Visa vya Wachamungu

Page 34

Visa vya wachamungu final Lubumba.qxd

5/15/2010

8:54 AM

Page 28

Visa vya wachamungu Alikwenda moja kwa moja hadi katikati mwa jiji (Msikitini) na akasema kwa sauti mbele ya umati wa Makureshi. “Nashuhudia kuwa hapana mola ila Allah na Muhammad ni mja na Mtume Wake. ” Waliposikia mwito huo kutoka kwa mtu wasiyemjua, watu wa Makka walimkimbilia upesi na kama Abbas bin Abdul Muttalib asingekuja kumuokoa wangemkatakata vipande vipande. Abbas alisema: “Huyu bwana ni wa kabila la Ghifar, na misafara ya biashara ya maquraishi kati ya Makka na Syria hupitia kwenye ardhi yao. Hamfikirii kwamba mkimuua mmoja wa watu wao hamtakubaliwa kamwe kupita kwenye nchi yao kwa amani? Abu Dhar aliokolewa kutoka mikononi mwao. Hata hivyo hakuridhika. Alisema, “Kwa mara nyingine nitarudia mwito huu wacha hawa watu wasikie kile ambacho hawataki kukisikia kabisa. Kama wakikisikia mara kwa mara watakizoea.” Kesho yake alirudia maneno yale yale tena. Wale watu wakamshambulia na Abbas ambaye alikuwepo hapo akamuokoa kutokana na ukatili wao. Baada ya hapo kulingana na amri ya Mtume (s.a.w.w), alirudi nyumbani na akaanza kulingania Uislamu miongoni mwa kabila lake. Wakati Mtume (s.a.w.w) aliguria Madina, Abu Dhar naye alikwenda na kubaki huko Madina hadi mwisho wa maisha yake. Alikuwa mkweli na mwenye msimamo na kutokana na sifa za uadilifu wake alifukuzwa na kuhamishwa wakati wa khalifa Uthman, mwanzoni kwenda Syria na baadaye mahali palipoitwa Rabdha karibu na Madina. Huko alifariki kifo cha upweke. Mtume (s.a.w.w) alikuwa amesema kuhusu yeye: “Mwenyezi Mungu amrehemu Abu Dhar! ataishi peke yake atakufa peke yake, na Siku ya Kiyama atafufuliwa peke yake.

28


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.