Page 1

1

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Yanayojiri katiba mpya …Na Musa Radoli

Mizozo inayozembea katika utekelezaji wake

M

iezi sita baada ya katiba mpya kupitishwa ni hatua chache imefikiwa kuhusu kutekelezwa kwa katiba hiyo mpya kutokana na mizozo kila kuchao. Mashiriki kijamii yameeleza wasiwasi kuhusu jinsi wabunge watakavyoweza kukabiliana na kuharakishwa kwa utekelezaji wa katiba. Kinachovunja moyo zaidi ni mizozo kati ya vyama viwili vikuu Party of National Unity (PNU) na Orange Democratic Movement (ODM) ambavyo vyote vimekuwa vikivutana kisiasa. Mashirika hao ya kijamii yanahofu kwamba miezi sita tangu katiba mpya kupitishwa, migawanyiko ya msimamo wa kisiasa katika serikali ya muungano yanadhihirisha wazi kwamba huenda lengo hilo halitafikiwa kwa wakati unaofaa. Mashirika ya kijamii yanahuzunishwa kuona kwamba tangu katiba mpya kupitishwa, mgawanyiko ulioko katika serikali ya muungano ambapo pande zote mbili zimeendelea kulumbana, unatia wasiwasi kuwezesha utaratibu huo uweze kufanikiwa. Kwenye kikao ya hivi majuzi cha mashirika ya kijami mjini Nairobi, ilibainika kwamba karibu vifungu 700 vya kisheria vinapaswa kushughulikiwa na afisi za mkuu wa sheria ili vikabidhiwe kwa bunge vipitishwe.

Mizozo ya Kisiasa Tume ya utekelezaji wa katiba mpya (CIC), imelalamika kwamba mkondo unaofuatwa, ulikuwa mwendo wa kinyonga kutokana na mizozo na maluumbano ya kisiasa ndani na nje ya bunge. Mwenyekiti wa tume hiyo, Bw Charles Nyachae alisema: “Licha ya utaratibu wa utekelezaji kuwa kwenye mwendo wa polepole baada ya katiba kupitishwa mnamo Agosti 27, 2010, sisi katika CIC tumejitolea kwa moyo wetu wote kuhakikisha kwamba utaratibu huo utatekelezwa kama ipasavyo kwa muhula wa miaka mitano ijayo kama ilivyopendekezwa.” Akaongeza: “Pia ni lengo letu kujiepusha kabisa na tume nyinginezo za hapo awali ambazo zimekuwa zikishughulikia maswala mengine ya kitaifa, na baada yake kuwaleta pamoja wadau wote kutoka ngazi zote ili hatimaye kuhakikisha kuwa Wakenya wanafurahia utaratibu ulio wazi, wa uhakika na wa uzingativu, ambao haujawahi kuonekana kwenye historia ya taifa hili.” Mwenyekiti huyo alisema licha ya mizozo ya

“Tumejitolea kwa moyo wetu wote kuhakikisha kwamba tumewaleta pamoja wadau wote na wa ngazi zote, ili kuhakikisha kwamba Wakenya wanafurahia katiba iliyo na uwazi ambayo haija onekana katika historia ya nchi hii.” — Bw Charles Nyachae, Mwenyekiti CIC

Wakenya wakisherekea kuapishwa kwa katiba mpya uwanjani Uhuru Park mnamo Agosti, mwaka jana. (Picha ya ndani) Ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji Katiba, Bw Charles Nyachae. kisiasa na malumbano mengineyo kati ya pande zote mbili kwenye serikali ya muungano, ilikuwa ni dhamira ya makamishna wa CIC kuhakikisha kwamba utaratibu wa utekelezaji wa katiba mpya hautavurugwa ama kuingiliwa kwa njia yoyote ile na makundi ya kisiasa yanayopingana

Utekelezaji Hofu ya jinsi utaratibu wa polepole wa utekelezaji wa katiba mpya inavyoendelea ni jambo lililozungumziwa kwa mapana na wadau kwenye mkutano huo kwa dhamira ya

kuchunguza ni ufanisi gani umepatikana tangu kuapishwa kwa katiba mpya. Mkutano huo uliofanywa chini ya mada: “Kuchunguza hali: Miezi sita ya katiba” ulidhaminiwa na mashirika ya Bridge Africa, Medeva Africa na Oxfam miongoni mwa mashirika mengineyo ya kijamii kukiwepo na lengo la kuboresha na kuchunguza jinsi katiba inavyopaswa kutekelelzwa na wale wasio serikalini. Wajibu mkubwa wa mpango huo ni kuchunguza kwa hisibati ustawi uliofanywa hadi sasa kwa utekelezaji wa katiba na kuchunguza Angalia uk.4

TAHARIRI

M

Akina mama wajitokeze kunyakua viti vikuu

namo Januari, mwaka huu, mashirika kadha wa kadha ya akina mama, yalilalamikia vikali hatua ya rais ya kufanya uteuzi wa vyeo kadhaa vikuu mahakamani. Katika kesi iliyowasilishwa kwenye mahakama kuu, akina mama hao, walieleza kuwa rais hakuzingatia usawa wa kijinsia alipowateua jaji mkuu, mkuu wa sheria, mkurugenzi wa mashtaka ya umma na cheo kile cha msimamizi wa bajeti. Hata hivyo, miezi miwili baadaye na hasa baada ya rais sasa kuamua

kutangaza nafasi ya vyeo hivyo mahakamani, majaji na mawakili wengine wamejitokeza kujaza nafasi hizo. Wagombezi ishirini na wanne walijitokeza kwa vyeo vya mkuu wa sheria na naibu wake. Hata hivyo, ilifedhehesha kwamba wanawake hawakutuma maombi kwa cheo kile cha mkurugenzi wa mashtaka ya umma. Matarajio yapo kuwa kati ya wale waliotuma maoimbi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na jaji mkuu aliyeondoka, Bw Evan Gicheru, kama iwapo mwanamke hatajaza na-

fasi hiyo, hapana shaka kile kiti cha naibu jaji mkuu, hakitawaponyoka. Kwenye maazimio ya katiba mpya, nafasi za kazi zitatangazwa, hivyo basi, wanawake sharti wawe macho na tayari kuhakikisha kuwa hawaachwi nyuma. Jambo la kutia moyo zaidi kwenye katiba hii ni kule kukumbatia jinsia katika afisi za utumishi wa umma. Hii inamaanisha kuwa kuajiriwa kwa maafisa serikalini kuanzia ngazi za chini hadi zile za juu, sio tu unazusha ushindani kati ya wake na waume, ila ni kwamba theluthi tatu ya

kazi hizo ni sharti kutengwa wa jinsia ya akina mama. Hata hivyo, kwa kazi ya ngazi za juu kwa afisi za umma, wanawake watapaswa kuwa na stakabadhi za kuhitimu za juu ili waweze kuajiriwa kulingana na uwezo wao kikazi. Zaidi ya hayo, wanawake watapaswa kuboresha uwezo wao wa kushirikiana kwenye nyanja za kitaalamu miongoni mwao. Hadi sasa maongozi ya kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika zoezi la uajiri wa kamishna, imefanywa kwa uwazi. Wakati umewadia kwa wanawake

wale walio na ari za viti vikuu vya kisiasa kujitokeza na kuhesabiwa kama alivyofanya aliyekuwa waziri wa sheria, Bi Martha Karua. Hawatapaswa kujikalia kitako hadi dakika za mwisho kisha kuwalaumu waume kwa madai wamekuhujumu juhudi zao za kutaka kuwakilisha wapiga kura wao. Ni jambo la kuvunja moyo kwamba hadi wakati huu, ni wanawake wachache tu wamejitokeza hadharani kutangaza nia ya kugombea viti vya magavana 47 ambavyo vitagombaniwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.


2

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Wanawake wahimizwa huu ndio wakati wa kuchukua vyeo vya uongozi Katiba mpya, hivyo inatoa nafasi kwa wanawake kisheria kunyakua viti vya uongozi kwa kauli lile la theluthi moja ya vyeo vyote ambavyo vitakuwa vimetangazwa. Wakati wa sherehe za kungamano la kimataifa ya wanawake mjini Eldoret, wanawake kadhalika walikariri wito wa watoto kuelimika. Walisema elimu ndio urithi bora zaidi kwa watoto wa kike na kiume kwa jumla. Ujumbe huo kadhalika ulikaririwa na wasemaji wengine kwenye hafla iliyowaleta pamoja wananchi wapatao 3000 waume kwa wake ambao walimsikia Dr Kiyapi akitoa mwito kwa wazazi wa sehemu hiyo kutowabagua watoto wa kike akieleza kuwa wasichana nao wana faida kwa uzinduzi za ujenzi wa taifa siku zijazo. “Unapomuelimisha mwanamke, unaelimisha jamii nzima,” akaongeza

Dr Kiyapi. Akihutubu pia kwenye sherehe hiyo, wakili mmoja anawake sharti wakutoka kituo maarufu cha hakikishe kutekelezKASS FM, Bi Grace Kiptui wa kwa katiba mpya aliwakumbusha wanawake kunalinda haki zao kwamba dhana kuwa haki zao zote.Usemi huu ni wake Dr Lucy Kizimeratibiwa kwenye katiba yapi, mhadhiri wa chuo cha afya ya mpya, haitoshi. umma katika Chuo Kikuu cha Moi “Katiba hii sharti itekelezambaye aliwahimiza wanawake kuwe kwa kuzingatia haki za Dr Lucy Kiyapi akimwonyesha Prof Margaret Kamar ngao ya utambulizi ya kundi hakikisha kuwa wanachukua vyeo akina mama, kama ipasavyo,” la Rural Women Peace Link, huku baadhi ya wanachama hao wakionyesha vyeti vya uongozi kama ilivyoratibiwa akasema Bi Kiptui. Hata hivyo, kwenye katiba hiyo. walivyokabidhiwa awali kutokana na juhudi zao. wakili huyo alitahadharisha Dr Kiyapi ambaye alikuwa mgeni usisitivu wa swala la elimu ya wamheshimiwa kwenye hafla moja ya lugha ya Kifaransa nchini, Bi Solenne sichana kabla ya watu kuanza sasa akina mama ilivyofanywa katika kikulalamika kuwa watoto wa kiume Huteau alisema kwamba wamewetuo cha Teachers Advisory mjini Elza kushirikiana na kundi la Rural ni kama wamesahaulika.” doret ambako alinukuu ibara 197(1) Women Peace Link (RWPL) kuan“Ni sharti tuhakikishe kuwa haki ya katiba mpya inayoeleza kuwa “sio za kiusawa zimedumishwa kati ya daa shereha hiyo kwa vile wanaamini zaidi theluthi moja ya wanachama watoto wa kike na wenzao wavula- kwamba ni ya muhimu mno kwa hali kwenye bunge za kaunti ama kamati yao ya siku za usoni. na,” akahimiza. kuu za utawala, itakuwa ya watu wa Kinara wa kundi hilo la RWPL, Naibu mkurugenzi wa chuo cha jinsia moja.” Bi Celline Korir alisema kuwa kundi Jambo hilo limekaririwa kwenye hilo lao lililoanzishwa mapema miaka kifungu cha uwakilishi kuhusiana na ’90, lengo kuu likiwa kupigania “Akina mama ndiyo nguzo ya jamii zote, na hivyo ya …Na Frank Ouma umma na utaratibu wa uchaguzi, likihaki za akina mama. sema katika ibara 81(b) “sio zaidi ya sharti waheshimiwe kama ipasavyo.” Kongamanohilopialilihudhuriwa theluthi mbili ya wanachama wa viti anawake wanaolea na waziri msaidizi, Prof Margaret — Bi Korir vya umma, watakuwa wa jinsia moja”. watoto wao gerezani, Kamar. wamelalamika vikali kutokana na changamoto kadha wa kadha wanazokabiliana navyo. Wakiongea wakati wa sherehe siku ya akina mama ulimwenguni, wanawake hao walisema changamoto kubwa ni kuwalea watoto wao wakiwa wangali kifungoni. kale ambazo kina mama walipaswa kufuata, na ya ya familia moja ambayo ilikumbwa na mzozo wa … Na Karani Kelvin Kwenye shairi lenye dibaji “Serikali pili hali ilivyokuwa baada uchaguzi mkuu uliopita kinyumbani ambapo badala ya mume kumpiga imuone mama huruma,” wafungwa hao wa 2007 uliokuwa na fujo na maafa. mkewe kwa madai kwamba “amekosea”, anamfuyimbo, shangwe, nderemo na viwalitaka serikali iwe ikiwapatia akina kuza arudi kwa wazazi wake. Wimbo huo unatoa Kwenye mchezo huo, kuna familia iliyo na gelegele vilivyoandamana na ngoma mama vifungo vyepesi. wito kwa waume kutokuwa wakatili dhidi ya wake mabinti wamili, msichana wa kwanza ambaye aliza kiutamaduni, hali kadhalika michMmoja wa wafungwa kama hao, zao na hata wanawake kwa jumla, na badala yake kuwa akilazimisha kuolewa , alibahatika kuponyoezo ya kuigiza kuelezea yale wanayBi Mary Onguku alisema aliwajibika kutafuta mbinu nyinginezo za kutatua matatizo ka, lakini mdogo wake hakuwa na bahati kwani oyapitia akina mama, zilitatandaa parwanja hapo kuwaacha watoto wake wachanga na yanayowakabili. anajipata akiolewa na mwanamume mzee. katika Teachers Advisory Centre mjini Eldoret mamake ambaye ni mzee ili kutumikia Msichina yule mkubwa hatimaye amerejea wakati wa maadhinisho ya kila mwaka ya wankifungo cha mwaka moja unusu. Mama Kunyanyasa akina mama nyumbani baada ya miaka kadhaa. Anapokea awake ulimwenguni. huyu mwenye watoto sita ambaye masomo na kujipatia utajiri ambapo mara ya Ujumbe kadha wa kadha ulipitishwa na Kadhalika wimbo huo huo unaeleza jinsi mumewe alifariki miaka kadhaa iliyopita, kwanza wazazi wake na dadake mdogo wanashmakundi mbalimbali ya wacheza ngoma hao. Moja wanawake walivyo muhimu mno kwa jamii. yumo gerezani kwa minajili ya kujaribu indwa kumtambua. Kumbe yeye anamipango na kati ya makundi sita yaliyotumbuiza, kulikuwepo “Jambo ninalowaeleza wazee ni kwamba waache kuwasimamisha mashemeji wake kujiunga na mambo ya siasa na ndoto yake ni na makundi manne ya akina mama wa ngoma za kunyanyasa akina mama, kwani bila wao, hatuwezi kumtimua toka shamba la mumewe kuchaguliwa kama seneta wa sehemu hiyo yao. kiutamaduni kutoka kaunti kadha. kuendelea mbele,” ndio baadhi ya mistari iliyoko marehemu. Nalo kundi la Saboti Traditional Dancers kutoKundi la Eldoret Muslim Women Dancers na kwenye wimbo huo. Wakati wa zogo hilo la kujaribu kuokoa ka mlima Elgon, liliimba wimbo mmoja wa kusifu lile maarufu la North Rift Cultural Young Talents, Mchezo wa kuigiza, kutoka kwa kundi la North kile anachoamini ni mali alioachiwa na Rural Women Peace Link kwa kuwasaidia vilivyo pia zilitumbuiza, Loripili Lomunyak Dancers kuRift Cultural Young Talents, kadhalika uliwavutia mumewe marehemu, matokeo yakawa ni na hata kuwarudisha nyumbani kundi la vijana toka Baringo ndio waliokuwa wa kwanza kwenye wengi. Mchezo wao ulikuwa ukigusia fujo za kwamba kutupwa gerezani. lililokuwa hapo awali limejiunga na makundi jukwaa wakiwa na ujumbe wa amani. Hata hivyo, kijiunsia, ndoa za mapema, elimu ya watoto wa “Sijui nitaelekea wapi baada ya haramu ya wavunja sheria. ilikuwa ni ule wimbo unaojulikana kama “Beatrice” kike na uwezo wa akina mama. kukamilisha kifungo changu. Ardhi Vile vile kulikuwepo na maonyesho toka kwa ndio uliowanata wananchi wengi wasikilizaji hata Wakati wa alasiri, wananchi walionyeshwa iliyokuwa yetu na marehemu bwanangu, Nandi Women Dancers na Cheptumut Dancers kuomba kurudiwe kwa mara ya pili. filamu mbili zinazohusiana na maswala la wanawake tayari imeuzwa na mashemeji wangu,” kutoka wilaya ya Pokot. Wimbo huo wa “Beatrice” ni kuhusu habari kwa jumla. Filamu ya kwanza ikielezea itikadi za akalia akisema. Afisa mkuu msimamizi wa gereza la Kapsabet, Bw Alfred Musila alieleza kwamba baadhi ya wafungwa wa kike huwa ni sharti kutumikia vifungo vyao wakiwa na watoto wao kwa vile wengine wao ni wachanga ambao hawawezi kuachwa mikononi mwa familia ama kuelndelea mbele na kunyakua nafasi “Tayari tumeanzisha hazina in- Mkuu wa Sheria inatayarisha mswada …Na Odhiambo Odhiambo jamaa zao. zilizoko za ustawi wa taifa hili. ayojulikana kama Women Enterprise ngeni ya kulinda familia, yaani Fam“ Kwa wakati huu tunawahudumia Usemi huo wa waziri ulikuwa kwe- Fund itakayohakikisha kwamba wa- ily Protection Bill ili kukabiliana na aajiri kwenye sekta ya watoto watano walio chini ya umri wa umma wametakiwa nye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake nawake wanapata mikopo waweze ongezeko na ugomvi wa kinyumbani miaka minne, ijapo wakati mwingine kuheshimu maslahi na waziri wake msaidizi, Bw Munyala kujiendeleza kiuchumi.” Akaongeza, ambao unahatarisha hali ya upendo idadi huwa inaongezeka,” akaongeza Bw ya wanawake ambapo Keya katika shule ya St. Gema Girls “ Lengo letu kuu ni kuhakikisha na utulivu nyumbani. Alieleza kuna Musila. kwa mujibu wa katiba mpya, wana- Secondary iliyoko eneo la Macalder, kwamba akina mama wasiojiweza na wengi wa wale ambao huathirika zaidi Alito mwito kwa jamaa na jamii kwa ni akina mama na watoto. paswa kutengewa asilimia 30 ya vyeo wilaya ya Nyatike wakati wa sherehe wale masikini tunawainua.” jumla, kusaidia kuwalea watoto kama za siku ya akina mama ulimwenguni. Waziri Shaaban alisema tume “Ningependa kuwahimiza vya uajiri serikalini. hao badala ya kuwaacha kuishi gerezani Bw Keya alikuwa amandamana na kadha zimebuniwa nchini ili kuimar- Wabunge wenzangu kupitisha Waziri wa Jinsia na Ustawi wa na mama zao. Kijamii, Dr Naomi Shabaan alihu- Mbunge wa Nyatike, Bw Edick Anyanga isha juhudi kama hizo kuhakikisha mswada huo mara tu utakapowasBw Musila alisema hayo alipojiunga zunishwa kupata kwamba wengi wa na Katibu ya Jinsia na Ustawi wa Kija- kwamba akina mama hawaachwi ilishwa kwenye meza kuu ya Bunge na wafungwa wengine wakati wa sherehe waajiri hawazingatii kanuni hiyo mii, Prof Collette Suda miongoni mwa nyuma kwenye nyanja za kujiende- ili tuweze kuwalinda akina mama na za siku ya akina mama ulimwenguni leza sio tu wao wenyewe kibinafsi, ila watoto.” muhimu ya kikatiba ambayo inael- maafisa wengine wakuu wa serikali. zilizosherehekewa ndani ya gereza hilo la Arifa ya Waziri Shaaban ilieleza pia na jamaa zao kwa ujumla. Waziri alitaka Wakenya kutupila eza wazi kwamba sharti akina mama Kapsabet, kitengo cha wanawake. “Jambo lingine la kuvutia mno ni kuti- mbali mila za kale zilizopitwa na wakawawe sehemu moja ya kiungo cha kuwa Serikali na washiriki wake wa Kwaya ya wafungwa hao ilikuwa na kimataifa, wamebuni maongozi na wa maanani kanuni ambapo akina mama ti kama vile upashaj tohara kwa watoto wafanya kazi serikalini. Hata hivyo, waziri huyo alisema mipango zenye lengo la kuboresha sasa wanaweza kumiliki ardhi, kadhalika wa kike, kwa Kimombo Female Geninyimbo yenye mistari wa kutoa wito kwamba akina mama wa Kenya sasa hali ya maisha ya akina mama kwa kupata uraia wa zaidi ya taifa moja.” kwa Serikali kuihimiza itafute mbinu za tal Mutilation (FGM), kadhalika ndoa wameamka ambapo kwa kauli moja jumla na hasa kutiliwa mkazo kwa kuhakikisha kuwa haki za akina mama Si hayo tu, akasema Bi Shaaban, za mapema ambazo hurudisha nyuma wameapa kutorusi nyuma na badala elimu ya watoto wa kike. zinalindwa. Serikali kwa wakati huu, kupitia afisi za elimu ya watoto wa kike. …Na Karani Kelvin

W

Ubaguzi wa kijinsia wajitokeza wazi

N

Waajiri wahimizwa kukumbatia maslahi ya akina mama

W

Wafungwa walalama kuhusu kuwepo na watoto wao gerezani

W


3

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Linah Jebii Kilimo

Shujaa anayevalia ukanda wakuzika FGM …Na Evelyne Ogutu

W

aziri Linah Jebii Kilimo ameyaona yote, mazuri, mabaya na ya kuhofia. Kuanzia ufukara nyumbani, uvindivu wa waume, mila za kiutamaduni za kuangamiza hatimaye hadi uwanja mchafu wa kisiasa. Licha ya yote hayo, hayajazamisha ari yake ya kujiendeleza maishani huku akifuata ndoto zake za tangu utotoni, kisha kuwa mmoja wa watu wasifika na mashuhuri katika taifa la Kenya. Linah mzaliwa wa kijiji cha Kartur, kata ya Kokwo Miso, wilaya ya Marakwet Mashariki ambako pia ndiko alikokulia. Siku yake ya kawaida ilikuwa ikianza alfajiri saa 12 kutafuta chumvi kwa malisho ya mifugo yao kwenye panda shuka za Kerio Valley, umbali wa kilomita tano toka nyumbani kwao. Harakati hizo zilikuwa za kuogofya, kwani katika sehemu hiyo hofu ya kushambuliwa na wanyama mwitu ilikuwa ya kutanda, lakini siyo kwa moyo wake Linah ambaye aliweza kupitia hayo yote kisha kunyakua kiti cha uongozi macho kwa macho toka kwa wanasiasa wakongwe na waliobebea kwenye fani hiyo kabla Waziri Jebii hajijitosa uwanjani. Katika mila na tamaduni za watu wa jamii ya Marakwet, ilikuwa ni nadra kwa mwanamke kujitokeza waziwazi kugombea kiti cha kisiasa, kisha afanikiwe, kama alivyofanya “Shujaa” huyu. Kama ilivyoelezwa kwenye utangulizi wa historia ya mwanasiasa huyu, yeye alipitia changamoto chungu nzima akiwa angali mdogo, kwani hata wakati wa kwenda kutafuta chumvi kulambwa na mifugo kwenye vilima vya Kerio, Lina hakukata tamaa. Zaidi ya yote hayo, njama ilikuwa imepangwa yeye aozwe akiwa na umri wa miaka tisa tu, na hata wakati huo, hakuwa ameanza shule ya msingi. “Katika mila zetu, wasichana hutahiriwa wakiwa hata na umri wa miaka tisa tu. Hii hufuatiwa na ndoa ya kimabavu ambapo mume mtarajiwa hutakiwa kutoroka na bikira huyo mdogo. Mimi sikutaka kupitia hayo yote, kwani kwangu mimi niliyaona kama mzigo mzito mno kwangu. Nililia sana, tena sana nikifikiria yale yatakayonipata, sawa na wenzangu wengine waliokuwa wamepitia njia hiyo hiyo,” akaeleza. Kwa karibu miaka kumi, Linah alikuwa mafichoni akihepa kisu hicho cha tohara ambacho kila msichana wa jamii ya Marakwet, alipaswa kukipitia enzi hizo zake.

Mawaidha ya mwalimu Hata hivyo, siku moja mwalimu mmoja ambaye alikuwa amejiunga na shule ambako Linah naye alianza kusomea, alimhimiza kuwa mzangitifu kwa masomo “kwa manufaa ya siku za usoni.” “Dhamira yangu ya manifikio kwa kweli ilianza nikiwa na umri wa miaka tisa ambapo nilikuwa hata niko tayari kuteketwa. Haya yote yalianza pale mwalimu wangu wa zamani, Ex Senior Chief Johnstone Labore alituzungumzia kiutu tukiwa wanafunzi wa darasa la nne. “Mwalimu Labore alikuwa wakati huo amehamishiwa shuleni mwetu na alitumia muda wa saa nzima kutuelezea yajayo akipinga vikali harakati za kuwateketa watoto wa kike. “Alisema wasichana wa Marakwet watapaswa kujiepusha kabisa na FGM ili kwamba siku za baadaye, nao pia wataweza kuendesha magari makubwa kama wanawake Wajaluo ambao hawakutahiriwa na huku wameelimika mno,” akaeleza kwa kijeli waziri huyu Msaidizi wa Vyama vya Ushirika na Masoko. Kwa kukumbuka miaka 37 iliyopita, mwanasiasa huyu mwenye umri wa miaka 46 na mama wa watoto watano- watatu wa kike

na wavulana wawili – anasema kwamba kama si mawaidha aliyoyapata toka kwa Mwalimu Labore, hapana shaka angeteketwa na hata kuolewa akiwa wa umri wa miaka tisa tu. Kuhepa kwake kisu cha mbarika kulimfanya hata kutengwa na jamaa zake ambao waliamini kuwa kitendo hicho chake kilikuwa ni cha ukaidi na laana. Miongoni mwa wasotaji wake alikuwa ni pamoja na babake Linah mzazi ambaye aliamini kwa dhati kwamba mila na tamaduni sharti kufuatwa na wasichana wake. “Nilikuwa nitekwe mnamo msimu wa Desemba 1975 ambapo matayarisho yote yalikuwa yamefanywa na hata nilikuwa kwenye foleni ya wasichana waliokuwa wakisubiri kutahiriwa siku hiyo. Hata hivyo, nililia fudufudu hata kuwafanya akina mama wazee waliokuwa wakihusika kwenye zoezi hilo, kunionea huruma wakisema mtu kulia hivyo, inamaanisha mkosi fulani huenda utatokea. “Jamii yangu inaamini kwamba mtu huweza kufariki iwapo atalia sana kabla ya kufika jandoni. Dhana hiyo ndiyo iliyoniokoa,” akasema. Hata hivyo, matatizo yake hayakuishia hapo. Mnamo mwaka wa 1976, badala ya yeye aendelee na masomo kujiunga na darasa la tano sawa na wanafunzi wenzake, aliondolewa darasani na kulazimishwa kwenda kumchunga mpwa wake huko nyumbani kwao. “Uamuzi huo wa wazazi ulinilazimisha kuacha shule kwa muda wa mwaka mmoja mzima nikiwa nyumbani nikilea mpwa wangu. Wakati huo, ndugu yangu mkubwa ambaye alikuwa muuguzi mjini Kakamega mkewe ailkuwa amejifungua na nikatumwa huko kwenda kumhudumia.” Baadaye ndugu huyo wake alipata uhamisho wa kikazi hadi Nairobi na ni wakati huo ndipo alipopata fursa ya kurudi shuleni. Mnano mwaka wa 1977 alijiunga na shule ya Madaraka Primary na kurodheshwa moja kwa moja hadi darasa la sita.

Mabadiliko maishani “Mimi sikukanyaga darasa la tano, lakini wakati nilipoufanya mtihani wa Certificate of Primary Education( CPE) mwaka uliofutia, nilipita vyema kwa alam 31 kati ya 36.” Kutoka hapo, aliitwa kujiunga na shule ya upili ya State House Girls High ambako kila siku alitembea akitoka shuleni hadi mtaa wa Madaraka alikokuwa akiishi nduguye. Jebii anasema alikuwa akihifadhi akiba ya Sh 2 alizokuwa akipewa kama nauli, badala yeye alikuwa akiamua kutembea kwenda na kurudi toka shuleni kwa miguu bila kulalamika. Japo wakati huo alikuwa akifurahia mazingira mema ya kuwa shuleni, lakini kumbe wimbi kama la simanzi lilianza kunukia. Wazazi wake walikuwa wametishia kwamba ni sharti, atahiriwe mara tu atakapomaliza kidato cha nne. Hata hivyo jambo alilofanya ni kwamba baada ya kumaliza kidato cha nne, hakurudi nyumbani Marakwet, ila kusalia Nairobi, kwani mwaka uliofuatia, alipita vyema mtihani huo na kuitwa kujiunga na Moi Forces Academy kwa

Ndiye huyu shujaa wa jamii ya Marakwet, Mheshimiwa Bi Jebii Kilimo ambaye kwa sasa ni Waziri Msaidizi wa Wizara ya Vyama vya Ushirika na Masoko. kidato cha tano na sita. Huo ulikuwa mwaka wa 1982. Jebii kadhalika anakumbuka kwamba baada ya kuufanya mtihani wa “O Level,” alienda kuishi na Wamishenari fulani mjini Mombasa, akisubiri matokeo ya mtihani huo, badala ya kurudi kwa wazazi willayani Marakwet. Hata hivyo, mwaka huo wa 1982 mwezi Agosti, unabakia kama kumbukumbu ya mwanzo mwingine mpya wa mabadiliko katika maisha yake, kwani aliweza sasa kupatana na kuridhiana na wazazi wake. Mhuri wa upatanishi huo ni kumbukumbu zaidi kwake, kwani punde si punde baba aligonjeka na kuaga dunia.

“Kuna wakati wakazi wa Marakwet walikuwa wakifa njaa na mimi singeweza kukaa kitako na kuona hoi yaliyokuwa yakiendelea. Nilikichukua kitabu changu kitukufu cha Biblia na kumwomba Mwenyezi Mungu anipe nafasi ya kuweza kuleta mabadiliko. Nilitaka pia niwe kama kigezo (leketio) kati ya jamii za Pokot na Marakwet ambazo zimekuwa zikizozana kwa muda mrefu .” — Jebii Kilimo, Mbunge wa Marakwet

Jebii alipomaliza masomo yake katika kidato cha sita, aliajiriwa kazi na Kenya Commercial Bank (KCB) kama karani. Alianza kufanya kazi hiyo hapo kuanzia 1985 hadi 1997 alipojiuzulu ili kukigombea kiti cha ubunge cha Marakwet Mashariki kwa tikiti ya chama cha Social Democratic Party (SDP). Hata hivyo alishindwa. Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2002, alijitosa tena uwanjani, na kwa bahati akachaguliwa mara ya kwanza kama mbunge wa eneo hilo kwa tikiti ya chama cha Narc. Katika uchaguzi wa mwaka wa 2007, alirejea bungeni kwa tikiti ya cham cha KENDA, akiwa ndiye mbunge wa pekee wa chama hicho nchini. Mbunge huyu ambaye ameolewa na mhandisi wa wizara ya barabara, Bw Philemon Kilimo, anasema sharti akina mama pale popote walipo, kupigania haki na wajibu wao na wasikubali kukandamizwa na waume. Jambo lingine ambalo huenda wengi wetu hawakuwa na habari ni kwamba wakati mmoja kabla ya kuundwa kwa serikali ya mahluti mnamo 2008, Bi Kilimo alikuwa ni waziri kamili wa Wizara ya Uhamiaji. Kushushwa kwake ngazi hadi cheo cha waziri msaidizi, kulitokana na hatua ya kuundwa kwa serikali ya mseto kati ya Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga mnamo 2008.


4

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Wanawake washauriwa wawe makini kwa mambo ya katiba …Na Musa Radoli

W

anawake wa Kenya wameshauriwa kuwa mstari wa mbele kupigania utekelezaji wa katiba mpya bila masharti na kwa sharti, ama sivyo hali hiyo inaweza ikatekwa nyara na wanasiasa fulani walafi. Akina mama wametakiwa kutokaa kitako ama kujistarehe ila waendelee na moyo ule uliowawezesha kupinga uteuzi haramu alioufanya Rais Mwai Kibaki kwa nafasi za kazi zilizohusu afisi za mkuu wa sheria, jaji mkuu, mkurugenzi wa mashtaka ya umma na ile ya msimamizi wa bajeti ya serikali. Kabla Rais kusalimu amri kutoka shindikizo kutoka nyanja mbalimbali, tayari muungano mmoja wa akina mama ulikuwa umewasilisha mahakamani kesi ya kulalamikia uteuzi huo.

Kikao cha jinsia Akihutubu kwenye kikao hicho, aliyekuwa wakati mmoja mbunge mteule, Bi Josephine Sinyo na ambaye wakati huu ni wakili na mwenyekiti wa United Disabled People of Kenya (UPDK), alisema: “Tumetoka mbali kufikia mahali tulipo sasa, lakini mapambano kamili ndio sasa yameanza kwa akina mama na makundi yale mengine ya wasiojiweza. “Tungali tukikabidhiwa na changamoto kadha wa kadha, hivyo ni sharti tujifunge vibwebwe kupigania haki zetu kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanawake hawaachwi nyuma kwenye dhamira za utekelezaji wa katiba mpya.” Bi Sinyo aliyekuwa mgeni mheshimiwa kwenye hafla hiyo, alieleza kwamba ule uteuzi alioufanya Rais ulionyesha dhahiri hali ya kutojali toka kwa afisi kuu ya taifa. “Wanawake wa Kenya sharti wawe macho wakati wote, isipokuwa tu pengine wakienda kulala. Watapaswa wawe wakichunguza kwa makini hatua baada ya hatua zinazofanywa kwenye utekelezaji wa katiba kwa muhula wa miak mitano ijayo,” akasema. Akaongeza: “Iwapo hatutasimama wima kuhakikisha kila kinachofanywa kinakuwa katika njia ya uwazi huku akina mama wakishirikiana na wadau wengineo, dhamira yetu kuu tuliyo ipa kipau mbele ni kuhakikisha kwamba haturudi nyuma kwenye enzi zile za kale ambapo akina mama alikuwa wamekanyagiwa chini. Wanawake walitakiwa kuongoza kwenye jitihada za uboreshaji wa katiba mpya inayotoa nafasi chungu nzima kwao.” Akihutubu pia kwenye sherehe hiyo, mwenyekiti wa Tume ya Utekelezaji Katiba (CIC), Bw Charles Nyachae, alisema kwamba chini ya mahitaji ya katiba mpya, maisha ya wanawake wa Kenya kutoka mashinani hadi ngazi za juu, yatabadilika vilivyo. “Katiba hii inatoa nafasi na kulinda haki za

Akina mama wakipokea nakili za katiba mpya kwenye mojawapo wa mikutano ya hadhara iliyokuwa ikifanywa na maafisa wa serikali kuelemisha wananchi kuhusu yale yaliyomo kwenye kurasa za katiba mpya katika sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Kenya.

“Wanawake wa Kenya ni sharti kuwa waangalifu na wangatifu wakati wote kuhakikisha kuwa wanachunguza kwa makini kwa hatua jinsi katiba itakavyo tekelezwa kwa muhula wa mpito wa miaka mitano ijayo.” — Bi Josephine Sinyo, aliyekuwa Mbunge mteule zamani wa KSC

akina mama kuanzia manyumbani mwao hadi pengine pia mashambani, maafisini na viwandani, kwani katiba ile ya zamani ilikuwa imewanyima baadhi ya nafasi hizo. “Maeneo muhimu na ya kuvutia kwenye katiba hii ni kama vile wanawake sasa wanaweza kurithi mali na ardhi.

Huko mashinani “Katiba ya zamani iliwanyima wanawake fursa ya kurithi ardhi ya familia na mali nyinginezo, jambo lililowafanya akina mama wengi kuwasilisha malalamiko yao katika mahakama kuu. Lakini hata baadhi ya wengine kufanya hivyo, walijipata bado wananyimwa haki hizo. Jambo lingine muhimu kwenye ibara za katiba hii mpya, ni kuwa na usawa kwenye vyeo vya uchaguzi maafisini ya umma. Katiba mpya inatoa nafasi za uteuzi wa moja kwa moja kwa viti kadha vilivyotengewa wanawake pamoja na wenzetu wasiojiweza kimaisha. Kongamano hilo lilidhaminiwa na wakfu

ya Kijerumani inayojulikana kama Heinrich Boil Foundation. Riaba kama hiyo imekuwa ikifanywa mara kwa mara kwa lengo la kusambaza hali ya hekima miongoni mwa akina mama kukiwepo pia na mkazo kuletwa kwa mabadiliko huko sehemu za mashinani. Kulingana na mshiriki kutoka wakfu huo, Bi Wanjiku Wakogi, hadhara hiyo ya kijinsia itaendelezwa karibu kila sehemu ya taifa hili ili kuhakikisha kwamba msingi bora umedumishwa kwa mahitaji ya taifa hili siku zijazo. “Mwaka huu pia una muhimu mno kwani ndio ule ambao tutakuwa na uchaguzi mkuu kabla ya mwisho wa mwaka kesho. Hali ya kisiasa kama ilivyo nchini kwa wakati huu, inatoa kielelezo cha jinsi sura kamili ya mambo yatakavyokuwa kabla na wakati wa uchaguzi huo,” akahofia Bi Wakogi. Msemaji huyo alisema kuwa ni wazi wanasiasa wengine hasa wale wa kiume wanafanya juu chini kuhakisha kwamba kesi ambazo huenda zinawakabili mahakamani, zimetupiliwa mbali.

Baadhi ya vizingiti kwenye utekelezaji wa katiba hii mpya Kutoka uk 1

kama kuna njia mgeni itakayowezesha kuboresha kwa utaratibu huo wa utekelezaji. Mnamo Februari 2011, Kenya ilisherehekea miezi sita tangu kuapishwa kwa katiba mpya. Utekelezaji wa katiba mpya uliwezesha taifa hili kuzaliwa upya na mwanzo mpya. Katiba mpya unatoa kwa mapana uwezekano wa kuwekwa kwa msingi thabiti ambao utaliwezesha taifa hili kuimarisha juhudi zake za kuimarisha haki za kibinadamu sawa wa kijinsia na demokrasia, uzingitifu kwa wananchi na hali nyinginezo za kimaendeleo. Mmoja wa wadau kwenye mkutano huo, Bw Jason Oyugi kutoka shirika la Bridge Africa alikuwa na swali moja tu muhimu : “Wakati tunaposhuhudia matatizo mbalimbali na mavutano

baina ya Wabunge kuhusiana na maswala ya utekelezaji wa katiba, je, ni yapi tuyatarajie baadaye?” Bw Oyugi aliamini kwamba uteuzi kama ule alioufanya rais kwa vyeo kadhaa vikuu serikalini ambao hatimaye ulizua kizaazaa kitaifa, hautapaswa kurudiwa tena. Washiriki kwenye mkutano huo walisisitiza kwamba Wakenya wakishirikiana na mashirika ya kijamii kati ya wadau wengine, ni sharti wawe kwenye mstari wa mbele kuhakikisha kuwa njia zote zinazopaswa kufuatwa kwa minajili ya utekelezaji ya utekelezaji huo wa katiba mpya. Shirika la Wataalamu wa Afrika Mashirika (ASEA) kupitia mmoja wa maafisa wake, Bw Gideon Ochanda alisema kuwa katiba mpya ina mipangilio wa kutekelezwa kwa kipindi kinachofuatana cha miaka mitano muda ambao mengi kati ya vifungu vya kisheria, zitapaswa ziwe zimekamilishwa kufikia

tamati ya muhula huo. Bw Ochanda alieleza kwamba kuna vifungu vipatavyo 700 na vingine zaidi ya 60 mpya ambavyo vyote vitapaswa kuchunguzwa upya ili kuhakikisha kuwa hatimaye yote hayo yanakuwa sembamba kikatiba. Alitoa wito kwa wasomi hao wataalamu kujizatiti kwenye nyanja zote zile ambazo zitawezesha utekelezaji katiba mpya haukumbwi na vizingiti. Kama alivyoeleza awali, mkurugenzi wa maongozi na miradi katika shirika la Bridge Africa, Bw Oyugi alisema tabia ya wanasiasa na wale wanaopigania viti vikuu serikalini kukiuka na kukaidi sheria wanazopaswa kufuata kama wananchi wengine wa kawaida, watapaswa kupuuzwa na wala sio kushangiliwa kila wanapowahutubia, hali wengi wa akina yakhe ni masikini hohe hahe wasio na mbele wala nyuma.


5

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Wanaume waliojitokezea kupigania haki za wanawake …Na Mercy Mumo

J

e, umewahi kusikia habari za wanaume wanaopigania haki za akina mama kwenye uwanja wa kisiasa? Ama kwa kweli jambo hili si la kawaida kwani waume wengi wamekuzwa wakijua kwamba hatimaye uongozi wote unapaswa kuwa wa wanaume na wala si wanawake. Waume kwa miaka mingi, wamejihusisha shingo upande kwa maswala yanayohusiana na hali ya kiutawala nchini. Si ajabu kupata kwamba wanaume wengine wangali wakisisitiza kuwa mahala pa wanawake kujenga taifa, ni jikoni! Hali ya kiutamaduni miongoni mwa jamii nyinginezo za nchini, pia imechangia ya kutohusisha akina mama kwenye nyanja za kimaendeleo kwa niaba ya jamii zao. Hata hivyo, mambo sasa yanaendelea yakibadilika kwani kundi linalBw Evans Gachie (katikati) akiwa pamoja na washiriki kwenye maandamano ya kupiga teke umasikini odhaminiwa na Caucus for Women katika ukoa wa Pwani Leadership, limewaleta waume kadha chini ya baraza lao linalojulikana kama Gender Warriors Programme. Baraza (Mashujaa wa Jinsia) lilibuniwa na bunge hizo mahitaji ya maongozi na siasa litahitaji kuzibwa hilo lilibuniwa manamo mwaka wa 2009 kwa len- ndogo za mikoani kwa minajili ya kupigania ili yote mawili yaweze kuzingatiwa kwa wakati go la kuwashirikisha pia wanaume kuhusiana na haki za akina mama kuhusiana na maswala ya mmoja. maswala ya kijinsia chini ya mradi unaojulikana usimamizi. “Ni jambo la kuhuzunisha mno kuona kwamkwa Kimombo kama Gender and Governance Hawa ni waume wa kati ya miaka 18 na 30 wa- ba akina mama wengine wangali wakishawishiwa naofanya kazi ya kuhimiza akina mama wa vikundi kwa hongo ndogo ndogo ambazo kwao hawaoni Programme (GGP 3). Wazo la kutaka kufanya kazi pamoja na wa- vyovyote vile kujitokeza na kushiriki kwenye shu- kama ni madhara bila kufahamu kuwa hazitawanaume, uliwazwa na kundi la Women’s Regional ghuli za utawala na maswala ya jinsia. Hadi sasa saidia kuboresha maisha yao siku za usoni,” akaelAssembly likiwa na lengo la kuleta mabadiliko ya kuna ‘Mashujaa wa Jinsia’ 28 katika Thika, Kwale, eza Bw Gachie. Karachuonyo, Homa- Bay, Makueni, Mombasa, Ilibainika kwamba wakati inakuwa rahisi kwa kiuchumi na kijamii nchini. wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano Kwa wakati huu, kuna ‘bunge ndogo’ 29 ka- Nakuru, Migori an Uasin Gishu. Mtetezi wa jinsia kutoka mkoa wa Pwani, ya kisiasa, ni wachache tu hujitokeza kuungana na tika sehemu mbalimbali za mikoa minane ya Kenya. Kundi hili linalojiita Gender Warriors Bw Evans Gachie alisema pengo lililoko kati ya mashirika ya kijami.

Elimu duni sasa imekuwa kikwazo kwa maswala ya ardhi nchini …Na Duncan Mboyah

S

wala la ardhi huwa ni la muhimu mno kwa mambo ya kiuchumi na kijamii kwa taifa hili. Ni ishara pia ya utajiri, kadhalika utambulizi kiutamaduni. Nchini Kenya maswala yanayohusiana na ardhi, yamekuwa kizunguti mkuu. Jamii nyingi na hata watu binafsi wanachukulia ardhi kama chambo cha kuwawezesha kuimarika na kunufaika kiuchumi. Haki za umiliki wa ardhi katika Kenya ni jambo ambalo huwa linashughulikiwa kwa marefu na mapana, sio tu miongoni mwa jamii, ila pia hata mahakamanijambo linaloonyesha wazi kwamba ardhi ni muhimu mno kwa maisha ya binadamu. Walioathirika zaidi ni wanawake ambao haki zao mara nyingi zimeondokea kupuuzwa na hasa miongoni mwa jamii nyingi za Kenya ambazo huwanyima wanawake haki zao za kimsingi. Wanawake wamejionea wazi wazi ubaguzi waliokuwa wakifanyiwa kwenye ugwaji mali, kitendo kilichokuwa hata ni kama kilihalalishwa na serikali za hapo awali. Maamuzi mengi yanayogusia maswala ya ardhi, huwa yanashu-

Wanawake wakifanya kazi shambani. Akina mama wengi hadi Agosti mwaka jana, hawakuwa wamekubalika kumiliki ardhi kama wenzao wa kiume. Walipata afueni hiyo baada ya katiba mpya kupitishwa. ghulikiwa na wanaume tu hata kama ni mambo ya kilimo kwa chakula cha matumizi nyumbani wajibu ambao unapaswa uachwe mikononi mwa akina mama. Kutokuwepo na hali ya usalama wa mali wakati waume wengi wanahamia sehemu za mijini na kuacha za kilimo kwa akina mama masham-

bani, imekuwa sasa kero. Linalovunja moyo ni kwamba licha wanawake kuachwa nyumbani kuangalia hali hiyo ya kilimo, hatimaye huwa hawana usemi wowote ule hata kama itafika swala la urithi wa ardhi kama hiyo. Hata hivyo, haya yote sasa yatabadilika baada ya kuidhinishwa kwa

katiba mpya ambapo kuna vifungu kadhaa ambavyo wajibu wake mkuu ni kuchunguza upya haki za urithi wa mali. “Ijapokuwa serikali imepiga hatua kubwa kwa mambo ya elimu nchini, lakini bado kuna changamoto nyingi hasa sehemu za mashambani ya kulinganishwa na wenzao walioko maeneo ya mjini,” alisema Bw Peter Ochola, meneja wa miradi kwenye kikao cha Cancus for Women Leadership. Bw Ochola alisema kwamba wanawake wakiwa miongoni mwa wale watakaonufaika zaidi na katiba mpya, lakini bado serikali itahitajika kuwaelimisha na hasa sehemu za mashinani ili kuelewa vyema wajibu wao na yale wanayopaswa kutimiza. Meneja huyo aliitaka serikali kuhakisha kwamba elimu ya umma mashinani kuhusu mambo ya ardhi, inapewa kipao mbele kwani wengi wa wananchi hawajapata fursa ya kujisomea kurasa za katiba mpya. Aliwalaumu wanasiasa akisema wengi wao wamesahau majukumu yaliyowafanya kupelekwa bungeni, na badala yake wanatumia muda wao mwingi kuchapa siasa za uchaguzi mkuu wa 2012.

Baadhi ya ‘mashujaa hao wa jinsia’

Evans Gachie: Pwani

Yeye alianza kama kiongozi wa vijana, kisha kuhitimu hadi kwenye maswala ya haki za akina mama. Anasema kuwa mahali kama mkoa wa Pwani iwapo mkutano utakuwa umeitishwa na kundi la Kiislamu, wanawake huwa hawaruhusiwi kushiriki wala kuhutubu kama vile hufanyika kwenye mikutano ya makundi mengine ya kijamii. Mashauri kati ya waume na wanawake wakiwa kwenye kikundi kimoja, pia hutatizika. Kazi yake kama ‘Shujaa’ imemwezesha kutoa mafunzo ya kuridhisha kwa wagombezi wachanga wa viti vya udiwani mashinani. “Ninajivunia kusema kwamba nimefanikiwa kulainisha maswala ya kijinsia kwa kiwango cha asilimia 50 kwa 50 na kuwezesha washiriki kujua jinsi ya kupigania haki zao.”

Steve Kanja: Thika

Shujaa huyu sio tu amehusishwa kwenye harakati za kupigania haki za akina mama mashinani, ila pia kuchunguza jinsi fedha za hazina ya ustawi wa maeneo ya bunge (CDF) na zile za serikali za mitaa, Local Authorities Trust Fund (LATF), zinavyotumika. Ijapokuwa amefanikiwa kutoa nafasi za kazi kwa theluthi tatu kwa wanawake, anakiri kwamba haikuwa rahisi kufanya hivyo. Kwa wakati huu anakabiliana na malalamiko kadhaa kutoka kwa wazee ambao wanamlaumu eti aliamua kupigania maslahi ya wanawake badala ya wanaume.

Khamisi Mohammed: Likoni

Khamisi amekuwa shujaa wa kutajika kwa muda wa mwaka mmoja. Yeye anahusishwa na shughuli za himizo za kijinsia kuleta usawa kama inavyokaririwa kwenye katiba mpya. Fulka ya maeneo mengine nchini, waume katika mkoa wa Pwani, wanamchukulia kama wakili wao ambaye anapigania haki zao kwa dhati. Hata hivyo, anasema, “Baadhi ya akina mama mkoani wangali wakipata pingamizi kutoka kwa waume wao wakati inapofika kiwango cha kuhudhuria mikutano na semina ambazo sisi huwa tunaandaa.” Licha ya hayo mkewe anamuunga mkono kwa dhati kwa kazi hiyo yake aifanyayo kwani hana tatizo mumewe kufanya kazi na wanawake wengine.


6

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Mashirika ya haki za kijamii yaililia ICC kuhusu akina mama kwenye kambi za wakimbizi nchini …Na Odhiambo Orlale

H

uku mjadala kuhusu tuhuma za washukiwa kwenye bahasha yake Bw Louis Moreno Ocampo ungali ukiendelea nchini, mashirika ya haki ya kijamii nayo yanaitaka Serikali isipuuze haki ya maelfu ya wakimbizi wa ndani kwa ndani (IDP), waliofurushwa makwao baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 na ambao kwa wakati huu wangali wakiishi ndani ya mahema yaliyochanika katika sehemu mbalimbali mkoani Rift Valley na hata kwingineko nchini. Mashirika hayo yana wasiwasi kwamba kesi zinazowakabili washtakiwa wale sita wa Ocampo huko Hague, huenda itaifanya Serikali kusahau kabisa kwamba waathiriwa hao wangali kambini, na hasa akina mama na watoto huku macho yote na fedha zikielekezwa kwa “Ocampo Six.” Kudhihirisha kwamba wao hawacheki na watu waliotuma waraka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukatalia mbali ombi kutoka kwa Serikali ya Kenya la kutaka kesi dhidi ya “Ocampo Six” zihairishwe kwa muda wa mwaka mmoja.

600 waliofurushwa Washtakiwa hao sita waliotajwa na Ocampo mnamo Desemba 15, mwaka jana kuhusiana na tuhuma za maafa yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 ambapo watu wapatao 1,333 walipoteza maisha yao na wengine zaidi ya 600,000 kufurushwa kutoka makwao huko mali ya thamani ya mabilioni, zikiharibiwa. Wahusika hao ni pamoja na Naibu wa Waziri Mkuu, Bw Uhuru Kenyatta, Mkuu wa Utumishi wa Umma, Bw Francis Muthaura, aliyekuwa waziri Bw William Ruto na mwenzake, Bw Henry Kosgey, kadhalika aliyekuwa Kamishna wa Polisi, Bw Hussein Ali na mtangazaji mmoja kutoka kituo cha radio cha KASS FM, Bw Joshua arap Sang. Kwenye taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa shirika la Centre for Rights Education Awareness (CREAW), Bi Anne Njogu, alilieleza baraza hilo hivi: “Tunaomba kwa hisani myakatilie mbali juhudi za washukiwa kukwepa sheria ikiwa ni pamoja na kuwaingilia mashahidi dhidi yao na hata kuvuruga utaratibu wa kisheria kwenye mahakama ya ICC.” Nyaraka hiyo ikaendelea kusema: “Kila mshtakiwa ana haki ya kupewa usawa wa kisheria mahakamani kuchunguza kama mhusika ana hatia au la. Hali kadhalika kila muathiriwa kwenye fujo zilizotokea nchini baada ya uchaguzi huo, anapaswa kutendewa haki.” Taarifa hiyo ambaye pia ilipokezwa mabalozi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wamehudhuria mkutano huo wa waandishi habari, ilitiwa sahihi na mashirika mengine nchini kama vile Kenya National Commission on Human Rights, Centre for Multi-Party Democracy, International Commission of Jurists, Kenyans for Peace with Truth and Justice, Centre for Rights and Awareness Education.

Wakenya waliobeba mabango wakipinga juhudi za Serikali ya Kenya za kutaka kesi zinazohusiana na machafuko yaliyotokea nchini baada ya uchaguzi mkuu uliopita kuahirishwa kutoka mahakama ya Hague. Kilio hicho cha waandamanaji kilisikizwa na Baraza la Umoja wa Mataifa kwa kutupilia mbali ombi hilo la Kenya.

“Kila mshtakiwa ana haki ya kanuni za sheria kuchunguza kama anahatia au la. Vilevile, kila muathiriwa wa machafuko yaliyotokea baada uchaguzi mkuu uliopita anapaswa pia asikizwe ili aone na ajisikie kuwa haki imetendeka ” — Bi Anne Njogu, Mwanaharakati na Mtetezi

Waathiriwa wateseka Mashirika hayo ya kijamii yameapa kuhakikisha kwamba haki za waathiriwa ambao wangali wakiteseka, zitashughulikiwa na wakati huo huo kuahidi kuona kwamba sheria zimefuatwa nao ukaidi dhidi ya sheria, umekomeshwa bara Afrika. Wanachama 15 wa baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa, ni pamoja na Marekani, Ufaransa, Urusi, Uchina, Uingereza, Bosnia na Herzegovina, Brazil, Gabon, Lebanon, Nigeria, Columbia, Ujerumani, India, Ureno na Afrika Kusini. Bi Njogu alieleza kwamba kazi ya ICC ilikuwa ya muhimu mno kuwezesha kukomesha

kabisa ukiukaji wa sheria na wakati huo huo kuhakikisha kwamba walioathiriwa wamepata haki yao. Kuhusu pendekezo lile la Serikali ya Kenya ya kutaka kesi za “Ocampo Six” zihairishwe kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao, Bi Njogu ambaye pia ni wakili alisema ijapo ni kweli kuwa katiba mpya iliyopitishwa nchini mnamo Agosti, mwaka jana ilipendekeza kuundwa upya shughuli za mahakama na mengineyo nchini, lakini ukweli ni kuwa hata muda huo wa mwaka mmoja unaopendekezwa, haitawezekana hayo kutendeka hapa.

Jambo lililokuwa la kutia moyo zaidi ni kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikataa mbali ombi hilo la Kenya likisema kuwa taifa hili lilifanya makosa kuliandikia badala ya kuwasiliana moja kwa moja na mahakama ya ICC. Mashirika ya kijami yanaeleza kwamba kazi ya ICC ni muhimu mno kuwezesha kukomeshawa kwa ukiukaji wa sheria na kuhakikisha kwamba wale wote walioathirika wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliopita, wametendewa haki kwenya mahakama hiyo ya kimataifa. Hata hivyo, mashirika hayo yanahuzunishwa kuona wanasiasa fulani Wakenya wanadai eti ICC inalenga mataifa tu ya Kiafrika kutokana na kesi zinazowasilishwa mbele ya jopo kazi ya majaji wa mhakama hiyo. Mashirika hayo kadhalika yameitetea ICC yakisema kuchunguzwa kwa kesi zilizo mbele yake wakati huu, kunadhihirisha wazi kwamba ICC siyo tu kuwa inapiga darubini kesi za kuhusu bara la Afrika.

Swala la Dafur Nne kati ya kesi tano zilikuwa zilitokana na ombi la mataifa ya Kiafrika yenyeweb ila tu kesi kama ile ya Dafur nchini Sudan iliyowasilishwa humo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo bara la Afrika liliwakilishwa vilivyo. Wawakilishi wao wengine kwenye swala la Dafur ni pamoja na Uganda na Jamhuri ya Kidomakrasia ya Congo (DRC). Bi Njogu alisema kwamba ijapo Kenya ilikuwa imeidhinisha katiba mpya ambayo inapendekeza mabadiliko mengi katika idhara ya mahakama, lakini sharti ikumbukwe kwamba mabadiliko hayo yote hayataweza kutokea kwa muda wa kipindi cha mwaka mmoja kama wanavyopiga pang’ang’a wakosoaji wa serikali ya muungano. Kuna idara kadhaa mpya za serikali ambazo zitahitaji kuundwa ili kutoa nafasi kwa

tume ile ya katiba iweze kurahisisha kazi yake. Kama alivyoeleza mwenyekiti wa tume hiyo, Bw Charles Nyachae alisema “ndoto ya vipengee vilivyomo kwenye katiba hiyo vitaweza tu kufanikishwa pale Wabunge na washikadau wote watakapo hakikisha kwamba wametimiza wajibu waliopewa chini ya katiba hiyo.” Baraza la Umoja wa Mataifa lilikuwa limepinga ombi lililowasilishwa humo na Makamo wa Rais, Bw Kalonzo Musyoka aliyejiwasilisha humo mwenyewe akiililia baraza hilo litoe wito kwa ICC kuhahirisha kesi zile zinazowakabili Wakenya mbele yake.

Msukumo kisiasi Kulingana na ibara ya sita katiba mpya inaangazia mambo ya uongozi na uzingatifu wa maisha na masilahi ya Mkenya. Kifungo 73 (2) (a) kinaeleza: “Msukumo wa uongozi unatokana na jinsi Wakenya wamekuwa wakielimishwa kwa maswala yanayohusiana na kuwepo na uchaguzi ulio na uwazi na uwajibikaji pasipo na malalamiko hatimaye.” Kwenye isibati hiyo hiyo inaelezwa kwamba maafisa wa serikali watahitajika kwa wakati wowote ule kuwa tayari kumweleza Mkenya yanayomhusu na yanayomfahisha kwa maswala hayo yote yanayohusiana na jinsia. Kama wanavyoelezea mara kwa mara wakosoaji wa maongozi ya serikali kwamba masilahi ya mtu wa chini ni kama huwa yanapuuzwa na Mbunge mara tu baada ya kuingia kwenye jumba hilo la kutunga sheria. Wakenya wengi wamebakia kusubiri miaka mingine mitano kuweza kupata fursa ya kupiga kura kumchagua mbunge mpya kwani wakati wa muhula wa kile kipindi cha uchaguzi uliokuwa wa kwanza masikini mwananchi ni kawaida hamwoni Mbunge wake ila hadi muda huo wa miaka mitano umekamilika ndipo wanasiasa kama hao hujitokeza mashinani kuomba kura kutoka kwa wananchi.


7

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Haki za akina mama chini ya katiba mpya …Na Claris Ogangah

K

wa mtoto wa kike, kupata elimu hapa nchini bado ni changamoto kubwa. Baada serikali kuanzisha mpango wa elimu ya bure katika shule za msingi, idadi ya watoto wa kike waliosajiliwa katika shule za msingi iliongezeka zaidi ya maradufu. Hata hivyo, ongezeko hilo halikutukia katika sehemu zote za nchini kwani katika sehemu za mashambani tamaduni za kienyeji bado zinashikilia kwamba mtoto wa kike hafai kwenda shule. Imani hizo pamoja na tamaduni nyingine za kikatili kama vile kumkeketa mtoto wa kike sehemu zake za siri na ndoa za mapema, vinaendelea kumzuia mtoto wa kike kupata elimu . Haya yanaonyesha wazi haja ya serikali ya kujitwika jukumu lake kubwa la kuhamasisha ufahamu katika sehemu za nyanjani kuhusu umuhimu wa mtoto wa kike kupata elimu.

Maongozi Kuna hatua pendekezi (kama vile kuratibu maongozi ya elimu)ambazo zinapaswa kuchukuliwa na serikali kuhakikisha kwamba watoto wote wa kike na wa kiume wanapata elimu. Tarakimu zinaonyesha kwamba ingawa kuna ongezeko kubwa la watoto wa kike wanaosajiliwa kujiunga na shule za msingi, idadi hiyo hupungua baada ya masomo ya shule ya msingi. Ni wasichana wachache tu ndio wanaojiunga na shule za upili. Hali hiyo inasababishwa na mambo kadha ikiwa ni pamoja na umaskini, ndoa za mapema na wakati mwingine ukeketaji wa wasichana. Serikali inapaswa kujitokeza na mbinu za kukabiliana na hali hii ya kusikitisha. Serikali inaweza kukabiliana na hali hiyo kwa kugharamia elimu ya sekondari ili elimu hiyo iwe ya gharama nafuu kwa wazazi wengi hasa wale wenye mapato haba. Serikali pia inapaswa kuchukua hatua thabiti za kukomesha vitendo vya kikatili dhidi ya mototo wa kike na ndoa za mapema. Sheria za kupambana na visa hivyo zipo (Sheria ya watoto ya mwaka 2001), lakini mengi yanapaswa kufanywa kuhusiana na utekelezaji wa sheria hizo hasa katika sehemu za mashambani.

Mapendekezo

Tunaishauri serikali ;• Ichukue hatua za kuhakikisha kupatikana kwa wepesi zaidi nafasi za wasichana na wanawake kupata elimu na mafunzo kama mbinu muhimu ya kufanikisha mabadiliko ya kijamii. • Kushughulikia chanzo cha tofauti za kijinsia katika usajili wa wanafunzi katika shule na kuhakikisha kudumishwa kwa wanafunzi wa kike katika viwango vyote vya elimu kote katika sehemu za mashambani na mijini, hasa kuhusiana na maswala ya mimba na dhuluma za kimapenzi. • Kushughulikia swala la ubora wa masomo hasa kwa jamii zinazoishi katika mazingira magumu kwa kuhakikisha wanapelekewa walimu wa kutosha katika sehemu hizo. • Kutekeleza maongozi ya kuwarejesha shuleni wasichana, kukiwemo na maongozi ya kuwasajili upya wanafunzi hao ambao waliacha shule kwa sababu ya kupata mimba.

Wanawake kazini Serikali imechukua hatua za kuhakikisha kukomeshwa kwa kila aina ya ubaguzi dhidi ya wanawake katika sehemu za kazi. Serikali ilipitisha sheria kuhusu kazi Namba 11 ya mwaka 2007 ambayo inaenda sambamba na kanuni za kongamano la mwaka 1998 la Shirika la Kazi Duniani (ILO). Sheria hiyo inafafanua, kuweka wazi na kutaka aina zote za ubaguzi katika sehemu za kazi kukomeshwa na wakati huo huo inasisitiza usawa katika masuala yote yanayohusiana na mambo ya kazi. Sheria hiyo inahakikisha yafuatayo;i) Inazuia na kukataza ubaguzi wa kila aina dhidi ya wanawake kazini ii) Inazuia na kukataza dhuluma za kimapenzi kazini iii) Inahakikisha malipo sawa ya mishahhara kwa wafanyakazi wote kwa kazi sawa. Sheria hii inaondoa hali iliyokuwepo awali kwamba mwanamke analipwa mshahara mdogo ikilinganishwa na mwanamume, hata kama kazi wanayofanya ni sawa. iv) Inatoa likizo ya miezi mitatu kwa mjamzito bila ya kuondoa haki yake ya kupata likizo ya mwaka. Sheria hii ni kinyume sana na sheria ya awali ambayo ilitoa likizo ya miezi miwili ya uzazi huku mama aliyejifungua akipoteza haki yake ya kupata likizo ya mwaka. Hizi zote ni sheria nzuri lakini bila ya kutekelezwa vyema mwanamke hataweza kuzifurahia. Serikali inahitajika kuanzisha idara au kitengo maalum cha kukagua na kukadiria mbinu za kuhakikisha kwamba waajiri wote wanatekeleza sheria hii namba 11 ya kazi iliyopitishwa mwaka 2007. Tungependa kusema hapa kwamba ingawa idadi ya wanawake wanaoajiriwa katika utumishi wa umma na katika kampuni za watu binafsi imeongezeka, bado kuna vikwazo vinavyowazuia wanawake kuingia katika sekta hizo. Pingamizi kubwa ni kupatikana kwa elimu inayofaa ambayo kwa sasa inawazuia kujiunga na sekta ya kazi za watu binafsi. Jambo hilo linawaacha wanawake kubaki katika vibarua vya kuajiriwa visivyo rasmi ambavyo havina ujira wa kutosha wa kujikimu kimaisha wao wenyewe na jamaa zao.

Mapendekezo

Tunaishauri serikali ;• Ishughulikie swala la mtoto wa kike kupata elimu; • Kuchukua hatua za haraka kukusanya tarakimu kukadiria idadi ya wanawake katika sekta za kazi zisizi za kilimo; • Kuchukua hatua za kuwahami wanawake na wanaume walio katika kazi za dhara dhidi ya athari za kiuchumi; • Kuchukua hatua za usimamizi wa kazi katika sekta za kazi zisizokuwa rasmi ambako wengi wa wafanyi kazi ni wanawake. Wanawake na uchumi na manufaa ya kijamii Kutokuwepo kwa usawa katika mambo ya kiuchumi kati ya wanawake na wanaume ndio msingi wa utaratibu wa jamii ya kisasa. Hapa Kenya kukosekana kwa usawa wa kiuchumi kati ya wanawake na wanaume kuna uhusiano mkubwa na hali halisi ya uhusiano wa kijinsia wa makundi hayo mawili. Kwa upande mmoja ni kwa kuwa wanawake wanapata mapato haba kuliko wanaume, na pia wanawake hubaki nyumbani zaidi wakiwatunza watoto. Kadhalika wanawake hufua-

Wanafunzi wa Kenya Girl’s High School wakifurahia matokeo mema ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka jana wa 2010 mara tu yalipotangazwa. Ijapokuwa tarakimu za hivi karibuni inaonyesha kwamba idadi kubwa ya wasichana wamo katika shule za msingi lakini si katika zile za upili. tilia shughuli za waume zao kuliko wanavyofanya wanaume kufuatilia shughuli za kikazi na kibiashara za wake zao. Na kama hawajaolewa, wanawake ni rahisi zaidi kubakia katika ufukara kuliko wanaume. Hali hiyo ni sehemu ya utamaduni mkubwa wa wanaume kuwakalia wanawake, jambo ambalo linawafanya wanawake kubaki katika kazi zao za kike katika maswala ya kijamii na kadhalika kiuchumi. Kama waekezaji, wanawake sawa na wanaume wanaweza kutumia nafasi zilizopo kuanzisha sekta maalum za kiuchumi kwa kuanzisha biashara. Wanawake hata hivyo, wanakabiliwa na mrundo wa vikwazo ambavyo vimewasaidia tu kubaki kwenye vibarua vya mapato ya chini. Biashara za wanawake kwa kawaida huanza zikiwa ndogo, zikakua polepole kuliko kazi wanazoanzisha wanaume. Kushiriki kwa wanawake hapa nchini pia ni kwa polepole katika sekta zinazohitaji mtaji mkubwa (hasa katika viwanda vya kutengeza bidhaa) ambako ilipatikana wanapata karibu asilimia 32 ya kile wanaume wanachopata. Tarakimu za taarifa kuhusu maswala ya kazi na taarifa ya uchunguzi wa makadirio ya kibajeti ya shirika la Kenya Intergrated Household Budget Survey ya mwaka 2008 inaonyesha kwamba kati ya Wakenya ambao wanashiriki kwa dhati kwenye shughulki za kiuchumi kwa watu wa kuanzia umri wa miaka 15 hadi miaka 64 ambao ni jumla ya milioni 12 na 700,000, milioni moja na 900,000 hawana kazi. Na wale wasiojushughulisha na kazi zozote ni milioni 5.3. Idadi kubwa ya wanaoshiriki katika shughuli za kiuchumi wako katika sehemu za miji kuliko wale wa sehemu za mashambani. Uchunguzi wa kijinsia ulionyesha kwamba idadi ya wanawake wanaojishughulisha na kazi katika sehemu za mashambani ni kubwa kuliko ya wanaume wa sehemu za mijini. Idadi ya wanawake wanaojishughulisha na kazi mashambani ni asilimia 77.1 ilhali wanaume wanaofanya kazi mijini ni asilimia 70.3. Hali hii inaweza kueleweka kwa kuwa wengi

wa wanawake wanaoishi katika sehemu za mashambani wanajishughulisha na kazi za kilimo. Hayo yanadhihirisha wazi mchango wa wanawake wa Kenya kwenye uchumi kupitia biashara na uekezaji. Sehemu kubwa ya mchango wa wanawake ni katika shughuli za kilimo kwa kuwa wengi wa wanawake wanaishi katika sehemu za mashambani. Kuna sababu mbili kubwa zinazowafdanya wanawake wasionekane kwenye harakati kuu za kiuchumi nchini. Kwanza ni asili mia moja tu ya hati za kumiliki mashamba ndizo zilizo katika mikono ya wanawake. Kiasi kingine cha asilimia kati ya tano na sita ya hati za kumiliki mashamba zinashikiliwa kwa ushirika wa wanawake na wanaume. Hii ina maana kwamba wengi wa wanawake hawawezi kupata mikopo kwa sababu hawana dhamana ya kupata mikopo katika benki kwa vile ardhi ndiyo dhamana kubwa inayopendelewa na mashirika ya pesa. Mbali na kutokuweza kumiliki ardhi imesemwa kwamba kwa sababu ya majukumu ya kijamii ya wanawake katika uchumi majumbani mwao na ukosefu wa kazi, hali yao imebaki ya umaskini daima. Mwanamke wa kawaida wa Kenya anafanya kazi mwa muda mrefu (masaa 13) kila siku ikilinganishwa na wanaume. Hatimaye huishia kulipwa mapato madogo kwa sababu saa ambazo anazitumia kwa shughuli zake za kibinafsi huwa hazina malipo. Zaidi ya hapo biashara nyingi nchini Kenya zinahitaji leseni kadha kutoka kwa serikali za mitaa na serikali kuu. Hitaji la leseni ni la kuhangaisha kwani linahitaji wakati na pesa. Hali hiyo humuathiri zaidi mwanamke kuliko mwanaume, kwa vile mwanamke hana wakati wa kutosha na pesa pia hana. Katika kutambua mashaka ya mwanamke katika biashara na uwekezaji, serikali ya Kenya mnamo mwaka 2006 ilianzisha hazina ya wanawakeinayofahamika kwa jina la Women Enterprise and Development Fund (WEDF), kama njia ya kupunguza umaskini kupitia kukabidhi uw-

ezo wa uchumi kwa wanawake. Lengo la hazina hiyo ni kutoa njia kwa wanawake ya kupata mtaji wa kujiendelezea kibiashara. Serikali kadhalika imeshughulikia swala la wanawake kupata mikopo kupitia mashirika mbali mbali ya pesa. Kenya imepitisha sheria mpya za kazi ambazi zinanuiwa kukomesha aina zote za ubaguzi katika sehemu za kazi. Sheria hizo zimewawezesha wanawake kuwa na haki sawa za kijamii na kiuchumi kama wenzao wanaume. Hata hivyo, kuna haja ya kutekeleza sheria hizo kikamilifu ili zipate kufurahiwa na wanawake wote kote nchini. Manufaa ya sheria hizo yanapaswa kufurahiwa na wote kuanzia mijini hadi katika sehemu za mashambani ambako wanawake wanashiriki katika sekta za kazi zisizo rasmi. Kuhakikisha usawa wa wanawake na wanaume katika maswala ya uchumi wa kijamii na kuhakikisha kwamba wanawake wananufaika vya kutosha kwa kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakibaguliwa. Habari zinasema kumekuwa na ongezeko la furaha kwa wanawake kuhusiana na manufaa ya uchumi wa kijamii wanayopata kutokana na uwezo wa kupewa mikopo na huduma nyingine za pesa. Hii hakika ni hatua kubwa, lakini ukweli bado upo kwamba wanawake wa Kenya bado hawajapata uwezo wa kiuchumi wa kuwawezesha kupata manufaa yaliyotajwa. Manufaa hayo yanafurahiwa na wachache miongoni mwa wanawake wa Kenya.

Mapendekezo

Tunaishauri serikali • Itekeleze sheria za kazi ili manufaa yake yafurahiwe na wanawake wote wa Kenya; • Kurekebisha sheria kuwaruhusu wanawake kumiliki ardhi na kuzitumia kama dhamana ya kutafutia mikopo; • Serikali ijitokeze na mipango mbinu ya kiuchumi na kuwapa uwezo wa pesa wanawake wa Kenya ili waweze kufurahia manufaa ya uchumi wa kijamii kama wenzao wanaume.


8

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Tohara ya FGM inavyozorotesha elimu …Na Fred Okoth

L

icha ya mamilioni ya pesa kutumiwa kwenye warsha kuhusu hatari ya kuwakeketa wasichana, pesa hizo hazijafanya lolote kubadilisha hali halisi ya mambo kuhusiana na tarakimu za ukeketaji nchini. Unapoingia mwezi wa Januari wa kila mwaka, mara tu baada ya mwezi Desemba shughuli hupamba moto eti za watoto wa kike kutolewa utotoni na kutiwa katika usichana. Shughuli ambazo husababisha wasichana wengi kuachishwa shule mapema kwani wazazi huchukua nafasi hiyo kuwaoza mabinti zao mapema ili wapate mali kwa kisingizio kwamba wasichana hao wamekuwa wanawake waliotosha kuolewa. Wengi wao hutolewa shule hata kama elimu yao haijafikia popote. Kwa sasa shule za msingi za Kuria ndizo zilizo na idadi ndogo ya kote nchini. Hali inakuwa mbaya zaidi wakati unapolinganishwa usajili wa watoto wa kike na wa kiume katika shule hizo.

Mshirikishi Huu ni ukweli halisi ambao Bi Denita Ghati, mwenyekiti wa Kituo cha Elimu cha Ustawi wa Wanawake anauhakikisha. Kituo hicho kinashughulika na vita vya kupambana na athari hizo mbaya na mshirikishi wa mipango ya kuleta mbinu mpya za kuwatoa watoto wa kike utotoni na kuwaingiza usichanani. “Kama utamaduni haumlindi watoto wa kike na wanawake, basi ni wajibu wa serikali kuingilia kati na kukomesha utamaduni kama huo,” asema Bi Ghati. Huku nyingi ya jamii za Kenya zikichukua hatua za kukomeshelea mbali ukeketaji wa wasichana, jamii ya Wakuria inaonekana kutupilia mbali mafanikio yaliyofikiwa katika vita vya kupambana na tamaduni hiyo potofu. Tarakimu zisizo rasmi kutoka idara ya utawala inaonyesha kwamba kwa mara ya kwanza baada ya mwongo mzima, idadi ya wasichana waliokeketwa huenda imepita ile ya wavulana waliopashwa tohara. Kulingana na afisa wa watoto wa Kuria Magharibi, Bw John Langat, kuongezeka kwa idadi hiyo kunafan-

ya hata idara za serikali kutofahamu ni kwa nini idadi ya wasichana wanaokeketwa inaongezeka. “Tukitazama tarakimu zilizopo, wakati mwingine nashangaa ni jamboi gani tunaloweza kulifanya dhidi ya wazazi hawa,” akasema Bw Langat. Maafisa hao wawili walikuwa wakizungumza kwenye dhifa ya kuwatoa watoto wa kike utotoni na kuwaingiza usichanani katika njia tofauti na ukeketaji katika misheni ya Komotobo huko Kuria Mashariki ambako wanaolaani utamaduni wa ukeketaji wa sehemu za siri za wasichana waliwahimiza wasichana na wazazi wao kupuuza tamaduni hiyo.

Ukeketaji Bw Langat alisema anasikitika kwamba wengi wa wazazi wa sehemu hiyo wanasita kuzuia ukeketaji wa wasichana licha ya jitihada za serikali za kukomesha kitendo hicho. Bi Ghati alisema hali hiyo ni ya kushtusha mno, akisema kwamba “Hatuelewi jinsi mafanikio yaliyopatikana kufuatia vita vya kupambana na ukeletaji huo yanavyoachwa kupotea.” Aliongeza kwamba katika visa vingi vya ukeketaji, wasichana hulazimishwa na wazazi wao. Mshirikishi wa kampeini ya kuangamiza ukeketaji katika sehemu za Kuria Mashariki na Magharibi Bw Mwita Samuel alikiri kwamba jitihada zilizofanywa katika sehemu hiyo kuzuia ukeketaji hazikuleta mafanikio yaliyonuiwa. “Tumejaribu kukomesha tamaduni hii bila mafanikio,” akaeleza Bw Mwita. Huku mandhari safi ya wasichana 400 wakiimba na kucheza kwenye dhifa ya mipango badala ya kuwatoa watoto wa kike kutoka utotoni kuingia usichanani ikipendeza, ukweli ni kwamba kuna gubiko kubwa linaloficha hali halisi ya mambo na kwamba kuna mengi yanayopaswa kufanywa kukomesha giza hiyo ya kitamaduni. Habari zimeenea kote kwamba watoto wa kike waliohudhuria warsha ya zaidi ya mwezi mzima kuwaingiza katika usichana, wanaporejea nyumbani hulazimishwa kukeketwa na hivyo basi kudhoofisha jitihada za kukomesha ukeketaji. Mambo yanazidi kufanywa maguni na idadi kubwa ya wasichana wa

Hawa ni baadhi ya wasichana 400 ambao waliokolewa kutoka kwenye minyororo ya shughuli potofu za ukeketaji.

“Hatuelewi ni kwanini faida zote zilizopatikana awali kwenye mapambano ya kukomesha ukeketaji wa wasichana hazitiliwi maanani. Kinachohuzunisha zaidi ni kwamba wazazi wa watoto kama hao wa kike ndiyo huwalazimisha kufanyiwa kitendo hicho.” Kitanzania ambao huvuka mpaka na kujiunga na shughuli za ukeketwaji wakati wa mapumziko ya Desemba, na kuwafanya wasichana wa Kenya ambao walikuwa wameepuka shughuli hiyo kubadili mawazo yao. Bi Ghati ambaye shirika lake lime-

shughulika na harakati za kuanzisha mipango mipya ya kuwaingiza watoto wa kike katika usichana pasi na kukeketwa katika muda wa miaka mitano iliyopita ni mwenye wasiwasi mkubwa. “Umefika wakati ambapo tunapaswa kuhakikisha kwamba hatua zinachukuliwa kuhusiana na ukeketaji huo,” akakariri, huku akiongeza kwamba ni vitendo vya aina hiyo ndivyo vinavyoifanya jamii hiyo kubaki nyuma katika hali zote za kimaisha. Alizishauri idara za serikali na mashirika yanayopigania kuangamizwa kwa ukeketaji wa wasichana kuongeza juhudi zao kukomesha kitendo hicho, akisema kwamba kuna mengi yanayostahili kufanywa, na hatupasi kukoma kwenye msemo kwamba serikali imepiga marufuku ukeketaji wa wanawake. Bi Ghati alisema kuna njia za kisheria za kuhakikisha kwamba haki ya mtoto wa kike inalindwa. Alieleza pia kwamba tayari Kenya imetia saini na kuidhinisha mikataba mingi ya kimataifa ya kulinda haki za watoto wa kike na akashangaa ni kwa nini jitihada thabiti hazichukuliwi kuhakikisha kutekelezwa kwa mikataba hiyo.

Kampeini kuhamasisha viwango vya elimu …Na Musembi Nzengu

M

afanikio makubwa yamepatikana kwenye kampeini iliyoanzishwa mwaka jana kuwazuia wasichana wasiache shule katika wilaya ya Mwingi Mashariki. Afisa tawala wa sehemu hiyo, Bw Martin Mwaro amesema kabla ya kampeini hiyo kuanzishwa katika nusu ya pili ya mwaka jana, wasichana wa shule za msingi walikuwa wakiacha shule kwa kiwango cha kushtua kwa sababu ya mimba na kuolewa mapema. Lakini licha ya kampeini hiyo kubwa, wasichana saba walifanya mtihani wa KCPE wakiwa na mimba. Bw Mwaro alisema kwenye mahojiano kwamba kampeini hiyo ya kumwokoa mtoto wa kike ilianzishwa na Halmashauri ya Elimu ya Wilaya (DEB), ambayo wanachama wake walisikitishwa na idadi inayoongezeka ya wasichana wanaoacha shule kwa sababu ya kuolewa mapema na

kupachikwa mimba. “Tulianza kampeini hii kati ya mwezi Juni na mwezi Julai ili kuhakikisha kwamba mtoto wa kike anabaki shuleni. Tuligundua ya kwamba kiwango cha wasichana wanaoacha shule katika madarasa ya shule za msingi kilikuwa cha kutisha,” akasema Mwaro . Alisema katika uchunguzi wao kwenye mpango uliowahusisha walimu wakuu wa shule, machifu na manaibu wao iliafikiwa kwamba walimu wakuu wapeleke habari kwa maafisa wa utawala kuhusiana na kutohudhuria masomo kwa wasichana katika njia ambayo haieleweki. Baada ya kupokea habari hizo, machifu na manaibu wao watafuatilia kwa wazazi na walezi wengine wa wasichana hao kuona kama waliolewa au walipata mimba. Bw Mwaro alisema kwamba katika visa vingi, iligunduliwa kwamba wasichana wengi walikuwa hawaendi shule kwa sababu ya kuwa na mimba

au kujiingiza katika mapema. Alisema, kupitia utaratibu huo baadhi ya wanaume ambao walikuwa na tabia ya kuwanyemelea wanafunzi wa shule, wameshtakiwa na baadhi ya kesi ziko mahakamani. Akaongeza, wengine walipatikana na hatia na wanatumikia vifungo gerezani. Matamshi hayo ya mkuu wa wilaya yalithibitishwa na afisa mmoja mkuu wa elimu kutoka sehemu hiyo, Bw John Maluki ambaye aliongeza kwamba ukeketaji wa wasichana na ubakaji ni miongoni mwa visa vinavyosababisha wasichana kuacha shule mapema. Bw Maluki ambaye ni afisa wa elimu anayehusika na tarafa ya Mui alisema tangu kampeini hiyo ilipoanzishwa, idara yake imeshughulikia visa ishirini na moja vya mimba na ndoa za mapema. Akizungumza kwa niaba ya afisa mkuu wa elimu wilayani, Bw Maluki alisema tayari kesi kumi na tano zimepelekwa mahakamani huko

Mwingi ilhali visa vingine sita vinachunguzwa na uchunguzi utakamilishwa hivi karibuni. Alisema visa hivyo viliwahusu wasichana kutoka shule ishirini za Mwingi Mashariki na akazitaja shule ambazo zimehusika na visa vingi zaidi vya wasichana kupachikwa mimba kama ni Kateiko, Kyangu, Kamulewa, Munyuni na Nzanzu. “Kwa ushirikiano na idara ya watoto na mashirika yasiyo ya serikali kama vile Can Do, wasichana waliohimili wamehimizwa kubaki shule hadi siku zao za kujifungua zitakapokuwa zimekaribia, na kurudi shule baada ya watoto wao kuacha kuamwishwa, “ akaeleza Bw Maluki. Alisema kwamba kutokana na wanaume waliohusika na kuwapachika mimba wasichana hao kuchukuliwa hatua kali, wengi waliokuwa na tabia hiyo wameacha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana wa shule na visa vya mimba na ndoa za mapema vimepungua.

Hofu iliyoko kwa wasichana wa Tanzania …Na Amelia Thomson-DeVeaux

K

wa wasichana wa Tanzania wanaojaribu kwenda shule , mambo ni magumu vya kushangaza kwenye malazi hatari ya muda ambako wasichana hao ni lazima waishi. Huwa wanakabiliwa na visa vya kuhangaishwa kimapenzi na wakati mwingine kubakwa. Visa vyao ni vya kusikitisha na mara nyingi matokeo yake ni kuacha masomo ambayo wamefanya kila jitihada kuyapata. Wanaume wanaowahangaisha na kuwapiga wasichana hao hutekeleza mambo hayo bila kujali, na ubakaji huo haujasababisha mashtaka ya aina yoyote.. “Hata tukipiga mayowe kuomba usaidizi, watu hawaji kutusaidia, alisema mmoja wa wasichana hao. Hadi wakati polisi wanapofika katika makazi yetu, watakuwa wamemaliza azma yao. Kwa hivyo wanaume hao hufanya vile wanavyotaka. Katika mwongo uliopita, shule kadha za sekondari zimefunguliwa kama mwitikio wa upanuzi wa shule za msingi. Lakini kwa kuwa ziko mbali na vijiji vingi, wasichana huchagua kuishi kwenye nyumba za kukodisha za bei rahisi katika mitaa ile inayofahamika kwa jina maarufu la ghetto ambazo ziko karibu na shule. Kuna usalama haba, lakini wasichana hao wanahatarisha maisha yao kwa ajili ya kupata elimu ambayo wengi wanaamini itawakwamua kutoka kwenye umaskini. Wakati wasichana wanapodhulumiwa kimapenzi matokeo yake yanaweza kuwa mabaya mno. Baadhi ya shule zimekumbwa na tatizo la wanafunzi kuacha shule kwa hadi kiwango cha asilimia ishirini kwa sababu ya mimba. Maafisa wana dhana kwamba mimba hizo zinatokana na kubakwa, visa ambavyo wakati mwingine havisemwi kwa sababu ya kuona fedheha. Wafanyikazi wa mashirika yasiyo ya serikali katika sehemu hiyo wamehimiza haja ya watu kuelimishwa kuhusu tatizo hili kubwa. “Haitoshi kujenga bweni kuwaweka wasichana salama. Ni dhana hii potofu kwamba wanaume wana haki kwa wanawake ambayo inahitaji kubadilishwa,” alisema Bi Rosie Martin, mkurugenzi mkuu wa shirika la African Initiatives.


9

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Mila yapewa kipaumbele zaidi

…Na Chrispinus Omar

E

limu ya mototo wa kike bado ni jinamizi kubwa katika sehemu za nchi zenye ukame. Hali huwa ngumu zaidi wakati wa kiangazi ambapo jamii huhama kutoka sehemu moja hadi nyingine wakitafuta malisho na maji. Wengi wa wazazi katika sehemu hii hawathamini elimu na huwa vigumu kwao kuwapeleka watoto wao shuleni, shule ambazo huwa haziko karibu. “Kuwatuma watoto wako kwenda kukusaidia kuleta chakula nyumbani na kuwapeleka shule kwa miaka kadha ambapo huna hakika ya kile watakachokuwa baada ya masomo hayo,” ni ndoto ambayo Mzee Tomuny Chelal hataki kuiota, na anauliza; “Ni lipi kati ya hapo mawili unaloweza kuchagua?” Dai hilo ndilo linalomfanya Mzee Chelel mkazi wa Pokot Mashariki kuwazuia watoto wake kwenda shule. Shinikizo kutoka kwa maafisa wa utawala ambao wanataka kutekeleza maongozi ya serikali kwamba elimu inatolewa bure na lazima katika shule za msingi limemfanya achague watoto wa kupeleka shule.

Wanachaguliwa Mzee Chelal ana wake watatu na kila mmoja anahitajika kumtoa mtoto mmoja kujiunga na shule. Watoto kama hao huwa wanachaguliwa maalum kwani ni lazima wawe ni wavivu ambao hawapendi kwenda kuchunga mifugo. “Mifugo ndiyo kiasili chetu kikubwa cha utajiri. Tunawatoa kama mahari, mbali na kuwafuga kwa ajili ya nyama na maziwa,” akasema Mzee Chelal. Wasichana hawana bahati kwani huozwa hata kabla ya kufikia balehe, kwa wanaume ambao ni wazee kama wazazi wao. Mnamo Februari 16, mwaka huu, mzazi mmoja aliyekuwa na hasira akiandamana na rafiki yake walivamia shule ya msingi ya wasichana ya Kakuma huko Turkana Magharibi. Alikuwa anataka kumtoa binti yake katika shule hiyo. Mzee huyo alizua zogo ambalo lilimfanya mwalimu wa msichana huyo kutafuta usaidizi wa mwalimu mkuu.

“Ilitubidi tuwaite polisi ambao walimkamata mzazi wa msichana huyo pamoja na kundi la watu waliokuwa wakipiga makelele ambao walidhamiria kumtoa shule msichana huyo kwa nguvu, ili akaanze maisha yake mapya ya kuwa mke wa mtu,” akalalamika Bw Korombori. “Msichana huyo wa Kiturkana bado ana wasiwasi kwa sababu ya tamaduni zilizopitwa na wakati. Msichana huyo hana haki ya kujiamulia hali yake ya baadaye. Wazazi wanaweza kuamua ni lini anapopaswa kuolewa na nani atakayemwoa.

Kupatanisha “Uamuzi unatokana na ni wapi kutakakotolewa mahari mengi zaidi,” akaongeza Bw Korombori. Alipendekeza kituo kianzishwe cha wasichana wanaokwepa ndoa za lazima na za mapema huku serikali ikijaribu kuwapatanisha na wazazi wao. Turkana ni eneo lenye matatizo makubwa. Wazazi wengi hawawezi kuwanunulia watoto wao sare za shule na vifaa vingine vinavyohitajika chini ya mpango wa elimu ya msingi bila malipo na msaada wa udhamini wa elimu ya sekondari . “Watoto kama hao wanahitaji kusaidiwa lau sivyo watashurutishwa na matakwa ya jamii zao ambazo zinaenda kinyume na haki zao. Kwa kawaida wengi wao hupuuzwa na wazazi wao kwa kuenda kinyume na utamaduni wa jamii zao,” asema Bw Korombori. Usajili wa wanafunzi huko Turkana bado ni haba na idadi ya wasichana wanaomaliza masomo ni ndogo mno kwa kuwa wanalazimishwa kuolewa mapema. “Ukeketaji hauendelezwi katika jamii hii lakini viwango vya watoto wa kike kuacha shule vinaanzia darasa la tatu kwa sababu wengi wao wanaji-

Maafisa kutoka wizara ya elimu walikuwa kwenye sherehe ya Siku ya Elimu, iliyofanywa katika shule ya Our Lady of Mercy Secondary wilayani Turkana Magharibi. (Picha ya ndani) Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kakuma Girls wakitumbuiza wageni, wazazi na wanafunzi wenzao wakati wa sherehe hiyo. Picha na: Chrispinus Omar

unga na shule wakiwa wamechelewa,” aeleza Bw Korombori. Kuna haja kwa viongozi kuwa katika msitari wa mbele kwenye vita vya kupambana na kutokuwa na elimu kwa vile wao ndio wanaoheshimiwa na jamii zao. “Viongozi wa eneo hilo wana wajibu mkubwa wa kutekeleza katika kubadilisha dhana ya jamii hiyo, ili watoto

“Msichana huwa hana hiari ya kujiamulia wazazi ndio huamua ni lini atapaswa kuolewa na nani. Uamuzi kama huo huwa unafikiwa inapotambulika ni wapi ng’ombe zaidi watapatikana” — Bw Wilson Korombori, Afisa wa Elimu Turkana Magharibi

wengi zaidi wajiunge na shule na kuendelea na masomo hadi watakapopata elimu ya kutosha,” akasema. Ingawa tamaduni zilizopitwa na wakati ni kikwazo kikubwa kinachozuia watu wa jamii za wafugaji za Turkana kupata elimu, tatizo lingine ni umbali wa shule ziliko. “Hatuna shule hapa sisi. Inatulazimu kutembea kilomita nyingi kupitia msituni. Njiani tunapambana na hatari ya wanaume wanaoweza kutuiba na kisha wasichukuliwe hatua yoyote kwa kuwa huwa wanatoa mahari yanayotakikana,” alisema Binti Margaret Longorikemer mwenye umri wa miaka 17 kutoka Pokot Kaskazini. Jamii inamchukulia msichana aliyebalehe au aliyekeketwa kuwa yuko tayari kuolewa. Katika jamii hii wasichana hawana haki. “Hawana haki kwa sababu utamaduni ni mkuu zaidi kuliko mambo

mengine yoyote ya kigeni.” Baada ya msichana kupashwa tohara, hakuna jambo lolote litakalonizuia kumuoa kama bado hajaolewa, asema Bw Julius Loitakori mwenye umri wa miaka 24.

Mheshimiwa Jambo lingine ambalo linawazuia watoto kwenda shule katika sehemu hiyo ni vipindi virefu vya ukame. Hivyo basi Mbunge wa Samburu Mashariki, Bw Raphael Letimalo, anasema serikali inapaswa kutekeleza kwa dhati maongozi ya elimu kuhakikisha kwamba watoto wote wa kike na wa kiume waliotimiza umri wa kwenda shule wanajiunga na shule kupitia mpango wa chakula shuleni ili wabaki shuleni hasa wakati wa kiangazi. Ni mradi ambao unapaswa kuendelezwa ili watoto wahakikishiwe kuendelea na masomo wakati wote, alisema Bw Letimalo.

Miradi ya wanasayansi wa kike Afrika zaboreshwa …Na Duncan Mboyah

S

hirika linalojulikana kama African Women in Agricultural Research and Development (AWARD), limetangaza udhamini kwa wanawake wanasayansi wa kilimo wa Afrika kutoka mataifa 11 za bara hili letu. Shirika hilo tayari limetuma maombi yao ya mwaka 2011 yanayotaka wanasayansi wanawake, ambayo mwisho ni mwezi huu wa Aprili. “Twataraji maombi mengi mwaka huu baada ya kupanuka hadi Liberia na kuenea kwa habari za manufaa ya shirika hilo kwa wanawake wanasayansi na taasisi za kilimo kote katika kanda hii,” amesema Bi Vicki Wilde ambaye ni mkurugenzi wa shirika hilo. Shirika la AWARD ambalo ni mradi wa jinsia na mpango wa ushauri kuhusu utafiti wa kilimo wa kimataifa (CGIRR), lilianzishwa kufuatia mradi wa majaribio wa miaka mitatu katika kanda ya mashariki mwa Afrika. Lengo la mradi huu ni kumtwika mwanamke wa Kiafrika katika sayansi

ya kilimo uwezo wa kutoa mchango thabiti na stadi kuangamiza umaskini na kuthibiti usalama wa chakula katika eneo la bara la Afrika linaloambaana na jangwa la Sahara. Karibu wanawake elfu mbili kutoka nchi kumi wameshiriki katika mashindano tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwaka 2008. Kati ya hao, kuna wanawake 41 wa Kenya ambao ni wanasayansi. Wanawake wapatao sabini wa Kiafrika ambao kwa sasa wanaendeleza utafiti wa kilimo katika nyanja mbali mbali watafikiriwa chini ya mradi huu. Udhamini huo unakusudiwa tu wanawake wanasayansi kutoka Afrika wanaofanya kazi za utafiti wa kilimo na maendeleo kutoka Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Rwanda, Tanzania, Uganda na Zambia, ambao wamekamilisha shahada za masomo za Bachelors, Masters, na udakitari katika mambo ya utafiti wa kilimo. “Lengo letu ni kuimarisha utafiti na maarifa ya uongozi ya wanawake Waafrika.”

“Tunafurahiwa na kuvutiwa mno na nafasi hii ya kipekee iliyotolewa kwa wanawake wanasayansi wa bara Afrika kujielimisha zaidi.” —Vicki Wilde, Mkurugenzi wa Shirika la AWARD

Mradi huu unadhaminiwa na wakfu wa Bill na Melinda Gates, Shirika la Amerika la Misaada ya Kimataifa (USAID) likishirikiana na lile la CGIAR. Bi Wilde anasema kwamba shirika lake linashughulikia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa wanawake ambao ni mifano mizuri kwa wengine, jambo ambalo linawazuia wanawake wa Afrika kutekeleza kwa vitendo wajibu wao katika masuala ya utafiti wa kilimo na kufikiria kujiingiza katika utafiti wa kilimo kama kazi ya manufaa. “Tuna furaha kubwa kutoa nafasi hii ya kipekee kwa wanawake Waafrika ambao ni wanasayansi wa kilimo ambao kazi yao ni muhimu sana,” akaeleza Bi Wilde. Karibu asilimia hamsini ya mifano bora ya shirika la AWARD, ni wanaume wa Kiafrika ambao wanashikilia mamlaka na madaraka makubwa ambao wametekeleza wajibu mkubwa katika kuleta mapinduzi ya kifikra kuhusu wajibu muhimu unaotekelezwa na wanasayansi wanawake wa Afrika.

AWARD ni mradi wa miaka mitano wa thamani ya dola milioni kumi na tano, wa kuwapa vihimizo wanasayansi wanawake katika bara la Afrika. Wanasayansi wanawake kutoka sekta za uchumi wa kilimo, uhandisi wa kilimo, sayansi inayohusiano na mambo ya wanyama na mifugo. Asilimali za kwenye maji na uvuvi, misitu, mazingira, ustawi wa mimea na wanyama, ukuima wa misitu, sayansi ya udongo, sayansi ya matibabu ya mifugo, maji na sayansi ya unyunyizaji maji mimea, miongoni mwa sekta nyinginezo zinazoshugulikiwa chini ya wakfu huo wa Bill na Melinga Gates wa huko Marekani. Chini ya shirika hilo, wanasayansi wanafanya kazi na wanawake katika sehemu za nyanjani na mashambani katika kupambana na umaskini na njaa kwa jumla. Kadhalika, shirika hilo linashughulikia ustawi wa sekta za masomo ya kazi na kuimarisha thamani ya miradi ya mafunzo ya kazi na kupalilia vipaji vya utafiti wa kilimo na maendeleo kupitia mradi huo wa ushirika.


10

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Wajane waacha tabia ya omba omba badala yake sasa wajitegemea

…Na Gilbert Ochieng

K

ifo kilipomnyang’anya mume, Bi Margaret Mugeni akiwa na umri wa miaka 49 na watoto saba miaka kumi na sita iliyopita, matumaini yake ya kuendelea na maisha yaligubikwa na giza. Hii ilikuwa nikwasababu alikuwa amempoteza mume aliyekuwa ndiye kiasili chake cha maishilio. Kifo cha ghafla cha mumewe ambaye alikuwa ni mwenye cheo cha Warrant Officer katika jeshi la nchi kavu la Kenya, mnamo mwaka 1994 kilimwacha katika hali ya kuchanganyikiwa, na hivyo basi kulazimika kuanza kibarua kigumu cha kuwatafutia wanawe mahitaji muhimu ya kimsingi ya elimu. Bi Mugeni alikuwa akiishi katika kijiji cha Busibwabo katika wilaya ya Busia. Kwa kuwa alikuwa hajafanya kazi yoyote maishani mwake, alitafakari njia za kumwezesha kupata chakula na kadhalika kuwapa elimu watoto wake na maisha mazuri. Yeye pamoja na wajane wenzake walifikia kwamba misaada midogo midogo haitawapeleka popote katika kuwalisha, kuwavisha na kuwalipia karo za shule watoto wao. Tafakuri zao ziliwapeleka kuanzisha kundi la akina mama waliloliita Busibwabo Widows and Orphans HIV and Aids Womens Group. Wakati lilipoanza lilikuwa na wanachama 17, watano wanaume na kumi na wawili wanawake. Baadaye kundi hilo liliongeza wanachama hadi wakafika 20, huku idadi ya wanawake ikifikia 16 ilhali wanaume

walipungua hadi wanachama wanne, huku likiwashughulikia mayatima 271 na watoto wengine wasiobahatika. Bi Mugeni ndiye mwenyekiti wa chama hicho kilichoundwa mwaka 2003 kwa lengo la kuwafariji wanawake waliofiwa na waume zao. “Wengi wetu tulifikiria ya kwamba maisha yetu yalikuwa yamefikia kikomo baada ya kuaga dunia kwa waume zetu ambao ndio waliokuwa tegemeo letu la maishilio,” akasema Bi Mugeni. “Hata hivyo, kwa vile sote tulikuwa tumefiliwa na waume, tulisaidiana wenyewe kwa wenyewe, na kundi limeimarika na hata kuhimizana sisi kwa wisi tufanye kazi kwa bidii zaidi,” akaongeza kinara huyo.

Kuishi na Ukimwi Kundi lake limefanikiwa kupata misaada ya chakula kutoka Shirika la Chakula la Ulimwengu (WFP) kukiwa na lengo la kuwapa wanachama chakula chenye lishe bora kwa wale ambao wanaishi na Ukimwi na virusi vya Ukimwi. Akina mama hao baada ya kuanzisha mradi wa ufugaji kuku ambao umepata mafanikio makubwa ni tabasamu iliyotanda katika nyuso zao. Hii ni kwa sababu wanauza kuku wao katika hoteli na mikahawa mbali za sehemu hiyo pamoja na kwa watu binafsi, na kwa ajili hiyo basi kuupiga teke umaskini. “Kwa hivi sasa tumeanzisha mradi wa ufugaji kuku kwa udhamini wa Sh 102,000 ambazo zilitolewa na Idara ya Kilimo katika mwaka wa 2006 chini ya mpango wa “Njaa marufuku Kenya”, akaeleza Bi Mugeni, na kuonge-

za kwamba kila mwanachama alipewa vifaranga watano, kuku wanne na jogoo mmoja. Mradi huo umewakwamua kutoka kwenye lindi la umaskini, na kutegemea kwao misaada kutoka kwa wafadhili hasa wanasiasa ambao dai ma wamekuwa wakitumia unyonge wao kujiendeleza kisiasa. Bi Mugeni anakumbuka kwamba wakati mumewe alipoaga dunia, mtoto wake wa kwanza wa Hawa ndio wanachama wa Busibwabo Widows and Orphans HIV/AIDS Women’s kiume alikuwa yuko karibu kujiunGroup ya wilayani Busia, wakionyesha baadhi ya kuku wanazofuga na kuuza ga na shule ya upili. Kupitia kundi kutoka vibanda vyao katika hali ya kujitegemea. Picha na Gilbert Ochieng hilo ameweza kuilipa karo za shule na sasa yuko katika chuo kikuu cha Egerton ambako anasomea masowauzia wenye maduka katika sehemu hiyo mumewe wake miaka mitano iliyopita. mo ya sayansi ya kompyuta. “Kati ya kuku 150 niliokuwa mbali na wanunuzi wengine wa kibinafsi. Watoto wengine wanasoma katika “Kadhalika tuna mradi wa ukuzaji shule mbali mbali za sekondari katika nao, niliuza 100 kwa bei ya Sh 600 kila jogoo mmoja na kupata jumla mboga na mtama na pia kuendesha mkoa wa Magharibi. Sawa na Bi Mugeni mwandishi ya Sh 60,000, ambazo ziliniwezesha mradi sawa na wa benki wa kutoa au katibu wa chama hicho, Bi Lillian kukamilisha ujenzi wa nyumba yetu mikopo kwa zamu, ambapo kila mwaVihenda, anasema mradi huo umem- ambayo ilikuwa imekwama baada ya nachama anapaswa kutoa mchango wezesha kuwasomesha watoto wake, mume wangu kuaga dunia, miaka mi- wa Sh 20 na kugawa pesa hizo kwa kuwanunulia sare za shule pamoja na tano iliyopita,” akakariri Bi Oduor ak- zamu,” akasema mwenyekiti huyo. Kundi hilo limo katika harakati za kushughulikia mahitaji yao ya kiafya iongeza kusema kwamba mradi huo kuwasajili mayatima zaidi na wajane tangu mumewe alipokufa miaka mi- umembadilishia maisha pakubwa. ili mao wapate kunufaika na mradi chache iliyopita. Dhamira kuu huo na kuweza kuinua hali zao za Hadi kufikia sasa kundi hilo lina kuku wapatao 420 katika mabanda “Tukiwa kama kundi hatuna la maisha na kujitegemea. Hata hivyo, tatizo kubwa linalolitofauti ya kufugia kuku. kujutia katika kuanzisha kwetu mradi Mmoja wa wanachama waliofaidi- wa kufuga kuku, kwa sababu kuna kumba kaundi hilo ni wezi wa kuku ka na mradi huo ni Bi Margaret Oduor soko kubwa la kuku,” asema Bi Mu- ambao mara kadha wamevunja aliyesema kwamba wakati wa majira geni, na anaongeza kusema kwamba: mabanda ya kufuga kuku na kuwaiba ya Krismasi, mnamo mwezi Desemba “Tuna dhamira kubwa ya kufanikisha wakati wa usiku. “Tunatoa mwito kwa idara ya kilkati ya kuku 150 alifanikiwa kuuza ma- mengi kupitia mradi huu.” jogoo 100 kwa bei ya Sh 600 kila moja. Mbali na mradi huo wa ufugaji imo na wafadhili kutusaidia kujenga Alitumia pesa hizo kukamilisha kuku, kundi hilo limeanzisha mradi wa mabanda thabiti zaidi ili kuhakikisha ujenzi wa nyumba yake ya mawe ambayo ukulima wa viazi ambavyo wanavitu- usalama wa kuku wetu ambao ndio kiilikuwa imekwama baada ya kifo cha mia kupikia chapati, keki na skonzi na ku- asili cha maishilio yetu,” wakaomba.

Misaada taruri yabadilisha hali ya maisha kwa wanawake …Na Gilbert Ochieng

W

anawake ndio wanaounda jumuiya kubwa zaidi ya maskini kote ulimwenguni, ingawaje inafahamika kwamba wanapopewa usaidizi mdogo wanawake wanaweza kuleta mabadiliko makubwa, aio tu mjumbani mwao bali katika jamii yake nzima. Maneno hayo yametekelezwa kwa vitendo na kundi la wanawake la Alakara ambalo kwa msaada mdogo wamefanikiwa kubadilisha hali zao za maisha. Ufanisi wao ni kisa halisi cha kujitoa katika ufukara mkubwa na kujiletea neema kubwa. Neno Alakara maana yake ni pamoja katika lugha ya Kiteso. Wanachama wa kundi hilo la akina mama la Alakara lililoko katika kaunti ya Busia lina furaha tele baada ya kupokea msaada wa Sh120,000 kutoka kwa Wizara ya Kilimo, chini ya mradi wa “Njaa Marufuku Kenya.” Pesa hizo zilitolewa mwaka 2006 kusaidia miradi ya kuleta mapato. Alakara ni moja ya makundi 15 ya kijamii ambayo yalinufaika na mradi huo ambao madhumuni yake ni kupunguza viwango vya umaskini katika eneo hilo. Ilitarajiwa kwamba pesa hizo zingewawezesha akina mama hao kujiingiza kwenye miradi ya kujiendelezea mapato kwa kushiriki kwenye miradi tofauti ya kuzalisha mapato. Katibu wa kundi hilo, Bi Florance Aunya anasema wana kila sababu ya kuwa na furaha kwa kuwa wanepata mafanikio makubwa. Sasa wanaweza kujitafutia njia za kujikimu wenyewe na jamaa zao bila ya kutegemea kurushiwa misaada. Kundi hilo la kujisaidia kaupitia mpango wa kukopeshana kwa zamu yaani merry-go-round. Lilianzishwa mwaka 1998 likiwa na wanachama watano wanaume na kumi wanawake na kusajiliwa na Idara ya Huduma za Jamii. “Mnamo mwaka 2001 kundi letu liliteuliwa na Idara ya Kilimo na wanachama wake wakapewa mafunzo ya kuchunguza na kukadiria ubora wa mihogo na viazi vitamu katika taasisi ya mafunzo ya kilimo ya Busia (ATC) chini ya udhamini wa Taasisi ya Kenya ya utafiti wa maendeleo ya viwanda,” akasema Bi Aunya. Walifundishwa pia utayarishaji wa uji wa unga wa mhogo, unga wa viazi vitamu na uji wa maharagwe aina ya Soya, miongoni mwa vyakula vingine. Kabla ya kupata msaada wa pesa kundi hilo lilikuwa likien-

Bi Florence Aunya, katibu wa Alakara Women’s Group akionyesha pakiti za unga ambazo wao hutengeza. Picha na Gilbert Ochieng

desha kibanda cha chakula katika kituo cha biashara cha Chepkube kwenye barabara ya kutoka Busia kwenda Kisumu. Lakini kufuatia msaada huo, mambo yalibadilika, na kuanzisha miradi mingine ya kuwaletea mapato zaidi. “Miongoni mwa bidhaa ambazo kundi hilo linatengeza ni pamoja na unga wa uji, unga safi wa mhogo, unga wa viazi vi-

“Mnamo mwaka wa 2001 kundi letu lilitambuliwa na Idara ya Kilimo ambapo wanachama wetu waliweza kupewa mafunzo jinsi ya kusaga mhogo na viazi vitamu .” — Florence Aunya

tamu wa uji, unga safi wa mtama, na siagi ya kupaka mkate kwa kutumia njugu,” asema Aunya. Makusudio hasa ya kuunda kundi hilo ilikuwa ni kuinua hali za maisha za wanachama na kuwapa uwezo wa kuanzisha miradi ya kujiletea mapato. “Msaada huo wa pesa umewawezesha wanachama kushiriki katika miradi mbali mbali wanayojichagulia wenyewe ambayo imewasaidia kupata uwezo wa kiuchumi, hivyo basi kuimarisha hali zao za maisha,” akaeleza Bi Aunya. Wengi wa wanachama wameweza kuwasomesha watoto wao kutokana na faida wanayopata. Wengi wao walikuwa wakiishi maisha ya kuhangaika, wakishiriki katika biashara za kijungu jiko ambazo hazingeweza kubadilisha maisha yao.. Mmoja wa wanachama wa kikundi hicho, Bi Wilkistah Emodo, ambaye ni mama wa watoto watano anasema, awali alikuwa akiuza mboga ya sukuma wiki. “Biashara hiyo haikuweza kunipa mapato ya kutosheleza mahitaji ya jamii yangu hasa kwa vile mume wangu alikuwa ni mfanya kazi za kibarua,” akaeleza Bi Emodo. “Msaada huo wa pesa pamoja na mkopo kutoka kwa kundi viliniwezesha kuanzisha biashara ya kuuza samaki, biashara ambayo imeniletea mapato makubwa.” Kundi hilo pia lina mradi wa kukopeshana kwa zamu kwa wanachama wake kwa faida ya shilingi kumi kwa mia. “Bidhaa zetu zinatafutwa sana na tunawauzia wenye maduka wa sehemu hii na kadhalika kwenye masoko ya hadhara kwa bei ya Sh 50 kila moja,” asema Bi Aunya. Mbali na kuuza bidhaa hizo kwa faida, kundi hilo linahimiza mtumiwaji wa bidhaa hizo kwa sababu bidhaa hizo zina lishe bora, sio kwa jamii bali hata kwa wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi. Hadi kufikia sasa, kundi hilo lina akiba ya Sh 86,000 katika benki moja ya hapa nchini. Kundi hilo lina mipango ya kununua mashini zao za kutayarishia bidhaa zao badala ya kutegemea ile iliyotolewa na shirika la utafiti wa maendeleo ya viwanda katika taasisi ya mafunzo ya kilimo ya Busia. Hata hivyo, Bi Aunya alilalamikia gharama kubwa za bidhaa wanazohitaji kutengezea bidhaa za kundi hilo, akisema ni ghali mno. Bi Aunya kadhalika alilalamika kuhusu ulaghai unaofanywa na baadhi ya makundi yenye nia mbaya kwa kuuza bidhaa zao na kuwaharibia masoko.


11

Toleo Namba 16 • Aprili 2011

Mtihani halisi kwa mwalimu darasani …Na Kipkoech Kosonei

H

uku utafiti uliofanywa na Baraza la Kitaifa la Mitihani nchini (NEC) kuhusu hali mbovu ya elimu ya msingi nchini ikiwa ni kashfa kubwa kwa wazazi, serikali na walimu, walimu ndio wanaostahili kashfa kubwa zaidi. Uchunguzi huo umeonyesha ya kwamba asilimia sitini ya wanafunzi katika darasa la tatu wamerudia darasa moja na kwamba zaidi ya moja miongoni mwa wale waliohojiwa hakuweza kusoma au kuandika kama inavyotarajiwa. Mfumo thabiti wa elimu na jamii ambayo inasisitiza ufanisi wa kimasomo, unatoa shinikizo kubwa kwa wanafunzi dhaifu, Hivyo basi, kuna haja kwa walimu kuwasomesha kwa uvumilivu mkubwa . Waalimu wanaendelea kulaumiwa kwa kutumia mbinu mbovu za kusomeshea darasani. Wanalaumiwa kwa kutumia mbinu za kawaida za mafunzo ambazo zinamfanya mwalimu kuwa muhimu zaidi huku mwalimu huyo akimhangaisha mwanafunzi. Wanafunzi hao hata kama kuna wale watakaobeba lawama ya ukosefu wa ustadi wa kazi, wanaoathirika vibaya zaidi ni wanafunzi wasioweza kushika chochote masomoni. Jinsi mwalimu anavyowatendea wanafunzi hao ndiyo changamoto kubwa zaidi ya mwalimu yeyote. Yapasa ifahamike kwamba wengi wa watu maarufu duniani walianza kwa ushinde mkubwa baada ya waongozaji wao – walimu na wazazi kuwapuuzilia mbali kuwa mbumbumbu au hawakuchukua hatua za kutosha za kuwapa vihimizo. Bw Albert Einstain na mwenzetu wa hapa nchini, Prof Ali Mazrui wanatujia katika kumbukumbu zetu kwa urahisi. Bw Einstain ndiye ‘mchawi’ maarufu wa fizikia na hesabu ambaye alikawia katika uundaji, lakini ndiye aliyeleta sheria maarufu ya mahusiano kati ya wakati nafasi na mwendo katika fizikia. Prof Mazrui ni msomi maarufu ambaye alianza kwa kunyimwa nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere kutokana na sababu za kipuuzi kwamba hawezi kufundishika, lakini hatimaye alikuwa mhadhiri mkuu akisomesha katika vyuo vikuu vitano mbali mbali duniani kwa wakati mmoja. Ni jambo lisiloingia katika fikra kwamba idadi kubwa ya watu ambao wangekuwa maarufu na ambao wangeweka historia, wamedidimia katika lindi la umaskini kwa sababu hawakupewa nafasi ya kusoma au walinyimwa vihimizo vya kujiendeleza kielimu na walimu wao na wazazi kwa kisingizio cha kutojiweza kimasomo. Halitakuwa jambo la kushangaza kama wengi wa watu hao ni wanawake na wasichana. Ingawa wanaojifunza wana nguvu na vipaji na matatizo. Ni wanafunzi hao wanaohitaji kupewa mafunzo peke yao ndio wanaoweza kujitokeza na ubora wao wote. Kupitia kuhimizwa na walimu, mwanafunzi aliye dhaifu kimasomo

ataweza kutumia nguvu zake za kiakili kukabiliana na udhaifu wake na kuimarisha uwezo wake. Je, kuna mbinu gani ambazo mwalimu au msimamizi wa mambo ya elimu anaweza kuzitumia anapokabiliwa na swala la kumwelimisha mwanafunzi dhaifu kimasomo? Wengi wamechukulia masomo ya ziada kama suluhisho la haraka kwa tatizo hilo. Masomo hayo mazuri ya ziada yamedhihakiwa vibaya. Ni manufaa gani yanayopatikana kwenye mafunzo ya ziada yanayorundika pamoja wanafunzi wa kila aina, yanayotumia mbinu za usomeshaji zilizofanyiwa majaribio kukiwa na lengo la kumaliza taratibu ya mpangilio wa masomo ili kumweka tayari mwanafunzi kwa mtihani anaoucha? Hakuna jitihada zozote ambazo zimefanywa kumsaidia mwanafunzi asiyeshika masomo kwa urahisi. Na bado baadhi ya walimu wanashauri kwamba watoto wasiofanya vyema warudie madarasa kama njia ya kukabiliana na wanafunzi hao. Wanaounga mkono mpango huo wa kuwafanya wanafunzi kurudia madarasa, wanasema wanafunzi wanaorudia hupata ushupavu na kuwa mahiri wanapopata matokeo mazuri baada ya kurudia. Lakini wanaousuta mpango huo wanasema kumlazimisha mwanafunzi kurudia humfanya kuvunjika moyo na kuwaaibisha wazazi wake ambao hujitia katika mkumbo huo wa kutoweza kujimudu kimasomo. Kwa hakika shule nyingi zimelaumiwa kwa kuwarudisha wanafunzi wasiofanya vyema kwenye madarasa yale yale na kuwasajili wanafunzi werevu na hivyo basi kwa hila kujipata wamo kwenye vichwa vya magazeti kwa shule zao kuwa na matokeo bora wakati matokeo ya kitaifa yanapotangazwa. Baadhi ya walimu wanazingatia mfumo wa kuwapandisha daraja wanafunzi pasi na kufanya vyema katika mitihani, lakini wapinzani wa mfumo huo wana hofu kwamba mpango huo huteremsha viwango vya elimu na kuua moyo wa kufanya bidii katika masomo. Hivyo basi, kuna haja ya kuleta usawa kati ya athari mbaya za kumfanya mtoto aregelee darasa na manufaa ambayo yanaweza kupatikana

Ni jambo la kuzungumkuti kufikiria idadi ya wale ambao wangebadilisha hali ya historia yetu kama wangeachwa nyuma bila kupelekwa shuleni na wazazi wao na hasa akina dada kwa kufuata eti itikadi kwamba elimu ni kwa wavulana wala si kwa dada zao

Mwalimu akiwa na wanafunzi darasani wakati wa masomo ya kawaida. Walimu wanahitajika kuhaimiza wanafunzi wa kike na wa kiume kutangamana badala ya utengemano na hasa iwapo hawafanyi vyema masomoni kupitia mpangilio wenye maana wa kumfanya mwanafunzi aregelee darasa baada ya mashauri kufanywa kati ya wazazi na walimu na mwanafunzi anayehusika. Wakati mwanafunzi anaporegelea darasa, basi atahitaji mafunzo maalum katika sehemu ambazo ana udhaifu. Mbali na hatua hizo mwanafunzi aliyerejeshwa darasa lake la awali anapaswa kupewa ushairi wa mwelekeo. Ushauri humfanya mwanafunzi akajitambua na kufahamu uwezo wake. Waandishi E.K. Mutie na P. Ndambuki katika kitabu chao kuhusu mwongozo na ushauri kwa shule na vyuo, wanasema mwongozo wa kibinafsi unapaswa kumsaidia mwanafunzi kupata hamasisho thabiti ili apate ufanisi wa kielimu. Kama madaktari ambao wamelaumiwa kwa kutibu ugonjwa wala sio mgonjwa, baadhi ya walimu huenda wana ufahamu katika kazi zao lakini wakawa hawajui jinsi ya kusambaza elimu katika mbinu ya kibinadamu inayofaa katika usomeshaji stadi. Si jambo la kawaida kwa walimu kushutumu darasa zima kwa kufanya vibaya kama kusema “kidato cha pili ni darasa bovu. Angalia huyu mwanafunzi alivyoniandikia. Mwanafunzi ambaye habari zake zinazungumziwa hatajwi kwa jina bali ni mwanafunzi na kidato cha pili.” Kadhalika kumpa mwanafunzi alama ya ‘D’ na kumwambia ‘vibaya sana’ si kumvunja moyo pekee lakini haina maana zaidi. Huku kila mtu akijua ya kwamba ‘D’ ina maana ya kutofanya vyema, ni mwalimu ambaye anasikitishwa na kutofanya vyema kwa mwanafunzi wake ndiko kunako mpa tumaini mwanafunzi na mwalimu anapaswa kumsaidia kwa mapendekezo mwanafunzi huyo ili ajikwamue kutoka kwenye kutofanya vyema.

Maadhimisho ya mishumaa ya Ukimwi ni hapo Mei 15

B

araza la Afya la Ulimwengu (GHC) na shirika la ulimwegu la watu wanaoishi na Ukimwi (GNP), yataadhimisha kumbukumbu za siku ya kimataifa ya Ukimwi mnamo tarehe 15 mwezi Mei. Maadhimisho hayo yataandaliwa na shirika la GNP kwa ushirikiano na baraza la GHC ili kuhakikisha ufanisi wa hali ya juu ya maadhimisho hayo. Kumbukumbu hizo ni chombo cha utetezi na uimarishaji wa masuala ya haki za binadamu huku kukitiliwa mkazo kupatikana kwa huduma za kukabiliana na Ukimwi kwa wote. Maadhimisho ya mwaka huu ya kuwasha mishumaa kwa ajili ya kuzidisha ufahamu juu ya Ukimwi yatafanywa kote ulimwenguni siku ya Jumapili Mei 15 kukiwa na wito usemao “Kugusa maisha .” Shirika hilo la kijamii limezagaa katika nchi 115 za ulimwengu na litatumia siku hii kuwakumbuka wote waliopoteza maisha yao kutokana na Ukimwi, kuwasaidia wale wanaoishi na virusi hivyo, na walioathiriwa na janga hilo na kuhimiza harakati za ufahamu dhidi ya ugonjwa huo. “Shirika la GNP ndilo shirika halisi linalofaa kuandaa kumbukumbu hizo za kimataifa za kuwasha mishumaa kwani tangu lilipoanzishwa limetoa jukwaa kwa watu wanaoishi na Ukimwi na walioathirika kwa sababu ya Ukimwi kutafakari na kupigania mabadiliko,” alisema Bw Jaffrey L Sturchio ambaye ni kinara wa baraza la afya la ulimwengu na afisa mkuu wa shirika hilo. “Tuna furaha huhamisha mradi huu wa nyanjani kwa Kevin Moody na wenzake na wana hakika kwamba chini ya uongozi wao mradi huo wa mwangaza wa mishumaa utaimarisha mafunzo ambayo watu wamejifunza na kuendelea kuleta sauti mpya kwenye kampeini ya kupambana na virusi vya Ukimwi. “Ukumbusho huo wa mwangaza wa mishumaa huongeza ufahamu kuhusu Ukimwi miongoni mwa jamii kote ulimwenguni huku watu wanaoishi na virusi. Hatua hiyo huimarisha ufahamu ambao husababisha watu kupata uwezo kwa ajili ya afya zao, kuheshimiwa kwa watu wanaoishi na Ukimwi na kuhimiza kutolewa kwa huduma za matibabu ya Ukimwi, kuzuia, kutunza na kusaidia,” alisema Bw Kevin Moody mshirikishi wa kimataifa na afisa mkuu wa shirika la GNP. “Shirika la GNP linajivunia kuimarisha na kuendeleza uongozi mashinani wa jamii katika kukabiliana na Ukimwi kupitia kumbukumbu za kuadhimisha maswala ya Ukimwi kupitia mwangaza wa mishumaa. Kumbukumbu za kimataifa za mishumaa kuhusiana na Ukimwi zilianzishwa mwaka 1983 nchini Amerika, na ndizo harakati kubwa zaidi za kimataifa dhidi ya Ukimwi na virusi vyake.

Mkurugenzi Mkuu: Rosemary Okello-Orlale Mhariri Mkurugenzi: Arthur Okwemba Mhariri Msimamizi: Jane Godia Wahariri Wasaidizi: Bob Okoth, Gunga Chea Waandishi: Mwanamke Mkenya ni toleo la African Woman and Child Feature Service Email: info@awcfs.org www.awcfs.org

Wapambe:

Musa Radoli, Kevin Karani, Frank Ouma, Odhiambo Odhiambo, Evelyne Ogutu, Duncan Mboya, Mercy Mumo, Odhiambo Orlale, Claris Ogangah, Fred Okoth, Musembi Nzengu, Amelia Thomson-Deveaux, Chrispinus Omar, Gilbert Ochieng, Kipkoech Kosonei Noel Lumbama and Bernadette Muliru (Noel Creative Media Ltd)

Jarida hili limechapishwa kutokana na usaidizi wa Hazina la Kidemokrasia la Umoja wa Mataifa (UNDEF)

Mwanake Mkenya Toleo la 16  

Mwanamke Mkenya ni toleo la African Woman and Child Feature Service. Jarida hili limechapishwa kutokana na usaidizi wa Hazina la Kidemokras...

Read more
Read more
Similar to
Popular now
Just for you