Sema Magazine September 2013

Page 6

10

Caroline Augostine

Veisi Ivan, Miaka 14. Ilikuaje mpaka ukajiunga na Mtandao wa Wanahabari Watoto Tanzania? Afisa elimu alikuja shule kuleta barua kwaajili ya mafunzo ya uandishi wa habari kutoka UNICEF na mkuu wa shule pamoja na wazazi wakakubali. Tulikaa UNICEF siku saba kwenye mafunzo haya.

Kama mwanahabari una majukumu gani? Nasaidia Katika kuandaa vipindi.

Umekutana na changamoto gani? Mwanzo nilikua sijui kutumia vifaa na nilikua ninaona aibu kujitambulisha. Pia, nilikua sijazoea kukaa mbali na nyumbani. Ukafanya nini kukabiliana na hili? Nilijitahidi kuzoea na kujifunza hadi nikaweza.

Kila mototo ana ndoto. Je, wewe ungependa kuwa nani ukiwa mkubwa? Ningependa kuwa mwanahabari redio na tv sanasana nishughulike na habari za watoto na kutetea haki za watoto. Tarehe 16 mwezi wa 6 ni Siku ya Mtoto wa Afrika. Unaielewaje siku hii? Watoto Afrika Kusini walipotezana na ndugu zao na wengi kuuwawa kwasababu ya kutetea haki zao. Siku hii hutusaidia kujua haki za watoto na kufahamiana. Ni mambo gani katika jamii za kiafrika unaona yana madhara kwa watoto? Mtoto wa kike kutopelekwa shule inamuumiza kisaikolojia.

Unaona kifanyike nini ili kuyatokomeza? Serekali itoe ushauri kwa jamii ili kuwepo na muamko kwamba mtoto ana haki ya kupendwa.

Unataka kuwaambia nini watoto wengine? Wapende kuhudhuria sikukuu hii maana kuna mengi ya kujifunza. Wasome ili wasaidie watoto wengine walioko katika hali ngumu.

Ilikuaje mpaka ukajiunga na Mtandao wa Wanahabari Watoto Tanzania? Nilikua mwenyekiti wa baraza la watoto, Kinondoni. Kati yetu, watoto 15 waliteuliwa kupata mafunzo ya uandishi wa habari UNICEF, mimi nikiwa mmoja wapo.

Kama mwanahabari una majukumu gani? Tunarekodi vipindi na kuvirusha hewani ili watu wajue haki za watoto. Nawaongoza wenzangu na tunasiadiana katika kuandaa vipindi. Umekutana na changamoto gani? Kipengele cha wanajamii kutoa maoni, wengine wanakataa. Watu hawajui kuhusu Mtandao wa Watoto Wanahabari. Ukafanya nini kukabiliana na hili? Tumewaambia Save the Children watoe elimu ili jamii ifahamu uwepo na umuhimu wetu.

Kila mototo ana ndoto. Je, wewe ungependa kuwa nani ukiwa mkubwa? Muhasibu na mwandishi wa habari.

Tarehe 16 mwezi wa 6 ni Siku ya Mtoto wa Afrika. Unaielewaje siku hii? Ni siku ambayo tunakumbuka vifo vya watoto wenzetu kule Soweto, Afrika Kusini. Hii siku ni muhimu kwasababu ni muda wa watoto kuona tuna faida na mchango katika jamii.

Ni mambo gani katika jamii za kiafrika unaona yana madhara kwa watoto? Mila ambayo ipo Mara ambapo mwanamke asiye na uwezo wa kuzaa anatoa mahari kwa familia yenye mtoto wa kike alafu anamuozesha. Yule binti akijifungua watoto, yule mama anawachukua kama wake kwa kua yeye alishamtolea mahari binti yule. Unaona kifanyike nini ili kuyatokomeza? Serekali ielimishe watu kuhusu jambo hili na madhara yake. Pia, watu wawe na hamasa ya kusikiliza wanachoelezwa juu ya mila kama hizi na watake mabadiliko.

Unataka kuwaambia nini watoto wengine? Siku ya leo kuna vitu vingi pamoja na maoni mengi na ningewashauri washiriki maana tuna mchango mkubwa katika jamii.

“Kuna msemo kua mbuyu ulianza kama mchicha na watoto hawa wanatuonyesha kwamba hata watu wenye umri mdogo wanaweza kufanya mambo makubwa.�


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.