Suala la madhehebu lilianza kuzungumzwa na Mtukufu Mtume SAW
mwenyewe katika hadithi zake tukufu: “Mayahudi walikuwa madhehebu
sabini na tatu baada ya Nabii Musa AS, na Wakristo madhehebu sabini na
mbili baada ya Nabii Isa AS, na Umma wangu huu utakuwa na madhehebu
sabini na moja baada yangu, na (madhehebu) zote (zitaingia) Motoni
isipokuwa moja.” Kutokana na kauli hii ya Mtume SAW ni kwamba suala
la madhehebu haliwezi kuepukika, lazima madhehebu zitakuwepo bali
changamoto moja tu iliyoko katika kauli hii ni kwamba madhehebu zote
hizo zitaingia Motoni isipokuwa moja. Suala hapa sasa ni kufanya utafiti
ili kujua ni madhehebu ipi hiyo itakayokuwa salama.