Page 1

JINSI YA KUOMBA NA KUPOKEA KUTOKA KWA BWANA


HATUA YA I: HAKIKISHA UMEOKOKA: Biblia inasema: “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.” (Yakobo 1:17-18) Na tena: “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” (Yohana 14:6). Hivyo kama unataka kupokea chochote kilicho chema kutoka kwa Mungu Muumba wako, njia ni moja tu nayo ni kupitia Mwanae wa pekee Yesu Kristo. Huu ndio ukweli na daima utabaki kuwa ukweli pekee! Mpokee Yesu maishani mwako kama Bwana na Mwokozi. Amini moyoni mwako kuwa Yesu alikufa kwa ajili yako na ukiri kwa kinywa chako kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu ili wewe uhesabiwe haki (Warumi 10:9). HATUA YA II: TUBU DHAMBI ZAKO: Hii ni kwa ajili ya yeyote anayetaka kuomba na kupokea miujiza. Tubu kila dhambi. Kwa mambo makubwa kama mauaji, uzinzi, uasherati, shiriksiha watumishi wa Mungu ambao watakuombea kwa Mungu. Achana na dhambi hizo na amini kuwa Mungu amekusamehe. Zaburi 66:18, 1 Yohana 1:9, Isaya 43:25 HATUA YA III: SOMA MAANDIKO: Dai ahadi zilizoandikwa kwenye Biblia, ziamini na uzikariri ahadi hizo na uzifanye kuwa zako pasipo mashaka yeyote. Yeremia 32:27, 2 Tim 3:16-17, Isaya 55:10-11. HATUA YA V: OMBA KWA IMANI: Ingia kwenye maombi. Acha mashaka, ni lazima umwamini Mungu na kuyaamini maombi yako kila unapoomba. Waebrania 11:6, Yakobo 1:6-8.


HATUA YA VI: AMINI: Mungu amekwishajibu maombi yako na tegemea kupokea miujiza. HATUA YA VII: AMINI KWAMBA MUNGU ANAKUPENDA: Amini kuwa Mungu anakupenda wewe na kwamba yuko nawe kila uendako. Yohana 3:16, Heb. 7:25. HATUA YA VIII: JIZOESHE MAOMBI YA MFUNGO: Jifunze kufanya maombi ya mfungo hususan kwa mambo makaidi au sugu. Mathayo 17:21. HATUA YA IX: SHUHUDIA MUUJIZA WAKO: Shuhudia kuwa Mungu amekujibu hata kama mazingira yanaonyesha kinyume. Mathayo 21:21-22, Marko 11:24. HATUA YA X: TII NENO LA MUNGU: Ishi maisha matakatifu, jifunze kutoa fungu la kumi, jifunze kumjaribu Mungu kupitia nadhiri na kumtolea mbegu- kwa imani. Epuka kutenda dhambi. Jifunze kuwashuhudia wengine Neno la Mungu. Jifunze kumtolea Mungu na kuwasaidia wengine pia. HATUA YA XI: DUMU KATIKA MAOMBI: Usiaache kuomba hadi pale unapopata majibu. Mshukuru Mungu na ukiri matokeo mema siku zote. Zaburi 125.


MAOMBI YALETAYO MIUJIZA 1. MAOMBI DHIDI YA UCHAWI NA MASHAMBULIZI YA KICHAWI Maandiko: Isaya 54:14-17, Zaburi 91. VIPENGELE VYA MAOMBI I. Moto wa Roho Mtakatifu (Rudia mara 7); Damu ya Yesu (Mara 7) II. Baba katika jina la Yesu, ninakuja kwako nikisihi damu ya Yesu itakase nafsi yangu, roho na mwili pia. III. Imeandikwa katika Isaya 54:17 kuwa: “Kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa.” Na ninatamka sasa kuwa kila silaha ya kichawi iliyo kinyume nami haitafanikiwa katika jina la Yesu IV. Popote pale ambapo jina langu, pesa zangu ama mali zangu zimechukuliwa katika ulimwengu wa roho, ninazidhoofisha nguvu hizo katika jina la Yesu (Rudia mara 2) V. Imeandikwa katika Mithali 18:10 kuwa: “Jina la Bwana ni ngome imara. Mwenye haki hukimbilia na kuwa salama.” Ninadai usalama wangu sasa dhidi ya kila nguvu ya adui katika jina la Yesu VI. Ninawafunga wachawi wote wanaoshambulia maisha yangu katika jina la Yesu VII. Ninawatosa adui zangu wote kwenye moto wa Roho Mtakatifu. Wakakose amani hadi pale watakapotubu. VIII. Kila mshale uliorushwa kwangu, ninauzuia kwa kutumia ngao ya Roho Mtakatifu na ninaamuru uwarudie walioutuma, katika jina la Yesu (Rudia mara 3) IX. Ninanyunyizia damu ya Yesu juu ya kioo watakachotumia


kutaka kuiiba taswira yangu na ninaamuru radi kutoka mbinguni ikivunjevunje, katika jina la Yesu (Rudia mara 2) X. Kupitia damu ya Yesu, ninafuta athari zote zitokanazo na vitu vyote vya kipepo watakavyonitupia ili nivikanyage, katika jina la Yesu XI. Hata kama wataniwekea sumu kwenye chakula changu ama kinywaji, ninaibatilisha sumu hiyo kwa kutumia damu ya Yesu (Rudia mara 2) XII. Ninaizamisha nafsi yangu, mwili na roho katika damu ya Yesu (Rudia mara 3) XIII. Ninaharibu kila nguvu ya kichawi iliyoko dhidi ya maisha yangu katika jina la Yesu (Rudia mara 3) XIV. Popote na kwa yeyote yule ambaye anatumiwa na Shetani, awe ni baba yangu, mama, dada, kaka, shemeji au wifi, ninawatamkia kutofanikiwa katika njia zao, katika jina la Yesu XV. Ninaifunika familia yangu, biashara na mali zangu zote kwa damu ya Yesu (Rudia mara 3) XVI. Baba, achilia malaika wako wanilinde mimi na vyote nilivyonavyo, katika jina la Yesu. ANGALIZO: Kama mashambulizi yatang’ang’ania, funga kuanzia saa 12 alfajiri hadi 12 jioni kwa siku tatu mfululizo huku ukiomba kila siku.


2. MAOMBI WAKATI WA SAFARI Maandiko: Zaburi 121, 2 Korint 10:4-6 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Katika jina la Yesu (mara 3), Damu ya Yesu (mara 3) II. Baba wa milele, mfalme wa wafalme, ninakuabudu na kukusujudia III. Bwana, ninaikabidhi safari yangu mikononi mwako. Chochote kile kilicho mikononi mwako kiko salama. IV. Ninaharibu nguvu za mapepo wanyonya damu walioko barabarani, katika jina la Yesu V. Ninawafunga na kuwatupia mbali na njia yangu mapepo wote wasababishao ajali, katika jina la Yesu (mara 3) VI. Ninanyunyiza damu ya Yesu juu ya njia nitakayopita (rudia mara 3) VII. Kwa wachawi wote watakaosimama kwenye njia yangu kutaka kuharibu maisha yangu, ninawafunga na kuamuru moto wa Roho Mtakatifu uwateketeze, katika jina la Yesu (rudia mara 2) VIII. Ninazamisha mwili wangu, nafsi na roho kwenye damu ya Yesu (mara 3) IX. Ninazamisha kila gari nitakalotumia niwapo safarini, dereva na abiria wote kwenye damu ya Yesu (mara 3) X. Ninawanyang’anya nguvu mawakala wote wa Shetani ambao watakuwa kwenye gari pamoja na mimi, katika jina la Yesu. (Rudia mara 3) XI. Ninabatilisha kila nuio la kipepo, katika jina la Yesu. (Rudia mara 3) XII. Asante Bwana kwa ajili ya rehema za safari na majibu kwa maombi yangu, katika jina la Yesu, amina


3. ULINZI KWA FAMILIA / WATOTO ANGALIZO: Watoto wengi hupagawa au kuingizwa kwenye ulimwengu wa kipepo wakiwa bado wadogo nyumbani au shuleni. Hivyo wanahitaji ulinzi wa Kiungu. Maandiko: Mithali 22:6, Kumb 6:19-21, Isaya 59:21, Isaya 1:18, Mithali 19:26, Ayubu 1:1-5 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Damu ya Yesu (mara 7) II. Baba wa rehema, ninamleta mwanangu/ninawaleta wanangu (taja majina) sawasawa na ilivyoandikwa kwenye Zaburi 127:3 kuwa: “Wana ndio urithi wa BWANA, uzao wa tumbo ni thawabu� III. Kila kilicho chema hutoka kwako na ndivyo ilivyo kwa watoto hawa ninawarudisha mikononi mwako, katika jina la Yesu IV. Ninapangua na kuharibu mipango yote ya Shetani ya kutaka kuwashambuliwa (taja majina) kwa maradhi/magonjwa na namna zinginezo, katika jina la Yesu (Mara 2) V. Ninamzamisha mwanangu (taja jina) kwenye damu ya Yesu (mara 3) VI. Ninazamisha mwili wake , nafsi na roho kwenye damu ya Yesu (Mara 3) VII. Ninabatilisha kila mpango wa Shetani kutaka kummiliki au kumfunda mwanangu (taja jina) kupitia wanafunzi wenzake, marafiki, ndugu, wapangaji wenzake n.k., katika jina la Yesu (Mara 3) VIII. Ninafunika kila chakula atakachokula ama kinywaji atakachokunywa kwa dmau ya Yesu (Mara 3)


IX. Ninaikabidhi hatma yake kwako. Yote uliyomwazia yatimie maishani mwake, katika jina la Yesu X. Fungua ufahamu wake, mpe kumbukumbu dhahiri iliyotulia na neema ya kufanikiwa katika yote atakayodhamiria kufanya, katika jina la Yesu XI. Baba panda upendo na hofu yako ndani yake. Mvute kwako, katika jina la Yesu XII. Ninamsalimisha kwako, mmiliki kama chombo chako, katika jina la Yesu (Mara 2) XIII. Bwana, pokea sifa na shukrani kwa maana umekwishanijibu katika jina la Yesu, amina.


4. KUFUNGUA MILANGO ILIYOFUNGWA Maandiko: Ufunuo 3:8, 2Kor 2:12, Malaki 3:10-12, Malaki 1:10 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Katika jina la Yesu (mara 3) II. Mwamba wangu wa kale, ninakuabudu. Uinuliwe katika jina la Yesu (mara 2) III. Milango yote iliyofungwa ninaimuru ifunguke, katika jina la Yesu (mara 2) IV. Ninaamuru radi toka juu ibomoe kila ufunguo uliotumika kuyafunga mafanikio yangu, katika jina la Yesu (mara 3) V. Ninaufungua mwili wangu, nafsi na roho kutoka katika kila kifungo cha Shetani, katika jina la Yesu (mara 3) VI. Ninaamuru udhihirisho wa baraka kutoka Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini, katika jina la Yesu (mara 3) VII. Milango yote inayoingiza uchafu ninaiamuru ifungike, katika jina la Yesu (mara 3) VIII. Ninaizamisha biashara yangu, mali na familia yangu kwenye damu ya Yesu IX. Utukuzwe Bwana kwa kuwa umeyajibu maombi yangu, katika jina la Yesu, Amina.


5. KUVUNJA MIKOSI NA KUKATISHWA TAMAA Maandiko: Zaburi 1:1-3, Kumb 28:6, Zaburi 5:12 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Moto wa Roho Mtakatifu (x7), damu ya Yesu (x3) II. Yehova El-Shadai, ninajikabidhi kwako, katika jina la Yesu III. Ninafunga kila roho isababishayo mikosi na kukatishwa tamaa, kwangu, familia yangu na biashara yangu, katika jina la Yesu. IV. Baba, ninaomba upendeleo wa Kiungu uyafunike maisha na biashara yangu, katika jina la Yesu V. Ninavunja nguvu ya mikosi na kukatishwa tamaa maishani mwangu katika jina la Yesu (x3) VI. Hivyo ninatamka upendeleo wa Kiungu na nguvu ya mafanikio isiyo ya kawaida maishani mwangu na kuamuru kukatishwa tamaa kugeuzwe kuwa mafanikio, katika jina la Yesu VII. Asante Baba kwa kuwa umetenda, katika jina la Yesu, Amina.


6. USHINDI WAKATI WA MITIHANI Maandiko: Kumb 28:12, Yak 1:5, Dan 1:17-20. VIPENGELE VYA MAOMBI I. Katika jina la Yesu (x3) II. Mungu mwenyezi uishie milele, mpaji wa maarifa na hekima, ninakubariki na kukuheshimu III. Bwana, ninaleta mbele yako mtihani, usaili ulioko mbele yangu. Ninakuomba unipe neema ya kujiandaa na kufaulu katika jina la Yesu IV. Nipe hekima na ufahamu wa kuelewa ni nini nijifunze, katika jina la Yesu V. Bwana, nipe kumbukumbu iliyotulia, katika jina la Yesu VI. Wewe ndiwe Mungu wa Danieli. Bwana, nipe ufahamu na hekima kama ile ya Danieli katika mtihani huu, katika jina la Yesu VII. Ninakuja kinyume na kila ujanja wa mwovu kutaka kunizuia nisifanye vema, katika jina la Yesu VIII. Kila udhaifu, uzembe katika kujiandaa kwangu, ninakuja kinyume nao katika jina la Yesu IX. Ninakataa maradhi au chochote kile kitakachonizuia nisiwe na afya kamili wakati wa mtihani/ usaili, katika jina la Yesu (x2) X. Bwana, acha mapenzi yako yatendeke, katika jina la Yesu (mara x3) XI. Ninawaleta wasimamizi/ wasaili mkononi mwako. Ninatamka kwamba watatumika upande wangu, katika jina la Yesu. XII. Ninadai mafanikio kwenye mtihani, usaili huu, katika jina la Yesu. XIII. Asante Bwana kwa mafanikio mazuri, katika jina la Yesu ninaomba, Amina.


7. UNAPOSIKIA SAUTI NGENI MASIKIONI MWAKO Maandiko: 1 Samweli 3:1-5 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Moto wa Roho Mtakatifu (x7), Damu ya Yesu (x3), katika jina la Yesu (x3) II. Baba, ninashukuru kwa kuwa wewe unatawala mbinguni na duniani. Uinuliwe katika jina la Yesu III. Kila pepo linaloingiza sauti masikioni mwangu, ninakufunga katika jina la Yesu (x3) IV. Haijalishi unatumia sauti ya ndugu aliyekufa, rafiki, mke/mme kaka au dada, ninakufunga na kukutupia mbali ya upeo wa macho yangu, katika jina la Yesu V. (Weka mikono masikioni mwako) Ninayafunika masikio haya kwa damu ya Yesu. Ninawaamuru ninyi masikio, msisikilize tena sauti zitakazo kwa yule mwovu na badal yake msikilize sauti kutoka kwa Mungu, katika jina la Yesu VI. Ninazamisha mwili wangu wote kwenye damu ya Yesu VII. Ninafunga kila pepo liliekezwa kuja kunichanganya, toka mbele yangu katika jina la Yesu VIII. Ninafunika biashara yangu, mali zangu na nyumba kwa damu ya Yesu. IX. Asante Bwana kwa kuwa umetenda, katika jina la Yesu, Amina


8. UNAPOONA VIUMBE VISIVYO VYA KAWAIDA Maandiko: Isaya 54:14-17, 1 Yohana 5:4 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Moto wa Roho Mtakatifu (x7), damu ya Yesu (x7), katika jina la Yesu (x3) II. Baba wa mbinguni, ninakushukuru kwa kuwa ulisema katika Zaburi 50:15 kuwa nikikuita siku ya mateso utanikionoa na wewe utanitukuza III. Baba, ninakuita leo uje unikomboe nisiwaone watu hawa wageni tena, katika jina la Yesu IV. Kila pepo lililojivisha sura ya ndugu yangu aliyekufa, rafiki, dada, mke/ mme (taja kile kinachohusika), ninakufunga na kukutupa mbali na upeo wa machu yangu, katika jina la Yesu (x3) V. Haijalishi ni jina gani unajiita, ninakukataa katika jina la Yesu VI. Ninakufunga ewe pepo ambaye hujinia mchana na usiku ninakukataa na kukutupilia mbali na upeo wa macho yangu katika jina la Yesu (x3) VII. Asante Yesu kwa kunikomboa, katika jina la Yesu. Amina ANGALIZO: Kama mashambulizi yatang’ang’ania funga kuanzia alfajiri saa 12 hadi 12 jioni kwa siku tatu mfululizo na kuomba kila siku.


9. MAOMBI YA KUFUNGUA TUMBO LILILOFUNGWA Maandiko: Zaburi 113:9, 127:3 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Damu ya Yesu (x7) katika jina la Yesu (x3) II. Mungu Mwenyezi, muumba wa mbingu na nchi, utukuzwe katika jina la Yesu III. Bwana uliniumba nikiwa mkamilifu. Ninakataa kila shambulizi la Shetani katika maisha yangu na ninapokea ukamilifu katika jina la Yesu IV. Baba, ulisema katika Mwanzo 1:28: “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambua, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiiisha.� Ahadi hii ni yangu pia. Ninaidai katika jina la Yesu V. Ninazifunga mamlaka zote zinazonizuia nisiwapate watoto wangu, katika jina la Yesu (x2) VI. Ninakufunga na kukuamuru utoke katika maisha yangu na mwenzi wangu, katika jina la Yesu (x3) VII. Ninawafungua watoto wangu kalika ulimwengu wa roho (x3) katika jina la Yesu VIII. Kila agano la kipepo ambalo nimeingia kwa kujua au kutokujua, ninabatilisha siku hii ya leo katika jina la Yesu (x3) IX. Ninajizamisha mimi na mwenzi wangu katika damu ya Yesu X. Ninazamisha vyumba vyangu, kitanda na vyote nilivyonavyo kwenye damu ya Yesu XI. Ninamuru moto wa Roho Mtakatifu ushuke juu ya kila mchawi ambaye amekuwa chanzo cha utasa wangu, katika jina la Yesu XII. Ninajifungua mimi na mwenzi wangu kutoka katika kila kifungo cha Shetani, katika jina la Yesu (x3)


XIII. Asante Bwana kwa kuwa umefanya, katika jina la Yesu, Amina. ANGALIZO: Kama hakuna mabadiliko yeyote ndani ya miezi 3, funga kuanzia saa 12 alfajiri hadi 12 jioni kwa siku saba mfululizo huku ukiomba kila siku.


10. MAOMBI KABLA YA KUFUNGA NDOA Maandiko: Mithali 18:22, Zaburi 37:5 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Moto wa Roho Mtakatifu (x3), katika jina la Yesu (x3) II. Mungu uishiye mahali pa juu na Baba wa milele, ninakusifu na kukuabudu. III. Imeandikwa kuwa “Apataye mke (mume) apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.� Hivyo basi, ninadai upendeleo katika yote ninayofanya, katika jina la Yesu IV. Bwana ninakuomba utufanyie njia mimi na mwenzi wangu. Tupatie fedha na usaidizi wa kutosha wenye kuleta mafanikio katika harusi yetu, katika jina la Yesu (x3) V. Ninamzamisha mke (Mume) wangu mtarajiwa kwenye damu ya Yesu VI. Ninampiga upofu Shetani na maajenti wake ili wasimwone, katika jina la Yesu (x3) VII. Tukinge na ajali katika njia zote tutakazoziendea, katika jina la Yesu VIII. Bwana, tujalie upendeleo wa Kiungu kwa kila tutakayemwendea, katika jina la Yesu IX. Ninakuja kinyume na falme na mamlaka zote zilizo kinyume na harusi yetu, katika jina la Yesu X. Ninavuruga kila mpango wa yule mwovu ulioandaliwa kuharibu ndoa yetu, katika jina la Yesu XI. Ninafunga kila pepo lililoandalowa kupinga ndoa yetu, katika jina la Yesu XII. Baba, ifanye harusi yetu kuwa yenye mafanikio, pokea utukufu katika jina la Yesu


11. UGONJWA USIOJULIKANA Maandiko: Kumb. 1:7-15, 3 Yohana 2, Isaya 10:27 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Damu ya Yesu (x7), Katika jina la Yesu (x7), Moto wa Roho Mtakatifu (x3) II. Yehova Rafa, ninakubariki katika jina la Yesu III. (Weka mikono juu ya sehemu husika) Kila kichopandikizwa na mwovu au wakala wake, ninaamuru kwa mamlaka ya jina la Yesu kiteketezwe na moto wa Roho Mtakatifu IV. Kila mbegu ya ugonjwa mwilini mwangu, ninaamuru ife katika jina la Yesu V. Chochote kinachotembea mwilini mwangu, ninakiamuru kiondoke katika jina la Yesu VI. Ewe pepo uliyetumwa kwangu, ninakuong’oa na kukuteketeza kwa moto wa Roho Mtakatifu, katika jina la Yesu VII. Sikia ewe ugonjwa usiyejulikana imeandikwa kuwa “Kwa kupigwa kwake mimi nimepona” Hivyo badi, ninakuamuru uachilie mwili wangu (toka katika jina la Yesu (x3) VIII. Asante Bwana kwa kuwa umeniponya, katika jina la Yesu, Amina. ANGALIZO: Kama ugonjwa utang’ang’ania funga kwa siku 3 mfululizo huku ukiendelea kuomba maombi haya.


12. MAOMBI WAKATI WA UJAUZITO Maandiko: Zaburi 127:3, Mwanzo 1:28 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Damu ya Yesu (x3) katika jina la Yesu (x3) II. Baba wa mbinguni, Muumba wa mbingu na nchi, ninakuabudu Bwana, ninayakabidhi kwako maisha yangu na ya mtoto aliyeko tumboni mwangu ili uyatawale, katika jina la Yesu III. Maendeleo yote ya mtoto huyu ninaayaacha mikononi mwako IV. Bwana tupatie fedha mimi na mume wangu ili tuweze kumlea na kumtunza mtoto huyu, katika jina la Yesu V. Ninaagiza moto wa Roho Mtakatifu uteketeze kila mkono mbaya utakaogusa tumbo hili kwa lengo la kuharibu ujauzito huu, katika jina la Yesu (x3) VI. Ninalipiga upofu kila jicho lenye hila dhidi ya mtoto wangu, katika jina la Yesu (x2) VII. Ninabatilisha kila shambulizi la kipepo dhidi ya mtoto wangu, katika jina la Yesu VIII. Popote pale ambapo kuna wachawi wanapanga kumchukua mwanangu, ninafutilia mbali jitihada zao hizo na kuamuru moto wa Roho Mtakatifu uwateketeze hadi pale watakapomwachia mwanangu, katika jina la Yesu IX. Ninaharibu kila hila za Shetani na mawakala wake huko hospitalini, nyumbani au popote pale, ambazo zimeandaliwa kunizuia nisijifungue salama, katika jina la Yesu (x3) X. Ninajizamisha damuni mwa Yesu mimi na mwanangu, katika jina la Yesu (x3) XI. Ninatamka na kudai usalama wa maisha yangu na mwanangu aliyeko tumboni katika jina la Yesu (x3)


XII. Ninaifunika kwa damu ya Yesu nyumba yangu pamoja na hospitali nitakayokwenda kujifungua (itaje jina) XIII. Ninatamka kuwa manesi na madaktari wa hospitali hii (itaje jina) watafanyika vyombo vya Mungu vitakavyonisaidia nijifungue salama katika jina la Yesu XIV. Asante Bwana kwa kuyajibu maombi yangu, katika jina la Yesu, Amina.


12. KUVUNJA LAANZA ZINAZOKUANDAMA KWENYE MAISHA YAKO Maandiko: Isaya 10:27, Mwanzo 27:40, Galatia 3:31 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Katika jina la Yesu (x3) Damu ya Yesu (x3) II. Yehova Elohim, ninaliheshimu na kuribariki jina lako III. Bwana, uliniumba ili nifanikiwe na kustawi, hivyo basi chochote kile kinachonizuia, ninakikataa katika jina la Yesu IV. Ninazivunja laana zote au ukoo na za mababu, katika jina la Yesu (x3) V. Ninatumia damu ya Yesu kufuta maagano yote yaliyofanywa na wazazi wangu kwa niaba yangu, katika jina la Yesu (x2) VI. Ninabatilisha kila agano nililofanya kwa kujua au kutojua, katika jina la Yesu (x2) VII. Imeandikwa katika 2Kor 5:17 kuwa “Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya.� Hivyo ninabatlisha kila ambukizo la laana lililosababishwa na dhambi za zamani kwenye maisha yangu katika jina la Yesu VIII. Ninazamisha damuni mwa Yesu, nafsi, roho na mwili wangu (x2) IX. Asante Bwana kwa kuwa umeyajibu maombi haya, katika jina la Yesu, amina


14. MAOMBI KWA AJILI YA KUPATA MWENZI (MKE/MME) Maandiko: Mithali 8:22, Mithali 10:24, Zaburi 37:5 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Katika jina la Yesu II. Baba wa mbinguni, ninatambua rehema na uaminifu wako maishani mwangu, utukuzwe katika jina la Yesu III. Imeandikwa katika Yeremia 29:11 kuwa “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA ni mawazo ya amani wala si ya mabaya kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” Hivyo basi ninaomba mapenzi yako yatimizwe maishani mwangu, katika jina la Yesu IV. Bwana, ninakuomba uniongoze/uniwezeshe kukutana na atakayekuwa mwenzi wangu, katika jina la Yesu (Mwambie Mungu yale jinsi unavyotamani mwenzi wako awe) Baba nakusihi uyatende haya katika jina la Yesu V. Imeandikwa katika Mithali 10:24b kuwa “Na wenye haki watapewa matakwa yao” katika jina la Yesu (x2) VI. Bwana, ninajitoa kwako ili mapenzi yako yatimie. Niwezeshe kukusikia na kukutii, katika jina la Yesu. VII. Ninawakataa wote ambao ni mawakala wa Shetani, katika jina la Yesu (x3) VIII. Ninakataa kila mpango ulioandaliwa na mwovu na mawakala wake ili kunipa mwenzi asiyestahili, katika jina la Yesu IX. Ninakuja kinyume na roho ya tamaa ya mwili maishani mwangu, katika jina la Yesu X. Imeandikwa katika Mithali 18:22 kuwa “Apataye mke (mume) apata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa BWANA” Hivyo ninaomba unipatie mwenzi sawasawa na mapenzi yako, katika jina la Yesu XI. Asante Bwana kwa kuwa umeyasikia na kuyajibu maombi yangu, katika jina la Yesu, Amina


15. KUHARIBU TABIA ZINAZOWEZA KUKUFANYA UTENDE DHAMBI Maandiko: Warumi 6, Isaya 10:27, Mwanzo 27:40 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Damu ya Yesu (x7), Moto wa Roho Mtakatifu, katika jina la Yesu II. Mungu Mtakatifu uishiye milele, ninakuabudu kwa kuwa uliniumba kwa sura na mfano wako, ushukuriwe milele katika jina la Yesu III. Shetani, nimekukataa wewe na vyote vilivyo vyako, toka katika maisha yangu, katika jina la Yesu IV. Ninakataa na kuja kinyume na kila tabia isababishayo dhambi maishani mwangu (taja tabia hizo) toka maishani mwangu katika jina la Yesu V. Imeandikwa kuwa “Wote waliompokea aliwapa uwez wa kufanyika kuwa watoto wa Mungu� Hivyo ninapokea uwezo wa kufanyika mwana wa Mungu na kuishi maisha ya ushindi juu ya dhambi, katika jina la Yesu (x3) VI. Ninafunga na kutupilia mbali kila pepo lililoelekezwa kuja kunifunga na vifungo vya dhambi, katika jina la Yesu (x3) VII. Ewe mamlaka uliyeagizwa kuniangamiza dhambini, ninakufunga leo na kukutupilia mbali na upeo wa macho yangu, katika jina la Yesu VIII. Ninakuja kinyume na roho ya tamaa za mwili (kwa ajili ya pesa au ngono au mali) maishani mwangu, toka katika jina la Yesu (x3) IX. Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu uteketeze kila tabia isababishayo dhambi maishani mwangu, katika jina la Yesu X. Asante Bwana kwakunipa ushindi dhidi ya tabia zisababishazo dhambi, katika jina la Yesu ninaomba, amina.


16. MAOMBI DHIDI YA KIFO CHA KABLA YA WAKATI Maandiko: Zaburi 23, Zaburi 91:14-16 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Katika jina la Yesu (x3) Damu ya Yesu (x3) II. Baba Mungu, ninakuja kwako katika jina la Yesu III. Imeandikwa katika Zaburi 91:16 kuwa “Kwa siku nyingi utanishibisha, nawe utanionyesha wokovu wako� Hivyo ninaidai ahadi hii iwe yangu katika jina la Yesu (x3) IV. Ninakuja kinyume na kila mchawi au wakala yeyote wa Shetani aliyetumwa kuyaharibu maisha yangu, katika jina la Yesu (x2) V. Ewe pepo la mauti unayeninyemelea, ninakuamuru utoke maishani mwangu, katika jina la Yesu (x3) VI. Ninajizamisha damuni mwa Yesu, mimi, familia yangu na ndugu zangu (x2) VII. Bwana, ninaomba uruhusu malaika zako wanilinde na mawakala wa yule mwovu, katika jina la Yesu VIII. Ninazamisha damuni mwa Yesu kila chakula nitakachokula (x3) IX. Ninamzamisha damuni mwa Yesu kila nitakayeshikana naye mkono, nikibatilisha kila shambulizi la kipepo, katika jina la Yesu (x2) X. Ninazamisha miguu yangu damuni mwa Yesu (x2) XI. Ninaizamisha damuni mwa Yesu kila sehemu nitakayoikanyaga, nikibatilisha kila shambulizi la kishetani, katika jina la Yesu (x2) XII. Ninafunika kila njia nitakayoiendea kwa damu ya Yesu


XIII. Ninatamka damuni mwa Yesu kila gari nitakalopanda (x2) XIV. Ninatamka kwamba hakuna baya litakakonifika, katika jina la Yesu XV. Ninadai maisha marefu sawasawa na Neno la Mungu, katika jina la Yesu (x2) XVI. Asante Bwana kwa kunipa maisha marefu na ushindi dhidi ya mipango yote ya yule mwovu, katika jina la Yesu, Amina.


17. UNAPOPATA MASHAMBULIZI NDOTONI/ UNAPOKOSA USINGIZI Maandiko: Kumb 28:25, Mithali 3:24, Zaburi 127:2 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Damu ya Yeu (x3) II. Yehova El- Shadai, ninalibariki jina lako kwa kuwa ni mapenzi yako nipate usingizi mtulivu, pokea sifa na shukrani, katika jina la Yesu III. Ninasimama kinyume na mipango yote ya yule mwovu inayotumika kunishambulia ndotoni ili kuyaharibu maisha yangu katika jina la Yesu IV. Ninapinga kila nguvu za giza zinishambuliazo wakati wa usiku, nikiziteketeza kwa moto wa Roho Mtakatifu, katika jina la yesu V. Ninamfunga kila mchawi ainukaye dhidi ya maisha yangu, ninamvua nguvu zake katika jina la Yesu VI. Ewe pepo unijiaye kwenye ndoto nikiwa nimelala, ninakufunga na kukutupilia mbali ya upepo wa macho yangu, katika jina la Yesu VII. Ninaifunika nyumba hii kwa damu ya Yesu VIII. Ninajifunika mimi na familia yangu kwa damu ya Yesu IX. Ninaizingira nyumba nzima kwa moto wa Roho Mtakatifu, katika jina la Yesu X. Ninatangaza usingizi uliojaa utulivu na amani siku zote za maisha yangu, katika jina la Yesu XI. Asante Bwana kwa kunijubu, katika jina la Yesu, Amina ANGALIZO: Kama mashambulizi yatang’ang’ania, funga kuanzia saa 12 alfajiri hadi 12 jioni huku ukiendelea kuomba maombi haya.


18. KUFANYA NGONO AU KULA CHAKULA UKIWA NDOTONI ANGALIZO: Hali hii inaashiria uchafu, inaweza kusababisha utasa kwa walioolewa na pia kuzuia kuolewa kwa wale ambao bado kuolewa. Unaweza kuingiwa na mapepo kupitia hali hii ya kula ukiwa ndotoni. VIPENGELE VYA MAOMBI I. Damu ya Yesu (x3) Moto wa Roho Mtakatifu (x3) II. Baba, ninakujia katika jina la Yesu. Ninajitoa kwako, mwili, nafsi na roho yangu naviweka vyote mikononi mwako. Tawala vyote katika jina la Yesu III. Ninakataa na kupinga kila pepo liniliajo kama mke/mume na kufanya mapenzi na mimi kwenye ndoto, katika jina la Yesu (x3) IV. Ninakataa na kupinga kila roho zinijiazo kama watoto, ninaagiza moto wa Roho Mtakatifi uwateketeze wote, katika jina la Yesu (x2) V. Ninazamisha damuni mwa Yesu mwili wangu, nafsi na roho yangu. VI. Kila sumu niliyokula nikiwa ndotoni, ninabatilisha utendaji wake kwa damu ya Yesu VII. Ninaamuru tabii hii ya kula nikiwa ndotoni ikome na isirudi tena, katika jina la Yesu VIII. Ninatangaza kuwekwa huru kuansia sasa, katika jina la Yesu IX. Asante Bwana kuwa kuwa umefanya, katika jina la Yesu ANGALIZO: Hali ikiendelea kuwepo, funga siku 2 mfululizo, kuanzia saa 12 alfajiri hadi 12 jioni, huku ukiendelea kuomba maombi haya.


19. UNAPOOTA UNAONA DAMU AU JENEZA VIPENGELE VYA MAOMBI I. Damu ya Yesu (X7) II. Baba wa milele, ninakuja kinyume na nguvu zote za giza zisababishazo uharibifu wa mimba zangu, katika jina la Yesu III. Ninatangaza kufuta mipango yote ya mwovu aliyokuwa ameipanga kusababisha ajali au kifo, kwangu na familia yangu, katika jina la Yesu IV. Ewe pepo wa mauti, ninakufunga na kukutupa mbali na maisha yangu, katika jina la Yesu V. Ninampiga upofu shetani na mawakala wake wote walio kinyume nami katika jina la Yesu VI. Ninajizamisha damuni mwa Yesu (mwili, nafsi na roho) x2 VII. (Kwa wanawake wajawazito) Ewe pepo usababishaye uharibifu wa mimba, ninakuamuru utoke maishani mwangu na familia yangu katika jina la Yesu (X3) VIII. Ninaangusha kila ngome ya adui iliyoko dhidi ya maisha yangu na familia yangu, katika jina la Yesu IX. Asante Bwana kunipa ushindi dhidi ya nguvu za giza, katika jina la Yesu, Amina ANGALIZO: Kama hali itaendelea, fanya maombi yakufunga kwa siku 3 mfululizo.


20. MAOMBI DHIDI YA NDOTO MBAYA VIPENGELE VYA MAOMBI I. Damu ya Yesu (x3) II. Mungu mwenyezi, ninakubariki kwa kuwa ni mapenzi yako mimi niote ndoto njema, uinuliwe katika jina la Yesu III. Ninakuja kinyume na kila ndoto mbaya katika maisha yangu, katika jina la Yesu IV. Ninatangaza kuwa hakuna ndoto yeyote mbaya itakayonijia tena, katika jina la Yesu V. Sikiliza shetani, imeandikwa kuwa “Ni mapenzi ya Mungu nistawi na kuwa na afya njema� Hivyo ninakataa kila ndoto iashiriayo kutostawi na kuwa na afya njema, katika jina la Yesu (x2) VI. Ninaamuru hofu na mashaka vitoweke, katika jina la Yesu VII. Ninadai ushindi kamili juu ya kila mpango wa mwovu ulioandaliwa dhidi yangu, familia yangu, wana wa Mungu, marafiki au majirabi, katika jina la Yesu VIII. Asante Bwana kwa kuwa umetenda, katika jina la Yesu, Amina.


21. MAMBI YA ALFAJIRI Maandiko: Zaburi 37:5, Zaburi 121 VIPENGELE VYA MAOMBI I. Mzee wa siku, ninakushukuru kwa kuniwezesha kuifikia siku hii ya leo, uinuliwe katika jina la Yesu II. Baba, ninashukuru kwa ajili ya ulinzi wako wa Kiungu ambao ulinizingira usiku wote. Utukuzwe katika jina la Yesu III. Imeandikwa katika Zaburi 27:5 kuwa “Umkabidhi BWANA njia yako, pia umtumiani, naye atafanya.” Hivyo ninaikabidhi siku hii mikononi wamko, Bwana itawale katika jina la Yesu IV. Imeandikwa katika Zaburi 37:23 kuwa “Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA” Hivyo ninakuomba Bwana uimarishe hatua zangu leo, katika jina la Yesu V. Baba, ninaomba kuwa maneno ya kinywa change, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, katika jina la Yesu VI. Ninadai ushindi juu ya mipango yote ya mwovu, katika jina la Yesu VII. Ninajizamisha damuni mwa Yesu VIII. Bwana, ninapokea nguvu na rehema ili niishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi na tamaa za mwili, katika jina la Yesu IX. Ninamkabidhi kwako mwenzi wangu, watoto wangu na familia yangu yote. Walinde na uwabariki, katika jina la Yesu X. Ninamleta kila mwana wa Mungu mikononi mwako, Bwana, walinde na uwastawishe , katika jina la Yesu XI. Ninakuja kinyume na kila mpango wa adui kutaka kusababisha ajali na vifo kwa ndugu zangu, katika jina la Yesu XII. Ninafunika wote kwa damu ya Yesu XIII. Bwana, ninaomba upendeleo wako wa Kiungu uwe juu


yangu ili nistawi katika kila nikatachokifanya siku ya leo, katika jina la Yesu XIV. Ninatakasa kwa damu ya Yesu kila chakula nitakachokula siku ya leo, katika jina la Yesu XV. Ninazamisha damuni mwa Yesu mali zangu zote, nyumba, biashara (ofisi) katika jina la Yesu XVI. Asante Bwana kwa kunipa ushindi siku hii ya leo, katika jina la Yesu, Amina


22. MAOMBI YA WAKATI WA KULALA (USIKU) Maandiko: Mithali 3:24, Zaburi 127:2 I. Katika jina la Yesu (x3), Damu ya Yesu (x3) II. Yehova EL-Shaddai, ninakusifu siku hii ya leo, Uinuliwe katika jina la Yesu. III. Bwana, samehe kila dhambi niliyofanya, iwe kwa maneno, matendo au mawazo (taja) katika jina la Yesu IV. Asante Bwana kwa ajili ya familia yangu. Pokea utukufu katika jina la Yesu V. Ninaukabidhi usiku huu mikononi mwako, ninaomba ulinzi wako wa Kiungu uwe juu yetu, katika jina la Yesu VI. Ninabatilisha na kufuta kila mpango uliopangwa na wachawi usiku huu wa leo, katika jina la Yesu VII. Ninaifunika familia yangu kwa damu ya Yesu VIII. Bwana, ninakuomba uachilie malaika wako watulinde usiku wa leo IX. Ninalifunika anga hili kwa moto wa Roho Mtakatifu na kulitangaza kuwa anga lisolopitika na nguvu za giza, katika jina la Yesu (x3) X. Ninakuja kinyume na kila ndoto chafu na mashambulizi yatokayo kwa shetani, katika jina la Yesu (x2) XI. Bwana, endelea kujifunua kwangu hata nitakapokuwa nimelala, katika jina la Yesu XII. Uinuliwe Bwana kwa kuwa umenijibu maombi yangu, katika jina la Yesu, Amina


Kwa msaada zaidi wa maombi, ushauri au swali lolote kuhusu maisha ya wokovu, wasiliana nasi: P.O. Box10874 – Dar es Salaam - Tanzania East Africa Cell: +255-713-757051/ +255-769-757051/ +255-783-757051 E-mail: info@ christconnectint.org Website: www.christconnectint.org

Maombi ya Kila Siku Yakuleteayo Miujiza  

Daily Miracle Prayers - Swahili Version

Maombi ya Kila Siku Yakuleteayo Miujiza  

Daily Miracle Prayers - Swahili Version

Advertisement