Page 1


FAHARASA MASHARIKI YA KATI Ushindi wa Ghaza utakuwa mwanzo na utangulizi wa kukombolewa Palestina..................................................................2 Katibu Mkuu wa OIC atahadharisha kuhusiana na hali mbaya Mashariki ya Kati.................................................................4 IRAN Mkutano wa Kilele wa Viongozi wa nchi 120 wanachama katika harakati za nchi zisizofungamana na Siasa za upande wowote NAM........................................................................5 Onyo kali la Iran kwa Maadui zake...........................................6 Iran yanuia kuwekeza Tanzania............................................7 Hafla ya kutoa misaada yafanyika Kituo cha Utamaduni cha Iran.............................................................................................10 Vijana wawili washiriki mashindano ya Qur' ani nchini Irani....................................................................................................11 MAKALA MAALUMU Kuzaliwa kwa Imam Mah'di (ATFS)......................................12 Ramadhani mwezi wa Qur' an...............................................16 JAMII Uislamu na Afya yako..............................................................20 Malezi mema kwa Watoto......................................................22 Kiigizo chema..........................................................................26 VIJANA Weledi juu ya Mustakbali wa Vijana.....................................28 KAZI Umuhimu wa Kazi Katika Uislamu.......................................30 MAPISHI Vipopoo vya Unga....................................................................34 Wali wa Nazi kwa .....................................................................34 MAONI BARUA Toa maoni yako..............................................................................36

MCHAPISHAJI Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran

MTAYARISHAJI

Kitengo cha Uhariri na Usanifu ANUANI: Al-Hikma Jarida Maridhawa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran S.L.P. 7898 Dar es Salaam Tanzania MKURUGENZI MKUU Morteza Sabouri MHARIRI / MSANIFU WA KURASA Maulidi Saidi Sengi WAANDISHI NA WATARJUMI Jopo Maalumu


Mashariki ya Kati

Ushindi wa Ghaza utakuwa mwanzo na utangulizi wa kukombolewa Palestina Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas amesema ujenzi mpya wa Ghaza ni kipaumbele cha kwanza cha serikali ya Palestina na kuongeza kuwa, Marekani na utawala wa Kizayuni unataka kuzuia ujenzi mpya wa Ghaza ili kwa njia hiyo uweze kuzusha malalamiko ya wananchi sambamba na kuwakatisha tamaa wananchi hao...

A

yatullahil Udh'ma Sayyid Ali (DI) Khamenei amesema tukio adhimu mno la ushindi wa wananchi wa Ghaza mbele ya jeshi la utawala wa Kizayuni linatokana na imani na jihadi na huku akipongeza moyo wa jihadi na kusimama kidete wa mpiganaji jihadi Ismail Hania, Waziri Mkuu wa serikali ya Palestina, Ayatullah Khamenei amesema kuwa, ni matumaini yetu kwa baraka za imani na moyo wa jihadi wa wananchi wa Palestina, Mwenyezi Mungu atajaalia ushindi huo kuwa utangulizi wa ushindi mwingine zaidi katika siku za usoni. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa vita havijamalizika huko Ghaza na kwamba vita vya kisiasa na vile vile vita vya kipropaganda na kisaikolojia bado vinaendelea. Ameongeza kuwa, wanamapambano wa Kiislamu wanapaswa kuwa macho kikamilifu, wajiandae vilivyo na wawe tayari kwa ajili ya hali yoyote inayoweza kutokea hata ya kuanza tena vita.

22

Ayatullah Khamenei aidha ameashiria njama na hila za adui katika vita vya kisiasa ambapo lengo la adui ni kutaka apate kile alichoshindwa kukipata katika medani ya vita na kusisitiza kuwa, ni lazima moyo wa kuwa na msimamo na kuwa tayari ( Muqawwama) pamoja na moyo wa jihadi ulindwe na ubakie vile vile kama ulivyo siku zote. Aidha amesisitiza kuhusu ulazima wa kuanza kwa haraka iwezekanavyo ujenzi mpya wa Ghaza na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kutoa


Mashariki ya Kati mchango wake katika uga huo na ama kuhusu vita vya kisaikolojia na kipropaganda vinavyoendeshwa na adui, amesema kwamba hizo ni njama za adui kupotosha uhakika wa mambo na kuficha ukweli ili kuibebesha lawama HAMAS na Muqaawama (harakati za mapambano) ya Kiislamu na kujaribu kuonesha kwamba wao ndiyo wahusika wa matatizo na masaibu ya wananchi wa Ghaza.

kuendelea na jihadi ya Ghaza na kuongeza kuwa, jihadi inahitaji kuwa na maamuzi thabiti na ya wazi na ni wakati huo ndipo nusura ya Mwenyezi Mungu inapoweza kuzaa matunda ya jihadi bila ya shaka yoyote.

Ayatullah Khamenei amewapongeza mashahidi wa Ghaza akiwemo sahidi Said Swiyam, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Palestina na kumuomba Allah azipe subira na Amesema jambo la kusikitisha ni ujira mwema familia za mashahidi kuona kuwa baadhi ya watawala wa hususan familia za mashahidi zenye nchi za Kiarabu zinazopakana na watoto wadogo wasio na hatia. Ghaza wanalikuza sana jambo hilo. Katika mazungumzo hayo, Khalid Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Mash'ali, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya

wa Palestina, anamshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na taifa kubwa lililojaa fakhari la Iran kwa msaada wao kisiasa, kisaikolojia na kifikra. Bwana Khalid Mash’ali amesisitiza kuwa, ni jambo lisilo na shaka hata chembe kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi kubwa katika ushindi wa wananchi wa Ghaza na kwa kweli inahusika katika ushindi huo. Mkuu huyo wa ofisi ya kisiasa ya HAMAS aidha amesema ushindi wa wananchi wa Ghaza dhidi ya adui Mzayuni ni muujiza kati ya miujiza ya Mwenyezi Mungu na kuongeza kuwa, katika mazingira hayo yaliyokuwa

Jambo lisilo na shaka hata chembe kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi kubwa katika ushindi wa wananchi wa Ghaza, na kwa kweli inahusika sana katika ushindi huo. amekumbusha kuwa, njia pekee ya kukabiliana na vita hivyo vya kinafsi na kipropaganda, ni kutangazwa kwa uwazi misimamo ya haki ya wanamapambano wa Kiislamu na wananchi wa Palestina ili njama hizo za adui zisiweze kufanikiwa. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa HAMAS na Muqaawama (Mapambano ya Kiislamu) wanapaswa kuviomba vyombo vya habari vya nchi za Kiarabu vitangaze vilivyo misimamo hiyo ya haki.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, HAMAS sambamba na kutoa ripoti kamili ya matukio ya kijeshi na kisiasa ya Ghaza na ya baada ya kumalizika vita (vya siku 22) amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawaunga mkono kwa kiasi kikubwa sana wananchi wa Ghaza na kwamba kwa niaba ya wananchi wa Ghaza na Muqaawama wa Kiislamu

magumu mno yasiyoelezeka kwa maneno, wananchi wa Ghaza walimtegemea Mwenyezi Mungu na huku wakikariri maradufu bila ya kuchoka aya ya Qur' ani isemayo: ُ َّ‫حسبنَا ه‬ ُ ‫الل وَن ِ ْع َم الْ َو ِك‬ ‫يل‬ ُ ْ َ Anatutosha Allah naye ni Mbora wa kutegemewa, walisimama kidete na kuonesha istikama ya hali ya juu; na

Aidha amesema ni jambo muhimu kufuatiliwa suala la kupandishwa kizimbani viongozi wa utawala wa Kizayuni kutokana na kutenda kwao jinai za kivita huko Ghaza na kusisitiza kuwa, inabidi suala hilo lifuatiliwe kwa uzito wa hali ya juu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema kuwa kulifuatilia jambo hilo ni sawa na 3


Mashariki ya Kati Mwenyezi Mungu Mtukufu Naye akawasaidia na kuwapa nusura wananchi hao waumini, wenye msimamo thabiti. Khalid Mash'ali ameongeza kuwa, Inshaallah ushindi huo wa Ghaza utakuwa ni mwanzo na utangulizi wa kukombolewa Palestina nzima na Qudsi Tukufu. Vile vile ameashiria kushindwa adui Mzayuni kufikia malengo yake wakati vita vilipokuwa vikiendelea na hivyo kulazimika kutangaza kusimamisha vita kwa upande mmoja tena bila ya masharti yoyote na baadae kutoka katika Ukanda wa Ghaza. Pia amekumbusha kuwa, hivi sasa vimeanza vita vya kisiasa, vita vya kuvunja mzingiro wa Ghaza na kufunguliwa njia zote za kuingia na kutoka katika ukanda huo. Amesema licha yakuwepo mashinikizo mengi na vita vya kisaikolojia, lakini serikali ya Palestina na Mapambano ya Kiislamu hawajakubaliana na masharti yoyote ya adui likiwemo la kuheshimu makubaliano ya mwaka 2005 kuhusu kivuko cha Rafah na kusimamisha vita milele. Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya HAMAS vile vile amesema ujenzi mpya wa Ghaza ni kipaumbele cha kwanza cha serikali ya Palestina na kuongeza kuwa, Marekani na utawala wa Kizayuni wanataka kuzuia ujenzi mpya wa Ghaza ili kwa njia hiyo uweze kuzusha malalamiko ya wananchi sambamba na kuwakatisha tamaa wananchi hao, lakini vyovyote itakavyokuwa serikali ya HAMAS itaanza kulijenga upya eneo hilo na haitaruhusu njama za maadui zifanikiwe.

njia ya kistratejia ya Muqawaama wa Kiislamu na makundi ya Palestina, ni jihadi na kuendesha mapambano dhidi ya adui Mzayuni na kwamba kamwe hawataachana hata kwa sekunde moja na lengo lao hilo. Katika mazungumzo hayo kulitolewa pia ripoti kuhusu hali ya mambo ndani ya Ghaza na Khalid Mash'ali pia amepongeza juhudi zinazofanywa misaada mbalimbali ya Mwenyezi Mungu kutoka ulimwengu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kuitisha kongamano wa ghaibu na moyo thabiti wa mapambano wa wananchi la kimataifa la ujenzi mpya wa Ghaza na kusisitiza kuwa, katika kipindi chote cha vita vya Ghaza.

Katibu Mkuu wa OIC atahadharisha kuhusiana na hali mbaya Mashariki ya Kati

Na: Salum Bendera

K

atibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ametahadharisha kuhusiana na hali mbaya Mashariki ya Kati hususan kuenea kwa vitendo vya kivamizi vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina. Profesa Ekmeleddin Ä°hsanoÄ&#x;lu amesema hayo katika hotuba yake kwenye kikao cha mawaziri wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM huko Sharm Sheikh Misri. Profesa Ekmeleddin ameashiria kuongezeka mivutano na migogoro Mashariki ya Kati hususan kuzidi vitendo vya kivamizi vya Israel dhidi ya Wapalestina na kutangaza kwamba, hatua ya Israel ya kuzikalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina inakinzana na sheria pamoja na mikataba ya kimataifa. Katibu Mkuu wa OIC amepokea kwa mikono miwili matukio ya kidemokrasia nchini Misri na kusisitiza juu wa ulazima kwa kufikiwa matakwa na malengo ya mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo. 44


Iran

Mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi

120

wanachama katika harakati za nchi zisizofungamana na Siasa za upande wowote NAM

K

iongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi 120 wanachama k a t i k a Harakati y a

Nchi Zisizofungamana na Siasa za Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) inapaswa kuwa na nafasi Upande Wowote NAM mjini Tehran. mpya katika kuunda mfumo mpya wa Katika hotuba hiyo muhimu mbele ya kimataifa na wanachama wa jumuiya viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa hiyo wanaweza kuwa na mchango na nchi za mabara matano ya dunia, Ayatullah nafasi ya kihistoria itakayokumbukwa Ali Khameni ameashiria hali nyeti ya sasa milele kwa ajili ya kuokoa ulimwengu na harakati ya dunia ya kuvuka kipindi kutoka katika hali ya ukosefu wa amani, muhimu sana cha kihistoria na ishara vita na ubeberu. za kuibuka mfumo mpya wenye pande kadhaa mkabala wa mfumo wa kibeberu Ayatullah Khamenei ameashiria hotuba wenye mwelelekeo wa kambi moja na iliyotolewa na waasisi wa Harakati ya akaeleza fursa zinazotoa bishara Nchi Zisizofungamana na Siasa za njema kwa nchi huru na thamani Upande Wowote ambaao walisema kuu za nchi wanachama katika msingi wa kuanzishwa jumuiya hiyo si jumuiya ya NAM na vilevile umoja wa kijiografia, kaumu au dini bali ishara za kufikia kikomo ni “umoja katika mahitaji” na akasema: subira ya walimwengu “haja hiyo bado ipo hivi sasa licha ya hususan mataifa ya maendeleo yaliyopo na kupanuka zaidi Magharibi kuhusu mfumo nyezo za ubeberu.” Amekumbusha wenye dosari, uliochakaa, mafundisho ya dini ya Uislamu ambayo usiokuwa wa kiadilifu inatambua maumbile ya wanadamu na usio wa kidemokrasia wote kuwa ni sawa licha ya tofauti zao wa muundo wa sasa wa za kikaumu, kilugha na kiutamaduni na kimataifa. Amesisitiza akasema kuwa, ukweli huo unaong’ara kuwa Harakati ya Nchi una uwezo mkubwa wa kuwa msingi

Inaendelea Uk: 15

5 5


Iran

Onyo kali la Iran kwa Maadui zake Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigadier General Ahmad Vahidi alisema siku yoyote Israel hawatakuwa na nafasi yoyote ile ndogo ya kupona na kuendelea kuishi baada ya wao kuanzisha shambulio la kijeshi dhidi ya Iran, kwani vikosi vya Jeshi vya Iran vitaifunika Israel yote kwa ujumla kwa maelfu ya makombora.

B

alozi wa Iran nchini Lebanon amesema kwamba, nchi yake ina uwezo mkubwa wa kufyatua maelefu ya maroketi kuelekea katika ngome za kijeshi za adui ikiwa kutatokea aina yoyote ile ya shambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislaam ya Iran. Ghazanfar Roknabadi amesema Iran inatizama kwa jicho la uangalifu sana uwezekano wowote ule wa tishio la kijeshi, na kwamba itatoa jibu kali kwa kutuma makombora elfu kumi na moja kuelekea katika sehemu zilizopangwa nchini Marekani, na Israel au sehemu yoyote ile kunapo patikana maslahi yao duniani kote endapo mitambo yake ya nyuklia itashambuliwa. Alisema Iran inafuata

msimamo wa kujihami ,akisisitiza kwa kusema kwamba pamoja na hayo nchi yake itajibu kwa nguvu zake zote katika shambulio lolote lile linalowezakana kutendeka. Naye Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigadier General Ahmad Vahidi alisema kwamba siku yoyote, Israel hawatakuwa na nafasi yoyote ile ndogo ya kupona na kuendelea kuishi baada ya wao kuanzisha shambulio la kijeshi dhidi ya Iran, kwani vikosi vya Jeshi vya Iran vitaifunika Israel yote kwa ujumla kwa maelfu ya makombora.

ya Kiislaam ya Iran itawafundisha wamarekani maana halisi ya vita na ni jinsi gani wanajeshi wanavyotakiwa kuwa. Marekani na Israel, pamoja na washirika wao, wanaituhumu Tehran kuwa ina malengo ya kutengeza silaha za kijeshi katika mpango wake wa nyuklia.

Washington na Tel Aviv mara kwa mara wamekuwa wakirudia rudia vitisho vyao dhidi ya Tehran kwamba zitatumika njia zote hata chaguo la kijeshi dhidi ya vituo Adui lazima ajibu swali hili, ni kwa vyake vya Nyuklia. muda gani amejiandaa kumaliza vita, na kajiandaa kupata hasara kiasi gani Iran inasema kuwa kama mmoja wapo kwa meli zake za kivita na vyombo wa nchi zilizotia saini Mkataba wa vyote vya majini kuzuia usambazaji wa silaha za nyuklia a l i v y o j i a n d a a na kama mwanachama wa Shirika la navyo pindi kimataifa la Nishati ya Nyuklia (IAEA), a t a k a p o j a r i b u ina kila haki ya kuendeleza na kupata k u i s h a m b u l i a teknolojia ya nyuklia kwa malengo (na Iran? Aliishauri matumizi) ya amani. Marekani na washirika wake IAEA mara kadhaa imefanya ukaguzi watambue uwezo mbalimbali wa mitambo ya nyuklia ya na nguvu kubwa Iran, lakini hakujapatikana ushahidi ya Iran, na wajue wowote ule unaoonyesha kuwa Mpango kwamba katika wa Nishati ya Nyuklia wa Tehran tukio lolote lile umekengeuka na kuelekea katika Waziri wa Ulinzi wa Iran General Ahmad Vahidi akikagua mitambo la kivita, Jamhuri uzalishaji wa silaha za Nyuklia. maalumu ya kurushia Makombora. ''Ole wenu Marekani na Wazayuni!

6


Iran

Iran yanuia kuwekeza katika huduma za kijamii Tanzania

Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Gharib Bilal (kushoto akitiliana saini na Makamu wa Rais wa Iran Mhe Muhammad Reza Rahimi (kulia), mwezi Mei 30, 2012. Kiongozi huyo wa Iran alikuwa nchini (Tanzania) kwa ziara ya kikazi.

H

Na: Lugenzi Makenya Kabale

istoria inaonyesha uhusiano kati ya Tanzania na Ghuba ya Uajemi (Iran ya leo) nchi ambayo jamii ya Washirazi inatoka ulianza takribani miaka 1,000 iliyopita. Hii ilitokea pale Washirazi na jamii nyingine kutoka Oman, Saudi Arabia na hata Yemen zilipokuja kufanya biashara katika Pwani ya Afrika Mashariki kutokea Pwani ya Somalia hadi kaskazini mwa Msumbiji.

raia wa Iran wenye asili ya Afrika Mashariki na hata majina yenye asili ya Pwani hiyo,� ndivyo alivyoeleza Balozi wa Iran katika mazungumzo na waandishi wa habari hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Anasema Iran ambayo ipo katika Ghuba ya Uajemi imehifadhi kumbukumbu mbalimbali zinazoonyesha uhusiano wake na Pwani ya Afrika Mashariki, hususani visiwa vya Zanzibar, Kilwa na Lamu nchini Kenya.

Balozi Muvahhedi anataja baadhi ya kumbukumbu ambazo zipo katika majumba ya makumbusho nchini Iran kama mitumbwi mikubwa ambayo ilitumika kama nyenzo za uchukuzi, bidhaa zilizopatikana Afrika ya Mashariki kama mawe yenye thamani yaliyotumika kwa “Ukijaliwa kutembelea kaskazini ujenzi na mapambo, vinyago na mwa Iran eneo ambalo Washirazi baadhi ya vifaa vya majumbani wanapotoka usishangae kukuta ambavyo vilikuwa vikitengenezwa Ni kwa kuithamini historia hiyo, ndiyo Balozi wa Iran nchini Tanzania, Bw. Mohsen Muvahhedi, anafanya kila juhudi kuhakikisha uhusiano wa Tanzania na nchi yake unaimarika kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Sasa Iran na Tanzania zimeamua kwa pamoja kujikita katika sehemu kuu nne ambazo ni kilimo, elimu, afya na diplomasia. Ni katika sekta hizo nne, Iran hivi karibuni imetoa ruzuku ya dola za Kimarekani billioni 10 (takribani Shilingi 16 bilioni za Kitanzania) kwa ajili ya kutekeleza miradi miwili ya afya na kilimo Tanzania (bara na visiwani). 7


Iran

Ukiacha mradi wa ujenzi wa hospitali za Kigamboni (Jijini Dar es Salaam) na Mjini Magharibi (Zanzibar), ruzuku ya dola milioni sita (takribani Shilingi bilioni 10) zitatumika kujenga chuo cha kisasa cha kilimo kitakachotumika kutoa mafunzo ya teknolojia ya kisasa ya kilimo cha umwagiliaji kiitwacho Irrigation Technology Transfer Centre. 88

kwa miti na wachongaji mahiri wa Afrika Mashariki. “Kwangu mimi baada ya kuteuliwa kuja kuiwakilisha nchi yangu hapa Tanzania nilijua nina jukumu la kihistoria, jukumu la kutoa mchango wangu katika kuimarisha uhusiano wa kihistoria wa nchi hizi mbili,” anasema Balozi Muvahhedi na kuongeza: “Mara baada ya kufika Tanzania niliweza kupata ukarimu na upendo halisi wa Watanzania.” Je, anasemaje kuhusu jukumu hilo la ujenzi wa uhusiano wa nchi hizi mbili? Balozi Muvahhedi anasema kwa sasa Iran na Tanzania zimeamua kwa pamoja kujikita katika sehemu kuu nne ambazo ni kilimo, elimu, afya na diplomasia. Ni katika sekta hizo nne, Iran hivi karibuni imetoa ruzuku ya dola za Kimarekani milioni 10 (takribani Shilingi bilioni 16za Kitanzania) kwa ajili ya kutekeleza miradi miwili ya afya na kilimo Tanzania (bara na visiwani). Katika fedha hizo zilizotolewa na Iran, dola milioni nne zitatumika kujenga hospitali mbili za kisasa katika maeneo ya Kigamboni (Dar es Salaam) na Mjini Magharibi kisiwani Unguja. “Ruzuku hiyo itajenga hospitali za kisasa kwa majengo na vifaa eneo la mji mpya wa Kigamboni na Unguja Mjini Magharibi,” anasema balozi Muvahhedi na kuongeza kuwa ni lengo la serikali ya Iran ni kuona ndugu zao wa Tanzania wanapata huduma bora za tiba kwa kadri nafasi ya kifedha inaporuhusu. Anasema kuwa mgonjwa anapokwenda hospitali huwa ni mtu ambaye amekata tamaa na anategemea zaidi mambo makuu matatu ili kuweza kurejesha matumaini ya maisha. Mambo hayo anayataja kuwa ni aina ya tiba atakayopata, mazingira ambayo atapata tiba hiyo na daktari atakayemhudumia ikiwa ni pamoja na vifaa vyake. “Kama anafika hospitali na kukuta mazingira mabaya, vifaa vibovu na daktari asiye na ari, basi mtu huyu huwa anahisi amekosa msaada na anaweza hata kuhisi ugonjwa wake unaongezeka badala ya kupungua akiwa hospitalini. Kwa kujua kasoro kama hizi, Serikali ya Iran itahakikisha hospitali za Kigamboni na Mjini Magharibi zinakuwa bora kwa majengo, vifaa na hata madaktari,” anasema Balozi huyo. Ukiacha mradi wa ujenzi wa hospitali za Kigamboni na Mjini Magharibi, ruzuku ya dola milioni sita (takribani Shilingi 10 bilioni) itatumika kujenga chuo cha kisasa cha kilimo kitakachotumika kutoa mafunzo ya teknolojia ya kisasa ya kilimo cha umwagiliaji kiitwacho Irrigation Technology Transfer Centre. Kwa mujibu wa balozi huyo, kituo hicho kitakuwa na vifaa vya kutolea mafunzo vya kisasa na wakufunzi toka Iran waliofuzu na uzoefu wa kufundisha taaluma ya umwagiliaji mashamba ya muda mrefu. “Chuo cha kufundishia taaluma ya umwagiliaji maji katika mashamba makubwa kitajengwa katika eneo ambalo Tanzania


Iran itaamua kwani Iran haiwezi kuamua kijengwe wapi. “Kama serikali rafiki wa Tanzania, Iran ipo tayari kwa utekelezaji wa mradi huu wakati wowote toka sasa na Tanzania inayo taarifa hii na imani yangu muda si mrefu tutaanza kujenga chuo kicho ili Watanzania wajifunze mbinu za kisasa za umwagiliaji maji mashambani na hivyo kuongeza maradufu uzalishaji mazao ya chakula na hata yale ya biashara,” anaongeza Balozi huyo. Amesema Iran kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika kilimo ikiwa ni pamoja na umwagiliaji maji mashambani, kulima na kuvuna kwa kutumia zana za kisasa za kilimo imeweza kufanikiwa kuzalisha mazao mara mbili hadi mara tatu kwa mwaka kutegemea na muda ambao zao husika linatumia kukua na kuweza kuvunwa. “Iran kwa sasa inazalisha sehemu kubwa ya mahitaji yake ya vyakula yenyewe na kuagiza kiasi kidogo sana kutoka nje kutokana na kufanikiwa kutumia kilimo cha kisasa. Lengo langu ni kuona kuwa Iran inashikana na Tanzania katika kubadili kilimo chake kupitia mpango wa Kilimo Kwanza,” anaeleza Balozi Muvahhedi. Anasema kuwa tayari serikali yake imetoa matreka 150 aina ya Power Tiller ili yaweze kuwapa nguvu wakulima wadogo wadogo bara na visiwani. Matreka hayo ambayo 50 yaligawiwa kwa Zanzibar na 100 yakatolewa kwa Tanzania Bara yana thamani ya Shilingi 4 milioni kwa kila moja, sawa na Shilingi 600 milioni kwa yote. Kwa upande wa elimu, Balozi Muvahhedi anasema kuanzia mwaka huu utaratibu uliokuwapo zamani wa baadhi ya Watanzania kwenda nchini Iran kusomea taaluma mbalimbali utarejeshwa. Na kwa kuanzia, mpango huo utahusisha Watanzania kumi watakaokwenda Iran kusomea taaluma mbalimbali.

Balozi Muvahhedi anataja baadhi ya kumbukumbu ambazo zipo katika majumba ya makumbusho nchini Iran kama mitumbwi mikubwa ambayo ilitumika kama nyenzo za uchukuzi, bidhaa zilizopatikana Afrika ya Mashariki kama mawe yenye thamani yaliyotumika kwa ujenzi na mapambo, vinyago na baadhi ya vifaa vya majumbani ambavyo vilikuwa vikitengenezwa kwa miti na wachongaji mahiri wa Afrika Mashariki.

Rais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Makamu wa Rais wa Iran Mhe. Rahimi (kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam. 9


Iran

Hafla ya kutoa misaada yafanyika Kituo cha Utamaduni cha Iran Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo, na sikieni, na t'iini, na toeni, itakuwa kheri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio waliofanikiwa. ( At-Taghabun: 16) maeneo husika. Naye Imam wa Msikiti wa Baabul Ilimi, Suleiman Abdallah, alisema wanakishukuru Kituo hicho, pamoja na Nyota Foundation kwa kuwapatia msaada huo kwa kuwa walikuwa na uhaba wa mabusati hayo. Aliwaomba wasiishie hapo bali waendelee kufanya hivyo kila wakati pale Mwenyezi Mungu anapowajaalia kwani misaada hiyo itasaidia zaidi kuwarahisishia Waislamu kufanya Ibada kwa utulivu na raha. Kwa msaada huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Zahra Foundation, Bi Fatma Ali Othman, yenye makao yake makuu maeneo ya Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, alitoa shukrani zake kwa Kituo cha Utamaduni cha Iran na Nyota Foundation kwa kusema: Mkurugenzi wa kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya “Napenda kutoa shukrani nyingi na za dhati kwa kituo Kiislamu ya Irani, Bw. Morteza Sabouri akiwa ofisini kwake cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Nyota Foundation kwa kutupatia msaada huu wa Zulia kwa ajili ya Na Maulidi S. Sengi Madrasatul Batul (AS). afla ya kutoa misaada ya mabusati ilifanyika katika Huo ni msaada uliofika wakati muafaka kwa ajili ya maandalizi Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Iran, Jijini Dar ya mwezi mtukufu wa Ramadhani , ambao pia utawasaidia es Salaam. Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Nyota watoto na kina mama ambao hufika pale (Madrasa ) kwa ajili Foundation nchini, jijini Dar es Salaam, wamekabidhi msaada ya kupata elimu na shughuli mbalimbali za kidini. wa mabusati kwa baadhi ya miskiti na taasisi nyingine nchini. Inshaallah Mwenyezi Mungu awalipe kheiri�.

H

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya msaada huo, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni, Bw. Morteza Sabouri alisema hayo ni maadalizi ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Alisema msaada huo unalenga kufika maeneo mbalimbali ikiwemo misikiti, shule na majumba ya watoto yatima ambapo mabusati hayo yatatumika katika nyumba hizo kwa ajili ya Ibada. Sabouri alisema miongoni mwa misikiti iliyopokea msaada huo kuwa ni pamoja na msikiti wa Baabul Ilimi uliyoko Kimara, Dar es Salaam na msikiti wa Hassanayn wa Mkoa wa Pwani. Alisema msaada huo haukomei kwenye mikoa hiyo miwili bali utaendelea katika mikoa mingine ambapo mabusati tayari yapo kinachosubiriwa ni hatua za kuyasafirisha katika 10 10

Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Bw. Sabouri akimkabidhi Ust. Suleiman Abdallah, msaada wa Busati, kushoto ni Sheikh Kaabi


Iran Iran

Vijana wawili washiriki mashindano ya Kimataifa ya usomaji wa Qur' an nchini Iran Tanzania kwenye mashindano hayo ni Saidi Idd Saidi na Omar Salumu ambapo sheikh huyo alisema safari hiyo imegharamiwa na serikali ya Iran ambapo vijana hao wakiwa nchini humo kwa siku saba watahudumiwa kila kitu bila malipo. Alisema Saidi anatarajiwa kushiriki katika ,mashindano hayo kwa upande wa kusoma kwa ‘Tajwid’ huku Salumu akishiriki kusoma kwa kuhifadhi (bila kuangakia kitabuni). “Leo tunawaaga vijana hawa na tunaamini kuwa watakwenda kufanya vizuri na watarudi wanang’ara kwa kupata ushindi,” alisema Sheikh Alna kuonesha ni muhimu kiasi gani. Pia Haadi. aliwaombea dua washiriki ili waweze kushika nafasi japo ya pili kama sio Al-Haad Salum anatarajia kuwa safari ya kwanza kwani alisema Tanzania hii vijana hao wataibuka na ushindi wa wanaweza sana, kwani mwaka jana kwanza ukilinganisha na nafasi ya waliweza kushika nafasi ya tano kati ya tano mwaka jana. Kheri na shime kwa wawakilishi wetu. nchi zaidi ya hamsini.

Sheikh Alhadi (wakwanza kushoto) baada ya kumkabidhi Tiketi ya Ndege Ustadhi Saidi Idi. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Irani, Bw. Morteza Sabouri akishuhudia tukio hilo

K

ituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran jijini Dar kilifanya Hafla fupi ya kuwaaga washindani wawili wa usomaji wa Qur'an. Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwa Sheikh wa Mko wa Dar es Salaam Sheikh Al-Haadi Musa Salimu kama mgeni Rasmi. Hafla ilifunguliwa kwa usomaji wa Qur ani na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sheikh Yahaya Foundation Ustadhi Muhammad Nassor. Baada ya kisomo, Mwenyeji wa shughuli Bw. Morteza Sabouri (Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran), aliwakaribisha wageni waalikwa. Kwanza alianza kwa kuwakaribisha kwa lugha ya kiswahili kwa kusema ''Karibuni sana''. Kisha akasema kwamba yeye binafsi, alifurahishwa sana na ujio wa Sheikh wa Mkoa Sheikh Al haadi Musa Salim kwani ujio wake ulilipa nguvu sana jambo hili

Akizungumza wakati wa kuwaaga vijana hao, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, AlHaadi Mussa Salum, alisema vijana hao wanapaswa kuwa makini k a t i k a mashindano hayo kwani wamebeba bendera ya nchi. Vijana walioiwakilisha

Mkurugenzi wa kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Irani, Bw. Morteza Sabouri akihojiwa na waandishi wa Habari kuhusu mashindano ya Qur' an. Kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Musa Salim 11


Makala Maalumu

Kuzaliwa kwa Imam Mah' di (ATFS) Na Sheikh Mulaba Swaleh Lulat

Nuru ya umaanawi ya uwepo wa Imam Mahdi AS imeenea hata katika wakati huu wa «ghaiba» wa kutokuwepo mtukufu huyo machoni mwa walimwengu. Miongoni mwa athari za nuru hiyo ni kwamba suala lenyewe tu la kusubiri kudhihiri kwa mwokozi huyo wa walimwengu kunafungua njia ya mustakbali bora

M

iongoni mwa itikadi ambazo waislamu wote kwa madhehebu zao wamekubaliana ni kwamba dunia haitamalizika na kiama kusimama mpaka aje Imam Mahdi kama khalifa wa Allah na kusimamisha serikali ya haki na uadilifu duniani kote baada ya kuwa imetawaliwa na dhulma na jeuri. Pamoja na kuwa suala hili lina nafasi ya pekee katika Uislamu, wengi Waislamu hawafahamu undani wake. Sababu za kisiasa na uadui dhidi ya umma ni miongoni mwa sababu zilizopelekea itikadi hii kusahaulika... Katika makala hii maalumu tutajitahidi kuweka wazi itikadi hii kwa hoja za Qur’ani, Sunnah na historia na kudhihirisha umuhimu wake wa pekee katika kujenga Ummah wa Kiislamu kama anavyotaka Allah na Mtume wake. A.- DALILI ZA QUR’AN NA SUNNAH Bila shaka Qur’an ni kitabu kinachobainisha na kupambanua kila kitu na mwongozo kwa walimwengu kama anavyosema Allah katika Surah Nahl, 16:89,: "…Na tumeteremsha kwako kitabu ambacho ni chenye kupambanua kila kitu na mwongozo na rehema na bishara njema kwa wanaojisalimisha". Kudhihiri Mahdi katika Akhirizzaman (zama za mwisho) ambaye atakayesimamisha Serikali moja ya Mwenyezi Mungu ulimwenguni kote na kwa uongozi wake kuleta ushindi wa Uislamu na haki dhidi ya kila aina ya dini na kuangamiza kila aina ya mfumo usio na msingi wa haki, ni tukio muhimu katika historia ya binadamu. Tukio kama hili lazima Qurani ilizungumzie. Hizi ni baadhi ya aya ndani ya Qur’ani zinazoashiria kuja kwa Imam Mahdi: 1.-Surah Anbiyaa, 21:105 ُ ِ‫الص ح‬ َ ََ َ ‫ُور ِم ْن ب َْع ِد ال ِّذ ْك ِر أ َ َّن األر‬ ‫الو َن‬ َّ َ‫ْض ي َِرثُ َها ِعبَا ِدي‬ ِ ‫وَلق ْد ك َت ْب َنا ِفي ال َّزب‬ “Na hakika tuliandika katika Zaburi baada ya ukumbusho kuwa: Ardhi (hii) watairithi waja wangu walio wema.” Aya hii inaashiria utabiri wa Mwenyezi Mungu kwa Mitume wake kwamba ardhi itarithiwa na waja wema na kwamba mapambano baina ya haki na batili yatamalizika kwa ushindi wa haki kutawala ulimwengu mzima. 2.- Surah Taubah, 9:32-33 , Surah Swaff, 61:9 ْ ُ ‫ين ُكلِّ ِه وَلَ ْو َكرِ َه مْال‬ ْ ‫ين حْالَقِّ لِ ُي‬ ‫شرِ ُكو َن‬ َ ْ ‫ُه َو الَّ ِذي أَر‬ ُ َ ‫س َل ر‬ ِ ِ‫سولَ ُه بِالْ ُه َدى وَد‬ ِ ‫ظ ِهرَ ُه َعلَى ال ِّد‬

12


Makala Maalumu “Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa mwongozo na kwa dini ya haki ili ishinde dini zote ingawa washirikina watachukia.” Said bin Jubayr, moja katika matabiina mashuhuri, alisema kuhusu tafsiri ya ‘kushinda dini zote’ inahusu zama za Mahdi katika kizazi cha Fatima (a). Ulamaa wa Tafsir wamekubaliana kwamba ayah hii inaashiria ya kwamba Uislamu ambao ndiyo dini ya haki lazima utashinda dini zote. Mifumo yote iliyobuniwa itapukutika na uislamu pekee ndio utaongoza dunia yote.

Hadithi hizo zinabainisha kwamba: Imam Mahdi (a) ni wa tisa katika kizazi cha Imam Husayn ibn 'Ali (a) Baba yake ni Imam Hasan 'Askari (a) Mama yake ni Bibi Nargis Khatun. Jina lake ni sawa na lile la Mtume (SAWW), na miongoni mwa sifa zake ni al-Mahdi, Al-Qaim, Al-Muntadhar... Atokana na kizazi cha Maimamu wa Ahlul Bayt (a) mmoja baada ya mmoja. Atazaliwa Samarra, na kuishi katika Ghaybah ndefu kama atakavyotaka Mwenyezi Mungu. Hatodhihiri mpaka baadhi ya alama zikamilike… Bishara hii bila shaka inamhusu Imam Atadhihiri wakati Dunia itakuwa imejaa Mahdi ambaye atadhihiri Akhirizzaman dhulma na atasimamisha haki na na kuongoza ushindi wa Haki dhidi usawa kote ulimwenguni. ya Batili na kusimamisha Serikali ya Atakapokuja, akiwa ameegemea Kaaba Mwenyezi Mungu kote duniani. atawaita wafuasi wake 313 na wote watahudhuria. Nabi Isa (a) atateremka 3.- Surah Zukhruf, 43:61 na kusali nyuma ya Imam Mahdi (a). َ ْ ْ َ َ‫م‬ َ َ ‫لس‬ ‫ون‬ َّ ‫ وَإِنَّ ُه ل ِعلمٌ ِل‬Imam wa Zama atasimamisha sheria ِ ‫اع ِة فال تت ُر َّن ِب َها وَاتَّ ِب ُع‬ َ ٌ َ َ ْ za kiislamu kote duniani na dunia ٌ‫صرَاط مُست ِقيم‬ ِ ‫هذا‬ “Na kwa hakika yeye ni elimu ya Kiyama itageuka kuwa kama Pepo. msikifanyie shaka na nifuateni: Hii ndio njia iliyonyooka. Baadhi ya wafasiri 1- Imam mahdi katika sihahu sittah wanasema ‘yeye’ ni dhamiri inayorejea (Vitabu Sita Sahihi vya Hadithi) kwa Nabi Isa (a). Ama Muqatil bin Imani ya Mahdi (a) ni itikadi ya kiislamu Sulayman na wengine kama Ibn yenye ushahidi wa Qur’ani na Sunnah. Hajar Haythamy, Shablanji, Safariini, Qanduzi, miongoni mwa ulamaa wakubwa wa kisunni wanathibitisha ayah hii inamhusu Mahdi (a) ambaye atadhihiri Akhirizzaman. Baada ya zama zake ndipo zitaanza ishara za Kiyama. B - DALILI ZA SUNNAH Maudhui ya Mahdi imezungumziwa kwa nafasi na umuhimu mkubwa. Zimepokelewa zaidi ya hadithi elfu moja (>1000) kutoka kwa Mtume (s) kwa njia mbali mbali, nyingi zikiwa ni kwa njia za masunni. Ulamaa wengi wa Kisunni wameandika vitabu mahsusi kuhusu Mahdi. Jumla ya hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (s) na maimamu wa Ahlul Bayt (a) zinazidi elfu tatu (3000).

Na kamwe si itikadi ya kishia kama vile baadhi ya wazushi walidai kwa maslahi yao ya kisiasa. Hizi ni baadhi ya hadithi za Mtume (s) kutoka katika Vitabu Sita Sahihi: 1-Kutoka kwa Ummu Salama anasimulia kwamba alimsikia Mtume (SAWW) akisema: “Mahdi (a) atokana na kizazi changu kwa kupitia kizazi cha Fatima (a).” Abu Dawud, An Nisai, Ibnu Maajah, Bayhaqy (AsSakhawiy, uk. 518) 2- Imam Ali (a) anasimulia kwamba Mtume (s) alisema: “lau kama ingebaki katika umri wa dunia ila siku moja, [basi Mwenyezi Mungu angeirefusha siku hiyo ili kumuwezesha ] mtu katika watu wa Nyumba yangu (Ahlul Bayt) [ ambaye ataitwa kwa jina langu] kuitawala Ardhi na kuijaza uadilifu kama ilivyojaa jeuri”. Abu Dawud, Ibn Maajah, Tirmidhy, Ahmad bin Hambal, Tabrani, Hakim,…, , (AsSakhawiy, uk. 522) 3-Kutoka kwa Abu Hurayra, Mtume (s) alisema: “mtakuwaje nyinyi pindi Isa bin Maryam (a) (atakapoteremka) atakapokuwa miongoni mwenu

Waumini wakiwa wakiwa katika maadhimisho ya kuzaliwa Imam Mah'di (AS) ambayo yalipambwa na msoma Qur' ani kwa kuhifadhi kutoka Pakistani Ustadhi Ali Khan. Maadhimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran jijini Dar es Salaam. 13


Makala Maalumu na Imam wenu akiwa baina yenu”. (Bukhary, Muslim.) 4- Miongoni mwa mambo ambayo ni ya yakini zama za kudhihiri Mahdi ni kuteremka Isa bin Maryam (a) na

kusali nyuma ya Imam Mahdi (a) na kuua ‘nguruwe’ na kuvunja ‘msalaba’. (AtTha’laby kuhusu tafsiri ya 43:61) Zipo hadithi nyingi ambazo zinaelezea kila zama za maisha ya Imam Mahdi (a). 2- Usahihi wa hadithi kuhusu Imam Mahdi (a) Uchunguzi wa hadithi zilizopokelewa kuhusu Imam Mahdi (a) unaonyesha kwamba: -Masahaba waliosimulia hadithi za Imam Mahdi (a) kutoka kwa Mtume (s) au ambao hadithi zao ni ‘mauquufa’ kwao na zenye hukumu ya kupandishwa kwa Mtume (s) ni wengi sana na lau ingethibiti kunukuliwa kutoka kwa asilimia 10 yao basi ingethibiti ‘tawaatur’ bila shaka. -Ulamaa na maimamu wakubwa wa hadithi wamenukuu hadithi kuhusu Imam Mahdi (a).Ni sahihi kabisa kusema kwamba hakuna mwanahadithi katika maimamu wa hadithi ambaye

hakutoa hadithi zinazohusu kudhihiri kwa Imam Mahdi (a) hapo Akhirizaman. Wengi wameandika vitabu mahsusi kumuelezea kwa mapana Imam Mahdi (a). -Ulamaa hao pia wamethibitisha kwamba hadithi hizo ni ‘Sahihi’ na ‘Mutawaatir’. Hawa ni baadhi yao na rai zao: 1- Al Imam Al Bayhaqiy, Ahmad bin Husayn (kaf. 458 H./1066 M.) Miongoni mwa maimamu wa hadithi. Miongoni mwa maFaqihi wakubwa wa kishafi‘i. Alizaliwa Khusrujard na kukulia Bayhaq na kufia Naysaabuur. Miongoni mwa vitabu vyake ni: Sunanul Kubra, Sunanus Sughra, Al Mabsuut… Alisema: “na hadithi kuhusu kutokeza kwa Mahdi, sanadi yazo ni sahihi zaidi” 2.- Al Qurtubiy Al Maaliky (kaf. 671H.) Ni miongoni mwa wenye kuthibitisha kwamba ni ‘mutawaatir’. Alisema kuhusu hadithi aliyoitoa Ibnu Maajah

Kwa idhini ya Allah Makala hii itaendelea Toleo lijalo

‫فثم يقوم القائم الحق منكم‬ * ‫وبالحق يأتيكم وبالحق يعمل‬ ‫صلوا على القائم المهدي من بهرت‬ *‫اياته وسما شانا على الرسل‬ ‫اتنسى حسينا وقد كاثرت‬ * ‫عليه العدا بالظبا واالسل‬ ‫أتنسى ابا صالح ثأركم‬ * ‫لطف فذاك لعمري اجل‬ ‫فعجل لتسحق جمع الطغاة‬ * ‫فانت لنا القائد الباسل‬ ‫اباصالح قم لمحو العصاة‬ ‫منقول منتدى الخالدون‬

14

‫ابا صالح قم لتشفي الغليل‬ * ‫ واجل‬... ‫ويهدأ قلب لنا‬ ‫اجل اننا في انتظار االمام‬ * ‫وذلك هو الحاكم العادل‬ ‫امام الزمان اتتك الجموع‬ * ‫ قائدنا الباسل‬... ‫النك‬ ‫ولدت لكي تنصر المسلمين‬ * ‫ الفاضل‬... ‫وانت امامهم‬ ‫فعجل لعلك تشفي السقام‬ * ‫ويحيا بك الميت الراحل‬ ‫وانت الكريم الذي يرتجى‬ *‫وفيك اختفى الجود والنائل‬ ‫اباصالح ياطبيب النفوس‬ * ‫بك استمطر البلد الماحل‬


Mkutano wa kilele (NAM) Inatoka Uk: 5 na nguzo ya kuunda jamii huru, zenye fahari, maendeleo na uadilifu na unaweza kuwa msingi wa ushirikiano wa kidugu kati ya mataifa mbalimbali. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa ushirikiano wa kimataifa unaojengeka juu ya msingi huo wa mawasiliano baina ya nchi kwa mujibu wa maslahi sahihi na ya pande zote utakuwa na maslahi ya kibinadamu na kuongeza kuwa, mfumo huo aali unakabiliana na mfumo wa kibeberu ambao katika karne za hivi karibuni madola ya kibeberu ya Kimagharibi na hii leo dola la kidhalimu la Marekani linaohubiri na kuuongoza. Ayatullah Ali Khamenei amesema malengo makuu ya Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote yangali hai licha ya kupita miongo sita sasa tangu jumuiya hiyo ianzishwe na akasema, kutimizwa kwa malengo hayo ni jambo linalotia matumaini na lenye matunda licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi. Amesema kuwa dunia iliopata ibra na tajiriba ya kihistoriaa ya kushindwa siasa za kipindi cha vita baridi na siasa za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja za baada ya kipindi hicho inaelekea katika mfumo mpya wa kimataifa unaozishirikisha pande zote na kutoa haki sawa kwa mataifa mbalimbali; na katika hali kama hii kuna udharura wa kuwepo mshikamano na umoja kati ya nchi wanachama wa NAM. Amesema kulindwa mshikamano na mfungamano kati ya wanachama wa jumuiya ya NAM katika mipaka ya thamani na malengo ya jumuiya hiyo ni miongoni mwa matunda makubwa. Ameongeza kuwa kwa bahati nzuri mustakbali wa matukio ya kimataifa unatoa bishara njema ya kijitokeza mfumo wa kambi kadhaa ambamo ndani yake kambi za kijadi za nguvu zitapoteza nafasi

Makala Maalumu

zao kwa majmui ya nchi, tamaduni na staarabu mbalimbali zenye mielekeo mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, na mabadiliko hayo yanazipa fursa nchi wanachama wa NAM ili ziweze kuwa na nafasi kubwa na yenye taathira katika nyanja za kimataifa na kutayarisha uwanja mzuri wa kuwepo uongozi wa kiadilifu na unaoshirikisha pande zote kote duniani. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, hali ya sasa ni fursa isiyokariri kwa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote. Amewaambia viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwamba kauli yetu ni kwamba usukani wa kuendesha masuala ya dunia haupaswi kushikwa na udikteta wa nchi kadhaa za Magharibi. Tunapaswa kuwa na uwezo wa kuzishirikisha pande zote kwa njia ya kidemokrasia katika uendeshaji wa masuala ya kimataifa na kudhamini suala hilo. Ayatullah Khamenei ameendelea kubainisha matatizo na muundo wenye dosari na usiofaa wa mfumo wa sasa wa kimataifa likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Amesema kuwa Baraza la Usalama lina muundo usiokuwa wa kimantiki, usio wa kiadilifu

na usio wa kidemokrasia. Mfumo wa baraza hilo ni udikteta wa wazi na hali iliyochakaa na kupitwa na wakati, amesisitiza Kiongozi Muadhamu. Amesema kuwa ni kwa kutumia muundo huo usiokuwa sahihi ndiyo maana Marekani na washirika wake wameweza kuitwisha dunia dhulma zao kwa kutumia vazi la maana nzuri na aali. Amesema kuwa, wanasema “haki za binadamu” wakikusudia maslahi ya nchi za Magharibi; wanazungumzia “demokrasia” na kuweka mahala pake uvamizi wa kijeshi katika nchi mbalimbali na wanazungumzia suala la kupambana na ugaidi huku wakiwashambulia kwa makombora na silaha nyinginezo watu wasiokuwa na ulinzi katika vijiji na miji mbalimbali. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria hatua ya Marekani na madola mengine ya kibeberu ya kuwagawa watu wa dunia kati ya watu wa daraja la kwanza, la pili na la tatu na akasema, roho za wanadamu katika Asia, Afrika na America ya Latini ni rahisi na zile za watu wa Marekani na Ulaya magharibi ni ghali. Usalama wa Marekani na Ulaya ni muhimu na usalama wa wanadamu wa maeneo mengine hauna umuhimu. Mateso na mauaji ya kigaidi

Katika Mkutano huo wa Tehran Tanzania iliwakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk. Muhammad Gharib Bilali Inaendelea Uk: 27 15


Makala Maalumu

Ramadhani mwezi wa Qur' an Na Salum Bendera

Kitabu kitakatifu cha Qur’ani ni muujiza mkubwa wa Mwenyezi Mungu na hati ya milele ya Uislamu. Kitabu hiki cha Mwenyezi Mungu licha ya kuweko hujuma na njama mbalimbali za kukipotosha lakini kimesalimika na njama zote hizo na licha ya kupita miaka na miaka lakini hadi leo kingali kinakwenda na wakati na kinawaongoza wanadamu katika njia nyoofu na kila mwenye kukifuata na kutekeleza kikamalifu mafundisho yake ataondoka katika kiza totoro la upotovu na kupata nuru ing'arayo ya uongofu.

S

ifa kuu na bora ya Qur’ani Tukufu ni kudhamini hidaya, uongofu na kumuongoza mwanadamu.. Kila mwenye kuifuata Qur’ani na mafundisho yake ataongoka na kuepukana na upotovu. Mwenyezi Mungu anasema katika katika Qur'ani kwamba: ‘’Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.’’ (Anfaal 8:24) Endapo mtu atairejea na kuitalii historia iliyojaa fakhari ya Uislamu, atapata athari nyingi zisizo na mithili na zenye mshangao za Qur’ani katika kuiongoza jamii ya mwanadamu. Wanahitoria wamefikia natija hii kwamba,

16

Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Bw. Morteza Sabouri (kushoto) akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete zawadi ya Qur' an ya Digital Ikulu Jijini Dar e Salaam alipomualika kwa ajili ya Futari siku ya Jumapili 29/7/2012

kabla ya kuja Uislamu, ulimwengu ulikuwa umezorota kielimu na kimaadili na watu walikuwa katika giza. Utumiaji mabavu, udikteta na dhulma ni baadhi tu ya mambo yaliyokuwa yametawala na kuenea katika mataifa mengi hasa baina ya Waarabu katika zama za ujahilia. Uporaji na unyang’anyi ulikuwa umeenea mno huku watu wakiwa wameshikamana na mila potofu na kufuata pamoja na kuabudu vitu ambavyo havikuwa na faida wala madhara kwao. Mwanamke alikuwa hathaminiwi hasa katika zama za ujahilia baina ya Waarabu. Wakati nuru ya Uislamu ilipoangaza, na Qur’ani ikaja katika medani na watu wakawa chini ya mafundisho aali na adhimu ya kitabu hicho kitakatifu na chenye kuleta uhai cha Mwenyezi Mungu, kulitokea mabadiliko makubwa katika jamii ya mwanadamu. Kwa muktadha


Makala Maalumu huo, Qur’ani ikawa imeleta maisha mapya na kuwatoa wanadamu katika ujahili wa kupindukia na kuwaleta katika maisha ya saada, izzah na utukufu. Ni hapo ndipo thamani ya mwanadamu ilipotambuliwa vyema na kuthaminiwa na hivyo kupelekea kuheshimiwa misingi ya akhlaqi na maadili na vile vile wanadamu kujishughulisha na kutafuta elimu yenye manufaa. Licha ya kuwa leo hii wale wenye mitazamo finyu wanajaribu kupuuza nafasi muhimu ya Qur’ani Tukufu katika kuyabadilisha maisha ya mwanadamu, lakini dhamiri zenye mwamko, insafu na uadilifu ulimwenguni zimekiri kuhusiana na nafasi hiyo adhimu ya Qur’ani.

kubainisha mitazamo na nadharia zake kuhusiana na jambo au elimu fulani, lakini haupiti muda mrefu, nadharia za mualifu na mtunzi wa kitabu hicho hupitwa na wakati, au hata mualifu mwenyewe kukiri kwamba, alikosea kutoa nadharia yake hiyo kuhusiana na jambo fulani. Amma kuhusiana na kitabu cha Qur’ani mambo ni kinyume kabisa. Licha ya kupita karne nyingi tangu kuteremshwa kwake na maendeleo makubwa yaliyopatikana katika uwanja wa elimu, si tu kwamba, Qur’ani haijapitwa na wakati na kuonekana kuwa ni kitabu cha kale, bali kimeonekana kuwa kinakwenda na wakati na hata katika baadhi ya mambo ambayo yanagunduliwa leo, Kwa hakika Qur’ani ni kitabu ambacho ukirejea Qur’ani unapata kuwa jambo kimebainisha na kuleta mambo ambayo hili lilikwishazungumziwa zamani na ni mahitaji ya lazima ya mwanadamu. kitabu hicho kisichojiwa na batili mbele Mwanadamu peke yake hawezi wala nyuma yake. kujiwekea sheria kuhusiana na mambo yote yanayohusu maisha yake, sheria Kitabu kitkatifu cha Qur’ani kikiwa na ambazo daima ziwe hai na zisizo na mipango maalumu na ratiba yenye mapungufu ndani yake na wala si malengo maalumu kimezungumzia mbalimbali. Qur’ani zenye kubadilikabadika. Mara nyingi maudhui tumeshuhudia mtu akialifu kitabu na imezungumzia kuhusu kumtambua Mwenyezi Mungu, viumbe, mbingu, ardhi na vilivyomo, historia ya waliotangulia, Manabii, akhlaqi (madili) haki za familia, muongozo wa kutawala na kuendesha serikali, mfumo wa kijamii, muamala, biashara na masuala ya kiuchumi na mambo mengine kadha wa kadha. Albert Einstein msomi na mwanafizikia wa Kijerumani anasema kuwa, ‘’Qurani sio kitabu cha aljebra na jiometri au hesabati, bali ni mjumuiko na mkusanyiko wa sheria ambazo humpeleka mwanadamu katika jiha na upande wa uongofu, njia ambayo, wanafalsafa wakubwa ulimwenguni wameshindwa kuianisha.’’ Mtambuzi na mtaalamu mmoja wa masuala ya Mashariki ya Kati wa Kijerumani anasema kwamba: ‘’ Qur’ani kwa mafundisho yake, ilikuwa na nafasi

muhimu ya kuinua fikra za Waislamu na ikawafanya Waislamu watutangulie katika kufikiri, utafiti, kubuni mambo na uvumbuzi katika masuala mbalimbali ya kielimu.’’ Wataalmu wa masuala ya kidini kwa upande wao wanaamini kwamba, Qur’ani imepita miujiza mingine yote. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana nyoyo zenye maandalizi huathirika haraka na maneno ya kitabu hicho adhimu. Gute Zeiten malenga na mwandishi wa Kijerumani anasema, Qur'ani ina taathira ya kustaajabisha, ambapo awali ibara zake zinaoneka kuwa ni nyepesi, lakini msomaji huathiriwa na kuvutwa haraka bila ya hiari yake na kuwa na uzuri usio na mwisho. Kwa miaka mingi makasisi wetu wametufanya tuwe mbali na uhakika wa Qur’ani tukufu pamoja na adhama yake.’’ Wanafikra wa Kiislamu nao kwa upande wao kila mmoja amezungumzia kwa namna yake muujiza wa Qur’ani. Allama Muhammad Hussein Tabatabai mwanafalsafa na mfasiri mkubwa wa Qur’ani katika zama hizi anasema: ‘’Qur’ani ni muujiza mkubwa katika balagha, ufasaha na hekima. Ni hazina na dafina yenye muujiza kwa wasomi na ni sheria ya kijamii kabisa kwa ajili ya watunga sheria. Kitabu hiki ni ubainisho wa siasa mpya na ambazo hazijawahi kushuhudiwa na wanasiasa.’’ Amma Jalaluddin al-Suyut msomi na alimu wa Kiislamu anasema kuwa, muujiza umegawanyika katika sehemu mbili. Muujiza wa kuhisika na wenye kuoneka na sehemu ya pili ni muujiza wa kiakili. Miujiza ya kuhisika na yenye kuonekana inawahusu Mitume waliotangulia. Amma Mtume Muhammad SAW akiwa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, muujiza wake ni wa kiakili yaani wa hoja za kiakili na wa milele na wala hauhusiani na jambo au tukio fulani. 17


Makala Maalumu

18


Cultural Centre of the Islamic Republic of Iran Dar es Salaam - Tanzania

Makala Maalumu

19


Jamii

Uislamu na Afya yako U Na: Sheikh Mulaba Saleh Lulat

islamu ni mfumo kamili aliyouweka Allah (swt) ili uwe ni muongozo kwa wanaadamu katika kila nyanja ya maisha yao iwe kiroho au kimwili.Allah (swt) alimuumba mwanadamu na kumjalia kuwa na kiwiliwili na roho. Uhai na maisha mazuri yanategemea afya njema ya mwili na roho. Ni dhahiri kabisa kwamba mwanadamu anahitaji afya njema ili aweze kufanya kazi na ibada yoyote ile. Kwa hiyo katika maisha ya mwanadamu suala la afya ni la msingi, kiasi kwamba neema hii ikitoweka, basi neema zote zimetoweka. Hakuna mtu binafsi, jamii au taifa, linalopiga hatua ya maendeleo iwe kielimu, kiuchumi au kisiasa ikiwa linakabiliwa na tatizo la afya. Kwa sababu hii tunakuta kwamba Qur’ani na pia Sunnah ya Mtume Muhammad (s) imezungumzia masuala ya afya na tiba kwa umuhimu wa pekee. Katika utangulizi huu tutanukuu baadhi ya aya na hadithi zinazozungumzia msingi huu muhimu wa mafanikio ya mwanadamu. 1-Uhai ni Amana ya Allah, lazima iheshimiwe na ihifadhiwe. Msingi wa Tawhiid unatufundisha ya kwamba muumbaji pekee ni Allah (swt). Yeye ndiye aliyeumba, na Yeye ndiye Mmiliki pekee wa uhai. Kwa sababu hiyo, Uhai ni amana na kila mtu ataulizwa

20

namna gani alivyo chunga amana hiyo. Ni haramu kabisa kwa mtu kujidhuru au kudhuru wengine. Ndani ya Qur’an, hizi ni baadhi ya aya zinazokataza kudhuru au kujidhuru kwa namna yoyote ile: Suratul Maida,5:32 Kuuwa nafsi kwa kudhamiria ni sawa na kuua watu wote, na kuhuisha nafsi ni sawa na kuhuisha watu wote Suratul Nisaa, 4:93 Kitendo cha kuua ni kibaya sana na hatari kwa uhai wa waliwengu kwa ujumla. Kwa sababu hiyo yeyote anayeua muumini kwa kudhamiria basi jaza yake ni ghadhabu na laana ya Allah

Uislamu ni mfumo kamili aliyouweka Allah (swt) ili uwe ni muongozo kwa wanaadamu katika kila nyanja ya maisha yao iwe kiroho au kimwili. Allah (swt) alimuumba mwanadamu na kumjalia kuwa na kiwiliwili na roho. Uhai na maisha mazuri yanategemea afya njema ya mwili na roho.

na kukaa milele motoni. Suratun Nisaa, 4: 29-30 Kama ilivyo haramu kuua, pia mtu hana haki ya kujiua na kukata uhai aliyopewa na Allah (swt). Surah Baqarah, 2:195 Katika ayah hii, Allah (swt) ameharamisha mtu kujidhuru kwa njia yoyote ile. Sheria nyingi zaKiislamu zinazohalalisha au kuharamisha zinasimama kwenye msingi huu muhimu. Hata katika masuala ya ibada. Hii ni baadhi ya mifano: ni haramu -mtu kufunga, kuhiji, kuoga (kwa mwenye janaba) ikiwa kufanya hivyo kutasababisha ugonjwa au kuhatarisha maisha yake. -kupuuzia kutumia dawa au kwenda hospitali na baadae kudhurika na ugonjwa. Suratul An’am, 6:151/ Suratul Israa, 17:31/ Suratul Takwir, 81:8 Katitka aya hizi Allah amekataza: - Mtu kumuua mtoto wake kwa sababu ya ufakiri, au kuogopa ufakiri -kuwaua watoto wachanga wa kike, kitendo cha kikatili kikifanywa zama za ujahilia, bara Arabu. Ama katika Sunnah ya Mtukufu Mtume (s), ikiwa ndiyo tafsiri ya Qur’an, haikuacha kutilia mkazo mafunzo ya kuheshimu uhai na viumbe vya Allah (swt). Hizi ni baadhi ya hadithi: 1-Miongoni mwa hadithi mashuhuri ni ile inasema: “kila mtu siku ya kiama ataulizwa kuhusu namna alivyotumia


Jamii 1. Mazingira Mwanadamu anaishi katika mazingira ambayo ndiyo yanampa mahitaji yake yote ya maisha. Mwanadamu kama khalifa wa Allah ndani ya ardhi anajukumu la kuheshimu na kutunza mazingira anayoishi ndani yake. Leo suala la uharibifu na uchafuzi wa mazingira kwa sababu ya maendeleo ya kisanyansi na kiteknolojia linathibitisha kwamba mwanadamu anaweza kujiangamiza ikiwa hataweza kuheshimu na kuchunga mazingira yake. maisha yake, alivyotumia elimu yake, namna alivyochuma mali yake, na namna alivyotumia afya yake”. 2-hata katika hali ya vita, Mtume (s) alihimiza mafunzo haya ya msingi kwa kusema: “ msiue watoto, wanawake na vikongwe. Msiwaguse watawa katika nyumba zao za ibada, msikate miti, wala kuua wanyama (ila kwa chakula). Msiwaue majeruhi na waliojisalimisha...” 3-katika ‘hijjatul wadaa’’ (hijja ya kuaga), Mtume akiwa Arafat alikumbusha na kuhusia msingi huu muhimu ambao ni nguzo ya ubinadamu, kwa kusema: “enyi watu, kama vile mnavyoutazama mwezi huu kuwa ni mtakatifu, na siku hii kuwa ni takatifu, na mji huu kuwa ni mtakatifu, basi hivyo hivyo tizameni uhai na mali na heshima ya kila muislamu kuwa ni amana takatifu...” 2-Uhai ni Amana ya Allah: Lazima itunzwe na ihuishwe Uhai unahitaji kutunzwa na kuhuishwa kwa kuchunga misingi bora ya afya. Afya njema ni Neema ambayo mwanadamu anatakiwa kuishukuru kwa kuitumia vyema. Ili kuwa na afya njema tunahitaji: - Kujiepusha na kila kinachoharibu na kudhuru afya

na shari anakuwa na wasiwasi, woga, hana subira, na akipata kheri ni mchoyo na mwenye kuzuia wengine (hali ambayo inazaa wasiwasi na matatizo zaidi). Ama yule mwenye imani, ibada, akamuogopa Allah na kuamini atalipwa siku ya Qiyama, anaishi kwa utulivu, amani na mapenzi kwa wanadamu wenzake. -Kujenga mwili kwa mazoezi Leo ni dhahiri kwamba mazoezi ni njia muhimu ya kujenga afya na kujiepusha na maradhi mengi hatari. Zipo aya kadha zinaonyesha fadhila ya kuwa 2. Chakula na lishe bora na nguvu, na kwamba wenye kufanya Kila mwanadamu anahitaji chakula jihadi ni bora kuliko wenye kukaa. bora ili aishi. Zaidi ya chakula, anahitaji Jihadi ya aina yeyote inahitaji nguvu za kuchunga adabu za kula. Bila shaka mwili na uwezo. Mwili kuwa na nguvu lishe duni ni tatizo, lakini tatizo la kula unahitaji mazoezi. kwa ulafi na israfu ni kubwa zaidi. Hizi ni baadhi ya aya kuhusu umuhimu wa Mtukufu Mtume (s) alitilia mkazo chakula na adabu za kula: suala la mazoezi na kujenga mwili. 1. Suratul Baqarah, 2:173 Katika moja ya hadithi anasema: Katika vyakula vilivyopo, mwanadamu “wafundisheni watoto wenu kuogelea, anahitaji kula vilivyo vizuri tu. kulenga mishale na kupanda farasi”. 2. Suratul Baqarah, 2:168 Vyakula vya kuliwa ni vile tu vilivyo halali na vizuri 3. Suratu Taha, 20:81 Katika kula na kunywa, lazima kujiepusha na kufanya israfu. 4. Suratul Rahman, 55:7-9 Kusimamisha mizani na kujiepusha na israf ni kanuni ya msingi katika maisha ya mwanadamu.

-kutafuta tiba pindi maradhi yanajitokeza Allah (swt) aliyeumba kila kitu, alikipa kila kiumbe umbile na mfumo maalum. Patholojia (hali ya ugonjwa) inasababishwa na fiziolojia (utendaji wa mfumo) kuwa na matatizo (kuingiliwa, kuvurugwa, kasoro...). Mfumo huo unapoingiliwa au kuwa na kasoro, lazima hali ya ugonjwa inajitokeza. Mtukufu Mtume (s) alifundisha kwamba 3. Hali ya kinafsi ‘kila ugonjwa una sababu na tiba. Kuwa na matumaini, utulivu, furaha na Hakuna ugonjwa isipokuwa Allah kutosheka ni hali inayojenga afya ya ameweka tiba yake.’ mwanadamu. Ama kuishi na wasiwasi, hasira, chuki, kukata tamaa, ni hali Aya nyingi zimezungumzia ubora wa inayoharibu afya na kusababisha baadhi ya vyakula na kutaja baadhi magonjwa hatari. Aya nyingi zimehimiza ya tiba kama vile Qur’an, funga, dua, kumuamini Allah na kumtegemea: asali... Suratul Maa’rij, 70:19-35 Aya hizi zinaonyesha hali mbili za InshaAllah, katika makala zijazo mwanadamu na matokeo yake. tutazungumzia kwa mapana nyanja Mwanadamu ni mwenye pupa, akifikwa mbalimbali za afya katika Uisalmu. 21 21


Jamii

Malezi mema kwa Watoto Na: Zahra Ally.

Kwa hali yoyote ile, ipo haja ya kutaja hapa kwamba, mazingatio ya Uislamu kwa watoto yameanza zamani na yanarejea nyuma zaidi ya miaka elfu moja na mia nne.Uislamu kwa mfululizo unaadhimisha na kuonyesha huruma yake kwa mtoto, si baada ya kuzaliwa tu, bali hata kabla ya kuzaliwa, na umeelezewa kwa makini haki zake.

W

akati wa utoto katika Uislamu umepewa picha ya ulimwengu mzuri wa furaha, uzuri, ndoto, mapenzi na ruya njema. Na aya za Qur'ani zinaonyesha mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa watoto, na ndipo akaapa Mwenyezi Mungu: "Naapa kwa mji huu, (wa Makkah). Na wewe utahalalishwa katika mji huu. Na (kwa) mzazi na alichokizaa." (90:1-3). Watoto wameelezwa katika Qur'ani kuwa ni bishara njema. Amesema Mwenyezi Mungu: "Ewe Zakaria tunakupa habari njema ya (kupata) mtoto jina lake ni Yahya…." (19:7). Pia watoto ni kiburudisho cha macho yetu. Amesema Mwenyezi Mungu: "Ewe Mola wetu, tupe katika wake zetu na watoto wetu watakaoyaburudisha macho yetu…."(25:74). Na watoto ni pambo la maisha katika ulimwengu huu: "Mali na watoto ni pambo la maisha ya duniani…." (18:16). Mtume (s.a.w.) anatudhihirishia ya kuwa ulimwengu wa utoto ni kama pepo, 22

pale aliposema: "Watoto ni vipepeo vya Peponi." Kuwatunza watoto ni jambo la lazima, na kuwapenda humleta mtu karibu na Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.) amesema: "Lau kama si watoto wanyonyeshwao, na wazee wanaorukuu (kwa kuswali) na wanyama walishwao mashambani, basi mngelipatwa na adhabu kali." Inaonyesha wazi kwamba huruma na uangalifu wa Mwenyezi Mungu kwa watoto ndiyo uliofanya Mwenyezi Mungu kuzuia adhabu juu ya watu wake. Kumjali mtoto hata kabla ya kuzaliwa: Kutilia maanani kwa Uislamu kuhusu malezi ya mtoto hakuanzi baada ya kuzaliwa tu, bali hata kabla hajaanza kupata umbo (tumboni) kwani Uislamu unamuamuru mtu kuoa mke mcha Mungu na mtulivu. Mtume (s.a.w.) amesema: "Jitahidi umpate mwenye kushikamana na dini, basi furaha zote ni zako." Uzuri, na utajiri si sifa pekee za kutosha kuchagua mke, sambamba


Jamii na sifa hizo, pia mke ni lazima awe na sifa zingine, kwa mfano kumpata aliye na dini, na awe ametoka kwenye nyumba yenye mema. Kwa sababu watoto wake atakaowazaa mke huyo watarithi tabia, adabu na mwenendo wake. Mwenyezi Mungu amekataza kuoa mwanamke mzuri tu asiye na tabia nzuri na nidhamu. Mtume (s.a.w.) amekataza: "Jihadharini na wanawake wazuri wenye sifa mbaya."

umepitia kutokana kwa muungano wa baba yake na mama yake, na ndipo Uislamu ukazitengeneza asili hizi kwa njia hiyo ili kumhifadhi mtoto awe ni kiumbe mwenye heshima na nidhamu, na hivyo kuepukana na upungufu wowote. Mara tu mtu anapoanza kufikiria kuoa na kutunza familia, Uislamu unamuongoza kupitia katika njia hizo.

ya wazazi na watoto wao, ni miongoni mwa uhusiano ulio imara na wenye daraja ya juu zaidi kuliko uhusiano wowote ule wa kibinaadamu. Uhusiano huo umehifadhiwa na Mwenyezi Mungu, naye amehakikisha kuwa unaendelea na kustawi; kwa sababu kufanya hivyo ni kuendelea kwa jamii ya binaadamu na uhai. Upendo wa wazazi kwa watoto wao hauna nafasi yoyote ya kutia Pendo la wazazi: shaka, kwani ni alama ya Mwenyezi Mtoto ni matokeo ya kimaumbile ya Mungu na ni neema Yake kubwa kwa Mtume (s.a.w.) ameweka mwongozo uhusiano imara wa wazazi, ubaba na walimwengu. kwa mwanamke ambaye yu tayari umama ni matamko mawili ambayo kuolewa: atafute mume mcha Mungu, Mwenyezi Mungu ameyazatiti kwa Mwenyezi Mungu amesema: "Na katika mwenye tabia za kidini, atakayeangalia ihsani na mapenzi Yake, akayatajirisha alama zake, ni huku kuwaumbia wake jamii yake kwa ukamilifu, kutekeleza na kuyapitia kwa maana ya kuungana zenu, kutoka miongoni mwenu ili mpate haki za mke, na kusimamia malezi watu wawili na kuendelea kuwa utulivu kwao, na akajaalia mapenzi na ya watoto. Mtume (s.a.w.) amesema: pamoja. Uhusiano wa karibu zaidi baina huruma baina yenu." (30:21).

Mtume (s.a.w.) mara kwa mara alikataza kuwapendelea watoto wa kiume zaidi ya wa kike pasi na sababu yoyote, kwa maana hiyo, ndiyo akaipa daraja la juu heshima ya watoto wa kike na akaipa nguvu thamani na staha yao. Amesema Mtume (s.a.w.): "Bora ya watoto wenu ni mabinti." Mtume (s.a.w.) alipopewa habari ya kuzaliwa bintiye Fatima (a.s.), nyuso za maswahaba zilionekana kuparama, Mtume (s.a.w.) akawaambia: "Mna jambo gani linalowahuzunisha? (kumzaa Fatima) ni kama kupata ua la mrehani niunusao, na riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu." "Atakapowajia mtu mtakayeridhishwa na dini yake, na tabia yake, basi muozeni, ama msipofanya hivyo, mtaleta fitina na ufisadi mkubwa duniani." Hii inaweza kuonekana kwamba Uislamu umezitangulia (kwa uvumbuzi) kanuni za kisayansi na elimu ya 'tabia zinazorithishwa' (Heredity) kwa kuonyesha umuhimu ulioko katika sehemu ya urithi wa tabia, na namna gani uteuzi mzuri wa watu wawili wanaooana utakavyopelekea kupata watoto ambao ni tuzo la Mwenyezi Mungu na furaha ya maisha. Kwa kuwa mtoto atachukua mwenendo wa wajomba na shangazi zake, asili ya undani ya baba yake na mama yake, na akajifunza kupitia kwa urathi ambao 23


Jamii Baadhi ya wafasiri wameeleza 'penzi' na 'huruma' hapa, kwa maana ya mtoto ambaye ameupa nguvu uhusiano baina ya wazazi na ameupa amani na usalama. Familia ndicho kitu cha kwanza ambacho Uislamu unakichukulia kuwa ni cha kwanza katika jamii ya watu. Familia huunda nyoyoni mwao penzi lisilo na kikomo kwa watoto wao, penzi hili ni nuru waliyopewa na Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.) aliwaambia maswahaba zake na huku akiwaonyesha mwanamke akasema: "Je Mnaweza kufikiria kwamba siku moja mwanamke huyu anaweza kumtupa mwanawe motoni?" Wao wakasema: "La", akasema: "Basi Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma zaidi kwa waja wake kuliko mama huyu alivyo na huruma kwa mtoto wake." Basi haya ni maumbile, na ni aina ya pendo la kiasili ambalo hapana yeyote awezaye kulizuia au kushindana nalo, na kwa sababu hii ndipo Mwenyezi Mungu akawausia wazazi kuwaangalia watoto wao. Mwenyezi Mungu amefanya kuwapenda watoto na kuwahurumia ni sehemu ya maumbile ya kiasili ya kibinaadamu yasioepukika. Pia ameziingiza hisia hizi thabiti ndani ya nyoyo za wazazi. Ni kwa ajili hii basi ndipo maelezo haya yote pamoja na wasia yameelekezwa moja kwa moja kwa watoto, kwa ajili ya kuwatendea wema na kuwapa heshima wazazi wao. Maelekezo haya amepewa mtoto ili kuzivutia hisia zake. Ni maelekezo ya hali ya juu ambayo yanategemeza uhusiano wa karibu na hisia ya kibinaadamu ambazo ndio sababu kubwa ya kuwepo kwetu duniani. Watoto wa kike: Kadri Uislamu unavyochukulia watoto kuwa ni kiburudisho cha macho yetu, 24

ni lazima hii idhihiri kwa vitendo na kwa njia zake. Usawa baina ya watoto hauna budi kutekelezwa hata katika kuwabusu. Uislamu unataka usawa ufanywe kulingana na maagizo yake matukufu. Siku moja Mtume (s.a.w.) alimwona baba ambaye alikuwa na watoto wawili, akambusu mmoja na kumwacha mwingine, kisha Mtume mtukufu akamuuliza: "Je huwezi kuwafanyia usawa?" Tukiangalia mvuto wa kumpendelea mtoto mmoja zaidi ya mwingine au jinsia moja (wa kike au wa kiume) zaidi ya nyingine, hii ni kinyume kabisa na maadili ya kiislamu, mila na fikra za usawa ambazo Uislamu umejengewa. Uislamu hautofautishi baina ya mwanamume na mwanamke, wala hautofautishi baina ya mvulana na msichana. Wote sawa, hapana yeyote ampitaye mwenzake ila kutokana na baadhi ya sifa alizonazo kitabia alizojipatia yeye mwenyewe, Mwenyezi Mungu amesema: "Mola akawakubalia (maombi yao), ya kwamba mimi sipotezi amali ya mwenye kutenda, awe ni mwanamume au mwanamke, baadhi yenu kwa baadhi nyingine‌."(3:195). Kwenda kinyume na misingi hii kunafuatia kwenda kinyume na fikra za usawa, maarifa, na haki. Kwa ajili hii, Uislamu unawaamuru

Waislamu kuwafanyia usawa watoto wao ili kwamba kusiwe na yeyote yule atakayekuwa na kinyongo au kusononeka. Kwa njia kama hiyo, Uislamu unazuia kuzagaa kwa chuki badala ya mapenzi, na kusema maudhi badala ya amani. Mambo haya iwapo yataendelea, hatimaye yataleta matatizo ya kinafsi, majonzi, na utengano, na haya yote huvunja hisia za moyo. Mtume (s.a.w.) mara kwa mara alikataza kuwapendelea watoto wa kiume zaidi ya wa kike pasi na sababu yoyote, kwa maana hiyo, ndiyo akaipa daraja la juu heshima ya watoto wa kike na akaipa nguvu thamani na staha yao. Amesema Mtume (s.a.w.): "Bora ya watoto wenu ni mabinti." Mtume (s.a.w.) alipopewa habari ya kuzaliwa bintiye Fatima (a.s.), nyuso za maswahaba zilionekana kuparama, Mtume (s.a.w.) akawaambia: "Mna jambo gani linalowahuzunisha? (kumzaa Fatima) ni kama kupata ua la mrehani niunusao, na riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu." Hapa Mtume (s.a.w.) kwa ubaba wake mtukufu alijaribu kubadilisha mawazo ya watu ya kuwapendelea watoto wa kiume zaidi ya watoto wa kike, tena hata aliwatanguliza watoto wa kike

Kwa kuwa upendo wa wazazi kwa watoto ni sehemu ya maumbile yao (wazazi) ya kiasili, ndipo ikawa hapana haja ya kuagizwa juu ya jambo hilo, kwa hivyo Uislamu umetilia mkazo zaidi umuhimu wa 'matunzo' ya watoto na ukaonya vikali wazazi wasizembee katika jambo hilo, ili familia na jamii ziweze kuishi kwa raha na furaha.


Jamii zaidi kwa kusema: "Mwenye kwenda sokoni, na kununua zawadi na kuwapelekea jamii yake, (familia yake) ni kama mtu aliyewapelekea sadaka wahitaji, basi aanze kuwapatia watoto wa kike kabla ya kiume." Mtume (s.a.w.) amejaribu kwa kadri awezavyo kuvutia penzi la watoto wa kike kama vile lilivyo penzi la asili kwa watoto wa kiume. Amesema: "Mwenye kuwalisha (kuwalea) watoto watatu wa kike ataingia Peponi." Akaulizwa: "Je wakiwa ni wawili?", akajibu: "Hata kama wawili", Akaulizwa: "Je mmoja", akajibu: "Hata kama ni moja." Matunzo ya mtoto: Matunzo ya mtoto wakati wa maisha yake yanahusiana na kumkinga kutokana na magonjwa na maradhi yaambukizayo na yote yale yawezayo kumpata mtu kutokana na uzembe, na kutojihusisha. Imesema Qur'ani: "Wala msijitie wenyewe katika maangamivu ‌." (2:195). Katika Aya iliyotangulia hapo juu, Mwenyezi Mungu amemkataza mwanaadamu kuchangia maangamivu yake mwenyewe kupitia kwenye vitendo ambavyo angevitenda kulingana na mwenyewe. Ijapokuwa mtu kujidhuru au kujiangamiza kunaonekana kwamba kunapingana na fikra zilizo timamu (yaani haiwezekani), lakini yaelekea kuwa kunaweza kutokea kutokana na uzembe ama kutojihusisha na kuchukua kinga zifaazo ili kuyachunga maisha yake mwenyewe.

hivyo hii ni pamoja na mtu kujihatarisha na magonjwa, maradhi yaambukizayo, ukosefu wa chanjo kutokana na maradhi yauwayo, na ukosefu wa uangalifu wakati wa shida na hatari. Vitendo hivyo vyote vilivyotangulia kutajwa vinachukuliwa kuwa ni kumchangia mtu katika maangamivu yake mwenyewe. Kwa sababu hiyo ndipo Uislamu ukaamuru kuchukua kinga zifaazo, na kutafuta matibabu kwa ajili ya magonjwa yote. Mtume (s.a.w.) amesema: "Mwenyezi Mungu hakuweka maradhi ila ameleta na dawa ya kuyatibu."

Mungu akawafanya wazazi kuwa ni dhamana kwa ajili ya kuwalinda watoto wao kutokana na magonjwa mbalimbali na hatari ambazo zingetishia maisha na makuzi yao. Imetajwa katika Hadith: "Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja ataulizwa juu ya kile akichungacho. Baba ni mlezi wa jamii yake. Mke ni mchungaji wa mali ya mumewe na watoto wake, na ndiye atakayeulizwa kuhusu akitunzacho. Mtumishi ni mtunzaji wa mali ya tajiri yake na ndiye atakayeulizwa kuhusu mali aitunzayo. Ndiyo, kila mmoja wenu ni mchungaji na ndiye atakayeulizwa juu ya anachokiangalia."

Sheria ya Kiislamu imewaamuru wazazi kuwa ni dhamana kwa maisha ya mtoto na makuzi yake. Kwa msingi wa kwamba, mtoto huchukuliwa kuwa ni dhamana waliyopewa, ambayo inapaswa kutunzwa nao kwani watakujaeleza mbele ya Mwenyezi Mungu (jinsi walivyoitunza amana waliyopewa). Mtoto mwanzoni mwa maisha yake huwa hajui hatari hasa ambazo zingehatarisha maisha yake. Kwa kuongezea ni kwamba yeye hawezi kujilisha na kuchunga maisha yake, kwa hivyo basi, ndipo Mwenyezi

Mbali na kuwa ni dhamana, ni wajibu wao pia kuwalisha watoto wao na kuwatosheleza mahitaji yao, hii inaweza kuwa kwa kuwachagulia kwa njia nzuri chakula chao, na kuwalinda kutokana na maradhi yote yatakayowadhuru. Miongoni mwa hatari zinazoweza kutishia maisha ya mtoto katika miaka yake ya mwanzoni ni uwezekano wa kupatwa na mojawapo ya maradhi yauwayo watoto kama: Ugonjwa wa kupooza (Polio), Surua (Ukambi), dondakoo (DPT au Diphtheria) n.k.

'Kujiangamiza' hapa, haina maana tu ya maangamivu yanayosababishwa na kiu, njaa, au mtu mwenyewe kujitoa mhanga kwa njia moja au nyingine kutokana na madhambi ayatendayo. 'Kuangamia' kwa maana hiyo, kunamaanisha kwamba kufanya ajizi kidogo tu, au kuzembea katika kujikinga, ndiko kujiangamiza. Kwa 25


Jamii

Kiigizo Na: Musabah Shaaban Mapinda

W

akati Waislamu wakishughulika na ujenzi wa Msikiti wa Mtume Muhammad s.a.w mjini Madina , walikuwa wakibeba mawe na vifaa vingine mbali mbali vya ujenzi ili kukamilisha jengo la msikiti. Mtume s.a.w naye kwa upande wake hakubakia nyuma katika kazi hiyo tukufu, bali alikuja akawa anabeba mawe.

mnacho kiigizo chema kwa Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, kwa yule mwenye kumtarajia Mwenyeezi Mungu na siku ya mwisho na akamkumbuka Mwenyeezi Mungu kwa wingi.” Qur 33:21.

Kuwalea Mayatima Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema: “Wanakuuliza (ewe Mtume) kuhusu mayatima. Waambiye: Kuwatendea Kwa bahati alikutana na sahaba mema ni bora. Na mkichanganyika nao aliyekuwa akiitwa Usaid bin Khudhair basi ni ndugu zenu…” Qur 2:120. ambaye alimwambia Mtume s.a.w kuwa: “Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu nipe Bila ya shaka uislamu ni utaratibu uliyo miye jiwe hilo nilibebe.” Bwana Mtume kamilika katika kila nyanja za maisha, s.a.w alijibu akamwambia: “Hapana kwani haukuwacha jambo lolote kubwa wewe nenda kachukuwe jiwe jengine.” au dogo isiipokuwa umelishughulikia. Ushiriki huu wa Mtume katika kazi ya Muundo wa jamii uliyomo ndani kubeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa ya uislamu, ni muundo unaojenga msikiti, ni dalili tosha inayotuonesha maingiliano kati ya makundi mbali mbali kuwa ujenzi wa msikiti ni jambo lenye ya wana jamii. malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, malipo ambayo Mtume s.a.w Muundo huo wa jamii ndani ya uislamu alikuwa akitaraji kuyapata kutokana na umepangika na hauna aina yoyote kazi hiyo. ile ya tofauti hasi. Kwa hali hiyo basi, kuwepo kwa mayatima ndani ya jamii Kadhalika kitendo hicho cha Mtume kwa kawaida linaweza likawa ni s.a.w ilikuwa ni njia ya kuwahamasisha jambo lenye kuleta mgawanyiko na wengine kuifanya kazi ile ya thawabu hasa inapozingatiwa kwamba kundi na ndiyo maana alimtaka Usaid bin la mayatima ni kundi lililo kosa walezi Khudhair kubeba jiwe jengine, badala au halina mtu wa kuwaliwaza na ya kumpokea lile alilokuwa amelibeba kuwaonesha upendo na huruma. yeye. Mwenyeezi Mungu anasema: “Bila shaka Sheria tukufu ya Mwenyeezi Mungu 26 26

imekuja ili kuweka utaratibu na mwongozo wa jinsi ya kuwalea na kuwatazama vyema mayatima hawa, bali imeandaa malipo mengi kwa yeyote mwenye kusimamia kazi ya kuwalea mayatima, awe mwana mume au mwana mke. Imamu Ali (a.s) Mlezi wa Mayatima . Katika mji wa Kufah pekee, Imam Ali bin Abii Talib alikuwa akiwalea mayatima zaidi ya mia mbili, na alikuwa akiwalisha kwa mkono wake mwenyewe na kuwaliwaza. Inasimuliwa kwamba; katika kipindi ambacho yule mal-uun Ibn Muljim alipompiga Imam Ali a.s kwa upanga wenye sumu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, tabibu aliyekuwa akimtibu Imam a.s aliagiza yaletwe maziwa amnyweshe ili kumpunguzia athari ya sumu mwilini mwake. Habari hizi zilienea mjini Kufah na mara ghafla mlangoni kwa Imam walifurika mayatima kwa wingi na kila mmoja akiwa amebeba maziwa na anataka kumpa Imam Ali a.s. Usia wa Imam Ali a.s kuhusu Mayatima. Hapo kabla tumeona ya kwamba Imam Ali a.s alikuwa mlezi wa mayatima. Historia inatuonesha pia kwamba jambo hilo


o chema inawapasa watu wote wake kwa waume kuisimamia kazi hiyo. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Maryamu Al ansari amesema: “Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu s.a.w amesema: Kwa hakika yatima anapolia Arshi tukufu (ya Mwenyeezi Mungu) hutikisika na Mola Mtukufu husema: Ni nani huyo anayemliza mja wangu niliye mnyang’anya wazazi wake wawili katika umri wake mdogo? Basi naapa kwa Utukufu Wangu hatamnyamazisha yeyote isipokuwa nitamuwajibishia pepo.” Kuna hadithi nyingine iliyosimuliwa Malipo ya wenye kuwalea Mayatima. Kuna hadithi nyingi za Mtume s.a.w na kutoka kwa Abu Ja’far a.s amesema Maimamu zinazowabashiria kheri nyingi kuwa: “Mambo manne akiwa nayo mtu, watu wanaofanya kazi ya kuwalea basi Mwenyeezi Mungu atamjengea mayatima, na zinaeleza kuwa jambo hilo mtu huyo nyumba peponi: Mwenye ni miongoni mwa mambo mema ambayo kumlea yatima, na mwenye kumhurumia alilisisitiza mno mpaka mwishoni mwa uhai wake hapa duiani akasema: “Allah Allah! Nakuhimzeni kuhusu mayatima, msiwaache na njaa na wala wasipotee mbele ya macho yenu (hali ya kuwa mnaona). Kwa hakika mimi nilimsikia Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu akisema: Yeyote mwenye kumlea yatima mpaka akaweza kujitegemea mwenyewe, basi Mwenyeezi Mungu amemuwajibishia pepo mtu huyo, kama alivyo wajibisha (adhabu ya) moto kwa mtu anaye kula mali ya yatima.”

Mkutano wa kilele (NAM) Inatoka Uk: 15

yanapofanywa na Marekani, Wazayuni na washirika wao huhalalishwa na kufumbiwa macho kwa kadiri kwamba vitendo viovu kabisa vinavyofanywa dhidi ya wafungwa wasiokuwa na ulinzi wala wakili wanaoshikiliwa bila ya kufikishwa mahakamani katika jela za siri za Marekani, haviamshi hisia zao.

Ayatullah Khamenei ameashiria maana isiyokuwa sahihi inayotolewa kwa baadhi ya mambo kama wasifu unaotolewa katika mfumo wa kibeberu wa mambo mazuri na yaliyomabaya na kusema, mabeberu hao wanayaita maslahi yao kwa jina la sheria za kimataifa na matamshi yao yasiyokuwa ya kimantiki wanayapachika jina la “jamii

ya kimataifa” na kuyatwisha mataifa mengine. Wanatumia kanali yao kubwa ya vyombo vya habari wanayoihodhi kwa ajili ya kubadili uongo na kuuita kuwa ni ukweli, batili wanaidhihirisha kuwa ni haki, dhulma zao wanaziita kuwa ni uadilifu; kila neno la haki linalofichua uongo wao wanaliita kuwa ni uongo na kila harakati ya kudai haki wanaipachika jina la uasi. Amesema hali hii yenye nakisi na dosari nyingi haiwezi kuendelea kuwapo na mataifa yote yamechoshwa na muundo huu wenye makosa wa kimataifa. Amesema kuwa Harakati ya 99 iliyoanzishwa na wananchi wa Marekani dhidi ya vituo vikuu vya utajiri na nguvu

mnyonge, na mwenye kuwahurumia wazazi wake wawili…..” Na ndani ya hadithi nyngine mashuhuri Mtume s.a.w.w anasema: “Yeyote mwenye kumlea yatima na akamlisha, basi mtu huyo atakuwa pamoja nami peponi mfano wa viwili hivi….” Mtume akaashiria kwa vidole vyake viwili cha kati na kile cha shahada. Shime enyi ndugu wa kike na wa kiume kuhusu jambo hili lenye malipo makubwa mbele ya Mwenyeezi Mungu. Itumiyeni vizuri fursa hii tukufu ya uhai mliyo nayo, kwani ni yenye kupita kwa haraka mno, kama ambavyo umri nao unapungua kadiri siku zinavyo kwenda. Basi je! Ni kitu gani tulicho kiandaa kwa ajili ya siku hiyo ya kutisha inayo tungojea?

nchini humo na malalamiko na upinzani wa wananchi wa nchi za Ulaya magharibi dhidi ya siasa na sera za kiuchumi za serikali katika nchi zao ni ishara ya kufikia kikomo subira na ustahamilivu wa mataifa mbalimbali mbele ya hali hiyo. Amesisitiza kuwa kwa msingi huo kuna udharura wa kutafutwa tiba ya hali hiyo isiyokuwa ya kimantiki. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa mshikamano madhubuti, wa kimantiki na wa pande zote wa nchi wanachama wa NAM katika kutafuta njia ya kutibu matatizo hayo una taathira kubwa. Ameashiria suala la ukosefu wa usalama na amani ya kweli kuwa ni miongoni mwa masuala tata ya Inaendelea Uk: 32 27


Vijana

Weledi juu ya Mustakbali wa Vijana Na: Hemedi Lubumba

Kizazi kipya mbinu mpya

K

una hotuba kutoka kwa Imam Ja’far ibn Muhammad as-Sadiq (a.s.) amesema: “Mtu ambaye anatambua kwa ukamilifu kile kipindi ambamo yeye anaishi, kamwe hatazidiwa na kiwewe (cha mambo yaliyomzunguka yeye).” Hii ina maana kwamba, yule mtu anayejua, ambaye anatambua na kuelewa ule wakati au kipindi ambamo anaishi, yeye hawezi kusumbuliwa na mkanganyiko au wasiwasi kuhusu mambo yanayotokea katika mazingira yake yanayomzunguka. Katika Hadith hii Imam (a.s.) ametwambia kwamba, “Kama mtu anatambua mazingira yake basi hatasumbuliwa kamwe na kuchanganyikiwa na kiwewe juu ya yale mambo ambayo yanamzunguka yeye, kiasi kwamba kwa wakati anaangalia na kusahau hata mikono na miguu yake mwenyewe, na akawa hana uwezo wa

28

kuzitumia nguvu na nishati yake mwenyewe wala hana uwezo wa kukusanya mawazo yake kuweza kutatua tatizo.” Hii kwa hakika ni Hadith mashuhuri sana. Viko vifungu vya maneno vingi vyenye umuhimu kama hiki katika Hadith hii ingawa sikuvihifadhi vyote, hata hivyo mstari mwingine unasema kwamba: “Mtu ambaye hatumii akili yake hatakuwa mwenye kufanikiwa, na yule mtu ambaye kwamba hana elimu hataweza kuitumia akili yake.” Maana ya akili ni nguvu au uwezo wa kuhitimisha na kuangalia jambo kwa mantiki na kuanzisha uhusiano kati ya hoja mbili – ikiwa na maana ya kutoa masharti juu ya jambo na kufikia uamuzi. Akili huchukua chanzo cha msukumo kutoka kwenye elimu na hivyo, akili ni taa ambayo mafuta


Vijana yake yanayoiendesha ni elimu. Hadith hii kisha inaendelea kusema: Hii ina maana kwamba, yeyote anayeelewa (jambo fulani), basi matokeo yake ni kwamba atakuwa na tabia njema na ya kuheshimiwa kwani matokeo ya hazina au bidhaa isiyo na thamani ya bei ni kupitia ile kazi inayoitanguliza mbele. Kwa hili ina maana kwamba tusiwe wenye kuiogopa elimu na ni lazima tusiifikirie elimu kuwa kama ni kitu ambacho ni cha hatari. Hata hivyo kwa hali halisi, sisi ni maana tofauti kabisa na udhihirisho wa Hadith hii, kwani wengi wetu hatutambui zile zama ambamo tunaishi. Tumejikalia chini tu, bila ya kutambua mazingira yetu, huku tukisinzia. Wakati mmoja tunakabiliwa kwamba, kwa mfano, ardhi hii ni lazima igawanywe na kwamba ardhi hii ni lazima isafishwe na kulimwa (ili kuifanyia matumizi). Bila kujua, inakuwa kana kwamba jambo hili (kuhusiana na usafishaji na ulimaji wa hiyo ardhi) linaanzisha machukizo juu yetu kwa vile hatuzitambui kabisa zile zama ambamo sisi tunaishi. Hatuna kule kuona mbali au makisio ya nini kinaweza kuja kutokea hapo baadae na hatukupanga lolote ili kuamua kwamba wajibu wetu utakuwa ni nini au ni kitu gani ambacho tunachotakiwa tuwe tunafanya.

Sisi, katika hali halisi, hatujui ni nini kinachoendelea katika ulimwengu huu na ni nini kinachofanyika nyuma ya mapazia. Tumekabiliana ghafla na suala la haki za kijamii za wanawake. Hapa, hatuna muda wa kutosha kufikiri juu ya hili na kuchambua vipengele vyake vyote ili kubaini umuhimu wake. Hivi wale wanaozitetea hizi haki za kijamii za wanawake wamedhamiria ukweli? Hivi kweli wanataka kuvutia mashabiki wengi?

mwote katika vipindi mbalimbali vya nyakati, na unatofautiana kulingana vile vikundi vya watu ambao tunafanya kazi nao. Hivyo, ni lazima tuondoe kabisa yale mawazo kutoka vichwani mwetu, kwamba kizazi hiki kipya lazima kiongozwe kwa kufuata zile taratibu zilizotumiwa na vizazi vilivyotangulia.

Kwanza kabisa, ni lazima tukielewe vizuri kabisa hiki kizazi kipya, na Kufahamu ni aina gani za sifa bainishi Au kuna faida nyingine yoyote na tofauti ambazo wanazo. Kuhusiana wanayonuia kuipata kutokana na na kizazi hiki, kuna namna mbili za kuibua masuala kama haya? Pamoja fikira ambazo ni za kawaida, na kwa na haya, yatakuja kutokeza mambo kawaida kuna njia mbili ambazo mengine yenye mashaka na mageni zinaweza zikashughulikiwa kwazo. yasiyojulikana kwetu sisi. Miaka sitini hadi mia iliyopita miongoni mwa nchi Kutokana na maoni ya baadhi ya nyingine za ulimwengu, hili suala watu, vijana hawa ni kundi la watu la kuwaongoza na kuwaelekeza ambalo lisilojali na fidhuli, ambao vijana lilikuwa limekwisha kufikiriwa, wamedanganywa na kupendezwa wamekuwa wakishughulika sana mno na tamaa zao duni. Wao ni wenye katika kulitafakari na kulijadili jambo kuabudu nafsi zao na wana maelfu hili kuliko sisi tulivyo sasa. (mengine) ya mapungufu. Hawa watu (wanaofikiria hivi juu ya kizazi hiki Ni nini ambacho ni lazima kifanyike? kipya) wakati wote wanawafinyia Kile ambacho ni muhimu sana kuliko nyuso na kila mara wanazungumza kuandaa mpango kwa ajili ya uongozi vibaya juu ya kizazi hiki. wa kizazi hiki ni kwamba, ni lazima tuziimarishe imani katika vichwa Hata hivyo, vijana hawa wanajiona vyetu wenyewe kwamba uongozi na wenyewe kama wako kinyume kabisa mwongozo wa kizazi hiki ni tofauti na hali (picha) hii. Vijana hawajioni katika utaratibu na mbinu zake, wenyewe kama ni wenye mapungufu

29


Vijana / Kazi yoyote. Wao wanajidhania kuwa ni sanamu (picha) la akili, sanamu la busara, sanamu la sifa za hali ya juu kabisa. Kizazi cha zamani kinafikiri kwamba kundi hili limeangukia kwenye utovu wa maadili na kwamba limetumbukia kwenye dhambi, ambapo hicho kizazi kipya kinadhani kwamba kizazi cha zamani wana akili nyepesi (mapunguani) na wajinga wasiojua kitu.

kwamba hawawaelewi! Kuzungumzia kwa kawaida jinsi mambo yalivyo, inawezekana kwamba kizazi kimoja kinaweza kukiona kizazi kilichotangulia kana kwamba ni watu wenye haki lakini pia inawezekana kwamba wakawaona kama waliopotoka.

Vijana wa Kisasa: Kizazi chetu kichanga cha leo kina sifa zote nzuri na kasoro kadhaa ndani yao. Kizazi hiki kina mlolongo wa uelewaji Kizazi cha zamani kinawaambia kizazi na hisia ambazo vizazi vilivyotangulia kipya kwamba wamejishusha wenyewe havikuwa nazo na kwa hiyo, sisi kwenye kuabudu nafsi zao wenyewe na lazima wakati wote tuwape faida ya wamekuwa watovu wa maadili, ambapo mashaka yao.Wakati huo huo, wao hicho kizazi kipya kinawaambia kizazi wanayo mawazo potovu na sifa bainifu cha zamani kwamba wao hawakijui za kimaadili za kinyume ambazo ni kile ambacho wanakisema na lazima ziondolewe kwenye tabia zao.

Haiwezekani kuziondoa sifa bainifu hizi kutoka kwao bila ya kuzingatia na kuziheshimu zile sifa nzuri ambazo vijana hawa wanazo – kwa maana ya kwamba, kule kuelewa kwao na hisia zao, na sifa bainifu zao bora na tabia hivyo ni lazima tuonyeshe heshima kwao kuhusiana na haya. Hakuna mwisho kabisa katika maisha. Katika vizazi vilivyotangulia, mawazo na akili za watu hazikuwa wazi kama za kizazi cha sasa. Hisia hizi na sifa nzuri hazikuwepo kwa watu wa siku za nyuma, na kwa hivyo ni lazima tuonyeshe heshima kwa vijana kwa ajili ya sifa zao bora – na ni Uislamu wenyewe, ambao umeonyesha heshima kwenye sifa bainifu hizi.

Umuhimu wa Kazi Katika Uislamu K utawakali kwa Mwenyezi Mungu na kumkabidhi Mola Mlezi kazi zetu, hakuna maana ya kwamba, mwanaadamu akae na kubweteka na kuacha kunufaika na suhula za kimaumbile zilizoko kwa ajili ya kufikia malengo yake. Kutawakali kwa Mwenyezi Mungu hakuna maana ya kutozishughulisha suhula zilizoko ambazo kimsingi ziko kwa ajili yetu. Mja muumini, hutawakali kwa Mwenyezi Mungu na hufadhilisha kumtegemea Mwenyezi Mungu Muumba badala ya kuwategemea asiyekuwa Yeye. Mwenyezi Mungu anazungumzia suala la kutawakali kwake katika Surat ya Aal Imran 30


Kazi aya ya 159 kwa kusema: «Na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.» Katika aya hii Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume Wake kwamba, baada ya kukata shauri kwa maana kwamba, baada ya kutathmini hali ya mambo na jambo lenyewe na kuandaa suhula za lazima, basi ifanye kazi hii hali ya kuwa unatawakali na kumtegemea Mola Muumba. Ayatullah Murtadha Mutahhari msomi mtajika katika ulimwengu wa Kiislamu anasema: «Mafuhumu ya kutawakali ni mafuhumu na fasili hai. Yaani kila mahala ambapo Qur'ani Tukufu inataka kumfanya mwanadamu afanye kazi na kumuondolea woga na hofu, humwambia kwamba, tawakali kwa Mwenyezi Mungu na umtegemee Yeye. Songa mbele na ufanye hima.» Mafuhumu na fasili ya kweli ya kutawakali ni hii kwamba, mwanadamu anapaswa kumfanya Mwenyezi Mungu Muumba kuwa tegemeo na kiegemeo chake cha pekee na kuwa na imani nae kamili na wakati huo huo atake msaada na kutumia suhula na nyenzo zote za kidunia ambazo ni nyenzo za kimaada kwa ajili ya kuboresha maisha yake. Na mtu mwenye kutawakali anapaswa kufahamu kwamba, nyenzo zote za kimaada ziko kwa ajili ya mwanadamu kwa mujibu wa mipango na irada ya Mwenyezi Mungu.

Hata alipofanikiwa kujenga kizuizi cha chuma baina ya watu na maadui alisimama na kusema: «Akasema: Hii ni rehema itokayo kwa Mola wangu Mlezi. Na itapofika ahadi ya Mola wangu Mlezi atauvunja vunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni kweli tu». Wakati mwingine mtu huandaa mipango kwa ajili ya kazi fulani na kuchunguza vizuri engo na pande za kazi hiyo na kidhahiri hupata natija kwamba, hakuna kizuizi cha kumfanya ashindwe kuifanya vizuri kazi hiyo na kufikia malengo aliyoyakusudia iwe ni kazi ya biashara au kazi ya ujenzi na kadhalika. Hata hivyo hutokea tukio dogo tu ambalo huja kuvuruga mahesabu yake yote na hivyo kuifanya kazi yake kutokuwa na natija. Hii inatokana na kuwa, elimu ya mwanadamu ina mipaka na mwanadamu hana habari na matukio au mishkili tarajiwa. Zaidi ya hayo, wakati mwingine mwanaadamu anapoamua kufanya kazi fulani au anapokata shauri kuiacha huwa hana habari ya maslahi yaliyoko katika kazi hiyo. Kwa mtazamo wa dini, mwanaadamu hukabiliwa na hakika yenye matumaini nayo ni kwamba, Mwenyezi Mungu ndiye mtawala mutlaki wa ulimwengu

na hekima na elimu isiyo na kikomo iko kwake. Mola Muumba ana uwezo wa kufanya kazi zote na vile vile ana ufahamu juu ya maslahi ya kweli ya waja wake. Hatua ya mja ya kutawakali kwa Mwenyezi Mungu mwenye sifa hizi humfanya ujudi wake ufungamane na nguvu isiyo na kikomo. Mja anayetawakali kwa Mwenyezi Mungu hushuhudia na kuona nguvu za Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu katika kazi na mambo yake na hunufaika na nguvu maalumu. Marhumu Allama Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai mfasiri mkubwa wa Qur'ani Tukufu anaandika hivi kuhusiana na kutawakali kwa Mwenyezi Mungu: «Wakati mwingine mwanadamu akiwa nia ya kufikia lengo lake fulani, huingia katika medani na kuona kuwa anayo mahitaji yote ya lazima, lakini baadhi ya sababu za kiroho kama kuwa na irada inayotetereka, woga, pupa na tajiriba ndogo huingia baina yake na kazi husika. Kama mtu atatawakali kwa Mwenyezi Mungu katika mazingira kama haya, irada yake huwa na nguvu, azma yake huwa thabiti na vizingiti vya kiroho huondoka.

Katika mazingira kama haya kutawakali kwa Mwenyezi Mungu hakuwezi kuwa sababu na hoja ya kuacha kufanya kazi na hivyo kuukumbatia uvivu. Katika Qur'ani Tukufu tunasoma kisa cha Dhul Qarnein na kuona jinsi gani alivyotumiwa nyenzo zote za kimaada alizopatiwa na Mwenyezi Mungu katika kupambana na dhulma na uonevu. 31


Kazi / Historia Mkutano wa NAM

Mkutano wa kilele (NAM) Inatoka Uk: 27 dunia ya leo. Amesema kuwa suala la kutokomezwa silaha za maangamizi ya umati na zinazosababisha maafa ni dharura na takwa la watu wote na nchi zinazojilimbikizia silaha za kuwaangamiza wanadamu katika maghala yao ya silaha hazina haki ya kujitangaza kuwa ni vinara wa usalama na amani duniani.

32 32

katika matumizi mbalimbali muhimu ya nchi na mataifa yao na kutotegemea nchi nyingine katika kutumia haki hiyo. Ayatullah Ali Khamenei ameashiria harakati inayotia shaka ya nchi kadhaa za Magharibi zinazomiliki silaha za nyuklia na zilizotumia silaha hizo kwa ajili ya kuhodhi uzalishaji na uuzaji wa fueli ya nyuklia na akasema: “Mchezo mchungu wa kuchekesha wa zama hizi Ayatullah Khamenei amesema nchi ni kuwa, serikali ya Marekani ambayo zinazomiliki silaha za nyuklia hazina ndiyo inayomiliki silaha nyingi zaidi za azma ya kweli ya kuondoa zana hizo maangamizi na za nyuklia na silaha za maangamizi katika sera zao za nyingine za mauaji ya halaiki mbayo kijeshi. Ameongeza kuwa fikra yoyote pia ndio nchi pekee iliyotumia silaha inayodhani kuwa silaha za nyuklia ni hizo dhidi ya binadamu, hii leo zinataka wenzo wa kuondoa vitisho na kigezo kubeba bendera ya kupinga uenezaji muhimu cha nafasi ya kisiasa na wa silaha za nyuklia. kimataifa cha nchi inayomiliki silaha hizo haiwezi kukubalika. Amesema kuwa Marekani na washirika wake wa silaha za nyuklia hazidhamini usalama Kimagharibi hawawezi kustahamili na amani na wala si alama ya uwezo kuona nchi zinazojitegemea zikitumia wa kisiasa bali ni tishio kwa viwili hivyo; nishati ya nyuklia kwa matumizi ya na matukio ya muongo wa 90 wa karne amani na zinapiga vita hata suala ya 20 yameonesha kwamba, kumiliki la uzalishaji wa fueli ya nyuklia silaha hizo za nyuklia hakuwezi kulinda kwa ajili ya kutengeneza madawa utawala kama Urusi ya zamani. (Radiopharmaceutical) na matumizi mengine ya kiraia.” Amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakutambua kutumia silaha za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi nyuklia, za kemikali na kadhalika kuwa ya Kiislamu ameashiria visingizio vya ni madhambi makubwa yasiyosameheka uongo vya Marekani na nchi kadhaa na kwa msingi huo ilitoa kaulimbiu ya za Magharibi kuhusu wasiwasi wao juu “Mashariki ya Kati isiyokuwa na silaha ya eti uzalishaji wa silaha za nyuklia za nyuklia” na inashikamana nayo nchini Iran na akasema: “Ninasisitiza barabara. kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina nia ya kutengeneza silaha za nyuklia Hata hivyo Kiongozi Muadhamu wa na kamwe haitafumbia macho haki ya Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza taifa lake ya kutumia nishati ya nyuklia kuwa hatua ya Jamhuri ya Kiislamu kwa matumizi ya kiraia. Kaulimbiu ya Iran ya kutoa kaulimbiu hiyo haina yetu ni ‘Nishati ya Nyuklia kwa Ajili maana ya kufumbia macho haki ya ya Wote, na Silaha za Nyuklia si kwa kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo Yeyote’. Tunashikamana barabara ya kiraia na kuzalisha fueli ya nyuklia. na mambo hayo mawili.” Ayatullah Amesema, kwa mujibu wa sheria za Khamenei amesema kuwa kuvunja kimataifa, utumiaji wa nishati ya nyuklia mzingiro wa nchi kadhaa za Magharibi kwa malengo ya amani ni haki ya nchi katika uzalishaji wa nishati ya nyuklia zote na watu wote wanapaswa kuwa sambamba na kuheshimu makubaliano na uwezo wa kutumia nishati hiyo ya kuzuia uzalishaji na uenezaji wa

silaha za nyuklia (NPT) kuna faida kwa nchi zote zinazojitegemea zikiwemo nchi wanachama katika Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote. Ameongeza kuwa tajiriba na uzoefu wa miongo mitatu ya kusimama kidete mbele ya madola ya kibeberu na mashinikizo ya pande zote ya Marekani na waitifaki wake umeifikisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kiwango cha kuamini kwamba, mapambano ya taifa lolote lenye umoja na azma kubwa yanaweza kushinda uhasama na uadui wote na kufungua njia yenye fahari ya kufikia malengo makubwa. Amesema kuwa maendeleo ya pande zote ya Iran katika kipindi cha miongo miwili ya hivi karibuni tena chini ya vikwazo na mashinikizo ya kiuchumi na hujuma za kipropaganda ni kielelezo kikubwa cha matokeo ya kusimama imara kwa taifa la Iran. Ameongeza kuwa, vikwazo ambavyo waropokaji wanaviita kuwa ni vya kudumaza, si tu kwamba havikuidumaza Iran wala havitaweza kufanya hivyo, bali pia vimezidisha kasi ya hatua za Iran, vimeimarisha hima ya taifa na kutia nguvu imani ya wananchi wa Iran kwamba uchambuzi wao ulikuwa sahihi na vikwazo hivyo vinaimarisha zaidi ari na azma ya taifa hilo. Amesisitiza kuwa taifa la Iran limekuwa likishuhudia kwa macho msaada wa Mwenyezi Mungu katika changamoto hizo. Suala jingine lililozungumziwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika hadhara ya viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa nchi wanachama wa NAM ni kadhia muhimu sana lakini inayoumiza jamii ya mwanadamu yaani kadhia ya Palestina. Ayatullah Khamenei amezungumzia njama hatari za nchi za Magharibi zikiongozwa na Uingereza katika kughusubu nchi inayojitegemea na


MASHARIKI HistoriaYA KATI yenye utambulisho wa wazi wa kihistoria ya Palestina na jinai za viongozi wa kisiasa na kijeshi wa utawala ghasibu wa Kizayuni katika kipindi cha zaidi ya miaka 65 iliyopita. Amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umeanzisha vita vya maafa makubwa, kuwaua wananchi, kukalia kwa mabavu ardhi za Kiarabu, kupanga ugaidi wa kiserikali katika Mashariki ya Kati na duniani na umekuwa ukifanya mauaji ya kigaidi, vita na shari nyinginezo kwa miaka mingi sasa. Pia unalituhumu taifa la Palestina linalopigania haki zake kuwa ni magaidi huku kanali ya vyombo vya habari vya Kizayuni na vyombo vingine vya habari vya Magharibi na vibaraka vikikariri uongo huo mkubwa. Vilevile viongozi wa kisiasa wanaodai kushika bendera ya kutetea haki za binadamu, wanaunga mkono utawala huo ghasibu kwa kufumbia macho jinai zake za kutisha na kudhihiri kama wakili wa upande wa utetezi. Amesisitiza kuwa njia zote zilizopendekezwa na kutekelezwa na nchi za Magharibi na washirika wao kwa ajili ya kutatua kadhia ya Palestina ni makosa matupu na haziwezi kufanikiwa. Ayatullah Khamenei ameashiria tena njia ya kiadilifu na ya kidemokrasia ya utatuzi wa kadhia ya Palestina iliyopendekezwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na akasema, kwa mujibu wa njia hiyo, Wapalestina wote sawa wale wanaoishi katika ardhi ya nchi hiyo au wale waliofukuzwa nchini kwao na kukimbilia nchi nyingine lakini wamelinda utambulisho wao wa Kipalestina, Waislamu, Wakristo na Wayahudi, wote wanapaswa kushiriki katika kura ya maoni itakayosimamiwa kwa uangalizi mkubwa na kuchagua muundo wa mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo; hapa ndipo amani itakapopatikana. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya

Kiislamu ameendelea na hotuba yake katika hadhara ya viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa jumuiya ya NAM kwa kutoa nasaha kwa wanasiasa wa Marekani ambao daima wamekuwa wakiutetea na kuulinda utawala ghasibu wa Israel.

tutazame kwa jicho la ibra kushindwa kwa tajiriba ya kambi ya ukomunisti miongo miwili iliyopita na kufeli kwa siasa zinaoitwa za demokrasia ya kiliberali za Magharibi katika kipindi cha sasa. Tunapaswa kuyatambua matukio ya kuporomoka madikteta waliokuwa tegemezi kwa Marekani na washirika Amewaambia utawala huo wa utawala wa Kizayuni wa Israel umewasababishia matatizo mengi, huko kaskazini mwa Afrika na vilevile kuwaingiza katika gharama kubwa na mwamko wa Kiislamu katika nchi za kuchafua sura yenu mbele ya mataifa ya eneo hilo kama fursa kubwa.� Mashariki ya Kati huku ukiwatambulisha kama washirika katika jinai za Mwishoni mwa hotuba yake mbele ya Wazayuni maghasibu. Hebu chunguzeni hadhara ya viongozi na maafisa wa ngazi pendekezo la Jamhuri ya Kiislamu za juu wa nchi 120 wanachama katika ya Iran kuhusu suala la kuitisha kura Harakati ya Nchi Zisizofungamana na ya maoni na jiokoeni kutoka kwenye Siasa za Upande Wowote, Kiongozi wa mkwamo usiokwamuka wa sasa kwa Mapinduzi ya Kiislamu ametilia mkazo kuchukua uamuzi wa kishujaa. udharura wa kuundwa sekretarieti madhubuti ya harakati hiyo na akasema, Hapana shaka kwamba watu wa tunaweza kutafakari kuhusu suala la Mashariki ya Kati na wanafikra huru kuzidisha nafasi ya kisiasa ya jumuiya kote duniani watakaribisha hatua hiyo. ya NAM katika uendeshaji wa masuala Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, ya kimataifa; tunaweza kutayarisha Ayatullah Ali Khamenei amezungumzia hati ya kihistoria kwa ajili ya kufanya umuhimu wa mkutano wa viongozi mabadiliko katika uendeshaji huo na wa nchi wanachama katika Harakazi kutayarisha nyenzo zake za utekelezaji ya Nchi Zisizofungamana Siasa za na tunaweza kuanzisha harakati ya Upande Wowote wa Tehran katika kuelekea kwenye ushirikiano mkubwa kipindi cha sasa na akasema, kwa wa kiuchumi na kubuni kigezo cha kushirikiana na kutumia vyema uwezo mahusiano ya kiutamaduni baina yetu. wao mkubwa, wanachama wa jumuiya hiyo wanaweza kuwa na mchango wa kihistoria utakaokumbukwa milele katika kuokoa dunia kutokana na ukosefu wa amani, vita na ubeberu. Amesema sharti la kufikiwa lengo hilo kubwa ni kuwepo ushirikiano wa pande zote kati ya nchi wanachama na kupeana uzoefu na tajiriba. Amesisitiza kuwa: “Tunapaswa kuimarisha azma zetu, kuendelea kuwa waamininifu kwa malengo yetu na tusiogope hasira za madola ya kidhalimu wala kughurika na tabasamu zao. Irada na matakwa ya Mwenyezi Mungu na kanuni za maumbile zitatuunga mkono, na 33 33


Mapishi

Vipopoo Vya Uwanga Na: Fatma Ali Othmani

Mahitaji: Uwanga ½ kilo Sukari kilo 1 Nazi 6 Hiliki kiasi

madonge madogo madogo halafu uyasokote. Baadae ukate vipopoo vidogo vidogo, kama chembe za mbaazi au hata vidogo kuliko hivyo.

3. Teleka sufuria utie maji, yakichemka vitie hivyo vipopoo vyote uache Namna ya kutayarisha na kupika 1. Uchunge (chekecha) uwanga uwe vichemke kidogo halafu vimimine kwa safi. Kuna nazi uchuje tui zito mbali na haraka katika chujio yatoke maji yote. jepesi mbali. Menya hiliki na uitwange. 4. Teleka tena sufuria utie tui jepesi, 2. Kanda uwanga kwa maji ya moto sukari, na hiliki upike na huku kisha ufinyange donge. Katakata unakoroga. Tui likianza kuchemka,

vitie vipopoo vyote uwe unavikoroga mpaka viwe vimeshakauka vizito vya kiasi viepue. Kupakua kwake tafuta sahani ndogo ndogo za shimo au vibakuli vidogo vidogo uvitie na baadae uviweke kwenye upepo vipate kuganda. Zingatio: Mlo huu ni maalum kwa ajili ya Futari katika mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini pia huliwa hata katika masiku mengine kama ukipenda.

Wali wa Nazi kwa Mchuzi wa Nyama Ng’ombe na Mchicha Wali Wa Mpunga

msongo (bunches) Bizari ya mchuzi (simba 2) kijiko 1 cha chai Namna ya kutayarisha na kupika Ndimu 1 kamua Mafuta ¼ kikombe 1. Osha mchele kisha 2. Bandika tui jikoni likichemka tia Chumvi kiasi mchele na chumvi. 3. Funika uchemke, tui likikauka wacha Namna ya kutayarisha na kupika: moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa 1. Weka nyama katika sufuri, tia tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi, ndimu na chemsha juu yake. nyama hadi iwive na ibakie supu yake kidogo. Mchuzi wa nyama Ng’ombe 2. Weka mafuta katika sufuri nyingine, Nyama kilo 1 Kitunguu thomu na tangawizi ilosagwa kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi tia majani ya mchuzi endelea kukaanga Vijiko 2 vya supu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi Viazi / mbatata 2 Kitunguu maji kilokatwakawa (slice (golden brown) 3. Tia nyanya/tungule, viazi/mbatata, ndogo) 2 Nyanya / tungule 4 endelea kukaanga mpaka nyanya ziive. Nyanya kopo vijiko 3 vya supu Majani ya mchuzi/mvuje 6 4. Tia nyama na supu yake kisha tia nyanya ya kopo, kotmiri, bizari ya Kotmiri ilokatwakatwa 3 34

mchuzi, chumvi uache mchuzi kidogo katika moto hadi viazi viive vikiwa tayari. Mboga Mchicha. Mchicha 4 michano/vifungu Kitunguu 1 Kitunguu thomu 3 Nyanya/tungule 2 Tui la nazi zito 1 kikombe cha chai Chumvi Namna ya kutayarisha na kupika: 1. Osha mboga iache ichuje maji. 2. Ikatekate kisha weka katika sufuria. 3. Katika kitunguu maji, kitunguu thomu kisage au kikatekate kidogodogo (chopped), nyanya. 4. Weka jikoni ipikike kwa maji yake na mvuke. 5. Tia tui endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi ikaribie kukauka ikiwa tayari.


MASHARIKI YA KATI

35


Maoni / Barua

FOMU YA MAONI Ili kuliboresha Jarida hili tafadhali jaza fomu hii ili utoe maoni yako kuhusu muundo mzima wa Jarida hili, kukosoa, kushauri au mapendekezo yoyote uliyonayo, bila shaka tutayafanyia kazi Maoni yako. Tutumie kupitia anuani zilizoko nyuma ya Jarida hili Jina kamili........................................................................................................................ Unapoishi (Mkoa / Wilaya / Kijiji)…………………………………………………….…...............… Sanduku la Posta………………………………………………………………………............................. Barua Pepe (E-mail)………………………………………………………………………….................…. Namba ya Simu…………………………………………………………………………............................ Weka alama katika moja ya masanduku utakayochagua A: Muonekano wa Jarida / Picha Mpangilio: Nzuri Nzuri kiasi Nzuri sana Mbaya Mbaya kiasi Mbaya sana B: Sifa za Jarida / Makala zote: Nzuri Nzuri kiasi Nzuri sana

Mbaya

Mbaya kiasi

Mbaya sana

C: Baadhi ya Makala: Nzuri Nzuri kiasi

Mbaya

Mbaya kiasi

Mbaya sana

Nzuri sana

Tumia nafasi hii kueleza chochote ulichonacho kuhusu Jarida hili .......................................................................................................................................... .......................................................................................................................................... .......................................................................................................................................... .......................................................................................................................................... .......................................................................................................................................... .......................................................................................................................................... .......................................................................................................................................... .......................................................................................................................................... .......................................................................................................................................... Mwisho tunatoa nafasi kwa yeyote mwenye Makala nzuri (za Dini, Jamii, Utamaduni Historia za Kiislamu nk.) atutumie na atapata zawadi kutokana na uzito wa makala. Pia tunakaribisha Barua za wasomaji ikiwa na anuani na picha ndogo (Passport Size) (kwa mwenye kutaka makala itoke na picha yake) Tutakuwa na utaratibu wa kukutumia Nakala (moja) ya Jarida hili kwa njia ya Posta. Pia unaweza kusoma Jarida hili kupitia mtandao (Web Site) kwa anuani hizi:http://issuu.com/al-hikma/docs/al-hikma_26 Asante kwa ushirikiano wako na kuchagua Jarida hili. 36


Profile for Maulidi Saidi

Al-hikma  

Al-Hikma ni Jarida Maridhawa la maarifa ya Kiislamu ambalo hutoa mwangaza kwa wasomaji wa afrika mashariki na nchi zingine zizungumzazo kis...

Al-hikma  

Al-Hikma ni Jarida Maridhawa la maarifa ya Kiislamu ambalo hutoa mwangaza kwa wasomaji wa afrika mashariki na nchi zingine zizungumzazo kis...

Profile for al-hikma
Advertisement