
1 minute read
Uwanjani kwawaka
Na Luke Kung’u
Ilikuwa kama vile msemo wa kisasa wa vijana… ‘mambo ni mengi, masaa ndio machache’, pale kiwanjani Strathmore Complex tarehe kumi na nane mwezi wa tatu mwaka huu, wakati KNHFC waliwaalika
Advertisement
Samwest Blackboots FC na kufunga mabao matatu kila upande kwa mechi. Hata hivyo KNHFC walijizolea alama moja na kufikia pointi kumi na mbili kwa mujibu wa chama cha mpira wa soka nchini Football Kenya Federation (FKF).
Waliotia mpira wavuni ni: Bw. Wilson Makena, Bw.Timothy Matanda na Bw. Collins Achieng. Hongera kwao.
Hapo awali, KNHFC kwa mwaliko wa timu ya Segera FC ilitwangwa mabao mawili kwa moja, walipocheza kwenye mchuano uwanjani Segera
Ranch mnamo tarehe kumi na mbili mwezi wa tatu mwaka huu. Hawakujinyakulia pointi yoyote. Mechi ifuatayo itachezewa uwanjani Strathmore Complex ambapo KNHFC itachuana na Ligi
Ndogo FC tarehe ishirini na tano mwezi huu wa tatu, ikiwa ni raundi ya tisa.
Tupatane uwanjani.