FAO Rabies Brochure

Page 1

Kwa mnyama • Unapohisi au unapoona mbwa au mnyama mwenye dalili za Kichaa cha Mbwa, toa taarifa kwa mtaalam wa mifugo au serikali ya kijiji/mtaa iliyo karibu na eneo lako. • Mbwa au mnyama afungiwe kwa muda usiopungua siku kumi akipewa chakula na maji ili kuona kama atakufa ama la. Endao atakufa ndani ya muda huo, kuna uwezekano mkubwa kuwa alikuwa na kichaa cha mbwa. • Toa taarifa mapema kwa mtaalamu wa mifugo kwenye eneo lako unapoona mnyama mwenye dalili kwa ufuatiliaji na udhibiti zaidi. • Kumtambua mwenye mbwa au mnyama aliyekung’ata kutasaidia uchunguzi zaidi • kufahamu endapo ana ugonjwa ama alishapatiwa chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa. JINSI YA KUZUIA KUENEA KWA UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA •

Kuna njia mbalimbali za kudhibiti Kichaa cha Mbwa. Njia hizo husaidia jamii kujikinga au kuepu-ka kupata ugonjwa huo, pia kuwakinga wanyama kama mbwa, paka na wengine dhidi ya ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa.

KUTOA KINGA TIBA DHIDI YA KICHAA CHA MBWA KWA MAKUNDI YAFUATAYO: • • •

Wafanyakazi wa maabara Watoa chanjo dhidi ya Kichaa cha Mbwa Wakusanyaji sampuli na mizoga ya wanyama

Kwa Wanyama • Mbwa na paka wapelekwe kuchanjwa dhidi ya Kichaa cha Mbwa kila mwaka au kulingana na ushauri wa mtaalamu wa mifugo. Chanjo ni njia pekee inayotumika kumkinga mbwa na wanyama wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya Kichaa cha Mbwa •

Zuia uzururaji wa mbwa na wanyama wengine wafugwao kwa kuwafungia katika mabanda, uzio au kuwafunga kamba kuanzia saa 12 alfajiri na kumfungulia saa 4 usiku.

Zingatia ufugaji bora wa mbwa kwa kuhakikisha kuwa anapatiwa haki zake za msingi (chakula cha kutosha, chanjo, tiba, kuogeshwa, nk).

Kuelimisha watoto wasicheze na mbwa wasiyemfahamu, pia kutoa taarifa kwa wazazi endapo watapata tukio la kukwaruzwa, kung’atwa au kulambwa sehemu yenye jeraha na mbwa anayehisiwa kuwa na Kichaa cha Mbwa. Epuka tabia hatarishi kama vile kumchokoza au kumpiga mbwa anayepita, anayekula au mwenye watoto.

Kichaa cha MBWA Chukua Hatua za Kujikinga

Kwa binadamu

FAHAMU KUHUSU

IMETOLEWA NA: Ofisi ya Waziri Mkuu Kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.