Page 1

RIZIKI

Sept-Dec/2017

Imani Ijaribiwapo

Mimi na wewe tunaweza kuwa na maswali mengi yanayosumbua imani yetu na kututilia wasiwasi mwingi wa kiroho; tunaweza kufadhaika sana na

kukata tamaa ya kufika mbinguni; hata tunaweza kujisikia kana kwamba tumepoteza imani kabisa nayo haipo. Lakini Yesu hajaondoka.


TAHARIRI

RIZIKI TOLEO 3, 2017

RIZIKI

S.L.P. 2696, Arusha Simu: +255 752 379 932 Barua pepe: editor.somabiblia@gmail.com Kamati ya Riziki: Anne Gihlemoen (mhariri) Hezron Mwasi Anza Amen Lema Philip Bach-Svendsen Cathbert Msemo Mary Bura Magdalena Mathayo Emmanuel Mollel Waandishi walioshiriki Gideon Mumo Mch. Gabriel Kimirei Layout: Cathbert Msemo Jalada: Kutoka KKKT Elerai, Arusha Nakala: 4500 Usambazaji

SOMA BIBLIA S.L.P. 2696, Arusha S.L.P. 12772 Dar es Salaam S.L.P. 1088 Iringa S.L.P. 6097 Mwanza S.L.P. 1062 Mbeya

Vita vya ndani

Anne Marken Gihlemoen

Yaliyomo: Ulimwengu kwa Kristo! Imechapwa na:

Imaging Smart - Dar es Salaam

Ukurasa 3-9: Ukurasa 10: Ukurasa 11-12: Ukurasa 13-15: Ukurasa 16-17: Ukurasa 18-19:

Mada: Maadui wanaposhambulia imani/Martin Luther Ushuhuda: Mahangaiko moyoni Watu wa Biblia: Mfalme Sulemani Kanisa la Nyumbani: Kutunza sauti ya roho Historia ya Wimbo: Ni salama rohoni mwangu Jamii: Mchungaji kama meneja 2

RIZIKI TOLEO 3, 2017

Maadui wanaposhambulia imani

“Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia. Bwana, usikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize sauti ya dua zangu” (Zab 130:3). Kama utakavyosoma kwenye ushuhuda katika toleo hili la RIZIKI, watu wengi wanaamini kwamba wakiokolewa, kila siku itakuwa ni kuimba haleluya, na hawatakutana na vikwazo vyovyote tena. Lakini, je, umewahi kukutana na Mkristo yeyote ambaye hajawahi kujaribiwa au kuhangaika moyoni? Mfalme Sulemani alikuwa mwenye hekima kupita mwanadamu mwingine awaye yote. Hata alitajirika sana katika fedha na mali pia. Hakukosa chochote. Na tungefikiri kwamba alikuwa na furaha kabisa. Lakini kinyume chake, anasema: “Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni; Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko” (Mhu 1:18). Vipo vita vya ndani mle moyoni mwa mwamini. Vinamletea maumivu makali na kumfadhaisha. Mimi na wewe tunaweza kuwa na maswali mengi yanayosumbua imani yetu na kututilia wasiwasi mwingi wa kiroho. Tunaweza kufadhaika sana na kukata tamaa ya kufika mbinguni. Hata tunaweza kujisikia kana kwamba tumepoteza imani kabisa nayo haipo tena. Lakini Yesu hajaondoka. Katika toleo hili la RIZIKI tutaelezea zaidi kuhusu kuhusu Mkristo anapohangaika moyoni kwa sababu imani yake inajaribiwa. Tunatumaini makala zitakusaidia ili imani yako ijengeke, na utiwe moyo na ufahamu zaidi wa kuwafariji na kuwashauri waamini wenzako. Ubarikiwe!

www.somabiblia.or.tz

MADA

Maadui wa imani

Magonjwa ya mwili tunayafahamu. Mwili unapoambukizwa na kuingiliwa na vidudu, dalili zake zinaonekana. Huwa mwili una vipingamizi fulani vinavyoupigania. Lakini mara nyingi havitoshi. Mgonjwa anahitaji kumeza dawa au kulazwa hospitali na kupata matibabu ili kupona. Vinginevyo atakufa. Magonjwa ya nafsi yapo pia, ingawa mara nyingi ni vigumu zaidi kuyatambua na kuyatibu. Jinsi gani, kwa mfano, kumsaidia yule aliyeshindwa kujitambua na kujiheshimu sawasawa, au yule aliyekata tamaa kabisa? Si rahisi, maana kwa kawaida ameathirika kwa kipindi kirefu, huenda kuanzia utoto wake. Haitoshi kuzungumza naye siku moja tu, au kumpa vidonge vya kuchangamsha. Vilevile roho ina mapambano yake. Daima hayo yanahusu uhusiano wa mtu na Mungu. Kinachoshambuliwa hapo ni imani yetu. Vipo vita vya ndani mle moyoni mwa mwamini. Vinamletea maumivu makali na kumfadhaisha. Ni suala la uzima au mauti, mbingu au jehahamu. Hata hivyo si kila mara tunatambua sawasawa vita hivyo vya kiroho, na kutafuta kuyatibu maumivu yake inavyotakiwa. Yaeleweka ikiwa asiyeamini haelewi sababu ya maumivu yake na kufikiri pengine ni ugonjwa wa kisaikolojia. Lakini sisi Wakristo tunapaswa kuyatambua mapambano hayo ya kiroho na kujua tukimbilie wapi ili kupata tiba. Maana tiba ipo – kwa uhakika ipo. Hebu tuangalie zaidi jambo hili.

Imani yetu ina maadui wengi. Shetani tunamfahamu. Njia zake za kushambulia ni nyingi. Kwa mfano Biblia inasema anatushawishi kuvitamani vitu badala ya Mungu (Mt 4:8-9). Pia anaturushia mishale yenye moto (Efe 6:16) na kunguruma kama simba mkali ili kututia hofu. Lakini shabaha yake ni moja tu: Shetani anashindana na imani yetu katika Yesu ili kuiondoa. Akifaulu, ameshinda. Vinginevyo tutasimama kama washindi. Dhambi ni adui mwingine wa imani. Kila wakati inatuotea mlangoni (Mwa 4:7). Tusipoiungama dhambi na kuiacha, tutakufa kiroho. Yesu asipopata kutusamehe na kuiondoa kwetu, dhambi itavunja ule uhusiano na Yesu tulio nao kwa imani. Pia ulimwengu, yaani, wasioamini wanafanya vita dhidi ya imani yetu, pengine bila hao kujua. Mfano moja unapatikana katika 2 Pet 3:4 ambapo walimwengu wanatuuliza: Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake Yesu? Swali lao ni kama mshale wenye moto kwenye imani yetu, maana tumaini la uzima wa milele ni tarajio la imani kuhusu siku zijazo. Maadui hawatukabili kutoka nje tu. Wanaye adui mwenzao ndani ya Mkristo. Huitwa Adamu wa kale, na Biblia inamtambulisha kama utu wetu wa kale au mwili wa dhambi (Rum 6:6). Msaliti huyo anatokea kwenye mlango wa nyuma, wakati maadui hao wengine wanataka kuingia kwetu kwa kuvunja mlango wa mbele. 3


MADA

RIZIKI TOLEO 3, 2017

MADA

RIZIKI TOLEO 3, 2017

Adui wa mwisho ni mauti. Biblia inasema kifo kina tanzi (Mit 14:27), kamba na mitego (Zab 18:5). Yaani, si mwili tu unaotiwa hatarini, adui huyu akitokea. Hata imani yetu inaweza kufa tunapokabiliana na mauti, tusipojua jinsi ya kupigana nayo na kuyashinda kiroho.

Yoshua mwenyewe hakusema lolote. Lakini nina uhakika kwamba alikuwa na mawazo mengi moyoni – mawazo yaliyomshtaki vilevile. Alipokuwa akisimama mbele za Mungu, zilionekana tena dhambi ambazo alifikiri zimekwisha kusahaulika. Na ilimbidi kukubali kuwa siyo tu kwamba alishindwa na dhambi; mara nyingine alishiriki hata kwa hiari yake kuzitenda dhambi hizi, na kwa namna fulani alizipenda. Alipokumbuka, Yoshua aliweza kusikia kicheko cha Adamu wa kale akisema: “Na wewe ulifikiri utanishinda? Kubali sasa kwamba umefeli kabisa, na mshindi ni mimi!” Kwa kweli Yoshua alikuwa na sababu ya kunyamaza tu. Maana aseme nini, wakati mashtaka yote aliyosomewa yalikuwa ya kweli! Lakini moyoni mwake, nafikiri Yoshua alilia: “Ole wangu! kwa maana nimepotea!” Huenda moyo wake ulilia kwa sauti nyingine pia: “Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.”

Maadui wanapoungana kuiondoa imani

Vita vikali zaidi vinatokea ambapo maadui hao wote wanashambulia imani ya Mkristo kwa wakati mmoja. Tunao mfano katika Zekaria 3. Hebu tumia muda kuusoma mlango huu kabla hujaendelea na makala hii! Je, uliona maadui wangapi wa imani? Bila shaka ulimwona Shetani aliyesimama mkono wa kuume wa kuhani mkuu, na ulielewa pia anataka nini: kushindana na Yoshua. Dhambi inaonekana kama nguo chafu. Yoshua anapovuliwa nguo hizi, anaambiwa kuwa ni uovu wake unaoondolewa (m.4). Bila shaka ni uovu huu ambao Shetani anakumbusha akimshtaki Yoshua mbele za Mungu. Wasioamini, sijui kama walikuwepo. Lakini ikiwa walimwona Yoshua, bila shaka walimshutumu: “Tazama huyu! Husifiwa kama mtumishi mtakatifu, lakini ni mchafu kama nani! Naye anasema anamtumikia Mungu! Mbaya kuliko sisi!” Bila shaka mauti alikuwepo pia. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti (Rum 6:23), na Yoshua alisimama kama mwenye dhambi mbele za Mungu mwenye haki.

Adui mkali kuliko wote

Hakuna adui wa imani asiye na nguvu. Lakini sasa tunakuja kwa adui mkali kuliko wote. Mpaka sasa sijamtaja. Ila yupo. Na yupo pale hasa ambapo tumesimama mbele za Mungu. Maana anaitwa Sheria – Sheria ya Mungu. Mashtaka ya Shetani si kitu kulingana na mashtaka ya Sheria, maana anayosema Shetani ni uongo isipokuwa yakithibitishwa na Sheria. Vilevile dhambi si kitu isipokuwa kwa sababu ya amri za Sheria. Hata mauti haipo tena, ikiwa Sheria hana la kusema. Maana Sheria ana neno

Vipi na kushindania imani? 4

5


MADA

RIZIKI TOLEO 3, 2017

Yesu hajaondoka imani ijaribiwapo

la mwisho kwa sababu anaongea na sauti takatifu ya Mungu. Sheria ndiye Mungu katika utakatifu wake. Ikiwa umesimama mbele za Mungu kama Yoshua, unajua kwa nini hakusema lolote ili kujinusuru na adhabu ya kifo. Unajua, kwa sababu pamoja na kusikia maumivu makali moyoni mwako, umejifunza kwamba Sheria hunena ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu (Rum 3:19).

Hebu angalia jambo moja zaidi katika habari za Yoshua! Wakati wote huyo malaika wa Bwana alikuwepo. Hakuondoka kwa sababu ya uchafu wa Yoshua wala mashtaka ya Shetani. Hiyo ni habari njema kwa sisi sote: Mimi na wewe tunaweza kuwa na maswali mengi yanayosumbua imani yetu na kututilia wasiwasi mwingi wa kiroho; tunaweza kufadhaika sana na kukata tamaa ya kufika mbinguni; hata tunaweza kujisikia kana kwamba tumepoteza imani kabisa nayo haipo. Lakini Yesu hajaondoka. Yuko karibu, na pamoja na Yesu upo pia wokovu wake. Ninaposikia habari hiyo njema, uhakika unachipuka na kukua moyoni mwangu kwamba nikiwa na Yesu tu, sitashindwa. Maadui wa imani hata wakishambulia kwa nguvu zote, hawatafaulu. Si kwa sababu ya imani yangu, kana kwamba ina nguvu ya kuwashinda, bali kwa sababu ya Yesu ninayemwamini. Yeye ndiye ushindi wangu. Ataniokoa - mimi pamoja na imani yangu.

Kiongozi wa kutuleta kwa Yesu

Nilimwita Sheria ‘adui mkali kuliko wote’. Kwa namna moja ni kweli, kwa namna nyingine sivyo. Maana Sheria ndiye pia yule kiongozi anayetuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani (Gal 3:24). Je, ulimwona Yesu pia uliposoma habari za Yoshua? Ndiye yule malaika wa Bwana, tena ni yule mtumishi wa Bwana aitwaye Chipukizi. Imeandikwa kuwa malaika wa Bwana aliamuru kwamba Yoshua avuliwe nguo chafu, na avalishwe mavazi ya thamani nyingi. Aliwezeje – bila kuvunja sheria takatifu ya Mungu? Aliweza, kwa sababu katika siku moja uovu wote wa dunia ulikuwa utaondolewa kwa njia ya yule mtumishi wa Bwana (m. 9). Ahadi hii ilitimizwa siku ile Yesu alipolia: “Imekwisha” (Yn 19:30)! Yeye asiyejua dhambi, Mungu alimfanya dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kusimama mbele za Mungu hali tumevikwa mavazi ya thamani nyingi ya haki ya Yesu (ling. 2 Kor 5:21).

MADA

RIZIKI TOLEO 3, 2017

Je, Martin Luther bado ana maana kwetu? Jibu tumwachie yeye mwenyewe, kwa sababu inaonekana kwamba alitaka kutoa ushuhuda baada ya kifo chake.

Mwaka 1522 aliandika: ”Naomba watu waache jina langu na wasijiite Walutheri, bali Wakristo. Maana Luther ni nini?

Philip Bach-Svendsen

6

7


MADA

RIZIKI TOLEO 3, 2017

Mafundisho siyo yangu! Wala mimi sijasulubiwa kwa ajili ya mtu yeyote (1 Kor 1:13). Paulo hakutaka kabisa Wakristo kujiita wa Paulo au wa Petro (1 Kor 3:2 na 21nk, angalia pia 1:12); walipaswa kuitwa Wakristo. Inakuwaje mimi – mfuko duni wa samadi inayonuka – nifike hapo ambapo watu wanaanza kuwaita watoto wa Kristo kwa jina langu la maafa?”1 Kwa hiyo kitu muhimu ni ”mafundisho”, na si Luther. Na mafundisho humaanisha mafundisho ya Neno la Mungu. Mara nyingi Luther alisema kwamba alikuwa tayari kufuta kila kitu alichosema – mradi tu ahakikishiwe kwa Neno la Mungu kwamba alichokisema si cha kweli. Hivyo tumerejea kwenye jambo kuu: Neno la Mungu lasema nini? Je, Luther alishuhudia kwa usahihi na kweli kuhusu Neno la Mungu? Hebu tunukuu neno moja zaidi. Liliandikwa muda mfupi baada ya hayo yaliyonukuliwa hapo juu. Luther anaandika: ”Ni kweli kwamba unapaswa kutokusema ‘mimi ni wa Luther’ au ‘mimi ni wa Papa’, kwa kuwa hakuna hata mmoja wao aliyekufa kwa ajili yako; ni Kristo tu aliyekufa kwa ajili yako. Lakini ikiwa umehakikishiwa kwamba mafundisho ya Luther ni ya Kiinjili, na kwamba mafundisho ya Papa si ya Kiinjili, basi, usimtupe Luther bila sababu ya kutegemewa, kwa kuwa ukimtupa hivyo unakataa mafundisho pamoja naye, na ni mafundisho haya ambayo unayatambua kuwa mafundisho ya Kristo. Hapana, sema hivi badala yake: ‘Ikiwa Luther ni mkorofi au mtakatifu, mimi sijali; mafundisho yake si yake yeye,

bali ni mafundisho ya Kristo’. Kumbuka unavyoona, jinsi madikteta walivyo na mipango ya kuondoa si Luther tu – lengo lao ni kumaliza kabisa mafundisho! Na ni kwa sababu ya mafundisho, wanakusuta na kuuliza ikiwa wewe ni wa Luther. Hapo inakubidi kutojibu kwa maneno laini, bali umkiri Kristo kwa unyofu!”2 Hakuna mtu aliyelazimika kuamini na kukiri jambo kwa kuwa Luther alilisema. Hata wakuu wanaweza kufanya makosa na kuwa watu wasiofuata utaratibu. Katika mambo mengi Luther aliyoyaandika na kuyasema, si vigumu hapa na pale kuona sababu ya kuuliza swali. Kwa hiyo Kanisa linalojitambulisha kwa jina lake halijafanya maneno ya Luther kuwa kigezo; Maandiko Matakatifu peke yake ndiyo kanuni, kipimo na kitu cha kuigwa! Kwanza na mwisho, ukuu wa Luther unapatikana katika kukiri kwake kwamba Maandiko Matakatifu peke yake yanastahili kuweka kanuni za imani – hakuna kitu kingine. Kristo pekee ni Mwokozi wetu, ambaye tunamwamini na kumkiri. Luther ni kiongozi wa kuaminika kwa wale wanaotaka kupata ule ukweli unaookoa, ukweli wa Maandiko Matakatifu kuhusu Yesu Kristo. Makala hii inatoka kutoka kitabu kipya cha “Theolojia ya Martin Luther”. Kinapatikana Soma Biblia 1.

Martin Luther. Verker i utvalg, I-VI. Ved Inge Lønning og Tarald Rasmussen, 1979nk Cl 2,308

2.

8

Luthers Werke in Auswahl, herausgegeben von Otto Clemen, I-VIII, 1950

MADA

RIZIKI TOLEO 3, 2017

KITABU KIPYA!

Kitapatikana kwenye maduka yote ya Soma Biblia. Dar es Salaam, Arusha, Iringa, Mbeya na Mwanza.

“Kwa nyakati hizi ambapo tunashuhudia upotoshwaji mkubwa wa Neno la Mungu, hasa kuhusu kiini cha wokovu wetu, kitabu hiki kitakuwa msaada mkubwa kwa Mkristo yeyote mwenye hamu ya kufahamu kwa undani kusudi na misingi ya Matengenezo ya Kanisa kama alivyofundisha Dk. Martin Luther mwenyewe. Ninapendekeza kitabu hiki kisomwe na watu wote”.

Askofu Dkt. Fredrick O. Shoo MKUU WA KKKT 9


USHUHUDA

RIZIKI TOLEO 3, 2017

RIZIKI TOLEO 3, 2017

MFALME SULEMANI:

Mahangaiko Moyoni

Utupu wa mahangaiko bila Mungu

Nilipompokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wangu, sikuwa na mawazo yoyote ya kukutana na vikwazo. Niliamini kila siku ni kuimba Haleluya. Kwa hiyo nilipohangaika moyoni, sikujua la kufanya.

Nimejifunza kuwa, kama vile vifaa vinavyotumia nguvu ya umeme, vinavyokosa maana kama havijaunganishwa kwenye umeme na kutumiwa kwa kazi iliyokusudiwa, vivyo hivyo maisha yetu Wakristo yanashambuliwa na kutawaliwa na mahangaiko mengi tusipojiunganisha kwa Mungu alinisaidia kupitia 1 Pet 5:6-11: Mungu wa mbinguni, ili tufanye mapenzi “… mkimtwika yeye fadhaa yake. Nguvu za ushindi zenu zote, kwa maana yeye ipo katika muunganiko hujishughulisha sana kwa Nimejifunza kuwa, kama vile wetu na Mungu daima. mambo yenu.” vifaa vinavyotumia nguvu ya Ukiendelea kuhangaika umeme, vinavyokosa maana Nikajifunza zaidi mambo kama havijaunganishwa kwe- peke yako, unajiumiza yanayoleta mahangaiko nye umeme na kutumiwa na kujitesa mwenyewe. moyoni, na kufanya nafsi ya kwa kazi iliyokusudiwa Kuhangaika hakutamtu kuinama. Mahangaiko tuii matatizo bali kuhumfanya mtu asitulie, awe jiongezea mzigo mzito na hofu au wasiwasi. Kwa zaidi usiobebeka. Fikiri kuwa tunaishi kwenye ulimunataka kusonga mbele, wengu wenye misukosuko, sote tunaweza lakini unabaki ukibembeabembea, yaani kulemewa na mahangaiko moyoni. Ya- unahangaikahangaika tu. Makosa yaliyonayosababisha mahangaiko ni pamoja pita yasikuhangaishe, bali mtwike Bwana na makosa ya wakati uliopita, mawazo Yesu fadhaa hizo. Kunyenyekea chini kuhusu wakati ujao na pesa. ya mkono wa Mungu ni dawa pekee ya moyo unaohangaika. Bwana Yesu anaseHangaiko katika moyo wa mtu huufan- ma: “Njooni kwangu, ninyi nyote mliolya uiname, lakini neno jema huufanya emewa na kusumbuka, nitawapumzisha” ushangilie. Neno jema hupatikana ka- (Mt 11:28-30). tika habari njema ya ufalme wa Mungu. Yesu asema kuwa tusihangaikie ya kesho Ninapomwendea Yesu namna hii, napewa (Mt 6:25,34). Ila tunapotafakari yale kufurahia msamaha wa dhambi zangu na mahangaiko, huwa tunaweza kusahau kushangilia wokovu wa Bwana, namtukujiunganisha na Mungu mweza yote, mikia kwa furaha ikiwa ni sehemu ya na mfadhaiko unapata nguvu na kutu- shukurani zangu kwake kwa yote aliyoniangusha. tendea. Na Magdalena Mathayo 10

WATU WA BIBLIA

Je, anaweza mtu kupata uradhi na pumziko la maisha kwa kuwa mwenye hekima, mwenye bidii na tajiri lakini bila kumjali Mungu? Mfalme Sulemani alikuwa na vyote hivi, zaidi kuliko wengi walioishi kabla na nyuma yake. Lakini licha ya kupata na kuogelea kwa raha zote za dunia, moyo wake ulibaki mtupu. Vyote vilikuwa “ubatili mtupu” (Mhu 1:2; 12:8). Ufuatao ni muhtasari wa mahangaiko yake.

Mungu alivyoongoza (1 Fal 6). Siku ya kuliweka wakfu Sulemani anatambua unyonge wake mwenyewe kulingana na ukuu wa Mungu (1 Fal 8:27). Kudumu katika kujitambua hivyo kunaweza kuutosheleza moyo wa binadamu, lakini Sulemani aliendelea na kutafuta kwake. Kisha Sulemani akajijengea nyumba za kifahari, akajipandia mashamba ya mizabibu na bustani zenye miti ya matunda ya kila aina, na kujenga birika za kuinyunyizia miti yake maji. Viungani mwa hivi vyote mfalme Sulemani alikuwa na utajiri wa ng’ombe, kondoo, na fedha kupita wote waliomtangulia Yerualemu (Mhu 2:4, 6-8).

Mfalme Sulemani alikuwa mwenye hekima kupita mwanadamu mwingine awaye yote (Mhu 1:16-17; 1 Fal 4:29-30). Hivyo basi kama kutosheka kungeletwa na hekima ya dunia, Sulemani alikuwa na nafasi ya kipekee. Lakini mwishowe anajuta akisema: “Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni; Naye aongezaye maarifa, huongeza masikitiko” (Mhu 1:18).

Kazi yote hii ilihitaji watenda kazi. Mfalme Sulemani alijipatia watenda kazi waliohitimu kwa kila kazi iliyohitajika (Mhu 2:7). Ila hakupata walioweza kuujenga na kuutosheleza moyo wake.

Baada ya kutofanikiwa kwa njia ya hekima na maarifa, Mfalme Sulemani aliamua kutafuta kuutosheleza moyo wake kwa kila aina ya anasa (Mhu 2:1). Ila mwishowe, hata furaha na anasa viliishia utupu. Havikufaa kitu (Mhu 2:2). Pia mvinyo haukufaa chochote (Mhu 2:3).

Mfalme Sulemani alijaribu burudani na muziki pia (2:8). Hapana shaka alikuwa amehadithiwa jinsi Daudi, baba yake, alivyocheza kinubi na kuutuliza moyo wa mfalme Sauli. Basi akawa na wengi wa kupiga, kuimba na kucheza mbele yake. Lakini hata muziki haukufaulu kujaza utupu wa moyo wake. Ni kitu gani kilichobaki?

Kisha Mfalme akafikiri angepata kuutosheleza moyo wake na kufikia makusudi ya maisha kwa kufanya miradi mikubwa ya kihistoria kwa nchi yake. Kwanza kabisa alianza kwa kumjengea Bwana Mungu wake hekalu huko Yerusalemu; nyumba iliyojengwa kwa ustadi kama Bwana

Mfalme Sulemani aliazimu kutafuta kuutosheleza moyo wake kwa wanawake. Basi akawaoa, sio wanawake tu, lakini binti za kifalme mia saba na kuongezea masuria 11


WATU WA BIBLIA

RIZIKI TOLEO 3, 2017

mia tatu, wote elfu! (1 Fal 11:3). Lakini moyo wake haukupata tiba.

Kwanza kabisa siyo dhambi kutafuta, tena kwa bidii, tunavyohitaji kwa maisha haya na kuvitumia kwa njia nzuri. Ila hakuna faida kama tukipata vyote, na kusifiwa na wote, lakini tukaishi maisha yasiyomjali Mungu na mpango wake kwa maisha yetu. Sulemani anafananisha maisha kama haya sawa na maisha ya mnyama ambaye mwisho wake ni kifo tu (Mhu 3:19). Ni maisha yasiyo na la ziada ila kula, na kunywa, na kucheka (Mhu 8:15); maisha yasiyo na tumaini baada ya kaburi.

Utakosea kama ukifikiri kwamba umaarufu wa Mfalme Sulemani ulijulikana Uyahudi tu. Biblia inasema alitawala siyo Israeli tu, lakini hata falme zote zilizomzunguka (1 Fal 4:21). Sifa za hekima na utajiri wake zilikuwa zimeenea ulimwe-ngu wote. Ndiyo maana watu wakuu, kama Malkia wa Sheba walifika Yerusalemu, kujionea na kuhakikisha kwamba yote waliyoyasikia kuhusu Mfalme Sulemani yalikuwa ya kweli (1 Fal 10:1-7,24). Lakini hata kutambulika na kusifika kimataifa hakukuutosheleza moyo wake. Huu pia ulibaki kuwa ubatili.

Pili, mioyo yetu haiponi kwa sababu tumetenda haya na yale. La hasha! Kama moyo ungelipona kwa njia hiyo, Sulemani angelikuwa wa kwanza kujiokoa. Lakini Biblia inasema twajikwaa sisi sote katika mambo mengi, na kama tukijitwaa katika neno moja, tumekosa juu ya yote (Yak 3:2; 2:10). Hivyo ni wazi kwamba hatuwezi kufidia kwa yale yote katika kutenda kwetu tunayoyaona kuwa si mazuri.

Kwa upande wa chakula, Mfalme Sulemani alikulia na kunywea kwa vyombo vya dhahabu (1 Fal 10:21). Nayo sehemu ya chakula chake cha kila siku kilikuwa ng’ombe kumi walionona, ng’ombe ishirini wa kawaida, kondoo mia, na ayala, na paa, na kuku walionona (1 Fal 4:22-24). Wa! Karamu ya kila siku.

Ujumbe mkuu ni kwamba tunahitaji kutoka kwa utupu wa birika tunazojenga wenyewe, na kukubali kupokea bure wokovu kutoka kwa Mungu. Mioyo yetu itaburudika na kupona, kwa maisha haya na kwa maisha ya baadaye, tukipokea msamaha unaopatikana kwa neema tu tunapomwamini Yesu Kristo (Rum 3:2022). Ama sivyo, anasema Sulemani, mahangaiko yetu yote yatakuwa ni bure, sawa na kujilisha upepo (Mhu 2:11,17).

Kwa muhtasari, Sulemani anasema, “... sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote” (Mhu 2:10). Maana yake kama kuna ukamilifu wa fahari, anasa, shibe, sifa na yote mazuri ya dunia hii, Mfalme Sulemani aliyatafuta na kuyafurahia pasipo kupimiwa. Lakini je, matukio yalikuwa nini? Utupu, ubatili, kuhangaika bila faida. Je, tunajifunza nini kutoka kwa maisha ya Mfalme Sulemani?

Mch. Gideon Mumo 12

KANISA LA NYUMBANI/MIMBARA

RIZIKI TOLEO 3, 2017

Kutunza sauti ya roho nyumbani na mimbarani Tujuavyo, sauti ni chombo cha mawasiliano mathalan kati ya mtu na mtu, na kati ya mtu na Mungu. Mungu ni Muumba na msingi wa kuwepo kwa watu. Mungu ni Roho, naye amekuwa akiwasiliana na watu tangu zama za “babu zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi” (Ebr 1:1).

kwa kupitia viongozi, wazazi na wadhamini wa vikanisa vidogo vidogo vichanga vinavyokua katika kaya zetu. Tena kwa viongozi na wahudumu wa Neno wasimamapo mimbarani kutoa ujumbe. Roho alijidhihirisha kwa kusudi la kutekeleza lengo lake la Yesu kuja humu duniani. Vivyo hivyo anajidhihirisha siku hizi ili Yesu aingie mioyoni mwa watu. Lengo ni lileile: “Nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yn 10:10b).

Hizo sehemu nyingi na njia nyingi zaweza sana kutokezwa na Mungu kupitia chochote au yeyote kama vile malaika, wafalme, na hata wanyama kama vile punda wa Balaam. Lakini siku hizi Mungu ana njia ya pekee anapoongea nasi. Njia hii ndiyo Mwana wake, Kristo Yesu. Ni muhimu sana kukaribishwa popote achaguapo na kubisha hodi, tukimwambia walivyofanya wale waliokwenda Emau: Karibu – “kaa pamoja nasi kwa kuwa kumekuchwa na mchana umekwisha” (Lk 24:29-31; Ebr 13:2).

Shughuli hii takatifu Bwana amewaachia Wakristo wote, wamshuhudia Mwokozi na Bwana wake. Wajibu wa pekee tumeachiwa sisi tulioitwa na kutengwa kwa kutiwa mikono ili tuifanye kwa bidii na kwa uaminifu. Ni shughuli endelevu humu kanisani (2 Tim 2:2). Wazazi Wakristo wameitwa kufanya vivyo hivyo nyumbani kwao. Ni muhimu sana kuisikia na kuisikiliza sauti ya Roho na kuitunza; kuitunza kwa maana ya kuiweka moyoni kwa kuizingatia kama alivyofanya Maria, mama wa Bwana wetu Yesu Kristo (Lk 2:51; Zab 119:10), akingojea muda na wakati muafaka wa kutekeleza hayo aliyoweka moyoni. Kimsingi kutunza sauti ya Roho, na kuizingatia kwa kuiweka moyoni, kuna maana ya kutii kwa kutekeleza madai yake, tena kwa furaha. Kwa furaha kwa sababu Mungu ni karimu mno.

Katika mazingira ya namna hii Mungu hujipatia fursa ya kuwasilisha ujumbe wake kwa sauti yake ambayo ni yeye mwenyewe. Mwenyeji wake, yule aliyemkaribisha, atafahamu hakika, tena kwa mshangao, kwamba sauti hii ni ya Mungu (Lk 24:31). Ndiyo kusema kuwa Mungu hujifunua kwa watu kwa namna apendayo, lakini anapotaka kuongea nasi ana kwa ana, hutumia neno la Biblia. Hivyo Mungu ndiye hiyo sauti inenayo 13


RIZIKI TOLEO 3, 2017

KANISA LA NYUMBANI/MIMBARA

Ona anavyowaitia walio wake shibe. Asema: “Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono; tegeni masikio yenu na kunijia; sikieni na nafsi zenu zitaishi” (Isa 55:2b3). Ni ukarimu ulioje huu? Roho anatoa nasaha kwa ufasaha kusema: Utakapotii, utitiri wa baraka utakufuata na kukupata. Hakuna sababu ya kuhangaika. Zenyewe baraka zitajua ulipo na kukujia (Kumb 28:1ff).

wafikie watumishi wa Mungu wanaotumika mimbarani na wazazi wote nyumbani, kugawa neema za Mungu kwa watu wake kwa uaminifu. Yatekelezwayo mimbarani huwa yanahusiana sana na nyumbani kwa namna mbalimbali. Hapo twapaswa kumwomba Mungu atuwezeshe, kwa sababu watumishi wote wa Bwana Mungu ni binadamu ambao nguvu za uovu haziachi kuwatembelea. Ni kwa sababu hii ni muhimu mtumishi na mwenzi wake wazingatie neno la Mungu, nabii Amos anaposema: “Je, watu wawili waweza kutembea pamoja wasipokuwa wamepatana?” (Amo 3:3) Bila shaka kupatana namna ya kuliendea jambo ni muhimu; la sivyo kila mmoja atafanya aonavyo kuwa sawa machoni pake, hali ambayo huleta kukawepo mvutano kati ya mtumishi na mwenzi wake jambo ambalo si jema popote, mimbarani wala nyumbani.

Lakini wahenga walipata kusema: “Hakuna masika yasiyo na mbu.” Isaya anathibitisha ukweli huu kwa kuonyesha upande wa pili wa shilingi katika onyo analowapa kanisa: “Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mtakataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga” (Isa 1:19). Wazo la kutunza sauti ya Roho kwa maana ya kuzingatia na kutii yaliyomo ndani ya sauti ile, si wazo la kibibilia tu. Linaonekana pia katika masimulizi mbalimbali ya makabila ya Kiafrika. Tunaloweza kujifunza na kutakiwa kulikumbuka ni kwamba kuna maana ya kutii na kutekeleza yaliyomo ndani ya sauti ya Mungu. Twapaswa kutunza na kuweka moyoni agizo tuliloagizwa na Mungu.

Ikitokea kukawepo jambo la namna hii katika nyumba ya mtumishi, hapo hamna budi kwenda magotini kwa moyo wote Bwana awahurumie. Ni pamoja na kutii sauti yake, akisema: “Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kuhangaishwa na mambo manyonge, msiwe watu wa kujivunia akili” (Rum 12:16). “Zaidi sana, msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno bali kwa unyenyekevu kila mtu amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake” (Flp 2:3-9). Ushauri huu ni muhimu mno katika nyumba za watumishi wa Mungu.

Ijulikane kuwa wito wa Mungu huandamana na kuwajibika (Amo 3:2). Hapo Mungu anawajibisha wote wasiotii. Kipekee wale wanaoshughulika mimbarani Mungu anawadai kuwajibika (Yak 3:1). Mada yetu, kutunza sauti ya Roho nyumbani na mimbarani, kumelengwa ku14

KANISA LA NYUMBANI/MIMBARA

Wito wa kutumika nyumbani na mimbarani hufaulu tu hapo hao wawili watakapokubaliana kwa dhati kwenda pamoja, na yule wa kiume akichunga sana roho ya ubeberu isikaribishwe nyumbani; badala yake unyenyekevu utawale, mume akimtii Muumba wake kuhusu kumpenda mke wake, kumsikiliza na kumtunza kama mwili wake mwenyewe.

RIZIKI TOLEO 3, 2017

ti ipasayo kutolewa na kupokelewa kwa hofu na kwa unyenyekevu. Huduma hii imefikia mahali ambapo mtu hatakosea kuiita chombo cha biashara ya walaghai ambao hunufaika kwayo, hasa tunapoona makanisa mengi ya vibanda vibanda vinavyoota kama uyoga siku hizi. Soko ni kubwa hapo kwa yeyote awezaye kuwalaghai watu kwa maneno ya kuvutia yaliyopangwa na kutayarishwa yatumike katika mkakati wa kuwapata wanyonge, na hasa wale wa uchumi mdogo na ambao kiwango chao cha elimu ya imani na hata elimu ile ya kawaida ni kidogo, na manabii na wahubiri “feki” ni wengi! Nao wanajipatia kula yao kwa namna hiyo.

Hii ni changamoto kwa wanaume wengi. Hasa kwa wanaume Waafrika hali hii inaonekana zaidi. Ila hakika ni jambo jema mume akimtunza mkewe kwa faida yao wenyewe na kundi alilopewa aliongoze (1 Pet 5:1-4). Mazingira ya namna hii ya mke kuonekana kwamba anaweza kushirikiana na mumewe na wote wawili kuwajibika katika wito wao, ndipo jibu la swali la nabii katika Amosi 3:3 linapata mashiko.

Kuthibiti hali hii ni changamoto, kwa sababu kiu ya kusikia Neno la uzima ni kubwa, na watumishi wa mimbarani waliotayarishwa vizuri vyuoni ni wachache. Hata hivyo kuna haja ya uongozi wa Kanisa kuona kama sasa ni wakati mwafaka wa kutathmini elimu ya Kikristo inavyofundishwa sharikani na elimu ya theolojia vyuoni kama inakidhi matarajio ya waumini.

Vivyo hivyo kwa habari ya huduma mimbarani, tukiangalia hali ya mtumishi wa Mungu na washarika anaowahubiria na kuwafundisha. Ikumbukwe kwamba hiyo ndiyo huduma ya Neno lihubiriwalo. Ni huduma ya Neno la Mungu. Na makanisa ya Matengenezo huitambua huduma hii kuwa chombo cha neema, na kuiweka maanani kuliko inavyofanyika katika makanisa mengine.

Sauti ya Roho nyumbani na mimbarani yapaswa kutiiwa na wote wanaohudumu nyumbani na mimbarani. Utiifu huu utasababisha mambo yatakayowafadhaisha, lakini wasisite kuyashughulikia. Hakuna lisilowezekana, ikiwa mtumishi na mwenzi wake watashirikiana kufanya maamuzi kwa kuongozwa na Roho anaponena nao katika Neno la Mungu, na wakiwa na maombi ya dhati.

Hii humaanisha nini kama si kuitendea haki hii huduma kwa kuitambua kuwa ina hadhi sawasawa na sakramenti za Ubatizo na Meza ya Bwana? Ni jambo la kusikitisha kuwa huduma ya Neno mimbarani ina taswira isiyofaa siku hizi. Imepoteza ule uzito na siha ya sakramen15

Mch. Gabriel Kimirei Chaplain Arusha Lutheran Medical Centre


HISTORIA YA WIMBO

RIZIKI TOLEO 3, 2017

Ni Salama Rohoni Mwangu

Wimbo huu umeandikwa na Horatio Spafford aliyeishi kati ya mwaka 1828 hadi 1888. Horatio Spafford alikuwa mwanasheria na alikuwa tajiri sana. Aliishi na kufanya biashara zake katika mji wa Chicago, Marekani. Mke wake aliitwa Anna, na walibarikiwa kuwa na watoto watano, mabinti wanne na mvulana mmoja. Horatio alikuwa ni Mkristo na mwanafunzi mzuri wa Maandiko Matakatifu. Katikati ya mafanikio yake, Horatio alikumbwa na matukio ya kuumiza. Kwanza alimpoteza mtoto wake akiwa na miaka miwili tu mwaka 1870. Akiwa bado kwenye maombolezo ya mwanae, mwaka 1871 moto mkubwa uliopewa jina la Moto Mkubwa wa Chicago (Great Chicago Fire), uliwaka. Moto huo uliteketeza karibu mji wote wa Chicago, na kusababisha vifo vya watu wengi, watu kukosa makazi na mali kuteketea. Pia Horatio ali-

poteza mali zake katika ajali hii ya moto. Wakati huo ulifuatiwa na anguko kubwa la uchumi la mwaka 1873, lililoendelea kumaliza biashara yake. Kutokana na magumu familia yake iliyokuwa inapitia, Horatio aliamua kuipeleka familia yake nje ya Marekani kwa ajili ya mapumziko. Wakaamua kwenda wote Uingereza ambako rafiki zake Moody na Sankey walikuwa wanafanya huduma ya kuhubiri Injili. Muda mfupi kabla ya safari yao, alipata udhuru, na ikambidi abaki ili kushughulikia masuala yaliyokuwa yamejitokeza katika biashara zake. Kwa kuwa muda wa safari ulikuwa umekaribia sana, aliiruhusu familia yake itangulie na kwamba yeye angefuata baadaye. Mke wake na binti zao wanne walianza safari na meli iliyokuwa ikielekea Ufaransa. Wakiwa safarini ndani ya bahari ya Atlantiki, meli ya Ville du Havre iligon16

HISTORIA YA WIMBO

gana na meli nyingine iliyoitwa Loch Ear. Watu 226 kati ya 313 waliokuwa ndani ya meli ya Ville du Havre, walipoteza maisha yao. Miongoni mwao wakiwemo watoto wote wanne wa Horatio. Mke wake alisalimika na alituma ujumbe kwa mumewe ulioeleza: “Ni mimi tu nimesalimika”. “Saved alone…” Wiki chache baadaye Horatio alianza safari kwenda Uingereza alikokuwa mkewe. Wakiwa njiani, kapteni wa meli aliyokuwamo aliwataarifu kuwa eneo walilokuwa wanapita, ndipo ilipotokea ajali iliyowaua watu wengi waliosafiri na meli ya Ville du Havre, wakiwapo pia watoto wake Horatio. Kwa majonzi na uchungu mkubwa, Horatio alichukua kalamu na karatasi, akaandika mashairi ambayo baadaye, baada ya kutungwa vizuri na Phillip Bliss, ulikuja kuwa wimbo uitwao “Ni Salama Rohoni Mwangu” ( “It is well

RIZIKI TOLEO 3, 2017

with my Soul” kwa Kiingereza). Spafford na mkewe walipata watoto wengine, na walihamia Nchi Takatifu na kuanzisha maisha mapya Yerusalemu. Hapo wakaanzisha kitu walichokiita “American Colony” (yaani, himaya ya Kimarekani). Ilikuwa jamii ya kikristo inayolenga kushiriki katika shughuli za kusaidiana kati ya Wayahudi, Waislamu na Wakristo. Baada ya miongo kadhaa kazi za huruma za American Colony zilikoma, na kubaki kuwa American Colony Hotel. Hii ni sehemu iliyotumika sana na Wapalestina na Waisraeli miaka ya karibuni kwa mazungumzo wakitafuta amani. Wimbo huu unaimbwa katika hali yoyote na mahali popote, lakini wengi hupenda kuimba wanapokuwa katika hali ngumu fulani, na kutafuta amani na faraja kutoka kwa Mungu pekee. Cathbert Msemo

Nionapo Amani kama Shwari (TUMW. Mungu 424 na Tenzi 23)

Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha Ni salama rohoni mwangu.

Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa msalabani; Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu.

Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.

Ee Bwana, himiza siku ya kuja; Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa; Ni salama rohoni mwangu.

Ingawa Shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu. 17


JAMII

RIZIKI TOLEO 3, 2017

Mchungaji kama Meneja Katika karne hii ya 21, kanisa la Mungu linapita katika changamoto mbalimbali ambazo zimeleta athari hasi katika ufanisi wa ukuaji na utoaji wa huduma zake. Changamoto hizi zimekuwa chimbuko kubwa la mahangaiko kwa kanisa. Kanisa ni watu, ni wafuasi wa Kristo. Mafundisho ya uongo, uasi, udhalilishaji na ukandamizwaji wa kanisa, pamoja na mambo mengine yote yanayowazuia wakristo wasimfuate Kristo, ni changamoto za sasa katika kanisa, yaani ni changamoto za wakristo katika mataifa yao, katika jamii wanazoishi na katika familia zao. Wachungaji pamoja na watumishi wengine wa kanisa wana wajibu mkubwa wa kulinusuru kanisa kutokana na changamoto hizi. Utimilifu wa kazi ya mchungaji huonekana vizuri pale ambapo anatumia vizuri nafasi yake kama mtumishi wa usharika na kanisa. Kimsingi, nafasi ya mchungaji inaweza kugawanyika katika sehemu kubwa tatu: Mchungaji kiongozi wa kiroho (mchungaji), ni mwalimu wa imani (mwanatheolojia), na pia ni meneja. Pale atakapotumia vizuri fursa hizi tatu, atachangia kwa kiasi kikubwa sana kuimarisha usharika na kanisa kwa ujumla. Katika makala hii nitaeleza juu ya Mchungaji kama Meneja.

Kanisa ni watu wa Mungu, lakini pia ni taasisi. Kwa hiyo mchungaji ni meneja. Ingawa sio wajibu wake wa kwanza. Mchungaji hutakiwa kuhakikisha kwamba rasilimali zote za kanisa zinatumika kwa usahihi na katika maeneo yaliyokusudiwa ili kufikia malengo ya kanisa. Suala likiwa rasilimali, watu wengi wanafikiri kwanza kuhusu fedha na malighafi za kanisa pamoja na majengo, magari n.k. Hapo mchungaji ana wajibu mkubwa wa kukumbusha kuwa rasilimali ya kanisa yenye maana zaidi ni waumini (wanasharika pamoja na wafanyakazi wa usharika). Pia rasilimali zingine kama mifumo mbalimbali ya kutolea huduma ilenge kuboresha ujuzi wao, maarifa yao n.k., na ipangwe ili kuwawezesha kutumia vizuri muda wao kwa manufaa ya usharika na jamii kwa ujumla. Matumizi sahihi ya rasilimali za wanasharika kama hizi huleta matokeo chanya katika huduma ya kanisa. Mchungaji anashauriwa kutumia fursa yake ya umeneja linapokuja suala la kupanga matumizi sahihi ya rasilimali za kanisa. Kimsingi, ili kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali, mchungaji anakuwa na majukumu makubwa manne, ambayo ni:

Meneja

Mchungaji ana wajibu wa kutambua na kuchagua kwa usahihi malengo na mipango mikakati ya kimaendeleo kwa ajili ya kanisa lake. Katika jukumu hili la kuweka mipango, mchungaji anatakiwa kufanya mambo matatu ya msingi, ambayo ni:

1. Kuweka Mipango

Meneja ni mtu anayewajibika katika usimamizi wa matumizi bora ya rasilimali za taasisi, mashirika, makampuni au miradi, ili kuwezesha taasisi na mashirika hayo kufikia malengo yake. 18

JAMII

RIZIKI TOLEO 3, 2017

a) Kuhakikisha kuwa malengo ya kanisa yanalingana na lengo kuu la Mungu kwa kanisa lake. b) Kuweka mpango mkakati utakaotekelezwa ili kufikia malengo yaliyobainishwa. Tunapozungumzia mpango mkakati, ni kuamua maswali yafuatayo: Jambo gani litafanyika? Litafanyika lini? Litafanyika wapi? Litafanyika kwa namna gani? Na litafanywa na nani? c) Kutambua maeneo ya msingi ya kupangilia rasilimali.

kama mafundisho na ushauri, mchungaji ana uwezo na pia wajibu mkubwa wa kuelezea kwa uwazi maono ya kanisa kwa wanasharika wenzake. Atumie huduma yake ya kichungaji kwa kutoa hamasa kwa watumishi wenzake na wote wengine wa usharika katika kutia bidii ili kufikia malengo ya kanisa. Wakati hamasa ya kampuni inaweza kuwa motisha ya fedha, safari, likizo, matibabu, ongezeko la mishahara na marupurupu mbalimbali, hamasa ya kanisa, na kipekee hamasa ya mchungaji ni zaidi ya hayo. Kwa mfano anaweza kusimamia semina za kuongeza ujuzi, kuwashukuru na kufanya maombezi kwenye ibada n.k. Na kila wakati awe tayari kuwasikiliza, si katika masuala ya kazi tu, bali yote. Motisha huchochea ubunifu, bidii na uzalishaji wa matokeo bora katika eneo la kazi.

2. Kuratibu

Kama meneja, mchungaji azingatie kuweka mfumo mzuri wa kimamlaka na mahusiano katika huduma za kanisa. Pamoja na viongozi wengine, anapaswa kuamua ni nani ataripoti jambo gani, na ataripoti kwa nani. Mifumo hii ionyeshe ni nani atakayewajibika endapo lengo lililokusudiwa halijatimizwa. Mchungaji akumbuke kwamba siye mwenye uamuzi wa mwisho usharikani, bali akiwa mtumishi mwenye karama za kuhubiri, kufundisha na kushauri alenge kuwawezesha viongozi wenzake kutoa uamuzi huo kwa hekima na maarifa ya kiroho. Asiwe muoga na dhaifu katika kusisitiza mambo muhimu na mema kulingana na mafundisho ya Neno la Mungu, ili kufikia malengo yaliyowekwa kwa ufanisi. Asikilize na kupokea ushauri. Itamsaidia kuwafahamu vizuri waumini wa usharika ili aweze kufanye kazi yake kwa busara kwa faida yao na kwa utukufu wa Mungu.

4. Kudhibiti

Pamoja na viongozi wenzake, mchungaji aweke mfumo madhubuti wa kufuatilia na kupima utekelezaji wa maazimio ya kanisa lake. Mfumo mzuri ni ule wenye uwazi na wa kuwawezesha kupata mrejeo kutoka kwa watendaji husika. Tena hapa mchungaji akumbuke kwamba ni meneja wa pekee mwenye wajibu wa kuangalia kwanza hali ya kiroho ya waumini. Katika toleo la RIZIKI litakalofuata, tutaendelea kuangalia huduma ya mchungaji kama kiongozi na mwanatheologia. Ninakushauri kusoma 1 na 2 Timotheo kama maandalizi!

3. Kuongoza

Kutokana na elimu yake katika mambo

Emmanuel Stephen Mollel 19


RIZIKI TOLEO 3, 2017

KITABU KIPYA!

Theolojia ya Martin Luther Soma kitabu hiki kwa makini, na utaelewa kuwa mafundisho yaliyoleta Matengenezo yana maana ileile hata leo kwa maendeleo ya Kanisa!

Je, unatafuta mifano ya kukusaidia kufafanua somo la mahubiri? Jossang alikuwa na kipawa maalumu. Pata mifano 115 yenye umaarufu.

Mifano toleo jipya

Vitabu hivi vinapatikana katika maduka yetu ya Soma Biblia: Dar, Arusha, Mwanza, Iringa na Mbeya. Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi

SOMA BIBLIA S.L. P 2696 Arusha +255 752 379 932 editor.somabiblia@gmail.com www.somabiblia.or.tz

SOMA RIZIKI “ONLINE�

www.issuu.com/riziki

Profile for RIZIKI

Riziki 3 2017 IMANI IJARIBIWAPO  

Mimi na were tunaweza kuwa na maswali mengi yanayosumbua imani yetu na kututilia wasiwasi mwingi wa kiroho; tunaweza kufadhaika sana na kuka...

Riziki 3 2017 IMANI IJARIBIWAPO  

Mimi na were tunaweza kuwa na maswali mengi yanayosumbua imani yetu na kututilia wasiwasi mwingi wa kiroho; tunaweza kufadhaika sana na kuka...

Profile for riziki
Advertisement