waandishi ebook 1688185843.33691

Page 1

NOVEL.................... MY VALENTINE- 22 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____


Kauli ya Mr Sule haikumtingisha tu Owen na Laureen bali hata Mr James na mkewe walitingishika vilivyo. Walijikuta wanapata shauku ya kutaka kujua kilichopo nyuma ya pazia kumuhusu Laureen. Siku zote walikuwa wanaishi nae lakini hawakuwahi kabisa kujua maisha yake ya nyuma. Walikuwa wanaona tu wema, unyenyekevu na ukarimu wa Binti huyo. Sasa walimpata mtu ambaye alitaka kuwaambia yale yaliyojificha nyuma ya Laureen.


"Kijana, kwanza kabisa nashukuru kwa kutaka kutujuza mimi na mke wangu yale tusiyoyajua kuhusu huyu Binti. Kwa sasa naomba unipatie business card yako ili nikutafute tuongee baada ya kumaliza hii sherehe.!" Mr James alizungumza kauli hiyo kufuatilia taarifa ya Mr Sule. "Mzee wangu, Simu yangu imevunjwa na kijana wako Owen kwenye ugomvi uliotokea dakika chache zilizopita. Owen


ameivunja kwa maksudi ili nisitoe ushahidi wa maovu ya huyu mwanamke. Nahisi kabisa hata Owen anafahamu kila kitu kuhusu huyu mwanamke.!" Mr Sule aliongea kauli hiyo "Sasa nitakupataje kijana wangu? Nahitaji uniambie kila kitu ila kwa sasa tumalize kwanza sherehe.!" "Usijali mzee wangu, mimi nitakusubiri kwenye parking ya magari hapo njee baada ya sherehe kumalizika.!"


Hayo yalikuwa mazungumzo mafupi kati ya Mr James na Mr Sule. Owen alijikuta tu anamtazama kijana mwenzake kwa hasira kubwa sana. Alitamani hata amrukie na amuue kabisa ilimradi tu siri iendelee kuwa siri. Baada ya maongezi yale hatimaye Mr Sule aliondoka. Mr James akawakata jicho kali Owen na Laureen kisha nae akaondoka. "Siku zote mficha maradhi kifo humuumbua. Haya sasa tukutane mahakamani vijana


wangu. Shahidi yupo tayari kutoa ushahidi wake.!" Mama yake Owen alizungumza kauli hiyo kisha akaondoka nae. Owen na Laureen walibaki wanatazamana tu huku wasijue kipi cha kufanya. Laureen alikuwa anatetemeka kuliko kawaida. Owen aliliona hilo hivyo akamtuliza mtoto wa kike kwa kumgusa na mikono yake mapajani kisha akasema, "Laureen, naomba ufikiri kuhusu mimi tu na sio kitu kingine. Kwa


sasa sina namna yoyote ya kumzuia Mr Sule asitoboe siri yako kwa wazazi wangu. Lakini naomba nikuahidi tu Laureen, hakuna kitu chochote kibaya kitakachokukuta wewe. Mimi nipo na wewe kwa kila hatua. Ulipo nipo kama sipo basi nipo njiani nakuja. Sitojali wazazi wangu wanakupenda au hawakupendi. Ninachojali mimi ni kukupenda wewe hivyo hivyo ulivyo. Tuendelee kusubiri sherehe iishe alafu tuondoke zetu.!" Owen alizungumza maneno hayo kumfariji na kumpa


moyo Laureen. "Kaka Owen, lakini wewe hapo si unajua kwamba mimi sio malaya eti?" Laureen alimuuliza Owen swali hilo kinyonge sana. "Ndio Laureen, najua kabisa wewe sio malaya. Wewe ni mwanamke wangu peke yangu. Nakupenda na nakuhitaji wewe tu. Hata wakisema wewe ni malaya haiwezi kunishtua kwa kuwa nilianza kujua hilo kabla sijaanza kukupenda. Kiufupi sijakupenda kwa bahati mbaya


Laureen, nilikuona machoni na kukuchagua moyoni.!" "Kaka Owen, Naomba usiniache tafadhali. Nakupenda sana My me. Kwa sasa wewe ndo kila kitu kwenye maisha yangu. Wewe ndo baba yangu, mama yangu, kaka yangu, ndugu yangu, rafiki yangu na kipenzi changu mimi. Wewe ndo dunia yangu babaa. Siku zote unaishi kwa kunizunguka tu. Popote nilipo nawe upo. Kiukweli kabisa kama itatokea utaniacha ili kukwepesha aibu kwenye familia


yenu basi nitakufa mimi. Nipo tayari kuishi na wewe kwenye mazingira yoyote yale ilimradi tu tuwe pamoja. Usiniache mimi My me, Nakupenda sana eti.!" Laureen alizungumza kauli hiyo kinyonge sana huku akitokwa na machozi. Owen alimtuliza Laureen na kumkumbusha kwamba pale walikuwa ukumbini na watu walikuwa wanawatazama. Laureen alitulia kisha wakaendelea kupata vinywaji. Hatimaye muda wa sherehe


kumalizika ulifika. Wenye sherehe yao walitoa shukrani za dhati kwa watu wote waliohudhuria. Kwa wale wafanyakazi wa kampuni ya Mr Jay Calvin walikumbushwa kwamba wiki mbili zijazo kutakuwa na tafrija maalumu kwa ajili yao kwenye ukumbi ule ule. Tafrija hiyo ilikuwa inafanyika kila mwaka kila ifikapo Februari 14 yani siku ya wapendanao duniani. Ile tarehe ndo ilikuwa inawadia wiki mbili zijazo na kampuni iliendelea na utaratibu wake wa


kuwakutanisha pamoja wafanyakazi wake ili kudumisha upendo miongoni mwao. Lakini kwa wale waliokuwa na wachumba walikuwa wanapata fursa ya kuwatambulisha wenza wao na hata kuwavisha pete. Lakini pia, kubwa zaidi ni kwamba siku hiyo ndo ilikuwa siku maalumu ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Owen ambaye alikuwa mmoja kati ya wafanyakazi kwenye ile kampuni. Kampuni iliamua kuunganisha sherehe zote mbili ndani ya ukumbi mmoja. Surprise kubwa


iliyokuwa inasubiriwa ni kijana Owen kumvisha pete mchumba 'ake ambaye alimueka kwenye mabano. Hakuna mtu ambaye alikuwa anamjua mchumba wa Owen isipokuwa Owen mwenyewe tu. Ukiachana na Owen, kuna mfanyakazi mwingine nae alikuwa na jambo lake la kumvisha pete mchumba 'ake siku hiyo hiyo. Tangazo maalumu kutoka kwa MC wa sherehe liliwashtua sana wale wanafanyakazi wa kike waliokuwa wanampenda Owen. Walijikuta wanaumia na kuhisi


kupata matumbo ya kuhara bila kutarajia. Baadhi yao walitamani hata hiyo siku isifike kabisa. Hawakutaka kumuona mwanamke mwenzao akivishwa pete na mwanaume wanaompenda wao. Baada ya MC kumaliza kutoa tangazo, watu walianza kuondoka ukumbini na kila mtu alienda alipopaki usafiri wake na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake. Owen aliwapakiza Laureen, Munira pamoja na ndugu zake kisha wakaanza safari kurudi nyumbani. Wakati wanatoka


eneo lile aliwaona wazazi wake wakiwa pamoja na Mr Sule wakizungumza jambo. Owen alielewa kila kitu kilichokuwa kinaendelea ila hakutaka kukipa kipaumbele. Alikanyaga spidi kuendelea na safari ya kurudi nyumbani kwao. Walifika nyumbani kwao wakaoga na kila mtu aliingia chumbani kwake kupumzika kwani usiku ulikuwa tayari umeshaingia. Owen alimkumbusha Laureen kuwa na amani kwani kila kitu kitakuwa sawa tu. Upande wa Mr & Mrs Robyson wao walienda rasmi


kuanza maisha yao ndoa kwenye nyumba waliyopewa na Mr Jay Calvin kama zawadi. Mr James na mkewe walichelewa kidogo kurudi nyumbani kwao na walipofika waliwakuta watu tayari wameshalala. Usiku ule ule waliwaamsha Laureen na Owen ili wazungumze jambo lao. Kwa namna walivyokuwa na hasira, hawakutaka kabisa kusubiri kukuche ili watapike nyongo. Owen na Laureen walitoka kwenye vyumba vyao na kwenda sebuleni walipokuwa wazazi. Owen ndo alikuwa wa kwanza


kufika sebuleni, aliwasalimia wazazi wake ila salamu yake iliitikiwa na baba yake tu. Mama aliuchuna kana kwamba hakusikia chochote. Owen alijua mama yake alikuwa na hasira hivyo akaamua kumpotezea. Owen aliketi kwenye kiti na dakika zile zile alitokea Laureen. Laureen nae alipofika tu aliwasalimia lakini salama yake haikuitikiwa kabisa. Huyo mama Owen alimkata jicho kali Laureen kisha akasonya. Hilo halikuwapa maswali Laureen na Owen kwa kuwa tayari walishajua sababu


ya wazazi kuwa vile. Laureen nae alikaa chini ili kusikia kile walichoitiwa. "Laureen, ulipoletwa hapa hatukuwahi kuambiwa kabisa kuhusu maisha yako ya awali uliyoishi huko mtaani. Lakini leo kwa mara ya kwanza kabisa tumeshaambiwa maisha yako ya awali kabla hujaingia ndani ya hii nyumba. Kila kitu kipo wazi mpaka kufikia muda huu. Tumeambiwa na kujionea kwa macho yetu wenyewe. Sasa nimekuita hapa ili tupate


uthibitisho zaidi kutoka kwako. Tunachohitaji hapa ni ukweli wako tu na sio kitu kingine. Binti. Naomba utuambie ukweli, kabla hujaingia ndani ya nyumba yangu ulikuwa unajishughulisha na kazi gani mtaani?" Mr James alimuuliza Laureen swali hilo huku akiwa amemkazia sura kweli kweli. Laureen alibaki ameganda tu maskini. Hakujua ajibu nini mtoto wa kike zaidi ya kuanza kutiririsha machozi mashavuni mwake.


NOVEL.................... MY VALENTINE- 23 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________


_____ "Wazazi wangu, Laureen ni....!" "Shiiiiiiiiiii!!!!!! Tulia Owen. Hili swali nataka lijibiwe na Laureen mwenyewe. Au nawe ulikuwa unajua ila ukaamua kutuletea aibu ndani ya nyumba yetu?" Owen alitaka kumjibia swali Laureen lakini alinyamazishwa kabla hajazungumza chochote. "Wazazi wangu, naomba nijibu tu hilo swali kwa kuwa hata mimi


nafahamu kila kitu kuhusu Laureen. Naomba nilijibu hilo swali tafadhali.!" "Owen! Kama ulikuwa unajua kila kitu mbona ulikuwa husemi siku zote? Hebu jaribu kuwa na heshima basi maana hilo swali ameulizwa Laureen. Wewe subiri swali lako utaulizwa.!" Mama Owen alizungumza kwa hasira na kumfanya Owen atulie. "Binti, machozi yako hayatoshi kujibu swali langu. Naomba unijibu kile nilichokuuliza, kabla


hujaingia hapa ndani ulikuwa unafanya biashara gani huko mtaani?" Mr James alimuuliza Laureen kwa mara nyingine. Laureen alijifuta machozi yaliyokuwa yanatiririka kwenye mashavu yake kisha akashusha pumzi ndefu na kuongea, "Baba na Mama, kwa kuwa mumeshaambiwa kila kitu kuhusu mimi na kujionea kabisa basi mimi sioni sababu ya kuzungumza chochote. Hiko mulichoambiwa na kujionea kina


ukweli ndani yake.!" Laureen alijibu kwa unyonge sana. "Anhaa! Kwahiyo ni kweli wewe ni kahaba Laureen?" Mama Owen aliuliza "Mama eeh, Mimi sio kahaba ila nilikuwa kahaba hapo awali.!" Laureen alijibu "Lakini wazazi wangu huyu Binti hakupenda kuwa kahaba ila ni ma...!" "Shut up! Shut up Owen.!


Naomba usizungumze chochote kile. Kumbe ulikuwa unajua Laureen ni mwanamke wa aina gani si ndio? Kwahiyo ulimuokota huko kwenye danguro ukaona utuletee hapa nyumbani tuishi nae si ndio? Hivi unajua ni aibu na fedhea kiasi gani tutaipata endapo maadui zetu watajua mmoja kati ya wanafamilia yangu ni kahaba? Haya vuta picha wapinzani wangu kwenye vyama wakijua Laureen ni mwanangu, mfanyakazi wangu au mkwe wangu kipi kitafuata? Unataka kuwapa nguvu


wapinzani wangu wanidhoofishe kupitia hili? Dah! Owen kijana wangu, kwa hili umenikosea sana mimi baba yako pamoja na mama yako. Kwanini umeleta kirusi ndani ya familia?" "Mzee wangu, Wewe ni kiongozi. Moja ya sifa ya kiongozi bora ni kusaidia watu. Mimi nilimleta huyu Laureen ili tumsaidie kwa nafasi tuliyonayo. Binti alikuwa anapitia kipindi kigumu sana cha maisha mpaka kufikia hatua ya kuwa kahaba. Sasa baba, Wewe ni kiongozi gani usiekuwa na


moyo wa kusaidia watu? Wewe ni kiongozi gani unayetaka watu wateseke? Zile kura za kukalia kiti unapewa na watu. Watu wenyewe ndo hawa unaotaka wateseke. Hivi unadhani siku ya uchaguzi hao watu watakuja kukuchagua? Hebu jaribu kujali shida za watu wengine kabla haujaangalia masilahi yako mzee wangu.!" "Hahah! Yani mimi nikae nianze kuwajali makahaba sio? Hivi dogo unadhani siasa ni kitu kinachoangalia huruma sio?


Kwahiyo huruma yangu kwa makahaba ndo itanipa kura eti? Sio kosa lako mwanangu, ni vile tu hujui chochote kuhusu siasa. Hizo kura za makahaba haziwezi kunikosesha kiti hata kwa bahati mbaya. Uwepo wa Laureen hapa ndani utachafua wadhifa wangu kwenye chama. Kesho ikifika naomba umrudishe Laureen kwenye danguro ulikomtoa.!" "Lakini mzee, mbona unakosa utu kisa cheo ulichopewa na Mola aliyemuumba huyu mtu? Huyu Binti alikuwa kahaba kwa


sababu ya shida na maisha aliyokuwa anapitia. Kwa sasa amebadilika kabisa na sio kahaba tena kama ilivyokuwa hapo awali.!" "Owen mwanangu, mazoea hujenga tabia. Huyu alishazoea ukahaba hivyo atabaki kuwa kahaba tu. Naomba umrudishe ulikomtoa asije kuwafundisha wanangu hizo tabia.!" Mama Owen alizungumza kauli hiyo "Mamaa! Sio kila mwanamke anayejiuza mwili anapenda


kufanya hivyo. Baadhi ya wasichana wanafanya hivyo kutokana na changamoto wanazopitia kwenye maisha. Kuna baadhi ya wasichana wadogo wanachukuliwa vijijini na kuletwa ndani ya jiji kwa ajili ya kufanya kazi za ndani lakini mwisho wa siku wanaingizwa kwenye madanguro ya ukahaba. Ukahaba sio tabia kama unavyodhani. Lakini pia ukahaba sio somo kwamba utafundishwa darasani. Huyo Laureen hawezi kufungua darasa la ukahaba kwa Catherine na Sharon hizo ni fikra


potofu mama yangu.!" "Owen.! Naomba unisikilize, Kesho asubuhi ukiondoka kwenda kazini na Laureen nae ataondoka kwenda kwenye danguro. Sisi hatuwezi kuishi na kahaba hapa ndani. Nyumba yangu sio danguro.!" Mr James alizungumza kauli hiyo kwa hasira. "Ok, Laureen ataondoka lakini hata mimi nitaondoka hiyo kesho. Siwezi kuishi kwenye nyumba ya watu wasiojali


thamani ya watu wengine. Kesho jioni nitakaporudi kutoka kazini nitachukua kila kilicho changu na kuondoka na Laureen.!" "Owen! Ikiwa utaondoka kwenye hii nyumba kisa huyo mwanamke basi sitokuwa na radhi na wewe. Kabla ujaondoka utamwambia mama yako akuoneshe baba yako halisi lakini sio mimi Mr James.!" Mr James aliongea kauli hiyo kwa hasira mno. "Owen! Hata mimi nitakupeleka kwa wakunga ukawaombe


wakuoneshe mama yako mzazi. Pengine labda mama yako alibadilishiwa mtoto wakati wa kujifungua.!" Mama Owen nae akapigilia msumari kauli ya mume wake. "Lakini wazazi wangu munakosea sana kuzungumza maneno hayo. Hivi kwanini munatumia vyeo vyenu kutukandamiza sisi watoto wenu? Kwanini kwenu nyie tunakosa uhuru wa kufanya maamuzi binafsi? Hata tukitaka kwenda kujitegemea kwenye


nyumba zetu binafsi bado munatuzuia, munataka tuendelee kuishi pamoja hata kama umri umeenda. Kwanini musitupe uhuru wa kwenda kupambana na changamoto zingine za maisha huko mtaani? Kwa sasa nahitaji kuondoka na kwenda kuishi maisha ya kujitegemea huko mtaani. Ndoa sio kipimo cha kunitoa kwenye nyumba yenu bali umri ndo unaniruhusu kuondoka hapa nyumbani. Hii ni nyumba yenu, acheni na mimi nikatafute nyumba yangu na nikaishi maisha yangu.!" Owen


alizungumza kauli hiyo kwa hekima na busara. "Owen! Kama utaondoka na huyo kahaba basi tunakufuta rasmi kwenye hii familia. Siwezi kukubali fedhea inayokuja mbele yangu.!" Mr James alizungumza kauli hiyo kisha akainuka na kwenda chumbani kwake. "Owen mwanangu.! Fikiria kwa kina kabla hujafanya maamuzi. Sisi ndo wazazi wako tuliokuzaa na kukulea. Ni wajibu wako kutusikiliza na kufuata kile


tunachokuambia.!" Mama yake Owen nae alizungumza kauli hiyo kisha akaondoka kumfuata mume wake chumbani. Pale sebuleni walibaki Owen na Laureen tu wakiwa vichwa chini. Kila mmoja alitafakari kwa upande wake kuhusiana na lile suala. Laureen alikuwa wa kwanza kuinua kichwa chake na kumtazama Owen. "Kaka Owen, Wazazi ndo nguzo muhimu kwenye hii dunia. Kwa sasa naomba tu tuepushe shari


kwa kukubali matakwa yao. Inawezekana ni kweli uwepo wangu unaweza kuchafua taswira nzima ya hii familia. Acha tu niondoke ili kuepusha aibu huko mbeleni. Kiukweli kabisa nakupenda sana Owen lakini sina budi kulivunja penzi langu kwako. Nataka uishi na wazazi wako kwa amani kaka Owen. Mimi nitaondoka hiyo kesho lakini bado nitaendelea kukukumbuka kwa wema wako. Kupitia wewe nimeionja raha ya maisha japo kwa muda mfupi. Mimi niseme tu asante kaka


Owen. Usigombane na wazazi wako kwa ajili yangu.!" Laureen alizungumza maneno hayo huku akitokwa na mvua ya machozi. Owen aliinua kichwa chake akamtazama Laureen. Aliweza kuona machozi ya mtoto wa kike yakidondoka kutoka kwenye mboni za macho yake. Owen alimsogelea Laureen na kuanza kumfuta machozi kwa kutumia viganja vyake vya mikono. "Laureen, Nakupenda sana mpenzi. Naomba usizungumze


tena kauli ya kulivunja penzi letu. Siku zote hakuna uhuru unaopatikana kwenye sahani ya dhahabu bila kuvuja jasho. Tunahitaji kushikamana na kupambania kile tunachokiamini sisi na sio wazazi. Maadam hakuna binadamu mkamilifu basi hata wazazi pia wanakoseaga kwa kuwa wao pia ni binadamu. Kwa hili najua kabisa wazazi wangu wanakosea hivyo nitahakikisha nawarudisha kwenye njia sahihi. Ni suala la muda tu Laureen hivyo tuendelee kusubiri. Muda ndo hakimu


sahihi wa maisha ya mwanadamu.!" "Lakini Owen, unadhani tutaweza kushindana na wazazi wako? Kama hawataki niishi hapa unadhani wataelewa ukija kuwaambia mimi ndo mwanamke unayempenda?" "Laureen, kila kitu kitakuwa sawa mpenzi wangu. Nachokuomba tu hakikisha siku ya Birthday yangu ambayo ndo itakuwa siku ya wapendanao duniani basi uwepo kwenye ule ukumbi uliofanyiwa


sherehe ya harusi ya Brother Robby. Kwa gharama yoyote ile hakikisha unakuwepo ndani ya ukumbi. Plan yangu ya kwanza itaanzia pale. Lakini pia Kesho jioni nikitoka kazini nitakuchukua na kukupeleka sehemu nyingine ya kuishi. Naomba usiondoke mpaka nitakaporudi kazini. Yani nakuahidi hakuna kitu chochote kitakachokukuta nikiwa hai, Nakupenda sana Laureen.!" Hayo yalikuwa mazungumzo mafupi kati ya Owen na Laureen pale sebuleni. Baada ya


mazungumzo hayo kila mtu alienda chumbani kwake kulala. Kwa kiasi fulani maneno ya Owen yalimpa matumaini Laureen. Siku iliyofuata asubuh na mapema, Owen alienda kazini. Alipofika kazini alikuta hali ya hewa imechafuka upande wake. Habari mpya ilikuwa ni kusambaa kwa picha chafu za Laureen ambaye ilisadikika moja kwa moja alikuwa mpenzi wa Owen. Kwa nyadhifa ya Owen kwenye ile kampuni, ilikuwa ni aibu sana kwake kuwa na mpenzi kahaba. Wale waliokuwa


wanamchukia Owen walizisambaza kwa wingi zile picha kwenye mitandao ya kijamii na kusindikiza na maneno ya kumchafua Owen pamoja na familia yake kwa ujumla. Siku nzima Owen alikosa nguvu na utimamu wa kufanya kazi. Mawazo yalikuwa mengi sana upande wake. Yote kwa yote hakutaka kumuuliza mtu yoyote kuhusu usambaaji wa zile picha. Aliamua kuacha mambo kama yalivyo kisha akaendelea na majukumu yake ya kazi. Muda wa kazi ulipoisha, Owen alirudi


nyumbani kwao. Baada ya kufika tu nyumbani alikutana na kizaa zaa kingine. Pale ndani hakumkuta kabisa Laureen. Alizama chumbani kwake hakukuta hata begi lake la nguo mtoto wa kike. Alijaribu kumpigia simu lakini haikupatika wakati haikuwa kawaida yake. Owen alirudi sebuleni akamkuta mama yake anaangalia taarifa ya habari huku akiwa na glasi ya juisi pembeni. Alipoangalia kwa umakini pale mezani aliona simu ya Laureen ambayo yeye ndo alimnunuliaga.


"Mamaa! Laureen yupo wapi?" "Kwahiyo hiyo ndo salamu sio?" "Mamaa! Niambie mtoto wa watu mumempeleka wapi?" "Kwahiyo Owen siku hizi tunafokeana humu ndani si ndio?" "Mamaa eeh! Nataka kujua mtoto wa watu mumempeleka wapi?" "Ok.. Yule kahaba muda huu yupo


kwenye Bus anaelekea nyumbani kwao Mwanza. Usiwe na wasiwasi kuhusu maisha yake Kwa sababu tumempatia fedha za kutosha ili akaanze maisha yake huko aendako.!" Mama Owen alizungumza kauli hiyo kwa nyodo za hali ya juu. "Eti nini? Sijasikia vizuri Mama, umesema Laureen anaenda wapi?" Aisee, Ni kama vile Owen hakusikia kauli ya mama yake ila kiukweli kabisa alisikia na


kuelewa. Moyo wa mtaalamu ulianza kudunda kwa spidi PAAH! PAAH! PAAH! PAAH! NOVEL.................... MY VALENTINE- 24 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM..............


@realsilentkiller_ _________________________________ _____ Owen alichanganikiwa sana baada ya kuambiwa ile taarifa. Alipata mashaka makubwa sana kuhusu hali ya Laureen. Alihisi pengine wazazi wake wamemfanyia kitu kibaya mtoto wa watu. Suala la kutekana na kuuana kwa wanasiasa ni jepesi kuliko kuvunja biskuti. Owen alipata hofu kubwa moyoni mwake. Alitoka fasta ndani ya


nyumba na kwenda getini kuonana na mlinzi. Alimkuta na kumuuliza kama alimuona Laureen akitoka nje ya geti. Mlinzi alimwambia Owen alimuona Laureen akipakiza begi lake kwenye gari na aliondoka na dereva wa mama mwenye nyumba yani mama yake Owen. Lakini pia Laureen kabla hajaondoka aliacha ujumbe kwenye karatasi na kumpatia mlinzi ili amkabidhi Owen pindi tu atakaporudi kutoka kazini. Mlinzi alimpa Owen karatasi chenye ujumbe wa maandishi na


Owen alipokea bila kupoteza hata sekunde. Alikifungua chap chap ile karatasi na kukutana na mwandiko wa Laureen wake. Hakuwa na mashaka na ule ujumbe kwa kuwa mwandiko wa Laureen alikuwa anaujua vyema sana na haikuwa mara ya kwanza kwa Laureen kumwandikia ujumbe wa maandishi kwenye karatasi. "Kaka Owen, Imekuwa ngumu sana kwangu kusema kwa kheri kaka. Lakini hakuna namna imenilazimu tu kusema kwa


kuwa hatima ndo zinatukutanisha na kututenganisha kwenye maisha. Kaka eeh, ulikuwa na nia thabiti ya kunipigania kwenye maisha haya mpaka kufikia ndoto zangu. Ulichokuwa unakitaka siku zote ni kuniona napata furaha na naishi kwenye maisha yanayomstahili binadamu kuishi. Naomba nikutoe tu wasiwasi kuhusu mimi kwani kuanzia leo nitaenda kuishi maisha yanayomstahili binadamu wa kawaida kuishi. Wazazi wako wamenipatia fedha nyingi sana


za kuniwezesha kwenda kuanza maisha yangu kwa sharti la kukaa mbali na wewe pamoja na familia yenu. Najua unanipenda sana na unatamani siku moja ningekuja kuwa mke wako. Lakini kwa sasa naomba tu unisahau mimi na uwaridhishe wazazi wako kwa kumuoa Juliette. Muoe Juliette ili kulinda na kukuza brand ya familia yenu Kaka Owen. Maadam binadamu tuna sifa ya kujongea basi ninaamini ipo siku mimi na wewe hapo tutaonana. Na pengine siku tukionana basi utakuwa tayari


una watoto wenye sura na roho nzuri kama ulivyo wewe Baba yao. Naomba uwe na furaha na usiumie kwa ajili yangu kaka Owen. Japo itakuwa vigumu kwangu kusahau penzi lako lakini nitajitahidi kuwa na furaha ili kutimiza matakwa yako kwangu. Owen My me, hakihitajiki kispika kuja kupaza sauti au kamusi kuja kukuelezea na kutafafsiri upendo wangu kwako. Najua unajua ni jinsi gani mimi hapa ninavyokupenda wewe. Bado utabaki kwenye dunia yangu My me.


Wako katika mapenzi, Laureen wa Owen. Untill we meet again Babaa, Bye byee..!" Aisee, Mpaka kufikia hapo Owen alifika nukta ya mwisho kabisa ya barua iliachwa na Laureen. Mpaka anamaliza kusoma barua tayari machozi yalishalowesha karatasi yote. Nguvu zilimuishia kabisa Owen na akajikuta anakaa chini bila kutarajia. Mlinzi wa geti alishangaa sana kumuona mwamba akimwaga machozi ya kiutu uzima. Owen alijua kabisa ile yote ilikuwa ni mipango ya


wazazi wake kutaka kumtenganisha na Laureen ili amuoe Juliette. Mtaalamu aliinuka pale chini na kwenda moja kwa moja chumbani kwake. Mpaka kufikia majira ya usiku hakutoka kabisa chumbani kwake. Hakutaka chakula wala stori na wazazi wake. Aliwaza ni namna gani afanye ili kumpata Laureen wake. Hata Catherine na Sharon waligoma pia kula siku hiyo. Suala la Laureen kuondoka pale ndani liliwahuzunisha sana. Walimzoea sana kwa ucheshi wake na upendo. Licha ya


kuambiwa kwamba alikuwa kahaba lakini hiyo haikutosha kumvua thamani Laureen. Walimpenda sana Bi mdada na walitamani hata angeolewa na kaka yao Owen. Owen aliwaza sana na ndipo akapata wazo la kumpigia simu dereva wa mama yake na kumuuliza alimpeleka Laureen mpaka wapi kwa kuwa yeye ndo aliondoka nae. Alimpigia simu na kwa bahati nzuri simu iliita na kupokelewa. Owen alizungumza na yule dereva na kumuuliza swali alilokuwa amekusudia. Jibu la


dereva lilitosha kumwaminisha Owen kwamba Laureen hakuwepo ndani ya jiji. Tayari alishapandishwa gari kuelekea Mwanza. Mbaya zaidi ni kwamba hakuwa na simu kwani alinyang'anywa na Mr James ili asiwasiliane kabisa na Owen. Lakini pia alipewa pesa na kuambiwa kama atathubutu kurudi tena ndani ya jiji au kumsogelea mtu yeyote kwenye ile familia basi maisha yake yatakuwa hatarini. Dereva aliamua kumfungukia Owen maneno hayo kwa kuwa


hakupenda kabisa kile alichofanyiwa mtoto wa kike. Kubwa zaidi alimwambia Owen kwamba wakati anamsindikiza Laureen, machozi hayakukatika kwenye mboni za mtoto wa kike. Muda wote alikuwa analia mpaka alipopanda kwenye Bus. Maneno yale yalimuumiza sana Owen mpaka akajikuta anapata hasira juu ya wazazi wake. Alitoka fasta chumbani na kwenda sebuleni ambako aliwakuta wazazi wake wamekaa huku wakitazama mikutano ya vyama vya siasa kwenye televisheni. Owen alienda


kusimama mbele yao kwa hasira kisha akasema, "Naona munafurahi sana wenyewe. Sasa nasema hivi, Ikiwa kuna baya lolote litamkuta Laureen basi wazazi wangu mutawajibika kwa hilo.!" Owen alizungumza maneno hayo kisha akaondoka kwa hasira pale sebuleni. "Owen..! Owen..!" Mama Owen alijaribu kumuita mwanae lakini Owen hakuitika


wala kusimama. "Hivi hili ritoto usikute siku hizi linavuta mibangi. Mbona ana ujasiri sana wa kutufokea sisi wazazi wake? Naona sasa hivi anaamua kututishia mpaka mpaka maisha. Yani kila tunachokifanya yeye anapinga wakati tunafanya kwa faida yake mwenyewe.!" Mr James aliongea "Mume wangu.! Kwa sasa Owen hajakua bado. Siku akikua ataelewa kwanini tunafanya haya yote.!" Mama Owen alimjibu


mume wake kauli hiyo kisha wakaendelea kutazama televisheni. Owen alipandisha ngazi na kwenda ghorofani kilipokuwa chumba chake. Kwa hakika usiku ule ulikuwa mrefu sana kwa Owen kutokana na kuwa na msongo mzito wa mawazo. Owen aliwaza sana mpaka akajikuta anafikia maamuzi ya kufunga safari kuelekea jijini Mwanza kwa lengo la kumtafuta Laureen tu. Wazo hilo alilipitisha katika akili yake. Safari ya Owen


kuelekea Mwanza ilianza rasmi mnamo majira ya alfajiri. Owen aliondoka bila kumuaga mtu yeyote na muda huo watu walikuwa bado wamelala. Ni mlinzi tu ndiye aliyejua kwamba Owen ameondoka ila hakujua anaenda wapi. Owen aliingia kwenye barabara kuu itokayo Dar es salaam kwenda Mwanza kupitia Morogoro. Mtaalamu aliendesha gari kwa spidi kubwa sana na alipofika nje kidogo ya ardhi ya Dar es salaam alifunga breki ya ghafla kisha akapaki gari pembeni. Kuna wazo fulani


lilimfika kichwani mwake juu ya safari yake. Alihisi kabisa safari yake haikuwa na utofauti na safari ya chizi kwa kuwa asingefanikiwa kurudi na chochote zaidi ya makopo. Suala la kumpata Laureen ndani ya jiji la Mwanza lisingekuwa rahisi kabisa kwake. Kwanza kabisa Mwanza ni miongoni mwa majiji makubwa sana nchini Tanzania. Pili hakujua wilaya wala mtaa aliokuwa anaishi Laureen. Jambo hilo lingempa tabu sana Owen na pengine ingemchukua muda mrefu kumtafuta mtu bila


mafanikio yeyote. Owen aliona ni bora tu arudi ndani ya jiji na akaendelee na kazi. Mtaalamu alijikuta anapata machungu ndani ya moyo kuona amempoteza mwanamke wa ndoto zake ikiwa ni mara ya pili tangu alipoingia kwenye ulimwengu wa mapenzi. Mwanamke wa kwanza alikuwa Diana na wa pili ni Laureen. Mpaka kufikia hapo alijua kabisa ule ndo ulikuwa mwisho wa yeye kuonana tena na Laureen. Wakati anajikatia tamaa, ni kama kuna sauti ilikuwa inamwambia


kwamba asikate tamaa wala kuvunjika moyo kwani Laureen hawezi kuishi bila yeye, Laureen hana ujasiri wa kuishi mbali na yeye, Kamwe hakunaga kitu kinachoweza kuvunja nguvu ya upendo kwa watu wawili wanaopenda kwa dhati. Sauti hiyo haikuwa ya kweli bali zilikuwa ni hisia tu za Owen. Kupitia zile hisia Owen alijikuta anapata nguvu kwa mara nyingine. Mtaalamu alikumbuka matukio na mambo kadha wa kadha waliyofanyaga na Laureen siku za nyuma. Owen aliweza


kubaini upendo mkubwa sana ndani ya moyo wa Laureen juu yake. "Ni kweli.! Ni kweli kabisa.! Mimi hapa mimi, naamini kwamba Laureen hawezi kwenda mbali na mimi.! Ninaamini kabisa Laureen hawezi kuishi bila mimi.! Yani naamini kabisa Laureen ananipenda mimi.! Kivyovyote vile naamini kabisa Laureen atarudi kwangu mimi.! Ijapokuwa ni ngumu lakini naamini kabisa Laureen


atakuwepo na mimi siku ya Valentine.! Na ninaamini kwamba Laureen ndo atakuwa My Valentine.!" Owen alijisemea maneno hayo kwa kujipa imani na matumaini kwamba vyoyote itakavyokuwa na iwe lakini Laureen lazima atakuwepo ndani ya ule ukumbi wa sherehe itakapofika ile siku ya wapendanao yani Valentine's Day. NOVEL.................... MY VALENTINE- 25


{Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____ Hatimaye Owen aliamua kugeuza


gari na kuliingiza tena ndani ya jiji. Muda ule alielekea moja kwa moja kazini kwa kuwa alikuwa hajachelewa bado. Kule kazini alikutana na vijembe vya chini chini kutoka kwa wafanyakazi wenzake juu ya sakata lililotokea kuhusu Laureen. Ulikuwa ni mkakati maalumu wa kumuumiza na kumtoa Owen kwenye ramani ya kazi. Ni vile tu Owen aliumbwa na uvumilivu lakini angekuwa mtu mwingine basi angekuwa ameshaanzisha vurugu ndani ya kampuni. Hata muda wa chakula ulipofika Owen


alijikuta anatengwa na wale marafiki zake wengi alikuwa anakaa nao meza moja. Kwa kipindi kile Owen alijikuta anabaki na marafiki wachache tu huku wengine wakigeuka kuwa maadui zake. Kuna muda fulani wakati anaendelea na majukumu ya kazi alitokea mwanadada Salma katika ofisi yake. Mara baada ya Salma kuingia pale ofisi akaanza kumzunguka Owen huku akitembea kwa madowido na kumringishia shepu yake. Owen hakutaka kuhangaika na mtoto wa kike. Alichokifanya ni


kuendelea kufanya kazi yake. "Hivi Owen, kwa huu uzuri wangu na shepu nililokuwa nalo, ulishindwa kweli kunipenda na ukaenda kumpenda yule changudoa? Yani kwenye hii kampuni wanawake wengi sana wapo single na wengine wapo tayari kuvunja hata mahusiano yao kwa ajili yako ila wote hao hukuwaona ukaamua kujidhalilisha kumpenda changudoa. Dah! Ama kweli mapenzi ni upofu, yani nilijua kwamba Owen una msimamo


kumbe ni zero kabisa. Ona sasa ulivyochafua jina lako kwa kitu kidogo tu. Yani kwa namna ulivyo smart, handsome, una elimu na na kipato kizuri hukutakiwa kabisa ku-date na kahaba.!" Salma alizungumza kauli hiyo kwenda kwa Owen. Owen aliendelea kufanya kazi yake kana kwamba hakusikia kabisa kauli ya Salma. "Owen, inamaana naongea peke yangu sio? Mbona huongei chochote.!" Salma alimuuliza


Owen kwa hasira. "Sikiliza wewe mwanamke, ongea peke yako ukimaliza nenda ofisi kwako ukaendelee na kazi iliyokuleta. Mimi sikuja hapa kutafuta mahusiano ya kimapenzi wala kujibizana kwenye mada za mapenzi. Kilichonileta hapa ni kufanya kazi tu. Kitu ambacho siwezi kukizuia ni watu kunisema iwe kwa mazuri au mabaya. Ongeeni kadri muwezavyo kwa sababu mumepewa vinywa na midomo. Ninachoshukuru mimi ni kwamba


hayo maneno yenu hayanitoboi mwili wala kunipotezea muda wangu. Zaidi na zaidi ni kwamba munajipotezea muda wa kuwaza na kufanya mambo yenu. Nakukumbusha tu Salma, hizo harakati zenu haziwezi kubadilisha moyo wangu dhidi yako wewe, Linda, Agnes na wengineo. Hakuna hata mmoja kati yenu anayeweza kuwa mwanamke wangu. Kaeni kwa kutulia, subirini februari 14 mutapata majibu yote ili mzidi kununa.!" Owen alimjibu Salma kauli hiyo huku akiendelea


kufanya kazi yake. Kwa hakika kipindi kile Owen alikutana na changamoto nyingi sana kule kazini. Lakini yeye hakuzipa uzito wowote kichwani mwake. Alijua kwamba ile ilikuwa ni sehemu ya maadui zake kumalizia hasira zao. Waliongea sana lakini mtaalamu hakurusha ngumi wala maneno makali dhidi yao. Aliwaambia kwamba wao wanakisia tu kwamba yupo kwenye mahusiano na Laureen lakini hawana ushahidi wowote. Hivyo basi aliwataka wasubiri


siku ya wapendanao ili awatambulishe rasmi mwanamke anayempenda. Kama anayempenda ndo huyo kahaba basi watamuona na kama kuna mwanamke mwingine tofauti basi watamuona pia. Wakati heka heka zile zikiendelea ndani ya kampuni, Diana yeye alikuwa na mapumziko ya wiki moja ya kufurahia ndoa yake pamoja na mume wake. Yale yaliyokuwa yanaendelea kwenye kampuni alipewa taarifa juu juu na wambea wake na aliwashinikiza wasiache kumchokonoa Owen


juu ya suala lile. Itoshe tu kusema kwamba Diana ni mwanamke ambaye alikuwa hapendi kumuona Owen akiwa na mahusiano na mwanamke yeyote yule. Sio Julliete, sio Laureen, sio Salma, sio Linda wala wengineo. Alichokuwa anakitaka yeye ni kumuona Owen anakuwa single siku zote. Hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa yanaendelea ndani ya kampuni ya Mr Jay Calvin. Taratibu siku zilisonga kuelekea tarehe 14 ya siku ya wapendanao duniani. Owen aliendelea kujipa imani


kwamba siku ya Valentine itakapofika ni lazima Laureen wake afike kwenye ule ukumbi kama alivyowahi kumwambiaga. Lakini pia kila siku alipotoka kazini alikuwa anatembea tembea kukatiza mitaa mbalimbali ya jiji kumtafuta Laureen. Hata kule uswahilini alipokuwa anaishi Laureen na marafiki zake hapo awali alienda lakini hakufanikiwa kabisa kumkuta Laureen wala wale marafiki zake. Alipojaribu kuuliza aliambiwa kwamba wale wanawake walishahama ule


mtaa na kuhamia mtaa wa pili ambako walianza maisha mapya kwa kujishughulisha na biashara ndogo ndogo. Owen alipewa maelekezo ya kufika kwenye makazi mapya ya wale marafiki wa Laureen. Baada ya kupewa maelekezo alianza safari kuelekea kule alipoelekezwa. Alipofika tu alishangaa sana kukuta maisha yamebadilika kwa wale wanawake. Wote kwa pamoja waliamua kujiajiri kwenye biashara ya kuuza chakula pembezoni kidogo mwa soko. Wale wadada


walipomuona Owen walimkumbuka vizuri sana. Kwanza kabisa walimshukuru kwa marefu na mapana kwa kuweza kuwatoa utumwani. Owen ndo mtu aliyewapatia maarifa na mtaji wa kufanya biashara halali badala ya kuuza miili yao. Kwa hakika wale wadada walimshukuru sana kwani biashara ya chakula ilibadilisha taswira nzima ya maisha yao kuanzia kwenye kipato mpaka kwenye maadili. Mpaka kufikia muda ule tayari wadada wawili kati yao walikuwa


wanaishi na waume zao japo ni kwa ndoa za kibongo bongo. Lakini pia kuna mmoja kati yao alikuwa anasubiri tarehe tu ya kuolewa ndoa ya kiislamu. Kwa hakika walifanikiwa kurejesha heshima yao kwenye jamii na ile tabia ya kugawa penzi kama njugu walishaiacha kabisa. Owen alijikuta anafurahi sana baada ya kuona mabadiliko chanya kwa wale wadada. "Ama kweli wakiwezeshwa wanaweza.!" Owen alijisemea kauli hiyo kimoyo moyo baada ya


kuona wale wadada wameweza kuacha ukahaba na kuwa wajasiriamali. Lakini sasa, Wakati anafurahia mabadiliko ya wale wanawake, ghafla huzuni ilirudi tena upande wake baada ya kuulizwa swali na wale wadada kuhusu hali ya Laureen. Hapo ndipo Owen alipokuja kugundua kwamba hata wale marafiki wa Laureen walikuwa hawajui mahali alipokuwa rafiki yao. Ni kweli, hakuna mtu ambaye alikuwa na taarifa za ukweli kuhusu


Laureen. Owen alijikuta anamkosa Laureen sehemu ambayo alihisi angeweza kumpata. Siku zilizidi kusonga hadi kufikia siku moja kabla ya tarehe 14 ya siku ya wapendanao duniani. Owen bado hakufanikiwa kabisa kumtia Laureen kwenye mboni za macho yake. Lakini kwa imani kabisa Owen aliamini Laureen atafika tu kwenye ule ukumbi haijalishi kama yupo Mwanza ama Nairobi. Alichokuwa anakitaka yeye ni kumuona tu Laureen wake na bado alikuwa na imani


Laureen hakuwa nje ya jiji la Dar es salaam. Aliamini kabisa Laureen yupo pale pale Dar es salaam. Naam! Ni kweli bwana, Imani ya Owen ilikuwa ya kweli kabisa. Laureen bado alikuwa ndani ya jiji la Dar es salaam wala sio Mwanza. Kwa mara ya kwanza kabisa Laureen alionekana akiwa pembezoni mwa bahari akitazama mawimbi ya bahari huku akiwaza mambo kadhaa yaliyotokea siku chache zilizopita. Alikumbuka ile siku alipandishwa kwenye Bus kuelekea jijini Mwanza. Njia


nzima alikuwa analia tu mtoto wa kike baada ya kuona ametenganishwa na mwanaume aliyekuwa anampenda kutoka moyoni. Aliwaza ni namna gani Owen alivyoipokea na kuisoma ile barua aliyomuandikia. Laureen alijua kabisa amemuacha Owen kwenye wakati mgumu sana wa maisha. Siku zote pesa inaweza kununua kitu chochote lakini sio amani ya moyo. Huwezi kupona donda la moyo kwa kutumia pesa. Huwezi kusalitiwa na mtu umpendae alafu ukatumia pesa zako


kurudisha furaha yako. Utanunua nini ili usahau maumivu? Chipsi? Nyama Choma? Biriani? Pizza? Au ukienda kununua mwanamke anayejiuza ndo utaweza kumsahau yule aliyekutenda? Hapana! Vipo vitu vya kununulika na pesa lakini sio amani ya moyo. Licha ya kwamba Laureen alikuwa na pesa nyingi mkononi mwake lakini hakuwa na furaha kabisa. Zile pesa hazikuwa chochote kwenye moyo wake mbele ya Owen. "Wamenipa pesa ili nikubali


kwenda kuishi mbali na Owen? Mbona Nina pesa lakini bado sina furaha? Mbona bado nalia mimi Laureen? Hapana! Hapana kabisa! Mimi siwezi. Siwezi mimi kuishi bila Owen. Siwezi mimi kuwa mbali na Owen. Kiukweli kabisa, Mimi hapa nampenda sana Owen. Kwangu mimi, Kaka Owen ndo My me wangu jamani. Nawezaje kwenda mbali nae mimi.!" Hayo yalikuwa mawazo ya Laureen wakati yupo ndani ya Bus kuelekea Mwanza.


Baada ya kuwaza hivyo ndipo Laureen alipoamua kufanya maamuzi magumu ya kuteremka njiani na kupanda gari lingine la kumrudisha ndani ya jiji la Dar es salaam. Baada ya kurudi ndani ya jiji, aliamua kwenda kupanga chumba uswahilini kwenye mitaa ambayo aliamini kabisa isingekuwa rahisi kuonekana na wazazi wa Owen. Alipata chumba akalipia kodi, akanunua tandiko, vyombo na kiasi kidogo cha pesa kilichobaki mkononi mwake aliamua kufanyia mtaji wa biashara. Hakuwaza tena


kurudi kwenye biashara ya ukahaba kwa kuwa tayari alikuwa na pesa ya kujiajiri kwenye biashara halali. Zile fikra za watu kudhania kwamba kahaba ni kahaba kwa maana ya kwamba hawezi kubadilika hazikuwa na ukweli wowote kwani Laureen aliweza kubadilika na kuonesha jamii kwamba ukahaba sio tabia wala kabila kwamba hauwezi kuondoka kwenye mwili au damu ya mtu. Ni vile tu baadhi ya wanawake wanakosa nyenzo za uzalishaji ama ajira ndo maana wanajikuta wanadondokea


kwenye hiyo kazi. Laureen aliamua kutumia kiasi cha pesa kilichobaki mkononi mwake kufanya biashara. Alipata wazo la kuuza samaki wabichi mitaani. Kila siku alikuwa anatoka alfajiri na kwenda baharini kununua samaki kwa wavuvi kisha anarudi kuwauza majumbani. Hiyo ndo ilikuwa kazi mpya ya mtoto wa kike. Aliamua kutumia nguvu zake kutafuta fedha halali kwa jasho lake mwenyewe. Mtoto wa kike aliweka uzuri wake pembeni kisha akaweka ndoo ya samaki kichwani na ikawa kutwa kucha


ni kiguu na njia yeye na samaki, samaki na yeye. Siku zote hakuacha kabisa kumkumbuka Owen japo alishindwa kupata ujasiri wa kumtafuta. Alijua kabisa wapi angempata mwanaume huyo lakini kila alipokumbuka vitisho vya wazazi wa Owen kwamba asithubutu kuisogelea ile familia aliishia kulia tu. Ukweli ni kwamba mtoto wa kike alikuwa anampenda sana Owen. Mara nyingi wakati anazunguka mitaani kuuza samaki alikutana na wanaume wengi waliomtongoza na


kumtaka kimapenzi lakini mtoto wa kike hakuwa tayari kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine. Akili na moyo wake ulikuwa kwa mwanaume mmoja tu ambaye ni Owen. Ni dhahiri shahiri, Laureen hakuwa tena malaya wala kahaba. Tayari alishautoa sadaka mwili wake kwa mwanaume mmoja tu. NOVEL.................... MY VALENTINE- 26 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY


DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____ {UKIMALIZA SOMA TANGAZO HUKO CHINI ILI KUEPUSHA MASWALI}


Hiyo ilikuwa ni kumbukumbu fupi ya Laureen alipokuwa kule baharini anayatazama mawimbi ya bahari. Wakati yupo pale baharini, Laureen alikumbuka kwamba siku inayofuata ndo ilikuwa siku ambayo aliombwa na Owen afike ndani ya ukumbi ulioshereheshaga harusi ya Robyson. Laureen aliwaza sana kuhusu lile suala. Alijaribu kuweka kwenye mzani vile vitisho vya wazazi wa Owen dhidi ya penzi lake na Owen. Wakati anaendelea kuwaza, ghafla alitokea mwanaume mmoja


nyuma yake, "Sister, mzigo wako upo tayari ila leo utaniongezea ela kidogo maana nimekuwekea samaki wakubwa sana tofauti na siku zote.!" Hiyo ilikuwa sauti ya yule mwanaume aliyetokea nyuma kwa Laureen. Mwanaume huyo alikuwa mvuvi na siku zote ndo alikuwa anamuuzia Laureen samaki. Laureen aliwakagua wale samaki kisha akalipia pesa kama ilivyokuwa desturi yao. Baada ya


kulipia alianza safari ya kurudi mtaani ili akawauze wale samaki. Siku nzima Laureen alikuwa anaiwaza kesho tu na sio kitu kingine. Bado hakuwa na maamuzi sahihi kwamba aende au asiende kule ukumbini. *** Muhenga aliyesemaga usiku wa deni haukawii kukucha wala hakukosea kabisa. Watu walilala kidogo tu ile kuja kushtuka tu Februari 14 hii hapa. Hatimaye ile siku iliyokuwa inasubiriwa


iliwadia bwana. Sherehe iliandaliwa kama ilivyokuwa imepangwa. Mapema tu kuanzia majira ya saa kumi jioni wahusika tayari walishajaa ukumbini. Wafanyakazi wote wa kwenye ile kampuni ya Mr Jay Calvin akiwemo Diana walikuwa wameshawasili tayari. Lakini pia familia nzima ya Mr James iliruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi kwa kuwa kijana wao Owen alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na pia alikuwa na surprise kwa wazazi wake pamoja na ndugu, jamaa na


marafiki. Surprise hiyo ilikuwa ni kumtambulisha na kumvisha pete mchumba 'ake. Hata Robyson pia alikuwepo ndani ya ukumbi wa sherehe kuona jambo la mdogo wake. Ukiachana na Owen kuna mfanyakazi mwingine pia alikuwa anatarajia kumvisha pete mchumba 'ake hivyo familia yake pia ilikuwepo ndani ya ukumbi. Juliette pia alihudhuria ile sherehe huku akiwa na asilimia kadhaa za kuamini pengine yeye ndo angevishwa pete na Owen. Hata wazazi wa Owen walitega macho na


masikio yao kusikia Owen akilitaja jina la Juliette. Ukumbi ulipendezeshwa kwa rangi nyekundu kwa kuwa hiyo ndo ilikuwa rangi maalumu kwa ajili ya wapendanao. Kwa hakika siku hiyo watu walivaa na kupendeza kweli kweli. Wenye couple zao walivaa nguo za kufanana ilimradi tu kudhihirisha upendo wao. Pengine naweza kukiri kwamba Owen ndo binadamu ambaye alikuwa smart na kupendeza zaidi kuliko watu wote ndani ya ukumbi. Hakunaga nguo iliyowahi kukataa kwenye


mwili wa Owen. Muonekano wa Owen uliwafanya wadada kutamani kupata japo mtoto kutoka kwa Mr handsome. Hata Diana alijikuta anajuta kwanini aliachana na Owen na kuwa na Robyson. Kuna muda alikuwa haamini kabisa kama ilikuwa ni akili yake kumuacha Owen na kwenda kwa Robyson. Owen alikuwa kijana mtanashati alafu ni bonge moja la handsome. Tukio la kwanza kufanyika lilikuwa ni tukio la Birthday party ambapo Owen alikata keki na familia yake pamoja na marafiki


zake. Siku hiyo Owen alijikusanyia zawadi kede kede na zawadi kubwa zaidi ilikuwa ni gari jipya na la kisasa kabisa kutoka kwa mrembo Juliette. Zawadi ya Juliette iliwafanya watu wote pale ukumbini kukuna vichwa na kuamini kabisa Juliette ndo mpenzi wa Owen. Ile zawadi hata Owen ilimshtua kuliko kawaida. Alishauelewa vizuri moyo wa Juliette juu yake. Mtaalamu aliamini kabisa kwamba Juliette alikuwa kichaa na mwendawazimu kwa ajili yake. Lakini sasa bado moyo wa


Owen ulikuwa kwa Laureen ambaye mpaka kufikia muda hakuonekana kabisa pale ukumbini. Baada ya watu kumaliza kumpa Owen zawadi, sasa ilikuwa zamu ya Owen kutoa zawadi iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu. Owen alikabidhiwa maiki ili amuite jukwani kipenzi chake kwa ajili ya kumvisha pete ya uchumba. Hapo sasa ukumbi wote ulikuwa kimya kusubiri kusikia na kumuona mwanamke mwenye bahati zake. Owen aliangaza macho ukumbi mzima lakini


hakufanikiwa kabisa kumuona mwanamke aliyekuwa anampenda. Alitupa macho kwenye mlango mkuu wa ukumbi kutazama huenda angemuona Laureen wake akiinga lakini wapi, hakumuona kabisa Laureen. Alichokifanya ni kufumba macho kwa imani na kuanza kumuomba Mungu atende miujiza ili amletee mwanamke anayempenda kutoka moyo. Akiwa anaendelea kusali huku akiwa amefumba macho, Ghafla alisikia sauti ikimuita,


"OoooWEN.!" Ilikuwa sauti ya kike iliyoita jina lake. Kwa hakika sauti ile ilimshtua sana Owen kwani aliijua vyema kuliko sauti ya mtu yeyote yule. Ilikuwa ni sauti ya mwanamke anayempenda na kumthamini kuliko hata maisha yake. Owen alihisi labda zilikuwa fikra zake tu na mawenge yake. Mtaalamu hakufumbua macho mpaka aliposikia akiitwa kwa mara ya pili na sauti ile ile. Hapo sasa akafumbua macho na kutazama kule mlango ilipokuwa


inatokea ile sauti. Aisee, mwamba hakuamini macho yake. Alihisi pengine alikuwa ndotoni lakini haikuwa kama alivyohisi. Ni kweli kabisa Laureen ndo alikuwa mbele yake na alishaanza kupiga hatua kumfuata kule jukwani. Mr James na mkewe hakuamini macho yao kumuona Laureen pale ukumbini. Walitegemea kwamba muda ule angekuwa jijini Mwanza kwa kuwa walishamsafirisha. Hapo sasa wakajua sherehe inaenda kuingia mchanga. Walichokifanya ni


kutoa amri kwa walinzi wamtoe nje Laureen kwa kuwa ile sherehe ilikuwa haimuhusu kabisa. Walinzi walimsogelea Laureen na kutaka kumzuia ili asimfuate Owen kule jukwani lakini Owen akawaambia wasimguse kabisa Binti huyo. Ilibidi walinzi watii amri ya Owen kwa kuwa kwa wakati ule ndo alikuwa mwenye jambo lake pale ukumbini. Laureen alizidi kupiga hatua kumfuata Owen huku akitokwa na machozi kama mtoto. Hata Owen alishindwa kabisa kuzuia machozi ya furaha


yasitiririke mashavuni mwake. Hakuamini kabisa kama Laureen angefika pale ukumbini tena kwa wakati muafaka kabisa. "Ahsante Mungu ahsante.! Kwa hakika nimeona utukufu wako Baba. Nilikuamini nawe umeipokea imani yangu. Baba eeh! Huyu ndo mwanamke ninayempenda mimi. Naomba umlinde na kumtunza mwanamke huyu kwa ajili yangu mimi.!" Owen alijisemea peke yake maneno hayo huku akijiandaa kumpokea Laureen na


kumkumbatia. Baada ya kufika jukwani Owen alimkumbatia kwa nguvu Laureen huku akiendelea kutokwa na machozi ya furaha kwenye mboni zake. "Laureen.! Ulikuwa wapi wewe? Eti mama'angu, ulikuwa wapi siku zote hizo? Hivi unajua ni jinsi gani nilivyoku-miss wewe? Kiukweli kabisa mimi hapa mimi, nilikumiss sana wewe.! Mimi hapa mimi, nilihangaika sana kukutafuta wewe kipenzi


changu.! Mimi hapa mimi, nimekusubiri sana wewe.!" Owen alizungumza maneno hayo kwa hisia kali za mapenzi huku akiendelea kutokwa na machozi. "My me.! Pengine labda mimi hapa mimi, nimeshachelewa kuja hapa?" Laureen alimuuliza Owen swali hilo kwa madeko huku akitaka kujua kama tayari Owen alishamtambulisha mwanamke mwingine kuwa ndo mpenzi wake. "Hapana! Haujachelewa bado.!


Wewe hapo wewe, bado haujachelewa mamaa! Umekuja muda sahihi kabisa mpenzi wangu. Pengine labda wewe hapo..... wewe hapo.... naweza kukuuliza swali mbele ya hawa watu wanaotutazama?" Owen alimuuliza Laureen kwa staili fulani ya kubembeleza. "Ndio Babaa! Unaweza kuniuliza na nipo tayari kukujibu mbele ya umati wa watu wanaotutazama.!" Laureen alimjibu Owen kwa unyenyekevu wa hali ya juu.


Baada ya Laureen kujibu hivyo, Owen aliingiza mkono mfukoni na kutoa kiboksi kidogo chenye pete. Pale pale mwanaume alipiga goti moja chini kisha akamtazama Laureen na kusema, "Laureen.! By any chance, Will You Marry Me?" Owen alimuliza Laureen swali hilo akiomba kumchumbia na ikibidi amuoe. Swali hilo lilitingisha ubongo wa watu wote pale ukumbini. Kila mtu alihisi labda Owen alikuwa


anaigiza muvi. Swali la Owen lilimfanya Laureen ashindwe kuzuia machozi kwenye mboni za macho yake. Kwa hakika alimuona Owen kama malaika aliyetumwa kwa ajili ya kumheshimisha na kumpa thamani kwenye dunia yenye watu walimvua thamani yake. Aseme nini Laureen zaidi ya kumkubalia Owen ombi lake. Hiyo nguvu ya kumkataa mwanaume wa ndoto ya kila mwanamke angeitoa wapi? Angepata wapi ujasiri wa kumkataa mwanaume


aliyewakataa maelfu kwa mamia ya wanawake wenye elimu na pesa zao na kumchagua yeye mbumbumbu, kahaba na muuza samaki mtaani? Laureen alifumba tu macho akamshukuru Mungu kisha akamtazama Owen na kusema, "Yes, I will marry you Owen. Nipo tayari kuolewa na wewe Owen.!" Laureen alijibu kisha akanyosha mkono wake na kuvishwa pete na Owen kwenye kidole cha uchumba.


Ni Catherine na Sharon tu ndo walipiga makofi ukumbi mzima. Wengine wote walibaki midomo wazi huku wakiwa hawaamini kile kilichokuwa kinaendelea. Kila mtu alikuwa haamini kama Owen aliamua kumchumbia yule mwanamke kahaba na mwenye status ndogo ya maisha. Baada ya kumvisha pete Laureen, Owen alikamata mkono wa mtoto wa kike kisha akaubusu. Baada ya hapo aliinuka kisha akakamata maiki na kuongea, "Wazazi wangu, Ndugu zangu,


jamaa zangu, marafiki zangu na bila kuwasahau maadui zangu. Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru na kuwakumbusha kwamba hapa hatupo location kwa ajili ya kushuti kwahiyo hiki kinachoendelea hapa mbele sio muvi wala sinema. Hapa tupo kwenye ukumbi wa sherehe tunaadhimisha siku ya wapendanao duniani yani Valentine's Day. Kwahiyo basi huyu mwanamke munayemuona mbele yenu anaitwa Laureen, Huyu ndo mwanamke muliyekuwa munamsubiria


niwatambulishe, Huyu ndo mwanamke ninayempenda kutoka moyoni.! She is My... My... My Valentine.!" NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 27 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Maneno ya Owen yaliharibu na kumaliza kabisa sherehe kabla ya muda uliopangwa. Taratibu kabisa watu walianza kutoka


ndani ya ukumbi huku wa kwanza akiwa Mr James na mkewe. Yule mfanyakazi ambaye nae alitaka kumvisha pete mchumba 'ake hakufanikiwa katika jambo lake maana tayari watu walishaondoka ukumbini. Ile fumba macho na kufumbua pale ukumbini walibaki watu tano tu ambao ni Owen, Laureen, Catherine, Sharon na Juliette. Juliette alikuwa amekosa hata nguvu ya kutoka mule ndani maana tayari alishapigwa KO. Sharon na Catherine walipiga hatua kwenda kule jukwani


walipokuwa wenye valentine yao, Owen na Laureen. Walipofika tu walimkumbatia Laureen kwa upendo wa hali ya juu sana. Kiukweli kabisa walikuwa wanampenda Laureen na walifurahi sana kuona amevishwa pete ya uchumba na kaka yao. Wao walishamridhia na kumpitisha moja kwa moja kuwa wifi yao. Wakati Laureen amekumbatiana na mawifi zake yani Catherine na Sharon, Owen alibaki tu akitazamana na Juliette. Juliette alikuwa amekaa kwenye kiti huku akilia baada ya


kushuhudia mwanaume aliyekuwa anampenda amemvisha pete ya uchumba mwanamke mwingine. Owen alipiga hatua kumfuata Juliette kule alipokuwa amekaa. Alipomfikia alimshika bega kwa staili fulani ya kumfariji kisha akasema, "Juliette, naomba unisamehe sana my dear. Nisamehe sana kwa kushindwa kuzipokea hisia zako. Nimeshindwa kuzipokea hisia zako sio kwa sababu hauna uzuri au sifa za kunipendeza


mimi, Lahasha! Ni kwa sababu tu ulichelewa kuja kwenye maisha yangu. Wakati ulipoanza kunipenda nilikuwa tayari nina Laureen moyoni mwangu. Naomba unisamehe kwa hilo Juliette na pia bado nakuhitaji upande wangu. Nakuhitaji kama rafiki na natumaini utakuwa rafiki mwema kwangu. Naomba tu uvute subra Mungu atakuletea mwanaume mwenye sifa kama zangu na pengine atakuwa bora kuliko hata mimi. Wewe ni mwanamke mwenye uzuri na sifa zinazomvutia kila mwanaume.


Keep in hope because GOD is there for you.!" Owen alizungumza maneno hayo kumfariji Juliette aliyekuwa anatokwa machozi. "Owen.! Naomba ile funguo ya gari.!" Juliette alizungumza kauli hiyo kinyonge akitaka arudishiwe ile funguo ya gari aliyompatia Owen kama zawadi ya Birthday. Owen hakupata tabu kumrudishia Juliette ule ufunguo kwani hata yeye alipanga kurudisha. Hakutaka kabisa


kuchukua ile zawadi kwa sababu mtoaji alitoa huku akitarajia malipo ambayo yalikuwa nje ya uwezo wake. Owen alifurahi sana kuirudisha ile funguo mikononi mwa Juliette ili kujiweka huru zaidi. Baada ya kurudishiwa ufunguo wake, Juliette aliondoka pale ukumbini na kuwaacha Owen, Laureen, Catherine na Sharon. Ni kama vile Owen bado alikuwa haamini kama Laureen alikuwa mbele yake. Alimkumbatia na kum'busu mara nyingi zaidi huku akimwambia awe na roho ya kijasiri kuanzia


muda ule kwani maadui zao ni wengi sana. Kuendelea kuwa dhaifu ni kutengeneza mpasuko ndani ya penzi lao. "Catherine na Sharon, asanteni sana ndugu zangu kwa kuwa upande wangu siku zote. Nawashukuru sana kwa kuonesha upendo kwa wifi yenu Laureen tangu siku ya kwanza alipoingia ndani ya nyumba yetu. Nyie ni waelewa sana ndugu zangu ndo maana nilipowasimulia mkasa wa maisha halisi aliyopitia Laureen


muliguswa na kunisisitiza nimtafute na nimuoe kabisa. Nashukuru sana dada zangu kwa ushirikiano wenu. Japo nyie ni wadogo lakini najivunia sana uwepo wenu. Kila sehemu najiona sipo peke yangu. Ila kuna kitu kimoja cha mwisho nataka kuwaambia muda huu maana inawezekana tusipate tena nafasi ya kukaa pamoja na kuzungumza.!" "Kitu gani hiko kaka na kwanini tusipate tena muda wa kuzungumza?" Catherine


alimuuliza Owen "Ni hivi ndugu zangu, haijalishi ni kitu gani kitatokea nyumbani lakini naomba mutambue kuwa mimi ni kaka yenu na nawapenda sana sana. Na kama siku moja sitokuwa karibu na nyie basi endeleeni kuishi kwenye misingi ya kumpendeza Mungu, kuwatii wazazi na kuwa na hekima kwa kila mtu. Siku zote nilikuwa nawaambia pesa sio kitu mbele ya utu. Watu ndo mtaji ndugu zangu. Kamwe musidharau watu kisa mumewazidi kipato.


Nawaomba sana endeleeni kuishi kwenye misingi hiyo hiyo hata kama nisipokuwepo.!" Owen aliongea kauli hiyo akiwaasa ndugu zake. "Lakini kaka, mbona unaongea hivyo? Kwani unataka kutuacha na kwenda mbali na sisi?" Sharon alimuuliza Owen "Sharon, Tukifika nyumbani mutaelewa vizuri kitu ninachomaanisha. Kwanza ngoja nikuulize mdogo wangu, unakumbuka Ile slogan (kauli


mbiu) yetu?" "Ndio kaka naikumbuka.!" "Hebu nikumbushe na mimi.!" "Ni FOHAD.!" "Safi sanaa.! Niambie kirefu chake sasa.!" "Ni Focus, Hard-working & Discipline.!" "Ikiwa na maana gani?"


"Zingatia ufanyacho, Chapa kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu.!" "Safi sana mdogo wangu, Mu-focus kwenye mambo yenu sio ya wazazi au watu wengine, Fanyeni kazi zenu kwa bidii huko shuleni ili mupate mali zenu na mwisho kabisa muwe na mwisho kabisa heshimu watu wote bila kuzingatia umri na status zao za maisha. Sawa?" "Sawa kaka tumekuelewa na tunakuahidi siku zote tutaishi kwenye misingi hiyo na kufuata


nyayo zako.!" "Munaniahidi?" "Yeah! Tunakuahidi kaka.!" "Ok, Twendeni nyumbani sasa.!" Owen alimaliza kwa kuzungumza maneno hayo kisha wakatoka ndani ya ukumbi. Walipotoka ndani ya ukumbi walienda moja kwa moja walipopaki gari kisha wakapanda na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao. Baada ya


mwendo wa dakika kadhaa walifika nyumbani na huko sasa ndo kulikuwa na kizaa kisichoelezeka. Picha linaanza walipoingia tu ndani ya nyumba, pale sebuleni waliwakuta wazazi wao, Robyson pamoja na mke wa Robyson yani Diana wakiwa kwenye kikao cha dharura kilichokuwa kinamjadili Owen. Vile vile kwa pembeni kulikuwa na begi la nguo la Owen pamoja na vitu vyake vingine. Owen alishajuaga nini kinaenda kutokea hivyo haikumshtua kabisa. Ni Catherine na Sharon tu


ndo walishtuka kuona vile. Wazee walionekana kuwa na hasira zisizoelezeka kwa maneno juu ya Owen na Laureen. Kwanza kabisa Catherine na Sharon walianza kukaa kwenye viti na pindi tu Owen na Laureen walipotaka kuketi walizuiliwa. Walizuiliwa kukaa kwenye viti na kuambiwa kwamba hawakuwa na haki ya kukalia viti vya ile nyumba. Owen na Laureen walisimama na hapo ndipo Mr James alipoanza kutema nyongo kwa Owen.


"Owen, ongea na mama yako muda huu mwambie akutajie jina la Baba yako halisi ili ukamtafute huko mtaani na umpelekee huyo kahaba uliyemchagua. Kuanzia leo mimi sio baba yako Owen. I'm no longer your father kid. Ninachojua mimi wajibu wa mtoto kwa mzazi ni kusikiliza na kutii yale anayoambiwa na mzazi wake. Wewe umeshindwa kunisikiliza mimi kwa maana ya kwamba kuna Baba yako mwingine unayemsikiliza. Naomba uondoke nyumbani kwangu. Siwezi kukubaliana na


aibu na fedhea uliyonipa mbele za watu.!" Mr James alizungumza kauli hiyo kwa hasira "Owen! Nenda kwenye hospitali ya taifa ya muhimbili ukawaambie wakunga wakuoneshe mama yako halisi. Kwa aibu uliyotuletea kwenye familia yetu naomba tu niseme kuanzia muda huu, sina radhi na wewe. Siwezi kumpokea mkwe kahaba ndani ya nyumba yangu.!" Mama Owen nae aliongea kauli hiyo kisha akainuka na kupiga


hatua kumfuata Owen na Laureen pale walipokuwa wamesimama. Alipowafikia tu alivuta mkono kisha akampiga kibao Owen. Owen hakutaka kukwepa wala kumzuia mama yake kumpiga. Mama alimtandika Owen kofi lingine, Owen aliganda vile vile bila kutingishika. Alimruhusu mama yake ampige pengine angepoza machungu aliyokuwa nayo. Baada ya kumtandika Owen, Mama alimsogelea Laureen sasa. Kwa hasira alivuta


mkono ili atandike kofi lakini Owen akadaka mkono wa mama yake. "Mamaa eeh! Huyu mwanamke hana hatia yoyote katika hili. Mimi ndo mwenye hatia naomba unipige mimi. Nipige tu mimi lakini huyu mwanamke hana kosa lolote kwenu. Makosa ni yangu mimi na nimekubali kupokea adhabu yoyote kutoka kwenu.!" Owen alizungumza kauli hiyo kisha akaushusha chini mkono wa mama yake.


Mama alimtazama Laureen kwa hasira na uchungu kisha akamwambia, "Binti, nakuchukia sana. Nakuchukia mno wewe kahaba uliyeamua kuleta aibu na mpasuko ndani ya familia yangu. Naona kabisa umetumwa kuja kuharibu maisha ya kijana wangu na kumpa maradhi tu. Tangu lini kahaba akawa mkweli kwenye mahusiano? Tangu lini kahaba akaolewa na mtu mwenye akili zake timamu? Kiukweli kabisa nakuchukia mpaka siku


nitakayoingia kaburini.!" Mama Owen alizungumza maneno hayo kwa hasira na jazba kubwa sana. "Mamaa eeh! Lakini kwa sasa mimi sio kahaba. Ni kweli kabisa hapo awali nilikuwa mwanamke ninaejiuza kwenye danguro. Huo ndo ulikuwa uhalisia wa maisha yangu mimi. Ni changamoto tu za maisha ndo zilinifanya niwe katika kazi ile. Lakini kwa sasa, nimebadilika mimi. Mimi sio tena yule mwanamke anayejiuza kwa kila mwanaume. Kwa sasa mwanaume wangu mimi kwenye


hii dunia ni Owen tu mamaa. Ikiwa munaamini kwamba mpaka sasa bado najiuza basi tambueni ni Owen tu ndiye mwenye dau la kuweza kuninunua mimi. Kiukweli kabisa mimi hapa, nampenda sana mwanao. Nampenda sana na nakuahidi tu mama mkwe nitakuwa mke bora kwa mwanao. Naomba mutupàtie baraka zenu wazazi ili tuweze kuoana.!" Laureen alizungumza kauli hiyo huku akitokwa na machozi. "Mshenzi kabisa wewe.! Yani


mimi niwapatie baraka ya nyie kuoana? Hilo halitokuja kutokea kamwe.! Yani mimi nitoe idhini na baraka kwa mtoto niliyembeba tumboni mwangu miezi tisa amuoe kahaba. Tena naomba unyamaze tu Binti usizungumze chochote. Tangu lini kahaba akawa mke bora? Labda ni bora kwa wahuni wenzake. Wewe unataka kusambaza kirusi cha ukimwi kwenye familia yangu sio bure.!" Muda wote Owen alikuwa kimya tu akitunga sheria zake kichwani.


"Bwana mdogo, Mimi kama kaka yako nakusihi tu uombe msamaha kwa wazazi kisha achana na huyo mwanamke. Huyo mwanamke hakufai na hawezi kuwa bora kwako. Ogopa sana wanawake wa kuwaokota okota kwenye madanguro, kumbi za starehe na vigodoro. Kwanza kabisa wanaweza kukupa maradhi na pili wanakupenda kwa kufuata pesa zako. Wewe msomi nilitegemea utapata mke huko chuoni ulipokuwa unasoma au kazini unapofanyia kazi. Hebu


achana na wahuni wahuni hao hawanaga mapenzi ya kweli. Tafuta msomi mwenzako na mwenye pesa ili upate ndoa bora.!" Robyson alizungumza maneno hayo na kumgusa pabaya Owen. Ile kauli ilikuwa kama mkuki moyoni mwa Owen maana kama mwanamke mwenye pesa na msomi alishampataga alipokuwa chuoni Ila mwisho wa siku akasaliti penzi kisa masilahi binafsi. Kauli ya Robyson ilifanya macho ya Owen na Diana


kukutana katikati maana ni kama iliwagusa. "Braza Robby, Wakati unaninyooshea kidole mimi kuhusu Laureen, naona kuna vidole vitatu vinakutazama wewe. Inawezekana ni kweli wanawake wa kuwaokota okota mitaani hawana upendo wa dhati na wana sifa ya usaliti, Lakini je hao wasomi munaowaoa wana upendo wa dhati? Je munafahamu historia zao za mahusiano ya nyuma? Braza, Mimi sitaki kuzungumza sana ila


ipo siku utaelewa tu. Utaelewa kwamba pesa na elimu sio nembo ya mke ama mume bora.!" Owen alimwambia Robyson maneno hayo yenye fumbo ndani yake. "Owen.! Begi lako la nguo pamoja na vitu vyako ndo vile pale vinakusubiri. Kuanzia leo hii hautambuliki kabisa kwenye hii familia. Kila kilichopo mikononi mwako kilichonunuliwa kwa pesa zangu naomba ukiache hapa. Acha mezani funguo ya gari nenda ukaanze kugombania


daladala huko barabarani. Pesa ulizonikopesha juzi sikulipi na kuanzia muda huu hautakuwa na ruhusa ya kutoa pesa kwenye akaunti ya familia. Ni rasmi sasa jina lako nalifuta kwenye kitabu cha urithi wa mali zangu. Huyo mwanamke ndo Baba yako na yeye ndo mama yako kwahiyo nenda ukaishi nae huko mtaani.!" Mr James aliamua kumaliza maneno kwa mwanae Owen. "BABA! Usiseme hivyo.! Usiseme hivyo tafadhali. Kaka Owen ni mwanao na sisi bado


tunamtambua kama kaka yetu.!" Catherine alizungumza maneno hayo huku akilia. "Catherine.! Ukithubutu kuzungumza tena upumbuvu wako nitakunyoosha sasa hivi. Naomba ukae kimya kama haujasikia chochote kile. Au na wewe ukitaka ondoka tu. Siwezi kukaa na watoto wapumbavu na washenzi washenzi.!" Catherine alitaka kuzungumza tena lakini Owen akamzuia asiendelee kuongea. Catherine


alitulia kwa kuwa alikuwa anamuelewa sana Owen kuliko mtu yeyote yule. Owen hakuona sababu ya kuendelea kujielezea tena kwa wazazi wake juu ya mwanadada Laureen. Alishajua siku zote binadamu wanapenda kusikia kile wanachotaka kukisikia wao na sio kile unachotaka kuwaambia. Alichokifanya ni kukubaliana na kile walichokuwa wanakitaka wao muda ule. Aliwatazama ndugu zake Catherine na Sharon, akamtazama kaka yake Robyson kisha akawatazama wazazi wake


na kusema, "Wazazi wangu.! Nimekuwa na huzuni kubwa sana kutamka maneno haya lakini sina budi tu kuyatamka. Naomba niseme tu ahsanteni sana kwa kunizaa na kunilea mpaka hapa nilipofikia. Nashukuru sasa nimekua na hatimaye leo naondoka nyumbani na kwenda kuanza rasmi maisha yangu binafsi. Naondoka muda huu lakini sibebi fikra kwamba nimefukuzwa bali nabeba fikra za kwamba mumeniruhusu kwenda


kutengeneza maisha yangu kwa kuwa umri pia unaruhusu. Kila nitakapokuwa nasali basi nitaendelea kuwaombea dua kwa Mungu ili aendelee kuwatunza na kuwapa maisha marefu zaidi wazazi wangu. Haijalishi nini kimetokea lakini mimi na mke wangu mtarajiwa, Laureen bado tunawapenda na tutaendelea kuwapenda. Mamaa eeh, nadhani unajua ni jinsi gani mwanao ninavyokupenda mama'angu. Huko ninapoenda, nitaendelea kukukumbuka sana mama'angu. Nitatamani japo


kukuona tu lakini ndo hivyo haitawezekana. Catherine na Sharon, nawapenda sana ndugu zangu. Naomba siku zote muishi kwenye ile formula ya FOHAD. Brother Robyson, nawapenda sana wewe na shemeji yangu Diana. Ishini mukimpendeza Mungu ili ndoa yenu iwe imara na bora siku zote. Kama familia naomba tu munisamehe kwa kufanya chaguzi ambalo hamjalipenda. Imenilazimu kuchagua kuishi na mwanamke ninayempenda mimi na sio munayemtaka nyie kwa sababu


waoaji sio nyie bali ni mimi. Naelewa mwanamke wangu hamumpendi ila nina imani kwamba ipo siku mutampenda tu. Nitaendelea kusubiri kwa sababu muda ndo hakimu sahihi wa maisha yetu wanadamu.!" Owen alizungumza maneno hayo kwa hisia kali sana huku akitokwa machozi kwenye mboni zake. Kwa hakika maneno ya Owen yalikuwa mazito kwa kila mtu aliyepata kuyasikia. Ni Mr James na Robyson tu ndo


hawakudondosha machozi pale ndani. Catherine, Sharon, Diana, Laureen na hata Mama Owen alijikuta anatokwa na machozi mpaka kuumwa na tumbo la uzazi. Mama alijua ni ukweli usiopingika kwamba alikuwa anapendwa sana na mwanae Owen pengine kuliko hata watoto wote. Kama unavyojua mapenzi ya mtoto wa kiume kwa Mama yake yanavyokuwa. Baada ya kuzungumza maneno yale, Owen alitoa ufunguo wa gari kisha akauweka mezani.


Akawasogelea wazazi wake kwenye sofa walipokuwa wamekaa kisha akachuchumaa na kuwashika miguu ikiwa ni ishara ya kuchukua baraka zao. Baada ya kufanya hivyo alilifuata begi lake la matairi, akaanza kulikokota kisha akakamkamata Laureen mkono na wakaondoka zao. Watu wote walibaki wanawasindikiza kwa macho wapendanao wenye Valentine Day yao. NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu}


EPISODE: 28 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Hatimaye Owen alihama rasmi kwa wazazi na kwenda kuanza maisha yake na mwanamke ampendae. Aliondoka yeye tu na nguo zake na hakuchukua kitu chochote kwa wazazi wake. Alinyang'anywa mpaka gari alilokuwa analitumia kuendea kazini na kwenye matembezi yake. Na kwa bahati mbaya alikuwa na kiasi kidogo sana cha


pesa kwani siku mbili zilizopita alimkopeshaga Baba yake kiasi fulani cha pesa ndo kile alichoambiwa kwamba halipwi. Lengo la Mr James lilikuwa kuona Owen anaenda kufeli kimaisha kule aendako ili ajutie kwa kitendo alichokifanya cha kuwapinga wao wazazi. Wazazi walitamani kuona siku moja Owen anarudi na kuomba msamaha baada ya maisha kumpiga vilivyo. Waliamini kabisa jambo hilo ni lazima lingetokea tu kwa kuwa Laureen asingeweza kumsaidia chochote


Owen. Licha ya kwamba Owen alikuwa na kiasi kidogo cha pesa lakini hakuwa na wasiwasi kwani bado alikuwa na uhakika kila mwisho wa mwezi angepokea mshahara kule kazini. Baada ya Owen na Laureen kuondoka kule kwa wazazi, walienda moja kwa moja kwenye chumba alichokuwa anaishi Laureen. Ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Owen kuishi uswahilini kwenye nyumba zilizochoka choka kuanzia nje mpaka ndani. Chumba cha Laureen bado kilikuwa hakijatimia kabisa kwani


kulikuwa na vyombo vichache sana. Godoro lilitandikwa chini kwa kuwa hakukuwa na kitandani. Ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Owen kuishi maisha aliyokuwa anayaonaga kwenye televisheni na kuyasoma kwenye vitabu. Owen alishazoea kiyoyozi nyumbani kwao lakini kwa mara ya kwanza alijikuta analala kwenye chumba chenye joto kali. Licha ya kwamba chumba kilikuwa na umeme lakini hakukuwa na feni ndani hivyo ilikuwa vigumu sana kwao kuepuka joto. Laureen


alishayazoea vyema yale maisha hivyo alijikuta tu anamuhurumia Owen kwa tabu alizokuwa anazipata pale chumbani. Muda wote mtoto wa kike alikuwa anamuomba msamaha Owen kwa kuwa yeye ndo alikuwa chanzo cha mwanaume kupitia yale mateso. "My me, naomba unisamehe mimi. Nisamehe sana kwa kukufanya uje kuishi maisha haya. Najua haya sio maisha unayostahili kuishi Babaa. Mateso yote unayopitia kwa sasa


ni kwa ajili yangu mimi tu. Nisamehe mimi Babaa.!" "Laureen, naomba usithubutu tena kuzungumza maneno hayo. Naomba... naomba... naomba.. usidiriki kuzungumza tena hayo maneno. Nilipokuambia nakupenda na nipo tayari kuishi na wewe kwenye maisha yoyote nilikuwa namaanisha hata porini naweza kuishi ilimradi tu uwe pembeni yangu. Haya maisha nimeyachagua mwenyewe nikiwa na akili zangu timamu kupitia upendo wangu kwako. Naomba


usijipe mzigo wa lawama usiostahili kuubeba. Mimi na wewe hakuna anayestahili kulaumiwa kwa kuwa njia tuliyoichagua ni sahihi.!" "Ni sawa Baba lakini mwenzako najikuta tu nakuhurumia. Haya maisha hukuyazoea kabisa.!" "Laureen, Kumbuka kwamba haya ni maisha ambayo Mungu amewaumbia wanaadamu na mimi pia ni miongoni mwa hao wanaadamu. Kwa sasa tunachotakiwa kufanya ni


kukubali uhalisia wa maisha tuliyonayo kisha tupange mikakati ya kuyaboresha. Haya ni maisha ya mpito tu Laureen. Tukipambana tutafika kule kule juu walipokuwa wao. Kwanza kabisa tunatakiwa tuishi kwa imani moja ya upendo Laureen wangu. Kuanzia muda huu tunatakiwa kuishi kama mume na mke na tuanze kutengeneza maisha kwa pamoja. Mkakati wangu wa kwanza kwako ni kukutafutia chuo ili ukatimize ndoto zako za kuwa Daktari. Utaanzia ngazi ya Diploma kwa


kutumia yale matokeo yako ya kidato cha nne. Baada ya hapo utaendelea na ngazi zinazofuata mpaka ufikie kule unapostahili kufika. Nina imani na kichwa chako Laureen wangu. Najua kabisa huwezi kuchezea hii nafasi. Hii ndo njia pekee ya kutengeneza status kubwa kama wale wanaokudharau. Kesho nitakuachia simu yangu utaingia mtandaoni kutafuta chuo kizuri kinachotoa kozi za afya kwa ngazi ya Diploma. Nikishapokea mshahara wangu mwisho wa mwezi nitakulipia ada ya chuo.!"


"My me, Ahsante sana kwa kukumbuka na kufufua ndoto zangu mimi. Nakuahidi tu mume wangu nitasoma kwa bidii mpaka kufikia malengo yangu. Hiyo nafasi kamwe sitoichezea babaa.!" Hayo yalikuwa mazungumzo kati ya Owen na Laureen katika usiku wao wa kwanza kabisa kuishi kama mume na mke. Asubuhi Ilipofika Owen alijiandaa kwenda kazini. Kabla hajatoka alimuachia Laureen kadi yake ya


benki na kumtaka atoe kiasi chote cha pesa kilichokuwa kimebaki kisha anunue kitanda, feni na baadhi ya vyombo vya ndani. Pesa itakayobaki waitumie kama akiba. Baada ya hapo Owen alimuaga Laureen kwa kum'busu kwenye paji la uso kisha akaondoka. Kwa hakika ndani ya zile siku mbili kila kitu kilikuwa kigeni kwa Owen. Kwa mara ya kwanza kabisa mtaalamu alijikuta anapanda daladala kwenda kazini na alikuwa hajui hata nauli ni shilingi ngapi kutoka kituo kimoja


kwenda kituo kingine. Baada mwendo wa dakika kadhaa alifanikiwa kufika kazini japo alichelewa kidogo kutokana na foleni. Alipofika tu kazini alienda kwa sekretari kusaini kama ilivyokuwa desturi yao siku zote. Alipofika kwa sekretari alivuta daftari ili asaini lakini alizuiliwa. "Mr Owen, Boss amesema ukifika tu nenda ofisi kwake kabla hujasaini.!" Sekretari alimwambia Owen kauli hiyo. Kauli ya Sekretari ilimshtua na


kumshangaza Owen kwani hakukuwa na mahusiano kati ya kusaini na wito wa Boss. Mtaalamu alianza kuhisi hali ya hatari. "Boss gani anaenihitaji?" Owen alimuuliza sekretari. "Madam Jay ndo anakuhitaji.!" Sekretari alimjibu Owen huku akimtazama kwa nyodo na dharau. Owen alishangaa sana kuona anahitajika kwenye ofisi ya


Meneja mwajiri. Huyo Madam Jay mwenyewe ndo Diana na hilo ndo lilikuwa jina alilokuwa anatumia pale kazini kwa kuwa Baba yake alikuwa anaitwa Mr Jay Calvin. Owen aliamua kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Meneja mwajiri kuitikia wito. Alipofika alimkuta Diana amekasirika kuliko kawaida yake. Owen alimsalimia Diana lakini salamu yake haikuitikiwa. Mtaalamu hakuona sababu ya kulazimisha salamu, alichokifanya ni kwenda kwenye point kuu iliyompeleka pale.


"Boss, nimeambiwa na Sekretari nije kukuona kabla sijasaini. Nimekuja kuitikia wito wako Madam.!" Owen alizungumza kauli hiyo kwa unyenyekevu wa hali ya juu. "Shika hii barau, soma utaelewa.!" Diana alizungumza kauli hiyo huku akimpatia Owen karatasi fulani. Owen alipokea ile karatasi kisha akaanza kuisoma taratibu kabisa huku kijasho chembamba


kikianza kumtoka kwenye paji la uso. Barua ile ilikuwa na dhumuni la kuvunja rasmi mahusiano yaliyopo kati ya Owen na ile kampuni. Kiufupi ni kwamba Owen alipewa barua ya kuachishwa kazi. "Boss.! Nimeshamaliza kusoma na nimeelewa dhumuni la barua. Lakini sasa bado sijaona sababu iliyofanya ni nifukuzwe kazi. Hivi kosa langu ni lipi haswa Boss?" "Owen, Nina mambo mengi ya kufanya muda huu hivyo nenda


kakabidhi ofisi kwa mfanyakazi atakaekaimu nafasi yako.!" "Diana.! Kwahiyo hii yote ni kwa sababu ya Laureen?" Owen alimuuliza Diana. "Owen, nimesema sina muda wa kukujibu maswali yako. Naomba uondoke kabla sijakuitia walinzi maana unaniletea fujo ofisini kwangu. Wewe si unajifanya Gentleman? Nenda sasa huko mtaani ukapambane na maisha kwa ajili ya kikahaba chako.!" Laureen aliongea kwa hasira kali.


"Mimi nitaondoka Diana lakini naomba tu unijibu swali langu moja tu. Hivi umeamua kunifanyia hivi kwa shinikizo la wazazi wangu au ni maamuzi yako mwenyewe?" Owen alimuuliza Diana kwa upole kabisa. "Unataka nikujibu sio? Ok haya ni maamuzi yangu binafsi kukufukuza kazi. Nenda sasa ukaoneshe ukidume wako huko mtaani. Nenda kachukue vyeti vyako ukaanze kuhangaika navyo


kwenye ofisi za watu. Si unahisi maisha ni rahisi ndo maana umejikabidhi mzigo usiokuwa na ulazima, haya sasa kampambanie mkeo.!" "Diana, Kumbe hata wewe unanichukia kiasi hiko? Hivi ni kitu gani kibaya nilichowahi kukufanyia Diana? Hebu niambie Diana, ni kitu gani kibaya nilichowahi kukifanya kwako kuanzia kipindi tulichokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mpaka kufika kwenye ushemeji. Hivi Diana, umesahau kabisa ule


upendo niliokuwa nauonesha kwako? Umesahau kabisa zile siku nilizokuwa nakufanya ufurahi? Umesahau kabisa zile siku nilizokuwa nakosa vipindi darasani kwa ajili ya kukuuguza ulipokuwa mgonjwa? Licha ya kukupenda, mbona nilikuwa na huruma na wewe Diana? Mbona wewe hauna huruma na mimi Diana? Hivi kwanini hutaki mimi nifurahi? Diana, uliniacha katika kipindi ambacho ulijua kabisa bado nakuhitaji lakini hukujali kuhusu machozi yangu. Yale maumivu uliyonipaga unaona


hayatoshi kwahiyo unaamua kupiga kampeni za kuniharibia furaha niliyonayo kwa sasa. Kwanini lakini unafanya hivyo Diana? Mbona mimi sikukuacha ila ni wewe mwenyewe ndo uliamua kuondoka na kwenda kuolewa. Wivu unatoka wapi sasa wakati tayari una ndoa yako? Anyway, Kama shida na matatizo yangu yanakupa furaha basi ongeza juhudi kwenye kampeni zako za kuniharibia. Naomba tu nikushukuru kwa kipindi chote tulichofanya kazi pamoja kwenye kampuni hii.


Nawatakia kila la kheri katika utendaji wa kazi na uzalishaji wa huduma bora katika nchi.!" Owen alizungumza kauli hiyo kisha akaanza kupiga hatua kuondoka kwenye ofisi ya Diana. Maneno ya Owen yalimgusa sana Diana mpaka akahisi maumivu ndani ya moyo. Alijikuta tu anakumbuka yale maisha waliyoishi kule Marekani walipokuwa masomoni. Alikumbuka upendo wa dhati wa Owen kwenye zile siku alizokuwa anaumwaga. Mtoto wa kike


alikuwa anadekezwa kwa kulishwa chakula na kunyweshwa mpaka uji. Ni kweli kabisa licha ya upendo lakini pia Owen alikuwa anamuhurumia sana kila alipokuwa anapitia vipindi vigumu hasa hasa vipindi vya homa. Diana alijikuta anasutwa na nafsi yake mwenyewe kwa kumtakia mabaya mtu ambaye alikuwa anaumia kwa ajili yake kwenye nyakati ngumu alizokuwa anapitia. "Owen Baba.! Hata mimi naumia


sana kuona nakuchukia jamani. Hizi chuki nashindwa kuzuia kila ninapokumbuka kwamba unapambana kwa ajili ya kumfurahisha mwanamke mwingine. Kiukweli kabisa sijui kwanini napata wivu kwako wakati tayari nimeshaolewa na mbaya zaidi aliyenioa ni kaka yako.!" Diana alijisemea moyoni kauli hiyo huku akimsindikiza Owen kwa macho. Owen alianza rasmi safari ya kurudi kwa mke wake Laureen huku akiwa amepoteza ile kazi


iliyokuwa inampa nguvu na matumaini ya kuendesha maisha na kutaka kumpeleka shule Laureen. Wahenga wanasema, wakati sahihi wa kujua upendo halisi wa mume ni pale tu mke anapokuwa mgonjwa. Na wakati sahihi wa kujua upendo halisi wa mke ni pale tu, mume anapopoteza kazi. NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 29 AUTHOR: HERRY DESOUZER


(Silentkiller) Owen alirudi kwenye chumba alichokuwa anaishi na kumkuta Laureen anaosha vyombo. Kwa hakika Laureen alishtuka sana baada ya kumuona Owen amerudi asubuhi ile tena akiwa mnyonge kuliko kawaida. Tayari alishajua kulikuwa na tatizo kubwa sana kwa mwanaume wake. Owen hakuzungumza kitu badala yake aliingia chumbani kwao moja kwa moja. Ilibidi mtoto wa kike aache shughuli ya kuosha vyombo kisha akamfuata


Baba watoto ndani ili ajue kipi kinamsibu. "Owen Mme wangu, mbona umerudi mapema na umekuwa mnyonge hivyo? Nini tatizo babaa?" Laureen alimuuliza Owen kwa unyenyekevu huku akimpapasa papasa begani. Owen aliwaza namna ya kumjibu Laureen ilimradi tu asivunjike moyo na kuumizwa na ile taarifa. "Unajua nini wife, kule kazini hali si shwari.!"


"Kivipi tena Baba?" "Yani ni kwamba mimi hapa kule kazini... kule kazini... nimefukuzwa kazi. Lakini usijali nitatafuta kazi nyingine maana mimi ni mtoto wa mjini na nina connection nyingi za kazi.!" "Dah! Pole sana Babaa.! Hili suala nilishaliona kabla hata hujatoka kwenda kazini. Nilishajua hili linaweza kutokea kwako na hiyo yote ni kwa sababu yangu mimi. Lakini


nakuomba sana baba, haijalishi tutapitia changamoto kiasi gani lakini naomba usinichukie mimi. Hii ni mipango tu ya watu kwa ajili ya kututenganisha sisi. Owen, naomba usiniache tafadhali kwani nakupenda sana mwenzako. Nipo tayari kuishi na wewe kwenye mazingira yoyote yale Baba.!" Laureen aliongea kauli hiyo huku akitokwa na machozi. "Laureen mke wangu, 'Sio kila unachokipoteza ni hasara.' Je unaikumbuka hiyo kauli?" Owen


alimuuliza Laureen. "Ndio Baba naikumbuka vizuri kwa sababu mimi ndo nilikuambiaga hiyo kauli.!" Laureen alimjibu Owen. "Basi tuweke imani zetu kwenye hiyo kauli mamaa.! Mimi naamini nimepoteza kazi lakini sijapata hasara kwa sababu kuna kitu kikubwa zaidi Mungu ameniandalia. Wao wanahisi wamenikomoa kwa kunifukuza kazi lakini wamesahau kwamba bado nina taaluma na ujuzi


mkubwa wa kufanya kazi sehemu yoyote ile. Naomba tuwe na subra tu mke wangu, kila kitu kitakuwa sawa. Nitapata kazi na yale malengo ya kukupeleka chuo yatatimia.!" "Sawa Babaa nimekuelewa mimi. Kamwe tusiyumbishwe na vitendo vya wanadamu kwani kwenye hii dunia mkubwa ni Mungu tu hivyo hili suala tulikabidhi mikononi mwake yeye. Kila siku nitasali na kukuombea mume wangu ili upate kile unachostahili. Hizi


changamoto za wanadamu ni kama ngazi tu kuelekea kilele cha mafanikio. Siku zote ili ing'ae basi ni lazima giza litande. Nina imani kabisa Mungu wetu ni mwema na atakuwa pamoja nasi Babaa.!" Hayo yalikuwa mazungumzo kati ya Owen na Laureen kuhusiana na sakata la Owen kufukuzwa kazi. Hivyo ndivyo Laureen alivyolipokea lile suala. Akiwa kama Baba mpya wa familia, Owen hakutaka tena kupoteza muda. Siku ile aliandaa vyeti


vyake vya taaluma pamoja na CV zake kwa ajili ya kuanza mchakato wa kutafuta ajira. Alianza kutuma maombi kwenye tovuti mbalimbali za ajira mtandaoni. Alituma maombi ya kazi kwenye taasisi nyingi nyingi tu huku akiamini angepata nafasi kwenye moja kati ya hizo taasisi. Lakini pia hakuishia hapo tu, siku iliyofuata aliondoka asubuhi na mapema akiwa na bahasha yenye vyeti vyake na kuingia kwenye makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuomba kazi. Ilibidi afanye hivyo kwani aliamini fursa


hazimfuati mtu nyumbani badala yake zinatafutwa. Siku nzima mtaalamu alitembea kwa miguu huku akiingia kwenye makampuni mbalimbali ya kazi kujaribu bahati yake. Lakini sasa, kila alipoenda alikosa nafasi. Waajiri walimwambia hakukuwa na nafasi za kazi na wengine walimpa tu matumaini kwamba kama kampuni itahitaji wafanyakazi hapo baadae basi atapigiwa simu. Owen hakukata tamaa kabisa kwani alitumia takribani mwezi mmoja kutafuta ajira lakini hakufanikiwa kabisa


kupata. Alituma barua kwenye kampuni mbalimbali lakini barua zake hazikujibiwa. Ilifikia hatua alikosa mpaka nafasi za kufanya kazi kwa kujitolea. Siku moja katika pita pita zake maofisi alikutana na Mwajiri ambaye alimpa matumaini kidogo. Alimsifia Owen kwa kuwa na vyeti vizuri vya taaluma hivyo akamtaka siku inayofuata aende kwenye ile kampuni kwa ajili ya kumfanyia interview na kama angefaulu basi angeajiriwa kabisa. Yule mwajiri alikuwa ni mwanamama mtu mzima


mwenye makamo yanayolingana na mama yake Owen. Kwa mara ya kwanza kabisa Owen alijikuta anafurahi na kupata matumaini kwani alikuwa anajiamini asingeweza kufeli kwenye interview. Taarifa ile Owen alimfikishia Laureen na Laureen alionekana kupata matumaini kwa kiasi fulani. Mtoto wa kike alimuombea sana Owen afanikiwe katika ile interview na apate kazi. Kulikuwa na kila sababu ya kumuombea Owen apate kazi maana tayari hali ya maisha ilishaanza kuwa mbaya


pale ndani. Mume hakuwa na kazi na mke alisitishwa kwa muda kufanya ile biashara yake ya kuuza samaki mtaani. Siku iliyofuata Owen aliamka mapema kwa ajili ya kwenda kwenye interview kama alivyokuwa ameambiwa. Laureen alimuandaa mume wake na kumtakia kila la kheri katika interview yake. Wote kwa pamoja walikuwa na imani kila kitu kingekuwa sawa siku hiyo. Owen aliondoka na kuwasili kwenye ile kampuni ndani ya muda maalumu uliopangwa. Alipofika


tu aliingia moja kwa moja kwenye ofisi ya Meneja mwajiri. Meneja mwajiri alipomuona tu Owen alimkaribisha huku akitabasamu. Owen alikaa kwenye kiti kisha akamsalimia yule mwanamke kwa kumwamkia kwa kuwa umri wake ulikuwa mkubwa. Cha ajabu ni kwamba yule mama hakutaka shikamoo ya Owen. Owen alishangaa kidogo lakini hakutaka kulijadili hilo kwa kuwa sicho kilichompeleka. "Sasa kijana wangu, nilipitia


vyema CV zako na nimeona zipo vizuri sana. Lakini pia nataka kukuambia kwamba kampuni yetu ina nafasi moja tu na mpaka sasa tumepokea maombi kutoka kwa watu takribani hamsini ukiwemo wewe. Kati ya hao watu hamsini, kuna watu wengi sana wana CV na ma-GPA makubwa kukuzidi wewe. Lakini sasa hii nafasi nataka nikupe wewe kwa upendeleo tena bila kukufanyia interview. Nimekuchagua wewe kwa sababu kuna kitu kimoja tu nimekipenda kutoka kwako.!" Mwajiri alizungumza kauli hiyo


na kumfanya Owen ashtuke kidogo. "Madam, Ni kitu gani hiko umekipenda kutoka kwangu?" Owen alimuuliza yule Meneja mwajiri. Meneja mwajiri aliinuka kwenye kiti chake na kumsogelea Owen kwenye kiti alichokuwa amekaa. Alipomfikia akaanza kumzunguka kisha akamshika shavuni na kuteremsha mkono mpaka kidevuni.


"Unajua nini Owen, wewe ni Gentleman na handsome boy kweli kweli. Tangu jana nilipokuona nimejikuta nakupenda wewe mtoto. Nataka uwe boy wangu unipe raha mimi. Endapo utakubali kuwa boy wangu basi nitakupa nafasi ya kazi na nitakuwa tayari kukufanyia chochote utakachotaka kwa pesa zangu mwenyewe.!" Yule Meneja alizungumza kauli hiyo huku akiendelea kumchezea kidevu Owen.


Owen alibaki ameganda kwa mshangao mkubwa huku akiwa haamini kile alichokuwa anakisikia. Kwa umri na wadhifa wa yule Meneja hakutakiwa kabisa kujidhalilisha kwa kijana mwenye makamo ya wanae aliowaacha nyumbani kwake. Owen aliwaza na kuwazua juu ya lile tukio lililokuwa linaendelea pale ofisini. Aliwaza ni maamuzi gani yangekuwa sahihi juu ya kauli ya yule Meneja. Kiukweli kabisa kazi alikuwa anaitaka kwani tayari hali ya maisha ilishakuwa mbaya kwake yeye na


mkewe Laureen. Lakini sasa, kumkubalia yule mama ilikuwa ni sawa na kumsaliti Laureen, kuvunja heshima kwa akina mama wote dunia pamoja na kujitafutia matatizo ya kiafya. Wakati Owen anaendelea kuwaza, Yule Meneja aliinamisha kichwa chake taratibu kabisa na kuanza kumpelekea mdomo Owen ili ampige busu. Owen aliganda huku akimtazama yule mama ambaye tayari alishazikaribia lipsi zake ili apate denda.!


NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 30 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Kabla yule Meneja hajazigusa lipsi za Owen, Owen alikwepesha mdomo wake kwa kugeuza shingo. Pale pale Owen aliinuka kwa hasira kwenye kiti. "Kwahiyo hutaki kazi sio?" Meneja alimuuliza Owen kwa hasira


"Kazi nataka lakini sipo tayari ku-date na wewe Madam. Wewe ni sawa na mama yangu kiumri hivyo sipo tayari kufanya hiko unachokitaka wewe.!" Owen alimjibu yule Meneja. "Ha ha ha! Naona una nyota ya umaskini sana kijana wangu. Yani mimi nakupa kazi na utamu kama kifungashio lakini wewe hutaki. Kwahiyo unataka nikusaidiaje sasa? Hivi unadhani kazi zinapatikana kirahisi rahisi sana? Ok, rudi


nyumbani kwenu ukanyonye mtoto mzuri. Hii nafasi wataichukua vijana wenzako wanaojua kula mashangazi.!" Meneja aliongea kauli hiyo kwa dharau. Owen hakuona sababu ya kuendelea kubaki pale ofisini. Aliamua kuondoka bila kuzungumza neno lolote. Tukio lile lilimfanya Owen awaze njia nzima. Sasa Owen ndo aligundua kwanini nchi imekuwa na changamoto kubwa kwenye sekta mbalimbali za uzalishaji


wa huduma kwa jamii. Kumbe changamoto zinatokana na ukosefu wa watu sahihi kwenye hizo sekta. Viongozi wa taasisi wanawaajiri watu kwa kuangalia undugu, ujamaa na rushwa. Rushwa ya ngono imekuwa ikitumika sana kama nyezo ya kupatia ajira. Uzuri, urembo na shepu ni vitu vinavyotumika kumpa mtu ajira mtu kuliko hata ujuzi na taaluma yake aliyosomea kwa miaka mingi. Mwisho wa siku taasisi zinawaacha watu sahihi wenye uwezo wa kufanya kazi kwa


ufanisi hivyo uzalishaji wa huduma bora kwenye jamii unakuwa changamoto. Hii ni kwa sababu taasisi zinakuwa zimeajiri wataalamu wasiokuwa na vigezo (Non qualified experts). Ubongo wa Owen ulifunguka na kujua sababu ya wasomi wengi kulalamika kukosa ajira licha ya kuwa na CV pamoja na GPA za juu kwenye vyeti vyao vya taaluma. Kwa mara ya pili tena Owen alirudi kwao kinyonge sana baada ya kushindwa masharti ya interview. Hakumficha jambo lolote


Laureen hivyo alimueleza kila kitu kilichotokea kule alipokwenda. Laureen alimfariji Owen na kumtaka asikate tamaa wala kuvunjika moyo ipo siku angepata tu kazi anayostahili. Kwa wakati ule ilibidi sasa Owen ajaribu kuangalia fursa zingine tofauti na zile za kwenye makampuni. Mwanaume aliamua kufungia kabatini vyeti vyake vya taaluma na kuamua kuingia mtaani kutafuta ridhiki kwa kutumia nguvu alizonazo. Alijua kabisa kama ataendelea kuhangaika na kazi za kwenye


makampuni basi maisha yangemuendea kombo. Mpaka kufikia muda ule hali ilishaanza kuwa tete upande wao. Huo mchango wa umeme tu ulishaanza kuwa changamoto upande wao. Tayari walishaanza kugombana na wapangaji wenzao kwa kushindwa kununua umeme kwa wakati. Sio siri maisha ya Owen na Laureen yalikuwa magumu kiasi kwamba hata baadhi ya wapangaji walikuwa wanawaonea huruma na wengine kuwacheka kabisa. Ni vile tu hawakujua Owen


ametoka kwenye familia ya aina gani ila laiti kama wangejua basi wasingemcheka. Ni rasmi sasa Owen alianza kuzurura kwenye machimbo ya kazi ili aweze kufanya kazi yoyote ilimradi tu apate pesa ya kujikimu na maisha. Takribani siku tatu alizurura bila kupata dili lolote la pesa. Laureen alimuomba Owen amruhusu arudi tena kwenye biashara yake ya kuuza samaki mtaani ili wapate chochote cha kusukuma familia. Ilibidi tu Owen akubali kumruhusu Laureen afanye ile biashara. Kulikuwa na


kiasi kidogo cha pesa kilichokuwa kimebaki kwenye akiba yao hivyo Laureen alikitumia kama mtaji. Kila siku asubuhi alikuwa anaenda baharini kununua samaki kwa wavuvi na kurudi nao mtaani kuwaauza. Owen yeye bado hakukata tamaa kwenda mtaani kutafuta madili ya pesa. Baada ya kusota kwa siku kadhaa, hatimaye alipata chimbo la kazi. Alipata kazi ya kuosha magari kwenye eneo moja maarufu kwa ajili ya shughuli hiyo. Mwanaume alianza kufanya kazi hapo kwa


kushirikiana na wenzake aliowakuta na kumkaribisha. Owen alifanya kazi bila kujali status ya maisha aliyokuwa nayo hapo awali wala elimu yake. Hakumwambia mtu yeyote kuwa yeye ni mtoto wa kiongozi fulani wa siasa wala hakutaja elimu yake. Kwa mara ya kwanza kabisa msomi wa shahada ya uzamili (Master's degree) na mtoto wa kiongozi mkubwa serikalini aliajiriwa kuosha magari ya watu. Owen aliishi vizuri na vijana wenzake pale kijiweni na taratibu kabisa


alianza kuyazoea yale maisha. Licha ya kwamba malipo yalikuwa madogo lakini afueni ilipatikana kidogo kwa kuwa ridhiki ilikuwa inapatikana. Haba ya Owen na haba ya Laureen ilijaza kibaba cha familia. Kiukweli kabisa Owen na Laureen waliridhika na maisha yao na kadri siku zilivyozidi kusonga ndivyo walivyozidi kupendana. Lakini sasa, changamoto mpya iliibuka tena katikati ya furaha yao. Laureen alianza kuugua na kupelekea kushindwa kwenda kwenye biashara yake. Ilibidi


sasa Owen awajibike kufanya shughuli zote za ndani, kumuuguza mwanamke wake na kwenda kibaruani kutafuta ridhiki. Kila siku Owen alikuwa anaamka mapema na kumwandalia mgonjwa wake chakula kisha akawa anaenda kijiweni kwake kuosha magari ili familia isikose tonge. Siku moja Owen akiwa kwenye kijiwe chake cha kazi, lilikuja gari moja la kifahari Kwa ajili ya kuoshwa. Owen alilisogelea lile gari kwa ajili ya kuliosha. Alichukua vifaa vya kazi ili aanze kuosha lile gari


lakini ghafla aliganda kama barafu. Aliganda punde tu kioo cha gari kilipofunguliwa. Ilikuwa ni uso kwa uso kati ya Owen, Robyson na Diana. Ndani ya lile gari kulikuwa na Robyson na Diana. Owen aliwasalimia lakini salamu yake haikuitikiwa badala yake walimshangaa tu. Owen hakutaka kuwajadili sana badala yake alifanya kazi yake kuosha lile gari huku akijisikia aibu kwa kiasi fulani. Kwa namna Owen alivyokuwa amebadilika, Diana alijikuta anaumia na kujiona mkosaji kwa kitendo cha


kumfukuza kazi Owen. Alijikuta tu anapata maumivu ya tumbo baada ya kumuona Owen akiwa katika hali ile. Na wakati huo tumbo la Diana lilishaanza kuwa kubwa kwani tayari miezi kadhaa ilishapita tangu alipopata ule ujauzito. Kwa hakika Owen alichakaa na kupauka kweli kweli. Alibaki tu anaonekana ni handsome kwa mbali lakini ule utanashati wote ulishapotea. Diana alikosa ujasiri wa kuendelea kumtazama Owen Ila Robyson aliendelea kumtazama mdogo wake akiwa anawaoshea


gari. Baada ya dakika kadhaa Owen alimaliza kazi yake. Alisogea dirishani kudai malipo kwa kazi yake. Robyson alimtazama Diana na kumwambia amlipe pesa Owen. Diana alitoa noti tatu za shilingi elfu kumi kisha akampatia Owen. Owen alipokea kisha akaichukua noti moja akaiweka mfukoni alafu zile mbili akawarudishia na kuwambia ile noti moja ndo halali kwa jasho alilotumia. Hakutaka huruma wala msaada wa mtu. Owen alitoka na kuwaacha wapendanao


wakimtazama. Robyson hakuongea kitu badala yake aliwasha gari na kuondoka huku akiwa na hasira. Tangu dakika zile Owen alijikuta anakosa amani ndani ya moyo. Alijua kabisa kitendo cha Robyson na Diana kugundua mahala anapofanyia kazi ni hatari sana upande wake. Alihisi kuna jambo baya litatokea upande wake. Ni kweli kabisa vile alivyohisi ndivyo ilivyokuwa. Siku iliyofuata wakati anafika tu kwenye kijiwe chake kuna gari nalo lilikuwa linatoka. Alipoangalia vizuri lile gari alilijua


vyema sana. Lilikuwa gari alilokuwa anatumia yeye kabla hajahama kwa wazazi. Owen alitupa macho kwenye kioo cha dirisha akaona kipara cha Baba yake wakati huo kioo cha gari kilikuwa kinamalizika kufungwa. Hapo sasa Owen akajua mambo yashakuwa vijimambo. Alisogea kule walipokuwa wenzake na alipowafikia tu aliambiwa kuanzia muda ule hatakiwi tena kuonekana pale kijiweni. Alipojaribu kuuliza sababu ya msingi ya kufukuzwa pale kijiweni hakujibiwa. Bosi


alimwambia tu Owen aondoke na hatakiwi kuonekana tena. Kwa hakika kilikuwa kipindi kigumu sana kwa Owen kwani ile ndo ilikuwa ofisi iliyokuwa inampa pesa ya kujikimu yeye na mke wake. Owen alijua kabisa hakuna neno analoweza kuongea na kueleweka kwa kuwa tayari wazazi wake walishatia mkono kwenye ile ile ofisi ili kuhakikisha anafeli kila sehemu. Owen aliona ni bora tu aondoke lakini kabla hajaondoka aliamua kuwashukuru wenyeji wake.


"Marafiki zangu, mimi nashukuru sana kwa wema na upendo wenu mulionionesha tangu siku ya kwanza muliponipokea na mpaka kufikia leo hii. Kiukweli kabisa sina cha kuwalaumu marafiki zangu kwa sababu najua hata nyie hamjafurahia mimi kuondoka. Nyie sio watu mulionifukuza mimi ila kuna mtu yupo nyuma ya hili. Huu ni mwendelezo tu wa vita nilizopigana tangu huko nyuma. Anyway, nawaombea tu kila la kheri katika majukumu yenu marafiki zangu. Ni wakati


mwingine kwangu kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.!" Owen alizungumza maneno hayo kwa huzuni kubwa moyoni. Wale wenzake walijikuta wanahuzunishwa sana na maneno ya Owen kwa kuwa walikuwa wanajuana vyema hali zao. Walijua kabisa mwenzao anaenda kukutana na msoto mwingine kwenye maisha kwa kuwa jiji lilikuwa gumu sana kwa mtu asiyekuwa na ajira. Owen aliondoka pale kijiweni na kuanza


rasmi safari ya kurudi nyumbani kwao. Hakupanda gari bali alitembea kwa mguu huku akitafakari hatima ya maisha yake na Laureen. Hakujua afanye nini ili azishinde zile changamoto. Tayari nyumbani alishamuacha Laureen akiwa mgonjwa na yeye ndo alikuwa anatumainiwa kupeleka tonge kwa mtoto wa kike. Kwa wakati ule hakuwa na pesa ya chakula na isitoshe kulikuwa na dawà alitakiwa akazinunue kwa ajili ya Laureen. Owen alijikuta anapata stress akiwa pembezoni mwa


barabara anatembea. Wakati anaendelea kuwaza, Ghafla kuna pikipiki ilitokea mbele yake. Owen alisogea pembezoni kabisa mwa barabara ili kumkwepa yule dereva lakini walimfuata huko huko. Dereva alionekana kudhamiria kumgonga na kumvunja kabisa mguu.Ile fumba macho na kufumbua Owen alijikuta mtaroni kwani tayari alishapitiwa na tairi la pikipiki mguuni kwake. NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu}


EPISODE: 31 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Yule jamaa alivyoona tayari amemgonga Owen hakusimama badala yake aliongeza spidi na kuondoka. Wasamaria wema waliokuwa karibu na eneo la tukio walimvuta Owen kutoka kule mtaroni na kumkagua majeraha mwilini mwake. Ni Mungu tu ndo aliweza kumnusuru Owen kwani hakupata jeraha kubwa


mwilizaidi ya michubuko tu. Lile tairi la pikipiki halikumgonga bali lilimparua tu na kumsukumiza mtaroni. Nguo alizovaa Owen zilichafuka kwa maji machafu ya mtaroni. "Kijana, kuwa makini sana maana inaonekana kuna watu wanakusakama. Yule boda alikusudia kabisa kukugonga maana hakukuwa na sababu ya msingi ya kukufuata mpaka pembezoni mwa barabara. NI dhahiri kabisa alikusudia kukuvunja viungo. Mshukuru tu


Mungu wako amekulinda.!" Hiyo ilikuwa kauli ya mmoja kati ya mashuhuda wa ile ajali. Owen aliwashukuru wale wasamaria wema waliomtoa pale mtaroni kisha akaondoka huku akiwa anachechemea. Alitamani kupanda daladala lakini alikosa ujasiri kwa kuwa nguo alizovaa zilikuwa zinatoa harufu mbaya ya maji machafu. Ilibidi tu atembee kwa miguu mpaka kwao licha ya kwamba kulikuwa na umbali kwa kiasi fulani. Alitembea kwa muda


usiopungua nusu saa mpaka kufika kwao na alipofika alimkuta Laureen bado amelala. Kwa mara nyingine tena Laureen alimshuhudia Owen akirudi nyumbani akiwa mnyonge sana tena awamu ile alikuwa anachechemea huku nguo zake zikiwa zimechafuka na kutoa harufu kali sana. Mtoto wa kike alijikuta anapata nguvu ya kuinuka kitandani na kumtazama Owen kwa umakini. Ilibidi amuulize nume wake ni kipi kilichomsibu mpaka amekuwa katika hali ile. Owen alimueleza


Laureen kila kitu kilichotokea kule atokako. Kwa mara nyingine tena Laureen alijikuta anamuhurumia Owen na kumuomba msamaha kwa yale yote yaliyokuwa yanamkuta. Laureen alijua kabisa yeye ndo alikuwa chanzo cha matatizo yote yaliyokuwa yanamkuta Owen. Zile miiba zote zilizokuwa zinapandikizwa kwenye njia za Owen zilikuwa na lengo la kumkumbusha Owen aachane na Laureen kisha amuoe Juliette ambaye ndo alikuwa chaguo la wazazi. Laureen alimfariji Owen


na kumwambia asikate tamaa na aendelee kupambana kwani kadri anavyopandisha ngazi kuelekea kilele cha mafanikio ndivyo kilima kinavyozidi kuongezeka. Kwa kuwa Laureen alikuwa bado anaumwa na Owen hakuwa na pesa ya kununua dawa walizoambiwa na Daktari, alichokifanya ni kwenda kwenye chumba cha mpangaji mwenzake na kuamua kumwekea bondi simu yake ili apate pesa ya dawa na chakula kwa ile siku. Makubaliano yalifanyika na ndipo Owen alipopata pesa ya kununua


dawa za Laureen pamoja na chakula. Siku iliyofuata Owen aliamka asubuhi na mapema kisha akaenda kutafuta madili ya pesa barabarani. Mwanaume alienda kwenye soko moja kubwa na maarufu sana ndani ya jiji. Alipofika pale akakuta baadhi ya vijana wakifanya kazi ya kushusha magunia kwenye magari yenye mazao kutoka shamba na kuingiza sokoni. Magari yalikuwa mengi sana yaliyobeba mazao tofauti tofauti kama vile viazi, ndizi, mahindi, matikiti, nyanya na bidhaa


zingine zitokazo shamba. Owen aliwafuata wahusika kisha akawaomba kazi ya kushusha magunia ili apate ridhiki. Kwa bahati njema, ombi lake lilikubaliwa hivyo alivua shati na kujifunga kichwani kama kilemba kisha akaanza kupiga kazi. Kwa mara ya kwanza kabisa Owen alijikuta anafanya kazi ngumu ambayo hakuwahigi kufikiria kama kuna siku angeifanya. Mpaka kufikia jioni tayari alishajipatia pesa hivyo akarudi nyumbani akiwa na kifurushi mkononi. Tangu siku hiyo Owen


alianza kufanya kazi hiyo na ilifikia hatua alishazoeleka pale sokoni na kujipatia marafiki. Kazi ilikuwa ngumu sana lakini Owen aliiona nyepesi kwa kuwa ilikuwa inasukuma gurudumu la familia japo kwa milo ya pasi ndefu. Bado kipato hakikuboresha maisha lakini angalau afueni ilikuwepo. Wenyewe waliendelea kufurahi na kumshukuru Mungu kwa kile kidogo alichokuwa anawapa. Wote kwa pamoja waliamini kwamba yale yalikuwa maisha ya mpito tu hivyo ipo siku Mungu angewainua mpaka kufika


kwenye kilele cha mafanikio. Walizidisha sala na maombi kwa Mungu ili azidi kuwalinda dhidi ya maadui zao. Siku moja Owen akiwa pale sokoni anaendelea na majukumu yake alimuona kibaka akikwapua mkoba wa mwanamke mmoja aliyekuwa pale sokoni kwa ajili ya kununua zaga zaga.Yule mwanamke alipiga kelele kuomba msaada lakini kila mtu alikuwa bize na mambo yake na ukizingatia sokoni kulikuwa na watu wengi sana hivyo sauti za watu zilikuwa hazisikilizani. Kwa kuwa Owen


alimuona kibaka akaamua kumuunganishia kwa nyuma. Alimkimbiza yule kibaka mpaka alipomkamata. Alianza kukabiliana nae mpaka akafanikiwa kumdhibiti na kumnyang'anya ule mkoba. Baada ya kuuchukua ule mkoba alirudi tena kumtafuta yule mwanamke lakini hakumkuta pale alipokuwa mwanzo. Owen alijaribu kuangaza angaza pale sokoni lakini hakumuona kabisa. Alitoka nje ya soko akamuona yule mwanamke amefungua mlango wa gari na anataka


kuingia ndani. Owen alimuwahi kwa spidi yule mwanamke kisha akasimama mbele yake huku akihema na jasho likiwa linamtoka kwa wingi. "Shangazi, Bila shaka huu ni mkoba wako. Hili soko lina vibaka wengi Shangazi hivyo unatakiwa kuwa makini. Yule mshenzi ameshazoea kuwaibia wateja mali zao na hii sio mara yake ya kwanza kufanya hivyo.!" Owen alizungumza hivyo huku akimkabidhi mkoba yule mwanamke


Yule mwanamke aliupokea chap ule mkoba kisha akafungua na kukagua kama vitu vyake vyote vilikuwemo. Alipokagua kwa umakini alikuta kila kitu kama alivyokiachaga. Yule mwanamke alimtazama Owen kisha akasema, "Ahsante sana kijana wangu. Nashukuru sana kwa wema wako maana ndani ya huu mkoba kulikuwa na vitu vingi sana vya thamani ambavyo havikupaswa kupotea. Kiukweli


kabisa nilichanganikiwa sana. Nashukuru sana mwanangu, Mungu akubariki kwa kuwa mwema na mwaminifu.!" "Sawa Shangazi, vipi vitu vyako vyote vimetimia lakini?" "Ndio mwanangu kila kitu kipo. Kadi zangu zote zipo na hata pesa haijapungua hata senti moja.!" "Ok, basi sawa Shangazi, ngoja mimi nikuache ila siku nyingine kuwa makini tu.!" Owen


alizungumza kauli hiyo kisha akaanza kupiga hatua kuondoka. "Kijana.! Hebu subiri kwanza.!" Yule mwanamke alimsimamisha Owen. Baada ya kumsimamisha alifungua mkoba wake na kutoa noti tatu za shilingi elfu kumi kumi na kumkabidhi Owen huku akimwambia ile ni kama shukrani kwa kwake. Huwezi kuamini yani, Owen aliikataa ile elfu thelathini ya kitanzania licha ya kuwa na shida zilizomzidi umri nyumbani


kwake. "Shangazi eeh, Siku zote msaada sio kazi ya malipo bali ni kazi ya kujitolea. Nikiwa kama binadamu mwenye moyo nafurahi sana pindi ninapotoa msaada kwa binadamu mwenzangu alafu akaniambia asante kaka Mungu akubariki. Kiukweli kabisa, Sipo tayari kupokea pesa za mtu ilihali sijamfanyia kazi yoyote ya malipo. Kwa hiki nilichokifanya kwako ilikuwa ni lazima tu nifanye kwa kuwa ulihitaji msaada na mimi ni mwanadamu


mwenye moyo wa kusaidia.!" Owen alimjibu yule mama. Dakika zile zile alitokea rafiki yake Owen aliyekuwa anafanya nae kazi. Yule rafiki alimwambia Owen kuna gari limeingia muda ule hivyo wanatakiwa wakashushe magunia. Yule mwanamke alivyosikia kauli ya yule mtu alimuuliza Owen anafanya kazi gani. Owen alimjibu kwamba yeye ni m'beba mizigo tu pale sokoni. Baada ya kuambiwa hivyo yule mwanamke akasema,


"Anha! Sasa naomba nikupe kazi kwa leo tu kijana wangu. Mimi nilikuja hapa kununua matunda lakini nilisitisha zoezi langu baada ya kuibiwa pesa. Ila muda huu nataka tena kurudi hapo ndani ili ninunue matunda kama nilivyokuwa nimepanga. Sasa basi kazi ninayotaka kukupa ni kunisaidia kubeba mzigo wa matunda na zaga zingine nitakazonunua na kuzileta kwenye gari. Nitakulipia kwa hiyo kazi.!" Yule mwanamke alizungumza maneno hayo


kwenda kwa Owen. Owen alimtazama yule mwanamke kisha akamgeukia rafiki yake na kumwambia akamchukue mtu mwingine wakashushe huo mzigo ulioletwa na gari. Yule jamaa aliondoka na alishajua Owen alipata dili lingine. Owen alimkubalia yule mama na kumwambia waingie sasa ndani ya soko. Wakati huo Owen alikuwa amechafuka kweli kweli kwani alikuwa na mavazi ya kazi. Wote wawili waliingia ndani na yule mama alianza kuchagua


zaga alizokuwa anazihitaji na kuziweka kwenye mfuko aliobebeshwa Owen. Walitumia takribani dakika ishirini kuzunguka sokoni huku wakinunua zaga tofauti tofauti. Walipomaliza Owen aliubeba mzigo na kuupeleka mpaka kwenye gari. "Ahsante sana kijana wangu kwa msaada ulionipa. Mwanzo nilisema kwamba nitakulipa lakini kwa sasa sihitaji tena kukulipa kwa kuwa najua hutaki malipo pindi unapotoa msaada.


Naomba tu upokee hii pesa kama shukrani yangu kwako. Haya sio malipo bali ni shukrani kwa hiki ulichonifanyia.!" "Lakini Shangazi unajua... unaju....!" Owen alitaka kuzungumza jambo lakini kabla hajamaliza kauli yake tayari alishawekewa pesa kwenye mfuko wa suruali yake. Yule mwanamke alijua kabisa Owen alitaka kukataa pesa licha ya kwamba alikuwa na dhiki kubwa kwenye maisha yake. Kwa


namna fulani yule mwanamke alimuhurumia Owen hivyo hakuona vyema kama angemuacha bila malipo. "Kijana wangu, roho yako inanifanya nitamani kujua mengi kuhusu wewe lakini muda wangu ni mchache sana. Kwa sasa naondoka ila nahisi wiki ijayo nitakuja tena hapa sokoni. Nitakuja kukuulizia kwenye kile kijiwe chenu. Si umesema unaitwa Owen eeh?" "Yeah! Owen ndo jina langu lakini


ukifika pale niulizie kwa jina la OLA. Hilo ndo jina langu maarufu hapa sokoni. Ukiniulizia kwa jina la Owen hutoweza kunipata.!" Owen alimjibu yule mwanamke.

Baada ya mazungumzo hayo yule mwanamke alipanda kwenye gari kwa ajili ya kuondoka. Kabla hajatoka Owen alisogea kwenye kioo cha dirisha na kusema, "Shangazi eeh, shukrani sana na Mungu akutangulie kwa kila jambo.!" Owen alimshukuru yule mwanamke kisha gari


likaondoka. Ilikuwa ni halali kabisa kwa Owen kumuita Shangazi yule mwanamke kwa kuwa alikuwa na umri mkubwa kama mama yake. Kitu pekee ambacho Owen alikigundua kwa yule mama ni kwamba alikuwa ni mtu mwenye pesa na roho nzuri sana. Owen alizihesabu zile pesa alizoachiwa na yule mama akakutana na elfu hamsini zilizonyooka. Mtaalamu alishukuru sana na kujisemea moyoni,


"Leo nitakula kuku na mke wangu.!" Baada ya kujisemea maneno hayo alienda kijiweni kwa ajili ya kuwaaga wenzake na kurudi nyumbani kwao maana tayari alishapata pesa. Aliwaaga wenzake kisha akaenda kununua kuku mzima kwa ajili ya kula na Laureen wake maana ni kitambo sana hawakula nyama. Kabla hajaenda kupanda gari alipitia kwenye duka fulani la viatu vya kike. Alipofika alinunua viatu kwa ajili ya Laureen wake. Ni viatu


fulani ambavyo Laureen alikuwa anavipenda na Owen alishamuahidi kwamba angemnunulia siku akipata pesa. Mwanaume alimnunulia kipenzi chake viatu kisha akaenda stendi kupanda daladala na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Kwa hakika siku hiyo alikuwa na furaha tele. Kumbe sasa, kule nyumbani siku ile Laureen alikuwa na mgeni. Mgeni huyo alikuwa ni mwanadada Juliette. Juliette alifanyaga utafiti wa kutosha mpaka akafanikiwa kufahamu mahala walipokuwa


wanaishi Owen na Laureen. Laureen hakuwa na kinyongo na Juliette hivyo alimpokea na kumkaribisha ndani kwake. Siku hiyo Juliette alishinda na Laureen kutwa nzima huku wakijadili mambo mengi kuhusu maisha. Juliette aligundua kwamba Owen na Laureen walikuwa wanaishi maisha duni na ya chini sana. Ni wanawake wachache sana wanaoridhikaga kuishi na mwanaume kwenye hali duni hivyo Juliette aliona atumie fursa ile kumshawishi Laureen aachane na Owen. Alichokifanya


ni kumpa Laureen nafasi moja adhimu sana ya kuuaga umaskini na kwenda kuishi maisha ya kifahari huku akiwa na nafasi ya kutimiza ndoto zake za kusoma. Juliette alimwambia Laureen hivi; "Laureen, Nipo tayari kukupa kiasi chochote cha pesa kama utakuwa tayari kumuacha Owen na kwenda kuishi mbali nae.! Umesema kwamba bado una ndoto za kurudi darasani, kwahiyo basi mimi nipo tayari kukutafutia chuo na kukulipia gharama zote za masomo


pamoja na pesa ya kujikimu mpaka pale utakapohitimu masomo yako kwa ngazi zote. Sharti ni moja tu kwako, kubali kuachana na Owen.! Lakini pia hata ukiamua kurudi kwenu Mwanza, nipo tayari kwenda kukujengea nyumba nzuri, kukupa mtaji mkubwa wa biashara na gari la kutembelea. Ila sharti ni moja tu, achana na Owen. Hii ni nafasi moja adhimu sana kwako endapo utaitumia vizuri basi utabadilisha status yako ya maisha. Nipo hapa nasubiri jibu lako Laureen and


the choice is yours. Take a risk or loose a chance.!"Juliette alizungumza kauli hiyo akimalizia kwa kumpa chaguo Laureen akubali kujitoa muhanga au kupoteza nafasi adhimu. NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 31 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Yule jamaa alivyoona tayari amemgonga Owen hakusimama


badala yake aliongeza spidi na kuondoka. Wasamaria wema waliokuwa karibu na eneo la tukio walimvuta Owen kutoka kule mtaroni na kumkagua majeraha mwilini mwake. Ni Mungu tu ndo aliweza kumnusuru Owen kwani hakupata jeraha kubwa mwilizaidi ya michubuko tu. Lile tairi la pikipiki halikumgonga bali lilimparua tu na kumsukumiza mtaroni. Nguo alizovaa Owen zilichafuka kwa maji machafu ya mtaroni.


"Kijana, kuwa makini sana maana inaonekana kuna watu wanakusakama. Yule boda alikusudia kabisa kukugonga maana hakukuwa na sababu ya msingi ya kukufuata mpaka pembezoni mwa barabara. NI dhahiri kabisa alikusudia kukuvunja viungo. Mshukuru tu Mungu wako amekulinda.!" Hiyo ilikuwa kauli ya mmoja kati ya mashuhuda wa ile ajali. Owen aliwashukuru wale wasamaria wema waliomtoa pale mtaroni kisha akaondoka


huku akiwa anachechemea. Alitamani kupanda daladala lakini alikosa ujasiri kwa kuwa nguo alizovaa zilikuwa zinatoa harufu mbaya ya maji machafu. Ilibidi tu atembee kwa miguu mpaka kwao licha ya kwamba kulikuwa na umbali kwa kiasi fulani. Alitembea kwa muda usiopungua nusu saa mpaka kufika kwao na alipofika alimkuta Laureen bado amelala. Kwa mara nyingine tena Laureen alimshuhudia Owen akirudi nyumbani akiwa mnyonge sana tena awamu ile alikuwa


anachechemea huku nguo zake zikiwa zimechafuka na kutoa harufu kali sana. Mtoto wa kike alijikuta anapata nguvu ya kuinuka kitandani na kumtazama Owen kwa umakini. Ilibidi amuulize nume wake ni kipi kilichomsibu mpaka amekuwa katika hali ile. Owen alimueleza Laureen kila kitu kilichotokea kule atokako. Kwa mara nyingine tena Laureen alijikuta anamuhurumia Owen na kumuomba msamaha kwa yale yote yaliyokuwa yanamkuta. Laureen alijua kabisa yeye ndo


alikuwa chanzo cha matatizo yote yaliyokuwa yanamkuta Owen. Zile miiba zote zilizokuwa zinapandikizwa kwenye njia za Owen zilikuwa na lengo la kumkumbusha Owen aachane na Laureen kisha amuoe Juliette ambaye ndo alikuwa chaguo la wazazi. Laureen alimfariji Owen na kumwambia asikate tamaa na aendelee kupambana kwani kadri anavyopandisha ngazi kuelekea kilele cha mafanikio ndivyo kilima kinavyozidi kuongezeka. Kwa kuwa Laureen alikuwa bado anaumwa na Owen hakuwa na


pesa ya kununua dawa walizoambiwa na Daktari, alichokifanya ni kwenda kwenye chumba cha mpangaji mwenzake na kuamua kumwekea bondi simu yake ili apate pesa ya dawa na chakula kwa ile siku. Makubaliano yalifanyika na ndipo Owen alipopata pesa ya kununua dawa za Laureen pamoja na chakula. Siku iliyofuata Owen aliamka asubuhi na mapema kisha akaenda kutafuta madili ya pesa barabarani. Mwanaume alienda kwenye soko moja kubwa na maarufu sana ndani ya


jiji. Alipofika pale akakuta baadhi ya vijana wakifanya kazi ya kushusha magunia kwenye magari yenye mazao kutoka shamba na kuingiza sokoni. Magari yalikuwa mengi sana yaliyobeba mazao tofauti tofauti kama vile viazi, ndizi, mahindi, matikiti, nyanya na bidhaa zingine zitokazo shamba. Owen aliwafuata wahusika kisha akawaomba kazi ya kushusha magunia ili apate ridhiki. Kwa bahati njema, ombi lake lilikubaliwa hivyo alivua shati na kujifunga kichwani kama kilemba


kisha akaanza kupiga kazi. Kwa mara ya kwanza kabisa Owen alijikuta anafanya kazi ngumu ambayo hakuwahigi kufikiria kama kuna siku angeifanya. Mpaka kufikia jioni tayari alishajipatia pesa hivyo akarudi nyumbani akiwa na kifurushi mkononi. Tangu siku hiyo Owen alianza kufanya kazi hiyo na ilifikia hatua alishazoeleka pale sokoni na kujipatia marafiki. Kazi ilikuwa ngumu sana lakini Owen aliiona nyepesi kwa kuwa ilikuwa inasukuma gurudumu la familia japo kwa milo ya pasi ndefu.


Bado kipato hakikuboresha maisha lakini angalau afueni ilikuwepo. Wenyewe waliendelea kufurahi na kumshukuru Mungu kwa kile kidogo alichokuwa anawapa. Wote kwa pamoja waliamini kwamba yale yalikuwa maisha ya mpito tu hivyo ipo siku Mungu angewainua mpaka kufika kwenye kilele cha mafanikio. Walizidisha sala na maombi kwa Mungu ili azidi kuwalinda dhidi ya maadui zao. Siku moja Owen akiwa pale sokoni anaendelea na majukumu yake alimuona kibaka akikwapua mkoba wa


mwanamke mmoja aliyekuwa pale sokoni kwa ajili ya kununua zaga zaga.Yule mwanamke alipiga kelele kuomba msaada lakini kila mtu alikuwa bize na mambo yake na ukizingatia sokoni kulikuwa na watu wengi sana hivyo sauti za watu zilikuwa hazisikilizani. Kwa kuwa Owen alimuona kibaka akaamua kumuunganishia kwa nyuma. Alimkimbiza yule kibaka mpaka alipomkamata. Alianza kukabiliana nae mpaka akafanikiwa kumdhibiti na kumnyang'anya ule mkoba.


Baada ya kuuchukua ule mkoba alirudi tena kumtafuta yule mwanamke lakini hakumkuta pale alipokuwa mwanzo. Owen alijaribu kuangaza angaza pale sokoni lakini hakumuona kabisa. Alitoka nje ya soko akamuona yule mwanamke amefungua mlango wa gari na anataka kuingia ndani. Owen alimuwahi kwa spidi yule mwanamke kisha akasimama mbele yake huku akihema na jasho likiwa linamtoka kwa wingi. "Shangazi, Bila shaka huu ni


mkoba wako. Hili soko lina vibaka wengi Shangazi hivyo unatakiwa kuwa makini. Yule mshenzi ameshazoea kuwaibia wateja mali zao na hii sio mara yake ya kwanza kufanya hivyo.!" Owen alizungumza hivyo huku akimkabidhi mkoba yule mwanamke Yule mwanamke aliupokea chap ule mkoba kisha akafungua na kukagua kama vitu vyake vyote vilikuwemo. Alipokagua kwa umakini alikuta kila kitu kama alivyokiachaga. Yule mwanamke


alimtazama Owen kisha akasema, "Ahsante sana kijana wangu. Nashukuru sana kwa wema wako maana ndani ya huu mkoba kulikuwa na vitu vingi sana vya thamani ambavyo havikupaswa kupotea. Kiukweli kabisa nilichanganikiwa sana. Nashukuru sana mwanangu, Mungu akubariki kwa kuwa mwema na mwaminifu.!" "Sawa Shangazi, vipi vitu vyako vyote vimetimia lakini?"


"Ndio mwanangu kila kitu kipo. Kadi zangu zote zipo na hata pesa haijapungua hata senti moja.!" "Ok, basi sawa Shangazi, ngoja mimi nikuache ila siku nyingine kuwa makini tu.!" Owen alizungumza kauli hiyo kisha akaanza kupiga hatua kuondoka. "Kijana.! Hebu subiri kwanza.!" Yule mwanamke alimsimamisha Owen.


Baada ya kumsimamisha alifungua mkoba wake na kutoa noti tatu za shilingi elfu kumi kumi na kumkabidhi Owen huku akimwambia ile ni kama shukrani kwa kwake. Huwezi kuamini yani, Owen aliikataa ile elfu thelathini ya kitanzania licha ya kuwa na shida zilizomzidi umri nyumbani kwake. "Shangazi eeh, Siku zote msaada sio kazi ya malipo bali ni kazi ya kujitolea. Nikiwa kama binadamu mwenye moyo nafurahi sana pindi ninapotoa msaada kwa


binadamu mwenzangu alafu akaniambia asante kaka Mungu akubariki. Kiukweli kabisa, Sipo tayari kupokea pesa za mtu ilihali sijamfanyia kazi yoyote ya malipo. Kwa hiki nilichokifanya kwako ilikuwa ni lazima tu nifanye kwa kuwa ulihitaji msaada na mimi ni mwanadamu mwenye moyo wa kusaidia.!" Owen alimjibu yule mama. Dakika zile zile alitokea rafiki yake Owen aliyekuwa anafanya nae kazi. Yule rafiki alimwambia Owen kuna gari limeingia muda


ule hivyo wanatakiwa wakashushe magunia. Yule mwanamke alivyosikia kauli ya yule mtu alimuuliza Owen anafanya kazi gani. Owen alimjibu kwamba yeye ni m'beba mizigo tu pale sokoni. Baada ya kuambiwa hivyo yule mwanamke akasema, "Anha! Sasa naomba nikupe kazi kwa leo tu kijana wangu. Mimi nilikuja hapa kununua matunda lakini nilisitisha zoezi langu baada ya kuibiwa pesa. Ila muda huu nataka tena kurudi hapo


ndani ili ninunue matunda kama nilivyokuwa nimepanga. Sasa basi kazi ninayotaka kukupa ni kunisaidia kubeba mzigo wa matunda na zaga zingine nitakazonunua na kuzileta kwenye gari. Nitakulipia kwa hiyo kazi.!" Yule mwanamke alizungumza maneno hayo kwenda kwa Owen. Owen alimtazama yule mwanamke kisha akamgeukia rafiki yake na kumwambia akamchukue mtu mwingine wakashushe huo mzigo ulioletwa


na gari. Yule jamaa aliondoka na alishajua Owen alipata dili lingine. Owen alimkubalia yule mama na kumwambia waingie sasa ndani ya soko. Wakati huo Owen alikuwa amechafuka kweli kweli kwani alikuwa na mavazi ya kazi. Wote wawili waliingia ndani na yule mama alianza kuchagua zaga alizokuwa anazihitaji na kuziweka kwenye mfuko aliobebeshwa Owen. Walitumia takribani dakika ishirini kuzunguka sokoni huku wakinunua zaga tofauti tofauti. Walipomaliza Owen aliubeba


mzigo na kuupeleka mpaka kwenye gari. "Ahsante sana kijana wangu kwa msaada ulionipa. Mwanzo nilisema kwamba nitakulipa lakini kwa sasa sihitaji tena kukulipa kwa kuwa najua hutaki malipo pindi unapotoa msaada. Naomba tu upokee hii pesa kama shukrani yangu kwako. Haya sio malipo bali ni shukrani kwa hiki ulichonifanyia.!" "Lakini Shangazi unajua... unaju....!" Owen alitaka


kuzungumza jambo lakini kabla hajamaliza kauli yake tayari alishawekewa pesa kwenye mfuko wa suruali yake. Yule mwanamke alijua kabisa Owen alitaka kukataa pesa licha ya kwamba alikuwa na dhiki kubwa kwenye maisha yake. Kwa namna fulani yule mwanamke alimuhurumia Owen hivyo hakuona vyema kama angemuacha bila malipo. "Kijana wangu, roho yako inanifanya nitamani kujua mengi


kuhusu wewe lakini muda wangu ni mchache sana. Kwa sasa naondoka ila nahisi wiki ijayo nitakuja tena hapa sokoni. Nitakuja kukuulizia kwenye kile kijiwe chenu. Si umesema unaitwa Owen eeh?" "Yeah! Owen ndo jina langu lakini ukifika pale niulizie kwa jina la OLA. Hilo ndo jina langu maarufu hapa sokoni. Ukiniulizia kwa jina la Owen hutoweza kunipata.!" Owen alimjibu yule mwanamke.

Baada ya mazungumzo hayo yule


mwanamke alipanda kwenye gari kwa ajili ya kuondoka. Kabla hajatoka Owen alisogea kwenye kioo cha dirisha na kusema, "Shangazi eeh, shukrani sana na Mungu akutangulie kwa kila jambo.!" Owen alimshukuru yule mwanamke kisha gari likaondoka. Ilikuwa ni halali kabisa kwa Owen kumuita Shangazi yule mwanamke kwa kuwa alikuwa na umri mkubwa kama mama yake. Kitu pekee ambacho Owen


alikigundua kwa yule mama ni kwamba alikuwa ni mtu mwenye pesa na roho nzuri sana. Owen alizihesabu zile pesa alizoachiwa na yule mama akakutana na elfu hamsini zilizonyooka. Mtaalamu alishukuru sana na kujisemea moyoni, "Leo nitakula kuku na mke wangu.!" Baada ya kujisemea maneno hayo alienda kijiweni kwa ajili ya kuwaaga wenzake na kurudi nyumbani kwao maana tayari


alishapata pesa. Aliwaaga wenzake kisha akaenda kununua kuku mzima kwa ajili ya kula na Laureen wake maana ni kitambo sana hawakula nyama. Kabla hajaenda kupanda gari alipitia kwenye duka fulani la viatu vya kike. Alipofika alinunua viatu kwa ajili ya Laureen wake. Ni viatu fulani ambavyo Laureen alikuwa anavipenda na Owen alishamuahidi kwamba angemnunulia siku akipata pesa. Mwanaume alimnunulia kipenzi chake viatu kisha akaenda stendi kupanda daladala na kuanza


safari ya kurudi nyumbani. Kwa hakika siku hiyo alikuwa na furaha tele. Kumbe sasa, kule nyumbani siku ile Laureen alikuwa na mgeni. Mgeni huyo alikuwa ni mwanadada Juliette. Juliette alifanyaga utafiti wa kutosha mpaka akafanikiwa kufahamu mahala walipokuwa wanaishi Owen na Laureen. Laureen hakuwa na kinyongo na Juliette hivyo alimpokea na kumkaribisha ndani kwake. Siku hiyo Juliette alishinda na Laureen kutwa nzima huku wakijadili mambo mengi kuhusu


maisha. Juliette aligundua kwamba Owen na Laureen walikuwa wanaishi maisha duni na ya chini sana. Ni wanawake wachache sana wanaoridhikaga kuishi na mwanaume kwenye hali duni hivyo Juliette aliona atumie fursa ile kumshawishi Laureen aachane na Owen. Alichokifanya ni kumpa Laureen nafasi moja adhimu sana ya kuuaga umaskini na kwenda kuishi maisha ya kifahari huku akiwa na nafasi ya kutimiza ndoto zake za kusoma. Juliette alimwambia Laureen hivi;


"Laureen, Nipo tayari kukupa kiasi chochote cha pesa kama utakuwa tayari kumuacha Owen na kwenda kuishi mbali nae.! Umesema kwamba bado una ndoto za kurudi darasani, kwahiyo basi mimi nipo tayari kukutafutia chuo na kukulipia gharama zote za masomo pamoja na pesa ya kujikimu mpaka pale utakapohitimu masomo yako kwa ngazi zote. Sharti ni moja tu kwako, kubali kuachana na Owen.! Lakini pia hata ukiamua kurudi kwenu Mwanza, nipo tayari kwenda


kukujengea nyumba nzuri, kukupa mtaji mkubwa wa biashara na gari la kutembelea. Ila sharti ni moja tu, achana na Owen. Hii ni nafasi moja adhimu sana kwako endapo utaitumia vizuri basi utabadilisha status yako ya maisha. Nipo hapa nasubiri jibu lako Laureen and the choice is yours. Take a risk or loose a chance.!"Juliette alizungumza kauli hiyo akimalizia kwa kumpa chaguo Laureen akubali kujitoa muhanga au kupoteza nafasi adhimu.


NOVEL: MY VALENTINE (MV14) {Kipenzi Changu} EPISODE: 32 AUTHOR: HERRY DESOUZER (Silentkiller) Ilichukua dakika moja tu kwa Laureen kujibu kauli ya Juliette ambaye alimtaka akubali kuachana na Owen. Ni kweli kabisa ilikuwa ni nafasi adhimu sana kwa Laureen kuweza kubadilisha maisha yake kutoka kwenye umaskini mpaka kufikia utajiri. Ile ndoto yake ya kusoma


ilikuwa inatimia endapo tu angekubali kupokea ofa ya Juliette. Lakini sasa masharti ya Julliete ndo yalimpa ugumu Laureen kukubali ile ofa. Suala la kumuacha Owen lilikuwa gumu kuliko hata kuupanda mlima Kilimanjaro kwa magoti. Kwanza kabisa Laureen alikuwa anampenda sana Owen kuliko hata ndoto zake. Pili alikuwa anapendwa sana na Owen kiasi kwamba Owen alishagombana na wazazi wake na kukubali kuishi maisha magumu kwa ajili yake. Laureen aliona kabisa


kama angekubali kumuacha Owen kisa pesa alizoahidiwa na Juliette basi usaliti wake ungekuwa mara kumi zaidi ya usaliti wa Yuda. Pigo ambalo angeliacha kwa Owen lingekuwa takatifu kuliko hata lile alilopewa na mwanamke wake wa kwanza (Diana). Laureen hakuona sababu ya kumuumiza mwanaume alieyatoa sadaka maisha yake kwa ajili yake. Mwanaume ambaye aliamua kupambana ili kutafuta maisha kwa ajili yake, Mwanaume ambaye alishaonesha nia ya


kumsaidia kutimiza ndoto zake katika masomo. Laureen hakuona sababu ya msingi ya kuweka kwenye mzani ofa ya Juliette dhidi ya penzi lake na Owen. Aliona kabisa penzi lao lilikuwa na uzito kuliko hata ile ofa. Alichokifanya ni kumtazama Juliette kisha akamjibu, "Juliette, Kwanza kabisa nashukuru sana kwa nafasi adhimu uliyonipa. Lakini naomba tu niseme kwamba, Mimi sipo tayari kuipokea hiyo nafasi. Kwa sasa nina furaha sana kuishi


kwenye haya maisha na mtu ninaempenda. Hizo mali, elimu na pesa hazitonipa furaha kama nitakosa nafasi ya kuwa na mtu ninaempenda. Katika hili nadhani hata wewe ni shahidi. Una elimu, pesa na mali lakini bado huna furaha kwa kumkosa tu mwanaume unaempenda. Kama ni pesa na mali basi nitazitafuta pamoja na Owen wangu. Uzuri ni kwamba bado hatujakata tamaa na ninaamini Owen wangu atapata pesa za kunipeleka darasani. Haijalishi itakuwa ni lini lakini nitasubiri tu. Nitasubiri


mpaka mume wangu atakapopata pesa. Na naomba nikuambie kitu Juliette, Mimi hapa nampenda sana Owen. Na Kama ikitokea tumeachana basi ujue yeye ndo atakuwa ameniacha mimi na sio mimi kumuacha yeye. Hata ukinishikia bastola muda huu na kuniambia nichague kifo au kuachana na Owen basi utaisikia tu sauti yangu ikisali sala zangu za mwisho. In my insane and foolish brain, Owen is Alfa. And in my darkest heart, He is Omega. Kiukweli kabisa, Mimi


hapa nampenda sana Owen.!" Hilo ndo lilikuwa jibu la Laureen kuhusiana na ofa aliyopewa na Juliette. Kauli ya Laureen ilimuumiza sana Juliette kwani ilikuwa inazima kabisa ndoto zake za kumpata Owen. Kumbe wakati Laureen anamjibu Juliette kauli ile, Owen alikuwa tayari ameshafika pale kwao na aliganda dirishani kusikiliza maongezi yale. Maneno ya Laureen yaliugusa moyo wake vilivyo kwani yalibeba tafsiri ya


mapenzi ya dhati kabisa. Mwanaume alijikuta anatokwa na machozi ya furaha baada ya kugundua kwamba hatimaye Mungu amempatia mwanamke mwenye moyo wa subra. Subra sio kitu ambacho kila mwanadamu ameumbiwa. Mtaalamu alijiuliza tu Juliette amepajuaje mahala pale. Hakutakaga kabisa watu wanaomfahamu hasa hasa wazazi wake na Juliette wajue makazi yake kwani hao ndo walikuwa wanampiga vita ili asifurahie maisha akiwa na


Laureen. Owen alitoka pale dirishani kisha akaenda mlangoni kubisha hodi. Laureen alimruhusu Owen kuingia ndani na alipoingia tu alimpokea kifurushi na kumkumbatia mume wake. Juliette alijisikia vibaya na wivu ulimtesa. Alitamani sana lile kumbatio angelipata yeye. Baada ya sekunde kadhaa Owen na Laureen walijitoa kwenye kumbatio. Hapo sasa mwanaume alianza kushughulika na Juliette kwa kuanza kumkaribisha kwa ukarimu. Ilibidi Juliette awe na heshima ndani ya


himaya ya watu waliochagua kuishi kama wanandoa. Siku hiyo Owen na Juliette waliongea mengi sana lakini kubwa zaidi lilikuwa lile la Juliette kumsisitiza Owen akubali kurudi kwenye maisha anayostahili kuishi na sio yale ya kimaskini. Juliette alimwambia Owen arudi kwa wazazi akaombe msamaha ili aendelee kutumikia nafasi yake kama mtoto wa kitajiri. Hilo suala Owen alilipinga na kulikataa katakata. Baada ya hilo kukataliwa, Juliette alimwambia Owen waungane kwenye


biashara zake lakini hata hilo Owen alilikataa. Alishajua ule ulikuwa mtego wa Juliette hivyo hakuwa tayari kunaswa. Mwisho kabisa Juliette alimwambia Owen atampatia kiasi fulani cha pesa ili afanye biashara yake binafsi na aachane na kazi za kuganga njaa barabarani. Hata hilo nalo Owen alikataa pia. Alimwambia Julliete kwamba alifanya maamuzi akiwa na akili zake timamu kuchagua yale maisha. Yale maisha anayafurahia sana hivyo haitaji huruma wala msaada wa mtu


yeyote yule. Alimtaka tu aendelee kupambana na biashara zake na sio kumfuatilia yeye. Huo ndo ulikuwa msimamo wa Owen dhidi ya Juliette ambaye alitaka kumsaidia kwa lengo la kudai fadhila hapo baadae. Wakati watu wanamuona Owen amefeli na kuyumba kimaisha, Owen yeye alikuwa anajiona amefanikiwa. Katika fikra zake aliamini kwamba mafanikio ni pamoja na kuwa au kuishi na yule unayempenda kwa dhati. **** Siku zilisonga na Owen


aliendelea kufanya kazi yake ile ile ya kubeba mizigo sokoni. Laureen alipona kabisa na alitaka kuendelea na shughuli yake ya kuuza samaki lakini Owen alimtaka mwanamke wake abaki nyumbani ili apate muda wa kutosha wa kupumzika. Owen aliendelea kufanya kazi na kwa qudra za Mwenyezi Mungu ridhiki iliendelea kupatikana japo kwenye mazingira magumu. Siku moja Owen alipokuwa kwenye majukumu ya kazi alidondokewa na gunia la viazi mguuni. Ni bahati tu hakuvunjika ila mguu


uliteguka na kumfanya ashindwe kuendelea na kazi. Siku hiyo alirudi nyumbani na alipofika Laureen alichemsha maji ya moto na kumkanda mtaalamu. Mwanzo walihisi ni mshtuko tu wa kawaida hivyo hawakuwaza kabisa kuhusu hospitali. Lakini siku iliyofuata mguu ulivimba na kumfanya Owen ashindwe kutembea. Hapo sasa waliamua kukusanya akiba yote iliyokuwa ndani kisha wakaenda hospitali. Walipofika hospitali gharama za matibabu zilikuwa kubwa kuliko hata pesa waliyokuwa nayo


mfukoni. Kwa hesabu za haraka haraka ilibidi waangalie rasilimali ya kuuza Ili wapate pesa ya kugharamia matibabu yale. Owen alitumia simu ya Laureen kumpigia yule jirani aliyemuekeaga bondi simu yake kisha akamuomba amalizie kiasi fulani cha pesa ili ainunue moja kwa moja. Shida na matatizo yalimfanya Owen auze simu yake yenye thamani ya shilingi laki tano za kitanzania kwa shilingi laki moja na elfu ishirini tu. Jamaa alitumia shida za Owen kama fursa ya kujipatia mali


kirahisi kabisa. Alijua kabisa Owen hakuwa na ujanja wowote katika lile. Baada ya biashara kufanyika, Owen aliweza kupata pesa za matibabu. Alilipia matibabu yote na walirudi nyumbani kwao siku ile ile. Lakini sasa, tazama namna Mwenyezi Mungu alivyokuwa mtenda haki, yule jirani aliyenunua simu ya Owen kwa dhuluma, alidondosha na kupoteza siku ile ile. Takribani mwezi mmoja Owen alikuwa hawezi kutembea vizuri hivyo hakutoka kwenda kutafuta ridhiki. Kwa kipindi hiko, Laureen


aliamua kurudi tena kwenye biashara Ila alianza kuuza mahindi ya kuchemsha mtaani. Hawakuwa na mtaji wa kutosha wa kufanyia biashara ya samaki ndo maana walizamia kwenye mahindi. Kiukweli kabisa, kwa kipindi hiko Owen na Laureen waliishi maisha magumu sana. Maisha magumu kuliko kawaida kwani biashara ilikuwa ndogo sana hivyo haikuweza kukidhi mahitaji yote ya familia. Bili ya maji na umeme ilishakuwa mtihani kwao. Ilifikia hatua hata chakula kwao kilishakuwa


changamoto. Hawakuwa na uhakika wa kula milo miwili kwa siku. Kwa hakika maisha yao yalitia huruma. Walishauza mpaka kitanda na kuanza kulala chini ilimradi tu wapate pesa ya kula. Wakati Laureen anauza samaki mtaani alikuwa anatongozwa na watu tofauti tofauti wenye pesa zao lakini mtoto wa kike hakuwa tayari kumsaliti Owen licha ya hali yao ya maisha kuwa duni. Alikuwa tayari kumvumilia Owen na kuamini kwamba ipo siku atapata pesa na watamiliki vitu


vyenye thamani kama watu wengine. Owen yeye alikuwa anaomba Mungu amponye kabisa ili aweze kwenda kutafuta pesa. Mpaka kufikia muda huo alikuwa na mawazo kuhusu kodi ya chumba ambayo alitakiwa kulipa mwisho wa mwezi ule. Siku moja akiwa amekaa na Laureen wanakula zao ugali kwa sukari, ghafla simu iliita. Kwa wakati huo Owen alikuwa ameweka laini zake kwenye simu ya Laureen. Alipoangalia alikutana na namba ngeni. Owen alipokea ile simu kisha akasikia


sauti upande wa pili ikisema, "Hello.! Bila shaka naongea na Owen James?" "Yes.! Ndo mimi mwenyewe.!" Owen alijibu "Ok, Mimi ni Meneja mwajiri kutoka kampuni ya SK GROUP. Tulishapokea barua yako ya kazi hivyo basi jumatatu ya tarehe tano, majira ya saa mbili kamili asubuhi tunakuomba ufike kwenye kampuni yetu kwa ajili ya interview. Njoo na vyeti vya


taaluma pamoja na CV zako.!" Hiyo ilikuwa sauti ya kike iliyosikika kwenye simu. Baada ya maongezi hayo simu ilikatwa. Kwa hakika taarifa ile ilimshtua Owen na kumpa furaha ambayo hakuitarajia kabisa. Sio Owen tu, hata Laureen alijikuta anafurahi na kupata matumaini mapya. Owen aliona miujiza imetokea upande wake kwani hakutarajia kabisa kama angeitwa kwenye interview ya kazi katika ile kampuni. Tayari ulishapita muda mrefu tangu


alipotumaga barua ya maombi ya kazi kwenye ile kampuni na alishakataga tamaa. Owen na Laureen walifanya sala na maombi ili Mungu awajalie katika jambo lile. Hiyo jumatatu ya interview haikuwa mbali, ilikuwa ni siku mbili tu mbele kutoka siku ile. Na ilipofika jumatatu Owen aliwasili mapema kwenye kampuni huku akiwa anachechemea mguu. Alipofika tu alishtuka kuwakuta wenzake kama hamsini nao wamefika kwa ajili ya interview ya kazi ile ile. Uwingi wa watu ulimkatisha


tamaa Owen na kuamini kwamba ingekuwa vigumu kwake kupata nafasi kwa kuwa ni chache na mara nyingi zilikuwa zinatolewa kwa kujuana au rushwa. Meneja mwajiri alianza kuita jina la kijana mmoja badala ya mwingine kwenye chumba cha mahojiano (interview). Aliitwa mmoja badala ya mwingine mpaka pale Owen aliposikia jina lake likiitwa. Owen alijivuta taratibu na kuingia ndani ya ofisi ya Meneja mwajiri. Alipofika tu alitupa macho mbele akajikuta anashtuka baada ya kuona sura


ya Meneja mwajiri. Sio Owen tu, hata Meneja mwajiri alishtuka sana baada ya kuona sura ya Owen. Hakuna mtu aliyetegemea kama wangekuja tena kukutana kwenye mazingira yale. Huwezi kuamini yani, Yule Meneja mwajiri ndo yule mwanamke aliyesaidiwa na Owen kule sokoni baada ya kuporwa mkoba wake na kibaka siku za nyuma. NOVEL.................. MY VALENTINE -33 (Kipenzi Changu)


AUTHOR.…..............HERRY DESOUZER (Silentkiller) SPONSORED BY.......SILENTKILLER STORIES TEL............. 0699470521/0713601762 INSTAGRAM............ @realsilentkiller_ "Ni wewe ama nakufananisha?" Yule Meneja alimuuliza Owen "Bila shaka ni mimi Madame. Naaminii kabisa hujanifananisha.!" Owen alimjibu yule mwanamke.


"Ok, Hebu kaa kwenye kiti kijana wangu.!" Yule Meneja alimkaribisha kiti Owen. Owen alikaa kwenye kiti kisha akatulia kumsikiliza Meneja. "Owen, Kwahiyo na wewe ni mmoja wa vijana waliokuja kwenye interview?" "Ndio.! Mimi ni miongoni mwao.!" "Duh! Kumbe wewe pia ni msomi Owen? Lakini kwanini sasa....


Anyway, tuyaache hayo, Naomba unipatie kwanza academic certificates pamoja na CV zako.!" Meneja alimuomba vyeti Owen. Owen akimkabidhi bahasha yule Meneja kisha akaanza kupitia vyeti vyake pamoja na CV. Yule Meneja alijikuta anashtuka kila alipokuwa anatazama vyeti vya Owen. Alishangaa sana kuona kijana alikuwa na vyeti vinavyoonesha alikuwa na ujuzi na taaluma kubwa sana kwenye suala la teknolojia ya habari na mawasiliano (IT). Kiufupi alikuwa


na uwezo wa kufanya kazi kwenye taasisi yoyote ya kiserikali au binafsi kwa sababu hakuna taasisi isiyokuwa na kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano. Iwe hospitalini, vyuoni, mashuleni, kwenye makampuni na hata jeshini. Owen alikuwa na ujuzi mkubwa kwenye masuala ya kompyuta. Meneja mwajiri alibaki ameduwaa kwa kuwa Owen aliyekuwa anamfahamu yeye alikuwa m'beba mizigo sokoni. Alishangaa sana kuona msomi mwenye Master's degree ya IT


kuwa m'beba mizigo sokoni. Mwisho kabisa Meneja aliamua kumfanyia Owen interview ili aone uwezo wake kwa vitendo. Akimkabidhi kompyuta kisha akamtaka amuoneshe kwa vitendo yale yaliyomo kwenye vyeti. Je ni kweli alikuwa na ujuzi kichwani au ni akili tu za kukariri masomo. Owen alivuta mashine na kuanza kuonesha utaalamu wake kwa vitendo. Kila alichoambiwa kukifanya alikifanya kwa usahihi na weledi mkubwa sana. Alikifanya kwa njia wanayoijua wao na akafanya


kwa njia anayoijua yeye tu kwa utundu wake. Meneja alishangaa sana kuona kijana anaonesha uwezo mkubwa. Kwa hakika Owen aliupiga mwingi mpaka Meneja akafurahia interview. "Owen hivi, unaweza kuniambia kwanini ulikuwa unafanya kazi ya kubeba mizigo ilihali una elimu na ujuzi wa kufanya kazi kubwa kwa manufaa ya taifa kwa ujumla?" "Madame, Aah! Mimi naweza kusema kwamba huu ni uhalisia


tu wa maisha yalivyo kwenye nchi yetu. Mimi ni muwakilishi tu kwani huko mtaani kuna akina Owen wengi sana ambao wana elimu na ujuzi mkubwa lakini wameshindwa kupata nafasi ya kutumia elimu na ujuzi wao kwa faida ya taifa kwa ujumla. Wapo akina Owen wengi sana wanaendesha bodaboda na degree zao za uhasibu, wapo akina Owen wanaosajili laini za simu mitaani na degree zao za uinjinia, wapo akina Owen wanaopiga debe kwenye daladala na degree zao za


uandishi wa habari, wapo akina Owen wanaolima nyanya na degree zao za ualimu, wapo akina Owen wanaouza machungwa na degree zao za udaktari, Na kuna sisi akina Owen tunaobeba mizigo na degree zetu za IT. Kwahiyo basi naomba usishangae mimi kubeba mizigo sokoni maana hayo ndo maisha yalivyo kwenye nchi yetu. Structure nzima ya ajira ndo inapelekea haya yote.!" Owen alimjibu Meneja "Ok, Naona umetumia sana hisia


kujibu swali langu Owen. Bado nauona ule moyo wako wa kujali watu wengine kwenye jamii. Swali lilikuwa upande wako lakini umeamua kuwagusa mpaka wengine wanaopitia changamoto kama zako. Hongera sana kwa kuwa na moyo wa kujali watu wengine. Kiukweli mwanangu una moyo wa kipekee sana. Nafikiri wazazi wako wanajivunia sana kuwa na mtoto kama wewe.!" Meneja alimpongeza Owen. "Madame, Nashukuru sana kwa


maneno yako ya busara.!" "Ok, sasa Owen mimi nimeshamaliza interview na wewe hivyo ni muda wa kuwapisha wenzako waje kuonesha kile walichonacho. Kiukweli kabisa, kampuni yetu ina nafasi tatu tu za kazi kwahiyo nyie wote muliokuja kwenye hii interview munashindania hizo nafasi. Wale watakaobahatika kupata nafasi basi tutawapigia simu na kuwapa maelekezo ya kuanza kazi. Lakini naomba nikuibie tu siri mwanangu, nenda


kajiandae kwa ajili ya kuanza kazi kwenye hii kampuni. Muda wowote tutakupigia simu hivyo hakikisha kuanzia sasa unakuwa hewani. Kiukweli kabisa unastahili kupata nafasi kwenye hii kampuni kwa kuwa una vigezo tunavyovihitaji. Lakini pia kaa ukijua kwamba, licha ya vigezo ulivyokuwa navyo ila kitu kikubwa kilichokupa hii nafasi ni utu uliokuwa nao. Kumbuka kwamba sio kwamba watakaokosa nafasi hawana vigezo tunavyovihitaji, La hasha! Vigezo wanavyo kama wewe lakini kinachokupa


kipaumbele wewe ni utu na uaminifu wako. Nadhani huu ni wakati wako wa kula matunda ya uaminifu wako. Nenda kajiandae kwa ajili ya kazi Mr Owen James.!" Naam! Hivyo ndivyo mambo yalivyokwenda katika ile interview aliyokwenda kuifanya Owen. Owen aliondoka kwenye ile kampuni na kurejea nyumbani kwao huku akiwa na furaha tele moyoni mwake. Alipofika alimueleza kila kitu Laureen wake na wote kwa pamoja


walimshukuru Mungu kwa kile kilichotokea. Japo simu ya kuitwa kazini ilikuwa bado haijapigwa lakini mpaka kufikia hatua ile waliamini kabisa walikuwa kwenye dakika za mwisho za ushindi. Kile kilichotarajiwa kutokea ndicho kilichotokea. Hatimaye baada ya siku moja kupita Owen alipigiwa simu na kuitwa kwenye ile kampuni. Owen alienda kuitikia wito na alipofika tu aliungana na wenzake wawili ambao walipita kwenye ile interview iliyofanyikaga. Uongozi wa


kampuni ulikubali kufanya kazi na vijana wapya waliochaguliwa lakini kabla hawajapewa mikataba ya kudumu walipewa miezi mitatu ya majaribio ili kuangalia ubunifu na uwezo waliokuwa nao. Walitaka kujua kama vijana wanaweza kuwa na mchango kwenye maendeleo ya kampuni au laa. Baada ya majaribio hayo, kwa wale ambao wangeonekana kuwa bora basi wangepewa mikataba ya kudumu na kuajiriwa moja kwa moja. Vijana walioneshwa ofisi zao na kukabidhiwa vitendea kazi


husika. Siku ile ile kazi ilianza. Owen alianza kazi huku akiwa bado anaishi na Laureen wake kule kule uswahilini. Katika kipindi hiko angalau sasa maisha yalibadilika kwa kuwa kila siku Owen alikuwa anapata posho kule kazini. Mtaalamu alimuhakikishia Laureen kwamba baada ya miezi mitatu maisha yao yatabadilika kabisa kwani aliamini ni lazima angepata mkabata wa kuajiriwa moja kwa moja. Alichokifanya Owen ni kuongeza juhudi katika kazi na kutumia maarifa yake yote katika


kubuni vitu mbalimbali vilivyopelekea Kampuni yao iwe juu zaidi kuliko wapinzani wao kwenye idara ya teknolojia. Ndani ya miezi miwili tu tangu Owen alipoanza kazi, teknolojia ya SK GROUP iliimarika na kuwa bora zaidi hali iliyopelekea upatikanaji wa huduma bora na kwa kiwango kikubwa sana. Kampuni ilijikuta inaingiza faida kubwa pamoja na kujipatia umaarufu kuliko hata wapinzani wao. Hiyo yote ilisababishwa na Owen James, kijana aliyezaliwa na kompyuta yake kichwani. Kampuni ya


SOPA's GROUP ambao walikuwa wapinzani wa kampuni ya SK Group walipeleleza ili kumjua mtu aliyekuwa nyuma ya mafanikio na maendeleo ya teknolojia ndani ya kampuni ya SK Group. Waliwatuma wapelelezi na walipofuatilia kwa umakini walikuja kumjua mtu aliyekuwa nyuma ya yale maendeleo. Kamera zao zilimnasa Owen na walipofuatilia kwa umakini kuhusu Owen waligundua kwamba kijana alikuwa mfanyakazi mpya kwenye ile kampuni na habari


njema ni kwamba bado alikuwa hajapewa mkataba wa kazi. Wapinzani waliona watumie njia za mkato ili kuhakikisha wanamchukua Owen na kumsainisha mkataba kwenye kampuni yao. Mpaka kufikia muda huo tayari walishapafahamu kule uswahilini alipokuwa anaishi Owen hivyo mabosi wa SOPA's GROUP waliamua kufunga safari na kumtembelea Owen. Owen alijikuta anawapokea wageni wa ghafla kule uswahilini alipokuwa anaishi. Watu wazito


walimtembelea na kumueleza dhamira yao ambayo ni kutaka kufanya kazi pamoja katika kampuni yao. Walimuahidi kumpa mkataba wa kudumu wenye mshahara mnono pamoja na marupurupu kila wiki. Lakini pia walimuahidi kumpa nyumba pamoja na gari la kutembelea. Owen alijikuta anavuta pumzi mzito juu ya ile ofa aliyopewa. Alichokifanya ni kutumia busara na kuwaambia wale watu wampe muda wa kufikiria juu ya ofa yao. Hakutaka kufanya maamuzi ya haraka bila kuwashirikisha watu


ambao walianza kumsaidia na kumfanya aonekane bora. Hata Laureen alimshauri mpenzi wake asikurupuke kukimbilia ofa ya SOPA's GROUP kabla hajasikiliza ofa ya SK Group ambao walimtoa kwenye mchanga na kumfanya aonekane. Owen alitaka kusubiri ile miezi mitatu ya majaribio iishe ili awasikilize mabosi wake watamwambia nini. Wale watu wa SOPA's GROUP waliondoka na kumwambia Owen muda wowote watakuwa tayari kumpokea. Kwa wakati ule Owen alikuwa kama dhahabu ambayo


kila mtu aliihitaji kuipata. Hata kwenye kampuni ya Mr Jay Calvin kulikuwa na pengo kubwa sana lililoachwa na Owen. Tangu Owen alipoondoka, kile kitengo cha teknolojia ya habari kilikuwa dhoofu mno. Mr Jay Calvin alikuwa anahangaika kuitafuta namba ya simu ya Owen ili amrudishe kwenye kampuni yake lakini hakuipata. Kwa wakati ule Owen alikuwa amebadilisha namba ya simu. Tukirudi upande wa kampuni ya SK Group, kumbe wakati SOPA's GROUP wanamvizia Owen na kufanya


nae mazungumzo ili wamnyakue, kuna watu wao walikuwa wanafuatilia kwa umakini lile suala. SK Group walishajua kila kitu kilichokuwa kinaendelea kati yao na Owen hivyo waliamua kufanya jambo kwa ajili ya kuhakikisha Owen hachukuliwi na wapinzani wao. Siku iliyofuata Owen alipofika tu kazini alikutana na mkataba mezani. Alipewa kwanza ausome kwa umakini kabla hajashusha saini. Kwa hakika Owen alishtuka sana baada ya kukuta kampuni imeamua kumpa mkataba


mnono sana wenye mshahara mkubwa tena ni mara mbili zaidi ya ule aliokuwa ameahidiwa na mabosi wa SOPA's GROUP. Mkataba ule ulikuwa na marupurupu mengi ndani yake huku pembeni yake kukiwa na kipengele cha kupewa nyumba na gari la kisasa kwa ajili ya kuendea kazini na kutembelea. Owen hakutaka kupoteza muda kuusaini ule mkataba. Aliutia saini ule mkataba huku taswira ya Laureen ikimjia kichwani. Chozi la furaha lilimtoka na kudondokea kwenye karatasi ya


mkataba aliokuwa anausaini. Mtaalamu alijisemea tu moyoni, "Kwa hakika wakati wa Mungu ndo wakati sahihi kwa kila ndoto ya mwanadamu.! Laureen mke wangu, hii ni kwa ajili yako wewe.! Ni wakati sasa wa mimi hapa kukununulia mawigi, simu na pochi zenye thamani ili na wewe ukawaringishie mke wangu. Sasa unakwenda kutembelea usukani, kwahiyo ni wakati wako wa kuwafungia vioo wale wote waliokudharau kipindi ulichokuwa unatembea kwa


miguu huku ukiwa na ndoo ya samaki kichwani.! Tuliteseka wote na sasa tutafurahi wote mke wangu.!" Owen alijisemea maneno hayo huku akitokwa na machozi ya furaha. NOVEL.................. MY VALENTINE -34 (Kipenzi Changu) AUTHOR.…..............HERRY DESOUZER (Silentkiller) SPONSORED BY.......SILENTKILLER STORIES TEL.............


0699470521/0713601762 INSTAGRAM............ @realsilentkiller_ Hatimaye Mwenyezi Mungu aliamua kumulika nuru na kuwaangazia Owen na Laureen waliokuwa kwenye maisha ya kiza. Baada ya subra ya muda mrefu hatimaye Mungu aliweza kuwafunulia ukurasa mpya waliokuwa wanatamani kuufikia. Mpaka kufikia hatua ile ilikuwa vigumu sana kwa binadamu yeyote kutumia nguvu ya kawaida ili kumuharibia kazi


Owen kwani ujuzi na utashi wake ulikuwa unahitajika kwenye makampuni mengi. Pengine ni nguvu za kiza tu ndo zilikuwa na uwezo wa kumkwamisha Owen kufanya kazi yake. Owen alimfikishia taarifa ile Laureen na kumwambia wajiandae kwa ajili ya kuhamia kwenye makazi mapya. Kwa hakika ilikuwa taarifa njema sana kwa mwanadada Laureen. Mtoto wa kike hakuamini kile alichokuwa anakisikia kutoka kwa Owen. Alijikuta tu anashindwa kuzuia machozi kutiririka kutoka kwenye


mboni zake. Yalikuwa ni machozi ya furaha na pengine ile ilikuwa ni miongoni mwa furaha kubwa alizowahi kukutana nazo kwenye maisha yake. Mtoto wa kike alimkumbatia Owen huku akiendelea kutoa machozi ya furaha. Hata Owen nae alijikuta anatokwa na machozi kutokana na mazito waliyoyapitia mpaka kufikia muda ule. "Laureen mke wangu, Ile siku ulipokuwa unamjibu Juliette kuhusiana na ile ofa yake nilisikia kila kitu. Nilisikia ukimwambia


Juliette huwezi kupokea ofa yake kwa sababu unanipenda sana mimi. Nilisikia ukimwambia haijalishi itachukua muda gani lakini utanisubiri nipate pesa ili nikupeleke masomoni. Laureen mke wangu, hatimaye sasa subira yako imefikia katika kilele. Zile pesa tayari nimezipata mimi. Sasa ni rasmi utaingia darasani ili kutimiza ndoto zako. Utasoma kwa pesa zako mwenyewe na sio za Juliette wala mtu mwingine.!" Ndani ya siku tatu mchakato mzima wa kuhama makazi


ulikamilika. Hatimaye Owen na Laureen walihama kule uswahili na kuhamia maeneo ya ushuani kulipokuwa na nyumba nyingi za watu maarufu. Kampuni iliamua kumpangia Owen nyumba moja ya kifahari yenye fenicha na huduma zote ndani yake. Lakini pia walimkabidhi gari la kisasa kwa ajili ya kuendea kazini na kutembelea. Owen na Laureen walijikuta mjengoni kwa mara nyingine tena. Kule uswahilini walipotoka waliacha somo kubwa kwa wapangaji waliokuwa wanawadharau siku zote.


Hakuna chombo walichoondoka nacho hivyo vitu vyote walivigawa kwa majirani zao. Wao waliondoka na nguo zao tu na kwenda kuanza upya kununua kitu kimoja kimoja. Ni rasmi sasa Owen na Laureen walianza kuishi maisha ya kula chochote walichokuwa wanakitaka. Owen aliendelea kufanya kazi kwa weledi mkubwa sana ndani ya kampuni ya SK Group na ulipofika mwisho wa mwezi alipokea mshahara wake kama walivyokubaliana kwenye mkataba. Mshahara wa kwanza


ule ule Owen aliamua kumlipia Laureen ada ya kujiunga na chuo. Laureen alianza rasmi safari yake ya masomo ya chuo katika ngazi ya Diploma (Astashahada) kwa masomo ya afya. Ndoto kubwa ya mtoto wa kike ilikuwa ni kuwa Daktari hivyo alianza rasmi safari yake kuelekea kwenye dunia ya ndoto zake. Wakati Owen anaenda kazini, Laureen alikuwa anaenda chuoni. Ilibidi tu wamtafute msichana wa kuwasaidia kufanya shughuli za nyumbani ikiwa ni pamoja na kutunza nyumba. Hivyo ndivyo


maisha yalivyokwenda kwa wawili wapendanao. Mabadiliko ya kipato hayakuweza kubadili tabia za mtu yeyote kati yao. Bado waliendelea kupendana kama ilivyokuwa hapo awali. Pesa zilimrudisha tena Owen kwenye muonekano wake wa siku zote hivyo bado aliendelea kukutana na changamoto ya kupendwa na wanawake kule kazini. Licha ya kupendwa lakini aliendelea kuwa na msimamo na kuwaambia kwamba nyumbani kwake alikuwa na mke. Lakini pia pesa ilimfanya Laureen anawiri


na kuzidi kuwa mzuri zaidi ya hapo awali. Kule chuoni alipokuwa alikutana na vishawishi vingi sana kutoka kwa wanafanzi wenzake wa kiume pamoja na walimu wake. Licha ya vishawishi alivyokutana navyo lakini aliweka msimamo thabiti na kuwaambia kabisa yeye ni mke wa mtu na anampenda sana mume wake. Kiukweli kabisa ilikuwa vigumu sana kwa Laureen kumsaliti Owen kwa sababu kama aliweza kukwepa vishawishi kipindi ambacho Owen hakuwa na pesa,


angewezaje kumsaliti kipindi ambacho amepata pesa. Laureen aliamua kusoma kiutu uzima huku akiwa na uchungu wa kukipata kile kilichompeleka chuoni. Alisoma kwa bidii sana huku akiendelea kutimiza wajibu wake kama mke wa Owen. Bado walikuwa na fikra ya kufunga ndoa lakini walisubiri muda ufike ili ndoa yao ipate idhini na ridhaa ya wazazi. Wenyewe walikuwa wanajua nini wanakifanya kwa wakati huo. Katika kipindi hiko cha maisha, Owen hakutaka kuwa na mawasiliano na wazazi


wake wala kaka yake Robyson. Mtu pekee aliyekuwa na mawasiliano na Owen ni Catherine tu na mawasiliano yao yalikuwa ya siri mno. Owen aliweza kumpata Catherine na kumpatia namba yake ya simu mpya kwa ajili ya kumpa taarifa za nyumbani kwao. Haikuwa ngumu kwa Owen kumpata Catherine kwa kuwa alikuwa anafahamu shule aliyokuwa anasoma. Kwa kipindi hiko Catherine alikuwa amebakisha siku chache tu kuingia katika mtihani wake wa mwisho wa


kidato cha sita. Hiyo ndo hali halisi ya maisha ilivyokuwa kwa wanafamilia. Siku zilisonga, wiki zikayoyoma, miezi ikapita na miaka ikakatika. Hatimaye ilipita takribani miaka saba. Ni miaka saba ilipita tangu Owen alipoajiriwa kwenye ile kampuni ya SK Group na Laureen kuanza masomo katika ngazi ya Diploma (Astashahada). Kubadilika kwa tarehe, miezi na miaka kulipelekea mabadiliko makubwa sana kwenye maisha ya watu. Umri na status za maisha zilibadilika kwa kiasi kikubwa


sana. Wapo waliokuwa wamepanda kimaisha na wengine walishuka. Tukianza na Catherine, tayari alishahitimu shahada (Degree) yake ya ualimu katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Lakini sasa, kutokana na masuala ya ajira kuwa changamoto, Catherine hakupata bahati ya kuajiriwa. Mtoto wa kike hakutaka kukaa nyumbani kusubiri ajira hivyo aliomba mtaji kwa wazazi wake na kwenda kufungua duka la nguo za watoto katikati ya jiji. Robyson na Diana wao waliendelea kuishi kwenye


ndoa na tayari walibahatika kupata mtoto wa kike ambaye alishatimiza miaka sita. Mtoto huyo alichagua kusadifu sura ya baba yake mdogo, Owen. Ni vile tu alikuwa wa kike, lakini kama angekuwa wa kiume basi watu wangehisi yule ni Owen ila aliamua tu kurudi utotoni. Hakuna mwanafamilia ambaye alishtuka kuona mtoto wa Robyson kusadifu sura ya baba yake mdogo badala ya wazazi wake. Waliona kawaida kwa kuwa Owen na Robyson walifanana kwa kiasi fulani na


pia ni kawaida sana kwa mtoto kutosadifu sura za wazazi wake na kusadifu sura ya mtu mwingine kwenye ile familia. Lakini sasa, katika kipindi hiko cha miaka saba mambo yalikuwa mabaya sana kwa Robyson katika upande wa siasa. Kulikuwa na uchaguzi mkuu ndani ya nchi na yeye alikuwa mmoja kati ya wagombea wa nafasi za ubunge. Lakini sasa, kwa bahati mbaya hakufanikiwa kuchukua Jimbo. Alijikuta anashindwa katika uchaguzi ule na kufanya zile ndoto zake za


kuwa Rais wa nchi kwa miaka ijayo kuyeyuka mazima. Kwa hakika lilikuwa ni pigo kubwa sana upande wake kwani alitumia pesa nyingi sana kwenye kampeni lakini mwisho wa siku alifeli. Kufeli kwa Robyson kwenye uchaguzi, kulimfanya Diana ajutie hata maamuzi yake ya kumuacha Owen na kuolewa na Robyson. Diana aliolewa na Robyson kwa lengo la kutaka kuwa mke wa kiongozi mkubwa nchini. Lakini sasa, kile alichokitarajia tayari kilishafeli na mbaya zaidi alikuwa anakosa


amani kila alipokuwa anamtazama mwanae. Ni kama alikuwa na siri nzito iliyomtesa moyoni juu ya binti yake aliyefahamika kwa jina la Careen. Lakini pia ile miaka saba haikumuacha salama Robyson tu, hata yule aliyesema hawezi kukosa uongozi kisa kura ya kahaba mmoja na kuamini kwamba pesa zake ndo zitampa nafasi ya uongozi, hatimaye alikosa kiti cha uraisi. Alikosa kiti kwa utofauti wa kura moja tu dhidi ya mpinzani wake. Ni kama vile Mwenyezi Mungu alijaribu


kumkumbusha Mr James kwamba mtu yeyote kwenye dunia haijalishi ni maskini, fukara, kahaba ama kichaa basi anaweza kuwa na mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yake. Pengine labda kama kahaba mmoja (Laureen) angempigia kura Mr James basi mzani wa matokeo ya uchaguzi ungekaa katikati. Mr James alijikuta anapata pigo zito sana kufuatia kushindwa katika uchaguzi. Chama chao kilishindwa kabisa kuking'oa madarakani chama tawala.


Kushindwa kwa Mr James kulipelekea anguko kubwa la kiuchumi katika familia. Pesa nyingi sana alizitumia katika kampeni zake huku akiwa na matumaini angezirudisha punde tu akiingia madarakani. Pesa nyingi alikopa kwenye taasisi za mikopo pamoja na kwa wafanyabiashara aliokuwa karibu nao ambao ni Mr Jay Calvin pamoja na Mr Evrat Gonzalo. Shida ilikuja kuibuka mwaka mmoja tu baada ya uchaguzi kupita ambapo zile taasisi za mikopo zilipohitaji pesa zao. Kwa


wakati huo tayari Mr James alikuwa ameshayumba tayari kiuchumi hivyo hakuwa na pesa ya kutosha kulipa madeni yote. Baada ya kuvumiliwa kwa kipindi kirefu bila kurejesha madeni, hatimaye Mr James alipewa mwezi mmoja tu wa kulipa madeni na kama angeshindwa basi nyumba yake ingekuwa sokoni. Tukirudi upande wa Laureen na Owen kwa hakika miaka saba ilikuwa ya baraka sana upande wao. Laureen alifanikiwa kutimiza ndoto zake za kuwa Daktari na tayari


alishapata ajira katika hospitali kuu ya Taifa. Alitumia miaka miwili kuhitimu masomo ya ngazi ya Astashahada (Diploma) na baadae alijiunga na masomo ya ngazi ya shahada (Degree) ambayo ilimchukua tena miaka minne kuhitimu ngazi hiyo. Ni takribani miaka sita alitumia kusomea udaktari na ulipofika mwaka wa saba aliajiriwa na kuanza kazi rasmi. Kama unavyojua mishahara ya madaktari ilivyo, Laureen alijikuta anamiliki pesa ndefu katika mkono wake. Upande wa Owen


mambo yaliendelea kuwa mazuri tangu alipoajiriwa kwenye ile kampuni ya SK Group. Tayari alishapandishwa cheo na kuwa mkuu wa idara katika kile kitengo alichokuwa anafanya kazi. Mshahara wa Owen ulikuwa unaongezeka kadri miaka ilivyozidi kukatika. Bado Owen na Laureen waliendelea kuishi kwenye nyumba moja kama mke na mume na mpaka kufikia muda huo tayari Laureen alikuwa na ujauzito wa miezi miwili. Wapenzi hao walikuwa miongoni mwa watu wenye pesa ndefu


sana ndani ya jiji. Tayari walishajenga nyumba kubwa ya kifahari na kutembelea magari yao. Lakini pia walikuwa wanamiliki miradi mikubwa sana ndani ya jiji. Walitumia mishahara yao kuwekeza kwenye maduka ya vifaa vya urembo na vipodozi, nguo, mikoba, viatu vya kike, saluni za kisasa za kike pamoja na hoteli na migahawa. Miradi yote iliwekezwa ndani ya majiji mawili ambayo ni Dar es salaam na Mwanza. Waliwatafuta vijana waaminifu kisha wakawaajiri kwenye


biashara zao. Owen na Laureen waliunganisha majina yao na kutengeneza brand waliyoitumia kwenye miradi yao yote. "OLA" ndo jina lililosomeka kwenye maduka na hoteli zao zote. OLA ni kifupi cha jina la Owen na Laureen. Kulikuwa na OLA's Hotel & Restaurants, OLA's Beauty & Cosmetics shops, OLA's Outfit and Classic Wear, OLA's Home Of Queens Shoes na kadhalika. Lakini sasa, hakuna ndugu yeyote wa Owen aliyekuwa anafahamu mmiliki wa ile brand. Ni Wafanyakazi tu waliokuwa


wameajiriwa kwenye ile miradi ndo walikuwa wanawajua mabosi wao na tafsiri ya neno OLA. Hivyo ndivyo maisha yalivyokuwa ndani ya miaka saba. Wale waliodhaniwa wangefeli ndo walifaulu na wale waliodhani wangefaulu ndo walifeli. NOVEL.................... MY VALENTINE- 35 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY


DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ Taarifa za Mr James na Robyson kushindwa katika uchaguzi mkuu, Owen alikuwa anazifahamu vyema sana kwa kuwa matokeo ya uchaguzi yalikuwa wazi kwa kila raia. Maumivu waliyoyapataga


wanafamilia hata Owen yalimpata kwa kiasi kile kile. Mtaalamu alijua kabisa wazazi wake pamoja na kaka yake walitumia nguvu na pesa nyingi sana kuwekeza kwenye ule uchaguzi hivyo kufeli kwao kulipelekea anguko kubwa sana kwenye familia. Owen hakuwahi kabisa kuomba mabaya yatokee kwenye familia yake licha ya kwamba aliondoka bila maelewano mazuri. Siku zote alikuwa anawatakia mema wazazi wake ili wazidi kusongesha gurudumu la familia.


Lakini pia licha ya kaka yake Robyson na mkewe Diana kuonesha chuki dhidi yake ila siku zote alikuwa anawaombeaga bahati njema kwenye harakati zao za maisha. Suala la nyumba ya Mr James kuwa kwenye hatihati ya kutaifishwa ili kulipia madeni, Owen alikuwa halifahamu kabisa. Alikuja kujua siku za mwisho kabisa kabla nyumba haijapigwa mnada. Alilijua suala lile baada ya kuambiwa na mdogo wake Catherine. Siku hiyo Catherine aliamua kumtafuta


Owen kwenye simu na kumfahamisha kila kitu kilichokuwa kinaendelea. "Kaka Owen, Wewe hapo na wifi yangu ni wazima kaka?" "Yeah! tupo vizuri kabisa dada, vipi wewe, Sharon na wazazi wetu hawajambo?" "Sisi wote ni wazima kaka japo baba akili yake haijakaa sawa kutokana na mawazo. Kiukweli kabisa kwa sasa familia yetu ipo kwenye wakati mgumu sana


kaka. Kumbe baba ana madeni makubwa sana na ameshindwa kuyalipa kwa muda mrefu sasa. Hivi navyokuambia amepewa mwezi mmoja tu kulipa madeni yote na kama atashindwa basi hii nyumba yetu itakuwa mnadani kaka.!" "What?" "Ndo hivyo kaka.! Huo ndo uhalisia wa maisha ulivyo sasa hivi. Muda wowote kuanzia sasa tutaenda kuishi kwenye vyumba vya kupanga. Na kwa namna


Baba alivyokuwa na mawazo nahisi kabisa anaweza kupata uchizi. Na mama nae sijui kama ile presha aliyonayo haitomletea shida.!" Hivyo ndivyo Owen alivyoipokea taarifa ya mambo yalivyokuwa nyumbani kwao. Mtaalamu alishtushwa sana na ile taarifa. Hakutegemea kabisa kama maisha yao yangebadilika mpaka kufikia hatua ile. Siasa iliweza kujenga maisha yao na siasa hiyo hiyo ilikuwa inakaribia kubomoa maisha yao. Mtaalamu


alijikuta anawaza kwa marefu na mapana juu ya maisha yatakavyokuwa kwa wazazi wake endapo ile nyumba ingeuzwa. Aliwaza namna ya kuikomboa nyumba yao pamoja na mali zingine licha ya kwamba jina lake lilishaondolewa kwenye kitabu cha urithi wa zile mali. "Kaka Owen, Lakini kwanini usirudi nyumbani kuja kutuona sisi? Miaka mingi imepita sasa au unahisi bado wazazi watakuwa na ugomvi na wewe?"


"Catherine mdogo wangu, hivi unahisi kwa sasa Baba na mama hawana hasira na mimi?" "Nahisi hivyo kaka.! Kiukweli kabisa Mama anakukumbuka sana kaka. Mara nyingi amekuwa mtu anayekutaja sana na naamini kabisa ndani ya moyo wake anakuombeaga dua njema licha ya kwamba alikutolea radhi. Ni kama vile mpaka sasa ana mgogoro wa nafsi kila akikumbuka maneno yake juu yako. Ukweli ni kwamba Mama alikuwa anatupenda sana watoto


wake, Ila wewe ndo alikuwa anakupenda na kukupendelea. Au umesahau kaka? Umesahau namna mama alivyokuwa anakupenda zaidi ya sisi wengine? Fanya urudi kaka, Mama anaku-miss sana mwanae.!" "Catherine mdogo wangu, kiukweli kabisa tangu nimeondoka nyumbani, mateso makubwa niliyokutana nayo mtaani na ambayo bado naendelea kukutana ni kumkumbuka mama pamoja na


ninyi hapo ndugu zangu. Kiukweli kabisa nam'miss sana mama, nam'miss sana mdogo wangu Sharon, nam'miss sana mzee wangu, nam'miss sana kaka Robyson na mwisho kabisa naku-miss sana wewe hapo dada yangu kipenzi. Kiukweli kabisa natamani kuwa pamoja na kushirikiana na nyie ndugu zangu. Natamani kuendelea kuona wazazi wangu wanajivunia uwepo wangu mimi. Huku nilipo kwa miaka yote naendelea kupambana huku nikijua kwamba kuna watu wananisubiri


nyumbani. Nitarudi dada nitarudi. Endeleeni kunisubiri nitarudi.!" "Lakini kaka Owen, jitahidi basi kaka yangu usichelewe tafadhali. Au unataka kuja siku ya kuwazika wazazi wako? Jitahidi urudi mapema kaka, hawa wazee hawatakiwi kufa kabla hawajafanya kitu kwa ajili yako. Ni lazima mumalize tofauti zenu either wewe uwaombe msamaha au wao wakuombe msamaha. Ni lazima mmoja kati yenu aombe msamaha ili kumaliza haya mabala yanayoendelea kwenye


hii familia.!" "Catherine, kile kilichonitoa nyumbani na kunileta huku mtaani tayari nimeshakikamilisha. Muda wowote kuanzia sasa nitarudi hapo nyumbani na nitakuwa tayari kuomba amani baina yangu na wazazi. Kama wazazi bado wataendelea kuamini mimi nilichagua njia isiyosahihi basi nitawaomba msamaha. Na kama njia yangu itakuwa sahihi basi sitohitaji waniombe msamaha bali nitawashukuru kwa kuwa


wao ndo walinionesha hii njia niliyopita. Nisubiri dada, nitarudi nyumbani muda si mrefu.!" Hayo yalikuwa mazungumzo kati ya Owen na mdogo wake Catherine. Mazungumzo hayo yalifanyika kwa njia ya simu. Mazungumzo hayo yalimfanya Owen atoe machozi baada ya kukumbuka maisha ya nyuma aliyoishi na wazazi wake. Alikumbuka sana ule upendo wa mama yake tangu alipokuwa mdogo mpaka kufikia umri wa utu uzima. Ni kweli kabisa Owen


ndo alikuwa mtoto aliyekuwa anapendwa sana na mama yake. Lakini pia aliwaza namna ya kukabiliana na lile suala la kutaifishwa nyumba yao ambayo Mr James aliiwekeaga rehani na kuitumia kama nyenzo ya kupatia mkopo. Wakati Owen anawaza namna ya kuikomboa nyumba yao, hata Robyson alikuwa kwenye mchakato wa kuikomboa hiyo nyumba. Mtu pekee ambaye aliamini angeweza kumsaidia katika lile ni Mr Jay Calvin ambaye ndo alikuwa Baba mkwe wake. Alijaribu kuongea nae


lakini Baba mkwe hakuwa tayari kutoa pesa zake kwa ajili ya kutatua tatizo lile. Kwanza kabisa Mr Jay Calvin alikuwa na hasira sana baada ya Robyson kushindwa kwenye uchaguzi mkuu. Kuna pesa nyingi sana alimpatia Robyson ili azitumie kwenye kampeni zake kuelekea uchaguzi lakini mwisho wa siku walidondokea pua. Mr Robyson alikula hasara kubwa na pia yale malengo yake ya kutaka kuwa Baba mkwe wa kiongozi mkubwa serikalini yalifeli. Kwa namna fulani alijuta kumuozesha Binti


yake kwa Robyson. Kwa hakika kile ndo kilikuwa kipindi ambacho Mr James alipata somo kubwa sana kwenye maisha yake. Sasa alielewa kwamba hakuna faida anayoipata mzazi kwa kumuozesha mwanae kwenye familia ya kitajiri. Mwanzo aliamini kama mwanae akioa kwenye familia yenye kipato kizuri basi ingekuwa rahisi kwake kupata msaada kutoka kwa wakwe wa mtoto wake. Kile alichotegemea kutoka kwa wakwe wa mtoto wao Robyson


sicho kabisa walichokipata. Mr Jay Calvin hakuwa tayari kutatua shida za Mr James. Mpaka kufikia siku moja kabla ya tarehe ya mwisho ya kulipa deni, Mr James alikuwa hajapata tumaini lolote la kulipa deni. Ni dhahiri kabisa Mheshimiwa alishakata tamaa na hakuona njia yoyote ya kuweza kuikomboa nyumba yake isipigwe mnada. Aliwaza sana kuhusu aibu ambayo ingemkuta mara baada ya nyumba yake kupigwa mnada. Ile brand ambayo hakutaka ichafuliwe na Binti kutoka kwenye familia ya


kimaskini hatimaye ilikuwa inaelekea kufa mazima. Siku hiyo walienda wanasheria kutoka serikalini pamoja na watu wa kampuni aliyochukuaga mikopo kisha wakamwambia ikiwa tarehe itabadilika kabla hajaweka pesa kwenye akaunti ya kampuni iliyokuwa inamdai basi siku inayofuata hawatakiwi kubaki kwenye ile nyumba. Wakusanye kila kilichokuwa chao kisha waondoke wakatafute makazi mapya. Ile nyumba isingekuwa mali yao tena bali ingekuwa mali ya kampuni. Walipewa tahadhari


mapema ili kuepuka usumbufu siku inafuata. Ikawa hivyo na siku iliyofuata ilipofika tu Mr James na familia yake walianza kujikusanya ili wahame rasmi kwenye ile nyumba na kwenda kutafuta makazi mapya kwenye nyumba za kupangisha. Hata Robyson na Diana walikuwa kwa Mr James muda ule wakiwasaidia wazazi wao kutoa fenicha ndani ya nyumba. Wakati wanaendelea kupanga vitu vyao vya ndani, Ghafla Mr James alipokea meseji kwenye simu yake. Alipoifungua ile meseji


alishtuka sana mzee mzima. Alishtuka baada ya kukutana na ujumbe kutoka kwenye ile kampuni aliyokuwa anadaiwa. Ujumbe ule ulikuwa wa kumpa pongezi kwa kufanikiwa kulipa deni lote alilokuwa anadaiwa na kampuni. Mr James hakuamini macho yake, alihisi labda ni wenge tu hivyo alimpa simu Robyson aisome ile meseji. Robyson alipoisoma ile meseji nae alishtuka. Hata yeye aliona kile kile alichokiona Mr James. "Mzee, deni lako lote limelipwa.!"


Robyson alizungumza kauli hiyo na kuwafanya wanafamilia wote kushtuka baada ya kusikia deni limelipwa. Dakika zile zile simu ya Mr James iliita na alipopokea alisikia sauti ya mfanyakazi wa kampuni aliyokopa mikopo ikiimpa hongera kwa kulipa deni na kumtaka aendelee kufurahia huduma za mikopo. Baada ya maongezi hayo simu ikakatwa. Mr James aliamua kuingia mtandaoni kwenye akaunti yake ya mikopo akakutana na ujumbe


mpya kwamba kampuni ya mikopo imepokea kiasi cha pesa kutoka kwa OLA TRADERS LIMITED kwa lengo la kulipa deni lake Mr James. Hapo sasa kabla ya kufurahi ilibidi kila mwanafamilia aanze kujiuliza maswali kichwani. Kwanini OLA TRADERS wamemlipia deni Mr James? Wamelipa lile deni kwa dhamira ipi? Wao walikuwa wanaifahamu sana ile brand ya OLA kwa kuwa ofisi zake zilizagaa pande zote za jiji. Ilibidi sasa wanafamilia wamuulize Mr James kuhusu mahusiano yake


na OLA. Mr James alisema hana mahusiano yoyote na huyo mtu wala hawajuani kabisa. Wote sasa wakabaki wanatazamana huku wakitafakari kuhusu mfanyabiashara OLA. Kila mtu aliwaza OLA ni nani na kwanini alimlipia deni Mr James. Alilipa deni kwa dhamira ipi. Wakati wanaendelea kutafakari, Ghafla walisikia sauti ya honi ya gari getini kwao. Mlinzi alifungua geti na lilionekana gari moja la kifahari likiingia ndani ya nyumba ya Mr James. Kila mwanafamilia alitupa macho kwenye mlango


wa geti kulitazama lile gari na kutaka kujua ni nani aliyekuwa anawasili nyumbani kwao muda ule. Wakati wanatazama, macho ya kila mtu yalitua kwenye plate number ya gari iliyokuwa na jina la 'OLA'. Hapo sasa walijua OLA ambaye alilipa deni la familia ndo mtu aliyekuwa anawasili muda ule. Macho na masikio ya kila mtu yalikuwa kwenye gari kusubiri kumuona huyo OLA akiteremka ndani ya gari. Ile fumba macho na kufumbua, milango ya mbele ya gari ilifunguka. Upande wa kulia


alitoka Owen, kushoto akatoka Laureen huku wote wakiwa wamevaa miwani nyeusi. Aisee, kila mtu aliyekuwepo ndani ya nyumba alihamaki na kupigwa na butwaa. Hakuna aliyeamini kile alichokuwa anakiona muda ule. NOVEL.................... MY VALENTINE- 36 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY......


SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ ____ "Kaka Ooowen.!" Sharon alimuita Owen kwa mshangao kisha akamkimbilia na kumkumbatia. Lilikuwa ni kumbatio la hisia kwa ndugu wawili waliokuwa wanapendana sana. Ni takribani miaka saba tayari ilishapita


tangu ndugu hao walipoachana. Kipindi hiko Sharon alikuwa mdogo mdogo tu na alikuwa anasoma shule ya msingi. Hatimaye sasa aliongezeka umri kwa kiasi fulani na tayari alishahitimu shule ya msingi na kufanikiwa kuingia sekondari. "Kaka Owen, ulikuwa wapi wewe? Ulikuwa wapi kaka? Nilikumiss sana eti.! Nilikumiss sana mimi.!" Sharon aliongea maneno hayo huku akitokwa na machozi. "Sharon mdogo wangu.! Usijali


kaka yako nimerudi tena nyumbani. Naona kabisa umeshakuwa mkubwa mdogo wangu. Nilikuacha mdogo ila sasa umeongezeka kimo na umezidi kuwa mzuriii.!" Owen alimjibu Sharon maneno hayo huku akimfuta machozi yaliyokuwa yanamtiririka. Muda ule Catherine nae alikuwa amemkumbatiana na Laureen huku wote wawili wakitokwa na machozi ya furaha. Ni muda mrefu ulikuwa umepita bila wawili hao kuonana. Ikumbukwe


kwamba wawili hao walishakuwaga marafiki wakubwa tena wa kutunziana siri kabisa. Mr James, Mrs James, Robyson na Diana walibaki wameganda kama mishumaa huku wakiwa hawaamini macho yao kwa kile walichokuwa wanakishuhudia. Mpaka kufikia muda ule hakuna mtu kati yao ambaye alihitaji Google au kamusi ili kupata jibu la swali walilokuwa wanajiuliza juu ya OLA. Tayari kila mtu alishaelewa OLA ni nani na kwanini alilipa deni la Mr James. Pale pale Mr


James alijikuta anapandwa na presha kisha akadondoka chini. Wanafamilia waliweza kumuona Baba mwenye nyumba amedondoka chini hivyo waligeuza macho na akili zao kwa mzee mzima. Chap chap Owen na Robyson walimnyanyua Mzee kisha wakamuingiza kwenye gari kwa ajili ya kumuwahisha hospitali. Safari ilianza kuelekea hospitali huku Robyson akiwa amekamatia usukani wa gari. Nyuma ya gari kulikuwa na Owen na mama yake ambao walimpakata Mr James


aliyekuwa mgonjwa. Wakiwa kwenye gari, Owen alikuwa anajaribu kumuongelesha Baba yake kwa maneno ya kumtia nguvu ili asife na kuiacha familia. Maneno ya Owen kwa Baba yake yalikuwa na tafsiri pana sana ya upendo mpaka mama yake alijikuta anadondosha machozi. Sio mama tu, hata Baba mwenyewe ambaye ndo alikuwa mgonjwa alijikuta anatokwa na machozi huku akijaribu kuinua mkononi ili auguse uso wa Owen. Mr James alijitahidi kuinua mkono lakini kabla hajaigusa


sura ya Owen alijikuta anakosa nguvu na kupoteza fahamu. Wakati Robyson akiendelea kukanyaga mafuta kumuwahisha Mzee hospitali, Nyuma yao kulikuwa na gari lingine lililokuwa linaendeshwa na Diana ambaye aliwapakiza Laureen, Catherine na Sharon ambao waliunga tela kuelekea kule kule hospitali. Safari yao ilikuwa ni kwenda katika hospitali ya taifa na baada ya mwendo wa dakika kadhaa walifanikiwa kufika hospitalini. Punde tu walipofika walipokelewa na madaktari kisha


mgonjwa akaingizwa fasta kwenye chumba cha matibabu. Dakika zile zile Laureen alizama kwenye chumba fulani walichokuwa wanakitumia madaktari kubadili mavazi yao kabla na baada ya kazi. Baada ya kuzama kwenye kile chumba hakuchukua hata dakika moja aliibuka akiwa na mavazi yake ya kazi. Japo kile kipindi alikuwa na likizo fupi lakini aliamua kuingia mwenyewe kwenye matibabu ya Mr James. Aliwataka wanafamilia wakae nje kisha yeye na madaktari wengine


waendelee kumtibu mgonjwa wao. Kitendo cha cha Laureen kuonekana na mavazi ya kidaktari huku akiwa na vifaa vya matibabu mkononi mwake kilifanya wanafamilia wote kushtuka kwa mara ya pili. "Eti? Laureen ni Daktari?" Hilo ndo swali ambalo kila mmoja alijiuliza huku akiwa mdomo wazi asiamini kile alichokuwa anakishuhudia. Ilikuwa vigumu sana kuamini kwamba Laureen alikuwa Daktari


katika hospitali kubwa ya Taifa, Muhimbili. Mama Owen ndo aliongoza kuduwaa kwa kile walichokuwa wanakiona. Ni kama vile alikuwa ndotoni anaota maana ilikuwa vigumu sana kwake kuamini yule kahaba wa kimaskini na asiyekuwa na elimu eti amekuwa Daktari. Kwa hakika yalikuwa ni zaidi maajabu ya Mussa kuigawanya bahari kwa fimbo. Laureen pamoja na madaktari mwenzake walimshughulikia Mr James na baada ya nusu saa zoezi lilikamilika. Laureen alitoka


kwenye chumba cha matibabu kisha akawafuata akina Owen. Aliwakuta wameketi kwenye benchi huku wakisubiri taarifa ya madaktari kuhusu hali ya Mzee wao. Laureen aliwatuliza kwanza maana walionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua kilichojiri katika chumba cha matibabu. Baada ya kuwatuliza aliwaambia kwamba matibabu yameenda vizuri hivyo mgonjwa amepumzika na baada ya muda ataamka na kuwa sawa kabisa. "Dokta, Naomba fanyeni kila


muwezalo kwa ajili ya uzima wa mume wangu jamani.!" Hiyo ilikuwa ni kauli ya Mama yake Owen kwenda kwa Laureen. Ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Mama Owen kumuita Laureen kwa heshima huku akiwa ameshusha sauti yake. Kauli ile iliwafanya wanafamilia kushtuka kwani hawakuwahi kabisa kusikia sauti ya unyenyekevu wala kuona sura ya upole ya Mama Owen dhidi ya Laureen. Kauli ile ilimfanya Laureen akaribie kudondosha


chozi mbele ya wanafamilia. Alichokifanya ni kutoka fasta eneo lile na kuingia chooni ambako alienda kumwagia machozi yake. Huko sasa alipata fursa ya kudondosha machozi yake kisha akasafisha uso kwa maji na kurudi kwenye majukumu yake. Ni kama vile kila mtu alijua kile kilichokuwa kimempeleka Laureen chooni. Siku nzima Laureen aliendelea kuwa karibu na Mr James ili kumfanyia matibabu kwa ukaribu zaidi. Mr James mwenyewe alipozinduka alishtuka sana kumuona Laureen


ndo alikuwa Daktari aliyekuwa anashughulika na matibabu yake. Mzee mzima alihisi pengine labda alikuwa anaota lakini kila alipofikicha macho alijikuta yupo kwenye uhalisia na sio ndotoni. Mshangao aliokutana nao pamoja na maswali aliyojiulizaga mke wake ndo hayo hayo aliyojiuliza kichwani mwake. Inawezekana vipi Laureen akawa Daktari? Hilo swali liligonga sana kwenye vichwa vya watu lakini bado halikuweza kubadilisha uhalisia wa Laureen kuwa Daktari. Siku ile Mr James


alilazwa pale hospitali na siku iliyofuata afya yake iliimarika na aliruhusiwa kurudi nyumbani. Baada ya miaka saba ya utengano, hatimaye familia nzima ya Mr James ilikutana kwa mara nyingine. Lakini pia kulikuwa na ongezeko la watu ndani ya familia ambao ni Diana, Laureen pamoja na Careen ambaye ni mtoto wa Robyson na Diana. Sura ya mtoto Careen ilimshtua sana Owen pamoja na Laureen. Walishtuka kwa sababu ilikuwa ni mara yao ya kwanza kumuona yule mtoto na sura


yake ilifanana kabisa na sura ya Owen. Laureen alijikuta anapata presha kwa kuhisi labda Owen alimpaga mimba msichana miaka saba iliyopita hivyo yule mtoto alipelekwa kulelewa kwa Bibi na babu zake. Presha ya Laureen ilishuka mara baada ya kuambiwa Careen ni mtoto wa Robyson na Diana. Lakini sasa, licha ya kusikia kwamba Careen ni mtoto wa Robyson ila upande wa Owen kijasho chembamba kiliendelea kumtoka kadri alivyokuwa anamtazama yule mtoto. Mapigo ya moyo ya Owen


yalidunda kwa kasi na spidi kubwa sana. Alijikuta anamtazama yule mtoto na ajabu ni kwamba hata yule mtoto alikuwa anamtazama sana Owen tena bila kupeoesa macho. Ilibidi tu Owen akwepeshe macho yake kwa yule mtoto licha ya kwamba mtoto aliendelea kumtazama. Owen aligeuza macho yake na kuanza kumtazama Diana lakini alikuta tayari macho ya Diana yanamtazama yeye. Ni kama vile mioyo yao ilikuwa inaongea kwa wakati huo kuhusiana na yule Careen. Utulivu na ukimya


ulitawala ndani ya nyumba. Mr James na mkewe walikuwa hawana ujasiri wa kuwatazama Owen na Laureen. Ni kama vile nafsi zilikuwa zinawasuta kwa wakati huo. Kila mmoja alikaa kimya kusubiri mtu wa kuanzisha maongezi. Mr James aliinuka kwenye sofa alipokuwa amekaa kisha akaanza kupiga hatua kumfuata Owen na Laureen kwenye sofa walilokuwa wamekaa. Mapigo ya moyo yaliwaenda mbio Owen na Laureen kwani walihisi mzee alikuwa anawafuata kwa shari.


Robyson alitamani kumfuata mzee ili amzuie maana alihisi pengine bado alikuwa na hasira na Owen. Lakini sasa, kitu cha kushangaza na kustaajabisha ni kwamba baada ya Mr James kuwafikia Owen na Laureen, alienda chini kisha akapiga magoti. Wakati watu wanaendelea kushangaa, Ghafla Mama mwenye nyumba nae alimsogelea Laureen kisha akampigia magoti. Kwa hakika lilikuwa ni tukio la kustaajabisha na kushangaza sana kwani sio rahisi kwa mzazi kumpigia


magoti mwanae pindi anapotaka kumuomba msamaha. Tukio hilo lilifanya mioyo ya watu kuacha kazi ya kusukuma damu na kuanza kusukuma mshangao. NOVEL.................... MY VALENTINE- 37 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................


0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ "Mwanangu Owen, Nina mengi sana ya kuzungumza juu yako lakini kabla sijaongea chochote naomba nitangulize ombi la msamaha kwako. Kiukweli kabisa nilikukosea sana kijana wangu.Nilidiriki kutengeneza kampeni za kukudhulumu haki yako ya msingi. Nilikuwa nafanya vile sio kwa kuwa nilikuwa


nakuchukia ila nilihisi kama nakutengenezea furaha na maisha bora ya baadae. Kiukweli kabisa sikujua kama kufanya vile nilikuwa nakudhulumu furaha yako. Najiuliza mpaka sasa, hivi mimi ni Baba wa aina gani? Nilikutolea radhi, nikakufukuza nyumbani na kama haitoshi nilikufuatilia mpaka mtaani kuja kukuharibia sehemu ulizokuwa unajipatia ridhiki. Nisamehe sana mwanangu kwa maovu yote niliyokutendea.!" Mr James alizungumza kauli hiyo huku akiwa ameinamisha kichwa chini


kwa aibu. Maneno ya Mr James yalimfanya Owen ashindwe kuzuia machozi yasitiririke mashavuni mwake. Mtaalamu alijifuta machozi kisha akasema, "Wazazi wangu, Hebu inukeni kwanza ili tuzungumze vizuri. Naona bado munafika mbali sana kwa kupiga magoti mbele yetu.!" Owen alizungumza kauli hiyo huku akiwanua wazazi wake.


"Owen na Laureen, Mimi binafsi sistahili kuzungumza na nyie wakati nimekaa au kusimama. Natakiwa kupiga magoti ili kutubu makosa yangu mbele yenu. Kwa hakika umejua kutunyoosha sana wazazi wako. Mwanzo tulijua njia uliyoichagua sio sahihi kumbe ni sisi ndo tulikuwa kwenye njia isiyo sahihi. Unajua sisi watu wenye vipato tunapenda sana vijana wetu waoe au kuolewa kwenye familia zenye vipato. Tunataka iwe hivyo kwa kuwa tunaamini itakuwa rahisi kwetu kusaidiana kwenye


matatizo. Lakini sasa, mpaka kufikia muda huu nimejifunza kitu kikubwa sana kupitia matatizo yaliyotokea kwenye familia yetu. Mwanangu Robyson ameoa kwenye familia ya kitajiri lakini wakwe zake wameshindwa kutusaidia sisi. Lakini kitu cha kushangaza msaada tumekuja kuupata kutoka kwako Owen uliyechagua kumuoa mwanamke kutoka kwenye familia ya kimaskini. Kiukweli kabisa naomba unisamehe sana mwanangu Owen.!" Mama Owen aliongea maneno hayo huku


akionesha kutotaka kuinuka pale chini alipokuwa amepiga magoti. Kauli ya Mama Owen ilimchokonoa Diana kwa sababu Baba yake aligoma kuisaidia familia ya mume wake. "Dah! Huwa nawaza sana hivi Owen ungekubali kufuata nyayo zetu za kuwa mwanasiasa leo hii tungekuwa wapi sisi? Nakumbuka tulikuwa tunakulazimisha uwe mwanasiasa kama sisi lakini ukapinga. Nakumbuka uliwahi


kusema sio vyema wanafamilia wote tukapita njia moja kwa sababu kama tutapandikiziwa miiba kwenye hiyo njia basi ni rahisi familia kupata anguko na kukosa usaidizi. Leo hii nimeamini ile kauli yako. Sisi wazazi wako pamoja na kaka yako tumekutana na pigo zito sana kwenye siasa. Tayari tulishapoteza dira na uelekeo lakini umejitokeza wewe mfanyabiashara umekuja kukomboa jahazi la familia. Pengine labda ungekuwa mwanasiasa basi leo hii dunia


ingetuelemea. Kwa hakika Owen una akili sana mwanangu. Yani kama tusingefanana sura basi ningeenda kupima DNA na wewe maana ningehisi wewe sio mwanangu. Hakuna mtu mwenye akili na maarifa kama yako kwenye ukoo wetu na hata ukoo wa mama yako. Hivi hizo akili umezipata wapi mwanangu? Dah! Kiukweli kabisa najivunia sana kuwa na mtoto kama wewe. Mimi ni mkubwa lakini harakati zako zimenifunza sana kwenye haya maisha. Sikuwahi kujua kama kuna madhara ya


kumlazimisha mtoto asomee kitu alichosomea mzazi, Sikuwahi kujua madhara ya kulazimisha ndoa kwa vijana kwa kufuata masilahi binafsi. Lakini pia sikuwahi kujua kama kura ya masikini mmoja ingeweza kunikosesha uongozi kwenye siasa. Owen mwanangu, Naomba uniombee msamaha kwa Laureen. Huyo Binti nilimdharau sana kutokana na status yake.!" Mr James alizungumza kauli hiyo kwa mara nyingine.


"Laureen Binti yangu, Kwanza kabisa naomba unisamehe kwa dharau na kejeli zote nilizokumwagia hapo awali. Pili, nakukumbusha kwamba nyuma ya mafanikio ya kila mwanaume kuna mwanamke. Haya mafanikio aliyonayo Owen yamesababishwa na wewe. Hiki alichokifanya Owen kinanikumbusha kauli ya marehemu mama yangu aliniambia kwamba 'mwanangu, usitafute mwanaume bora bali mfanye mwanaume ulienae kuwa bora'. Alichokifanya Owen ni


kutohangaika kutafuta mwanamke mwenye status nzuri ya maisha badala yake ameamua kukutengenezea status wewe uliyekuwa mkononi mwake. Kwa hatua muliyoifikia sasa haipingwi. Nyie ni washindi wanangu. Naona kabisa Mwenyezi Mungu amewafunga kwenye hatima moja. Yani ni rahisi kuzuia mvua isinyeshe kuliko kuzuia penzi lenu. Nikiwa kama Mama mzazi niliyembeba Owen tumboni mwangu basi natoa idhini akuoe Laureen.!" Hiyo ilikuwa kauli ya Mama Owen


kwenda kwa Laureen Laureen alijikuta anashindwa kuyazuia machozi yasitiririke kwenye mboni za macho yake. Kwa namna alivyokuwa amenyanyaswa na Mama yake Owen hakuamini kabisa kama kuna siku angekuja kuombwa msamaha na kukubalika kama mkwe. Kutoka kuwa kijakazi mpaka kuwa mke wa mtoto wa bosi sio jambo jepesi na rahisi. Baada ya Mama Owen kumalizana na Laureen alimgeukia mwanae Owen.


Alipomtazama tu alijikuta anatokwa na machozi. Ni mwanae kipenzi aliyetowekaga kwenye mboni za macho yake kwa takribani miaka saba. Zaidi na zaidi ni kwamba ndo alikuwa mtoto aliyekuwa anampenda kuliko wote. "Owen babaa! Umebadilika sana mwanangu. Kiukweli kabisa nilikutoa akilini mwangu lakini kamwe sikuwahigi kukutoa moyoni mwanangu. Mara nyingi nilikuwa nakuota kwenye njozi na kila nilipokuwa nashtuka nilikuwa


nafanya maombi kwa ajili yako. Hakuna siku niliyosali nikashindwa kulitaja jina lako mwanangu. Maovu yote yaliyokuwa yanafanywa na Baba yako kuja kukuharibia kwenye viajira vyako mimi sikuhusika kabisa. Maumivu uliyokuwa unayapata kipindi ulichokuwa mbali nami hata mimi niliyapata pia. Nilikuwa naku-miss sana mwanangu. Nilikuwa najiuliza upo wapi, unafanya nini, upo kwenye hali gani na unaishije mwanangu. Nashukuru sasa umerudi tena mwanangu. Safari


hii sitaki nikupoteze tena. Sitaki kupitisha siku bila kukuona babaa. Naomba unisamehe kwa kauli zangu chafu juu yako. Mimi ndo mama yako na wewe ni mwanangu. Kuanzia sasa nakupa idhini ya kumuoa mwanamke unayempenda kwa dhati ndani ya moyo wako. Ni ruksa sasa muoe huyo Valentine wako.!" Mama Owen alizungumza kauli hiyo kisha akamkumbatia mwanae Owen. Walimkumbatiana kwa muda kisha wakaachiana. Owen


aliwatazama wazazi wake kisha akashusha pumzi na kuongea, "Wazazi wangu, Nadhani kwa sasa anayepaswa kuombwa msamaha ni huyu Laureen tu ingawa najua ameshawasamehe ndo maana pesa tuliyotumia kulipa deni, asimilia sabini ni ya kwake yeye. Mimi nimetoa mfukoni mwangu asilimia thelathini tu ili nyingine yote imelipwa na Laureen. Aah.. Mimi kwa upande wangu sina ninachowadai wazazi wangu zaidi ya idhini tu ya kumuoa


mwanamke ninayempenda kwa dhati. Sihitaji muniombe msamaha kwa kuwa hamjanikosea ndo maana hata ile siku nilipoondoka hapa niliwaambia kwamba siondoki na fikra kwamba mumenifukuza ila naondoka huku nikijua mumeniruhusu kwenda kutafuta maisha huko mtaani. Kiukweli kabisa nawashukuru kwa kunifukuza nyumbani kwa sababu mulinifungulia mlango na kunionesha njia ya kwenda kutafuta mtaani. Tabu na mateso niliyopitia huko mtaani


yamenifunza mengi sana katika maisha. Kubwa zaidi nililojifunza mtaani ni kuwaheshimu watu pamoja na kuithamini shilingi kwa kuitunza na kuitumia leo kwa faida ya kesho. Mitaa imenifunza kujua kwa vitendo utofauti kati ya maskini, fukara na tajiri. Naweza kusema kwamba kila kitu kinatokea kwa sababu hivyo kuondoka kwangu kulikuwa na faida kubwa sana. Najua kabisa kama ningebaki hapa ningebweteka tu kula ugali wa bure wala nisingepata uchungu wa kutafuta ugali


wangu. Hebu fikirieni, Kama ningebaki hapa, Je leo hii kungekuwa na OLA TRADERS LIMITED? Je hili deni la familia nani angelipa? Kwahiyo nachoweza kusema ni kwamba mafanikio yangu yamesababishwa na nyie wazazi wangu. Muliponifukuza nyumbani kwenu hamkunikomoa bali mulinitaka nikapambanie maisha mtaani.!" Owen alizungumza maneno hayo kwa unyenyekevu wa hali ya juu. "Hapana mwanangu, Mimi


nilikufukuza kwa ubaya kijana wangu. Kama haitoshi nilikufuata mpaka mtaani nikaanza kukuharibia kwenye vibarua vyako. Kwa ajili yangu ulikosa kibarua kilichokuwa kinakupa pesa ya kujikimu. Sasa unawezaje kusema nimechangia mafanikio yako huko mitaani.!" "Hahah! Mzee wangu, wakati mwingine sio kila unachokipoteza ni hasara. Vingine huwa ni faida kwa kuwa unapata nafasi ya kukaribisha kitu kingine ambacho kinaweza


kuwa bora zaidi. Inawezekana ningeendelea kuosha magari basi huenda nisingepata wazo la kwenda kufanya kazi sokoni ambako nilikutana na mtu asiyenipiga kampani kwenye maisha yangu. Kiufupi ni kwamba ulivyonipiga teke muda ule hukuniumiza tu bali ulinisaidia kusogea mbele zaidi nilipokuwa natamani kufika. Kwa hilo nashukuru sana mzee wangu. Unajua kwa sisi wanaadamu, kadri changamoto zinavyozidi ndivyo wigo wa kufikiri unavyozidi kutanuka. Yote


kwa yote, Mimi na Laureen wangu tunawapenda sana wazazi pamoja na ndugu zetu wote. Kwa sasa tumerudi tena kuomba idhini yenu ili tuweze kuoana. Kama vigezo vyenu ni status ya maisha basi niwambie tu, huyu niliemleta mbele yenu sio tena Laureen. Huyu ni Dr Laureen kutoka Hospitali Ya Taifa, Muhimbili.!" Hiyo ilikuwa kauli ya Owen. "Owen kijana wangu, mama yako tayari ameshakubali hivyo na mimi kama Baba mwenye


nyumba nasema kwamba Laureen amepitishwa bila kupingwa. Kwa sasa tujadili tu kuhusu ndoa hayo mengine yabaki tu kama historia. Napendekeza kabisa hiyo ndoa ifungwe miezi miwili ijayo kwenye tarehe na mwezi ule ule mliotulazaga na viatu miaka saba iliyopita. Nataka kufuta kumbukumbu za huzuni kila ifikapo ile tarehe. Kiukweli kabisa kila ifikapo Februari 14 ya siku ya wapendanao nimekuwa nakumbuka surprise iliyoniumizaga moyo kutoka


kwenu wapendanao. Sasa nataka nikafute kumbukumbu mbaya na kujenga kumbukumbu nzuri juu ya ile siku. Sasa ni rasmi natangaza kwamba ndoa yenu (Owen na Laureen) itafanyika kwenye Valentine Day ijayo na maandalizi yataanza kuanzia kesho.!" Hiyo ilikuwa ni kauli ya Mr James. Baada ya kauli hiyo wote walifurahi isipokuwa Diana na Robyson tu wao walionekana kuwa tofauti kidogo. Diana yeye bado aliendelea kuwa na ile roho


ya kutotaka mwanamke yeyote awe karibu na Owen. Ukweli ni kwamba bado alikuwa anampenda sana Owen. Kwa miaka yote aliyoishi na Robyson bado alishindwa kufuta kumbukumbu za Owen kichwani mwaka. Lakini pia Robyson nae hakufurahi kabisa juu ya kauli ya baba yake. Alichokifanya ni kutengeneza tu tabasamu la uongo usoni mwake ili kuonesha kwamba amefurahi kumbe alichukia. Ukweli ni kwamba hakufurahi kabisa kuona wazazi wake wakim'mwagia sifa Owen


kwamba ndo mtoto mwenye akili nyingi kuliko wote. Lakini pia hakufurahi kwa sababu moyoni mwake alikuwa na siri nzito kuhusu Laureen ndo maana hakuwahigi kabisa kuunga mkono suala la Owen kumuoa Laureen. Ni kama vile alishawahigi kufahamiana na Laureen hata kabla hajaingia nyumbani kwao kwa mara ya kwanza kabisa. Kama unakumbuka Robyson alishawahi kumwambia Owen aachane na wanawake wa kuwaokota okota mitaani na alisema vile akiwa na


sababu zake binafsi. Wakati Owen na Diana wana siri yao, kumbe hata Robyson na Laureen nao walikuwa na siri yao. NOVEL.................... MY VALENTINE- 38 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762


INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ ____ Hatimaye sasa ile sintomfahamu kati ya wazazi dhidi ya Owen na Laureen ilimalizika. Ilimalizika kwa Owen na Laureen kuibuka washindi na waliweza kupewa idhini ya kuoana. Ni rasmi sasa Laureen alikubalika kwa wazazi wa Owen. Furaha nyingine iliongezeka kwa wazazi wa Owen baada kujua kwamba tayari Laureen alikuwa na mjukuu wao


tumboni mwake. Ilikuwa ni taarifa njema sana kwa wazazi, Catherine na Sharon. Lakini kwa upande wa Robyson na Diana ni kama waliongezewa machungu. Japo walikuwa na machungu lakini machungu yao hayakuweza kubadili ratiba wala kuharibu maandalizi ya ndoa. Suala lilibaki vile vile kama lilivyopangwa na kilichokuwa kinasubiriwa ni siku tu ya harusi. Siku ile Owen na Laureen walishinda na kulala kule kule kwa wazazi wao. Robyson na Diana wao walirudi nyumbani


kwao. Owen na Laureen wao walikaa kwa wazazi kama wiki moja hivi na uzuri ni kwamba wote walikuwa na likizo fupi. Likizo zao walizitumia pamoja na familia huku wakikumbushana mambo kadha wa kadha waliyoyafanyaga miaka ya nyuma. Kiufupi ni kwamba furaha ilirejea tena ndani ya nyumba. Baada ya wiki kumalizika Owen na Laureen walirudi kwenye nyumba yao na kuendelea na majukumu yao ya kazi. Ile siku ya kwanza kabisa kwa Laureen kurudi kazini alikabidhiwa faili la


mgonjwa mmoja ambaye hakuweza kutibiwa kutokana na ndugu zake kushindwa kulipia gharama za awali za matibabu. Mgonjwa huyo alikuwa na hali mbaya sana na alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa ini. Baada ya hospitali zilizopo jijini Mwanza kushindwa kutibu tatizo la mgonjwa huyo ilibidi asafirishwe mpaka Dar es salaam katika Hospitali Ya Taifa Muhimbili. Baada ya kufikishwa Muhimbili, tatizo lake lilionekana kuhitaji kiasi kubwa sana za pesa. Tatizo ni kwamba kiasi cha


pesa kilichokuwa kinahitajika kilikuwa kikubwa kuliko uwezo wa ndugu wa mgonjwa. Lakini pia madaktari walitoa masaa sita tu kwa ndugu wa mgonjwa kuhakikisha wanapata pesa ili mgonjwa wao afanyiwe matibabu. Tofauti na hapo wangekabidhiwa mgonjwa wao na kurudi nae nyumbani kwao kitu ambacho kingehatarisha uhai wa mgonjwa. Kutokana na umaskini na hali duni ya maisha, wale ndugu wa mgonjwa walibaki tu wakitia huruma kwa madaktari na kuwaomba


wamfanyie matibabu mgonjwa wao. Dada wa mgonjwa alionekana akimlilia mmoja kati ya madaktari aliyetoka kwenye wodi aliyokuwa amelazwa mgonjwa wake. Dada huyo alipiga magoti chini huku akimuomba Daktari amtibu kaka yake na kama pesa wangezileta. Yule Daktari hakumsikiliza yule mwanamke badala yake alienda kwenye wodi za wagonjwa wengine kuendelea na majukumu yake. Wakati yule mwanamke amepiga magoti pale chini, Dr Laureen nae alikuwa anapita


eneo lile. Alishangaa sana kumuona mwanamke mwenzake akiwa chini amejipigia magoti mwenyewe. Laureen alimsogelea yule mwanamke kisha akampa mkono ili kumuinua pale chini. Yule mwanamke alipokea mkono wa Laureen kisha akavutwa na kuinuka. Ile kutazamana tu, kila mtu alishtuka. Walishtuka kwa kuwa walikuwa wanafahamiana na ilishapita miaka mingi sana tangu walipoonana. Licha ya kwamba Laureen alishakuwa na sura ya kiutu uzima na kunawiri kutokana na pesa lakini hilo


halikumzuia yule mwanamke kumtambua Laureen. Ni Laureen ambaye alimpa kila aina ya manyanyaso na mateso kwenye nyumba yake. Ni yule yule Laureen ambaye ndo mtoto wa kaka yake aliyempokeaga ndani ya jiji la Dar es salaam akitokea jijini Mwanza. Ni yule Shangazi yake Laureen. Shangazi alijiuliza, imekuaje tena Laureen amekuwa Daktari? Kwa hakika aliona miujiza ya aina yake. Yule Shangazi alihisi labda alikuwa njozini lakini haikuwa kama alivyohisi. Kile alichokuwa


anakiona ndo kilichokuwa kwenye uhalisia. Lakini pia hata Laureen alimtambua vizuri yule Shangazi na kukumbuka mateso na manyanyaso aliyoyapata chini ya himaya yake. Ni mwanamke ambaye ndo alimtelekezaga bila huruma katika ya jiji la Dar es salaam bila hata senti tano. "Laureen mwanangu.!" Shangazi alimuita Laureen kwa mshangao. Laureen alisikia vyema akiitwa jina lake na allishamtambua yule mwanamke lakini akabadili sura


yake na kujifanya kama hamjui kabisa. Huwezi kuamini yani, Laureen alimkana yule mwanamke na kujifanya hamjui kabisa. Yule mwanamke alimsogelea Laureen na kumkagua sura kwa umakini kabisa na akajidhihirishia kwamba ndo yule yule Laureen mtoto wa kaka yake. "Ni wewe kabisa Laureen mtoto wa kaka yangu. Najua kabisa kwanini unajifanya unijui mimi. Lakini Laureen, naomba utusaidie kwa leo tu mwanangu.


Sisi tupo hapa hospitali kwa ajili ya baba yako wewe. Baba yako ni mgonjwa wa ini na hali yake ni mbaya sana hivyo anahitaji apate matibabu ya haraka. Tangu jana tumefika hapa hospitali lakini mpaka sasa hajafanyiwa matibabu kwa kuwa madaktari wanataka pesa na pesa inayohitajika ni kubwa sana kuliko uwezo wetu. Naomba ufanye kitu kwa ajili ya Baba yako. Okoa maisha ya Baba yako Laureen.!" Yule Shangazi aliongea maneno hayo na kumfanya Laureen apige hatua


kurudi kwenye chumba chake huku machozi yakimtoka. Laureen alifika kwenye ofisi yake (chumba cha Daktari) huku machozi yakiwa yanaendelea kumtoka. Maneno ya Shangazi ndo yalizidi kumchoma kwani alikumbuka namna Baba yake alivyomkana na kusema kwamba yeye sio mwanae. "Laureen! Kwahiyo unataka kujua kwanini nimebadili mwenendo wangu juu yako si ndio? Ok ngoja sasa nikuambie ukweli.


Nimebadilika ghafla kwa sababu wewe sio mwanangu wa damu. Mama yako alikuwa ananisaliti mpaka akabeba ujauzito nje ya ndoa. Kwahiyo kuanzia sasa, elewa kwamba mimi sio baba yako mzazi.!" "Laurine, nadhani sasa umeshajijua wewe ni nani kwa kaka yangu. Kwahiyo basi kuanzia sasa utaishi hapa kama upo kwa bosi wako na sio shangazi yako. Majukumu yako ndani ya nyumba yangu ni kuhakikisha nyumba inakuwa


safi kila dakika. Kila siku utakuwa unamuandaa mwanangu kabla hajaenda shule. Kama hutaki basi ni ruksa kuondoka, geti lipo wazi kwa ajili yako. Na kama utachagua kubaki basi tambua kwamba mimi ni bosi wako na sio shangazi yako tena. Umesikia wewe mpumbavu?" Hizo zilikuwa kumbukumbu za Laureen kuhusiana na matukio yaliyotokea miaka ya nyuma dhidi ya baba yake pamoja na Shangazi yake. Maneno hayo


Laureen aliyakumbuka vyema sana na bado hayakufutika kichwani mwake. Alikumbuka vyema sauti ya baba yake, aliikumbuka vyema sauti ya Shangazi yake. Mtoto wa kike alijikuta anaumia sana baada ya Shangazi kumwambia yeye ni mtoto wa kaka yake. Yale maneno yalikuwa ya kinafiki sana. Yani Shangazi huyo huyo ndo aliwahi kumwambia Laureen kuwa yeye sio mtoto wa kaka yake lakini ghafla amebadilika na kumwambia yeye ni mtoto wa kaka yake. Laureen alitamani


kuendelea na mambo yake lakini kuna roho ya ubinadamu ilimuingia juu ya afya ya baba yake. Kwanza alianza kukumbuka yale mazuri ambayo aliwahi kufanyiwa na Bwana Laurence. Kuna maisha fulani ya upendo waliishi kwenye familia yao kabla hata mchepuko hajaingilia ndoa ya wazazi wake. Kiukweli kabisa Bwana Laurence alishawahi kuonesha mapenzi ya dhati kwa mke wake Zuwena na mwanae Laureen. Hata safari ya Laureen kwenye masomo aliianzishaga yeye na


alimpigania mwanae kwa kila hatua ili kuhakikisha anatimiza ndoto zake. Lakini sasa ndo hivyo baadae alitokea mchepuko akaharibu kila kitu kwenye familia. Laureen alitamani kuwa mkatili dhidi ya wale watu lakini alijikuta anaingiwa na roho ya huruma. Licha ya kwamba Bwana Laurence alimkana Laureen kwamba sio mwanae lakini Laureen bado aliamini Bwana Laurence ndo alikuwa baba yake mzazi. Hata mama yake enzi za uhai wake hakuwahi kumuonesha baba mwingine


zaidi ya Bwana Laurence. Uzito wa damu ulimfanya Laureen aguswe na maradhi ya baba yake. Mtoto wa kike hakutaka kutoa hukumu kwa mzazi wake hivyo aliamua kumsaidia na kuiacha kesi mikononi mwa Mola ili atoe hukumu yake. Laureen alilipitia lile faili la yule mgonjwa na akaliona kweli jina la baba yake likiwa limeandikwa juu ya jalada. Laureen alijikuta anatokwa na machozi kwa sababu alijua baba yake alikuwa anapitia maumivu makali kutokana na yale maradhi


aliyokuwa nayo. Dakika zile zile Laureen alianza kufanya mchakato wa kugharamia matibabu yote ya Bwana Laurence. Baada ya kukamilisha hilo akawadokeza madaktari wenzake kuhusu mahusiano yake na yule mgonjwa hivyo aliwaomba wapambanie maisha yake kwa gharama yoyote ile. Baada ya madaktari kujua mahusiano ya Dr Laureen na Bwana Laurence, chap chap waliingia kwa wingi kwenye chumba cha matibabu kwa ajili ya kumfanyia upasuaji wa ini


Bwana Laurence. Laureen alikuwa miongoni mwa madaktari walioshiriki kwenye ule upasuaji. Takribani masaa sita yalitumika mpaka kumaliza zoezi la upasuaji wa ini la Bwana Laurence. Kwa bahati nzuri zoezi lilienda vizuri kabisa kama ilivyotarajiwa. Madaktari walitoka kwenye chumba cha upasuaji wakiwa hoi bini kuchoka. Laureen aliwafuata ndugu waliokuwa pale hospitali kwa ajili ya kumuuguza Bwana Laurence ili kuwapa ripoti ya mgonjwa wao. Alipofika alimkuta Shangazi


pamoja na baba zake wadogo ambao aliwahigi kuwaona zamani sana alipokuwa mdogo. Laureen hakutaka stori nao hivyo aliwaambia tu kwamba mgonjwa wao amefanyiwa matibabu hivyo waendelee kusubiri mpaka atakapoamka wataambiwa nini cha kufanya. Baba wadogo nao walijifanya kumkumbuka Laureen lakini Laureen aliwaambia kwamba wanamfananisha maana yeye hawafahamu kabisa wala hakuwahi kuishi Mwanza. Licha ya Laureen kuzungumza vile lakini walimshukuru sana


kwa kuwa walijua yeye ndo alifanya Bwana Laurence apate matibabu. Zilimchukua takribani siku tatu Bwana Laurence kuzinduka tangu alipofanyiwa upasuaji wa ini. Siku zote alikuwa anakula kupitia mirija. Ndani ya hizo siku Laureen alikuwa karibu sana na Baba yake ili kuhakikisha anakuwa salama. Kiufupi Daktari alikuwa yeye, Nesi yeye na muuguzi akawa yeye mwenyewe. Kila baada ya lisaa moja alikuwa anaenda kwenye wodi aliyolazwa baba yake kutazama kama mashine zilikuwa zinaendelea


kufanya kazi kwa usahihi. Mpaka ile siku ya tatu ambayo Bwana Laurence alifumbua macho Laureen ndo alikuwa binadamu wa kwanza kabisa kuonekana kwenye mboni za macho ya Bwana Laurence. Bwana Laurence alijikuta anashtuka baada ya kumuona Laureen mbele yake tena akiwa kama Daktari aliyekuwa anamtibia. Ilikuwa ni uso kwa uso kati ya Baba na mwana. NOVEL.................... MY VALENTINE- 39


{Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____ Bwana Laurence alihisi pengine


labda ugonjwa ndo ulikuwa unamfanya afananishe sura ya daktari yule na sura ya mwanae Laureen. Hakutaka kabisa kuamini kama mwanae Laureen ndo alikuwa Daktari anayeshughulika na matibabu yake. "La.. La.. Lau..reen.!" Bwana Laurence aliliita jina la Laureen kwa tabu sana. Laureen alisikia lakini hakuitikia badala yake alimtuliza mzee na kumtaka apumzike. Hakutaka


kumkana mzee kwa sababu angemuanzishia matatizo mengine ya kiafya. Alichokifanya ni kuonesha upendo kwa mgonjwa ili kumjenga kisaikolojia asiathiri afya yake. Matibabu yaliendelea kwa Bwana Laurence na kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo hali ilivyozidi kuimarika. Lakini sasa, gharama za kuishi pale hospitali zilikuwa kubwa sana. Gharama zote zilikuwa chini ya Laureen kwa kuwa waliompeleka mgonjwa hospitali hawakuwa na pesa za kutosha. Laureen aliamua kujitoa


kwa ajili ya Bwana Laurence kwa kuwa alijua ni baba yake mzazi. Hakuona sababu ya kuiga ubaya kwa kuwa alitendewa ubaya. Takribani mwezi mmoja Bwana Laurence aliishi kule hospitalini na baada ya hapo aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali yake kuimarika kidogo. Lakini sasa alipewa wiki mbili mpaka tatu za kutembelea hospitali ili kuangalia maendeleo yake. Kwa mantiki hiyo Bwana Laurence alitakiwa kubaki ndani ya jiji la Dar es salaam kwa zile wiki mbili na sio kurudi Mwanza.


Changamoto ilikuwa ni mahala pa kwenda kuishi kwa kipindi chote ambacho angekuwa anatembelea hospitali. Ile miaka saba ya mabadiliko haikuweza kumuacha salama Shangazi. Zile mali alizokuwa anajivunia na kumnyanyasia Laureen hazikuwepo tena mikononi mwake. Yule mume wake aliuawa kwenye fumanizi alipokuwa na mke wa mtu. Baada ya mume kufariki zile mali zote pamoja na nyumba zilichukuliwa na wazazi pamoja na ndugu wa yule mume kwani


zilikuwa mali za familia. Mtoto wa marehemu alichukuliwa na ndugu wa marehemu na kwenda kulelewa huku Shangazi akiondoka na nguo zake tu. Baada ya hapo alianza maisha kwenye chumba cha kupanga na tangu muda huo alianza kuishi maisha ya kuungaunga huku akitumiwa na wanaume bila kuolewa. Kiufupi maisha yalimuendea vibaya sana Shangazi. Kwa wakati ule hakujua mahala pa kuwapeleka kaka zake Bwana Laurence pamoja na yule mwingine


aliyekuwa anamuuguza Bwana Laurence. Lakini pia hata angepata mahala pa kuwahifadhi, bado kungekuwa na changamoto kubwa kwenye suala la chakula. Kiufupi Shangazi alishapotea kabisa kwenye ramani ya maisha. Ilibidi tu wamfuate Laureen na kumpigia magoti kumuomba hifadhi kwa kipindi kile. Laureen alijua kabisa wale watu walikuwa wanahitaji sana msaada na mtu pekee aliyekuwa na uwezo wa kuwasaidia ni yeye tu. Alichokifanya mtoto wa kike ni


kumshirikisha Owen kwenye lile suala. Owen alimwambia Laureen akubali tu kuwasaidia maadamu bwana Laurence ni baba yake na alikuwa anapigania uzima sio mafanikio. Ilibidi sasa Laureen amchukue baba yake mzazi na kumpeleka nyumbani kwake alipokuwa anaishi na Owen. Yule Baba mdogo alipewa nauli ya kurudi Mwanza kuendelea na shughuli zake zingine. Laureen na Owen waliamua kuchukua jukumu la kumpa uangalizi Bwana Laurence mpaka pale ambapo


hali yake ingeimarika. Walimpa Bwana Laurence upendo na mahitaji yote ya msingi bila kuangalia historia ya nyuma. Mzee alikula chochote alichohitaji tena kwa wakati maalumu. Alilala sehemu nzuri ambayo hakuwahigi kulala hapo awali. Walimsisitiza na kumkumbusha kunywa dawa kwa wakati ili asiharibu dozi. Walimuheshimu kama mzee wao huku wakimfariji kwamba hali yake ingerudi kama ilivyokuwa hapo awali. Kila baada ya siku tatu Laureen alimchukua mzee


na kwenda nae hospitali kumfanyia vipimo ili kujua maendeleo yake kiafya. Kwa upendo aliokuwa anauonesha Laureen kwa Baba yake, Mzee alijikuta anasutwa na nafsi yake mwenyewe. Kila alipokuwa anakumbuka mabaya aliyomtendeaga Binti yake alijikuta tu anapata maumivu makubwa moyoni. Kila jema alilokuwa anafanyiwa na Laureen lilikuwa linamchoma moyoni na kumtoa machozi bila kutarajia. Zile wiki mbili za kutembelea hospitali ziliisha na vipimo


vilionesha hakuna hali yeyote ya hatari inayoweza kujitokeza tena kwa Bwana Laurence. Ni rasmi sasa Bwana Laurence aliruhusiwa kurudi nyumbani kwao akaendelee kujitazamia afya yake. Baada ya ripoti ile kutoka, Laureen alimwambia Bwana Laurence ratiba za hospitali zimeisha hivyo anatakiwa kurudi sasa jijini Mwanza akaendelee na maisha yake. Kauli hiyo aliitoa kwa Bwana Laurence mnamo majira ya usiku. Muda huo hata Owen alikuwemo ndani ya nyumba na


maongezi hayo yalifanyika sebuleni. Baada ya Laureen kuongea kauli ya kumtaka Bwana Laurence arudi nyumbani kwao, Bwana Laurence alianza kwa kupiga magoti chini kisha akaanza kuongea, "Laureen mwanangu, naomba unisamehe kwa mabaya yote niliyokutendea mwanangu. Kiukweli kabisa maisha niliyopitia mpaka kufikia muda huu ni malipo tosha kwa dhambi nilizowahi kuzifanya kwenye familia yangu. Haikuwa dhamira


yangu kuwatelekeza wewe na mama yako ila nahisi nililogwa mimi. Niliwatelekeza wewe na mama yako na kwenda kuishi na mchepuko nilieamini amenibebea kiumbe tumboni mwake. Nilisitisha huduma kwako mwanangu na kuanza kumuhudumia mtoto ambaye baadae nilikuja kugundua kuwa hakuwa wangu. Yule mshenzi alinipukutisha kila kitu nilichokuwa nacho na mwisho wa siku akaniacha. Tangu muda huo ni kama nililaaniwa kwenye maisha yangu. Kila nilichokuwa


nakifanya kilifeli. Ilifikia hatua hata nikigusa pesa ziligeuka na kuwa majani. Nikigusa sukari inageuka kuwa mchanga. Siku zote nimekuwa najiwa na taswira ya mama yako kichwani mwangu. Niliwahi kuja ndani ya hili jiji miaka kadhaa iliyopita kuja kukutafuta lakini jitihada zangu zilifeli. Tangu miaka hiyo nilijikuta naingia kwenye ulevi mpaka kufikia hatua ya kuharibu ini langu. Laureen, wewe ni mwanangu kabisa. Naomba unisamehe sana Baba yako. Naomba tusahau yaliyopita na


tuanze upya kuishi kama familia. Nahitaji kufurahia siku zangu zilizobaki hapa duniani na wewe mwanangu. Naomba unisamehe mwanangu ili nikawe na kauli thabiti mbele ya Mola wangu. Nisamehe sana mwanangu.!" Bwana Laurence alizungumza kauli hiyo huku akitokwa na machozi kama mtoto mdogo. Kauli ya Bwana Laurence ilimfanya Laureen alie kama mtoto. Alikumbuka sana namna Baba yake alivyogeukaga na kuwa mbogo. Mtoto wa kike


alijikuta analia tu kila alipokumbuka namna baba yake alivyomkana na kumkatisha tamaa kwenye safari yake ya masomo. "Sikiliza wewe mpumbavu, naomba iwe mwanzo na mwisho kunipigia simu na kuniuliza maswali ya kijinga. Tangu awali nilishakuambia wewe sio wa kusoma. Subiri upate mume huko Dar na uolewe kabisa. Nakupa onyo, Ishi huko huko na usirudi tena nyumbani kwangu. Kama Ukithubutu kuja


nitakufanyia kitu kibaya kabla kitu kibaya hakijatokea kwenye ndoa yangu. Kiufupi ni kwamba mimi na wewe tulishamalizana.!" "Laureen! Kwahiyo unataka kujua kwanini nimebadili mwenendo wangu juu yako si ndio? Ok ngoja sasa nikuambie ukweli. Nimebadilika ghafla kwa sababu wewe sio mwanangu wa damu. Mama yako alikuwa ananisaliti mpaka akabeba ujauzito nje ya ndoa. Kwahiyo kuanzia sasa, elewa kwamba mimi sio baba yako mzazi.!"


Hayo ni maneno aliyowahigi kutamka Bwana Laurence kwa mwanae Laureen. Maneno hayo yalijirudia mno kichwani kwa Laureen kila alipokuwa anamtazama Baba yake. Laureen alijikuta anazidi kulia tu kufuatia kumbukumbu zile. Owen alimsogea Laureen na kuanza kumnyamazisha huku akiwa amemkumbatia. Alimsihi sana akaze roho kisha afikiri kuhusu yule aliyekuwa mbele yake kutubu makosa yake. Ni dhahiri kabisa Bwana Laurence


alionesha nia thabiti ya kuhitaji msamaha wa mwanae. Sio kwamba alihitaji msamaha kwa kutaka mali au pesa, alihitaji msamaha ili apate nafasi ya kuitwa Baba kabla hajafa. Ukweli ni kwamba Laureen ndo alikuwa mtoto pekee katika uzao wa Bwana Laurence. Owen alimsihi Laureen amsamehe mzee wake ili maisha mengine yaendelee. Kwa namna sura ya Bwana Laurence ilivyokuwa inaonekana kwa wakati ule, ilihitajika roho ya kikatili sana kushindwa kumsamehe. Laureen


alimtazama Baba yake kisha akamwambia, "Baba eeh, Mimi hapa nakupenda sana baba yangu. Mama yangu mimi hakuwahi kabisa kunionesha baba mwingine zaidi yako wewe tu. Nikianza na makosa yako kwa mama yangu siwezi kuyahukumu kwa sababu siwezi jua ni kipi haswa kilichokuwa kinaendelea chumbani kwenu. Pengine labda mama yangu mimi alikuwa na madhaifu mengi ndo maana ulienda nje ya ndoa. Kama


unahisi ulimkosea mke wako basi utaenda kumuomba msamaha yeye mwenyewe juu ya kaburi lake. Mimi kwa upande wangu nahisi kabisa haujanikosea bali ulinisaidia kwa kiasi kikubwa sana kufikia ndoto zangu. Nahisi kabisa ilibidi tu nipite kwenye ile njia ili nifikie ndoto zangu. Naamini kabisa Pengine labda usingenifukuza nyumbani basi leo hii nisingekuwa kwenye hii nyumba wala nisingekutana na huyu kijana. Naomba tu nikushukuru baba yangu kwa kunipitisha


kwenye ile njia ambayo ndo ilinikutanisha na mwanaume wa ndoto zangu. Mwanaume ambaye aliamua kuvuja jasho lake kwa ajili ya kuhakikisha nafurahia maisha kama binadamu wengine. Baba eeh, huyu unayemuona hapa ndo mtu aliyeniokota jalalani na kunifanya kuwa Daktari. Huyu ndo mwanaume aliyefanya miujiza yote unayoiona kwangu. Yeye ndo mwanaume wa maisha yangu na jukumu lako la kwanza ukiwa kama mzazi wangu basi naomba idhini niweze kuolewa


na huyu mwanaume. Huyu mwanaume ndo dunia ya mwanao Laureen.!" Laureen alizungumza kauli hiyo kisha akamuinua Baba yake pale chini alipokuwa amepiga magoti. Bwana Laurence aliinuka na kumkumbatia mwanae Laureen huku akitokwa na machozi. Alimshukuru sana kwa kumsamehe na kumpa heshima ya mzazi kama ilivyokuwa hapo awali. Bwaña Laurence alimsogelea Owen kisha akamshukuru kwa kuchukua


jukumu zito la kumpambania binti yake. "Kijana wangu, mamlaka ya kutoa idhini kwa Laureen kuolewa yapo mikononi mwako. Wewe ndo utaamua binti yetu tunamwozesha au hatumwozeshi. Wewe ni mchumba na pia ni Baba wa Laureen. Yani hata ningekuta tayari umemuoa basi nisingehoji kuhusu mahari. Kwahiyo basi ninachoweza kusema ni kwamba maamuzi yapo mikononi mwenu wenyewe wanangu. Mimi


nasubiri kusikia tarehe ya ndoa tu hapa wala sihitaji hata kula mahari.!" Bwana Laurence aliongea na kuwafanya Owen na Laureen kucheka. Kwa mara ya kwanza kabisa Owen na Laureen walimchekea Bwaña Laurence na Bwana Laurence alitabasamu mbele ya Laureen na Owen. Owen alimshukuru Bwana Laurence kwa kuridhia amuoe Binti yake. "Mzee wangu, kwa kuwa umenizalia mke bora kwenye hii


dunia basi nitakujengea nyumba ya kisasa na pia nakukabidhi OLA Hotel iliyopo kule Mwanza ili ikusaidie kuendeshea maisha yako. Hiyo ni sehemu ndogo tu ya shukrani yangu kwako. Ahsante sana mzee wangu kwa kunikabidhi Binti yako. Nakuahidi nitaendelea kumpenda na kumtunza mpaka pumzi yangu ya mwisho.!" Owen alizungumza kauli hiyo ili kumuonesha Bwana Laurence thamani ya mtoto wake aliyemdharau na kumkana bila huruma.


Bwana Laurence alijikuta haamini kabisa kwa kile alichokisikia kutoka kwa Owen. Hakuwahi kabisa kufikiri kama Mwenyezi Mungu alim'bariki kupitia uzao wake. Hakuwahi kabisa kudhania kama Binti yake alikuwa mrembo na wathamani sana kwenye maisha ya watu wengine. Hakuwahi kabisa kudhania kama Mwenyezi Mungu alimuandalia mafanikio kupitia uzao wake. Bwana Laurence alishindwa kuamini aisee. Ni kama vile aliokota Bus na abiria ndani yake, abiria ambao hata


nauli walikuwa bado hawajatozwa. Kwa hakika ulikuwa ni wakati wa Mungu kumuonesha mwanadamu kwamba wakati mwingine juhudi zako kwenye kutafuta zinaweza zisikupe mafanikio ila ukaja kuyapata hayo mafanikio kupitia uzao wako. NOVEL.................... MY VALENTINE- 40 {Kipenzi Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER


{Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____ Wakati nyumbani kwa Owen, Laureen na baba yake wakipatana, kuna watu wengine walikuwa kwenye mgogoro mkubwa sana wa kifamilia.


Katika hali isiyotarajiwa, ugomvi mkubwa sana uliibuka katikati ya ndoa ya Robyson na Diana. Ugomvi huo uliibuka mara baada ya Diana kuletewa mtoto wa nje ya ndoa na mwanamke mwenzake aliyedai kuzaa na Robyson. Taharuki kubwa ilizuka ndani ya ndoa. Ukweli ni kwamba Robyson alikuwaga na mahusiano ya siri na mwanamke huyo lakini hakuwa na uhakika kama yeye ndo alimpachikaga ule ujauzito. Hakuwa na uhakika kwa kuwa alishawahi kumfumania yule mwanamke


akiwa na mwanaume mwingine. Kiufupi ni kwamba ulikuwa ni usaliti ndani ya usaliti. Mpaka mtoto alipozaliwa Robyson hakupeleka huduma kwa kuwa aliamini yule mtoto hakuwa wake. Aliamua kuachana na yule mwanamke kisha akatulia kwenye ndoa yake na Diana. Lakini sasa, Yule mwanamke aliamini kabisa yule mtoto ni wa Robyson hivyo alianza kupeleleza mpaka alipogundua mahala alipokuwa anaishi Robyson. Baada ya kupafahamu alimchukua mwanae kisha


akampeleka mpaka ndani ya nyumba na kumueleza Diana kila kitu kuhusu yule mtoto. Siku hiyo Robyson alichelewa kurudi kwenye majukumu yake na pindi tu aliporudi alikutana na hiko kizaazaa nyumbani kwake. Alimkuta mkewe Diana amekasirika huku pembeni kukiwa na mgeni ambaye ndo yule mchepuko wake pamoja na mtoto mdogo aliyesadikika kuwa wake. Robyson alijua sasa kila kitu kimeharibika pale ndani baada ya kumuona yule mwanamke. Alichokifanya


Robyson ni kumkana yule mwanamke pamoja na mtoto ili kunusuru ndoa yake. Licha ya kwamba Robyson alikana lakini suala lile halikumalizika krahisi kabisa. Diana aliamua kushikilia point kwamba Robyson alizaa na yule mwanamke. Akaenda mbali zaidi akamwambia Robyson kwamba ule ndo ulikuwa mwisho wa ndoa yao kwani hakuwa mwaminifu. Ukweli ni kwamba tangu muda mrefu Diana alikuwa anatafuta sababu ya kuachana na Robyson. Ile ndoa yake na Robyson ilifungwa kwa ajili ya


masilahi binafsi. Katika moyo wake hakuwahi kabisa kumpenda Robyson. Mwanaume pekee ambaye alikuwa ndani ya moyo wake alikuwa Owen lakini ndo hivyo tayari alishampoteza kwa tamaa zake mwenyewe. Diana alimtaka Robyson akubali kwamba yule mtoto ni wake au waende kwenye vipimo vya DNA ili kupata uthibitisho. Kwa kutaka kuthibitisha kwamba yule mtoto hakuwa wake, Robyson alikubali kwenda kupima DNA na yule mtoto. Mwanaume hakutaka kabisa kumpoteza mke wake.


Ilibidi sasa waongozane kwa pamoja mpaka hospitalini ili kufanya vipimo vya DNA. Walipofika walieleza nia yao na madaktari walichukua sampuli ya damu ya Robyson pamoja na yule mtoto. Baada ya zoezi hilo kukamilika waliambiwa watulie na wasubiri majibu ili wajue kama Robyson na yule mtoto walikuwa Baba na mwana. Baada ya kusubiri kwa muda fulani majibu yalitoka sasa na yaliwekwa wazi kwa kila mtu. Ripoti ya kweli ilionesha kwamba yule mtoto hakutoka kwenye


uzao wa Robyson. Yule mtoto hakuwa wa Robyson. Baada ya majibu hayo kutolewa, kila mtu sasa alielewa nafasi yake. Yule mchepuko aliumbuka kwa marefu na mapana. Lakini pia ni kama vile mpango wa Diana kutaka kuachana na Robyson ulikuwa umefeli. Kilichofuata hapo ni kuanza safari ya kurejea nyumbani kwao. Lakini sasa kabla hawajatoka pale hospitali, yule Daktari aliyewafanyia vipimo Robyson na yule mtoto alimuita Robyson kwenye chumba cha siri kwa ajili ya kuzungumza nae.


Robyson alimuacha nje Diana kisha akaenda kumsikiliza Daktari. Baada ya dakika tano kupita Robyson alitoka kwenye chumba cha Daktari akiwa amenyong'onyea sana. Mwanaume alitembea kwa kujikokota huku akiwa na sura ya huzuni. Lakini punde tu alipomfikia Diana aliamua kujikaza na kutengeneza tabasamu la bandia usoni mwake. Walipanda ndani ya gari na kuanza safari ya kurudi kwao. Diana alikuwa na hasira sana juu ya Robyson. Licha ya kwamba


vipimo vilionesha kwamba yule mtoto hakuwa wa Robyson lakini alichukia kujua Robyson alikuwa anachepuka na yule mwanamke. Lakini pia alitamani sana vipimo vingetoa majibu kwamba yule mtoto ni wa Robyson ili kusudi apate sababu yenye nguvu ya kudai talaka yake. Wakati Diana ana hasira zake, hata Robyson nae alikuwa na hasira zake. Safari iliendelea na hakuna kati yao aliyethubutu kumsemesha mwenzake. Robyson alionekana kuwa na mawazo mengi sana kuliko hata Diana. Kuna kitu


ambacho aliambiwa na Daktari kilimkosesha sana raha. Baada ya kufika nyumbani kwao, Diana aliteremka kwenye gari na kumuacha Robyson ndani ya gari akiwa ameegemea usukani. Mwanaume alianza kukumbuka maneno aliyoambiwa na Daktari muda ule alipoitwa. "Kijana mwenzangu, baada ya kufanya vipimo vya DNA niligudua kwamba yule mtoto sio wa kwako kwa sababu wewe hauna uwezo wa kumpa ujauzito mwanamke yeyote yule. Kwa


ufupi ni kwamba una changamoto kubwa kwenye mfumo wako wa uzazi.!" Hayo ndo yalikuwa maneno ya Daktari aliyomwambiaga Robyson muda ule alipomuita. Maneno hayo yalimfanya mwanaume ashtuke kwa marefu na mapana. Alishtuka sana kuambiwa kwamba hakuwa na uwezo wa kumpa ujauzito mwanamke hali ya kuwa nyumbani alimuacha mtoto. Suala lile lilimfanya Robyson akose furaha huku akianza


kumdadavua mwanae Careen kwa marefu na mapana. Siku nzima Robyson hakuwa na furaha kabisa kutokana na kuandamwa na msongo mzito wa mawazo. Usiku ukipofika usingizi haukupanda kabisa machoni mwake. Aliwaza na kuwazua mpaka ilipofika asubuhi. Asubuhi hiyo Diana alienda zake kazini huku nyuma Robyson alimchukua mwanae Careen na kwenda nae hospitali. Alipofika hospitali alieleza dhamira yake ikiwa ni kupita DNA yeye na yule mtoto. Daktari


alichukua sampuli ya damu ya Robyson na Careen kisha akapeleka maabara kwa ajili ya vipimo. Masaa kadhali baadae majibu yaliyotoka. Kwa hakika yalikuwa majibu mazito mno kwa Robyson. Kumbe miaka yote alikuwa anamlelea mtoto wa mwanaume mwenzake huku akijua ni wake. Mwanaume alikasirika sana. Alirudi nyumbani kwake na yule mtoto kisha akaanza kumsubiri Diana kwa udi na uvumba ili amwambie ukweli kuhusu baba halisi wa Careen. Majira ya jioni Diana


aliporudi kutoka kazini alimkuta mumewe Robyson akiwa sebuleni ameketi huku mkononi akiwa ameshika glass yenye pombe kali. Juu ya meza kulikuwa na chupa za bia pamoja na kisu. Diana alishtuka sana baada ya kukutana na ile hali kwani mume wake hakuwa mtumiaji wa pombe. Kwa namna fulani alihisi kulikuwa na jambo baya linaendelea pale ndani. Bila uwoga alimsogelea Robyson pale alipokuwa amekaa. Robyson nae alipomuona Diana aliinuka na kisu mkononi kisha akamvuta


Diana karibu yake na kumwekea kisu shingoni. "Diana.! Umenidanganya vya kutosha kwahiyo muda huu sihitaji tena kusikia uongo kutoka kwako. Naomba uniambie, Careen baba yake halisi ni nani? Tayari nimeshajua Careen sio damu yangu, kwahiyo usiposema ukweli nakuchinja hapa hapa.!" Robyson alizungumza kauli hiyo kwa sauti ya juu huku akiwa amemwekea Diana kisu shingoni. Diana alijikuta anatetemeka


mwili mzima. Hakuwahi kabisa kuona hasira za Robyson ila kwa mara ya kwanza aliziona. Mpaka kufikia hapo alishajua kila kitu kilikuwa kimeharibika. Kumbe hata yeye alikuwa anajua kwamba Careen hakuwa mtoto wa Robyson kwa kuwa alishawahi kufanya vipimo vya DNA kupitia damu ya Careen na mswaki wa Robyson. Kadri Diana alivyozidi kuwa kimya juu ya swali la Robyson ndivyo kisu kilivyozidi kupenya kwenye shingo lake. Robyson alionekana kudhamiria kutenganisha kichwa


cha Diana na kuwiliwili. Mkojo ulianza kumtoka Diana na alioona kabisa asiposema ukweli basi maisha yake yalikuwa yanafikia tamati muda ule. "Diana.! Careen Baba yake halisi ni nani?" Robyson alimuuliza Diana kwa mara nyingine huku akizidi kupenyeza kisu kwenye shingo la Diana. Ilibidi tu Diana afungue kinywa chake na azungumze ukweli ili kunusuru maisha yake. Kwa tabu sana alisikika akisema,


"Ca..Ca..Careen... Careen ni... ni... ni mtoto wa Owen.!" Diana alimjibu Robyson huku akiwa anahema kwa tabu sana. "Owen? Owen yupi unayemzungumzia?" Robyson alimuuliza Diana kwa mshangao "Ni huyo huyo unayemjua wewe. Ni Owen mdogo wako wewe.!" Diana alijibu kauli hiyo na kumfanya Robyson kulegea mwili mzima.


Mwanaume alikosa nguvu na kuanza kuhisi kizunguzungu. Alijikuta tu anakaa chini huku akiwa na kisu chake mkononi. Jibu la Diana lilimfanya ajihisi yupo kuzimu. Alikaa pale chini huku akiwa haamini kabisa kile alichokuwa amekisikia kutoka kwa Diana. Alianza kulitaja jina la mdogo wake, Owen kwa kurudia mara mbili mbili. NOVEL.................... MY VALENTINE- 41 {Kipenzi Changu}


AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ _________________________________ _____ Kimya kirefu kilipita bila kusikika sauti yoyote mule ndani. Robyson hakuhitaji vipimo vya


DNA kuthibitisha kauli ya Diana kuhusu Careen kuwa mtoto wa Owen. Ule mfanano wa Owen na Careen ulitosha kuamini kauli ya Diana kwamba Owen ni baba wa Careen. Robyson aliinuka kwenye sakafu alipokuwa ameketi kisha akakaa kwenye sofa. Aliamua kutupilia mbali kile kisu ili kumsogeza mbali shetani kwa wakati ule. Alimuomba Diana kwa utuvu aketi pale kwenye sofa. Diana alikaa huku akiwa anatetemeka. "Diana mke wangu! Naomba


uniambie kwanini ni Owen? Kwanini asiwe mtu mwingine wa mbali? Inamaana miaka yote mulikuwa munanizunguka mimi? Kumbe ulikuwa na mahusiano ya siri na mdogo wangu? Diana, naomba uniambie kwanini unicheat na mdogo wangu?" Robyson alimuuliza Diana maswali hayo kwa uchungu mkubwa. Diana alionekana kufuta machozi kisha akaanza kumsimulia Robyson ukweli wote kuhusu mahusiano yake ya awali na


Owen. Alimsimulia mpaka ile mara ya mwisho alipolala na Owen ikiwa ni siku mbili tu baada ya Owen kurudi kutoka masomoni. Robyson alijikuta anachoka kupitia ile stori ya Diana. Sasa alianza kukumbuka matukio kadhaa yaliyotokeaga miaka ya nyuma baada ya Owen kurudi masomoni. Alikumbuka Owen aliwaambiaga kwamba atamtambulisha mpenzi wake siku ambayo Robyson angemvisha pete mchumba 'ake. Lakini ule utambulisho haukufanyika kwa sababu penzi


la Owen na mwanamke wake lilifikia tamati kabla ya siku ya utambulisho. Robyson alikumbuka namna Owen alivyokuwa anapitia wakati mgumu baada ya kuachwa na mpenzi wake katika kipindi kile. Kumbe mwanamke mwenyewe ndo alikuwa Diana aliyemvishaga pete. Sasa alianza kuelewa kwanini Owen na Diana walikuwa wanatazamana kama watu wanaofahamiana kwenye ile siku ambayo alimvisha pete Diana. Aliikumbuka vyema sura ya Owen akagundua kwamba lile


tabasamu alilotoaga lilikuwa la bandia. Alikumbuka pia namna Owen alivyotoa maua na kumkabidhi Diana kwenye ile siku ya ndoa yao. Hapo sasa Robyson alipata picha halisi kuhusu Owen na Diana. Robyson alimruhusu Diana aende chumbani akabadili nguo na kuendelea na shughuli zake zingine. Yeye alibaki pale sebuleni huku akiendelea kunywa pombe na kutafakari kitu cha kufanya. Siku hiyo Robyson alikunywa pombe kweli kweli. Alikunywa mvinyo ilimradi tu apunguze mawazo kichwani.


Mwanaume hakujua nini cha kufanya juu ya Diana, Owen na Careen. Taratibu sasa alianza kuelewa kwanini Owen alimwambia kwamba wakati anamnyooshea kidole kuhusu Laureen basi afikiri kuhusu vidole vitatu vinavyotazama yeye kuhusu Diana wake. Sasa aliamini kwamba sio kila mwanamke msomi na mwenye pesa ni mwaminifu katika mapenzi, hata wasomi na wenye pesa ni wasaliti sana katika mapenzi. Hakuna somo la mapenzi ya dhati vyuoni wala


mashuleni hivyo mke au mume bora anapatikana popote pale na hapimwi kwa kiwango chake cha elimu au pesa. Sasa Robyson alielewa kwamba Diana alikuwa mshenzi wa tabia pengine kuliko hata Laureen. Yote kwa yote Robyson alitaka kumuuliza mdogo wake Owen kwanini aliamua kuificha ile siri. Siku iliyofuata ilikuwa ni jumapili hivyo wafanyakazi hawakwenda kazini. Robyson alimuita Owen nyumbani kwake na alimtaka aende na Laureen. Mpaka kufika muda huo, zilikuwa zimebaki siku


chache tu kuelekea harusi ya Owen na Laureen. Kiufupi ni kwamba ile siri ilifichuka kwenye wakati mbaya sana. Kulikuwa na uwezekano mkubwa sana wa kuathiri ndoa ya Owen na Laureen kutokana na uzito wa lile jambo. Owen na Laureen waliwasili nyumbani kwa Robyson kuitikia wito maalumu. Walipofika walikaa kitako katika sebule. Kulikuwa na Robyson, Diana, Owen na Laureen. Yule mtoto Careen aliambiwa akacheze ili asisikie maongezi ya watu wazima. Muonekano wa


Robyson na Diana ulitosha kutoa tafsiri kwa Owen na Laureen kwamba pale ndani hapakuwa shwari. Ilibidi tu wasubiri kusikiliza ajenda kuu ya ule wito. Robyson alimtazama sana Owen kisha akaanza kuzungumza kwa kumuuliza, "Bwana mdogo, Hivi unamjua baba halisi wa Careen?" Robyson alimuuliza Owen swali la kushtua kidogo. "Ndio namjua, si wewe hapo Broo.!" Owen alijibu huku tayari


akiwa na wasiwasi "Hapana, Sio mimi.! Baba halisi wa Careen ni wewe na nadhani unalifahamu hilo.!" Robyson aliongea huku akiwa amekaza sura. Kauli ya Robyson ilimshtua sana Owen na Laureen. Owen alianza kutokwa na jasho huku Laureen akibaki amepigwa na butwaa zito. "Brother Roby, ujue bado sijakuelewa. Yani unamaanisha...


unamaanisha Careen ni mto.. mtoto wangu? Mtoto wangu ki vipi yani?" Owen aliuliza huku akiwa na kigugumizi "Diana, hebu mwambie mzazi mwenzio kuhusu mtoto wenu.!" Robyson aliongea huku akimgusa bega Diana. "Owen! Ile siku ya mwisho tuliyolala mimi na wewe ndo siku ambayo mimba ya Careen ilipatikana.!" Diana alizungumza kauli hiyo huku akimtazama Owen.


Kwa hakika kauli ya Diana ilienda kugusa sehemu mbaya sana kwenye mwili wa Owen na kumfanya anyong'onyee mazima. Laureen nae alijikuta anachoka mno kufuatia kauli ile. Hapo sasa alielewa kwanini Careen alifanana na Owen kwa kila kitu isipokuwa jinsia tu. Lakini sasa alijiuliza ni kwanini Owen aliamua kulala na mke wa kaka yake? Kwanini Owen aliamua kufanya ule uchafu? Laureen alimtazama Owen huku akitokwa na machozi. Siku zote alijua


Owen ni mwanaume msafi sana kumbe haikuwa kama alivyofikiria. Kumbe Owen alikuwa na madudu mengi machafu aliyoyaficha nyuma ya pazia. Laureen alianza kulia huku Owen akiwa amejiinamia. Ilikuwa vigumu sana kwa Owen kupinga juu ya ile kauli licha ya kwamba hakufanyiwa vipimo vya DNA kati yake na Careen. Ule muonekano wa Careen ulitosha kumthibitishia kwamba Careen alikuwa mwanae. Ilibidi sasa Robyson amuulize Owen kwanini aliamua kumfanyia ule mchezo


mchafu mpaka kufikia hatua ya kumpachika mimba shemeji yake. Owen alivuta pumzi ndefu kisha akaanza kusimulia historia kuhusu mahusiano yake na Diana kuanzia mwanzo mpaka ile siku walipoachana. Stori ya Owen ilimshtua sana Laureen kwani miaka yote aliyoishi na Owen hakuwahi kabisa kujua kama yule mwanamke aliyemsalitigi Owen miaka kadhaa iliyopita kumbe alikuwa Diana. Yule mwanamke ambaye alisababisha Owen anywe pombe nyingi mpaka kuzamia kwenye


danguro la makahaba kumbe ni Diana. Laureen alivuta kumbukumbu ya maneno aliyozungumzaga Owen ile siku ya kwanza kabisa walipokutana na kwenda pamoja Gesti. Alikumbuka Owen alisema ni bora yule mwanamke (Diana) angeenda mbali kuliko kuchukuliwa na mtu wake wa karibu. Hapo sasa Laureen alielewa picha nzima ilivyo. Kumbe siku zote Owen alikuwa na siri nzito juu ya Diana. Kumbe Owen na Diana walikuwaga wapenzi na waliamua kuificha ile


siri. Kwa upande wa Robyson, maneno ya Owen yalikuwa kama marudio tu kwani alisimulia kile kile alichosimulia Diana. Kupitia ile simulizi, Robyson aliona kosa la Owen lilikuwa moja tu ambalo ni kuficha ile siri mbele yake. Robyson alimuuliza Owen kwanini hakumwambia kwamba Diana ndo alikuwa mpenzi wake na ndo huyo huyo aliyemsalitigi. Owen alimjibu Robyson kwamba aliamua kuficha ile siri kwa kuwa hakutaka kuharibu ndoa yao. Alijua kabisa Robyson alikuwa anampenda sana Diana hivyo


hakutaka kuikatisha furaha yake. Hakutaka kabisa kumuona kaka yake anakosa furaha kwa kuharibika ndoa yake. Lakini pia wazazi wake walishafanya maandalizi kwa ajili ya harusi ya kaka yake hivyo hakutaka kabisa kuharibu ratiba za watu wazima ndo maana akakubali kuwa mbuzi wa kafara. Lakini pia alishaombwa na Diana aifiche ile siri kwani alihitaji sana kuolewa na Robyson. Kwa kuwa Diana alionesha kutohitaji tena mahusiano na Owen, Owen akaamua kumwacha mtoto wa


kike aende kwa mwanaume anayempenda na akakubali kumtunzia siri yake. Maneno ya Owen yalimuingia vyema Robyson. Robyson alimtazama Owen kisha akasema, "Ndugu yangu, ahsante sana kwa kuonesha upendo wako kwangu. Kwa hakika nimeuona upendo wako kwangu. Kwa ajili ya furaha yangu ukakubali kuitoa sadaka furaha yako. Lakini pia naomba unisamehe sana kwa kukudhulumu mwanamke wako. Sikujua kama ulikuwa unapitia


kipindi kigumu kwa ajili ya ndoa yangu. Owen, Una akili sana ndugu yangu. Hili alilofanya Diana lilikuwa linatengeneza uadui mkubwa baina yetu sisi ndugu. Kama ungekuwa mtu mwingine basi ungenichukia mazima lakini wewe haukunichukia badala yake uliendelea kunipenda kaka yako. Kiukweli kabisa, sina tatizo na wewe Owen ila nina tatizo na Diana. Sijui kuhusu hatima ya Careen lakini kuhusu ndoa yangu nafikiri hapa ndo imefikia tamati. Siwezi tena kuendelea na hii


ndoa ili kuepusha aibu huko mbele.!" Robyson aliongea kauli hiyo kwa majonzi makubwa "Brother eeh, Mimi sifikiri kama hayo ni maamuzi sahihi kwenye hili suala. Kwanza kabisa unatakiwa kujua damu ni nzito kuliko maji. Mimi na wewe ni ndugu wa damu kabisa hivyo mwanangu ni mwanao na mwanao ni mwanangu. Mimi naomba tuendelee kuishi kama ilivyokuwa hapo awali. Endelea kumtazama Careen kama mwanao kwa sababu tayari


Careen anajua wewe ndo baba yake na hata wazazi na watu wengine wanajua hivyo. Naomba tuungane kwa pamoja tuendelee kuizika hili siri kwenye mioyo yetu. Me naomba uendelee tu kuishi katika ndoa yako kwa sababu mimi na Diana tulishamalizana kabla hata hamjaoana. Kwa sasa mimi nina mwanamke wangu na nafurahia mahusiano yangu hivyo siumizwi kabisa na ndoa yenu.!" Owen alizungumza kauli hiyo. "Owen! Huna haja ya kutumia


nguvu zako kutengeneza tena ndoa yetu. Mimi mwenyewe naunga mkono hoja ya Robyson kuhusu mustakabali wa hii ndoa. Huu ndo mwisho wa ndoa yangu na Robyson. Kiukweli kabisa sikuolewa na Robyson kwa mapenzi yangu. Nilikubali kwa sababu ya tamaa zangu pamoja na shinikizo la Baba yangu. Kiukweli kabisa ndani ya moyo wangu kuna mwanaume mmoja tu ambaye ni wewe Owen. Katika kipindi chote nilichoishi na Robyson nimeshindwa kukusahau kabisa. Yale uliyowahi


kuyafanya kwangu yameacha kumbukumbu za maumivu kwenye moyo wangu. Siwezi kukulaumu wala kukuchukia kwa kuwa nilikupoteza kwa tamaa zangu mwenyewe na sina uwezo wa kukupata tena. Ninachoshukuru sasa hivi ni kwamba umeniachia kiumbe chako hivyo nafurahi kwa hilo. Ninachoenda kukifanya muda huu ni kwenda na mwanangu mbali na ardhi ya hii nchi ili kuepusha aibu katika familia zetu. Naondoka lakini nitawaletea binti yenu baada ya


miaka kadhaa kupita.!" Diana aliongea kauli hiyo kwa uchungu. "Diana.! Nilikuoa kwa kuamini kwamba ulikuwa unanipenda. Ila kwa sasa acha tu niseme safari njema na kila la kheri huko uendako. Naomba ukampe malezi mema mwanetu. Careen ni damu yetu na ndo mjukuu wa kwanza kabisa kwenye familia ya Mr James.!" Robyson alizungumza kauli. Baada ya kuzungumza kauli hiyo, Robyson alimtazama Laureen


kisha akamtazama Owen. "Unajua nini Bwana mdogo, ukiachana na tamaa za Diana kutusambazia raha sisi ndugu, Lakini pia hata sisi tulifanya kosa. Kosa letu kubwa ni kutotambulishana wachumba wetu ilihali sisi ni ndugu. Usiri wetu ndo ulipelekea tujikute tunashea mwanamke mmoja. Kama ungenitambulishaga huyu Diana au kunitumia hata picha yake basi nisingethubutu kumchumbia Diana na kumuoa kabisa. Kuanzia sasa sihitaji tena


kuificha siri yeyote kwako. Vyovyote itakavyokuwa ni sawa lakini ngoja nikuambie kitu usichokijua kuhusu mimi na shemeji Laureen. Tangu siku ya kwanza nilikuwa napinga mahusiano yako na Laureen kwa sababu mimi ndo nilikuwa wa kwanza kabisa kumfahamu Laureen kabla yako. Ukweli ni kwamba mimi na heshima zangu zote nilikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanaenda kununua wanawake kwenye danguro la makahaba. Huyu shemeji Laureen ni miongoni mwa


wanawake niliowahi kuwanunua na kulala nao. Nimeamua kuzungumza hili ili kila kitu tukiweke sawa hapa hapa. Sihitaji tena kuishi na vifundo moyoni mwangu.!" Robyson alizungumza kauli hiyo na kumfanya Laureen na Diana kushtua. Wakati Laureen na Diana wanashtuka, Owen yeye aliipokea taarifa ile bila mshtuko wowote ule. Alimtazama Laureen kisha akamtazama Robyson na kusema,


"Brother Roby, Ile siku ulipokuwa unazungumza na Laureen na kukuomba umtunzie siri yake nilikuwa mahali nimebana na kusikiliza. Nilimsikia Laureen akikuomba usiniambie kama ulishawahi kulala nae kwenye danguro. Kiufupi ni kwamba nilikuwa nalitambua hilo na nilianza kumpenda wakati nayajua madhaifu yake yote. Brother eeh, Huyu mwanamke mimi nampenda sana na nilichagua kuyavumilia madhaifu yake. Ukiwa kama kaka yangu,


nategemea baraka na support yako kuelekea sherehe yangu ya harusi.!" Owen alizungumza maneno hayo huku akiwa na tabasamu katika uso wake. Kauli ya Owen ilimfanya Laureen aamini kabisa moyo wake ulikuwa sehemu sahihi kabisa. Hakuwahi kabisa kudhania kama Owen alikuwa anafahamu siri yake na Robyson. Kumbe miaka yote waliyoishi pamoja Owen alikuwa anajua kila kitu. Ni vile tu mwanaume alichagua kuishi na Laureen ndo maana aliyapokea


madhaifu yote ya mtoto wa kike kisha akayawekea uzio ili yasijitokeze tena. "Owen! Asante Baba.! Nakupenda sana wewe mwanaume.!" Laureen alijikuta anazungumza maneno hayo huku akitokwa na machozi. Owen hakumjibu Laureen badala yake alimtazama Diana na kumwambia, "Diana! Naomba sana umtunze Careen wetu na usimuhusishe


kabisa kwenye ugomvi wetu. Mimi sina uadui na wewe na wala sijawahi kukuchukia. Najua unajua jinsi gani nilivyokupendaga. Hapo awali nilifikiri na kudhani utakuja kuwa mke wangu lakini historia imechagua njia tofauti. Zile ndoto nilizotarajia ningetimiza na wewe hatimaye naenda kutimiza na mwanamke mwingine ambaye sikuwahi hata kumdhania. Laureen ndo mwanamke pekee aliyethibitishwa kwenye maisha yangu mimi. Wiki ijayo kwenye siku ya wapendanao duniani,


nakukaribisha sana kwenye ukumbi ule ule uliovishwaga pete mbele ya macho yangu. Hiyo siku nami nitakuwa na jambo langu kwa mwanamke ninayempenda.!" Owen aliongea kauli hiyo iliyokwenda moja kwa moja kukita kama msumari wa moto kwenye moyo wa Diana. Kama utani vile Diana alijikuta anadondosha machozi aisee.! NOVEL.................... MY VALENTINE- 42 {Kipenzi


Changu} AUTHOR................. HERRY DESOUZER {Silentkiller} SPONSORED BY...... SILENTKILLER STORIES TEL................ 0699470521/0713601762 INSTAGRAM.............. @realsilentkiller_ ______________FINAL____________ ______ Hiyo ndo hali halisi ya mambo yalivyokuwa. Ndugu wawili,


Robyson na Owen walimaliza tofauti zao na kuapeana ahadi kwamba wangekuwa bega kwa bega kwa kila jambo. Kilichokuwa kinasubiriwa sasa ni harusi tu kati ya Owen na Laureen. Macho na masikio ya kila mtu kwa wakati ule yalikuwa sawia kusubiri Februari 14 ili kushuhudia ndoa ya wapendanao waliopitia kwenye misukosuko mizito sana. Kabla ya siku ya ndoa kufika, Diana alimchukua mwanae Careen na kwenda kuishi nae nje ya nchi. Hakutaka kabisa kusubiri kuona


ndoa ya Owen na Laureen. Ilifikia hatua alimchukia mpaka Baba yake mzazi, Mr Jay Calvin ambaye alishirikiana na wazazi wa Robyson kutengeneza ndoa ya family friend iliyolenga masilahi badala ya upendo. Diana alilaani vikali ndoa ya aina hiyo kwani ilimfanya ampoteze mwanaume aliyekuwa anampenda kutoka moyoni. Maandalizi ya ndoa yaliendelea huku kadi za mialiko zikisambazwa kwa wingi kwa ndugu, jamaa na marafiki ndani na nje ya jiji. Mpaka kufikia muda


huo tayari Bwana Laurence alishakutanishwa na wazazi wa Owen na kuzungumza kiutu uzima zaidi. Siku ziliyoyoma kwa kasi na hatimaye ilifika ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu. Ni siku ya wapendanao duniani yani Valentine's Day ambayo Owen na Laureen walitarajia kufunga pingu za maisha. Shughuli nzima ilianzia kanisani ambako kiongozi wa kanisani alitumia wadhifa wake kutoa kibali kwa Owen na Laureen kuishi kama mke na mume kupitia maandiko matakatifu.


Zoezi lilikamilika na hatimaye Owen Laureen walikuwa Mr na Mrs ama mke na mume. Baada ya shughuli kumalizika kanisani, sherehe nzima ilihamishiwa ukumbini sasa. Huko sasa mambo ndo yalitaradadi na kunoga kweli kweli. Watu walifurika ukumbini kama kumbikumbi kushuhudia ndoa ya kihistoria ya kijana kutoka familia ya kitajiri ambaye aliangukia kwenye penzi la mwanamke kahaba kutoka familia ya kimaskini. Ile sherehe haikuwa ya kibaguzi kwani watu wa hadhi


zote waliruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi kupata chakula, vinywaji na burudani mbalimbali. Hata wale marafiki wa Laureen waliokuwaga pamoja kwenye danguro la ukahaba waliweza kuhudhuria ile sherehe. Kila aliyekumbuka historia ya Laureen aliishia kudondosha machozi. Ilikuwa vigumu sana kuamini kama yule Laureen aliyekuwa kahaba hatimaye amekuwa Daktari na tayari ameshaolewa na kijana msomi, mfanyabiashara na mwenye pesa zake. Kwa hakika haikuwa


rahisi kwa Laureen kufikia yale mafanikio kwani alipitia kwenye njia ngumu sana yenye tabu, mateso, manyanyaso, dharau na masimango ya kila aina. Imani, subra na uvumilivu ndo vitu pekee vilivyopelekea kumpa ushindi katika dakika za mwisho kabisa. Siku hiyo Laureen alipokea zawadi nyingi sana kutoka kwa marafiki zake ambao wengi walikuwa madaktari na wale aliosoma nao vyuoni. Owen nae alipokea zawadi nyingi sana kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa kampuni ya SK


GROUP. Pongezi zilikuwa nyingi sana kwao. Familia nzima ya Mr James ilifurahi sana. Bwana Laurence pia alifurahi kuona Binti yake ametengeneza status nzuri kwenye familia yao. Ule uvumi kwamba Laureen alikuwa kahaba haukuwa na nguvu tena kwenye vinywa vya watu. Kila mtu aliishia tu kutoa pongezi kwa wapendanao kwa hatua kubwa waliyofikia. Watu walikula, wakanywa na kupata burudani ya mziki laini kabisa. Kwa kuwa ilikuwa siku ya wapendanao, kila mmoja alionekana kudansi na


kipenzi chake pale ukumbini huku nyimbo mbalimbali za mahaba zikipigwa. Owen na Laureen wao walikuwa jukwani kabisa wakidansi kwa pamoja. Mkono mmoja wa Owen ulikuwa begani kwa Laureen na mwingine ulikuwa umeshikilia kiuno cha mtoto wa kike. Laureen yeye alikuwa ameweka mikono yake yote mabegani kwa Owen huku akimtazama kwa kurembua na kudansi kwa madowido kabisa. Wakati wanaendelea kudansi walianza kupiga stori kwa sauti za mahaba huku wakisindikizwa


na wimbo wa maalumu wa Valentine's Day, "My me, mwenzako mimi bado siamini Babaa.!" "Huamini nini Mamaa.!" "Siamini kama mimi hapa, tayari nimeshakuwa mke wako.!" "Kwanini huamini sasa?" "Kwa sababu wewe hapo ni hensamu Babaa. Wanaokutaka ni wengi tena ni wazuri kuliko hata


mimi.!" "Hapana mke wangu, wewe hapo ni mzuri kuliko hata hao unaowasema. Kiukweli kabisa mimi hapa mimi, sijakupenda wewe kwa kuwa eti mapenzi ni upofu, macho yangu mimi yalikuona wewe na moyo wangu ukakuchagua.!" "My me, Ahsante sana kwa kunipenda mume wangu.!" "Ok, Ahsante pia kwa kushukuru na kuniridhia niwe mume wako.!"


"Ila unajua nini Chibaba wangu.!" "Walaa! Sijui hata Chimama wangu.!" "Ni hivi, Mwaka mzima una siku takribani 365. Lakini sasa, kwangu mimi Februari 14 ndo siku pendwa na bora kabisa kwenye maisha yangu.!" "Lakini kwanini wewe hapo umeichagua hiyo siku kuwa bora zaidi kwako.!"


"Ni kwa sababu hiyo ndo siku ambayo tulianzisha rasmi harakati za kupigania penzi letu. Siwezi kusahau ile siku ulivyowatangazia watu kwenye huu ukumbi kwamba mimi hapa ndo Valentine wako. Ile ndo siku ambayo tuliingia rasmi kwenye vita dhidi ya walimwengu ambao walikusudia kuidhulumu haki yangu ya kupendwa na wewe. Lakini pia ndo hii hii siku ya leo ambayo umeniheshimisha kwa watu waliodhani mkono wangu mimi hauna kidole kinachostahili kuvaa pete ya ndoa kutoka


kwako. Kiukweli kabisa nitaendelea kuikumbuka na kuiheshimu Valentine's Day.!" "Ni kweli Chimama wangu, Upo sahihi kabisa katika hilo. Hii ni siku spesho sana kwetu na nafikiri tufanye kitu kwa ajili kuienzi na kuiwekea kumbukumbu kabisa.!" "Enhee, Kitu gani hiko tufanye Chibaba wangu?" "Naomba ukijifungua mtoto wa kiume basi tumuite VALENT na


kama atakuwa wa kike basi tumuite VALENTINA.!" "Waooh! Umewaza mbali sana Baba Valent.!" "Hahah! Kwahiyo ndo ushaanza kulitumia kabisa jina la Valent. Je kama kijacho wetu ni wa kike?" "Hahah! Huyu ni wakiume maana wa kike tayari tunae Careen wetu.!" "Hahah! Unajua nini Mrs wangu.!"


"Hata sijui Mr wangu.!" "Mwenzako mimi nime-miss eti.!" "Ume-miss nini Mr wangu?" "Nime-miss kusikia ukiniita 'Kaka Owen.! Kiukweli kabisa nime-miss mimi.!" "Dah! Umenikumbusha mbali sana mume wangu. Ama kweli mapenzi ni safari kwani tulipotoka ni mbali sana huku tukikatiza milima na mabonde. Kwa imani moja tuliamini


kwamba tutafika lakini hakuna hata mmoja wetu aliyejua siku, mwezi wala mwaka ambao tungefika. Kaka Owen eeh...!" "Naam.!" "Kaka Owen eeh..!" "Naam.!" "Kaka Owen eeh.!" "Naam, Dada Laureen.!" "Mimi hapa mimi, Nakupenda


sana wewe. Nakupenda sana Kaka Owen. Lakini Kaka Owen, Will you be my forever valentine ?" Laureen alimuuliza swali Owen lililobeba tafsiri ya kwamba 'unaweza kuwa mpenzi wangu wa milele?' Owen alijikuta anatabasamu baada ya kusikia lile swali. Kwanza kabisa alim'busu Laureen kwenye paji la uso kisha akamjibu kwa sauti yenye hisia kali kutoka ndani ya moyo, "Yes, I Will.! I will be your


Valentine till my last breath. The day I will stop loving you is the day when I close my eyes forever. I love you My Laureen. I love you now and then..!" Owen alihitimisha maongezi kwa kumjibu Laureen maneno hayo yaliyobeba tafsiri ya kwamba 'Ndio nitakuwa.! Nitakuwa kipenzi chako mpaka pumzi yangu ya mwisho. Siku nitakapoacha kukupenda ndo siku nitafumba macho yangu milele. Nakupenda sana Laureen wangu. Nakupenda sasa hivi na kuendelea..


#NYIEEE...! IT WAS MV14. NITAKUFA MIMI ILA RIWAYA ZANGU ZITAISHI NA MTAKUJA NA MASHADA SIKU YANGU YA MAZISHI. NIPENI RAMBIRAMBI ZANGU NIZILE NIKIWA HAI. MPAKA KUFIKIA HAPO NAWEKA CHINI KALAMU YANGU KUHITIMISHA RIWAYA YETU YA "MY VALENTINE" NYUMA YA CAMERA NILIKUWA MIMI MTAALAMU WAKO HERRY DESOUZER AKA SILENTKILLER/


INSANITY GENIUS/MR IG/SK97. MENGI NIMEYAZUNGUMZA LAKINI CHUKUA YALIYO MEMA KISHA ISHI NAYO, YALE MABAYA NIACHIENI MWENYEWE JINIAZ MPUMBAVU NITAISHI NAYO. NAKARIBISHA COMMENTS ZA UKOSOAJI ILI NIJUE WAPI NIFANYE MABORESHO.ILI NIWALETEE KAZI NZURI ZAIDI. HUU MWAKA NI MWENDO WA MAWE TU. TULIENI HAPA HAPA.....


KWA MAONI NA USHAURI NICHEKI KUPITIA, 0699470521 {Normal call/SMS} 0713601762 {WhatsApp only} NI-FOLLOW INSTAGRAM @realsilentkiller_ #HerryDesouzer #Silentkiller #InsanityGenius #MrIG #Sk97







Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.