
1 minute read
Ngumi ndogo ikipunga
BY KAREN HINES
MAZUNGUMZO KWA WALE WANAOSITASITA KUPATA CHANJO...
... na wale wanaowapenda
“Katika janga hili lote lengo letu limekuwa kuwatumia wasanii ili kutusaidia kuelewa nyakati hizi za sisizo za kawaida. Kwa hivyo, wakati
Dr. Peter Centre ilipotufikia kuhusu kufanya kazi katika mradi kuhusu watu wanaositasita kupata chanjo, ilitubidi kusema ndiyo — kwa sababu tunaona kwamba suala la chanjo linagawanya marafiki, familia na jamii. Kama wasanii tunataka kufanya sehemu yetu kuleta watu pamoja, na kupigana na kile tunachoona kama athari mbaya zaidi ya janga hili — mafarakano na migawanyiko inayoibuka katika sehemu nyingi za jamii.
Pamoja na Majadiliano ya Wanasitasita Kupata
Chanjo na Wale Wanaowapenda, tuliagiza waandishi wanne wa tamthilia ambao mambo waliyokuwa wamepitia maishani yangeweza kutoa maarifa na uelewaji kuhusu baadhi ya hali ngumu zaidi ambazo sote tunakabili. Tunafikiria haya kama mazungumzo ya kuigiza yanayojumuisha hali ngumu ambazo wengi wetu tunajikuta ndani yake. Iwe ni mjadala unaofanya pamoja nawe mwenyewe, au mtu fulani katika mduara wako, tunatumai michezo hii mifupi itakusaidia kuabiri suala hili kwa fadhili na huruma.”
SHERRY J YOON JAY DODGE Artistic Director Artistic Producer
Boca del Lupo Boca del Lupo