibilisi. 108. Lakini hatuwezi kudhuriwa kwa hisi za majaribu tu mradi iwe kinyume cha mapenzi yetu na tuwe tungependa sana kuwa mbali nayo. Iwapo hatukulihisi jaribu, basi, haliwezi kuitwa jaribu kabisa. Lakini ukilikubali, utalipatia hatamu hiari, hutaliasi wala kuomba msaada dhidi yalo.
109. Kwa hiyo, sisi Wakristo lazima tujizatiti na tujiandae kwa ajili ya mashambulizi yanayotujia bila kukoma. Mtu yeyote asije akafikiria kwamba, yu salama na kuwa asiyejali kana kwamba, Ibilisi yu mbali nasi. Lakini wakati wote tuyatarajie mapigo yake na tuyazuie. Ingawa sasa mimi ni mnyofu, mvumilivu, mwema, na imara katika imani, Ibilisi yu tayari wakati huu kuufyatua mshale wa jinsi hiyo moyoni mwangu ili nisiweze kusimama kabisa. Kwa maana, 1495 Efe. 6:16
1496 Mfano na shauri lililo katika kitabu cha ‘Vitae patrum’ (‘Maisha ya akina Baba’): watu hawawezi kuwazuia ndege wasiruke juu ya vichwa vyetu, lakini wanaweza kuwazuia vizuri ndege wasijenge viota vyao juu ya vichwa vyetu.
477
yeye ni adui asiyekoma au asiyechoka. Shambulizi moja linapokoma, mengine mapya hutokea. 110. Nyakati kama hizo, msaada wako wa pekee na faraja iwe ni kuikimbilia Sala ya Bwana na kumwita Mungu kutoka moyoni mwako: “Babangu mpendwa, uliniagiza kuomba; usiniruhusu niingie majaribuni!” 111. Kisha utaona kwamba, majaribu yamekoma na yamekubali kushindwa hatimaye. Vinginevyo, ukijaribu kujisaidia mwenyewe kwa mawazo na mashauri yako, utayaharibu mambo na utampatia Ibilisi mwanya mkubwa zaidi. Kwa maana, yeye ana kichwa cha nyoka, akiupata mwanya wa kujipenyezea, basi, mwili mzima utafuatia bila kizuizi. Lakini sala inaweza kumzuia na kumfukuza.
OMBI LA MWISHO
112. “Lakini utuokoe na yule mwovu. Amina.”1497
113. Katika Kiyunani,1498 ombi hili husomeka: “Utuokoe au utulinde na yule Mwovu au Mpotovu.” Ombi hili linaonekana kuzungumzia Ibilisi kama jumla ya maovu yote ili muhtasari mzima wa sala uweze kuelekezwa dhidi ya adui mkuu wetu. Kwa maana, ni yeye anayezuia kila kitu tukiombacho kwa ajili ya jina au utukufu wa Mungu, ufalme wake, mapenzi yake, mkate wetu wa kila siku, na dhamiri safi yenye furaha na kadhalika. 114. Kwa hiyo, tunahitimisha kwa kusema: “Babangu mpendwa, utusaidie tusipatwe na balaa hizi zote!” 115. Hata hivyo, ombi hili hujumlisha maovu yote ambayo yanaweza kutupata chini ya ufalme wa Ibilisi: yaani, umaskini, aibu, kifo, na kwa ufupi, tanzia zote za huzuni na maumivu makali yasiyopimika hapa duniani. Kwa kuwa Ibilisi ni mwongo, na mwuaji, 1499 huyatafuta maisha yetu daima na kuitoa hasira yake kwa kusababisha ajali na madhara miilini mwetu. Licha ya hayo, yeye huzivunja shingo za watu wengi na kuwafanya wengine vichaa. Baadhi huwafisha maji, wengine huwashurutisha wajinyonge au huwafanya wajihusishe na maangamizi mengine ya kutisha sana. 116. Kwa sababu hiyo, hatuna la kufanya hapa duniani isipokuwa kusali bila kukoma dhidi ya huyo adui mkuu. Kwa maana, Mungu asipotusaidia, hatutaweza kuwa salama hata kidogo.
117. Hivyo, unaona jinsi Mungu anavyotutaka tumwombe kila kitu kinachoathiri ustawi wa miili yetu na kutuagiza tusitafute wala kuutarajia msaada 1497 Mwisho wa kawaida katika Sala ya Bwana––‘kwani ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele’–haupatikani katika maandiko ya zamani sana ya Agano Jipya. Hii ndiyo sababu haukutumika pia katika utaratibu wa asili wa ibada. Baadaye, sehemu hii ya sifa ilipokelewa katika Kanisa. 1498 Katika maandiko ya asili ya Kijerumani, Luther alitumia Kiebrania badala ya Kiyunani: ‘In Ebräischen lautet das Stücklin also.’ Kilatini/Kiyunani katika Katekisimo Kubwa kinasomeka:– ‘Graeci codices hoc loco ita habent.’ 1499 Yn. 8:44
478
kutoka kwa mwingine yeyote isipokuwa Yeye. 118. Lakini ameliweka ombi hili kuwa la mwisho. Maana, tukitaka kulindwa na kukombolewa kutoka kwa maovu yote, lazima jina lake litakaswe, ufalme wake uje, na mapenzi yake yafanyike kwanza miongoni mwetu. Halafu, atatuokoa kutoka dhambini, aibu, na lolote linalotudhuru au kutuumiza.
119. Hivyo, kwa ufupi, Mungu ameweka mbele yetu mateso yote ambayo yanatusumbua wakati wote ili tusiwe na udhuru wowote wa kutojali kusali. Lakini uwezo wa sala u1natutaka pia tujifunze kusema, “AMINA” kwayo. Yaani, kutokuwa na mashaka kwamba, maombi yetu yatasikika na yatajibiwa hakika. 120. Neno hili ni thibitisho la imani isiyotetereka kwake yeye asiyesali kwa kubahatisha. Badala yake, anajua kabisa kwamba, Mungu hasemi uongo kwani ameahidi kumpatia matakwa yake. Ambapo imani ya jinsi hiyo haipo, maombi ya kweli hayawezi kuwepo. 121. Kwa hiyo, ni madanganyo ya kudhuru watu wanaposali kwa njia ambayo hawathubutu kusema, “ndiyo” kwa moyo wao wote. Si hayo tu, wanahitimisha kwa mashaka kwamba, Mungu atayasikia maombi yao, lakini wanaendelea kuwa na mashaka wakisema: “Kwa nini niwe jasiri sana kujigamba kwamba, Mungu huyasikia maombi yangu? Mimi ni mkosaji maskini tu!” 122. Maana ni kwamba, hawaioni ahadi ya Mungu. Badala yake, wanaona matendo na stahili zao wenyewe kiasi kwamba, wanamdharau Mungu na kumshtaki kuwa mwongo. 123. Kwa hiyo, hawalipokei lolote jinsi Mt. Yakobo asemavyo: “Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.”1500 124. Tazameni, huo ndio umuhimu anaouambatisha Mungu katika kuwa kwetu na hakika kwamba, hatutasali bure na kwamba, tusiyadharau maombi yetu.
SEHEMU YA NNE: UBATIZO
1. Sasa tumekwisha kumaliza sehemu tatu kuu za mafundisho yetu ya pamoja ya Kikristo. Sasa inabakia kuzungumzia kuhusu sakramenti mbili zilizoanzishwa na Kristo. Kila Mkristo anapaswa kuwa na angalau mafundisho mafupi ya kwanza yanayozihusu sakramenti hizo. Kwa maana, bila hizo hakuna anayeweza kuwa Mkristo ingawa, kwa bahati mbaya, katika siku zilizopita hakuna lolote lililofundishwa kuzihusu. 2. Kwanza, tutajishughulisha na Ubatizo ambao kwao, tunapokelewa kwanza katika jamii ya Wakristo. Ili uweze kufahamika upesi, tutaushughulikia kwa utaratibu na kujihusisha tu na yale ambayo ni ya lazima
1500 Yak. 1:6-7
kwetu kuyajua. Jinsi unavyoweza kudumishwa na kutetewa dhidi ya waasi na watu wa madhehebu mengne, tutawaachia wataalamu.
3. Kwanza kabisa, na zaidi ya yote, lazima tuyajue maneno ambayo ni msingi wa Ubatizo, ambayo kwayo, kila lisemwalo linauhusu. Yaani, mwishoni mwa Mathayo ambapo Kristo Bwana anasema: 4. “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na Roho Mtakatifu.”1501
5. Kadhalika, katika Marko sura ya mwisho1502 anasema: “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.”
6. Kwanza, chunguza kwa makini kwamba, maneno haya yana amri na agizo la Mungu. Basi, usiwe na shaka kwamba, Ubatizo umeasisiwa na Mungu, na si tendo lililobuniwa na kugunduliwa na mwanadamu. Ninavyoweza kusema kweli ni kwamba, Amri Kumi, Ukiri wa Imani, na Sala ya Bwana havikufanyizwa kutokana na dhana ya mtu yeyote bali vilifunuliwa na kutolewa na Mungu mwenyewe. Hivyo, ninaweza pia kujisifu kwamba, Ubatizo si tendo la kuchezewa na binadamu bali umeanzishwa na Mungu mwenyewe. Aidha, imeamriwa kwa heshima na kwa kweli kwamba, ni lazima tukubali kubatizwa. La sivyo, hatutaokolewa. Basi, tusiuangalie kama tendo lisilokuwa na maana sawa na kulivalia koti jekundu jipya. 7. Ni jambo lenye maana kubwa kwamba, tunauheshimu Ubatizo kama tendo bora sana, tukufu, na lililosifika sana. Hii ndiyo sababu kuu ya mashindano na mapambano yetu. Kwa maana, sasa, ulimwengu umejaa madhehebu yanayotangaza kwamba, Ubatizo ni tendo la nje na kwamba, vitu vya nje havina manufaa. 8. Haidhuru ulivyo wa nje, hapa pana Neno na amri ya Mungu ambavyo vimeuanzisha, vimeuimarisha, na kuuthibitisha Ubatizo. Ambalo Mungu amelianzisha na kuliamrisha haliwezi kuwa bure. Ni kitu chenye thamani kubwa sana, ingawa ni bure ghali katika kuonekana kwake kwote. 9. Ikiwa watu walifikiria kwamba, lilikuwa tendo bora kwa Papa kuviuza vyeti vya upatanisho na kuyaweka wakfu madhabahu na makanisa peke yake, kwa nguvu ya barua zake na mihuri, basi, tunapaswa kuuheshimu Ubatizo kama tendo bora na la thamani zaidi. Kwa maana, Mungu ameuamrisha, na licha ya hayo, unafanyika katika jina lake. Hivyo, maneno yanasema, “enenda, ubatize,” siyo katika jina lako ila “katika jina la Mungu.”
10. Kubatizwa katika jina la Mungu si kubatizwa na wanadamu bali na Mungu mwenyewe. Ingawa unafanywa kwa mikono ya wanadamu bado ni tendo la Mungu mwenyewe kweli. Kutokana na ukweli huu, ni hakika kwamba, kila
1501 Mt. 28:19
1502 Mk. 16:16
mmoja anaweza kuhitimisha rahisi kwamba, ni tendo la thamani kubwa zaidi kuliko kazi ya mtu au mtakatifu yeyote. Kwa maana, ni kazi gani inayoweza kufanywa na mwanadamu ambayo ni bora zaidi kuliko kazi ya Mungu? 11. Hapa, Ibilisi anajiingiza kazini ili kutufanya vipofu kwa sura za uongo na kutuongoza kutoka katika kazi ya Mungu na kutupeleka katika kazi zetu. Anaifanya sura ing’are sana wakati Wakerthusi wanafanya kazi nyingi kubwa na ngumu nasi sote tunauweka umuhimu mkubwa zaidi katika mafanikio yetu na stahili zetu wenyewe. 12. Lakini Maandiko Matakatifu yanafundisha kwamba, tungerundika kazi zote za wamonaki/watawa wa kiume wote, haidhuru zinavyokuwa za thamani kubwa na zazinavyong’ara, hazingekuwa na ubora na uzuri sawasawa na kama Mungu angeokota jani kavu. Kwa nini? Kwa sababu mtu anayelitenda tendo hili ni bora na wa kufaa zaidi. Hapa tunapaswa kutathmini, siyo mtu kulingana na kazi, bali kazi kulingana na mtu ambaye kwaye, lazima zipate thamani. 13. Lakini uendawazimu hujitokeza mbio, kwa kuwa Ubatizo haung’ari kama kazi tuzifanyazo, huuchukulia kwamba, hauna thamani.
14. Labda, sasa unaweza kufahamu jinsi ya kulijibu vyema swali: Ubatizo ni nini? Si maji ya kawaida tu, bali ni maji yaliyoambatana na kutakaswa na Neno na amri ya Mungu. Si lingine lolote isipokuwa maji ya kimungu. Siyo kwamba, maji yenyewe ni bora kuliko maji mengine bali ni kwamba, Neno na amri ya Mungu vimeongezewa kwayo. 15. Kwa hiyo, ni uovu mtupu na kufuru ya Ibilisi wakati roho zetu mpya,1503 ili kuukashifu Ubatizo, zitalipuuza Neno la Mungu, agizo lake, hazitalidhukuru lolote isipokuwa maji yaliyotekwa kutoka kisimani, na baadaye kuboboka: “Ni vipi gao la maji huisaidia nafsi?” 16. Naam, mwenzangu mpendwa! Nani asiyejua kwamba, maji ni maji, ikiwa utengano kama hilo ni sahihi? Lakini wewe unathubutuje kuligeuza agizo la Mungu hivyo na kuirarulia mbali bizimu hiyo yenye thamani mno ambayo kwayo, Mungu ameikaza na kuifunga, na ambayo kwayo, hataki agizo lake litengwe? Kwani asili iliyo ndani ya maji ni Neno au amri na jina la Mungu. Hii ni hazina kubwa na bora kuliko mbingu na nchi.
17. Basi, ifahamuni tofauti: Ubatizo ni tofauti sana na maji mengine yoyote. Siyo kutokana na asili ya kiini cha maji yenyewe bali kwa sababu kitu bora zaidi kinaongezwa kwayo. Mungu mwenyewe anahatarisha heshima, nguvu, na uwezo wake katika Ubatizo. Kwa hiyo, si maji ya asili tu bali ni ya kimungu,
1503 Kijerumani: ‘Unsere neue Geister.’ Hapa, Luther alimaanisha watu waliokataa sakramenti ambao katika Kijerumani waliitwa, ‘Schwarmgeister’ au ‘Schwärmer.’ Wakristo wa aina hiyo walifikiria kwamba, Roho Mtakatifu hufanya kazi yake mara moja bila vyombo vya neema. Yaani, Neno la Mungu, na Sakramenti Takatifu vilivyoanzishwa na Bwana Yesu Kristo kuwa vyombo au silaha za wokovu wetu.
ya kimbingu, matakatifu, na yaliyobarikiwa–yasifuni kwa istilahi1504 zozote uwezavyo. Haya yote ni kwa ajili ya Neno, ambalo ni la kimbingu, Neno takatifu ambalo hakuna mtu yeyote awezaye kulisifu vya kutosha kwani lina na linauwasilisha utimilifu wote wa Mungu. 18. Kutokana na Neno, yanapata asili yake kama sakramenti jinsi Mt. Agostino alivyofundisha: “Accedat verbum ad elementum et fit sacramentum.”1505 Kumaanisha kwamba, Neno linapoongezewa katika kitu cha asili au dutu ya asili, inakuwa sakramenti. Yaani, kitu kitakatifu, cha kimungu, na ishara.
19. Kwa hiyo, tunafundisha daima kwamba, sakramenti na vitu vyote vya nje vilivyoamriwa na kuanzishwa na Mungu ni lazima viheshimiwe, si sawa na inavyokuwa barakoa chafu ya nje–jinsi tulionavyo ganda la kokwa–bali kama lile ambamo kwamo, Neno la Mungu limefungiwa. 20. Vivyo hivyo, tunaizungumzia asasi ya wazazi na mamlaka ya serikali. Tukiwaheshimu watu hawa kuhusiana na pua, macho, ngozi, nywele, nyama, na mifupa yao, hawana tofauti na Waturuki na Wapagani. Mtu fulani anaweza kuja na kusema, “Kwa nini nimjali mtu huyu zaidi kuliko wengine?” Lakini ni kwa sababu amri imeongezewa: “Umheshimu baba na mama.” Ninamwona mtu tofauti, aliyepambwa na kuvikwa enzi na utukufu wa Mungu. Ninasema, amri ndiyo mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Naam, taji kichwani mwake linalonionyesha namna na kwa nini niheshimu mwili na damu hii. 21. Kwa njia iyo hiyo na hata zaidi, unapaswa kuuheshimu na kuusifu Ubatizo kwa ajili ya Neno. Kwa kuwa, Mungu mwenyewe ameuheshimu kwa maneno na matendo na ameuthibitisha kwa maajabu kutoka mbinguni. Unadhani ilikuwa masihara mbingu zilipofunguka Kristo alipokubali kubatizwa na kwamba, Roho Mtakatifu alishuka dhahiri na kwamba, utukufu na enzi ya Mungu vilifunuliwa kila mahali? 22. Kwa hiyo, ninakuonya tena kwamba, hivi viwili Neno na maji, lazima visitenganishwe kimoja kutoka kwa kingine kamwe. Ambapo Neno linatenganishwa na Ubatizo, maji yanayobakia si tofauti na anayoyatumia kupikia mtumishi mwanamwali. Hakika, unaweza kuitwa maji ya kuogea tu. Lakini, Neno linapokuwepo kulingana na agizo la Mungu, Ubatizo unakuwa sakramenti na unaitwa Ubatizo wa Kristo. Asili kuhusu kiini na heshima ya hii Sakramenti Takatifu ndilo jambo la kwanza kusisitizwa.
23. Kwa kuwa sasa tunajua Ubatizo ni nini na unavyopaswa kuheshimiwa, lazima tujifunze pia ulianzishwa kwa shabaha gani katika nafasi ya pili. Yaani, unaleta faida, karama, na athari zipi? Wala hatuwezi kuyaelewa haya zaidi
1504 Neno litumikalo kwa ufupi badala ya maneno mengi ya kiufundi kulingana na elimu fulani.
1505 ‘Neno linaingia maji na kuwa sakramenti;’ Agostino aliandika, ‘accedit’ badala ya ‘accedat’ jinsi Luther alivyoyadondoa maneno yake. Agostino katika ‘Tractatus 80 in Jn. Cap. 3’ (Makala 80 kuhusu Yn. 3).
482
ya maneno ya Kristo yaliyodondolewa hapo juu: “Aaminiye na kubatizwa ataokoka.”1506 24. Kwa maelezo rahisi, nguvu, matokeo, faida, tunda, na shabaha ya Ubatizo ni kuokoa. Hakuna mtu anayebatizwa ili awe mtawala bali “aokolewe” jinsi maneno yasemavyo. 25. Tunajua kwamba, kuokolewa ni kuondolewa kutoka kwa dhambi, kifo, na Ibilisi. Isitoshe, tunaingia katika ufalme wa Kristo na kuishi naye milele na milele. 26. Hapa unaona tena jinsi Ubatizo unavyopasa kuchukuliwa kuwa kitu cha thamani na muhimu. Maana, tunapata hazina isiyoelezeka katika huo. Hii inaonyesha kwamba, si maji matupu tu wala ya kawaida, kwa sababu maji ya kawaida hayangekuwa na matokeo ya namna hiyo. Lakini Neno lina matokeo. Inaonyesha pia–jinsi tulivyosema hapo juu–kwamba, jina la Mungu li ndani ya maji hayo. 27. Palipo na jina la Mungu, lazima pawe na uzima na wokovu pia. Hivyo, yanaelezewa kama maji ya kimungu, yaliyobarikiwa, yenye kuzaa matunda, na yenye neema kwa sababu, kwa njia ya Neno, Ubatizo huipata nguvu ya “kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya,” jinsi Mt. Paulo anavyouita katika Tit. 3:5.
28. Lakini wajuaji wetu, zile nafsi mpya1507 hudai kwamba, imani peke yake huokoa na kwamba, matendo, na mambo ya nje hayachangii lolote katika wokovu. Tunajibu: Ni kweli, hakuna lolote ndani yetu linalookoa isipokuwa imani jinsi tutakavyosikia baadaye. 29. Lakini viongozi hawa wa vipofu1508 hawapendi kuona kwamba, imani lazima iwe na jambo la kuamini, jambo ambalo kwalo, lazima iweze kuambatana na kusimama kwalo. Hivyo, imani huambatana na maji, na huyaamini kuwa Ubatizo ambao kwao, kuna wokovu na uzima tu. Si kwa njia ya maji, jinsi tulivyoelezea vya kutosha, bali kwa njia ya mwungano wake na Neno, agizo, na jina la Mungu linalounganishwa nayo. Ninapoliamini hili, kuna lipi lingine ila kumwamini Mungu kuwa yeye alilipanda Neno lake katika agizo hili la nje, na akalitoa kwetu ili tuweze kuifahamu hazina iliyomo?
30. Sasa, watu hawa ni wapumbavu kiasi cha kuitenga imani na maji. Imani imejiambatisha na imejifungamanisha nayo kwa sababu kwamba, haya ni ya nje. Naam, lazima yawe ya nje ili yaweze kutambuliwa, kufahamika kwa hisi, na hivyo yaingizwe moyoni, jinsi Injili yote ilivyo mahubiri ya nje na simulizi. Kwa ufupi, lolote Mungu atelindalo ndani yetu, hulitenda kwa njia ya maagizo ya nje. Naam, haidhuru anakosemea, lengo la kusema, na njia aitumiayo kusema Mungu,
1506 Mk. 16:16
1507 Luther alimaanisha wafuasi wa Huldrych Zwingli (1484-1531) huko Zürich, aliyekana pamoja na Waanabaptisti maana ya Ubatizo kama kuzaliwa kwa pili. Hata hivyo, Zwingli aliwapinga Waanabaptisti na alikubali adhabu za kifo za wakuu wao. Wafuasi wa Zwingli na Waanabaptisti walikubali kwamba, Ubatizo ni alama ya imani peke yake wala si tendo la Mungu la kuzaliwa kwa pili kwa wokovu wetu. Wafuasi wa Zwingli waliukubali Ubatizo wa watoto wachanga na kwa sababu hiyo walipingana sana na Waanabaptisti.
1508 Mt. 15:14
483
lazima imani iangalie na ishikilie hapo. 31. Hapa tuna maneno: “aaminiye na kubatizwa ataokoka.” Maneno haya yanalirejea lipi isipokuwa Ubatizo. Yaani, maji yanayojumuishwa katika agizo la Mungu? Hivyo, inafuatia kwamba, yeyote anayeukataa Ubatizo analikataa Neno la Mungu, imani, na Kristo ambaye hutuelekeza na kutuunganisha katika Ubatizo.
32. Baada ya kujifunza faida kubwa na nguvu ya Ubatizo, acheni tuchunguze zaidi ni nani ambaye huzipokea karama hizi na faida za Ubatizo katika nafasi ya tatu. 33. Hili limeelezewa vizuri sana na kwa uwazi katika maneno yayo hayo tena: “Aaminiye na kubatizwa ataokoka.” Yaani, imani peke yake humfanya mtu kustahili kuyapokea maji ya kuburudisha, na ya kimungu kwa njia ya kufaidi. Kwa sababu baraka hizi zimetolewa na kuahidiwa katika maneno yanayoandamana na maji, haziwezi kupokelewa hadi tuziamini kwa moyo wote. 34. Ubatizo hauna maana bila imani, ingawa wenyewe ni hazina isiyokuwa na mwisho na ya kimungu. Hivyo basi, usemi huu mmoja tu “aaminiye,” ni muhimu sana kiasi kwamba, huyaacha na kuyakataa matendo yote ambayo tunaweza kuyafanya kwa shabaha ya kuustahili wokovu kwayo. Kwa maana, ni wazi kwamba, lolote lisilokuwa imani halichangii lolote katika wokovu na halipokei lolote.
35. Hata hivyo, kuna ukinzani mara kwa mara: “Iwapo Ubatizo wenyewe ni tendo, na unasema kwamba, matendo hayana maana katika wokovu, imani ifanyiwe nini?” Kuhusu jambo hili, unaweza kujibu: “Ndiyo, ni kweli kwamba, matendo yetu hayana maana katika wokovu. Hata hivyo, Ubatizo si tendo letu ila ni tendo la Mungu. Kwa maana, kama ilivyosemwa, lazima utofautishe wazi kabisa kati ya Ubatizo wa Kristo na maji ya kuogea.” Hata hivyo, matendo ya Mungu yanafaa, ni ya lazima kwa wokovu, na hayatengi bali hutukaribisha1509 kwenye imani, kwa sababu bila imani, hayangeeleweka. 36. Hivyo, huupokei Ubatizo unaporuhusu umwagiwe maji tu kwa njia hiyo ambayo haikufaidi. Lakini unakufaidi ukiupokea kama amri na agizo la Mungu, ili unapobatizwa katika jina la Mungu, uweze kuupokea wokovu ulioahidiwa kwa njia ya maji. Jambo hili haliwezi kutendwa kwa mkono wala kwa mwili bali moyo lazima uliamini. 37. Hivyo basi, unaona wazi kwamba, Ubatizo si tendo ambalo tunalitenda bali ni hazina tupewayo na Mungu nayo imani huushikilia. Hili ni kulingana na jinsi uwepo wa Bwana Kristo msalabani usivyokuwa tendo bali hazina tutunukiwayo na tupewayo katika Neno na tunaipokea kwa imani. Kwa sababu hiyo, hawatendi haki wanapopiga kelele dhidi yetu kana kwamba, tunahubiri dhidi ya imani. Kwa kweli, tunaisisitiza imani peke yake kuwa ya lazima sana kiasi kwamba, bila
1509 Kijerumani: ‘fodern,’ istilahi ya Luther inaweza kumaanisha ‘fordern,’ (dai) au ‘fördern’ (saidia) au (jenga). Maana hizi mbili lazima ziwe katika tafsiri.
hiyo, hakuna tunaloweza kulipokea au kulifurahia.
38. Hivyo basi, tumeyazinghatia mambo matatu ambayo lazima yajulikane kuhusu sakramenti hii hasa kwamba, ni agizo la Mungu na lazima iheshimiwe kabisa. Hili peke yake lingetoshea, ingawa Ubatizo ni tendo la nje kabisa. Kadhalika, amri: “Waheshimu baba yako na mama yako,” inahusu mwili na damu ya binadamu. Hata hivyo, hatuutazami mwili na damu bali amri ya Mungu ambayo kwayo, imejumuishwa kwa sababu ambayo inaufanya mwili huu kuitwa baba na mama. Vivyo hivyo, kama hatungekuwa na lingine lolote isipokuwa maneno haya,“Nendeni na mkawabatize,” bado tungekubali na kuutii Ubatizo kama agizo la Mungu. 39. Lakini hapa tuna amri, katazo, na ahadi ya Mungu. Kwa hiyo, ni tukufu zaidi kuliko jambo lolote aliloliamuru na kulibariki Mungu. Kwa ufupi, umejaa faraja na neema kasi kwamba, mbingu na dunia haviwezi kuuelewa. 40. Ufahamu maalumu unahitajika ili kuuamini kwa sababu si hazina inayokosekana. Linalokosekana ni kwamba, Ubatizo lazima ufahamike na uzingatiwe kwa uthabiti.
41. Kwa hiyo, katika Ubatizo, kila Mkristo ana mambo ya kutosha kujifunza na kuyatenda katika maisha yake yote. Kila mara ana mambo ya kutosha kumfanya aamini kwa uthabiti yale ambayo Ubatizo huahidi na kuleta. Hayo ni: ushindi dhidi ya kifo na Ibilisi, msamaha wa dhambi, neema ya Mungu, mkamilifu Kristo, na Roho Mtakatifu na karama zake. 42. Kwa ufupi, baraka za Ubatizo hazina mpaka kiasi kwamba, ikiwa hali ya asili yenye hofu inazifikiria, inaweza kuwa na mashaka iwapo zote zinaweza kuwa za kweli. 43. Chukulia kwamba, kulikuwa na tabibu ambaye angekuwa na ustadi kiasi kwamba, watu hawangekufa au ingawa wangekufa, baadaye wangeishi milele. Basi, fikiria jinsi ulimwengu ungemwangushia na kumnyeshea fedha kama dhoruba ya theluji. Kwa sababu ya umati wa matajiri, hakuna mtu mwingine yeyote ambaye angeweza kumkaribia. Sasa, katika Ubatizo, kila mtu ameletewa dawa ya bure yenye thamani kuu mlangoni pake ambayo inakimeza kifo na kuyaokoa maisha ya watu wote. 44. Ili tuufurahie na kuutumia Ubatizo barabara, lazima tuchote nguvu na faraja kutoka kwa huo wakati dhambi au dhamiri zetu zinatukandamiza na lazima tuseme: “Lakini nimebatizwa! Kama nimebatizwa, nina ahadi kwamba, nitaokolewa na kuwa na uzima wa milele nafsini na mwilini.” 45. Ndiyo sababu haya mambo mawili hutendwa katika Ubatizo: kwanza, mwili humwagiwa maji, ingawa hauwezi kulipokea lolote isipokuwa maji, pili, Neno hutamkwa ili nafsi iweze kulifahamu. 46. Kwa kuwa, maji na Neno pamoja vinaufanyiza Ubatizo mmoja, mwili na nafsi vitaokolewa na kuishi milele. Nafsi, kwa njia ya Neno ambalo huliamini, na mwili, kwa sababu umeunganishwa na nafsi, na
huuelewa Ubatizo kwa njia ya pekee. Kwa hiyo, hakuna johari kubwa ambayo inaweza kuurembesha mwili wetu na nafsi kuliko Ubatizo. Maana, kwa njia ya Ubatizo, tunaupata utakatifu na wokovu kamili, ambao hakuna namna yoyote ya maisha na hakuna matendo ulimwenguni yanayoweza kuupata. Basi, yaacheni haya yatoshee kama jibu la shabaha ya sasa kuhusu asili, faida, na matumizi ya Ubatizo.
[UBATIZO WA WATOTO WACHANGA]
47. Hapa, tunalirejelea suala ambalo kwalo, Ibilisi anaukanganya ulimwengu kwa njia ya madhehebu yake. Yaani, suala la Ubatizo wa watoto wachanga. Je, watoto wanaamini pia, na ni halali kuwabatiza? 48. Tunalijibu hili kwa ufupi: Waacheni watu wa kawaida waliondoe suala hili kutoka akilini mwao na waliachie wasomi. Lakini ukipenda kulijibu, basi, useme: 49. Imethibitishwa vya kutosha kwamba, Ubatizo wa watoto wachanga unampendeza Kristo kutokana na kazi yake mwenyewe. Mungu amewatakasa wengi waliobatizwa kwa njia hii na amewapa Roho Mtakatifu. Hata leo kuna wengi ambao mafundisho na maisha yao yanashuhudia kwamba, wana Roho Mtakatifu. Vivyo hivyo, kwa neema ya Mungu, tumepewa nguvu ya kuyafasiri Maandiko Matakatifu na kumfahamu Kristo, hali ambayo haiwezekani bila Roho Mtakatifu. 50. Sasa, ikiwa Mungu hakukubali Ubatizo wa watoto wachanga, hangekuwa amempatia yeyote Roho Mtakatifu wala sehemu yake yoyote. Kwa ufupi, tangu wakati huo hadi leo, hakuna mwanadamu duniani ambaye angeweza kuwa Mkristo. Kwa kuwa, Mungu ameuthibitisha Ubatizo kwa njia ya kipaji chake cha Roho Mtakatifu, jinsi tulivyotambua katika baadhi ya akina baba, kama vile Mt. Bernardo, Gerson, Yohana Huss na wengineo.1510 Kwa kuwa Kanisa Takatifu la Kikristo litadumu mpaka mwisho wa dunia, wapinzani wetu ni lazima wakubali kwamba, 1510 Bernardo wa Clairwaux (1090-1153) aliingia katika daraja kali sana la wamonaki/watawala wakuu la Citeaux huko Ufaransa na baadaye alikuwa mkuu wa jumba la watawa huko Clairwaux ambalo alilianzisha. Daraja la Bernardo lilikuwa moyo muhimu wa kiroho wa Matengenezo ya Kanisa la Magharibi. Bernardo alikuwa Mkristo wa maombi, mahubiri, na taamuli takatifu. Katika vitabu na mahubiri yake, alitilia mkazo sana maana ya mateso ya Bwana Yesu Kristo. Kama Mkristo wa upendo wa kimungu wa wakati wake, aliyasuta kabisa mateso ya Wayahudi huko Ulaya. Yohana Huss (1372-1415) alitoka Bohemia huko Ulaya na aliyatangulia Matengenezo ya Kanisa la Magharibi. Alisomea katika Chuo Kikuu cha Prag na alibarikiwa na daraja la mapadre mwaka wa 1400. Alijifunza maandiko ya John Wyckliffe (1330-1384) na aliendelea kuhubiri zaidi na zaidi dhidi ya hali ya upotovu wa mapadre na Kanisa lote. Alitengwa na Kanisa kwa agizo la Papa wa Roma mwaka wa 1407 na mwaka wa 1411. Alifungwa katika Sinodi ya Konstanzo na alichomwa moto nguzoni 6.7.1415, licha ya ahadi rasmi ya Sigismundo, aliyekuwa Kaisari wa Ujerumani. Alifariki kwa ujasiri mkubwa. Kitabu chake muhimu kinaitwa, ‘De Ecclesia’ (Kuhusu Kanisa) ambamo aliyadondoa maandiko ya Wyckliffe sura kwa sura. Baada ya kifo cha Huss, vita vikali viliendelezwa huko Bohemia dhidi ya Kaisari na watawala wa Kanisa huko Roma. Mwishowe, wafuasi wa Huss waliruhusiwa kuipokea Sakramenti ya Ekaristi katika aina mbili, yaani, mkate na divai tangu mwaka wa 1433 hadi mwaka wa 1567.
486
Ubatizo wa watoto wachanga unampendeza Mungu. Kwa maana, hawezi kamwe kujifarakisha mwenyewe, kuunga mkono uongo na maovu, au kuitoa neema yake na Roho Mtakatifu wake kwa mambo ya aina hiyo. 51. Hili ndilo thibitisho bora na thabiti sana kuliko yote kwa watu wa kawaida na wasioelimika. Kwa maana, hakuna awezaye kutunyang’anya au kulibatilisha fungu hili lisemalo: “Naamini kanisa takatifu la Kikristo lililo moja tu, ushirika wa watakatifu.”
52. Licha ya hayo, kimsingi, hatujishughulishi na iwapo mtu aliyebatizwa anaamini au haamini. Maana, katika uwezekano huo wa pili, Ubatizo haukomi kuwa halali. 53. Kila kitu kinategemea Neno na amri ya Mungu. Labda, hii ni hoja nyeti lakini msingi wake ni yale niliyokwisha kusema kwamba, Ubatizo ni maji hasa na Neno la Mungu pamoja. Yaani, wakati Neno linaambatana na maji, Ubatizo unakuwa halali ingawa imani haipo. Kwani imani yangu haifanyizi Ubatizo bali inaupokea. Ubatizo haukosi uhalali hata kama umepokewa au umetumiwa visivyo kwani haufungamanishwi na imani yetu bali na Neno. 54. Ingawa Myahudi atakuja leo, adanganye, awe na nia mbaya, na tumbatize kwa nia nzuri, lazima tukiri kwamba, Ubatizo wake ulikuwa halali. Kwani maji na Neno la Mungu vitakuwepo ingawa atashindwa kuupokea inavyostahili. Vivyo hivyo, wale wanaoshiriki Meza ya Bwana isivyostahili wanaipokea sakramenti ya kweli ingawa hawaamini.
55. Kwa hiyo, unaona kwamba, ni upuuzi nafsi potovu zinapokataa Ubatizo wa watoto wachanga. Jinsi tulivyosema, ingawa watoto wachanga hawaamini–hali ambayo si ya kweli hata hivyo, jinsi tulivyothibitisha–bado Ubatizo wao unakuwa halali na yeyote asiwabatize tena. Vivyo hivyo, Sakramenti ya Meza ya Bwana haibatilishwi ikiwa mtu anaijia akiwa na kusudi baya. Isitoshe, asiruhusiwe kuirudia wakati uo huo kwa ajili ya matumizi hayo mabaya, kana kwamba, hakuwa kweli ameipokea sakramenti mara ya kwanza. Hilo lingekuwa ni kukufuru na kuiaibisha sakramenti kwa njia mbaya mno. Tunathubutuje kufikiria kwamba, Neno na agizo la Mungu ni mbaya na siyo halali kwa kuwa tunalitumia vibaya? 56. Kwa hiyo, ninasema, ikiwa hukuamini awali, basi, amini sasa na ukiri: “Kwa kweli, Ubatizo ulikuwa halali, lakini kwa bahati mbaya, sikuupokea vyema.” Mimi mwenyewe na wote waliobatizwa lazima tuseme mbele za Mungu: “Ninakuja hapa katika imani yangu, na katika imani ya wengine. Hata hivyo, siwezi kuutegemea ukweli kwamba, ninaamini na watu wengi wananiombea. Juu ya hili, ninaamini kwamba, ni Neno na amri yako.” Ninaenda kwa Sakramenti ya Meza ya Bwana vivi hivi tu, siyo kwa nguvu ya imani yangu mwenyewe, bali katika nguvu ya Neno la Kristo. Ninaweza kuwa imara au dhaifu. Hilo ninaliacha mikononi mwa Mungu. Hata hivyo, ninalijua hili kwamba, ameniamuru niende,
nile, na ninywe, na kadhalika na kwamba, hunipa mwili wake na damu. Hatasema uongo wala hatanidanganya. 57. Tunafanya vivyo hivyo katika Ubatizo wa watoto wachanga. Tunamleta mtoto tukitumainia kwamba, anaweza kuamini, na tunamwomba Mungu ampe imani. Lakini hatumbatizi kwa sababu hiyo bali kwa Agizo la Mungu tu. Kwa nini? Kwa sababu tunajua kwamba, Mungu hasemi uongo. Kwa ufupi, mimi, jirani yangu, na watu wote wanaweza kukosea na kudanganya lakini Neno la Mungu haliwezi kudanganya.
58. Kwa hiyo, ni nafsi zenye kiburi tu na pumbavu zinazohitimisha kwamba, ambapo hapana imani ya kweli, Ubatizo wa kweli hauwezi kuwepo pia. Kadhalika, ninaweza kuitoa hoja kwamba: “Ikiwa sina imani, basi, Kristo si kitu.” Au tena: “Ikiwa mimi si mtiifu, basi, baba, mama, na mahakimu si kitu.” Je, ni sahihi kuhitimisha kwamba, ikiwa mtu yeyote hafanyi lililompasa, analolitumia vibaya halina uwepo wala thamani? 59. Rafiki yangu, afadhali uugeuze ubishi na uhitimishe barabara kwa sababu umeupokea Ubatizo visivyo, licha ya huo kuwa na uwepo na thamani. Usemi unakuwa: “Abusus non tollit, sed confirmat substantiam.” Yaani, “Utumishi mbaya hauharibu kitu, lakini unathibitisha kiini chake.” Dhahabu haiachi kuwa dhahabu kwa sababu kahaba anaivalia katika dhambi na aibu.1511
60. Kwa hiyo, acheni hitimisho liwe kwamba, daima, Ubatizo hubakia kuwa halali na hudumisha uadilifu wake ingawa mtu mmoja tu alibatizwa, na hakuwa na imani ya kweli aidha. Kwa maana, agizo na Neno la Mungu haliwezi kubadilishwa au kugeuzwa na mwanadamu. 61. Lakini hawa walokole wamepofushwa kiasi kwamba, hawaifahamu amri na Neno la Mungu. Wanauona Ubatizo tu kama maji yaliyo ndani ya kijito au ndani ya jungu, na mahakimu kama watu wa kawaida tu. Kwa kuwa hawaoni imani wala utiifu, wanahitimisha kwamba, haya maagizo yenyewe si halali. 62. Hapa, Ibilisi mchochezi na mchongezi amejibanza na angependa kuyanyakua mataji kutoka kwa watawala na kuyakanyagia chini ya miguu. Licha ya hayo, angependa kuyapotosha na kuyabatilisha matendo na maagizo yote ya Mungu. 63. Kwa hiyo, ni lazima tuwe waangalifu na tujiandae vya kutosha tusije tukapotoshwa kutoka kwa Neno linahusiana na Ubatizo kama alama tupu tu, jinsi walokole wanavyoota.
64. Mwisho, ni lazima tujue Ubatizo unamaanisha nini na ni kwa nini Mungu aliiamuru hii alama na adhimisho la nje kwa ajili ya sakramenti ambayo kwayo, tunapokelewa kwanza katika Kanisa la Kikristo. 65. Tendo au adhimisho hili lina asili yake katika kuzamishwa majini ambayo yanatufunika kabisa na kutolewa
1511 Lugha ya methali.
nje tena. Sehemu hizi mbili–kuzamishwa majini na kutolewa nje1512 tena–zinaonyesha nguvu na matokeo ya Ubatizo ambayo ni kuuawa tu kwa Adamu wa kale na ufufuo wa mtu mpya. Matendo yote mawili lazima yaendelee maishani mwetu. Hivyo basi, maisha ya Mkristo ni Ubatizo wa kila siku, unaoanzishwa mara moja na kuendelea siku zote. Kwa maana, lazima tufanye hivyo daima, tukiliondoa lolote linalomhusu Adamu wa Kale ili lolote la mtu mpya liweze kujitokeza. Mtu wa kale ni nini? 66. Yeye ni lile lililozaliwa ndani yetu kutoka kwa Adamu, mwepesi wa hasira, mwenye chuki, mwenye husuda, mwasherati, mlafi, mkunguni, mwenye kiburi, na asiyeamini. Anashambulia kwa maovu yote na kwa asili hana lolote zuri ndani yake. 67. Sasa, tunapoingia katika ufalme wa Kristo, uovu huu hauna budi kupungua siku kwa siku ili tunapoendelea kuishi tuzidi kuwa watulivu, wapole, na wema. Isitoshe, tuendelee kujitenga na uchoyo, chuki, wivu, na majivuno.
68. Haya ndiyo matumizi mema ya Ubatizo miongoni mwa Wakristo, yanayodhihirishwa kwa Ubatizo wa maji. Ambapo masahihisho haya ya maisha hayatokei, lakini mtu wa kale anapewa nguvu uhuru na anaimarika daima, basi, Ubatizo hautumiwi bali unaasiwa. 69. Wale walio nje ya Kristo wanaweza tu kuzidi kuwa wabaya siku kwa siku. Ni jinsi methali ifuatayo inavyosema kweli kabisa: “Umri ukiongezeka, uovu huzidi.” 70. Ikiwa mwaka mmoja uliopita mtu alikuwa sodai na mchoyo, mwaka huu atazidi kuwa mbaya zaidi. Kwa hiyo, maovu hukua na kuongezeka ndani yake kutoka ujana wake na kuendelea. Mtoto mdogo, ambaye hana ovu maalumu, huwa mwovu na mwasherati anapokua. Anapokuwa mtu mzima, maovu halisi huzidi kuwa na nguvu siku kwa siku. 71. Basi, mtu wa kale huiandama mielekeo ya asili yake ikiwa hazuiwi na kukandamizwa kwa nguvu ya Ubatizo. Kwa upande mwingine, tunapokuwa Wakristo, mtu wa kale hupungua siku zote hadi anaangamizwa mwishowe. Hii ndiyo maana ya kutumbukia katika Ubatizo na kutokezea tena kila siku. 72. Hivyo, ishara ya nje imeteuliwa, si kwa sababu ya lile inalolitoa kwa nguvu, lakini kwa ajili ya inalolidhihirisha pia. 73. Ambapo kuna imani pamoja na matunda yake, hapo, Ubatizo huwa si ishara tupu bali matokeo yanayoandamana nao. Lakini ambapo hakuna imani, Ubatizo unabakia kuwa alama tu isiyozaa matunda.
74. Unaona hapa kwamba, kwa nguvu na kwa maana yake, Ubatizo huitambua pia sakramenti ya tatu iliyojulikana zamani kama toba, ambayo hakika ni Ubatizo. 75. Maana ya toba ni kumshambulia kwa dhati mtu wa kale na kuingia katika maisha mapya? Kwa hiyo, ukiishi katika toba, unatembea katika Ubatizo ambao 1512 Kawaida, watoto wachanga walibatizwa katika karne ya kumi na tano kwa njia ya mzamo. Yaani, walizamishwa majini mara tatu. Wakati wa majira ya baridi kali desturi hii ilikuwa hatari kwa maisha ya watoto wachanga.
unayatangaza maisha haya mapya, unayatoa, unayaanzisha na unayaendeleza. 76. Katika Ubatizo, tunapewa neema, Roho Mtakatifu, na nguvu za kumkandamizia mtu wa kale ili mpya aweze kutokezea na kukua kwa nguvu. 77. Kwa hiyo, Ubatizo hudumu milele. Ingawa tunaanguka na kutenda dhambi, hata hivyo, daima tuna njia ya kuurudia ili tuweze tena kumshinda mtu wa kale. 778. Lakini hatuhitaji tena kumwagiwa maji. Ingawa tutazamishwa majini mara mia moja, bado Ubatizo utakuwa mmoja tu na matokeo na maana ya Ubatizo ingeendelea na ingebaki. 79. Kwa hiyo, toba ni kuurejea na kuujongelea Ubatizo, kuanza tena, na kujizoeza lile lililokuwa limeanzishwa mapema na halafu likaachwa.
80. Ninasema hivi kwa shabaha ya kulisahihisha wazo ambalo limeenea miongoni mwetu kwamba, Ubatizo wetu ni tendo lililopita, ambalo hatuwezi kuendelea kulitumia baada ya sisi kuanguka tena dhambini. Tuna dhana kama hiyo kwa sababu tunauchukulia Ubatizo kuwa tendo lililotendwa mara moja tu. 81. Naam, wazo hili linamhusu Mt. Hieronimo kwa maana aliandika: “Toba ndio ubao wa pili ambao ni lazima tuutumie kuogelea mpaka pwani wakati wa maangamizi ya meli baharini.” ambayo tuliipanda tulipoingia katika Kanisa la Kristo.1513 82. Ufasiri huu unauondolea Ubatizo thamani yake na kuufanya usiwe na faida kwetu. Kwa hiyo, kauli hii si sahihi. Meli haiangamii kwani, jinsi tulivyosema, ni agizo la Mungu na si matendo yetu. Lakini inatokea kwamba, tunateleza na kuanguka kutoka melini. Ikiwa mtu yeyote anaanguka, inampasa aharakishe kurudi melini, iendee meli mara moja na kuishikilia mpaka apande tena na aendelee kusafiri ndani yake jinsi alivyofanya mwanzoni.
83. Hivyo, tunaona jinsi Ubatizo ulivyo tendo kubwa na bora sana, ambalo linatunyakua kutoka kinywani mwa Ibilisi na kumfanya Mungu kuwa wetu. Unazishinda na kuziondolea mbali dhambi na kumwimarisha mtu mpya kila siku. Unabakia daima hadi tupite kutoka tabu tuliyo nayo sasa na kutuingiza katika utukufu wa milele. 84. Kwa hiyo, mwache kila mtu auchukulie Ubatizo wake kama vazi la kila siku ambalo analivalia wakati wote. Kila siku ni lazima awe katika imani na miongoni mwa matunda yake. Awe anamkandamiza mtu wa kale na kukua katika yule mpya daima. 85. Ikiwa tunataka kuwa Wakristo, ni lazima tujizoeze tendo linalotufanya tuwe Wakristo. 86. Lakini ikiwa mtu yeyote ataanguka kutoka kwenye Ubatizo wake, acha aurudie. Jinsi Kristo, aliye kiti cha neema,1514 hajiondoi kutoka kwetu au hatukatazi kumrudia ingawa tunatenda
1513 Hieronimo (342-420) Ep. 122, 130, 147 na maelezo kuhusu Is. 3:8-9. Kulingana na maoni ya Hieronimo, Sakramenti ya Ubatizo iliondoa dhambi ya asili na makosa yaliyotendeka kabla ya Ubatizo peke yake. Sakramenti ya Toba ilihitajika ili kuondoa dhambi zilizotendeka baada ya Ubatizo. Maoni ya namna hiyo yalikataa zaidi maana na thamani ya Sakramenti ya Ubatizo na yalihitaji kurekebishwa. 1514 Rom. 3:25; Ebr. 4:16.
dhambi. Hivyo, hazina zake zote na vipaji vyake hubakia. Jinsi tulivyoupata msamaha wa dhambi katika Ubatizo, vivyo hivyo msamaha unavyobakia siku kwa siku wakati wote wa maisha yetu. Yaani, tunapombeba Adamu wa Kale shingoni mwetu.
SEHEMU YA TANO: SAKRAMENTI YA MADHABAHU
1. Jinsi tulivyoushughulikia Ubatizo Mtakatifu chini ya vichwa vitatu, vivyo hivyo tutaishughulikia hii sakramenti ya pili, Sakramenti ya Madhabahu: maana yake, manufaa yake, na anayestahili kuipokea. Haya yote yanathibitishwa kwa maneno ambayo Kristo aliyasema alipoianzisha. 2. Kwa hiyo, yeyote anayenuia kuwa Mkristo na kuishiriki sakramenti lazima ayajue haya. Kwa maana, hatukusudii kuwaruhusu na kuwagawia hii sakramenti wasiojua wanalolitafuta au sababu ya kushiriki kwao. Yafuatayo ndiyo maneno yenyewe:
3. “Bwana wetu Yesu Kristo usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema: ‘Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu uliotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”
“Vivyo hivyo pia alichukua kikombe baada ya kula, akashukuru, kisha akawapa, akisema: ‘Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagwa kwa ajili yenu kwa ondoleo la dhambi. Fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.””1515
4. Wakati huu hatunuii kuzozana na kubishana na wanaokufuru na kuinajisi sakramenti hii. Lakini, sawa na katika Ubatizo, tutajifunza lililo muhimu zaidi kwanza. Yaani, Neno, agizo, au amri ya Mungu iliyo kuu na ya kuzingatiwa. 5. Maana, Chakula cha Bwana hakikubuniwa au kushauriwa na mtu yeyote. Kilianzishwa na Kristo bila ushauri au kusudi la mtu. Jinsi ambavyo Amri Kumi, Sala ya Bwana, na Ukiri wa Imani huhifadhi asili na thamani yao ingawa hatuvitimizi, hatuviombi, au hatuviamini, vivyo hivyo hii sakramenti yenye baraka haiharibiwi na haidhuriwi ingawa tutaitumia na kuishughulikia isiyostahili.
6. Je, unafikiri Mungu anajali sana kuhusu imani na mwenendo wetu kiasi cha kuviruhusu viliharibu agizo lake? La hasha! Vitu vyote visivyodumu vinabaki jinsi Mungu alivyoviumba na kuviamrisha bila kujali tunavyovishughulikia.
7. Lazima hili lisisitizwe kila mara, kwani katika kufanya hivyo, tunaweza kuukanusha ubobokaji wa wenye nafsi asi wanaoichukulia sakramenti kama matendo ya binadamu kinyume cha Neno la Mungu.
1515 1 Kor. 11:23-25; Mt. 26:26-28; Mk. 14:22-24; Lk. 22:19-20
8. Sakramenti ya Madhabahu ni nini? Jibu: Ni mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo Bwana katika mkate na divai ambavyo sisi Wakristo tumeagizwa kula na kunywa kwa Neno la Kristo. 9. Jinsi tulivyosema kuhusu Ubatizo ni kwamba, si maji matupu. Vivyo hivyo, tunasema hapa kwamba, sakramenti ni mkate na divai lakini si mkate au divai tupu jinsi inavyotolewa mezani. Ni mkate na divai iliyojumuishwa na kuunganishwa na Neno la Mungu. 10. Ninasisitiza kwamba, ni Neno linaloipambanua kutoka kuwa mkate na divai tupu na kuifanya kuwa sakramenti ambayo, kwa usahihi, inaitwa mwili na damu ya Kristo. Inasemekana: “Accedat verbum ad elementum et fit sacramentum”–“Neno likiunganishwa na kitu cha asili cha nje, litakuwa sakramenti.’1516 Usemi huu wa Mtakatifu Agostino ni sahihi na umesemwa vizuri sana na ninashuku kama amepata kulisema lolote zuri zaidi kuliko hili. Lazima Neno likifanye kitu cha asili kuwa sakramenti. La sivyo, kinabakia kuwa kitu cha asili tu. 11. Hili si neno na agizo la mtawala au Kaisari. Ni Neno la Enzi ya Mungu ambayo lazima ipigiwe kila goti chini ya miguu yake na ikiriwe, ikubaliwe kwa uchaji, hofu, na unyenyekevu jinsi anavyosema. 12. Kwa Neno hili, unaweza kuitia dhamiri yako nguvu na kutangaza: “Waacheni mashetani mia moja elfu na walokole wote wa dini wasiofikiri, wajitokeze haraka na kusema: “Inawezekanaje mkate na divai kuwa mwili na damu ya Kristo?” Bado ninajua kwamba, nafsi na wataalamu wote pamoja, wana hekima ndogo zaidi kuliko ile iliyo katika kidole kidogo cha Enzi ya Mungu. 13. Hapa tuna Neno la Kristo: “Twaeni mle huu ni mwili wangu. Nyweni nyote katika hiki, hii ni agano jipya katika damu yangu.” Hapa tutakuwa na msimamo wetu na kuona ni nani anayethubutu kumshauri Kristo na kulibadilisha alilolisema. 14. Naam, ni kweli kabisa kwamba, ukilitoa Neno kutoka katika vitu vya asili au ukivitazama mbali na Neno, utakuwa na mkate na divai ya kawaida tu. Lakini maneno yakibakia, jinsi ilivyo sahihi na lazima, basi, utakatifu upatikanao kwayo ni mwili na damu halisi ya Kristo. Ndivyo ilivyo kwa maana jinsi tulivyo nayo kutoka kinywani mwa Kristo, hawezi kusema uongo au kudanganya.
15. Hivyo, ni rahisi kuyajibu maswali ya kila aina ambayo sasa yanawasumbua watu. Kwa mfano, maswali kama, je, mchungaji mbaya anaweza kuitoa sakramenti? 16. Hitimisho letu ni: ingawa mlaghai ataipokea au kuitoa, bado ni sakramenti ya kweli–yaani, mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo–halisi sawa na wakati mtu anaitumia kwa heshima kuu mno. Kwa maana, haina msingi wake katika utakatifu wa mwanadamu lakini katika Neno la Mungu. Naam, kwa kuwa hakuna mtakatifu duniani wala hakuna malaika mbinguni awezaye kugeuza mkate na divai kuwa mwili na damu ya Kristo, vivyo hivyo, hakuna hata mmoja 1516 Taz. rejeo la 69.
anayeweza kuigeuza au kuibadilisha sakramenti ingawa itatumiwa isivyostahili. 17. Kwa maana, Neno ambalo liliianzisha sakramenti halifanyiki kuwa uongo kwa sababu ya kutostahili au kutoamini kwa mtu. Kristo hasemi: “Ukiamini, au ukistahili, unapokea mwili na damu yangu,” bali, “Twaa, kula na kunywa, huu ni mwili na damu yangu.” Hali kadhalika, yeye husema: “Fanyeni hivi, yaani, ninalolifanya ninalolianzisha, ninalokutolea, na ninalokuagiza ulichukue sasa.
18. Hii ni sawa na kusema: “Haidhuru, ustahili au usistahili, hapa una mwili na damu ya Kristo kwa sababu ya maneno haya ambayo yameunganishwa na mkate na divai.” Lizingatieni na likumbukeni hili vizuri. 19. Kwa maana, maneno haya ndiyo msingi wa ubishi wetu wote, ulinzi, na kinga dhidi ya upotovu na hila zote ambazo zimepata kutokea au zitakazotokea.
20. Tumeichunguza sehemu ya kwanza kwa ufupi, yaani, kiini cha hii sakramenti. Sasa tutazungumzia nguvu na faida yake ambayo iliifanya sakramenti hii kuanzishwa hasa kwa sababu ni lazima sana kujua tunalolitafuta na tunalolipata hapa. 21. Haya ni dhahiri kabisa kutoka kwa maneno yaliyonukuliwa: “Huu ni mwili na damu yangu, uliotolewa na kumwagwa kwa ajili yenu kwa ondoleo la dhambi.” 22. Kwa maneno mengine, tunaishiriki sakramenti kwa sababu tunaipokea hazina kubwa ambayo kwayo, tunapata ondoleo la dhambi. Kwa nini? Kwa maana, kuna maneno ambayo kwayo, inatolewa. Kristo hunialika kula na kunywa ili sakramenti iweze kuwa yangu na iweze kuwa chemchemi ya baraka kwangu kama ahadi na alama imara, naam, kama zawadi iyo hiyo ambayo amenipatia dhidi ya dhambi zangu, kifo, na maovu yote.
23. Kwa hiyo, kinastahili kuitwa chakula cha nafsi kwani kinamlisha na kumtia nguvu mtu mpya. Kwa kuwa ni kweli kwamba, kwa njia ya Ubatizo, tunazaliwa upya mara ya kwanza, hali yetu ya ubinadamu haijapoteza sura yake ya kale. Kuna vikwazo na majaribu mengi ya Ibilisi na ulimwengu kiasi kwamba, mara nyingi tunachoka, tunanyong’onyea, na wakati mwingine hata tunajikwaa. 24. Chakula cha Bwana kinatolewa kama chakula na mlo wa kila siku ili imani yetu iweze kuburudika na kuimarika yenyewe na isidhoofishwe katika mapambano bali izidi kuwa hodari daima. 25. Kwa maana, maisha mapya lazima yawe yale yanayokua na kuendelea siku zote. Wakati uo huo, maisha haya lazima yapatwe na upinzani mwingi. 26. Ibilisi ni adui mwenye ghadhabu kali mno. Akiona kwamba, tunampinga na kumshambulia mtu wa kale, na asipoweza kutushinda kwa nguvu, yeye hunyemelea na hujifichaficha kila mahali, akizijaribu aina zote za hila, na hakomi mpaka mwishowe atuchoshe ili tuikane imani yetu au kukubali kumtumikia Ibilisi sana1517 na kuwa wasiojali au watu wasiokuwa na subira. 27. 1517 Lugha ya methali: kuacha kufanya kazi/kukubali kumtumikia Ibilisi sana.
Faraja ya Chakula cha Bwana inatolewa kutupatia nguvu na kiburudisho mioyo yetu inapoona maumivu ya kugandamizwa.
28. Basi, hapa tena, nafsi zetu zenye akili zaidi hujipotosha zenyewe kwa elimu ya juu na hekima, zikinguruma na kufoka: “Mkate na divai vinawezaje kusamehe dhambi au kuimarisha imani?” Hata hivyo, zinajua kwamba, hatulidai hili kutoka kwa mkate na divai, maana, wenyewe, mkate ni mkate, bali kuhusu huo mkate na hiyo divai ambavyo ni mwili na damu ya Kristo na vinavyounganishwa na maneno. Tunasema, hivi tu ndivyo hazina ambayo kwayo, msamaha wa dhambi unapatikana. 29. Hazina hii inajulishwa na kuwasilishwa kwetu kwa njia ya maneno: “uliotolewa na iliyomwagika kwa ajili yenu.” Hapa una kweli zote mbili, yaani, mwili na damu ya Kristo, na kwamba, hivi ni vyako kama hazina na zawadi. 30. Mwili wa Kristo hauwezi kuwa wenye hauzai matunda, kitu ovyo, mpungufu, wala usiokuwa na maana. Hata hivyo, haidhuru hazina hii yenyewe ilivyo kubwa, lazima ijumuishwe katika Neno na itolewe kwetu kwa njia ya Neno na. La sivyo, hatungeweza kuielewa au kuitafuta.
31. Kwa hiyo, ni upuuzi kusema kwamba, mwili wa Kristo hautolewi na damu yake haimwagiki kwa ajili yetu katika Chakula cha Bwana, na kwamba, kwa sababu hiyo, hatuwezi kuupata msamaha wa dhambi katika sakramenti. Ingawa kazi ilitimizwa na msamaha wa dhambi ulipatikana msalabani, hata hivyo, haiwezi kutujia kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kwa njia ya Neno. Tungewezaje kujua kwamba, hili limetimizwa na kutolewa kwetu kama halikutangazwa katika mahubiri kwa Neno la kinywa? Wataanzia wapi kuujua msamaha, na watawezaje kuufahamu na kujitwalia isipokuwa waamini kweli Maandiko Matakatifu na Injili?
32. Sasa, Injili yote na mafungu ya Ukiri: “Naamini Kanisa Takatifu la Kikristo, na msamaha wa dhambi,” yamejumuishwa katika hii sakramenti na kutolewa kwetu kwa njia ya Neno. Basi, kwa nini tuiruhusu hazina hii iondolewe kutoka katika sakramenti? Wapinzani wetu lazima watubu bado kwamba, haya ndiyo maneno yayo hayo tunayoyasikia kila mahali katika Injili. Wanaweza kusema kwamba, maneno haya hayana thamani katika sakramenti jinsi wanavyothubutu kusema kwamba, Injili yote au Neno la Mungu halina thamani mbali na Sakramenti.
33. Kufikia hapa, tumeishughulikia sakramenti kwa kusisitiza kiini, matokeo, na faida zake. Kwa ufupi, jinsi tulivyosema hapo juu kuhusu Ubatizo na mahali pengine pengi, jibu linakuwa: ni yule anayeamini lile maneno yalisemalo na yalitoalo, kwa sababu hayasemwi au hayahubiriwi kwa mawe na miti bali kwa wanaoyasikia, ambao Kristo huwaambia: “Twaeni, mle,” na kadhalika. 34. Kwa sababu yeye hutoa na huahidi msamaha wa dhambi, hauwezi kupokelewa ila kwa imani. Yeye mwenyewe huidai imani hii katika Neno anaposema: “Uliotolewa
kwa ajili yenu,” na “iliyomwagika kwa ajili yenu,” kana kwamba, alisema: “Hii ndiyo sababu ninaitoa na kuwaamuru kula na kunywa ili mwichukue kama yenu kabisa na mwifurahie.” 35. Yeyote ambaye huyaruhusu maneno haya yasemwe kwake na kuamini kwamba, ni ya kweli, ana lile maneno yanayolitangaza. Lakini ambaye haamini hana lolote kwa maana anauachilia mbaraka huu utolewe kwake bure na hukataa kuufurahia. Hazina hii imefunguliwa na imewekwa mlangoni mwa kila mmoja. Naam, mezani mwa kila mmoja, lakini ni wajibu wako pia kuichukua hakika kwa imani jinsi maneno yanavyokuambia.
36. Sasa basi, haya ndiyo maandalizi yanayohitajika kwa Mkristo ili aipokee hii Sakramenti inavyostahili. Kwa sababu hazina hii inatolewa kikamilifu katika maneno, inaweza kufahamika na kutwaliwa na moyo tu. Zawadi ya namna hiyo na hazina ya milele haviwezi kushikwa kwa mkono. 37. Kufunga, kuomba, na matendo kama hayo yanaweza kuwa na nafasi kama maandalizi ya nje na kama mazoezi ya watoto ili mwili wa mtu uweze kuwa na mwenendo mzuri na uwe na heshima kwa ajili ya mwili na damu ya Kristo. Lakini lile linalotolewa ndani na pamoja na sakramenti haliwezi kueleweka na kutwaliwa na mwili. Hili linatendwa na imani ya moyo ambayo huitambua na kuitamani hazina hii. 38. Sasa, ya kutosha yamesemwa kuhusu mafundisho yote ya kawaida kuhusu mambo ya msingi ya hii sakramenti. Mambo mengine zaidi yataweza kusemwa wakati mwingine.
39. Hitimisho, kwa kuwa sasa tuna ufafanuzi na mafundisho sahihi kuhusu sakramenti, kuna haja kubwa pia ya onyo dogo na kusihi kwamba, hazina kubwa ya namna hiyo, ambayo inatolewa na inagawiwa Wakristo kila siku, isipuuzwe.
Ninamaanisha kwamba, wale ambao hudai kuwa Wakristo lazima wajiandae kuipokea hii sakramenti yenye mbaraka kila mara. 40. Kwa kuwa tunaona kwamba, watu wanakuwa walegevu na wazembe kuhusu upokeaji wa sakramenti hii. Watu wanaoisikiliza Injili, wanauacha mwaka upite, miwili, mitatu, au zaidi bila kuipokea sakramenti, kana kwamba, wao ni Wakristo imara kiasi cha kutoihitaji. Sasa, upuuzi wa Papa umepigwa marufuku na tuko huru kutokana na ugandamizwaji na mamlaka yake. 41. Wengine hujiruhusu wazuiwe na wavunjwe moyo nayo kwa sababu tumefundisha kwamba, mtu asiiendee mpaka ajihisi kwamba, ana njaa na kiu kinachomsukuma kwenda kuipokea. Wengine hulifanya kuwa suala la hiari, lisilokuwa la lazima, na kwamba, inatosha kama wanaamini tu. Hivyo, wengi huwa mbali kimawazo kiasi cha kuwa washenzi na mwishowe huidharau sakramenti na Neno la Mungu. 42. Tunarudia, sasa ni kweli kwamba, hakuna mtu yeyote awezaye kuzuiwa kwa nguvu au kulazimishwa kwa namna yoyote, tusije tukayaanzisha machinjo mapya ya nafsi. Hata hivyo,
lazima ieleweke kwamba, watu ambao hujinyima na hujizuia wenyewe makusudi kuishiriki sakramenti kwa muda mrefu, wasichukuliwe kuwa Wakristo. Kristo hakuianzisha sakramenti ili ichukuliwe tu kama tamasha bali aliwaamuru Wakristo wake kula na kunywa na kumkumbuka kwa njia hiyo.
43. Naam, Wakristo wa kweli ambao huitunza na kuiheshimu sakramenti watajihimiza na kujilazimisha kuishiriki kwa hiari yao. Hata hivyo, ili watu wa kawaida na wanyonge, ambao wangependa kuwa Wakristo wavutiwe kuona sababu na haja ya kuipokea Sakramenti, itatubidi tuwe makini kiasi kuhusu suala hili. 44. Sawa na mambo mengine yanayohusu imani, upendo, na uvumilivu, haitoshi kufundisha na kuagiza tu. Badala yake, lazima pawe na ushawishi kila siku, lazima tuendelee kuhubiri kuhusu somo hili ili watu wasije wakalipuuza na kuchoshwa. Kwani, kutokana na uzoefu tunajua kwamba, daima, Ibilisi hulipinga hili na kila tendo la Mkristo, akiwawinda na kuwawinga watu awezavyo waiache sakramenti.
45. Kwanza, tuna matini wazi katika maneno ya Kristo: “Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Haya ndiyo maneno ya maagizo na amri, yanayowaamuru wote watakaokuwa Wakristo waishiriki Sakramenti. Ni maneno yaliyosemwa kwa wanafunzi wake Kristo. Hivyo, yeyote atakayekuwa mmoja wao pia, mwache aishikilie hii Sakramenti kwa uaminifu, si kwa kulazimishwa au kushurutishwa na watu bali kwa kutii na kumpendeza Kristo Bwana. 46. Hata hivyo, unaweza kusema: “Lakini maneno ‘kila mnywapo’ yameongezewa. Kwa hiyo, hamshurutishi mtu yeyote bali ametuacha hivyo ili tuwe huru kuchagua.” 47. Ninajibu: Hayo ni kweli lakini hayasemi hatupaswi kuishiriki kamwe. Naam, maneno yenyewe, “kila mnywapo” yanamaanisha lazima tufanye hivyo kila mara. Yameongezewa kwa sababu Kristo anaitaka sakramenti iwe huru. Anataka isifungamanishwe na wakati fulani maalumu kama Pasaka, ambayo Wayahudi walilazimika kula mara moja kila mwaka, jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi mpevu wa kwanza, bila kuibadilisha siku hata moja. Kristo anamaanisha: “Ninawaanzishia Pasaka au chakula mtakachokifurahia, si usiku huu mmoja kila mwaka, bali kila mara, wakati wowote, na mahali popote mpendapo, kulingana na wasaa na haja ya mtu, bila kufungamanishwa na nafasi au wakati wowote maalumu.” 48. Hata hivyo, baadaye, Papa aliipotosha na kuibadilisha kuwa sherehe ya Kiyahudi.1518
49. Hivyo, unaona kwamba, hatupatiwi uhuru wa kuidharau sakramenti. Wakati mtu, anauruhusu muda mrefu upite bila kuihitaji sakramenti, na bila
1518 Mwaka wa 1215, sinodi ya nne ya Laterano iliagiza kwamba, ikiwezekana, inambidi kila Mkristo kupokea, kwa heshima, Sakramenti ya Chakula cha Bwana wakati wa Pasaka.
kuzuiwa na lolote, ninaliita tendo hilo kuidharau sakramenti. Iwapo unataka uhuru wa namna hiyo, unaweza pia kuwa na uhuru wa kutokuwa Mkristo. Kisha, huhitaji kuamini au kuomba kwa sababu kila moja ni sawa na amri ya Kristo. Lakini kama unataka kuwa Mkristo, lazima uitimize na uitii amri hii kila wakati. 50. Kwa sababu amri hii lazima ikusukume kuyachunguza maisha yako ya ndani na kuakisi: “Tazama, je, mimi ni Mkristo wa aina gani? Kama ningekuwa mmoja wao, kakika ningekuwa na haja ndogo angalau kulifanya lile Bwana wangu ameniamuru nilifanye” 51. Naam, kwa kuwa tunaionyesha chuki kubwa ya namna hiyo kwa sakramenti, watu wanaweza kuhisi, kwa urahisi hasa, tulikuwa Wakristo wa namna gani tulipokuwa chini ya Upapa, tulipoishiriki sakramenti kwa kushurutishwa tu, tulipoogopa amri za watu bila furaha na upendo, na bila hata kuijali Amri ya Kristo. 52. Lakini hatumlazimishi wala hatumshurutishi mtu yeyote wala hatumhitaji aishiriki sakramenti kwa kututumikia au kutupendeza. Linalopasa kukusukuma na kukushurutisha ni ukweli kwamba, Kristo analitaka na linampendeza. Usikubali kulazimishwa na watu katika jambo linalohusiana na imani au tendo zuri. Yote tunayoyafanya ni kukuhimiza uweze kufanya ambalo unapaswa kulifanya, si kwa ajili yetu bali kwa ajili yako mwenyewe. Anakualika na kukuchochea. Ulikidharau tendo hili, itakubidi ulijibu wewe mwenyewe.
53. Hili ni wazo la kwanza hasa kwa manufaa ya waliorudia mazoea mabaya na wasiojali ili wajirudi na kuamka. Jinsi nimeona katika uzoefu wangu mwenyewe na jinsi kila mmoja atakavyojionea mwenyewe, ni kweli kabisa kwamba, mtu akijitenga na sakramenti siku kwa siku, atakuwa baridi zaidi na zaidi, atapoa, na mwishowe ataidharau kabisa. 54. Ili kuepukana na hayo, lazima tuichunguze mioyo na dhamiri zetu. Isitoshe, lazima tutende kama watu wenye ari kweli ya kuwa wenye haki mbele za Mungu. Tukifanya hivyo zaidi na zaidi, ndivyo mioyo yetu itakavyozidi kupashwa moto na kuamshwa ili isipoe kabisa. 55. Lakini, iwapo unasema: “Itakuwaje nikijihisi kwamba, sistahili?” Jibu: “Hili ni jaribio langu pia, hasa nililorithi kutoka kwa daraja la awali chini ya Papa, tulipojitesa wenyewe ili tuwe safi kamili ili Mungu asipate hata waa dogo ndani yetu. Kwa hiyo, tulikuwa waoga sana kiasi kwamba, kila mmoja wetu alikuwa katika mshangao mkuu akisema, “Lo, sistahili!” Kisha, asili na akili huanza kutofautiana na kutostahili kwetu kwa njia ya hii baraka kuu na ya thamani kubwa na kuonekana kama taa nyeusi inayohitilafiana na jua linalong’aa sana au kama samadi kinyume cha johari. 56. Kwa kuwa, asili na akili huliona hili, watu kama hao wanakataa kuishiriki sakramenti na wanangojea wajitayarishe. Kisha, juma moja inapita hadi nyingine, nusu mwaka inapita, na nyingine tena. 57. Ukichagua kujiona ulivyo mzuri na safi, ukijishughulisha na wakati ambapo lolote halitaichoma dhamiri yako, hutaishiriki kamwe.
58. Kwa hiyo, tunapaswa kutofautisha kati ya watu. Wasiokuwa na haya na wakaidi hawana budi kuambiwa wakae mbali kwa sababu hawafai kuupokea msamaha wa dhambi kwani hawautamani na hawataki kuwa wema. 59. Baadhi wasiojali na walio mafisadi lakini wangependa kuwa wema, wasijitenge nayo wenyewe, ingawa wao ni dhaifu na wanyonge kwa vyovyote. Jinsi mtakatifu Hilario1519 alivyosema: “Isipokuwa mtu awe ametenda dhambi inayoweza kumfanya atengwe na Kanisa na inayomfanya alipoteze jina la Kikristo, hana budi kujizuia kuishiriki sakramenti, asije akajinyang’anya uzima mwenyewe. 60. “Hakuna mtu yeyote atakayeendelea kiasi cha kutobakia na aina nyingi za udhaifu wa kawaida katika hali yake ya ubinadamu.”
61. Watu wenye mashaka ya namna hiyo ni lazima wajifunze kwamba, ni hekima kubwa kuliko zote kufahamu kwamba, hii sakramenti haitegemei ustahiki wetu. Hatubatizwi kwa sababu tunastahiki na tu watakatifu wala hatuji kwa ungamo tukiwa safi na bila dhambi. Kinyume chake, tunakuja kama watu maskini na wanyonge hasa kwa sababu hatustahiki lolote. Jambo la pekee ni mtu asiyetaka kupokea neema na ondoleo la dhambi na hana nia ya kuyarekebisha maisha yake. 62. Mtu anayetaka kupokea neema na faraja kwa moyo, lazima ajilazimishe kuishiriki na asimruhusu yeyote kumzuia akisema: “Ningependa sana kustahiki, lakini naja, si kwa sababu ya ustahiki wangu wowote, bali kwa sababu ya Neno lako kwani wewe umeagiza hivyo na ninataka niwe mwanafunzi wako, haidhuru udogo wa ustahiki wangu ulivyo.” 63. Hili ni gumu kwa sababu kila wakati tunashindana na kizuizi na kipingamizi hiki cha kushikilia kwamba, tunajimakinikia sana kuliko tunavyomakinikia maneno yatokayo kinywani mwa Kristo. Asili ingetaka kutenda kwa njia ambayo kwayo, ingejipumzisha na kujitegemea yenyewe kikamilifu. La sivyo, hukataa kwenda hatua moja. Basi, yaacheni haya yatoshee kuhusu wazo la kwanza.
64. Jambo la pili ni kwamba, ahadi, ambayo ingetuvuta na kutuchochea kwa nguvu, imeambatanishwa na agizo jinsi tulivyosikia hapo juu. Maneno ya rehema na ya kupendeza ndiyo haya: “Huu ndio mwili wangu uliotolewa kwa ajili yako;” “hii ndiyo damu yangu, iliyomwagika kwa ajili yako kwa ondoleo la dhambi.”
65. Nimesema, maneno haya hayahubiriwi kwa miti au mawe ila kwako wewe na kwangu mimi. La sivyo, Kristo angenyamaza na hangeianzisha sakramenti. Sasa fikiria, kisha ujijumuishe katika neno “yenu” ili asiseme nawe bure. 66. Katika sakramenti hii anatupatia hazina yote aliyotuletea kutoka mbinguni ambayo kwayo, anatualika mahali pengi kwa rehema jinsi anavyosema katika Mt. 11:28: 1519 Hilario wa Poitieso (mnamo 315-367), Athanasio wa Magharibi. Kauli hii haitoki katika maandiko ya Hilario. Hata hivyo, inapatikana chini ya jina lake katika ‘Decr.Grat. P. III D. 2 c. 15.’ Kauli iyo hiyo inapatikana katika nyaraka za Agostino Ep. 53 c. 3.
498
“Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” 67. Hakika ni dhambi na aibu kwamba, anapotuita kwa upole na uaminifu na anatusihi kwa ajili ya faida yetu ya juu na kubwa kuliko zote, tunaitikia shingo upande na kuipuuza pakubwa kiasi kwamba, tunapoa kabisa, tunakuwa wasiojali, na tunapoteza hamu na upendo wote kwayo. 68. Hatupaswi kuichukulia sakramenti kama kitu chenye madhara ambacho lazima tukitoroke. Badala yake, tuichukulie kama dawa safi, yenye kuponya, ya kutuliza, inayotusaidia, na kutuchangamsha mwili na nafsi.1520 Kwa sababu, ambapo nafsi inaponywa, mwili unanufaika hapo pia. Basi, kwa nini tunajifanya kana kwamba, sakramenti ni sumu ambayo ingetuua tungeishiriki?
69. Naam, ni dhahiri kwamba, wanaoidharau sakramenti na wanaoishi maisha yasiyokuwa ya Kikristo, wanaipokea kwa hasara na laana yao.1521 Lolote halitaweza kuwa jema au lenye manufaa kwa watu kama hao, jinsi ilivyo kwa mgonjwa ambaye anajua kwamba, makusudi, anakula na kunywa alivyokatazwa na tabibu. 70. Lakini wanaouhisi udhaifu wao, na wanaotamani sana waepukane nao na kuhitaji msaada, wanapaswa kuichukulia na kuitumia sakramenti kama kiuasumu chenye thamani kubwa kinachoiharibu sumu katika viwiliwili vyao.1522 Kwa sababu katika sakramenti, mnapokea msamaha wa dhambi kutoka kinywani mwa Kristo, ambao una na unatuletea neema ya Mungu, Roho Mtakatifu, na vipawa vyake vyote, yaani, ulinzi, kinga, na nguvu dhidi ya kifo, Ibilisi, na maovu yote.
71. Kwa hiyo, kutoka kwake Mungu una amri na ahadi ya Kristo Bwana. Wakati uo huo, wewe ungehitaji kuchochewa na upungufu wako mwenyewe, unaoning’inia shingoni mwako, na ambao ndiyo sababu ya dhati ya amri hii, yaani, mwaliko na ahadi. Kristo mwenyewe anasema: “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.”1523 72. Yaani, wanaosumbuliwa na kulemewa na dhambi, wanaoogopa kifo, na mashambulizi ya mwili na Ibilisi. Iwapo umelemewa na unauhisi udhaifu wako, ishiriki sakramenti kwa furaha na upokee viburudisho, faraja, na nguvu. 73. Ukingojea hadi utakapoondolewa mzigo wako ndipo uweze kuishiriki sakramenti ukiwa safi na aliyestahiki, itakubidi ujitenge nayo milele. 74. Katika hali hiyo, Kristo anaitamka hukumu: “Ukiwa safi na mnyofu, huna haja nami na sina haja nawe.” Kwa hiyo, wasiostahiki ni wale wasiouhisi udhaifu
1520 Yaani, kwa mwanadamu mzima si kwa sehemu yake tu.
1521 Yaani, katika Chakula cha Bwana, washiriki wote walioamini hupokea mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo kwa ondoleo la dhambi na baraka zote. Wasioamini, hupokea hasara na hukumu. (Kilatini: ‘manducatio infidelium’). Taz. 1 Kor. 11:27
1522 Kama mtu aliyeumwa na nyoka.
1523 Mt. 9:12
wao na wasiokubali kuwa wao ni wenye dhambi.
75. Iwapo utasema: “Nitafanya nini iwapo sihisi haja hii, wala njaa, wala kiu cha sakramenti?” Jibu: Watu walio katika hali ya namna hiyo ya moyo, ambao hawawezi kuihisi, sina shauri zuri zaidi kwao kuliko kupendekeza waiweke mikono yao kifuani mwao na wajiulize kama wameumbwa wakiwa na hali ya ubinadamu. Ukigundua kwamba, una ubinadamu, basi, kwa faida yako mwenyewe usome Waraka wa Paulo kwa Wagalatia na ujue matunda ya mwili ni yapi: “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo.”1524 76. Kwa hiyo, kama huwezi kuuhisi upungufu, basi, angalau yaamini Maandiko Matakatifu. Hayatakudanganya, nayo yanaujua ubinadamu wako vyema kuliko unavyoujua wewe mwenyewe. Ndivyo Mt. Paulo anavyohitimisha katika Rum. 7:18. “Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema.“ Sasa, iwapo Mt. Paulo anaweza kusema hivyo kuhusu mwili wake, tusijifanye kuwa wazuri wala watakatifu kumshinda. 77. Lakini ni vibaya zaidi kuwa hatuzitambui dhambi zetu kwa sababu ni dalili kwamba, miili yetu ni yenye ukoma usiohisi lolote ingawa ugonjwa unaendelea kwa ukali na machungu sana. 78. Jinsi tulivyokwisha kusema, ingawa umekufa kabisa dhambini, angalau yaamini Maandiko Matakatifu yanayoitamka hukumu hii juu yako. Kwa ufupi, unavyopungukiwa kuhisi dhambi na udhaifu wako, ndivyo unavyokuwa na sababu zaidi ya kuishiriki sakramenti na kuitafuta tiba.
79. Tena, yatazame mazingira yako uone kama wewe u duniani pia. Kama hujui waulize majirani zako. Kama u duniani, usifikirie kwamba, hakutakuwepo na dhambi na mahitaji. Jaribu tu kujifanya kwamba, unataka kuwa mwema, ishike Injili, na uone kama hutapata maadui wa kukudhuru, kukudhulumu, kukuumiza, na kukusababishia dhambi na maovu. Kama hujaupata uzoefu huu, basi, usikie kutoka katika Maandiko Matakatifu ambayo kila mahali yanautoa ushuhuda huu kuhusu dunia.
80. Licha ya mwili na dunia, hakika utakuwa na Ibilisi anayekuzunguka. Hutamponda kabisa miguuni mwako kwa sababu Bwana wetu Kristo hakuweza kumwepuka kabisa. 81. Ibilisi ni nani? Maandiko Matakatifu yanamwita mwongo na mwuaji.1525 Mwongo anayeushawishi moyo uliache Neno la Mungu, anayekufanya kipofu, anayekufanya usiweze kuihisi haja yako au usije kwake Kristo. Ni mwuaji anayeionea wivu kila saa ya maisha yako. 82. Ungeweza kuona
1524 Gal. 5:19-21 1525 Yn. 8:44
wingi wa visu, mikuki, na mishale inayokulenga kila wakati, ungependa kuishiriki sakramenti kila inapowezekana. Sababu ya pekee inayotufanya tuendelee kwa usalama tulivyo na bila uangalifu ni kwamba, hatukiri wala hatuamini kwamba, tu katika mwili au chini ya himaya ya Ibilisi au katika dunia hii mbovu.
83. Kwa hiyo, lijaribu hili na ulifanyie mazoezi kikamilifu. Jichunguze mwenyewe tu, tazama ulipo kidogo, na yashike Maandiko Matakatifu vizuri. Iwapo hutalihisi lolote bado, utakuwa na sababu kubwa zaidi ya kumlilia ndugu yako na kumlilia Mungu. Yapokeeni mashauri ya wengine na yatafute maombi yao, na usikate tamaa kamwe hadi jiwe liondolewe kutoka moyoni mwako. 84. Hapo haja yako itakuwa dhahiri na utagundua kwamba, umezama mara mbili, yaani, kama mwenye dhambi na kama maskini mwingine yeyote anayehitaji sana hii sakramenti ili upambane na tabu zako. Kwa bahati mbaya, huioni tabu hii ingawa Mungu hukupatia neema yake makusudi ili uwe mwepesi wa kuhisi na upate njaa zaidi ya kuishiriki sakramenti. Hili hutokea hasa kwa sababu Ibilisi hukusonga kila wakati, hukuotea ili akutege na akuangamize nafsi na mwili, ili usiwe salama naye hata kwa saa moja. Anaweza kukuingiza katika dhiki na tabu upesi jinsi gani wakati hukutazamia hata kidogo!
85. Basi, liacheni hili liwe kama ushauri, si kwetu tu ambao tumekuwa watu wazima na tuna miaka mingi, ila kwa vijana ambao pia wanatakiwa walelewe katika mafundisho ya Kikristo na ufahamu wake mzuri. Kwa njia ya mafundisho kama hayo, itakuwa rahisi zaidi kwetu kuwafundisha Amri Kumi, Imani, na Sala ya Bwana ili wayapokee kwa furaha, kwa moyo, na wayatende na kuyazoea kutoka ujana wao. 86. Kwa maana, ni wazi kwamba, ni bure kujaribu kuwageuza wazee. Hatuwezi kuyaendeleza mafundisho haya na mengineyo bila kuwafundisha watu watakaokuja baada yetu ili waiendeleze huduma na kazi yetu, ili baadaye nao wafaulu kuwalea watoto wao vizuri. Kwa njia hiyo, Neno la Mungu na Kanisa la Kikristo litahifadhiwa. 87. Kwa hiyo, mwache kila bwana wa kaya akumbuke kwamba, kwa njia ya agizo na amri ya Mungu, ni wajibu wake kuwafundisha watoto wake wanayotakiwa kuyajua. Kwa kuwa, wamekwisha kubatizwa na kupokelewa katika Kanisa la Kikristo, lazima wao waufurahie ushirika huu wa hii sakramenti ili waweze kututumikia na kuwa wa manufaa. Kwa sababu lazima wao wote watusaidie kuamini, kupenda, kuomba, na kupigana na Ibilisi.
USHAURI MFUPI KUHUSU UNGAMO
1. Kuhusu ungamo la dhambi, daima tumefundisha kwamba, linapasa kuwa la hiari na linaloutakasa udhalimu wa Papa. Tumewekwa huru kutoka kwa ushawishi wake, na kutoka kwa mzigo usioweza kustahimilika, uliolazimishwa katika Kanisa la Kikristo. Mpaka sasa, jinsi sote tujuavyo kwa njia ya uzoefu, hapajakuwepo sheria yenye ukandamizaji kamwe kama ile iliyomlazimisha kila mmoja aungame kwa ajili ya makali ya dhambi ya mauti baya sana kuliko zote. 2. Aidha, ulizilemea na kuzitesa dhamiri za watu kwa uorodheshaji wa aina zote za dhambi, kiasi kwamba, hakuna hata mmoja aliyeweza kuziungama vya kutosha hasa. 3. Baya zaidi kuliko yote ni kwamba, hakuna aliyefundisha au kufahamu ungamo ni nini na jinsi lilivyo la manufaa na faraja. Badala yake, lilifanywa kuwa maumivu matupu na mateso ya Jehanumu kwa kuwa watu walilazimishwa kuungama japo hapakuwa na lolote lililowachukiza. 4. Sasa, mambo haya matatu yameondolewa na kufanywa kuwa ya hiari ili tuweze kuungama bila ushawishi au woga. Si hivyo tu, tumefunguliwa kutoka kwenye mateso ya kuziorodhesha dhambi zote kinaganaga. Aidha, tuna heri ya kujua jinsi ya kulitumia ungamo kwa njia inayofaa ili kuzifariji na kuziimarisha dhamiri zetu.
5. Kila mmoja analijua hili sasa. Kwa bahati mbaya, watu wamejifunza hili vizuri kupita kiasi. Wanalifanya lolote linalowapendeza na kuutumia uhuru wao kwa manufaa yao, wakijifanya kana kwamba, hawahitaji au hawatamani kwenda kwa ungamo tena. Tunalifahamu haraka lolote linalotufaidi, na tunalishika kwa urahisi usiokuwa wa kawaida lolote lililo laini na pole katika Injili. Lakini jinsi nimesema, nguruwe kama hao, hawastahili kujitokeza mbele ya Injili au kuipata sehemu yake yoyote. Wanastahili kubakia chini ya Papa na wajisalimishe kusukumwa, kuadhibiwa, kuungama, na kufunga zaidi kuliko wakati wowote wa awali. Kwa maana, ambaye hataiamini Injili, hataishi kwayo, hatatenda jinsi inavyompasa Mkristo, na hapaswi kufurahia hata kidogo faida yake yoyote. 6. Kungetokea nini kama ulitaka kuifurahia faida za Injili lakini hukufanya lolote kuihusu na hukuilipia chochote? Kwa kuwa hatutayatoa mahubiri wala hatutawaruhusu watu kama hao kushiriki na kufurahia sehemu yoyote ya uhuru wetu bali tutamwacha Papa au anayefanana naye awagandamize na kuwashurutisha jinsi afanyavyo mdhalimu. Akina yahe ambao hawataitii Injili wanastahili tu mlinda gereza kama Ibilisi na chakari wa Mungu. 7. Hata hivyo, kwa baadhi wanaoisikiliza kwa furaha, inatulazimu kuhubiri, kushauri, kutia moyo, na kuwashawishi daima ili wasiipoteze hii hazina ya thamani na inayofariji ambayo inatolewa na Injili. Kwa hiyo, lazima tuliseme jambo kuhusu
ungamo ili kuwaelimisha na kuwaonya watu wa kawaida.
8. Kwa kuanzia, nimesema kwamba, kwa kuliongezea ungamo hili tunalolijadili, kuna aina mbili zaidi za ungamo ambazo zina hata haki kubwa kuitwa ungamo la pamoja la Wakristo. Ninarejea mazoea ya kuungama kwa Mungu pekee yake au kwa jirani yetu peke yake tukimwomba msamaha. Aina hizi mbili zimeelezwa katika Sala ya Bwana tunaposema: “Utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyowasamehe wanaotukosea.” 9. Naam, Sala ya Bwana nzima ni ungamo la jinsi hiyo. Kwa maana, sala yetu ni ungamo ambalo hatuna, hatutendi inavyotupasa, na hatuombi kwa ajili ya neema na dhamiri yenye furaha? Aina hii ya ungamo inapasa na lazima isemwe daima kadiri tunavyoishi. Kwa sababu asili ya kweli ya maisha ya Kikristo ni kutambua kwamba, sisi ni wenye dhambi na tuiombe neema.
10. Kadhalika, ungamo la pili ambalo kila Mkristo analitoa kumhusu jirani yake linajumuishwa katika Sala ya Bwana. Tunapaswa kuungama makosa yetu mmoja mbele ya mwenzake na kusameheana wenyewe kwa wenyewe kabla ya kuja mbele za Mungu kumwomba msamaha. Sasa, sisi sote ni wadeni mmoja kwa mwenzake. Kwa hiyo, inatupasa na tunaweza kuungama hadharani mbele ya kila mmoja, bila yeyote kuwa na wasiwasi kwa ajili ya mwenzake. 11. Kwa maana, ni kweli jinsi methali inavyosema: “Ikiwa mtu mmoja ni mnyofu, ndivyo walivyo wote.” Hakuna anayemtendea Mungu au jirani yake linalompasa. Hata hivyo, licha ya hatia ya wote pia, kuna iliyo maalumu wakati mtu amemkasirisha mwenzake na anahitaji kumwomba radhi. 12. Kwa hiyo, tuna ondoleo la dhambi maradufu katika Sala ya Bwana: madeni yetu kwa Mungu na kwa jirani yetu yanasamehewa tunapomsamehe jirani yetu na kupatanishwa naye.
13. Licha ya ungamo hili la hadharani, la kila siku, na la lazima, kuna pia ungamo la siri linalofanyika faraghani mbele ya ndugu mmoja peke yake. Wakati tatizo moja au ugomvi unamfanya mtu mmoja kumkaba mwenzake koo na hatuwezi kuusuluhisha, na tunajipata kuwa hatuna uthabiti wa kutosha kiimani, tunaweza kuweka lalamiko letu mbele ya ndugu wakati wowote na mara nyingi tunavyonuia, tukiutafuta ushauri wake, faraja, na nguvu. 14. Ungamo la aina hii halikuingizwa katika amri kama zile nyingine mbili, lakini limeachwa kwa kila mmoja kulitumia anapolihitaji. Hivyo, kwa agizo la Mungu, Kristo mwenyewe amelikabidhi Kanisa la Kikristo ondoleo la dhambi na kutuamrisha tumsamehe kila mmoja wetu dhambi zake.1526 Kwa hiyo, kama kuna moyo unaohisi dhambi zake na kutamani faraja, una kimbilio la hakika hapa unaposikia katika Neno la Mungu kwamba, kwa njia ya mtu, Mungu humfungua na kumwondolea dhambi
1526 Mt. 18:15-19
503
504 zake.
15. Basi, kumbukeni jinsi nilivyosema mara nyingi kwamba, ungamo lina sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni kazi na tendo langu, ninapoomboleza kwa ajili ya dhambi zangu na kuhitaji faraja na uponywaji wa nafsi yangu. Sehemu ya pili ni kazi ambayo Mungu huifanya, anaponiondolea dhambi zangu kwa njia ya Neno ambalo limewekwa kinywani mwa mtu. Hili ndilo jambo lililo kubwa na zuri kushinda yote lilifanyalo ungamo liwe la ajabu na lenye faraja. 16. Zamani, tuliitilia mikazo yote juu ya kazi zetu peke yake na lililotushughulisha tu lilikuwa iwapo tuliungama halisi vya kutosha. Hatukutambua wala hatukuhubiri sawasawa kuhusu sehemu ya pili muhimu. Ilikuwa kana kwamba, maungamo yetu yalikuwa kazi nzuri tu ambayo kwayo, tungeweza kumridhisha Mungu. Ambapo ungamo halikufanywa kikamilifu na kuwa timilifu kinaganaga, tuliambiwa kwamba, ondoleo la dhambi halikuwa halali na dhambi haikusamehewa. 17. Kwa hiyo, watu walifikishwa mahali ambapo kila mmoja, bila budi, alikata tamaa ya kuungama halisi– ambako hakukuwezekana–na hakuna hata mmoja aliyejihisi kuwa na amani katika dhamiri yake au kuwa na imani katika ondoleo lake la dhambi. Hivyo, ungamo la awali lilikuwa mzigo na chungu kwa madhara wazi na uharibifu wa nafsi. 18. Basi, lazima tujihadhari kuzibainisha sehemu hizo mbili. Inatupasa kuiweka thamani ndogo katika matendo yetu na kulitukuza na kulikuza Neno la Mungu. Tusitende kana kwamba, tulitaka kuitenda kazi nzuri ya kumkabidhi yeye, bali tukubali na kupokea hasa kitu kutoka kwake. Huwezi kuthubutu kuja na kusema jinsi ulivyo mwema au ulivyo mwovu. 19. Ukiwa Mkristo, hili ninalijua vyema vya kutosha, usipokuwa Mkristo, bado ninalijua vyema zaidi. Lakini likupasalo kulifanya ni kuyasikitikia mahitaji yako na kujiruhusu mwenyewe usaidiwe ili uweze kupata moyo na dhamiri yenye furaha. 20. Licha ya hayo, yeyote asithubutu kukukandamiza kwa mahitaji. Afadhali yeyote aliye Mkristo au apendaye kuwa mmoja, aupate ushauri mwaminifu hapa kwenda na kuipokea hii hazina yenye thamani. Iwapo wewe si Mkristo wala huitamani faraja ya namna hiyo, basi, tutakuacha chini ya mamlaka ya mwingine. 21. Kwa hiyo, tunaubatilisha udhalimu, amri, na ushawishi wa Papa kwani hatuvihitaji. Kwa kuwa, jinsi nilivyosema, mafundisho yetu ndiyo haya: Mtu awaye yote asipokwenda kwa ungamo kwa hiari, na kwa ajili ya ondoleo la dhambi, basi, mwache alisahau kabisa. Naam, ikiwa mtu yeyote atategemea usafi wa ungamo lake, naye aache kulikaribia. 22. Hata hivyo, tunakusihi uungame na uyataje mahitaji yako, si kwa sababu ya kulitenda tendo fulani, bali kwa kulisikia analotaka kukuambia Mungu. Ninasema, Neno au ondoleo la dhambi ndilo unapaswa kulimakinikia, ukilikuza na kulitunza kama hazina kuu ya ajabu ifaayo
kukubaliwa kwa sifa na shukrani zote.
23. Kama haya yote yangeelezwa kwa uwazi, na wakati uo huo, iwapo haja zinazopasa kutusukuma na kutushawishi kuungama zingeonyeshwa wazi, hapangekuwa na haja ya ushawishi na nguvu. Dhamiri ya mtu mwenyewe ingemshurutisha na kumfanya awe na hofu kiasi kwamba, angefurahi na kutenda kama mwombaji duni maskini asikiaye kwamba, zawadi kubwa ya pesa au nguo itatolewa mahali fulani. Hangehitaji msimamizi wa mali kumpeleka na kumpiga, bali angekimbia huko haraka iwezekanavyo ili asiikose zawadi hiyo. 24. Fikiria sasa, iwapo mwaliko ungebadilishwa kuwa amri kwamba, waombaji wote lazima wakimbie mahali hapo, bila sababu yoyote kutolewa na bila kutajwa lolote la kupokewa. Mwombaji angeenda kwa ukinzani kwa kuwa hangetarajia kupokea lolote, ila tu kufanya watu wote wamwone alivyo maskini na mwenye huzuni. Furaha au faraja nyingi haitapatikana katika hili, bali uhasama mkubwa dhidi ya amri hiyo.
25. Vivyo hivyo, wakati uliopita, wahubiri wa Papa walikaa kimya kuhusu sadaka hii ya ajabu, yenye utajiri mwingi, na hii hazina isiyoelezeka. Wamewasukuma watu tu kwenye makundi ya ghasia kuonyesha tu jinsi walivyo najisi na wachafu. Ni nani angeenda katika ungamo kwa hiari? 26. Kinyume chake, sisi hatusemi kwamba, watu lazima watazame jinsi wewe ulivyojaa uchafu, wakikufanya kuwa kioo cha kujitafakaria wenyewe. 27. Badala yake, tunashauri: Ukiwa maskini na mwenye huzuni, basi, nenda ukaitumie dawa ya kuponyesha. Yeyote anayehisi tabu na haja zake, ataikuza tamaa ya jinsi hiyo kwa ajili ya ungamo kiasi cha kulikimbilia kwa furaha. Lakini ambao hawalijali na wasiolijia kwa hiari yao wenyewe, tunawaacha waende zao. Hata hivyo, inawapasa wajue kwamba, hatuwahesabu kuwa Wakristo.
28. Hivyo, tunafundisha jinsi ungamo lilivyo jambo la ajabu, lenye thamani, la kufariji, na tunahimiza kwamba, baraka ya thamani ya jinsi hiyo isidharauliwe hasa tukikumbuka haja yetu kubwa. Ukiwa Mkristo, huhitaji shurutisho langu wala amri ya Papa wakati wowote. Lakini, utajishurutisha mwenyewe na kuniomba tu heshima ya kulishiriki. 29. Hata hivyo, ukiidharau na kukaa mbali na ungamo kwa fahari tu, basi, tutahitimisha kwamba, wewe si Mkristo na hupaswi kuipokea sakramenti. Kwa sababu unalidharau lile ambalo Mkristo yeyote hawezi kulidharau na hapo unaonyesha kwamba, huwezi kuwa na msamaha wa dhambi. Hii ni dalili ya hakika kwamba, unaidharau Injili pia.
30. Kwa ufupi, hatuuidhinishi ushawishi. Hata hivyo, ikiwa mtu awaye yote anakataa kusikia na kufuata maonyo ya mahubiri yetu, hatutakuwa na haja naye
wala hapaswi kuishiriki Injili kwa njia yoyote. Ukiwa Mkristo, unapaswa kufurahi kukimbia zaidi ya maili mia moja kwa ajili ya ungamo, si kwa kushurutishwa bali kuja na kutulazimisha tulitoe. 31. Kwa sababu hapa, lazima shurutisho liwe kinyume. Lazima tuwe chini ya amri nawe lazima uupate uhuru. Hatumlazimishi mtu yeyote, lakini tunajiruhusu wenyewe kulazimishwa jinsi tunavyoshurutishwa kuhubiri na kutoa huduma ya sakramenti pia.
32.Hivyo basi, ninapokuhimiza uliendee ungamo, ninakuhimiza tu uwe Mkristo. Nikikufikisha hapa, basi, nimekufikisha kwenye ungamo pia. Ambao wanataka kweli kuwa Wakristo wazuri, waliowekwa huru kutoka kwa dhambi zao, na wenye furaha katika dhamiri zao, tayari wana njaa na kiu cha kweli. 33. Wanaunyakua mkate kama ayala anayewindwa, wakiungua kwa joto na kiu jinsi Zab. 42:1 isemavyo: “Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji, vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, ee Mungu.” Yaani, jinsi ayala atetemekavyo kwa hamu ya kupata chemchemi safi, vivyo hivyo nami ninalionea shauku Neno la Mungu, ondoleo la dhambi, sakramenti na kadhalika. 34. Unaona, kwa njia hii, ungamo lingefundishwa vizuri, tamaa na upendo kulihusu vingechochewa kiasi kwamba, watu wangetukimbilia kulipokea zaidi ya vile ambavyo tungependa kulitoa. Tutawaacha wafuasi wa Papa wajihangaishe na wajitese wenyewe na watu wengine wanaoipuuza hazina kama hiyo na kujitenga nayo wenyewe. 35. Hata hivyo, kutuhusu sisi, tuacheni tuiinue mikono yetu katika sifa na shukrani kwa Mungu kwamba, tumeipata hii hekima takatifu ya ungamo.
SHAURI LA MWAFAKA
Takriri na maelezo makamilifu, dhahiri, sahihi, na makataa ya baadhi ya mafungu ya Ukiri wa Augsburg, Baadhi ya wanatheologia waliokubaliana na Ukiri wamejadiliana kwa muda fulani kuhusu ufafanuzi wa mafungu haya ambayo yanatatuliwa na kukubaliwa kwa Neno la Mungu na kwa mujibu wa mafundisho yetu ya Kikristo ya yaliyomo makuu
SEHEMU YA KWANZA: MUHTASARI
1527
wa mafungu yaliyojadiliwa miongoni mwa wanatheologia walioukubali Ukiri wa Augsburg ambapo ukiri unarudiwa na mabishano yanatatuliwa na wanapatana kwa njia ya Kikristo kulingana na Neno la Mungu
MUHTASARI, KANUNI, NA SHAURI LA MAFUNDISHO
kadiri mafundisho yote yanavyopaswa kupimwa na mabishano yaliyojipenyeza yanavyopaswa kutatuliwa na kuamuliwa katika njia ya Kikristo!
1. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, maandiko ya unabii na ya kimitume, ya Agano la Kale na Agano Jipya ndiyo kanuni na shauri la pekee ambalo kwalo, mafundisho yote na walimu wote kamili lazima wapimwe na waamuliwe kama jinsi ilivyoandikwa katika Zab. 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.” Naye Mtume Paulo anasema katika Gal. 1:8, “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiria ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria, na alaaniwe.”
Maandiko mengine ya walimu wa kale na wa sasa, bila kuyajali majina yao, hayawezi kuwa sawa na Maandiko Matakatifu. Kila moja ya hayo lazima yawekwe chini ya Maandiko Matakatifu. Isitoshe, lazima lipokelewe si kwa njia nyingine, bali kama ushahidi wa umbo ambalo kwalo, mafundisho ya manabii na ya mitume yalihifadhiwa baada ya nyakati za mitume.
1527 Kilatini: ‘Epitome articulorum.’
2- 3. Punde tu baada ya wakati wa mitume, kwa kweli, tayari katika wakati wa uhai wao, walimu wa uongo na wazushi walilivamia Kanisa. Dhidi ya wapinzani hawa, Kanisa la Zamani liliunda alama, yaani, kiri fupi na kamili za imani, ambazo zilikubaliwa kuwa imani ya umoja, kikatoliki, ya Kikristo ya Kanisa lenye imani sahihi na ya kweli, ambazo ni: Ukiri wa Mitume, Ukiri wa Nikea, na Ukiri wa Athanasio. Sisi wenyewe tunaweka amana katika kiri hizi. Hivyo, tunakataa uzushi wote na mafundisho ambayo yameingizwa katika Kanisa la Mungu kinyume cha kiri hizo.
3. 4. Kanisa la wakati wetu liligawanyika/lilifarakana kwa sababu ya masuala ya kiimani. Kwa hiyo, tunadhukuru hasa dhidi ya ibada za kukufuru, ibada za sanamu, na ushirikina wa wafuasi wa Papa. Kinyume cha madhehebu mengine, tunachukulia kwamba, maelezo ya msimamo wetu wa pamoja wa maafikiano, tangazo la imani yetu ya Kikristo, na ukiri wetu wa kisasa ni Ukiri wa Augsburg usiobadilishwa, uliotolewa kwa Kaisari Karolo wa V wakati wa Baraza la Augsburg mwaka wa 1530, pamoja na Utetezi wake, na mafungu ya imani yaliyotungwa huko Smalkaldi mwaka wa 1537, ambayo wanatheologia hodari zaidi wa wakati huo waliyaidhinisha kwa kutia sahihi zao.
5. Kwa kuwa mambo haya yanawahusu Wakristo wa kawaida na wokovu wa nafsi zao, tunakiri hadharani kwamba, tunazikubali katekisimo zote mbili za Dk. Martin Luther, yaani, Katekisimo Ndogo na Katekisimo Kubwa jinsi zilivyoandikwa katika majuzuu yake. Hizi ni kama Biblia ya Wakisto wa kawaida. Katekisimo hizi zinajumlisha, kwa ufupi, yote ambayo Maandiko Matakatifu yanayaelezea kwa urefu na ambayo lazima Mkristo wa kawaida ayafahamu kwa ajili ya wokovu wake.
Mafundisho yote lazima yalingane na vipimo vilivyowekwa hapo juu. 6. Lolote lililo kinyume cha hayo lazima likataliwe na lilaaniwe ikiwa linapingana na azimio la pamoja la imani yetu.
7. Kwa njia hii basi, tofauti kati ya Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale, Agano Jipya, na maandiko mengine inahifadhiwa. Maandiko Matakatifu yanabakia kuwa mwamuzi, kanuni, na kaida ya pekee na kwamba, ni kigezo ambacho, mafundisho yote lazima yachunguzwe na yapimwe kama ni mazuri au mabaya, ni ya kweli au ya kukufuru.
8. Alama au kiri na maandiko mengine yaliyotajwa hapo juu si halali kutumiwa kama mamlaka sawa na Maandiko Matakatifu. Badala yake, yatumiwe hasa kama mashahidi tu na maelezo ya imani yakionyesha jinsi walimu wa Kanisa la Mungu walivyoyaelewa na walivyoyafafanua Maandiko Matakatifu nyakati katika
nyakati zao, kuhusu mafungu yaliyobishaniwa na jinsi mafundisho yaliyopinga Maandiko Matakatifu yalikataliwa na kulaaniwa.
I. DHAMBI YA ASILI
Status controversiae – Ajili ya Ubishi
1. Je, ni kweli kwamba, dhambi ya asili ni asili ya kibinadamu iliyopotoka, kiini, na ariki ama ni sehemu yake kuu na nzuri ya nafsi yake? Yaani, ni nafsi yenye busara katika hali yake ya juu kabisa na nguvu zake? Au, je, kuna tofauti hata baada ya anguko kati ya dhambi ya asili na kiini cha ubinadamu, asili, dhati, mwili, na nafsi kwa upande mmoja na dhambi ya asili kwa upande mwingine kiasi kwamba, asili ya ubinadamu na dhambi ya asili ni kitu kimoja, kinachoshikamana na asili iliyopotoka na kuiharibu?
Affirmativa - Makubaliano
Mafundisho, Imani, na Ukiri Safi kulingana na Maelezo Mapana na Sanifu Yaliyotajwa
1. I. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, kuna tofauti kati ya asili ya ubinadamu na ya dhambi ya asili. Tofauti hii haihusu tu asili ya ubinadamu katika hali yake ya mwanzoni, yaani, jinsi ilivyoumbwa na Mungu kuwa safi, takatifu, na bila dhambi. Badala yake, inahusu pia asili yetu ya sasa baada ya anguko. Asili yetu inabaki kuwa kiumbe cha Mungu hata baada ya anguko. Tofauti kati ya haya mawili ni kubwa jinsi ilivyo baina ya tendo la Mungu na tendo la Ibilisi.
II. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri pia kwamba, ni sharti tuihifadhi tofauti hii kwa makini kwasababu mtazamo uliochukulia kwamba, hakuna tofauti kati ya asili ya ubinadamu iliyopotoka na dhambi ya asili unapinga na hauwezi kuwekwa pamoja na mafungu makuu ya imani yetu ya Kikristo. Yaani, uumbaji, wokovu, utakaso, na ufufuo wa miili yetu.
4. Mungu hakuumba tu mwili na nafsi ya Adamu na Hawa kabla ya anguko, bali aliumba miili na nafsi zetu pia baada ya anguko. Ingawa hivyo viwili vilipotoka, Mungu bado anavikubali kama tendo lake, jinsi ilivyoandikwa: “Mikono yako imeniumba na kunifinyanga; nawe utageuka na kuniangamiza?” (Ayu. 10:8)1
5. Zaidi ya hayo, katika muungano wake wa binafsi,1528 Mwana wa Mungu aliitwaa asili hiyo hiyo ya kibinadamu ingawa haikuwa na dhambi. Hakuuchukua mwili wowote mgeni bali mwili wetu sisi na Kulingana na huo mwili wetu, hakika amekuwa ndugu yetu kweli. Waebrania 2:14,16,17 inasema: “Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki hayo hayo, . . . Maana ni hakika, hatwai asili ya Malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote,” isipokuwa dhambi.
6. Kwa hivyo, Kristo ameikomboa asili ya kibinadamu kama kiumbe chake mwenyewe. Anaitakasa, na anaihuisha kutoka kwa wafu, na kuipamba kwa utukufu kama uumbaji wake mwenyewe. Hata hivyo, hakuiumba dhambi ya asili, hakuitwaa, hakuikomboa, wala hakuitakasa. Hataifufua dhambi ya asili katika wateule kutoka kwa wafu, hataitukuza wala hataiokoa kamwe. 7. Kinyume chake, itaangamizwa kabisa katika ufufuo.
Hoja hizi zinaonyesha wazi tofauti kati ya asili yenyewe iliyopotoka na upotovu uliopo katika asili na ambao umeiharibu asili.
8 III. Kwa upande mwingine, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, dhambi ya asili si upotovu mdogo tu wa asili ya mwanadamu. Badala yake, ni upotovu wa kina sana wa asili ya kibinadamu kiasi kwamba, hakuna chochote timamu au kisichoharibika kilichosalia katika mwili au nafsi, uwezo wa ndani au wa nje wa mtu. Ni jinsi Kanisa liimbavyo: “Kwa anguko la Adamu, asili na ariki ya ubinadamu vimepotoka kabisa.”1529 9. Madhara haya yasiyoelezeka hayawezi kutambuliwa kwa mchakato wa busara bali kwa nuru ya Neno la Mungu peke yake. 10. Hakuna yeyote anayeweza kuitenganisha asili yenyewe kutoka katika upotovu wetu isipokuwa Mungu peke yake. Hili litafanyika kabisa katika kifo na ufufuo. Kisha, asili tuliyo nayo sasa itafufuka na kuishi milele bila dhambi ya asili. Itakuwa imetenganishwa na kuondolewa kwayo, jinsi ilivyoandikwa katika Kitabu cha Ayubu (Ayu. 19:26,27): “Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; nami nitamwona mimi nafsi yangu, na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine.”
1528 Kilatini: ‘Unio personalis.’ 1529 Wimbo uliotungwa mwaka wa 1524 na mwandishi wa Baraza la Nürnberg, Lazaro Spengler (+1534) ambao unaanza: ‘Durch Adams Fall ist ganz vorderbert menschlish Natur und Wesen.’
Negativa – Uhakiki Hasi
Kuyakataa Mafundisho ya Uasi Yanayopinga Mafundisho Safi
1. Basi, tunakataa, na kuyalaani mafundisho ya kwamba, dhambi ya asili ni hatia1530 tu na deni tunalodaiwa kwa ajili ya makosa ya mtu mwingine bila aina yoyote ya upotovu wa asili yetu wenyewe.
2. Kadhalika, tunakataa mafundisho kwamba, tamaa mbaya si dhambi, bali ni tabia za kiariki za asili ya mwanadamu zilizoumbwa tena. Mafundisho kwamba, upungufu au madhara haya yaliyotajwa, si dhambi ya kweli kwa sababu ya mtu aliye nje ya Kristo ni mwana wa gadhabu.1531
3. Kadhalika, tunakataa uasi wa wafuasi wa Pelagio unaodai kwamba, asili ya mwanadamu si potovu hata baada ya anguko, hasa kwamba, katika mambo ya kiroho, uwezo wake wa asili1532 unabaki kuwa mwema na safi kabisa.
4. Kadhalika, tunakataa mafundisho kwamba, dhambi ya asili ni waa dogo ambayo limerashiwa kwa nje lisilokuwa na maana au dosari. Licha ya hayo, asili ya mwanadamu imehifadhi nguvu zake zisizoharibika kwa ajili ya mema na hata katika mambo ya kiroho.
5. Kadhalika, tunakataa mafundisho kwamba, dhambi ya asili ni kizuizi cha nje tu cha uweza mwema wa kiroho wa mwanadamu na si unyimwaji kabisa au upotevu wa uweza huo, sawa na yalivyo maji ya kitunguu saumu, yakipakwa kwenye sumaku, huzuia lakini hayaondoi nguvu ya asili ya sumaku.1533 Kadhalika, tunaukana mtazamo kwamba, dosari hii ya asili inaweza kuondolewa tu kwa urahisi kama jinsi doa linavyoweza kuoshwa kutoka usoni au baka la rangi kutoka ukutani.
6. Kadhalika, tunakataa kwamba, asili na ariki ndani ya mwanadamu haijapotoshwa kabisa, bali kwamba, bado mtu ana wema fulani ndani yake mwenyewe hata katika mambo ya kiroho. Kwa mfano, uwezo, stadi, akili au uwezo wa kuanzisha, kutekeleza au kushirikiana katika mambo ya kiroho.
7. Kwa upande mwingine, tunaukataa pia uasi wa wafuasi wa Mani
1530 Kilatini: ‘Reatus.’
1531 Efe. 2:3. Sinodi ya Trento, kikao cha tano cha mwaka wa 1546, sura ya tano.
1532 Maandiko ya asili: ‘In naturalibus.’ Pelagio, mtaalamu wa theologia kutoka Uingereza aliyefundisha theologia huko Roma mwanzoni mwa karne ya tano. Wapelagio waliamini hiari kuwa katika wokovu na waliikataa dhambi ya asili. Agostino wa Hippo (354-430) wa Kaskazini mwa Afrika, askofu na Baba wa Kanisa la Zamani aliyapinga mafundisho ya Wapelagio kwa bidii sana. Kanisa la Magharibi liliyakataa mafundisho haya na liliwaharamisha Wapelagio katika karne ya tano.
1533 Maoni ya kawaida ya wakati huo.
wanaofundisha kwamba, dhambi ya asili ni kitu cha lazima, kisichoumbwa, kinachomiminwa na kuchanganywa na Ibilisi katika asili ya mwanadamu jinsi inavyokuwa wakati sumu na divai vinachanganywa pamoja.1534
8. Kadhalika, tunakataa kwamba, si mtu wa asili mwenyewe anayetenda dhambi bali ni kitu fulani cha nje na kigeni kilicho ndani yake. Kwa hiyo, si asili ya mtu inayoshtakiwa bali ni dhambi ya asili tu iliyo ndani yake.
9. Tunayakataa na kuyalaani pia kama uzushi wa Wamani mafundisho kwamba, dhambi ya asili ni na kwa kweli, iliharibu utu, asili, na dhati ya mwanadamu bila tofauti yoyote, kiasi kwamba, tofauti yoyote haipaswi kufanywa hata akilini, kati ya asili ya mwanadamu yenyewe na dhambi ya asili baada ya anguko, na kwamba, hivyo viwili haviwezi kutofautishwa akilini.
10. Ni kweli kwamba, Luther anaiita dhambi ya asili: ‘dhambi ya kimaumbile,’ ‘dhambi ya binafsi,’ na ‘dhambi ya lazima.’ Hata hivyo, hamaanishi kwamba, asili, nafsi, na dhati zenyewe ziwe sawa na dhambi ya asili bila tofauti yoyote. Badala yake, kwa matumizi ya istilahi hizi, aonyeshe tofauti kati ya dhambi ya asili inayoshikamana na asili ya mwanadamu na dhambi nyingine zinazoitwa, ‘dhambi halisi.’1535
11. Maana dhambi ya asili si dhambi ambayo mtu anaitenda. Imefungamanishwa katika asili, kiini, na dhati yake kiasi kwamba, ingawa fikira mbaya haingetoka moyoni mwa mtu mpotovu kamwe, hangesema neno la upuuzi, au hangetenda ovu au tendo baya, lakini asili ya mwanadamu imeharibiwa kupitia dhambi ya asili.
Hii ni dhambi ya asili ya maumbile tuliyoirithi kwa njia ya mbegu yetu ya maumbile ya dhambi na chemchemi ya dhambi zingine zote za mauti, kama vile: mawazo, maneno, na matendo mabaya jinsi ilivyoandikwa: “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya,” na kadhalika na “Mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake.”1536
12. Inatubidi kutambua maana tofauti za neno ‘asili.’ Kwalo, Wamani wanauficha uzushi wao na kupotosha watu wengi wa kawaida. Wakati mwingine, neno hili linamaanisha asili ya mtu jinsi tunavyosema, “Mungu ameiumba asili ya mtu.” Basi, wakati mwingine, neno hili linamaanisha uzuri au ubaya 1534 Mani (mnamo 216-276), alianzisha dhehebu lake lenye asili ya maoni ya Ugnostiki pande za Uajemi na Uhindi. Alifundisha kwamba, uhalisia umegawanyika kabisa katika sehemu mbili zinazoshindana daima. Matthias Flacius Illyricus (1520-1575) na wafuasi wake walishtakiwa na wapinzani wao, hasa na Viktorino Strigel (1524-1569) kuwa wafuasi wa Mani.
1535 Kilatini: ‘Peccatum actale.’
1536 Mt. 15:19; Mwa. 8:21, 6,5.
unaoambatana katika asili au tabia ya kitu jinsi tunavyosema, “Ni tabia ya nyoka kuuma” na “Ni asili au tabia ya mtu kufanya dhambi” au “asili ya mtu ni dhambi.” Neno ‘asili’ hapa halina maana ya dhati ya mtu, bali kitu kinachoambatana katika asili au ariki yake.
13. Kuhusu maneno ya Kilatini substantia1537 na accidens,1538 hizi si istilahi za Maandiko Matakatifu. Isitoshe, Wakristo wa kawaida hawazifahamu. Kwa hiyo, hazipaswi kutumiwa katika mahubiri kwa watu wa kawaida wasioelimika bali watu hao waepushwe nazo.
Lakini, kwaajili manufaa, istilahi hizi zinaweza kutumiwa katika mijadala kuhusu dhambi ya asili shuleni na miongoni mwa wataalamu kwa sababu wao wanazifahamu na hazileti hisia zozote za uongo. Badala yake, zinaonyesha wazi tofauti kati ya asili ya kitu fulani na kitu kinachohusika nacho bila kukusudiwa.
Hivyo basi, istilahi hii inaonyesha wazi tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya Ibilisi. Ibilisi hawezi kuumba dutu yoyote ila tu anaweza, kwa kibali cha Mungu, kuiharibu dutu ambayo Mungu ameiumba.
II. HIARI
Status controversiae – Ajili ya Ubishi
1. Hiari ya mtu inaweza kujadiliwa katika hali nne tofauti: 1. Kabla ya anguko 2. Baada ya anguko 3. Baada ya kuzaliwa upya, na 4. Baada ya ufufuo wa mwili. Basi, katika ubishi huu, suala la kimsingi linahusu hiari na uwezo wa binadamu katika hali ya pili: Je, mwanadamu ana uwezo gani katika mambo ya kiroho baada ya anguko la wazazi wetu wa kwanza na kabla ya kuzaliwa upya? Je, kwa uwezo wake mwenyewe, na kabla hajazaliwa upya kwa njia ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anaweza kupanga na kujitayarisha mwenyewe kuipokea neema ya Mungu? Je, anaweza au hawezi kuipokea neema ya Mungu iliyotolewa katika Neno na katika Sakramenti Takatifu?
Affirmativa - Makubaliano
Mafundisho Safi kuhusu Fungu hili katika Msingi wa Neno la Mungu
1. Tunafundisha, tunaamini, na tunakiri kwamba, ufahamu na 2. akili za binadamu ni upofu katika mambo ya kiroho na kwamba, kwa uwezo wake halifahamu lolote jinsi ilivyoandikwa: “Basi mwanadamu wa tabia ya asili
1537 ‘Dutu’ au ‘kiini.’
1538 ‘Mbadiliko umbo.’
hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu,” wakati anapimwa kuhusu mambo ya kiroho.1539
2. Kadhalika, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, hiari 3 ya mwanadamu isiyozaliwa upya, haikataliwi tu na Mungu lakini imekuwa adui wa Mungu pia. Hivyo, anayatamani na anayataka tu yale yaliyo maovu yanayopingana na Mungu jinsi ilivyoandikwa: “Maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake.”1540 Kadhalika: “Nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.”1541 Jinsi maiti isivyoweza kujiamsha kimwili na kuwa na maisha ya dunia hata kidogo, ndivyo mtu ambaye amekufa kiroho, kwa njia ya dhambi, hawezi kujifufua mwenyewe hata kidogo na kuwa na maisha ya kiroho jinsi ilivyoandikwa: “Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo.”1542 Kwa hiyo, sisi si wenyewe. “Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu” (2 Kor. 3:5).
3. Hata hivyo, Mungu Roho Mtakatifu hautekelezi uongofu bila 4 vyombo, bali kwa kusudi hili, anatumia mahubiri na kulisikiliza Neno la Mungu jinsi ilivyoandikwa: “Injili ni uweza wa Mungu uuletao wokovu” (Rum. 1:16); kadhalika, “imani, chanzo chake ni kusikia Neno la Mungu” (Rum. 10:17).1543 Ni mapenzi ya Mungu kwamba, wanadamu 5 walisikilize Neno lake na wasiyazibe masikio yao.1544 Roho Mtakatifu yumo katika Neno hili na huifungua mioyo jinsi ule wa Lidia ulivyofunguliwa katika Mdo.16:14. Wanalisikiliza Neno na wanaongolewa kwa njia ya neema na uweza wa Roho Mtakatifu. Maana, uongofu wa mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu pekee.
Bila neema yake ‘hiari na juhudi zetu,’1545 yaani, kuzipanda 6 mbegu na kunyunyizia maji kwetu ni bure mpaka ‘azikuze.’1546 Hivyo, Kristo anasema: “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”1547 Katika maneno haya machache, anakataa nguvu zote za hiari na anahusisha kila kitu kwa neema ya Mungu ili yeyote asijisifu mbele za Mungu.1548
1539 1 Kor. 2:14. 1540 Mwa. 8:21. 1541 Rum. 8:7. 1542 Efe. 2:5. 1543 ‘Union Version:’ ‘Basi imani, chanzo chake kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.’ 1544 Zab. 95:8. 1545 Rum. 9:16. 1546 1 Kor. 3:7. 1547 Yn. 15:5. 1548 1 Kor. 9:16.
Negativa – Uhakiki Hasi
Kuyakataa Mafundisho ya Uasi Yanayoyapinga Mafundisho Safi
Kwa hiyo, tunayakataa na tunayalaani makosa yafuatayo yote 7 ambayo ni kinyume cha kanuni1549 ya Neno la Mungu:
1. Kwanza, payo ya wanafalsafa wa Stoa na vifijo vya Wamani 8 waliofundisha kwamba, lolote linalotokea lazima litokee na haliwezi kutokea vinginevyo. Kwa maana wakati wote mwanadamu anatenda, akiwa chini ya shurutisho, hata katika matendo yake ya nje na kwamba, huyafanya matendo maovu na vitendo kama uzinzi, unyang’anyi, mauaji, wizi, na dhambi zinazofanana.
2. Tunakataa pia kosa la Wapelagio wapumbavu wasiosita 9 kufundisha kwamba, kwa uwezo wake mwenyewe na bila neema ya Roho Mtakatifu, mwanadamu mwenyewe anaweza kumgeukia Mungu, kuiamini Injili, kuitii sheria ya Mungu kwa moyo wote, na hivyo kustahili msamaha wa dhambi na uzima wa milele.
3. Tunakataa pia kosa la Wapelagio Nusu, 10 wanaofundisha kwamba, kwa uwezo wake, mwanadamu anaweza kutengeneza mwanzo wa kuongoka kwake, lakini hawezi kuukamilisha kabisa bila neema ya Roho Mtakatifu. 1550
4. Kadhalika, tunakataa fundisho kwamba, kabla ya kuongoka 11 kwake, mwanadamu mwenyewe ni dhaifu kabisa kuweza kuchukua hatua za mwanzo kwa hiari za kuweza kumgeukia Mungu kwa uwezo wake mwenyewe na kuitii sheria ya Mungu kwa moyo wake wote. Lakini baada ya Roho Mtakatifu kuanza, kwa njia ya kulihubiri Neno, na anaitoa neema yake kwalo, mara moja, hiari ya mwanadamu, kwa uwezo wake wa asili, inaweza kuongezea kitu kusaidia, kushiriki, kujiandaa yenyewe kwa neema, kujipanga yenyewe, kushika na kuipokea, na kuiamini Injili japo kwa udogo na udhaifu..
1549 ‘Kanuni’ katika maana ya neno la Kiyunani: ‘κανων,’ yaani, ‘kipimo.’ 1550 Kilatini: ‘Semipelagii.’ Agostino wa Hippo na Pelagio (mnamo 340-420), aliyetoka Uingereza, walijadiliana vikali juu ya nia ya ubinadamu katika uongofu wa wanadamu. Pelagio aliitetea hiari ya ubinadamu dhidi ya mafundisho ya Agostino. Baada ya kulaaniwa na sinodi za Afrika, Kaisari wa Roma, na Papa wa Roma pia, Pelagio alipotea kutoka jukwaa la historia. Askofu Yuliano wa Eclanum (mnamo 386-454), huko Italia, aliendelea kupigana na Agostino na alimshtaki kuwa mfuasi wa Mani kwa sababu ya kumkataza binadamu uwezo wowote katika uongofu wake. Askofu Yuliano alilaaniwa na sinodi kadhaa na alifukuzwa kutoka kwa kiti chake cha uaskofu. Wapelagio Nusu walifundisha kwamba, hiari ya binadamu inaweza kuchukua hatua za kwanza katika uongofu. Kisha, Neema ya kimungu itatimiza mfuatano wa wokovu: Kassiano wa Marseilles (420), Vinkentio wa Lerinum (+ kabla ya 450), Fausto wa Riez (mnamo 470). Watetezi wa mafundisho wa Agostino walikuwa hasa mwanafunzi wake, Prospero wa Akuitania (mnamo 390-mnamo 463) na baadaye Fulgentio wa Ruspe na Kaisario wa Arles, walioathiri Sinodi ya Orange iliyoyalaani mafundisho wa Wapelagio Nusu. Halafu mafundisho ya Agostino yalikuwa mafundisho rasmi ya Kanisa la Magharibi. Hata hivyo, mafundisho ya Pelagio na wafuasi wake mbalimbali yalistawi katika theologia ya Uwanazuoni.
5. Kadhalika, tunakataa kwamba, baada ya kuongoka kwake, 12 mwanadamu anaweza kuishika sheria ya Mungu kabisa na kikamilifu. Utimizaji huu unajumuisha haki yetu mbele za Mungu ambayo kwayo, tunastahili uzima wa milele.
6. Isitoshe, tunalikataa na kulilaani kosa la walokole 13 wanaodhania kwamba, Mungu anawavutia watu kwake mwenyewe, anawaangaza, anawahesabia haki, na anawaokoa bila vyombo vyovyote. Yaani, bila kulisikia Neno la Mungu na bila kuishiriki Sakramenti Takatifu. Walokole1551 ni wale wanaoungojea mwangaza wa Roho wa mbinguni licha ya mahubiri ya Neno la Mungu.
7. Kadhalika, tunayakataa mafundisho kwamba, katika kuongoka 14 na katika kuzaliwa upya, Mungu anaharibu kabisa kiini na dhati ya Adamu wa Kale hasa nafsi ya akili na kwamba, katika kuongoka na katika kuzaliwa upya anaiumba kiini kipya cha nafsi kutoka kwa ombwe tupu.
8. Vivyo hivyo, wakati kauli hizi zinatolewa bila maelezo husika 15 kwamba, “hiari ya mwanadamu kabla, katika, na baada ya kuongoka inampinga Roho Mtakatifu,” na kwamba, “Roho Mtakatifu hutolewa kwa wanaompinga makusudi na kwa kuendelea.” Basi, katika kuongoka, Mungu anawafanya watu wasiokuwa na imani kuwa na imani na hukaa ndani ya walio tayari kama jinsi Agostino asemavyo.1552
Baadhi ya walimu wa kale na wa sasa wametumia misemo 16 kwamba, “Mungu huvuta, lakini anamvuta mtu aliye tayari/radhi” au “hiari ya mwanadamu si zembe katika kuongoka bali hufanya jambo fulani.”1553 Kwa kuwa, misemo hii imetumiwa kuthibitisha wajibu wa hiari ya asili katika kuongoka kinyume cha mafundisho ya neema ya Mungu, tunakataa kwamba, maelezo haya hayakubaliani na mafundisho mabruki.1554 Kwa hiyo, ni vyema kuiepuka misemo hii katika majadiliano kuhusu kumgeukia Mungu.
Kwa upande mwingine, ni halali kusema kwamba, katika 17 uongofu, Mungu anawabadilisha watu wagumu na wasiopenda kuamini kwa njia ya mvuto wa Roho Mtakatifu. Baada ya uongofu, hiari ya mtu iliyozaliwa upya haiwi zembe katika mazoezi ya toba ya kila siku bali inashiriki katika matendo yote ambayo Roho Mtakatifu anayatenda kwa kupitia sisi.
1551 Kijerumani: ‘Enthusiasten;’ Kilatini: ‘Enthusiastae.’
1552 Dhidi ya barua mbili za Wapelagio kwa Bonifasio I, 19, 37.
1553 Kilatini: ‘Deus trahit, sed volentem trahit;’ ‘Hominis voluntas in conversione non est otiosa sed agit aliquid.’ Yohana Krisostomo ‘De laudibus S. Pauli hom. IX; Basileio Mkuu ‘Hom. de paenitentia XXXI; (Basileio Bandia).
1554 Kijerumani: ‘gesunde Lehre.’ ‘Mabruki:’ -enye kuleta afya.
9. Hali kadhalika, kauli ya Luther ni kwamba, hiari 18 ya mwanadamu ni imepoa kabisa1555 isipolitenda lolote. Kauli hii lazima ieleweke kwamba, inahusu neema ya kimungu inayochochea misukumo mipya1556 katika hiari. Maana yake: Roho wa Mungu, kwa njia ya Neno lililosikika au kwa njia ya Sakramenti Takatifu, anaidhibiti hiari ya mwanadamu na kusababisha kuzaliwa upya na uongofu ndani yake. Mara tu baada ya Roho Mtakatifu kuyatenda na kuyafanikisha haya, na hiari ya mwanadamu imebadilishwa na kufanywa upya kwa uwezo na utendaji wa Mungu peke yake, hiari mpya ya mwanadamu inakuwa chombo na njia ya Mungu Roho Mtakatifu, kiasi kwamba, mwanadamu haipokei neema tu, bali pia anashirikiana na Roho Mtakatifu katika matendo yanayofuata.
Basi, kabla ya uongofu wa mwanadamu, kuna sababu mbili tu za 19 athari,1557 yaani, Roho Mtakatifu na Neno la Mungu. Neno ni chombo cha Roho Mtakatifu ambapo analeta uongofu. Mtu lazima alisikilize Neno hili ingawa hawezi kulipokea, kwa imani, kwa uwezo wake binafsi, bali kwa neema tu na uwezo wa Mungu Roho Mtakatifu.
III. HAKI YA IMANI MBELE ZA MUNGU
Status controversiae – Ajili ya Ubishi
1.Makanisa yetu hukiri kabisa kwa maafikiano na kwa msingi wa Neno la Mungu na kulingana na yaliyomo katika Ukiri wa Augsburg kwamba, sisi wakosaji maskini tunahesabiwa haki mbele za Mungu na tunaokolewa tu kwa imani katika Kristo na kwamba, Kristo peke yake ndiye haki yetu. Yeye ndiye Mungu wa kweli na mwanadamu wa kweli kwani katika yeye asili ya kimungu na ya kibinadamu zinaunganika kwa njia ya binafsi (Yer. 23:6; 1 Kor. 1:30; 2 Kor. 5:21). Kwa hiyo, swali lililotangulia ni: Je, Kristo ni haki yetu kulingana na asili ya kimungu au ya kibinadamu? Hivyo, mafundisho mawili ya uongo na yapinganayo yamevamia baadhi ya makanisa.
Kundi moja linaona kwamba, Kristo ni haki yetu tu kwa njia ya 2 asili yake ya uungu anapokaa ndani yetu kwa imani.1558 Kinyume cha uungu huu unaokaa ndani yetu kwa imani, dhambi za watu wote zinaonekana kama tone la maji likilinganishwa na bahari kubwa. Kinyume chake, wengine wameshikilia
1555 Luther, WA 18, 697; WA 2, 421. Kilatini: ‘pure passive.’
1556 Kilatini: ‘respectu divinae gratiae in accendendis novis motibus.’
1557 Istilahi ya Aristotele, Kilatini: ‘Causa efficiens.’
1558 Andrea Osiander (1498-1552). Jean Calvin (1509-1564), katika ‘Institutio christianae religionis’ III.11.i,v-xii, xxiii.
517
kwamba, Kristo ni haki yetu mbele za Mungu kwa njia ya asili ya kibinadamu tu.
Affirmativa - Makubaliano
Fundisho Safi la Kanisa la Kikristo dhidi ya Haya Makosa Mawili
1. Katika kuyapinga makosa haya mawili yaliyosimuliwa karibuni,3 tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwa ridhaa kuu kwamba, Kristo ni haki yetu kweli, si kulingana na asili ya uungu wala kulingana na asili ya ubinadamu peke yake. La hasha! Kwa njia ya asili zote mbili, Kristo kwa ujumla, kwa njia ya asili zote mbili ni haki yetu kabisa katika utiifu wake ambao, akiwa Mungu na mwanadamu, alimwonyesha kutoka kwa Baba yake hata mpaka kifo chake chenyewe. Kwa hiyo basi, alitupatia msamaha wa dhambi na uzima wa milele, jinsi ilivyoandikwa: “Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mtu mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki” (Rum. 5:19).
2. Kwa hiyo, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, haki4 yetu mbele za Mungu ni kwamba, Mungu anatusamehe dhambi zetu kwa neema peke yake bila ustahili wowote au ustahiki wa matendo yaliyotangulia, yaliyopo, ama yatakayokuja. Mungu anatukirimia na anatuhesabia haki ya utiifu wa Kristo. Kwa ajili ya haki hii, Mungu anatupokea katika neema yake na kutunachukuliwa kuwa wenye haki.
3. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, imani ni njia na 5 chombo pekee ambacho kwacho, tunamkubali Kristo na katika Yeye tunapokea “haki inayofaidi mbele za Mungu.” Kwa ajili ya Kristo, “imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki” (Rum. 4:5).
4. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, imani hii si ujuzi6 mtupu tu wa kihistoria kuhusu Kristo, bali ni karama ya Mungu, ambayo kwayo, tunamtambua Kristo kwa Neno la Injili kama Mkombozi wetu na tunamtegemea na kumwamini kwamba, kwa ajili ya utiifu wake pekee na kwa neema, tuna msamaha wa dhambi na tunatambuliwa na Mungu Baba kama watakatifu, wenye haki, na tutakaokolewa milele.
5. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, kulingana na 7 matumizi ya Maandiko Matakatifu, katika fungu hili, neno ‘hesabia haki’ linamaanisha ‘ondolea la dhambi,’1559 yaani, kutangaza uhuru kutoka dhambini. “Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; 1559 Kijerumani: ‘absolvieren;’ Kilatini: ‘absolvere.’
518
hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA” (Mit. 17:15). Vivyo hivyo, “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki” (Rum. 8:33). Jinsi ilivyo katika ‘Utetezi wa Ukiri wa Augsburg,’ neno, ‘regeneratio’ (‘kuzaliwa upya’) na ‘vivificatio’ (‘kuhuisha’) zinatumiwa badala ya ‘kuhesabiwa haki,’ kuwa na maana hiyo hiyo. Ingawa, kwa upande mwingine, istilahi hizi zinarejelea urekebishaji wa mwanadamu na zinautofautisha kutoka kwa kuhesabiwa haki kwa imani.
6. Pia tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, ingawa 9 waumini halisi na ambao walizaliwa upya hubaki na udhaifu na upungufu mwingi hadi makaburini mwao, kwa hakika bado hawana sababu ya kuionea mashaka haki waliyohesabiwa kwa njia ya imani au wokovu wa nafsi zao. Badala yake, hawana budi kuiheshimu kama hakika kwamba, kwa ajili ya Kristo, wana Mungu wa neema katika msingi wa ahadi na Neno la Injili Takatifu.
7. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, ikiwa 10 tutahifadhi mafundisho safi kuhusu haki ya imani mbele za Mungu, lazima tuwe makini kuhusu vishirikishi maalumu.1560 Yaani, kwa maneno hayo ya Mt. Paulo yanayotenganisha kabisa stahili za Kristo kutoka kwenye matendo yetu na kumpatia Kristo peke yake utukufu wote. Hivyo, Mt. Paulo anaitumia misemo ya pekee kama: ‘kwa neema,’ ‘bila ustahili,’ ‘bila sheria,’ ‘bila matendo,’ ‘si kwa matendo,’ na kadhalika.1561 Kwa kweli, misemo hii yote inasema jambo moja tu kwamba, tunahesabiwa haki na kuokolewa “katika Kristo kwa imani peke yake.”1562
8. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, majuto 11 yanayotangulia kuhesabiwa haki na matendo mema yanayofuatia,1563 hayahusiki na fungu la kuhesabiwa haki mbele za Mungu. Hata hivyo, hatupaswi kudhania aina fulani ya imani katika uhusiano huu ambayo ingedumu sambamba na nia ovu ya kufanya dhambi na kutenda kinyume cha dhamiri ya mtu. Kinyume chake, baada ya kuhesabiwa haki kwa imani, mwanadamu ana imani ya kweli iliyo hai, yaani, “imani itendayo kazi kwa upendo” (Gal. 5:6). Hivyo, matendo mema hufuatia imani inayohesabia haki na inayoonekana kweli, kwa vile imani hii ni ya kweli na hai wakati wote haiko peke yeke kamwe bali inaambatana na upendo na tumaini wakati wote.
1560 Kilatini: Partculae exclusivae.’
1561 Rum. 6:4; 3:20, 21, 24, 28; 11:6; Gal. 2:16; Efe. 2:9; Tit. 3:5.
1562 Kilatini: ‘Sola fide.’
1563 Kilatini: ‘Nova obedientia,’ yaani, ‘utiifu mpya.’
Tabaini au Uhakiki Hasi
Kuyakataa Mafundisho yaliyo Kinyume
Kwa hiyo, tunayakataa na tunayalaani makosa yote yafuatayo: 12
1. Kristo ni haki yetu kulingana ya asili yake ya kimungu tu. 13
2. Kristo ni haki yetu kulingana ya asili yake ya ubinadamu tu. 14
3. Kwamba, wakati haki ya imani inazungumziwa 15 katika matamko ya manabii na mitume, maneno ‘kuhesabia haki’ na ‘kuhesabiwa haki’ hayamaanishi kuondolea na kuondolewa kutoka dhambini na kupata msamaha wa dhambi. Badala yake, yanamaanisha kufanywa wenye haki kweli mbele za Mungu kwa ajili ya upendo na uadilifu uliyokwisha kumiminwa na Roho Mtakatifu na matendo yanayotokana nayo.
4. Imani haitazamii utiifu wa Kristo tu bali pia asili yake ya 16 kimungu (kadiri inavyokaa na kufanya kazi ndani yetu) na kwamba, huko kukaa kwake kunazificha dhambi zetu.
5. Kwamba, imani ni aina ya tegemeo katika utiifu wa Kristo 17 ambalo linaweza kuwepo na kubakia ndani ya mtu, ingawa hatubu kweli na haonyeshi ushahidi wowote wa matokeo ya upendo wowote unaojitokeza, lakini anaendelea kufanya dhambi dhidi ya dhamiri yake.
6. Kwamba, ni vipawa vya kimungu tu vikaavyo ndani 18 ya waumini na si Mungu mwenyewe.
7. Kwamba, imani inaokoa kwa sababu kwayo, kufanyika upya 19 kunaanzishwa ndani yetu ambako kunategemea upendo wa Mungu na wa wanadamu wenzetu.
8. Kwamba, kwa kweli, imani ina wajibu mkuu sana katika 20 kuhesabiwa haki. Lakini kufanyika upya na upendo pia vinahusiana na haki yetu mbele za Mungu, si kana kwamba, ilikuwa sababu ya kimsingi ya haki yetu, lakini kwamba, haki yetu mbele za Mungu si yote na kamilifu bila upendo huo na kufanywa upya huko.
9. Kwamba, waumini wanahesabiwa haki mbele za Mungu na 21 wanaokolewa kwa ajili ya haki ya Kristo iliyohesabiwa kwao na kwa ajili ya uanzishaji wa utiifu mpya, au kwa kiasi fulani kwa kuhesabiwa kwao haki ya Kristo na kwa kiasi fulani kwa ajili ya uanzishaji wa utiifu mpya.
10. Kwamba, ahadi ya neema inakuwa yetu mioyoni mwetu kwa 22 imani na
pia kwa njia ya kumkiri Kristo kwa vinywa vyetu pamoja na maadili mengineyo.
11. Kwamba, imani haiwezi kuhesabia haki bila matendo mema. Matendo haya mema ni ya lazima kwa ajili ya haki na kwamba, bila matendo mema, mwanadamu hawezi kuhesabiwa haki.
IV. MATENDO MEMA
Status controversiae – Ajili ya Ubishi
Suala Kuu la Mabishano kuhusu Matendo Mema
Mabishano mawili yamejitokeza katika baadhi ya makanisa 1 kuhusu mafundisho ya matendo mema: ubishi wa kwanza miongoni 2 mwa wanatheologia ulitokana na kundi moja lililodai kwamba, “matendo mema ni ya lazima kwa wokovu.” “Huwezi kuokolewa bila matendo mema.” “Hakuna hata mmoja aliyeokolewa bila matendo mema.”1564 Kinyume chake, wengine wameandika: “Matendo mema ni ya madhara kwa ajili ya wokovu.”1565
Kisha, ubishi wa pili uliibuka miongoni mwa baadhi ya 3 wanatheologia kuhusu matumizi ya maneno ‘lazima’ na ‘huru.’ Kundi moja lilishikilia kwamba, hatupaswi kulitumia neno lazima wakati tunazungumzia utiifu mpya kwa sababu halitokani na lazima au shurutisho bali linatokana na nafsi ya hiari. Isitoshe, kuhusu neno ‘lazima,’ kundi jingine lilishikilia kwamba, utiifu mpya si suala la hiari yetu bali watu waliozaliwa upya wanalazimika kuonyesha utii huo.
Mwanzoni, suala hili lilikuwa la kisemantiki tu. Baadaye, 4 mabishano halisi yaliibuka. Kundi moja lilishikilia kwamba, sheria haipaswi kabisa kuhubiriwa kwa Wakristo bali watu wote lazima waonywe kuyatenda matendo mema tu kwa msingi wa Injili Takatifu. Kundi jingine la wanatheologia liliyapinga mafundisho haya.
Affirmativa - Makubaliano
Mafundisho Safi ya Kanisa la Kikristo kuhusu Mabishano Haya
Ili kuyaelezea mabishano haya na kuyamaliza kabisa, imani, 5 mafundisho, na ukiri wetu ndio huu:
1564 Georg Major ( - ). 1565 Nicholas von Amsdorf ( - ).
1. Kwamba, imani ikiwa ya kweli, hai, na isiyokufa, kwa kweli na 6 bila mashaka yoyote, inayazaa matendo mema kabisa jinsi mti bora unavyoyazaa matunda mema.
2. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, matendo mema 7 lazima yaachwe nje kabisa ya majadiliano ya fungu la wokovu wetu wa milele na vile vile yaachwe nje ya fungu la haki yetu mbele za Mungu jinsi mtume anavyoshuhudia kwa maneno yaliyo wazi: “Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo, heri waliosamehewa makosa yao, na waliositiriwa dhambi zao” (Rum. 4:6-7). Mahali pengine: “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu” (Efe. 2:8,9).
3. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri zaidi kwamba, watu wote 8 wanalazimika kuyatenda matendo mema, hasa waliozaliwa na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.
4. Kwa hiyo, istilahi ‘lazima,’ ‘sharti,’ na ‘inabidi’ zimetumiwa 9 kihalali na kwa njia ya Kikristo kabisa kuhusu watu waliozaliwa upya. Istilahi hizi haziipingi lugha sanifu hata kidogo.
5. Hata hivyo, istilahi ‘lazima’ na ‘sharti’1566 zikitumika kwa 10 waliozaliwa upya hazimaanishi shurutisho bali ni utiifu ambao waumini huuonyesha kadiri wanavyozaliwa upya, si kwa shurutisho au sharti la sheria bali kutoka kwa nafsi ya hiari kwa kuwa “hamuwi chini ya sheria, bali chini ya neema.”1567
6. Kwa hiyo, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, si 11 halali kuifafanua kauli“Waliozaliwa upya hutenda matendo mema kwa hiari” kana kwamba, iliachiwa mtu aliyezaliwa upya achague kwa hiari kama atayatenda mema au maovu na kwamba, anaweza kukaa katika imani yake hata kama atadumu katika dhambi kwa makusudi.
7. Lakini hili linapaswa kueleweka kabisa jinsi Kristo na mitume 12 wenyewe wanavyolielezea kwamba, linahusu tu nafsi iliyowekwa huru ambayo huyatenda matendo mema, si kwa kuogopa adhabu kama mtumwa, bali kwa upendo kama wana wa Mungu (Rum. 8:15).
8. Basi, katika watoto wateule wa Mungu hiari hii si kamilifu, 13 bali bado wanalemewa na udhaifu mwingi, jinsi Mt. Paulo anavyolalamika mwenyewe
1566 Kilatini: ‘Necessitas, necessarium.’ 1567 Rum. 6:14; 7:6; 8:14.
katika Rum. 7:14-25 na Gal. 5:17.
9. Hata hivyo, Bwana hauhesabu udhaifu huu kwa wateule wake 14 kwa ajili ya Kristo jinsi ilivyoandikwa: “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Rum. 8:1).
10. Pia tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, imani na 15 wokovu huhifadhiwa na kudumu ndani yetu, si kwa matendo ila kwa njia ya imani kwa ajili ya Roho Mtakatifu peke yake. Basi, matendo mema ni ushahidi wa kuwepo na kukaa kwa Roho Mtakatifu ndani yetu.
Negativa - Uhakiki Hasi
Mafundisho ya Uzushi ya Kuyapinga Mafundisho Yaliyotangulia
1. Tunakataa na tunalaani taratibu zinazofuatia 16 zinazofundisha kwamba, matendo mema ni ya lazima kwa wokovu na kwamba, hakuna mtu yeyote aliyewahi kuokolewa kamwe bila matendo mema na kwamba, haiwezekani kuokolewa bila matendo mema.
2. Tunakataa na tunalaani kauli hii ya kuchukiza sana na yenye 17 madhara kwenye nidhamu ya Kikristo kwamba, matendo mema ni yana madhara kwa wokovu.
Katika nyakati hizi za mwisho, inatulazimu hasa kuwasihi watu 18 waitafuate nidhamu ya Kikristo na matendo mema. Isitoshe, wakumbushwe jinsi ilivyo lazima kujizoeza wenyewe katika matendo mema kama ushahidi wa imani yao na shukrani zao kwa Mungu, kama kuwaonya watu dhidi ya mchanganyiko wa matendo mema katika fungu la kuhesabiwa haki. Watu wataweza kuangamia kwa ushawishi wa Epikuro1568 kuhusu imani sawa na tegemeo la Wafarisayo na wafuasi wa Papa kwa matendo na stahili zao wenyewe.
3. Tena, tunakataa na tunayalaani mafundisho haya kwamba 19 imani na kuwepo kwa Roho Mtakatifu ndani yetu haviwezi kumfanya mtu atende dhambi makusudi. Lakini kwamba, watakatifu na wateule humhifadhi Roho Mtakatifu ingawa wanaanguka katika uzinzi na dhambi nyinginezo na kuendelea kutenda dhambi hizo.
1568 Epikuro ( - K.K.), mwanafalsafa Myunani aliyefundisha kwamba, maana ya maisha ya ubinadamu ndiyo anasa.
V. SHERIA NA INJILI
Status controversiae – Ajili ya Ubishi
Swali limekuwa: Je, kuihubiri Injili Takatifu hasa ni kuihubiri neema tu, yaani, mahubiri ya msamaha wa dhambi au pia ni mahubiri ya toba na makaripio kwa wasioamini, kwa kuwa wasioamini wanahukumiwa na Injili pekee na si sheria?
Affirmativa - Makubaliano
Mafundisho Safi ya Neno la Mungu
1. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, tofauti kati ya 2 Sheria na Injili ni mwanga adhimu mno unaobidi kudumishwa katika Kanisa kwa uangalifu mkuu zaidi ili Neno la Mungu ligawanywe kwa uhalali1569 jinsi Mt. Paulo anavyosihi.
2. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, sheria ni 3 mafundisho ya kimungu hasa yanayofundisha yaliyo mema, yaani, yampendezayo Mungu. Isitoshe, sheria inalikemea lolote ambalo ni dhambi na lililo kinyume cha mapenzi ya Mungu.
3. Kwa hiyo, katika Maandiko Matakatifu, lolote linalohukumu 4 dhambi linahusika na mahubiri ya sheria.
4. Lakini kusema kweli, Injili ni aina ya mafundisho5 yanayofundisha mambo ambayo mtu ambaye hajashika sheria na anahukumiwa nayo anapaswa kuyaamini. Yaani, kwamba, Yesu Kristo ameridhia na amefidia dhambi zote na bila stahili yoyote ya mwanadamu, amepata na amestahili msamaha wa dhambi na “haki inayonufaisha mbele za Mungu” (Rum. 1:17; 2 Kor. 5:21) pamoja na uzima wa milele.
5. Mjadala huu umeanza kwa sababu neno ‘Injili’ halitumiki kwa 6 maana 1569 Linganisha na 2 Tim. 2:15. Katika historia ya Uprotestanti, aya hii imepata maana isiyokuwa halisi kwa ajili ya mafundisho ya J.N. Darby (1800-188?) na wafuasi wake, hasa katika mafundisho ya C.I. Scofield (18? -19? ). Katika kitabu chake kiitwacho, ‘Rightly Dividing the Word of Truth’ (Kuligawanya Neno la Ukweli kwa Haki) na katika toleo lake la Biblia, ‘The Scofield Reference Bible’ (Biblia Marejeo ya Scofield). Scofield anafundisha kwamba, shabaha ya Paulo ni kutofautisha baina ya maana za aya za Agano Jipya zinazohusu Wayahudi tu na aya zinazohusu Wakristo wa mataifa au Kanisa la Kikristo kama Bibi Arusi. Ili kuliepuka kosa hili, toleo la ‘Union Version’ linatafsiri 2 Tim. 2:15: “. . . ukitumia kwa halali neno la kweli.” Katika huu muktadha wa 2 Tim., maana ya ‘kugawanya’ ni sawa na kuwapatia watu chakula, si kutofautisha baina ya yaliyomo mbalimbali ya andiko fulani. Utofautishaji wa Sheria na Injili haumaanishi kuligawanya andiko lenyewe katika sehemu ndogondogo, bali ni kuelewa athari tofauti za kinyume cha Neno lilo hilo la Mungu kama Sheria na Injili.
moja tu katika Maandiko Matakatifu. Kwa hiyo, tunafundisha, tunaamini, na tunakiri kwamba, pale ambapo neno ‘Injili’ linafahamika kuwa mafundisho mazima ya Kristo aliyoyatangaza mwenyewe katika huduma yake ya kufundisha na vile mitume wake walivyofanya, ndiyo halali kusema kwamba, Injili ni tangazo la yote mawili, yaani, toba na msamaha wa dhambi. Neno hili linatumiwa kwa maana hii katika Mk. 1:15 na Mdo. 20:24.
6. Wakati sheria na Injili vinatolewa kama zinazopingana, kwa 7 mfano, pale ambapo Musa, kama mwalimu wa sheria na Kristo kama mhubiri wa Injili, hapo basi, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, Injili si mahubiri ya toba na adhabu, bali, kweli, si kitu chochote kingine isipokuwa mahubiri ya kuitangaza faraja na habari yenye furaha mno. Haiadhibu wala kuogofya, bali inazifariji dhamiri zinazotiwa hofu na sheria. Inauonyesha ustahili wa Kristo pekee, na inaziinua tena dhamiri zenye hofu kwa mahubiri matamu ya neema na huruma ya Mungu katika Kristo.
7. Kuhusu habari ya dhambi, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri 8 kwamba, utaji ule wa Musa1570 huyafunika macho ya watu wote wakati wote ambapo wao husikia mahubiri ya sheria tu, bila kulisikia lolote kuhusu Kristo hivyo, hawafahamu dhambi zao kwa njia halisi. Hivyo, wanakuwa wanafiki wenye kiburi kama Wafarisayo, au wanakata tamaa kama Yuda alivyofanya, na kadhalika. Kwa hiyo, Kristo anachukua sheria mikononi mwake mwenyewe na kuielezea kwa njia ya kiroho (Mt. 5:21-48; Rum. 7:14). Hivyo ndivyo, “ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu” (Rum. 1:18) ili wajifunze kuufahamu ukali wake kwa sheria. Basi, kwa njia ya sheria, wanaongozwa kuifahamu sheria, na wanajifunza kutoka sheria kwa mara ya kwanza kufahamu dhambi zao kweli. Musa asingeweza kamwe kuubinya ufahamu huo kutoka kwao.
Kwa hiyo basi, mahubiri ya mateso na kifo cha Kristo, aliye 9 Mwana wa Mungu, ni mahubiri na tangazo kakamavu1571 na la kuogofya sana kuhusu ghadhabu ya Mungu ambayo kweli huwaongoza watu ndani ya sheria. Baada ya utaji wa Musa kuondolewa kutoka kwao, wanaanza kuelewa kwa njia halisi uzito wa madai ya Mungu katika sheria yake. Sisi hatuwezi kutimiza dai hata moja. Kwa sababu hiyo, hatuna budi kuitafuta haki yetu katika Kristo peke yake.
8. Hata hivyo, wakati mateso ya Kristo na kifo chake vinaiweka 10 ghadhabu ya Mungu mbele ya macho na kumtisha mwanadamu, hapo huwa bado hakuna mahubiri ya kweli ya Injili, bali mahubiri ya Musa na ya sheria. Kwa hiyo, ni 1570 2 Kor. 3:13-16. 1571 Yaani, zito.
‘kazi ngeni’1572 ya Kristo ambayo kwayo, huja kwenye huduma yake maalumu, ambayo ni kuhubiri neema, kufariji, na kuhuisha. Haya yote ni sifa maalumu za mahubiri ya Injili.
Negativa - Uhakiki Hasi
Mafundisho Mapotovu/kinyume Yaliyokataliwa
Kwa hiyo basi, tunakataa mafundisho ambayo tunayaona kuwa 11 mapotovu na yenye madhara, endapo watu wanafundishwa kwamba, Injili kamili ni mahubiri ya toba na adhabu na si mahubiri ya neema peke yake. Kwa hiyo, Injili inageuzwa tena kuwa mafundisho ya sheria, inauficha ustahili wa Kristo na Maandiko Matakatifu. Wakristo wananyang’anywa faraja yao ya kweli, na milango hufunguliwa tena kwa Upapa.
VI. MATUMIZI YA TATU YA SHERIA
Status controversiae – Ajili ya Ubishi
Sheria imetolewa kwa watu kwa sababu tatu zifuatazo: (1) Kutunza 1 nidhamu ya nje dhidi ya watu wakaidi na wasiokuwa watiifu. (2) Kuwafundisha watu kufahamu dhambi zao (3) Watu waliozaliwa upya kuweza kupanga na kutawala maisha yao yote kwa sababu bado wako katika mwili. Kuhusiana na kazi ya tatu ya sheria, mabishano yametokea kati ya baadhi ya wanatheologia. Je, sheria inabidi kuhubiriwa kwa Wakristo waliozaliwa upya au la? Kundi moja lilikubali ilihali kundi lingine lilikataa.
Affirmativa - Makubaliano
Mafundisho sahihi ya Kikristo katika mabishano haya
1. Tunaamini, tunafundisha na tunakiri kwamba, ingawa watu 2 ambao wanaamini kweli na ambao Mungu amewaongoa kweli, tena wamewekwa huru katika Kristo kutokana na laana na nguvu ya sheria, hawako kwasababu hiyo bila sheria. Kinyume chake, wamekombolewa na Mwana wa Mungu ili wapate kuitafakari mchana na usiku (Zab. 119:1; Zab. 1:2). Kama jinsi ilivyokuwa kwa wazazi wetu wa kwanza, kabla ya anguko, hawakuishi bila sheria kwa kuwa sheria ya Mungu iliandikwa mioyoni mwao walipoumbwa kwa mfano wa Mungu
1572 Kulingana na Isa. 28:21.
(Mwa. 2:16; 3:3). 1573
2. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, sheria 3 isihubiriwe kwa bidii tu kwa wale wasioamini na wasiotubu, bali pia kwa watu wanaoamini kweli, walioongoka kweli, waliozaliwa upya, na waliohesabiwa haki kwa imani.
3. Kwa maana, ingawa mmezaliwa upya na ‘mfanywe wapya 4 katika roho ya nia ´zenu,’1574 kuzaliwa upya na kufanywa upya hakuwezi kuwa kamili katika ulimwengu huu, bali kwa hakika ndio kwanza imeanza, na katika ‘Roho ya nia’ ya hao wanaoamini inapigana vita daima dhidi ya mwili, yaani, uharibifu wa asili, ambao unawang’ang’ania mpaka kifo.1575 Adamu huyu wa Kale, anayeendelea kukaa katika akili, nia, na uwezo wake wote, yu tayari kufuata desturi za kiibada zilizobuniwa na dini ya kibinadamu. Kwa hiyo, ni lazima sheria ya Bwana ituwakie daima.1576 Adamu wa Kale hapaswi kuyafuata mapenzi yake mwenyewe. Kinyume chake, lazima alazimishwe dhidi ya nia yake mwenyewe, si kwa maonyo na vitisho vya sheria tu bali pia kwa adhabu zake na mateso, ili kufuata uongozi wa Roho na kuwa mateka mwenyewe (1 Kor. 9:27; Rum. 6:12; Gal. 6:14; Zab. 119:1; Ebr. 13:21).
4. Kuhusu tofauti kati ya matendo ya sheria na matunda ya Roho, 5 tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, matendo yanayofanywa kulingana na sheria, yanaitwa matendo ya sheria, na ndivyo yalivyo, wakati kumbukumbu ya adhabu na tisho la ghadhabu ya Mungu vinagandamiza kutoka kwa watu chini ya sheria.
5. Kinyume chake, matunda ya Roho, ni matendo yale ambayo 6 Roho wa Mungu anayekaa ndani ya waumini hutenda kazi. Wale wanaoamini na kuzaliwa upya, wanayafanya matendo haya kwa hiari, kana kwamba, hawasikii kitisho wala thawabu yoyote kuhusu amri. Kwa hiyo, watoto wa Mungu “wanaishi katika sheria”1577 na kutembea kulingana na sheria ya Mungu. Katika nyaraka zake, Mt. Paulo anaiita sheria ya Kristo na sheria ya nia. Hata hivyo basi, watoto wa Mungu “hawako chini ya sheria, bali wako chini ya neema” (Rum. 7:25; 8:1,14).
6. Maana, sheria inadumu kuwa moja tu kwa wote wawili, yaani, 7 kwa waliotubu na wasiotubu, kwa waliozaliwa upya na wasiozaliwa upya, kwa kuwa sheria nayo ni mapenzi ya Mungu yasiyobadilika. Tofauti inahusu utiifu, yaani, mwanadamu peke yake kwa maana mwanadamu asiyezaliwa upya huitii sheria
1573 Taz. pia Rum. 2:15.
1574 Efe. 4:23.
1575 Gal. 5:17; Rum. 7:21,23.
1576 Rum. 2:7-8.
1577 Zab. 119:1.
mshindani kwa lazima sawa na mtu aliyezaliwa upya. Kadiri anavyoishi katika mwili, hufanya yale anayodaiwa na sheria kwa kulazimishwa na si kwa matakwa yake. Lakini, kadiri muumini alivyozaliwa upya, kwa nafsi ya hiari ambayo hakuna kitisho chochote cha sheria ambacho kingeweza kumshawishi kutenda, hufanya bila kulazimishwa.
Negativa - Uhakiki Hasi
Mafundisho mapotovu/yaliyo kinyume
1. Hivyo, tunayakataa mafundisho ya uzushi yenye madhara mno, yanayopinga maadili ya Kikristo na uchaji wa kweli yanayofundisha kwamba, sheria isihubiriwe jinsi ilivyoelezewa hapo juu, kwa Wakristo na wanaoamini kweli kweli, ila tu kwa wasioamini, wasiokuwa Wakristo na wasiotubu.
VII. CHAKULA KITAKATIFU1578 CHA KRISTO
1. Ingawa walimu walio wafuasi wa Zwingli hawahesabiwi kati ya wanatheologia waliotambuliwa na Ukiri wa Augsburg, kwa sababu walijibagua wenyewe tayari wakati Ukiri1579 ulipowasilishwa. Lakini, kwa sababu wanajaribu kujipenyeza miongoni mwetu na wameanza kueneza uzushi wao chini ya jina hili la Ukiri wa Kikristo, tumeona ni vyema kuyaelezea pia mabishano haya kwa ufasaha unaohitajika.
Status controversiae – Ajili ya Ubishi: kiini cha mabishano kati ya mafundisho yetu na ya wanaoidharau sakramenti1580
2. Swali ni: Je, katika Chakula Kitakatifu, kuna mwili wa kweli na damu ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambavyo vyote vipo katika kiini chao kweli na vikigawiwa katika mkate na divai na kama vitapokelewa na kunywewa kwa midomo ya wote wanaoitumia hii sakramenti, aidha wawe waliostahili au wasiostahili, wacha Mungu au wasiomcha Mungu, wanaoamini au wasioamini, kwamba, kwa wanaoamini kwa faraja na uzima, na kwa wasioamini hukumu? Wanaoidharau sakramenti husema: ‘Hapana!’ Sisi tunasema: ‘Ndiyo!’
3. Ili kuyatatua mabishano haya, kwanza kabisa inatubidi kujua kwamba, 1578 Kijerumani: ‘heiliges Abendmah;’ Kilatini: ‘Coena Domini.’ 1579 Miji minne ya kusini magharibi mwa Ujerumani, yaani, Strassbourg, Memmingen, Konstanzo, na Lindau iliwasilisha ‘Confessio Tetrapolitana’ (‘Ukiri wa Miji Minne’) kwa Kaisari Karolo V huko Augsburg mwaka wa 1530. Huldrych Zwingli alituma ‘Ratio Fidei’ (‘Uwiano wa Imani’) kama ukiri wake wa binafsi. 1580 ‘Wanaoidharau sakramenti:’ Kijerumani: ‘Sakramentierer;’ Kilatini: ‘Sacramentarii.´
528
kuna aina mbili za watu wanaoidharau sakramenti. Baadhi yao ndio wagumu.1581
Hawa husema wazi kwa maneno ya Kijerumani wanaloliamini mioyoni mwao, yaani, kwamba, katika Chakula Kitakatifu, ni mkate na divai tu ndivyo vinavyopatikana na vinavyogawiwa na kupokelewa na kunywewa kwa kinywa. 4. Lakini wengine, ndio werevu,1582 wenye madhara kuliko wote, ambao kwa njia fulani huzungumza, lugha yetu kwa kudhania, na kusingizia kuamini kwamba, mwili hai wa kweli na damu hai ya kweli ya Kristo vinakuwepo kweli katika Chakula Kitakatifu. Lakini wanadai kwamba, haya hufanyika kwa njia ya kiroho kwa imani. Lakini watu wa aina hii huendelea kulizingatia chini ya kauli hizi za udanganyifu wazo gumu lililotajwa awali kwamba, ndani ya Chakula Kitakatifu hakuna lolote isipokuwa mkate na divai ndivyo vilivyomo na ndivyo hupokelewa na kunywewa kwa midomo.
5. Kulingana na lugha yao, neno ‘kiroho’ halimaanishi lolote lingine isipokuwa kuwapo kwa Roho ya Kristo au nguvu ya kutokuwepo kwa mwili wa Kristo au pia ustahili wa Kristo. Badala yake, mwili wa Kristo hauwezi kuwepo hapa kwa njia yoyote, bali unakaa tu huko juu mbinguni kabisa, ambako tunapaswa kujiinua kwa mawazo ya imani yetu na kwenda kwake huko mbinguni. Kisha, tuutafute mwili wake na damu yake na siyo katika mkate na divai ya Chakula Kitakatifu.
Affirmativa - Makubaliano
Ukiri wa mafundisho sahihi kuhusu Chakula Kitakatifu dhidi ya wanaoidharau sakramenti
1. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, mwili na damu ya Kristo vimo kweli katika kiini chao kwenye Chakula Kitakatifu, na kimsingi vinagawiwa na kupokelewa kweli kwa mkate na divai.
2. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, maneno ya agano la Kristo yasieleweke kwa njia nyingine isipokuwa kwa maana yake halisi. Yaani, mkate haumaanishi mwili wa Kristo usiokuwepo na divai haimaanishi damu ya Kristo isiyokuwepo, bali kwamba, kwa sababu ya muungano wa kisakramenti1583 vimekuwa mwili na damu ya Kristo kweli.1584
1581 Rejea wanatheologia wa Geneva (Yohana Calvin, Theodoro Beza), Zürich (Huldrych Zwingli na Heinrich Bullinger) na Heidelberg (wanatheologia walio katika kitala cha Mtawala Mchaguzi Fredrik III).
1582 Rejea wafuasi wa siri wa Philipp Melanchthon katika majadiliano baada ya kifo cha Dk. Luther.
1583 Kilatini: ‘Unio sacramentalis.’
1584 Nakala nyingi za matoleo ya Dresden ya mwaka wa 1580 zina istilahi ‘kweli’ mara mbili. Martin Chemnitz: ‘typographicum erratum,’ yaani, kosa la uchapishaji.
3. Kuhusu kuibariki elementi, tunaamini, tunafundisha, na kukiri kwamba, hakuna tendo lolote la kibinadamu, wala si maneno ya kasisi wa Kanisa, yanayosababisha mwili na damu ya Kristo kuwepo katika Chakula Kitakatifu, bali uweza wenye enzi wa Bwana wetu Yesu Kristo pekee yake uhesabiwe.
4. Lakini wakati huo huo, tunaamini, tunafundisha, na kukiri kwa kauli moja kwamba, katika kushiriki Chakula Kitakatifu, maneno ambayo Kristo aliyatumia kuanzisha karamu hii yasiachwe kwa njia yoyote ile, bali yatamkwe hadharani, kama iliyoandikwa: “Kikombe kile cha baraka tukibarikicho” (1 Kor. 10:16; 11:23-25). Kubariki huku kunatokea katika kuyatamka maneno ya Kristo.
5. Katika mabishano haya dhidi ya wanaoidharau sakramenti, tunasimama katika msingi uliowekwa na Dk. Luther katika Ukiri wake Mkuu: 1585
“Msingi wa kwanza: Fungu la imani yetu ya Kikristo. Kwa mujibu wa ariki na asili yake, Yesu Kristo ni Mungu wa kweli na timamu na binadamu wa kweli na timamu katika nafsi moja. Asili hizi haziwezi kutenganishwa wala kugawanywa.1586
Msingi wa pili: Mkono wa kuume wa Mungu u kokote. Kristo aliketi katika mkono huu katika asili yake ya kweli ya ubinadamu na bado anatawala na mikononi mwake na chini ya miguu yake ana vyote vilivyoko mbinguni na duniani. Hakuna mwanadamu mwingine wala malaika ambaye amewekwa katika mkono wa kuume wa Mungu isipokuwa Mwana wa Mariamu. Kwa hiyo basi, ana uweza wa kuyafanya mambo haya.
Msingi wa tatu: Neno la Mungu si uongo na wala halidanganyi.
Msingi wa nne: Mungu anazo na anazijua njia mbalimbali za kuwepo mahali fulani. Si njia moja tu ambayo wanafalsafa wanaiita njia ya mahali maalumu au ndani ya mipaka mahsusi.”1587
6. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, sisi hatupokei mwili na damu ya Kristo kwa njia ya kiroho tu, yaani, kwa imani, bali pia kwa kinywa; siyo kwa jinsi ya Kikapernaumu1588 ila kwa sababu ya muungano wa Kisakramenti kwa
1585 Vom Abendmahl Christ, Bekenntnis, (‘Ukiri Mkuu wa Chakula Kitakatifu cha Kristo’) WA, 261-509 mwaka wa 1528.
1586 Ukiri wa Sinodi ya nne ya kiekumeni huko Khalkedon mwaka wa 451: ‘αδιαιρετως, αχωριστως.’
1587 Kilatini: ‘modus localis’ na ‘circumscriptus’ (Kijerumani: ‘räumlich’); kiini chochote kilichozuiwa katika mipaka isiyobadilika na nafasi maalumu, bila kushirikiana na kiini kingine.
1588 Wapinzani wa mafundisho ya Kilutheri waliwashtaki walimu Walutheri kwamba, jinsi watu wa Kapernaumu walivyoyatafsiri maneno ya Yohana 6:26,52 kumaanisha kula kwa njia ya kimwili tu. Vivyo hivyo, walidai kwamba, mafundisho ya Kilutheri yalimaanisha kwamba, washiriki ‘wanaichana nyama ya Kristo kwa
530
namna ipitayo asili, yaani, namna ya kimbingu. Maneno ya Kristo hulifundisha jambo hili wazi yanapotuagiza kuchukua, kula, na kunywa. Yote yalifanyika kwa mitume, maana imeandikwa “wakakinywea wote” (Mk. 14:23). Kadhalika, Mt. Paulo anasema “mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?”1589 Yaani, yeyote aulaye mkate huu anakula mwili wa Kristo. Hili ndilo fundisho kuu walilolikubali walimu wakuu wa Kanisa la Zamani kwa ridhaa, kama vile Krisostomo, Sipriano, Leo I, Gregorio, Ambrosio, na hata Agostino.1590
7. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, licha ya waaminio kweli na wanaostahili, hata wasiostahili na wasioamini wote hupokea mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo, ingawa si kwa kuwapa uzima na faraja bali kwa hukumu na taraa kama hawajaongoka na hawajatubu.
Kwa kuwa wanaomfukuza na kumkataa Kristo kama Mwokozi, hawana budi kumpokea kama hakimu mkali ingawa ni kinyume cha matakwa yao. Jinsi auletavyo uzima na faraja katika mioyo ya waaminio na wanaostahili, vivyo hivyo, huwahukumu wageni wasiotubu.
8. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, kuna aina moja tu ya wageni wasiostahili, nao ni wasioamini kwani imeandikwa: “asiyeamini amekwisha kuhukumiwa.”1591 Matumizi ya hii sakramenti yasiyostahili yanaanzisha, yanakuza, na yanauongeza ubaya na ukali wa hukumu hii (1 Kor. 11:27, 29).1592
9. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, hakuna aaminiye kweli, hata awe dhaifu kiasi gani. Kadiri ya imani hai, atapokea Chakula Kitakatifu kwa hukumu yake. Chakula Kitakatifu kilianzishwa hasa kwa ajili ya Wakristo dhaifu katika imani, walio tayari kutubu ili wafarijiwe na waimarishwe katika udhaifu wa imani yao.
10. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, ustahilifu wa pekee wa wageni katika meza ya karamu hii ya kimbingu ni utiifu mtakatifu zaidi na ustahili kamili wa Kristo ambao tunaufanya kuwa wetu wenyewe kwa njia ya imani ya kweli. Sakramenti inayaimarisha haya. Ustahili wetu hausimami hata kidogo katika wema wetu wenyewe wala katika maandalio yetu ya ndani wala ya nje.
meno yao na kuisaga kama chakula kingine chochote.’ Wengine pia walithubutu kubuni kwamba, Walutheri ni wala watu.
1589 1 Kor. 10:16.
1590 Taz. Tamko Thabiti 7,60,66.
1591 Yn. 3:18.
1592 Martin Bucer alitofautisha baina ya ‘walioamini wasiostahili’ (‘indigni’) na ‘wasiomini wasiomcha Mungu’ (‘impii’).
Negativa - Uhakiki Hasi
Mafundisho mapotovu yaliyokataliwa ya wanaoidharau sakramenti
Kwa upande mwingine, tunayakataa na kuyatupilia mbali kwa kauli moja mafundisho yote yafuatayo ya uzushi. Haya ni kinyume na yanayopingana na mafundisho yaliyowekwa hapo juu na imani yetu sahili, na ukiri wetu kuhusu Chakula Kitakatifu.
1. Mafundisho ya wafuasi wa Papa kuhusu mageuzo-uwamo.1593 Wao hufundisha kwamba, mkate na divai hupoteza kiini chao na ariki yao ya kiasili1594 katika Chakula Kitakatifu hata huangamizwa kabisa kwa namna ambayo kugeuzwa kuwa mwili wa Kristo na kitu ambacho hubakia tu ni sura ya nje.1595
2. Dhabihu ya Misa kwa ajili ya dhambi za walio hai na wafu.
3. Kufuru hii kwamba, Wakristo wa kawaida huipokea aina moja tu ya Sakramenti. Wao hunyimwa kikombe, kinyume cha Neno dhahiri la agano la Kristo. Hivyo, wananyimwa damu ya Kristo.
4. Mafundisho yasemayo kwamba, maneno ya agano la Kristo yasieleweke na kuaminiwa kwa njia sahili, ila ni kauli ya iliyo kwenye giza ambayo maana yake inabidi kutafutwa kwingineko katika Maandiko Matakatifu.
5. Mwili wa Kristo haupokelewi katika Chakula Kitakatifu kwa kinywa pamoja na mkate, ila kwamba, tunapokea mkate na divai tu kwa kinywa. Mwili wa Kristo hupokelewa kwa njia ya kiroho pekee yake kwa imani.1596
6. Mkate na divai katika Chakula Kitakatifu ni alama tu ambazo kwazo, Wakristo hupata kufahamiana.1597
7. Mkate na divai ni alama, mifano, na taswira tu za mwili na damu ya Kristo asiyekuwepo.
8. Mkate na divai ni alama za kutukumbusha kama mihuri na dhamana. Shabaha yao ni kutuhakikishia kwamba, imani yetu inapopaa mbinguni, itashiriki huko mwili na damu ya Kristo jinsi tunavyokula mkate na kunywa divai katika Chakula Kitakatifu.1598
1593 ‘Transsubstantiatio,’ yaani, mageuzo ya elementi. 1594 Kilatini: ‘substantia atque naturalis sua essentia.’ ‘Sura ya nje,’ Kilatini ‘accidens,’ yaani, ‘mbadiliko umbo’ kinyume cha ‘substantia,’ yaani, ‘kiini;’ istilahi za falsafa ya Aristotele. 1595 Sinodi ya Laterano ya mwaka wa 1215 iliamua kwamba, mafundisho haya ni ya lazima kwa imani ya kweli. Sinodi ya Trento, kikao cha 13, mwaka wa 1551, Fungu la Nne, liliuthibitisha mfumo huu wa imani.
1596 ‘Consensus Tigurinus’ (‘Mwafaka wa Zürich’), Fungu la IX. 1597 Zwingli, De vera et falsa regione (Opera, III. 145, n.k).
1598 Wazo la Calvin kuhusu 1 Kor. 11:23 ( C.R., 49:483).
532
9. Imani yetu inaimarishwa na kuthibitishwa katika Chakula Kitakatifu kipekee na ishara za nje, yaani, mkate na divai na si uwepo wa mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo.
10. Kwamba, katika Chakula Kitakatifu, ni uwezo, utendaji, na ustahili tu wa mwili wa Kristo na damu ya Kristo isiyokuwepo ndivyo vinavyogawiwa.1599
11. Mwili wa Kristo umefungiwa mbinguni kiasi kwamba, hauwezi kuwepo kwa njia yoyote hapa duniani wakati huo huo katika mahali pengi, licha ya mahali pote, ambapo Chakula Kitakatifu chake kinasherehekewa.1600
12. Kristo asingeweza kuahidi na kutekeleza kuwepo kiasili kwa mwili wake na damu yake katika Chakula Kitakatifu. Kwa kuwa asili na sifa za ubinadamu wake aliouchukua haungeweza kuruhusu wala kukubali jambo hili.
13. Mungu na uenyezi wake hawezi - kwa tamko la kutisha - kusababisha mwili wa Kristo kuwepo wakati mmoja katika mahali pengi badala ya pahali pamoja tu.1601
14. Kwamba, uwepo wa mwili na damu ya Kristo katika Chakula Kitakatifu unatekelezwa na kufanywa na imani na si maneno yenye enzi zote ya agano la Kristo.
15. Wanaoamini wasitafute mwili wa Kristo katika mkate na divai ya Chakula Kitakatifu, bali wainue macho yao kutoka kwenye mkate kuelekea mbinguni na huko wautafute mwili wa Kristo.1602
16. Kwamba, Wakristo wasioamini na wasiotubu hawapokei katika Chakula Kitakatifu mwili na damu ya Kristo, ila wao hupokea mkate na divai tu.1603
17. Ustahilifu wa wageni katika chakula hiki cha kimbingu hautegemei tu imani ya kweli katika Kristo, bali pia maandalizi ya nje ya wanadamu.1604
18. Kwamba, waaminio kweli, walio na imani1605 hai ya kweli katika Kristo, 1599 Calvin, ‘Institutio,’ IV, 22, 18. 1600 ‘Consensus Tigurinus’ Fungu la III. 1601 Theodoro Beza katika ‘Creophagia,’ na Petro Martiro Vermigli katika ‘De utrague omn Chisto natura,’ uk. 14.
1602 ‘Consensus Tigurinus,’ mafungu ya XXI na XXV.
1603 Kwa kuwa, ariki ya sakramenti haitegemei imani ya ubinadamu bali neno la Kristo, Walutheri walisisitiza kwamba, wasioamini na wasiostahili hupokea mwili na damu ya Kristo kwa kweli katika sakramenti (‘manductio infidelium/indignorum’). Kanisa la Kiangilikana linafundisha katika Mafungu 39 kinyume cha mafundisho haya ya Ukiri wa Kilutheri.
1604 Aya 17, 18, na 19 zinakusudia mafundisho ya Roma.
1605 Andiko la Kijerumani: ‘wahrhaftigen, lebendigen, reinen glauben’ ( ‘ya kweli, hai, imani safi’). Kulingana na Martin Chemmitz, hili lilikuwa kosa la mpangaji herufi ambaye aliweka ‘reinen’ badala ya ‘einen,’ kosa
533
na wanaodumu katika imani hii, wanaweza pia kuipokea sakramenti kwa hukumu yao kwa sababu bado hawajakamilika katika mwenendo wao wa nje.1606
19. Elementi za nje zinazoonekana, yaani, mkate na divai, katika Sakramenti Takatifu zisujudiwe.1607
20. Hali kadhalika, tunayakabidhi maswali na matamko yote ya upekuzi na yenye kufuru, ambayo hayawezi hata kukaririwa bila chukizo hukumuni mwa haki ya Mungu. Wale wanaoidharau sakramenti wamesema kuhusu siri za juu za asili na za kimbingu za sakramenti hii kwa njia ya kukufuru na ya kuchukiza mno, kwa njia ya ukali na kimwili ya Wakapernaumu.
21. Basi, sisi tunakataa na tunalaani mafundisho kuhusu kuula mwili wa Kristo yaliyobuniwa na Wakapernaumu. Wao hudhania kwamba, mwanadamu huurarua mwili wa Krisrto kwa meno yake na kuimung’unya sawa na chakula chochote. Wale wanaoidharau sakramenti wanalisisitiza hili makusudi na kwa njia ya kuchukiza sana dhidi ya ushuhuda wa dhamiri zao wenyewe na dhidi ya kukataa kwetu kwa wingi kwamba, sisi tunakubaliana nao. Kwa hiyo basi, wasikilizaji wao wanataka kuyafanya mafundisho yetu kuwa madharau. Kinyume chake, tunashikilia na kuamini kweli kulingana na maneno rahisi ya agano la Kristo ingawa yanapita akili zetu kwamba, tunaula mwili wa Kristo na kuinywa damu yake kweli, lakini kwa njia ipitayo asili ambayo haitambuliwi na akili na hisia za kibinadamu. Hapa, akili zetu zinashikwa mateka katika kumtii Kristo, jinsi tunavyofanya katika mafungu mengine yote. Siri hii imefunuliwa katika Neno la Mungu peke yake na kupokelewa kwa imani peke yake.
VIII. NAFSI YA KRISTO
Kutokana na majadiliano kuhusu Chakula Kitakatifu, ugomvi umezuka kati ya wanatheologia thabiti wa Ukiri wa Augsburg na wafuasi wa Calvin,1608 ambao wamewapotosha baadhi ya wanatheologia kuhusu nafsi ya Kristo, asili zake ambalo waliopitia nakala hizo walishindwa kuligundua. Nakala za kwanza hazina neno hili lililoongezewa. Neno hili halipo pia katika andiko la Kilatini.
1606 Sinodi ya Trento, Kikao cha 13, fungu la 7
1607 Ibid. fungu la 5 na la 6.
1608 Jean Calvin (1509- 1564) aliyetoka Noyon, Ufaransa. Baada ya uamsho wake wa kiroho mwaka wa 1533 alisikia wito wake wa kulitengeneza Kanisa katika hali yake ya asili. Alikimbilia Uswisi mwaka wa 1535 kwa sababu ya hatari ya mateso ya Waprotestanti huko Ufaransa. Alihamia mjini Geneva huko Uswisi mwaka wa 1536 lakini alifukuzwa mwaka wa 1538 kwa ajili ya uongozi wake mkali. Alikuwa kiongozi wa mji wa Geneva tena mwaka wa 1541 na tangu mwaka wa 1555 alitawala kama dikteta. Aliandika vitabu vingi vya ufafanuzi wa Biblia. Kitabu chake muhimu mno ni ‘Institutio christianae religionis’ (‘Mafundisho ya Dini ya Kikristo’), kilichoandikwa mwaka wa 1536 na kilichohaririwa mara nyingi mpaka mwisho wa maisha yake.
534
mbili, na sifa za asili hizo.
Status controversiae – Ajili ya Ubishi
Swali kuu ni: Je, asili ya kimungu na asili ya kibinadamu na sifa zao zimeungana katika nafsi ya Kristo kwa ajili ya muungano wa kibinafsi kwa njia iliyo kweli, yaani, katika tendo na ukweli na zimeunganishwa kwa kiasi gani?
Wale wanaoidharau sakramenti wanasingizia kwamba, asili ya kimungu na ya kibinadamu zimeunganishwa katika Kristo kwa njia ya jina peke yake. Kwa kweli, sifa hizo mbili za asili haziambatani kwazo zenyewe. Wao husema wazi: ‘Muungano wa kibinafsi unayafanya majina bia.’1609 Mungu anaitwa binadamu na binadamu anaitwa Mungu. Hata hivyo, Mungu hana lolote la pamoja na wanadamu wala wanadamu hawana (yaani, katika tendo na kweli), lolote la pamoja na Mungu na enzi yake na sifa zake. Dk. Luther na wafuasi wake wameshindana kwa maoni tofauti dhidi ya wanaoidharau sakramenti.
Affirmativa - Makubaliano
Mafundisho safi/sahihi ya Kanisa la Kikristo kuhusu Nafsi ya Kristo.
Ili kuyaelezea na kuyamaliza mabishano haya, tunayatoa haya yafuatayo kama mafundisho, imani, na ukiri wetu.
1. Asili ya kimungu na kibinadamu zimeunganishwa katika Kristo kiasi kwamba, hakuna Kristo wawili, ambapo mmoja ni Mwana wa Mungu na mwingine mwana wa Adamu. Ni Mwana wa Mungu mmoja peke yake, ambaye ndiye mwana wa Adamu (Lk. 1:35; Rum. 9:5).
2. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, asili ya kimungu na ya ubinadamu hazichanganywi kuwa ariki moja wala asili moja haibadiliki kuwa nyingine, bali asili hizi mbili zinahifadhi sifa za ariki zao, ambazo haziwi sifa za asili ya nyingine kamwe.
3. Sifa za asili ya kimungu ni uenyezi, umilele, pasipo mwisho na (kulingana na sifa za asili na ariki ya kiasili katika asili hii yenyewe) kuwa kokote, kuyajua yote na kadhalika, ambazo kamwe zitakuwa sifa za asili ya mwanadamu.
4. Sifa za asili za mwanadamu ni kuwa kiumbe chenye mwili, kuwa nyama na damu, kuwa mwisho, kuwa mpaka, kuteseka, kufa, kupaa, na kushuka, kuhama kutoka mahali pamoja mpaka pengine, kuona njaa, kuhisi kiu, baridi, joto, na
1609 Kilatini: ‘Unio faciat communia nomina.’
mambo mengine ambayo kamwe hayajawahi kuwa sifa za asili ya kimungu.
5. Kwa kuwa asili hizo zote mbili zimeungana kibinafsi, yaani, katika nafsi moja, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, muungano huu si mchanganyiko au muungano wa aina ambayo zote haziwi na uhusiano wowote kibinafsi, kama jinsi mbao mbili zinavyounganishwa kwa gundi na haiwi kwamba, ubao huu unatoa au unachukua lolote kutoka kwa ubao mwingine, wakati ushirika wa kweli wa Mungu na wa mwanadamu ni ushirika wa juu kuliko zote. Muungano huu wa kibinafsi unauzaa ushirika wa juu sana usioelezeka. Kutoka katika ushirika huu, yanafuatia yote ambayo yanaweza kusemwa na kuaminiwa kuhusu ubinadamu wa Kristo kama Mungu na yote ambayo yanaweza kusemwa na kuaminiwa kuhusu uungu wa Kristo kama mwanadamu. Akina baba wa kanisa wa kale wameufafanua muungano na ushirikiano huu wa kiasili kwa mifano ya chuma kinachong’aa kwa sababu ya moto mkali pamoja na ushirikiano wa mwili na roho ndani ya mwanadamu.
6. Kwa hiyo, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, Mungu ni mwanadamu na mwanadamu ni Mungu. Hali hii ya mambo isingeweza kuwa hivyo kama asili ya kimungu na ya kibinadamu zisingekuwa na ushirikiano wowote wa kweli.
Basi, ni kwa njia gani mwanadamu, yaani, mwana wa Mariamu,anaweza kuitwa Mungu kweli, au Mwana wa Mungu aliye juu kuliko wote, kama ubinadamu wake usingekuwa umeungana kweli,1610 yaani, katika tendo na kweli na Mwana wa Mungu, na usiwe na lolote kweli la pamoja na Mwana wa Mungu isipokuwa jina la Mungu peke yake?
7. Kwa hiyo, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba,Mariamu hakuichukua mimba na hakumzaa mtu tu, bali aliichukua mimba na kumzaa Mwana wa kweli wa Mungu. Kwa hiyo ni haki kumwita kweli Mama wa Mungu1611 kwani ndivyo alivyo.
8. Kwa hiyo, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri pia kwamba, hakuwa mtu wa kawaida tu aliyeteseka, akafa, akazikwa, akashuka kuzimuni, akafufuka kutoka kwa wafu, akapaa mbinguni, tena akainuliwa kwenye utukufu na enzi kuu ya Mungu, bali ni mtu ambaye asili yake ya ubinadamu imeungana na kushiriki na Mwana wa Mungu kwa njia iliyo juu mno na isiyoelezeka, hata kuwa nafsi 1610 Andiko la Kijerumani na Kilatini: ‘realiter.’ 1611 Θεοτοκος: Sinodi ya Efeso ya mwaka wa 431 dhidi ya mafundisho ya Nestorio (+ mnamo 451 katika Misri ya Juu), Askofu Mkuu wa Konstantinopoli 428-430. Nestorio alisisitiza dhidi ya muungano wa binafsi wa asili za Kristo (ενωσις) mwingiliano (συναφεια) wa asili. Badala ya tunakiri ushirikiano wa kiariki (ενωσις καθ’ υποστασιν) alipendelea kufundisha mwingiliano wa nia (συναφεια καθ’ ευδοκιαν).
536
moja pamoja naye.
9. Kwa hiyo, Mwana wa Mungu ameteseka kweli kwa ajili yetu. Yaani, kulingana na sifa za asili ya ubinadamu aliyoichukua katika umoja wa nafsi yake ya kimungu na kuifanya kuwa yake, ili apate kuteseka na kuwa Kuhani wetu Mkuu kwa ajili ya upatanisho wetu na Mungu, jinsi ilivyoandikwa katika 1 Kor. 2:8: “Wamemsulibisha Bwana wa utukufu,” na katika Mdo. 20:28. “Tumekombolewa kwa damu yake Mungu mwenyewe.”
10. Kwa hiyo, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, Mwana wa Adamu ameinuliwa kweli kweli,1612 yaani, katika tendo na hakika na asili yake ya ubinadamu kwenye enzi zote za Mungu. Kwa hiyo, alitwaaliwa katika uungu alipochukuliwa mimba kwa Roho Mtakatifu katika tumbo la uzazi la mama yake, na asili yake ya ubinadamu iliungana kibinafsi na Mwana wa Aliye juu sana.1613
11. Kwa ajili ya muungano binafsi, alikuwa na utukufu huu wakati wote, lakini katika hali ya yake ya unyenyekevu alijitolea kwao.1614 Kwa hiyo basi, alizidi kweli kuongezeka katika kimo, hekima, na neema mbele za Mungu na wanadamu,1615 kwa maana, wakati wote, hakuifunua enzi yake ila tu ilipompendeza. Hatimaye, baada ya kufufuka kwake, aliiacha kabisa hali ya utumwa1616 lakini si asili ya ubinadamu. Kisha alikabidhiwa matumizi yote ya ufunuo na dhihirisho la enzi yake ya kimungu. Hivyo, aliingia katika utukufu wake. Sasa anayajua yote si kama Mungu tu, bali pia kama mwanadamu na anaweza kuyafanya yote. Yuko kwa viumbe vyote na vyote ambavyo vinapatikana viko chini ya miguu yake na mikononi mwake mbinguni na duniani (Yn.13:3), jinsi anavyoshuhudia mwenyewe: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”1617 (Mt. 28:18). Pia, jinsi Mt. Paulo asemavyo, alipanda “ juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote.”1618 (Efe. 4:10). Anaweza kuutumia uwezo wake kokote kila mahali, anaweza kulifanya lolote, na anajua kila kitu.
12. Vivyo hivyo, akiwepo ataweza, hata kwa urahisi, kutugawanyia mwili
1612 Andiko la Kijerumani: ‘realiter, das ist, mit Tat und Wahrheit.’ 1613 Nakala ya mwanzo ya Andreae inayaongezea yafuatayo: “Kwa sababu hiyo asingeinuliwa zaidi baada ya kufufuka kwake, kwa maana hakulazimika kusubiri mpaka kufufuka kwake ndipo awe Mungu, au asili yake ya ubinadamu iungane pamoja na Mwana wa Mungu; lakini alikuwa Mungu na mwanadamu mara alipotungwa mimba katika tumbo la mama yake.”
1614 Toleo la ‘Union Version:’ “Alijifanya kuwa hana utukufu;” ‘Living Bible:’ “Alikubali kuyaacha yote.” Tafsiri hizi zinaifuata tafsiri ya toleo la ‘King James Version.’ Flp. 2:7 inalitumia neno linalomaanisha ‘kujimimina,’ kujifanya kuwa mtupu kabisa kutoka utukufu unaoonekana, Kiyunani κενωσις.
1615 Lk. 2:52.
1616 Flp. 2:8.
1617 Ebr. 2:8; Yn. 3:31; Mt. 28:18. 1618 Efe. 4:10.
wake wa kweli na damu yake ya kweli ambavyo vimo ndani ya Chakula Kitakatifu. Si kulingana na jinsi au sifa ya asili ya kibinadamu, bali kulingana na jinsi na sifa ya mkono wa kuume wa Mungu jinsi Dk. Luther anavyosema kulingana na mafundisho yetu ya Kikristo kwa watoto.1619 Kuwepo kwake Kristo kusieleweke kwa njia ya kidunia, hata kwa njia ya Kikapernaumu ingawa ni kweli na kiariki jinsi maneno ya agano la Kristo yanavyosema: “Huu ndio mwili wangu.”
Mafundisho, imani, na ukiri wetu haugawanyi asili za nafsi ya Kristo, jinsi Nestorio alivyofanya. Alikataa muungano binafsi, yaani, umoja wa kweli wa sifa za hizi asili mbili katika Kristo. Hivyo basi, aliigawanya nafsi kama Luther anavyoelezea katika kitabu chake ‘Sinodi na Makanisa.’1620 Sisi pia hatuzichanganyi asili hizo na sifa zao na kuwa kiini kimoja, jinsi Eutykhe1621 anavyofundisha kwa makosa. Aidha hatukatai au hatuondoi asili ya ubinadamu katika nafsi ya Kristo, au kudai kwamba, asili hizi mbili hubadilika na kuwa nyingine. Kristo ndiye na anabaki kuwa huyo huyo milele, Mungu na mwanadamu katika nafsi moja isiyogawanyika. Baada ya Utatu Mtakatifu, hili ndilo fumbo la juu kuliko yote, jinsi mtume anavyoshuhudia (1 Tim. 3:16) na katika msingi wa pekee wa faraja, uzima wetu, na wokovu wetu.
Negativa – Uhakiki Hasi
Mafundisho yaliyo kinyume na mapotovu kuhusu nafsi ya Kristo
Hadi hapa, tunayakataa na kuyatupilia mbali mafungu haya yafuatayo kama kinyume na imani yetu ya Kikristo na Neno la Mungu.
1. Mungu na mwanadamu si nafsi moja katika Kristo, bali kwamba, Mwana wa Mungu ni nafsi moja na Mwana wa mtu ni nafsi nyingine, jinsi huyo chale Nestorio, anavyodai.
2. Asili ya kimungu na ya kibinadamu huchanganywa kuwa kiini kimoja na kwamba, asili ya kibinadamu inabadilika kuwa ya kimungu, jinsi Eutykhe anavyobabaika.
3. Kuhusu asili, Kristo si Mungu wa kweli na wa milele jinsi Ario alivyoshikilia.
1619 Luther, ‘Dass diese Worte Christi (Das ist mein Leib) noch fest stehen wider die Schwarmgeister’ (kwamba maneno ya Kristo (huu ndio mwili wangu) yanasimama imara dhidi ya roho za kilokole’) mwaka wa 1527. ‘Vom Abendmahl Christi, Bekenntnis’ (‘Ukiri kuhusu Chakula cha Kristo’) mwaka wa 1528.
1620 ‘Von den Konziliis und Kirchen’ mwaka wa 1539. 1621 Eutykhes (mnamo 378-454) mwanzilishi wa mwenendo wa asili moja, yaani, asili ya kimungu ya Kristo. Mwenendo huu ulipinga mafundisho ya Katoliki ya Sinodi ya Khalkedon mwaka 451 na ulikuwa wa kuyatwaa makanisa ya Misri na Uhabeshi.
538
4. Kristo hakuwa na asili ya kweli ya ubinadamu yenye mwili na nafsi, jinsi alivyodhania Marcion.
5. Muungano binafsi unayafanya majina na vyeo kuwa vya pamoja1622 tu.
6. Kusema, “Mungu ni mwanadamu na mwanadamu ni Mungu” ni usemi tu na ni jinsi ya kusema,1623 kwa hakika,1624 uungu hauna lolote la pamoja na ubinadamu, wala ubinadamu hauna lolote la pamoja na uungu.
7. Kusema, “Mwana wa Mungu alikufa kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu au kwamba, Mwana wa Adamu amefanyika Mwenyezi”1625 ni mawasiliano ya maneno1626 tu.
8. Asili ya ubinadamu ya Kristo imefanyika vile vile, jinsi ilivyo uungu kuwa ariki isiyokuwa na mwisho, na asili hiyo inakuwako kokote jinsi ilivyo asili ya uungu kwa sababu uwezo huu na sifa hii iliyotengwa na uungu na kuwasilishwa pamoja na kuingizwa katika asili ya ubinadamu.
9. Asili ya ubinadamu imeinuliwa mintarafu ya kiini, ariki, na sifa zao za kiariki kuwa sawa na asili ya Mungu.
10. Asili ya ubinadamu ya Kristo imeenezwa kujaza kila mahali mbinguni na duniani (jambo ambalo kwa vyovyote si halali kuihesabia kwenye asili ya kimungu).
11. Sifa za asili ya ubinadamu zinammyima Kristo awepo wakati huo huo sehemu zaidi ya moja na kidogo zaidi kuwepo kila mahali kwa njia ya kimwili.1627
12. Asili ya ubinadamu ya Kristo tu ndiyo iliteswa kwa ajili yetu na kutukomboa. Mwana wa Mungu hakuwa na ushirika wowote na asili ya ubinadamu. Mateso haya hayakumuhusisha yeye kabisa.
13. Kristo yu pamoja nasi ulimwenguni katika Neno, katika sakramenti, na katika huzuni zetu zote kwa kulingana na uungu wake peke yake. Kuwepo kwake hakuhusu asili yake ya ubinadamu. Baada ya kutukomboa kwa mateso yake na kifo chake, hana lolote tena la kufanya pamoja nasi mintarafu ya asili yake ya ubinadamu.
14. Mwana wa Mungu aliyeichukua asili ya ubinadamu, baada ya kuweka
1622 Kilatini: ‘Unio personalis facit tantum communia nomina.’
1623 Kilatini: ‘Phrasis et modus loquendi.’
1624 Kilatini: ‘realiter.’
1625 Dhidi ya Zwingli, Opera II, 1, 449.
1626 Kilatini: ‘communicatio verbalis.’
1627 Calvin, Institutio IV, 17, 26, 29.
kando hali ya utumwa, hafanyi kazi zozote katika asili yake ya ubinadamu kama Mwenyezi, ila kwa uchache na mahali pale tu, ambapo asili yake ya ubinadamu inapatikana.
15. Licha ya maneno thabiti ya Kristo yasemayo, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani,”1628 na pia licha ya tamko la Mt. Paulo lisemalo, “katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu” (Kol. 2:9), asili yake ya ubinadamu haiwezi kabisa kuwa yenye uwezekano wa uenyezi na sifa zingine za asili ya kimungu.
16. Kweli, Kristo amepewa uwezo mkuu zaidi mbinguni na duniani. Yaani, mkuu zaidi kushinda malaika wote na viumbe vingine kwa jumla. Hata hivyo, hashiriki katika uenyezi wa Mungu, hajapewa hiyo. Wanaodai hivyo, hubuni pia kwamba, uwezo wa kati unaopatikana baina ya uenyezi wa Mungu na uwezo wa viumbe vingine na wanadhani kwamba, katika kuinuliwa kwa asili ya ubinadamu ya Kristo ilipokea uwezo ulio chini kuliko uenyezi wa Mungu, lakini mkubwa kuliko uwezo wa viumbe vingine.1629
17. Roho wa ubinadamu wa Kristo ana kiwango fulani cha ujuzi. Anafahamu tu mambo yale anayopaswa kuyafahamu na anayoyahitaji katika huduma yake kama hakimu.
18. Hadi sasa, Kristo bado hana ufahamu kamili wa Mungu na matendo yake yote, ingawa imeandikwa kwamba, katika Yeye zimefichwa “hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.”1630
19. Roho wa ubinadamu wa Kristo hawezi kujua lolote 38 lililokuweko tangu umilele, mambo gani yanayofanyika siku hizi kila mahali, wala yatakayofanyika katika umilele ujao.
20. Yeyote akifundisha, akifafanua vibaya, na akivuruga kwa kukufuru maneno ya Kristo, “Nimepewa mamlaka yote” (Mt. 28:18) kumaanisha kwamba, katika kufufuka na kupaa kwake, uwezo wote mbinguni na duniani ulirudishwa tena kwa Kristo mintarafu ya asili ya kimungu, kana kwamba, katika hali ya unyenyekevu alikuwa ameyaweka kando na kuyaacha kulingana na uungu wake.
Mafundisho haya si lingine lolote zaidi ya kuyapotosha maneno ya agano la Kristo na kuufungulia njia uzushi wa Kiariano uliolaaniwa, unaokataa uungu wa milele wa Kristo. Hivyo basi, tunampoteza Kristo kabisa na heri yetu ya milele ikiwa hatutakingwa kabisa na msingi imara wa Neno la Mungu na kwa imani 1628 Mt. 28:18.
1629 Kilatini: ‘media potentia.’ 1630 Kol. 2:3.
yetu ya mvuto wa Kikristo.
IX. KUSHUKA KUZIMUNI1631 KWA KRISTO
Status controversiae - Ajili ya Ubishi kuhusu fungu hili
1. Baadhi ya wanatheologia walioungana na Ukiri wa Augsburg wamebishana kuhusu fungu hili: kulingana na imani yetu ya rahisi ya Kikristo, ni lini na kwa njia gani Kristo alienda kuzimuni? Je, ilitokea kabla au baada ya kifo chake? Je, ni nafsi yake tu iliyoshuka huko, au ni uungu wake tu, au alishuka huko katika mwili na nafsi yake? Je, alishuka kwa njia ya kiroho au kimwili? Je, fungu hili linaambatana na mateso ya Kristo au na ushindi wake wa utukufu na shangwe?
2. Fungu hili la imani, sawa na lile lililotangulia, haliwezi kueleweka kwa hisia au akili zetu, ila ni lazima litambuliwe kwa imani peke yake. Kwa hiyo, ni maoni yetu ya pamoja kwamba, lisiwe shabaha ya mabishano, liaminiwe, na lifundishwe kwa urahisi wote jinsi Dk. Luther, mwenye kumbukumbu ya heri, alivyofundisha katika mahubiri yake huko Torgau mwaka wa 1533. Anakataa maswali yote yasiyokuwa na faida, yasiyohitajika, na anawaonya Wakristo wote kuifuata imani ya mvuto.1632
3. Inatosha kujua kwamba, Kristo alishuka kuzimuni, aliiharibu kuzimu kwa wote wanaoamini, na amewakomboa kutoka katika mamlaka ya kifo, ya Ibilisi, na ya laana ya milele ya mapatilizo ya kuzimu. Lakini tunaliahirisha hili swali mpaka ulimwengu ujao kwa njia gani yote haya yalivyofanyika. Basi, ambapo tutafunuliwa mafumbo mengine mengi, ambayo tuliyaamini tu kwa imani rahisi kuhusu fumbo hili, kwa sababu hatukuweza kuyaelewa katika maisha haya kwa akili na ufahamu wetu mpofu.
1631 Kijerumani: ‘Höllenfahrt;’ Kilatini: ‘Descensus ad inferos.’ 1632 WA, 37,62-67.
X.
MATUMIZI
YA KANISA YAITWAYO MAMBO YASIYOKUWA YA LAZIMA KUYAJALI1633
Mabishano yametokea pia miongoni mwa wanatheologia wanaoukiri Ukiri wa Augsburg kuhusu kaida au matumizi ya Kanisa yasiyokuwa na amri wala katazo la Neno la Mungu, bali yaliyoingizwa kanisani kwa ajili ya utaratibu bora na ustawi wa jumla.
Status controversiae – Ajili ya Ubishi
Sababu ya mabishano imekuwa: Je, mintarafu ya ukiri na wakati wa mateso, inawezekana tena kupokea, chini ya ukandamizaji na madai ya wapinzani wa Injili, baadhi ya kaida zilizoachwa ambazo zenyewe ni mambo yasiyokuwa ya lazima kuyajali? Yaani, mambo ambayo hayana amri au katazo la Mungu? Je, tungeweza kuafikiana na wapinzani kuhusu kaida na mambo ambayo si lazima kuyajali? Hivyo, wapinzani, kama maadui wa Injili, watakubali kupatanishwa nasi kuhusu mafundisho? Sehemu moja inasema ‘ndiyo’ na sehemu nyingine inasema ‘la’.
Affirmativa - Makubaliano
Mafundisho sahihi, ya kweli, na ukiri kuhusu fungu hili
1. Ili kuyahitimisha mabishano haya, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwa maafikiano kwamba, kaida au matumizi ya Kanisa ambayo hayajaamrishwa wala kukatazwa katika Neno la Mungu, bali yaliyoasisiwa tu kwa ajili ya ustawi wa hadhara na utaratibu bora, yenyewe hayawi ibada. “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” (Mt. 15:9).
2. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, makanisa ya Mungu1634 yana haki kila wakati na kila mahala kuzibadilisha kaida hizo, kulingana na faida na ustawi mkuu wa makanisa ya Mungu.
3. Lakini katika jambo hili, upuuzi wote na machukizo hayana budi kuepukwa. Hasa walio dhaifu katika imani waangaliwe kwa huruma.1635
4. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, wakati wa mateso ambapo ukiri wa wazi wa imani unahitajika, haturuhusiwi kumwepuka adui hata katika
1633 ‘Adiaphora,’ Kijerumani: ‘Mitteldinge’ (‘mambo ya kati’).
1634 Kulingana na andiko la Kilatini. Kijerumani, ‘Geimende’ (‘jumuiya’).
1635 1 Kor. 8:9-13; Rum. 14:13 n.k.
mambo ambayo si lazima kuyajali, jinsi Mtume Paulo anavyoandika: “Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.” “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi?” “. . . ambao hata saa moja hatukujitia chini yao, ili kwamba kweli ya Injili ikae pamoja nanyi.”1636 Hali ya namna hiyo haihusu jambo ambalo si lazima kulijali, bali inahusu kabisa ukweli wa Injili na uhuru wa Kikristo. Aidha tutaithibitisha ibada ya miungu mingine hadharani au kuwaimarisha wale walio dhaifu katika imani yao. Katika hali hiyo, tusiepuke hata kidogo, bali inatupaswa kushuhudia wazi ukiri wetu na kuwa tayari kwa mateso yatakayotokea kutoka kwa Mungu au akiruhusu maadui wa Neno lake kutuumiza.
5. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, hakuna Kanisa linalopaswa kulilaani lingine kwa sababu kwamba, kuna kaida chache au nyingi zaidi za nje ambazo hazijaamriwa na Mungu, ikiwa yanaafikiana katika kila fungu la mafundisho na matumizi ya Sakramenti Takatifu.1637 Kauli inayotambulika husema: “Kutokubaliana kuhusu kufunga hakuwezi kuharibu makubaliano katika imani.”1638
Uhakiki Hasi
Fundisho la uzushi1639
Kwa hiyo basi, tunakataa na kulaani mafundisho yafuatayo kama uzushi na yaliyo kinyume cha Neno la Mungu kabisa:
1. Maagizo na amri za kibinadamu zinapaswa kutambuliwa katika Kanisa kama ibada ya kimungu1640 au sehemu yake.
2. Wakati kaida, maagizo, na amri za jinsi hiyo zimewekwa kwa nguvu katika Kanisa la Mungu kama mambo ya lazima na kukiuka uhuru wa Kikristo kuhusu mambo ya nje.
3. Wakati wa mateso ambapo ukiri wa hadhara unahitajika,inawezekana
1636 Gal. 5:1; 2 Kor. 6:14; Gal. 2:5.
1637 Ukiri wa Augsburgu, Fungu la 7.
1638 ‘Dissonantia ieuinii non dissolvit consonatiam fidei;’ Ireneo kwa Askofu Viktor wa Roma kulingana na Eusebio ‘Historia ya Kanisa’ V, 24, 13.
1639 Msimamo wa kweli wa Walutheri (‘Gnesiolutheraner’) dhidi ya Melanchthon na wanatheologia wake katika kitala cha Mtaala Mchaguzi wa Sachsen, hasa katika makubaliano ya ‘Augsburg Interim’ (‘Hati ya Muda ya Augsburg’) mwaka wa 1548 baina ya Walutheri na wafuasi wa Papa wa Roma.
1640 Kulingana na Andiko la Kilatini: ‘cultus Dei.’ Neno linalomaanisha ‘ibada’ katika Kijerumani, ‘Gottesdienst’ (‘huduma ya Mungu’) tayari lina maana hii ya ‘kimungu.’
543
kufanya ridhaa au kufikia maelewano na maadui wa Injili takatifu katika mambo ambayo si lazima kuyajali au kaida za dini. (Mambo haya yanadhoofisha ukweli).
4. Kaida za nje na mambo mengine ambayo si lazima kuyajali hutolewa kwa kusudi hili kwamba, Kanisa la Mungu haliwezi kuwa huru kwa kuifuata desturi moja au baadhi yazo kama jinsi Kanisa linavyohitaji faida katika kila fursa.
XI. MAJALIWA YA MILELE NA UCHAGUZI WA MUNGU
Hakuna mfarakano wa hadhara ulioendelea miongoni mwa wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg kuhusu fungu hili. Fungu hili ndilo lenye faraja sana ilimradi linafafanuliwa kwa usahihi. Kwa hiyo ili kuuepuka mfarakano mkubwa mbeleni, tulitaka kuyaingiza maelezo yake hapo.
Affirmativa - Makubaliano
1. Kwanza kabisa, tofauti kati ya utambuzi wa mbele1641 na Majaliwa,1642 yaani, uchaguzi wa milele wa Mungu havina budi kuangaliwa kwa umakini.
2. Utambuzi wa mbele wa Mungu si lingine zaidi ya kwamba, Mungu huyajua yote kabla hayajatokea jinsi ilivyoandikwa, “Lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho” (Dan. 2:28).
3. Ufahamu huu wa mbele wa Mungu unanena sawa juu ya wacha Mungu na watu wabaya. Hata hivyo, wenyewe si chanzo cha ubaya au makosa mengine mabaya. Chanzo chao ni Ibilisi pamoja na nia mbaya ya wanadamu iliyopotoka. Ufahamu huu wa mbele si sababu ya maangamizi ya watu wabaya, bali wao wenyewe ndio wenye lawama. Ufahamu wa mbele au Majaliwa ya Mungu inaudumisha tu utaratibu bora katika mambo mabaya na kuyawekea mipaka kwa muda wake ili kwamba licha ya ubaya wake wote, hayana budi kueneza wokovu wa wateule wake.
4. Majaliwa au uchaguzi wa milele na wa kipekee wa Mungu unawahusu watoto wacha Mungu na wapendwa wake na kuwa chanzo cha wokovu wao. Majaliwa huutekeleza wokovu na mambo yote ambayo huhusika nao. Katika msingi huo, wokovu wetu umeimarishwa zaidi hata “milango ya kuzimu haitalishinda.” 1643
5. Majaliwa haya yasichunguzwe katika shuri ya siri ya Mungu, bali hayana 1641 Kilatini: ‘praescientia’). 1642 Kilatini: ‘praedestinatio.’ 1643 Yn. 10:28; Mt. 16:18.
544
budi kutafutwa katika Neno lake ambamo ameyafunua.
6. Lakini Neno la Mungu hutuongoza kwenda kwake Kristo, ambaye ndiye ‘Kitabu cha Uzima.’1644 ambamo wote watakaookolewa milele wameandikwa na kuteuliwa jinsi ilivyoandikwa: “. . . kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.”1645
7. Huyu Kristo mwenyewe anawaita kwake wakosaji wote na huwaahidi kiburudisho. Anatamani sana kwamba, watu wote waje kwake na waruhusu kusaidiwa1646 anapojitoa mwenyewe katika Neno lake. Mapenzi yake ni kwamba, walisikie Neno na wasiyazibe masikio yao au kulidharau. Licha ya hayo, anaahidi nguvu na utendaji wa Roho Mtakatifu , msaada wa kimungu kwa ajili ya uthabiti na uzima wa milele.
8. Kwa hiyo, tusiuhukumu huu uchaguzi wetu kwa uzima wa milele aidha kulingana na akili au sheria ya Mungu. Aidha hii inaweza kutupeleka sisi katika maisha makali na yenye fujo ya Waepikureo, au katika hali ya kuwafanya watu wafe moyo na kuyaamsha mawazo hatari katika mioyo yao. Kadiri watu wanavyozifuata akili zao, hawawezi kuzikwepa fikira za jinsi hiyo: “Kama Mungu amenichagua kwa wokovu sitaweza kuadhibiwa milele na kufanya nitakavyo.”
Au: “Kama sijachaguliwa kwa uzima wa milele, zuri lolote nilifanyalo haliwi la manufaa; kila kitu ni bure katika hali hiyo.”
9. Hatuna budi kujifunza mafundisho haya kuhusu Kristo katika Injili takatifu peke yake, ambayo hushuhudia wazi kwamba: “Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.”1647 Mungu hataki mtu yeyote apotee,1648 bali kwamba, kila mmoja apate kuongoka kwa toba na kumwamini Bwana Yesu Kristo.1649
10. Mafundisho haya ni ya manufaa na yenye faraja kubwa kwa mtu yeyote anayehusika na mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa na huchunguza utaratibu ambao Mt. Paulo huufuata katika Waraka kwa Warumi. Hapo, kwanza, anawaelekeza watu kutubu, kutambua dhambi zao, kumwamini Kristo, na kumtii Mungu. Basi, baada ya hayo, anaizungumzia siri ya uchaguzi wa milele wa Mungu.
11. Aya hii, “waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache,”1650 haimaanishi
1644 Flp. 4:3; Ufu. 3:5; 20:15. 1645 Efe. 1:4.
1646 Mt. 9:2, 9, 22, 29, 35, 37; 11:28.
1647 Rum. 11:32.
1648 Eze. 33:11; 18:23. 1649 1 Tim. 2:6; 1 Yoh. 2:2. 1650 Mt. 20:1-16; 22:14.
545
kwamba, Mungu hataki kumwokoa kila mmoja. Sababu ya hukumu ni kwamba, aidha watu wengi hawalisikilizi Neno la Mungu kabisa, ila kwa makusudi wanalidharau na kufunga masikio yao na mioyo yao. Kwa hiyo, wao huzuia njia ya kawaida ya Roho Mtakatifu ili asiweze kufanya kazi yake ndani yao. Wakilisikiliza Neno watalipeperusha katika upepo bila kulijali. Kosa halipo kwa Mungu wala katika uchaguzi wake, bali katika ufisadi wao.1651
12. Mkristo ajihusishe mwenyewe na fundisho la uchaguzi wa milele wa Mungu pekee maadamu limefunuliwa katika Neno la Mungu, ambalo hutuonyesha Kristo kama ‘Kitabu cha Uzima.’ Kwa njia ya mahubiri ya Injili takatifu, Kristo anatufungulia na kutufunulia kitabu hiki, kama ilivyoandikwa:
“Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita.”1652 Katika Yeye, inatubidi kuutafuta uchaguzi wa milele wa Baba ambaye aliamua katika baraza lake la milele kwamba, hatamwokoa hata mmoja isipokuwa wale ambao wanamfahamu Mwana wake, Yesu Kristo, na huamini kweli katika Yeye na kuyakataa mawazo mengine yote yasiyotoka kwa Mungu, bali yanayoongozwa na adui mwovu. Anajaribu kutudhoofisha sisi au kuturubuni kabisa kutoka katika faraja tamu ya mafundisho haya. Yaani, kwamba, tunajua kuwa tumekwisha kuchaguliwa kwa uzima wa milele kwa neema safi katika Kristo na bila ustahili wetu sisi, na kwamba, hapana yeyote anayeweza kutunyakua kutoka katika mikono yake. Bwana hakutuhakikishia uchaguzi huu wa neema kwa maneno matupu, bali kwa kiapo chake na kwa muhuri wa sakramenti takatifu. Inatubidi kuzikumbuka hizo ili kujikumbusha na kujifariji wenyewe katika dhiki zetu kuu, na hivyo kuizima mishale ya moto ya Ibilisi.
13. Zaidi ya hayo, inatubidi kuishi kwa bidii zaidi kulingana na mapenzi ya Mungu na “kuhakikisha wito wetu,” jinsi Mt. Petro asemavyo.1653 Hasa tunahitajika kulishika Neno lililofunuliwa ambalo haliwezi na halitaweza kutudanganya.
14. Maelezo haya mafupi ya mafundisho ya uchaguzi wa milele wa Mungu, humpa Mungu utukufu wake kwa ukamilifu na utimilifu. Ni yeye peke yake anayetuokoa sisi kwa neema yake safi tu bila ustahili wetu wowote kulingana na lengo la mapenzi yake.1654 Zaidi ya hayo, mafundisho haya kamwe hayawezi kumpa yeyote nafasi, aidha ya kukata tamaa au kuyaongoza maisha bila kujali na yasiyomcha Mungu.
1651 2 Pet. 2:2 n.k.; Lk. 11: 25,49; Ebr. 12:25.
1652 Rum. 8:30.
1653 2 Pet. 1:10. 1654 Efe. 1:11.
Antithesis - Uhakiki Hasi
Mafundisho ya uzushi kuhusu fungu hili
Tunaamini na tunakiri kwamba, kama watu ambao huyatoa 16 mafundisho ya uchaguzi wa neema ya Mungu kwa uzima wa milele, kwa njia ambayo Wakristo wenye huzuni hawawezi kupata faraja kwayo, bali wanaingizwa katika mashaka na kukata tamaa, au kwa njia ambayo wasiotubu wanatiwa nguvu katika ukaidi wao, hawahubiri mafundisho haya kulingana na Neno na mapenzi ya Mungu bali wao huzifuata akili zao na uchochezi wa Ibilisi aliyelaaniwa kabisa. Kama vile Mt. Paulo anavyoshuhudia kwamba: “yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufindisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.”1655 Kwa hiyo, tunayakataa makosa yafuatayo:
1. Mafundisho kwamba, Mungu hataki watu wote watubu na kuiamini
Injili.1656
2. Kwamba, Mungu akituita kuja kwake, hamaanishi kwa hakika kwamba, watu wote waje kwake.
3. Kwamba, Mungu hataki kila mtu aokolewe, bali kwamba, kwa nia, lengo, na mapenzi ya uamuzi wake tu, pasipo kuangalia dhambi zao, Mungu ameazimia tangu awali watu fulani wahukumiwe ili wasiweze kuokolewa.1657
4. Kwamba, sababu na chanzo cha uchaguzi wa Mungu si huruma ya Mungu tu na ustahili mtakatifu mno wa Kristo, bali kwamba, ndani yetu kuna sababu ya kuchaguliwa na Mungu kwa uzima wa milele.
Haya yote ni mafundisho ya kufuru na ya kutisha ya uzushi, kwani huwapokonya Wakristo faraja yao yote ambayo wanayo katika Injili Takatifu na katika matumizi ya Sakramenti Takatifu. Hivyo, yasivumiliwe katika Kanisa la Mungu.
Haya ndiyo maelezo mafupi na rahisi ya maandiko mbalimbali ambayo, kwa muda, wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg wamekuwa wakiyajadili na kuyafundisha kwa mvutano.
Kila Mkristo wa kawaida anaweza kuelewa wazi kutokana na mwelekeo wa Neno la Mungu na katekisimo, lipi ni kweli na lipi ni uongo, kwani hatujaweka
1655 Rum. 15:4.
1656 Hasa dhidi ya Jean Calvin, Inst. III, 21, 5.
1657 Mafundisho ya Calvin ya Majaliwa maradufu yaliyoandaliwa kwa ukamilifu zaidi na Theodoro Beza (1519-1605) mfuasi wa Calvin huko Geneva. ‘Confessio Gallica’ (Ukiri wa Kifaransa) mwaka wa 1561, XII.
mafundisho safi tu, bali tumeonyesha pia mafundisho ya uzushi yanayopinga mafundisho haya safi. Kwa hiyo basi, mabishano mabaya yametatuliwa kabisa.
Mungu Mwenyezi, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo atujalie neema ya Roho Mtakatifu wake kwamba, sisi sote tuweze kuwa na moyo mmoja katika yeye na kudumu katika mwafaka huu wa Kikristo na umpendezao Mungu. Amina.
XII. MADHEHEBU MENGINE NA MAFARAKANO AMBAYO HAYAJAUKIRI KAMWE UKIRI WA AUGSBURG
Katika maelezo yaliyotangulia hatukutaja Wakristo wa mafarakano fulani wanaofundisha dhidi Imani ya Kikristo na ukiri. Ili wasiunganishwe nasi kimya mwishoni kabisa, hapa tunataka kutaja mafungu ambamo wanakosea na kupingana na imani yetu.
Mafungu ya uasi ya Waanabaptisti1658
Waanabaptisti wamegawanyika katika vikundi vingi ambavyo baadhi yavyo huyatetea makosa mengi na vingine huyatetea machache zaidi. Lakini kwa jumla basi, wao huyafundisha mafundisho ambayo hayawezi kuvumiliwa aidha kanisani, serikalini, katika madaraka ya dunia, au katika uchumi.1659
Mafungu ambayo hayawezi kuvumiliwa kanisani
1. Kristo hakutwaa mwili na damu yake kutoka kwa Bikira Mariamu, bali alikuja navyo kutoka mbinguni.
2. Kristo si Mungu kweli, bali alikuwa tu na karama zaidi za Roho 4 Mtakatifu kuliko mtu mtakatifu mwingine yeyote.
3. Mbele za Mungu, haki kwetu haitegemei kabisa upekee wa ustahili wa Kristo, bali katika kufanywa kwetu upya na katika uchaji wetu, yaani, mwenendo wetu. Kwa sehemu kubwa, uchaji wa namna hiyo ni maisha maalumu ya kiroho yaliyochaguliwa nasi wenyewe ambayo kimsingi si lingine lolote, bali aina mpya ya umonaki.
4. Mbele za Mungu, watoto wasiobatizwa si wenye dhambi ila ni wenye haki
1658 Jina la madhehebu mbalimbali yaliyokataa Ubatizo wa watoto wachanga na kwa hiyo, waliwabatiza Wakristo mara ya pili. 1659 Kilatini: ‘Ecclesia, politia, oeconomia.’
548
na wasiokuwa na hatia. Bila welekevu, hawahitaji Ubatizo bali wanaokolewa bila huo kulingana na mtazamo huu. Kwa hiyo, wanayakataa mafundisho yote ya dhambi ya asili na kila kitu kinachohusika.
5. Kwamba, watoto wasibatizwe kabla ya kuwa na welekevu na kabla ya kuweza kuikiri imani yao binafsi.
6. Watoto wa wazazi Wakristo na wenye imani ni watakatifu na ni watoto wa Mungu kabla na bila Ubatizo. Kwa hiyo, wao hawathamini sana Ubatizo wa watoto wala hawauhitaji licha ya Neno la ahadi ya Mungu linalohusu wale ambao hawalidharau, bali hulishika agano lake (Mwa. 17:4-8, 19-21).
7. Usharika si wa Kikristo kweli kama wakosaji bado wanapatikana ndani yake.
8. Wakristo hawapaswi kulisikiliza hubiri hata moja au kuzuru mahekalu ambayo misa za wafuasi wa Papa zilisomwa na kusherehekewa awali.
9. Wakristo wasihusike na watumishi wa Kanisa wanaohubiri Injili kulingana na Ukiri wa Augsburg na kuwaonya watu kwa ajili ya mahubiri na makosa ya Wanabaptisti. Watu hawapaswi kuwatumikia au kuwafanyia kazi katika njia iwayo yote, bali wanapaswa kuwakimbia na kuwakwepa kama wapotoshaji wa Neno la Mungu.
Mafungu yasiyovumiliwa katika madaraka ya dunia
1. Wakati wa Agano Jipya, mamlaka kuu si cheo kimpendezacho Mungu.
2. Hakuna Mkristo anayeweza kutumika na kufanya kazi katika huduma yoyote ya mamlaka kuu kwa dhamiri njema.
3. Mkristo hawezi kuwapinga watu waovu katika huduma ya mamlaka kuu bila kuivunja dhamiri yake katika kadhia za kufaa. Kadhalika, raia hawapaswi kuiita mamlaka kuu kwa wao kuhitaji msaada na ulinzi ambayo hata hivyo, wameyapokea mamlaka kutoka kwa Mungu kwa shabaha hii.
4. Mkristo hawezi kula kiapo kwa dhamiri njema wala kutoa yamini ya uaminifu kwa mtawala wake au kwa mamlaka kuu.
5. Mamlaka kuu haiwezi kuwa na dhamiri njema ya kuwahukumia wahalifu kifo wakati wa Agano Jipya.
Mafungu yasiyovumiliwa katika uchumi na jamii
1. Mkristo hawezi kumiliki mali binafsi kwa dhamiri njema, bali inambidi kutoa kila kitu kwa jamii.
2. Mkristo hawezi kuwa na dhamiri njema kwa mtunza hoteli, mfanyabiashara au mtengeneza silaha.
3. Mume na mke wanapaswa kutalikiana kwa sababu ya imani. Wanapaswa kuachana na kuoa au kuolewa na mwingine aliye na imani hiyo hiyo.
Makosa ya wafuasi wa Schwenkeld1660
1. Wote wasemao kwamba, mwili wa Kristo uliumbwa, hawana ufahamu wa kweli wa Kristo kama mtawala na mfalme wa mbinguni.
2. Mwili wa Kristo ulizitwaa sifa zote za kimungu katika utukufu wake hata kuwa Kristo ni sawa kabisa na Baba na Neno kuhusu tabaka na hali ya ariki yake mintarafu ya ubinadamu wake. Yeye ndiye aliye na mamlaka, nguvu, enzi, na utukufu huo huo. Ariki, sifa, nia, na utukufu wa asili zote mbili ni huo huo wa Kristo. Mwili wa Kristo pia unahusika na ariki ya Utatu Mtakatifu.
3. Huduma ya Kanisa na Neno lililohubiriwa na kusikilizwa si njia ambayo kwayo, Mungu Roho Mtakatifu anawafundisha watu na kuumba ndani yao ufahamu wa Kristo uokoao, wongofu, toba, imani, na utiifu mpya.
4. Bwana Mungu hayatumii maji ya Ubatizo kuwa muhuri wa utoto wetu na njia ya kuzaliwa mara ya pili.
5. Kwamba, mkate na divai katika Chakula Kitakatifu si njia ambayo kwayo, Kristo anatoa mwili na damu yake.
6. Mkristo aliyezaliwa upya kweli, kwa Roho wa Mungu, anaweza kuwa mkamilifu katika kutunza na kutimiza sheria ya Mungu katika maisha haya.
7. Usharika ambao watu hawatengwi na Kanisa na adhabu kubwa ya kutengwa na Kanisa haitumiki hadharani, si usharika wa kweli wa Kikristo.
8. Mtumishi wa Kanisa1661 hawezi kufundisha kwa faida au kutunza sakramenti za kweli na halisi isipokuwa yeye mwenyewe awe amezaliwa tena kweli na awe mwenye haki na mchaji.
1660 Caspar Schwenckfeld (1490-1561) mchaji wa fumbo na mwanatheologia aliyewapinga Walutheri vikali kuhusu mafundisho ya Ekaristi na Kristologia. 1661 Kijerumani: ‘Diener der Kirche;’ Kilatini: ‘Minister ecclesiae.’
550
Uzushi wa Waariano wapya1662
Kwa mujibu wa kiini na asili yake, Kristo si Mungu wa kweli mwenye ariki hiyo hiyo ya milele na Mungu Baba na Roho Mtakatifu, bali ndiye aliyeumbwa mwenye enzi ya kimungu chini na kando ya Mungu Baba.
Kosa la Wapinga Utatu1663
Hili ndilo dhehebu jipya kabisa lisilojulikana awali katika Ukristo. Wao huamini, hufundisha, na hukiri kwamba, hakuna ariki moja ya kipekee na ya milele ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Jinsi Mungu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu walivyo nafsi tatu tofauti, hivyo kila nafsi ina ariki yake tofauti ya kimungu mbali na nafsi zingine za Mungu. Hata hivyo, nafsi hizi tatu ni sawa kuhusiana na uweza, hekima, enzi, na utukufu, jinsi watu watatu walivyo tofauti na wanavyohitilafiana mmoja kwa mwingine kuhusu ariki zao. Baadhi hushikilia kwamba, nafsi hizo tatu si sawa mintarafu ya ariki na nafsi bali Baba peke yake ndiye Mungu wa haki na wa kweli.
Mafungu haya, yote yanayofanana nayo, makosa yao, na yanayotokana nayo, tunayakataa na kuyalaani kama mafundisho yasiyokuwa halisi, ya uongo, na uzushi unaopinga kabisa Neno la Mungu, kiri tatu kuu, Ukiri wa Augsburg, Utetezi, Mafungu ya Smalkaldi, na Katekisimo za Luther. Wakristo wachaji wote wa cheo cha juu na chini hawana budi kujiepusha na haya ikiwa wanapenda sana wokovu na heri ya nafsi zao.
Haya ndiyo mafundisho, imani, na ukiri wetu sote jinsi tutakavyotoa hesabu yake siku ya mwisho mbele za hakimu mwenye haki, yaani, Bwana wetu Yesu Kristo. Sisi hatutaki kusema au kuandika kwa siri, wala hadharani kitu chochote kinyume chake, bali tunakusudia kukaa nao kwa neema ya Mungu. Tumetia sahihi kwa mikono yetu wenyewe kwa fikira kamili katika hofu ya Mungu na maombezi kwake.
Berg, Mei 29, 1577.
Dk. Yakobo Andreae aliitia sahihi yake
Dk. Nikolao Selnecker aliitia sahihi yake
Dk. Andrea Muskulo aliitia sahihi yake
Dk. Kristoforo Kornero aliitia sahihi yake
Daudi Khytreo
k.Martin Chemnitz
1662 Waliokataa Utatu Mtakatifu, wapinga Utatu. 1663 Kijerumani: ‘Antitrinitarier;’ Kilatini: ‘Antitrinitarii.’
SEHEMU YA PILI: SOLIDA DECLARATIOTAMKO THABITI
Takriri na maelezo ya kawaida, dhahiri, sahihi, na makataa ya baadhi ya mafungu ya Ukiri wa Augsburg, Baadhi ya wanatheologia wamejadiliana kwa muda fulani kuhusu ufafanuzi wa mafungu haya ambayo yanatatuliwa na kukubaliwa kwa Neno la Mungu na kwa mujibu wa yaliyomo makuu ya mafundisho yetu ya Kikristo
1. Kwa neema na huruma maalumu ya Mwenyezi Mungu, mafundisho kuhusu mafungu makuu ya imani yetu ya Kikristo ambayo yalifichwa kwa njia ya kuogofya sana na mafundisho na maagizo ya kibinadamu chini ya upapa, kwa mara nyingine yalielezwa wazi kwa msingi wa Neno la Mungu na kuchujwa na Dk. Luther kwa kumbukumbu ya heri na takatifu. Aliukashifu uzushi, matumizi mabaya, na ibada za miungu mingine. 2. Hata hivyo, wapinzani, waliyaelewa matengenezo haya safi kama mafundisho mapya na waliyashtaki kuwa kinyume kabisa na Neno la Mungu na utaratibu wa Kikristo kabisa. Wakayashambulia kwa ukali matengenezo haya na wakaibua visingizio visivyokuwa na mwisho na uchongezi dhidi yavyo. 3. Kwa hiyo basi, watawala wachaguzi,1664 watawala wengine, vyeo vya heshima vya dola ambavyo tayari vilikubali mafundisho safi ya Injili Takatifu na kuyatengeneza makanisa yao kulingana na Neno la Mungu, waliagiza maandalizi ya Ukiri wa Kikristo kwa msingi wa Neno la Mungu na kuupeleka mbele ya Kaisari Karolo V wakati wa Baraza la Augsburg mwaka wa 1530. Waliutoa ukiri wao wa Kikristo wa wazi na usiokuwa na sahaka, wakiielezea imani na mafundisho ya Makanisa ya Kiinjili ya Kikristo kuhusu mafungu makuu, hasa ambayo yalikuwa katika mabishano kati yao na wafuasi wa Papa. Maadui wakauchukua mtazamo wa uadui katika Ukiri huu. Hata hivyo, Mungu ashukuriwe kwani, mpaka leo, haujakanushwa wala kuangushwa.
4. Kwa hiyo basi, sisi tunakiri tena kwa moyo wote ufuasi wetu wa Ukiri wa Kikristo wa Augsburg uliojengwa kwa njia thabiti sana juu ya Neno la Mungu. Tunabaki kuwa waaminifu kwa maneno yake wazi, dhahiri, na safi. Tunaukubali ukiri huu kuwa imani1665 halisi ya Kikristo ambayo Wakristo wote wa kweli wanapaswa kuipokea wakati huo baada ya Neno la Mungu. Nyakati za kale, imani au kiri za Kikristo ziliundwa katika Kanisa la Mungu wakati mabishano mabaya, walimu safi, na wasikilizaji wao walikiri imani hizi kwa moyo na kwa
1664 Watawala wachaguzi (Kijerumani, ‘Kurfürst’) walimchagua kaisari wa dola.
1665 Andiko la Kijerumani na Kilatini: ‘Symbolum.’ Istilahi hii ni sawa na istilahi ‘ukiri,’ kama ‘Symbolum apostolicum,’ ‘Imani ya Mitume.’
kinywa. 5. Basi, kwa neema ya Mwenyezi, tunakusudia kukiri huu ukiri wetu wa Kikristo mpaka mwisho jinsi ulivyotolewa kwa Kaisari Karolo V mwaka wa 1530.1666 Sisi hatukusudii kutoka katika ukiri uliotajwa hata kidogo wala katika andiko hili wala la baadaye. Hatuna shabaha yoyote pia ya kuutoa ukiri mwingine mpya.
6. Japo mafundisho ya Kikristo katika huu ukiri yamebaki bila changamoto ya kiutendaji, isipokuwa kwa upande wa wafuasi wa Papa, hata hivyo, inatubidi kukubali kwamba, baadhi ya wanatheologia wamepitia mafungu fulani muhimu na yenye maana sana, kwa sababu aidha wameshindwa kuelewa maana yao ya kweli au hawakudumu kwayo. Baadhi yao, walikuwa wakitoa tafsiri ya uongo kwa maandiko haya walipothubutu kujigamba kukubaliana na kuutegemea Ukiri wa Augsburg. 7. Hali hii ilisababisha mizozo mizito na hatari katika Makanisa ya kweli ya Kiinjili, jinsi ilivyokuwa wakati wa mitume watakatifu. Makosa ya kuogofya sana yalijitokeza miongoni mwa waliojifanya kuwa Wakristo na wakajitukuza katika mafundisho ya Kristo. Wengine walitaka kuwa wenye haki na kuokolewa kwa matendo ya sheria (Mdo. 15:1-5,10,24). Baadhi walikanusha ufufuo wa wafu (1 Kor. 15:12), na hata wengine walikataa kwamba, Kristo si Mungu wa milele1667 kweli. Mitume watakatifu walilazimika kwa nguvu zote kuwashutumu vikali hawa wote kwa mahubiri na maandiko yao. Japo kulikuwa na mabishano makali kwa sababu makosa haya makubwa mno yaliwaudhi sana wakati ule, wasioamini na waumini dhaifu pia. 8. Kadhalika, sasa, maadui wetu, yaani, wafuasi wa Papa, wanafurahia sana mizozo iliyotokea miongoni mwetu tulio wenye tumaini duni lisilokuwa la Kikristo kwamba, mikwaruzo hii hatimaye inaelekea kwenye maangamizi ya mafundisho ya kweli. Walio dhaifu katika imani, kwa upande mwingine, wataudhiwa hata kuwa na mashaka kama mafundisho ya kweli yanaweza kupatikana miongoni mwetu pamoja na migawanyiko ya jinsi hiyo. Wengine husita wasijue waunge mkono kundi lipi kati ya makundi yanayobishana kwa ajili ya mafungu ya imani yanayojadiliwa. 9. Basi, kwa kuwa mabishano haya si jinsi wengine wanavyoweza kufikiri kwamba, ni sintofahamu tu au upinzani kuhusu maneno, jinsi kikundi kimoja kwa kudhania, hakikuelewa shabaha ya kingine hivi kwamba ushindani ulitokea kwa baadhi ya maneno maalumu yasiyokuwa na maana sana. Kinyume chake, mabishano haya yanahusiana na mambo mazito na muhimu, ni ya asili kiasi kwamba, maoni ya kundi linaloasi hayakuweza kuvumiliwa katika Kanisa la Mungu, na akali zaidi, 1666 Rejea mabadiliko ya Philipp Melanchthon ya mwaka wa 1541. Toleo hili jipya liliitwa ‘Ukiri wa Augsburg Uliobadilika’ (‘Confessio Augustana variata’). Toleo la asili, lililoendelea kutumiwa katika Makanisa ya Kilutheri mpaka sasa linaitwa ‘Ukiri wa Augsburg Usiobadilika’ (‘Confessio Augustana invariata’). 1667 Labda waandishi walikuwa wakifikiria kuhusu Yud. 4:8; 2 Pet. 2:1-10; Kol. 1 na 2; na 1 Tim. 2:5.
553
hayawezi kutetewa wala kusamehewa.
10. Kwa hiyo, muhimu kabisa ni kwamba, mafungu yanayobishaniwa yafafanuliwe kwa Neno la Mungu na kwa maandiko yanayojulikana kuwa ya kuaminika ili kila mmoja mwenye maelewano bora ya Kikristo aweze kuona ni wazo lipi linaungana na Neno la Mungu, katika mambo yanayobishaniwa. Yaani, Ukiri wa Kikristo wa Augsburg, ili Wakristo wema wanaohangaikia ukweli wapate kujua jinsi ya kujilinda na kujihifadhi wenyewe dhidi ya makosa, na uzushi ambao umeingia miongoni mwetu.
MUHTASARI WA MAFUNDISHO, MSINGI, KAIDA, NA KANUNI
jinsi ya kuyahukumu mafundisho yote kwa Neno la Mungu na lazima makosa yote yaelezwe na kutatuliwa kwa njia ya Kikristo Umoja wa kimsingi na wa kudumu katika Kanisa unalazimisha 1 kuwa na ufupisho makini na muundo, uliohakikiwa kwa pamoja, ambao mafundisho yaliyojumlishwa na kuvutwa kutoka katika Neno la Mungu yanaungamwa na makanisa ya dini halisi ya Kikristo. Kwa lengo hilo hilo, Kanisa la Kale lilikuwa na miundo yao maalumu ya imani1668 wakati wote. Muundo huu wa imani hauwezi kutegemeza maandiko ya mtu yeyote binafsi tu, bali vitabu vya jinsi hiyo vilivyopata kuandikwa, kuthibitishwa, na kupokelewa na makanisa ambayo yalikiri mafundisho na dini hiyo hiyo. Sisi pia tumetamka pamoja kwa mapatano yatokayo mioyoni mwetu na kwa midomo yetu kwamba, hatutataka kuutunga wala kuupokea ukiri maalumu mpya wa imani yetu, bali tunakiri ufuasi wetu wa maandiko yote ya hadhara na yanayojulikana, yanayokubaliwa, na yanayotumiwa kama miundo ya imani katika makanisa yote ya Ukiri wa Augsburg jinsi kiri za watu wote na wakati wote hadi mabishano kadhaa yalitokea miongoni mwa wafuasi wa Ukiri wa Augsburg. Yaani, wakati mafungu yote ya mafundisho safi ya Neno la Mungu yalishikwa kwa maafikiano jinsi Dk. Luther mwenye kumbukumbu yenye heri alivyoyafafanua.
1. Kwanza kabisa, maandiko ya unabii na ya kimitume ya Agano la Kale na Agano Jipya, kama chemchemi safi na wazi ya Israeli, ambayo ndiyo kanuni pekee ya kweli, ambayo kwayo, walimu na mafundisho yote hawana budi kupimwa na kutathminiwa.
1668 Andiko la Kijerumani na la Kilatini: ‘Symbolum.’
2. Tangu nyakati za kale, mafundisho ya kweli ya Kikristo kama yalivyoeleweka kwa usahihi na ukamilifu, yaliandikwa kutokana na Neno la Mungu katika mafungu mafupi au sehemu kuu kinyume cha mafundisho bandia ya wazushi. Pili, tunazikubali kama kiri zetu miundo mitatu ya imani iliyokiriwa mahali kote, yaani Imani ya Mitume, Imani ya Nikea, na ya Athanasio kama kiri tukufu za Kikristo za imani zenye maneno machache, na zilizojengwa juu ya Neno la Mungu ambamo uzushi wote unakanushwa wazi na kwa ukamilifu uliojitokeza wakati ule katika Kanisa la Kikristo.
3. Tatu, Mungu wa huruma nyingi, kwa neema yake maalumu na kwa huduma aminifu ya mtu wa Mungu, Dk. Luther, nyakati hizi za mwisho, ameuleta mwangani tena ukweli wa Neno lake uliofichwa na akina Papa wa Roma katika giza la kuogofya sana. Mafundisho haya yaliyoandikwa kutokana na kuambatana na Neno la Mungu, yamejumlishwa katika mafungu na sehemu kuu za Ukiri wa Augsburg kinyume cha upotovu wa upapa na wa madhehebu mengine. Kwa hiyo, tunakiri kushikamana kwetu na toleo la kwanza na lisilobadilika la Ukiri wa Augsburg. Hatufanyi hivyo ka sababu lilitolewa na wanatheologia wetu bali kwa sababu yaliyomo ndani yake yalichukuliwa kutoka kwenye Neno la Mungu na kusimikwa imara juu yake. Basi,tunamaanisha ukiri jinsi ulivyoandikwa mwaka wa 1530, na kutolewa kwa Kaisari Karolo V huko Augsburg na baadhi ya Watawala Wachaguzi, watawala wengine, na vyeo vya heshima vya Dola la Roma kama ukiri wa makanisa yote ya matengenezo.1669 Muundo huu wa imani umetofautisha Makanisa yetu ya Matengenezo na Makanisa ya Upapa na madhehebu mengine yaliyohukumiwa kukanushwa kama uzushi. Tunaomba Ukiri wa Augsburg jinsi ilivyokuwa desturi katika Kanisa la Kale kwamba, sinodi za baadaye, maaskofu, na walimu wa Kikristo kukiri ufuasi wao wa Imani ya Nikea.
4. Mintarafu ya maana halisi na kweli ya Ukiri wa Augsburg, Utetezi uliandaliwa kirefu na kuchapishwa mwaka wa 1531.1670 Unaelezea wazi maana ya asili na halisi ya Ukiri wa Augsburg, kwa lengo la kutoa mafundisho, kinyume cha wafuasi wa Papa kwa uwazi na ufanisi zaidi na pia kuzuia uwezekano kwamba, chini ya jina la Ukiri wa Augsburg mtu angeweza kudiriki kwa hila kupenyeza makosa ndani ya Makanisa ya Mungu ambayo yalikuwa yamekataliwa tayari. Kwa hiyo, tunakiri kwa maafikiano, ufuasi wetu wa huu utetezi, kwa sababu Ukiri wa Augsburg uliotajwa haukufafanuliwa na kutetewa tu nao, bali unauthibitisho wazi kwa shuhuda dhahiri na zisizopingwa kutoka katika Maandiko Matakatifu. 1669 Kijerumani: ‘reformiert;’ Kilatini: ‘reformata.’ Matumizi ya jumla ya jina halisi la kuelezea makanisa ya Zwingli na Calvin ni ya chimbuko la baadaye. 1670 Lengo la hii sifa ni kueneza mamlaka ya toleo la kwanza pekee.
5. Tunakiri pia ufuasi wetu wa mafungu yaliyotolewa katika 7 mkutano mkuu wa wanatheologia huko Smalkaldi mwaka wa 1537 ambapo mafungu haya yalikubaliwa na kupokelewa na jinsi yalivyochapishwa.1671 Yalikusudiwa kutolewa mbele ya sinodi huko Mantua au kokote ambapo ingefanyika, kama jinsi maelezo ya Ukiri wa Augsburg, kwa majina ya Watawala Wachaguzi mashuhuri mno na watawala na vyeo vya heshima adhimu sana. Hawa waliazimia kubaki kuwa waaminifu kwayo kwa neema ya Mungu. Mafundisho haya ya Ukiri wa Augsburg yanarudiwa katika mafungu haya na mafungu fulani yanaelezwa zaidi kwa Neno la Mungu. Licha ya hayo, misingi na sababu zimeelezewa, kwa urefu uliohitajika, ambazo zimetulazimu kukataa uzushi na aina fulani za ibada za miungu mingine katika Upapa, na kwa sababu gani tusishirikiane nazo. Isitoshe, kwa nini hatukupata wala hatukujaribu kufikia maafikiano na Papa katika mambo haya.
6. Kwa kuwa mambo haya muhimu yanahusu watu wa kawaida 8 pia, yaani, Wakristo wa kawaida, ambao inawabidi watofautishe kati ya mafundisho ya kweli na ya uongo kwa ajili ya wokovu wao, tunakiri kwa maafikiano pia kwamba, ufuasi wetu wa Katekisimo Ndogo na Katekisimo Kubwa ya Dk. Luther, jinsi zilivyoandikwa naye na kuambatanishwa na maandiko yake yote. Maadamu, zilikubaliwa kwa ridhaa kuu na kutumiwa hadharani kanisani, shuleni, na nyumbani na makanisa haya yote yanayodumu katika Ukiri wa Augsburg, kwa sababu katekisimo hizi hujumlisha kwa usahihi mafundisho ya Kikristo kuhusu msingi wa Neno la Mungu kwa Wakristo wa kawaida katika muundo sahihi na rahisi hasa, lakini kwa uwazi wa kutosha.
Maandiko yaliyotajwa awali, yaliyopokelewa hadharani, na kwa ujumla, yamechukuliwa daima na makanisa na shule zilizofundisha kwa njia safi kwamba, muhtasari na muundo wa mafundisho ambayo Dk. Luther mwenye kumbukumbu yenye heri aliyaelezea wazi katika maandiko yake kuhusu msingi wa Neno la Mungu dhidi ya Upapa na madhehebu mengine. Tunalalamikia maelezo yake ya kinaganaga katika maandiko yake ya mafundisho na ya mabishano, jinsi alivyofanya mwenyewe katika utangulizi wa toleo la Kilatini la maandiko yake yaliyokusanywa.1672 Ametukumbusha kwa njia ya Kikristo na ya lazima kwamba, Neno la Mungu halina budi kubaki kama kipimo na kanuni kamili ya mafundisho yote, na kwamba, hakuna maandiko ya mwanadamu yeyote yanayothubutu kuwekwa sambamba nalo ila kwamba, kila kitu lazima kiwe chini yake.
1671 Baadaye, wanatheologia Walutheri walitoa pamoja na Mafungu ya Smalkaldi makala ya Melanchthon kuhusu Ukuu wa Papa kutoka kwa uo huo mwaka wa 1537. 1672 Toleo la Wittenberg katika Kilatini (1545-1561) na Kijerumani (1539-1561). WA 54:179-187.
556
Sisi hatumaanishi kwamba, vitabu vingine vizuri, vinavyofaa sana na safi, kama vile ufafanuzi wa Maandiko Matakatifu, ukanusho wa makosa, na maelezo ya mafungu ya imani viachwe kabisa. Ikiwa vinaafikiana na muundo wa mafundisho uliotajwa, havina budi kupokelewa na kutumika kama maelezo na fafanuzi za kufaa sana. Mintarafu ya yaliyotajwa hapo juu kuhusu muhtasari huu wa mafundisho yetu ya Kikristo, yanalenga tu muundo thabiti wa mafundisho, uliokubaliwa na unaokiriwa kote na kwa maafikiano makubwa kuwa halisi na unaokiriwa na makanisa yetu yote ya Kiinjili, ambao kwao, maandiko yote yanapaswa kuchunguzwa na kupimwa. Kwa kuwa, muundo huu umepokelewa kutoka katika Neno la Mungu, utaamua pia kwa kiasi gani vitabu vingine vyote vitaweza kukubaliwa na kutumiwa.
Basi, tumevikusanya vitabu vilivyotajwa. Yaani, Ukiri wa Augsburg, Utetezi, Mafungu ya Smalkaldi, Katekisimo Ndogo, na Katekisimo Kubwa ya Luther, kama muhtasari uliofikiriwa kwa kuzingatia mafundisho yetu ya Kikristo. Kwa sababu vitabu hivi vilichukuliwa wakati wote na mahali pote kuwa msimamo wa pote na uliokubaliwa na wote katika makanisa yetu. Vilitiliwa sahihi za wanatheologia wakuu na mashuhuri sana wa wakati huo na kupokelewa na makanisa yote na shule zote za Kiinjili. 12 Vitabu hivi vyote vilitungwa na kutolewa kabla ya mafarakano yaliyojitokeza miongoni mwa wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg. Kwa hiyo basi, vinatambuliwa kuwa viadilifu na hakuna hata sehemu moja katika majadiliano haya inayoweza au itakayoweza kuvikataa. Hakuna mfuasi yeyote mnyofu wa Ukiri wa Augsburg atakayeyapinga maandiko haya, bali atayakubali na kuyapokea kwa furaha kama ushuhuda wa kweli. 13.Hakuna hata mmoja anayeweza kutulaumu sisi kwa ajili ya kuyatumia maandiko haya ili kutuelezea na kuenezea maamuzi yetu kuhusu mafungu ya imani yaliyojadiliwa. Jinsi tunavyojenga mafundisho yetu juu ya Neno la Mungu kama ukweli wa milele, ndivyo tunavyoyataja maandiko haya kwa sababu yanatoa ushuhuda wa kweli, msimamo wa pamoja, na usahihi wa waliotutangulia ambao walibaki imara katika mafundisho safi.
Mafungu yaliyojadiliwa, tabaini, yaani, mafundisho ya uzushi yaliyopingwa
14. Ili kuhifadhi mafundisho safi na mwafaka, imara, na umpendezao Mungu kanisani, ni lazima tuyatoe mafundisho ya kweli na safi kwa usahihi, na pia kuwapinga maadui wanaofundisha vinginevyo (1 Tim. 3:9; Tit. 1:9; 2 Tim. 2:24; 3:16). “Wachungaji waaminifu,” jinsi Luther anavyosema, “lazima wote wawili wachunge au walishe kundi la kondoo na kulilinda dhidi ya mbwa mwitu
ili wapate kuepuka sauti ngeni na watenganishe kitu cha thamani na kibaya.”1673
15. Kwa hiyo basi, tumefikia mapatano ya msingi pamoja na kujulisha dhahiri kwamba, wakati wote, inatubidi kutofautisha kati ya mashindano yasiyohitajika na yasiyokuwa na faida ambayo yanaangamiza kuliko kujenga vizuri, yasiruhusiwe kulisumbua Kanisa na tena majadailiano ya lazima yanayohusu mafungu ya imani, yaani, sehemu maalumu za mafundisho ya Kikristo. Sawia, hatuna budi kukanusha mafundisho yaliyo kinyume na yenye makosa ili kuutetea ukweli.
16. Maandiko yaliyotajwa yanatosha kabisa kumwelezea msomaji wa Kikristo anayeugua kwa ajili ya upendo wa ukweli wa kimbingu, kwa njia wazi na dhahiri kuhusu mafungu yote na ya kipekee ya dini yetu ya Kikristo. Yaani, mambo ambayo hana budi kuyakubali na kuyapokea kuwa sahihi na kweli kulingana na kanuni ya Neno la Mungu. Yaani, maandiko ya manabii na mitume, na mambo ambayo lazima ayakatae, ayakimbie na ayaepuke. Ili ukweli huu uweze kuhifadhiwa kwa usahihi na dhahiri bila utata wowote na ili tofauti zozote zisiweze kujificha nyuma ya kauli bia, tumeonyesha dhahiri wenye tofauti zote kuhusu mafungu yote makuu na ya maana sana ambayo yalikuwa yamejadiliwa kwa wakati huu. Hivyo, watu wa kisasa na vizazi vitakavyokuja vitapata ushuhuda yakini na wazi, kuhusu maoni na hukumu katika maafikiano ya makanisa yetu sasa na baadaye. Yaani:
1. Kwanza, tunakataa na kulaani uzushi na makosa yote ambayo 17 Kanisa la Kale na lenye mafundisho sahihi lilikataa na kulaani kwa msingi yakini na imara wa Maandiko Matakatifu ya kimungu.
2. Pili, tunakataa na kulaani madhehebu yote na aina zote za 18 uzushi zinazokataliwa katika maandiko yaliyotangulia kutajwa.
3. Tatu, wakati wa miaka ishirini na mitano kwa ajili ya ‘Interim’ (‘Hati ya Muda’) na mambo mengine,1674 migawanyiko kadhaa imetokea miongoni mwa baadhi ya wanatheologia waliojiunga na wa Ukiri wa Augsburg. Kwa hiyo, tumeelezea imani na ukiri wetu katika majadiliano yote na kila suala mojamoja, 1673 Yn. 10:12-16, 27; Yer. 15:19. 1674 Andiko la Kilatini, miaka thelathini. Muda wa miaka ishirini na mitano ulihesabiwa tangu vita vya Smalkaldi (1546-1547) na ‘Augsburg Interim’ (Hati ya Muda ya Augsburg) iliandikwa mwaka wa 1548. Kaisari Karolo V aliamuru hati hii baada ya kushinda Watawala Walutheri katika Vita vya Smalkaldi. Andiko la (Hati ya Muda ya Augsburg) ilitungwa na wanatheologia wa Roma. Yaani, Pflug na Helding pamoja na mwanatheologia Mlutheri Yohana Agricola kutoka Brandenburg. Waprotestanti wachungaji walikubaliwa kufunga ndoa na Wakristo wote walikubaliwa kuinywa divai katika Ekaristi, lakini ahadi hizo zilikuwa za muda tu mpaka wakati wa sinodi iliyofuatia. Mwaka uo huo, Kaskazini mwa Ujerumani, Melanchthon na wengine walitunga ‘Interim of Leipzig’ (Hati ya Muda ya Leipzig) chini ya Mtawala Mchaguzi Moritz. Andiko hili lilizua mabishano kuhusu ‘adiaphora.’
558
kwa unyofu, kwa uwazi, na dhahiri kwa njia ya hoja na tabaini, 1675 Yaani, kuelezea kwa usahihi mafundisho halisi na pia mafundisho yasiyokuwa halisi. Hivyo basi, msingi wa ukweli wa kimungu unafunuliwa katika mafungu yote ya imani, na kila fundisho lisilokuwa sahihi, lenye mashaka, la kukufuru, na lililolaaniwa liweze kuwekwa wazi, haidhuru wapi au katika vitabu gani, linaweza kupatikana au nani aliweza kulisema au kuliunga mkono. Kwa uaminifu, tunataka kumwonya kila mmoja mapema dhidi ya makosa yaliyomo hapa na pale katika maandiko ya wanatheologia fulani. Mtu yeyote asirubuniwe na heshima ya wanatheologia hawa. Msomaji Mkristo akilichunguza tamko hili kikamilifu na akililinganisha na maandiko yaliyotangulia kutajwa, ataona kwamba, mambo yaliyokiriwa tangu mwanzo na halafu kuelezewa katika nyakati fulani katika muhtasari wa dini na imani yetu na sasa kurudiwa katika kitabu chetu si mafundisho ya mvutano fulani, bali ni ukweli huo huo ulio rahisi, usiobadilika, na wa kudumu. Sisi hatuelekei kutoka katika fundisho moja hadi lingine, jinsi maadui zetu walivyotushutumu kwa uongo. Kinyume chake, tunatamani kuonekana kwamba, tumekuwa waaminifu katika Ukiri wa Augsburg jinsi ulivyotolewa mara moja na kufafanuliwa kwa maafikiano na kwa njia ya Kikristo. Kwa neema ya Mungu, tunataka kuendelea kuwa thabiti na imara katika ukiri huu na kustahimili kwake dhidi ya udanganyifu wake wote uliojitokeza.
I. DHAMBI YA ASILI1676
Kwanza, kumekuwa na mfarakano miongoni mwa wanatheologia 1 kadhaa walio wafuasi wa Ukiri wa Augsburg kuhusu dhambi ya asili inavyoeleweka na hasa ni nini. Baadhi yao,1677 wametoa hoja ifuatayo: Kwa kuwa, anguko la Adamu lilipotosha asili na kiini cha ubinadamu kabisa, dhambi ya asili imekuwa asili, kiini, na dutu1678 ya mwanadamu jinsi ilivyokuwa baada ya anguko angalau kuwa sehemu muhimu na kuu mno ya kiini chake. Yaani, nafsi yake katika kiwango chake cha juu kabisa na nguvu zake maalumu. Dhambi ya asili imekuwa ikiitwa ‘dhambi–asili’ au ‘dhambi ya binafsi’ kwa sababu si wazo, neno, au tendo, bali ni asili yenyewe hasa ambayo kwayo, mzizi na chanzo cha dhambi nyingine hutokea. Sasa basi, kwa kuwa baada ya anguko asili ya mwanadamu imepotoka kwa sababu ya dhambi, hakuna tofauti kati ya asili ya mwanadamu au kiini chake na dhambi ya asili. Vinginevyo, haku-
1675 Andiko la asili: ‘In thesi et antithesi.’
1676 Kilatini: ‘Peccatum originale;’ Kijerumani: ‘Erbsünde’ (‘dhambi ya kurithiwa’).
1677 Matthias Flacius Illyricus (1520-1575) na wafuasi wake tangu mahojiano yake na Viktorino Strigel (15241569) huko Weimar Agosti mwaka wa 1560.
1678 Rejea wimbo wa Lazaro Spengler (1479-1534) aliyekuwa katibu wa mji wa Nürnberg: (1523)
na tofauti kati ya asili ya mtu au nafsi na dhambi ya asili.1679
Basi, wengine1680 wameendelea kufundisha kwamba, dhambi ya 2 asili si asili, dutu, wala kiini cha ubinadamu kama mwili na nafsi, ambavyo hata baada ya anguko vinabaki kuwa kazi na viumbe vya Mungu ndani yetu. Badala yake, dhambi ya asili ni kitu fulani katika asili ya mtu, katika mwili, nafsi na nguvu zake zote. Yaani, upotovu wa kuogofya sana, wa kina na usioelezeka. Mwanadamu anapungukiwa na haki ambayo katika hiyo asili aliumbwa. Katika mambo ya kiroho ni mfu kwa yaliyo mazima na amegeukia kwenye kila kitu kilicho kibaya. Kwa sababu ya upotovu huu na dhambi hii ya kuzaliwa ambayo hushikamana katika asili yake, dhambi zote halisi hutiririka kutoka katika moyo wake. Kwa hiyo basi, ni lazima kutofautisha kati ya asili na kiini cha mtu aliyeanguka. Yaani, kati ya mwili na nafsi yake ambavyo vinabaki ndani yetu kama viumbe vya Mungu hata baada ya anguko na kwa upande mwingine, dhambi ya asili ambayo ni kazi ya ibilisi, na hii imeipotosha asili ya ubinadamu.
Mabishano haya kuhusu dhambi ya asili si mabishano yasiyokuwa 3 na maana. Kinyume chake, mafundisho haya yakitolewa wazi kutoka na kulingana na Neno la Mungu, kwa njia ya kuyaepuka makosa yote ya Wapelagio na Wamani, tutajifunza zaidi na zaidi, jinsi Utetezi unavyoelezea kufahamu na kutukuza fadhili za Kristo, ustahili wake wa thamani na kazi ya thamani ya Roho Mtakatifu. Isitoshe, tunamtukuza Mungu tunapotofautisha kazi na uumbaji wake na kazi ya Ibilisi iliyopotosha asili ya ubinadamu kwa njia halisi. Hivyo, ili kuyaelezea 4 mabishano haya kwa njia ya Kikristo, yaani, kulingana na Neno la Mungu na kuyahifadhi mafundisho halisi na sahihi kuhusu dhambi ya asili, tutatoa, kwa mafungu makuu na mafupi na kwa msaada wa maandiko yaliyokwisha kutaja hoja na tabaini hapo juu. Yaani, mafundisho ya kweli na mafundisho ya uasi yanayopingana nayo.
Kwanza, ni kweli kwamba, Wakristo lazima waone na watambue 5 kwamba, dhambi si kukosea Amri za Mungu tu, bali pia ni ugonjwa wa kuogofya na wa kutisha mno unaorithiwa ambao umeipotosha asili yote. Kwa hakika, ni dhambi kuu hasa ambayo ni mzizi na chemchemi ya makosa yote. Dk. Luther anaiita dhambi hii ‘dhambi ya asili’ au 6 ‘dhambi ya binafsi’1681 ili kuonyesha kwamba, 1679 Hoja ya Matthias Flacius Illyricus, Cyriacus Spangenberg, Christian Irenaeus, Francis Coelestinus, na wengineo.
1680 Martin Chemnitz, Joachim Mörlin, Tilemann Heshusius, Johann Wigand, na Nikolao Selnecker; wakiungwa mkono na Simon Musaeus, Jacob Andreae, na wengineo.
1681 Katika mahubiri kuhusu Injili, kwa ajili ya Karamu ya tohara ya Bwana wetu, katika mabishano kuhusu muundo mzima wa Kipelagio Luther alisema kwamba, hapatakuwa na ‘dhambi ya kutendwa’ bila ‘dhambi ya asili,’ na kwamba, kwa ajili ya ukombozi wetu kutoka kwa dhambi ya asili, Kristo alitahiriwa si katika mkono au ulimi - kuonyesha kwamba, dhambi haina maneno na matendo, bali katika asili yetu iliyopotoshwa. WA,
ingawa mtu hangeyafikiria maovu, hangesema maovu, au hangetenda maovu ambayo, baada ya anguko la wazazi wetu wa kwanza, haiwezekani kwamba, dhambi ya asili imetia sumu na kuipotosha asili ya ubinadamu kabisa katika maisha haya na mbele za Mungu kama ukoma wa kiroho. Sheria ya Mungu inaishtaki na kuihukumu asili yetu. Yaani, nafsi yetu, kwa ajili ya upotovu huu kwa sababu ya anguko la mtu wa kwanza. Hivyo basi, tu “wana wa ghadhabu kwa asili tu,”1682 wana wa kifo na wa laana mpaka tukombolewe kutoka katika hali hii kwa njia ya ustahili wa Kristo.
Pili, ni dhahiri na kweli pia kama jinsi Fungu la XIX la Ukiri wa 7 Augsburg linavyofundisha kwamba, Mungu si muumbaji, mwanzilishi au chanzo cha dhambi, bali dhambi ni tendo la Ibilisi, “kwa mtu mmoja dhambi iliingia duniani” (Rum. 5:12; 1 Yoh. 3:8). Hata sasa, katika hali ya upotovu huu, Mungu haumbi na hatengenezi dhambi ndani yetu, bali ni kazi ya asili ambayo bado Mungu anaiumba na kuitengeneza hata sasa. Tumeambukizwa dhambi ya asili kwa njia ya kuchukuliwa mimba na kuzaliwa kwetu kimwili kutokana na mbegu ya dhambi kutoka kwa akina baba na mama zetu.
Tatu, jinsi Mafungu ya Smalkaldi yanavyosema, akili yoyote 8 haiwezi kujua na kufahamu aina ya uharibifu huu uliorithiwa. Badala yake, lazima kujifunza na kuamini kutokana na ufunuo wa Maandiko Matakatifu.1683 Utetezi1684 unalijumlisha jambo hili chini ya vichwa vifuatavyo:
1. Upotovu huu uliorithiwa ndio hatia, yaani, kwamba, sisi sote, 9 kwa sababu ya kutotii kwa Adamu na Hawa, tuko chini ya hasira ya Mungu na “tu watoto wa ghadhabu kwa asili,” jinsi Mt. Paulo asemavyo (Rum. 5:12).
2. Licha ya hayo, dhambi ya asili ndiyo upungufu mkamilifu au 10 ukosefu kabisa wa haki ya asili ya Paradiso na mfano wa Mungu ambao kulingana nao, mwanadamu wa asili aliumbwa katika ukweli, utakatifu, na haki.1685 Wakati huo huo ni upungufu na upumbavu katika mambo yote yanayomhusu Mungu. Katika Kilatini: ‘Deescriptio peccati originalis detrahit naturae non renovatae et dona et vim seu facultatem et actus inchoandi et efficiendi spiritualia’1686 (‘Maelezo ya dhambi ya asili hukataa kwamba, asili isiyofanywa upya kuwa na vipawa, nguvu, na uwezo wote wa kuanzisha na kutekeleza chochote katika mambo ya kiroho.’)
51:354; 46:39, 40.
1682 Efe. 2:3
1683 ‘Mafungu ya Smalkaldi,’ III, 1.
1684 ‘Utetezi wa Ukiri wa Augsburg,’ II, 2-50.
1685 Efe. 4:24.
1686 Fasili ya Utetezi wa Ukiri wa Augsburg II, 2-3. Martin Chemnitz aliitumia fasili hii katika kitabu chake kiitwacho, ‘Corpus doctrinae Julianum’ huko Wofenbüttel-Brauschweig mwaka wa 1576.
3. Dhambi ya asili katika asili ya ubinadamu sio tu ukosefu tele 11 wa mema yote ya kiroho katika mambo ya kimungu, bali wakati huo huo, inashika nafasi ya mfano wa Mungu uliopotea ndani ya mwanadamu pamoja na upotovu wa kiini cha uovu mbaya kabisa wa kina kirefu mno, usiofahamika na usioeleweka, wa asili yake kamili katika nguvu zake zote, hasa nguvu za juu na za kwanza za nafsi katika akili, moyo, na nia. Kama matokeo yake, tangu anguko la mwanadamu, kila mmoja hurithi mielekeo mibaya ya kuzaliwa, uchafu wa ndani wa moyo, tamaa mbovu, na mwelekeo mbaya. Hivyo basi, kwa upande wa asili yake, kila mmoja wetu hurithi kutoka kwa Adamu moyo, maono, na mawazo ambayo, katika nguvu zake za juu na katika mwanga wa akili, kwa asili vinampinga kabisa Mungu na amri zake hata kuwa na uadui dhidi ya Mungu hasa katika mambo ya kimungu na ya kiroho. Ni hakika, 12 mwanadamu bado anamiliki kipimo cha akili, nguvu, na uweza katika mambo ya asili na ya nje yaliyo chini ya akili, ingawa kwa kiasi kikubwa, vimedhoofishwa vibaya. Kwa sababu maradhi ya kurithiwa yamevitia sumu na doa, havitafaa chochote mbele za Mungu.
4. Adhabu ya dhambi ya asili ambayo Mungu anailipiza juu ya 13 wana wa Adamu na juu ya dhambi ya asili ni kifo na laana ya milele.1687 Isitoshe pia, ni pamoja na balaa zingine za kimwili, kiroho, kidunia na za daima, udhalimu na utawala wa Ibilisi, kwa kuwa asili ya ubinadamu imewekwa chini ya utawala wa Ibilisi na kukaa kama mfungwa katika ufalme wake. Ibilisi hupotosha na hukosesha watu wengi wakuu na wenye hekima katika ulimwengu huu kwa makosa, uzushi, na upofu wa kutisha, na anawaendesha kwa kishindo katika aina yoyote ya uovu.
5. Uharibifu huu wa kurithiwa ni mkubwa na wa kuogofya sana 14 kiasi kwamba, Mungu peke yake anaweza kuufunika na kuusamehe jinsi anavofanya kwa ajili ya Kristo Bwana tu kwa waaminio na kubatizwa. Asili ya ubinadamu iliyopotoka na kuharibika inaweza kutibiwa kwa njia ya kuzaliwa upya na kurekebishwa na Roho Mtakatifu. Ukarabati huu unaanzia tu katika maisha haya na hautakamilika mpaka maisha ya baadaye.
Mambo haya, ambayo tumeyatoa katika muundo wa jumla, 15 yataelezwa kwa undani zaidi katika mafundisho yetu ya Maandiko ya Kiri za Kikristo.
Mafundisho haya lazima yahifadhiwe na yalindwe ili yasianguke 16 kwa upande wa Wapelagio au Wafuasi wa Mani. Kwa hiyo, kwa ufupi, inatubidi kutaja mafundisho yaliyo kinyume ambayo yamekataliwa na kulaaniwa katika makanisa yetu:
1687 Tahakiki ya wanatheologia wa Preussen ilidai kwamba, hukumu ya milele iwe imetajwa hasa ili watu waelewe kwamba, dhambi ya asili hustahili kifo na hukumu ya milele pia.
1. Kwanza, tunapinga na kukataa maoni na mafundisho ya 17 uzushi wa Wapelagio wote wa zamani na wapya, ambayo hufundisha kwamba, dhambi ya asili ni hatia iliyorithiwa peke yake kwa ajili ya tendo la mtu mwengine bila upotovu wa asili yetu.
2. Kwamba, tamaa mbaya za dhambi si dhambi, bali masharti ya 18 dhambi na sifa za kiini za asili1688 zilizoumbwa.
3. Kwamba, upungufu na hasara hii iliyotajwa si dhambi ya 19 kweli kabisa mbele za Mungu, ilikwa kivyovyote, mwanadamu awe mwana wa ghadhabu, kuzimu, ndani ya ufalme wa Ibilisi, na chini ya mamlaka yake bila Kristo.
4. Makosa yatakayofuatia na mengine ya aina hiyo yanapingwa 20 na kukataliwa: Baada ya anguko, asili ni halisi bila upotoshaji wowote, hasa ni nzuri kabisa na safi, na kwa upande wa sifa zake za asili, ni kamilifu kabisa.
5. Dhambi ya asili ni doa ndogo au waa la nje, lililonyunyiziwa 21 juu yake tu, au ‘corrurptiotantum accidentium aut qualitatum,’ yaani, upotovu wa sifa za muda za asili ya ubinadamu. Licha ya hayo, asili yenyewe inabaki na uzuri na nguvu zake katika mambo ya kiroho pia.1689
6. Dhambi ya asili haimaanishi hasara au ukosefu wa nguvu 22 nzuri za kiroho za mwanadamu, bali ni kizuizi chao cha nje tu, ni sawa na maji ya kitunguu saumu yaliyopakwa juu ya sumaku yasiyoweza kuharibu nguvu ya asili ya sumaku ila kuizuia tu,1690 au kwamba, madoa yaliyozungumziwa yanaweza kuoshwa kwa urahisi, sawa na doa la uchafu kutoka usoni mwa mmoja au rangi kutoka ukutani.
7. Vivyo hivyo, pia tunapinga na kukataa wote wanaofundisha 23 kwamba, ingawa asili imedhoofishwa na kuharibiwa kwa kiasi kikubwa na anguko, hata hivyo, haijapoteza uzuri wote unaohusika na mambo ya kimungu na maisha ya kiroho. Wao husisitiza kwamba, wimbo tunaouimba katika Kanisa letu, unavyoelezea si kweli, “Kwa anguko la Adamu asili imepotoka kabisa,” kwamba, asili yetu, tangu kuzaliwa kwa kimwili na sifa fulani, ina kilicho kizuri hata kama ni kidogo na hafifu. Yaani, kama vile welekevu wepesi, ustadi, au uwezo wa kuanzisha na kutekeleza jambo fulani katika mambo ya kiroho au kukishirikisha ndani.1691 Katika fungu litakalofuatia, tutaelezea nafasi ya kutekeleza 24 shughuli za nje na za ulimwengu huu ambazo zi chini ya akili ya ubinadamu.
1688 Petro Lombardo (sent. II, dist. 30. c. 6) na madaktari wa Uwanazuoni wengine. Ukanusho wake, Martin Chemnitz, ‘Examen Concili Tridentini’ miaka ya 1566-1575, 1:311-374.
1689 Sinodi la Trento, Kikao cha tano, tamko kuhusu dhambi ya asili, sura ya 5. Huldrych Zwingli aliyatoa maoni yayo hayo katika kitabu chake kiitwacho, ‘Fidei ratio’ (1530).
1690 Viktorino Strigell aliutumia mfano huu wa itikadi ya umma katika majadiliano ya Weimar. 1691 Kwa sehemu, dhidi ya Viktorino Strigell na Philipp Melanchthon.
563
Tunayalaumu na kukataa mafundisho kama haya na 25 yanayofanana nayo ambayo huupinga ukweli, kwa kuwa Neno la Mungu linafundisha kwamba, asili iliyopotoka, yenyewe haiwezi kuzaa lolote lililo zuri katika mambo ya kiroho na ya kimungu, hata jambo dogo kabisa kama wazo moja lililo safi. Kinyume chake, yenyewe inaweza kutenda dhambi tu mbele za Mungu (Mwa. 6:5; 8:21).
Kwa upande mwingine, mafundisho haya pia hayana budi 26 kulindwa dhidi ya upotovu wa Wamani. Kwa hiyo, mafundisho yafuatayo ya uzushi na yanayofanana nayo yanakataliwa:
1. Tangu anguko na hata sasa, asili ya ubinadamu mwanzoni iliumbwa safi na kamilifu. Kisha baadaye, Ibilisi anamimina na kuichanganya dhambi ya asili kutoka nje kama kitu muhimu katika asili ya mtu jinsi sumu inapochanganywa na maji.
Mintarafu ya Adamu na Hawa, asili yao mwanzoni ilikuwa 27 imeumbwa safi, nzuri, na takatifu. Lakini dhambi haikuivamia asili yao kwa jinsi ambayo Wamani hudhania katika utashi wao, kwamba, Ibilisi angeumba au kutengeneza kitu yakinifu kilicho kibaya na amekichanganya na asili yao. Kwa usahihi zaidi ni kwamba, mwanadamu alipoanguka kwa sababu ya ushawishi wa Ibilisi alipoteza haki iliyoumbwa na kurithiwa kama adhabu ya hukumu ya Mungu. Hii hasara, upungufu, udhaifu, na ulemavu ambao Ibilisi ameuleta, umepotosha na kuozesha mno asili ya mwanadamu kama ulivyoelezewa hapo juu kwamba, watu wote, waliochukuliwa mimba na kuzaliwa katika hali ya asili kutoka kwa baba na mama, sasa wanarithi asili pamoja na upungufu na upotovu huo huo. Kwa maana, tangu anguko, asili ya 28 mwanadamu haijawa kama jinsi ilivyoumbwa mwanzoni, yaani, safi na takatifu. Imepotoka baadaye tu kwa njia ya dhambi ya asili. Mwanzo wa kuchukuliwa mimba kwetu, mbegu ambayo kwayo, mtu ameumbwa, ina dhambi na imepotoka. Hivyo, dhambi ya asili si kitu fulani kinachoishi peke yake ndani au nje ya asili ya mtu aliyepotoka, jinsi kiini, mwili, nafsi, au mtu mwenyewe asivyokuwa. Hivyo basi, si halali na 29 haiwezekani kabisa kutofautisha kati ya dhambi ya asili na asili mwanadamu iliyoozeshwa na dhambi hii. Hata asili ya mwanadamu ingeonekana kuwa safi, njema, takatifu, na isiyopotoka mbele za Mungu, wakati dhambi ya asili tu ambayo hukaa ndani yake ndiyo mbovu.
2. Tunakataa pia kosa ambalo Agostino aliwahesabia Wamani1692 30 kwamba, si mtu aliyepotoshwa mwenyewe ambaye hutenda dhambi kwasababu ya dhambi ya asili ya kuzaliwa kwake, bali ni kitu kigeni na cha nje kilicho ndani ya mtu. 1692 Agostino, Maungamo, V. 10, 18; Maelezo ya Zaburi 140:9 na kwa jumla wakati wote maandiko yake dhidi ya Wamani na Wapelagio.
Kulingana na haya, Mungu hashtaki na hahukumu, kwa sheria yake, asili ya ubinadamu iliyopotoshwa na dhambi, bali dhambi ya asili peke yake. Jinsi ilivyoelezewa katika andiko lililotangulia, tulipoyajadili mafundisho sahihi ya dhambi ya asili, asili yote ya kila mwanadamu aliye hai, aliyezaliwa katika hali asili kutoka kwa baba na mama yake, ameozeshwa na kupotoshwa na dhambi ya asili katika mwili na nafsi, katika nguvu zake zote kutoka mwanzo hadi mwisho mintarafu ya uzuri, ukweli, utakatifu, na haki iliyotolewa wakati wa uumbaji katika Paradiso. Hii haimaanishi kwamba, asili ya mwanadamu imeharibiwa kabisa au imegeuka kuwa kiini fulani kingine ambacho ni tofauti na asili yetu na hivyo haina kiini hicho hicho nasi.1693
Sheria inashtaki asili yote ya mwanadamu kwa sababu ya 31 upotovu huu na kuilaumu ikiwa dhambi haisamehewi kwa ajili ya Kristo.
Hata hivyo, sheria haishtaki na kuiadhibu asili yetu kwa sababu 32 kwamba, tuliumbwa na Mungu kuwa wanadamu, bali kwa sababu ya dhambi na maovu yetu. Asili yetu haihukumiwi kwa sababu na kwa kadiri ya asili na kiini chetu, ni tendo na kiumbe cha Mungu hata baada ya anguko, bali kwa sababu na kwa kadri asili yetu imetiwa sumu na kupotoshwa na dhambi.
Ingawa, kwa maneno ya Luther,3 dhambi ya asili kama sumu na 33 ukoma wa kiroho imetia sumu na kuipotosha hasa asili yote ya mwanadamu, hata kuwa muhali kugawanya asili yetu iliyopotoka katika sehemu mbili tofauti za kutazamiwa, hata hivyo basi, ni mambo mawili yasiyofanana. Yaani, asili iliyopotoka au kiini cha mtu aliyepotoka, mwili na nafsi au mtu mwenyewe jinsi alivyoumbwa na Mungu, ndani ambamo dhambi ya asili inakaa na kupotosha asili na kiini. Naam, mwanadamu kamili, si mfano mmoja na dhambi ya asili ambayo inakaa katika asili au kiini cha ubinadamu na kuipotosha. Kama mwili ulionajisiwa na ukoma na ukoma unaokaa ndani ya mwili, hayo ni mambo mawili tofauti. Hali kadhalika, tukiyatumia maneno katika maana yao maalumu, hatuna budi kutofautisha kati ya asili yetu iliyoumbwa na kutunzwa na Mungu, ambamo dhambi hukaa na dhambi ya asili inayokaa katika asili yetu. Kulingana na Maandiko Matakatifu, inatubidi kutofautisha kati yao katika mafundisho na imani.
Mafungu makuu ya imani yetu ya Kikristo hutulazimisha na 34 hutushurutisha kushikilia tofauti hizo. Kwanza, fungu linalohusu uumbaji linashuhudia kulingana na Maandiko Matakatifu kwamba, Mungu hakuumba asili ya ubinadamu tu kabla 1693 Kilatini: ‘Non tamen in aliam substantiam genere aut specie diversam, priori abolita, transmutata est.’ 3 WA, 36: 682; 44:472, 489, 506, na kadhalika. Tafsiri ya neno kwa neno.
565
ya anguko, bali pia kwamba, baada ya anguko, asili ya mwanadamu inaendelea kuwa kiumbe na kazi ya mikono yake Mungu (Kum. 32:6; Isa. 45:11; 54:9; 64:8; Mdo. 17:25, 26; Ufu. 4:11). Ayubu anasema: “Mikono yako imeniumba na 35 kunifinyanga; nawe utageuka na kuniangamiza? Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena? Je! wewe hukunimimina kama maziwa, na kunigandisha mfano wa jibini? Umenivika ngozi na nyama, na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa. Umenijazia uhai na upendeleo, na maangalizi yako yameilinda roho yangu” (Ayu. 10:8-12).
Naye Daudi anasema: “Nitakushukuru 36 kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.1 Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana, mifupa yangu haikusitirika kwako, nilipoumbwa kwa siri, nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado” (Zab. 139:14-16).
Katika Kitabu cha Mhubiri tunasoma: “Nayo mavumbi kuirudia nchi 37 kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa” (Mhu. 12:7).
Aya hizi huonyesha wazi kwamba, hata baada ya anguko, Mungu 38 ni Muumbaji wa mtu anayemuumbia mwili. Kwa hiyo, mtu aliyepotoka hawezi kuwa tofauti bila dhambi yenyewe, la sivyo, Mungu angekuwa Mwumbaji wa dhambi. Katika maelezo ya Sharti la Kwanza la Imani katika Katekisimo Ndogo tunakiri: “Ninaamini ya kwamba, Mungu ndiye ameniumba mimi na vyote vilivyoko, kwamba, amenipa na anahifadhi mwili na nafsi yangu, viungo vyote na akili; mawazo yangu na welekevu wangu wa akili.” Vile vile imeandikwa katika Katekisimo Kubwa: “Ninashikilia na kuamini kwamba, mimi ni kiumbe cha Mungu; yaani, kwamba, amenipa na daima huutunza mwili wangu, nafsi, na uhai, viungo vyangu vidogo na vikubwa, hisi zote na akili na busara yangu, na kadhalika.”1694 Ni kweli kwamba, kiumbe hiki na kazi ya mikono ya Mungu imepotoshwa na dhambi kwa njia ya kutisha sana. Kwa sababu, vifaa ambavyo kwavyo, Mungu humwumba na kumtengeneza mtu vimepotoka na kupotoshwa katika Adamu na vinarithiwa nasi pia.
Kwa hiyo, inabidi mioyo ya Wakristo wacha Mungu kuutafakari 39 sana wema wa Mungu usioelezeka kwamba, hatupi kwa haraka katika moto wa Jehanamu vifaa hivi vilivyopotoka na kuharibika na vyenye dhambi, bali katika huo, anavifinyanga na kutengeneza kwavyo asili ya sasa ya kibinadamu ambayo imeharibiwa vibaya sana na dhambi ili apate kuiosha kutoka dhambini, kuitakasa, na kuiokoa kwa njia ya Mwanawe mpendwa.
Fungu hili linaonyesha tofauti madhubuti na wazi katika asili na 40 dhambi 1694 Kurasa.
566
ya asili. Dhambi ya asili haitoki kwa Mungu wala Mungu si Mwumbaji au Mwanzilishi wa dhambi. Dhambi ya asili si kiumbe wala kazi ya mikono ya Mungu. Kinyume chake, dhambi ni kazi ya Ibilisi. Kama hakungekuwa na tofauti yoyote kati ya asili ya mwili na nafsi 41 iliyoharibiwa na dhambi ya asili na dhambi ya asili yenyewe iliyoipotosha asili yetu, ingetokea kwamba, ama kwa vile Mungu ndiye Muumbaji wa asili yetu hii, ameumba na kuitengeneza dhambi ya asili ambayo inaweza kuwa kazi ya mikono na kiumbe chake. Au kwamba, kwa kuwa Ibilisi ni mwanzilishi wa dhambi, Ibilisi ni mwumbaji wa asili yetu, mwili, na nafsi yetu ambayo inaweza kabisa kuwa kazi ya mikono au kiumbe cha Ibilisi jinsi asili yetu potovu ilivyo mfano mmoja na dhambi yenyewe. Majumlisho hayo yote mawili yamekuwa kinyume cha Sharti la Kwanza la Imani yetu ya Kikristo.
Kwa hiyo, ili tutofautishe kiumbe na kazi ya mikono ya Mungu 42 ndani ya mtu kutoka kwa kazi ya Ibilisi, tunatangaza kwamba, ni kazi ya uumbaji wa Mungu kwamba, mwanadamu ana mwili na nafsi. Hali kadhalika, ni kazi ya Mungu kwamba, mwanadamu anaweza kufikiri, kusema, kutenda, na kufanya lolote, kwa sababu “ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu” (Mdo. 17:28). Kinyume chake basi, kwanza, ni kazi ya Ibilisi kwamba, asili yetu imepotoka na mawazo, maneno, na matendo yetu ndiyo maovu. Kwa kuwa, Ibilisi amekipotosha, kwa dhambi, kiumbe cha Mungu ndani yake Adamu. Upotovu huu umetufikia kwa njia ya kurithi.
Pili, katika fungu kuhusu ukombozi wetu, Maandiko Matakatifu 43 yanashuhudia kwa nguvu kwamba, Mwana wa Mungu aliichukua asili ya ubinadamu, japo bila dhambi. Katika mambo yote, alifanywa kuwa sawa nasi, tulio ndugu zake, isipokuwa dhambi pekee (Ebr. 2:17). Kuhusu mambo haya, walimu wa kale walisema: “Kristo yu na asili yenye kiini hicho hicho pamoja nasi, ndugu zake, mintarafu ya asili ambayo aliichukua. Asili hii ni ya aina, jinsi na kiini hicho hicho na asili yetu licha ya dhambi. Wanayalaani yanayoyapinga mafundisho haya kuwa 44 uzushi dhahiri.”1695 Kwa hiyo basi, kama hapakuwa na tofauti yoyote kati ya asili na kiini cha mwanadamu aliyepotoshwa na dhambi ya asili, na kwa upande mwingine, dhambi ya asili yenyewe, ingebidi ifuate kwamba: Kristo hakuichukua asili yetu, kwa kuwa hakuichukua dhambi. Kwa sababu, Kristo aliichukua asili yetu, aliichukua pia dhambi. Maoni haya yote 1695 Dondoo hili ni mkusanyiko mfupi wa kauli za akina Baba wa Kanisa zilizojumlishwa na Martin Chemnitz katika kitabu chake kiitwacho, ‘De duabus naturibus in Christo’ (‘Asili zote Mbili katika Kristo’) mwaka wa 1580): “Christum nobis, fratribus suis, conssubstantialem esse secundum assumptam naturam, quia naturam, quae, excepto peccato, eiusdem generis, soeciei et substantiae cum nostra est, assumpsit, et contrariam sententiam manifeste haeresos damnarunt.”
567
mawili ndiyo kinyume cha Maandiko Matakatifu kabisa. Kwa sababu Mwana wa Mungu aliichukua asili yetu na si dhambi ya asili, ni dhahiri kwamba, hata baada ya anguko, asili ya mwanadamu ni kitu tofauti kabisa ikilinganishwa na dhambi ya asili, bali lazima vitofautishwe kwa kila kimoja na kingine.
Tatu, katika fungu la utakaso, Maandiko Matakatifu 45 yanashuhudia kwamba, Mungu anamwosha, anamsafisha, na kumtakasa mwanadamu kutoka dhambini, na kwamba, Kristo analiokoa taifa lake kutoka katika dhambi zao. Kwa hiyo basi, dhambi haiwezi kuwa kwenye mfano mmoja na mtu mwenyewe. Kwa sababu Mungu humpokea mtu katika neema yake kwa ajili ya Kristo, bali anabaki adui wa dhambi wakati wote milele. Kwa hiyo, ni kuupinga Ukristo na ni jambo la kuchukiza sana kusema kwamba, dhambi ya asili inabatizwa katika jina la Utatu Mtakatifu, inatakaswa, na inaokolewa na maelezo mengine yanayofanana na hayo ambayo kwayo, hatutaki kuwachukiza watu wasiofundishwa ingawa yanapatikana katika maandiko ya Wamani wapya.1696
Nne, katika fungu la ufufuo, Maandiko Matakatifu yanashuhudia 46 kwamba, kiini halisi cha mwili huu wetu kitafufuka, ila bila dhambi. Tutakuwa katika uzima wa milele na hii nafsi hiyo hiyo ya kudumu, ingawa bila dhambi.
Kama hakuna tofauti yoyote kati ya mwili wetu na nafsi yetu 47 iliyopotoka na dhambi ya asili, ingekuwa kinyume cha fungu la imani yetu ya Kikristo, ama mwili wetu hautafufuka siku ya mwisho na kwamba hatutakuwa katika uzima wa milele na kiini hiki cha mwili na nafsi yetu. Badala yake, tutakuwa na kiini kingine au nafsi nyingine kwa vile hatutakuwa na dhambi huko; au dhambi pia itafufuka, itakua na itabaki ndani ya wateule katika uzima wa milele.
Kutokana na haya, ni dhahiri kwamba, ni lazima kuyakataa 48 mafundisho haya na yote yanayohusika nayo. Yaani kwamba, dhambi ya asili ndiyo asili, kiini, kitovu, mwili au nafsi ya mwanadamu aliyepotoka, kiasi kwamba, hakuna tofauti yoyote kati dhambi ya asili, kiini, na kitovu cha asili iliyopotoka. Kwa kuwa mafungu makuu ya imani yetu ya Kikristo huonyesha, kwa nguvu na uzito mno, kwa nini tunapaswa kushikilia tofauti kati ya asili au kiini cha mtu, ambayo imepotoshwa na dhambi, na dhambi yenyewe ambayo kwayo, mtu amepotoka. Basi, 49 yaacheni haya yatoshee hapa kama maelezo rahisi kwa njia ya hoja na uhakiki hasi wa mafungu yanayopingana. Hatuujadili hapa kwa urefu, bali tunazielezea hoja kuu za mafungu haya pekee.
1696 Katika kazi yake, Kristiano Irenaeo ‘Examen Libri Concordiae’ anaelekea kuwa na msimamo huu. Flacius aliifundisha mitazamo hii wazi (‘Clavis Scripturae,’ I ,1299), bali wenzake walimfikiria kuwa kitendawili kwamba, “dhambi ya asili lazima ibatizwe katika jina la Utatu Mtakatifu.”
568
Kuhusu maneno yenyewe na kauli, inafaa sana na ndiyo njia 50 yakini ya kuifuata mifano ya maneno mabruki yanayotumiwa katika Maandiko Matakatifu na vitabu vilivyotajwa hapo juu na vinavyoyatumiwa kulielezea fungu hili.
Ili kuepuka mabishano yote kuhusu maneno,1697 ni muhimu 51 kuelezea kwa uangalifu na kwa uwazi sana maneno na kauli zinazotumiwa katika maana nyingi.1698 Hivyo basi, katika kauli, “Mungu anaumba asili ya mtu,” neno, ‘asili’ maana yake ndiyo kiini, mwili, na nafsi ya mwanadamu. Mara nyingi tena, sifa nzuri ya ubaya wa kitu fulani inaitwa asili yake kama katika kauli: Ni asili ya nyoka kuuma na kutia sumu.” Ni katika maana hii ya mwisho ambayo Luther anaandika kwamba, dhambi na kutenda dhambi ni sifa na asili ya mtu.1699
Kwa hiyo, tukisema kiuhalisia, dhambi ya asili ndiyo upotovu wa 52 kina wa asili yetu jinsi ilivyoelezewa katika Mafungu ya Smalkaldi.1700 Pengine, neno hili linatumika katika maana pana ya kumhusisha mtu au kiini cha binafsi.1701 Yaani, mtu mwenyewe pamoja na mwili na nafsi yake ambamo dhambi inakaa na kuganda ndani yake kwa sababu mtu amepotoshwa na kuliwa na dhambi. Kwa hiyo, Luther anaweza kusema: “Kuzaliwa kwako, asili yako, kiini chako kwa jumla ki dhambi, yaani, ni vyenye dhambi na visivyokuwa safi.”1702
Luther mwenyewe anaelezea kwamba, anazitumia istilahi 53 ‘dhambi ya asili,’ ‘dhambi ya binafsi’ na ‘dhambi ya kiini’ kumaanisha kwamba, si matendo tu yaliyo dhambi, bali kwamba, asili nzima, nafsi yote ya kiini vimepotoshwa kabisa na kuwa dhambi ya asili.1703
Kuhusu maneno ya Kilatini, yaani, ‘substantia’ na ‘accidens,’ 54 Wakristo wa kawaida wahurumiwe nayo katika mahubiri ya hadhara, kwa sababu hawayafahamu. Lakini wataalamu wanapozitumia istilahi hizi miongoni mwao wenyewe au kwa watu wengine wanaozifahamu vizuri, kama Eusebio, Ambrosio, na hasa Agostino na madaktari wengine wengi hodari wa Kanisa walivyolazimika kufanya walipolielezea fundisho hili dhidi ya wazushi,1704
1697 Andiko la Kilatini linatumia neno la Kiyunani, ‘λογομαχιας .’
1698 Kilatini: ‘Aequivocationes vocabulorum.’
1699 Katika maelezo yake kuhusu Zab. 51:3 (WA, 2:728; 18:501) Luther anasema kwamba, wazo la asili ya mtu hutofautiana na sifa ya mchunguzi. Kwa hakimu, asili ya mtu ni kuwa katika matatizo halali, kwa mganga, asili ya mtu ni afya yake dhaifu, kwa wanafalsafa, asili ya mtu ni kufikiri kwake. Lakini mwanatheologia huiona asili kuwa nafsi ya mtu katika hali ya dhambi zake.
1700 Mafungu ya Smalkaldi III, 1,3.
1701 Andiko la Kijerumani: ‘Concretum’ au ‘Subjectum.’
1702 WA, 12-403; 40 (II) 322, 380. Kila kundi lilikuwa limesihi maandiko ya Luther kuhalalisha matumizi ya istilahi hizi tatu.
1703 WA, 10 II, 1: 508; 40 II: 327, 385.
1704 Eusebio, ‘Praeparatio Evangelica.’ VII, 22; Ambrosio, ‘Hexaemeron,’ I, 8, 28; Maelezo kwa Warumi (Rum. 7:18); Agostino, ‘De natura et gratia,’ 19, 21, 20, 22 na kadhalika.
569
walizitumia kwa maana ya ugavi kamili1705 bila istilahi ya katikati kwa njia ya kuigawanya istilahi katika vinyume vyake. Kulingana na haya, lazima kila kitu kiwe ama ‘substantia,’ yaani, kitu kinachopatikana kupitia kwake kwenyewe au ‘accidens’ kisichopatikana kupitia kwake kwenyewe, ambacho kinaambatana na kitu kingine kinachopatikana katika chenyewe na kinachoweza kutofautishwa nao. Kirillo na Basileio pia walitumia ugavi huo.1706
Kauli za kimsingi, ambazo ndizo yakini na zisizokuwa na 55 ukinzani wowote katika theologia zinadai kwamba, kila ‘substantia,’ yaani, kitu kinachopatikana katika chenyewe kama kiini ni ama Mungu mwenyewe au kiumbe cha Mungu. Kwa hiyo, Agostino alihukumu na kukataa kwa makusudi na kwa uzito kauli hii, pamoja na wanatheologia wengi wa kutegemewa, katika maandiko yake mengi dhidi ya Wamani: “Dhambi ya asili ndiyo kiini au asili ya mwanadamu.”1707 Wataalamu na watu hodari wote baada ya Agostino wameshikilia kwamba, hakuna kitu chochote wala kiini kisichopatikana kwa njia ya chenyewe au kama sehemu ya kitu kinachoishi kwa njia ya chenyewe, bali kinapatikana kama sifa isiyodumu ya kitu kingine kisichokuwa kiini, yaani, kitu fulani kinachopatikana katika chenyewe, bali ni mbadiliko umbo,1708 yaani kitu fulani cha bahati mbaya. Kwa hiyo, mara kwa mara, Agostino 56 anatumia kauli hii: “Dhambi ya asili si kitu kama asili ya mwanadamu mwenyewe, bali ni upungufu na uharibifu wa nasibu katika asili.”1709 Kabla ya mabishano haya, wanatheologia waliongea hivyo katika shule na makanisa yetu, wakifuata kanuni za upembuzi kwa uhuru na bila kuchochea mashaka wala kulaumiwa na Dk. Luther au na mwalimu yeyote wa kweli wa makanisa yetu safi ya Kiinjili.
Hivyo basi, ukweli usiopingika ni kwamba, kila kitu 57 kinachopatikana ni ama kiini au nasibu, yaani kitu kinachopatikana katika chenyewe au kitu fulani cha bahati mbaya. Ukweli huu ulionyeshwa awali kidogo na kuthibitishwa na shuhuda za Madaktari wa Kanisa, na haujapata kutiliwa mashaka na mtu yeyote aliye hodari. Basi, hatuna budi kusema kwamba, iwapo yeyote angeuliza kama dhambi ya asili ni kiini, yaani, kitu ambacho kinapatikana katika chenyewe au kama ni kitu cha bahati, yaani, kitu ambacho hakipatikani katika chenyewe, bali kilichoambatana katika kitu kingine na hakiwezi kupatikana katika chenyewe, lazima akiri wazi na dhahiri kwamba, dhambi ya asili si kiini, bali ni kitu cha
1705 Kilatini: Divisio immediata.’
1706 Kirillo wa Iskanderia (+444) na Basileio Mkuu (mnamo 330-379).
1707 Kilatini: ‘Peccatum originis est substantia vel natura.’ Agostino, ‘Maungamo’ (‘Confessiones’) V, 10, 18.
1708 Kilatini: ‘Accidens.’
1709 Kilatini: ‘Accidens vitium in natura.’
bahati tu.1710
Kwa hiyo, makanisa ya Mungu hayatapata amani ya kudumu 58 katika mabishano haya kamwe. Kinyume chake, ugomvi peke yake utaongezeka na kukuzwa iwapo wahudumu wa Kanisa watakuwa na mashaka iwapo kama dhambi ya asili ni kiini au nasibu katika maana sahihi na halisi ya neno.
Kwa hiyo basi, ni lazima kabisa kuwaelimisha watu wote katika 59 masuala haya ili makanisa na shule ziwe huru kutoka katika mabishano haya mabaya na ya hasara kubwa.
Lakini ikiulizwa zaidi, ni nasibu gani ya dhambi ya asili? Swali 60 hili ni tofauti na hakuna mwanafalsafa, hakuna mfuasi wa Papa, hakuna mtalaamu wa ghiliba au akili ya kibinadamu, iliyo hodari kiasi cha kuweza kulitoa jibu. Maelezo na jibu linatolewa katika Maandiko Matakatifu peke yake. Maandiko Matakatifu yanashuhudia kwamba, dhambi ya asili ni upotovu usioelezeka na uharibifu wa jinsi hiyo ya asili ya mwanadamu kwamba, hakuna kilicho safi wala kizuri kilichobakia ndani yake chenyewe na katika vyote, nguvu zake za ndani na nje, bali kwamba, vyote kwa pamoja vimeozeshwa. Kwa sababu ya dhambi ya asili, mwanadamu hana maisha ya kiroho mbele za Mungu na licha ya nguvu zake zote za kutenda mema, yeye ni kama maiti.
Inatokea hapa kwamba, matumizi ya istilahi ‘nasibu’ kuhusu 61 dhambi ya asili hayatapunguza dhambi ya asili iwapo istilahi itaelezwa kwa mwafaka wa Neno la Mungu, jinsi Dk. Luther alivyoandika kwa bidii katika ufafanuzi wake kwa Kilatini kuhusu sura tatu za Kitabu cha Mwanzo1711 dhidi ya kuidhoofisha dhambi ya asili. Istilahi hutumika sasa tu ili kuelezea tofauti kati ya kazi ya Mungu, yaani, asili yetu, licha ya upotovu wake, na kazi ya Ibilisi, ambayo ndiyo dhambi iliyofungamana na kiumbe cha Mungu na kukiharibu kwa kiasi kisichoelezeka.
Kwa kweli, Luther hakuyaacha maneno kama ‘nasibu’ na 62 ‘sifa’1712 bali aliyatumia yote mawili katika suala hili. Wakati huo huo, ameelezea na kuhifadhi kwa uzito maalumu na juhudi kubwa kuwa sifa hii na nasibu ya kuogofya mno ambayo haikuchafua asili ya ubinadamu peke yake, bali iliipotosha kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba, hakuna kilichobakia kuwa safi ndani yake. Katika ufafanuzi wake wa Zab. 90:12 anaandika: “Tunaita dhambi ya asili kuwa sifa au ugonjwa; ndiyo ni hasara mbaya mno. Tutateseka kwa sababu ya ghadhabu
1710 Mazungumzo haya kuhusu ‘substantia’ na ‘accidens’ yanafuata aina ya falsafa ya Aristotele.
1711 WA XLII, 123-125.
1712 Kilatini: ‘Qualitas.’
ya milele ya Mungu na kifo cha milele, hata bila kutambua kile kinachotufanya tuteseke”1713 Tena katika Mwa. 3, “Uchungu wa dhambi ya asili umetutia sumu hadi kwenye taji la kichwa chetu kwa kuwa hata sasa hii itaangukia ukamilifu wa asili.” 1714
II. HIARI AU UWEZO WA UBINADAMU
1. Kumekuwa na majadiliano kuhusu hiari, si kati ya wafuasi wa Papa na wenzetu tu, bali pia miongoni mwa wanatheologia fulani wa Ukiri wa Augsburg. Kwa hiyo, kwanza kabisa, tutaelezea wazi uhalisia wa Mabishano haya.
2. Kuhusiana na hiari, mwanadamu anaweza kuonekana na kutazamiwa katika hali nne tofauti kabisa.1715 Suala hili halihusu mwanadamu kabla ya anguko, wala uwezo wake katika mambo ya nje ya maisha haya ya dunia, baada ya anguko na kabla ya uongofu. Hatujadiliani pia kwamba ana hiari gani katika mambo ya kiroho baada ya kuzaliwa upya na Roho Mtakatifu na kuanza kutawaliwa naye, au atakuwa na hiari gani atakapofufuka kutoka kwa wafu. Suala kuu ndilo hili tu: welekevu na akili ya mwanadamu asiyezaliwa upya vinaweza kufanya nini kwa nguvu zake zenyewe ambazo zimebakia baada ya anguko katika kuongoka na kuzaliwa upya kwake mwenyewe? Wakati Neno la Mungu linahubiriwa na neema ya Mungu inatolewa, je, mtu anaweza kujiandaa mwenyewe kwa neema ya jinsi hiyo, kuipokea na kuikubali? Baadhi ya wanatheologia waliokubaliana na Ukiri wa Augsburg wamejadiliana kuhusu suala hili kwa muda wa miaka mingi.1716
3. Kundi moja1717 lilishikilia na kufundisha kwamba, ingawa kwa nguvu zake na bila kipawa cha Roho Mtakatifu, mtu hawezi kutimiza amri za Mungu, kumtegemea Mungu kweli, kumwogopa, na kumpenda yeye, hata hivyo, mtu bado ana mengi ya nguvu zake za asili kabla ya kuzaliwa kwake upya. Anaweza, 1713 EA, Opera, Exegetica XVIII, 320, 321: “Sive igitur peccatum originis qualitatem sive morbum vocaverimus, profecto extremum malum est non solum pati aeternam iram et mortem, sed sgnoscere quidem, quid pateris.”
1714 WA XLII, 123: “Qui isto veneno peccati originis a planta pedis usque ad verticem infecti sumus, siquidem in natura adhuc integra accidere.”
1715 Hali hizi nne tofauti huyafuata mafundisho ya Petro wa Lombardia: ‘Liber sententiarum’ II, dist. 25 cap 6. Agostino pia alizitofautisha itibari nne: kabla ya sheria, chini ya sheria, chini ya neema, na ndani ya amani. Maelezo ya maazimio kadhaa kutoka Rum. 13 - 18, ‘Enchiridion kwa Laurentio’ 118.
1716 Ushambuliaji wa kwanza wa Nikolao wa Amsdorf dhidi Yohana Pfeffinger wa mwaka wa 1556. Mwaka wa 1558, vitabu vingi vilitolewa kuhusu mabishano haya.
1717 Wafasiri wakuu wa shauri hili walikuwa Philipp Melanchthon tangu mwaka wa 1535, katika nakala zake za baadaye za kitabu kiitwacho, ‘Loci communes’ na katika Ukiri wa Augsburg uliobadilika (‘Confessio Augustana variata’), Fungu la XVIII mwaka wa 1540. Pia Yohana Pfeffinger, Viktorino Strigel, Paulo Eber, Georg Major, na vitivo vya theologia katika vyuo vikuu vya Wittenberg na Leipzig miongo ya 1560 na 1570.
572
kwa kiasi fulani, kujiandaa mwenyewe kwa neema na kuikubali ingawa kwa udhaifu, lakini bila ya kipawa cha Roho Mtakatifu hataweza kutimiza lolote kwa nguvu hizi bali atashindwa katika mapigano.
4. Kwa upande mwingine, walokole wa zamani1718 na wapya wamefundisha kwamba, Mungu humwongoa mwanadamu kwa Roho wake Mtakatifu na kumleta kwenye ufahamu wa wokovu wa Kristo bila njia na vyombo vyovyote vya maumbile. Yaani, bila mahubiri ya nje wala kulisikia Neno la Mungu.
5. Madaktari safi wa Ukiri wa Augsburg1719 wamesisitiza na kufundisha dhidi ya vikundi hivi viwili kwamba, mwanadamu amepotoka kwa sababu ya anguko la wazazi wetu wa kwanza katika mambo ya kimungu kuhusu uongofu na wokovu wa nafsi yake hata kuwa kipofu kabisa. Hivyo basi, haelewi na hataweza kulielewa Neno la Mungu linapohubiriwa. Badala yake, analichukulia kuwa ni upumbavu. Kwa ari yake mwenyewe, hatajisogeza kwa Mungu bali amekuwa na amebaki kuwa adui wa Mungu, mpaka Roho Mtakatifu na nguvu yake na kwa Neno linalohubiriwa na kusikilizwa, kwa neema safi tu, bila mwanadamu kushiriki kwa namna yoyote, amemtekelezea kuongoka, imani, kuzaliwa upya, na mageuzi ya kufanywa mpya.
6. Ili kuyatatua mabishano haya kwa njia ya Kikristo na kulingana na Neno la Mungu na kuyatimiliza kwa njia ya neema ya Mungu, tunayatoa mafundisho yafuatayo, imani, na ukiri wetu. Akili, moyo, na nia ya mtu asiyezaliwa upya kwa uwezo wake wa asili haiwezi, kuelewa, kuamini, kupokea, kuwaza, kutaka, kuanza, kutenda, kufanya, kuvuta, au kushirikiana na lolote katika mambo ya kiroho na ya kimungu. Kinyume chake, amekufa na kuharibika kabisa kuhusu jambo lolote jema. Baada ya anguko na kabla ya kuzaliwa upya, hakuna hata chembe ya uwezo wa kiroho hata kidogo iliyobaki au kupatikana ndani ya asili ya mwanadamu ambayo kwayo, angeweza kujiandaa mwenyewe kwa neema ya Mungu au kuipokea neema iliyotolewa. Hana uwezo wowote wa kuipokea neema na hawezi kujifanya mwenyewe kuwa nao. Kwa uwezo wake mwenyewe, hata kwa msaada wake wowote, yaani, wote, nusu, au kwa kiwango chake kidogo, hawezi kutenda, kuvuta, au kushirikiana katika kuongoka kwake ikiwa, “yeye mwenyewe kama kuja kutoka kwake mwenyewe”1720 ila ni mtumwa wa dhambi (Yn. 8:34), na mfungwa wa Ibilisi anayemwendesha (Efe. 2:2; 2 Tim. 2:26). Kwa hiyo basi, hiari ya asili inaweza kutenda lile ambalo linamchukiza Mungu tu na 1718 Hawa ni miongoni mwa watu wa zamani katika karne ya kumi na sita, yaani, Wamesaliano au Waeukhito, Walutheri waliwalaumu Gaspar Schwenckfeld na Ulrich Zwingli kwa kosa hilo. 1719 Matthias Flacius (mpaka 1560) Nikolao wa Amsdorf, Tilemann Heshusius, Yohana Wigand, Simon Musaeus, Joachim Mörlin, na Nikkolao Gallus. 1720 2 Kor. 3:5.
ndilo lililo dhidi ya mapenzi yake kulingana na jinsi na asili yake iliyopotoka.
8. Tamko hili na jibu kuu kwa swali lililoulizwa mwanzoni mwa fungu hili na Ajili ya Ubishi, vinathibitishwa na sababu zifuatazo kutoka katika Neno la Mungu. Ni kweli kwamba, zinapinga kiburi cha akili na falsafa, ila pia tunajua kwamba “hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu,”1721 na kwamba, mafungu ya imani yanapaswa kuhukumiwa kwa Neno la Mungu peke yake.
9. Kwanza, ingawa akili ya mwanadamu au ujuzi wa asili bado una chembe hafifu ya ufahamu kutoka katika fundisho la sheria (Rum. 1:19-21, 28, 32) kwamba, Mungu hupatikana, hata hivyo, akili ndiyo ujinga, upofu, na upotovu. Hata watu wenye akili sana na walioelimika zaidi hapa duniani ambao labda husoma au husikia Injili ya Mwana wa Mungu na ahadi ya wokovu wa milele, hawawezi, kwa nguvu zao wenyewe, kuifahamu, kuitambua, kuielewa, au kuiamini na kuipokea kama ukweli. Kinyume chake, kadiri wanapozidi kutambua mambo haya ya kiroho kwa akili zao, kwa bidii, na kwa moyo, ndivyo watatambua na kuamini kidogo zaidi. Wataona kwamba, yote ni upumbavu na uongo mtupu hadi Roho Mtakatifu anapowaangazia na kuwafundisha. 10 Ni kama jinsi Mt. Paulo anavyosema katika 1 Kor. 2:14: “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.” Tena “Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuuzi wa lile Neno linalohubiriwa” (1 Kor. 1:21). Wengine, ambao hawajazaliwa upya na Roho wa Mungu, “. . . katika ubatili wa nia zao; ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarakanishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao” (Efe. 4:17-18). “. . . wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni” (Mt.13:13, 11). “Hakuna afahamuye; hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja” (Rum. 3:11-12). Kwa hiyo, Maandiko Matakatifu humwita mtu wa asili “giza” kwa urahisi katika mambo ya kiroho na ya kimungu (Efe. 5:8; Mdo. 26:18). “Nayo nuru yang’aa gizani (yaani, katika giza, dunia pofu ambayo haimjui wala haimtambui Mungu), wala giza halikuiweza” (Yn.1:5)1. Kadhalika, Maandiko Matakatifu hufundisha kwamba, mtu aliye ‘dhambini’ si mnyonge na mgonjwa tu, bali kwamba, kwa kweli hana uhai na ni mfu (Efe. 2:1, 5; Kol. 2:13).
11. Sawa na maiti ambayo haitaweza kujiandaa au kujifadhili yenyewe, kupata tena maisha yake ya duniani, kwa nguvu zake, vivyo hivyo, mtu aliye mfu kiroho 1721 1 Kor. 3:19.
katika dhambi hataweza kujiandaa mwenyewe na kwa uwezo wake mwenyewe. Isitoshe, hataweza kuipokea haki ya kiroho, ya kimbingu, na ya uzima, isipokuwa Mwana wa Mungu awe amemweka huru kutoka kifo cha dhambi na amfanye mzima.
12. Hivyo basi, Maandiko Matakatifu yanakataa kabisa welekewu, moyo, na nia ya mtu wa asili, uwezo wowote, ustadi, werevu, na upeo wa kufikiri, kuelewa, kuanzisha, kutaka, kuchukua hatua, kutekeleza, kuvuta peke yake au pamoja, kitu chochote kilicho chema katika mambo ya kiroho: “Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu” (2 Kor. 3:5). “Wote hawana uwezo” (Rum. 3:12) “Neno langu halimo ndani yenu (Yn. 8:37). “Giza halikuiweza” (Yn. 1:5). “Mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei au, jinsi neno la Kiyunani lisemavyo hasa, hawezi kufumbata au kushikilia au kutambua mambo ya Roho wa Mungu yaani, hana uwezo katika mambo ya kiroho; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu.”1722 13. Zaidi sana, hakika, hataweza kuiamini Injili, kuiitikia, na kuihesabu kuwa ukweli. Nia ya asili ya binadamu “ni uadui juu ya Mungu; kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii” (Rum. 8:7). 14. Lile Mwana wa Mungu alisemalo litabaki milele kama muhtasari wake: “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”1723 Mt. Paulo anasema: “Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema” (Flp. 2:13). Aya hii ni tamu kwa Wakristo wacha Mungu ambao hugundua katika mioyo yao cheche ndogo na shauku ya neema ya Mungu na wokovu wa milele. Ni faraja kubwa kwao kujua kwamba Mungu mwenyewe ameuamsha mwanzo huu wa uchaji wa kweli ndani ya mioyo yao na anataka pia kuendelea kuwaimarisha katika hali yao ya udhaifu mkubwa na kuwasaidia ili wapate kustahamili kubakia katika imani ya kweli mpaka mwisho wao.
15. Hapa, maombi yote ya watakatifu kwa mafundisho, mwanga, na utakaso wa Mungu. Kwa maombi haya, wanaonyesha kwamba, hawawezi kuyapata wanayomwomba Mungu kwa uwezo wao wa asili. Zab. 119 peke yake imeyataja maombi ya Daudi zaidi ya mara kumi,1724 akimwomba Mungu ampatie yeye ufahamu ili aweze kutambua na kujifunza mafundisho yake ya kimungu kwa usahihi. Nyaraka za Mt. Paulo pia zimeyataja maombi ya jinsi hiyo (Efe. 1:17,18; Kol.1:9; Flp. 1:9, 10). Maombi na kauli hii kuhusu ujinga na udhaifu wetu havikuandikwa ili tuwe walegevu na wavivu katika kusoma, kusikia, na
1722 1 Kor. 2:14.
1723 Yn. 15:5 1724 Zab. 119:7,18, 19, 26, 27, 33, 34, 66, 124, 125, 135, 144, 169, 171.
kutafakari Neno la Mungu. Kinyume chake, viliandikwa ili kutuwezesha, zaidi ya mambo yote, kumshukuru Mungu kwa mioyo yetu yote kwa ajili ya kutukomboa kupitia kwa Mwanawe kutoka kwa giza la ujinga, kifungo cha dhambi, kifo, kutuzaa upya, na kutuangaza kwa Ubatizo na Roho Mtakatifu.
16. Baada ya Mungu kutuwashia na kututendea mwanzo wa imani ya kweli na maarifa yake, kwa Roho Mtakatifu wake katika Ubatizo, tunapaswa kumwomba daima ili atuhifadhie imani na vipawa vyake vya kimbingu ndani yetu, kwa Roho na neema yake hiyo hiyo, kwa njia ya mazoezi na masomo ya kila siku ya Neno lake, akiviimarisha siku kwa siku na kuvihifadhi mpaka mwisho. Mahali ambapo Mungu mwenyewe si mwalimu, hatuwezi kusoma au kujifunza lolote linalompendeza Yeye na lenye manufaa kwetu na kwa wengine.
17. Pili, Neno la Mungu, linashuhudia kwamba, katika mambo ya kimungu, akili, moyo, na nia ya mwanadamu wa asili, havijajitenga tu na Mungu, bali vimepotoka dhidi ya Mungu kwa upande wa maovu yote. Akili, moyo, na nia si dhaifu tu, hafifu, potovu, na vivu kwa ubora, bali pia vimeharibiwa vibaya sana na dhambi ya asili, vimetiliwa sumu na kupotoshwa kabisa kiasi kwamba, tabia na asili zao ni mbaya na kaidi na maadui kweli kweli wa Mungu. Wakati huo huo, zina nguvu, uzima, na juhudi sana katika mambo yote ambayo hayampendezi Mungu na mapenzi yake. “Mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake” (Mwa. 8:21). “Moyo [wa mtu] huwa mdanganyifu na mbaya mno,” yaani, umepotoka sana na umejaa taabu kiasi kwamba, hakuna anayeweza kuuelewa (Yer. 17:9). Mt. Paulo anaifafanua aya hii: “Nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu” (Rum. 8:7), na tena, “Na roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana” (Gal. 5:17). “Twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi” (Rum. 7:14). Baadaye kidogo, Mt. Paulo anasema: “Najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; . . . kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani (ambao Roho Mtakatifu ameuumba); lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka wa ile sheria ya dhambi” (Rum. 7:18, 22, 23).
18. Iwapo nia ya asili au kimwili ya Mt. Paulo na watu wengine waliozaliwa upya inapigana dhidi ya sheria ya Mungu, hata baada ya kuzaliwa kwao upya, lazima iwe kaidi na hasimu zaidi kupambana na sheria na mapenzi ya Mungu kabla ya kuzaliwa upya. Kutokana na haya, ni dhahiri jinsi tunavyoonyesha kwa kirefu zaidi katika fungu hili kuhusu dhambi ya asili - ambalo kwalo, tunataka kurejelea kwa ajili ya ufupi – kwamba, hiari pamoja na uwezo wake wa asili haviwezi kutenda pekee. Isitoshe, haviwezi kutekeleza pamoja chochote kwa
kuongoka kwa mwanadamu, kuhesabiwa haki, wokovu, kufuata, kuamini, na kukubali wakati Roho Mtakatifu anamkaribisha kwenye neema na wokovu wa Mungu kwa njia ya Injili. Kinyume chake, kwa sababu ya asili mbaya na kaidi ambayo alizaliwa nayo, yeye hupiga vita kushindana na Mungu na mapenzi yake mpaka Roho Mtakatifu amwangazie na amtawale.
19. Kwa hiyo basi, Maandiko Matakatifu huilinganisha mioyo ya watu wasiozaliwa upya na jiwe gumu,1725 ambalo hushindana kuliko kuzaa katika njia iwayo yote mtu alishikapo, au ambao hawachunwi,1726 au na mnyama wa mwitu asiyekatwa.1727 Kusema haya, hakumaanishi kwamba, tangu anguko, bado mtu si kiumbe chenye akili, au kwamba, aliongoka kwa Mungu bila kusikia na kutafakari kuhusu Neno la Mungu, au kwamba, haelewi au hatendi kwa hiari na kiasi mema na mabaya katika mambo ya nje na ya dunia.
20. Ni jinsi Luther asemavyo katika ufafanuzi wake kuhusu Zab. 911728 “Katika mambo ya dunia na ya nje yanayoathiri malezi na mahitaji ya mwili, mtu amekuwa kweli mjanja sana, mwerevu na mwenye shughuli nyingi sana. Hata hivyo, katika mambo ya kiroho na ya kimungu, ambayo yanahusu wokovu wa nafsi yake, binadamu ni kama nguzo ya chumvi, kama mke wa Lutu, naam, kama gogo au jiwe, kama sanamu isiyokuwa na uhai, isiyotumia mdomo wala macho wala akili wala moyo, 21. Kwa kuwa mtu haoni au hatambui hasira ya Mungu iliyo ya kuogofya na katili juu ya dhambi na kifo. Badala yake, yeye husonga mbele zaidi bila hofu1729 hata kwa ujuzi wote na makusudi kabisa, na kwa hiyo, hujiingiza katika maelfu ya hatari, mwisho katika kifo, na hukumu ya milele. Maombi yote, haja zote, na maonyo yote ni batili. 22. Haifai kutisha, kukaripia, au hata kufundisha na kuhubiri,” mpaka Roho Mtakatifu amwangaze, amgeuze, na amzae upya, hali ambayo kwayo, mtu peke yake aliumbwa wala si jiwe au gogo. Mungu ameziacha kabisa na milele roho mbaya zilizoanguka, kwa hukumu yake kali na ya haki. Hata hivyo, katika huruma yake safi na maalumu, ametamani kwamba, asili ya kibinadamu iliyo maskini, iliyoanguka, na iliyopotoka iweze tena kuwa mshiriki katika uongofu, neema ya Mungu, na uzima wa milele, si kwa ustadi wa wepesi, uwezo, au ustahimilivu, kwa kuwa asili yetu ya kibinadamu
1725 Eze. 36:26; 5:3.
1726 Hos. 6:5.
1727 Zab. 73:22.
1728 Dondoo hili si halisi kutoka kwa ‘Ufafanuzi wa Zaburi 90’ wa Luther ila ni fasili iliyoongezewa kutoka kwa maelezo yake kuhusu Hosea 6 na mahubiri yake kuhusu somo la waraka la Siku ya Krismasi (Tit. 3) na pia Somo la Injili la Jumapili ya tatu baada ya Epifania (Mt. 8:1-13). Andiko la pembeni katika tafsiri ya Kilatini la mwaka wa 1584 linayaorodhesha madondoo haya yote kwa uaminifu.
1729 Kijerumani: ‘Sicherheit; ‘Kilatini: ‘Securitas,’ yaani, ‘uthabiti’ (‘batili’) hali iliyoko bila hofu na ghadhabu ya Mungu.
imo katika ukaidi wa uadui dhidi ya Mungu. Bali inafanyika kwa neema peke yake, kwa njia ya kazi ya Roho Mtakatifu yenye neema na nguvu. 23. Dk. Luther anaiita ‘uwezo’1730 ambao anauelezea ifuatavyo: “Wakati mababa wanaitetea hiari, wanasema kwamba, uwezo huu unaweza kuupata uhuru kwa njia ambayo neema ya Mungu inaweza kuigeuza kuelekea wema hata kuupata uhuru wa kweli, shabaha ambayo kwayo, iliumbwa1731 kiasili. Agostino aliandika katika mwelekeo huo huo katika kitabu chake cha pili kiitwacho, ‘Dhidi ya Yuliano.’1732
24. Awali, amekuwa akiangazia kuzaliwa upya, kufanywa upya, na kuvutwa na Roho Mtakatifu, kiukweli, mwanadamu mwenyewe kwa nguvu zake za asili, hawezi kufanya lolote linalohusu jambo moja la kiroho katika kuongoka au kuzaliwa kwake upya ingawa jiwe, boriti au bonge la udongo1733 linaweza. Ijapokuwa anaweza kumiliki viungo vya mwili wake, kusikiliza Injili, na kuitafakari kwa kiasi kidogo na pia anaweza hata kuizungumzia, jinsi inavyoonekana kwa Mafarisayo na wanafiki, hata hivyo, anaifikiria kuwa ni upuuzi na hawezi kuiamini. Kwa hili, yeye ndiye mbaya kuliko boriti kwa sababu ni mpinzani na adui wa mapenzi ya Mungu mpaka Roho Mtakatifu atende kazi ndani yake kwa kumwashia, kumtekelezea imani na utii, na mema mengine yanayompendeza Mungu.
25. Tatu: Maandiko Matakatifu hayahesabu nguvu za kibinadamu za hiari ya asili, uongofu, imani katika Kristo, kuzaliwa, kufanywa upya, na kila linalohusika na mwanzo na mwisho wake, iwe kamilifu au nusu au kidogo au kipande kidogo mno, bali ni ‘solidum,’ yaani, kazi ya Mungu tu na Roho Mtakatifu, kama Utetezi unavyotamka.1734
26 Kwa kiasi fulani, akili na hiari vinaweza kuzaa maisha ya nje ya kimaadili. Lakini Roho Mtakatifu peke yake huzaa upya na huutekeleza uzima wa ndani, yaani, yeye huujalia1735 moyo mpya, nia, na nafsi. Yeye hufungua moyo na ufahamu wa kuelewa Maandiko Matakatifu na kulitii Neno la Mungu, jinsi ilivyoandikwa katika Lk. 24:45: “Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.”
1730 Kilatini: ‘capacitas.’ Kwa asili, istilahi hii ilifuatwa na “non activam sed passivam” (“uwezo usiokuwa hai bali baridi”). Maneno haya yaliondolewa kutoka kwa aya ya Kijerumani ya toleo la mwaka wa 1580 baada ya capacitatem. Mkazo katika maana hii ni kwamba, mtu hafanyi lolote, ila kwamba, tendo fulani limefanywa kwake. Istilahi yenyewe haionyeshi kwamba, uvumilivu huu umekusudiwa. Hivyo, hali yake nzuri na ya kustahili ina maana tu kwamba, ni kiumbe ambacho kinaweza kuongoka tena (subjectum convertendum).
1731 Kilatini: “Quando patres liberum arbitrium defendunt, capacitatem libertatis eius praedicant, quod scilicet verti potest ad bonum per gratiam Dei et fieri revera liberum, ad quod creatum est.” Toleo la Jena la mwaka wa 1556, Buku la kwanza, uk. 236; WA 2, 647, 28-31.
1732 ‘Contra Julianum,’ 2, 8, 23-30.
1733 Yn. 6:44; Isa. 45:9; 64:7; Yer. 18:6.
1734 Utetezi, 18, 7, 8. 1735 Yaani, tunakirimu.
Vivyo hivyo, “Lidia . . . akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo” (Mdo. 16:14). “Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu” (Flp. 2:13). Mungu anatoa toba (Mdo. 5:31; 2 Tim. 2:25). Tena, anatoa imani kwa kuwa “Imetolewa kwenu na Mungu kwamba mweze kuamini” (Flp.1:29). “Ni kipawa cha Mungu” (Efe. 2:8). “Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye” (Yn. 6:29). Mungu anatoa moyo wa kuelewa, macho yanayotazama, na masikio yanayosikia (Kum. 29:4; Mt. 13:15). Roho Mtakatifu katika Roho wa “kufanya upya” (Tit. 3:5,6). Mungu huondoa moyo mgumu wa jiwe na kuweka moyo wa mpya nyama na mwororo ili tuweze kutembea katika amri zake (Eze. 11:19; 36:26; Kum. 30:6; Zab. 51:12); anatuumba sisi katika Kristo Yesu kwa matendo mema (Efe. 2:10); na anatufanya viumbe vipya (2 Kor. 5:17; Gal. 6:15). Kwa ufupi, kila karama njema hutoka kwa Mungu (Yak. 1:17). Hakuna yeyote awezaye kuja kwa Kristo mpaka Baba amvute kwake (Yn. 6:44). “. . . hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia (Mt. 11:27). “. . . hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu” (1 Kor. 12:3). “. . . maana pasipo mimi,” Yesu anasema, “ninyi hamwezi kufanya neno lo lote” (Yn. 15:5). “. . . utoshelevu wetu watoka kwa Mungu” (2 Kor. 3:5). “Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? (1 Kor. 4:7). 27 Ni aya hii pekee ambayo, kwa kauli yake mwenyewe, Mt. Agostino, ilimshawishi kukataa wazo lake la awali lenye kosa kama alivyoandika katika andiko lake ‘Majaliwa:’1736 “Nilikosea hapa nilipofikiri kwamba, neema ya Mungu inajumuishwa katika hili tu, kwamba, Mungu hufunua mapenzi yake kwa njia ya kuuhubiri ukweli, ili kuiitikia Injili hii inapohubiriwa pia na kazi yetu inayotegemea nguvu zetu.” Kadhalika: “Nilikosea kabisa niliposema kwamba, kuiamini Injili na kujivunia mambo mema vipo ndani ya nguvu zetu. Ni kazi ya Mungu kutoa uwezo wa kutekeleza kitu fulani kwa wale wanaoamini na kutaka.”
28. Mafundisho haya yamejengwa juu ya Neno la Mungu na yanatamkwa na Ukiri wa Augsburg na maandiko mengine yaliyotajwa hapo juu, jinsi ushuhuda ufuatao utakavyoonyesha:
29. Fungu la Ishirini la Ukiri wa Augsburg huelezea hivi: “Kwani bila Kristo, imani, na Roho Mtakatifu, wanadamu wako chini ya nguvu za Ibilisi anayewahimiza washiriki katika dhambi mbalimbali. Kwa hiyo, tunaanza na mafundisho ya imani. Kwa hayo, Roho Mtakatifu ametolewa kuonyesha kwamba, Kristo hutusaidia na kutulinda dhidi ya Ibilisi.” Kitambo kidogo baadaye 1736 ‘De predestinatione’ 3,7.
inaeleza kwamba: “Bila Kristo, unyonge wa akili na uwezo wa mwanadamu ni wa aina hii, kwamba, hawezi kumpinga Ibilisi ambaye huwashawishi watu kutenda dhambi.” 1737
30. Kauli hizi huonyesha wazi kwamba, Ukiri wa Augsburg haukubali kwamba, nia ya kibinadamu ni huru katika mambo ya kiroho. Kinyume chake, unaelezea kwamba, mtu ni mfungwa wa Ibilisi. Kwa hiyo, ni vipi mtu anaweza kuitegemea Injili au Kristo kwa nguvu zake mwenyewe?
31. Utetezi wa Ukiri wa Augsburg hufundisha ifuatavyo kuhusu hiari: “Pia tunatamka kwamba, kwa kiasi fulani akili ina hiari. Kwani katika mambo ambayo yanaweza kutambuliwa na akili, tuna hiari.” Kitambo kidogo baadaye inaeleza: “Mioyo ambayo haina Roho Mtakatifu haina hofu ya Mungu, haina imani, haitegemei au haimwamini Mungu kwamba, anaisikia, kwamba, anasamehe dhambi zao, au kwamba, anaisaidia katika matatizo. Kwa kweli, mioyo hii haina Mungu kabisa. Mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mema, na bila imani hakuna yeyote awezaye kumpendeza Mungu. Kwa hiyo, ingawa tunakubali kwamba, inabaki ndani ya nguvu zetu na kufanya kazi za nje, tunatangaza kwamba, katika mambo ya kiroho, hiari na akili zetu haviwezi kufanya lolote.”,1738 Kutokana na haya, tunaona wazi kwamba, aidha Utetezi haukubali hiari ya mtu au uwezo wowote wa kuanzisha kitu kizuri au kushiriki kwacho kwa hoja yake yenyewe.
33. Mafungu ya Smalkaldi huyakataa makosa yafuatayo kuhusu hiari: “Kadhalika, mwanadamu ana hiari hata kuamua ama kutenda mema au kuyaacha mabaya.” Kitambo kidogo baadaye: “Haikuandikwa katika Maandiko Matakatifu
1737 ‘Ukiri wa Augsburg’ 20:28-34 kulingana na Toleo la Quarto la Wittenberg lililosahihishwa sana mwaka wa 1531.
1738 ‘Ukiri wa Augsburg’ 18:4-6 kulingana na Toleo la Quarto. Sehemu hii hulingana na tafsiri hii: “Basi, sisi hatukatai kabisa hiari ya binadamu. Hiari ya binadamu ina uhuru katika matendo na mambo yanayoeleweka kwa akili ya binadamu. Kwa kiasi fulani, inaweza kuitengeneza haki ya raia au haki ya matendo. Inaweza kumzungumzia Mungu na kumwabudu kwa njia fulani kwa matendo ya nje. Inaweza kuwatii mahakimu na wazazi. Inaweza kuuacha uuaji, uzinzi, au wizi kwa njia ya nje. Kwa kuwa asili ya ubinadamu bado ina ufahamu na hukumu kuhusu mambo yanayohusu hisi, inaweza kubakia na nia, hiari kuchagua katika mambo haya, na uhuru na uwezo wa kutekeleza haki ya raia. Maandiko Matakatifu yanaliita jambo hilo haki ya kimwili inayotengenezwa na asili ya kimwili, yaani, asili yenyewe bila Roho Mtakatifu. Hata hivyo, nguvu ya ashiki mbaya ni ya jinsi hiyo hata huwafanya watu wazitii tamaa mbaya zaidi kuliko akili timamu. Licha ya hayo, Ibilisi, anayefanya kazi, kulingana na maneno ya Mt. Paulo, haachi kuuhimiza udhaifu huu wa asili katika makosa mbalimbali katika wana wa kuasi. Kwa hiyo, haki ya raia huadimika sana kati ya watu, jinsi tulivyoona kwamba, hata wanafalsafa ambao walionekana kuitafuta haki hii, hawakuifuata. Lakini ni uongo kabisa kusema kwamba, mtu hatendi dhambi akitenda matendo ya amri nje ya neema. Licha ya hayo, wanaongezea kwamba, kadiri ya matendo haya, huustahili msamaha wa dhambi na haki kwa kuwa mioyo ya binadamu, bila Roho Mtakatifu, pia haina hofu na tegemeo kwa Mungu. Haiamini kwamba, inasikilizwa, inasamehewa, inasaidiwa, na inahudumiwa na Mungu. Kwa sababu mioyo hii ni miovu: “Mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mema;” na, “bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu.
kwamba, Roho Mtakatifu na vipawa vyake ni muhimu kwa tendo jema.”1739
34. Mafungu ya Smalkaldi husema zaidi: “Toba ya Wakristo itadumu hadi kifo, kwa kuwa inaipinga dhambi iliyobaki katika mwili wakati wa maisha yote. Jinsi Mt. Paulo anavyoshuhudia katika Rum. 7:23, anapigana vita na sheria katika viungo vyake, na anafanya hivyo, si kwa nguvu zake mwenyewe, bali kwa karama ya Roho Mtakatifu ambayo hufuatia msamaha wa dhambi. Daima, karama hii hung’oa na kufagia dhambi ambayo imebakia na hufanya kazi kwa bidii ili kumwezesha mwanadamu kuwa safi na mtakatifu kabisa.”1740 35 Maneno haya hayasemi lolote kuhusu nia yetu hata kidogo, wala hayasemi kwamba, hata kwa waliozaliwa upya, nia inaweza kufanya lolote, bali yote yanajumuisha kipawa cha Roho Mtakatifu, ambaye huwasafisha wanadamu na kila siku huwafanya watu kuwa wacha Mungu na watakatifu zaidi. Nguvu zetu zenyewe zimetolewa hapa kabisa.
36. Imeandikwa pia katika Katekisimo Kubwa ya Dk. Luther: “Katika jamii hii ya kanisa la Kikristo, mimi nami ni sehemu na kiungo pia, mshiriki, na mwenzi katika mibaraka yote inayomiliki. Nililetwa humo na Roho Mtakatifu na kuunganishwa kwa ukweli kwamba, nimelisikia na ningali ninalisikia Neno la Mungu ambalo ndilo hatua ya kwanza ya kuingilia. 37. Kabla ya kuendelea kiasi hicho, tulikuwa wa Ibilisi kabisa na hatukujua kitu kumhusu Mungu na Kristo. Hadi siku ya mwisho, Roho Mtakatifu hubaki pamoja na jamii takatifu au Wakristo. Kwa njia yake, hutukusanya akitumia kulifundisha na kulihubiri Neno. Kwa njia yake, yeye huumba na kuongezea utakaso, akiusababisha ukue kila siku, uwe imara katika imani, na katika matunda ya Roho.”1741 38.Kwa maneno haya, Katekisimo haitaji lolote kuhusu nia yetu au mchango wetu, bali inayaweka yote kwa Roho Mtakatifu. Yaani, kwamba, anatuleta katika Ukristo1742 kwa njia ya huduma ya mahubiri, anatutakasa ndani yake, na anasababisha kwamba, tukue katika imani, na tuyatende matendo mema zaidi na zaidi kila siku.
39. Ingawa waliozaliwa upya wakiwa bado katika maisha haya, hufikia kiwango cha hata kuweza kutamani wema na kuufurahia na zaidi, kweli hasa huutekeleza wema na kuzidi kwao. Hata hivyo, jinsi ilivyotajwa hapo juu, mambo haya hayatoki kwa nia au uwezo wetu wenyewe, bali Roho Mtakatifu, huzaa na hufanya nia na tendo jinsi hiyo kama vile Mt. Paulo asemavyo (Flp. 2:13). Anaihesabu kazi hii kwa Mungu peke yake pia jinsi asemavyo katika Efe. 2:10: “Tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo
1739 ‘Mafungu ya Smalkaldi’ 3:1, 5, 10.
1740 ‘Mafungu ya Smalkaldi’ 3:3, 40.
1741 Katekisimo Kubwa: ‘Ukiri wa Imani’ 52-53.
1742 Andiko la Kijerumani: ‘Christenheit;’ Andiko la Kilatini: ‘Ecclesia’ (‘Kanisa’).
tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”
40. Katika Katekisimo Ndogo ya Dk. Luther, imeandikwa: “Ninaamini ya kwamba, kwa akili au nguvu zangu mwenyewe, siwezi kumwamini Bwana wangu Yesu Kristo, wala kumfikia. Lakini Roho Mtakatifu ameniita kupitia Injili, ameniangaza, amenipa vipaji vyake, amenitakasa, na kunilinda ili nishike imani ya kweli. Vivyo hivyo, huwaita Wakristo wote ulimwenguni, huwakusanya, huwaangaza, huwatakasa, na kuwalinda wakae wakimshika Yesu Kristo kwa imani ya kweli iliyo moja tu.”1743
41. Maneno haya yanapatikana katika maelezo ya ombi la pili ya Sala ya Bwana: “Hili linafanyikaje? Jibu: Wakati Baba wa mbinguni anatupatia Roho Mtakatifu wake ili, kwa neema yake tuweze kuliamini Neno lake takatifu na kuishi maisha ya kimungu, wakati huu na baadaye milele.”1744
42. Shuhuda hizi huthibitisha wazi kwamba, kwa nguvu zetu wenyewe, sisi hatuwezi kumfikia Kristo, bali kwamba, Mungu lazima atupatie Roho Mtakatifu ili atuangazie, atutakase, na atulete kwa Kristo katika imani ya kweli na kutulinda katika yeye. Shuhuda hizi hazitaji lolote kuhusu hiari na kushiriki kwetu. 43 Hapo, tunaongezea kauli moja kutoka katika andiko la Dk. Luther liitwalo ‘Ukiri Mkuu wa Chakula cha Bwana’1745 ambapo anarudia kutangaza, kwa maneno yafuatayo, katika shahada yake kwamba, anakusudia kuyashika mafundisho haya mpaka mwisho wake: “Vivyo hivyo, ninakataa na kulaani kama kosa tu, kila fundisho ambalo huitukuza hiari yetu, kwa kuwa linapinga wazi mafundisho yanayotangaza msaada na neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Yaani, kifo na dhambi vimo nje ya Kristo. Mabwana wetu na Ibilisi ni mungu na mtawala wetu. Hakuna nguvu au uwezo, hakuna werevu au ufahamu, ambao kwao, tunaweza kujiandaa wenyewe kwa haki na maisha au kuvitafuta. Kinyume chake, hatuna budi kubaki vipofu, wafungwa, na mali ya dhambi na Ibilisi, hata kufanya na kufikiri yanayowapendeza wao na ambayo ndiyo kinyume cha Mungu na amri zake.”
44. Dk. Luther, mwenye kumbukumbu ya heri na takatifu, kwa maneno haya, haikubali nia yetu kuwa na nguvu yoyote ya kujiandaa sisi wenyewe kwa haki na kuitafuta. Badala yake, anasisitiza kwamba, mtu ambaye ni kipofu na mateka hutenda tu mapenzi ya Ibilisi dhidi ya Bwana Mungu. Kwa hiyo, nia ya mwanadamu haina nafasi yoyote ya kuusonganisha uongofu wake. Mungu
1743 ‘Katekisimo Ndogo:’ Ukiri, 6.
1744 ‘Katekisimo Ndogo:’ Sala ya Bwana, Ombi la Pili.
1745 Kijerumani: ‘Grosser Bekenntnis vom Abendmahl Christi’ mwaka wa 1528; WA, 26: 502, 35-503, 24.
582
mwenyewe lazima amvute mwanadamu na kumzaa upya. Bila hivyo, moyo wetu wenyewe haufikiri hata mara moja kuigeukia Injili takatifu na kuipokea. Dk. Luther analijadili suala hili lote katika kitabu chake kiitwacho,‘Utumwa wa Hiari.’1746 Alikiandika kitabu hiki chenye maelezo bora na kamili dhidi ya Erasmus. Jambo hili lilielezwa kwa uangalifu mkubwa na kwa undani kabisa. Tena, katika ufafanuzi wake bora wa Kitabu cha Mwanzo, hasa sura ya 26, anarudia na kulielezea wazo hilo hilo.1747 Katika maandiko haya, anachukua pia mambo fulani mengine ya kujadiliwa ambayo Erasmus aliyatoa, kwa mfano, ‘mambo kamili ya lazima’,1748 jinsi Luther alivyotaka yaeleweke na kupokelewa dhidi ya sintofahamu na uasi wote. Kwa hiyo, tunayataja maandiko haya na pia kuyarejelea kwa watu wengine.
45. Kwa hiyo, watu wanafundishwa vibaya wakielezwa kwamba, mwanadamu mwenyewe ana uwezo uliobaki wa kutosha hata kutaka kuipokea Injili na kujifariji nayo, na kwamba, nia yake inasaidia katika kugeuka angalau kidogo tu. Wazo la namna hiyo linayapinga Maandiko Matakatifu ya Mungu, Ukiri wa Augsburg wa Kikristo, Utetezi wake, Mafungu ya Smalkaldi, Katekisimo Kubwa na Ndogo ya Luther, na maandiko mengine ya mwanatheologia huyu mashuhuri na aliyeangaziwa sana.
46. Walokole na wa aina ya Epikuro, hutumia vibaya na kwa njia isiyokuwa ya Kikristo mafundisho haya kuhusu udhaifu na uovu wa nia yetu ya kiasili, na pia kwamba, kuongoka na kuzaliwa upya ni kazi ya Mungu peke yake na si ya uwezo wetu sisi. Kama matokeo ya maneno yao, watu wengi wamekuwa waovu katika uhuni, uvivu, na uzembe katika mazoezi ya Kikristo na nyinginezo kama sala, kusoma vitabu, na taamuli1749 za Kikristo. Wanajadiliana kwamba, kwa kuwa hawawezi kumgeukia Mungu wenyewe, kwa nguvu zao za asili, wataendelea kushindana na Mungu kwa ukaidi wao au mpaka lazima Mungu awaongoe kwa nguvu kinyume cha hiari yao. Wao hujadiliana kwamba, kwa vile kila kitu kinatokea kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, wenyewe hawawezi kufanya lolote katika mambo haya ya Kiroho, hawalijali Neno na sakramenti ila watasubiri mpaka Mungu awamwagie vipawa vyake kutoka mbinguni, bila vyombo vya neema ili waweze kusikia na kugundua kwamba, Mungu amewaongoa kweli.
47. Kwa upande mwingine, watu wenye mioyo yenye woga wanaweza
1746 ‘De servo arbitrio;’ WA, 18:600-727. Luther alikiandika kitabu chake mwaka wa 1525 dhidi ya kitabu cha Erasmus wa Rotterdam (1466-1536) ‘Diatribe de libero arbitrio’ (‘Tahakiki Kuhusu Hiari’) mwaka wa 1524.
1747 ‘Ufafanuzi wa Kitabu cha Mwanzo’ miaka ya 1535-1546; WA, 43:457-463.
1748 Kilatini: ‘De absoluta necessitate.’
1749 Kuhoji, kutafakari.
kuanguka katika mahangaiko makubwa na mashaka, na kutojua kweli iwapo Mungu amewachagua na anapenda kutekeleza ndani yao vipawa vya Roho Mtakatifu wake, kwa kuwa hawafahamu imani imara, motomoto, na utiifu, ila tu wanafahamu udhaifu, mashaka, na taabu.
48. Kwa hiyo basi, kutokana na Neno la Mungu, tutaelezea jinsi mtu anavyomgeukia Mungu, vipi na kwa vyombo gani. Yaani, Neno la kinywa, sakramenti takatifu, na Roho Mtakatifu anataka kuwa na ufanisi wa kufaa ndani yetu kwa kutupatia na kuitekeleza toba ya kweli, imani, nguvu, uwezo mpya wa kiroho, kuyatenda matendo mema, na vipi tunapaswa kujihusisha wenyewe kwa wenyewe na kuvitumia vyombo hivyo.
49. Si mapenzi ya Mungu kwamba, mwanadamu yeyote ahukumiwe, bali watu wote wamgeukie na kuokolewa milele. “Kama mimi niishivyo, . . . sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi” (Eze. 33:11). “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”1750
50. Kwa hiyo, katika wema na huruma zake zisizopimika, Mungu anaruhusu kuihubiri hadharani sheria yake ya kimungu, sheria ya milele, na shauri lake la ajabu sana la kutukomboa. Yaani, Injili Takatifu iokoayo peke yake ya Mwanawe wa milele, Mwokozi na Mkombozi wetu pekee, Yesu Kristo. Hivyo basi, Mungu analikusanya kwake Kanisa la milele kutoka kwa walimwengu. Kwa hiyo basi, ndani ya mioyo ya watu, anatekeleza toba ya kweli, utambuzi wa dhambi zao, na imani ya kweli katika Mwana wa Mungu, Yesu Kristo. Kwa vyombo hivi, Mungu anataka, yaani, Neno lake takatifu linalosikika katika mahubiri au linalosomwa, na Sakramenti zinazotumiwa pia kulingana na Neno lake na, si kwa njia zingine, kuwaita watu kwa wokovu wa milele, kuwavutia kwake, kuwaongoa, kuwazaa upya, kuwatakasa1751 Kwa hiyo, na si katika njia nyingine: 51. “Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuuzi wa lile Neno linalohubiriwa” (1 Kor. 1:21). “Petro atawahubiri maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote” (Mdo. 11:14). “. . . imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa Neno la Kristo” (Rum. 10:17). “Uwatakase kwa ile kweli; Neno lako ndiyo kweli . . . Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao” (Yn. 17:17, 20).
1750 Yn. 3:16.
1751 Kitabu cha Torgau kimezungumzia kusikia, kusoma, na kutafakari kuhusu Neno, ila rejeo kwenye tafakuri liliondolewa ili kuyakwepa matumizi kwamba, mtu asiyeongoka anaweza kutafakari kuhusu Neno kwa njia ifaayo.
Kwa hiyo, Baba wa milele analia kutoka mbinguni: “... msikieni yeye” (Mt. 17:5). Kwa neno ‘yeye,’ anamaanisha Mwanawe mpendwa na pia wote wahubirio toba na ondoleo la dhambi kwa jina lake.
52. Wote wanaotaka kuokolewa lazima wayasikie mahubiri haya. Maana, mahubiri ya Neno la Mungu na kuyasikia ni vyombo vya Roho Mtakatifu ambavyo kwavyo,1752 anataka kuifanya kazi yake kwa nguvu, anataka kuwaongoa wanadamu kwa Mungu ili wawe watu wake, na kuwatekeleza ndani yao waweze kunuia na kutenda.
53. Mtu ambaye bado hajamgeukia Mungu na hajaongoka, anaweza kulisikia na kulisoma Neno hili kwa njia ya nje kwa sababu, jinsi ilivyosemwa hapo juu, hata baada ya anguko, bado mtu anaendelea kuwa na nia kiasi katika mambo ya nje, kwamba, anaweza kwenda kanisani, akasikiliza mahubiri, au asiyasikilize.
54. Basi, kwa vyombo hivyo, yaani, mahubiri na kulisikia Neno, Mungu anajishughulisha na wanadamu. Anaivunja mioyo yetu, na anawavuta watu kwake ili, kwa mahubiri ya sheria, mtu ajifunze kutambua dhambi zake na hasira ya Mungu. Moyo wake husikia hofu kuu, majuto makubwa, na huzuni ya kweli. Halafu, atasikia Injili Takatifu inayotangaza msamaha wa dhambi wenye neema tele katika Kristo. Hivyo basi, cheche ya imani inawashwa ndani yake. Anapokea msamaha wa dhambi kwa ajili ya Kristo na kujifariji kwa ahadi ya Injili. Kwa hiyo, Roho Mtakatifu anayeyatenda haya yote, anaingizwa mioyoni.
55. Hata hivyo, mhubiri apande na kumwagilia maji, msikilizaji akimbie na kutamani. Haya yote yatakuwa batili, iwapo nguvu na kazi ya Roho Mtakatifu havijaongezwa, ambaye kwa Neno linalohubiriwa na kusikilizwa huangaza mioyo ili watu waliamini Neno hili na kuliitikia.
Kusema hivyo hakumaanishi kwamba, mhubiri au msikilizaji hawi na mashaka kuhusu neema hii na kazi ya Roho Mtakatifu. Kinyume chake, lazima wawe na uhakika kwamba, wakati Neno la Mungu linahubiriwa kwa usafi na ukweli, kulingana na agizo na mapenzi ya Mungu, na wakati watu wanalisikia na kulitafakari kwa uangalifu na bidii, kwa uhakika, Mungu yupo na kwa neema yake, anatoa kile ambacho, kwa nguvu zake, mtu mwenyewe hawezi kukichukua au kukitoa. 56. Daima, mwanadamu hapaswi na hawezi kutoa hukumu juu ya kuwepo, kazi na karama za Roho Mtakatifu kwa hisia yake.1753 Yaani, kwa msimimko wa moyo. Kwa sababu, mara nyingi, kazi ya Roho Mtakatifu imefichika na hutokea kama gamba la udhaifu mkuu. Hatuna budi kuwa na uhakika, kwa
1752 Kijerumani: ‘Bei, mit und durch’ (‘kwa, pamoja na, kupitia kwa, kwa njia ya ’). 1753 Kilatini: Ex sensu.’
sababu ya na kuhusu msingi wa ahadi yake, kwamba, Neno linalosikilizwa na kuhubiriwa ni ofisi na kazi ya Roho Mtakatifu, ambaye, kwa hakika, ana nguvu na ni mtendaji katika mioyo yetu (2 Kor. 2:14).
57. Mahali ambapo mtu hataki ama kuyasikia mahubiri au kulisoma Neno la Mungu, bali hulidharau Neno na jamii ya Mungu, hata kufa katika hali hii na kupotea katika dhambi zake, hataweza kujifariji mwenyewe kwa uchaguzi wa milele wa Mungu ama kuipata huruma yake. Kwa maana Kristo ambaye katika yeye, tumechaguliwa, anatoa neema yake kwa watu wote katika Neno na sakramenti zake takatifu. Mapenzi yake imara ni kwamba, tulisikie Neno hili, na ameahidi kwamba, wanapokusanyika pamoja, wawili au watatu, katika jina lake takatifu, yeye yu katikati yao.1754
58. Lakini, mtu asiyeamini,1755 akidharau vyombo vya Roho Mtakatifu na asipotaka kusikia, atatendewa udhalimu wowote kama Roho Mtakatifu hajamtolea nuru bali amemwacha abaki katika giza la kutokuamini kwake na kupotea, jinsi ilivyoandikwa: . . . ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!” (Mt. 23:37).
59. Katika maana hii, inanipasa kusema kwamba, mtu si jiwe au boriti. Jiwe au boriti havishindani na mtu anayelisukuma wala havielewi au kuhisi vinavyotendewa jinsi mwanadamu anavyopingana na Bwana Mungu kwa nia yake mpaka awe ameongoka. Hata hivyo, ni kweli kwamba, kabla ya kuongoka kwake, bado mtu ni kiumbe chenye akili, busara, na hiari ingawa hana ufahamu wa mambo ya kimungu na hana mapenzi ya kutenda mema au lolote kwa uongofu wake. Kwa hiyo, amekuwa mbaya zaidi kuliko jiwe au boriti kwa kuwa anapingana na neno na mapenzi ya Mungu mpaka Mungu amfufue kutoka kwa kifo cha dhambi, ampatie nuru na amfanye mpya kabisa.
60. Ingawa Mungu hamshurutishi1756 yeyote kwa uchaji, kwa kuwa wote wanaompinga Roho Mtakatifu daima na kukataa ukweli, jinsi Stefano anavyowaelezea Wayahudi wakaidi (Mdo. 7:51), hawataongoka. Hata hivyo, Bwana Mungu anamvuta kwake mtu ambaye anapenda kumwongoa, na humvuta yeye kwa njia ambayo welekevu wake uliotandwa na giza utaangazwa na nia ya upinzani itakuwa nia sikivu. Maandiko Matakatifu yanaiita kazi hii uumbaji wa 1754 Mt 18,20.
1755 Kilatini: ‘Homo profanus.’
1756 Katika Majadiliano ya Weimar Viktorino Strigel alishikilia kwamba, kwa jumla, kuondolewa kwa nguvu za binadamu katika uongofu hakuepukiki. Kuufunga uongofu ni shurutisho. Kwa hiyo, alisisitiza jinsi mtu anavyoweza kufanya (modus agendi), busara ambayo humtofautisha na hayawani, na alishikilia kwamba, inategemea matumizi ya namna ya matendo ya mtu kama anaitikia au haitikii mwito wa Injili.
586
moyo mpya.
61. Kwa hiyo, si sawa kusema kwamba, kabla ya kuongoka kwake, mtu ana namna ya kutenda.1757 Yaani, namna au fursa ya kuyatekeleza mambo mema yanayohusu wokovu. Kabla ya kuongoka kwake, mtu ni mfu kabisa katika dhambi (Efe. 2:5). Hivyo basi, hana uwezo wowote wa kuufanya wema au namna yoyote ya kutenda katika mambo ya kiroho.
62. Ila, iwapo mtu anajadili suala la jinsi Mungu anavyofanya ndani ya mtu, ni sahihi kusema kwamba, Bwana Mungu ana njia moja ya kutenda ndani ya mtu aliye kiumbe chenye busara, na namna nyingine tofauti katika viumbe visivyokuwa na busara au katika jiwe au boriti.1758 Hata hivyo, mwanadamu hawezi kuhesabiwa namna yoyote ya kutenda mema katika mambo ya kiroho kabla ya kuongoka kwake.
63. Badala yake, baada ya mtu kuongoka na hivyo, kutiwa nuru, na nia yake kufanywa upya ndipo atakapotaka lililo jema ilimradi amezaliwa upya na amekuwa mtu mpya. Atafurahia sheria ya Mungu kulingana na nafsi yake ya ndani (Rum. 7:22). Kisha, atafanya mambo mema kadiri Roho Mtakatifu anavyompa nia jinsi Mt. Paulo asemavyo: “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.”1759 64 Msukumo huu wa Roho Mtakatifu haumaanishi ‘coactio,’ yaani, shurutisho au sharti, kwa sababu mtu aliyeongoka hufanya yaliyo mazuri kwa hiari jinsi Daudi asemavyo: “Watu wako wanajitoa kwa hiari, siku ya uwezo wako.”1760 Hata hivyo, maneno ya Mt. Paulo yanadumu pia kwa waliozaliwa upya: “Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapigana vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu” (Rum. 7: 22-23). Kadhalika: “Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi” (Rum. 7: 25). Tena: “Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka” (Gal. 5:17).
65. Linalofuatia kutokana na hili ni kwamba, jinsi tulivyosema, mara tu Roho Mtakatifu aianzishapo kazi yake ya kutufanya tuzaliwe upya na kufanywa wapya kwa neno na Sakramenti Takatifu, ni hakika kwamba, tunaweza na 1757 Kilatini: ‘Modus agendi.’
1758 Mkazo huu unaonyesha hasa kinyume cha neno la Nikolao von Amsdorf, ambaye, katika kujaribu kwa juhudi zaidi, ameelezea kutekwa kwa hiari ya mtu akiihukumu kauli ya Strigel, kwamba, “Mungu anafanya tofauti na mtu kuliko viumbe vingine.”
1759 Rum. 8:14. 1760 Zab. 110:3.
lazima tushiriki katika nguvu ya Roho Mtakatifu, ingawa bado tunafanya hivyo kwa udhaifu mkubwa. Ushirika wa jinsi hiyo hauibuki kutokana na nguvu zetu za kimwili na za asili, bali kutoka kwa nguvu mpya na vipawa ambavyo Roho Mtakatifu amevianzisha ndani yetu katika uongofu, 66 jinsi Mt. Paulo anavyotukumbusha kwa baraka na kwa moyo: “Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.”1761 Hii inapaswa ieleweke si katika maana nyingine zaidi ya kwamba, mtu mwongofu hutenda mema kwa wingi, kadiri Mungu anavyomtawala, anavyomwongoza, na anavyomlinda kwa Roho Mtakatifu. Mungu akiuondoa mkono wake wa neema, mtu hawezi kubakia kuwa mtiifu kwa Mungu hata kidogo. Lakini jambo hili lingeeleweka kana kwamba, mwongofu anashirikiana bega kwa bega na Roho Mtakatifu, jinsi farasi wawili wanavyoivuta gari pamoja, mtazamo wa jinsi hiyo hauwezi kukubalika bila hasara katika ukweli wa kimungu kwa vyovyote.
67. Kwa hiyo, kuna tofauti kubwa kati ya watu waliobatizwa na watu wasiobatizwa kwa sababu, kulingana na mafundisho ya Mt. Paulo: “Nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Gal. 3:27) na kweli, wamezaliwa upya. Kwa hiyo basi, nia yao iliwekwa huru,1762 yaani, jinsi Kristo asemavyo, wamewekwa huru tena.1763 Kwa hiyo, hawasikilizi tu Neno la Mungu, bali pia wanaweza kuliitikia na kulipokea, japo ni kwa udhaifu mkubwa.
68. Kwa kuwa katika maisha haya tunapokea tu matunda ya kwanza ya Roho, na kuzaliwa kwetu kupya bado si kukamilifu, vita vya mwili dhidi ya Roho huendelea pia katika wateule na waliozaliwa upya kweli. Hivyo, tofauti kubwa hazionekani tu baina ya Wakristo. Mmoja akiwa dhaifu na mwingine akiwa mwenye nguvu katika Roho. Badala yake, katika maisha yake, Mkristo mmoja anagundua kwamba, wakati fulani, ana furaha katika Roho, muda mfupi baadaye yeye ni mwenye hofu na woga, wakati fulani, yeye ni mwenye bidii katika upendo, mwenye nguvu katika imani na tumaini, na wakati mwingine ni baridi na dhaifu.
69. Lakini wote waliobatizwa, waliotenda kinyume cha dhamiri zao, walioruhusu dhambi kuwatawala wenyewe, waliomhuzunisha, na kumpoteza Roho Mtakatifu ndani yao, hawahitaji kubatizwa tena. Badala yake, lazima waongoke tena kabisa, jinsi tulivyoarifu vya kutosha hapo juu.
70. Ni kweli kabisa kwamba, mabadiliko yanatokana na uongofu wa kweli. Welekevu, nia, na moyo vinasukumwa na vinatenda kwa njia mpya kabisa. Moyo 1761 2 Kor. 6:1.
1762 Kilatini: ‘Arbitrium liberatum.´ 1763 Yn. 8:36.
unafahamu dhambi, unaogopa hasira ya Mungu, unageuka kutoka dhambini, unaelewa, na unapokea ahadi ya neema katika Kristo. Mawazo mazuri ya kiroho yatatokana na makusudi ya Kikristo, uangalifu, na kupigana dhidi ya mwili na kadhalika. Ikiwa mambo haya hayatokei au hayapo, hakuna uongofu wa kweli.
71. Lakini swali linahusu chanzo cha athari, 1764 yaani, ni nani anayeyasababisha haya yote ndani yetu, mtu anavipata vitu hivi wapi, na anavikaribia jinsi gani?1765 Jibu kwa mafundisho yetu ndilo hili: Kwa sababu uwezo wa asili wa mwanadamu hauwezi kuchangia lolote au kueneza mema yaliyotajwa hapo juu kwa njia yoyote (1 Kor. 2:4-12; 2 Kor. 3:4-12), Mungu, katika wema na huruma zake zisizopimika, hutangulia kuyaanzisha kwa njia ya kuihubiri Injili yake takatifu kwetu, ambayo kwayo, Roho Mtakatifu anataka kutenda uongofu na kufanywa upya ndani yetu. Ndani yetu, Mungu huwasha imani na maadili mengine ya kumpendeza Mungu kwa mahubiri na kwa kulitafakari Neno lake. Haya yote ndiyo vipawa na kazi pekee ya Roho Mtakatifu. 72. Fundisho hili linatuongoza kwenye vyombo ambavyo kwavyo, Roho Mtakatifu anapenda kuanzisha na kutenda haya yote. Kadhalika, linatukumbusha sisi jinsi anavyohifadhi, anavyotutia nguvu, anavyoviongeza vipawa hivi, na pia kutuonya tusipokee neema hii ya Mungu kwa ubatili. Badala yake, tujizoeze wenyewe kuwaza jinsi dhambi inavyohuzunisha, inavyozuia, na inavyopingana na kazi hizo za Roho Mtakatifu.
73. Basi, mafundisho haya makamilifu kuhusu hiari yanatusaidia mwishowe kuupata ufumbuzi wa maswali ambayo yametia wasiwasi katika makanisa ya Ukiri wa Augsburg kwa miaka mingi: Iwapo mtu anampinga Roho Mtakatifu kabla, katika, au baada ya uongofu wake na kama hafanyi lolote kabisa, bali yu mlegevu tu na analisubiri lile alikamilishalo Mungu ndani yake? Iwapo mtu ni kama boriti katika uongofu wake? Iwapo Roho Mtakatifu ametolewa kwa wote wanaompinga yeye? Iwapo uongofu umefanyika kwa njia ya shurutisho kiasi kwamba, Mungu anawalazimisha watu kuongoka kwa nguvu kinyume cha mapenzi yao?1766 Katika mtazamo wa majadiliano yaliyotangulia, mtu anaweza kuwa tayari kutambua, kuonyesha, kukataa, na kuyahukumu mafundisho ya uongo na makosa kama haya:
1. Upuuzi wa wafuasi wa Stoa1767 na Wamani katika kushikilia 74 kwamba, 1764 Kilatni: ‘Causa efficiens.’
1765 Mjadala huu ulibuniwa kuijibu nadharia ya Viktorino Strigel ya muundo wa kulitenda ambalo mtu asiyeongoka analo. Katika neno la falsafa, swali lililofikiwa ‘causa efficiens’ ni: Je, Mungu peke yake ana sababu ifaayo ya uongofu wa mtu au mtu ana namna ya kufanya ‘modus agendi?’
1766 Kilatini: “An homo ante, in, post conversionem Spiritui Sanctorepugnet? vel pure passive se habeat? An homo convertatur ut truncus? An Spiritus Sanctus detur repugnantibus? et an conversio hominis fiat per modum coactionis?
1767 Kundi la Falsafa lililoanzishwa na Zenon takribani mwaka wa 300 K.K.
kila kitu lazima kitokee jinsi kilivyo na kwamba, mtu anafanya tu chini ya shinikizo.1768 Hata katika matendo ya nje, nia ya mwanadamu haina uhuru au uwezo wa kupokea kipimo chochote cha haki ya nje, tabia ya heshima, na nidhamu. Haiwezi kuiepuka dhambi na maovu yaliyo dhahiri. Nia ya mwanadamu inashurutishwa katika kufanya matendo maovu kama uzinzi, wizi, na uuaji.
2. Kosa la Wapelagio wakorofi ndilo hili kwamba, hiari inaweza 75 kujiongoa yenyewe kwa Mungu, kuiamini Injili, na kuitii sheria ya Mungu, kwa moyo kabisa, kwa nguvu zake za asili, na bila Roho Mtakatifu. Kwa utiifu huu wa hiari, mwanadamu aweze kuustahili msamaha wa dhambi na uzima wa milele.
3. Kosa la wafuasi wa Papa na madaktari wa Uwanazuoni1769 76 walifundisha kwa upambanuaji kwamba, kwa nguvu zake za asili, mwanadamu anaweza kuanzisha kuongoka kwake vyema. Lakini, kwa sababu mwanadamu ni dhaifu mno kuukamilisha, Roho Mtakatifu anakuja mbio kutoa msaada kwa ajili ya mema ambayo mtu aliyaanzisha kwa nguvu zake za asili.
4. Fundisho la Wasynergisti,1770 wanaoshikilia kwamba, katika 77 mambo ya kiroho, mwanadamu hajafa kabisa kuelekea lililo jema, bali amejeruhiwa vibaya na ni nusu mfu tu. Hata hivyo, matokeo yake ni kwamba, nia yake ni dhaifu mno kuweza kulianzisha lolote kwa nguvu zake mwenyewe, kujiokoa mwenyewe na kuitii sheria ya Mungu moyoni. Hata hivyo, baada ya Roho Mtakatifu kuwa mwanzilishi, anatuita kwa njia ya Injili, anaitoa neema, msamaha wa dhambi, na heri ya milele. Ndipo nia itaweza kukutana na Mungu kwa kiwango fulani na kwa nguvu zake za asili ingawa, kwa kiasi kidogo, kwa njia dhaifu, husaidia, hushiriki, na hujiandaa yenyewe kwa neema ya Mungu, huifahamu, huipokea, huiamini Injili, na kwa nguvu zake yenyewe baadaye hushiriki pamoja na Roho Mtakatifu katika kuendeleza na kuhifadhi kazi hii ndani yetu.
Hapo juu,1771 tumeonyesha uwezo wa jinsi hiyo dhidi ya 78 mafundisho haya kwamba, facultas applicandi se ad gratiam, yaani, kujiandaa kwa neema kwa mtu hakuji kutokana na nguvu zetu za asili, bali tu kutokana na kazi ya Roho Mtakatifu.
1768 Kilatini: ‘Hominem coactum omnia facere.’
1769 Peter Lombard, ‘Liber Sententiarum,’ II, 26 - 28; Sinodi ya Trento, kikao cha 6, sura 1 na 5.
1770 Kiyunani: ‘συνεργειν:’ kuathiri, kufanya, kutenda, au kutekeleza pamoja. Istilahi ya kitheologia inayomaanisha kwamba, Mungu na binadamu hufanya kazi pamoja katika uongofu na wokovu. 1771 ‘Tamko Thabiti’ 2,5-15.
590
5. Vivyo hivyo, tunakataa mafundisho ya Papa na wamonaki1772 79 /watawa wa kiume kwamba, baada ya kuzaliwa upya, tayari mwanadamu anaweza kuitimiza sheria ya Mungu kwa ukamilifu katika maisha haya, na kwa utii mkamilifu wa jinsi hiyo wa sheria, anastahiki haki na uzima wa milele mbele za Mungu.
6. Kwa upande mwingine, ni lazima kuwaulaumu walokole kwa 80 ukali na juhudi zote. Wanaobuni kwamba, Mungu humvuta mtu kwake na kumwangazia, kumhesabia haki, na kumwokoa bila kutumia vyombo vyovyote, yaani, bila kulisikia Neno la Mungu na bila matumizi ya Sakramenti Takatifu, hao wasivumiliwe kabisa katika makanisa ya Mungu.
7. Vivyo hivyo, wote wanaofikiri kwamba, katika kugeuka na 81 kuzaliwa upya, Mungu anauumba moyo mpya na mtu mpya katika njia ambayo kiini na dhati ya Adamu wa kale, na hasa nafsi yenye busara, kwa jumla, inaharibiwa na asili mpya ya roho inayoumbwa kutoka tupu.1773 Mt. Agostino analilaani kosa hili kwa maneno dhahiri katika ufafanuzi wake kuhusu Zab. 25 ambamo anataja na kuyaelezea maneno ya Paulo: “Mweke mbali mtu wa kale,” kama ifuatavyo: “Isije ikawa yeyote akafikiri kwamba asili au nafsi ya mtu lazima iwekwe pembeni, yeye mwenyewe anaeleza ina maana gani kumweka kando Adamu wa kale na kumvaa mtu mpya kwa kuongeza, ‘Kwa hiyo uvueni uongo, mkaseme kweli.’ Tazama, huku ni kumvua mtu wa kale na kumvaa mtu mpya.”1774
8. Pia tunazikataa kauli zifuatazo zikitumika bila maelezo: 82 kwamba, nia ya mtu kabla, wakati, na baada ya uongofu hupingana na Roho Mtakatifu na kwamba, Roho Mtakatifu anatolewa kwa wanaompinga.
83. Kutokana na maelezo yaliyotangulia, ni wazi kwamba, wakati Roho Mtakatifu anapokuwa hazai mabadiliko kabisa kwa ajili ya mema katika akili, nia, na moyo, wakati mtu haamini ahadi na haandaliwi na Mungu kwa neema anapoendelea daima kulipinga Neno, uongofu hauwezi kupatikana. Uongofu unamaanisha mabadiliko ya akili, nia, na moyo wa mwanadamu kwa njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hata mtu ataweza kuipokea neema iliyotolewa kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Hivyo basi, wote walio wakaidi na wanaoipinga misukumo
1772 Sinodi ya Trento, Kikao 6, kanuni ya 32.
1773 Dhidi Flacius jinsi waliotunga Shauri la Mwafaka walivyouelewa msimamo wake.
1774 Kilatini: “Deponite veterem hominem.” . . . Ne aliquis arbitretur, deponendum esse aliquam substantiam, exposuit, quid esset: Deponite veterem hominem et induite novum etc., cum dicit in consequentibus: quapropter deponentes mendacium loquimini veritatem. Ecce, hoc est deponere veterem hominem et induere novum etc. Ufafanuzi wa Zab. 25: 1, 2.
na matendo ya Roho Mtakatifu, yanayotokana na Neno, hawatapokea Roho Mtakatifu bali watamhuzunisha na kumpoteza.
84. Hata hivyo, upinzani unaendelea hata miongoni mwa walioongoka jinsi Maandiko Matakatifu yanavyosema kwamba, tamaa za mwili zinaipinga nafsi. Isitoshe, sheria iliyomo katika viungo hushindana na sheria ya akili.1775
85. Kwa hiyo, mtu asiyezaliwa upya hupingana kikamilifu na Mungu na ni mtumwa wa dhambi kabisa. Basi, katika sheria ya Mungu, mtu aliyezaliwa upya hufurahia kulingana na utu wake wa ndani, ingawa katika viungo vyake, anaona pia sheria ya dhambi ikishindana na sheria ya akili yake. Kwa hiyo basi, akilini mwake anaitumikia sheria ya Mungu ilihali mwilini mwake anaitumikia sheria ya dhambi (Rum. 7: 22, 23, 25). Kwa hiyo, inawezekana na ni lazima kuelezea na kufundisha wazo sahihi katika jambo hili kwa ukamilifu, uwazi, na ubora.
86. Kuhusu kauli: “Hiari ya mwanadamu si zembe katika uongofu, bali pia inafanya kitu. Mungu humvuta yeye apendaye kuja.”1776 Kwa kawaida, kauli hizi zinatumiwa kupambana na mafundisho kuhusu neema ya Mungu kuonyesha kwamba, nia ya asili na huru inatekeleza sehemu yake katika uongofu. Kutokana na mjadala uliotangulia, inashuhudiwa kwamba, nafasi hii haipatani na muundo wa fundisho lenye uzima bali inapingana nalo tu. Kwa hiyo, ni sahihi uongofu wa mwanadamu kwa Mungu kukwepwa katika mijadala yote.
87. Naam, uongofu wa nia yetu iliyopotoka ni uamsho wa nia yetu kutoka kifo cha kiroho. Kwa hiyo basi, uongofu ni kazi ya Mungu peke yake jinsi ufufuo wa mwili unahesabiwa kuwa wa Mungu peke yake, jinsi ilivyoelezewa kikamilifu hapo juu kwa shuhuda wazi za Maandiko Matakatifu.
88. Hapo juu, imeelezwa vya kutosha jinsi Mungu anavyofanya katika uongofu. Anawavuta watu wanaopinga na kuwafanya kuwa wepesi kwa Roho Mtakatifu. Basi, baada ya uongofu huo, nia ya mwanadamu haiwi zembe katika zoezi la toba ya kila siku, bali hushiriki katika kazi zote ambazo Roho Mtakatifu anafanya katika sisi.
89. Tena, wakati Luther anasema kwamba, katika uongofu wake na kwa njia baridi kabisa,1777 mtu anatenda, yaani, hafanyi lolote bali ndiye shabaha ya
1775 Gal. 5:17; 1 Pet. 2:11; Rum. 7:23.
1776 Kilatini: ‘Hominis voluntas in conversione non est otiosa, sed agit aliquid. Trahit Deus, sed volentem trahit.’ Kauli hizi zinatokana na Yohana Krisostomo (‘De laudibus S. Pauli hom. 9) na Basileio Mkuu (‘Homilia de paenitentia’ 3) na zilidondolewa kutoka kitabu cha Melanchthon ‘Loci Communes’ mwaka wa 1543.
1777 Kilatini: ‘Pure passive’ Luther alitumia istilahi ‘pure passive,’ na ‘subjectum convertendum’ kwa maana ya uwanazuoni ili kuonyesha tu kwamba, mtu hashiriki katika uongofu wake, bali yeye ni kitu ambacho
592
matendo ya Mungu, hakumaanisha kwamba, uongofu unatokea bila mahubiri na bila kulisikiza Neno la Mungu. Isitoshe, hakumaanisha kwamba, Roho Mtakatifu hasababishi mienendo mipya na misukumo ya kiroho ndani yetu. Badala yake, anamaanisha kwamba, mtu mwenyewe au kwa nguvu zake za asili, hawezi kufanya lolote na hawezi kusaidia katika njia iwayo yote katika uongofu wake. Uongofu si kwa sehemu tu, bali kwa ukamilifu wake, kazi, kipawa, karama, na tendo la Roho Mtakatifu peke yake. Roho Mtakatifu anakamilisha na kuifanya nia na moyo wa mwanadamu kwa nguvu na uwezo wake kwa njia ya kulitumia Neno katika akili, sawa na ‘in subiecto patiente,’1778 yaani, kiima kilichoathiriwa. Maana yake: Mtu hatendi au hafanyi lolote. Badala yake, anaathiriwa, ingawa si kama jiwe lichongwalo sanamu, au nta wakati muhuri umekandamizwa ndani yake kwani hivi havijui lolote kuhusu kinachoendelea au kupata au kutaka lolote kwa jambo hili, bali kwa njia na baada ya hali iliyoelezewa na kufafanuliwa kwa ufupi hapo juu.
90. Wanafunzi wachanga katika vyuo vyetu vikuu wamepotoshwa kwa kiasi kikubwa mno na fundisho la sababu tatu katika uongofu wa mwanadamu kwa upande wa Mungu. Yaani, Neno la Mungu linalohubiriwa na kusikilizwa, Roho Mtakatifu, na nia ya kibinadamu.1779 Kutokana na maelezo yaliyotangulia, ni wazi kwamba, kwa upande wa Mungu, uongofu unatendwa na Roho Mtakatifu tu ambaye ni fundi wa kweli, ambaye anatenda mambo haya peke yake, ambaye anatumia mahubiri na usikivu wa Neno Takatifu kama njia na vyombo vyake vya kawaida. Kinyume chake, akili na nia ya mtu asiyeongoka ni ‘subiectum convertendum,´ yaani, kiima kinachoongolewa, kwa kuwa ndiyo akili na hiari ya mtu ambaye ni mfu kwa njia ya kiroho, Roho Mtakatifu anafanya kazi ya uongofu ndani yake na kufanywa upya. Nia ya mtu atakayeongolewa haifanyi lolote, bali humwacha Mungu afanye kazi ndani yake, mpaka aongoke. Ndipo anashiriki pamoja na Roho Mtakatifu katika matendo mema kwa kufanya yampendezayo Mungu, katika hali na kiwango kilichoelezwa kwa kina hapo juu. kimeongoka. WA, 18, 697. Martin Chemnits, Examen Concilii Tridentini, I, 5 Wenye shauku waliliombea hili tungo ili kuunga mkono mtazamo wao kwamba, Roho Mtakatifu anaongoa bila kutumia nyenzo.
1778 Kirai cha Melanchthon na cha Flacius.
1779 ‘Loci’ ya Melanchthon ya mwaka wa 1535 na wa 1543 (C.R., XXI, 376, 658) inahusika na “sababu tatu zinazolandana huhusu matendo yetu mazuri.” Mwanzoni, tungo hili lilitumika kwa jumla kwa utakaso katika maana finyu sana. Sababu tatu huitwa “ustadi” katika andiko lake ‘Elementa Rhetorices’ (C.R. XIII, 426 n.k.) Wafuasi wa Melanchthon huzungumzia kuhusu sababu tatu za ustadi zilizooana katika uongofu wa mtu moyoni. Waandishi wa ‘Shauri la Mwafaka’ wanakubali sababu tatu zinazolandana katika uongofu, ilimradi nia ya binadamu imeelezewa kama ‘causa materialis in qua et circa quam.’
593
III. HAKI YA IMANI MBELE ZA MUNGU
1. Ubishi wa tatu uliojitokeza kati ya wanatheologia fulani wa Ukiri wa Augusburg linahusu haki ya Kristo au ya imani ambayo Mungu huwahesabia maskini waovu kuwa wenye haki katika neema kwa imani.1780
2. Baadhi yao1781 wameshikilia kauli ya kwamba, haki ya imani, ambayo Mtakatifu Paulo anaiita haki ya Mungu,1782 ni haki ya undani wa Mungu. Haki hii ni Kristo mwenyewe kama Mwana kweli, halisi, Mwana wa asili wa Mungu, ambaye, kwa njia ya imani, anakaa ndani ya wateule, anawahimiza wao kufanya yaliyo mema na kwa njia hii ni haki yao. Dhambi za watu wote zikilinganishwa na haki hii, ni kama tone la maji likilinganishwa na bahari kubwa.
3. Kwa upande mwingine, baadhi walishikilia na kufundisha kwamba, Kristo ni haki yetu kulingana na asili ya ubinadamu peke yake.1783
4. Dhidi ya vikundi hivi viwili, baadhi ya walimu wa Ukiri wa Augsburg1784 walishikilia kwa maafikiano makubwa kwamba, Kristo ni haki yetu, si anapokuwa katika asili ya kimungu tu, au si anapokuwa katika asili ya kibinadamu tu bali akiwa katika asili zote mbili. Kama Mungu na mwanadamu tu, kwa utiifu mkamilifu, Kristo ameweza kutukomboa kutoka kwa dhambi zetu, ametuhesabia haki na kutuokoa. Kwa hiyo, haki ya imani ni msamaha wa dhambi, kupatana na Mungu, na uhakika kuwa tumefanywa wana wa Mungu hasa kwa sababu ya: utiifu wa Kristo tu ambao kwa njia ya imani tu, waaminio wanahesabiwa neema kama wenye haki, na kwamba, wamesamehewa maovu yao yote kwa sababu ya utiifu huo.
5. Kwa ajili ya wakati na vinginevyo, mabishano mengine mengi yanayohusu fungu la kuhesabiwa haki yaliibuliwa. Mabishano haya yatatatuliwa hapa chini katika tabaini, ambapo maoni yanayoyapinga mafundisho safi yatatolewa katika maneno ya Utetezi.
6. Jinsi Utetezi wa Ukiri wa Augsburg usemavyo, fungu hili la kuhesabiwa haki kwa imani ni “mfumo maalumu wa imani ya Kikristo,”1785 ambalo
1780 Kilatini: ‘Per fidem ex gratia.’
1781 Andrea Osiander na wafuasi wake.
1782 Rum. 1:22.
1783 Franzisko Stancaro ambaye, sawa na Petro Lombardo, alishikilia kwamba, Kristo ni mpatanishi wetu kulingana na asili yake ya ubinadamu.
1784 Hasa Philipp Melanchthon, Joachim Mörlin, Justus Menius, Matthias Flacius, Nicholas von Amsdorf, Nicholas Gallus, na Matth. Lauterwaldt. Kutokana na ombi la Mtawala Albrecht wa Preussien lililotaka kuwepo na kauli ya kitheologia kuhusu Ukiri wa Osiander, idadi kubwa ya wanatheologia kutoka pande zote za dola walitoa changamoto dhidi ya msimamo wa Osiander.
1785 ‘Utetezi wa Ukiri wa Augsburg’ 4, 2.
likikosekana, hakuna dhamiri dhaifu inayoweza kuwa na faraja yoyote idumuyo au inayoweza kuuelewa utajiri wa neema katika Kristo kwa namna hiyo hiyo. Dk. Luther aliandika: “Mahali ambapo fungu hili pekee linabaki safi, Ukristo wote utabaki safi katika umoja ulio safi, na bila mafarakano yoyote. Lakini mahali ambapo halibaki safi, haiwezekani kulizuia kosa lolote au roho ya uzushi.”1786 7.Paulo anasema wazi kuhusu fungu hili kwamba, chachu kidogo hulichachusha donge zima.1787 Kwa hiyo, kwa hamu kubwa, anatumia misemo kama vishirikishi vya pekee1788 hapa. Yaani, maneno ambayo kwayo, matendo yote ya wanadamu yanawekwa mbali. Kwa mfano: “bila sheria,” “bila matendo,” “kwa neema tu.” Anayasisitiza maneno haya kwa bidii ili aonyeshe umuhimu wake ulivyo kwamba, sambamba na mafundisho ya kweli, tabaini yake ndiyo mafundisho ya uzushi, ambayo tunayaonyesha, tunayalaumu na tunayatupilia mbali wazi.
8. Hivyo, ili kuutatua ubishi huu kwa njia ya Kikristo, kulingana na Neno la Mungu na kwa neema yake, tunathibitisha fundisho, imani, na ukiri wetu ifuatavyo:
9. Kuhusu haki ya imani mbele za Mungu, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwa maafikiano kulingana na jumlisho la imani yetu ya Kikristo na ukiri ulioelezwa hapo juu1789 kwamba, mkosaji maskini anahesabiwa haki mbele za Mungu. Anachukuliwa na kutangazwa kuwa huru kabisa kutoka kwa dhambi zake zote na kutoka kwa hukumu ya laana ya milele aliyowekewa na kufanywa mwana wa Mungu na mrithi wa ufalme wa milele bila sifa yoyote njema au ustahili wowote kutoka kwetu, bila matendo yaliyotangulia, yaliyopo, au yatakayofuatia kwa neema peke yake, kwa njia ya ustahili wa utiifu, maumivu makali, kifo, na kufufuka kwa Kristo, Bwana wetu, ambaye utiifu wake unahesabiwa kuwa haki kwetu.
10. Roho Mtakatifu anatoa hazina hizi kwetu kwa ahadi ya Injili. 11.Imani ni njia ya pekee ambayo kwayo, tunaweza kuzitambua, kuzipokea, na kuzitumia hazina hizi wenyewe na kuzifanya kuwa zetu. Imani ni zawadi ya Mungu, ambayo kwayo, tunajifunza kumfahamu Kristo Mkombozi wetu, kwa njia halisi katika Neno la Injili na kumtegemea. Basi, kwa imani, kwa ajili ya utiifu wake peke yake, na kwa neema tu, tunajua kwamba, tuna msamaha wa dhambi, tunahesabiwa haki, tu watakatifu, na tutapatiwa heri ya milele na Mungu Baba.
1786 Toleo la Jena 5, 159; WA 22, 255.
1787 1 Kor. 5:6.
1788 Kilatini: ‘Particulae exclusivae.’
1789 Yaani, Kiri, ‘Ukiri wa Augsburg’ na Utetezi wake, ‘Mafungu ya Smalkaldi,’ na Katekesimo mbili za Luther. Tazama juu, ‘Tamko Thabiti,’ “Jumlisho la Kanuni,” 1-9.
12. Hivyo, maelezo ya Mt. Paulo yanayofuata yanatakiwa kufikiriwa na kupokelewa kama yaliyo na maana moja: “Tunahesabiwa haki kwa imani” (Rum. 3:28), au “Imani inahesabiwa kama haki kwetu” (Rum. 4:5) au anaposema kuwa inatuhesabia haki kwa ajili ya utiifu wa Kristo, Mtetezi wetu pekee, au kwamba, “tendo la haki la mtu mmoja linamwezesha mtu kuachiliwa dhambi na uzima kwa watu wote” (Rum. 5:18).1790 13. Kwa kuwa, imani haihesabii haki kwa sababu ya kuwa tendo lililo jema na ndiyo wema unaomfurahisha Mungu. Badala yake, inashikilia na kupokea ustahili wa Kristo katika ahadi ya Injili Takatifu. Inatubidi kuupokea ustahili huu kuwa wetu na kufanywa wetu kwa njia ya imani kama tutahesabiwa haki kwa huo. 14. Kwa hiyo basi, haki ambayo, kwa neema inahesabiwa kwa imani au kwa waaminio ni utiifu, mateso, na ufufuo wa Kristo alipoitimiza sheria kwa ajili yetu na kulipa ridhaa kwa ajili ya dhambi zetu. 15. Kwa kuwa Kristo si mwanadamu tu, bali ni Mungu na mwanadamu katika mtu mmoja asiyegawanyika. Yeye hakuwa chini ya sheria, maana yeye ndiye Bwana wa sheria, kwani angekuwa amelazimika kuteseka na kufa kwa ajili ya ubinadamu wake.1791 Kwa hiyo, utiifu wake haumo tu katika mateso na kifo chake tu, bali pia katika hiari yake ya kuwa chini ya sheria badala yetu na utunzaji wake wa sheria kikamilifu kiasi cha kutuhesabu kuwa wenye haki. Mungu anatusamehe dhambi zetu na anatuhesabu kuwa watakatifu na wenye haki, na hutuokoa milele kutokana na utiifu huu mtimilifu, ambao Kristo alituonyesha kwa Baba yake wa mbinguni katika kutenda na kuteseka, katika uhai na kifo. 16. Haki hii hutolewa kwetu na Roho Mtakatifu kwa njia ya Injili na Sakramenti. Inahesabiwa kwetu sote kwa imani, inatolewa kuwa mali yetu na kupokelewa nasi. Kwa hiyo basi, waaminio wamepatanishwa pamoja na Mungu, wamesamehewa dhambi zao, wamepokea neema ya Mungu, uwana wa Mungu na wao ndio warithi wa uzima wa milele.
17. Kwa hiyo, neno “kuhesabia haki” lina maana ya kutangaza haki na uhuru kutoka dhambini na kutoka katika adhabu ya milele ya dhambi hizi kwa sababu ya haki ya Kristo ambayo Mungu anaihesabu kuwa imani (Flp. 3:9). Na haya ndiyo matumizi ya kawaida na maana ya neno hili katika Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na Agano Jipya. “Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.” (Mit. 17:15). “Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, 1790 Toleo la Kijerumani la mwaka wa 1580 linafuatia tafsiri ya asili ya Luther, “kwa njia ya haki ya mtu mmoja, haki ya imani imefika kwa watu wote.” Walakini, maneno ya Kilatini kulingana na Kiyunani, yana “haki ya uzima.”
1791 Huu ni upinzani wazi dhidi ya Georg Karg (Parsimonius), aliyesisitiza kwamba, ‘utiifu wenye bidii’ wa Kristo hauna thamani kwa wengine kwani Kristo wa asili ya ubinadamu alilazimika kuitunza sheria.
watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo; wampao haki mwenye uovu, ili wapewe ijara, na kumwondolea mwenye haki haki yake!” (Isa. 5: 22-23). “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki” (Rum. 8:33), yaani, anazichukua na kuziachilia dhambi.
18. Maana neno ‘kuzaliwa upya’1792 wakati mwingine linatumika badala ya ‘kuhesabiwa haki.’1793 Kwa hiyo, ni lazima kabisa kulielezea kwa uhalisi neno hili ili kufanywa upya huko kunakofuatia baada ya kuhesabiwa haki, kuweze kutofautishwa kikamilifu kutoka kwingine.
19. Naam, neno ‘kuzaliwa upya’ linatumika kwa njia mbili: kwanza, linatumika kumaanisha msamaha wa dhambi hasa kwa ajili ya Kristo na kufanywa upya kunakofuatia baadaye ambako Roho Mtakatifu anakufanya ndani ya waliohesabiwa haki kwa imani. Lakini neno hili pia linatumika kiasi kumaanisha msamaha wa dhambi na kufanywa kwetu kuwa wana wa Mungu.1794 Pili, linatumika katika Utetezi sana na mara nyingi kwamba, “kuhesabiwa haki ni kuzaliwa upya.”1795 Yaani, kuhesabiwa haki mbele za Mungu ni kuzaliwa upya, sawasawa na jinsi Mt. Paulo anavyolitumia neno kwa uainisho anaposema: “Alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.” (Tit. 3:5).
20. Vivyo hivyo, neno ‘uhuishaji’1796 yaani, kufanywa hai limetumika wakati mwingine kwa maana hiyo hiyo moja.1797 Kwani, iwapo Roho Mtakatifu amemfanya mtu kuamini na kumhesabia haki, kuzaliwa upya kumekwisha kutendeka kwa sababu amembadilisha mwana wa ghadhabu kuwa mwana wa Mungu na hivyo kumhamisha kutoka kifoni na kumwingiza uzimani jinsi ilivyoandikwa: “Tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo” (Efe. 2:5). “Mwenye haki ataishi kwa imani” (Rum. 1:17). Maneno ya Utetezi yanalitumia neno hili mara nyingi katika maana hii.1798
21. Mara nyingi neno “kuzaliwa upya” linamaanisha utakaso au kufanyika upya kunakofuatia baada ya kuhesabiwa haki kwa imani jinsi Dk. Luther
1792 Kilatini: ‘Regeneratio.’
1793 Kilatini: ‘Iustificatio.’
1794 Kilatini: ‘Remissio peccatorum et adoptio in filios Dei.’
1795 3 Fungu hili la maneno halijitokezi katika maneno ya Utetezi ingawa wazo limo katika maneno ya Utetezi 4: 72, 78, 117.
1796 Kilatini: ‘Vivificatio.’
1797 Wakati wa Majadiliano ya Altenburg, wanatheologia kutoka Jena hawakukubaliana na ulinganifu wa kauli za kuhesabiwa haki (iustificatio) na uhaishaji (vivificatio) uliofanywa na Kitivo cha Wittenberg kwa kudai kwamba, huu ulikuwa ukosefu wa kuyapambanua maneno ambayo unachukuliwa kuyakanganya.
1798 Mfano, maneno ya Utetezi, 4: 250; 7,31.
alivyolitumia neno hili katika kitabu chake kiitwacho, ‘Masinodi na Makanisa na mahali pengine.1799
22. Tunapofundisha kwamba, tunazaliwa upya na kuhesabiwa haki kwa njia ya kazi ya Roho Mtakatifu, hatumaanishi kwamba, katika kiini na maisha yao wale ambao wamehesabiwa haki na kuzaliwa upya, hakuna udhalimu unaoambatana nao. Badala yake, tunasisitiza kwamba, kwa utiifu wake mkamilifu, Kristo anaesitiri dhambi zao zote ambazo bado zinaambatana na asili yao ya maisha yote. Mbali na kudumu kwamba, kwa upande wa asili yao, wakosaji huyatenda yaliyopotoka mpaka kaburini. Hata hivyo, wao hutangaziwa na kutazamiwa kuwa wacha Mungu na wenye haki kwa imani na kwa ajili ya utiifu wa Kristo, ambao alituonyesha kwa Baba yake tangu utoto wake hadi kifo chake cha aibu msalabani kwa ajili yetu. Wala si kwa upande mwingine, kumaanisha kwamba, tunaweza au tunalazimika kuzifuata njia za dhambi, kudumu na kuendelea kukaa ndani yake bila toba, kubadilika na kufanya vizuri zaidi.
23. Kwa maana majuto ya kweli ni lazima yatangulie. Kwa kutokana na neema tu, kwa ajili ya Kristo, Mpatanishi pekee, kwa imani peke yake, bila matendo au sifa njema, wanahesabiwa haki mbele za Mungu - yaani, wanapokelewa ndani ya neema - wanapewa Roho Mtakatifu, ambaye anawafanya wapya na kuwatakasa na kuwaumbia upendo ndani yao kwa Mungu wao na kwa ndugu zao. Lakini kwa sababu kufanyika upya katika maisha haya bado si kamili, dhambi inaendelea kukaa ndani ya mwili hata katika hali ya kuzaliwa upya. Asili ya haki ya imani mbele za Mungu ni sisi kuhesabiwa neema kwa haki ya Kristo, bila matendo yetu, na dhambi zetu zinasamehewa na kufunikwa na hazihesabiwi kwetu (Rum. 4:6-8).
24. Vile vile, hapa, iwapo fungu linalohusu kuhesabiwa haki linatakiwa kubaki safi, tunatakiwa hasa kuwa waangalifu ili tusichanganye au kuingiza kitu cha kuitangulia imani au kuifuata imani kwenye fungu la kuhesabiwa haki. Kwa kuwa hatuwezi kuzungumza kwa njia moja na inayofanana kuhusu wongofu na kuhusu kuhesabiwa haki. 25. Kwa maana si kila kitu kinachohusiana na uongofu kinakuwa pia sehemu ya kuhesabiwa haki wakati huo huo. Mambo ambayo yanahusiana na yaliyo muhimu kwa kuhesabiwa haki, ni neema ya Mungu, ustahili wa Kristo, na imani inayoyapokea haya yote kwa ahadi ya Injili, na ambayo kwayo, haki ya Kristo inahesabiwa kwetu. Hivyo basi, tunapata msamaha wa dhambi, upatanisho na Mungu, tunakuwa wana wa Mungu na warithi wa uzima wa milele.
1799 Kitabu cha Luther kilichotolewa mwaka wa 1539; WA, 50:599; 625 n.k.
26. Hivyo basi, imani halisi ya kuokoa haiwezi kupatikana ndani ya wale wafanyao kwa kukusudia bila majuto na masikitiko kubaki na kudumu katika dhambi. Kwa maana majuto ya kweli yanatangulia na imani ya kweli inakuwa pamoja na toba ya kweli.
27. Upendo ni tunda ambalo halina budi na sharti liifuate imani ya kweli. Maana iwapo mtu hapendi, hii inaonyesha wazi kwamba, mtu huyo hajahesabiwa haki ila bado yu kifoni, au kwamba, amepoteza tena haki ya imani, jinsi Mt. Yohana anavyosema, (1 Yoh. 3:14). Lakini Mt. Paulo anaposema, “Tumehesabiwa haki kwa imani pasipo matendo,”1800 anaonyesha kwamba, si majuto yanayotangulia wala matendo yanayofuatia yamekuwa sehemu ya fungu la kuhesabiwa haki kwa imani. Kwa maana matendo mema hayatangulii kuhesabiwa haki, ila yanafuata, kwani mtu anatakiwa kwanza awe mwenye haki kabla ya kutenda matendo mema.
28. Vivyo hivyo ingawa kufanyika upya na utakaso ni kipawa cha Kristo, Mpatanishi, na ni kazi ya Roho Mtakatifu, matukio hayo hayawi fungu au jambo la kuhesabiwa haki mbele za Mungu. Yanafuata hasa baada ya kuhesabiwa haki, kwa sababu katika maisha haya, utakaso hauwi safi kabisa na kamili kamwe, kwa sababu ya mwili wetu wa dhambi. Katika ufafanuzi wake mzuri na wa uangalifu kutoka Waraka kwa Wagalatia Dk. Luther anaelezea: 29 “Hakika, tunakubali kwamba, tunatakiwa kufundisha kuhusu upendo na matendo mema pia. Lakini lazima hayo yafanyike wakati na mahali panapotakiwa. Yaani, tunapoyashughulikia matendo mema mbali na suala hili la kuhesabiwa haki. Kwa maana hiyo, suala kuu ambalo kwalo, tunatakiwa kujiuliza ni: vipi mtu anaweza kuhesabiwa haki na kuokolewa mbele za Mungu. Ndipo tunajibu pamoja na Mt. Paulo kwamba, njia ya matendo ya sheria au njia ya upendo - si kwamba, tunayakataa kabisa matendo na upendo – jinsi wapinzani wanavyotusingizia na kutulaumu kwa uongo - bali ili tusipotoshwe, jinsi Ibilisi anavyopenda. Kutokana na suala muhimu ambalo tunalishughulikia, tunaingia kwenye jambo lingine geni ambalo halihusiani na fungu hili kabisa. Kwa hiyo, kwa sababu tunajishughulisha na fungu hili la kuhesabiwa haki, tunayakataa na kuyatupilia mbali matendo, kwani asili halisi ya fungu hili haiwezi kulikubali shauri au hoja ya matendo. Kwa hiyo, tunalikataa rejeo la aina yoyote la sheria na la matendo ya sheria katika muungano huu.”1801 Luther alikomea hapo.
30. Si kwa ajili hii tu, bali pia kwa kuiweka mioyo yenye masikitiko ili ipate faraja yenye kutegemewa, yenye kuaminika, na yenye kutoa heshima kwa ustahili wa Kristo na neema ya Mungu. Maandiko Matakatifu ndiyo yanayofundisha
1800 Rum. 3:28. 1801 WA 41:240.
31. Wala si majuto, upendo, wema wowote unaoweza kuwa njia na chombo ambacho kwacho, tunaweza kupata na kupokea neema ya Mungu, ustahili wa Kristo, na msamaha wa dhambi vilivyoahidiwa katika Injili na vinavyotolewa na kupokelewa nasi bali ni kwa njia ya imani tu.
32. Ni sahihi kabisa kusema kwamba, waliohesabiwa haki kwa njia ya imani katika Kristo kwanza, wana haki ya imani inayohesabiwa kwao katika maisha haya. Kisha, pia wana haki ya utiifu mpya inayozinduliwa au ya matendo mema. Lakini mambo haya mawili hayatakiwi kuchanganywa au kuwekwa pamoja katika fungu la kuhesabiwa haki mbele za Mungu. Kwa maana haki inayoanzishwa au kufanyika upya ndani yetu si kamili na si safi katika maisha haya kwa sababu ya mwili. Isitoshe, hakuna hata mmoja atakayeweza kusimama mbele za hukumu ya Mungu akiitegemea haki hii, bali atasimama katika haki ya utiifu inayohesabiwa kwa imani, mateso, na kifo cha Kristo. Hivyo, hata baada ya kufanyika upya, baada ya kufanya matendo mengi yaliyo mema, na kufaulu katika maisha yake, mtu ataweza kumpendeza Mungu, kupokelewa katika fadhila zake, na kuishi kama mwana na mrithi wa uzima wa milele kwa sababu ya utiifu wa Kristo peke yake.
33. Andiko la Mt. Paulo kuhusu Ibrahimu linahusika na muktadha huu. Anasema kwamba, Ibrahimu alihesabiwa haki mbele za Mungu kwa imani tu kwa ajili ya Mpatanishi bila nyongeza ya matendo yake mwenyewe. Wala, kwa mara ya kwanza, hakuongolewa hapo kutoka katika ibada ya miungu ya uongo na bila matendo mema, bali vile vile baadaye, wakati Roho Mtakatifu alimfanya upya na kumvika fahari ya matendo mema mengi (Rum. 4:3; Mwa. 15:6; Ebr. 11:8). Naye Mt. Paulo analiibua swali hili katika Rum. 4:1 kwamba, msingi wa kuhesabiwa haki mbele za Mungu wa Ibrahimu ambaye alikuwa na Mungu wa neema na alimpendeza na kukubalika kwake kwa maisha ya milele ulijengwa katika nini,?
34. Anajibu: “Kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtaua, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa
600 kwamba, haki ya imani mbele za Mungu inafanyika kwa upatanisho wa neema peke yake au msamaha wa dhambi uliopokelewa kwa neema tu kwa ajili ya ustahili wa Kristo aliye Mpatanishi wetu na inayopokelewa kwa imani katika ahadi ya Injili tu. Kwa hiyo basi, imani haitegemei kuhesabiwa haki mbele za Mungu, toba, upendo, au wema mwingine wowote. Badala yake, inamtegemea Kristo tu, hasa utiifu wake mkamilifu kwamba, alitimiza sheria ya Mungu kwa ajili yetu na inayohesabiwa kwa waumini kuwa ni haki.
haki.”1802 Pia Daudi anasema, wokovu ni wa mtu yule tu ambaye Mungu humhesabia haki bila nyongeza ya matendo. 35. Hata hivyo, kufanyika upya na utakaso umezinduliwa katika walioongoka na kuamini na wenye upendo, wema, na matendo mema. Haya yote hayawezekani na hayapaswi kuchukuliwa kuwa sawa au kuchanganywa na fungu la kuhesabiwa haki mbele za Mungu. Lazima Kristo Mkombozi wetu apate utukufu wake na dhamiri zilizohuzunika zipate faraja ya kudumu. Utiifu wetu mpya si mkamilifu na safi kwa kusudi hili.
36. Hii ndiyo shabaha ya Mt. Paulo anapolifafanua fungu la haki ya imani kwa njia ya kutumia kauli ambazo zinatoa maana ya matendo, yaani, vishirikishi vya pekee,1803 ‘pasipo matendo,’ ‘pasipo sheria,’ ‘bure,’ ‘si kwa matendo.’ Haya yote yanaweza kufupishwa katika sentensi moja: tunahesabiwa haki mbele za Mungu na kuokolewa ‘kwa imani tu.’ Hivyo basi, maana ya matendo imekanushwa. Hata hivyo, hakuna imani ya kweli bila toba ya kweli. Pia lazima kukubali kwamba, matendo mema yanafuatia imani kama matunda imara yasiyokataliwa, au kana kwamba, waaminio hawana budi na wanapaswa kufanya mema. Jambo la kuzingatia vyema ni kwamba, matendo mema yanawekwa mbali na fungu la kuhesabiwa haki ili wakati wa kushughulika na kuhesabiwa haki kwa mkosaji maskini mbele za Mungu yasije yakachukuliwa, yakatungwa, au yakachanganywa kama mambo ya lazima. Kauli zilizoorodeshwa hapo juu kuhusu mafundisho ya kuhesabiwa haki1804 lazima zitambuliwe kwa njia hii na zisisitizwe kwa juhudi na uzito katika kulishughulikia andiko hili:
1. Matendo yetu yote yanaondolewa nje kabisa katika fungu la 37 kuhesabiwa haki pamoja na ustahili, thamani, majisifu, na tegemeo lote kwa matendo yetu. Hivyo basi, matendo yetu yasitazamiwe ama kama chanzo cha kustahili kuhesabiwa haki, ambacho lazima Mungu akizingatie anapotuhesabia haki au ambacho kwacho, tunaweza na tunapaswa kukitegemea. Matendo yetu hayana maana yoyote katika kuhesabiwa haki, (si yote, nusu, au hata kwa kiwango kidogo tu).
2. Ofisi na sifa ya imani pekee ndiyo njia ya kuwa chombo au 38 silaha ambayo kwayo, neema ya Mungu na ustahili wa Kristo katika ahadi ya Injili vinafahamika, kupokelewa, na vinatiliwa kwetu. Katika kutiliwa na kujitwalia upendo huku, wema na tendo lolote viwekwe mbali kabisa.
3. Kufanyika upya, utakaso, wema, wala matendo mema 39 havitazamiwi kuwa haki inayompendeza Mungu, wala haviwezi kufanywa na kuwa
1802 Rum. 4:5,6.
1803 Kilatini: ‘Particulae exclusivae; absque operibus, sine lege, gratis, non ex operibus.’
1804 Kilatini: ‘Particulae exclusivae in articulo iustificationis.’
sehemu au chanzo cha kuhesabiwa haki.1805 Visichanganywe kwa kisingizio chochote, haki, au kwa jina lolote na fungu la kuhesabiwa haki kama kuwa vya lazima. Haki ya imani ni msamaha wa dhambi kwa neema tu, kwa ajili ya ustahili wa Kristo peke yake. Hazina hizi zinatolewa katika ahadi ya Injili, zinapokelewa, zinakubaliwa, zinatumiwa nasi, na zinafanywa zetu kwa imani tu.
40. Hali kadhalika, utaratibu unahifadhiwa baina ya imani na matendo mema. Vile vile kati ya kuhesabiwa haki na kufanyika upya au kutakaswa.
41. Matendo mema hayaitangulii imani, wala kutakaswa hakutangulii kuhesabiwa haki. Kwanza, Roho Mtakatifu huiwasha imani ndani yetu tunapoongoka kwa njia ya kuisikia Injili. Imani inashika na inaifahamu neema ya Mungu katika Kristo ambayo kwayo, mwanadamu anahesabiwa haki. Basi, baada ya kuhesabiwa haki, Roho Mtakatifu humfanya kuwa mpya, humtakasa, na kutokana na kufanyika tena upya huku na utakaso, matunda ya matendo mema hufuatia. Hata hivyo, hii isieleweke kana kwamba, kuhesabiwa haki na kutakaswa vinatenganishwa katika njia ambayo pengine imani ya kweli inaweza kuwepo sambamba na nia mbaya. Hii huonyesha tu utaratibu ambao kila mmoja huutangulia au huufuata. Kwa maana kauli njema ya Dk. Luther inabaki kuwa kweli: “Imani na matendo mema yanapaswa kuwa pamoja vizuri. Lakini imani peke yake inashika baraka bila matendo. Na bado hakuna wakati imani inakuwa peke yake.”1806 Jambo hili limekwisha kufafanuliwa hapo juu.
42. Majadiliano mengi yanaweza kusuluhishika pia kwa njia ya manufaa na vizuri kwa msaada wa mabishano haya jinsi Utetezi unayvyojadili kuhusiana na Yak. 2:24.1807 Tukizungumzia imani inayohesabia haki, fundisho la Mtume Paulo ni kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani peke yake bila matendo. Kwa kuwa imani inautilia na kuufanya ustahili wa Kristo kuwa mali yetu jinsi tulivyosema hapo juu. Wakati swali linaulizwa: vipi Mkristo anaweza kujitambulisha, ama kwake mwenyewe au kwa upande wa wengine, kuwa na imani ya kweli iliyo hai na kuitofautisha na imani ya kuiga iliyokufa? Wakristo wengi wavivu hujidanganya wenyewe na kufikiria kwamba, wana imani wakati hawana imani ya kweli. Utetezi unatupatia jibu lifuatalo: “Yakobo alisema kwamba, imani isiyozaa
1805 Kilatini: ‘Tamquam forma au pars au causa iustificationis.’
1806 WA, 43:255: “Et haec non ita divellitur quasi vera fide aliquando et aliquamdiu stare possit cum malo propositio, sed ordine causarum et effectuum antecedentium et consequentium ita distribuuntur; manet enim quod Lutherus recte dicit: Bene conveniunt et sunt connexa inseparabiliter fides et opera, sed sola fides est, quae apprehendit benedictionem sine operibus, et tamen numquam est sola.” 1807 Utetezi 4,244.
602
matunda mema imekufa.”1808 Wakati huo huo, Utetezi wa Kilatini unasema: “Yakobo anafundisha kwa usahihi anapokanusha kwamba, tunahesabiwa haki kwa imani iliyoko bila matendo, jambo ambalo ni imani iliyokufa.”1809
43. Lakini, jinsi Utetezi unavyosema kwa uthabiti, Yakobo anasema kuhusu matendo mema ya waliokwisha kuhesabiwa haki na Kristo, ambao wamepatanishwa na Mungu na ambao wameupokea msamaha wa dhambi katika Kristo. Lakini tunapouliza imani itapata wapi sababu yake ya kuhesabia haki, kuokoa na yanayoambatana nayo, itakuwa ni uongo na si sahihi kujibu:
- Imani haiwezi kuhesabia haki bila matendo.
- Imani huhesabia haki au humfanya mtu kuwa mwenye haki ilimradi ihusishwe na upendo, upendo ambao huiumba imani.
- Matendo mema lazima yapatikane sambamba na imani ambayo peke yake haitoshi kumhesabia mwanadamu haki mbele za Mungu.
- Matendo mema lazima yapatikane katika fungu la kuhesabia haki jinsi ambavyo ni lazima yatangulie kuhesabiwa haki kama chanzo ambacho kikikosekana mtu hataweza kuhesabiwa haki. Kwa hiyo, yasitolewe kutoka katika kuhesabiwa haki kwa njia ya kutumia vishirikishi vya pekee jinsi Mt. Paulo alivyofanya, kama vile ‘mbali na matendo’ na kadhalika.1810 Kwa maana, imani inahesabia haki inaposhika na kuipokea neema ya Mungu na ustahili wa Kristo kwa njia ya ahadi ya Injili ikiwa kama chombo na kifaa.
44. Haya na yatoshee kama muhtasari wa maelezo ya mafundisho ya kuhesabiwa haki. Mafundisho haya yamewekwa mbele kwa undani katika maandiko yaliyotajwa hapo awali. Kutokana na maandiko hayo pia, tabaini1811 yake, yaani, uzushi, umekuwa wazi. Juu ya makosa ambayo yamekwisha kutajwa lazima tupinge, tuadhibu, tuhukumu, na tukatae makosa yafuatayo yanayofanana na yaliyo kinyume cha maelezo yaliyotangulia, yakifundishwa hivyo:1812
1. Upendo wetu au matendo yetu mema ni ustahili ambao kwao, 45
1808 Utetezi: 4,248.
1809 Kilatini:‘Iacobus recte negat nos tali fide iustificari, quae est sine operibus.‘ Tafsiri ya Kijerumani ndiyo ufafanuzi kuliko kuwa tafsiri kamili.
1810 Kilatini: ‘Fidem non posse iustificare sine operibus; vel fidem, quatenus caritatem, qua formetur, coniunctam habet, iustificare;vel fidei, ut iustificet, necessariam esse paesentiam bonorum operorum; vel bona opera esse causam sine qua non, quae particulas exclusivas ex articulo iustificationis non excluduntur.‘ Taz. istilahi kuu ya theologia ya Roma‚ ‘fides caritate formata,’ yaani, ‘imani iliyoumbwa kwa upendo.’
1811 ‘Antithesis.’
1812 Mashindano ya uongo yamenenwa yakielekezwa dhidi ya ‘Makosa ya Waroma’ ingawa pia lilikuwa lengo lake Andrea Osiander.
tunahesabiwa haki mbele za Mungu, ama kwa jumla au kwa sehemu.
2. Kwa njia ya matendo mema, mtu lazima ajistahilishe na afae 46 ili ahesabiwe ustahili wa Kristo.
3. Haki yetu ya kweli mbele za Mungu ndiyo upendo wetu wa 47 kufanyika upya ambao Roho Mtakatifu hutenda na yu ndani yetu.1813
4. Haki inayompendeza Mungu ina vipande au sehemu mbili. 48 Yaani, msamaha wa dhambi wenye neema na pia kufanyika upya au utakaso.
5. Imani huhesabia haki tu kwa sababu haki inaanzishwa ndani 49 yetu kwa imani, au kwamba, imani inapewa kipaumbele katika kuhesabiwa haki lakini kwamba, kufanyika upya na upendo hali kadhalika vinahusu haki yetu mbele za Mungu. Kwa kweli, imani hii ni chanzo kikuu bali, kuhesabiwa haki kwetu mbele za Mungu hakujakamilika au hakujawa safi kabisa bila upendo na kufanyika upya.1814
6. Waaminio wanahesabiwa haki mbele za Mungu na ndio wenye 50 haki wakati huo huo kwa njia ya haki ya Kristo inayohesabiwa kwao. Isitoshe, kwa njia ya utiifu wao mpya, ulioanzishwa na ulio na mwanzo wake ndani yao, au kuwahesabia haki ya Kristo kwa sehemu na kwa njia ya mwanzo wa utiifu mpya ndani yao1815 kwa nyingine.
7. Tunaipokea ahadi ya neema ya Mungu kwa imani ya moyo, 51 ukiri wa kinywa, na kwa njia ya wema mwingine.1816
52. Vile vile ni kosa inapofundishwa kwamba, mtu huokolewa kwa njia tofauti au kwa chombo tofauti kuliko kuhesabiwa haki mbele za Mungu, kana kwamba, kweli tunahesabiwa haki kwa imani bila matendo lakini kwamba, hatuwezi kuokolewa bila matendo au kwamba, wokovu hauwezi kupatikana bila matendo.
53. Hili ndilo kosa kwa sababu linapingana kabisa na maelezo ya Mt. Paulo kwamba, wokovu ni kwa mtu ambaye Mungu humhesabia haki bila matendo (Rum. 4:6). Sababu ya Mtume Paulo ni kwamba, tunayapokea mambo yote mawili, yaani, haki yetu na wokovu wetu kwa njia hiyo hiyo moja. Kwa kweli, 1813 Dhidi ya Osiander aliyesema kwamba, “haki ndiyo kitu kinachowafanya wenye haki kutenda matendo ya haki.” Sentensi katika Kilatini: ‘Formalem nostram iustitiam coram Deo esse inhaerentem nostram novitatem seu caritatem.’
1814 Kilatini: ‘Fidem iustificare tantum initialiter, vel partialiter, vel pricipaliter; et novitatem vel caritatem nostram iustiificare etiam coram Deo vel ompletive, vel minus pricipaliter.’
1815 Kilatini: ‘Credentes coram Deo iustificari vel coram Deo iustos esse simul et imputatine et inchooatione, v el partim imputatione partim inchoatione novae oboedientiae.’
1816 Kilatini: ‘Applicationem promissionis gratiae fieri et fide cordis et confessione oris ac reliquis virtutibus.’
604
tunapohesabiwa haki kwa imani, mara tutakuwa wana na warithi wa uzima wa milele na heri. Kwa hiyo, Paulo anatumia vishirikishi vya pekee vinavyoyatenga kabisa matendo na ustahili wetu wenyewe kwa nguvu, kama vile:‘kwa neema’ na ‘pasipo matendo’ kuhusu fungu la heri na la kuhesabiwa haki.
54. Kadhalika, hatuna budi pia kuelezea majadiliano kwa usahihi kuhusu kusakini1817 kwa dhati haki ya Mungu1818 ndani yetu. Kwa upande mmoja, ni kweli kabisa kwamba, Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ambaye daima dawamu ni haki ariki, anaishi kwa imani ndani ya wateule ambao wamekwisha kuhesabiwa haki katika Kristo na wamepatanishwa na Mungu, kwa kuwa Wakristo wote ni mahekalu ya Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ambaye anawasukuma watende kwa haki. Lakini, kwa upande mwingine, huku kukaa kwa Mungu ndani ya wanadamu si haki ya imani anayoizungumzia Mtume Paulo na ambayo anaiita haki ya Mungu,1819 ambayo kwayo, tunatangaziwa kuwa wenye haki mbele za Mungu. Huku kukaa kwa Mungu ndani ya wanaoamini kunafuatia haki ya imani. Haki hiyo basi, ni msamaha wa dhambi na kuhurumiwa kwa neema kwa mkosaji maskini kwa ajili ya utiifu na ustahili wa Kristo.
55. Kwa kuwa, inajulikana wazi miongoni mwa wanatheologia wote katika makanisa yetu wanaokubaliana na Ukiri wa Augsburg kwamba, haki yetu inatoka kwa Kristo Bwana peke yake bila stahili, matendo, wema, na cheo chetu au watu wengine, inatubidi kuchunguza kwa uangalifu ni kwa njia ipi Kristo anaitwa haki yetu katika jambo hili la kuhesabiwa haki? Haki yetu si asili yake moja au nyingine bali ndiyo nafsi nzima ya Kristo na haki yetu, ambaye peke yake, ndiye kama Mungu, mwanadamu, na mtiifu mkamilifu.
56. Kwa maana hata kama Kristo alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu bila dhambi na alizaliwa, katika asili ya kibinadamu peke yake, alitimiza haki yote, asili, utiifu, na mateso yake ya ubinadamu visingeweza kutuhesabia haki kama hangekuwa Mungu wa milele kweli. Kadhalika, asili ya kimungu ya Mwana wa Mungu isingeweza kuwa haki yetu pekee kama hakufanyika mwanadamu. Kwa hiyo, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, utiifu wa jumla wa nafsi nzima ya Kristo, alioutoa kwa Baba yake wa mbinguni hata katika aibu kuu mno ya mauti ya msalaba vinahesabiwa kwetu kuwa haki. Kwani, bila asili ya kimungu, asili yake ya kibinadamu isingeweza kujitolea kwa Mwenyezi Mungu wa milele kwa utiifu na maumivu ya ridhaa kwa ajili ya dhambi za dunia
1817 Kukaa, kuishi; Kilatini: ‘Inhabitatio.’
1818 Hii ilihusisha fumbo la msingi la fundisho la Osiander kuhusu fundisho la kuhesabiwa haki, ambalo alilisema kwa uthabiti dhidi ya neno lenye maana ya kutohusiana na mambo mengine ‘kuhesabia’ fundisho (‘imputatio’).
1819 Kilatini: ‘Iustitia Dei.’
nzima. Kwa upande mwingine, uungu peke yake, bila ubinadamu usingeweza kutupatanisha na Mungu.
57. Jinsi tulivyotaja hapo juu, utiifu wa Kristo ndio utiifu wa nafsi yake nzima. Basi, unamaanisha, ridhaa tele na upatanisho wa wanadamu wote. Unatosheleza madai yote ya haki ya kimungu ya milele isiyobadilika, na iliyofunuliwa kwa njia ya sheria. Utiifu huu ndio haki yetu iliyofunuliwa katika Injili na inayokubalika mbele za Mungu ambayo imani inategemea na Mungu huhesabia kwa imani kama jinsi ilivyoandikwa: “Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki” (Rum. 5:19), na: “damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote” (1 Yoh. 1:7), na tena: “. . . mwenye haki ataishi kwa imani yake” (Hab. 2:4).
58. Hivyo basi, asili ya kimungu au ya kibinadamu havihesabiwi mojamoja kuwa haki yetu, bali haki yetu ya pekee ndiyo utiifu wa nafsi nzima ambayo ni Mungu na wakati huo huo mwanadamu. Kwa hiyo, imani hutazama nafsi ya Kristo jinsi alivyowekwa chini ya sheria kwa ajili yetu. Alizitwaa dhambi zetu, na aliporudi kwa Baba yake, akatolewa kama mwakilishi wetu sisi wakosaji maskini kwa njia ya utiifu wake tele tangu kuzaliwa kwake kutakatifu hadi kifo chake. Hivi, akafunika kutotii kwetu, ambako kunakaa ndani ya asili yetu, katika mawazo, maneno, na matendo yetu, ili kutohesabiwa kwetu kusiwe laana yetu bali kuwe kusamehewa na kuachiliwa kwa neema safi kwa ajili yake Kristo peke yake.
59. Kulingana na hayo, kwa ridhaa kuu, tunakataa na kulaani zaidi makosa yaliyokwisha kuelezwa hapo awali, makosa ya uzushi yafuatayo na yanayofanana nayo kwamba, ni kinyume cha Neno la Mungu, mafundisho ya manabii, mitume, na imani yetu ya Kikristo:
1. Ikifundishwa kwamba, Kristo ndiye haki yetu mbele za Mungu 60 kwa upande wa asili yake ya kimungu tu.
2. Kristo ndiye haki yetu kwa upande wa asili yake ya 61 ubinadamu tu.
3. Wakati manabii na mitume wanazungumzia haki ya imani, maneno, ‘kuhesabia haki’na ‘kuhesabiwa haki’hayana maana ya ‘kuondoa dhambini’ na ‘kusamehewa dhambi.’ Badala yake, walimaanisha kufanywa halisi na wenye haki kweli kwa ajili ya upendo na wema ambavyo wanamwagiwa na Roho Mtakatifu na matendo mema yanayofuatia.
4. Imani haitazami utiifu wa Kristo tu, bali pia uungu wake kadiri 62
anavyokaa na kutenda kazi ndani yetu, na kwamba, kwa kukaa huku, dhambi zetu hufunikwa mbele za Mungu.1820
5. Imani ndiyo aina ya tegemeo katika utiifu wa Kristo kwamba, 63 inaweza kuwa na kudumu ndani ya mtu asiyetubu kweli na ambayo haifuatiwi na upendo lakini kushindana na dhamiri hubakia dhambini.1821
6. Mungu hakai ndani ya waumini bali ni karama zake Mungu peke yake.1822
66. Tunayakataa kwa ridhaa kuu makosa haya na yote yanayofanana na haya kuwa ni kinyume cha Neno la Mungu lililo wazi. Kwa neema ya Mungu tutabaki waaminifu siku zote katika fundisho la kuhesabiwa haki kwa imani mbele za Mungu jinsi ilivyowekwa mbele, ikafafanuliwa, na kuthibitishwa wazi kutoka katika Neno la Mungu kwenye Ukiri wa Augsburg na baadaye kufuatiwa na Utetezi.
67. Fungu hili kuu na muhimu mno la kuhesabiwa haki ambalo kwalo, wokovu wa nafsi zetu wategemea, ikiwa likihitajika kufafanuliwa zaidi, tunapendekeza ufafanuzi mzuri na mtamu wa Dk. Luther, kwa wote, kuhusu Waraka wa Mt. Paulo kwa Wagalatia. Kwa upande wetu, tunaridhika kuurejea kwa sababu tunaupenda ufupi wa maelezo yake.
IV. MATENDO MEMA
1. Kadhalika, mabishano yametokea miongoni mwa wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg kuhusu matendo mema. Upande mmoja umetumia maneno na kauli kama vile “Matendo mema ni ya lazima kwa ajili ya wokovu,” na “haiwezekani kuokolewa bila matendo mema,” na “hakuna aliyewahi kuokolewa bila matendo mema,”1823 kwa kuwa matendo mema yanahitajika kwa waaminio wa kweli kama matunda ya imani kwa kuwa imani bila upendo imekufa, ingawa upendo wa jinsi hiyo si chanzo cha wokovu.
2. Upande wa pili1824 ulisisitiza kinyume chake kwamba, ijapokuwa ni kweli kwamba, matendo mema ni ya lazima, hata hivyo, si kwa ajili ya wokovu bali kwa sababu nyingine. Kwa hiyo, si halali kuruhusu matumizi ya kauli au misemo iliyotangulia katika Kanisa kwa sababu haviwi kulingana na mafundisho
1820 Dhidi ya ukiri wa Andrea Osiander. 1821 Sinodi ya Trento, Kikao cha 6, sura ya 15, kanuni ya 28.
1822 Philip Melanchthon, katika ‘Loci,’ 1535 (C.R., XXI, 479); Georg Major, hasa katika kitabu chake kiitwacho, ‘Sermon von S. Pauli und aller Gottfürchtigen menschen bekerung zu Gott’ (Leipzig, mwaka wa 1553); na Justus Menius.
1823 P. Melanchthon katika toleo la mwaka wa 1535 la ‘Loci Communes,’ na tena G. Major. 1824 N. von Amsdorf, M. Flacius, N. Gallus na Yoh. Wigand.
607
na misemo mabruki na imekuwa ikitumiwa na wafuasi wa Papa walipopinga mafundisho yetu ya imani yetu ya Kikristo tunamokiri kwamba, imani peke yake inahesabia haki na kuokoa. Hivyo basi, tujihadhari kwamba, ustahili wa Mwokozi wetu Kristo usije ukapunguzwa, na ili ahadi ya heri ihifadhiwe kwa uiimara na uthabiti kwa waaminio.
3. Katika majadiliano haya, baadhi ya wanatheologia1825 wametumia kauli ya kuelekea kuleta mabishano: “Matendo mema hutia hasara katika wokovu.” Wengine pia wameshikilia kwamba, matendo mema si ya lazima bali ni huru, kwani hayazaliwi na hofu au adhabu ya sheria, bali lazima yatokee kutoka kwa roho ya hiari na moyo wenye furaha. Kundi lingine lilichukua mtazamo tofauti kwamba, matendo mema ni ya lazima.
4. Mwanzoni, mabishano haya yalihusu maneno ‘lazima’ (‘necessitas’) na ‘uhuru’ (‘libertas’). Naam, neno ‘lazima’ halimaanishi tu utaratibu wa milele usiobadilika unaowalazimu na kuwafunga watu wote kuwa watiifu kwa Mungu. Wakati mwingine, lina maana ya nguvu ambayo kwayo, sheria huwalazimisha watu kutenda matendo mema.
5. Basi, baadaye, kadiri muda ulivyokwenda, hayakuwa maneno tu yaliyojadiliwa bali mafundisho yenyewe yalizongwa vikali kwa hoja kama utiifu mpya wa waliozaliwa upya usiokuwa wa lazima kulingana na utaratibu wa kimungu uliotajwa hapo juu.
6. Ili kuyataja majadiliano haya kwa njia ya Kikristo, kulingana na Neno la Mungu, na kwa neema ya Mungu kuyamaliza kabisa, tutayatoa yatakayofuatia kama mafundisho, imani, na ukiri wetu.
7. Kwanza kabisa, hatuna mabishano yoyote miongoni mwetu kuhusu mafungu yafuatayo:
- Wale waaminio lazima waishi kulingana na mapenzi, utaratibu, na amri ya Mungu kwa njia ya kutenda matendo mema.
- Matendo mema si ambayo mtu binafsi huyabuni kwa shabaha nzuri au yanayotendeka kulingana na kanuni zilotungwa na wanadamu lakini ambayo yameagizwa na yameamuriwa na Mungu mwenyewe katika Neno lake.
- Matendo mema ya kweli hayafanywi na binadamu kwa nguvu zake za asili bali tu baada ya kupatanishwa na Mungu kwa imani na kutiwa nguvu na Roho Mtakatifu, au jinsi asemavyo Mt. Paulo, “Tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema” (Efe. 2:10). 1825 N. von Amsdorf.
8. Wala hakuna mabishano miongoni mwetu iwapo matendo mema yanapendeza na kukubalika kwa Mungu, ingawa si safi bado na yana upungufu katika mwili wetu huu. Yanakubaliwa kwa ajili ya Kristo Bwana kwa imani, kwa sababu nafsi inayotenda inakubalika kwa Mungu. Lakini matendo haya si matendo yanayohusu uthabiti wa nidhamu ya nje na ambayo wasioamini na wasioongoka wanaweza na wanatakiwa kutenda pia ambayo husifiwa na dunia, na hata Mungu atayapatia tuzo kwa kitambo katika dunia hii. Lakini kwa kuwa hayatiririki kutoka kwa imani ya kweli, ni dhambi na yamenyunyiziwa dhambi machoni pa Mungu. Mungu anayaona sawa na dhambi na unajisi kwa sababu mtendaji amepotoka bila kupatanishwa bado na Mungu. Mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri,1826 na “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi” (Rum. 14:23). Kwanza, mtu lazima ampendeze Mungu, kwa ajili ya Kristo, kabla matendo ya mtu huyo hayajawa ya kumpendeza.
9. Kwa hiyo, imani ndiyo mama na chanzo cha matendo mema ya kweli na ya kumpendeza Mungu, ambayo Mungu huyapatia tuzo hapa na katika ulimwengu ujao. Kwa hiyo, Mt. Paulo anayaita ya kweli matunda ya imani na ya Roho.1827
10. Kwani, jinsi Luther aandikavyo katika utangulizi kwa waraka wa Mtakatifu Paulo kwa Warumi:1828 “Imani ndiyo kazi takatifu ya Mungu ndani yetu inayotubadilisha na kutuzaa upya kutoka kwa Mungu. Inamuua Adamu wa kale, inatufanya kuwa watu tofauti kabisa moyoni, rohoni, akilini, katika nguvu zetu zote, na inakuja na Roho Mtakatifu. Lo! imani ndiyo hai, ina kazi nyingi, ni yenye juhudi, ni yenye ukuu, na yenye nguvu nyingi hata haiwezekani ibakie daima bila kufanya lililo jema. 11 Kadhalika, imani haiulizi ikiwa matendo mema hayana budi kufanywa, bali kabla mtu hajauliza, imani inakuwa tayari imetekeleza na daima ni hodari katika kutenda. Yeyote asiyetenda matendo mema kama haya ni mtu asiye na imani, anayebisha hodi kwa kuzungukazunguka kama kipofu akitafuta imani na matendo mema bila kujua ama imani ni nini au matendo mema ni yapi, huku akipayapaya na kukanganyika sana kuhusu imani na matendo mema. 12. Imani ndiyo tegemeo hai na lenye ujasiri kwa neema ya Mungu hata kuwa tayari kufa mara elfu kwa ajili yake. Tumaini hili na itikadi hii kuhusu neema ya Mungu hutufanya wenye furaha, wakaidi, na wenye mikogo mingi mbele za Mungu na viumbe vyote. Hii ,Roho Mtakatifu ambaye yumo katika imani, anafanya kazi. Kwa hiyo, bila kizuizi chochote, mtu atakuwa tayari na mwenye kutamani kutenda mema kwa mtu yeyote, kumtumikia kila mtu, kuteseka kwa kila mtu kwa ajili ya upendo wa Mungu na kwa utukufu wake, 1826 Mt. 7:18.
1827 Gal. 5:22; Efe. 5:9. 1828 EA 63, 124.
ambaye amekuwa mwenye neema kwake. Kwa hiyo, haiwezekani kutenganisha matendo na imani jinsi isivyowezekana kutenganisha joto na mwanga kutoka katika moto.”
13. Kwa kuwa hakujawa na mabishano miongoni mwetu kuhusu mambo haya, hatutaendelea kuyajadili zaidi bali tutatekeleza mambo ambayo yanabishaniwa kwa urahisi na kwa uwazi.
14. Katika nafasi ya kwanza, ni dhahiri kwamba, katika kulijadili swali kama matendo mema ni lazima au hiari, Ukiri wa Augsburg na Utetezi kuzitumia kauli kama: “Matendo mema ni ya lazima;” tena, “Ni lazima kufanya matendo mema kwa sababu huwa ni lazima yatafute imani na upatanisho;” tena, “Imetupasa na ni lazima kuyafanya matendo mema ambayo Mungu ameyaagiza.” Vile vile, Maandiko Matakatifu yenyewe yanatumia maneno kama “ulazima,” “lazima,” “iliyotakiwa,” “pasa,” na “hatuna budi,” kuonyesha ambayo tunapaswa kuyatenda kwa sababu ya utaratibu wa Mungu, agizo, na mapenzi yake (Rum. 13:5, 6, 9; 1 Kor. 9:9; Mdo. 5:29; Yn. 15:12; 1 Yoh. 4:11).1829
15. Basi, wengine hulaumu kauli hizi bila sababu bora na kuzikataa. Hata hivyo, inatumiwa katika maana yao halisi na ya Kikristo. Badala yake, afadhali yatumike kwa usahihi kwa shabaha ya kulikaripia na kulikataa kosa la wafuasi wenye kupenda anasa wa Epikuro, kwani watu wengi hujitolea wenyewe dhidi ya ndoto ya imani iliyokufa au ushirikina, bila toba na bila matendo mema, kana kwamba, ingewezekana kuwa na imani sahihi na kauli mbaya kuendelea katika moyo mmoja na kudumu katika dhambi, jambo ambalo haliwezekani. Au kana kwamba, mtu angeweza kuwa nayo na kushika imani ya haki, na wokovu hata kama bado anaendelea kuwa mti tasa na mgumba usiozaa matunda mema yoyote. Anadumu katika dhambi kinyume cha dhamiri au kwa hiari anajiingiza tena katika dhambi kama hizo, jambo ambalo ni uongo na udanganyifu kabisa. 16. Inatulazimu kutilia maanani tofauti. Yaani, kwamba, neno ‘lazima’ litumikapo katika matumizi haya, lisieleweke kama lenye kumaanisha shurutisho, bali limaanishe tu utaratibu wa mapenzi ya Mungu yasiyobadilika, ambayo sisi tu wadeni wake,1830 jinsi amri inavyoelezea Mungu anapoagiza kiumbe kumtii Muumba wake. 17.Penginepo, kama katika 2 Kor. 9:7; Flm. 14; 1 Pet. 5:2, neno ‘lazima’ limetumiwa kulielekeza lile ambalo mtu amelifanya kinyume na matakwa yake, kwa kushurutishwa au vinginevyo, kiasi kwamba, atekeleze kwa nje kwa hila, ambalo kweli, yeye hakuwa tayari, au hata kinyume cha mapenzi
1829 ‘Ukiri wa Augsburg’ 5; 20; Utetezi 4: 183-400.
1830 Kilatini: ‘Necessitas ordinis mandati et voluntatis Christi ac debiti nostri, non autem necessitas coactionis.’
610
yake. Mambo kama haya ya kujifanya Mungu hayataki. Kinyume chake, watu wa Agano Jipya wanapaswa kuwa watu wanaojitoa wenyewe kwa hiari (Zab. 110:3), wanaoleta matoleo kwa hiari (Zab. 54:6), si kwa sababu ya kutopenda wala kwa kushurutishwa bali kwa utiifu kutoka moyoni (2 Kor. 9:7; Rum. 6:7). Maana “Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” (2 Kor. 9:7). 18. Kwa maana hii na kwa shabaha hii, ni sahihi kusema na kufundisha kwamba, matendo mema kweli yatafanywa kwa hiari au yatakuja yenyewe kutoka rohoni, yakiwa yenye hiari ambayo Mwana wa Mungu ameiweka huru. Ilikuwa ni kwa moyo wa kupenda hili hasa, wengi walilitetea azimio kwamba, matendo mema ni ya hiari.
19. Lazima pia kuona hapa tofauti ambayo Paulo anaizungumzia katika Rum. 7:22,23, kwamba, anaifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, na kwa upande mwingine katika viungo vyake anaona sheria ambayo haiwi tu kwamba, haiko tayari bali kweli inaipiga vita sheria ya akili zake. Kuhusu mwili huu usiotaka na mpinzani, Paulo anasema: “Nautesa mwili wangu na kuutumikisha” ( 1 Kor. 9:27). Tena, walio wa Kristo wameisulubisha,” yaani, wao huinyima miili yao na mateso, tamaa mbaya, na matendo yao (Gal. 5:24; Rum. 8:13). Lakini si halali na ni lazima yakaripiwe. Pia wengine wakisisitiza kwamba, matendo ya wanaoamini ni ya hiari kwa maana kwamba, jambo liko mikononi mwao kuchagua kwa hiari iwapo wanaweza kutenda au kutotenda au watu wakifundisha kwamba, neema na ukereketwa wa Mungu vinaweza kuhifadhiwa japokuwa ndiyo njia ya kutenda dhidi ya mapenzi ya Mungu.
21. Pili: Ikifundishwa kwamba, matendo mema ni ya lazima inapaswa kuelezewa kwa sababu gani ni ya lazima jinsi ilivyofanywa na Ukiri wa Augsburg na Utetezi.
22. Lakini inatubidi kuangalia hapa vizuri matendo yasije yakaingizwa na kuchanganywa na fungu la kuhesabiwa haki na la wokovu. Kwa hiyo basi, inatufanya kuzikataa kauli kwamba, matendo mema ni ya lazima kwa wokovu wa amwaminiye, au kwamba, haiwezekani kuokolewa bila matendo mema, kwa sababu kauli kama hizi zinapinga vishirikishi vya pekee.1831 Yaani, maneno ambayo kwayo, Mt. Paulo anayatenga matendo yetu kabisa na ustahili wetu nje ya fungu la kuhesabiwa haki, kuokolewa, na kutangaziwa kwamba, haya yote hutendwa na neema ya Mungu kwa ajili ya ustahili wa Kristo, jinsi ilivyoelezewa katika fungu lililotangulia. 23. Kadhalika, kauli hizi zinanyima faraja ya Injili, dhamiri zilizojaribiwa na kusumbuliwa, yanazisababisha kuwa na mashaka, ni hatari kwa njia nyingi, yanaimarisha kiburi cha kutegemea haki ya binadamu mwenyewe 1831 Kilatini: ‘Particulae exclusivae in articulo iustificationis et salvationis.’
611
na kutegemea haki na matendo ya mtu mwenyewe. Kauli hizi zinakubaliwa na kutumiwa na wafuasi wa Papa kwa faida yao binafsi dhidi ya fundisho safi la kuokolewa kwa imani peke yake. 24. Hivyo basi, kauli hizi ndizo kinyume cha mfumo wa Neno safi, jinsi ilivyoandikwa kwamba, yanayomhesabia haki ya hiari kamili ya wokovu mtu tu ambaye Mungu humhesabia haki mbali na matendo (Rum. 4:6), au maelezo katika fungu la sita la Ukiri wa Augsburg: “Tunaokolewa bila matendo kwa imani tu.” Pia Dk. Luther amezikataa na kuzilaani kauli hizo:
1. Kuwa kauli za manabii wa uongo miongoni mwa 25 Wagalatia.1832
2. Kuwa kauli za wafuasi wa Papa katika mahali pengi.1833 26
3. Kisha pia katika maandiko yake dhidi ya Waanabaptisti ambao 27 waliuendeleza ufafanuzi huu kwamba, kwa kweli, imani isitegemee ustahili wa matendo mema, lakini inatupasa kuyapokea kama masharti ya lazima ya wokovu.
4. Zaidi ya hayo, kwa habari ya baadhi ya wafuasi wake 28 mwenyewe waliojaribu kuielezea kauli kwa kusema kwamba, ingawa tunahitaji matendo mema kama ya lazima kwa wokovu; hata hivyo, hatuwafundishi watu kuweka tegemeo lao katika matendo (Ufafanuzi wa Kitabu cha Mwanzo, sura 22).
29. Kwa hiyo na kwa sababu zilizotajwa hapo juu, ni sahihi kwa makanisa yetu kuendelea kuushikilia msimamo huu kwamba, kauli zilizokwisha kutajwa hazitafundishwa, hazitatetewa, wala hazitaachwa, bali zitaondolewa na kukataliwa na makanisa yetu kuwa za uongo na si sahihi. Ni kama katika nyakati za mateso ambapo ukiri sahihi ulihitajika dhidi ya aina zote za mafundisho bandia ya fungu la kuhesabiwa haki, uliingizwa na kuchukuliwa tena kuwa mada ya majadiliano kama katika andiko la ‘Interim’ (Hati ya Muda).1834
30. Tatu: Pia yametokea majadiliano kuhusu matendo mema kama yangekuwa ya lazima katika kuuhifadhi wokovu, yaani, katika kuhifadhi imani, haki, na heri kuwa vyetu? Kwa kweli, hili ni swali zito na muhimu kwani ni “Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka” (Mt. 24:13), na “Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho” (Ebr. 3:14). Kwa hiyo, ni muhimu kuelezea kinaganaga jinsi haki na wokovu vinahifadhiwa ndani yetu ili tusivipoteze tena.
31. Kwa hiyo, kwanza, hatuna budi kuikataa kwa makaripio makali ndoto
1832 Ufafanuzi wa Waraka wa Mt. Paulo kwa Wagalatia, sura za 2 , 3 na 5. 1833 Ufafanuzi wa Kitabu cha Mwanzo, sura ya 22. 1834 Hati ya Muda ya Augsburg na ya Leipzig za mwaka wa 1548.
612
za uongo za wafuasi wa Epikuro ambapo wengine huota kwamba, baada ya kupokelewa haiwezekani kupoteza kipawa cha imani, haki, na wokovu ijapokuwa matendo mabaya ya dhambi yaliyotendeka makusudi. Kulingana na maono yao, Mkristo ataweza kuibakiza imani, neema ya Mungu, hali, na wokovu hata kama ataishi kulingana na tamaa zake mbaya hadharani na bila kuona aibu. Licha ya hayo, yeye humpinga Roho Mtakatifu, na anaendelea kujiweka makusudi dhambini dhidi ya dhamiri yake.
32. Ili kuukanusha, lazima Wakristo waliohesabiwa haki kwa imani wasisitiziwe vitisho vya kweli visiyvobadilika vya kimungu, na makaripio, na maonyo ya kweli: “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; washerati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji wala walawiti” (1 Kor. 6:9). “. . . Watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu” (Gal. 5:21; Efe. 5:5). “Kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa” (Rum. 8:13). “Kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu” (Kol. 3:6) juu ya wana wote wa kuasi.
33. Utetezi unatoa mfano mzuri wa ni lini na vipi mahimizo ya kutenda matendo mema yanaweza kufundishwa bila kutia giza mafundisho ya imani na fungu la kuhesabiwa haki kwa msingi wa yaliyotangulia. Utetezi unapofafanua aya ya 2 Pet. 1:10: “Jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu,” unasema: “Petro anafundisha kwa nini tunapaswa kufanya matendo mema, yaani, kuthibitisha wito wetu kiasi kwamba, tusianguke kutoka katika wito wetu na kupotea tena katika dhambi. Anasema: ‘Naam, Petro anazungumzia kuhusu matendo yanayoufuata msamaha wa dhambi na kufundisha kwa nini matendo haya yatendeke kwa ajili ya kuthibitisha wito wao. Maana yake: wasije wakaanguka tena kutoka katika wito wao kwa njia ya kutenda dhambi tena. Fanyeni matendo mema ili kuvumilia katika wito wako na si kupoteza karama zake, ambazo ulipewa kabla ya matendo yako na si kwa sababu ya hayo matendo ambayo sasa yameshikwa na imani. Imani haibaki katika wale ambao wamepoteza Roho Mtakatifu na kuiacha toba.” 1835
34. Lakini ufafanuzi huu haumaanishi kwamba, imani hupokea haki na wokovu mwanzoni peke yake. Kisha, matendo yafuatie tena, kana kwamba, matendo yanaweza kuitunza imani, hali iliyopokelewa na wokovu. Paulo anasema kwamba, imani si kuingia kwetu katika neema tu bali pia ndiyo hali yetu ya sasa ya neema na “kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu” (Rum. 5:2), yaani, kuwa mwanzo, katikati, na mwisho. Hivyo basi, ahadi kuhusu haki na heri 1835 Utetezi 20,12.
lazima viwe yakini. Vivyo hivyo, anasema: “Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako” (Rum.11:20). “Awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; mkidumu tu katika ile imani” (Kol. 1:22-23). “Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu,” na tena “katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu” (1 Pet. 1:5, 9).
35. Kwa hiyo, inajulikana wazi katika Neno la Mungu kwamba, imani ni njia halisi na ya pekee ya kupokelea haki na wokovu. Pia, Mungu anavihifadhi kuwa vyetu kwa imani peke yake. Basi, tuna sababu zote za kukataa amri za Sinodi ya Trento,1836 na maoni mengine yoyote ya kuelekea kwenye wazo hilo hilo. Yaani, kwamba, matendo yetu mema huhifadhi wokovu, au kwamba, matendo yetu hutegemea, na hutunza haki ya imani kwa jumla au kwa sehemu, ambayo tumeipokea ama hata imani yenyewe.
36. Ingawa kabla ya ubishi huu, walimu wengi safi walizitumia kauli hizi au zile zizofanana katika ufafanuzi wa Maandiko Matakatifu bila shabaha yoyote ya kulithibitisha kosa la wafuasi wa Papa lililotangulia. Hata hivyo, kwa vile majadiliano yalitokea baadaye, kauli hizo, jambo ambalo lilisababisha kuongeza chumvi nyingi mbaya, ni bora kabisa kulifuata shauri la Mt. Paulo la kuushikilia muundo wa maneno yanayokubalika na ‘fundisho la kweli lenyewe.’1837 Hivyo basi, mabishano yasiyohitajika yataweza kumalizwa na Kanisa kulindwa kutokana na mabaya mengi.
37. Nne, kuhusu kauli kwamba, matendo mema yanadhaniwa kuwa ya hasara kwa wokovu,1838 tunatangaza msimamo wetu kwa uwazi: Iwapo mtu yeyote atayachanganya matendo mema na fungu la kuhesabiwa haki na kutegemea haki na tumaini la wokovu kwayo, na kudhania aweze kustahili neema ya Mungu kwayo, si sisi bali Paulo mwenyewe, ambaye anarudia kutamka mara tatu katika Flp. 3:7 na kadhalika kwamba, matendo mema hayafai na ni kipingamizi kwa mtu wa jinsi hiyo, bali pia ni yenye madhara hasa. Hata hivyo, kosa halitokei kwa ajili ya matendo mema yenyewe, bali ni tumaini la uongo ambalo linawekwa kinyume cha Neno halisi la Mungu.
38. Lakini matokeo yake siyo hitimisho kwamba, ingetubidi kusema tu kabisa1839 kwamba, matendo mema ndiyo hasara kwa waaminio kadiri ya wokovu wao. Kinyume chake, matendo mema yakifanyika kwa ajili ya sababu sahihi
1836 Sinodi ya Trento ya mwaka wa 1545-1563, kikao cha sita, kanuni ya 24, 32. 1837 2 Tim. 1 :13. 1838 N. von Amsdorf. 1839 Kilatini: ‘Simpliciter.’
na kwa kusudi sahihi,1840 yaani, kwa lengo kwamba, Mungu anayahitaji katika maisha ya waliozaliwa upya, na ni dalili za wokovu katika wanaoamini (Flp. 1:28). Ni mapenzi na amri wazi ya Mungu kwamba, wanaoamini hawana budi kutenda matendo mema ambayo Roho Mtakatifu anatenda ndani yao. Mungu anataka kupendezwa nayo kwa ajili ya Kristo na anaahidi kuwapatia tuzo angavu katika maisha haya na yatakayokuja.
39. Kwa hiyo basi, makanisa yetu pia yanailaumu na kuikataa kauli hii, kwa kuwa ni ya uongo na ya makurufu. Inaweza kudhoofisha adabu na heshima, na badala yao, kuyaleta na kuyahakikisha maisha ya kinyama katika hali ya kutojali wokovu kwa njia ya wafuasi wa Epikuro. Kwa bidii kubwa, mwanadamu anapaswa kuepuka lolote lililo la hasara kwa wokovu wake.
40. Kwa kuwa Wakristo hawasitishiwi kutoka kwa matendo mema, bali wanaonywa na kuhimizwa kwa bidii sana na kuelezewa kujishughulisha wenyewe na matendo mema, hatuwezi na hatupaswi kuivumilia, kuifundisha, au kuitetea kauli hii katika makanisa yetu.
V. SHERIA NA INJILI
1. Tofauti kati ya sheria na Injili ni mwanga wa heri unaometameta sana ili Neno la Mungu ligawanywe kwa uhalali,1841 na maandiko ya manabii na ya mitume yafafanuliwe na yaeleweke vyema. Basi, inatubidi kuichunguza tofauti hii kwa makini ili tusiyachanganye mafundisho haya mawili na kuibadilisha Injili kuwa sheria. Hii itautia giza ustahili wa Kristo na kuzinyang’anya dhamiri zinazosumbuka faraja ambayo zingepata katika Injili Takatifu ikihubiriwa katika uwazi na usafi wake bila mkanganyiko, kwani kwayo, Wakristo wanaweza kuitegemea dhidi ya hofu kuu ya sheria wanapopata majaribu makubwa.
2. Katika jambo hili, kumekuwa na majadiliano baina ya wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg. Kundi moja hudai kwamba, Injili si mahubiri ya neema tu, bali wakati huo huo ndiyo mahubiri ya toba yanayokemea dhambi kubwa zaidi, yaani, kutoamini.1842 Kundi lingine linazingatia na kushikilia kwamba, Injili si mahubiri ya toba na adhabu. Wanasema kwamba, kazi hii ndiyo ile ya sheria ya Mungu inayoadhibu dhambi zote na kutoamini, ambapo Injili ndiyo mahubiri ya neema na huruma ya Mungu kwa ajili ya Kristo, ambapo mahubiri yake
1840 Kilaini: ‘Propter veras causas et ad veros fines.’
1841 Dokezo la 2 Tim. 2:15.
1842 Rejea mafundisho ya Yohana Agricola yaliyoitwa ‘antinomia,’ yaani, upingaji wa sheria. Melanchthon alifundisha hivyo pia katika kitabu chake kiitwacho, ‘Loci Communes’ ambamo anaita Injili kuwa mahubiri ya toba na ahadi.
615
yanawahakikishia watu waliotubu na kumgeukia Kristo kwamba, kutokuamini kwao kunakokemewa na sheria ya Mungu kumesamehewa.1843
3. Tukichunguza majadiliano haya kwa makini, tunapata kuona kwamba, yanasababishwa na matumizi tofauti ya neno moja dogo ‘Injili’ ambalo halitumiki kwa njia moja tu bali linatumika katika maana mbili katika Maandiko Matakatifu ya Neno la Mungu na maandiko ya wanatheologia wa kale na wa siku hizi. 4. Kwa upande mmoja, neno ‘Injili’ limetumika katika maana ya mafundisho yote ya Kristo, Bwana wetu ambayo alifundisha katika huduma yake ya mahubiri hapa duniani na yote aliyoamuru yazingatiwe katika Agano Jipya. Hapa Injili inatumika kufafanua sheria na kuitangaza huruma na neema ya Mungu, Baba yetu wa mbinguni kama ilivyoandikwa katika Mk. 1:1: “Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.” Kisha muhtasari wa mafungu makuu yanatangazwa, yaani, toba na ondoleo la dhambi (Mk. 1,4). Vile vile, baada ya kufufuka kwake Kristo, alipowaamuru mitume wake kuihubiri Injili katika ulimwengu wote (Mk.16:15), alijumlisha mafundisho yake kwa maneno machache kama katika Luka 24:46-47: “Ndivyo ilivyoandikwa kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi.” Kadhalika, Mt. Paulo anayaita mafundisho yake yote kuwa ‘Injili’ (Mdo. 20:24) na anaifupisha kwa vichwa hivi: Toba kwa Mungu na imani katika Kristo. 5. Katika maana hii, ni halali kusema kwamba, Injili ndiyo mahubiri ya toba na msamaha. Hapa Injili ni fasili ya ‘ahlabu’1844 ikitumiwa kwa upana licha ya tofauti iliyopo kati ya Injili na sheria. Hivyo, ni sahihi kutumia neno Injili kama mahubiri ya toba na msamaha wa dhambi. Kwa kuwa Kristo, Yohana, na mitume walianza mahubiri yao kwa toba na wakaelezea na kusisitiza ahadi ya ondoleo la dhambi na sheria takatifu.
6. Kisha, neno ‘Injili’ linatumika katika maana nyingine, yaani, katika maana yake halisi. Halijumuishi tangazo la toba, bali linahubiri kuhusu neema ya Mungu peke yake. Haya yanaonekana baadaye katika Marko 1:15 Kristo anaposema: “. . . tubuni, na kuamini Injili.”
7. Tena, matumizi ya neno dogo ‘toba’ hayana maana moja tu katika Maandiko Matakatifu. Mahali pengine katika Maandiko Matakatifu, neno hili linamaanisha uongofu wote wa mwanadamu kama katika Lk. 13:5: “Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo,” na tena katika Lk. 15:7: “Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.” 8. Lakini katika dondoo lililotajwa katika Mk. 1:15, 1843 Watetezi wa msimamo huu walikuwa: Matthias Flacius, Matthayo Yudex, na Yohana Wigand. 1844 Kilatini: ‘Definitio generalis.’
na mahali pengine ambapo toba na imani katika Kristo (Mdo. 20:21), au toba na msamaha wa dhambi (Lk. 24:46) yanatajwa moja kwa moja, neno ‘kutubu’ linamaanisha mwanadamu anatambua dhambi zake, anakuwa na majuto na anaziacha. 9. Ufahamu huu ndio hutokana na sheria, lakini bado hautoshi kwa uongofu mabruki1845 kwa Mungu. Hivyo, lazima imani katika Kristo iingie. Wote waliovunjika na mahubiri ya sheria na wako tayari kutubu, mahubiri yenye faraja ya Injili Takatifu yanawatolea ustahili wa Kristo ili upokelewe kwa imani. Hivyo, Injili haihubiri msamaha wa dhambi kwa mioyo isiyojali na isiyokuwa thabiti, bali kwa mioyo ‘iliovunjika’ au iliyo tayari kutubu (Lk. 4:1). Ili majuto au woga unaoletwa na sheria usiwe wa kukatisha tamaa, lazima mahubiri ya Injili yaongezwe ili yawe “toba iletayo wokovu isiyo na majuto” (2 Kor. 7:10).
10. Kuihubiri sheria tupu bila Kristo huzaa watu wenye kiburi wanaoamini kwamba, wanaweza kutekeleza madai ya sheria kwa uwezo wao binafsi au yanamwelekeza mwanadamu kukata tamaa kabisa. Hivyo, Kristo anajichukulia sheria mikononi mwake na kuifafanua kwa njia ya kiroho (Mt. 5:22 n.k.; Rum. 7:6, 14). Anaidhihirisha ghadhabu yake katika ukubwa wake kutoka mbinguni kwa wakosaji wote. Kwa hiyo basi, kwa kweli, wakosaji wanapaswa kuzitambua dhambi zao kwa sheria, jambo ambalo Musa hangeweza kuwashurutisha walifanye kamwe. Naam, mtume anashuhudia kwamba, ingawa torati ya Musa inasomwa, “utaji alioutia juu ya uso wake,” hautaondolewa, ili wasione sheria kwa njia ya kiroho, au kiasi kinachodaiwa kwetu, au jinsi sheria inavyotulaani kwa njia ya jehanamu kwa sababu tumeshindwa kuitimiza. “Wakati wowote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa” (2 Kor. 3:13-16).
11. Kwa hiyo, Roho wa Kristo hapaswi kufariji tu, bali kwa njia ya huduma ya sheria, lazima aushutumu ulimwengu juu ya dhambi.1846 Hata katika Agano Jipya, lazima Roho atende linaloitwa na nabii ‘kitendo cha kigeni,’1847 yaani, kuadhibu, hadi aichukue kazi yake halisi,1848 yaani, ya kufariji na kuhubiria neema. Kwa hiyo basi, Kristo amepatiwa Roho na Baba yake na amemtuma kwetu. Kwa hiyo pia, anaitwa Mfariji1849 jinsi Dk. Luther anavyoelezea katika ufafanuzi wake wa Injili ya Jumapili ya Tano baada ya Utatu kwa maneno yafuatayo:
12. “Mahubiri yote yanayohubiri juu ya dhambi zetu na ghadhabu ya Mungu bila kujali ni lini au ni vipi inatendeka, ni utangazaji wa sheria. Kwa upande
1845 Kilatini: ‘Salutaris.’ 1846 Yn. 16:8.
1847 Isa. 28:21; ‘Union Version:’ ‘Kitendo cha ajabu.’ Kilatini katika Toleo la Vulgata: ‘Opus alienum.’
1848 Kilatini: ‘Opus proprium.’ 1849 Yn. 16:7.
mwingine, Injili ni utangazaji unaotuonyesha na kutupatia neema na ondoleo la dhambi katika Kristo bila kulijua lolote lingine. Wakati huo huo, ni kweli tena ni haki kwamba, mitume na wahubiri wa Injili, jinsi Kristo mwenyewe alivyofanya, wathibitishe utangazaji wa sheria na waanze na sheria kwa wale ambao, tangu awali, hawajafahamu dhambi zao wala kuhofia ghadhabu ya Mungu, jinsi anavyosema katika Yn. 16:8-9: ‘Naye akiisha kuja, huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu, . . . kwa sababu hawaniamini mimi.’ Kwa kweli, ni wapi ambapo mahubiri kuhusu ghadhabu ya Mungu yamedhihirisha wazi isipokuwa katika mateso na kifo chake Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee? Walakini isipokuwa haya yote yanatangaza ghadhabu ya Mungu na kuwaogofya wanadamu, hayo si Injili wala si tangazo la Kristo mwenyewe, ila ni tangazo la Musa na sheria inayotangazwa kwa ambao hawajatubu. Kwa kuwa Injili pamoja na Kristo haikuwekwa wakfu ili kutuogofya, wala kutuhukumu, bali kwa kutufariji na kuwainua ambao wana hofu na wenye huzuni kubwa.” Tena: “Kristo anasema: 13.‘Roho atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi,’1850 jambo ambalo haliwezi kufanywa bila ufafanuzi wa sheria.”1851
14. Pia, Mafungu ya Smalkaldi yanasema: Agano Jipya linadumisha na kutekeleza huduma hii ya sheria kwa njia ya kudhihirisha dhambi na ghadhabu ya Mungu.1852 Lakini katika huduma hii inaongeza mara moja ahadi ya neema ya Mungu kwa njia ya Injili. 15 Tena Utetezi unasema kwamba, mahubiri ya sheria hayatoshi kwa toba halisi, lazima Injili iongezwe kwayo.1853 Hivyo, mafundisho haya mawili yako pamoja sambamba, na yote mawili lazima yatiliwe maanani pamoja, lakini iwe kwa utaratibu mwema na kutofautisha kwa usahihi. Kwa hiyo, kwa haki, tunakemea wapinga na wapinzani wa sheria1854 wanaokataa mahubiri ya sheria katika makanisa na kudai kwamba, dhambi ilaumiwe na majuto na huzuni visifundishwe kutokana na sheria, bali kutokana na Injili.
16. Lakini ili kila mtu afahamu kwamba, hakuna kitu tunachokificha katika mabishano haya ya kisasa na tunaweka kila kitu kwa njia safi na wazi kwa wasomaji Wakristo, tunayawasilisha haya:
17. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwa ridhaa kuu kwamba, kwa kweli, sheria ni mafundisho ya kimungu yanayodhihirisha haki na mapenzi ya Mungu yasiyobadilika. Inaonyesha jinsi hali ya mtu inavyopaswa katika
1850 Yn. 16:8.
1851 Toleo la Jena, Buku la pili, sahifa ya 455.
1852 Mafungu ya Smalkaldi 3:3. Toba.
1853 Utetezi, IV, 257.
1854 Kijerumani: ‘Gesetzstürmer,’ kutokana na analogia ya ‘Bilderstürmer,’ (wapinga sanamu), ‘Iconoclast’. Kilatini: ‘Antinomi,’ adversari legis.’
mawazo, maneno, na matendo ili awe mwenye kumfurahisha Mungu na wa kupokelewa naye. Pia, inawatisha ambao wameivunja sheria kwa ghadhabu ya Mungu pamoja na hukumu ya muda na ya milele jinsi Luther anavyosema dhidi ya wapinga sheria:1855 “Chochote kinachokemea dhambi ni na kinatokana na sheria, na kina kazi ya kushutumu dhambi na kuelekezea watu kwa ufahamu wa dhambi” (Rum. 3:20; 7:7). Kwa kuwa kutoamini ni mzizi na chanzo cha dhambi zote zinazostahili kuadhibiwa, sheria inakushtaki pia. 18. Lakini pia ni kweli kwamba, Injili inaelezea na kufafanua sheria na mafundisho yake. Hata hivyo, kazi halisi ya sheria ni kuishtaki dhambi na kutoa maelezo ya matendo mema.
19. Hivyo basi, sheria hushtaki kutoamini, yaani, mtu asipoamini Neno la Mungu. Kwa kuwa Injili peke yake ambayo, kusema kweli, hufundisha na kuamuru kumwamini Kristo, ndiyo Neno la Mungu, Roho Mtakatifu, kwa njia ya huduma ya sheria inayoshtaki pia kwa ajili ya kutoamini kunakowafanya watu wasimwamini Kristo. Hata hivyo, kwa kweli, Injili tu ndiyo inayofundisha kuhusu imani iokoayo katika Kristo.
20. Injili ni mafundisho yanayofundisha anayopaswa kuyaamini mtu ili aweze kupata ondoleo la dhambi kutoka kwa Mungu, kwa kuwa mtu ameshindwa kuishika na ameivunja sheria ya Mungu kwa asili potovu, mawazo, maneno, na hupingana na sheria kila mara. Kwa hiyo, anastahili ghadhabu ya Mungu, kifo, mateso ya muda, na adhabu ya moto wa kuzimuni. Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, Bwana wetu, aliichukua laana ya sheria mwenyewe, akaifidia na akailipia kwa ajili ya dhambi zetu zote kiasi kwamba, katika yeye, tunaingia tena katika neema ya Mungu, tunapata ondoleo la dhambi, tunakuwa huru kutoka katika kifo, kutoka katika adhabu zote za dhambi, na tunaokolewa milele pia kwa imani.
21. Kuhusu lolote linalofariji, linalotoa huruma na neema ya Mungu kwa wale ambao wamevunja sheria, kusema kweli ndiyo Injili, habari njema yenye furaha kwamba, Mungu hapendi kuiadhibu dhambi, bali anaisamehe kwa ajili ya Kristo.
22. Kulingana na hayo, kila mkosaji aliyejuta lazima aamini. Yaani, amtegemee Bwana Yesu Kristo kabisa, “ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili mpate kuhesabiwa haki.”1856 “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.”1857 Alifanywa kwetu haki itokayo kwa Mungu. Alikuwa haki yetu, kwa sababu wakati wa hukumu ya Mungu, utiifu wake unahesabiwa kwetu kuwa haki yetu. Hivyo, jinsi ilivyoelezewa awali, sheria ni huduma inayoua na
1855 WA 39:348. Toleo la Erlangen 13:153. 1856 Rum. 4:25. 1857 2 Kor. 5:21.
inayoitangaza laana kwa herufi.1858 Injili ni “uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye.”1859 Injili ndiyo inatangaza haki na kupatia Roho.1860 Dk. Martin Luther anaelezea kwa makini tofauti hii katika maandiko yake yote. Ameonyesha kwa upana tofauti iliyoko kati ya ufahamu wa Mungu unaotokana na Injili na unaofundishwa kutokana na sheria. Kwa kuwa kutokana na sheria ya asili, kwa kiasi, Wapagani wana ufahamu kuhusu Mungu ingawa hawakumwelewa sawasawa wala hawakumheshimu ipasavyo (Rum. 1:21).
23. Tangu mwanzo wa ulimwengu, mahubiri haya mawili yamekuwepo yakifundishwa bega kwa bega katika Kanisa la Mungu lakini kwa njia tofauti halisi. Wahenga wetu na uzao wao wenyewe walikumbuka kwamba, mwanzoni Mungu alimwumba mwanadamu akiwa mwenye haki na mtakatifu. Kwa sababu ya udanganyifu wa nyoka, mwanadamu alilivunja agizo la Mungu na akawa mwenye dhambi. Akapotoka mwenyewe pamoja na uzao wake na akaanguka katika mauti na uharibifu wa milele. Pia, wahenga walithibitishwa na wakafarijiana wenyewe kwa mahubiri kwamba, uzao wa mwanamke utakiponda kichwa cha nyoka.1861 Kadhalika, katika uzao wa Ibrahimu, mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.1862 Mwana wa Daudi, atauinua ufalme wa Israeli na kuwa nuru ya mataifa.1863 “Alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.”1864
24. Tunaamini na tunakiri kwamba, mafundisho haya mawili1865 lazima yasisitizwe katika Kanisa la Mungu mpaka ukamilifu wa dahari pamoja na tofauti hii bora: ni wajibu wa huduma ya Agano Jipya kuihubiri sheria. Lazima watu wasiotubu waogopeshwe kwa vitisho vya sheria hata wapate kutambua dhambi zao na kutubu kweli. Lakini wasikatishwe tamaa wala wasifanywe kufa mioyo. Naam, “torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani” (Gal. 3:24). Hivyo, haitutoi, bali inatuonyesha na kutuongoza kwa Kristo ambaye “ni mwisho wa sheria” (Rum. 10:4). 25. Mahubiri ya Injili takatifu kuhusu Kristo Bwana wetu, yatawafariji na kuwatia moyo tena kwa uhakikisho kwamba, wakiamini Injili, Mungu atawasamehe dhambi zao zote kwa njia ya Kristo na atawapokea kuwa watoto wake na kuwatafanya wenye haki na heri ya milele kwa neema tu bila ustahili wao wowote. Hii haimaanishi kwamba, watu
1858 Yaani herufi ya sheria, siyo herufi kamilifu ya Maandiko Matakatifu.
1859 Rum. 1:16.
1860 2 Kor. 3:9.
1861 Mwa. 3:15.
1862 Mwa. 22:18; 28:14.
1863 Zab. 110:1; Isa 40:10; 49:6.
1864 Isa. 53:5.
1865 Yaani, Sheria na Injili.
wanaweza kuitumia vibaya neema ya Mungu na kutenda dhambi kinyume chake. 26. Tofauti hii iliyoko kati ya sheria na Injili imeelezwa kwa makini na ujasiri na Mt. Paulo katika 2 Kor. 3:7-9.
27. Kwa hiyo basi, ili mafundisho haya mawili ya sheria na Injili yasichanganywe, sifa ya fundisho moja isihesabiwe kwa fundisho lingine. La sivyo, ustahili na fadhili za Kristo vitatiwa giza kwa urahisi. Injili itakuwa mafundisho ya kisheria tena, jinsi ilivyofanyika wakati wa Upapa, na hivyo kuwanyang’anya Wakristo faraja ya kweli waliyo nayo katika Injili dhidi ya hofu inayoletwa na sheria. Kwa hiyo, milango inafunguliwa tena kwa Upapa katika makanisa ya Mungu. Kwa hiyo, tofauti baina ya sheria na Injili lazima ihifadhiwe wazi na ifundishwe kwa bidii. Lazima tujihadhari kikamilifu dhidi ya yote ambayo yangeweza kusababisha mchanganyo wa sheria na Injili na kuvikoroga kuwa fundisho moja tu.1866 Ni hatari na kosa kubwa sana kuifanya Injili iliyo tofauti na sheria kuwa mahubiri ya toba na adhabu kwa jina lake halisi. Kwa hali yoyote mahali pengine, kwa kawaida, inaeleweka kama mafundisho kwa jumla, mafundisho yanayopatikana katika Utetezi.1867 Isitoshe, Injili inaitwa mahubiri ya toba na ondoleo la dhambi. Lakini, Utetezi1868 unaonyesha kwamba, katika maana yake halisi, Injili ni ahadi ya ondoleo la dhambi na kuhesabiwa haki katika Kristo, ambapo kinyume chake, sheria ni ujumbe unaokemea na kuihukumu dhambi.
VI. MATUMIZI YA TATU YA SHERIA
Inajulikana wazi kwamba, Sheria ya Mungu inatumika: 1.
1. Sio tu kwa shabaha ya kudumisha nidhamu na heshima ya nje dhidi ya watu washenzi na wasiotii,
2. bali inawaleta watu katika ufahamu wa dhambi zao.
3. Ambao wamekwisha kuzaliwa upya katika Roho Mtakatifu, ambao wameongoka katika Bwana, na ambao utaji wa Musa umekwisha kuondolewa kutoka kwao, wanajifunza katika kuishi1869 na kutembea katika sheria. Mabishano yametokea kati ya wanatheologia wachache kuhusu matumizi haya ya tatu na ya mwisho ya sheria.
1866 Kilatini: ‘Confusio inter legem et evangelium.’
1867 Kwa mfano, Utetezi 4, 62, 257; 12, 31, 45.
1868 Kwa mfano, Utetezi 4, 40, 57; 12, 45, 52, 73, 76.
1869 Maneno “jifunze katika sheria ya kuishi,” hayamo wala hayalingani na ya mwanzoni katika Kijerumani. Katika Kilatini tafsiri yake ni: ‘lege docentur ut in era pietate vivant et ambulant.’
2. Kundi lingine1870 lilifundisha na kushikilia kwamba, waliozaliwa upya, hawajifunzi utiifu mpya, matendo yapi ndiyo mema, na wanapaswa kutembea kutoka kwa sheria. Isitoshe, fundisho hili halipaswi kuwa na msingi wake katika sheria, kwa njia yoyote ile. Kwa kuwa wamefanywa huru na Mwana wa Mungu na wamekuwa mahekalu ya Roho wake. Hivyo basi, wako huru kadiri jua lichomozavyo lenyewe na kukamilisha mwendo wake wa kawaida bila nguvu yoyote ya nje ya kulisukuma. Pia nao, kwa hiari, kwa maongozi, na mvuto wa Roho Mtakatifu, hulifanya lile ambalo Mungu analolihitaji kwao. 3. Kinyume chake, kundi lingine1871 lilifundisha kwamba, ijapokuwa wenye imani halisi wanaongozwa kweli na Roho Mtakatifu, kulingana na utu wao wa ndani, hufanya mapenzi ya Mungu kutokana na Roho aliye huru. Hata hivyo, Roho Mtakatifu hutumia sheria iliyoandikwa kwa shabaha ya kuwafundisha. Kwa hiyo, hata wenye imani halisi wanajifunza kumtumikia Mungu si kulingana na nia zao, bali kulingana na sheria yake ilivyoandikwa na Neno ambalo ni kanuni na shauri la kuaminika katika maisha ya kimungu na mwenendo unaopatana na mapenzi ya Mungu ya milele yasiyobadilika.
4. Ili kuyaelezea dhahiri na kuyatuliza mabishano haya, tunaamini kwa umoja, tunafundisha, na tunakiri kwamba, ingawa Wakristo wenye imani ya kweli, ambao wamekuwa waongofu halisi wa Mungu, waliothibitishwa kuwa wana haki, wamekwisha kufanywa kuwa huru na kufunguliwa kutoka kwa laana ya sheria, lazima waendelee kufanya mazoezi daima katika Sheria ya Mungu jinsi ilivyoandikwa: “Heri mtu yule aendaye katika sheria za BWANA na sheria yake huitafakari mchana na usiku” (Zab.1:1, 2; 119:1, 35, 47, 70, 97). Kwa maana sheria ndiyo kioo ambacho kwacho, mapenzi ya Mungu na lile linalompendeza linadhihirishwa sawasawa. Ni muhimu waaminio kuishika sheria hii kwa nguvu machoni pao na kuisisitiza kwao siku zote kwa bidii.
5. Ni kweli kwamba, sheria haitolewi kwa watu wenye haki, jinsi Mt. Paulo anavyosema, bali kwa wasiokuwa wacha Mungu.1872 Lakini hili lisieleweke bila kikwazo kana kwamba, wenye haki wanapaswa kuishi bila sheria. Kwa kuwa sheria ya Mungu imeandikwa mioyoni mwao, maana hata mtu wa kwanza, mara tu baada ya kuumbwa, aliipokea sheria ili apate kujiongoza kwayo. Kwa maana kusudi la Mt. Paulo ni kwamba, sheria haiwezi kuwatwika mzigo wa laana ambao wamekwisha kupatanishwa na Mungu katika Kristo. Isitoshe, sheria haiwezi kuwatesa ambao wamezaliwa mara ya pili kwa njia kushurutisha kwake, kwa kuwa, kwa njia ya utu wa ndani, wanaifurahia sheria ya Mungu.
1870 N. von Amsdorf, A. Poach, A. Otho. 1871 J. Mörlin, J.Wigand. 1872 1 Tim. 1:9.
6. Iwapo watoto wa Mungu waaminio na waliochaguliwa, wangekuwa wamefanywa wapya kabisa katika maisha haya na Roho akaaye ndani yao, na kwa upande wa asili yao kuwa na nguvu zao huru kabisa kutokana na dhambi, hawangehitaji mwendeshaji. Bila mafundisho, mashauri, uongozi, na hima yoyote ya sheria, wangetenda kabisa lile ambalo linawapasa kulingana na mapenzi ya Mungu kwa hiari, jinsi jua, mwezi, na nyota zote za mbinguni zikamilishavyo mienendo yao kulingana na utaratibu ambao Mungu aliuweka wakati wote kwa hiari, bila kutatanisha, bila onyo lolote la upole, shauri, shurutisho, uzuizi, au masharti, na jinsi malaika wapendwa wamtiivyo Mungu kwa hiari halisi.
7. Lakini katika maisha haya, Wakristo hawafanywi wapya kabisa na wakamilifu1873 ingawa dhambi zao zimefunikwa katika utiifu mkamilifu wa Kristo na haziwezi kuhesabiwa kwa wale waaminio kwa njia ya laana ya milele. Ingawa Roho Mtakatifu ameanza kumwua Adamu wa Kale na kufanya upya roho yake nao, hata hivyo, Adamu wa kale bado anashikamana na hali yao ya asili na vipaji vyao vyote vya ndani na nje. 8 Kulihusu hili, mtume anaandika: “Najua ya kuwa ndani yangu, . . . halikai neno jema,” na tena, “lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.” Kadhalika: “Katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi.” Vilevile: “Mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.”1874
9. Kwa hiyo basi, watoto wa Mungu waliochaguliwa, walio na imani halisi, waliozaliwa upya, katika maisha haya, kwa ajili ya tamaa za mwili, hawahitaji tu mafundisho, onyo na tishio la kila siku, bali mara nyingi pia wanahitaji adhabu zinazowasukuma mbele kumfuata Roho wa Mungu jinsi ilivyoandikwa: “Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, nipate kujifunza amri zako.” Tena: “Nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” Tena: “Kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.”1875 Dk. Martin Luther analielezea hili kikamilifu na kwa urefu zaidi katika sehemu ya kiangazi cha ‘Postilla ya Kanisa’ kuhusu waraka wa Jumapili ya Kumi na Tisa baada ya Utatu.1876
1873 Kilatini: ‘Completive vel consummative.’
1874 Rum. 7:18, 19, 23; Gal. 5:17.
1875 Zab. 119:71; 1 Kor. 9:27; Ebr. 12:8. 1876 WA, 45:161-164. ‘Postilla:’ ´Post illa verba sacrae scripturae;’ ‘baada ya maneno ya Maandiko Matakatifu.’ Mahubiri au ufafanuzi wa maneno ya Biblia yaliyokwisha kusomwa, baadaye mkusanyiko wa mahubiri katika kitabu fulani. Dk. Luther alikuwa na ‘Postilla ya Kanisa’ kwa wahubiri na pia ‘Postilla ya Nyumbani’ kwa Wakristo wa kawaida. Hasa ‘Postilla ya Nyumbani’ ilikusanywa kutoka hatimkato ya wanafunzi wa Luther
10. Inatubidi pia kuelezea zaidi katika kila kipengele jinsi Injili huzaa, huumba, hufanya, na hutekeleza utiifu mpya katika waaminio pamoja na kazi ambayo sheria hufanya katika matendo mema ya waaminio.
11. Kwa kweli, sheria inatuelezea kwamba, ni mapenzi ya Mungu na amri kwamba, inatupasa kutembea katika maisha mapya lakini haitoi nguvu na uwezo wa kuyaanzisha au kuyaendeleza. Roho Mtakatifu ambaye hatolewi na hapokelewi kwa njia ya sheria, huifanya mioyo kuwa mipya, na hupokelewa kwa njia ya mahubiri ya Injili (Gal. 3:2, 14). 12Kisha, Roho Mtakatifu anaitumia sheria kwa mafundisho ya waliozaliwa upya, kuwaarifu na kuwaonyesha mapenzi ya Mungu yanayokubalika ni yapi katika Amri Kumi (Rum. 12:2). Isitoshe, anawaarifu na kuwaonyesha matendo mema ambayo Mungu ameyatayarisha ambayo kwayo, wanapaswa kutembea ni yapi (Efe. 2:10). Yeye pia huwaonya kuyatenda haya. Wakati wamekuwa wazembe, wasahaulifu, na wakaidi kwa ajili ya mwili, Roho Mtakatifu huwashutumu kwa njia ya sheria. Roho Mtakatifu ana huduma mbili: “Huua, naye hufanya kuwa hai; hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.”1877 Kazi yake si ya kufariji tu, bali pia ni ya kukemea, jinsi ilivyoandikwa: “Naye (Roho Mtakatifu) akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu (ambao unahusu Adamu wa kale) kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.”1878 13 Dhambi ni yote yaliyo kinyume cha sheria ya Mungu. Mt. Paulo anasema: 14. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao.”1879 Lakini shutuma ndiyo kazi halisi ya sheria. Kwa hiyo, aghalabu Wakristo wanapokosea, wanashutumiwa na Roho wa Mungu kwa mujibu wa sheria. Lakini Roho huyo huyo anawafufua tena na kuwafariji kwa mahubiri ya Injili Takatifu.
15. Ikiwezekana, inatubidi kuepuka kila sintofahamu na kudumisha mafundisho yetu tofauti hasa kati ya matendo ya sheria na ya Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, lazima kuchunguza, kwa juhudi maalumu ni lini tunatenda matendo mema ambayo yanapatana na sheria ya Mungu. La sivyo, hayawezi kuwa matendo mema. Hapa neno ‘sheria’ lina maana moja. Yaani, mapenzi ya Mungu yasiyobadilika, ambayo kwayo, mwanadamu atajiongoza katika maisha haya.
16. Lakini kuna tofauti kati ya matendo kulingana na tofauti baina ya watu wanaojikakamua kutekeleza sheria na mapenzi ya Mungu. Kwa maana, mwanadamu ambaye hajazaliwa upya huishi kulingana na sheria, na hufanya kazi yake tu kwa sababu ya agizo au kwa ajili ya hofu ya adhabu au tumaini la thawabu. Bado yu chini ya sheria. Mt. Paulo anaiita kazi ya mtu wa namna hiyo alipohubiri nyumbani kwa jamaa na marafiki zake.
1877 1 Sam. 2:6,7.
1878 Yn. 16:8.
1879 2 Tim. 3:16.
‘kazi za sheria’1880 kwa sababu matendo yake mema yanazaliwa na sheria jinsi yalivyokuwa matendo ya watumwa. Watu kama hawa ni watakatifu wa aina ya Kaini.1881
17. Lakini mwanadamu anapozaliwa upya kwa Roho wa Mungu na kuwekwa huru kutoka kwa sheria, yaani, mtu atakuwa huru kutoka kwa mwendeshaji huyo na ataendeshwa na Roho wa Kristo, ataishi kulingana na mapenzi ya Mungu yasiyobadilika na yaliyoandikwa katika sheria, na atayatenda yote kwa roho huru, yenye furaha, taraa,1882 na atazaliwa upya. Si halali kuyaita matendo haya kazi za sheria, bali ndiyo kazi na matunda ya Roho jinsi Mt. Paulo anavyoziita sheria za nafsi na sheria ya Kristo. Kulingana na Mt. Paulo, watu kama hawa hawamo tena chini ya sheria, bali chini ya neema (Rum. 6:14; 8:2).
18. Hivyo basi, kwa sababu waaminio hawajafanywa upya kikamilifu katika maisha haya, Adamu wa kale huambatana nao hadi makaburini. Yaani, vita kati ya Roho na mwili huendelea ndani yao. Kulingana na nafsi ya ndani kabisa, wanaifurahia sheria ya Mungu, lakini sheria iliyo ndani ya viungo vyao inafanya vita dhidi ya sheria ya nafsi zao. Hivyo, hawako bila sheria wala chini yake kamwe, bali wanaishi na kutembea katika sheria ya Bwana, lakini hawafanyi lolote kwa shurutisho la sheria.
19. Badala yake, Adamu wa kale ambaye bado anaambatana na anahusika nao, lazima azuiliwe kwa nguvu si kwa sheria tu lakini pia kwa taabu kuu kwa sababu huyu hufanya kila tendo kinyume cha mapenzi yake na kwa shurutisho, jinsi wasioongoka wanalazimishwa kuwa na utiifu kwa vitisho vya sheria (1 Kor. 9:27; Rum. 7:18, 19).
20. Licha ya hayo, waaminio wanahitaji mafundisho ya sheria ili wasianguke katika utakatifu na uchaji wao wenyewe katika kuzichagua na kuzipanga ibada zao wenyewe bila Neno la Mungu kwa kisingizio cha Roho Mtakatifu. Imeandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati: “Msifanye . . . kila mtu kama aonavyo vema machoni pake; nikuagizayo yote yatunze na kuyasikiza. Usiliongeze, wala usilipunguze” (Kum. 12:8, 28, 32).
21. Licha ya hayo, waaminio wanahitaji mafundisho ya sheria. La sivyo, wangeweza kudhania kirahisi kwamba, matendo yao na maisha yao yote ni makamilifu kabisa. Lakini sheria ya Mungu huonyesha kama kioo kwamba, matendo yetu mema si makamilifu katika maisha haya tena ni machafu.
1880 Rum. 2:15; 3: 20; Gal. 2:16; 3:2,10. 1881 Kilatini huongezea: yaani, wanafiki. 1882 Yaani, ‘kwa sharti.’
Tuseme pamoja na mpendwa Paulo: “Sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo.”1883 Wakati Paulo anawahimiza ambao wamezaliwa upya wayatende matendo mema, mbele yao, anazishika Amri Kumi sawasawa (Rum. 13:9). Isitoshe, yeye mwenyewe hujifunza katika sheria kwamba, matendo yake bado ni mapungufu na machafu (Rum. 7:18,19). Daudi anasema: “Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako” (Zab. 119:32),1884 lakini kwingineko tena anasema: “. . . usimhukumu mtumishi wako, maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki” (Zab. 143:2).
22. Sheria hudai utiifu mkamilifu na safi kabisa kuwa wa kumpendeza Mungu. Haitufundishi kwa nini na kwa sababu gani matendo mema ya waaminio yanampendeza Mungu ingawa katika maisha haya, bado haijawa kamilifu na ni chafu kwa sababu ya dhambi iliyomo katika miili yetu. Kinyume chake, Injili inatufundisha kwamba, kafara zetu za kiroho zinakubalika kwa Mungu kwa imani kwa ajili ya Kristo (1 Pet. 2:5; Ebr. 11:4; 13:15). 23. Kwa heshima hiyo, Wakristo hawako chini ya sheria, bali chini ya neema kwa sababu nafsi zao zimefanywa huru kutokana na laana na hukumu ya sheria kwa imani katika Kristo. Ingawa matendo mema ya mtu hayajawa makamilifu na bado ni machafu, yanakubalika kwa Mungu kwa ajili ya Kristo. Kulingana na nafsi yake ya ndani, anafanya yanayompendeza Mungu si kwa shurutisho la sheria, bali kwa radhi na hiari ya kutoka moyoni kwa kufanywa upya na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, daima anaendelea katika vita dhidi ya Adamu wa kale.
24. Adamu wa kale ni punda asiyeweza kuongozwa na ni mkaidi sana. Mafundisho ya sheria, maonyo, hima, na vitisho havimtoshi. Licha ya haya, lazima ashurutishwe katika utiifu wa Kristo kwa bakora ya adhabu na taabu, mpaka mwili wa dhambi uwekwe nje kabisa na mtu afanywe mpya kabisa katika ufufuo. Hapo, hatahitaji mafundisho ya sheria wala kitisho na adhabu kamwe. Kadhalika, hatastahili Injili kamwe kwa kuwa bado yu katika maisha haya yasiyokuwa makamilifu.
25. Lakini watamwona Mungu uso kwa uso. Wakati huo basi, wataweza kuyatekeleza mapenzi ya Mungu kwa msaada wa Roho wa Mungu aliye ndani yao. Watayafanya mapenzi yake kwa hiari bila kushurutishwa na kuzuiliwa. Badala yake, watafurahia huko milele na milele kwa utimilifu, ukamilifu, na kwa furaha kuu.
Kwa hiyo, tunakataa na tunayahukumu mafundisho haya ya uasi yaliyoelezewa hapo juu, ambayo hudhuru kweli, yaliyo kinyume kabisa cha maadili ya Kikristo, 1883 1 Kor. 4:4. 1884 Kilatini: ‘Viam mandatorum tuorum cucurri.’
626
na uchaji wa kweli kwamba, sheria isihubiriwe kwa Wakristo, wenye imani halisi, wakweli, bali tu kwa wasioamini, wasiokuwa Wakristo, na wasiotubu.
VII. CHAKULA KITAKATIFU
1. Inawezekana kwamba, maoni ya maelezo mengine ya fungu hili hayapaswi kuunganishwa katika makataa haya, ambapo tunanuia kujishughulisha tu na mafungu yaliyokuwa katika mabishano kati ya wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg. Mapema sana, karibu mwaka wa 1530, wakati Ukiri wa Augsburg ulitungwa na kutolewa kwa Kaisari, walioidharau Sakramenti walikanusha na waliuacha kabisa Ukiri wa Augsburg na waliutoa ukiri wao wenyewe.1885
Hata hivyo, kwa bahati mbaya, miaka iliyopita baadhi ya wanatheologia na Wakristo wengine waliojigamba kushikamana na Ukiri wa Augsburg, walithibitisha wazi misimamo ya wanaoidharau sakramenti.1886 Kinyume cha dhamiri zao wenyewe, walijaribu kuuvuruga na kuughushi ufafanuzi wa Ukiri wa Augsburg ili upate kuonekana kuwa mojawapo ya makubaliano kamili ya mafundisho ya wanaoidharau Sakramenti. Kwa hiyo, hatuwezi wala hatupaswi kuzuia kutoa ushuhuda kuhusu ukweli wa kimungu kwa njia ya ukiri wetu katika andiko hili. Hii ndiyo sababu na wajibu wetu wa kimungu usioweza kuepukika wa kuukiri ukweli wa kimungu katika makataa haya na kutoa ushuhuda wake. Kwa shabaha hiyo, tutarudia tena ufahamu na ufafanuzi halisi wa maneno ya Kristo na Ukiri wa Augsburg katika fungu hili. Kwa msaada wa Mungu, tutafanya yote tuwezavyo kulihifadhi kwa ajili ya uzao wetu na kwa uaminifu wa kuwaonya wasikilizaji wetu na Wakristo wengine wanaomcha Mungu dhidi ya uasi huu wenye madhara, ambao kwa ujumla, ndio kinyume cha Neno Takatifu la Mungu, Ukiri wa Augsburg, na ambao umelaaniwa mara kwa mara.
Status Controversiae – Ajili ya Ubishi
Majadiliano makuu kati ya mafundisho yetu na ya wanaoidharau sakramenti katika fungu hili
2. Baadhi ya wanaoidharau Sakramenti, wanajaribu kwa uangalifu kutumia msamiati ambao unakaribiana sana na kanuni na mitindo ya usemi wa Ukiri wa 1885 ‘Ukiri wa Miji Minne,’ ‘Confessio Tetrapolitana’ na andiko la Zwingli ‘Fidei ratio.’ Ukiri huu ulikubaliwa na Zürich . . .
1886 Wakalvinisti wa siri waliokuwa maprofesa wa theologia, utabibu, na sheria katika vyuo vikuu vya Wittenberg na Leipzig. Walihusika na maandiko ‘Catechesis Wittebergica’ (1571), ‘Grundfest,’ na ‘Dresdner Abschied’ (1571) na ‘Exegesis perspicua’ (l574), kati yao wakiwemo Wolfang Crell, Caspar Cruciger, Joachim Eger, Christop Pezel, Caspar Peucer, Erasmus Rüdinger, Hieronymus Schaller, Georg Krakow, Johann Stössel, Johann Hermann, na Christian Schütz (Sagittarius).
627
Augsburg na wa makanisa yake. Wanakiri kwamba, kwa kweli, waaminio hupokea mwili wa Kristo katika Chakula Kitakatifu. Lakini tukiwataka walifafanue wazo lao maalumu kwa dhahiri, uaminifu, na uwazi, wote wanatangaza kwa ridhaa kuu kwamba, asili ya mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo ina nafasi kubwa zaidi katika mwili na damu iliyobarikiwa mezani jinsi mbingu zilivyo juu kuliko dunia. Kwani maneno yao wenyewe yanadai: “Tunasema kwamba, mwili na damu ya Kristo i mbali zaidi kiishara na kwa nafasi kubwa jinsi mbingu zilivyo juu kuliko dunia.”1887 3. Kwa hiyo, wanaelewa uwepo wa mwili wa Kristo si kwamba, unaichukua nafasi hapa duniani, bali kuwa jambo linalohusu imani tu, ‘in respectu fidei:’ imani yetu inakumbushwa na kuhuishwa na ishara inayoonekana kwa namna hiyo jinsi Neno linavyohubiriwa. Hivyo basi, imani hujiinua yenyewe, hupanda katika mbingu yote, hupokea, na kushiriki kweli na asili, lakini bado ni ya kiroho tu. Kwa kuwa mwili wa Kristo ambao u huko mbinguni, ndio mwili wa Kristo mwenyewe na wenye fadhili zake zote. Jinsi ambavyo mkate na divai viko hapa duniani na si mbinguni, kadhalika, sasa, mwili wa Kristo u mbinguni na si duniani. Kwa hiyo, hauwi kingine, bali mkate na divai vinavyopokelewa na kuliwa katika Chakula Kitakatifu.
4. Mwanzoni, walitoa hoja kwamba, Chakula Kitakatifu kilikuwa ishara ya nje tu ambayo kwayo, Wakristo wangeweza kutambuliwa.1888 La sivyo, hakikuwa zaidi ya mkate na divai tupu ambavyo ni ishara tupu za kutokuwepo kwa mwili wa Kristo, na ambavyo vinagawiwa. Kwa kuwa wazo hili halikuweza kushikiliwa, walikiri kwamba, Kristo aliye Bwana kweli yu katika Chakula Kitakatifu, communicatio idiomatum,1889 yaani, kulingana na asili yake ya kimungu tu, lakini si kulingana na mwili na damu yake.1890
5. Baadaye, walipolazimishwa kwa maneno ya Kristo, walikiri kwamba, mwili wa Kristo u katika Chakula Kitakatifu. Bado hawakuuelewa na wakauelezea tu kama kitu kinachopokelewa kwa njia ya kiroho peke yake. Yaani, kulingana na nguvu, kazi, na fadhili zake zinazopokelewa kwa imani. Wanasema kwamba, kwa njia ya Roho wa Kristo ambaye yu kila mahali, miili yetu, ambamo Roho wa Kristo anaishi hapa duniani, huunganika na mwili wa Kristo ambaye yu mbinguni.
6. Kama matokeo, watu mashuhuri wamekanganywa na kutiwa kiwi na maneno haya wanapodai na kujisifu kwamba, hawana wazo lingine isipokuwa kwamba, kweli, Kristo Bwana yu katika Chakula Kitakatifu chake katika asili na 1887 Consensus Tigurinus, 25: ‘Abesse Christi corpus et sanguinem a signis tanto intervallo dicimus, quanto abest terra ab altissimis coelis.’
1888 Vivyo hivyo, Zwingli katika andiko lake la ‘Fidei Ratio.’
1889 Kilatini: ‘per commucationem idiomatum.’
1890 Vivyo hivyo, ‘Grundfest’ (1571), 175b; ‘Catechesis Wittebergica’ (l571), 83, 128.
uhai. Walakini, kwa upande wa asili yake ya kimungu tu na si kwa mwili na damu yake, ambavyo sasa vipo mbinguni na si penginepo. Pamoja na mkate na divai, Kristo hutupatia mwili wake na damu yake ya kweli ili tule, kwa njia ya kiroho, kwa imani, na si kwa njia ya mwili kwa kinywa.1891
7. Watu hawa hawaelewi maneno ya Chakula cha Bwana, “Huu ndio mwili wangu,”1892 kama jinsi maneno yenyewe yanavyosikika hasa kulingana na herufi zake, lakini kama lugha ya kitamathali. Wanafasiri kwamba, “kula mwili wa Kristo” kunamaanisha ‘kuamini.’ Nao ‘mwili’ unamaanisha ‘alama,’ yaani, ishara au mfano wa mwili wa Kristo ambao haupo katika ushirika duniani bali mbinguni. 8. Wanalifafanua neno ‘NI’1893 kwa maana ya Sakramenti au kwa njia ya tamathali wakimaanisha kwamba, mwili wa Kristo umeunganishwa na mkate na kwamba, wakati Wakristo wacha Mungu na wenye imani hula mkate kwa vinywa vyao, kwa imani, wanashiriki mwili wa Kristo kiroho ambao upo mbinguni.1894 Lakini wao hulaani na kuhukumu, kama ukafiri makuruhu, mafundisho kwamba, mwili wa Kristo wenyewe, katika asili yake, upo hapa duniani pia katika Chakula Kitakatifu ingawa, kwa njia isiyoonekana, na isiyoeleweka, hupokelewa na wanafiki au Wakristo bandia pia.1895
9. Kinyume chake, Ukiri wa Augsburg unafundisha kulingana na Neno la Mungu: “Mwili na damu ya Kristo vipo hapa kwa kweli, na vinatolewa kwa wale wanaoshiriki Chakula cha Bwana. Unawakataa wanaofundisha vinginevyo.”1896 Yaani, mafundisho ya wanaoidharau Sakramenti, ambao wakati huo huo walimtolea Kaisari ukiri wao wenyewe huko Augsburg. Katika ukiri wao, wanasisitiza kwamba, baada ya kupaa mbinguni, kwa kweli, mwili wa Kristo haupo katika asili yake hapa duniani katika Sakramenti. 10. Dk. Luther anatoa dhahiri wazo sawa katika Katekisimo Ndogo kwa maneno yafuatayo: “Sakramenti ya Madhabahu ni mwili wa kweli na damu ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo katika mkate na divai, iliyoanzishwa na Kristo mwenyewe
1891 Vivyo hivyo, ‘Exegesis perpicua’ (l574), kur. 17 n.k. 1892 1 Kor. 11 :24. 1893 Au ‘ndio.’
1894 Andiko la Kijerumani lina sehemu ya Kilatini hapa: “sacramentaliter seu modo significativo.” Msimamo wa wafuasi wa H. Zwingli na J. Calvin ni kwamba, sakramenti ina maana ya kitamathali tu na haina kiini cha kweli cha maneno jinsi Walutheri wanavyokiri kuhusu sakramenti. “. . . ne quis rem cum signis ita putet copulari, ut Christi quoque caro nunc in terris adsit modo quodam invisibili et imcomprehensibili,” yaani, “Mtu yeyote asifikirie kuhusu jambo la ishara kwamba, mwili wa Kristo unaweza kuwepo hapa duniani pia kwa njia fulani isiyoonekana au isiyoeleweka.” Kauli ya Sinodi ya Bern 47, Ukiri wa Basel 97:36 n.k., ‘Confessio Helvetica Prior’ 107:23 n.k., 35 n.k., Ukiri wa Zürich 158:7, ‘Consensus Tigurinus’ 10:161, Katekisimo ya Heidelberg, 102:105 n.k., Calvin Inst. 4:17,18.
1895 J. Calvin, Inst. 4: 17, 26, ‘Consensus Tigurinus’ 26.
1896 Ukiri wa Augsburg, 10.
629
kwa ajili yetu Wakristo katika kula na kunywa.”1897 11. Na bado, katika Utetezi, haijawekwa wazi zaidi na tena inatia hamasa hapo kwa maneno ya Paulo katika (1 Kor. 10:16) na katika dondoo kutoka kwa Kirillo ifuatavyo: Fungu la Kumi limekubaliwa tunapokiri maoni yetu kwamba, mwili na damu ya Kristo vipo katika Chakula cha Bwana kweli na kwa uthabiti1898 na vinatolewa pamoja na vitu vinavyoonekana, yaani, mkate na divai, kwa wale wanaoipokea Sakramenti. Basi, Paulo anasema: “Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo, na kadhalika. Roho Mtakatifu peke yake akiwepo katika Chakula Kitakatifu na si mwili wa Kristo, itafuatia kwamba, mkate ni ushirika katika Roho wa Kristo na si katika mwili wake. Tunajua vizuri kwamba, si Kanisa la Roma tu bali Kanisa la Kiyunani pia linafundisha kuwepo kwa mwili wa Kristo katika Ushirika Mtakatifu.”1899 Kisha, kauli ya Kirillo inadondolewa kwamba, Kristo anakaa ndani yetu kwa njia ya mwili katika Chakula Kitakatifu kwa njia ya kututolea mwili wake kuwa chakula chetu.
12. Baadaye, waliokuwa huko Augsburg walipoutoa ukiri wao wenyewe kuhusu fungu hili na walipoonekana kuukubali Ukiri wa makanisa yetu, wanatheologia wa Sachsen na Kusini mwa Ujerumani walilitunga ‘Shauri la Mwafaka’1900 la Kikristo huko Wittenberg mwaka wa 1536.1901 Dk. Martin Luther na wanatheologia wengine wa vikundi vyote viwili walitia sahihi zao:
13. “Tumesikia jinsi Bwana Martin Bucer alivyoelezea maoni yake kuhusu Sakramenti Takatifu ya mwili na damu ya Kristo na ya wahubiri wengine waliokuja pamoja naye kutoka mijini.
14. Wanakiri, kulingana na maneno ya Irenaeo1902 kwamba, kuna vitu viwili katika Sakramenti hii. Yaani, kimoja cha mbinguni na kingine cha duniani. Hadi, wanashikilia na kufundisha kwamba, mwili na damu ya kweli ya Kristo vipo, vinagawiwa, na kupokelewa pamoja na mkate na divai, japo wao huyakana mageuzo-uwamo.1903 Yaani, kiini cha mkate na divai vibadilishwe kuwa mwili na damu ya Kristo. Hawaamini pia kwamba, mwili na damu ya Kristo vimo katika mkate katika mahali pao1904 au vimo kwa njia nyingine vikiwa vimeunganika na kudumu pamoja mbali na kuipokea Sakramenti.1905 Hata hivyo, wanakubali
1897 Katekisimo Ndogo, 6: 2.
1898 Kilatini: ‘Vere et substantialiter.’
1899 Dondoo hili halifuati maneno ya Utetezi kikamilifu.
1900 Kilatini: ‘Formula Concordiae.’
1901 Mwafaka wa Wittenberg, l536.
1902 Irenaeus, Haer. 4:18, 5.
1903 Kilatini: ‘Transsubstantiatio.’
1904 Kilatini: ‘Localiter.’
1905 Kijerumani: ‘Niessung,’ kupokea kwa njia ya kula na kunywa. Kilatini: ‘Extra usun,’ (mbali na
kwamba, kwa njia ya muungano wa sakramenti, mkate ndio mwili wa Kristo na kadhalika. 15 Lakini nje ya kupokelewa au kama mkate unatiwa kando au unaingizwa kisandukuni1906 au unapelekwa na kuonyeshwa katika maandamano jinsi wafuasi wa Papa wanavyofanya, hawashikilii kwamba, ni mwili wa Kristo.1907
16. Pili, wanashikilia kwamba, sakramenti hii itadumu katika Ukristo kwa sababu ilianzishwa na Kristo. Sakramenti hii haitegemei ustahimilivu au kutostahili kwa mtumishi anayeigawa Sakramenti au aipokeaye, kwa kuwa jinsi Mt. Paulo anavyosema, wasiostahiki wao hupokea sakramenti pia. Kwa hiyo, wanashikilia kwamba, mahali pale ambapo uanzishaji na amri ya Kristo vinatolewa, mwili na damu ya Kristo kweli vinagawanywa kwa wasiostahiki na kwamba, wanavipokea kwa kweli. Lakini wakiipokea, wanaipokea kwa hukumu, jinsi Mt. Paulo anavyosema. Kwa sababu wanatumia vibaya Sakramenti Takatifu, maana wanaipokea bila toba ya kweli na bila imani. Kwa kuwa, Sakramenti hii ilianzishwa ili ishuhudie kwamba, neema na fadhili za Kristo zinaambatana nao, na wanaunganishwa katika Kristo, na wanaoshwa na damu ya Kristo katika toba ya kweli na faraja ya imani katika Kristo.”
17. Mwaka uliofuatia wanatheologia hodari mno wa Ukiri wa Augsburg walikusanyika kutoka pande zote za Ujerumani katika Smalkaldi ili kuchunguza ni mafungu gani ya mafundisho wangeweza kuyatoa katika sinodi kuu. Kwa makubaliano, Dk. Martin alitunga Mafungu ya Smalkaldi ambayo wanatheologia wote waliyatilia sahihi zao. Mafundisho halisi yanatolewa katika mafungu haya kwa ufupi na dhahiri kwa maneno yanayokubaliana sawasawa kabisa na maneno ya Kristo. 18 Wanaoidharau Sakramenti waliwahi kulifafanua ‘Shauri la Mwafaka’ lililotungwa mwaka uliotangulia kwa manufaa yao wenyewe. Walikwisha kusema kwamba, mwili wa Kristo pamoja na fadhili zake zote vinagawiwa katika mkate halisi sawasawa na ilivyo katika Neno la Injili. Walisisitiza pia kwamba, muungamo wa Sakramenti unakusudiwa kumaanisha kuwepo kwa Kristo Bwana kiroho peke yake katika imani.1908 19. Milango yote ya kutokea na mianya yote ilizibwa kabisa kwa maneno kwamba, “mkate na divai katika Chakula cha Bwana ni mwili na damu ya kweli Kristo. Vinatolewa na kupokelewa siyo tu na wacha Mungu bali pia na hata Wakristo waovu.” matumizi).
1906 ‘Ciborium’
1907 Maandamano ya Mwili wa Kristo, ‘Corpus Christi,’ yaliainishwa siku ya Alhamisi iliyofuatia Jumapili ya Utatu. Sherehe hii ilianzishwa katika Kanisa la Magharibi kwa ajili ya agizo la Papa Urbano IV mwaka wa 1264. Papa Urbano IV alifuata vishawishi vya madai ya maono ya mmonaki Yuliana huko Ubelgiji mwaka wa 1230. Wakuu wa Matengenezo ya Kanisa waliiacha sherehe hii kwa sababu ya mafundisho mabaya kuhusu aina moja ya sakramenti ya Chakula cha Bwana.
1908 Mafungu ya Smalkaldi, sehemu ya tatu na nne.
631
20. Dk. Luther anaelezea na kuthibitisha msimamo huu kwa upana zaidi kutoka kwa Neno la Mungu katika Katekisimo Kubwa. Anaandika ifuatavyo: “Sasa, Sakramenti ya Madhabahu ni nini? Jibu: Ni mwili wa kweli na damu ya kweli ya Bwana wetu Kristo ndani na chini ya mkate na divai ambavyo sisi Wakristo tumeagizwa kwa Neno la Kristo kula na kunywa. Jinsi tulivyosema kuhusu Ubatizo kwamba, si maji matupu, vivyo hivyo, tunasema hapa kwamba, Sakramenti ni mkate na divai, lakini si mkate au divai tupu, jinsi inavyotolewa mezani. Ni mkate na divai iliyopambanuliwa na Neno la Mungu na kuunganishwa kwalo.” 21 Tena: Ni Neno, ninasisitiza, linaloipambanua kutoka kuwa mkate na divai tupu na kuifanya kuwa Sakramenti ambayo kwa usahihi inaitwa mwili na damu ya Kristo.” 22. Na baadaye: “Kwa Neno hili unaweza kuitia dhamiri yako nguvu na kutangaza: “Acheni mashetani mia moja elfu, pamoja na walokole wote wa dini, wasiofikiri, wajitokeze haraka na kusema: ‘Inawezekanaje mkate na divai kuwa mwili na damu ya Kristo?” Bado ninajua ya kwamba, roho zote na wataalamu wakiwa pamoja, wana hekima ndogo zaidi kuliko aliyo nayo enzi ya Mungu katika kidole chake kidogo. Hapa tuna Neno la Kristo: “Twaeni mle huu ni mwili wangu. Nyweni nyote katika hiki, hili ni Agano Jipya katika damu yangu,” n.k. Hapa tutaweka msimamo wetu na kuona ni nani anayethubutu kumshauri Kristo na kubadilisha alilolisema. 23. Ni kweli kabisa kwamba, ukitoa Neno kutoka kwa vitu vya asili au ukivitazama mbali na Neno, huna lolote, bali mkate na divai ya kawaida. Lakini maneno yakibaki, jinsi ilivyo sahihi na lazima, basi katika uwezo ulio ndani yake, ni mwili na damu halisi ya Kristo. Jinsi sisi tulivyo nayo kutoka kwa kinywa cha Kristo, ndivyo yalivyo; hayawezi kusema uongo au kudanganya.”1909
24. Kwa hiyo basi, ni rahisi kabisa kuyajibu maswali ya aina zote ambayo kwayo, watu wanajisumbua sasa, kwa mfano, iwapo kasisi mwovu atahudumu na kutoa sakramenti, na maswali kama hayo. Mwisho wetu ni kwamba, ingawa mlaghai huipokea au huitoa Sakramenti, ni Sakramenti ya kweli, yaani, mwili na damu ya Kristo. Hakuna tofauti hapa kati ya anayeitunza kwa njia ya hadhi mno. Kwani Sakramenti haitegemei msingi wa utakatifu wa kibinadamu, bali Neno la Mungu. Hakuna mtu mtakatifu hapa duniani, au hata malaika wa mbinguni, hawezi kuubadilisha mkate na divai kuwa mwili na damu ya Kristo. Kadhalika, ingawa inatumiwa vibaya, mtu yeyote anaweza kuiharibu au kuibadilisha Sakramenti kidogo sana.
25. Neno la kuanzishwa kwa Sakramenti haliwezi kugeuzwa kuwa uongo kwa sababu ya nafsi ya ubinadamu au kutokuamini kwake. 1909 ‘Katekisimo Kubwa’ 5:8-14.
26 Kristo hasemi, “Mkiamini au mkiwa wenye hadhi, mtapokea mwili na damu yangu.” Badala yake, anasema: “Twaeni, mle na kukinywa, huu ndio mwili wangu na hii ndiyo damu yangu.” Vile vile anasema: “Fanyeni hivi,” yaani, lile ninalolifanya sasa, ninalianzisha, ninawapeni, na kuwaamuru mlichukue. Hii ni sawa na kusema: “Ingawa una hadhi au huna hadhi, hapa una mwili na damu yake kwa uwezo wa maneno hayo ambayo yanaongezewa kwa mkate na divai.”
Lizingatie hili na ulikumbuke vyema, kwani katika maneno hayo, ndimo mna mabishano yetu yote, tunzo, na ulinzi dhidi ya makosa yote na uongo ambao umetokea au pengine unaweza kutokea.”1910
27. Kwa Neno la Mungu, Katekisimo Kubwa inaimarisha kwamba, mwili na damu ya Kristo vipo kwa kweli katika Chakula Kitakatifu si juu ya waaminio na wenye hadhi tu bali pia wasioamini na wasiokuwa halali.
28. Kwa kuwa mtu huyu aliye na maarifa zaidi aliona mbele katika Roho kwamba, baada ya kifo chake wengine watajaribu kumfanya mshukiwa kwa kutoa maoni kwamba, ameondoka kutoka kwa mafundisho haya na mafungu mengine ya Kikristo,1911 mwishowe alilitoa hakikisho1912 lifuatalo kwa andiko lake la ‘Ukiri Mkuu:’ 29. “Ninaona kwamba, mafarakano na makosa yanaongezeka kulingana na mpito wa wakati na kwamba, hakuna mwisho wa hasira na ghadhabu kali za Ibilisi. Kwa hiyo, wakati wa uhai wangu au baada ya kifo changu, mwache mtu yeyote aniite au atumie vibaya maandiko yangu kuthibitisha uzushi jinsi wanaoidharau Sakramenti na Waanabaptisti walivyoanza tayari kufanya. Kwa hiyo, kwa makala haya, ninatamani kuikiri imani yangu mbele za Mungu na mbele ya ulimwengu wote sehemu kwa sehemu. Ninaimarishwa kudumu katika hiyo hadi kifo changu na hivyo, Mungu unisaidie katika imani hii niondoke katika dunia hii na nionekane mbele ya kiti cha hukumu cha Yesu Kristo Bwana wetu. Kwa hiyo, baada ya kifo changu, mtu yeyote asiseme kwamba, iwapo Dk. Luther angeishi sasa angefundisha na kulishikilia fungu hili au lile tofauti kwa sababu hakuwa amelifikiria sawasawa na kadhalika. 30 Jinsi nilivyosema, niache niseme sasa kwamba, kwa neema ya Mungu, kwa uangalifu mkubwa, nimeyatafuta mafungu haya yote kutoka katika Maandiko Matakatifu. Nimeyachunguza tena na tena katika mwanga huo, na nilitaka kuyatetea hayo yote jinsi ninavyoitetea Sakramenti ya Madhabahu sasa. 31Sijalewa wala sijakurupuka. Ninajua
1910 Taz. ‘Katekisimo Kubwa’ 5: 12-19.
1911 Kabla ya kifo cha Luther, uvumi ulikuwa umekwisha kuenea kwamba, aliwaagiza marafiki zake hasa kufanya mabadiliko kuhusu mawazo yake ya ndani sana kuhusu sakramenti kwa taratibu za kutoa mafundisho yaliyorekebishwa. Hili lilijulikana kwa Walutheri kama ‘Roorback ya Heidelberg’ (Heidelberger Landlüge).
1912 Kilatini: ‘Protestatio.’
633
ninalolisema. Ninafahamu vizuri hili linamaanisha nini kwangu katika hukumu ya mwisho wakati wa kuja kwake Kristo Bwana. Mtu yeyote asije akalifanya hili kuwa mzaha au mazungumzo ya upuuzi. Ninakaribia kufa na kwa neema ya Mungu, nimejifunza kumfahamu Ibilisi kiasi. Kama anaweza kuchafua na kuvuruga Neno la Mungu, ni lipi litakalomshinda kufanya kwa maneno yangu au ya mtu mwingine?”1913
32. Kulingana na hakikisho hili, marehemu Luther aliongezea yafuatayo miongoni mwa mafungu mengine: “Kwa hiyo, nami pia ninasema na tunakiri ya kwamba, katika Sakramenti ya Madhabahu, mwili na damu ya Kristo huliwa kweli na hunywewa katika mkate na divai ingawa makasisi wanaovigawa au wanaovipokea hawaamini. Kwa upande mwingine, Sakramenti hutumiwa vibaya. Haitegemei imani ya mtu au kutoamini kwake isipokuwa inategemea Neno na agizo la Mungu. Labda kwanza, walibadili Neno la Mungu, agizo, na kuvitafsiri vibaya jinsi maadui wa Sakramenti wanavyofanya wakati huu. Kweli, wao wana mkate na divai peke yake, kwani hawana Neno wala utaratibu halisi wa Mungu tena ila wamepotoshwa na kuibadili kulingana na mawazo yao wenyewe.”1914
33. Dk. Luther, aliyefahamu kweli na vyema kusudi la Ukiri wa Augsburg kuliko mtu yeyote, alidumu kwalo kwa uthabiti na kulilinda kila wakati mpaka akafa. Mara tu kabla ya kifo chake, katika ukiri wake wa mwisho, aliitetea imani yake katika fungu hili kwa bidii kubwa na kuandika ifuatavyo: “Wanaoidharau Sakramenti, ninawaoka wote wakiwemo walokole kama keki moja. Wao ndio watu wa jinsi hiyo kwa sababu hawataki kuamini kwamba, katika Chakula Kitakatifu, mkate wa Bwana ni mwili wake wa kweli na wa asili, ambao wasiomcha Mungu au akina Yuda huupokea kwa kinywa sawasawa na Mt. Petro na watakatifu wote. Ninasema kwamba, yeyote ambaye hataliamini hili afadhali aniache na asitarajie ushirika nami. Hili ndilo mwisho.1915
34. Kutokana na maelezo haya na hasa katika maelezo ya Dk. Luther, kama mwalimu mkuu wa Ukiri wa Augsburg, kila mtu mwenye akili na anayependa ukweli na amani anaweza kuelewa zaidi ya mashaka yote maana halisi ya Ukiri wa Augsburg na nia katika fungu hili ambalo limeendelea kuwa hivyo.
35. Kauli kama “mkate katika Chakula Kitakatifu ni mwili wa kweli wa Kristo” au “kushiriki katika mwili wa Kristo” zinatokana na maneno ya Kristo na ya Mt. Paulo.1916 Pamoja na haya, tunazitumia pia kauli kama “chini ya mkate,
1913 WA 26:499, 500.
1914 WA, 26:506.
1915 WA, 54:155, 156.
1916 Mt. 26:26; Lk. 22:19; Mk. 14:22; 1 Kor. 11:24, 10,16.
634
pamoja na mkate, ndani ya mkate.”1917 Tunafanya hivyo kwa shabaha ya kukataa mafundisho ya mageuzo-uwamo ya wafuasi wa Papa na kuonyesha wazi kwamba, kiini cha mkate na mwili wa Kristo kisichobadilika, kimeunganika kwa njia ya kisakramenti. 36.Kwa njia hiyo hiyo, kauli, “Neno alifanyika mwili”1918 inaelezewa kwa matumizi ya kauli zenye maana hiyo hiyo kama hizi, “Neno akakaa kwetu,” au “Katika Kristo unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili,” au “Mungu alikuwa pamoja naye,” au, “Mungu alikuwa ndani ya Kristo,” na maneno kama hayo.1919 Kwa hiyo, inaelezewa kwamba, asili ya kimungu haijabadilishwa kuwa asili ya kibinadamu lakini asili zote mbili zisizobadilika zimeungana katika muungano wa kinafsi. 37.Walimu wengi wa zamani waliokuwa maarufu kama Justino, Sipriano, Agostino, Leo, Gelasio, Krisostomo na wengine, wameelezea umoja wa kinafsi wa maneno ya agano la Kristo, “Huu ndio mwili wangu,” kwa mfano unaofuatia: Jinsi asili zote mbili zisizobanduka na zisizobadilika zilivyoungana kwa njia ya kutobanduliwa, kadhalika basi, katika Chakula Kitakatifu, asili mbili, yaani, mkate wa kawaida, mwili wa kweli, na wa asili wa Kristo, vipo hapa duniani katika tendo la Sakramenti lililoagizwa, 38. ingawa muungano wa mwili na wa damu ya Kristo katika mkate na divai si umoja wa kinafsi, jinsi asili mbili zilizomo katika Kristo zilivyo. Badala yake, ni muungano wa kisakramenti,1920 jinsi Dk. Luther na wanatheologia wetu wanavyouita katika Shauri la Mwafaka la mwaka wa 15361921 na kwingineko. Hivyo basi, walitaka kuonyesha wazi kwamba, walipozitumia kauli tofauti kama ‘katika mkate,’ ‘chini ya mkate,’ ‘pamoja na mkate,’1922 hata hivyo, waliyaelewa maneno ya Kristo kwa maana yao halisi na jinsi yanavyosomeka. Hawakufikiria kwamba, maneno ya wasia wa Kristo, “Huu ndio mwili wangu,” yalieleweka kama tamathali, yaani, kauli zenye maana nyingi1923 lakini kinyume chake kabisa, yenye maana maalumu ya peke kabisa,1924 39. jinsi Justino alivyosema: “Tunapokea huu, si kama mkate wa kawaida au kinywaji cha kawaida, lakini tunaamini kwamba, jinsi Kristo, Mwokozi wetu, alivyofanyika mwanadamu kupitia Neno la Mungu na kwa ajili ya wokovu wetu akawa na mwili na damu, hivyo, chakula kilichobarikiwa naye kwa njia ya Neno na sala ni mwili na damu ya kweli ya Bwana Yesu Kristo.”1925
40. Katika ‘Ukiri Mkuu,’ Dk. Luther alitetea na hasa ukiri wake wa mwisho
1917 Kilatini: ‘In, cum et sub.’
1918 Kilatini: ‘In, cum et sub.’
1919 Yn. 1:14; Kol. 2:9; Mdo. 10:38; 2 Kor. 5:19. ‘
1920 Kilatini: ‘Unio sacramentalis.’
1921 Juu, sehemu ya 12.
1922 Kilatini: ‘In pane, sub pane, cum pane.’
1923 Kilatini: ‘Praedicatio figurata.’
1924 Kilatini: ‘Praedicatio inusitata.’
1925 Justinus Martyrus Apol. 1:66.
kuhusu Chakula Kitakatifu, kwa juhudi kuu na raghba kauli ya Kristo katika Chakula Kitakatifu cha kwanza.1926 Kwa juhudi kuu na kwa bidii, Dk. Luther alitaja utaratibu ambao Kristo aliutumia katika Chakula cha Bwana.
41. Kwa kuwa, Dk. Luther anapaswa kustahiwa kama mwalimu mkuu zaidi katika makanisa ambayo yanaufuata Ukiri wa Augsburg. Yaliyomo yote katika mafundisho yake kwa jumla, yametolewa katika mafungu ya Ukiri wa Augsburg uliokwisha kutajwa na kutolewa kwa Kaisari Karolo wa V. Kwa hiyo basi, maana halisi na kusudi la Ukiri wa Augsburg haliwezi kupatikana kwa usawa au ubora zaidi kutoka katika chanzo kingine, isipokuwa kutoka kwa mafundisho ya Dk. Martin Luther mwenyewe na maandiko ya majadiliano.
42. Msimamo uliowekwa wazi hapo juu una msingi wa mwamba wa ukweli pekee, ulio imara, na usiobadilika. Msingi wake ndiyo maneno ya uanzishwaji wa Neno la Mungu Takatifu. Waandishi watakatifu wa Vitabu vya Injili, mitume, wanafunzi, na wasikilizaji wao waliyafahamu mafundisho haya kwa maana hii kabisa, walikuwa wameyafundisha na kuyarithisha pia kwa vizazi vijavyo.
43. Ndiye Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo ambaye kwake, kama mwalimu wetu wa pekee, amri ya dhati imetolewa kwa watu wote kutoka mbinguni: “Msikieni yeye.”1927 Yeye si mwanadamu wala malaika tu. Yeye si kweli pekee, mwenye busara, na mwenye uwezo, lakini mwenyewe ni ukweli wa milele, na hekima katika nafsi yake na Mungu Mwenyezi. Anafahamu vyema nini, vipi lazima azungumze, na kwa uwezo mkubwa, anaweza kutimiza na kufikisha lile alisemalo na kuliahidi jinsi anavyosema: “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe,” na tena, “nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.”1928
44. Baada ya chakula cha jioni, alipokuwa mwanzoni mwa mateso na kifo chake cha uchungu kwa ajili ya dhambi zetu na kwenye huzuni, wakati huu wa mwisho wa maisha yake, huyu mwenye ukweli na Bwana Mwenyezi, Muumbaji wetu na Mkombozi Yesu Kristo, alichagua maneno yake kwa uangalifu mkubwa na kwa tahadhari alipoianzisha Sakramenti hii adhimu. Hivyo, Sakramenti hii inapaswa kutumiwa kwa heshima kuu na utiifu mpaka mwisho wa dunia. Sakramenti hii ndiyo kumbukumbu ya kudumu ya mateso yake makali, uchungu, na kifo na kwa fadhili zake zote, muhuri wa Agano Jipya, faraja ya mioyo yote yenye huzuni, na mafungo ya kweli na muungano wa Wakristo pamoja na Kristo aliye kichwa chao na kati yao wenyewe. Kwa hiyo, kuhusu mkate uliobarikiwa
1926 WA, 26:271 n.k., 379 n.k., 54:149 n.k.
1927 Kilatini: ‘Hunc audite.’ Mt. 17:5; Lk. 3:22.
1928 Lk. 21:33; Mt. 28:18.
na kutolewa, Kristo alikuwa amesema: “Twaeni mle, huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu.”1929 Na kuhusu kikombe au divai alisema: “Hii ndiyo damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.”1930
45. Hii ndiyo sababu, ni wajibu wetu kutoyatafsiri na kutoyafafanua maneno haya ya Mwana Mwenyezi wa milele na wa ukweli wa Mungu, Yesu Kristo, Muumba na Mkombozi aliye wa milele, kama kirai cha tamathali au cha mafumbo, kama jinsi yanavyoonekana katika akili zetu. Badala yake, hatuna budi kukubali, katika imani rahisi na utii unaostahili, katika nguvu yao na maana halisi, jinsi yanavyosomeka. Wala hatuthubutu kuliruhusu katazo lolote au pingamizi la kibinadamu, lenye kujitokeza kulingana na akili ya kibinadamu kututenga na maneno haya, haijalishi jinsi akili yetu inavyoweza kuliona.
46. Naam, Ibrahimu alikuwa na msingi wa kutosha wa kubishana aliposikia maneno ya Mungu kuhusu kumtoa mwana wake. Kwa sababu maneno haya dhahiri yalikuwa kinyume cha akili, sheria ya kimungu ya asili, fungu kuu la imani kuhusu mbegu iliyoahidiwa, Kristo ambaye angezaliwa, na Isaka. Ibrahimu angeweza kuuliza kama agizo hili lingefahamika kulingana na Neno kamili au kama lingeweza kufafanuliwa kwa nia laini na yakuvumilika zaidi.
Lakini ilivyokuwa awali, wakati Ibrahimu aliipokea ahadi ya mbegu iliyobarikiwa ya Isaka, ingawa hii ilionekana kuwa muhali katika akili yake, alimpa Mungu heshima ya kweli zaidi katika moyo wake kwamba, lile aliloliahidi Mungu, alikuwa na uwezo wa kulifanya pia.
47. Hivyo, Ibrahimu alielewa na kuamini Neno na agizo la Mungu kwa njia ya wazi na dhahiri, jinsi maneno yanavyosomeka katika herufi zake. Aliyakabidhi mambo yote kwa uwezo na hekima ya Mungu, akijua kwamba, Mungu ana namna na njia nyingi zaidi za kuzitimiza ahadi zote zinazohusu mbegu ya Isaka kuliko jinsi anavyoweza kufahamu kwa njia ya akili yake ya upofu. Sisi pia hatuna budi kuamini katika uvumilivu wote na katika utiifu ulio dhahiri, thabiti, wazi, na wa maneno ya kweli na maagizo ya Muumbaji na Mkombozi wetu bila mashaka yoyote au majadiliano kuhusu yoyote jinsi yanavyoweza kupatanishwa na akili zetu kwa sababu au labda jinsi yanavyowezekana. Bwana ambaye ameyasema maneno haya, mwenyewe ndiye hekima na ukweli usiokuwa na mwisho na bila shaka anaweza kulikamilisha na kulifanikisha lolote analoliahidi.
48. Hali zote za uanzishwaji wa chakula hiki zinashuhudia kwamba, maneno
1929 Mt. 26:26; Lk. 22:19. 1930 Mk. 14:24; Lk. 22:20; Mt. 26:28.
haya ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, ambayo yenyewe ni ya kawaida, dhahiri, bainifu, thabiti, na yasiyo na shaka, yanaweza na yanapaswa kueleweka tu kwa matumizi yake halisi na maana ya kawaida inayokubalika. Kwa kuwa Kristo alilitoa agizo hili mezani wakati wa chakula cha jioni, inawezekana kusiweko na shaka kwamba, alikuwa anauzungumzia mkate wa kawaida kweli na divai ya kawaida kweli na vile vile kula na kunywa kwa kutumia kinywa. Hivyo, haiwezekani kuwa sitiari, yaani mabadiliko ya maana, kwa neno ‘mkate, ‘kana kwamba, mwili wa Kristo ulikuwa mkate wa kiroho au chakula cha kiroho cha mioyo.
49. Kadhalika, Kristo mwenyewe alikuwa mwangalifu kutoutumia uhawilisho wa maana1931 katika neno ‘mwili’ ili lisiwe na maana ya ishara ya mwili wake, wala mifano ya uwezo wa mwili wake, na kwa faida zote ambazo alitushindia kwa njia ya dhabihu ya mwili wake. Alikuwa anazungumzia kuhusu mwili wake wa kweli wenye kiini chake ambao aliutoa kwa njia ya kifo kwa ajili yetu na damu yake ya kweli yenye kiini chake iliyomwagika msalabani kwa msamaha wa dhambi.
50. Kwa kweli, hakuna mfafanuzi mwaminifu au wa kuaminika wa maneno ya Yesu Kristo kuliko Kristo Bwana mwenyewe, ambaye anafahamu maneno, moyo, na shabaha yake vyema kuliko wote. Yeye pia anaweza kuyaelezea maneno yake kwa hekima na busara mno. Anapotangaza mapenzi yake ya mwisho na kuanzisha wosia wake, agano lake, na umoja wa kudumu, hatumii tamathali. Badala yake, anayatumia maneno yanayofaa zaidi, rahisi, ya hakika, na wazi kadiri anavyofanya katika mafungu yote ya imani na katika ishara zingine zote za agano na ishara za neema na Sakramenti, kama tohara, dhabihu nyingi mbalimbali za Agano la Kale, na Ubatizo Mtakatifu. Ili kusiwe na utata katika maneno haya, aliyaelezea mambo wazi zaidi na kuyaongezea maneno yafuatayo: “unaotolewa kwa ajili yenu, inayomwagika kwa ajili yenu.” 51 Alitaka wanafunzi wake wakae katika ufahamu safi unaoyafuata maneno na akawaamuru mitume wake wayafundishe mataifa yote kuyashika yote aliyowaamuru.
52. Kwa hiyo, wainjilisti wote watatu, Mathayo (26:26), Marko (14:22), na Luka (22:19) - na Mt. Paulo pia, aliyezipokea habari hizo hizo baada ya kupaa kwake Kristo (1 Kor. 11:25) – kwa umoja, na kwa maneno hayo hayo na silabi hizo hizo, waliyatoa maneno angavu, dhahiri, thabiti, na ya kweli kuhusu Kristo: “Huu ndio mwili wangu.” Wanarudia kwa njia moja hiyo hiyo kabisa maneno kuhusu mkate uliobarikiwa na kutolewa bila tafsiri na mabadiliko yoyote. 53. Kwa hiyo basi, hakuna shaka kwamba, katika sehemu ya pili ya Sakramenti, 1931 Kilatini: ‘Metonymia.’
638
maneno ya Luka na Paulo, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu,” (Lk. 22:20; 1 Kor. 11:25) hayana maana nyingine kuliko yale ambayo Mt. Mathayo na Mt. Marko wametupatia. Yaani, Mathayo na Marko wanasema “‘hii´ ambayo mnainywa kwa vinywa vyenu katoka kwa kikombe, ni damu yangu ya Agano Jipya, ninauanzisha wosia wangu, ninapiga muhuri, na kuthibitisha nanyi Agano Jipya, yaani, msamaha wa dhambi.”1932
54. Pia marudio, thibitisho, na ufafanuzi wa maneno ya Kristo yanatolewa na Mt. Paulo katika 1 Kor. 10:16: “Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je, si ushirika wa damu ya Kristo?” Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Maneno haya yanashuhudia dhahiri kabisa kwamba, mwili na damu ya Kristo vinapatikana na kugawanywa kwa kweli katika Chakula Kitakatifu katika kiini chao. Hivyo basi, tunajifunza wazi kwamba, si kikombe tu ambacho Kristo alikibariki katika Chakula Kitakatifu na si mkate tu ambao Kristo mwenyewe aliumega na kuugawa. Lakini pia ni kwamba, tunaumega na kuubariki ushirika katika mwili na damu ya Kristo, kiasi kwamba, wote wanaoula mkate huu na kukinywea kikombe hiki, kwa kweli, humpokea na hushiriki mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo. 55. Kwa kuwa, mwili wa Kristo usipokuwepo kweli katika kiini chake na kupokelewa tu kulingana na wema na utendaji wake, basi, mkate haungeitwa ushirika katika mwili. Badala yake, ungeitwa ushirika katika roho, wema, na faida za Kristo, kadiri Utetezi unavyobisha na kukamilisha.1933 56. Iwapo Paulo alikuwa anasema tu kuhusu ushirika wa kiroho katika mwili wa Kristo kwa njia ya imani, jinsi wanaoidharau Sakramenti wanavyoighushi kauli hii, asingesema kwamba, ndio mkate bali ndiyo roho au imani ambayo ni ushirika katika mwili wa Kristo. Badala yake, anasema kwamba, mkate ni ushirika katika mwili wa Kristo. Maana yake ni kwamba, wote wanaoupokea mkate uliobarikiwa, kadhalika wanashiriki pia mwili wa Kristo. Kwa hiyo, bila shaka, haiwezekani kwamba, anazungumzia ulaji wa kiroho, bali ulaji wa Sakramenti au na kula kwa kinywa, mwili wa Kristo ambao wote wanaomcha Mungu na wasiomcha Mungu wanaushiriki.
57. Kulingana na madhumuni na miktadha yote ya mahubiri ya Mt. Paulo katika 1 Kor.10:18-33, inaeleweka wazi kwamba, alikuwa na fikra ya watu waliokula dhabihu za miungu na kuushiriki ukafiri wa ibada za Ibilisi ambao vilevile walikuwa wakienda kwa Chakula Kitakatifu na kushiriki mwili na damu ya Kristo. Alikuwa akiwakatisha na kuwaonya dhidi ya kupokea mwili na damu ya Kristo kwa adhabu na hukumu yao wenyewe. Kwa kuwa, wote wanaoshiriki
1932 Mt. 26:28; Mk. 14:24. 1933 Utetezi wa Ukiri wa Augsburg 10:1.
mkate uliobarikiwa na kumegwa katika Chakula Kitakatifu, wanashiriki katika mwili wa Kristo, bila shaka, Mt. Paulo asingeweza kuuzungumzia ushirika wa kiroho pamoja na Kristo, kwa kuwa hakuna yeyote ambaye angeweza kuutumia vibaya na kwamba, mtu hapaswi kuonywa dhidi yake.
58. Kwa hiyo basi, akina baba wetu wapendwa waliotutangulia, kama Luther na walimu wengine safi wa Ukiri wa Augsburg, walielezea kwa njia rahisi zaidi fungu hili la maneno ya Paulo na kwa maneno yanayokubaliana na ya Kristo kwa kusema “Mkate tuumegao ni mwili wa Kristo uliotolewa, au mwili wa kawaida wa Kristo hugawiwa kwa ambao huupokea mkate uliomegwa.”
59. Tutadumu katika maelezo rahisi, yaliyothibika, na ya ushuhuda bora katika 1 Kor. 10:16. Tumeshangazwa kwamba, wengine wana ujasiri wa kuitumia kauli hiyo ambayo zamani, waliiendeleza dhidi ya wanaoidharau Sakramenti ili kuuweka msingi wa uasi wao. Yaani, kwamba, mwili wa Kristo Bwana, hupokelewa katika Chakula Kitakatifu kwa njia ya kiroho tu. Wanaandika ifuatavyo: “Mkate ndio ushirika katika mwili wa Kristo (yaani, Kanisa), au ni njia ambayo kwayo, sisi waumini tunaunganishwa na Kristo jinsi Neno la Injili, linaposhikwa kwa imani. Ni njia ambayo kwayo, tunaunganishwa kiroho na Kristo na tunafanywa wamoja ndani ya mwili wa Kristo, yaani, Kanisa.”1934
60. Lakini Mt. Paulo anafundisha wazi kwamba, si Wakristo wacha Mungu wanaoamini tu, ambao hupokea kwa vinywa mwili na damu ya kweli ya Kristo katika Sakramenti. Badala yake, ni wasiostahili na wanafiki wasiomcha Mungu, kama Yuda na wengine kama yeye ambao hawana ushirikiano wa kiroho pamoja na Kristo. Hawa huja katika Chakula Kitakatifu bila toba ya kweli na shabaha ya kumgeukia Mungu. Kwa njia ya kula na kunywa kwao kusikofaa, hukosea vibaya dhidi ya mwili na damu ya Kristo. Mt. Paulo anasema, “kila aulaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili” ( 1 Kor. 11:27) hutenda dhambi dhidi ya mkate, divai, ishara na alama, mifano ya mwili na damu, pia huwa na hatia ya kutoheshimu, kutumia vibaya, na kunajisi mwili na damu ya Bwana Yesu Kristo aliyepo. Bila shaka, mtu kama huyo hutenda dhambi kama Wayahudi walivyofanya kwa kweli walipoiweka mikono yao juu ya mwili wa Kristo na kumuua. Akina baba Wakristo wa zamani na walimu wa Kanisa walielewa na kuielezea kauli hii kwa mwafaka.1935
1934 Kilatini: “Panis est communicatio corporis Christi, hoc est id, quo fit societas cum corpore Christi (quod est ecclesia), seu est medium, per quod fideles unimur Christo, sicut verbum evangelii fide apprehensum est medium, per quod Christo spiritaliter unimur et corpori Christi, quod est ecclesia, inserimur.”
1935 Hapa kitabu cha Torgau kilianzisha nukuu kutoka kwa Basileio, ‘De baptismo’ 1: 3, 3; I2: 3; Yohana Krisostomo, ‘In epistola 1 ad. Corinthios homilia’ 27:5, 5; Agostino Bandia ‘Contra Fulgentiam Donatistam;’
61. Basi, kuna aina mbili za ulaji wa mwili wa Kristo. Moja ni ulaji wa kiroho ambao Kristo anauzungumzia zaidi katika Yn. 6:48-58. Hili hutokea kwa njia ya Roho na imani katika kuhubiri na kutafakari Injili, na katika Chakula Kitakatifu. Kweli ina manufaa halisi, wema, na ni lazima kwa wokovu wa Wakristo wote wakati wowote. Bila ushirika huu wa kiroho, hata Sakramenti au ulaji wa Chakula Kitakatifu kwa njia ya kinywa hauwi mwema, lakini kwa kweli unakuwa madhara yenye hukumu ya milele.
62. Ulaji huu wa kiroho ni imani. Yaani, Neno la Mungu linalotutolea Kristo, Mungu kweli na mwanadamu kweli, pamoja na vipawa vyake vyote ambavyo ametutafutia kwa njia wa kutoa mwili wake kwa ajili yetu katika kifo na kwa kumwaga damu yake kwa ajili yetu. Vipawa vyake ndivyo neema ya Mungu, msamaha wa dhambi, haki, na uzima wa milele. Sisi basi, tunalisikia Neno na kumpokea Kristo kwa imani na kumshika kweli. Kwa ajili ya Yesu Kristo Bwana wetu, tuna Mungu mwenye huruma na heri ya milele. Tunaitegemea faraja hii imara yenye tegemeo halisi katika ugumu wote na majaribu.
63. Aina nyingine ya kula kwa mwili wa Kristo ni ambayo inafanywa kwa kinywa au kwa njia ya Sakramenti. Wote wanaokula mkate uliobarikiwa na wanaokunywa divai iliyobarikiwa hupokea kwa kinywa mwili na damu halisi ya Kristo katika kiini chake. Waaminio hupokea, bila shaka dhamana na thibitisho la kwamba, dhambi zao zimesamehewa kweli na Kristo anakaa na kuishi ndani yao. Lakini wale wasioamini, hula na hupokea pia kwa vinywa yote ambayo Kristo aliyasema alipokianzisha Chakula Kitakatifu, lakini kwa njia ya hukumu na laana yao.
64. Hivyo ndivyo maneno ya Kristo ya uanzishwaji yanavyosema. Akiwa mezani na wakati wa chakula cha jioni aliwapatia wanafunzi wake mkate wa kawaida na divai ya kawaida, ambayo aliita mwili na damu yake ya kweli na akasema “mle na mnywe.” Ilivyo, amri hii inaweza kueleweka kuhusu ulaji na unywaji halisi kwa kinywa peke yake lakini si kwa njia ya ushenzi, na mwili Kikapernaumu.1936 Badala yake, kwa njia inayopita akili zetu na isiyofahamika.
65. Basi, Kristo anaongezea amri nyingine na katika nyongeza ya ulaji kwa kinywa anaagiza ulaji wa kiroho, anaposema, “Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Kwa maneno haya basi, anahitaji imani.
Agostino, ‘De baptismo contra Donatistas’, V, 8; ‘Epistula’ 43 (162), 8, 23; ‘Contra Donatistas post collationem,’ 7: 9; 20: 27; ‘Sermo 71 (11) de verbis Domini, Quisquis blasphemaverit,’ 11, 17. 1936 Huko Kapernaumu (Yn. 6:52-65), Wayahudi waliyafahamu maneno ya Kristo kama kula mwili wake hasa. Katika karne ya kumi na sita lugha tata ya ‘Kikapernaumu’ ilikuwa neno la kunguruma ambalo lilidokeza imani katika mkazo kwamba, mkate na divai hubadilika kimaumbile kuwa mwili na damu.
641
66. Hivyo basi, kulingana na maneno haya ya uanzishwaji ya Kristo na maelezo ya Mt. Paulo kuhusu maneno hayo, walimu wa Wakristo wote wa zamani na Kanisa zima Takatifu la Wakristo wamefundisha kwa ridhaa kuu kwamba, mwili wa Kristo hupokelewa kwa njia ya kiroho, imani nje ya Sakramenti, na hata kwa njia ya kinywa pia. Mwili wa Kristo hupokelewa hivyo pia na wasiostahili, wasioamini, wanafiki, Wakristo waovu sawa na wanaomcha Mungu na wachaji.1937 Kuziorodhesha shuhuda hizi ni kazi ngumu sana. Shabaha yetu ni maelezo mafupi. Kwa hiyo, tunapendekeza vitabu vyenye maarifa mengi zaidi kwa msomaji Mkristo.
67. Kutokana na haya, ni dhahiri jinsi wanaoidharau Sakramenti kwa inda wanamdhihaki Kristo Bwana, Mt. Paulo, na Kanisa zima. Kuhusu ulaji kwa kinywa na wasiostahili kuupoea mwili wa Bwana, wametumia kauli za kukufuru mno ambazo Mkristo anayemcha Mungu anapaswa kuona aibu kuzitafsiri.1938
68. Ni vyema kuwaelezea wageni kwa uangalifu mkuu ni wangapi wasiostahili kula chakula hiki.1939 Wao ndio wanaokuja katika sakramenti bila toba na majuto ya kweli kwa ajili ya dhambi zao na bila imani ya kweli na kusudi jema la kuyarekebisha maisha yao. Kwa njia ya kula mwili wa Kristo kwa vinywa vyao, wanajiweka chini ya hukumu na kupokea adhabu za maisha haya na za milele na kupokea hatia kwa ajili ya mwili na damu ya Kristo.
69. Washiriki wa kweli na wenye stahili ni Wakristo walio dhaifu katika imani, wenye woga, na huzuni. Mioyoni mwao wanatishwa kwa sababu ya dhambi zao nyingi na kubwa. Ni wanaojihesabu wenyewe kutostahili hazina hii bora na fadhili za Kristo kwa sababu ya kutokuwa safi sana, na wanafahamu unyonge wao katika imani, wanalia moyoni mwao, na wangependa kumtumikia Mungu kwa nguvu, imani kunjufu, na utiifu ulio safi zaidi. 70. Sakramenti hii adhimu zaidi ilianzishwa na kuamriwa kwanza kwa washirika kama hawa, jinsi Kristo anavyosema: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mt. 11:28). Na tena: “Wenye afya hawahitaji
1937 Hapa kitabu cha Torgau kilianzisha nukuu kutoka kwa Theodoroto, ‘Interpretatio epistolae 1. ad Corinthios, ad 11, 27’; Yohana Krisostomo, ‘Sermo 3’ in Ephesos 1; ‘Homilia 59’ in Matthaeum; in epistola 1. ad Corinthios homilia 27: 5; Homila 11 ad Populum; Homilia 21’; Sipriano, ‘De lapsis’ 26, 27; Leo, ‘Sermo 91 ( 6), de ieiunio’; Gregorio Mkuu, Dialogi, 4:58; Homilia in evangelia 27:7, Ambrosio (hajulikani ni yupi), Agostino, ‘Epistola’ 54 (118), 4, 8.
1938 ‘Duo pili caudae equinae et commentum, cuius vel ipsum Satanam pudeat’ (nywele mbili za mikia ya farasi na ufumbuzi ambao hata Ibilisi mwenyewe anaweza kuuonea aibu) na ‘Excrementum Satane, quo diabolus sibi ipsi et hominibus illudat’ (Kinyesi ambacho Ibilisi hujivika mwenyewe na kudanganya watu). Virai hivi vilitumiwa na Theodoro Beza, mfuasi wa Calvin (1519-1605).
1939 Wakalvinisti huwatofautisha washiriki wa aina tatu, (1) Wanaostahili (digni) ambao wana imani imara, (2) Wasiostahili (indigni) ambao wana imani dhaifu, na (3) Wasiomjua Mungu (impii) ambao hawana imani hata kidogo.
642
tabibu, bali walio hawawezi” (Mt. 9:12). Kadhalika: “Uweza wangu (Mungu) hutimilika katika udhaifu” (2 Kor. 12:9). Na tena: “Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, . . . kwa maana Mungu amemkubali” (Rum. 14:1,3). Kwani kila mtu amwaminiye Mwana wa Mungu, hata kama imani yake ni imara au nyonge, anao uzima wa milele.1940
71. Kustahili hakutegemei unyonge au uhakika wa imani, kuwe kukubwa au kudogo, lakini tu kunategemea ustahili wa Kristo. Baba mwenye imani dhaifu (Mk. 9:29) alikushiriki jinsi alivyofanya Ibrahimu, Paulo, na wengine waliokuwa na imani changamfu na imara.
72. Acha hili litoshee kuhusu kuwepo kwa kweli na kushiriki aina mbili za mwili na damu ya Kristo. Kwanza, kwa njia ya imani na ya kiroho. Pili, kwa njia ya kinywa. Aina hizi hufanyika katika hali zote za wanaostahili na wasiostahili.
73. Pia, kumetokea sintofahamu na mabishano kati ya walimu wengine wa Ukiri wa Augsburg kuhusu kuzibariki elementi na kanuni ya kawaida kwamba, hakuna sakramenti isipokuwa matumizi yaliyoasisiwa. 74 Katika suala hili, tumeyafikia maelewano na maafikiano yafuatayo kati yetu, kwa pamoja na kwa njia ya kidugu: Hakuna neno la mwanadamu au kazi, iwe yenye ustahili au kauli ya mtumishi, uwe ulaji na unywaji au imani ya washiriki, inayoweza kudhuru kuwepo kweli kwa mwili na damu ya Kristo katika Chakula Kitakatifu. Hili lipo tu kwa njia ya Neno na Mungu Mwenyezi mwenye nguvu zote. Pia lipo kwa uanzishwaji na agizo la Bwana wetu Yesu Kristo.
75. Maneno ya kweli na ya enzi ya Yesu Kristo ambayo aliyanena kwanza katika uasisi, bado yanaudumisha uthabiti wake na nguvu zao zinazofaa kokote ambako Chakula cha Bwana kinafuatwa kulingana na uanzishwaji wa Kristo, na mahali kokote ambako maneno yake yanatumika na mwili na damu ya Kristo vipo kweli, vinagawiwa, na vinapokelewa kwa uwezo na nguvu za maneno hayo hayo ambayo Kristo aliyanena katika Chakula cha Bwana cha kwanza. Kwa kuwa, kila mahali tunaadhimisha uanzishwaji wake, tunapoyasema maneno yake kuhusu mkate na kikombe na kugawiwa mkate na kikombe vilivyobarikiwa, Kristo mwenyewe yu mwenye uwezo katika maneno yanayosemwa kwa uwezo wa uasisi wa kwanza, na ambayo anataka yarudiwe.
76. Katika mahubiri ya Juma Takatifu Krisostomo anasema: “Kristo mwenyewe anaitayarisha Meza hii na kuibariki. Hakuna mwanadamu, bali Kristo mwenyewe aliyesulibiwa kwa ajili yetu, ndiye anayeweza kufanya mkate na divai vilivyoandaliwa mbele yetu kuwa mwili na damu ya Kristo. Maneno 1940 Yn. 3:16.
643
yanasemwa kwa kinywa cha kasisi, lakini kwa nguvu na neema ya Mungu kwa njia ya maneno anayoyasema, “Huu ni mwili wangu.” Vyombo vilivyoandaliwa mbele yetu katika Chakula cha Bwana, vimebarikiwa. Ni kama asili na yanafanya vitu vikue na viongezeke. Hivyo basi, neno hili lilisemwa mara moja, lakini linafaa kama maneno yasemayo, “zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi” (Mwa.1:28) yaliyosemwa mara moja tu, lakini yanaendelea kufaa mpaka siku hizi, na hadi kurudi kwake, kuna mkazo kwamba, mwili na damu ya kweli vimo katika Chakula cha Bwana cha Kanisa.”1941
77. Naye Luther anasema: “Amri yake hii na uasisi vinaweza na vinaleta lile tusiloliweza kuligawa katika kupokea mkate na divai ya kawaida tu, bali vinaleta mwili na damu yake, jinsi maneno yake yanavyosema, “Huu ndio mwili wangu, “na kadhalika. “Hii ndiyo damu yangu,” na kadhalika Hivyo basi, si kazi yetu au kuzungumza kwetu. Ni amri na agizo la Kristo lisemalo kwamba, tangu mwanzo wa ushirika wa kwanza mpaka mwisho wa dunia, Kristo huufanya mkate kuwa mwili na huifanya divai kuwa damu ambavyo kila mara vinagawiwa kwa njia ya huduma na kazi yetu.”1942
78. Tena: “Kuhusu mikate yote ningesema, “huu ndio mwili wa Kristo,” lolote halingeweza kufanyika. Lakini tukifuata uasisi na amri yake katika Chakula cha Bwana na kusema, “huu ndio mwili wangu,” basi, ndio mwili wake na si kwa sababu ya kunena kwetu au kwa neno letu linalofaa, bali kwa sababu ya amri yake ambayo kwayo, ametuambia tuseme na tufanye na ameshikamanisha amri na matendo yake mwenyewe katika kunena kwetu.”1943
79. Katika huduma ya Chakula Kitakatifu, maneno ya uasasi wake lazima yasemwe au yaimbwe wazi na dhahiri mbele ya ushirika, na hayawezi kuachwa kwa hali yoyote. 80. Hatuna budi kuitii amri ya Kristo: “Fanyeni hivi.” 81. Inatubidi kuiamsha, kuiimarisha, na kuithibitisha, imani ya wasikilizaji katika maana hii halisi na faida za Sakramenti kwa maneno ya Kristo. Yaani, kuwepo kwa mwili na damu ya Kristo, msamaha wa dhambi, faida zote ambazo Kristo ametushindia kwa kifo chake, na kuimwaga damu yake ambayo anatupatia katika wosia wake.
82. Hivyo basi, lazima kuzibariki elementi. Yaani, mkate na divai kwa matumizi haya matakatifu kwamba, mwili na damu ya Kristo hugawiwa kwetu kwa njia ya kula na kunywa, jinsi Paulo anavyosema, “Kikombe kile cha baraka tukibarikicho” (1 Kor. 10:l6). Hili linafanyika sawasawa kwa njia ya marudio na
1941 Yohana Krisostomo, ‘De proditione Iudae,’ 1: 6.
1942 Toleo la Jena 6:99; WA, 38:240.
1943 Toleo la Jena 3:446; WA, 26:282 n.k.
644
83. Lakini baraka hii au masimulizi yenyewe ya asasi ya maneno ya Kristo, iwapo tendo zima la Chakula cha Bwana jinsi Kristo alivyoamuru halifuatwi, halifanyi sakramenti.1944 Kwa mfano, mkate uliobarikiwa haugawiwi, haupokelewi, na hauliwi bali unafungiwa katika sanduku la Sakramenti, hutolewa kama dhabihu, au umebebwa huku na huko katika maandamano. 84. Hatuna budi kuifuata amri ya Kristo, “fanyeni hivi,” ambayo inalihusisha tendo zima au kaida ya Sakramenti hii: katika mkusanyiko wa Wakristo, mkate na divai vinachukuliwa, vinabarikiwa, vinagawanywa, vinapokelewa, vinaliwa, na divai inanywewa, na hapo ndipo kifo cha Bwana kinatangazwa. Lazima kuishika amri hii bila kuliondoa au kulibadili lolote. Kwa hiyo basi, Mt. Paulo anaweka wazi tendo zima la umegaji wa mkate, au la ugawaji na upokeaji mbele ya macho yetu katika 1 Kor. 10:16.
85. Kuna kanuni na kipimo bora kwa shabaha ya kuyalinda mafundisho ya kweli ya Kikristo kuhusu Sakramenti na kuepukana na makosa na ubadhirifu wa kipagani na kuuondoa kabisa: “Hakuna Sakramenti pasipo matumizi yake yaliyoanzishwa na Kristo au pasipo tendo lililoanzishwa na Mungu.”1945 Hakuna Sakramenti yoyote ambapo asasi ya Kristo haifuatwi jinsi ilivyoanzishwa naye. Kwa vyovyote, kanuni hii haiachwi kwa sababu kwamba ndiyo inafaa Kanisa la Mungu na inastahili kusisitizwa zaidi. 86 Maneno haya ‘matumizi’ au ‘tendo,’ kimsingi hayamaanishi imani, au ulaji kwa kinywa pekee. Badala yake, ni tendo zima la nje na la hadhara la Chakula cha Bwana jinsi kilivyoanzishwa na Kristo: uwekaji wakfu au maneno ya asasi na zaidi ugawaji au upokeaji, au ulaji mkate kwa kinywa na unywaji divai vilivyobarikiwa. Yaani, mwili na damu ya Kristo.
87. Hakuna Sakramenti bila matumizi yake. Kwa mfano, katika misa ya wafuasi wa Papa, mkate haugawanywi bali unatolewa kama dhabihu, unafungiwa ndani ya sanduku kwa shabaha ya kuabudiwa na watu au unabebwa katika maandamano. Hakuna Ubatizo ambapo kengele hazijabarikiwa kwa maji ya Ubatizo au ukoma kutibiwa kwayo au maji haya yanaabudiwa. Kanuni iliyotajwa hapo juu ilitungwa mwanzoni ili kukinga ubaridhifu wa wafuasi wa Papa na ilikuwa imefafanuliwa na Dk. Luther.1946
88. Licha ya hayo, hatuna budi kukumbuka kwamba, wanaoidharau
1944 Tendo la sakramenti tangu mwanzo mpaka mwisho wake katika liturgia ya Ekaristi, Kilatini: ‘Actio sacramentalis.’
1945 Kilatini (Melanchthon): ‘Nihil habet rationem sacramentum extra usum a Christo institutam seu extra actionem divinitus institutam.’
1946 Toleo la Jena 4; WA, 32: 254, 255; ‘Mafungu ya Smalkaldi,’ Seh. III, 15:4.
645 matamshi ya maneno ya asasi.
Sakramenti wamevuruga kanuni hii bora na ya manufaa sana. Kwa msaada wake, wamejaribu kukanusha kabisa kwamba, mwili wa Kristo upo kweli katika kiini chake na hata hapa duniani, wanaostahili na wasiostahili huupokea kwa vinywa vyao. Wanaifafanua maana ya Sakramenti kuwa matumizi ya kiroho na matumizi kwa imani ya ndani1947 peke yake ili wapate kukana kweli ya kuwepo halisi kwa ulaji wa mwili wa Kristo kwa kinywa, ambao wanaostahili na wasiostahili wanaushiriki hapa duniani. Hii inamaanisha kwamba, wasiostahili hawaipokei Sakramenti. Kula kwa mwili wa Kristo kunachukua nafasi tu kwa njia ya kiroho kwa imani, au kwamba, imani inadhuru kuwepo kwa mwili wa Kristo katika Chakula Kitakatifu na kwamba, wasiostahili na wanafiki wasioamini hawapokei mwili wa Kristo kwa sababu haupo kwa ajili yao.
89. Sakramenti haifanywi na imani yetu bali na maneno ya uanzishwaji ya Mungu Mwenyezi na Mwokozi wetu Yesu Kristo tu. Maneno haya yanaendelea daima kuwa na uwezo wao katika Ukristo bila kutegemea stahili au udhaifu wa mtumishi wa ibada. Kutoamini kwa mtu anayeipokea hakuwezi kuitoa na kuitangua. Jinsi Injili inavyosalia kuwa Injili ya kweli hata kama wasikilizaji wasiomcha Mungu hawaiamini, ila tu kwamba, kwao, haizai wokovu. Hivyo basi, ijapokuwa wanaoipokea Sakramenti wanaamini au hawaamini, Kristo anabaki kuwa mkweli katika maneno yake anaposema: “Twaa ule; huu ndio mwili wangu.” Hii haipokei imani yetu bali enzi yake.
90. Basi, kwa ajili ya ukavu wao, wengine wanaendelea kuutetea uasi wao mpotovu. Wanaivuruga kwa hila kanuni ya kawaida ya imani yetu. Wao hufikiria kwamba, imani yetu ndiyo inayoweza kuufanya mwili wa Kristo uwepo na upokelewe. Hivyo basi, wanashikilia imani yetu kuwa na uwezo zaidi kuliko Yesu Kristo aliye Bwana, Mwokozi, na Mwenyezi wetu.
91. Mintarafu ya sababu zote za kudhania na hoja duni za wanaoidharau Sakramenti kuhusu tabia za kiini na za asili za mwili wa binadamu, kuhusu kupaa kwa Kristo, na kuhusu kutoka kwake ulimwenguni humu, na mengine kama hayo, yamebatilishwa na Dk. Luther kwa upana kwa msingi wa Neno la Mungu katika maandiko yake ya mjadala kama ‘Dhidi ya Manabii wa Mbinguni,’ kwamba, maneno haya, ‘Huu ndio mwili wangu,’ yanasimama imara.’ Kadhalika pia, ‘Ukiri Mkuu na Mdogo kuhusu Chakula Kitakatifu’ na maandiko yake mengine.1948 Baada ya kifo chake, pepo hawa walokole hawakuweza kutoa mambo yoyote mapya. Kwa ajili ya ufupi unaopendwa sana, tunamrejesha msomaji Mkristo kwa maandiko haya ili ajifunze vizuri.
1947 Kilatini: ‘Usus spiritualis:’ ‘Usus fidei internus.’ 1948 WA 17:62-214; 18:64-320; 19:482-523; 26:261-509; 30:595-626; 54:141-167.
92. Sisi hatutaki, hatuwezi, au hatupaswi kamwe kuyaruhusu mashauri ya mtu yeyote mwerevu, haijalishi fungu au sifa anazoweza kuwa nazo, kutuongoza mbali na uelewa sahihi, wa uwazi, na wa dhahiri wa Neno la Kristo na agano lake. Kwenye maana iliyo ngeni na tofauti kadiri barua zinavyosomeka, jinsi inavyoelezwa hapo juu, tutazielewa na kuziamini kwa maana rahisi.
93. Sababu ambazo kwazo, tunarejea tena na tena katika jambo hili na majadiliano yote yanayotokana nalo ndiyo yale ambayo Dk. Luther aliyaelezea zaidi dhidi ya wanaoidharau Sakramenti mwanzoni kabisa kwa maneno yafuatayo: “Misingi yangu ambapo ninasimama katika jambo hili, ni ifuatayo:
1. Sababu ya kwanza ni fungu hili la imani yetu kwamba, kwa 94 upande wa kiini na asili yake, Yesu Kristo ndiye Mungu mkamilifu na mwanadamu katika nafsi moja asiyetenganishwa au kugawanyika.
2. Mkono wa kuume wa Mungu ndio upo pahali pote. 95
3. Neno la Mungu halisemi uongo wala halidanganyi. 96
4. Mungu ana njia mbalimbali tofauti na anajua jinsi ya kuwepo 97 mahali fulani, si moja tu, ambayo walokole huifikiria, ambayo wanafalsafa huiita kuwa ya mahali.1949 98. Kadhalika, mwili mmoja wa Kristo una jinsi tatu tofauti au zote tatu pamoja za kuwa mahali fulani:
99. Njia ya kwanza ya kuwepo kwa mwili ni njia ya kushika au ya kimwili, jinsi alivyotembea kimwili ulimwenguni na kujaza nafasi kulingana na ukubwa wake. Akipenda angeweza kutumia njia ya kuwepo, jinsi alivyofanya baada ya kufufuka kwake na jinsi atakavyofanya Siku ya Mwisho, jinsi Mt. Paulo anavyosema: “Kutokea kwake kutafanyika wakati ufaao na Mungu mwenye heri” (1 Tim. 6:15), na: “Kristo atakapofunuliwa aliye uhai wetu” (Kol. 3:4). Basi, kulingana na jinsi hii, hayumo ndani ya Mungu au pamoja na Baba au mbinguni, bali jinsi nafsi mwendawazimu anavyoota. Mungu si nafasi ya kimwili au mahali fulani. Hii ndiyo maana ya aya ambazo pepo walokole hutaja kuhusu Kristo anapouacha ulimwengu na kwenda kwa Baba na kadhalika.
100. Pili, tunaitaja njia isiyofahamika ya kuwepo kiroho. Kristo hahitaji nafasi yoyote. Badala yake, hupenyeza ndani ya kila kiumbe, popote apendapo. Kwa njia ya vielelezo vingine vya kawaida: maoni yangu hupenya hewani, nuruni, au majini, lakini hayajazi au hayaondoi nafasi yoyote, jinsi sauti ya muziki au toni hupita kwenye hewa au maji au ubao na ukuta na wala haijazi au haiondoi nafasi. Vivyo hivyo, nuru na joto hupitia hewani, majini, kwenye bilauri, fuweleni, na
1949 Kilatini: Localis.’
647
kadhalika, na vipo bila kujaza au bila kuondoa kitu kwenye nafasi. Kuna vielelezo vingi kama hivi. Alitumia jinsi hii ya kuwepo alipoliacha kaburi lililofungwa, alipotokea ambapo milango ilikuwa imefungwa, alipopatikana katika mkate na divai katika Chakula cha Bwana, na jinsi watu wanavyoamini, alipozaliwa na mama yake, na kadhalika.1950
101. Tatu, kuna jinsi ya kimungu na kimbingu. Kwa sababu yeye ndiye nafsi hiyo hiyo na Mungu, viumbe vyote lazima viweze kupenyezwa zaidi na kuwepo kwake kuliko jinsi vilivyo kulingana na jinsi ya pili. Kwa kuwa iwapo ni kulingana na jinsi ya pili, anaweza kuwepo ndani ya viumbe kwa njia ambayo hawahisi, hawagusi, hawapimi, au hawatambui, kwa kiwango cha kushangaza wakati akiwa ndani ya viumbe vyote kulingana na jinsi hii ya tatu ya kimungu, kwa njia ambayo haviwezi kumpima au kumtambua, lakini pale anapoviweka mbele yake mwenyewe, huwapima na huwafahamu. Lazima uielewe nafsi hii ya Kristo jinsi ilivyo moja na Mungu bila kutengwa, huwa mbali zaidi kupita viumbe, jinsi Mungu anavyoviangalia kutoka juu. Lazima uelewe kwa undani na ukaribu sana zaidi ya viumbe vyote kwamba, Mungu alivyo ndani ya viumbe, ndivyo mtu asiyeonekana yu pamoja na Mungu, na mahali ambapo Mungu yupo, ni lazima na pia awepo, la sivyo imani yetu haitakuwa ya kweli.
102. Lakini ni nani awezaye kuelezea au hata kutafakari jinsi hii inavyofanyika?
Tunajua kweli kwamba, yeye ndiye aliye ndani ya Mungu mbali zaidi kushinda viumbe vyote na ndiye aliye nafsi moja na Mungu. Lakini hatujui, jinsi hili linavyofanyika. Linashinda maumbile na mantiki, ujuzi wa malaika wote wa mbinguni, linajulikana kwa Mungu, na kufahamika kwake peke yake. Kwani hili ni kweli ingawa halijulikani kwetu. Tusiweke uongo katika maneno yake mpaka tujue jinsi ya kuthibitisha ukweli kwamba, kwa vyovyote vile, mwili wa Kristo hauwezi kuwa mahali ambapo Mungu yupo, na kwamba, jinsi hii ya kuwepo kwake ni udanganyifu. Waacheni walokole waithibitishe lakini itafanyika abadani!
103. Labda Mungu anajua namna zingine za kuwepo kwa mwili wa Kristo mahali fulani. Mimi sitaki kuyakanusha haya lakini kusudi langu la pekee lilikuwa kuonyesha jinsi walokole wetu walivyo wapumbavu kwa sababu wanakubali jinsi ile ya kwanza tu ya kushikika ya kuwepo kwa mwili wa Kristo, ingawa hawana uwezo wa kuthibitisha kwamba, hata jinsi hii ni kinyume cha maoni yetu. Kwa sababu sitaki kukanusha kwa namna yoyote kwamba, nguvu ya Mungu ina uwezo wa kufanya mwili kuwa mahali popote wakati huo huo, ingawa mwili u katika hali inayoshikika. Kwani ni nani basi anayetaka kujaribu kuthibitisha 1950 Taz. chini, 8, 24.
kwamba, Mungu hawezi kulifanya hilo? Ni nani aliyewahi kuona mwisho wa nguvu yake? Kwa kweli, walokole wafikiria kwamba, Mungu hawezi kuifanya, lakini ni nani atakayeziamini fikira hizo? Watathibitisha vipi fikira zao kuwa za kweli?” Mpaka sasa ni Luther tu.1951
104. Maneno haya ya Dk. Luther pia yanaonyesha dhahiri kwa nini makanisa yetu yanatumia neno ‘kiroho’ katika muktadha huu. Kwa wanaoidharau Sakramenti, neno hili ‘kiroho’ linamaanisha ushirika wa kiroho ambao unaanzishwa wakati Roho, kwa njia ya imani ya waumini wa kweli, anaunganishwa katika Kristo na kufanyika kweli kuwa mshirika wa kiroho wa mwili wake.1952 105. Badala yake, wakati Dk. Martin Luther au sisi tunapolitumia neno ‘kiroho’ katika mjadala huu, tunalielewa kumaanisha namna ya kiroho na ya kimbingu ipitayo asili jinsi Kristo alivyo katika Chakula Kitakatifu. Namna hiyo ya kiroho haifanyi tu faraja na uzima kwa waumini bali pia hulipiza/hutoa hukumu kwa wasioamini. Hivyo basi, tunakataa mawazo machafu ya Kikapernaumu. Yaani, kuwepo kwa mwili kwa njia ya kawaida ambayo wanaoidharau Sakramenti wanatoa na kulazimisha makanisa yetu licha ya ushuhuda wetu wa hadharani na unaorudiwa mara kwa mara kinyume chao. Katika fikira hii, pia tunatumia neno ‘kiroho’ tunaposema kwamba, mwili na damu ya Kristo vinapokelewa katika Chakula Kitakatifu. Mwili unaliwa na damu inanywewa kiroho, kwani ingawa ulaji wa aina hiyo hufanyika kwa kinywa, ni wa jinsi ya kiroho.
106. Hivyo basi, katika fungu hili, imani yetu kuhusu kuwepo kwa kweli kwa mwili na damu ya Kristo katika Chakula Kitakatifu, inajengwa juu ya ukweli na uenyezi wa kweli wa Mungu wa milele, Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Msingi huu ndio imara kabisa kuithibitisha na kuiimarisha imani yetu katika mahangaiko yote yanayohusu fungu hili. Kwa upande mwingine, msingi huo hupindua na huyakanusha mabishano yote yaliyokwisha kuwasilishwa na vipingamizi vya wanaoidharau, haijalishi jinsi itakavyoweza kuonekana kuipendeza akili ya mwanadamu. Kwa kweli, msingi huu pia unauwezesha moyo wa Mkristo kuutegemea na kuuamini kwa kweli na kwa uhakika.
107. Kulingana na hayo, tunakataa na kulaani, kwa moyo na kinywa, kila kosa ambalo halilingani na au mafundisho yaliyokwisha kutajwa ambayo yamejengwa katika msingi wa Neno la Mungu, kuwa uongo, udanganyifu, na upotoshaji. 108. Kwanza, mafundisho ya mageuzo-uwamo 1953ya wafuasi wa Papa wa Roma, wanaofundisha kwamba, mkate na divai vilivyowekwa wakfu
1951 WA, 26:335 n.k.
1952 Taz. ‘Consensus Tigurinus,’ 6, 9.
1953 Au ‘mageuzo ya elementi;’ Kilatini: ‘Transsubstantiatio.’
au vilivyobarikiwa katika Chakula Kitakatifu vinapoteza kabisa kiini na ariki1954 zao na vinageuzwa kuwa kiini cha mwili na damu ya Kristo. Vinavyobakia huwa sura tu ya mkate na divai.1955 Mwili wa Kristo unaendelea kuwepo katika sura ya mkate hata baada ya tendo la Sakramenti,1956 wakati mkate unafungiwa ndani ya sanduku la sakramenti1957 au unabebwa katika maandamano maalumu ili watu wauone na kuuabudu. Lakini hatuna Sakramenti yoyote isipokuwa kwa amri ya Mungu, agizo, na matumizi ambayo yametolewa katika Neno la Mungu jinsi ilivyoonyeshwa hapo juu.
109. Pili, tunakataa na kulaani pia matumizi yote mabaya ya wafuasi wa Papa wa Roma kuhusu Sakramenti hii, hasa machukizo makuu ya dhabihu ya misa kwa ajili ya walio hai na wafu.
110. Hali kadhalika, tunakataa na kulaani kwamba, aina moja tu ya Sakramenti inatolewa kwa Wakristo wa kawaida kinyume cha amri dhahiri na uasisishwaji wa Kristo, na kadhalika. Matumizi haya mabaya ya wafuasi wa Papa wa Roma tayari yamekataliwa kwa upana katika ukiri wa kawaida1958 wa makanisa yetu, Utetezi, Mafungu ya Smalkaldi, na maandiko yetu mengine, kwa msingi wa Neno la Mungu na shuhuda za Kanisa la Zamani.
111. Kwa njia ya andiko hili, kwanza, tunakusudia kutoa ukiri wetu na maelezo kuhusu kuwepo kweli kwa mwili na damu ya Kristo dhidi ya wanaoidharau Sakramenti, ambao wengine wao wana ukavu wa kupenyeza katika makanisa yetu kama wafuasi waaminifu wa Ukiri wa Augsburg. Kwa hiyo basi, kwanza, tutayatoa maelezo kuhusu Sakramenti na hivyo tunawaonya wasomaji wetu kwamba, wanaweza kuepukana na hayo sasa.
112. Kwa hiyo, tunakataa na kulaani, kwa kinywa na kwa moyo, kama uongo, uzushi, na upotofu, maoni na mafundisho ya wanaoidharau Sakramenti na mafundisho ambayo hayalingani na hayakubaliani nayo. Au yaliyo kinyume cha mafundisho yaliyotajwa hapo juu yenye msingi wa Neno la Mungu.
1. Wanasisitiza kwamba, maneno ya uanzishwaji hayapaswi 113 kueleweka kwa wepesi kwa namna yake halisi, jinsi yanavyosomeka, kuhusu kuwepo kwa kweli halisi kwa mwili na damu ya Kristo katika Chakula Kitakatifu.
1954 Kilatini: ‘Substantia et essentia.’
1955 Kilatini: ‘Accidentia sine substantia.’
1956 Kilatini: ‘Actio (sacramentalis).’
1957 Kilatini: ‘Sacrarium.’ Awali mikate iliyobarikiwa ilihifadhiwa katika kishubaka ukutani mwa Kanisa. Baada ya utambulisho wa sherehe ya ‘Corpus Christi’ mwaka wa 1264, mahali pa kishubaka hicho palichukuliwa na mnara mdogo ulionakshiwa sana na ulioitwa ‘sacrarium,’ nyumba ya sakramenti au tabenakulo.
1958 ‘Ukiri wa Augsburg.’
Badala yake, kama ‘tropos’1959 au kitamathali, inaweza kupewa maana tofauti, mpya, na isiyofahamika. Tunayakataa madai ya jinsi hiyo ya wanaoidharau Sakramenti, na maoni yao yanayopingana, hata yakiwa ya jinsi gani na mengi vipi.
2. Kadhalika, ukanaji wa ulaji wa mwili na damu ya Kristo kwa 114 kinywa katika Chakula Kitakatifu, ni mafundisho yaliyo kinyume chake kwamba, katika Chakula Kitakatifu, mwili wa Kristo unashirikiwa kwa njia ya kiroho tu kwa imani na kwamba, katika Chakula Kitakatifu vinywa vyetu hupokea mkate na divai tu.
3. Kadhalika, mafundisho kwamba, mkate na divai katika 115 Chakula cha Bwana si zaidi ya alama ambapo Wakristo wanatambuana au
4. kwamba, ni mifano tu au mithali, na ishara ya mwili wa Kristo ulio mbali sana. Maana ni kwamba , mkate na divai vilivyo chakula cha nje cha mwili wetu, ndivyo mwili wa Kristo ambao pamoja na ustahili wake ni chakula cha kiroho cha nafsi zetu.
5. Au kwamba, mkate na divai si zaidi ya vitu vya mfano na 116 ukumbusho wa mwili wa Kristo ambao haupo, na kwamba, kwa njia ya ishara hizi sawa na kwa njia ya muhuri, tunathibitishwa kwamba, imani yetu inapoondoka kwa Chakula Kitakatifu na kupanda juu ya mbingu zote, na kushiriki mwili na damu ya Kristo, kwa kweli, jinsi ilivyo katika Chakula Kitakatifu, tunapokea ishara za nje kwa vinywa vyetu. Hilo ni hakikisho na thibitisho la imani katika Chakula Kitakatifu linalobuniwa kwamba, linafanyika, si kwa njia ya uwepo wa kweli wa mwili na damu ya Kristo vinavyogawiwa kwetu, bali kwa njia ya ishara za nje.
6. Au kwamba, katika Chakula Kitakatifu, imani inagawiwa 117 sehemu tu kwa uwezo, nguvu, na ustahili wa mwili wa Kristo ulio mbali sana, na kwamba, kwa njia hii tunashiriki mwili wake ambao haupo. Kulingana na hayo, istilahi ‘muungano wa kisakramenti’1960 inapaswa kueleweka katika analogia ya ishara na kitu kilichodhihirika.1961 Kwa maneno mengine, kwa jinsi hiyo tu ambayo mkate na divai vina uhusiano na mwili na damu ya Kristo.
7. Au kwamba, mwili na damu ya Kristo vinapokelewa tu na 118 kushirikiwa kwa njia ya kiroho kwa imani peke yake.
1959 Kiyunani: ‘τροπος,’ yaani, ‘mwelekeo,’ ‘sifa.’
1960 Kilatini: ‘Unio sacramentalis.’
1961 Kilatini: ‘Analogia signi et signati.’
8. Kadhalika, mafundisho kwamba, kwa sababu ya kupaa kwa 119 mwili wake mbinguni, Kristo amefungiwa kabisa na kuzuiwa na nafasi fulani huko mbinguni, wala hawezi au hakusudii kuwepo kwa uhalisi kweli pamoja nasi katika Chakula Kitakatifu ambacho kinasherehekewa kulingana na uanzishaji wa Kristo hapa duniani. Badala yake, anaishi mbali jinsi mbingu na nchi zinavyotengana kila moja na nyingine. Baadhi ya wanaoidharau Sakramenti ili kuuthibitisha uzushi wao na kwa sababu ya ukorofi wao, waliyaghushi maneno haya ya Mdo. 3:21, “ilimpasa Kristo kupokelewa mbinguni” kwamba, “Kristo lazima apokelewe mbinguni –yaani, Kristo lazima atwaliwe ndani au azuiliwe au afahamike mbinguni. Maana, kwa vyovyote vile, hawezi na hatamani kuwa pamoja nasi duniani katika asili yake ya ubinadamu.
9. Kadhalika, kwamba, Kristo hangeweza kuahidi, kutekeleza, 120 au kutamani kuwa na uwepo halisi na wa kweli wa mwili na damu yake katika Chakula Kitakatifu kwa sababu asili na sifa zake za asili ya kibinadamu ambayo imejitwalia, haitoi nafasi wala hailiruhusu hili.1962
10. Kadhalika, mafundisho kwamba, si maneno na enzi ya 121 Kristo bali ni imani ndiyo inayofanya uwepo wa mwili wa Kristo katika Chakula Kitakatifu. Kwa hiyo, wengine huyaruka maneno ya uanzishwaji wakati wa tendo la Sakramenti.1963 Hata hivyo, sisi tunapinga na kulaani kuwekwa wakfu kwa wafuasi wa Papa wa Roma ambao wanasingizia neno na kazi ya kasisi kuwa na nguvu inayotolewa kuitekeleza Sakramenti. Maneno ya uanzishwaji hayawezi na hayapaswi, kwa namna yoyote, kurukwa katika tendo la Chakula Kitakatifu, jinsi ilivyoonyeshwa hapo juu katika maelezo yaliyotangulia.
11. Kadhalika, kwamba, wanaoamini wasitafute mwili wa 122 Kristo katika mkate na divai kulingana na maneno ya Kristo ya uanzishwaji katika Chakula Kitakatifu. Badala yake, hushauriwa kutazama mbali zaidi ya mkate wa Chakula Kitakatifu. Yaani, kwa imani yao, watafute mahali mbinguni ambapo Kristo Bwana yuko na mwili wake na hapo ndipo watamshiriki.1964
12. Sisi tunakataa pia mafundisho kwamba, wasioamini, 123 wasiotubu, na walio Wakristo waovu wamebeba jina la Kikristo tu lakini hawana haki,
1962 Kauli ya Theodoro Beza (1519-1605).
1963 Caspar Schwenckfeld (1490-1561).
1964 ‘Consensus Tigurinus’ mwaka wa 1549, 11: J. Calvin, G. Farel, H. Bullinger; ‘Confessio Helvetica Posterior’ mwaka wa 1566, 21: H. Bullinger.
652
ukweli, maisha, na imani iokoayo, wanapokea mkate na divai tu katika Chakula Kitakatifu na si mwili na damu ya Kristo. Kwa kuwa, kuna wageni wa aina mbili tu katika chakula hiki cha kimbingu, walio halisi na wasiokuwa halisi, basi, tunakataa, kufanya utengano kati ya wasiostahili ambao wanaitwa na Waepikuro kuwa wasiomcha Mungu na wenye kulidharau Neno la Mungu, na walio katika umoja wa nje wa Kanisa, wakipokea tu mwili na damu kwa matumizi katika Chakula Kitakatifu na si mwili na damu ya Kristo kwa hukumu yao.1965
13. Pia tunakataa mafundisho kwamba, ustahili hautegemei 124 imani ya kweli tu bali pia unategemea matayarisho ya mwanadamu mwenyewe.1966
14. Kadhalika, mafundisho kwamba, hata waaminio wa kweli 125 walio na imani halisi na ya kweli, hawafai kwa maana hushindwa kufikisha zaidi matayarisho yao wenyewe. Hivyo, wanaweza kupokea Sakramenti hii kwa hukumu, sawa na wengine wasiostahili.1967
15. Kadhalika, inapofundishwa kwamba, elementi, yaani, sura 126 inayoonekana ya mkate na divai vilivyobarikiwa, vinapaswa kuabudiwa.1968 Kwa kweli, hakuna mtu yeyote, isipokuwa mzushi Mwariano, awezaye au apendaye kukataa kwamba, Kristo mwenyewe, Mungu wa kweli na mwanadamu wa kweli, yupo kweli katika kiini chake katika Chakula Kitakatifu. Tunamwabudu katika Roho na ukweli ikiwa Chakula Kitakatifu kinatumiwa vizuri. Tunamwabudu popote lakini hasa mahali ambapo Kanisa lake limekusanyika.
16. Tunakataa na kulaani pia maswali na maneno yote 127 matakatifu, yenye kufuru na dhihaka, yanayozungumza kwa njia ya ujinga, ya kimwili, na ya Kikapernaumu kuhusu siri za kimbingu zinazoshinda asili katika Chakula Kitakatifu.1969
1965 Kauli ya Profesa Paul Eber (1511-1569) huko Wittenberg ya mwaka wa 1562.
1966 Sinodi ya Trento, kikao cha 13, sura ya 7, kanuni ya 11.
1967 Sinodi ya Trento, kikao cha 13, sura ya 7, kanuni ya 11.
1968 Ibada ya elementi inaitwa ‘artolatria.’
1969 Ukiri wa Torgau wa mwaka wa 1571 unaorodhesha baadhi ya maswali haya: 1. Lini na vipi mwili wa Kristo unakuwa mkate au unakuwa katika hali ya mkate? 2. Vipi au mwili wa Kristo una tofauti gani na mkate? 3. Mwili wa Kristo umefichwaje katika mkate? 4. Muungano wa sakramenti huendelea kwa muda gani? 5. Lini mwili wa Kristo unaachana na mkate? 6. Je, mwili wa Kristo ambao tunaupokea unaingia katika miili na matumbo yetu na je, unameng’enyeka humo? 7. Unasagwa na kutafunwa kwa meno? 8. Je, ni mwili hai au mfu kwa kuwa tunaupokea katika mkate, na unakuwa umetengwa na damu katika divai?” 9. Kwa kweli, kuwepo kwa Kristo kimwili kuna faida gani? 10. Bwana Kristo anatekeleza nini katika mtu ambaye huipokea sakramenti kwa njia isiyostahili na kukufuru? 11. Je, mwili wa mtu aliyepokea mwili wa Kristo unabadilishwa kwa njia ya asili na mwili wa Kristo?
653
Tukiyajumlisha mabishano haya, tunakataa tabaini za uzushi ambazo tayari zimelaaniwa na kukataliwa katika maelezo yanayoendelea. Kwa ajili ya uchache wa maneno, hatuna tumaini la kuyarudia haya wakati huu. Maoni yoyote yaliyokataliwa na yanayoweza kuongezewa, au maoni ya uzushi yanayoweza kuwepo, yanaweza kujulikana na kutambuliwa kwa jina kwa njia ya maelezo yaliyotangulia. Kwa kuwa, tunakataa na kulaani vitu vyote ambavyo havilingani na ambavyo ni kinyume cha au havipatani na mafundisho yaliyotolewa hapo juu, yenye msingi wake uliojengwa katika Neno la Mungu.
VIII. NAFSI YA KRISTO
1. Mabishano yamezuka pia kati ya wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg kuhusu nafsi ya Kristo. Mabishano haya hayakutokea kati yao, bali yalitokea miongoni mwa wanaoidharau Sakramenti.
2. Kwa kuwa, wakati Dk. Luther alishikilia kuwepo kweli kwa kiini cha mwili na damu ya Yesu Kristo katika Chakula Kitakatifu, kwa msingi wa maneno ya uanzishwaji, wafuasi wa Zwingli walimpinga kwa kusema kwamba, mwili wa Kristo hauwezi kuwa kweli na halisi mwili wa binadamu ikiwa yu mbinguni na wakati huo huo yuko katika Chakula Kitakatifu hapa duniani kwani enzi ya jinsi hiyo inamhusu Mungu pekee na mwili wa Kristo hauna uwezo huo.1970
3. Jinsi mafundisho na maandiko yake ya mabishano yanavyoonyesha wazi kuhusu Chakula Kitakatifu, Dk. Luther alipinga na kukataa, ambapo tunatangaza uaminifu wetu waziwazi.1971 4. Lakini baada ya kifo chake, wanatheologia wachache wa Ukiri wa Augsburg, bila kuwa tayari kujitolea wenyewe hadharani na dhahiri, kwa upande wa ukiri wa wanaoidharau Sakramenti kuhusu mafundisho ya Chakula Kitakatifu, waliendelea nayo na walitumia msingi wa mabishano hayo hayo1972 kuhusu nafsi ya Kristo ambayo kwao, wanaoidharau Sakramenti walithubutu kuondoa kutoka kwa Chakula Kitakatifu, kuwepo kweli mwili na damu ya Kristo na kwa uhalisi. Walisema kwamba, hakuna kitu kinachoweza kuhesabiwa kwa asili ya ubinadamu katika nafsi ya Kristo ambacho huvuka mipaka au hupingana na asili yake ya kawaida. Walienda mbali sana na kutupa mafundisho ya Dk. Luther, na ya wale waliofuata kama waliokuwa katika umoja
1970 Huldrych Zwingli, Opera, II/1, 64-320.
1971 ‘Mahubiri kuhusu sakramenti ya mwili na damu ya Kristo yalipambana na walokole’ mwaka wa 1526, ‘Kwamba, maneno haya ya Kristo ‘huu ndio mwili wangu’ yalisimama imara kupambana na walokole’ mwaka wa 1527, ‘Chakula Kitakatifu’ cha Kristo, Ukiri wa mwaka wa 1528.
1972 Rejea andiko la Wakalvinisti wa siri miongoni mwa Walutheri lililoitwa ‘Grundfest,’ yaani, (hoja ya kimsingi) ya mwaka wa 1571. Waliotetea mafundisho ya Luhter walishtakiwa kwa kuitwa wafuasi wa Markion, Paulo wa Samosata, Sabelliano, Ario, Nestorio, Eytykhe na Monothelete.
na Neno la Mungu, na karibu mashtaka makubwa ya aina zote za uzushi wa zamani.
5. Kusudi majadiliano haya yatatuliwe kwa njia ya Kikristo kulingana na Neno la Mungu na kulingana na imani yetu ya Kikristo iliyo wazi, na kuyatuliza mafundisho yetu sawasawa kwa neema ya Mungu, imani, na ukiri wetu wa pamoja ni kama ifuatavyo:
1. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, ingawa Mwana 6 wa Mungu ndiye nafsi maalumu, tofauti, na kamilifu ya kimungu, ndiye Mungu wa kweli, wa kiini hicho hicho na mkamilifu pamoja na Baba na Roho Mtakatifu tangu milele. Lakini wakati ulipowadia, alijichukulia asili ya ubinadamu katika umoja wa nafsi yake. Hilo halimaanishi kwamba, sasa ama nafsi mbili zinazopatikana au Kristo wawili, lakini kwamba, Kristo Yesu anayeishi, ni mwenye nafsi moja iliyo ya Mungu kweli wa milele, aliyezaliwa na Baba tangu mwanzo, na vile vile mwanadamu wa kweli, aliyezaliwa na Bikira Maria ambaye kweli ni wa kusifiwa sana, jinsi ilivyoandikwa “Na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, ni ambaye Mungu aliye juu ya vyote, aliyebarikiwa milele” (Rum. 9:5).
2. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, katika nafsi hii 7 moja isiyoweza kugawanyika sasa, kuna asili mbili tofauti. Yaani, asili ya kimungu ambayo ni ya tangu milele yote, na asili ya kibinadamu ambayo ilitwaliwa katika umoja wa nafsi ya Mwana wa Mungu. Asili hizi mbili zisitenganishwe abadani katika nafsi ya Kristo. Tangu sasa, zisichanganywe pamoja, au moja isibadilishwe kuwa nyingine, lakini katika nafsi ya Kristo, kila moja hubaki katika asili na kiini chake milele na milele.1973
3. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri pia kwamba, asili na kiini 8 cha nafsi zote mbili zilizotajwa, hubaki bila kuchanganywa na bila kuondolewa kabisa. Badala yake, kila moja hubaki na sifa zake za kiasili na zenye kiini chake. Milele, hazitapoteza sifa zao. Sifa za kiini cha asili moja hazitabadilishwa kamwe kuwa sifa za kiini cha asili nyingine.
4. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri pia kwamba, sifa za asili 9 ya kimungu ni kwamba, mwenyezi wa milele, asiyekuwa na mwisho, huwa kila mahali wakati mmoja katika uhalisia. Yaani, kulingana na sifa ya asili na ya kiini
1973 Kanuni ya Sinodi ya Khalkedon ya mwaka wa 451 kuhusu asili mbili za Kristo mmoja: bila kuchangannywa ασυγχυτως, ατρεπτως (kupambana na Eytykhes ) na bila kugawanywa αδιαιρετως, αχωριστως (kupambana na Nestorio). Mwaka wa 1570, Martin Chemnitz alitoa (toleo lililoongezewa mwaka wa 1578) katika kitabu kikubwa kiitwacho,‘De duabus naturibus in Christo’ (‘Asili Mbili katika Kristo’). Kitabu hiki kilitolewa katika Kiingereza mwaka wa 1971 (‘The Two Natures in Christ’).
655
cha asili, kuwepo halisi kwa njia yake mwenyewe1974 na kuyajua mambo yote. Sifa hizi haziwezi kamwe kuwa za asili ya kibinadamu.
5. Kwa upande mwingine, sifa za asili ya ubinadamu ni: kiumbe 10 cha kimwili, chenye mwili na damu, mwisho na mipaka, kinachoteseka na kufa, kinachopaa na kushuka, kinachotoka mahali na kwenda mahali pengine, kinachoona njaa, kinachohisi kiu, baridi kali, na joto na kadhalika. Sifa hizi haziwezi kuwa za asili ya kimungu kamwe.
6. Kadhalika, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, 11 baada ya umwilisho1975 wake kati ya asili hizi mbili za Kristo, hakuna hata moja inayoendelea kuwepo yenyewe kiasi kwamba, inakuwa au inaanzisha nafsi halisi. Badala yake, asili zote mbili ziliungana kwa hiyo kwamba, zinamfanya kuwa nafsi moja. Katika nafsi hii moja, asili ya kimungu na asili ya kibinadamu iliyotwaliwa zinakuwepo kwa njia ya binafsi. Kwa hiyo, baada ya umwilisho, haiwi tu asili yake ya kimungu, bali pia asili yake ya kibinadamu inayotwaliwa katika nafsi nzima ya Kristo. Nafsi ya Kristo au ya Mwana wa Mungu mwenye mwili wa ubinadamu, yaani, ambaye amejitwalia mwili na amekuwa mwanadamu, si kamilifu bila asili yake ya kibinadamu. Hali kadhalika, nafsi ya Kristo si kamilifu bila asili yake ya kimungu. Kwa hiyo, Kristo si nafsi mbili tofauti bali ni nafsi moja, ijapokuwa, kwa hakika, ni asili mbili tofauti zenye viini vyao na sifa zao zinazopatikana ndani yake bila kuchanganywa.
7. Licha ya hayo, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, 12 asili iliyotwaliwa ya ubinadamu katika Kristo inaendelea kuwa na kuhifadhi sifa zao za asili na za kiini. Kwa njia ya muungano wa binafsi pamoja na uungu, asili hii iliinuliwa baadaye kwa njia ya kupandishwa au kutukuzwa katika mkono wa kulia wa enzi, uwezo, na utawala juu ya kila jina linalotajwa siyo tu katika zama hii bali pia katika zama itakayokuja.1976
8. Kristo hakuipokea enzi hii ambayo kwayo, aliinuliwa kwa 13 upande wa ubinadamu wake ila baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu na kupaa kwake, lakini alipochukuliwa mimba katika tumbo la mama yake na kuwa mwanadamu, ndipo asili ya kimungu na ya kibinadamu zilipoungana pamoja.
9. Muungano huu wa kibinafsi usieleweke, jinsi wengine 14 walivyouelezea kimakosa, kana kwamba, nafsi zote mbili, ile ya kimungu na ile ya kibinadamu, zimeungana pamoja kama vibao viwili vilizoshikanishwa pamoja kwa gundi.
1974 Kijerumani: ‘Für sich selbst gegenwärtig sein.’ Kilatini: ‘Per se ubique praesentem esse.’
1975 Kilatini: ‘Incarnatio .’
1976 Efe. 1:21.
Kwa hiyo basi, asili zote mbili hazina ushirikiano wa kweli na halisi kamwe 1977. 15 Hili ndilo lililokuwa kosa na uzushi wa Nestorio na wafuasi wa Paulo wa Samosata1978 kulingana na ushuhuda wa Suda1979 na Theodoro, mzee1980 wa Kanisa la Rhaitu.1981 Walifundisha kwamba, nafsi zote mbili hazina ushirikiano kamwe.1982 Hii inamaanisha kwamba, asili zote mbili hazina ushirikiano wowote na zenyewe kwa kuwa asili hizi zimetenguka moja kwa nyingine na hivyo kuwafanya Kristo wawili. Moja ni Kristo na nyingine ndiye Mungu, yaani, Neno, anayedumu katika Kristo.
16. Mzee Theodoro, aliandika: “Wakati wa Mani,1983 Paulo fulani aliyezaliwa huko Samosata, ambaye alikuwa msimamizi1984 wa Antiokia katika Shamu, alifundisha kwa njia ya kukufuru sana kwamba, Kristo Bwana alikuwa mwanadamu wa kawaida ambaye ndani yake Neno la Mungu lilidumu kama ilivyokuwa katika kila mmoja wa manabii. Pia alishikilia kwamba, asili ya kimungu na ya kibinadamu zimetengana na zi mbali na kila mmoja na kwamba, katika Kristo hazina ushirikiano kabisa, kana kwamba, Kristo ni mmoja na Mungu na Neno anayedumu kwake ni mwingine.”1985
17. Kinyume cha uzushi huu uliolaaniwa sana, Kanisa la Kikristo wakati wote limeamini na kushikilia kwa njia rahisi kwamba, asili ya kimungu na ya kibinadamu zimeungana katika nafsi ya Kristo kwa njia ambayo kwayo, zina ushirikiano wa kweli. Katika ushirikiano huo, asili zote mbili hazichanganyiki
1977 Andiko la Kijerumani linatumia neno la Kilatini: ‘realiter.’
1978 Nestorio (+ mnamo mwaka wa 451) alitoka Shamu, tangu mwaka wa 428 Askofu Mkuu wa Konstantinopoli. Alilaaniwa katika Sinodi ya Efeso mwaka wa 431 na akafukuzwa mwishowe kutoka kwa nyumba ya watawa huko Misri. Alifundisha kwamba, asili zote mbili katika Kristo ziliunganishwa kwa njia ya nia ‘ευδοκια’ na siyo kwa njia ya kiini ‘υποστασις.’ Hivyo, alifundisha kwamba, asili mbili katika Kristo haziwezi kuunganishwa katika nafsi ya Kristo. Paulo wa Samosata, askofu wa Antiokia, tangu mwaka wa 260 na aliondolewa madarakani mwaka wa 268. Mafundisho yake yalitangulia ya Nestorio.
1979 Suda ‘η Ζουδ’), ‘ngome ya ujuzi,’ ensaiklopidia ilikusanywa na wataalamu wa Byzantio mnamo karne ya kumi.
1980 Kiyunani: ‘πρεσβυτερος,’ yaani, kasisi au mchungaji na si mwanakamati asiyebarikiwa kuwa mchungaji jinsi neno hili linavyofahamika kimakosa siku hizi.
1981 Mtawa katika Rhaitu huko Sinai (+ kati ya miaka ya 638 na 649) na baadaye askofu wa Pharan, mtunzi wa kitabu kiitwacho, ‘Προπαρασκευη κτλ,’ yaani, (‘Maandalio’) n.k.
1982 Kiyunani: ‘Δυο φυσεις ακοινωνητους προς εαυτας πανταπασιν.’ Kilatini: ‘Hoc est, naturas omni modo incommunicabiles esse.’
1983 Mwaka wa 216-276 kutoka Seleukia-Ktesiphon huko Uajemi, alianzisha dini mpya kwa elementi za Ugnostiki. Mani alifundisha kwamba, kuna misingi miwili ya milele: msingi wa wema na wa ubaya vikishindana daima.
1984 Kijerumani: ‘Vorsteher.’ Andiko la Kilatini: ‘Antistes.’
1985 “Paulus quisdam iisdem, quibus Manes, temporibus, Samosatenus quidem ortu, sed Antiochiae Syriae antistes, Dominum impie dixit nudum fuisse hominem, in quo Deus Verbum sicut et in singulis prophetis habitavit, ac proinde duas naturas separatas et citra omnem prorsus inter se communionem in Christo esse, quasi alius sit Christus, alius Deus Verbum in ipso habitans.” MSG 91, 1496 D, dondoo huru.
657
katika asili moja bali katika nafsi moja, jinsi Dk. Luther anavyoandika. 18. Kwa sababu ya umoja na ushirika huu, walimu wa Kanisa la Zamani, kabla na baada ya Sinodi ya Khalkedon, mara nyingi, walitumia neno ‘mchanganyiko’1986 kwa njia nzuri, ya kweli, na tofauti kabisa. Ikihitajika, tutaweza kuzitaja shuhuda nyingi za akina baba kuhusu jambo hili. Shuhuda hizi zinapatikana katika maandiko yetu kwa wingi.
19. Ili kuuelezea muungano wa binafsi na ushirika, wanatumia mifano ya mwili na nafsi na ya chuma cha kinachowaka.1987 Mwili na nafsi, vile vile chuma kinachowaka, vinashirikiana kwa kweli, siyo tu kwa njia ya kirai cha tamathali, bali katika tendo na ukweli, si kwa kirai au njia ya kusema kwa maneno tu bali kwa ukweli kabisa.1988 Hata hivyo, asili ama hazichanganyiki au hazisawaziki,1989 jinsi pombe ya asali itokanayo na asali na maji havipambanuliwi kuwa maji au asali. Badala yake, huwa mchanganyiko wa kinywaji. Umoja wa asili ya kimungu na ya kibinadamu katika nafsi ya Kristo ndio tofauti kabisa.
Ushirika na muungano huu kati ya asili ya kimungu na ya kibinadamu katika nafsi ya Kristo ni tofauti kabisa, wa juu sana, na usioelezeka. Hivyo basi, katika muungano na ushirika huu, Mungu ndiye mwanadamu na mwanadamu ndiye Mungu bila nafsi au sifa zake kuchanganywa. Kinyume chake, kila asili inadumisha kiini na hali yake.
20. Muungano huu wa binafsi, unamaanisha ushirika wa kweli wa asili. Kwa hiyo basi, haikuwa asili tu ya ubinadamu, ambayo hali yake ni kuteswa na kufa, iliyoteseka kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu, bali pia Mwana wa Mungu mwenyewe ameteseka na kufa kweli. Hii ndiyo imani yetu rahisi. Mwana wa Mungu ameteseka na kufa katika asili ya kibinadamu ambayo alijitwaa ingawa asili ya kimungu kamwe haiwezi kuteswa na kufa.
21. Dk. Luther tayari amelielezea hili zaidi katika ‘Ukiri Mkuu kuhusu Chakula Kitakatifu’ dhidi ya mafundisho ya kukufuru ya Zwingli yanayoitwa ‘alloiosis.’1990 Zwingli alifundisha kwamba, asili moja ni lazima ichukuliwe na kueleweka kuwa nyingine. Luther aliliita jambo hili kinyago cha Ibilisi na kulilaani hadi kina cha kuzimuni.1991
1986 Kilatini: ‘mixtio;’ k.m. Gregorio wa Nazianzo, Gregorio wa Nyssa, Athanasio, Tertulliano na Agostino.
1987 Kilatini: ‘anima et corpus; ferrum cadens:’ Yustino Shahidi, rejea barua ya 137 ya Agostino. Origene ‘Περι αρχων’ 2:6, 6.
1988 Kilatini: ‘Non per phrasin aut modum loquendi aut verbaliter, sed vere et realiter.’
1989 Kilatini: ‘Confusio aut exaequatio naturarum.’
1990 Istilahi ya balagha: mabadiliko ya sehemu moja kuwa nyingine.
1991 WA, 26:317 n.k. Taz. chini sehemu ya 39.
658
22. Kwa hiyo, walimu wa Kanisa la Zamani, kama Ireneo, Athanasio, Hilario, Basileio kulingana na Theodoro, Gregorio wa Nyssa, na Yohana wa Dameski, walipoielezea siri hii, waliyaunganisha maneno haya mawili, yaani, ‘ushirika’ na ‘umoja’ na kulielezea moja kushinda lingine.1992
23. Kwa sababu ya muungano na ushirika huu wa asili ya kimungu na wa kibinadamu katika Kristo, tunaamini, tunafundisha na tunakiri kulingana na imani yetu ya Kikristo iliyo wazi, yote yanayosemwa kuhusu enzi ya asili ya ubinadamu ya Kristo anapoketi katika mkono wa kuume wa Mungu Mwenyezi, na yote yanayofuatia. Ikiwa muungano na ushirika wa asili zote mbili katika nafsi ya Kristo havikuwako kwa tendo na kwa ukweli, haya yote yangekuwa bure wala hayangeweza kudumu.
24. Kwa ajili ya muungano na ushirika huu wa binafsi, Mariamu, bikira aliyesifiwa sana, hakushika mimba ya mwanadamu wa kawaida, bali ya mwanadamu ambaye kweli ni Mwana wa Mungu aliye juu mno, jinsi malaika anavyoshuhudia. Alionyesha enzi yake ya kimungu hata katika tumbo la mama yake na alizaliwa na bikira bila kuharibu ubikira wake. Kwa hiyo, yeye kweli ni Mama wa Mungu1993 na alibaki kuwa bikira.1994
25. Kwa hiyo basi, Kristo alifanya miujiza yake yote na kuonyesha enzi yake ya kimungu kulingana na mapenzi yake mema, muda, na kwa jinsi alivyotaka. Alifanya hivyo, baada ya kufufuka, na kupaa kwake katika hali ya fedheha. Kwa mfano, wakati wa arusi huko Galilaya,1995 alipotimiza umri wa miaka kumi na miwili alikuwa kati ya wataalamu,1996 katika bustani, kwa neno moja, alifapofadhaishwa aliwachapa maadui zake na wakaanguka,1997 na katika kifo, hakufa tu kama mwanadamu yeyote, bali kwa njia ambayo, kwa kifo chake, alishinda dhambi, mauti, Ibilisi, kuzimu, na hukumu ya milele. Asili ya ubinadamu haingeweza kuyatimiza hayo kama haingeungana na asili ya kimungu na kuwa na ushirika nayo.
1992 Kiyunani: ‘Κοινωνια’ na ‘ενωσις:’ Kilatini: ‘Communio’ na ‘unio.’ Ireneo, Adv. Haer. 4:37; Athanasio Barua yake kwa Epikteto, Hilario ‘Utatu;’ Yohana wa Dameski ‘Πηγη γνωσεως’ 3:19.
1993 Kijerumani: ‘Gottes Mutter;’ Andiko la Kilatini kulingana na Kiyunani: ‘θεοτοκος.’
1994 Kauli maarufu katika Kilatini: ‘Unde et vere θεοτοκος, Dei genitrix, est, et tamen virgo mansit.’ ‘Kitabu cha Mwafaka’ kinajiunga hapa na mafundisho ya Kanisa la Magharibi na Mashariki kwamba, Mariamu aliendelea kuishi katika hali ya ubikira baada ya kuzaliwa kwa Yesu. Hata hivyo, baadaye aliwazaa watoto wengine, kwa mfano, Yakobo, aliyeitwa nduguye Bwana. Tunaweza kuelewa mafundisho haya kumaanisha kwamba, Kanisa la Kikristo linafahamu na tunamkiri tu Mariamu kama mama mzazi wa Mungu katika hali yake ya ubikira. Wakati uo huo, ndoa yake na Yusufu inaisifu sana ndoa kama hali takatifu iliyoumbwa na Mungu kwa shabaha takatifu ya upendo, heri, na kuvizaa vizazi vipya.
1995 Yn. 2:1-11.
1996 Lk. 2:41-52.
1997 Yn. 18:6.
26. Kwa hiyo pia, asili ya ubinadamu iliinuliwa baada ya kufufuka kutoka kwa wafu, juu ya viumbe vyote huko mbinguni, na hapa duniani. Inamaanisha kwamba, ameiweka kando kabisa sura ya utumwa hata hivyo, bila kuweka kando asili ya ubinadamu, ambayo itadumu milele na milele. Katika asili hii ya ubinadamu aliyojitwalia, anaimiliki na kuitumia kabisa enzi ya kimungu. Alikuwa na enzi hii mara moja tu wakati alichukuliwa mimba katika tumbo la mama yake, lakini jinsi mtume anavyoshuhudia, aliiweka kando.1998 Jinsi Dk. Luther anavyoielezea,1999 aliiweka ikafichika wakati wa fedheha yake na hakuitumia wakati wote, ila tu wakati ambapo alitaka kufanya hivyo. 27 Lakini sasa, kwa kuwa alipaa mbinguni, si kama watakatifu wengine, bali kulingana na maneno ya mtume,2000 amepaa juu sana kupita mbingu zote kiasi kwamba, aweze kujaza vitu vyote. Yu kila mahali akitawala, si kama Mungu tu, bali pia kama mwanadamu, kutoka bahari hadi bahari mpaka miisho ya dunia jinsi manabii wanavyotabiri2001 na jinsi mitume wanavyoshuhudia kwamba, alifanya kazi pamoja nao kila mahali na kuthibitisha lile Neno na ishara zilizofuatana nalo.2002
28. Hata hivyo, hili halikutekelezwa kwa njia ya ulimwengu huu, lakini jinsi Dk. Luther anavyoelezea, kwa njia ya mkono wa kulia wa Mungu, ambapo si mahali fulani huko mbinguni, jinsi wanaoidharau sakramenti wanavyoshikilia bila thibitisho kutoka kwa Maandiko Matakatifu. Mkono wa kuume wa Mungu ni nguvu halisi ya Mungu Mwenyezi ambayo inajaza mbingu na dunia, ambamo Kristo amekwisha kusimikwa kulingana na ubinadamu wake kwa matendo na kwa kweli bila mchanganyiko wowote au usawa wa asili zote mbili katika kiini na hali ya miliki yake.2003
29. Kwa sababu ya nguvu hii inavyowakilishwa, anaweza na kweli yu pamoja na mwili na damu yake katika Chakula Kitakatifu, kwa nguvu ya agano lake, ambalo kwalo, ametuongoza kwa njia ya Neno lake. Hakuna mwanadamu mwingine anayeweza kufanya hili, kwa sababu hakuna mwanadamu ambaye ameungana kwa jinsi hii na asili ya kimungu na amewekwa katika kazi ya kimungu, mwenye enzi tukufu na nguvu zote kwa njia ya muungano wake wa asili zote mbili katika Kristo, jinsi Yesu, Mwana wa Mariamu alivyo.
30. Katika yeye, asili ya kimungu na ya kibinadamu zimeungana zenyewe kwa njia ambayo katika Kristo, ukamilifu wote wa uungu na uanadumu kimwili
1998 Flp. 2:7.
1999 ‘Makala kuhusu maneno ya mwisho ya Daudi’ mwaka wa 1543, WA, 54:50.
2000 Efe. 4:10.
2001 Zab. 8:6; 93:1; Zek. 9:10.
2002 Mk. 16:20.
2003 Kilatini: ‘Realiter sine confusione et exaequatine naturarum.’
660
(Kol. 2:9). Katika muungano wake huu, kuna namna ya ushirika ulioinuliwa, ndani, na ushirika usioelezeka ambao hata malaika wanaustaajabia. Wanapata furaha yao na shangwe wanapoutazama, jinsi Mt. Petro anavyoshuhudia.2004
Tutalijadili hili kwa urefu zaidi hapa chini.
31. Fundisho la muungano wa binafsi2005 linamaanisha kwamba, asili ya kimungu na asili ya kibinadamu, yaani, zinaungana moja na nyingine katika nafsi ya Kristo kwamba, si majina tu yanayofanana, bali pia zina ushirika kwa matendo kati yao bila mchanganyiko wowote au usawa wa asili ya kiini. Mafundisho kuhusu mawasiliano ya sifa2006 yanatokana na msingi huu. Licha ya hili, tutasema mengi hapa chini pia.
32. Kwa kuwa ni kweli kwamba, kila asili inadumisha sifa zake za kiini,2007 na pia hazitengani kutoka kwa asili moja na kumwagwa katika asili nyingine, jinsi maji yanavyomwagwa kutoka chombo kimoja hadi kingine, mabadiliko ya hali hii hayawezi kufanyika au kuendelea ikiwa muungano au mawasiliano ya sifa katika nafsi ya Kristo haukuwepo kweli. 33. Mafundisho haya ndiyo siri kubwa zaidi mbinguni na duniani inayofuata fungu la Utatu Mtakatifu, jinsi Mt. Paulo anavyosema: “Siri ya utauwa ya dini yetu ni kuu: Mungu alidhihirishwa katika mwili” (1 Tim. 3:16). 34 Mt. Petro anashuhudia kwa maneno yaliyo wazi kwamba, sisi ambao Kristo yu ndani yetu kwa neema tu, tunamiliki siri hii katika Kristo: “Tupate kuwa washirika wa tabia ya Uungu.”2008 Ni uhusiano gani na asili ya kimungu unapaswa uwe ambao mtume anasema kwamba: “Katika yeye (Kristo) unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.”2009 Mungu na mwanadamu ni nafsi moja.
35. Ni muhimu sana kwamba, fundisho hili la mawasiliano ya sifa2010 katika nafsi mbili litachukuliwa kwa makini na kwa upambanuzi halisi kwa sababu kauli au matamko2011 yanayohusu nafsi ya Kristo, asili, na sifa zake si ya aina na namna moja. Kauli hizi zikizungumziwa bila upambanuzi halisi, mafundisho yanaweza kuwa na matatizo na msomaji wa kawaida anaweza kupotoshwa kwa urahisi. Utoaji ufuatao wa hoja unapaswa kufuatwa kwa uangalifu sana. Kwa ajili ya utoaji bora na rahisi, hoja zinaweza kueleweka chini ya vipengele vikuu vitatu.2012
2004 1 Pet. 1:12.
2005 Kilatini: ‘Unio personalis.’
2006 Kilatini: ‘Communicatio idiomatum.’
2007 Kilatini: ‘Quod propria non egrediantur sua.’
2008 2 Pet. 1:4.
2009 Kol. 2 :9.
2010 Kilatini: ‘Communicatio idiomatum.’
2011 Kilatini: ‘Propositiones vel praedicationes.’
2012 Mgawanyo katika aina (‘genus’) tatu unamrejelea Martin Chemnitz. Maelezo ‘genus idiomaticum, genus
36. Kwanza, Kristo yu na asili mbili zilizo wazi na zinabaki bila kugeuzwa, kubadilika, na bila kuchanganyika katika asili na sifa zake. Asili zote mbili hufanyika kwa nafsi moja tu. Hivyo basi, ingawa ni ya asili, sifa yoyote inaelezewa. Haihusiki tu na asili inayolingana, bali inahusika na nafsi nzima ambayo kwa wakati huo huo ni Mungu na mwanadamu, ingawa anaitwa Mungu au mwanadamu.
37. Katika jinsi hii,2013 si kwamba, lolote linalohusu nafsi moja, wakati huo huo ni sifa ya nafsi zote mbili bali lazima ielezewe dhahiri kwamba, ni kulingana na asili gani sifa fulani inahesabiwa kuwa nafsi nzima. Hivyo basi, kwa mfano, Mwana wa Mungu alizaliwa kimwili katika ukoo wa Daudi (Rum. 1:3). Naye Kristo aliuawa katika mwili na aliteseka kwa ajili yetu katika mwili (1 Pet. 3:18; 4:1).
38. Lakini wanaoidharau Sakramenti kwa siri au hadharani, wanauficha uzushi wao wa kupotosha chini ya maneno haya: inatupasa kuitolea nafsi nzima kilichohusu asili moja. Hata hivyo, wanaielewa asili moja na wanaiacha nyingine. Kwa mfano, nafsi moja tu ndiyo iliyoteseka kwa ajili yetu, jinsi Dk. Luther anavyoelezea katika ukiri wake mkuu: “Ukiri Mkuu kuhusu Chakula Kitakatifu cha Bwana,” aliouandika kuhusu ‘alloiosis’ ya Zwingli.2014 Hapa tunayataja maneno ya Dk. Luther mwenyewe, ili Kanisa la Mungu lipate kulindwa dhidi ya kosa hili. Maneno yake yanasomeka ifuatavyo:
39. “Zwingli anaiita ‘alloiosis’ wakati kitu kinachosemwa kuhusu uungu wa Kristo ambacho kwa vyovyote ni cha ubinadamu, au kinyume chake kabisa. Kwa mfano, je, haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? (Lk. 24:26). Hapa Zwingli anafanya hila na kuibadilisha nafsi ya ubinadamu kuwa Kristo. 40. Jihadharini, jihadharini, ninasema kuhusu hii ‘alloiosis,’ kwamba, ni kinyago cha Ibilisi. Mwishowe, kitatunga aina ya kristo ambapo baadaye sitataka niitwe Mkristo. Hivyo, ni Kristo ambaye si zaidi ya mateso na kifo kuliko kuwa mtakatifu mwingine, lakini nikiamini kwamba, asili ya ubinadamu tu ndiyo iliyoteseka, kwa ajili yangu, basi, Kristo mwenyewe atahitaji Mwokozi. Kwa ufupi, inashangaza mno, anachojaribu kukifanya Ibilisi kwa ‘alloiosis.”2015 maiestaticum’ au (auchematicum) na ‘genus apotelesmaticum’ yalitokea baadaye. Kwa jumla, aina ya kwanza inazungumzia sifa za asili mbili kwa nafsi nzima. Kipengele cha pili hasa katika mabishano haya, kinahusu mwelekeo wa ukuu wa enzi ya kimungu kwa Kristo kulingana na asili yake ya ubinadamu. Aina ya tatu, inahusu wazo kwamba, katika utendaji wa kazi yake ya kuokoa, Kristo alitumia hali ya asili mojawapo au asili zote mbili kulingana na kazi inayozungumziwa.
2013 Kilatini: ‘In hoc genere.’
2014 Istilahi ya balagha: mabadiliko ya sehemu moja kuwa nyingine. 2015 WA, 26:319.
662
41. Na baadaye anaelezea: “Ikiwa mchawi mzee,2016 Bibi Asili, yule nyanya wa ‘alloiosis’ atasema kwamba, uungu kwa kweli hauwezi kuteseka na kufa, basi, ni lazima ujibu na kusema, hiyo ni kweli, lakini kwa kuwa uungu na ubinadamu ni nafsi moja katika Kristo, kuhusu uungu, Maandiko Matakatifu yanasema na kwa sababu ya muungano huo, yote yanayofanyika kwa mwanadamu, yanafanyika pia katika nafsi ya uungu. 42. Hili ni katika ukweli huo, kwani ni lazima useme kwamba, ukimwelekeza mtu kwa Kristo, huteseka hadi kufa. Lakini mtu huyu kweli ni Mungu, na kwa hiyo, ni vyema kusema, Mwana wa Mungu huteseka. Japo, kwa kuizungumzia sehemu moja, yaani, uungu, haiwezi kuteseka, lakini mtu huyu ambaye ni Mungu kweli anateseka katika sehemu nyingine, yaani, katika ubinadamu. Kwa kuwa, Mwana wa Mungu kweli alisulibishwa kwa ajili yetu, yaani, mtu huyu ambaye ni Mungu, ndivyo alivyo mtu huyu, ninasema anasulibishwa kulingana na ubinadamu. Ikiwa ‘alloiosis’ ya Zwingli inasimama, basi, Kristo lazima wawe watu wawili mmoja wa kimungu na mwingine wa kibinadamu. 43.Kwa kuwa Zwingli anatumia kauli zote juu ya mateso kuhusu asili ya ubinadamu peke yake na kuigeuzia kabisa asili ya kimungu. Lakini ikiwa kazi zimegawanywa na kutengwa, nafsi pia itatengana kwa kuwa matendo yote na mateso hayahesabiwi kwa asili, bali kwa nafsi. Basi, ni nafsi ambayo hufanya na huteseka kwa vitu vyote, kitu kimoja kulingana na asili hii na kingine kulingana na asili nyingine. Hayo yote wataalamu wanayafahamu vyema. Kwa hiyo, tunamstahi Bwana wetu Kristo kama Mungu na mwanadamu katika nafsi moja, bila kuchangamana na asili hizo wala kutengana na nafsi.”2017
44. Kadhalika, Dk. Luther anaelezea katika kitabu chake kiitwacho ‘Masinodi na Makanisa:’2018 “Sisi Wakristo lazima tujue kwamba, Mungu asipokuwa yuko katika mizani na atupe uzito kwa uzani sawa, tutazama mpaka chini pamoja na mizani yetu. Ninamaanisha hili, ikiwa si kweli kwamba, Mungu alitufia, bali mwanadamu ndiye aliyekufa tu, kweli tumepotea. Lakini ikiwa kifo cha Mungu na Mungu mfu hulalia upande mwingine wa mzani, basi, upande wake unaenda chini, nasi tunaenda juu kama mwanga na kikaango kitupu. Kwa kweli, anaweza pia kwenda juu au kuruka kutoka kwa kikaango chake. Lakini hangeweza kuketi ndani ya kikaango chake, isipokuwa amekuwa mwanadamu kama sisi, kiasi kwamba, liweze kunenwa: ‘Mungu mfu,’ ‘mateso ya Mungu,’ ‘damu ya Mungu,’ na ‘kifo cha Mungu.’ Kulingana na asili ya Mungu, hawezi kufa. Walakini kwa kuwa Mungu na mwanadamu wameungana katika nafsi moja, ni sawa
2016 Kijerumani: ‘Wettermacherin,’ yaani, mtendaji wa hali ya hewa.
2017 WA, 26: 321, 322. Rejea kanuni ya Sinodi ya Khalkedon ya mwaka wa 451 (Kilatini): ‘Non confudendo naturas nec dividendo personam.’
2018 ‘Von den Conciliis nd Kirchen’ mwaka wa 1539.
kukizungumzia kifo cha Mungu, wakati huyo mwanadamu anakufa ambaye ni kitu kimoja au nafsi moja na Mungu.”2019 45. Basi, hadi hapo, kutokana na hili, ni dhahiri kwamba, Luther ameeleweka vibaya kwamba kwa kusema au kuandika kwamba nahau zilizotajwa “Mungu aliteseka,” na “Mungu alikufa,” ni maneno matupu2020 tu ambayo hayalingani na ukweli. Kwani ukiri wetu wa Kikristo ulivyo wazi unatufundisha kwamba, Mwana wa Mungu ambaye alifanywa kuwa mwanadamu aliteseka kwa ajili yetu, akafa, na anatukomboa kwa damu yake.
46. Pili: Kristo anapoitunza huduma yake, nafsi yake haitendi ndani, pamoja, au kulingana na asili moja tu, bali katika, kulingana, pamoja na, kwa njia ya asili zote mbili, au jinsi Sinodi ya Khalkedon inavyotangaza kwamba,2021 kila asili hulingana na hali yake yenyewe na hufanya kazi kulingana na nyingine. 47. Hivyo, Kristo ni Mpatanishi wetu, Mkombozi, Mfalme, kuhani mkuu, kichwa, mchungaji, na kadhalika. Siyo kulingana na asili moja tu, wala ya uungu au ya ubinadamu, bali kulingana na asili zote mbili, kama tulivyotoa maelezo haya hapo awali.2022
48. Tatu: Suala lililo tofauti linaloshughulikiwa katika mjadala huu ni hili: Je, asili zote zilizounganishwa katika nafsi ya Kristo zina sifa zao za asili za kiini chao peke yake? Hapo juu tumefundisha kwamba, zinazo na sifa hizo zinadumu.
49. Kwa kuwa Mungu habadiliki (Yak. 1:17), hivyo hakuna kilichoongezewa au kilichotolewa kwa hali na miliki ya asili ya kimungu katika Kristo. Hapo, katika umwilisho,2023 asili ya kimungu halisi haikupunguzwa wala kuongezewa. 50. Jinsi ambavyo asili ya ubinadamu inayotwaliwa katika nafsi ya Kristo ilivyo, baadhi2024 walitaka kushindana kwamba, hata katika muungano wa binafsi na uungu, asili ya ubinadamu haina lolote. Wala zaidi kuliko sifa zake za asili muhimu na za pekee ambazo, katika kila hali, zimefanywa kuwa kama ndugu zake na kwamba, kwa hiyo, hakuna kitu chochote kinachoweza kuhesabiwa asili ya ubinadamu katika Kristo ambacho inashinda au linazuia sifa zake za asili ingawa ushuhuda wa Maandiko Matakatifu unaelekeza upande huo.
51. Lakini kwa msingi wa Neno la Mungu, ni dhahiri kabisa kwamba, wazo hili ni la kupotosha na la uongo. Hata washiriki wao wenyewe wanakataa na kulipinga kosa hili. Maandiko Matakatifu na akina baba wa zamani, kwa msingi
2019 WA, 50:590.
2020 Kilatni: ‘Praedicatio verbalis.’
2021 Hii si fasiri ya mkutano wa Khalkedon, bali kauli katika Tome na Leo ambayo ilithibitishwa na mkutano.
2022 Juu, III, 56.
2023 Yaani, kufanyika mwili. Kijerumani: ‘Menschwerdung;’ Kilatini: ‘Incarnatio.’ 2024 Wafuasi wa siri wa Calvin huko Wittenberg, katika andiko la ‘Grundfest’ la mwaka wa 1573.
664
wa Maandiko haya, wanashuhudia zaidi kwamba, kwa kuwa asili ya kibinadamu iliungana yenyewe na asili ya kimungu katika Kristo, na ilitukuzwa na kuinuliwa baada ya sura ya mtumishi na fedheha kuachwa, ilipokea na kuongezea kwa asili katika mkono wa kuume wa utukufu wa Mungu, hali, mali, uzuri, utukufu, ukubwa wake wa ajabu, usiochunguzika na usioelezeka, pamoja na haki ya mbinguni2025 na fadhila katika enzi, utukufu, nguvu na uwezo juu ya majina yote yanayotajwa siyo tu wakati huu, bali pia wakati ujao.2026 Basi, kwa kazi ya huduma ya Kristo, asili ya kibinadamu katika Kristo inatumika kadiri ya umbo lake pamoja na lingine, na ina nguvu2027 na manufaa yake, siyo tu kutokana na kulingana na hali na sifa, au jinsi ambavyo uwezo wake unavyopanuka tu, bali kwanza, kutokana na kulingana na enzi, utukufu, nguvu, na uwezo ambao asili ya ubinadamu imepokea kupitia kwa umoja wenyewe, utukufu na kuinuliwa. Hata maadui hawathubutu zaidi kulikataa hili. 52. Hata hivyo, wanabishana kwa juhudi kwamba, ni vipawa vipi ambavyo asili ya ubinadamu inaviweka na kuvipamba katika Kristo na vipawa vilivyoumbwa,2028 kama jinsi ilivyo kwa watakatifu. Kwa msingi wa hesabu na mabishano yao, na zaidi, wanapojaribu kuonyesha ushahidi wao na kuweka mipaka ya kile ambacho asili ya ubinadamu katika Kristo inaweza au lazima iwe na uwezo au isiwe na uwezo bila kuharibiwa.
53. Nja nzuri na iliyo salama kwa kweli kabisa katika mabishano haya ni kutambua kwamba, hakuna mtu yeyote anayeweza kujua zaidi na kwa ukamilifu zaidi kuliko Kristo Bwana mwenyewe yale ambayo yeye ameyapokea kwa njia ya muungano wa binafsi na kwa kutukuzwa na kuinuliwa. Anajua pia kwamba, asili yake ya ubinadamu iliyotwaliwa imepokea nini kushinda sifa za asili bila kupotea. Kwa neno lake, Kristo ametufunulia kadiri tunavyohitaji kujua katika maisha haya. Kwa kuwa, tumepokea shuhuda wazi na hakika, tunaamini bila shaka na bila kubishana kwa kusisitiza kwamba, asili ya ubinadamu katika Kristo haina uwezo huo.
54. Bila shaka, kauli hii ni halisi na ya kweli kwamba, asili ya kibinadamu ya Kristo ina vipawa vyote vilivyoumbwa ambavyo imepewa na kushiriki. Lakini vipawa hivi havikadirii enzi ambayo Maandiko Matakatifu na akina baba wa zamani, kwa msingi wa Maandiko, waliihesabia asili ya ubinadamu katika Kristo.
55. Kwa kutoa uzima, kutekeleza hukumu yote, kuwa na mamlaka yote mbinguni na duniani, kuwa na vitu vyote vilivyokabidhiwa mkononi mwake, 2025 Kilatini: ‘Praerogativae.’
2026 Efe. 1:2.
2027 Kilatini: ‘Efficacia.’
2028 Kilatini: ‘Finitae qualitates,’ yaani, sifa zenye mipaka.
kuwa na vitu vyote chini ya miguu yake, kusafisha dhambi na vinginevyo, si vipawa vilivyoumbwa, bali ni sifa za kimungu zisizokuwa na mwisho. Ingawa kulingana na maelezo ya Maandiko, Kristo mwanadamu amepatiwa na kuachiwa hali hizi, (Yn. 5:21, 27; 6:39, 40; Mt. 28:18; Dan. 7:14; Yn. 3:31, 35; 13:3; Mt. 11:27; Efe. 1:22; Ebr. 2:8; 1 Kor. 15:27; Yn. 1:3, 10).
56. Kuna hoja tatu ngumu zisizoweza kukanushwa ambazo huonyesha kwamba, mawasiliano haya siyo jambo la maneno,2029 tu bali lazima yaeleweke kuhusu nafsi, siyo kulingana na asili ya kimungu tu, bali pia kulingana na asili ya kibinadamu. Hizi ndizo hoja zifuatazo:
57. Kwanza, ni kanuni inayokubaliwa kwa ridhaa kuu na Kanisa la Zamani lote lenye imani ya kweli kwamba, lolote ambalo Maandiko Matakatifu yanashuhudia kwamba, alilopokea Kristo katika zama za ulimwengu, hakulipokea kulingana na asili yake ya kimungu. Kwa mujibu wa asili yake ya kimungu, alimiliki yote tangu milele na milele. Badala yake, nafsi ya Kristo ilipokea haya kulingana na asili ya ubinadamu aliyojichukulia.2030
58. Pili, Maandiko Matakatifu yanashuhudia dhahiri (Yn. 5:21, 27; 6:39, 40) kwamba, nguvu ya kufufua wafu na kutekeleza hukumu amepatiwa Kristo kwa sababu yeye ndiye Mwana wa Adamu mwenye mwili na damu.
59. Tatu, Maandiko Matakatifu hayasemi aghalabu tu kuhusu nafsi ya Mwana wa Adamu, bali yanaonyesha asili yake ya kibinadamu ya kawaida inayochukuliwa anavyosema: “Damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote” (1 Yoh. 1:7). Hilo halielezi tu kuhusu ustahili ambao ulikwisha kufanyika msalabani mara moja. Mahali hapo, Yohana anasema kwamba, sisi hatuhesabiwi kuwa wenye haki tu kwa ajili ya asili ya kimungu katika Kristo, bali damu yake ya kweli2031 yatusafisha dhambi zote. Kadhalika, Yn. 6:48-58 inasema kwamba, mwili wa Kristo ni chakula kitoacho uzima, na hivyo, Sinodi ya Efeso ilikiri kwamba, mwili wa Kristo una nguvu kutoa uzima. Shuhuda nyingine za kupendeza za Kanisa la Zamani lenye imani ya kweli kuhusu fungu hili zimeandikwa kwingineko. 2032
60. Inatubidi na ni lazima tuamini kwamba, Kristo aliyapokea haya yote kulingana na asili yake ya kibinadamu, na kwamba, yote yalitolewa na kuwasilishwa katika asili ya kibinadamu ambayo yalitwaliwa na Kristo kwa kuwa Maandiko Matakatifu yanafundisha hivyo. Lakini kama tulivyosema hapo
2029 Kilatini: ‘Non per phrasin aut modum loquendi.’ ‘Grundfest’ 121, 122, 127, 132.
2030 Kilatini: ‘Ratione et respectu humanae naturae.’
2031 Kilatini: ‘Per modum efficaciae.’ 2032 ‘Catalogus testimonium.’
juu, asili hizi zote katika Kristo zimeungana kiasi kwamba, hazipatani pamoja au nyingine haibadilishwi kuwa nyingine. Kila moja inadumisha hali na asili ya nafsi yake kwa njia ambayo sifa za asili moja haziwezi kuwa zile za asili nyingine kamwe. Mafundisho haya lazima yaelezewe vizuri na yatetewe kwa bidii dhidi ya mafundisho yote ya uasi.
61. Hapa, sisi hatubuni mafundisho yetu mapya, lakini tunakubali na kurudia maelezo ambayo Kanisa la Zamani lenye imani halisi liliyatoa kwa msingi wa fungu thabiti la Maandiko Matakatifu. Asili ya kibinadamu ya Kristo iliyotwaaliwa imepatiwa nguvu, maisha, mamlaka, enzi, na utukufu wa kimungu. Si halisi kuchanganya jambo hili pamoja na ukweli huu kwamba, tangu milele, Baba alimwasilishia Mwanawe kiini chake na sifa zake zote za kimungu, kiasi kwamba, kwa mujibu wa asili yake ya kimungu, Kristo ni asili moja na Baba, na ni sawasawa pia na Mungu. Kwa kuwa, kwa mujibu wa asili yake ya kimungu, Kristo ni sawa na Mungu, lakini kwa mujibu wa asili yake ya kibinadamu iliyotwaaliwa, yeye yu chini ya Mungu. Kutokana na hili, ni dhahiri kwamba, sisi hatuchanganyi wala hatusawazishi au hatuzitangui asili za Kristo.2033 Hivyo, uwezo wa kutoa maisha haumo katika mwili wa Kristo pia kama sifa yake ya asili jinsi ilivyo katika asili yake ya kimungu.
62. Mawasiliano haya au ugavi huu haumaanishi pia kwamba, sifa za asili ya kimungu zigawe kwa njia ya kawaida au ya kiini kwa asili ya kibinadamu ili ubinadamu wenyewe wa Kristo uzimiliki mbali na uungu. Asili ya Kristo haikuacha pia sifa zake za asili na ya kiini hata asili hii ya Kristo ama ibadilike kuwa kama uungu au kwa njia ya miliki hizi zilizowasilishwa na kufanyika kuwa halisi sawasawa na Mungu. Mafundisho haya hayamaanishi pia kwamba, sifa tendaji za asili na za kiini za asili hizi mbili zimekuwa hizo hizo au hata zinafanana. Mafundisho haya ya uzushi tayari yamekataliwa na kuhukumiwa katika sinodi za zamani zilizokubaliwa.2034 Hakuna njia yoyote ya kufundisha au kukubali kwamba, asili za Kristo au sifa zao za kiini zinaweza kubadilishwa au kuchanganywa au kutazamiwa kuwa sawa.
63. Istilahi hizi ‘mawasiliano halisi,’ na ‘kuwasiliana kwa kweli’2035 zisichanganywe kamwe na ‘mawasiliano ya maumbile’ au ‘upaji wa kiini’2036 ambamo asili tofauti zinachanganywa kuwa kiini kimoja chenye sifa zake kuu. Hivyo ndivyo walivyofanya baadhi ya wapinzani wetu wakorofi wenye hila kinyume cha dhamiri zao zenyewe ili kufanya mafundisho sahihi kuonekana kuwa
2033 Kilatini: ‘Confusio,’ ‘exaequatio,’ ‘abolitio.’
2034 Kwa mfano, mkutano wa pili wa Konstantinopoli, kanuni ya 7 dhidi ya Origeno.
2035 Kilatini: ‘Realis communicatio,’ ‘realiter communicari.’
2036 Kilatini: ‘Physica communicatio,’ ‘essentialis transfusio.’
667
ya uongo. Wameweka ‘mawasiliano ya maneno’2037 dhidi ya mafundisho haya yetu ya ‘mawasiliano halisi.’ Maana ya ‘mawasiliano ya maneno’ ni kirai au namna ya kusema tu, yaani, si zaidi ya neno tupu, kichwa,2038 au jina. Wamelisisitiza hili kwa nguvu sana kiasi kwamba, hawataki kujua kuhusu mawasiliano yoyote ya aina nyingine. Ili kuieleza enzi ya Kristo kwa njia halisi kabisa, tumezungumzia ‘mawasiliano halisi’ ili tuonyeshe hapo kwamba, mawasiliano ya aina hiyo yalifanyika kwa uhalisi na kwa kweli bila mchanganyiko wowote wa asili na sifa zao za kiini.
64. Kwa hiyo basi, tunashikilia na kufundisha pamoja na Kanisa la Zamani lenye imani halisi, jinsi fundisho hili lilivyoelezewa kuhusu msingi wa Maandiko Matakatifu kwamba, asili ya kibinadamu katika Kristo imepokea enzi hii kulingana na namna ya umoja wa binafsi.2039 Kwa kuwa, utimilifu wote wa Mungu unakaa katika Kristo,2040 kwa njia ya kimwili, jinsi ilivyo katika mwili wake wa binafsi lakini si jinsi ilivyo kwa wanadamu wengine watakatifu, Mungu, au kwa malaika. Ukamilifu huu hung’ara katika asili inayotwaliwa pamoja na enzi yake yote, nguvu, utukufu, na uwezo wake, kwa hiari yake, yaani wakati na mahali apendapo. Ndani, pamoja na kwa njia ya asili ya kibinadamu Kristo hubainisha, huonyesha, na hutumia nguvu yake ya kimungu, utukufu, na uwezo, jinsi nafsi inavyofanya katika mwili na moto katika chuma chekundu, mifano ambayo Kanisa la Zamani zima lilitumia kwa kuelezea fundisho hili kama jinsi tulivyoelezea hapo juu.2041 65. Wakati wa kufedheheshwa kwake, enzi yake ilisitiriwa na kuzuiliwa.2042 Lakini sasa, kwa sura ya utumwa, imekwisha kuwekwa kando, inafanyika kikamilifu kwa nguvu na wazi mbele ya watakatifu wote mbinguni na duniani. Katika maisha ya ulimwengu ujao, tutapata kuuona utukufu wake uso kwa uso (Yn. 17:24).
66. Hivyo basi, Kristo yu na hubakia kuwa na uenyezi wa kimungu peke yake, nguvu, enzi, na utukufu ambao ni sifa pekee ya asili ya kimungu. Asili hii inang’ara mbele na kujidhihirisha yenyewe kikamilifu, ijapokuwa kwa hiari, siku zote, ndani, pamoja, na kwa njia ya asili ya ubinadamu iliyoinuliwa. Jinsi ilivyo katika chuma chekundu, nuru na mwako si nguvu mbili - nguvu ya nuru na ya mwako hutokana na hali ya moto - lakini kwa kuwa moto umeungana na chuma, inaonyesha na kudhihirisha nguvu yake ya nuru na mwako ndani na kwa njia ya
2037 Kilatini: ‘Verbalis communicatio.’
2038 Kilatini: ‘Phrasis, modus loquendi.’
2039 Kilatini: ‘Unio hypostatica.’
2040 Kol. 2:9.
2041 Taz. juu, 8, 18.
2042 Andiko la Kilatini linaongezea maneno haya: ‘Maiori ex parte,’ ‘kwa sehemu kuu.’
668
chuma, kwa njia ambayo kwayo, na kwa njia ya umoja huu, chuma chekundu huwa na nguvu ya moto na mwako bila mabadiliko yoyote ya asili ya hali ya moto wala chuma.
67. Kwa hiyo, tunaelewa ushuhuda wa Maandiko Matakatifu unaozungumzia enzi ambayo asili ya ubinadamu wa Kristo imekwisha kuinuliwa. Enzi hii tukufu, ambayo ni hali ya asili ya uungu wa Mwana wa Mungu, inapaswa kuhesabiwa kuwa nafsi ya Mwana wa Adamu bila kulingana tu na asili yake ya uungu. Enzi hii haihesabiwi pia katika asili ya ubinadamu katika Kristo kwa hiyo tu kwamba, asili yake ya kibinadamu ishiriki katika cheo na jina kwa njia ya kirai au jinsi ya kusema2043 tu lakini katika tendo na ukweli haipaswi kuwa na ushirikiano wa kweli.
68. Mungu ndiye kiini cha kiroho kisichogawanyika. Kwa hiyo, yu popote katika viumbe vyote. Popote anapopatikana yu na enzi yake, hasa katika waaminio na watakatifu. Inaweza kusemwa kwa uhalisia na kwa ukweli kwamba, Mungu yu katika viumbe vyote, lakini hasa kwa waaminio ambao Mungu anaishi ndani yao. Vivyo hivyo, ukamilifu wa uungu unaishi humo kimwili, hazina yote ya hekima na elimu vimefichwa humo, na mamlaka yote mbinguni na duniani yametolewa2044 kwao kwa sababu Roho Mtakatifu ambaye ana uwezo wote, ametolewa kwao. 69. Kwa hiyo, hakuna tofauti inayoweza kuwekwa kati ya Kristo kulingana na asili yake ya kibinadamu na watakatifu wengine. Hivyo, Kristo atanyang’anywa utukufu wake, ambao ameupokea kama mwanadamu na kulingana na asili yake ya kibinadamu juu ya viumbe vyote. 70. Kwa sababu hakuna kiumbe chochote, awe mwanadamu au malaika, awezaye au apaswaye kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mt. 28:18). Kwa maana, ni kweli kwamba, Mungu pamoja na ukamilifu wa uungu wake wote, alio nao daima, anaishi katika waaminio. Lakini Mungu haishi katika waaminio wake kwa njia ya kimwili wala kwa njia ya kuunganishwa nao na kuwa nafsi moja jinsi ilivyo katika Kristo. Kwa sababu ya muungamo wa binafsi, katika asili yake ya kibinadamu Kristo anasema: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mt. 28:18). Vivyo hivyo, “Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake” (Yn. 13:3). Vivyo hivyo, “Katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Kol. 2:9). Vivyo hivyo, “Umemvika taji ya utukufu na heshima, umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake” ( Ebr. 2:7, 8), na “kwa kuwa, alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake” (1 Kor.15:27).
2043 Kilatini: ‘Per phrasin et modum loquendi.’ 2044 Kol. 2:9; Mt. 28:18.
71. Hatuamini, hatufundishi, na hatukiri kwa njia yoyote kumiminwa kwa enzi ya Mungu na sifa zake zote ndani ya asili ya ubinadamu wa Kristo kwa jinsi hiyo kwamba, asili ya kimungu imedhoofishwa au kutolewa kitu chake fulani bila kukitunza kwa ajili yake. Hatufundishi kwamba, asili ya kibinadamu, katika kiini na dhati yake, imepokea enzi iliyo sawa, iliyotengana, au iliyogawanywa kutoka kwa asili na dutu ya Mwana wa Mungu. Si jinsi maji, divai, au mafuta humwagwa kutoka katika chombo kimoja hadi kingine. Kwa kuwa asili ya ubinadamu, sawa na kiumbe chochote mbinguni au duniani, haina uwezo wa kuishika enzi ya Mungu, kiasi kwamba asili ya ubinadamu yenyewe iweze kuwa na enzi hii au sifa za enzi hii. Kwa njia ya kuyashikilia haya, asili ya ubinadamu wa Kristo itakanushwa na itabadilishwa kabisa kutoka kwa ile ya kimungu. Hili ni kinyume kabisa cha imani yetu ya Kikristo na mafundisho yote ya manabii na mitume.
72. Badala yake, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, Mungu Baba alimpa Kristo Mwana wake mpendwa Roho wake katika asili yake ya kibinadamu iliyotwaliwa - hapo anaitwa Masihi, au aliyewekwa wakfu2045lakini si kwa kipimo jinsi watakatifu wengine walivyovipokea vipawa vya kiroho. Kwa mujibu wa uungu wake, Kristo ndiye mwenye kiini hicho hicho kama Roho Mtakatifu. Kulingana na asili yake ya kibinadamu inayotwaliwa, “Roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza roho ya maarifa . . . ” anashuka juu ya Kristo Bwana.2046 73. Matokeo yake hayakuwa kwamba, kama mwanadamu, anafahamu na anaweza kufanya tu mambo fulani kwa njia ambayo watakatifu wengine wanaweza kuyafahamu na wanaweza kuyafanya kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye anawajaza tu vipawa vilivyoumbwa. Kwa mujibu wa uungu wake, yeye ndiye nafsi ya pili katika Utatu Mtakatifu na Roho Mtakatifu hutoka kwake, jinsi anavyotoka kwa Baba. Kwa hiyo, yeye anabakia kuwa katika umilele wote, katika Roho wake, na katika roho wa Baba mwenyewe, ambaye hatengani na Mwana kamwe. 74 Vivyo hivyo, ukamilifu wote wa Roho umetolewa kwa Kristo katika muungamo wa binafsi kupatana na mwili ambao umeungana wenyewe na Mwana wa Mungu, jinsi akina baba wa zamani wanavyosema.2047 Kwa hiari pamoja na nguvu yote, ukamilifu huu huthibitisha na hudhihirisha wenyewe ndani, pamoja, na kwa njia ya asili ya kibinadamu. Matokeo si kwamba, Kristo, kama mwanadamu angejua na angeweza kufanya mambo fulani tu bila ujuzi na uwezo kuhusu vitu vingine vyote bali, kwa kweli,
2045 Yn. 1:41; 4:25.
2046 Isa. 11:2; 61:1. 2047 Cyril wa Aleksandria “muunganiko wa uungu na ubinadamu wa Yesu Kristo (Hypostatic)” uliofafanuliwa na baraza la Chalcedon 451
ninafahamu yote kwamba, Kristo ni mwenye uwezo wa kutenda lolote. Baba alimmiminia Roho wake wa hekima na nguvu bila kipimo. Katika muungamo wa binafsi, kama mwanadamu mwenyewe kweli, amepokea ufahamu wote na nguvu zote. Kwa hiyo basi, hazina yote ya hekima imesitirika ndani yake, amepewa mamlaka yote, na ameinuliwa katika mkono wa kuume wa enzi na nguvu ya Mungu.2048
75. Katika vitabu vya historia inajulikana kwamba, wakati wa Kaisari Valens,2049 dhehebu maalumu lilipatikana miongoni mwa Waariano lililoitwa ‘Wajinga’2050 kwa sababu walifundisha kwamba, Mwana, Neno la Baba, anayafahamu mambo yote kwa kweli, lakini kwamba, kulingana na asili yake ya kibinadamu iliyotwaliwa, mambo mengi hayafahamiki kwake. Kwa ajili ya kupinga dhehebu hili, Gregorio Mkuu pia aliandika 2051 yafuatayo:
76. Kwa sababu ya muungano huu wa binafsi wa kweli wa asili ya kimungu na ya kibinadamu, katika nafsi ya Kristo na kwa ajili ya na mawasiliano yanayotokea kwao, sifa ambazo haziwezi kuuhusu mwili wake, kulingana na kiini chake cha asili mbali na muungamo huu, zinahesabiwa kwa Kristo, kwa mujibu wa mwili wake. Kwa kuwa mwili wake ndicho chakula cha kweli kitoacho uzima, nayo damu yake ndicho kinywaji cha kweli kitiacho uzima, jinsi akina baba mia mbili walivyoshuhudia katika Sinodi ya Efeso kwamba, mwili wa Kristo ni mwili utoao uzima.2052 Hivyo, kweli, ni mwanadamu huyu tu na hakuna mwanadamu mwingine mbinguni na duniani awezaye kusema, “. . . walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao” (Mt. 18:20), vivyo hivyo, “mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” (Mt. 28:20).
77. Hatuuelewi ushuhuda huu kwa kumaanisha uungu wa Kristo peke yake na kuwepo kwake katika Kanisa na Usharika wa Kikristo na kuwepo huko kwa Kristo, kwa vyovyote, hakuhusiki na kuwepo kwake kimwili. Iwapo ni kweli, Petro, Paulo, na watakatifu wote mbinguni pia wangekuwa pamoja nasi duniani kwa sababu Mungu ambaye yu popote, anakaa ndani yao. Maandiko Matakatifu yanaelezea kuwepo kwa Kristo kwa jinsi hiyo tu, na si kwa mwanadamu yeyote.
78. Badala yake, tunashikilia kwamba, maneno haya yaliyotajwa yanaelezea dhahiri jinsi ya enzi ya Kristo mwanadamu, ambayo Kristo aliipokea kama
2048 Kol. 2:3; Mt. 28:18; Ebr. 1:3.
2049 328-378; Kaisari tangu mwaka wa 364.
2050 Kiyunani: ‘Αγνωητοι;’ Kilatini: ‘Agnoetae.’
2051 Gregorio Mkuu, Ep. X 35, 39.
2052 Sinodi ya Efeso mwaka wa 431, kanuni ya 11, Kilatini: ‘Carnem Christi esse vivificam seu vivificatricem.’
mwanadamu katika mkono wa kulia wa enzi na nguvu ya Mungu. Kulingana na hii asili yake ya kibinadamu iliyotwaliwa, Kristo anaweza na yu popote apendapo, na hasa yu pamoja na Kanisa lake na usharika wake hapa duniani kama Mpatanishi, Kichwa, Mfalme, na Kuhani Mkuu, siyo kwa sehemu tu au nusu tu ya nafsi ya Kristo, lakini mtu mkamilifu ambaye ni asili zote, ya uungu na ya ubinadamu zilizotwaliwa. Kwa mujibu wa asili yake ya ubinadamu, yeye ndiye ndugu yetu na sisi nyama ya nyama yake na mifupa ya mifupa yake.2053
79. Ili kuwa na uhakika na matumaini maradufu ya ukweli huu, alikianzisha Chakula chake Kitakatifu ili aweze kuwa pamoja nasi, afanye makao yake ndani yetu, afanye kazi yake, na awe na nguvu juu yetu kulingana na asili hiyo ambayo humiliki mwili na damu.
80. Ambayo Dk. Luther mwenye kumbukumbu iliyobarikiwa, ameyaandika kuhusu enzi ya Kristo katika asili yake ya kibinadamu, yanasimama juu ya msingi huo thabiti.
81. Katika ‘Ukiri Mkuu kuhusu Chakula cha Kristo’2054 anayaandika yafuatayo kuhusu nafsi ya Kristo: “Kwa kuwa yeye ndiye mwanadamu wa jinsi hiyo na kwa kuwa hakuna Mungu bila mwanadamu huyu, ni lazima ifuatie kwamba, kulingana na jinsi ya tatu ipitayo akili,2055 yeye yu na anaweza kuwa popote alipo Mungu na kwamba, kwa njia ya, na kulingana na ubinadamu wake pia, vitu vyote vimejaa Kristo, si kulingana na uwezo wa kueleweka kwa njia ya kimwili, bali kulingana na jinsi ya kimungu ipitayo akili kabisa.
82. Hapa, huna budi kusimama na kusema kwamba, popote alipo Kristo kulingana na uungu wake, yeye yu katika nafsi ya asili na ya kimungu pia, jinsi kuchukuliwa mimba kwake katika tumbo la mama yake kunavyoithibitisha asili bila mashaka. Kama Mwana wa Mungu, ilimbidi kuwa katika tumbo la mama yake katika asili na nafsi ya kuwa mwanadamu. Akiwa katika asili na nafsi yake popote alipo, basi, lazima awepo kama mwanadamu pia, kwa kuwa hana nafsi mbili tofauti, bali nafsi moja tu. Popote nafsi hii ilipo, ni moja na haigawanyiki. Ukiweza kusema, “Huyu ni Mungu,” basi, ni lazima pia useme, “Kristo mwanadamu yupo pia.” Ukiweza kunionyesha shemu hata moja ambapo Mungu yupo na si mwanadamu, basi, tayari, nafsi imegawanyika na kweli, mara moja ningeweza kusema, “Ni Mungu ambaye si mwanadamu na hajawahi kuwa mwanadamu.” 83. Lakini simfahamu na simwabudu Mungu wa jinsi hiyo! Kwa kuwa kutokana na hili, itafuatia kwamba, nafasi na mahali patupu vingeweza 2053 Efe. 5:30 kulingana na ‘Vulgata’ na ‘Textus Receptus,’ yaani, andiko lililokubaliwa la Erasmus wa Rotterdam.
2054 ‘Grosse Bekenntnis vom Abendmahl Christi’ 1528.
2055 Taz. juu, 7, 98-102.
kutenganisha asili mbili, moja kutoka kwa nyingine na hivyo kuigawanya nafsi, ingawa kifo na Ibilisi vyote pamoja havikuwa na uwezo wa kutenganisha na kuvirarua vipande vipande. 84.Kwangu, atabakia kuwa Kristo aliye maskini ikiwa alikuwepo tu katika pahali pamoja kama nafsi ya kimungu na ya kibinadamu, na ikiwa pahali pengine pote patakuwa si kitu zaidi ya kuwa Mungu mtupu aliyetenganishwa na nafsi ya kimungu bila ubinadamu. La hasha! Rafiki, kwangu, kila unapomweka Mungu chini, ni lazima pia uuweke ubinadamu chini. Hatawaacha watenganishwe na wagawanywe mmoja na mwingine. Amekuwa nafsi moja na hautenganishi ubinadamu unaotwaliwa kutoka kwake kamwe.”2056
85. Katika kitabu chake kidogo kiitwacho,‘Maneno ya Mwisho ya Daudi,’ ambacho alikiandika punde tu kabla ya kifo chake, Dk. Luther anaelezea: “Kulingana na kuzaliwa kwake mara ya pili kama mwanadamu hapa duniani, pia alipatiwa uweza wa milele wa Mungu kwa njia ya dunia, si tangu milele. Kwa kuwa ubinadamu wa Kristo haujakuwepo kama uungu wake tangu milele, lakini kulingana na kalenda yetu, Yesu mwana wa Mariamu, ana umri wa miaka 1543 mwaka huu. Lakini kutoka wakati huo ni kwamba, uungu na ubinadamu viliungana katika mwanadamu huyu mmoja, mwana wa Mariamu, anayeitwa Mungu Mwenyezi wa milele, mwenye uweza wa milele na ameumba na kuhifadhi vitu vyote. Huu ndio ukweli kwa ajili ya mawasiliano ya sifa,2057 kwa sababu mwanadamu ndiye nafsi moja pamoja na uungu na ndiye Mungu wa kweli. Hilo ndilo analomaanisha anaposema, ‘Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu’ (Mt. 11:27), na ‘Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani’ (Mt. 28:18). Ni nini maana ya ‘mimi?’ Kwangu, Yesu wa Nazareti, ndiye mwanawe Mariamu, aliyezaliwa na mwanadamu. Tangu milele, nina mamlaka haya kutoka kwa Baba kabla sijawa mwanadamu, lakini nilipokuwa mwanadamu, niliyapokea kwa wakati, kulingana na ubinadamu na nikayaficha mpaka kufufuka kwangu na kupaa, wakati yalikusudiwa kufunuliwa na kuthibitishwa, jinsi Mt. Paulo anavyosema: ‘Amedhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu’ (Rum. 1:4), na Yohana analiita tendo hili ‘kutukuzwa’ (Yn. 7:39; 17:10).”2058
86. Kuna ushuhuda mwingi wa aina hii katika maandiko ya Dk. Luther, hasa katika kitabu chake kiitwacho, ‘Kwamba Maneno Haya Yangali Yanasimama Imara’ na katika kitabu chake kingine kiitwacho,‘Ukiri Mkuu Kuhusu Chakula cha Bwana.’ Kwa ufupi, hapa, inafaa tuvirejelee vitabu vilivyotajwa, ambavyo vinaelezea kinaganaga enzi na wosia wa Kristo. Ana enzi hii anapoketi katika mkono wa kuume wa Mungu. Jinsi tulivyotaja awali, haya yanahusu fungu la 2056 WA, 26: 332, 333.
2057 Kilatini: ‘communicatio idiomatum.’ 2058 WA, 54: 49, 50.
Chakula Kitakatifu pia.
87. Hivyo, tunalifikiria kuwa kosa chungu kumnyima Kristo enzi hii kulingana na ubinadamu wake. Kufanya hivyo ni kuwaibia Wakristo faraja yao kuu, waliyopatiwa katika ahadi waliyoitiwa ya kuwepo na kukaa ndani yake kama Kichwa chao, Mfalme, na Kuhani Mkuu ambaye aliahidi kuwa pamoja nao, si katika uungu wake usiofunuliwa tu, ambao kwetu maskini wenye dhambi ni kama moto uunguzao, ulio katika mashina ya majani makavu, bali kama mwanadamu aliyezungumza nao, ambaye ameonja taabu katika asili yake ya ubinadamu iliyotwaliwa, na ambaye kwayo, anaweza kutuhurumia kama wanadamu na ndugu zake. Pia, anataka kweli kuwa pamoja nasi katika masumbuko yetu yote kulingana na asili hiyo ambayo kwayo, yeye ni ndugu yetu nasi tu nyama ya nyama yake.2059
88. Kwa hiyo, tunakataa na kulaani kwa vinywa, mioyo, na kwa ridhaa kuu makosa yote ambayo hayalingani na mafundisho ambayo hapa, yamewekwa mbele kama kinyume cha maandiko ya manabii na mitume, ya Kiri za Imani Halisi, na ya Ukiri wa Augsburg wetu wa Kikristo:
1. Ikiwa mtu yeyote angeamini au kufundisha kwamba, kwa 89 sababu ya muungano wa binafsi, asili ya kibinadamu imechanganywa na asili ya kimungu au imebadilika kuwa hiyo nyingine.
2. Vivyo hivyo, kwamba, asili ya kibinadamu katika Kristo 90 inapatikana kila mahali kwa njia sawa na uungu, asili isiyokuwa na mwisho, kwa njia ya asili ya nguvu au sifa zake za asili.
3. Vivyo hivyo, kwamba, asili ya ubinadamu katika Kristo 91 imesawazishwa2060 naye na amekuwa sawa kwa asili ya kimungu kwa mujibu wa kiini, dhati, au sifa zake za kiini.
4. Vivyo hivyo, kwamba, ubinadamu wa Kristo umepanuliwa 92 kutoka mahali maalumu kila mahali mbinguni na duniani, jambo ambalo si vyema kuhesabiwa hata kwa Mungu. Katika enzi yake ya kimungu, Kristo anaweza kuwepo popote katika mwili wake ambao kwao, anaketi katika mkono wa kuume wa enzi na uweza wa Mungu, popote apendapo na hasa ambapo ameahidi kuwepo kwake katika Neno lake jinsi ilivyokuwa katika Chakula Kitakatifu.2061
5. Vivyo hivyo, kwamba, asili ya kibinadamu ya nafsi ya Kristo 93 peke yake
2059 Efe. 5:30 kulingana na ‘Vulgata’ na ‘Textus Receptus.’
2060 Kilatini: ‘Exaequare.’
2061 Tabaini zilizoorodheshwa katika vipengele 1-4 vya mashtaka ambayo Wanasakramenti waliyatoa dhidi ya Walutheri.
iliteseka kwa ajili yetu na akatukomboa bila ushirikiano wowote wa Mwana wa Mungu katika hali ya mateso.
6. Vivyo hivyo, kwamba, Neno linapohubiriwa, na matumizi 94 halisi ya Sakramenti Takatifu, Kristo yu pamoja nasi duniani kwa uungu wake tu, na kwamba, kuwepo kwake, kamwe hakuhusu asili yake ya ubinadamu iliyotwaliwa kwa njia nyingine.
7. Vivyo hivyo, kwamba, asili ya ubinadamu iliyotwaliwa katika 95 Kristo, haishiriki nguvu takatifu, uwezo, hekima, enzi, na utukufu kwa uhalisi na ukweli, bali ina jina tupu tu na jina la kawaida pamoja naye.
8. Tunakataa na kulaani mafundisho haya na mengineyo ya 96 uzushi yanayopinga na kuzuia mafundisho ya imani ambayo yalielezewa hapo juu kuwa kinyume cha Neno safi la Mungu, maandiko ya manabii watakatifu na mitume, pamoja na Imani na Ukiri wetu wa Kikristo. Maandiko Matakatifu humwita Kristo siri2062 ambayo kwayo, walimu wote wa uasi hupasua vichwa vyao. Kwa hiyo basi, tunawaonya Wakristo wote kutokupeleleza akili zao katika siri hii. Badala yake, tudumu pamoja na mitume wapendwa katika imani rahisi kwa njia ya kuyafumbua macho na akili zetu zenye kufungwa kwa kumtii Kristo kabisa. Faraja na furaha yetu ya daima ni kwamba, mwili na damu yetu vimeinuliwa tayari katika Kristo, kuketi juu zaidi katika mkono wa kuume wa enzi na uweza wote wa Mungu. Kwa hiyo basi, hakika, tutaweza kutafuta faraja ya kudumu katika mateso yote na tutalindwa vyema dhidi ya uzushi wenye kudhuru.
IX. KUSHUKA KUZIMUNI KWA KRISTO
1. Baadhi ya wanatheologia wetu, sawa na baadhi ya walimu wa zamani wa Kanisa la Kikristo, tayari wamelielezea fungu linalohusu kushuka kuzimuni kwa Kristo kwa njia tofauti. Hivyo basi, tunashikilia imani yetu sahili ya Kikristo kwa njia ambayo Dk. Martin Luther alituonyesha wazi katika mahubiri yake aliyoyatoa katika Ngome ya Torgau mwaka wa 1533:2063 “Ninaamini katika Kristo Bwana, Mwana wa Mungu, aliyekufa, akazikwa, na akashuka kuzimuni.” Ukiri wetu unatofautisha kati ya kuzikwa na kushuka kuzimuni kama mafungu tofauti. 2. Kwa imani yetu sahili tunakiri kwamba, nafsi nzima ya Kristo, yaani, Mungu na mwanadamu ilishuka kuzimuni baada ya kuzikwa kaburini, akamuangamiza Ibilisi, akaharibu nguvu ya kuzimuni, na akamnyang’anya Ibilisi uwezo wake wote.
2062 Kol. 1 :27.
2063 WA, 37:62-67. Nukuu hili linaonekana kuwa lilichukuliwa neno kwa neno kutoka kwa mahubiri ya Luther.
3. Sisi hatuwajibiki kujishughulisha sana kwa mawazo ya juu na tambuzi jinsi tendo hili lilivyotendeka, kwa sababu fungu hili haliwezi kueleweka kwa akili zetu na kwa milango yetu mitano ya fahamu. Fungu hili lililotangulia haliwezi kueleweka kirahisi kuliko lile linalofuatia, jinsi Kristo alivyofanywa kuketi katika mkono wa kuume wa Mungu Mwenye enzi yote. Tunapaswa kuamini na kushikilia neno hili tu. Hivyo basi, tutahifadhi kiini na faraja ya fungu hili kwamba, ama kuzimuni au Ibilisi hawezi kuwafunga au kumdhuru yeyote anayemwamini Kristo.
X. KAIDA ZA KANISA, ZINAZOITWA ADIAPHORA, YAANI, MAMBO AMBAYO SI LAZIMA KUYAJALI2064
1. Pamekuwepo na mabishano miongoni mwa baadhi ya wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg kuhusu kaida na mitindo ya Kanisa ambayo haikuamriwa wala haikukatazwa katika Neno la Mungu. Bali, mambo haya yameingizwa katika Kanisa kwa shabaha ya kuueneza utaratibu na ustawi2065 bora au kuuhifadhi uchaji wa Kikristo. 2. Upande mmoja2066 ulishikilia kwamba, hata wakati wa mateso na hali ya kukiri,2067 wakati maadui wa Injili hawakubaliani nasi kuhusu mafundisho ya imani. Mtu anaweza kuwa bado na dhamiri safi, kwa matakwa ya adui, kurejesha tena kaida zilizotangulia ambazo zenyewe ni mambo ambayo si lazima kuyajali, ambayo hayakuamriwa, hayakukatazwa na Mungu na kwamba, mtu anaweza kukubaliana na mambo haya ambayo si lazima kuyajali. 3. Hata hivyo, upande mwingine2068 umesisitiza kwamba, wakati wa mateso na wa majadiliano yanayohusu ukiri, hasa wapinzani wanapojaribu kuyagandamiza mafundisho safi katika Kanisa letu na kuingiza tena mafundisho yao ya uzushi kwa polepole, ama kwa nguvu na shurutisho, au kwa hila, mambo ambayo si lazima kuyajali2069 hayawezi kukubaliwa bila hasara kwa dhamiri na ukweli wa kimungu.
4. Kwa shabaha ya kuyatatua mabishano haya, na kuyasuluhisha kabisa kwa neema ya Mungu, tunayatoa maelezo yafuatayo kwa wasomaji Wakristo:
5. Wakati mambo yanaitwa ‘adiaphora’ kwa kisingizio cha kuwa mambo ya nje tu, tutaweza kutafuta msingi unaolipinga kabisa Neno la Mungu chini ya vipodozi hivi.2070 Mambo haya yasitazamiwe kama mambo ambayo si lazima
2064 Kijerumani: ‘Mitteldinge,’ (mambo ya kati); Kilatini: ‘res mediae et indifferentes.’
2065 Andiko la Kilatini linatumia neno la Kiyunani: ‘ευταξια.’
2066 Hasa Philipp Melanchthon, Yohana Bugenhagen, Georg Major na Caspar Cruciger.
2067 Kijerumani: ‘Fall der Bekenntnus,’ yaani, (Ukiri wa Imani) unapohitajika.
2068 Hasa Matthias Flacius, Yohana Wigand, Nikolao Gallus, ? Hesshusius, na Antonio Corvinus.
2069 Yaani, ‘adiaphora.’
2070 M. Flacius alimaanisha vipodozi vya makahaba.
676
kuyajali bali lazima yaepukwe kama yote yaliyokataliwa na Mungu. Hii ndiyo sababu, kaida ambazo hukusudia kuifanya dini yetu kuoneakana kama Upapa au kuufanya Upapa uonekane kuvumilika kwetu kwa shabaha ya kuyaepusha mateso, zisihesabiwe kuwa mambo ya dhati ambayo si lazima kuyajali. Shabaha ya kaida za namna hiyo ni kuzileta katika makubaliano dini zile zinazopingana kabisa ili zikue kama mwili mmoja nasi turudi tena ndani ya Upapa na moja kwa moja, kuacha mafundisho safi ya Injili na dini ya kweli.
6. Kuhusu jambo hili, lazima tuyasikilize mafundisho ya Mt. Paulo yasemayo: “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha.”2071
7. Maonyesho ya chale yasiyokuwa na faida ambayo hayasaidii kueneza utaratibu bora, nidhamu ya Kikristo, na uchaji wa Kiinjili katika Kanisa, kwa kweli ni mambo ambayo si lazima kuyajali kamwe.
8. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, mambo ambayo si lazima kuyajali kwa kweli, jinsi yalivyoelezewa hapo juu,2072 ni kaida ambazo hata sehemu zake si ibada zenyewe, bali lazima tutofautishwe nayo kikamilifu jinsi ilivyoandikwa, “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” (Mt. 15,9).
9. Hivyo basi, tunaamini, tunafundisha, na tunakiri kwamba, usharika wa Mungu, popote na wakati wote una haki, mamlaka, na nguvu kubadilisha, kupunguza, au kuongezea kaida kulingana na hali yake, ilimradi ufanyike kwa njia halisi, bila upuuzi na hatia, bali kwa utaratibu wenye kufaa. Kwakuwa wakati wowote unaweza kuonekana wenye faida zaidi, wenye manufaa na msaada kwa utaratibu mzuri, nidhamu bora ya Kikristo, uchaji wa Kiinjili, na kulijenga kanisa. Paulo anatufundisha jinsi tunavyoweza kukubali, kwa dhamiri nzuri, na kujitoa katika imani katika mambo ambayo si lazima kuyajali kwa walio dhaifu (Rum. 14) na kulionyesha hilo wazi kwa mfano wake mwenyewe (Mdo. 16:3; 21:26; 1 Kor. 9:l0).
10. Tunaamini, tunafundisha, na tunakiri zaidi kwamba, wakati tunakiri, wakati maadui wa Neno la Mungu wanakuwa na nia ya kuyagandamiza mafundisho
2071 2 Kor. 6:14,17.
2072 Matthias Flacius: mikarara, masomo, saa, na mahali pa ibada, hali ya mtu anayeshiriki, mavazi na upigwaji wa kengele. Miongoni mwa mambo ya kibinafsi, aliongezea kufunga, saa maalumu za sala, kujiepusha kwa muda, kukaribiana kati ya mke na mume, au kutokula vitu vitamu, mtu kupunguza wingi wa chakula alichozoea kula kwa sababu ya sala au mazoezi ya kiroho n.k.
677
sahihi ya Injili takatifu, jamii nzima ya Mungu, yaani, kila Mkristo na zaidi, wahudumu wa Neno kama viongozi2073 wa jamii ya Mungu, wanalazimika kukiri wazi kwamba, si kwa maneno tu bali pia kwa matendo yao, kwa mafundisho ya kweli, na lolote linaloambatana nayo, kulingana na Neno la Mungu. Katika hali ya jinsi hiyo, tusikubaliane na wapizani wetu hata katika mambo ambayo si lazima kuyajali, wala kuvumilia uingizaji wa ibada za jinsi hiyo za wapinzani wetu, kwa madhumuni ya kudhoofisha ibada halisi za kumwabudu Mungu na pia kuanzisha na kuthibitisha kwa nguvu na kwa hila ibada zao za miungu mingine. 11. Imeandikwa: “Katika ungwana huo Kristo alituhesabu huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa” ( Gal. 5:1). Na tena: “Bali kwa ajili ya ndugu za uongo walioingizwa kwa siri; ambao waliingia kwa siri ili kuupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Kristo Yesu, ili watutie utumwani, ambao hata saa moja hatukujitia chini yao, ili kwamba kweli ya Injili ikae pamoja nanyi (Gal. 2:4, 5). 12. Hapa, Paulo anazungumzia tohara ambayo kwa wakati huo, ilikuwa jambo ambalo halikuwa lazima kulijali (Gal. 2:3; 1 Kor. 7:18, l9) na ambayo aliitumia kwingine katika uhuru wake wa Kikristo (Mdo. 16:3). Lakini wakati mitume wa uongo walidai tohara na kuitumia vibaya kwa shabaha ya kuyathibitisha mafundisho ya uongo kuwa kazi za sheria zinahitajika kwa haki na wokovu, Paulo alisema kwamba, hangekubali kamwe hata kidogo ili ukweli wa Injili uhifadhiwe (Gal. 5:2).
13. Hivyo, kwa ajili ya walio dhaifu, Paulo alikubali mambo yanayohusiana na chakula, majira, na siku (Rum. 14:6). Lakini hakukubaliana kamwe na mambo ambayo si lazima kuyajali na mitume wa uongo waliotaka kuingiza mambo haya ili kuziwajibisha dhamiri za watu kana kwamba, yalihitajika kuwa ya lazima: “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato” (Kol. 2:16). Wakati Petro na Barnaba walipokuwa katika hali hiyo, walikubali kiasi kwamba, Paulo aliwakosoa hadharani kwa sababu hawakuwa wazi kuhusu ukweli wa Injili ( Gal. 2:14).
14. Hapa, hatujishughulishi zaidi na mambo ya nje ambayo si lazima kuyajali ambayo, kwa mujibu wa asili na kiini, yanabaki kuwa huru na pia hayana sheria inayotulazimisha kuyatumia au kutoyatumia. Tunajishughulisha hapa na fungu kuu la imani yetu ya Kikristo, jinsi mtume anavyoshuhudia: ukweli wa Injili uhifadhiwe (Gal. 2:5). Lolote linalopotosha au linalotia giza katika fungu hili, kwa njia ya shurutisho na sheria, kwa sababu maadui watajitokeza na kudai mambo
2073 Kijerumani, ‘Vorsteher,’ lililotafsiriwa katika Kilatini kwa maneno haya: ‘ii quos Dominus ecclesiae suae regendae praefecit.’
haya ambayo si lazima kuyajali, kwa shabaha ya kuyathibitisha mafundisho ya uongo, ya uganga, ya ibada ya miungu mingine, ya kuyagandamiza mafundisho sahihi, na uhuru wa Kikristo, au watayatumia vibaya na kuyatafsiri vinginevyo.
15. Wakati huo huo pia, jambo hili linahusu fungu la uhuru wa Kikristo. Fungu ambalo Roho Mtakatifu, kwa njia ya kinywa cha mtume, kwa uzito aliagiza lihifadhiwe katika Kanisa, jinsi tulivyosikia hapo juu. Mara tu baada ya fungu hili kudhoofishwa na sheria za kibinadamu kuingizwa kwa nguvu katika Kanisa kana kwamba, kutojali kwa sheria hizi au dhambi, wakati huo mlango utafunguliwa kwa ibada za miungu mingine na mwishowe, sheria za kibinadamu zitaongezeka. Kwa hiyo basi, kuyafuata maagizo ya wanadamu kutachukuliwa kuwa ibada ya Mungu, kwa njia ya ufuasi wa Amri za Mungu.
16. Hivyo basi, kukubali kushindwa katika mambo ya nje, hata kabla ya makubaliano sahihi kuhusu mafundisho ya kweli ya Kikristo, kunaimarisha tu ibada za miungu mingine. Kwa upande mwingine, kutahuzunisha na kukashifu waaminio wa kweli, hata kudhoofika katika imani zao. Kila Mkristo na aepuke matokeo haya mawili kwa ajili ya wokovu na heri yake ya milele, jinsi ilivyoandikwa: “Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!” na tena, “bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.”2074
17. Inatubidi tuyatafakari maneno ya Kristo hasa: “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni” (Mt. 10:32).
18. Ushuhuda ufuatao umedondolewa kutoka kwa Mafungu ya Smalkaldi, yaliyoandikwa na kukubaliwa mwaka wa 1537 na wa 1540, na yanayoonyesha wazi kwamba, haya yamekuwa mafundisho sahihi na yalisadikishwa kabisa na kwamba, ni ukiri wa walimu wakuu wa Ukiri wa Augsburg kuhusu mambo haya ambayo si lazima kuyajali. Ndiyo sababu, kwa neema ya kustahimili katika ukiri wao tunanuia, na tunatembea katika nyayo zao.
19. Mafungu ya Smalkaldi ya mwaka wa 1537, yanatuambia yafuatayo kuhusu hili (‘Kanisa’): “Sisi hatukubali kamwe kwamba, wao (maaskofu wafuasi wa Upapa) ni Kanisa, wakati sivyo. Wala hatutasikiliza yale waamuruyo au wayakatazayo kwa jina la Kanisa. Tunamshukuru Mungu, mtoto wa umri wa miaka saba anajua Kanisa ni nini: ni waaminio watakatifu na “kondoo
2074 Mt. 18:6,7.
wanaoisikia sauti ya mchungaji wao.”2075
Kabla ya hilo: “Maaskofu wangetaka kuwa maaskofu wa kweli, kutunza Kanisa na Injili vizuri, tungeweza kukubali kwa ajili ya upendo na umoja. Hata hivyo, jambo hili si lazima kwamba, wangebariki na kuwasimika wahubiri wetu kwa sharti kwamba, watayafanya haya bila unafiki na majivuno yasiyokuwa ya Kikristo. Hta hivyo, sasa wao si maaskofu wa kweli na hawapendi kuwa maaskofu wa jinsi hiyo bali wao ni malodi na watawala wa dunia. Hawahubiri, hawafundishi, hawabatizi, hawatunzi Chakula cha Bwana, au hawafanyi kazi au huduma yoyote katika Kanisa. Kinyume chake, wanawatesa na kuwahukumu ambao wameitwa kufanya huduma za jinsi hiyo. Lakini Kanisa halipaswi kuachwa bila wahudumu kwa ajili ya maaskofu.”2076
20. Katika fungu kuhusu Ukuu au Mamlaka ya Papa, Mafungu ya Smalkaldi yanasema: “Jinsi ilivyo, hatuwezi kumwabudu Ibilisi mwenyewe kama bwana na mungu wetu. Hivyo, hatuwezi kumvumilia mtume wake, Papa, ama Mpinga Kristo na utawala wake kama kichwa au bwana. Kwa maana, utawala wake ni uongo, uuaji, na uangamizaji wa milele wa mwili na roho.” 2077
21. Makala Kuhusu Mamlaka na Ukuu wa Papa yanayojumlisha sehemu ya kiambatisho cha Mafungu ya Smalkaldi, ambayo wanatheologia wote waliokusanyika huko Smalkaldi waliyaweka sahihi kwa mikono yao, tunapata kauli ifuatayo: Mtu yeyote asijichukulie ubwana au mamlaka ya Kanisa, wala asililemee Kanisa kwa mzigo wa mapokeo, wala mamlaka ya yeyote yasionekane kuliko Neno la Mungu.2078 Punde tu baada ya hayo: 22. Kwa hivyo, hiyo ndiyo hali. Wakristo wote ni sharti wajihadhari, wasishiriki mafundisho ya uongo, kufuru, na ukatili wa Papa usiokuwa wa haki. Hawana budi kumwacha na kumlaani Papa na wafuasi wake kama ufalme wa Mpinga Kristo jinsi alivyoamuru Kristo: “Jihadharini na manabii wa uongo.” 2079 Paulo pia aliamuru kwamba, walimu wasiokuwa wachaji inapaswa waepukwe na wachukiwe kama waliolaaniwa.2080 Isitoshe, katika 2 Kor. 6:14 anasema pia: “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini,2081 kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi?
2075 ‘Mafungu ya Smalkaldi’ III, 12. 2076 ‘Mafungu ya Smalkaldi’ III, 10. 2077 ‘Mafunngu ya Smalkaldi’ II, 4, l4.
2078 ‘Makala Kuhusu Mamlaka na Ukuu wa Papa’ 11.39. 2079 Mt. 7:15. Taz. pia Ukiri wa Augsburg, Fungu la 28, 22-28. 2080 Tit. 3:10.
2081 Kulingana na Andiko la Kijerumani lililofuatia ‘Vulgata.’ Andiko la Kilatini: ‘Ne sitis consortes infidelium’ (Msiandamane na wasioamini).
680
23 Kutokubali muafaka wa nchi nyingi, na kuitwa watu wa mafarakano ni jambo lililo zito. Lakini mamlaka ya kimungu inawaamuru watu wote wasijihusishe na wasiunge mkono kufuru na ukatili usiokuwa wa haki.” 2082
24. Katika tamko lake maalumu, Dk. Martin Luther aliandika kuhusu kaida kwa jumla na hasa kuhusu mambo ambayo si lazima kuyajali katika Kanisa la Mungu.2083 Alitoa tamko hili tena katika mwaka wa 1530.2084
25. Kutokana na maelezo haya, kila mmoja anaweza kujifunza usharika wa Kikristo ni nini, Mkristo binafsi, na hasa wahubiri wanaweza kuifanya au kutokuifanya wakiwa na dhamiri safi kuhusu mambo ambayo si lazima kuyajali, hasa wakati wa ukiri, ili wasiichokoze hasira ya Mungu, wakiuke upendo wa Mungu, na wathibitishe maadui wa Neno la Mungu na kuwakashifu walio wanyonge katika imani.
1. Kwa hiyo, tunakataa na kulaani tena wazo lisilokuwa halali 26 kwamba, agizo la mwanadamu lizingatiwe kama ibada ya kumwabudu Mungu au sehemu yake.
2. Pia, tunakataa na kulaani kama dhuluma, agizo la jinsi hiyo 27 likiingizwa katika usharika wa Mungu kwa nguvu kana kwamba, ni la lazima.
3. Tunakataa na kulaani, tena kama dhuluma wazo la 28 wanaoshikilia kwamba, wakati wa mateso, tunaweza kukubali kushindwa na maadui wa Injili takatifu, au tunaweza kukubaliana nao kuhusu mambo mabayo si lazima kuyajali, kwa kuwa utekelezaji wa namna hii unauhatarisha ukweli.
4. Kadhalika, tunaichukulia kama dhambi inayostahili adhabu 29 iwapo, wakati wa mateso, lolote litafanyika kuhusu mambo ambayo si lazima kuyajali au si mafundisho ya Kanisa au kwa vyovyote, si mambo ya dini, ili kuwafurahisha maadui wa Injili kwa namna nyingine kabisa kinyume cha Ukiri wa Kikristo.
5. Pia tunakataa na kulaani utaratibu kwamba, mambo ambayo si 30 lazima kuyajali yanatangulizwa, kana kwamba, usharika wa Mungu hauna uhuru wa kutumia ama moja au mengi zaidi wakati wowote na mahali popote, kulingana na hali ya mambo na manufaa kwa Kanisa.
6. Kulingana na haya basi, yaliyoelezewa hapo juu, makanisa 31 yasilaumiane kwa sababu ya tofauti za kaida, wakati ambapo Kanisa fulani linazitumia nyingi
2082 Makala 41, 42.
2083 Ripoti kwa rafiki yake kuhusu aina zote mbili katika Ekaristi (1528), WA, 26: 560-618.
2084 Toleo la Jena Tom. 3, fol. 523, Tom. 5. Wa 32, 268-356. Barua zilizoandikwa na Luther kupelekwa Augsburg kati ya Juni na Septemba, mwaka wa 1530, katika WA, Briefwechsel, Juzuu la 5.
au chache zaidi katika uhuru wake wa Kikristo ilimradi makanisa yanakubaliana katika mafundisho na katika mafungu yake na pia katika matumizi halisi ya Sakramenti Takatifu, kulingana na kauli inayojulikana vizuri: “Kutokubaliana kuhusu kufunga hakupaswi kuharibu makubaliano kuhusu imani.” 2085
XI. MAJALIWA YA MILELE NA UCHAGUZI WA MUNGU
1. Bado hapajakuwepo mabishano mapana ya hadharani na kuleta kashfa kati ya wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg kuhusu Uchaguzi wa milele wa watoto wa Mungu. Hata hivyo, mahali pengine, tayari fungu hili limejadiliwa vikali na miongoni mwetu pia, mabishano yameanza kusikika.2086 Hata wanatheologia hawaitumii lugha dhahiri. Kwa hiyo, kwa neema ya Mungu, katika fungu hili tunapaswa kuzuia mapema tuwezavyo kutengana na kufarakana katika kizazi kijacho. Tumekusudia kuyaweka wazi maelezo ya fungu hili katika andiko hili ili watu waelewe tufundishayo, tuyaaminiyo, na tunayoyakiri katika fungu hili. 2. Mafundisho ya fungu hili yakitunzwa kulingana na Neno la Mungu na mifano itolewayo, basi, hayataweza kuchukuliwa kama yasiyokuwa na faida au yasiyokuwa na maana, au yenye madhara na hasara fulani, kwa sababu Maandiko Matakatifu hayalitaji fungu hili mara moja tu kwa mpito. Badala yake, Maandiko Matakatifu huyazungumzia kikamilifu maeneo mengi. 3. Kwa hiyo, mtu asikwepe wala asipuuze mafundisho ya Neno la Mungu kwa sababu watu wengine hulitumia na kulielewa visivyo. Kinyume chake, ili tuweze kuzuia matumizi mabaya na kulielewa visivyo, tunapaswa kuweka maana sahihi kuhusu msingi wa Maandiko Matakatifu. Yaliyomo ya mafundisho haya yajumlishwe kama ifuatavyo:
4. Kwanza kabisa, lazima tufahamu tofauti kati ya ufahamu wa mbele2087 wa milele wa Mungu na uchaguzi wa milele wa wana wa Mungu kwa wokovu wa milele. Kwa maana daima, Mungu huona na hujua kila kitu kabla hakijatokea. Ufahamu wa mbele wa Mungu unahusu viumbe vyote, vizuri na viovu. Mwanzoni, Mungu anajua na kuona yote yalivyo na yatakavyokuwa, yote yatokeayo au yatakayotokea, mema na maovu, kwa kuwa vitu vyote vilivyoko au vya baadaye huonekana wazi kwa Mungu jinsi ilivyoandikwa: “Je! mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua
2085 Kilatini: “Dissonantia ieiunii non dissolvit consonantiam fidei.” Irenaeo dhidi ya Askofu Victor wa Roma, kulingana na Eusebio, ‘Historia ya Kanisa,’ V, 24, 13.
2086 Rejea shambulizi la Tilemann Heshusius dhidi ya Jean Calvin na Theodoro Beza, mabishano kati ya Walutheri na Wakalvini huko Strasbourg kabla ya mwaka wa 1563, na majadiliano makali ya suala hili katika mkoa wa chini ya Sachsen.
2087 Kijerumani: ‘Vorshenung;’ Kilatini: ‘Praescientia,’ ‘praevisio.’
682
Baba yenu” (Mt.10:29). Kadhalika, “Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; kitabuni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado” (Zab.139:16). Na pia, “Lakini najua, kuketi kwako, na kutoka kwako, na kuingia kwako; na ghadhabu yako uliyonighadhibikia” (Isa. 37:28).
5. Majaliwa ya milele ya Mungu2088 yanamaanisha kwamba, Mungu anaamuru wokovu kwa mwanadamu. Majaliwa haya hayahusu wakati huo huo waliomcha Mungu au waovu, bali watoto wa Mungu ambao wamechaguliwa na kupewa uzima wa milele, “kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” jinsi Mt. Paulo asemavyo, “Kama vile alivyotuchagua katika yeye . . . alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo” (Efe.1:4, 5).
6. Ufahamu wa awali wa Mungu (praescientia) huona na hujua maovu kabla, lakini si kwa njia ya jinsi hiyo kana kwamba, yalikuwa matakwa ya Mungu kwamba, yangepaswa kutokea. Kwa hakika, yeye hujua na huona kabla nia na makusudi mabaya ya Ibilisi na jinsi watu watakavyojaribu kufanya na kutekeleza. Lakini hata katika matendo na kazi potovu, ufahamu wa Mungu hufanya kazi kiasi kwamba, Mungu huweka mipaka na vipimo kwa uovu ambao haupendi – jinsi utatenda, muda gani vitastahimili, lini na kwa namna gani ataingilia na kuadhibu. Kwa maana, Mungu anatawala kila kitu mpaka kimerudisha utukufu wa jina lake na wokovu kwa wateule wake, na kwa wasiomcha Mungu wanafedheheka
7. Ufahamu huu wa Mungu si chanzo au sababu ya uovu, kwa kuwa Mungu hakuumba wala hakuuathiri, hakuusaidia, na hakuueneza uovu. Makusudi mapotovu na mabaya ni matokeo ya nia ya Ibilisi na watu iliyopotoka jinsi ilivyoandikwa: “Haya ndiyo maangamizo yake, Ee Israeli, ya kuwa wewe u kinyume changu mimi, kinyume cha msaada wako” (Hos. 13:9). Kadhalika, “Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya” (Zab. 5:4).
8. Hata hivyo, majaliwa ya milele ya Mungu, hayamaanishi tu kwamba, Mungu anaona na kujua mbele wokovu wa wateule. Badala yake, majaliwa haya ndiyo sababu ya wokovu wetu. Mapenzi ya Mungu na fadhila yake yenye huruma katika Kristo Yesu, vinaumba na kuathiri yote, vinasaidia na kueneza yote yaliyoambatana na wokovu wetu. Kwa majaliwa haya ya milele wokovu wetu umewekewa msingi hapa kwa maana kwamba, hata “milango ya kuzimu” haiwezi kuishinda (Mt. 16:18), jinsi ilivyoandikwa, “. . . wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu” (Yn.10:28), na pia, “. . . nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini” (Mdo. 13:48).
9. Majaliwa haya ya milele yasitazamiwe kwa mujibu wa mpango wa siri 2088 Kilatini: ‘Praedestinatio.’
wa kimungu na ushauri usioweza kuchunguzika kana kwamba, hakuna lolote au la ziada linaloingizwa, au hakuna la zaidi la kuhusiana nalo, au kwamba, hakuna lolote zaidi linaloweza kufikiriwa kuhusiana nalo licha ya haya kwamba, Mungu ameona mbele ni akina nani na ni wangapi watakaokolewa, na ni akina nani watakaotupwa. Tusifikirie kwamba, kama amiri jeshi, Mungu atapiga gwaride: “Huyu lazima aokolewe, yule lazima atupwe, huyu atastahimili, yule hatastahimili!”
10. Maoni haya yanazaa na kuunda mawazo mageni hatari na mapotovu kwa watu wengi, ambayo ama yanazaa na kuongeza usalama wa uongo na ufidhuli au yanazaa na kuongeza wasiwasi na kukata tamaa. Matokeo yake ni kwamba, watu hujisumbua kwa sababu ya fikra na mashaka haya na kusema: “Kama vile (Mungu) alivyotuchagua katika yeye ‘kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu . . .’ (Efe.1:4) na kwa kuwa ufahamu wa mapema wa Mungu hauwezi kushindwa na hakuna awezaye kuubatilisha au kuuzuia (Isa. 14:27; Rum. 9:19,11). Kwa hiyo, kama nimetambuliwa mapema kwa ajili ya wokovu, haitaniumiza iwapo nitaishi maisha ya aibu ya dhambi mbalimbali na bila toba, madharau ya Neno la Mungu na Sakramenti, na bila kujali Neno, imani, sala, na uchaji. Kinyume chake, nitaokolewa kwa maana ufahamu wa Mungu lazima utendeke. Lakini kama sikutambuliwa, kila kitu ni ubatili mtupu, ingawa nitadumu katika Neno, nitatubu, nitaamini na kadhalika. Kwa maana siwezi kuzuia au kutangua utambuzi wa mbele wa Mungu.”
11. Mawazo kama hayo yanaweza kutokea kwa mioyo ya waliomcha Mungu pia, ingawa kwa neema ya Mungu wana toba, imani, na maamuzi mema kuishi maisha ya uchaji. Hasa wanapoona udhaifu na mfano wa jinsi hiyo kadiri wasivyoweza kuvumilia lakini wakaanguka tena, wanaweza kufikiri: “Kama hukutambuliwa kabla ya kuurithi wokovu na uzima, kila kitu ni ubatili.” Wazo kama hili linaweza kuzaliwa hasa wakati mwanadamu anatambua udhaifu wake mwenyewe na kuona kwamba, wengine hawakudumu mpaka mwisho. Badala yake, wameiacha tena imani.
12. Lazima tupinge mawazo na fikira za uongo kuhusu msingi ulio wazi, usiokuwa na mashaka, na usioshindwa kama ifuatavyo: Maandiko yote yaliyovuviwa na Mungu lazima yaongoze siyo kwa usalama bandia au wa hali ya kutotubu, bali “kwa kuwaonya, kuwaongoza, na kuwafundisha” (2 Tim. 3:16). Licha ya hayo, kila kitu katika Neno la Mungu kimeandikwa kwa ajili yetu, siyo ili lituongoze kukata tamaa, bali: “. . . ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini” (Rum.15:4). Kutokana na hili, ni wazi kwamba, mafundisho kuhusu ufahamu wa milele wa Mungu hayawezi ama kuelewa au kutumiwa kwa
njia halisi ikiwa mafundisho haya yanazaa hali ya kutotubu au ya kukata tamaa. Pengine, Maandiko Matakatifu pia hayaongozi mafundisho haya isipokuwa yanatuelekeza moja kwa moja kwa Neno (Efe. 1:13,14; 1 Kor. 1:21, 30, 31), kutufanya tutubu (2 Tim. 3:16), kutufanya tuwe watakatifu (Efe. 1:15 n.k.; Yn. 15:16,17, 3, 4, 10, 12), kuimarisha imani yetu na kutuhakikishia wokovu wetu (Efe. 1:9, 13, 14; Yn. 10:27-30, 2 The. 2:13-15).
13. Kwa hiyo basi, tukitaka kufikiri au kusema kwa njia iliyo sahihi na iliyozaa matunda mema kuhusu Uchaguzi wa milele au kuchaguliwa tangu asili na kuagizwa kwa watoto wa Mungu kwa uzima wa milele au kuhusu haki ya uzima wa milele, itatubidi kuepuka kuutafakari ufahamu wa Mungu ulio mtupu, uliofichwa kwa siri, na usiotambulika. Badala yake, inatupasa kuchunguza ushauri, shabaha, na mipango ya Mungu katika Kristo Yesu, ambaye kwa kweli ndiye ‘Kitabu cha Uzima’ aliyefunuliwa kwetu kwa Neno.2089 14. Hii inamaanisha kwamba, daima, lazima tuchukue kama sehemu moja ya mafundisho yote kuhusu shabaha, ushauri, mapenzi, na mipango juu ya wokovu, wito, na kuhesabiwa haki kwetu, jinsi Paulo asemavyo na kuelezea aya hii (Rum. 8:28 n.k.; Efe. 1:4 n.k.), pia jinsi Kristo alivyofanya katika mfano (Mt. 20:2-14) kwamba, Mungu, katika shabaha na maonyo yake, ameyaamuru yafuatayo:
1. Uwanadamu umekombolewa na kupatanishwa kweli na 15 Mungu wakati Kristo kwa utiifu, mateso, na kifo chake alitustahilia bila hatia “ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (Rum. 1:17; 2 Kor. 5:21) na tupate uzima wa milele.
2. Stahili na vipawa vya Kristo vinatolewa, vinatolewa, na 16 vinagawanywa kwetu kwa njia ya Neno lake na sakramenti zake.
3. Mungu na Roho Mtakatifu wake wanataka kutenda kazi ndani 17 yetu, kwa nguvu, kwa njia ya Neno linapohubiriwa, linaposikilizwa, na linapotafakariwa. Ataweza kuiongoa mioyo iwe na toba ya kweli, na ataitaalamisha katika imani ya kweli.
4. Mapenzi yake ni kuwafanya wote wawe na haki na neema, 18 kukubali kuwapokea watoto wake na warithi wa uzima wa milele ambao, baada ya kutubu kwa kweli, humpokea Kristo kwa imani ya kweli.
5. Anataka pia kuwatakasa kwa upendo wote waliokuwa 19 wamehesabiwa haki, jinsi Paulo asemavyo katika (Efe. 1:4).
6. Anataka kuwalinda katika hali yao ya udhaifu mkuu dhidi ya 20 Ibilisi, 2089 Flp. 4:3; Ufu. 3:5; 20:15.
dunia, na mwili. Anawaelekeza na kuwaongoza katika njia yake, kuwainua tena wanapoanguka, kuwafariji, kuwatunza chini ya msalaba, na katika majaribu.
7. Anataka kuimarisha na kuongeza kazi njema aliyoianza kwao 21 na kuwalinda mpaka mwisho, iwapo watadumu katika Neno la Mungu, wataomba kwa makini, watavumilia kwa neema ya Mungu, na watavitumia vipawa walivyovipokea kwa uaminifu.
8. Mwisho, anataka kuwapatia uzima, heri, na utukufu wa 22 milele aliowateua, aliowaita na aliowahesabia haki.
23. Kwa mashauri haya ya milele, shabaha, na mpango wa Mungu, si kwamba, ameandaa wokovu kwa ujumla. Badala yake, amefikiria pia na kuchagua, kwa ajili ya wokovu wa mtu binafsi, kati ya wateule ambao wataokolewa kwa njia ya Kristo kwa neema. Amewaamuru kwamba, kwa hali ambayo imeelezewa jinsi apendavyo kwa neema, karama, na matendo yake ya maana, atawaletea wokovu, atawasaidia, atawatunza, na atawatia nguvu.
24. Kulingana na Maandiko Matakatifu, haya yote yameunganishwa katika mafundisho ya Majaliwa ya Mungu ya milele ya kuwafanya wanadamu wawe watoto wake wenye wokovu na heri2090 ya milele. Mambo haya yanapaswa kufahamika kama yaliyounganishwa ndani na yasitolewe au yasiachwe kamwe tunapozungumzia shabaha, ufahamu wa mapema, chaguo, na mpango wa Mungu kwa wokovu wa milele. Tukiyafuata Maandiko Matakatifu na kuyarekebisha mawazo yetu kulingana na fungu hili, tutaweza kujielekeza ndani yake kwa neema ya Mungu.
25. Jibu kwa swali lifuatalo ni muhimu kwa maelezo na matumizi sahihi ya mafundisho kuhusu ufahamu wa mapema wa Mungu kwa wokovu. Kwa kuwa ni wateule tu, “wale . . . ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima”2091 wataokolewa. Mtu atawezaje kufahamu jinsi na wakati wa kuokolewa, na nani au ni wapi mtu ataweza kutambua, au ni wateule wepi watapaswa na wataweza kujifariji kwa fundisho hili? Hatupaswi kutoa hukumu kwa msingi wa mawazo yetu, au kwa msingi wa sheria, au kwa msingi wa vitu vya nje. Wala tusijiruhusu kujaribu kuvumbua siri na shimo la ufahamu wa mapema wa Mungu uliofichika. Badala yake, tuyasikilize mapenzi ya Mungu ambayo ameyafunua na “ametujulisha siri ya mapenzi yake” na ameileta kwa Kristo ili iweze kuhubiriwa (Efe. 1:9, 10; 2 Tim. 1:9-11).
2090 Kijerumani: ‘Seligkeit’ ni zaidi ya wokovu tu. Istilahi hii inamaanisha hali ya mwisho baada ya kuokolewa kutoka dhambini, mautini, na kutoka kwa Ibilisi. Hii ndiyo sababu, katika Kiswahili, istilahi ‘heri’ imeongezewa.
2091 Flp. 4:3; Ufu. 20:15.
27. Hili limefunuliwa kwetu, jinsi Paulo asemavyo: “Maana wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki” (Rum. 8:29, 30). Sasa, Mungu haiti tu mara moja bila vyombo, badala yake, yeye huita kwa Neno, jinsi alivyoamuru mahubiri ya toba, na msamaha wa dhambi.2092 Paulo anashuhudia jambo hilo hilo anaposema: “Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; . . . mpatanishwe na Mungu” (2 Kor. 5:20). Sawa na wageni ambao mfalme aliwakaribisha katika arusi ya mwanawe, Mungu huwaita kwa njia ya wajumbe, ambao huwatuma wengine mwanzoni, wengine saa mbili, saa tatu, saa sita, saa tisa na hata saa kumi na moja (Mt. 20:1-16; 22:2-14).
28. Basi, tukitaka kutafakari kwa njia ya manufaa kuhusu Majaliwa yetu ya milele kwa wokovu, kwa vyovyote, hatuna budi kabisa kushika kwa ushupavu na uthabiti ukweli kwamba, jinsi mahubiri ya toba huenea kwa watu wote (Lk. 24:47), kadhalika ahadi ya Injili itaenea. Hivyo basi, Kristo alituamuru tuhubiri “toba na msamaha wa dhambi katika jina lake kati ya mataifa yote.” “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee” (Yn. 3:16). Kristo amezichukua dhambi za ulimwengu (Yn. 1:29), ameutoa mwili wake “kwa ajili ya uzima wa ulimwengu” (Yn 6:51); damu yake ni kipatanisho . . . kwa dhambi za ulimwengu wote” (1 Yoh. 1:7; 2:2). Kristo anasema: “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mt. 11:28). “Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote” (Rum. 11:32). “. . . maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba” (2 Pet. 3:9). “. . . maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao” (Rum. 10:12). “Haki “ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio” (Rum. 3:22). “Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele . . .” (Yn. 6:40). Amri ya Kristo ni kwamba, wote pamoja ambao kwao, toba imehubiriwa lazima wawe na ahadi ya Injili iliyohubiriwa kwao (Lk. 24:47; Mk. 16:15).
29. Tusiuchukulie wito huu wa Mungu ambao hufanyika kwa njia ya mahubiri ya Neno kuwa kama udanganyifu Badala yake, tujue wazi kwamba, Mungu ameyafunua mapenzi yake kwa njia hii. Ambao amewaita anataka waangaziwe kwa Neno, waongoke, na waokolewe.
Kwa maana mahubiri ya Neno ambayo kwayo, tumeitwa, “ni huduma ya Roho” (2 Kor. 3:8), ambayo hutoa Roho na “uwezo wa Mungu uuletao
2092 Lk. 24:47.
wokovu” (Rum. 1:16). 2093 Kwa kuwa, Roho Mtakatifu anataka kuwa na uwezo, kutuimarisha, kutupatia nguvu, na ufahamu kwa njia ya Neno, ni mapenzi ya Mungu kwetu kwamba tunapaswa kulipokea Neno, tunaliamini na kulifuata.
30. Hivyo, wateule wanaelezwa ifuatavyo: “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele.” (Yn. 10:27, 28). Wale waliofanywa urithi, ‘kulingana na shabaha ya Mungu,’ huisikia
Injili, humwamini Kristo, huomba, na kutoa shukrani. Isitoshe, wanatakaswa kwa upendo, wana matumaini, uvumilivu, na faraja chini ya msalaba (Efe. 1:11, 13; Rum. 8:25). Ingawa bado ni dhaifu, hata hivyo, wana njaa na kiu ya haki (Mt. 5:6).
31. Hivyo basi, Roho wa Mungu hutushuhudia tulio wateule kwamba, sisi ndio watoto wa Mungu na tunapokosa kufahamu jinsi ya kuomba ipasavyo, Roho mwenyewe hutuombea “kwa kuugua kusikoweza kutamkwa (Rum. 8:16-26).
32. Kwa hiyo, Roho Mtakatifu pia hutuhakikishia kwamba, Mungu aliyetuita atakuwa mwema baada ya “kazi nzuri aliyoianzisha kwetu,” ataiendeleza pia mpaka mwisho na kuikamilisha, ikiwa sisi wenyewe hatutamwacha, bali “tutakuwa imara mpaka mwisho wa maisha yaliyokwisha kuanza” ndani yetu. Katika hali hiyo, ameiahidi neema yake (1 Kor. 1:8; Flp. 1:6 n.k.; 2 Pet. 3:9; Ebr. 3:14).
33. Inatubidi kuyatafakari mapenzi haya ya Mungu yaliyofunuliwa, tuyafuate, na tuwe waangalifu kwayo kwa sababu Roho Mtakatifu hutupatia neema, nguvu, na uwezo kwa Neno ambalo kwalo, alituita. Hatupaswi kuvumbua shimo la ufahamu wa Mungu uliofichika. Kadhalika, jinsi Kristo alivyojibu swali, “Bwana, watu wanaookolewa ni wachache?” kwa kusema, “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba” (Lk. 13:23, 24). Luther pia anasema hivyo hivyo: “Ufuate utaratibu katika Waraka wa Warumi. Jihusishe na Kristo na Injili yake ili ujifunze kuzitambua dhambi zako na neema yake. Kisha, pigana vita dhidi ya dhambi jinsi Paulo afundishavyo kutoka fungu la kwanza hadi la nane. Baadaye, katika fungu la nane, unajaribiwa chini ya msalaba na mateso, katika fungu la tisa, la kumi, na la kumi na moja unajaribiwa jinsi ufahamu wa kabla wa Mungu ulivyo wenye faraja, na kadhalika.2094
34. Sababu ya kuwa “waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache wamechaguliwa”2095 si kwamba, ipo katika wito wake uliofanyika katika Neno.
2093 ‘Ukiri wa Augsburg’ 5.
2094 Dibaji kwa Waraka kwa Warumi, EA, 63:135. 2095 Mt. 20 :16; 22 :14.)
Mungu alikusudia kusema: “kwa kweli ninawaita wote kabisa kwa Neno, niwapao Neno langu katika ufalme wangu, lakini ndani ya moyo wangu simaanishi wote, bali wachache tu. Ingawa ni kusudi langu kuwaita wengi miongoni mwa niwaitao kwa Neno, hawapaswi kuangaziwa au kuongoka. Badala yake, wawe na wabaki chini ya laana ingawa nilisema tofauti katika wito wangu kwao.” 35. Mafundisho ya jinsi hiyo yanamaanisha kwamba, Mungu ambaye ni ukweli wa milele anajipinga mwenyewe.2096 Mungu mwenyewe bado anawaadhibu watu kwa makosa yao wasemapo jambo fulani, wafikiriapo, na wakusudiapo jambo lingine tofauti mioyoni mwao (Zab.5:10,11; 12:3,4). 36. Kweli, hili litaharibu na kushusha msingi muhimu na unaofariji, ambao kila siku hutukumbusha na kutuonya tujifunze na tuzingatie mapenzi ya Mungu yatuthibitishayo na kutuahidi hasa kutoka kwa Neno lake ambalo kwalo, anashughulika nasi na hutuita kiasi kwamba, tunapaswa kuliamini kwa uhakika kabisa na hivyo kutokuwa na mashaka.
37. Kwa hiyo, Kristo pamoja na mahubiri ya ahadi za Injili kwa ujumla, aliunganisha Sakramenti kama muhuri wa ahadi na ambazo hushuhudia kila muumini binafsi.
38. Kwa hiyo basi, kama Ukiri wa Augsburg unavyoelezea katika fungu la kumi na moja, tunahifadhi ondoleo la dhambi la binafsi na kufundisha kwa amri ya Mungu kwamba, “tunaamini ondoleo la dhambi na kwa ujasiri, tunadumu kwamba, wakati tunaamini Neno la ondoleo la dhambi, tunakuwa tumepatanishwa pamoja na Mungu kweli kana kwamba, tumesikia sauti kutoka mbinguni,” jinsi fungu kuhusu Utetezi lielezeavyo.2097 Tutapoteza kabisa faraja hii iwapo hatutaweza kushikilia mapenzi ya Mungu katika wito wake ambayo hutujia sisi kwa Neno na kwa sakramenti.
39. Msingi huu wa imani yetu ungegeuzwa pia, yaani kwamba, Roho Mtakatifu anapenda kuwepo kabisa pamoja na Neno linapohubiriwa, linaposikilizwa, na linapokaririwa na anataka kutuathiri kwalo kwa nguvu. Kadhalika, jinsi tulivyotoa maoni hapo awali ni kwamba, wataweza kuwa wateule ambao hulidharau, hulipuuza, hulikufuru, na kulitesa Neno (Mt. 22:5; Mdo. 13:40 n.k, 46),2098 au ambao huifanya mioyo yao migumu (Ebr. 4:2, 7), humkatalia Roho Mtakatifu (Mdo. 7:51), hudumu dhambini bila toba (Lk. 14:18, 24), wasioamini kweli katika Kristo (Mk.16:16), wafanyao tu uongo ulio wazi (Mt. 7:15; 22:12), au watafutao njia nyingine za kuhesabiwa haki na wokovu nje ya Kristo (Rum. 2096 Kilatini: ‘Hoc enim esset Deo contradictorias voluntates affingere.’
2097 Tafsiri ya Kijerumani ya ‘Utetezi wa Ukiri wa Augsburg,’ XI, 2, ilifupishwa kidogo na kukubaliwa.
2098 Ya mwanzo inahusu Mdo. 15 kimakosa.
41. Kwa maana, wachache ndio wanaolikubali na kulitii Neno, wengi hulikataa, hulidharau na hukataa kuja arusini.2100
Sababu ya kulikataa Neno hakutokani na ufahamu wa Mungu. Badala yake, kunatokana na matakwa ya mwanadamu ya ukaidi, ambayo hukataa na kuasi njia na chombo cha Roho Mtakatifu ambacho Mungu hutoa kwake kwa njia ya wito na kumkatalia Roho Mtakatifu apendaye kuwa wa manufaa na mtendaji kwa njia ya Neno jinsi Kristo alivyosema: “Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja . . . lakini hamkutaka ?” (Mt. 23:37).
42. Wakati huo huo, wengi “hulipokea lile neno kwa furaha” lakini baada ya muda mfupi “hujitenga” (Lk. 8:13). Lakini sababu yake si kwamba, Mungu hapendi kugawa neema ya uvumilivu kwa ambao mioyoni mwao“alianza kazi njema.” Hili linapingana kabisa na Mt. Paulo katika Flp. 1:6. Sababu yake ni kwamba, hugeuka na kuacha agizo takatifu, humhuzunisha, na humkasirisha Roho Mtakatifu makusudi, na hushiriki tena uchafu mbaya wa dunia, na hupamba mioyo yao kuwa hema ya Ibilisi. Hivyo tamaa yao ya awali itakuwa mbaya zaidi ya mwanzoni (2 Pet. 2:10; Lk. 11:24, 25; Ebr. 10:26; Efe. 5:3-11, 18).
43. Mpaka hapa, Mungu ametufunulia siri ya kujua mambo kabla katika Neno lake. Sisi tukidumu na kulishika, kwa kweli ni mafundisho mazuri yanayofaa kutufariji na kutuletea wokovu. Mafundisho haya yanaliimarisha fungu ambalo kwalo, tunahesabiwa haki na kuokolewa bila matendo au stahili zetu wenyewe bali kwa neema kabisa, kwa ajili ya Kristo pekee yake. Kabla ya wakati wowote wa dunia hii, kabla ya kupatikana kwetu na “kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Efe. 1:4). Kabla hatujaweza kutenda tendo lolote zuri, Mungu alituteua kwa wokovu wake kadiri ya “makusudi yake” kwa neema katika Kristo (Rum. 9:11; 2 Tim.1:9). 44. Basi, mafundisho haya, hayatapinga kabisa maoni yote ya uzushi na mafundisho mapotovu kuhusu uwezo wa mapenzi yetu
2099 Mt. 20:16; 22:14. 2100 Mt. 22:5; Lk. 14:18-20.
690 9:31). 40. Kinyume chake, jinsi Mungu asemavyo katika maelekezo yake ni kwamba, Roho Mtakatifu ataweza kuita, kuangaza, kuongoa wateule kwa njia ya Neno, na kwamba, atawahesabia haki na kuwaokoa wamkubalio Kristo kwa imani ya kweli. Amekata pia shauri lake kwamba, atawafanya wagumu, atawakataa na kulaani wote ambao wanapoitwa kwa Neno, hulitupilia mbali na kumkatalia kabisa Roho Mtakatifu ambaye angependa kufanya kazi ndani yao kwa bidii, kwa njia ya Neno. Hii ndiyo maana ya, “Waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.”2099
ya asili.2101 Kwa maana, mashauri yake Mungu yamekusudia na yameamuru kabla ya ulimwengu kwamba, ataumba na kubadilisha kila kitu kwetu ambacho kinahusu kuongoka kwetu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwa njia ya Neno lake.
45. Mafundisho haya pia huiwezesha faraja bora na ya kufurahisha sana ya kwamba, Mungu anahusika sana na uongofu wa kila Mkristo, haki, na wokovu wake. Kwa uaminifu, alikumbuka “hata kabla ya msingi wa ulimwengu kuwekwa,” alishikilia mashauri, na aliyafanya “kwa kadiri ya makusudi yake yeye”2102 jinsi ya kunileta ndani na kunitunza humo. 46. Licha ya hayo, Mungu alitaka kunihakikishia wokovu wangu ili upate kuwa wa hakika na imara kwa sababu udhaifu na uovu wa mwili wetu ungeweza kuponyoka kutoka mikononi mwetu. Kutokana na uongo na ukatili wa Ibilisi na dunia, unaweza kusongwa na kuchukuliwa kutoka mikononi mwetu. Kwa hiyo, kwa ufahamu wake wa mapema, aliukabidhi wokovu ambao hauwezi kushindwa au kuondolewa mikononi mwa Yesu Kristo, Mwokozi wetu, ambaye kwake, hakuna awezaye kutupokonya (Yn. 10:28). 47. Kadhalika, Paulo anasema kwamba, kwa kuwa tumeitwa kulingana na kusudi la Mungu, “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo?” (Rum. 8:35).
48. Kadhalika, mafundisho haya yatatupatia faraja tukufu wakati wa msalaba na majaribu. Kwa maana, katika shauri lake kabla ya msingi wa ulimwengu, Mungu alikusudia na kutamka kuwa atatusaidia katika mahitaji yetu yote, atatupatia busara, faraja, atatuumbia tumaini, na kutuandalia mwisho ambao utaweza kutuokoa. 49. Hali kadhalika, Paulo anatuletea faraja kuu anapoelezea kwamba, kabla ya ulimwengu kuwepo, Mungu aliahidi katika mashauri yake ambayo kwayo, msalaba maalumu na mateso vitamtia moyo kila mteule kwa ‘sura ya Mwana wake,’ na kwamba, kwa kila njia, mateso yanapaswa na ni lazima ‘kutenda mema kwa pamoja’ kwa sababu “yalikuja kwa mujibu wa mapenzi yake.” Katika hili, Paulo anatoa jumlisho lisilokuwa na mashaka kwamba, “shida, au adha, au njaa, . . . wala mauti, wala uzima, na kadhalika, wala kiumbe kinginecho hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu” (Rum. 8:28, 29, 35, 38, 39).
50. Pia fungu hili hutupatia ushuhuda mtukufu kwamba, Kanisa la Mungu litadumu na kuendelea kuwepo dhidi ya “milango ya kuzimu” (Mt. 16:18). Wakati huo huo, hutufundisha kuhusu Kanisa la kweli lilivyo, ingawa tunapingwa na majivuno ya nje ya kanisa la uongo (Rum. 9:8 n.k.).
51. Isitoshe, fungu hili lina maonyo na mashauri makuu. Miongoni 2101 Taz. juu, ‘Tamko Thabiti,’ II, 7, 90. 2102 Efe. 1:4; 2 Tim. 1:9.
mwa hayo ni: “walilipinga shauri la Mungu dhidi yao wenyewe” (Lk. 7:30). “maana ninawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeonja karamu yangu” (Lk. 14:24); vilevile, “kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache” (Mt. 22:14); vilevile, “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie” (Lk. 8:8). “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo” (Lk. 8:18). Hivyo, katika fungu hili, inawezekana kuyatumia mafundisho kwa njia nzuri ya manufaa na ya faraja.
52. Lakini inatubidi kubainisha kwa makini tofauti kati ya ambayo Mungu aliyafunua katika Neno lake na ambayo hakuyafunua. Mbali na mambo ambayo yamefunuliwa katika Yesu Kristo na ambayo tumeyazungumzia mpaka sasa, kuna mambo mengi katika siri hii ambayo Mungu amebaki kimya kwayo, na ambayo hakuyafunua lakini ameyatunza tu kwa sababu ya hekima na ufahamu wake. Hatupaswi kuyachunguza, wala hatupaswi kuyafuata mawazo yetu katika suala hili na kutoa hitimisho la mawazo yetu, bali tunapaswa kushikamana kabisa na Neno lililofunuliwa.
53. Onyo hili ni muhimu kabisa. Katika mawazo yetu, tunaangalia zaidi njia zetu wenyewe pamoja na mambo ambayo hatuwezi kuyalinganisha kwa kweli. Hatuna ruhusa kufanya hivyo mbali na mawazo hayo ya suala ambalo Mungu amelifunua kwetu katika Neno lake.
54. Hivyo, hakuna mashaka kwamba, kabla ya wakati wa ulimwengu huu, Mungu alifahamu sawasawa kabisa na kusema kwa hakika kabisa, na mpaka sasa anaendelea kufahamu kuwa kati ya walioitwa, kuna watakaoamini na wasioamini. Vile vile, anajua ni nani kati ya waongofu watakaovumilia na ambao hawatavumilia. Ambao, baada ya anguko watarudi na ni nani, ambao wameanguka kabisa katika hali ya ugumu wa moyo. 55. Mungu anajua pia wangapi watakuwa katika pande hizo mbili. Lakini Mungu anayaweka haya kuwa siri ya hekima yake bila kutufunulia lolote katika Neno. Bado, ametuamuru kuichunguza kwa njia ya hisia zetu, lakini ametuonya kabisa (Rum. 11,33). Hivyo basi, kwa msingi wa hisia, hatupaswi kupunguza lolote, kutoa hitimisho, au maoni juu yake, bali tunapaswa kudumu katika Neno lililofunuliwa na tuliloelekezwa kwalo.
56. Bila shaka, Mungu anajua na amekusudia kwa kila mtu saa na wakati wa wito na kuongoka kwake. Lakini kwa kuwa hakulifunua hili kwetu, lazima tukubali amri yake na kutenda sawasawa ndani ya Neno, wakati tunaacha mambo ya muda na saa kwa Mungu (Mdo. 1:7).
57. Kadhalika, tunapoona kwamba, Mungu amelitoa Neno lake kwa upande mmoja na kwamba, si mwingine, analiondoa kutoka upande mmoja
lakini analiacha libaki katika upande mwingine au kwamba, mtu huwa na moyo mgumu, kipofu, na hutolewa kwa mawazo mapotovu ambapo mwingine, aliye katika hali iyo hiyo ya kuwa mkosaji, huokolewa tena. 58. Kwa maswali haya na mengine ya jinsi hii, Paulo anaweka mpaka jinsi tunavyoweza kuenenda: katila upande mmoja, tunapaswa kuona hukumu ya Mungu (Rum. 9:14 n.k.; 11:22 n.k.). Kweli, ni adhabu ya dhambi inayostahilika wakati Mungu ataadhibu nchi au watu fulani kwa sababu ya kulidharau Neno lake. Adhabu hiyo inaendelezwa vile vile katika vizazi vyao, sawasawa na Wayahudi. Hivyo basi, katika historia ya baadhi ya mataifa na baadhi ya watu, Mungu katika ukali wake anaonyesha watu wake yale ambayo sisi sote tunastahili kuyapata na kutunukiwa kwa sababu ya kukosa dhidi ya Neno la Mungu na mara nyingi kumkasirisha Roho Matakatifu. Hili litatufanya tuishi katika woga wa Mungu, tutambue, tutukuze wema wa Mungu bila kutegemea bila na kinyume cha stahili zetu, kwa ambao huwapatia na hulitunza Neno lake, ambao hawafanyi mioyo yao kuwa migumu na kulikataa.
60. Kwa kuwa, asili yetu yenye hatia, ilipotoshwa na dhambi na kustahili hasira ya Mungu na laana yake ya milele, Mungu hawajibiki kutupatia Neno lake, Roho wake, wala neema yake. Kusema kweli, anapotupatia hivi kwa huruma yake, tunavitupilia mbali na kujifanya kwamba, hatustahili uzima na milele (Mdo. 13:46). Hii ndiyo sababu, Mungu anaturuhusu kuangalia haki yake na hukumu iliyostahiliwa katika nchi, mataifa, na watu fulani binafsi ili tunapojilinganisha nao, tujikute kwamba, tunastahili hukumu hiyo hiyo, ili tujifunze hasa kutambua na kutukuza kwa bidii, neema ya Mungu isiyostahilika kabisa kwa ‘vyombo vya huruma.’2103
61. Hivyo basi, hakuna dhuluma iliyotendwa kwa ambao wanaadhibiwa na ‘kuupokea mshahara wao wa dhambi.’ Kuhusu watu wengine ambao Mungu huwapatia na hulitunza Neno lake, humo, huwapa mwangaza, huwaongoa, na kuwatunza. Mungu huamuru utakatifu wake, neema, na huruma zisizostahilika.
62. Katika fungu hili, tukiendelea mpaka hapa, tu katika njia bora jinsi ilivyoandikwa: “Haya ndiyo maangamizo yako, Ee Israeli, ya kuwa wewe u kinyume changu mimi, kinyume cha msaada wako” (Hos. 13:9). 63. Lakini iwapo katika mazungumzo kuhusu suala hili, jambo litaonekana kuzidi au kuvuka mipaka, tutaweka vidole vyetu vinywani kama Paulo na kusema, “Wewe u nani umjibuye Mungu.”2104
64. Mtume mkuu Paulo anashuhudia kwamba, hatuwezi wala hatutaweza kuchunguza na kulielezea fungu hili kinaganaga. Baada ya maelezo marefu
2103 Rum. 9:23; 11:5. 2104 Rum. 9:20.
ya fungu hili, kulingana na Neno la ufunuo wa Mungu, anakoma na kukata mazungumzo haya mara anapofikia kuonyesha kuhusu sehemu ambayo Mungu aliificha kwa hekima yake kwa maneno yafuatayo: “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana . . . ”2105 yaani, nje na mbele kushinda ambayo Mungu ametufunulia kwa Neno lake.
65. Hivyo, Majaliwa ya milele lazima yatazamiwe ‘katika Kristo,’ na si nje au mbali na Kristo. Kwa kuwa kulingana na ushuhuda wa Mt. Paulo, tumeteuliwa katika Kristo “kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Efe. 1:4); pia jinsi ilivyoandikwa, Ametuneemesha katika huyo Mpendwa (Efe. 1:6). Uteuzi huu umefunuliwa mbinguni kwa njia ya Neno lililolohubiriwa wakati Baba alisema: “Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe,” (Lk. 3:22). Na Kristo anasema: “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mt. 11:28). Na kuhusu Roho Mtakatifu, Kristo anasema: “Atanitukuza mimi” (Yn.16:14), na atawakumbusha kila kitu ambacho niliwaambia. 66. Hivyo, Utatu Mtakatifu wote, Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, huwaelekeza watu wote kwa Kristo. Yeye ndiye Kitabu cha Uzima ambamo wanapaswa kutafuta chaguo la milele la Baba. Kwa kuwa, kutoka milele, Baba ameamua kwamba, yeyote atakayemwokoa atamwokoa kwa njia ya Kristo, jinsi Kristo mwenyewe asemavyo: “Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi” (Yn. 14:6), vile vile: “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka” (Yn. 10:9). “Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba” (Yn. 1:18), ameyatangaza mapenzi ya Baba na vile vile uteuzi wetu wa milele anaposema: “. . . ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili” (Mk. 1:15), na vile vile asemapo: “Mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele” (Yn. 6:40); na tena, “Mungu aliupenda ulimwengu” na kadhalika. (Yn. 3:16).
68. Mapenzi ya Baba ni kwamba, watu wote wasikie mahubiri haya na waje kwa Kristo, na kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe, Kristo hatawafukuza: “yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe” (Yn. 6:37).
69. Ili tuweze kufika kwake Kristo, Roho Mtakatifu anaiumba imani ya kweli kwa njia ya kulisikia Neno la Mungu, jinsi mtume ashuhudiavyo anaposema: “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Rum. 10:17). Yaani, linapohubiriwa kwa uwazi na kwa usafi.
70. Hivyo, yeyote apendaye kuokolewa asijisumbue na kujiumiza na
2105 Rum. 11:33, 34.
mawazo kuhusu mashauri ya siri ya Mungu, ikiwa ameteuliwa na kuchaguliwa kwa ajili ya uzima wa milele. Kwa hiyo, Shetani asumbuaye anakusudia kujaribu na kuchokoza mioyo ya wachaji. Badala yake, wanapaswa kumsikiliza Kristo, ambaye ndiye ‘Kitabu cha Uzima’ na Majaliwa ya watoto wa Mungu kwa uzima wa milele, na ashuhudiaye watu wote bila ubaguzi kwamba, Mungu hupenda watu wote wenye kulemewa na mizigo mizito ya dhambi waje kwake ili wapewe pumziko na kuokolewa naye.2106
71. Kulingana na mafundisho haya ya Kristo, lazima waachane na dhambi, watubu, waamini ahadi, na kujikabidhi mikononi mwake kabisa. Kwa maana, hatuwezi kufanya hivyo kwa uwezo wetu wenyewe. Roho hupenda kufanyiza kazi ya toba na imani ndani yetu kwa Neno na sakramenti. 72. Ili tuweze kumaliza vizuri na kudumu kwa uvumilivu, lazima tumwombe Mungu neema yake ambayo alituhakikishia katika Ubatizo Mtakatifu. Isitoshe, tusiwe na wasiwasi kwamba, atatupatia ahadi yake. Tuna Neno lake lisemalo: “Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki . . . akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” (Lk. 11:11-13).
73. Roho Mtakatifu anayekaa ndani ya walioteuliwa na kuipokea imani, anaishi kama katika hekalu lake, na si kwamba, ni mvivu kwao. Badala yake, anawahimiza waitii Amri ya Mungu. Vivyo hivyo, wanaoamini wasiwe wavivu, wala wasiyapinge maonyo ya Roho wa Mungu hata kidogo. Lazima wajizoeze katika maadili ya Kikristo na katika utakaso wote, kiasi, haki, subira, na upendo wa ndugu na kwa unyenyekevu watafute ‘uthibitisho wa wito na uteuzi wao,’ 2107 ili jinsi wanavyozidi kujizoeza uwezo na nguvu za Roho ndani yao, ndivyo wanavyopunguza mashaka kuhusu uteuzi wao. Kwa maana, kwa wateule, Roho anashuhudia kwamba, ni “watoto wa Mungu” (Rum. 8:16). 74. Iwapo, kwa bahati mbaya, watoto hutumbukia katika shimo la majaribu ambamo watajisikia kuwa hawapo tena katika uzoefu wa nguvu yoyote ya kuishi kwa Roho wa Mungu na kusema kama Daudi, “Nami nalisema kwa haraka yangu, nimekataliwa mbali na macho yako; . . . ” (Zab. 31:22). Vile vile, mbali na waliyozoea wao wenyewe, kwa vyovyote, wanapaswa kuungana na Daudi katika maneno yafuatayo: “Lakini ulisikia sauti na dua yangu wakati nilipokulilia” (Zab. 31:22).
75. Kuteuliwa kwetu kwa uzima wa milele hakutokani na uchaji au maadili yetu. Badala yake, kunatokana na ustahili wa Kristo na mapenzi ya neema ya 2106 Mt. 11:28. 2107 2 Pet. 2:10.
695
Baba. Baba hawezi kujipinga mwenyewe kwa maana habadiliki katika mapenzi na kiini chake. Hata hivyo, watoto wanapoasi na kujikwaa katika utiifu, anapanga kuwaita kwa toba kwa Neno na kwa njia ya Roho Mtakatifu, anapenda kuwawezesha wapate kutubu kwa kweli. Iwapo watamrudia kwa toba na imani ya kweli, daima atawaonyesha moyo huo huo wa kale wa ubaba wake kwa wote wanaolitetemekea Neno lake na kwa ukunjufu wa moyo, hurudi kwake jinsi ilivyoandikwa: “Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! mtu huyo atamrudia tena? je, nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? asema BWANA” (Yer. 3:1).
76. Maandiko Matakatifu ambayo yanasema kwamba, hakuna awezaye kumfikia Kristo isipokuwa Baba amlete kwake, ni sahihi na kweli.2108 Lakini Baba hataki kuyatenda hayo bila vifaa. Kwa hiyo basi, ameanzisha Neno na sakramenti kama vifaa na vyombo vya kawaida. Si mapenzi ya Baba au Mwana kwamba, mwanadamu akatae kusikia mahubiri ya Neno lake au kuyadharau na asubiri tu mpaka Baba amlete bila Neno na Sakramenti.2109 Kweli, kwa nguvu, Baba huleta Roho Mtakatifu. Lakini kulingana na utaratibu wake wa kawaida na agizo lake la kulisikia Neno lake takatifu, ambalo ndilo kama wavu, ambalo huwavuta wateule kutoka katika meno ya Ibilisi. 77. Kila mkosaji maskini lazima alishughulikie, aweze kulisikiliza kwa makini, na kwa vyovyote, asiwe na mashaka kumkaribia Baba kwa sababu Roho Mtakatifu, pamoja na uwezo wake, hupenda kuwemo katika Neno na kutenda kazi yake kwalo. Na huku ndiko kuvuta kwa Baba.
78. Si mapenzi ya Mungu kwamba, wasikilizaji wengine wa Neno hawataamini. Hivyo, wataanguka zaidi ndani ya vina vya laana. Ni kosa lao wenyewe kwa sababu walisikia Neno la Mungu si kwa shabaha ya kujifunza bali kulidharau, kulikufuru na kulidhihaki.Waliendelea kumpinga Roho Mtakatifu aliyependa kutenda kazi yake ndani yao, jinsi lilivyokuwa suala la Mafarisayo wakati wa Kristo.2110
79. Hivyo, kwa makini, Paulo hutofautisha kati ya kazi ya Mungu, ambaye mwenyewe hutayarisha vyombo vya heshima, na kazi ya Ibilisi na ya mwanadamu, ambaye, kwa njia ya shinikizo la Ibilisi na si la Mungu, mwenyewe amejifanya kuwa chombo kisichofaa. Imeandikwa: “Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu
2108 Yn. 6:44.
2109 Taz. juu, ‘Tamko Thabiti,’ 4, 80.
2110 Mt. 23:26; Lk. 11:39; Yn. 7:48; 8:13; 9:16, 41; 12:42.
mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu; tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu” (Rum. 9:22, 33).
80. Hapa, Mtume anasema dhahiri kabisa kwamba, Mungu “alivumilia vyombo vya ghadhabu kwa uvumilivu sana.” Yeye hasemi kwamba, Mungu aliwafanya wao kuwa vyombo vya hasira. Iwapo hayo yangekuwa mapenzi yake, hangekuwa na subira nyingi. Sababu ya kuangamia ni Ibilisi na mtu mwenyewe wala si Mungu.
81. Matayarisho yote kwa jehanamu yanatokana na Ibilisi na mwanadamu kwa njia ya dhambi na kamwe si kutoka kwa Mungu, asiyependa mtu yeyote apotee. Vipi anaweza kumtayarisha mwanadamu kwa laana yake? Mungu si chanzo cha dhambi, wala si sababu ya adhabu, yaani, laana. Sababu ya Jehanamu ni dhambi. Kwa maana “mshahara wa dhambi ni mauti” (Rum. 6:23).2111 Kwa kuwa, Mungu hakusudii dhambi na hafurahii dhambi, hivyo pia hapendi kifo cha mkosaji na hafurahii laana yake. Hapendi “mtu yeyote apotee, bali wote waifikilie toba” (2 Pet. 3:9). Imeandikwa katika Ezekieli: “Je! mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?” (Eze. 18:23; 33:11). 82 Mt. Paulo hushuhudia kwa maneno wazi kwamba, uwezo na utendaji wa Mungu huweza kubadilisha vyombo visivyostahili kuwa vyombo vya heshima anapoandika: “Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema” (2 Tim. 2:21). Kila ambaye atajitakasa lazima awe asiyekuwa safi na hivyo chombo kisichokuwa na heshima. Kuhusu ‘vyombo vya huruma’ anasema wazi kwamba, Bwana mwenyewe “alivitengeneza tangu zamani vipate utukufu” (Rum. 9:23). Hasemi hili kwa ajili ya waliolaaniwa, ambao Mungu hakuwatayarisha, bali wale ambao wamejitayarisha kuwa vyombo vya laana.
83. Lazima ifikiriwe kwa umakini kwamba, Mungu hurudi dhambi kwa dhambi. Anawaadhibu kwa ushupavu wa moyo na upofu walioongoka kwa sababu ya usalama bandia, kutotubu, na dhambi zilizotendeka makusudi. Hili halipaswi kutafsiriwa kwamba, mapenzi mema ya Mungu hayakuwepo kamwe kwamba, watu hawa wasiufikie ufahamu wa kweli na kuokolewa. Mapenzi ya Mungu yamefunuliwa kuwa mambo haya mawili: kwanza, atawapokea kwa neema wote watubuo na kumwamini Kristo, pili, atawaadhibu wote ambao hurudi
2111 Hili linalengwa dhidi ya mafundisho ya Jean Calvin kuhusu kuchaguliwa kwa aina mbili, na hasa dhidi ya Theodoro Beza.
nyuma makusudi kutoka kwa amri2112 takatifu na kujiingiza wenyewe katika uovu wa dunia hii (2 Pet. 2:20), humwandalia Ibilisi mioyo yao (Lk. 11:24, 25), na humdhihaki Roho Mtakatifu (Ebr. 10:29), na hivyo atawafanya wagumu, vipofu, na kuwalaani milele.
84. Kuhusu Farao imeandikwa: “Nilikusimamisha wewe kwa sababu hii hii, ili nikauonyeshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote” (Kut. 9:16; Rum. 9:17). Hakuangamia kwa sababu Mungu hakupenda kumpatia wokovu au kwa sababu ilikuwa furaha ya Mungu kwamba, ilimpasa kutupwa na kupotea. Kwa maana Mungu, “hapendi mtu yeyote apotee,” wala, “hafurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi” (2 Pet. 3:9; Eze. 33:11).
85. Lakini kwamba, Mungu aliushupaza moyo wa Farao aendelee kutenda dhambi na kadiri alivyozidi kuwa mkaidi, ndivyo alivyozidi kukaripiwa na kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi iliyofuatia. Mungu alifanya hivyo ili utawala na ukatili wake mbaya, ambao uliwatesa wana wa Israeli kwa hila nyingi zisizokuwa za ubinadamu, na za aina tofauti kinyume cha sauti ya dhamiri yake. Lakini baada ya Mungu kupanga kwamba, hili Neno lake lihubiriwe na mapenzi yake yafunuliwe kwa Farao, na kwa kuwa aliasi dhidi ya maonyo na maangalizi yote, Mungu aliondoa mkono wake kutoka kwake. Hivyo, moyo wake ukawa mgumu na sugu na Mungu alitekeleza hukumu yake juu yake, ambayo, kwa kweli, ilikuwa ya mkosaji wa ‘moto wa Jehanumu.’2113
86. Mtume mtakatifu hutumia tu mfano wa Farao kwa sababu ya kuonyesha haki ya Mungu ambayo Mungu huifunua kwa wasiotubu na wanaliodharau Neno lake. Hakuna njia ambayo Paulo anatutaka tufahamu kwamba, Mungu hakupenda kumpatia Farao au mtu yeyote uzima wa milele, au kwamba, kwa siri Mungu, amemfanya awe katika laana ya milele ili Farao asije akaokolewa.
87. Majaliwa ya milele na ya kuokoa ya watoto wa Mungu walioteuliwa yakifundishwa na kuelezewa, Mungu atapatiwa heshima yake kamili na timilifu. Yataonyesha kwamba, atatuokoa ‘kadiri ya makusudi yake’ na mapenzi yake kwa njia ya rehema tele katika Kristo bila stahili na matendo yetu mema, jinsi ilivyoandikwa: “Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa” (Efe. 1:5, 6).
2112 Nakala nyingi za misaada na maandiko ya Kijerumani zilizochapishwa mwaka wa 1580 husomeka ‘Gebet’ (sala), lakini hili ni kosa la matamshi ya neno ‘Gebot’ (amri), tafsiri ya Kilatini: ‘mandatum.’ 2113 Mt. 5:22.
88. Kwa hiyo, ni uongo na kosa kubwa watu wafundishapo kwamba, sababu ya Majaliwa yetu si tu huruma ya Mungu na ustahili mtakatifu wa Kristo, na kusema kwamba, kuna chanzo cha uteuzi wa Mungu. Kwa hiyo, Mungu ametuteua kwa uzima wa milele. Kwa kuwa Mungu alituteua tu si kabla hatujatenda mema na kabla hatujazaliwa (Rum. 9:11). Kwa kweli, “kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Efe. 1:4). Mungu alituteua katika Kristo, ili shabaha ya uteuzi huo iendelee, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya wito wake. Aliambiwa, “mkubwa atamtumikia mdogo,” jinsi ilivyoandikwa, ‘Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia” (Rum. 9:11-13; Mwa. 25:23; Mal. 1:2, 3).
89. Kwa hiyo basi, mafundisho haya hayatoi sababu ya mtu yeyote ama ya simanzi au ya kiburi na maisha yasiyozuiliwa. Badala yake, watu wanafundishwa kutafuta Majaliwa yao ya milele katika Kristo na katika Injili yake takatifu kama ‘Kitabu cha Uzima.’ Injili haimtengi mkosaji yeyote atubuye, bali inawakaribisha na kuwaita maskini wote wenye mizigo ya dhambi walemewao watubu, wapate ufahamu wa dhambi zao na imani katika Kristo, na kuwaahidi Roho Mtakatifu ili awatakase na kuwafanya wapya. 90. Mafundisho haya huitoa faraja idumuyo kwa watu wenye huzuni na waliojaribiwa ili wajue kwamba, wokovu wao hautokani na mikono yao. Ikiwa hii ingekuwa njia, wangeupoteza zaidi kuliko Adamu na Hawa walivyofanya huko Paradiso. Kweli, wangeupoteza kila wakati na kila saa. Wokovu wao unapatikana katika neema ya Majaliwa ya Mungu ambao aliufunua kwetu katika Kristo ambaye katika mkono wake, ‘hakuna wa kutupokonya’ (Yn. 10:28; 2 Tim. 2:19).
91. Kwa hiyo, mafundisho haya kuhusu Majaliwa ya Mungu ukitangazwa kwamba, Wakristo waliohuzunishwa hawawezi kupata faraja kwayo bali wanafanywa kukata tamaa, au wakati wasiotubu wanaimarishwa katika uovu wao, bila shaka, hapo huwa ni wazi kwamba mafundisho haya hayakuwekwa kwa mujibu wa Neno na mapenzi ya Mungu, bali kulingana na akili ya kibinadamu na kwa tashititi ya Ibilisi mpotovu.
92. Kwa maana, mtume hushuhudia kwamba: “Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini” (Rum. 15:4). Lakini inadhihirika kabisa kwamba, kila ufafanuzi wa Maandiko Matakatifu ambayo hudhoofisha na kuondoa faraja hii na matumaini haya ni kinyume cha shabaha na mapenzi ya Roho Mtakatifu.
93. Tutadumu katika maelezo haya rahisi, wazi, na yenye kufaa sana ambayo, daima yamejengwa juu ya msingi imara wa mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa. Tunakimbia na kuepuka maswali na majadiliano yote matakatifu na ya ghiliba.
699
Tunapinga na kulaani mambo yote yanayopinga maelezo haya ya kweli, rahisi, na murua.
94. Mpaka hapa tumeyachuja mafungu yaliyozaa majadiliano kati ya wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg kwa muda wa miaka mingi na ambamo baadhi yao wamekosea na upinzani mkali umeibuka kuhusu dini. 95. Kutokana na maelezo yetu, marafiki na maadui wataelewa kabisa kwamba, hatuna nia na hata mamlaka pia ya kutoa lolote la Mungu la ukweli milele na lisilobadilika kwa ajili ya amani ya muda, utulivu na patano la nje. Amani na mwafaka wa namna hiyo uliopinga ukweli na kulenga kuudhulumu, hauwezi kudumu. Pia bado hatukutaka kuyapaka rangi nyeupe au kuyafunika mafundisho yoyote yaliyoghushiwa kinyume cha ukweli na uzushi uliolaaniwa hadharani. 96. Badala yake, basi, tufunarahia kweli na tungependa, kwa moyo wa ukunjufu, mwafaka wa kweli unaolinda utukufu wa Mungu usiudhiwe, bila kupunguza lolote katika ukweli wa Injili takatifu na kutoa nafasi kwa hata kosa dogo. Kwa hiyo basi, wakosaji maskini husaidiwa kutubu kweli, kuwapa moyo wenye simanzi na kuwaimarisha wanaoamini katika utiifu mpya. Hivyo wakosaji watakuwa wenye haki na heri ya milele kwa ajili ya ustahili wa Kristo peke yake.
XII. WAASI NA MADHEHEBU MENGINE YASIOKUBALI UKIRI WA AUGSBURG KAMWE
1. Hatukutaja katika maelezo haya madhehebu na vikundi vingine ambavyo havikukubaliani Ukiri wa Augsburg kamwe, yaani, Waanabaptisti, wafuasi wa Schwenckfeld, Waariano wapya, na wanaokataa Utatu Mtakatifu. 2. Kwa sababu makanisa yote yanayodumu katika Ukiri wa Augsburg, yamelaani makosa yao, hatukutaka kuyataja hususani makosa haya katika maelezo haya.
3. Wapinzani wetu walikuwa wanadai na kutangaza kwa nguvu na ukavu kwa ulimwengu wote kwamba, kati ya makanisa na walimu wetu, hatuna wahubiri wawili ambao hukubaliana na kila fungu la Ukiri wa Augsburg lakini hutengana kwa Ajili ya Ubishi mwingi. Maana mwishowe wao wenyewe hawajui hata Ukiri wa Augsburg ni nini na maana yake ni ipi. 4 Kwa hiyo, hatukutaka kurudia tu ukiri wetu kwa maneno machache matupu au kwa sahihi zetu. Badala yake, tulitaka kutunga maelezo ya mafungu yetu yote kwa wazi, dhahiri, na kamili ambayo yalikuwa na utata miongoni mwa wanatheologia wa Ukiri wa Augsburg.
5. Tulitaka kila mmoja aweze kuona kwamba, hatukupendekeza au hatukuficha lolote ili kudanganya hata makubaliano yetu yawe tendo la kusingizia tu. 6. Tulitaka kuyatatua mambo yote kwa njia ya kimsingi na kuonyesha kwa
uwazi zaidi msimamo wetu na maadui zetu wangepaswa kukubali kwamba, katika maswali haya yote, tunayashikilia kwa ukweli, urahisi, asili, na kwa maana halisi ya Ukiri wa Augsburg. Na kwa neema ya Mungu tunatamani kubaki imara katika uwajibikaji wetu katika ukiri huu mpaka mwisho. Kulingana na huduma yetu, hatutakubali kuangalia kwa woga au kusimama kimya wakati mambo yanayopinga Ukiri wa Augsburg yanaingizwa makanisani na shuleni mwetu, ambamo Mwenyezi Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ametuweka kuwa walimu na wachungaji.
7. Kama matokeo ya kimya chetu, mtu yeyote asituhesabie uzushi uliolaaniwa wa vikundi na madhehebu yaliyokwisha kutajwa hapo juu. 8.Kwa kiasi kikubwa, yamejipenyeza yenyewe kwa siri, kulingana na asili ya roho hizi katika sehemu hizo na hasa kwa muda huo ambapo Neno safi la Injili Takatifu halikuruhusiwa kupata nafasi, eneo, wala mahali walimu wa kweli na wanaokiri Injili walikuwa wakiteswa, wakati giza kubwa la Upapa lilitawala, na wakati watu maskini wa kawaida walilazimishwa kushiriki ibada wazi za sanamu na imani za uongo za Upapa. Kwa bahati mbaya, kwa sababu ya ujinga wao, walikubali lolote lililoitwa Injili na si la Upapa. Hivyo, tunaona kwamba, lazima kusadikisha hadharani mbele ya Ukristo mzima kwamba, hatuhusiki na makosa yao, yawe machache au mengi. Kinyume chake basi, tunapinga na kulaani makosa haya yote kuwa mabaya ya uzushi, na kuwa kinyume cha Ukiri wa Augsburg wetu ambao ni wa Kikristo na una msingi wa Biblia.
MAFUNGU MAPOTOVU YA WAANABAPTISTI
9. Tunakataa na kulaumu mafundisho yenye makosa na uzushi ya Waanabaptisti2114 ambayo hayawezi kukubaliwa au kuvumiliwa katika makanisa, jumuiya, jamii, na uchumi. Wao hufundisha yafuatayo:
1. Haki yetu mbele za Mungu haifanyiki tu kwa utiifu halisi na 10 ustahili wa Kristo, bali pia kwa kufanyika kwetu upya, uchaji wetu, na maisha yetu mbele za Mungu. Lakini kwa kiasi kikubwa, uchaji wao unaonekana kuwa maagizo ya kanuni zao zilizochaguliwa, yaani, kama aina ya umonaki mpya.
2114 Waanabaptisti walikuwa wa aina mbili: 1. Waliojaribu kujenga Ufalme wa Mungu hapa duniani kwa njia ya mapinduzi na vita, kama Melchior Hoffmann (+1543) na David Joris (+1556). Bernt Rothmann, Jan Beuckelssen, na Jan Matthys walijaribu kujenga Sayuni huko Münster, Westfalen. Watu walibatizwa mara ya pili kwa nguvu na mitala iliingizwa kulingana na mifano ya Agano la Kale. Mji wa Münster ulichukuliwa na majeshi ya watawala mwaka wa 1535. 2. Waanabaptisti wenye amani waliouonaUkiristo kama jambo la ndani peke yake. Walikuwa na mashaka kuhusu muundo wa jamii na serikali: Wafuasi wa Menno Simons (14961561) na Fausto Sozzini (1539-1604), baadaye wafuasi wa Jakob Arminius (1560-1609) na wengine wengi. Mahali pengi, Waanabaptisti waliteswa na Wakatoliki, Walutheri, wafuasi wa Zwingli na Calvin.
2. Watoto wasiobatizwa hawana dhambi mbele za Mungu, bali ni 11 wenye haki na wasiokuwa na hatia. Katika hali ya maasumu, wataokolewa bila Ubatizo kwa maana hawauhitaji. Hivyo basi, huyakataa na kuyapuuza mafundisho yote ya dhambi ya asili na yote yanayoelezwa humo.
3. Watoto wasibatizwe mpaka wapate uwezo fulani wa kufikiri 12 na wawe na uwezo wa kuikiri imani yao.
4. Kwa sababu ya kuzaliwa na wazazi Wakristo na wanaoamini, 13 watoto wa Wakristo ni watakatifu na ni watoto wa Mungu hata bila kubatizwa kwanza. Kwa hiyo, hawauthamini Ubatizo wa watoto wadogo na hawana hamu kutenda kinyume cha maelezo ya maneno ya ahadi ambayo huwafikia tu ambao hulishika agano na hawalidharau (Mwa. 17:4-8, 19-21).
5. Hakuna usharika au mkusanyiko halisi wa Kikristo ambapo 14 katikati yake bado kunapatikana wakosaji.
6. Mtu asisikilize au asihudhurie mahubiri katika mahekalu hayo 15 ambamo misa za kipapa zilikuwa zimeongozwa.
7. Kwa njia yoyote, mtu asihusike na wahudumu wa Kanisa 16 ambao wanahubiri Injili Takatifu kulingana na Ukiri wa Augsburg na kuyalaumu makosa ya Waanabaptisti. Wanasema kwamba, mtu asiwahudumie kamwe na kuwafanyia kazi kabisa, bali mtu na awakimbie na kuachana nao kama watu wanaolipotosha Neno la Mungu.
8. Mamlaka kuu hazimpendezi Mungu wakati wa Agano Jipya. 17
9. Mkristo yeyote hawezi kuzihudumia Mamlaka kuu bila 18 kuivunja dhamiri yake.
10. Mkristo yeyote hawezi kuwapinga watu waovu katika 19 huduma ya mamlaka kuu bila kuivunja dhamiri yake hata kama kazi ya namna hiyo ni wajibu wake. Hali kadhalika, raia huomba msaada wa serikali.
11. Mkristo yeyote hawezi kutoa kiapo kwa dhamiri safi 20 mahakamani au kuweka nadhiri ya uaminifu wake kwa ajili ya watawala au mabwana wake wakuu.
12. Mamlaka kuu haziwezi kuamuru adhabu ya kifo kwa watenda21 maovu, kwa dhamiri safi.
13. Hakuna Mkristo ambaye, kwa dhamiri safi, anaweza kupata 22 au kumiliki mali binafsi, bali anapaswa kutoa mali yake kwa jumuiya.
14. Hakuna Mkristo ambaye, kwa dhamiri safi, anaweza kuwa na 23 hoteli au mfanyibiashara, mlinzi, na muuza nyembe au majambia.
15. Waume na wake huruhusiwa kutalikiana kwa sababu ya 24 imani, kutengana, na kuingia katika ndoa mpya na mtu mwingine mwenye imani hiyo hiyo.
16. Kristo hakupata mwili na damu yake kutoka kwa Bikira 25 Mariamu, bali alikuja nao kutoka mbinguni.2115
17. Kwamba, Kristo si Mungu kweli kwa mujibu wa kiini chake, 26 bali ana vipawa na utukufu zaidi ya wanadamu wengine.
27. Wana mafungu mengi kama haya. Lakini kati yao, wamegawanyika wenyewe katika vikundi vingi. Kikundi kimoja kinashikilia makosa mengi zaidi, na kingine kinashikilia makosa machache. Hivyo, dhehebu lote linaweza kutambulika kama aina mpya ya umonaki.
MAFUNGU MAPOTOVU YA WAFUASI WA SCHWENCKFELD
28. Kadhalika, tunakataa na kulaani makosa ya wafuasi wa Schwenckfeld2116yasemayo:
1. Wanaoutazama mwili au ubinadamu wa Kristo kuwa vitu 29 vilivyoumbwa, kwa kweli, hawamfahamu Kristo kama Mfalme Mtawala wa mbinguni. Kristo alipotukuka, mwili wake ulijichukulia sifa zote za kimungu na kwa njia zote na mintarafu ya wadhifa wake sawasawa na Baba na Neno la milele, ukawa wenye uwezo, nguvu, enzi, na utukufu. Hivyo, kiini na sifa zote za asili mbili za Kristo, mapenzi na utukufu ni moja. Kwa hiyo, mwili wa Kristo unaandamana na kiini cha Utatu Mtakatifu.
2. Huduma ya Kanisa, Neno linalohubiriwa na kusikika, si njia 30 ambayo Mungu, na Roho Mtakatifu hufundisha watu kuhusu ufahamu mabruki wa wokovu wa Kristo, uongofu, toba, na imani au hufanya kazi ya utiifu mpya ndani yao.
3. Maji ya Ubatizo si njia ambayo Bwana Mungu huitumia 31 kuufungia utoto wake na kuwa tendo la kuzaliwa mara ya pili.
4. Mkate na divai katika Chakula cha Bwana si njia ambayo 32 Kristo 2115 Hasa, Melchior Hoffmann. 2116 Kaspar Schwenckfeld (1489-1561), mwenye cheo cha lodi, mfuasi wa Luther, lakini baadaye aliiacha imani ya Kilutheri iliyojengwa juu ya neno kamili la Biblia. Badala yake, Schwenckfeld alifundisha dini ya ndani bila herufi ya Neno la Mungu.
703
5. Mkristo ambaye kweli amezaliwa upya, kwa njia ya Roho wa 33 Mungu, anaweza kuifuata na kuitimiza sheria ya Mungu kwa ukamilifu katika maisha haya.
6. Usharika ambamo uteuzi au adhabu kubwa ya kutengwa 34 hautendeki hadharani, hauwezi kuwa usharika halisi wa Kikristo.
7. Mhudumu wa Kanisa asiyefanyika upya na kuwa mwenye haki35 na mcha Mungu, kwa hakika, hawezi kufundisha wala kuwapa Wakristo sakramenti ya kweli.
MAFUNGU MAPOTOVU YA WAARIANO WAPYA2117
36. Kadhalika, tunakataa mafundisho ya Waariano Wapya ambao hufundisha kwamba, Kristo si Mungu wa kweli, si mwenye ariki, si asili ya Mungu, si wa milele, na si mwenye asili moja ya kimungu. Badala yake, amepambwa tu na enzi ya kimungu chini na kando ya Mungu Baba.
MAFUNGU MAPOTOVU YA WAPINZANI WAPYA WA UTATU
1. Kadhalika, tunakataa baadhi ya wapinzani wa Utatu 37 wanaokataa na kupinga kiri za kale za Nikea na za Athanasio. Zote mbili, huhusu maneno na yaliyomo yao. Badala yake, wanafundisha kwamba, hakuna asili moja ya milele, ya kimungu, ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Wanafundisha kwamba, jinsi kuna nafsi tatu za Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, kadhalika, kila nafsi ina kiini chake tofauti kinachohitilafiana na kingine. Nafsi hizi zote tatu ni kama wanadamu watatu tofauti kabisa. Zina nguvu sawa, hekima, uadhama, na utukufu, wakati wengine hufundisha kwamba, nafsi tatu katika Utatu, hazilingani katika asili na hali.
2. Baba peke yake ndiye Mungu halisi na wa kweli. 38.
39. Mafungu haya yote na yanayofanana, na lolote liunganishwalo na mafungu haya au linalolingana nayo, tunayapinga na kuyalaumu kama yenye uongo, upotovu, uzushi, ni kinyume cha Neno la Mungu. Isitoshe, ni kinyume
2117 Michael Servet + 1553, Matteo Gribaldi + 1564, Giovanni Valentino Gentile + 1566, Georg Blandrata + mnamo 1585, Franz Davidis + 1579, Lelio Sozzini (1525-1562), Fausto Sozzini (1539-1604).
704 huutoa mwili na damu yake.
cha Kiri tatu, ni kinyume cha Ukiri wa Augsburg na Utetezi, ni kinyume cha Mafungu ya Smalkaldi, na ni kinyume cha katekisimo za Luther. Wakristo wote wachaji wanapaswa na wanatakiwa kuachana nayo iwapo wanaipenda heri ya nafsi zao na wokovu wao.
40.Hivyo basi, mbele za Mungu na mbele ya Wakristo wote wa sasa na vizazi vyetu vijavyo, tungependa kushuhudia kwamba, maelezo haya ya mafungu yaliyojadiliwa na kuelezewa awali, yanalingana kabisa na mafundisho, imani, na ukiri wetu. Kwa neema ya Mungu, tunataka kuonekana mbele ya kiti cha hukumu cha Yesu Kristo, kuwa wenye mioyo thabiti na kuitoa hesabu yake. Sisi hatutaki kusema na kuandika kinyume chake, kwa siri wala hadharani. Badala yake, kwa neema ya Mungu, tunakusudia kuyazingatia. Kwa maneno haya, tumeshauri na tunatia sahihi zetu kwa mikono yetu wenyewe, kwa hofu ya Mungu na maombi mengi.
Dk. Yakobo Andreae, ametia sahihi
Dk. Nikolao Selnecker, ametia sahihi
Dk. Andrea Musculus, ametia sahihi
Dk. Christoforo Cornerus, ametia sahihi
Daudi Chytraeus, ametia sahihi
Dk. Martin Chemnitz, ametia sahihi
ORODHA YA SHUHUDA
TESTIMONIA PATRUM
CATALOGUS TESTIMONIORUM
KWA MSOMAJI MKRISTO
Wengine wamesingizia bila msingi wowote kwamba, Kitabu cha Mwafaka2118 kinapiku, kauli, na njia za kusema2119 za Kanisa la Zamani lenye imani halisi na mababa wao hasa katika fungu la Nafsi ya Kristo. Kinyume chake, kimeziingiza kauli mpya na ngeni ambazo hazikutumiwa wala hazikusikika. Hata hivyo, Kitabu cha Mwafaka kina shuhuda za Kanisa la Zamani na za mababa. Kuziambatisha hizo shuhuda zote na Shauri la Mwafaka kungekifanya kitabu hiki kuwa kikubwa zaidi. Baadaye, shuhuda hizi zilichaguliwa kwa uangalifu na kutolewa kwa baadhi ya watawala wachaguzi na watawala wengine.
Sasa, mikusanyiko tele ya shuhuda hizi imegawanywa katika sura fulani na imeambatishwa mwishoni mwa kitabu hiki ili msomaji Mkristo apate maelezo ya kweli na kamili. Katika orodha hii, inajulikana na kusadikika kwamba, kitabu hicho kilichotajwa hakina mafundisho mapya na kauli mpya. Badala yake, hii siri inafundishwa na kusemwa kwanza, jinsi ilivyo Maandiko Matakatifu na pili, jinsi ilivyo Kanisa la Zamani lenye imani halisi.
Kwanza kabisa, Shauri la Mwafaka linazungumzia kuhusu umoja wa nafsi ya Kristo. Pili, linazungumzia kuhusu tofauti za dhati za sifa zake zote mbili za asili jinsi Kanisa la Zamani safi, mababa, na sinodi zao zilivyofanya. Kristo ndiye mmoja na hana nafsi mbili. Naam, hii nafsi moja ina asili mbili. Yaani, asili
2118 Kilatini: ‘Liber Concordiae.’
2119 Kilatini: ‘Phrases et modi loquendi.’
ya kimungu na ya kibinadamu. Asili hizi mbili zenyewe haziwezi kutenganishwa wala hazichanganywi. Moja haibadiliki kuwa nyingine. Badala yake, asili hizo mbili zina sifa zao za dhati na zinahifadhi sifa hizo bila kuziacha kamwe. Sifa za asili moja, ambazo kwa njia halisi na kulingana na ukweli, zinahesabiwa kuwa za nafsi nzima, hazitakuwa sifa za asili nyingine kamwe. Ukweli huu unashuhudiwa na kanuni za sinodi za zamani zenye imani halisi zifuatazo:
Sinodi ya Efeso2120 kanuni ya nne: “Alaaniwe mtu atakayeyagawa maneno ya Maandiko Matakatifu yanayohusu Kristo kati ya nafsi au viini viwili ili kumhesabia maneno fulani kama binadamu bila mazingatio ya Neno la Mungu, maneno fulani yanayotazamiwa kuwa sawa na hadhi ya Mungu na Neno la Mungu Baba peke yake.”
Kanuni ya tano: “Alaaniwe mtu atakayethubutu kusema kwamba, Kristo ndiye anayembeba Mungu2121 bila kumwita yeye kuwa Mungu, jinsi alivyo Mwana lazima aitwe kulingana na ukweli kwa ajili ya asili yake kwa sababu Neno alifanyika mwili na mshiriki wa mwili na damu kama sisi wenyewe.”
Kanuni ya sita: “Alaaniwe mtu asiyekiri kwamba, Kisto huyo huyo ndiye Mungu na mwanadamu, kwa kuwa, kulingana na Maandiko Matakatifu, Neno alifanyika mwili.”
Kanuni ya kumi na mbili: “Alaaniwe mtu asiyekiri kwamba, Neno la Mungu aliteswa katika mwili, alisulibiwa katika mwili, alionja kifo katika mwili, na alikuwa mtoto wa kwanza aliyefufuka kutoka kwa wafu kwa sababu kama Mungu, ndiye uzima na huutoa uhai.”
Sinodi ya Khalkedon2122 kulingana na Evagrio (2,4): “Kulingana na mifano ya mababa watakatifu, sisi tunamkiri Mwana wa pekee Bwana wetu Yesu Kristo. Tunatangaza kwa sauti moja kwamba, yeye ndiye kamili katika umwilisho wake. Yeye ndiye Mungu wa kweli na mwanadamu wa kweli mwenye mwili na nafsi yenye akili. Kwa mujibu wa uungu wake, yeye ndiye mwenye kiini icho hicho na Baba. Kwa mujibu wa ubinadamu wake, yeye ndiye sawa nasi katika yote. Hata hivyo, hana dhambi. Kwa mujibu wa uungu wake, alizaliwa na Baba kabla ya mwanzo wa nyakati zote. Kwa mujibu wa ubinadamu wake, alizaliwa na Bikira Mariamu, aliye ???2123 mwishoni mwa nyakati kwa ajili yetu na kwa ajili ya wokovu wetu. Yeye ndiye Yesu Kristo wa pekee, Mwana, Bwana, aliyezaliwa pekee, anayejulikana katika asili mbili, bila kuzichanganya, kuzibadilisha,
2120 Katika mwaka wa 431.
2121 Kiyunani: Θεοφορος.
2122 Katika mwaka wa 451.
2123 Kiyunani: Θεοτοκος.
kuzigawanya, na kuzitenganisha.2124 Tofauti baina ya asili zake haipotei hata kidogo katika muungano wa binafsi. Badala yake, sifa za asili zote mbili zinadumu na zinaifanya nafsi moja. Hakugawanyika kuwa nafsi mbili, bali yeye ndiye Mwana mmoja na wa pekee, Mungu, Neno, na Bwana Yesu Kristo. Manabii watakatifu walifundisha vivyo hivyo zamani. Kristo mwenyewe alitufundisha sisi tumfahamu yeye hivyo. Ukiri wa Imani ulitupatia mafundisho haya.”
Waraka wa kumi wa Leo kwa sinodi2125 pia unafundisha: “Wakati sifa za asili zote mbili zilihifadhiwa na kuunganishwa kuwa nafsi moja, basi, enzi ilijichukulia udhalili, uwezo ulijichukulia udhaifu, umilele ulijichukulia mauti. Ili kuyalipia madeni yetu, asili isiyoudhika ilijiunga na asili inayotaabika ili Mkombozi wetu, yaani, Mkombozi mmoja wa pekee, aliyekufa kwa mujibu wa asili yake moja, hata hivyo, ndiye asiyekufa kwa mujibu wa asili yake nyingine.”
Licha ya hayo: “Yeye aliye Mungu wa kweli, ni mwanadamu wa kweli pia kwa kuwa, udhalili wa binadamu na utukufu wa Mungu ni mamoja katika nafsi moja. Uungu haubadiliki. Hata hivyo, anatuhurumia na ubinadamu hauyeyuki katika utukufu wa Mungu kwa sababu asili zote mbili zinatenda kazi yao pamoja lakini kulingana na sifa zao. Neno na mwili vinatenda kazi zao kulingana na sifa zao. Wakati moja inametameta kwa utukufu katika miujiza, nyingine inajitolea kwa udhalimu. Yeye ndiye Mungu kwa sababu alikuwa Neno mwanzoni. Neno alikuwa Mungu na vyote vilifanyika kwa njia ya huyo (1 Yoh.1). Yeye ndiye binadamu, kwa sababu Neno alifanyika mwili na alizaliwa na mwanamke ili tupate kuelewa umoja wa nafsi moja katika asili zote mbili. Mwana wa Adamu alishuka kutoka mbinguni. Hata hivyo, Mwana wa Mungu alijichukulia mwili katika Bikira Mariamu. Tena: “Inasemekana kwamba, Mwana wa Mungu alisulibiwa na akazikwa. Hata hivyo, hakufa katika uungu wake ambao ndio wa kiini icho hicho na Baba, bali katika asili yake dhaifu ya ubinadamu.”
Mpaka hapa, kuna kanuni za sinodi mbili, yaani, sinodi ya Efeso na ya Khalkedon. Mababa watakatifu wote wanakubaliana nazo. Wakati wote, wataalamu katika vyuo vikuu vyetu wametaka kuonyesha na kuyaelezea haya kwa njia wazi walipoyatumia maneno ’thabiti’ na ‘la kuwazika.’2126 Shauri la Mwafaka linawarejea kwa ufupi: “Jinsi wataalamu wanavyoyajua haya yote vizuri.” Maneno haya lazima yatumiwe katika maana yao halisi katika vyuo vyetu.
2124 Kiyunani:
2125 Askofu wa Roma ( ).
2126 Kilatini: ‘Concretum’ na ‘absractum.’
Maneno hayo ndiyo thabiti.2127 Yanamaanisha nafsi nzima ya Kristo, kama ‘Mungu’ na kama ‘binadamu.’ Maneno ya kuwazika2128 ndiyo yanayokusudia na yanayomaanisha asili za nafsi ya Kristo kama ‘uungu’ na kama ‘ubinadamu.’
Kulingana na tofauti hii, ni halisi kuitumia kauli thabiti: “Mungu ndiye mwanadamu, na mwanadamu ndiye Mungu.” Badala yake, si halisi kuitumia kauli ya kuwazika: “Uungu ndio ubinadamu, na ubinadamu ndio uungu.”
Hii ndiyo inayohusu sifa za kiini. Sifa za asili moja haziwezi kuhesabiwa kwa njia ya asili nyingine kwa kuwazika, kana kwamba, sifa hizi ni zake. Kwa sababu hiyo basi, kauli zinazofuatia zingekuwa batili na za uongo: “Asili ya ubinadamu ndiyo yenye majaliwa na hupatikana tangu milele.” Sifa haziwezi pia kuhesabiwa kwa njia ya zingine. Kwa mfano, kwa kusema: “Hali ya kuweza kufa ndiyo hali ya kutoweza kufa na hali ya kutoweza kufa ndiyo hali ya kuweza kufa. Kwa njia ya kauli za namna hiyo, tofauti kati ya asili na sifa zao zibatilishwe, asili zichanganywe hasa, moja ibadilishwe kuwa nyingine, na hivyo basi, asili hizi zisawazishwe na kufanywa kuwa za jinsi iyo hiyo.
Si wajibu wetu hasa kuyajua haya na kuyasadiki kabisa kwamba, asili ya ubinadamu ya nafsi ya Kristo inatamalaki na daima dawamu inahifadhi kiini chake na sifa zake za asili. Jambo hili ni muhimu mno, kwa kuwa faraja kuu ya Wakristo ni kujua na kuamini bila mashaka yoyote kwamba, asili yake ya ubinadamu imeinuliwa kweli katika muungano wa binafsi kwenye enzi hii na kushiriki binafsi katika enzi hii. Jambo hili limeelezewa kikamilifu katika Shauri la Mwafaka.
Tunadhamiria kuziorodhesha shuhuda zifuatazo ili mtu yeyote aweze kuona kwamba, kwa upande huu pia, kitabu kilichotajwa hakitoi, kwa Kanisa la Mungu, mifumo ya imani na kauli mpya, zisizosikika kamwe na zilizobuniwa na watu. Kwanza, tutatoa shuhuda kutoka kwa Maandiko Mtakatifu. Kisha, tutatoa shuhuda za walimu safi wa kanisa wa zamani, hasa za mababa waliokuwa kama viongozi katika sinodi nne kuu muhimu sana. Shuhuda hizi zitaonyesha wazi jinsi walivyojadiliana kuhusu mambo haya.
Shuhuda hizi zimeorodheshwa ifuatavyo katika vichwa fulani ili msomaji Mkristo aweze kuzitafuta bila tatizo na kuzihukumu kweli.
I2127 Kilatini: ‘Concreta vocabula.’
2128 Kilatini: ‘Abstracta vocabula.’
Kwanza: Maandiko Matakatifu na mababa pia, wanapoizungumzia enzi iliyopatiwa asili ya ubinadamu ya Kristo katika muungano wa binafsi, wanayatumia maneno communicatio, communio, participatio, donatio, traditio, subjectio, exaltatio, dari, na kadhalika. Yaani, ‘mawasiliano,’ ‘usharika,’ ‘kushiriki,’ ‘utoaji,’ ‘hawilisho,’ ‘kuweka miguuni,’ ‘kutawaza,’ ‘kupa,’
Dan. 7:13,14: “Nikaona katika njonzi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu . . . Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, . . . mamlaka yake ni mamlaka ya milele.”
Yn. 13:3: “. . . hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake . . .”
Mt. 11:27: “Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu . . .”
Mt. 28:18: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.”
Flp. 2:9: “Mungu akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina.”
Efe. 1:22: “Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake.”
Zab. 8:7; 1 Kor. 15:27; Flp. 2:9: “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, . . .”
Eusebio (‘Demonstratio evangelica’ 4,13): “Neno aliifanya asili ya ubinadamu ambayo aliichukua, kuwa kushiriki katika yeye mwenyewe, yaani, Logos, bila mwenyewe kushiriki katika asili yenye kufa. Kwa hiyo basi, Neno aliifanya asili yenye kufa ambayo aliichukua kuwa kushiriki katika uweza wa Mungu bila kulichukua lolote la asili yenye kufa.”
Sura ya 14: “Neno aliifanya asili ya ubinadamu ambayo aliichukua kustahili kuwa kushiriki katika uzima wa milele, yaani, uungu na uanaheri.”
Athanasio (‘Epistula ad Epictetum’): “Neno halikufanyika mwili ili uungu wake ukue, bali ili mwili ufufuke kutoka kwa wafu. Neno hakufanyika mwili ili lipate kuinuiliwa katika cheo bora zaidi, bali ili asili ya ubinadamu iinuliwe wakati Neno alishikiriki na kujiunga naye.
Epifanio (‘Panarion, uzushi 69’): “Mwili, uliotoka kwa Mariamu, yaani, jamii yetu, umepata utukufu na kuupokea utukufu, heshima, na ukamilifu wa kimungu na fahari ya kimbingu. Tangu mwanzo, mwili haukuwa na sifa hizi, bali umezipokea kwa njia ya kujiunga na Neno.”
Kirillo (‘De Trinitate, Dial. 5’): “Mwili wa Kristo unatuhuisha vipi? Jibu: Kwa kuwa umejiunga na Neno lililo hai, ambalo linayafanya mambo ya asili yake kuwa yale ya mwili wake pia, yaani, mambo ya pamoja nao.”
710
Theodoreto (‘Kwa Waefeso): ” Kweli, mwujiza unaopita yote ni kwamba, asili yetu ilikabidhiwa washiriki katika utukufu uo huo pamoja naye aliyeichukua kuwa yake. Hakuna tofauti katika ibada yake, bali inatubidi tuuabudu uungu usioonekana kwa njia ya asili inayoonekana.”
Yohana wa Dameski (‘De fide orthodoxa III, 7 na 15’): “Asili ya kimungu inaufanya mwili kuwa kushiriki katika utukufu na sifa zake. Lakini, hata hivyo, bila tamaa na mateso yake.
Licha ya sura ya 19: “Mwili unashiriki uungu mtendaji katika Neno kwa kuwa uungu mtendaji aliutumia mwili kama kifaa chake. Hivyo basi, mmoja yuyo huyo huitenda kazi yake kwa njia ya kimungu na kibinadamu. Inatubidi kujua kwamba, Roho Mtakatifu2129 wake anafanya kazi yake ya kawaida kwa njia zake wakati anashiriki katika uungu wa Mwana ambao huitenda na kuitawala kazi yake. Kwa hiyo basi, Roho Mtakatifu wake hufahamu, hujua, na huutawala ulimwengu wote si kama roho mtupu wa ubinadamu, bali kwa kuwa amekuwa mamoja na Roho wa Mungu katika muungano wa binafsi.”
II
Kristo ameipata enzi hii wakati huu, si kwa mujibu wa uungu wake au asili yake ya kimungu, bali kwa mujibu wa asili ya ubinadamu au mwili ambao aliuchukua, kama mwanadamu au kama Mwana wa Adamu.2130
Ebr. 1:3: “Akiisha kufanya utakaso wa dhambi, kupitia kwake mwenyewe,2131 aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu.”
Ebr. 2:8-9: “Twamwona . . . Yesu kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima.” Amewekwa juu ya matendo yote ya mikono ya Mungu, na yote yamewekwa chini ya nyayo zake.
Lk. 22:69: “Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi.”
Lk. 1:32-33: “. . . Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na falme wake utakuwa hauna mwisho.”
2129 Kiyunani: ‘αγιος νους’ badala ya jina la kawaida ‘πνευμα αγιον.’ 2130 Kilatini: ‘Humanitus, ratione corporis seu humanitatis, propter arnem, quia homo aut filius hominis.’
2131 ‘Δι εαυτου,’ baadhi ya miswada ya kale. Maneno haya yanapungua katika toleo la Kilatini la Vulgata na katika matoleo ya kisasa ya Biblia.
Athanasio kulingana na Theodoreto (‘Dial.’ I 2): “Maneno ya Maandiko Matakatifu kuhusu yale ambayo ameyapokea au ameyaadhimisha, daima yanamaanisha ubinadamu na si uungu wake.”
Yn. 5:26-27: “Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake. Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.”
Athanasio (‘Oratio contra Arianos’ 2, 4): “Maandiko Matakatifu hayamaanishi kwamba, kiini cha Neno kimeinuliwa, bali jambo hili linahusu ubinadamu wake. Inasemekana kwamba, ameinuliwa kwa kuwa ana mwili. Kwa sababu mwili wake umeinuliwa, ni halisi kabisa kusema kwamba, yeye mwenyewe ameinuliwa kama binadamu kwa mujibu wa mwili na ubinadamu wake. Amepokea yale ambayo mwili umepokea. Neno limeyashika mambo haya daima kwa ajili ya uungu na ukamilifu wake ambao ameupokea kutoka kwa Baba. Kwa hiyo, anasema kwamba, ameyapokea, kama binadamu, mamlaka ambayo alikuwa nayo daima kama Mungu. Yeye ambaye huwapa wengine wote utukufu, anasema: “Unitukuze.” Kwa hiyo, anaonyesha wazi kwamba, ana mwili ambao unahitaji utukufu. Kwa kuwa, mwili wa ubinadamu wake unatukuzwa, anazungumza jinsi yeye mwenyewe angetukuzwa. Inatubidi tuzingatie kokote kwamba, ambayo anayasema ameyapata wakati huu, hakuyapokea kwa maana hii kwamba, hangekuwa nayo awali. Kama Mungu na kama Neno, amekuwa nayo daima. Lakini sasa anasema kwamba, ameyapokea haya kama binadamu ili mwili wake uyapokee haya yote na sisi pia tuyapokee kutoka kwa mwili wake kuwa rasimali yetu.”
Mwandishi yuyo huyo anayasema maneno yayo hayo kuhusu Kristo kuuchukua ubinadamu dhidi ya maneno ya Apollinario: “Petro anaposema kwamba, Mungu amemfanya Yesu kuwa Bwana na Kristo, hamaanishi uungu wa Yesu bali ubinadamu wake. Daima, Neno amekuwa Bwana. Hakuwa Bwana baada ya mateso yake msalabani tu. Badala yake, uungu wake uliufanya ubinadamu wake kuwa Bwana na Kristo.”
Kadhalika: “Yoyote yanayosemwa na Maandiko Matakatifu kwamba, Mwana amejipokea, yanahusu mwili wake ambao ni mzaliwa wa kwanza wa Kanisa. Kwa hiyo, kwanza, Bwana aliuamsha na kuuinua mwili wake na halafu viungo vya mwili wake.” Kwa hiyo basi, Athanasio aliyaelezea ambayo aliyatumia kwa njia yake kuhusu Kanisa zima.
Basileio Mkuu “Dhidi ya wafuasi wa Eunomio” Kitabu cha Nne: “Tukisema ili tumtukuze Bwana kwamba, amelipokea jina lenye hadhi ya juu kuliko majina
yote na akisema: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani;” “nami ni hai kwa Baba;” “Unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao kabla ya ulimwengu kuweko,” na kadhalika. Haya yote lazima yaeleweke kuhusu kuzaliwa kwake kuwa mwanadamu na si kuhusu uungu wake.”
Ambrosio “Imani Vitabu Vitano” Kitabu cha tano, 6: “Umejifunza kwamba, anaweza kuyaweka yote chini yake kwa nguvu ya uungu wake. Sasa basi, jifunze pia kwamba, kwa mujibu wa mwili wake, anayapokea yote kuwa chini yake jinsi ilivyoandikwa katika Efe. 1. Vyote vimewekwa chini ya miguu yake kulingana na mwili wake.”
Kadhalika, katika Kitabu cha Tano, 2: “Kutoka kwa Mungu, mitume hawakupata haki ya kuketi katika kiti chake cha enzi. Badala yake, Kristo amepewa haki ya kuketi katika kiti cha Mungu hata kama alikuwa mwanadamu.”
Sura ya sita: “Asili yetu yote ya ubinadamu imestahiki haki mahsusi ya kuketi katika kiti cha mbinguni katika Kristo.”
Krisostomo “Kwa Waebrania” Mahubiri: “Baba alimaanisha umwilisho wa Kristo aliposema: “Na wamsujudia malaika wote wa Mungu.”
Theofilakto Yn. 3: “Baba, . . . naye amempa vyote mkononi mwa Mwana –mikononi mwa mwanadamu.”
Oikumenio akimnukuu Krisostomo Ebr. 1: “Kama Mungu, Mwana ana kiti cha enzi cha milele: ‘Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele.’ Kama Mungu, hakutazamiwa kustahili utukufu huu baada ya mateso yake ya msalabani tu, bali kama mwanadamu, aliupata utukufu huo alio nao kama Mungu.” Baadaye kidogo: “Kama mwanadamu aliyasikia maneno haya: ‘Uketi mkono wangu wa kuume.’ Yaani, kama Mungu aliyekuwa tayari na mamlaka yote.”
Kirillo ‘Thesaurus 9:3: “Amepaa kama mwanadamu katika mamlaka yake.”
11:17: “Alijiombea utukufu huo aliokuwa nao daima kama Mungu. Haya hayangesimuliwa juu yake kamwe kama angekuwa hana utukufu wake. Alitaka kulibeba hekalu lake mwenyewe katika utukufu ambao ulikuwa wake daima kama Mungu.”
Yuyo huyo “Ad Reginas” 2: “Kuupokea kwake utukufu, mamlaka, na ufalme, kunamaanisha ubinadamu wake.”
Theodoreto katika Zab. 2: “Kwa mujibu wa asili yake ya kimungu, Kristo ndiye Bwana, lakini hata kama binadamu, anayapokea mamlaka yote na ufalme.”
Katika Zab. 110: “Uketi mkono wangu wa kuume.’ Maneno haya yanahusu ubinadamu wake. Jinsi alivyo na mamlaka ya milele kama Mungu, kadhalika, anavipokea kama mwanadamu vyote alivyo navyo kama Mungu. Kama mwanadamu, anayasikia maneno haya: ‘Uketi mkono wangu wa kuume.’ Basi, ana ufalme wa milele kama Mungu.”
Yuyo huyo katika Ebr. 1: “Kwa kuwa, Kristo ndiye Mungu daima, malaika wamemwabudu na kumsujudia, lakini sasa wanamsujudia kama mwanadamu.”
Leo, Waraka 23 katika Efe. 1: “Labda wapinzani wa ukweli waulize: ‘Lini Baba Mwenyezi alimtukuza Mwanawe juu yote au kulingana na asili gani? Alivipokea vyote chini ya kiini gani? Ni kweli kwamba, vyote viliwekwa chini ya uungu kwa sababu yeye ndiye Mwumbaji! Mamlaka yake yakiongozwa au enzi yake ikiinuliwa, itamaanisha kwamba, amepunguka kuliko huyu anayemwinua na hana utajiri wa asili ambao aliuhitajia ukarimu wake.’ Ario huwanyakua watu wanaozitoa hoja za namna hiyo.
Yuyo huyo Waraka 83: “Ukweli ni kwamba, uungu na ubinadamu unaiunda nafsi moja pekee katika Kristo. Hata hivyo, tunaelewa kwamba, kutukuzwa na jina lenye hadhi ya juu kuliko majina yote vinahusu sura ile ambayo ilibidi iufanye utajiri kwa njia ya kuipa utukufu mkuu wa namna hiyo. Kwa kweli, Neno hakupoteza lolote alipofanyika mwili, ambalo Baba angelazimika kumrudishia tena. Lakini ‘namna ya mtumwa’ inamaanisha mtu wa chini aliyeinuliwa katika uweza na utukufu wa Mungu ili mwanadamu ashiriki katika matendo yake yote ya kimungu na Mungu ashiriki katika matendo yake yote ya ubinadamu.”
Kadhalika: “Vyote ambavyo Kristo amevipokea ulimwenguni, amevipokea kama mwanadamu. Mtu anaweza kupatiwa vyote ambavyo hakuwa navyo awali. Kuhusu mamlaka ya Neno, Mwana ana vyote kama Baba bila ubaguzi wowote.”
Vigilius “Dhidi ya Eytykhes” 5: “Asili ya kimungu haihitaji kutukuzwa kwa takrima au kuongezewa heshima yake au kuyapata mamlaka huko mbinguni na hapa duniani kwa ajili ya utiifu wake. Amevipata hivi kwa mujibu wa mwili wake au asili yake ya ubinadamu, ambavyo hakupungukiwa kamwe kwa sababu ya kuwa kwake Neno. Je, ingewezekana kwamba, Mwumbaji alipungukiwa uweza na mamlaka ya kutawala juu ya uumbaji wake na kuvipata hivi mwishoni mwa nyakati?
Nikeforo. 1:36: “Wakati wanafunzi walimwona Kristo mlimani huko Galilaya, aliwathibitishia kwamba, Baba amempa mamlaka makuu hapa duniani kama mwanadamu, na huko mbinguni.”
Maandiko Matakatifu, mababa wa Kanisa la Zamani lenye Imani Halisi huzitumia kauli dhahania2132 kuhusu hii siri. Yaani, maneno ambayo yanamaanisha hasa asili ya ubinadamu ya Kristo. Kristo ana asili hii kwa ajili ya muungano wa binafsi. Basi, inasemekana kwamba, asili ya ubinadamu, kwa kweli kabisa, imeipokea enzi ya namna hiyo na huendelea kuitumia.
Yn. 6:54-56: “Mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu,. . . anao uzima wa milele.”
1 Yoh. 1:7: “Damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.”
Ebr. 9:14: “Damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu.”
Mt. 26:26-28: “Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu . . . Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano.”
Eustakhio kulingana na Theodoreto (Dialogus II): “Basi, alibashiri kwamba, (yaani, Kristo kama mwanadamu) ataketi juu ya kiti kitakatifu. Alimaanisha kwamba, angeketi juu ya kiti hicho hicho kama Roho wa Kimungu,2133 kwa kuwa Mungu anakaa ndani yake bila ubaguzi wowote.”
Huyo huyo kulingana na Gelasio: “Kristo mwanadamu aliyezidi kukua katika hekima, kimo, na neema, amejipatia mamlaka yote.”
Kadhalika: “Kristo alikuja katika mwili wake kwa mitume wake na akasema: ‘Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.’ Hekalu la Neno liliyapokea mamlaka, si Mungu ambaye alilijenga hekalu hilo rembo, yaani, mwili wake.”
Athanasio kuhusu Ukiri wa Kiario na Kikatoliki: “Mungu hakubadilika kuwa mwili au kiini cha ubinadamu. Badala yake, aliitukuza asili hiyo katika yeye mwenyewe ambayo aliichukua. Hivyo, mwili na asili dhaifu ya ubinadamu yenye kufa vimepokea utukufu wa kimungu. Mwili huu na asili hii vimepokea mamlaka yote mbinguni na duniani, ambayo vilipungukiwa kabisa kabla ya Neno kuyachukua.
2132 Kilatini: ‘Vocabula abstracta.’
2133 Kilatini: ‘Spiritus divinissimus’ (Roho wa Kimungu mno). Andiko la Kijerumani: ‘Gottheit’ (Uungu).
Huyo huyo dhidi ya Apollinario kuhusu kujichukua mwenyewe kwa ubinadamu: “Katika Flp. 2 Paulo anaizungumzia hekalu ambalo ndilo mwili wa Kristo. Kwa kweli, yeye aliye juu ya yote hainuliwi bali mwili. Aliuita mwili wake kwa jina lilishindalo kila jina ili kila goti lipigwe kwa jina la Yesu na kila ulimi ukiri kwamba, Yesu Kristo ni Bwana, kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Athanasio anaiambatisha kanuni ya kawaida hapa: Maandiko Matakatifu yanapozungumzia kutukuzwa kwa Kristo, yanamaanisha asili yake ya ubinadamu, yaani, mwili wake. Asili hii ya ubinadamu inaupokea utukufu huu. Yoyote aliyoyapokea Mwana kwa maneno ya Maandiko Matakatifu, yanamhesabia ubinadamu na si uungu wake. Kwa mfano, mtume akisema kwamba, “katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili,”2134 lazima ieleweke kwamba, maneno haya yanamaanisha kwamba, utimilifu huu unapatikana katika mwili wa Kristo.
Huyo huyo kulingana na Theodoreto (Dialogus 2): “Bwana alisema, ‘uketi mkono wangu wa kuume,’ kwa mwili.”
Athanasio ‘De incarnatione,’ kulingana na Kirillo (‘utetezi wa lana ya nane’) na pia kulingana na kitabu ‘De recta fide ad Reginas:’ “Mtu akisema kwamba, si halali kuuabudu mwili wa Bwana wetu kwa sababu ndio mwili wa mwanadamu na licha ya hayo akisema, si halali kuuabudu mwili huu kama mwili wa Bwana na Mungu, atalaaniwa na Kanisa takatifu Katoliki.”
Huyo huyo: “Yote ambayo Maandiko Matakatifu yanasema kwamba, Mwana ameyapokea, yanaeleweka yakimaanisha mwili wake. Mwili wake ndio mzaliwa wa kwanza wa Kanisa. Kwanza, Bwana aliuamsha na kuutukuza mwili wake, halafu viungo vya mwili wake pia.”
Hilario 9: “Mwanadamu Yesu Kristo hukaa katika utukufu wa Mungu Baba, kwa kuwa mwili umejiunga na utukufu wa Neno na kuendelea kuwa na utukufu wa Neno.”
Eusebio wa Emesa (“Mahubiri ya sikukuu sita baada ya Pasaka”): “Yeye ambaye, kwa mujibu wa uungu wake, daima ametawala yote pamoja na Baba na Roho Mtakatifu, aliyapokea yote pia chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa ubinadamu wake. Mwanadamu yule ambaye awali kidogo aliteswa, sasa anaendelea kutawala mbinguni na duniani na kuyatenda yote kulingana na mapenzi yake mwenyewe.”
Gregorio wa Nyssa kulingana na Gelasio na Theoodoreto (Dial. 2): “Basi, 2134 Kol. 2:9.
ametukuzwa, kwa mkono wa kuume wa Mungu (Mdo. 2). Ni nani wa chini au wa juu aliyetukuzwa? Ni nani aliye wa chini isipokuwa binadamu? Ni nani aliye wa juu isipokuwa Yeye wa kimungu? Mungu hahitaji kutukuzwa kwa sababu yeye ndiye aliye wa juu. Basi, mtume anasema kwamba, asili ya ubinadamu wa Kristo imetukuzwa kwa kuwa mwanadamu alifanyika kuwa Bwana na Kristo. Mtume hataki kusema kwamba, kiini cha milele kilifanyika Bwana. Badala yake, anaizungumzia asili duni ya Kristo ambayo ilitukuzwa kuliko yote, yaani, kwa mkono wa kuume wa Mungu.” Baadaye kidogo: “Mkono wa kuume wa Mungu ulioyajenga yote, yaani, Bwana mwenyewe, ambaye kwake, yote yalifanyika. Bila yeye hakuna lolote linaloweza kudumu. Mkono huu ulijiunga na mwanadamu na alimwinua kwa umoja huu mpaka akaufikia utukufu wake mwenyewe.”
Basileio Mkuu (“Dhidi ya Eunomio 2”): “Petro aliposema kwamba, Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo,2135 anakirejea kiwakilishi kionyeshi “huyo” kinachomaanisha asili ya ubinadamu ya Yesu iliyoonekana kwa wote. Baadaye kidogo: “Petro aliposema kwamba, Mungu amemfanya kuwa Bwana na Kristo, alimaanisha kwamba, Baba alimpatia cheo cha mtawala na mamlaka yote ya asili ya ubinadamu.”
Epifanio (“Dhidi ya Wafuasi wa Ario”): “Huyo Yesu mliyemsulibisha.” Neno lisiloumbwa na lisiloshiriki katika mateso halikutaka kulipanua agano lake takatifu na mwili. Badala yake basi, iliubidi mwili kujiunga na Neno lisiloumbwa huko juu. Kwa hiyo, Mungu alimfanya kuwa Bwana na Kristo huyu aliyezaliwa na Mariamu na kujiunga na uungu.”
Ambrosio (“Juu ya Roho Mtakatifu 3:12): “Malaika hawauabudu uungu wa Yesu Kristo peke yake, bali hata pandio lake pia.” Licha ya hayo: “Nabii anasema kwamba, lazima kuiabudu hata ardhi ambayo Bwana Yesu aliichukua kuwa sehemu yake mwenyewe alipouchukua mwili. Pandio lake linamaanisha ardhi, na ardhi inamaanisha mwili wa Kristo, ambao hata leo, bado tunauabudu na mitume waliuabudu katika Bwana Yesu jinsi nilivyokwisha kusema awali.”
Agostino: (‘Maneno ya Bwana; Mahubiri 58): “Kwa mujibu wa asili yake, Kristo akiwa si Mungu bali kiumbe tu, asitukuzwe wala asiabudiwe kama Mungu pia. Lakini labda hao watajibu: Mbona, basi, pamoja na uungu wake unauabudu mwili wake pia uliokiri kwamba, umeumbwa?
Huyo huyo katika (Zab. 98): “Sujuduni penye kiti cha miguu yale,” yaani, 2135 Mdo. 2:36.
717
nchi.2136 Yaani, Kristo aliichukua ardhi kutoka ardhini kuwa mwili wake. Mwili unatokea ardhini. Aliuchukua mwili kutoka mwili wa Mariamu. Alitembea hapa katika mwili huo. Alitupatia sisi mwili huo kuwa chakula chetu ili tuokolewe. Hakuna yeyote atakayeula mwili huu bila kuusujudia kwanza. Kwa hiyo basi, tutaitafuta njia bora kabisa ya kukisujudia kiti cha miguu yake. Sisi hatukisujudii bila dhambi, bali hata tutatenda dhambi tusipokiabudu.”
Krisostomo (Ebr. 2): “Kwa kweli, jambo lililo kuu, la ajabu, na la kutushtusha sana ni kwamba, mahuluki2137 mwenye mwili wetu huketi huko juu na anaendelea kuabudiwa na malaika, malaika wakuu, maserafi, na makerubi. Nikiyatafakari haya, nitashtuka sana mara kwa mara.”
Huyo huyo katika (2 Kor. 10): “Mamajusi waliusujudia ulipolala katika hori . . . Walikuja kutoka mbali na waliuinamia kwa hofu na mitetemeko.”
Huyo huyo, kulingana na waraka wa Leo (‘Ep. 95’): “Je, Baba alisema kwa asili gani: Uketi hapo mwenyewe katika kiti changu cha enzi?” Alisema kwa asili hiyo hiyo, ambayo ilisemwa: “Kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”2138
Theofilakto akimnukuu Krisostomo (Mt. 28): “Kwa kuwa asili ya ubinadamu iliyohukumiwa awali ilijiunga kwa njia ya binafsi na Neno, aliye Mungu, na anaendelea kuketi kule mbinguni na kuabudiwa na malaika, asili hii ndiyo ina haki ya kusema: ‘Nimepewa mamlaka yote mbinguni.’ Awali, asili ya ubinadamu ilipatikana katika hali ya utumwa, lakini sasa inapatikana katika Kristo aliye mtawala wa yote.”
Huyo huyo katika (Yn. 3): “Baba amempa vyote mkononi mwa Mwanawe, yaani, mkononi mwa mwanadamu.”
Kirillo (“De Incarnatione”): “Neno liliingia katika hali ambayo halikuwa nayo awali ili asili ya ubinadamu iliingie katika hali ambayo halikuwa nayo awali. Hivyo basi, asili yetu inang’ara fahari ya Enzi ya Kimungu kwa ajili ya muungano kwa kuwa imeinuliwa kuliko hali yake ya kwanza bila kumvuta Mungu asiyebadilika chini ya asili yake.
Kanuni ya Sinodi la Efeso (11): “Alaaniwe mtu asiyekiri kwamba, mwili wa Bwana unatuhuisha, kwa sababu umekuwa mwili wa Neno linaloyahuisha yote.”
2136 Zab. 99:5.
2137 Yaani, kiumbe, binadamu. 2138 Mwa. 3:19.
Kirillo anapoifafanua kauli ya laana hii anasema: “Nestorio hakutaka kukubali kwamba, mwili wa Kristo unatuhuisha. Badala yake, alizifafanua kauli za Yn. 6 kumaanisha uungu wake peke yake.”
Theodoreto (Dial. 2): “Mwili huo umetazamiwa kustahili cheo cha kuketi kwa mkono wa kuume wa Mungu. Uumbaji wote unausujudia kwa sababu unaitwa kuwa mwili wa asili ya Mtawala, yaani, mwili wa Mungu.”
Huyo huyo katika (Zab. 8): “Asili ya ubinadamu imepokewa kutoka kwa Mungu na heshima ya namna hii katika Kristo, yaani, cheo cha mtawala wa uumbaji wote.”
Leo (Waraka 2): “Ubinadamu aliouchukua Mungu haukuinuliwa bali ubinadamu uliouchukua uungu. Kwa hiyo tena, Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe . . . , na kila ulimi ukiri ya kuwa, YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”2139
Yohana wa Dameski (3:18): “Nia ya kimungu ya Kristo ndiyo haina mwanzo na inayatenda yote. Lakini nia yake ya ubinadamu imepata mwanzo wake wakati huu. Nia hii ina mihemuko yake maasumu2140 ya kiasili na haina mwenyeji kwa mujibu wa asili yake. Lakini, kwa kweli, baada ya kuwa nia ya Neno na nia ya Mungu kwa upande wa asili yake, nia ndiyo mwenyeji kabisa.” Jinsi mfafanuzi mmoja anavyosema, hii inamaanisha kwamba, mapenzi ya Mungu yana mamlaka kwa ajili ya asili yake mwenyewe kulitenda lolote analopenda. Kinyume chake, mapenzi ya ubinadamu ya Kristo hayana mamlaka haya kwa upande wa asili yake, lakini kwa sababu yamejiunga na Mungu, naam, Neno.
Licha ya hayo, sura ya 21: Mwili unawasiliana na uungu wa Neno unaotenda kazi yake, kwa kuwa uungu unautumia mwili kama kifaa chake. Hivyo basi, yuyu huyu mmoja huitenda kazi yake kwa njia ya kimungu na kibinadamu. Inatubidi kujua kwamba, Roho Mtakatifu wake hutenda kazi yake kwa matendo yake mwenyewe wakati anashiriki katika uungu wa Neno ambao hutenda kazi yake na kutawala. Kwa hiyo basi, Roho Mtakatifu wake huushika, huufahamu, na huupanga uumbaji wote. Hafanyi hivyo kama nafsi ya mwanadamu peke yake, bali kwa sababu amekuwa mamoja katika muungano wa binafsi na katika Roho wa Mungu.”
Licha ya hayo, sura ya 21: “Asili ya ubinadamu wa Kristo haujui wakati ujao kwa ajili ya kiini chake mwenyewe bali kama nafsi ya Bwana iliyojiunga
2139 Flp. 2:9-10.
2140 Yaani, bila kosa na hati.
na Neno lenyewe na kuwa muungano wa binafsi pamoja naye. Kwa hiyo, imetajirika na imekirimika mbali na mambo yote ya kimungu kwa uwezo wa kuyajua mambo yatayokuja.” Mwishoni mwa sura: “Basi, tunasema kwamba, Mtawala wa uumbaji wote na Bwana, Kristo aliye mmoja kama Mungu na mwanadamu, anayajua yote, ‘ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.”2141
Nikeforo (18:36): “Wanafunzi walipomwona Kristo mlimani kule Galilaya, aliwahakikishia kwamba, Baba alimpatia mamlaka huko mbinguni na humu duniani kama mwanadamu.”
IV
Maandiko Matakatifu na mababa watakatifu hawakuielewa enzi ya Kristo ambayo aliipokea wakati huo kuwa yenye vipawa vilivyoumbwa peke yake.2142 Enzi hii ndiyo utukufu wake wa kawaida wa kimungu. Asili yake ya ubinadamu imeinuliwa kwenye enzi hii na utukufu huo katika nafsi ya Mwana wa Mungu. Kwa hiyo, asili yake ya ubinadamu imepokea uweza na ufanisi wake ambao ni wa kawaida na asili ya kimungu.
Yn. 17:5: “Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.”
Kol. 2:9: “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.”
Hilario (“Utatu 2:3): “Neno lililofanyika mwili lilisali kwamba, ule uliopata mwanzo wake wakati huo, upate utukufu na enzi vilivyopatikana tangu milele.”
Gregorio wa Nyssa kulingana na Gelasio na Theodoreto (“Dial.” 2): “(Mdo. 2:33) Mkono wa kuume wa Mungu ulijiunga na mwanadamu na ulimwinua kwa msaada wa muungano huu kwenye utukufu wake.”
Huyo huyo (“De anima”): “Mungu au Neno halibadiliki kuwa kitu kingine chochote. Hata hivyo, linawasiliana na mwili na nafsi bila kuushiriki udhaifu wao. Yeye anavipatia nguvu ya uungu wake mwenyewe, lakini anadumu kuwa huyo huyo aliyekuwako kabla ya kuzaliwa kwake.”
Basileio kuhusu kuzaliwa kutakatifu kwake Kristo: “Uungu unapatikana vipi katika mwili? Jinsi moto katika chuma usivyobadilika kwa njia ya kuushirikisha.
2141 Kol. 2:3.
2142 Kilatini: ‘De finitis qualitatibus.’
Moto hauhami kutoka katika chuma lakini unakitolea chuma nguvu zake kinapokaa ndani yake. Moto haupungui bali wenyewe unakijaza kabisa chuma ambacho kinaushiriki moto.”
Epifanio (‘Ancoratus’): “Kwa kuushirikisha mwili wa dunia katika nguvu hiyo hiyo ya kimungu, aliviunganisha kuwa uweza mmoja, yaani, uungu mmoja. Yeye ambaye ndiye Bwana mmoja wa pekee na Kristo mmoja, alifanya hivyo si kama Kristo wawili au Mungu wawili.”
Kirillo (Yoh. 4:23): “Si itakuwa ujinga wenu mkikataa kwamba, mwili hauwezi kuhuisha? Mwili wenyewe hauwezi kuhuisha lolote kwa kuwa unahitaji kuhuishwa wenyewe. Baada ya kuichunguza siri ya umwilisho2143 kwa uangalifu na baada ya kujifunza kuelewa kwamba, uzima wenyewe unaishi katika mwili, hamna budi kuamini kwamba, mwili umekuwa mtoa uzima. Hata hivyo, katika yeye, hauwezi kufanya lolote wenyewe. Baada ya kujiunga na Neno linalotoa uzima, mwili umekuwa mtoa uzima. Haukulivutia Neno katika asili yake ya uharibifu, bali mwili wa Kristo umeinuliwa kwenye nguvu ya asili iliyo bora zaidi. Hata hivyo, asili ya mwili yenyewe haiwezi kulihuisha lolote. Inaweza kufanya hivyo kwa sababu imeyapata mamlaka yote ya Neno. Mwili wa Paulo, Petro, na mtu fulani hauwezi kufanya hivyo isipokuwa mwili wake ambaye mwenyewe ndiye Uzima na ambaye utimilifu wote wa Mungu unakaa kwa jinsi ya kimwili.2144 Kwa hiyo basi, mwili wa wengine kwa kweli haufai kitu.2145 Mwili wa Kristo peke yake unaweza kuhuisha, kwa sababu Mwana wa Mungu wa pekee huishi ndani yake.”
Agostino (“Dhidi ya Felikiano Mwariano” 11): “Tunajua kwamba, mwili wake umetukuzwa kwa enzi ya kimungu, lakini sikubali kwamba, walipouharamisha mwili wake, uungu wake pia ulikuwa umeharamishwa.”
Theodoreto (katika sura ya “Mpingakristo”): “Neno alipofanyika mwanadamu, hakuonyesha asili ya ubinadamu ambayo aliipokea sehemu ya neema tu, bali ilimpendeza Mungu kuwa utimilifu wote ukae ndani yake.”2146
Huyo huyo katika (Zab. 21): “Asili iliyopokelewa ikijiunga na uungu wake aliyejiunga nayo, asili hiyo itapata pia kushiriki katika hekima na utukufu huo huo.
Huyo huyo katika (Ebr. 1): “Baada ya ufufuo ubinadamu pia umepokea
2143 Kilatini: ‘Incarnatio.’
2144 Kol. 2:9. 2145 Yn. 6:63. 2146 Kol. 1:19.
utukufu wa kimungu.”
Yohana wa Dameski (3:7.15): “Asili ya kimungu inaushirikisha mwili katika utukufu wake na sifa zake mwenyewe bila kushiriki katika tamaa na mateso ya mwili.”
VKama Mungu, Kristo ndiye mwenye enzi yenyewe ya kimungu kwa njia ya kiini, yaani, kama sifa ya kiini chake mwenyewe. Kama mwanadamu, anaimiliki kwa njia tofauti, yaani, kwa muungano wa binafsi na siyo kwa ajili ya kulingana na kiini chake.
Yn. 14:6: “Mimi ndimi uzima.”
Yn. 5:26-27: “Baba . . . alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake . . . kwa sababu ni Mwana wa Adamu.”
Kirillo (“Thesauro” 12:15): “Hali na sifa za kiumbe na Mwumbaji ni tofauti kabisa. Lakini asili ya ubinadamu ya Mwana wa Mungu imepita mipaka yake na imehamishwa kwa neema katika hali yake ambayo ameichukua.”
Huyo huyo katika (Yoh. 2:144): “Kristo anaongezea sababu ambayo kwayo alisema kwamba, Baba alimpatia uzima na hukumu: ‘Kwa sababu ni Mwana wa Adamu.’ Hivyo basi, anatufundisha kwamba, amekabidhiwa vyote kama mwanadamu. Badala yake, Mwana wa pekee hashiriki katika uzima kwa kuwa yeye ndiye uzima.”
Huyo huyo katika (Yoh. 3:37): “Mwili wa Kristo huhuisha kwa sababu ndio mwili wa Uzima wenye uweza wa Neno aliyefanyika mwili. Kweli, unajaa nguvu ambayo hufanya vyote viwepo na kuishi.”
Huyo huyo katika(Yoh. 4:14): “Kwa kuwa, mwili wa Mwokozi umejiunga na Neno la Mungu ambaye kwa mujibu wa asili yake ni uzima, mwili huu umekuwa pia mtoa uzima.”
Licha ya hayo: “Nimeujaza mwili wangu uzima. Nimeuchukua mwili mfu. Kwa kuwa, mimi ambaye kwa mujibu wa asili yangu ndimi uzima, ninaishi katika mwili mfu, nimeubadilisha kabisa kufuatia uzima wangu mwenyewe.”
Sura ya 24: “Asili ya mwili yenyewe haiwezi kuhuisha lakini sisi hatufikirii kwamba, asili hii inapatikana katika Kristo peke yake. Mwana wa Mungu ambaye, kwa mujibu wa kiini chake, ndiye uzima, amejiunga nayo. Kristo
anapouita mwili wake mtoa uzima, hamaanishi kwamba, mwili huu una uweza wa kutoa uzima kwa njia hiyo hiyo kama yeye mwenyewe au kusema kikamilifu zaidi, roho wake. Ni Roho ambaye huhuisha, lakini mwili huipokea nguvu hii unapojiunga na Roho. Inafanyikaje? Akili yetu haiwezi kuelewa na hatuwezi kusema kwa lugha yetu, bali tunaupokea ukweli huu, imani ya kimya, na thabiti.”
Huyo huyo katika (Yoh. 10:13): “Mwili wa uzima uliofanyika mwili wa Mzaliwa pekee, umeupokea uweza wa uzima.”
Huyo huyo katika (Yoh. 11:21): “Mwili wa Kristo wenyewe haukuwa mtakatifu, lakini baada na kujiunga na Neno ulibadilika kuwa kama Neno mwenye nguvu na ulikuwa chemchemi ya wokovu na utakaso kwa wale walioushiriki. Sisi hatudai kwamba, mwili kama mwili mtupu uweze kutenda jinsi Mungu anavyotenda, bali uweza huu ndio ule wa asili ya Neno.”
Huyo huyo katika (“De Trinitate” Dial. 6): “Baba anamtukuza yeye, si kwa sababu yeye ndiye Mungu, bali kwa sababu yeye ndiye mwanadamu. Kama mwanadamu, uweza wa kimungu wa kutenda kazi yake, haukuwa kwa mujibu wa asili yake, lakini kwa njia nyingine, aliupata kuwa wake wakati Neno la Mungu alijiunga na kuambatana na ubinadamu kwa njia ya kushangaza sana.”
Huyo huyo katika (“De recta fide ad Theodosium”): “Aliuficha uzima wake mwenyewe ndani ya mwili aliouchukua kwa njia ya muungano wa asili zote mbili.”
Licha ya hayo: “Kwa kuwa, Neno alizaliwa kwa njia ya kushangaza sana na Baba aliye na uzima, Neno pia anahuisha. Inatubidi kutambua kwamba, nyakati zingine nguvu ya utukufu wa Mungu huitwa nguvu ya mwili wake.” Isitoshe: “Hakuna maana kukiri kwamba, mwili wa dunia huhuisha tukimaanisha asili ya mwili wenyewe.”
Epifanio (“Contra Ariomanitas”): “Ubinadamu wa Kristo haupatikani kwa njia ya kutengwa. Hakusema wakati uungu na ubinadamu ulitengwa lakini wakati ubinadamu ulijiunga na uungu na kuwa mahuluki mmoja mtakatifu. Hivyo basi, katika yeye mwenyewe, ubinadamu wake ulihisi mambo yote kwa njia halisi kwa sababu ulijiunga na uungu na katika muungano huu, ulikuwa mmoja na uungu.”
Agostino (“De verba Domini,” mahubiri): “Ninauabudu mwili wa Bwana au ubinadamu timamu wa Kristo kwa njia ya kusujudu kwa kuwa uungu uliuchukua huo na ulikuwa mmoja na uungu. Mimi simkubali Mungu na mwanadamu waliotengwa, bali ninakiri kwamba, Mwana mmoja pekee wa Mungu ndiye Mungu na mwanadamu. Sasa, ukimtenga mwanadamu na Mungu, sitamwamini
na sitamwabudu mwanadamu wa namna hiyo kamwe.”
Licha ya hayo: “Hatuzungumzii ubinadamu mtupu peke yake. Lakini mtu akiudharau ubinadamu uliojiunga na uungu, Mwana peke yake wa Mungu, aliye Mungu wa kweli, na mwanadamu wa kweli, na kukataa kumsujudu, yeye kweli amestahili kifo cha milele.”
Huyo huyo (“De civitate Dei” 10:24): “Mwili wa Kristo wenyewe hausafishi waumini. Wao husafishwa na Neno aliyeuchukua mwili.”
Kanuni 11 ya Sinodi la Efeso: “Alaaniwe mtu asiyekiri kwamba, mwili wa Bwana hutuhuisha kwa sababu umekuwa mwili wa Neno anayeyatolea yote uzima.”
Theofilakto (Yn. 3): “Baba amempa vyote mkononi mwa Mwana, yaani, mkononi mwa mwanadamu. Kauli hii ina maana gani ikiulenga uungu wake? Baba alimkabidhi Mwana vyote kwa ajili ya asili, si kwa ajili ya neema.”
Huyo huyo katika (Mt. 28): “Maneno haya ‘mimi nimepewa mamlaka yote’ yakichukuliwa kumaanisha Neno ambaye ndiye Mungu, maana yake itakuwa kwamba, wapende wasipende, wote walionitumikia, waliokuwa watiifu awali, wananikiri sasa kwamba, mimi ndimi Mungu. Maneno haya yakiilenga asili ya ubinadamu, lazima yaeleweke hivyo: ‘mimi ambaye nilikuwa na asili iliyohukumiwa, ndimi Mungu baada ya kujiunga na Mwana bila kuzichanganya asili zote mbili na nimepewa mamlaka yote.”
Yohana wa Dameski (3:17): “Mwili wa Bwana huyatenda matendo ya kimungu, si kwa nguvu yake wenyewe, bali kwa nguvu ya Neno aliyejiunga na mwili. Kwa njia ya mwili, Neno hudhihirisha jinsi Neno anavyoitenda kazi yake. Chuma kinachoungulika hakichomi kwa sababu chuma chenyewe kinachoma kwa mujibu wa asili yake. Chuma kimepata nguvu hii kwa njia ya kuunganishwa na moto. Hivyo basi, mwili wa Bwana wetu wenyewe ni mfu, lakini umepata uweza kuhuisha kwa kuwa umejiunga na Neno kuwa nafsi moja.”
Huyo huyo 18: “Mapenzi ya kimungu ya Kristo ni hayana mwanzo na yanayatenda yote . . . lakini mapenzi yake ya ubinadamu yalianza wakati huo. Mapenzi haya yamekuwa na jazba za kiasili na safi bila kuwa mwenyezi. Kwa kweli, baada ya kuwa na kwa mujibu wa asili yake, mapenzi ya Neno yenyewe, yaani, ya Mungu, ndiyo yanakuwa mwenyezi.” Maana yake ni jinsi mfafanuzi mmoja alivyoelezea: Mapenzi ya Mungu yana mamlaka kwa ajili ya asili ya kutekeleza yote yanayotaka. Lakini mapenzi ya ubinadamu ya Kristo hayakuwa na uweza huu kwa ajili ya asili yake bali kwa sababu yamejiunga na Mungu,
yaani, Neno.
Isitoshe 21: “Asili ya ubinadamu ya Kristo haijui wakati ujao kwa ajili ya kiini chake, lakini kama nafsi ya Bwana wetu iliyojiunga na Neno mwenyewe na kuwa muungano wa binafsi. Kwa hiyo, imetajirika na iliyapokea mambo yote ya kimungu pamoja, uweza wa kuyajua mambo yatakayokuja.” Mwishoni mwa sura hii: “Basi, tunasema kwamba, Mtawala na Bwana wa uumbaji, Kristo mmoja, ambaye ndiye Mungu na mwanadamu, anayajua yote. Naam, ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.”2147
Huyo huyo 2:22: “Hata hivyo, nafsi ya ubinadamu wa Bwana wetu ni moja pamoja na asili ya kibinadamu ambayo haijui wakati ujao. Imejiunga kuwa nafsi moja na Neno, yaani, Mungu ambaye huyajua yote, na kwa hiyo, ameyajua yote, si kwa neema bali kwa ajili ya muungano wa binafsi.” Baadaye kidogo: “Kwa kuwa, asili zote mbili za Bwana wetu Kristo hazihitilafiani, ujuzi wa asili ya kimungu unahitilafiana na ujuzi na nia ya asili ya kibinadamu.”
VI
Enzi, nguvu, na uweza wa Kristo ni sifa za asili yake ya kimungu. Sifa hizi zinadumu lakini uungu unaziruhusu kujulikana na kuzitenda kazi zao kwa njia ya na katika ubinadamu uliojiunga na uungu hata kuwa nafsi moja. Ubinadamu uliipokea enzi hii ili utimilifu wote wa Mungu ukae kwa njia ya binafsi katika mwili na damu ya Kristo, ambavyo uungu ulivipokea.
Rum. 3:25: “Ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake.”
Rum. 5:9: “Tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake.”
Kol. 1:20: “Kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake.”
Athanasio (“Mahubiri dhidi ya Waariano” 5): “Kwa nini hatukuruhusiwa kuuabudu mwili wa Bwana? Neno alimpatia mkono wake wa kimwili na akamponya mtu mwenye homa. Kwa sauti ya ubinadamu alimwamsha Lazaro. Kwa mikono yake msalabani, alimshinda mfalme yule wa uweza wa anga.”
Huyo huyo (“Utatu, Dial.” 5): “Neno ambaye ndiye Mungu, anaitenda miujiza yake kwa njia ya kujiunga na ubinadamu bila wao. Kwa kuwa ilimpendeza Neno
2147 Kol. 2:3.
kuuruhusu uweza wake wa kimungu kutenda kazi yake kwa njia ya ubinadamu, kwa msaada wa ubinadamu, na katika hao.” Baadaye kidogo: “Ilimpendeza kumfanya mahuluki huyu kuwa mkamilifu kwa njia ya masharti ya kiasili na na hivyo kuwa mwanadamu wa kweli, yaani, mnyama mwenye akili.”
Kirillo (“Imani halisi kwa Theodosio”): “Nafsi ya Kristo iliyojiunga na Neno, ilishuka kuzimuni. Huko, aliwatangazia wafungwa kwa uweza na nguvu yake ya kimungu: ‘Ondokeni kabisa!”
Huyo huyo (“Kwa Regina”): “Kristo mwenyewe anahuisha kama Mungu kwa mwili wake.”
VII
Utoaji wa enzi hii ya kimungu kwa asili ya kibinadamu inafanyika kwa njia hii kwamba, hata katika utukufu wa kimbingu, asili ya kibinadamu haitachanganywa na asili ya kimungu, haitapotea, na kuwepo kwake hakutakataliwa.
Mt. 16:27: “Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake.”
Mdo. 1:11: “Atakuja jinsi hiyo hiyo kama mlivyomwona akienda zake mbinguni.”
Athanasio (“Utatu” Dial. 5): “Ilimpendeza kumfanya mwanadamu huyu kuwa mkamilifu juu ya masharti ya kiasili na hivyo kuwa mwanadamu wa kweli, yaani, kiumbe mwenye akili.”
Theofilakto, akimnukuu Krisostomo katika Mt. Mathayo (Mt. 28): “Mimi mwenye asili iliyohukumiwa awali, nikiwa Mungu kulingana na muungano wa asili zisizochanganywa pamoja na Mwana wake Mungu, nimepewa mamlaka yote.”
Kirillo, 4: 24: “Ameonyesha kwamba mwili Wake wote umejaa nguvu ya kuhuisha ya Roho, si kwa sababu umepoteza asili ya mwili na kubadilishwa kuwa Roho, lakini kwa kuwa, ukiunganishwa na Roho, huzipokea nguvu zote za kuhuisha.”
Yuyo huyu, kuhusu Umwilisho, 8: “Kama kielelezo, kwa njia ya makaa ya mawe, tunaweza kuona jinsi Mungu aliye Neno, Amejiunganisha kabisa na ubinadamu, na Ameibadilisha asili Aliyojitwalia kuwa utukufu na ufanisi wake. Kama vile moto unavyoshikamana na kuni, ndivyo Mungu anavyojiunganishwa na ubinadamu kwa namna ambayo haiwezi kufahamika, akiipa asili hiyo tendo
la asili Yake pia.”
Theodoreto, (Dial. 2): “Na kwa sababu hiyo, mwili wa Bwana ulifufuka pasipo kuharibika, bila kuteseka, usioweza kufa, na kutukuzwa kwa utukufu wa kiungu, na unaabudiwa na mamlaka ya mbinguni. Hata hivyo, ni mwili, uliowekewa mipaka mwanzoni.”
Yuyo huyu, katika (Dial. 3), huidhinisha kwa kabuli kauli hii ya Apollinario: “Ikiwa kuchanganywa kwa moto na chuma, ambako huonyesha uangavu wa chuma, ili yaliyo ya moto yatendwe pia, hakuibadilishi asili ya chuma, kwa hiyo, basi, wala muungano wa Mungu na mwili hautabadilisha mwili, ingawa utaupatia mwili utendaji wa kimungu.”
Yohana wa Dameski, (3:17): “Mwili wa Bwana ulipambwa kwa matendo matakatifu kwa ajili ya muungano wake kamili wa kibinafsi na Neno, bila kuharibiwa wenyewe kwa mambo yake ya asili.”
Yuyo huyu, (2:22): “Kwa maana ingawa (nafsi ya Bwana) ilikuwa ya asili isiyoyajua ya wakati ujao, hata hivyo, ikiwa imeunganishwa kibinafsi na Mungu Neno, ilikuwa na ujuzi wa mambo yote, si kwa neema, bali kwa sababu ya muungano wake binafsi.” Na muda mfupi baadaye: “Na kwa kuwa asili ni tofauti katika Bwana wetu Yesu Kristo, basi, nia ya asili ya kimungu na nia ya asili ya ubinadamu, pia, zinatofautiana.”
VIII
“Kadhalika ni kwamba, kulingana na asili na kwa sababu ya muungano wa kibinafsi, asili ya kibinadamu ni mshiriki na ina uwezo wa enzi ya kimungu ambayo ni ya Mungu.”
Kol. 2:9: Katika yeye unakaa utimilifu wote wa Uungu, kwa jinsi ya kimwili. Ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimefichwa.
Yustino, (Expositio Fidei): “Hatusemi kwamba Yeye yu ndani ya Baba jinsi alivyo ndani ya wengineo; si kwa sababu asili iliyo ndani ya wengineo imepunguzwa, bali kwa sababu ya uwezo mdogo wa kuweza kuupokea Uungu.”
Pia: “Kwa kuwa mwili ulionajisika haupokei miale yote ya Uungu.”
Na muda mfupi baadaye: “Kisaha lifikilie Jua la Uadilifu katika hali ya kila kitu, kwa vile Yeye ni Mungu; bali sisi sote, tulio dhaifu na macho yetu yamepofushwa na uchafu wa dhambi, hatuwezi kuipokea nuru nzima bali kidogo
tu; lakini hekalu lake mwenyewe, yaani, jicho lake lililo safi kabisa, laweza kupokea nuru yote, kwa sababu limeumbwa na Roho Mtakatifu na limetengwa kabisa na dhambi.”
Origene, (“De Principiis” 2:6): “Nafsi yote ya Kristo hulipokea Neno lote, na hupokewa katika nuru na fahari Yake.”
Yuyo huyo 4: “Nafsi ya Kristo, ikiunganishwa na Neno la Mungu, imekuwa na uwezo kamili wa kumpokea Mwana wa Mungu.”
Agostino, (Waraka wa 57): “Ingawa Mungu yupo pia katika viumbe vyote, na anakaa hasa ndani ya waumini, hata hivyo hawampokei Yeye kikamilifu, lakini, kulingana na tofauti ya uwezo wao, baadhi humpata na kumpokea Yeye zaidi, na wengine kidogo. Lakini kuhusu Kichwa chetu, Kristo, mtume husema: Katika Yeye unakaa utimilifu wote wa Uungu, kwa jinsi ya kimwili.”
IX
Ijapokuwa inajulikana na haikanushiki kwamba Uungu, pamoja na enzi yake, haupaswi kuwekewa mipaka na mwili, kana kwamba umefungiwa ndani ya chombo, jinsi Athanasio, Origene, Gregorio wa Nyssa, na wengine walivyoandika kwa usahihi, na kama vile Kitabu cha Mwafaka [uk. 1019 kinavyokataa kwa uwazi kama kosa mafundisho kwamba ubinadamu wa Kristo umepanuliwa kila mahali katika maeneo yote, au kwamba, kwa muungano wa kibinafsi, asili ya kibinadamu katika Kristo imebadilishwa kuwa kiini kisicho na mwisho, - hata hivyo, tangu asili ya uungu na ya ubinadamu zimeunganishwa kibinafsi na bila kutenganishwa katika Kristo, Maandiko Matakatifu na mababa watakatifu wanashuhudia kwamba popote Kristo alipo, hakuna nusu ya nafsi yake, au nusu moja tu, au sehemu tu ya nafsi yake, kwa mfano, uungu peke yake, kando na mtupu, bila ya ubinadamu Wake wa kutwaaliwa kuunganishwa au kutengwa nayo, na nje ya muungano wa kibinafsi na ubinadamu; bali nafsi yake yote, yaani, kama Mungu na binadamu, kwa mujibu wa mtindo wa muungano wa kibinafsi na wanadamu, ambao ni siri isiyoweza kuchunguzwa, upo kila mahali kwa njia na kipimo kinachojulikana na Mungu.
Efe. 4:10: Alipaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote. Hili Oikumenio anaeleza hivi: “Kwa maana, kwa hakika, tangu zamani alivijaza vitu vyote uungu Wake mtupu; na baada ya kufanyika mwili, ili Ajaze vitu vyote kwa mwili Wake, alishuka na kupaa.”
Naye Theofilakto, kwenye kifungu kile kile: “Ili apate kuvijaza vitu vyote kwa mamlaka yake na kazi yake, na kwamba, katika mwili, tangu awali alivijaza vitu vyote na uungu wake. Mambo haya, hata hivyo, yanapingwa na Paulo wa Samosata na Nestorio.
Leo, (Walaka wa 10): “Kanisa la Kikatoliki (la Wakristo wote) li hai na huendelea mbele katika imani hii, kwamba katika Kristo Yesu, ubinadamu hauaminiki bila uungu wa kweli wala uungu hauaminiki bila ubinadamu wa kweli.”
Yuyo huyo, katika Mahubiri ya 3, Juu ya Mateso ya Yesu Kristo: “Imani ya Kikatoliki (ya Wakristo wote) hulifundisha, na hulitaka hili, tujue kwamba katika Mwokozi wetu, asili mbili zimeunganika, na kwamba, wakati sifa zao zilibaki, muungano kama huo wa dutu zote mbili umetokea kwamba, tangu wakati ambapo Neno alifanyika mwili ndani ya tumbo la Bikira Mariamu, hatupaswi kumfikiria Mungu bila hii, kwamba Yeye ni mwanadamu; wala tusimfikirie mwanadamu bila hili, kwamba Yeye ni Mungu.”
Kadhalika: “Kila asili, kwa utendaji bainifu, inatangaza uhalisi wake, lakini haijitengi yenyewe kutoka kwa uhusiano na nyingine; hapa hakuna lililo la asili moja lisilopatikana katika asili nyingine; lakini Mungu alimtwaa binadamu mzima, na hivyo akajiunganisha Mwenyewe kwa binadamu na binadamu akajiunganisha na Yeye, kwamba kila asili imo ndani ya nyingine, na wala asili moja haigeuki kuwa ile nyingine kwa kupoteza sifa zake binafsi.”
XKwa kuwa katika fungu hili la maneno, mafundisho kama hayo yameelekezwa hasa kwenye hatima ili tupate kujua ni wapi tunapaswa kutafuta na tupate kuifahamu nafsi nzima ya Mpatanishi, Mungu na mwanadamu, Kitabu cha Mwafaka, hutuelekeza sisi, jinsi mababa wengine wote watakatifu, hufanya pia, si kwa gogo au jiwe au kitu kingine chochote, bali kwa yale ambayo Kristo Ametuonyesha na kutuelekeza katika na pamoja na Neno Lake.
Kirillo, katika Mt. Yohana 2:32: “Mavazi ya Kristo yaligawanywa katika mafungu manne, na joho Lake pekee lilibaki bila kugawanywa, ambalo, naweza kusema, lilikuwa ishara ya siri. Kwa maana pembe nne za dunia, zilizoletwa kwenye wokovu, zimeshiriki vazi la Neno, yaani, wakiushiriki mwili Wake, miongoni mwao kwa njia ambayo haujapata kugawanywa. Kwa maana Mwana wa Pekee, akipita ndani ya kila mmoja ili kushirikiwa na kila mmoja, na kutakasa
nafsi na miili yao kwa mwili Wake, Yuko katika wote bila kugawanyika na ni mzima, kwa kuwa, akiwa mmoja, Yu kila mahali bila kugawanyika.”
Theofilakto, katika Mt. Yohana 19: “Kwa hiyo mwili mtakatifu wa Kristo haugawanyiki. Pembe nne za dunia zikiugawanya na kuushiriki; umegawanywa miongoni mwa kila mmoja kwa njia zote, na umeitakasa nafsi ya kila mmoja kwa mwili. Akiwa kila mahali; Aliye Mzaliwa Pekee kwa mwili Wake binafsi Yuko mzima na hagawanyiki ndani ya wote; kwa maana hajagawanywa kamwe, kama Paulo asemavyo.”
Krisostomo, Mahubiri Waebrania 17 (na Ambrosio: “Ad Hebraicos 10): “Kwa kuwa wanamshiriki kila mahali, je, kuna Kristo wengi? La, hasha! Lakini Kristo mmoja yuko kila mahali, akiwa mwili mmoja halisi hapa na pale. Kwa maana yeye wanamshiriki kila mahali alivyo mwili mmoja, wala si miili mingi, Yuyo huyu naye ni dhabihu moja. Yeye ndiye Kuhani Mkuu wetu ambaye ametoa dhabihu inayotutakasa. Sisi pia sasa tunatoa kile ambacho, baada ya kutolewa wakati huo, hakikuharibiwa. Hili linafanywa kwa ukumbusho wa lile ambalo lilifanyika wakati huo. Akasema, ‘Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.’ Maana hatutoi dhabihu nyingine, kama afanyavyo kuhani mkuu, bali ni ileile siku zote. Heri tuuamili ukumbusho wa dhabihu hii.” (Tazama: Dhidi ya dhabihu ya upatanisho ya Misa ya Wafuasi wa Papa.)
HITIMISHO
Msomaji Mkristo, shuhuda hizi za walimu wa kale wa Kanisa zimeelezwa hapa, si kwa maana hii kwamba imani yetu ya Kikristo imejengwa juu ya mamlaka ya wanadamu. Kwa maana imani ya kweli iokoayo haitakiwi kujengwa juu ya waalimu wowote wa kanisa, wa zamani au wapya, bali juu ya Neno la Mungu tu na peke yake, ambalo linapatikana katika Maandiko ya manabii na mitume watakatifu, kama mashahidi wasio na shaka wa ukweli wa Mungu. Lakini kwa sababu roho za kilokole, kwa hila maalum na isiyo ya kawaida ya Shetani, wanataka kuwaongoza watu kutoka katika Maandiko Matakatifu - ambayo, mshukuru Mungu! hata mlei wa kawaida sasa anaweza kusoma kwa manufaa yake - kwa maandishi ya mababa na waalimu wa kale wa kanisa kama ndani ya bahari pana, hivi kwamba yeye ambaye hajasoma hawezi kujua kwa usahihi kama wao na maandishi yao ni kama hawa waalimu wapya wanavyoyanukuu maneno yao, na hivyo kuachwa katika mashaka makubwa, - tumelazimishwa kwa njia ya Katalogi/Orodha hii kutangaza, na kuonyesha kwa maoni ya wote, kwamba fundisho hili jipya la uwongo lina msingi mdogo katika waalimu wa
730
zamani wa kanisa katika Maandiko Matakatifu, lakini kwamba inapingana nayo kikamilifu. Shuhuda zao wanazinukuu kwa maana ya uwongo, kinyume na mapenzi ya mababa, kama vile kwa makusudi na bila kupenda kupotosha maneno sahili, yaliyo wazi na dhahiri ya agano la Kristo na shuhuda safi za Maandiko Matakatifu. Kwa sababu hii Kitabu cha Mwafaka kinaelekeza kila mtu kwenye Maandiko Matakatifu na Katekisimo rahisi; kwa maana yule anayeshikilia muundo huu sahili kwa imani ya kweli na sahili hutoa kilicho bora zaidi kwa ajili ya nafsi yake na dhamiri yake, kwani imejengwa juu ya Mwamba thabiti na usiotikisika, Mt. 7 na 17; Gal. 1; Zab. 119.
Maandishi haya yalibadilishwa kuwa maandishi ya ASCII ya Mradi wa Wittenberg na Mchungaji Thomas Von Hagel na yanapatikana kwa umma.
Faharasa ya Mada
Nambari za kurasa zilizoandikwa katika italiki zinarejea sehemu zile za Utetezi zinazopatikana tu katika Toleo la Princeps la Septemba, mwaka wa 1531.
Adamu, 83.5; 85; 317.1; 384.10; 385.14; 389.14; 471.65; 476.100; 488.64; 509.4; 537.10; 539.7; 561.9; 562.11; 564.27; 566.38, 42; 666.58; 669.67; 699.90; 708; 711; 712; 722; 726; anguko la, 10.1; 82.2; 319.4; 559.1; 563.23; Ibilisi alimbadilisha kuwa mlokole, 329.5; 330.9; mwanzoni alifanywa kuwa na majuto makubwa, kisha aliipokea Injili ya Kristo, 188.53, 55; hakuupokea msamaha wa dhambi kwa njia ya adhabu, 188.55; 210.155; Adamu wa kale, tazama Adamu wa Kale; Kiumbe wa Kale
Adamu wa Kale, imani humwua, 609.10; anapaswa kuuawa kila siku kwa njia ya uwezo wa Ubatizo, 488.65–66. Tazama pia Kiumbe wa Kale
Adhabu, kwa dhambi ya asili: mauti, laana ya milele, maovu ya kimwili na ya kiroho, utawala wa ibilisi, 89.46; 562.13; 563.19; baadhi ya watakatifu huteswa na zilizo dhahiri zinazolazimishwa na Mungu kama mfano, 210.156; funguo hazina uwezo wa kuzilazimisha, 214.176; wahubiri wasichanganye mapatilizo ya raia na adhabu ya kiroho ya kutengwa na kanisa, 331; tazama
pia Kutengwa na Kanisa. Tazama pia Hukumu; Sheria; Adhibu Afya, haki ya asili ilikusudiwa kuwa pamoja na afya kamili kwa jumla, 85.17
Agizo (Maagizo), Agizo la Mungu haliwezi kubadilishwa na binadamu, 488.60; linatakiwa kutiifuwa kwa heshima yote, 485.38; ibilisi hujaribu kuyapotoa na kuyabatilisha maagizo yote ya Mungu, 488.62; kila akifanyacho Mungu na kukitekeleza kwetu hutamani kukifanikisha kwa njia ya maagizo ya nje, 483.30; Wakristo wanaruhusiwa kuyatumia maagizo ya raia, 175.50; Injili haiharibu taifa au kaya lakini hutuamuru tuvitii kama maagizo matakatifu, 230.5; Injili hututiifusha kwa serikali ya ulimwengu jinsi ambavyo tumewekwa chini ya sheria za majira kama maagizo matakatifu, 230.6; Waiaminio Injili hawayahakiki maagizo ya kisiasa, 246.2; tazama pia Mamlaka; Ufalme wa Raia; Serikali; Watawala; upendo wa jinsia moja kwa nyingine hakika ni agizo takatifu, 250.7; tazama pia Upendo wa Asili; agizo la Kristo katika aina zote mbili katika Chakula cha Bwana, 246.2; haliwezi
kubatilishwa au kubadilishwa na kanisa, 246.2; 248.14; si chaguo la binadamu, 248.15; maagizo ya kanisa, tazama Maagizo ya Kanisa; agizo la Mungu katika wokovu, tazama Uchaguzi. Tazama pia Amri
Agnoetai, Dhehebu la (Wasiojua), 671.75; Wafuasi wa Theofronio walioona kutojua kuwa sababu ya umwilisho wa Kristo na waliofundisha kwamba, katika umwilisho wa Kristo, kuna nafsi moja katika asili mbili.
Ahadi
A. Asili: ahadi na sheria ni sehemu mbili za Biblia, 91.5; 108.102; 120.183; 188.53; 319.4; 618.14; tazama pia Sheria, ni Injili, tazama Injili; yaliyomo yake ni msamaha wa dhambi, 97.43; 108.102; 275.69; 601.39; imetolewa kwa sababu tumeshindwa kuishika amri, 99102; imetolewa tayari kwa Adamu na kwa mababa wakuu, 99.57; 188.53; 272.55; ahadi ya Injili ni ya ulimwengu wote, 687.28
B. Kujitwalia: iwapo kungehitaji sheria na hali ya stahili zetu, kungekuwa bure, 97.42; iwapo kungetegemea matendo yetu, hakungekuwa imara, 235.10; kujitwalia kunawekwa na Mungu kwa sababu ya uaminifu wa Mungu na siyo kwa sababu ya matendo yetu, 106-7; wale wanaohesabu kuhesabiwa haki na upendo
hukukomesha, 109.110; 286.17; 290.34; kunaweza kupokewa kwa imani tu, 97.43; 98.50; 101.70; 104.84; 111.127; 194.80; 275.70; 599.30; 604.51; imani inakuidhinisha, 98.50; 110.113; tazama pia Imani, kutokukuamini humkasirisha, humfedhehesha, na kunamshtaki Mungu kwa kudanganya, 464.21
C. Katika maana pana: ahadi inayoambatanishwa na Amri ya Kwanza, 404.29; 406.39; kwa Amri ya Nne, 420.131; 425.164; kwa amri Kumi, 451.333; haja zao, 318.1; ahadi za ndoa, 217.14; za sala, 217.16; 240.20; 464.19; za huduma ya Neno, 216.11; 585.56
Alama, tazama pia Ishara; za kanisa, tazama Kanisa; za Wakristo, tazama Chakula cha Bwana, Sakramenti; za wateule, tazama Uchaguzi; za imani, tazama Imani
Alexandria, 40.41; 43.41; 349.62; mshona viatu katika, 291.38; makasisi katika, 315.9; kanisa katika, 332.3; Baba Askofu (Mkuu) wa, 339.12; 341.18-19
Alloiosis (Αλλοιωσις), Ubadilishaji (Zwingli), 654; 674; ni nini, 658.21; ilikataliwa na Luther, 654; ililaaniwa kama barakoa ya ibilisi, 658.21; 662.40
Altenburg, Kongamano la Wataalamu la (1568–1569), 597
733
Amani, pamoja na Mungu: humaanisha kuwa na dhamiri tulivu na ya furaha, 106.91; siyo kwa njia ya matendo bali imani, tazama
Imani, Matendo; kanisani: haviwezi kupatikana kwa kuuacha ukweli wa Mungu wa milele usiobadilika, 700.95
Amri, kwa amri ya Mungu ya milele isiyobadilika, binadamu wote wa- nalazimika na sharti wamtii
Mungu, 616.4; amri ya Mungu haiwezi kubatilishwa na nadhari, 53.18; 34.24; jinsi ilimwengu na miendo ya nyota vilivyo amri za Mungu hakika, vivyo hivyo serikali halali ni amri za Mungu hakika, 175.50; Injili haiharibu utaratibu wa kisiasa, 230.6; mam- laka yote ya kisiasa, serikali nzuri, sheria, na utaratibu mwema vimeumb- wa na kuanzishwa na Mungu, 20.1; tazama pia Ufalme wa Raia; Uumbaji; Serikali; Watawala; Mungu hataki amri zake zidharauliwe, 252.19; amri za kanisa, tazama Maagizo ya Kanisa; amri sahihi baina ya imani na maten- do mema, na baina ya kuhesabiwa haki na utakaso, lazima zidumishwe, 602.40; kwa sababu ya makosa kuhusu kujipatia neema, amri mpya za utawa zilibuniwa kila siku, 52.1–3; watawa wa kiume huzieneza stahi-li za amri zao, 241.29; watawa wa kiume wote na madaraja matakatifu hayawezi kujigambia kumpata mmoja, 442.278; tazama pia Majumba ya
734
Watawa; Maisha ya Utawa; Nadhiri za Utawa; Watawa wa Kiume. Tazama pia Agizo (Maagizo)
Amri (Sheria)
A. Mungu amezitoa ili kutenganisha mema na maovu, 427.183; zinaweza kutokataliwa, 204.134; hakuna mwanadamu awezaye kuzibatilisha, 52- 58.22, 24; 214.175; hubaki na asili na thamani yao ingawa hatuziweki kamwe, 622.5; zinapasa kusharifiwa zaidi kuliko desturi zote, 32; haziwezi kubadilishwa na nadhiri au sheria yoyote ya binadamu, 33-35.8; 34-37.24; 50-53.18; 293.51; zimefichwa na Mapokeo ya binadamu, 46-49.8; 207.145; 225.25; 306.4; kwa njia ya maisha ya utawa, 57-61.49; katika mafundisho ya papa, hakuna lolote kabisa kuzihusu, 316.14; anataka maagizo yake na sheria vichukue nafasi ya kwanza, 220.6. Tazama pia Sherehe; Kaida za kibinadamu; Nadhiri za Utawa, Watawa wa Kiume; Matendo; Ibada
B. Hazihesabii haki, 195.87; 222.17; hakuna binadamu awezaye kuzishika zote, 318.6; hatuwezi kuzishika kwa uwezo wetu wenyewe, 451.2-3; asili ya binadamu ni hasimu (kinyume) cha hizo, 595.11; 603.43; zinatushtaki daima, 447.310; hatuwezi kuzishika mbali na Roho Mtakatifu anayetushurutisha kuzitii, 232.2; 695.73; tunahitaji moyo mpya wenye mtazamo sahihi kwake Mungu, 449.324; 578.26; imani ya
kweli haizidharau, 203.131
C.Amri Kumi za Mungu (Decalogus), 23-26.2; 362-364; 401,402.1-10; 400; muhtasari wa mafundisho matakatifu, 447.311; watu hawawezi kutoa mafundisho, utangamano wa jamii, au kazi inayolingana nazo, 448.317; 451.333; zimeandikwa katika mioyo ya watu wote, 461.67; zinatuonyesha ni nini mapenzi ya Mungu, 624.12; matendo mema halisi, 624.12; 625.21; chemchemi ya kweli na njia ya matendo mema yote, 447.311; tunapaswa kuziweka daima machoni petu na katika kumbukumbu zetu, 402.14; 451.331; matabaka yote ya watu lazima yazishike, 448.317; mikono yetu itajaa tukizishika, 447.313; 448.317-318; wale wanaozifahamu kikamilifu wanayafahamu Maandiko Matakatifu yote, 396.17; hakuna awezaye kuishika hata moja jinsi inavyopasa kushikwa, 448.316; kuhusu mpangilio wa amri, 407.50; 416.103; 427.180; 4430.200; 433.223; 434.255; 449.324
1. Amri ya Kwanza, 404.12;; 449.324; huuagiza moyo na hufundisha imani, 407.50; Imani ni mwitiko na ukiri wa Wakristo unaioihusu, 452.10; amri zingine zote zinatokana nayo, 449.324; chanzo muhimu na asili inayozipenya zingine zote, 450.329; sawasawa na bizimu au pete ya shada la maua, 450.326; tukiiweka,
zingine zitafuatia zenyewe, 407.48; Zaburi nzima ni taamuli na mazoezi yanayoihusu, 402.18; hakuna awezaye kuiweka isipokuwa Kristo, 185.37; Mungu ameiambatisha na tishio la kuogofya na ahadi nzuri ya kufariji, 404.29
2. Amri ya Pili, 362.3-4, 407; 491.5; 496.45; kuanzisha matendo ya ibada bila amri ya Mungu na bila mfano wa Maandiko Matakatifu ni kinyume chake, 280.89
3. Amri ya Tatu, 362.5-6, 412; tazama pia Siku
4. Amri ya Nne, 362.7-8, 416; kazi kubwa zaidi kuliko zote tunayoweza kuifanya baada ya kumwabudu Mungu ambayo imefupishwa katika amri za kwanza tatu, 419.125; inajumuisha utiifu kwa watu wote walio mamlakani, 422.141; asili ya wajibu wa wazazi, 425.167; ni mkufu wa dhahabu ulio shingoni na taji lililo kichwani mwa mzazi, 482.20; lazima isisitizwe kwa watoto na kwa watu wa kawaida, 359.18; pia kwa watawala wenye mamlaka na kwa wazazi, 359.19; vijana wanapaswa kuipa kipaumbele, 418.115; yeyote asiyeitii atawajibika kwa chakari na kwa mvunaji aogofyaye, 421.13536; 423.149; Mungu ameambatisha kwayo ahadi nzuri sana, 420.131; 425.164; chini ya upapa haikutiliwa maanani wala haikufundishwa, 421.140
735
5. Amri ya Tano, 363.9-10, 427; Mungu ameiweka kama ukuta, ngome, na kimbilio kwa majirani zetu, 428.185; muhtasari: hatupaswi kumdhuru yeyote kwa mkono, tendo, ulimi, au moyo, 428.188; inavunjwa pia wakati tunashindwa kuwatendea majirani zetu mema au kuwanusuru kutoka madhara, 429.189-194; Mungu anatuamuru tuwe na upendo na huruma kwa maadui zetu, 429.194; lakini lile inalolikataza linahusu watu binafsi, si watumishi wa serikali wenye madaraka rasmi, 427.181
6. Amri ya Sita, 363.11-12 ; 430
7. Amri ya Saba, 363.13-14; 433; lazima isisitizwe kwa mafundi mchundo, wenye maduka, wakulima, wafanyakazi wa nyumbani, na vibarua wa siku, 359.18; 434.225; 436.237; Kiti Kitakatifu cha Roma na wafuasi wake wameikiuka, 435.230; hutuamuru tuwasaidie maskini, 437.247; wajibu wa watawala na mahakimu, 438.249
8. Amri ya Nane, 363.15-16; 438; hutukataza kumhukumu na kumshutumu jirani hadharani, 440.265; isipokuwa mahakimu wa raia, wahubiri na wazazi, 441.274
9. Amri ya Tisa na Kumi, 364.17-20; 444; inakataza kutamani, 444.293; 446.307, 447.310; uhusiano na Amri ya Saba, 444.296; zinatolewa si kwa majangili waovu bali kwa watu
wanyofu sana, 445.300
10. Hitimisho kwa Amri, 369.2122, 447; 451.333
Anfechtung, tazama Mateso Anguko, uharibifu wa asili ya binadamu kwa ajili ya hilo, 10.1; 86.24; 317.4; 561.8; 563.23; 564.26; 573.5; asili ya binadamu ni na inabaki kuwa kiumbe cha Mungu hata baada ya hilo, 509.2; 559.2; 566.38; kwa kiasi fulani, katika mambo ya kinje, watu wana hiari hata baada ya hilo, 585.53; adhabu ya hilo, 89.46; 251.13; wazazi wetu wa kwanza hawakuishi bila sheria hata baada ya hilo, 526.2
Ariki (Asili), katika mafundisho ya dhambi ya asili, tazama Asili ya Binadamu; Dhambi ya Asili; katika mafundisho ya Utatu Mtakatifu: kuna nafsi tatu katika ariki ile ile moja isiyogawanyika, 9.1-3; 81.1 (I); 669.68; kosa la Wapinzani wa Utatu Mtakatifu, 551.29; 704.37; katika Kristologia: tazama Kristo, A; kufuatana na asili yake takatifu, Kristo ni wa ariki moja na Baba na Roho, 670.73; kosa la Waario Wapya, 551.28; 704.36; kufuatana na ubinadamu wake, Kristo ni wa ariki moja nasi, 567.43; asili takatifu na ya binadamu hazijachanganywa kuwa ariki moja, 535.6; 538.18, 21, 27; 670.71; kosa la wafuasi wa Schwenckfeld, 550.21; 551.29
Aristotele, -a 82; 99; 161; 517; 532;
736
571; 589;
Ashiki Mbaya (tamaa mbaya, uasherati mbaya) (Concupiscentia), asili yake, 86.24; si jambo la katikati/lisiloegemea upande wowote, 88.42; dhambi, siyo tu mapatilizo, 88.38; jinsi ilivyoumbwa, tamaa mbaya siyo sifa bainifu za lazima za asili yetu, 517.12; ashiki hubaki baada ya Ubatizo, 87.35; tazama pia Mwili; unatafuta mambo ya mwili kinyume cha Neno la Mungu, 86.26; siyo tu tamaa za mwili bali pia hekima ya mwili na haki, 86.26; huuamsha upendo wa asili (tamaa), 251.13; 251.16; uwezo wake, 249.5; uashe–rati mbaya unafukuzwa kutoka moyo–ni kwa njia ya Roho Mtakatifu, 1011. Tazama pia Upendo wa Asili; Dhambi ya Asili 735
Asili, asili mbili za Kristo, tazama Kristo
Asili ya Kibinadamu, 81-89; 509-512; 512-516; 559-571; 572593; maana ya neno “asili,” 512.22; 569.51; kwanza iliumbwa njema, 564.27; lakini imeharibiwa sana na dhambi ya asili (iliyoirithiwa), 317.3; 510.8; 560.5; 564.30; ni yenye dhambi (iliyoharibiwa kabisa) 560.6; 562.11- 14; 569.53; tazama pia (Dhambi ya maumbile”; “Dhambi ya mtu”; lakini haijafutwa au kugeuzwa kabisa kuwa katika kiini kingine, 564.30; tazama pia Ubadilisaji Umbo (Accidens), Kiini;
737
fulani lazima atofautishe baina ya asili ya binadamu na dhambi ya asili, 509.2; 512.19; 560.2; 565.33; 567.41; Kristo aliichukua asili yetu ya kibinadamu bila dhambi, 510.5; 567.43; hata baada ya anguko bado ni na hubaki kuwa kiumbe cha Mungu, 509.2; 560.2; 565.32, 34; kazi ya Mungu lazima itofautishwe na kazi ya Ibilisi, 513.25, 560.3; 567.42; 696.79; i katika uwezo wa Ibilisi anayeisukuma kwenye dhambi nyingi, 25.32; 89.47; 232.5; 562.13; 565.29; 567.44; iliyokwamishwa sana dhambini kiasi kwamba, haiwezi kuziona au kuzijua zote, 45.9; sheria ya Mungu huishtaki na kuilaani, 560.6; 565.32; “Tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira” (Efe.2:3), 560.6; kwa kiasi fulani, katika mambo ya nje na ya asili, hubakiza welekevu wake, uwezo, na kipaji, 562.12; tazama pia Mapenzi; lakini haina cheche ya uwezo wa kiroho, 573.7; 575.12; haina uwezo, ustadi, kipaji, ufarisi, au ukubwa wa kuanzisha au kutekeleza jambo katika mambo ya imani au kushirikiana katika matendo kama hayo, 511.16; 563.23; tazama pia wongofu; haiwezi kumpenda, kumwogopa, kumwamini, au kumtegemea Mungu kwa moyo wote, 22.2; 82.7ff; inampinga Mungu kabisa, 562.11; 567.44; Kristo ni Mwokozi wa asili ya binadamu iliyoharibika, 95.30; Kristo ameikomboa na kuitakasa,
559.6; kuzaliwa upya na kufanywa upya tu kwa Roho Mtakatifu kunaweza kuiponya, 562.14; Kristo amezifunika dhambi zetu zote lakini
bado zinakaa ndani yake wakati wa maisha haya, 598.22; mafundisho ya uongo ya wanatheologia wanazuoni, 89.43; 317.4; 511.11; 563.17; tazama
pia Dhambi ya Asili; ya Wapelagio, 511.13; 563.17; 563.20; ya Wafuasi wa Mani, 512.19; 564.26; Tazama
pia Mwili; Moyo; Dhambi ya Asili; Akili; Mapenzi
Augsburg, Baraza la (1530), 6.1; 6.5–6; 229.52; 308.10; 315.16; 394.8; 508.4; 552.3; 556.5; 682.1; Muda, 611; 594; 595
Jiwe, wongofu hautokei kama taswira inayochorwa katika jiwe kwa kutumia asidi, 592.89. Tazama
pia Pande la Mti au Jiwe
Kipimo, Maandiko Matakatifu pekee hubakia kuwa kipimo ambacho kwacho, mafundisho yote yanapasa kupimwa, 508.7
Kiumbe wa Kale, 624.12; ni yupi, 498.66; kama punda mpumbavu, mkaidi, 626.24; huwaning’inia waumini hadi kaburini, 623.7; 625.18; tunambeba kila siku shingoni mradi tunaishi, 476.102; 490.86; kwa sababu yake, asili ya binadamu potovu hutuning’inia hadi mautini, 527.4; haangamizwi kabisa katika wongofu, 516.14; 591.81; lazima auawe kwa njia ya
uwezo wa Ubatizo, 371.12; mateso humsikitikia, 471.66; hupungua kila siku miongoni mwa Wakristo, 489.71; kwa njia ya sheria na mapatilizo, lazima ashurutishwe kumfuata Roho, 527.4; 625.19; 626.24. Tazama pia Adamu wa Kale
Mwito, kila mtu anapaswa kutenda kufuatana na mwito wake, 48-50.10; bila imani na Kristo, asili ya binadamu ni nyonge sana kujishughulisha kwa makini katika miito halali, 2628.33-37; watu wote, wanapaswa kuutafuta ukamilifu, yaani, kukua katika kicho cha Mungu, imani, upendo kwa majirani zao bila kujali mwito wao, 289.37; na kwa kujitolea katika mwito wao, 57-61; 289.27; wapinzani wameipatia desturi (matendo) kipaumbele kuliko kazi za mwito anaoutaka Mungu, 225.25; 293.48; katika kila binadamu, tendo jema la mwito halisi linapasa kuifuata imani, 254.32. Tazama pia Ukamilifu; Kazi
Nadhiri za Utawa, 52–62; 312–31; 283; 333; mabishano, 285.9; kwanza, yalikuwa ya hiari, lakini yakawa jela, 52–57.2; nadhiri haipaswi kulazimishwa bali inapasa kuwa ya hiari katika mambo yaliyo chini ya uwezo wa binadamu, 54–59.27; lakini inajulikana vyema ni kwa kiasi gani usafi wa kudumu unakuwa katika uwezo wa binadamu, 54–59.28; nadhiri haziwezi kubadilika au kukomesha asili za binadamu,
738
250.8; 251.16; 257.51; wala haziwezi kubadilisha au kubatilisha Neno la Mungu, utaratibu, na amri, 33.8; 35–37.24; 57–58.18; 293.51; nadhiri dhidi ya uchaji (kafiri), inayofanywa kinyume cha amri ya Mungu, ni ile iliyobatilika, 60.40; chini ya Upapa, kwa kujigamba, ilisemekana kwamba, nadhiri za utawa ni sawa na Ubatizo, 52–57.11; 287.20; 220.3 (XIV); zilisifiwa zaidi kuliko ubatizo, 52–57.13; ilidaiwa kwamba, zinapokea msamaha wa dhambi, 285.11; 296.65; 347.48; 220.3 (XIV); 60–66.43; 289.30; ni tusi kwa Injili, 285.11; nadhiri za utawa ni kinyume cha Injili, 19–20.4; 59.36; huduma za Mungu zisizofaa na danganyifu, 55–60.39; matendo ya ibada yasiyomjua Mungu, 296.65; yaliyobatilika, 55–59.36; 294.57; kuna dhana nyingi zisizokuwa za kumcha Mungu na makosa yanayoambatishwa nazo, 56–62.61; nadhiri zinazofanywa katika vijana, 34.26; 37.26; 285.9; kanuni fulani za kanisa na sheria za Kuhani Mkuu wa Roma zinabatilisha nadhiri zinazotolewa chini ya umri wa miaka kumi na mitano, 59–64.31. Tazama pia Maisha ya Utawa; Watawa wa Kiume; Nadhiri Nadhiri, nadhiri ya usafi imesababisha uasherati usiowahi kutokea na ubaya wa kuchukiza sana, 34–37.18; nadhiri zote za usafi zilizo nje ya ndoa zinalaaniwa na kubatilishwa na Amri ya Sita; tazama
pia Amri, nadhiri zinazofanywa miongoni mwa vijana, 34-37.26. Tazama pia Nadhiri za Utawa
Nafsi, mtu wa asili, tazama Asili ya Binadamu; Dhambi ya Asili; Nia; mtu wa kale, tazama Adamu wa Kale; Asili ya Binadamu; Kiumbe wa Kale; mtu mpya, (kiumbe), 371.12; 587.63; 591.81; tazama pia Maisha, Mapya; Kuzaliwa Upya; mtu wa ndani katika wale wanaomwamini Kristo, 621.3; katika imani ya Utatu Mtakatifu, tazama Mungu, katika Kristologia, tazama Kristo, Kristo kama binadamu: haki yetu hutegemea nafsi nzima ya Kristo, 585.55; imani huitumainia nafsi ya Kristo, 606.58; nafsi ya binadamu: kuna tofauti baina ya nafsi ya kiumbe binadamu na dhambi ya asili, 512.20; hata hivyo, mtu mzima amepotoshwa na dhambi ya asili, 560.6; 569.53; tazama pia Asili ya Binadamu; Dhambi ya Asili; mtu lazima akubaliwe mbele za Mungu kwa sababu ya Kristo pekee kabla ya matendo yake ya kumpendeza Mungu, 609.8; tazama pia Imani; Kuhesabiwa Haki; Matendo; Mungu haijali sala kwa sababu ya mtu, bali kwa sababu ya Neno lake, 463.16
Nafsi, si yenye afya kwa sababu ya dhambi, 318.11; tazama pia Asili ya Binadamu; Dhambi ya Asili; katika wongofu na kuzaliwa kwa pili, Mungu haiangamizi kabisa na huiunda ariki mpya ya nafsi kutoka
ombwe, 516.14; 591.81; tazama pia wongofu; Kuzaliwa kwa Pili; Chakula cha Bwana ni mlo wa nafsi, 493.23; mwili na nafsi jinsi kama kielelezo cha muungano wa binafsi, tazama Kristo, nafsi katika Purgatorio, tazama Purgatorio; majadiliano iwapo Kristo alishuka kuzimuni katika nafsi yake tu, au katika uungu wake tu, au akiwa na mwili na nafsi, 541; Siku ya Watakatifu Wote, 309.12; Kuoga kwa Nafsi, 309.12
Nathani, 188.56
Ndoa, 382-386; 430-433; ni agizo la kimungu, sheria ya kiasili isiyobadilika, 250.9; iliyoanzishwa mwanzoni, wakati wa uumbaji wa binadamau, 217.14; kusudi lake: Mungu alimuumba binadamu kwa kuzaa, 33.5; ni muhimu siyo tu kwa sababu ya kuzaa lakini pia kama dawa kwa ashiki mbaya, 251.13; ili kuepukana na makosa ya kutisha, uzinifu, uasherati, na uovu mwingine, 33-35.3-9; 3437.15; 432.212; kuwawezesha watu kuwa safi, 252.19; inampendeza Mungu, 256.48; Mungu huiheshimu na huisifu, 431.206; ni takatifu katika waumini kwa sababu imetakaswa kwa Neno la Mungu, 253.28; si chafu, jinsi wapinzani wanavyodai, 253.26; kabla na juu zaidi ya kazi zingine, 431.209; ni hali ya ulimwengu, 382.1; 382.3; hata hivyo, ina Neno la Mungu
740
ubavuni mwake na si ubunifu au asasi ya binadamu, 382.3; inapaswa kuhesabiwa mara mia moja kuwa ya kiroho zaidi kuliko hali ya utawa, 382.3; Mungu ameibariki sana zaidi ya kazi zingine zote, 431.208; katika Maandiko Matakatifu, Mungu aliiamuru isharifiwe sana, 34-37.19; huonyesha ndoa ya Kristo na kanisa, 385.16; ubikira ni kipawa bora sana lakini si ubikira wala ndoa hustahili kuhesabiwa haki, 254.38-39; 260.69; amri na uumbaji wa Mungu huwaelekeza wote wasiobarikiwa kuwa na kipawa cha ubikira waoe, 53- 58.20; mafundisho yanayokataza ndoa ni mafundisho ya Ibilisi (pepo wabaya), 34-37.22; 47-51.29; 258.63; haipaswi kutanguliwa/kuvunjwa, 252.23; 258.63; 260.71; talaka iliruhusiwa katika Agano la Kale, 444.295; lakini imekatazwa katika Agano Jipya, 446.306; si hata kwa sababu ya tofauti katika imani (dhidi Waanabaptisti), 550.19; 703.24; wajibu wa watu waliooa, 363.11-12; 377.6-8; tazama pia wazazi; Mungu ameuweka msalaba katika cheo hiki, 385.14; Ibilisi husababisha huzuni nyingi katika hiyo, 383.5; matumizi mabaya ya jina la Mungu katika mambo ya ndoa, 408.53; 410.68; ni jambo la ulimwengu, na kila mji na nchi inapasa kuruhusiwa kuendeleza desturi zake, 382.1; yeyote anayetaka kuiita sakramenti, anapasa kuitofautisha bado na zile
zilizo ishara bainifu za Agano Jipya na shuhuda za neema na msamaha wa dhambi, 217.14; maaskofu wana uwezo na mamlaka katika mambo ya ndoa kwa haki ya binadamu lakini wanapoupuuza wajibu huo, watawala wanapaswa kutoa haki kwa watawaliwa wao, 64–71.29; mwanzoni, hukumu ya mambo ya ndoa ilikuwa ya mahakimu, 352.77; kwa kuwa maaskofu wamezitunga sheria fulani zisizokuwa za haki kuhusu ndoa na wanazitumia katika vitala vyao, uanzishwaji wa michakato mingine ya haki inahitajika, 353.78; sheria kama hizo zisizokuwa za haki ni pamoja na desturi kuhusu mahusiano ya kiroho, yanayokataza kuoa au kuolewa tena kwa mtu asiye na hatia ya uasherati katika ndoa baada ya talaka, na kuziidhinisha ndoa za siri katika kuzivunja haki za wazazi, 353.78
Ndoa za Makasisi, 33-37; 248-260; 332; makatazo yake ni jambo la sheria ya kibinadamu hasa, 257.56; za pekee kwa udhalimu wa Kuhani Mkuu wa Roma, 252.25; hawakuwa na mamlaka wala haki ya kuzikataza, 332.1 (XI); sheria hii haina haki, 352.78; kinyume cha Neno la Mungu na amri yake, 34-37.18; kwa agizo na amri ya Mungu, 432.213; kwa sheria takatifu na ya asilia, 249.6; 258.60; hasa kuzitangua ndoa zilizoko, 33-36.13; 249.3; 252.23; pia kinyume cha kanuni za kanisa na sinodi, 33-36.13; 249.3, 6;
252.23; 258.60; sheria ya useja wa kudumu ni “mafundisho ya pepo wabaya,” 258.58; 258.63; alama ya ufalme wa Mpinga Kristo, 252.25; isiyokuwa ya Kikristo, 332.1 (XI); nyakati za zamani, ilikuwa kawaida kwa makasisi kuwa na wake, 3335.10; 259.67; hata Papa Pio wa Pili aliiunga mkono, 33.2; 34.13; useja ilianzishwa kwa lazima, 33-35.12; makasisi wengi wasiokuwa na hatia wameuawa, 34-37.23; 249.3; 257.57; 260.70-71; useja haustahili kuhesabiwa haki kuliko ndoa, 253.26; 254.36; sheria haikatazi ndoa bali ashiki mbaya, na kwa hiyo, useja si lazima uwe mtakatifu, 254.35; una uovu wa kujisingizia tu wa uchaji, 249.5; nadhiri ya useja imesababisha makosa, uzinifu, uasherati, ubaya wa kuchukiza sana, kashfa, dhambi, na uharibifu wa maadili ya umma, 34-37.18; 249.6; 257.51; 332.1 (XI); 347.48; 432.213-216; Mungu hulipiza kisasi kwa wale wanaokidharau kipawa cha Mungu mwenyewe na agizo kwa kuikataza ndoa, 257.53; sheria ya useja ni ya ushirikina na hatari, 249.6; 253.26; 256.50; 258.60; wapinzani hubisha kwa sababu moja tu, udhibiti wao (utawala), 249.5; 258.60; makasisi waiaminio Injili wameoa ili kuepukana na makosa, uzinifu, na kashfa za umma, 3335.3; waseja wachafu, wanapaswa kuwa waume safi, 259.66. Tazama pia Useja; Usafi, Ndoa; Ubikira;
Nadhiri
Neema, ya mwanzo (neema ya awali), 93.17; 120-122; 144; kwa usahihi zaidi, imani inaweza kuitwa “neema inayotufanya tumpendeze Mungu,” 110.116; msaada wa neema, 85.23; neema kwa wote, tazama Uchaguzi, Mungu haitoi kwa yeyote mbali na Neno la kinje (dhidi ya Walokole), 329.3; Mungu huitoa kwa njia ya Ubatizo, 485.41; sakramenti ni ishara zake, tazama Sakramenti; Mungu hatuwii neema, 693.60; wataalamu wa uanazuoni wamedai kwamba, kwa lazima, Mungu huitoa kwa wale wayatendao matendo mema, lakini wazo hili linakataliwa, 92.11-12; hata wale ambao wamehesabiwa haki tayari, hawaistahili kwa njia ya Mapokeo ya binadamu, 221.12; mapenzi ya kibinadamu hayawezi kulifanya lolote ili kujitayarisha yenyewe kuipokea kwa uwezo wake wenyewe, 515.11; 572.3; 590.77; tazama pia Kazi ya Mungu na Binadamu Pamoja; hatuwezi kufahamu ukuu wake hadi tuzitambue dhambi zetu kwanza, 87.33; tunaipokea kwa imani, 39.28; 66-73.52; tazama pia Imani, ni lazima kuitegemea, yaani, rehema za Mungu anayeahidi kwamba, kwa ajili ya Kristo, tunakubaliwa, dhambi ya asili hutufanya tukate tamaa kwayo, 83.8; dhambi zetu humzuia Mungu kuwa mwenye rehema kwetu, kwa sababu hatutubu, 305.14; Mungu
huiahidi kwa wale wanaompenda na wanaomtegemea kwa mioyo yao yote, 364.22; 405.32; neema wakati wa vyakula, tazama Baraka Mezani. Tazama pia Kuhesabiwa Haki; Rehema; Ahadi Nyundo ya Mungu, sheria, 318.2
Neno (Logos), katika mafundisho kuhusu Mungu na Kristo, 9–10.6; 635.36; 657.16
Neno la Mungu, tazama pia Injili; Sheria; Biblia; Agano
A. Hakika na uwezo: haviwezi kudanganya, 488.57; 530.13; ni kweli ya milele, 557.13; huanzisha pekee mafungu ya imani, 310.15; kanuni ya kuongoza tu na utawala wa mafundisho yote, 556.9; katika msingi wake tu ndipo maamuzi kuhusu mafungu ya imani yanaweza kufanywa, 574.8; si zembe wala haijafa, bali inafaa na ni hai, 416.101; haitokei bila matunda, 416.101; itafanikisha alilolikusudia Mungu, 216.11; ni mzamili wa zaidi ya sanaa elfu mia moja, 395.12; humshinda, humwangamiza, na humfukuza ibilisi, 394.10–12; 416.102; huwachopoa wateule kutoka mataya ya ibilisi, 696.76
B. Matokeo: Mungu hafanyi kazi bila hayo, 516.13; kadhalika Roho Mtakatifu, tazama Roho Mtakatifu, Mungu hawezi kushughulikiwa na hawezi kufahamika kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kwayo,
101.67; hatuwezi kuthibitisha lolote kuhusu mapenzi ya Mungu bila hayo, 222.17; 457.38; na kanisani, 458.52; ufalme wa Mungu hutujia kwayo, 469.53; Mungu huwaitia binadamu wokovu, huwaongoa, huwapatia kuzaliwa upya, na huwatakasa kwayo, 584.50; 688.33; 690.44; imani inatolewa kwayo, tazama Imani, na msamaha wa dhambi, 494.31; 503.14; katikati ya majuto makubwa, tunahuishwa kwa neema itolewayo nayo, 187.49; Mungu huhuisha kwayo, 186.40; hutufanya sote kuwa watakatifu, 414.92
C. Mahusiano: Neno na Kanisa, tazama Kanisa, na sakramenti, 220.5; 327.1; 10; 482.18; 485.45–46; 491.4, 9; 492.10; 632.21; Neno la Mungu tu ndilo lionyeshalo ibada sahihi, tazama Ibada; ni hazina inayokifanya kila kitu kitakatifu, 414.91
D. Neno lisemwalo: kwalo, msamaha wa dhambi unahubiriwa ulimwenguni kote, 327; linafaa kwa sababu ya agizo na amri ya Kristo, hata wakati linahubiriwa na watu waovu, 14.2; 168.19. Tazama pia Huduma; Wahubiri; Kuhubiri; Tangazo
E. Kusema: ni jambo la kweli takatifu, 414.91; johari na madhabahu matakatifu, 418.117; ni mapenzi ya Mungu kwamba, watu walisikie, 415.95; 514.5; 586.57; na wajifunze 415.98; lazima tuliweke
743
moyoni mwetu daima, midomoni mwetu, na masikioni mwetu, 415.100; ni lazima kuomba kwamba, Mungu aimarishe imani kwa njia ya mazoezi ya kila siku katika kulisoma na kulitumia, 576.16; mtu ambaye bado hajamgeukia Mungu na hajazaliwa mara ya pili anaweza kulisikia na kulisoma kwa nje, 585.53; ibilisi huroga na kudanganya mioyo mingi ili aweze kuichukua tena, 415.99; kusudi la ibilisi ni kutufanya tulibeze na kulidharau, 476.104; shaka kulihusu neno huishikilia asili ya binadamu, 96.35; kulipuuza ni miongoni mwa matunda ya dhambi ya asili, 318.2; wengi wanalidharau, 690.41; lazima lipitie mateso na kukufuru, 439.262; 443.289; Mungu atawaadhibu wote wanaolidharau na kukataa kulisikia na kujifunza, 415.95; inatupasa tuitambue hukumu ya Mungu wakati Mungu anaindoa mahali, 692.57; 693.58; wanaolibeza hufa na kuangamia katika dhambi zao, 586.57; Mungu huwafanya wagumu, huwakataa, na huwalaani wanaolidharau, 690.40
F. Ufasiri: Kristo mwenyewe ndiye mwaminifu kuliko wote na mfasiri walo wa kutegemewa 638.50; wapotoshaji hulipotosha kwa uovu ili lizifae ndoto zao zisizofaa, 202.123
Nguzo, kisahihi, kanisa linaitwa “nguzo . . . ya ukweli” (1Tim.3:15), 168.20; si papa, 169.27; katika
mambo ya kiroho na matakatifu, binadamu ni kama nguzo ya chumvi, 577.20
Nidhamu, ya mwili, tazama Mazoezi; nidhamu ya kinje ya sheria, tazama Sheria, haki ya raia aina hiyo ni nzuri, lakini inabidi itofautishwe na haki ya kiroho, 216.9; tazama pia Haki, Watu Waiaminio Injili hawaikatai, 48- 51.30; nidhamu ya kanisa, tazama Maaskofu; Kutengwa na Kanisa,
Nidhamu ya Kanisa, tazama Kutengwa na Kanisa
Nikea, Sinodi ya (325), 2; 3; 9-10.1; 34; 36; 173.42; 339.12-13; 340.17
Njia, Mungu hajishughulishi nasi isipokuwa kwa njia ya kinje ya Neno la nje na sakramenti, 330.10; 516.13; 550.22; 573.4; 583.46; 696.76; 703.30-32; njia za Roho, tazama Roho Mtakatifu; imani pekee ndiyo njia ambayo kwayo, tunamshika Kristo, ahadi ya Injili, neema ya Mungu, na msamaha wa dhambi, 518.5; 595.10; 600.31; 601.38; tazama pia Imani
Njia, Uislamu, 9
Nta, wongofu hautokei kama mhuri unaobanwa kwa nta, 592.89
Nyenyekea, Unyenyekevu, sala ya tano ya Sala ya Bwana linatumika kutufanya wanyenyekevu, 475.90; haki ya imani inafichwa wakati watu wanavutiwa na unyenyekevu
744
wa uongo wa watawa wa kiume, 55-61.48; chini ya Upapa, watu waliambiwa kwamba, unyenyekevu katika kuhesabiwa kwa dhambi, hakika kungestahili neema ya Mungu, 322.19
Nyimbo za Dini, Nyimbo za Dini za Kijerumani katika Misa, 38-41.2; 260.3-4; 403.25
Nyumba/Kaya, 422.142; tazama pia Amri Odysseo, 276.71-72
Ofisi/huduma, 19–22; 229–231; Mkristo anaweza kuwa na huduma serikalini akiwa na dhamiri nzuri na wazi, 702.18–19; huduma za kanisa: huduma ya askofu ni kuihubiri Injili, kusamehe dhambi, kuichunguza imani, na kuwatenga na jumuiya ya Kikristo ambao maisha yao ya kutomcha Mungu ni wazi, 64–70.21; tazama pia Maaskofu; ya makasisi, tazama Makasisi; ya funguo, tazama Ondoleo la Dhambi; Funguo; ya kuhubiri, 13; Mungu aliianzisha, 12.1; manufaa ya milele hayawezi kupatikana isipokuwa kwa hii, 63–70.8–9; haiingilii amani ya umma na mamlaka ya ulimwengu, 63–70.10; sasa, imekuwa huduma tofauti kabisa kuliko ilivyokuwa chini ya papa, 361.26; huhusisha masumbufu na kazi, hatari nyingi, na mashambulizi, lakini Kristo mwenyewe atakuwa zawadi, 361.26–27; tazama pia Injili;
Huduma; Wahubiri; Kuhubiri; Neno la Mungu; huduma yote ya kanisa lazima ithaminiwe sana, 329.2 (VIII); wanafiki na wasiomcha Mungu wanaweza pia kuwa na huduma kanisani, 164–176; hata Mpinga Kristo, 165.4; huduma ya Kristo, tazama Kristo; ya Roho Mtakatifu, tazama Roho Mtakatifu; ya sheria na Injili, tazama Injili, Sheria. Tazama pia Wito; Kazi
Ondoleo la dhambi, 177.1; 177.2; 197.99; 371; si lolote isipokuwa Injili, 185.39; 190.61; si hukumu bali usimamiaji wa karama ya mtu mwingine, 198.105; si neno la mtu bali Neno la Mungu (sauti kutoka mbinguni), 43-44.3-4; 186.40; 197.99; 689.38; ni uwezo wa funguo, 185.39; 329.1 (VIII); tazama pia Funguo, sehemu kuu katika ungamo, 190.61; linaweza kuitwa sakramenti ya toba, 186.41; 216.4; hupatanisha na Mungu, 689.38; ni faraja na msaada dhidi ya dhambi, 329.1 (VIII); kimbilio la kweli kwa moyo unaohisi dhambi, 503.14; huhitaji imani, 43-44.4; 177.2; 190.61; lilianzishwa na Kristo, 329.1 (VIII); limeagizwa na Mungu, 216.4; halipaswi kukanwa, uhifadhi wa daawa haupaswi kulizuia, 214.177; liliamuriwa na Kristo, 503.14; amri ya kusamehe dhambi, si ya kudadisi siri, 197.104; mtu wa kawaida mmoja anaweza kulitoa kwa mwenzake, 350.67; ondoleo la dhambi la faragha halijaagizwa, bali
limetolewa kama msaada, 503.13; linapasa kuhifadhiwa, 16-17.1; 197.100; 329.2 (VIII); kama hazina ya thamani kubwa, 504.20,22; lilifichwa chini ya upapa, 177.2; 201.122; 225.25; 322.20; 501.1; uwezo wa ondoleo la dhambi haukuelezwa kwa waungamaji, 322.20; lilibakia kuwa lenye mashaka, 504.17; miongoni mwa Waiaminio Injili, mbaraka wa ondoleo la dhambi umeelezewa kijuujuu na umeleta faraja, 177.2. Tazama pia Ungamo; Funguo
Opus Operatum, rai ya walokole kuhusu opus operatum ya sakramenti imesababisha matumizi mabaya mengi, 218.23; huduma ya Roho hupigana na matumizi ya opus operatum 273.59. Tazama pia kwa njia ya tendo lenyewe
Papa (Askofu wa Roma, Upapa, Kuhani Mkuu wa Roma), 313–316; 337–354
A. Kujifanya: hutaka kuitwa “bwana mwenye neema sana,” 313.2; wapinzani wanadai uwezo usiokuwa na mipaka kwa Baba Mtakatifu wa Roma, 169.23; hudai kuwa kichwa cha kanisa kulingana na haki ya kimungu, 315.13; mwakilishi wa Kristo duniani, 337.3; bwana wa ulimwengu wote, 169.23; 315.13; kama mungu wa kidunia, 315.13; mwenyewe amejiweka kuwa sawa na, na hata kuwa mkuu kuliko Kristo, 313.4;
315.13; 345.40; anadai kuwa nguzo na msingi wa kweli (1 Tim. 3:15), 169.27; kuwa na mamlaka juu ya nafsi baada ya maisha haya, 345.40; na hata kuwaamuru malaika mbinguni, 315.13; huhamisha funguo kwa utawala wa ulimwengu, 344.36; hudai kuwa na panga zote mbili, wa kiroho na wa kidunia, 169.23; 337.2; hutaka kumsimamia Kaisari, 169.23; 347.50; hudai uwezo wa kutunukia na kuhamisha mamlaka ya kifalme, 169.23; 337.2; aliwasumbua watawala kwa kuwatenga na kanisa na kwa vita visivyokuwa vya haki, 343.35; alijaribu kunyakua himaya, 343.35; hudai ukuu kwa haki ya kimungu juu ya maaskofu wote, 337.5; huweka mamlaka yake juu ya hukumu ya sinodi na ya kanisa lote, 345.40; 347.49; hapendi kuhukumiwa na yeyote, 345.40; 347.50; hudai mamlaka ya kutengeneza sheria zinazohusu ibada, mabadiliko katika sakramenti, na mafundisho, 169.23; 337.6; 345.40; hudai kwamba, Wakristo hawawezi kuokolewa hadi wamtii yeye katika mambo yote, 313.4; 315.12; 337.3; 337.6; 344.36
B. Shughuli kanisani: chini ya Upapa, imani ilifichwa kabisa na hakuna aliyemtambua Kristo kama Bwana, wala Roho Mtakatifu kamaanayetufanya watakatifu, 457.43; katika mafundisho ya papa, hakuna lolote kabisa kuhusu Kristo, imani, na amri za Mungu,
746
316.14; papa huuficha utukufu wa Kristo, huziiba dhamiri za maliwazo yakini, na huangamiza ibada ya kweli, 346.44; hamtaki Kristo, does not want Christ, 305.15; huyabuni maumbo ya ibada yasiyokuwa ya kumcha Mungu na kufundisha kinyume cha Injili, 169.23; 316.14; 344.38; 348.57; tazama pia Misa; Watakatifu; mafundisho ya papa yanatoa maagizo katika kazi rahisi na kazi ya mpumbavu, 316.14; 334.4–5; kwa vyovyote vile, imetolewa kutoka sheria ya kifalme na ya kipagani, 316.14; ilianzisha mwaka wa jubilii wa kuleta pesa, 323.25; huuza stahili za Kristo pamoja na stahili nyingi mno za watakatifu, 311.24; ndiye kichwa na mlinzi mkuu wa wezi wote, 435.230; jinsi alivyofuja pesa nyingi zaidi ndivyo koo lake lilivyokuwa kubwa, 323.25; tazama pia Vyeti vya Upatanisho; ni bawabu wa gereza, ibilisi wa Mungu na chakari, 502.6; angependa kuuona Ukristo wote wameangamia na kila nafsi imelaaniwa kuliko kujiruhusu mwenyewe kuongolewa, 302.3; haruhusu majadiliano ya kikanisa kuamuliwa kwa usahihi, 347.49; huwafungisha watumishi wake kwa viapo vya kutisha na laana kwa kusudi la kuutetea udhalimu wake, 348.55; huyatetea makosa yake ya kuogofya na uovu kwa vurugu, 345.40; 347.49; 347.51
C. Uhakiki: Kristo hakuwapatia mitume uwezo wa upanga wala haki
ya kuanzisha, kumiliki, au kutupilia mbali falme za ulimwengu, 343.31; papa hawezi kuwa mkuu kulingana na haki ya kimungu katika kanisa lote wakati kanisa linamteua na wakati desturi ilikuja kuenea polepole kiasi kwamba, Kaisari alimthibitisha, 341.20; Injili inaonyesha kwamba, Askofu wa Roma si mkuu kwa haki ya kimungu kwa maaskofu na wachungaji wengine, 338.7–11; jinsi ushuhuda wa historia ufanyavyo, 339–341; hakukuwa na ubwana wala ukuu miongoni mwa mitume, 338.8; Petro hakuwa na mamlaka maalumu yoyote, cheo kikubwa, au ubwana miongoni mwa mitume, 342.24; kanisa lilikuwa bila papa kwa zaidi ya miaka mia tano, 313.4; katika makanisa ya Kiyunani na ya Kilatini, kuwekewa mikono na kipaimara havikuhitajika kutoka Askofu wa Roma, 340.15; sinodi nyingi za kale yaliitwa na kufanyika ambayo hakuyaongoza, 340.17; Sinodi ya Konstanz liliwaondoa akina papa watatu na lilimteua wa nne, 314.7; Sinodi ya Nikea liliamua kwamba, askofu wa Roma angesimamia tu makanisa ya “viungani,” 339.12; Hieronimo na Gregorio waliupinga ukuu wa Askofu wa Roma, 340.18–19; papa si kichwa cha kanisa “kulingana na haki ya kimungu,” 313.1; 314.7; 315.13; Melanchthon alikuwa tayari kumpatia papa ukuu wake juu ya maaskofu “kwa haki ya
kibinadamu,” kwa ajili ya amani na umoja, 333; kanisa halihitaji kichwa ulimwenguni, 314.5; kanisa haliwezi kuongozwa vyema na kulindwa kuliko iwapo sote tungeishi chini ya kichwa kimoja, Kristo, 315.9; papa hana uwezo wa kuyatoa maagizo dhidi ya mwafaka wa manabii, 191.66; ni askofu tu, au mchungaji wa kanisa la Roma, 313.1; Upapa si wa lazima kanisani, kwa sababu hautumii ofisi yoyote ya Ukristo, 314.6; Kristo, manabii, na mitume hulifasili kanisa kwa njia tofauti sana kuliko ufalme wa Papa ufanyavyo, 169.26; Upapa ulihuishwa na ibilisi, 314.5; papa ni mtume wa ibilisi, 315.14; 680.20; Mpinga Kristo, 222.18; 315.10, 14; 345.39; 348.57; 680.20, 22; laana, anathema, 344.38; kwa hiyo, fulani asimtii bali anapaswa kumpinga, 315.14; 316.16; 344.38; 346.41; 348.57; 680.20; jinsi Kristo alivyoamuru, 346.41; fulani asije akawa mshiriki katika mafundisho yake yasiyokuwa ya kumcha Mungu, kukufuru, na ukatili usiokuwa wa haki, 346.41; 348.59; 680.22; watawala lazima wauzuie ukorofi wa mababawatakatifu na lazima wamkemee papa anapoepa na kuzuia upelelezi wa kanisa na hukumu ya kweli, 348.56
Paradiso, 561.10
Pasaka, 67.57; 173.40; 174.43; 171174; 496, mbele ya Baraza la Nikea,
wengine waliifuata Pasaka wakati mmoja, baadhi wakati mwingine, 48-52.43; 171.32; 173.42. Tazama pia Siku; Mabishano ya Pasaka ya Wayahudi
Paulo, 463.15; 671.77; mtetezi thabiti wa mafundisho ya Injili kwamba, Mapokeo ya binadamu si za lazima kwa kuhesabiwa haki, 228.50; anaizungumzia imani tofauti na wafanyavyo wataalamu wa ghiliba, 296.67– 68; alijichukulia mwenyewe kama mwenye haki, kwa njia ya neema, kwa sababu ya Kristo, 145; hakuwekewa mikono wala kuthibitishwa na Petro, 338.10; maneno ya Yakobo hayapingani na ya Paulo; ni baba wa kiroho, 424.158–425.160; aliapa daima, 410.66
Paulo, 147; majuto yake makubwa, 181.8; 185.36; kukata tamaa kwake, 320.7; sababu ya kuangamia kwake, 407.45–46
Petro, 342.27–28; 343.29–30; 463.15; 634.33; 671.77; imani ilifanya tofauti baina ya majuto yake makubwa na ya Yuda, 181.8; 185.36; tazama pia Majuto Makubwa; msamaha wa Petro baada ya kukana kwake ni mfano wa rehema ya Mungu, 237.5; 243.36; na Kornelio, 330.8; azimio lake kuhusu ukuhani wa kifalme (1 Petro 2:9), 351.69; onyo lake kuhusu manabii wa uongo (2 Petro 2:1), 249.5; alibashiri kutokea kwa maaskofu wasiomcha Mungu siku
748
zijazo (2 Petro 2: 13-15), 354.82; neno lake linawekwa dhidi ya wanaofasiri kuhusu Sentensi/Fetwa, 192.70; alijiita mwenyewe mzee wa kanisa/mpresbyteri, 349.62; mwito wa Paulo haukutegemea mamlaka ya Petro, na Paulo hakumtambua kama mkuu wake, 338.10; Paulo anakana kwamba, mamlaka ya Petro yanayashinda yale ya wengine au yale ya kanisa, 339.11; katika misemo mingi, anawakilisha kundi lote la mitume, 341.22; 341.23–24; “mwamba” (Mathayo.16:18) si mamlaka yake bali huduma ya ungamo lake, 342.25; imani yake na ungamo (kufuatana na Krisostomo na Hilario) 342.28; 342.29
Pinga, wale wanaompinga Roho Mtakatifu kwa kuchagiza hawataongolewa, 586.60; 591.83, tazama pia Wongofu; Wakristo wanapompinga Roho Mtakatifu, wanapoteza imani, neema ya Mungu, haki, na wokovu, 612.31. Tazama pia Maasi
Polifemo, 242.35
Poluksi, 242.32
Purgatorio, 182.13; 183.26; 200.118; 204.132; 204.136; 207.147; 210.156; 212.167; 274.64; 280.90; 309.12; 322.22; 323.26
Riba, 304.12
Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu pekee anaitwa Roho Mtakatifu,
456.36
A. Nafsi ya Roho Mtakatifu
Nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, 2-3.7; 3-5; 305; 366.5-6; 399.13; 456-460; katika shauri la Ubatizo, 365.4; 391.28; 390.21; 480.4; katika shauri la ondoleo la dhambi, 373.28; litokalo kwa Baba na Mwana, 3.7; 4.22; 305; 670.73; si mwendo ulioumbwa katika viumbe vyote, 9-10.6
B. Kazi ya Roho Mtakatifu
1. Kazi: 366.6; watakatifu hujaliwa vipawa vilivyoumbwa, 670.73; huanza na kila siku huuongeza utakatifu katika nchi kwa njia ya Kanisa la Kikristo na msamaha wa dhambi, 459.59; hutenda kazi iliyo ngeni (kuhukumu) ili kuja katika kazi sahihi ya Roho (kufariji na kutangaza neema), 617.11; 624.14; kutolewa na hupokewa si kwa njia ya sheria lakini kwa njia ya Injili, na hufanya moyo kuwa mpya, 624.11; lakini wapinzani hufikiria kwamba, Roho Mtakatifu anaweza kutolewa bila athari yoyote, 100.63; hutolewa kwa njia ya Ubatizo, na huanza kuiua ashiki mbaya na kuiunda misukumo mipya katika binadamu kiumbe, 87.35; hushindana na (hukataa, hufisha) mabaki ya dhambi ya asili katika asili ya binadamu, 89.45; 114.146; 326.40; 326.44; 581.34; hufisha matendo ya mwili, 113.143; hutoa msamaha wa dhambi, 366.6;
459.55; humfunua Kristo, 112.132; 460.65; hutuita na kutuongoza hadi kwa Kristo kwa njia ya Injili, 366.6; 457.38; hutuongoza hadi kwa ufalme wa neema, 468.52; huleta vipawa vya upendo, sala, shukrani, usafi, uvumilivu na kadhalika, 112.132; sheria haiwezi kuwekwa bila Roho Mtakatifu, 101.70; 112.130; tazama pia Sheria;wala hatuwezi kuogopa, kupenda, na kumwamini Mungu kuliko vitu vyote, 21-22.2-3; 84.10; 112.130; huumba ndani yetu upendo kwake Mungu na kwa jirani yetu, 598.23; matendo na matunda ya Roho, 625.17; huishi katika wateule na huwalazimisha kuzitii amri za Mungu, 695.73; watu wanatenda mema tu kiasi kwamba na mradi tu Roho Mtakatifu awalazimishe, 587.63; matendo mema ni ushahidi wa uwepo na Roho Mtakatifu aliye mioyoni mwao, 523.15
2. Masharti ya kazi:
a. Roho Mtakatifu, Neno na sakramenti: hutolewa kwa njia ya Neno la Mungu (Injili), 21-22.3; 112.135; 585.54; Mungu hampi yeyote Roho Mtakatifu mbali na Neno la nje (dhidi ya Wenye Shauku), 13.4; 329.3; Roho Mtakatifu anatolewa kwa njia ya kuihubiri Injili na utoaji wa sakramenti, 12.1-2; 63-69.9; kwa njia ya Ubatizo, 87.35; 485.41; hakuna nabii aliyempokea Roho nje ya au bila neno lisemwalo la
Amri Kumi, 330.10-11; lolote linalojigamba kwamba, limetoka kwa Roho mbali na Neno la nje na sacramenti ni la Ibilisi, 330.10; Neno ni huduma ya Roho, 687.29; kazi na tendo la Roho Mtakatifu, 585.56; hutenda kazi kwa njia ya Neno (kuhubiri kwa Injili), 186.44; 457.38; 459.58; 514.4; 573.5; 581.38; 585.55; 696.77; kwa njia ya neno (Injili) na sakramenti, 13.12; 275.70; 513.1; 587.65; 596.16; Neno (Injili) na sakramenti ndivyo njia (vyombo) vya Roho Mtakatifu, 13.1-2; 514.4; 516.13; 517.19; 573.4; 584.48
b. Roho Mtakatifu na kanisa, 164175; 456-460; matendo kwa njia ya kanisa, 456.37; 460.61; vitabaki na jumuiya takatifu hadi Siku ya Mwisho, 458.53. Tazama pia Kanisa
c. Roho Mtakatifu hutolewa na hupokewa kwa njia ya imani, 25-28.29; 97.45; 111.125, 94-97; 119.175; 236.15; waliozaliwa mara ya pili hupokea Roho Mtakatifu, 194.82; Mungu hutoa Roho Mtakatifu pia kwa watoto wadogo waliobatizwa, 176.3
d. Uongozi wa Roho Mtakatifu si wa shurutisho bali ni wa hiari, 587.64; 609.12; 621.3; 623.6; 625.17; 626.25; wakati Roho Mtakatifu ametekeleza na amefanikisha kuzaliwa upya na wongofu, nia ya binadamu mpya ni chombo na ala ya Roho Mtakatifu, 517.18; tunapokea
tu matunda ya kwanza ya Roho katika maisha haya, 588.68; vita vya mwili dhidi ya Roho huendelea hata katika wateule, tazama Mwili; wale ambao wamehesabiwa haki mara moja wanaweza kumpoteza Roho Mtakatifu, 17.7; kwa njia ya dhambi ya makusudi (kutenda dhidi ya dhamiri), 523.19; 588.69; kwa njia ya kuutupilia mbali upendo 126.219; imani haibaki katika wale wanaompoteza Roho Mtakatifu, 236.13; wakati dhambi inalitenda lolote ilitakalo, basi Roho Mtakatifu hayupo, 326.43; hatupaswi kuikwamisha na kuikataa kazi ya Roho Mtakatifu, 589.72
e. Roho Mtakatifu huendelea kufanya kazi bila kukoma hadi Siku ya Mwisho, 460.61-62
c. Roho wa Kristo: siyo tu Roho wa Kristo apatikanaye katika mkate wa Chakula cha Bwana bali pia ni mwili wa Kristo (dhidi ya Walioidharau Sakramenti), 630.11; wala kuwepo kwa mwili wa Kristo kunamaanisha kwamba, kwa njia ya Roho wa Kristo, miili yetu, iishiyo ulimwenguni imeunganishwa na mwili wa Kristo ulio mbinguni, 628.5; Kristo hulitawala Kanisa kwa Roho wa Kristo, 165.5; 167.16; ufalme wa Kristo ni ule ambao Kristo huufanya hai kwa Roho wa Kristo, 167.18
Roma, 34.18; 48–52.43; 201-203; 257.52, 54; 314.8; 315; 323.24; 323.25;
Rozari, 23–26.3; 182.14; 243.37; 294.53
Saa (za sala), tazama Saa Saba za Kikanuni
Saa Saba (Saa za Sala za Kikanuni), 65–72.41; 393.3
Saa za Sala za Kikanuni, tazama Saa Saba
Sababu/Ajili, ya dhambi, tazama Dhambi ya Asili; Dhambi; ya uchaguzi, tazama Uchaguzi; ajili ya tatu ya wongofu, tazama Wongofu
Sabato, maana ya neno la Kiyahudi, 412.79. Tazama pia Jumapili
Sadaka, imani inahitajika katika kuzitoa, 140.279; kutoa sadaka kunakompendeza Mungu ni kule kunakofuata kuliko kule kunakotangulia upatanisho, 133; zinaweza kuchukuliwa kama sakramenti, 217.17; lakini hazimfanyi mtu kuwa huru kutoka dhambini na mautini kwa njia ya tendo lenyewe, 133; hutumiwa vibaya na watawa na maaskofu, 220.5; 353.80
Sakafu ya Kupuria Nafaka, taswira ya kanisa, 164.1 Umeta wa Mungu, sheria, 319.2
Sakramenti, 17–18; 215–218; tazama pia Ubatizo; Chakula cha Bwana
A. Asili: 275.68–70; ni kaida zilizo na amri ya Mungu na ambazo kwazo,
751
ahadi ya neema imeongezewa, 215.3; huwa na sehemu mbili, ishara na Neno, 275.69; tusiziangalie kufuatana na barakoa bovu la nje bali kama vile ambavyo zimezungukwa kwa Neno la Mungu ndani yake, 482.19; Neno likiongezewa elementi linafanyiza sakramenti, 327.1; 368.10; 374.8; 482.18; 492.10; “Neno linaloonekana,” 216.5; tofauti baina ya sakramenti na dhabihu, 263.17–18; pepo chochezi, kinyume cha Neno la Mungu, huichukulia sakaramenti kama tendo tulifanyalo, 491.7
B. Matokeo: sakramenti na kanisa, tazama Kanisa; bila hivyo viwili, hakuna awezaye kuwa Mkristo, 479.1; si alama za ungamo tu 18.1; 215.1; bali ni ishara na shuhuda za mapenzi ya Mungu kwetu, 18.1; 215.1; 275.69; ishara za Agano Jipya na shuhuda za neema na msamaha wa dhambi, 186.42; 217.14; 271.49; 638.50; ishara na “mihuri” ya ahadi, 218.20; 275.70; 689.37; uchaguzi wetu umetiwa mhuri nazo, 546.13; zimeteuliwa kwetu kama ishara za nje, 476.98; kuamsha imani yetu na kufariji dhamiri zetu, 39–42.30; 476.98; Neno na kaida vina matokeo sawa, 216.5; kaida ni taswira ya Neno, 216.5; Roho Mtakatifu na imani hutolewa kwazo, tazama Imani; Roho Mtaktifu; imani inalishwa kwazo, 186.42; imani hupokea linaloahidiwa jinsi litolewavyo huko kwazo, 218.19;
Kristo huitoa neema yake kwa watu wote kwazo, 586.57; stahili na faida za Kristo zinatolewa, zinapewa, na kugawiwa kwetu kwazo, 685.16; huutoa msamaha wa dhambi, 186.42; 275.69–70; 276.75; 459.54
D. Matumizi sahihi: 217.18; 275.68–70; kwa njia ya imani, si kwa njia ya tendo lenyewe; 39–42.29; 182.12; 183.25; 217.18; tazama pia Misa; imani katika sakramenti, si sakramenti yenyewe, huhesabia haki (Agostino) 218.23; Misa huharibu matumizi ya sakramenti, 280.91
E. Uhalali: zinafaa kwa sababu ya agizo na amri ya Kristo, 14–15.2; hakuna sakramenti iliyo nje ya matumizi yake kufuatana na asasi nzima ya Kristo, 643.73; 645.85; 649.108; hazitokani na utakatifu wa binadamu au ustahiki bali katika Neno la Mungu, 492.16; 498.61–63; hazitegemei kuamini au kutokuamini kwa binadamu bali katika Neno na agizo la Mungu, 633.25; 634.32; 646.89; hazipotezi manufaa yao zinapotolewa na watu waovu, 14–15.2; 164.3; 168.19; 492.16; hata wasiofaa (waovu) huzitoa kwa niaba ya na mahali pa Kristo, 170.28; 175.47; hata wale wanaozipokea isivyostahiki hupokea sakramenti ya kweli ingawa hawaamini, 487.54; yeyote haruhusiwi kuzitoa bila mwito sahihi, 17–18; 218.1; uchungaji ni huduma ya sakramenti
752
inayotolewa kwa wengine, 216.7, 9; huu ni wa uwezo wa funguo au wa maaskofu, 62–69.5; 299.13; 349.60. Tazama pia Maaskofu; Chakula cha Bwana; Huduma
Idadi ya sakramenti: 215–218; toba kama sakramenti, tazama Ondoleo la Dhambi; Toba, papa huudai uwezo wa kuyafanya mabadiliko ndani yazo, 337.6; watawa wa kiume wamezibuni sakramenti kwa uhamisho wa stahili zao, 164-165
Sala ya Bwana, 366-369; 398.14; 461-481; ni aula kuliko sala zingine zote tunazoweza kuzibuni, 464.23; wachungaji wanapaswa kuiomba wenyewe na wakazi wao wa usharika, 392.3; hutuonyesha haja yetu inayopasa kutusukuma na kutulazimisha kuomba, 464.24; 465.27; ni ungamo, 503.9; katika hiyo, tuna ondoleo la dhambi mara mbili, 503.12; lazima itusaidie iwapo tutazishika Amri Kumi, 448.316; 452.3; mafungu ya kwanza matatu, 471.68; kuisema mara tano kama ridhaa, 322.21; tazama pia Ridhaa
A. Asili: katika utendewaji wake, Wakristo si lazima waelekezwe kwenye msingi na asili isiyokuwa Maneno ya Asasi ya Kristo, maneno haya yanapasa kufafanuliwa si kama tamathali, bali jinsi yanavyosimama, katika maana yao, sahihi, dhahiri, sisisi, 529.7; 532.25; 629.7; 635.38; 637.45; 650.113; mafundisho ya Wanaoidharau Sakramenti, 528-
534; 627-653; mafundisho kwamba, mkate ni kushiriki katika mwili wa Kristo tu katika maana ya kushiriki kanisani kunakataliwa, 640.59; jinsi lilivyo fundisho kwamba, imani inaelekezwa mbali kutokwa kwa mkate kuushiriki mwili wa Kristo mbinguni, 652.122; kuwepo kwa kweli kwa mwili na damu ya Kristo katika Chakula cha Bwana, 16-17; 528-534; 627-653; 660.29; Hoja za Walioidharau Sakramenti tu kuhusu uwepo wa mwili wa Kristo baada ya ufufuo zinakanushwa, 646.91; 652.119; 674.92; madhanio ya Kristologia (Uchunguzi kuhusu Nafsi ya Kristo), tazama Kristo, mkate na divai si alama tu ambayo kwayo, Wakristo wanajitambua wao kwa wao, 651.115; wala si viwakilishi tu, ishara, na taswira za mwili usiokuwepo na ulio mbali na damu ya Kristo, 532.28; 651.115; wala si ishara tu au makumbusho ya mwili wa Kristo usiokuwepo, 651.116; ni njia ambazo kwazo, na pamoja nazo Kristo hugawa mwili na damu yake (dhidi ya Wafuasi wa Schwenckfeld), 550.24; 703.32; mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo, 328.1; 492.12–14; mageuzo uwamo yanakanushwa, 328.5; 532.22; 630.14; 634.35; 649.108; mwili wa Kristo huwepo tu katika utolewaji wa nje wote wa Chakula cha Bwana kinachoonekana, jinsi Kristo alivyokianzisha, 645.86-87; kuabudu kwa elementi
753
kunakanushwa, 534.40; 631.15; 645.87; 649.108; 653.126; mwili na damu ya Kristo vipo kwa kweli na halisi na vinagawanywa kwa vitu vinavyoonekana, mkate na divai, 176.1; chini ya mkate na divai, 372.2; 629.9; “chini ya mkate,” “pamoja na mkate,” “katika mkate,” 634.35; vinaunganika kwa njia ya muungano wa sakramenti, 529.7; 530.15; 630.14; 631.18–19; 634.35, 651.117; siyo kushiriki kwa kiroho kwa mwili wa Kristo, bali kushiriki kwa kinywa, 651.114; 651.118; siyo mapokezi ya kiroho bali mapokezi ya sakramenti au ya mwili wa Kristo kwa kinywa, 639.56; tazama pia Mapokezi; kufuatana na maneno ya asasi, 637.48; lakini si katika mtindo wa Kikapernaumu, 530.15; 534.41; 538.17; 641.64; 649.105; 653.127
B. Matokeo: 493.20; 636.44; si ishara tu ya mapenzi ya watu miongoni mwao wenyewe, bali ni ishara ya mapenzi ya Mungu kwetu, 275.69; agano la Kristo, 246.2; 529.7; 638.53; 660.29; mhuri na ushuhuda wa msamaha wa dhambi, 271.49; Injili nzima imejumuishwa ndani yake, 494.32; wanaoupokea wanafanywa hai kwa kuunganishwa na Kristo, 247.10; huimarisha imani yetu, 125.210; 186.42; hutoa msamaha wa dhambi, 186.42; 280.90; 493.22; 499.70; 638.53; na neema na Roho wa Mungu, 499.70; chakula cha kuihuisha nafsi, 493.23; 666.59; 671.76; chakula cha kila
siku na riziki, 493.24; chenye afya, dawa itulizayo, 499.68; huamsha na huimarisha imani yetu na hufariji dhamiri yetu, 38-41.7; 39-42.30; matokeo mara mbili: maliwazo kwa dhamiri na shukrani au sifa, 276.7475
C. Uhalali: mkate na divai ambavyo ni mwili na damu ya Kristo na ambavyo vinafuatana na Neno ni hazina ambayo kwayo, msamaha unapatikana, 494.28-29; kiini kikuu ni Neno la Mungu na agizo au amri, 491.4; bila Neno, elementi si kitu ila mkate na divai ya kawaida, 492.14; si nguvu za binadamu wala kukariri kwa mchungaji (hata hivyo, kukariri huku ku lazima) kunakotimiza uwepo wa mwili na damu ya Kristo, 530.8; 643.74; 652.121; badala yake, ni uwezo wa Mungu na maneno, asasi, na mpangilio wa Kristo, 643.74; si imani, bali maneno na uenyezi wa Kristo pekee, 652.121; sakramenti haitegemei kuamini au kutoamini kwa binadamu bali katika Neno na agizo la Mungu, 634.32; wala katika utakatifu wa binadamu, 492.16; wala katika ustahili wetu, 498.61; 631.16; hubaki isiyoharibika na isiyodhurika ingawa tutaitumia na kuishughulikia isivyofaa, 491.5; 492.16; hata wasiofaa hutoa na hupokea mwili na damu ya Kristo, 170.28; 175.47; 328.1; 629.8; 631.16, 19; 632.24, 27; 634.32; 639.57, 60; 641.63; 652.123
D. Mapokezi sahihi: yanatolewa kwa wale wanaohitaji maliwazo, 40.33; mtu anayeamini lisemwalo na litolewalo na maneno hupokea uwezo na faida zake, 494.33, 35; dhamiri zilizotishwa ndizo zinazoyastahiki, 276.73; 642.69; mtu aliye na imani katika maneno “kwako,” anastahiki, 373.10; 494.33-35; ustahili pekee unakuwa katika utiifu na stahili za Kristo tunazozifanya zetu wenyewe kwa njia ya imani, 531.20; hauwi pamoja na matayarisho yetu, 373.10; 653.124; hisia zetu za kutostahiki hazipaswi kutuzuia, 497.55-56; 497.57; hazitegemei ustahiki wetu, 498.61; 631.16; matumizi yake mabaya, 498.61; 499.69, 74; 531.18; 640.60; 642.68; kuipokea isivyofaa ni kualika hukumu na laana, 178.5; 499.69; 531.16; 631.16; 639.57; 652.123
E. Nafasi katika maisha ya Mkristo: hakuna anayepaswa kulazimishwa kuipokea, 360.21; 495.42; jinsi ilivyo chini ya Upapa, 497.51; matokeo ya shurutisho ni mauaji ya watu, 495.42; hakipaswi kufungamanishwa na wakati maalumu (uliotengwa), 178.5; 496.47; kwa sababu si kila mmoja anayejitayarisha kwa njia sawa wakati uo huo, 178.5; lakini inatupasa kujitayarisha wenyewe kukipokea mara kwa mara, 495.39; maneno ya Kristo hutuagiza na kutuamuru kufanya hivyo, 496.45;
na ahadi ya Kristo, 498.64; haja yetu (mzigo) hutulazimisha, 360.23; 499.72-73; watu wanapaswa kukipokea baada ya kuchunguzwa na kusamehewa, 39.6; 45-46.1; 260.1; wasiojua wanachokitafuta au kwa nini wanakijia wasikipokee, 491.2; wala wasiotaka kujifunza katekisimo, 358.11; 397.5; wala wanaojitenga na ungamo, 505.29; wala walio waovu wazi wazi, wajeuri, au watundu, 178.4; 498.58
F. Nafasi katika ibada ya umma: ni agizo takatifu, 174.46; tendo zima la uanzishaji wa Kristo lazima lifuatwe, 643.75; 645.83; lazima kitolewe katika aina zote mbili, 31-33; 245-248; 328.2; 532.24; 650.110; hili si jambo linaloachiwa chaguo la binadamu, 248.15; maana Kristo alianzisha elementi zote mbili kwa kanisa zima, 245.1-2; chini ya Upapa, aina zote mbili za elementi hazikutolewa ili kutukuza hadhi za wachungaji, 247.9; Maneno ya Uanzishaji yanapaswa kusemwa au kuimbwa dhahiri na wazi, 644.79; mafundisho kwamba, elementi zinapaswa kuabudiwa kunakataliwa, 534.40; 653.126; kujipatia komunyo mwenyewe hakuruhusiwi, 308.8; maana ya “Ushirika wa watu wa kawaida,” 247.8. Tazama pia Misa; Sakramenti
Sala ya Jioni, 374.4-5
Sala, Maombi, Maombezi, 367–369; 373–375; 398.14; 461–479; ina
755
amri ya Mungu, 206.143; 217.16; 462.5; Mungu anatutaka tuombe vitu vingi na muhimu, 469.56; ina ahadi ya Mungu, 217.16; 240.20; 464.19; Mungu husikia na kujibu, 463.18; 465.32; inaweza kuitwa sakramenti, 217.16; uwezo wake, 465.29–32; hutupatia silaha kumpinga ibilisi, 465.29–32; 478.113; sawa na ukuta wa chuma ulio upande wetu, 465.31; usalama wetu wote na ulinzi unapatikana katika sala pekee, 465.30; hautegemei utakatifu wetu, 462.10; 462.11, 15; si tendo jema, 464.25; si umbo la ibada kwamba, kwa njia ya tendo lenyewe, hutoa heshima kwa Mungu na kufidia mauti ya milele, 206.143; tegemeo katika ahadi takatifu na katika stahili za Kristo lazima zitoe msingi kwayo, 240.20; 464.21; 479.122; Roho huwaombea wateule, 688.31; Mungu haiheshimu kwa sababu ya mtu, bali kwa sababu ya Neno lake, 463.16; 463.17; tunaweza tu kuthubutu kuomba tunapojua kwamba, dhambi zetu zinasamehewa, 475.92; sala bila imani si sala, 236.13; 479.120; wale wasioiamini ahadi wanamkasirisha, wanamwaibisha, na kumshataki Mungu kwa kusema uongo, 464.21; 479.122; hivyo ni kuibahatisha sala na kumunyamunya bila lengo maalumu, 463.14; lazima tuakisi na kuhisi haja yetu kwa moyo kabisa, 464.24; 404.26; sala za watawa wa kiume na makasisi zimekataliwa,
462.7; 464.25; lazima tujifunze kuthamini sala kama tendo kuu la thamani na lazima tutofautishe kikamilifu baina ya kubwabwaja bure na kukiomba kitu, 466.33; hatupaswi kuipurukusha, 465.27; 583.46; hakuna lililo la lazima kama kumwita Mungu bila kukoma, 461.2; kutoka ujana na kuendelea, tunapaswa kuwa na mazoea ya kuomba kila siku, 373–375; 398.16–17; 465.28; kutoomba ni kutoamini, 469.58; sala ni tunda la toba, 205.139; “ubani” na “sadaka safi ” 267.32; ibada ya kweli, 267.29; ndoa, vyakula, na vitu kama hivyo vinatakaswa nayo, 253.30; Sala ya Bwana ni kubwa sana kuliko zingine zote tunazoweza kuzibuni, 464.23; tunapaswa kuomba kwa agizo takatifu, nuru, na utakaso, 575.15; kwamba, Mungu aweze kutupatia, kuhifadhi, na kuongeza imani ndani yetu na utimizaji wa Amri Kumi, 461.2; kwamba, Mungu aimarishe imani na kuhifadhi vipawa vyake vya mbinguni ndani yetu, 576.16; kwa mahitaji ya mwili na maisha yetu duniani, 472–474; kiini chote cha sala yetu kinaelekezwa dhidi ya Ibilisi, 478.113, 116; wachungaji wanapaswa kuomba Sala ya Bwana kwa wao wenyewe na kwa wakazi wao wa usharika (parokia), 393.3; tunapaswa kuwaombea wengine, 465.28; sala kwa watakatifu, tazama Watakatifu; kwa wafu, tazama Wafu
Samehe, tazama Ondoleo la
Dhambi; Fungu
Sanamu za Miungu Mingine, Ibada ya Sanamu, ni tegemeo na imani ya moyo pekee ifanyayo Mungu na sanamu, 400.2; 404.28; wapagani huunda fikira na ndoto zao kumhusu Mungu kuwa sanamu, 403.20; pesa/ mamoni ndiyo sanamu ya kawaida sanakatika nchi, 401.6; kimsingi, ibada ya sanamu ni jambo la moyo, litafutalo msaada na maliwazo kutoka viumbe, watakatifu, na maibilisi, 403.21; 239.16; 294.53; 312.26; 346.47; na malaika, 312.26; ibada ya sanamu iliyo kubwa sana ni kuutafuta wokovu katika matendo yetu wenyewe, 403.22; kushurutisha amri za binadamu kanisani kama lazima huiruhusu ibada ya sanamu, 679.15; hii ibada ya sanamu itabaki hadi Kristo arudi na kuuangamiza ufalme wa Mpinga Kristo, 283.98; matumizi mabaya ya Misa ni ibada ya sanamu, 283.98; Misa imekuwa kuu na ya thamani kubwa sana kuliko ibada za sanamu anuai za baba mtakatifu, 307.1; na imezaa ibada za sanamu anuai, 309.11; ibada ya sanamu ya rozari, 294.53; ulimwengu haufuati lolote isipokuwa ibada ya uongo na ibada ya sanamu, 402.17; ibada ya sanamu ya chini ya upapa, 307.1; 508.4. Tazama pia Imani; Mungu; Ibada
Santiago de Compostela, Mahali pa Hija huko Uhispania Shetani, tazama Ibilisi
Sauti za Thrasonia, 247.11
Serikali, serikali nzuri ni kipawa (baraka) kutoka Mungu, 368.14; 453.15; wakati mwingine Mungu huuruhusu wema mwingi zaidi kuwajia watu hata kwa njia ya mdhalimu au mwovu, 313.3; Injili haiipindui, 19-20.5; badala yake, Injili huiidhinisha na hututiifusha kwayo, 230.6; tazama pia Injili; mafundisho ya uongo ya Waanabaptisti, 549.12-16; 702.1721. Tazama pia Mamlaka; Ufalme wa Jamii; Watawala; Upanga
Shahidi, tazama Ushuhuda
Shaka, wale wanaomwamini Kristo hawapaswi kutilia shaka haki yao, waliyopatiwa kwa njia ya imani, 519.9; wala neno la ondoleo la dhambi, 371.16; afanyaye hivyo humtusi Kristo, 114.149; na hawezi kusali 195.89; 479.123; hatupaswi kutia shaka kwamba, sala humpendeza Mungu, 464.22; wanaotia shaka, wanaanguka wakitanguliza kichwa kuelekea ukataji tamaa, 195.89; wapinzani huwaamuru watu watie shaka iwapo wamepokea msamaha wa dhambi, 110.119; 346.44; watu wema wengi wangeteseka hadi mautini kwa urahisi kuliko kulivumilia hili, 203.128. Tazama pia Hakika; Dhamiri; Kukata Tamaa; Imani
Shauku, tazama Hamu ya Asili (στοργη φυσικη)
Shauri la Mungu, siri na lililofunuliwa, 553.6; 683.9; 685.13; lilitambulisha wongofu wetu, 691.44, 48; aliloliagiza Mungu kabla, 682- 685; lisimhudumie yeyote isipokuwa wale wamwaminio Kristo, 546.13. Tazama pia Uchaguzi
Shauri la Mwafaka, 507-553; halikusudiwi kuwa ukiri mpya au kuuacha Ukiri wa Augsburg, 552.5; halizikaidi kiri zingine za Kiinjili, 558.20; huwakilisha mapatano ya pande mbili kuhusu maelezo ya mafungu muhimu sana ambayo yameingizwa katika mabishano, 558.16
Sherehe/Kaida fulani, 18-19; 4552; 54. 65-72.36; 67.61; 74.57; 76.5; 219; 259.64; 333-334; 542544; 676-681
A. Maana: ni mambo yasiyokuwa ya lazima kuyajali, 295.58; tazama pia mambo yasiyokuwa ya lazima kuyajali; si ya lazima na hakuna kumwabudu Mungu, 62-67.53; 226.32; 542.3; 543.9; 677.8; mchezo wa mtoto na tendo la mpumbavu, 316.14; si ya lazima kwa msamaha wa dhambi, 199.113; kwa kuhesabia haki, 48-52.41; 170.31; 223.20; 225.29- 30; si pamoja na utakatifu wa kanisa, 332.3; haki ya sheria ilibobeshwa kwayo, 170.31; ufalme wa Kristo si uzingatifu wa nje wa hayo, 166.13; ni wazo la Kiyahudi au kipagani kufikiria kwamba,
tunahesabiwa haki kwayo, 67-74.61; 223-21; 217.18; 221.10; 225.28; 272.52; utaji wa Musa, 112.133; tazama pia Musa; kwa hiyo kazi ya Kristo inafichwa, 221.10; 223.20; 294.54; yanakusudiwa kutenda kazi ya kuwafundisha watu, 3841.3; 260.3; 294.55; na kudumisha amani kanisani, 48-52.40; 67-73.53; 171.33; 218.1; 542.1, 3; 676.1; usawa si wa lazima, 15.3; 48-52. 166.10; 170.30; 222.18; 543.7; 681.31; “kaida halisi za dini” na “kaida za dini za ulimwengu wote” 170.30
B. Faida: si za haki ya kimungu, 173.40-41; katika Agano la Kale, baadhi zilikuwa za lazima, 226.32; katika Agano Jipya, zilibatilishwa (ziliondolewa), 67-74.59; 221.10; 255.41; 259.64; kanisa li huru kuhusiana nazo, 48-52.41; 199.113; 543.10; na linaweza kuzibadilisha wakati wowote, 542.4; 677.9; Kristo hakuamuru ubunifu wa zingine mpya, 67-74.61; mitume waliutetea uhuru, 255.42; 678.11; maaskofu hawana uwezo kuzianzisha zingine mpya, 64-71.30; 65-71.34; tazama pia maaskofu; hata hivyo, hizo ambazo zinapaswa kuzingatiwa zinaweza kuzingatiwa bila dhambi, 219.1; tazama pia Maagizo ya Kanisa; chini ya upapa, 294.55; 316.14; miongoni mwa Waiaminio Injili, 38-41.2; 48-52.40; 228.44; 260.1. Tazama pia mambo yasiyokuwa ya lazima kuyajali;
758
Mapokeo ya binadamu
Sheria na Injili 91.5; 524-527; 615621; tofauti baina ya sheria na Injili ni nuru adhimu ambayo kwayo, Neno la Mungu linagawanywa kikamilifu, 524.2; 615.1; Biblia nzima imegawanywa katika sehemu hizi mbili, 91.5; 108.102; 121.186; 188.53; tangu mwanzo wa dunia, matamko haya mawili yamewekwa kandokando moja kwa nyingine yakiwa na tofauti sahihi baina yao, 620.23; hadi mwisho wa dunia, lazima tofauti sahihi zifundishwe siku zote, 620.24; tofauti baina yao, 91.5; 115-116; 121.186; 188.53; kuna tofauti kubwa baina ya maarifa ya Mungu yapatikanayo kutoka Biblia na yale yapatikanayo kutoka sheria, 619.22; Injili hutangaza haki ya imani iliyo tofauti na haki ya sheria, 97.43-44; 131; tazama pia Haki; kwa kawaida, akili ya binadamu huifahamu sheria, kwa kiasi fulani, 91.7; kwa hivyo, wapinzani huiteua, na kwayo, wanatafuta msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki, 91.7; wanafundisha sheria pekee na si Injili, 128.229; 185.34; mafundisho yao yanajengwa juu ya msingi hafifu wa sheria, 325.39; hatuhesabiwi haki kwa sheria, 90-120; 189.79; 220.8; 286.14; 307.4; Mungu hata haipatii sheria heshima ya kustahili uzima wa milele, 289.30; utumwa katika sheria si wa lazima kwa kuhesabiwa haki, 66-73.51; shughuli sahihi ya sheria ni kushutumu dhambi
na kufundisha matendo mema, 619.18; kufunua, kushtaki, kutia hatiani, na kulaani dhambi, 108.103; 109.106; 187.48; 188.53; 319.4; 524.4; 617.11; 619.17; kushtaki, kulaani, na kutisha dhamiri, 96.38; 119.179; 185.33-34; 195.88; hulaani kutokuamini, 619.17, 19; hushtaki na hulaani asili ya binadamu, 560.6; 565.32; ni radi na nyundo ya Mungu, 318.2; tangazo la ghadhabu ya Mungu, 617.12; tangazo la ghadhabu ya Mungu, 103.79; 112.128; 618.14; huleta ghadhabu, 96.38; 123.204; 195.88; 320.5; huleta mauti na jehanamu, 320.7; husukuma kiburini na kukata tamaa, 195.89; 320.7; 617.10; kwa njia ya kuihubiri sheria, watu huhisi kitisho halisi, hujutia, na huwa na huzunu mioyoni, 585.54; ni ya lazima kwa toba ya kweli kuongezewa katika
Injili, 135-138 inayotuita kutoka sheria na kutupeleka kwenye ahadi; kwa njia ya tangazo la sheria na
Injili, Mungu hutekeleza toba na imani ya kweli mioyoni mwa binadamu, 584.50; 585.54; Agano Jipya hubaki na ofisi hii ya sheria, 319.1; sheria haikomeshwi na imani, bali huthibitishwa, 236.14; Kristo na sheria, tazama Kristo
2. Matumizi maradufu ya sheria, 318-319; matumizi mara tatu, 526.1; 621.1; matumizi ya kwanza: tazama Haki, kudhibiti dhambi kwa njia ya kitisho cha mapatilizo na ahadi ya upendeleo, 318.1; sheria
759
kama mdhibiti nidhamu wetu, 94.22; huwafanya watu wengine kuwa wabaya zaidi, 318.2; huwazaa wanafiki na watakatifu wa uongo, 318.3 (II); matumizi ya tatu: 526528; 621-626; sheria ilitolewa si kwa wenye haki (maasumu), bali kwa wasiokuwa wenye haki (wavunja sheria na wakaidi), 94.22; 622.5; kabla ya kuishika, lazima tupokee msamaha wa dhambi na upatanisho kwa imani, 115-116; waliozaliwa mara ya pili hawako chini ya sheria tena lakini wako chini ya neema, 625.17; wana wa Mungu wanaishi katika sheria na hutembea kufuatana nayo, 527.6; wanataka kuifuata kufuatana na nafsi yao ya ndani, 611.19; 625.18; lakini hawaishi bila sheria yoyote, maana sheria ya Mungu imeandikwa mioyoni mwao, 622.5; wanapaswa kuzidi kuishika, 111.124; 113.136; wamekombolewa ili waweze kuifuata, 526.2; kwa sababu ya tamaa za mwili, wanaihitaji ili waweze kuchochewa kumfuata Roho wa Mungu, 623.9; ni kioo kinachopasa kushikiliwa mbele ya waumini daima, 622.4; 625.21; huwaagiza na kuwaadhibu, 624.12; ni ushauri yakini wa waliozaliwa mara ya pili, 526.1; ili wasirudi nyuma kwa utakatifu na uchaji Mungu wao, 625.20. Tazama pia Amri; Haki; Matendo
Sheria, hakuna binadamu mwenye haki kuivunja sheria iliyotokana na sheria takatifu, 54–58.24
Dhana:
A. Sheria ya asili na iliyofunuliwa: iliandikwa mioyoni mwa wazazi wetu wa kwanza hata kabla ya anguko, 526.2; imeandikwa kwenye mioyo ya wenye haki, 622.5; sentensi ya sheria imeandikwa moyoni, 187.48; kwa kawaida, akili ya binadamu huifahamu kwa kiasi fulani, kwa kuwa akili ina hukumu sawa iliyoandikwa akilini na Mungu, 91.7; sheria takatifu, ya milele, 584.50
B. Sheria ya Kaida Mbalimbali (kanuni za Walawi, ibada za Walawi): 264.21; 268.34, 36; ingefikia kikomo kwa ufunuo wa Injili, 265.24; Wakristo wamefanywa huru kutoka kwayo, 65-73.39-41; 67-74.59; 255.41; 286.15-16; 295.58. Tazama pia Kaida; Mapokeo ya Kibinadamu
C. Sheria ya jamii (dunia): 18-19; 63-70.13; 229-231; Injili haianzishi sheria mpya kwa ufalme wa jamii, 229.3; Wakristo wanapaswa kuzitii sheria za sasa (dhidi ya Karlstadt), 229.3. Tazama pia Mamlaka; Ufalme wa Jamii; Serikali
D. Yaliyomo na utimizaji: mbao mbili za amri kumi alizopewa Musa na Mungu (Amri Kumi), 84.14; 95.34; 112.131; 129.231; 235.7; Amri Kumi za Mungu zinahitaji siyo tu matendo ya kinje na ya raia ambayo akili inaweza
kuyazaa kwa kiasi fulani, 91.8; 112.134; bali pia matendo mengine yaliyowekwa mbali, nje ya uwezo wa akili, 91.8; 94.27; matendo mema hayaziridhishi, 162-164; yanadai utiifu kamili, mtimilifu, safi, 626.22; yanatutaka tumwogope na tumpende Mungu kwa kweli, 94.27; 206.142; upendo ni utimizaji wazo, 114.147; 116.159; kwa kawaida, akili ya binadamu huzifahamu, kwa kiasi fulani, 91.7; tazama pia haki, wengine hufikiria wanaweza kuzishika kwa uwezo wao wenyewe, 318.3 (II); kwazo, wanatafuta msamaha wa dhambi na kuhesabiwa haki, 91.7; 93.18; utiifu kwazo ungekuwa haki iwapo tungezishika, 115-116; lakini hakuna awezaye kuzishika kikamilifu, 93.18; 97.40; 125-6; 195.88; 206.142; 590.75; haiwezekani kuzishika bila Kristo, 111.126; 112.135; 120.184; 185.37; 194.86; na Roho Mtakatifu, 97.45; 101.70; 111.126; 112.135; 194.82; imani hutokana na utimizaji wazo wetu, 98.46; 111-113; 125-6; 194.82; kwanza, lazima tupatanishwe na ahadi kabla ya kuzishika, 194.80–82; hatuwezi kuzishika hadi tuwe tumezaliwa mara ya pili, 111.126; hata baada ya kuzaliwa kwa pili, hatuwezi kuzishika kikamilifu katika maisha haya, 114.146; 516.12; 550.25; 591.79; 704.33; hata baada ya kufanywa kwetu upya, zinatuhukumu daima, 120; mafundisho ya uongo: matendo ya
zaidi ya kadiri ipasayo kwa haki, tazama Washauri wa Injili; Matendo; mafundisho ya wafuasi wa Pelagio kwamba, isipokuwa Roho Mtakatifu, watu wanaweza kumpenda Mungu na kuishika sheria “kufuatana na kiini cha tendo,” 232.2; kwamba, utimizaji wazo baada ya kuzaliwa kwa pili huanzisha haki yetu mbele za Mungu, 516.12; 591.79; tazama pia Haki
Hulka na ofisi: 618.17; ni fundisho takatifu linalotoa maagizo kuhusu mapenzi ya Mungu, 524.3; 624.11, 15; ni kioo kinachosawiri mapenzi ya Mungu sahihi, 622.4
Shule, wakati mmoja, majumba ya watawa yalikuwa shule, 53–58.15; 284.5; 313.1
Shurutisho, Mungu hawashurutishi watu dhidi ya mapenzi yao ya kuongolewa, 586.60; 589.73; watu walioongolewa kwa Mungu kwa kweli wamefanywa huru kutoka shurutisho la sheria, 526.2; 622.5; utiifu wao haupo kwa ajili ya shurutisho la sheria, 522.10; 609.12; 610.17; Mungu
Sifa, katika mafundisho ya dhambi ya sili, 563.21; 571.62; tazama pia Dhambi ya Asili; wapinzani wanapinga kwamba, asili ya binadamu ya Kristo imejaliwa tu kwa vipaji vilivyoumbwa au sifa zenye mpaka zinazopatikana katika watakatifu, 665.52
Sifa za Kimsingi, za asili mbili za Kristo, 667.62; kila asili inabaki na sifa za kimsingi za lazima zake, na haziondolewi na kuhamishwa kwa asili nyingine, 661.32
Siku, siku ya mwisho (ukamilisho wa ulimwengu), 20-21; 231; 366.6; 458.53; tazama pia hukumu; siku takatifu (siku za sherehe, Siku ya Bwana, Jumapili): 411415; zinashikwa kwa sababu ya umuhimu wao kwa jumuiya, ili watu waweze kujua wakati wanapaswa kukusanyika na vitu vyote viweze kufanywa kwa utaratibu mwema, 17-19; 67-74.60; 173.40; 223.20; 227.38; zinapaswa kuwaelimisha watu wa kawaida na kupitisha kumbukumbu ya matukio muhimu ya historia ya Injili, 171.33; 173.40; lakini hatuwezi kupokea neema au kufanya ridhaa kwa dhambi kwa njia ya kuzishika (hazihesabii haki), 18-19; 23-26.3; 65-72.39; 227.38; zisilazimishwe kwa dhamiri kana kwamba ni za lazima, 678.13; kuiweka siku kuwa takatifu kunamaanisha kuitenga kwa maneno, matendo, maisha matakatifu 413.87; Wakristo wanapaswa kuifanya kila siku kuwa takatifu, 413.89. Tazama pia Sherehe; Kaida, Mapokeo ya Kibinadamu; Jumapili
Siku Takatifu, tazama Siku
Siku ya Bwana, tazama Siku; Jumapili
Silika (katiba ya jumla), katika ufasili wa dhambi ya asili 86.24; tazama pia Dhambi ya Asili; ya upendo; 93.17; 101.66; 103.81
Sinodi, zinapasa kushughulikia mambo muhimu katika matabaka ya kiroho na ya kidunia yanayompinga Mungu na kusahau mambo ya upumbavu, 305.13; hukumu zao ni hukumu za kanisa, si za mababa watakatifu, 348.56; papa hutaka kuyaweka mamlaka yake juu ya hukumu zao, 345.40; 347.49; watu
Waiaminio Injili wanaitamani sinodi ya Kikristo ya jumla na huru, 8.2124; 304.10; ingawa haziulizi kwa ajili yazo zenyewe, 304.10; kaisari anazitamani, 7.16; lakini kitala cha Roma kinaziogopa sana, 302.3; katika sinodi kama hizo, Watu
Waiaminio Injili hawangeweza kusimama mbele ya Kaisari jinsi ilivyokuwa huko Ausgburg, bali wangefanya hivyo mbele ya Papa na Ibilisi mwenyewe, 316.16; huenda Kristo ataifanya sinodi ya malaika iweze kuishambulia Ujerumani, 304.11
Sinodi ya (1078), askofu wa, tazama Papa; Kiti Kitakatifu cha Roma ni kichwa na mlinzi mkuu wa wezi wote, 435.230; ulimwengu ni mkuu kuliko Roma, 340.18
Siri, iliyo kubwa sana ni Utatu Mtakatifu, 538.18; 661.33; iliyo kubwa sana baada ya hii ni muungano wa binafsi wa Kristo, 538.18;
762
661.33; 675.96; uwepo wa Kristo katika Chakula cha Bwana ni siri isiyoweza kufahamika isipokuwa kwa imani, 534.42; 653.127
Smalkaldi, Kongamano la (1537), 352; 509.4; 555.7; 631.17; Vita (1546–47), 557
Soko, tazama Biashara
Speyer, Baraza la (1526), 8.15; Mkutano wa, 8.17; 32
Strasbourg, Tazama pia Wittenberg (Mwafaka)
Sumaku, dhambi ya asili haiwezi kulinganishwa na kuipaka sumaku juisi ya kitunguu saumu, 511.15; 563.22
Sybaris, 257.54
Taji la Miiba, huonyesha kupinduliwa kwa ufalme wa kiroho wa Kristo na ufalme mwin gine wa ulimwengu kwa kujisingizia uwezo wa kanisa la Kikristo, 343.32
Tamaa, Mbovu, tazama Ashiki Mbaya (Concupiscentia)
Tamaa Mbaya (Concupiscentia), tazama Ashiki Mbaya
Tamathali, 115.152
Tangazo, kwa njia ya tangazo la Neno la hadharani, Mungu alikusanya kanisa la milele, 584.50; kanisa linajengwa juu ya ungamo alilolitoa Petro, ambalo kwalo, alimkiri Yesu kuwa Kristo, 342.25;
tangazo la Neno ni njia Roho Mtakatifu, 577.22; 585.52; 589.71; 589.72; 703.30; kwa njia ya tangazo la Injili, Mungu huiwasha imani, 267.32; 589.71; wote wanaotaka waokolewe wanapaswa kulisikiliza, 585.52; iwapo watu hawataki kulisikia, hawawezi kupata faraja wala rehema katika uchaguzi wa milele wa Mungu, 586.57; Mungu anawataka wote walisikie, 694.68; ni dhabihu halisi ya kila siku, 269.38; Misa ilianzishwa kwa ajili ya hilo, 269.35; mapambo ya kweli ya makanisa, 271.51. Tazama pia Huduma; Kuhubiri
Taswira za watakatifu, tazama Watakatifu
Tegemeo (Fiducia), Amri ya Kwanza inaihitaji, 400.4; ni lazima kwa sala, 475.92. Tazama pia Imani; Tegemeo
Tegemeo, imani ni tegemeo katika rehema, 189-190; tazama pia Imani, ni faraja, 180-191; tegemeo kwa Mungu huwa ni taswira ya Mungu katika binadamu, 81.18; kwa yaliyomo ya Sheria, tazama Amri, Sheria; Kristo hulaani tegemeo katika matendo yetu, lakini halaani tegemeo katika ahadi yake, 153.339; tegemeo katika utimizaji sheria ni kutomcha Mungu, lakini tegemeo katika ridhaa ya Kristo ni lazima, 120-121; lazima tuweke tegemeo katika maombezi ya Kristo kwa sababu hayo pekee ndiyo yana ahadi ya Mungu, 243.31; wenye dhambi
763
wanaotubu wote wanapaswa kuweka tegemeo lao katika Kristo pekee, 619.22; tegemeo katika matendo, tazama Matendo, tegemeo katika watakatifu, tazama Watakatifu
Thamani, tazama Malipo; Hazina Ukuu, wa Papa, tazama Papa
Thawabu, Mungu huiheshimu haki ya akili kwa thawabu za dunia hii, 94.24; matunda mema ya toba yana thawabu zao, 213.174; matendo si yenye kustahili kwa msamaha wa dhambi, lakini ni yenye kustahili kwa thawabu zingine za kimwili na za kiroho, 213.172-174; Mungu huahirisha thawabu nyingi hadi baada ya maisha haya kwa sababu Mungu anawataka watakatifu katika maisha haya waimarishwe kwa njia ya kumdhalilisha kiumbe wa kale, 213.172-174; jinsi uzima wa milele unaitwa thawabu, 156.357; 213.172174. Tazama pia Stahili
Toba, tazama Majuto Makubwa; Toba; Ridhaa Toba, tazama Majuto Makubwa; Toba PenteKoste, 25; 67.57; 173.40; 224; 302.1; 400
Toba, 16–17; 180–197; 319–326
A. Maana: ndiyo mada kuu ya mafundisho ya Kikristo, 271.46; huhusu mada kuu ya Injili, yaani, msamaha wa dhambi, 182.10; ndiyo sauti ya Injili kweli, 180.1–3; mafundisho yake yanapasa kuwa dhahiri na wazi iwezekanavyo, 244.41; mafundisho kuihusu na
mafundisho kuhusu kuhesabiwa haki yanakaribiana sana, the teaching on it and the teaching on justification are closely related, 180; tunamwangusha papa na kila kitu kilichojengwa juu ya matendo yetu mema kwa mafundisho kuihusu, 325.39; chini ya Upapa, mafundisho kuihusu yalikanganya kupita kiasi, 181.4
B. Toba ya uongo ya wafuasi wa Kanisa Katoliki: 180–182; 320–326; tazama pia Ungamo; Majuto Makubwa; Ridhaa; yalitokana na mafundisho ya uongo ya matendo, 207.145–146; 321.12; na mafundisho ya uongo ya sheria, 181.8; 185.34; 192.75; hakika, hayatambui ni nini dhambi, 320.10; yanasema kwamba, mtu mwenye majuto au mtu mwenye kutubu hulipokea tendo la upendo kutoka Mungu na tendo hili hustahili mapokezi ya msamaha wa dhambi, 192.75; yanafundisha kwamba, imani huitangulia toba, lakini hayaifahamu imani kama yenye inahesabia haki, bali kama imani ya jumla kwamba, Mungu yupo na huwatisha wasiomcha kwa mapatilizo, 189.60; toba yao haijakamilika au ni hafifu, 325.36; inamaanisha kutubu daima lakini bila kuifikia toba, 323.23
C. Mafundisho ya Kiinjili kuhusu toba: kwanza, yalielezewa wazi na Luther, 181.4; mafundisho sahihi, proper teaching, 319.1–3;
imani lazima ihitajike katika kila aya kuhusu toba, 120-122; huziita dhamiri kutoka sheria hadi kwenye
Injili na kutoka tumaini katika matendo yetu wenyewe hadi kwenye tumaini katika ahadi na katika Kristo, 193.76; katika kuhubiri juu yake, tangazo la sheria halitoshi lakini ni lazima pia kuiongezea Injili, 114.146- 148; Injili huitangaza, 184.30; 294.54; lakini hayo siyo
Injili huyatangaza, 526.11; 616.4–6; tazama pia Injili; katika kuifundisha toba, yote mawili, yaani, sheria na Injili lazima yafundishwe pamoja lakini katika utaratibu sahihi na utofautishaji unaofaa, 618.15; katika aya fulani za Biblia, inaeleweka kama wongofu mzima, lakini ambapo inalinganishwa na imani, inamaanisha kuzitambua dhambi, kuzisikitikia, na kuepukana nazo, 184. 28; 616.7–8; ni ya kinafiki na ya uongo isipokuwa ifuatwe na matunda mema, 150-52; lazima liwe badiliko kwa mema ya maisha yote ya fulani, 213.170; ni shambulio lenye bidii katika kiumbe wa kale na kuingia katika maisha mapya, 489.75; kutembea katika Ubatizo, walking in baptism, 489.75; kuurudia na kuukaribia Ubatizo, 490.79–86; toba ya ndani haimaanishi lolote isipokuwa pia iishie kuonekana katika usahihishaji mkali wa mwili, 203.131; ina sehemu mbili: majuto makubwa na imani, 16-17.3–5; 180.1; 184.28; 185.35; 186.44;
188.52; 189; 189.60; 196.91; 197.98; vitisho na maliwazo, 188.52; imani huwa ndani yake, 186.45; 113.142; kuihubiri kwake kunawaandaa watu waipokee neema, 320.5; na huzitisha dhamiri zinazopatwa na ghadhabu ya Mungu, 100.62; 113.142; 184.29; haya ndiyo mapatilizo ya kweli ndani yake, 208.148; si “majuto makubwa mashughuli” bali “majuto makubwa baridi,” 319.2; tazama pia Majuto Makubwa; hujumuisha hasa kila kitu kama dhambi, 325.36; matendo mema (matunda) yanapasa kuifuata, 203.131; 213.174; Amri Kumi zinafundisha matunda mema ni yapi, 213.174; ni maisha mapya yote, 186.45; 204.132; toba huvumilia miongoni mwa Wakristo hadi kufa kwa sababu hushindana dhidi ya dhambi zinazobaki mwilini, 326.40; 581.34
D. Kama sakramenti ya tatu: 186.41; 216.4; 489.74; toba na ondoleo la dhambi, tazama Ondoleo la Dhambi; toba inawezekana kwa waliotenda dhambi baada ya Ubatizo, 16–17.1; 17.9
Tofauti, baina ya sheria na Injili, tazama Sheria, baina ya vyakula, tazama Vyakula; ya siku, tazama Siku, ya thawabu, tazama Thawabu
Tohara, haikupashwa kwa ajili ya kuhesabiwa haki, 123.201; 218.19; wakati walimu wa uongo wanaidai, huwa si jambo la lazima kulijali tena, 678.12; tohara ya kiroho, 186.46
765
Toledo, Sinodi ya (577), 246.4
Torati, 317-319; 524-528; 615-621
Torgau, Mahubiri ya Luther huko (1533), 10; 541.2; 584; 640; 642; 654; 675.1; Mafungu, Kongamano (1576), Kitabu
Trento, Sinodi ya (1545-63), 76; 511; 532; 534; 563; 590; 591; 607; 614; 653
Tumaini, imani na tumaini ni tofauti kwa sababu imani hupokea msamaha wa dhambi na upatanisho sasa, lakini tumaini limeelekezwa kwenye wema wa siku zijazo na wokovu, 142-143; ndani ya kila Mkristo, wakati mmoja tumaini huwa baridi na wakati mwingine huwa nyonge, within each Christian, 588.68
Ubatili ((ןוא), ibada katika misingi na makazi ya watawa, 313.2
Uasherati, Uovu, tazama Ashiki Mbaya Waganga, 402.12
Ubatizo, 3; 15; 175-176; 327; 37010; 387-391; 399.21-22; 479-491
A. Maumbile: si jambo la nje lisilokuwa na maana (dhidi ya wenye shauku) 480.7; bali ni wa asili takatifu, 480.6; agizo la Mungu, 485.38; 480.60; Mungu ameuthibitisha kwa njia ya miujiza, 482.21; hazina itolewayo na Mungu, 484.34; 484.37; Neno la Mungu katika maji, 327.1; “kusafishwa kwa Neno,” (Efe. 5:26), 166.7; 327.1;
uwezo wake, 370.10; 483.27; maji (matakatifu) ya Mungu, 481.14, 17; kuoga kwa mbinguni, 389.13; tendo lenyewe la Mungu, 480.10; 484.35; Mungu hutubatiza, 263.18; 480.10; yeyote anayeukataa, hukataa Neno la Mungu, imani, na Kristo, 484.31; matumizi yake mazuri, 489.68; imani ni yake, 370.8; 483.28, 34; lakini imani haiusababishi bali huupokea, 487.53; 488.60; huwepo milele, 490.77; kwa hiyo, hakuna kubatizwa tena, 588.69; tazama pia Ubatizo wa watoto wachanga, mafundisho ya uongo ya wafuasi wa Tomaso na wa Skota, 327.2-3; ya Waanabaptisti, 548; 549.8; 701.9; ya wafuasi wa Schwenckfeld, 550.23; 703.31
B. Matokeo, 370.5-6; 388.8; 482.23-25; 485.41; 490.83; ni kusafishwa kwa dhambi, 388.14; maji ya uzima, 370.10; kuoshwa kwa kufanywa upya (kuzaliwa upya), 370.10; 483.27; hutoa kuzaliwa upya, 391.30; humfanya fulani kuwa mtakatifu kabisa na aliyebarikiwa, 485.46; ni wa lazima kwa wokovu, 15.1; 175.1; 480.6; kupokewa katika jumuiya ya Wakristo, 389.9; 479.2; 488.64; hutufanya wana wa Mungu, 387.2; 388.8; 484.37; 490.83; humtoa Roho Mtakatifu, 87.35; 485.41; hutekeleza kufanywa upya (kuzaliwa upya), 10.2; 370.10; 489.13; 483.27; huiondoa hatia ya dhambi ya asili, 87.35; huutoa uhai mpya, 489.75; huutoa ushindi dhidi ya Ibilisi, tazama Ibilisi; dhidi ya
766
mauti, 488.6; 485.41; 485.43; hutoa nguvu na faraja, 485.44; dhambi hubakia baada ya huo, 87.35; 588.69; lakini wale waliobatizwa huzaliwa upya, 588.67, wana hiari, 588.67; wanaotenda dhambi baada ya Ubatizo hupokea msamaha wa dhambi wakati wanatubu, 1617.1; 180.1; sharti uendelee ndani yetu maishani, 488.65; 490.83; ni Ubatizo wa kila siku, 488.65; ni vazi la kila siku, 490.84; huonyesha kuuawa kwa kila siku kwa kiumbe wa kale (Adamu wa kale), 371.12; 488.65
C. Ubatizo wa Kristo: 482.21
D. Ubatizo wa maji matupu: 482.22; 484.35
E. Ubatizo kwa kengele: 334.4; 645.87
Ubatizo wa Watoto Wachanga, 16; 175-176; 327.4 (V); 387.1; 486-490; ni wa lazima, haki, na wa kufaa (dhidi ya Waanabaptisti), 16; 175-94; 349.6- 7; 349.8; 702.11-13; ni thibitisho la kutosha kwamba, unampendeza Kristo kutokana na ukweli kwamba, Mungu amewatakasa wengi waliobatizwa kwa jinsi hiyo na amewapatia Roho Mtakatifu, 486.49; Ubatizo wa watoto wachanga na imani, 487.5253. Tazama pia Ubatizo
Ubikira, (kuitawala tamaa) huhitaji kipawa maalumu, 252.19; ni kipawa bora zaidi kuliko ndoa,
254.38; 260.69; lakini hatuhesabiwi haki kwa sababu ya ubikira wala ndoa, 254.36; 260.69; si ukamilifu wa Kiinjili, 289.27; ni chafu kwa wasiomcha Mungu, 254.34; ubikira si usafi bila imani bali ndoa ni safi kwa sababu ya imani, 259.64; unasifiwa kwa sababu ya taamuli na kujifunza, 255.40; unaweza kupendekezwa lakini hauwezi kuamriwa, 252.20; wasiobarikiwa kuwa na kipawa cha ubikira kwa tendo maalumu la Mungu wanapaswa kuoa, 53–58.20; 251.16. Tazama pia Useja; Usafi; Ndoa
Uchaguzi (Majaliwa ya Milele), 544-547; 586.57; 682-701
A. Lazima utofautishwe na Ujuzi wa mbele wa Mungu ya kutokea jambo, 544.2; 682.4; maana ya kweli haiwezi kupatikana kutoka akili au sheria, bali kutoka Injili tu, 545.910; 686.25; usitafutwe katika ushauri wa siri wa Mungu bali katika Neno lililofunuliwa, 545.6; 683.9; 686.25; 689.36; 690.43; 692.52; katika Kristo, 546.13; 685.13; 694.65; maana yake, 690.43; 699.89; ni mafundisho muhimu na ya kufariji, 544.1; 546.11, 13; 690.43; faraja miongoni mwa majaribu, 546.13; 691.48; matumizi sahihi ya fundisho hili yanatuonya tutubu, 684.12; 691.51; 695.71; hulielekeza Neno, huhimiza wema, huimarisha imani, na kutuhakikishia wokovu, 684.12; huthibitisha fungu la kuhesabia haki,
767
690.43
B. Hulikumbatia tendo zima la Mungu la kuokoa 544.5; 683.8; hautegemei haki yetu bali mapenzi ya rehema ya Mungu tu na ustahili wa Kristo, 695.75; 699.88; Mungu ameuthibitisha kwa kiapo na ameutia mhuri kwa sakramenti, 546.13; ahadi ya Injili ni ya ulimwengu wote, 687.28; Mungu anawataka watu wote watubu, waiamini Injili, na waokolewe, 545.10; 547.17; 697.81; Mungu amenuia kutomwokoa yeyote isipokuwa kwa imani katika Kristo, 546.13; matayarisho yote kwa ulaanifu yanaanzia kwa Ibilisi na binadamu, si kwa Mungu, 546.12; 696.78, 80-81; kwa njia ya kulidharau na kulibeua Neno la Mungu, 546.12; 690.40; 696.78; uchaguzi ni neema ya Mungu isiyostahili lakini ukosefu wa uchaguzi ni haki ya Mungu, hukumu inayostahili, 693.60-61; uchaguzi wa Mungu huwafikia tu wana wa Mungu, 544.5; 683.5; ishara zake, 686.25-26; 687.27
Uchaji, ya watawa wa kiume, tazama Maisha ya Utawa; Watawa wa Kiume; kwa Waanabaptisti, 548.5; 701.10; ya waseja, tazama Ndoa ya Makasisi. Tazama pia Kazi
Uchumi, tazama Biashara
Uchungu, tazama Mateso; Msalaba; Adhibu
Udhalimu, Mdhalimu, wakati
mwingine Mungu huruhusu wema mwingi kuwajia watu kwa njia ya mdhalimu, 313.3; ibilisi hujaribu kuigandamiza na kuipotosha Injili kwa kuwachochea wadhalimu, 299–300; udhalimu wa papa, 252.25; 280.91; 302.3; 504.21. Tazama pia
Ukatili
Udugu, 23.3; 26.3. tazama pia
Mashirika
Uenyezi/Kudura, wa/ya Kristo, tazama Kristo
Ufahamu wa mbele wa Mungu (Praescientia), 544.2-4; 682–684; ufahamu wake Mungu wa milele lazima utofautishwe kutoka uchaguzi wa milele wa Mungu, 544.2; 682.4; huvifikia viumbe vyote, vizuri na viovu, 544.4; 682.4; si sababu ya uovu, badala yake huutoa utaratibu miongoni mwa uovu na huuwekea kikomo, 544.4; 573.6; si sababu ya dharau kwa Neno, 690.41; kulifahamika katika mafundisho ya uchaguzi wa milele wa Mungu, 686.24. Tazama pia Uchaguzi
Ufalme wa Mpinga Kristo, 222.18; 252.25. Tazama pia Ufalme wa Baba Mtakatifu
Ufalme wa Mungu, wa Kristo, ni ufalme wa kiroho na lazima utofautishwe na ufalme wa raia (ufalme wa ulimwengu), 214.176; 229.2; 343.31; tazama pia Mamlaka; Ufalme wa Raia; Serikali; Watawala; Upanga; si Baraka ya dunia hii
768
iharibikayo bali hazina ya milele yenye thamani kuu, 469.55; wokovu wetu kwa njia ya Kristo, 468.51; haki ya moyo na kipawa cha Roho Mtakatifu, 166.13; ule ambao Kristo huufanya hai daima kwa Roho, 167.18; haki na uzima moyoni, 289.27; siyo tu uzingatifu wa kinje wa kaida fulani za dini, 166.13; 289.27; unaweza kufunuliwa au unaweza kufichwa chini ya msalaba, 167.18; ingawa mbwa mwitu na walimu wasiomcha Mungu wataenea kanisani, bado wao si ufalme wa Kristo, 169.22; huja kwa njia mbili: kwanza, huja hapa, mapema, kwa njia ya Neno na imani, na pili, katika ukweli wa milele, huja kwa njia ya ufunuo wa mwisho, 469.53; fundisho kwamba, kabla ya ufufuo wa wafu, watakatifu na watu wenye haki pekee watakuwa na ufalme wa ulimwengu limekataliwa, 19- 20.5
Ufalme wa Papa, 169.23–24. Tazama pia Papa
Ufalme wa raia, lazima utofautishwe na ufalme wa Kristo, 229.2; tazama pia Ufalme wa Mungu, wa Kristo; Injili haianzishi sheria mpya kwa ajili ya ufalme wa raia, 229.3; 230.6; tazama pia Injili. Tazama pia Mamlaka; Serikali; Watawala; Upanga
Ufufuo, wa wafu, 3.10; 20–21.1; 231; 366.6; 510.10; 626.24; wa mwili, 2.8; 366.5; 391.25; 456.34; 460.60; 568.46–48; 592.87;
Ubatizowa kila siku si lolote isipokuwa kumuua Adamu wa kale na ufufuo wa kiumbe mpya, 488.65; hutokea kwa njia ya imani, 133.250; 187.46
Ugomvi, kanisani, tazama Mabishano
Ugonjwa, dhambi ya asili ni ugonjwa wa maumbile, 11.2
Uharibifu, wa asili ya binadamu, tazama Ashiki Mbaya; Asili ya Binadamu; Dhambi ya Asili; ajili ya uharibifu; tazama uchaguzi; Dhambi ya Asili
Uharibifu, wa kanisa, tazama Mpinga Kristo; uharibifu wa kweli siyo kwamba, madhabahu yanasimama bila mapambo, bali ni kutoijua Injili, 270.44-45
Uhuru (Libertas), wa mapenzi, tazama Hiari (Arbitrium); Uhuru wa Kikristo: lazima uhifadhiwe kanisani, 66–73.51; 679.15; lazima udumishwe kuhusu sherehe za nje na Mapokeo ya binadamu, 4852.42; 299.15-16; 542.6, 10, 12; tazama pia Sherehe; Siku; Mapokeo ya binadamu; mitume hawakuharibu uhuru wa Injili, 174.44; mfano wake ni ukomeshaji wa kuishika Sabato, 67-74.60; uhuru unapaswa kutumiwa kwa kiasi, ili wasiokuwa na ujuzi wasiudhike, 228.51; kutumiwa vibaya na watu, 357.3; na wachungaji, 393.3
Ujazo, kuhusiana na wongofu, 578.23. tazama pia Wongofu
Ukamilifu, watawa wa kiume walijidai kuwa katika hali ya ukamilifu, 55–60.46; 285.9; tazama pia Maisha ya Utawa;Watawa wa Kiume; usiopatikana katika Mapokeo ya binadamu, tazama Mambo Yasiyokuwa ya Lazima Kuyajali; Sherehe; Mapokeo ya binadamu; haumaanishi kuondoka nyumbani na kuiacha familia, kujiepusha na mali na milki, au kujizuia kutoka shughuli za raia, 19–20.4; 233.9; 292.45; wala useja au uombaji, 56–61.50; u katika kumfuata Kristo, 293.48; kukua katika kicho cha Mungu katika imani, upendo kwa jirani, na kujitolea katika wito wa fulani, 19–20.4; 56–61.49; 233.9; 289.27; 291.37; watu wote bila kujali wito wao, lazima wautafute, 291.37; mshona viatu katika Mji wa Iskanderia, 291.38; lakini kila mahali, Maandiko Matakatifu yanasema kwamba, tunapungukiwa sana katika huo, 206.142; tazama pia Sheria, mafundisho kwamba, wengine wanaweza kuupata katika maisha haya yanakataliwa, 17.7. Tazama pia Sheria; Kazi
Ukataji Tamaa, tunda la dhambi ya asili, 317.2; Ibilisi anaweza kutudanganya na kutupotosha kwa huo, 369.18; ambao hawajasikia lolote kuhusu neema ya Kristo na wale wanaoshuku kwamba, wana
769
msamaha huanguka kwa huo, 4650.13; 195.89; mafundisho ya wapinzani, mafundisho ya sheria, ni mafundisho ya ukataji tamaa, 195.89; bila Kristo, tangazo la sheria pekee, huwasukuma watu kwa huo, 617.10; na mafundisho ya kuzihesabu dhambi moja moja, 180.10; 346.45; na fundisho la uongo la uchaguzi, 545.9; 547.16; 684.10; tazama pia
Uchaguzi
Ukatili, wa maaskofu, 219.2; wa papa, 347.49. Tazama pia Udhalimu
Ukiri wa Athanasio, tazama Kiri
Ukiri wa Augsburg, 6-77; 362; 507.1; 549.11; 551.30; 552.4; 552.5-6; 554.10; 555.5-6; 555.7; 557.11-12; 559; 561.7; 579.28-30; 583.45; 588.66; 594.1,6; 605.55; 607.66; 607.1; 627. Mapatano yake na Maandiko Matakatifu, 7.8; na Ishara za zamani, ni imani takatifu ya Kikristo, 552.4; ni pamoja na karibu idadi nzima ya mafundisho yote ya Kikristo, 202.124; ni imani yetu (ishara) kwa kizazi hiki, 508.4; 555.5; 557.11; litabaki kuwa msingi wa mafundisho ya makanisa ya Kiinjili, 552.5; 563.20; 700.6; lilichangiwa na baraza la huko Smalkaldi, 354; na tena baraza la huko Naumburg, toleo la kwanza lisilobadilishwa, 508.4; makosa yamesambazwa chini ya jina lake, 528.1; fasiri yake sahihi itapatikana kutoka maandiko ya Luther, 634.34; 636.41; makanisa ya, 572.2; 574.8;
770
589.73; wanatheologia wa, 528.1; 534.1; 541.1; 542.1; 544.1; 547.22; 558.19; 559.1; 572.1; 594.1; 605.55; 607.1; 615.2; 627.1; 631.17; 654.1, 4; 676.1; 682.1; 700.94; 700.4; walimu wa, 373.5; 594.4; 640.58; 643.73; 679.18
Ukiri wa Miji Minne (Strassbourg, Memmingen, Lindau, na Konstanz) (Confessio Tetrapolitana), ya Wanatheologia hasa ya Martin Bucer na Wolfgang Kapito, Walioidharau Sakramenti, 627; 629.9, 630.12
Ukiri wa Mitume, 2; 12.6; 90.1; 98.51; 306; 365–366; 394.11-13; 451–461; 508.3; 552.4. Tazama pia Mafungu ya Imani
Ukiri wa Nikea, tazama Kiri
Ukiri wa, Kiri za Imani, huwaalika wengine waamini 123; huliheshimu jina la Mungu, 410.70; kanisa limejengwa juu ya huduma ya ukiri alioufanya Petro, 342.25; Kiri tatu za Kiekumeni ndizo kiri takatifu za imani, 552.4; Kiri za Watu Waiaminio Injili, 508.4-5; 551.30; 552.3-4; 552.5-6; 552.2; 552.5; 704.39. Tazama pia Imani; Ishara
Ukoma, dhambi ya asili ni kama ukoma wa kiroho, 559; 565.33; Uungwana, tazama Uhuru
Ukwasi, iwapo kweli tunaamini kwamba, Baraka na vipawa vyote vinatoka kwa Mungu, hatupaswi kujigamba na kujivuna kana kwamba,
tuna ukwasi wetu wenyewe, 454.21. Tazama pia Baraka; Miliki; Mali
Ukweli, katika msingi wa muungano wa binafsi, mtakatifu na asili za binadamu za Kristo zinahusishwa kwa njia ya mwandani moja na nyingine katika ukweli, 535.2; 536.11; 537.15; 667.63; tazama pia Kristo, umuhimu wa huu kwa
Kristologia, 659.23
Ulegevu (Ακηδεια), 415.99
Ulimwengu, umetafuta kujifunza ni nini Mungu anaweza kuwa na anafikiria kulitenda lakini haujafanikiwa, 460.63; hauamini, 406.42; haumtambui Mungu kama
Bwana na Muumbaji, 454.21; hulaani na kutesa kweli na watoto wa Mungu, 439.262; haujizoezi lolote isipokuwa ibada za uongo na kuabudu sanamu, 402.17; umejaa kukufuru, madhahebu, walimu wa uongo, na mafundisho maovu, 89.49; 467.47; mafundisho ya uongo ya matendo huushikilia, 124.206; hautambui matendo mema yanayompendeza Mungu, 444.290; haya si muhimu wala hayavutiifu machoni pake, 447.313; hutumia vibaya Baraka zote za Mungu kwa ajili ya fahari yake yenyewe tu, pupa, furaha, na anasa, 454.21; hauchukulii mifumo mingi ya wizi kuwa dhambi, 446.304; ni zizi kubwa pana lililojaa wezi wakuu, 435.228; unaendelea kuwa mwovu zaidi, 36.14; hujaribu kutupotosha
771
tuamini uongo, kukata tamaa, hasira, na kutosubiri, 369.18; 476.103; kujiingiza mwenyewe katika jumba la watawa kulisemekana kuwa kuutoroka na kuyatafuta maisha matakatifu, 56–61.57
Ulinganifu, Ustahili wa, tazama Ustahili/Stahili
Umaskini, umaskini wa Injili si pamoja na kuacha mali, lakini ni kutokuwepo na tamaa na tegemeo katika ukwasi, 293.46. Tazama pia Maisha ya Utawa, Nadhiri za Utawa; Watawa wa Kiume; Mali; Matendo; Ibada
Umma, 239.16; 307.5; 393.4
Unafiki, Wanafiki, uhusiano wao na kanisa; tazama Kanisa; na sakramenti, tazama Chakula cha Bwana, Sakramenti; mradi tu watu wanasikia mahubiri ya sheria na hakuna lolote kuhusu Kristo, wanakuwa wanafiki wenye kiburi, 525.8; na wanamhukumu Mungu kutokuwa mwenye haki katika kuwaadhibu wao, 198.108. Tazama pia Wasiomcha Mungu; Waovu
Ungamo (la dhambi), 16; 4344; 177-180; 180-210; 368369; 501-506; huwa na sehemu mbili: tunaungama dhambi zetu na tunapokea ondoleo la dhambi, 371.16; ya kwanza ni kazi yetu, ya pili ni kazi aifanyayo Mungu, 503.15; kazi ya Mungu ni kamili na nzuri ambayo hulifanya ungamo
liwe la kuajabia na la kufariji, 4344.3; 503.15; chini ya upapa, kazi yetu pekee ilisisitizwa, 504.16; ya hadharani na ya faragha, 502.8; yote yamejumlishwa katika Sala ya Bwana, 502.8-9; aina hii ya ungamo lazima ifanyike bila kikomo, 503.9; si lazima kuziorodhesha dhambi zote kwa kuwa haiwezekani, .16 (IX); 44-45.10-11;177.1; 178.6; 183.23; 197.102; 322.19; 328.1-2 (VII); 329.2 (VIII); 346.45; watu binafsi hawapaswi kutafuta au kuzibuni dhambi wasije wakalibadilisha ungamo kuwa mateso, 373.24; mbele ya mwungamishi, inatubidi tuziungame tu zile dhambi ambazo tunazijua na zinazotusumbua, 371.18; ungamo linalofanywa kwa Mungu kwa moyo ni majuto makubwa, 198.107; linajumuisha dhambi zote, 325.37; hatuupokei msamaha kwa sababu ya ungamo letu, 197.95, siyo kwa njia ya tendo lenyewe, 182.12; lakini kwa sababu ya Kristo, 197.95; ungamo la faragha halijaamriwa, 503.14; halijaamriwa katika Maandiko Matakatifu lakini limeanzishwa na kanisa, 44-45.12; linapasa liwe huru kutoka ushawishi, 178.5; 501.1; 504.21; lilikuwa maumivu matupu na mateso mabaya mno chini ya upapa, 502.3; tunafahamu jinsi ya kulitumia kwa ajili ya kufariji na kuimarisha dhamiri yetu, 502.4; ushawishi si lazima, 504.23; 506.32; ni kimbilio la kweli kwa moyo
unaohisi dhambi zake, 503.14; dawa ya kutibu, 505.26; halikosi kuwa na hakika, 325.37; kwa vyovyote, halipaswi kuruhusiwa kutotumika kanisani, 43-44.1; 4445.13; 329.1 (VIII); kwa uhuru wao, watu hujinufaisha kulihusu, 502.5; yeyote anayelidharau si Mkristo na hapaswi kuipokea sakramenti, 505.29-30; maagizo na umbo fupi, 368-369; miongoni mwa waandishi wa kanisa, 199.112; ugomvi baina ya watawa wa kiume na wachungaji kwa ajili ya kulisikiliza ungamo, 7576.2; 179.8. Tazama pia Ondoleo la Dhambi, Funguo
Ungamo la Faragha, tazama Ondoleo la Dhambi; Ungamo
Upanga, papa hudai kumiliki panga zote mbili, wa kiroho na wa duniani, 169.23; 333.2; tazama pia Papa, uwezo wa maaskofu unapasa kutofautishwa na upanga wa duniani, 72–71; tazama pia Maaskofu; Uwezo wa Kanisa; Kristo hakuwapatia mitume uwezo wa upanga, 343.31; upanga wa duniani (wa kuonekana), tazama Mamlaka; Utawala wa Raia; Serikali; Adhabu, Adhibu
Upapa, tazama Papa
Upendo, ni utimizaji wa sheria, 114.147; 116.159; upendo kwa Mungu na jirani ndiyo maadili mema zaidi kuliko yote, 128.226; lakini hatupokei msamaha wa dhambi na upatanisho kwa sababu ya huo,
110.111-112; 114.147; hauhesabii haki, 116.159; 193.78; 195.87; 520.15; 599.27; 601.38; tazama pia Kuhesabiwa Haki; maana kama ulifanya hivyo, hakungekuwa na haja ya Kristo kama msuluhishi; hatupendi tunavyopaswa, 109.110; 153.342; mtu hawezi kupenda bila haki ya imani na msamaha wa dhambi, 93.18; 96.36; 109.110; wapinzani wanahubiri kuuhusu, lakini hawauonyeshi, 130.236; huifuata imani kama tunda fulani na la lazima, 102.74; 110.111; 185.37; 194.82; 236.14; 519.11; 599.27; watu wote wanapaswa kutafuta kukua katika upendo kwa jirani yao, 291.37; unapopotea, imani na Roho Mtakatifu hupotea, 126.219; 128- 129; 520.17; bila huo, imani inakufa, 607.1. Tazama pia Imani
Upendo wa Asili, upendo wa jinsia moja kwa nyingine ni agizo takatifu, 250.7–13; ashiki mbaya huuamsha ili uhitaji dawa ya ndoa sasa, 251.13; 251.16; tamaa mbaya, tazama Ashiki Mbaya; Dhambi ya Asili Naumburg, Mapatano (1561)
Usafi, tazama Utakaso
Usafi, 430-433; yaliyomo ya amri ya usafi, 431; neema ya Mungu inahitajika kuudumisha, 432.212; jinsi Roho Mtakatifu na imani ilivyo, 112.132; 170.31; 222.15; unapaswa kudumishwa kwa njia ya ndoa, 252.19; 432.212; usafi wa kudumu haupatikani katika uwezo wa
773
binadamu, 54-59.28; huificha haki ya imani, 55-61.48; nadhiri zote za usafi zilizo nje ya ndoa zinalaaniwa na Amri ya Sita, 432.216. Tazama pia Useja; Amri, Ndoa za Makasisi; Nadhiri za Utawa; Ubikira; Nadhiri
Usafi, Kristo huwakemea Mafarisayo kwa kufikiria kwamba, wanatakaswa mbele za Mungu, kwa kutawadha mara kwa mara, 141.282; usafi hukirejelea kitu kinachokubalika na kuidhinishwa mbele za Mungu, 254.33; ndoa ni safi, 254.33; Injili huhitaji usafi wa moyo si usafi wa nje wa sheria, 259.64; usafi wa moyoni na wa kuufisha uasherati mbaya, 254.35; utakaso wa nje unapaswa kutafutwa katika matendo yaliyoamriwa na Mungu na si katika Mapokeo ya binadamu kama kutawadha katika sherehe, 141.283; usafi mkubwa wa moyo unaweza kuwepo katika mtu aliyeoa kuliko katika wengi wa wale wanaoitawala tamaa kweli, 254.35; 259.64; “Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi” (Tito 1:15a), 254.34; 255.41; 259.64; hatuchukuliwi kuwa wenye haki kwa sababu ya usafi wetu wenyewe, 105.86. Tazama pia Useja; Usafi; Ndoa ya Makasisi; Ubikira
Usalama, huwa katika sala pekee, 465.30 Watakatifu
Useja, hauhesabii haki, 287.21; haustahili msamaha wa dhambi, 248-250; watu wachache wana kipawa hiki, 34-37; 293.51;
watawa wa kiume waliutukuza kana kwamba, ulikuwa namna ya maisha ya kimalaika, 255; lakini useja wa watawa wa kiume na makasisi unasababisha utovu wa adabu; 286.16; 432.214; nadhiri za, 3337; 332.1-3 (XI); nadhiri ya jinsi hiyo si sahihi kwa wasiokuwa na kipawa, 293.51. Tazama pia Usafi; Ndoa za Makasisi; Nadhiri za Utawa; Ubikira; Nadhiri
Usharika, tazama Kanisa
Ushirika wa Platon, kanisa si jamhuri fulani ya Platon, 168.20; akili ya wajima haina amri ya Mungu (dhidi ya watawa wa kiume), 238.13; semi “kuua” na “kuhuisha” hazipaswi kueleweka kiakili, 187.46
Ushirika wa Wakristo, tazama Kanisa
Ushirika/Komunyo/Ekaristi
Takatifu, tazama Chakula cha Bwana, Umoja wa Watakatifu, tazama Kanisa hayataki matendo yaliyo chini ya shurutisho, 610.17; kuongoza kwa Roho Mtakatifu si shurutisho, 587.64
Ushuhuda, Roho huwapatia wateule ushuhuda kwamba, wao ni watoto wa Mungu, 688.31; 695.73; matendo ni shuhuda za imani, 120.184; wa uwepo na Roho wa kukaa ndani, 523.15; tazama pia Matendo; sakaramenti kama shuhuda za neema na msamaha wa dhambi, tazama Sakramenti; Ishara ni ushuhuda wa
774
imani na wa ukweli, 510.8; 557.13; 558.16 Ukiri wa Miji Minne, tazama “Confessio Tetrapolitana”
Ustahiki, tunapatanishwa na Mungu kwa sababu Mungu huuahidi na si kwa sababu ya ustahiki wa matendo yetu, 98–100; tazama pia Matendo; Mungu hutusamehe dhambi zetu bila ustahiki wowote wetu wenyewe, 518.4; na hutuhifadhi, hutukirimia, na hutulinda, 362.2; wasioitumainia ahadi ya Mungu bali ustahiki wao wenyewe hawawezi kuomba, 479.121– 122; imani pekee humfanya mtu astahiki kuupokea Ubatizo, 484.33; Ustahiki wa Chakula cha Bwana, tazama Chakula cha Bwana
Ustahili (stahili), kukataa kwa mafundisho ya wapinzani kwamba, watu wanapokea msamaha wa dhambi kwa sababu ya stahili zao wenyewe, 90-164; tazama pia Sherehe; Mapokeo ya binadamu; Nadhiri za Utawa; Watawa wa Kiume; Nadhiri; Matendo; ya majuto madogo, 183.18; 191.68: 215.178; wa ulinganifu na wa hadhi, 93.19; 114.146; 142-143; 166-7; 156.356; wa zaidi ya kadiri ipasayo kwa haki, 171-2; 285.9; 288.24; wa watakatifu, 236-245; 311.24; wote wanaojaribu kujipatia msamaha wa dhambi kwa sababu ya stahili zao wenyewe wanaikomesha ahadi ya Kristo na wanamtelekeza Kristo, 286.17; na wanaiponda Injili, 290.34;
stahili na kuhesabiwa haki, tazama Kuhesabiwa Haki; imani katika stahili zetu haileti tegemeo kwa Mungu, 97.44, 46; lakini katika ustahili wa Kristo, tazama Kristo, ndani yake, imani huishikilia na huikubali ahadi ya Injili, 603.43; stahili za Kristo ndizo gharama na dhabihu ya kupatanisha, 99.53; tuna Mungu wa rehema kwa hizo, 12–13.3; Kristo huziweka dhidi ya ghadhabu ya Mungu, 286.17; zinatolewa kwetu, 130.238; 262.12; tunahesabiwa haki kwa tegemeo letu kwazo, 239.19; tunakombolewa kwa njia ya ustahili wa Kristo, 560.6; uchaguzi wetu unaitegemea, 547.20; 695.75; tazama pia Uchaguzi; mafundishao ya Waanabaptisti kwamba, haki yetu mbele za Mungu haiutegemei tu bali pia hukutegemea kufanywa upya kwetu kunakokataliwa, 548.5; 701.10; ustahiki wote wa wageni katika meza ya mlo wa mbinguni wa Kristo ni na ni wa ndani yake pekee, 531.20; 643.71; tegemeo katika stahili za Kristo lazima zitoe msingi wa sala, 240.20; ustahili wa Kristo haupatikani kwa njia ya tendo au pesa zetu, bali kwa njia ya imani kwa neema, 311.24; lazima tuitenganishe kabisa na matendo yetu, 519.10; hatupaswi kuichanganya katika ustahili wa ridhaa, 210.157; itawabidi watu waitambue kwa njia ya mafundisho sahihi ya dhambi ya asili, 560.3; mafundisho ya wapinzani kuhusu dhabihu ya Misa
huutangua ustahili wa kuteseka kwa Kristo, 273.57; ustahili wa Kristo unafichwa kwa njia ya kuichanganya sheria na Injili, 549.11; 621.27. Tazama pia Thawabu
Utaji wa Musa, tazama Musa Veno, 402.18
Utakaso, uhusiano wake na kuhesabiwa haki, 601.39–41; si sehemu ya haki ya imani mbele za Mungu, 601.39; 604.48; bali hutokana nao, 597.21; 599.28; 602.41; kwa njia ya Injili tunatakaswa kwa damu ya Kristo aliyeuawa na kuhuishwa, 269.38; Kristo hulitakasa kanisa, 165.5; ndoa, chakula, na vitu kama hivyo “vinatakaswa kwa Neno la Mungu na sala,” 253.30. Tazama pia Mtakatifu; Maisha, Mpya; Kufanywa Upya
Utaratibu wa Kikanisa, tazama Maagizo ya Kanisa Watumishi wa Kanisa, tazama Wachungaji Utumishi wa Kanisa, tazama Huduma
Utatu Mtakatifu, ni siri kubwa kuliko zote, 538.18; 661.33; Utatu Mtakatifu wote unawaelekeza watu kwa Kristo, 668.66. Tazama pia Kristo; Mungu; Roho Mtakatifu
Utekelezaji wa Sheria kama Mamlaka, ya Maaskofu, 349-353; huwa na mamlaka kuhusu kesi za ndoa kwa haki ya binadamu, 352.77. Tazama pia Maaskofu Wanasheria, 250.9, 11; 439.261; 445.299. Tazama
pia Mawakili
Utetezi wa Ukiri wa Augsburg, 81-301; 349; 349.60; 354; 518.7; 580.31; 561.8; 574.25; 580.31-32; 583.45; 594.6; 597.19-20; 602.42; 603.43; 607.66; 610.14; 613.21; 613.33; 618.15; 621.27; 624.11; 639.55; 650.110; 689.38; 705.39; ilitambuliwa kama mwafaka na maelezo ya mafundisho ya Kikristo, 509.4; 553.6; 554.10
Utiifu, Tii, kwa Mungu: binadamu wote wanalazimika na sharti wamtii Mungu, 608.4; miili yetu inapasa kuwa dhabihu ili kuonyesha kutiifu kwetu, si kugharamia mauti yetu ya milele, 211.160; Amri Kumi za Mungu zinahitaji kumtii Mungu katika mauti na katika mateso yote, 91.8; tazama pia Mateso; Msalaba; kuitii sheria kungekuwa haki iwapo tungeishika sheria, lakini hatuwezi kuishika, 118-119; imani ni kutiifu kwa Injili na inahesabiwa kama haki kiasi kwamba, kuitii sheria kunampendeza Mungu tu kwa sababu tunaamini kwamba, Mungu ni mwenye rehema kwetu kwa ajili ya Kristo, 141-142; utiifu mpya, 14; 111–121; tazama pia Sheria, Maisha, Mapya; binadamu viumbe waliozaliwa mara ya pili sharti wauonyeshe, 521.3, 10; ambacho Injili inakifanya kuutekeleza lazima kitofautishwe kutoka kile sheria ikifanyacho, 624.10; kwa wazazi: tazama Amri Kumi za Mungu, kwa
serikali: lazima tujizoeze upendo kwa njia ya utiifu wetu kwa sheria za sasa, iwe zimebuniwa na wapagani au na wengine, 229.3; tazama pia Mamlaka; Ufalme wa Raia; Serikali; Watawala; kwa maaskofu: tazama Maaskofu; kwa papa: tazama Papa; watawa wa kiume wanajigambia utiifu wao, 286.16; lakini bora tu usiwe mchafu, ni sura ya nidhamu isiyokuwa ya lazima, 287.21; tazama pia Nadhiri za Utawa; utiifu wa Kristo, 605.56, 58; tazama pia Kristo
Utukufu, wa Mungu, tazama Mungu; wa Kristo, tazama Kristo, wa watakatifu, tazama Watakatifu
Uumbaji, Viumbe, 452-454; Mungu alituumba kutukomboa na kutufanya watakatifu, 460.64; Kristo ni muumba wetu, 636.44; tu viumbe wake Mungu, 453.13; hata baada ya anguko, asili ya kibinadamu ni na inabaki kuwa kiumbe cha Mungu, 509.2, 4; 560.2; 565.32, 34; kazi na uumbaji wa Mungu lazima vitofautishwe na kazi ya ibilisi, 513.25; 560.3; 567.42; 696.79; uwezo wa binadamu hauwezi kustawisha au kubadilisha uumbaji wa Mungu bila kipawa maalumu chake Mungu, 33-35.6; hanjamu ni uumbaji wa Mungu, 249-251; 252.19; 332.2 (XI); tazama pia Hamu ya Asili; uumbaji wa Mungu na amri vinaelekeza vyote kwa asasi ya ndoa kwa ambao hawajabarikiwa kuwa
na kipawa cha ubikira, 53-58.20; tazama pia Ndoa; Ubikira; maagizo halali ya raia ni uumbaji bora wa Mungu, 229.1; kujua kwa milele kwake Mungu kabla kunahusu viumbe vyote, 573.4; Mungu na Kristo wapo katika viumbe vyote, 538.16; 648.101; Mungu hutoa msaada kwa viumbe vyote kwa kuvipatia manufaa na mahitaji ya maisha; viumbe ni mikono, njia na namna ambazo kwazo Mungu huzitoa Baraka, 404.26; kutafuta msaada na maliwazo kutoka viumbe ni kuabudu sanamu, 403.21
Uvumba, fulani hawezi kutoa uvumba bora zaidi dhidi ya Ibilisi kuliko kujishughulisha mwenyewe na amri na maneno ya Mungu, 394.10
Uwepo Kila Mahali, wa Mungu, tazama Mungu; wa Kristo, tazama Kristo
Uwepo, wa Mungu, tazama Mungu, wa Kristo katika Chakula cha Bwana, tazama Chakula cha Bwana; wa Kristo ndani yetu, tazama Kristo Uwezo, wa asili ya mtu, tazama Asili ya Binadamu; Mapenzi
Uyahudi, -a Kiyahudi, Uyahudi wa Raghba 217.18; 220.4 (XV)
Uzazi, Mpya, tazama Kuzaliwa Upya
Uzima
A. Uzima wa Mkristo: chini ya Upapa ulichukuliwa kuwa uzingatifu wa mapokeo, 46-50.8-9; si lolote isipokuwa Ubatizo wa kila siku, 488.65
B. Uzima wa milele: unatolewa pamoja na kuhesabiwa haki kwa njia ya rehema kwa sababu ya Kristo, 145; mwili wetu utahuika ukiwa na utakatifu kamili na mkamilifu ndani yake, 459.57; Injili ni mwanzo wake katika mioyo ya waumini, 230.6; Neno la Mungu na Roho Mtakatifu huitekeleza moyoni, 299.10; kwa maana gani Maandiko Matakatifu huuita tuzo, 156.356; 157-160
C. Uzima Mpya: 111-121; Roho hufanya kazi ndani yetu, 112.132; 273.59; Ubatizo huuzaa, huuanzisha, na huufuata, 489.75; imani huuzaa mioyoni mwetu, 111.125; hukua kutokana na majuto makubwa na imani (toba), 186.45; 204.132. Tazama pia Ubatizo; Wongofu; Imani; Roho Mtakatifu; Kuhesabiwa Haki; Kiumbe Mpya; Kuzaliwa kwa Pili; Toba
D. Maisha ya kiroho: chini ya upapa, yeyote aliyezizingatia desturi alisemekana kuwa aliishi maisha ya kiroho, 46-50.8-9
Uzushi, Wazushi, 479.2; Ibilisi anajaribu kuikandamiza na kuipotosha Injili kwa kuwachochea, 299-300; acheni farakano na uadui (chuki) kanisani, 129.232;
131.242; ulokole ndicho chanzo, uwezo, na nguvu yake 330.9; kiri za imani zinawekwa mbele dhidi ughushi wa wazushi, 554.4; wale wanaowatenga, wanaowakataa, na wanaowaepa Waiaminio Injili kama wazushi wanaenda kinyume cha umoja na upendo wa Kikristo, 28-29.1; papa, wanatheologia, na wanasheria, wanayaita mafundisho ya Kiinjili uzushi, , 326.41; wahubiri wanyofu na Wakristo lazima wavumilie kuitwa wazushi na ulimwengu, 439.262; wale wanaotiwa mikono hata na wazushi lazima pia wachukuliwe kama na wanabaki waliotiwa mikono, 331.3
Vifaa vya Dhambi vya Moto, 83.7; 88.42. Tazama pia Dhambi ya Asili Zaka, kanisani, 59–64.29; katika Israeli, 264.21
Vijana, wanapaswa kulelewa katika kicho na heshima ya Mungu, 411.75; 451.330; wajibu wao, 378.12; wanapaswa kufundishwa katekisimo kikamilifu, 357.6; 397.3; 400.26; 449.321; 501.85; wanapaswa kuhudhuria mahubiri hasa wakati mahubiri kuhusu katekisimo yanatolewa, 400.26; katekisimo itakapokuwa imefahamika, fulani anaweza kuwapatia zaburi au nyimbo za dini ili kuongezea na kuyathibitisha maarifa yao, 399.25; wanapaswa kuwa na tabia ya kuomba kila siku, 465.28; wanajaribiwa hasa na mwili, 477.107; wanapasa kuoa
na kuolewa kwa heshima, 433.218; nadhiri wakati fulani yu kijana, 3437.26; 54–59.29
Vita, vinasababishwa na Ibilisi, 302; 473.80; Wakristo wanaweza kupigana vita vya haki bila dhambi, 19–20.2; 229.1; kulipiza kisasi faraghani kunakataliwa lakini si haki ya hadharani ambayo ni pamoja na vita, 230.7; mfalme mkuu anaweza kuufuata mfano wa Daudi katika kupigana vita na Waturuki, 29.1
Vita vya Mafalahi, (mapinduzi) (1525), 302; 325; 329
Vyakula, tofauti za, 45-55; 6065.39; 225.30; ni desturi ya binadamu, 141.283; 172.35; tazama pia Mapokeo ya binadamu; kwa hiyo si tendo la sala linalohesabia haki wala ukamilifu, 288.26; jambo ambalo si lazima kulijali, 678.13; kufikiria kwamba, watu wanaweza kujipatia neema au kufanya ridhaa kwa dhambi kwa njia ya hivyo ni kinyume cha Injili, 16- 17.4; kwa kufaa, Chakula cha Bwana kinaitwa chakula cha nafsi, 493.23
Vyeo vya Heshima, utengano miongoni mwa watawala na vyeo vya heshima, 304.12
Vyeti vya Upatanisho, wapinzani wanadai kutumia stahili za watakatifu kwa watu katika hivyo, 240.23; vinasemekana kusamehe radhi, 204.135; 323.24; awali vilihusika na msamaha wa toba ya hadharani,
214.175; lakini vimeelezewa visivyo kama ukombozi wa nafsi kutoka Purgatorio, 183.26; 214.175; vyeti vya upatanisho kwa wafu, 182.15; 323.24; 323.26; katika mazoea ya ungamo, 43.5; ingawa papa aliwafundisha watu wavitegemee, aliufanya mchakato kutokuwa wa hakika, 323.27; ni uongo usioghushiwa uliobuniwa kwa faida, 346.46
Vyombo, tazama
Vyombo, vya heshima na visivyokuwa vya heshima, 696.79; vya ghadhabu na vya rehema, 696.79
Waaguzi wa Sibylla Sodoma, 304.11
Waanabaptisti, 13.4; 15; 16.3; 17.7; 19.3; 20-21.4; 101.66; 175-176.3; 217.13; 548-1; 412.27; 633.29; 700.1, 701.9; madhehebu yaliyo maisha mapya ya utawa, 548.5; 701.10; 703.27
Waandishi, 14–15.2; 324.29
Wapelagio Wasio Kamili, 510.10
Waandishi wa vitabu vya ungamo, 46–50.14; 171.32; 179.7; mateso ya wajumlishaji, 179.9
Waariano, 3; 9-10.5; 540.39; 653.126; 671.75; 551.28; 700.1; 704.36
Wachungaji, wa wapinzani hawajaomba kikamilifu kamwe, 464.25; wapinzani wanadai
kwamba, cheo cha wachungaji ni cha juu kuliko cha Wakristo wa kawaida, 247.9; wakati uliopita, kulikuwa na majadiliano kuhusu ni nani aliyekuwa kasisi halisi kati ya makasisi wa kawaida na makasisi wa madaraja fulani, 179.8. Tazama pia Maaskofu; Makasisi; Huduma; Watawa wa Kiume; Ofisi; Wachungaji; Wahubiri; Kuhubiri; Makasisi
Wachungaji, kanisa lina mamlaka ya kuwateua wao, 217.12; ni watumishi wa Neno na viongozi wa jumuiya ya Mungu, 677.10; wote ni sawa, na yeyote hawezi kutawala kama kabaila au kuwa na cheo kikubwa kanisani, 376.11; wana amri ya kutangaza ondoleo la dhambi, na si kupeleleza siri, 197-198; wanapaswa kuwafundisha na kuwachunguza vijana hadharani, 227.41; kutofaa kwao hakuwadunishi kutokana na kufaa kwa sakramenti, kwa sababu hata wasiofaa wanatenda kwa niaba ya na pahali pa Kristo, 170.28; 175.47; isipokuwa kwa walimu wasiomcha Mungu walio Wapinga Kristo, 175.48; kosa la Wafuasi wa Schwenckfeld, 550.27; 704.35. Tazama pia Maaskofu; Wachungaji; Wahubiri
Wachungaji, nyakati zilizopita, waliteuliwa na watu, 351.70; kubarikiwa kuwa mchungaji hakukuwa lolote isipokuwa kuthibitishwa na askofu, 351.70;
779
wote wanaoyaongoza makanisa waligawanya uwezo wa kanisa la Kikristo, wawe wanaitwa wachungaji, wazee wa kanisa (wapresbyteri), au maaskofu, 349.61; kubarikiwa kuwa mchungaji kunakofanywa na mchungaji katika kanisa lake mwenyewe ni halali kwa haki takatifu, 350.65; mamlaka halali ya kawaida ya kutenga na kanisa ni ya wachungaji, 352.74; zamani, walikuwa na ugomvi usiokwisha na watawa wa kiume; ndoa ya wachungaji, tazama Ndoa za Makasisi; wajibu wao, 375.2; lazima wajifunze katekisimo wenyewe kila siku, 393.3; 396.19; wawafunze watu katekisimo, hasa vijana, 227.41; 358.6; waombe Sala ya Bwana wao wenyewe na kwa wakazi wao wa usharika (parokia), 393.3; kwa bahati mbaya, walimu wengi hawana ustadi na hawajimudu kabisa, 357.2; wazembe katika kufundisha, 392.1; wachungaji ni kipawa cha Mungu, 342.26; 350.67; kusanyiko la Wakristo linapasa kuwatii, 74.55; miongoni mwa malodi kuna wengine wanaotangaza kwamba, hawawahitaji, 393.6; papa si mkuu kwao kwa haki takatifu, 338.7. Tazama pia Wachungaji; Ofisi; Wahubiri; Kuhubiri
Wachungaji, wachungaji wa kweli huwalisha kondoo na huwakinga mbwamwitu, 557.14. Tazama pia Wachungaji; Wahubiri
Wadhamini wa Ubatizo, tazama Wadhamini
Wadhamini (Wadhamini wa Ubatizo), wenye kuhusu Ubatizo, 387–391; ni haki na ni sahihi kutowateua wadhamini bure wa wa ubatizo, 388.8; wasiotaka kujifunza katekisimo wasiwe wadhamini katika Ubatizo 358.11; ndoa baina wadhamini wa ubatizo wawili, “wadhamini wa ubatizo” katika kaida kama vile kengele za ubatizo na mawe ya madhabahu, 334.4
Wadominikano, wamebuni maumbo maovu ya aina hiyo ya ibada kama vile rozari, 223; 294.53; mafundisho ya uongo ya Ubatizo, 327.2 (V)
Wadonatio, 15.3; 170.29; 175.49
Waenkratito, 223.21; 256.45, 50
Waepikuro, 583.46; 652.123; ushawishi wa Epikuro, 523.18; 613.31; maisha, life, 545.9; 615.39; anasa, 610.15
Waeunomio, 9-10.5
Wafalme, tazama Watawala
Wafransiskano, 86; 92; 206; 207; 223; 283; 327; 327.3; hadithi ya Yohana Hilten, 283.1-3
Wafu, kuhusu wao, hatujapokea amri wala fundisho, 309.12; maombi kwa ajili yao hayakatazwi, 281.94; 282.96; Misa si dhabihu na haistahili msamaha kwa ajili yao, 39-41.22;
780
262.11; 274.64; lazima tukatae mafundisho ya wataalamu wa ghiliba na Wakanunisti kuhusu vyeti vya upatanisho na dhabihu ya Misa kwa
ajili yao, 182.15; 280.89; 309.12; wale wanaoishi katika majumba ya watawa wanasherehekea Misa kwa niaba yao ili kujipatia fedha, 294.53; watawa wa kiume huvalia ukaya ili kuthibitisha kwamba, stahili za mwingine zimetumiwa kwao, 162163
Wafuasi (Wanafalsafa)
Wakakamavu wa Stoa, 515.8; 589.74
Wafuasi wa (Paulo) Samosata, 9–10.6; 657.15
Wafuasi wa Calvin, 349.61; 517.2; 534.1; 627; 642; Kifaransa, Wafuasi wa siri wa Calvin, 654; tazama pia
Wafuasi wa Philipp Melanchthon. Tazama pia Walioongoka; Wanatheologia Walioshikilia kwamba, Mkate na Damu katika Ekaristi ni Mwili na Damu ya Kristo Kisitiari tu; Wafuasi wa Zwingli
Wafuasi wa Mwanatheologia
Philipp Melanchthon, Watetezi wa Siri wa Philipp Melanchthon,529; 557; mafundisho kuhusu kazi pamoja na wafuasi wa Philipp Melanchthon, tazama Kazi ya Mungu na Binadamu pamoja, 79; 204; 334; 337; 355; 529; 554; 564; 572; 594; 676
Wafuasi wa Novatiano, 17–18.9
Wafuasi wa Pelagio, 10.3; 83; 93.19; 95.29; 109.106; 232.1–3; 236.14; 511.13; 515.9; 515; 516; 560.3; 562; 564; 590.75
Wafuasi wa Schwenckfeld, 550.20–27; 700.1–2; 703–704
Wafuasi wa Wycliffe, 170.29
Wafuasi wa Zwingli, 84; 88; 215; 245-246; 275; 349; 355; 356; 483; 528; 529; 532; 539; 554; 563; 627; 628; 629; 654; Tazama pia
Wafuasi wa Calvin; Walioongoka; Wanaoidharau Sakramenti
Wafuasi wenye Rai kwamba, Wakristo Wanafanywa Huru kutokana na Haja ya Kuzingatia Kanuni Yoyote ya Mema na Mabaya, tazama Wapinga Sheria
Wagumu wa Moyo, mapatilizo ya Mungu kwa wagumu wa moyo, 697.83. Tazama pia Wasiotubu
Wahubiri, wazazi na wenye mamlaka ya kutawala katika serikali wanapasa kusaidia kuwafundisha watoto kama wahubiri, 360.20; majumba ya watawa yanapasa kurudishwa kwa matumizi kama hayo, 313.1; wanapasa kuisisitiza katekisimo, hasa kwa vijana, 357.6; hawapaswi kuionea shaka neema na shughuli ya Roho Mtakatifu, 585.55; hakuna anayepaswa kuhubiri hadharani bila mwito sahihi, 18; 218.1; kuwabariki wachungaji, 331–332, tazama pia
Bariki; wa uongo hutukana na kulinajisi jina la Mungu, 408.54; 466.41; na dhambi dhidi ya Amri ya Nane, 440.263; wajibu wao, 375.2; hawapaswi kuchanganya mapatilizo ya raia na adhabu ya kiroho ya kutenga na Kanisa, 331; tazama pia Kutengwa na Kanisa; watu wa kawaida wanapaswa kuwatendea mema na kuwapatia chakula chao, 425.161; lakini kila mmoja anapinga kwa sababu ya hofu kwamba, matumbo yao wenyewe yatauma, 425.162; watu wanapaswa kuwaombea, 465.28; wengine miongoni mwa malodi wanaarifu kwamba, hawawahitaji, 393.6; na wanawaacha wateseke kwa dhiki na njaa, 393.6; wengine wanawalaumu, wanawaelewa vibaya, na kuyapotoa mambo kwa njia mbaya zaidi, 443.289; wahubiri wanyofu lazima wavumilie kwa kuitwa wazushi na ulimwengu, 439.262. Tazama pia
Wachungaji; Huduma; Kuhubiri; Walimu
Waislamu, 9–10.5; 289.27; misemo ya Mwislamu kanisani, 289.27
Wajane, 296.64; wajibu wao, 378.13
Wakati wa Mwisho, u sasa, 34.14; 202.126; 257.53
Wakazi wa Sachsen, Sachsen, 472; ziara za Kanisa la Sachsen, (1527–28), -a Chini, wa mwinyi, tazama pia
Walutheri halisi; wenye kuchagua, 543, 749tazama pia Wafuasi wa
Philipp Melanchthon
Wakerthuso, yaani, Wafuasi wa Mt. Bruno, matendo yao yana sura nzuri sana, 481.11; lakini kutimiza amri ni heri kuliko utakatifu wao, 411.74; 418.118; 419.120; 430.197
Wakfu, katika Chakula cha Bwana, tazama Chakula cha Bwana
Wakristo, mafungu matatu ya Imani yanayatofautisha hayo kutoka watu wengine wote, 460.66; na mambo ya jamii, 19-20; 175.50; 229-231; tazama pia Mamlaka; Wito; Ufalme wa Raia; Serikali; Ofisi, Uwezo; Mali; Upanga; Kazi
Wakristo wa Kawaida, wakati wa dharura, hata Mkristo wa kawaida hulitangaza ondoleo la dhambi, 350.67; anapaswa kupokea aina zote mbili za Chakula cha Bwana, 31-35; 245-248; 632.24; 650.110; katekisimo za Luther ni Biblia ya Watu wa Kawaida, 508.5; 556.8
Walimu, yeyote asifundishe hadharani bila mwito sahihi, 18; ni vipawa vya Mungu, 342.26; Biblia hutuonya kwamba, waovu watazuka kanisani, 164-165; 168.22; mitume walipokuwa bado hai, walimu wa uongo walilivamia kanisa, 509.3; ili kuhifadhi mafundisho safi kanisani, ni muhimu kuwakemea wanaolipinga, 557.14; wasiomcha Mungu hawatendi tena kulingana na nafsi ya Kristo bali wao ni Wapinga Kristo, 175.48; na lazima
782
waepukwe, 175.48; watengwe na wakanwe hadharani kuwa wamelaaniwa, 346. 41
Waliorudia Nyuma, 199.113
Waliotengenezwa, papa angependa zaidi kuwaona Wakristo wote wakiangamia na nafsi zote zikilaaniwa kuliko kuvumilia mwenyewe au wafuasi wake kutengenezwa, 302.3; kuhusu Waiaminio Injili: Ukiri wa Augsburg ni ukiri wa Makanisa ya Matengenezo, 555.5; kuhusu Wafuasi wa Zwingli na wa Calvin: 627-654 tazama pia Wafuasi wa Calvin; Wanaoidharau Sakramenti; Wafuasi wa Zwingli. Tazama pia Mabishano
Walokole, wanafundisha kwamba, Mungu huwaongoa binadamu bila njia yoyote ya kuumbwa, isipokuwa Neno na Sakramenti, 516.13; 573.4; 591.80; wanajigamba kwamba, wana Roho isipokuwa Neno, 329.3; kwa njia ya matayarisho fulani yao wenyewe, 221.13; wanalaani Neno la milele, na bado wao wenyewe hawanyamazi, 330.6; wanayatumia vibaya mafundisho ya udhaifu na uovu wa hiari yetu ya asili, 583.46; Ibilisi aliwabadilisha Adamu na Hawa kuwa walokole, na ulokole unawaandama wazao wao, 329.5; 330.9; ni chanzo, uwezo, na nguvu ya uzushi wote, 330.9; cheo cha papa ni shauku pia, 329.4. Tazama pia Waanabaptisti; Walokole;
783
Wanatheologia Wanaoidharau sakramenti; Madhehebu fulani
Walokole, Pepo za Kilokole, 245.43; 326.42; 467.47; 488. 61, 63; 492.12; 632.22; 648.102; Tazama pia Wenye Shauku; Ugomvi Baina ya Vikundi; Madhehebu
Walutheri Halisi
Wamani, 9-10.5; 232.1; 512.17, 19, 22; 515.8; 560.3; 562.16; 564.26–27, 30; 570.55; 589.74; wapya, 568.45
Wana wa Mungu, wanaishi katika sheria, si chini ya sheria, 527.6; Roho aliye mioyoni mwao huwalazimisha kutiifu, 623.6; 695.73; lakini wao si watimilifu bado, 522.13; 623.7; kwa hiyo, wanahitaji sheria, 623.9; tazama Sheria, Tazama pia Kuzaliwa Upya, Watakatifu
Wanafunzi, tazama Mitume
Wanaodharau Sakramenti, 538–534; 535.3; 627–653; 654.1–4; 660.28; 662.38; tazama pia Wafuasi wa Calvin; Warefomu, Wafuasi wa Zwingli; Majadiliano ya Wanadharau Sakramenti
Wanaokataa Utatu Mtakatifu, wapya, 551.29; 700.1; 704.37; 704.38 mara kwa mara, wanamatengenezo waliurejelea Uislamu kama uasi wa wafuasi wa mifumo ya Kikristo inayokubaliana tu na kuikataa imani ya Utatu Mtakatifu, 9.5
Wanyonge, Kristo alikianzisha
Chakula cha Bwana hasa kwa
Wakristo walio wanyonge katika imani lakini wanaotubu ili kuwafariji na kuimarisha imani yao nyonge; 531.19; 642.69
Waovu, wasitengwe na kanisa 164–175; tazama pia Kanisa. Tazama pia
Wasiomcha Mungu
Wapagani, walikuwa na ufahamu fulani juu ya Mungu kutoka sheria ya asili, lakini hakika, hawakumjua wala hawakumheshimu Mungu, 619.22; waliifanya miungu kutokana na kile moyo wao ulikitamani sana, na kwa hiyo, hata katika akili zao, kuwa na mungu kunamaanisha kutegemea na kuamini, 402.18; tegemeo lao haliwi katika Mungu mmoja, 403.19; kwa hiyo, wanaziunda fikira na ndoto zao kumhusu Mungu kuwa sanamu, 403.20; kutokana na kuelezewa vibaya kwa desturi ya uaskofu mkuu, walizitwaa mila, ikiwa ni pamoja na dhabihu za binadamu, katika kujaribu kumpatanisha Mungu, 264.23; walikuwa na fidia fulani za dhambi ambazo kwazo, walipatanishwa na Mungu kwa kudhania, 200.114. Tazama pia
Watu wa Mataifa
Wapayukaji, tazama Walokole
Wapinga Sheria (Nomoklast), Wafuasi wenye Rai kwamba, Wakristo Hufanywa Huru kutoka
Haja ya Kuzingatia Kanuni yoyote ya Mema na Mabaya, 624.15, 17;
Warekabi, 295.59–62; 296.63
Wasaidizi, hatupaswi kuwachukulia watu watakatifu kama wasaidizi wakati wa haja, 312.26; 401.11. Tazama pia Watakatifu
Washiriki, wa kanisa, 129.232; 164176; 581.36; wafalme na watawala ndio washiriki maarufu sana wa kanisa, 348.54. Tazama pia Kanisa
Wasiomcha Mungu, huiamini historia ya Kristo lakini si msamaha wa dhambi, 24–27.23; Tazama pia Imani, na sakramenti, tazama
Chakula cha Bwana, Sakramenti; ingawa zina ishara fulani za kinje kwa ajili ya wote, wao si ufalme wa kweli wa Kristo, kwa kuwa wao ni washiriki wa ufalme wa ibilisi, 168.19; 170.29; Kristo atakaporudi siku ya mwisho kuhukumu, watatupwa kuzimuni na katika mapatilizo ya milele, 19–20.3; Tazama pia Waovu
Wasiostahili, watu hutoa na kupokea Chakula cha Bwana, tazama Chakula cha Bwana
Wasiotubu, sheria inapasa kuhubiriwa kwa wasiotubu, 617.12; 620.24; tazama pia Sheria. Tazama pia Ugumu wa Moyo
Wataalamu wa Ghiliba, 81.17; 153.341; 181.9; 183.16; 184.28; 262.13; 267.31; 320.9; 328.2 (VI); hulipotosha Neno la Mungu, 202.123; 202.124; wameficha
mafundisho ya dhambi ya asili, 87.32; hakuna awezaye kutoa maelezo sahihi ya sifa (accidens) ni aina gani ya dhambi ya asili, 571.60; hawaifahamu imani, 152.335–337; 296.68. Tazama pia Wataalamu wa Uwanazuoni
Wataalamu wa Uwanazuoni, 82-90; 91.9; 111.121; 128.229; 138.271; 138.269; 147.304; 148.312; 154.344; 160.378; 161.383; 177.2; 178.3; 181.9; 183.16; 184.28; 186.41; 199.110; 200.117; 201.120; 203. 217.18; 218.23; 244.40-41; 318.3; 590.76; istilahi ya uanazuoni, theologia ya uwanazuoni, vimechanganya mafundishho ya Kikristo na maoni ya kifalsafa, 84.12–13; 89.43; mitazamo yao ilipeleka mafundisho ya toba kwenye usahaulifu, 180.3. Tazama pia Wapotoshaji
Watakatifu
A. Katika maana ya jumla: ushirika wa watakatifu, tazama Kanisa; Neno hutufanya sote kuwa watakatifu si tendo la kinje, 414.92; hawawezi kupata aina ya maisha ya juu na mazuri kuliko Amri Kumi zinavyofundisha, 447.312, 283; hawawezi kuzishika sheria kikamilifu, tazama Sheria; ni shida kwao kubaki na imani ya kweli, 233.8; hawamchi na kumwamini Mungu vya kutosha, 288.25; hawajastahili msamaha wa dhambi kwa matendo, 123.203;
785
wanatawaliwa na mauti na mateso yetu yote ya kawaida, 209.151; ndani yao mateso huzima na hudhalilisha ashiki mbaya, 209-210; mateso na matendo yao mema ni dhabihu za ekaristi, 265.25; watakatifu wa mlia wa Kaini, 624.16
B. Katika maana maalumu: madhehebu ya watakatifu, 23-26.3; 30; kuwaomba watakatifu, 236–245; 311–312; baadhi ya wapinzani huwahesabia utukufu wa Mungu, 238.11; wapinzani huwafanya wapatanishi na wasuluhishi, 238.14; staha yao hujitwalia mahali pa Kristo, 294.53; iwapo tutategemea kwamba, tunaokolewa kwa stahili zao, basi wanafanywa kuwa sawa na Kristo, 240.23; katika maoni ya umma, Bikira Mbarikiwa ameichukua nafasi ya Kristo kabisa, 241.27–28; hii huwapatia watakatifu heshima ambayo ni ya Kristo, 238.14; hatuhesabiwi haki kwa kuzitegemea stahili za Bikira mbarikiwa au mtakatifu mwingine yeyote, 241.31; Biblia haitufundishi kuwaita au kuwaomba msaada, 28.2; 238.10; 241.31; 242.33; 311.25; kuwaomba pia hakuungwi mkono na waandishi wa kale, 237.3; 242.33; na hakutokani na imani, 239.17; kunagongana na fungu la kwanza kuu la imani, 311.25; kunatumiwa na watawa wa kiume tu kwa kujipatia pesa, 294.53; ni kuabudu sanamu, 235; 312.26; 346.47; 403.21; huwapatia
watakatifu heshima ambayo ni ya Mungu pekee, 312.26; ni mojawapo ya matumizi mabaya ya Mpinga Kristo, 311.25; kosa kwamba, tufe maalumu la shughuli limetolewa kwa kila mtakatifu lilitokana wazi na mifano ya wapagani, 242.32; labda watakatifu duniani na mbinguni hutuombea, 312.26; mbinguni, wao huliombea kanisa kwa jumla, jinsi walivyoliombea kanisa lote walipokuwa hai, 237.9; tunapaswa kuwapatia watakatifu heshima, 237.4; lakini hatupaswi kuwaomba, kufunga na kuwafanyia sherehe, au kuwachukulia kama wasaidizi wakati wa haja, 312.26; wakumbukwe ili tuweze kuimarisha imani yetu tunapoona jinsi walivyojipatia neema na jinsi walivyosaidiwa na imani, 30.1; mambo makuu waliyoyafanya yanatumika kama mifano, 243.36; lakini watu wanapojaribu kuwaiga, mara nyingi huwa wanayaiga mazoea ya nje, bali si imani yao, 224.24; ingawa tungekuwa na mifupa yao yote, haingetusaidia, kwa kuwa ni vitu vilivyokufa ambavyo haviwezi kumfanya yeyote mtakatifu, 414.91; tazama pia Masalio; staha ya taswira zao, 242.34
Watawa wa Kiume, Maisha ya Utawa, 52–62; 283; 312; 333
A. Kusudi la maisha ya utawa: “Watawa wa kiume wanajitahidi sana kuishi kufuatana na Injili,”
286.12; 291.39; kuishika sheria mpya ya Kristo, 286.16; kushika yote mawili, amri na mashauri ya injili, 56–62.61; 285.9; 288.24; 291.39; tazama pia mashauri ya Injili; kuwa katika hali ya ukamilifu, 52–58.16; 55–60.46, 49; 291.39; 430.197; Gersoni alilisahihisha hili na alisema kwamba, ni hali ya kujipatia ukamilifu, 290.36; yalisemekana kuwa mazuri kuliko njia yoyote ya maisha, 288.24; watawa wa kiume waliyadharau mambo ya umma, 229.4; na shughuli za umma na za faragha, 231.13; yalitumainiwa kushinda na kuzifuta dhambi mbele za Mungu kwa matendo yao wenyewe, 321.14; kustahili uzima wa milele, 289.28; hata hudai kuyatoa matendo yao mema kwa wengine, 54–60.44; kuhamisha stahili zao kwa wengine, 171-2; hata kuuza stahili zao za zaidi ya kadiri ipasayo kwa haki, 241.29; 288.24; 292.39; 324.28; tazama pia Ustahili (Stahili)
B. Uhakiki: mabishano, 285.9; maisha ya utawa hayastahili msamaha wa dhambi au uzima wa milele, 286.14; 288.23; 289.28–29; 292.40; watawa wa kiume wameanguka kutoka Kristo, 286.17; wanamfedhehesha Kristo, 290.30; na huiponda injili, 290.34; mfumo wote wa utawa unajaa kujifanya, unafiki, na mitazamo ya uongo, 286.16; 292.44; 294.56; ushikaji kanuni za utawa si matendo ya
mashauri ya injili, 288.26; maisha ya utawa hayana amri ya Mungu, 231.13; hakuna ushahidi kutoka
Neno la Mungu kwamba, Mungu huyaidhinisha, 288.23; ni ubunifu wa kibinadamu usiomcha Mungu, usiokuwa na msingi katika Biblia, 382.3; utakatifu wa watawa wa kiume ni kama ule wa Mafarisayo na waandishi wa sheria, 324.29; wa uongo na wa kinafiki, 430.197; matendo yao ni matendo ya kitoto, 23–25.3; kuzishika amri katika kazi za fulani ni bora kuliko maisha ya utawa, 417.112; 418.118; 422.144–145; matendo ya kujibunia wenyewe ya watawa wa kiume ni kinyume cha amri ya Mungu, 418.119; 432.213; hawawezi kujigamba kumpata ndugu hata mmoja, 442.278; matendo yao yote si mazuri na mema kana kwamba Mungu angeokota jani kavu, 481.12; tabaka la utawa linapasa kuchukuliwa kuwa la dunia na la tamaa za mwili kuliko yote, 382.3; ingawa watawa wa kiume wanadai kuwa waseja, wanashiriki kila anasa, 295.59; ama wanajihusisha na uasherati wazi na wenye aibu au hata wanayafanya maovu zaidi kisirisiri, 432.214; ingawa wanadai kuwa maskini, wanaishi katika anasa tele, 295.59; mahali pengi, wanahusika katika kuwaua watu waadilifu, 284.7; ilikuwa baada ya watawa wa kiume waombaji kutawala ambapo Misa za Faragha zilienea, 261.7;
787
wachungaji wamekuwa na ugomvi nao usiokwisha kuhusu kusikiliza ungamo na mambo mengine; 179.8; kufifia kwa utawala wa utawa kulitabiriwa na Hilten, 283.1–3; kimsingi, madhehebu ya Waanabaptisti si lolote ila maisha mapya ya utawa, 703.27. Tazama pia Majumba ya Watawa; Maisha ya Utawa; Nadhiri za Utawa; Kazi
Watawala (wafalme), chini ya Upapa, matendo yao yalichukuliwa kuwa njia ya maisha ya “ulimwengu na yenye dosari,” 45–50.10–11; Wakristo wanaweza kuwa watawala wasiokuwa wenye dhambi, 21.2; haja ya kwanza ya wafalme inapasa kuwa kuuinua utukufu wa Mungu, 348.54; kuhifadhi mafundisho mema na kuwatetea wanaofundisha kwa haki, 245.44; ni lazima hasa kwao, kama washiriki mashuhuri wa kanisa, kulihudumia na kuhakikisha kwamba makosa yameondolewa, 348.54; maaskofu wanapopuuza mamlaka yao, wanalazimika kutenda haki kwa raia wao kwa ajili ya amani, 64–71.29; wanapaswa kuwafukuza nchini wasiotaka kujifunza katekisimo, 358.11; ofisi yao inadai ulinzi na kinga kwa raia wao, 30.1; ingefaa kama nembo ya kila mtawala mnyofu ingepambwa kwa mkate kama ukumbusho kwamba, ni kwa njia ya ofisi ya mtawala ambapo wote wanafurahia kinga na amani, 472.75; mafundisho ya Kiinjili huongeza heshima kwao,
kwa sababu hutuza mamlaka yao
kwa sifa kamilifu, 297-301; dhambi za watawala dhidi ya Amri ya Saba, 435.230. Tazama pia Ufalme wa Raia; Serikali; Upanga
Watetezi wa Siri wa Philipp Melanchthon, tazama wafuasi wa
Philipp Melanchthon
Watoto, wajibu wao, 377.9; 456.103ff; hawapaswi kuoa bila wazazi wao kujua, 353.78; malezi yao, 411.75-77; 425.167-170; 426.171-174; tazama pia wazazi; Vijana; wanapaswa kulelewa katika kicho na maarifa ya Mungu, 426.174; wamefundishwa katekisimo, 397.1; 398.16; 501.87; walipelekwa shuleni, 359.19; walifunzwa kuwa wachungaji, wahubiri, watumishi wa serikali, na kadhalika, 400.20; 426.174
Watu wa Mataifa, 222.15-16; 249.3; 268.34; 338.8; kanisa ni watu wa kiroho wanaotofautishwa nao si kwa ajili ya kaida za raia bali kwa waliozaliwa mara ya pili kwa njia ya Roho, 167.14; walikuwa na dhabihu walizorithi kutoka Mababa Wakuu, lakini walifikiria matendo hayo yalikuwa dhabihu za kupatanisha, 124.206; msamaha wa dhambi uliahidiwa kwao kwa sababu ya Kristo, 135. Tazama pia Wapagani
Watu Waiaminio Injili, si wazushi, 29.1; hawajasema lolote jipya,
90.50; hawafundishi lolote lililo kinyume cha Maandiko Matakatifu au kanisa la ulimwenguni kote, 29.1; 76.5; 87.32; au kwa Kanisa la Rumi, kadiri inavyoweza kuonekana katika maandiko ya Mababa, 29.1; kwa bidii sana wanataka kuanzisha mwafaka, 258.59; lakini lazima wamtii Mungu, 258.59; 346.42; hawatakubaliana na fungu la msamaha licha ya vitisho, mateso, na mapatilizo, 233.9
Waturuki, 6.1; 460.66; 482.20; wanamruhusu yeyote anayetaka kuwa na imani katika Kristo, 315.11; Kaisari anaweza kuufuata mfano wa Daudi katika kupigana vita dhidi yao, 28.1; tunaweza kuowaombea watawala ili waweze kuwa washindi dhidi ya Waturuki, 490.77
Waudiano, 174.43
Wavalentino, 9–10.5
Wayahudi, Uyahudi, 41.32; 188.53; 200.114; 320.8; 405.35; 413.85; 439.258; 444.293; 445.300; 451.331; 487.54; 586.60; 640.60; watu wa Uyahudi, 430.201; serikali, 444.294; huduma (ibada), 74.61; Pasaka, 60,173.42-43; 496.47; 496.48; mafundisho (mitazamo) 1920.5; visasili, 66-73.46; ndoto ya ufalme wa Masihi, 230.7; ingawa wanamwamini na kumwabudu Mungu wa kweli mmoja, hata hivyo, hawajui mtazamo wa Mungu ulivyo kwao, 460.66; wapinzani
788
wanaukazia uangalifu wao haki ya sheria, jinsi Wayahudi walivyofanya kuhusu uso wa Musa uliofunuliwa, 94.21; 193.78; kuhusu uzingatifu wa nje, amri ya tatu ilitolewa kwao pekee, 412.80-81; wao ni mfano wa hukumu ya Mungu kwa wale wanaolidharau Neno la Mungu, 693.58; kanisa la kweli litatenganishwa na taifa zima la Uyahudi, 168.19. Tazama pia Israeli Yuda, 282-283.91-92
Wazazi, Mungu ameupatia ubaba na umama cheo maalumu cha heshima kilicho karibu na Yeye mwenyewe, 416.105; 419.126; ni wawakilishi na hutenda kazi kwa niaba ya Mungu, 416.108; 427.182; mamlaka yote wameyapata na yamekuzwa kutokana na mamlaka yao, 422.141; umama, ubaba, na mamlaka ya serikali huitegemea amri ya Mungu, 482.20; 485.38; amri ni mkufu wa dhahabu ulio shingoni mwao na taji lililo juu ya vichwa vyao, 482.20; ndio mabwana na mabibi wa kaya, 422.142; amri ya Mungu ni kuwaheshimu, kuwahudumia, kuwatii, kuwapenda, na kuwastahi, 346.7–8; 397.4; 416–427; 450.327; kuwatii ndilo tendo kuu na bora sana kuliko yote baada ya kumtii Mungu, 418.116; ndio hazina ya thamani kuliko zote ulimwenguni, 417.109; kazi zao, 46–50.10; wajibu wao, 368.12; 359.19; 377.8; 416–418; wanapaswa kuwafundisha watoto wao (watumishi) katekisimo,
789
357–378; 397.4; 397.17; 501.87; na kuomba asubuhi na jioni, 373374; chini ya upapa, kazi ya uzazi ilichukuliwa kuwa hali ya maisha ya “ulimwengu na yenye dosari,” 46–50.10; wazazi wabaya hustahili jehanumu kulingana na jinsi wamewalea watoto wao, 426.176
Watu, tofauti baina ya watu wa sheria na kanisa ni kwamba, kanisa ni watu wa kiroho, siyo watu wanaotofautishwa kutoka mataifa kwa kaida za raia, 167.14; watu wa Sheria, tazama Israeli; watu wa Agano Jipya wanapaswa kuwa watu walio tayari, 587.64; 610.17; desturi za kibinadamu zinatumika ili umma uweze kujua wakati wa kukusanyika na jinsi ya kufanya mambo kwa utaratibu, 173.40; 223.20; mwafaka utachanguka wakati wowote maaskofu watailazimisha mizigo inayozidi kwa umma, 129.233; hukumu ya Mungu kwa watu, 693.58, 60
Wema, upendo kwake Mungu na jirani ni mkubwa kuliko vyote kwa sababu hiyo ndiyo amri kuu kuliko zote, 128.226; wema wa sheria hayahesabii haki bali imani ndiyo inahesabia haki, tazama pia Imani; Kuhesabia Haki; waumini wanapaswa kuyafuata mema yote ya Kikristo, 695.73. Tazama pia Haki
Wema, hakika, vyote vilivyo vyema humwagika kutoka Mungu, 403.25; Luther alidai kwamba,
katika Kijerumani, jina la Mungu linatokana na neno “wema,” (Güte, gut) 403.25; mbali na Amri Kumi, hakuna tendo au maisha yanayoweza kuwa mema, 447.311; kutenda mema, tazama Matendo; tunatupaswa kumtegemea Mungu kwa kila kitu chema, na tunapaswa kuvitumia vipawa vya Mungu vyote tu kwa ajili ya mahitaji yetu ya mwili, bila kukiruhusu chochote cha vitu hivi kuwa bwana au sanamu, 407.47; tazama pia Baraka; Ukwasi
Wiki ya Misa, 344.12
Wito, tusiuchukulie mwito utokao kwa Mungu kama aina ya uongo bali tunapaswa kufahamu kwamba, Mungu hupenda kutenda kazi kwa huo unaotokea kwa njia ya kulihubiri Neno, 687.29; 688.34; tazama pia Uchaguzi; Kristo anawaita kwake wenye dhambi wote na huwaahidia kiburudisho, 545.8; tunapaswa kushindana kwa makini tuwezavyo ili kuuthibitisha wito wetu, 546.14; 695.73; kwa njia ya matendo mema yanayofuatia imani, 221.12-13; 613.33; hadi kwa cheo cha kuhubiri, 331–332; tazama pia Wachungaji; Wahubiri; yeyote hapaswi kufundisha, kuhubiri, au kuzitoa sakramenti hadharani bila wito sahihi, 18; 218.1
Wittenberg, 304.8; Vurugu (1521–22), Katekisimo (1525), Mwafaka (1536),39; 76; 79; 229; 352; 387; 409; 409-410; 554; 571; 580; 597;
627; 630.12; 631.18; 635.38; 653; Wizi, ndiyo hila ya kawaida sana na ushirika mkubwa sana wa mafundi duniani, 435.228
Wokovu, Okolewa, kuokolewa si lolote isipokuwa kutolewa dhambini, mautini, na kutoka ibilisi, kuingia katika ufalme wa Kristo, na kuishi na Kristo milele, 483.25; sababu ya uchaguzi wa Mungu, tazama Uchaguzi; Mungu anawataka watu wote waokolewe, tazama Uchaguzi; Mungu hutuokoa kwa njia ya Kristo, tazama Kristo, hatuwezi kushirikiana, tazama kazi pamoja; si sahihi kufundisha kwamba, watu lazima waokolewe kwa njia nyingine kuliko kuhesabiwa haki mbele za Mungu, 604.52; tazama pia Kuhesabiwa Haki; wokovu na matendo mema, tazama Matendo, unaweza kupotea kwa njia ya dhambi ya makusudi, 612.31; hauwi mikononi mwetu bali katika uchaguzi wa rehema wa Mungu, 699.90; katika mkono wa enzi wa Yesu Kristo Mwokozi wetu, 691.46
Wongofu,
A. Asili: katika wongofu wa kweli, lazima pawe na mabadiliko katika akili, mapenzi, na moyo, 588.70; 591.83; toba, 183-184; 203.131; sehemu mbili: majuto makubwa na imani, 184.28; 187.46; 188.56; moja inaweza kuiongezea sehemu ya tatu: matunda yastahiliyo toba,
184.28; humaanisha kuua na kuhuisha, 174.46; uamsho wa mapenzi yaliyoharibiwa kutoka mauti ya kiroho, 592.87; lakini Mungu haharibu kabisa kiini na iriki ya Adamu wa kale na kuumba iriki mpya kutoka ombwe, 516.14; 591.81; si sawa na kuhesabiwa haki, 598.24; amri ya wongofu kuhusu kuhesabiwa haki na utakaso, 602.41; inarudiwa, 588.69
Utambuzi wa wongofu: 583-584; Mungu amempangia kila muumini wakati na saa ya wongofu, 692.56; shughuli takatifu na kazi ya Roho Mtakatifu pekee, 578.25; wongofu na neema, 577.22; Roho Mtakatifu huutekeleza kwa njia ya Neno (na sakramenti), 514.4; 573.5; 589.71; 695.71; ajili mbili madhubuti (si tatu): Roho Mtakatifu na Neno la Mungu, 517.19; 593.90; uwezo wa binadamu haushirikiani kama ajili ya tatu, 515.9; 517.19; 593.90; mtu aliyeoongolewa hashiriki kando kando mwa Roho Mtakatifu jinsi farasi wawili huvuta rikwama pamoja, 588.66; kuhusu mafundisho sahihi, ni kinyume kusema, “hiari ya binadamu si zembe katika wongofu lakini huchukua hatua pia,” au “Mungu huwavuta, lakini huwavuta wale wanaotaka, 592.86; au kwamba, katika msingi wa uwezo wao wa asili, watu wanaweza kuchukua hatua ya kwanza kwa huo, 590.76; au kwamba, kwa neema, fulani ana uwezo wa kujitolea mwenyewe kwa
urahisi, 590.78; Mungu amewasha hata hamu kwa neema yake, 575.14; ni kinyume kusema kwa mafundisho sahihi kwamba, hiari inaweza kumkuta Mungu kwa uwezo wa asili yake yenyewe baada ya Roho Mtakatifu kuanza, 590.77; hiari ya binadamu si mashughuli kabisa, 517.18; 592.89; sawa na bonge la jiwe au mti, 577.19; 586.59; 587.62; lakini bado una uwezo kutokuwa mashughuli, 578.23; Mungu hawalazimishi binadamu kuongoka, 586.60; lakini Mungu huwabadilisha watu wasiopenda kuwa watu wanaopenda kwa njia ya uwezo wa mvuto wa Roho Mtakatifu, 516.17; 586.60; 592.88; badiliko kama hilo katika akili ya binadamu, mapenzi, na moyo kwa shughuli ya Roho Mtakatifu kwamba, binadamu anaweza kukubali neema itolewayo, 591.83; mara tu Roho Mtakatifu anapokuwa ameanza kazi yake, hiari ya binadamu inapaswa kushirikiana katika matendo yote ya Roho, 516.17; 587.65; mafundisho kuhusu udhaifu wa hiari yetu ya asili na mafundisho kwamba, wongofu wetu ni kazi ya Mungu pekee haupaswi kuwafanya watu wawe wapotovu au wasiotii amri, 583.46
Worms, Mapatano baina ya Raia na Watawala wa Kanisa la Kikristo ya (1122), Kongamano la Wataalamu la (1557), 20; 331
Wosia, Chakula cha Bwana ndicho
wosia wa Kristo, 246.2; 638.53; maneno ya wosia wa Kristo, 529.7; 532.25; 534.39; 635.38; 638.50; 647.92; 660.29; Agano la Kale lilikuwa na taswira au vifuli vya mambo yajayo, 269.36; dhabihu za Agano la Kale hazikustahili upatanisho bali ziliionyesha dhabihu ijayo, 272.56; jinsi tunavyokifahamu “kivuli” katika Agano la Kale, vivyo lazima tukitafute kinachomaanishwa katika Agano Jipya, 269.37; dhabihu ya kila siku ya Agano la Kale humsawiri Kristo na ibada nzima ya Agano Jipya, 269.36; katika Agano Jipya, hakuna dhabihu inayohusiana na dhambi za wengine hubakia nje ya dhabihu moja ya Kristo, 272.56; tazama pia Kristo; Dhabihu; katika Agano Jipya, dhabihu, ukuhani, na sherehe za Agano la Kale vinabatilishwa, tazama Sherehe; Mchungaji; Dhabihu; katika Agano la Kale jinsi ilivyo katika Agano Jipya, watakatifu walihesabiwa haki kwa imani katika msingi wa ahadi ya msamaha wa dhambi unaotolewa kwa ajili ya Kristo, 272.55; tazama Maaskofu Wakuu; Agano Jipya hubaki na ofisi ya sheria ambayo inaifunua dhambi iliyorithiwa na matunda yake, 319.1; hata hivyo, Agano Jipya huongezea mara moja katika ofisi hii, ahadi ya neema ya kuliwaza kwa njia ya Injili, 319.4; sakramenti ni ishara za Agano Jipya,
186.42; 217.14
Yuda (Iskariote), alikata tamaa chini ya sheria, bila nyongeza ya Injili, 320.7; 525.8; tofauti baina ya majuto makubwa yake na yale ya Petro, 181.8; 185.36; alipokea mwili wa kweli na damu ya kweli ya Kristo kwa kinywa wakati wa Chakula cha Bwana, 634.33; 640.60; papa kama “Yuda mlaaniwa,” 311.24
Yuno (mungu wa kike wa Warumi), 242.32 Yupita (Mungu Mkuu wa War mi), 402.18
Zaburi, hutukuza imani kama ibada iliyo kuu kuliko zote, 99.57; katekisimo inapofahamika vyema, fulani anaweza kuwapatia baadhi ya vijana zaburi ili kuongezea na kuthibitisha imani yao, 399.25
Zaburi, ni taamuli na mazoezi yanayoihusu Amri ya Kwanza, 399.18
Ziara, katika makanisa na shule. Tazama pia wakazi wa Sachsen Uhaishaji, tazama Kufanya Hai
Zürich, 524; 627; 629; Mwafaka (1549), Tazama pia Waanabaptisti; Wafuasi wa Calvin; Walioongoka;Wanaoidharau Sakrament; Wafuasi wa Zwingli
Agano la kale
Mwanzo
Mwa. 1:11 - 250
Mwa. 1:27 - 85
Mwa. 1:27 – 35, 385
Mwa. 1:28 – 33, 250, 644
Mwa. 2:16 - 527
Mwa. 2:18 – 54, 58, 384
Mwa. 2:21 -384
Mwa. 3: 1, 14 - 330
Mwa. 3:3 - 527
Mwa. 3:6 - 317
Mwa. 3:15 – 89, 295, 620
Mwa. 3:16-19
Mwa. 3:19 - 718
Mwa. 4:7 - 232
Mwa. 4:10 - 260
Mwa. 6:5 - 564
Mwa. 8:21 – 512,514
Mwa. 15:6 – 564, 600
Mwa. 17:4-8 – 549, 702
Mwa. 17:19-21 - 549
Mwa. 18 – 257
Mwa. 19 – 257, 702
Mwa. 22 - 124
Mwa. 22:18 - 620
Mwa. 25:23 - 699
Mwa. 28:14 - 620
Kutoka
Kut. 3:2 - 330
Kut. 9:16 - 698
Kut. 20:2-17 - 362
Kut. 20:5-6 – 364, 404, 449
Kut. 20:6 - 138
Faharasa ya Biblia
Kut. 20:7 - 39
Kut. 20:12 – 158,295
Kut. 20:15 - 293
Kut. 20:17 – 288
Kut. 29:38-39 - 269
Kut. 32:6 - 264
Kut. 33:20 - 317
Mambo ya Walawi
Law. 1-7 - 264
Law. 5 - 264
Law. 19:18 - 143
Law. 20:2 – 124
Hesabu
Hes. 6:2-21 - 295
Hes.14:18 - 151
Hes. 28:4 – 269
Kumbukumbu la Torati
Kum. 4:24 - 151
Kum. 5:6-21 - 362
Kum. 6:5 – 112, 143, 206, 288
Kum. 6:6-8 - 395
Kum. 6:8-9 – 451
Kum. 11:20 – 451
Kum. 12:8 - 625
Kum. 12:8 - 625
Kum. 12:32 – 625
Kum. 16:10 - 278
Kum. 21:18-20 - 427
Kum. 24:1-4 - 444
Kum.29:4 - 579
Kum. 30:6 - 579
Kum. 32:6 - 566
Waamuzi
Amu. 13
Amu. 13
1 Samweli
1 Sam. 2:6 - 624
1 Sam. 2:36 - 247
1 Sam. 16:14 - 456
1 Sam. 16:23 - 456
1 Sam. 28:20 - 320
1 Sam. 31:34 - 320
1 Sam. 2:6 – 188
2 Samweli
2 Sam. 1-2:13
2 Sam. 6:17 - 264
2 Sam. 12:13 – 187,189
2 Sam. 12:13-14 -
2 Sam. 22:5 – 208
2 Sam. 12:14 – 189
1 Wafalme
1 Fal. 12:26-28 - 222
2 Wafalme
2 Fal. 23:10 – 124
Mambo ya Nyakati
2 Nya. 20:30 – 224
Ayubu
Ayu. 9:28 - 151
Ayu. 10:8 - 509
Ayu. 10:8-12 - 566
Ayu. 19:26-27 – 510
Zaburi
Zab. 1:1-2 - 622
Zab. 1:2 - 526
Zab. 2 – 622, 713
Zab. 2:10 - 348
Zab. 4:6 - 267
Zab. 5:4 - 683
Zab. 5:10-11 - 689
Zab. 6:1 - 209
Zab. 6:2-3 - 184
Zab. 7:8 - 151
Zab. 8 - 719
Zab. 8:6 - 660
Zab. 8:7 - 710
Zab. 12:3-4 - 689
Zab.19:12 – 16, 43, 45, 179, 328
Zab. 21 - 721
Zab. 25 - 591
Zab. 25:1-2 - 591
Zab.31:22 - 695
Zab.32:1-2 – 103,108,117
Zab. 32:2 - 118
Zab. 32:5 -198
Zab. 32:6 - 118
Zab. 37:1 - 123
Zab. 37:5 – 44,45
Zab. 38:4 - 184
Zab. 38:8 - 184
Zab. 39:6 - 267
Zab. 40 - 267
Zab. 42:1 - 506
Zab.45:12 - 239
Zab. 49 - 267
Zab. 50:8 - 124
Zab. 50:13 - 267
Zab. 50:15 – 100, 138, 267, 410, 464
Zab. 50:18 - 267
Zab. 51 - 267
Zab. 51:3 - 569
Zab. 51:4 - 198
Zab. 51:5 - 317
Zab. 51:12 -579
Zab. 51:16-17 -
Zab.54:6 - 611
Zab.56:12 - 265
Zab. 68:18 - 113
Zab. 72:11 - 239
Zab. 72:15 - 239
Zab. 73:22 - 577
Zab. 82:6 - 245
Zab. 90 - 577
Zab. 90:12 - 571
Zab. 91 - 577
Zab. 93:1 - 660
Zab. 95:8 - 514
Zab. 98 - 717
Zab. 99:5 - 718
Zab. 35 - 622
Zab.47 - 622
Zab. 76 - 622
Zab. 97 - 622
Zab. 109:13 - 421
Zab. 110 - 714
Zab. 110:1 - 620
Zab. 110:3 – 587,611
Zab. 111:4-5 - 276
Zab. 115:17 - 267
Zab. 116:11 – 87,288
Zab. 118: - 277
Zab. 118:18 - 187
Zab. 119 – 575,731
Zab. 119:1 – 526,527
Zab. 119:7 - 575
Zab. 119:18 - 575
Zab. 119:19 - 575
Zab. 119:26 - 575
Zab. 119:27 - 575
Zab. 119:28 - 188
Zab. 119:32 - 626
Zab. 119:33 - 575
Zab. 119:34 - 575
Zab. 119:46 - 61
Zab. 119:50 – 63
Zab. 119:66 - 575
Zab. 119:70 - 682
Zab. 119:71 - 623
Zab. 119:105 - 507
Zab. 119:124-125 - 575
Zab. 119:135 - 575
Zab. 119:144 - 575
Zab. 119:169 - 575
Zab. 119:171 - 575
Zab. 121:8 - 390
Zab. 129 - 320
Zab. 130:3 – 99, 151
Zab. 130:3-5 - 100
Zab. 130:7 - 320
Zab. 136:1-25 - 375
Zab. 139:14-16 - 566
Zab. 139:16 - 683
Zab. 140:9 - 564
Zab. 143:2 – 118,151,193,329,626
Zab. 145:15-16 - 374
Zab. 147:9-11 - 375
Zab. 147:11 - 450
Mithali
Mit. 10:12 - 131
Mit. 17:15 – 519,596
Mit. 18:22 - 385
Mit. 19:17 - 438
Mit. 20:9 - 151
Mit. 27:23 - 198
Mhubiri
Mhu. 12:7 - 566
Isaya
Isa. 1:13 – 313
Isa. 1:16-18 - 135
Isa. 1:16-19 - 212
Isa. 1:19-20 - 232
Isa. 5:22-23 - 597
Isa. 11:2 - 670
Isa. 11:10 - 239
Isa. 14:27 - 684
Isa. 25:5 - 456
Isa. 26:16 - 210
Isa. 28:16 - 191
Isa. 28:21 – 211, 188, 617, 526
Isa. 29:20 - 313
Isa. 37:28 - 683
Isa. 38:10-13 - 184
Isa. 40:6 - 260
Isa.40:6-7 - 152
Isa. 40:10 - 620
Isa.41:29 - 313
Isa. 45:9 - 578
Isa. 45:11 - 566
Isa. 48:20 - 348
Isa. 49:6 - 620
Isa. 52:11 – 348, 259
Isa. 53:5 – 306, 620
Isa. 53:5-6 - 620
Isa. 53:6 – 306, 234
Isa. 53:10 – 272, 264
Isa. 53:11 - 107
Isa. 54:5 - 566
Isa. 54:11 - 217
Isa. 58:7 – 135, 134
Isa. 58:8-9 - 158
Isa. 58:9 - 134
Isa. 61:1 - 670
Isa. 64:7 – 566
Yeremia
Yer. 2:8 - 282
Yer. 2:26 - 282
Yer. 3:1 - 696
Yer. 3:5 - 232
Yer. 7:22 - 124
Yer. 7:22-23 - 266
Yer. 7:31 - 124
Yer. 10:24 - 269
Yer. 15:19 – 138, 558
Yer. 17:1 - 282
Yer. 17:9 – 43, 45, 576
Yer. 18:6 - 578
Yer. 23:6 - 517
Yer. 23:29 - 319
Yer. 31:19 - 87
Yer. 31:33 – 111, 126
Yer. 35:6 - 295
Yer. 49:12 - 211
Yer. 51:45 – 348
Ezekieli
Eze. 5:3 - 577
Eze. 7:26 - 248
Eze. 11:19 - 579
Eze. 18:21-22 - 136
Eze. 18:23 – 545, 697
Eze. 18:31-32 - 232
Eze. 20:18-19 - 221
Eze. 20:25 - 290
Eze. 33:11 – 545, 584, 697, 698, 196
Eze. 36:26 – 577
Danieli
Dan. 2:28 - 544
Dan. 2:28 - 272
Dan. 3:29 - 136
Dan. 4:24 – 134,136
Dan. 4:27 – 136, 134
Dan. 7:13 – 710
Dan. 7:14 – 666, 710
Dan. 8:11-12 - 269
Dan. 9:18-19 - 152
Dan. 11:31 – 270, 271
Dan. 11:36-39 - 169
Dan. 11:37 - 253
Dan. 11:38 – 272, 222
Dan. 11:43 - 323
Dan. 12:11 – 269, 271
Hosea
Hos. 6 - 577
Hos. 6:5 - 577
Hos. 13:9 – 683, 693
Hos. 13:14 - 206
Yona
Yona. 2:8 – 152
Yona. 3:10 – 212
Mika
Mika 2:11
Habakuki
Hab. 1:3 – 313
Hab. 2:4 – 606, 107, 187
Zekaria
Zek. 1:3 - 138
Zek. 1:12 - 237
Zek. 2:13 - 151
Zek. 3:2 - 317
Zek. 9:10 - 660
Zek. 10:2 – 313
Malaki
Mal. 1:2-3 - 699
Mal. 1:11 - 267
Mal. 3:1 - 324
Mal. 3:3 – 268
Tobiti
Tob. 4:5 - 140
Tob. 4:11 - 140
Tob. 4:19 - 140
Wamakabayo
Wak. 15:14 – 238
Agano Jipya Mathayo
Mt. 3:7 - 325
Mt. 3:8 – 136, 184, 201, 204
Mt. 3:12 – 164, 165, 168
Mt. 4:17 - 204
Mt. 5:3 - 293
Mt. 5:6 - 688
Mt. 5:10 - 123
Mt. 5:13 - 284
Mt. 5:21 - 525
Mt. 5:22 – 617, 698
Mt. 5:31 – 444, 446
Mt. 5:32 – 353, 446
Mt. 5:39 - 230
Mt. 5:46-47 - 429
Mt. 5:48 - 417
Mt. 6:7 - 294
Mt. 6:913 - 367
Mt. 6:14 - 475
Mt. 6:33 - 470
Mt. 7:3-5 - 305
Mt. 7:7 – 389, 462
Mt. 7:7-8 - 464
Mt. 7:12 - 443
Mt. 7:15 – 64, 71, 175, 346, 680, 689
Mt. 7:18 – 233, 609
Mt.8:1-13 - 577
Mt. 9:2 – 545
Mt. 9:9 - 545
Mt.9:12 – 499, 643
Mt. 9:22 - 545
Mt.9:29 - 545
Mt. 9:35 - 545
Mt. 9:37 - 545
Mt. 10:29 - 683
Mt. 10:32 – 679
Mt. 11:27 – 579, 666 545, 687, 186, 239, 498, 642
Mt. 12:1-8 - 226
Mt. 13:11 - 574
Mt. 13:13 - 574
Mt. 13:15 - 579
Mt. 13:24-30 - 175
Mt. 13:36-43 - 175
Mt. 13:47-50 - 175
Mt. 13:38 - 168
Mt. 13:47 – 164,168
Mt. 14:3-4 - 446
Mt.15:3 - 47
Mt. 15:9 – 51, 54, 55, 60,206,207, 220, 288, 292, 297, 307, 334, 512, 677
Mt. 15:11 – 47, 51, 298
Mt. 15:13 – 66, 73
Mt. 15:14 – 66, 73, 483
Mt. 16:10 - 169
Mt. 16:15 - 342
Mt. 16:16 - 342
Mt. 16:18 – 165, 344, 544, 683, 691
798
Mt. 16:18-19 – 190, 262, 342
Mt. 16:19 – 163, 214, 341, 344, 345
Mt. 16:27 - 726
Mt. 17:5 – 148, 636
Mt. 17:21 – 48, 51
Mt. 18:1-4 - 338
Mt. 18:6-7 679
Mt. 18:15 - 442
Mt. 18:15-19 - 503
Mt. 18:16 - 442
Mt. 18:18 – 328, 344
Mt. 18:19 - 442
Mt. 18:20 - 327, 351, 394, 586, 671
Mt. 19:3-9 – 446
Mt. 19:6 – 253, 252, 258, 384
Mt. 19:7 - 444
Mt. 19:11 – 33, 35, 251
Mt. 19:12 – 252, 255
Mt. 19:17 – 111, 138
Mt. 19:21 - 292
Mt. 19:29 – 289, 292
Mt. 20:1-16 – 546, 687
Mt. 20:2-14 – 685, 687
Mt. 20:16 - 688
Mt. 22:5 – 689, 690
Mt. 22:12 - 689
Mt. 22:14 – 546, 688
Mt. 22:21b - 376
Mt. 22:37 - 128
Mt. 23:2 - 15
Mt. 23:3 - 301
Mt. 23:5 - 451
Mt. 23:24 305
Mt. 23:26 - 696
Mt. 23:37 – 232, 586, 690
Mt. 24:13 - 612
Mt. 24:15-18 - 348
Mt. 25:1 - 168
Mt. 25:21 - 237
Mt. 25:23 - 237
Mt. 25:35 - 159
Mt. 25:41 - 471
Mt. 25:42-43 – 429, 671, 639
Mt. 26:26 – 634, 637
Mt. 26:26-28 – 491, 715
Mt. 26:27 – 31, 32
Mt. 26:28 – 275, 637
Mt. 26:63-64 - 410
Mt. 27:5 – 320
Mt. 28 – 618, 724, 726, 673
Mt. 28:18 – 636, 666, 669
Mt. 28:19 – 176, 398, 399, 480
Mt. 28:19-20 – 343, 370
Mt. 28:20 – 671
Marko
Mk. 1:1 - 616
Mk. 1:4 - 616
Mk. 1:15 – 186, 201, 319, 525, 616, 694
Mk. 6:17 - 446
Mk. 9:29 - 643
Mk. 10:2-19 - 446
Mk. 10:11 - 353
Mk. 10:13-16 - 390
Mk. 10:29 - 292
Mk. 13:14-16 - 348
Mk. 14:7 - 232
Mk. 14:22 - 634
Mk. 14:22-24 - 491
Mk. 14:23 - 531
Mk. 14:24 -639
Mk. 16:10 – 263
Mk. 16:15 – 63, 399, 616, 687
Mk. 16:16 -330, 398, 480, 483, 689
Mk. 16:20 - 660
799
Luka
Lk. 1:8-19 - 331
Lk. 1:32-33 - 711
Lk. 1:35 - 535
Lk. 1:41-44 - 331
Lk. 2:41-52 - 659
Lk. 2:52 - 537
Lk. 3:22 – 636, 694
Lk. 4:1 - 617
Lk. 6:23 - 156
Lk. 6:37 - 135
Lk. 7:30 - 692
Lk. 7:37 - 475
Lk. 7:48 - 189
Lk. 7:50 – 115, 189
Lk. 8:13 - 690
Lk. 10:16 – 64, 170, 175, 186, 300
Lk. 11:11-13 - 695
Lk. 11:24-25 – 690, 698
Lk. 11:25 – 546
Lk. 11:25 -546
Lk. 11:39 - 696
Lk. 11:41 - 116
Lk. 12:14 – 63, 70
Lk. 12:31 – 470
Lk. 13:4 - 616
Lk. 13:23 - 688
Lk. 13:23-24 - 688
Lk. 14:18-20 - 690
Lk. 14:24 - 689
Lk. 13:31-32 - 290
Lk. 15:7 - 616
Lk.16:18 -353, 446
Lk. 17:10 – 13, 14, 152
Lk. 18:1 - 462
Lk. 21:33 - 636
Lk. 21:34 – 51, 228
Lk. 21:36 - 462
Lk. 22:19 – 39
Lk. 22:19 – 634, 637
Lk. 22:19-20 – 275, 186, 491
Lk. 22:20 – 637, 639
Lk. 22:25-26 – 338
Lk. 22:69 -711
Lk. 24:17 - 201
Lk. 24:26 - 662
Lk. 24:35 - 246
Lk.24:45 - 578
Lk. 24:46 - 617
Lk. 24:47 – 100, 184, 320, 687
Yohana
Yn. 1:3 - 666
Yn. 1:5 – 574, 575
Yn. 1:10 – 666
Yn. 1:14 - 635
Yn. 1:16 - 325
Yn. 1:18 - 694
Yn. 1:29 – 306, 308, 687
Yn. 1:41 - 670
Yn. 2:1-11 - 659
Yn. 3 - 482
Yn. 3:3 - 388
Yn. 3:5 - 388
Yn. 3:16 – 584, 643, 694
Yn. 3:18 - 531
Yn. 3:31 – 537, 666
Yn. 3:35 - 666
Yn. 4:25 - 670
Yn. 5:21 - 666
Yn. 5:27 - 666
Yn. 6:29 - 579
Yn. 6:35 - 277
Yn. 6:37 - 694
Yn. 6:39-40 - 666
Yn. 6:40 – 666, 687, 694
Yn. 6:44 – 578, 579, 696
Yn. 6:48-58 – 641, 666
Yn. 6:51 - 687
Yn. 6:52-65 - 641
Yn. 7:19 - 326
Yn. 7:39 - 673
Yn. 7:48 - 695
Yn. 8:34 - 573
Yn. 8:36 - 588
Yn. 8:37 - 575
Yn. 8:44 – 22, 23, 37, 478, 500
Yn. 10:3 - 332
Yn. 10:9 - 694
Yn. 10:12-16 - 558
Yn. 10:27 – 558, 688
Yn. 10:27-30 - 685
Yn. 10:28 – 544, 683, 688, 691, 699
Yn.13:3 – 537, 666, 669, 710
Yn. 14:6 - 24
Yn. 14:16 - 694
Yn. 15 - 381
Yn. 15:3-4 - 685
Yn. 15:5 – 25, 28, 514, 575, 579
Yn. 15:12 – 610, 685
Yn. 15:16-17 – 381, 685
Yn. 16:17 - 617
Yn. 16:8 – 319, 618, 624
Yn. 16:8-9 – 617, 618
Yn. 16:14 - 694
Yn. 17:10 - 673
Yn. 17:17 – 584
Yn. 17:24 - 668
Yn. 18:6 - 659
Yn. 18:36 - 343
Yn. 20:23 – 342, 344
Yn. 21:15 - 343
Yn. 21:17 – 341, 343
Matendo ya Mitume
Mdo. 1:7 - 692
Mdo. 1:11 - 726
Mdo. 2 - 717
Mdo. 2:33 - 790
Mdo. 2:36 - 717
Mdo. 2:38 - 222
Mdo. 3:21 - 652
Mdo. 4:12 - 306
Mdo. 5:29 - 20, 75, 610
Mdo. 5:31 - 579
Mdo. 7:51 -586, 689
Mdo. 10:2 -330
Mdo. 10:38 - 635
Mdo. 10:43 - 191, 234
Mdo. 10:44 - 192
Mdo. 11:14 -584
Mdo. 13:40 - 689
Mdo. 13:46 - 693
Mdo. 13:48 - 683
Mdo. 15 - 255, 689
Mdo. 15:1 -5 - 553
Mdo. 15:9 - 141
Mdo. 15:10 - 51, 66, 226, 298, 553
Mdo. 15:10 -11 -47, 72
Mdo. 15:20 - 68
Mdo. 15:23 - 29 - 75
Mdo. 15:24 - 553
Mdo. 15:29 - 65, 68, 301, 344
Mdo. 16:3 - 677, 678
Mdo. 16:14 - 514, 579
Mdo. 17:22 - 289
Mdo. 17:25 - 566
Mdo. 17:26 - 566
Mdo. 17:28 – 567
Warumi
Rum. 1:3 -662
Rum. 1:4 - 673
Rum. 1:16 – 63, 70, 101, 217, 395, 514, 620, 688
Rum. 1:17 – 187, 524, 597
Rum. 1:18 – 319, 525
Rum. 1:19 - 574
Rum. 1:21 - 620
Rum. 1:22 - 594
Rum. 1:28 - 574
Rum. 1:32 - 574
Rum. 2:6 - 159
Rum. 2:7-8 - 527
Rum. 2:10 – 159, 159
Rum. 2:13 – 111, 133
Rum. 2:14-15 - 91
Rum. 2:15 – 527, 625
Rum. 3 – 12, 235
Rum. 3:10-12 - 325
Rum. 3:11-12 - 574
Rum. 3:12 - 575
Rum. 3:20 - 619
Rum. 3:20-21 – 519, 619
Rum. 3:21 - 519
Rum. 3:21 - 96
Rum. 3:19-20 - 319
Rum. 3:22 - 687
Rum. 3:23-25 – 95, 307
Rum. 3:24 – 235, 519
Rum. 3:25 – 161, 190, 725
Rum. 3:26 – 306
Rum. 3:28 – 102, 105, 306, 519, 596, 599
Rum. 3:31 – 119, 236
Rum. 4 – 12, 112, 235
Rum. 4:1 - 666
Rum. 4:1-6 - 106
Rum. 4:3 – 144, 600
Rum. 4:5 – 144, 518, 596
Rum. 4:5 – 147, 518, 601
Rum. 4:6 – 601, 604, 612
Rum. 4:6-7 - 522
Rum. 4:6-8 - 598
Rum. 4:7 - 117
Rum. 4:9 - 106
Rum. 4:9-22 - 123
Rum. 4:11 - 276
Rum. 4:13 - 144
Rum. 4:14 - 142
Rum. 4:15 – 96, 138, 195, 319
Rum. 4:16 – 98, 105, 190, 194, 235
Rum. 4:17 - 298
Rum. 4:18 - 150
Rum. 4:20 - 148
Rum. 4:25 – 306, 619
Rum. 5:1 – 24, 27, 126, 147, 150, 185, 262, 280
Rum. 5:1-2 – 122, 142
Rum. 5:2 – 134, 138, 145, 149, 185, 190, 613
Rum. 5:9 – 725, 725
Rum.5 - 380
Rum. 5:12 – 317, 561
Rum. 5:18 - 596
Rum. 5:19 – 518, 606
Rum. 5:20 – 108, 115, 237, 319
Rum. 6:4 - 519
Rum. 6:7 - 611
Rum. 6:9 - 177
Rum. 6:12 - 527
Rum. 6:14 – 522, 625
Rum. 6:19 – 201, 204
Rum. 6:23 – 156, 697
Rum. 7:5 - 87
Rum. 7:6 – 522, 617
Rum. 7:7 – 88, 105, 619
Rum. 7:10 – 320
Rum. 7:14 – 525, 576, 617
Rum. 7:14-25 - 523
Rum. 7:18 – 500, 576, 625
Rum. 7:18-19 – 569, 623, 626
Rum. 7:19 – 118, 625, 626
Rum. 7:21 - 527
Rum. 7:22 – 576, 587, 592, 611
Rum. 7:22-23 – 576, 587, 592
Rum. 7:23 – 88, 326, 328, 329, 527, 581
Rum. 7:25 – 118, 527, 587
Rum. 8:1 – 114, 148, 184
Rum. 8:2 - 625
Rum. 8:3 - 256
Rum. 8:7 – 514, 575, 576
Rum. 8:7-8 - 95
Rum. 8:10 – 155, 209
Rum. 8:12-13 - 114
Rum. 8:13 – 611, 613
Rum. 8:14 – 159, 522
Rum. 8:15 - 522
Rum. 6:21-3 - 379
Rum. 7 - 381
Rum. 8:16-26 – 688, 695
Rum. 8:17 – 156, 158
Rum. 8:25 - 688
Rum. 8:28 – 685, 691
Rum. 8:29 - 687
Rum. 8:29-30 – 687, 691
Rum. 8:30 – 122,157, 546
Rum. 8:33 – 519, 597
Rum. 8:34 – 29, 117
Rum. 8:35 - 691
Rum. 8:38-39 - 691
Rum. 9:5 – 535, 655
Rum. 9:8 - 691
Rum. 9:11- 699
Rum. 9:11-13 – 690, 699
Rum. 9:14 - 693
Rum. 9:16 - 514
Rum. 9:17 - 698
Rum. 9:19 - 684
Rum. 9:20 - 693
Rum. 9:31 - 689
Rum. 9:33 - 242
Rum. 10:3-4 - 95
Rum. 10:4 – 159, 620
Rum. 10:10 – 161, 218
Rum. 10:12 - 687
Rum. 10:17 – 101, 186, 216, 514, 584, 694
Rum. 11:6 – 97, 519
Rum. 11:20 - 614
Rum. 11:32 – 545, 687
Rum. 11:33 – 693, 694
Rum. 12:1 – 204, 228, 266, 280
Rum. 12:2 - 624
Rum. 12:5 - 177
Rum. 12:12 - 462
Rum. 12:19 - 230
Rum. 13:1 - 230
Rum. 13:1-4 - 376
Rum. 13:5 – 230, 610
Rum. 13:5-7 - 376
Rum. 13:9 – 378, 610, 626
Rum. 14 – 677
Rum. 14:1 - 643
Rum. 14:3 - 643
Rum. 14:6 - 678
Rum. 14:13 - 542
Rum. 14:17 – 47, 51, 172
Rum. 14:23 – 96, 195, 222, 288, 609
Rum. 15:4 – 547, 684
Rum. 15:16 – 268, 699
803
1 Wakorintho
1 Kor. 1:8 - 688
1 Kor. 1:21 - 574, 585, 685
1 Kor. 1:30 - 105, 517
1 Kor. 1:30 - 31 - 147, 681
1 Kor. 1:31 – 333
1 Kor. 2:4 - 12 - 589
1 Kor. 2:8 - 537
1 Kor. 2:11 - 456
1 Kor. 2:14 - 21, 22, 86, 233, 514, 574, 575
1 Kor. 3:4 - 8 - 339
1 Kor. 3:7 - 514
1 Kor. 3:8 - 122, 158, 241
1 Kor. 3: 12- 168
1 Kor. 3:19 - 574
1 Kor. 3:21 - 22 - 339
1 Kor. 4:1 - 277
1 Kor. 4:4 - 117, 329, 626
1 Kor. 4:7 - 579
1 Kor. 4:13 - 265, 426
1 Kor. 4:15 - 424
1 Kor. 5 - 165
1 Kor. 5:6 - 595
1 Kor. 6:9 - 613
1 Kor. 7:2 - 33, 35, 53, 58, 251, 258, 293
1 Kor. 7:5 - 255
1 Kor. 7:9 - 33, 35, 251
1 Kor. 7:10 - 11 - 446
1 Kor. 7:14 - 253
1 Kor. 7:18 - 19 -678
1 Kor. 7:32 - 255
1 Kor. 7:37 - 232
1 Kor. 8:8 - 288
1 Kor. 8:9 - 13 - 542
1 Kor. 9:9 - 610
1 Kor. 9:10 - 677
1 Kor. 9:14 - 375
1 Kor. 9:16 - 514
1 Kor. 9:27 - 48, 228, 572, 611, 623,625
1 Kor. 10:16 - 328, 530, 531, 630, 639, 640, 644, 645
1 Kor. 10:17 - 177
1 Kor. 10:18 - 33 - 639
1 Kor. 11:5 - 67, 73
1 Kor. 11:20 - 31, 32 42
1 Kor. 11:23 - 533
1 Kor. 11:23 - 24 - 246
1 Kor. 11:23 -25 - 399, 491, 530
1 Kor. 11:24 - 276, 629, 634
1 Kor. 11:25 - 218, 360, 638,639
1 Kor. 11:26 - 125, 269
1 Kor. 11:27 - 38, 178, 281, 499, 531, 640
1 Kor. 11:28 - 246, 328
1 Kor. 11:29 - 178, 531
1 Kor. 11:31 - 138, 211
1 Kor. 11: 33 - 40
1 Kor. 12:3 - 579
1 Kor. 12:22 - 23 - 443
1 Kor. 13:2 - 111, 126
1 Kor. 13:13 - 128
1 Kor. 14:2 - 38
1 Kor. 14:9 - 38
1 Kor. 14:30 - 67
1 Kor. 14:32 - 232
1 Kor. 14:40 - 67
1 Kor. 15:12 - 553
1 Kor. 15: 56 - 57 - 103, 210
1 Kor. 15:57 - 207, 666, 669, 710
1 Kor. 16:1 - 122
2 Wakorintho
2 Kor. 1:9 - 210
2 Kor. 1:23 - 410
2 Kor. 1:24 - 343
2 Kor. 2:14 - 586
2 Kor. 3:4 - 12 - 589
2 Kor. 3:5 - 515, 573, 575, 579
2 Kor. 3:6 - 273
2 Kor. 3:7 - 621
2 Kor. 3:8 – 687
2 Kor. 3:13 -16 - 525, 617
2 Kor. 3:15 - 17 -112
2 Kor. 3:18 - 155, 289
2 Kor. 4:16 - 209
2 Kor. 5:2 - 3 -155
2 Kor. 5:17 - 579
2 Kor. 5:19 - 635
2 Kor. 5:20 - 277, 687
2 Kor. 5:21 - 147, 517, 524, 691, 685
2 Kor. 6:1 - 588
2 Kor. 6:14 - 346, 543, 677, 680
2 Kor. 6:17 - 348
2 Kor. 7:10 - 617
2 Kor. 9:6 - 158
2 Kor. 9:7 - 232, 610, 611
2 Kor. 9:12 - 278
2 Kor. 10 - 718
2 Kor. 10:4 - 343
2 Kor. 10:4 - 5 - 63, 70
2 Kor. 10:8 - 273
2 Kor. 12:9 - 211, 643
2 Kor. 13:2 - 15 - 128
2 Kor. 13: 8 - 64, 71
2 Kor. 13:10 - 64, 66
Wagalatia
Gal. 1:2 - 731
Gal. 1: 7 - 9 - 351
Gal. 1:8 - 64, 71, 300, 310, 344, 507
Gal. 1:9 - 175
Gal. 1:20 - 410
Gal. 2 - 380
Gal. 2: 2- 338
Gal. 2:3 - 678
Gal. 2:4-5 - 678
Gal. 2:5 - 543, 678
Gal. 2:6 -399, 338
Gal. 2:14 - 678, 112
Gal. 2:16 - 519,
Gal. 2:16-17 - 625, 106
Gal. 2:17 - 149, 221
Gal. 2:19 - 184
Gal. 2:21 - 95
Gal. 3:2 - 624, 625
Gal. 3:10 - 625
Gal. 3:13 - 119
Gal. 3:14 - 12, 624
Gal. 3:15 - 221
Gal. 3:18 - 105
Gal. 3:22 - 104, 194
Gal. 3:24 - 94, 620
Gal. 3:27 - 588
Gal. 4:9 - 163
Gal. 5 - 381
Gal. 5:1 - 66, 73, 226, 300, 543, 678
Gal. 5:2 - 543, 678
Gal. 5:4 - 55, 60, 95, 220, 285
Gal. 5:6 - 110, 519
Gal. 5:7 - 163
Gal. 5:17 - 118, 149, 523, 527, 576, 587, 592, 623
Gal. 5:19-21 - 500
Gal. 5:21 - 613
Gal. 5:22 - 609
Gal. 5:24 - 611
Gal. 6:6-7 - 376
Gal. 6:14 - 527
Gal. 6:15 - 579
Waefeso
Efe. 1 - 713, 714
Efe. 1:2 - 665
Efe. 1:4 - 545, 684, 685, 690, 691, 694, 699
Efe. 1:4-5 - 683
Efe. 1:5-6 - 698
Efe. 1:6 -694
Efe. 1:7 - 139
Efe. 1:9 - 685, 686
Efe. 1:-10 - 686
Efe. 1:11 - 546, 688
Efe. 1:13 - 685, 688
Efe. 1:13-14 - 685
Efe. 1:15 - 685
Efe. 1:17-18 - 575
Efe. 1:21 - 656
Efe. 1:22 - 313, 666, 710
Efe. 1:22-23 - 165
Efe. 2:1 - 574
Efe. 2:2 - 167, 232, 573
Efe. 2:3 - 511, 561
Efe. 2:5 - 514, 574, 587
Efe. 2:8 - 24, 106, 579
Efe. 2:8-9 - 26, 102, 106, 220, 522
Efe. 2:9 - 519
Efe. 2:10 - 597, 581, 608, 624
Efe. 4:4-5 - 14
Efe. 4:5-6 - 14
Efe. 4:8 - 350
Efe. 4:10 - 537, 660, 728
Efe. 4:11 - 350
Efe. 4:15 - 313
Efe. 4:17-18 - 574
Efe. 4:23 - 527
Efe. 4:24 - 561
805
Efe. 4:28 - 212
Efe. 5:3-11 - 690
Efe. 5:5 - 613
Efe. 5:8 - 574
Efe. 5:9 - 609
Efe. 5:18 - 690
Efe. 5:22 - 377
Efe. 5:22-24 - 384
Efe. 5:25 - 313
Efe. 5:25-27 - 165
Efe. 5:25-29 - 384
Efe. 5:25-33 - 433
Efe. 5:26 - 327
Efe. 5:30 - 672, 674
Efe. 5:32 - 386
Efe. 6:1-3 - 377
Efe. 6:2-3 - 122, 420
Efe. 6:4 - 377
Efe. 6:5-8 - 378
Efe. 6:9 - 378
Efe. 6:16 - 395, 477
Wafilipi
Flp. 1:6 - 688, 690
Flp. 1:9-10 - 575
Flp. 1:28 - 615
Flp. 1:29 - 579
Flp. 2 - 716
Flp. 2:7 - 537, 660
Flp. 2:8 - 537
Flp. 2:9 - 710
Flp. 2:9-10 - 719
Flp. 2:13 - 575, 579, 581
Flp. 2:14 - 67
Flp. 2:25 - 278
Flp. 3:7 - 614
Flp. 3:9-10 - 596
Flp. 3:20 - 63, 70
Flp. 4:3 - 545, 685, 686 Wakolosai
Kol. 1 - 553
Kol. 1:9 - 575
Kol. 1:13 - 158
Kol. 1:19 - 721
Kol. 1:20 - 725
Kol. 1:22-23 - 614
Kol. 1:27 - 675
Kol. 2 - 553
Kol. 2:3 - 540, 671, 720, 725
Kol. 2:8 - 163
Kol. 2:9 - 540, 635, 661, 668, 669, 716, 720, 721, 727
Kol. 2:10 - 120
Kol. 2:11 - 186
Kol. 2:12 - 133, 212
Kol. 2:13 - 574
Kol. 2:14 - 108, 155, 187
Kol. 2:16 - 47, 51, 286, 678
Kol. 2:16-17 - 172, 255
Kol. 2:16-23 - 51, 66
Kol. 2:17 - 269
Kol. 2:18 - 256, 313
Kol. 2:20-21 - 47
Kol. 2:20-23 - 73, 299
Kol. 2:23 - 224
Kol. 3:4 - 647
Kol. 3:6 - 613
Kol. 3:10 - 85, 155
Kol. 3:13 - 131
Kol. 3:14 - 129
Kol. 3:18-19 - 433
Kol. 3:19 - 377
Kol. 4:2 - 462
1 Wathesalonike
1 The. 4:4 - 255, 259
1 The. 5:12-13 - 376
1 The. 5:17 - 462
2 Wathesalonike
2 The. 2:4 - 165, 315, 345
2 The. 2:13-15 - 685
2 The. 2:16-17 - 239
1 Timotheo
1 Tim. 1:5 - 132
1 Tim. 1:9 - 94, 622
1 Tim. 2:1 - 378, 462
1 Tim. 2:1-3 - 377
1 Tim. 2:5 - 29, 553
1 Tim. 2:6 - 545
1 Tim. 2:15 - 253
1 Tim. 3:2 - 33
1 Tim. 3:2-4 - 375
1 Tim. 3:2-6 - 35
1 Tim. 3:6 - 375
1 Tim. 3:9 - 557
1 Tim. 3:15 - 168
1 Tim. 3:16 - 538, 661
1 Tim. 4:1 - 66, 220, 258, 289, 332, 346
1 Tim. 4:1-3 - 35, 37, 48, 51, 257
1 Tim. 4:2-3 - 163
1 Tim. 4:5 - 253
1 Tim. 4:8 - 287
1 Tim. 5:5-6 378
1 Tim. 5:8 - 296
1 Tim. 5:9 - 296
1 Tim. 5:11 - 296
1 Tim. 5:17 - 425
1 Tim. 5:17-18 - 376
1 Tim. 6:8 - 472
1 Tim. 6:15 - 647
2 Timotheo
2 Tim. 1:9 - 690, 691
2 Tim. 1:9-11 - 686
2 Tim. 1:13 - 614
2 Tim. 2 - 381
2 Tim. 2:15 - 121, 524, 615
2 Tim. 2:19 - 699
2 Tim. 2:21 697
2 Tim. 2:24 - 557
2 Tim. 2:25 - 579
2 Tim. 2:26 - 573
2 Tim. 3:16 557, 684, 685
2 Tim. 4:8 - 157
Tito
Tit. 1:5-7 - 349
Tit. 1:9 - 375, 557
Tit. 1:14 - 66, 73, 334
Tit. 1:15 - 254, 255, 259
Tit. 2:14 - 201
Tit. 3 - 577
Tit. 3:1 - 377
Tit. 3:5 - 389, 483, 519, 597
Tit. 3:5-6 - 579
Tit. 3:5-8 - 371
Tit. 3:10 - 346, 680
Filemoni
Flm. 14 - 610
Waebrania
Ebr. 1 - 713, 714, 721
Ebr. 1:3 - 671, 711
Ebr. 1:14 - 264
Ebr. 2 - 718
Ebr. 2:7-8 - 669
Ebr. 2:8 - 537, 666
Ebr. 2:8-9 - 711
Ebr. 2:14-17 - 510
Ebr. 2:17 - 567
Ebr. 3:14 - 612, 688
Ebr. 4:2 - 689
Ebr. 4:7 - 689
Ebr. 4:14-16 - 104
Ebr. 4:16 - 490
Ebr. 5:1 - 272
Ebr. 7-9 - 216
Ebr. 9:14 - 715
Ebr. 10:1 - 167, 269
Ebr. 10:5-16 - 264
Ebr. 10:10 - 39, 264
Ebr. 10:14 - 39
Ebr. 10:26 - 690
Ebr. 10:29 - 698
Ebr. 11:1 - 27, 148
Ebr. 11:4 - 123, 526,
Ebr. 11:6 - 134, 138, 159, 233
Ebr. 11:8 600
Ebr. 12:8 623
Ebr. 12:25 - 546
Ebr. 13:15 - 266, 626
Ebr. 13:17 - 300, 376
Ebr. 13:21 - 527
Yakobo
Yak. 1:6 462
Yak. 1:6-7 - 479
Yak. 1:17 - 579, 664
Yak. 1:18 - 132
Yak. 2:19 - 146, 153, 186
Yak. 2:22 - 133
Yak. 2:24 - 131, 133, 602
Yak. 3:5 - 444
Yak. 5:13 - 462
Yak. 5:16 - 198
1 Petro
1 Pet. 1:2 - 269
1 Pet. 1:5 - 162, 614
1 Pet. 1:9 - 156, 614
1 Pet. 1:12 - 661
1 Pet. 2:4-6 - 130
1 Pet. 2:5 - 265, 626
1 Pet. 2:6 - 190
1 Pet. 2:9 - 351
1 Pet. 2:11 - 592
1 Pet. 2:13-14 - 377
1 Pet. 3:5-6 - 377
1 Pet. 3:7 - 377
1 Pet. 3:18 - 662
1 Pet. 4:1 - 662
1 Pet. 4:8 - 130, 432
1 Pet. 4:17 - 209
1 Pet. 5 - 381
1 Pet. 5:1 - 349
1 Pet. 5:2 - 75, 610
1 Pet. 5:3 - 68, 339
1 Pet. 5:5-6 - 378
2 Petro
2 Pet. 1:4 - 661
2 Pet. 1:10 - 235, 546, 613
2 Pet. 1:21 331
2 Pet. 2:1-10 - 553
2 Pet. 2:2 - 546
2 Pet. 2:10 - 690, 695
2 Pet. 2:20 - 698
2 Pet. 3:2 - 249
2 Pet. 3:9 - 687, 688, 697, 698
1 Yohana
1 Yoh. 1 - 708
1 Yoh. 1:7 - 606, 666, 687, 715
1 Yoh. 1:8 - 151, 327
1 Yoh. 2 - 381
1 Yoh. 2:1 28, 29
1 Yoh. 2:2 - 545, 687
1 Yoh. 2:12 - 139
1 Yoh. 3:8 - 113, 561
1 Yoh. 3:9 - 327
1 Yoh. 3:14 - 599
1 Yoh. 4:11 - 610
1 Yoh. 4:19 - 113
1 Yoh. 5:10 - 190, 195
1 Yoh. 5:10-12 - 145
1 Yoh. 5:18 - 327
2 Yohana
2 Yoh. 1 - 349
3 Yohana
3 Yoh. 1 - 349
Yuda
Yud. 4-8 - 553
Yud. 20 - 462
Ufunuo
Ufu. 3:5 -545, 685
Ufu. 4:11 - 566
Ufu. 10:3 -314
Ufu. 12:3 - 309, 330
Ufu. 12:9 - 329, 330
Ufu. 16:12 - 247
Ufu. 18:4 - 348
Ufu. 19:8 - 265
Ufu. 20:2 - 309
Ufu. 20:15 - 545, 685, 686