Ulinzi wa miti

Page 1

ulinzi wa miti Tatizo: Ndovu kuharibu miti Ndovu wanahitaji kula miti na majani ili wapate virutubisho, lakini pia wanaweza wakaharibu moja kwa moja miti mikubwa yenye umuhimu – wanabandua magome, wanavunja matawi na kung’oa kabisa miti.

Miti mikubwa ya kihistoria ni muhimu kwa uchumi, utamaduni na wakati mwingine hata sababu za kimatibabu. Inahusika moja kwa moja na maisha ya msituni, wanyama, na mimea. Kwa mfano, huko kusini mwa Afrika, tafiti zinaonyesha kuwa ndovu wanapenda kutumia miti kama ya Marula, Knob thorn na Red bushwillow kupata virutubisho.

1.

Kwa mfano miti ya Marula iliyopo Afrika Kusini ni miti muhimu inayozaa matunda na yana thamani kubwa ya kiuchumi. Uharibifu wa miti hii ni chanzo cha migogoro baina ya wanadamu na ndovu. Ndovu wanaweza kubandua magome. Kuvunja matawi au kusukuma miti wakiwa wanakula – ndovu dume wanaweza kusukuma miti mingi zaidi kuliko ndovu jike.

Miti ambayo imepunguzwa au kuvunjwa huweza kuwaathiri wadudu au kushika moto.

Kulinda miti dhidi ya uharibifu wa ndovu ni muhimu kwa mfumo mzima wa ikolojia. Kuharibu miti mikubwa hupelekea kupungua kwa anuai ya ndege, popo na mamalia wadogo.


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.