Falsafa ya Mageuzi ya Imam Hussein (a.s)

Page 33

Falsafa ya Mageuzi ya Imam husein (a.s).qxd final

Lubumba.qxd

7/1/2011

3:25 PM

Falsafa ya Mageuzi ya Imam Husein wa ile falsafa halisi ya ‘Qayam-e-Imam Husein’ – Mageuzi ya Imam Husein (a.s.).

Matatizo katika kulichanganua tukio la Karbala Kutokana na maelezo yaliyopita, ni dhahiri kwamba kuna umuhimu kwa sisi kuchanganua yale mageuzi ya Imam Husein (a.s.). Sio kwamba mageuzi yenyewe yanahitaji uchanganuaji wetu, bali ni sisi ambao tunahitaji kuyachanganua mageuzi haya. Bila ya uchambuzi huu sisi hatuwezi kukifikia kina chake, hiyo iwe ni leo ama kesho. Ni jambo ambalo haliwezekani kwamba bila ya uchambuzi huu mtu anaweza kwa kweli kuifahamu hoja ya kimantiki kwa ajili ya mageuzi haya. Umejionea mwenyewe kwamba tangu wakati ule wa mageuzi yenyewe hadi leo hii kila mtu ametoa maelezo tofauti juu ya sababu ya mageuzi haya kutegemeana na mitazamo na uelewa wao. Vile vile hatuwezi tukadai kwamba bila ya kujali juhudi zote hizi za kielimu na kitafiti, sisi tumeelewa sawasawa ule uhalisia wa mageuzi haya. Kwa upande mwingine ni muhimu kwamba tuwe tunatambua baadhi ya uchambuzi wake na kwamba tuna uelewa fulani kuhusu uhalisia wake na ule moyo ambao kwawo huo hili lilitukia. Hata hivyo, kwa upande mwingine tena tunakabiliwa na matatizo kadhaa makubwa katika kutafsiri matukio ya namna kama hii.

Tatizo la Kwanza – Maoni Binafsi: Nitawasilisha mbele yako la kwanza kati ya matatizo kama hayo ambalo kwa kweli lenyewe ni msiba mkubwa kwa haki yake. Tatizo ni kwamba kwa tukio kama la Karbala, ambalo lilikusudiwa kuwa la hadhara na limekuwa maarufu miongoni mwa watu, linakuwa ni muathirika wa maoni ya watu. Wakati tukio linapokuwa la wazi kwa kiasi kama hicho, basi linakuwa limeanikwa kwenye uchunguzi wa ummah na linakuwa ni eneo la maoni ya ummah na mitazamo ambayo huongezwa kwenye tafsiri yake. Hebu tuliweke pembeni tukio la Karbala na tuangalie jambo jingine ambalo pia ni maarufu na ni somo la uchunguzi wa ummah, ambalo matokeo 27

Page 27


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.