Page 1

Ijumaa Februari 22, 2012

KUWAUNGA A MKONO WADAU WA MAPINDUZI YA kilimokwanza@guardian.co.tz Wasiliana nasi bure kwa ujumbe mfupi kwenye simu andika KILIMO kwenda 15774

RUKA JUU IMERUDI TENA

“

Ikiwaletea kwa mara nyingine fursa kwa maisha yote kwa vijana ...Ruka JUU, changamoto ya biashara kwa vijana, sasa imerudi tena. Ni kwa vijana juu ya Biashara Kilimo.


Ijumaa Februari 22, 2013

Ijumaa Februari 22, 2013

UJUMBE WETU

2

MAISHA

Kilimo Kinalipa

47’! ‘Yeah’, simulizi zangu zinafanana mno na simulizi za maisha yangu. Hata ukiniuliza ni lini haswa nilianza kujihusisha na kilimo, nitakwambia SIJUI. Nilipata akili nikajikuta tayari nakwenda shamba na watu wote katika familia yetu! Nimezaliwa na kukulia katika familia yenye watu wengi na ilipotimu saa ya shamba wagonjwa na watoto wachanga tu ndio ‘waliosamehewa’! Hata tulipokuwa tumeshatawanyika katika shule mbalimbali za bweni – wakati wa likizo kila mmoja alitengewa ‘pande’ lake na aliyemaliza aliruhusiwa kuorodhesha mahitaji yake ya shule na kupewa fedha. Kilimo kilikuwa ndiyo mpango mzima na hakuna aliyelalamika wala kusononeka! Tulikuwa tukifahamu fika kwamba mahitaji yetu yote – kuanzia ada za shule hadi msosi – yalipatikana shamba.Tulifahamu pia kwamba sisi ndiyo nguvukazi ambayo wazazi wetu walijivunia na kuitegemea na kama tusingeifanya kazi hiyo hakuna mtu yeyote ambaye angekuja kuifanya kwa niaba yetu. Nilikuwa nikifanya kazi ‘usiku na mchana’ ili nimalize kipande changu mapema, nipate japo siku chache za kutembelea ndugu na jamaa kabla ya kurudi shule. Maisha yaliendelea kwa mtindo huo mpaka wote tukahitimu masomo yetu. Leo hii, tumetawanyika sehemu mbalimbali nchini, tukifanya kazi tofauti – wengine ofisini, wengine shamba na wengine kotekote! Waliochagua kuendelea na kilimo, uzoefu wao wa utotoni umewasaidia kuifanya kazi hiyo vizuri sana na wamekuwa wakulima bomba vibaya mno! ‘Ukinitupa’ shambani leo hii, hutoamini kwamba ndiye yuleyule Pendo Mashulano, unayemsoma kila leo katika Fema! Sina ugeni wowote katika anga hizo, utashangaa! Nashukuru sana kwa uzoefu nilioupata wakati na kua kwa nini na ujuzi wa ziada ambao naweza kuutumia wakati wowote!!

Ardhi itumike kuvutia vijana kujiajiri

T

ANZANIA inakabiliwa na tatizo la ajira katika sekta rasmi, umaskini kwa wananchi wake na upungufu wa chakula katika baadhi ya maeneo.

Baadhi ya vijana wenye nguvu za kutosha wamekuwa wakirandaranda mitaani na kukaa vijiweni mijini na vijijini kwa kile kinachodaiwa kuwa hawana shughuli za kufanya. Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali kuanzia ngazi ya vyeti hadi shahada, wanahitimu kila mwaka na kujikuta wakihangaika kutafuta ajira katika sekta rasmi huku wengi wao hawafanikiwi kwa sababu ya ufinyu wa nafasi hizo. Kundi la watu hao ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, baadhi yao hujikuta wakizurura au kufanya shughuli ambazo hazina tija au zile za bora mkono uende kinywani. Hawaboreshi maisha yao, kuchangia pato la familia na uchumi wa taifa. Ushahidi uko wazi kuwa wakati mwingine vipaumbele vyetu havielekezwi katika maeneo sahihi. Kwamba wapi tuanze na wapi tumalizie. Mathalani, katika eneo la kilimo, maelezo

na mipango mingi imekuwa ikielezwa kuwa inalenga kubadilisha kilimo chetu kutoka jembe la mkono ambalo limekuwa linatumiwa na wakulima wengi kwa mikoa mingi na kuelekea katika kilimo cha kisasa chenye tija. Kaulimbiu mbalimbali zimekuwa zikitolewa kutoka Siasa ni Kilimo hadi Kilimo Kwanza, lakini mapinduzi ya kilimo yamekuwa yakibadilika kwa kasi ndogo sana. Kilimo kinaelezwa kuwa ni uti wa mgongo wa taifa na kinaajiri zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania ambao wanaishi vijijini. Kwa hiyo eneo hili linatakiwa kupewa kipaumbele cha uhakika ili kuleta mapinduzi ya kweli na kuwafanya wakulima waongeze uzalishaji, kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, kuongeza usalama wa chakula na kupunguza kiwango cha umaskini kinachowakabili watu wengi. Haiaminiki hata kidogo leo hii kusikia baadhi ya maeneo yakiwamo yale yanayopakana na maziwa na mito, watu wanaishi kwa kula mlo mmoja huku wakikabiliwa na umaskini wa kiwango cha kutisha. Kilimo cha umwagiliaji kimekuwa kinatajwa kuwa kitasaidia sana kutuondoa katika utegemezi wa mvua ambazo miaka ya hivi kari-

buni, mvua zimekuwa hazitabiriki sana kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima na kushusha kiwango cha uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali. Tunaweza kulima kilimo cha uhakika kwa sababu ya neema ya maji tuliyonayo kwa sababu nchi imezungukwa na mito, mabwawa na maeneo nyevu nyevu mengi karibu kila kona ya nchi. Hata hivyo, utekelezaji bado hauendi kwa kasi inayozungumzwa. Kwa hiyo, tunatakiwa kupima kwa makini vipaumbele vyetu na uwekezaji ili kuhakikisha kuwa nguvu kazi ya vijana tuliyonayo inatumika kuzalisha kwa tija na kutuondoa hapa tulipo. Matumizi ya teknolojia rahisi na mitambo kama itapatikana kwa urahisi ni kwamba kilimo kitavutia vijana na watu wengi kwa sababu ya faida inayotarajiwa kupatikana. Wakati unapopitishwa uamuzi wa kutekelezwa Kilimo Kwanza ili kuinua uzalishaji na kuleta mapinduzi katika kilimo, yaliingizwa matrekta na baadhi ya mitambo . Tuna ardhi kubwa yenye rutuba na uhakika wa soko la chakula ni mkubwa hata katika

nchi jirani za Afrika Mashariki na kwingineko. Kinachotakiwa ni kutoa mikopo yenye riba ndogo kama ilivyosemwa kuwa itaanzishwa benki ya kilimo, inatakiwa ionekane kweli ni tegemo la wakulima. Hali kadhalika, ufugaji mdogo mdogo kama wa kuku, nyuki na mwingineo, unaoweza kufanywa na watu wengi kwa mtaji mdogo, ni muhimu ukahimizwa na kuhamasishwa vilivyo. Pia kilimo cha mazao mchanganyiko ya bustani ikiwamo mboga mboga, matunda na maua kwa wakulima wanaofanya miradi hiyo, umechangia mabadiliko ya kuboresha maisha na kuchangia pato la familia na taifa kwa ujumla.

Jesse Kwayu Mhariri

Na Pendo Mashulano

NDANI

Bustani: Rasilimali kubwa, fursa nyingi

Umoja ni nguvu!

4

Tatizo la ufugaji wanyama na mabadiliko ya tabia nchi

7

15

Nikiwa kinda la miaka mitatu na ‘vijino’vyangu vichache tu kinywani, tayari nilishakuwa ‘mkulima’ ”, anasema Geoffrey Martin Sadana, mwanafunzi wa shule ya sekondari Nkasi, mkoani Rukwa. “Katika kigizagiza cha kuelekea pambazuko, mama alininyanyua kutoka kitandani, akanitupia mgongoni na kunifunga vizuri kwa mbeleko. Kisha alibeba jembe lake, tayari kwa safari ya shamba kilometa kadhaa kutoka nyumbani. Sikujua kilichokuwa kinaendelea kwani ilikuwa usiku nalala kitandani lakini kila nilipoamka nilijikuta shamba.” “Tukiwa shamba nilichezea chochote kilichokuwa karibu nami, kuanzia udongo hadi mabua na mama hakunizuia, aliniacha nicheze, ilimradi sikitu kinachoweza kunidhuru. Kwa kutumia kijiti au jiwe lenye ncha, nili-

tifua ardhi na kupanda mbegu au mimea, kama nilivyokuwa nikiona wazazi wangu wakifanya! Niliweza kujaza hata mahindi kumi kwenye shimo moja na kufukia, yalipoota kila mtu alijua ni mimi. Kwa ufupi, kilimo kilikuwa ndiyo mchezo wangu wa utotoni,” “Nilipotimiza miaka mitano, wazazi wangu walinitengenezea jembe la saizi yangu, nikaanza kusaidia kazi ndogondogo za shamba kama palizi, kuchimbia vitunguu na nyingine za namna hiyo. Kadri miaka ilivyokwenda ndivyo umaridadi wangu katika kilimo ulivyoongezeka.” “Nilipotimiza miaka saba nilikuwa na uwezo wa kulima hadi yadi 6 x 20. Nilijifunza kilimo kwa kupiga mzigo, siyo kwa kutazama. Kadri miaka ilivyokwenda ndivyo uwezo wangu ulivyoogezeka na kila baada ya muda wazazi wangu waliniongezea ukubwa wa eneo la kulima; hivyo ndivyo

walivyonifundisha kazi. Nawashukuru sana.” “Tangu wakati huo, kilimo kikawa ndiyo maisha yangu, nikajua kwamba ni kutokana na kilimo tu napata chakula, elimu, mavazi, na mahitaji yote ya familia. Leo hii, japokuwa niko shule, lazima niutafute muda wa kuungana na familia katika kazi za shamba, japo wikiendi na wakati wa likizo,” Geoffrey anamalizia. Bahati naye anasimulia Ndiyo! Ni dada Bahati Yule yule wa Fema TV Talk Show. Ni ‘mkali’ shambani kama alivyo ‘mkali’ kwenye runinga, sikiliza simulizi yake. “Wakati nakua, nakumbuka, shamba la familia lilikuwa ‘hatua’ kidogo kutoka nyumbani. Jogoo la kwanza tu lilipowika, tulidamka, tukaosha nyuso zetu na chapchap tulikamata jembe tayari kwa safari ya shamba pamoja na wazazi wetu.”

3

“Ukiacha shamba kubwa la familia, tulikuwa na eneo kubwa mbele ya nyumba yetu na yeyote katika familia aliyetaka kulima pale aliruhusiwa.” “Nilikuwa na kibustani changu pale, nikilima mboga za majani – spinachi, ‘chainizi’, au kabichi. Mboga hizi zilikuwa zikitumika kwa msosi wa familia lakini niliruhusiwa kuuza kiasi na kutumia fedha kununua chochote nilichohitaji.” “Kutokana na biashara hii ndogo, nilikuwa na pocket money yangu muda wote na nilikuwa na uwezo wa kujinunulia pamba za ukweli wakati wowote nilipohitaji. Wazazi wangu walikuwa wakijivunia sana juhudi zangu! Nani atathubutu kusema kilimo hakilipi?” Simulizi zetu zinafanana mno Muda wote ninapozungumza na Geoffrey na Bahati kwa ajili ya makala hii, akili yangu inakumbuka mbaaaali sana. Nakumbuka enzi zileeee ‘mwaka

Wewe je? Baadhi yenu wanafunzi tayari mnajishughulisha na kilimo, lakini wengine pengine hamjawahi hata kugusa jembe. Sawa? Je, unafahamu kwamba kilimo ni maisha? – kila kitu, kuanzia ada ya shule, ‘vocha’ za simu, nguo na chakula, vyote vinatoka shamba! Je, umewahi kufikiria kulima kijishamba chako mwenyewe? Unaweza kupata mshiko wa ziada na kuchangia katika ‘pocket money’ yako kama alivyofanya Dada Bahati enzi zake! Je, umewahi kujiuliza ni kiasi gani cha fedha unaweza ‘kutengeneza’ kwa kulima japo eneo dogo tu la mbogamboga? Tafakari na uanze sasa! Kuwa mjanja! Kilimokinalipa! Kumbuka: Kujishughulisha na kilimo wakati ukiwa masomoni kutakupatia wewe na familia yako kipato cha ziada. Tumia muda wako wa jioni, ‘wikiendi’ na wakati wa likizo kwa kulima na ukifanye kilimo kuwa sehemu ya maisha yako. KUMBUKA, chakula, vitabu, nguo, ada ya shule na hata ‘pocket money’ –vyote vinatoka shamba. Baadaye katika maisha yako, unaweza ukawekeza zaidi katika kilimo na kutengeneza faida kubwa kibiashara. KUNA FURSA ZA MAANA KATIKA KILIMO!!! Tuma maoni yako bure ukianza na neno LIFE kwenda namba 15774


Ijumaa Februari 22, 2013 A

BUSTANI

4

Ijumaa Februari 22, 2013 A

BUSTANI

5

Bustani: Rasilimali kubwa, fursa nyingi Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Bustani Tanzania (Taha) , Jacqueline Mkindi anazungumzia masuala mbalimbali ikiwamo mipango, mikakati na uwekezaji katika sekta hiyo kama alivyofanyiwa mahojiano na Mwandishi wa Kilimo Kwanza: SWALI: Je kuna aina gani ya kuwapo fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa kilimo cha bustani? Je, wanaweza kuzungumzia mahitaji ya masoko? JIBU: Uzalishaji wa matunda na mboga kwa ajili ya masoko ya ndani na Kimataifa katika Tanzania ni ya chini sana ikilinganishwa na rasilimali inayopatikana kwa uzalishaji nchini. Mahitaji ya soko ya mboga zenye thamani yapo juu (kijani maharage, mbaazi, mtoto mboga, pilipili ) na matunda kama vile maembe, avocados na mananasi yamekuwa yakiongezeka. Kujenga mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji ili wawekeze katika sekta ya maua, TAHA imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na serikali kuhusu masuala kadhaa kama vile kuhamasisha wakulima wadogo na wa kati wa kuzalisha na huduma ya mahitaji ya soko. Pamoja na wakulima wadogo, TAHA ina jukumu la kuhamasisha na kujenga uwezo wa wakulima hawa na kuunganisha na wanunuzi au makandarasi, kutoa mafunzo juu ya kuzingatia viwango kwa ajili ya kukabiliana na ushindani katika soko. Hivi karibuni, TAHA ilitambuliwa mwekezaji aliyekuja kuwekeza katika soko la nje la mboga na mpango wa kununua hadi tani 100 za mboga ya kila siku ili kuongeza mauzo ya nje na ikilinganishwa na hali ya sasa ya wastani wa tani 50 kwa siku. Ingawa mwekezaji huyu

anaelekeza nguvu katika eneo la Kaskazini (Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida).Kuna wawekezaji wengine ambao wanalenga mikoa mingine. TAHA imekuwa ikifanya kampeni ya kuhamasisha wakulima wadogo na wa kati ukubwa kuzalisha kwa ajili ya kukabili soko hili. SWALI: Kwa kifupi unaweza kueleza hatua za mkakati, mbinu za uzalishaji, viwango, kuongeza thamani na upatikanaji wa masoko kwa ajili ya wazalishaji wa mananasi? JIBU: Upatikanaji wa masoko umekuwa kikwazo kwa wakulima wa bustani katika sehemu mbalimbali za nchi kutokana na miundo mbinu duni, vifaa na uwezekano wa kupata fedha. Moja ya malengo ya TAHA ni kuimarisha uhusiano kati ya mnunuzi na muuzaji. Moja ya malengo ya mchakato huo mwaka huu ni kuwaunga nisha wazalishaji wa Chama cha Wazalishaji Mananasi wa Kiwangwa (KIPA) na wenzao kutoka kanda ya Ghuba, ambao wako tayari kununua kontena tano kwa wiki kutoka kwa wakulima hao. Taha itaendelea kuhamasisha wakulima kuhakikisha wanatumia teknolojia sahihi. Chama pia kinafanyia kazi kuhakikisha kiwango cha uzalishaji kinaongezeka, aina, na viwango vya kuendeleza soko hili. SWALI: Je, una mkakati wa Ushirikiano kuhakikisha kuongeza uwezo katika sekta ndogo ya kilimo cha mazao ya bustani, mboga na matunda? JIBU: TAHA ina dhamana ya kupanua huduma zake kwa kuwafikia wakulima wa mazao ya bustani, mboga na matunda na wadau wengine ikiwa pamoja na kutoa msukumo kwa kulenga katika masoko ya kilimo katika kanda kwa kutumia majukwaa mbalimbali. Jukumu la TAHA ni kuongeza uwezo wa wakulima ili waweze kushiriki kwa ufanisi na kuwa na uhusiano endelevu. Ili kufanikisha hilo, TAHA imekuwa ikishiriki katika ubia na mashirika mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha kwamba huduma za msaada wa biashara unatolewa kwa sekta. Ni kwa suala hili kuwa chama waliungana na Kilimo Trust, ili kufanya kazi pamoja na kutambua usalama wa chakula na kuongeza mchango wa kilimo ili kutokomeza umaskini, kama

vile kuongeza tija na faida za kampuni za biashara ndogo. TAHA na Kilimo Trust wametia saini makubaliano ya kushiriki katika juhudi za pamoja ili kuhakikisha ongezeko la tija na ushirikiano wa sekta ndogo ya mazao ya bustani na mbogamboga nchini Tanzania katika kanda na mnyororo wa dunia. Tunafanya hivyo kwa kutumia faida ya fursa kubwa ya ardhi nchini na rasilimali za ardhi na maji kufikia hatua kuelekea kwa muuzaji nje wa mazao ya kilimo. SWALI: Unaelezeaje namna mnavyojipanga kuanzisha mafunzo ya vitendo kuhusu kilimo cha bustani katika kituo cha ubora (PTC)? Unadhani itafanikiwa ? Kwa namna gani? JIBU: TAHA imetia saini makubaliano na serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Aprili 2012, ardhi imetengwa kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kujitegemea cha ubora kwa mafunzo ya bustani kwa vitendo (PTC). PTC watakuwa wanatoa mafunzo kwa maeneo mbalimbali ya mnyororo wa uzalishaji wa mazao ya bustani, maua na matunda, mbinu bora za kisasa na huduma nyingine za msaada wa kiufundi kwa wakulima. Kwa sasa , TAHA hutoa mafunzo juu ya mbinu bora za kilimo, kilimo kama mbinu ya biashara, uvunaji na baada ya mavuno, miongoni mwa wengine. Kwa hiyo, TAHA inasukuma gurudumu, lakini badala ya kutumia kituo cha mafunzo kuimarisha mafunzo ya sasa na kuwa na "maabara" na mchakato mzima wa mnyororo wa thamani. PTC itakuwa chombo endelevu na vyombo sahihi binafsi na serikali wakati wa kudumisha dhamira yake kwa wakulima wa bustani . TAHA imeanzisha mfululizo wa shughuli na kuanza utekelezaji wa mradi huu. Maendeleo ya kituo hiki itakuwa kwa awamu. Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa majengo, mboga mboga kwa vitendo na viwanja vya mbegu na kisha shamba vitendo / viwanja kwa ajili ya matunda . Wakati awamu ya tatu itahusisha maendeleo ya mashamba kwa ajili ya maua maua. Tuma maoni yako bure ukianza na neno HORTICULTURE kwenda namba 15774


Ijumaa Februari 22, 2013

Ijumaa Februari 22, 2013

A

6

Na Gaure Mdee

A

TABIA

UMOJA

Jishughulishe shambani ufanikiwe

Mama alifariki nikiwa na umri wa miaka 17. Hii ilikuwa ni miaka sita baada ya baba kufariki, wakati huo nikiwa ndiyo kwanza nimehitimu darasa la saba huku mdogo wangu wa kike akiwa darasa la nne. “Hatukuwa na chanzo cha mapato na nilihitaji kumaliza kidato cha nne kwa namna yoyote ile. Tulikuwa na hekari tatu za shamba na sikuwa na uhakika wa kulifanyia nini shamba hilo au nitalitumiaje,” anafafanua mkulima Frank Kalezi. Kwa sasa Frank ana miaka 32, mke na watoto watatu. Alilitumia shamba hilo kwa kilimo akiwa na dada yake na watoto wake wawili. Alilitumia kupata faida ya ziada. “Changamoto nilizokutana nazo wakati ule na ninazokutana nazo sasa zinafanana. Kwa kifupi naweka mkakati na nakabiliana nazo tofauti sasa. Nilifanikiwa kupitia kujitambua, bahati na msaada kutoka kwa maofisa kilimo,” anasema. Kwa wanaojipanga kuingia kwenye kilimo ili kupata faida siku fulani au wale ambao tayari tunafanya shughuli hiyo itakuwa ni busara kuzingatia ushauri huu. Jiandae. Zifuatazo ni mbinu za kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika kilimo.

Changamoto: Ukosefu wa ufahamu na maarifa Wakulima wengi wanakosa maarifa ya kukipeleka kilimo katika hatua nyingine. Wanaridhika mara tu wanapopata fedha kidogo. Frank alitaka msaada wa Ofisa Ugani aliyemfundisha jinsi ya kulima kwa faida. Aliuza magunia manane ya

Umoja ni nguvu! •

kama utapanda kabla ya kipindi cha unyevunyevu,” anasema Frank. Katika kundi lako, wanachama wanaweza kufuata pembejeo kwa mawakala wilayani au mkoani. Kama mtakumbushana mara kwa mara mambo yanaweza kutekelezwa mapema.

Changamoto: Ukosefu wa sehemu za kuhifadhi mazao Uhifadhi na uchakataji wa mazao ni njia nzuri ya kuongeza thamani ya mazao yako; hasa kama unasubiri hadi bei ya zao iongezeke sokoni, na hapo utapata bei nzuri. •

Suluhisho: Frank alikua anatunza mazao yake uvunguni na sebuleni, kitu ambacho mkewe alikuwa hapendi. Baadaye, alipata nafasi ya kuhifadhi ghalani. Watu katika vyama vya wakulima huweza kupata sehemu ya kuhifadhia mazao au mnaweza kupunguza gharama za kusafirisha mazao kwa ajili ya kupeleka ghalani. Pia mbinu zaidi za kijadi katika uhifadhi wa mazao kama vile Vihenge hutumika kuokoa jahazi.

Changamoto: Uhaba wa masoko Kutafuta soko la bidhaa zako kunaweza kuwa changamoto kubwa, umbali kutoka shambani hadi sokoni au wakati mwingine kutopata kile unachohitaji. Frank huhakikisha kwamba kila anapokwenda sokoni tayari anakuwa na wateja wa kuwauzia mazao yake na kama mnunuzi hajaridhika na bei anayotaka basi huamua kufanya uchakataji kwa kusaga mahindi kuwa unga na kisha kuuza kwa watu kwa bei nzuri zaidi.

Changamoto: Mtazamo hasi kuhusu kilimo Watu wengi wanakatishwa tamaa na hali ya unyanyapaa kuhusu kilimo. Tunasikia watu wakisema “Kilimo ni uchafu, ni kwa watu masikini na wasio na elimu!” Hata katika shindano la Bongo Star Search baadhi ya majaji wanawakatisha tamaa washiriki kwa kuwaambia warudi shamba kama kwamba kilimo ni kitu cha kutia aibu. Mawazo haya yako mbali mno na ukweli. Hakuna kitu cha aibu ukiwa mkulima mjanja na unayejiongezea kipato kihalali. Frank anasema “tabia hii inapoteza dhana ya kilimo kwenye taifa hili” Inafanya vijana wengi kukipa mgongo kilimo na kuona kama si shughuli ya maana kwao, mwisho wake wanajikuta wamepotea. Suluhisho Kilimo kina thamani na kinaweza kuwa sekta yenye faida kubwa kwa sababu watu wanahitaji kula, soko la bidhaa za kilimo linakuwapo kila wakati hususani mazao ya chakula. Kila sekta inalipa kwa wale tu ambao hujitoa na kufanya kazi kwa bidii na ndiyo ilivyo hata kwenye kilimo. Hivyo usiogope jembe kwa sababu kilimo ni fedha. Kifanye kuwa shughuli yako rasmi.

7

mahindi kwa mara ya kwanza na kununua hekari nyingine, “…baada ya kupata hekari nyingine nilijikuta ghafla nimeanza kupata fedha nyingi, na nilihakikisha kwamba naweza kumsomesha dada yangu.” •

Suluhisho: Kila kijiji kiwe na fursa ya kupata ushauri wa bwana au bibi shamba katika eneo lao. Hawa wana utaalamu wa kuelewa ni zao lipi linalofaa zaidi katika eneo husika, aina gani ya mbolea na viuatilifu utumie shambani kwako. Kazi yao

ni kusaidia wakulima na una haki ya kupata msaada wao. Tafuta makundi ya kilimo katika jamii unayoishi ambako pamoja mtabadilishana mawazo na kushauriana juu ya kilimo. Kama hakuna shirikiana na jirani yako kuanzisha kikundi. Umoja ni nguvu!

Changamoto: Upungufu wa Pembejeo Mbolea na mbegu wakati mwingine hutolewa na serikali kupitia ruzuku; hata hivyo hufika zikiwa

zimechelewa. •

Suluhisho: Jinunulie mbolea yako. Frank kamwe hakusubiri ruzuku ya pembejeo; huenda na kununua mwenyewe. Uliza katika kundi la wakulima wenzio au kwa bwana au bibi shamba juu ya mazingira yako. Fahamu muda mzuri wa kupanda ili kuepuka wadudu waharibifu na jinsi ya kujitengenezea mboji. “Mazao yanakuwa imara zaidi kuhimili mashambulizi ya wadudu

Suluhisho: Panga kabla: Jadiliana kuhusu bei na fanya makubaliano ya bei na mteja wako au dalali kabla ya kuufikisha mzigo. Kuwa na mkakati mbadala: Kama mnunuzi hakubaliani na bei yako, peleka biashara yako sehemu nyingine au tafuta njia nyingine ya kuuza bidhaa zako. Ni vyema kuanzisha chama ili muweze kujadiliana na kupata bei nzuri ya pamoja.

Kumbuka. Kilimo ni kazi yenye changamoto kama zilivyo kazi nyingine. Unaweza kupata fedha nzuri na kupata mafanikio kama utajituma na kuongeza bidii kutatua changamoto zinazojitokeza. Hata hivyo kama ilivyo kwa kazi zingine unahitaji vitu vitatu – Uvumilivu, Mipango na Nia ya dhati ili kufikia kileleni. Kuwa mjanja, jipange! Nenda..chukua jembe, ondoka kivulini uende shamba. Tuma maoni yako bure ukianza na neno DIG kwenda namba 15774

Na Gaure Mdee

H

apo zamani za kale palikuwapo na joka kubwa. Viumbe wadogo, wadogo waliliwa hadi likanenepa sana, kiasi cha kushindwa kuenea katika shino lake. Hivyo likalazimika kutafuta shimo jingine. Joka lilifika katika kichuguu cha siafu na kusema “Mimi ni nyoka nina nguvu sana nipisheni katika shimo hili nataka kuishi hapa.” Siafu wakasema “Tumewekeza nguvu nyingi kujenga mji wetu, tutaondokaje?” Joka likasisitiza lazima waondoke likiwa na uhakika kuwa siafu kwa udogo wao hawawezi kumfanya kitu. Alikosea. Siafu wakatambua udhaifu wao, ila wakapanga mpango, “Tushirikiane wote kwa pamoja” walinong’onezana. Wote wakapanda kwenye mwili wa joka lile, na mara moja wakaenea mwili mzima. Wakaanza kuliuma. Joka kuona vile likashindwa kuvumilia maumivu na kukimbia ili kuokoa maisha yake. Kwa umoja, siafu wadogo, wakafanikiwa kulishinda joka kubwa. Pamoja mnaweza Kama walivyo Siafu, wakulima walioungana huwa na nguvu na uwezo wa kukabiliana na changamoto ngumu. Mfano halisi ni wakulima wa miwa wa huko Mtibwa. Mwaka jana walipoona wanalipishwa kodi wasiyostahili, kwa kutumia Chama cha Wazalishaji Miwa Mtibwa ( MOA), kilichukua hatua ya kwenda Baraza la

Kilimo Tanzania (ACT) kutafuta msaada. “Tuliwaambia ACT kwamba wakulima wa Kilombero wanalipa kodi kidogo kuliko sisi katika mzigo wa aina moja wa miwa. Hii siyo haki kwetu. ACT walilichukua suala hili na kulifikisha serikalini. Waziri Mkuu aliagiza kodi hizo zirekebishwe, nasi tukapata msamaha,” anasema Hadija Kondo, Mwenyekiti wa MOA. Unganisheni nguvu kwa faida ya wote Kujiunga katika klabu, vyama au makundi kuna manufaa mengi. Na kama hutuamini basi shika haya kutoka kwa Mbunge anayetushirikisha uzoefu wa jambo hili. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, anasema pembejeo za kilimo zilichelewa sana mwaka uliopita na kuhakikisha kuwa zinafika mapema msimu unaofuta kwa kuwapa ushauri wakulima jimboni kwake. “Niliwaambia waungane na wajipange vizuri. Hakuna njia mbadala katika hili. Mnahitaji kuungana katika kundi kubwa, na kama kungekuwa na shida niliwashauri pia wawahusishe waandishi wa habari kama wanaweza.” Ushauri wa Zitto unajidhihirisha kuwa na manufaa katika mfano ufuatao. Kikundi cha walikuma cha wanawake kilichojipanga vizuri huko Ijombe mapema mwaka jana, walijikuta katika wakati mgumu baada ya kuambiwa kwamba ardhi waliyokuwa wakilima kwa miaka yote si mali yao tena.

“Viongozi wa kijiji walikodisha ardhi kwa watu wengine na kuchukua fedha katika mchakato huu. Tulienda kuomba msaada kwenye Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kituo cha Mbeya. Walikuja na waandishi wa habari walioripoti suala hili na kuwapa kashkash viongozi wa kijiji na hatimaye waliturejeshea ardhi yetu,” anasema Salome Simon, Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wakulima cha Ijombe, mkoani Mbeya. Pengine hili lisingetokea bila nguvu na nia ya dhati ya kina mama wale, na msaada kidogo kutoka kwa Diwani aliyehakikisha kuwa anakutana na

viongozi wa kijiji. Mfano wa uongozi bora ulionekana. “Fedha zilizochukuliwa kutokana na kukodishwa ardhi yao zilirejeshwa na kupelekwa kufanya kazi ya ukarabati wa shule,” anasema Said Mohamed Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Mbeya.

Niliwaambia waungane na wajipange vizuri. Hakuna njia mbadala • katika hili. Mnahitaji kuungana katika kundi kubwa, na kama kungekuwa na • shida niliwashauri pia wawahusishe waandishi wa habari kama wanaweza •

Manufaa ya kujiunga na vikundi! Gharama ndogo za uendeshaji: Kama kikundi mnaweza kununua pembejeo kwa pamoja. Mara nyingi pembejeo huuzwa kwa punguzo maalum na hivyo mnaweza kuchangia gharama za usafirishaji na hivyo kujiongezea faida! Kuwa Mjanja! Nguvu zaidi ya kupanga bei: Kukabiliana na madalali wanaopandisha na kushusha bei kiholela inaweza kuwa rahisi kama wakulima mtakuwa wamoja wenye sauti ya pamoja. Kama kikundi mnaweza kupanga bei na kulazimisha ikubalike. Tumieni nguvu yenu! Kutenda pamoja (kama siafu): Umoja ni nguvu. Kama mna tatizo au mnadhani mmefanyiwa visivyo, msikae kimya, unganisheni nguvu na mzungumze kwa sauti moja. Pamoja mtashinda. Kufanya maamuzi ya pamoja: Kuwa katika kikundi kunawafanya kujifunza na kupata mbinu bora za kilimo. Pia mtafanya maamuzi mazuri juu ya masuala yanayowaathiri wakulima wote. Mtaonekana: Serikali za mtaa au kijiji na asasi binafsi zikitambua

uwapo wenu mara nyingi ni rahisi kusaidia makundi kuliko mtu mmoja mmoja. Kifanyeni chama au kikundi chenu kifahamike. Manufaa mengine ni kwamba unakuwa na kazi chache za kufanya mnapofanya kazi pamoja! Changamoto hazitakosekana Wakati mwingine kuna watu hutaka kuwa vinara, msiruhusu hili litokee katika kundi lenu. Msiruhusu mtu mmoja kutumia mwanya huo kwa manufaa binafsi au kuwa na nguvu kuliko wengine. Wekeni mambo wazi kadri inavyowezekana na hakikisheni kila mmoja anawajibika. Ndiyo, mtu yeyote anaweza kujaribu kukimbia na fedha hivyo Kuweni makini na uchaguzi wa wanakikundi, si kila mtu ni mwaminifu. Kuweni na uvumilivu; Kwa kweli mnatakiwa kuwa na uvumilivu wa hali ya juu kwa kila mmoja. Ikiwezekana muwe na katiba au muweke sheria zitakazoliongoza kundi lenu ambazo kila mwana kikundi atalazimika kuzifuata. Muheshimiane, bila hivyo mambo hayatasonga. SEMA NA FEMA. Kwa uzoefu wako kuunda kikundi au klabu kuna faida? NDIYO, HAPANA? Tuandikie na utuambie kwa nini?

• • •

Tuma maoni yako bure ukianza na neno FORCES kwenda namba 15774


Ijumaa Februari 22, 2013

Ijumaa Februari 22, 2013

A

8

Na Rebeca Gyumi

U

nakumbuka shindano la ujasiriamali la Ruka Juu kwenye runinga mwaka 2011 lilikutanisha vijana machachari sita walioshindania nafasi ya kubadili maisha yao? Ni shindano ambalo kinyozi kutoka Kibaha, Idrissa Mannah aliibuka kidedea? Sasa sikia, habari ya mjini ndiyo hii, shindano la Ruka Juu limerudi tena…na sasa ni kuhusu vijana wanaofanya kilimo kibiashara zaidi. Kilimo ni bomba! Tumetembelea vijana makini wajasiriamali nchi nzima wanaotumia kilimo kujenga maisha yao. Kila mtu anahitaji ajira itakayomletea kipato, ila fursa za ajira zinaweza kuwa ngumu kupatikana. Wakati fursa za ajira katika sekta nyingine zinaweza kuwa chache, kilimo kina fursa kibao kwa vijana. Kilimo cha kisasa ni muhimu, kama kijana mmoja anavyosema “ udongo unanukia pesa, sema watu hawaoni tu”. Femina tunataka kukusaidia kugundua fursa iliyojificha kwenye kilimo, usije ukapitwa kwa kilimo kinaweza badili maisha yako. Shindano la kwenye runinga Ruka Juu limerudi, na msimu huu pia tuna kipindi cha radio, Fema Radio, ambavyo vitakwenda sambamba. Kwa hiyo usikose kuangalia TV na kusikiliza radio yako, upate ujanja wa kilimo.

Timu ya Ruka Juu Amabalis a.k.a ABC: Ulimpenda mtangazaji wetu mchangamfu kwenye msimu wa kwanza, utampenda zaidi katika msimu huu wa pili. Muda huu anakuja amekamilika na maujanja ya shamba. ABC atatuonesha njia na kututhibitishia kuwa kilimo ni bomba. Bwana Ishi: Hautamani kujua Bwana Ishi anatafuta nini shambani? Haswaa, mchekeshaji Bwana Ishi anaingia kwenye kilimo, atakutana na siri na changamoto za kilimo, usikose kuangalia. Dada Bahati: Washiriki na watazamaji wa msimu wa pili wa Ruka Juu wote wana nafasi ya kushinda. Wasiliana na Bahati, ubahatike. Tuna majaji katika kila kipindi cha Ruka Juu cha kwenye runinga, lakini wewe pia uliyeko nyumbani unaweza kupiga kura na kura yako ni muhimu. Rebeca: Ulimuona Rebeca akitangaza kipindi cha Fema TV Talk show, akiwa na ABC. Sasa utamsikia kwenye radio atakua mtangazaji mwenza wa Fema Radio. Michael Baruti: Unaweza ukakumbuka sauti yake maridhawa, nzito kidogo wakati akifanya kazi kama mtangazaji wa East Africa radio. Msubirie Michael, sasa ana-mix kwa mtindo wa Fema. Pia utakutana na vijana wengi wakulima na wataalam kutoka pande mbalimbali za Tanzania wanaoishi na kufurahia zawadi ya ardhi. Kwa timu hiyo machachari usikose kufuatilia

A

HABARI YA MBELE

HABARI YA MBELE

9

Ruka JUU Imerudi Tena “ Ruka Juu II, itakupagawisha.

• •

• •

Kwa nini Kilimo? Kilimo ni maisha: chakula kinajenga miili yetu, kinatupa nguvu. Kwa kutumia chakula tunakuwa, tunakidhi njaa zetu, tunaponya magonjwa mbalimbali. Tupo tulivyo kwa sababu ya chakula. Kilimo ni utajiri: Kila mtu ni lazima ale ili aishi kwa hiyo soko la kilimo haliishi na hivyo basi hakuna kazi nyingine yenye umuhimu kuliko kilimo. Lima kwa usahihi na ubora, kuna pesa ya uhakika kwenye kilimo. Ardhi kubwa yenye rutuba: Nchi yetu imebarikiwa ardhi yenye fursa kibao za kuendeleza kilimo. Wakulima wajanja wanaofahamu nini cha kufanya kubadilisha ardhi hii kuwa pesa. Kilimo ni uti wa mgongo: Unafahamu kuwa asilimia 85 ya Watanzania wanaishi kwa kutege-

mea ardhi. Nchi hii inategemea kilimo. Sasa ni muda muafaka wote tuweke msisitizo kwenye kilimo na kukifanya kiwe na faida zaidi.

Wengi wenu

Bomba! Unaweza kuita kil• Kilimo imo bomba au Kilimo Kwanza, mlituomba tuendelee kama kampeni inayoendeshwa na serikali. Tuungane wote na kukipa kilimo kipaumbele. Tulishe kizazi kijacho, tujenge maisha yetu.

Tumetembea, tukajifunza, tukafurahi ‘Tembea uone’ni msemo wa Kiswahili wenye maana, ukitembea unajifunza mambo mengi. Na ndivyo ilivyotokea kwa timu ya msimu wa pili wa Ruka Juu wakati wakitafuta washiriki katika mikoa ya Arusha, Morogoro na Rukwa. Kutoka kwenye barabara korofi ya Rukwa mpaka zenye vumbi ya Karatu timu ya msimu wa pili wa Ruka Juu ilikutana na vijana wengi wakulima

na vipindi na kuongelea vijana na kilimo cha biashara. Kwa hiyo 2013 Machi tutazindua msimu mpya, weka macho na masikio yako wazi

(miaka 18 – 30), wakiendesha maisha yao na wale wawapendao kwa kutumia kilimo. Timu imechagua wakulima

sita kutoka Monduli, Karatu, Kilosa, Mvomero, Sumbawanga na Nkasi ambao watashiriki katika shindano la runinga. Tutakutana na wengi zaidi kupitia kipindi cha radio.

pili wa Ruka Juu! Angalia, piga kura, na jifunze kwa kiasi gani kilimo bora kinabadilisha maisha ya vijana nchini Tanzania. Kilimo ni bomba, na tunasikia harufu ya pesa kwenye kilimo.

Shindano la TV Washiriki ambao kwa sasa wanalima mazao mbalimbali ya chakula kwa ajili ya kujiingizia kipato, wataweka stadi zao za kilimo na ujasiriamali kwenye majaribio watakapokuwa wanapewa changamoto za shamba. Vipindi vimerekodiwa katika mazingira ya kawaida ya washiriki. Utakutana na familia zao, marafiki, kuangalia uwezo wao wa ushiriki na pia utashiriki katika kuchagua mshindi. Utaona jinsi shamba, linavyomtoa ushamba mtu wa shamba. Na zaidi ya yote utapata mawazo mapya kuhusu kilimo.

Ruka Juu ni nini? Ruka Juu ni moja ya zao la Femina lenye lengo la kuhamasisha upatikanaji wa ajira na kipato. Kwenye runinga, Ruka Juu ni shindano la ujasiriamali linatumia maisha halisi. Msimu wa kwanza ulionyeshwa mwaka 2011, na kutokana na maoni yenu ulifurahisha sana. Wengi wenu mlituomba tuendelee na vipindi na kuongelea vijana na kilimo cha biashara. Kwa hiyo 2013 Machi tutazindua msimu mpya, weka macho na masikio yako wazi.

Usikose Ungana nasi kwenye msimu wa

Tuma maoni yako bure ukianza na neno BUSINESS kwenda namba 15774


Ijumaa Februari 22, 2013

Ijumaa Februari 22, 2013

A

10

A

VECO

VECO

11

Mpango kuboresha uhakika wa chakula, mabadiliko ya maisha

Na Mwandishi Maalum, Ansaf

K

uboreshwa soko na msingi ya uzalishaji inachangia kuleta mabadiliko ya mapato kwa idadi kubwa ya wafugaji kuku wadogo wadogo katika jamii za vijijini. Ufanisi huo umethibitishwa na mpango wa VECO katika wilaya ya Same, Kilimanjaro. Mwaka 2007, Tanzania Veco iliunga mkono programu ya miaka mitano kuhusu usalama wa chakula katika wilaya za Simanjiro na Same kwa lengo la kufanya kilimo ni shughuli yenye faida na manufaa kwa jamii zisizo na mazingira bora Mpango huo ulirekebishwa mwaka 2008 na Veco katika mbinu kuelekea kuimarisha usalama wa chakula kwa familia za wakulima. Mbinu ya SACD ,wote walihusika wa moja kwa moja katika shughuli za ndani ya mnyororo wa bidhaa katika mpangilio maalum. Mbinu ya awali ya kilimo endelevu kwa ajili ya usalama wa haikuchukuliwa kwa uzityo mkubwa . Ilionekana ni kwa ajili ya ustawi wa familia za wakulima 'kusababisha kuacha baadhi ya masuala muhimu na vikwazo kutafutiwa ufumbuzi.. Jinsi inavyofanya kazi Mpango wa kuunga mkono utekelezaji na makundi kupangwa katika kata nne za Kihurio, Makanya iliyopo, Maore na Same. Hii ilikuwa miaka mitatu wa mpango mkakati kusaidia Wakulima Family ulioandaliwa (awamu ya pili) kuboresha maisha yao. Veco, kupitia mdau wake wa utekelezaji ( halmashauri ya wilaya Same), iliwezesha shirika na uimarishaji wa vikundi vya wakulima, kwa kuimarishwa utoaji rahisi ya huduma za ugani, mafunzo , uzoefu na kupunguza gharama kwa kikundi.

Mafunzo yanayotolewea ni pamoja na ufugaji bora, uzalishaji na usimamizi, masoko, kutunza kumbukumbu, biashara ujuzi wa usimamizi, malezi ya kundi na uimarishaji wa makundi. Mafunzo yanalenga kuwezeshwa wakulima kufanya biashara na kuboresha ubora na wingi wa kuku wa asili. Pia kuboreshwa stadi za ujasiriamali na uwezeshaji katika biashara ya kuku. Ujasiriamali miongoni mwa wafugaji kuku ukawa ni ujuzi mpya na njia ya maisha kwa ajili yao. Wakulima si tu walipewa mafunzo kwa uzalishaji na kuuza kuku, lakini mengi zaidi juu ya namna bora wanaweza kuweka makampuni yao hai. Wakulima wamekuwa wakitumia

stadi hizi ili kuboresha ustawi wa familia zao na jamii kwa ujumla, na wao kuendelea kuwekeza na kupanua biashara zao. Wajasiriamali walibadilishana wanunuzi na uzoefu mbalimbali . Wakulima wadogo wadogo sasa wanawekeza katika mradi kuzaliana unaoonekana kuwa na faida zaidi. Athari za muda mrefu. Athari za muda mrefu za kusaidia kupangwa vikundi vya wakulima umechangia thamani ya ziada kiuchumi ni kwamba sehemu kubwa ya idadi ya watu maskini ni kupunguza umaskini . Baadhi ya mafanikio ni pamoja na kuwatumia kuku kibiashara, mradi wa kilimo na kuboresha maisha ya watu. Danstan Kihedu ni mkulima anayeishi na mke na watoto wake

watatu katika kijiji cha Mpirani , kata ya Maore , wilaya ya Same. Amekuwa akiwatunza kuku tu shughuli ya kujifurahisha tu tangu mwaka 1998. Kama alivyosema, "Mimi nilikuwa natunza kuku tu kwa ajili ya mahitaji ya mayai na nyama kwa ajili ya familia yangu. "Nilikuwa nafuga kuku si zaidi ya tano kwa wakati. Sikujua kwamba kuku asili inaweza kubadilisha maisha yangu kiuchumi. Ghafla, mradi wa kuku umeboresha kabisa maisha yangu. Shukrani kwa mpango huu. " Kihedu alijiunga na Muungano wa kundi mapema mwaka 2008. Kupitia kundi hili lililoingiliwa na Veco mpango katika kata ya Maore, alifanikiwa kuwabadilisha kuku wake kutoka wa kujikimu na kuwa katika kwa uzalishaji wa kibiashara.

Hii ilikuwa baada ya kupokea mafunzo ya kiufundi kuhusu kilimo na ufugaji wa biashara ya kuku kutoka Baraza la Wilaya ya Same. Alisema kuwa, kilimo cha biashara kimepanua maarifa na ujuzi wake. Kwa upande wa mapato ya Kihedu yaliongezeka na akawa elimu ya kutosha. Hatimaye akageuka katika usambazaji wa vifaranga katika kijiji chake mwenyewe na vijiji jirani nje ya kata ya Maore. Soko kuu la vifaranga vyake ni Same, Hedaru na Makanya. Anaweza kuuza hadi vifaranga 400 kwa mpigo. Ana uwezo wa kuchanja vifaranga kabla ya kuwauzia wateja wake na hivyo kufanya vifaranga wake waaminike pamoja na vifaa wake. "Mimi pia kuwapa ushauri wa jinsi ya kuwatunza," aliongeza.

biashara amegeuza maisha yake. Yeye kujenga nyumba mbili na alikuwa na uwezo wa kulipa ada za shule kwa watoto wake. Kihedu anasema: "Kuku ni mali" maana kuku ni utajiri. Kupitia ujasiriamali, uzalishaji ,mafunzo ya ujuzi na kibiashara ya kuku, Danstan Kihedu amepanua maarifa na ujuzi ambao umembadilisha kutoka kujikimu na kuwa mkulima wa kibiashara. Pia, Shogholo ni mkulima anayeishi na familia yake katika kata ya Same wilayani Same. Alianza kufuga kuku mwishoni mwa mwaka 2008 baada ya kujiunga na Umoja wa kikundi chake. Alipata motisha baada ya kuona baadhi ya wanachama waanzilishi wa kikundi hicho wakinufaika na mafunzo na nyinginezo baada

ya Veco kuingilia mpango unaotolewa kwa kundi. Awali, hakuweza kushiriki katika kutunza kuku, kwa sababu alikuwa bado mgeni katika mradi. Baada ya kushiriki katika ziara ya mafunzo huko Mfiduo, alianza kufuga kuku 10. Polepole mradi ukaanza kupanuka kwa kufuga vifaranga zaidi waloikuwa wanazalishwa kutokana na usimamizi bora na huduma. Yeye sasa anamiliki hadi kuku 300 kwa wakati mmoja. Anauza mayai, kuku na vifaranga na kuboresha maisha. Anaweza kupata hadi sh.350,000 kwa mwezi kama mapato kutokana na biashara hiyo. Kutokana na mapato hayo ameweza kutatua mahitaji ya familia kama vile ada ya shule, chakula na mahitaji mengineyo. Shogholo pia alijengwa nyumba ya

familia. Sasa ana mipango ya kupanua biashara yake na kuwa na kundi kubwa la kuku. Miongoni mwa faida zilizopatikana kutoka kuingilia mpango kwamba kamwe hawezi kusahau mafunzo ya kiufundi na ujuzi alioupata kuhusu uzalishaji wa kuku kibiashara. Alisema, kwa njia ya mafunzo mbalimbali na Mfiduo, amepata maarifa na ujuzi mwingi ambayo anaona kuna zaidi ya fedha. Maoni yake ni kwamba: "maarifa na ujuzi uliopatikana ni mbegu kuelekea mafanikio ya kiuchumi na kijamii." Magreth Mashambo ni mkulima anayeishi katika wilaya ya Same mwenye watoto wake watano kati yao wasichana wawili na wavulana watatu. Alianza kufuga kuku baada ya mo-

tisha alioupata kupitia mpango huo mwaka 2008. Awali, alikuwa akifuga kuku kama chanzo cha mayai na nyama kwa familia yake. Baadaye akaanza ufugaji wa kibiashara wa kuku asili na kuwa kuwa chanzo kikuu cha mapato na kumsaidia mama moja; "Tumepanuka kibiashara . Watoto hupata mahitaji yao yote kutoka biashara hiyo. Biashara ni kazi yangu. " Mashambo ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa kundi na mkulima aitwaye Muungano. Kundi lilianzishwa mwaka 2008 kwa njia ya uwezeshaji wa mpango Veco wilaya ya Same. Kundi lina wanachama 30, wanawake 25 na wanaume wa tano. Kupitia mafunzo mbalimbali ya kiufundi kuhusu uzalishaji wa kukuwa kibiashara, Mashambo imeweza

kuanzisha mradi wa kuku. Alianza na kuku 50. Sasa ana makazi bora ya kisasa kutokana na kuku.Alikuwa akichangia matofali ya ujenzi, maji na kazi wakati Veco imechangia saruji, bati na mbao za kujengea. Ujenzi wa upanuzi wa makazi kuimarishwa ya uzalishaji. Aliweza kuongeza idadi ya kuku hadi 150 ikiwa ni pamoja na baadhi ya majogoo anaowakuza kwa miezi 3-4 kabla ya kuuzwa kwa sh. 8000 kila mmoja. Anaweza kuendelea hadi majogoo 15 wakati huo. Kupitia mikopo midogo kutoka Benki ya Kijiji kundi lake na Jamii, limeweza kuendesha biashara vizuri. Hutoa vifaranga 50 kila mwezi. "Mimi pia kuuza mayai. Naweza kupata hadi trei nne ya mayai kwa mwezi. Trei kila kuuzwa katika sh. 7500 kwa hiyo, mimi hupata 30,000 kutokana na mayai. Vifaranga huuzwa sh 1000 kila mmoja. Mimi kupata kiwango cha chini cha sh. 50,000 kutoka biashara ya vifaranga "Anasema kwa wastani anaweza kulipwa hadi sh. 150,000 kwa mwezi. " Ninawahudumia watoto wawili walio katika shule za sekondari, mvulana na msichana. Biashara hii imesaidia sana tangu mume wangu aliponiacha na watoto. Watoto hutegemea kila kitu kutoka kwangu, "anaongeza. Mume wa Mashambo kaenda Morogoro kuangalia ajira tangu mwaka 2007 na hajarudi nyuma. Licha ya hadhi yake ya ndoa, Mashambo alikuwa na uwezo wa kutunza watoto wake wawili wanaosoma shule ya sekondari. Pia amekarabati nyumba yake. Tuma maoni yako bure ukianza na neno INITIATIVE kwenda namba 15774


Ijumaa Februari 22, 2013 A

12

BIASHARA

Kilimo biashara ndiyo mpango mzima Na Majuka Ololkeri

tu

engi yanasemwa kuhusu kijana au mtu anayejihusisha na kilimo. Wengine wanakiponda kilimo na wakati mwingine wana sababu zinazoweza zikakushawishi kukubaliana nao. Tulifika Kilosa na kuzungumza na vijana kuhusu kilimo, soko lake, namna ya kujiendeleza katika kilimo na mengineyo.

Nini kifanyike? Sekta zinazohusika zitoe elimu ya kilimo biashara ili wakulima wanufaike na kilimo Kuwe na msukumo wa matumizi ya teknolojia sahihi za kilimo kama vile kilimo cha umwagiliaji, mbegu sahihi kulingana na udongo na hali ya hewa ya eneo lako. Wakulima wajifunze namna ya kutafuta masoko na biashara juu ya kilimo stahiki kinacholenga hitaji la soko na walaji Kuwaunganisha wakulima kwenye masoko kwa kutumia teknolojia na mawasiliano mfano vipindi vya redio, simu za mkononi na mengineyo. Kufanya tafiti za kuendeleza kilimo biashara Miundombinu ya barabara, vyombo vya usafiri na mengineyo iboreshwe Elimu ya usindikaji itolewe kwa wakulima Suala la kilimo biashara lipewe kipaumbele katika ngazi zote ili wakulima waweze kuingia katika soko la ushindani Huduma za pembejeo za kilimo zisogee zaidi vijijini na ziwalenge wakulima

M

Changamoto zinazowakabili wakulima ni hizi Wakulima wengi wanalima bila kuwa na malengo Hakuna mfumo wa taarifa za masoko kuwawezesha wakulima kufahamu watauza wapi mazao yao Elimu ndogo juu ya uongezaji wa thamani ya mazao wanayolima kama vile usindikaji Hakuna utunzaji mzuri wa mazao Kutojihusisha kwenye vikundi na taasisi za kifedha kama vile SACCOS na VICOBA Kukosa uwezo wa kupanga bei ya mazao Miundombinu ya barabara na mawasiliano mbovu Ukosefu wa vyombo vya usafirishaji kutoka maeneo ya uzalishaji Kutojua namna ya kutumia simu za mikononi kibiashara ili kupata taarifa Ubora wa mazao kupungua yanapofika sokoni

• • • • • • • • • • • • • •

Madhara yake ni nini? Vijana wengi hukata tamaa kujishughulisha na kilimo kwa madai kwamba hakilipi Wakulima hukata tamaa kuendeleza kilimo hata kuuza mashamba Vijana kukimbilia mijini bila kuwa na malengo Wengi hulima kwa ajili ya chakula

• • • • • • • • •

Swali Je ni changamoto zipi wanazokutana nazo wakulima wa eneo lako? Unadhani nini kifanyike kutatua changamoto hizo? Swali hili linaendana zaidi na makala hii. Je, ni fursa zipi za kilimo biashara zinapatikana katika eneo lako? Unadhani zinakidhi mahitaji ya wakulima? Tuambie kwa kutumia mawasiliano hapa chini; Barua pepe: simchezo@feminahip.or.tz Sms: 0715568222 S.L.P. 2065, Dar es Salaam.

Ijumaa Februari 22, 2013 A

PROMO

13


Ijumaa Februari 22, 2013 A

14

Ijumaa Februari 22, 2013 A

MBEGU

MBEGU

15

Wakulima wazuiwa kutunza na kubadilishana mbegu bora Na Mwandishi Maalum, Ansaf

S

erikali imepitisha sheria inayozuia wakulima kuchagua, kutunza, na kubadilishana mbegu bora na familia zao, marafiki na majirani; imefahamika. Mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni katika mfumo wa kisheria kuhusu Haki Miliki juu ya mbegu na mimea mbalimbali.. Wakati hali hii inaonekana kama si muhimu sana na kuachiwa wanasheria, inakuwa muhimu zaidi wakati asilimia 70 ya wananchi wanategemea kilimo kwa maisha yao. Mabadiliko hayo ni pamoja na Sheria mpya ya Haki ya Mimea 2012, kusaini Mkataba wa Kimataifa juu ya Aina ya Mimea (UPOV 1991), na utumiaji wa mfumo wa kisheria kupitia uanachama wa Shirika la Hakimiliki kanda ya Afrika (Aripo). Mapendekezo ya mabadiliko ya sheria zote tatu yataimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kudhibiti mauzo ya mbegu duniani, na zaidi hasara kwa wakulima wadogo ambao wanategemea mbegu kuwaokoa kwa usalama wa chakula chao. Serikali imekuwa ikisaidia sana ushiriki wa sekta binafsi katika kilimo cha kisasa, na mfano kiasi kikubwa cha kilimo cha kisasa na mashamba makubwa kama muktadha wa kilimo katika nchi unabadilika. Jamii ya Biashara ya kimataifa imekuwa ikijihusisha na kuwekeza katika kilimo nchini Tanzania. Hii inaleta njia mpya ya kufanya kazi na changamoto, kampuni za kimataifa za mbegu yanatafuta hakimiliki ya sheria zilizo na mpya katika mimea ili kujitengenezea faida kupitia mauzo ya mbegu, dawa na mbolea.

Ajenda ya Mapinduzi mapya ya kijani Jamii ya Biashara ya kimataifa imekuwa ikijihusisha na kuwekeza katika kilimo nchini Tanzania. Hii inaleta njia mpya ya kufanya kazi na changamoto, kampuni za kimataifa za mbegu zinatafuta hakimiliki ya sheria mpya katika mimea ili kujitengenezea faida kupitia mauzo ya mbegu, dawa na mbolea. Wapinzani wa ‘mapinduzi mapya ya kijani’ hawajaacha utekelezaji katika kilimo, lakini wamewapa jukumu mabingwa kusoma jinsi gani sheria katika nchi za kiafrika zinaweza kubadilishwa ili kuanzisha modeli mpya ya kilimo. Wamebainisha kanda za biashara na mikata yaa kimataifa kama sehemu ya kuanzia. Nchi za kiafrika zinajipanga katika makundi yakiwamo EAC, SADC, na Comesa ni kama rutuba kwa ajili ya kupanda sera ya mbegu na sheria za kanda kwa ajili ya kuunga mkono utashi wa kampuni ya kimataifa. Badala yake, wakulima wamekuwa wakifuatiliwa na ‘polisi wa mbegu’, mawakala wa kampuni kubwa ambao kazi zao ni kuchunguza wakulima na kuwapeleka kwenye sheria wale wote wanaotunza mbegu. Hapa katika Afrika zaidi ya asilimia 80 ya mauzo ya mbegu zinazozalishwa zinasambazwa bila ya utaratibu rasmi,kutoka kwa mkulima kwenda kwa mkulima. Wakulima wadogowadogo katika Afrika Mashariki

wanatunza asilimia 60-70 ya mbegu zinazotumiwa shambani, wananunua asilimia 30-40 ya mbegu zao kutoka kwa ndugu na jirani na chini ya asilimia 10 per cent zinapatikana katika sekta rasmi kwa mfano kutoka kwa wauzaji wa zana za kilimo. Ukweli ni kwamba wakulima wadogo ni wazalishaji na watumiaji wakubwa wa mbegu katika Afrika na wamefanikiwa kulima na kuvuna mazao kwa miongo mingi. Mfumo wa mbegu wa mkulima kwa mkulima Mfumo wa mbegu wa mkulima kwa mkulima unapunguza gharama za uzalishaji kwa kutunza uhuru kutoka sekta ya biashara ya mbegu, wakati ubadilishanaji wa mbegu unahakikisha mtiririko wa rasilimali, kuchangia maendeleo ya mbegu sahihi za asili na mazao kwa ujumla. Tunahitaji kuunga mkono maendeleo ya mfumo huu, ambao ni rasilimali muhimu kwa kilimo cha kisasa na cha asili. Kuna utambuzi mpana wa umuhimu wa mfumo wa wakulima wadogowadogo kumudu mbegu na fursa muhimu kwa wanawake kuendeleza. Kwa hifadhi ya mbegu za shambani zinatambuliwa katika mikataba ya kimataifa kama vile the International Treaty on Plant Genetic Resources (ITPGRFA) na the Convention on Biological Diversity (CBD). Tanzania imetia saini kuridhia mikataba yote miwili , lakini inashindwa kutambua mchango wa wakulima na haki zao katika kushiriki au kunufaika na faida katika wimbi jipya la sheria mpya iliyotiwa saini. Sheria ya The Plant Breeders Rights Bill 2012 imepitishwa kuwa sheria za Tanzania. Zitatumika kuimarisha haki za sekta ya biashara ya mbegu na kuwabana jamii ya wakulima, na kuathiri maisha ya watu wengi na usalama wa chakula kwa wakulima wadogo wa Tanzania. Sehria hiyo inatoa haki ya kuuza mbegu kwa wale wanaoanzisha aina mpya. Kwa kina inaruhusu tu wakulima kutumia “ mbegu zilizovunwa (kupatikana katika mimea yao) kwa ajili ya dhamira ya propaganda katika himaya yao”. Hii inamaanisha kuwa wakulima hawawezi kutunza, kubadilisha na kuuza mbegu kutoka katika aina zilizozuiwa. Kwa mfano katika modeli ya Mapinduzi ya kijani, kampuni za mbegu za kimataifa zimmetuma wanasayansi wake nchini Tanzania ili kuendeleza mbegu zilizoboreshwa. Wanachukua mbegu za asili zinazoendelea kuwapo licha ya mazingira magumu na kuziboresha kwa kuzichanganya na nyinginezo au kwa kuanzisha aina nyingine ya kufanikiwa. Kisha wanazisajiri kama aina mpya ya mbegu chini ya Sheria na kisha kuwa na haki pekee za kuuza mbegu hizo kwa miaka 25-30. Kama mkulima anataka kutumia mbegu hizo anatakiwa kuzinunua kutoka kwenye kampuni za mbegu. Kama mimea, hatakiwi kutunza mbegu zilizovunwa kwa namna yoyote ile zaidi ya matumizi yake. Hawezi kutoa au kubadilishana baadhi na jirani na hawezi kuuza kwa namna yoyote ile. Pia mazao ya mbegu

hizo zilizoboreshwa zinapoteza uasili wa wazazi wake na hivyo mbegu zinakuwa hazina maana. Kununua mbegu mwaka hadi mwaka Sasa wakulima wanalazimika kununua mbegu mwaka hadi mwaka kutoka kwa wauzaji wa zana za kilimo, ambao wanawahimiza kuongeza mbolea na dawa ambazo wanaziuza. Na hakuna utambuzi kwa jukumu la wakulima katika uendelezaji wa mbegu zilizopo. Hazina ya akiba ya mbegu katika sekta isiyo rasmi inatekelezwa na hivyo mbegu pekee zinazopatikana ni aghali kuzinunua. Fursa mbadala katika suala hili ni kwa wakulima kufanya kazi na wafanyakazi wa nchini na taasisi za kilimo za utafiti kufanya majaribio, kuchagua na kuzalisha zaidi mbegu bora na kuzisajiri na Tanzania Official Seed Certification Institute (TOSCI), na kisha kuwa na uwezo wa kubadilishana na kuuza mbegu kwa wakulima na vijiji vya jirani, ambao wanatambua mbegu hizi kuwa zina ubora wa hali ya juu, na watafanikiwa katika mazingira ya nchi yao. Bei zitakuwa chini, na wakulima wa nchini (wanaume na wanawake) watakuwa na udhibiti kwa mbegu zao na chakula, huku wakirutubisha bionuwai ambayo Tabnzania imekuwa ikifurahia (Tanzania ni nchi ya 11 kwa kuwa na bionuwai bora zaidi dunia). Haki ya kumiliki itabakia kuwa mali ya umma. NJia hii tayari inafanya kazi katika baadhi ya maeneo ya Tanzania, na hadi sasa imekuwa ikitiwa nguvu na serikali chini ya mfumo ujulikanao the Quality Declared Seed system. Kama mbegu hizo zitasajiriwa chini ya sheria mpya( PBR Bill) zoezi hili litafanikiwa. Mabingwa wa mbegu duniani Kwa mujibu wa kundi linalojiendesha bila ya faida- ETC Group, wazalishaji sita wakubwa wa zana za kilimo, ambao wanamiliki karibu asilimia 75 ya soko la dawa za wadudu na mimea duniani ndiyo mabingwa wanaoshikilia sekta ya mbegu. Monsanto, kampuni kubwa zaidi ya mbegu ni ya tano kwa uzalishaji wa zana za kilimo. Syngenta, kampuni ya pili kwa ukubwa ya zana za kilimo pia ni kampuni ya tatu kwa uzalishaji mbegu duniani. Bayer, kampuni kubwa ya uzalishaji wa zana za kilimo pia ni kampuni ya saba kwa uzalishaji wa mbegu. Na DuPont, kampuni kubwa ya pili dunia ya uzalishaji wa mbegu pia ni kampuni ya sita kwa uzalishaji wa zana za kilimo. Kampuni zinajishughulisha kusafirisha nje duniani

Utafiti unaoongozwa na sekta binafsi unaweza kutosheleza nmahitaji ya wakulima...

na yanaungwa mkono na serikali zao ambayo yanahitaji mapato kwa ajili ya kurekebisha nakisi zao. Faida nyingine ni wawekezaji wakubwa duniani ambao wanachangia katika kukabiliana na ongezeko la bei ya chakula, ongezeko la nyama (kulisha wanyama) kwa ongezeko la ghafla la daraja la kati la uchumi, na kuhamia kutoka kwa matumizi ya gesi ukaa na matumizi ya nishati ya mafuta ya mimea. Uwekezaji huo mkubwa wa mabilioni ya dola yamekuwa yakifadhili miradi mkubwa ya mashamba katika ardhi ambazo ni bei rahisi – na hawapati sehemu nyingine kwa bei rahisi kama Tanzania. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Kuhusu Haki ya Chakula, Olivier de Schutter, anatahadharisha “utaalamu wa kupandikiza mbegu na kutenganishwa katika kilimo unaongoza katika hatua za haraka za mfumo wa biashara wa mbegu, pamoja na mfumo wa mbegu wa wakulima kuitia kwa wakulima wa jadi unatunza, kubadilisha na kuuza mbegu katika mfumo usio rasmi” Faida za ukiritimba Kuhama huku unatoa fursa za muda kwa wapandaji wa mimea na haki miliki kuitia Haki miliki, kama njia za kuhimiza utafiti na upandikizaji wa mimea. Katika mchakato huu, hata hivyo wakulima maskini wataendelea kuwa tegemezi katika pembejeo za bei mbaya, kujihatarisha katika madeni makubwa na kujikuta katika mapato yasiyotengemaa. Utafiti unaoongozwa na sekta binafsi unaweza kutosheleza nmahitaji ya wakulima na katika nchi zilizoendelea na kuwapuuzia wale wakulima maskini waliopo katika nchi zilizoendelea. Mfumo wa mbegu kwa wakulima wanawezakujikuta katika changamoto licha ya kwamba wakulima wengi katika nchi zilizoendelea bado wanategemea katika mfumo huo licha ya kuwa wakulima wengi katika nchi zilizoendelea bado wanategemea katika mfumo huo ambao kwao ni chanzo cha uhuru wa uchumi na tegemeo kwa tishio kama la wadudu, magonjwa na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa ujumla, zana za kilimo zinaweza kutishiwa na kutiwa moyo masuala ya biashara ya aina mbalimbali. Wakulima, wakiwamo wakulima wanawake, wanahitaji haki halisi kutoka kwa watunga sera na wenye dhama ya maamuzi? Je kwa nini Tanzania imetia saini? Sasa ni muhimu kutambua kwa nini Tanzania imetia saini mkataba wa kimataifa (UPOV 1991) ambao unalinda haki za kampuni za kimataifa zinazojishushulisha na zana za kilimo na kudhoofisha haki za wakulima. Hivi karibuni, Tanzania ilijiunga na the International Union for the Protection of New Varieties of Plants (UPOV 1991). Sasa ni nchi ya pili Kusini ya jangwa la Sahara Afrika kufanya hivyo baada ya Afrika Kusini. Mawakala huru wamekuwa wakipiga kelele kutahadharisha kuhusu kujiunga na UPOV. Grain, kama taasisi ya kimataifa isiyozalisha faida inayofanya kazi ya kuunga mkono wakulima wadogo wadogo kati-

ka mapambano yao dhidi jamii zinazoathiriwa na mfumo usiozingatia bionuwai inasema kuwa: “UPOV inapuuzia haki za wakulima. Haki ya uhuru wao wa kutunza mbegu kutokana na mavuno yao. Katika maana pana ni kwamba, UPOV haitambui wala kuunga mkono haki za jamii kwa bionuwai na nafasi yao ya kutekeleza. “Kampuni za nchi za Kaskazini zitachukua mfumo wa taifa wa mbegu katika nchi za Kusini. Kampuni za taifa na kampuni za wazalishaji wengine wa mbegu zitanunuliwa na kampuni za nje. Kampuni za Kaskazini zitapata haki ya bionuwai ya Kusini bila ya kujali kugawana faida. “UPOV haitoi fursa kwa faida kushirikiana kutoka Kaskazini kwa baionuwai ya Kusini. Wakulima wa kusini watajikuta wakilipwa tu mirahaba kwa ajili ya mali zao ambazo zimechakachukuliwa na kupangwa upya na Kaskazini.” “ Kigezo cha UPOV kwa ulinzi kitachangia mmomonyoko wa baionuwai. Hii itachangia kushusha mavuno na kusababisha usalama mdogo wa chakula. Kujiunga na UPOV maana yake ni kwamba kushiriki katika mfumo ambao unaunga mkono haki za wenye viwanda wakubwa na kukandamiza wakulima. “UPOV imeundwa kufanikisha ukiritimba katika uzalishaji wa mbegu. Licha ya miaka 35 ya Mapinduzi ya Kijani na UPOV, ya Kusini pamoja hakuna usalama wa chakula. Kujiunga na mfumo kama UPOV utahakikisha kuwa Kaskazini inamiliki mfumo wa masoko yanayoongezeka lakini si kwa faida ya nchi ambazo zina njaa sasa.” Graham Dutfield, Profesa wa Utawala wa Bora Kimataifa katika chuo kikuu –‘Leeds University School of Law’, anasema , “wachambuzi wanachambua mfumo wa UPOV kwamba haufai kwa kilimo katika nchi zinazoendelea.” Lakini UPOV inafaa kuendeleza mfumo wa viwanda na kuunga mkono sekta ya mbegu ya kibiashara (ikiwamo kuendeleza kilimo kwa pembejeo za viwandani) dhidi ya wakulima wadogo na maarifa ya jadi. Mkazo katika sekta ya mbegu Wengi wanatilia mkazo katika sekta ya mbegu kwa karibu miongo miwili, wakisema kwamba mkazo huo ukiwamo Hakimiliki ya kulingana na ulinzi wa hakimiliki na ulinzi wa mbegu haiendi sambamba na haki za binadamu. Wachambuzi wanasema kuwa uboreshaji wa mavuno tangu UPOV ilipoanza kufanya kazi unatoa kipaumbele zaidi kwa maendeleo ya sayansi kuliko ulinzi wa hakimiliki na kwa hiyo hii inakwenda sambamba na kupotea kwa bionuwai. Mfumo wa UPOV hautambui mchango wa mkulima kwa miongo kwa ajili ya maendeleo ya mazao mapya, na kwamba maendeleo ya mazao na uboreshaji umetokea tangu kilimo kianze hata kabla ya kuwapo kwa hakimiliki. Dutfield ametahadharisha, “Inavyoonekana ni kuwa idadi ya nchi zinazoendelea zinajiunga na UPOV kwa sababu za kisiasa na msukumo wa kiuchumi, bila ya kufikiria kwa makini kama uanachama wa UPOV utachangia kwa muda mrefu katika

sera za nchi katika maeneo muhimu katika maeneo muhimu yakiwamo ya maendeleo ya uchumi, usalama wa chakula na bionuwai.” Rasimu ya Aripo ni jaribu jingine ya kuhusisha UPOV 91 katika nchi 14 za Afrika, ikiwamo Tanzania. Mfumo wa sheria hautoi fursa kwa maendeleo muhimu yanayofaa kwa kutekeleza mahitaji ya kikanda. Ni kiasi cha kulinda sekta binafsi kwa maslahi ya wakulima wadogo. Mfumo huu wa kisheria , kama ukitekelezwa utaifunga Tanzania kwa UPOV 91 na aina yoyote ye sheria ya nchi itafanyakazi kwa kuzingatia mazingira hayo. Kuhamia kwa kilimo-viwanda Kwa pamoja, mabadiliko ya sheria hizo tatu yanatoa fursa kwa njia ya kuhama kuelekea kwenye viwanda vya kilimo, na kufanya kampuni kubwa kutekeleza maslahi ya wadau wenye hisa, lakini wawajibika kidogo kwa mahitaji ya mamilioni ya wakulima wadogo ambao wanategemea mfumo wa mbegu kwa maisha yao. Kinachovutia ni kwamba, Umoja wa Afrika (AU) umetoa modeli ya sheria kwa masuala haya, ambayo yanatoa usalama kwa wakulima wadogo na kutambua nafasi yao muhimu katika kulinda bionuwai na maendeleo ya mbegu. Wanaoandaa rasimu mpya wamepuuzia ushauri wa AU na kuona kuwa wanazingatia sana suala la haki za wenye viwanda. Modeli ya AU inatilia mkazo hakimiliki dhidi ya maarifa ya jadi na kuzuia hakimiliki za maisha yote na mchakato wa kibiolojia. Pia unalinda haki za wakulima kutunza, kutumia, kubadilishana na kuuza mbegu zao. Mapendekezo ya fursa sawa Kwa hiyo, hapa kuna mapendekezo machache ya kusaidia kuweka uwanja sawa ikiwamo kutazama upya rasimu hiyo- Plant Breeders Rights Bill, na kuubadilisha na mwingine unazozingatia modeli ya AU-African Union Model Law – ambao unatoa uwiano sawa na umuhimu wa kulinda kampuni za mbegu ikiwamo mahitaji ya kulinda haki za wakulima. Kuchelewesha kujiunga na UPOV 1991 hadi sekta ya kilimo ya Tanzania inaendelezwa katika nafasi ambayo taifa litanufaika kutokana na UPOV na kuanza kusikiliza sauti za huru wanasayansi huru wa dunia, Umoja wa Mataifa na AU, wanaopinga kilimo kwa ajili ya kilimo cha viwanda na kuunga mkono ikolojia ya kilimo. Pia inapendekeza kupanua ukweli kwamba sheria hii inashinikizwa na kampuni za zana za kilimo za kimataifa na wawekezaji ambao wanataka kutumia fursa ya uwekezaji katika eneo ambalo kwa sasa linahitajika sana duniani. Kilimo cha Afrika. Mwisho kabisa ni kwamba , inajumuisha kundi la wakulima wa Tanzania kikamilifu katika maendeleo ya sheria kuhakikisha kuwa inatekeleza hasa mahitaji ya jamii ya wakulima,watu ambao wanalisha taifa. Tuma maoni yako bure ukianza na neno SEEDS kwenda namba 15774


Ijumaa Februari 22, 2013 A

SAFU

16

Tatizo la ufugaji wanyama na mabadiliko ya tabia nchi Kwetu Afrika

Na Nicolas

K

Begisen

UNA hatari nyingi zinazoyakabili maisha katika dunia hii. Wataalam wameainisha vitisho sita vikubwa zaidi katika zama zetu yaani mabadiliko ya tabia nchi, uhaba wa maji, uhaba wa chakula, bahari kuchemka, ukataji wa misitu na upotevu wa bionuwai. Ingawa vitisho hivi vinaweza kusababisha madhara. Uwapo wake unaweza kusababisha madhara makubwa kwa dunia hii na kupoteza maisha katika sayari. Leo hii, hebu tujadili kuhusu idadi. Hesabu inaweza sana kuvutia mara kwa mara, lakini si mara zote wao watakuachia tabasamu usoni na hii itakuwa moja ya nyakati hizo. Mabadiliko ya tabianchi ni suala linalojitokeza sana katika jitihada za

kukabiliana na hali hiyo na juhudi kubwa zimekuwa zikichukuliwa katika kukabiliana nayo. Je, unajua kwamba moja ya sababu ya msingi ya mabadiliko ya hali ya hewa ni ufugaji wa mifugo? Karibu asilimia 51 ya uzalishaji wa binadamu unaosababisha kuzalisha gesi chafu zinaelekezwa kwenye mifugo na mazao yake. Sekta ya ufugaji ni chanzo kikuu cha uzalishaji wa hewa ukaa na nitrojeni ambayo ni mara 300 zaidi kuliko hewa ukaa (kaboni dioksidi). Ufugaji wa mifugo pia ni sababu ya kuwapo mgogoro wa chakula. Karibu nusu ya nafaka inayozalishwa duniani hutumiwa kwa ajili ya malisho na kunenepesha mifugo. Hii ni kwa gharama ya watoto milioni 11 duniani kote katika nchi zinazozalisha nafaka hizi; ambao hufa kutokana na njaa kila mwaka.

Wanasayansi wanasema kuwa kupunguza mifugo kutasaidia kuwezesha nafaka hizo ziweze kutolewa kwa watu kukabiliana na ongezeko la idadi ya watu na hivyo kuondokana na mgogoro wa chakula. Kuna mambo mengi ambayo huchangia mgogoro huu wa chakula, ambao tayari ni wa kutisha katika nchi maskini na tishio kwa matajiri. Moja ya kashfa ya mfumo wetu wa chakula duniani ni kwamba karibu watu bilioni moja wanakabiliwa na njaa na utapiamlo. Wanyama karibu bilioni 67 kwa mwaka wanatumiwa kwa ajili ya maziwa ya unga, na mayai. Ufugaji ni kuwajibika kwa asilimia 18 kimataifa katika uzalishaji wa gesi chafu ambayo huchangia katika mabadiliko ya hali ya hewa ya hatari. Zaidi ya asilimia 30 ya nafaka kimataifa ikiwa ni pamoja na ngano na mahindi na asilimia 90 ya soya hutumiwa kulisha mifugo. Kuzalisha kilo moja ya nyama ya aina ya nyama, kilo kumi ya malisho ya wanyama ni kutumia kilo tano za nafaka kuzalisha kilo moja ya nyama ya nguruwe na kilo tatu ya nafaka kuzalisha kilo moja ya chakula cha kuku. Sasa, umri wa wastani wa ng'ombe aliyekua vizuri na kufikia uzito wa kilo 300, hii itahitaji kilo 3000 ya malisho ya wanyama kwa mazao hayo. Kama mkulima mwenye mifugo alikuwa na mifugo 100, alitumia kilo 300,000 za nafaka kulisha wanyama. Kisha jiulize tena jinsi watoto wengi na kwamba kama kiasi hicho wangepe-

wa watoto wakala kwa sababu baada ya ng'ombe kuchinjwa nyama inakuwa ghali kuinunua kwa ajili ya watu wengi na kujikuta haiwanufaishi watu maskini. Moja kwa moja nafaka zinaweza kulisha idadi ya watu wote wa dunia kwa urahisi. Ufumbuzi mwingine rahisi kusaidia kurekebisha hali hii ni kwa ajili ya wakazi kupunguza ulaji wa jumla wa nyama na maziwa, na kuchagua bidhaa za wanyama tu kutoka mifumo ya juu ya ustawi ambayo hulipwa zaidi kuhusu ulinzi wa mazingira na ustawi wa wanyama. Ripoti ya programu ya Umoja wa Mataifa ya Mazingira ya Juni 2010 na Tume ya Ulaya ilihitimisha kwamba punguzo kubwa la athari za mazingira inawezekana kwa mabadiliko makubwa duniani kote ya chakula na bidhaa za wanyama wote. Kila mtu lazima kutoa kipaumbele kwa sehemu yake katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la joto duniani. Kipaumbele isiwe tu kwa sifa ya kiuchumi au kisiasa wa mataifa kwa mtu binafsi au sisi kuweza kupoteza maisha yote juu ya sayari yetu; binadamu, wanyama, mimea, miti na mengineyo. "Kama wanadamu, sisi ni hatari kuwachanganya mno na kutokutabirika. Katika uzoefu wetu wa kila siku, kama kitu fulani hakijawahi kutokea kabla, sisi ni salama katika kuchukua hatua na haitaweza kutokea katika siku zijazo, lakini isipokuwa inaweza kukua wewe na mabadiliko ya tabia nchi, " anasema Al Gore.

KILIMO KWANZA DIRECTORY WATER AND SANITATION Dar es Salaam Water and Sewerage Authority (DAWASA) – Tel: +255 22 276 0006 Dar es Salaam Water and Sewarage Corporation (DAWASCO) Tel: +255 22-2131191/4 Drilling and Dam Construction Agency (DDCA) Tel: +255 22 2410430/2410299 Energy and Water Utilities Regulatory Authority Tel: +255 22 2123850, 22 2123853 Ministry of Water Tel: +255 22 245 1448 INDUSTRY SUPPORT AND ASSOCIATIONS Small Industries Development Organization (SIDO) – Email: dg@sido.go.tz, info@sido.go.tz Agricultural Non State Actors Forum, P.O Box 33562, Dar es Salaam, TEL: + 255 22 2771566 / 2775970 Agricultural Council of Tanzania Tel: 255 22 2124851 CNFA - info@cnfatanzania.org TCCIA Iringa Regional Chamber Tel: +255 26 2702486. Tractors Limited Cells: +255 784 421606, 786 150213 Export Processing Zones in Tanzania (EPZ) Tel: +255 22 2451827-9 Agricultural Economics Society of Tanzania (AGREST) – Tel. +255-23 260 3415 Tanzania National Business Council (TNBC) Tel: +255 22 2122984-6 Tanzania Agriculture Partnership (TAP) Tel: +255 22 2124851 Tanzania Milk Processors Association (TAMPA) Tel: +255 222 450 426 Rural Livelihood Development Company (RLDC) Tel: +255 26 2321455 Tanzania Cotton Board Tel: +255 22 2122564, 2128347 AGRO-PROCESSING TANEXA, Samora Avenue, N.I.C Investment House 6th Floor, Wing A, P. O BOX 1175 Dar es Salaam Tanzania info@tanexa.com, www.tanexa.com Tel:+255-732-924564 Fax: +255-22-2125432 ERTH Food - Tel: +255 22 2862040 Tanzania Organic Agriculture Movement PO Box 70089 DSM. Tel: 0732975739 ASAS Diaries Limited - Tel: +255 26 2725200 Tanga Fresh – Tel +255 27 2644238 NatureRipe Kilimanjaro Limited Tel: +255 22 21 51457 EQUIPMENT Gurudumu Tatu Limited Tel: +255 22 2865632 / 2863699 National Service Corporation Sole (SUMAJKT) Cell: +255 717 993 874, 715 787 887 FINANCE Private Agricultural Sector Support (PASS) Tel: 023-3752/3758/3765 Community Bank Association Tel: +255 22 2123245 AGRO-INPUTS Minjingu Mines & Fertilizers Ltd Tel: +255 27 253 9259 250 4679

Imefadhiliwa na

www.best-ac.org

www.ansaf.or.tz

Nipashe Kilimo Kwanza issue number 48  

Nipashe Kilimo Kwanza issue number 48 SEND YOUR COMMENTS FOR FREE TO 15774 BY STARTING WITH THE WORD “KILIMO” FOLLOWED BY YOUR COMMENTS

Read more
Read more
Similar to
Popular now
Just for you