TAMKO KWA UMMA:JUKWAA LA KATIBA

Page 1

JUKWAA LA KATIBA TANZANIA P. O. Box 9354, Dar Es Salaam, TANZANIA Telephone: +255 22 2780 765, +255 22 2781 443, Cell: 0788 758581 (Chairman), E-mail: jukwaa.katiba@gmail.com, Web site: www.katibaforumtz.com

TAMKO KWA UMMA MAONI YA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA KUWEKA UTARATIBU NA VYOMBO VITAKAVYOHUSIKA KATIKA KURATIBU MCHAKATO WA KATIBA MPYA TANZANIA, 2011 Jukwaa la Katiba Tanzania ambalo ni Jumuiko la Wananchi wanaoongozwa na asasi 150 za Kiraia kupigania Katika Mpya Tanzania, linapenda kuwasilisha maoni na mapendekezo ya wananchi juu ya Muswada wa Sheria ya kuweka utaratibu wa mabadiliko ya Katiba Tanzania. Maoni haya ni matokeo ya uchambuzi wa JUKWAA LA KATIBA TANZANIA wa maoni yaliyokusanywa kutoka kwa watanzania walioshiriki midahalo, semina, makongamano na mahojiano mbalimbali yaliyoandaliwa na JUKWAA LA KATIBA TANZANIA, asasi wanachama wake na makundi mengine ya Kijamamii tangu muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba wa mwaka 2011 ulipotoka na kusomwa bungeni mwezi Aprili mwaka huu. Uchambuzi huu pia unahusu Muswada Mpya wa Sheria ya Mapitio ya Katiba, 2011 uliochapishwa katika gazeti la serikali Nambari 41 vol 92 la 14 October 2011. Jukwaa la Katiba Tanzania linatambua juhudi ambazo zimefanywa na serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria za Serikali (CPD) na kwa kuweza kuzingatia baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia Mwezi April, 2011 pale Muswada wa awali uliposomwa kwa mara ya Kwanza ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila mafanikio na ukaondolewa rasmi kwenye mchakato wa kusomwa bungeni mpaka ukaandikwe upya, tena kwa Kiswahili. Ni dhahiri kuwa yapo mambo ambayo angalau yameweza kubadilika kulingana na maoni yaliyotolewa na wasomi, wataalam na wananchi juu ya Muswada wa mwezi Aprili. Hata hivyo, Inasikitisha kuwa kumekuwa na kusuasua katika kuukamilisha tena Muswada huu kwa ajili ya kuwasilishwa tena Bungeni. Ikumbukwe kuwa Muswada huu Mpya awali ulipangwa kuwasilishwa katika Mkutano wa Bajeti uliokamilika mwezi Agosti, 2011. Ni kutokana na kusuasua kwa ukamilishaji wa Muswada ndipo Bunge likaamua kufuta ratiba ya kujadili Muswada mwishoni mwa Mkutano wa Bajeti. Hata katika awamu hii, Muswaada umecheleweshwa sana kuchapishwa katika gazeti la serikali na kunyima fursa ya wananchi kuuona, kuuchambua na kuujadili, kabla kwenda Bungeni kwenda kusomwa kwa mara ya Kwanza. Ikumbukwe kuwa ilipendekezwa na wananchi wengi kuwa Muswada Mpya

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

ujadiliwe si tu katika vituo vitatu vya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar bali angalau kuwe na kituo cha Kujadili Muswada katika kila Mkoa. Hili nalo limeshindikana. Kutokana na mambo yaliyojitokeza katika maandalizi ya Muswada huu mpya, na kwa kuzingatia maudhui yaliyomo katika Muswada wenyewe, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tuna Maoni yafuatayo: 1. Licha ya juhudi zilizofanywa na Serikali kuandaa Muswada huu, Jukwaa la Katiba Tanzania bado linasikitishwa na kitendo cha Serikali kuchelewesha kutoa na kusambaza Muswada kwa umma ndani ya muda wa kutosha kuwezesha wananchi walio wengi kupata fursa ya kushiriki majadiliano ya kina na kutoa maoni yao juu ya (kuhusiana na) maudhui ya Muswada kabla haujawasilishwa rasmi Bungeni. Tunatoa rai kuwa Muswada huu ni wa Katiba ya Watanzania katika Jamhuri yote ya Mungano wa Tanzania na hauwezi kuendelea kupitishwa bila ridhaa pana ya Watanzania. 2. Muswada kama huu uliwasilishwa na kukataliwa Bungeni katika kikao chake cha Aprili, 2011. Kwa mantiki hiyo muswada huu wa sasa ni mpya na hivyo ungetarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeni mwezi huu. Hivyo basi, pendekezo kuwa mswada huu utawasilishwa Bungeni na utakuwa ukisomwa kwa mara ya pili na ya tatu ni upotoshaji. Muswada huu ni mpya kwa hiyo unatakiwa uwasilishwe Bungeni kwa mara ya kwanza. Tofauti ya Muswada kusomwa kwa mara ya kwanza na mara ya pili ni kwamba ukisomwa kwa mara ya kwanza kuna fursa ya wananchi kutoa maoni yao, wakati ukisomwa kwa mara ya pili basi hakuna ulazima wala fursa ya Wananchi kutoa maoni yao. Kitaalam, Muswada huu ulisomwa Bungeni kwa mara ya kwanza mwezi Aprili bila mafanikio na hauwezi kuletwa kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya pili kana kwamba ulisomwa wa mafanikio. 3. Jina la Muswada bado ni tatizo na halishabihiani na maudhui makuu ya Muswada na lengo la tunachotaka kufanya kama nchi; huu si Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba bali Muswada wa Sheria ya Kuweka utaratibu, mchakato na vyombo vitakavyohusika katika kuandika Katiba Mpya Tanzania. Jina lake la sasa ni batili .Tunapendekeza kuwa Jina la Muswada huu liwe: MUSWADA WA SHERIA YA KUWEKA UTARATIBU NA VYOMBO VYA KURATIBU MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA TANZANIA. Hii itasomeka kwa Kiingereza kama – TANZANIA CONSTITUTION MAKING PROCESS BILL, 2011. 4. Kuna vipengele vingi vinavyoonyesha Serikali kukosa umakini katika kuandaa Muswada huu. Kwa mfano, mapendekezo kuwa Bunge Maalum la Katiba litaundwa na wajumbe wanaojumuisha wabunge wote wa Bunge la Tanzania na wawakilishi wote wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na halafu kuongeza wajumbe wa nyongeza kuwa ni pamoja na Waziri wa Sheria na Katiba na Mwanasheria Mkuu wa serikali ni marudio yasiyo na sababu ya msingi. Kwa mfumo wetu, Waziri tayari ni Mbunge. Hii inaonyesha kuwa imechukuliwa kutoka katika nchi ambayo mfumo wake unaruhusu kuwa na Mawaziri wasio wabunge. Vivyohivyo, kwa wadhifa wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali tayari ni Mbunge. Na hii ni kwa pande zote za Muungano. FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

5. Kwa mwitikio na maudhui yake, Muswada huu unadhihirisha kuwa Serikali bado ina mtazamo kuwa inaandika Katiba ya dola (yake). Ukweli ni kuwa katika suala hili Serikali inapaswa kutambua kuwa ni mdau kama wadau wengine ila mwenye jukumu la kuwezesha wananchi kuandika Katiba ya Nchi yao. Kuendelelea kufanya mambo kwa usiri na vificho hakutaleta tija yoyote katika mchakato huu muhimu wa Kuandika KATIBA YA WATANZANIA. Aidha, marekebisho ya KATIBA si ajenda ya wananchi wala ya Bunge la Tanzania. 6. Pamoja na vigezo vingine muhimu, Katiba ya Nchi sharti ijibainishe kama 'waraka wa kisiasa'. Lakini mapendekezo mengi yaliyomo kwenye Muswada huu yanaonesha kuwa Katiba itakayoandaliwa, kama ilivyo ya sasa, itakuwa zaidi 'waraka wa kisheria' na 'waraka wa kiutawala' tu (mamlaka makubwa ya Rais ni kielelezo). Sifa ya Katiba kama muafaka wa kitaifa na kijamii unaoleta maridhiano inakosekana katika Muswada huu. Endapo dalili za kukosekana kwa muafaka wa Kitaifa na wa Kijamii zitaanza kujionyesha sasa, kunaweza kutokea mgawanyiko mkubwa wa kitaifa huko tuendako. 7. Muswada haujaweka lengo kuu la kuanzishwa kwa mchakato wa kuandika Katiba mpya. Hili ndio tatizo kuu la Muswada wenyewe na JUKWAA LA KATIBA TANZANIA hatutapitisha Muswada usiolenga kuandika Katiba Mpya. Kwetu sisi, viraka katika katiba iliyopo vinatosha na tunaona kuwa itakuwa ni kupoteza muda na rasilimali za taifa kuanzisha Mchakato utakaoishia kuzaa marekebisho mengine Katika Katiba ya Nchi. Ikumbukwe kuwa Katiba iliyopo ya Tanzania tayari imefanyiwa marekebisho mara kumi na nne (14) tangu mwaka 1977. Kutokana na Maoni haya tunatoa mapendekezo yafuatayo: Utolewe muda na fursa ya kutosha kwa wananchi kupata muswada na kuujadili kabla ya kuwasilishwa kwa majadiliano rasmi Bungeni. Ili hilo litokee, Muswada utamke kuwa unakwenda kusomwa kwa mara ya kwanza na kwamba baada ya kusomwa, kitakachofuata ni Kamati ya Bunge kufika kila Mkoa kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Muswada huu muhimu. JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tuko tayari kusaidia kuandaa Wananchi kwa ajili ya utoaji wa Maoni katika Kila Mkoa. Jina la Muswada libadilishwe na kuwa "Muswada wa Sheria ya Kuweka Utaratibu, Mchakato na Vyombo vitakavyohusika katika Kuandika Katiba Mpya Tanzania". Serikali ioneshe umakini kwa kuondoa vipengele vyote vinavyobainisha kutoandaliwa kwa umakini kama ilivyoainishwa katika uchambuzi wetu wa Kina (ulioambatishwa). Maudhui na mwitikio wa lugha ya Muswada vionyeshe na kubainisha kuwa wananchi wa Tanzania ndio wanaoandaa Katiba yao, siyo Serikali, hivyo, vifungu vyote vinavyoonesha Serikali kupora mamlaka ya raia wa Tanzania kuandaa Katiba yao vikaratibiwe au kuhaririwa ili viakisi ukweli wa mambo na matarajio ya Wananchi wa Tanzania. Hii ni pamoja na kupunguza kabisa, mamlaka kadhaa ya Rais katika mchakato huu wa kuandaa Katiba mpya ya Tanzania. Kwa mfano, itakuwa ngumu FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

kwa Rais kutoa hadidu za Rejea kwa Tume ya KATIBA. Hadidu za Rejea lazima ziwe sehemu ya Muswada huu. Pia, itakuwa ngumu kwa Rais kuteua wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Ipo haja ya kuweka wazi kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la KATIBA watachaguliwa na kupendekezwa na makundi wanakotokea kabla ya majina yao kuchapishwa katika gazeti la Serikali pamoja na yale ya wajumbe wengine kutoka Bunge la TANZANIA na Baraza la wawakilishi Zanzibar. Yatosha kabisa kwa Tume ya Katiba kupeleka majina hayo kwenye gazeti la serikali. Aidha, ili kurahisisha jinsi ya upatikanaji wa wajumbe wa Bunge MAALUM la Katiba, wachaguliwe wajumbe wawili (mmoja akiwa Mwanamke na mwingine mwanaume) kutoka kila wilaya, Tanzania Bara na Zanzibar ili kuwakilisha wilaya zao katika Bunge Maalum la Katiba. Mfumo mzima na mchakato wa kupata wasimamizi wa vyombo vya mamlaka ya mpito kuandaa Katiba mpya usiingizwe, kuchanganywa wala kumezwa na mfumo wa sasa wa uendeshaji wa Serikali. Kwa mfano, Sheria hii iunde Tume Maalum ya uchaguzi kwa ajili ya kusimamia na kuendesha shughuli zote za upigaji kura katika mchakato wa kuandaa katiba mpya. Sambamba na hilo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lipewe jukumu la kusimamia kasi ya mchakato huu ili kuhakikisha kuwa hakuna kusuasua. Watendaji katika vyombo hivi waajiriwe kwa kufuata kanuni za ushindani na masharti ya utumishi wa umma. Kwa kutimisha, tunapenda kutoa rai kwa watanzania wote kujitokeza na kuchangia kwa hali na mali katika Mchakato huu muhimu utakaopelekea watanzania kuandika Katiba yao. Muhimu zaidi, tunapenda kutoa wito kwa wasomi wa ngazi mbalimbali kujitokeza kusaidia kuhamasisha na kuelimisha umma wa Watanzania juu ya namna Katiba Mpya itakavyopatikana. Ni vema tukawezesha uelewa na uwazi ili wananchi wenyewe washiriki mchakato huu. Kwa upande wetu, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tuko mbioni kuunda na kutangaza jopo la wataalam wa masuala ya Katiba ambalo litakuwa na kazi ya kulishauri taifa kuhusu Mchakato huu kuanzia sasa mpaka tutakapopata Katiba Mpya ya Nchi. Tunawaomba mtakaoteuliwa kukubali kutumikia taifa letu kwa moyo na uadilifu Mkubwa. Pamoja na Shukrani na kwa niaba ya JUKWAA LA KATIBA TANZANIA,

Deus M Kibamba MWENYEKITI JUKWAA LA KATIBA TANZANA 02 NOVEMBA 2011

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

UCHAMBUZI WA MUSWADA NA MAPENDEKEZO KWA KILA KIFUNGU KIFUNGU

UCHAMBUZI WA VIFUNGU

Kifungu cha 1

Jina la Muswada (Sheria Mabadiliko ya Katiba, 2011).

PENDEKEZO ya Isomeke; Sheria ya Kuweka Utaratibu, mchakato na Vyombo vitakavyohusika Kuandika Katiba Mpya Tanzania, 2011

Kifungu cha 4

Kifungu hiki hakijaonyesha dhumuni kuu la kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya. 4(l) ina dhumuni la kuanzisha mfumo wa kisheria utakaowezesha Rais kuunda Bunge la Katiba. 4(h), vyama siasa vimeachwa

Dhumuni kuu la Muswada liwe kuweka/kuanzisha utaratibu wa mchakato wa kuandika Katiba Mpya. 4(l), kuanzisha mfumo wa kisheria utakaowezesha kuunda Bunge la Katiba (Neno Rais liondolewe). Vyama vya siasa viongezwe

Kifungu cha 6(1)

6(1) Wajumbe wa tume wanaoteuliwa na Rais

6(1) wajumbe wateuliwe na Rais wathibitishwe na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 6(3)(d) Jinsia kwa wajumbe wa Tume iwe asilimia 50 Kwa 50

Kifungu cha 6(3)(d) 6(3)(d) imetaja neno jinsia tu, lakini haijataja uwiano

Kifungu 7

Nafasi ya Mwenyekiti na makamu Endapo mwenyekiti atakuwa mwanamke, basi makamu wa Tume awe mwanaume

Kifungu cha 8 (1),(3)

Hadidu za rejea zitatolewa na Rais

Sheria hii hii ndio iainishe hadidu za rejea ambazo zitatajwa tena kwenye

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

waraka wa uteuzi na ziambatanishwe kwenye sheria hii. Kifungu cha 9

Majukumu ya Tume yameainishwa Kuna mkanganyiko kati ya lakini hadidu za rejea zitatolewa Majukumu ya tume na hadidu za rejea na Rais zitakazotolewa na Rais. Tunasisitiza umuhimu wa hadidu za rejea kuambatanishwa na Sheria hii.

Kifungu cha 13

Ni lazima Katibu wa sekretareti Nafasi ya Katibu wa Tume itangazwe kwa umma na awe mtumishi wa serikali mchakato wa uajiri wake na masharti yasimamiwe na Tume ya Utumishi wa umma (Majukumu ya Rais yapunguzwe).

Kifungu cha 13(5)

Waziri anateua watendaji wengine Watendaji wengine waajiriwe na Tume ya wa Sekretarieti Utumishi wa Umma.

Kifungu cha 16(1)

Hadidu za rejea

Kifungu 18

Rasimu na ripoti vitawasilishwa Rasimu ya Katiba Mpya na taarifa ya Tume kwa Rais vitawasilishwa Bungeni na Bunge litoe Azimio la kukabidhi kwa Bunge la Katiba na nakala kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri na wa Zanzibar.

Kifungu cha 20

Hadidu za rejea ziambatanishwe na sheria hii.

Rais asihusike kutamka wala kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba.

Sheria hii inapaswa itamke kuundwa Bunge la Katiba.

Kifungu hiki hakitoi vigezo bayana vya kuwateua wajumbe wa Bunge la Katiba.

Sheria hii iainishe jinsi Bunge hilo la katiba litakavyoundwa. Kuwe

na

uchaguzi

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

wa wazi wa kidemokrasia kila Wilaya za Kiserikali kutoa wawakilishi wawili kwa kuzingatia Usawa wa kijinsia. Tume ya mpito ya uchaguzi iundwe na kusimamia uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba.(Tume hii iundwe na Majaji wakuu wastaafu wa Bara na Visiwani, Spika wastaafu, Viongozi wakuu wa dini wasiozidi 4). Kifungu cha 21(1)

Spika, naibu spika wa Bunge la Usawa wa kijinsia: endapo Spika ni mwanamke Naibu Katiba Spika awe mwanaume.

Kifungu cha 21(4)

Kiapo cha Spika na Naibu Spika kwa kutumia Kanuni za kudumu za Bunge.

Spika na Naibu Spika wasiape kwa kutumia Kanuni za kudumu za Bunge, bali Sekretarieti iandae Kanuni mahsusi kwa ajili ya kuongoza Bunge la katiba.

Kifungu cha 22(1)

Katibu wa Bunge

Katibu wa Bunge la Katiba atapatikana kwa kuzingatia vigezo na ushindani (kwa kufuata Sheria ya Utumishi wa Umma).

Kifungu cha 22(2)

Uchaguzi wa Katibu na Naibu Katibu wa Bunge la Katiba.

Katibu wa Bunge la Katiba atasimamia upatikanaji wa Naibu Katibu wa Bunge la Katiba.

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Kifungu cha 22(4)

Uteuzi wengine Katiba.

watumishi Bunge la

Watumishi wengine wa Bunge la Katiba wataajiriwa kwa kufuata masharti ya Sheria ya Utumishi wa Umma

Kifungu cha 22(5)

Kiapo cha Katibu na Naibu Katibu

Katibu na Naibu Katibu wa Bunge la Katiba waape mbele ya Spika wa Bunge la Katiba.

Kifungu cha 23 (1)

Bunge la Katiba kuwa na mamlaka ya kutunga upya Katiba

Bunge la Katiba halitungi katiba bali linapitisha katiba.

Kifungu cha 22(3)

Utaratibu wa kufanya kazi wa Katibu na Naibu Katibu wa Bunge

Katibu na Naibu Katibu wa Bunge la Katiba watafanya kazi kwa kuzingatia masharti/ ajira utumishi wa Umma.

Kifungu cha 24(1)

Bunge la Katiba linaweza kuandaa kanuni kwa ajili ya kuendesha shughuli katika Bunge la Katiba.

Bunge liandae kanuni kwa ajili ya kuendesha shughuli zake.

Kifungu cha 25

Imetajwa; Sheria yoyote ya Bunge la Katiba

Neno Sheria yoyote ina maana sheria itakayotungwa.

Kifungu cha 26

Kuvunjwa kwa Bunge la Katiba

Bunge la Katiba likimaliza kazi yake ikiwa ni pamoja na kupitisha masharti ya mpito muda wake utakua umekoma rasmi.

Kifungu cha 26(2)

Kuvunjwa na kukoma kwa Mamlaka ya Bunge la Katiba, Rais kuitisha tena Bunge la Katiba kwa

Kipengele kiondolewe

wa wa

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

hiki

siku za usoni. Kifungu cha 27

Uendeshaji wa kura ya maoni kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Tume ya Uchaguzi ya mpito isimamie zoezi zima la uendeshaji wa kura ya Maoni

Kifungu cha 27(2)

Tume ya Uchaguzi Zanzibar itaandaa, kuendesha,kusimamia na itawasilisha matokeo kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Zoezi la kuendesha na kusimamia upigaji wa Kura ya Maoni utasimamiwa na Tume ya Mpito ya Uchaguzi.

Kifungu cha 28(1)

Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itatayarisha na kuchapisha swali litakaloamuliwa kwa kura ya maoni

Bunge la katiba litapendekeza na kujadili swali la kupigiwa kura ya maoni ya Katiba Mpya.

Kifungu cha 28(2)

Kutayarishwa kwa Swali la kura ya Kifungu kiondolewe Maoni

Kifungu cha 29(1)

Tume ya Uchaguzi ya Taifa na ya Zanzibar kuhamasisha wananchi na kusimamia zoezi la upigaji kura ya maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya

Tume ya mpito ya uchaguzi isijihusishe na suala la kuelimisha na kuelimisha wananchi kuhusu upigaji kura ya maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya Pande mbili za makundi ya kijamii zinazounga mkono na kupinga katiba mpya ndiyo zifanye kazi ya kuhamasisha wananchi, Tume ihusike katika kuratibu mchakato

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

wa maoni. Kifungu cha 29(2)

Tume kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha wapigaji kura ya maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya.

Wananchi kupitia vyama vya siasa, vyama vya kijamii watatoa elimu ya uraia kuhamasisha wapigaji kura ya maoni.

Kifungu cha 29(3)

Usimamizi wa Kura za Maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya.

Tume ya mpito iajiri wasimamizi wa kura ya maoni katika kila Wilaya ya Jimbo la Uchaguzi.

Kifungu cha 30

Haki ya Kupiga kura ya maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya

Watanzania wote wapige kura ya maoni kwa uhuru mahali popote walipo kwa kutambuliwa ukazi wao au mahali pa kazi. Mahabusu na Wafungwa wote wanaotumikia vifungo Magerezani pia wapewe fursa ya kupiga kura ya maoni ya Katiba Mpya.

Kifunga cha 31

Utaratibu wa kuendesha kura ya Maoni

Bunge la katiba litaandaa utaratibu wa kisheria wa kupiga kura ya maoni ya katiba mpya

Kifungu cha 32

Matokeo ya kura ya maoni kutangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa

Matokeo yatatangazwa Tume ya Mpito Uchaguzi yataheshimiwa wananchi wote.

Kifungu cha 32(2)

Matokeo ya kura ya maoni

na ya na na

Matokeo ya Kura ya maoni iamuliwe bila

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

kubagua Tanzania Bara na Zanzibar, bali kura asilimia hamsini kwa ujumla bara na visiwani iamue matokeo(siyo kuhesabiwa kwa kubagua Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar). Kifungu cha 32(3)

Kura ya ikishinda

maoni

ya

HAPANA Bunge la Katiba kuitishwa upya

Kifungu cha 32(4)

Kurudiwa kwa kura ya maoni

Mchakato wa kura ya maoni utarudiwa upya na Bunge la Katiba kupitisha.

Kifungu cha 33

Ukomo wa Tume ya Katiba

Tume

Kifungu cha 34(2)

Kuanza kutumika kwa katiba

Kuwepo na Sheria itakayoelezea jinsi ambavyo utekelezaji wa Katiba utafanyika.

Kifungu cha 34(4)

Matumizi ya Sheria na Lugha.

Sheria ya Kiswahili ndio toleo rasmi la kurejea na Kiingereza iwe lugha ya pili (ya tafsiri).

na Kamati zote zitafikia ukomo baada ya kumaliza majukumu yake.

FOUNDING STEERING COMMITTEE Tanzania Citizens’ Information Bureau (TCIB); The Leadership Forum (TLF); Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA); Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Tanzania Gender Networking Programme (TGNP); Legal and Human Rights Centre (LHRC); Tanzania Ecumenical Dialogue Group (TEDG); Youth Partnership Countrywide (YPC); Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP); Pemba Association of NGOs (PACSO); Association of NGOs – Zanzibar (ANGOZA); Trade Union Confederation of Tanzania (TUCTA); Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.