Ebook tanzania tanzanian islam imân na uislam

Page 77

vijana ili waweze kusoma. Pia vitabu vinavyofichua malengo ya madui ya Uislam vinafaa kusambazwa.] Wanachuoni wa Ahl-I sunna walioonyesha waislam wote njia ya sahih duniani na kutuongoza kujielimisha dini ya Muhammad ‘alaih salam’ bila mabadiliko yoyote au kuongeza kitu ni wachuoni wa madhehebu manne ambao walifikia daraja la ijtihadi. Watu hawa wane ni: Abu Hanîfa Nu’mân ibn Thâbit ‘rahmahu-Allahu ta’âla’. Alikuwa mmoja kati ya wanachuoni wa kiislam wakubwa. Alikuwa kiongozi wa Ahl-I sunna. Wasifu wake umeandikwa kwa urefu kwenye vitabu kama Se’âdet-I Ebediyye na Faideli Bilgiler. Alizaliwa kûfa mwaka wa 80 H. (699 M.) na mnamo mwaka wa 150 H. (767) aliuliua kwenye mji wa Bagdad. Wa pili ni Imâm Mâlik bin Enes ‘rahmahu-Allahu ta’âla’, ni âlim mkubwa. Alizaliwa mwaka 90 H. kwenye mji wa Madina, na mwaka 179 H. (795 M.) alifarik dunia huko Madina. Imeandikwa katika Ibni Âbidîn kwamba aliishi miaka 89. Mâlik bin Abî Âmir ni babu yake. Wa tatu ni Imâm Muhammad bin Idrîs Shâfi’î ‘rahmahu-Allâhu ta’âla’ ambae alipendwa na wanachuoni wa kiislam wote. Alizaliwa mwaka 150 M. (767 M.) nchi ya Palestine mji wa Ghazza na alikufa mwaka 204 H. (820 M.). Wa nne ni Imâm Ahmad Ibn Hanbal ‘rahmah-Allahu ta’âla’. Alizaliwa mwaka wa 164 H. (780 M.) kweneye mji wa Baghdad na kwenye mji huo huo mwaka 241H. (855M.) alikufa. Ndio nguzo za jingo la Uislam ‘rahmahumllah ajma’ên’. Leo mtu asifuata mmoja kati ya maimam wane hao yupo kwenye hatari kubwa. Ametoka kwenye njia sahih. Zaidi ya hawa, maulamâ wa Ahl-I sunna wengine wapo wengi. Nao pia madhehebu yao ya kweli ilikuwepo. Lakini bada ya mda madhehebu yao ilisahauliwa. Haijandikwa kwenye vitabu. Kwa mfano (Fukahâ-u sab’a) wâlimu Saba wakubewa wa mji wa Madina na Umar bin Abdul’azîz, Sufyân bun Uyaina[1], Is’hâq bun Râhawa, Dâwûd atTâ’î, Âmir bun Sharâhil ash-Sha’bî, Layth ibn Sa’d, ‘A’mash, Muhammad bun Jarîr at-Tabarî, Sufyân ath-Thawrî[2] na [1] Sufiyân bun Uyaina mwaka 198 H. (813 M.) alikufa kwenye mji wa Makka. [2] Sufiyân ath-Thawrî alifariki dunia mwaka 161 H. (778 M.) kwenye mji wa Basra.

– 77 –


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.