Page 1

RIZIKI Feb/2018 - Apr/2018

Mwishindanie IMANI waliokabidhiwa WATAKATIFU mara moja tu YUDA. 1:3


TAHARIRI

RIZIKI TOLEO 1, 2018

RIZIKI S.L.P. 2696, Arusha Simu: +255 752 379 932 Barua pepe: editor.somabiblia@gmail.com Kamati ya Riziki: Anne Gihlemoen (mhariri) Hezron Mwasi Anza Amen Lema Philip Bach-Svendsen Cathbert Msemo Mary Bura Magdalena Mathayo Elias Byabato Waandishi walioshiriki Gideon Mumo Rev. George Mark Fihavango Elieshi Kisinza Monica Ndege Justin Oforo Layout: Cathbert Msemo Jalada: ginosphotos/iStockPhoto Nakala: 4500

Usambazaji

SOMA BIBLIA S.L.P. 2696, Arusha S.L.P. 12772 Dar es Salaam S.L.P. 1088 Iringa S.L.P. 6097 Mwanza S.L.P. 1062 Mbeya www.somabiblia.or.tz

Ulimwengu kwa Kristo! Imechapwa na:

Imaging Smart - Dar es Salaam

”Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu ...?” (Mwa 3:19) Bila shaka unakumbuka neno hili la shetani na jinsi wanadamu wa kwanza walivyokubaliana naye. Tangu hapo sisi binadamu tumetaka kugeuza ukweli wa neno la Mungu ili lifaae mawazo, mahitaji na mipango yetu. “Hivi ndivyo alivyosema Mungu...?” Kama utavyosoma katika toleo hili la RIZIKI, muda sio mrefu baada ya kupaa kwa Yesu, kulitokea watu wadanganyifu wenye ”hoja nyepesi” kuhusu Yesu na imani ya Kikristo. Ili kushindania imani waliyokabidhiwa, na kwa kutumia fundisho la Mitume katika Agano Jipya, Wakristo wa kwanza walitunga maneno machache yanayoelezea kiini cha imani ya kweli ya Kikristo. Na hatimaye tulipata Imani ya Mitume kama ilivyo leo. Hiyo ni muhimu, hasa nyakati zetu ambapo Wakristo wanakutana na mafundisho mengi potofu. Kwa sababu, je, nini itatokea kwa imani yetu, ikiwa kila kizazi huibadilisha tu kulingana na mawazo, mahitaji na mipango yake? Ukiri huu utatusaidia kusimama imara, na pia kukemea kwa nguvu zote mafundisho hayo potofu. Utatusaidia kushindania imani yetu. Katika matoleo yajayo ya RIZIKI, tutaendelea kuangalia Imani ya Mitume sehemu kwa sehemu. Tunatumaini itakuwa ukumbusho mzuri kwa watumishi wote wa Mungu, wapate kuzingatia imani yetu ya Kikristo ni nini. “...mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu” (Yuda 1,3b) Mungu akubariki, Anne Marken Gihlemoen

Yaliyomo: Ukurasa 3-5: Ukurasa 6-7: Ukurasa 8- 9: Ukurasa 10 : Ukurasa 11: Ukurasa 12-13: Ukurasa 14-15:

Mada: Mwishindanie Imani Mada: Historia ya Imani ya Mitume Watu wa Biblia: Adamu Kanisa la Nyumbani: Nyumbani mahali pa... Ushuhuda: Nilipookoka tu... Historia ya wimbo: Yesu kwa Imani Jamii: Wazazi kukosa Watoto 2

MADA

RIZIKI TOLEO 1, 2018

Mwishindanie Imani Utangulizi

ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliokabidhiwa watakatifu mara moja tu.”

Waraka wa Yuda kwa watu wote ni barua fupi sana na haifahamiki sana na watu wengi, ingawa ina ujumbe muhimu kwetu. Mapokeo ya Kanisa yanamtambulisha mwandishi kama ndugu yake Yesu, lakini mwenyewe anaandika ni mtumwa wa Kristo. Kwa kujishusha hivyo, Yuda anabainisha kuwa ujumbe wa waraka haujatungwa na yeye mwenyewe, bali umetoka kwa Bwana wa Kanisa.

Mstari huu wa tatu ndio kiini cha Waraka wa Yuda, na sababu ya kuandikwa kwake. Yuda aliandika kuitetea imani ya Kikristo ambayo watakatifu walikabidhiwa mara moja tu kwa njia ya fundisho la Mitume (Mdo 2:42). Aligundua kuwa kuna mafundisho ya uongo yaliyoingia kuharibu imani ya Kikristo, hivyo akajitokeza kama mlinzi wa imani hiyo na Wakristo wenyewe kwamba imani yao binafsi katika Kristo Yesu iimarike.

Kwa utangulizi wa waraka (mst. 1-2), Yuda anataka Wakristo duniani kote wajitambue kuwa: A. Ni watu walioitwa na Mungu. Wameitwa kwa wajibu maalum wa utumwa na utumishi kwa Kristo. Lakini pia wanaitwa kwa ajili ya siku ya mwisho ambapo wengine watakaribishwa kwa sherehe, na wengine kwa hukumu ya mateso ya milele.

Kwa nini itetee imani ya Mitume na kuwaagiza Wakristo waishindanie? Kwa kufuata ufafanuzi wa William Barclay1, zipo sababu nne . Nimezijadili hapa chini. i. Imani ya Kikristo haijagunduliwa na Wakristo, bali wamekabidhiwa kama kitu cha thamani mno wanachopaswa kukitunza. Ni urithi wa pekee mno. Inarithishwa toka kizazi hadi kizazi, ama kutoka imani hadi imani. Na inarithishwa siyo kwa maandishi tu, bali kwa njia ya kushirikiana sisi kwa sisi. Wimbo toka Tumwabudu Mungu Wetu namba 75 unasema: “Mikononi mwa Mitume kazi ilifanywa”. Sasa ni wajibu wetu kuipokea na kusogeza mbele.

B. Ni watu waliopendwa na Mungu. Wanaitwa ili waishi katika upendo wake, na kuwapenda wengine kama itikio la wao kupendwa na Mungu. C. Wakristo wamehifadhiwa na Mungu katika Yesu Kristo. Hawapo pekee yao, wapo ndani ya Kristo, na Kristo ndani yao. Yuda 1:3

“Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu

ii. Imani ya Kikristo tulikabidhiwa 3


MADA

RIZIKI TOLEO 1, 2018

MADA

RIZIKI TOLEO 1, 2018

Maonyo ya Yuda 1:4-25

mara moja tu. Wakristo wasitegemee kuwa wanaweza kugundua imani nyingine ama kubadili fundisho la mitume. Mtume Paulo aliwaambia Wakristo kwamba msingi umeshawekwa na Mungu, na hakuna msingi mwingine, na msingi huo ni YESU KRISTO (1 Kor 3:10-15; 1 Kor 15:1-11).

Katika mistari hii inayofuata, Yuda anaonyesha mazingira yaliyosababisha awaandikie ili watetee imani ya Kikristo. Walijiingiza watu kwa siri kupotosha imani (mst. 4). Ndipo akatoa maonyo akitumia mifano ya Agano la Kale kuhusu jinsi walivyoadhibiwa wale waliopotosha kundi la Mungu lililotoka Misri, adhabu dhidi ya malaika walioanguka na jinsi Sodoma na Gomora zilivyoangamizwa (mist. 5-7).

iii. Imani ya Kikristo ilikabidhiwa na Mungu kwa wakatifu. Imani haijakabidhiwa kwa mtu mmoja ama kiongozi fulani, imekabidhiwa kwa Kanisa la Mungu ambalo ni sawa na waaminio wote. Inapokelewa ndani ya kanisa na kurithishwa toka imani hadi imani ndani ya kanisa, sisi tunaomwamini Yesu tunapoikabidhi kwa wengine kwa njia ya kukiri imani yetu, kuwashuhudia na kuwafundisha mambo ya imani.

Pia Yuda anawalinganisha hawa wanaopotosha imani ya Kikristo na manabii wa uongo na ndoto zao. Hao manabii wa uongo walinajisi miili yao na kudharau malaika wa Mungu. Yuda anazileta habari za kufa kwa Musa zilizoandikwa katika Kumbukumbu 34:1-6, kwamba mwili wa Musa ulizikwa na malaika Mikaeli baada ya malaika huyu kushindana na shetani kuhusu huo mwili. Hoja ya Yuda ni kwamba hata malaika Mikaeli hakumshutumu shetani, alisema tu: “Bwana na akukemee”. Lakini hawa watu wananena mambo wasiyopaswa kuyanena kwani hawayafahamu mambo matukufu ya Mungu (mist. 8 na 10). Yuda anasema watu hawa wanatembea katika njia ya Kaini aliyemuua ndugu yake Habili (Mwa 4:1-15), na katika njia ya Balaamu wakati alipokubali kuajiriwa na Balaki ili awalaani wana wa Israeli (mst. 11).

iv. Imani ya Mitume lazima ilindwe na kushindaniwe. Kila Mkristo anao wajibu wa kuilinda na kuitetea imani ya Kikristo. Kwa vile inarithishwa toka kizazi hadi kizazi kingine, ni wajibu wa kila kizazi kuitunza katika utakatifu wake na kuikabidhi kizazi kijacho. Sio wajibu mdogo huu. Kazi ya kuitetea imani ya Kikristo siyo nyepesi, kwani kuna nyakati katika vizazi vya babu zetu iligharimu maisha yao. Na hata leo bado kuna Wakristo sehemu mbalimbali za dunia wanaoteswa na kuuawa kila siku, kwa sababu ya imani yao.

Baada ya hapo Yuda analeta picha ya watu hawa waliopotoka. Ni kama miamba yenye hatari, mawingu yasiyo na maji, miti iliyopukutika isiyo na matu-

Picha: www.pixabay.com

nda, mawimbi ya bahari na nyota zipoteazo (mist. 12-16). Akawaasa sasa Wakristo wayakumbuke maneno yaliyonenwa zamani na Mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kati ya mambo waliyoonywa na Mitume ni kwamba siku za mwisho watatokea watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe zenye upotevu. Hawa ndio wanaoleta matengano, na hawana Roho.

wengine wakiwahurumia (mist. 17-23). Hivyo ni wajibu wetu kulinda imani tuliyokabidhiwa na Mungu kupitia fundisho la Mitume na kuitetea dhidi ya mafundisho ya uongo yanayojipenyeza katika kanisa la Mungu. Yuda anamalizia waraka wake kwa wimbo wa sifa ambao unaeleza ni kwa jinsi gani tutaishindania imani hiyo hata tushinde. Anamwelezea Mungu kama mwenye uwezo, ambaye anaweza kuwatunza Wakristo wasijikwae, na hatimaye waje kusimama mbele ya utukufu wake pasipo mawaa na kwa furaha kuu. Yeye ndiye Mungu pekee aliyetuokoa kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu (mist. 24 -25).

Ili Wakristo wasichukuliwe na uongo huo na kupoteza yote waliyokabidhiwa, inabidi wajijenge juu ya imani iliyo takatifu sana na kuomba katika Roho Mtakatifu. Na wanapaswa kujilinda katika upendo wa Mungu, huku wakingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hadi wapate uzima wa milele. Lakini pia wawasaidie

Rev. Dr. George Mark Fihavango, Msaidizi wa Askofu 1. “The Daily Study Bible. The letters of John and Jude.” William Barclay. New Delhi: Rekha Printers. 1976. Reprinted 2006.

4

5


MADA

RIZIKI TOLEO 1, 2018

MADA

RIZIKI TOLEO 1, 2018

Historia ya Imani ya Mitume Utangulizi

pale Mtume Petro anapokiri Kristo kama Bwana na Mwokozi. Mtume Paulo anaweka msingi wa kutambua Mkristo wa kweli kwa kusema: “Ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Rum 10:9). Kama ilivyo wakati wetu, pia waliobatizwa wakati wa Mitume walipaswa kukiri hivyo. Soma kwa mfano Mdo 16:30-31, 1 Kor 12:3 na 1 Yoh 4:2. Ndivyo tunavyofanya hata sasa wakati wa ubatizo na kipaimara.

Shabaha ya mada hii ni kukumbushana jinsi sisi kama Kanisa tulivyopata Imani ya Mitume, na kwa nini Kanisa enzi za Mitume kama Paulo na Petro liliendeleza desturi ya kukiri imani yake kwenye ibada na makusanyiko yao. Ni matumaini yetu kuwa tutakapopata historia ya Imani ya Mitume, tutaendeleza kuikiri kila tukutanapo, na hivyo kuzidi kumjua yeye tunayemwamini na kwa nini tunaamini. Hiyo ni muhimu, hasa nyakati zetu ambapo Wakristo wanakutana na mafundisho mengi potofu. Ukiri huu utatusaidia kusimama imara, na pia kukemea kwa nguvu zote mafundisho hayo potofu.

Historia

Historia ya Imani ya Mitume kama tuliyo nayo leo, ilifikia sura hiyo hatua kwa hatua kulingana na mahitaji ya wakristo Kwa nini inaitwa kuweza kumwabudu Imani ya Mitume? Mungu wao, kumChangamoto ya Kanisa shuhudia na kuwaelezea Historia ni wazi kuwa kupambana na uzushi baada ya Yesu kupaa, watu wengine imani ya Kanisa halikuweka kiKikristo, kwa mfano na mafundisho potofu kao cha kutunga mawakati wa kuwafundisha ilichangia sana kwa neno yaliyopo kwenye waliotaka kubatizwa. Pia kuwepo kwa Imani ungamo hili. Sehemu changamoto ya Kanisa ya Mitume. za ungamo zilikuwepo kupambana na uzushi tangu enzi za Mitume. na mafundisho potofu Luka katika Mdo 2:42 ilichangia sana kwa kuakieleza ibada ya Kanisa la kwanza, anase- wepo kwa Imani ya Mitume. Turejee ma walikuwa wanadumu katika “fundisho matukio kadhaa ya kihistoria katika mala mitume, na katika ushirika, na katika pambano hayo yaliyochangia kuwepo kwa kuumega mkate, na katika kusali”. Unga- ungamo hili katika sura tuliyo nayo leo. mo hili limesheheni yote waliyofundisha Mitume kuhusu Mungu wa Utatu. Miaka kama 40 baada ya kufariki Mtume Yohana, ambaye alikuwa ndiye Katika Mt 16:16 msingi unawekwa mwanafunzi wa mwisho kufariki kati

ya wale wanafunzi 12 wa Yesu, alitokea yaliyoandikwa yenye maana zaidi wakati mzushi mmoja aliyeitwa Markion (kama wa kukiri imani yao kwa ufupi. 85-160 b.K.). Yeye alipinga kuwa Yesu hakuzaliwa na mwanamke. Yesu hakuwa Hitimisho mwanadamu kweli ila Kimsingi ungamo la alionekana tu machoni Imani ya Mitume lilipapa watu kana kwamba tikana kuanzia mwaka Msingi mkuu ni mwanadamu. Ndi140. Kama mwaka 200 yo maana mababa wa b.K. lilikuwa limeshapawa ungamo hili ni Kanisa wakaingiza kweta sura yake kamili, laNeno la Mungu. nye ungamo kuwa Yesu kini ni kuanzia karne ya alizaliwa na Bikira Manane tu kwamba liliparia. Uzushi huu uliibuka tikana kwa maandishi mwaka wa 140 baada ya katika sura tuliyo nayo kuzaliwa kwa Yesu. leo. Kama tutakavyoona Markion pia alifundisha kuwa Yesu kwenye mada zitakazofuata katika toleo hakuteswa na kufa msalabani, na ndiyo hili la RIZIKI, msingi mkuu wa ungamo maana Kanisa likaweka kwenye ungamo hili ni Neno la Mungu. kwamba Yesu Kristo aliteswa chini ya Kanisa limeweza kuweka kwa kifupi kautawala wa Pontio Pilato, akasulubiwa, bisa kile ambacho Biblia inakifundisha akafa, akazikwa na siku ya tatu akafufu- kuhusu Mungu Mtakatifu katika utatu ka. Mzushi Markion alifundisha pia kuwa wake. Mungu wa Agano la Kale si yule yule wa Agano Jipya; hao wawili ni tofauti. Ndi- Ukiri huu umekuwa kipimo halisi cha yo maana Kanisa katika maungamo yake mtu yeyote yule anayekiri kwamba amelikakaza kuwa Mungu ni mmoja: Baba, mwamini Yesu, na kwamba anastahili Mwana na Roho Mtakatifu. ubatizo na sakramenti nyingine zinazotolewa na Kanisa. Ungamo hili pia ni Aliyelisaidia sana Kanisa kuweka msi- ushuhuda kwamba Kanisa la Bwana ni mamo wenye misingi ya Biblia, ni mwali- moja na la ulimwengu wote. Pia ni kinga mu wa Neno la Mungu wa wakati huo halisi dhidi ya mafundisho potofu. Mtu aliyeitwa Origeni. Yeye alizaliwa Afrika ya yeyote anayekiri chochote kinyume na Kaskazini mwaka wa 180 b.K. ungamo hili, amepotoka wala kweli ya Kristo haimo ndani yake. Tumwogope Upekee wa Imani ya Mitume ni kwa- kama ukoma na kumpinga kwa nguvu mba maneno yake yote yanapatikana ka- zetu zote. tika Biblia. Wakristo walikusanya tu yale Mch. Justin Oforo

6

7


WATU WA BIBLIA

RIZIKI TOLEO 1, 2018

WATU WA BIBLIA

RIZIKI TOLEO 1, 2018

ADAMU “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu …” (Mwa 1:26)

Tofauti na viumbe vyote, Adamu aliumbwa kwa mfano na sura ya Mungu (Mwa 1:26-27). Hali ya kuwa na mfano na sura ya Mungu vilimpatia Adamu uwezo na nafasi ya kipekee ya kuyatambua mapenzi ya Mungu, na kuwa na usharika binafsi wa fahamu naye.

kwa kweli, ni kwa sababu hiyo nyoka alitangaziwa hukumu inayopatikana katika Mwa 3:15. Lakini licha ya ushawishi wa Shetani, ni Adamu aliyechagua kuasi amri ya Mungu, na kwa sababu hiyo akawa mwenye dhambi, na wanadamu wote nyuma yake (Rum 3:23).

Mungu alipanda shamba la Edeni kuwa makao yake, na kuchipusha kila aina ya miti ya matunda kwa chakula chake. Shamba la Edeni lilimpa Adamu kila kitu alichohitaji kwa maisha yake (Mwa 2:8-9). Adamu na Hawa hawakuhitaji nguo, kwani shamba hili halikuwa joto wala baridi. Kama Baba mpenzi, Mungu alihakikisha Adamu aliishi kwa wingi wa mali, furaha na amani. Zaidi ya yote, Adamu alifurahia ushirika wake na Mungu.

Baada ya anguko hili kubwa, Mungu aliwahukumu Adama na Hawa (Mwa 3:14-24). Kwa sababu ya dhambi ya Adamu, wanadamu wote wakawa chini ya laana. Uhusiano wetu na Mungu ulivunjika, tukapoteza utimilifu tuliofurahia shambani Edeni, ikawa tule na kunywa kwa jasho na taabu; miaka yetu ya kuishi ikapunguzwa na kifo kikawa sehemu ya kila mwanadamu (Rum 5:14; 1 Kor 15:22). Dhambi ilimfanya Adamu kumkimbia Mungu (Mwa 3:8). Kwa sababu ya dhambi, Adamu na mkewe waliona aibu na kumwogopa Mungu (Mwa 3:10). Adamu hakuwa na nia, wala uwezo wa kufuta dhambi yake. Kama Mungu asingelimtafuta, Adamu angelipotea milele. Ama kwa kweli, pasipo Mungu kututafuta, wote wa uzao wa Adamu tumepotea milele. Hakuna amtafutaye Mungu, wala hakuna atakayefaulu kuulipia wokovu wake (Rum 3:9-23).

Adamu na Hawa walikuwa huru kula matunda yote shambani, isipokuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mungu alimwonya Adamu na kusema: “Siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika” (Mwa 2:17). Mungu aliweka mbele ya Adamu kuchagua kutii amri hii na kupata uzima, au kuchagua kutoitii na kupata kufarakana na Mungu, uchungu wa maisha, na kifo. Walakini Shetani alipomtokea na kumjaribu, Adamu alikula matunda ya mti waliokatazwa na Mungu (Mwa 3:1-6). Ni kweli kwamba Shetani alihusika pakubwa kwa kusababisha dhambi ya Adamu. Ama

Swali langu, na lako, aliuliza Ayubu pia: “Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele za Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?” (Ayu 25:4). 8

Kama Mungu asingelimtafuta, Adamu angelipotea milele. Ama kwa kweli, pasipo Mungu kututafuta, wote wa uzao wa Adamu tumepotea milele. Picha: www.pixabay.com

Sawa na Mungu alivyoahidi Adamu na uzao wake (Mwa 3:15; Isa 7:14; Lk 1:3031), Yesu Kristo, aliye uzao wa mwanamke, alikuja katika mwili kwa njia ya kuzaliwa na Mariamu (Lk 2:7; Flp 2:57). Kwa kuishi katikati yetu, Yesu aliye chapa ya Mungu, aliukamilisha ufunuo wa Mungu Baba na mpango wake wa wokovu kwa mwanadamu aliyepotea (Ebr 1:1-3). Na basi, wakati ulipotimia, Yesu alijitoa kufa kifo cha msalaba, na kuwa fidia ya wenye dhambi sawa na mpango wa Mungu kwa wokovu wetu (Isa 53:112; Mk 10:45).

Hivyo basi, kuna habari njema kwa wote wa uzao wa Adamu! Ni habari njema kwamba kwa kifo chake msalabani, Yesu Kristo alibeba laana zetu. Ni habari njema kwamba Yesu Kristo alipata adhabu ya makosa yetu. Ni habari njema kwamba Yesu alikufa kifo chetu. Na ni habari njema kwamba kila aaminiye na kutubu dhambi zake, ataepuka adhabu ya Mungu na kuupata uzima - hata uzima wa milele (Yn 1:12, 3:16, 3:36). Tendo hili la Yesu Kristo msalabani linanipa kila sababu ya kuishindania imani hii; imani ya pekee iletayo wokovu. Mch. Gideon Mumo 9


KANISA LA NYUMBANI

RIZIKI TOLEO 1, 2018

Nyumbani – mahali pa kurithisha imani yetu kwa kizazi kingine Ikiwa baba na mama hawashiki nafasi zao, itachukua mowa wa kizazi kimoja tu Mungu kusahaulika. Kama ilivyoandikwa katika Waamuzi 2:10: “Kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli”. Maisha ya imani ni kama mbio za kupokezana kijiti. Fanya bidii kuwapa kizazi kinachokuja nyuma yako imani ya thamani uliyo nayo. Nyumbani kwenye familia, ndicho kituo cha Mungu duniani. Hapa ndipo mahali watu hupewa jina, hupata lugha na hupokea mtazamo kuhusu maisha, hayo yakiwa pamoja na Mungu, uumbaji, wanadamu na shetani. Nyumbani kukiwa imara, kanisa ni imara, na taifa ni imara.

kusikia mashauri yako. Muda wako na watoto wako ni wa thamani kuliko fedha utakazowapatia, japo fedha zinahitajika. Tena Petro anasema imani hiyo, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, hujaribiwa (1 Pet 1:7). Ukijua kwamba imani ya watoto wako itajaribiwa, basi wekeza kwao, ili siku ya kujaribiwa kwao waweze kusimama. Kuna kizazi kisichomjua baba katika maisha yao. Hata kuna kizazi kisichomjua mama vizuri. Kizazi hiki kinakosa ladha ya upendo na kuhurumiwa na wazazi. Mzazi asiyekuwepo, mzazi anayefanya kazi mbali na watoto wake, mzazi anayepeleka watoto wadogo shule za bweni kwa kisingizio cha kazi – wanayofanya hawa wote ni maandalizi ya kizazi chenye kasoro, maana hakipokei upendo wa mzazi na huruma za mzazi na maonyo ya mzazi. Mzazi, tafakari na fanya maamuzi kuwa karibu na familia na watoto wako.

Umuhimu kwa wazazi kuwepo katika maisha ya watoto

Baba wa nyumbani ni mfano wa Mungu. Ndiye kichwa cha familia aliyepewa wajibu mkuu wa kutekeleza agiza lifuatalo: “Maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo” (Kum 6:6-7). Chukua nafasi urithishe kizazi chako imani uliyo nayo. Imani utakayorithisha uzao wako, haiharibiki. Petro anaiita imani yenye thamani: “… kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani …” ( 2 Pet 1:1). Baba, wanacholilia sana watoto wako si fedha, lakini wanakulilia wewe! Wanahitaji muda na wewe. Wanahitaji

Mashindano

Siku hizi kuna mashindano katika familia. Nani ana nguvu? Nani apewe kipaumbele? Je, ni TV? Je, ni simu na mitandao yote iliyopo? Au wewe mzazi, uko tayari kuweka madhabahu ya Mungu nyumbani kwa msisitizo, ili kumheshimu Mungu na kurithisha 10

... inaendelea ukurasa 11

USHUHUDA

RIZIKI TOLEO 1, 2018

Nilipookoka tu, nikapewa faraja ya msamaha! Kwangu mimi kuokoka ni TUKIO MAHUSUSI! Linapita kabisa upeo wa mtu kuwa mshirika tu wa kanisa. Mimi, hilo lilinipata yapata miaka 58 iliyopita. Nilikuwa darasa la 6, na umri wa miaka 16, kwenye ‘Middle School’ iliyoitwa Kigarama, huko Bukoba. Mkuu wa shule hiyo aliitwa Felix Kataraiya, ambaye kumbe naye alikuwa ameokoka tangia akiwa mwanachuo wa Chuo cha ualimu Katoke Bukoba. Ilitokea kwa mahubiri ya Waganda kadhaa waliookoka. Je, lilinitokeaje?

Lilikuwa muujiza mtupu! Felix alimwalika mhubiri Mwanglikana kutoka Uganda ili atuhubirie sisi wanafunzi Ijumaa-Jumapili. Aliitwa Mch. Elishafati Matovu, naye ameokoka. Wanafunzi zaidi ya 200 tulimsikiliza Mch. Matovu kwa kituo. Kwa uchungu alisema zipo hatima mbili tu baada ya maisha duniani. Ndizo uzima wa milele kwa kila anayemkubali Yesu, na ziwa la moto wa milele kwa kila mtu anayemkataa Yesu. Kisha akataja dhambi za vijana kama vile uongo, wizi, tamaa mbaya ... kutoka ukurasa 10

imani yako kwa kizazi kijacho? Wape watoto wako kijiti cha imani. Nyumbani ni mahali pa kushindania imani (Yud 1:3). Ebu kila mzazi arudi kwenye nafasi ya kuisimamisha madhabahu ya Mungu aliye hai katika familia yake. Hakuna badala ya mzazi. Hakuna mtu wa kukaimu nafasi ya mzazi. Nafasi ya nyumbani ni wajibu ambao kila mzazi

n.k. Hapo aliniumbua mimi mubashara. Hapo nikajiuliza: “Mch. Matovu amejuaje kwamba mimi ni mwizi?” Ghafla sauti ngeni karibu nami ikaniambia: “Mch. Matovu hajui, ila ni Mungu anakuambia kupitia Mch. Matovu.” Nikashtuka sana; nikaogopa na kutetemeka mno, huku nikitiririkwa machozi, na anayenijibu simuoni. Hakika nilijiona wazi kwamba naenda motoni. Nilitubu dhambi zangu zote wazi wazi kwa machozi. Hapo ndipo Mungu akatimiza ahadi zake: Kwanza, AMANI TELE ilimiminwa ndani yangu, ikawa mhuri wa kutosha wa ‘FARAJA YA MSAMAHA’ kutoka kwake. “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako” (Isa 43:25). Pili, Roho Mtakatifu alihamia ndani yangu, na tangu hapo huniongoza na kunitia kwenye kweli yote (Yn 16:13). Siku ya unyakuo NAAMINI HATANIACHA (1 The 4:17). HALELUYA! Mw. Elias Byabato

amepewa na Mungu. Mzazi akiiacha nafasi yake, adui shetani huidaka kwa haraka. “Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.” 2 Timotheo 1:5 Mary Bura na Elieshi Kisinza 11


HISTORIA YA WIMBO

RIZIKI TOLEO 1, 2018

HISTORIA YA WIMBO

RIZIKI TOLEO 1, 2018

Yesu kwa Imani Eng.: “My faith looks up to Thee”. Tumwabudu Mungu Wetu na. 179, Tenzi za Rohoni na.14. Ray Palmer, aliyezaliwa Novemba 12, 1808, na kufariki 1887, huko Little Compton, Rhode Island USA, ndiye mwandishi wa wimbo huu, “Yesu kwa Imani”. Wimbo una mafungu manne. Sehemu ya 1 na 2 zinafaa sana katika huduma ya kuungama na kusamehewa. Fungu la kwanza huanzisha ukiri; Fungu la pili ni jibu kwa maneno ya msamaha na uhakika. Na fungu la 3 na 4 ni sala za uongozi kama Mkristo anayeendeleza safari ya kuelekea katika utukufu.

Karibu tuimbe wimbo huu

fulani akiwa mwalimu katika shule ya wasichana huko New York, alikuwa na wakati mgumu ulioambatana na ugonjwa na upweke mkubwa. Hapo alipata nafasi ya kutafakari juu ya shairi fulani kutoka Ujerumani lililoeleza maisha ya mkosaji aliyepiga magoti mbele ya msalaba wa Kristo. Hapo Palmer na maneno ya wimbo huu yalianza kumjia rohoni akiwa ametawaliwa na mawazo ya ukombozi na wokovu. Palmer aliandika maneno hayo katika daftari ndogo ambayo aliiweka katika mfuko wake, akaitunza tu bila kujua nini zaidi cha kufanya. Miaka miwili baadaye alimtembelea rafiki yake, Lowell Mason, aliyekuwa mwanamuziki. Mason alimjulisha Palmer kuwa alikuwa akijiandaa kuchapisha kitabu cha nyimbo, na kumwuliza kama ana chochote angependa kuchangia. Hiyo ilisababisha Palmer kukumbuka shairi lake. Baada ya kumpa rafiki yake daftari ayaone yale maneno, Mason alitunga sauti na kutengeneza muziki. Wimbo huu umekuwa maarufu sana duniani na umeingizwa katika vitabu vingi vikubwa vya nyimbo za Kikristo, kama alivyotabiri Mason, mtunzi wa sauti, akimwambia Palmer: “Unaweza kuishi miaka mingi na kufanya mambo mengi. Lakini nadhani utajulikana kwa vizazi vingi kama mwandishi wa 'Yesu kwa Imani'”.

Wakati Ray Palmer akiwa kijana, familia yake ilikumbwa na hali ngumu ya kiuchumi, na alilazimika kukatisha masomo na kufanya kazi katika duka la bidhaa mbalimbali huko Boston. Pamoja na kazi hiyo, Palmer alijiunga na Kanisa, na hiyo ilimfanya azinduke na kuipenda huduma. Alijiunga na mafunzo mbalimbali ikiwemo chuo cha Yale, New Haven, ambapo alihitimu mwaka wa 1830. Mwaka 1835 akawa mchungaji wa Kanisa la Central Congregational Church, Bath, mkoani Maine, na pamoja na nafasi nyingi katika kulitumikia Kanisa, alihudumu pia kama katibu wa Umoja wa Kanisa Marekani. Palmer alikuwa mhubiri maarufu na mwandishi, akiandika mashairi ya awali pamoja na kutafsiri nyimbo. Wakati

1. Yesu kwa imani, Nakutumaini, peke yako; Nisikie sasa, Na kunitakasa, Ni wako kabisa Tangu leo.

3. Hapa nazunguka Katika mashaka, Na matata; Palipo na giza Utaniongoza Hivi nitaweza Kufuata.

2. Nipe nguvu pia Za kusaidia Moyo wangu; Ulikufa wewe, Wokovu nipewe Nakupenda wewe, Bwana wangu.

4. Takuwa mzima Nivushe salama Mautini; Sina hofu kamwe Ukiwapo nami Nami nikwandame Siku zote.

Picha: www.pixabay.com

Cathbert Msemo 12

13


JAMII

RIZIKI TOLEO 1, 2018

JAMII

RIZIKI TOLEO 1, 2018

Wazazi Kukosa Watoto Mume na mke wanapokutana kimwili kwa muda wa miezi 12 bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi na bado kushika mimba au kupata ujauzito hakujatokea, wataalamu wanaanza kuongea kuhusu ugumba, ambao ni hali ya mwanamume au mwanamke kutokuwa na uwezo wa kuzaa licha ya kufikia umri wa kuweza kufanya hivyo. Kuna imani iliyotawala katika jamii nyingi kuwa endapo mwanamke hapati mimba, yeye ndiye mwenye tatizo, na hutuhumiwa kuwa mgumba. Lakini ukweli ni kwamba asilimia 30-40 ya matatizo yote ya ugumba huwakumba wanaume, wakati asilimia 40-50 ya tatizo hilo huwakumba wanawake. Asilimia 1030 iliyobakia ya tatizo hili, husababishwa kwa pamoja kutokana na matatizo kati ya mume na mke, ila hapa sababu halisi hazijulikani.

Tatizo lingine ni kutofahamu ni lini hasa muda mwafaka wa kufanya tendo la ndoa, ili kushika mimba kwa urahisi. Kuna wanawake ambao hawajui hata mzunguko wao wa hedhi (yaani hawajui wanaanza na kumaliza hedhi lini, na muda wa hedhi ni wa siku ngapi. Mwanamke akijua wakati wa ovari zake kutoa yai (ovulation), anaweza kuongeza nafasi ya kushika ujauzito. Ni vizuri kufanya tendo la ndoa angalau kila siku ya pili wakati wa kuelekea yai kutoka, na kuendelea siku 2-3 baada ya hilo kutoka. Ovari hutoa yai wiki 2 kabla ya kupata hedhi. Kama mwanamke ana mzunguko wa hedhi wa siku 28 (yaani kila baada ya siku 28 anapata hedhi), basi ni vizuri kujamiiana angalau kwa siku 3 kati ya siku ya 7-18 baada ya kupata hedhi.

Ushauri nasaha na kuwaelimisha wazazi wote wawili

• Acha kunywa pombe, kuvuta sigara, kuacha matumizi ya madawa ya kulevya nk. • Hakikisha kwamba hasa mwanamke anapata kupumzika vizuri, na mwanamume asikae tu bila kufanya mazoezi ya kimwili. • Punguza unene uliopitiliza. • Kuwa na mume/mke mmoja mwaminifu. Sababu ni maradufu: Hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya zinaa yanayoweza kusababisha ugumba. Huleta raha ile iliyo muhimu kwa mwanamke hasa ili kushika mimba. • Kula mlo kamili na wenye virutubisho vyote muhimu kwa afya njema.

• Nendeni kupima kwa daktari ili kuhakikisha hamna magonjwa kwenye mfumo wa uzazi. Zipo dawa za kutibu.

• Ombeana. Mfano mzuri ni Isaka aliyeendelea kumwombea Rebeka miaka 20 (Mwa 25:21). Licha ya kuwa vyema kumleta kwa Mungu, inampa pia mwenzako raha kusikia maombi yako na kutiwa uhakika kwamba humlaumu wala kutaka kumwacha kwa sababu ya ugumba wenu. • Kumbuka kwamba hata kama Mungu asipokujalia mtoto hapo unapotaka, bado anakubariki kwa namna nyingine nyingi unapomwamini (Yak 1:2-4). Mwombe akusaidie kuona baraka hizo. Kwa vyovyote vile mnaweza kutegemea kwamba Mungu ana mawazo ya amani tu kwenu si ya mabaya, na lango lake ni hili tu kuwapa ninyi tumaini siku zenu zote (Yer 29:11).

Ushauri wa kichungaji kwa wanandoa wote

• Usitafute msaada kwa waganga wa kienyeji, bali mtegemee Mungu na kumwabudu yeye peke yake, maana anataka kukubariki pia katika suala la ugomba (Kut 23:25-26). • Kuwa tu na hamu ya kupata watoto na kuomba muujiza wa Mungu. Usiwe na wasiwasi kwamba anaweza kuushinda ugumba wako. Lakini wakati huohuo uwe mnyenyekevu na kuomba mapenzi ya Mungu yatimizwe kwa wakati wake.

Monica Ndege, mkunga na muuguzi

Ushauri mwingine wa kidaktari kwa wanandoa wote

Ni vizuri kwa wote wawili, mke na mume, kuchukuliwa vipimo ili kujua ni nani baina yao aliye na tatizo. Matatizo mengi ya ugumba hutokea kutokana na uelewa au ufahamu mdogo wa elimu ya uzazi na ya kujamiiana kwa wanandoa. Kuna wanaume ambao hufika kilele haraka wakati wa tendo la ndoa, na kutoa shahawa mapema kabla ya muda muafaka ili shahawa itolewe nje ya uke. Hii husababisha kutopata ujauzito. Kitaalamu ni wazi kwamba tatizo liko kwa mwanamume, lakini kwa kosa mara nyingi lawama zote huelekezwa kwa mwanamke. 14

Picha: Lesli Lundgren www.freeimages.com 15


RIZIKI TOLEO 1, 2018

Shindano la uandishi wa kitabu kwa vijana Soma Biblia hushiriki katika wito wa kuwaletea vijana habari njema ya Biblia kuhusu Yesu Kristo ili wamwamini na kumfuata. Kwa hiyo tunawakaribisha wote wenye vipawa vya uandishi waandike kitabu kwa vijana wenye umri wa miaka 13-19.

Masharti kwa mswada:

Ahadi ya Soma Biblia:

• Lugha iwe ya Kiswahili, na ieleweke kwa walengwa • Mfumo wa uandishi uwe simulizi • Ukubwa wa kitabu usizidi kurasa 50 zenye Maneno 400 • Yaliyomo yakidhi malengo yaliyotajwa hapo juu

• Mswada utakaoshinda utachapwa kama kitabu kwa gharama za Soma Biblia • Pamoja na heshima ya kuwa mshindi, mwandishi wa kitabu hicho atalipwa mrabaha wa asilimia 10 • Waandishi wengine wote watarudishiwa mswada wao, ukiwa pamoja na maoni machache; hatutautumia kwa namna nyingine isipokuwa kwa idhini ya mwandishi

Tuma mswada wako kwa Soma Biblia, S.L.P. 2696, Arusha publishingmanager.somabiblia@gmail.com

Tarehe ya mwisho kutuletea mswada ni 31 Machi 2018 SOMA BIBLIA S.L. P 2696 Arusha +255 752 379 932 editor.somabiblia@gmail.com www.somabiblia.or.tz

SOMA RIZIKI “ONLINE”

www.issuu.com/riziki

Riziki 1 2018 MWISHINDANIE IMANI  

Je, nini itatokea kwa imani yetu, ikiwa kila kizazi huibadilisha tu kulingarna na mawazo, mahitaji na mipango yake?

Riziki 1 2018 MWISHINDANIE IMANI  

Je, nini itatokea kwa imani yetu, ikiwa kila kizazi huibadilisha tu kulingarna na mawazo, mahitaji na mipango yake?

Advertisement